You are on page 1of 8

Ufupisho wa kusali kama

alivyo Sali mtume wako


Alayhis sswalaatu
wassalaam

Muandishi wa Risala hii ni;


Al-akh Abuw Raslaan kilongozi Muwsa chibwiko
NATAKA KUJIFUNZA KUSWALI JE NIFANYEJE?

1- MAANA YA SWALA

2- FADHILA ZA SWALA

3-HUKUMU YA SWALA

4-JINSI YA KUSWALI MWANZO MPAKA MWISHO.

5-MAKOSA BAADHI YA WENYE KUSWALI.

1-MAANA YA SWALA;

Swala kwa lugha ya kiarabu ni DUA (YA KHERI)

Kisheria swala ni;IBADA YENYE KAULI NA VITENDO,HUFUNGULIWA KWA KUTOA


TAKBIRA(ALLAAHU AKBAR)NA HUMALIZIWA KWA KUTOA SALAMU.

2-FADHILA ZA SWALA

1-Ni Ibada kubwa katika ibada zilizo kubwa iliyokusanya ndani yake mambo
mengi,mf;TAKBIRA,TASBIH,TAHMID,KUSOMA QUR’AN,KUMSALIA MTUME ALAYHIS
SALAAM,KUSIMAMA,KURUKUU,KUSUJUDU,KUKAA.DUA NK.

2-Imefaradhishwa nakuwajibishwa kwa mtume(swallallaahu alayhi wasallam)juu ya umma huu


kutoka mbinguni kabla ya kuhamia madina kwa miaka mitatu,kinyume na ibada zingine kwani
zenyewe zimefafaradhishiwa Ardhini.

3-Amepewa kwayo mtume wetu(swallallaahu alayhi wasallam) moja kwa moja kutoka kwa
mola wake,kinyume na ibada zingine kwani zenyewe zimepitia kwa jibriylu(malaika anaye
teremsha ufunuo kwa mitume)alayhis salaam

4-Inakataza machafu na maovu;kwa maana Yule mwenye kuitekeleza anakuwa ni mwenye


kujiweka mbali na mambo machafu ya madhambi na maovu.

5-Inayasafisha madhambi;mfano wa Yule anaye oga kwa kila siku mara tano haiwezekani
kubakia kwenye mwili wake uchafu.

6-Inafuta madhambi;kati ya swala na swala ukifanya dhambi lisilokuwa kubwa basi swala
inayofuatia inayafuta makosa uliyoyafanya.

7-Unanyanyuliwa madaraja na kuwa katika madaraja ya juu.

8-Kuingia peponi nakuwa pembeni ya mtume alayhis salaam

9-Malaika hukuombea dua muda wa kuwa ukiwa katika mahala pa ibada.

10-Kwenda kwako msikitini unaandikiwa mema na kupandishwa madaraja.


3-HUKUMU YA SWALA

Kwa utukufu wa ibada hii na ujira wake jinsi ulivyo kuwa mwingi,Yule atakaye ipinga ibada hii na
kuikanusha mtu huyu kisheria huzingatiwa ni KAFIRI(mpingaji wa haki)kwa kuwa amepinga
jambo ambalo lajulikana katika dini kuwa ni katika mambo ya lazima mtu kuyajua,

Ama Yule atakaye iacha swala kwa UZEMBE au UVIVU hapa wanawachuoni wametofautiana
katika kumuhukumu mtu huyu,na Qauli iliyo ya sawa ni kama ya kwanza kuwa ni KAFIRI,sawa
sawa atazembea kwenye swala moja au mbili au ijumaa mpaka ijumaa nk.

4-JINSI YA KUSWALI

1-Ninapoanza kuswali ni lazima niwe nimesafishika mwili,nguo,sehemu ya kuswalia,

2-Ni lazima nichukue udhu kama alivyofundisha mtume(swallallaahu alayhi wasallam) na


wakafanya hivyo maswahaba zake Allah awaridhie,

3-Yanipasa baada ya hayo nielekee kibla(MAKKAH)katika swala zangu za aina yoyote ile.

4-Ni wajibu kwangu kusimama ninaposwali swala ya faradhi,kwa maana nisimame kama
inavyojulikana,si kwa maana ile ya kusema usimame pale unapo soma kitu.

5-Ni wajibu kwangu mimi mwenye kusali kutia nia ya swala,na kuiainisha hiyo swala katika moyo
wangu,wala nisitamke nia yangu kwani kufanya hivyo nitakuwa nimekwenda kinyume na jinsi
alivyo swali mtume wangu(swallallaahu alayhi wasallam),kwani haijapokelewa riwaya yoyote
sahihi inayo onyesha kuwa alitia nia yake kwa kutoa sauti.na pia nitakuwa nimekwenda kinyume
na maimamu wanaofuatwa katika madhehebu.

6-Kisha niwajibu kwangu kutoa Takbira kwa kusema ALLAAHU AKBAR.

7-Ninyanyue mikono yangu wakati wa kutoa takbira,usawa wa mabega yangu au usawa wa


masikio bila ya kugusisha kidole gumba katika njewe za masikio.

8-kisha niweke mkono wangu wa kulia juu ya mkono wa kushoto na yote ikiwa juu ya kifua,na
wala nisiweke mikono yangu juu ya kitovu changu.

9-kisha niangalie mahala pa kusujudia tu pasi na kuangalia kuliani kwangu wala kushotoni
mwangu pasi na kuzungusha shingo langu,na ilhali nimeinamisha kichwa changu chini.

10-Kisha inapendeza nisome dua ya ufunguzi kama ifuatavyo;

‫ اللَّ ُه َّم‬،‫س‬ َّ ‫ض ِم ْن‬


ِ َ‫الدن‬ ِ ِ ِ ‫اي َك َما بَاعَ ْدت بَيْ َن ال َْم ْش ِر ِق َوال َْمغْ ِر‬
َ َ‫ اللَّ ُه َّم نَ ِّقني م ْن َخطَاي‬،‫ب‬
ُ ‫اي َك َما يُنَ َّقى الث َّْو‬
ُ َ‫ب ا ْْلَبْي‬ ِ ِ
َ َ‫اللَّ ُه َّم بَاع ْد بَيْني َوبَيْ َن َخطَاي‬
ِ ‫اي بِال َْم ِاء َوالثَّل‬
‫ْج َوالْبَ َرِد‬ ِ ِ ِ
َ َ‫اغْسلْني م ْن َخطَاي‬

(ALLAAHUMMA BAAID BAYNIY WABAYNA KHATWAAYAY KAMAA BAA’DTA BAYNAL MASHRIQ


WAL MAGHRIB,ALLAAHUMMA NAQQINIY MIN KHATWAAYAAY KAMAA YUNAQQAA
THAWBUL ABYADH MINAD DANASI,ALLAAHUMMA IGHSILNIY MIN KHATWAAYAAY BIL MAAI
WATHTHALAJ WAL-BARAD)
11-Nikimaliza kusoma dua hii nijikinge na Shaytwaan na nisome Bismillaahir Rahmaanir
Rahiym,kwa ukimya huku nikitikisa midomo yangu hali ya kuashiria kuwa ninasoma kitu.na
niisome kwa siri siri katika kila swala,sawa sawa ni swala za wazi au za kimya.

12-Kisha nisome suwrat Al-faatiha kwa ukamilifu wake mahala husika na kwa hukumu zake bila
kubadilisha maana wala kugeuza herufi,naisoma katika kila rakaa nitakayo kuwa nimesimama.na
baada ya hapo nisome sura nyingine kwenye rakaa ya kwanza na ya pili.

13-Kisha nitakwenda kurukuu kwa kusema ALLAAHU AKBAR huku nimenyanyua mikono
yangu,na nitauinamisha mgongo wangu mpaka kulingana kwake bila ya kuinuka mbele au
kuinama sana chini kana kwamba natizama kitu nyuma katikati ya miguu miwili.Na huku
nimeshikilia magoti yangu mawili kwa mikono yangu miwili huku nimevipanua vidole vyangu vya
mikono.

14-Nikiwa katika hali hii nitasema ;;(‫ ) سبحان ربي العظيم‬SUBHAANA RABBIYAL ADHWIYM)

hii nitaisema mara tatu au zaidi au pungufu kama mara moja.

15-Kisha nitaunyanyua mgongo wangu kwenda kusimama na ilhali nimenyanyua mikono


tena,kisha nitasema;‫( سمع هللا لمن حمده‬SAMIALLAAHU LIMAN-HAMIDAH)Na hii nitaisema pindi
nikiwa naswali peke yangu,ama nikiwa naswali nyuma ya imam sinto paswa kuitamka bali
nitatosheka nahii ifuatayo hapo mbele.kisha nitasema tena;‫( ربنا ولك الحمد‬RABBANAA WALAKAL
HAMDU).

16-Na nitalingana sawa katika kusimama kwangu huko.

17-Kisha nitasema ALLAAHU AKBAR huku nikielekea kusujudu(kuweka paji langu la uso ardhini).

18-Na nikiwa naelekea kusujudu ninatakiwa nitangulize mikono miwili yangu kabla ya magoti
mawili.

19-Na kusujudu kwangu ninatakiwa nigusishe chini viungo vyangu saba,ambavyo ni;

(1)uso (2)viganja viwili ya mikono (3)magoti mawili (4)ncha mbili za vidole vya miguu huku
vidole vikielekea kibla,na kugusanisha visigino vyangu.ukihesabu vyote kwa kila kimoja
kimoja utakuja kukuta idadi yake ni saba.

20-Na kwa upande wa vidole vya viganja vyangu vinatakiwa nivibananishe na hali vikiwa
vimeelekea kibla.

21-kisha nikiwa katika sijda ninatakiwa niseme hivi;‫( ُس ْبحَ انَ رَ ِّبيَ اَ ْْلَعْ لَى‬subhaana Rabbiyal
A’alaa),mara tatu au zaidi au pungufu nayo ni mara moja.

22-Na sijda yangu inatakikana ikaribiane kiurefu na rukuu yangu,na ni vizuri nikithirishe dua
nyingi katika sujuwd,na vizuri zaidi nisome kwa lugha ya kiarabu hasa hasa zile dua alizokuwa
akizisoma Mtume wetu (swallallaahu alayhi wasallam) .Na haifai kusoma Qur’an katika sujuwd.

23-Na kipindi hiki ncha za miguu yangu zinatakiwa ziguse ardhi.na ziwe zimebanana na wala
zisiwe zimeachana.
24-Kisha nitatoa takbira kwa kusema (ALLAAHU AKBAR)kwa ajili ya kunyanyuka na kukaa.na hili
ni wajibu kwangu kulifanya.

25-kikao changu hiki kinatakiwa niwe nimeunyanyua mguu wangu wa kulia kwa kunyanyua
vidole vyake huku nimevipindisha vikiwa vinatizama qibla,na mguu wa kushoto nimeuweka chini
ya Makalio nimeukalia kwa kuulaza huku tumbo la mguu likiwa juu,na hili ni lazima kwangu
kulitekeleza.

26-Na hiki kinaitwa kikao katikati ya sijda mbili,na ninatakiwa nitulie mpaka kirejee kila kiungo
mahala pake.

27-Na ninatakiwa niseme katika kikao hiki ‫( رَ بِّ ا ِْغفِرْ لِي‬RABBI IGHFIR LIY)na nitasema kadri
nitakavyo jaaliwa kusema,kwa idadi nitakayo iweza.

28-kisha nitatoa Takbira tena (ALLAAHU AKBAR)kwa ajili ya kuelekea kwenye sijda ya pili.

29-Nitasujudu sijda ya pili,na hapa nitafanya jinsi nilivyofanya kwenye sijda ya kwanza.

30-Na nitakapo nyanyua kichwa changu kutoka katika sijda ya pili,na nikakusudia kusimama
nakuendelea na Rakaa ya pili basi nitatoa Takbira,Na sinto nyanyua mikono yangu.

31-Na katika Rakaa yangu ya pili nitainuka kwa kuegemea mikono yangu miwili,na nitafanya
kama nilivyofanya rakaa ya kwanza ispokuwa hapa sinto soma ile dua ya ufunguzi.

32-Na rakaa hii inakuwa ni fupi kuliko ya kwanza.

33-Nikiimaliza Rakaa hii ya pili kwa kusujudu sijda ya pili,hapa nitakaa kikao changu kwa ajili ya
kuleta Tashahhud,na hili nilazima nilifanye.na nitakaa kama nilivyo eleza jinsi ya kukaa kwenye
nambari 25.

34-Na nitaweka kiganja changu cha mkono wa kulia juu ya paja langu la kulia mwishoni mwa
goti.na kiganja changu cha kushoto nitakiweka juu ya goti langu la kushoto.

35-Na haitofaa kwangu nitakapo kuwa nakaa vikao hivi nikawa nimeegemea kwa mikono hasa
hasa mkono wa kushoto.

36-kisha nitanyoosha kidole changu cha shahada cha mkono wa kulia.na hili ni wajibu
kwangu,huku nikitamka maneno yafuatayo kwa siri bila kunyanyua sauti yangu;

‫ أَ ْش َه ُد‬, َ‫هللاِ اَلصَّالِحِين‬ ِ َّ َ ‫ اَلس َََّلم َعلَيْك أَ ُّيهَا اَل َّن ِبيُّ َورَ حْ َم ُة‬,‫َات‬
َّ َ ‫ اَلس َََّل ُم َعلَ ْي َنا َو َعلَى ِعبَا ِد‬,‫هللا وَ بَرَ َكا ُت ُه‬ ُ ‫الط ِّيب‬َّ ‫ َو‬,‫ات‬ ُ ‫صلَ َو‬ َّ ‫ َوال‬,ِ‫ت ِ َّلِل‬ ُ ‫حيَّا‬ِ ‫اَل َّت‬
‫ َوأَ ْش َه ُد أَنَّ ُمحَ َّم ًدا َع ْب ُدهُ َورَ سُول ُ ُه‬,ُ ‫هللا‬
َّ َ ‫أَنْ َل إِلَ َه إِ َّل‬

(ATTAHIYYAATU LILLAAHI,WASSWALAWAATU,WATTWAYYIBAATU,ASSALAAMU A’LAYKA


AYYUHAN NABIYYU WARAHMATULLAHI WABARAKAATUH,ASSALAAMU A’LAYNAA WAA’LAA
I’BAADIL LAAHIS SWAALIHIYNA,ASH-HADU AN-LAA ILAAHA ILLA LLAHU,WA ASH-HADU ANNA
MUHAMMADAN A’BDUHU WARASUWLUHU).

37-Ikiwa hii niliyoswali hapa ni swala yenye rakaa Nne basi nitafupizika na kusema hivi bila ya
kuongeza kitu chochote zaidi ya dua zilizothibiti kwa mtume (swallallaahu alayhi wasallam).
38-Na ikiwa ni swala yenye rakaa mbili tu hapa nita ongeza dua ya kumswalia mtume
wetu(swallallaahu alayhi wasallam) ,na hili ni wajibu kwangu, kuisoma kama ifuatavyo;

‫ َكمَا‬,‫َاركْ َعلَى ُمحَ مَّد َو َعلَى آ ِل ُمحَ مَّد‬


ِ ‫ َوب‬,‫جيد‬ َ ‫آل إِ ْبرَ اهِي َم إِ َّن‬
ِ ‫ك حَ مِيد َم‬ ُ ‫صلَّي‬
ِ ‫ْت َعلَى‬ َ ‫اَللَّ ُه َّم‬
ِ ‫ص ِّل َعلَى ُمحَ مَّد َو َعلَى‬
َ ‫ َكمَا‬,‫آل ُمحَ مَّد‬
‫جيد‬ َّ ِ ‫بَارَ ْكتَ َعلى‬
َ ‫ إِن‬,‫آل إِ ْبرَ اهِي َم‬
ِ ‫ك حَ مِيد َم‬ َ

(ALLAAHUMMA SWALLI A’LAA MUHAMMADIN WAA’LAA AALI MUHAMMADIN,KAMAA


SWALLAYTA A’LAA AALI IBRAAHIYMA INNAKA HAMIYDUN MAJIYDUN,WABAARIK A’LAA
MUHAMMADIN WA A’LAA AALI MUHAMMADIN,KAMAA BAARAKTA A’LAA AALI
IBRAAHIYMA,INNAKA HAMIYDUN MAJIYDUN).

39-Na ikiwa ni swala yenye rakaa Tatu au Nne basi ile rakaa ya mwisho nitakapokuwa nimekaa
kikao changu cha kumalizia swala basi nitayatamka maneno yaliyo kwenye nambari 36 kisha
nikiyafuatia na maneno niliyoyasoma kwenye nambari 38.

40-Na katika kusoma kwangu hii Tashahhud na kumsalia Mtume (swallallaahu alayhi
wasallam),natakiwa niwe nimekaa mkao maalumu,nao ni kuyakalia makalio chini hali nikiwa
nimeunyanyua mguu wangu wa kulia na vidole vya miguu vikiweka matumbo yake juu ya Ardhi
huku vikielekea kibla,ama mguu wangu wa kushoto wenyewe nitaupitisha kwenye muhundi wa
mguu wa kulia,ilhali tumbo la mguu huo likiwa limejitokeza kwa chini,na mgongo wa mguu huo
ukiwa umelalia chini.

41-Kisha nikimaliza kumswalia Mtume(swallallaahu alayhi wasallam) nitasoma dua ya


kujikinga na mambo manne kama ifuatavyo;

ْ ِ ‫ َومِنْ فِ ْت َن ِة اَ ْل َمحْ يَا َوا ْل َممَا‬,‫ب اَ ْل َقب ِْر‬


ِ ‫ َومِنْ َع َذا‬,‫ب جَ َه َّن َم‬
ِ ‫لِل مِنْ َع َذا‬ ُ ‫أَع‬
ِ َّ َ ‫ُوذ ِبا‬
ِ ِ‫ َومِنْ فِ ْت َن ِة اَلمَس‬,‫ت‬
‫يح اَلدَّجَّ ا ِل‬

(A’UDHU BILLAAHI MIN A’DHAABI JAHANNAAM,WAMIN A’DHAABIL QABRI,WAMIN FITNATIL


MAH-YAA WAL-MAMAATI,WAMIN FIT-NATIL MASIYHID DAJAAL)

42-Kisha nitaomba dua niipendayo baada ya hii,na zote hizi zinatakiwa nizitamke kwa lugha ya
kiarabu.

43-Baada ya hapa nitatoa salamu kwa kuanzia upande wangu wa kulia kwa kugeuza shingo
langu mpaka kuonekane weupe wa shavu langu,kisha upande wa kushoto mpaka uonekane
weupe wa shavu langu la kushoto,hata kama itakuwa ni swala ya jeneza.

44-Ikiwa nitakuwa ni imamu basi nitainyanyua sauti yangu ya kutoa salamu,na tamshi lenyewe
la salamu ni kusema;(ASSALAAMU A’LAYKUM WARAH-MATULLAHI),na kama nitakuwa naswali
mimi mwenyewe basi sinto nyanyua sauti yangu.nitaisema kwa siri.

َّ َ ‫اَلس َََّل ُم َعلَ ْي ُك ْم َورَ حْ َم ُة‬


ِ‫هللا‬

5-BAADHI YA MAKOSA WANAYO YAFANYA WENYE KUSALI

1-Wanaponyanyua mikono yao kwa ajili ya kutoa Takbira utawaona wakigusisha vidole gumba
kwenye masikio.hili halijapokelewa usahihi wake,hivyo ni vyema kujiepusha nalo.
2-Kusikika baadhi ya wenye kusali akiwa amesimama kusali nakuanza kuitamka nia kwa sauti
kwa kusema mfano;

(USWALLIY FARADHAS SWALAATI ADH-DHUHR ARBA’ RAKA’ATI LILAAHI TA’ALA IMAAMAN


ALLAAHU AKBAR),Hili nalo halina mafundisho yoyote kutoka kwa Mwalimu wetu Muhammad
(swallallaahu alayhi wasallam) wala kwa wanafunzi wake wabora.bali ni mambo yaliyowekwa
na watu tu wasio tegemewa kutunga sharia.

3-Katika makosa waliyonayo wenye kusali utawasikia wakirefusha Tamshi la Allah kwa kiwango
kirefu,na hili hutokea wakati wakitoa Takbira ya kuhama kwenda sehemu nyingine.

4-Pia utawasikia baadhi neno la AKBAAR wakilivuta mpaka kulitoa katika maana yake halisi.

5-Na katika makosa mengine ni kusoma kwa haraka sana suwrat Al-faatiha kiasi cha kwamba ile
maana inakoswa.

6-Nikupatikana baadhi wa waswaliji kubadilisha herufi za neno,mfano kwenye neno

َ‫ب َعلَي ِْه ْم وَ َل الضَّالِّين‬


ِ ‫َغي ِْر ا ْلم َْغضُو‬

Badali ya kuitamka herufi DHWAAD)‫ (ض‬utamsikia akiitamka herufi DHWAA )‫(ظ‬

7-kuelekea viungo vya baadhi ya wenye kusali kusiko kuwa Al-ka’aba(Makkah),ima yatakuwa ni
mabega,miguu miwili wakati wa kusimama,mikono miwili wakati wa kusujudu.nk.

8-kuacha kutoa sauti walau ya chini kwa chini kipindi unapo Sali peke yako ile swala ya
kudhihirisha kisomo.

9-Utamsikia mtu akisema wakati imamu anasoma aya ya mwisho katika suwrat Al-faatiha,akiwa
katika tamshi lile la mwisho akisema;( َ‫) َو َل الضَّالِّين‬utasikia naye asema(RABBIGH FIRLIY).Hakuna
katika mafundisho sahihi ya mtume wetu (swallallaahu alayhi wasallam) jambo kama hili.

10-Nikupatikana wenye kusali pale wanapofikia kumswalia mtume (swallallaahu alayhi


wasallam) kwenye Tashahud ya mwisho,basi huongeza Tamshi la (‫)سيدنا‬SAYYIDINAA.

11-kupatikana baadhi ya wenye kusali pale wanapotoa salamu utawasikia wakisema(sssss)na


ilhali wananyanyua kichwa juu kwanza na kukiteremsha chini kisha ndio wakielekeze kuliani
mwao na kushotoni mwao,na haya hayana mafundisho kutoka kwa mtume wetu (swallallaahu
alayhi wasallam) .

12-Na utawaona pia wakinyanyua mikono yao katika sehemu tofauti tofauti ndani ya swala
wakiashiria kuomba dua,mfano;wanapoinuka kutoka katika rukuu,na pale wanapotoa salamu
hukimbilia kunyanyua mikono nakuipaka kwenye uso.hili ni kosa.

Sifa njema zote ni zake muumba wangu aliyeniwafikisha kulitekeleza moja katika malengo
yangu,nalo ni la kuiandika risala hii kwa ufupi sana,nikiwa nimeacha vipengele vingi,nikitaraji
afaidike na risala hii kila muislamu wa kiwango cha chini kabisa anaye hitaji kuijua ibada hii,

Nikiwa nafahamu yakuwa yapo mas’ala ambayo yana ikhtilafu ndani yake,nami nimechagua yale
ninayo yaona yanawafikiana na Dalili sahihi,Nikiwa nataraji kwa Mola wangu atakapo nijaalia
nafasi nyingine niweze kuandika yaliyobakia,au kusherehesha risala hii kwa upana kiasi na
kuziba mianya ya yale niliyo yaacha kwa kuhofia kurefusha,pia nikitaraji kuandika risala zingine
zinazo husiana na Twahara ya muislamu,kuanzia Udhu,kuoga janaba,na vitu ambavyo ni Najisi
na jinsi ya kujisafisha navyo nk.pia mas’ala ya zakaa Na muomba Mola wangu Mkarimu
aniwafikishe niyafikie malengo yangu haya na mengine mengi.

Na tegemeo kubwa la risala hii nimeegemea kwenye risala mbili tu ,ya sheikh MUHAMMAD
NAASIR AL-BAANI ALLAH AMREHEMU,Inayo itwa (‫)تلخيص صفة صَلة النبي‬pia risala ya sheikh ABDUR
RAHMAAN NAASIR AS-SA’D ALLAH AMREHEMU,inayoitwa(‫)منهج السالكين‬

Mwisho kabisa nawashukuru wale wote walioshirikiana nami katika kukamilisha jambo hili.

Nimeianza kazi hii 26/04/2020M jumapili.ambayo ni sawa na 03/Ramadhani/1441H,nakuimaliza


kwa kuiandika Tarehe 04/05/2020M,ambayo ni sawa na Tarehe 11/Ramadhani/1441H.

Muandishi ni;

Abuw Raslaan Muwsa Kilongozi Chibwiko

Tanzania,Dodoma,Masjid Manyema,barabara ya 07

You might also like