You are on page 1of 7

SHINA LA UKOO NA URITHI.

Imeandaliwa na mr.luhwago shadrack c mwanafunzi wa sayansi ya chakula na


teknolojia SUA (2013-2016)
Mawasiliano: 0764444277, luhwagoshadrack17@gmail.com
UTANGULIZI.
Somo hili ni pana na lina mafundisho jinsi ya kutambua jinsi dhambi mbali mbali
zinavyoweza kutoka kizazi kimoja kwenda kizazi kingine , Bila ya kizazi chenyewe
kutambua
MAANA YA SHINA LA UKOO URITHI
Katika kichwa hiki cha somo tunatakiwa tujue maana ya maswali yafuatayo
a/ nini maana ya shina
b/nini maana ya shina la ukoo
c/nini maana ya urithi
d/nani anarithishwa
e/ sifa za mwenye kurithishwa
A.MAANA YA SHINA
Shina lina maana ya
chanzo,
beginnner,
a source,
anzilishi
B.URITHI
ni hali ya kupokea sifa, tabia, umbo, namna, kutoka kwa wazazi wako au ndugu yako
its known as inheritance(utu wa ndani) genotypic characters

thus its automatically


urithi huu huambatana na Damu(watu wa Damu moja yaani ndugu)
katika maisha yetu kuna watu wawili(mtu wa ndani ambaye yupo rohoni na mtu
wa nje ambaye yupo katika ulimwengu wa mwili)
ndiyo maana utasikia mwili wa marehemu fulani..kwani yeye anakuwa yupo
wapi..?
MWANZO WAKO NI UPI NA UKOJE..?
Kila kitu na mwanzo wake, kusema kweli ni vigumu sana kuelewa mwanzo wako wa maisha
na wakati mwingine unakata tamaa ya kutokuendelea kufuatilia the orign of life.
Maisha yangu (luhwago shadrack c) kusema kweli nilipata shida sana namna ya kuweza
kupata habari na taarifa yakinifu juu ya kuzaliwa kwangu, juu ya ukoo wangu , kwa nini sisi
ni akina luhwago, je neno luhwago lina maana gani?, nani mwanzilishi wa jina hilo? Na
alikuwa anamaanisha nini juu ya jina hilo? Unajua nini. TAMANI KUJUA.
Siku moja katika huduma yangu ya kufundisha injili nilikutana na mtoto mmoja ambaye ni
mgonjwa tukamuombea lakini ilishindikana. nikamuuliza mama yake juu ya kuzaliwa kwa
mtoto wake akanambia kuwa kipindi amezaliwa mtoto wake aliugua sana karibu kufa ndipo
alipochukua hatua ya kwenda kwa miungu na kumlaza kwenye ngozi ya kondoo iliyochunwa
muda huohuo ndipo akapona tujiulize je alipona ? ..hapana maana kukua kwake
kuliandamana na kuugua.
Pia kuna dada mwingine katika ukuaji wake alishawahi kuugua kiasi cha kubadilika sura
yake akapelekwa kwa mganga wa kienyeji. Alipoolewa alipata uwezo wa kuzaa mtoto, cha
kushangaza mtoto Yule alikuwa hakui(mwaka mmoja bado alikuwa ana kilogram
4).kilichofanyika ni kumpeleka kwa yule mganga wa kienyeji na wakatamka maneno
yafuatayo na nukuu(tuliyemleta kipindi kile sasa anamtoto tunaomba na huyu mtoto
apokelewe pia).baada ya hapo anaendelea kukua hadi muda huu ninavyoandika
makala hii. Je huyu mtoto ataishije..?

B. KIZAZI CHA TERA.


Labda ili uelewe ngoja nikupitishe katika maandiko . tuangalie kizazi cha Tera
mwazo11:24. Na kuendelea..

Mwanzo 11:24 Tera anazaliwa na

anazaa (Abrahamu ,Nahori

na Harani) na

wengineo akiwemo sarai


Abraham akamuoa sarai(akawa tasa)
Rahani akamzaa milka
Nahori akamwoa milka akamzaa bethuel na wengineo
Sarai akamruhusu Abraham kuzaa na hagari kijakazi wake

akazaliwa Ishmael

Kipindi hagari ni mjamzito wakagombana na bibi yake sarai


Bethuel akamzaa Rebeka na Labani
Kwa imani sarai akapata ujauzito uzeeni akamzaa isaka
Isaka akamuoa Rebeka(akawa tasa)
Kwa kuomba na kumlilia Mungu rebeka akapata ujauzito akazaliwa Esau na
Yakobo
Esau akapoteza nafasi yake ya uzaliwa wa kwanza, yakobo akabarikiwa.
Labani akamzaa Lea na Rahel

Yakobo akamuoa Lea na Rahel (rahel akawa tasa na ni mrembo) na siyo Lea
Esau akaoa mkaanani akaleta uchungu ndani ya nafsi ya wazazi wake
(Mungu aliweka agano na Abraham kwamba wasije wakaoa wakaanani)
Lea akapewa uwezo wa kuzaa hata kama ana sura mbaya.(akamzaa Reuben, simeoni,
lawi na Yuda) kila aliyezaliwa isipokuwa Yuda , lea anasema ili Yakobo mumewe
ampende (yaani kamsahau Mungu) na Yuda ndipo aliposema nitamsifu Bwana
Rahel anaruhusu Yakobo azae na kijakazi wake Bilha ili apate uzao
Kwa kumlilia Mungu Rahel akapata mimba akamzaa Yusufu.
Lea naye anaruhusu kijakazi wake zilpa aanze kuzaa na mumewe yakobo
(wanashindana kuzaa sasa) , wivu, tamaa, upendo unakosekana ndani ya hizi
familia
Katika hili reubeni akalala na kijakazi wa aliyewahi kuzaa na baba yake yakobo
(yakobo akamlaani) akapoteza pia nafasi yake ya uzaliwa wa kwanza.
Yuda anazini na mkwewe tamari akijua ni kahaba wa mitaani na anazaliwa zera na
pelesi
(wanagombana tumboni)
Mkono wa Mungu unakuwa mzito juu ya Eri na onani kwa maana wametenda
maovu mbele za Bwana
LABDA NIKUACHE HAPA KWA YUDA , SASA TUANGALIE MAMBO
YALIYOMO NDANI YA KIZAZI HIKI:
A.

Utasa

B.

kuzaa na mjakazi (wajakazi) , uzinzi,

C.

kukosekana kwa upendo

D.

wivu na tama

E.

Uchungu

F.

Hasira

G.

Laana

SABABU ZA KUATHIRIWA KWA KIZAZI CHA TERA


Tera alikuwa mganga wa kienyeji (Joshua 24:2) 2 Yoshua akawaambia watu wote, Bwana,
Mungu wa Israeli, asema hivi, Baba zenu hapo zamani walikaa ng'ambo ya Mto, maana Tera,
baba yake Ibrahimu, naye ni baba yake Nahori; wakaitumikia miungu mingine.
3 Nami nikamtwaa Ibrahimu baba yenu toka ng'ambo ya Mto, nikamwongoza katika nchi
yote ya Kanaani; nikaongeza uzao wake, nikampa Isaka.
4 Kisha nikampa huyo Isaka, Yakobo na Esau; nami nikampa Esau mlima Seiri aumiliki;
Yakobo na watoto wake wakashuka Misri.
5 Kisha nikawatuma Musa na Haruni nikaipiga nchi ya Misri, kwa hayo yote niliyoyatenda
kati yake; hatimaye nikawatoa ninyi.
hivyo kizazi chote cha Tera kilichofuata kilipata kuathiriawa na vitu vifuatavyo, Utasa ,
kuzaa na mjakazi (wajakazi), kukosekana kwa upendo(29:30-31), wivu na tamaa(30:1),
uchungu(26:34-35) , hasira(27:41) , Laana(49:3-4) na uzizi.
Kwa wewe unayesoma makala hii hakuna dhambi yenye madhara na machukizo makubwa
kwa Bwana kama kuabudu miungu mingine. Tazama haya.,
YEREMIA 17:5-6
5 Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye
mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana.
6 Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani
palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu
AYUBU (3:1)
Ayubu anailaani siku ya kuzaliwa kwake kwa sababu ya taabu aliposema Siku ya kuzaliwa
kwangu na ipotelee mbali, nao usiku ule iliposemekana, Mtoto wa kiume amezaliwa!
ZABURI 16:4)
Mtu asipo okoka au anaye abudu miungu mingine ugumu wa maisha utaongezeka au mabaya
yataongzeka
MITHALI 4:18
Mungu ansema usikubali kurithi upumbavu( maovu) Mjinga hurithi upumbavu

MAMBO YA WALAWI 18:13


inasema usifunue umbu la mama yako hili linawalenga wanaozini na dada zao au wale
ambao hawajaoa na kufanya uasherati katika umri wao wa ujana au wazee wanaozini na
ndugu zao
EZEKIELI 16:44
Katika maisha unatakiwa kuvunja madhabahu za urithi zinazo risishwa kupitia maziwa ya
mama kama inavyozungumziwa katika hapa .inavyosema tabia ya mama itarithiwa na
mtoto wake
ZABURI 51:5
5 Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani.
YEREMIA 6:16
16 Bwana asema hivi, Simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize habari za mapito ya
zamani, I wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi
zenu. Lakini walisema, Hatutaki kwenda katika njia hiyo.
MAOMBOLEZO 5:7
7 Baba zetu walitenda dhambi hata hawako; Na sisi tumeyachukua maovu yao
Sasa utakuwa umeanza kuelewa ninachozungumza, Mungu akupe macho ya rohoni sana ili
uweze kuelewa maada hii: kwa muda huu tafuta majibu ya masuali haya; familia yako ina
ugomvi?, ina magonjwa yanayosumbua? Au wewe mwenyewe unasumbuliwa gonjwa
ambalo huponi?, kichwa au tumbo lako linakusumbua?, kuna tatizo la kuolewa au kuoa
katika familia yako?, katika familia yako kuna shida katika elimu?, familia yenu kuna roho ya
uzizi?, wivu?, ukahaba?, uchoyo?, tama?, vifo?, uchungu ndani ya nafsi yako?,ulishanenewa
maneno ya laana?, mabaya?, ya kutokufanikiwa?, je jina lako lina maana gani?, lilitoka wapi
na nani alikutajia?,hali ya imani ikoje katika familia yako?, wanamwabudu Mungu yupi?,
wanapopata matatizo wanakwenda wapi?, chukua hatua, ya kuokoka, kutafuta toba ya kweli
lasivyo maisha yako yatakuwa ya tabu.(soma kumb 28. yote namna laana na Baraka juu ya
maisha yako).

MAMBO YA KUFANYA KUEPUKA ROHO ZA URITHI.


kuepukana na laana zote hizo hapo juu ambazo hadi leo hii zinaendelea na hasa katika familia
na koo zetu ambazo tumezaliwa
Kwanza kabisa peleleza mambo ya zamani (Yeremia 6:16)
Nenda mbele za Mungu kwa Toba ( Matendo 3:17)
Kwa hiyo yafuatayo ni mambo unaweza kuyafanya ili kujiokoa na urithi wa mambo yaliyo
orodheshwa hapo juu.
KWANZA KABISA NI KUMPOKEA YESU KUWA BWANA NA
MWOKOZI WA MAISHA YAKO.

kufunga na kuomba (I Nyakati 7:14)

kutoa sadaka

ibada na kusali(misa

You might also like