Professional Documents
Culture Documents
tz
Facebook:annuurpapers@yahoo.com
Sauti ya Waislamu
ISSN 0856 - 3861 Na. 1112 RABIUL THAN 1435, IJUMAA , FEBRUARI 14-20, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs
Uk. 16
Balozi mdogo wa Marekani nchini Sudan, Joseph D. Stafford (mwenye kilemba cha kijani na picha ndogo chini) akiwa nchini Sudan.
2
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam
Tahariri/Makala
AN-NUUR
v i t a d h i d i ya u g a i d i lishafanyiwa kazi sana. Hakuna kiongozi wa nchi leo anaweza kuwa na udhuru wa kusema kuwa alikuwa hajui. Ukiacha haya yanayoelezwa hivi sasa juu ya Al Qaida na Al Shabab, wanaweza kurejea katika historia waone wenzao walivyofanyiwa katika nchi za Nicaragua, Guaetamala, El Salvador, Chile, Cuba na Panama. Nchi zilivurugwa magaidi wa kuundwa wakifanya mauwaji ya
AN-NUUR
hatimaye mnajikuta mmekaliwa na mtandao wa kikachero na kijeshi kutoka kwa mabeberu. Hamfanyi jambo mpaka muelekezwe la kufanya. Rasilimali zenu zinaporwa na mnakuwa hamna kauli ila kwa yale mnayoruhusiwa kufanya. Kwa nchi zetu za Afrika Mashariki, ukiacha Al Qaidah, hivi sasa tumeletewa adui mwingine, Al Shabab. Wote hawa ni katika ule mkakati kwamba adui anahitajiwa kuwezesha agenda ya kijeshi ifaulu ambayo inakuwa ni kuwafuata Al Qaida na Al Shabab. Katika mchezo huu, tunahadaiwa tunaletewa m a g a i d i , wa n a t u u wa na kuharibu mali. Kisha tunapewa mafunzo (polisi) ya kupambana na magaidi. Tunajazwa ukatili wa kutuwezesha kumlaza mwananchi mwenzetu kitandani na kumpiga risasi kichwani tukiwa tumemfunga pingu. Tunajazwa mafunzo ya kututoa ubinadamu wetu kuwa baada ya kumuua mwananchi mwenzetu asiye na hatia kwa kumpiga r i s a s i s i t a k i c h wa n i , tunakosa soni bali tunavaa uso wa kihayawani kumsingizia kuwa ni gaidi hatari tuliloliuwa baada ya kutushambulia kwa risasi. Alipotukosa, tukamuwahi. H a y a n d i y o y a n a y o w a k u t a wa n a o t u h u m i wa k wa u g a i d i n c h i n i K e n ya hivi sasa. Haya ndiyo wanayofanya askari wa ATPU Kenya. Hatima ya yote haya, ni vurugu na kuuwana Wakenya kwa Wakenya. Analohakikisha beberu ni kuwa watuhumiwa wa ugaidi hawakosekani kila uchao, na askari katili wa ATPU wanazidi kupewa mafunzo na posho zao kupitia msaada wa mamilioni ya dola kutoka kwa mabeberu kila mwaka. Ya p o m a m b o m t u unaweza kufanya kwa ujinga. Lakini hili la
vile vile na hii nikuonyesha wazi uadilifu na utukufu wa dini hii amesema Mwenyezi Mungu (na piganeni katika njia ya Mwenyezi Mungu wale ambao wanaopigeni nyinyi na wala msivuke mipaka hakika mwenyezi Mungu hawapendi wavukao mipAka). Surat Al-bakarat aya ya (190) Jee, hapo kuna ugaidi? Bali wengine wanaotaka kujibu uadui kwa kuuweka Uislamu kwenye ncha ya ugaidi basi mizani yao imegeuka kwani magaidi ni wale ambao wanaovuka mipaka duniani kwa kuzifanyia uadu ardhi nafsi na rasilimali bila ya haki. Na miongoni mwao wa p o wa n a o i g a a m b a o wanawasikiliza wanaoutaka Uislamu bila ya kuilazimisha nafsi yake kutafuta uhakika wa Uislamu na wanakiri na kujitambulisha kutokana na vyanzo vya asili na wala hawazigeukii kauli za wana chuoni wasio Waislamu katika Elimu nyingi na matunda ya elimu toka katika Qur ani na suna na wanatosheka na wanayoyasikia toka kwa wa n a o t u k a n a d i n i wa l e ambao wana malengo yao na maslahi katika kuupakazia Uislamu mabaya. Bali hakika Dini ya Uislamu nayo ni Dini ambao amekuja nayo nabii wote nabii Nuhu amesema (Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Wa i s l a m u ) n a I b a h i m u amesema (nimenyeyekea kwa Mola wa Ulimwengu) amesema Nabii Yakubu kuwambia watoto wake (hakika Mweneyezi Mungu amekuchagulieni Dini musife isipokuwa mufe Waislamu) amesema Suleimani (na nijilieni mimi Waislamu) na Issa (Wamesema (na shuhudilieni kwamba mimi ni Muislamu) na akasema Mussa (na kwa Mwenyezi Mungu tegemeeni ikiwa nyinyi ni Waislamu) na aya nyingine za Qur-an zinashuhudia juu ya hilo. Mwenyezi Mungu ndiye muwezeshaji.
Habari
AN-NUUR
Inatoka Uk. 1 Kundecha, amesema mchakato huo utawahusu Makadhi watakaofanya kazi chini ya Jumuiya na Taasisi za Kiialamu. Tu n a wa o m b a wa l e wote waliohitimu masomo ya Shariya (Digrii ya Sharia) katika vyuo mbalimbali kuwasilisha vyeti na wasifu (CV) katika Ofisi za Baraza Kuu na Ha-y-at, wakati tukielekea katika mchakato wa kuanzisha vituo vya Kadhi kwa mujibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu. Amesema Amir Kundecha. Na Hassan Kombo
KUNA mfuko wa Rais Bush wa Kupambana na Ugaidi Afrika Mashariki (President Bushs East African Counterterrorism Initiative). Pia kuna Scholarship za B a l o z i k wa wa s i c h a n a (The Ambassadors Girls Scholarship Program). Usisahahu pia Mfuko wa elimu Afrika (African education initiative). Unajua misaada na mifuko hii inavyowaathiri Waislamu na Dini yao? Wanazitumia pesa hizo kuwasomeshea Wa a l i m u wa K i i s l a m u , kuandaa mitaala na vitabu, kuwalipa mishahara waalimu, na viongozi wa jamii, na kusaidia pia kipesa watoto wa masikini. Wameanzisha pia Kituo cha Vitabu vya rejea vya madrasa Zanzibar (The Zanzibar Madrasa Resource Centre). Misaada hiyo Marekani kwa kupitia mradi wa MKEZA (Mradi wa Kuendeleza Elimu Zanzibar) imekwisha kujenga madrasa 16 (mpaka mwaka 2007) moja ya madrasa hizo aliyotembelea mke wa Bush, Laura, Julai 2005. Na kwa mujibu wa USAID wenyewe M a r e k a n i n i wa f a d h i l i wakubwa kwenye nyanda ya elimu huko Zanzibar. Kwa upande wa Tanzania bara, USAID kwa kushirikiana n a B A K WATA wa m e t o a kitabu cha Mwongozo wa kufundishia walimu wa Kiislamu. USAID pia imetoa mafunzo kwa walimu 54 wa madrasa ya kuwafundisha watoto wa Kiislamu namna ya kupambana na UKIMWI. Mwongozo huo wa vitabu 2,500 uligawanywa kwa walimu wa madarasa Dar es Salaam na Iringa. (Taarifa hizi zote zimepatikana kutoka katika tovuti ya USAID/
watakaokidhi haja katika taaluma hiyo. Sasa kinachofuata ni kutafuta Makadhi katika utaratibu unaokubalika kisheria kasha tutafanya nao semina tayari kwa kuanza kazi rasmi kwa mujibu wa Jumuiya na Ta a s i s i z a K i i s l a m u . Alisema. Alisema, zoezi hilo litasimamiwa na Msheikh kutoka Hay-at Ulamaa katika mchakato wa kuwachuja Makadhi hao, ambao watakuwa wakifanya kazi chini ya Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T).
mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu. (TaHa 20:124) Amesema Allah (Sw): Na Mtume alikuwa akisema: Ee Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wameifanya hii Qur'ani ni kihame. (Al Furqan25:30) Baadhi ya maswahaba wa l i s h a n g a a u k u u l i z a vipi wameihama (Kuipa mgongo) Quran hali yakuwa wanaisoma? Alisema Mtume (Saw) Umekuwa mzigo kwa mama yako ewe! Ziad, nilikuwa ninakuona kuwa ni mtu m we n ye u f a h a m u z a i d i katika Maddina (Je, Nyinyi sio kama) Mayahud na Manasara ambao mkononi mwao wana Tourati na Injili wala hawanufaiki navyo nachochote. (Ahmad) K wa h i v y o p a m o j a n a kuwa nayo Quran lakini hatunufaiki nayo kibinafsi wala kijamii, kama sawa na Mayahud na Manasara. Katika hali halisi tuliyo nayo viongozi wa kitwaaghuut ambao hawana ufunuo kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Taala) ndio ambao ambao wanaotuundia mfumo wa maisha yetu vile wao wanavyoataka tuwe. Pamoja na kwamba matwaaghuut wana mchango mkubwa wa kutufanya tuweze kuipa mgongo Quran, lakini sisi wenyewe kwa sehemu kubwa pia tunao mchango wetu kwa kufuata hawaa za nafsi zetu kwa kuisaliti Quran. Hivyo inatupasa kujiuza na kupatia majibu mambo yafuatayo; Je, pale tunapoisoma au kuisikiliza Quran kwenye swala nk. Tunakuwa tupo hadhiri na kufahamu kile Inaendelea Uk. 7
4
Na Shaban Rajab
A M A k we l i M we n ye z i Mungu humjaalia amtakaye neema zake, kwa vigezo a m b a v y o n i s i r i ya k e mwenyewe muumba. Wakati mwingine utajiri si kwa uhodari, akili nyingi au ujanja wa mtu, bali ni kwa hiari yake mwenyewe Allah (sw). Hata hivyo lililo dhahiri k wa m wa n a d a m u k wa mujibu wa mafundisho ya Mwenyezi Mungi, ni kwamba utajiri au ukwasi, ni mtihani mkubwa kwa mwanadamu. Kwamba rizki za watu wengine kwa namna moja au nyingine, zimehifadhiwa ndani ya utajiri wa mtu. Hata hivyo, rizki na haki za wengine zilizohifadhiwa k wa m k wa s i , z i n a we z a zikapatikana iwapo aliyepewa dhamana hiyo na Mwenyezi Mungu, atatambua hadhi ya aliyempa utajiri huo, yaani Mwenyezi Mungu, akawa mwadilifu na mwenye busara katika kuutendea haki ukwasi aliojaaliwa, ili na wengine waweze kupata rizki zao wa l i z o p a n g i wa k u p i t i a ukwasi huo. Kinyume cha tajiri kushindwa kufanya uadilifu katika mali yake, basi ni kuangukia katika majaribu n a m i t i h a n i m i k u b wa , ikiongozwa na kibri, fahari, israafu, ria, dhulma, dharau nk. Alhaj Aliko Dangote, alizaliwa April 10, 1957 katika jimbo la Kano lililopo Kaskazini mwa Nigeria. Dkt. Dangote ambaye maskani yake yapo jijini Lagos, alipata taaluma ya biashara katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar cha jijini Cairo nchini Misri. Kwa sasa ndiye mmiliki, Mwenyekiti na Mtendaji M k u u wa k a m p u n i ya Dangote Group. Inaelezwa kwamba utajiri wa D k t . D a n g o t e h a d i kufikia Novemba mwaka jana (2013) ulikuwa ni dola za Kimarekani bilioni 20.8, kiasi kilichomfanya kuwa tajiri namba moja Afrika kwa muda wa miaka mitatu mfululizo, kwa mujibu wa jarida maarufu la Fobes. Alhaj Dangote ni mtoto wa mzee Mohammed Dangote na mama Mariya Sanusi Dantata. Amelelewa na wazazi wake katika maadili kamili ya Kiislamu. Familia ya Dangote ni miongoni mwa familia zilizokuwa na uwezo huko Kano. Kampuni ya Dangote Group iliyoanzishwa mwaka 1977, shughuli zake zikiwa ni kuuza bidhaa mbalimbali nchini Nigeria, hususan bidhaa za vyakula. Le o k a mp u n i h i y o si ya kuuza bidhaa tu, bali ni kampuni inayomiliki
Makala
AN-NUUR
Aidha kuna haja ya Taasisi za Kiislamu z i na z o a m i ni k a , k uwa na utaratibu rasmi wa kutoa zaka, ambao utawashirikisha pia wakwasi ili kufikia malengo yanayotakikana. Tukirejea katika enzi za Khalifa Umar (ra)
kuhusu suala la zaka, hakika tutafika pale kila Muislamu anapopatamani kufika, kuikomboa jami ya Kiislamu dhidi ya umaskini na ufukara.
Habari za Kimataifa
AN-NUUR
BANGUI Mashirika ya kutoa misaada Jamhuri ya Afrika ya Kati yameonya kuwa endapo Waislamu nchini humo wataendelea kulihama taifa hilo, njaa itawamaliza raia wa Taifa hilo. Taarifa kutoka Bangui zinaeleza kwamba tayari masoko nchini humo yameanza kuwa matupu na bidhaa za vyakula kuwa haba. Mashirika ya kutoa misaada ya Oxfam na lile la Action Against Hunger, yamesema kuwa ni chini ya maduka kumi ya jumla ndiyo yaliyosalia katika mji mkuu wa nchi hiyo huku wa f a n ya b i a s h a r a we n g i wakiendelea kutoroka taifa hilo. Umoja wa Mataifa umekadiria kwamba watu milioni 1.3, ikiwa ni zaidi ya robo ya idadi ya watu nchini humo wanahitaji msaada wa haraka wa chakula kufuatia machafuko ambayo jamii ya kimataifa nayo imeonekana kushindwa kudhibiti hali na wafanyabiashara wakiwa wameondoka na biashara zao. Immeelezwa kuwa Waislamu ndio wanaomiliki sehemu kubwa ya biashara katika nchi hiyo kutoka nchi za jirani, na ndio ambao wamekuwa wakisambaza huduma muhimu za bidhaa za vyakula kama sukari, unga wa mahindi na ngano, sabuni, mafuta ya kupikia na vitoweo kwa watu zaidi ya 800,000 wa mji wa Bangui na miji mingine nchini humo. Bei za bidhaa za vyakula zimepanda kwa asilimia ishirini tangu Novemba, huku bei ya nyama ikiwa imepanda zaidi ya mara mbili ya bei iliyokuwepo awali kufuatia wafugaji kukimbilia porini na mifugo yao. Katika soko la Petevo, lililopo karibu na ukingo wa mto Oubangui Kusini mwa mji wa Bangui, limebaki tupu huku huduma ya kitoweo ikififia tangu kuondoka Waislamu, ambao ndio waliokuwa wanamiliki biashara za mifugo kutoka Chad. Imeelezwa kwamba kitoweo pekee kilichopo ni nyama ya nguruwe ambayo ni kidogo sana kutokana na nguruwe kufugwa kwa uchache na wenyeji. Kwa sasa kuna upungufu mkubwa wa nyama kwa sababu wafugaji wamekimbilia msituni na wakati wanapochinja mifugo yao, bei huwa ghali sana. Tuna mashaka makubwa s a n a k wa s a b a b u i wa p o upungufu huu utaendelea kidogo tu, tutakufa kwa njaa, alinukuliwa akisema
WAISLAMU nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wakihama nchi hiyo kuelekea nchi jirani za Chad na Cameroon. zinasema kuwa mamia ya Shirika la Medecins Sans ya Makosa ya Jinai ilisema malori yaliyosheheni chakula Frontiers (MSF) limesema siku Ijumaa iliyopita kwamba yamekwama katika mpakani za hivi karibuni limewatibu i n a k u s u d i a k u f u n g u a mwa nchi hiyo na Cameroon, watu 100 majeraha ya risasi mashataka ya awali kutokana kwa sababu madereva wengi na mapanga katika kambi n a k u we p o u we z e k a n o ambao ni Waislamu, wana iliyopo jirani na uwanja wa mkubwa wa makosa ya kivita wasiwasi wa kushambuliwa. ndege wa Bangui ambako katika machafuko hayo. Shirika hilo la Oxfam, kuna wakimbizi 100,000. Umoja wa Mataifa limesema kuwa endapo Watu wanakuja hapa umesema kuwa zaidi ya watu raia waliosalia hawatapewa bila pua, masikio, chuchu, 2,000 wameuliwa na zaidi ulinzi wa kutosha, hali nchini alisema Lindis Hurum, ya elfu 800,000 wamekimbia Jamhuri ya Afrika ya Kati msimamizi miradi wa MSF nchi, huku nusu ya watu hao huenda ikawa mbaya zaidi. Mahakama ya Kimataifa wakitoka mji wa Bangui.
KHARTOUM Balozi mdogo wa Marekani nchini Sudan, Joseph D. Stafford, amefutwa kazi ghafla mara tu baada ya kusilimu na kuingia katika dini tukufu ya Kiislamu. Hata hivyo msemaji wa ubalozi wa Marekani mjini Khartoum, amedai kuwa balozi huyo aliamua kujiuzulu yeye mwenyewe na kuachia nyadhifa zote za kisiasa. Habari zilizochapishwa na World Bulletin, zimeeleza kuwa Bw. Joseph D Stafford, alijiuzulu nafasi yake baada ya kuamua kusilimu na kuwa Muislamu. Lakini vyanzo vya vyombo vya habari nchini Sudan vimesema kuwa Balozi huyo wa Marekani alilazimishwa kujiuzulu baada tu baada ya kubainika taarifa zake za kusilimu. Stafford mwenyewe ameieleza Idara ya Mambo ya Nje ya Marekani kuwa ameamua kujiuzulu kwasababu zake binafsi, lakini vyanzo vya habari nchini Sudan vimedai kuwa balozi huyo alilazimishwa kujiuzulu baada ya kuamua
Aliyekuwa Balozi mdogo wa Marekani nchini Sudan, Joseph D. Stafford. kusilimu. Vyanzio hiyo vilibainisha kwamba Bw. Stafford alikuwa akirekodiwa kila alipokuwa anatembelea Makao Makuu ya Ansar alSunnah nchini Sudan, ziara ambazo ziliweza kuanzisha uhusiano wa karibu na idadi
kubwa ya viongozi wa dini ya Kiislamu kufuatia ziara za mara kwa mara za balozi huyo. Idara ya Mambo ya Nje ya Marekani haijatoa maelelzo yeyote kuthibitisha ama kukanusha habari za kusilimu na kuacha kazi Bw. Joseph Stafford. Mara baada ya kujiuzulu, Bw. Stafford aliandika habari katika jarida la Sudan Tribune akisema, "Mke wangu na mimi tumekuwa na bahati ya kukutana na watu wengi wazuri hapa Sudan, ambao tulikuwa na nia na lengo muhimu la kuimaridha jamii zao. Siku zote tutawakumbuka na nchi yenu nzuri, na natambua kuwa mtaendelea kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kufikia maisha bora, kama mnavyosema kila siku 'Fi Kulu Harakah Baraka' kila hatua ina Baraka zake. Marekani haijawahi kuteua balozi kamili katika Ubalozi wake wa Khartoum nchini Sudan tangu mwaka 1998 na kwa muda wote huo, shughuli zote za kibalozi n c h i n i h u m o z i l i k u wa zikisimamiwa na balozi mdogo (charge daffaires).
6
DAD, do you believe i n h e a ve n ? H i l o n i swali ambalo kijana mdogo Jeffrey siku moja alimuuliza baba yake wakati wakiwa katika matembezi na kupunga upepo ufukweni (beach). Swali hili kwa lugha na msamiati wa Kiislamu ni sawa na kumuuliza je, unaamini kuwa kuna Pepo? M u u n d o wa s wa l i ukilinganishwa na umri wake wakati huo, ulidhihirisha jambo moja: kuwa ni mdadisi na mtu wa logic na haikushangaza wengi alipokuja kuwa profesa wa hesabu akiwa muhadhiri katika Chuo Kikuu cha Kansas. Dr. Jeffrey Lang ni Profesa wa hesabu katika Chuo Kikuu cha Kansas (University of Kansas), moja ya vyuo v i k u u v i k u b wa s a n a katika Marekani. Safari yake ya kutafuta dini ya haki inaanzia Januari 30, 1954, alipozaliwa katika familia ya Kikatoliki huko Bridgeport, Connecticut. Katika miaka 18 ya kwanza ya maisha yake aliitumia katika shule za Kikatoliki (Catholic schools), hata hivyo, masomo katika shule hi zo, yal i mwac h a n a maswali mengi badala ya kupata majibu na kwa hakika kumchanganya zaidi kuhusu dhana ya Mungu na uhusiano wake na binadamu au viumbe kwa ujumla. Kama kuna Mungu, na huyu Mungu ni Mungu wa upendo na mwenye huruma, kwa nini anawaacha baadhi ya watu wanaishi maisha ya tabu hapa duniani, magonjwa, njaa na hata kuonewa na wanadamu wenzao ( k a m a wa l i v y o k u wa Wa m a r e k a n i We u s i wakibaguliwa na kuonewa na Wazungu wa Marekani). Kwa nini asituchukue tukaishi huko mbinguni tukaepukana na tabu za dunia hii? Kwa nini aumbe watu ili wataabike? A n a s e m a , m a s wa l i kama haya, yaligonga akili yake kila siku na hakupata majibu. Anasema, akiwa sekondari-Notre Dam Boys High, alikuwa akihoji sana juu ya Mungu na wakati mwingine kukataa majawabu aliyokuwa akipewa na walimu na wachungaji akisema kuwa hayana mantiki wala hayakubaliani na akili ya
Makala
AN-NUUR
Jeffrey Lang ni Profesa wa hesabu katika Chuo Kikuu cha Kansas (University of Kansas)
kawaida. K a d i r i a l i v y o f a n ya mjadala na Mchungaji wa shule (school Priest), wazazi wake na wanafunzi wake, hawakuweza kabisa kutosheleza kiu yake ya k u m j u a M u n g u . K wa hiyo, kwa mshangao wa mchungaji na wazazi, akatangaza kuwa yeye s a s a h a a m i n i j u u ya M u n g u . Wa k a t i h u o alikuwa na umri wa miaka 18. Na akabaki hivyo kwa miaka 10. Kwa maana mpaka alipokuwa na umri wa miaka 28, alikuwa haamini juu ya kuwepo kwa Mungu wala alikuwa hashughuliki na kwenda kanisani si Jumapili, Krisimasi, Pasaka wala mwaka mpya. Akiwa anafundisha katika Chuo Kikuu cha San Francisco (University of San Francisco), alikutana na mwanafunzi Muislamu akiitwa Mahmoud Qandeel akiwa mmoja wa wanafunzi wake
akiwafundisha hesabu. Alijikuta akiwa karibu sana na mwanafunzi huyu na kuwa marafiki hasa kutokana na mwenendo wake. Urafiki wa Profesa na mwanafunzi wake ukapelekea urafiki kuingia katika familia zao. Hata hivyo, katika muda wote walipoanza urafiki wa kifamilia, kila familia hizi mbili zilipokutana, dini haikuwa kabisa moja ya mada katika mazungumzo yao. Hata hivyo, baadae kabisa familia ya Kiislamu ya mwanafunzi wake, walimzawadia Dr. Jeffrey Lang Quran. Japo hakuwa na hamu ya dini, lakini akaona ngoja tu asome kama kitabu kingine chochote. You cannot simply read the Quran, not if you take it seriously. You either have surrendered to it already or you fight it. It attacks tenaciously, directly, personally; it debates, criticizes, shames, and
challenges. From the outset it draws the line of battle, and I was on the other side. Hayo ni maelezo yake baada ya kuipitia Quran kidogo. Anasema, ukiisoma Quran, utakuta ikikushambulia (kama unafanya mambo yasiyo kubalika), ikijadiliana na wewe juu ya mambo mbalimbali, ikikulaumu, ikikupa changamoto na nasaha, na hata kukuaibisha kwa matendo yako. Kwa hiyo anasema, alijikuta akiwa vitani na Q u ra n . A n a p a m b a n a nayo. I was at a severe disadvantage, for it became clear that the Author knew me better than I knew myself. Hata hivyo anasema kuwa alijikuta akizidiwa nguvu kwani ilielekea kana kwamba mwandishi wa Quran alikuwa akimjua vizuri pamoja na maswali yake yote aliyokuwa nayo kichwani.
7
Inatoka Uk. 6 maana yake, lakini mara akipuuza na kuiacha kama ilivyo. Hivi naota tena au nipo macho, anasema alijuliza akiwa ndani ya swala ilipomjia ile picha ya ndoto aliyokuwa akiota zamani ikiwa sawasawa na jinsi watu walivyokuwa katika chumba kile kidogo wakiswali naye akiwa mmoja wao. Ni kutokana na ndoto hii na historia yake kupitia kwenye Ukatoliki hadi kukanusha Mungu, Dr. Lang anasema, hawezi kusema kuwa amefanya juhudi kubwa sana kutafuta ukweli juu ya Uislamu, ila anamshukuru Mwenyezi Mungu kuwa ndiye pekee a l i ye m w o n g o z a h a d i kusilimu. Mtoto kama baba Baba kwa nini tunaswali (Daddy, why do we pray)? Hili ni swali ambalo binti wa Dr. Lang aitwaye Jameellah akiwa na miaka minane (8), siku moja alimuuliza baba yake baada ya kumaliza swala ya dhuhuri. Sikutarajia kuulizwa swali hili kutoka kwa mtoto wa miaka minane na kwa hiyo sikuwa na jawabu la haraka. Anasema Dr. Lang, hata hivyo akisema kuwa swali la binti yake huyo mdogo, linamkumbusha swali la kiudadisi kama hilo ambaye naye alimuuliza baba yake Mzee Lang. Yeye alimuuliza, unaamini kuwepo kwa Pepo? Anasema, swali kama hilo la kimantiki na kitafiti, l i n a m p a f a r a j a k u wa huenda binti yake huyo akawa msomi wa kiwango cha hali ya juu. Wasomi wa kiwango cha juu kabisa katika fani mbalimbali, ndio wanatakikana katika ulimwengu wa leo kufanya D a wa h n a h a o n d i o watakaouhuisha Uislamu ukarejesha heshma yake. Baada ya kutafakari k wa m u d a , a l i m j i b u : Tunaswali kwa sababu Mwenyezi Mungu anatutaka tuswali. Jameellah akauliza tena, lakini kwa nini? Kwa nini Mungu atuamrishe kuswali? Swala ina faida gani kwetu? M a s wa l i ya l i k u wa mazito na uzito wake unakuwa kwamba Dr. Lang alikuwa akipata tabu ni kwa vipi na kwa maelezo gani mepesi atatumia binti yule wa umri mdogo apate
kuelewa. Binti yangu ninaye kupenda sana, ni vigumu kueleza kwa mtoto mdogo kama wewe ukaelewa. We endelea tu kuswali swala tano kila siku, nina uhakika itafika siku utaelewa kwa n i n i t u n a s wa l i . H a t a hivyo, ngoja nijaribu kukufahamisha. Huku akimshika kichwa kwa upendo akasema: Honey Binti yangu, si unaona nakupenda, lakini Mungu ndiye chanzo cha upendo, huruma, ukarimu, hekma, busara na uzuri wa kila kitu kinachotuzunguka katika maisha. Kama unavyoona, jua ndio chanzo cha mwanga tunaouona wakati wa mchana. Lakini Mungu ndiye chanzo cha vyote hivyo na vingine usivyovijua. Kwa hiyo, upendo nilio nao kwako, kwa dada zako na kwa mama yako, unatoka kwa Mungu, ni Mungu kanipa. Tunajua kuwa Mungu ni mkarimu sana kwa kutupa yote mazuri katika maisha yetu. Tunaposwali tunapata hisia za upendo wa Mungu na ukarimu wake kwetu kwa namna ya kipekee kabisa na yenye athari kubwa katika mioyo yetu. Binti yangu, chukua mfano huu: unajua k u wa m a m a ya k o n a mimi tunakupenda sana na tunafanya kila tuwezalo kukuhudumia, kukuhurumia na kukulinda. Lakini tunapokukumbatia na kukubusu, bila shaka unapata hisia za upendo wa hali ya juu na za ndani kabisa jinsi tunavyokupenda. Ni vivyo hivyo, tunajua Mungu anatupenda sana na ni mkarimu kwetu, lakini tunaposwali, tunapata hisia za ndani kabisa na za kipekee juu ya upendo, huruma na ukarimu wake kwetu. Hayo yalikuwa maelezo ya Dr. Lang kwa binti yake Jameellah aliyetaka kujua ni kwa nini tunaswali. Does praying make you a better daddy? Je, swala inakufanya kuwa baba mwema zaidi, inakufanya kuwa baba mzuri zaidi (kwetu na kwa mama?) Jameellah alimuuliza tena
Makala
AN-NUUR
B a a d a ya k u s i l i m u Dr. Lang anajitahidi kufuata Uislamu kama unavyoagiza. Anaswali swala tano na anasema, hakuna sakina, utulivu wa nafsi, burudani na faraja anayopata kama ile anayopata akiswali na kusoma Quran. Anasema, hata asiyejua tafsiri ya Quran, akiisoma kwa imani na kwa utulivu, n a ye h u p a t a u t u l i v u na sakina kama mtoto mchanga anapokumbatiwa na mama yake. Dr. Lang ana Shahada ya Uzamili na ya Uzamivu ( m a s t e r s a n d d o c t o r a l degrees) katika hesabu kutoka Chuo Kikuu cha Purdue (Purdue University). Lang anasema, anapenda sana hesabu kwa sababu Maths is logical. Kwamba hesabu ni logiki. Ni kutafuta ukweli na majibu sahihi na ya wazi yasiyo na utata. Na kwamba, kwake yeye anapokutana na mambo yasiyo na maelezo ya
Inatoka Uk. 3
na hata kuelewa kuwa imamu alisoma sura gani baada ya kusoma Suratul Fatiha. Lakini jiulize jinsi unavyoweza kueleza kwa ufasaha mara baada kumalizika mpira u liok u wa uk i ut i z a ma katika TV/Runinga, na mtu akitokea na kukuuliza ni timu ipi iliyoshinda? Utajibu kwa ufasaha kabisa timu iliyoshinda, mfungaji wa goli, aliyempatia pasi, dakika Fulani na beki au
kipa wa adui aliyesababisha makosa yaliyopelekea timu yao kufungwa au jiulize jinsi unavyoweza kuelezea Filamu na wakati mwingine hata hiyo lugha inayozungumzwa huifahamu bali utaweza
na akili itakuwa yapo nje ya swala na inafikia mahali hata hufahamu upo kwenye rakaa ya ngapi na bali utashituliwa na imamu akitoa salamu ndio utakumbuka kwamba ulikuwa upo kwenye swala,
kutaja wahusika wakuu na wadogo na kila mtu nafasi au dhima yake ilikuwa ni ipi. Au hata wanafunzi wengi wanapokuwa mbele ya mwalimu ni tofauti kabisa
na wanavyokuwa mbele ya kioo cha TV/Runinga. Je, kwa muda wa mwaka mzima tumeisoma Quran aya ngapi na kuzifanyia kazi? Je, kwa muda wa mwaka mzima kwenye matatizo yetu ambayo ya m e t u t o k e a k we n ye Nyanja ya siasa, uchumi, maadili na mizozo yetu nk. Tumeweza kuirejea Quran mara ngapi ili kuweza kututatulia matatizo yetu? S wa l i l a m s i n g i l a kujiuliza wapi tunakwenda na mustakabali wetu dunia na akhera ni upi? Kwa mantiki hiyo ni ukweli halisi kwamba tumeidhara Quran na tuko mbali nayo kabisa.
Makala
AN-NUUR
Usiombe kuingia anga ya polisi wa ugaidi Sheikh alingolea macho, sehemu za siri Mchezo wa danganya toto jinga waendelea
KHUBAIB A. Rogo, mtoto wa Marehemu Abdul Rogo. alihojiwa na kutishwa wakiwemo wale wa FBIAwali serikali ya Kenya n a m a k a c h e r o we n g i Wazungu. ilikuwa imetangaza kuwa
A l i G i t o n g a a l i k u wa mmoja wa magaidi wa Al Shabab waliovamia Westgate Shopping Mall na kwamba alikuwa amejeruhiwa katika mapambano na polisi. Hata hivyo Ali Gitonga alikuwa kijana dereva aliyekuwa ameajiriwa na tajiri mmoja Nairobi na kwamba siku ya tukio, alikuwa amewapeleka watoto wa tajiri yake katika duka la Nakumatt kufanya manunuzi. Aliposikia risasi zikirindima ndani, ilibidi aingie ndani kujaribu kuwaokoa watoto wa tajiri yake na ndio akapigwa risasi na kujeruhiwa na magaidi. Kama alivyojieleza hapo juu, wakati anatolewa katika ile hali ya uchungu, na akidhani ndio anakufa, akawa anashahadia. Askari waliposikia anatamka Laailah ilallah, wakasema huyu ni gaidi. Serikali ya Kenya ikamtangaza kuwa ni gaidi aliyejeruhiwa. Akasota ndani wiki tatu. Haya ni baadhi ya mambo a m b a y o ya m e f i c h u k a Inaendelea Uk. 9 Muda mfupi baadae maafisa wa polisi (ATPU) walimlaza Sheikh Said k i t a n d a n i m wa k e n a kumpiga risasi sita kichwani akiwa amelala kifudifudi na pingu mikononi. Hivyo ndivyo anavyosimulia mchunguzi wa KTN kutokana na maelezo aliyopewa na mke wa marehemu pamoja na shemeji yake, Twalha Hassan. Katika taarifa ya uchunguzi wa KTN wanasema kuwa baada ya kufanya mauwaji hayo, askari hao wa ATPU, walizidisha unyama wao kwa kumkamata m k e n a m t o t o wa k e mdogo eti nao magaidi kando na kuwa silaha haramu. Silaha ambazo ni za kumbambikizia na kumkamatisha mkononi. Akisimulia kisa hicho cha kusikitisha mke wa marehemu anasema, yeye binafsi walimpiga sana kabla hawajamuuwa Inaendelea Uk. 9
kufanya mauwaji kinyama na kuepuka (mkono wa sheria kutokana na) maovu hayo. Hivyo ndivyo mwendesha kipindi anavyofungua makala ya Jicho Pevu cha televisheni ya K T N , m a d a i k i wa Wagigisi wa Mauwaji. Mwendesha kipindi katika ufafanuzi wake alisema kuwa wagigisi wa m a u wa j i n i wa t u wanaojifanya kuwa wao ni walinzi wa usalama wa raia (Polisi), lakini hao hao ndio wanaofanya mauwaji ya kutisha na ya kinyama, halafu hakuna hatua zozote wanazochukuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi. H u k u akiwatahadharisha watazamaji kuwa makala hiyo itakuwa na picha za kutisha, hasa
Wagigisi wa mauwaji
kutokana na maiti za Masheikh waliouliwa kikatili, akafungua mada kwa kueleza masaibu ya Waislamu wa Mombasa katika hiki kinachoitwa vita dhidi ya magaidi. Kisa cha kwanza k ue lezwa ni k il e cha k u u l i wa S h e i k h S a i d Mohammed Njiro wa Kiembeni, Mombasa. Makala inafunguka kwa kuonyesha chakula k i s h a t e n g wa m e z a n i . Kama ilivyo kawaida ya wanawake wa Pwani, mkewe Sheikh Said kafunika chakula kwa kawa imeandikwa, Siringi ni tabia yangu. Kwa vile wakati wa dhuhri ulishakaribia, Sheikh Said akamwambia mkewe kwamba anakwenda kwanza msikitini kuswali halafu atakula akirejea. Lakini
Sheikh Said Mohammed Njiro, hakuwahi kula chakula hicho kilichoandaliwa na mkewe kipenzi, Rahma Hassan, wa l a h u k o m s i k i t i n i hakuwahi kufika. Askari wa kikosi cha ATPU walimkamata njiani, wakamfunga pingu na kumrejesha nyumbani. Kwa mujibu wa maelezo ya majirani waliokuwa katika eneo la tukio akiwemo msichana Agnes Kanga, ili kuficha ushahidi, polisi walifukuza watu wote walio jirani na eneo hilo. Baada ya kupekuwa nyumba nzima na kukosa silaha walizodai kuwa zipo katika nyumba hiyo, wa l i m c h u k u a S h e i k h wakamlaza kitandani kwake kifudifudi wakiwa wamemfunga pingu wakampiga risasi sita kichwani.
Makala
AN-NUUR
Inatoka Uk. 8 wakati tukifuatilia tukio la kuvamiwa Waislamu waliokuwa masjidi Mussa, Mombasa na watu kadhaa kuuliwa. Awali katika taarifa zetu tulikuwa tukisema kuwa hakukuwa na picha za kamera zilizo wanasa waliodaiwa kuwa magaidi. Hata hivyo, pamoja na picha nyingi kuharibiwa na kufichwa, lakini jicho la uchunguzi la kituo kimoja cha televisheni, Kenya kimepata picha nyingi zikionyesha tukio hilo, na hasa magaidi hao walivyofanikiwa kutoroka huku jengo likizingirwa na jeshi la Kenya-Kenya Defense Force (KDF). Kama itakavyoonekana katika makala hii huko mbeleni, mtafaruku uliotokea baina ya polisi n a wa n a j e s h i k a t i k a operesheni ya Westgate, huenda ndio uliopelekea baadhi ya polisi kutoa picha hizo kwa baadhi ya waandishi wa habari zilizokuwa zimedhibitiwa ili kulipiza kisasi kwa wanajeshi. Lakini jingine ambalo tumelipata katika ufuatiliaji wetu tukio la Masjid Mussa ni kuwa unyama wa kutisha hadi sasa umeshafanywa dhidi ya Waislamu wa Inatoka Uk. 8 mumewe. Wa l i n i p i g a s a n a mpaka nikafura uso (uso ukavimba). Wakanilazimisha nilale chini. Kulikuwa na begi la nguo za mtoto wangu. Walichukua silaha wakatia silaha (katika begi ile) wakanyanyua wakaniuliza, we mama waona hii nini? Nikawaambia mimi sijui. Wakanitoa wakaniweka sitting room wakaniambia nikae hapo hapo nisiinuke, nikiinuka wataniuwa baadae wakanipeleka ndani wakaniambia twende ukaone, tumemuuwa (mumeo). Baada ya kukamilisha operesheni hiyo, tunaambiwa kuwa polisi h a o wa l i f a n ya k a m a walivyozoeya. Kuita waandishi wachache wa magazeti,
Kenya katika zile jitihada za serikali hiyo kujisajili kwa Marekani kwamba inapambana na magaidi. Taarifa za uchunguzi zilizokusanywa na kituo cha televisheni KTN, katika kipindi chake maarufu Jicho Pevu, zinaonyesha kuwa waliomuuwa Sheikh Aboud Rogo ni polisi wa kikosi cha kupambana na magaidi-Anti Terrorism Police Unit (ATPU) na kwamba aliuliwa jirani kabisa na kituo cha polisi cha Bamburi. Na baada ya mauwaji hayo polisi wawili waliomuuwa waliingia katika kituo hicho cha
redio na runinga w a n a o a m i n i k a kutumikia maofisa wa polisi wanaochapisha taarifa bandia na porojo kama wanavyotakiwa zinazochapishwa na kitengo hicho na kutumwa kwa wanahabari hao. K wa h i y o , k u p i t i a wanahabari hao, polisi wakasema kuwa wamemuuwa mtuhumiwa wa ugaidi Sheikh Said Mohammed katika mapambano makali ya kurushiana risasi na polisi!!! Mke na mtoto wake kwa muda wa siku sita akawa yupo rumande katika gereza la Shimo la Tewa, kisha akapelekwa
Wagigisi wa mauwaji
mahakamani akituhumiwa kuwa yeye ni gaidi hatari anayemiliki silaha. Kutokana na kilio cha mama huyo, Bi Rahma Hassan, mahakama ikampa dhamana, lakini bado akibaki na tuhuma za ugaidi na kukutwa na silaha (silaha ambayo alikamatishwa na polisi). Mwingine kufikwa na mkasa kama huu ni Sheikh Mohamed Aboud Rogo. Huyu aliuliwa tarehe 27 Agosti, 2012. Akisimulia kisa cha mauwjai yake, Mohammed Ali anasema: A g o s t i 2 7 , 2 0 1 2 ndiyo siku ambayo familia, ndugu, jamaa na marafiki wa Sheikh Mohammed Aboud Rogo,
Mombasa na siku kadhaa baadae, aliokotwa katika msitu wa Tsavo, maiti yake ikiwa imenyofolewa macho na sehemu zake za siri. Walioshuhudia tukio la kutekwa kwake wanasema, alitekwa na polisi wa ATPU mara tu alipovuka kivuko cha Likoni. Wananiambia tutakufanya kama huyu. Awali polisi walikuwa wa m e k a n u s h a k a b i s a kuhusika na kumteka Samir na kisha kumuuwa. Lakini sasa wanatumia picha za Samir baada ya kufanyiwa unyama
kuwatisha watoto wa Sheikh Aboud Rogo. Pengine nitaje hapa tena kisa cha kuuliwa Sheikh Said Mohammed. Huyu aliuliwa Mombasa. Polisi wa l i m k a m a t a wa k a t i akielekea msikitini kuswali dhuhri, wakamrejesha nyumbani. Wakapekua wakidai wanatafuta silaha, walipokosa kitu wa k a m f u n g a m i k o n o kwa nyuma wakamlaza kifudifudi kitandani mwake na kisha kumpiga risasi sita kichwani. Taarifa ikadai kuwa aliuliwa akipambana na polisi. (Yote haya ni kwa mujibu wa taarifa za Jicho PevuKTN). Na hayo ni baadhi tu ya matukio ya mauwaji ya kutisha waliyofanyiwa Waislamu kabla ya hili la juzi la Masjid Mussa. Pengine sasa tuangalie lile shambulio la Westgate Shopping Mall, ili tutizame linahusiana vipi na matukio kama haya ya kuvamia misikiti na kushambulia Waislamu. Mpaka sasa yapo maswali mengi ambayo bado hayajapatiwa majibu kufuatia shambulio la kigaidi pale Westgate Shopping Mall, Nairobi. Moja ya maswali hayo ni hili: Kama magaidi waliuliwa, maiti zao ziko Inaendelea Uk. 10 ni polisi wa kikosi maalum walijitokeza nje kidogo ya barabara wakamfyatulia risasi. Maelezo ya mtafiti wa KTN yanasema kuwa waliomuuwa ni watu wa kikosi maalum wanaopewa mafunzo kutoka Marekani, Uingereza na Israel na kwamba kikosi hicho kina kambi zake Nairobi, ila kukiwa na operesheni kama hiyo, hupewa ndege wakaingia Mombasa wakafanya kazi yao na kurejea Nairobi b i l a ya k u t a m b u l i k a . KTN katika Jicho Pevu wanasema, katika operesheni chafu kama hizo, Marekani, Uingereza na Israel, hucheza kadi zao kinyumenyume ili wasigundulike. Wa n a o i n g i a k a t i k a orodha hii ni watu wengine sita ambao nao wameuliwa Inaendelea Uk. 10
hawataisahau kamwe. Siku ambayo kiongozi wa dini aliyekuwa na ufasaha na ustadi wa kusema na kuvutia hadhira, alizimwa kwa mtutu wa bunduki. Je, aliuliwa vipi? Maelezo yanatolewa kuwa aliuliwa kiasi mita 200 kutoka kituo cha polisi cha Bamburi. Baada ya yeye kupita eneo fulani kukaribia kituo hicho cha polisi, polisi walikuwa wamepangwa kana kwamba kulikuwa msafara wa Rais. Njia zote zikafungwa. Hakuna gari inayokuja mbele yake wala nyuma yake katika barabara ya MalindiMombasa. Hapo ndio watu wanaodaiwa kuwa
10
Makala
AN-NUUR
wapi? Pili, magaidi hao ni akina nani? Tatu, kwa nini polisi wa kawaida na vikosi maalum waliondolewa ghafla na badala yake likaletwa jeshi (KDF)? Kwa nini jeshi halikuingia kuanza mashambulizi bali likasubiri usiku kucha muda ambao unadhaniwa ndio waliotumia magaidi kutoka? Taarifa ya uchunguzi wa K T N i n a o n y e s h a kuwa hadi kufikia jioni ya siku ya shambulio, polisi walikuwa wamefanikiwa kuwaokoa watu wote, kwa hiyo ndani kukabaki magaidi peke yao. Na taarifa hiyo inaonyesha jinsi ndani kulivyokuwa kupitia kamera za C C T V. Wa n a o n e k a n a watu (magaidi) wanne tu wakiwa na silaha zao wakirandaranda bila hata ya kuwa na wasiwasi. Mohammed Ali, mchunguzi na mtayarishaji kipindi wa KTN, anasema kuwa pamoja na mafanikio hayo, lakini jambo lisilokuwa la kawaida na lisilokuwa limetarajiwa likafanyika. Ilitangazwa k u wa j e s h i l i n a i n g i a kuongoza operesheni. Kilichotokea ni kuwa walijikuta wakiuwana Inatoka Uk. 9 kinyama wakituhumiwa kwa ugaidi. Mmoja wao ni Sheikh Samir Hashim Khan, Imam wa msikiti. Huyu alitekwa na maofisa wa polisi akiwa na Sheikh Mohamed Kassim (kipofu). Walitekwa katika kivuko cha Likoni muda wa saa 6 mchana tarehe 10 Oktoba, 2012. Siku sita baadae mwili wa Sheikh Samir uliokotwa katika msitu wa Tsavo ukiwa na majeraha ya kuteswa, macho pamoja na sehemu za siri zikiwa zimenyofolewa. Aidha, uso ulikuwa umeharibika ikidhaniwa kuwa alimwagiwa tindi kali katika kuteswa au baada ya kuuliwa. Hadi makala haya ya Wagigisi wa Mauwaji inakamilika, Kassim alikuwa hajapatikana, si maiti au japo kusikia yupo wapi. Pengine nimalizie kwa masaibu yanayowakuta watoto wawili wa kiume wa marehemu Sheikh Aboud
Rogo. Hawa ni Khubaib A Rogo na Dhulkifli Aboud Rogo. Katika maelezo yao vijana hawa wanasema kuwa polisi wamekuwa wakiwajia na kuwasumbua mara kwa m a r a wa k i wa t u h u m u kuwa wanaficha silaha na kwamba wao walishakwenda Somalia na kujifunza ugaidi. Katika kuwatisha huwa wakiwaletea picha ya baba yao na masheikh wengine waliouliwa na miili yao kuharibika vibaya, kisha huwaambia kuwa watawafanya kama hao au kuwafanyia vibaya zaidi. Waliniwekea bunduki juu ya meza wakaniambia niifungue,wakati wakinitisha, wananiletea picha ya Samir wakati n i m z i m a n a wa k a t i
Wagigisi wa mauwaji
washamchoma kwa asidi, washamuuwa, wakasema unaona vile tulimfanya huyu, basi na wewe tutakufanya hivi au kukufanyia unyama zaidi. Baada ya hapo wakaniletea picha ya baba yangu wakati yupo hai, wakaniuliza wamjua huyu, nikawaambia ndio baba yangu, kisha hunionyesha picha wakati washampiga risasi. Hayo ni maelezo ya K h u b a i b a k i e l e z a alivyokuwa akipata wageni mara kwa mara kutoka kikosi cha ATPU wakiongozwa na kamanda wa kikosi hicho Mombasa, Elijah Rop, mara baada ya baba yake kuuliwa na hata sasa. Khubaib anasema katika mambo ambayo hatayasahau, ni kauli ya Elijah Rop alipomwambia kuwa wao, ATPU, ndio waliomuuwa baba yake. Kisha akamwambia, naye akileta kidomodomo watamuuwa kama walivyomuuwa baba yake. Khubaib anasema, yeye hajawahi kwenda Somalia na wala hana mpango huo, ila yeye ni Mwana Sunna. Ni Muislamu. Sasa kama atauliwa kwa ajili hiyo, hana la kusikitika. Ila anasema, akiitwa katika kituo chochote cha polisi, hatakwenda. Kama ni kumuuwa waje wamuue mbele ya mama yake, k a m a wa l i v y o m u u wa baba yake mbele ya mkewe (mama yake Khubaib). Mama yake ajue kwamba mwanawe kauliwa na polisi.
hao wakiingia wakiwa wa m e s h i k a b u n d u k i , lakini wanapotoka kila mmoja kashika mifuko ya Rambo utadhani wanatoka kufanya manunuzi (shopping). Katika tukio moja wanaonekana wakielekezana duka la kuingia kupora kwa hiyo wakati wanatoka, kila mmoja anaingia hapo na kuchukua kitu kabla ya kutoka. Katika kilele cha operesheni hiyo, wakati wa na nchi wa k i jiul i z a ilikuwaje jeshi likaitwa na nini kinaendelea ndani ya Westgate, ukaonekana moshi mzito ukitokea duka la Nakumatt. Waziri wa Usalama akasema kuwa hao walikuwa magaidi waliokuwa wamechoma magoro kutaka k u wa b a b a i s h a a s k a r i na kwamba moto huo ungezimwa mara moja. Hata hivyo, haukupita muda ikaonekana kuwa haukuwa moto wa magodoro bali ulikuwa u k i wa k a n j e s e h e m u ya juu ya kuegesha magari na mara jengo likaporomoshwa kutoka ghorofa ya tatu mpaka chini. Wa k a t i h a l i i k i z i d i kutatiza, mara jina la Samantha Louise Inaendelea Uk. 12 Maelezo ya mtoto Dhulkifli nayo ni ya namna hiyo hiyo. Naye anasema AT P U wa n a m wa m b i a kuwa yeye ni komandoo la magaidi waliohitimu mafunzo Somalia. Katika tukio la kuvamiwa Masjid Mussa wiki mbili zilizopita, Dhulkifli anaonekana mbele ya msikiti akiwa kashikishwa bendera ya Al Shabab huku polisi wenye silaha wakimzingira. Katika picha moja iliyopigwa kupitia simu ya m k o n o n i , a m b a y o nimeishuhudia na kuisikiliza, mtoto huyo wa Sheikh Rogo anasikika a k i l a l a m i k a k wa m b a kashikishwa bendera hiyo na polisi. Na katika mahojiano yake na KTN anasema, afya yake ni mgogoro mtupu, kama anavyoonekana (unene usio wa kawaida). Kisha anahoji, hivi na mwili huu mazoezi gani ya kijeshi/kigaidi naweza kufanya.
11
Mohammed Makimu K U J I H U S I S H A na madh-hab flani imekuwa ni dhana na itikadi inayoshadidiwa miongoni mwa Waislamu walio wengi. Kwa dhana hi yo, i m ef ikia hatua mtu kuwaaminisha waislamu wasiojitambua na kuufahamu Uislamu sahihi na wale ambao si Wasilamu waamini kwamba bila kuwa na dhehebu katika Uislamu wewe si Muislamu. Ni seme t u kwamba dhana hii ni dhanifu na daima haikubaliki katika Uislamu. Suala la kuwa na dhehebu flani, ni wazo na zao la mtu binafsi (Personal and Private opinions). Mwenyezi Mungu (SWT) na Mtume wake, hawakutuamrisha tujitenge kimakundi kama tulivyojitenga sasa hivi. Kwa kuangalia ubaya wa jambo hili, Mwenyezi Mungu (SWT) hakuacha kutuonya tusifanye hivi pale aliposema ndani ya Quran: Nyenyekeeni Kwake na mcheni, na simamisheni swala wala msiwe katika washirikina. Katika wale walioitenga dini yao na wakawa makundi, kila kikundi kinafurahia kilichonacho (30:30-31). Kwa kuirejea aya hiyo na nyingine ambazo sijazinukuu katika makala haya, hakuna mahala suala la madhehebu limebainishwa. Na si lazima kuwa mfuasi wa Hanafi, Shafii, Maliki au Hanb ali. Hawa ni wanazuoni na maimamu waliofanya na kuonesha juhudi zao katika dini na hawakuwaamrisha watu watengeneze makundi na kupigana ima kutukanana kama tufanyavyo sisi. Na waliweza kuhitilafiana lakini hawakugombana, kuzomeana, kutukanana, kukufurishana na kufanyiana uhasama na uadui kama tufanyavyo sisi leo hii. Jambo moja la msingi la kufuata si Shekhe wala Imam Fulani, bali ni kuitafuta njia iliyobainishwa kwetu kama Wa i s l a m u . M we n ye z i Mungu anasema ndani ya Quran: Sema: Hii ndio njia yangu, ninaita (ninalingania) kwa Mwenyezi Mungu k wa u j u z i wa k we l i , mimi (nafanya hivi) na (kila) wanaonifuata. Na Mwenyezi Mungu ametakasika na kila
Makala/Tangazo
AN-NUUR
upungufu, wala mimi sio miongoni mwa wanaomshirikisha (Mwenyezi Mungu) (12:108). Mwenyezi Mungu (SWT) ametuamrisha tushikamane na kuwa kitu kimoja (3:103). Na ametoa tahadhari kwamba iwapo tusipokuwa pamoja na letu likawa moja kama Waislamu tunaomfuata Mtume mmoja nini kitatufika. Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake wala msizozane (msigombane), msije mkaharibikiwa na kupotea nguvu zenu, na vumilieni (mstahamiliane). Bila shaka Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanaovumilia Quran (8:46) Katika miongoni mwa kauli za Imam Maliki anasema mawazo a u m t a z a m o wa m t u yeyote waweza kubalika pale yakiendana na Quran na Hadithi na yanaweza kupingwa pale yanapokuwa kinyume ispokuwa ya huyu aliyelazwa hapa kaburini. (Akaashiria kaburi la Mtume Muhammad s.a.w). Maimam wote wane wa Fiq-hi wamesema katika kauli zao kwamba kama Hadithi sahihi itabainika kuliko haya maoni yangu, hivyo basi hiyo itakuwa ndio madhehebu yangu (Idhaa swah-hal-hadiith fahuwa madh-habii). Hii ina maana kwamba hadithi sahihi ikibainika katika masala wanayoyafutu, ndio i t a k u wa n j i a ya wa o kufuata. Si maoni yao tena. Na walihimiza na kusisitiza s a n a wa t u wa ya p i m e maneno na mitazamo yao kwa uzani wa Quran na Sunnah, ikibainika wao kwenda kinyume, watu wasiwafute kwa ushabiki kwa kuwa wanawapenda, bali wayaachilie mbali maneno yao. Ugonjwa unaowasibu Waislamu wengi sasa hivi ni kuifuata dini kibubusa na kuwa washabiki wa dini. Suala la umaamuma katika Uislamu linaishia katika swala tu. Na hata katika umaamuma katika swala, ni lazima na wewe un ayes walis h wa u ju e namna ya kuswali. Sio kwamba anatakiwa kujua
Madhehebu
Imam pekee. Kama ilivyo wajibu kwa Imamu kusoma Suratul Fatha na kujua taratibu zote za swala, ndivyo hivyo anavyotakiwa kuwa maamuma. Kwa hiyo, kila Muislamu anawajibu wa kuusoma na kuufahamu Uislamu sahihi k u t o k a k we n ye v ya n z o vyake (Quran na Sunnah) si kushabikia. Waislamu walio wengi wamekuwa ni wafuasi wa madhehebu mbalimbali. Mbaya zaidi hakuna lolote wanalojua juu ya huyo wanayemnasibisha na dhehebu wanalolifuata. Si Shafii, Hanbali, Maliki wala Hanafi. Hakuna wanachokifahamu wafuasi wa madhehebu hayo zaidi ya kujua jina tu ima huyu ni Shafii, Maliki, Hanbali au Hanafi. Ukiwauliza kipi unafahamu juu ya yale yaliyozungumzwa na Imam
huyu, hana jibu la msingi. Ndugu zangu katika dini hii iliyofundishwa na Mitume wote, bado inatutaka tuitumikie kama inavyotufundisha. Tu i r e j e e k i l a k i p e n g e l e chake kimatendo. Huu ni muda wa kuacha tofauti zetu kwa kuangali Uislamu unafundisha nini si watu wanasemaje. Ishi na Muislamu mwenzako kama ndugu yako, penda yamfike mambo ya kheri kama wewe mwenyewe unavyopenda katika nafsi yako. Nihitimishe makala yangu kwa kuirejea hadithi iliyosimulia na Irbad bin Sariya katika SahihtTirmidh. Anaeleza kwamba Siku moja Mtume (s.a.w) alituawaidhi waadhi ambao ulishtua nyoyo za watu baada ya swalat Fajr ambao ulibubujisha watu machozi, na nyoyo zikapatwa khofu,
CHUO KIKUU CHA WAISLAMU CHA MOROGORO KINATANGAZA NAFASI ZA MASOMO KWA NGAZI ZA DIPLOMA NA CERTIFICATE KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015 MASOMO YA TOLEWAYO NI:1) Diploma and Certificate in Science and Laboratory Technology 2) Diploma and Certificate in Journalism 3) Diploma and Certificate in Islamic Banking and Finance 4) Diploma and Certificate in Procurement and Logistics Management 5) Diploma and Certificate in Law and Shariah 6) Diploma and Certificate in Islamic Studies 7) Certificate in Medical Laboratory Technology 8) Certificate in Information Technology 9) Certificate in Chinese Language 10) Certificate in Sign Language 11) Certificate in Arabic Language SIFA ZA KUJIUNGA:KWA NGAZI YA DIPLOMA. MWANAFUNZI ANATAKIWA AWE NA FORM SIX ONE PRINCIPLE PASS NA SUBSIDIARY, SIFA ZA MUOMBAJI ZIENDANE NA KOZI ANAYOOMBA. AU AWE NA NTA LEVEL 4 CERTIFICATE YA KOZI INAYOFANANA NA IWE YA CHUO KINACHOTAMBULIKA NA SERIKALI. KWA NGAZI YA CERTIFICATE. AWE NA ANGALAU D NNE ZA KIDATO CHA NNE ZINAZOFANANA NA KOZI ANAYOOMBA AU AWE NA VETA LEVEL 3 CERTIFICATE INAYOFANANA NA KOZI ANAYOOMBA FORM ZA KUJIUNGA NA CHUO ZINAPATIKANA MUSLIM UNIVERSITY OF MOROGORO AU KATIKA WEBSITE YA CHUO, www.mum.ac.tz AU KUPITIA MAWAKALA WETU. MASOMO YATAANZA RASMI TAREHE 12/05/2014. MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI NI TAREHE 31/03/2014 KWAMAELEZO ZAIDI NA KWA KUPATA ORODHA YA MAWAKALA WALIPO KARIBU YAKO PIGA SIMU AU TUMA UJUMBE MFUPI KWA NAMBA ZIFUATAZO: - 0712277598, 0655003744 AU 0785330002 IMETOLEWA NA NAIBU MAKAMU MKUU WA CHUO TAALUMA CHUO KIKUU CHA WAISLAMU CHA MOROGORO
12
Mashairi/Makala
Mhariri samahani, niweke japo pembeni, Nitoe yangu maoni, kwa wananchi nchini, Katiba ninabaini, jadidi mada mezani, Katiba mpya si hoja, hoja ni uadilifu !
Bunge lile tambueni, la katiba li njiani, Wajumbewe kwa yakini, wiki jana si zamani, Amiri-Jeshi nchini, wote aliwabaini, Katiba mpya si hoja, hoja ni uadilifu ! Si kwa majina kwa nduni, baadhi nakujuzeni, Wanasiasa kundini, pamwe na wanazuoni, Kadhalika wa kidini, viongozi nao ndani, Katiba mpya si hoja, hoja ni uadilifu ! Juma lijalo nadhani, yumkini li hewani, Bilhaki kwa yakini, wengi mwalitumaini, Kwa mengi matumaini, tena yaso na kifani, Katiba mpya si hoja, hoja ni uadilifu ! Kwa finyu wangu uoni, sina nalotumaini, kutoka humo bungeni, la utendi si uneni, Yanenwayo katibani, matendoni siyaoni, Katiba mpya si hoja, hoja ni uadilifu ! Mifano nitakupeni, toka ile ya zamani, Kwa ibara katibani, msijedhani nabuni, Tisashara namba 'wani', 'UHURU WA KIIMANI', Katiba mpya si hoja, hoja ni uadilifu ! Waminywa huu na nani, uhuru wa kiimani, Katiba au insani, jibu mnalo vichwani, Hapo ina kosa gani, katiba nijulisheni, Katiba mpya si hoja, hoja ni uadilifu ! Kadhalika rejeeni, moja tatu namba 'wani', 'USAWA WA SHERIANI', haki ya kila insani, Nao waminywa na nani, katiba au insani, Katiba mpya si hoja, hoja ni uadilifu ! Shekhe pale kizimbani, kupandishwa kulikoni, Mchungaji mitaani, yu 'apeta' ni kwanini, Hapo ina kosa gani, katiba nijulisheni, Katiba mpya si hoja, hoja ni uadilifu ! Moja nane kwa makini, kifungu 'a' durusuni, Waandishi kitanzini, watiwa sasa kwanini, Mwigamba muulizeni, vyema atakujuzeni, Katiba mpya si hoja, hoja ni uadilifu ! Pamwe na wenza safuni, walikamatwa kwanini, Japo kesi 'waliwini', wiki ya juzi kotini, Kilichowaminya nini, katiba au insani, Katiba mpya si hoja, hoja ni uadilifu ! Aidha likumbukeni, 'MWANAHALISI' si geni, 'linasota' kifungoni, hadi leo ni kwanini, 'UHURU WA KIMAONI', wa 'Bongo' u mashakani, Katiba mpya si hoja, hoja ni uadilifu ! Japo sasa i hewani, kifungoche dhukuruni, Redio yetu 'IMANI', 'ilisota' gerezani, Kwa ghaidhi ya insani, si sheria katibani, Katiba mpya si hoja, hoja ni uadilifu ! Mwisho nakukumbusheni, cha Njozi mwanazuoni, KITABU kilobaini, mauaji ya insani, Dawamu marufukuni, kwa amri yake 'Beni', Katiba mpya si hoja, hoja ni uadilifu ! Usuli au kiini, cha tatizo katibani, Adala na si uneni, ya insani matendoni, Kwa yangu mimi maoni, jipya hasa silioni, Katiba mpya si hoja, hoja ni uadilifu ! Kwa kina tafakarini, kuhusu yangu maoni, Yapimeni 'kwa mizani', si 'kwa alosema nani', Kaditama kwaherini, wa Bara na Visiwani, Kalamu naweka chini, mwisho wa yangu maoni. ABUU NYAMKOMOGI - MWANZA.
Inatoka Uk. 10 Lewthwaite, maarufu White Widow, likaanza kusikika katika vinywa vya wanahabari na serikali k wa m b a a l i h u s i k a n a shambulio hilo. Wakenya walijisahau wakashika hilo. K T N i n a s e m a k u wa kuletwa jina la Samantha ilikuwa namna nyingine ya danganya toto jinga k u w a f a n y a Wa k e n y a wasihoji mambo ya msingi kwani japo mama huyo alishawahi kufika Kenya huko nyuma, lakini madai ya kushiriki mashambulio hayo ilikuwa ni porojo tupu. Katika kuhitimisha kadhia hiyo, Waziri wa Usalama akatangaza kuwa k u l i k u wa n a m a g a i d i 10 mpaka 15. Naye Rais Uhuru Kenyatta siku ya Jumanne, siku moja baada ya kutolewa tangazo kuwa operesheni imekamilika, alisema kuwa magaidi wa l i o u l i wa wa l i k u wa watano na 11 walikuwa wamekamatwa na kushikiliwa na polisi. Hata hivyo, picha za kamera za CCTV ambazo hatimaye zilifika mikononi mwa waandishi wa habari, zilionyesha kuwa kulikuwa na magaidi wanne tu. Lakini jingine la kutaja hapa ni kuwa japo taarifa ya serikali ilitangaza kuwa m a g a i d i 5 wa l i u l i wa , haikuweza kuonyesha picha za maiti hao. Aidha, hadi leo haikuweza pia kuonyesha hao magaidi 11 waliokamatwa na kushikiliwa na polisi. Kinyume chake, kama ilivyoripotiwa katika gazeti la Daily Nation la Jumatatu iliyopita Februari 10, 2014, serikali sasa inasema magaidi waliouliwa eti toka wakati huo, maiti zao zinashikiliwa na FBI wakizifanyia uchunguzi!!! Ajabu ya mambo! Akitoa taarifa hiyo Mkuu wa Jeshi la Kenya, Generali Julius Karangi, anasema: Here it from me, these fellows were killed on Monday morning. It happened on Saturday. We f i n i s h e d t h e m o n Monday morning and their bodies are with the FBI somewhere. Swali ni je, iweje magaidi wauliwe na jeshi la Kenya, serikali ishindwe k u o n ye s h a m i i l i ya o , lakini muda wote huo toka Septemba mwaka
AN-NUUR
katika hizi dola kutoka Marekani. Ambalo kila wakati la kujikumbusha ni kuwa vita hii dhidi ya ugaidi ina malengo makuu mawili. Kwanza ni kwa ajili ya kuendeleza agenda ya mabeberu ya kuzitia utumwani nchi mbalimbali duniani ili zipate kudhibitiwa na kuwatumikia mabeberu. Pili, ni kuhujumu Uislamu. Wanapouliwa Masheikh na vijana wa Kiislamu, Uislamu unahujumiwa kwa kuporwa nguvu kazi yake. Lakini unapowaonyesha magaidi kama wale pale Westgate, eti wanaswali Isha, baada ya kuuwa watoto wachanga na wanawake wasio na hatia, unahujumu Uislamu kwa kutangaza kuwa ni dini inayofundisha ukatili na hivyo unahalalisha hatua zozote zinazoweza k u c h u k u l i wa k u u p i g a v i t a U i s l a m u . Ta t u , u n a p o f a n ya n j a m a z a entrapment, unawafanya vijana wa Kiislamu na nguvu kazi ya Waislamu, badala ya kufanya kazi za kimaendeleo kwa ajili ya dini yao na dunia yao, wabaki kila mara ni watu wa kupambana na polisi na kufanya ghasia mitaani. Unapouwa Sheikh, unawatia ghadhabu Waislamu na hasa vijana, kwa hiyo unawafanywa wawe na msimamo mkali zaidi dhidi ya serikali na hata wasio Waislamu. Wanabaki kuwa watu wa kuongozwa na hasira za kujihami badala ya kukaa kupanga na kufanya mambo ya maendeleo. Matokeo yake ni kuwaingiza katika chambo na ndoano ya Free Islamic Army, kwa maana ya jeshi la mujahidina lisilo na malengo maalum ya nchi maalum wala kuwa na udhibiti wa serikali yoyote duniani. Wao wakisikia mahali kuna vita wanatafuta hoja za kujiridhisha (kujidanganya) kuwa ni jihad, wanakwenda. Kwa mtindo huu ndio linaibuka tatizo jingine la hatari la kuwaangamiza Waislamu: Kutumiwa kama jeshi huru la kimataifa la kupigana proxy war ya mabeberu. Ndio walioko Afghanistan, Iraq, Libya, Pakistan, Somalia na sasa Syria.
13
Makala
AN-NUUR
MWAKA 2013 ulimalizika kwa kali ya aina yake katika medani za siasa hapa nchini Tanzania, hasa baada Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutoa Rasimu ya Pili ya Katiba mpya ambayo ina ibara 271. Katika ripoti ya tume hiyo ambayo ilikabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein, hakuna kitu kilichovuta hisia za watu wengi na kusubiriwa kwa hamu kama suala la mundo wa Muungano wa Tanzania. Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Warioba katika hotuba yake fupi aliyoitoa katika viwanja vya Kareemje, alikiri kuwa suala la muundo wa Muungano wa Tanzania ndilo lililoipasua kichwa Tume hiyo. Kwa kauli yake Tume hiyo ilichukua muda mrefu katika kuyafanyia uchambuzi maoni ya wananchi yaliyokusanywa na Tume hiyo juu ya suala la muundo wa muungano na kulazimika kufanya utafiti zaidi. Kama hiyo haitoshi katika kujiridhisha juu ya suala la muundo wa muungano, Tume hiyo ililazimika kupitia ripoti za tume na kamati mbalimbali zilizoundwa na kutoa mapendekezo juu ya suala la muungano, kama vile Tume za Jaji Kisanga, Tume ya Amina, Tume ya Shelukindo na nyenginezo. Jaji Warioba alihitimisha kutoa matokeo ya maoni ya Watanzania juu ya muundo wa m u u n g a n o a m b a p o kwa Zanzibar asilimia 0.1 (ambazo ni sawa na watu 25) walipendekeza serikali moja, asilimia 34 walipendekeza serikali mbili na asilimia 60 walipendekeza serikali ya mkataba. Kinachoshangaza ni kwamba wapo baadhi ya watu ambao kwa fikira zao na wanavyojihisi kuwa wao ni Wazanzibari zaidi kuliko wengine huku wakisema suala la serikali tatu katu asilan, abadan haliwezekani, h u k u wa k i a p a k u l i n d a mfumo wa serikali mbili uliopo, ambao umechokwa na Wazanzibari. Kinachosumbua kila ukiwafikiria watu hawa unajiuliza masuala mawili mawili, hivi kweli wana udhati wa kuipenda Zanzibar? Ama wanashikilia suala la serikali mbili kuendeleza maslahi yao binafsi na wale wanaowatuma kufanya hivyo? Wakati Rais Jakaya Kikwete akihitimisha matembezi ya maadhimisho ya miaka 50 ya mapinduzi, yaliyoratibiwa na Umoja wa Vijana wa CCM pale katika viwanja vya Maisara, viongozi wa umoja huo walikula yamini kuendelea kulinda mfumo wa serikali mbili. Nilikuwa pembeni kusikiliza kwa makini sababu za vijana hao kwanini waseme
HAYATI Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. tuendelee na serikali mbili, lakini nilikuja kubaini kuwa wao ni makuwadi wa kisiasa ni watumwa wa kundi fulani ambalo linapenda liendelee k u wa m a d a r a k a n i k wa manufaa binafsi kama vile suala la ulua limekuwa teule kwao kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Nathubutu kuwaita makuwadi wa kisiasa kwa sababu ni mambumbu, wenye ufinyu wa mawazo, uwezo na upeo mdogo wa kifikiri, kwa ujumla nilibaini wanaugua maradhi yaitwayo ufinyu wa mawazo. Katika ripoti yake Jaji Warioba ameainisha sababu kadhaa za kimantiki na sio zile za kiporojo kwanini Tanzania iwe na mfumo wa serikali tatu na sio mbili kama ilivyo hivi sasa au serikali moja ambayo maoni yake hapa Zanzibar yalitolewa na watu 25 tu, sina shaka hawa ni watu wenye asili ya Tanzania bara. Sikuwa na shaka k u wa U V C C M n a wa l e wanaowatuma hapa Zanzibar wanaugua gonjwa la uoni finyu, kwani dalili kubwa ya kuugua ugonjwa huu ni kushindwa kutoa sababu za kimantiki ambazo tutazikubali Wazanzibari kwanini tuendelee muundao wa serikali mbali. Ipo hoja nyengine inayoendelea kutumiwa na wahafidhina wanaotaka serikali mbili nayo ni kutokwenda kinyume na m a wa z o ya m a r e h e m u walioasisi muungano mzee Abeid Amani Karume na Mwalimu Nyerere. H i i n i h o j a ya k a m a wale waliopigiwa mifano katika kur-ani, hawajui wanachokifanya au waliodai kufuata waliyowakuta nayo babu zao wakaambiwa na Kuran, hata kama babu zao walikuwa wajinga au hawajui kitu? Hivi jamani mpaka lini tukiwa katika karne hii tutaongozwa na fikra za tuliokwisha kuwazika na sasa ni hitma tu juu yao? Wanasahau kuwa mzee Karume alipokuwa akielezea madhila ya muungano wa serikali mbili aliwahi kutamka kuwa koti likikubana livue, akimaanisha uwezekano wa kujitoa kwenye muungano wa serikali mbili wenye mizengwe. Kwa upande wake marehemu Nyerere wakati alipokuwa hana jinsi ya kuzima kasi ya wabunge waasi G55 mwaka 1993 waliokuwa wanataka Tanganyika yao, aliwatuliza kwa kile kilichoelezwa kuwa muelekeo ni kutoka serikali mbili kuelekea moja. Lakini ni sababu zipi hasa zinazotufanya tuendelee kuyaabudu, kuyaenzi, kuyanyenyekea na kuyaendeleza mawazo ya wafu? Wazanzibari wamechoka na mfumo wa serikali mbili kwa sababu hautoi haki, inakuwaje Muungano ujipanue unavyotaka kuchota mamlaka ya Zanzibar, wakati Zanzibar ikigusa tu wanakuja juu, suala la muungano huu pia limewakera baadhi ya viongozi wa Zanzibar. Nimepitia kitabu cha Rais wa Pili wa Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi kiitwacho The Partner Ship , katika kitabu hicho i n a o n e k a n a wa z i m z e e huyo hakuwa muumini wa serikali mbili na amebainisha wazi kuwa katiba ya muda ya mwaka 1965 ilikuwa na vipengele vilivyoeleza Tanzania kuwa nchi ya shirikisho kwamba kuna s e r i k a l i ya M u u n g a n o , serikali ya Zanzibar na serikali ya Tanganyika.
wa riziki za Wazanzibari? Mbona wanatuuzia mchele wa Kiyela ghali kuliko ule unaotoka Thailand, Pakistan, India na China. Mbona saruji inayotoka Oman na Urusi rahisi kuliko ya Wazo Hill ama kiwanda cha Tanga Cement. Mbona vitunguu thomu vya India rahisi kuliko vya Tanzania bara. Nguzo ya uchumi wa visiwa duniani ni uingiza bidhaa zaidi importation kulikokusafirisha e x p o r t a t i o n . K wa n i n i liwasumbue vichwa enyi wenye mawazo mgando? Mwanafalsafa Aristotle, alipokuwa akitoa tafsiri ya maana neno ujinga, alisema ujinga ni kutokuwa na habari za undani juu ya kitu fulani ama to be a mere lack of information, hili ndilo tatizo la UVCCM na CCM kwa ujumla wake. Dunia imebadilika na hii si jamii ya Wazanzibari ambao wanatosheka na sababu kuambiwa waendelee na mfumo wa serikali mbili eti kwa sababu tu sera na ilani zinaeleza hivyo. Wazanzibari wanafahamu kuwa sera na ilani sio misahafu kutoka kwa Mungu. Hawaoni jinsi Zanzibar ilivyokaliwa shingoni kama ngoma ya kimanga haupumui kwa kila kitu si kwa uchumi, siasa, utamaduni, diplomasia. Mbona wanaCCM wenyewe wanalalamika chini kwa chini kulichoka suala la Rais wa Zanzibar kuchaguliwa Dodoma? Sera ya amani na utulivu si ya CCM, hiyo ni sera yenye uasili wa Wazanzibari tangu zama za kale nashangaa hivi sasa kuwa kufanywa ndio dira. Msingi wa amani na utulivu unatokana na wananchi na sio nguvu za kisiasa. Angalizo liliopo ambalo linapaswa kungaliwa kwa makini ni kwamba hata Zanzibar iwe na siasa safi kiasi gani, hata iwepo amani na utulivu kiasi gani, bila ya uchumi imara ambao mizizi na mihimili yake imekaliwa na serikali ya muungano ipo siku amani na utulivu h u o u t a t o we k a b i l a ya kipingamizi. Suala la uchumi ni muhimu na likiwezekana hilo ndipo amani na utulivu utakapodumu lakini kama mnasisitiza amani na utulivu mnajilia kuku huku wananchi wakishinda hata kupata kishina cha muhogo hapo litatokezea tatizo. Tungalie kwa makini majanga yanayotunyemelea ikiwemo lile la kujaliwa kuwa na vijana ambao hawana ajira, na haiwezekani vijana hao kupata ajira endapo uchumi utataendelea kuwa na serikali mbili. Kwa wale wanaodhani kuwa Wazanzibari wamelala wanakosea, Wazanzibari wanaona mbali, Wazanzibari wanaona mbele na sio kama ngombe anayeona mbele haoni mbali.
14
H A PA N A S H A K A kila aliyesoma au kusikiliza ile simulizi ya mama wa Kiislamu aliyekuwa Masjid Mussa, Mombasa atasikitika na kupandwa na ghadhabu. Maelezo ya mama huyo t u l i ya c h a p i s h a w i k i iliyopita ukurasa wa 3 ikiwa na kichwa cha habari, M a m a a l i ye k u we p o Masjid Mussa aeleza kilichotokea. B a a d a ya k u e l e z e a kwa urefu kilichojiri na yaliyosemwa na vyombo v ya d o l a v ya K e n ya , sasa hebu tuangalie upande wa pili. Kwa maana ya kutumia jicho pevu kufanya tathmini, uchambuzi na kuona iwapo Waislamu walipatia au kuna tatizo. Siku kadhaa kabla ya kufanyika muhadhara huo ulioleta maafa makubwa kwa Waislamu, kulisambazwa kipeperushi kuhimiza watu kufika. Katika sehemu moja kipeperushi hicho kinasema: Alhamdulillah Jihad haiko mbali sasa, na Inshaallah maadam maIkhwa wameshaanza kuwauwa majasusi, dalili ya kuanza Jihad Kenya zaanza kudhihiri. Kisha kipeperushi kikaeleza kuwa vijana wa Jihad wamemuuwa adui wa Uislamu (Ahmed Abdullah Bahshuweiny.) Juu ya kipeperushi hicho ikachapishwa picha ya Ahmed Abdullah Bahshuweiny, waliyedai kuwa adui mkubwa wa Waislamu na hivyo ikatajwa kuwa aliuliwa na Mujahidina na kwamba mkusanyiko wa Masjid Mussa siku ya Jumapili, ilikuwa ni katika kujenga umoja wa vijana wanaopenda Jihad na kuweka mikakati na mipango ya kuwauwa makafiri na maadui wa Uislamu. Moja ya mada zitakazozungumzwa ikatajwa kuwa ni A h k a m u l - J i h a d . Nyingine ni Hukumu ya Shaheed. Kipeperushi kikaandika chini ya picha ya Ahmed Abdullah kuwa Allah awahifadhi (vijana wapenda Jihad) wenye k u f a n ya k a z i h i i ( ya kuwauwa watu kama Ahmed) na awape nguvu juu ya makafiri. Ili kuhakikisha wanapatikana watu wengi, kipeperushi kikatoa motisha, kikasema:
Makala
AN-NUUR
15
Makala
AN-NUUR
Na Rashid Abdallah, MUM WAANDISHI wote wa historia wameshuhudia j u u ya U c h a M u n g u wake, uadilifu na huruma yake, pamoja na uwezo wake mkubwa wa kuongoza kwa haki na kuibadilisha hali ya umma kutoka katika umasikini uliopindukia na kuiweka katika hali njema inayoendelea kuzungumziwa mpaka wakati wetu huu. H u y o s i m we n g i n e ila ni Omar bin Abdull Aziz, ambaye baadhi ya wanazuoni wanamuita kuwa ni Khalifa wa tano baada ya wale wanne wakubwa, ambao ni Abuu Bakar, Omar, Othman na Ally (Rehema za Allah ziwe juu yao). A l i k u w a
Inatoka Uk. 16 Mwezi wa Ramadhani ulipokwisha nilipata muda wa kutosha kufikiri na kujiuliza, kwanini navaa hijab katika mwezi wa Ramadhani pekee na sio muda wote? Kuanzia hapo nilianza mwenyewe kujizoesha kuvaa hijab kila nilipotoka nyumbani. Siku hizi siwezi hata kutoka nje bila kuwa na hijab na sijisikii raha nikiikosa. Hijab imekuwa sehemu ya maisha yangu na inanipa hamasa na ufahamu mimi ni nani na nini lengo la kuumbwa kwangu hapa duniani. Nilikuwa nikivaa kama wanavyovaa wanawake wengi wanavyovaa katika mji. Nimekulia jijini Dar es Salaam. Nilihisi naonekana wa kisasa (up to date) kwa fasheni, lakini nimekuja kutambua
Huyo ndiye Omar Bin Abdull Aziz, cha kushangaza kama si kufurahisha hayo yote aliyafanya ndani ya miaka MIWILI TU. Historia hii ya Omar ni nzuri sana kwa viongozi wa sasa wa Tanzania na hata Duniani haijalishi uwe Muislamu ama siyo Muislamu. Chakuzingatia ni kuwa aliyeondosha umasikini k wa m i a k a m i w i l i ni Binaadamu kama wewe. Siku moja Fatima binti Abdul Malik mke wa Omar bin Abdul Aziz alipoingia chumbani na kumkuta mumewe akiwa juu ya msala akilia. Alimuuliza; 'Mume wangu una nini mbona unalia namna hii? Omar akamjibu; Ewe Fatima! Mimi nimepewa jukumu kubwa katika jambo hili. Nawaza juu ya fakiri mwenye njaa na mgonjwa asiyejiweza, na yule asiyekuwa na nguo ya kuvaa, na yatima asiyekuwa na wa kumtazama, aliyedhulumiwa asiyeweza kujitetea, mgeni asiyekuwa na pa kulala na mateka na wazee na vizuka na
kwamba sisi wanawake wa Kiislamu ni viumbe wanaovutia. Mwenyezi Mungu anapenda tujihifadhi kwa hijab zetu. Hijab ni ulinzi wetu wa nje dhidi ya uovu wa maisha. H a k u n a m t u anayetukandamiza na dunia inahitaji kuona kuwa hatuhitaji kuokolewa au kuwekwa huru. Ndio maana msingi huu ni bora kabisa na ninauunga mkono kwa asilimia mia m o j a n a u t a wa s a i d i a wanawake wasiokuwa Wa i s l a m u k u o n a n i namna gani tunajisikia hasa kwa kuvaa vazi hili tulilolichagua kulivaa. N i k i wa m wa n a m k e wa Kiislamu ninatambua kuwa vazi hili sio nguo tu ya kuvaa, lina maana nyingi kwetu na tunatumaini litawasukuma wanawake wengine kuelekea katika hali ya kujiweka vizuri wenyewe, Insha Allah. Mrs. Mwanaidi Mohamed Ali.
16
AN-NUUR
MAKALA
16
AN-NUUR
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema wakati umefika kwa Wi z a r a ya K a t i b a na Sheria kuandaa sera itakayozingatia maslahi ya walimu wa madrasa, ili kuthamini juhudi zao za kuwafundisha watoto. Maalim amesema, walimu wa madrasa wana kazi kubwa ya kuisaidia jamii katika malezi na kuwajenga wa t o t o k i m a a d i l i , hivyo hakuna budi kuthaminiwa kwa kazi hiyo ambayo muda wote wamekuwa wakiifanya kwa kujitolea. Akizungumza katika hafla ya maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) yaliyoandaliwa na madrasatMuumin Islamiya ya M u e m b e s h a u r i , Maalim Seif amesema hatua hiyo itasaidia kuwapa moyo walimu hao na kuzidisha ari ya kufundisha. Kwa upande mwengine Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesisitiza suala la umoja na mshikamano miongoni
malezi iko katika ngazi ya familia. Katika kuunga mkono juhudi za madrasa hiyo, Maalim Seif ameahidi kutoa kompyuta mbili pamoja na mifuko ya saruji kwa ajili ya kuiendeleza madrasa hiyo. Mapema akisoma risala ya madrasa hiyo ustadh Baiya Maulid, amesema madrasa hiyo iliyoanzishwa mwaka 1995, kwa sasa inakusudia kuanzisha miradi itakayosaidia kukidhi mahitaji ya kuendeleza madrasa yao. Amesema tokea kuanzishwa kwa madrasa hiyo wameweza kupata mafanikio mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuimarisha jengo la madrasa, kuhifadhisha kuran, pamoja na kukuza mashirikiano baina ya walimu na wazazi. Hata hivyo wamesema bado wanakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo uchakavu wa vifaa vyao vya ofisi pamoja na kutaka kunyanyua jengo lao. H i v y o wa m e i o m b a serikali pamoja na wahisani we n g i n e
kuweza kuungana nao katika kutatua kero hizo, ili kuwawezesha watoto kusoma katika mazingira mazuri.
wote, dini mara zote imekuwa ufunguo katika familia yangu, lakini nikuwa navaa hijab katika siku za sherehe za kidini pekee kama sherehe ya ndoa au kwenye Maulid n.k. B a a d a ya k u o l e wa mwaka 2009 nilijaribu kuvaa hijab na jambo la kufurahisha, ni mume wangu ambaye alikuwa kila mara akinieleza kuwa nikivaa hijab naonekana mwanamke mzuri zaidi na mwenye heshima. Inaendelea Uk. 15
Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na POA Printing Works LTD, S.L.P. 4605, Dar es Salaam.