You are on page 1of 17

DARUBINI YA IMANI

Harakati za Utume kwa Ndugu wa Kiislam

Na. Mchungaji Dominic Mapima

Apologetics materials prepared by Adventist Muslim Relation office of Eastern Tanzania


Conference Writtern by Pr. Dominic Mapima Director
Mobile: 0754-527143

“Gundua Ukweli”

Hivi Yesu ninani kwa mujibu wa Qur-an na


Biblia!Kweli ni Mungu “ Mtume” au alikuwa
mtu wakawaida tu!
Utangulizi

Amani ya Mwenyezi Mungu iwe pamoja nawe ndugu msomaji wangu mpendwa wa
nakala hiii ya “Tarumbeta ya vitabu”.

Ninazo shukrani za pekee kwa Mola Mtukufu kwaajili ya upendeleo wake wa pekee wa
kutupatia uhai sote mimi pamoja nawe msomaji wa makala hii, katika hayo ninapenda
kukili kuwa hakuna yaliyo makubwa tulioyafanya mbele zake ila ni kwa Qudra na
rehma zake tu twajipatia uzima.

Kwaajili ya hilo ninapenda kuchukua fursa hii kukualika katika familia ya wasomaji na
wafuatiliaji wa makala mbalimbali za Darubini ya Imani lakini haswa katika makala hii
muhimu inayo zungumzia mada hii nzito ihusuyo ukweli juu ya Bwana Yesu kuwa
yeye ni nani haswa kiasili? Kimsingi mada hii ni miongoni mwa mada zenye utata
mkubwa katika ulimwengu wa Imani na Dini mbalimbali, maoni na mitazamo tofauti
imetolewa na watu wa Dini juu ya namna wanavyoelewakuhusu mada hii.

Ndugu mpendwa! Makala hii itakuwa msaada mkubwa sana kwako ili kukuwezesha
kutambua ukweli haswa juu ya mtu huyu aitwaye “Yesu” andaa tu moyo wako na akili
ili vitabu viweze kuzungumza ndani yako na hatimaye kujipatia ufumbuzi na upana wa
mawazo katika mada hii kwaajili ya maisha ya milele (Jannat) Mwenyezi Mungu
mwingi wa rehma akubariki.
Yaliyomo
Sura ya 1:

Mitazamo mbalimbali ya Kidini kuhusu Bwana Yesu

Sura ya 2.

Asili na kuzaliwa kwa Bwana Yesu (Issa) ndani ya Qur-an na


Biblia.

Sura ya 3.

Je! Yesu ni nani haswa?

Sura ya 4.

Ubinadamu wa Yesu, kwanini aitwe Mwana wa Mungu?

Hitimisho
Sura ya 1. kuangalia mitazamo hiyo mbalimbali ya
madhehebu juu ya Bwana Yesu.

Mitazamo mbalimbali ya Kidini


kuhusu Bwana Yesu.
Jehova’s Witnesess
Hili ni dhehebu lililoanzishwa na Ndugu
 Kama inavyoeleweka katika historia, Charles Taze Russel dhehebu hili huzalisha
Bwana Yesu ni mmoja kati ya watu majarida mbalimbali chini ya kitengo chake
mashuhuri walio wahi kuishi katika cha uchapaji kiitwacho Watch tower Bible
ulimwengu huu, pengine Bwana Yesu and tract Society kitengo hiki kinatoa
anaonekana kuwa na mvuto mkubwa zaidi majarida mbalimbali ambayo ndiyo yanayo
katika historia ya kidini na hata ya kidunia. elezea imani na mtazamo wa dhehebu hili juu
Mvuto huo wa Bwana Yesu unatokana na ya Bwana Yesu dhehebu hili humwelezea Yesu
mambo makuu ya ajabu na ya kustaajabisha kama kiumbe tu wa Mungu aliyepewa
aliyo yatenda katika dunia hii wakati wa upendeleo kwa kuumbwa kabla ya kiumbe
kipindi cha maisha yake ya kumkomboa yeyote mwingine (mzaliwa wa kwanza ) nao
mwanadamu. hudai kuwa Bwana yesu husimama kimamlaka
katikati ya viumbe na Mungu lakini kamwe
hana mamlaka ya kiasili ya Uungu. Mshahidi
wa Yehova hukataa pia fundisho la kuwepo
kwa utendaji wa Mungu katika nafsi tatu (3) za
milele.

Ndugu msomaji wangu hiyo ndiyo imani ya


dhehebu hili la mashahidi wa Yehova makala
hii ya Tarumbeta ya Vitabu itaweka wazi na
kutoa ufumbuzi juu ya mada hii ya msingi
kupia vitabu mbalimbali vya dini hususani
qur-an na Biblia Takatifu.

Jamii ya Waislam
Jamii ya waislam imejengwa chini ya msingi
 Umashuhuri wa kiongozi huyu wa Kidini wa mafundisho na maelekezo ya Qur-an
umepelekea watu mbalimbali wa madhebu Tukufu, dini hii ya Uislam imeanzishwa rasmi
ya dini kumgombania na kila mmoja mnamo mwaka 622BK mwaka ambao
akitaka kuitwa kwa jina lake (mfuasi wa Muhammad alihama toka mji wa Makka
Yesu). Hali hiyo imepelekea kuzalika kwa kwenda Madina (Yathrib) akihofia
mitazamo mbalimbali inayo lenga mashambulizi aliyofanyiwa na Waarabu
kumwelezea kiongozi huyo haswa juu ya pamoja na Wayahudi mara tu alipotangaza
mamlaka aliyokuwa nayo kiasili. kuanzisha Imani hii ya Kiislam.
Mitazamo hiyo pia inaonekana kugongana
kwa kiwango cha hali ya juu kutokana na Sehemu ya mafunuo ya Kiislam yaani Qur-an
uelewa wa uchambuzi wa kimaandiko Tukufu huonekana kumtaja na kumwelezea
unaonekana kutofautiana na hivyo kuleta Yesu kwa jina lile la Isa Ibn Mariam, lakini
migongano hiyo. Hebu tutumie fursa hii maandiko hayo humueleza Bwana Yesu (Isa
Ibn Mariam) kama nabii tu na mtume wa Hivyo Yesu aitwapo kwa majina hayo mbali
Mungu kama walivyo mitume wengine. mbali hulenga kuhashiria tu vile alivyo
jishusha na kufukia kiwango na nafasi
inayolingana na kumfikia mwanadamu
(Emmanuel – God with us) ili kutekeleza
Qur-an Surat Al-maida 5:75 Masihi bin mpango wa mbingu wa kumkomboa
Mariam si chochote ila ni mtume (tu). mwanadamu ambao lazima ufanywe na
Bila shaka Mitume wengi wamepita mamlaka kuu toka mbinguni lakini
kabla yake ………………….. iliyojishusha.
Imani na maelezo hayo ndiyo yanayo
chukuliwa zaidi na Ummah wa Kiislam na Maelezo hayo yahusuyo imani ya wakristo juu
kutia mkazo zaidi kuwa Bwana Yesu yeye ni ya bwana Yesu na mamlaka yake hukaziwa na
Mtume tu na hana cheo kingine au nafasi waalimu wa Kikristo kupitia maneno ya Yesu
nyingine yeyote kimamlaka zaidi ya hiyo ya mwenyewe anapotamka katika Maandiko:-
kiutume.

Pamoja na hayo jamii na Ummah huu wa


kiislam unayochangamoto kubwa na mambo
ya kutafakari kwa kina juu ya mamlaka haswa
ya Bwana Yesu (Isa Ibn Mariam) hii ni Sura ya 2.
kutokana na upande wa pili wa maelezo ndani
ya Mafunuo na aya kadhaa za Qur-an ambazo
huonekana kumfunua Yesu na kumpa Asili na kuzaliwa kwa Bwana
heshma na mamlaka ya juu zaidi Yesu (Isa ) ndani ya Qur-an na
yanayoonekana kupita uwezo wa utendaji
wa kiutume ama nabii tu. Maandiko hayo Biblia.
yatatusaidia sana kupitia jarida hili ili kupata
ufumbuzi wa kina zaidi kuhusiana na asili na Maelezo juu ya kuzaliwa kwa Yesu (Isa)
mamlaka haswa ya Bwana Yesu (Isa). yanaelezwa kwa upana zaidi kupitia maandiko
ya vitabu vyote yaani ndani ya Qur-an katika
Jamii ya Kikristo sura ile ya 19 surat Mariam na kibiblia ni
Jamii ya Wakristo (Manaswara ) wao pasipo katika kitabu cha Injili ya Mtume luka 1:26 na
hofu ukubaliana na vyeo pamoja na majina kuendelea, hebu tuanze na mafunuo ya Qur-an
kadha wakadha aliyonayo Bwana Yesu kama tukufu vile yanavyoeleza kwa ujumla juu ya
aitwavyo. tukio hili la kihistoria.
 Nabii - Yohana 4:19
 Mfalme - Filipi 2:10 Qur-an Surat Mariam 19:19 Malaika
 Mchungaji - Yohana 10:15 aksema hakika mimi ni mjumbe Wa
Mola wako ili nikupe mwana Mtakatifu.
 Njia - Yohana 14:6
 Mwalimu - Marko 9:38
 Bwana - Yohana 13:13
Qur-an hapa ina kubaliana na mawazo ya
n.k.
kimsingi juu ya tukio la malaika wa Mungu
kupeleka ujumbe maalumu wa kuzaliwa kwa
Lakini pamoja na hayo huamini kuwa Bwana
Yesu kwa binti huyu Mariam, katika aya za
Yesu anayo mamlaka kuu zaidi ya hapo kiasili,
mbele ndani ya andiko hilo huonyesha tukio la
yeye si mwanadamu wa kawaida tu. Pengine
Mariam kuhofia juu ya uwezekano wa kupata
hilo tutalitazama mbele kidogo katika
mtoto hadi anapo hakikishiwa juu ya nguvu na
uchambuzi wa mada hii ili vitabu vyote vya
mkono wa Mwenyezi Mungu Mwenyewe
Dini viweze kusaidiana na hatimaye kutupatia
kushiriki na kuwezesha jambo hilo lisilo
majibu sahihi na ya uhakika zaidi.
kubalika kibaolojia na kisayansi.
Mafunuo haya ya Qur-an hukamilisha tukio Hayo ndiyo mawazo ya kimsingi juu ya uzazi
zima hadi kuzaliwa kwa masihi kuanzia aya ile wa Bwana Yesu yanayopatikana katika
ya 17 na kuendelea hadi 22 katika sura mafunuo hayo ya Qur-an, pamoja na hayo bado
hiyohiyo ya 19 (surat Mariam). Qur-an itatusaidia kujua asili haswa ya Bwana
Yesu (Isa) mbele kidogo ya mada hii muhimu
naomba ufuatilie kwa makini.

Maelezo ya Kibiblia

Mambo ya Kimsingi yanayoelezwa hapo. Luka 1:26 mwezi wa sita malaika Gabriel
Pamoja na tofauti ndogondogo tunazoweza alitumwa na Mungu kwenda mji wa
kuziona lakini bado Qur-an hapo ufunua Galilaya jina lake Nazaret, kwa
mambo ya kimsingi yahusikanayo na tukio la mwanamwali bikira jina lake Mariam
kuzaliwa kwa masihi Yesu (IsaIbn Mariam) ………(2) utapata mimba na kuzaa mtoto
kama ifuatavyo. mwanamume, naye ataitwa Yesu huyo
atakuwa mkuu ataitwa Mwana wa aliye
Yohana 8:23 Ninyi ni wachini mimi ni juu.
wajuu. Ninyi ni wa
Ulimwengu huu mimi si wa Mtume wa Mwenyezi Mungu Luka Mtakatifu
Ulimwengu huu. akiongozwa na roho mtakatifu (Ruh’ L-Qudus)
anaweka wazi juu ya tukio hilo muhimu,
- Malaika alitumwa kupeleka taarifa ninayo imani kuwa Qur-an imepata habar
rasmi ya kuzaliwa kwa Bwana Yesu kadha …….
kwa Mariam kuhusu kuzaliwa kwa Bwana Yesu kupitia
(Aya 17) Mtume huyo Luka Mtakatifu kama Qur-an
- Mariam alihofia juu ya kuwezekana inavyojieleza yenyewe katika aya ifuatayo:-
kwa mpango huo ila alifahamishwa
kuwa uzazi huo ni wa mkakati Qur-an surat Al-Alaa 87:18 yaliyomo ndani
maalumu wa Mungu hivyo asihofu. ya Qur-an yamo katika vitabu vilivyo
- Uzazi wa Bwana Yesu (Isa) ni tangulia, vitabu vya Musa, Isa na Manabii
wakimuujiza kwa Ulimwengu na wengine.
niwa aina ya kipekee.

Mtume Luka anaweka wazi kuwa mamlaka ya Kumbuka


Mbinguni ilimwagiza rasmi malaika mkuu Yesu alisema mimi ni wajuu ninyi ni
Gabriel ili kuleta taarifa hiyo kwa Mariam juu wachini, Ninyi ni wa Ulimwengu
ya kupata mimba na kumzaa mtoto ambaye huu mimi si wa Ulimwengu huu.
anamtaja jina kuwa ni Yesu.
Pamoja na hayo aya za mbele zaidi huonyesha
kuwa Bwana Yesu ataitwa mwana wa aliye
juu, hapa pia huleta utata juu ya cheo na nafasi
Je Yesu (Isa) ninani Kiasili?
haswa ya Bwana Yesu, lakini kimsingi
maandiko yanaonyesha kuwa jina hilo la
mwana wa Mungu Bwana Yesu analipata Watu wengi wanaopenda kutafiti habari za
baada ya tendo lake hilo la kuzaliwa na Yesu wamekuwa wakifanya kosa kubwa la
Mariam lakini bado ipo asili haswa kutotaka kujua asili ya Yesu kabla ya uzazi
inayomhusu Yesu isiyotokana na vyeo au sifa
alizopewa kutokana na kazi yake ya Utume wa
Kidunia (Cross Culture witnessing) wake wa kidunia, wengi wamekuwa wakifanya
kosa hilo kubwa la kuhitimisha ufahamu wao
juu ya Yesu kwa kuishia tu kumjadili mara Ibrahimu - Habiba llahu ………
baada ya kutwaa mwili pengine jambo hilo kipenzi cha Mungu
hutokana na kutokuwa na shauku ya kujifunza
zaidi. Lakini nabii Isa huonekana kuwa na sifa mbili
ya kwanza ni ile ya kuitwa
Lakini makala hii itatupatia mwanga. Maana Kalimatu llahu - Neno la
tutavipa nafasi vitabu vyote viwili viweze Mungu
kueleza Mamlaka haswa aliyokuwa nayo Yesu Ruh” llahu - Roho
kabla ya kupewa majina ya Utume wake wa itokayo kwa Mungu
kidunia
Hivyo baada ya kufahamu hilo ni vyema sasa
tukaangalia na kuchunguza kwa upana juu ya
sifa hii ya “Neno” Je inatueleza nini juu ya
Qur-an Tukufu inasemaje! asili na mamlaka haswaa ya Yesu (Isa)
kabla ya kuja hapa duniani.
Qur-anSurat al-Imran 3:45 aliposema
malaika ewe Mariam Mwenyezi Mungu Je Biblia inasema nini?
anakupa habari njema za “neno” litokalo
kwake “jina lake” ni Masihi Isa Ibn Baada ya kuona wazo hilo la Qur-an hebu
Mariam, mwenye heshma katika Dunia na tuone Biblia nayo inasema nini juu ya hilo?
akhera ………….
Yohana 1:1-3 hapo Mwanzo kulikuwako
Andiko hilo la Qur-an linaonyesha na kufunua neno naye neno alikuwa kwa Mungu,
kwa wazi juu ya kauli ya Malaika kwa vyote vilifanyika kwa huyo wala pasipo yeye
Mariam iliyomtaka kujua juu ya mamlaka hakikufanyika chochote kilichofanyika.
inayotakiwa kukaa ndani ya tumbo lake na
hapa Qur-an huitaja mamlaka hiyo kuwa ni
Mwana aitwaye Isa Ibn Mariam. Lakini Katika sura na Aya hizo Biblia nayoinaeleza
Qur-an hutaja mwana huyo (Isa) kama “Neno” juu ya habari ya “Neno” (logos) pia
litokalo kwake (Mungu ). Katika maneno ya inatupeleka mbele zaidi maana inasema kuwa
Kiarabu ni:“Kalimatu minhu” - Neno huyo “Neno” (kalimatu) ni Mungu (rej
litokalo kwake (Mungu) …….Yohana 1: 1-2 naye neno alikuwa
Mungu) Je hii inamaana kuwa huyo Neno ni
Katika upana wa lugha neno “kalimatu” Yesu! Na je inamaana Yesu ni Mungu kiasili?
limetumika kama kisifa kinacho mwelezea
“Mtu” maana imetumika kauli ya umoja, Ndugu yangu mpendwa msomaji ukiwa ni
“Kalimatu” - Neno, kwa Waarabu huita Muislam au Mkristo yawezekana hilo likawa
“Mufrada” yaani umoja hivyo aya haikusudii ndiyo swali lako. Ninakuomba kuwa makini
“Maneno” ya kutamkika ila ni sifa na cheo zaidi tunapoingia sehemu hii ngumu na
cha mtu (Isa Ibn Mariam) kama Neno katika inayosumbua watu wengi.
umoja na siyo wingi (Jami-u) hivyo Isa (Yesu)
katika Qur-an hutambuliwa kuwa na cheo au Hebu kwanza tumfuatilie huyu Neno Je
sifa iitwayo Neno kabla ya zile za kibinadamu, Biblia inasemaje juu ya Neno?
katika Uislam manabii mbalimbali wamepewa
……. Zaburi 33:6 kwa “Neno” la Bwana
Mbingu zilifanyika na Jeshi lake lote
kwa
vyeo na sifa mfano:- Pumzi ya kinywa chake.
Musa huitwa - Takalama llahu………
aliyeongea na Mungu Biblia hapo inaonyesha kutaja tena habari ya
“Neno” na huyu neno hapo anaonekana kuwa
na sifa ya kuumba, lakini ninayo imani kuwa
Biblia inapotaja habari ya “Neno” bado ingali Maswali hayo ni mazuri ikiwa yapo katika
inazungumzia juu ya Mungu mmoja tu katika fikra zako ndugu msomaji wangu mpendwa.
upana wa utendaji (Nafsi) hivyo Neno ndiye
Mungu huyo. Kumbuka
Mungu ufahamika kwa vigezo na sifa maalumu
Je Neno la Mungu ndiye Mungu huyo? zinazomfanya aitwa Mungu vigezo na tabia
hizo kamwe havipaswi kumhusu mwanadamu.
Ndiyo ni kweli ndugu msomaji wangu hebu Vinginevyo ikiwa yuko anayeonekana kuwa
nikupe mfano:- mwanadamu lakini vitabu halali vya Kidini
Kwa kutumia kielelezo cha Neno lakawaida yaani Qur-an na Biblia vikampa sifa za
tunajifunza juu ya neno kama nafsi fikiri kimungu hiyo anapaswa kutazamwa upya na
huenda ulimuudhi mtu Fulani naye kwa kwa umakini, asije akawa ni Mungu pamoja
kughadhibika akaamua kukushitaki kwa kosa nasi (Emmanuel).
la kumtamkia “Neno” baya Swali! Je polisi
watakapo kuja kukukamata watakamata Kumbuka
“Neno” lako lililosema vibaya au Mungu alijifunua kwenye kijiti na kusema na
utakamatwa wewe mwenyewe? mtumishi wake nabii Musa (Qur-an 20:911)
Kulingana na ukuu na uweza wa Mungu
Jibu:- Niwazi kuwa utakamatwa wewe huenda hilo lilikuwa ni jambo duni na
mwenyewe na hiyo ni kwasababu! Neno na lakushangaza ila Musa alipaswa tu kutambua
mwenye Neno ni kitu kimoja. kuwa alikutana na kuzungumza na Mungu na
Kielelezo hicho kinawiana fika na mamlaka ya ndiyo sababu leo hii Musa huitwa katika
Yesu kama Neno la Mungu huwezi Uislam.
kumtenganisha kiasili na mamlaka ya Uungu,
yeye (Yesu) ni Neno kama nafsi (logos) ya Takalama llahu - aliyeongea na
utendaji wa Mungu, alikuwako kabla ya vyote. Mungu

Kubuka Musa alipoona ule moto alifikiri hata


kuutumia kwa mambo binafsi lakini laajabu
Pamoja na hayo ninaamini bado unajiuliza kumbe moto ule ulisitiri mamlaka ya Mungu
maswali haya. aliye hitaji kuzungumza naye.
Je! Huyu Yesu ninani haswa na je vitabu vyote
vya dini vina uwazi gani kuhusu Yesu kama ni Sura ya 3
Mungu, na je kweli zipo dalili na sifa za
Uungu wake?
Je Yesu (Isa) ninani haswa? Mwanadamu
Katika sehemu ya mwishoni sura ya 2 ya jarida Tabia shirikishi Tabia zisizo shirikishi
hili nimezungumzia juu ya kuwepo kwa sifa Commucable Un communicable
zinazo mfanya Mwenyezi Mungu (Allah) altibuties altibuties
kuitwa Mungu, na nikaeleza kuwa sifa hizo Upendo Uumbaji
kamwe haziwezi kuwa za binadamu hebu tuone Amani Uweza
mifano michache ya tabia hizo ambazo:- Furaha Umilele
Hakima Kuabudiwa/kutukuzwa
Communicable altibuties - tabia Utu wema Nuru ya Mbingu na Dunia
shirikishi Maarifa Kuokoa
Un communicable altibuties- tabia Mamlaka ya Mbingu na
zisizo shirikishi Dunia

Mungu Ni za Mungu pekee Hivyo ili Mungu aitwe Mungu lazima awe na
umshirikisha sifa ambazo kamwe Mwanadamu hawezi
kuzifikia, hivyo basi ili kujua asili haswa ya Pengine jambo hilo tutaliongelea zaidi mbele
Yesu na mamlaka yake ni vyema tuka fuatilia ya jarida hili la “Darubini ya Imani” katika
kwa makini kupitia tabia hizo, haswa zile mfululizo wa mada hii makini na yenye utata
zinazo mhusu Mungu pekee na kuchunguza kwa watu wengi, zaidi sana wale wasio soma
kwa makini kuwa je! Yesu alikuwa nazo sifa na kuchunguza maandiko kwa makini.
hizo hata aitwe Mungu?
Pamoja na hayo ndugu msomaji wangu Hebu sasa kwa makini tuanze kuchunguza
ninakuomba kuwa na moyo laini na wa ukubali taratibu vigezo hivyo vya msingi katika
kwa kadri maandiko yatakavyo zungumza na mchakato wa mada hii.
kubainisha ukweli haswa wa mada hii tata hebu
sasa tuanze safari yetu taratibu na kwa uhakika (1,1) Uumbaji
ili tuweze kuvuna maarifa haya ya ajabu. Kwa ujumla Mungu yeye ni Mungu tu
kwa asili kama alivyo Mungu, lakini
Je! Ni sifa zipi basi zimhusuzo Mungu, sisi wanadamu tunavyo vigezo vinavyo
alizonazo Bwana Yesu? Je Qur-an na Biblia tusaidia kumtambua katika kikomo
vinasema nini? chetu cha ufahamu wa kibinadamu
hivyo moja kati ya sifa kuu
Sifa tutakazo zichunguza kwa muktasari. zinazomtambulisha Mwenyezi Mungu
(1) Uumbaji kwetu ni tendo hili kuu “Uumbaji”.
(2) Mamlaka ya Mbingu na Dunia
(3) Kutukuzwa na viumbe vyote na Uumbaji umweleza Mungu vyema
kusujudiwa sana katika akili ya Mwanadamu
(4) Nuru ya Mbingu na ardhi (Ibn adam), kupitia tendo hili la
(5) Kuokoa uumbaji wanadamu hujifunza na
(6) Umilele kutambua kuwa:-

Hizo ndizo baadhi ya sifa tutakazo zipitia kwa - Mungu ndiye asili (Chanzo) ya
makini ili zitusaidie kugundua ukweli haswa vyote viijazavyo dunia.
juu ya Bwana Yesu kuwa Je! Ni kweli - Yeye kwa hakika ndiye asili na
anastahili kuitwa Mungu? Tutakubaliana chanzo cha uzima maana yeye
ndugu msomaji wangu mpendwa kuwa sifa mwenyewe ni uzima.
hizo zote nilizo zitaja ambazo ndizo tutakazo - Kuwepo kwetu kunatokana na
zipitia zote zinamhusu Mungu pekee na kamwe kuwepo kwake kusiko na mwanzo
haziwezi kumhusu binadamu yeyote wala mwisho
wakawaida vinginevyo kama yupo anaonekana - Yeye ndiye mwenye mamlaka juu
ni binadamu lakini anasifa hizo basi atakuwa ya maisha yetu awezaye kuyazuia
na asili inayopita ubinadamu alionao, maana au kuyaruhusu kuendelea, ni
hata Mungu anauwezo wa kuchukua mwanzilishi ndiye mtoa uhai nasi
mwonekano wowote hata ule usio eleza kabisa tunaishi ndani yake.
mamlaka yake ili kujifunua kwa watu wake.

Rejea “ Qur-an 20:9-11


Mungu alijifunua kwenye kijinga cha moto
na kuongea na Musa
Hata malaika wa Mungu uweza kutwaa
maumbile mbalimbali.

Soma” Qur-an 19:17 ………… Malaika


akajimithilisha (kujibadili-kujifunua )
kwake kwa sura ya binadamu aliye kamili.
Sifa na mamlaka hii kuu ihusuyo uumbaji
kamwe haiwezi na wala haitoweza Katika sura nyingine ya Qur-an kuna maneno
kumhusu mwanadamu wa asili ya Dunia yanayo mwelezea Mungu kwa kauli
hii, Mungu Mwenyewe alisema. inayosema “hakuna anaye fanana naye hata
mmoja “

Isaya 42:8 “Mimi ni Bwana ndilo jina Qur-an Surat nnasi 114:4
langu na utukufu wangu sitampa mtu Katika aya nyingine ndani ya mafunuo ya Qur-
mwingine wala sitawapa sanamu sifa an bado huweka na kutia mkazo mkuu juu ya
zangu” swala hili la Uumbaji namna linavyohusika na
Vitabu vyote vya maandiko ya kidini Mungu pekee, pamoja na hayo, Qur-an
uelezea kwa upana juu ya umaalumu huonyesha kuwa kazi yeyote ihusuyo Kuumba
wa sifa hii ya uumbaji ni vile hata nzi (mdudu mdogo) inahusika na Mungu
isivyopaswa wala kustahili ya uungu maana ni uanzishaji wa kiumbe (uhai).
hebu tufuatilie ushahidi wa kimaandiko
haswa tukianza na mafunuo ya Qur-an
Qur-an surat Al-hajj 22:73 Enyi watu!
pamoja na Biblia Takatifu na kisha
Unapigwa mfano, basi usikilizeni, hakika
tutaangalia kwa makini kuwa Je!
wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi
Bwana Yesu anasifa hiyo ya uumbaji ili
Mungu hawawezi kuumba (hata) nzi
aitwe Mungu?
……………………………
Uumbaji sifa ya Mungu Pekee.
Katika mafunuo ya Qur-an zipo habari Hivyo mkazo mkuu wa Aya hizo za Qur-an ni
kadha wa kadha na maelezo ya namna kuonyesha umakini na upekee wa tendo hilo
mbali mbali juu ya uumbaji, katika linalo mfanya Mungu kuwa Mungu kwa watu
sehemu hii tutachunguza kwa makini wake, hivyo katika sehemu hii tutaangalia kwa
ili kuweza kuona uzito na umakini wa makini kuwa Je! Kweli Bwana Yesu anaweza
tendo hili la Uumbaji na yakuwa ni nani kuwa na sifa hiyo ya kuumba inayo onekana
pekee anaye husika na mwenye uwezo kwa mkazo mkubwa kuhusika na Mungu
huo wa kuumba. pekee?

Pamoja na Aya hizo za Qur-an pia tunaweza


Muumbaji ni nani? kuona Biblia nayo ikiweka mkazo juu ya
umaalumu wa tendo hilo la Uumbaji, na
yakuwatendo hilo na mengineyo yatendwayo
Qur-an surat Yunus 10:34 sema je na Mungu hulenga kufanya wanaadamu
(yuko)katika hao mnaomshirikisha wamche Mungu kutokana na uwezo wake huo
Mwenyezi Mungu aliyeanzisha kuumba wa kiutendaji ambao kamwe hauwezi kufikiwa
viumbe, kasha atavirejeshea? Sema na mwanadamu.
“Mwenyezi Mungu ndiye aliye anzisha
viumba kisha atavirejesha. Basi
Mhubiri 3:14 Najua ya kwamba kila kazi
mmegeuziwa wapi? ………………
aifanyayo Mungu itadumu milele,
haiwezekani kuzidisha kitu, wala
kupunguza kitu, nayo Mungu ameifanya
Andiko hilo kama lilivyoonekana kujieleza ili watu wamche yeye.
linaonyesha kuwa hakuna uwezekano kwa
Mwanadamu Kuumba, na yakuwa ni Mungu
pekee awezaye kuumba na kuhuwisha atahivyo
tendo lolote la kumhusisha mwingine awaye Hapo Biblia inaonyesha wazi kuwa zipo kazi
yote katika sifa hiyo ya Uumbaji ni kujitenga zinazohusika na kufanywa na Mungu (Aya 14-
na ukweli wa Mungu. Kila kazi aifanyayo Mungu) bila shaka Biblia
hapo hulenga kuonyesha kuwa kuna mambo
kadha wa kadha ambayo kamwe hayapo chini
ya uwezo wa binadamu maana awezaye
kuyatenda ni Mungu pekee naye hamshirikishi
mwanadamu.
Ndugu mpendwa hivyo ndivyo qur-an
Pia Biblia hutaja sababu zinazopelekea inavyoeleza juu ya kile alichokifanya Isa Ibn
matendo hayo kuhusika na Mungu pekee nayo Mariam, hapo kunajambo kuu na lakimsingi
ni kuwa watu wamche Mungu pekee (ili watu kwa wale wanao chunguza maandiko kwa
wamche yeye) hivyo basi tendo hili la kuumba makini na kutafakari.
na mengineyo ya mhusuyo Mungu humfanya
Mungu kustahili kuabudiwa. Andiko hilo la Qur-an linaeleza kuwa Isa Ibn
Mariam aliwaeleza watu wa taifa la Israeli
Hebu tuone mkazo wa Aya nyingine. mambo ya fuatayo.
1. Amewajia na hoja kutoka kwa mola
Isaya 44:24 BWANA, Mkombozi wako, (mbinguni)
yeye aliye kuumba tumboni asema hivi, 2. Yakuwa anaouwezo wa kuumba
mimi ni Bwana, nifanyaye vitu vyote: kiumbe kwa udongo
nizitandazaye
Ndugu msomaji mbingu
wangupeke
badoyangu:
Biblia 3. Anao uwezo wa kukipa uhai hicho
niienezaye kuonyesha
inaendelea nchi ni naniumakini
aliye pamoja
na upekee alichoumba na kukipulizia pumzi ya
nami?
wa tendo hilo, hapo Biblia inafunua mambo uhai.
yafuatayo:-
Ndugu msomaji wangu bilashaka umeanza
 Vitu vyote vinavyoonekana ni matokeo kufunguka masikio kupitia Aya hiyo yaQ-an
ya kazi iliyofaywa na Mungu. katika Aya hiyo inaonekana orodha ya matendo
 Kuwepo kwetu duniani kunatokana makuu ambayo Bwana Yesu (Isa) anatangaza
tendo la Uumbaji mkuu uliofanywa na kuwa na uwezo wa kuyatenda bila shaka
Mungu matendo hayo ikiwa umeyachunguza kwa
 Tendo hilo la Uumbaji kamwe siyo makini, yanaonekana kuhusika na uwezo wa
tendo (tabia) shirikishi bali hutendwa kiutendaji wa Mungu Mwenyezi, sasa hebu
na Mungu pekee (niienezaye nchi ni tufuatilie kwa makini.
nani aliye pamoja nami? Rejea Isaya
44:24)
Nukuu kwa muktasari Qur-an 3:49
Hivyo yeyote anayeumba katika mfanano wa
utendaji wa kiuungu kunahaja ya kumchunguza
kwa makini ili kujua asili yake na mamlaka a) Nakuambieni katika udongo kama sura
aliyonayo ni ya namna gani haswa. ya ndege.
bila shaka tendo hili hufanana fikiri na kile
Je Yesu (Isa ) anasifa ya Kuumba ili aitwe alichofanya Mungu pindi aliokuwa
Mungu? akimuumba Adamu maandiko yanaonyesha
kuwa Mungu alifinyanga udongo na
kumuumba Adamu vivyo hivyo Isa (Yesu)
Qur-an 3:49 na atamfanya mtume kwa wana nae anafanya Uumbaji kwa kufinyanga
wa Israel awaambie nimekujieni na hoja udongo kwa sura ya ndege.
kutoka kwa mola wenu ya kuwa Qur-an 22:5…… tulikuumbeni kwa
Ref: Mwanzo 2:7udongo
“ninakuumbieni”katika Bwana kama
Mungu sura ya udongo mzee wenu Nabii Adamu ………
akamuumba
ndege kisha mwanadamu
“nampulizia” kutoka katika
mara anakuwa
udongo wa ardhi Hivyo Yesu anafanya tendo la Uumbaji kwa
hatua zinazo fanana fika na kile alichofanya
Mungu (kufinyanga udongo).
Katika tafsiri ya kawaida Neno “Idhini”
b) Kisha nampulizia mara anakuwa ndege. humaanisha “ruhusa” au “Ukubali”
Ndugu mpendwa yawezekana liletendo la
kufinyanga udongo lisiwe na nguvu sana Hivyo Qur-an inapomnukuu Nabii Isa akisema
kwa wajenga hoja , lakini hapa ndipo kwa “idhini” inaleta maana tu ya ukubali,
panapo nishangaza zaidi Qur-an ruhusa toka kwa Mungu.
inapoonyesha wazi kuwa Isa aliweza
kupulizia udongo nao ukapata uzima na Swali:- je kwanini apewe ruhusa na hali yeye
kuwa kiumbe hai. ni Mungu? Au Je kuna miungu wangapi?

Wanasansi huu ndio uumbaji na wanabaiolojia Jibu:- katika mafunuo ya Biblia mara kadhaa
wamejitahidi kuumba na kutengeneza mtu Bwana Yesu ametumia kauli hiyo ya
lakini wamegonga mwamba inapofikia hatua kuruhusiwa au kukubaliwa na Mungu (eg:
ya kumfanya kuwa kiumbe hai, aweze Yohana 5:30) mara kadhaa Yesu alisema
Kutembea, Kunusa, kuona n.k “ninenalo si neni yaliyoyangu nisikiavyo
ndivyo nihukumuvyo”
Lakini maandiko ya Qur-an ufunua siri hii ya
ajabu, bilashaka tendo hili la kupuliza pumzi Kwanini aseme hivyo (kwa idhini)?
na kitu kikawa hai ndiyo uleta maana halisi ya Kwa msingi ujio wa Yesu hapa Duniani
Uumbaji na hili ndilo tendo linaloleta maana na ulimlazimu kufunika uwezo na mamlaka yake
uzito haswa unaofanya tendo hilo kuwa rasmi ya asili ya Kimungu, ilimpasa kumwelekeza
na kumhusu Mungu pekee. mwanadamu kwa vielelezo hai vya
kimwenendo, hali na mazingira hayo
Mafunuo ya Qur-an huonyesha kuwa tendo yalimfanya kujipa cheo cha chini mara kadhaa
hilo haswa ndilo alilotenda Mungu alipokuwa alipozumngumza na watu.
akimuomba Adamu nalo ni tendo la kutoa uhai
(Maisha) kwa kuomba. Rejea Qur-an 20:9-11 Mungu alijifunua
kwa Musa kupitia kichaka cha moto
Qur-an surat 15:27 bila shaka alichukua ufinyu huo ili
kuwa Asili na mwanadamu.

Tunajua fika juu ya tabia ambazo Mungu Pamoja na hayo Bwana Yesu akuadhimu mara
umshirikisha mwanadamu na pamoja na hayo chache kufunua taratibu mamlaka aliyonayo
zipo zile ambazo Mungu kamwe hawezi kiasili, mfano ni pale aliposema.
kumshirikisha mwanadamu, lakini katika
andiko hilo tunaona Yesu akitenda kazi hiyo Yohana 10:30 mimi na Baba tu umoja.
kuu yenye uhusiano kwa asilimia miamoja na Kauli hiyo iliwafunulia mafarisayo juu ya
uwezo wa Kiuungu bilashaka huyo Yesu anayo mamlaka ya Yesu ya Kimungu, lakini haikuwa
asili inayopita ubinadamu aliokuwa nao na siyo jambo rahisi kwao kukubaliana na hilo
asili ya kawaida.

Je! Mbona Qur-an inasema aliumba kwa


idhini ya Mungu?
Inawezekana ndugu msomaji wangu ukawa na
swali la namna hiyo ndani ya moyo wako hebu
niruhusu sasa niweze kuondoa mashaka
uliyonayo.

Je! Neno kwa idhini humaanisha nini?


na katika aya hiyo tunaona wakiadhimu Andiko hilo la Qur-an linasema kuwa
kumpiga mawe kwa kujiita yeye ni Mungu. - “Ati yeye aliyeumba (Mungu) atakuwa sawa
na wasio umba”?
Bilashaka Yesu alitambua saikolojia ya imani
ya watu hao anaowajua hata mioyo, hivyo Jibu :- la” aliyeumba hawezi kuwa sawa
Yesu aliamua kushuka kwa kumtaja Mungu wasioumba bali aliye umba anakuwa sawa na
wanayemdhani kama Mungu aliye ng’ang’ana aliyeumba hivyo ikiwa Yesu aliumba je yeye ni
Mbinguni tu lakini kwa hakika hiyo ndiyo asili nani?
yake binafsi.
Qur-an kamwe haimpi sifa au usawa kiumbe
Ndiyo maana alisema kwa Idhini. yeyote asiye na sifa inayohusika na Mungu,
Katika wazo hilohilo ndiyo maana Yesu maana sifa inayomhusu Mungu haswa ile ya
Utumia neno kwa “Idhini”alipenda watu kuumba ndiyo humfanya Mungu kuitwa
watambue mamlaka yake katika utendaji wake Mungu kamwe hawezi kupewa Mwanadamu.
zaidi kuliko katika maneno yake
Pamoja na hayo jambo la kushangaza ni pale
Hata hivyo neno kwa “Idhini” halimaanishi Qur-an inapoo nekana kuweka wazi kuwa
kwa “uwezo” Idhini na uwezo ni mambo Nabii “Isa Ibn Mariam” naye alikuwa na sifa
mawili yanayo tofautiana sana hiyo inayo mhusu Mungu maana naye aliweza
kuumba
Mfano:- wewe unaweza kupewa Idhini ya (rejea neno nakuumieni Qur-an 3:49)
kuhubiri lakini usiweze (usiwe na uwezo ) wa
kuhubiri hivyo idhini( ruhusa ) na uwezo Na kutokana na kile kichosemwa na aya
nitofauti kulingana na maandiko tabia ya Yesu tuliyoisoma punde Nabii Isa anaonekana kuwa
ihusuyo Uumbaji uonekana akiwa nayo katika sawa na Mungu au kwa lugha rahisi naya ufupi
asili (Yohana 1:1-3) hivyo ni tabia ya kiuwezo yeye ni Mungu Muumbaji aliye adhimu
na mamlaka yake ya Kimbinguni kabla ya kuvaa ubinadamu, lakini ana mamlaka inapita
kujishusha na kuvaa ubinadamu (nitalieleza huo ubinadamu (yeye ni neno, muumbaji).
mbele kwaupana ) na kuja hapa duniani.
(2,2) Mamlaka ya Mbingu na Dunia
Neno idhini Isa (Yesu) analitumia anapo kuwa Baada ya kuona sifa hiyo ya kwanza ya
hapa Duniani kama sehemu ya hatua yake ya Mungu ihusuyo Uumbaji ambapo
kujishusha na kutwaa ubinadamu kwaajili ya tumeona wazi vile ambavyo Bwana
kuokoa, lakini bado tendo la uumbaji linarejea Yesu anavyohudika nayo, nivyema
asili na mamlaka yake kama Muumbaji na si sasa tukaenelea na mchakato huu wa
wa ndege tu bali Dunia kwa ujumla (Yohana mada hii yeye utata kwa kuangalia
1:1-3) kigezo cha pili kihusucho mamlaka ili
kuendelea kuona kama bwana Yesu
Qur-an inampa cheo gani Yesu (Isa) kwa tendo anayo mamlaka hiyo ikiwa yeye ni
la Kuumba? Mungu?

Uandishi au kuchapaji mwandishi na Mamlaka ni kitu gani?


mengineyo ya kimsingi. Kwa ufupi mamlaka huashiria hali ya
kiutawala anayokuwa nayo mtu juu ya
Qur-an 16:17 …….Ati yeye eneo sehemu au mazingira fulani, hali
aliyeumba (naye ni Mwenyezi hiyo humpa mtu huyo uwezo wa
Mungu ) atakuwa sawa na wale kuamua na kuongoza pasipo kikwazo
wasio umba je hamkumbuki? mwingine awayeyote.

Moja kati ya sifa zimhusuzo Mungu ni


tendo hili la kuwa na mamlaka juu ya
mbingu na Dunia niwazi kuwa hakuna Qur-an 3:45 ………. Mwenyezi Mungu
kiumbe yeyote asiye na sifa ya kimungu anakupa habari njema ya “Neno”
anayeweza kuwa na mamlaka juu ya litokalo kwake
Mbingu na Dunia, sifa hii kama ilivyo Jina lake ni Masihi Isa Mwana
ile ya kuumba uhusika na Mungu wa Mariam – mwenye “heshima”
Mwenyewe. katika “Dunia” na “akhera”
…………
Kuashiria kuwa hii ni mamlaka ya
Mwenyezi Mungu pekee tunaweza Qur-an hapo inataja ninaouona ni
kuona mifano ya wanadamu wa upekee au mamlaka ya Bwana Yesu
kawaida waliojaribu kujifanya kuwa pale inapoeleza kuwa ana “heshma”
nao wanamamlaka kile kilichowapata katika “Dunia na Akhera”. Katika Qur-
baada ya tendo hilo. an ni marachache kuona mtu yeyote tu
akielezwa katika namna kama hiyo
Mfalme Nebkadneza – mfalme huyo …………..
alifanyakazi ya kuujenga mji wa
……………… Hilo linaonyesha kuwa kuna upekee na
Na baada ya kujenga vyema kwa kitu cha ziada kinacho pelekea sifa hizi
kuweka mabustani ya angani n.k. kuu za kimamlaka kuangukia kwa
alijisikia kiburi na kudai kuwa ndiye Bwana Yesu …………… na kama
mwenye mamlaka na muumba wa mji tulivyoona yeye kwa hakika ni Mungu.
huo, tendo hilo halikuwa jema machoni
pa mwenye mamlaka halisi yaani
Mungu.

Kama matokeo ya kufuru hiyo ya wizi


wa mamlaka na uwezo wa Kimungu
Mfalme hivyo
aliambulia…………………

Lakini tunaposoma ndani ya Biblia


hiyohiyo, maandiko Matakatifu ya
Sura ya 4
Biblia yanapo mzungumzia Bwana
Yesu sehemu kadhaa huonyesha vile
alivyo kuwa na mamlaka sehemu ya Ubinadamu wa Yesu na
maandiko kama: sababu ya kuitwa Mwana
Mathayo 28:19-2 Bwana Yesu wa Mungu toka mamlaka
mwenyewe anatamka ya Uungu.
“Nimepewa mamlaka yote
Mbinguni na Duniani” Ndugu mpendwa msomaji
Sehemu nyingine ni katika mafunuo ya tutakubaliana kuwa hilo ni moja kati ya
Qur-an yenyewe katika maneno yasiyo maswali nyeti yanayoulizwa na watu
fanana sana na hayo ya Kibiblia lakini wengi wanao hoji na kutafiti mamlaka
nayo inaonyesha upekee aliokuwa nao haswa ya Bwana Yesu.
Yesu (Isa bin Mariam ) “Ubinadamu wake”

Chanzo cha maswali yote yanayo


ulizwa juu ya Bwana Yesu kinaanzia
Hebu fuatialia aya ifuatayo:- mara tu Yesu alipovaa mwili wa
kibinadamu tendo hilo kwa fikra za
haraka tu linaweza kudhaniwa kuwa mawasiliana ya Mungu kwa wanadamu,
ndilo linaloshusha mamlaka yake ya pazia hii maanisha ni kitu
asili kama Mungu. Pamoja na hayo kinachofunika ili kuzuia kuonekana
mimi binafsi nichoelewa ni kuwa tendo kwa uhalisi wa jambo kwa lugha
hilo kamwe halishushi mamlaka bali nyingine Mungu wakati Fulani huamua
linafunika mamlaka aliyokuwa nayo kufunika uhalisi wake kwa kujifunua
kwa kadri ya sababu………… nyuma ya “Pazia”.

“Pazia ni nini Kibiblia?”


Waebrania 10:20 ……….. ipitayo
Ifuatayo:- katika “Pazia” yaani mwili wake.
Mungu aliwahi kujifunua wazi katika
nyakati za nyuma na wanadamu Katika Biblia Pazia huashiria mwili wa
wakaangamia Bwana Yesu, hivyo hiyo ni njia ya
kimawasiliano kati yake na binadamu
Fuatilia:- kutoka 19:14-19 “swali la inayofunika mamlaka yake ya Asili ya
kujiuliza” Uungu ili binadamu kumudu kukutana
Je! Mungu aje katika hali gain ili naye.
mwanadamu aweze kuikabili?  1Timotheo 3:16 Mungu
“Jibu” alidhihirishwa katika mwili
Ni lazima uje katika hali inayofunika  Ebrania 10:5 Mwili uliniwekea
uwazi wa mamlaka yake iliyo ya utisho tayari
kwa mwanadamu mdhambi.  Filipi 2:7 alijifanya hana
utukufu …….. akawa na mfano
Fuatilia kutoka 33:18-20 mwanadamu wa mwanadamu.
hataniona akaishi ……………..
Sababu hiyo ya kimsingi ndiyo
inayofanya Bwana Yesu kuchukua
mwili wa kibinadamu kupitia Mariam
kama tulivyo kwishaona. Hivyo mwili
ya Bwana Yesu ulisitiri mamlaka kuu
ya Uungu wake ambao hainge kuwa
busara kuufunua na kufanya binadamu Kwanini aitwe Mwana naye ni
kuangamia badala ya kuokolewa naye. Mungu?
Kwa kauli nyingine ni kuwa Mungu Tendo la Bwana Yesu kuitwa Mwana
(Yesu) alitumia mwili huo ili kuwafikia wa Mungu linaanzia kwenye chanzo
waja wake kama tulivyoona hapo cha kutwaa mwili.
nyuma jinsi Mungu alivyojifunua hata Yohana 1:14 naye neno akafanyika
kwa kichaka kwa kadri ya Qur-an mwili akakaa kwetu nasi tukaona
tukufu. “Ubinadamu ni njia ya Mungu utukufu wake utukufu
kusema na waja wake:” kama wa Mwana pekee atokae
kwa baba …………..
Qur-an 42:51 ……….. Mungu
husema na wajawake kwa njia ya:- Andiko hii linaonyesha hatua kuu
1. Ilhamu – sauti ya mbili yaani:-
ndani ya moyo ya Mungu  Kufanyika mwili
2. Nyuma ya pazia – ishara ya  Kuitwa mwana atokae
kufunika mamlaka. Mbinguni.
Kwa kadri ya Aya hiyo tunaona Qur-an Sababu kuu
ikitaji “Pazia” kama chombo cha
Tendo la Yesu kuamua kuchukua
jukumu la kutuokoa lilimladhimu siyo
kufunika Utukufu wake (Uungu ) tu
kwa mwili bali pia kubadili Hitimisho
kitambulisho chake cha mamlaka

“Fatilia mfano huu” Kwa mahitaji ya elimu na


Maji yanaweza kugeuka katika hali ufafanuzi wa mada mbalimbali
mbalimbali katika kile ninachojua maji zenye utata tafadhali niandikie
hayo mara yanapo badili hali tu pia au wasiliana nami kupitia
tendo hilo huambatana na kubadilli jina,
anuani zangu kama
yaani mfano maji yanapoganda
hanayoitwa tena maji bali huitwa barafu nilivyoonyesha hapo chini.
Masomo na vijarida mbalimbali
Swali:- Je barafu si maji? vya huduma vimebariki watu
Jibu:- la barafu ni maji ila yamebadili wengi uwe mmoja wapo na
asili kwa muda na baadae hurejea. Mungu atakujazi.
Sababu ya Bwana Yesu kuitwa mwana
inatokana na kusudi lake tu la kuja
Duniani Kutukomboa hivyo alifanyika
barafu toka asili ya maji (alifaninyika Lecture Prepared By Pr. Dominic
mwana toka asili ya Uungu kama Mapima
njia ya Ukombozi) lakini asili yake ya Muslim areas Evangelism Instructor.
Uungu inabaki palepale. Mobile: 0754-527143
Email: dominicmapima@yahoo.com

Fuatilia ushauri mwingine juu ya


Uungu wa bwana Yesu katika
mafungu yafuatayo:-
Yohana 14:7-10……… aliyeniona
mimi amemwona Baba
Tito 2:13 ……. Yesu Mungu mkuu na
mwokozo wetu.
Yohana 20:28 Bwana wangu (Yesu)
na Mungu wangu.

Ndugu mpendwa ninaamini hofu na


mashaka ya moyo wako juu ya mada hii
yamepingwa na uondolewa kupitia
uchambuzi huu, fanya maamuzi yako
leo kwa kujenga upya imani yako juu
ya mamlaka ya Bwana Yesu kama
tulivyo jifunza.

You might also like