You are on page 1of 3

Nadharia ya ikolojia ni nadharia ya mazingira.

Inachambua kzi za fasihi kwa kuangalia


mazingira na kuchunguza uhusiano uliopo kati ya fasihi na mzingira .Nadharia hii ilianza
miaka ya 1900 na kushika kasi miaka ya 1990. Waasisi wa nadharia hii ni
Buell(1995),Crlolfelly(1996) na mawazo makuu ya nadharia hii inaangalia jinsi fasihi
inavyotumika kutetea au kunusuru mazingira yanayotuzunguka ,inapigania haki za kimazingira
,vipengele mbalimbali vinayojitokeza katika fasihi kwa kuangali mazingira mfano
wadudu,mito,miti,vichaka .Pia katika nadharia hii kuangalia kazi husika inavyomuonesha
mwanadamu kuwa sehemu ya mazingira .Lazima kuangalia vipengele vinavyolenga
kumuelimisha msomaji kuwa ni muhimu katika kutunza mazingira .Nadharia hii ya ikolojia
inayotambuliwa katika riwaya hii ya “Marimba ya majaliwa “iliyoandikwa na Edwin Semzaba
inahusu uhusiano kati ya binadamu na mazingira yake .Riwaya hii inawasilisha mawazo makuu
ya nadharia ya ikolojia kupitia uhusiano uliopo kati ya mazingira na binadamu .Mawazo makuu
ya nadharia ya ikolojia katika “Marimba ya Majaliwa” hii ni pamoja na:.

Nadharia ya kiekolojia inatumika katika jamii kwa njia kadhaa ,ikiwa ni pamoja na hoja
zifuatzo.

Nadharia ya kiekolojia inasaidia kupunguza umaskini :Nadharia hii ya ekolojia inaweza


kutumika kusaidia kupunguza umaskini katika jamii.kwa kuelewa rasilimali za mazingira
zinavyohitajika kwa Maisha ya kibinadamu na kwa kuzingatia haki na uwiano .Mwandishi wa
riwaya ya “Marimba ya Majaliwa”,nadharia hii imesawiri mazingira yalivyotumika katika
riwaya hii mfano Kijiji cha Mafia watu wengi wanajikita katika shughuli za kiuchumi za
kiuchumi kama vile Uvivu kupitia bahari ambapo ilileta biashara miungoni mwao. Hivyo
nadharia ya Okolojia imesaidia kupunguza umaskini kwa watu katika jamii pale ambapo
wameweza kuzitumia rasimali hizi vzuri pasipo kuharibu mazingira.

Nadharia ya Ekolojia imesaidia kupanga maendeleo endelevu: Waasisi wa


Nadharia hii ambao ni Buell na Glotfelty na Fromm 1996, wao wanasema kwamba Ekolojia
inasaidia kupanga maendeleo endelevu kwa kuzingatia mahitaji ya mazingira katika mipango
ya maendeleo. Katika fasihi tunaona kwamba wapo waandishi wanaelezea ekolojia kwa namna
mbalimbali ili kuweza kudhibiti mazingira yao. Mfano Riwaya ya “Marimba ya Majaliwa”
Mwandishi ameweza kupanga maendeleo endelevu kwa kuonyesha jinsi shughuli za uzalishaji
mali zinazofanyika. Mfano katika riwaya hii mwandishi pia ameonyesha shughuli za uvivu
endapo zikitumika vizuri zinaweza kuwa endelevu katika Maisha ya watu wanaozunguka
sehemu hiyo, Pia tunaona kuwa mipango endelevu inasaidia maendeleo kama vile shughuli za
utalii wa majini, katika riwaya ya Marimba ya Majaliwa tunaona pale majilwa akiwa baharini
“aliona meli kubwa imebeba watalii ikielekea Afrika Kusini “(UK 7). Hivyo tukitunza
mazingira vizuri tunaweza kupanga maendeleo endelevu.

Nadharia ya Ekolojia imesaidia Utafiti wa masuala ya Mazingira. Nadharia hii inaweza


kutumika katika kufanya utafiti wa masuala ya mazingira yanayoathiri jamii. Mfano
kwakutumia nadharia hii tunaweza kufanya masuala ya kitafiti ya kimazingira namna
yanavyoathiriwa na jinsi ya kuyatunza. Masuala hayo yanaweza kuwa kama uchafuzi wa hewa
kutokana na uzalishaji wa viwandani , sehemu za masoko mfano soko la samaki linasababisha
uharibifu wa wa maji machafu na harufu mbaya , ambapo tusipochukia hatua mapema tunapata
milipiko ya magonjwa kama vile kipindupindu. Riwaya ya “Marimba ya Majaliwa” mwandishi
anaonyesha pale bibi yake Majaliwa alikumba meza na kuvunja chupa ya wahudumu
waliojitokeza na kumuomba aziondoe kwa sababu zitaathiri mazingira ya binadamu.(UK 20)

Uharibifu wa mazingira unaosababishwa ni shughuli za binadamu katika riwaya ya


malimba mwandishi anaonesha kuwa shughuli za kibinadamu kama kukata miti ovyo uvivu
haram una matumizi mabaya ya rasilimali zinaweza kusababisha kuharibu mazingira kwa
viumbe hai wanaoishi katika mazingira hayo. Mfano katika riwaya mwandishi ameonyesha
Kisiwa cha Mafia jinsi shughuli za uvuvi zinavyoharibiwa na wavuvi kwa kufanya uvuvi
haramu. Hata kwenye jamii ya sasa kuna uharibifu wa mazingira unaosababishwa na shughuli
za binadamu zinazoendelea katika mazingira yetu.

Utegemezi wa binadamu kwa Mazingira: Pia katika riwaya hii ya “Marimba ya


Majaliwa” inaonesha jinsi binadamu anavyotegea mazingira yake kwa kuishi na kujipatia
riziki. Kijiji cha Majaliwa kinategemea uvuvi kwa Maisha yao ya kila siku. Kwahiyo bahari ni
sehemu ya Maisha yao na wanategemea rasilimali hii kwa ajili ya kujipatia kipato. Hata katika
jamii yetu swala la utegemezi wa binadamu kwa mazingira kwaajili ya kujipatia kipato hasa
watu wa tabaka la chini.

Nadharia ya Ekolojia pia uhusisha uhusiano wa ubinadamu wa Wanyama pori:


Nadharia ya Ekolojia inajadili masuala ya kimazingira kwa kuangalia Uoto wa asili na namna
kazi mbalimbali za kazi za fasihi zinavyoweza kunusuru mazingira. Katika Riwaya hii ya
“Marimba ya Majaliwa”, mwandishi Edwin Semzaba anaonyesha kuwa ikiwa binadamu
anataka kuishi kwa amani na ustawi ni lazima atunze mazingira yanayomzunguka. Kuna
uhusiano kati ya binadamu na mazingira kwa sababu vitu vyote hivi vinategemeana: mfano
Wanyamapori wanahama kutokana na mabadiliko ya mazingira kama ukame, mvua, n,k ,Pia
binadamu anategemea Wanyamapori kwa ajiri ya chakula kama vile nyama. Kwa upande
mwingine shughuli za binadamu zinapofanywa bila kuzingatia mazingira sahihi zitaathiri
mazingira kwa sababu vitu vyote vinategemeana.

Nadharia ya ikolojia inasisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya binadamu na


mazingira yake. Riwaya inaonyesha kuwa ikiwa binadamu wanataka kuishi kwa amani na
ustawi, wanahitaji kutunza mazingira yao na kuchukua hatua za kudumisha usawa wa ikolojia.
Mfano katika riwaya hii inaeleza umuhimu wa elimu ya mazingira, utunzaji wa rasimali na
uhamasishaji wa jamii ili kuwezesha kuwepo kwa mfumo endelevu wa Ikolojia. Mfano katika
riwaya hii mwandishi kaeleza ushirikiano uliopo kati ya binadamu na mazingira yake endapo
ataweza kuyatunza vizuri ataweza kupata mambo mazuri au faida kutoka katika mazingira
atakayo yatunza. Hata kwenye jamii ya sasa nadharia ya ikolojia inasisitiza umuhimu wa
ushirikiano kati ya binadamu na mazingira yake.

Nadharia hii ya ikolojia katika riwaya ya Marimba ya Majaliwa ina muhimu katika mazingira
tunayoishi. Nadharia ya ekolojia endapo ikitumika vizuri katika jamii itasaidia utunzaji mzuri
wa mazingira. Pia tunaweza kutunza mazingira vizuri kwa kutumia njia ambazo zinaweza
kunusuru viumbe wa majini. Hata hivyo masuala ya ukataji wa miti linatakiwa lichukuliwe
hatua Madhubuti ili kunusuru uoto wa asili ambayo hutusaidia nishati mvua n.k. Kwa ujumla
nadharia hii ya ikolojia imeweza kusawiri vizuri riwaya ya mwandishi Edwin Semzeba kwa
kuangalia nadharia hii imetumikaje katika jamii.

You might also like