You are on page 1of 2

BARAZA LA KIROHO LA MAHALI LA WA-BAHAI WA

DAR-ES-SALAAM
S. L. P. 585, Dar-es-Salaam, baruapepe: royqudsi@gmail.com

Wa-Bahai Duniani kote Washerehekea Naw-Rz (Mwaka Mpya)

Naw-Ruz (Mwaka Mpya) katika Imani ya Bahai ni mojawapo ya


siku tisa zinazosherehekewa na Wa-Bahai duniani kote. Naw-Rz
huashiria ujio wa musimu wa mchipuo katika mzingo wa Kaskazini.

Naw-Rz ni siku ya kwanza ya kalenda ya Ki-Bahai ambayo pia ni


maarufu kama Badi (nzuri ajabu) kalenda. Katika siku hii, Wa-
Bahai hawaendi kazini wala shuleni. Mtukufu Bb, Mtangulizi wa
Bahaullah, Mtume Mwanzilishi wa Imani ya Bah, aliteua siku
hiyo kama siku takatifu na kuishirikisha na Jina Kuu Kabisa la
Mungu. Kalenda ya Ki-Bahai imethibitishwa na Baha'u'llah.

Kalenda ya Ki-Bahai ina jumla ya miezi 19 ambayo kila moja ina


siku 19 (jumla siku 361). Zaidi ya hapo zipo Siku za Kati (4 katika
mwaka wa kawaida na 5 katika mwaka mrefu) kati ya mwezi wa 18
na 19 kwa ajili ya kuurekebisha mwaka kufuata kalenda ya mwaka wa
jua. Mnamo mwezi wa mwisho wa Ki-Bahai, Wa-Bahai hufunga na
hawali chakula wala kunywa chochote kutoka alfajiri hadi jioni, na
pia husali, hutafakari na kujitahidi kurekebisha tabia zao, kutakasa
mioyo yao na kufikia kiwango cha juu zaidi cha kujitenga na vitu vya
duniani. Sherehe ya Naw-Rz hufika mwisho wa mwezi wa kufunga
wenye siku 19.

Bahaullah amekuja kuleta umoja, kuunganisha jamii nzima ya


wanadamu katika Hoja moja, Imani moja ya ulimwengu, kutokomeza
kila aina ya ubaguzi na kuleta utambuzi kuwa sisi sote ni ndugu. Kwa
uhakika, Bahaullah anatuambia, Mwangaza wa Umoja una Uwezo
mkubwa sana kana kwamba unaweza kuangaza dunia nzima.
Yeye anatuambia kwamba sisi sote ni kama matunda ya mti mmoja,
majani ya tawi moja, mawimbi ya bahari kuu moja, maua ya bustani
moja maridhawa ya jamii ya wanadamu.
Mnamo Naw-Ruz, Wa-Bahai hukusanyika kwa furaha kubwa kabisa
kwa sababu huu siyo tu mwanzo wa Mwaka Mpya, bali ilivyoelezwa
na Abdul-Bah, mwanae Bahullh na Kiolezo Kamilifu wa Imani
ya Bahai, Sasa ndio mwanzo wa duru la Uhalisi, Duru Jipya,
Zama Mpya, Karne Mpya, Wakati Mpya na Mwaka Mpya. Kwa hiyo
umebarikiwa sana.

Katika zaidi ya maeneo 120,000 ambamo zaidi ya Wa-Bahai milioni


6 huishi ulimwenguni kote, sherehe za kuadhimisha Mwaka Mpya wa
Ki-Baha'i zinachukua maumbile tofauti.

Jamii Bahai ya Dar es Salaam itasherehekea Naw-Rz siku ya


Jumapili, tarehe 19 Machi, 2017 saa 12:30 jioni katika Bahai Senta,
iliyopo katika Mtaa wa Mfaume, Upanga Magharibi. Kila mmoja
anakaribishwa kwa moyo mkunjufu katika sherehe hii yenye furaha
na nderemo. Ratiba itakuwa na sehemu ya maombi ambamo sala na
dua za Ki-Bahai zitasomwa na kuimbwa katika lugha mbalimbali,
kinafuata ni kujuana hali na kuburudika pamoja. Karibuni tena.

Bi. Qudsiyeh Roy


Afisa Matangazo
Baraza la Kiroho la Wa-Bahai wa Dar es Salaam
Simu: 0784-381565; 0659-604744

You might also like