You are on page 1of 118

A THREAD BY FORTUNATUS BUYOBE

MAJARIBIO MATATU YA KUIANGUSHA SERIKALI YA MWALIMU NYERERE

UTANGULIZI
Kwa Uelewa wa Wengi,Wanahesabu matukio yafuatato kama majaribio ya kuiangusha
serikali ya Mwalimu JULIUS KAMBARAGE NYERERE

i/Maasi ya kijeshi ya Mwaka 1964

ii/Uhaini uliowahusisha kina BIBI TITI,OSCAR KAMBONA na wenzake Mwaka 1969

iii/Tukio la uteji wa ndege ya Boeing 737 uliofanywa na vijana wa kitanzania wakishinikiza


Nyerere aachie madaraka mwaka 1982

iv/Uhainiwa mwaka 1983 Ulipangwa na PIUS MUTAKUBWA LUGANGIRA na wenzake

Nimeorodhesha Visa Vinne Na nitaanza kwa kusimulia kisa kimoja baada ya kingine katika
series hii ya masimulizi ninayoipa jina la FAILED ATTEMPTED COUPS

Tuanze na Kisa cha kwanza.

MUTINY-MAASI YA KIJESHI
Mutiny ni kitendo cha kikundi cha Wanajeshi kuasi na kupinga amri au uongozi wa juu wa
kijeshi. Pia hali hii hutokea kwenye Maswala ya Ubaharia ambapo officers wa chini huasi
maelekezo ya Uongozi wa melini.

Kuna siku ambazo historia rasmi ya Tanzania haipendi kuzikumbuka, lakini haitaweza kukaa
bila kuzikumbuka
Januari 20, 1964, siku kulipotokea maasi ya kijeshi katika Tanganyika, ni miongoni mwa siku
hizo. Hiyo ilikuwa ni wiki moja tu baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12.
Hata Mwalimu Nyerere alijua kuwa ni vigumu kusahau, ingawa inawezekana kwa kuificha
historia. Kwa huzuni Nyerere alikaririwa na jarida TIME (Jan. 31, 1964), chini ya makala
yake, The Rise of the Rifles, akisema: “Itachukua miezi, na hata miaka, kufuta katika bongo
za walimwengu kile walichosikia kuhusu matukio ya juma hili.” Hata hivyo imeshaanza
kufutika katika bongo za walimwengu.

Kwa maneno mengine tunaweza kusema haya yalikuwa ni Mapinduzi ya Tanganyika. Tofauti
kati ya Mapinduzi ya Zanzibar yale ya Tanganyika ni kwamba: Mapinduzi ya Zanzibar
yaliruhusiwa yafaulu, lakini Mapinduzi ya Tanganyika hayakuruhusiwa kufaulu.

January 20, 1964 kulitokea zahama mjini Dar es Salaam katika Kambi ya jeshi ya Colito (sasa
inajulikana kama Lugalo), ambalo lilisambaa hadi kambi nyingine nchini.

Baada ya tukio hilo, maswali mengi yaliulizwa. Ingawa tayari mengi yamejibiwa, majibu hayo
ni ya ‘kuzunguka mbuyu’. Je, yalikuwa ni mapinduzi ya serikali (kama yale ya Zanzibar)?
Yalikuwa ni maasi tu ya kijeshi? Ulikuwa ni mgomo tu wa wanajeshi waliotaka kuongezwa
mishahara?

Majibu yaliyotolewa na wale walioitwa—au waliojiita—wanasayansi wa siasa yalijaribu


kupunguza uzito wa maasi hayo kutoka katika mapinduzi ya serikali na kuyafanya yaonekana
kana kwamba yalikuwa ni mgomo tu wa kutaka kuongezwa mishahara na vyeo.

Tafsiri zao zilikuwa hivi: kama ingekuwa ni mapinduzi, ilikuwa ni lazima kwanza wanajeshi
walioasi wangeteka maeneo yote muhimu ya kama Bunge na Ikulu. Ilikuwa ni lazima
wawakamate mawaziri, jambo ambalo hawakufanya. Hawakuwa wamemtangaza kiongozi
wa nchi.

Ilidaiwa kuwa aliyekuwa afaidike na maasi hayo ni Waziri wa zamani wa Ulinzi na Mambo ya
Nje wa Tanganyika, Oscar Kambona ambaye alikuwa na uhusiano wa karibu sana na Kaasim
Hanga wa Zanzibar.

Tupate Historia kidogo kujua tulifikaje hapa?

Tanganyika ilirithi jeshi kutoka kwa wakoloni wa kiingereza baada ya Uhuru Dec 9 1961
likijulikana kama KING’S AFRICAN RIFLES(KAR) na baadae kuitwa TANGANYIKA RIFLES(TR)
Baada ya Uhuru,ili kukidhi matarajio ya watanganyika,zilitakiwa nafasi zote za juu za utawala
nchini,zikabidhiwe kwa wazarendo.Ulikuwa ni utamaduni uliojengeka kwa nchi zote
zilizopata uhuru kufanya hivyo.
Mwalimu Nyerere akiwa ni waziri mkuu wa serikali mpya,hakuchukua hatua hizo kwa
haraka.Hata aliyekuwa waziri wake wa mambo ya ndani GEORGE KAHAMA hakuchukua
hatua zozote kubadilisha uongozi wa Waingereza ndani ya Jeshi la polisi.

Yakaanza malumbano ndani ya kamati Kuu ya TANU kuwa mwalimu Nyerere alikuwa
anaikumbatia serikali ya kikoloni.
Ili kuhepuka malumbano hayo ambayo yangevunja mshikamano baina ya
wanachama,Mwalimu akaachia madaraka na kurudi kijijini kwake kukiimarisha chama kama
mwenyekiti wa TANU. RASHIDI KAWAWA akampokea kijiti katika nafasi ya Waziri mkuu na
OSCAR KAMBONA aliyekuwa waziri wa elimu,akachukua madaraka ya waziri wa mambo ya
ndani nafasi ambayo ilikuwa mwanzoni inashikiliwa na GEORGE KAHAMA.
Uongozi huu mpya ukabebeshwa mzigo wa kuleta hayo mabadiriko ya kuwatoa wazungu na
kuwaweka watanganyika katika madaraka serikalini.
Haraka sana,KAMBONA akamtimua kamishna wa polisi Mwingereza na kumteua ELANGWA
SHAIDI kuchukua nafasi hiyo. Kasi hii ilianza kuishtua jumuiya ya kimataifa.

Desemba 1962,ulifanyika uchaguzi mkuu na Mwalimu akachaguliwa kama rais wa kwanza


wa Tanganyika na January 1963 alipokuwa madarakani,alisitisha zoezi la kuwaondoa
wazungu madarakani na kuwapa madaraka hayo wazarendo(Africanisation)

Jambo hili liliwaudhi wengi hasa Wanajeshi wa TANGANYIKA RIFLES wazarendo na vyama
vya wafanyakazi.
Hali iliendelea namna hiyo hadi mwaka uliofuata ambapo January 12 1964 kulitokea
mapinduzi ya Zanzibar na Abeid Karume akakimbilia bara.
Kuanzia January 13 1964 Nyerere akawa busy na mgogoro wa Zanzibar ambapo alimshauri
Karume arudi Zanzibar kwani kukimbia kwake kutamfanya aonekane ni mwoga.

John Okelo aliyeongoza mapinduzi yale akamtangaza Karume kuwa rais asiye mtendaji huku
akimtaka ajitokeze popote alipo mafichoni aende akachukue madaraka yake. Binafsi Okello
akajitangaza kuwa Kiongozi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Jumatatu Jan 14 1964 OSCAR KAMBONA ambaye alikuwa ni waziri wa mambo ya nje na
Ulinzi,akiwa nchini Kenya alimpigia simu Mwalimu na kumwambia serikali za Kenya na
Uganda zimeitambua Seikali ya mapinduzi Zanzibar ja ni yeye tu (MWALIMU) amebaki
kuitambua serikali hiyo. Mwalimu akamkatalia kwa kusema bado hana uhakika kama
Karume yupo madarakani.
Jumanne,January 15 Mwaka 1964 Mwalimu akasafiri kwenda Nairobi ili kukutana na Waziri
mkuu wa Kenya JOMO KENYATTA kujadili kuhusu shirikisho la Afrika Mashariki na
kuzungumzia msimamo wake juu ya Zanzibar

Jumatano, Jan 16 Sultan aliyepinduliwa Zanzibar akawa ametia nanga Dar Es salaam baada
ya Kenya kukataa kumpokea. Mwalimu akampokea ili akamilishe mipango ya kuhamia
Uhamishoni Uingereza

Alhamisi Jan 17, MBWANA KARUME,ABDULAHAMAN BABU,na KHASSIM HANGA walikutana


na Mwalimu Nyerere Ikulu Dar es salaam wakiwa na Ombi mwalimu awaongezee msaada
wa askari 300 kisiwani Zanzibar kwani hali ya kisiasa ilikiwa bado ni tete kule.Ni Siku hihihihi
ambapo JOHN OKELO alitengua Uteuzi wa Karume Kama Raisi wa Zanzibar kwa hoja kuwa
hakushiriki lolote kwenye mapinduzi yale. Badala yake Okelo akajiteua yeye kuwa Rais
Mtendaji wa Zanzibar.

Siku mbili zilizofuata yaani ijumaa Tarehe 18 na Jumamosi Tarehe 19 zilikuwa za utulivu kwa
Mwalimu kwani hakuwa na fatiki yoyote. Katika kipindi hiki, askari wa FFU 300 waliwasili
Zanzibar wakitokea Tanganyika. Mwalimu hakujua kabisa kuwa alikuwa amejipunguzia Ulinzi
wake kwa Tukio ambalo lingefuatia tarehe 20 kuamkia tarehe 21.
Ni Tarehe 20 Ambapo Mwalimu Nyerere alikuwa Ikulu kwenye Mazungumzo na JOHN
OKELO ambaye ndiye aliyeongoza mapinduzi ya Zanziba(Mpaka leo haijasemwa kokote jinsi
Okelo alivyoondoka baada ya jaribio hili)
Maasi haya yalitokea wiki moja tu baada ya mapinduzi ya umwagaji damu ya Zanzibar,
Januari 12, 1964; na usiku huo wa maasi hayo, Kiongozi wa Mapinduzi ya Zanzibar “Field
Marshal” John Gidion Okello, alikuwa na mazungumzo na Mwalimu Nyerere Ikulu, Dar es
Salaam, katika hali ya kubadilishana mawazo juu ya hali ya Zanzibar ambapo Mwalimu,
alimshauri Okello afanye kazi kwa imani na Rais Abeid Amani Karume

Wakati jeshi hilo likiasi; siku hiyo hiyo, na saa hiyo hiyo, majeshi ya Kenya na Uganda nayo
yaliasi kwa staili hiyo hiyo. Maasi yote ya nchi tatu hizo yalizimwa na majeshi ya Uingereza
siku moja na wakati huo huo.

Hali Ilikuwaje Usiku Huo wa Tarehe 20 Kwa Upande wa Kambi ya COLITO?


saa 7:50 alfajiri, Januari 21, Mkuu wa Kikosi cha kwanza cha TR, Brigedia Patrick Sholto
Douglas, aliamshwa nyumbani kwake na sauti ya baruji (buggle) na ving’ora, karibu na kambi
ya Jeshi ya Colito (sasa Lugalo Barracks).

Alipotoka nje, aliona askari wake 12 wakikamatwa na wenzao wenye silaha na kutiwa
mahabusu. Ndipo alipofahamu kwamba, nusu ya askari 800 wa Kikosi hicho walikuwa
wameasi. Aliweza kutoroka yeye na familia yake hadi katikati ya jiji, akaiacha familia kwa
Balozi wa Australia, kisha akakakimbilia kwa Afisa mwenzake, eneo la Oyster Bay.

Akiwa huko, akampigia simu Oscar Kambona, akamwomba, naye akakubali, kupeleka ndege
tatu Kikosi cha Pili huko Tabora, kuleta askari waliokuwa bado waaminifu kwa Serikali.
Douglas na Kambona hawakujua kwamba, tayari waasi walikuwa wamefunga barabara
iendayo uwanja wa ndege; kwa hiyo, marubani walirudi mbio; naye Douglas akakimbilia
kwenye Ubalozi wa Uingereza, akajificha kwa siku tano hadi Januari 25.
Douglas alikuwa amempigia simu Mkuu wa Polisi, ambaye alikwenda moja kwa moja
nyumbani kwa Makamu wa Rais, Rashidi Kawawa, eneo la Ikulu na kumwamsha, kisha hao
wawili kwa pamoja, wakaenda kumpa habari Mwalimu.

Mwalimu alipokeaje taarifa hizo?

Mwalimu alipoelezwa juu ya maasi hayo, alilipuka kwa hasira na ghadhabu kubwa papo
hapo; akataka kwenda yeye mwenyewe kukutana na Waasi hao ili wamweleze sababu za
kitendo hicho cha aibu. Mama Maria Nyerere, kwa machozi na kwa kupiga magoti, alimsihi
mumewe asitoke kwenda kukutana na watu wenye silaha, lakini hakufanikiwa kumgeuza
nia.
Ndipo watu wa Usalama walipojenga hoja nzito kumzuia, na hoja hiyo ikamwingia; akakubali
kuteremka dari ya chini, kisha yeye, Kawawa na Mama Maria Nyerere, wakatorokea mahali
kusikojulikana. Wakati huo, tayari waasi walikuwa kwenye lango kuu la Ikulu wakimtafuta.
Bado ni kitendawili kuhusu mahali Mwalimu na wenzake walikokuwa wamejificha. Wapo
wanaodai alijificha Misheni au Kanisani; wapo pia wanaosema alijificha kwenye nyumba ya
Balozi mmojawapo Jijini.
Wengine wanasema alijificha kwenye kibanda kidogo sana (Kigamboni?) karibu na Pwani; na
baadhi wanadai alikwenda Arusha au Nairobi. Lakini wapo pia wanaosema alijificha kwenye
meli. Wala haielezwi kama John Okello aliondokaje Ikulu usiku huo baada ya mazungumzo
au kama maasi yalimkuta Ikulu usiku huo.

Upande wa Jeshini hali iliendeleaje?


Kufikia saa 9:00 alfajiri, waasi walikuwa wamekamata kambi ya Colito, kisha wakajigawa
vikundi vitatu na kuingia mjini. Kikundi kimoja kilibakia kulinda kambi ya Colito, kikundi cha
pili, kikiongozwa na Sajini Francis Higo Ilogi, ndicho kilichokwenda Ikulu kumtafuta Rais;
wakati kikundi cha tatu kililinda barabara kuu zote mjini.
Kikundi cha Sajini Ilogi kilipofika Ikulu, kilishauriwa na mmoja wa Maafisa Usalama wa Taifa,
wamwone kwanza Waziri wao wa Ulinzi, Oscar Kambona; nao wakakubali kufanya hivyo.
Wakaenda hadi kwa Kambona na kumleta Ikulu, na kumweleza kwamba walikuwa
wamewakamata na kuwaweka mahabusu maafisa wake (Wanajeshi) 16; na kwamba, kama
(Kambona) alikuwa tayari kusikiliza malalamiko yao, afuatane nao hadi Colito. Kambona
alikubali.
Ni ujasiri gani huo; ni kujiamini vipi kwa Kambona, kwamba bila ulinzi wala woga, tena
akiwa amepanda gari la Mkuu wa Polisi tu, aliweza kukubali kuandamana na askari wenye
silaha, na hasira kali, kwenda Colito Barracks?

Ukimwondoa Nyerere na Kawawa, ambao walikuwa na kila sababu ya kujificha, kulikuwa na


Waziri wa Mambo ya Ndani, Job Malecela Lusinde; kwa nini Kambona hakumshirikisha,
kama aliona mambo yalikuwa salama kiasi hicho? Hapo ndipo baadhi ya watu wanakwenda
mbali zaidi kusema kwamba, huenda Kambona alihusika na maasi hayo.
Huko Colito Barracks, walimweka Kambona “kiti moto”, wakimtaka aamue papo hapo,
pamoja na mambo mengine, kuondolewa mara moja kwa Maafisa wa Kiingereza Jeshini, na
nafasi zao zishikwe na Wazalendo. Walitaka pia mishahara iongezwe, kutoka 105/= hadi
260/= kwa mwezi.
Bila kuonyesha kwamba ameyakubali au kuyakataa madai yao, Kambona aliomba wateue
wawakilishi wachache ili wafuatane naye hadi Ikulu kwa mashauriano na Mwalimu Nyerere.
Ndipo Kiongozi wa waasi, Francis Higo Ilogi, alipokataa na kusema, “Tunataka kila kitu leo
hii”, Yowe zikasikika, “Apigwe risasi, apigwe” (Kambona) huyo!”.
Pengine kwa kuingiwa na hofu, kwamba lolote lingeweza kumtokea, Kambona akauliza:
“Mnataka nani awaongoze?” Lilitajwa jina la Alex Nyirenda; lakini likakataliwa kwamba
alikuwa na majivuno. Akatajwa Luteni Elisha Kavana, akapitishwa kwa kauli moja na
kuvishwa kofia ya Brigedia Douglas.
Kambona alikataa kutia sahihi makubaliano, kwa madai kwamba mpaka ashauriane kwanza
na Rais. Ndipo kikundi chote cha Ilogi kikafuatana naye kwenda Ikulu.
Walipofika huko, askari hao walijipanga barabara yote iingiayo Ikulu, lakini Sgt Ilogi
aliwakataza wasiingie ndani, wakamruhusu Kambona pekee. Wakati huo Nyerere alikuwa
ametoroka zaidi ya saa mbili zilizopita.
Baada ya mashauriano kwa muda na wasaidizi wa Rais pamoja na mama mzazi wa Mwalimu,
Kambona alitoka nje na kuwatangazia waasi hao kuwa Rais ameyakubali madai yao. Lakini
askari hao wakapiga kelele “mwongo huyo! Rais hayumo ndani; mpige risasi, mwongo
huyo!
Hata hivyo, waliondoka wameridhika, wakarejea kambini siku hiyo. Hima, Kambona
aliwaondoa maafisa wa Kiingereza na kuwasafirisha kwao kupitia Nairobi.
Akiwatangazia wananchi kupitia Redio “Tanganyika Broadcasting Corporation” (TCB),
Kambona alisema: “Huyu ni Waziri wenu wa Mambo ya Nje na Ulinzi; Serikali ingalipo…
Kumekuwa na kutoelewana baina ya askari Waafrika na maafisa wa Kiingereza katika
Jeshi. Baada ya kuingilia kati shauri hili, sasa askari wamerudi kambini”. Hata hivyo,
hakusema lolote juu ya Nyerere, wala mahali alikokuwa.
Je, ni kweli mambo yalikuwa yamekwisha? Kwa nini Nyerere hakutokea hadi siku mbili
baada ya askari kurejea kambini? Kwa nini askari hao waliasi tena siku nne baadaye na
Nyerere kulazimika kuita majeshi ya Uingereza kuja kuzima maasi?

Siku ya tatu baada ya maasi ya kikosi cha kwanza, Jumatano, Januari 23 asubuhi, ghafla
Nyerere akatokea hadharani amepanda gari la wazi akiwa na Mama Nyerere na Waziri wa
Mambo ya Ndani, Job Lusinde, akatembelea kila sehemu ya mji iliyoathiriwa na maasi.
Alhamis ya Januari 24, ilikuwa shwari; lakini Ijumaa, Januari 25, mazungumzo kati ya Serikali
na waasi yalionekana kuanza kuvunjika, wakaasi tena. Ni nani alikuwa kiongozi wa maasi
haya awamu ya pili? Sajini Higo Ilogi tena?

Tofauti na maasi ya Januari 21, ambayo hayakushirikisha wanasiasa, wala kugubikwa na


hisia au shabaha ya kisiasa, maasi haya mapya yaliingiliwa na wapiga filimbi wa kisiasa.
Taarifa za kiusalama zilionyesha kwamba, viongozi wa vyama vya wafanyakazi, kupitia
Chama Kikuu (Shirikisho) cha Wafanyakazi (TFL), walikuwa wakikutana kwa siri na askari
walioasi kwenye kambi ya Colito; na kwamba vyama hivyo vilikuwa vimeandaa mgomo nchi
nzima mwishoni mwa wiki kuungana na askari hao.
Maasi haya ya pili yaliweza kuambukiza majeshi ya Kenya na Uganda, nayo yakaasi vivyo
hivyo, siku hiyo hiyo, wakati huo huo, na kwa mtindo huo huo. Marais Kenyatta na Obote
walizisoma alama za nyakati ukutani; nao wakajiandaa kuita Jeshi la Uingereza kuzima
maasi. Nyerere hakutaka; hakuamini kwamba Jeshi lake mwenyewe lingeweza kumhujumu,
yeye na Serikali yake.
Alianza kuhisi hatari mbele pale maofisa usalama walipomuonesha orodha ya mawaziri
wanaotarajiwa iwapo Serikali yake ingepinduliwa, iliyoandaliwa na waasi. Mmoja wa watu
wake wa karibu alikwenda mbali zaidi kumwambia kwamba, alikuwa ameombwa na waasi
akubali kuwa Makamu wa Rais baada ya Mapinduzi. Mwalimu akalowa; akayaamini maneno
hayo, kwamba Serikali yake ilikuwa hatarini.
Ndipo, yapata saa 11:30 jioni siku hiyo, Mwalimu akamwita Ikulu Naibu Balozi wa Uingereza,
Bwana F. Stephen Mills; akamwomba msaada wa Kijeshi wa nchi yake naye Mills, bila
kuchelewa, akapeleka taarifa London na kujibiwa kwamba maombi ya Nyerere yalikuwa
yamekubaliwa bila masharti yoyote.
Naye Oscar Kambona akaenda mbio kwenye Ubalozi wa Uingereza, kumtafuta Brigedia
Douglas ambaye alikuwa amejificha humo kwa wiki nzima, kumwomba msaada wa kuratibu
mipango. Usiku wa siku hiyo, Douglas na ofisa mwingine, walinyatia hadi kwenye manowari
Centaur iliyokuwa imefichwa Pwani.
Jumamosi, Januari 26; saa 12:20 asubuhi, helikopta sita kutoka manowari Centaur zilichukua
askari 60 (akiwamo Brigedia Douglas) hadi eneo karibu na kambi ya Colito. Dakika kumi
baadaye, saa 12:30, manowari hiyo, na meli nyingine ya vita, Cambrian, iliyokuwa ikisubiri
Pwani; zilianza mashambulizi kwa kupiga mizinga kuwatisha waasi.
Kutoka umbali wa mita 20 hivi, na kwa ujasiri mkubwa, Douglas akatangaza kwa kipaza sauti,
kwamba alikuwa ameshika madaraka yake tena; akatoa amri askari wote watoke nje
kambini “mikono juu” na kukaa chini barabarani.
Baada ya dakika 10 bila kuona kitu, Brigedia Douglas akaanza kuhesabu, “moja, mbili…..
kumi”, askari wa Kiingereza wakafyatua roketi hadi kambini. Waasi wakaanza kujisalimisha.
Dakika 10 zingine zilizofuata askari 150 walijisalimisha, na wengine 150 baada ya saa moja.
Kufikia saa 1:30 asubuhi, wote walikuwa wamesalimu amri; maasi yakawa yamezimwa
katika zoezi ambalo askari walioasi, watano waliuawa na wengine watano kujeruhiwa.
Hakuna askari wa Kiingereza kati ya 60 walioongoza mapambano, aliyedhurika. Na kwa juma
lote la maasi, raia wasiopungua 17 waliuawa.

Wakati wanajeshi wa Jeshi la Uingereza wakiwadhibiti askari waasi wa Tanganyika, huko


Uganda na Kenya nako, Jeshi lilikuwa linachukua hatua kama hiyo, muda, saa hiyo hiyo na
kwa staili hiyo hiyo kwa askari walioasi Jinja (Uganda), na katika kikosi cha 11 cha Bark-Lanet
(Kenya).

Kwa Kambi ya Tabora hali ilikuwaje?

Siku hiyo ilipokelewa taarifa kwamba, Kikosi cha Pili cha Jeshi kilichokuwa Tabora nacho
kilikuwa kimeasi, baada ya kupata habari kwamba wenzao wa Collito walikuwa wameasi.
Inawezekana, ama walikuwa hawajapata taarifa kwamba wenzao wa kambi ya Colito
walikuwa wamerejea kambini; au walifahamu, lakini wakataka nao watekelezewe mambo
kadhaa kwenye Kikosi chao.

Wakati Kikosi cha Tabora kikiendelea na maasi, ilipokelewa hapo Tabora, simu ya maandishi
(telegraph) kutoka kwa Kambona, kwamba alikuwa amemteua Kapteni Mirisho Sam Hagai
Sarakikya, kuwa Mkuu wa Kikosi cha Tabora. Wakati huo Sarakikya na maafisa wengine
walikuwa wamekamatwa na kuwekwa mahabusu na askari walioasi hapo Tabora.
Sarakikya akatolewa mahabusu, akaomba simu hiyo isomwe kwa sauti; kisha akatoa amri
wasimame “Mguu sawa”, wafungue beneti na kutoa risasi. Nao wakamtii. Usiku huo,
Sarakikya alifanya mipango ya kuwasafirisha maafisa wa Kiingereza kutoka Tabora kwenda
Dar es Salaam na hatimaye makwao.
Tukio la Januari 21, na lile la Tabora pamoja na hali ya hatari ilivyokuwa huko Kenya, Uganda
na Zanzibar, lilifanya Serikali ya Uingereza ichukue tahadhari ya ziada kwa kupeleka askari
2,000 zaidi ukanda wa Afrika Mashariki.

Kwa hiyo, manowari iliyoitwa Rhy, ikawa imetia nanga hima Pwani ya Dar es Salaam, na
nyingine Centaur; iliyobeba ndege, iliwasili na askari 600.

Haielezwi ni jinsi gani Sajini Higo Ilogi aliweza kuponyoka, akaonekana mjini asubuhi hiyo
kwenye jumba la Simu za Nje za Kimataifa (Extelcoms), akituma simu ya mandishi kwa
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) U Thant, kuomba msaada. Simu hiyo ilisomeka hivi:
“Majeshi ya Tanganyika yametekwa na askari wasiojulikana saidia haraka kuleta Majeshi
ya Umoja wa Mataifa LUTENI KANALI ILOGI, MKUU WA JESHI”.

Turejee kwenye swali letu la msingi: Nani alichochea maasi ya jeshi letu mwaka 1964? Oscar
Kambona? John Okello?
Kambona alikuwa Waziri mwenye dhamana ya ulinzi wakati huo, ambapo Jeshi lilikuwa chini
ya wizara yake. Kwa sababu hii, kushiriki kwake katika kutuliza maasi ya awamu ya kwanza,
hakuwezi kuchukuliwa kwamba alikuwa na hisa au kwamba alijua mpango huo wa maasi
hayo.
Ni ujasiri wake tu uliomtuma kukabiliana na hali hiyo. Kama kweli angekuwa na nia mbaya
kwa Serikali; na kwa kuzingatia pia jinsi alivyodhibiti hali hadi askari wakamkubali,
angeshindwaje kupindua nchi ambayo ilikuwa mikononi mwa Jeshi kwa siku mbili mfululizo
kama alikuwa na nia hiyo?
Je, ni Field Marshal John Okello? Hapa tena jibu ni HAPANA. Yeye hakuwa na muda huo, kwa
sababu kwa kipindi chote tangu Mapinduzi ya Zanzibar, alikuwa katika hati hati za kulinda na
kuimarisha utawala wake visiwani kutokana na tishio la kuenguliwa na wahasimu wake
ambao alidai hawakushiriki katika Mapinduzi. Okello aliongoza Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar kwa miezi miwili mfulilizo kabla ya kuenguliwa na Karume kwa kushirikiana na
Mwalimu Nyerere.

Wala haishangazi kwamba, maasi ya askari hawa yaliweza kuambukizwa kwa wenzao wa
Kenya na Uganda, ikizingatiwa kuwa majeshi ya nchi hizi tatu yamezaliwa na Jeshi la
Wakoloni wa Kiingereza waliotawala nchi hizo. Kwa hiyo, kwa kipindi hicho, na kwa
mazingira ya kazi ya wakati huo, malalamiko yao yalifanana kuwafanya wadai haki zao kwa
njia na kwa mtindo unaofanana.

Nakubaliana na maoni ya Balozi Abbas Kleist Sykes (akinukuliwa mahali fulani mwaka 2001),
kwamba, “Maasi ya Jeshi la Tanganyika Rifles (TR) mwaka 1964, yalitokana kwa sehemu
kubwa na kuchelewa kuwaondoa makamanda wa kizungu na kuwapandisha vyeo waafrika”,
kama ilivyofanyika kwa Jeshi la Polisi na watumishi wengine serikalini. Na ndivyo ilivyokuwa
kwa maasi ya Kenya na Uganda.
Wala haishangazi kwamba, viongozi wa vyama vya wafanyakazi waliungana na waasi awamu
hii ya pili kutaka kuiangusha Serikali, kutokana na ukweli kwamba, tangu Mwalimu
alipositisha zoezi la “Africanisation” Januari 1963, wao walikwishaapa mapema kutolala
usingizi “mpaka kieleweke”.
Kutokana na maasi hayo, Mwalimu alikifuta Kikosi chote cha Kwanza (Colito Barracks) na
kuwafukuza kazi askari 100 wa kikosi cha pili, Tabora. Alifukuza pia asilimia 10 ya askari
polisi 5,000 waliokuwapo, kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao wa kudhibiti maasi.

Watu zaidi ya 400 walikamatwa na kuhojiwa, wakiwamo viongozi wa vyama vya


wafanyakazi; na wengine 500 walitiwa nguvuni chini ya Sheria ya kuzuia hali ya hatari, lakini
wengi waliachiwa.
Nalo lililokuwa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TFL) lilifutwa, badala yake
kikaundwa Chama cha National Union of Tanganyika Workers (NUTA) kama Jumuiya ya
Chama tawala – TANU. Mwalimu alimteua Mirisho Sam Hagai Sarakikya kuwa Mkuu mpya
wa Jeshi na kumpandisha cheo kuwa Brigedia.
Mwanzoni mwa Aprili 1964, Majeshi ya Uingereza yaliondoka na nafasi yake kuchukuliwa na
Kikosi cha Tatu cha Jeshi la Nigeria, chini ya Luteni Kanali James Pam. Sajini Francis Higo Ilogi
alipatikana na hatia ya uasi wa Jeshi na kufungwa miaka 15, ambapo washirika wake wakuu
13 wakafungwa kifungo kati ya miaka mitano hadi 10.
Waswahili walisema, “Kila ovu lina baraka zake”. Mwalimu aliongeza kima cha chini cha
mishahara kwa wanajeshi kutoka shilingi 105 hadi 240/= kwa mwezi. Lakini la muhimu
kuliko yote ni kwamba, maasi hayo yalitusaidia kujihoji na kufahamu aina ya Jeshi
lililotakiwa kwa nchi kama yetu. Yalituwezesha kujenga Jeshi upya, tukapata “Jeshi la Ulinzi
la Wananchi wa Tanzania” (JWT), kwa maana halisi ya Jeshi la Wananchi na kwa ajili ya
Wananch

Hata wakati Mapinduzi ya Zanzibar yanafanyika, Hanga aliondoka haraka kwenda Dar es
Salaam kuzungumza na Kambona kuhusu matukio ya Zanzibar. Hadi leo mazungumzo hayo
yamekuwa siri.

Baada ya Mapinduzi Hanga alikataa kutoa sababu zozote za yeye kwenda kuonana na
Kambona na hakutaka kuzungumzia jambo walilojadiliana. Alichosema, alipohojiwa na
mwandishi wa Kiingereza, Keith Kyle, kwa mujibu wa gazeti The Spectator, Februari 14,
1964, “...Nilikuwa kazini.”

Kambona walikutana tena na Kassim Hanga siku moja kabla ya maasi ya kijeshi yaliyotokea
mjini Dar es Salaam usiku wa January 20, 1964 ambayo yalitokea juma moja tu baada ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Inawezekana Mwalimu Julius Nyerere alijua jambo fulani kuhusu mapendekezo ya Kambona
kumsaidia Kassim Hanga, lakini hakujua jambo lolote kuhusu maasi ya kijeshi yaliyotokea
Dar es Salaam na kumfanya yeye akimbilie mafichoni Kigamboni.

Kambona alijua kuhusu mpango wa maasi ya kijeshi na, kwa mujibu wa Anthony Clayton
katika kitabu chake, The Zanzibar Revolution, “...Kambona alitazamia kufaidika kisiasa
kutokana na machafuko ambayo yangetokea.”

Haikuelezwa ni namna gani angefaidika. Lakini wasiwasi wa baadhi tu ya watu waliofuatilia


mambo hayo wanadai kuwa Mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa yamepangwa kufanyika wakati
mmoja na Maasi ya Dar es Salaam yaliyoanzia katika Kambi ya Colito (Lugalo).

Kwa maana nyingine kuna watu waliokuwa wamepanga kufanya mapinduzi huko Zanzibar
usiku wa Januari 20, siku ambayo kulitokea machafuko katika mji wa Dar es Salaam, lakini
John Okello akawazidi ‘kete’.

Kwamba Mapinduzi ya Zanzibar yalipangwa kufanywa na Kassim Hanga na watu wake huko
Zanzibar usiku wa Jumamosi ya Januari 18 kuamkia Jumapili ya Januari 19 na usiku huo huo
Kambona, au watu waliohusiana naye, wangefanya Mapinduzi ya Dar es Salaam ni jambo
lililozua gumzo wakati huo.

Kama yote hayo ni ya kweli, Mapinduzi ya Unguja na yale ya Dar es Salaam yalipangwa
kufanywa siku moja—usiku wa Januari 18—19, 1964. Mipango hiyo ilikuwa imeandaliwa
kwa muda mrefu.

Hata mijadala fulani fulani, kama ile ya kuwajadili Wacuba walioonekana Dar es Salaam na
Unguja katika kipindi hicho—ilifanyika Bagamoyo na maeneo mengine ambayo
hayakujulikana haraka.

Kwa kawaida Kambona alijua au alikuwa amearifiwa mapema kuhusu maasi ya Dar es
Salaam katika vitengo vya usalama vya Tanganyika na maofisa wa Kiingereza ambao bado
walikuwa wakiitumikia Serikali ya Tanganyika, lakini hakuchukua hatua yoyote kuikabili hali
hiyo hadi pale ilipotokea. Mmoja wa maofisa hao ni Luteni Kanali Rowland Mans.

Ilidaiwa kuwa mara kwa mara, Kambona, akiwa Waziri wa Ulinzi, alikuwa akiwatembelea
maofisa wa ngazi za chini katika kambi ya Colito, na mara nyingine bila kuonana na viongozi
wakubwa wa kambi hiyo.

Pia, kwa sababu zisizojulikana dhahiri lakini ambazo inawezekana ni njia ya kumsaidia
Kassim Hanga, Kambona alitenga silaha na zana nyingine za vita zilizotoka Algeria na
kuwasili Dar es Salaam Jumatano ya Januari 3, 1964 na kupakuliwa chini ya ulinzi maalum.
Silaha hizo ziliwasili siku tisa kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar na wiki mbili kabla ya maasi ya
Dar es Salaam.
Silaha hizi, baada ya maasi yaliyotokea Dar es Salaam, inadaiwa—na hii inadaiwa tu—
zilichukuliwa na kutoswa baharini na Jeshi la Maji la Uingereza lililoombwa na Serikali ya
Tanganyika Jumamosi ya Januari 25, 1964, kukomesha maasi ya jeshi Dar es Salaam.

Hata hivyo nyingi za silaha hizo zilitumiwa wakati wa Vita Kuu II Kaskazini mwa Afrika.
Zilitumiwa na Waingereza, Wajerumani, na Waitalino na zingekuwa vigumu kutumiwa katika
miaka ya 1960 kwa kuwa hazikuwa na vipuri.

Inasemekana kwamba silaha hizo ziliagizwa na Serikali ya Tanganyika kwa ajili ya chama cha
Frelimo cha Msumbiji. Zilipowasili Dar es Salaam, pamoja na kwamba maofisa wakubwa wa
Jeshi la Tanganyika walikuwa ni Waingereza, silaha hizo zilipakuliwa na wanajeshi Waafrika
tu.

Inasemwa pia kwamba silaha hizo hazikuhifadhiwa kama ilivyopaswa, kwa hiyo zikawafanya
Waingereza washtuke. Walipozichunguza sana wakagundua kuwa zana nyingine zilitiwa
alama ya msalaba mweusi, wakachukulia kwamba hizo zilizotiwa alama zilikusudiwa
kupelekwa Zanzibar kumsaidia Kassim Hanga kulingana na tetesi walizokuwa wamezipata
hapo awali. Lakini silaha hizo hazikuwahi kufika Zanzibar. Je, zilikusudiwa kutumika wakati
wa maasi yaliyotokea Dar es Salaam?

Kwa mujibu wa utafiti wa Ndugu Nestor Luanda katika kitabu Tanganyika Mutiny, Kambona
alianza kufika mara kwa mara katika Makao Makuu ya Jeshi mwishoni mwa 1963 na
aliwaambia maofisa wa kijeshi wa Kiingereza kwamba alitaka wawe wameondoka nchini
ifikapo mwishoni mwa 1964.

Kambona alitaka maofisa wengi wa Kitanganyika wapewe vyeo haraka, jambo ambalo
Waingereza walidai haliwezi kutendeka kwa ghafla kama alivyotaka. Kuanzia hapo maofisa
hao wakaanza kuwa na wasiwasi kuwa chochote kinaweza kutokea.

Ingawa uhusiano wa maofisa wa kijeshi wa Uingereza na Waziri Kambona ulianza kupungua,


huo si ushahidi wa kutosha kueleza kuwa Kambona alihusika kwa njia ya moja kwa moja au
isiyo ya moja kwa moja.

Hata hivyo, usiku ule wa maasi maofisa wengi wa Kiingereza walikamatwa na ‘kutiwa ndani’
katika Kambi ya Colito’ ambako kwa wakati huo umeme tayari ulikuwa umekatwa.

Kikosi cha kiasi cha wanajeshi 25 waliondoka kambini hapo kwenda Ikulu kumfuata Rais
Julius Nyerere kikiongozwa na mwanajeshi machachari, Sajenti Francis Hingo Ilogi, mzaliwa
wa Bukene, Tabora.

Wakati huo huo, Mkuu wa Tawi Maalum, Emilio Mzena, baada ya kuambiwa yaliyotokea na
kwamba wanajeshi walio na silaha wameelekea Ikulu, aliwaarifu watu wake waliokuwa Ikulu
na kuwaambia wamtoroshe Rais.
Mzena aliambiwa kuhusu maasi hayo majira ya saa 8:00. Nusu saa baadaye, saa 8:30, baada
ya kuamshwa na walinzi wao, Rais Nyerere, akiongozana na Makamu wake, Rashidi
Kawawa, waliondoka Ikulu kupitia mlango wa nyuma. Walipishana na wanajeshi hao kwa
sekunde chache tu.

Baadaye wanajeshi hao walipelekwa kwa Oscar Kambona, wakamchukua kwenda naye
kambini kwao, Colito. Wakati huo ghasia na uporaji wa mali za raia tayari ulikuwa umetanda
katika mitaa ya mji wa Dar es Salaam.

Wakati hayo yakitokea, tayari walikuwa wameanza kupeana vyeo huko huko kambini.
Wengine walipokea vyeo hivyo lakini wengine hawakuharakisha kupokea. Kwa mfano, Ilogi
ambaye alikuwa na cheo cha Sajini alijikuta katika cheo cha Luteni Kanali na wengine
walimtaka mtu kama Kapteni Alex Nyirenda kuwa Brigedia.

Maasi hayo yalisababisha ghasia nyingi mitaani, hususan Mtaa wa Msimbazi maeneo ya
Kariakoo. Maeneo mengi ya katikati ya mji risasi zilirindima. Mwarabu mmoja eneo la
Magomeni, kwa kuona duka lake linavamiwa, alimpiga risasi mwanajeshi mmoja
aliyejulikana kwa jina la Kassim.

Koplo Nashon Mwita, ambaye alishuhudia mauaji hayo, alirudi kambini kujizatiti.
Akiongozana na askari mwingine, Luteni Mwakipesile, pamoja na wanajeshi wengine,
walifika Magomeni na kummiminia risasi Mwarabu huyo.

Kana kwamba haikutosha, waliiteketeza nyumba yake kwa moto. Katika nyumba hiyo,
inasemekana, Mwarabu huyo aliteketea na familia yake ya watu 15.

Maasi hayo yalianza kusambaa haraka. Siku moja baadaye, Jumatatu ya Januari 20, yalifika
hadi kambi ya jeshi ya Tabora ambako wanajeshi wengi, kama Mrisho Kapteni Sarakikya,
Luteni David Msuguri na Luteni Abdallah Twalipo walikuwa wamepandishwa vyeo.

Jumanne ya Januari 21, maasi hayo yakafika Nachingwea—kambi ambayo ndiyo kwanza tu
ilikuwa imeanzishwa, ikiongozwa na Meja Temple Morris.

Jumamosi ya Januari 25, 1964, baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya, Mwalimu Nyerere
aliomba msaada kutoka Serikali ya Uingereza kunyamazisha maasi ya kijeshi yaliyokuwa
yanazidi kusambaa katika Tanganyika. Hatimaye makomandoo wa Uingereza waliwasili kwa
helikopta na kuwanyang’anya silaha waasi. Jioni ya siku hiyo hiyo maasi ya Tabora nayo
yakazimwa.

Maasi hayo, hasa katika kambi ya Colito, yalizimwa baada ya makomandoo hao wa
Uingereza kutua na kuanza kulipua lango la mbele la kambi hiyo. Mara moja askari walioasi
walijisalimisha.

Kikosi cha Uingereza kiliongozwa na Brigedia Patrick Sholto Douglas. Waasi watatu waliuawa
katika operesheni hiyo. 20 walijeruhiwa na wengine 400 walikamatwa, kwa mujibu wa
‘TIME’ (Jan. 31, 1964). Wengine walitoroka.

Kwa njia hiyo Rais Nyerere alirejea madarakani, lakini historia ya Tanganyika ikabadilika
moja kwa moja.

Jioni ya Januari 25, baada ya kutembelea mitaa ya Dar es Salaam kujionea uharibufu
uliofanywa na wanajeshi walioasi, Mwalimu alisikika moja kwa moja Tanganyika
Broadcasting Corporation (TBC) akisema:

“Jana nililazimika kuomba msaada wa Mwingereza. Kwa bahati akakubali. Asubuhi hii kikosi
cha kwanza kikawasili …yote sasa ni shwari. Nasikia maneno ya wajinga kwamba eti
Waingereza wamerudi Tanganyika.”

Zaidi ya hilo aliwachekesha waliokuwa wakimsikiliza. Alisema: “…Askari wametuvua nguo.


Tuko uchi. Jamaa wanasema tuazime nguo, nasema nguo ya kuazima bwana! …Unaweza
kwenda kuazima ukapata baibui.”

Wiki tatu baada ya maasi (Feb. 16, 1964), aliitisha mkutano wa hadhara Viwanja vya
Jangwani na kuwaambia Watanganyika hivi: “…(Wanajeshi walioasi) Walidanganywa.
Wendawazimu walikuwa wawili, watatu. Wale wengine waliswagwa tu. Wakivutishwa
bangi, wakaja mjini kutenda maovu. Tukaenda kwa Mwingereza. Bwana Mwingereza
tusaidie utuondolee balaa hili.”

Baada ya maasi hayo, Mwalimu Nyerere alianza kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa
hakuna kosa linalorudiwa. Hatua ya kwanza, kwa mujibu wa jarida TIME (Feb. 07, 1964)
alianza kukamata wote waliohusika, kisha akapiga marufuku gazeti Nation la Kenya
linalomilikiwa na Aga Khan kutouzwa katika Tanganyika.

Kwanini marufuku hayo? TIME linasema hivi: “Gazeti hilo (Nation) lilitoa taarifa sahihi lakini
yenye raghba kuhusu kuangushwa kwa serikali yake. Kupunguza uwezekano wa mfarakano
wa mawazo, amewabadilisha makamanda wa Kiingereza akaweka wa Kiafrika. Wakati huo
huo, ameteua kamati ya kutafakari mabadiliko ya kikatiba ambayo yataifanya Tanganyika
kuwa nchi ya kidemokrasia ya ‘chama kimoja kisheria na kiuhakika.”

“…Uso wake ulikuwa na simanzi. Hakuna hata Mtanganyika mmoja aliyeuawa kwa miaka
yote 17 ya kupigania Uhuru wa Tanganyika. Lakini sasa baada ya uhuru Watangayika
wameuawa,” likasema TIME (Jan. 31, 1964)

Jumanne ya Aprili 21, Mwalimu Nyerere alimwapisha Sir Ralph Wildham ndani ya Ikulu ya
Dar es Salaam kuwa Jaji Mkuu wa Tanganyika, na kumwambia awashughulikie kikamilifu
wanajeshi waliofanya jaribio la kuipindua serikali yake hapo Januari 19, 1964. Ndipo Sir
Wildham akatangaza rasmi kuwa wanajeshi wa Kambi ya Colito waliotaka kuiangusha
serikali watafikishwa mahakamani siku ya Jumatatu, Aprili 27, 1964.
Wakati huo huo Rais alimteua Kapteni Abdallah Twalipo (35) na Kapteni Lukias Shaftaeli
(39), wote wakiwa ni wanajeshi wa jeshi la Wananchi, kuwa wajumbe wa mahakama ya
kijeshi. Sir Wildham akawa Rais wa mahakama hiyo. Baada ya uteuzi huo, Mkurugenzi wa
Mashitaka, Herbert Wiltshire Chitepo, alisema angewaita mashahidi 25.

Kesi hiyo iliendeshwa kwa siku chache na hatimaye hukumu ikatolewa. Ijumaa ya Mei 15,
1964, siku 19 baada ya kufanyika kwa Muungano wa Tanzania, wanajeshi walioasi katika
Kambi ya Colito walihukumiwa, lakini adhabu zao zilikuwa tofauti.

Sajini Francis Hingo Ilogi alihukumiwa kifungo cha miaka 15 jela, Koplo Aliche miaka kumi,
Koplo Baltazar miaka kumi, Private Jonas Chacha miaka kumi, Private Pius Francis miaka
kumi.

Wengine ni Private Patric Said John aliyehukumiwa miaka kumi, Sajini Lucas miaka kumi,
Kapteni Kamaka Mashiambi miaka kumi, Kapteni Benito Manlenga miaka kumi, Private
Dominicus Said miaka kumi, Kapteni Andrea Dickson miaka mitano, Private Hamidus miaka
mitano na Roger Mwanaloya miaka mitano.

Wanajeshi walioshitakiwa lakini hawakupatikana na hatia na hivyo kuachiwa huru ni Koplo


Peter Mbasha, Private Ernao Msafiri, Private Gerado Raphael, Kapteni Mahara Magom na
Kapteni Moses Kawanga.

MWISHO WA SEHEMU YA KWANZA

********************
PART 2
JARIBIO LA PILI/UHAINI WA KWANZA(Bibi Titi,Kambona and co.)

2nd Coup Attempt and 1st TREASON


Baaada ya Uasi wa kijeshi wa mwaka 1964 kuzimwa. Hali ilirudi kama kawaida nchini.

Ilifikia hatua Mwalimu Nyerere alijiamini na kuweza kutoa kauli hii mwaka 1966 “I have
been one of the luckiest presidents in Africa.My colleagues are very loyal to me"

Mwalimu hakujua kama Upepo ulikuwa unaenda kubadirika kipindi cha miaka miwili tu
mbeleni.
Katika miaka hii miwili mbeleni,wengi wa waliokuwa kwenye baraza lake la mawaziri
walikuwa wamewekwa Vizuinini na zaidi ya yote,rafiki yake Mkubwa alikuwa amekimbilia
uhamishoni.

Ndiyo,Mwaka 1967,OSCAR KAMBONA mmoja wa waasisi wa TANU,alijiuzuru nafasi zake


zote ndani ya chama na serikalini na kwenda kuishi kama mkimbizi Uingereza.
Sasa Issue Nzima ilianza hivi,

Inasemekana OSCAR KAMBONA ambaye ndiye alitajwa kama muhusika mkuu wa mpango
huu,alikuwa akiendesha harakati za kutaka kumpindua Mwalimu Nyerere akiwa huko huko
uamishoni Uingereza.
KAMBONA alinukuliwa na chombo kimoja cha habari akidai kuwa Rafiki yake wa
zamani(Nyerere) ameanza kuwa dictator.
Hivyo kambona akatajwa kuwa alikuwa akituma kiasi kikubwa sana cha pesa kwa watu
wanaomuunga mkono nchini Tanzania ili ziweze kusaidia katika nia yao ya kumng'oa
Nyerere madarakani.

Walimshawishi Mr. POTLAKO LEBALLO ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa chama cha


wapigania uhuru wa Afrika kusini kiitwacho Pan African Congress Of South Africa
kilichokuwa kimeweka makao yake makuu Dar es salaam.
Wahusika Wengine katika Mpango huo walikuwa wakitumia majina ya bandia,na
kuyabadilisha mara kwa mara ili isiwe rahisi kuweza kugundulika kirahisi. Wahusika hao na
majina yao ya bandia ni;
1. GRAY LIKUNGU MATTAKA,Huyu alikuwa ni Mhariri wa gazeti la TANU lililokuwa
likiitwa “THE NATIONALIST “ Pia aliandikia gazeti la Uhuru. Majina ya bandia
aliyokuwa akitumia ni CHAIMA,KAVUMA,MIKAYA au EDWARD KAVUMA.
2. MICHAEL MARSHALL MOWBRAY KAMALIZA.Huyu alikuwa ni Mlemavu wa ugonjwa
wa Polio. Alikuwa waziri wa zamano wa Kazi na pia raisi wa chama cha wafanyakazi
NUTA. Majina ya bandia aliyotumia ni PERIJEKANTU,BWANA MIGUU,WAMALIZA au
HAKUNA KITU
3. JOHN DUNSTAN LIFA CHIPAKA,alikuwa katibu wa zamani wa chama cha Congress,
Majina yake ya uficho yalikuwa ni M.M CHIMWALA, CHIMWALA CHING-WACHENE,
CHIMWALA au PADRE JOHN CHIMWALA
4. BIBI TITI MOHAMED,alikuwa ni mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT.
Majina yake ya uficho yalikuwa ni AUNT,MAMA MKUU au MWAMBA
5. ELIYA DUNSTAN CHIPAKA,alikuwa mdogo wa JOHN CHIPAKA na alikuwa ni afisa wa
jeshi wa zamani
6. WILLIAM MAKORI CHACHA, alikuwa ni Kanali wa Jeshi. Majina yake ya bandia ni BEN
TASU au KITUMBO
7. ALFRED PHILIP MILINGA huyu alikuwa ni afisa wa zamani wa Jeshi.
Mhusika wa nane kwenye njama hizi ndiye alikuwa OSCAR SELATHIE KAMBONA ambaye
alikuwa ughaibuni.
Wahusika hawa walitajwa kuwa walianza mkakati wao wa kula njama za kuipindua
serikali ya Mwalimu Tangu November 1968 wakifanyia mikutano yao maeneo mbali
mbali ikiwepo Nairobi,Zanzibar,London na kwenye Night clubs Dar Es salaam.

Katika vikao vyao,Walikuwa wakitumia majina ya Uficho,na hata katika barua


walizokuwa wakiandikiana walikuwa wanatumia mafumbo ndio maana ilikuwa vigumu
sana kuwabaini katika hatua za asali za mipango yao.

Mipango yao ilifikia kilele kati ya tarehe 10 hadi 15 October 1969 ambapo waliendesha
vikao vyao mfululizo wakati Mwalimu Nyerere akiwa ameambatana na wasaidizi wake
wengi nje ya nchi akiwemo Major General wa JWTZ SAM SARAKIKYA.
Aliyelipua mipango hii sio mwingine,bali ni POTLAKO LEBALLO ambaye walimuingiza
kwenye mpango wao bila kujua kama jamaa alikuwa akiwachota baada ya kumwamini
na yeye akawa anatoa taarifa hizo kwa Usalama wa taifa.

Issue Ilianza Kubumbuluka Jijini Nairobi nchini Kenya ambapo POTLAKO LEBALLO alikutana
na GRAY MATTAKA ambaye alimwambia ana ujumbe wake kutoka kwa KAMBONA
aliyemtaka awaunge mkono kwenye Mpango wao wa mapinduzi. MATTAKA alimuhakikishia
POTLAKO kuwa watu wengi tu walio kwenye serikali ya Nyerere walikuwa nyuma ya
Mpango huo.

POTLAKO labda kwa kutambua Umuhimu wa serikali ya NYERERE iliyokuwa imekiifadhi


chama chake cha wapigania uhuru Kusini mwa Afrika PAC akaona akawape siri hiyo Watu
wa serikali ya Tanzania ambao walimuunganisha na watu wa Usalama wa taifa.

Watu wa Usalama, Walipokutana na POTLAKO wakamwambia aendelee na vikao na


wahusika ili kujua hasa wamepanga vipi kutekeleza mipango yao.
Hapo ndipo Mr. POTLAKO akaendelea na mipango akawa hadi anaminika na wale
waliopanga hadi akawa anakutana mara kwa mara jijini London na OSCAR KAMBONA huku
akichota taarifa na kuzifikisha kwa watu wa Usalama.
MR. POTLAKO LEBALLO aliwaeleza Usalama wa Taifa jinsi alivyokutana na OSCAR KAMBONA
nchini Uingeleza ambapo alimpatia dola za marekani 700 huku akimuahidi kuwa angepata
zaidi kutoka “zilikotoka" Kama KAMBONA angeamua tu kuwasiliana na watu wa United
States Information Service walioko pale pale London. Yote hii ilikuwa ni njia ya kumshawishi
POTLAKO LEBALLO aungane na mpango ule.
LEBALLO akazidi kusaga kunguni kuwa hata waziri wa mambo ya nje wa Serikali ya Kikaburu
kule Afrika kusini Mr. HILGALF MULLER alikuwa anawasiliana na KAMBONA kuhusu mpango
huo wa mapinduzi.

Watu wa Usalama walianza kwanza kwa kumkamata GRAY MATTAKA aliyekuwa Jijini
Nairobi.
POTLAKO alipoenda kukutana tena na KAMBONA Uingereza,KAMBONA akamwambia
wameamua kuachana na mpango huo baada ya GRAY MATTAKA kukamatwa. Kambona
hakujua kama alikuwa amekaa meza moja na mtu aliyekuwa akimuuza.
Baada ya hapo,Huku Tanzania,Watu walikuja kushangaa tu Mwezi October 1969 wahusika
wa mipango hiyo wanakamatwa.
Yalipotajwa majina ya wahusika watu walipigwa na butwaa hasa waliposikia jina la BIBI TITI
MOHAMED. Pia Wale kina ELIYA CHIPAKA na JOHN CHIPAKA watu walikuja kujua baadae
kuwa walikuwa ni Wapwa wa OSCAR KAMBONA.

Wahusika hawa zaidi ya kupanga kumuondoa madarakani mwalimu Nyerere,Pia


walisemekana walipanga kumuua. Hii ni kutokana na Ujumbe wa siri uliokamatwa ambao
JOHN DUNSTAN LIFA CHIPAKA alikuwa ameandika “We are going to Eliminate him"
Mambo yakazidi kufunuka zaidi baada ya ndugu wa JOHN,hapa namaanisha ELIYA DUNSTAN
LIFA CHIPAKA kukutwa na Orodha ya Watu 37 waliokuwa washawishiwe kuingizwa ndani
ya Mpango ule. Hata alipobanwa kuhusu Orodha ile alidai kuwa ile ilikuwa ni “Wedding list”
yaani watu aliotarajia kuwaalika kwenye sherehe ya ndoa.
Kilichombana zaidi ni kuwa kuwa list ile ilikuwa imejaa majina ya Wanajeshi na zaidi,kwenye
moja ya jina la Mtu aliyekuwa na cheo cha Kanali,kulikuwa na maelezo yakisema
“Dissatisfied,but his stand is not known". Maelezo haya hayakuwa na uhusiano wowote na
mambo ya harusi.
Pia ilikamatwa nyaraka ambayo ilikuwa imeorodhesha maeneo yote ya muhimu ambayo
yalitakiwa kushikiliwa haraka siku ya Mapinduzi hayo kama vile,Shirika la
Umeme,Tanganyika Broadcasting Corporation,Bank kuu ma viwanja vya ndege.
Tarehe 8 July, 1970 Wahusika 7 wa mpango huu walifikishwa mahakamani na kushtakiwa
kwa kosa la Uhaini mbele ya Jaji Mkuu PHILIP GEORGES.
Mshtakiwa wa Kwanza Ambaye alikuwa ni OSCAR KAMBONA hakuwepo wakati mashtaka
haya yanasomwa kwa kuwa alikuwa ukimbizini Uingereza .
Tetesi zilisema kuwa Serikali ya Tanzania ingeweza kuwaomba Uingereza kumrudisha
KAMBONA ili kuja kujibu mashtaka yake lakini haikufanya hivyo. Sijui kama Uingereza
wangelikubali ombi hilo.
Wakati kesi inaendekea Mkurugenzi wa upepezi wa jinai GEOFFREY SAWAYA aliieleza
mahakama hatua kwa hatua njama hizo zilivyopangwa,wahusika na ushaidi wa POTLAKO,
Pia alikabidhi mahakamani maelezo ya kukiri kosa ya baadhi ya wahusika wa mpango ule.

Baada ya Kesi kuendeshwa kwa jumla ya siku 127, GRAY MATTAKA,ELIA CHIPAKA,JOHN
CHIPAKA na BIBI TITI MOHAMED walihukumiwa kifungo cha maisha.
Pia MICHAEL KAMALIZA na WILLIAM CHACHA walihukumiwa kifungo cha miaka 10
Kwa Upande wake ALFRED MILINGA aliachiliwa huru baada ya kutokutwa na hatia
akapokewa kwa furaha na ndugu zake baada ya kuwa Kizuizini kwa miezi zaidi ya 16 wakati
kesi hii ikiendelea.
Hata hivyo,Jaji katika kesi hii aliilaumu serikali kwa Kutunga sheria hiyo ya Kizuizi na kisha
ikapitishwa na Bunge kwani iliweza kumweka mtu kizuizini bila kumfikisha mahakamani kwa
hisia tu kuwa mtu anahatarisha usalama wa nchi.
OSCAR KAMBONA hakuhukumiwa kwa kuwa hakuwepo mahakamani hivyo hakujitetea .
Miaka saba baadae BIBI TITI aliachiwa kwa msamaha wa rais akiwa katika gereza la Isanga
dodoma. Inasemekana ni baada ya kumwandikia barua Nyerere ya kuomba msamaha
ambayo haikujibiwa.

Pia mwaka 1978 ndugu wa OSCAR KAMBONA waliokuwa wamewekwa kizuizini nao

waliachiwa na Mwalimu Nyerere. Ndugu hao ni MATTIYA KAMBONA na OTINI KAMBONA.

Waliachiwa pamoja na wengine 22 waliokuwa kizuizini. Pia siku hiyo waliachiwa huru

wafungwa wengine 7,000 kwa msamaha wa Rais.

Wote hawa waliachiwa huru katika maadhimisho ya kwanza ya kuzaliwa kwa CCM na miaka

11 ya Azimio la Arusha. Otini na Mattiya hawakufikishwa mahakamani na kwa sababu hiyo

hawakuhukumiwa, bali walikuwa wamewekwa kizuizini ambako walikaa kwa miaka 10 tangu

Desemba 1967 kwa sababu walikuwa wakimuunga mkono kaka yao, Oscar Kambona, na

kwa kutumia gazeti alilomiliki la ‘Ulimwengu’ kuendesha propaganda za kisiasa.

Gazeti hilo lilikuwa likichapisha pia makala zilizoandikwa na Oscar Kambona akiwa

uhamishoni Uingereza. Kambona mwenyewe hakuwahi kukamatwa, na wala hakukuwahi


kufanyika jitihada zozote za kumrejesha nchini ili ashtakiwe pamoja na wale aliotuhumiwa

kula nao njama.

Aliendelea kukaa nchini Uingereza hadi aliporejea nchini kwa hiari yake mwenyewe mwaka
1992 ulipoanzishwa mfumo wa vyama vingi.

MWISHO WA PART 2
*********************

PART 3

JARIBIO LA TATU KUMTOA


NYERERE MADARAKANI

This wasn't a coup,Lilikuwa ni tukio


la Utekaji wa ndege ya ATC
ambapo vijana watano ndugu na
mashemeji zao waliteka ndege ili
kumshinikiza Mwalimu Nyerere
ajiuzuru madarakani.

Ijumaa Tarehe 27 February 1982


Taifa lilitikisika tena.
Hii ni baada ya Kupata taarifa kuwa
ndege ya Boeing 737 Mali ya shirika
la ndenge la Tanzania iliyokuwa na
safari ya kutoka Mwanza Kuelekea
Dar es Salaam,Ilikuwa Imetekwa na
kuelekezwa Nairobi baada ya
kuruka mwanza Mida ya saa 6 na
dakika 35.
Kama Coincidence,Ndege hiyo
liyokuwa na "Call sign" 5-HATC
ilitua katika Uwanja wa Nairobi
katika muda sawa na ndege
iliyokuwa imembeba waziri wa
mambo ya Nje wa Kenya wakati
huo DR. ROBERT OUKO ambaye
alijipa jukumu la kuzungumza na
watekaji kujua madai yao.
Kwa mawasiliano ya radio,Watekaji
walijitambulisha kuwa wao ni
wanachama wa ‘Harakati za
Kidemokrasia za Vijana wa
Tanzania.’ na kuwa walitaka Rais
Julius Nyerere ajiuzulu kwa sababu
“...Watanzania wanaishi katika hali
ya shida na hawana
chakula.”

Majadiliano na waziri OUKO


yalichukua masaa saba na wakati
huo Serikali ya Tanzania ilimteua
waziri wake wa Mawasiliano na
Uchukuzi kwenda Kenya kufatilia
sakata hilo. Watekaji waliishurutisha
serikali ya kenya iwaruhusu waruke
kuelekea JEDDAH,Saud Arabia

Utekaji ule ulitokea muda mbaya


ambapo mahusiano ya KENYA na
Tanzania hayakuwa
mazuri Tangu kuvunjika kwa
Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mgogoro kati ya Kenya na Tanzania


ambao ulioanza taratibu kuanzia
mwaka 1974, ulifikia kilele chake
mwaka 1977 wakati nchi zote
mbili—Tanzania na Kenya—
zilipogoma kutoa michango yake ya
uanachama wa jumuiya hiyo. Kwa
kukosa bajeti yake ya mwaka wa
fedha wa 1977-1978,

Serikali ya Tanzania ilishinikiza


Kenya wasiiruhusu ndege ile kuruka
lakini Kenya waliiruhusu baadae
baada ya watekaji kutishia
kuwauwa mateka wao.

Mtekaji mmoja aliyedhani kuwa


muda unawatupa mkono, kwa
hasira kali alifoka: Tutailipua ndege
hii sasa hivi … Tutakufa sasa.
Baada ya kuizuia ndege hiyo kwa
muda
wa saa kadhaa, usiku wa
manane,Kenya iliona haina la
kufanya, na hivyo ikaiachia ndege
hiyo iondoke Kenya ikatue nchi
nyingine.
Kabla haijaondoka, watekaji hao
waliiachia familia moja ya Kiarabu
ya watu sita kutoka katika ndege
hiyo. Mmoja wa mateka hao,
Khadija Mohammed Hassan,
alisema waliruhusiwa na watekaji
kutoka katika ndege hiyo kwa
sababu mtoto wake wa miezi 18,
Mselem, alikuwa hanyamazi kulia,
na kwa sababu hiyo watekaji
walimwona kama anawasumbua
kwa hiyo wakamwacha aondoke.
Lakini maofisa wa serikali ya
Tanzania waliitilia mashaka familia
hiyo. Wasiwasi huo uliongezeka
zaidi wakati familia hiyo iliposema
kuwa ilikuwa ikisafiri kwenda Dubai,
na kwa kuwa tayari walikuwa
Kenya, ingekuwa rahisi zaidi kwao
kufika huko kupitia Mombasa. Bila
wao kutaka, familia nzima
ililazimishwa kupanda ndege ya
Jeshi la Tanzania na kupelekwa Dar
es Salaam. Akiwa kama kiongozi
wa kushughulikia utekaji nyara huo,
Waziri Malecela alitoa taarifa hizo
hizo kwa Rais Nyerere kuwa
v

Wateka nyara hawakutoa madai


yoyote. Kwa kuwaamini maofisa
wake, Nyerere aliamini pia kile
walichomwambia kuhusiana na
utekaji huo. Kikundi cha maofisa wa
serikali ya Tanzania waliopiga
kambi nyumbani kwa Mwalimu
Nyerere, Msasani, kulingana na
taarifa walizokuwa wakipokea,
walianza kuchukulia kwamba utekaji
huo haukuwa na kusudio lolote la
kisiasa. Kwa kuwa hawakujua kisa
halisi cha kutekwa kwa ndege hiyo,

....walibuni vya kwao.

Walianza kuambizana wenyewe


kwa wenyewe; wakamwambia na
Rais Nyerere pia kwamba
‘inawezekana’ watekaji hao
walikuwa na kiasi kikubwa cha
dhahabu na almasi walizotaka
kuzitoa nchini. Waliamini pia
kwamba walitumia utekaji huo
kuvusha mali hizo na kwamba
familia ya Kiarabu iliyotaka kwenda
Dubai kupitia Mombasa ilikuwa ni
sehemu ya
utekaji huo. Kitendo cha kuiruhusu
ndege hiyo kuondoka mjini Nairobi
kiliongeza idadi ya maswali. Lakini
serikali ya Kenya haikujiingiza kwa
undani katika kulizungumzia sana
jambo hilo. Wakati watu wakitafakari
kilichotokea, ‘Kilimanjaro’ ilikuwa
ikiambaa ambaa angani kuelekea
Jeddah, Saudi Arabia. Ilipopata
habari, Serikali ya Saudi Arabia
iliikatalia ndege hiyo ruhusa ya
kutua na kwa kuonyesha kuwa
haikuwa ikitania, iliufunga uwanja
wake. Lakini wakati Kapteni Deo
Mazula alipowasiliana kwa redio na
uwanja huo na kuwaambia kuwa
ndege yake imekwisha safiri umbali
wa kiasi cha maili 1,600 tangu
ilipoondoka Nairobi na kwamba
haikuwa na mafuta zaidi ambayo
yangeiwezesha kuendelea na safari
nyingine,

Saudi Arabia ilifyata mkia.

Ndege hiyo iliruhusiwa kutua


kwenye uwanja
wa ndege wa Jeddah. Ruhusa hiyo
ilikuwa ni kwa ajili ya kujaza mafuta
tu. Walinyimwa hata ruhusa ya
kufungua mlango wa ndege hiyo.
Wakati huu hali ya hewa katika
ndege ilishaanza kuwa afadhali.
Viyoyozi vilikuwa vimeanza kufanya
kazi tena na watekaji walijaribu
kuwasemesha abiria na kuwaambia
shabaha yao ya kuiteka ndege.
Sasa niwatajie Wahusika wa utekaji
huu,

1.Yassin Membar(21),
2.Mohammed Tahir(21),
3.Abdallah Ali Abdallah(22),
4.Mohammed Ally Abdallah(26)

na kiongozi wao
5.Musa Membar(26)

Kwa Kuangalia umri wao utaona


kabisa wote walikuwa ni vijana
wadogo
Mwisho wa mazungumzo yao
waliwaambia abiria kuwa
wamekusudia kuipeleka ndege hiyo
nchini Marekani. Wakati wakisema
hayo, watekaji hao walikumbuka
kuwa kuna abiria mmoja(MR
MUSHUMBUSHI),alitoa bastola
yake walipokuwa Uwanja wa Ndege
wa Mwanza na kuikabidhi chumba
cha marubani. Ilikuwa Ni utaratibu
katika viwanja vya ndege vya
Tanzania kwa abiria yeyote kuitoa
silaha yake na kuikabidhi kwa
wafanyakazi wa ndege hadi mwisho
wa safari. Walipokumbuka hilo,
mmoja wa watekaji hao alimfuata
Kepteni Mazula na kumtaka
awapatie bastola hiyo. Mmoja wao,
Mussa Memba alipoipokea
alionekana kubabaika kidogo kana
kwamba hakuwa na ujuzi wowote
wa namna ya kuitumia silaha hiyo

Mwanzoni watekaji waliteka ndege


wakiwa na bastora mbili bandia
zilizotengenezwa kwa mbao,Bomu
la kurushwa kwa mkono la bandia
na walikuwa na mishumaa miwili
iliyoungwa na
kuonekana kama bomu la kujitoa
mhanga. Pia walikuwa na visu viwili.

Ndipo wakapata bastora ya kweli.

Alipokuwa amejikunja upande


mmoja wa chumba cha rubani
akiishika shika bastola hiyo,
pengine akiishangaa au
kuichunguza, ghafla risasi ilifyatuka.
Risasi iliyofyatuka iliuparaza
mgongo wa Oscar Mwamaja, rubani
msaidizi wa Kepteni Mazula na
kumjeruhi.

Baada ya kujaza mafuta kwenye


Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Mfalme Abdulaziz mjini Jeddah,
kituo cha tatu kilikuwa ni Athens,
Ugiriki. Pamoja na maombi mengi
ya Serikali ya Tanzania ya kutaka
ndege hiyo ishikiliwe ili isiondoke,
maofisa wa Serikali ya Ugiriki
walitangaza mapema kabisa, hata
kabla Boeing 737 haijatua, kwamba
ingeruhusiwa tu kujaza mafuta na
kuondoka mara moja bila kuikawiza.

Turejee nyuma Kidogo Ili Mjue


Mazungumzo
yalivyokuwa Pale Kenya na ni kipi
hasa Kilitokea hadi watekaji
wakaruhusiwa kuruka tena.

Baada ya maofisa wa Serikali ya


Kenya kupata habari kuwa ndege
hiyo aina ya Being 737 ya Air
Tanzania itatua kwenye Uwanja wa
Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini
Nairobi, polisi waliufunga na
wanajeshi kuuzingira uwanja huo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya,


Robert Robert Ouko (51), ndio
kwanza alikuwa ametua uwanjani
hapo akitokea jijini Addis Ababa,
Ethiopia na hiyo ilikuwa muda mfupi
baada ya ndege hiyo ya Tanzania
kutua.
Alipopewa habari za yaliyotokea, Dk
Ouko hakusita kwenda moja kwa
moja kwenye chumba cha
kuongozea ndege ambako alijaribu
kulishughulikia jambo hilo kwa
kuwasiliana na watekaji. Ndege hiyo
ilikaa
katika uwanja huo kwa saa sita
tangu ilipotua hadi ilipoondoka.

Akizungumza kupitia redio ya


mawasiliano ya ndege hiyo. Kwa
mujibu wa jarida la The Weekly
Review, mmoja wa watekaji
alijitambulisha kwa jina la Luteni
Wami na kusema yeye ni ofisa wa
Jeshi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ).sawa

‘Luteni Wami’ alisema ni lazima


Rais Nyerere ajiuzulu “la sivyo
tutailipua ndege hii”. Dk Ouko
alijaribu kujadiliana na mtekaji huyo,
lakini baadaye alijibiwa kuwa “tayari
nimeshaua abiria watatu, na
nitaendelea kuwaua wengine zaidi”.

Dk Ouko alishtushwa na kauli hiyo.


Alilazimika kumsihi mtekaji huyo
kwa kumwambia: “Usiendelee kuua
zaidi.”
Lakini ukweli wa mambo, hapakuwa
na mauaji yoyote hadi kufikia wakati
huo.
Kupitia mawasiliano ya redio yao ya
upepo, mtekaji huyo alimwambia
Waziri Ouko: “Sasa namuua huyu
rubani.” Rubani mwingine aliyekuwa
akisaidiana na Kepteni Mazula ni
Oscar Mwamaja.

Dk Ouko alimjibu mtekaji huyo kwa


kumwambia kuwa ikiwa atafanya
kitendo cha kumuua rubani wa
ndege hiyo atakuwa amefanya
ujinga kwa sababu “atahitajika
kuirusha ndege hiyo kwenda
kwingine”.
Pakatoa Ukimya kidogo, Kisha
likaibuka jibu hili

“Ninaweza kuiendesha ndege hii


mimi mwenyewe,” akafoka
mtekaji huyo, “Mimi ni luteni wa
anga.”
Kadiri muda ulivyosogea, kiwango
cha uvumilivu cha mjadala kati ya
Dk Ouko na watekaji kilianza
kuzorota.

Walianza kuonekana kama


wanarukwa na wazimu. Mtekani
mmoja aliyedhani kuwa muda
unazidi kuwatupa mkono, kwa
hasira kali alifoka: “Tutailipua hii
ndege sasa hivi. Tutakufa sasa
hivi. Leteni majeneza 100 sasa
hivi.”

Kuona hana jingine la kufanya, Dk.


Ouko alikubaliana na matakwa ya
watekaji hao. Baada ya kuizuia
ndege hiyo kwa muda wa saa
kadhaa, ilipofika usiku wa manane
Serikali ya Kenya iliona haina la
kufanya. Ikaona ni heri wairuhusu
hiyo iondoke ikatue nchi nyingine.

Mabishano yaliyodumu kwa saa


kadhaa yakafikia mahali ambako
watekaji hao
walidai ndege hiyo ijazwe mafuta
kwa ajili ya safari ya kwenda Saudi
Arabia. Ndege ilijazwa mafuta tayari
kwa safari ya Saudi Arabia.

Wakati huohuo, jijini Dar es Salaam


kumbukumbu za kijeshi zilianza
kuchunguzwa kutafuta jina la Luteni
Wami. Jina hilo, kwa mujibu wa
jarida la Africa Now, halikupatikana
popote, na wala hakukuwa na cheo
chochote cha LUTENI WA ANGA
nchini.

Kwa upande mwingine, hata baada


ya majina ya watekaji hao
kujulikana, Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa
Jeshi la Polisi Tanzania, Joseph ole
Muturu Lemomo, wakati huo akiwa
na miaka 45, alisema katika taarifa
yake kwa vyombo vya habari
kuwa....

“majina ya vijana hao ni ya kawaida


na si rahisi kugundua mara moja
katika
kumbukumbu za polisi iwapo
waliwahi kuhusika na uhalifu
wowote”.

Joseph Lemomo, mzaliwa wa


Wilayani Monduli mkoani Arusha,
alikuwa ameteuliwa mwaka mmoja
uliopita (1981) kuchukua nafasi ya
Menolf Mwingira
Watekaji walipokuwa Ugiriki
walishangaa Jinsi Kijana mmoja wa
watekaji MUSA MEMBA alivyokuwa
anaongea kwa ufasaha Lugha ya
Kigiriki. Wapelelezi wakaanza
kusaka Taafifa zake na ikabainika
MUSA MEMBA alikuwa ni baaria wa
muda mrefu na alishakuwa dereva
taxi

Sasa Mke ndegeni, Mmoja wa


abiria wa daraja la kwanza alikuwa
ni aliyekuwa Askofu mteule Dk.
METHOD MUTEGEKI
NKYABONAKI KILAINI. Askofu
huyu ambaye aliweka rekodi kwa
kupata upadirisho akiwa mdogo wa
miaka 24 tu,Alikuwa anasafiri
kutoka Mwanza hadi Dar ili
akatibiwe nje ya
nchi

Kwa upufi ni kwamba Askofu


KILAINI alikuwa ametoka kupata
ajari mbaya sana ya gari aliyoipata
huko Pasiansi, mkoani Mwanza
ambapo aliumia vibaya na kupoteza
fahamu kwa muda wa wiki moja.
Alipochunguzwa na Daktari Bingwa
ilibainika kuwa fuvu la kichwa chake
lilikuwa kimepasuka na
kugawanyika likishikiliwa na ngozi
tu.

Ajari hiyo alipata akiwa na viongozi


wenzake wa kiroho wakielekea
uwanja wa ndege kupanda ndege
kuelekea Dar-Es-Salaam kwenye
mkutano.

Wenzake katika ajari hiyo walikuwa


ni Askofu Castol Sekwa ambaye
alivunjika mguu,Gombera wa
Seminari ya Rubya Padre
Simon Rutatekululwa,Padre Peter
kutoka Rulenge na Padre
Deogratias Rweyemamu ambaye
naye aliumia vibaya.
Baada ya ajali hiyo majeruhi wote
walipelekwa katika hospitali ya
Bugando ambapo Dokta MAKWANI
alimchunguza afya yake na kukuta
kichwa kimepasuka.

Askofu alikaa hospitalini Bugando


kwa muda wa mwezi mmoja kabla
ya kwenda kwenye hospitali ya
KCMC kwa matibabu zaidi. Mwaka
Uliofuata askofu akatakiwa kwenda
Rome Italy ili kupata matibabi zaidi
ndio akajikuta "anapewa lift" na
watekaji wale.

Ndio Alipewa Lift, Badala ya


kwenda Dar ili apande ndege
nyingine mpaka Rome,Yeye
alipelekwa mpaka Uingereza

Akiwa safarini From Mwanza yo Dar


es salaam ndipo alikumbwa na
mkasa huu wa kutisha kwani ndege
aliyopanda ilitekwa na maharamia
hawa niwasimuliao
Akielezea mkasa huo uliotokea
Februari 27, 1982 Askofu alisema
kuwa akiwa amepanda ndege ya
ATC kutoka Mwanza kwenda Dar-
Es-Saalam ambapo alitarajia
kupanda ndege nyingine kwenda
Roma ,

ndege hiyo haikuweza kufika Dar-


Es-Saalam na badala yake ilitekwa
ikiwa njiani na kupelekwa Nairobi,
Kenya, ikaelekea Jeddah, kisha
Athens, Ugiriki.

Huku ikitua tu na kuweka mafuta


katika maeneo hayo na sehemu
nyingine ikinyimwa, ilikwenda moja
kwa moja London, Uingereza.
Ndege hiyo ilitekwa na wahaini
watano, wawili kutoka Zanzibar na
wengine Tanzania Bara
Alisema yeye alipata msukosuko
zaidi kwani kwa vile alikuwa na tiketi
ya daraja la kwanza (first Class)
hivyo alidhaniwa kuwa ni
mwanasiasa.

Alisema walipofika London, Waziri


Mkuu wa Uingereza enzi hizo akiwa
Magreth Thatcher alitoa amri
kwamba ndege iachiwe iingie lakini
kwa vyovyote isiruhusiwe
kuondoka.

Alisema maongezi ya kina


yalifanyika kati ya Serikali ya
Uingereza na watekaji hao na hapo
ndipo waliporuhusiwa kutelemka
kwenye ndege hiyo na kuanza
kupata huduma nchini humo, lakini
wakiwa wameshateseka kwa njaa
vya kutosha

Baada ya mkasa huo, Askofu


mteuele alisema kuwa serikali ya
Tanzania ilitaka watu wake kurudi
nchini lakini kwa vile yeye alikuwa
na vyeti vya daktari,paspoti na
vitambulisho vingine vilivyoonyesha
alikuwa akienda Roma
kwa matibabu, kwake tukio hilo
likageuka kuwa lifti, japo ...

....yenye "kasheshe" kwani


aliruhusiwa kuendelea na safari
yake.

Akiwa huko alifanyiwa uchnguzi wa


kichwa na kukutwa hakina matatizo
makubwa na kwamba anaweza
kuendelea na kazi bila matatizo.

Sitaweza kuusahahu mkasa huo,"


hiyo ni sentensi yake ya mwisho
baada ya hadithi hiyo.

Ndege ilipokuwa chini ya kuzuizi


pale Uingereza,watekaji walimtaka
OSCAR KAMBONA ndio ashiriki
kwenye Majadiliano yale. Kwa kuwa
walikaa muda mrefu bila kula
chakula,walianza kukata tamaa juu
azma yao ya kumshinikiza Mwalimu
Nyerere ajiuzuru na hivyo
wakaanza kuwaachia mateka wao
kwa makundi.

Baadae wao wakaomba wapewe


Ukimbizi wa kisiasa lakini waliishia
kukamatwa na kushtakiwa katika
mahakama za kule kule Uingereza.

Serikali ya Tanzania iliomba


warudishwe nyumbani lakini serikali
ya Uingereza ilikataa ombi hilo.
Mahakama iliwakuta na hatia hivyo
wakahukumiwa kifungo cha miaka
mitatu Jela kule kule Uingereza.

Walipotoka YASIN MEMBAR


alienda kufanya kazi katika kampuni
moja ya sheria na baadae akasoma
degree ya sheria kule kule
Uingereza.

Ndugu zake waliporudi Tanzania


walikamatwa na kuwekwa kizuizini
na baadae kuachiwa lakini MUSA
MEMBAR alifia gerezani mwaka
1992 katika Mission nitakayokuja
kuielezea binasfi.
YASIN MEMBAR aliporudi alijisajiri
kwenye Chama cha wanasheria
Tanganyika na alifariki baadae
Mwaka 2018

MWISHO

JARIBIO LA NNE NA LA MWISHO


LA MAPINDUZI

2ND TREASON &2ND COUP PLOT

Chanzo Kilikuwa Nini?

Kwa Mujibu wa mmoja wa


waliopanga Tukio hili ambaye ni
mwanajeshi alisema hivi:-
“Mambo yalianza kwenda mrama
kwa upande wa jeshi tangu
walipoenda kupigana vita vya
Kagera.”

Alidai hakukuwa na sababu za


msingi kuhalalisha vita vile,bali
mazungumzo tu yangemaliza
mzozo uliokuwepo.

Akarndelea kudai kuwa, Shabaha


kubwa ya Mwalimu kuingiza nchi
vitani ilikuwa tu ni kutaka kumsaidia
Rafiki yake MILTON OBOTE
ambaye alikuwa amepinduliwa na
IDD AMIN,arudi madarakani.
Kutokana na hili wanajeshi
walinung'unika kutumiwa vibaya hali
iliyoleta hali ngumu kiuchumi baada
ya vita.

Pia wanajeshi walilalamikia


upendeleo jeshini ambapo wasio na
elimu waliweza kupandishwa vyeo
hata mara mbili kwa wiki huku
Wenye Elimu hasa kutokea kanda
ya kaskazini wakiwekwa benchi.

Hali ilizidi kuwa mbaya baada ya


kuchagizwa na kukosekana kwa
bidhaa muhimu madukani

Wakiwa Wanaendelea na
manung'uniko huku wakiandaa
"mchoro" wa kumpiga "spana" Baba
mkuu, ndipo wakakutana na PIUS
MUTAKUBWA LUGANGIRA
ambaye alikuwa ni mfanya biashara
mkubwa mwenye asili ya kitanzania
nchini Kenya.

PIUS MUTAKUBWA LUGANGIRA


alikuwa ni Mwalimu wa Chemistry
hapo awali mkoani Kagera, Baba
yake alikosana na Nyerere kitambo
tu na akaamua kukimbilia Uganda.

Rais YUSUPH LULE hakuwa na


mahusiano mazuri na
Mwalimu,hivyo PIUS LUGANGIRA
alihisiwa kuwa alikuwa ni "Infomer"
wa Uganda
Hii yote Ni kwa kuwa Mwalimu
alitegemea baada ya Vita,OBOTE
angerudishiwa madaraka lakini
YUSUF LULE ndie akasimikwa
badala yake. Mbaya zaidi
Mwanajeshi wa Tz Komandoo
MOHAMED MUSSA TAMIMU
akaasi jeshi na kuwa mlinzi wa rais
LULE(Nitafafanua mbeleni)

Basi PIUS MUTAKUBWA


LUGANGIRA akapata misukosuko
hadi akaamua kukimbilia Uganda
alikokuwa baba yake na hivyo
akawa na chuki za wazi dhidi ya
serikali ya nyumbani kwao
Tanzania.
Alipokutana na wapangaji wa
mipango hii akafurahi sana. Kwa
kuwa PIUS MUTAKUBWA
LUGANGIRA alikuwa na pesa za
kutosha alikubali kufadhili mpango
huu. Pia akajipa Nickname ya
UNCLE TOM au FATHER TOM ili
asigundulike kwa urahisi.

Mipango hii ilianza kusukwa Tangu


November 1982 na ilipanga
Kutekelezwa January 9 mwaka
1983

Katika Mipango hiyo,ilipangwa


Baada ya Mapinduzi,Mwalimu
Nyerere auwawe na pia "Plotters"
wa mpango hui walimuahidi Fr.
TOM kuwa atakuwa mkuu wa nchi
baada ya Mapinduzi.

Ni katika kipindi hicho ambapo


Komandoo MOHAMED MUSSA
TAMIMU alirudi Bongo Kimya kimya
na kufikia kwenye nyumba moja
Kinondoni Mkwajuni. Alikuwa hatoki
mchana hata kidogo bali anatoka
usiku tu kwenda vikaoni maeneo ya
DRIVE INN

Ni Katika Wakati karibu na huo


ambapo PIUS MUTAKUBWA
LUGANGIRA aliingia jijini Dar na
kufikia hotel ya Motor Agip.
Pia kwa nyakati mbili Tofauti
aliwasiliana na mpwa wa Mshirika
mwenzake aitwaye CHRISTOPHER
NGAIZA. Kipindi hicho Ngaiza
alikuwa Kigali Rwanda

CHRISTOPHER NGAIZA akiwa


Rwanda aliitaka familia yake
iliyokuwa Ikiishi dar Pale Drive Inn
iende ikaungane naye Bukoba ili
kusherehekea Sikukuu ya Noel.

Huku nyuma kwenye nyumba yake


alibaki STEPHEN BUBERWA
aliyepigiwa simu mara mbili na
UNCLE TOM
Mara ya Kwanz LUGANGIRA
alimpigia simu BUBERWA kuwa
maji pale MOTEL AGIP yalikuwa
yamekatika hivyo alikuwa anataka
aende pale nyumbani akaoge. Kwa
kuwa Buberwa alikuwa amkifahamu
LUGANGIRA kama mjomba wake
hakukataa.

Siku nyingine LUGANGIRA kapiga


simu kwa BUBERWA na kumtaarifu
kuna wageni ataend kuongea nao
biashara pale nyumbani,walienda
wageni Tisa wakiwa
wanazungumza kwa sauti za chini
hivyo BUBERWA hakusikia wala
kuhisi lolote. Waliondoka Saa za
jioni kabisa.
LUGANGIRA alifika tena kesho
yake asubuhi kisha wakafuatia
wageni wake nane,wakaendelea na
"mkutano wao wa biashara" na
walikaa tena mpaka jioni.

Wakati vikao hivi vikiendelea


kwenye Nyumba nyingine mali ya
GEORGE BANYIKWA pale pale
Drive Inn vikao vingine viliendelea.

Kwenye Vikao hivi Vyote Komandoo


MOHAMED MUSSA TAMIMU
alikuwa anakuwepo kama katibu
Muhtasi aliyekuwa anachukua
summary za vikao.
Mmoja wa "plotters" aliyekuwa
hakosi vikaoni alikuwa ni rubani wa
ndege ndogo Captain HATIBU
HASSAN GANDHI mwenye jina la
uficho la HATTY MCGhee

Sasa huyu Captain HATIBU


HASSAN GANDHI aka HATTY
MCGhee alikuwa na kawaida ya
kukodi Taxi ya dereva ABDALLAH
SHABANI MHANDO aliyekuwa
akimpeleka sehemu mbali mbali
kwenye Vikao vyao vya siri. Pia
alikuwa akiwabeba wageni wengine
walioambatana na MCGhee.

Dereva Taxi ABDALLAH SHABANI


MHANDO alianza kuhisi vikao vile
lazima vingekuwa Nyeti sana kwani
watu aliowabeba walionekana ni
"watu wazito" kutokana na matumizi
makubwa ya fedha waliyokuwa
wakiyafanya wakati akiwa
anawaendesha. Mkumbuke kipindi
hicho kulikuwa na "UKATA"
mkubwa

Siku Moja MHANDO akiwa


anampeleka MCGhee
Airport(Alikuwa anaenda
Zanzibar)ndipo wakapiga story mbili
tatu na MCGhee akamgusia kuwa
Nchi iko kwenye hali mbaya hivyo
wanahaji kufanya "Overhaul".
Kipindi hicho MCGhee alikuwa
kapata kilaji kidogo

Kauli ile ilimshtua MHANDO hata


hivyo alificha hisia zake. Punde tu
alipomuacha MCGhee Airport
haraka akamtafuta Mwandishi wa
Daily News na Sunday News
CHARLES KIZIGHA na kumpa
mchapo ule.

CHARLES KIZIGHA
akamuunganisha na Mkurugenzi wa
Usalama wa Taifa AUGUSTINE
MAHIGA

Pamoja na KIZIGHA kumsaidia


MHANDO kupiga simu kwa
MAHIGA, hawakuweza kuonana
kwa muda waliokubaliana kwa
sababu gari lake (Mhando)
liliharibika na hivyo akashindwa
kufika sehemu waliyokubaliana
kukutana

Baada ya kushindwa kumwona


Mahiga siku hiyo, ilimchukua tena
muda kuonana naye kwa sababu
Ijumaa, Desemba 17, 1982
alilazimika kusafiri kwenda Harare,
Zimbabwe, kwa muda wa majuma
mawili.

Ilikuwa ni mpaka January 2 ndipo


AUGUSTINE MAHIGA alifanikiwa
kukutana na dereva taxi kipenyo
MHANDO.

MHANDO alimwelezea kuwa kuna


watanzania wawili waishio Kenya
amekuwa akiwachukua kwenye gari
lake lakini mwenendo wao umempa
mashaka.

Aliwataja watanzania hao ni


HATIBU GANDHI na Captain
MARTIN

Mhando alimwelezea MAHIGA


kuwa watu hao walikuwa hawatoki
mchana na walikuwa wakiendesha
mikutano ya siri mingi ikihusisha
raia na wanajeshi wengi pia
wamekuwa wakijifungia wakiwa
mikutanoni.

MAHIGA,baada ya kuelezwa hayo


alimuomba Mhando amwonyeshe
moja ya nyumba zilizokuwa
zikitumika kwa mikutano hiyo na
nyumba ambayo MHANDO
alimuonyesha ilikuwa karibu na
Drive Inn Cinema.

Baada ya Kusikia hayo,MAHIGA


alimwagiza MHANDO aendelee
kuwasiliana na naye kuhusu yale
aliyokuwa akisikia kutoka kwa watu
hao na hasa alimsisitiza ajaribu
kukumbuka majina ya watu hao na
wengine kama watakavyokuwa
wakitajwa,”

MAHIGA na wenzake Idarani


walianza kuifanyia kazi taarifa hiyo
Januari 3, 1983, kwanza kwa
kuifanyia uchunguzi kuithibitisha.
Aliamua kuishughulikia taarifa hiyo
akiwa na wasaidizi wake wawili—
Mkurugenzi wa Usalama wa Ndani
na Mkuu wa Idara ya Ulinzi.

Katika Kufatilia Mkasa huu MAHIGA


alijiita MR. X na Mkuu wa Idara ya
Ulinzi alimpa Jina Y(ilikuwa ni kwa
sababu ya unyeti wa majukumu yao
hivyo kutotambulika kirahisi kwa
raia. Majina haya waliyatumia pia
mahakamani kwenye kesi hii)

Mr. ‘Y’ ndiye aliyepewa jukumu la


kuratibu utekelezaji na ufuatiliaji wa
taarifa hiyo na kwamba baadaye
alimchukua ‘Y’ na kumtambulisha
kwa Mhando na kumwagiza taarifa
zote za kila siku ampatie ‘Y’ badala
ya yeye.

Kesho yake,yaani Januari 4,


1983,Mr. ‘Y’ alimpa MAHIGA taarifa
aliyoipata kutoka Makao Makuu ya
JWTZ iliyohusu kuwapo nchini na
kutambulika kwa CAPTAIN
MOHAMED MUSSA TAMIMU
ambaye ndiye aliyekuwa akijiita
CAPTAIN MARTIN kulingana na
taarifa za MHANDO.

Taarifa hiyo ilisema alikuwa


ameonwa na Luteni Kanali Mbwile
na kwamba Mbwile alishapeleka
taarifa hiyo kwa Mkurugenzi wa
Usalama Jeshini.

Mr.Y’ alimwambia MAHIGA kuwa


Jeshi lilikuwa likitaka kumkamata
Tamimu na kumshtaki kwa kosa la
utoro akiwa jeshini,

Lakini Mr ‘Y’ aliwaeleza wasifanye


hivyo kwa sababu kulikuwa na
uchunguzi uliokuwa ukiendelea
kuhusu watu waliokuwa wakiishi
katika nyumba aliyokuwa
ameonyeshwa na Mhando,

Baadaye uchunguzi ulipokuwa


ukiendelea ilifahamika kuwa,
nyumba iliyo karibu na Drive In
Cinema ilikuwa ya George
Banyikwa.

siku hiyo hiyo ya Januari 4, 1983,


alipelekwa tena taarifa na MR.‘Y’
kwamba mwanajeshi mmoja kwa
jina la SAJENTI TEMU,alienda Ikulu
kutoa taarifa kuwa amekuwa
akishawishiwa na mkuu wake wa
kazi, KAPTENI MBOGORO,ashiriki
katika mipango ya kuipindua
serikali.
KAPTENI MBOGORO alimpa
jukumu SAJENTI TEMU jukumu la
kutafuta askari watano wa
kuwaongezea kwenye mpango
wao.

MR. Y’ alimpa jukumu SAJENTI


TEMU la kuendelea kuhudhuria
mikutano hiyo na kuendelea kutoa
taarifa kila siku kwake,

SAJENTI TEMU alihudhuria mmoja


wa mikutano hiyo kwa kupelekwa
na Mbogoro ambako alitambulishwa
kwa wajumbe wa mkutano huo.
Wakati haya yanaendelea,Mwalimu
Nyerere alikuwa ametoka safarini
nje ya nchi na sijui kama ni kwa
kupenyezewa taarifa au la,
Aliunganisha moja kwa moja kijijini
kwake Butihama ambako alikaa
kwa siku kadhaa.

"Wazee wa Mipango" nao walikuwa


wakiendelea na "vikao vya
biashara" huku wakiharisha kwa
mara tatu zoezi lao kwa sababu
mbali mbali.

Kwanza walipanga walianzishe


Jumatatu tarehe 3 January
wakahairisha mpaka Jumatano
tarehe 5
Baadae wakasema lazima iwe
Jumapili tarehe 9 kwani kwa
kuendelea kuhairisha wanazidi
kuwashirikisha watu wengi hivyo
hatark ya siri yao kuvuja ingekuwa
nje nje

Sasa "Wazee wa mipango"


walikipanga kikosi chao cha mizinga
ambacho kilienda Pale Msasani
bonde la chumvi(MAYFAIR PLAZA)
Ili kusurvey na kangalia jinsi ya
kuweka mizinga yao pale juu ya
magugumaji ili "Mzee" akipita pale
waruke naye Jumlajumla. Kikosi hiki
kilijumuisha watu watatu ambao ni
Captain METUSELA SULEIMAN
KAMANDO, captain EUGENE
MAGANGA na Luteni
CHRISTOPHER KADEGO. Huyu
Captain EUGENE MAGANGA
alikuwa amejizolea umaarufu
mkubwa kwenye vita vya Kagera
kwenye maswala ya Mizinga. Kikosi
hiki kilikuwa tegemeo lao. Sasa pale
Bonde la chumvi,ambapo ndipo ilipo
MAYFAIR PLAZA kwa
sasa,kulikuwa na wamakonde
waliokuwa wakienda kucheza
"unyago" mabinti wao wakivunja
ungo. Wakati wa zoezi hilo wazee
wa kiume walikuwa wanakaa juu ya
maghorofa mabovu ya Drive Inn
kucheki "soo"
Wale wazee wakiwa juu ya
maghorofa,waliwaona "kikosi cha
mizinga" wakiwa busy kuchora
"ramani ya vita" kwa siku tatu
mfululizo hivyo wakawatilia
mashaka na kwenda "kuwapa
michano" maafisa usalama

Sasa Kwenye Mpango ule,Pia


ilikuwemo familia ya Hayati RPC
HANS POPE. yaani watoto wake
wawili ambao ni HARRY HANS
POPE aliyekuwa ni rubani wa kikosi
cha Anga cha 613 KJ AIRWING na
kaka yake ZAKARIA HANS POPE
aliyekuwa Captain wa kikosi cha
mizinga. Wote hawa walipigana
Kagera.
Baba yao alikuwa ni RPC wa iringa
na baadae akaenda mkoa wa west
lake (Kagera) ambapo aliuwawa na
majeshi ya Idd Amin katika uvamizi
wa mwanzoni kabisa wa mwaka
1971. Kwa kuwa huyu alikuwa ni
chotara wa Kijermani amini alitumia
picha yake kueneza propaganda
kuwa Tz ina mamluki.

Mwili wake ulirudishwa na kuzikwa


chini mwaka 1979 kipindi hicho rais
mstaafu Mkapa akiwa ni waziri wa
mambo ya nje.

TUSITOKE NJE YA MADA


Turudi kwa wanae, Hapa nitasimulia
moja kwa moja what transpired on
the fateful day with the help of
narrations from one of Plotters.

Sasa "Wazee wa Mipango"


walikuwa wameshaivisha mipango
yao.

Naam, Ilishaiva Sasa Ilikuwa rasmi


lazima waruke na "mzee" Jumla
jumla siku ya Ijumaa.

Jamaa(Ndani ya mpango) anasema


walishapata taarifa kuwa "Mzee"
anarudi Dar Ijumaa tarehe 7
January 1983 kutoka Butiama.
Anasema walikuwa wamekubaliana
wakutane "RV" mida ya Saa 9
mchana ili kuweka Mambo sawa
kwani hawakutaka kuhairisha tena.
Walishapanga Usiku wa Tarehe 8
Jan kuamkia Jumapili tarehe 9
"wanaikomboa" nchi na "Mzee"
"wanamtoa kwenye picha"

Jukumu la kumtoa "Mzee kwenye


picha" alikabidhiwa KOMANDOO
MOHAMED MUSSA TAMIMU
ambaye pia alikuwa ni "Mdunguaji"
aliyeiva.

Kwa wasiojua maana ya RV,hii ni


lugha ya kijeshi inayomaanisha
RENDEZVOUS au "maeneo ya
makutano kwa muda maalumu"

Kwa "Wazee wa mipango" RV yao


ilikuwa ni Kinondoni
Mkwajuni,Kwenye nyumba ya
KOMANDOO MOHAMED MUSSA
TAMIMU na Muda ulikuwa ni saa 9
mchana.

Msimuliaji anadai alikuwa


amebakiza mita chache tu kufikia
Nyumba ya MUSSA TAMIMU
akashangaa anaona Movie Moja
kali sana.

Ni kwamba Jamaa aliona


KOMANDOO TAMIMU akiwa
anaonyesha Umahiri wake wa
mapigano akitupiana mikono na
Maafisa vipenyo kibao huku mara
kwa mara akikwepa risasi. Ni kama
vile umuonavyo "Staring" ndani ya
Movie.

Noma sasa Ikawa imehamia


barabarani baada ya jamaa
kuwatoka maafisa.

Ni kwamba,kumbe ile nyumba


ilikuwa chini ya surveillance Tangu
tarehe 3 January 1983 ni tangu
ilipofahamika kuwa mtu "mbaya"
KOMANDOO MOHAMED MUSSA
TAMIMU karudi nchini baada ya
kuliasi jeshi Uganda na zaidi ya
yote anaendesha vikao vya siri
visivyoeleweka.

Tamimu na maafisa vipenyo


walipambana kwa MASAA MAWILI
katika umbali mfupi tu wa kutoka
Kindondoni Mkwajuni mpaka Drive
In Cinema, Na kuna wakati
TAMIMU "alichupa" Juu ya Pickup
iliyobeba bia" na bado alizigeuza
kuwa siraha yake kwa Umahiri
mkubwa. Maafisa Vipenyo walikuwa
wamepewa maelekezo mapema
kabisa(Na MR. X) kuwa "That was
Operation to CAPTURE and Not
to KILL" kwani "maiti huwa
haiongei" nao lengo lao ni kumpata
TAMIMU waijue mipango kwa kina.
Lakini kwa mbinu aliyokuwa
anawafanyia TAMIMU, afisa
kipenyo Mmoja(Mzee SIMBA
rip),akajua pale wakizubaa,TAMIMU
atawatoroka ndipo Afisa kipenyo
SIMBA aka"open fire aimed at
target" kwenda kwa TAMIMU

Yule Jamaa Ambaye alikuwa ni


Mmoja wa wanamipango, alikuwa
kajificha sehemu tu anafatilia tukio
zima pia analifatilia hadi alipoona
TAMIMU "katumiwa vijana
wenzake" I mean risasi
Mazee😂😂 Funny bt not funny.

Yes TAMIMU sasa alilala chini pale


mitaa ya Drive In Cinema.
"Jamaa yangu" akaendelea tu
kuangalia jinsi jamaa walivyokuwa
wanalaumiana kwa nini
wamemrushia risasi,hadi
walivyombeba haraka kwenye gari
yao kwenda nao Mhimbili Hospitali.

"Jamaa yangu, hakulaz damu naye


akatafuta usafiri na kuwafatilia watu
wale hadi Mhimbili

Kule Mhimbili jamaa akaona


TAMIMU akishushwa kwenye gari
kisha akaitwa daktari, kwa mbali
jamaa akaona dokta akiuangalia
mwili na kutoa maelekezo ambayo
hakuyasikia kutokana na umbali,
lakini aliyaelewa baada ya Kuona
TAMIMU akibebwa na kuelekea
uelekeo wa mortuary

Mpaka muda huo jamaa hakuwa na


hofu yoyote kama mipango inaweza
kutibuka hata kama TAMIMU
kauwawa. Hivyo baada ya wale
vipenyo kuondoka yeye akaenda
kuzungumza na Mhudumu wa
mortuary

Jamaa akampa kitu kidogo


mhudumu wa Mortuary kisha
akaomba autazame Mwili wa
KOMANDOO MOHAMED MUSSA
TAMIMU na akakubaliwa. Jamaa
alaangalia majeraha ya risasi
alizopigwa tamimu akafurahi sana.
Alifurahi kwa kuwa alijua,kwa
majeraha yale,ni hakika
KOMANDOO MOHAMED MUSSA
TAMIMU lazima alifariki pale pale
bila kupana hata muda wa kuweza
kuhojiwa. Hivyo alikuwa na hakika
siri yao bado haijavuja.

Lakini baadae Furaha hii ilikatika


ghafla.

Ndio ilikatika! Ni kutokana na


ujumbe ambao yule mhudumu
alimpatia.

Ujumbe ule ukamfungua macho


"jamaa yangu" akakumbuka jinsi
alivyowaona wale maafisa usalama
walivyotoka kwenye chumba cha
maiti wakiwa wametaharuki

Muhudu alimwambia Yule


mwanajeshi aliye kwenye mpango
wa mapinduzi kuwa, Maafisa
vipenyo waliusachi mwili wa
KOMANDOO MOHAMED MUSSA
TAMIMU na kuna karatasi
walimkuta nayo
TAMIMU(kumbukeni TAMIMU ndio
alikuwa mtunza kumbukumbu wa
vikao) Jamaa baada ya kuambiwa
hivyo akatoka nduki

Jamaa haraka akaenda kuwacheki


"waasi" wenzake kwenye mpango
ule majumbani mwao lakini
hakuwakuta,hilo halikumtatiza sana
kwani walishakubaliana kuwa
wakishakutana RV haikutakiwa
yeyote kurudi nyumbani kwake
mpakaka "H Hour"

"H Hour" lilikuwa ni neno lao la


uficho lililokuwa likimaanisha "Muda
wa kuanza mashambulizi"

Mashambulizi haya yalipangwa


kuwa, baada ya mdunguaji kumpata
"mzee",Vikosi vyote kuanzia
Mizinga,Anga,maji na miguu
vilitakiwa "kuengage" na kuanza
kushika maeneo ya muhimu.

Jamaa akaamua kurudi kule


RV(Kinondoni Mkwajuni) na
alipofika akakuta nyumba nzima
imezungukwa na askari wengi
sana,wakiwemo wenye Uniforms na
wasio na Uniforms.

Kwa upande Mwingine,baada ya


Purukushani baina ya TAMIMU na
maafisa vipenyo, MR X alimwamuru
mkuu wa polisi atume askari
wailinde ile nyumba na kumkamata
na kumhoji mtu yeyote ambaye
angekuwa anaingia au kutoka
katika nyumba ile.

Mkuu wa polisi akayashusha


maagizo yale Kituo cha Polisi
Oysters Bay na maelekezo yale
akaachiwa SAJENTI JEREMIAH
ambaye alituma askari wawili Wote
wakiwa ni DETECTIVE
CONSTABLES SHINDO
MWALUKA na HARIRI LOWOO
kwenda kulinda nyumba ile ya
Mkwajuni.

Hawa DETECTIVE CONSTABLES


wakiwa lindo ndipo alipofika Mtu
mmoja mnene mweusi(Captain
METUSELA SULEIMAN
KAMANDO) ndipo alipofika pale na
kusema anataka kwenda kumuona
"mpwa" wake aliyedai yuko ndani ya
nyumba ile.

"Jamaa yangu" alikuwa kajibanza


sehemu tu kwa mbali na
alishuhudia jinsi "mzee wa
mipango" mwenzake Captain
METUSELA SULEIMAN KAMANDO
akiwekwa chino ya Ulinzi ma
baadae akamwona "mwenzake"
mwingine Luteni CHISTOPHER
KADEGO naye akifika pale na
kuwekwa chini ya ulinzi.

Baadae wakafika pale wadada


wawili waliosema wanamuulizia
ndugu yao binti aitwaye
HOPE(alikuwa mpenzi wa
Komandoo TAMIMU) nao
wakawekwa chini ya Ulinzi.

Hadi kufikia hapo jamaa akajia


"mission" imefail kwa sababu
waliokamatwa walikuwa ni
wataalamu wa mizinga
waliowategemea sana.
Watu wale wote walichukuliwa na
kupelekwa kwa mkuu wa Upelelezi
wa kituo cha Oyster bay ASP DAUD
MFALINGUNDI.

"Jamaa yangu" aliweza kuwaona


wenzake kwenye mission wakiwa
nao wamejibanza maeneo tofauti
wakishuhusia "picha zima" na
akaamua kuwafata na kuwaeleza
alichokijua.

Jamaa anasema tayari ilikuwa


imeshatimia saa 2 usiku na baada
ya mashauriano na wenzake akajua
hawangeweza kufanya lolote
kuokoa mpango wao bali sasa
ilitakiwa kila mmoja apiganie nasfi
yake.

Jamaa akaanza kuwawaza Mke


wake na binti yake wa mwaka
mmoja.

Story hii ni ndefu kwa hakika.

Mjue Watu wa usalama walikuwa


katika wakati Mgumu sana kubaini
wahusika wote wa Mpango ule na
hali ya Kuaminiana ndani ya
vyombo vya usalama ilijitokeza kwa
kila mtu akimshuku mwenzake
inawezekana alikuwa ni sehemu ya
mpango ule. Hali hii ilizidi
kujibainisha baada ya baadhi ya
waasi waliokuwa wamewekwa chini
ya Ulinzi,kufanikiwa kutoroka.

Ndio,Capt. EUGENE MAGANGA na


Lt. CHRISTOPHER KADEGO
walitoroka chini ya Ulizi,wakatumia
gari la mkaa kusafiri hadi
Tanga,Mombasa na Kuishia
Nairobi.

Kama hiyo haitoshi, PIUS


MUTAKUBWA LUGANGIRA
aliyekuwa kinara wa kundi lile
haramu, na HATIBU HASSAN
GANDHI aka Hatty MCGhee
walitoroka gerezani Keko na wao
pia Kukimbilia Kenya. Sasa Tujiulize
hawa watu wenye kesi nzito hivyo,
wangewezaje kuukimbia Ulinzi bila
kuwa na hujuma?

Tuachane na hao watoro kwani


tutawarudia baadae.

"Jamaa yangu" Anasema yeye


hakuona sababu za kukimbia nchi
(kama baadhi ya wenzake
walivyofanya)na kuiacha familia
yake.

Anasema Yeye alikamatwa saa 9


usiku siku hiyo hiyo na kupelekwa
police "Central"

Alishangaa kumkuta mdogo wake


naye akiwa tayari amekamatwa na
kuwekwa mle ndani. Mdogo wake
alikuwa na cheo cha Captain na pia
alikuwa ni rubani wa ndege za jeshi.

Jamaa akajua baadar kuwa Mdogo


wake alikamatiwa kwenye Kikosi
cha Anga "Airwing"

Pia akaelewa kwa nini wanajeshi


walipajua kwake na kwenda
kumkamata(hawakuwa wakipajua
kwake). Kumbe mdogo wake baada
ya "kuminywa" ndiye aliyewatajia
anapoishi kaka yake.

Mle mahabusu walikuwa wamejaa


wanajeshi kibao na baadhibya raia
waliohusishwa na jaribio lile.
Jamaa anasema Siku ya
kukamatwa kwake familia yake yote
ilitolewa nje ya nyumba,kisha
nyumba ikafungwa. Kwesho yake
nyumba yake ilipekuliwa yeye
akiwepo lakini hawakukuta
chochote.

Jamaa aliambiwa anashtakiwa na


mkuu wa majeshi lakini hakutajiwa
kosa lake lakini baade akagundua
kuwa alikamatwa kwa kuwa jina
lake na cheo chake lilikutwa kwenye
orodha ya majina aliyokutwa nayo
Marehemu KOMANDOO
MOHAMED MUSSA TAMIMU
alipopekuliwa.
Anasema ndani ya mahabusu
hakupata mateso yoyote zaidi ya
kutishiwa maisha yake na ya familia
yake.

Kilichowaokoa wasiteswe ni ile


skendo iliyotokea mwaka mmoja tu
uliokuwa umepita ambapo kuna
watu waliteswa na kufa kashfa
iliyomfanya aliyekuwa Waziri wa
Mambo ya ndani,Rais mstaafu Ali
Hassan Mwinyi kujiuzuru pamoja na
aliyekuwa waziri wa Utawala bora
SIYOVELWA.

Kutokana na kashfa hiyo RPC na


maafisa wengine wa Polisi na
Magereza walishtakiwa na
kuhukumiwa vifungo vya kati ya
miaka 3 hadi 8.

Kuhepuka hali hii isijirudie ndio


maana hawakuteswa.

Anakumbuka siku ya tano tangu


akamatwe,Kuna afisa usalama wa
taifa alienda Maabusu kwa nia ya
kumchukua kwa mahojiano lakini
mkuu wa kituo SSP MWAMAKUSA
alimgomea kata kata.

Baadae jamaa akarudi na mabosi


wawili kutoka Ikulu lakini bado SSP
MWAMAKUSA akaendelea na
msimamo wake.
Zikapita siku mbili bila
mahojiano,ndipo jamaa alikuja
kugundua kulifanyika kikao
kilichohusisha vyombo vyote vya
Usalama na ikaamuliwa mahojiano
yote ni lazima yafanyike chini ya
Uangalizi wa Maafisa wa Polisi.

Watu wa kwanza Kutorokea Kenya


walikuwa ni Lt. CHRISTOPHER
KADEGO na Capt. EUGENE
MAGANGA. Walikaa kwa Miezi
kumi kama wakimbizi wa kisiasa pia
wakipanga mbinu mpya za
mapinduzi.

MAGAGA akaendea kudai,kwa


muda wote huo hawakujua
chochote kilichokuwa kinaendelea
kwa wenzao waliowaacha Dar es
salaam. Wao walienda kwenye
Embassy ya marekani pale Kenya
na kuomba wawasaidie kuanzisha
kambi pale kwa ajiri ya kuja tena
kufanya mapinduzi lakini
walikataliwa.

Siku moja kwenye pita pita zao


mitaa ya Nairobi wakashangaa
wanakutana na wenzao wawili
waliowaacha Dar. Watu hao ni
PIUS MUTAKUBWA
LUGANGIRA(Uncle Tom) na
HATIBU HASSAN
GANDHI(MCGhee) waliokuwa
wametoroka gereza la keko.
Kwa kuwa Uncle Tom alikuwa ni
mfanya biashara mkubwa pale
Kenya,maisha yao hayakuwa
mabaya lakini Uncle Tom
akawaambia ana wasiwasi serikali
ya kenya inaweza kuwageuka hivyo
inabidi wafanye kipango waende
Malawi.

UNCLE TOM akasafiri kwenda


Uingereza ili akirudi ashughurikie
mipango hiyo.

Ni kama machale yalikuwa


yamemcheza vile...

Mnajua wakati Ule kuna wanajeshi


wakenya wawili walikuwa
wametorokea Tanzania baada ya
jaribio lao la Kumuua rais ARAP
MOI mwaka 1982 kutofanikiwa.

Wanajeshi hao ambao ni LANCE


CORPORAL OCHUKA na
SERGEANT PANCRAS OTEYO
walipofika Tanzania walipewa
ukimbizi wa kisiasa.

Sasa kwa hatua hii kila Nchi ilikuwa


imemshika mwenzake pabaya. Kila
nchi ilikuwa "ikifuga" mahasimu wa
maraisi wa pande zote mbili.

Kilichofata ilikuwa ni mabadirishano


tu(EXTRADITION).
Wakina MAGANGA,MCGhee na
KADEGO bila kujua kama
"wameuzwa kwa bei nafuu"
walidanganywa kuwa wanapelekwa
sehemu salama zaidi hivyo
wakafungwa vitambaa kichwani na
kutiwa pingu.

Walikuja tu Kujikuta kwenye Gereza


la Isanga Dodoma. MAGANGA
alisema walikuta kuta zote za selo
yao zimepakwa kinyesi na pia
walilazwa chini na kufungwa pingu
wa siku tatu bila kuoga. Maaskari
magereza hawakuruhusiwa
kuongea nao kwani walionekana ni
watu wenye ushawishi sana.
Ilihofiwa wasije wakawashawishi
askari kujiunga nao.

Lakini MAGANGA anasema hilo


halikuwezekana kwani walifanikiwa
kuandika barua na kuwapa askari
wakaitume kwenda Ubarozo wa
Marekani.

Barua hiyo ilikuwa inaujulisha


ubalozi kuwa wamekamatwa tangu
November 1983 "kimya kimya".

Hadi muda ambao maria inawafikia


watu wa ubalozi wa marekani,tayari
ilikuwa ni October 1984 hivyo
walikuwa kwenye "Detention" kwa
muda wa mwaka mzima bila mtu
yeyote kujua zaidi ya vyombo vya
usalama vya Tanzania na Kenya.

Ni mpaka January 1985 ndipo


wahusika wote wa mpango wa
maasi yale walianza kufikishwa
mahakamni baada ya Vyombo vya
nje kuanza kupiga kelele kupinga
sheria ya "Detention" iliyokuwa
hairuhusu "HABEAS CORPUS"
Yaani mahakama kushinikiza
maabusu aachiwe bila masharti au
ashitakiwe

Kesi ilianza na walipandishwa


mahakamani jumla ya washtakiwa
30. Baina yao walikuwepo
Wanajeshi 21 na raia 9.
Kwa upande wa wanajeshi kulikuwa
na maluteni kanali 3, Meja
1,Makapteni 8,Maluteni 8, na
Sajenti 1

Major Alikuwa ni REVELIAN


BUBERWA aliyetokea Kikosi cha
MGULANI.

Sasa hapa kuna kitu nitataka


mkielewe,Haikujulikana ni kwa
sababu gani KOMANDOO
MOHAMED MUSSA TAMIMU
aliwadanganya wanamipango
wenzake kuwa HATIBU HASSAN
GANDHI aka HATTY
MCGHEE,kuwa ni mwanajeshi
mwenye cheo cha KAPTENI wakati
alijua si kweli bali ni raia tu.
HATIBU HASSAN GANDHI ambaye
kabila lake ni mbondei wa Tanga
mkoa ambao pia ndipo alitokea
TAMIMU, alikuwa ni rubani tu wa
ndenge ndogo nchini kenya na
ndipo walipokutana na TAMIMU na
kujenga urafiki hadi akamjumuisha
kwenye mipango hii.

Anguko kubwa la mipango hii


lilitokea kwa huyu HATTY MCGHEE
ambaye inasemekana kwa kuwa
alikuwa ni raia,hakujua "protocals"
za kutunza siri. Ndipo akaropoka
aliyoropoka kwa MHANDO ambaye
alikuwa ni dereva taxi na mipango
ikaharibikia hapo.
Raia waliofikishwa mahakamani
walikuwa ni,PIUS MUTAKUBWA
LUGANGIRA(40),HATIBU HASSAN
GANDHI(37),CHRISTOPHER
PASTOR NGAIZA(52)Huyu alikuwa
mshauri wa Nyerere,JAYANTILAL
PRAGJI RAJAN(53),ROBERT
BAYONA(29)Huyu alikuwa Meneja
mauzo kiwanda cha viatu cha
Tanzania(BORA)

Wengine ni,THADEO BONIFACE


MUTAKWAYA
BUNGINGO(37),Huyu alikuwa wa
UDSM,RAMADHANI
OTTO(46)huyu alikuwa fundi
makanika mkazi wa Ilala Bungoni,
GEORGE BANYIKWA na ZERA
BANYIKWA hawa wanandoa
walikuwa ndio wenye nyumba ya
Drive Inn ambao vikao vilikuwa
vinafanyikia.

Kesi hii Ilikuwa na mvuto sana


mahakamani,Ukizingatia ilikuwa ni
zamani,lakini taifa letu lilikuwa
limepika wasomi walioiva. Sio
upande wa mawakili wa serikali
wala wa Utetezi kila upande ulikuwa
umejitosheleza na ulikuwa ukijenga
hoja nzito sana mbele ya jani
MZAVAS.

Hadi Kesi inafikia hatima yake Ni


watu 8 tu ndio waliokutwa na hatia
na kuhukumiwa vifungo vya maisha.
Ni mpaka mwaka 1995 ikiwa
ambapo rais Mwinyi aliwaachia kwa
msamaha wafungwa wote
waliohusika na kesi hii.
MWISHO

You might also like