Professional Documents
Culture Documents
Uhalisia Wa Kijamaa
Uhalisia Wa Kijamaa
Hii ni mbinu ya utunzi na uhakiki inayomzingatia binadamu kama uti wa mgongo wa kuwepo
kwa ulimwengu na maana ya ulimwengu ule, hii ni dhana ya njogu na wafula (2007). Kwa
ujumla tunaweza sema kwamba uhalisia wa kijamaa ni nadharia ya uhakiki ianyozingatia
maendeleo ya jamii na maendeleo ya kitabaka ,vilevile nadharia hii huonyesha jinsi uhusiano
kati ya tabaka la mabwenyenye na wachochole huleta mgongano unaosababisha kutokea kwa
mapinduzi . mapinduzi haya huwa ni juhudi na mikakati za wanajamii kupambana na
ukandamizaji wa kilimwengu.
Mihimili yake
Husawiri matukio kihistoria ,hutekeleza matendo ya kitabaka. Hufanya hivi kimakusudi au bila
fahamu ,la mno kwao ni kwamba tabaka la wanyonge linajiimarisha ili kujipa mamlaka na nguvu
za kiuchumi ,kwa mfano hata kama Amani na Imani wanateseka kwa muda mrefu katika utawala
wa kidikteta wa Mtemi Nasaba pamoja na wanasokomoko wengi wanajifunga kibwebwe
kukabiliana na hali hiyo na mwishowe wanakuwa washindi.
Huonyesha matumaini ya kupatikana kwa ushindi baada ya dhiki kuu ya kupigania ukombozi.
Huonyesha kuwa ambaye anakandamizwa yaani mchochole mwishowe huishia kuwa ndiye
mshindi kwenye vita vya ukombozi. Katika tamthilia ya kilio cha haki kundi ambalo
linaongozwa na akina Lanina Musa Na Dewe ndilo linaloshida na katika mwisho wa tamthilia
tunadokezwa vile kaburu Delamon pamoja na wasaliti na vibarakala wake kama Tekeri,Shindo
Na Matovu wanavyouawa.Katika tamthilia ya mstahiki Meya vilevile tunamwona mstahiki meya
pamoja na wanyonyaji wenzake wanavyoshindwa na kundi la wachochole ambalo lilikuwa
limeongozwa na daktari Ziki.
Nadharia ya uhalisia wa kijamaa huelezea hadithi kikweli. Nadharia hiii hueleezea changamoto
zinazomkumba mwanadamu katika harakati zake za maisha. Nadharia hii huonyesha vile
wanajamii huusiana na wenzao ,kwa mfano katika tamthilia ya mstahiki Meya tunaelewa kuwa
katka jamii yetu ama nchi yetu, viongozi wengi wamejitumbukiza kwa siasa chafu za
kuwadhulumu wananchi waliowachagau. Mstahki meya ni mhusika ambaye amewekwa pale
kuonyesha vile viongozi wa nchi za kiafrika ni wafisadi na uwa wanatumia mamlaka yao
kuijinyakulia mali yasiyo halali ,vilevile katika riwaya ya kichwamaji inaonyesha vile jamii zetu
ama nchi zetu zinavyokandamizwa na viongozi wabaya wa serikali kwa mfano tunamwona
Manase akitumia mamlaka yake vibaya kupeana kazi katika afisi yake ya mkuu wa wilaya.