You are on page 1of 2

HALMASHAULI YA (W) SENGEREMA

Balaza la aridhi kata ya chifunfu


26/09/2023
Yah: Shauri namba moja . Mgogorowa eneo kati ya ndugu kokino –
MTAHIGWA dhidi ya mzee wamtilana kokino wote wakazi wa luchanga
A. Wajumbe walio kuweko kusikiliza shauli hili
1. HELENA J. KIBUNGOSHO (KE)
2. JULIUS N. SUMUNI (ME)
3. LAURIAN M. GASPAL (KE)
4. SADIKI SANZU (ME)
5. IRINE P. MANENGERO (KE)
6. MAGRETH FULUGENCI (KE)
7. STEOFN JUSTINE (ME)
B. Maelezo ya mdai
Bwana kokino Mtahigwa
Dini R.c
Umri 50.
Maelezo ya mdai
Mimi kokino mtahigwa ni msimamizi wa mirathi ya
marehemu mzee kokino Nduri naambatanisha ruksa ya
kusimamia mirathi hiyo kutoka mahakama ya mwanzo kasenyi.
Ni kwamba kipindi cha uhai wa mzee kokino nduri
alibahatika kuwa na wanawake wawili., wa kwanza alikuwa
nyakwantazi lukonza na wa pili alikuwa kahabi msobozi –
aliishinao tangu akiwa kwenye mahame. Na ndipo ilipoingia
operation vijiji vya mwaka 1974 alihama na kuja kugomwa hapo
ambapo pana mgogoro kwa sau, hivyo alihama na familia yake
wote yam wake wawili na kuanza maisha mapya mnamo mwaka
1974 marehem kokino nduri alikuwa na familia ya watoto 18 mke
mkuu watoto 8 mke mdogo watoto 10 , hapo alienderea kuishi
kwa na familia yake vizuri.
Mnamo mwaka 1998 alimfukuza kijana wake mkubwa (mtahigwa
kokino) Baada ya kushindana kitabia na walio baki walienderea
kuishi hapo. Wasichana wao waliolewa wale walio kuwa wakubwa
na wale walio kuwa wadogo waliendelea kuishi hapo,
1982 marehemu kokino nduri aliugua na kufariki dunia., Baada
ya kufariku dunia eneo lote lililo kuwepo lilibaki chini ya watoto
wa marehemu. Pia baada ya kufariki watoto wa marehemu
waligawana mashamba ya pembeni, kila watoto walienderea
kumiliki mashamba yaliyo kuwa yanamilikiwa na mama zao , na
hata wakagawana eneo la mahame kwa kufuata mama zao hivyo
waligawana kati kwa kati

You might also like