You are on page 1of 5

SEMINA YA KUJIFUNZA LITURGIA YA IBADA YA SIKU YA

BWANA
1. MAANDALIZI; Maandalizi ya ibada yafanyike wiki nzima kuanzia jumapili jioni hadi jumamosi, ili
kubaini matukio muhimu mapema kama vile matengenezo na siku ya watakatifu n.k,
 Ili kuweza kuimba litrugia vizuri bila kigugumizi, na kuandaa nyimbo mapema kufuatana
na majira na matukio husika katika kalenda; inashauriwa kuwa ni vema nyimbo za
jumapili ijayo itangazwe kwa wakristo na makundi ya kwaya ili wafanyie mazoezi pamoja
na wakristo ili kuondoa kigugumizi ndani ya ibada kwa kulinda uchaji wa ibada.
2. ALAMA ZA MADHABAUNI YAANI LITURGIA YA IBADA; Kariri alama za madhabauni mapema na
utofautishe alama ya kugeukia madhabauni na alama za kugeukia usharika,
-mkono wa kugeukia madhabahu ni mkono wa kushoto(bayshani) na mkono wa kugeukia
usharika ni mkono wa kulia (dakw do /ayma)
 Hii inaonesha kuwa huna kitu unataka kutoka kwa MUNGU na unapeleka matatizo ya
wakristo kwa MUNGU
 Na mkono wa kulia (dakw do /ayma) hii inaonesha unaleta majibu ya mahitaji yetu
kutoka kwa MUNGU.
3. MAELEZO; Alama ni kwaajili ya mchungaji au kiongozi wa ibada kuonesha kuwa wakati
huo ageukie madhabahuni, akilenga msalaba wa madhabahu bila kupinda pinda
 Alama ni kuonesha kuwa wakati huo ageukie usharika na mgongo wake
uelekee msalaba bila kupinda pinda
4. MADHABAHU; Madhabahu iandaliwe mapema na wahudumu wa kanisa walioko zamu
wahakikishe kila kilichopo madhabahuni ni sahihi na ipo kwenye majira yake
 NB; Kama wahudumu wa kanisa wamekosekana wazee waandae madhabahu vizuri.
 NB; Kama wote hawapo mwenyekiti wa idara ya wanawake au katibu wa mtaa ata
andaa madhabahu isipokuwa siyo watu wa kudumu.
5. MAOMBI YA OFISINI KABLA YA IBADA KUANZA; Wafuatao wafanye maombi pamoja wakiwa
ofisini wote wawepo,ikiwa mtu mmoja amekosekana wakati wa maombi hayo akaingia ibadani
wakati ni muhusika na yupo zamu, hairuhusiwi kutumika siku hiyo.
I. Kiongozi wa ibada akiwa tayari amevaa vazi la ibada.
II. Mhubiri wa ibada akiwa tayari amevaa vazi la ibada.
III. Wazee wa zamu wakiwa tayari wamevaa vazi la ibada.
IV. Wahudumu wa zamu wakiwa tayari wamevaa vazi la huduma.
V. Mchungaji kama yupo akiwa amevaa vazi la ibada.
VI. Msomaji wa somo la 1.
6. KUZINGATIA NAMBA WAKATI WA KUINGIA IBADANI; Mtiririko huu ufuatwe wakati wa kuingia
ibadani.
I. Wahudumu watangulie mbele wakati wa kuingia ibadani.
II. Wazee watafuata baada ya wahudumu.
III. Msomaji wa somo la kwanza.
IV. Kiongozi wa ibada na muhubiri watafuata,watakuwa wa mwisho pamoja na mchungaji
kama yupo
7. KUINGIA MLANGO WA KANISA; Wazee, wahudumu, msomaji, kiongozi wa ibada na muhubiri
wataingia na wimbo wakati huo wakristo wote wawe wameingia ndani na wote wasimame.
8. KABLA YA KUPANDA MADHABAHUNI; Wahudumu wa zamu wakifika ngazi ya kwanza ya
madhabahu wasogee hatua moja pembeni,moja kulia na mwingine kushoto,
 Wazee wa zamu wakifika ngazi ya kwanza ya madhabahu wote pamoja na wahudumu
watasogea pembeni hatua moja kila mmoja na msomaji.
 Kiongozi na mhubiri watasimama katikati na kiongozi wa ibada akielekea msalaba wa
madhabahuni wote wainame pamoja na wakristo mara moja tu.
9. KUPANDA MADHABAHUNI; Kiongozi wa ibada atatangulia na mhubiri atafuata, wakati kiongozi
wa ibada akiwa madhabahuni na mhubiri,kiongozi wa ibada atasimama katikati akielekea
msalaba wa madhabahuni bila kupinda pinda kisha watasali sala ya kimya au kwa sauti ya chini,
NB; Angalia Tumwabudu MUNGU wetu ukurasa wa 249 maandishi mekundu.
 Kama waliopanda madhabahuni ni watatu, wawili watasimama pembe ya madhabahu
na wasimame wakielekeana kisha kiongozi wa ibada ataanza ibada.
10. WAHUDUMU,WAZEE MSOMAJI; kiongozi wa ibada na muhubiri wakipiga magoti au kusimama
madhabahuni, wahudumu,wazee na msomaji watumie fursa hiyo kutawanyika kabla kiongozi
hajageukia usharika
 Watatawanyika kwa utaratibu huu; mzee mmoja na mhudumu mmoja watasimama
nyuma ya wakristo kwa safu ya wakristo.
 Mzee mmoja na mhudumu mmoja watasimama mbele ya wakristo kwa safu ya
wakristo.
 Walioko mbele watalinda usalama wa madhabahu na isipite dakika mbili bila kuaangalia
madhabahuni;wajue ishara ya kuita.
 Kama kuna jambo la kuwakilisha madhabahuni, wazee au mzee na mhudumu walioko
mbele ni kazi yao, watumie eneo la pembeni kunong’onezana.
 Mzee na mhudumu waliokaa nyuma ya wakristo watatatua matatizo ya wakristo,
(hairuhusiwi mkristo kupanda madhabahuni wakati ibada inaendelea ,matatizo yao ya
tatuliwe na wazee na wahudumu) hasa yale yasiyo subiri baada ya ibada.
11. IBADA; Kiongozi wa ibada ageukia usharika na aseme ‘’
wapenda katika bwana tuanze ibada ya siku ya bwana katika jina la baba nala mwana nala roho
mtakatifu na asiangalie kitabu aangalie usharika na wote waseme amen’’
 Kiongozi wa ibada afuate muongozo wa litrugia bila kupayuka payuka au kukosea.
 Msaada wetu ni katika jina la bwana isomwe siyo kuimba.
12. UNGAMO LA DHAMBI; Wakati wa maungamo ya dhambi usharika watasimama au kupiga
magoti.
 kiongozi wa ibada lazima apige magoti mbele ya madhabahu akielekea msalaba.
 Tutakiane amani ya bwana kwa kupungiana mikono ili kumfikia kila mmoja.
13. MSOMAJI WA SOMO LA KWANZA; Msomaji wa somo la kwanza atasoma somo la kwanza tu na
afunge kwa kusema ‘’hili ndilo neno la mungu’’ na wakristo wote waitike ‘’Tumshukuru mungu’’.
14. UKIRI WA IMANI; Kiongozi wa ibada wakati wa ukiri wa imani atangaze namba ya ukiri-Imani ya
mitume au imani ya nikea na kiongozi ageukie usharika bila kufunga macho wakitazamana
macho kwa macho.
15. MATANGAZO; kiongozi wa ibada atangaze mbele ya madhabahu mgongo wake uelekee msalaba
na kusema ‘karibu mzee wa kanisa kwa kutoa matangazo ya kanisa na hii iwe ni desturi ya
kiongozi wa ibada kusimama mbele ya msalaba wa madhabahuni,akitaka kutangaza wimbo au
kukaribisha kwaya.
 Matangazo mengine yasiyohusika madhabuhuni yatangazwe kwenye mimbara ya
matangazo.
16. MZEE WA ZAMU AU MHUDUMU; Kabla ya kupanda madhabahuni atainama kuelekea
madhabahuni, akimaliza kutoa matangazo ataelekea madhabahuni na kuinama tena kwa kuaga
mdhabahu.
 Mzee au mhudumu anapotaka kutoa matangazo atangulize kuwakaribisha usharika
kusikia matangazo ili wawe tayari na makini kusikiliza matangazo,utulivu uwepo.
 Hairuhusiwi kwa mzee au mhudumu kutoa matangazo ya kanisa bila vazi la ibada au
kanzu.
 Haipendezi kwa mzee au mhudumu kuwa mgeni wa matangazo au kusoma matangazo
kwa wasiwasi .
17. MAHUBIRI; Mambo muhimu katika kuandaa mahubiri ni kama yafuatayo;
 Mhubiri ni lazima akubali kuwa mwanafunzi wa biblia ili awe na ujuzi dhabiti wa kitabu
chochote cha biblia.
 Mhubiri ajihoji kwanza kuhusiana na somo la mahubiri na kujituliza katika maombi
Ezekieli 2:8:3:3, Ufunuo 10:8-11
 Muhubiri aandae mahubiri yake kuanzia jumapili hadi jumamosi hakikisha usikurupukie
mahubiri.
 Sala za kutosha zifanyike kwani madhabahu inavita usipokuwa makini unapigwa.
 Fikiria kuhusu wasikilizaji wako kwani kila mmoja ana hitaji lake na upana wa uelewa wa
mtu ni lazima mhubiri afundishe jambo linaloeleweka kwa wasikilizaji wake.
 Panua uwanja wa somo lako la mahubiri na kufahamu mipaka ya somo lako na utumie
mifano inayoeleweka kwa wasikilizaji wako.
 Andika mahubiri yako katika daftari kwa kuzingatia alama ya furaha au huzuni wakati wa
kuhubiri.

MUHUBIRI AZINGATIE YAFUATAYO

a) Hubiri habari za kweli naya uhakika kutoka neno la mungu au kwakushuhudia.


b) Muhubiri atambue kuwa wasikilizaji wake wana haja na kiu ya kusikiliza mambo mapya
na uponyaji kwa mioyo iliyo jeruhika.
c) Hakikisha kuwa watu wote wanasikia lugha yako na kuielewa barabara.
d) Muhubiri afuate hatua zinazotakiwa kwa mahubiri yake bila kupayuka payuka au
kwenda mbele na kurudi nyuma.
e) Namna ya kufuata mtiririko ni mfano;
I. Utangulizi; Inaweza kuwa ni wimbo,au ushuhuda na kichwa cha kalenda.
II. Mahubiri yenyewe; Chukua mambo muhimu sana yatakayo wasaidia
watu/wasikilizaji.
III. Hitimisho; ni mambo machache ya kukazia.
 Maombi yafanyike pale unapoongozwa na roho mtakatifu wa mungu na uwe na
uhakika kuwa ni roho mtakatifu wa mungu siyo matakwa yako.
18. MATOLEO YA SADAKA; Mambo yafuatayo ni lazima yazingatiwe wakati wa kutoa sadaka.
I. Wazee watatoa maelekezo ya namna ya kutoa sadaka ili wakristo wasigongane.
II. Wakristo wanapotoa sadaka waelekee madhabahu na wasizungukie chombo cha
sadaka.
III. Wazee watangulie na wahudumu kutoa sadaka.
IV. Wazee/wahudumu watasimama nyuma ya chombo cha sadaka ili kuelekeza na
kupokea sadaka za wakristo (hairuhusiwi mkristo kuweka sadaka yake chini badala
yake wazee wapokee na kuweka kwenye ngazi ya kwanza ya madhabahu ) huku
mzee mmoja wa zamu akiendelea kulinda sadaka za wakristo.
V. Viongozi wa ibada wataaga madhabahu na kwenda kutoa sadaka zao kwa kuandika
vi(V)yenye nukta katikati watazunguka upande wa kushoto (dakw do bayshani)
watatoa sadaka kwa kuelekea madhabahuni na watarudi kwa mkono wa kulia (dakw
do /ayma) kisha watainama nakuja madhabahuni.
VI. Kabla sadaka haijaombewa mimbara ya sadaka isogezwe isionekane tena, kisha
wazee na wahudumu warudi kwenye nafasi zao.
VII. Kiongozi wa ibada atapiga magoti wakati wakuombea sadaka.
19. SHUKRANI; Wazee na wahudumu watasimama mbele ya wakristo wakati huo chombo cha
sadaka iandaliwe madhabahuni kwenye ngazi ya kwanza au mwisho.
 Wakiwa madhabahuni watasogea hatua moja pembeni ilikuruhusu viongozi wa ibada
kusimama katikati.
 Kisha wakristo watakao toa shukrani watakuja mbele na watasimama kwenye ngazi
namba moja.
 Wakristo watainua sadaka zao na maombezi yatafanyika,kisha wakristo watatoa sadaka
zao na wazee na wahudumu watapokea mikononi mwao.
 Wakristo waliotoa sadaka yao ya shukrani watapewa Baraka na kiongozi wa ibada au
kiongozi mkuu
20. BARAKA ZA MUNGU; Wakati wa kutoa Baraka ni lazima itifaki izingatiwe kama ifuatavyo
I. Kama kiongozi wa ibada ni mkristo na mhubiri ni mzee wa kanisa, kiongozi wa ibada
atampa nafasi mzee wa kanisa kutamka Baraka za mungu.
II. Kama kiongozi wa ibada ni mhudumu wa kanisa na mhubiri ni mzee wa kanisa kiongozi
wa ibada atampa nafasi mzee wa kanisa kutamka Baraka za mungu.
III. Kama kiongozi wa ibada ni mzee wa kanisa na mhubiri ni mwinjilisti, mzee ampe nafasi
mwinjilisti.
IV. Mtoa Baraka ni mungu,hivyo kiongozi anapotamka maneno ya Baraka awageukie
washarika na kuwa tazama barabara bila kuangalia kitabu ajiamini.
V. Wakati wa kupokea Baraka za mungu wakristo wote wainamishe vichwa vyao kama
ishara ya unyenyekevu.
VI. Kiongozi afunge ibada kwa sala ya shukrani .
21. KUTOKA; Kiongozi wa ibada na mhubiri wataaga madhabahu kwa kuinamisha vichwa vyao na
kisha watashuka madhabahuni na kuungana na wazee na wahudumu kwenye ngazi ya kwanza
watainama pamoja na wakristo kisha kiongozi wa ibada atangulie na wengine wafuate.
 Wote washiriki neema ya bwana pale nje.
22. SALA YA SHUKRANI; Wote waliohudumu madhabahuni waombe sala ya shukrani kwa pamoja
wakiwa ofisini.
 Baada ya sala kiongozi wa ibada na mhubiri watavua vazi la ibada.
 Wazee na wahudumu hawatavua vazi la huduma yao badala yake watahamisha chombo
cha sadaka kwaajili ya kuhesabu sadaka na wahudumu watazima mshumaa na mambo
yakusogeza yakiwepo, kisha watavua vazi la huduma.

MASWALI
1. Je wakati wa kusali ni lazima kufunga macho? Jadili.
2. Kuabudisha kabla ya mahubiri(kuabudu) inaleta faida gani? Na je ni lazima?
3. Je ni lazima matangazo ya kanisa isubirishwe baada ya ibada au kabla ya mahubiri? Jadili.

You might also like