You are on page 1of 5

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

TAMKO KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU


NCHINI, PAMOJA NA MLIPUKO WA UGONJWA WILAYANI CHEMBA NA
KONDOA, MKOANI DODOMA, LILILOTOLEWA NA MHE. UMMY MWALIMU
(MB); WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO,
TAREHE 04 JULAI, 2016

Ndugu wanahabari,
Serikali kupitia Wizara yangu imeweka na utaratibu wa kutoa taarifa ya
mwenendo wa magonjwa ya mlipuko yanayoikumba nchi yetu kwa
wakati

husika

ili

kutoa

elimu

na

kuifahamisha

jamiii

hatua

zinazochukuliwa na Wizara kudhibiti magonjwa hayo.


Ugonjwa wa kipindupindu ulioanza tangu Agusti 2015, bado upo nchini na
hadi kufikia tarehe 03 Julai 2016, jumla ya wagonjwa 22,216 wametolewa
taarifa. Kati yao ndugu zetu 345 wamepoteza maisha.
Takwimu za wiki iliyopita kuanzia tarehe 27 Juni hadi 03 Julai 2016
zinaonesha kuwa, kasi ya ugonjwa wa kipindupindu imepungua sana
ambapo idadi ya wagonjwa wapya walioripotiwa wiki hiyo ni 31, na
pametokea kifo 1,

ikilinganishwa na wagonjwa 365 bila kifo walioripotiwa

wiki iliyotangulia ya Juni 20 hadi 26, 2016. Mkoa ambao bado umeendelea
1

kuripoti ugonjwa wa kipindupindu ni mmoja tu nao ni Morogoro katika


Halmashauri ya Kilosa (23) na Morogoro Vijijini (8). Aidha, katika wiki hii
kumeripiotiwa kifo cha mtu mmoja kilichotokana na ugonjwa wa
kipindupindu kutoka Halmashauri ya Kilosa.
Ndugu wanahabari
Pamoja na changamoto za utoaji taarifa sahihi

na utunzaji wa

kumbukumbu za taarifa za wagonjwa wa Kipindupindu kupitia mfumo wa


ufuatiliaji wa magonjwa ya milipuko, tafsiri kubwa tunayoipata kutoka
kwenye takwimu hizi ni kwamba kwa sasa ni dhahiri kuwa mlipuko huu wa
ugonjwa wa kipindupindu uliodumu kwa miezi 10 unakaribia kuisha, ila
kuna haja ya jitihada za ziada katika mkoa wa Morogoro ili kuutokomeza
ugonjwa huu katika nchi nzima.
Pamoja na muelekeo huo, ninatoa rai kwa viongozi wa ngazi za vituo vya
kutolea huduma za afya, wilaya na mikoa kuendelea kutoa taarifa sahihi
na kwa wakati za wagonjwa wa Kipindupindu ili kufanikisha juhudi za
kupambana na mlipuko huu hapa nchini. Aidha katika hali ya sasa ya kuwa
na

wagonjwa

wachache,

natoa

agizo

kwamba

wagonjwa

wote

wanaohisiwa kuwa na ugonjwa huu wa kipindupindu wathibitishwe kwa


vipimo vya maabara na kupatiwa matibabu. Aidha napenda kusisitiza
kwamba hatua za Kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakaebainika
kutotoa taarifa sahihi za wagonjwa wa Kipindupindu na magonjwa
mengine ya mlipuko.
Vile vile nasisitiza kwamba ni budi Mikoa yote kuendelea kuchukua hatua
za tahadhari ili kuzuia maambukizi, na pia kuendelea kutoa taarifa sahihi
2

kila siku na kusimamia kikamilifu hatua mbalimbali za udhibiti wa mlipuko


huu.
Ndugu wanahabari,
Tunaendelea kuisihi jamii kuungana na Halmashauri, Mikoa pamoja na
Wizara katika juhudi za kupambana na kuenea kwa ugonjwa wa
kipindupindu kwa kuzingatia yafuatayo:
Utoaji na upatikanaji wa takwimu sahihi za ugonjwa kwa kuzingatia
miongozo iliyotolewa na Wizara bila kuingiliwa na viongozi wa kisiasa
au kiserikali.
Kujenga na kutumia vyoo bora katika maeneo yote ya mjini na vijijini ili
kupunguza hatari ya kuenea kwa ukongwa huu.
Kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kupitia Mamlaka za
maji zilizopo katika ngazi zote.
Kuhakikisha utunzaji salama wa maji ya kunywa yaliyotibiwa.
Kuwahi kupata matibabu mapema katika vituo vya kutolea huduma.
Kuhakikisha upatikanaji na matumizi sahihi ya ORS katika maeneo
mbali mbali nchini ili kupunguza athari za ugonjwa.
Ndugu wanahabari,
Wizara yangu pia inaendelea kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu ugonjwa
usiofahamika, ulioripotiwa mnamo tarehe 13 Juni 2016, katika Wilaya ya
Chemba mkoani Dodoma.
Hadi kufikia tarehe 03 Julai 2016, kulikuwa na jumla ya wagonjwa 43, na
watu 11 wamekwishapoteza maisha kutokana na ugonjwa huu. Mikoa ya
3

Dodoma na Manyara ndiyo iliyoripoti wagonjwa kutoka katika Halmashauri


za Chemba (34), Kondoa (4), Dodoma Manispaa (1), Chamwino (1) na
Kiteto (3). Vifo 10 viliripotiwa na Halmashauri ya Chemba, na kifo kimoja
na Halmashauri ya Kiteto.
Kama tulivyowataarifu siku chache zilizopita, uchunguzi wa awali wa
kimaabara wa baadhi ya vyakula walivyotumia wagonjwa ulibaini kuwa
vyakula hivo vilikuwa na sumu kuvu (Aflatoxins). Aidha Timu yetu ya
wataalamu kutoka sekta mbalimbali imekuwa mkoani Dodoma na Manyara
kwa uchunguzi wa Kiepidemiolojia. Vile vile sampuli za damu kwa
uchunguzi zaidi zimekwisha pelekwa nchini Marekani katika Kituo cha
Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Centres for Disease Control and
Prevention - CDC). Pindi tutakapopata matokeo ya

sampuli hizo za

wagonjwa pamoja na ripoti ya uchunguzi unaoendelea kufanywa na


wataalumu wetu tutawajulisha matokeo hayo. Kufuatia mlipuko wa
ugonjwa huu, napenda kusisitiza mambo yafuatayo:
a) Tunaendelea kushirikiana na mamlaka husika za kitaifa, kimkoa na
kiwilaya ili kuhakikisha kuwa nafaka ambazo zina sumukuvu kwa
kiasi kisichokubalika hazitumiwi kwa chakula;
b) Tunaendelea kutoa Elimu kwa wananchi juu ya njia sahihi za
uandaaji wa chakula utakaosaidia kupunguza kiasi cha sumukuvu
(aflatoxin) kwa nafaka ambazo hazijaharibika sana. Njia hizi ni
pamoja na kuchambua nafaka zilizoharibika (zilizooza, kuvunjika,
zilizobadilika rangi), kukoboa mahindi kabla ya kusaga au kuacha
kutumia nafaka zitakazoonekana kuharibika sana.
4

c) Serikali itaendelea kuimarisha mikakati ya kitaifa ya kupunguza


uchafuzi wa sumukuvu katika vyakula, ikiwa ni pamoja na kujenga
uwezo wa kupima sumukuvu katika damu na mkojo miongoni mwa
taasisi za ndani ya nchi.

d) Tunaendelea kutoa matibabu kwa wanachi walioathirika na Ugonjwa


huu, kwenye Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na Hospitali ya Wilaya
ya Kondoa.
e)

Tunaendelea kushirikiana na wataalamu wa sekta mbalimbali,


Mashirika ya Kimataifa, Mikoa na Halmashauri katika kudhibiti
ugonjwa huu.

Hitimisho
Wizara inaendelea kuwapongeza na kuwashukuru wadau wote kwa
jitihada za dhati zinazoendelea kutekelezwa katika kusimamia kikamilifu
miongozo inayotolewa na Wizara ili kutokomeza magonjwa ya milipuko,
ikiwa ni pamoja na wataalamu wa sekta mbalimbali, Mashirika ya
Kimataifa, Watumishi, Mikoa na Halmashauri pamoja na waandishi wa
habari na wananchi kwa ujumla.
Asanteni kwa kunisikiliza

You might also like