You are on page 1of 11

SHULE YA SANAA NA SAYANSI JAMII

IDARA YA KISWAHILI NA LUGHA NYINGINE ZA KIAFRIKA


BEWA LA MASENO
AKI 102: UTANGULIZI WA FASIHI YA KISWAHILI
(INTRODUCTION TO KISWAHILI LITERARURE)
MHADHIRI: DKT. DEBORAH NANYAMA AMUKOWA
KUNDI LA 48
MAJINA YA WANAKUNDI

JINA NAMBARI YA USAJILI NAMBARI YA SAHIHI


SIMU
SETH ONYANGO OPIYO EAR/00093/023 0768141540
OCHIENG STEPHEN OMEDO EAR/00481/023 0110907861
BRIAN ETINDI EAR/00575/023 0703465751
JACKSON OLOOKO EAR/00731/023 0758866754
JOSPHINE WACHIENG EAR/00053/023 0106598943
DAMARIS MORAA EAR/00872/023 0745959721
ROBINA KERUBO ONDATI EAR/00018/023 0743680490
SHEILA MORAA EAR/00212/023 0719458235
VIVIAN ATIENO EAR/00480/023 0743032769
NYAUMA KELVIN EAR/00825/023 0718491070
OKWANYO

SWALI LA UTAFITI:
‘Patashika zinazosheheni katika NDOA YA PATASHIKA si za ndoa tu’.
Thibitisha kauli hii.
UTANGULIZI
Patashika ni nini?
Patashika ni aina ya kitu au mwenendo ambao unakusumbua au kukuletea matatizo
katika maisha yako. Inaweza kuwa shida au changamoto ya kiafya, kihisia, kifedha au
katika maeneo mengine ya maisha. Ni jambo ambalo linaweza kukuletea wasiwasi au
kukufanya ujisikie vibaya. Katika lugha ya mtaani, patashika inaweza kutumika
kumaanisha hali ngumu au ya kutatanisha. Patashika zinazosheheni katika ndoa ya
patashika ambazo si za ndoa ni zifuatazo;

1. Umaskini/Ufukara/Ukabwela.
1. Galacha anakiri kwamba pamoja na kuhama kutoka nyumba yao ya kifahari, hali
yao ilididimia ikawa uchwara. Mambo ya kifahari yakawapa kisogo. (uk.1)
2. Galacha anasema kwamba baada ya mamake na yeye kutimiza kipimo chao cha
kilio, mamake alimbadilishia nguo akamvisha fulana iliyoraruka tumboni na kaptura
iliyotiwa kiraka upande wa nyuma ungedhani kiota cha ndege. (uk.2)
3. Sare za wanafunzi wa shule ya msingi ya Chekeleni zilimtia Galacha huruma.
Wengine walivalia kaptura zilizosetiri mbele na kusahau kuficha siri za nyuma.
Ziliunda madirisha mawili mawili katika sehemu za nyuma na kuyaacha makalio
yakiwachungulia wapitanjia. (uk.18)
4. Wanafunzi hawa wa shule ya Chekeleni vilevile walitembea miguu chuma yenye
nyayo iliyoweza kubana misumari. (uk.18)
5. Galacha anaongeza tena kwa kusema kuwa Chekeleni iliwaweka watoto wa
makabwela hohehahe wasiokuwa na mbele wala nyuma. (uk.18)
6. Galacha anasema kwamba mafanikio yao kula samaki hayakuwa juhudi za Masika
kwani yeye hakudhihirisha mfano wowote wa ulalaheri. (uk.40)
7. Godoro ambalo mamake Galacha alilazwa pale hospitali Jaribuni lilikuwa kuukuu
sana. Umeme nao haukuwa unatambulika popote katika hospitali hiyo. (uk.22)

2. Ukosefu wa Mapenzi.
1. Galacha analalamika kwa kukosa mapenzi ya baba mzazi na hili linabua maswali
mengi akilini mwake. (uk.1)

2. Upweke.
1. Baada ya Galacha kutoka katika ulimwengu wa kusadikika na kufikirika, mazingira
yale ya kifahari yalipata kumpa kisogo akahisi upweke kila mara alipojikuna au
kushtuka juu ya kiti chao cha mbao kilichyumbayumba kila mara. (uk.9)
2. Galacha anahisi upweke baada ya mamake na Rama kukosa kurudi nyumbani
baada ya kuenda hospitalini. Babake pia hakuwa anamwona tena. Alijihisi kama mtu
asiye na jamaa wala utambulisho. (uk.29)
3. Bwana Dola anahisi upweke baada ya mkewe kuaga dunia. (uk. )

4. Ulevi.
1. Babake Akoth anatambulika kama mlevi wa kila kileo akawa mtu wa kuzua
kimondo kila baada ya kulewa. (uk.12)
2. Bw. Dola anaambulia ulevi baada ya kifo cha mkewe. Anausaliti hadi wokovu
wake kwa kuwacha kumtumikia Mungu. (uk.143)

5. Matatizo ya Elimu.
1. Baada ya serikali kuisitisha mpango wa masomo bila malipo, Galacha na Rama
waliachishwa shule kutokana na hali ya mama yao kutokuwa na uwezo wa kuufadhili
masomo yao. (uk.16)
2. Galacha analinganisha hali ya shule ya msingi ya Chekeleni na hali ya shule ya
msingi ya Bidii. Anasema kuwa shule ilijengwa vibaya vibaya nao walimu
wakiongozwa na mwalimu mkuu wakakosa kufanya jambo katika kuimarisha shule.
Walimu walifunza kama ambao walilazimishwa kufanya kazi hiyo. (uk.17)
3. Amadi Madiewe tangu kuokotwa kwake Patashika hakuwahi kumpeleka shuleni na
hii ndiyo maana hakuwa mweledi wa lugha ambayo akina Galacha walizungumza.
(uk.80)

6. Mabadiliko ya mkondo wa Maisha/Hali ya Maisha.


1. Galacha anasema kwamba kilichowabadilisha hali ghafla kilibaki kitendawili.
Maisha ya kifahari yaliyowapa kisogo bado yalikuwa mabichi katika kumbukumbu
zao. Waliyakabidhi na kuyapokea maisha ya ukabwela ambayo hawakuyazoea shingo
upande.

7. Upungufu wa Kiafya.
1. Galacha anasema kuwa tangu watoke malishoni kwa mabwanyenye,
wameonyeshwa upungufu wa kiafya. Mili yao iliyonenepa kama nguruwe hapo awali
ilisinyaa kama puto lililochomwa na mwiba. (uk.18)

8. Maradhi/Magonjwa/Ndwele.
1. Mamake Galacha anakuwa muwele/mgonjwa pale Chekeleni. Galacha anasema
kwamba waliporudi kutoka kwa mama Hussein, yeye na Rama pamoja na mama
Hussein, mamake alizidiwa na jasho na kila mara alipojaribu kuinuka, mwili
ulimchezacheza akajiangusha tena kitandani. (uk.20)
2. Rahab alipofika kwa mzee Abdi, babake halisi, alizipokea habari kwamba babake
aliaga dunia miezi sita iliyotangulia baada ya kusumbuka kutokana na maradhi ya
UKIMWI. (uk.36)
3. Kijana mmoja wa kike aliyeabiri gari ambalo akina Galacha waliabiri, alisema
kuwa yeye ndiye aliyempima utingo wa gari hilo virusi vya UKIMWI na baada ya
kubaini virusi hivyo kwake akamwelekeza namna ya kuishi na kuyapanga maisha
yake vizuri. Suala hili lilimtia utingo huyo fedheha akaufungua mlango wa gari na
kutokomea mbali. (uk.41)
4. Galacha anasema kuwa walipata kusikia taarifa redioni kuhusu vifo vilivyotokana
na maradhi yasiyotibika. (uk.127)
5. Galacha anasema kuwa katika eneo la Majimbo mapenzi yaliendelezwa kwa hiari
na watu wakapata magonjwa kwa hiari bali si kwa kulazimishwa. (uk.129)

9. Vurugu.
1. Masika anazua vurugu hospitalini huku akitaka malipo yake baada ya kusafirisha
mamake Galacha hadi hospitalini. Daktari anajaribu kumkemea lakini anaendelea bila
kukoma. (uk.23)
2. Kulitokea vurugu kati ya babake Hussein na mamake Hussein eti kwamba mamake
Hussein aligundua bwanake alikuwa na macho ya nje tukio ambalo lilisababisha
utangano baina yao. (uk.33)
3. Bwana Mashaka anamfurusha Patashika kutoka kibandani na kwa wakati huo
alikuwa amechapa mtindi akalewa chakari. Alimbebea upanga mkononi sababu eti ni
kodi ya nyumba.
4. Kawaka anazua vurugu kwa kumwahi mamake Galacha kofi usoni. Patashika
alipoingilia kati, Kawaka alikwishamkanyaga mamake Galacha tumboni. Haya yote
alitenda kwa madai kuwa Patashika alimwoa mamake Galacha kama mke wake wa
pili. (uk.100)
5. Kawaka anamvamia mamake Galacha kwa madai kuwa aliskia uvumi ukienezwa
eti kwamba ni mchawi. (uk.132)
6. Galacha anasema kwamba Rahab ndiye alikuwa mtetezi wake pale mchezoni kwani
wakati mwingine vurugu ingetokea. Anaongeza kwa kusema kuwa Mokaya ndiye
aliyejulikana kwa tadi na hili lilimfanya kupigwa siku moja na Rashid kwa kumwita
mtoto wa mlevi. (uk.26)

10. Utengano
1. Utengano kati ya Galacha na mamake pamoja na Rama unazua maswala mengi
akilini mwa Galacha, maswali ambayo yana mpeleka kumwuliza mama Hussein hali
ya mzazi wake baada ya kutengana naye mwezi mmoja. Pia, alitaka kujua siku
ambayo mama pamoja na Rama wangwrejea nyumbani (uk. 28).
2. Galacha anakiri kwamba kuna mambo ambayo yanavuruga akili yake ambayo
hayawezi kuyasahau na mambo haya ni kutoweka kwa baba yake miaka miwili
iliyopita na miezi saba kwa mamake na Rama (uk. 39).
3. Galacha anaondoka Chekeleni na kutenganaa na Rahab. Rahab anampungia hali
akilengwa machozi. Moyo wa Galacha ulisumbuka (uk.74).

11. Ubaguzi.
1. Rahab alibaguliwa na babake aliyemwoa mamake baada ya kutengana na mchumba
wake wa kwanza ambaye hakuwahi kuwa naye katika ndoa halisi (uk. 35).
2. Mamake Rahab alimpa kibarua kigumu cha kwenda kumtafuta babake halisi katika
mtaa wa Chekeleni baada ya kukataliwa na babake aliyemwoa mamake (uk.35).
3. Kazi ya Patashika ya utabibu ilimfanya kujua juwabagua wale wa kutibu na wale
wa kutowatibu mpka wakati mmoja akalalamikiwa na umma (uk.95).
4. Patashika kazi yake imo kabla ya kuhamishwa kwenda Chekeleni kufuatia fununu
kwamba alikuwa akiwatibu wagonjwa wa kike na kuwapuuza wa kiume (uk. 95).

12. Ukiukaji wa Haki.


1.Mama Akoth alipoandamana na Rahab hadi nyumbani kwake aliahidi kwamba
angempa kila alichohitaji lakini ikatokea kwamba kiburi cha Mashaka, babake Akoth
haingemsabili kutia guu lake shuleni. Kwake Rahab alifaa ujakazi kuliko usomi (uk.
37)
2.Maafisa wa polisi wanamwagiza Galacha kuamka waende na hawataki kujali kama
Galacha alipona au hajapona. Hili linafanyika wakati ambapo Galacha alikuwa
amepata nafuu lakini hakuwa amepona vizuri (uk. 158).

13. Kifo/Vifo/Mauti.
1. Galacha anasema kwamba siku moja alipokuwa akidurusu ukurasa mmoja wa
gazeti la taifa leo pale maktabani mwao shuleni aliweza kukutana na ujumbe
uliozungumzia kuhusu kifo cha utingo ambayo alijitia kitanzi. Utingo huyo ndiye
alikuwa katika lile gari waliloliabiri siku ambayo Galacha alipelekwa shuleni (uk. 47).
2. Galacha anasema kwamba tangu mwanafunzi mmoja kwa jina la Falcao kumpiga
mwenzake kwa jina la Mtushi na kumzamisha majini hadi kifo, kulisitishwa kwa
onyo kali kutoka kwa mkuu wa polisi wilayani mwao (uk. 88).
3. Kifo cha Jefrey Masika kinatangazwa, habari ambayo inamsikitisha Galacha sana
(uk. 110).
4. Jioni moja akina Glacha walipata taarifa ya dau ziwani lililoenda mrama kisha
kumwaga wavuvi ndani ya ziwa Viktoria. Watatu walinusurika huku wenzao watatu
wakizama na kupotea majini (uk. 127).
5. Mokaya anatiwa kitanzi na kuaga dunia baada ya kusomewa hukumu ya kifo pale
mahakamani. (uk. 142).
6. Rahab alipompeleka Galacha nyuma ya nyumba, aliufungua mlango mijawapo ya
choo. Galacha aliweza kuona kiwiliwili cha Dola kikiwa kimening’inia mle. Ulimi
kautoa nje, macho yake yakakodoka, miguu ikakaika huku nguo zimetulia mwilini
(uk. 150).

14. Usaliti.
1. Hussein anakunja uso wake kwa maasi na pingamizi kwamba mamake amemsaliti
baada ya kumchukua Masika kama babake Hussein. (uk.32)
2. Galacha anasema kuwa hakuzungumza wala kufurahia chochote tena katika kikao
kile cha wazazi wao waliokuja kuwatembelea shuleni baada ya kusikia kwamba
mamake alimchukua mwanamme mwengine kama baba yao. (uk.55)
3. Mamake Galacha anawaka na kuwafurusha nje Galacha na Rama usiku kwa madai
kwamba aliwauliza baba yao ni nani wakajibu ni Philip Bidika. Hili lilikuwa kinyume
kwa sababu hapo awali mama yao alikuwa anawapenda. (uk.97)
4. Patashika baada ya kuondokewa na Kawaka anayapunguza mapenzi yake kwa
mamake Galacha na akina Galacha. Huu ni usaliti kwa kuwa hapo mwanzo
aliwapenda. (uk.138)
5. Patashika anawatema akina Galacha kabisa kwa madai kwamba wamemsababishia
bahati mbaya nyumbani kwake. (uk.139)
6. Mokaya anawasaliti wazazi wake kwa kujiingiza katika kitendo kibaya cha ubakaji.
Kisa hiki kilimwezesha kufikishwa mahakamani na kisha baadaye kusababisha kifo
cha mamake Mokaya. (uk.141)
7. Bwana Dola anausaliti wokovu wake kwa madai kwamba amejaribu kanisa lakini
haijamsaidia, Mungu amemwacha kufilisika. (uk.143)
8. Patashika anamdunga Galacha dawa inayochukua fahamu zake zote. Baadaye
inagunduliwa na Mwuguzi mwengine kuwa alimwachilia sumu mwilini. (uk.157)
9. Rahab anamsaliti Galacha kwa kuungana na Patashika kutoa ushahidi ambao si wa
ukweli dhidi ya Galacha. Hili alilitenda ili Galacha apate kufungwa ili abaki na
Patashika kama mpenziwe. (uk.164)

15. Udanganyifu.
1. Galipata alipata kusikia kwamba babake alipoteza maisha yake vitani kutoka kwa
babu mzaa mama baada ya mamake kumdanganya kwamba baba yao alienda ulaya.
(uk.66)

16. Mimba za Mapema.


1. Galacaha anasema kuwa mamake aligwia mimba kabla ya kufanya mtihani wake
na kumzaa Rama. Baada ya kugwia mimba alifukuzwa na wazazi wake akaenda zake.
(uk.67)

17. Uchawi na Ushirikina.


1. Eneo zima la Imo ambao akina Galacha walihamia kutoka hospitali Jaribuni
lilibeba walozi wa kila aina. Mchawi wa usiku angeingia ndani ya nyumba ya
wenyewe kwa njia ya kustaajabisha. (uk.82)
2. Inasemekana kwamba huko Imo kulikuwa na wachawi hatari zaidi; wale
waliolenga kuyahatarisha maisha ya watu. (uk.83)
3. Ilidaiwa kwamba warembo hao wale waliomtembelea Patashika kila mara alikuwa
akiwapumbaza na dawa aliyopewa na mganga mmoja kutoka Subawanga,
Tanganyika. (uk.96)
4. Galacha na Rama waliamka alfajiri moja kujitayarisha kwenda shule. Galacha
alihisi uvundo wa aina yake mle chumbani mwao mwa kulala. Mara akawasha tochi.
Kwa mshangao, mtu mweusi tititi alitoka nje mbio. Uchi wa mnyama alikimbia.
(uk.107)
5. Galacha anasema kuwa iliaminika kuwa wavuvi wengine walishiriki ushirikina ili
kuwapata wasichana. Walitumia dawa za waganga kuwapumbaza wakawa vifuu kisha
matokeo yakawa mimba na ndoa za lazima au hata maradhi. (uk.109)
6. Siku moja mamake Galacha alipokuwa akimlisha mtoto wake mdogo barazani,
Kawaka alipita hapo akamwangalia kwa macho makali. Baadaye tumbo la mtoto
lilianza kufura polepole likizidi, hadi likafika hatua ya kupasuka. (uk.121)
7. Inasemekana kwamba baada ya tumbo la mtoto kufura ilimbidi mama Galacha
kumtafuta mwuguzi wa kienyeji. Mtoto alinyweshwa dawa ya kumaliza urogi.
(uk.121)

18. Uyatima.
1. Inasemekana kwamba wazazi wake Amadi waliaga dunia miaka mingi iliyopita
akiwa na umri wa miaka mitatu tu. (uk.83)
2. Wazazi wake Yasmin waliaga dunia katika siku yake ya kuhitimu uuguzi katika
chuo kikuu cha Mwangaza. (uk.187)

19. Vita dhidi ya Jamii.


1. Amadi alikuja kuambiwa baada ya vifo vya wazazi wake kuwa vilitokana na vita
vya wenyewe kwa wenyewe kati ya jamii ya Watupatupa na Wazuavita. (uk.84)
2. Achayo, dadake Patashika alifurushwa na mumewe baada ya kufurushwa kwa
Kawaka kutoka Imo. Huu ndio ukawa mwanzo wa uhasama kati ya jamii ya
Wanamajimarefu na Waimo. (uk.134)

20. Ukahaba.
1. Patashika alikuwa akiwaleta wanawake na wasichana wa kila maumbile hapo
kwake. (uk.95)
2. Rahab anamwandikia Galacha barua na kumweleza kuwa Bw. Masika mbali na
kujihusisha na Bi. Rehema, alijihusisha na wasichana wengine ambao sasa wanahofia
maisha yao baada ya kifo chake. (uk.114)
3. Hussein baada ya kuzifuata sinema ndani ya nyumba yao kati ya babake na
mamake, aliamua kujipa kidosho wa rika yake. Kuna siku kidosho huyo alikuja
kumtembelea Hussein akamkosa kisha akanyemelewa na kunajisiwa na Masika.
(uk.115)
4. Rahab anapomwandikia Galacha mpenziwe barua, anamfahamisha kwamba
ukahaba umeenea kotekote Chekeleni. Anaongeza kusema kwamba unaenezwa hata
na watoto waliozaliwa jana. (uk.116)
5. Inasemekana kwamba ukahaba ulileta hasara Chekeleni. Zaidi ya watu wawili
walipoteza maisha kila wiki. (uk.126)

21. Chuki na Wivu.


1. Inasemekana kwamba chuki na wivu yalimwasha Kawaka ndani kwa ndani kila
siku. Hakukosa la kunena, kuwe kusiwe na Patashika pale nyumbani. Alisikika
akinung’unika peke yake. (uk.103)
2. Achayo aliporudi kwao Imo, aliwaambia akina Galacha kwamba Kawaka aliahidi
kuutekeleza utengano wa Patashika na mama yao kwa vyovyote vile. (uk.134)
3. Nduguye Masumbuko, babake halisi wa Rahab, baada ya kumfunulia Rahab habari
za kifo cha babake Masumbuko, hakumkaribisha hata ndani ya nyumba hata kwa
kopo la uji. Mazungumzo yote baina yao yakawa yametekelezwa chini ya mti. (uk.36)
4. Inasemekana kwamba nyumbani alikozaliwa mamake Rahab kulikuwa hakukaliki.
Babu na nyanya tayari walikwishaaga dunia na waliobaki walikuwa wajombaze
waliosheheni kila aina za tabia zilizowafanya jamaa zao kuwagura kwa hiari. (uk.36)

22. Ubakaji.
1. Rahab alipomwandikia Galacha barua alimfahamisha kwamba kila mtu Chekeleni
anatembea na roho yake mikononi kwa hofu ya kubakwa na wahasiriwa walipizao
kisasi. (uk.116)
2. Rahab alimfahamisha Galacha kuwa Mokaya alihusika katika ubakaji baada ya
kupotea kwa siku nyingi. Alimzuia mtoto wa miaka kumi njiani akitoka dukani saa
moja jioni na kumdhulumu kimapenzi mara kadha wa kadha. Mtoto hatimaye aliaga
dunia. (uk.141)
3. Hussein anakamatwa kwa sababu ya kumbaka msichana mdogo mwenye umri wa
miaka kumi na miwili. Kesi dhidi yake iliamuliwa na akasomewa kifungo chake cha
maisha. (uk.161)

23. Utundu.
1. Rahab alimfahamisha Galacha kwamba Mokaya aliamua kuwacha shule na
kutoroka nyumbani. (uk.127)

24. Mapenzi ya Kiholela.


1. Galacha anasema kuwa mjomba wake aliwasili Majimbo kuwatembelea na katika
harakati hizo, akawa mpenzi wa msichana mmoja hapo Majimbo. Mjomba huyo
aliaga dunia wakamzika kwa sababu aliambukizwa ugonjwa katika harakati za
kumtibu mgonjwa wake. (uk.130)
2. Galacha anasema kwamba alipokuwa katika chuo kikuu aliwaona akina dada
wakiipa anasa kipaumbele badala ya masomo. (uk.141)

25. Ukosefu wa Chakula


1. Watoto wa mitaani wanaojulikana kama chokoraa walishinda wakiyachokora
mabiwi ya takataka angalau kupata chakula kule mtaa wa mabanda. (uk.9)

26. Ukatili/Unyanyasaji.
1. Wafungwa wengine waliokuwa kwenye chumba kile cha jela ambamo Galacha
aliingizwa, walimkaribisha kwa masimango na ndweo punde tu aliposukumwa ndani.
Walimkaribisha kwa makonde na mateke. Kwa zamu, waliunyanyasa mwili wake
uliolegea. (uk.159)
2. Askari wawili walioenda kumchukua Galacha akiwa kwa jela ili aweze kutiwa
kitanzi, walimsakata ngumi na mateke kama yule ambaye kazi yake ilikwisha duniani
kabla ya kumwelekeza katika chumba chake cha mauti. (uk.169)
3. Rahab anamfahamisha Galacha kwamba mama Akoth yumo hospitalini baada ya
kuraruliwa kisu na mumewe. (uk.115)
4. Kawaka alichukua vitu vya mamake Galacha vyote na mamake Galacha
alipomwuliza, ndiye huyo chui kupanua mdomo wake tayari kummeza. (uk.102)
5. Amadi anakipokea kipigo cha Patashika siku moja alipotoka uvuvini kwa cheleo
akawa amechelewa kutekeleza majukumu yake mengine kama vile kukama na
kuwapeleka mifugo malishoni. (uk.93)
6. Patashika alimpiga Amadi na kumnyima chai. Wakati huo alikuwa amekomewa
mlango kama mahabusu. (uk.93)
7. Mkubwa wa wale wafungwa alikisukuma kichwa cha Galacha ndani ya ndoo yenye
mkojo huku akidai kwamba anamkaribisha “breakfast” ama kiamshakinywa kwa
lugha ya Kiswahili. (uk.159)

You might also like