You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA MAKAMU WA RAIS


Anwani ya simu: MAKAMU,
Simu Na. +255 2116919
Fax Na. +255 2116990

Barabara ya Luthuli,
P.O Box 5380,
Dar es Salaam.

Barua Pepe: km@vpo.go.tz

TANZANIA.
17/4/2016

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali haina nia ya


kumwonea mtu inapochukua hatua ya kutumbua majipu kwa watumishi wa
umma.
Samia ameyasema hayo jana Jumamosi baada ya kupokea taarifa ya mkoa
wa Morogoro iliyosomwa na Mkuu wa mkoa huo Dk. Steven Kebwe akiwa
katika ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani humo.
Alisema lengo la kutumbua majipu ni kurekebisha na kurejesha nidhamu,
uadilifu na uwajibajikaji serikalini kama ilivyoangizwa katika Ilani ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM) ili Watanzania wote wafaidike na matunda ya nchi yao.
"Mtasikia katika serikali tunarekebisha, majipu yanatumbuliwa... kwa kweli
hatuna nia ya kumwonea mtu, tunarekebisha kama ilivyoagizwa katika Ilani
yetu ya Chama Cha Mapinduzi ili Watanzania wote wafaidi matunda ya nchi
yao," alisema.
Makamu wa Rais alisema katika marekebisho hayo serikali imechukua hatua
ya kukata mishahara ya walio juu na kunyanyua ya walio chini sana waje juu
kidogo na kwamba jitihada zote hizo ni katika kufanya mambo yaende vizuri
nchini.
"Tunapozungumzia amani na utulivu ni pamoja na kuhakikisha kwamba walio
chini wapo vizuri, wasipokuwa vizuri hakuna amani na utulivu, kazi itawapata
watu wa kamati ya ulinzi na usalama, kuwatuliza kila siku na hawatatulizika
kwa sababu wana shida." alisema Makamu wa Rais na kuongeza

"lakini tukiwatuliza kwenye mambo yao wana maji, wana umeme, wana
chakula, mtoto anaenda shule vizuri, anapata afya, akienda zahanati dawa
zipo, watatulia tu."
Alisema kwa hivi sasa kuna tatizo la watumishi hewa na wengine wamediriki
kumdanganya mkuu wao wa kazi na hayo ndiyo mambo ambayo hayaleti
picha nzuri katika serikali.
Aliwataka wakuu wa mikoa na wilaya nchini kuunga mkono jitihada hizo za
serikali ili kurejesha nidhamu na uwajibaikaji kwa watumishi wote.
Wakati huo huo, Makamu wa Rais jana alitembelea kiwanda cha kutengeneza
nguo cha Mazava ambapo aliutaka uongozi wa kiwanda hicho kuzingatia
masharti ya ajira na wafanyakazi kuchapa kazi kwa bidii ili Taifa liweze
kupata kodi na wao wapate mapato.
Akizungumza na wafanyakazi, Samia aliuhakikishia uongozi wa kiwanda
hicho kuwa serikali itazifanyia kazi changamoto za eneo na ukosefu wa ujuzi
kwa kuwapeleka vijana wengi kwenye Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) kujifunza
ushonaji.
Alisema Serikali ya Awamu ya Tano imeweka mkazo kwenye viwanda na
kusisitiza kwamba kupitia mpango wa EPZ viwanda vingine vinatarajiwa
kujengwa mkoani humo jambo ambalo litaongeza ajira kwa vijana.
Kiwanda hicho ambacho kilianza uzalishaji mwaka 2010 kina wafanyakazi
zaidi ya 2,000 na kwamba asilimia 100 ya nguo zinazozalishwa kiwandani
hapo zinauzwa nje ya nchi ambapo soko kuu liko Marekani.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Morogoro
17/4/2016

You might also like