You are on page 1of 114

HUENDA

TUKAONGOKA:
(Toleo la Pili)

Uharamu na Ukubwa wa dhambi ya


Ushirikina

Abuu Farheen Farid na IbnuRajab Allhassany

1
HUENDA TUKAONGOKA: (Toleo la Pili)
Uharamu na Ukubwa wa dhambi ya
Ushirikina

Barua pepe: faridhamad78@gmail.com


Simu: +255 748 202 226
Whatsapp: +255 777 002 226
Tanga, Tanzania.
ISBN: 978-9912-40-

Kimerejelewa na:
1. Mohamed Rajab (IbnuRajab Allhassany)
Khartom Sudan
2. Mohamed Abdallah Kifosha
Tanga, Tanzania

Mpiga chapa:
Truth Printing Service
0764 425 704/0692 637 282
geofreymakula@gmail.com
Ubungo, Dar es Salam
Tanzania

2
Kutoka kwa Swahaba Abuu Khurayra (Radhi za
Allah ziwe juu yake) amesema; Amesema
Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake):
Amesema Allah (Subhanahu) (katika Hadith
Qudsi): “Mimi nimejitosheleza na washirika
kutokana na ushirikina, yoyote atakaefanya
mwengine pamoja nami mshirika, katika jambo
hilo, basi namuacha yeye na ushirikina wake.”

Amepokea Imam Muslim

3
YALIYOMO
3. KUHUSU KITABU:................................................. 6
4. MAKOSA YA CHAPA NA UANDISHI: .............. 8
5. SHUKRANI:............................................................. 9
6. DIBAJI:...................................................................12
7. UTANGULIZI ........................................................17
8. MAANA, MISINGI NA CHIMBUKO LA
USHIRIKINA ........................................................23
Ushirikina Mkubwa: ...................................................29
Ushirikina Mdogo: .......................................................30
9. UFAFANUZI WA USHIRIKINA NDANI YA
QUR‟AN ..................................................................32
10. HUKMU ZA USHIRIKINA NDANI YA QUR‟AN
..................................................................................37
11. KAULI ZA WANACHUONI JUU YA UKUBWA
NA UHARAMU WA USHIRIKINA, DUNIANI NA
MBELE YA ALLAH ................................................42
12. USHIRIKINA NA JAMII ZETU ........................49
Ushirikina katika kuomba Dua ...............................50
Ushirikina katika kuomba Maiti na Wafu ...........55
Ushirikina katika Ndoa..............................................59
Ushirikina katika Kazi na Biashara .......................67
Ushirikina katika Michezo ........................................73
Aina za watu katika Mazoezi na Michezo .......74

4
Hukumu ya michezo katika Uislamu ................75
Uwajibu wa Michezo katika Uislamu:..............75
Uharamu wa Michezo ndani ya Uislamu: .......76
ATHARI ZA USHIRIKINA ..........................................80
Athari za Ushirikina katika Imani .........................80
Athari za ushirikina katika Jamii ...........................89
13. KWANINI JAMII INAINGIA KATIKA
USHIRIKINA ........................................................93
14. VIPI TUTAJIKWAMUA KUTOKA KATIKA UOVU
WA USHIRIKINA UNAPOTUPATA ...............100
Alama kumi za kumtambua tabibu mchawi
(Mshirikina) na muongo:........................................105
15. HITIMISHO: .......................................................112

5
KUHUSU KITABU:
„Huenda Tukaongoka‟ ni muendelezo wa
machapisho ambayo hubeba maudhui tofauti yenye
athari za moja kwa moja ndani ya jamii. Mtiririko wa
chapisho hili, ulianzia katika toleo la kwanza ambalo
liliangazia kuhusu Riba na athari zake ndani ya jamii
na dhana za Uchumi. Kupitia toleo hilo (la kwanza)
tulifafanua kwa kina juu ya maana, aina, hukmu za
riba ndani ya Qur‟an, Hadithi za Mtume (Rehma na
Amani ziwe juu yake), pamoja na Fatwa za wanazuoni
mbali mbali wa Kiislamu. Kadhalika, kupitia toleo hilo
tulifanya uchambuzi juu ya athari hasi za Riba ndani
ya jamii, sambamba na athari zake hasi katika
Uchumi kwa ujumla. Tunataraji kwa Allah
(Subhanahu) lengo na nia ya kuandaa chapisho hili
litafikiwa na jamii itaongoka kwa idhini yake.

Mtiririko wa „Huenda Tukaongoka‟ umerudi tena


katika toleo lake la pili, ikija na anuani „Uharamu na
Ukubwa wa dhambi ya Ushirikina‟ ikifanya uchambuzi
na ufafanuzi wa kina juu ya dhambi ya ushirikina.
Toleo hili la pili limedadavua kwa weledi na uzamivu
namna na sura tofauti za ushirikina ndani ya jamii
zetu. Sambamba na kutoa elimu na mafunzo muhimu
kwa jamii, elimu ambayo tunataraji kwa Allah
(Subhanahu) itatoa nuru kwa jamii katika kujikinga na
kujiweka mbali na ushirikina kwa ujumla wake. Kila

6
nukta katika chapisho (toleo) hili ni muhimu kwako
wewe msomaji na jamii kwa ujumla na huenda ikawa
ni tajamala (fursa) ya kutambua uharamu na ukubwa
wa dhambi ya ushirikina kwa kila sura na aina zake
kwa idhini ya Allah (Subhanahu).

7
MAKOSA YA CHAPA NA UANDISHI:
Alhamdulillah, sifa zote anastahiki Allah (Subhanahu)
muumba wa mbingu na ardhi. Ambaye ameturuzuku
neema ya Uislamu na Qur‟an kuwa ni Dira na
Muongozo wa maisha yetu. Mbali na neema hizo zote,
yeye ndiye alietuumba wanadamu katika umbile lililo
bora na kisha akatujalia sifa ya upungufu katika kila
jambo tulitendalo.

Kwa minajili hiyo, natanguliza samahani kwa kila


nukta ambayo itabainika kuwa na mapungufu katika
hatua zote, hakika ukamilifu ni wake Allah
(Subhanahu) kila kazi ama amali ya mwanadamu
haikosi kuwa na mapungufu. Hivyo nawaomba ndugu
zangu wasomaji kunipa udhru katika nukta yoyote
ambayo itabainika kuwa na makosa katika uandishi
ama uchapaji. Namuomba Allah (Subhanahu) awape
elimu yenye manufaa na ufahamu thabiti wa kuweza
kuyafanyia kazi yale mema yatakayopatikana ndani ya
Kitabu hiki na kuacha yote maovu yaliyobainishwa na
mengine nje ya chapisho hili.

Abuu Farheen Farid Bakari Hamad

8
SHUKRANI:

ALHAMDULILLAH! Sifa na stahiki zote za shukrani na


ibada zinamstahiki Allah (Subhanahu) ambae
ametupa hidaya ya uhai, afya, na maarifa mema.
Akatujaalia neema ya elimu na juhudi za kukusanya
maarifa mbali mbali, kisha akasafisha nia zetu kuweza
kufanya hili tunalolifanya kwa ajili yake na jamii zetu.
Sala na Amani zimuendee mtukufu wa darja, Mtume
(Rehma na Amani ziwe juu yake), na ahli na
maswahaba zake na wote waliomfuata kwa wema
hadi siku ya kiyama.

Baada ya kutanguliza shukrani hizo za pekee kwa


mstahiki, napenda kuchukua fursa hii aidha,
kumshukuru Ndugu yangu, msharafu katika fani ya
sharia na muandishi mwenza wa chapisho hili,
Mohamed Rajab (IbnuRajab Allhassany) kwa juhudi
zake na kujitoa kwake katika kuhakikisha kitabu hiki
kinakamilika na kufikia lengo lililokusudiwa. Kadhalika,
namshukuru sana kwa mchango wake wenye thamani
kubwa ndani ya chapisho hili; ikiwamo uandishi bora
wa Dibaji yenye kutoa dira na muangaza wa wazi juu
ya anuani ya Kitabu hiki. Mbali na uandishi huo mzuri
wa Dibaji, napenda kutoa shukrani na kukiri kuwa
ukamilishaji wa chapisho hili umechagizwa kwa kiasi
kikubwa na mchango wake katika ukusanyaji wa
9
maudhui ya Ushirikina katika Michezo na Mazoezi.
Namuomba Allah (Subhanahu) amuhifadhi na kuweka
juhudi zake katika mizani ya mema yake.

Nitakua mchoyo wa fadhila, kama sitafikisha shukrani


zangu za pekee kwa wasomaji wote wa vitabu vyetu.
Kuanzia „Haya ndiyo Qur‟an Imenifunza‟ hadi „Huenda
Tukaongoka‟ kwa hakika wanamsukumo mkubwa
sana kwetu. Kwa hakika uwepo wenu ni hidaya na
tajamala kwetu. Namuomba Allah (Subhanahu)
awalipe kila kheri na awape nuru ya elimu na maarifa
mema ya dini. Kadhalika, kila gharama mlizotumia
kununua nakala za vitabu vyetu, Allah (Subhanahu)
azifanye kuwa ni sadaka na kuziweka katika mizani ya
mema yenu na Allah (Subhanahu) awape Baraka
belele.

Napenda kufikisha shukrani pia kwa familia yangu


kwa ujumla, pamoja na wadau wote ambao kwa
namna moja ama nyengine wamechochea katika
ukamilishaji wa Chapisho hili. Namuomba Allah
(Subhanahu) awahifadhi na kuwapa kila hitaji la kheri
la nyoyo zao. Alkadhalika, napenda kukiri kuwa
kukamilika kwa kitabu hiki, kulihitaji zaidi mchango
wa ndugu yangu, Mohamed Abdallah Kifosha, ambae
kwa namna ya pekee napenda nikiri kuwa
nimekifanya kitabu hiki kuwa ni zawadi kwake.

10
Namuomba Allah amuhifadhi na kumpa kila kheri
katika maisha yake.

Amin.

Abuu Farheen Farid Bakari Hamad

11
DIBAJI:
Bismillahi Rahmani Rahiim
Kila sifa njema ni za Allah aliemtuma Mtume wake
Muhammad (Rehma na Amani ziwe juu yake) kwa
dini ya haki ili awatoe waja kutoka katika kiza cha
ushirikina na kuwapeleka katika nuru ya Tauhidi,
kisha sala na amani zimfikie mwalimu wa Ummah huu
Mtume Muhammad (Rehma na Amani ziwe juu yake)
pamoja na Ahli zake na Maswahaba zake na wale
watakao mfuata kwa wema mpaka siku ya Kiyama.
Hakika yule atakaezingatia katika uumbaji wa Allah
(Subhanahu) wa mbingu na nchi na vilivyomo ndani
yake, ataona maajabu na alama kubwa sana ambazo
zinathibitisha uwepo wa Allah na upekee wake katika
kuumba na kustahiki kuabudiwa. Moja ya viumbe
vyake vya ajabu sana na vyenye mpangilio mzuri wa
maumbile ni binadamu, ambaye amemfanya kuwa ni
kiumbe kitukufu kuliko kiumbe chochote, endapo
atasimamia yale aliyoamrishwa na muumba wake.
Aidha, kiumbe huyo huenda akawa dhalili na duni
kushinda hata mnyama endapo atakiuka yale yote
alioamrishwa na muumba wake kwa kufanya au
kuacha.

12
Kisha Allah (Subhanahu) amemuumba mwanadamu
na kumbainishia njia ya haki na njia za batili:

﴾ٖ﴿ً‫ٱلسبِيل إِ َّما َشاكِراً وإِ َّما َك ُفورا‬ ِ


َ َ َّ ُ‫إنَّا َى َديْػنَاه‬
"Hakika sisi tumemuongoza mwanadamu njia, ama
mwenye kushukuru au mwenye kukufuru" (76:03)
Pamoja na hayo yote Allah (Subhanahu) amempa
mwanadamu utashi na mamlaka ya kuchagua baada
ya kubainishiwa na kusimamishiwa hoja kwa kutuma
Mitume, lakini utashi wa mwanadamu uko chini ya
utashi wa Allah (Subhanahu)

﴾ٖٓ﴿ً‫وما تَ َشآءو َن إِالَّ أَن ي َشآء ٱللَّو إِ َّن ٱللَّو َكا َن َعلِيماً ح ِكيما‬
َ َ ُ َ َ ُ ََ
"Wala hamwezi kutaka ila atakapo Allah. Hakika Allah
ni mwenye Elimu, Mwenye Hikima" (76:30)
Yote hayo ambayo Allah amemneemesha
mwanadamu kwa neema na tunu anazoziona na zile
asizoziona, bado mwanadamu amekuwa ni mkaidi
sana kwa Mola wake kwa kufanya mambo
yasiyomridhisha muumba wake. Mwanadamu
akaabudu asiekuwa Yeye. Hakika, huu ni uhasama wa
wazi anautafuta mwanadamu, kwani kaumbwa na
Allah lakini anamuabudu mwingine. Riziki akapewa na
Allah lakini anamshukuru mwingine, Allah
anamshushia heri zake yeye anampandishia shari kwa
maasi yake. Kadhalika, Allah (Subhanahu)

13
anamuonesha mapenzi kwa neema mbalimbali yeye
anamuudhi kwa kumuasi, pamoja na hivyo Allah
(Subhanahu) bado ni mkarimu kwa mwanadamu.

ِ ِ
َ ‫﴾ َوإِنَّوُ َعلَ ٰى ٰذل‬ٙ﴿‫نسا َن لَربِّْو لَ َكنُود‬
﴾ٚ﴿‫ك لَ َش ِهيد‬ ِ ِ
َ ‫إ َّن ٱإل‬
"Hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola
wake. Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni
shahidi wa hayo!" (100:6-7)
Ndugu zangu, ikiwa mwanadamu hapendi ushirika
katika vitu anavyovimiki, iweje amshirikishe kiumbe
mwingine katika ibada anayostahili Allah.

‫ت أَِْيَانُ ُك ْم ّْمن ُشَرَكآءَ ِِف َما‬ ِ


ْ ‫ب لَ ُك ْم َّمثَالً ّْم ْن أَن ُفس ُك ْم َى ْل لَّ ُك ْم ّْمن َّما َملَ َك‬
َ ‫ضَر‬
َ
﴾ٕٛ﴿‫رَزقْػنَا ُكم فَأَنتُم فِ ِيو سوآء‬
ََ ْ ْ َ
"Amekupigieni mfano kutokana na nafsi zenu, Je!
Katika hao iliyo wamiliki mikono yenu ya kulia mnao
washirika katika hivyo tulivyo kuruzukuni mkawa
nyinyi katika hivyo sawasawa." (30:28)
Jibu ni hapana, na wala hakuna anaekubali kuchuma
mali kisha aje mtu mwingine ashiriki katika mali yake
kirahisi, aidha, mtu akusanye mali kisha akaoa mke
wake mzuri anaempenda, kisha asikie kuna mtu
mwingine anapendwa na mkewe na anapewa
heshima kubwa kuliko anayopewa yeye, je! atakubali
kufanyiwa hilo? Kama yeye hakubali hilo basi Allah

14
anachukia zaidi kushirikishwa katika ibada zake kwa
namna yoyote ile.
Kutokana na jamii kujiweka mbali na maswala ya
kielimu, imepelekea kufungua mlango mpana wa
kupokea fikra tofauti. Kwamaana, inasemwa kuwa;
mkataa pema pabaya panamuita. Halkadhalika, akili
isiposhughulishwa na jambo la maana, basi
itajihusisha na jambo lisilo na maana. Yakiwemo
maswala ya ushirikina, ambao kwa sasa umechukuwa
nafasi kubwa sana kuliko juhudi binafsi. Kitabu hiki
kitakwenda kurekebisha fikra potovu za ushirikina
katika jamii na kutoa muongozo juu ya nini kifanyike
ili kuondokana na changamoto hizi. Mtunzi, (Allah
amhifadhi) amegusa mambo muhimu sana ambayo
yanaikabili jamii yetu kisha akatoa mifano na njia
elekezi zitakazosafisha mawazo machafu katika jamii.
Hakika jamii yetu inahitaji elimu zaidi kuliko
inavyohitaji mambo mengine ambayo yanapewa
kipaumbele. Mwisho nasema kwamba; endapo
tutapuuza miongozo ya Allah na Mtume wake, basi
lolote baya linaweza kutupata ikiwemo kuenea kwa
ushirkina, kwani amesema Allah (Subhanahu);
ِ َّ ِ ِِ
َ ‫صدّْق لّْ َما َم َع ُه ْم نػَبَ َذ فَ ِريق ّْم َن ٱلذ‬
ْ‫ين أُوتُوا‬ َ ‫َولَ َّمآ َجآءَ ُى ْم َر ُسول ّْم ْن عند ٱللَّو ُم‬
﴾ٔٓٔ﴿‫ٱلْ ِكتَاب كِتَاب ٱللَّ ِو ورآء ظُهوِرِىم َكأَنػَّهم الَ يػعلَمو َن‬
ُ ْ َ ْ ُ ْ ُ َ ََ َ َ
“Na alipowajia Mtume kutoka kwa Allah, mwenye
kuthibitisha yale waliyo nayo, kundi moja miongoni

15
mwa wale waliopewa kitabu lilitupa Kitabu cha Allah
nyuma ya migongo yao kama kwamba hawajui.”
(02:101)
Baada ya kupuuza kitabu cha Allah ambacho ndani
yake kuna mafundisho kwao wakaangukia katika
jambo baya zaidi ambalo ni ushirikina, Allah akasema
katika aya iliyofuata:
ِ ِ ِ ِ
‫ني‬ ُ ‫َوٱتػَّبَػعُواْ َما تَػْتػلُواْ ٱلشَّيَاط‬
َ ‫ني َعلَ ٰى ُم ْلك ُسلَْي َما َن َوَما َك َفَر ُسلَْي َما ُن َولَػٰك َّن ٱلشَّْياط‬
﴾ٕٔٓ﴿‫ٱلسحر‬
َ ‫َك َفُرواْ يػُ َعلّْ ُمو َن ٱلن‬
َ ْ ّْ ‫َّاس‬
“Na wakafuata yale waliyokuwa wakiyasoma
mashetani katika ufalme wa Suleiman, na hakukufuru
Suleiman lakini mashetani ndio wamekufuru kwa
kuwafundisha watu uchawi.” (02:102)
Haujaenea ushirikina katika jamii ispokuwa baada ya
kupuuza mafundisho ya Quran na yale ya Mtume
(Rehma na Amani ziwe juu yake)
Wa billahi Taufiqi
Allhamdulillahi Rabbil Àlamiin
Imeandikwa na:
IbnuRajab Allhassany
Khartoum|Sudan
ibnurajabalhassany@gmail.com
‫بِس ِْم ه‬
ِ ‫َّللاِ ٱلرهحْ م ٰـ ِن ٱلر‬
‫هح ِيم‬

16
UTANGULIZI
Kila sifa njema anastahiki Allah Mola mlezi wa viumbe
vyote, kisha sala na amani zimfikie Mtume wetu
Muhammad (Rehma na Amani ziwe juu yake) pamoja
na ahli na maswahaba zake na wote watakaomfuata
kwa wema mpaka siku ya mwisho. Nausia nafsi
yangu, pamoja na kuwausia ndugu zangu wasomaji
juu ya suala zima la kumcha Allah (Subhanahu), na
miongoni mwa njia za kumcha Allah (Subhanahu) ni
pamoja na kukataza na kuelimishana juu ya dhambi
ya Ushirikina.
Nawasalimu kwa maamkizi ya Amani ndugu zangu
wasomaji, Assalam Alaikum Warahmatullah
Wabarakatu. Kitabu hiki tutagusia kwa uchache
makatazo na ufafanuzi juu ya Shirk (Ushirikina)
kupitia kitabu Kitukufu cha Qur‟an na Sunna za
Mtume wa Allah. Sambamba na kutoa ufafanuzi mbali
mbali juu ya kauli za Allah katika Sura tofauti ndani ya
Qur‟an na Sunna.
Kwa hakika katika dhambi kubwa mbele ya Allah ni
ushirikina, kwa ukubwa wake Allah (Subhanahu)
amebainisha makatazo mbali mbali kupitia Sura
tofauti ndani ya Qur‟an, pamoja na kubainisha adhabu
na matokeo mabaya ambayo ameyaandaa kwa
viumbe ambao watajihusisha na ushirikina, iwe
kwenye Ibada, Dua ama ushirikina wa sihri na
uganga.

17
Kwani, Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah
(Radhi za Allah ziwe juu yake) kwamba Mtume
(Swalla Allahu Alaiyh wa Sallam) amesema:
((Jiepusheni na mambo (Madhambi) saba
yanayoangamiza!))
Wakauliza: Ni yepi hayo ee Rasuli wa Allah?
Akasema: ((Ni kumshirikisha Allah,
sihri [uchawi], kuua nafsi Aliyoiharamisha Allah
isipokuwa kwa haki, kula Riba, kula mali ya yatima,
kukimbia wakati wa kupambana na adui na
kuwatuhumu uzinifu wanawake Waumini
waliohifadhika walioghafilika)). [Al-Bukhaariy na
Muslim]
Imam Bin Baaz (Radhi za Allah ziwe juu yake)
amesema wakati akitoa ufafanuzi juu ya Hadith hii
kuwa; dhambi hizi zinauzito kwa kadiri ambavyo
Mtume (Swalla Allahu alaiyh wa Sallam) alivyozitaja
na ameanza kwa kutaja shirki (Ushirikina) ikiwa ni
dhambi kubwa yenye daraja la kwanza katika dhambi
hizo saba. Ndani ya kumshirikisha Allah (Subhanahu)
kumefungamanishwa mambo mawili muhimu ambayo
yote yanalenga na kufungamanishwa na Tawhid.
Ushirikina unaweza kuwa ni ule wa kumjaalia Allah
kuwa na wenza, pamoja na kukusudia ibada za shida
kwa viumbe wengine wasio kuwa Allah (Subhanahu).
Ama kwa upande mwengine ambao hauna tofauti
sana, huelekezwa kwenye uchawi, mizimu na sihri

18
ambazo zote wafanyaji huzitegemea kwa kuomba
kinga na haja zao bila kuwakusudia katika ibada.
Shaykh Al-Fawzan (Allah amhifadhi) katika ufafanuzi
wake wa kitabu cha Misingi Minne ya Shirk; ameeleza
kuwa shirki ina misingi minne ambayo katika kuitaja
akasema; Msingi wa kwanza ni ule ushirikina wa
makafiri ambao walimpinga Mtume wa Allah, huku
wakiamini kuwa Allah ndiye Muumba na Mlezi wa
viumbe wote na Imani yao hiyo isiwafae chochote
katika kuikubali dini ya Uislamu. Na msingi huu
akauthibitisha kwa kauli ya Allah ndani ya Surat
Yunus aliposema;

‫ٱْلَ َّى‬
ْ ‫ِج‬ ِ ِ ‫ٱلسم‬
ِ ‫آء َوٱأل َْر‬
ُ ‫ص َار َوَمن ُُيْر‬ َ ْ‫ٱلس ْم َع وٱألَب‬ َّ ‫ك‬ ُ ‫ض أ ََّمن ِيَْل‬ َ َّ ‫قُ ْل َمن يػَْرُزقُ ُكم ّْم َن‬
ْ ‫ت ِم َن‬
َ‫ٱْلَ ّْى َوَمن يُ َدبػُّْر ٱأل َْمَر فَ َسيَػ ُوولُو َن ٱللَّوُ فَػ ُو ْل أَفَال‬ َ ّْ‫ِج ٱلْ َمي‬
ِ ِ
ُ ‫م َن ٱلْ َميّْت َوُُيْر‬
﴾ٖٔ﴿‫تَػتَّػ ُوو َن‬

“Sema: Ni nani anaye kuruzukuni kutoka mawinguni


na kwenye Ardhi? Au ni nani anaye miliki kusikia na
kuona? Na nani amtoae hai kutoka maiti, na akamtoa
maiti kutoka alie hai? Na nani anae yadabiri mambo
yote? Watasema: Allah. Basi sema: Je! Hamchi?
(10:31)

Akaendelea kusema kuwa; Msingi wa pili wa shirki ni


kwa wale wapagani (Wasio muamini Allah na Mtume

19
wake) na wanaosema kuwa “hatuwaabudu (Miungu
ya uongo) na wala hatuwategemei isipokuwa kwa
lengo la wao kutukurubisha kwa Allah” Al-Fawzan
akaongeza kuwa; msingi huu unawafanya watu wa
kundi hili kuwa hawamshirikishi Allah katika Uungu
wake, bali hufanya ushirikina katika ibada zake, kwa
sababu wao hawaamini kwamba miungu yao hiyo
inaweza kuwadhuru wala kuwanufaisha. Na msingi
huu akauthibitisha kupitia Qur‟an ndani ya Surat Az-
Zumar aliposema;

‫ين َّٱَّتَ ُذواْ ِمن ُدونِِو أ َْولِيَآءَ َما نػَ ْعبُ ُد ُى ْم إِالَّ لِيُػ َوّْربُونَآ إِ ََل ٱللَّ ِو ُزلْ َف ۤى إِ َّن ٱللَّوَ ََْي ُك ُم‬ ِ َّ
َ ‫َوٱلذ‬
‫بػَْيػنَػ ُه ْم ِِف َما ُى ْم فِ ِيو َُيْتَلِ ُفو َن إِ َّن ٱللَّوَ الَ يػَ ْه ِدى َم ْن ُى َو َك ِاذب َكػفَّار‬

“Na wale wanao wafanya wenginewe kuwa ni walinzi


wakisema: Sisi hatuwaabudu ila wapate kutujongeza
tu kumkaribia Allah- Hakika Allah atahukumu baina
yao katika wanayo hitalifiana. Hakika Allah
hamwongoi alie kafiri, muongo” (39:03)
Aidha, akaeleza kuwa msingi wa tatu, ni wale
wanaomshirikisha Allah kwa ibada za viumbe wake,
kama vile Malaika, Mitume, Mawali, Mizimu, Mawe,
Miti, na wengine wakiabudu jua na mwezi. Na
akasema kuwa; Mtume wa Allah ametumwa
kuwabainishia uovu huu na katika hao wote
akawaweka katika kundi moja, japo kuwa wao
kutokana na imani zao hawana usawa wowote wa
ibada, kila mmoja anaabudu kile anacho kiamini.

20
Kundi hili la washirikina mfano wake ni kama vile mtu
mwenye mabwana wengi, asiyejua yupi amridhishe,
kila mmoja ana matakwa yake kwa manufaa yake.
Hivyo Allah akasema ndani ya Surat Az-Zumar;
ِ ‫ضرب ٱللَّو مثَالً َّرجالً فِ ِيو ُشرَكآء متَ َشاكِسو َن ورجالً سلَماً لّْرج ٍل ىل يستَ ِوي‬
ً‫ان َمثَال‬َ ْ َ ْ َ ُ َ َ ُ ََ ُ ُُ َ ُ َ ُ َ ََ
“Allah amepiga mfano wa mtu mwenye mabwana
washirika wanao gombana, na mtu mwengine alie
husika na bwana mmoja tu. Je! Wako sawa katika hali
zao?” (10:29)
Shaykh akasema; msingi wa nne wa shikri, ni wa
washirikina ambao walikuwa wakifanya ushirikina
katika kipindi cha furaha na utulivu na wakimrudia na
kumuabudu Allah (Subhanahu) katika kipindi cha
shida. Msingi huu akauthibitisha pia kupitia Qur‟an
ndani ya Surat Al-„Ankabut, Allah amesema;

‫ََّاى ْم إِ ََل ٱلْبَػّْر إِذَا ُى ْم‬ ِِ ِ ِ


ُ ‫ّْين فَػلَ َّما ّم‬ َ ‫فَِإ َذا َركبُواْ ِِف ٱلْ ُف ْلك َد َع ُواْ ٱللَّوَ ُمُْلص‬
َ ‫ني لَوُ ٱلد‬
﴾ٙ٘﴿‫ي ْش ِرُكو َن‬
ُ
“Na wanapo panda katika merikebu, humwomba Allah
kwa kumsafia utiifu. Lakini anapo wavua wakafika
nchi kavu, mara wanamshirikisha” (29:65)
Allah amesema pia ndani ya Surat Al-Isra akibainisha
msingi huu;

21
ْ ‫ض َّل َمن تَ ْد ُعو َن إِالَّ إِيَّاهُ فَػلَ َّما ّمََّا ُك ْم إِ ََل ٱلْبَػّْر أ َْعَر‬
‫ضتُ ْم‬ َ ‫َوإِذَا َم َّس ُك ُم ٱلضُُّّر ِِف ٱلْبَ ْح ِر‬
﴾ٙٚ﴿ً‫وَكا َن ٱ ِإلنْسا ُن َك ُفورا‬
َ َ
”Na inapo kufikieni taabu katika bahari, hao mnao
waomba wanapotea, isipokuwa Yeye tu. Na anapo
kuvueni mkafika nchi kavu, mnageuka. Ama
mwanadamu ni mwingi wa kukanusha” (17:67)
Akaendelea kueleza kuwa msingi huu wa ushirikina
umekuja kuwa na afadhali kwani wao humcha Allah
katika kipindi cha shida. Lakini ubaya mkubwa
umeonekana katika washirikina wa zama zetu ambao
wao, hufanya ushirikina katika kipindi cha raha na
amani huku ushirikina wao ukizidi zaidi wakiwa katika
shida na misukosuko.
Haya yote hubainika ndani ya jamii zetu, ushirikina
umefika katika hatua ya juu, huku wengi wao
wakiingia ndani ya kundi la nne ambalo humshirkisha
Allah katika hali zote, wakikumbwa na maradhi
huwaendea waganga na makuhani kutafuta tiba,
wakikosa riziki huelekeza shida zao kwa mizimu,
misukosuko ya ndoa hutatuliwa kwa nyota. Aidha,
hayo yote yakiwandokea na kuwa na amani basi
hurudi kutoa shukurani za kafara na zawadi kwa
mizimu na majini.
Kutokana na nukta hizi na nyengine nyingi, ndio
sababu ya kuandaa chapisho hili, huenda Allah

22
(Ta‟ala) akatuongoa kutoka katika ushirikina wa aina
zote.

MAANA, MISINGI NA CHIMBUKO LA


USHIRIKINA
Katika kuelezea kwa ufasaha maana halisi ya
ushirikina itatupasa kujua chimbuko la shirki kwamba
imetokana na nguzo kuu ya itikadi sahihi ya Muumini
ya „Kumuamini Allah‟ kwamaana kinyume na kutakidi
juu ya msingi huu adhimu, hapo kiumbe huingia
kwenye ushirikina. Maana ya Kumuamini Allah
(Subhanahu), imesemwa na Sheikh Abdulaziz
Abdallah Ibn-Baaz (Radhi za Allah ziwe juu yake)
kuwa; “Kumuamini Allah (Subhanah) ni kuamini kuwa
yeye ndiye Mungu wa kweli, anaestahiki kuabudiwa
badala ya kila kisichokuwa yeye, kwa sababu yeye
ndiye Muumba wa waja, Mfadhili wao, Mwenye
kuzisimamia riziki zao, Mwenye kuzijua siri na dhahiri
zao, Mwenye uwezo wa kumpa thawabu mwenye
utiifu na kumuadhibu mwenye kufanya uasi.”

Hivyo kinyume na kumuamini Allah basi hupelekea


kumuhusisha na kiumbe ama kitu chengine. Hakika
Allah (Subhanahu) amewaumba wanadamu kwa
lengo maalumu. Kama ambavyo ameumba majini na
viumbe wengine, wote wakiwa wamewekewa
utaratibu na makusudio mahasusi. Haya

23
yanathibitishwa na Qur‟an kupitia Surat Adh-Dhariyat
kuwa:

ِ ‫ٱْلِ َّن وٱ ِإلنس إِالَّ لِيػعب ُد‬


﴾٘ٙ﴿‫ون‬
ُْ َ َ َ ْ ‫ت‬ ُ ‫َوَما َخلَ ْو‬
“Nami sikuwaumba majini na wanadamu isipokuwa
waniabudu Mimi” (51:56)
Amewaumba viumbe hawa kwa lengo moja tu,
kumuabudu Yeye na ni sawa ambavyo Allah
(Subhanahu) alivyowatuma Mitume kutafsiri na
kufafanua maamrisho na makatazo yake. Hivyo hivyo,
Allah (Subhanahu) akateremsha vitabu vitukufu
vilivyofungamanishwa na risala ya uongofu kwa
viumbe wote. Vitabu hivyo vikafanywa kuwa ni
nyenzo za kuwajenga viumbe kumjua na kumuabudu
yeye.
Mbali na neema zote hizo, viumbe hawakuacha
kuwapiga vita Mitume hao wa Allah (Subhanahu)
sambamba na kukanusha yale waliyokuja nayo. Haya
yote sababu ikiwa ni namna ambavyo waliwakataza
juu ya Ushirikina wa aina zote. Kwani ushirikina ni
dhambi kubwa na yenye kuangamiza. Mbali na hivyo,
ushirikina, ni dhulma anayozulumiwa Allah
(Subhanahu), kwa kuchukuwa haki ya kuabudiwa na
kupewa kiumbe mwengine asiyekuwa Yeye. Allah
(Subhanahu) amelieleza hili wazi wazi ndani ya
Qur‟an, akinukuu maneno ya Mtume wake Luqmani

24
(Alaihi Salatu wa Salam) akiwa anampa mwanawe
waadhi, nae alisema:

﴾ٖٔ﴿‫َن الَ تُ ْش ِرْك بِٱللَّ ِو إِ َّن ٱلشّْرَك لَظُْلم َع ِظيم‬ ِ ِِ َ َ‫َوإِ ْذ ق‬


ََّ ‫ال لُ ْو َما ُنِ البْنو َوُى َو يَعظُوُ ٰيػبُػ‬
ْ
“Na Luqman alipo mwambia mwanawe kwa kumpa
waadhi: Ewe mwanangu! Usimshirikishe Allah. Kwani
hakika ushirikina bila shaka ni dhulma iliyo kubwa”
(31:13)
Ushirikina umekuwa ni dhulma kubwa, kwakuwa
kiumbe anamdhulumu Muumba kwa kuchukuwa sifa
zake za kuabudiwa akampa asiyekuwa Allah
(Subhananu). Ushirikina ni kujaalia asiyekuwa Allah,
mshirika, msawa ama aliyekuwa darja sawa au haki
sawa na Allah katika yale mambo ambayo
yanamkusudia Mmoja tu, ambaye ni Allah
(Subhanahu).
Ushirikina ni kumjaalia Allah mshirika mwenza katika
yale ambayo ni mahasusi kwake, ikiwa ni katika
Uungu wake ilihali wakijua kuwa Allah (Subhanahu)
ndiye Muumba. Aidha, ndiye anaeyaendesha mambo
yote. Sambamba na kuelewa hayo yote, viumbe
wakamshirikisha Allah (Subhanahu) katika mambo
ambayo kwa yakini mfanyaji na msimamizi ni Yeye.
Watu wakamshirikisha Allah (Subhanahu) katika
kuelekeza shida zao kwa viumbe wengine, kama vile
kuomba mvua, utajiri, poza za maradhi, na mengine

25
katika mahitaji ya viumbe (wanadamu) kwa viumbe
wengine pasi na kumuomba Allah (Subhanahu).
Haya yote ni katika ushirikina, ambao kwa yakini
mwisho wake ni majuto, udhalili na uhasama baina ya
watu hapa duniani na ni majuto na udhalili mkubwa
mbele ya Allah (Subhanahu). Kwani imethibiti ndani
ya Qur‟an tukufu kuwa viumbe ambao
watamshirikisha Allah hapa duniani, watatambua na
kukiri kuwa wamekua miongoni mwa walio katika
maangamivu makubwa. Kama alivyosema Allah ndani
ya Surat Ash-Shuara‟

﴾ٜٛ﴿‫ني‬ ِ ٍ ِ‫ضالَ ٍل ُّمب‬


ّْ ‫﴾ إِ ْذ نُ َس ّْوي ُك ْم بَِر‬ٜٚ﴿‫ني‬ ِ ِ
َ ‫ب ٱلْ َعالَم‬ َ ‫تَٱللَّو إِن ُكنَّا لَفى‬
“Wallahi! Kwa yakini tulikuwa katika upotovu ulio
dhihiri, Pale tulipo kufanyeni ni sawa na Allah, Mola
mlezi wa walimwengu wote.” (26:97-98)
Hivyo, ndugu yangu msomaji, kila Imani juu ya haki
ya Allah (Subhanahu) na Uungu wake ambao
atapewa mwengine asiekuwa Yeye ni ushirikina.
Kuamini na kutakidi kuwa yupo mwengine ambae
anaweza kutoa riziki, anaeweza kuzuru ama
kunufaisha, mwenye kuweza kutatua shida yoyote ile,
anaeweza kuleta mvua, ama mengine yote
yasiyokuwa hayo mbali na Allah (Subhanahu) basi
tambua umeshazama ndani ya kina kirefu cha
ushirikina.

26
Kadhalika, kufanya ushirikina katika matendo yote ya
ibada, pia tambua unaendelea kudidimia ndani
dhambi ya ushirikina na dhulma kubwa kwa Muumba
wako. Kwani, ibada na matendo yote mema ni katika
stahiki za Allah (Subhanahu), ukijumuisha matendo
yote kama vile dua, kwani dua ni ibada ambazo
mkusudiwa ni Allah (Subhanahu), kwani anasema
ndani ya Surat Ghafir:

‫ب لَ ُك ْم‬ ِ ‫ال ربُّ ُكػم ٱدع ِوِن أ‬


ْ ‫َستَج‬
ْ ۤ ُ ْ ْ َ َ َ‫َوق‬
“Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni
nitakuitikieni.” (40:60)
Allah (Subhanahu) amesema aidha:

‫ان فَػلْيَ ْستَ ِجيبُواْ َِل‬


ِ ‫َّاع إِذَا دع‬
َ َ ِ ‫يب َد ْع َوةَ ٱلد‬
ِ ِ ِ ِ ِ َ‫وإِذَا سأَل‬
ُ ‫ك عبَادى َع َّْن فَإ ِّّْن قَريب أُج‬
َ َ َ
﴾ٔٛٙ﴿‫ولْيػ ْؤِمنُواْ ِِب لَعلَّهم يػر ُش ُدو َن‬
َْ ْ ُ َ َُ
“Na waja wangu watakapo kuuliza habari zangu,
waambie kuwa Mimi nipo karibu. Naitikia maombi ya
mwombaji anapo niomba. Basi waniite Mimi, na
waniamini Mimi, ili wapate kuongoka.” (02:186)
Yamkini, ibada zote ambazo tunazifanya kwa kupitia
mafundisho sahihi ya Qur‟an na Sunna za Mtume
wake, zinamstahikia Yeye. Kama ilivyo ibada ya dua,
basi tambua hata kuchinja, sala na ibada zote
nyengine ambazo zimekuja katika misingi sahihi ya
Imani, basi mkusudiwa ni Allah (Subhanahu). Kama

27
ilivyokuja ndani ya Qur‟an kupitia Surat Al-An‟am
kuwa Allah amesema:

﴾ٕٔٙ﴿‫ني‬ ِ ّْ ‫اى َوِمََاتِى لِلَّ ِو َر‬


َ ‫ب ٱلْ َعالَم‬
ِ ِ ‫قُل إِ َّن‬
َ َ‫صالَتى َونُ ُسكى َوََْمي‬
َ ْ
“Sema: Hakika Sala zangu, na ibada zangu (kuchinja),
na uhai wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Allah,
Mola Mlezi wa viumbe wote.” (06:162)
Ukitazama kwa jicho la yakini, utagundua kuwa jamii
yetu imeingia katika kiza kinene cha ushirikina. Na
huenda haya yote ni kwa sababu jamii imeshindwa
kutambua ubaya na ukubwa wa dhambi ya ushirikina.
Ukirudi katika historia utaona kuwa ushirikina
umezaliwa kwa asili ya kuwatukuza watu wema kiasi
cha kuvuka mipaka. Kama ambavyo Qur‟an
inatuthibitishia juu ya kisa cha mabwana wakubwa
watano katika watu wa Mtume Nuhu. Allah anasema
ndani Surat Nuh:

﴾ٕٖ﴿ً‫وق ونَسرا‬ ِ
َ ُ‫َوقَالُواْ الَ تَ َذ ُر َّن آِلتَ ُك ْم َوالَ تَ َذ ُر َّن َوّداً َوالَ ُس َواعاً َوالَ يػَغ‬
ْ َ َ ‫وث َويػَ ُع‬
”Na wakasema: Msiwaache miungu yenu, wala
msimwache Wadda wala Suwaa‟ wala Yaghutha,
wala Yau‟qa, wala Nasra.” (71:23)
Mabwana hawa walikuwa ni watu wema katika kizazi
cha watu wa Mtume Nuhu (Alaihi Swalat wa Salam)
ambapo baada ya kufa kwao, wanadamu kwa
ushawishi wa shetani wakawafanya ni kimbilio la

28
shida zao. Kama ambavyo tunaona katika nyakati
zetu (tutaelezea mbeleni) namna ambavyo watu
wanavyotoka katika mipaka ya Allah (Subhanahu)
mfano ambavyo walifanya miongoni mwa wajinga
waliopita. Kwa msingi huu, jamii inapaswa kuamka
kutoka katika dhambi ya ushirikina, tuchunge
kuchupa mipaka ya Allah (Subhanahu), tuwe werevu
katika kusoma na kujua uwanda wa ushirikina katika
kila tendo ambalo tunalifanya. Tuhakikishe
tunamfanyia ibada yule anaestahiki kufanyiwa na
kujikataza na yale ambayo yatatuingiza katika
ushirikina na huenda yakatutoa katika dini zetu.
Kwani ushirikina huporomosha matendo yote mema.

Katika istilahi za kisharia, zipo aina mbili za ushirikina.


Ambazo 1. Ushirikina Mkubwa 2. Ushirikina Mdogo,
ambazo zote ni makosa makubwa sana mbele ya
Allah.
Ushirikina Mkubwa:
Ni aina ya Ushirikina ambao mtendaji hutoka kwenye
Mila sahihi ya Kiislamu na imesemwa kwamba damu
yake na mali yake ni halali. Aina hii ya Shirki ni
kujaalia kiumbe ama kitu chengine kwa ajili ya
kukusudia haja na maombi, mbali na Allah
(Subhanahu). Hili, limebainishwa ndani ya Qur‟an
kwamba Allah (Subhanahu) hamsamehe kiumbe
yoyote baada ya kufa bila ya kufanya tawba ya

29
ushirikina mkubwa na hufuta na kuporomosha
matendo na ibada zote za mja huyo. Kauli ya Allah;

‫ك لِ َمن يَ َشآءُ َوَمن يُ ْش ِرْك بِٱللَّ ِو فَػ َو ِد‬ ِ ِ ِ


َ ‫إِ َّن ٱللَّوَ الَ يػَ ْغفُر أَن يُ ْشَرَك بِِو َويػَ ْغفُر َما ُدو َن ٰذل‬
﴾ٗٛ﴿ً‫ٱفْػتَػر ٰى إِْْثاً َع ِظيما‬
َ
“Hakika Allah Hasamehe kushirikishwa; na husamehe
yaliyo duni ya hilo kwa amtakae. Na anae mshirikisha
Allah, basi hakika amezua dhambi kubwa.” (04:48)
Ibn Kathir (Radhi za Allah ziwe juu yake) katika tafsiri
yake ya Qur‟an, amemnukuu Imam Ahmad kuwa
amemsikia Abu Dhar‟ kwamba Mtume wa Allah
amesema katika Hadith Quds, Allah amesema; “Enyi
waja wangu! Siku ukitutana na Mimi hali ikiwa dunia
yako imejawa na dhambi isipokua ya kunishirikisha,
basi utakutana na Mimi nikiwa nimejawa na msamaha
wa dhambi zako.”
Ushirikina Mdogo:
Ni aina ya ushirikina ambayo pia hujulikana kama
„Riyaa‟ kwamaana ya kufanya ibada ama matendo
mema kwa nia ya kujionesha kwa watu ama kundi
fulani, huku akiacha kufanya ibada kwa ajili ya Allah.
Riyaa ni miongoni mwa tabia ambazo muislamu
anatakiwa kujiepusha nazo ili aweze kutimiza
malengo ya uhakika wa ibada zake na matendo yake
kwa Allah, ili yawe yenye malipo mbele ya Allah.

30
Imepokelewa kutoka kwa Mahmuwd bin Labiyd
ambae amesema: Rasul Allah (Alaihi Swalatu
Wasalam) amesema: “Hakika ninachokihofia kwenu
zaidi ni Shirki ndogo. Wakasema “ni ipi hiyo Shirki
ndogo?” Akasema: Ar-Riyaa. Allah („Azza wa Jalla)
Atawaambia watu siku ya Qiyama pale watakapolipwa
malipo yao: Nendeni kwa wale mliokuwa mkijionesha
kwa „amali‟ zenu duniani kisha tazameni je, mtakuta
kwao malipo yoyote?
 Imam Ahmad na Shaykh Al-Albaaniy (Radhi za Allah
ziwe juu yao wote) wameisahihisha Hadith hii.

Kwa kauli hii ya Mtume wa Allah ni dhahiri kwamba


Ar-Riyaa ni kitendo kibaya ambacho kinaweza
kuwaathiri wengi miongoni mwa waumini. Kwa
maana katika ibaada mbali mbali kama vile swala,
sadaka, pamoja na amali nyengine njema. Zote hizo
zinaweza kuonekana kana kwamba mtu anafanya kwa
ajili ya Allah, na kumbe lengo lake ni kuwaonesha
watu kwa minajili aweze kusifiwa ama kupewa
heshima fulani ndani ya jamii. Mtume wa Allah
aliogopea sana waumini kuingia kwenye aina hii ya
ushirikina. Kadiri zama zinavyokwenda ndivyo imani
za waumini zinazidi kuporomoka kutokana na
kuhafilika na kuacha misingi imara ya itikadi
aliotuachia Mtume kupitia misingi ya Qur‟an na Sunna
zake zilizotakasika.

31
UFAFANUZI WA USHIRIKINA NDANI YA
QUR‟AN
“Hakika Shirki ni dhulma kubwa mno” Allah
(Subhanahu) amekemea na kufafanua kwa uwazi juu
ya uovu wa ushirikina kwa viumbe wake. Akaeleza juu
ya matokeo yake kwa kiumbe yoyote atakae
shirikisha, ama kwa shirki ya aina yoyote ile kwa
maana ni kukataa haki Yake ya kuabudiwa yeye na
yeye tu. Tunaweza kusema kwamba ushirikina unao
uwanda mpana sana kwenye kupambanua maana,
mbinu na njia tofauti ambazo hutumika na viumbe
waliochagua kuenda kinyume na maelekezo na
makatazo ya Allah na Mtume wake, katika kuyatenda
matendo ambayo kwa jicho la kawaida huonekana
yapo kwenye njia ya uongofu lakina kwa siri huwa
yamejaa ghadhabu na laana za Allah.
Katika nyakati za Mtume wa Allah na Maswahaba
zake, Shirki kubwa ilikua ni kumshirikisha Allah
(Subhanahu) na masanamu, ama viumbe wengine wa
Allah kama vile jua, mwezi ama moto. Hivyo ilikuwa
wazi katika ubainifu wa kutambua nani haswa ni
mshirikina na nani ni Muumini, ukiacha kundi la
wanafiki ambalo walijificha kwenye mbavu za
waumini.
Kwa nyakati zetu za sasa, huenda tukawa
tumenusurika kwa kiasi kikubwa na shirki hii, ila kuna
mazito ambayo yanaendelea kwenye ushirikina

32
ambayo naweza kusema kwamba athari yake ni
kubwa zaidi kuliko ile ya awali kwa maana kipindi kile
tunasema ni kipindi cha ujinga. Kwa nyakati zetu,
uchafu mkubwa umeelekea kwenye imani za kichawi
na mizimu na kuamini katika ulinzi wa mashetani na
mizimu na hata kufikia hatua ya wachache
kuogopewa na jamii inayowazunguka kutokana na
matumizi mabaya ya viumbe hawa wa Allah
(Subhanahu) ambao wameumbwa kwa lengo moja
linalofanana na wanadamu la kumuabudu. Allah
anasema;

ِ ‫ٱْلِ َّن وٱ ِإلنس إِالَّ لِيػعب ُد‬


﴾٘ٙ﴿‫ون‬
ُْ َ َ َ ْ ‫ت‬ ُ ‫َوَما َخلَ ْو‬
“Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu
Mimi.” (51:56)
Ibn Kathir (Radhi za Allah ziwe juu yake) amefafanua
maana ya kauli ya Allah “Ila waniabudu Mimi” na
kusema kuwa; maana yake ni kwamba Allah hahitaji
kwa viumbe hawa chochote naye aliwaumba na
kuwaamrisha wamuabudu. Ali bin Abi Talhah (Radhi
za Allah ziwe juu yake) aliskia kwamba Ibn Abbas
(Radhi za Allah ziwe juu yake) akisema juu ya kauli hii
ya Allah kuwa; “Wameumbwa viumbe hawa
wamuabudu Allah kwa hiyari ama kwa lazima kwa
maana wanawajibika kufanya hivyo.”
Ubaya na uovu ulioenea sasa nikwamba viumbe hawa
wameacha madhumuni hayo ya kuumbwa na badala

33
yake baina yao wakapatika watumwa wakuwatumikia
wengine na wakapatikana mabwana wakukusudiwa
shida za wengine. Jambo lakusikitisha zaidi kwa sasa
ushirikina umetamalaki katika hatua nyengine ambayo
ni mbaya zaidi kwa baadhi ya washirikina
kujinasibisha na kitabu kitukufu cha Qur‟an,
kujinasibisha huko ni kwasababu ya kuficha maovu ya
ushirikina wao wa kutumia mgongo wa Ruqya na
Dua. Ila kwa kupitia chapisho hili, tunawapa tanbihi
kwamba Allah alishawatambuwa mbinu zao tangu
kipindi cha Mtume wa Allah na ndio maana Allah
amesema;

﴾ٜ﴿‫ُُيَ ِاد ُعو َن ٱللَّو وٱلَّ ِذين آمنُوا وما َُيْ َد ُعو َن إِالَّ أَنْػ ُفسهم وما ي ْشعرو َن‬
ُُ َ َ َ ُ َ ََ َ َ َ َ
“Wanatafuta kumdanganya Allah na wale walio amini,
lakini hawadanganyi ila nafsi zao; nao hawatambui.”
(02:09)
Kunasibishwa huku ni pamoja na kupiga ramli na
kutumia baadhi ya vitabu vya dua ambavyo kwa
hakika madhumuni ya waandishi wa vitabu hivyo
hayakua katika chochote miongoni mwa
wanavyovitumia. Mfano mzuri katika hili ni kitabu cha
Ahlil Badri; ambacho kimeorodhesha majina ya
Maswahaba (Radhi za Allah ziwe juu yao wote)
waliopigana sambamba na Mtume wa Allah katika vita
ya Badri. Watu hawa wamekuwa na athari kubwa

34
katika jamii na wakiaminika kwamba ni masheikh
wenye kuwafanyia watu dua mbali mbali za shida zao.
Hakuna chochote wanachojinasibisha nacho
kimethibiti ndani ya Qur‟an na Sunna isipokua
ushirikina na dhulma. Na hutumia mwanya huo
kujinathibisha na Qur‟an kufanya ramli na kutumia
majini wawe ni msaada wa kutatua shida za wateja
wao. Hivyo basi, kwa kila muhusika wa kundi hili
atambue kua yumo katika uovu mkubwa wa
ushirikina, na kwa upande mwengine wale wenye
kuwaendea watu hawa wajue pia nafasi zao mbele ya
Allah (Subhanahu), nafasi ambazo zina majuto na
hasara kemkem. Kwani Mtume wa Allah amesema
katika Hadith sahihi kuwa;
((Atakaekwenda kwa mtabiri akamuuliza kitu
hazitokubaliwa Swalaa zake kwa siku arubaini))
[Muslim]
Pia Mtume amesema;
((Atakae mwendea kahini au mchawi akasadiki
(akaamini na kutekeleza) yale anayoyasema basi
amekufuru ambayo Ameteremshiwa nayo Muhammad
(Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) [Tafsiyr Ibn
Kathiyr; Hadithi hii ina isnaad ya upokezi Sahihi na
kuna Hadithi zinazokubaliana na hii]
Ndugu yangu msomaji, acha nikubainishie nukta hizi
muhimu ambazo tutazibainisha kwa upana mbeleni ili

35
kila mmoja wetu awe ni mwerevu kwenye kuhakikisha
tunaepuka kiunzi cha kuingia kwenye mtego huu;
 Ruqya ya Kisheria humtegemea moja kwa
moja Allah kwa maana yeye ndiye mtatuaji wa
shida za viumbe.
 Ruqya ya Kisheria haihitaji kuchoma chungu,
kutupa mayai, kuvunja nazi wala kitabu
chochote isipokua Qur‟an kwani ndiyo ponyo
na utatuzi. Kwa Kauli ya Allah;

‫ِف آ َذاِنِِ ْم َوقْػر َوُى َو َعلَْي ِه ْم‬ ِ


ۤ ِ ‫ين الَ يػُ ْؤمنُو َن‬
ِ َّ ِ
َ ‫ين َآمنُواْ ُى ًدى َوش َفآء َوٱلذ‬
ِِ
َ ‫قُ ْل ُى َو للَّذ‬
ٍ ِ‫ان بع‬ ِ
‫يد‬ ٍ َ ِ‫َع ًمى أ ُْولَػٰئ‬
َ ‫ك يػُنَ َاد ْو َن من َّم َك‬
“Sema: Hii Qur‟an ni uwongofu na poza kwa wenye
kuamini. Na wasio amini umo uziwi katika masikio
yao, nayo kwao imezibwa hawaioni. Hao wanaitwa
nao wako pahala mbali. ”(41:44)
Allah amesema pia;
ِ ِ ُ ‫آن ما ىو ِش َفآء ور ْْحة لّْْلم ْؤِمنِني والَ ي ِز‬
ِ ِ
َ ‫يد ٱلظَّالم‬
َّ‫ني إَال‬ َ َ َ ُ َ ََ َ ُ َ ‫َونػُنَػّْزُل م َن ٱلْ ُو ْر‬
﴾ٕٛ﴿ً‫خسارا‬
ََ
“Na tunateremsha katika Qur‟an yaliyo ni matibabu na
Rehema kwa Waumini. Wala hayawazidishii
madhaalimu ila khasara.” (17:82)
Kwa kaui hizi za Allah unaweza kupata ubainifu juu ya
nukta hizi muhimu na kwa hakika Qur‟an inatosha

36
kuwa ni suluhisho la kila tatizo. Sharti la msingi ni
Imani ya kweli juu ya Allah. Amesema Sheykh „Abdul-
Rahman As Sa‟adiy (Radhi za Allah ziwe juu yake)
“Poza iliyokusanywa katika Qur‟an, kwa ujumla ni
poza ya moyo, na mwili kutokana na maumivu yake
na huzuni.

HUKMU ZA USHIRIKINA NDANI YA QUR‟AN


Katika kuonesha uzito wa dhambi hii, Allah
(Subhanahu) ametoa makatazo ndani ya Qur‟an
kupitia Aya 126, zote zikionesha na kukemea viumbe
juu ya kujihusisha na aina yoyote ya ushirikina.
Hakika ushirikina ni dhulma kubwa mno mbele ya
Allah, Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah (Radhi za
Allah ziwe juu yake) amesema: “Hakika kila
Alichokikataza Allah kinarejea katika dhulma na kila
Alichokiamrisha kinarejea katika uadilifu, na ndio
maana Allah (Subhanahu) Amesema:

‫َّاس بِٱلْ ِو ْس ِط‬


ُ ‫وم ٱلن‬
ِ ِ
َ ‫اب َوٱلْم َيزا َن ليَػ ُو‬
ِ ِ
َ ‫لَ َو ْد أ َْر َس ْلنَا ُر ُسلَنَا بِٱلْبَػيّْػنَات َوأ‬
َ َ‫َنزلْنَا َم َع ُه ُم ٱلْكت‬
“Kwa hakika tuliwatuma Mitume wetu kwa dalili
waziwazi, na tukateremsha Kitabu pamoja nao na
Mizani, ili watu wasimamie uadilifu.” (57:25)
Hivyo basi, kuusiana na kupeana waadhi juu ya
kuachana na kujiepusha na ushirikina ni uadilifu kwa
Allah (Subhanahu) kwani humfanya mtu kuchunga
haki za Allah, na kwa upande mwengine kuendelea na
kudidimia ndani ya ushirikina kwa matendo ni

37
kuendelea kuchochea dhulma kwa Muumba wetu na
mwisho wake ni madhara kwetu na nafsi zetu.
Qur‟an tukufu imefafanua na kubainisha juu ya
Hukmu za dhambi ya ushirikina huku ikionesha kwa
kina juu ya namna ambavyo Allah (Subhanahu)
anavyochukia kushirikishwa.

Surat Az-Zumar:

‫ت لَيَ ْحبَطَ َّن َع َملُ َك َولَتَ ُكونَ َّن ِم َن‬ ِ َ ِ‫ك وإِ ََل ٱلَّ ِذين ِمن قَػبل‬ ِ ِ
َ ‫ك لَئ ْن أَ ْشَرْك‬ ْ َ َ َ ‫َولَ َو ْد أ ُْوح َى إلَْي‬
﴾ٙ٘﴿‫اس ِرين‬ ِ ْ
َ َ‫ٱْل‬
“Na kwa yakini yamefunuliwa kwako (Ewe Mtume) na
walio kuwa kabla yako: Bila shaka ukimshirikisha Allah
matendo yako (mema) yataanguka, na lazima utakua
miongoni mwa wenye kuhasirika” (39:65)
Ibn Kathir (Radhi za Allah ziwe juu yake) amefafanua
katika Tafsiri yake kuwa; miongoni mwa sababu za
kushuka Aya hii pamoja na ya nyuma yake,
imenukuliwa kutoka kwa Ibn Abi Hatim kwamba Ibn
Abbas amesema makafiri katika upotevu wao
walimwita Mtume wa Allah kwamba wakubaliane
aende kuabudu miungu yao kwa kipindi fulani, kisha
wao watakubali kumuabudu Allah kwa kipindi
maalumu. Na ndio Allah akashusha Aya hii ya katazo
kwa Mtume wake na Waumini kwa ujumla.

38
Surat Al-Bayyinah:
ِ ‫اب وٱلْم ْش ِركِني ِِف نَا ِر جهنَّم خالِ ِد‬ ِ َّ ِ
َ ِ‫ين ف َيهآ أ َْولَػٰئ‬
‫ك ُى ْم‬ َ َ َ ََ
ِ ِ
َ ُ َ ِ َ‫ين َك َفُرواْ م ْن أ َْى ِل ٱلْكت‬
َ ‫إ َّن ٱلذ‬
﴾ٙ﴿‫َشُّر ٱلْ َِبيَِّة‬
َ
“Na hakika waliokufuru miongoni mwa waliopewa
kitabu, na washirikina basi hao makazi yao ni moto
wadumu humo milele na hayo ni jaza mbaya kuliko
zote” (98:06)
Katika Aya zote ambazo Allah amezibainisha kukataza
ushirikina na matokeo yake amekuwa akitoa kauli za
kutisha sana juu matokeo ya watu hao, hapa Allah
anasema “Hao makazi yao ni moto na watadumu
humo milele” Katika kufafanua maana ya kauli hii, Ibn
Kathir (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema
kwamba maana yake ni kusema watabakia ndani ya
moto huo na hakutakuwa na njia yoyote ya kutoka na
adhabu ndani yake hazitosimama.
Surat Luqman:

﴾ٖٔ﴿‫َن الَ تُ ْش ِرْك بِٱللَّ ِو إِ َّن ٱلشّْرَك لَظُْلمع ِظيم‬ ِ ِِ َ َ‫َوإِ ْذ ق‬


ََّ ‫ال لُ ْو َما ُنِ البْنو َوُى َو يَعظُوُ ٰيػبُػ‬
َ ْ
“Na Luqman alipo mwambia mwanawe kwa kumpa
waadhi; Ewe mwanangu! usimshirikishe Allah. Hakika
ushirikina bila shaka ni dhulma kubwa mno.” (31:13)
Nabii Luqman (Rehma za Allah ziwe juu yake) Alikua
ni Mtume mwenye busara na taqwa ya juu sana na

39
hapa unaweza kuona Allah anamsimulia Mtume
Muhammad (Rehma na Amani ziwe juu yake) juu
waja waliokuwa na taqwa. Aya hii inaweza kutupa
funzo kwamba Taqwa kwa watoto hujengwa na
wazazi, hivyo wazazi wana nafasi kubwa juu ya
Taqwa ya watoto wao. Na Aya hii inaonesha uzito wa
ushirikina ambapo kiumbe mwenye kumpenda mtoto
wake basi kila wakati atamuusia na kumuelekeza
mtoto juu ya kujiweka mbali na kumshirikisha Allah.
ِ ‫ك بِِو عِ ْلم فَالَ تُ ِطعهما وص‬
‫احْبػ ُه َما ِِف‬ َ َ َ ُْ َ َ‫س ل‬ ِ ِ
َ ‫اى َد َاك َعلَ ٰى أَن تُ ْشرَك ِب َما لَْي‬ َ ‫َوإِن َج‬
‫َل َم ْرِج ُع ُك ْم فَأُنػَبّْئُ ُك ْم ِِبَا ُكنتُ ْم‬
ََّ ِ‫َل ُُثَّ إ‬
ََّ ِ‫اب إ‬
َ َ‫يل َم ْن أَن‬ِ ِ
َ ‫ٱلدنْػيَا َم ْعُروفاً َوٱتَّب ْع َسب‬
ُّ
﴾ٔ٘﴿‫تَػعملُو َن‬
َْ
“Na pindi wakikulazimisha kunishirikisha na ambayo
huna elimu nayo, basi usiwatii. Lakini kaa nao kwa
wema duniani, nawe ishike njia ya anae elekea
kwangu. Kisha marejeo yenu ni kwangu Mimi, na
Mimi nitakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda.”
(31:15)
Kwa wafuatiliaji wa Qur‟an unaweza kuona kwamba
Allah mtukufu amewapa cheo cha juu wazazi wawili
na katika Aya tofauti amewausia viumbe juu ya
kuwatendea wema wazazi wawili. Na mara nyingi
Allah hufunganisha wema kwa wazazi na ibada yake
kutokana na darja za juu alizowapa wazazi, kwa uzito
huo na uzito wa ushirikina, unaweza kuona kupitia

40
kauli hii ya Allah; mbali na darja alizowapa (wazazi)
ila bado haziwezi kuwa ni sababu ya wao
kukuamrisha kumshirikisha Allah.
Ibn Kathir (Radhi za Allah ziwe juu yake) amenukuu
kisa cha Swahaba wa Allah Sa‟ad; Sa‟ad (Radhi za
Allah ziwe juu yake) alikuwa ni mtu anae waheshimu
sana wazazi wake, wakati ameingia kwenye Uislamu,
mama yake alimwambia: „Ewe Sa‟ad! Ni kitu gani hiki
kipya ninachokuona unafanya na kuacha dini yako na
ya wazazi wako, Nakuamrisha uache bila hivyo
sitakula wala kunywa chochote hadi nifariki, na watu
watakushangaa kwa kitu ulichomfanyia mama yako.
Sa‟ad akasema; Usifanye hivyo mama yangu, kwani
sitoacha dini ya haki kwa chochote.‟ Hivyo aliamua
kukaa kwa siku mbili bila kula wala kunywa na kuanza
kuonekana kuwa na hali mbaya. Sa‟ad akasema;
„Nilipoona hali hiyo, nikamuambia, “Ewe mama yangu,
kwa jina la Allah, hata kama ungekua na nafsi mia
moja na zikaanza kutoka moja baada ya nyengine,
Sitoweza kuacha dini ya haki, kwa chochote, hivyo
unaweza kuendelea kuacha kula ama kuamua kula,
Mwisho aliamua kula.
Hivyo basi, ni dhahiri kuwa ushirikina ni dhambi
kubwa mbele ya Allah (Subhanahu) na ni jambo
ambalo tunapaswa kujiweka mbali nalo (kama
alivyosisitiza Mtume wa Allah). Qur‟an imefafanua na
kubainisha wazi kuwa ushirikina ni haramu kwa

41
uthibitisho ndani Qur‟an, Hadithi sahihi za Mtume
(Swalla Allahu alaihi wa Sallam) pamoja na
makubaliano ya wanazuoni wote wa sasa na
wazamani.

KAULI ZA WANACHUONI JUU YA UKUBWA NA


UHARAMU WA USHIRIKINA, DUNIANI NA
MBELE YA ALLAH
Katika kubainisha uchafu na uovu wa ushirikina,
wanachuoni mbali mbali wametoa fafanuzi na fatawa
nzito juu ya ushirikina huku wakiashiria kima cha uzito
wa dhambi hii mbele ya Allah (Subhanahu). Ufafanuzi
huu utatupatia ubainifu juu ya uzito wa ushirikina ili
iwe ni sababu kwa kila ambae ameteleza kwa kujua
ama kutokujua na kujikuta ametumbukia kwenye
shimo lenye kiza kinene. Lengo letu ni kuhakikisha
jamii ya kiislamu ina twahirika na ushirikina, kwani
kila mmoja wetu akipata elimu na kujua ubaya,
uharamu na dhambi ya ushirikina, basi tunaweza
kutahamaki washirikina wamekosa wateja. Tukianza
na ufafanuzi huu, tuangalie kauli na nasaha za Al-
Alaamah Swaahil bin Fawzan (Allah amhifadhi)
aliulizwa katika Fatawah zake;
((Mwenye kutubu kwa ushirikina kama wa uchawi
anasamehewa? Vipi kujumuisha baina ya Aya (Kwa
hakika Allah Hasamehe) na baina ya Aya za
Tawbah?)) Al-Fawzaan (Allah amhifadhi) akajibu;
((Kwa hali yoyote, mchawi anauawa. Asimamishiwe

42
adhabu, adhabu haikomeki kwake. Ama kutubu
kwake, ni baina yake na Allah. Ikiwa kama ni mkweli,
basi amri yake iko kwa Allah. Ama adhabu, haikomeki
kwake hata akifanya Tawbah))
Shaykh Al-Fawzaan (Allah amhifadhi) alisema pia
katika nasaza zake; ((Mtu asitamani kupona na
akachukulia sahali (wepesi) masuala haya (ya
ushirikina katika dua). Akaenda kuchukua (dawa) kwa
wachawi na akachukua nasaha zao. Wakamfanyisha
ushirikina na kumshirikisha Allah („Azza wa Jalla) kwa
madai ya kutamani kupona kwa maradhi. Na
wanaweza wakasema baadhi yao ya kuwa hii ni
dharura. Hii sio dharura. Allah (Jalla wa „Alaa)
Hakufanya dawa yetu kwa yale aliyotuharamishia. Hii
sio dharura kwa kuwa Allah hakufanya dawa ikawa
katika Haramu. Vipi tusemeje kuhusu ushirikina?
Hakuna dharura. Allah amewawekea Waislamu Ruqya
ya kisharia, Ruqya yenye kunufaisha na Ruqya yenye
manufaa. Ni juu yao waishie katika aliyoyaweka Allah
na ndani yake kuna kheri nyingi. Na lau wangelitumia
aliyoruhusu na kuweka Allah na huku wakamuamini
Allah (Subhanahu), basi Allah angeliwafaa kwahilo na
dawa ingelipatikana kwa idhini ya Allah (Subhanahu).
Imam Ibn Baaz (Radhi za Allah ziwe juu yake) nae
akatoa ufafanuzi juu ya suala la kuchinja kwa ajili ya
asiekuwa Allah. Haya tunayaona mara nyingi
yakifanyika katika tiba za kishirikina, akasema moja

43
kwa moja kwamba huo ni ushirikina na ni munkari
mkubwa. Shaykh, aliulizwa kuwa; ((Kuchinja kwa ajili
ya asiekuwa Allah inajuzu? Kwa kuwa huku kwetu
watu wanamchinjia mtu ambae anaitwa “Mujalliy”
tunaomba utupe faida.)) Imam Ibnu Baaz (Radhi za
Allah ziwe juu yake) akajibu kuwa; ((Kuchinja kwa
ajili asie kuwa Allah ni munkari mkubwa na ni
ushirikina mkubwa, sawa ikiwa kachinjiwa Nabii,
Walii, Nyota, Jinni, Sanamu au visivyokuwa hivyo.
Kwa kuwa Allah (Subhanah) Anasema:

َ ‫ٔ﴾الَ َش ِر‬ٕٙ﴿‫ني‬
ُ‫يك لَو‬
ِ ّْ ‫اى َوِمََاتِى لِلَّ ِو َر‬
َ ‫ب ٱلْ َعالَم‬
ِ
َ َ‫صالَتى َونُ ُسكى َوََْمي‬
ِ ‫قُل إِ َّن‬
َ ْ
﴾ٖٔٙ﴿‫ني‬ ِِ ِ َ ِ‫وبِ ٰذل‬
َ ‫ت َوأَنَاْ أ ََّو ُل ٱلْ ُم ْسلم‬
ُ ‫ك أُم ْر‬ َ
“Sema: Hakika Sala zangu, na ibada zangu, na uhai
wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Allah, Mola
Mlezi wa viumbe wote. Hana mshirika wake. Na hayo
ndiyo niliyo amrishwa, na mimi ni wa kwanza wa
Waislamu.” (06:162-163)
Akaendelea kueleza kuwa; Allah (Subhanahu)
anaeleza kuwa kuchinjiwa ni kwa ajili yake kama
Swala ilivyo yake. Atakaechinja kwa ajili ya asiekuwa
Allah, ni kama alieswali kwa ajili ya asiekuwa Allah.
Atakuwa kamshirikisha Allah („Azza wa Jalla). Ibaada
ni haki ya Allah pekee; na kuchinja ni miongoni mwa
ibada, kutaka msaada ni katika ibada na swala ni
katika ibada na imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla
Allahu alayhi wa sallam) ya kwamba amesema:

44
((Allah Amlaani mwenye kuchinja kwa ajili ya
asiekuwa Allah.)) Sahih Muslim, Hadith kutoka kwa
Aliy (Radhi za Allah ziwe juu yake). Ni juu yenu
kuwakataza watu hawa na kuwafunza ya kwamba
huu ni ushirikina mkubwa na kwamba lililo la wajibu
juu yao ni kuacha hilo.
Baadhi ya wanazuoni wanasema kuwa; hata kama
ataambiwa mtu kutoa mnyama ili achinjwe kwa ajili
ya kafara ya matatizo yake, basi ni juu yake kuchunga
juu ya uhalali wa kafara hiyo na ni juu yake pia
kutambua ni kweli mkusudiwa wa kichinjwa hicho ni
Allah (Subhanahu) au anakusudiwa mwengine
miongoni mwa viumbe vyake. Kama kichinjwa hicho
ni kwa ajili ya asie kuwa Allah (Subhanahu) basi
atambue anafanya jambo ambalo linampelekea katika
ushirikina wenye kuangamiza matendo na Imani
yake.
Kwa kuongozea katika kauli za Imam Ibn Baaz (Radhi
za Allah ziwe juu yake), aliulizwa pia kuhusu uvaaji
wa hirizi kama inavyoelezwa: Aliulizwa muulizaji
kuwa; ((Ipi hukumu ya mwenye kuswali au
kutekeleza Ibada yoyote katika Ibada nae mkononi
mwake amevaa hirizi?)) Ibn Baaz (Radhi za Allah ziwe
juu yake) akajibu kuwa; ((Hirizi ni Haramu na wala
haijuzu. Na ni katika ushirikina mdogo, na inaweza
kwenda katika ushirikina mkubwa. Swala yake ni

45
sahihi, ikiwa hakuufanya moyo wake kuitegemea hirizi
hiyo na akaitakidi kuwa inadhuru na kunufaisha.
Hajatumbukia katika Shirki kubwa. Shirki ndogo
haiporomoshi matendo (yote), isipokuwa Riyaa tu
ndiyo inaporomosha amali iliyochanganyika nayo.
Wanawavalisha watoto wao kuwakinga na kijicho,
jinni na huenda akavalishwa hata mgonjwa. Yote
haya ni makosa na hayajuzu. Amesema Mtume
(Swallah Allahu Alayhi wa sallam): ((“Yeyote
atakaevaa hirizi (au ataejiambatanisha na kitu, basi
Allah Hatomtimizia matakwa yake kutimia kamwe. Na
yule atakaevaa au kutundika chaza ndogo (au aina
yoyote ya hirizi.”)). Ni wajibu kwa Muislam kutubu
kwa Allah ikiwa amefanya hili. Hali kadhalika muumini
mwanamke atubu kwa Allah kwa jambo hili na akate
hirizi hii na mtu atahadhari nayo kabisa.))
Katika ufafanuzi huu kwa hakika kuna nukta ya
kuizingatia, tunawezaje kutofautisha na kujiweka
mbali na kujifunganisha na hirizi tunazozivaa kuwa
hatuzitegemei. Ilihali tumezitafuta na kuzinunua kwa
thamani kubwa wakati mwengine. Uamuzi wa kuvaa
au kutundika hirizi ni kwasababu tumeamini na
kuaminishwa kuwa zinaweza kutukinga ama
kutuepusha na jambo fulani, n ahata wahusika
watoaji wa hirizi kutoa huku wakifunganisha na
hakiba ya maneno „Ivae na uitunze hii‟ ili ufanikiwe,
Je! Hatuoni kuwa tayari tumeingia katika ushirikina.

46
Ushirikina wakutegemea ulinzi wa kitu pasi na Allah
(Subhanahu). Na ipi hali ya ibada zetu ambazo
tunazifanya huku tukiwa na mfuko wa hirizi kiunoni
au kikasha kikubwa cha hirizi kwenye maeneo yetu.
Basi hii ndio maana halisi ya Hadithi hii ya Mtume
(Rehma na Amani ziwe juu yake).
Ndugu zangu hizi ni baadhi ya fatwa za wanazuoni na
namna ambavyo wamefafanuwa kwa undani juu ya
masuala tofauti juu ya ushirikina. Natambua kwamba
wapo baadhi ya watu ndani ya jamii wanaamini na
kutakidi kwamba maradhi yoyote ya kichawi basi
hutibiwa kwa uchawi, hili ni miongoni mwa makosa
ambayo Al-Alaamah Fawzaan (Allah amhifadhi) pia
amelitolea ufafanuzi kama alivyo ulizwa; ((Nataka
bayana na kuwekewa wazi katika masuala ya hukumu
ya kutibu uchawi kwa kutumia uchawi mfano wake,
kwa kuwa tumesikia baadhi ya wanaodai wana elimu
wakisema ya kwamba hilo linajuzu.?))
Sheikh Al-Fawzaan (Allah amhifadhi) akajibu kuwa;
((Kutibu uchawi kwa kutumia uchawi mfano wake
haijuzu na ni kufuru kwa kuwa uchawi ni kufuru sawa
kujifunza nao ama kuufunza na kuutumia. Sawa
anautumia ili kutibu uchawi au kautumia ili
kuwadhuru watu. Anasema Allah (Subhanahu):
ِ ِ
َ ‫ني بِبَابِ َل َى ُار‬
‫وت‬ ِ ْ ‫ٱلس ْحر وَمآ أُنْ ِزَل َعلَى ٱلْملَ َك‬
َ َ َ ّْ ‫َّاس‬ َ ‫ني َك َفُرواْ يػُ َعلّْ ُمو َن ٱلن‬َ ‫َولَػٰك َّن ٱلشَّْياط‬
‫َح ٍد َح َّ َّٰت يػَ ُووالَ إََِّّنَا َْْم ُن فِْتػنَة فَالَ تَ ْك ُف ْر‬ ِِ
َ ‫وت َوَما يػُ َعلّْ َمان م ْن أ‬
َ ‫َوَم ُار‬

47
“Lakini shetani ndio waliokufuru; wanawafundisha
watu uchawi na yaliyoteremshwa kwa Malaika wawili
(katika mji wa Baabil, Haaruwt na Maaruwt. Na (hao
Malaika wawili) hawamfundishi yoyote mpaka
wamueleze: “Hakika sisi ni fitna (mithani), basi
usikufuru (kufanya uchawi))”. (02:102)
Hii ni dalili kwamba uchawi ni kufuru na kama Aya
hiyo ilivyoishia;
ِ ‫ولَ َو ْد علِمواْ لَم ِن ٱ ْشتػراه ما لَو ِِف‬
‫ٱآلخَرةِ ِم ْن َخالَ ٍق‬ ُ َ ُ ََ َ ُ َ َ
“Na kwa hakika walielewa kwamba ataenunua
(ataefanya biashara ya uchawi) hatopata katika
Akhera fungu lolote.” (02:102)
Yani, hana katika Pepo fungu na hili haliwi isipokuwa
kwa kafiri. Allah atukinge. Vipi atajitokeza mwenye
kusema ya kwamba inajuzu kutumia uchawi? Yani
mtu ajitibu kwa kufuru? Mtume (Swalla Allahu alayhi
wa sallam) anasema; ((“Msijitibu kwa haramu.”))
Na uchawi ni haramu kubwa. Na Ibn Mas‟uud (Radhi
za Allah ziwe juu yake) anasema – kama ilivyo katika
Sahihi al-Bukhaariy: ((“Kwa hakika Allah Hakufanya
dawa yenu katika yale Aliyowaharamishia.”)) Uchawi
una dawa isiyokuwa kufuru na uchawi.
Nukta hizi tumezileta ili tuweze kulipambanua jambo
hili. Jamii imekua ikiendelea kupeana mawazo maovu
kama haya, watu wengi wakiusiana na kusisitizana

48
kwamba hakuna dawa ya uchawi isipokuwa uchawi
mfano wake au kama msemo maarufu unaotumika
kuwa „Dawa ya moto ni moto‟ hakika hizi ni dhana
potofu katika jicho la sharia ya Kiislamu. Dhana
ambazo zinapaswa kusafishwa ndani ya vichwa vya
watu. Hakuna tiba wala utatuzi wa jambo lolote
inayopatikana kupitia dhambi kubwa kama ushirikina
na hili tunapaswa kulitambua kwa uwazi na
libainishwe kwa vinywa vipana hata kama watachukia
wasiopenda haki.

USHIRIKINA NA JAMII ZETU


Makemeo na makatazo ya ushirikina yamedharauliwa
ndani ya jamii zetu. Hatuna budi kutahazarishana na
kukemeana juu ya dhambi hii na tufanye juhudi mbali
mbali kuwaita watu kuachana kabisa na ushirikina.
Wanazuoni mbali mbali waliifanya juhudi ya kukataza
ushirikina kuwa ni faradhi (Lazima) kwao huku
wakiieleza jamii kwa kauli na maandishi. Lengo kubwa
likiwa ni kuisafisha jamii juu ya ushirikina, kwani
imeonekana ni kama jambo la kawaida ambalo
linapatikana kwa bei nafuu.
Ndani ya jamii zetu kwa sasa ushirikina umeenea zaidi
katika maeneo makubwa matano, ambayo yanagusa
sehemu kubwa ya jamii zetu. Ushirikina umekithiri
katika Dua, Kuomba maiti, ushirikina katika ndoa,
ushirikina katika kazi na biashara pamoja na ushirkina
mkubwa katika michezo. Hizi ni nyanja tano ambazo

49
zinagusa kila mmoja wetu. Bila ya elimu na nasaha za
mara kwa mara tunaweza tahamaki kila mmoja wetu
ameguswa na vumbi la ushirikina.
Ushirikina katika kuomba Dua
Tulitangulia kueleza kuwa Dua ni miongoni mwa
Ibada ambazo mkusudiwa ni Allah (Subhanahu).
Ubaya ulioje katika matendo ya ibada za dua, ndani
yake yakachanganywa mengi miongoni mwa matendo
maovu ya ushirikina. Kwa jicho la kawaida
yakionekana kana kwamba ni miogoni mwa
yanayokubalika katika visomo vya dua za tiba. Walio
wengi hutumia mwanya wa Ruqya (Kisomo cha
Kisharia) kufanya na kuwafanyisha watu ushirikina,
huku wakijinasibisha na Kitabu kitukufu cha Qur‟an.
Yote haya, yanadhihiri wazi wazi ndani ya jamii zetu
kwa kuyaona na kuyasikia. Wengi miongoni mwa
washirikina hutumia vibaya mwemvuli wa dua kwa
kufanya hadaa na kificho cha kuwaficha wahitaji,
huku wakihusisha ushirikina mkubwa wa kutumia
majini na mbinu mbali mbali za kichawi. Hujificha
ndani ya mwamvuli wa dua za kisharia wakipiga ramli,
kutumia majini na hata kuomba mizimu na wafu.
Hebu tafakari, kisha jipe jibu juu ya hili, Kuna
mahusiano gani kati ya Dua kwa Allah (Subhanahu)
na ndimu! Kuna mahusiano gani katika Dua na
kuvunja nazi! Kuna mahusiano gani kati ya Dua kwa
Allah (Subhanahu) na kuchinja mnyama mwenye sifa

50
maalumu! Je! Hizi zote ni Dua kwa Allah (Subhanahu)
au kuna kiumbe mwengine anakusudiwa? Huenda
akawakurubisha Kwake! Wengi wameenda kwa
wasoma dua kisha kurudi na vifurushi kwa ajili ya
kuvizika ama kuchoma au hata hirizi za kuzivaa au
kutundika sehemu tofauti.
Hivyo basi, hizi ni miongoni mwa aina za ushirikina
katika Dua zinazofanyika, tena kwa kiwango kikubwa
sana ndani ya jamii zetu. Lakini tunalipi la kwenda
kueleza mbele ya Allah (Subhanahu) juu ya kuomba
kupitia viumbe wengine visivyokuwa Allah
(Subhanahu), basi hata nafsi na akili zetu hazipati
taabu wakati tukiyafanya haya. Tunashuhudia
utaratibu na mambo mengi ndani ya hizo zinazoitwa
Dua au visomo, wagonjwa wakizungushiwa kuku juu
ya vichwa vyao, mara nyingi hujiuliza kuna uhusiano
wowote katika kutesa kiumbe hicho (Kuku) kwa
kumzungusha na Dua ambayo anayeombwa ni Allah
(Subhanahu).
Majumba mengi ndani ya jamii zetu, hukosi kuona
vikaratasi vimetundikwa mlangoni kwa minajili ya
ulinzi juu ya ubaya dhidi ya nyumba hizo. Ni nani
haswa mwenye dhamana ya ulinzi wa viumbe wote.
Kuna jibu jengine zaidi ya Allah (Subhanhu). Tunaona
namna jamii na nyumba nyingi zinavyokosa Baraka na
ulinzi, mbali na kuwa na hayo wanayoyaamini, bado
matatizo na misukosuko mikubwa inawakumba.

51
Tunaona namna jamii inavyokosa Baraka na
kuongezeka kwa dhiki na umasikini hadi wa chakula,
kutokana na kutumia vibaya neema za Allah
(Subhanahu). Tunayo malalamiko chungu nzima juu
ya kupanda kwa bei za vyakula, bado hatujatanabahi
wapi tunakosea! Huwezi kukosa kuona nazi
zikitapakaa barabarani kwa dhana na Imani chafu za
kishirikina huku wahusika wakila chakula cha
kuchemsha. Na yote hayo akinasibishwa na kuveshwa
vazi la dua na visomo vya kisharia.
Ibada za Dua zimekumbwa na wimbi kubwa la
ushirikina na zimekuwa zikifanywa kama ni njia ya
kudhuru wengine. Yote ni kwasababu ya
kuwajumuisha mashetani na majini katika kutatua
shida za wateja wao. Uovu zaidi ni pale ambapo
wahusika wakubwa wakiwa ni watu wenye nafasi
ndani jamii au mara nyengine ni miongoni mwa
viongozi wa nyumba tukufu za ibada. Kwa mujibu wa
duru za kijamii, zinasema kwamba kundi kubwa la
washirikina ni katika wale ambao Allah (Subhanahu)
amewapa neema ya elimu ya Qur‟an kwa uchache.
Hakika huu ni msiba mzito. Tunamuomba Allah
(Subhanahu) atuongoze ili kuepukana na aina hii ya
ushirikina.
Nikinukuu maneno ya Imam Al-Fawzan (Allah
amhifadhi) alisema kuwa; ((Watu wengi hawajali ni
aina ipi ya Ruqya wanayotumia. Bali kila ambae

52
yasemekana kuwa anasomea watu na kuwatibu watu,
wanaenda kwake. Bila kwanza kuhakikisha usomaji
wake, wakajua misimamo (Aqida) yake katika dini na
wakajua anachotumia katika Ruqya; je, ni ya Kisharia
au Ushirikina? Wengi hawahakikishi mambo haya.
Kinyume chake, wanachoamini wao ni umaarufu (wa
usomaji) na utajo wake kwa watu. Wanawatia
hatarini ndugu na jamaa zao na Dini yao (kwa
kwenda kwa watu kama hao). Suala hili ni hatari
sana.))
Hivyo, kwa ufafanuzi huu wa kielimu ni dhahiri kuwa
tunayo haja ya kuhakikisha tunachagua kwa
kuangalia misingi ya aqida, matendo na aina ya
visomo vya yule ambae tunamuendea katika kutafuta
dua za shida na masuala mbali mbali yanayotusibu,
na kuacha kufata mkumbo wa umaarufu wa mtu ama
sifa zake katika jamii ambayo haitambui misingi ya
dua na visomo vya kisharia.
Kwa upande mwengine, ibada za dua ambazo
zinakusudiwa kutatua shida ya mhitaji imefanywa
kuwa ni biashara na kitega uchumi cha wafanyaji,
tunaona jamii inavyo hangaika kwa umasikini na
maradhi huku zile rasilimali chache zikichangishwa ili
kulipwa msomaji dua, na mwisho wake wakaingizwa
katika ushirikina wa kupwa na kujaa. Yamkini,
kuibuka kwa biashara katika ibada za dua ni miongoni
mwa sababu kuu iliosababisha kufungua mlango wa

53
washirikina kuingia ndani yake, huku wakijinasibu na
kujitangaza kuwa wao ni watibabu wa kisharia.
Haiwezekani kwa mwenye akili, kukusudia shida au
maradhi kwa Allah (Subhanahu) kupitia dua ilihali
mbele yake kuna chungu kinachemka kwenye jiko la
mkaa, haiwezekani kwa mtu timamu mwenye lengo la
kumkusudia Allah (Subhanahu) juu ya shida zake kwa
dua huku amepewa nazi za kuvunja njia panda, ama
mayai mabovu (mayai viza). Duru za kijamii
zinatufahamisha kuwa, wapo wauzaji maalumu wa
mayai viza katika masoko yetu na ni miongoni mwa
biashara zinazofanya vizuri sana ndani ya jamii
kutokana na uhitaji kuwa mkubwa. Taarifa za ndani
kutoka kwenye sekta hiyo zinatupa takwimu kuwa
kwa wastani huuzwa kuanzia trea tano hadi kumi kwa
siku, huku bei ya yai moja viza ikionekana kua kubwa
ya ile ya yai zima. Hizi zote ni ishara za uthibitisho wa
uovu uliogubika jamii yetu.
Hakuna mafungamano yoyote kwa hakika, kati ya dua
anayokusudiwa Allah (Subhanahu) na jambo lolote
ambalo halikuthibiti katika sharia za Kiislamu. Tuwe
na tahadhari katika kuwaendea watu hawa, na kila
mmoja wetu achunge misingi iliyowekwa ya dua za
shida na maradhi. Allah (Subhanahu) hakuweka
katika tiba ama suluhisho la yote hayo kupatikana
katika haramu. Tuhimizane na kukatazana kwa nguvu
zote katika kuyaendea yote yalioharamishwa huku

54
kipaumbele kikiwa ni kujikinga na kuwakinga ndugu
zetu na ushirikina katika ibada za dua.
Ushirikina katika kuomba Maiti na Wafu
Allah (Subhanahu) amesema katika Surat Yunus;
ِ ِ ُ ‫َجيعاً ُُثَّ نػَ ُو‬
َِ ‫ويػوم َْْم ُشرىم‬
َ ‫ول للَّذ‬
‫ين أَ ْشَرُكواْ َم َكانَ ُك ْم أَنتُ ْم َو ُشَرَكآ ُؤُك ْم فَػَزيػَّْلنَا بػَْيػنَػ ُه ْم‬ ْ ُُ َ َْ َ
﴾ٕٛ﴿‫آؤىم َّما ُكنتُم إِيَّانَا تَػعب ُدو َن‬
ُْ ْ ْ ُ ُ ‫ال ُشَرَك‬
َ َ‫َوق‬
“Na siku tutakapo wakusanya wote, kisha
tutawaambia walio shirikisha: Simameni mahali penu
nyinyi na wale mlio wafanya washirika. Kisha
tutawatenga baina yao. Na hao walio washirikisha
watasema: nyinyi hamkuwa mkituabudu sisi. (10:28)
Imam Al-Fawzan (Allah amhifadhi) amesema katika
fatawa zake kuwa; ((Ni bida‟a kuomba dua kwa jaha
au kwa haki ya fulani. Na ni njia inayopelekea katika
ushirikina. Kwani jambo hili limekusanya mambo
mawili: Kwanza, ni bidaa kwa kuwa ni kufanya jambo
lisilokuwa na dalili kutoka katika Qur‟an na Sunna. Pili,
ni njia nyepesi inayompelekea mtu katika ushirikina.
Kwani hao wafanyao hayo, sababu kubwa kama
walivyoanza kwa kutawasali kwao, kisha ndio
wakajikurubisha kwao kwa kuwafanyia ibada na
utiifu. Hivyo, wakawa wametumbukia katika ushirikina
mkubwa.))
Ukilifungua dirisha la aina hii ya ushirikina, hakika
kuna mengi ambayo yanaweza kukutisha na

55
kukuogopesha juu ya ibada za uovu zinazofanyika
katika makaburi. Wahusika wakiamini na kutakidi
kuwa ni ibada miongoni mwa ibada ambazo kupitia
hao wanataraji fadhila zao, basi watawakurubisha
kwa Allah (Subhanahu). Kwa kua walikuwa ni waja
wema ama ni mawalii au masharifu wakubwa. Uovu
wa kupindukia mipaka hadi kufikia kuamini kwamba
bila kuwaomba wao (Maiti) ambao ni mabwana,
huwezi kumfikia Mtume (Swalla Allahu alaiyh wa
Sallam). Hivyo, kupitia fadhila zao, wao ndio watakao
wasogeza na kuwaonesha njia sahihi ya kumfikia
Mtume wa Allah.
Ndani ya jamii zetu, wapo wengi wanaokwenda kulia
na kugaragara makaburini kwa mababu zao
wakiomba msaada, wakiomba poza na hata ushauri
mara nyengine. Je! Tumekuwa wajinga kiasi hicho!
Imam Ibn Taymiyyah (Rehma za Allah ziwe juu yake)
alishangaa na kusema ndani ya kitabu chake cha Al-
Ubudiyya kuwa; ((Yawaje aliye hai, anamuomba
msaada kiumbe aliyekufa!))
Imefika hatua hata neema za mali ambazo Allah
(Subhanahu) ameturuzuku, ni lazima zipelekwe
kwenye makaburi ya mabwana wakubwa kupewa
Baraka zao. Huu ni msiba mzito, kwani badala ya sisi
kuwaombea dua na rehema za Allah wale waliokufa.
Tumekuwa tukitaraji na kuomba msaada kwa wafu.
Ilihali hatujui hata mafikio yao ni ya aina gani huko

56
makaburini kwao. Ibada hizi hufanywa na kuhimizwa
kuzifanya wakiamini wanao waomba wanasikia na
kuweza kutatua shida zao. Hali ya kuwa jambo hili
limegaragazwa vibaya sana ndani ya Qur‟an kupitia
Surat Fatir:

‫س َوٱلْ َو َمَر ُكلّّ ََْي ِرى‬ ِ َ ‫َّها ِر ويولِج ٱلنػ‬ ِ ِ


ْ ‫َّه َار ِف ٱلْلَّْي ِل َو َس َّخَر ٱلش‬
َ ‫َّم‬ ُ ُ َ َ ‫يُول ُج ٱلْلَّْي َل ِف ٱلنػ‬
‫ين تَ ْد ُعو َن ِمن ُدونِِو َما ِيَْلِ ُكو َن ِمن‬ ِ َّ ‫ألَج ٍل ُّمس ِّمى ٰذلِ ُكم ٱللَّو ربُّ ُكم لَو ٱلْم ْل‬
َ ‫ك َوٱلذ‬ ُ ُ ُ ْ َُ ُ َ َ
﴾ٖٔ﴿‫قِطْ ِم ٍي‬

“Anauingiza usiku katika mchana, na anauingiza


mchana katika usiku. Na amelifanya jua na mwezi
kukutumikieni. Kila kimoja wapo kinakwenda kwa
muda maalumu. Huyo ndiye Allah, Mola Mlezi. Ufalme
ni wake. Na hao mnao waomba badala yake
hawamiliki hata ugozi wa kokwa ya tende.” (35:13)
Kama hivyo ndivyo, wanaweza kusema kuwa
wakiwaomba wanasikia au wanawajibu maombi yao.
Hili pia Allah (Subhanahu) amelijibu na kulifafanua
vizuri kupitia Aya zinazofuata baada ya hiyo ya awali
aliposema:

‫ٱستَ َجابُواْ لَ ُك ْم َويػَ ْوَم ٱلْ ِويَ َام ِة يَ ْك ُفُرو َن‬ ِ


ُ ‫إِن تَ ْد ُع‬
ْ ‫وى ْم الَ يَ ْس َمعُواْ ُد َعآءَ ُك ْم َولَ ْو ََسعُواْ َما‬
﴾ٔٗ﴿‫ك ِمثْل خبِ ٍي‬ ِ ِ
َ ُ َ ُ‫بِش ْركػ ُك ْم َوالَ يػُنَبّْئ‬
“Mkiwaomba hawasikii maombi yenu: na hata
wakisikia hawakujibuni. Na siku ya Kiyama watakataa

57
ushirikina wenu. Na hapana atakae kua na habari
vilivyo kama Yeye mwenye habari.” (35:14)
Haya ni katika matendo maovu ya ushirikina, na
hayana tofauti na ya wale walio unda miungu katika
zama za Nabii Ibrahimu (Alaihi Salatu wa Sallam)
kama ilivyokuja ndani ya Qur‟an kupitia Surat Ash-
Shuarah (Soma kuanzia Aya 70-82). Ipo haja ya
kuachana kabisa na ibada hizi za kishirikina hakika
hazina zaidi ya ghazabu za Allah (Subhanahu) na
haya ni matendo ya wale wenye kuchupa mipaka.
Tambua kuwa hao maiti hawadhuru wala kunufaisha,
hawasikii wala kujibu chochote zaidi ya kuwaongezea
uzito wa maisha yao katika makaburi.
Jamii ielimike na kutambua kuwa ushirikina hauna
nafasi ndani ya jamii zetu kwani unavunja msingi
mkuu wa taqwa na kumpwekesha Allah (Subhanahu)
na mwisho wake ni kutoka katika Uislamu. Na wale
viongozi na waratibu wa ziara hizi waache upotoshaji
kwa wafuasi wao na jamii kwa ujumla kwa kutumia
hekaya za uongo. Kama vile mtu aliyesomeshwa
Qur‟an nzima na maiti (Walii). Ama yule ambae
alikwenda Umra bila ya kutegemea baada tu ya
kwenda kuzuru (Kutembelea) kaburi la Walii. Kwa
sababu, haya huchochea kuporomosha Imani za jamii
na kujikuta wimbi kubwa limejielekeza ndani ya
ushirikina wa kuabudu na kuomba maiti.

58
Mara nyingi, ukisoma ndani ya Qur‟an tukufu, kupitia
zile Aya ambazo Allah (Subhanahu) amezungumzia
Ushirikina, basi utaona mwisho Allah hufunga Aya
hizo na suali kuwa‟Je! Hamna akili‟hili linatokana na
upeo mdogo wa akili za washirikina. Kwani ndani ya
mambo mengi yanayo nasibishwa na ushirikina,
huhitaji maarifa madogo kuweza kuyabaini. Hivyo
basi, kila mmoja wetu atafakari kisha aseme na nafsi
yake juu ya kuachana na ibada za kumshirikisha Allah
(Subhanahu) na huenda kwa idhini ya Allah
akatuongoa kutokana katika dimbwi la ushirikina.
Ushirikina katika Ndoa
Ndoa kwa hakika ni ibada na Sunna ya Mtume (Swalla
Allahu alaiyh wa Sallam) na pia ni miongoni mwa
ukamilishaji wa Neema za Allah (Subhanahu) kwa
viumbe wake. Allah (Subhanahu) ameifanya ndoa
kuwa ni miongoni mwa dalili za Uungu wake. Kama
ilivyokuja ndani ya Qur‟an kupitia Surat Ar-Rum:

ً‫َوِم ْن آيَاتِِو أَ ْن َخلَ َق لَ ُكم ّْم ْن أَن ُف ِس ُك ْم أ َْزَواجاً لّْتَ ْس ُكنُػۤواْ إِلَْيػ َها َو َج َع َل بػَْيػنَ ُكم َّم َوَّدة‬
﴾ٕٔ﴿‫ات لّْ َووٍم يػتَػ َف َّكرو َن‬ ٍ ‫ور ْْحةً إِ َّن ِِف ٰذلِكَ آلي‬
ُ َ ْ َ َ َ ََ
“Na katika ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake
zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao.
Nae akajaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika
katika haya bila shaka zipo Ishara kwa watu wanao
fikiri.” (30:21)

59
Malengo makubwa ya ndoa ni kama yalivyoelezwa
ndani ya nukuu ya Aya hapo juu, kuwa ni chanzo cha
maingiliano ya mapenzi, na huruma huku Allah
(Subhanahu) akajalia pumziko na ndani yake
kupatikana kizazi cha watoto. Kama ambavyo Mtume
(Swalla Allahu alayihi wa Sallam) alivyo sisitiza katika
Sunna zake kuwa:
((Oeni wanawake wenye mapenzi, wenye uzazi,
kwani nitashindana na Mitume wengine kwa idadi ya
wafuasi siku ya Kiyama)) Sahihi Bukhary
Mbali na hayo yote niliyoyatanguliza na kufafanua juu
ya neema ya Allah (Subhanahu) kwa viumbe wake,
viumbe hao wamebadili malengo ya ndoa kutoka
kwenye kuifanya kuwa kisima cha utulivu, mapenzi na
huruma, na kuifanya kuwa ni kitovu cha ushirikina.
Ushirikina ndani ya ndoa, huanza kuchepua mizizi
yake katika hatua za awali za ndoa. Kinyume na
kutumia msingi sahihi alioiacha Mtume (Swalla Allahu
alaiyhi wa Sallam) katika kuchagua mchumba kama
ilivyokuja katika Hadithi kuwa;
Imepokewa kutoka kwa Abuu Khurayra kwamba
Mtume (Swalla allahu alaiyh wa Sallam) amesema:
((Pindi atakapo chumbia kwenu mtu ambae
mumeridhia dini yake na tabia yake, basi muozesheni.
Msipofanya hivyo basi itakuwa fitna kubwa na ufisadi
mkubwa katika ardhi.))

60
Viumbe wakaacha utaratibu huu, sasa uchumba
huchagulia kwa waganga wenye kuangalia nyota.
Mizimu na mashetani yatakapo ridhia juu ya uchumba
wao, basi ndoa hupita. Ndio maana tunaona
misukosuko mingi ndani ya ndoa, na hakikia hii ndio
ile fitna na ufisadi aliousema Mtume wa Allah. Kwani
kwa hakika itaachaje ndoa hiyo kukosa matatizo na
misukosuko ilihali ilishakabidhiwa kwenye mikono ya
ushirikina hali ikiwa ni changa. Hakika hilo ni jepesi
sana, ushirikina unaofanywa katika ndoa yenyewe
(baada ya uchumba na posa kupita) ni wa kiwango
kikubwa kiasi cha baadhi kuichukia ndoa ndani ya
usiku wa kwanza. Ndoa nyingi hugubikwa na shirki
nzito ndani yake huku wengine wakizifanya kwa siri
mbali ya kwamba Mtume (Swalla Allahu alaiyh wa
Sallam) ameusia kuificha posa na kuidhihirisha ndoa,
ila hufanyika haya yakiwa ni masharti ya wazee
(Wataalamu) wa kishirikina.
Aidha, Allah (Subhanahu) ameifanya ndoa kuwa
chanzo cha kupata kizazi, kwa wale ambao
amewaruzuku, na kuwanyima wengine ambao
amewapimia kwa hikima zake, kama alivyosema
ndani ya Qur‟an tukufu kuwa:

‫ب لِ َمن‬ ِ ِ ‫ض َُيْلُق ما يشآء يػه‬ ِ َّ ‫لِلَّ ِو م ْلك‬


ُ َ َ ُ َ َ َ ُ ِ ‫ٱلس َم َاوات َوٱأل َْر‬
ُ ‫ب ل َمن يَ َشآءُ إنَاثاً َويػَ َه‬ ُ ُ
‫ٗ﴾ أ َْو يػَُزّْو ُج ُه ْم ذُ ْكَراناً َوإِنَاثاً َوََْي َع ُل َمن يَ َشآءُ َع ِويماً إِنَّوُ َعلِيم‬ٜ﴿‫ٱلذ ُك َور‬
ُّ ‫يَ َشآء‬
ُ
﴾٘ٓ﴿‫قَ ِدير‬

61
“Ufalme wa mbingu na ardhi ni wa Allah; anaumba
apendavyo, anamtunukia amtakae watoto wa kike, na
anamtunukia amtakae watoto wa kiume, Au
huchanganya wanaume na wanawake, na akamfanya
amtakae tasa. Hakika Yeye ni Mjuzi Mwenye uweza.”
(42:49-50)
Uovu ulioenea ndani ya jamii zetu, wameshindwa
kukubali kudura za Allah (Subhanahu) juu ya mmoja
kati yetu kunyimwa ama kucheleweshewa neema hii
ya watoto. Badala ya kubaki katika ibada za Allah
(Subhanahu) kwa kusali na maombi, walio wengi
huchupa mipaka Yake na kuelekeza shida zao kwenye
ushirikina. Wahanga wakubwa wakiwa ni wake, dada
na mama zetu ambao kwa yakini aidha, kwa
kushawishiwa ama kuamua tu kufanya na
kufanyishwa ushirikina. Sambamba na mambo mengi
machafu, maovu, na yakudhalilisha ambayo
hufanyiwa mhitaji (waandishi wameshindwa
kuyabainisha) kwa dhana ama Imani ya kupata
watoto.
Pindi mtu akiruzukiwa watoto, huwapeleka pia kwa
waganga na kufungwa hirizi, eti ziwape ulinzi wa
mambo mbali mbali. Ajabu ilioje, huoni kuwa mtoto
huyo alikuwa na ulinzi wa Allah (Subhanahu) kwa
miezi tisa (au zaidi) tumboni kwa mama yake, bila
dhara lolote kumpata isipokuwa lile aliloliandika.
Iweje amezaliwa akiwa salama na afya njema, kisha

62
mtu anaenda kumtafutia ulinzi wa hirizi pasi na Allah
(Subhanahu). Itoshe kwetu mifano ya waja wema na
Mitume wa Allah (Subhanahu) tuliyofafanuliwa ndani
ya Qur‟an. Tunaona namna na njia walizotumia
kwenye nyakati za shida zinazofanana na hizi,
hawakuenda kwa wazee wala wataalamu,
hawakuzuru makaburi wala kuvunja nazi, bali kubwa
na la busara walimuomba Allah (Subhanahu) kwa
Imani na Taqwa huku wakiwa na yakini ya kujibiwa
na kutatuliwa shida zao.
Angalia namna Allah (Subhanahu) alivyopiga mfano
wa Nabii Zakariya (Alaihi Salatu wa Sallam) ndani ya
Surat Maryam, akimbainishia Mtume wake (Swalla
Allahu alaiyhi wa Sallam):

‫ب‬ َ ِ‫ْس َشْيباً َوََلْ أَ ُك ْن بِ ُد َعآئ‬


ّْ ‫ك َر‬ َّ ‫ب إِ َِّّن َوَى َن ٱلْ َعظْ ُم ِم َّْن َوٱ ْشتَػ َع َل‬
ُ ‫ٱلرأ‬ ّْ ‫ال َر‬َ َ‫ق‬
﴾ٗ﴿ً‫َش ِويا‬
ّ
“Akasema: Mola wangu Mlezi! Mafupa yangu
yamedhoofika, na kichwa kinameremeta kwa mvi;
wala, Mola wangu Mlezi, sikuwa mwenye bahati
mbaya kwa kukuomba Wewe.” (19:04)
Aidha katika Surat Al-Anbiya, Allah amesema kuwa:

﴾ٜٛ﴿‫ني‬ِ ّْ ‫َوَزَك ِريَّآ إِ ْذ نَ َاد ٰى َربَّوُ َر‬


َ ‫َنت َخْيػُر ٱلْ َوا ِرث‬
َ ‫ب الَ تَ َذ ْرِِّن فَػ ْرداً َوأ‬

63
“Na Zakariya alipo mwita Mola wake Mlezi: Mola
wangu Mlezi! Usiniache peke yangu, na Wewe ndiye
Mbora wa wanao rithi.” (21:89)
Nabii wa Allah Zakariya, alijieleza kwa siri katika ibada
zake za usiku kwa Allah (Subhanahu) na akaendelea
kuwa:

﴾٘﴿ً‫ك ولِيا‬ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ‫وإِ ِّّْن ِخ ْفت ٱلْمو‬


ّ َ َ ْ‫ب َِل من لَّ ُدن‬
ْ ‫اَل من َوَرآئى َوَكانَت ْٱمَرأَتى َعاقراً فَػ َه‬
َ ََ ُ َ
“Na hakika mimi nawahofia jamaa zangu baada
yangu. Na mke wangu ni tasa. Basi nipe mrithi kutoka
kwako.” (19:05)
Ukisoma mtiririko wa maombi yake unaweza kuona
Taqwa ya Allah ndani ya maombi yake na hakuna
chochote miongoni mwa itikadi chafu za kishirikina.
Hata ukifatilia Aya inayofuata baada ya maelezo hayo
kuwa lengo la kuhitaji hilo hitaji lake (mtoto) ni jema
zaidi. Sasa angalia majibu ya Allah kwake. Na hii ni
kwa sababu ya kujiepusha kwake na ushirikina na
kutambua kuwa mtoaji wa riziki na neema hiyo ni
Yeye. Hakuna mshirikina wala mganga mwenye
uwezo wa kutoa mtoto wa kufungua kile
kilichofungwa miongoni mwa vizazi vya wale ambao
Allah (Subhanahu) amevifunga ama kuvichelewesha
kwao. Hakika ni Allah (Subhanahu) pekee, Mola Mlezi,
Mwenye kujibu na kutatua miongoni mwa shida hizo.
Hebu ona majibu ya Allah (Subhanahu) kwa Mja wake
Zakariya pale alipomkusudia kwa shida zake:

64
﴾ٚ﴿ً‫ٱَسُو ََْي َٰي ََل َّْمعل لَّو ِمن قَػبل ََِسيا‬ ٍ ِ
ّ ُ ْ ُ َ ْ َ ُ ْ ‫ٰيػَزَك ِريَّآ إِنَّا نػُبَشُّْرَك بغُالَم‬
“(Akaambiwa): Ewe Zakariya! Hakika Sisi
tunakubashiria mwana; jina lake ni Yahya. Hatujawahi
kumpa jina hilo yoyote kabla yake.” (19:07)
Hatupaswi kutafuta katika Rehema za Allah, kama vile
watoto katika njia za Haramu na zakumshirikisha
Yeye. Bali tunafundishwa kutumia njia sahihi kama
vile Dua kama zilivyokuja katika dalili pamoja na tiba
zilizothibiti kwetu kutoka kwa Mtume (Swalla Allahu
alaiyh wa Sallam).
Kwa upande mwengine, Allah (Subhanahu) ameifanya
ndoa kuwa ni kimbilio la mapenzi, huruma, na utulivu
kama ambavyo tunatambua kuwa ndoa sahihi,
iliyofuata utaratibu na misingi sahihi basi haiwezi
kusababisha huzuni, matatizo na misukosuko kwa
idhini ya Allah (Subhanahu). Mapenzi na huruma
ndani ya ndoa, ndio asili ambayo Allah (Subhanahu)
ameijaalia kwa viumbe wake. Lakini kwa masikitiko
makubwa uovu wa ushirikina ukaendelea kuingizwa
ndani yake kwa kumshirikisha Allah (Subhanahu)
katika kutafuta dawa za kichawi za kuongeza mapenzi
(Limbwata), wanadamu wakahadaika kwa kutafuta
dawa za kumtuliza Mume (Mke), wakakesha kwa
washirikina kutafuta dawa za kumfunga Mume (Mke)
asitoke ndani ya ndoa yake, haya yote yakasababisha
madhara makubwa kwa wakusudiwa. Yamkini, huu

65
wote ni ujinga mkubwa. Kwani, hakika hakuna
mapenzi yanayozalishwa na ushirikina, wala hakuna
utulivu unao patikana nje ya mipaka ya Allah
(Subhanahu) isipokuwa adhabu zake na matatizo
yasiyoisha.
Matendo haya yote ni maovu, na hakika yanaakisiwa
vyema na namna ambavyo vizazi (watoto) wetu
wanavyokuwa na akili za ushetani. Wanavyokuwa na
uthubutu mchafu wa kufanya mambo makubwa
maovu ambayo hata Ibilisi (Laana za Allah ziwe juu
yake) anavishangaa (ikiwamo kupatikana kwa
makundi dhalimu ya wanayojiita watoto wa Ibilisi).
Hizi zote ni dalili kwamba kuna sehemu tulimkosea
Allah (Subhanahu) katika kubadilisha dhamira yake ya
huruma na mapenzi katika ndoa na kuifanya kuwa ni
nakama na kituo cha ushirikina. Ipo haja katika ndoa
zetu kujipamba kwa mapenzi ya dhati, huruma yenye
mfano, sambamba na kujilazimisha katika uaminifu na
ihisani.
Kadhalika, ushirikina umeenea pia ndani ya ndoa
kutokana na chuki na uhasidi baina ya wake (wenza)
wengi wamekuwa wakipeana madhara kwa njia ya
ushirikina kwa uchoyo na hasadi zilizowajaa, wivu na
ubinafsi umetamalaki ndani ya ndoa nyingi ambao
kwa kiasi kikubwa huzalisha fikira chafu
zinazowapeleka kwenye ushirikina. Ushirikina ambao
aidha kumdhuru kiumbe mwenzake (mke mwenza) au

66
kumdhuru mume kimawazo na kumfanya zezete. Na
wengine wakienda mbali zaidi hadi kufikia hatua ya
kuwadhuru watoto wasio na hatia. Hakika huu ni
udhalimu na ukosefu wa akili timamu.
Unawezaje kuchukia na kumshirikisha Allah
(Subhanahu) kwa jambo ambalo limeruhusiwa, ndoa
ni misingi ya kisharia na uke wenza ni ruhusa
iliyotolewa kwa mwenye uwezo. Unaingia katika
ushirikina kwa sababu ya jambo lililoruhusiwa na Allah
(Subhanahu). Tuandae majibu ya kumjibu Allah
(Subhanahu) siku ambayo watasimamishwa mbele
yake na hao waliokuwa wakiwafanya washirika wa
Allah.
Ushirikina katika Kazi na Biashara
Katika ustawi wa wanadamu hapa duniani, ni lazima
kujishuhulisha katika kutafuta sababu za riziki za
Halali. Kiumbe (Mwanadamu) kufanya kazi ama
biashara ni miongoni mwa mambo yanayopendeza.
Kwani ndani yake ndimo hupatikana kipato kwa ajili
yake na wale wategemezi. Sharti la msingi ni
kuhakikisha kuwa kazi ama biashara hizo hazitoki nje
ya misingi ya Kiislamu. Misingi mingi ya kisharia
imewekwa na kushurutishwa kwa wafanyaji ili
kuhakikisha inachunga mipaka ya sharia za Uislamu
sambamba na Taqwa ya Allah (Subhanahu). Misingi
mikuu ikiwa ni kuepukana na ushirikina, dhulma,
hadaa, viapo vya uongo nakadhalika.

67
Kadiri karne na zama zinavyokwenda, ndivyo
ambavyo kila jambo limefunganishwa na ushirikina
ndani yake. Kama ambavyo tumeona namna
ushirikina ulivyo enea katika nyanja tulizozifafanua
hapo awali. Hivyo hivyo, ushirikina umekuwa ni
msingi mkubwa katika nyanja ya kazi na biashara.
Maeneo haya pia hayakuachwa salama na uchafu wa
ushirikina kama yalivyo maeneo mengine. Tamaa za
nafasi za juu na utajiri wa haraka umeshika hatamu
na ndio kwa kiwango kikubwa umesababisha kuingiza
dhana na imani za kishirikina ndani yake. Haya yote
yakaifanya jamii kuhitaji nguvu ya ziada katika kazi na
biashara zao.
Tunayo mifano na ushahidi wa wazi wa namna
ambavyo wafanyakazi wanavyotumia ushirikina ili
wapate nafasi fulani ama cheo fulani katika maeneo
yao. Mbali na kupupia huko, matokeo yake ni kukosa
Baraka na neema za Allah (Subhanahu) katika hayo
wanayoyakimbilia. Tunaona matukio ya wazi namna
wafanyakazi wanavyozuriana wao kwa wao ili mmoja
wao aondoke katika nafasi aliyopewa ili mwengine
aweze kuishika nafasi hiyo, huku wakiwasababishia
wengine madhara makubwa kwa ugonjwa na hata
kifo mara nyengine. Tunasahau kuwa Allah
(Subhanahu) amesema ndani ya Qur‟an;

68
‫ٱلدنْػيَا ِِف‬
ُّ ُ‫ٱْلَيَاة‬
ْ ‫ٱلدنْػيَا َوَما‬ ْ ِ‫ٱلرْز َق لِ َم ْن يَ َشآءُ َويػَ َو ِد ُر َوفَ ِر ُحواْ ب‬
ُّ ِ‫ٱْلَيَاة‬ ّْ ‫ط‬ُ ‫ٱللَّوُ يػَْب ُس‬
ِ
﴾ٕٙ﴿‫ٱآلخرةِ إِالَّ متَاع‬
َ َ
“Allah humkunjulia riziki amtakaye, na humkunjia kwa
kipimo. Na wamefurahia maisha ya dunia. Na uhai wa
dunia kwa kulingana na Akhera si kitu ila ni starehe
ndogo.” (13:26)
Tambua kila ambacho umekipata ama kukuepuka
katika huu ulimwengu ndio hisabu ya Allah
(Subhanahu) na kinachokutosha kwa kadiri ya
mahitaji yako. Hakuna haja wala hitaji la
kumshirikisha Allah (Subhanahu) kwa waganga na
makuhani kwa lengo la kupata ziada. Pia tambua hata
hao washirikina unaowaendea wanashida zao nyingi
ambazo kwa kadiri wanavyojinasibu na misaada yao
wangeanza kujisaidia wao wenyewe kwanza.
Kwa upande mwengine, biashara nazo zimekuwa
zikifanywa kwa msaada mkubwa wa ushirikina. Hadi
kufika hatua ya kugubikwa na dhulma kubwa kiasi
cha mtu kuwa tayari kutoa kafara ya uhai wa mtoto
wake wa kumzaa. Jamii ya wafanyabiashara imekua
ni jamii chafu kwa ushirikina zaidi ya kundi au jamii
yoyote nyengine. Tamaa za mali na utajiri wa haraka
ukaenda kuvua utu katika nafsi zao. Wakafikia hadi ya
kuwa tayari kulala (kimapenzi) na mama mzazi kwa
lengo la kupata utajiri na mafanikio ndani ya biashara
zao.

69
Wengi, miongoni mwa wafanyabashara wamewafanya
watoto wao misukule (mataahira) kwa lengo la
kuvutia wateja kwa njia za kishirikina. Jambo la
kushangaza, bado wameedela kuwa duni kama
ambayo walikuwa kabla ya hapo. Ushirikina ndani ya
biashara umeenea, kiasi cha kwamba imeonekana ni
jambo la kawaida. Wengi miongoni mwa
wafanyabiashara ni matajiri wakubwa, ilihali katika
jamii anaendelea kuonekana duni na dhaalili, yote
ikiwa ni kufuata masharti ya uovu wa washirikina kwa
kukatazwa kuvaa na kuishi vizuri.
Ndugu yangu msomaji, kama hayo utaona
yamefichikana, tunaona vikaratasi vikining‟inizwa
madukani, vilivyoandikwa kwa wino wa rangi
nyekundu. Haujiulizi kuna mahusiano gani kati ya
vikaratasi hivyo na biashara inayofanyika. Hakuna jibu
lengine zaidi ya ushirikina, na hizi zote ni hirizi za
kichawi zilizofunganishwa na ushetani mkubwa, ili
kuwa ni msaada wa kuwavuta wateja na kunawirisha
biashara kama wanavyo amini. Tunafahamu pia, ile
midoli, vipicha, ama viatu vya mguu mmoja
vinavyoning‟inizwa ndani ya magari ya biashara, vyote
vimekuwa ni hadaa kwa wasio jua, ilihali vikiwa ni
hirizi na tarasimu za kishirikina kwa ajili ya
kunawirisha biashara hiyo.
Hakuna kazi wala biashara katika nyakati zetu
ambayo imesalimika na ushirikina. Duru za kijamii

70
zinatueleza kuwa; ushirikina umetamalaki katika sekta
ya uvuvi ambapo kwa vinywa vipana wanathibitisha
kuwa; ili chombo cha uvuvi kiende baharini ni lazima
kifanyiwe zunguo la kishirikina ili kukilinda na
kuwalinda wahusika na shari za ajali pamoja na shari
za samaki wakubwa wenye madhara. Kadhia hizi sio
hadithi za kusadikika, bali ni duru za uhakika ambazo
waandishi wamezikusanya kutoka kwa wakusika wa
sekta hiyo.
Tunatambua kuwa wapo wafanyabiashara wa sekta
ya hii ambao walipotea baharini kwa kipindi fulani,
tahamaki wamerudi na kuwa waganga wakubwa
wenye nyenzo na zana murua za kuagua na kutibu
ushirikina kwa kutumia ushirikina waliopewa na majini
wa bahari. Tunatambua pia kuwa wapo
wafanyabiashara wa madini ambao hawawezi
kuchimba mgodi bila ya kupitisha ushirikina, huku
wengine wakiwatoa kafara vibarua wao ili kumwaga
damu kwa kutimiza masharti ya makuhani na
waganga wao.

Magwiji wa biashara za nyama na wachinjaji


wanatueleza kuwa; jamii inapaswa kuwa makini na
kundi la wafanyabiashara hawa kwani ni rahisi kwao
kutoa kafara za viumbe hai (kama mwanadamu) ili tu
biashara zao ziwe na mafananikio. Jamii hiyo
inatufahamisha kuwa ni jambo la kawaida kwao kutoa

71
kafara za kishirikina hadi kwa mke au mtoto ili kulinda
maslahi ya biashara zao. Wakausia pia kuwa; walio
wengi miongoni mwao sio watu wazuri hata kufanya
miamala ya kijamii nao. Sasa ndugu yangu msomaji
hii ndio hali halisi, ni nani ambae kasalimika na
ushirikina ndani ya jamii zetu? Hatuna budi isipokua
kuzilainisha nyoyo zetu kwa misingi ya sharia,
kuzirovya nyoyo zetu rovyorovyo kwa maji na
chemchem za taqwa ili kuachana na uchafu huu
ambao utatuangamiza.
Mambo yote haya yamekatazwa ndani ya Qur‟an na
Sunna za Mtume (Swalla Allahu alaiyhi wa Sallam)
kama ilivyothibiti katika Hadithi ya Imam Ahmad
(Radhi za Allah ziwe juu yake):
Amepokea Imam Ahmad (Radhi za Allah ziwe juu
yake) katika Musnadi wake, kutoka kwa Uqba ibnu
Aamir (Radhi za Allah ziwe juu yake) kutoka kwa
Mtume, amesema: ((“Yeyote atakaetundika hirizi basi
Allah asimtimizie mambo yake na ataetundika hirizi
basi amefanya ushirikina”))
Matokeo mabaya ya ushirikina ambayo yanaakisi
laana za Mtume wa Allah tunayaona wazi wazi. Hali
za biashara kuwa ngumu, maisha kuwa na dhiki,
vipato visivyotosheleza ni mrejesho mbaya wa
ushirikina tulioufunganisha ndani ya kazi na biashara
zetu. Malalamiko na masikitiko mbali mbali ya
wafanyabishara tunayashuhudia. Haya yote ni kwa

72
sababu Allah (Subhanahu) hatutimizii mambo yetu
katika vichumo na vipato vyetu kutokana na uovu wa
ushirikina. Miongoni mwa njia za kujinasua ni pamoja
na kuvunja miiko na mizizi yote ya ushirikina ambayo
tumeiweka ndani ya kazi na biashara zetu, pamoja na
kuomba msamaha wa dhati kwa Allah (Subhanahu)
kwa hatua ambayo tulitanguliza ushirikina mbele ya
Kadari na Taqwa Yake.
Ushirikina katika Michezo
Kabla ya kuzungumzia ushirikina katika michezo,
napenda kuzungumzia mtazamo wa Uislamu juu ya
michezo na mazoezi kwa ujumla. Uislamu ni dini
ambayo imekusanya kila kitu. Miongoni mwa dalili juu
ya ukusanyaji wa uislamu katika kila jambo ni kumtilia
umuhimu binadamu katika upande wa kiroho na
kimwili. Ukaiwekea roho haja zake na mambo yake
ambayo inahitaji na inafurahi kutokana na mambo
hayo. Wakati huo huo, Uislamu haukupuuza upande
wa mwili na yale ambayo yanaupa nguvu mwili na
kuuacha ukiwa na muonekano mzuri na salama.
Uislamu ukahamasisha kutilia umuhimu kwa kufanya
kila ambalo litaufanya mwili kuwa na nguvu na afya
njema.
Kwani; Amepokea Imam Muslim hadithi kutoka kwa
Mtume (Swalla Allahu alayhi wa Sallam) akisema:
(("Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendeza
zaidi kwa Allah kuliko muumini dhaifu, na wote wawili
ni bora (kuna kheri ndani yake)"))

73
Pia amesema Mtume (Swalla Allahu alayhi wa
Sallam): (("Na mwili wako pia una haki zake juu
yako"))
Maneno haya aliyasema kumwambia swahaba
ambaye alisema hatolala usiku wala hatokula mchana
wala hatomkaribia mkewe. Mtume (Swalla Allahu
alayhi wa Sallam) akamuelekeza jambo bora zaidi
kwake na kumpa msingi mkubwa kwamba kama roho
yako ilivyokuwa na haki ya kufurahia ibada ya
kisimamo cha usiku na funga za mchana basi mwii
wako pia una haki zake ikiwemo kupumzika usiku,
kula chakula na kukidhi matamanio yake ya kijinsia.
Na huu ndio msingi ambao Uislamu umeuweka katika
kuonesha umuhimu wa mazoezi kama nyenzo ya
kuutia nguvu mwili.
Aina za watu katika Mazoezi na Michezo
Aina ya Kwanza: Wale ambao wanaona kwamba
mazoezi yanatakiwa kufanywa na tabaka maalumu la
watu, au michezo fulani ni ya watu fulani au dini
fulani, wakajiweka mbali na michezo moja kwa moja
na hawakujihusisha nayo.
Aina ya Pili: Wale ambao wanaona mazoezi ni jambo
la hiari na wanafanya kulingana na haja. Wakiwa
hawashughulishwi na mazoezi au michezo mpaka
wakaacha kutekeleza mambo ya wajibu juu yao katika
ibada na kusimamia majukumu yao upande wa
familia.

74
Aina ya Tatu: Wale ambao wamefanya mazoezi na
michezo kuwa ni sehemu ya maisha yao. Wakijaalia
michezo na mazoezi kuwa sehemu kubwa katika
wakati wao mpaka wakaacha kutekeleza wajibu wao
kwa Allah (Subhanahu) na familia zao. Aidha, hawa ni
wale ambao wanafanya mazoezi mpaka vipindi vya
swala pamoja na wajibu mwengine yakawa na
sehemu duni katika maisha yao.
Hukumu ya michezo katika Uislamu
Kutokana na aina za watu katika mazoezi tunaweza
kupata hukumu ya mazoezi kutokana na athari
zitakazopatikana. Hukumu ambazo zitategemea
malengo na makusudio ambayo mtu ameyaweka
katika mazoezi ama michezo hiyo. Aidha, napenda
ifahamike kwamba asili ya michezo au mazoezi
kisharia ni (MUBAAH) yani; mtu akifanya hapati
dhambi wala thawabu, ila hutegemea nia na
makusudio ya kuingia katika michezo husika.
Uwajibu wa Michezo katika Uislamu:
Mazoezi yanakuwa wajibu endapo yanamjenga mtu
na kumuandaa kwa ajili ya kupigania dini ya Allah.
kama Allah alivyosema katika surat An-Faal: 60

﴾ٙٓ﴿‫ٱْلَي ِل تػُرِىبو َن بِِو َع ْد َّو ٱللَّ ِو‬ ِ ِ ٍ ِ


ْ ‫َوأَع ُّدواْ َِلُ ْم َّما‬
ُ ْ ْ ْ ‫ٱستَطَ ْعتُ ْم ّْمن قُػ َّوة َومن ّْربَاط‬
“Na jiandaeni kwa ajili ya maadui kwa kadri
muwezavyo katika nguvu na kupanda farasi
muwaogopeshe maadui wa Allah na maadui zenu.”
(08:60)

75
Katika Aya hii imetajwa nguvu kwa ajili ya kupambana
na maaduni na inaingia katika kujiandaa kwa kila aina
ya mazoezi na michezo ambayo itamfanya mtu kufikia
malengo hayo yaliyowekwa. Katika nukta hii,
hujumuishwa michezo na mazoezi ya aina zote, kama
kukimbia kwa ajili ya pumzi, kulenga shabaha kwa
kila aina ya silaha, kupigana karate na kutumia silaha
kwa aina zote hata hizi za kisasa, kama inavyoingia
elimu ya zana za kisasa.
Pia imenukuliwa kutoka kwa Mtume (Swalla Allahu
alayhi wa Sallam) akilenga shabaha kwa mishale na
mikuki. Kadhalika, alicheza mchezo wa kukimbia na
farasi na ngamia kama ambavyo alishiriki katika
mchezo wa mieleka na alishuhudia maonesho ya
wahabeshi walipokuwa wanachezea mikuki. Yote haya
yanathibitisha uwepo wa michezo na mazoezi katika
zama za Mtume na ni jambo linalokubalika katika
sharia endapo litafanyika katika misingi sahihi.
Uharamu wa Michezo ndani ya Uislamu:
Uharamu wa michezo umekuja baada ya
kujumuishwa ndani yake mambo mengi ambayo kwa
namna moja ama nyengine yanaitoa katika usahihi
wake. Mambo ya msingi ambayo yanaweza kupelekea
michezo kuingia katika uharamu ni pamoja na
kujumuishwa ushirikina, michezo kufanywa kua ni
kipaumbele zaidi kuliko ibada za Allah (Subhanahu)
kama vile swala, kujumuishwa ndani yake kutangaza
ama kuhamasisha mambo mengine maovu kama vile

76
kamari, na mengineyo yasiyokua hayo katika
yaliyoharamishwa.
Mchezo wowote ule utakapo jumuishwa na maswala
ya ushirikina unakuwa haramu kushiriki mchezo huo
kwa namna yoyote ile. Sawa sawa, kwa kucheza au
kuongoza kama mwalimu au kusaidia wachezaji labda
kama mtu hafahamu kwamba kuna ushirikina
umehusika katika mchezo hiyo.
Michezo mingi hivi sasa imekuwa ikihusishwa na imani
za kishirikina kwa kutoa kafara za aina mbalimbali
kwa lengo la ushindi. Bila ya kutambua kuwa kafara
kisharia hutolewa kwa ajili ya Allah (Subhanahu) iwe
ni kuchinja au kufunga
Allah anasema;

َ ‫ٔ﴾ الَ َش ِر‬ٕٙ﴿‫ني‬


ُ‫يك لَو‬
ِ ّْ ‫اى َوِمََاتِى لِلَّ ِو َر‬
َ ‫ب ٱلْ َعالَم‬
ِ
َ َ‫صالَتى َونُ ُسكى َوََْمي‬
ِ ‫قُل إِ َّن‬
َ ْ
﴾ٖٔٙ﴿‫ني‬ ِِ ِ َ ِ‫وبِ ٰذل‬
َ ‫ت َوأَنَاْ أ ََّو ُل ٱلْ ُم ْسلم‬
ُ ‫ك أُم ْر‬ َ
“Sema hakika ya kuswali kwangu na kuchinja kwangu
ni kwa ajili ya Allah mola mlezi wa viumbe wote, hana
mshirika katika hilo, kwa hilo nimeamrishwa na mimi
ni wa mwanzo kujisalimisha kwake.” (06:162-163)
Pia Allah amesema;

﴾ٕ﴿‫ك و ْٱْمَر‬ ِ َ‫ف‬


ْ َ َ ّْ‫ص ّْل لَرب‬
َ
“Swali kwa ajili ya mola wako mlezi na uchinje kwa
ajili yake” (108:02)
77
Yoyote atakaefanya vitu miongoni mwa hivi kwa
asiekuwa Allah (Subhanahu) basi anakuwa amefanya
ushirikina kwa kutekeleza jambo hilo kwa asiekuwa
Allah. Mbali na hilo kuna jambo jingine kubwa
linalofungamana na ushirikina, ambalo ni ubadhirifu
katika mali, pia hupelekea katika uharibifu wa
mazingira ambayo mshirikina huufanya kwa kuchoma
baadhi ya vitu au kuvunja vingine. Yote hayo ni katika
mambo yaliyoharamishwa na sharia na kushiriki
katika mchezo au mazoezi ambayo yamekusanya
mambo haya ni sawa na kushiriki katika ushirikina.
Duru za kijamii katika michezo, zinatuarifu uwepo
kikundi maalumu cha watu ndani ya timu ama vilabu
mbali mbali vya michezo, vikundi ama mjumuiko huo
uliopewa jina la Kamati ya Ufundi. Kamati ambayo
hujumuisha manguli wakuu katika ushirikina, ambao
uwepo wao ndani ya vilabu hivyo ni kuhakikisha
ushindi nje ya uwanja. Tunaposema ushindi nje ya
uwanja, tunamanisha ni kutumia njia zozote
ziwezekanazo katika kuisadia au kuiwezesha timu
fulani kupata matokeo wanayoyahitaji (Ushindi).
Ufundi ambao kwa kiasi kikubwa ni kutumia makuhani
na washirikina.
Tunazo taarifa kutoka kwa baadhi ya wachezaji
ambao walipewa sharti la kushiriki katika ushirikina ili
wapate nafasi za kucheza ndani ya timu hizo, ikiwamo
kufungwa hirizi miguuni, ama viunoni, au wengine
wakiamrishwa kuzika ama kufukia vitu vya kishirikina
katika uwanja ambao unakusudiwa kutumika katika
mchezo huo. Tunazo taarifa ndani ya jamii yetu za
78
wachezaji wenye uwezo mkubwa sana kwenye
mchezo husika ila kwa kutumia ushirikina, uwezo ule
hufungwa na kuonekana dhaifu wakati mchezo
ukiendelea. Watu wakimlaumu na kumtuhumu juu ya
kipaji chake, kumbe ukweli uliofichwa ni kufungwa
kwa kipaji chake na uwezo wake ili asiwe tishio kwa
timu pinzani ndani ya mchezo husika. Matukio yote
haya huratibiwa na kusimamiwa na kamati maalumu
uliyowekwa (Kamati ya Ufundi) kufanya dhulma kwa
Allah (Subhanahu) na mara nyengine kuwadhulumu
baadhi ya wachezaji wapinzani wanaonekana kuwa ni
tishio katika matokeo ya michezo.
Kwa minajili hii, ndipo michezo inakuwa haramu, na
kutolewa katika jambo ambalo linapendeza na
kuruhusiwa na sharia. Jambo lolote ndani ya Uislamu,
hukosa haki ya kisharia pale ambapo litahusishwa na
ushirikina ndani yake. Haijalishi, jambo hilo liwe ni
Ibada, Kafara, Biashara ama michezo. Hivyo basi,
tufanye michezo na mazoezi bali tuchunge kuingiza
ndani yake chembechembe za ushirikina. Tushiriki
mazoezi na michezo mbali mbali bali kwa sharti la
kuchunga msingi huu mkuu.
Angalizo: Kanuni katika kujua uharamu wa michezo
au uhalali wake ni kuangalia mchezo husika natija
yake ni nini baada ya mtu kushiriki. Je, unamuweka
mbali na ibada, je unamfanya asifanye mambo ya
wajibu kisheria haya na mengineyo yakikosekana basi
hakuna shida kushiriki katika michezo.

79
ATHARI ZA USHIRIKINA
Athari za Ushirikina katika Imani
Shaykh Al-Islam Ibn Taymiyyah (Rehma za Allah ziwe
juu yake) amesema: Miongoni mwa ufisadi mkubwa
katika Ardhi ni kumshirikisha Allah (Subhanahu) na
kutokumfuata Mtume (Swalla Allahu alayhi wa
Sallam). Akaongeza kuwa; kwa ujumla ushirikina na
kuomba dua kwa asiekuwa Allah (Subhanahu) pamoja
na kumuabudu asiekuwa Yeye, au mwenye kutiiwa na
kufuatwa asiekuwa Mtume wa Allah ni ufisadi
mkubwa kabisa katika Ardhi. Hakuna kutegemea kwa
watu wake isipokua Allah (Subhanahu) awe Ndiye
muabudiwa pekee na kuombwa dua na si
mwenginewe. Utiifu na kufuata (kama ilivyopokelewa
miongozo) ni wa Mtume wa Allah pekee.
Katika mlango huu, baada ya kunukuu maneno ya
mwanazuoni huyo, tutabainisha baadhi ya athari za
ushirikina katika Imani ya mwanadamu pamoja na
kuonesha dalili na hoja mbali mbali ambazo
zinathibitisha athari hizo kwa watendaji wa ushirikina
huo. Athari hasi za ushirikina katika Imani ni nyingi
mno, hivyo tulizozikusanya ni baadhi yake ambazo ni
kwa tawfiq yake Allah (Subhanahu) kuweza
kuzikusanya na kuzinukuu.

80
i. Ushirikina unabatilisha (unaporomosha
Amali (Matendo mema)
Amali ama matendo yote mema ambayo
yatahusishwa na kufunganishwa na ushirikina ndani
yake, hukosa thamani mbele ya Allah (Subhanahu).
Huenda mtendaji aliwezeshwa na Allah (Subhanahu)
katika kutekeleza ibada zake, kama vile sala, funga,
sadaka na mengine miongoni mwa mambo ya heri.
Yanapofunganishwa na ushirikina, basi huporomoka
na kukosa thamani kwa Allah (Subhanahu). Haya
yameelezwa na kuthibitishwa kwa dalili zifuatazo:
Allah (Subhanahu) anasema:

﴾ٕٖ﴿ً‫وقَ ِدمنَآ إِ َ َٰل ما َع ِملُواْ ِمن َعم ٍل فَجع ْلنَاه ىبآء َّمنثُورا‬
ً ََ ُ َ َ َ ْ َ ْ َ
“Na tutayaendea yale waliyo yatenda katika vitendo
vyao, tuvifanye kama chembechembe za mavumbi
yaliyo tawanyika.” (25:23)
Ufafanuzi wa kauli hii ya Allah (Subhanahu) amesema
Al-Imam Ibn Kathir (Rehma za Allah ziwe juu yake)
kuwa; Allah anatueleza kwamba matendo yote ya
mwanadamu ambayo yalifanywa kwa ajili ya asiekuwa
Yeye, ama yalifanywa kinyume na utaratibu wa
kisharia, yote yatabatilishwa na kufutwa na hakutakua
na hisabu ya chochote ndani matendo hayo.
Akaendelea kueleza kuwa; namna yatakavyo

81
batilishwa mithili ya vipande vya majani makavu
yanavyo peperushwa na upepo mkali.
Aidha, kuhusu kuporomoka kwa Amali ya washirikina,
Allah (Subhanahu) anasema pia:

‫ك َولَتَ ُكونَ َّن ِم َن‬


َ ُ‫ت لَيَ ْحبَطَ َّن َع َمل‬ ِ َ ِ‫ك وإِ ََل ٱلَّ ِذين ِمن قَػبل‬ ِ ِ
َ ‫ك لَئ ْن أَ ْشَرْك‬ ْ َ َ َ ‫َولَ َو ْد أ ُْوح َى إلَْي‬
﴾ٙ٘﴿‫اس ِرين‬ ِ ْ
َ َ‫ٱْل‬
“Kwa yakini umefunuliwa Wahy kwako (Mtume) na
kwa wale waliokua kabla yako kwamba: Bila ya shaka
ukimshirikisha Allah amali zako zitaanguka, na lazima
utakuwa miongoni mwa wenye kuhasirika.” (39:65)
Allah amesema pia:

َ ِ‫َولَ ْو أَ ْشَرُكواْ َْلَب‬


‫ط َعْنػ ُه ْم َّما َكانُواْ يػَ ْع َملُو َن‬

“Na kama wangelimshirikisha, bila shaka


yangeporomoka yale yaliyokuwa wakitenda.” (06:88)
Hizo ni miongoni mwa dalili ndani ya Qur‟an ambazo
zinathibitisha kuwa ushirikina bila ya shaka
huporomosha amali za mtendaji, aidha, Mtume
(Swalla Allahu alaiyh wa Sallam) ametaja Hadithi Al-
Qudsiy kuwa:
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhi za
Allah ziwe juu yake) kwamba Mtume (Swallah Allahu
alayhi wa Sallam) amesema: ((Allah (Ta‟ala)
amesema: “Mimi ni mwenye kujitosheleza kabisa,

82
sihitaji msaada wala mshirika. Kwa hiyo yule afanyae
amali kwa kunishirikisha na mtu, nitaikanusha pamoja
na mshirika wake.”)) Yaani hata pata ujira wowote wa
amali hiyo. [Imesahihishwa na Imami Muslim na Ibn
Maajah]
Tutambue ndugu zangu wasomaji, tunaposema
ushirikina tunajumuisha pamoja yale matendo yote
ambayo mwanadamu huyafanya hapa duniani kwa
kujionesha (Riyaa) kwani Riyaa ni kigawanyo
miongoni mwa vigawanyo vya ushirikina. Allah
(Subhanahu) ameitaja wazi wazi namna ambavyo
riyaa inavyopelekea kubatilisha na kuyaporomosha
kabisa matendo yote. Kwani Allah amesema ndani ya
Qur‟an:

ِ ‫ص َدقَاتِ ُكم بِٱلْ َم ّْن َوٱألَذَ ٰى َكٱلَّ ِذى يػُْن ِف ُق َمالَوُ ِرئَآءَ ٱلن‬
‫َّاس‬ ِ
َ ْ‫ين َآمنُواْ الَ تػُْبطلُوا‬
ِ َّ
َ ‫يٰأَيػُّ َها ٱلذ‬
ِ ٍ ِ ِ ِ ِ ِ
ُ‫َصابَوُ َوابِل فَػتَػَرَكو‬
َ ‫ص ْف َوان َعلَْيو تُػَراب فَأ‬ َ ‫َوالَ يػُ ْؤم ُن بٱللَّو َوٱلْيَػ ْوم ٱآلخ ِر فَ َمثَػلُوُ َك َمثَ ِل‬
﴾ٕٙٗ﴿‫ص ْلداً الَّ يػ ْو ِدرو َن َعلَ ٰى َشي ٍء ِّْمَّا َكسبواْ وٱللَّو الَ يػه ِدى ٱلْ َووم ٱلْ َكافِ ِرين‬
َ َْ ْ َ ُ َ َُ ْ ُ َ َ
“Enyi mlio amini! Msibatilishe sadaka zenu kwa
masimbulizi na udhia kama yule ambaye anatoa mali
zake kwa kujionesha kwa watu wala hamwamini
Allah. Siku ya Kiyama, mfano wake ni kama jabali juu
yake pana udongo, kisha likapigwa na mvua kubwa
ikaliacha tupu. Hawana uwezo juu ya lolote katika
waliyoyachuma. Na Allah hawaongoi watu makafiri.”
(02:264)

83
Kwa upande mwengine, Mtume (Swallah Allahu alayhi
wa Sallam) amefundisha kupitia Hadithi:
Imepokelewa kutoka kwa Jundub bin Abdillah bin
Sufyaan (Radhi za Allah ziwe juu yake) ambaye
amesema; Mtume (Swallah Allahu alayhi wa Sallam)
amesema: ((Mwenye kudhihirisha amali yake kwa
riyaa, Allah atamfedhehesha siku ya Kiyama, na
mwenye kuwafanyia watu riyaa [Kwa amali njema ili
aonekane mtukufu] Allah atadhihirisha siri zake siku
ya Kiyama.)) [Imesahihishwa na Al-Bukhari na
Muslim]
ii. Ushirikina humuingiza mtu katika wafanyao
madhambi makubwa.
Tulifafanua awali juu ya wasia wa Mtume (Swallah
Allahu alayhi wa Sallam) kuhusiana na kujikinga na
mambo saba yenye kuangamiza. Miongoni mwa
mambo hayo, ushirikina ulikaa nafasi ya kwanza.
Ushirikina ni miongoni mwa dhambi kubwa ambayo
mfanyaji hujihakikishia ghazabu na maangamizi ya
Allah (Subhanahu). Aidha, ushirikina ni miongoni mwa
dhambi ambayo Allah (Subhanahu) haisamehe bila ya
toba ya kweli.
Amesema Allah (Subahanahu):

‫ك لِ َمن يَ َشآءُ َوَمن يُ ْش ِرْك بِٱللَّ ِو فَػ َو ِد‬ ِ ِ ِ


َ ‫إِ َّن ٱللَّوَ الَ يػَ ْغفُر أَن يُ ْشَرَك بِِو َويػَ ْغفُر َما ُدو َن ٰذل‬
﴾ٗٛ﴿ً‫ٱفْػتَػر ٰى إِْْثاً َع ِظيما‬
َ
84
“Hakika Allah hasemehe kushirikishwa, na husamehe
yaliyo duni ya hilo kwa amtakae. Na anae mshirikisha
Allah hakika amezua dhambi kubwa.” (04:48)
Kadhalika Allah (Subhanahu) amesema:

‫ك لِ َمن يَ َشآءُ َوَمن يُ ْش ِرْك بِٱللَّ ِو فَػ َو ْد‬ ِ ِ ِ


َ ‫إِ َّن ٱللَّوَ الَ يػَ ْغفُر أَن يُ ْشَرَك بِِو َويػَ ْغفُر َما ُدو َن ٰذل‬
﴾ٔٔٙ﴿ً‫ضالَالً بعِيدا‬
َ َ ‫ض َّل‬ َ
“Hakika Allah hasamehe kushirikishwa na kitu. Lakini
Yeye husamehe yasiyo kuwa hayo kwa amtakae. Na
anae mshirikisha Allah basi huyo amepotea upotovu
wa mbali.” (04:116)
Nikimnukuu Imam ibn Uthaymin (Rehma za Allah ziwe
juu yake) alisema kuwa; Allah hasamehe ushirikina
kamwe (asipotubia mtu kabla ya mauti) kwani ni jinai
juu ya haki ya Allah (Subhanahu) nayo ni Tawhid.
Katika Hadithi ilio sahihishwa na Al-Bukhari na
Muslim; Mtume (Swalla Allahu alayhi wa Sallam)
amesema: ((Je, hivi nikufahamisheni madhambi
makubwa kabisa? Ni kumshirikisha Allah
(Subhanahu).
iii. Ushirikina unamuharamishia mtu kuingia
katika Pepo (Jannah)
Kila amali njema ambayo mwanadamu hufanya juhudi
kuifanya, hutegemea malipo kwa Allah (Subhanahu).
Kama ambavyo ameahidi malipo kemkem kwa

85
wafanyao amali njema. Allah (Subhanahu) akaweka
na kutoa muongozo wa namna ambavyo atalipa kila
amali njema ya mja. Akaeleza kupitia Qur‟an na
mafundisho ya Mtume (Swalla Allahu alayhi wa
Sallam) kuwa atalipa kila jema moja kwa wema kumi
hadi sabini mfano wake. Mbali na yale mema ambayo
ameyaficha malipo yake, kama yalivyofichwa malipo
ya funga. Kisha kwa Rehema zake atawaingiza
kwenye pepo zake kwa sababu ya wema
walioutanguliza duniani.
Ila, kwa amali ambazo ndani yake zimegubikwa na
ushirikina, hazitakua na malipo wala Rehema yoyote
katika Rehema zake za pepo. Badala yake zitamfanya
afanyae ushirikina kuwa miongoni mwa waja ambao
wameramishiwa kuingia ndani ya pepo (Allah
atuhifadhi na kutulinda kuwa miongoni mwa watu
hao). Kutokana na dhambi ya ushirikina, malipo na
mafikio ya watu hawa yatakuwa ni moto (Jahannam)
ambao ndani yake watadumu milele. Ushahidi wa hili
unadhihirishwa ndani ya Qur‟an, ambapo Allah
(Subhanahu) anasema;

‫َنصا ٍر‬ ِ ‫ٱْلنَّةَ ومأْواه ٱلنَّار وما لِلظَّالِ ِم‬ ِ ِ ِ ِ


َ ‫ني م ْن أ‬
َ َ َ ُ ُ َ َ َ َْ ‫إنَّوُ َمن يُ ْش ِرْك بٱللَّو فَػ َو ْد َحَّرَم ٱللَّوُ َعلَيو‬
“Kwani anae mshirikisha Allah, hakika Allah
atamharamishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na
walio dhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru.”
(05:72)

86
Hivyo hivyo, Imepokelewa kutoka kwa Abdallah bin
Mas-uwd (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema:
Mtume (Swalla Allahu alayhi wa Sallam) amesema:
((Atakae kufa akiwa katika hali ya kumuomba
asiekuwa Allah (mshirikina), anamfanyia mlinganishi
(mshirika) ataingia Motoni.)) Al-Bukhari na Muslim.

Kadhalika, katika kuendelea kufafanua namna


ambavyo washirikina wataharamishiwa Pepo. Allah
(Subhanahu) akakataza na kukemea vikali hata
kuwaombea dua wazazi ambao walifariki wakiwa
katika hali ya ushirikina wa aina na sura yoyote. Mbali
na kuwa miongoni mwa jambo jema na lenye
kumfaidisha mzazi aliefariki ni dua za mtoto mwema.
Lakini katika ushirikina Allah (Subhanahu) amelikataza
na kuliwekea hukmu ndani ya Qur‟an, kama
alivyosema ndani ya Qur‟an kuwa:

‫ني َولَ ْو َكانػُۤواْ أ ُْوَِل قُػ ْرَ ِٰب ِمن بػَ ْع ِد َما‬ِ ِ ِ
َ ‫ين َآمنُػۤواْ أَن يَ ْستَػ ْغفُرواْ ل ْل ُم ْش ِرك‬
ِ َّ ِ‫ما َكا َن لِلن‬
َ ‫َِّب َوٱلذ‬
ّْ َ
﴾ٖٔٔ﴿‫ٱْل ِحي ِم‬
َْ ‫اب‬
ُ ‫َص َح‬
ْ ‫ني َِلُ ْم أَنػ َُّه ْم أ‬
َ َّ ‫تَػبَػ‬
“Haimpasi Nabii na wale walioamini kuwaombea
msamaha washirikina japokuwa ni jamaa zao wa
karibu baada ya kuwabainikia kwamba wao ni watu
wa Moto uwakao vikali mno.” (09:113)
Hivyo hivyo, pia washirikina wamebebeshwa sifa
nyingi mbaya ndani ya Qur‟an. Mara zote Allah

87
(Subhanahu) anapowataja washirikina hufunganisha
na sifa mbaya kemkem, kama vile analivyowaita kuwa
ni vipofu, viziwi, mabubu, pamoja na kuwaita watu
wasiotumia akili. Kutokana na kufuru yao, Allah
(Subhanahu) akawafafanisha na wanyama, na mara
nyengine akawashusha kwa udhalili na uduni na kuwa
chini zaidi ya wanyama. ushahidi wa ufafanuzi huu ni
kama ambavyo Allah anasema ndani ya Qur‟an:
ِ
َ ‫َن أَ ْكثَػَرُى ْم يَ ْس َمعُو َن أ َْو يػَ ْعولُو َن إِ ْن ُى ْم إِالَّ َكٱألَنْػ َع ِام بَ ْل ُى ْم أ‬
‫َض ُّل‬ َّ ‫ب أ‬
ُ ‫أ َْم ََْت َس‬
﴾ٗٗ﴿ً‫سبِيال‬
َ
“Je, unadhania kwamba wengi wao wanasikia au
wanatia wakilini? Wao si chochote isipokuwa kama
wanyama bali wao wamepotea zaidi njia.” (09:44)
Haya yote ni kwasababu ya ujinga na upofu wao.
Kwani Allah (Subhanahu) anasema aidha:

‫َنزَل ٱللَّوُ قَالُواْ بَ ْل نػَتَّبِ ُع َمآ أَلْ َفْيػنَا َعلَْي ِو آبَآءَنَآ أ ََولَ ْو َكا َن آبَ ُاؤُى ْم‬ ِ ِ
َ ‫يل َِلُ ُم ٱتَّبِعُوا َمآ أ‬
َ ‫َوإذَا ق‬
﴾ٔٚٓ﴿‫الَ يػع ِولُو َن َشيئاً والَ يػهتَ ُدو َن‬
َْ َ ْ َْ
“Na wanapoambiwa: “Fuateni aliyoyateremsha Allah”
Husema: “Bali tunafuata tuliyowakuta nayo baba
zetu.” Je, japo kuwa baba zao walikuwa hawaelewi
kitu chochote na wala hawakuongoka?” (02:170)

88
Athari za ushirikina katika Jamii
Athari hasi za ushirikina haziishi tu katika Imani ya
mtendaji, bali pia huzalisha madhara makubwa ndani
ya jamii nzima. Jamii ambayo imegubikwa na dhambi
ya ushirikina ni jamii ovu, yenye kila aina ya laana za
Allah (Subhanahu). Miongoni mwa athari hasi za
ushirikina katika jamii ni pamoja na kusababisha
umasikini na ufukara, kuzalisha chuki na uhasama
baina ya jamii ama familia pamoja na kuchochea
matendo maovu na umwagaji damu.
i. Ushirikina husababisha umasikini na kukosa
Baraka katika rasilimali.
Ndugu yangu msomaji, kwa hakika jamii yoyote
iliyokumbatia ushirikina siku zote haina maendeleo.
Mbali na kuzagaa kwa matangazo ya dua (za
kishirikina) na visomo kadhaa vya utajiri ama kuvuta
wateja kwenye biashara, bado tunaona jamii
inaendelea kuwa duni kuliko walio duni. Ushirikina
husababisha umasikini kwa mantiki ya kwamba, ndani
ya ushirikina hupelekea matumizi mabaya ya rasilimali
zilizochumwa kwa jasho na damu. Ushirikina
hupelekea mtu kuwa mtumwa wa waganga na majini
huku akishurutishwa kugharamia kafara mbali mbali
za wanyama kwa mali nyingi.
Mali na rasilimali nyingi hutumika ndani ya ushirikina
kuliko namna ambavyo hutumika katika kustawisha
familia na jamiii inayowazunguka. Hili kwa kiasi

89
kikubwa huzalisha umasikini na utegemezi kwa kiasi
kikubwa. Aidha, chumo lolote ambalo hupatikana kwa
njia za ushirikina (kama pesa za majini), Allah
(Subhanahu) huziondolea Baraka na kuwaacha
wahusika kutofaidika na chochote ndani ya mali hizo.
Kadhalika, mali na rasilimali hupotea kwa ushirikina
kwa ahadi za uongo, huku wahusika wakitaraji wema
na mafanikio kama walivyo ahidiwa na washirikina.
Hakuna mafanikio (hapa duniani) kupitia ushirikina
kama ambavyo hakuna malipo ya matendo ya
washirikina mbele ya Allah (Subhanahu). Kwani
jambo lolote linalokosa malipo mbele ya Allah, kwa
yakini haliwezi kunawirisha wala kustawisha hapa
duniani. Hakika huwezi kutegemea ustawi na
maendeleo katika jamii ambayo neema za Allah
(Subhanahu) kama vyakula (Nazi) hutupwa na
kutelekezwa barabarani. Tusitegee neema na Baraka
zake katika utafutaji riziki hapa duniani, hali ya kuwa
tumekuwa tukifunganisha ibada mbali mbali na
ushirikina kama ambavyo watu huchinja kwa kafara
kwa asiekuwa Allah (Subhanahu).
ii. Ushirikina huzalisha uhasama na uadui
baina ya jamii.
Miongoni mwa athari nyengine za ushirikina ndani ya
jamii. Mara nyingi, huzalisha uhasama na uadui
mkubwa baina ya watu. Ndoa, familia, hata
mahusiano ndani ya jamii huathirika kwa kiasi

90
kikubwa pale ambapo ushirikina utaanza kuonesha
makucha yake. Hakuna salama ndani ya jamii yoyote
ambayo ushirikina umeshika hatamu. Bali jamii hiyo
itagubikwa na uonevu, udhalimu mkubwa baina yao.
Wengi wametengeneza ama kutengenezewa uadui
baina yao ikiwa ni matokeo mabaya ya ushirikina na
ramli chonganishi na za uongo. Wengi ndani ya jamii
zetu wameingia katika uhasama baina yao na rafiki
zao, baina yao na familia zao, bali hadi baina yao na
wazazi wao kwa sababu za Imani za ushrikina ambazo
zimewatoa katika kuamini kadari za Allah
(Subhanahu). Biashara na rasilimali nyingi zimeingia
katika hasara mbali mbali kwa Imani ovu za
kishirikina ama kwa uchafu wa hasara
zilizosababishwa na chuma uele (Kopera). Hizi zote ni
katika namna ambayo ushirikina umekuwa
ukitengeneza uhasama na kuondoa tangamano jema
ndani ya jamii zetu, kwani uadui wa ushirikina mara
nyingi ni mkubwa. Ushrikina mara nyingi umekuwa
ukisababisha chuki na kuondoa Imani baina ya jamii
huku jamii hizo zikiachwa na mabaki ya hofu, hasadi
na uchoyo.
iii. Ushirikina huzalisha matendo maovu na
umwagaji wa damu.
Jamii imeondokewa na Imani huku ikuvuliwa utu kwa
sababu ya ushirikina. Kila uchwao tunashuhudia
kushamiri kwa matendo maovu ambayo asili yake ni

91
kukithiri kwa ushirikina. Tulishuhudia, hapo awali,
ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi wakifanyiwa
matendo mabaya na ya kikatili kwa kukatwa baadhi
ya viungo vyao kwa dhulma kubwa. Wimbi hili
likakithiri na kuongeza hofu baina ya jamii hiyo huku
wakikosa fursa zao za msingi za kutangamana na
uhuru wa kufanya shuhuli zao. Hili ikawa ni pigo
kubwa kwa jamii ambalo lilizalishwa na uovu wa
ushirikina.
Ushirikina haukuwaacha salama vikongwe (wazee),
ambao walikuwa dhaifu ndani ya jamii kwa kuuwawa
bila hatia yoyote kwa Imani ovu za kishirikina. Jamii
nayo ikaingia katika msukosuko mkubwa huku damu
za wasio na hatia zikamwagika bila ya haki, yote
yakawa ni matokeo mabaya na machafu ya ushrikina.
Watoto wachanga wakatolewa kafara kwa kuwatupa
ama kuwakabidhisha kwa mizimu huku wakiiachwa
wazazi katika buguziko na hangaiko kubwa la moyo.
Hivi karibuni, tumeshuhudia pia watu wakidhalilishana
wazi wazi kwa kufanyiwa unyama mkubwa na wa
aibu kwa sababu ya Imani potofu za ushirikina
zilishikanishwa na wivu na ndoa. Haya na mengine
mengi ni matokeo ya athari hasi za ushirikina,
ambazo ipo haja ya jamii yetu kuelezwa ili wafahamu
ukubwa na uharamu wa ushirikina. Hivyo basi kupitia
Chapisho hili kwa idhini ya Allah (Subhanahu) huenda

92
tukaongoka na kuachana na ushirikina kwa ujumla
wake.

KWANINI JAMII INAINGIA KATIKA


USHIRIKINA
Ushirikina umekatazwa na makatazo yake
yamekokotezwa kwa uzito wake ndani ya Qur‟an na
Sunna za Mtume wa Allah. Mbali na makatazo hayo,
sambamba na athari zake hasi kemkem, kama
ambavyo tumezibainisha baadhi hapo juu. Bado jamii
zetu zinaonekana kuendelea kuukumbatia kwa kasi
kubwa. Ushirikina umekithiri ndani ya jamii zetu hadi
kufikia hatua (kama tulivyobainisha) kuonekana ni
haki ambayo tunapaswa kuipupia ili kujikwamua
katika mambo mbali mbali ndani ya jamii. Tukasahau
kuwa Allah (Subhanahu) ameshatoa ahadi yake kuwa,
kwa yoyote ambaye ataiacha na kuifumbia macho
haki na kuendelea kushikamana na batili (kama ya
ushirikina), basi ameandaliwa matokeo makubwa
mawili kama alivyosema ndani ya Qur‟an;

﴾ٕٔٗ﴿‫ضنكاً وَْْم ُشره يػوم ٱلْ ِويام ِة أ َْعم ٰى‬ ِ


َ ِ‫ض َعن ذ ْك ِرى فَِإ َّن لَوُ َمع‬
َ َ َ ْ َ ُُ َ َ ً‫يشة‬ َ ‫َوَم ْن أ َْعَر‬
“Na atakae jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa
yakini atapata maisha ya dhiki (Duniani). Na siku ya
Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” (20:124)
Jambo la msingi katika mlango huu, ni kubainisha
kwa mujibu wa ufatiliaji na utafiti wa kina ambao
ulifanyika ndani ya jamii zetu, uliolenga kujua sababu
93
haswa kwanini jamii zetu zinaendelea kuingia ndani
ya ushirikina. Mbali na kwamba makatazo yake yapo
wazi, athari zake hasi zinaonekana na madhara
makubwa (kama tulivyobainisha) yanaendelea kuisibu
jamii yetu. Kwa uchache wake tutabainisha sababu
muhimu na za msingi ambazo zinasababisha jamii
zetu kuingia ndani dimbwi hili refu la ushirikina
ambazo ni kama tunavyozibainisha hapa chini.
Awali ya yote, jamii inaingia katika ushirikina
kwasababu imeshindwa kuwa na Taqwa ya kweli kwa
Allah (Subhanahu). Imani potofu na chafu ndizo
zimetawala katika nafsi za wengi ndani ya jamii.
Wakasahau kuwa wanaweza kupata nusura ndani ya
mipaka Allah (Subhanahu). Wakaamini kuwa dhiki na
umasikini huweza kutatuliwa na kiumbe ama viumbe
wengine pasi na Allah (Subhanahu). Ndio ukaona
shida nyingi za viumbe (wanadamu) kama vile riziki,
mafanikio ndani ya biashara, vizazi na mengine
yasiyokuwa hayo yanaweza kutatuliwa kupitia njia
chafu za ushirikina. Jamii ikaamini na kutaraji poza za
maradhi kupitia waganga, ikaamini kuwa kufunguliwa
kwa milango ya riziki na mali katika biashara na kazi,
hupatikana kupitia ushirikina huku wakikutana na
udhalili mkubwa wa masharti kandamizi ya mizimu.
Watu wengi miongoni mwa jamii zetu wakaamini
kuwa uzazi na neema ya watoto huweza kutatuliwa
kupitia njia za ushirikina kama vile uganga ama

94
kuomba wafu miongoni mwa mawalii. Huku
wakidharau na kupuuza maamrisho ya Allah
(Subhanahu) na mafundisho ya Mtume wake juu ya
umuhimu wa kutegemea na kukusudia shida zote kwa
Allah. Wakasahau kuwa Yeye ndiye alietuumba na
kutupangia kila kitu katika maisha yetu hapa duniani.
Tukaacha itikadi sahihi za kuamini kudra za Allah
(Subhanahu), tukapuuza kukumbuka kuwa Yeye
ndiye anaeturuzuku uhai na nafasi ya maisha hapa
duniani na kwamba Yeye Allah (Subhanahu) ndiye
aliyetupangia kila riziki yetu kuanzia tukiwa
matumboni mwa mama zetu hali tukiwa duni kabisa,
kisha tukazaliwa na kuendelea kuyaendesha maisha
yetu kwa kadiri alivyotupangia.
Yawaje, tukose kuamini juu ya Uungu wake na kuwa
wapinzani wa Muumba wetu bila haki. Kama
alivyosema Allah (Subhanahu) ndani ya Surat An-
Nah‟l kuwa:

ِ ‫خلَق ٱ ِإلنْسا َن ِمن نُّطْ َف ٍة فَِإ َذا ىو خ‬


﴾ٗ﴿‫صيم ُّمبِني‬
َ َُ َ َ َ
“Amemuumba mtu kwa tone la manii. Nae mara
amekuwa mshindani Dhahiri.” (16:04)

Hivyo basi, ni juu yetu kujipamba na Taqwa ya Allah


(Subhanahu) na kuachana na ushirikina kwani kwa
hakika muongoaji ni Yeye. Ni jukumu letu kuamini na

95
kutakidi kuwa hakuna dhara ambalo linaweza
kutukuta wala neema ambayo inaweza kutufikia bila
ya Allah (Subhanahu) kutaka na kuipangilia kwetu.
Kama ambavyo imethibiti kutoka katika Hadithi,
Mtume (Swallah Allahu alaiyhi wa Sallam) alimwambia
Ibn Abbass (Radhi za Allah ziwe juu yake) kuwa;
((Watu wote wakijikusanya kukunufaisha, hawawezi
kukunufaisha kwa kitu isipokuwa kile Allah
alichokiandika. Na wakitaka kukudhuru hawawezi
kukudhuru isipokuwa katika kile alichokiandika Allah.
Kila kitu kimeshaandikwa na kila kitu kimekamilika.))
Msingi mkubwa ni kumtegemea Allah (Subhanahu)
katika kila jambo na kujenga vyema Imani zetu
Kwake. Kwani katika kumtegemea ndio mafanikio ya
yale yote ambayo tunayakimbilia hupata ufumbuzi.
Kwa muumini (Muislamu) anahimizwa kumtegemea
Allah (Subhanahu) na kuacha uchafu wote ambao
humuondoa katika Uislamu kama ambavyo ushirikina
huporomosha matendo yote mema. Kwani Allah
amesema;
ِِ ِ
َ ‫َو َعلَى ٱللَّو فَػتَػ َوَّكلُۤواْ إِن ُكنتُم ُّم ْؤمن‬
‫ني‬

“Na mtegemeeni Allah ikiwa nyinyi ni Waumini.”


(05:23)
Aidha, sababu ya pili ambayo husababisha jamii zetu
kuingia ndani ya ushirikina, ni kukosekana kwa elimu

96
sahihi juu ya dhambi ya ushirikina. Jahazi la jamii
yetu imekuwa ikienda ubenibeni (kombo) kwa kukosa
kujua haswa upana, ukubwa na uharamu wa
ushirikina. Hakika mwenye kulijua jambo kwa undani
wake basi kwake ni wepesi kulikimbia na kutahadhari
nalo. Watu wengi miongoni mwa jamii zetu huingia
ndani ya ushirikina bila ya kujua. Wakiamini kuwa
wapo katika njia iliyo sawia. Ipo haja ya wahadhiri na
viongozi mbali mbali wa dini ya Kiislamu kuendelea
kuibainishia jamii upana wa ushirikina na sura zake.
Ili iwe ni wepesi kwa jamii zetu kubaini na kutanabahi
juu kila hatua ama viashria vya ushirikina.
Elimu sahihi ikitolewa kwa jamii itasaidia wengi katika
kubaini na kujikinga na kuingia ndani yake.
Imethibiti Hadithi ya Khudhaifa ibn Yaman kuwa
alisema: ((Walikuwa watu wakimuuliza Mtume (Swalla
Allahu alaiyh wa Sallam) kuhusu matendo mema na
heri, lakini mimi, nilikuwa nikimuuliza kuhusu shari na
maovu kwa kuhofia kuingia ndani yake bila kujua.))
Sambamba na hilo, Muislamu haswa hapaswi kuwa
mjinga katika mambo ya msingi kama vile Ibada,
hupaswa kuhakikisha anatafuta elimu sahihi juu ya
jambo kabla ya kuliingia. Hivyo, inasisitizwa pia
kujibidiisha katika kuisoma dini yetu, kusoma misingi
ya ibada zetu pamoja na kujitahidi katika kujikuza
kielimu ya mambo mbali mbali ambayo
yanamafungamano ya moja kwa moja na ibada. Hii

97
itasaidia katika kuepuka na kutahamani tumeingia
katika mambo ambayo mwisho wake ni uovu na
maangamizi bila ya kujua.
Kadhalika, miongoni mwa sababu ambazo zinaifanya
jamii kuingia ndani ya ushirikina ni uovu na uchafu wa
nafsi za wengi miongoni mwa jamii. Duru za kijamii
zinaeleza kuwa kwa kiwango kikubwa watu hufanya
ushirikina kwa lengo la kujitibu kutokana na madhara
makubwa na madogo ambayo yamesababishwa na
ufisadi wa wengine wenye nafsi chafu na korofi.
Uchawi ama ushirikina kwa kiasi kikubwa hutumiwa
na watu kuwadhuru wengine, hivyo kutokana uhaba
wa elimu na Imani ndani ya jamii wengine huamini
kuwa uchawi hutibiwa kwa kutumia uchawi mfano
wake.
Dhana ambayo ni ovu, na yakupigwa vita sana
miongoni mwa jamii zetu. Waliowengi huenda katika
ushirikina kwa lengo la tiba za maradhi ambayo mbali
na yale ya kawaida, kuna yale ambayo
yamesababishwa na hasadi, kijicho ama uovu tu
mwengine wa kichawi. Wakaacha njia sahihi ya Ruqya
ya kisharia na kuingia ndani ya ushirikina. Ajabu ilioje,
wapo miongoni mwa wanadamu wanathubutu
kuwadhuru wengine kwa kutumia ushirikina, na kwa
kukosa Imani sahihi ya taqwa ya Allah (Subhanahu)
waliodhuriwa wakaelekea kwa waganga kupata tiba
ambazo zinawaingiza pia katika ushirikina mkubwa.

98
Wengi huingia katika ushirikina kwa aidha, kujitibu
ama kulipiza kisasi cha uovu waliofanyiwa. Wakaacha
njia sahihi zilizowekwa za tiba na kumtegemea Allah
(Subhanahu). Lakini msingi mkubwa kuwa, kwanini
umdhuru mtu kwa ushirikina. Na mara nyingi sababu
zikiwa ni dhaifu ambazo haziendani na kima cha
dhara ambayo utamsababishia mwingine.
Sababu ya tatu ambayo inaifanya jamii yetu kuingia
kwa kasi kubwa ndani ya ushirikina, ni kuibuka kwa
wimbi kubwa la wanganga na wapiga ramli na
watumiaji wakubwa wa tarasimu, ambao kwa namna
moja ama nyengine wamejivesha vazi la tiba za dua.
Wimbi hili limekuja kwa baadhi yao kujinasibisha na
Qur‟an kwa dhahiri huku kwa siri wakitumia uchawi
na majini katika visomo ama tiba zao. Kutokana na
jambo hili likaifanya jamii kushindwa kutambua na
kutofautisha kwa wazi yupi yupo katika tiba ya
kisharia na yupi kati yao ni mshirikina.
Haya huyafanya kwa adhma maalumu, kwa sababu
wanatambua kwa asilimia kubwa sasa jamii
imeelimika japo kwa uchache juu ya uovu na ubaya
wa ushirikina. Hivyo wakidhirihisha matendo yao,
huenda jamii ikawakataa. Kwa msingi huo,
wakajipamba kwa mavazi na matangazo yenye dua
na Qur‟an, wakajivesha vazi la Imani kuihadaa jamii,
na mwisho kuwafanyisha ushirikina na uchawi bila ya
wao kujua. Wakitahamaki, wanapewa hirizi, ama

99
tarasimu za kuvaa au kutundika. Wakitahamaki
wanatakiwa kufanya kafara ya wanyama mwenye sifa
fulani.
Kwa masikitiko makubwa sana, wimbi hili limekuwa
likiongezeka na kushamiri maradufu, huku
wakisaidiwa vyema na uwepo wa mitandao ya kijamii.
Hutumia mwanya huo kujitangaza na kutangaza uovu
wao bila ya kujali wala kuhofia ghadhabu za Allah
(Subhanahu). Hivyo basi, kwa kulijua hili ipo haja
sasa jamii kuwa makini na kuchukua tahadhari kubwa
ya kuchagua ni wapi na kwa nani unaenda kwa ajili
tiba za kisharia. Kwa ubainifu huu, tunategemea jamii
itatambua uovu wa ushirikina, itatambua mbinu
zinazotumika kuwahadaa na kuwavuta kuingia ndani
ya ushirikina na kila mmoja atakua na tahadhari.
Kwani Mtume (Swalla Allahu alaiyh wa Sallam)
amesema, kama ilivyokuja Katika Sahihi Al-Bukhari:
((Imepokewa kutoka kwa Abuu Khurayra (Radhi za
Allah ziwe juu yake) kuwa Mtume (Swalla Allahu
alaiyh wa Sallam) amesema: Haumwi (Hadhuriki)
Muislamu katika tundu moja mara mbili.))

VIPI TUTAJIKWAMUA KUTOKA KATIKA UOVU


WA USHIRIKINA UNAPOTUPATA
Athari na dalili za Hadithi sahihi za Mtume (Swalla
Allahu alayhi wa Sallam) zinathibitisha kuwa uchawi
upo, na mtu anaweza (kwa idhini ya Allah) kusibiwa
na uchawi (Ushirikina) ama majini kutokana na aidha

100
shari za viumbe wengine ama kwa namna nyengine
yoyote. Uislamu haukuacha wala kulikalia kimya
jambo hili, bali ulitoa njia sahihi na za kisharia za
kujikwamua katokana na sihri au ushirikina. Ama kwa
upande mwengine zile dhana za kuwa uchawi
huondolewa kwa kutumia uchawi mfano wake, ni
dhana na mila potofu ambazo hazina nafasi ndani ya
sharia na miongozo ya Kiislamu.

Hivyo, uchawi ama sihri (Ushirikina) upo, na kama


tulivyo tangulia kusema kuwa huenda mtu akapata
dhara kutokana na uchawi na kumsababishia maradhi
mbali mbali, kama vile wasiwasi, jinni ama ukichaa
(Kwa idhini ya Allah). Ila jambo la msingi ni
kuhakikisha mtu huyo hatumii wala hawaendei
wanganga, washirikina wala makuhani ili kutibu na
kuondoa tatizo hilo, bali anafanya kile ambacho
kimeruhusiwa na sharia katika kutafuta poza za
kisharia. Kutokana na kukosekana kwa Imani hii,
ndipo kundi kubwa ndani ya jamii hukata shauri na
kuwaendelea wanganga na washirikina bila ya kujua
anajiingiza katika maradhi mengine na hasara kubwa.
Mbali na maradhi ya ushirikina yaliyowakumba,
akaongeza maradhi mengine makubwa ya maasi ya
ushirikina ndani ya nafsi yake na wale
wanaomzunguka.

101
Kutokana na Imani hizi potovu, ndipo jamii ikaamini
kuwa huwezi kuishi hapa ulimwenguni bila ya kuwa
na mganga (Babu) au waganga mara nyengine wa
masuala tofauti. Tunatambua kuwa ndani ya jamii
zetu, wapo watu wanao waganga hadi kumi, huku
kila mmoja akiwa na kazi yake maalumu, kati yao
yupo wa kulinda mali, wa kulinda familia, na mengine
yasiyokuwa hayo. Kwa hakika haya yote ndiyo haswa
yanayo endelea ndani ya jamii zetu. Ndani ya jamii
zetu tunatambua kuwa wapo watu wengine
wanaumwa hata na malaria, badala ya kuenda
hospitali, kwanza huanza kupiga ramli na kutazamia
nyota.
Watu wengi husibiwa na maradhi makubwa ambayo
kwa hakika (kwa idhini ya Allah) yalihitaji tiba sahihi
za hospitali, lakini waliishia kufanyishwa ushirikina
hadi yakawagharimu uhai wao. Haya yote huzalishwa
na nyoyo chafu, zilizochafuliwa kwa Imani ovu za
kishirikina. Aidha, haya yote yamekuwa yakitokea
ndani ya jamii zetu huku mali nyingi zikipotea kwa ajili
ya kununua mbuzi, ng‟ombe na vitu vyengine na
kumuacha mtu akiwa dhalili kwa maradhi, dhambi
pamoja na umasikini.
Kutokana na ukweli kuwa mambo yote haya hayana
athari wala hayakufundishwa ndani ya sharia za
Uislamu. Je! Uislamu umetufundisha njia zipi sahihi za
kuweza kujikwamua pale mmoja wetu anaposibiwa na

102
sihri ama uchawi. Uislamu umekamilisha kila kitu
katika mifumo ya maisha pamoja na mifumo ya tiba
sahihi za kujitibu kama vile ulivyofundisha na
kusisitiza kuwaona madaktari (Hospitali) na hata
kutumia njia za tiba za miti shamba ambayo
imeruhusiwa, huku ukiweka sharti kwamba ni lazima
njia hizo (tiba mbadala) ziwe zimeruhusiwa na sharia
za Uislamu.

Tukiwa tunaufungua mlango huu, tutambue kuwa


jambo la kwanza na la msingi ni kutambua kwamba
uchawi ama sihri (ushirikina) hutibiwa (kwa idhini ya
Allah) kwa kutumia Qur‟an, sambamba na dua
ambazo zimethibiti ndani ya Hadithi sahihi za Mtume
(Swalla Allahu alaiyh wa Sallam) pamoja na dawa
sahihi ambazo zimetajwa na matabibu wa kisharia wa
Kiislamu. Katika miongoni mwa tiba na kinga bora
iliotajwa na Mtume (Swalla Allahu alayhi wa Sallam)
ni kama vile mtu kula tende punje saba aina ya Ajwa
kila siku asubuhi. Hili limethibiti katika Hadithi ya
Abuu Hurayrah:
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhi za Allah ziwe juu
yake) amesema: Amepokea kutoka kwa Mtume
(Swallah Allahu alayhi wa Sallam) amesema: ((Yule
atakaekula asubuhi tende saba za Ajwa, haitamdhuru
yeye siku hiyo sumu wala uchawi))

103
Ama katika Hadithi nyengine:
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhi za
Allah ziwe juu yake) amesema; Amesema Mtume
(Swallah Allahu alayhi wa Sallam) amesema:
((Shetani haingii katika nyumba ambayo husomwa
ndani yake Surat Al-Baqarah.))
Aidha, katika riwaya nyengine Mtume (Swallah Allahu
alayhi wa Sallam) Amesema kwamba: ((Dumuni
kuisoma Surat Al-Baqarah kwani kuichukua ni Baraka
na kuiacha ni masikitiko na ni majuto kwani wachawi
hawaiwezi Sura hiyo.))
Kadhalika, imethibiti kuwa uchawi ama sihri hutibiwa
na kubatilishwa kwa kutumia pia sura nyengine ndani
ya Qur‟an; kama vile Surat N‟asi, Falaq, Ikhlas pamoja
na Ruqya ya kisharia na kufanya adhkari za asubuhi
na jioni, mara kwa mara. Jambo linalosisitizwa zaidi
katika mlango huu, ni mtu kushikamana na adhkari
katika maeneo na miamala tofauti kama vile wakati
wa kuamka, kulala, kutoka nyumbani, kurudi
nyumbani, kuingia chooni, wakati wa kutembea
barabarani, kuvaa nguo na kuvua, pamoja na nyakati
zote ambazo zimefundishwa adhkari za wakati huo.
Kwani kwa kudumu na adhkari hizi, mtu hujihakikishia
anaishi na kutembea na ulinzi wa Allah (Subhanahu)
na kwa idhini yake, uchawi wala sihri haitamkumba
(kwa idhini ya Allah).

104
Ndugu yangu msomaji, jambo la pili na la msingi
katika nukta hizi, ni kutafuta tabibu ama msomi wa
ruqya ambaye anatambulika kuwa ni mwenye elimu
juu ya tiba za kisharia. Tabibu ambae hatomuingiza
katika ushirikina na kutahamaki badala ya kutafuta
radhi na rehema za Allah (Subhanahu), anaingia
katika hasira na maangamivu Yake. Ni sharti la msingi
kumuendea mtu sahihi ambae hafanyi wala
kujumuisha ushirikina ndani ya tiba zake. Kwamaana
wapo wengi katika matabibu ambao wanajinasibu
kufanya tiba hizi, lakini kwa hakika wapo mbali kabisa
na sharia zilizowekwa.
Wanazuoni wa tiba za kisharia, wamebainisha alama
kumi za kuweza kumjua na kumtambua tabibu
mchawi na ambae hujumuisha ushirikina ndani ya tiba
zake. Wakazibainisha kwa lengo la kuisaidia jamii
kuweza kuwaendea watu sahihi pale wanaposibiwa na
sihri ama uchawi. Mtu anapokwenda kwa tabibu wa
visomo ama dua, achunge na kubaini alama hizi,
endapo atabaini yoyote kati ya hizi ambazo
tutazibainisha basi atambue kuwa huyo ni tabibu
mchawi na dhalimu.
Alama kumi za kumtambua tabibu mchawi
(Mshirikina) na muongo:
i. Anapokwenda mgonjwa kwa tabibu wa visomo
na kukuta anakuliza jina lako pamoja na jina la

105
mama - tambua huyo tabibu ana
chembechembe za shirki ndani ya tiba zake.
ii. Anapokwenda mgonjwa kwa tabibu na
kumtaka kuleta athari ya kitu chochote kutoka
kwake kama vile nywele, nguo, mtandio ama
kitu chengine chochote – tambua huyo tabibu
ana chembechembe za shirki ndani ya tiba
zake.
iii. Anapo omba tabibu kutoka kwa mgonjwa wake
mnyama mwenye sifa maalum kwa ajili ya
kumchinja wakati tiba – tambua huyo tabibu ni
mshirikina.
iv. Anapo ambiwa mgonjwa na kupewa sharti la
kujitenga na watu kwa muda fulani na wala
asikae sehemu ambayo atapata jua. Tambua
huyo ni tabibu mshirikina.
v. Anapopewa sharti la kuacha kuoga ama
kushika maji kwa muda fulani – tambua huyo
tabibu ni mshirikina.
vi. Anapo pewa mgonjwa na tabibu wake
makaratasi ambayo yameandika kwa wino wa
rangi nyekundi maandishi yasio eleweka wala
kusomeka na kumuamuru kuenda kuyachoma
ama kujifukiza nayo – tambua huyo ni tabibu
mchawi.
vii. Anapo pewa mgonjwa na tabibu wake vitu
fulani kama ni chupa ama vifurushi na
kumuaru kuvizika pahala fulani kama vile chini

106
ya mlango, baharini, chumbani ama sehemu
yoyote ile– tambua huyo ni tabibu mchawi.
viii. Anapo omba huyo tabibu kutoka kwa mgonjwa
wake kumpa kiganja chake cha kulia ama
kushoto ili atazame – tambua huyo ni tabibu
mchawi.
ix. Anapo omba kutoka kwa mgonjwa picha yake
ama tarehe ya kuzaliwa – tambua huyo ni
tabibu mchawi
x. Anapo kuandikia vitu au kumsikia anasoma vitu
ambavyo havieleweki ni lugha gani wala ni
maneno gani – tambua huyo ni tabibu mchawi
na muongo.
Alama hizi zinaenda sambamba na sharti tatu za
msingi amabazo wanazuoni wamezibainsha, kama
ambavyo Shaykh Al-Fawzan (Allah amhifadhi)
amezifafanua na kuzibainisha. Imam Al-Fawzan (Allah
amhifadhi) alieleza kwa ufasaha juu ya masharti
makuu ya kuzingatia katika kuitambua Ruqya
(Dua/Kisomo) cha Kisharia. Aidha akaeleza masharti
hayo kuwa ni kama yafuatayo;
Ruqya iwe inatokana na Kitabu cha Allah (Subhanahu)
(Qur‟an) na Sunna za Mtume wake (Swalla Allahu
alaiyh wa Sallam) na dawa zinazoruhusiwa, au dawa
zinazoafikiana na zile zilizowekwa. Kisomo hicho
kisiwe ndani yake na dawa za kishirikina au dawa za

107
kizushi, isipokua iwe dawa zenye kunufaisha,
zilizotakasika na ushirikina.
Aidha, akaeleza kuwa, sharti la pili ni kuwa msomaji
(wa Ruqya) awe ni katika watu wa Tawhid,
wanachuoni na watu wenye Aqida iliyo salama. Mtu
asiende kwa waganga, mashetani na wachawi
akaomba Ruqya kutoka kwao, hata kama watu
wanawataja watu hawa na kuwaelekeza watu kwao,
wasiwaendee. Kwani watu hawa ni makuhani,
wachawi, na ni washirika wa mashetani. Au huenda
pia ni wajinga wasiojua haki kutokana na batili, wao
wanachotaka ni mali tu na wala hawaulizi kuwa ni
haki wala batili. Watu hawa mara nyingi
wanawaamrisha wanaowaendea kuchinja kwa ajili ya
asie kuwa Allah, kisha ndio wanawafanyia mahitajio
yao. Na hilo ni ushirikina mkubwa unaomtoa mtu
katika Uislamu.
Kadhalika, sharti la tatu, akaeleza pia kuwa Ruqya
anayoisoma msomaji iwe kwa maneno ya kiarabu
yanayofahamika. Ruqya isiwe kwa matamshi ya kigeni
au matamshi yasiyotambulika maana yake. Sababu
kuu huenda yakawa ni majina ya mashetani na
majini, anawaomba huyu mchawi badala ya Allah
(Subhanahu). Wakati huo msomewaji hafahamu
lugha yake na wala hajui akisemacho. Watu hawa
husema maneno wasiyoyafahamu waliohudhuria pale

108
wala mgonjwa. Hakika watu hawa wametoka kwenye
sharti hili na haijuzu (haifai) kwenda kwao.
Ama baada ya kuhakikisha kuwa umempata tabibu
ambae ni sahihi na ameepukana na mambo hayo
kumi tuliyoyaabainisha na amechunga masharti ya
Ruqya ya kisharia. Wanazuoni wa tiba za kisharia
wakaweka misingi mitatu ya kuizingatia baada ya
hapo. Wakasema kuwa; kuna kanuni na taratibu za
kuchunga kabla ya tiba kuanza, kanuni za kuchunga
wakati tiba inaendelea na kanuni za kuchunga baada
ya tiba kukamilika na poza kupatikana. Hizi ni hatua
tatu muhimu ambazo wote, tabibu na mgonjwa
inawapasa kuzihifadhi, kwani ndio misingi
inayotofautisha kati ya tiba za kisharia na tiba za
kishirikina.
i. Kanuni za kuchunga kabla ya tiba kuanza
Ni wajibu wa mtu anaetafuta poza ya maradhi ya sihri
ama maradhi mengine ambayo yanatibiwa na ruqya
ya kisharia, kuepuka kuamini na kutakidi kuwa poza
ama ponya la maradhi yanayomsibu itatokana na
tabibu huyo pasi na Allah (Subhanahu). Bali
anapaswa kuamini kuwa poza, tiba na kinga
zinatokana na Allah (Subhanahu). Kama Allah
(Subhanahu) alivyosema ndani ya Qur‟an:

ِ ‫ت فَػ ُهو يَ ْش ِف‬


﴾ٛٓ﴿‫ني‬ ْ ‫َوإِ َذا َم ِر‬
َ ُ‫ض‬

109
“Na ninapo ugua ni Yeye ndiye anae niponesha.”
(26:80)
Aidha, katika kanuni hii, mtu ahakikishe kabla ya
kutafuta poza la sihri ama uchawi, awe amejiweka
mbali na maovu yote; ya matendo na meneno. Na
katika mazingira yote. Kwani haiwezekani kupata
poza kutoka kwa Allah (Subhanahu) huku ukiwa
umedumu kwenye maasi na kuacha ibada. Pia
itampasa mtu kueleza kwa tabibu wake, baadhi ya
hali ambazo anakumbana nazo ama zinamtokea,
katika nyakati tofauti kama vile akiwa amelala ama
nyakati nyengine.
ii. Kanuni za kuchunga wakati tiba inaendelea
Wakati tiba ikiwa inaendelea, ni lazima tabibu
kuchunga na kuzingatia kutumia kisomo ama dua
ambazo zimethibiti ndani sharia. Kisomo ambacho
ndani yake hakitakua na chembechembe za
ushirikina; kama matumizi ya hirizi wala ramli. Kisomo
ambacho hakitakuwa na matumizi ya mayai, nazi,
vyungu, na vyengine ambavyo havikuthibiti ndani ya
sharia ya Uislamu katika mlango wa ruqya na
kuombeana, kwani hakuna mahusiano yoyote katika
dua inayoombwa kwa Allah na vitu hivyo.
Aidha, mtu atambue kuwa wakati kisomo
kinaendelea, kuna baadhi ya mambo yanaweza
kujitokeza, kama vile ile sihri ama jinni kudhihiri

110
katika mwili wa mgonjwa ama kuendelea bila
kudhihiri kwake. Nukta hii tumeibanisha kwa sababu,
baadhi ya watu hukosa Imani na tiba husika kutokana
na kuona kuwa kisomo kinaendelea na hakuna kitu
chochote ambacho kimetokea kwa mgonjwa ama
athari zozote. Hivyo inaweza kumtoa mtu katika
uvumilivu na kuamua kurudi katika tiba za kishirkina
ambazo zimegubikwa na uongo na hadaa nyingi.
Hivyo, mtu atambue na achunge kanuni ya kwanza,
na atakidi kuwa mwenye kuleta poza ya maradhi ni
Allah (Subhanahu). Kadhalika, itambulike kuwa
shetani miongoni mwa tabia zake ni uadui, uongo na
kueneza ubaya, hivyo pale anapodhihiri katika mwili
wa mgonjwa ni muhimu kuchunga juu ya kuamini
maneno yake. Kwani lengo lao mara nyingi ni kuleta
chuki na kuzalisha uhasama baina ya watu. Kwani
Allah (Subhanahu) amesema ndani ya Qur‟an:

‫َح َس ُن إِ َّن ٱلشَّْيطَا َن يَ َنزغُ بػَْيػنَػ ُه ْم إِ َّن ٱلشَّْيطَا َن َكا َن‬ ِ ِ ِ


ْ ‫َوقُل لّْعبَادى يػَ ُوولُواْ ٱلََِّّت ى َى أ‬
﴾ٖ٘﴿ً‫ان َع ُدواً ُّمبِينا‬ ِ ‫لِ ِإلنْس‬
ّ َ
“Waambie waja wangu waseme maneno mazuri,
maana shetani huchochea ugomvi baina yao. Hakika
shetani ni adui alie dhahiri kwa mwanadamu.”
(17:53)

111
iii. Kanuni za kuzingatia baada ya tiba
kukamilika na poza kupatika kwa idhini ya
Allah (Subhanahu)
Baada ya Allah (Subhanahu) kuleta rehema zake, na
poza kupatikana, mtu anapaswa kuhakikisha
anashikamana na kudumu kusoma sana Qur‟an,
haswa kudumu kusoma Surat Baqarah (kama
tulivyoeleza dalili juu ya hili). Mtu atapaswa
kuhakikisha anadumu na kumtaja Allah (Subhanahu)
kwa wingi sambamba na kudumu kufanya adhkari za
kila wakati kama ambavyo zimefundishwa. Pia
ahakikishe anadumu katika kutekeleza yale yote
ambayo kila wakati yatamueka karibu na Allah
(Subhanahu). Kadhalika, jambo la msingi baada ya
poza kupatikana mtu atapaswa kuhakikisha
anasimamisha sala tano kwa jamaa, pale ambapo
inawezekana. Pia anapaswa kuhakikisha anakuwa
mstari wa mbele katika kujiepusha na mambo yote
maovu yanayo kinzana na maamrisho ya Allah
(Subhanahu).

HITIMISHO:
Allah (Subhanahu) amefafanuwa kwa uwazi juu ya
makatazo na uzito wa ushirikina ndani ya Qur‟an
Tukufu na kwa yakini ghadhabu za Allah kwa kiumbe
ambaye anamshirikisha ni kubwa sana. Nasi kwa
upande wetu tumefafanua kwa kadiri ambavyo Allah
ametuwezesha kukusanya anuani ya Chapisho hili.

112
Hivyo, kwa hatua hii, jamii inapaswa kutambua ubaya
wa ushirikina, uwe wa kuabudu kiumbe ama kitu
chengine ama ya kumshirikisha Allah kwa uchawi.
Jamii inapaswa kuacha na kujiweka mbali na misingi
mengine isiyo halali katika dua, biashara, ndoa,
pamoja na miamala yote ambayo imewekewa
utaratibu wa ushirikina ndani yake. Kwani, hakika ni
dhulma kubwa kwa haki ya Allah. Tunapaswa kuamini
kadari za Allah kwamba kheri na shari zote zinatoka
kwake na kwa hakika yeye ndiye anazipangia ukomo
wake na haiwezi kumpata mtu ubaya wowote ispokua
Allah ameandika umfike na wala hakuna kiumbe
yoyote anae weza kukunufaisha isipokua kwa rehema
za Allah. Tutambue kuwa, milango ya Allah ipo wazi
kwa yoyote anaekusudia kurudi kwake na kuacha
maovu ya ushirikina na maovu mengine, pia
tutambue tiba na suluhisho la misukosuko yote ya
miamala ya maisha yanayo miongozo ndani ya
Uislamu mbali na ushirikina. Hivyo hatuna haja ya
kukata tamaa juu ya Rehema za Allah. Kwa kauli ya
Allah;

‫َسَرفُواْ َعلَ ٰى أَن ُف ِس ِه ْم الَ تَػ ْونَطُواْ ِمن َّر ْْحَِة ٱللَّ ِو إِ َّن ٱللَّوَ يػَ ْغ ِفُر‬
ْ ‫ين أ‬
ِ َّ ‫قُل يٰعِب ِاد‬
َ ‫ى ٱلذ‬ َ َ ْ
﴾ٖ٘﴿‫ٱلرِحيم‬ ِ ِ ُ‫ٱلذن‬
ُ َّ ‫ور‬ َ ُّ
ُ ‫وب ََجيعاً إنَّوُ ُى َو ٱلْغَ ُف‬
“Sema: Enyi waja wangu mlio jidhulumu nafsi zenu!
Msikate tamaa na Rehema za Allah. Hakika Allah

113
husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwenye
kusamehe, Mwenye kurehemu.” (39:53)
Kwa kauli hii ya Allah, anawaita viumbe wote ambao
wamekata tamaa kutokana na maovu yote ikiwemo
ya kumshirikisha, basi warudi kwake kwa tawba ya
kweli na kutoa ahadi ya kutokurudia makosa yao
kabla ya hayajawafikia mauti. Hakika Allah
(Subhanahu) ni msamehevu na mwenye huruma kwa
waja wake. Tumuombe na tumgemee, sambamba na
kujiweka mbali na ushirikina kwa kila aina zake na
sura zake. Tuelimishane na kukumbushana juu
uharamu na ukubwa wa dhambi ya ushirikina,
tupeane nasaha huku tukishauriana katika kutumia
njia salama za kujikwamua kutoka katika dhiki za
maradhi na misukosuko. Tuelekezane na kusimuliana
matatibu wa kisharia na tuwapuuze na kuwakataa
wote wanaojinasibisha na visomo vya Ruqya huku
wakiwafanyisha watu ushirikina. Tukishikamana na
haya yote na mengine mengi katika mafunzo juu ya
utambuzi wa ushirikina, kwa idhini ya Allah
(Subhanahu) Huenda Tukaongoka.
Alhamdulillah
Wabillah Tawfiq

114

You might also like