You are on page 1of 16

www.annuurpapers.co.

tz

Sauti ya Waislamu

ISSN 0856 - 3861 Na. 1153 SAFAR 1436, IJUMAA ,

NOV. 28-DES. 4, 2014

Dhulma ilishashtadi

Ya Escrow ni tabia
BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Sheikh Ponda ashinda


kesi Mahakama Kuu

Uk. 2

SHEIKH Ponda Issa Ponda.

Vigogo wa Mamlaka
kamili waunguruma
BAADHI ya Waislamu wakiwa nje ya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam wakiendelea na dua wakati kesi ya Sheikh
Ponda Issa Ponda ikiendelea kuunguruma ndani ya Mahakama hiyo Novemba 26, 2014.

'Ndio itaangamiza lengo la Mapinduzi


Wahoji ile sababu ya kumtoa mkoloni
Hakuna maendeleo kwa mfumo uliopo

Wanasiasa, magazeti
wanapandikiza ugaidi
Wabaya kuliko watuhumiwa ugaidi Uk. 8
Tujifunze kutoka Kenya na ATPU yao
Kama tukifuata nyayo, tumeangamia

MZEE Salum Rashid, Katibu


wa kwanza wa Baraza la
Mapinduzi. Uk. 3

Tahariri/Habari

2
AN-NUUR

S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786


Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.
www.annuurpapers.co.tz
E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top
Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Dhulma ilishashtadi

Ya Escrow ni tabia

KATIKA maadili ya Kiislamu,


ni mwiko mtu kudhulumu
au hadhulumiwa.
Ni marufuku kumdhulumu
mtu kwa kigezo chochote kile,
hata kama unatofautiana
naye katika imani. Wala mtu
asikubali kudhulumiwa na
yeyote awaye.
Hii ni kwa sababu
d h u l m a k wa a i n a z a k e
zote imeharamishwa na
kukaripiwa vikali kabisa
ndani ya Qurani tukufu na
suna ya Mtume (Hadithi)
Msidhulumu wala
msidhulumiwe. [2:279].
Na atakayedhulumu
miongoni mwenu, tutamuonjesha
adhabu kubwa. [25:19].
Na Allah hawapendi
madhalimu. [3:57]
Na Allah amesema tena
katika hadithi Quds,
Enyi waja wangu, hakika
Mimi nimejiharamishia
d h u l m a n a n i m e i f a n ya
(dhulma) kuwa ni yenye
kuharamishwa baina yenu,
basi msidhulumiane.
(Muslim).
Hiyo ni baadhi ya mifano
tu katika Quran Tukufu na
Hadith za Mtume Muhammad
(s.a.w), ambayo kwa pamoja
ndio muongozo sahihi katika
maisha ya Muislamu na
binadamu wote kwa ujumla.
Hapa unaonekana utukufu
wa hali ya juu wa Uislamu,
dini ya haki, uadilifu na
usawa. Hakika hii ni dini
ambayo inayochukia dhulma
na madhalimu na inaamrisha
uadilifu, kufanya hisani na
inakataza uchafu na uovu na
dhulma.
Kama mwanadamu
angekubali kutii na kukua
katika maadili ya dini, maadili
kama haya yanayokataza
kikamilifu dhulma miongoni
m wa wa n a d a m u k a t i k a
maisha yake yote duniani,
basi ni wazi haki ingeshtadi
katika jamii na yeyote
anayedhulumu angetahayari.
Tunaweza tukaielezea na
kuianisha dhuluma kuwa
ni kile kitendo cha mtu au
kikundi cha watu kuchupa
mipaka ya Allah (sw) na
kuitumia au kuikalia haki
ya mtu au watu wengine bila
uhalali.
Na mara nyingi dhulma
h u f a n y i wa m n y o n g e a u
dhaifu asiyeweza kujinusuru
nayo. Dhulma hutokana na
kiza kilichoko moyoni mwa
mtu, na kiza hiki ndicho
kinachomzuia kuiona haki
n a k u h e s h i m u h a k i ya
mwenziwe. Akachukua kitu
kisichokuwa chake, iwe cha
mtu binafsi, cha serikali
(jamii), bila ya kuona vibaya.
Ukosefu wa mwongozo
na imani ya dini ni jambo
jingine linalofanya dhulma
iongezeke. Wanaodhulumu
hufanya hivyo kwa kibri na
jeuri yao ya kimamlaka waliyo

nayo juu ya watu wengine.


Katika hali kama hii,
lau moyo wa dhalimu
ungelikuwa na nuru, basi
angeweza kuzingatia haki ya
wengine na kuziheshimu na
asingelikuwa na ujasiri wa
kumdhulumu yeyote.
Zipo dhulma za aina tatu.
Kuna dhulma hupatikana
kwa mja kumkufuru
Mwenyezi Mungu Mtukufu
na kumshirikisha. Dhuluma
ya mja kwa nafsi yake na
kuna dhuluma ya mtu kwa
wenziwe au kwa viumbe
v i n g i n e v ya M w e n y e z i
Mungu.
Aina hii ya tatu ya dhuluma
hasa ndio tunayokusudia
kuielezea hapa, ambayo
hupatikana pale mtu
atakapowafanyia maudhi
wenziwe kwa kuwavunjia
heshima au kuchukua mali
zao. Iwe ni kwa nguvu alizo
nazo, kwa ukwasi alio nao,
kwa cheo alicho nacho, kwa
elimu aliyo nayo au kwa roho
yake mbaya tu ya kibinafsi na
choyo.
Dhulmati huyu anaweza
kufanya dhulma hata kwa
kuwadhuru watu katika miili
au hisia zao, kwa kutwaa mali
zao pasi na uhalali au haki.
Haya ndio matatizo
ya l i y o t u s i b u h i v i s a s a ,
ambapo watu waliopewa
dhamana na Watanzania,
watachukua mabilioni ya
fedha isipo haki ambapo
pesa hizo zingetumika kwa
kununulia madawa na kutoa
huduma nyingine za kijamii.
Kwenye huduma kama ya
umeme, wananchi wanajikuta
wakilipa gharama kubwa,
kumbe katika gharama hizo,
wamejumlishiwa pia na zile
fedha za wizi na zinazotumika
kifisadi badala ya kuboresha
huduma na kupunguza
gharama za uendeshaji. Ndio
haya tunayosikia ya akaunti
ya Tegeta Escrow.
Tu k u m b u s h e k u wa
dhuluma hizi hazikuanza
leo. Ni tabia ya muda mrefu
kwa watendaji wa serikali
na wenye mamlaka, ambao
n a f s i z a o z i n a o n g o z wa
na tamaa, choyo, ubinafsi
uliopindukia kiasi kwamba
sasa kudhulumu imekuwa
jambo la mazoea na tabia.
Watanzania wanakumbuka
vyema sakata la ununuzi wa
ndege ya Rais katika awamu
ya Rais Benjamin Mkapa na
lile la rada na vijisenti vya
chenji yake.
Katika Awamu hii ya
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
muendelezo wa dhulma
kubwa uliendela ambapo
masalia ya walafi walikuja
na mpango mwingine wa
kudhulumu kupitia akauti
ya madeni ya Nje (EPA).
Katika kashfa hii, dhulma
kubwa ilifanywa na
wateule wachache dhidi ya

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 2014

Watanzania, kufuatia wateule


hao kutumia mamlaka yao
kuiba fedha nyingi, zaidi ya
bilioni mia moja katika akauti
hiyo.
Haukupita muda, dhulmati
wengine wakakwapua
mabilioni ya fedha kupitia
mikataba mibovu na ya wizi
katika kashfa ya Richmond.
H a t u j a k a a s a wa , h i v i
karibuni tu, watu wakatumia
m wa n ya wa o p e r e s h e n i
ya Ta i f a ya k u p a m b a n a
na ujangili, kudhulumu
kwa kukwapua mifugo ya
wafugaji, kukwapua fedha
z a o k u p i t i a r u s h wa z a
kulazimisha nk. Wengine
waliokaidi kudhulumiwa
wakaishia kupoteza mifugo
yao na baadhi yao kuteswa
barabara.
Tuseme tu kwamba, haya
yamekuwa mazoeya, kwamba
sasa dhulma ni jambo la
kawaida kwa baadhi ya
wanasiasa na viongozi wetu.

We n g i h a w a a m i n i k i
na wamejaa tamaa za fisi.
Wanapata madaraka kupitia
migongo ya Watanzania,
halafu wanatumia nafasi
tulizowapa kudhulumu ili
kukidhi tamaa zao huku
wakiwaumiza Watanzania
zaidi ya milioni 46.
Pamoja na jitihada za Bunge
kujaribu kuwabana, badi
tatizo halionekani kwisha
kwa kuwa wanaodhulumu
walishakosa mioyo ya
imani katika dini, (hawana
m w o n g o z o wa k i d i n i ) ,
wameonja tamu ya dhulma
na wameshazoea.
Katika mioyo yao, hakuna
huruma wala maadili.
Zaidi wanaonyesha wapo
kinadharia zaidi kuliko
vitendo.
Hata hivyo awali tuliona
dawa sahihi iliyoonekana
kuwa mwarobaini wa dhulma
inayofanywa na viongozi

na wenye mamlaka dhidi


ya wananchi, ilikuwa ni
rasimu ya katiba iliyokuwa
imependekezwa na Tume ya
Jaji Joseph Warioba.
Kwa sababu Rasimu ya
Warioba ilikuwa ni rasimu
iliyowapa wananchi mamlaka
zaidi ya kuwasimamia na
kuwawajibisha viongozi wao.
Hata hivyo walengwa
walitambua hilo na
kuivunjavunja na kuondoa
kabisa ile azma ya rasimu ya
kuwawajibisha dhulmati.

Na Bakari Mwakangwale

wa n a z u o n i wa n a o e l e wa
masuala ya Uislamu, bali
wa n a a m i n i z a i d i m a d a
zitolewazo katika mitandao,
na fatwa anayoikuta huko
ndio unakuwa msimamo
wake.
Akasema Mwalimu Filambi
kuwa hilo ni tatizo kubwa
linaloweza kuwaangamiza
Waislamu.
Filambi alisema, Waislamu
wanapaswa kuzama zaidi
katika mafunzo ya Uislamu
kutoka kwa wanazuoni wenye
taaluma ya masuala ya dini na
si kwa tafsiri ya juu juu tu
kisha wakachukua maamuzi
na kuanza kuyafanyia kazi.
F i l a m b i , a l i s e m a k wa
kawaida watengeneza agenda
au mada za kuwagonganisha
Waislamu, huwa wanaangalia
palipo na mwanya wa
kuwagonganisha Waislamu
na hutumia njia hiyo kwa
kujinasibisha na Uislamu kwa
lengo la kuwavuruga.
Akinukuu maelezo ya
Profesa Hamza Njozi, katika
Bunge la Katiba, alisema
kwa haya yanayoendelea
nchini huivi sasa hadhani
kama Tanzania inaweza kuwa
salama, kwa sababu agenda
zinawekwa na mabwana
wakubwa hivyo Uislamu
unakuwa ni njia tu kama
daraja la kuwafikisha katika
ajenda zao.
Kwa sababu, alisema baada
ya vita na Warusi, mabwana
wakubwa hao walitangaza
wazi kuwa, vita iliyobaki ni
dhidi ya Uislamu kwa sababu
ndio dini pekee inayoweza
kuwa kikwazo katika malengo
yao.
Akitoa maoni yake
kutokana na hali ilivyo sasa
hususani kwa Waislamu
Abdallah Waziri, alisema
Uislamu ni dini ya kiutu
zaidi kwani umefundisha
kuishi na mtu hata asiyekuwa
Muislamu.
A l i s e m a , Wa i s l a m u
wanapaswa kufahamu na
kujifunza kutoka kwa Mtume
Muhammad (s a w), kwani

aliweza kuishi na Mayahudi,


Washirikina pamoja na hila
zao za ukandamizaji dhidi ya
Waislamu na Uislamu.
Mfumo wa Kiislamu
sio fikra za mtu binafsi
bali kuna mfumo rasmi
ambao Mwenyezi Mungu
ameushusha ambao
unapatikana katika Qur an,
na si vinginevyo. Hivyo
linapokuja suala kuhusu
Uislamu ni lazima litolewe
fatwa na wanazuoni si
kila mmoja anaweza kutoa
msimamo, jambo ambalo
linaweza kuwaingiza
Waislamu katika matatizo
makubwa. Alisema Ust.
Waziri.
Akasema, ukiangalia
suala zima la Jihadi, kuwa
linatafsirika zaidi katika Sira,
kwamba katika matukio
yaliyogusa Waislamu na
Uislamu Mtume (s a w)
alifanya nini, na inapolazimu
kwenda kupigana Mtumie,
alitumia vigezo, adabu na
Sharia zipi.
Alitolea mfano sakata la
kundi la Boko Haram la nchini
Nigeria, linalosadikiwa kuwa
lipo katika Jihadi, akasema
katika Uislamu hakuna Jihadi
ya kuwateka wanawake
(mabinti) na kuuwa watu
hovyo kama magaidi na
maharamia.
Katika uhai wake, AlMaruhum, Mwalimu Jafari
Siraji, aliwahi kuwataka
Wa i s l a m u k u wa m a k i n i
sambamba na kuchukunguza
m we n e n d o wa m a t u k i o
yanayoshajihishwa na
Waislamu au Uislamu, kisha
kurejea katika sira na Fiqh,
kwamba Mtume (s a w)
aliyaendea vipi masuala ya
Jihadi.
Katika makongamano
yake mbalimbali Mwalimu
Siraji, alikuwa akieleza kuwa
kilichopo hivi sasa ni mitego
iliyotengenezwa na makafiri
kisha kuiingiza kwa Waislamu
wakilenga kuwashawishi na
kuwaingiza katika mapigano
ya wenyewe kwa wenyewe.

Bila ya kuwa na katiba


inayowawajibisha wenye
mamlaka na viongozi,
hatudhani kama Bunge
letu la sasa pamoja na
kuonyesha jitihada zake

za kudhibiti walafi hawa,


watafanikiwa kuondoa
mazoea yaliyokwishajengeka
kwa watendaji wakubwa
serikalini kuwadhulumu
wananchi.

Njama za makafiri kuangamiza


Waislamu kupitia jihad bandia
WA I S L A M U n c h i n i
wameaswa kuwa makini na
propaganda ya dhana ya
Jihadi kwani ni mipango
maalum ya Mataifa ya Ulaya
inayowalenga Waislamu
katika kutekeleza vita dhidi
ya Uislamu.
Tahadhari hiyo imetolewa
na Muhadhiri wa Chuo Kikuu
Cha Waislamu Morogoro,
Mwalimu Suleiman Filambi,
akizungumza katika kipindi
cha Mwangaza wa Jamii
kinachorushwa na Radio
Imaan, ya Mjini Morogoro.
Filambi amesema, jamii
ya Wa i s l a m u h i v i s a s a
inapaswa kuiangalia dhana
ya Jihadi kwa umakini zaidi
kuliko kukurupuka jambo
ambalo linaweza kuwaingiza
Wa i s l a m u k a t i k a m t e g o
uliokusudiwa na watunga
sera dhidi ya Uislamu na
Waislamu.
Tatizo lililopo hivi sasa ni
kwamba, jamii inayolengwa
ambayo ni ya Waislamu,
wengi wao hawafahamu
kuwa wanalengwa na hizi
propaganda zinazoendelea
za uwepo wa Jihadi katika
Mataifa ya Afrika. Alisema
Mwl. Filambi.
Alisema, kuibuka kwa
mitandao ya kijamii hivi
sasa, imekuwa ni tatizo kwa
Waislamu wengi hususani
kwa vijana kwani wamekuwa
wakiipa kipaumbele
wanadhani kuwa kwa kusoma
madai fulani kupitia mitandao
hiyo ndio inatosheleza kupata
ufumbuzi wa masuala na
matatizo ya Waislamu.
Matokeo yake Waislamu
wenyewe kwa wenyewe
wameingia katika mgongano
wa kimtazamo, wapo
ambao wanatafsiriwa kuwa
hawataki Jihadi na wengine
wa n a o n e k a n a wa n a t a k a
Jihadi, sasa wananyoosheana
vidole. Alisema Mwl.
Filambi.
Alisema, hivi sasa Waislamu
wamewaweka kando

Habari

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 2014

Vigogo wa Mamlaka kamili waunguruma


Na Salma Alghaithiyyah.

IMEELEZWA kuwa kura ya Ndio


kwa katiba inayopendekezwa
itaviza malengo yote ya mapinduzi
na kuleta maangamizi Zanzibar
kama nchi.
Aidha, Zanzibar isitarajiwe kuwa
na maendeleo ya kiuchumi, kama
hali itabaki kama ilivyo Wazanzibari
wakiwa wametiwa kwapani na
serikali ya muungano, ambayo
inatajwa kuwa ndiyo ya Tanganyika
iliyojivika koti la Tanzania katika
muungano wa serikali mbili.
Hayo ni katika hoja zilizotolewa
katika kongamano lililofanyika
mapema wiki hii katika Hoteli ya
Bwawani ambapo ilielezwa kuwa
imekuwa bahati mbaya kwamba
Zanzibar imekosa mtetezi hivi sasa
kwa vile Rais amekuwa akisimamia
zaidi masilahi ya CCM.
Ikiwa Rais atalichukulia hili
kichama na sio ki-nchi na ikafika
kupigwa kura ya maoni, wafahamu
kwamba sote tupo katika jahazi moja
pengine viongozi wao kwa maslahi
yao binafsi, wanahisi wawe hewallah
bwana kwa lolote wanaloambiwa
Dodoma. Ndugu zangu wanachama
wa CCM, nawaheshimu sana na
n a h e s h i m u m s i m a m o wa o n a
kuchagua chama wanachotaka,
lakini nawasihi katika hili watafanya
makosa makubwa kama watasema
Ndio.
Mzee Rashid anasema akishangaa
kuwa watu walokwenda mbio kutaka
Muingereza awaachie nchi yao hadi
wakaachiwa kukafanyika Mapinduzi,
lakini hali hiyo imebadilika kwa kuwa
Zanzibar hivi sasa haina mamlaka
yoyote kinyume na dhamira yake ya
Mapinduzi na watu hawalioni hilo.
Mzee Salum Rashid ambaye
alikuwa Katibu wa kwanza wa
Baraza la Mapinduzi, alisema
Wazanzibari wengi hawaridhishwi
na mambo yanavyokwenda na kutaka
kurejeshwa mamlaka ya Zanzibar na
sio wananchi tu bali hata viongozi
wakiwemo Baraza la Mapinduzi na
kuna nyaraka mbali mbali ambazo
zinaitaka Tanganyika kurejesha
mambo mbali mbali Zanzibar.
Zanzibar iwe nchi huru,
tuligombania uhuru na tunagombania
mamlaka hivi sasa, sio kwa sababu ya
ukorofi, lakini tunafanya hivyo kwa
sababu ya kurejesha hali ya uchumi
wa Zanzibar, tunataka kurejesha hali
ya vijana wetu kuwainua katika ajira
na kuifanya nchi vizuri, kurejesha
mfumo wa elimu, kurejesha afya bora
na mambo mengine ambayo sasa
hayapo kutokana na hali ya uchumi,
alisema.
Zanzibar bila ya mamlaka kamili
na bila ya sera mbadala haiwezi
kusonga mbele na kama Zanzibar
inataka kuendelea, basi ifuate mfano
wa Mauritius na isifate mfano
wa Tanganyika, alisema huku
akishangiriwa kwa makofi.
Katibu huyo wa zamani wa Baraza
la Mapinduzi, amesema, mchakato
wa katiba umeifanya Zanzibar isiwe
na msemaji wake katika kipindi hiki
muhimu cha historia ya visiwa hivi.
Akizungumza katika kongamano
hilo la kitaifa lililoandaliwa na
Kamati ya watu sita ya kusimamia
Maridhiano ya kisiasa lililofanyika
Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani,

aliwanasihi Wazanzibari kuinusuru


nchi yao katika kipindi hiki cha
kutafuta katiba.
Mimi nilifikiria wakati huu wa
mchakato, Rais wa muungano ambaye
anawakilisha Tanganyika na Rais wa
Zanzibar watafanya mazungumzo
kwa kila khatua ambayo wote ni
viongozi wakubwa wa chama cha
CCM, watafanya mazungumzo
ili kutupatia katiba na mamlaka
kamili kama tulivyokusudia, lakini
wamefanya mazungumzo kama
viongozi wa CCM, sasa jee huu
utaratibu ni mwafaka? Jee, hii katiba
ya nchi au ni katiba ya chama?
Alihoji.
Alisema ukitizama zile tunu za taifa
ni sera za Chama Cha Mapinduzi, na
sio za taifa ambapo, Rashid aliwaonya
Wazanzibari kabla ya kufanya
maamuzi ya kupiga kura ya Ndio
itakayoitosa nchi yao, wanapaswa
kufahamu kwamba hizi ni nchi mbili,
Tanganyika na Zanzibar zilizoungana
miaka 50 iliyopita.
Zanzibar mwaka 1963 Muingereza
alipokata shauri ya kutupa uhuru
wetu, vyama vyote viwili tulitakiwa
watu saba tukaandika katiba ya uhuru
wa 1963, lakini Zanzibar hawaitaki,
eti ilikuwa imetaja Sultan kwa nini
haibadilishwi badala ya Sultani
tukaweka Rais katiba hiyo iliandikwa
na Afro Shirazi na Hizbu, ilitoa haki
za binaadamu kwa kila raia, uteuzi
kila miaka mitatu baada ya mapinduzi
ikatubidi sisi tusimamishe katiba kwa
kuwa hatukuweza kuitekeleza maana
serikali ya kimapinduzi haiwezi
kutekeleza katiba.
Alisema kwa wakati ule khatima
ya Zanzibar haikuweza kuamuliwa
na chama kimoja, lakini khatima
ya Zanzibar ilikuwa iamuliwe na
vyama vyote na Wazanzibari wote
na ndio maana Wazanzibari wote

waliheshimika na kuamua jambo la


nchi yao.
Alisema, Zanzibar inapaswa
kutetea mamlaka yake na kukataa
kuamuliwa na Dodoma kwa kuwa
Zanzibar ina mamlaka yake na
haihitajiki kuamuliwa jambo lake
Uingereza wala Dodoma.
Mamlaka ya Zanzibar ni muhimu
na wala sio u-CUF Mzanzibari kuitetea
nchi yake, alisisitiza Katibu huyo wa
zamani wa Baraza la Mapinduzi.
Alisema katiba ni jambo muhimu
sana na sio jambo la kuchezea, sio la
maskhara au la mzaha.
Rashid anasema anashangaa kuwa
watu walokwenda mbio kutaka
Muingereza awaachie nchi yao hadi
wakaachiwa kukafanyika Mapinduzi,
lakini hali hiyo imebadilika kwa kuwa
Zanzibar hivi sasa haina mamlaka
yoyote kinyume na dhamira yake ya
Mapinduzi.
Katibu huyo wa zamani alisema
Wazanzibari wengi hawaridhishwi
na mambo yanavyokwenda na kutaka
kurejeshwa mamlaka ya Zanzibar na
sio wananchi tu bali hata viongozi
wakiwemo Baraza la Mapinduzi na
kuna nyaraka mbali mbali ambazo
zinaitaka Tanganyika kurejesha
mambo mbali mbali Zanzibar.
Kwa upande wake Bwana
Mohammed Mugheiry (Eddy Riamy)
ametuma salamu zake kwa Rais
wa Zanzibar ambapo alisema Dk.
Shein anavurugiwa nafasi yake
na hao wapambe wake ambao
wanafanya kampeni chini kwa chini
kumuangusha ambapo huenda Mkoa
wa Kaskazini na kupachua bendera
za Uamsho lengo ni kumchafulia Rais
Dk. Shein ili aonekane uongozi wake
una matatizo.
Wanaokwenda kushusha bendera
ili watu waichukie serikali yako
ndio wabaya, lakini wewe umeshika

kuitukana Kamati ya Maridhiano


kila ukipanda jukwaani na wale
wanaokwenda kuandika Maskani
Kisonge kuwa Wapemba wahame
na waondoke, ndio hao hao watu
wako ambao wanakwambia wewe
mwenyewe uhame, alisema Eddy
Riamy.
Mimi nikitiwa ndani, mwengine
anyanyuke aseme hatufai tusikubali,
lakini hatukubali katiba yetu ya
Zanzibar iharibiwe na tutakwambia
hatufai kwa sababu gani wamekwenda
Dodoma kutaka katiba yetu ya
Zanzibar ifutwe? Alisema na kuhoji.
Aidha Eddy alisema CCM
Zanzibar wanapanda katika
majukwaa na kuwatukana Waarabu
tu, lakini wanasahau kwamba
akina (Mheshimiwa Wziri Mkuu)
Pinda, (Waziri Wiliam (Lukuvi)
na (Mheshimiwa Spika wa Bunge)
Anna Makinda, wanakwenda Oman
huko huko kwa Waarabu huku akina
Shamhuna wakibaki kazi yao kubeba
mikoba.
Akizungumza katika Kongamano
hilo, Masoor Yussuf Himid, alisema
lazima Wazanzibari waache woga
n a k u k a t a a k u wa c h o n g a n i s h a
Wazanzibari kwani Maridhiano
ni kheri na Mwenyeenzi Mungu
amehimiza umoja na mshikamano.

Na Seif Msengakamba

amekubaliana nasi kwamba


ushahidi ambao ulitolewa katika
mahakama ya Kisutu, umebainika
kwamba hapakuwa na ushahidi
wowote unaoweza kuthibitisha
shitaka ambalo ametiwa hatiani,
la kuingia katika eneo lililokuwa
na migogoro kule Markaz
C h a n g o m b e k wa k u t u m i a
nguvu. Alisema Wakili Nassor
jana mahakamani hapo.
Kwa msingi huo, Mahakama
Kuu iliridhika kwamba kwa
ushahidi uliokuwa umetolewa,
haukuonyesha kuwa kulikuwa
matumizi ya nguvu.
Hukumu ya Jaji Shangwa
ilikwenda mbele zaidi na kuona
kwamba Sheikh Ponda, pamoja
na Waislamu ambao walikuwa
wamefika Markazi Changombe,
walitumia njia mbalimbali za
kidiplomasia kwa maana ya
kuongea na huyo ambaye ndiye
aliyenunua eneo hilo, pamoja
na kuchukua namba ya simu ya
shahidi namba tano Bw. Othmani
kwa ajili ya kufanya mazungumzo.
Alisema, mazungumzo
yalifanyika katika Msikiti wa
Mtambani kwa hali ya utulivu
mpaka pale polisi walipokuja

kuwakamata wale Waislamu kule


Changombe.
Sababu nyingine iliyokuwa
hoja ya msingi ya kufuta hukumu
ya Sheikh Ponda iliyotolewa na
Mahakama ya Kisutu, ni kwamba
kesi ile ilikuwa inahusu mgogoro
wa ardhi na haikustahili kuwa kesi
ya kijinai.
Wakili wa utetezi Juma Nassoro,
alisema kimsingi jeshi la Polisi
lilipaswa kumshauri mlalamikaji
aende katika mahakama ya
ardhi ili akathibitishe uhalali wa
eneo lake, na kama kuna mtu
alikuwa anapaswa kushtakiwa,
basi alipaswa kushitakiwa katika
mahakama ya ardhi kwa maana
ya kesi ya madai.
Aidha, ilionekana kuwa
Mahakama ya Kisutu
haikujielekeza katika kuweka
mizani sawa kwa washtakiwa
wote, yaani fare trial.
Ilionekana kuwa kutokana na
ushahidi uliokuwepo, hapakuwa
na sababu yeyote ya kuwaachia
washitakiwa arobaini na tisa
kwa ushahidi ule ule uliotumika
kuwaachia washitakiwa wengine,
Inaendelea Uk. 4

Kuna watu wazito lakini


wanaogopa kuzungumza kwa kuwa
wapo katika nyadhifa za serikali,
ukiwaambia wanasema wakati
haujafika, lakini tunawaambia wakati
ni huu wa kusema na tusisubiri kufa,
alisisitiza Mansoor.
Mansoor amesema wanaoimba
Mapinduzi Daima, bila ya kuyafanyia
kazi kwa kuleta uhuru na maendeleo,
hao ni wanafiki kwa sababu lengo
la mapinduzi ni uhuru na kuleta
mamlaka ya Zanzibar.

Sheikh Ponda ashinda kesi Mahakama Kuu


MAHAKAMA KUU ya Tanzania
imefuta hukumu iliyokuwa
imetolewa awali na Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini
Dar es Salaam Mei mwaka jana
dhidi ya Sheikh Ponda Issa
Ponda, ambayo ilimtia hatiani na
kumhukumu kifungo cha nje na
watuhumiwa wenzake wengine
49 wakiachwa huru.
Uchambuzi wa hoja
zilizowasilishwa, umeifanya
Mahakama Kuu kufuta hukumu
iliyokuwa imetolewa na
Mahakama ya Kisutu na kwa
sasa Sheikh Ponda yuko huru,
hana hatia yeyote kwa mashtaka
ambayo ameshtakiwa.
Hukumu hiyo iliyotolewa
kufuatia rufaa iliyowasilishwa
mahakamani hapo na wakili wa
upande wa utetezi Juma Nassor.
Mahakama ilitoa sababu
takriban sita za kupinga hukumu
iliyomtia hatiani Sheikh Ponda
katika Mahakama ya Kisutu.
K wa b a h a t i n z u r i r u f a a
hiyo imekubalika, hoja zetu
zimeonekana ni za msingi, Jaji

Makala
Na Salum Bendera

KATIKA nchi kama Jamhuri ya


Kenya uhuru wa kuabudu ni jambo
ambalo limekuwa likiheshimiwa
na ndio maana ukienda katika nchi
hiyo utakuta kuna dini mbalimbali.
Wananchi wa dini mbalimbali
wamekuwa wakiishi kwa amani kwa
miaka nenda rudi na hatujasikia
vita vya kidini katika nchi hiyo.
Mfano wa wazi ni kupata makanisa
hata katika miji ambayo kimsingi
ni ya Waislamu kama Mombasa.
Uhuru wa kuabudu umepelekea
kuweko utitiri wa makanisa na hata
makanisa sasa yameondoka katika
mkondo wa nyumba za ibada na
kuwa miliki za watu. Kwa maana
kwamba, makanisa sasa nchini
Kenya ni sehemu ya vitega uchumi
vya wahubiri. Nyote bila shaka
mmesikia mkasa wa hivi karibuni
wa utapeli katika kanisa moja huko
Kenya. Kali zaidi ni ule mkasa
wa Embakasi, Nairobi ambapo
mhubiri alimnunua dada mmoja na
kumuahidi kumlipa kitita kizuri cha
pesa. Alichotakiwa kufanya dada
huyo ni kuja akiwa amepindisha
mdomo ambapo mhubiri baada ya
kufanya maombi na mikogo ya hapa
na pale, dada hunyoosha mdomo
wake na mhubiri hupayuka kwa
nguvu HALELUYA, KWA JINA LA
YESU, AMEPONA.
Tabani kesi kama hizo ziko
pia nchini Tanzania, Uganda na
kwingineko Afrika Mashariki, ingawa
kwa Kenya masuala ya kutapeliwa
waumini makanisani yamekithiri.
Nimedokeza hayo ili kutoa taashira
ya jinsi Wakristo walivyokuwa na
uhuru wa kufanya mambo yao pasi
na kubughudhiwa kinyume kabisa
na Waislamu.
Tukio la kufungwa misikiti minne
ya Mussa, Sakina, Swafaa na Minaa
huko Mombasa Kenya hivi karibuni
na polisi ya nchi hiyo kutoruhusu
waumini kutekeleza ibada zao
za kila siku katika misikiti hiyo,
ni habari ambayo ilimgusa kila
Mwislamu mwenye dhamira safi.
Sababu inayotolewa na vyombo vya
usalama vya Kenya ya kuhalalisha
hatua hiyo ya kufunga misikiti katika
Kaunti ya Mombasa ni kwamba,
hatua hiyo imechukuliwa katika
mlolongo wa vita dhidi ya ugaidi
na sababu za Kiuslama. Kwa mujibu
wa polisi, misikiti hiyo imekuwa
ikitumiwa kueneza misimamo mikali
ya kidini na vitendo vya ugaidi.
Taarifa ya polisi imedai kwamba,
imepata silaha pia katika misikiti
hiyo. Waislamu wa Kenya na hata
wa nchi nyingine ambao wanapinga
kufungwa misikiti hiyo wanasema
kuwa, kufungwa kwa misikiti
hiyo kunaweza kuchochea hisia za
chuki na kuwafanya vijana kuwa na
siasa kali. Aidha wanasema hizo ni
harakati zisizokubalika na zinaweza
kuongeza hali hiyo kwa kuwaudhi
vijana zaidi na kushadidisha hisia
miongoni mwao kwamba, serikali
iko dhidi yao, hivyo kuwafanya kuwa
na siasa kali zaidi. Wenye mtazamo
huo wanahoji kwamba, kama misikiti
hiyo ina kamati zake zinazoongozwa
na viongozi ambao mipango yao
ni kuingiza ajenda za siasa kali
na kuwaandikisha vijana kwa ajili
ya kuwapeleka Somalia kujiunga
na kundi la al-Shabab, kwa nini
serikali isingeingilia kati kuhakikisha
kamati hizo zinabadilishwa badala ya
kufunga misikiti hiyo? Je hatua hiyo
sio kinyume kabisa na uhuru? Kwa
nini waumini wengine wa Kiislamu

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 2014

Kufungwa Misikiti Kenya

Mlolongo wa njama dhidi ya Waislamu


Sawa Wazayuni kule Baytul Muqaddas

MOJA ya Misikiti iliyofungwa nchini Kenya hivi karibuni.


wanyimwe haki ya kwenda kufanya Septemba 11.
Mwenyekiti wa Baraza Kuu
ibada katika misikiti hiyo kwa sababu
la Waislamu nchini SUPKEM,
ya makosa ya watu wachache?
Bila shaka uamuzi wa busara Profesa Abdul-Ghafur Al-Busaidy
ungeweza kutumika nao ni serikali akizungumzia sakata la kufungwa
kusaidia kamati hizi kutwaa tena misikiti hiyo alisema, ingekuwa
udhibiti wa misikiti hii kuliko jambo la busara kama serikali ingeketi
kwenye meza ya mazungumzo
kuifunga.
Swali ambalo limekuwa likiulizwa na viongozi wa kaunti na wa
na wengi ni kwamba, kufunga kidini nchini Kenya ili kulitafutia
misikiti hiyo kunamaliza ugaidi au ufumbuzi jinamizi la ugaidi na
kutashadidisha? Je walioshambulia vijana kushawishiwa kujiunga na
bari la abiria Mandera na kuua watu makundi yenye misimamo mikali,
28 wasio na hatia walikuwa waumini
wa misikiti ya Mussa, Sakina, Swafaa
au Minaa?
Jambo jingine linalolalamikiwa
na Waislamu wa Mombasa na wa Inatoka Uk. 3
Kenya kwa ujumla katika kadhia ukamtia hatiani mshitakiwa
nzima ya kufungwa misikiti minne Sheikh Ponda.
ya Mussa, Sakina, Minaa na Swafaa
Pia kulikuwa na hoja kwamba
ni jinsi polisi wanavyovamia misikiti ushahidi wa kielelezo ambacho
hiyo na kuingia na viatu katika kilidaiwa kuwa Sheikh Ponda
nyumba hizo za ibada. Kitendo cha alikiri makosa, ulikuwa sio
polisi hao kuingia na mabuti yao na ushahidi wa kweli na hakuna
kuivunjia heshima misikiti hiyo hata kielelezo ambacho Sheikh Ponda
kama ni kwenda kukamata magaidi, alipokiri makosa kwa mashitaka
a m b a y o a l i s h i t a k i wa k u wa
hakikubaliki hata kidogo. Msikiti ni aliingia kwa nguvu huko Markaz
nyumba tukufu ya ibada na polisi Changombe.
wanapoingia katika maeneo hayo
H i v y o , i l i o n e k a n a k u wa
hata kama wanakwenda kumkamata Mahakama ya Kisutu ilikosea
gaidi aliyejificha humo wanapaswa kusema kwamba Sheikh Ponda
kuheshimu nyumba hizo za ibada na alikiri makosa.
Kwa ujumla Jaji alizichukua
kuacha kujeruhi hisia za Waislamu.
Hatua hiyo ya polisi ya Kenya haina sababu zote hizo na nyingine
tofauti na hujuma na vitendo vya na kuziweka katika hoja moja
kuyavunjia heshima matukufu ya kwamba je, kulikuwa na ushahidi
Kiislamu zinazofanywa na askari wa kutosha wa kumtia hatiani
wa utawala wa Kizayuni kila siku Sheikh Ponda kwa mashitaka
huko Baytul Muqaddas. Jeshi la
Israel huvamia msikiti mataktifu a m b a y o a l i y o s h i t a k i wa n a
wa al-Aqswa kibla cha kwanza kuhumiwa?
Mwisho ndipo Jaji alichambua
cha Waislamu huko Palestina na
ushahidi
na ikathibitika kwamba
kuingia na viatu, jambo ambalo
limekuwa likilalamikiwa kila kona ushahidi ule haukutosha na
haikupaswa kumtia hatiani na
ulimwenguni.
Ni kutokana na ukweli huo hatia ile imefutwa na rasmi.Katika
ndio maana Waislamu kote Afrika kushrehesha hukumu hiyo, Jaji
Mashariki wanalitathmini suala la Shangwa alimwelezea Sheikh
kufungwa misikiti minne ya Mombasa Ponda kuwa yeye ni zaidi ya
kwamba, ni katika mlolongo ule Sheikh, kwani ni yake ya kutetea
ule wa kuwaandama Waislamu haki za Waislamu ni sahihi.
Jaji Shangwa alisema
lakini katika kivuli cha kisingio cha
anavyofahamu,
ni kweli katika
kupambana na ugaidi. Vita ambavyo
jiwe lake la msingi liliwekwa na Uislamu mali ya Wakfu haiuzwi.
Marekani baada ya mashambulio ya Alifafanua kuwa anavyofahamu

badala ya kuvamia maeneo ya ibada


na kuwakamata waumini kiholela.
Matamshi hayo yaliungwa mkono
na Khelef Khalifa Mwenyekiti wa
Shirika la Kiislamu la Kutetea Haki za
Binadamu nchini Kenya (MUHURI),
ambaye alisisitiza kuwa, ugaidi ni
suala la idiolojia ambalo linafaa
kutafutiwa ufumbuzi kwa kutumia
sera za kiaidiolojia.
Hakuna Mwislamu wa kweli
anayeunga mkono kutumiwa maeneo
ya ibada kuendeshea harakati za
kufurutu ada; kwani Uislamu
unapinga suala zima la misimamo
ya kupindukia ambayo imekuwa
ikitumiwa vibaya na watu wenye fikra
finyu na uelewa mbaya kuhusiana
na Uislamu na kadhia nzima ya
jihadi katika Uislamu. Fikra za kuua
watu bila sababu au kwa kuwa sio
Waislamu au kwa sababu hawajui
kutamka shahada mbili na mikasa
mingine kama hiyo inayonukuliwa
kufanywa na baadhi ya makundi ya
kigaidi kama ya al-Shabab Somalia,
Daesh Iraq, Jabhat al-Nusra Syria na
kwingine, ni fikra na mitazamo finyu
na potofu na ambayo haikubaliwi na
mafundisho sahihi ya Uislamu. Hata
hivyo haya yote bado hayalalalishi
vitendo vinavyofanywa na polisi ya
Kenya vya kuvamia misikiti kiholela,
kuivunjia heshima kwa kuingia
na viatu na kuwakamata waumini
kiholela pasi na ya sababu kwa
tuhuma za ugaidi na mengineyo.
Mbona makanisa yanayotapeli
waumini kila leo nchini Kenya
hayafungwi? Kwani sheria sio
msumeno? Au ndio chambilecho
Waswahili, mkuki kwa nguruwe kwa
binadamu mchungu?

Sheikh Ponda ashinda kesi Mahakama Kuu

Mujahidina katika Uislamu, ni

mtu ambaye yuko radhi kuitetea


dini yake, jambo ambalo alisema
kuwa ni sahihi kabisa.
Hivyo alimshauri baada ya
kumaliza suala lake, akafungue
kesi ya madai katika mahakama
ya ardhi kudai haki ya Waislamu
ambayo ni wakfu.
Hata hivyo, bado Sheikh
Ponda ataendelea kukabiliwa
na kesi nyingine dhidi yake
iliyofunguliwa katika mahakama
ya Morogoro.
Imeelezwa kuwa Sheikh Ponda
hawezi kuwa huru kwa sasa
maana ya kutoka mahabusu
baada ya kushinda rufaa yake,
kwasababu kule Morogoro jeshi la
Polisi limemshitaki tena kwa kosa
jingine wakidai kwamba alifanya
uchochezi mjini Morogoro na
vile vile amekiuka mashariti ya
hukumu ya mahakama ya Kisutu.
Wa k i l i w a J u m a N a s s o r
alisema hizo zilikuwa kesi mbili
tofauti, lakini kushinda rufaa ya
Mahakama Kuu ni jambo ambalo
linaathiri kesi ya Morogoro,
k wa k u wa k i m s i n g i t a ya r i
inaonekana shitaka la kukiuka
hukumu ya Mahakama ya Kisutu
halitakuwepo tena.
Wakili huyo alisema kuwa
wataichukua hukumu ya rufaa
yao kutoka Mahakama Kuu na
kuipeleka Morogoro ili kunaiomba
mahakama hiyo, nayo vile vile
kwa mujibu na kadiri sheria
itakavyoruhusu kumwachia huru
mteja wao.

Habari za Kimataifa

Huu ni mzuka wa polisi kuua watoto Marekani


Muuaji hana kesi, vurumai zatawala
Wamuua mwingine wa miaka 12

JOPO lililoteuliwa na mahakama


kutoa maamuzi katika jimbo la
Missouri nchini Marekani juu ya
polisi aliyemuua kijana wa miaka
17 huko Marekani, limeamua
kutomfungulia mashitaka
ofisa huyo wa polisi, ambaye
alimpiga risasi na kumuuwa
kijana mweusi asiyekuwa na
silaha Michael Brown, yapata
miezi minne iliyopita.
B a a d a ya m a a m u z i h a y o
kutangazwa, hali katika mji wa
Ferguson imekuwa tete huku
waandamanaji wakitupia mawe
na chupa magari ya polisi na
mengine kuchomwa moto, huku
Polisi nao wakijibu kwa kutumia
gesi ya kutoa machozi.
Ghasia hizo zilifuatia tangazo
la mwendesha mashitaka wa
kitongoji cha Missouri, Robert
McCulloch, Jumatatu usiku wiki
hii kutangaza kwamba jopo hilo
halikuona sababu yoyote ya
kumfungulia mashitaka polisi
Darren Wilson.
Wilson alikuwa ofisa wa polisi
aliyempiga risasi na kumuuwa
kijana Michael Brown Agosti 9,
2014.
Mauaji hayo yalisababisha
mvutano mkali kati ya wakazi
ambao wengi wao ni jamii ya
watu weusi wa eneo la St. Louis,
ambalo hufanyiwa doria na polisi
ambao wengi wao ni Wazungu.
Baada ya maamuzi kutangazwa
Jumatatu usiku, familia ya
Michael Brown ilisema kwamba
wamesikitika sana.
Mawakili wa Darren Wilson
walisema jopo la majaji
walioteuliwa limekubaliana
kwamba hatua za polisi huyo
zilifuata sheria na taratibu za
polisi.
Wakati machafuko katika
eneo la Ferguson huko Marekani
yakiwa bado hayajapoa kutokana
na afisa huyo wa polisi kumpiga
risasi na kumuua kijana asiye na
silaha, habari nyingine zinasema
Polisi katika jimbo la Cleveland
wamemuua kwa kumpiga risasi
mtoto wa kiume mwenye mri wa
miaka 12 mwishoni mwa wiki
iliyopita.
Tamir Rice, alipigwa risasi
katika viwanja vya michezo vya
Cudell Commons Park Jumamosi,
baada ya kumtaka asalimishe
silaha aliyokuwa akiichezea kwa
kuwatishia watu, Cleveland.com
imeripoti.
Polisi walisema Rice alishika
bunduki yake kiunoni alipotakiwa
ajisalimishe na walidhani alikuwa
akichomoa silaha ya kweli.
Hata hivyo mnyetishaji wa
taarifa za Rice kuwa na silaha na
kutishia watu, alisema silaha hiyo
ilionekana kama si halisi.

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 2014

Moon aunga mkono


kuundwa taifa huru
la Palestina

Polisi kumwona kijana huyo


akipeleka mkono kiunoni kutoa
silaha yake walimpiga risasi
mbili tumboni.
Kwanini wasingemtishia,
Gregory Henderson alihoji katika
mkutano na waandishi wa habari
kufuatia mauaji ya mwanaye.
Alipigwa risasi mara mbili,
sio mara moja na mwishowe
hakuna aliyepiga risasi miguuni,
walimpiga sehemu za juu za
mwili.
Ofisa huyo wa polisi alidai
kuwa, alimpiga risasi kijana
huyo baada ya kuchomoa silaha

yake na kudai kuwa alitishia


kumshambulia, hivyo alifyatua
risasi ili kujilinda.
Hata hivyo watu waliokuwepo
karibu na tukio hilo walisema
kuwa mtoto huyo mdogo, hakuwa
amemtishia kwa njia yoyote ofisa
huyo wa polisi, si kwa maneno na
wala si kwa vitendo.
Kuanzia Agosti 9 mwaka huu,
mji wa Ferguson na miji mingine
ya Marekani imegeuka uwanja
wa maandamano makubwa na
ghasia, raia wakilalamikia ukatili
wa polisi wa nchi hiyo dhidi ya
raia.

KATIBU Mkuu wa Umoja wa


Mataifa ameunga mkono juhudi za
kuundwa nchi huru ya Palestina.
Akihutubia vyombo vya habari,
Ban Ki-moon, amelaani jinai
zilizofanywa na majeshi ya utawala
wa Kizayuni wa Israel katika vita
vya siku 50 katika eneo la Ukanda wa
Gaza na kusisitiza juu ya umuhimu
wa kuungwa mkono kimataifa
kukarabatiwa eneo hilo.
M k u u h u y o wa U m o j a wa
Mataifa amelaani vikali mapigano
yanayoendelea huko Baitul Muqaddas
hasa suala la kuvunjiwa heshima
matukufu ya Waislamu katika eneo
hilo takatifu.
Ameongeza kuwa, ujenzi wa
vitongoji vya walowezi wa Kizayuni
katika ardhi zilizoghusubiwa licha ya
kuwa si wa kisheria, bali unazuia pia
kupatikana amani na utulivu katika
eneo hilo.
Wakati Katibu Mkuu UN akitaka
kuundwa Taifa huru la Wapalestina,
Misri kwa upande wao wanakoleza
kitanzi cha mzingiro kwa Wapalestina
hao.
Hii ni kutokana na kitendo cha Jeshi
la Misri kutangaza kuwa limeharibu
njia za chini kwa chini zaidi ya elfu
moja na mia nane zinazounganisha
eneo la mpaka wa nchi hiyo na
Ukanda wa Ghaza.
Taarifa ya jeshi la Misri imedai
kuwa, hatua hiyo imechukuliwa ili
kuzuia kile kinachodaiwa kuwa ni
kuingia makundi ya wanamgambo
wa kigaidi nchini humo.
Jeshi la Misri linadai kuwa
makundi 13 ya kigaidi yakiwemo
ya Answar Baitul Muqaddas, al
Qaeda na mengineyo yamekuwa na
harakati za kuingiza silaha nchini
humo, kwa lengo la kutoa mafunzo
kwa wanamgambo wa makundi hayo
waliomo ndani ya ardhi ya Misri.
Naye Majidi al Basyuni, Naibu
Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani
wa Misri ameeleza kuwa, maeneo ya
Sinai yamekuwa yakitumiwa na
makundi ya kigaidi yanayofanya
njama za kutaka kujitenga na ardhi
ya Misri.

JAMHURI ya Kiislamu ya Iran


imezindua ndege nyingine isiyo
na rubani (drone) ya kisasa kabisa
iliyotengenezwa nchini humo,
ambayo inaweza kutumika katika
operesheni za upelelezi.
Drone hiyo iliyopewa jina la
Ababil-3 imezinduliwa katika siku
ya nne katika Maonyesho ya saba ya
Kimataifa ya Sekta ya Vyombo vya
Anga nchini humo, katika kisiwa cha
Kish katika ghuba ya Uajemi Kusini
mwa Iran.
Taarifa zinaeleza kuwa Drone
hiyo inaweza kuruka kwa saa nane
mfululizo katika eneo lenye ukubwa
wa kilomita 250 na kupaa kwa umbali
wa futi 15,000 juu angani, huku
ikituma picha katika kituo cha mbali.
Wiki iliyopita, Iran pia ilizindua
drone nyingine inayoshabihiana

na ile ya Marekani iliyolazimishwa


kutua Iran miaka mitatu iliyopita.
Drone hiyo ya Iran inashabihiana
na ile ya Marekani ya RQ-170
isiyoonekana kwenye rada.
Mwezi Septemba, Iran ilionyesha
drone yake nyingine iliyotengenezwa
na wataalam wa ndani wa nchi hiyo
iliyoitwa 'Sadeq 1', katika maonyesho
ya kijeshi katika hifadhi ya mwasisi
wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran,
marehemu Imam Khomeini, huko
kusini mwa Tehran.
Sadeq 1 ina uwezo wa kuruka
umbali wa kwenda juu angani wa
futi 25,000 kwa mwendo kasi sana
(supersonic speeds).
Drone za Iran zimekuwa
zikitengenezwa kwa ajili ya majaribio
ya rada na mifumo ya ki-electronic
na kwa ajili ya kutathmini mafunzo.
Katika siku za hivi karibuni, taifa

hilo limeelezwa kuwa limepiga hatua


kubwa katika maendeleo ya viwanda
vya usafiri wa anga, hasa katika
kubuni na kuunda ndege zisizokuwa
na rubani.
Wakati huo huo Iran leo imezindua
chanjo iliyotengenezwa hapa nchini
katika sherehe iliyohudhuriwa na
Rais Hassan Rouhani.
Chanjo hiyo ya watoto ina uwezo
wa kukinga magonjwa matano
hatari ambayo ni pamoja na Homa
ya H a e m o p h i l u s - B , K i f a d u r o ,
Pepopunda, Hepatitis B na Dondakoo.
Maafisa wa Iran wamesema wana
uwezo wa kuzalisha asilimia 60 ya
chanjo zinazohitajika nchini humo.
Shirika la Afya Duniani WHO,
limeitaja Iran kuwa nchi iliyofanikiwa
zaidi katika eneo la Mashariki ya
Kati katika kuwapa watoto chanjo ya
ugonjwa wa kupooza, Polio. (www.
almanar.com)

Michael Brown (picha ndogo) aliyeuawa na askari wa Marekani


(mwenye picha kubwa).

Iran yazindua drone nyingine

Makala

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 2014

Dk. Bana, ni udini tu au udhaifu wako kitaaluma?

Na Majidi Mussa Kimaro, Arusha

KATIKA ngazi za kitaaluma,


mwanataaluma wa Chuo Kikuu
anayefanya kazi yake ipasavyo
na kwa weledi, anaweza kupanda
kufikia ngazi ya Profesa Mshiriki
(Associate Professor ) katika
kipindi cha miaka 9 tangu
aajiriwe Chuo Kikuu. Aidha,
inamchukua miaka 3 zaidi
kufikia ngazi ya Profesa Kamili
(Full Professor ). Inapotokea
mwanataaluma akajinadi kuwa
kafundisha Chuo Kikuu zaidi
ya miaka 38 na wakati huo
huo akabakia kama Mhadhiri
Mwandamizi (Senior Lecturer),
basi hii ina tafsiri mbili tu,
kwamba mhusika ni dhaifu sana
au mvivu mno.
Ni kweli kwamba kuna fani
ambazo ni vigumu kufanya
utafiti na kuandika machapisho
yanayoweza kumpandisha mtu
kufikia ngazi za uprofesa katika
kipindi kifupi. Tafiti nyingine
huchukua muda mrefu na ni za
gharama mno. Hata hivyo, tafiti
hizi si zile za sayansi ya siasa
(Political Science). Huhitaji fedha
nyingi wala muda mrefu kufanya
utafiti na kuandika machapisho
yanayohusu hali ya siasa nchini.
Inatosha kusikiliza redio na
kuandika paper. Huo ndio ukweli!
Nimelazimika kuanza na
utangulizi huu ili kuweka bayana
upotoshaji unaofanywa na baadhi
ya wanataaluma ambao hujiita
wataalam na wachambuzi wa
siasa, kupitia vyombo mbalimbali
vya habari huku wakijua wazi
kuwa uwezo wao kitaaluma
ni mdogo. Vyuo Vikuu vyote
duniani vinaongozwa na kauli
mbiu ya You either publish or you
perish yaani andika/chapisha
au ufe kitaaluma. Kimsingi,
mwanataaluma ambaye haandiki
au kuchapisha ni mfu kitaaluma.
Kwa bahati mbaya sana, baadhi
ya watu waliokufa kitaaluma
kutokana na kutokuandika
machapisho kwenye majarida ya
kimataifa wameona njia bora ya
kuwalaghai Watanzania kuwa ni
wakali kitaaluma, ni kukimbilia
kwenye vyombo vya habari
na kujifanya wachambuzi wa
masuala ya kisiasa na kijamii.
Jiulize, huo uchambuzi kwa nini
wasiupeleke kwenye majarida
ya kimataifa? Ni wazi kuwa
hawawezi kuthubutu kwa kuwa
wanajua kuwa uchambuzi huo
ni dhaifu, hauna viwango na
hauwezi kukubalika.
Dr Benson Bana ni Mhadhiri
Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam. Mwanataaluma
huyu mzee ni miongoni
mwa watu wanaopenda sana
kuonekana kwenye vyombo vya
habari wakifanya kile wanachodai
wenyewe kuwa ni uchambuzi wa
masuala ya kisiasa na kijamii. Hata

hivyo, mara nyingi uchambuzi wa


mwanataaluma huyu umekuwa
ukikosolewa na watu wengi katika
jamii kutokana na kulalia upande
mmoja au kukosa hoja zenye
mashiko.
Katika mtandao mmoja wa
kijamii, mmoja wa wachangiaji
aliwahi kuandika hivi kumhusu
Dr Bana:
Mtu kama huyu Benson
katika nchi ni hatari sana kuliko
watu wanavyotambua. Huyu
ni mropokaji anayefundishwa
au kujipendekeza ili aendelee
kutimiza malengo yake
ya kipropaganda kama
anavyotumwa na '---'. Report
zake ni za kuegemea mlengo wa
chama kilicho madarakani na siku
zote ametoa report sizizoungwa
mkono na sehemu kubwa ya
jamii yetu, labda wasomi anao
wadanganya kwa ufundishaji
wake. Si mchambuzi mkweli. kwa
umri wake ni janga kwa wasomi
wadogo wanaomtizama. Simply
said benson is a ccm puppet.
Mchangiaji mwingine
akaandika: Jamaa nilimsikiliza na
nikamshangaa mpaka mwanangu
akaniuliza....Baba unafikiri nini?
Ama kweli jamaa ni janga kwa
wanafunzi wake na Taifa letu.
Mwingine naye akaandika hivi:
Kimsingi nimekuwa nikitilia
shaka wakati wote uchambuzi
wa huyu dk. Kumbuka tafiti
zenye kuhusu mvuto wa viongozi,
hata maoni yake juu ya kujivua
gamba kwa RA ni utata mtupu.
Nashukuru kwa taarifa kwamba
mdau ni mwenye mlengo
wa CCM, hivyo nimetambua
ni kwanini uchambuzi wake
unaonekana kubeba upande
mmoja na kuponda mwingine
kiaina. Hatari sana kwa wasomi
kama hawa kutosimamia kweli.
Wakati utawaumbua.
Mwingine akamkejeli Dr Bana:
Uchambuzi wa BANA utadhania
ni uchambuzi uliofanywa na
bibi (nyanya) yangu kule kijijini
ITIMBI.
Dr. Bana ni mwalimu wangu.
Hata hivyo, naomba nikiri kuwa
sikuwahi kumwelewa hata siku
moja katika ufundishaji wake!
Ufundishaji wake zaidi ulikuwa
wa ubabaishaji. Huwezi kumweka
Dr. Bana katika kundi la magwiji
kama kina Profesa Issa Shivji,
Haroub Othman, Mwesiga Baregu
na hata wanafunzi wake kama
kina Dr. Bashiru Ali. Na hii ndio
sababu sishangai kuwa kwa
nini katika kipindi cha miaka 38
anayodai kufundisha Chuo Kikuu
ameshindwa kusogea kutoka
ngazi moja hadi nyingine.
Maoni ya Dr. Bana kufuatia
waraka wa Wizara ya Elimu wa
tarehe 11 Novemba 2014 uliotaka
wanafunzi katika vyuo vikuu
kupewa haki yao ya kikatiba ya
kufanya ibada kwa siku za Ijumaa

PROFESA Issa Shivji.


na Jumamosi kama ilivyo kwa siku
za Jumapili, ni ushahidi mwingine
juu ya uwezo mdogo wa Mhadhiri
huyu katika kupambanua mambo.
Inaonesha dhahiri kuwa Daktari
huyu ni mvivu wa kujenga
hoja na anasukumwa zaidi na
chuki, choyo na hisia badala ya
kuzingatia ukweli na uhalisia wa
mambo.
Katika kupinga waraka wa
s e r i k a l i B a n a a n a d a i k u wa
wanafunzi wake siku za Ijumaa
na Jumamosi hawezi kuwakatalia
kwenda kuabudu. anaongeza
Hili si suala la Serikali kutoa
waraka ni la mwafaka kati ya
mwalimu na mwanafunzi.
Inawezekana kwamba Mwalimu
wangu Bana amebadilika siku
hizi (tofauti na ninavyomfahamu
mimi) - kwamba siku hizi anajali
haki ya wengine kuabudu kama
yeye.
Hata hivyo, kama si kwa
makusudi, basi mwalimu wangu
amekurupuka. Hakusoma waraka
husika na kujua chimbuko
lake. Kwamba kumekuwa na
malalamiko kutoka kwa baadhi
ya wanafunzi na viongozi wa dini
kwamba wananyimwa haki ya
kuabudu. Shughuli za masomo
ikiwemo mitihani inapangwa
kwa makusudi nyakati za Ibada.
Mahafali katika vyuo vingi
yanaanza saa sita siku za Ijumaa
na maombi ya kubadili hali hii
yamekuwa yakigonga mwamba!
Hoja kwamba yeye anawaruhusu
wanafunzi wake kuabudu haiwezi
kumaliza tatizo. Je; ruhusa ya Bana
pekee ndio suluhu ya ubaguzi

wa kidini unaofanywa dhidi ya


baadhi ya wanafunzi Tanzania?
Ningemuelewa vizuri sana
Dr. Bana kama angechukulia
changamoto hii kama eneo la
utafiti ili kupata ukweli juu ya
utekelezaji wa haki ya kuabudu
vyuoni badala ya kukurupuka na
hoja zilizochoka.
Bana anadai kuwa eti Serikali
inachokoza jambo ambalo tayari
lina utamaduni wake. Kwamba
inapotoa mwongozo maana
yake inafanya wengine nao
wadai. Anaongeza kuwa eti
kinachofanywa sasa ni kutoa jini
kwenye chupa. Sielewi kwamba
Bana anakusudia nini anaposema
utamaduni wake. Utamaduni
upi? Wa kuwanyima uhuru
wa kuabudu baadhi ya watu?
Hivi kuna tatizo gani serikali
kukumbusha taasisi zake kufuata
sheria na taratibu kwa kuwapa
wananchi haki zao za msingi? Leo
Serikali ikitoa waraka kukemea
rushwa na uzembe kazini, Bana
atadai kuwa jini anatolewa
kwenye chupa kwa kuwa tayari
kuna utamaduni wa rushwa?
Bana anaonyesha chuki za
wazi dhidi ya waislamu anapodai
kuwa Haya mambo yanaweza
kuibua hisia za makundi kama ya
Waislamu wenye msimamo mkali
kuibuka na kudai Ijumaa isiwe
siku ya kazi. Watataka wapumzike
kama wenzao wanaopumzika
Jumapili, ndio maana nasema
hili jambo halipaswi kuingiliwa
na serikali, liachwe walimu na
wanafunzi wenyewe waone
Inaendelea Uk. 7

Makala

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 2014

Huyu mnyama kutoka ardhini mnyama gani?


Na Khaitib Juma Mziray

HISTORIA za dini,
zinatufahamisha kuwa, kila
Mwenyezi Mungu alipoleta
Mtume au Mitume, (Manabii),
waharibifu chini ya ibilisi
wa l i i n g i l i a k a t i k u h a r i b u
miongozo ya Mwenyezi Mungu
a l i y o p i t i s h i a k wa M i t u m e
hao. Baada ya uharibifu huo,
Mwenyezi Mungu alituma
mjumbe mwingine. Na kama vile
mlezi wa mototo, humwanzisha
mtoto shule kwa darasa la
kwanza nakuendelea, ndivyo
Mwenyezi Mungu alivyowaletea
wanadamu ujumbe kulingana na
nyakati zao.
Ujumbe wa Nabii Musa a.s
ulivurugwa mara nyigi, na
wavurugaji waliamini kuwa
wataufuta kabisa, ili sheria zao
ziwe ndizo zinazo tawala. Mfano
mdogo ni wa mfalme wa Ugiriki
na wa Rumi waliotaka imani
zao ndio zitawale. Ni pamoja
na wana wa Israeli kuibadilisha
Torati na kutengeneza kitabu
chao cha Talmudi. Hiyo ndiyo
maana Nabii Isa (Yesu) A.S. akawa
hakusomeshwa katika chuo
chochote, bali Mwenyezi Mungu
alimjuvya elimu iliyokuwa
katika Torati na ndiyo maana
hakupewa kitabu, bali alipewa
Injili (Mahubiri) yaliyotoka
kwa Mwenyezi Mungu kupitia
kichwani kwake:
Mimi siwezi kufanya neno
mwenyewe; kama nisikiavyo
ndivyo nihukumuvyo; na hukumu
yangu ni ya haki, kwa sababu
siyafuati mapenzi yangu mimi,
bali mapenzi yake aliyenipeleka.
(Yohana 5:30.)
Waandishi, Mafarisayo na
Masadukayo, walishtuka na
kukasirika baada ya kuona
kuwa anawahubiri sheria zile
zile za Torati ambazo waliamini
wamezivuruga sana, kwa kuwa
alikuwa akiwaambia kuwa:
Msidhani ya kuwa nalikuja
kuitangua Torati au Manabii la,
sikuja kutangua, bali kutimiliza.
Kwa maana, amini, nawaambia,
mpaka mbingu na nchi
zitakapoondoka, yodi moja wala
nukta moja ya Torati haitaondoka,
hata yote yatimie. (Mathayo
5:20.)
Ndiyo maana wakapanga
mbinu za kumwuuwa mapema
tu baada ya kukabidhiwa Utume
akiwa na miaka 30 kwa kuwa
walihofia kua akiendelea kuishi
wataumbuka. Na kwa kuwa Yesu
hakuwa na kitabu, mahubiri yake
ya miaka mitatu hayakuandikwa
a k i we p o , wa k i a m i n i k u wa
wakimuuwa mafundisho yake
yatakuwa ndio mwisho:
Tu n a f a n ya n i n i ? M a a n a
mtu huyu afanya ishara nyingi.
Tukimwacha hivi, watu wote
wa t a m wa m i n i ; n a Wa r u m i
watakuja, watatuondolea

mahali petu na taifa letu. Mtu


mmoja miongoni mwao, Kayafa,
aliyekuwa Kuhani mkuu mwaka
ule, akawaambia, ninyi hamjui
neno lolote wala hamfikiri
yakwamba yafaa mtu mmoja afe
kwa ajili ya watu, wala lisiangamie
taifa nzima. (Mathayo 11:40-50)
H a p o B wa n a Ye s u
aliposulibiwa, ilidhaniwa
kwamba dini ya Kikristo hapana
budi itakoma mara moja. Yeye
Kristo alikuwa hakuwaachia
wanafunzi wake chuo chochote
alichokiandika, wala Imani
(Creed) yoyote aliyoitengeneza.
(Historia ya Kanisa, cha Canon
H.J.E. Butcher, uk. 1.)
Ndiyo maana, ile dhana hiyo
ya kufutika mafundisho ya dini
itokayo kwa Mwenyezi Mungu
ikamilike, Paulo alipewa kazi ya
kuwasaka wale wanafunzi wa Yesu
ili wauawe wasije wakaendeleza
yale mafundisho yake. Wa kwanza
kuuawa, ni Stefano; wanafunzi
wakatawanyika na kukimbilia
nchi za jirani, Paulo akaomba
kibali cha kwenda kuwasaka:
Lakini Sauli (Paulio),
akazidi kutisha na kuwaza
kuwaua wanafunzi wa Bwana
(Yesu), akamwendea Kuhani
Mkuu, akataka apewe barua za
kwenda Dameski zilizoandikwa
kwa masinagogi, ili akiona
watu wa njia hii (wanaofuata
mafundisho ya Yesu), waume
kwa wake, awafunge na kuwaleta
Yerusalemu. (Matendo. 9:1-2.)
Biblia na historia ya Kanisa,
vinatuonesha kuwa, mwanafunzi
wa Ye s u a l i ye i t wa Yo h a n a
Mtakatifu,
walishindwa
kumwuwa; au ni kwa mipango
ya Wa r u m i , Wa ya h u d i n a
Wagiriki hicho ni kizungumkuti,
maana kazi kubwa ya mambo
yanayoihangaisha dunia hii,
ya l i p a n g i wa h u k o , n a d i n i
iliyokusudiwa, ikaanzishiwa
huko, kama nilivyo nukuu hapo
juu. Na yule mwuwaji mkuu wa
wanafunzi wa Yesu, akawa ndiye
mkufunzi mkuu. Na injili zake
zikawa ndizo za kwanza kutolewa
na kufundishia dini:
Bali, kinyume cha hayo,
walipoona yakuwa nimekabidhiwa
Injili ya wasiotahiriwa, kama
vile Petro ya waliotahiriwa;
(Galatia 2:6-10.)
Ndugu zangu, nanena kwa
jinsi ya kibinadamu. Lijapokuwa
ni agano la mwanadamu, hata
hivyo likiisha kuthibitika,
hakuna mtu alibatilishaye, wala
kuliongeza neno. (Gal 3:15)
Paulo amewaandikia wafuasi
wake huko Glatia mnamo mwaka
wa 57, A.D. yeye akiwa Efeso
au Makedonia. Utangulizi wa
barua kwa Wagalatia; Biblia ya
Imprimatur.
M k u m b u k e Ye s u K r i s t o
aliyefufuka katika wafu, wa uzao
wa Daudi kama inenavyo Injili
yangu. (1.Timotheo 2:8.)

Paulo amemwandikia Timotheo


mwaka wa 65, A.D. akiwa Rumi,
na ndizo zilizo fundishia Ukristo
kabla ya hizi Injili nne tunazoziona
katika Biblia hivi leo.
Injili na Ufunuo wa Yohana
viliandikiwa gerezani, katika
visiwa vya Patimo Yohana akiwa
gerezani. Sina hakika kuwa,
mfungwa huyu aliyeshindikana
kuuawa kwa lengo la kufuta
mafundisho ya Yesu; ilitokea
nini askari wamruhusu kuandika
yale yaliyokuwa yamekataliwa,
n a wa a n d i s h i , M a f a r i s a y o ,
Masadukayo na Makaisari wa
Ugiriki na Rumi. Lakini ngoja
waandishi watusaidie:
Wanafunzi wengi hudhani ya
kwamba kitabu hiki kiliandikwa
kwenye mwaka wa 95 (A.D.) na
Yohane Mtume, alipohamishwa
na wakubwa wa Dola katika
kisiwa kiitwacho Patmo.
Wengine husema yakwamba
h a k i k u a n d i k wa n a Yo h a n e
mwenyewe, ila mfuasi wake
fulani. Sababu ni kwamba lugha

ni tofauti na lugha ya Injili, ijapo


mawazo ni ya Yohane. Wengine
hus e m a ya k wa m b a k i t a b u
kiliandikwa na Yohane akisaidiwa
na karani ambaye hakutawala
sana lugha ya Kigiriki.
Utangulizi wa Ufunuo wa
Yohane; Bibli ya Imprimatur.
Ufunuo huu umebeba madhila
m e n g i , ya l i y o , ya n a y o n a
yatakayoikumba dunia hii, iwe
ni kwa maana halisi ya Ufunuo,
au kwa ufunuo wa kupangwa kwa
ajili ya kuwadhulumu wanadamu
na kuwaangamiza viumbe kwa
jumla, chini ya kivuli cha dini:
Ikaonekana ishara nyingine
mbinguni; na tazama, joka kubwa
jekundu, lilikuwa na vichwa
saba na pembe kumi,nyoka wa
zamani aitwaye Ibilisi na Shetani.
(Ufunuo 12:1-17)
Kisha nikaona mnyama alitoka
katika bahari, mwenye pembe
kumi, na vichwa saba, na juu ya
pembe zake ana vilemba kumi,
na juu ya vichwa vyake majina ya
makufuru. (Ufunuo 13:1-4)
Itaendelea toleo lijalo

Dk. Bana, ni udini tu au udhaifu wako kitaaluma?


Inatoka Uk. 6
namna ya kulitekeleza.
Huo ni uchambuzi wa mtu
mwenye PhD! aliyefundisha
Chuo Kikuu kwa miaka 38!
Hawezi kuona kwamba hapa
hana hoja zaidi ya ubaguzi wa
wazi na chuki iliyotamalaki!
Kwani hamna Wakristo wenye
siasa kali? Kama si unafiki, mtu
mwenye chuki kama huyu kweli
atamruhusu Muislamu akafanye
ibada? Hivi dawa ya kuzuia mtu
asidai kitu ni kuhakikisha kuwa
unamkandamiza na kuhakikisha
kuwa hapati haki yake ya msingi?
Kwa hoja kiwete kama hizi, hivi
ni jarida (Journal) lipi litakubali
paper (maandiko) ya Dr Bana?
Dr Bana anauliza mbona
miaka kumi iliyopita haya mambo
hayakuwepo? Eti hakumbuki
Waislamu kudai jambo hili!
Kama ni kweli kwamba Bana
hakumbuki, basi ni dhahiri
kwamba akili yake imechoka kiasi
kwamba kuendelea kwake kubaki
Mlimani huku akilipwa mshahara
ni kitendo cha kuliibia taifa.
Madai ya wanafunzi Waislamu
kuruhusiwa kufanya ibada ni
ya kihistoria, lakini yamekuwa
yakipuuzwa bila sababu za msingi.
Hata hivyo, ni kujidhalilisha
pale msomi wa PhD anayejifanya
mchambuzi wa masuala ya kisiasa
na kijamii anapotaka kutuaminisha
kuwa hatutakiwi kushughulishwa
na mambo ambayo hayakuwepo
siku za nyuma. Kwa hoja yake
anataka tuamini kwamba hata
yeye anajishangaa kuvaa viatu
kwa kuwa miaka 50 iliyopita

mguu wake ulikuwa haujui


kiatu! Kwamba anashangazwa
na mchakato unaoendelea wa
katiba kwa kuwa haukuwepo
miaka kumi iliyopita! Hii ndiyo
hoja ya msomi kweli? Kwa hoja
mfu kama hizi, kwa nini asibaki
kwenye ngazi moja ya kitaaluma
kwa zaidi ya miaka 20?
Namheshimu sana Mwalimu
wangu Dr Bana. Hata hivyo,
sitamtendea haki endapo
sitamkumbusha kuwa anapwaya
mno kitaaluma, na kwamba
pengine alipotea njia na kujikuta
katika fani ya uwanataaluma. Ndio
maana hata wanafunzi wake wengi
aliowafundisha wako mbali katika
ngazi za taaluma kulinganisha
naye. Pengine anaamini kuwa
maoni yake kupitia vyombo vya
habari yanamjengea umaarufu.
Ukweli ni kwamba maoni haya
yanammaliza na kuanika udhaifu
wake mbele ya jamii. Kwa hali
hiyo itabidi mwalimu wangu
aendelee kusherehekea miaka 30
ya kuwa mhadhiri mwandamizi
mkongwe zaidi hapa Tanzania.
Mwisho, kama mdau naunga
mkono hatua ya wizara kutoa
waraka unaoelekeza vyuo vikuu
kuzingatia haki na uhuru wa watu
kuabudu. Haiwezekani wakati
Taifa linalia na mmomonyoko
wa m a a d i l i , wa we p o wa t u
wanaowanyima raia wengine
uhuru wa kuabudu. Hamna dini
inayoruhusu ufisadi, rushwa,
wizi, ulevi, umalaya, uuaji nk. Na
haya ndiyo maradhi makubwa
yanayolisumbua Taifa letu.

Makala

8
Na Omar Msangi
NINGEPENDA kuanza kwa
kuwaombea kwa Mwenyezi
Mungu wale waliodhulumiwa
uhai wao kwa kupigwa risasi
katika tukio la mwishoni mwa
wiki kule Kenya. Katika tukio
hilo tunaambiwa kuwa watu
wanaodhaniwa kuwa ni magaidi
waliteka basi na kuuwa watu 28.
Aidha, nawapa pole wale
ndugu, jamaa na marafiki wa
marehemu ambao wamekatizwa
uhai wakiwa safarini kuelekea
Nairobi. Taarifa za vyombo
v ya h a b a r i z i n a f a h a m i s h a
kuwa basi lililokuwa likielekea
Nairobi, lilipofika katika mji
wa Mandera, ulio mpakani na
Somalia, lilivamiwa na kutekwa
na watu wenye silaha. Taarifa
zaidi zinadai kuwa watekaji hao
waliwatenganisha Waislamu
na Wakristo kisha wakawauwa
Wakristo 28, waliokuwa kati ya
abiria 60 wa basi hilo.
Waliwajua vipi Wakristo?
Baadhi ya vyombo vya habari
vikasema kuwa waliwataka
watu wote watamke Shahada
mmoja mmoja, walioshindwa
wakatambulika kuwa ni Wakristo.
Magazeti mengine yakasema kuwa
abiria waliambiwa kusoma Quran,
walioshindwa kusoma japo sura
au aya yoyote, wakatambulika
kuwa sio Waislamu.
The hijackers demanded the 60
passengers aboard recite the Shahada,
a tenet of Islam. The 28 -- 19 men
and nine women -- who were unable
to recite the passage where shot
to death. (Agence France-Presse
reported)
Wakati AFP wakisema kuwa
a b i r i a wa l i t a k i wa k u t a m k a
Shahada, BBC wao walikuwa na
haya ya kusema:
Gunmen separated out nonMuslims by asking passengers to read
from the Koran, officials and witnesses
said. Those who failed were then shot
in the head.
Ripoti ya polisi Kenya ni sawa
na ile ya AFP ambapo Mkuu
wa P o l i s i , D a v i d K i m a i y o ,
alisema kuwa waliouliwa ni wale
walioshindwa kutamka Shahada.
Taarifa ya haraka haraka ya
polisi, wanasiasa na vyombo vya
habari, zilidai kuwa wahusika wa
shambulio hilo ni Mujahidina wa
al-Shabab, wengine wakisema ni
magaidi wa al-Shabab.
Sababu zilizotolewa ni mbili,
moja ni kwamba pamoja na ile
sababu ya siku zote kwamba
wanafanya mashambulizi hayo
kulipiza kisasi kutokana na hatua
ya serikali ya Kenya kupeleka jeshi
Somalia, lakini sababu nyingine
i m e t a j wa k u wa wa n a l i p i z a
kisasi kwa tukio la wiki iliyopita
ambapo polisi walivamia Msikiti
Mombasa, wakauwa kijana mmoja
na kuwakamata wengi kwa
mamia. Katika operesheni hiyo,
iliyomalizika kwa kupigwa kufuli
misikiti minne na kuwa marufuku
kupiga Adhana na kuswali au
kufanya Ibada yoyote katika
Misikiti hiyo, polisi walidai kuwa

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 2014

Wanasiasa, magazeti
wanapandikiza ugaidi

Wabaya kuliko watuhumiwa ugaidi


Tujifunze kutoka Kenya na ATPU yao
Kama tukifuata nyayo zao, tumeangamia

RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

MAKAMU wa Rais William Ruto

wamekamata shehena kubwa ya


silaha msikitini.
Kwa upande wake Rais

Uhuru Kenyatta amesema kuwa


wanachotaka magaidi hao wa
al-Shabab ni kupandikiza vita

Wataalamu wa kupambana
na magaidi watatuangamiza
Na Omar Msangi
TAARIFA za wiki hii kutoka
Nigeria zinafahamisha kuwa
washambuliaji wawili wa kike
wa kujitoa muhanga (suicide
bombers), walilipua bomu katika
soko lililojaa watu katika mji
wa Maiduguri, na kuuwa kwa
uchache watu 45.
Taarifa ya Shirika la Habari la
AFP ikidai kunukuu mashuhuda
waliokuwa eneo la tukio ilidai
kuwa wasichana wadogo chini ya
miaka 20 waliokuwa wamevalia
hijabu walijilipua katikati ya watu
sokoni hapo.
Japo hakuna kikundi hadi
sasa kilichodai kuhusika na
shambulio hilo, vyombo vya
usalama vya Nigeria vinadai
kuwa watuhumiwa watakuwa ni
Boko Haram.
Tukio hilo linakuja baada ya
miaka mingi kwa serikali ya
Nigeria na vyombo vyake vya
dola kutangaza hatua kali za
kupambana na Boko Haram, lakini
pia na kuwekewa bajeti kubwa ya

msaada kutoka Marekani kwa ajili


hiyo.
Shambulio hilo linakuja pia
wakati mji huo na Jimbo zima la
Borno lipo chini ya hali ya hatari
(state of emergency) kutoka Mei
mwaka jana.
US Government Sent Nigeria $20
Million To Fight Boko Haram Since
2012, hiyo ni taarifa ya mwandishi
Clement Ejiofor, ambaye anaeleza
kuwa mwaka 2012 serikali ya
Marekani ilitoa Dola milioni 20
sawa na Naira (pesa ya Nigeria)
bilioni 176 (N3.176 billion) kwa
ajili ya kusaidia polisi, idara za
usalama na jeshi kupambana na
Boko Haram.
Bajeti hiyo imekuwa ikiongezeka
mwaka hadi mwaka, lakini zaidi
ikiandamana na mafunzo ya
kijeshi na kikachero, yakiwemo
mazoezi ya pamoja na uundaji wa
vikosi maalum. Hata hivyo, sote
hali tunaiona. Kama ilivyo kwa
Yemen, Pakistan na Afghanistan,
msaada huo haujaweza kuondoa
Inaendelea Uk. 9

ya kidini baina ya Waislamu na


Wakristo. Na hiyo ni kutokana na
jinsi walivyoendesha shambulio
hilo kwamba waliwalenga abiria
Wakristo tu.
Kwa upande mwingine baadhi
ya vyombo vya habari vikadai
kuwa al-Shabab wamedai katika
mtandao wao kwamba wanauwa
Wakristo kwa sababu walifurahia
kitendo cha polisi kuvamia
Misikiti na kuifunga.
Taarifa ya serikali ya Kenya
imesema k uwa harakati za
kuwasaka na kuwaangamiza
washambuliaji hao zinaendelea
n a k wa m b a j e s h i l a K e n ya
limefanikiwa kushambulia na
kuangamiza baadhi ya kambi za
magaidi ambapo al Shababu 100
wameuwawa. Hiyo ni kwa mujibu
wa taarifa ya Makamo wa Rais wa
Kenya William Ruto.
Hata hivyo inadaiwa kuwa
msemaji mmoja wa al-Shabab
aliyetajwa kwa jina la Abdi Aziz
Abu Mus'ab, amekanusha madai
hayo ya Ruto na kusema kuwa ni
uwongo mtupu.
"Our mujahedeen are safe and
didn't face any attack whatsoever
after the successful operation they
carried out by the grace of Allah,"
amenukuliwa Mus'ab akidaiwa
kuongea na Al Jazeera.
Kwa upande wake serikali
ya Marekani haraka haraka
ililani shambulio hilo na kusema
kwamba ipo pamoja na Kenya
katika kupambana na magaidi wa
al-Shabab.
"The United States condemns in
the strongest terms today's horrific
attack in Kenya by the terrorist group
al-Shabab against innocent civilians."
Alisema Bernadette Meehan
ambaye ni msemaji wa Baraza
la Usalama la Taifa (National
Security Council) la Marekani.
"The United States stands with
our Kenyan partners in the effort to
counter the threat of terrorism and
affirms our ongoing commitment to
working with all Kenyans to combat
these atrocities."
Bibie Bernadette Meehan,
aliongeza katika taarifa aliyoitoa
huko Washington.
Kinachoelezwa katika habari
hii kwanza ni kufahamishwa
juu ya kuwepo magaidi wa alShabab na pili juu ya ubaya wao
na ukatili wao. Na hilo huelezwa
kupitia tukio lao la kuuwa abiria
28. Lakini katika hilo kuna kitu
kinapandikizwa, sio tu kwamba
magaidi hao ni Waislamu, lakini
magaidi wanaolenga kuwaangaza
Wakristo na hivyo kuchochea vita
ya kidini, baina ya Waislamu na
Wakristo.
Taarifa hizi zinatufahamisha pia
jinsi serikali ya Kenya ilivyojizatiti
kupambana na magaidi wa alShabab, lakini pia jinsi Sekali ya
Marekani inavyoguswa na jambo
hili na azma yake ya kushirikiana
na Wakenya katika kupambana
na magaidi.
Yapo mambo kadhaa hapa ya
kutizama. Kwanza ni kuwa yapo
makosa makubwa yamefanywa
Inaendelea Uk. 9

9
Inatoka Uk. 8
huko nyuma na wanasiasa wetu,
ambayo ndiyo yanayopelekea
kupandikiza kitisho katika nchi
zetu. Na kikishapandikizwa,
kikakubalika kwamba kipo, hizi
kauli za polisi, jeshi, Rais wa nchi
kwamba tutapambana vikali
na magaidi, ni kauli za bure tu.
Hazina maana yoyote. Kadiri
watakavyojidai kupambana,
ndivyo na ugaidi wenyewe
utakavyoongezeka. Mfano wala
haupo mbali, upo kwa Goodluck
Jonathan na Boko Haram yake.
Aliwahi kusema aliyekuwa
Waziri wa Mambo ya Nje wa
Uingereza, Robert Finlayson
"Robin" Cook , kwamba, al-Qaida
ni magaidi wa kubuni na wa
kutumiwa na mabeberu kwa
malengo yao. Mabeberu wakiacha
mkakati huo wa kutumia magaidi
katika mipango yao, na ugaidi
unaporomoka siku hiyo hiyo.
Huo ndio ukweli. Sio kwa ATPU
au jeshi la Kenya kukaza buti
kupambana na magaidi.
Nigeria walikaza sana buti
toka Boko Haram walipokuwa
wakidaiwa kuwa wanarusha
mabomu ya mafuta ya taa na baruti
za kutengeneza kienyeji, sasa
wana magari ya kivita na mizinga
ya kutungulia ndege! Swali ni
je, wamezipata wapi silaha hizi?
Zimetoka wapi na zimeingia vipi
Nigeria hadi kuwafikia?
Al-Shabab halikuwa tatizo
la Kenya, Uganda, Tanzania
Inafahamika wazi kuwa pamoja
na matatzo waliyokuwa nayo
Somalia, vita vyao havikuwa
tatizo la Kenya, Uganda, Zanzibar
wala Dar es Salaam, ukiacha
tatizo la wakimbizi kama walivyo
wale kutoka Rwanda, Burundi
na Congo DRC. Inafahamika pia
kuwa juhudi zote za inayoitwa
Jumuiya ya Kimataifa kuleta
amani Somalia, zilikwama. Na
inafahamika kuwa ni Wasomali
weyewe hatimaye waliofanikiwa
kurejesha amani kama CCM na
CUF walivyofanikiwa kuleta
muafaka Zanzibar ikatulia,
wakati huko nyuma miafaka yote
iliyopata baraka na iliyosimamiwa
na serikali ya muungano na ile
Jumuiya ya Kimataifa, ikasainiwa
kwa mbwembwe ilikwama.
Ni jambo linalofahamika wazi
pia kwamba hawa wanaotoa
machozi kuwalilia Wakenya
waliouliwa na wanaosema
k u wa wa t a k u wa b e g a k wa
bega na Kenya kupambana na
magaidi, ndio waliovuruga
amani iliyochipua Somalia na
ikawa ndio sababu ya kuibuka
al-Shabab. Lakini inafahamika
wazi pia kuwa ilikoanzia alShabab, ni wananchi wa Somalia
waliokuwa wakipinga serikali
waliyoita kibaraka iliyoweka na
wale walioondoa serikali yao ya
umoja iliyoweza kurejesha amani
na usalama Somalia.
Lakini kilichotokea ni kuwa
wakati al-Shabab na serikali
ya mpito (Transitional Federal
Government-TFG), ilikuwa ni

Makala

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 2014

Wanasiasa, magazeti
wanapandikiza ugaidi

WATU 28 wanaodaiwa kuuliwa na magaidi nchini Kenya.


tatizo la Somalia, tukasomeshwa
na mabeberu kuimba kuwa alShabab ni magaidi wanaohusiana
n a a l - Q a i d a h . Tu k a u p o k e a

wimbo tukaimba kwa juhudi na


mbwembwe nyingi bila maarifa
wala kutumia akili japo kidogo.
Matukio yakapatikana ya kudaiwa

Inatoka Uk. 8
tatizo la ugaidi wa Boko Haram.
Inakuwa kana kwamba kila
unapopewa msaada zaidi, ndio
ug a id i u n a v y o o n g e z e k a n a
magaidi kuwa na uwezo mkubwa
zaidi.
Tuliambiwa kuwa kule Iraq
walitumia Salvador Option na
tunafahamu kilichotokea pale
wa l i p o k a m a t wa m a k a c h e r o
wawili wa Uingereza wakijifanya
ni magaidi wa Mehdi Army wa
kujitoa muhanga. Hakuna namna
nyingine unaweza kuelewa
kitendawili hiki cha Boko Haram,
zaidi ya kutizama uhusiano wa
ugaidi wa Iraq na matukio hayo
ya Salvador Option.
Kule Mombasa tumeambiwa
kuwa polisi walivamia msikiti
kwa sababu kulikuwa na taarifa
za ki-intelijensia kuwa kuna
silaha na watu wanaojifunza
ugaidi. Ukifanya harakati kama
zile, kwa maana ya kuvamia
msikiti na kisha kuufunga na
kupiga marufuku watu kuswali,
jambo ulilo na uhakika nalo ni
kuwa litazuka zogo na vijana
(Waislamu) wanaweza kuja juu
kutaka kulipiza kisasi.
Swali ni kuwa kwa nini polisi
walifanya harakati ile wakijua
matokeo yake?
Lakini mara baada ya tukio
hilo, tunaambiwa kuwa magaidi

wa al-Shabab wameuwa abiria 28


Wakristo baada ya kufanya zoezi
la kuwatambua wakisafiri katika
basi. Na tunaambiwa kuwa alShababu hao ambao wamejitaja
kama Mujahidina, wanafanya
hivyo kulipiza kisasi uvamizi
wa misikiti kwa madai kuwa
Wakristo walifurahia Waislamu
walipovamiwa na polisi. Hapa
kuna mambo mawili. Ukisema
kuwa waliofanya ni Mujahidina,
wa t u h a o h a wa we z i k u wa
Waislamu kwa sababu hakuna
mahali popote katika mafundisho
ya Uislamu panapo ruhusu jambo
hilo kufanyika. Hata kwa kutumia
lile tukio la Mombasa kuwa ni
hasira, wanalipiza kisasi, bado
haipo katika hukumu za Kiislamu.
Lakini ukirudi katika tukio la
Mombasa na jinsi lilivyofuatana
na hili la kuuliwa abiria na hoja
zinazotolewa, na ukizingatia
madai ya watu wa Mombasa
kuwa polisi wanapandikiza silaha
Msikitini, na ukizingatia pia kuwa
hakuna Muislamu anayeweza
kufanya unyama huo kwa jina
la Uislamu, wa kushusha abiria
wasio na hatia na kuwapigha risasi
za kichwa, tukio hili linakuwa tata
kama lile la Westgate. Bali itabidi
uchunguzi ufanyike kujua, nani
kauwa abiria hawa 28 Wakristo?
H u m a n R i g h t s Wa t c h n a

Wataalamu wa kupambana
na magaidi watatuangamiza

Inaendelea Uk. 10

kuthibitisha hilo.
Shambulio la Westgate
Shopping Mall Nairobi
Yapo matukio mengi ambayo
ilidaiwa kufanywa na magaidi wa
al-Shabab likiwemo lile shambulio
la Kampala tarehe 11 Julai, 2010
ambapo watu 74 walikufa na
wengine 70 kujeruhiwa wakati
wapenzi wa mpira wakitizama
mechi za kombe la dunia. Lakini
hayo tuyaache kwanza tutizame la
Westgate Shopping Mall, Nairobi.
Tuliambiwa magaidi kati ya 10 na
15 kutoka Somalia waliigia Kenya
wakiwa na gari lililosheheni silaha
wakaingia katika kituo hicho
maarufu cha kibiashara na kuanza
kuuwa watu. Walivamia tarehe
21 Septemba 2013, na kudumu
katika jengo hilo hadi 24 Septemba
ambapo ilidaiwa kuwa watu 67
waliuliwa na wengine zaidi ya 175
kujeruhiwa.
Polisi, vikosi maalum vya polisi,
Idara za Usalama za Ndani na
Nje ya Kenya na jeshi la Kenya,
w o t e h a o wa l i k u wa k a t i k a
operesheni ya kukabiliana na
magaidi hao 15 kutoka Somalia!
Vifaru na silaha nyingine nzito
za kijeshi, vikaonekana vikiranda
na kuzingira Nakumati. Na
tunaambiwa kuwa kituo hicho
cha kibiashara kinamilikiwa na
raia wa Israel. Lakini pia wapo
Wayahudi kwa uchache wanne
ambao wamekodi katika jengo
hilo wakiendesha migahawa.
Zaidi ni kwamba, Kenya ina
makubaliano na Israel ya kiulinzi
na hivyo makachero wa mwanzo
kuingia katika operesheni hiyo ya
kukabiliana na magaidi 15 kutoka
Somalia, walikuwa makachero wa
MOSSAD. (Tazama: International
Business Times)
Hata hivyo, vikosi vyote hivyo
havikufanikiwa japo kukamata
au kuuwa hata gaidi mmoja
n a k u o n y e s h a m a i t i ya k e !
Magaidi wakafanya waliyofanya,
wakajiondokea zao wakaacha
huku nyuma wanajeshi,
serikali na wananchi wa Kenya,
wakiparurana kuwa badala ya
kupambana na magaidi, wanajeshi
walikuwa wakipora mali na
kulewa. Picha zikasambazwa
kuonyesha walichokuwa
wakifanya wanajeshi hao wakiwa
ndani ya Nakumati. (Pflanz, Mike.
"Kenyan army admits that soldiers
looted Westgate during siege".
London. Retrieved 29 October
2013.)
Taarifa za kuingia magaidi
Nakumati, Westgate, Nairobi,
zilipambwa na kusindikizwa na
visa vyingi vilivyonogeshwa zaidi
na vyombo vya habari vikiwa vile
vilivyopigiwa zumari kuonyesha
jinsi magaidi hao al-Shabab
walivyokuwa katili kwa Wakrsito.
TV na magazeti yakaandika na
kupamba kwamba magaidi hao
walikuwa wakiwapa mateka wao
mtihani, anayefaulu kuthibitisha
kuwa ni Muislamu anaachwa,
a n a y e f e l i a n a p i g wa r i s a s i
Inaendelea Uk. 10

10
Inatoka Uk. 9
kichwani. Lakini tukaambiwa
pia kuwa hata watoto wadogo
wakithibitika kuwa ni Wakristo,
walikuwa wakibamizwa vichwa
vyao katika ukuta au mikono yao
kukatwa ikachongwa na kufanywa
kalamu za kuandikia huku damu
ikifanywa wino. Vyombo vya
habari vikasherehesha sana habari
hizi.
K wa h i y o , m p a k a t u k i o
linamalizika, ishawekwa
ushahidi kuwa wapo magaidi
wanaoitwa al-Shabab weye uwezo
wa kushinda polisi, Idara ya
Usalama ya Kwenya na Jeshi
lote la Kenya likipewa msaada
kutoka Israel na Uingereza!
Lakini maadhali tuliambiwa kuwa
walikuwepo makachero wenye
silaha nzito wa MOSSAD na wale
wa Uingereza (na Marekani?), ni
kwamba tukio liliweka muhuri pia
kuwa magaidi hao ni hatari mno
kiasi kwamba hata wazito hao wa
kidunia katika vita na ukachero,
hawana ubavu wa kukabiliana
nao!
Maadhali ushaweka msingi
huo, na maadhali ushakubali
kuwa una kitisho hicho cha
ugaidi wa kiwango hicho, katika
ulimwengu huu wa Vita dhidi
ya Ugaidi, yaliyosalia au tuseme
yatakayokuja kufanyika baadae
ili kuendeleza vita ya wenyewe
mabeberu dhidi ya ugaidi, wala
hutakuwa na udhibiti nayo. Huo
ndio ukweli. Ndio pale nikasema
kuwa kauli ya Rais Uhuru Kenyatta
na mwenzake William Ruto, wala
hazina maana yoyote. Silaha
zitaendelea kupatikana Misikitini,
iwe ni kwa njia ya kupandikizwa
(dubious terrorism sting tacticsDubious Entrapment ), kwa maana
ya kughilibu baadhi ya watu au
kuwanunua na kuwafanyisha
vitendo vitakavyothibitisha kuwa
kuna ugaidi. Na kwa sababu
hiyo, matukio yanayodaiwa
ya Wakristo kutenganishwa
na Waislamu, kisha Wakristo
kuuliwa, yataendelea kuwepo.
Ile kukubali propaganda
kuwa al-Shabab wanaopambana
n a m a j e s h i ya u va m i z i ya
Ethiopia yaliyovamia nchi yao
na kuweka serikali kibaraka,
ni magaidi hatari kwetu; kosa
namba moja. Vile tulivyopokea
shambulio la Westgate, pamoja
na utata wote ulioligubika kama
inavyoelezwa katika ile makala
ya Jicho Pevu (KTN), kosa la
pili la msingi. Mtu anadaiwa
kupigwa risasi ya mgongoni,
lakini picha inamwonyesha hana
damu inayotiririka, bali doa tu
jekundu inakodaiwa kupita risasi.
Lakini zaidi anatembea. Ajabu
ya mambo. Kwa ujasiri mkubwa
tv zinaonyesha na magazeti
yaliandika na kusherehesha, ikiwa
ni pamoja na yule aliyedaiwa
kupigwa risasi ya kisigino, lakini
soksi haina damu na anatembea
mwenyewe!
Kuuliwa Masheikh
Kenya yamefanyika mauwaji

Makala

Wanasiasa, magazeti
wanapandikiza ugaidi

BASI linalodaiwa kutekwa na magaidi na kuua abiria 28 Wakristo.

Wataalamu wa kupambana
na magaidi watatuangamiza

Inatoka Uk. 9
Columbia Law School, wamefanya
utafiti na kutoa ripoti ya kurasa
214 waliyoipa jina "Illusion of
Justice: Human Rights Abuses in US
Terrorism Prosecutions.
Ndani ya ripoti hiyo
wanaonyesha jinsi FBI
wanavyotumia njia mbovu na
zisofaa (Dubious Entrapment
Arrests/terrorism sting tactics.)
kuwatia katika jinai ya ugaidi
watu ambao wala hawakuwa na
mawazo ya kufanya uhalifu huo.
Ripoti hiyo inaeleza kwa
undani jinsi serikali ya Marekani
inavyowahujumu Waislamu na
kuwachonganisha na jamii ya
Wakristo. Na hiyo ni kwa sababu
ya kuwafanyia vitendo vingi vya
entrapment na kuwatangaza
kuwa ni magaidi.
The report also shows how
government tactics are antagonizing
American Muslims. "The U.S.
government has on the one hand
claimed that American Muslim
communities are essential partners,
while at the same time placing them
under surveillance and treating them
as suspects. The impact of those
practices has been quite serious,
alienating some communities and
leading to fear and suspicion in places
like mosques and community centers
that should be places of refuge."
(Andrea Prasow, deputy Washington
director for HRW)
Kama tutakumbuka vizuri
katika matukio yote yaliyowahi

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 2014

kutokea hapa nchini yenye


harufu ya ugaidi likiwemo lile la
kuuliwa Padiri Zanzibar na lile la
kulipuliwa bomu kanisani Arusha,
tuliambiwa kuwa wazoefu FBI
wanakuja kutusaidia. Lakini
ripoti ya Human Rights Watch
inatuambiwa kuwa:
The FBI will identify someone who
fits a possible terrorist profile; urge
that person to participate in an attack;
provide the necessary materials; then,
finally, make an arrest. In many of
the sting operations we examined,
informants and undercover agents
carefully laid out an ideological basis
for a proposed terrorist attack, and
then provided investigative targets
with a range of options and the
weapons necessary to carry out the
attack. Instead of beginning a sting
at the point where the target had
expressed an interest in engaging
in illegal conduct, many terrorism
sting operations that we investigated
facilitated or invented the target's
willingness to act before presenting
the tangible opportunity to do so."
Ufupi wa maneno ripoti hiyo
inasema kuwa ni makachero wa
FBI wanaowatia watuhumiwa
wazimu wa kufanya ugaidi na pia
kuwasaidia kwa vifaa watu hao
na kisha baadae baada ya kuweka
ushahidi, ndio huwakamatisha.
Na kwamba wala hawasubiri
kumpata mtu ambaye anaonekana
kuwa na mawazo ya kigaidi, bali
wao ndio hupandikiza mawazo
Inaendelea Uk. 12

mengi ya viongozi wa kidini.


Taarifa za uhakika zinaonyesha
kuwa viongozi hao waliuliwa na
kikosi maalum cha kupambana na
magaidi (Anti Terror Police UnitATPU), lakini serikali inasema
haijui nani kafanya mauwaji hayo.
Au pale wanapokiri kuwa Sheikh
kauliwa na ATPU, basi wanadai
kuwa Sheikh huyo alikuwa gaidi
aliyeuwawa wakati akirushiana
risasi na polisi, wakati ukweli wa
mambo Sheikh huyo alivamiwa
nyumbani kwake akapigwa
risasi za karibu kichwani. Hata
wa n a wa k e wa l i o va a h i j a b u
wamedaiwa kuwa na silaha na
kupambana na polisi!
Kuna na haya ya juzi ambapo
baadhi ya watu wanadai kuwa
polisi walifanya kupandikiza
silaha walizodai kuzikamata
msikitini na kisha kuvamia. Na
wanaodai haya sio watu wa
mitaani tu. Hata ile Tume ya Haki
za Binadamu Kenya, imekuja na
madai hayo pia na kuonya kuwa
matumizi ya njia hizo chafu,
zitaiangamiza Kenya.
Hapa kwetu kumekuwa na
mtindo, chambilecho, nyimbo
mbaya haimbiwi mwana.
Atasimama mwanasiasa katika
jukwaa, iwe la kisiasa au la kidini
na kuwafananisha, kwa mfano
Masheikh wa UAMSHO na Boko
Haram. Au atazungumza katika
namna ambayo, anakazia uwepo
wa kitisho cha magaidi, iwe alQaida au al-Shabab. Katika masiku
ya hivi karibuni, ukaja na mtindo
mwingine wa kuchochea chuki na
uhasama baina ya Waislamu na
Wakristo. Tuliwahi kutangaziwa
hapa kwamba ulinzi wa polisi
utaimarishwa makanisani ili
kuwalinda Wakristo wakati wa
ibada. Ilimuradi linapandikizwa
jambo ambalo katika hali halisi
ya maisha mitaani halipo kabisa.
Sasa tuna hiyari, kujifunza
kutoka Kenya na Nigeria
tusalimike au tukimbilie jahazi
linalozama ambalo nadhani
wenzetu watakuwa wanataka
k u t a f u t a n a m n a ya k u t o k a
kujinusuru, lakini hawaioni.
Walisema wasomi na maprofesa
k u t o k a N i g e r i a wa l i o k u wa
katika ile semina ya Muslim
University of Morogoro (MUM),
kuwa mkisharuhusu hali kama
hii kujengeka, basi mmekwisha
kwa sababu yaliyobaki mtakuwa
hamna udhibiti nayo. Kila
siku watapatikana watu wa
kushambulia, kulipua na kuuwa
watu, wala hamtajua nani kafanya,
ila mtatangaziwa kuwa ni alShabab (Boko Haram).
S e r i k a l i n a v i k o s i v ya k e
ikisharuhusu yote haya
yakafanyika, inakuwa kama
mnyama aliyekiwisha zingwa na
chatu, hana pa kutokea tena.
H i y o n d i y o h a l i . K e n ya
imezama wala haitoki. Labda
wanasiasa watanabahi na wakae
kitako na kuja na mkakati mpya,
lakini sio huu wa Ruto na afande
David Kimaiyo.

11

Makala
Na Mwandishi Wetu

NIKIWA kama mgeni mwalikwa


katika Haqika ya kijana wetu
mmoja (Allah sw amuhifadhi
) maeneo ya Nsumba jijini
Mwanza, ulizuka mjadala juu
ya umuhimu wa Jihadi. Mmoja
kati wageni waalikwa alizusha
mjadala mkubwa wa kuwalaumu
wa s o m i wa n a o b e z a j i h a d i
akisema hapa namnukuu:
Kupinga, kubeza, au
kudhihaki jihadi ni ukafiri na
a nayef anya h ivy o an ain g ia
kwenye ukafiri. Wamezuka watu
na magazeti yao waliyoyapa
majina ya Allah, eti kazi yao ni
kuwabeza vijana wanaofanya hijra
sehemu mbalimbali duniani kwa
ajili ya jihadi hawajui Uislamu
utasimama kwa mambo matatu
(i) imani (ii) hijra (iii) jihadi?
Someni vizuri dini. Mwisho wa
kumnukuu.
Hoja katika mjadala haijawahi
kuwa Jihad na nafasi yake katika
Uislamu. Hakuna Muislamu
aliyetamka Shahada ambaye
atapinga Jihad. Kusema kuwa
kuna watu wanapinga Jihad ni
upotoshaji. Kinachohojiwa ni je,
wanayofanya Boko Haram, ni
Jihad?
Wiki iliyopita tuliambiwa kuwa
IS wamechinja watu 18, lakini
wameweka pia katika mtandao
wao cl i p ya video ambap o
wapiganaji wa IS wanaburura
maiti za watu waliowaua mitaani.
Wamefunga maiti katika pikipiki
k wa k a m b a n d e f u , h a l a f u
wanapita kwa kasi mitaani, maiti
zikibururwa nyuma ya pikipiki
huku watu wakisimama na
kushangaa. Swali ni je, haya ya
IS ni Jihad?
Kwa anayetaka kujua ukweli,
ushahidi upo wa kutosha kuwa
IS wanapewa mafunzo, pesa na
silaha kutoka Marekani na NATO,
na hata majeruhi wao wanatibiwa
katika hospitali za Israel. Na moja
ya picha katika mitandao na
magazeti ya Israel anaonekana
Waziri Mkuu wa Israel, Binyamin
Netanyahu akiwatembelea baadhi
ya majeruhi hao katika hospitali
za Israel.
Je, USA, NATO, Israel, inaweza
kusimama bega kwa bega na
Mujahidina kusimamisha Dola ya
Kiislamu?
Kama hilo linawezekana, basi
tungeona hilo likitokea Libya na
Afghanistan. Lakini walioitwa
wapiganaji wa Kiislamu,
walitumika kufanikisha malengo
ya mabeberu, sasa Libya ni vurugu
t u p u . M a b e b e r u wa n a v u n a
mafuta bila ya kuwa na serikali
madhubuti ya kuwadhibiti japo
walipe kodi.
Hivi kuwahamasisha watu
kuuwa na kupora mali za kafiri,
ndio Jihad? Wapi yanapatikana
mafundisho hayo katika Uislamu.
Abu Baghdadi anayedaiwa
kuwa Amir wa IS aliibukia katika
gereza la Bucca (biggest U.S.
detention camp in Iraq) mwaka
2009 alikokuwa akishikiliwa na
askari wa Marekani waliokuwa
Iraq. Siku alipoachiwa alimuaga
mkuu wa kambi ile, Col. Kenneth
King akimwambia, tutaonana

Hoja sio Jihad, tusipotoshe

WAZIRI Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.


New York (Ill see you guys in
New York).
Kamanda Kenneth King
anasema hakuwa ameelewa
alichomaanisha Abu Baghdadi
kwa wakati ule. Alikuja kuelewa
alipokuja kuona kuwa kapewa
tenda ya kuongoza ISIS walio
foot soldiers na intelligence
assets wa ubeberu wa Marekani
na Israel.
Pengine na sisi turudi nyuma
tutizame, hawa Akhiy wetu,
walio makamanda wetu na
wanaotuhimiza kuwa na AK-47
nyumbani, kama hatuna tuuze
TV tununue, wameibuka kutoka
wapi? Miaka mitatu, minne
hadi mitano nyuma, walikuwa
wapi? Tuvinjari mpaka kule
Mabatini, tuulize, ipi rekodi ya
maisha yao? Na pengine kama
tutaweza kufuatilia tutafute tujue,
walipopotea kwa muda, walikuwa
wapi kabla ya kuibuka wakiwa
wamezaliwa upya? Wamesoma
na kupata mafunzo haya ya Jihad
wanayotuhimiza kutoka wapi?
Mwenendo wa maisha ya
Mtume (s.a.w) ulijijenga katika
kile wataalamu wamekiita (six
C ) mambo sita yanayofasiri
mwenendo wa maisha
ambayo ni, kwanza, Concience
(dhamira ). Dhamir yao
iliwapelekea wakatulea katika
kile wanachokiamini. Dhamira
iliwaambia iko siku Uislamu
utasimama hivyo hawakukubali
kuvuka hatua moja kwenda
nyingine.
Mtume (s.a.w) alipokea
maagizo kutoka kwa Allah s.w
akayafundisha vilivyo ndani ya
miaka mitatu tena kwa siri katika
Darul- Arkamu ( nyumba ya
Arkamu ). Malengo na matarajio

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 2014

ya Mtume (s.a.w) ilikuwa ni


kuiona jamii siku moja ikitoka
kwenye giza totoro, na yeye
Mtume ( s.a.w) kapewa jukumu
la kuwawashia taa.
Hivyo ndivyo Mtume (s.a.w)
na maswahaba zake na dhamira
zao ziliwapelekaea kuwatoa watu
katika madhila makubwa. Kabla
hatujaingia kipengele cha pili,
tujitazame dhamira zetu sisi vijana
tunaohemkwa kupigana jihadi.
Hivi ni kweli kijana dhamira yako
imetulia kabisa kwamba familia
yako umeifundisha Uislamu na
wanaujua na kuufuata Uislamu
vizuri, sasa wanakiendea kila
kipengele cha maisha yao kwa
mujibu wa mafundisho ya Mtume
(s.a.w)? Wanachuma na kutumia
mali zao kama alivyofundisha
Mtume? Wanalala na kuamka
kama alivyofundisha Mtume?
Wanakula na kutembea kama
Mtume? Hawadhulumu katika
biashara na mengine kama hayo?
Ni muhimu sana kijana wa
Kiislamu kujiuliza maswali
h a ya k wa n i n d i v y o s i l s i l a
iliyowavukisha Mtume (s.a.w) na
maswahaba zake (r.a), vinginevyo
ni kuvuka hatua na kuvuka hatua
hasara zake ni kubwa katika jamii.
Ni hatua hii pekee iliyompelekea
Mtume (s.a.w) akamwandaa mtu
wa kuingia naye hatua ya pili.
Kijana wa Kiislamu, hebu vuta
hisia Mtume (s.a.w) kamfikisha
pahala Abubakari (r.a) yuko tayari
kutoa mali yake yote kwa ajili
ya Allah (s.w) hata alipoambiwa
na Mtume (s.a.w) anatakiwa
kuhama pamoja naye alionyesha
utayari wa hali ya juu. Kijana
wa Kiislamu, unanye Abubakari
wako wa kuhama naye? Angalia
Abubakari alivyoiandaa familia
yake Asmaa binti Abubakar
(r.a) anapeleka chakula pangoni
usiku anakutana na maadui
wanamtafuta Mtume (s.a.w) na

baba yake, wanamuuliza rejea


majibu aliyowajibu binti yule
alivyoandaliwa kwa silabasi ya
Mtume (s.a.w). Wewe unae Asmaa
wako ?
La pili nni Compassion
(Huruma) maandalizi hayo
yaliwapelekea wakaharumiana
kwa kiwango cha juu sana.
Hawakukubali kufanya jambo
lolote lenye kuleta maangamizi
katika jamii hata walipoingia
katika mapambano. Huruma
iliwapelekea wakachunga
mipaka katika mapambano.
Hawakuwadhuru wale
wasiohusika. Hayakuwagusa
wazee, watoto, wanawake na nk
Hawakuharibu miundo mbinu
yoyote. Sote ni mashahidi katika
hizi zinazodaiwa kuwa jihadi za
IS, Jabhat Islamia, Boko Haram
na watu kama hao, zinazoendelea.
K wa wa t u k u k o s a h u r u m a
tunashuhudia maangamizi
makubwa kwa watu wasiohusika.
Tunashuhudia uharibifu mkubwa
wa miundo mbinu. Hii ndiyo
tofauti kubwa kati ya jihadi ya
kweli na ile bandia, isiyokuwa na
dhamira nzuri wala malengo ya
Kiislamu.
Kuna kitu kinaitwa Couragekwa maana ya ushujaa au uthubutu.
Kwa vile walijiandaa vyema na
walihakikisha wanayepambana
naye ndio adui halisi wa Dini yao,
walionyesha ushujaa wa hali ya
juu lakini pia walifikia uwiano wa
wingi uliotajwa katika Kurani wa
mmoja kumi.
Jingine la muhimu ni
Consideration, yaani kufikiri
kabla ya kutenda. Mtume (s.a.w)
akiwa kwenye maandalizi , kila
akipima nguvu za waumini
anagundua bado siyo za
kupambana, aliwasubirisha.
Hata pale walipotokea baadhi ya
Waislamu wanataka mapambano,
bado aliwasubirisha kwani akiona
viwango bado kwa kulinganisha na
nguvu ya makafiri. Leo sisi vijana
tukiambiwa tufikiri vizuri hii jihadi
ya kurushiwa silaha na Amerika
akidai amekosea, tunaambiwa ina
lengo la kutufanya tujiangamize
wenyewe, tunaporomosha matusi,
kutukanana Waislamu kwa hoja
kuwa baadhi yetu wanapinga
jihad!
C nyingine inasimama kwa neno
Control, ikimaanisha kujidhibiti.
Pamoja na hali iliyowakabili
Waislamu wakati wa Mtume
ya kuteswa sana na makafiri,
walijidhibiti na kujizuiya hadi
walipoona kuwa sasa wanaweza
kuwakabili. Walizuiya mikono
yao wakabaki kuzidisha ibada
na Dawa kupata waumini wengi
zaidi.
Confidence, inamaana ya
kujiamini. Mtume (s.a.w) na
swahaba zake waliamini kwa
kufuata utaratibu wa mafundisho
ya Allah, iko siku kafiri atakuwa
chini na Uislamu utakuwa juu.
Na ndicho kilichotokea ndani ya
miaka 23. Sisi kwa kutokujiamini,
kijana una miaka arobaini, hata
siku moja hujawahi kuwaita
m a j i r a n i z a k o u k a wa a m b i a
kuhusu uzuri wa Uislamu, wala
maisha yako hayajawa kigezo
c h e m a k wa m a j i r a n i wa s i o
Waislamu waupende Uislamu
kwa tabia zako njema, utu na
uadilifu wako.

12

Barua/Mashair

UFISADI WA VIONGOZI AKAUNTI YA 'ESCROW'

Naanza kumhimidi, Mola wangu SUBHANA,


Yu pweke tena wahidi, aso mke wala mwana,
Mwenye aali weledi, kwa ghaibu na bayana,
UONGOZI ni DHAMANA, si TUNU ya UFISADI.
Insani hatuna budi, kutafakari kwa kina,
Kwa kila letu kusudi, la siri na la bayana,
La kinywa na la fuadi, si kunga kwa SUBHANA,
UONGOZI ni DHAMANA, si TUNU ya UFISADI.
Uongozi njema sudi, kwa anolenga 'ubwana'
Hukazana kwa juhudi, kukwepa nongo utwana,
Lengole ni kufaidi, si dhima kwa SUBHANA,
UONGOZI ni DHAMANA, si TUNU ya UFISADI.
Jambole kulisanidi, vyovyote atang'ang'ana,
Kwa uvumba au udi, ili liweze kufana,
Hata kama kwa kutadi, mipaka ya SUBHANA,
UONGOZI ni DHAMANA, si TUNU ya UFISADI.
Ahadi ataahidi, lukuki tena mwanana,
Keshoye huzikaidi, na nyingine huzikana,
Kuulizwa hana budi, na Allahu SUBHANA,
UONGOZI ni DHAMANA, si TUNU ya UFISADI.
Kitini hanayo budi, hugeuka kuwa 'bwana',
Husimika yake jadi, ya asili huikana,
Kwa kujitenga baidi, na mila ya SUBHANA,
UONGOZI ni DHAMANA, si TUNU ya UFISADI.

Hujali wake mradi, wa juzi, leo na jana,


Japo ni wa kifisadi, huhisi wa kiungwana,
Kwa ya kwake itikadi, u mwema kwa SUBHANA,
UONGOZI ni DHAMANA, si TUNU ya UFISADI.
'ESCROW' walofaidi, wang'oke kwenye dhamana,
Wafilisiwe nukudi, na mali walozivuna,
Na mwisho hapana budi, na kortini kuwabana,
SI TUNU YA UFISADI, UONGOZI NI AMANA.
ABUU NYAMKMOGI- MWANZA.

GAIDI NAMBARI 'WANI'!


Kalamu nimeishika, gaidi kumbaini,
Batini alofichika, mumtambue bayani,
Si mwingine Amerika, ukipenda marekani,
Gaidi nambari 'wani', duniani AMERIKA.
Kwa jahara huoneka,yuna kiu ya amani,
Kumbe yu gaidi fika, ukijasusi kwa ndani,
Kwa ngozi alojivika, muhali kumbaini,
Gaidi nambari 'wani', duniani AMERIKA.
Mipaka yuaivuka, hata ya ughaibuni,
Kwa majeshi kupeleka, ya vita ulimwenguni,
Katu damu kumwagika, hajutii ya insani,
Gaidi nambari 'wani', duniani AMERIKA.
Kwa 'ishuze' za kupika, dunia ameiwini,
Sasa yuaaminika, kwa kila anolibuni,
Dunia yaghururika, kwa puyaze kuamini,
Gaidi nambari 'wani', duniani AMERIKA.
Aula ikakumbuka, IRAQ alokibuni,
Katu hazikuoneka, silaha alozibuni,
Kwalo ikighafilika, atazidi kuiwini,
Gaidi nambari 'wani', duniani AMERIKA.
Kwa sasa yuaibuka, na la tenge tahanani,
Yu tena akurupuka, kwa kunadi hadharani,
Si jingine kwa hakika, la Syria tambueni,
Gaidi nambari 'wani', duniani AMERIKA.
Eti yuna uhakika, na ushahidi mezani,
Bilhaki kwa hakika, kwayo mimi siamini,
Kwa la IRAQ kupika, yu bado mwamuamini?
Gaidi nambari 'wani', duniani AMERIKA.
IRAQ alitamka, tena kwa kujiamini,
"Ndanimwe zimefichika, silaha ziso kifani",
Na nembo kuzipachika, "za hilaki kwa insani",
Gaidi nambari 'wani', duniani AMERIKA.
Ikaja kubainika, kwa ukaguzi makini,
Kwa wakaguzi kuweka, mambo yote hadharani,
"Adaicho Amerika,sicho tulokibaini",
Gaidi nambari 'wani', duniani AMERIKA.
Mara akawakiuka, kwa wake ufirauni,
Kwa majeshi kupeleka , angani na ardhini,
Umma ukahujumika, kwawo wake 'uhaini',
Gaidi nambari 'wani', duniani AMERIKA.
Wanawake kwa hakika, wakahiliki vitani,
Na watoto kadhalika, pasi na kosa jamani,
Namba 'wani' nikimweka, yu gaidi ni kosani?,
Gaidi nambari 'wani', duniani AMERIKA.

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 2014

Wataalamu wa kupambana
na magaidi watatuangamiza
Inatoka Uk 10

hayo. Na zaidi ripoti


inasema:
Some of th e p e op le
targeted suffer from mental
illness or financial problems.
It said they were given the
motive and the means to
commit crimes they might
never have ever considered.
N a r i p o t i ya H RW
inanukuu kesi mbili
ambapo baada ya Majaji
kusikiliza kesi na ushahidi
uliowasilishwa na FBI,
walikuwa na haya ya
kusema:
of one suspect, that
only the government could
have succeeded in making a
terrorist out of him -- because
his "buffoonery is positively
Shakespearean in scope
."The government came up
with the crime, provided
the means, and removed all
relevant obstacles."
Hawa ni Majaji wa
N e w Yo r k k a t i k a i l e
kesi mashuhuri ambapo
vijana wanne Waislamu
walituhumiwa kutaka
kudungua ndege ya kijeshi
na kulipua synagogue la
Wayahudi.
Kama hawa ndio
wataalamu wanaowapa
mafunzo ATPU wetu,
tutawaamini vipi polisi wa
Kenya katika zile habari
zao kuwa wamekamata
silaha msikitini.
Tutawaamini vipi ATPU
wakituambia kuwa
magaidi wameuwa abiria
Wakristo 28. Kwanini
tusiwe na wasiwasi kuwa
yaweza kuwa ni moja ya
zile Sting Operations.
Tu f a h a m u k u wa
kwa mtindo huu
unaozungumzwa katika
ripoti ya Human Rights
Wa t c h , k wa m b a : T h e
government came up with the
crime, provided the means,
and removed all relevant
obstacles", huenda ndio
unaosababisha leo Nigeria
kuzama katika tope la
Boko Haram, lakini ndio
pia utakaoitosa Kenya, na
sisi huku iwapo tutafuata
nyayo.
Yapo maneno hapa
ya n a t a k a k u t a f a k a r i
kwa kina kidogo. Hebu
yasome. Human Rights
Watch wanasema:
Some of th e p e op le
targeted suffer from mental
illness or financial problems.
It said they were given the
motive and the means to
commit crimes they might
never have ever considered.
Ambapo maana yake
ni kuwa hawa marafiki
zetu na wataalamu
wetu wa kutegemewa
katika kupambana
na ugaidi, moja ya
m b i n u wa n a z o t u m i a

ni kuwatafuta vijana
maadhura walio
punguwani kidogo, kama
wavuta bangi vile na
wenye matatizo ya kipesa.
Hawa hujazwa fikra za
ugaidi, kulipua mabomu
na Jihad feki halafu
ndio baadae hukamatwa
ikadaiwa kuwa ni magaidi
Waislamu.
Sasa kwa mtindo huu,
kama tutakwenda na
mtiz a m o k uwa ha wa
vijana ndio maadui hatari
wa amani ya nchi yetu,
kadiri tutakavyofanya
operesheni
za
kuwakamata na kuwatesa,
haitatusaidia sana.
Haitatusaidia kwa sababu
tuta kuwa tunahangaika

na majani, wala si matawi


tukiacha shina na mizizi
yake ikiendelea kunawiri
na kuzalisha matawi zaidi
na zaidi. Vijana maadhura
na wenye shida ya pesa
wataendelea kuwepo.
Tusipohangaika na huyu
anayewatumia katika
Sting Operations zake,
kinyume chake tukamfanya
ndio wa kutusaidia katika
kupambana na magaidi,
itakuwa sisi, kwa maana ya
serikali na vyombo vyake
vya dola pamoja na wale
watuhumiwa wa ugaidi,
wote tutakuwa sawa tu
mbele ya mabeberu hawa.
Tutakuwa tunatumiwa na

kufadhiliwa kila mmoja


kwa namna yake, lakini
kwa kutimiza lengo lile
lile. Kupandikiza ugaidi
na kuleta machafuko
katika nchi zetu kwa
manufaa ya mabeberu.
Yapo maneno mengine
ya kuzingatia sana katika
ile ripoti ya HRW. Sikiliza
inavyosema katika
kipande hiki cha ripoti:
In many of the sting
operations we examined,
informants and undercover
agents carefully laid out
an ideological basis for a
proposed terrorist attack, and
then provided investigative
targets with a range of options
and the weapons necessary to
carry out the attack. Instead
of beginning a sting at the
point where the target had
expressed an interest in
engaging in illegal conduct,
many terrorism sting
operations that we investigated
facilitated or invented the
target's willingness to act
before presenting the tangible
opportunity to do so."
Leo ukisikia kwa mfano
anasimama mtu, Ustadh/
Sheikh msikitini anahimiza
watu kuwa na silaha kwa

a j i l i ya k u p a m b a n a n a
makafiri au Wakristo au
hata kwenda Somalia, mtu
huyu anasimama katika
misikiti miwili, mitatu na
a n a d u m u k wa m a s i k u
kadhaa, bila ya vyombo
husika kuchukua hatua,
kwa nini Waislamu wasiwe
na wasiwasi kuwa ni katika
zile zile mbinu za marafiki
zetu FBI za dubious
entrapment? Rejea ile ripoti
ya HRW iliposema: The
government came up with the
crime, provided the means, and
removed all relevant obstacles."
Kama walivyosema HRW,
Sting Op erations hizi

ndio zinapandikiza ugaidi.


Pili, zinawatia uhalifu
Waislamu ili serikali
ipate kuwahujumu. Na
tatu, inawachonganisha
na wananchi wenzao wa
dini nyingine na hatimaye
kuleta machafuko katika
nchi.
Kufuatia tukio la
kuuliwa abiria 28
Wakristo, Rais Uhuru
Kenyatta amesema kuwa
waliofanya mauwaji hayo
wanalenga kuleta vita ya

kidini baina ya Waislamu


na Wakristo. Kwa muda
mrefu, Kenya imekuwa
mshirika wa karibu wa
vyombo ya usalama vya
Marekani katika kupambana
na ugaidi kuliko ilivyo
Tanzania. Washirika hao
ndio wanaowapa mafunzo
na kuwafadhili ATPU. HRW
nao wanatuambia kuwa
washirika na marafiki
h a o wa K e n ya k a t i k a
kupambana na ugaidi,
kawaida yao ni kupandikiza
ugaidi ili kuwanasa magaidi
na hufanya mambo ambayo
yanaleta uhasama baina ya
Waislamu na Wakristo.
Kauli ya Rais Kenyatta na
ile ya Makamu wake William
Ruto, haitawasaidia Wakeya

kubaki salama kama


ambavyo ile ya Goodluck
Jonathan na mabilioni ya
Dola anayopewa kutoka
Washington, haijasaidia
Nigeria hadi sasa
kuondokana na k itisho

cha Boko Haram.


Kenya kulikuwa na
migogoro sugu ya kikabila
kutokana na suala nyeti
la ardhi, lakini sio hii ya
kidini na ugaidi. Wajitizame
upya kwa makini. La
kama wamekubali kuwa
sehemu ya Dubious
Entrapment Arrests na Sting

Operations za ki-FBI,
hakuna wa kuwasaidia
wala wasitafute mchawi.

13

TANGAZO

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 2014

Bismillahir Rahmanir Rahiim

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE


NAFASI ZA KIDATO CHA KWANZA 2015

Waislamu kote nchini mnatangaziwa nafasi za kidato cha Kwanza kwa shule zifuatazo:
Mkuzo Islamic High School - Bweni tu - SONGEA
Kirinjiko Islamic Sec. School - Bweni tu SAME - KILIMANJARO
Nyasaka Islamic Sec.School - Bweni tu - MWANZA
Ubungo Islamic High School - Kutwa tu DAR ES SALAAM

1. Shule hizi ni za Kiislamu, zenye lengo la kuwapa watoto elimu bora na kuwalea kwa malezi mazuri ya Kiislamu.
2. Masomo yanayofundishwa ni haya yafuatayo:
Elimu ya Dini ya Kiislamu, Usomaji Quran na mafunzo yake, Hadithi za Mtume(s.a.w), Lugha ya Kiarabu, Kiswahili, English, Basic Mathematics, Physics, Chemistry, Biology, Geography,
History, Civics, Book keeping na Commerce.
3. Patakuwa na mtihani tarehe

29/11/2014 saa2:00asubuhi katika vituo mbali mbali kote nchini. Muombaji anaweza kufanyia mtihani katika kituo chochote.

4. Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 28/11/2014.


5. Fomu za Maombi zinapatikana kwa gharama ya shilingi 10,000/= katika vituo vilivyoorodheshwa hapa chini.
6. Pia, fomu zinapatikana kwenye Tovuti: www.ipctz.org. Ikumbukwe kuwa atakayepata fomu kupitia tovuti (download) atatakiwa kulipia wakati wa kurejesha siku ya mtihani.

Arusha

- Ofisi ya Islamic Education Panel, Jambo Plastic, Ghorofa ya 2 mkabala na


msikiti Mkuu Bondeni : 0763 282 371/ 0783552414.

Kilimanjaro

- Moshi: Msikiti wa Riadha : 0654 723 418.


- Same Juhudi Studio mkabala na Bank ya NMB Same: 0757 013344.
- Same: Kirinjiko Islamic Secondry School: 0784 296424/0655 697 075
- Usangi- Falhum Kibakaya : 0787 142054.
- Ugweno Kifula Shopping Centre- Yusuph Shanga : 078458776.

Tanga

- Twalut Islamc Centre Mabovu Darajani : 0715 894111/0789 410914.


- Uongofu Bookshop: 0784 982525
- Korogwe: SHEMEA SHOP : 0754 690007.
- Mandia Shop - Lushoto: 0782257533.


Mwanza

- Nyasaka Islamic Secondary School : 0717 417685/0786 417685.


- Ofisi ya Islamic Education Panel Mtaa wa Rufiji mkabala na Msikiti Al-Amin 0785 086 770.

Musoma - Ofisi ya Islamic Ed Panel -Mtaa wa Karume,Nyumba Na. 05 : 0784721015/0765024623


Kagera
- Bukoba: Alhuda Caf Kwa mzee Kinobe karibu na ofisi za TRA. : 0684 701175.
Shinyanga
- Msikiti wa Majengo karibu na Manispaa ya Shinyanga Mjini :0752180426
- Kahama ofisi ya AN NUUR Karibu na msikiti wa Ibadhi : 0753 993930.

Dar es Salaam
- Ubungo Islamic High School : 0712974428/0712033556.
- Ofisi ya Islamic Ed. Panel Temeke -Msikiti wa Nurul Yakin : 0655144474.
Morogoro
- Wasiliana na Ramadhani 1
Chale : 0715704380.
Dodoma
- Hijra Islamic Primary School : 0716 544757/0718 661992.
Singida
- Ofisi ya Islamic Education. Panel karibu na Nuru snack Hotel : 0786 425838/0784 928039.
Manyara - Ofisi ya Islamic Ed. Panel Masjid Rahma: 0784 491196

Kigoma

Lindi

Mtwara

- Amana Islamic S.S: 0715 465158/0787 231007.

Songea

- Kwa Kawanga Karibu na Msikiti wa NURU : 0713249264/0683670772.


- Mkuzo Islamic High School : 0717348375.

Mbeya

- Ofisi za Islamic Education Panel Uhindini 0785425319.

- Msikiti wa Mugera Mwandiga: 0714 717727.


- Kibondo Islamic Nursery School: 0784 442860.
- Kasulu: Murubona Isl.SS: 0714710802.

- Wapemba Store: 0784 974041/0783 488444/0653 705627.

- Rexona Video mkabala na Mbeya RETICO: 0713 200209/0785425319.


Rukwa

- Sumbawanga: Masjid TAQWA: 0717082 073.

Tabora

- Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784 944566.

Iringa

- Madrastun Najah: 0714 522 122.

Pemba

-Wete: Wete Islamic School : 0777 432331/0712772326.

Unguja
- Madrasatul Fallah: 0777125074.
Mafia
- Ofisi ya Ust. Yusufu Ally jirani na msikiti mkuu : 0773580703.
Handeni - Nassoro Mafiga: 0782 105735/ 0657 093983

USIKOSE NAFASI HII ADHIMU WAHI KUCHUKUA FOMU SASA!


MKURUGENZI
WABILLAH TAWFIIQ

14

Makala

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 2014

Chimbuko la maradhi ya kisukari ni chakula kisichofaa


Na Juma Kilaghai

CHAKULA ambacho ni bora


kabisa kwa mtu mmoja,
kinaweza kuwa sumu baridi
kwa mtu mwingine, na kumletea
madhara endelevu katika maisha
yake. Kwa muktadha huu basi,
hakuna chakula bora kwa kila
mtu! Chakula ni bora kwa mtu
kama baada ya kukitumia mwili
utakipokea vizuri, ukafyonza
virutubisho, na kikasaidia
kuimarisha afya ya mlaji.
Ni vigumu kujua aina ya
chakula inayokufaa, bila kujua
jinsi mwili wako unavyochakatua
c h a k u l a . K i m s i n g i wa t a f i t i
wamebaini makundi makuu
m at at u ya watu k uh us ian a
na jinsi miili inavyochakatua
chakula. Kundi la kwanza ni la
wachakatuaji wa protini. Hawa
miili yao inakubaliana zaidi na
vyakula vya protini. Kwa watu wa
kundi hili vyakula vya wanga, na
hususan vile vilivyochakatuliwa
n a k u c h u j wa k wa k i wa n g o
kikubwa (highly processed and
refined), ni sumu baridi ambayo
itawapelekea kuugua maradhi
mengi ya kimfumo.
Kundi la pili ni la wachakatuaji
wa wanga. Hawa miili yao
inakubaliana zaidi na vyakula
vya wanga. Kwa watu wa kundi
hili vyakula vya protini, na
hususan vile vilivyochakatuliwa
na kuhifadhiwa kwa ajili
ya kuwa na muda mrefu wa
matumizi, ni sumu baridi ambayo
itawapelekea kuugua maradhi
mengi ya kimfumo. Kundi la tatu
ni la wachakatuaji wa vyakula vya
protini na wanga kwa viwango
sawa. Kundi hili kidogo lina
bahati kwa maana halidhuriwi
kwa wepesi na vyakula vilivyoko
katika yale makundi mawili ya
mwanzo.
Moja ya magonjwa
yanayosababishwa na
mkanganyiko huu katika kula ni
ugonjwa wa kisukari. Mchakatuaji
wa protini anapokula chakula cha
wanga, kasi ya kuchakatua wanga
huo ni kubwa mno ikilinganishwa
na mlaji mwenzake ambaye ni
mchakatuaji wa wanga. Kasi hiyo
hupelekea kiwango cha sukari
kinachoingia katika mzunguko wa
damu ndani ya muda mfupi kuwa
kikubwa sana. Kutokana na hali
hii kongosho hulazimika kufanya
kazi ya ziada kuzalisha kiwango
kikubwa cha insulin (homoni ya
kuondoa sukari kwenye damu
na kuipeleka kwenye seli ili
itumike kutengenezea nishati),
ili kukabiliana na ongezeko hilo.
Hali hii ikijirudia rudia mara
kwa mara kongosho huchoka
na kuanza kufanya kazi chini ya
kiwango; au wakati mwingine
vipokezi vya sukari katika seli
(receptors) hushindwa kuendana
na kasi ya kuletewa sukari kwa
ajili ya matumizi ya seli, na

huishia kuikataa sukari hiyo.


Hali hii kitaalamu hujulikana
kama insulin resistance, au
pingamizi dhidi ya insulin kwa
tafsri isiyo rasmi. Kuna baadhi ya
nyakati yote mawili hutokea kwa
wakati mmoja, yaani kongosho
linafanya kazi chini ya kiwango,
na pia mgonjwa anakabiliwa na
pingamizi dhidi ya insulin.
Hivi karibuni imebainika
kuwa moja ya sababu kubwa
sana zinazopelekea vipokezi vya
seli vikashindwa kupokea sukari
inayoletwa ni uvimbe mwako
(inflammation). Vichocheo vya
kusababisha uvimbe mwako
kwenye seli viko vingi lakini baadhi
ya hivi ni vyakula tunavyokula
kila siku. Vyakula hivi ni pamoja
na sukari, wanga uiliochakatuliwa
kwa kiwango kikubwa, na mafuta
ya mbegu (alizeti, ufuta, karanga,
pamba, mawese, nakadhalika)
yanapotumiwa kwa ajili ya
kupikia. Sababu nyingine ni
maambukizi ya vimelea vya
maradhi mbalimbali.
Wataalamu wameyagawanya
magonjwa ya kisukari katika
makundi makuu matatu. Makundi
haya ni:
1. Kisukari cha aina ya kwanza
(type 1 diabetes). Hiki ni kisukari
kinachojitokeza mapema (kwa
kawaida kabla ya mtu kufika
miaka 40), mara nyingi ikiwa ni
katika kipindi cha utoto na ujana
wa chini ya miaka 20. Katika aina
hii ya kisukari mwili wa mhusika
unaacha kuzalisha kabisa homoni
ya insulin na hivyo kumlazimu
mgonjwa kuishi kwa kudunga
sindano za insulin kila siku.
2. Kisukari cha aina ya pili (type
2 diabetes). Kiashiria kikubwa
katika aina hii ya kisukari ni
kwamba mwili hauzalishi insulin
ya kutosheleza mahitaji, au
vipokezi (receptors) vya sukari
katika seli havifanyi kazi kwa
kiwango kinachotakiwa. Zaidi ya
asilimia 90 ya wagonjwa wote wa
kisukari duniani wanaugua aina
hii ya kisukari.
3. Kisukari cha ujauzito
(gestational diabetes). Hiki ni
kisukari kinachowakumba baadhi
wanawake pale wanapokuwa
wajawazito. Wakati wa ujazito
baadhi ya wanawake huwa na
kiwango kikubwa cha sukari
kwenye mzunguko wa damu
kuliko inavyotakiwa na wanaweza
wakalazimika kutumia matibabu
ili wasidhurike. Kutotambua
kuweko kwa kisukari hiki na
kukitibu kunaweza kusababisha
matatizo wakati wa kujifungua.
Moja ya madhara ya aina hii
ya kisukari ni kuzaliwa watoto
wenye miili mikubwa kuliko
kawaida.
Kisukari ni ugonjwa unaotisha.
Ni ugonjwa unaotisha kutokana
na sifa zake. Sifa hizi ni pamoja na
kutokuwa na dawa ya uhakika,
kumlazimisha mgonjwa abadilishe

mwenendo wake wa maisha


kwa kiasi kikubwa, kusababisha
mlolongo wa madhara mengine
kibao ya kiafya ndani ya mwli,
kuongeza gharama za maisha kwa
mgonjwa, na ile hali ya kugeuka
kuwa janga la kijamii.
Tunasema kisukari hakina dawa
ya uhakika kwa kuwa ulimwengu
wa tiba za kisasa umeshindwa
kuja na dawa za aina hiyo hadi
sasa. Dawa zilizoko ni zile za
kumsaidia mgonjwa kushusha
sukari iliyolundikana kwenye
damu yake, ili iende katika
viwango vinavyokubalika. Hata
hivyo historia inaonyesha kuwa
baadhi ya dawa hizi siyo salama,
na hatima yake zinamsababishia
mtumiaji madhara mengine
ya kiafya ikiwa ni pamoja na
kumwongezea uwezekano wa
kupoteza maisha.
Avandia (rosiglitazone) ni moja
ya dawa hizo. Mauzo ya dawa
hii ambayo enzi zake ilikuwa ni
moja ya dawa maarufu sana za
kifamasia kwa ajili ya ugonjwa
wa kisukari, yalifikia kiasi cha
dola za Kimarekani bilioni 3.2
mnamo mwaka 2006. Baada ya
hapo ziliibuka taarifa za kitafiti
k wa m b a d a wa h i i i l i k u wa
inasababisha madhara makubwa
ya kiafya kwa mtumiaji kama vile
ongezeko la hatari ya shambulizi
la moyo (heart attack), wepesi wa
kuvunjika mifupa na hususan
ile ya mikononi juu ya kiwiko,
uharibifu wa macho, kiharusi
na uharibifu wa ini kutokana na
ongezeko la sumu. Inakadiriwa
kuwa ndani ya Marekani peke
yake kati ya mwaka 1999 na
mwaka 2006 dawa hii ilisababisha
mashambulizi ya moyo (heart
attacks) na vifo kati ya 60,000 na
200,000.
Japokuwa baadhi ya matatibu
wa dawa za asili na zile za
tiba mbadala wanadai kuwa
wanatibu ugonjwa huu, madai
haya yanapaswa kuchukuliwa
kwa tahadhari. Ni kweli kuwa
mtu anaweza kuwa na dawa ya
kuondoa sababu moja au zaidi

ya kisukari na hivyo kumsaidia


mtumiaji kuondokana na dalili
zote za ugonjwa huo. Hata hivyo
hii haina maana kwamba dawa
hiyo itamtibu kila mgonjwa
wa kisukari. Kwa kifupi ni
kwamba kundi la wenye kisukari
kilichosababishwa na sababu
zinazoguswa na dawa husika
watapona, na wengine wenye
kisukari kilichosababishwa na
sababu zisizoguswa na dawa hiyo
hawatapona.
M a z o e a ya n a t a b u s a n a .
Tulio wengi hatuli chakula kwa
kuzingatia kanuni za afya bali
tunakula kwa ajili ya mazoea
na kulenga ladha. Mgonjwa
wa kisukari mwenye nia ya
kuidhibiti hali hiyo analazimika
kuachana kabisa na kula kwa
mazoea na kulenga ladha.
Anatakiwa ajue kuwa vyakula
vyote vya wanga, na hususan vile
vilivyochakatuliwa kwa kiwango
kikubwa, vina madhara makubwa
kwake na anatakiwa kuviendea
kwa tahadhari kubwa. Hali hii
huwa ni chanzo kikubwa cha
kufadhaika kwa baadhi ya watu
ambao wamepata ugonjwa wa
kisukari. Baadhi yao huuliza kwa
ghadhabu : sasa utakula nini???!
na kuendelea kula vyakula vyao
walivyozoea huku wakisaidiwa
kisaikolojia na kimwili na vidonge
wanavyopewa hospitalini na
madaktari wao. Waathirika wengi
wa madawa kama avandia ni wale
wanaoangukia katika kundi hili.
Kisukari pia kinatisha kwa
kuwa kinasababisha mololongo
wa matatizo mengine kibao
ya kiafya. Matatizo haya ni
pamoja na uharibifu wa macho
unaotambulishwa na magonjwa
kama glaucoma (uharibifu wa
neva za jicho), cataracts (ukungu
kwenye lenzi ya jicho), retinopathy
(uharibifu mkubwa katika retina
ya jicho), nakadhalika. Matatizo
ya miguu yanayotambulishwa
na magonjwa kama neurapathy
(maumivu yatokanayo na
uharibifu wa mishipa ya
Inaendelea Uk. 15

15

MAKALA/TANGAZO

AN-NUUR

SAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 2014

Chimbuko la maradhi ya kisukari ni chakula kisichofaa


Inatoka Uk. 14

fahamu), ulcers (vidonda sugu),


g a n g r e n e ( m k u s a n y i k o wa
tishu zilizokufa kutokana na
kutofikiwa na mzunguko wa
damu), nakadhalika. Matatizo
mengine ni yale ya magonjwa ya
ngozi na magonjwa ya moyo.
Faraja ya ugonjwa wa sukari
ni kuufatilia kwa makini. Hii ina
maana kuwa ni muhimu kufanya
kipimo kila siku, ikiwezekana
hata mara mbili au tatu kwa siku.
Kutokana na hali hii gharama za
kuufuatilia ugonjwa huu ni kubwa
na huathiri kwa kiasi kikubwa hali
ya kiuchumi ya mgonjwa. Kwa
mfano tu, hivi sasa katika zahanati
na vituo vingi vya afya, gharama
za kupima kisukari kwa mara
moja ni kati ya shilingi 2,000.00 na
shilingi 2,500.00. Unapomwambia
mtu apime mara tatu kwa siku
maana yake atumie kati ya shilingi
6,000 na shilingi 7,500.00 kila siku!
Mwisho kisukari kinatisha
kwa sababu taratibu kinaonekana
kunyemelea hadhi ya kuwa ni
janga kubwa sana la kijamii.
Katika pande zote za dunia
kisukari kinaongezeka badala
ya kupungua. Kwa mujibu wa
Shirika la Afya Duniani, dunia
inatarajiwa kuwa na wagonjwa wa
kisukari 366,000,000 mwaka 2030
kutoka wagonjwa 171,000,000
waliokuwepo mwaka 2,000. Hili ni
ongezeko la aslimia 53! Tanzania,
ambayo mwaka 2,000 ilikuwa na
wagonjwa 201,600 inatarajiwa
kuwa na wagonjwa 605,000
mwaka 2030, ikiwa ni ongezeko
la 66.7%
Hata hivyo janga la kisukari
linaoonekana kuzikumba zaidi
zi l e nchi ambazo raia wao
wanapendelea mno vyakula vya
wanga katika mitindo tofautisoda, pasta, doughnut, keki,
mikate, lambalamba, nakadhalika.
Nchi kama Italy uwiano kati ya
Wataliano wanaoumwa kisukari
n a wa l e a m b a o h a wa u m w i
ni 1:14!. Inawezekana sababu
kubwa ikawa ni piza, pasta
na spaghetti. Hivi ni vyakula
vinavyotengenezwa kwa ngano
na Wataliano wanavifakamia kwa
wingi.
Marekani uwiano wao ni 1:17. Hii
nayo ni jamii ambayo imelogewa
soda, doughnut, chips, pizza,
na vyakula vingine vya wanga
vilivyochakatuliwa kwa kiwango
cha juu. India uwiano wao ni 1:39.
Hawa nao ni mabingwa wa vitu
vitamu. Wahindi ni wafakamiaji
wa tamutamu za kila aina na sifa
kuu ya tamutamu hizi ni wingi wa
sukari, ngano, mafuta na rangi.
Ta n z a n i a i n a u w i a n o wa
1:238. Huu ni uwiano mzuri
sana ukilinganisha na nchi
tulizotangulia kuzitaja. Sababu
ya uwiano huu mzuri ni nini
wakati kimsingi sehemu kubwa ya
Watanzania ni wala wanga zaidi
kutokana na hali zao za kiuchumi?

Nadhani sababu kubwa ni ukweli


kwamba Watanzania wengi ni
wakaazi wa vijijini na kimsingi
pamoja na kwamba sehemu
kubwa ya chakula chao ni wanga,
lakini kutokana na sababu za
kiuchumi, wanalazimika kuula
wanga huo katika mfumo ambao
haujachakatuliwa.
Kuepukana na ugonjwa wa
kisukari ni muhimu kufanya
kipimo cha kutambua aina ya
mwili wako katika kuchakatua
v ya k u l a ( m e t a b o l i c t y p i n g
test) na iwapo utagundulika
kuwa wewe ni mchakatuaji wa
protini, haraka uchukue hatua
za kupunguza kwa kiwango

kikubwa ulaji wa wanga, na hasa


ule ambao umechakatuliwa kwa
kiwango kikubwa. Nafasi ya
wanga (kwa ajili ya kuzalisha
nishati ya matumizi ya mwili)
ichukuliwe na mafuta bora ya
kula nazi, siagi, samli, zaituni.
Nafasi ya wanga kwa ajili ya
kujaza tumbo ichukuliwe na
mboga mchanganyiko za majani,
na pale ambapo uwezekano upo,
sehemu kubwa ya mboga hizo iwe
mbichi (salad). Mafuta ya kawaida
(yale tuliyoyazoea) tunaweza
kuendelea kuyatumia (siyo kwa
kupikia) bali kwa kupambia saladi
(salad dressing).
Aidha kama wewe tayari ni

mgonjwa wa kisukari, utanufaika


s a n a k wa k u o n d o a wa n g a
uliochakatuliwa katika orodha
ya vyakula vyako na ukaingiza
wanga ambao haujachakatuliwa,
tena kwa kiwango kidogo sana
kama mbadala wake. Kwa ajili ya
kuupatia mwili nishati punguzo
hilo la wanga lichukuliwe na
ongezeko la mafuta bora ya kula
nazi, siagi, samli, na zaituni. Aidha
nafasi ya kushiba ichukuliwe
na wingi wa mchanganyiko wa
mboga za majani, ikiwezekana
sehemu kubwa ya mboga hizi iwe
mbichi (salad).
Kama ilivyo kwa yule
anayelenga kukwepa kuugua
kisukari, mafuta ya kawaida (yale
tuliyoyazoea) tunaweza kuendelea
kuyatumia (siyo kwa kupikia) bali
kwa kupambia saladi. Ushauri
huu kuhusu mafuta ni kinyume
kabisa na ushauri mnaopatiwa na
madaktari wenu kuhusu mafuta
ya kula. Hata hivyo kisayansi ndio
ushauri sahihi. Mungu akipenda
post yetu ijayo itazungumzia
jambo hili kwa kina ili kuliweka
katika mazingira ya kueleweka
zaidi.
Herbal Impact
1574/144 Mosque Street,
Kitumbini, Dar es Salaam.
P.O. Box 70949, Dar es Salaam,
Tanzania.
Tel: +255 (22) 2134757
Mobile: 0754281131/065528113
1/0779281131/0686281131
E-mail: enterprisesnovel@
yahoo.com.

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE

NAFASI ZA KUJIUNGA NA KOZI FUPI YA UALIMU


KATIKA VYUO VYA UBUNGO NA KIRINJIKO-2015
Sifa na masharti ya kujiunga
Muombaji atimize sifa na masharti yafuatayo:
(i) Awe Muislamu aliye tayari kuishi Kiislamu
(ii) Awe anajua kusoma Quran kwa ufasaha.
(iii) Awe amemaliza juzuu ya 1 na 2 ya Maarifa ya Uislamu, Darasa la Watu
Wazima kabla ya kujiunga.
(iv) Awe na uwezo wa kusoma na kuandika lugha ya Kiswahili kwa ufasaha.
(v) Awe amehitimu darasa la saba au kidato cha nne na awe anafundisha
madrasa au kipindi cha dini katika shule za Msingi au Sekondari.
Patakuwa na usaili na mtihani siku ya tarehe 29/11/2014 saa 2:00 asubuhi
katika chuo cha Ubungo na Kirinjiko na katika vituo mbalimbali vya mitihani kote
nchini.
Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 28/11/2014.
Fomu inalipiwa shilingi 5,000/- tu.
Fomu zinapatikana katika vituo vilivyoorodheshwa ukurasa wa 13 wa gazeti hili.
MKURUGENZI

AN-NUUR

16
16

16

MAKALA

SAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 2014

AN-NUUR

Soma
gazeti la
AN-NUUR kila Ijumaa

SAFAR 1436, IJUMAA NOVEMBA 28-DES. 4, 2014

Hujuma kwa Waislamu zazidi kupamba moto


Maduga aachiwa kwa masharti
Alidaiwa kufadhili magaidi Moro
Atakiwa kuripoti polisi miaka 2

Na Bakari Mwakangwale
MWENYEKITI wa Taasisi
ya Kiislamu ya DaarulHijra ya Mjini Morogoro,
S h e i k h Wa z i r i A m a n i
Maduga, ameachiwa huru
na Mahakama ya Wilaya
ya Morogoro baada ya
kukamatwa kwa tuhuma
za Ugaidi.
Mbali ya Sheikh
Maduga, pia Mahakama
hiyo imewaachia Waislamu

wengine wanne, Jumatatu ya


wiki hii ambao walikamatwa
pamoja naye mapema wiki
iliyopita wakiwa katika
shughuli zao mjini huo.
Hatua hiyo imefikiwa
na Mahakama hiyo, baada
ya upande wa mashitaka
(Serikali) kuieleza
Mahakama kuwa Waislamu
hao sio washitakiwa bali ni
wajibu maombi.
Akiongea na An nuur,
Amir wa Baraza Kuu
la Jumuiya na Taasisi za

Kiislamu, Mkoani humo,


Sheikh Ayoub Salim
Muwinge, alisema taarifa
kutoka Mahakani hapo
zilieleza kuwa, upande wa
mashitaka unawatuhumu
Wa i s l a m u h a o k wa
kujihususha na Magaidi,
kwa kuwahifadhi na kuwapa
msaada wa kifedha.
Tuhuma zao zinahusishwa
na masuala ya Ugaidi, lakini
katika maelezo yao upande
wa mashitaka wamesema
kwamba si washitakiwa

Watuhumiwa ugaidi, kesi yaanza Mahakama Kuu Dar


Sheikh Mselemu azushiwa kifo!

Na Seif Msengakamba
KESI dhidi ya watuhumiwa
wa ugaidi ambayo awali
iliwasilishwa katika
Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu kwa zaidi
ya mwezi mmoja uliopita,
imefikishwa Mahakama
Kuu ya Tanzania Jumatatu
wiki hii Novemba 24 ikiwa
chini ya Jaji Twaibu Faudhi.
Hata hivyo kesi hiyo
imeahirishwa hadi Desemba
4 mwaka huu, baada ya
mawakiliwa wa upande wa
Jamhuri kuiomba mahakama
hiyo kuwapa muda wa
kuleta majibu ya maombi
yaliyoletwa na upande wa
utetezi katika mahakama
hiyo.
Jaji Faudhi alikubaliana na
hoja ya upande wa Jamhuri
na kuwaamuru kuleta majibu
yao Novemba 28.
Wakili wa upande wa
utetezi, Abubakari Salim,
alimwelezea mwandishi
wa gazeti hili baada ya
kuahilishwa kwa kesi hiyo
kuwa, upande wa Jamhuri
ulioongozwa na wakili
Peter Njike, awali waliomba
kupewa muda zaidi wa
kuleta majibu ya maombi
ya u p a n d e wa u t e t e z i
yaliyowasilishwa mahakami
hapo.
Wamepewa tarehe 28
Novemba walete majibu
yao na sisi kama tuna hoja
za nyongeza, tumetakiwa
kuleta Desemba 1 na shauri
litasikilizwa Desemba 4
mwaka huu. Alisema Wakili

SHEIKH Mselem (katikati).


huyo.
Wa k a t i k e s i ya
watuhumiwa hao wa
ugaidi ikianza kusikilizwa,
kulikuwa na taarifa
z i l i z o k u wa z i m e z a g a a
katika mitandao ya simu
kuwa Sheikh Mselem Ali
Mselem amefariki.
Uzushi huo uliibuka
siku ya Jumanne, ikiwa
ni siku moja baada ya
watuhumiwa hao, akiwemo
Sheikh Mselem kurejeshwa
rumande kutoka Mahakama
K u u a m b a p o k e s i ya o
ilikuwa ikisikilizwa.
Taarifa hizo zilikuwa
zikisambazwa kwa njia
ujumbe mfupi wa simu na
katika mitandao ya kijamii.
Gazeti hili lilifanikiwa
kuzungumza na mmoja wa
mawakili wanaowatetea
watuhumiwa hao, Abdalah
Juma, ambaye naye alisema
yeye yupo Zanzibar.
Hata hivyo aliwasiliana

na mawakili wenzake
waliokuwa Dar es Salaam
ambao walimhakikishia
kwamba Sheikh Msellem
alikuwa salama.
Taarifa hizo za mitandao
ya simu na kijamii ni za uzushi
na uvumi unaoenezwa bila
kuchunguzwa. Niwatoe hofu
Waislamu juu ya afya ya
Sheikh Mselemu, afya yake
ni safi na imeimarika na
inaendelea vizuri.
W a k i l i
h u y o
aliwahakikishia Waislamu
a k i wa o m b a wa t u l i e n a
kuwataka kutosikiliza taarifa
zisizokuwa rasmi na ambazo
hazijachunguzwa.
Kila mmoja atakufa, ya
nini umzushie mwenzako
hali ya kuwa yu hai, alihoji
Wakili Juma.
Alisema watuhumiwa
wote walifika mahakamani
na afya zao zinaendelea vizuri
hivyo kuwataka Waislamu
kuendelea kuwa na subra.

bali ni watuhumiwa
kwamba Serikali ilikuwa
inawatuhumu tu na wao
ni wajibu hoja kujitetea.
Alisema Sheikh. Mwinge.
Kiongozi huyo wa
Waislamu Mkoani humo,
alisema ilibainika Mahakana
hapo kuwa Waislamu hao
walikamatwa na watu wa
uchunguzi wa mabomu
wa Kimataifa, ambao ndio
wanaendelea na zoezi hilo
kwa sasa hata hivyo hakuna
ushahidi wowote uliotolewa
kwa tuhuma hizo.
Alipoulizwa kama
Waislamu hao walipata
nafasi ya kujitetea juu
ya tuhuma hizo, Sheikh
Mwinge, alisema, kutokana
na upande wa mashitaka
kuweka wazi kuwa haikuwa
kesi hawakuwa na papara
ya kutafuta Wakili kwa ajili
ya utetezi au wao wenyewe
kujitetea.
Waislamu
hao
wameachiliwa kwa mashariti
kadhaa kufuatia upande
wa mashitaka kuiomba
Mahakama, miongoni mwa
mashariti hayo kuwataka
wasifadhili Magaidi,
wasiwasaidie na wasitoe
msaada wa kifedha kuwapa
magaidi.
Aidha, Mahakama hiyo
iliombwa iwatake Waislamu
hao kuwa walinzi wa amani
kwa muda wa miaka mitatu,
sambamba na mashariti
magumu ambayo yatatolewa
na Mahakama.
Mashariti mengine
yametajwa kuwa, kila mjibu
m a o m b i ( m t u h u m i wa )
alitakiwa kusaini mkataba
wa udhamini wenye thamani
ya Shilingi Milioni tatu,
sambamba na wadhamini
watatu huku wakitakiwa
kuripoti kituo cha Polisi kwa
RCO, kila baada ya miezi
mitatu.
Sheikh Mwinge, alisema
mashariti yote yalitimizwa
k wa wa t u h u m i wa h a o
kwa kusaini mkataba wa
kulinda amani na dhamana
ya shilingi milioni tatu kwa
maandishi pia walipatikana
wadhamini watu kwa kila
mmoja siku hiyo hiyo
Mahakamani hapo, baada
ya Mahakama kukubaliana
na upande wa mashitaka.
Lakini Mahakama
ilipinga muda wa miaka
mitatu na badala yake
ikawapa miaka miwili.
K wa h i y o k wa m u j i b u
wa makubaliano hayo ya

kimahakama, wataanza
kuripoti kwa RCO, kuanzia
Februari 25, 2015, kwa hiyo
tokea jana (Jumatatu wiki
hii) wakawa huru. Alisema
Shkh. Mwinge.
A k i z u n g u m z i a
k a m a t a k a m a t a h i y o ya
Serikali na kuwahusisha na
Ugaidi, Sheikh Muwinge,
alisema hayo ni matunda
y a Ta n z a n i a k u u n g a
mkono sheria ya Ugaidi,
kwa madai ya kupiga vita
Ugaidi bila kujua gaidi
wanayemkusudia ni nani.
Mchakato ule wa sheria
ya Ugaidi matokeo yake ndio
haya na kwa kutokana na
hali ya Waislamu tuliyonayo
sasa na kanuni za sheria
h i y o , n i wa z i k wa m b a
Waislamu tupo katika kuti
kavu ndani ya nchi yetu.
Alisema Muwinge.
Kubwa niseme kwamba
utulivu unahitajika, subra
inahitajika hekma inahitajika
katika suala zima la kufikisha
u j u m b e wa M w e n y e z i
Mungu, vinginevyo
tunaweza kujikuta tunaingia
katika mitego iliyokusudiwa
kwetu. Alisema na
kutahadharisha.
Sheikh Waziri Maduga,
n a Wa i s l a m u w e n g i n e
wanne walikamatwa usiku
wa J u m a t a t u k u a m k i a
Jumanne ya wiki iliyopita,
kisha walisafirishwa
hadi Jijini Dar es Salaam,
ambapo Novemba 23, 2014
( Jumapili) walirudishwa
Mjini Morogoro na hatimaye
Novemba 24 (Jumatatu wiki
hii) walifikishwa Mahakama
ya Wilaya ya Morogoro.
Waislamu
hao
walikumbwa na kadhia hiyo
ni Sheikh Waziri Amani
M a d u g a ( K i o n g o z i wa
Kiislamu), Othman Saidi
Masanga (Dereva SUA),
Shabani Ramadhani Mussa,
Ally Ahmada Kahena
(wafanyabiashara Sokoni
Morogoro) , Msagomora
Faraji Msagomora, wote
wa k i wa n i wa k a z i wa
Morogoro.
Sheikh Waziri Maduga,
ni Mwenyekiti wa Taasisi ya
Daarul Hijra iliyopo Mafisa
Mjini Morogoro, ambayo
inaendesha na kusimamia
Shule za Awali na Msingi
za Taasisi hiyo, pia Shekh
Maduga, ni muhadhiri wa
Dini ya Kiislamu.

You might also like