You are on page 1of 46

TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A.

MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

UTANGULIZI
Tamthilia ya Kimya Kimya Kimya iliandikwa na Said.A. Mohamed mnamo (2011) nchini
Tanzania. Imechapishwa na “Printing Services Ltd”. Tamthilia hii inazungumzia juu ya
Ubinafsi wa uongozi ambao umechukua muda mrefu na ukaishia kuwaongoza vibaya
wananchi kwa kuwadhulumu na kuwanyima haki zao. Wananchi wanaongozwa na Mpya
katika harakati za kupigania haki zao, Mpya anampinga babake Bw.Binafsi.Wahusika
wanaopatikana ni kama vile; Bw. Binafsi, Bi.Shoo, Mpwa, Mussa, zanga, Bw. Naona,
Bw.Taja, Bw.Salimina, Bi.Mgeni, Bwa.Subira, Bw.Sikilivu, Mpishi, Fumbo, Kushoto, Kulia,
Mkemeo, Wananchi na Sauti.

UCHAMBUZI WA JALADA / KIFUNIKO CHA TAMTHILIA


Jalada la tamthilia lina kichwa cha “Kimya Kimya Kimya” ambacho kinawakilisha
yaliyomo ndani. Pia, Jalada lina jina la Mwandishi ambaye ni Said A. Mohamed. Waaidha,
Jalada limepambwa na picha mbili za watu waliorembekwa kwa rangi mbili yaani nyeusi na
nyeupe. Mtu katika rangi nyeusi anamwashiria kidole mwenzake eti asiseme yaani abaki
kimya kimya kimya akiwa gizani lakini yule katika rangi nyeusi anamchekelea na kuonyesha
kutaka kusema, kuzileta njia mpya za kujitoa gizani maana rangi nyeupe inaashiria mwanga
wa wazalendo.Picha za watu hao zimefungwa na picha ifananayo na nyoka kiasi kuonyesha
kuwa watu hao wanatoka katika familia majo na kuna msaliti baina yao. Aidha, jalada
linafananua dhamira ya mwandishi na linaonyeshs eti limepambwa na “Longhorn
Publisher.”

PLOTI YA TAMTHHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA Ploti ni mtiririko wa matukio


au matendo kutoka mwanzoni hadi mwishoni. Ploti ya tamthilia hii ni sahili kwa sababu
matukio yanasababishana.Ploti ya tamthilia ya Kimya Kimya Kimya inaanzia katika kisima
tunapowaona Kushoto na Kulia wakisema eti kiu na njaa vinawadhoofisha. Wakiwa hapo
wanaisikia sauti ya kisima inayowashangaza kwa kusema eti waijali na waitetee nchi yao
kwa kuwa ni tamu kuliko Siasa. Wanabaki hapo wakisukumana na kugandamana kimpongo.
Mpya anaelekea kisimani na kuikumbusha hadhira kuwa wakati wa wakusema umewadia
kwa sababu kusema ni haki ya uzawa wa kila kiumbe, binadama na hata wanyama. Baada ya
Mpya kuwaona wakijongeleana kimgongo, anawaambia eti fikra zao ziungane. Mpya
anapewa maji ya ujasiri kutoka kimani anayanywa halafu Kulia na Kushoto wanabagukana
na kusema eti watajitoa mhanga kujotetea. Baada ya hayo, tunawaona Bi.Shoo, Zanga,
Mpya na Mussa wameketi nyumbani mwao wakivitazama vyakula bila kuvinusa na kuvionja
kwa kuwa wamemgonjea Bw.Binafsi. Wakiwa na subira, vyombo vinaanguka na kumfaya
Mpya aseme. Bw.Binafsi anaingia na kuketi, halafu anaombea chakula na vinywaji kwa
majivuono. Mpya anaonekana amekataa kula vyakula. Katika wakati wa kuka, Bw.Binafsi
anawaamuru kumwonyesha utiifu. Wote wanafanya hivyo ila Mpya ambaye anamwambia

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 1


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

vitendo vyake vya ubinafsi. Bw. Binafsi anakasirika. Anaamuru walinzi wamtoe, mama mtu
anaingilia katikati kumtetea ingawa naye anakemewa, na wote wawili wanaondoka.Baada ya
suluhu, Zanga anaonekana amelala kitandani kisha anaamshwa na Mussa anayemwambia ati
amechoka kuwa kimya na sasa anataka kusema. Wakiwa wanapeana maneno, sauti ya Mpya
wanaisikia ikiwaaambia eti wajitohe mhanga na waanze kusema. Baada ya haya, tunawaona
Bw.Naona na Bw.Salimina wakimwambia ukweli Bw.Binafsi kuwa watu wamechoka
kusubiri na wameamka kupigania haki zao. Wanamwambia ati viongozi wa vurugu ni
watoto wake Bw.Binafsi anawaambia kuwakamata. Sauti ya mpya inasikika ikiwajulisha
wananchi juu ya mkutano utakaotekelezwa kupigania haki zao. Wananchi wanakubaliana
naye, wanaishia kukubaliana kwamba mkusanyiko wao hautakuwa na fujo, ghasia na
uchokozi bali wa amani tu. Bw.Naona na Bw.Salimina wanaonekana katika ofisi ya
Bw.Binafsi wakiulizwa ikiwa wameshawakamata wachochezi wa mpomo. Bw.Naona kama
anavyoona anamwambia eti wamejificha katika umma na hawawezi kuonekana. Hatimaye,
Bw.Binafsi na Bi.Shoo wanakabiliwa na umma kwa nguvu na kelere. Wana hofu, na majuto
wakiona mwisho wao umefika. Bw.Binafsi utawala wake unaishia hapo, kushoto na kulia
wanaimba wimbo wa ukombozi wa wanaarifi wananchi kuisimamia nchi yao.

MUHTASARI WA MAONYESHO KATIKA TAMTHILIA YA KIMYA KIMYA


KIMYA.
Kifunguzi (Uk 8 -17)
Wapotea njia……Kisimani--Kulia na Kushoto.
Katika kifunguzi Kushoto analalama akisema eti kule anakotoka hakuna maisha, kiu na njaa
vimemsakama. Akiwa hapo anasikia Sauti ya Kisima kinachomwambia kuwa hakuna uhai na
chakula, kinawaambia kuijali nchi yake na kuitetea kwa sababu nchi ni tamu kulia siasa.
Kulia naye anaingia akiwa amechoka vibaya kwa safari ya myaka ya kuutafuta uhuru ingawa
hajapata pahali pa kusimama, naye analalamikia kiu na njaa vinavyokaririwa.
Kulia pia anashangazwa na Sauti ya Kisima kinachomwambia eti anakotoka ni kukavu na
hakuoti kitu, kinamwambia eti asitazame nyuma bali atazame mbele aijali nchi yake kuliko
siasa.
Kushoto anatoka kichakani ambapo amekuwa amejificha na kuzungumza naye wakisema ya
kwamba nafsi zao ni mbaya lazima zisafishwe kwa kuizima kiu yao. Kulia anamwambia
kushoto kuwa dunia imejaa ukweli uliojaa uwongo. Wanasongeleana, Kushoto anataka
kubaki kushoto lakini anapelekwa kulia, na Kulia anataka kwenda kushoto lakini
anang’ang’anizwa kulia, wanabaki hapo wamegongona na wanasukumana kimgongo
mgongo.
Ni haki kujifudisha kusema, hasa ikiwa hakuna mema!
Onesho la 1 (UK19-24)

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 2


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

Onesho hili linatendeka kisimani. Mpya (Kijana wa kike) anawapita Kulia na Kushoto bila
kuwajali wakiwa wanapingana vile vile. Kulia anamwuliza Kushoto aina na ya hali ya
anayotakoa kushirikia, na Kushoto anamwambia aina na hali ya mpya ya uhuru wa kusema,
kuandika, kulalamika, kukataa na kutoa maoni mwafaka. Mpya anaelekea kisimani halafu
anaikumbusha hadhira ati kusema ni haki ya uzawa kwa kila kiumbe, binadamu hata
wanyama. Kisima nacho kinamshabika na kumwita ili apewe maji ya ujasiri.
Baadaye, anawaonyesha kidole Kulia na Kushoto na kuuliza kwani wanapeana na kusuguana
migongo. Anaendelea kusema kuwa itakadi inakuja na dawa ya taifa ni uzalendo.
Anawaambia ya kwamba, wanalazimika kuungana.
Mpya anaelekea kisimani,na kunywa bakuli la maji na kuwaonyesha wananchi kuwa
anakunywa maji ya ujasiri kwa niaba yake na yao, anawaambia kuwa maji yanasafisha woga,
baada ya kuyanywa maji, anajimwagia yaliyobaki, Kulia na Kushoto wanabagukana na
kusema kuwa hakika nchi ni tamu kuliko siasa. Wote kwa pamoja wanakariri kauli kwa
kusema eti ndio wa kujitolea mhanga.
Giza totoro na totoro ya giza
Onyesho la 2 (UK 26-43)
Katika onyesho hili, Mkemeo ananyamazisha hadhira kwa msisitizo, katika familia ya Mzee
Binafsi, Mpya anaonekana
aneketi upande wake pekee, Mussa na Zanga upande mwingine,mama yao Bi.Shoo
kwenye ncha ya meza, Bw.Binafsi hajaonekana, kiti chake kitupu. Vyakula vya kila aina
vinaonekana mezani, wamemsubiri mwenye nyumba. Wakiwa hapo, chuma kinaanguka
sakafuni ghafla kwa mpasuao mkali.
Mpya anasema kwamba chuma kimeangushwa lakini Sauti inamwambia eti kwao
hawaruhusiwi kusema. Mpya anasema eti yeye ni mwananchi, mzalendo na mkereketwa
ameanza. Vyombo vinammwagia ungao ambao unamfanya aseme.
Mpya anasema eti baba yake ni mtu wa ajabu na nafsi yake mwenyewe. Anaendelea kusema
ati amechoka kusubiri, kungojea na kunyamaza, kwa sababu vinamkandamiza. Mamake
Bi.Shooaliyeketi katika ukingo mwennye hofu anataka kumsimamisha kusema lakini
hawezi.
Baada ya muda, Bw.Binafsi anaingia na walinzi wake baada ya kuketi, yeye na Mpya
wanatumbuliana macho. Bwa.Binafsi anamwamuru Mpya kuwa na adabu na kumkemea
akimwita kigege na mtoto wa ukorofi. Anamwambia eti hakutaka mimba yake iingie. Mpya
ankataa katakata kuinamisha kichwa. Baada ya hayao, Bw.Binafsi anawamuru kumwonyesha
utiifu kwake. Mama yao Bi.Shoo anaanza na kumsihi kwa mapenzi yake. Zanga anafuata
kwa wasiwasi kidogo na kuzungumzia utegemeo wake, anamshukuru kwa kuwatunza vizuri.
Anasema kuwa baba yao ni kil kitu yaani, ni mwalimu wao, ni mganga wao, ni sheshe, ni
padre na msema.Muda wa Mpya unapofika,hasemi bali anaguna wake na kumkumbusha juu
ya vitendo vyake.

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 3


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

Bw.Binafsi anaamrisha walinzi kumburura, Bi.Shoo mamake anajaribu kumhurumia lakini


anakatishwa na mumewe. Bi.Shoo anasema eti hawezi kumtupa mtoto wake na hivyo
wanatoweka pamoja.
Mdogo humfundisha mkubwa kusema
Onyesho la 3 (UK 45-55)
Onesho hili linaanza tukiwaona Zanga, Mussa na mama yao wanamrudia Bw.Binafsi baada
ya suluhu isipokuwa Mpya. Wakati ni usiku wa mamane, Zanga amejilalia chumbani mwaka,
halafu anaamshwa na Mussa kwa kugonga mlango. Zanga anaashiria kidole chake kinywani
akimtarajia anyamaze. Mussa anapojaribu kumjibu alikokuwa na kwa nini anatoroka,
anatumia Sauti ya juu. Zanga anamwambia kuwa anyamaze au atakiona cha mtema
kuni.Mussa anamwambia kuwa wao wanaonyamazishwa lazima watoke na kuzitafuta haki
zao za utoto- haki za binadamu. Haki aliyozaliwa nayo mtu, ya kusema pasi hofu na woga.
Anaendelea kujiuliza mpaka lini atakuwa mtoto, ameamua kusema na ameamua kupiga
kelele. Mpya sauti yake inawaambia eti kila kitu huanza kama mchezo yaani mwanzo wa
ngoma ni lele. Mpya anaendelea kusema eti jambo hilo ni la kusema na kutetea haki za kila
mtu. Onyesho linaishia tukiwaana wote wakisema eti wataungana na wanaojua kusema
wawafundishe kusema kwa kuwa wanaojua kusema ni wengi kuliko wasiokujua kusema.
Kero na wanaokereka….Ndani kumezaa nje, Na nje kumezaa mchakatao wa umma!
Onesho la 4 (UK 57- 61)
Onyesho hili linatendeka katika bustani ya taifa kijijini. Wenye msimamo wa kusema na
kupigania haki zao yaani Bw.Taja, Bi.Subira, Bw.Sikilivu, Bi.Mgeni, Mpya pamoja na
wananchi wamekusanyika kwa Mkutano wa dharura. Katika mkutano huo, Bi. Subira kwa
wazi anasema hana subira tena, yuko tayari kuyafichua yale yaliyofichika.
Bi.Subira anasema eti nchi imekaa kama msitu wa watoro, imejaliwa na waharifu. Wenzake
wanamwunga mkono. Bi. Subira anawaelezea eti hawawezi kujikomboa bila ya kusema.
Anasema vile vile eti nchini mwao, watu wanakata miti ovyo na kujenga nyumba bila vibali.
Aidha, viwanja vya watu vinachukuliwa kwa nguvu, kila pahali pamechafukika, anaendelea
kusema kuwa uzalendo umefifia, wanauza nchi yao kwa bei rahisi…..
Bw.Taja anamwingilia kati na kusema eti orodha ni ndefu hawezi kuimaliza. Naye Bw.Taja
anayataja yale yanayomwuma, akisema kuwa wamepoteza uraia na utaifa wao. Anasema
kuwa wageni ndio wanaojaliwa na kuheshimiwa lakini wao wanaposema, hawasikilizwi.
Wakiwa wapo wanalalamikia mambo yasiyo na kikomo, kundi la wananchi linaloongozwa
na Mpya linaingia. Mpya anawaambia kukomesha fujo kwani inaweza kuwaharibia mambo.
Wananchi kwa ari ya kujikombo,wanasema kwamba hawatasita, hatakoma, wanasema
mpaka kufa kwao.
Wasiwasi wa wazee.
Onesho la 5 (UK 63-70)

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 4


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

Katika ofisi ya kiongozi mkuu (Bw. Binafsi) waziri wa nchi (Bw. Naona) na ofisa wa
usalama (Bw. Salimina) wanaonekana humo. Bw. Naona hafichi mambo yoyote, anasema
kinaganaga jinsi mambo yalivyo. Anapoulizwa kinachotokea Bw. Naona, anamwambia eti
watu wameanza kuamka. Anaendelea kumwambia eti chini ya uongozi wake, watu
wameamshwa na mengi na ni lazima wawe macho.
Pia, Bw.Salimina anapoulizwa jinsi anavyoona mambo, naye kwa msimano thabiti
anamwambia kuwa watu wamekuwa wamelala na sasa wameamka, anaendelea kumwambia
eti elimu aliyoisambaza ni ya uhange inayotukuza uongoza wake, na kwa hiyo wanataka
wairekebishe katiba na waiandike upya. Bw. Binafsi anakasirika na kuanza kulipuka kwa
maneno akiwadharau wananchi eti wamelala fofofo na wanalolijua ni kula mhogo.
Anandelea akionyesha kuwa yeye ndiye kiongozi peke. Anauliza visababishi vya zogo.
Bw. Naona anamwambia eti mambo yalianzwa na Mpya, Mussa na Zanga watoto wake
wenyewe ambao wamewaongoza wananchi. Bw.Binafsi anaahidi kuwa wakirudia vurugu
hizo wakamatwe bila kumbagua yeyote wakiwa ni watoto wake au la kwani mtoto akililia
wembe mpe, ukimkata ajuta mwenyewe.
Wakati ukifika watu husema wakati umewadia!
Onyesho la 6(UK 72-75)
Njiani, watu wanapiga huku na huku, wanasita kuisikia Sauti ya Mpya ambayo inasikika
kokote ikisema kwamba wao wananchi wameamua kesho yake wakutane tena kulalamikia na
kutetea haki zao. Sauti ya umma nayo inaendelea kusema ati hawatki na fujo bali inasikika
ikikubaliana naye eti wako tayari kuingia barabarani na kusema kwa amani.
Mpya kwa utondoti anayesema wazi bila kuficha yatayoshughulikiwa kama vile, kupitia
upya katiba yao, kusimama kidete kudai kugeuza mwendo wao wa kutojali masilahi yao,
kuhakikisha wananchi wanapata hunduma za kijamii, kupigana vita kwa ushujaa kuondoa
ufisadi na kulinda rasilimali zao zinazoimbwa kiholera. Watu au wananchi wanakubaliana na
kuvifanya hivyo.
Baba anataka kuwala watoto wake
Onyesho la 7 (uk77-82)
Onesho hili linatendeka katika ofisi ya Bw.Binafsi. Bw.Binafsi anaonekana
amechanganyikiwa, anatembea huku na huku na kupiga hatua za masafa kama
mwananajeshi. Anazisikia sauti za wananchi zikiimba wimbo wa mapinduzi. Anajaribu
kuwanyanyamazisha lakini sauti zinamchekelea.
Anawauliza Bw.Naona na Bw.Salimina wakiwa wameshawapata wapigaji kelele kama
walivyoagizwa. Bw.Naona anamwambia ukweli kuwa hawajawapata kwa sababu
wamefichwa na umma lakini nyumba kwa nyumba na hatimaye watashikwa. Kwa ghadhabu,
anawafukuza akisema hawezi kuvumilia, anawataka watoto wake kwa lolote.
Wananchi wanaonyesha kuwa wamejitayarisha na wako sawa kwa lolote. Bw.Binafsi
anabaki katika ziwa la fikra na majuto yaliyojaa huzuni. Anaanza na kusema na yoo,

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 5


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

analiomba limkejeli na kumsamehe yaani anaona amebaki peke yake kwa kuwa watoto wake
wamemkimbia, watu wake wamemsusia na kumwendea kinyume. Yoo linamwambia eti
lilimwonya lakini masikio akayatilia komango na kumdharau na hayo ndiyo matokeo yake.
Bw. Binafsi anaanguka chini.
Si shwari tena
Onesho la 8 (uk 84-89)
Nchi inanguruma Bw.Binafsi na Bi.Shoo wana jitimai na hofu wanapozisikia sauti za
wananchi zinagonga kuta za nyumba. Sauti zao zinadai haki zao, wamesubiri miaka 50 lakini
hakuna linalofanyika.Bi.Shoo anamwambia mumewe kuwa wameshamwambia kujiuzulu
kwa masilahi ya nchi na umma lakini yeye bado anang’ang’ania, anaendelea kumwelezea eti
wameshapoteza watoto wao, heshima udhibiti wao wan chi na hawawezi kusikilizwa na
hawawezi kusilizwa na mtu yeyote. Baadaye, tunawaona wananchi wakiikabilia ana nguvu
na kelele nyumba ya Bw.Binafsi. Bw.Binafsi anaonekana akijuta, mwisho wake umefika.
Hatimaye, tunawaona Kulia na Kushoto katika kufungio wakiimba kwa hoi hoi na nderemo.
Wanafurahia mwisho wa utawata wa Bw. Binafsi. Wanaona lililobaki ni wananchi wenyewe
kuisimamia nchi yao.
DHAMIRA YA MWANDISHI
Mwadishi wa tamthilia ya kimya kimya kimya andhamiria kuonyesha baadhi ya viongozi
wenye ubanafsi wanaochukua muda mrefu katika uongozi. Viongozi hawa wana uongozi
mbaya unaodhalimu na kuwatesa wananchi na kuwaonyesha wapiganiaji haki wakijaribu
kujikomboa juu ya uongozi mbaya ambao wanaongozwa na Mpwa.
MAUDHUI KATIKA TAMTHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA
 Maudhui ni kile kinachosemwa katika kazi ya fasihi.
 Aidha, Maudhui ni ujumbe muhimu unaopatikana kwa msomaji kutoka kazi ya mwandishi.
 Isitoshe, Maudhui ni ile mada inayoendelezwa na wahusika katika mazungumzo yao.
 Hali kadhalika, maudhui ni jumla ya mawazo yote yanayozungumzwa pamoja na mtazamo
wa mwandishi juu ya mawazo hayo.
 Maudhui hujumuisha mawazo pamoja na mafunzo tofauti yaliyomsukuma msanii hadi
akatunga na kusani kazi ya fasihi.
Hivi basi maudhui yafuatayo yanapatikana katika kazi ya “Kimya kimya kimya” ;
1. Kimya/ Unyamavu.
* Kimya ni hali ya mtu kunyamaza au kunyamazishwa ili asiseme chochote. Bila shaka, kimya
ndiyo maudhui kuu inayoendeleza tamthilia hii. Katika tamthilia hii, wahusika wengi
wanalilia kusema maana wamebaki kimya kwa muda mrefu. Kwa mfano, tunamwona
Kushoto anamwambia mwenzake Kulia eti anataka kubaki kushoto kwa namna na hali mpya
ya uhuru wa kusema, kuandika, kulalamika, kukataa na kutoa maoni mwafaka. Bila shaka,
maneno kama haya yanaoynesha kuwa hajasema hivyo maudhui ya kimya (UK 19).

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 6


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

* Pia, maneno ya Mpya yanaonyesha maudhui ya kimya kwa mfano, tunamwona anasema,
“Umeshafiki…..umeshafika…umeshafika wakati wa kusema….” Anaendelea kusema
kuwa kusema ni haki ya uzawa kwa kila kiumbe, binadamu hata wanyama, anatamani siku
moja kila mtu aseme, atoe madukaku yake. Bila kudanganya, haya yanaonyesha kuwa watu
wamekuwa wamenyamazishwa hivi kuthibitisha maudhui ya kimya (UK 20-21).
* Isitoshe, maswali ya Mpya nayo yanaonyesha maudhuli ya kimya. Kwa mfano, tunamwona
anauliza Kulia na Kushoto, “Jamani nyinyi nani? Nyinyi nani mnaonyamanza kimya?”.
Kwa ukweli, maswali haya yanathibitisha maudhui ya kimya (UK21)
* Bila shaka, amri ya Mkemeo nayo lazima inatetea maudhui ya kimya. Kwa mfano,
tunamwona ananyamazisha hadhira akisema, “Kimyaaaa! Kimyaaa! Nyamazeeeni!
Anaendelea na kusema, “nasema kimya! Hamsikii?” Kwa dhahiri, hadhira inanyamazishwa
hivi kuhakikisha maudhui ya kimya (UK26).
* Vile vile, baada ya Mpya, Zanga, Mussa na mama yao Bi.Shoo kunyamaza kwa muda mrefu,
ghafla chuma kinaanguka na kumfanya Mpya aseme wazi na kelele mara ya kwanza katika
maisha yake.Mathalani, tunamwona anasema, “ Kikaango cha chuma kimeangushwa
hatimaya!” Baada ya kauli hii, Sauti inajitokeza ikiuliza ni nani amemruhusu kusema kwani
kwao hawasemi waziwazi wala hawasemi kwa kelele. Mpya anajibu kuwa yeye ameanza
(UK 26-28)
* Kimya ni maudhui yanayothibitishwa na maneno ya Mpya. Kwa mfano, Sauti inajitokeza na
kumkumbusha eti yeye ni mtoto wa Bw.Binafsi na Bi.shoo ambaye huruhusiwi kusema
lakini yeye anajibu kuwa upeo umeanza kuvisemesha vyumba, kukisemesha kila kitu na
kuzisemesha nafsi zao. Maneno haya yanadhihirisha kuwa watu wamekuwa kimya (UK 28).
* Fauka, katika familia ya Bw. Binafsi, wanafamilia wameyamaza, Mpya anajaribu kuelezea
matendo ya babake na kusema, “Mtu wa ajabu! Nafsi yake ni yake mwenyewe. Lakini nafsi
zetu si zetu ni …..aaa sisemi…. Siruhusiwi kusema!” Pia, anaendelea kusema ati amechoka
kusubiri na kunyamaza. Kwa wazi, vitendo hivi vinaonyesha maudhui ya kimya (UK 30-31).
* Kimya lazima ni maudhui ambayo imetawala tamthilia ya Kimya Kimya Kimya. Kwa
mfano, tunamwona Mpya, anatwelezea kuwa mamake Bi.Shoo ameketi katika ukingo wa
dunia, angekuwa na la kusema lakini hasemi. Mathalani, anajaribu kumnyamazisha Mpya
yaani anasema, Mm Mpya…..maneno yake yanapotelea pote na kubaki kimya (UK32).
* Juu ya hayo, Mpya anatufafanulia kuwa na ndugu zake, kaka na dada yake wanatetemeka
kwa hofu ingawa nao wana hamu ya kusema. Hiki bila shaka, kinaonyesha eti wapo kimya
na kudhihirisha maudhui ya kimya (UK32)
* Kimya yenye uzito inadhihirishwa na maneno ya Zanga wakati anapoonyesha utiifu wake
kwa baba yake. Kwa mfano, anasema, “…….unatoka kijasho kwa ajili yetu. Unafikiri kwa
ajili yetu. Unasema kwa ajili yetu. Sisi tumenyamaza tu……” Zanga hapa anaonyesha
kimya kwani baba yao anawasemea (UK37).

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 7


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

* Ghalibu, tunamwona Zanga anamyamazisha Mussa ambaye amekuja usiku wa manane. Kwa
mfano, Mussa anagonga mlango kwa nguvu huku akimwita na kumwamsha Zanga. Zanga
anainuka na kuweka mto mdomoni kuzuia maneno yasitoke kwa nguvu yaani ‘‘Shhhhhhh!
Kimya ….kimya ……kimya…” Bila mzunguko, haya yanathibitisha maudhui ya kimya (UK
45)
* Hali kadhalika, tunamwona Mussa anaendelea na kusema eti anataka kusema na kuondoa
Unyamavu. Mathani, tunamwona anasema, … “ nimeamua nisema. Nimeamua kupiga
kelele….” Mambo haya yanaonyesha kuwa Mussa amekuwa kimya kwa muda mrefu (UK48)
* Waaidha, wananchi wanaoimba wimbo wakupigania haki zao, wananyamazishwa na Bw.
Binafsi kwa ukali. Kwa mfano, anageukia hadhira na kuiamrisha, “Kimya, kimya, kimya!
Mnaimba nini nyinyi? Mnanifanyia inda siyo?” lazima huu ni unyamavu (Uk 77-78).
* Katika maudhui sambamba, Mpya anawashauri wenzake yaani Zanga na Mussa ambao
hawajui kusema kwamba wafundishwe na wale wanaojua kusema. Sauti ya Mpya nayo
lazima inawahimiza kuwa sasa wanaojua kusema ni wengi kuliko wasiojua kusema. Kwa
kweli, ikiwa watu hawajaanza kusema kweli wamenyamaza, vivi hivi kutetea maudhui ya
unyamavu (UK 54-55
2. Upiganiaji haki/ Uzalendo.
 Uzalendo ni hali ya mwanamchi kuwa tayari kuifia na kuipiginia nchi yake kwa hali yoyote
bila kukata tama. Wahusika wengi katika tamthilia hii wanaonyesha uzalendo kwa kuupinga
uongozi mbaya mathalani sauti ya ndani ya kisima inaonyesha uzalendo yaani inamwambia
Kushoto eti atazame mbele asitazame nyuma, aijali yake na kutetea. Hivi vyote vinaonyesha
uzalendo (UK 8).
 Aidha, maneno ya Kushoto nayo yanaonyesha uzalendo. Kwa mfano, tunamwona
anamwambia Kulia ya kwamba anataka kubaki kushoto kwa namna ya upya yenye uhuru wa
kusema, kaundika, kulalamika, kukataa na kutoa maoni mwafaka. Kwa ukweli maneno haya
yanathibitisha maudhui ya uzalendo katika tamthilia ya Kimya Kimya Kimya (UK19)
 Waaidha, Mpya naye kweli ni mzalendo, yaani anaonekana bila hofu akisema,
“Umeshafika…. Wakati wa kusema ingawa mimi peke yangu sina uzito wa kusema. Mimi
pweke, kusema ni haki ya uzawa kwa kila kiumbe, binadamu na hata wanyama. Natamani
siku moja kila mtu aseme.” Maneno haya bila kudanganya yanahakikisha uzalendo wake
(Uk21).
 Hali kadhalika, wanapomwita Mpya kumnyweshe maji ya ujasiri anaitikia vizuri kuonyesha
misimamo thabiti, mathalani tunamwona anasema kuwa lazima yuko njiani. Pia, anaendelea
kusema ati lazima mmoja ajitolee muhanga ndipo usasa utakapomheshimu naye kuuheshimu.
Haya yote yanadhihirisha uzalendo (UK21)
 Vile vile, uzalendo wa Mpya unaonekana anapokunywa maji ya ujasiri na kuyajimwagia
Mwilini. Kwa mfano, anatekea kiamo na kugugumia maji ya ujasiri jambo ambalo analiita

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 8


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

tambiko la uhai wa nchi yake. Baada ya kuyanywa, hayo, anasafisha hofu na woga ndipo
Kulia na Kushoto wanabagukana (UK23)
 Pia, baada ya Kulia na Kushoto kubaguana, wanasema kauli zinazodhilirisha uzalendo, yaani
wanasema kuwa nchi ni tamu kuliko siasa, wanaendelea kusema wao ndio watawala,
wataliwa wenye unchungu wa nchi na watajitolea mhanga kuipigania. Bila shaka, hivi vyote
vinaonyesha uzalendo (UK 24).
 Bado juu ya uzalendo, Mpya ni mfano mzuri wa kuonyesha maudhui haya. Kwa mfano,
anapoambiwa na sauti kuwa kwao watu hawasemi waziwazi na kupiga kelele, Mpya
anasema, ‘mimi nimeanza. Mimi mwananchi. Mimi mzalendo’ na hivi uzalendo
katikatamthilia hii (UK 27-28)
 Bila shaka, Mpya hajachoka kuonyesha uzalendo wake. Kwa mfano, tunamwona akisema eti
ameshoka kusubiri, amechoka kugonjea, amechoka kunyamaza. Anaendelea kusema ati
kunyamaza kunamwangamiza na anauliza, “Kwa nini kila siku tugonjee? Tugonjee,
tugonjee mpaka lini?”. Kwa kweli, matendo kama haya yanarejesha uzalendo (UK31)
 Katika maudhui sambamba, Mvutano kati ya Bw.Binafsi, Mpya na Bi.Shoo nao unaonyesha
uzalend. Bi.Shoo anasema kishujaa akimwambia Bw.Binafsi ya kuwa hana ujasiri mbele ya
mtoto wake. Anaendelea kumwambia eti unchungu wa mwana amjuaye ni mzazi. Mvutano
huu unajitokeza kwa sababu Mpya amekataa kakata kuonyesha utiifu kwa babake. Hatimaye,
tunamwona Bi.Shoo anasema, “Siwezi kumtupa mtoto wangu hasa kwa sababu ni msema
kweli. Heri tuondoke sote”. Lazima huu ni uzalendo (UK43)
 Bila kurandagatana, Mussa naye ni mzalendo yaani tunamwona anajiuliza eti mpaka lini
atakuwa mtoto wa kuongozwa na mawazo ya mtu mwingine. Anamwambia Zanga ya kuwa,
watoke watafute ukimbizi za binadamu, haki aliyozaliwa nayo kila mtu ya kusema pasi na
hofu wala woga. Anaonekana akisema ya kwamba aneamua kusema na kupiga kelele. Bila
shaka, hivi vyote vinathibitisha maudhui ya uzalendo (uk 47-48)
 Fauka, Zanga Mussa na Mpya wote pamoja ni wazalendo. Kwa mfano, tunawaona
Wakisema ya ati wameshatambua. Mussa anamwambia Zanga kuwa wawatembelee
wajuaokusema wawafundishe kusema ili waache kunong’onanong’ona na kugumaguguma
wapiganie haki zao. Sauti ya Mpya inawahimiza ya kuwa wanaojua kusema ni wengi kuliko
wasiojua kusema. Wahusika hawa kwa ukweli ni wazalendo (uk 54)
 Kuongeza hapo, wananchi wanaonyesha uzalendo wao. Mathalani, wanajumuika
wakiongozwa na Mpya kupigania haki zao. Kwa mfano, wanaonekana katikati ya uwanja wa
bustani wakisema, “Kimya kimya kimya wananchi kmya kimya wananchi. Kimya
tusiharibu mambo” wanaendelea kusema ya kuwa hawatasita, hawatakoma mpaka kufa
kwao. Vivi hivi huonyesha uzalendo (uk 61)
 Fauka ya haya, Mpya bado anadhihirisha uzalendo wake anapoongoza uchochezi wa mgomo.
Kwa mfano, tunamwona anasema kuwa wananchi wameamua keshoye kukutana na

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 9


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

kulalamikia haki zao bila fujo bali kukutana na kulalamikia haki zao bila fujo bali kuweka
wazi kere zao. Wananchi nao kweli wanakubaliana na kauli yake (uk 72-73)
 Ghalibu, wimbo wa wananchi nao unaonyesha uzalendo. Kwa mfano, tunawaona
wanamwimbia Bw.Binafsi wimbo wa kupigania haki zao. Mathalani, wanasema, “Haki ni
kama upanga Usipotekeleza utajutia leo na kesho ndiyo……….” (uk 77)
 Bila kuchoka, wananchi ni wazalendo halisi yaani wanamkabilia Bw.Binafsi nyumbani
mwake bila woga. Mathalani, wakisema kwamba wanadai haki zao, wamesubiri miaka zaidi
ya 50 hakuna la maana linalofanyika. Wanaendelea kusema kuwa hawatasubiri tena kwa
hiyo, matendo haya yanahakikisha maudhui ya uzalendo. (uk 84)
 Ghalibu ya hayo, mambo matano muhimu yanayowekwa na Mpya wazi kupigania haki zao
yanaonyesha uzalendo. Kwa Mfano, tunamwona, anawaambia wananchi ya kuwa watapitia
upya katibu kwa masilahi ya wamanchi, watasimama kidete kudai kugeuza mwendo wao
kutojali masilahi yao, wahakikishe wananchi wanapata huduma za kijamii kutonoa masilahi
yao, wapigane vita kwa ushujaa kuwondoa ufisadi na kuzilinda rasilimali zao. Kwa wazi,
haya yanatetea maudhui ya uzalendo (Uk 73-74)
 Bw.Naona naye anaonyesha uzalendo kwa kusema kama anavyoona. Kwa mfano,
anamwambia Bw.Binafsi wazi kwamba watu wamekuwa wamelala lakini sasa wameamka.
Anaendelea kumwamba ukweli eti anaelewa kwamba chini ya uongozi wake watu
wameamshwa na mengi, kwa hivyo wanapaswa wawe macho.Na kwa hiyo, anawashabika
kupigania haki zao na hiki kinaonyesha kuwa naye ni mzalendo (uk 63)
 Uzalendo kadhalika unathibitishwa na msimamo thabiti wa Bw.Taja ambaye anaongezea juu
ya mambo maovu yanayofanywa na siasa ya Bw.Binafsi. Kwa mfano, anamshabika kwa
kusema kwamba wamepoteza uraia na utaifa wao lakini wageni ndio wanaojaliwa na
kuheshimiwa. Anaendelea na kusema kuwa wao wakisema hawasikilizi.(uk 60)
 Bw.Sikilivu naye anahakikisha ya kuwa matatizo yapo lazima na yanamiminika. Hivi basi
anataka wananchi wajumuike, waungane mikomo ili waweze kupigania haki zao
wajikomboe (uk 58)
 Kwa kutamatisha, Bi. Mgeni naye ni mzalendo hususan tunamwona anamwunga mkono
Bi.Subira eti nchi yao kwa ukweli haina uongozi kwa sababu uongozi uliopo ni wa kiubinafsi
(Uk 58).
2. Ubinafsi
 Ubinafsi ni tabia ya mtu kuyajali masila yake mwenyewe bila kuwajali wengine. Hiki lazima
kinaomekana wazi na jina la Bw.Binafsi. Bw.Banafsi hataki wananchi wapiganie haki zao.
Kwa mfano, wananchi wanapodai kubadilisha katiba ya nchi, Bw.Binafsi anawadharau kwa
kuwaita vinyangarika wanaolala fofofo kama pono. Anaendelea kusema eti wao.
Wanachokijua ni kula mhogo tu. Pia, tunamwona akisema, “katiba ni ya viongozi na
kiongozi ni mmoja” yaani yeye. Bila shaka huu ni ubinafsi (uk 66)

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 10


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

 Kuongeza katika ubinafsi, maneno ya Mpya nayo yanaonyesha kuwa nchi yao ni ya mtu
mmoja. Kwa mfano, anasema, “tunataka nchi iwe yetu sote. Isiwe tena nchi ya watu
wachache wanaoiba mali na kwenda kuikindika katika mataifa ya nje”. Bila kudanganya,
maneno haya yanaonyesha ubinafsi (uk 74)
 Vile vile, Bi.Subirti naye anaonyesha kuwa nchi yao imejaa ubinafsi. Mathalani, tunamwona
anasema kuwa ofisi zao ni chafu, makazi machafu, vijiji vichafu, mwenendo mchafu, nafsi
zao chafu kwa sababu ubinafsi ndio unaowatia ujinga. Bila shaka, ubinafsi ni maudhui katika
tamthilia ya Kimya Kimya Kimya (uk 59)
3 Uongozi.
 Uongozi ni hali ya mtu kuchukua mamlaka miongoni mwa wenzake. Katika tamthilia hii,
kuna aina mbili za viongozi, viongozi wanaoendeza uongozi mbaya na viongozi wanaojali
masilahi ya wananchi. Uongozi mbaya ni ule usioegemea masilali ya wananchi. kwa mfano,
Bw. Binafsi ni kiongozi mbaya ambaye amejaa ubinafsi, ufisadi, mateso, dhuluma na
kadhalika. Mathalani, tunamwona hataki wananchi wapiganie haki zao yaani anaamrisha
askari kuwapiga rungu (uk 61)
 Vile vile, Bw.Binafsi ni kiongozi mbaya anayetesa familia yake. Kwa mfano, anamtesa
Mpya kwa sababu amepinga uongozi wake mbaya. Mathalani, tunamwona anaamrisha
walinzi kumwendea Mpya na wanamburura kama gunia la makaa na kumfukuzia nje (uk
41)
 Aidha, Bwana Binafsi ni kiongozi mbaya ambaye ananyima wananchi haki zao. Kwa mfano,
wananchi wanapomwomba kubadilisha katiba yeye analipuka kwa matusi bila kuwajali. Kwa
mfano, tunamwona anawaita vinyangarika wanaojua kulala na kula mhogo. Anawaambia
kuwa wao hawajui lolote juu ya katiba kwani wao si viongozi wala kiongozi ni mmoja. Hivi
hivi, vinathibitisha uongozi mbaya (uk 66)
 Kwa upande mwingine, kuna viongozi ambao wanajali masilahi ya wananchi na hivi
wanajaribu kuwaunga mkono ili wajikomboe juu ya uongozi mbaya wa myaka mingi. Kwa
mfano, Bw. Naona (anasema kama mambo yalivyo), huyu ni waziri wa nchi Bw.Naona,
Bw.Salimia naye ni kiongozi anayefanya kazi kama ofisa wa usalama (uk 63)
4. Njaa na Kiu.
 Njaa ni hali ya kukosa vyakula. Katika tamthilia hii tunaona wahusika wanalalamikia njaa.
Kwa mfano, tunamwona Kushoto anasema kwamba kule anakotoka hakuna maisha kwa
sababu ya njaa na kiu (uk 8).
 Aidha, Kulia naye anaihisi njaa na kiu vibaya. Kwa mfano, tunamwona anasema ,
“…..naisikiliza nafsi yangu, lakini. Siisikii. Nahisi nafsi ya mtu mwingine ndiyo
inayoniongoza. Njaa, njaa,. Kiu, kiu, kiu ….” (uk 11).
 Bila shaka, maneno ya Bi.Subira nayo yanatetea maudhui ya njaa. Kwa mfano, tunamwona
akisema, “…. Chakula kimekuwa ghali kupatikana. Kila mtu analia njaa, njaa, njaa na

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 11


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

mashamba tunayo”. Baada ya kuangalia mambo kama haya hatuna budi kusema kuwa kuna
maudhui ya njaa. (uk95)
5. Migogoro.
 Migogoro ni mikinzano au mivutano miongoni mwa wahusika yanayosababishwa na
kutokubaliana. Kwa mfano, katika tamthilia ya Kimya Kimya Kimya tunaona mgogoro kati
ya Kulia na Kushoto unaosababishwa na hamu ya kujikomboa. Mathalani, tunawaona
wanagonganisha migongo na kusukumana. Kushoto anamsukuma Kulia aruda Kulia na
Kushoto anasukumwa aende kushoto (uk 15).
 Mgogoro mwingine unajitokeza katika ya Mpya na bakake Bw.Binafsi. Kwa mfano, baada
ya Bw.Binafsi kuingia mwake, wengine wanainamisha vichwa ila Mpya jambo ambalo
babake linamfanya kumkaripia kwa mfano, Binafsi anamwita Mpya Mtoto wa Ukorofi,
kigego na hata anajuta kwa kumzaa (uk 34)
 Juu ya hayo, Bw.Binafsi na Mpya nao wanaonyesha mgogoro katika mlo. Wakiwa wanakula,
Bw. Binafsi anaamri watoto wake na mkewe kuonyesha utiifu wao kwake lakini yeye Mpya
anaguna na halafu anambwambia vitendo vyake vibaya jambo ambalo. Linamkera. Anawaita
walinzi ambao wanakuja kumburura kama gunia la makaa (uk 39-41)
 Hali kadhalika, kuna mgogoro kati ya Bi.Shoo na mumewe. Kwa mfano, tunamwona
Bi.Shoo akijaribu kumtetea mtoto wake lakini Bw.Binafsi anamwingilia, Bi. Shoo anamshika
mtotowe mkono wanaondoka pamoja (uk 43).
 Fauka, wananchi na askari polisi nao wanaonyesha mgogoro. Wananchi wanapojumuika
kuambiana jinsi watakavyopigania haki zao, wakiwa katika uwanja wa bustani, askari polisi
wanajitokeza wakiwa wamebeba virungu na kuwatandika viboko. Kwa kweli huu ni
mgogoro wazi (uk 61).
 Mgogoro mwingine unajitokeza kati ya wananchi na Bw.Binafsi. Kwa mfano, wananchi
wanamwendea kwake wakinguruma, sauti zao zinasikika kwa vitisho na kusema kwamba
wanataka haki zao. Wanaendelea kusema eti wamesubiri zaidi ya myaka hamsini na hakuna
linalofanyika. Kundi lao linaonekana limebeba mabango. Kwa uhakika kuna maudhui ya
mgogoro (uk 84)
6. Mapenzi ya dhati.
 Ni hali ya kuwa na moyo wa kumtakia mema mwenzako. Kwa kurejelea tamthilia hii,
tunamwona Mpya akionyesha mapenzi yake kwa mamake (Bi.Shoo) yaani anamtakia mema.
Mathalani, amhurumia chini ya mateso mbaya wa Bw.Binafsi kwa mfano, tunamwona
akisema eti mamake ameketi katika ukingo wa dunia, ana hofu za kuanguka na kuangamia,
kwa hiyo anamtetea. Hiki kinaonyesha mapezi (uk 32)
 Waaidha, kama wasemavyo wahenga, “Mtenda mema hulipwa mema”, naye Bi.Shoo
mamake Mpya anamtetea dhidi ya ukatili wa babake. Kwa mfano, Bw.Binafsi
anapomkaripia, Bi.Shoo anaingilia kumtetea mtoto wake na ndivyo tunamwana anasema,
“Uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi.” kweli haya ni mapenzi (uk 42)

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 12


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

 Vile vile, mamake Mpya anaonyesha mtoto wake mapenzi. Kwa Mfano, tunamwona
anasema, “siwezi kumtupa mtoto wangu hasa kwa sababu ni msema kweli. Heri tuondoke
sote” kauli kama hii inahakikisha uchungu wa mwana aujuaye mzazi yaani mapenzi (uk 43)
 Bi.Shoo naye anaonyesha mapenzi yake kwa mumewe Bw.Binafsi. Hiki kinafanyika
anapoonyesha utiifu wake kwake. Mathalani, anasema kuwa Bw.Binafsi alisheheni mapenzi
kwake. Pia, anamshukuru kwa kuwa nguzo nzuri kwa familia yao na kuwa fahari kwake. (uk
36).
7. Utajiri
 Ni hali ya kuwa na mali na pesa za kutosha. Familia ya Bw.Binafsi ni tajiri kwani inaonekana
ina vyakula vya kila aina, ina mlinzi (uk 27).
 Pia, maneno ya Bw.Binafsi yanadhihirisha utajiri wake. Kwa mfano, anaposhukuru Mungu
kwa kumtia imani kuitunza familia yake anasema, “….fumbueni macho muone ukosefu,
njaa, na maradhi yalivyojaa dunia nzima. Tazameni majirani. Hawana cha kutegemea.
Lakini kwenu vimejaa vitu tele vya manufaa. Mnakula mnachokitaka mnavaa
mnavyopenda mnakwenda vyuoni kuelimika” (uk 34).
 Mwandishi Said A. Mohamed anausawiri kikamilifu utajiri wa Bw. Binafsi. Kwa mfano,
anasema eti chumbani mwa vijana wawili wa kiume Mussa na zanga kina vitanda vya kisasa,
kuna samani na mapambo yakitajiri. Anasema kuwa chumba ni cha kitajiri.na kwa hiyo, ni
bora kusema eti kuna maudhui ya utajiri katika tamthilia ya kimya kimya kimya (uk 45).
8. Nafasi ya mwanamke/ usawiri wa mwanamke/ hadhi ya mwanamke.
Nafasi ya mwanamke ni jinsi mwanamke anavyosawiriwa na mwadindishi au hadhi
anayopewa katika jamii. Katika tamthilia hii, mwanamke anasawiriwa;
 Kama mzalendo, mzalendo ni yule mtu ambaye yuko tayari kuipinia na kuifia nchi yake kwa
hali yoyote. Kwa mfano, Mpya naye kweli ni mzalendo yaani anaonekana bila hofu akisema,
“umeshafika, umeshafika…. Umeshafika …..umeshafika wakati wa kusema ingawa mimi
peke yangu sina uzito wa kusema. Natamani siku moja kila mtu aseme” maneno haya bila
kudanganya yanahakikisha uzalendo wake (uk 21)
 Pia, wahenga wanapomwita Mpya kumnywesha maji ya ujasiri, anaitikia vizuri kuonyesha
kuwa yuko tayari kuipigania na kufia nchi yake. Mathalani tunamwona anasema kuwa
lazima yuko njiani. Pia, lazima anaendelea kusema eti mmoja ajitolee mhanga ndipo usasa
utakapomheshimu naye kuuheshimu. Haya yote yanadhihirisha uzalendo wake (uk 21).
 Vile vile, uzalendo wa Mpya unaonekana apokunywa maji ya ujasiri. Kwamfano, anateka
kiamo na kugugumia maji ya ujasiri jambo ambalo analiita tambiko la uhai wa nchi yake.
Baada ya kunywa maji hayo, anasafisha hofu na woga wake na wa wananchi (uk 230).
 Bila shaka, Mpya ni mfano mzuri wa kuonyesha uzalendo. Kwa mfano, anapoambiwa na
Sauti kuwa kwao watu hawasemi waziwazi, anasema ‘mimi mwananchi. Mimi mzalendo na
mkereketwa’. Kwa kweli, haya yanaonyesha uzalendo wake (uk 27-28)

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 13


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

 Isitoshe, Mpya anaonyesha uzalendo wake anaposema eti amechoka kusubiri, amechoka
kugonjea, amechoka kunyamaza. Anaendelea kusema ati kunyamaza kunamwangamiza na
anauliza, “kwa nini kila siku tugonjee? Tugonjee, tugonjee mpaka lini?” Kwa kweli
maswali haya yanahakikisha uzalendo wa kijana wa kike Mpya (uk 31).
 Hali kadhalika, Mvutano baina ya wanawake (Mpya na Bi.Shoo) na Bw.Binafsi unathibitisha
uzalendo. Kwa mfano, tunamwona Bi.Shoo anaonyesha uzalendo wake kishujaa
anapomwambia Bw.Binafsi ya kuwa hana ujasiri mbele ya mateso ya mwanake. Anaendelea
kumwambia ati uchungu wa mwana aujuaye mzazi. Mvutano huu unajitokeza kwa sababu
Mpya amekataa katakata kuonyesha utiifu wake kwa babake. Hatimaye, tunamwona Bi.
Shoo anasema, “Siwezi kumtupa mtoto wangu hasa kwa Sababu ni msema ukweli. Heri
tuondoke sote” Kwa kweli huu ni uzalendo (uk 43).
 Waaidha, Bi.Mgeni naye ni mzalendo hususan tunamwona anamwunga mkono Bi.Subira eti
kwa ukweli nchi yao haina uongozi kwa Sababu uongozi uliopo ni uongozi wa kibinafsi na
kwa hiyo, wanaungana na kuupinga uongozi wa Bw.Binafsi (uk58).
 Bila shaka, maneno ya Subira yanaonyesha uzalendo wake hususa anaposema kuwa
wamekusanyika kwa madhumuni ya kujifungua dhidi ya uongozi mbaya. Anaendelea
kusema eti hawawezi kujikomboa bila ya kusema na ni lazima waseme hivi basi ni mzalendo
(uk 59).
 Ghalibu ya hayo, mambo matano muhimu yanayowekwa wazi na Mpya yanaonyesha kuwa
mwanamke kwa kweli ni mzalendo. Kwa mfano, tunamwona anawaambia wananchi ati
wanataka kuipitia katiba upya kwa masilahi ya wananchi, watasimama kidete kudai kugeuza
mwendo wao wa kutojali masilahi yao, wahakikishe wananchi wanapata huduma za kijamii
kutonoa masilahi yao, wapigane vita kwa ushujaa kuondoa ufisadi na kuzilinda rasilimali
zao. Umilisi wa kusimama kidete na kuyataja haya wazi unatetea uzalendo wa mwanamke
katika tamthilia ya Kimya Kimya Kimya (uk73-74)
 Fauka ya hayo, mwanamke (Kijana wa kike) Mpya anadhilihirisha uzalendo wake wakati
anapoongoza uchochezi wa mgomo. Mgomo huu unalenga kumwondoa Bw.Binafsi katika
uongozi. Kwa mfano, tunamwona Mpya anasema ati wananchi wameamua kesho yake
kukutana na kulalamikia haki zao bila fujo bali kuweka wazi kereo zao. Wananchi hao
lazima uanakubaliana na kauli yake. Haya yote yanamshauri Mpya kama kijana mzalendo
(uk 72-73).
 Kando na uzalendo, mwanamke pia anasawiriwa kama mwenye mapenzi. Mapenzi ni hali ya
kuwa na upendo na kutakiana mema. Kwa mfano, tunamwona Mpya akiyaonyesha mapezi
yake kwa mamake. Mathalani, anamhurumia chini ya uongozi mbaya wa babake. Kwa
mfano, anasema eti, mamake ameketi katika ukingo wa dunia, ana hofu za kuanguka na
kuangamia. Kwa hiyo, anamtetea na kuonyesha kujali, hayo ni mapenzi (uk 32)
 Waaidha, kama wasemavyo wahenga, “mtenda mame: hulipwa mema”, Bi. Shoo naye
anaonyesha mapenzi yake kwa mtoto wake Mpya wakati anapomtetea dhidi ya ukatili wa

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 14


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

babake wa kumkaripia Mpya. Bi.Shoo anaingilia kati kumtete na ndivyo tunamwona


anasema “Uchungu wa mwana aujuaye mzazi”. Kwa kweli, hayo ni mapenzi (uk 24)
 Juu ya mapenzi ya mama, Bw.Binafsi anapomfukuza nyumbani Mpya, tunamwona anasema,
“Siwezi kumtupa mtoto wangu kwa sababu ni msema kweli. Heri tuondoke sote”, kauli
kama hii kweli inaonyesha mapenzi ya mwanamke (uk 43)
 Bi.Shoo naye kuna pale ambapo kweli anadhihirisha mapenzi yake kwa mumewe
Bw.Binafsi. Hiki kinafanyika anapoonyesha utiifu wake kwake. Mathalani, anasema kuwa
Bw.Binafsi alisheheni mapenzi kwake. Pia, anamshukuru kwa kuwa nguzo nzuri kwa familia
yao na kuwa fahari kwake (uk 36)
 Vile vile, mwanamke anasawiriwa kama mvumilivu. Mvumilivu ni yule anayestahimihili
mambo kwa muda mrefu bila kukata tamaa. Kwa mfano, Bi.Shoo na Mpya wanavumilia
mateso ya Bw.Binafsi. Mathalani, tunamwona Mpya akifafanua eti mamake Bi.Shoo ameketi
katika ukingo wa dunia, ana hofu za kuannguka na kuangamia, anaihofu ndoa kwa sababu
anamwogopa mumewe Bw.Binafsi. Haya yote Anayavumilia hivi kuonyesha uvumilivu
wake (uk 32)
 Mpya naye anavumlia mateso ya babake Bw.Binafsi. Mathalani, Mpya anapomwambia
vitendo vyake yaani uongozi mbaya, Bw.Binafsi anakasirika na kumkaripia halafu anawaita
walinzi wake kuja kumburura na kumfukuza. Mateso haya anayavumilia hivi kuonyesha
uvumilivu (wake uk 41)
 Bado juu ya uvumilivu, wananchi wa jinsia ya kike wanavumilia ugonzi mbaya wa
Bw.Binafsi kwa muda wa miaka hamsini na zaidi. Kwa mfano, Mpya (Kijana wa kike),
Bi.Shoo, Bi.Subira, Bi.Mgeni tunawaona wakiyataja mambo ambayo wamevumilia kama
vile njaa, kiu, ufisadi, udhalimu, kuchukua ardhi yao, kutawaliwa kiumbinafsi na kadhalika
(uk 59)
 Kando ya uvumilivi, mwanamke ana hadhi ya kuikomboa nchi yake yaani anasawiriwa kama
mkombozi. Kwa mfano, Mpya ni mkombozi ambaye anachochea wananchi kupigania haki
zao jambo ambalo linasababisha Bw.Binafsi kuondolewa katika uongozi. Kwa mfano,
tunamwona Mpya akiwajulisha wananchi ya kuwa wameamua kesho yake wakutane
kulalamikia haki zao (uk 72)
 Bi.Shoo lazima naye ni mkombozi (anasababisha mapinduzi) kwa mfano, tunamwona
anautetea ukweri wa Mpya. Mathalani, Bw.Binafsi anapomfukuza Mpya, Bi.Shoo anasema,
“Siwezi kumtupa mtoto wangu hasa kwa sababu ni msema kweli. Heri tuondoke sisi sote”.
Hivi basi, Bi.Shoo naye anajua kuwa Mpya ni msema keli (uk 43)
 Waaidha, Bi.Shoo ni mkombozi kwani tunamwona anamwambia mumewe kujiuzulu. Pia,
anamwambia eti hawezi kuwa katika upande wake. Kwa mfano, Bw Binafsi anapomwuliza
akiwa yuko katika upande wake, Bi.Shoo anasema, “Unataka niwe pamoja na wewwe vipi?
Huoni kwamba ninakuzindua kwamba hatari iko karibu nasi? Huoni kwamba mwisho

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 15


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

wetu umefika?”. Maneno haya yanadhihirisha kuwa Bi.Shoo anasababilisha mapinduzi (uk
86-87)
 Bi.Subira, Bi.Sikilivu na Bi. Mgeni nao ni wakombozi yaani wanasababisha mapinduzi. Kwa
mfano, tunawaona wamekusanyika katika bustani ya taifa jijini kwa mkutano wa dharura.
Pia, tunamwona Bi.Subira akisema kuwa hana subira tena, hawawezi kujikomboa tusiposema
(uk 57-59)
 Kwa upande mwingine, mwanamke anasawiriwa kama mwaminifu wa utamaduni wake.
Kwa mfano, Mpya anamini mambo ya ukale (utamaduni) yaani tunamwona wahenga
wanamnywesha maji ya ujasisi ili aweze kusafisha hofu na woga vinavyomzuia kupigania
uhuru (uk 23)
 Juu ya nafasi ya mwanamke, anasawiriwa kama mchochezi wa mgomo. Mchochezi ni yule
ambaya anasababisha wengine wagome. Uchochezi wake unathibitishwa na maneno yake
akisema kwamba wananchi wameamua eti keshoye wakutane tena kulalamikia haki zao (uk
72)
 Pia, tunamwona Mpya akiwanyamazisha na kusema ati fujo ndiyo itakayoharibu mambo yao
katika harakati za kupigania haki zao (uk 61).
 Juu ya mengine kama haya, tunamwona akiwaambia Mussa na Zanga kuwa wanaojua
kusema ni wengi kuliko wasiojua kusema hivi wawaendee wafundishwe kusema. Lazima
huyu ni mchochezi mzuri (uk 55)
 Isitoshe, mwanamke anasawiriwa kama mjenzi wa familia. Kwa mfano,tunamwona Bi.Shoo
anawapenda na kuwatetea watoto wake. Kwa mfano, anamtetea Mpya dhidi ya mateso ya
babake. Mathalani, tunamwona Mpya anapofukuzwa, mamake anaondoka naye. Kwa ukweli
Bi.Shoo ni mjenzi wa familia (uk 43).
 Ghalibu ya hayo, mwabamke anasawiriwa kama msaliti. Msaliti ni yule anayemtendea
kinyume mtu mwingine kulingana na makubaliano. Kwa mfano, Mpya ni kijana msaliti
ambaye anongoza mikutano ya uchochezi wa kumwondoa babake katika uongozi (uk 86).
 Bila shaka, mwanamke anasawiriwa kama shujaa/ jasiri. Ni yule anayetenda bila kuogopa na
kujali maisha yake. Kwa mfano, Bi.Shoo ni shujaa ambaye hajamwogopa kumwambia
Bw.Binafsi uso kwa uso kujiuzulu wakati wanapokabiliwa na umati wa wananchi (uk86)
 Aidha, Mpya naye ni jasiri yaani hajamwogopa kumwambia babake juu ya vitendo vyake
viovu. Kwa mfano, wakati wakuonyesha utiifu wake kwa babake, anamwambia vitendo
vyake. Pia, tunamwona anakatataa katakata kumwinamia baada ya kuingia. Mpya haogopi,
hata kamwe (uk34-39).
 Juu ya hayo, wanawwake ni jasiri kwani wanajitolea nmhanga kupigania haki nchi yao. Kwa
mfano, Mpya, Bi.Mgeni, Bi.Sikilivu na Bi.Subira wanaonyesha wazi kuwa wamechoka na
uongozi uliojaa ubinafsi, mateso , ufisadi, udhalimu, wakionyesha kumpinga Bw. Binafsi (uk
57)

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 16


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

 Waaidha, mwanamke anasawiriwa kama mpenda amani. Mpya lazima ni yule mtu
asiyependa fujo. Kwa mfano, tunamwona anawaambia kutenda mambo yao bila fujo kwa
sababu fujo huweza kuwaharibia mambo. Mathalani, anasema, “………..sisi wananchi
timeamua kwamba kesho tukutane tena kulalamika na kutetea haki zetu. Hatutaki fujo
lakini” (uk 72).
 Pia, mwanamke anasawiriwa kama kiumbe cha kudharauliwa na mwanamume. Kwa mfano,
Mpya anapokataa kumwinamia babake, anamkaripia akisema, ……… “wewe kigego, mtoto
wa ukorofi. Sikutaka mimi uingie mimba mwa mamako mtotot wewe. Mtoto wa kike
anafaida gani? Na ilipoingia mimba sikujua kama ungezaliwa hivi. Umekuja duniani
kuniondolea furaha” (uk 34).
 Bila kudanganya, mwanamke anasawiriwa kama mtiifu. Mtiifu ni yule anayesikiliza na
mwenye kutoa heshima. Kwa mfano, Bi.Shoo ni mtiifu yaani anaonyesha utiifu wake kwa
mumeme akisema, “Bwana uliyesheheni mapenzi kwangu, baba wa watoto wangu,
mwenzangu katika safari ngumu…… Nakumbuka kuguma tulikotoka na najua wapi
tulipo leo…..kama si wewe, usingetimu ujanajike wangu……umama wangu …..fahari
yangu kwako!” (uk 36)
 Juu ya hayo, Mpya naye ni mtiifu. Kwa mfano, tunamwona anawatii wahenga. Wahehenga
wanapomwita kumnyesha maji ya ujasiri, Mpya anaitikia kwa kusema yuko njiani hatua kwa
hatua kichwa juu miguu chini au miguu juu kichwa chini. Mathalani, tunamuona anapeleka
kiamo kinywani na kugugumia maji ya ujasisi na yaliyobaki anajimwagia mwilini (uk 21-
23).
 9. Uvumilivu.
 Ni hali ya mtu kustahimili mambo magumu kwa muda mrefu bila ya kukata tamaa. Kwa
mfano, Bi.Shoo na Mpya wanavumilia mateso ya Bw.Binafsi. Mathalani, tunamwona Mpya
akifafanua eti mamake Bi.Shoo ameketi katika ukingo wa dunia, ana hofu za kuanguka na
kuangalia, anaihofu ndoa kwa sababu anamwogopa Bw.Binafsi. Haya yote Bi.shoo
anayavumilia na kwa hiyo, ni mvumilivu (uk 32)
 Hali kadhalika, wananchi ni wavumilivu. Kwa mfano, wananchi (wote) kama vile, Bw.Taja,
Bw.Salimina, Bw.Naona, Kushoto, Kulia, Bi.Subira, Bi.Sikilivu, Bi.Mgeni, Mpya, Bi.Shoo,
Mussa, Zanga na wengine wanavumilia uongozi wenye maovu. Kwa mfano, njaa, kiu,
ufisadi, udhalimu, kuchukua ardhi zao, kukata miti ovyo, kutawaliwa kiubinafsi matendo
haya na mengine wanayavumilia, na kwa hiyo ni maudhui ya uvumilivu (uk 59)
 Bila shaka, Mpya naye ni mvumilivu ambaye amevumilia mateso ya baba yake. Mathalani,
Mpya anapomwambia babake vitendo vyake yaani uongozi mbaya, Bw.Binafsi anakasikika
na kumkaripia vibaya. Kwa, mfano, tunawaona walinzi wakiitwa na baada ya kuja,
wanamburura Mpya kama gunia la makaa na kamfukuza. Haya Mpya anavumilia (uk 41).
 10. Usaliti.

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 17


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

 Usaliti ni hali ya kumtendea mtu kinyume cha makubaliano. Kwa mfano, Bw.Binafsi ni
msaliti kwa kutendea kinyume cha makubatiano nchi yake. Aidha, Mpya, Mussa na Zanga
nao ni wasaliti kwa mfano wanachochea mgomo wa wa kumwondoa baba yao katika
uongozi. Kwa mfano, tunaona Mpya ndiye anayeongoza mikutano ya wananchi ili wapiganie
haki zao. Kwa kweli wanamsaliti baba yao (uk 72-75).
 11. Ujasiri
Bi. Shoo ni Jasiri, kwa mfano, hajamwogopa Bw.Binafsi kumwambia uso kwa uso eti
ajiuzulu wakati wanapokabiliwa na wananchi (uk 34-59)
 Juu ya hayo, Mpya naye ni jasiri yaani hajamwogopa babake kiongozi mkuu kumwambia
vitendo vyake. Pia, tunamwona anakataa kumwinamia baada ya kuingia. Hiki kinaonyesha
ujasiri wake (uk 57)
 Kwa ujumla, wananchi nao ni jasiri. Kwa mfano, hayajaogopa kuanzisha mikutano ya
kujikomboa polepole wakielekea katikati ya uwanja wa bustani (uk 61). Pia, wanaonekana
akimkabila Bw.Binafsi nyumbani mwao bila kuogopa hata kamwa. Tunawaona wameshika
mabango yenye maandiko. Hiki kweli kinaonyesha maudhului ya ujasiri (uk 84)
 12. Utiifu
 Ni hali ya kutenda kile kinachotakiwa. Kwa mfano, Mussa ni mtiifu yaani anaonyesha utiifu
wake kwa babake. Anapoamurishwa na babake kuonyesha utiifu wake kwake, anaitikia
vizuri na kuanza kumsifu kwa kutokonga na kusema eti hakuna anayefanana naye duniani au
nchini (uk 36- 37).
 Juu ya utiifu, Zanga naye ni mtiifu yaani anatenda kile anachoagizwa. Kwa mfno, wakati
anapoagizwa na babake kumwonyesha utiifu wake, naye anaitikia vizuri na kuanza kumsifu
babake kwakuwa tegemea kwao (uk 37)
 Bila kudaganya, Bi.Shoo naye ni mtiifu. Kwa mfano, anamtii muwewe Bw.Binafsi
Mathalani,tunamwona akitoa utiifu wake kwa mumewe akisema, “Bwana uliyesheheni
mapenzi kwangu, baba ya watoto wangu, mwenzangu katika safari ngumu…. Nakumbuka
kugumu tulikotoka na sasa tulipo leo…..kama si wewe, usingetimu ujanajike
wangu….Umama wangu….fahari yangu kwako!” (uk 36).
 Juu ya hayo, Mpya naye ni mtiifu. Kwa mfano, tunamwona anawatii wahenga. Wahenga
wanapomwita, kumnyesha maji ya ujasiri, Mpwa anaitikia kwa kusema kuwa yuko njiani
hatua kwa hatua, kisha juu miguu chini au miguu juu kichwa juu. Mathalani, tunamwona
anatetkea kiamo kinywani na kugugumia maji ya ujasiri na yaliyobaki anayajimwagia
mwilini. Hivi basi ni maudhui ya utiifu (uk 21-23)
 Hali kadhalika, wananchi nao lazima ni watiifu. Kwa mfano, Mpya anapowaita kuja
kukutana juu ya hali za kujikomboa, tunawaona wanaitikia na kuja. Pia, katika mikutano yao,
tunamwona Mpya akisema waache fujo, nao wanaziacha yaani wanatumia mabango yenye
maandiko (uk 84).
 13. Msimamo thabiti.
P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 18
TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

 Ni hali ya kusisitiza jambo bila kubadilikabadilika. Kwa mfano, Mussa ni mwenye msimamo
thabiti yaani tunamwona akimwambia Zanga ati mameno yake yanaweza kuwa na utata
lakini hayana ugumu. Pia, tunamwona anasema kuwa ameamua kupiga kelele na baada ya
haya anaonekana akiongoza mgomo. Huo ni msimamo thabiti (uk 48)
 Pia, Zanga naye ni mwenye msimanio thabiti yaani tunamwona anajiunga na Mpya na Mussa
ati wafundishwe kusema na baadaye tunawaona wanasema wanapoongoza mgomo wa
kupigania haki zao na kuupinga uongozi wa baba yao (uk 54-67)
 Bila shaka, naye Mpya ni mwenye msimamo thabiti yaani tunamwona anasisitiza kuuondoa
uongozi mbaya wa baba yake na hatimaye anaikomboa nchi yake. Msimamo wake na
unaonekaa anaposema kuwa amechoka kunyamaza. Kwa hiyo, kuna maudhui ya msimamo
thabiti (uk 31)
 14. Ujenzi wa familia
 Ni hali ya kuitunza familia vilivyo. Kwa mfano, ujenzi wa familia unaonekana na Bi.Shoo
ambaye anawapenda na kuwatetea watoto wake. Aidha, Bw.Binafsi naye ameijenga familia
yake kwani anawaelimisha watoto wake vyuoni, maneno kama haya lazima yanaonyesha
maudhui ya ujenzi wa familia (uk34).
 15. Uchochezi wa mgomo.
 Ni tabia ya kuwaambia wengine ili waweze kupigana. Kwa mfano, Bi.Subira ni mchochezi
wa mgomo kwa sababu tunamwona akianzisha vurugu wakati anaposema eti amechoka
kusubiri na kusema eti anadhani nchi yao haina viongozi (uk 67).
 Vile vile, Mpya, Zanga na Mussa nao ni wachochezi wa mgomo na wananchi ambao
wameamua kusema. Pia, wanaonekana wakisema eti wanataka kuwaendea wale wanaojua
kusema eti wafundishwe kusema na huko ni kuchochea mgomo.
 Bila shaka, Mpya ni mchochezi wa mgomo. Kwa mfano, tunamwona akisema ati wananchi
wameamua kututana kulalamikia haki zao katika bustani ya nchi (uk 73-74)
 16. Ukombozi
 Ni hali ya kusababisha vitendo au vita vyo kuokoa maisha ya watu. Kwa mfano, ukombozi
unathibitishwa na vitendo vya Bi.Subira. mathalani, kwa mfano, tunamwona akisema ya
kwamba ameamua kusema na hataki kusubiri kwa sababu mtu hawezi kujikomboa asiposema
na kwa hiyo hii ni maudhui a ukombozi (uk 49)
 Pia, Mussa naye ni mkombozi kwani anaungana na Mpya, Zanga na wananchi wanaongoza
mgomo wa kupigania haki zao. Kwa mfano, tunamwo Bw.Naona akisema kuwa watoto wake
Bw.Binafsi ni waasisi wa kupigania haki zao na za wananchi (uk 67)
 Fauka, Bi.Shoo ni mhusika ambaye anadhihirisha maudhui ya ukombozi. Kwa mfano,
tunamwona akitetetea ukweli wa Mpya akimwambia babake juu ya vitendo vyake vibaya.
Mathalani, tunamwona akisema eti hawezi kumtupa mtoto wake kwa sababu amesema
ukweli. Na hiki kinamfichua kuwa naye Bi.Shoo ni Mkombozi (uk 43)

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 19


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

 17. Uharibifu wa mazingira


 Ni uchafuzi wa mazingira. Kulingana na tamthilia hii, uharibibu wa mazingira
unadhihirishwa na maneno ya Bi.Subira. kwa mfano, anaelezea kuwa watu kwao wanafanya
wapendavyo, wanakata miti ovyo, wanachafua mazingira katika kile eneo, uchafu umejaa,
uchafu ni wa kila aina, makazi yao machafu. Mameno ya namna hii lazima yanaonyesha
uharibifu wa mazingira (uk 59)
 18. Elimu
 Ni hali ya kuwa na uwezo wa kujua kusoma na kuandika. Maudhui ya namna hii huthibishwa
na maneno ya Bw.Binafsi. Mathalani, katika majivuno yake akimshukuru Mungu kwa kumpa
kila kitu anasema ati watoto wake wanakula wanachokitaka, wanavaa wanavyopenda na hata
wanaenda vyuoni kuelimika. Kwenda vyuoni kuelimika kunadhihirisha maudhui ya elimu
(uk 34)
 Ghalibu ya hayo, Bw.Binafsi anasema kuwa elimu yote ameisambaza nchi mwote ingawa
Bw.Salimina anamwambia kuwa watu wanasema kwamba elimu ni ya kuutukuza uongozi
wake badala ya kukuza taifa (uk 64)
 Hali kadhalika, majina ya wafanya-kazi yanayotolewa na Bw.Naona yanaonyesha eti baadhi
ya watu lazima wameelimika. Kwa mfano, anasema kuwa kila aina ya raia imejumuika
kupigania haki zao kama vile, wazee, vijana, wanawake na wanaume, wagonjwa na wazima,
wa mjini, majijini na mashambani, waliosoma na wasiosoma, walimu, madaktari, mawakili
na kadhalika (uk 67)
 19. Ubabedume.
 Ni ujanja na hila za kutumia nguvu au mashavu mwanamume anayoonyesha mwanamke au
mtu wa jinsia ya kike. Kwa mfano, Bw.Binafsi ni mwenye ubabedume yaani anamdharau
bintiye Mpya akisema, “Wewe kigego, mtoto mkorofi. Sikutaka uingi mimba mwa mamako
mtoto wewe. Mtoto wa kike anafaida gani? Na ilipoingia mimba sikujua kama ungezaliwa
hivi wewe. Ningekung’oa mimba mwa mamako. Umekuja dunia kuniondolea furaha” ( uk
34).
 20. Imani.
 Ni kuamini au kukubali mambo kuwa ni ya kweli na mtu kupaswa kuyaheshimu. Pia, ni
itikadi. Kwa kurejelea tamthalia, hii Kushoto kweli ni mwaminifu yaani anaamini sauti ya
kisima. Mathalani, tunamwona akisema eti katika kisima hicho ndipo pahala patakatifu
walipokutania wahenga kujadili mateso na kutafuta njia ya kuyaondoa. Na kwa hiyo, ni bora
kusema eti kuma maudhuli ya imani (uk 9)
 Kuongeza hapo, Kulia naye ni mwaminifu wa kisima cha ajabu. Kwa mfano, tunamwona
baada ya kisima kusemam, anasema eti hapo ndipo palipobubujika maji yaliyonguruma
mpaka ulaya (uk 12)

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 20


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

 Aidha, naye Mpya ni mwaminifu wa kisima. Mathalani, Sauti ya kisima inajitokeza ikimwita
eti aje anywe maji ya ujasiri yenye kuzitoa hofu na woga naye anaamini. Kwa mfano,
tunamwona akisema, “niko njiani wahenga.” Katika ukurasa unaofuata, tunamwona
akipeleka kiamo kinywani na kuonyesha maudhui ya imani (uk 21-23).
 Bila kutetema, Bw.Binafsi naye ni mwaminifu. Yaani anaamini mambo ya Mungu kwa
mfano, tunamwona akimshukuru kwa kumtia imani ili aitunze familia yake. Aidha, anasema
kuwa Mungu amempa nguvu na uwezo wa kuihudumia familia yake. Haya yote lazima
yanahakikisha maudhui ya imani (uk 34)
 Bw. Binafsi anaonyesha imani yake anapomkaripia mtotowae, Mpya na mamake Bi.Shoo
kwa mfano, tunamwona anasema kwamba Mungu atawalaani ikiwa hawamtii. Anaendelea
kusema eti Dini zote duniani zinahubiria utakaso wao kupitIa kwa wazazi na wazee. Hivi
basi, hakuna budi kusema kuwa kuna maudhui ya imani katika tamthilia ya Kimya Kimya
Kimya (uk 38-39). (Bw. Binafsi pia anaamini yoo).
 21. Utengano.
 Ni hali ya kuachana baina ya watu na kusosa ushirikiana. Kwa mfano, Mpya ametengana na
baba yake kwa sababu ya kupigania haki. Mathalani, tunamwona Mpya anaupinga uongozi
mbaya wa babake jambo ambalo linamtetea kufukuzwa kwa mfano, tunamwona Bw.Binafsi
anawaita walinzi kuja kumburura kama gunia la makaa na kumtenganisha naye (uk 41)
 Maudhui ya utengano pia huonekana baina ya Bw.Binafsi na wananchi. kwa mfano,
wananchi wanajitenga naye na kuanza kukutana katika bustani ya taifa ili waweze
kumwondoa kwa uongozi wake mbaya. Mathalani, tunawaona wakimkabilia vibaya na
mabango wakidai haki zao. Pande hizi mbili kweli hazishirikiani hata kamwe hivi utengano
(uk 84).
 Zanga na Mussa bila shaka nao wametengana na baba yao wakimlaumu kuwanyamazisha
kwa muda mrefu. Watoto wake hawa, wanashirikiana kuweza kufundishwa kusema ili
waweze kumfukuzia mbali baba yao (uk 54)
 22. Janga / balaa la ukame
 Ukame ni ukaukaji wa maji. Kulingana na tamthilia hii, ukame unahahikishwa na maneno ya
sauti ya kisima. Kwa mfano, sauti inamwambia Kushoto eti hakuna uhai, anakotoka hakuma
chakula na hata hakuna maji anakotoka. Ndiyo sababu tunamwona Kushoto analalamikia kiu.
Isitoshe, Kulia naye analalamika kwa sababu ya kiu., Sauti ndani ya kisima inamwambia
kuwa alikotoka kukavu, kote kumedamirika, hakuoti kitu wala kuzaa kitu. Na kwa hiyo, ni
kweli kusema eti kuna maudhui ya janga la ukame (uk 8-11)
 23. Ukatili
 Ni hali ya kumtendea mtu kitendo bila huruma yoyote. Kwa mfano, Mpya anatendewa
kikatili na baba yake hususa pale anapoita walinzi kuja na kumburura kama gunia la makaa.
Anatendewa hivi, kwa sababu amesema kuwa vitendo vya Bw.Binafsi ni vibaya na kuupinga
uongozi wake (uk 41)
P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 21
TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

 Fauka, wananchi nao wanatendewa vibaya na Bw.Binafsi. Kwa mfano, wakati wananchi
wanapojikusanya ili waweze kujadiliana jinsi ya kujikomboa, askari wanaingia
wakimiminika kama mchanga katika bustani, wakiwa wameshika virungu na kuwatandika
mmoja baada ya mwingine (uk 61)
 24. Majivuno
 Ni hali ya kujisifu au kuwafanya watu wakusifu. Bw.Binafsi kwa ukwelii anaonekana kama
mwenye majivuno. Mathalani, anashukuru Mungu akiwa anawarejeshea na maneno ya
kukera wale wenye njaa. Kwa mfano, anasema, “kabla hatujafungua kinywa inapasa
tumshukuru Mungu wakati huu wa dhiki kwa kunitia mimi imani ili nitunze familia
yenyewe. Mungu kanipa mguvu na uwezo wa kuihudumia familia yangu. Fumbueni
macho muone jinsi ukosefu, njaa na maradhi yalivyojaa dunia nzima. Tazameni majirani.
Hawana cha kutegemea. Lakini kwenu vimejaa vitu tele vya manufaa. Mnakula
mnachokitaka. Mnavaa mnaavyopenda. Mnakwenda vyuoni kuelimika. Na yote hayo
mimi sina ninachokuombeni nyini……’’ . (uk 34)
 Vile vile, Bw. Binafsi pia, anaonekana na majivuno baada ya kuingia nyumbana. Kwani
anawaambia kumsifu ingawa yeye Mpya anakataa (uk 37-38)
 25. Unyanganyaji
 Ni kuchukua mali ya mtu kwa kutumia nguvu kwa mfano, Bi.Subira anatwambia ati wanauza
nchi yao kwa bei rahisi kabisa, wamekuwa wajinga wa kuporwa raslimali zao, ardhi
zinauzwa au zinakodishwa kwa miaka mia mbili ……….(uk 59)
 26. Mazingaombwe.
 Ni utendaji wa vitu au mambo yenye maajabuu. Mambo haya yanashangaza watu. Kwa
mfano,tunaona ndani ya kisima kunajitokeza sauti inayosema kuwa Kushoto anakotoka
hakuna uhai , hakuna chakula, hakuna maji, hakuna ari ya kusema. Kusema kwa kisima
kunamshangaza Kushoto hivi anajiuliza, “Aaaa, hiki ni kisima cha aina gani, kisima
kinachosema. Kwa kweli haya ni mazigaombwe” (uk 8-9)
 Isitoshe, mazingaombwe mengine yanajitokeza kati ya Kushoto na Kulia. Kwa mfano,
Kushoto anageuka kuelekea Kulia na Kulia anageuka kuelekea Kushoto……wanagusana
mgongo kwa mgongo, lakini wanapojariribu kubanduka hawawezi.vile vile, tunawaona
wamemsukuma Kulia arudi kulia na Kulia anamsukuma Kushoto aende kushoto, mwishowe,
wanagandamana kitu kumoja. Haya yote ni mazingaombwe (uk15-17).
 Hali kadhalika, kisima kumwita Mpya kikampa maji ya ujasiri haya ni maajabu kweli.
Tunanamwona Mpya anaitwa na sauti ndani ya kisima eti aje apewe maji ya ujasiri ya
kumwondoa hofu na woga, Mpya anaitikia mwito. Kwa mfano, tunamwona anapeleka kiamo
kinywani na kugugumia maji ya ujasiri na kujimwagia yaliyobaki mwilini. Jambo la ajabu
mmo ni kwamba, baada ya Mpya kuyanywa maji hayo, Kushoto na Kulia wanabagukana na
kugeukiana na kutazamana uso kwa uso. Hakuna kudanganya hapa mtu akisema kuwa
tamthilia hii ina maajabu (uk 21-23)

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 22


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

 Hali kadhalika, waliosema kuwa maajabu hayatakwisha hawakudanganya na hivi maajabu


yanajitokeza katika tamthilia ya Kimya Kimya Kimya maajabu haya yanahakikishwa na
kuanguka kwa vyuma bila kuonekana mtu anayeviangusha. Kwa mfano, katika familia ya
Bw.Binafsi wakiwa wamemsubiri kuingia, ghafla chuma kinaanguka sakafuni pahali fulani
kwa mpasuko mkali unaopasua vigoma vya masikio na watu wanashangaa (uk 27)
 27. Athari za utandawazi.
 Utandawazi ni mfumo wa kimataifa ambao unarahisisha mawasiliano na mahusiano katika
nyanja kwenye maendeleo ya teknolojia. Kwa mfano, Kushoto anatwambia ya kuwa nguvu
za utandawazi zimemzuia kwenda atakapokwenda yaani anasema ni Mungu mpya
anajiyeficha kwa jina la utandawizi (uk 16)
 Mwandishi pia anauona utandawazi kama “utandawizi” yaani mfumo ambao viongozi
wanatumia kuiba rasilimali za watu na kuwafanya wasiweze kutambua.
 28. Utamaduni
 Ni mila, desturi, asili, jadi, imani na itikadi za kundi la watu au jamii fulani. Kwa mfano,
inasemekana ya kuwa hapo zamani, jamii ilikuwa na kisima hicho, jamii ingekutania hapo
kujadii mateso ya kutafuta njia ya kuyaondoa na ndiko patakatifu. Uaminifu wa kisima
unaonyesha utamaduni (uk 9)
 Maneno ya Kulia pia yanathibitisha maudhui ya utamaduni. Kwa mfano, anaendea kuelezea
ya kuwa, katika kisima hicho, wazee wangekutania hapo kutoa simulizi zao, na palikuwa na
bubujika la maji yaliyonguruma mpaka ulaya. Pia, anasema wazee wangeamshana kutoka
usingizini na hata ndoto mpya zingetolewa hapo. Haya yote yanaonyesha utamaduni (uk 12).
 Aidha, Mpya naye anathibitisha utamaduni kulingana na uaminifu wake wa jadi. Kwa mfano,
Sauti ndani ya kisima inasikika ikimwita kumpa maji ya ujasiri. Na ndipo tunamwona Mpya
akisema, “Niko njiani wahenga”. Na baada ya kuyanywa maji hayo, anajitoa hofu, woga na
woga wa mananchi ndiyo sababu wanazinduka uzingizini kupigania haki zao (uk 21 na 23)
 Vile vile, matambiko yanazotolewa nayo lazima yanaonyesha utamaduni. Kwa mfano,
tunamwona Mpya akisema, “Mimi ninayeshika kiamo kilichosafishwa kwa moshi wa
vifuu. Kiamo cha kutekea maji ya ujasiri. Hilo ndilo tambiko letu. Tambiko la uhai wanchi
.Tambiko la kusema ukweli bila ya kuhofu wala kuogopa” matambiko haya zinahakisha
maudhui ya utamaduni (uk 23)
 Imani ya mazingaombwe nayo inadhihihirisha maudhui ya utamaduni. Kwa mfano,
tunamwona Bw.Binafsi anaamini Miungu yaani yoo. Baada ya kukabiliwa vibaya na
wananchi, tunamwona akiliendea hilo na kusema nalo akiliomba kumkusoa kumhakiki,
kumkejeli, kumsibabi na kumlaumu. Baadaye, tunaliona yoo likisema eti lilimwambia lakini
hakusikia (uk 80-82)
 Utamaduni kadhalika unaonekana wakati vyuma vinapoanguka. Inaaminika ya kuwa
kuanguka kwa vyuma ndiko kunakosababisha watu kusema. Kwa mfano, tunamwona

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 23


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

Mkemeo akimwambia Bw.Binafsi eti upepo unaangusha vyuma naye anamjibu eti aviache
vianguke kelele zienee nyuma na mbele, awaache waende wanaotaka kwenda (uk 43)
 29. Utabiri.
 Ni hali ya kutaja mambo yatakavyotokea. Kwa kujejelea tamthilia ya Kimya Kimya Kimya,
Bw.Binafsi ni mtabiri. Kwa mfano, tunamwona anasema, “………..Nasema wacha waende!
Najua watarudi kichwa chini maguu juu. Najua watarudi kuja kuomba radhi”. Baada ya
Bw. Binafsi kusema maneno haya, tunawaona Bi.Shoo na watoto wake wa kiume wamerudi
kuomba radhi isipokuwa Mpya (uk 43 na 45)
 Utabiri kadhalika unathibitishwa na maneno ya yoo. Kwa mfano, tunaliona likisema ya kuwa
lilimwambia eti akitawala kwa wema atamalizia wema lakini akitawala kwa maovu
ataangamia. Kwa ukweli tunamwona Bi.Binafsi anatawala kwa maovu kama vile, kujaa
ubinafsi, ufisadi, unyanyasaji, ukatili na hatimaye anangamia. Na kwa hiyo, ni kweli kuna
maudhui ya utabiri (uk 82)
 30. Ufisadi.
 Ni utumiaji mbaya wa mali ya shirika au serikali, tabia ya ubadhirifu. Kwa kuirejelea
tamthilia hii, Bw.Binafsi anatumia vibaya mali ya Serikali. Kwa mfano, anajishughulisha na
ukataji wa miti ovyo, anawakubali watu kujenga nyumba bila vibali, anachukua ardhi na
viwanja vya watu, anawaacha watu kuchafua mazingira, anachafua ofisi za wananchi(uk 59)
 31. Unyanyasaji na mateso.
 Ni hali ya kumfanyia mtu vitendo vya dharau na dhuluma kwa kumnyima haki zake. Kwa
mfano, Bw.Binafsi anamnyanyasa Mpwa ambaye anapigania haki zake. Kwa mfano, baada
ya Mpya kumpinga na kumwambia vitendo vyake viovu, Bw.Binafsi anawaamuru walinzi
kuja na kumburura kama gunia la makkaa. Huu ni unyanyasafi (uk 41)
 Aidha, wananchi nao wananyanyaswa kwa kunyimwa haki zao, kuwafisidi, kuwadharau,
kuwatesa, kunyang’anya ardhi na wanapojaribu kujitetea, anawaonyesha cha mtema kuni.
Kwa mfano, wananchi wakiwa katika mkutano wao wa kupigania haki zao katika bustani ya
taifa, askari wanakuja na virungu na kuwatandika na lazima haya ni mateso (uk 61)
UTENDAJI/ SIFA/ HULKA/ WASIFU WA WAHUSIKA.
Sifa ni namna mhusika anavyosawiriwa kulingana na matendo yake na mavazi yake.
Wafuatayo ni wahusika na sifa zao;
1 Bw. Binafsi.
Huyu ni kiongozi mkuu wa taifa, mumewe Bi.shoo na Baba yao Mpya, Zanga na Mussa. Ana
sifa kama vile;
Kwanza, Bw.Binafsi ni kiongozi mbaya asiyeegemea masilahi ya wananchi. kwa mfano, amejaa
ubinafsi, ufisadi, mateso, dhuluma na kadhalika, mathalani tunamwona hataki wanchi wapiganie
haki zao yaani anaamrisha askari kuwapiga wote virungu. Na kwa hiyo, huo ni uongozi mbaya
(uk 61)

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 24


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

 Aidha, Bw.Binafsi ni kiongozi mbaya ambayae anawanyima wananchi haki zao kwa mfano,
wananchi wanapomwambia kubadilisha katiba, yeye analipuka kwa matusi bila kuwajali.
Kwa mfano, tunamwona akiwaita vinyangarika wanaojua kulala fofofo na kula mhogo.
Anasema kuwa wao si viongozi wala kiongozi ni mmoja. Hivi basi, kiongozi Bw.Binafsi ni
mbaya mbaya (uk 66)
 Vile vile, Bw.Binafsi ni kiongozi mbaya ambayae anawatesa wananchi. kwa mfano,
tunamwona akiwatesa wananchi ambao wanajaribu kujitetea. Mathalani, Mpya
anapomwambia ati amechoka na vitendo vyake Bw.Binafsi ananung’unika vibaya na
kuwaamuru walinzi kuja na kumfukuza. Walinzi wakati wanapokuja, wanamburura Mpya
kama gunia la makaa bila huruma.kulingana na matendo yote ya Mheshimiwa kama kiongozi
mbaya.
 Pia, Bw.Binafsi ni mwenye ubinafsi. Ni yule mwenye uchoyo na kujitakia mwenyewe wa
mfano, wananchi wanapodai kubadilisha katiba ya nchi, Bw.Binafsi anawadharau kabisa kwa
kuwaita vinyangarika ambao wanalala fofofo kama pono. Anaendelea kusema , “Katiba ni ya
viongozi na kiongozi ni mmoja” yaani yeye mwenyewe. Bila Shaka, hiki kinatetea ubinafsi
wa Bw.Binafsi (uk 66)
 Isitoshe, Bw.Binafsi ni mwenye ubinafsi ambaye anasema kwa niaba ya wananchi. kwa
mfano, anasema kuwa taifa lake ni taifa ambalo wananchi hawaruhusiwi kusema. Pia,
ubinafsi wake unaonekana wakati ambao anaongoza nchi kwa muda mrefu bila kuwajali au
kuwapatia wananchi bahati ya kuongoza. Kwa mfano, tunawaona wananchi wakigoma na
kusema eti wamesubiri zaidi ya miaka hamsini na kuchoka. Hiki kinaonyesha ubinafsi.
 Hali kadhalika, Bw.Binafsi ni mtabiri. Ni yule anayetaja mabo yatakavyokuwa. Kwa mfano,
kulingana na tamthilia hii, tunamwona Bw.Binafsi akisema, “…..Nasema wacha waende!
Najua watarudi kuja kuomba radhi” Baada ya muda mfupi, Bi.Shoo na watoto wake wa
kiume waliokuwa wamekimbia wanakuja tena kuomba radhi ila Mpya (uk 43 na uk n auk 45)
 Juu ya sifa zake, ni mwenye majivuno. Yaani watu wanamsifu. Kwa mfano, Bw.Binafsi kwa
kweli anaonekana kama mwenye majivuno. Hiki kinathibitishwa na maneno yake akiwa
anasema, “Kabla hatujafungua kimya inapasa tumshukuru Mungu wakati huu wa dhiki
kwa kunitia mimi imani ili nitunze familia yenyewe. Mungu kanipa nguvu na uwezo wa
kuhudumia familia yangu. Fumbueni macho muone jinsi ukosefu, njaa na maradhi
yalivyojaa dunia nzima. Tazameni majirani. Hawana cha kutegemea. Lakini kwenu
vimejaa vitu tele vya manufaa. Mnakula mnachotaka. Mnavaa mnavyopenda. Mnakwenda
vyuoni kuelimika. Na haya yote mimi sina ninachokuombeni nyinyi....” ombi la namna hii
kweli linadhihirisha majivuno ya Bw.Binafsi yaani, anafurahia hali mbaya ya wananchi (uk
34)
 Bila Shaka, Majvuno ya Bw.Binafsi mengine yanaonekana baada ya kuingia kwake
nyumbani. Kwa mfano, anamurisha wanafamilia yake kumsifu. Mathalani, tunaona waliomo

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 25


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

Bi.shoo, Zanga na Mussa wanamsifu (wanaonyesha utiifu kwake) lakini yeye Mpya anakataa
katakata (uk 37-38)
 Hali kadhalika, Bw.Binafsi ni mkaidi. Ni yule mwenya tabia ya kukataa kusikiliza ushauri
wa mtu. Kwa mfano, Mpya anapomwambia vitendo vyake, yeye badala ya kubadilisha
matendo yake, anamkaripia. Pia, tunamwona akisema eti labda si mtoto wake ingawa
anaujwa ukweli fika eti ni wak, huo ni ukaidi (uk 40)
 Ukaidi wake pia unaonekama anapomwambia Mpya kuwa, “Wewe kigego, Mtoto wa
ukorofi. Sikutaka mimi uingie mimba mwa mamako mtoto wewe. Mtoto wa kike anafaida
gani? Na ilipoingia mimba sikujua kama ungezaliwa hivi wewe. Ningekung’oa mimbani
mwa mammako! Umekuja duniani kuniondolea furaha.” Hivi basi, Kumwambia mwanake
maneno haya ni ukaidi (uk 34)
 Bw.Binafsi ni mwenye ubabedume. Ubabedume ni ujanja na hila za kutumia nguvu au
maonevu mwanamume anayoonyesha jinsia ya kike kwa kujionelea juu yake. Kwa mfano,
tunamwona akimwambia mtowe Mpya, “Wewe kigego, Mtoto wa ukorofi. Sikutaka mimi
uingie mimba mwa mamako mtotowe. Mtoto wa kike ana faida gani? Na ilipongia mimba
sikujua kama kamaungezaliwa hivi wewe. Ningekung’oa mimbani mwa mamako!
Umekuja dunuia kuniondolea furaha “ (uk 34)
 Vile vile, ni mwaminifu. Kwani anaamini Mungu na mambo ya kiutamaduni. Kwa mfano,
Bw.Binafsi anaamini mazingombwe. Pia, anaamini. Mungu yaani yoo, jambo ambalo ni la
utamaduni. Mathalani, baada ya kukabiliwa vibaya na wananchi, Bw.Binafsi anaogopa na
kuliendea hilo yoo ili liweze kumsibabi na kumlaumu ingawa mwishowe yoo linamjibu eti
lilimwambia lakini hakusikia (uk 80-82)
 Waaidha, maneno yake juu ya shukrani ambazo anatoa yanadhihirisha kuwa ni
mwaminifu wa Mungu. Kwa mfano, tunamwona akimshukuru Mungu kwa kumtia imani
ili aitunze familia yake. Pia, anamshukuru kwa kumpa nguvu na uwezo wa kuihudumia
familia yake (uk 34)
 Aidha, Bw.Binafsi ni mwenye dharau. Kwa mfano, tunamwona anamdharau mwanamke
(mtoto wake wa kike Mpya) yaani anasema eti hakumtaka aingie mimba mwa mamake kwa
sababu mtoto wa kike hana faida yoyote na hiyo ni dharau (uk 34).
 Vile vile, anawadhurau wananchi yaani anakataa wananchi kubadilisha katiba akisema wao
ni vinyangarika, hawajui kitu kuhusu uongozi, anaendelea kusema eti wamelala fofofo kama
pono na wananchokijua ni kula mhongo tu. Lazima huyu ni mwenye dharau (uk 66)
 Waaidha, Bw.Binafsi ni katili. Ni yule anayetenda kitendo cha kinyama kisicho na huruma
yoyote. Kwa mfano, Bw.Binafsi anamtesa mtoto wake wa kike Mpya hususa pale
anapowaita walinzi kuja na kumburura kama gunia la maka. Anamtendea hivi kwa sababu
Mpya ameupinga uongozi wake mbaya (uk 41)
 Vile vile, Bw.Binafsi anaonyesha ukatili wake kwa wananchi. Mathalani, wananchi
wanapojikusanyia katika bustani ya taifa ili waweze kujikomboa, anawaamru walinzi ambao

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 26


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

wanaingia na virungu na kuwatandika bila huruma. Bila shaka, tendo kama hili kwa kweli
linamwonyesha kama katili (uk 61)
 Kuongeza hapo, Bw.Binafsi anajulikana kama tajiri yaani ana mali na pesa za kutosha. Kwa
mfano, familia yake ina vyakula vya kila aina (uk 27)
 Aidha, mwandishi wa Kimya Kimya Kimya ameusawiri kikamilifu utajiri wa Bw. Binafsi
kwa mfano, anasema ati chumbani mwa vijana wawili wa kiume yaani Mussa na Zanga,
kuna samani na mapambo ya kitajiri. Anasema kuwa chumba ni cha kitajiri. Na kwa hiyo, ni
kweli kusema ati Bw. Binafsi ni tajiri.
 Juu ya hayo, utajiri wa Bw.Binafsi kweli unadhihirishawa na maneno yake mwenyewe
wakati anapomshukuru Mungu. Kwa mfano, akiwa anamshukuru Mungu kwa kumtia amani
kuitunza familia yake anasema, “……….fumbueni macho mwone jinsi ukosefu, njaa, na
maradhi yalivyojaa dunia nzima.Tazameni majirani. Hawana cha kutegeme. Lakini
kwenu vimejaa vitu teele vya manufaa. Mnakuula mnachokitaka. Mnavaa mnavyopenda.
Mnakwenda vyuoni kuelimika” (uk 34)
 Bw.Binafsi kwa kweli ni mwepesi wa kukasirika. Ni yule anayepandwa hasira kwa urahisi.
Kwa mfano, mtoto wake wa kike Mpya anapokataa kumwinania, tunaona Bw.Binafsi
anapandwa na hasira na kuanza kumkaripia akisema eti Mpya ni mtoto kigego, mtoto wa
ukorofi hana faida yoyote. Anaendelea kusema kuwa angejua, angemng’oa mimba yake mwa
mamake. (uk 34).
 Kukasirika kwake pia, kunaonekana wakati Mpwa anapokataa kuonyesha utiifu wake kwa
babake. Bw.Binafsi anapandwa hasira kubwa na kuwaita walinzi eti waje wamfukuze na
ndiyo sababu tunawaona wanamwendea Mpya, wanamshika mkono na kumburura kama
gunia la makaa (uk 41)
2 Mpya

Ni mtoto wao wa kike Bw.Binafsi na Bi. Shoo na ni dada zao Mussa na Zanga. Ana hulka
zifuatazo;

 Kwanza kabisa, Mpya ni mzalendo. Ni yule ambaye yuko tayari kupigania na kuifia nchi
yake kwa hali yoyote bila kuogopa. Kwa mfano, tunamwona anasema wazi bila ya kuogopa,
“Umeshafika……Umeshafika……….umeshafika wakati wa kusema ingawa mimi peke
yangu sina uzito wa kusema. Mimi pweke kusema ni haki ya uzawa wa kila kiumbe
binadamu na hata wanyama. Natamani siku moja kila mtu aseme”. Maneno haya lazima
yanamsawiri Mpya kama mzalendo (uk 21)
 Hali kadhalika, uzalendo wake unaonekana anapokubali kuyanywa maji ya ujasiri. Sauti
ndani ya kisima inamwita Mpya kumnywesha maji ya kumsafisha hofu wake na woga. Mpya
anaitikia akisema kuwa yuko njiani. Aidha, anaonekaona akisema ati lazima mmoja ajitolee
mhanga ndipo usasa utakapomheshimu naye kuuheshimu. Hivi vyote, vinamsawiri Mpya
kama mzalendo (uk 21)

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 27


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

 Aidha, Mpya ni mzalendo kwani aambiwapo na sauti ati kwao hawasemi, waziwazi na
kupiga kelele, Mpya anasema, “Mimi nimeanza. Mimi mwananchi mimi mzalendo na
mkereketwa”. Kwa ukakika, maneno ya Mpya haya yanamtetea kama mzalendo (uk 27-28)
 Bado katika uzalendo, Mpya anaonyesha uzalendo wake wazi wazi Kwa mfano, tunamwona
akisema ati amechoka kusubiri, amechoka kugonjea, amechoka kunyamaza.
Anakomwangamiza na hivyo anauliza, “kwa nini kila siku tugonjee? Tugonjee, tugonjee
mpaka lini?” Maswali haya ya balagha lazima yanadhihirisha uzalendo wake Mpya (uk 31).
 Fauka ya hayo, Mpya bado anadhihirisha uzalendo wake anapoongoza uchochezi wa
mgomo. Kwa mfano, tunamwona anasema ati wananchi wameamua keshoye kukutana na
kulalamikia haki zao bila fujo bali kuweka wazi kero zao. Wananchi nao kwa mwitiko wao
wanakubaliana na maneno yake. Bila kudanganya mhusika Mpya ni mzalendo (uk 72-73)
 Ghalibu ya hayo, mambo matano ambayo Mpya anayataja wazi ya kupigania haki kweli
yanauonyesha uzalendo. Mathalani, tunamwona anawaambia wananchi kuwa watapitia upya
katiba kwa masilahi ya wananchi, watasimama kidete kudai kugeuza mwendo wao kutojali
masilahi yao, wahakikishe wananchi wanapata huduma za kijami kutonoa masilahi yao,
wapigane vita vya ushujaa kuondoa ufisadi na kulinda rasilimali zao. Haya yote, Mpya
anayataja na kuyafafanua bila kuogopa hata kamwe na ndiyo sababu tunamsawiri kama
mzalendo (uk 73-74)
 Isitoshe, uzalendo wa Mpya lazima unadhihiriswa na maneno ambayo anayaamibia babake
Bw.Binafsi. Kwa mfano, anamwambia kuwa wamechoka na vitendo vyake. Hivi basi Mpya
ni mzalendo.
 Juu ya sifa, Mpya ni mwaminifu wa mambo ya ukale. Kwa mfano, anaamini kisima.
Mathalani, sauti ndani ya kisima inajitokeza na kumwita eti aje apewe maji ya ujasiri yenye
kumtoa hofu na woga. Baada ya kuitwa, hapotezi muda bali anaamini kuwa maji hayo
yanaweza kumwokoa maisha yake,. Kwa mfano, anasema, “nikonjiani wahenga”. Baadaye,
tunamwona anatia kiamo kinyawani na kuyagugumia maji hayo. Na kwa hiyo Mpya pia ni
mwaminifu wa kisima (uk 21-23)
 Mpya pia ni mwenye msimamo thabiti. Hii ni kwa sababu anasisitiza jambo fulani bila
kubadilika na kukata tama. Kwa mfano, tunamwona akisisitiza kuondoa uongozi mbaya wa
babake na mwihowe anaikomboa nchi yake, msimamo wake unaonekana anaposema kuwa
amechoka kusubiri, amechoka kunyamaza kwa sababu kunyamaza kunamwangamiza (uk 31)
 Fauka, Mpya ni mpenda ushirikiano yaani anashauri watu kuwa na umoja ili waweze kufaulu
katika kupigania haki zao. Kwa mfano, tunamwona akiwashauri Kushoto na Kulia kwamba
wameambatana na kusuguana migongo kuwa wanalazimika kuungana, shabaha zao ziwe za
nchi zisiwe za mtu binafsi (uk 22)
 Bila Shaka, Mpya ni mpenda amani. Ni yule anayetanda bila fujo. Kwa mfano, tunamwona
katika upiganiajai haki za wananchi ananyamazisha wananchi ambao wanapiga kelele.

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 28


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

Anasema eti wameamua kukutana katika bustani ya taifa kulalamikkia haki zao bila fujo (uk
72-73).
 Ghalibu, Mpya ni mpenda utamaduni wake. Ni yule anayependa mila, desturi, asili, jadi,
imani na itikadi za kundi la watu au jamii fulani. Kwa mfano, Mpya anadhihirisha utamaduni
kulingana na kisima wakati kinapomwita kumnywesha maji ya ujasiri anaitika na kusema,
“Niko njiani wahenga”. Hiiki kinahakikisha eti ni mpenda utamaduni wake (uk 21na 23)
 Juu ya haya, mpya anamini mtambiko ya utamaduni, na ndiyo sababu anautetea utamaduni
wake. Kwa mfano, tunamwona akisema, “Mimi ninayeshika kiamo kilichosafishwa kwa
moshi wa vifuu. Kiamo cha kutekea maji ya ujasiri. Hili ndilo tambiko letu. Tambiko la
kusema ukweli bila ya kuhofu wala kuogopa”. Bila ya kudanganya, Mpya ndiye mshusika
ambaye anaaminika kuwa anaupenda utamaduni wake kuliko wengine. Na kwa hiyo, Mpya
ni mpenda utamaduni katika tamthilia ya Kimya Kimya Kimya (uk 23)
 Mpya ni msomi. Ni yule mwenye uwezo wa kusoma na kuandika. Kwa mfano, ni mmoja wa
watoto wa Bw.Binafsi ambao wanaenda chuoni kuelimika. Hivi vinathibitishwa na shukrani
anazotoa Bw. Binafsi akimshukuru Mungu (uk 34).
 Katika mada sambamba, Mpya ni mvumilivu. Ni yule anayestahimili mambo mengi magumu
kwa muda mrefu. Kwa mfano, Mpya ni mvumilivu ambaye anavumilia mateso ya babake.
Kwa mfano, Mpya anapomwambia babake vitendo vyake, Bw.Binafsi anamkaripia na
kuwaita walinzi eti waje wamwondoe na wanakuja na kumburura. Haya yote, Mpya
anayavumilia (uk 41)
 Pia. Mpya ni jasiri. Ni yule anayetenda kishujaa yaani bila kuogopa. Mathalani, Mpya
hajamwogopa kumwambia babake kuwa anatendea wananchi vibaya. Pia, Mpya kweli ni
jasiri yaani tunamwona akikataa katakata kumwinamia babake baada ya kuingia. Vile vile,
Mpya ni jasiri ambaye hajamwogopa babaye yaani anajiunga na wananchi kupinga babake
(uk 34-39)
 Mpya kwa ukweli ni msaliti. Msaliti ni yule anayetenda mtu kinyume cha makubaliano. Kwa
mfano, Mpya ni msaliti ambaye anamtendea kinyume baba yake katika uongozi. Mathalani,
tunamwona anawashawishi Mussa na Zanga eti wawatafute wanaojua kusema wafundishwe
kusema. Aidha, anamsaliti babake, kwa kuuongoza mgmo wa kupigamia haki za wananchi.
hiki kinamshauri Mpya kama msaliti (uk 72-75)
 Hali kadhalika Mpya ni mkombozi. Ni yule anayesababisha vitendo au vita vya kuokoa
maisha ya watu. Kwa mfano, tunamwona akianzisha harakati za kuikomboa nchi yake juu ya
uongozi mbaya wa babake. Mathalani tunamwona akinywa maji ya ujasiri ili asiweze
kuogopa kupigania haki.
 Waaidha, Mpya ni mchochezi wa mgomo. Mchochezi ni yule ambaye anawasababisha
wengine wagome. Mathalani, Mpya ndiye kiongozi mkuu wa kuchochea mgomo. Kwa
mfano, uchochezi wake unadhihishwa na maneno yake anaposema ati wananchi wameamua
ati keshoye wajumuike tema walalamikie haki zao bila fujo (uk 72).

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 29


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

 Aidha, tunamwona akiwashawishi kaka zake Mussa na Zanga kwamba wawatafute wale
wanaojua kusema wawafundishe kusema. Baadaye, tunawaona wote wamejumuika
kuchochea mgomo. Pia, Mpya anaonekana akiwaongoza wananchi kugoma ingawa kwa
muda huu bila fujo yoyote. Mathalani, anasema ya kuwa hataki fujo, Mpya ni mchochezi wa
mgogo (uk 55 na 61)
 Juu ya haya, Mpya ni mwenye mapenzi. Ni yule mwenye upendo na kuwatakia mema. Hiki
kinathibitishwa na maneno yake mwenyewe. Mathalani, anasema, “ mimi nawapenda na
kuwaheshimu sana wazazi wangu.” Anawapenda lakini anasema tatizo lao ni kwamba
wamesahau kuwa wao ndio vijana na wazee wa kesho (uk 51-52)
 Mpya pia ni mdini. Anamini na kumjua Muumba wake wa mbinguni. Kwa mfano,
tunamwona akiwaambia maneno ya Mungu wazazi wake. Mathalani, anasema, “Na haki ya
mja imeandikwa mbinguni.” (uk 51)
 Kwa kweli, Mpya ni mwenye busara. Ni mwenye uamuzi wa hekima katika mambo tofauti .
kwa mfano, anaamua kusababisha mapinduzi ya kupigania haki zake na wananchi wenzake
na baadaye, tunamwona anaikomboa nchi yake.
 Hatimaye, Mpya ni mtiifu. Ni yule anayefuata kile kinachotakiwa. Kwa mfano, anawatii
wahenga. Wahenga wanapomwita kumnywesha maji ya ujasiri, Mpya anaitikia vizuri.
Mathalani, tunamwona akisema kuwa yuko njiani hatua kwa hatua kichwa juu miguu chini
au miguu juu kichwa chini. Baadaye, tunamwona akishika kiamo na kunywa maji (uk 21-23)
3 Bi.Shoo
Ni mkewe Bw. Binafsi na mama yao Mpya, Mussa na Zanga. Sifa zake ni zifuatazo;

 Kwanza, Bi.Shoo ni mwenye mapenzi. Ni mwenye mvuto na upendo kwa mtu mwingine
(Mpya) Kwa mfano, anaonyesha mapenzi yake kwa mumewe Bw.Binafsi wakati
anapoonyesha utiifu wake kwake. Aidha, anasema kuwa Bw.Binafsi amesheheni mapenzi
kwake. Mathalani, anasema kuwa amekuwa nguzo nzuri kwa familia na kuwa fahari kwake.
Kulingana na maneno haya, Bi.Shoo anampenda mumewe (uk 36)
 Fauka, Bi.Shoo anaonyesha mtoto wake Mpya Mapenzi. Kwa mfano, Bw.Binafsi
anapomfukuza Mpya, mamake anaondoka naye na jambo hili linaonyesha mapenzi yake.
Mathalani, anasema, “Siwezi kumtupa mtoto wangu hasa kwa Sababuu ni msema kweli.
Heri tuondokae sote”. Bi.Shoo ni mwenye mapenzi (uk 43)
 Bila Shaka, Bi.Shoo ni mwoga. Hana ukakamavu. Kwa mfano, tunamwona Mpya akituelezea
eti mamake ameketi katika ukingo wa dunia, ana hofu za kuanguka. Anamhofu mumewe
anaogopa ndoa yake kwa kweli kuvunjika (uk 32)
 Bi.Shoo ni mvumilivu. Ni yule anayestahimila masharti na mateso ya mumewe. Kwa
mfano,tunamwona kweli anayavumilia mateso ya mumewe. Mathalani, tunamwona Mpya
anatufafanulia kuwa mamake Bi.Shoo ameketi katika ukingo wa dunia, ana hofu za
kuanguka, anamhofu mumewe Bw.Binafsi, ana hofu ya ndoa maama yake watoto wake

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 30


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

kuvunjika, na kuvunjika kwa ndoa maana yake watoto wake wanavunjika. Hivi vyote,
Bi.Shoo kweli anavivymilia (uk 32)
 Kwa kweli, Bi.Shoo anamtii mumewe Bw.Binafsi. kwa mfano, tunamwona akitoa utiifu
wake kwa mumewe akisema, “Bwana uliyesheheni mapenzi kwangu, baba ya watoto
wangu, mwenzangu katika safari ngumu …..Nakumbuka kuguma tulikotoka nanajua
wapi tulipo leo…... kama si wewe, usingetimu ujanajike wangu….umama wangu….fahari
yangu kwako!” (uk 36)
 Ni mwenye huruma. Ni yule mwenye moyo wa amani, wema na upole mwenye moyo wa
kujali. Kwa mfano, anamwonea hisani mtotowe Mpya. Mathalani, tunamwona anamtetea
Mpya dhidi ya mateso ya Bw.Binafsi. Kwa mfano, tunamwona akiambia mumewe kuwa
Mpya ni mtoto tu ….akili zake hazijatulia mtotowe akiteswa. Tunamwona anamshika mkono
anaondoka naye (uk 41-43).
 Vile vile, Bi.Shoo ni jasiri. Ni yule anayefanya jambo la kishujaa ambalo huweza kuhatarisha
maisha. Kwa mfano, Bi.Shoo ni jasiri ambaye hajamwogopa Bw.Binafsi uso kwa uso
kujiuzulu wakati wa dhiki za wananchi , kweli kinamwonyesha Bi.Shoo kama jasiri (uk 86)
 Ni mjenzi wa familia. Ni yule anayetunza familia yake vizuri. Kwa mfano, tunamwona
Bi.Shoo akiwapenda na kuwatetea watoto wake. Mathalani, anamtetea, Mpya dhidi ya
mateso ya babake Bw.Binafsi. Kwa mfano, tunamwona anaondoka naye Mpya
anapofukuzwa na lazima hiki kinamwonyesha kama mjenzi wa familia (uk 43)
 Ni mzalendo pia. Ni yule ambaye yuko tayari kuifia na kuipigania nchi yake. Kwa mfano,
Bi.Shoo tunamwona akimwambia mumewe kujuizulu na auache uongozi Bi.Shoo
anaonekana akiwa na kauli tofauti yaani, naye anawashabiki wananchi. kwa mfano,
tunamwona anamwambia eti hawezi kuwa katika upando wake akisema, “unataka niwe
pamoja na wewe vipi? Huoni kwamba ninakuziundu kwamba hatari iko karibu nasi?” (uk
87)
 Fauka ya haya, Bi.Shoo ni mkombozi (anayasababisha mapinduzi). Kwa mfano, tunamwona
anautetea ukweli wa Mpya. Mathalani, Bw. Binafsi anapomfukuza Mpya, Bi.Shoo anasema,
“Siwezi kumtupa mtoto wangu kwa sababu ni msema ukweli. Heri tuondoke sisi sote.”
Kwa hiyo, Bi.Shoo anajua kwamba Mpya ni mtu anayesema ukweli hivi kuonyesha
Ukombozi (uk 43)
4 Mussa.
Ni mtoto wa kiume wa Bw.Binafsi na Bi.Shoo, ni kaka yake Mpya na Zanga. Mussa ana
sifa zifuatazo;
 Kwanza, Mussa ni mvumilivu. Ni yule ambaye anastahimili kwa muda mrefu akiwa
anangojea mabadiliko. Kwa mfano, anayavumilia mateso ya baba yake Bw.Binafsi. Pia,
tunamwona amesubiria chakula kwa muda mrefu. Aidha, tunamwona Mpya akisema eti kaka
zake wana hamu ya kusema lakini hawajasema, na Mussa ni kaka yake kinamaanisha eti
naye amevumilia kusema (uk 32)

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 31


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

 Bila kudanganya, Mussa ni mtiifu. Ni yule anayetenda kinachotakiwa. Kwa mfano,


tunamwona wakati anapoambiwa na Bw.Binafsi (Babake) kumwonyesha utiifu wake,
anaitikia vizuri na kuanza kuonyesha utiifu wake babake akimsihi kwa kutokonga na akiuliza
eti ni nani atakayefanana na babake (uk 36-37).
 Aidha, ni mwenye msimamo thabiti yaani anayasisitiza anayoyasema na kutenda bila
kubadilikabadilika. Kwa mfano, tunamwona akimwambia Zangu ya kuwa maneno yake
yanaweza kuwa na utata lakini hayana ugumu. Anaendelea kusema eti ameamua kusema na
kupiga kelele na ndivyo tunamwona anataka kuwatafuta wa kumfundisha kusema (uk 48 na
54).
 Isitoshe, Mussa ni mzalendo. Ni yule ambaye yuko tayari kuipingania haki nchi yake na
kuifia kwa hali ile yoyote. Kwa mfano, tunamwona akiambia Zanga ya kuwa watoto
watafute haki zao za utoto- haki za binadamu. Haki aliyozaliwa nayo kila mtu, haki ya
kusema bila hofu wala woga. Anaendelea akijiuliza ati mpaka lini atakuwa mtoto akingojea
kusema (uk 47)
 Mussa ni Msomi. Ni yule anayejua kusoma na kuandika. Kwa mfano, ni mmoja wa
wanafunzi (watoto) wa Bw.Binafsi ambao wanasomea chuoni. Hiki kweli kinathibitishwa na
maneno ya babake. Kwa mfano, Bw. Binafsi anasema, “Mnakwenda vyuoni kuelimika” (uk
34)
 Aidha, Mussa ni mkombozi (anasababisha mapinduzi) . ni yule anayesababisha matendo au
vita vya kuokoa watu kutoka kwenye hai mbaya yenye mateso au hali ya unyonge. Kwa
mfano, anajiunga na Mpya, Zanga na wananchi kuendeleza mgogoro wa kupigania haki zao.
Mathalani, tunamwona Bw.Naona akisema “Watoto wa nyumba kuu, Mpya, Mussa na
Zanga ndio waasisi wa fikra hizi Mpya na mabaya” (uk 67)
 Mussa ni jasiri. Ni yule anayelifanya jambo la kishujaa ambalo huweza kuhatarisha maisha
yake. Kwa mfano, hajamwogopa baba yake. Kwa mfano, anapinga uongozi wake wazi (uk
67)
 Ni mchochezi wa mgomo.
 Ni msaliti.
5 Zanga
Ni mtoto wa kiume wa Bw.Binafsi na Bi.Shoo. ni kaka yake Mpya na nduguye Mussa.
Anatenda kama ifuatavyo;
 Kwanza, ni mvumilivu. Ni yule ambaye anastahimili mambo kwa muda mrefu akingojea
mabadiliko. Kwa mfano, anayavumilia mateso ya babake.mathalani, ni mmoja wapo wa kaka
zake Mpya anaotwambia eti wanacho cha kusema lakini hawajasema hivi ni kuvumilia. Pia,
tunamwona akisubiria chakula kwa muda mrefu (uk 26 na 32)
 Zanga kwa ukweli ni mwoga. Ni yule mwenye hofu ya kufikwa na jambo linaloweza
kuhatarisha mtu. Kwa mfano, Mussa anapokuja usiku wa manane na kumwamsha,

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 32


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

tunamwona Zanga anainuka na kuweka mto mdomoni kuzuia maneno yasitoke kwa nguvu.
Hiki kunaonyesha woga wake (uk 45).
 Naye Zanga ni msomi. Ni yule anayejua kusoma na kukuandika. Mathalani, ni mmojawapo
wa watoto wa Bw.Binafsi ambao wanasomea chuoni. Kwa mfano, tunamwona Bw.Binafsi
akisema eti watoto wake wanaenda vyuoni kuelimika (uk 34)
 Hali kadhalika, Zanga ni mchochezi wa mgomo. Ni yule mwenye tabia ya kuwaambia watu
habari ili wapate kugombana, kupigana au kutukana. Kwa mfano, anaonekana pamoja na
Mpya na Mussa wakiendeleza vita vya kumpinga baba yao (uk 67).
 Pia, Zanga naye ni mtiifu. Ni yule anayetenda kinachotakiwa. Kwa mfano, babake
anapomwamru kumsifu, tunamwona anaitikia vizuri na kuanza kumshukuru kuwa tegemeo
leo (uk 37).
 Kadhalika, ni mwenye msimamo thabiti. Ni yule ambaye anayasisitiza na kuyatenda bila
kubadilikabadilika. Kwa mfano, tunamwona akijiunga na Mpya na Mussa eti wafundishwe
kusema na baadaye tunawaona wanasema wakiongoza mgomo wa kupigania haki zao na
kuupinga uongozi wa baba yao (uk 54-55 na 67)
 Zanga lazima ni msaliti. Ni yule ambaye anatenda kinyume na makubaliano. Kwa mfano,
anamsaliti Babayake na kujiunga na wananchi kumwondoa katika uongozi. Mathalani,
tunamwona kulingana na maneno ya Bw.Naona ni miongoni mwa waasisi wa uchochezi wa
mgomo (uk 67)
 Bila kuchoka, Zanga ni jasisi. Ni yule anayelifanya jambo la kishujaa ambalo linaweza
kuhatarisha maisha yake. Kwa mfano, hajamwogopa babake. Mathalani, tunamwona
akipinga uongozi wake anapoongoza mgomo na wenzake (uk 67)
 Hatimaye, Zanga ni mzalendo. Ni yule ambaye yuko tayari kuipigania na kuifia nchi yake
kwa hali ile yote. Mathalani, tunamwona akiuliza jinsi ambavyo anaweza kujua kusema ili
aanze kusema. Aidha, ni mfano mzuri wa wale wanaoongoza mgomo wa kupigania haki za
wananchi (uk 54-55) na uk 67)
6 Bi.Subira.
Ni kijana wa kike ambaye anajali masilahi ya wananchi wenzake. Sifa zake ni zifuatayo;
 Ni mvumilivu. Ni yule anastahimili mambo kwa muda mrefu akiyasubiri mabadiliko. Kwa
mfano,kulingana na jina lake, inaonekana eti ameanza kusubiria uongozi mbaya wa
Bw.Binafsi kubadilika kwa muda mrefu (uk 58).
 Pia, ni mchochezi wa mgomo. Ni mwenye tabia ya kuwaambia wananchi habari ili wapate
kupigania haki zao, Kwa mfano, tunamwona akianzisha vurugu wakati anaposema eti
amechoka kusubiri na kusema eti anadhani nchi yao haina viongozi. Baada ya hayo, wengine
wanaanzia hapo (uk 58)
 Aidha, Bi.Subira ni mkombozi. Ni yule ambaye anasababisha vitendo au vita vya kuokoa
maisha ya watu. Kwa mfano, tunamwona akisema eti amechoka kusubiri hivi kuamua
kusema. Anaendelea kusema eti mtu asiposema hawezi kujikomboa (uk 59)

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 33


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

 Bi.Subira kwa upande mwingine ni jasiri. Ni yule anatenda kwa ukakamavu bila kuogopa
hatari yote. Kwa mfano, wakiwa katika mkutano wa dharura katika bustani ya wananshi
(taifa), Bi.Subira anaingia na kusema wazi bila kuogopa eti amesubiri na kuchoka, a nasema
hatasubiri tena (uk 58)
 Ni mwenye msimamo thabiti. Ni yule anayesisitiza mambo bila kubadilikabadilika. Kwa
mfano, anaanza kusema ili aweze kwa ukweli kuukomesha uongozi mbaya wa Bw.Binafsi.
 Bila Shaka, Bi.Subira ni mwerevu yaani ni kwenye kuamua na kutambua mambo jinsi
yanavyoonekana. Kwa mfano, Tunamwona akiyatambua matendo maovu katika uongozi wa
Bw.Binafsi. kwa mfano, tunamwona anasema kuwa, kwao, watu wanafanya wapendavyo
yaani kukata miti ovyo, kujenga nyumba bila vibali, kuchukua ardhi na viwanja kwa nguvu,
kuchafua mazingira, kuchafua ofisi za watu na kadhalika (uk 59).
7 Kushoto.
 Ni mwenye njaa. Ni mhusika ambaye anaonyesha kuwa amekosa chakula na kinywaji kwa
muda mrefu. Kwa mfano, tunamwona akisema “kiu, kiu, kiu……….Njaa, njaa, njaa …
huko nitokako kumepoteza maisha” (uk 8).
 Kushoto ni mzalendo. Ni yule ambaye yuko tayari kuifia na kuipigania nchi yake. Kwa
mfano, tunamwona akisema eti nchi ni tamu kuliko siasa na yuko tayari kujitolea mhanga (uk
23-24)
 Kushoto ni mwimbaji yaani tunamwona yuko pamoja na Kulia wakiimba wimbo wao wa
ukombozi,
“Mwisho maana yake mwisho”
Mwisho hawezi kuwa mwanzo…..
Mwisho unapokuwa mwisho yaani yuko hali ile yoyote. Kwa
Hauwezi kurudiwa
Hauwezi kurejea nyuma……”
8. Kulia.
 Ni mwenye njaa. Ni mhusika ambaye anayeonsha kuwa amekosa chakula kwa muda mrefu.
Kwa mfano, tunamwona akisema eti anahisi nafsi yake lakini haisiki, anahisi nafsi ya mtu
mwingine ndiyo ambayo ina mwongoza, njaa njaa njaa. Kiu, kiu, kiu (uk 11)
 Kama kushoto, naye ni mzalendo yaani yuko tayari kuifia na kuipigania nchi yake kwa hali
ile yoyote. Kwa mfano, tunamwona akisema eti nchi ni tamu kuliko siasa na yuko tayari
kujitolea mhanga (uk 23-24)
 Aidha, Kulia ni mwimbaji yaani tunamwona yuko pa Kushoto wanaimba wimbo wa
ukombozi wakiimba’
“Mwisho maana yake mwisho”
Mwisho hawezi kuwa mwanzo…..
Mwisho unapokuwa mwisho yaani yuko hali ile yoyote. Kwa
Hauwezi kurudiwa

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 34


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

Hauwezi kurejea nyuma……”


9. Bw. Naona.
Ni waziri wa nchi, mwenye mwelekeo wa ukombozi. Sifa zake ni;

 Ni mzalendo. Kwa mfano, anasema mambo kana yalivyo yaani anamwambia Bw.Binafsi
bayana kuwa watu wamekuwa wamelala lakini sasa wameamka. Anaendelea kusema ukweli
kuwa chini uongozi wake yeye anaona wananchi wameamshwa na mengi, kwa hivyo
wanapawa kuwa macho. Anawaunga mkono kulingana na maneno yake hivi kuonyesha
uzalendo(uk 63)
 Bw.Naona ni jasiri. Ni yule anayeweza kusema, kutenda bila kuogopa hata kamwe. Kwa
mfano, hajamwogopa mheshimiwa mkuu Bw.Binafsi kumwambia ukweli kuwa suala la
kupigania haki limeanzishwa na watoto wake (uk 67)
 Ni mvumilivu yaani anastahimili uongonzi mbaya wa Bw.Binafsi yaani tunamwona mengi
na wanapaswa wawe macho. Kauli hii inaonyesha kuwa naye anayaona matendo maovu
lakini ameyavumilia (uk 63)
 Pia, Bw.Naona ni mwenye busara kwa sababu anaamua kutowashika wale ambao
wanachochea mgomo.
 10. Bw.Salimina
Ni kiongozi anayesimamia taifa kama ofisa wa usalama. Ana sifa zifuatazo;
 Ni mwenye busara kwa sababu anaamua kutowashika wale wanaopigania haki zao ili
waweze kujikomboa.
 Ni jasiri kwa mfano, tunamwona akiambia Bw.Binafsi ya kweli eti watu wanasema elimu
anayodhani anasambaza inatukuza uongozi wake badala ya kukuza taifa lenyewe ambalo
wanaliona si taifa (uk 64).
 Bw.Salimina ni mpiganiaji haki yaani tunamwona akiagizwa na Bw.Binafsi kuwakamateni
wanachochea mgomo lakini anakataa na kusema eti uchochezi wa mgomo hauna viongozi
bali unajiongoza (uk 69)

FANI/ MBINU/ TAMATHALI ZA SEMI KATIKA TAMTHILIA YA KIMYA KIMYA


KIMYA

Fani ni jumla ya mbinu za kisanaa/ lugha ambazo mwamdishi anazitumia kuwasilisha ujumbe
wake kwa hadhira. Mwandishi wa Kimya Kimya Kimya Said A Mohamed ametumia mbinu
zifuatazo;

1) Mrudio/ Takriri

Ni mbinu ya kurudiarudia ya maneno kusisitiza ujumbe . Kwa mfano ;

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 35


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

 Mbinu hii inayonyesha Kushoto na Kulia wakikariri neno “njaa” na “kiu”. Mathalani,
Kushoto anasema “Kiu,Kiu,Kiu…Njaa, njaa, njaa… huko nitokako kumepoteza maisha
(uk8). Kwa upande wa Kulia anasema, “Nahisi nafsi ya mtu mwingine ndiyo
inayoniongoza. Njaa, njaa, njaa. Kiu, kiu, kiu……” Wahusika hawa wanasisitiza ukosefu
wa maji na chakula (uk 11)
 Aidha, tunamwona Kulia akisisitiza neno “Kiza” Kwa mfano,anasema, “Kiza, Kiza ndani ya
kisima mna ombwe” (uk 12)
 Pia, tunamwona Kulia anarudiarudia neno “hapo”. Kwamfano, anasema, “…..Mimi nataka
kwenda kushoto, lakini kwa sababu fulani inaning’aniza kulia. Nazuiwa “hapohapo”
kulia kifikra (uk 16).
 Isitoshe, mwandishi naye amerudia neno “Mgongo.” Kwa mfano, anasema, “Bada
wamegandamana kitu kimoja, lakini wanasukumana ‘Kimgongomgongo’ (uk 17)
 Bila Shaka, takriri inaonekana kutokana na maneno ya Mpya akisema…. “Umeshafika”….
“Umeshafika” wakati wa kusema ingawa mimi peke yangu sina uzito wa kusema’’ (uk
20)
 Waaidha, maneno yanayotoka ndani ya kisima yanakariri “Ishara njema”. Kwa mfano, Sauti
inasema, “Ishara njema…..ishara Njema”…. “Ishara njema”….. Njema Njema, njema, “
Ishara njema”. 9uk 21)
 Mpya pia amerudiarudia kira “tazameni”. Kwa mfano, anasema, “Tazameni”, Tazameni’
enyi walimwengu ‘Tazameni” wananchi hii. “Tazameni watoto, wajukuu,vitukuu,
virembe, virembwekeza na vinying’inya” (uk 23)
 Hali kadhalika, mbinu ya takriiri inathibitishwa na kishazi cha Mpya akisema eti amekoka.
Kwa mfano, anasema, “Nimechoka kusubiri”, ‘Nimechoka kugonjea’. ‘Nimechoka’
kunyamaza”. Anaendelea kurudia kiunganishi ‘na’ wakati anapotaja mambo yakuombea
ruhusa, kwa mfano, anasema, “Tungojee, tungojee mpaka lini? Kula, kulala, kuamka,
kubaki ndani, kushoto nje, kwenda na kurudi, kwenda haja kubwa na ndogo, kuuza na
kununua……na, na, na…..kila kitu! (uk 31)
 Isitoshe, Bw.Binafsi anakariri kitenzi ‘cheka’ wakati Mpya anapomchekelea. Kwa mfano,
“mnaona ananicheka? Ananicheka kimoyomoyo…… binafsi yangu. Ananicheka mimi.
Wewe mimi”(uk 40)
 Baada ya kicheko hicho, bw.Binafsi anamfukuza akisema atoke. Kwa mfano, anasema,
“Toka toka toka……” (uk 41)
 Zanga anapomyamazisha Mussa wakati anapiga kelele, anasema, “shhhhhhhh! Kimya,
Kimya, Kimya…..” (uk 45) na kadhalika.
2) Uhaishaji/ tashihishi

Ni mbinu ambayo kitu kisichokuwa na uhai hupewa sifa za kiumbe mwenye hai. Kwa mfano;

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 36


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

 Sauti inajitokeza ndani ya kisima. Kwa kweli kisima hakiwezi kusema lakini kimepewa sifa
za kiumbe mwenye uhai. Kwa mfano, kinaambia Kushoto kuwa anakotoka hakuna uhai
(uk 8). Adha, Kinamwambia Kulia kuwa alikotoka kukavu, kote kumedamirika (uk 11)
 Aidha, Mpishi anaonekana akizungumza na vyombo. Kwa mfano, anasema, “Nyinyi vyomba
mmetumwa nini kuja kunisemesha mimi? (uk 29)
3) Utohozi
 Ni mbinu ya kuswalihisha maneno yasiyo ya kishwahili yatamkwe kama ya kishwahili. Kwa
mfano, neno “familia” limetoholewa kutroka neon la kingereza “family” (uk 26)
 Pia, mwandishi ametumia mbinu ya utohozi kurembesha kazi yake.kwa mfano, tunamwona
akisema, “Hatimaye ‘memba’ wa familia yake….” Neno memba linatokana na neno
“member” la Kiingereza (uk 30)
 Mwandishi pia ametumia utohozi anaposema hapo Bw.Binafsi anaketi hapo, lakini ghafla
anasimama hapo anamwona seketari wake anayetangaza kuingia kwa Bw.Naona na ofisa wa
Usalama Bw. Salimina. Neno ‘Seketari’ linatokana neno ‘Secretary’ na ‘Ofisa’ linatokana
na ‘Officer’ yote ya kiingereza (uk 78)
4) Kejeli.
 Ni mbinu ya maneno ya kuudhi mtu kwa masihara au kumfanyia kero. Kwa mfano, Baada ya
Mpya kukataa kumwinamia, babake, Bw.Binafsi anamkaripia na maneno ya kejeli.
Mathalani, tunamwona akisema, “Wewe kigego, mtoto wa ukorofi – Sikutaka mimi uingie
mimba mwa mamake wewe. Mtoto wa kike ana faida gani? Na ilipoingia mimba sikujua
kama ungezaliwa hivi wewe. Ningekung’oa mimbani mwa mamake!” (uk 34)
 Aidha, Mpya anapomwambia baba yake Vitendo vyake, babayake anamkaripia akisema,
“Fumba kijaliba chako! Nani kakuruhusu kufungua domo lako chafu hapa?” (uk 39).
 Vile vile, wananchi wanapomjulisha kiongozi mkuu eti wanataka kubadilisha katiba.
Bw.Binafsi anawamiminia bahari ya kejeli. Kwa mfano, tunamwona anasema eti wao ni
vinyangarika wamelala fofofo kama pono na wanachokijua ni kula mhogo tu (uk 66)
5) Alama za dukukuku/ Mdokezo.
 Ni mbinu ya kifani au sanaa ambayo kwayo mtu husema baadhi ya silabi, neno au maneno na
kuacha mengine. Hali kama hii inasababishwa na; kilio, kicheko, hofu, hasira au kutojua
ukweli wa mambo. Kwa mfano, Kushoto na Kulia wanadokeza maneno. Mathalani,
tunawaona wanasema, “kiu, kiu, kiu…… Njaa, njaa, njaa…..” (uk 8)
 Aidha, Kulia anapotaka kwenda kushoto tunamwona anasema, “lakini siku hizi
hawanong’oni licha ya kusema…….aaaa, wazimu ……(anasita, halafu……) (uk 11)
 Waaidha, tunamwona Kushoto naye anatumia alama za dukuduku. Mathalani, anasema,
“Mbona siendi mbele? Najitahidi …..Najivuta. Najisukuma. Natumia nguvu zanga zote,
lakini…..(uk 15)

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 37


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

 Vile vile, Kushoto anapomwuliza ikiwa utandawazi ulikuweko. Zamani, Kulia anajibu kwa
mdokezo bila kumaliza anasema, “ndiyo ulikuweko kwa kiasi fulani na kwa nguvu ndogo
mno, lakini sasa…….”(uk 17)
 Isitoshe, kwa hofu mwingi Bw.Binafsi anapomwuliza Bw.Salimina ikiwa wananchi
wanadhani bado wamelala, Bw.Salimina anajibu na kusema, “Wao wanasema kwamba
elimu yenyewe inayotolewa ni elimu ya uhange. Ni elimu
inayo…..inayo….inayotukuza……aaaa……….” (uk 64)
6) Nahau.
 Ni mafungu ya maneno yenye maana fiche ambayo hutumiwa na mwandishi ili kuweka
maadili katika matamshi. Kwa mfano, Mwandishi anasema kwamba Kushoto “ametoa
Macho”. ‘‘Toa macho” ni nahau ambaye inamaanisha “kuona wazi’’ (uk 8)
 Fauka, katika maneno yake Kushoto ametumia nahau. Kwa mfano, tunamwona akisema,
“Labda hapa ndipo baadaye palipochotwa maji kukata kiu na kuzima joto iliyomo ndani
ya nafsi zao”. “kata kiu” ni nahau inayomanisha “zima kiu” (uk 9)
 Hali kadhalika, tunamwona Mpya anatumia nahau akisema, “lazima mtu mmoja wetu
ajitolee mhanga” . “Kujitoa mhanga” ni nahau ya inayotumiwa mtu akimaanisha ‘‘kuwa
tayari kufanya kitu kwa hali yoyote” (uk 21)
 Vile vile, mwandishi naye ametumia nahau akielezea hali ya Kushoto na Kulia. Kwa mfano,
anasema, “Kulia na Kushoto wanabagukana kutazamana uso kwa uso”. ‘‘Kutazamana
uso kwa uso”ni nahau yenye maana ya, “kuonana” (uk 23)
 Isitoshe, baada ya Bw.Binafsi kumshukuru Mungu na kuombea chakula, wote “wanakula
kwa pupa na hamu”. ‘‘ Pupa na hamu” ni nahau inayomaanisha ‘‘kuwa na hamu nyingi
sana” 9uk 35).
 Zanga naye anatumia nahau anapomwonya Mussa akiwa anapiga kelele. Kwa mfano,
anasema, “Ukija kusikika utakiona cha mtema kuni”. “Cha mtema kuni’’ ni nahau
inayomaanisha “Kuadhibiwa kwa sababu ya kosa” (uk 46)
 Bila shaka, mwandishi ametumia nahau akiwa anafafanua hali ya Bw.Binafsi. kwa mfano,
anasema, “Anaonekana kakata tama na huzuni nyingi zimemvaa”. “Kata tama” ni nahau
inayomaanisha “ Kupoteza matumaini” (uk 87)
 Fauka ya hayo, Bw.Salimina naye ametumia nahau anapofafanua vurugu ya wananchi.
Mathalani, anasema, “polisi waliwatimua Kwa virungu tu, na wananchi wakatimka ovyo
ovyo…..mambo yak’enda segemnege….sambejambe! .“Enda segemnege” ni nahau
inayomaanishe “ kuharibu mambo” (uk 69)
 Bw.Naona akiwa anamfafanulia nahau akisema eti lazima wananchi “wawe macho”, “ kuwa
macho’’ humaanisha, “kutambua” (uk 63)
7) Tabaini/ Ukinzani

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 38


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

 Ni mbinu ya usemi wenye maana ya ukinzani lakini maana ya msingi haitengeki. Kwa
mfano, wakati Kushoto anapomwuliza Kulia anasema, “kulia au kulia kucheka?” Swali hili
lina ukinzani kwa sababu neno “kulia” hapo linachukua maana tofauti kama vile;
* “Kulia” kwa kutoa machozi
* “kulia” kama upande wa mwili mkono au mguu
* “kulia kutokana na kitenzi “la” (uk 13)
 Aidha, sauti ya Mpya nayo inaonyesha mbinu ya tabaini. Kwa mfano, inasema, “usiwe
utawala wa mtu na familia yake finyu ingawa pana”. Anachomanisha hapa ni eti,
Bw.Binafsi asijibinafsishe na uongozi wa nchi bali awaachie wananchi nao waongoze (uk
53)
8) Uzungumzaji nafsi/ uzungumzi nafsi.
 Ni mbinu ya lugha ambayo mhusika anazungumza pepe yake. Kwamfano, Mpya anaoneka
akizungunmza peke yake. Mathalani wakiwa wanasubiria baba yao, Mpya anajisemea “huyu
ndiye babangu (Anaigeukia hadhira huku kaketi vile vile juu ya kiti na huku familia yake
inamkana. Sauti inaendea). Mtu wa ajabu! Nafsi yake ni yake mwenyewe. Lakini nafsi zetu
si zetu ……….Nafsi zetu ni……….aaaa sisemi …….. siruhusiwi kusema ………” (uk 30)
 Pia, Kushoto anaoneka akisema peke yake baada ya kushangazwa na Sauti inayotoka ndani
ya kisima. Kwa mfano, anasema, “Aaa, hiki ni kisima cha aina gani, kisima
kinachosema?.....”(uk 9)
 Aidha, Kulia naye anaonekana akisema peke yake. Kwa mfano, anasema, “Nimechoka
vibaya kwa safari ya miaka. Sijasita hata siku moja. Mchana na usiku niko mbioni -kiguu
na njia, kutafuta sehemu yangu ya uhuru……” (uk 11)
9) Kuchanganya ndimi/ Mseto.
 Ni mbinu ambazo lugha za kigeni zinatumika katika maneno au sentensi za Kiswahili. Kwa
mfano, Bw.Binafsi ametumia mbinu ya mseto anapoambia Bw.Salimina kuwa hakuna
kikundi kisicho na kiongozi. Kwa mfano, tunamwona anasema, “kuna kikundi gani cha
maana kisicho na uongozi …..Labda” Mass eruption”. “Mass eruption” ni lugha ya
Kiingereza (uk 69)
10) Chuku/ Udamisi
 Hii ni mbinu ya lugha ambayo mwandishi au mhusika. Kwa mfano, mhusika Mpya anatumia
chuku katika maneno yake. Mathalani, anasema, kuwa mama yake ameketi katika ukingo
wa dunia. Hii ni chuku kwa sababu dunia haina ukingo (uk 32)
 Pia, Zanga naye ametumia mbinu ya udamisi katika maneno yake. Mathalani, anasema,
“Hupiga kelele mpaka bahari ijae kwa machozi yangu ya huzumi na hamaki” Hii ni
Chuku kwani machozi ya huzuni hayawezi kujaa bahari (Uk 49)
 Ghalibu ya hayo, Mwandishi Said. A Mohamed ametumia mbinu ya chuku katika kazi yake.
Kwa mfano, anasema kuwa katika mkutano wa wananchi, askari wanamiminika na kuingia

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 39


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

bustanini na virungu. Ukweli ni kwamba, watu hawawezi kumiminika lakini wanajitokeza


ghafla, hivi ni kuonyesha chuku (uk 61)
 Waaidha, Sauti A Mohamed ametumia mbinu ya chuku. Kwa mfano, anasema kuwa
Bw.Naona kwani videvu haviwezi kuanguka . Videvu haviwezi kuanguka (uk 67)
 Bila shaka, mwandishi ametumia chuku anapoelezea mchanganyiko wa Bw.Binafsi hususa
anaposema kuwa ameanza kushuka matao yao chini na kuijongea hadhira na anaonekana
ameonekana kakata tama na huzuni nyingi zimemvaa. Chuku imetumiwa hapa kwa kuwa
huzuni haziwezi kuvaa mtu (uk 87).
 Hali kadhalika, tunamwona Bw.Taja naye anatumia mbinu ya chuku akiwa anamwuliza
Bi.Subira hali. Mathalani anasema, “Vipi Bi.Subira, Naona umekuja moto! Naona Sauti
yako inapasua hewa bali kupita katika hewa (uk 58)
11) Nyimbo
 Ni maneno na sauti zilizopangwa na zinazopigwa kama ngoma ambazo huwa ni mziki.
Mathalani, watu (wananchi) wanaonekana wakiimba wimbo fulani. Wanaimba wimbo fulani
wakiwa wamesimama nyuma ya hadhira (uk 77)
 Pia, tunawaona Kulia na Kushoto wanaimba pamoja wimbo wa ukombozi. Kwa mfano,
waanasema,
“Mwisho maana yake mwisho
Mwisho hauwezi kuwa mwanzo………..
Mwisho unapokuwa mwisho
Hauwezi kurudiwa
Hauwezi kurujea nyuma …..” (uk 89)
12) Tashtiti .
 Ni mbinu ya lugha ambayo kwayo mhusika anauliza swali huku akijua jibu lake.Kwa mfano
tunamwona Kushoto anarejea kisimani,anainama na kuchungulia.anasema tena huku sauti
yake inasikika kidogokidogo… halafu ghafla, anapiga ukwezi, lakini mwangwi wa kisima
haumjibu kisha anauliza, “ kunatokea nini katika dunia hii. Hatia visima vimepoteza
Mwangwi? Havinatena sauti kujibu na kuongeza?” (KU 10).
 Kushoto naye anayauliza maswali huku akijua majibu yake. Mathalani, anauliza na kujipatia
jibu kwa mfano, baada ya kufikia kisima na kuisikia sauiti yake anasema ‘‘Hapa wapi?
Pameelekea kama za wazee. Na kile nini? Si kisimakile? Aaa, ndichi kujiuliza swali na
kujijibu kunaonyesha mbinu ya tashtiti (UK 12).
13) Tanakali sauti / Onamatopia
 Ni mbinu ambayo sauti zinazotolewa huiga milio, au sauti za viumbe vyenye hai na visiyo
hai. Kwa mfano,Mwandishi anasema kuwa Mpya anaibuka kisimani, “koroa rovurovu”.
“roa rovurovu” ni tanakali ya sauti (uk 22)
 Ghalibu, mwandishi Said. A Mohamed ametumia tanakali ya sauti akijaribu kuonyesha
mandhari. Kwa mfano, anasema, “Giza totoro’’ akimaanisha “Kiza kali sana” (uk 260 .

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 40


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

 Hatimaye, tunamwona Bw.Binafsi naye kweli ametumia tanakali ya sauti anapowadharau


wananchi wanaojaribu kupigania haki yao ya kubadilisha katiba na kusema hawana kitu
wanachokijua kuihusu katiba kwa sababu wao si viongozi.Anaendelea kuwaita vinyangarika
ambao “wamelala fofofo”kama pono’’. “Lala fofofo” ni tanakali ya sauti (uk66)
14) Methali
 Ni mbinu ya sanaa au kifasihi inayotumia mafumbo .Kwa ufupi, methali ni kifungu cha
maneno ya hekima yenye maana fiche. Ubora wa hekima hiyo hutegemea muktadha ambako
imetumika. Kwa mfano, BI.shoo ametumia maarifa ya wahenga akijaribu kumtetea Mtowe
Mpya dhidi ya mateso ya walinzi walioagizwa na Bw.Binafsi kwa sababu ya kutomhashimu.
Kwamfano anasema, “uchungu wa mwana aujuaye mzazi” akiwa anamaanisha kuwa
anamhurumia Mpya kwa sababu ndiye aliyeyahisi maumivu ya uzazi wake(uk 42). Pia,
Bw.Binafsi naye ametumia methali akiwa anawaonya wanaotaka kuleta mapinduzi nyumbani
mwake. Kwa mfano, anatumia methali ya, “kikulacho kumbe ki nguoni mwako..”
akimaanisha kuwa wanaomsumbua ndio walio karibu naye (uk 42)
 Aidha, Bw.Binafsi ametumia methali nyingine akiwa anawaambia Bw.Salimina na
Bw.Naona kuwahusu wananchi wanaodai kuwa wanataka wapewe uhuru wa kusema. Kwa
mfano, anasema, “kumbe fadhili za punda ni mazushi” (uk 65)
 Bw.Binafsi aidha, ametumia maarifa ya wahanga akiwa anaambia Bw.Naona na Bw Sikilivu
ati wanaochochea mgomo wote wakamatwe bila ubaguzi wote ikiwa ni wake au la yeye
hataki kujua. Anasema, “mtoto akililia wembe mpe” akiwa na maana kuwa watoto wake
wakiwa wanataka kuhatarishwa awaache wahatarishwe (uk 70)
 Pia, anaendelea kutumia methali ya “asiyesikia la mkuu huvunjika mguu” akimaanisha
kuwa ikiwa hawataki kusikia watajuta baadaye (uk 70)
 Wakati Bw.Binafsi anapomlilia / anapolilia yoo linamwambia eti lilimwambia lakini
hakusikia. Linamkuumbusha kuwa lilimwambia eti akitawala vema atamalizia vema na
akitawala vibaya atashia vibaya .Kwa mfano,linamwambia, “pendapo mema huirudia
mema” yaani mtenda jamala huliwa jamala (uk 82 )
 Hatimaye, Bw.Binafsi anatumia methali nyinngine wakati Mkewe Bishoo anapomwambia eti
ajiuzulu watoke, Bw. Binafsi anamjibu, “Muungwana hakimbii vita” akiwa na ukakamavu
wa kuonyesha ujasiri wake (uk 86)
15) Maswali ya balagha
 Haya ni maswali yanayoulizwa na mhusika ambayo hayahitaji majibu .kwa mfano, maswali
ya Mpya anayojiuliza akiwashusu Kulia na Kushoto ambao wamepeana migongo.Kwa
mfano anauliza, “Kwa nini wamepeana migongo? Kwa nini wanasuguana migongo? Kwa
nini wanachagua pande tofauti kabla ya kujali taifa? Kwa nini hawasimami pamoja
ingawa wana misimamo tofauti?” Maswali haya ni ya balagha kwa sababu Mpya hawezi
kujibiwe (uk 22).

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 41


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

 Ghalibu, Mpishi naye anauliza maswali ya balagha akiwa anauliza vyuma. Kwa mfano,
anasema “Nyinyi vyombo mmetumwa nini kuja kunisemesha mimi? Kuja kunimwagia
unga. Mimi sijapata kusema namna hii . Mnasema nyinyi na kunisemesha na mim nini?
(uk 29)
 Hali kadhalik,a maswali Mpya anayojiuliza nayo ni ya balagha akiwa anasema eti hataki
kusubiri siku tena. Kwa mfano, anauliza, “Kwanini kila siku tugonjee ? Tugonjee,tugonjee
mpaka lini?...” (uk 31).
 Maswali ya balagha mengine yanalizwa na Bi.Shoo akiwa anaonyesha utiifu wake kwa
mumewe. Kwa mfano, anasema, “..nani atafanana na we nchini humu? Nani atafanana
na wewe dunia hii? (uk 37).
 Fauka ya hayo, Mussa naye anatumia mbinu ya maswali ya balagha anapouliza maswali
yasiohitaji majibu. Kwa mfano, anauliza, “Mpaka lini nitakuwa mtoto? Mpaka lini
nitangojea siku ya kusema? Mpaka lini nitaongozwa na mawazo ya mtu mwingine?
Mpaka lini nitasema anavyotaka mtu mwingine?” (UK 47).
 Maswali mfulilizo ya Bw.Binafsi ni ya balagha. Anauliza maswali baada ya kuambiwa na
Bw.salimina kuwa wananchi wanasema kuwa elimu yake inatukuza uongozi wake bali si
taifa. Analipuka kwa maswali na kuuliza, “si taifa? Taifa linolojulikana vizuri duniani kote
sitaifa? Taifa linaloendeshwa kwa usalama si taifa? Taifa ambalo watu wake wanakula na
kushiba si taifa? Taifa ambalo watu wake wanatibiwa wakiumwa si taifa? Taifa ambalo
watu wake hawasemi ovyo ovyo si taifa? Kama hii si taifa lipi basi taifa? Kama hiti si taifa
lipi basi taifa?” (uk 64)
16) Taaashira/Metonomia
 Ni aina ya tamathali ya semi ambayo kitu kinachohusiana na kingine hutumiwa kuashiria
kitu kingine kama hicho. Kwa mfano “Mungu Mpya’’ ni jina ambalo limetumiwa kuashiria
“utandawazi” (uk 16)
 Pia, Kushoto na Kulia kupeana migongo na kugusana huashiria umoja (uk 19)
17. Nidaa
 Ni tamathali ya semi ambayo inaonyesha kushanga au kushangazwa kwa jambo fulani kwa
mfano, baada ya Kushoto kuisikia sauti ya kisima kinachosema anashangaa. Mathalani
anasema “Nachungula kama sichungulii. Humu mna utupu. Labda mna mazingaombwe
.Labda mazigazi . Lolote liwalo, nashangazwa na kisima hiki kinachosema! (uk 9)
 Kulia naye anashangazwa na kisima hicho ambacho kinasema. Kwa mfano, anasema, “Na
kile nini? Si kisima kile? Aaaa, ndicho!” (uk 12)
 Aidha, Mkemeo naye sauti yake inashangaza anpoamuru hadhira kunyamaza. Kwa mfano,
“Kimyaaaaa! Kimyaaaa! Kimyaaaa!”(uk 26)
 Waaidha, Bi.Shoo anapomtetea mtoto wake Mpya dhidi ya babake. Bw.Binafsi
anamyamazisha kwa mshangao na sauti ya kutisa kwa mfano, ananguruma, “shaaaarab!”
(uk 26)

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 42


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

 Pia, Zanga ananeokana ametumia mbinu ya nidaa anapomnyamazisha Mussa eti asipige
kelele. Kwa mfano, anasema, “Shhhhhhhh! Kimya…Kimya…Kimya…” (uk 45)
 Mussa anaposema kuwa amechoka na vitendo vya babake, anasema akiwa na hasira. Kwa
mfano,Mungu mbele yangu! Mimi sijawaa kinyago cha mpapure. Wala sitawai kuwa!(uk
47)
18. Tasfida
 Ni tamathali ambayo kwayo maneno yanayotumika yanapunnguza ukali, aibu na kero za
msemaji. Pia, inajumuisha maneno yanayotoa heshima . Mathalani, “mzee” (uk 28), salamu
ya “Asalaam aleykum”(uk 57), mwitiko wa salamu “Aleykum salaam” (uk 57)
“Bwana”(uk 57), “Kujifungua” kwaa maana ya “kujikomboa “mheshimiwa” (uk 63)
19. Kisengele nyuma / Mbinu rejeshi/Kiangaza nyuma
 Ni mbinu ambayo mwandishi anarudi nyuma na kusimulia yaliyotokea awali .Kwa mfano,
mbinu hii inathibitishwa na maneno ya yoo. Mathalani,yoo linasema kuwa lilimwambia
Bw.Binafsi mwendo wake .lakini akalidharau. Lilimwambia ya kuwa yeye si malaika na
lilimwambia ya kwamba akitawala kwa wema atamalizia wema na kinyume chake (uk 32)
 Juu ya hayo, Bi.Shoo akiwa anamsifu au anaonyesha utiifu wake kwa mumewe Bw.Binafsi
anatuonyesha kuwa anakumbuka kugumu walikotoka. Hivi basi anatumia mbinu ya
kisengele nyuma (uk 36)
 Kuongeza hapo, zamani wazee walikuwa na kisima ambapo walikuwa wanasimulia hadithi
zao. Pia, anatuonyeshana ati katika kisima hicho ,palikuwa na bubuko la maji
yaliyonguruma. Na ni katika kisima hicho ambapo wazee walienda na kuamshana kutoka
kwa usingizi wa miaka mingi waliolala (uk 12)
 Mbinu vejeshi pia inathibitishwa ha maneno ya Kushoto kukihusu kisima. Mathalani
anasema eti ndicho kisima ambapo Fumo Liongo alifanyia tambiko kuhifadhi nafsi yake.
Katika kisima hicho, alipokimbilia kunya maji ya kuokoa maisha yake, baada ya kuchomwa
na shazia ya kitovu na mwanawe mwenyewe (uk 10)
20. Taniaba
 Ni taamathali ambayo kwayo jina la mtu / kiumbe mmoja wakati mwingine hutumiwa kwa
watu wengine wenye tabia, hali au mwendo kama wa mtu huyo. Kwa mfano, Bi.Subira
anasema, “……Afadhali hao masimba na mafisi wanaohujumu na kula viumbe”. Na kwa
hiyo, “Viongozi wakali na wanyonyaji” hapa wanawakilishwa na “Masimba na Mafisi” (uk
58)
21. Taharuki
 Ni mbinu ya kumwachia msomaji na hamu au mvuto ya kuendelea kusoma kazi ili aone
yanayofuata. Kwa mfano, Bw.Binafsi anapokataa kujiuzulu yoo linamwambia ya kuwa
halitasema tena. Hapa taharuki inajitokeza katika kuanguka kwake. Hii ni kwa sababu
hatuelewi vizuri kinachomwangusha na katika onyesho linalofuata tunamwona na hivi
hatuelewi anavyoamka (uk 82).

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 43


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

 Taharuki pia inajitokeza mwishoni mwa tamthilia. Kwa mfano, hatuonyeshi vizuri
Bw.Binafsi anavyoondolewa katika uongozi na wananchi. tunaona anaomboa jumba
kuporomoka na kumfunika au kutamani ardhi kupasuka na halafu tunawaona Kulia
wakiimba wimbo wa ukombozi, hivi, Bw.Binafsi ameuawa au amemezwa na ardhi? Hii ni
taharuki (uk 89)
22. Tashibihi/ Mishabaha
 Ni tamathali ya semi ambayo vitu viwili au zaidi vyenye sifa tofauti hulinganishwa kwa
kutumia viunganishi kama vile; “Kama”, “Kama kwamba”, “Mfano wa”, “fanana na”,
mithili ya” na “Kuliko”. Kwa mfano, Zanga anatumia mbinu hii mfulilizo baada ya kuisikia
Sauti ya Mpya. Mathalani, anasema, “ Inasikikia popote au Kokote! Inapasua kama radi
yenye hasira. Inakereza viini. Vya masikio kama msumeno wenye makali” (uk 49)
 Pia, Mpya anasema, “Kila siku vitu vingi haunza kama mchezo” (uk 50)
 Aidha, Bi.Subira naye ametumia mbinu hii. Kwa mfano, analinganisha nchi na msitu wa
watoro. Anasema, “nchi imekaa kama msitu wa watoro. (uk 58)
 Isitoshe, Bw.Salimina naye ametumia mbinu ya tashbihi. Kwa mfano, anasema, “………tena
watairebisha wao, maana wao wanajua kuiandika katiba kauli hiyo akiwa na hasiri na
kusema, “Wamelala fofofo kama pono kasha wanadai wanajua?” (uk 66)
 Juu ya hayo, mwandishi Mohamed naye ametumia mbinu hii akiifafanua hali ya Bw.Binafsi.
Kwa mfano, anasema, “anapiga hatua za masafa kama wanajeshi. Halafu anageukia
kushoto. Anapiga hatua za masafa kama mwanajeshi. Sasa anafuliza kutembea huku na
huku kama askari mlinda doria” uk 77)
 Katika mbinu sambamba, wananchi wanapomwendea Bw.Binafsi wanamwambia na kusema,
“Tuko sawa kama sahani na Kawa” (uk 80).
 Waaidha, wananchi wanapoenda kumkabili uso kwa uso Bw.Binafsi. Bw.Binafsi anaruka
hapo alipoketi kama mkizi na kutua mbele ya hadhira (uk 84)
 Mpya naye kwa ukweli anasema ati uwili wake umeshapata mifupa. Mbele hauendi, nyuma
hausongoei. Amebaki kimya kama maji ya mtungi (uk 53).
 Baada ya Mpya kutomwinamia babake Bw.Binafsi, Bw.Binafsi anawaamrisha walinzi wake
kumwendea Mpya, wanamshika mkono na kumburura kama gunia la makaa! (uk 41)
23. Dhihaka.
 Ni tamathali ya semi ambayo kwayo mtu kwa makusudi husema maneno kumbeza mtu
mwingine. Kwa mfano, Bw.Naona anapaka mafuta kwa mgongo wa chupa kwa ajali ya
kupata usamehevu maalumu anapomwita mtukufu. Hii ni dhihaka (uk 68)
 Aidha, Bw.Binafsi anapomtusu mtotowe Mpya akisema eti Mpya si mtoto wake, Sauti ya
Mpya inasikika ikimchekelea kicheko cha mfulilizo ha, ha, ha…… Kicheka cha Mpya ni cha
dhihaka (uk 40)
24. Aklonimu.

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 44


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

 Ni mtindo wa lugha ambao unajihusisha na matumizi ya vifupisho. Kwa mfano, mwandishi


ametumia mbinu hii katika majina ya wahusika kama vile Bw.Binafsi(Bwana Binafsi), Bw.
Naona (Bwana Naona), Bw. Salimina (Bibi Salimina), Bi.Mgeni (Bibi Mgeni), Bi.Subira
(Bibi Subira), Bi. Shoo (Bibi Shoo), Bw. Taja (Bwana. Taja), Bw. Sikilivu (Bwana Sikilivu)
(uk 57-58) na (uk 64-65).
 Pia, kuma matumizi ya aklonimu yaani GMO’s (uk 59)
25. Taswira/ jazanda.
 Ni mkusanyiko wa picha zinazoundwa na maelezo ya msanii katika kazi yake ya ubunifu.
Taswira hujengwa na matumizi ya tamathali za semi hususan sitiari na tashbiha. Kwa mfano;
maneno ya mwandishi njaa ya miaka yanajenga picha ya umaskini katika akili mwa
mshomaji (uk 8)
 Aidha, maneno ya Mpya nayo inajenga picha ya uzalendo akilini mwa msomaji. Kwa mfano,
anaposema kuwa amechoka kusubiri, amechoka kugonjea na hata amechoka kunyamaza (uk
31).
 Maneno ya Bw.Binafsi nayo yanajenga picha ya ukatili akilini musa msomaji. Kwa mfano,
anamwita mtoto wake kigego na ukorofi. Anaendelea kusema kuwa angejua kwamba
angezaliwa hivyo, angemng’oa mimbani mwa mamake (uk 34)
26. Majazi/Majina ya Lakabu.
» Ni upaji wa mhusika jina kulingana na kazi yake, tabia yake, maneno yake, umri wake,
mavazi yake pamoja na matendo yake. Kwa Mfano;
 Mpya ambaye anatenda mambo mapya.
 Bw.Sikilivu ambaye anachukua muda akisikiliza maneno yanayosemwa.
 Bw.Naona ambaye anasema mambo kama yalivyo.
 Kushoto ambaye anatoka upande wa kushoto.
 Kulia ambaye anatoka upande wa kulia .
 Bi.Subira ambaye amesubiria uongozi mbaya na kuchoka.
 Bw.Binafsi ambaye anaiongoza nchi yake kwa ubinafsi.
 Bw.Taja ambaye anataja ukweli wa mambo.
Maswali ya majalibi.
1. (a) “Mpya ni mhusika anaye linganishwa na vijana wengine katika nchi yako.” Tetea kauli
hii ukitoa mifano kutoka tamthilia na nchi yako.
(b) Fafanua jinsi wahusika wanavyopigania haki zao?
2. “Wanawake wamefanya yanayostahili kuikomboa nchi yao.” Jadili kauli hii ukitoa mifano
kuntu.
3. Elezea sifa na umuhimu wa wahusika wafuatao;
a) Mpya
b) Bw.Binafsi
c) Bi.Shoo

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 45


TAMHILIA YA KIMYA KIMYA KIMYA NA SAID A. MOHAMED

MHAKIKI: MWALIMU FAGIL FARAJA MONDE


Piga 0756040644/0785090252/0780947386

d) Bw.Naona
e) Mussa
f) Zanga.
4. Linganisha na ulinganue maisha ya tamthilia ‘Kimya Kimya Kimya’ na maisha ya jamii
yako ukitoa mifano maridhawa.
5. “Uongozi wa Bw.Binafsi umejaa mambo na matendo maovu”. Tetea kauli hii ukiyataja na
kuyelezea hayo matendo.
6. Jadili vipengele vifuatavyo ukirejea tamthilia ya Said. A. Mohamed.
a) Umaskini
b) Umoja
c) Kinaya
7. “Kimya Kimya Kimya ni kichwa ambacho kinaona na ujumbe uliomo.” Tetea kauli hii ukitoa
mifano mwafaka kutoka tamthilia.
8. ‘‘Tamthilia ya Kimya Kimya Kimya ni kichwa ambacho kina mafunzo mengi kwa wananchi
wako.” Fafanua mafunzo unayoyapata kutoka tamthilia husika.
9. “umoja ni ngunvu utengano ni udhaifu” Kwa kurejelea tamthilia ya Said. A Mohamed, Jadili
kauli hii ukitoa mifano maridhawa.
10. Elezea malengo ya mwandishi wa tamthilia ya ‘Kimya Kimya Kimya’ ukitoa maelezo
mwafaka.

P320/2 KIMYA KIMYA KIMYA. Mwalimu Fagil Faraja Monde Page 46

You might also like