You are on page 1of 30

1

Kitabu
Kisichokuwa
na
Shaka ndani yake
Quran tukufu inaweka wazi katika Sura ya 2:2

‫اب َل َريْ َب ِفي ِه ُهدًى �لِّلْ ُمتَّ ِق َني‬


ُ َ‫َٰذلِ َك الْ ِكت‬
Hiki ni Kitabu kisicho kuwa na shaka ndani yake; ni
uwongofu kwa wachaMungu,”

Hii ni kwa mujibu wa Tafsiri ya Quran Tukufu


kama ilivyotafsiriwa na Shekhe Abdallah Farsy.
Lakini tunaposoma tafsiri ya aya hii katika Tafsiri
ya Quran kama ilivyotafsiriwa na Waislamu wa
Madhehebu ya Ahmadiyya inasema kwamba.

“Hicho ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni


uwongofu kwa wachaMungu”

Ukichunguza vizuri maneno haya ya Kiswahili,


utagundua kwamba kuna tofauti ya maana. Neno
lililotumiwa na Abdallah Farsy katika Tafsri yake
ni “Hiki ni Kitabu”, wakati maneno ya Tafsri ya
Ahmadiyya ni “Hicho ni Kitabu”. Tofauti hapa ni
kwamba, neno hiki linaashiria kitu kilicho karibu
(mkononi) wakati ambapo, neno hicho, linaashiria
2
kitu kilicho mbali siyo kilichopo mkononi. Ili
kuondoa utata wa utofauti huu wa maneno haya
mawili ni vizuri kuangalia neno halisi lililotumika
katika lugha ya asili, lugha ya Kiarabu ambayo ndiyo
lugha ya Quran.

Neno lililotumika hapa ni ‫( َٰذلِ َك‬Dhaalika). Neno hili


dhaalika, kwa kiarabu linaitwa “ismu ishaaratu lil bai’di”
yaani jina la kuashiria kitu kilicho mbali, maana yake
kwa Kiswahili ni “Hicho”.

Neno lingine linalofanana na hili ni َ‫( اَذه‬Hadha),


maana yake ni “hiki”. Kwa hiyobasi tafsiri sahihi
ya aya hiyo ni ile inayosomeka ““Hicho ni Kitabu
kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wacha
Mungu”. Hii inamaana kwamba, aya hii haikusudii
Quran ni kutokana na historia yenyewe ya uteremsho
wa Quran. Inasadikika kwamba, Muhammad alipata
utume wake katika mwaka wa 610 AD. Waislamu
wanaamini kwam ba Wahyi, ama ufunuo kwa
Muhammad ulikuja kidogo kidogo. Kwakuwa
hakujua kusoma wala kuandika ilibidi akalili maneno
aliyofunuliwa, na pia aliwakalilisha masahaba zake.
Inadaiwa kwamba, Wahyi (ama ufunuo) ulikuja kwa
Muhammad kwa kipindi cha miaka 23.

Muhammad alifaliki katika mwaka wa 634


AD. Hadi anafaliki hakukuwa na kitabu hiki
kiitwacho Quran, bali ujumbe huo ulikuwa
umehifadhiwa vifuani mwa masahaba, ambao
waliitwa muhafidhuuna (Wenye kuhifadhi). Baada ya
Muhammad kufariki, alitawala Khalifa (kiongozi)
wa Kwanza wa Umma wa Kiislamu aliyekuwa
3
akiitwa, Abbakar Sadik. Yeye aliwaongoza Waislamu
katika vita vya Yamama mwaka huo 634. Katika vita
hivi, walikufa masahaba wengi waliohifadhi Quran
wapatao 70, hivyo kukawa na hofu kubwa ya kupotea
kwa Quran iwapo muhafidhuuna wote wange kufa.
Hivyo Uthuman bin Afan, swahaba mwingine wa
Muhammad, akapendekeza kwa Abbakar kwamba
waikusanye Quran na kuiandika. Ndipo Abbakar
akachagua kamati ya watu 12 ikiongozwa na Zaid
ibn Thabit. Pamoja naye walikuwepo katika kamati
hiyo, Uthman ibn Affan, Ali ibn Abi Talib, Talha ibn
Ubaydullah, Abdullah ibn Masood, Ubayy ibn Kab,
Khalid ibn al-Walid, Hudhaifah and Saliim.

Kamati hii ndiyo kwa mara ya kwanza ikawaitisha


masahaba wote waliokuwa wamehifadhi Quran na
kila mmoja alisema aya aliyohifadhi, ndipo watu hawa
wakaandika aya hizo na ikapatikana hii Quran yenye
Sura 114 na aya 6,236 na maneno yapatayo 323,000.
Kufuatia historia hii, ni uwazi kwamba, hakukuwa
na kitabu cha Quran wakati wa Muhammad, kwa
hiyo aya hii ya Sura ya 2:2 haiwezekani kabisa kuwa
ilikusudia Quran (ambayo haikuwepo wakati huo)

Je, Quran sura ya 2:2 inakusudia kitabu gani hasa?

Ni wazi kwamba wakati wa Muhammad


kilikuwepo kitabu tayari kilichoandikwa chenye
kukusanya maneno ya Mwenyezi Mungu ambayo
yalifunuliwa kwa Manabii wa kale.

Muhammad mwenyewe aliambiwa katika Quran.


4
َ ‫للاَ َو َل نُ ْش ِر‬
‫ك‬ َّ ‫ب تَ َعالَوْ ا إِلَ ٰى َكلِ َم ٍة َس َوا ٍء بَ ْينَنَا َوبَ ْينَ ُك ْم أَ َّل نَ ْعبُ َد إِ َّل‬ ِ ‫يَا أَ ْه َل ْال ِكتَا‬ ْ‫قُل‬
‫للاِ ۚ فَإِن تَ َولَّوْ ا فَقُولُوا ا ْشهَدُوا‬ َّ ‫ُون‬ ِ ‫د‬ ‫ن‬ ‫م‬
ِّ ‫ًا‬ ‫ب‬ ‫ا‬َ ‫ب‬ ْ‫ر‬َ ‫أ‬ ‫ًا‬
‫ض‬ ْ
‫ع‬ َ ‫ب‬ ‫َا‬ ‫ن‬ ‫ض‬
ُ ‫ع‬ ْ َ ‫ب‬ ‫َش ْيئًا َو َل يَتَّ ِخ َذ‬ ‫بِ ِه‬
َ‫بِأَنَّا ُم ْسلِ ُمون‬

“Sema: Enyi Watu wa Kitabu! (cha Mwenyezi Mungu.


Mayahudi na Manasara) Njooni kwenye neno lilio sawa
baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila
Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; …..”
(Quran Sura 3:64)

Hii inaonyesha kwamba, tayari kulikuwa na kundi


la watu ambao waliitwa WATU WA KITABU, na
kamba kitabu hicho ni “cha Mwenyezi Mungu”, hii
ikiwa na maana kwamba walikuwa na kitabu chenye
maneno ya Mwenyezi Mungu. Na Watu hao ni
Mayahudi na Manasara (yaani Wakristo)

Je Kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu walichokuwa


nacho Mayahudi na Masanara ni kipi?

Katika Quran sura ya 2:113 Tafsiri ya Shekhe Ali


Muhsin Al-Barwan wa Madhehebu ya Suni tunasoma
kwamba;

‫ت ْاليَهُو ُد َعلَ ٰى‬ ِ ‫صا َر ٰى لَ ْي َس‬ َ َّ‫ت الن‬ِ َ‫َي ٍء َوقَال‬ ْ ‫صا َر ٰى َعلَ ٰى ش‬ ِ ‫ت ْاليَهُو ُد لَ ْي َس‬
َ َّ‫ت الن‬ ِ َ‫َوقَال‬
‫اللُ يَحْ ُك ُم بَ ْينَهُ ْم‬ َ ِ‫َاب ۗ َك ٰ َذل‬
َّ َ‫ك قَا َل الَّذِينَ َل يَ ْعلَ ُمونَ ِم ْث َل قَوْ لِ ِه ْم ۚ ف‬ َ ‫َي ٍء َوهُ ْم يَ ْتلُونَ ْال ِكت‬
ْ ‫ش‬
َ‫يَوْ َم ْالقِيَا َم ِة فِي َما كَانُوا فِي ِه يَ ْختَلِفُون‬

Na Mayahudi husema: Wakristo hawana lao jambo. Na


Wakristo husema: Mayahudi hawana lao jambo. Na ilhali
wote wanasoma Kitabu hicho hicho (Biblia). Na
kadhaalika walisema wale wasio jua kitu mfano wa kauli
yao hii. Basi Mwenyezi Mungu atahuku mu baina yao
5
Siku ya Kiyama katika yale waliyo kuwa wakikhitilafiana.
(Quran Sura 2:113

Hivyo ni wazi kwamba wakati wa Muhammad


kilikuwepo kitabu ambacho kitabu hicho ni cha
Mwenyezi Mungu, nacho Shekhe Barwan anasema
kinaitwa Biblia.

Je Mashekhe na Wanachuoni wakubwa ndani ya


Umma wa Kiislamu wanatafsri kuwa Sura ya 2:2
inakusudia kitabu gani kisichokuwa na Shaka?

Tuangalie baadhi ya Mashekhe wengine wanasemaje


kuhusu aya hii.

Tafsiri ya Ibn Kathiyr juu ya Sura ya 2:2

‫وقد ذهب بعض المفسرين فيما حكاه القرطبي وغيره أن ذلك إشارة إلى القرآن‬
‫الذي وعد الرسول صلى هللا عليه وسلم بإنزاله عليه أو التوراة أو اإلنجيل أو‬
‫نحو ذلك في أقوال عشرةا‬

Ibn Kathiyr anasema; Baadhi ya wafasiri kama vile


wale waliotajwa na imam Kurtuby na wengine kwamba
neno dhaalika, linaashiria Quran iliyoshushwa kwa mtume
Muhammad s.a.w ua Taurati au Injili na nyingine kama
hizo.

Tafsiri At-Twabariy juu ya Sura ya 2:2

‫ َوإِ ًذا َوجْ ه تَأْ ِويل‬, ‫ال ْن ِجيل‬


ِ ْ ‫ك ْال ِكتَاب } يَ ْعنِي بِ ِه التَّوْ َراة َو‬ َ ِ‫ { َذل‬: ‫َوقَ ْد قَا َل بَعْضه ْم‬
‫ك « يَ ُكون ِحينَئِ ٍذ‬ َ ِ‫ك ِلَنَّ « َذل‬ َ ِ‫ك إلَى هَ َذا ْال َوجْ ه فَ َل ُم ْؤنَة فِي ِه َعلَى ُمتَأ َ ِّوله َك َذل‬
َ ِ‫َذل‬
‫صحَّة‬ ِ ‫إخبَارًا ع َْن غَائِب َعلَى‬ ْ
6
Baadhi ya Wafasiri wa Quran wamesema neno “dhaalika
l-Kitaab”, yaani ni Tautati na Injili.

Hivyo basi tunaona kwamba wanachuoni wa


Kiislamu wamekhitilafiana juu ya ni kitabu gani hasa
kisichokuwa na Shaka kilichokusudiwa katika Sura
ya 2:2 ndani ya Quran. Baadhi wanadai kitabu hicho
ni Quran, na Baadhi wanasema kuwa kitabu hicho ni
Tautati na Injili yaani Biblia.

Kutokana na maelezo hapo juu, yaani tunapochunguza


Lugha asili ya Kiarabu juu ya neno lililotumika dhaalika,
naTunapoangalia historia ya Quran, pamoja na tafsiri za
baadhi ya wanachuoni wa Kiislamu, ni dhahiri kwamba;
Kitabu kisichokuwa na Shaka kilichokusudiwa katika
sura ya Quran Sura ya 2:2 ni Biblia Takatifu.

Je twaweza kuiamini Biblia?

Leo hii wengi wanatilia Mashaka usahihi wa Biblia,


Wengi hawaamini kama Biblia ni Maneno ya Mungu,
baadhi ya watu wanadhani kwamba Biblia ni kitabu
tu kinachoelezea historia ya Wana wa Israeli, na Visa
vya watu na wafalme mbalimbaali wa kale. Baadhi
wanaamini kwamba kumewahi kuwa na Maandiko
sahihi ya Mungu hapo zamani Kamavile Torati ya
Musa, Zaburi ya Daudi, na Injili ya Bwana Yesu,
lakini sasa maandiko hayo yameharibiwa na watu na
hivyo si ya kuamini tena. Hoja wanayo jaribu kujenga
hapa ni kwamba; Tunafahamu wazi kwamba Mungu
alituma manabii na kuwapatia vitabu ambavyo
vilihifadhi neno lake, kwa mfano wanasema, Musa
7
alipewa Torati, Daudi alipewa Zaburi na Yesu
alipewa Injili Takatifu na Muhammad akapewa
Furkan. Sasa Swali la Msingi huwa ni kwamba je, hii
Biblia alipewa nabii gani? Hoja nyingine inayoletwa
na watu wenye kutilia mashaka Biblia ni kwamba,
hata kama Biblia ina maneno ya mwenyezi Mungu, si
kwa usahihi wote kwani yawezekana kabisa kwamba
maneno hayo yameharibiwa au kuchafuliwa.

Tutajifunza kuhusu Biblia yenyewe hasa ni nini


na ilitoka wapi? Je imetufikiaaje sisi leo? Usahihi wa
kitabu hiki kiitwacho Biblia, na pia ikibidi tutaleta
mashahidi wa mambo haya kwa kuwa tunaambiwa
katika Kumb. 19:15 na Math. 18:16 “Jambo na
lithibitishwe kwa vinywa vya mashahidi wawili, au
watatu”

Je Biblia ni nini hasa?

Neno hili Biblia, Siyo neno la Kiswahili, bali ni


neno la Kiyunani (Kigiriki) yaani biblia. Neno hili kwa
Kiyunani ni wingi wa neno biblos, ambalo lina maana
ya gombo. Hivyo biblia ni mkusanyiko wa magombo
ambayo yalitumika zamani kuandikia. Watafisiri wa
Biblia walitumia neno hilo hilo kumaanisha kwamba
Biblia si kitabu kimoja bali ni mkusanyiko wa Vitabu
vingi. Biblia ni mkusanyiko wa vitabu vipatavyo 66,
vilivyogawanyika katika sehemu mbili yaani agano
la kale vitabu 39 na agano jipya vitabu 27.

Kabla ya Yesu, vitabu hivi viligawanyika


kutokana na waandishi wake. Kwa mfano, Vitabu
vilivyoandikwa na nabii Musa jumla vitabu 5 viliitwa
8
Torati ya Musa. Kisha kulikuwa na manabii wengine
walioandika vitabu kama jinsi walivyofunuliwa
ufunuo na Mwenyezi Mungu, vitabu vyao
vilikusanywa kundi moja na kuitwa Manabii. Kisha
sehemu ya mwisho ya mgawanyiko huu iliitwa
Zaburi iliyoandikwa na Daudi. Hivyo mtu aliweza
kusema Torati, Zaburi na Manabii, kumaanisha Biblia
nzima ya wakati huo. (Tazama Luka 23:27, 44).

Yesu alipokuja hapa duniani, mafundisho yake


yalikusanywa na kuunda mkusanyiko mwingine
wa vitabu ujulikanao kama Injili. Vitabu vinne
viliweza kupatikana na kuitwa majina kutokana na
wakusanyaji wa mafundisho hayo ya Yesu. Mitume
wa Yesu ambao pia walipewa uvuvio kwa njia ya
Roho mtakatifu kama ilivyokuwa ahadi ya Yesu
(Tazama Luka 24:49 na Matendo 1:8) waliweza
kuandika kundi lingine la mkusanyiko wa vitabu
lijulikanalo kama Nyalaka. Quran inathibitisha
katika Sura ya 5:111 kwamba wanafunzi wa Yesu
walipewa ufunuo (Wahyi) na Mwenyezi Mungu.

َ‫اريِّينَ أَ ْن آ ِمنُوا بِي َوبِ َرسُولِي قَالُوا آ َمنَّا َوا ْشهَ ْد بِأَنَّنَا ُم ْسلِ ُمون‬
ِ ‫ْت إِلَى ْال َح َو‬
ُ ‫َوإِ ْذ أَوْ َحي‬

Hivyo tunaweza kuwa na ujasiri wa kusema kuwa


maandiko yao waliyoandika ni Wahyi (Ufunuo) wa
Mwenyezi Mungu. Maandiko hayo yalikuwa kwa
mfumo wa Nyaraka mbali mbali zilizotumwa kwa
Makanisa ambako wanafunzi hao walihudumu, hii
ilikamilisha sehemu ya Biblia ijulikanayo leo kama
agano jipya.

Je Vitabu hivi vya Biblia vilipatikanaje?


9
Ufunuo wa Mungu kwa Wanadamu:- Hapo
mwanzo kabla ya dhambi kuingia duniani, Mungu
alizungumza na watu ana kwa ana Mfano tazama
Mwanzo 2:15,19. Lakini dhambi ilipoingia duniani,
kulitokea utengano kati ya Mungu na Mwanadamu.
Tunaona katika Mwanzo 3:9-10 Mwanadamu
anajificha usoni pa Mungu na Mungu Mwenyewe
akaamua kumfukuza atoke usoni pake Mwanzo
3:24. Mungu mwenyewe anasema katika Isaya 59:2
“Lakini maovu yenu yemewatenga ninyi na Mungu
wenu, dhambi zenu zimewaficha ninyi uso wake, ili
asisikie.”

Hivyo Mungu akatafuta njia nyingine mbadala ya


kuwasiliana na wanadamu na hii ni njia ya Manabii.
Tunasoma katika Waebrania 1:1 “Zamani Mungu
alisema na baba zetu kwa njia ya manabii mara
nyingi na kwa njia mbalimbali,” Pia tunaambiwa
kwamba “BWANA alimtumia nabii kumpandisha
Israeli kutoka Misri, kwa njia ya nabii alimtunza.”
Hosea 12:13

Je nabii ni nani?

Tunasoma katika 1Samweli 9:9


“Zamani katika Israeli, kama mtu alikwenda kuuliza
neno kwa Mungu, angalisema, “Njoo na twende kwa
mwonaji, kwa sababu nabii wa wakati huo alikuwa akiitwa
mwonaji

Tunaona hapa kwamba nabii ni mwonaji, kwa


maana ya kwamba huweza kuona na kuhabarisha
mambo ya usoni ambayo hayajatokea bado. Mungu
10
analo kusudi la kufunua mapenzi yake ya siku za
usoni kwa watu wake.
“Mimi ndimi Mungu, wala hakuna mwingine, Mimi
ndimi Mungu, wala hakuna mwingine aliye kama mimi.
Nitangazaye mwisho tangu mwanzo, naam, tangu zamani
za kale, mambo ambayo hayajatendeka” Isaya 46:9-10.

“Hakika BWANA hatafanya neno lolote bila kuwafunulia


watumishi wake manabii siri yake.” Amosi 3:7

Hivyo karama ya unabii ndiyo njia sahihi na


yenye mamlaka ya juu ambayo Mungu alichagua
kuwasiliana nasi. Kupitia njia hii ya manabii Mungu
huongea na watu wake. Maneno yanayotoka kwa
manabii ni maneno ya Mungu na siyo maneno ya
manabii. Yawezekana manabii wakawa na madhaifu
ya kibinadamu, hii haimanishi kwamba ujumbe wao
una mapungufu. Mara kwa mara manabii walitangaza
kwa watu asili ya ujumbe wao wakisema “Neno la
Bwana likaniijia”, “Bwana asema”, “lisikieni neno la
Bwana”. Wakati mwingine Mungu alitawala midomo
ya manabii walipozungumza maneno, mfano Ezekiel
3:26,27; Isaya 50:4-5; 57:19. Hawa manabii wa Mungu
waliongozwa na Roho wa Mungu kunena. 1Petro
1:20-21

Mungu alipowapatia manabii ufunuo wake


aliwaamurisha kuandika maneno hayo. Tunaona
Mungu akitoa amri hii ya kuyaandika maneno katika
kitabu tunaposoma kwa mfano katika Kutoka 34:27
Musa aliaambiwa aandike, kadhalika Yoshua (Yoshua
8:32,34;24:26), Daniel (Daniel 7:1), Isaya (Isaya 30:8),
Habakuki (Habakuki 2:2), Yeremia (Yeremia 36:2,30:2)
11
Yohana (Ufunuo 1:10-11) na manabii wengine.

Hii yaonyesha kwamba manabii wa mwenyezi


Mungu walijua kusoma na kuandika. Kamwe
hakukuwa na nabii wa Mwenyezi Mungu asiyejua
kusoma na kuandika. Mungu alikusudia hivyo ili
kwamba neno lake lisije likaharibiwa. Kama nabii
asingejua kusoma na kuandika uwezekano mkubwa
ungekuwapo mwandishi wake kuandika mambo
ambayo nabii hakuyatamka kwake na nabii huyo
asigundue.

Neno la Mungu lililoandikwa na Musa na manabii


wengine likawa ndiyo njia pekee ambayo Mungu
alijidhihirisha kwa Israeli na kwa mataifa yote.
Ilikuwa ni mpango wa Kimbingu kwamba vitabu
hivi vitasomwa na kusikiwa na mataifa yote katika
vizazi vijavyo ili kwamba watu wamjue Mungu kama
muumbaji na mwokozi kwa kutii neno lake wapate
mibaraka. (Tazama Yoshua 1:8)

Maandiko hayo ya manabii yalikusanywa pamoja


na kuitwa BIBLIA, yaani mkusanyiko wa vitabu vya
manabii wa Mwenyezi Mungu.

Je Biblia yaweza kuaminika.

“Mwaminini BWANA Mungu wenu hivyo mtathibitika,


wasadikini manabii wake nanyi mtafanikiwa” 2Nyakati
20:20

Ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa watu wake siku


zote umekuwa “wasadikini Manabii”
12
Tunasoma pia katika Qurani 2:136 kwamba

َ ُ‫ق َويَ ْعق‬ َ ‫نز َل إِلَ ٰى إِ ْب َرا ِهي َم َوإِ ْس َما ِعي َل َوإِ ْس َحا‬ُ ُ َّ ِ‫قُولُوا آ َمنَّا ب‬
‫وب‬ ِ ‫نز َل إِلَ ْينَا َو َما أ‬
ِ ‫اللِ َو َما أ‬
َ‫ق بَيْن‬ُ ِّ‫اط َو َما أُوتِ َي ُمو َس ٰى َو ِعي َس ٰى َو َما أُوتِ َي النَّبِيُّونَ ِمن َّربِّ ِه ْم َل نُفَر‬ ِ َ‫َو ْالَ ْسب‬
َ‫أَ َح ٍد ِّم ْنهُ ْم َونَحْ نُ لَهُ ُم ْسلِ ُمون‬

“Semeni: Tumemwamini Mwenyezi Mungu na


tulichotelemshiwana alichotelemshiwa Ibrahimu, na
Ismaili na Is’haka na Yakub na Wajukuu na alichopewa
Musa na Isa, na walichopewa manabii wote na Mola wao.
Hatutofautishi baina ya mmoja wao, na sisi ni wenye
kumnyenyekea yeye”

Mwenyezi Mungu hapendi tuvitilie mashaka


vitabu vyake. Ni dhambi kubwa kutilia mashaka
vitabu vya Mwenyezi Mungu na kuwaongoza watu
kufanya hivyo. Tunaambiwa katika Quran 32:22
kwamba

“Na ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule


anayekumbushwa aya za Mola wake kisha akazikataa?
Hakika sisi ni wenye kuchukua kisasi kwa waovu”.

Mungu anachukua kisasi kwa waovu wanaokataa


maneno yake au kuyatilia mashaka. Ikiwa tumeona
katika vitabu kwamba vitabu hivi viliandikwa na
manabii waliopokea uvuvio kutoka kwa Mwenyezi
Mungu, basi kutilia mashaka ni sawa na kujitakia
kisasi kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Kwa kuzingatia ushauri tuliopewa katika Kumb.


19:15 na Math. 18:16 ya kwamba
13
“Jambo na lithibitishwe kwa vinywa vya mashahidi
wawili, au watatu”

Basi tutaleta mashahidi mbali mbali ili kushuhudia


juu ya Usahihi wa Biblia

Shahidi wa Kwanza: Manabii wa Mwenyezi Mungu.

Hebu tuangalie Manabii wa Mwenyezi Mungu,


je kuna nabii yeyote alipokuja akatia mashaka juu
ya Maandiko ya nabii Mwenziye aliyemtangulia au
ya manabii wengine waliotangulia? Kabla ya yote
tunataka kuthibitisha ukweli huu, kwamba “Roho
za Manabii huwatii Manabii” 1Wakorintho 14:32.
Nabii yeyote wa kweli wa Mwenyezi Mungu hawezi
kuwapinga manabii waliomtangulia. Hii ni kwa
sababu, Roho aliyewavuvia manabii waliotangulia
ni Roho huyo huyo anaye wavuvia manabii wa
Mwenyezi Mungu. Kinyume chake iwapo atazuka
nabii kuwapinga manabii waliotangulia, tuwe
na uhakika kabisa kwamba huyo siyo nabii wa
Mwenyezi Mungu.

Imani ya Manabii juu ya Biblia:

Nabii Yoshua na Imani juu ya Maandiko Matakatifu

Huyu ni Nabii aliyefuata baada ya Musa, Je yeye


alikuwa na hofu yoyote ya Maandiko ya Torati ya
Musa? Hapana, bali aliamini Torati ya Musa kuwa
ni Maneno ya Mungu Tunaambiwa katika Yoshua
8:35 kwamba “Hakuna neno lo lote katika yale yote
ambayo Musa alikuwa ameamuru ambalo Yoshua
14
hakulisomea kusanyiko lote la Israeli, ikiwa ni
pamoja na wanawake na watoto na wageni walioishi
miongoni mwao”

Mwenyezi Mungu mwenyewe alimwambia


Yoshua kulishika Neno kama lilivyoandikwa na
Musa katika Torati. Yoshua 1:8 “Usiache Kitabu hiki
cha Torati kiondoke kinywani mwako, bali yatafakari
maneno yake mchana na usiku, ili upate kuwa
mwangalifu kufanya kila kitu sawasawa na yote
yaliyoandikwa ndani yake”

Baada ya Miaka Mingi kupita Tunaambiwa katika


kitabu cha Wafalme 22 kwamba Nabii Hilkia alikiona
kitabu cha Torati ndani ya Hekalu na hakuwa na
shaka nacho, kisha alikipeleka kwa mfalme, na
mfalme akapiga mbiu kuwakusanya watu waje
kukisikia kikisomwa masikioni mwao (Soma 2Falme
22 hadi 23)

Daudi na Imani juu ya maandiko matakatifu

Aliamini yote yaliyonenwa katika Torati na


sehemu nyingi katika Zaburi yake ananukuu Torati.
Kwa mfano Zaburi 77 hadi 78

Yesu na Imani juu ya maandiko matakatifu

Yesu Mwenyewe alipokuja baada ya miaka


mingi katika Mafundisho yake hatuoni mahali
popote akipuuzia Maandiko Matakatifu ya manabii
waliomtangulia. Mahali fulani aliwalaumu watu
wanaopuuzia Maandiko matakatifu akisema
15
“Mwapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala
uweza wa Mungu”. Kumbe kuyapuuzia maandiko
ni kujiletea upotevu. Shetani kwa kulijua hili
atawaongoza watu kuyapuuzia maandiko ili wapotee.

Katika mafundisho yake mengi Yesu aliwasisitiza


watu kusoma maandiko ama yeye mwenyewe
kunukuu sehemu nyingi za Maandiko ya maanabii.
Mfano ni katika aya zifuatazo.

Marko 12:26 linganisha na Kutoka 33:2-6, Luka 4:17


linganisha na Isaya 61:1-2 Mariko 12:10 linganisha na
Zaburi 118:22-23, Yohana 7:48 linganisha na Isaya 44:3
Yohana 13:18 linganisha na Zaburi 41:9

Hizi ni aya chache tu ndani ya Biblia zinazonyesha


jinsi Yesu alivyothamini maandiko Matakatifu. Ikiwa
Hadi wakati wa Yesu Maandiko matakatifu yalikuwa
sahihi kiasi cha Yesu Mwenyewe kuyatumia katika
maafundisho yake. Iweje leo watu wengine wazuke
kutupotosha eti Maandiko ya Mungu hayako sahihi.
Hakika hii ni Mbinu ya Mwovu Ibilisi kuwakosesha
watu. Yesu aliwahi kufundisha kwamba, usomaji wa
maandiko Matakatifu huongoza kwenye uzima wa
milele. Yohana 5:39

“Mwayachunguza maandiko…kwasababu…mna uzima


wa milele ndani yake…”.

Ni ujanja wa Shetani kuwaongoza watu kuyauuza


Maandiko Matakatifu ili waukose uzima wa milele.

Shahidi wa Pili: Quran Tukufu.


16
Mtume Mhammad S.A.W na Imani juu ya Maandiko
Matakatifu.

Muhammad S.A.W alizaliwa katika mwaka wa


570BK na anadaiwa kuwa alipata utume wake katika
mwaka wa 610BK. Hadi kufikia wakati huo tunaweza
kupata ushahidi kwamba Biblia ilikuwa Sahihi kabisa
isiyo na Mashaka ndani yake. Hii ni kwa sababu,
Muhammad mwenyewe alifunuliwa yakuwa

“Kama watu wa Kitabu (Wayahudi na Wakristo)


wangeamini na kumcha (Mwenyezi Mungu) bila shaka
tungaliwafutia makosa yao na kuwaingiza katika bustani
zenye neema. Na kama wangelisimamisha Taurati na
Injili na yale yaliyoteremshwa kwao kutoka kwa Mola wao,
hakika wangelikula vya juu yao na vya chini ya miguu
yao, wako watu miongoni mwao washikao njia njema…”
Qurani 5:65-66

Kwa mujibu wa aya hii ni wazi kuwa Muhammad


S.A.W anabainishiwa kwamba Kama watu wa
kitabu watasimamisha Taurati na Injili na yote
yaliyoteremshwa kwao wangeweza kuneemeka.
Haiwezekani Mwenyezi Mungu amletee Muhammad
maneno haya iwapo hadi kufikia wakati wake Biblia
ingekuwa imechafuliwa au kutiwa mikono kama
watu wanavyodai sasa.

Kisha Muhammad akaendelea kufunuliwa ya


kwamba awasisitize watu wa Kitabu (Mayahudi na
Wakristo) Kusimamisha Taurati na Injili.

“Sema: Enyi watu wa Kitabu! Hamna chochote mpaka


17
msimamishe Taurati na Injili (maana yake wafanye kama
isemavyo Torati na Injili) na yaliyoteremshwa kwenu
kutoka kwa Mola wenu” (kwa maana ya Maandiko ya
manabii wengine) Qurani 5:68.

Na ndipo akahitimisha kwa kusema wale


Mayahudi na Wakristo wafanyao vitendo vizuri
hawatakuwa na hofu wala hawatahuzunika

‫اللِ َو ْاليَوْ ِم‬


َّ ِ‫صا َر ٰى َم ْن آ َمنَ ب‬
َ َّ‫إِنَّ الَّذِينَ آ َمنُوا َوالَّذِينَ هَادُوا َوالصَّابِئُونَ َوالن‬
َ ‫ْال ِخ ِر َو َع ِم َل‬
َ‫صالِحًا فَ َل َخوْ فٌ َعلَ ْي ِه ْم َو َل هُ ْم يَحْ َزنُون‬

“Hakika walioamini, na Mayahudi na Masabihi, na


Wakristo watakao mwamini Mwenyezi Mungu, na siku ya
Mwisho, na wakafanya amali njema, basi wao hawatakuwa
na hofu wala hawatahuzuninka” Qurani 5:69

Ni dhahiri kwamba Biblia ilikuwa ikingali sahihi


hadi wakati wa Mtume Muhammad S.A.W.

Kupitia ufunuo aliopewa Muhammad S.A.W


aliwafundisha wafuasi wake akisema

“Wala msibishane na watu wa Kitabu ila kwa yale


yaliyobora, isipokuwa wale waliodhurumu miongoni
mwao. Na semeni: Tunaamini yaliyotelemshwa kwetu na
yaliyotelemshwa kwenu, na Mungu wetu na Mungu wenu
ni Mmoja nasi ni wenye kunyenyekea kwake” Qurani
29:46.

Hapa ni wazi kwamba Qurani inasisitiza waumini


kuamini yale yote ambayo watu wa kitabu walipewa
yaani, Taurati, Zaburi, Injili na Manabii wengine.
18
Haiwezekani Mtume Muhammad awaambie watu
wake kusema “tunayaamini yaliyoteremshwa kwenu”
ikiwa Torati na Injili vingekuwa vimechafuliwa.

Itakuwa vyema kusikiliza maneno ya Mwenyezi


Mungu kuliko kufuata matamanio ya watu
wanaojaribu katika nyakati hizi kutuchanganya
na kutugombanisha. Ni hakika kwamba yeyote
anayefundisha kuwa Biblia si kitabu cha Mwenyezi
Mungu huyo anajikinai mwenyewe nafsi yake na
kusudi lake ni kuwapotosha watu. Huyo ameikana
imani wala haamini kitabu chochote, kwani kusema
hivyo ni kupingana hata na Qurani yenyewe.

Shahidi wa Tatu: Sunna za Mtume Muhammad


S.A.W

Mtume alitumia Torati, Zaburi na Injili katika


mafundisho yake na pia alihukumu kwa vitabu
hivyo. Hapa ni baadhi ya mifano michache tu
kuonyesha Muhammad hakuwa na mashaka juu ya
vitabu vilivyotangulia.

‫ ع َْن‬،‫ أَ ْخبَ َرنَا َعلِ ُّي بْنُ ْال ُمبَا َر ِك‬،‫ َح َّدثَنَا ع ُْث َمانُ بْنُ ُع َم َر‬،‫ار‬ ٍ ‫َح َّدثَنِي ُم َح َّم ُد بْنُ بَ َّش‬
‫ب‬ِ ‫ قَا َل َكانَ أَ ْه ُل ْال ِكتَا‬،َ‫ ع َْن أَبِي هُ َر ْي َرة‬،َ‫ ع َْن أَبِي َسلَ َمة‬،‫ير‬ ٍ ِ‫يَحْ يَى ب ِْن أَبِي َكث‬
َِّ ‫اإل ْسالَ ِم فَقَا َل َرسُو ُل‬
‫للا‬ ِ ِ ‫ل‬ ْ
‫ه‬ َ ‫أل‬ ‫ة‬
ِ َِّ ‫ي‬ ‫ب‬ ‫ر‬
َ ‫ع‬
َ ْ
‫ال‬ِ ‫ب‬ ‫ا‬َ ‫ه‬َ ‫ن‬ ‫ُو‬
‫ر‬ ‫س‬
ِّ َ ‫ف‬ُ ‫ي‬ ‫و‬ ‫ة‬ َّ ‫ي‬ ‫ن‬ ‫ا‬ ‫ر‬
َ ‫ب‬ْ ‫ع‬ ْ
َ ِ ِ ِ ِ‫يَ ْق َرءُونَ التَّوْ َراةَ ب‬
‫ال‬
َّ ِ‫ َوالَ تُ َك ِّذبُوهُ ْم َوقُولُوا‏{‏آ َمنَّا ب‬،‫ب‬
ِ‫الل‬ ِ ‫ص ِّدقُوا أَ ْه َل ْال ِكتَا‬ َ ُ‫صلى هللا عليه وسلم‏»‏ الَ ت‬
‫‏‬.َ‫‏ اآليَ ‏ة‬.‫َو َما أُ ْن ِز َل إِلَ ْينَا َو َما أُ ْن ِز َل إِلَ ْي ُك ْ‏م}‏‏»‏‏‬

“Imepokelewa kutoka kwa Ubu Huraira: amesema, watu


wa Kitabu walikuwa wakisoma Taurati kwa Kiebrania
na wakawatafasiria Waislamu kwa Kiarabu. Mjumbe wa
Allah akasema (kuwaambia Waislamu), msiwaakubalie
19
watu wa Kitabu, wala msiwakatalie, lakini semeni
‘Tumemwanini Mwenyezi Mungu na yale yaliyofunuliwa
kwetu na yale yaliyofunuliwa kwenu” Sahihi Bukhari
Hadithi na. 7362

Hadithi hii yaonyesha kwamba, hadi wakati


wa Muhammad, Taurati ilikuwa sahihi kiasi cha
Muhammad kuwaambia waafuasi wake waiamini.

Katika Sahihi Bukhari Juzuu ya 4 hadithi namba


3635 tunasoma;

Amesimulia Abdullah bin Umar: Wayahudi walikuja


kwa mjumbe wa Allah na kumwambia kwamba,
Mwanamme mmoja na mwanamke kutoka miongoni
mwao alifanya uzinzi. Mjumbe wa Allah akawauliza, “Je
mmekuta imeandikwaje katika Torati juu ya adhabu ya
Ar-Rajm (kuponda mawe)?” Wakajibu, “tunatangaza kosa
lao kisha tunawachapa viboko. Abdullah bin Sam akasema
“nyie ni waongo; Torati ina amri ya Rajm”. Wakaleta na
kufungua Torati, na mmoja wao akaweka mkono juu ya
aya ya Rajm na akasoma aya iliyokuwa kabla yake na ile
iliyofuata. Abdullah bin Sam akasema, “ondoa mkono
wako”, alipoondoa mkono wake, Aya ya Rajm ilikuwa
imeandikwa hapo. Kisha wakasema, “Muhammad amesema
kweli; Torati inayo aya ya Rajm. Kisha Mtume akatoa amri
kwamba wote wapigwe mawe hadi kufa. (Abdullha bin
Umar akasema, “Nilimwona mwanamme akilala juu ya
mwanamke ili kumkinga asipigwe mawe”)

Kisha Mwenyezi Mungu akateremushia aya hizi;


20
Na watakuwekaje kuwa hakimu na wanayo Taurati
yenye hukumu za Mwenyezi Mungu? Kisha baada ya hayo
wanakataa, na hao si wenye kuamini (Sura 5:43) Hapa
tunaona kuwa hadi wakati wa Muhammad Torati
ilikuwa sahihi kiasi cha kutegemewa katika hukumu,
na Mwenyezi Mungu anamwonyesha mtume kuwa
Torati ni sahihi.

Hadithi zifuatazo zinaonyesha Muhammad alikuwa


akitumia Biblia katika Mafundisho yake.

‫ ع َْن أَبِي‬،‫ ع َْن هَ َّم ِام ب ِْن ُمنَبِّ ٍه‬،ٌ‫ أَ ْخبَ َرنَا َم ْع َمر‬،ِ‫للا‬
َّ ‫ أَ ْخبَ َرنَا َع ْب ُد‬،‫َح َّدثَنَا ُم َعا ُذ بْنُ أَ َس ٍد‬
ُ ‫للاُ أَ ْع َد ْد‬
‫ت‬ َّ ‫هُ َر ْي َرةَ ـ رضى هللا عنه ـ ع َِن النَّبِ ِّي صلى هللا عليه وسلم قَا َل‏ ‏» قَا َل‬
»‫َر‏‬
ٍ ‫ب بَش‬ ِ ‫ َوالَ َخطَ َر َعلَى قَ ْل‬،‫ت‬ ْ ‫ َوالَ أُ ُذنٌ َس ِم َع‬،‫ت‬ ْ َ‫لِ ِعبَا ِدي الصَّالِ ِحينَ َما الَ َعيْنٌ َرأ‬

“Imepokelewa kutoka kwa Abu Huraira (r.a): Amesema


Mtume (s.a.w), Allah amesema, ‘nimewaandalia waja
wangu, mambo (mazuri) ambayo, jicho halijawahi kuona,
wala sikio halijapata kusikia, wala moyo wa mwanadamu
hauwezi kufikiria”

Linganisha maelezo haya na Biblia:

“Lakini kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho


halijawahi kuona, wala sikio halikuyasikia, (wala
hayakuingia katika moyo wa mwanadamu) Mambo ambayo
Mungu aliwaandalia wampendao” 1Wakorintho 2:9

‫للاَ َع َّز َو َج َّل‬ َّ َّ‫ ((إِن‬:‫للاُ َعلَ ْي ِه َو َسلَّ َم‬َّ ‫صلَّى‬ َ ِ‫للا‬َّ ‫ قَا َل َرسُو ُل‬:‫ع َْن أَبِي هُ َر ْي َرةَ قَا َل‬
َ‫ك َوأَ ْنت‬َ ‫ قَا َل يَا َربِّ َكيْفَ أَعُو ُد‬.‫ت فَلَ ْم تَ ُع ْدنِي‬ ُ ْ‫ يَا ابْنَ آ َد َم َم ِرض‬:‫يَقُو ُل يَوْ َم ْالقِيَا َم ِة‬
‫ك‬ َ َّ‫ض فَلَ ْم تَ ُع ْدهُ أَ َما َعلِ ْمتَ أَن‬
َ ‫ قَا َل أَ َما َعلِ ْمتَ أَنَّ َع ْب ِدي فُ َلنًا َم ِر‬. َ‫َربُّ ْال َعالَمِين‬
َ‫ قَا َل يَا َربِّ َو َكيْف‬. ‫ط ِع ْمنِي‬ ْ ُ‫ك فَلَ ْم ت‬ ْ ‫يَا ابْنَ آ َد َم ا ْست‬. ُ‫لَوْ ُع ْدتَهُ لَ َو َج ْدتَنِي ِع ْن َده‬
َ ُ‫َط َع ْمت‬
‫ك َع ْب ِدي فُ َلنٌ فَلَ ْم‬ ْ ‫ قَا َل أَ َما َعلِ ْمتَ أَنَّهُ ا ْست‬. َ‫ك َوأَ ْنتَ َربُّ ْال َعالَمِين‬
َ ‫َط َع َم‬ ْ ُ‫أ‬
َ ‫ط ِع ُم‬
21
َ ُ‫ يَا ابْنَ آ َد َم ا ْستَ ْسقَ ْيت‬. ‫ك ِع ْن ِدي‬
‫ك فَلَ ْم‬ َ ِ‫ط َع ْمتَهُ لَ َو َجدْتَ َذل‬ ْ َ‫ك لَوْ أ‬ ْ ُ‫ت‬
َ َّ‫ط ِع ْمهُ أَ َما َعلِ ْمتَ أَن‬
ٌ‫ك َع ْب ِدي فُ َلن‬ َ ‫ قَا َل ا ْستَ ْسقَا‬. َ‫ك َوأَ ْنتَ َربُّ ْال َعالَمِين‬ َ ‫ قَا َل يَا َربِّ َكيْفَ أَ ْسقِي‬. ‫تَ ْسقِنِي‬
‫ك ِع ْن ِدي)) مسلم‬ َ ِ‫ك لَوْ َسقَ ْيتَهُ َو َجدْتَ َذل‬ َ َّ‫فَلَ ْم تَ ْسقِ ِه أَ َما إِن‬

“Amesimuria Abu Huraira (r.a), “Amesema mjumbe wa


Mwenyezi Mungu (S.A.W) Hakika Mwenyezi Mungu
S.W atasema siku ya kiyama. Ee mwanadamu, nilikuwa
mgonjwa lakini hukuja kuniona. Atasema: Ee Bwana
wangu, nitawezaje kukutembelea ikiwa wewe ni Bwana
wa ulimwengu? Allah atasema, je hukujua kwamba mja
wangu huyu na yule alikuwa mgonjwa lakini hukuenda
kumtembelea? Na je hukulifahamu hili kwamba kama
ungemtembelea ungenikuta mimi kwake? Ee mwanadamu,
nilikuomba chakula lakini hukunilisha. Naye atasema,
Bwana wangu nitawezaje kukulisha hali wewe ni Bwana
wa ulimwengu? Atasema Mwenyezi Mungu, Je hukujua
kwamba mja wangu huyu na yule alikuomba chakula
lakini hukumlisha? Je hukufahamu kwamba, kama
ungemlisha ungenikuta mimi kando yake? Allah atasema
tena, Eee mwanadamu, nilikuomba maji lakini hukunipa.
Naye atasema, Eee Bwana wangu ningewezaje kukupa
wewe maji nawe ni Bwana wa ulimwengu? Allah atasema,
mja wangu huyu na yule alikuomba maji lakini, na kama
ungemnywesha maji, ungenikuta mimi karibu yake”
Sahihi Muslim Kitabu 32 Hadith Namba 6232

Linganisha na maneno haya ya Yesu ndani ya Biblia

“Mwana wa Adamu atakapokuja katika utukufu


wake na malaika wote watakatifu pamoja naye, ndipo
atakapoketi juu ya kiti cha enzi cha utukufu wake. Mataifa
yotewatakusanyika mbele zake, naye atawatenga kama
mchungaji anavyotenga kondoo na mbuzi.Atawaweka
22
kondoo upande wake wa kuume na mbuzi upande wake
wa kushoto.Ndipo Mfalme atawaambia wale walioko
upande wake wa kuume, ‘Njoni, ninyi mliobarikiwa na
Baba yangu, urithini Ufalme ulioandaliwa kwa ajili yenu
tangu kuumbwa kwa ulimwengu. 35Kwa maana nilikuwa
na njaa mkanipa chakula, nilikuwa na kiu mkaninywesha,
nilikuwa mgeni mkanikaribisha, 36nilikuwa uchi
mkanivika, nilikuwa mgonjwa mkanitunza, nami nilikuwa
kifungoni mkaja kunitembelea.’Ndipo wale wenye haki
watakapomjibu wakisema, ‘Bwana, ni lini tulikuona una
njaa tukakulisha au ukiwa na kiu tukakunywesha?Lini
tulikuona ukiwa mgeni tukakukaribisha au ukiwa uchi
tukakuvika? Tena ni lini tulikuona ukiwa mgonjwa
tukakutunza au ukiwa kifungoni tukakutembelea?’ “Naye
Mfalme atawajibu, ‘Amin, amin ninawaambia, kwa jinsi
mlimvyotendea mmojawapo wa hawa ndugu Zangu walio
wadogo, mlinitendea Mimi.’Kisha atawaambia wale walio
upande Wake wa kushoto, ‘Ondokeni kwangu, ninyi
mliolaaniwa, nendeni kwenye moto wa milele alioandaliwa
kwa ajili ya ibilisi na malaika zake. Kwa maana nilikuwa na
njaa hamkunipa chakula, nilikuwa na kiu hamkuninywesha,
43nilikuwa mgeni nanyi hamkunikaribisha, nilikuwa
uchi hamkunivika, nilikuwa mgonjwa hamkunitunza na
nilikuwa gerezani nanyi hamkuja kunitembelea.’Ndipo
wao pia watajibu, ‘Bwana ni lini tulikuona ukiwa na njaa
au kiu, au ukiwa mgeni au uchi , au ukiwa mgonjwa na
kifungoni na hatukukuhudumia?’Naye atawajibu, ‘Amin,
amin nawaambia, kwa jinsi ambavyo hamkumtendea
mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo,
hamkunitendea mimi.’Ndipo hawa watakapoingia kwenye
adhabu ya milele, lakini wale wenye haki wataingia katika
uzima wa milele” Mathayo 25:31-46
23
Muhammad alifundisha Sala ya Bwana kwa
wafuasi wake

‫ ع َْن‬،‫ ع َْن ِزيَا ِد ب ِْن ُم َح َّم ٍد‬،‫ْث‬ ُ ‫ َح َّدثَنَا اللَّي‬،‫ب ال َّر ْملِ ُّي‬ ٍ َ‫َح َّدثَنَا يَ ِزي ُد بْنُ خَالِ ِد ب ِْن َموْ ه‬
ُ ‫ قَا َل َس ِمع‬،‫ ع َْن أَبِي الدَّرْ دَا ِء‬،‫ضالَةَ ب ِْن ُعبَ ْي ٍد‬
‫ْت‬ َ َ‫ ع َْن ف‬،‫ب ْالقُ َر ِظ ِّي‬ ٍ ‫ُم َح َّم ِد ب ِْن َك ْع‬
ُ‫للاِ صلى هللا عليه وسلم يَقُو ُل‏»‏ َم ِن ا ْشتَكَى ِم ْن ُك ْم َش ْيئًا أَ ِو ا ْشتَكَاهُ أَ ٌخ لَه‬ َّ ‫َرسُو َل‬
‫ض َك َما‬ ِ ْ‫ك فِي ال َّس َما ِء َواألَر‬ َ ‫ك أَ ْم ُر‬
َ ‫َّس ا ْس ُم‬َ ‫للاُ الَّ ِذي فِي ال َّس َما ِء تَقَد‬ َّ ‫فَ ْليَقُلْ َربُّنَا‬
َ‫ض ا ْغفِرْ لَنَا حُوبَنَا َو َخطَايَانَا أَ ْنت‬ ِ ْ‫ك فِي األَر‬ َ َ‫ك فِي ال َّس َما ِء فَاجْ َعلْ َرحْ َمت‬ َ ُ‫َرحْ َمت‬
»‫ك َعلَى هَ َذا ْال َو َج ِع فَيَ ْب َرأُ‏‬ َ ِ‫ك َو ِشفَا ًء ِم ْن ِشفَائ‬ َ ِ‫َربُّ الطَّيِّبِينَ أَ ْن ِزلْ َرحْ َمةً ِم ْن َرحْ َمت‬

“Imepokelewa kutoka kwa Abu Darda: amesema,


‘nilimsikia mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) akismea
‘ikiwa mmoja wenu anaumwa ugonjwa wowote, au ndugu
yake anaumwa, basi na aseme, Bwana wetu ni Allah
aliyeko mbinguni, Jina lako ni Takatifu, amri zako zatawala
mbinguni na duniani, kama rehema zako zilivyo mbinguni
utujaalie rehema hapa duniani. Utusamehe dhambi na
makosa yetu, wewe ni Bwana wa watu wema. Tuma
rehema kutokana na rehema zako na uponyaji kutokana
na ponyo lako, ili kwamba ugonjwa huu uweze kupona.”
Sunan Abu Daud Hadithi na. 3892

Katika Quran, hakuna hata aya moja inayosema


kwamba, Taurati, Injili na Zaburi virikuwa
vimeharibiwa hadi kuja kwa Muhammad.
Badala yake ndani ya Quran kumejaa maneno
yanayoonyesha kuwa Vitabu hivi ni ufunuo sahihi
kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

“Hakika tulitelemsha Taurati yenye muongozo na nuru,


ambayo kwayo Manabii waliojisalimisha (kwa Mwenyezi
Mungu waliwahukumu Mayahudi na watawa na
maulamaa, kwa sababu waliktakiwa kuhifadhi Kitabu cha
24
Mwenyezi Mungu, na walikuwa mashahidi juu yake. Basi
msiwaogope watu, bali mniogope (Mimi), wala msiuze
aya zangu kwa bei ndogo na wasio hukumu kwa yale
aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio Makafiri”
(Sura 5:44)

“Na tukamfuaatisha Isa bin Maryam katika nyao zao,


kuyahakikisha yaliyokuwa kabla yake katia Taurati, na
tukampa Injili iliyomo ndani yake muongozo na nuru
inyaosadikisha yaliyokuwa kabla yake katika Tautati na
muongozo na mawaidhsa kwa wenye kumcha” (Sura 5:46)

Ni wazi kutokana na aya hizi kwamba Taurati na


Injili ni Nuru kwa ajili ya wale wamchao Mwenyezi
Mungu. Ikiwa watu wanatokea na kukuambia
usiziamini tena Taurati na Injili, ni hakika watu hawa
wanakunyang’anya Nuru aliyotupatia Mwenyezi
Mungu na wanataka utembea gizani na Mwisho
utaangamia katika Moto.

Katika Sura ya 5:46 tumeona kwamba, nabii Isa


alikuja kusadikisha yaliyokuwa kabla yake, yaani
Taurat na Injili. Mafundisho ya Nabii Isa (Yesu)
yanaonyesha kuwa hadi kufikia wakati wake, Taurat
na Zaburi vilikuwa sahihi kiasi cha yeye mwenyewe
kusema.

“Mwayachunguza maandiko…kwasababu…mna uzima


wa milele ndani yake…”. Yohana 5:39

Yesu alifundisha kwamba, Taurat, Zaburi na


Manabii haviwezi kutanguliwa (kubadirishwa),
mpaka mbingu na nchi zitakapopita;
25
“Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii,
la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana amin,
nawaambia, mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi
moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote
yatimie. Mathayo 5:17-18

Shahidi wa Nne: Historia inathibitisha kwamba


Biblia haijawahi kuharibiwa

Mwanahistoria Flavius Josephus (Karne ya


Kwanza) akiandika katika mwaka wa 90 alitaja
vitabu 24 vilivyokusanya historia ya Wayahudi ya
kila ambacho kiliaminika kama Uvuvio.

Vitabu 5 vilindikwa na Musa, Vitabu 13 viliandikwa


kati ya Musa na Mfalme Atashasta (Artaxerxes) wa
Waajemi. Vitabu 4 vilikuwa vimejumuisha mashairi
(vitabu vya Mashairi) na Nyimbo, Zaburi, Methali,
Mhubiri, Maombolezo (Against Apion 1:38-40)

Kisha Josephus akaendelea kusema

“Ni kweli kwamba Historia yetu imekuwa ikiandikwa


toka wakati wa Atashasta, lakini maandiko hayo
hayajachukuliwa kuwa ni maandiko sawa na maandiko ya
kale ya Mababu zetu. Hii ni kwa sababu, hakuna mfuatano
wa Manabii toka wakati huo.Na ni kwa kiasi gani
tumekuwa na msimamo mkali na kuaenzi maandiko hayo
na kuchunga asije mtu akaongeza katika maandiko—Toka
wakati huo, haijawahi kutokea mtu kuongeza maandiko
hayo au kupunguza au kufanya badiriko lolote ndani yake.”
(Against Apion 1:38-40)
26
Wayahudi hadi kufikia mwaka wa 100 walikuwa
na uhakika kabisa kwamba vitabu vya manabii kama
walivyopokea toka kwa Mwenyezi Mungu viko sahihi
na havijawahi kuchafuliwa ama kutiwa mikono kama
watu wengine wanavyotaka kutuaminisha siku hizi.

Shahidi wa Tano: Uvumbuzi wa Mabaki ya kale

Magombo kando ya Bahari mfu (Dead sea Scrolls)

Mnamo mwaka 1947 Kijana mmoja wa Kiarabu


aliyekuwa akichunga kondoo, alipoteza kondoo
wake mmoja. Katika harakati za kumtafuta alianza
kutupa mawe katika pango lililokuwa mlimani, ndipo
aliposikia sauti mfano wa kuvunjika kwa vyungu.
Kisha akamwita mchungaji mwenzie waliyekuwa
wakisaidiana naye. Wote wawili waliingia katika
pango hili ambamo ndani yake walikuta mitungi
ya vyungu vyenye urefu wa inchi 25 hadi 29 na
upana wa inchi 10. Ndani yake waliona Magombo
ya ngozi yaliyovingilishwa. Vijana hawa walidhani
ya kwamba wameokota hazina zilizositirika na hivyo
walianza kutembea mjini Yerusalemu kutafuta wateja
bila mafanikio. Ndipo walipofanikiwa kuyauza kwa
Padre Athanasius Samweli wa Kanisa la Watawa wa
Mt Mariko wa Orthodox Syria. Magombo mengine
waliyauza kwa Dr. John C. Trever Mkurugenzi wa
American School of Oriental Research. (TheThompson
chain Reference Bible, Fifth Improved Edition uk.
1740)

Baadaye eneo hili lilifanyiwa uchunguzi na


wataalamu wa mambo ya kale, uchimbaji na utafiti
27
ulifanyika zaidi na kugundua magombo zaidi ya
800 katika eneno hili. Utafiti zaidi ulionyesha kuwa
magombo haya yaliachwa pale tokea karne ya 1
(Mwaka 100AD) na Wayahudi wa kundi la Wa-Esene.
Hawa inasadikiwa kuwa walikuwa wayahudi wenye
msimamo mkali waliojitenga kutoka kwa wayahudi
wengine ili kuepuka uchafu na ufisadi wa kidini
uliofanywa na Wayahudi waliomwasi Mwenyezi
Mungu. Wao waliamini kwamba wameitwa na
Mungu kuitengeneza njia ya Bwana na kuyanyosha
mapito yake. Yohana mbatizaji anadaiwa kuwa
alikuwa miongoni mwa watu wa kundi hili.

Utafiti wa magombo yote yaliyogunduliwa


toka mwaka 1947 hadi mwaka 1952 umeonyesha
kuwa Karibia vitabu vyote 66 kama tulivyonavyo
leo kwenye Biblia vimepatikana katika magombo
mbalimbali. Hii inatoa ushahidi mwingine kwamba
hakuna andiko lolote lililopotea ama kuharibiwa
katika Biblia. Neno linasema “Nasi tunalo pia neno
la hakika zaidi la unabii, ambalo mtafanya vyema
kuliangalia kwa bidii kama vile nuru inayong’aa
gizani, hadi kupambazuka na nyota ya asubuhi
itokee mioyoni mwenu” 2Petro 1:19

Rafiki yangu napenda kukutia moyo endelea


kuisoma Biblia yako ukiwa na uhakika kwamba,
unashikilia mkononi mwako, MANENO YA
MWENYEZI MUNGU ALIYE HAI, yaliyonenwa
kupitia vinywa vya manabii wake. Tembea kifua
mbele na uhakika kwamba, neno hilo lililoandikwa
humo ni kama lilvyotoka kwa Mwenyezi Mungu
28
tokea wakati wa manabii hao hadi sasa. Iamini Biblia
kama kiongozi wako katika maisha ya kiroho na
kwamba “ndani yake mna uzima wa milele”. Yohana
5:39
Kwa maelezo zaidi
Wasiliana nasi kwa simu:

+255 674 461 761

You might also like