You are on page 1of 21

TUME YA USHINDANI NA SHERIA KATIKA

KUMLINDA MLAJI

MAADHIMISHO YA SIKU YA HAKI ZA MLAJI DUNIANI

SHERIA YA KUMLINDA MLAJI

OFISA WA KUMLINDA MLAJI

MACHI, 2020

KIGOMA
1
TUME YA USHINDANI
HISTORIA YA HAKI ZA MLAJI
• Tarehe 15, Machi 1962
• Raisi wa Marekani katika kikao cha Bunge
aliasisi haki nne za walaji kutokana na
hotuba yake juu ya utetezi wa watumiaji
wa bidhaa na huduma.
• John F. K – Aliasisi Haki (4) za awali za Mlaji
Haki ya Usalama, Haki ya Kuchagua, Haki ya kupata
Taarifa,Haki ya Kusikilizwa
2
TUME YA USHINDANI
HISTORIA YA SHERIA ZA KUMLINDA
MLAJI TANZANIA

Serikali ilipendekeza na Bunge likakubali


kuwa Sheria zote nne za udhibiti wa
mashirika ya huduma na miundombinu na
ile ya ushindani pia ziweke utaratibu wa
utetezi wa mlaji.
Hivyo wakati serikali ilipokuwa ikianzisha
Mamlaka za Udhibiti na Ushindani, iliamua
pia kuunda mabaraza ya Ushauri kwa mlaji
katika kila moja ya mamlaka hizo.
3
TUME YA USHINDANI
HISTORIA YA SHERIA ZA KUMLINDA
MLAJI TANZANIA
Kwa Sheria ya Ushindani, Sheria iliunda
Baraza a Taifa la Kusimamia Uwakilishi na
Maslahi ya Mlaji Kisera na Kisheria (National
Consumer Advocacy Council-NCAC).
Chombo hiki kilipewa mamlaka kisheria
kuunda Kamati za Mikoa na kushauriana
nazo na kumuwakilisha Mlaji katika vikao na
mipango ya Sera na mikakati yenye maslahi
kwa mlaji.
4
TUME YA USHINDANI
Sheria mbalimbali
zinazomtetea Mlaji Tanzania
(i) Katiba ya Jamhuri ya Muungano
Tanzania:
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
1977 (Ibara ya 11, 14 na 18), pamoja na sheria
mbalimbali ambazo zimeundwa kwa mujibu wa
Katiba hiyo zinatambua haki na wajibu wa
mlaji. Kimsingi Katiba imejikita zaidi katika
kuelezea haki za raia, ambaye pia ni mlaji, za
kupata mahitaji muhimu ya kibinadamu.
5
TUME YA USHINDANI
Sheria mbalimbali
zinazomtetea mlaji Tanzania
(ii) Sheria Nyingine:
Baadhi ya sheria zinazomlinda mlaji wa
nchini Tanzania ni pamoja na Sheria ya
Ushindani ya mwaka 2003, Sheria ya Alama
ya Bidhaa ya mwaka 1963, Sheria ya
Viwango ya mwaka 1975, Sheria ya
Chakula, Dawa na Vipodozi ya mwaka 2003
na Sheria ya Vipimo ya mwaka 2002.

6
TUME YA USHINDANI
Utetezi wa Mlaji kwa Mujibu wa
Sheria ya Ushindani ya mwaka 2003
Kati ya sheria zote zilizotajwa hapo juu, Sheria
ya Ushindani ya mwaka 2003 ndiyo sheria kuu
inayohusika na masuala ya kumlinda
mlaji/mtumiaji nchini.
Katika nchi nyingine, masuala ya ushindani na
masuala ya kumlinda mlaji husimamiwa na
sheria tofauti. Lakini hapa Tanzania masuala
ya ushindani ya kumlinda mlaji yapo kwenye
sheria moja.
7
TUME YA USHINDANI
Utetezi wa Mlaji kwa Mujibu wa
Sheria ya Ushindani ya mwaka 2003
Hata hivyo, nchi nyingi zina mfumo
unaojumuisha katika taasisi moja masuala ya
kumlinda mlaji na yale ya ushindani.
Nchi hizo ni pamoja na Marekani, Australia,
Zambia, Nigeria, Tanzania, Afghanistan,
Azerbaijan, Brunei Darussalam, Denmark,
Finland, France, Ireland, Italy, Netherlands,
Poland, South Korea, Gambia, Guyana,
Malawi, Malta na Mongolia.
8
TUME YA USHINDANI
Utetezi wa Mlaji kwa Mujibu wa
Sheria ya Ushindani ya mwaka 2003
Nchi nyingine ni pamoja na Panama, Papua
New Guinea, Seychelles, Singapore, Zanzibar
na Zimbabwe.

Pia kuna Jumuiya za Kikanda kama vile


COMESA, Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),
Jumuiya ya Ulaya (EU), nk, ambazo pia
zinashughulikia kwa pamoja masuala ya
ushindani na kumlinda mlaji.
9
TUME YA USHINDANI
Haki za Mlaji
Mlaji ana haki zinazolindwa kwa mujibu wa
Sheria za Kitaifa na Kimataifa.

Kimataifa: Msingi wa Haki za Mlaji ni


Mwongozo wa Umoja wa Mataifa wa Kumlinda
Mlaji (UNGCP)-Toleo la Dec 22, 2015.

10
TUME YA USHINDANI
Haki za Mlaji
1. Haki ya mahitaji muhimu
2. Haki ya usalama
3. Haki ya kupatiwa taarifa
4. Haki ya kuchagua
5. Haki ya kusikilizwa
6. Haki ya kutatuliwa malalamiko
7. Haki ya mazingira bora na endelevu
8. Haki ya kupatiwa elimu

11
TUME YA USHINDANI
Wajibu wa Mlaji
• Kuhakiki bidhaa na huduma kwa kuuliza maswali ili
kujua ubora na usalama wake kabla ya kununua;
• Kutafuta taarifa sahihi kuhusu bidhaa (kuifahamu)
kabla ya kufanya maamuzi ya kuinunua;
• Kufanya manunuzi kwa busara kwa kuzingatia
mahitaji na matakwa;
• Kudai na kupatiwa risiti sahihi kwa kila manunuzi ili
kuweka kumbukumbu ya manunuzi;
• Kuanzisha lalamiko usiporidhishwa na bidhaa au
huduma;
• Kutunza mazingira.

12
TUME YA USHINDANI
Maeneo yanayohusu utetezi wa mlaji katika
Sheria ya Ushindani yameainishwa katika
vifungu mbalimbali kama ifuatavyo:
KIFUNGU MAELEZO
15 - 21 Udanganyifu na upotoshaji katika mwenendo wa
biashara, bidhaa au huduma katika bei au mauzo.
22 - 24 Biashara ambayo si ya haki: Matangazo ya kuvutia
bila kukusudia kuuza kama tangazo linavyodai.
25 Tabia ya uonezi, hila au ujanja dhidi ya mtu
ambaye ama hajui au hana upeo unaotarajiwa
katika suala la biashara.
26 - 36 Mikataba ya mlaji na ubora wa bidhaa na huduma;
fidia ya hasara ya kuvunja mkataba wa mlaji
37- 47 Wajibu wa mzalishaji kwa bidhaa ambazo
zinagundulika baadaye kuwa hazifai.

13
TUME YA USHINDANI
Vipengele vya Kumlinda Mlaji
KIFUNGU MAELEZO
48 - 52 Utaratibu kuhusu usalama wa bidhaa na taarifa
muhimu zinazopaswa kuoneshwa kwenye bidhaa.

53 Utaratibu wa kuondosha bidhaa katika soko kwa


hiari au kwa mujibu wa sheria .

92 - 95 Uanzishwaji wa Baraza la Ushauri kwa Mlaji, kazi


zake, uendeshaji wake na masuala ya kifedha.

14
TUME YA USHINDANI
UTEKELEZAJI WA SHERIA KATIKA
KUMLINDA MLAJI
Maamuzi ya kesi na malalamiko ya mlaji
(sehemu ya tano na baadhi ya vipengele vya
sehemu ya sita ya FCA) hayafanywi na Tume
ya Ushindani, bali Mahakama za kawaida.

Kwa mashauri ya aina hii, Tume


huyashughlikia kwa kuchukua hatua za awali
za upatanishi na kutoa ushauri wa namna ya
kutetea haki za mlaji kwa mujibu wa sheria.
15
TUME YA USHINDANI
UTEKELEZAJI WA SHERIA KATIKA KUMLINDA
MLAJI
 Elimu kwa wadau mbalimbali tangu 2007

Kuanzisha vilabu vya kumlinda mlaji katika shule za


msingi Dodoma na Morogoro, 2017 & 2018

Elimu kupitia maonesho mbalimbali tangu 2007

Uhamasishaji kupitia Siku ya Mlaji Duniani tangu 2009

 Utatuzi wa migogoro baina ya wafanyabiashara na


walaji

 Usajili wa mikataba ya walaji


16
TUME YA USHINDANI
Muono Mbele
• Katika mabadiliko ya sheria ya ushindani ya 2003,
inapendekezwa kwa baadhi ya malalamiko ya
walaji ambayo yako katika sehemu ya IV,V,VI na
VII ambayo yanaelekezwa mahakamani, kuipa
nguvu Tume ya kusikiliza na kutatatua kwa njia ya
usuluhishi.
• Kurekebisha Kanuni za Kudhibiti Mikataba ya Mlaji
(2014) ili kuingiza vipengele vya kulinda haki za
mlaji katika biashara mtandao na taarifa za
faragha za mlaji, pamoja na mambo mengine

17
TUME YA USHINDANI
Inaendelea…
• Iwapo mabadiliko tajwa hapo juu yataridhiwa
na vyombo husika, yataleta faida zifuatazo;
– urahisi wa kufikiwa na walaji wa kipato cha
chini.
– Malalamiko ya walaji kutatuliwa kwa muda mfupi
kwa utaratibu mbadala wa utatuzi wa migogoro
(ADR).
– Kupunguza gharama kwa mlaji za kupeleka
shauri mahakamani.

18
TUME YA USHINDANI
Inaendelea…
– Walaji wasio na taaluma ya sheria watapata
fursa ya kuwasilisha malalamiko yao.
– Itapunguza bidhaaa hafifu au zisizokuwa na
kiwango sokoni.

19
TUME YA USHINDANI
HITIMISHO
Tume ya Ushindani imejizatiti katika kutetea na
kusimamia haki za mlaji kwa njia na mikakati
mbalimbali.
Elimu ya mlaji mashuleni, elimu kupitia vyombo
vya habari vya umma, maonesho, semina,
warsha na makongamano ya wawakilishi wa
vyombo vya walaji na wafanyabaishara, ni
baadhi ya mikakati inayotumiwa na Tume ili
kuongeza mwamko wa walaji katika kuchukua
hatua za kutetea haki zao, na wafanyabaishara
kuzizingatia wawapo sokoni.
20
TUME YA USHINDANI
MWISHO

ASANTENI KWA
KUNISIKILIZA!

21
TUME YA USHINDANI

You might also like