You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA MAKAMU WA RAIS


Anwani ya simu: MAKAMU,
Simu Na. +255 2116919
Fax Na. +255 2116990

Barabara ya Luthuli,
P.O Box 5380,
Dar es Salaam.

Barua Pepe: km@vpo.go.tz

TANZANIA.
28/4/2016

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Serikali ya Urusi imeahidi kuongeza fursa za masomo ya elimu ya juu kwa
wanafunzi wanaotoka Tanzania.
Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Urusi, Denis
Manturov wakati alipokutana na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, leo
Ikulu, ambapo alimkabidhi ujumbe wa Rais John Magufuli kutoka kwa Rais
Vladmir Putin wa Urusi.
Alisema serikali yake kwa mwaka jana ilitoa nafasi kumi kwa wanafunzi
wanaotoka Tanzania kujiunga na vyuo vya elimu ya juu nchini Urusi na
kwamba wameahidi kuongeza idadi ya wanafunzi watakaofaidika na masomo
Urusi.
Manturov alitumia fursa hiyo kumweleza Makamu wa Rais kuwa Warusi wako
tayari kuwekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali zikiwemo za kilimo,
viwanda, utalii, nishati, mafuta na gesi.
Katika mazungumzo hayo, Makamu wa Rais alimweleza Waziri huyo kwamba
Tanzania ina fursa nyingi za uwekezaji na kusema upande wa mafuta na gesi
serikali itaangalia maeneo muafaka kwa Urusi kujenga viwanda.
Akizungumzia mapendekezo ya kuanzishwa kwa Tume ya Pamoja ya
Ushirikiano kati ya Tanzania na Urusi Samia alimwakikishia Waziri huyo
kwamba Mkataba wa Makubaliano waliouleta unapitiwa na Wizara ya Mambo
ya Nje kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kisheria katika ushirikiano huo.
Alisema Tume hiyo ni muhimu katika kudumisha na kuimarisha mahusiano ya
muda mrefu ya kiuchumi na kijamii kati ya nchi hizo mbili.
Katika suala la utamaduni Makamu wa Rais alishauri mafunzo ya lugha za
kiswahili na Kirusi yatolewe kwa pande zote mbili ili hatimaye yarahisishe
sekta ya utalii.
Imetolewa na

Ofisi ya Makamu wa Rais


Dar es salaam
28/4/2016

You might also like