You are on page 1of 14

‫آداب ﺗـﻼوة اﻟـﻘـﺮآن اﻟـ�ﺮﻳـﻢ‬

Muhusika: Kamati Ya Kudumu Ya Kutoa Fatwa Chini Ya Uongozi Wa


Mwanachuoni Mkubwa Abdul-aziz Bin Baz -allah Amrahamu –

Tarjama: Abuu Thurayah Ismail Seiph Mbonde-Allah amuhifadhi


Imekusanywa na: fawaidusalafiyatz.net
◾️ ‫سـئلـت اللّجنة الدائمة لإلفتاء‬
ُ
ّ ‫شــي ُخ‬
‫رحمهُ هللا‬- ‫العّلمــة عـبدُ الـعَ ِزيـز بن بـاز‬ َّ ‫برئاسة ال‬
Iliulizwa kamati ya kudumu ya kutoa fatwa chini ya uongozi
wa mwanachuoni mkubwa Abdul-Aziz bin Baz -Allah
amrahamu –

‫مـا هـي آداب تـالوة الـقـرآن الـكـريـم ؟‬


Ni zipi adabu za kusoma qurani tukufu?
ُ‫ــــــواب‬
َ ‫ال َج‬
Jawabu :
‫لـتـالوة الـقـرآن آداب مـنهـا‬
Kusoma qurani kuna adabu katika hizo (ni):
‫ وال‬، ‫ ال ريـاء وال سـمعة‬، ‫للا‬
ُ ‫صا لـوجه‬
ً ‫– أن يـكون قـارئ الـقرآن عـمله خـال‬١
‫يـطلب بـه أجـرة ؛ ألن عـبادته تـقربًا إلـى للا‬
1- Awe msomaji qurani matendo yake ni kwa ajili ya kutafuta
radhi za Allah, si kwa kujionesha na wala si kwa kutaka
kusikika na wala asitake ujira kwa huko (kusoma qurani) kwa
sababu ibada yake ni kwa ajili ya kujiweka karibu na Allah.

‫– مـن آداب تـالوة الـقرآن أن يـستعيذ بـاهلل مـن الـشيطان الـرجيم عـند ابـتدائه‬٢
‫ ويـقرأ بـسم للا الـرحمن الـرحيم إذا كـان ابـتداء قـراءته مـن أول‬،ُ ‫للـقراءة‬
‫الـسورة عـدا سـورة الـتوبة‬
2- Miongoni mwa adabu za kusoma qurani ni (msomaji)
ajikinge kwa Allah kutokana na Shetani aliyefukuzwa katika
1
rehema za Allah wakati wa kuanza kwake kusoma ,na
atasoma "kwa jina la Allah mwingi wa rehema mwenye
kurehemu " ikiwa mwanzo wa kusoma kwake ni mwanzoni
mwa sura isipokuwa suratu ttaubah.

‫ فـإن كـانت‬،ُ ‫– يـستحب لـقارئ الـقرآن عـند قـراءته أن يـكون عـلى وضـوء‬٣
‫قـراءته مـن مـصحف وجـب عـليه الـوضوء ؛ لـقوله ﷺ‬
«‫»ال يمس القرآن إال طاهر‬
3- Ni suna kwa msomaji wa qurani wakati wa kusoma kwake
awe na udhu ,na kukiwa kusoma kwake ni katika (kuushika)
msahafu ni wajibu juu yake achukue udhu kwa kauli yake-
swala na salamu za Allah zimfikie- :
"Asiiguse qurani ila aliyekuwa twahara "

Maelezo ya mfasiri :
Hizi ni miongoni mwa adabu za kusoma qurani ambazo
wamezitaja wanavyuoni hawa na wameweka idadi yake ni
kumi na moja (11):
1- Aitakase nia yake pindi anaposoma qurani kwa maana
asome kwa ajili ya kutaka thawabu na radhi za Allah na bila
shaka neema kubwa kabisa peponi ni kuuona uso wa Allah -
mtukufu .
2- Na anapoanza kusoma qurani ajikinge kwa Allah na shetani
aseme hivi:
‫أعوذ باهلل من الشيطان الرجيم‬

2
(Najikinga kwa Allah kutokana na Shetani aliyefukuzwa
katika rehema za Allah).
Na anapoanza mwanzo wa sura asome :
ِ‫الر ِح ْي ِم‬
َّ ‫ن‬ِِ ‫الر ْح ٰم‬
َّ ِ‫للا‬
ِ ‫بِس ِِْم‬
(Kwa jina la Allah mwingi wa rehema na mwenye kurehemu).
Isipokuwa mwanzo wa suratu ttaubah asianze na Bismillah.
3- Ni suna anaposoma qurani awe na udhu kwa yule
anayesoma bila ya kushika msahafu au akatumia msahafu wa
mtandaoni, ama yule atakayeshika msahafu huyo ni lazima
achukue udhu kwa sababu ni haramu kuishika qurani bila ya
udhu.

‫ى هـيئة حـسنة ولـباس حـسن‬


ُ ‫– يـستحسن أن يـجلس عـند قـراءة الـقرآن عـل‬٤
‫مـستقبل الـقبلة‬
‫ق بالـقرآن‬
ُ ‫وفـي مـكان مـحترم يـلي‬
4- Ni suna pindi anaposoma qurani aketi mkao mzuri na (avae)
mavazi mazuri (aketi) hali ya kuelekea qibla na katika sehemu
yenye kuheshimika inayonasibiana na quran.

، ‫– يـستحب أن يـقرأ بـخضوع وخـشوع وتـمهل وتـدبر وتـفكر فـي آيـاته‬٥


‫ وال يـقطع الـقراءُة بـكالم‬،ُ ‫ن الـقرآن‬
ُ ‫ف بـقلبه وحـواسه لـما يـقرأ مـ‬
ُ ‫ومـنصر‬
‫اآلدمـيين مـن غـير حـاجة‬
5- Inapendeza asome kwa unyenyekevu na utulivu wa viungo,
kwa upole, kuzingatia na kufikiria katika aya zake na

3
aupeleke moyo wake na viungo vyake kwa kile anachokisoma
katika quran na wala asikate kisomo kwa Sababu ya
kuzungumza na wanadamu bila ya haja.
Maelezo ya mfasiri:
Adabu ya nne (4):
Ni kuisoma qurani kwa adabu zilizotajwa hapo na kufanya
hivyo ni katika kukitukuza kitabu cha Allah na hivyo ndivyo
walivyokuwa wema waliopita mfano:
‫ رحم ُه للا‬- ‫كان أبو العالية الرياحي‬
Alikuwa Abuu Al-'aliyah Arriyahiy -Allah amrahamu -
‫ واستقبل القبلة‬،‫ وارتدى ثيابه‬،‫ لبس عمامة‬،‫إذا قرأ اعت ّم‬
Pindi anaposoma qurani huzungusha kilemba kichwani (yaani)
huvaa kilemba na huvaa nguo yake (nzuri) na huelekea
(upande wa) kiblah.
٢٧/١ ‫تفسير القرطبي‬

Kwa hiyo unapotaka kusoma qurani vaa nguo yako nzuri paka
manukato unukie, na tafuta sehemu nzuri yenye utulivu wala
usisome qurani sehemu ambayo inapigwa mziki au
yanafanyika maovu, na kaa mkao mzuri hali ya kuelekea kibla
kwa sababu ni suna kuelekea kibla katika vikao mbalimbali na
haswa vikao vya ibada, na ubora huu umethibiti katika kauli
yake Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie-:
«ُ‫ست ُ ْق ِب َِل ِب ِِه ْال ِق ْبلَ ِة‬ ِ ِ ‫ف ْال َم َجا ِل‬
ْ ‫س َما ا‬ َِّ ِ‫ َوإ‬،ً‫ن ِل ُك ِِل ش َْيءِ ش ََرفا‬
َِ ‫ن ش ََر‬ َِّ ِ‫»إ‬

4
Hakika kila kitu kina kitukufu chake, na hakika kikao
kitukufu ni kile (kikao) kilichoelekezwa kiblah.
‫عنه‬
ُ ُ‫ي للا‬
َُ ‫ض‬
ِ ‫عبَّاسُ َر‬
َ ‫ْن‬
ُِ ‫ن اب‬
ُِ ‫ع‬
َ ‫رواه الطبراني في الكبير‬
Adabu ya tano (5):
Aisome qurani kwa mazingatio na unyenyekevu na kufikiria
maana za aya kama alivyosema Allah -aliyetukuka -:
َُ ‫ِك َٰت َبُ أَنزَ ْل َٰنَهُ ِإلَي‬
ِ َ‫ْك م َٰبَ َركُ ِلّيَدَّبَّر ٓوُاْ َءا َٰيَتِِۦه َو ِليَت َ ُذَ َّك َُر أ ْولوُاْ ْٱأل َ ْل َٰب‬
ُ‫ب‬
(Na hiki) Kitabu; tumekiteremsha kwako,chenye baraka
nyingi ;ili wapate kuzizingatia Aya zake,na ili wenye akili
wawaidhike.
٢٩ ‫ص‬
Hii ni dalili kuwa wenye kuisoma qurani na wakazifiria aya
zake na kuzizingatia na wakawaidhika nayo basi hao ndio
wenye akili yaani akili ya uongofu na bila shaka kusudio
kubwa la kuteremshwa qurani ni kuwaidhika nayo.

‫– يـستحب أن يـرتل الـقرآن بـصوت حـسن مـع تـبيين الـحروف والـحركات‬٦


‫والـعناية بـأحكام الـتجويد حـسب قـدرته‬
6- Ni suna aisome quran kwa utaratibu na kwa sauti nzuri
pamoja na kuzibainisha herufi na haraka na kutilia umuhimu
hukumu za taj-widi kadri ya uwezo wake.

‫ فـينبغي أن ال يـزعجهم‬، ‫– إذا كـان أحـد يـسمعه وهـو يـقرأ الـقرآن أو يـصلي‬٧
‫ بـرفع الـصوت أو يـشوش عـلى مـن يـصلي‬.
5
7- Kukiwa kuna yeyote anayemsikia na hali huyo (mtu pia)
anasoma quran au anaswali basi inatakikana asiwashughulishe
(watu) hao kwa kunyanyua sauti au kumchanganya yule
anayeswali.
Maelezo ya mfasiri :
Adabu ya ya sita katika adabu za kusoma qurani ni kuwa
msomaji anatakiwa aisome qurani kwa utaratibu, na kwa
sauti nzuri, na kwa kuziweka wazi herufi kama kaaf,alifu n.k
na pia kuziweka wazi haraka kama dhwammah ,fat'hah
n.k ,na pia atilie umuhimu hukumu za taj-wid, kwa sababu
Allah -aliyetukuka-amemuamrisha Mtume wake -swala na
salamu za Allah zimfikie- aisome Qur'an kwa uzuri na upole
na kuzingatia pale aliposema:
ً ‫ل ْالق ْرآنَُ ت َ ْر ِت‬
ُ‫يال‬ ُِ ّ ‫َو َر ِت‬
Na soma Qur'an kwa utaratibu /kwa utungo .
٤ ‫المزمل‬

Na vile vile Mtume - swala na salamu za Allah zimfikie-


amehimiza kuisoma qurani kwa sauti nzuri pale aliposema:
‫ز ِيّنوا القرآنَُ بأصواتِكم‬
Kipambeni (kisomo cha) Qur'an kwa sauti zenu .
: ٧٤٩‫صحيح ابن حبان |الصفحة أوالرقم‬

Na adabu ya saba ni kuwa mtu anapokuwa anasoma Qur'an na


kukawa na mtu au watu wanaomsikia na hali hao watu pia
6
wanasoma Qur'an au wanaswali basi anatakiwa asinyanyue
sauti katika kusoma kwake qurani kwa sababu hilo litapelekea
kuwachanganya hao wenzake wanaosoma Qur'an au
wanaoswali na imethibiti hadithi kuwa siku moja Mtume -
swala na salamu za Allah zimfikie- alikuwa amekaa itikafu
msikitini akawasikia Maswahaba wakinyanyua sauti zao kwa
kusoma Qur'an na hali Mtume akiwa katika jengo lake la
itikafu basi akafungua panzia na akasema:
َُّ َ‫ وال يرفع‬، ‫ضا‬
ُ‫ن بعضكم على بعض‬ َُّ ‫ فال يؤذ‬، ‫إن كلَّكم مناجُ ربَّ ُه‬
ً ‫ِين بعضكم بع‬ َُّ ‫أال‬
ُِ‫في الصالة‬: ‫بالقراءةُِ أ ُو قال‬
Sikilizeni hakika nyote (nyinyi kila mmoja) ana mnong'oneza
Mola wake,basi baadhi yenu wasiwaudhi baadhi na wala
baadhi yenu wasinyanyue sauti juu ya baadhi kwa kusoma
(Qur'an). Au alisema katika swala.
11915 ‫أخرجه أحم ُد‬

‫ السنن الكبرى‬، ‫والنسائي في‬

8092 ‫باختالف يسي ُر‬

Ufafanuzi:
Ni haramu kunyanyua sauti kwa kusoma Qur'ani likiwa
hilo litamchanganya mtu anayeswali kwa maana ikithibiti
kuwa hiyo sauti inawaudhi na kuwachanganya basi itakuwa ni
haramu ,na kama hiyo sauti haiwachanganyi na kuwaudhi basi
jambo hilo linachukiza.

‫ وال يـمططه ويـمده‬، ‫– ال يـهذ الـقارئ الـقرآن هـذًّا فـال يـفهم عـنه مـا يـقول‬٧
ً ‫ بـل وسـ‬، ‫مـدًّا يـخل بـألفاظه فـيخرجه عـن الـمقصود مـن تـالوته‬
‫طُا بـين ذلـك‬
7
8- Msomaji Qur'ani asiisome haraka haraka hii Qur'an (akawa)
hakifahamu kile anachokisema na wala asizirefushe (herufi)
na kuvuta (herufi) uvutaji unaoharibu (maana ya) matamko
yake akaitoa katika makusudio yake ya kuisoma, bali (aisome)
kati na kati baina ya hivyo.

‫ وال بـترجيع‬، ‫ق‬


ُ ‫ كـألحان أهـل الـفس‬، ‫ن بـألحان الـغناء‬ ُ ‫– ال يـقرأ الـقرآ‬٩
‫ فـإن ذلـك كـله ال يـجو ُز‬، ‫الـنصارى وال نـوح الـرهبانية‬
9- Na wala asiisome Qur'an kwa sauti za miziki,kama sauti za
waovu na wala (asisome) kwa sauti za Manaswara na wala
(kwa) vilio vya watawa na hakika yote hayo hayafai
Maelezo ya mfasiri:
Adabu ya nane katika adabu za kusoma Qurani ni msomaji
kuisoma Qur'an polepole bila ya kuharakisha kwa sababu
akisoma kwa haraka itampelekea asizingatie maana yake, na
wala asivute herufi za kuvuta kupita kiasi na wala
asizikate ,na kuna nasaha alizozitoa ibn Masud -Allah
amridhie kuhusu hili pale aliposema:
َ ‫ َو َح ِ ّركوا بِ ِهُ ْالقل‬،‫ع َجائِبِ ِه‬
،‫وب‬ َُ َ‫ ِقفوا ِع ْن ُد‬،‫ش ْع ِر‬
ّ ِ ‫الَ تَهذوهُ هَذ ال‬ ُ ‫ل َو‬ ُِ ‫الَ ت َ ْنثِروهُ نَثْ َُر الدَّ ْق‬
ُ
‫ورة‬
َ ‫س‬ ِ ‫الَ يَكونُ َه ُُّم أ َ َحدِك ُْم‬
ُّ ‫آخ َُر ال‬ ُ ‫َو‬
Msiitawanye hiyo (Qurani) utawanyaji wa tende zilizochakaa
na wala musiisome kwa haraka (kama) yanavyosomwa
mashairi kwa haraka, simameni katika maajabu yake na
zitingisheni (nyoyo) kwa hiyo (Qur'an) na wala yasiwe
makusudio ya mmoja wenu (kufika) mwisho wa sura.

8
٨٧٣٣( ‫أخرجه ابن أبي شيبة في المصنف‬

Ufafanuzi:
Hapa ibn Masud -Allah amridhie- anatutahadharisha kuwa
tusisome Qur'an kwa haraka ikawa inasikika sauti lakini
haifahamiki maana yake kama vile tende zilizochakaa na
kukauka pindi zinaposambazwa hutoa sauti za kugongana
gongana, na vile vile tusisome Qur'an kwa haraka kama
washairi wanaposoma mashairi yao ambao malengo yao ni
kusifiwa kwa ufasaha na uhodari waliokuwa nao na wala
hawazingatii kile wanachokisoma.
Na akatuamrisha pindi tunaposoma Qur'an tuzingatie maana
yake na maajabu yaliyomo ndani na maana mbalimbali na
uongofu, na vilevile nyoyo zetu zitingishike kama
zinavyotingishika ndimi zetu pindi tunaposoma kitabu cha
Allah ,na wala isiwe pupa ya msomaji ni kumaliza sehemu
aliyoikusudia kuisoma kwa haraka bila ya kuzingatia bali
asome kwa kuzingatia na kuifanyia kazi.
Adabu ya tisa ni mtu kutoisoma Qur'an kwa sauti za miziki,
au sauti za Manaswara au sauti za vilio vya watawa wao
kufanya hivyo ni haramu

‫ن يـمسك عـن القراءة إذا تـثاءب حـتى يـذهب‬ ُ ‫– ومـن آداب الـقراءة أ‬١٠
‫ والـتثاؤب مـن الـشيطان‬، ‫الـتثاؤب ؛ تـعظي ًما هلل ؛ ألنـه مـخاطب ومـناج لـربه‬
10 - Na katika adabu za kusoma (Qur'an msomaji) ajizuie
na kusoma pindi atakapo piga miayo mpaka imuondoke

9
miayo kwa kumtukuza Allah kwa sababu huyo (msomaji)
ni mwenye kumsemesha na Kumnong'oneza Mola wake
mlezi na kupiga miayo ni kunatokana na Shetani.

‫ وأن‬، ‫ن آداب الـقراءة أن يـقف عـند آيـة الـرحمة فـيسأل للا مـن فـضله‬ ُ ‫– ومـ‬١١
‫ وعـند آيـة الـتسبيح فـيسبح‬، ‫يـقف عـند آيـة الـعذاب والـوعيد فـيستجير بـاهلل مـنه‬
، ‫وذلـك فـي غـير الـصالة الـمفروض ُة‬
11- Na katika adabu za kusoma (Qurani) ni msomaji
kusimama wakati wa aya ya rahmah na amuombe Allah
katika fadhila zake na asimame wakati wa aya ya adhabu
na makemeo na ajikinge kwa Allah kutokana na hiyo
(adhabu) ,na wakati wa aya ya tasbih alete tasbih ,na hilo
(asilifanye) katika swala za faradhi.

Maelezo ya mwandishi:
Adabu ya kumi katika adabu za kusoma Qur'an ni msomaji
ajizuie kusoma pindi anapopiga miayo mpaka amalize kupiga
miayo kwa sababu kufanya kwake hivyo ni kumtukuza Allah
kwani msomaji Qur'an anamsemesha Mola wake Mlezi na ana
mnong'oneza na kupiga miayo kunatokana na Shetani ,kama
alivyosema Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie-:
«‫ان‬ َ ‫ش ْي‬
ُِ ‫ط‬ َّ ‫التَّثَاؤبُ ِمنَُ ال‬، .. »
“Kupiga miyayo kunatokana na Shetani...”
‫البخاري‬

10
Kupiga miayo ni alama ya kuchoka na Shetani huipenda hali
hii kwa muumini na pia mtu anatakiwa aache kusoma Qur'an
anapokuwa na usingizi mpaka akawa anasinzia anatakiwa
aache kusoma Qur'an kwa muda huo kwa sababu anaweza
akachanganya herufi au akakosea kusoma au aya
zikachanganyika, au akataja herufi isiyokuwepo kama
alivyosema Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie:
‫ فليضطجع‬،‫ فلم يدر ما يقول‬،‫ فاستعجم القرآن على لسانه‬،‫إذا قام أحدكم من الليل‬
Pindi mmoja wenu atakaposimama usiku Qur'an ikawa ngumu
katika ulimi wakeُ(akawa)ُhajuiُkileُanachokisema,basiُalale”
‫رواه مسلم وغيره‬
Adabu ya kumi na moja na ya mwisho katika adabu
walizozitaja hawa wanavyuoni ni adabu ya msomaji Qur'an
kusimama pindi anaposoma aya inayotaja rahma za Allah na
amuombe Allah katika rehma zake na fadhila zake, na pia aya
ya adhabu ajikinge na adhabu zake, na aya iliyotaja tasbih
yaani kumtakasa Allah anatakiwa amtakase Allah, na huu
ndiyo mwenendo wa Mtume -swala na salamu za Allah
zimfikie -kama anavyosema Hudhaifah bin l-Yaman akielezea
kisomo cha Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie - :
‫مر بآيةِ فيها‬ َِّ ‫ و إذا‬، َ‫مر بآي ِِة خوفِ تعوَّ ِذ‬
َِّ ‫ و إذا‬، ‫مر بآي ِِة َرحمةِ سأ َِل‬ َِّ ‫كان إذا‬
ِِ ُ‫تَنزي ِه‬
َِ َّ‫للا سب‬
‫ح‬
Alikuwa pindi anapopita aya ya hofu (adhabu) hujikinga, na
anapopita aya ya rehma huomba, na anapopita aya ndani yake
kuna kumtakasa Allah humtakasa.

11
٤٧٨٢: ‫صحيح الجامع |الصفحة أو الرقم‬

Mwisho :
Msomaji wa Qur'an anapokuwa nje ya swala ni suna kwake
kufanya hivyo moja kwa moja kwa maana hakuna tofauti ya
wanavyuoni katika hilo, ama akiwa ndani ya swala
wanavyuoni wametofautiana na wanachuoni hawa wameitia
nguvu kauli ya ibn Qudam katika Mahanabilah kwa maana
atafanya hivyo katika swala ya suna si faradhi, ama
madhehebu ya kishafii ni suna katika swala zote za faradhi na
za suna kama anavyosema Annawawiy :
‫يسن للقارئ في الصالة وخارجها إذا مر بآية رحمة أن‬: ‫قال الشافعي وأصحابنا‬
‫يسأل للا تعالى الرحمة‬...
Amesema Shafiy na watu wetu : Ni sunnah kwa anayesoma
Qur'an ndani ya swala na nje yake pindi anapopita aya ya
rahmah amuombe Allah rehma ...
‫ويستحب ذلك لإلمام والمأموم والمنفرد‬...
Na ni suna (kufanya) hivyo kwa imamu na maamuma na
anayeswali peke yake ...
‫ألنه دعاء فاستووا فيه كالتأمين‬
Kwa sababu hiyo ni dua wakalingana wote kama vile kuitikia
aamiin
‫وقال بمذهبنا جمهور العلماء من السلف ممن بعدهم‬: ‫ثم قال‬

12
Kisha akasema (Annawawiy): Na wanachuoni wengi zaidi
wanameshika madhehebu yetu katika (wale wema) waliopita
na wale waliokuja baada yao.
٦٦/٤: ‫المجموع‬
١٨٦٧٦ ‫الفتوى رقم‬

Kwa faida mbali mbali ungana nasi katika mitandao


ya kijamii Facebook,Instagram,Youtube,Twitter
@fawaidusalafiyatz
Telegram:t.me/fawaidussalafiyatz
Tovuti : www.fawaidusalafiyatz.net

13

You might also like