You are on page 1of 23

AZIMIO LA ARUSHA

DIRA YA MAPAMBANO YA
WAVUJAJASHO

Kimehaririwa na
Sabatho Nyamsenda

1
AZIMIO LA ARUSHA
DIRA YA MAPAMBANO YA
WAVUJAJASHO

Kimehaririwa na:
SABATHO NYAMSENDA

2 iii
YALIYOMO
SURA YA KWANZA:
TUMWENZI MWALIMU NYERERE KWA KUDAI
AZIMIO LA ARUSHA....................................................................... 1-14

SURA YA PILI:
AZIMIO LA ARUSHA: UJAMAA NA KUJITEGEMEA............. 15-35

NYONGEZA:
BADO NATEMBEA NALO..................................................................36

Kitabu hiki kiliandaliwa kwa ajili ya Kongamano la Kumbukizi


ya miaka 19 baada ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius
K. Nyerere, lililofanyika tarehe 14 Oktoba 2018 jijini Dar es
Salaam.

2018

iv v
1
SURA YA KWANZA

TUMWENZI MWALIMU NYERERE KWA


KUDAI AZIMIO LA ARUSHA

M
waka 1967 utabaki kuwa na historia ya kipekee Tanzania
Bara. Ni mwaka ulioleta matumaini mapya kwa
Watanzania wa tabaka la chini; matumaini ya ujenzi
wa nchi mpya, yenye mfumo wa utu, uhuru na usawa.
Japokuwa Tanzania Bara ilijipatia uhuru wake 9 Desemba 1961, uhuru
huo haukuonekana kama ni uhuru kamili. Tanzania Bara iliendelea
kunyonywa na kuporwa na nchi za kibeberu chini ya mfumo
wa ukoloni mambo leo. Na ndani ya nchi viongozi walioongoza
mapambano ya uhuru sasa wakawa watawala serikalini: mawaziri,
makatibu wakuu, wabunge, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya,
mabalozi, n.k. Tena walipambana ili wazungu wote waliobaki
kama watumishi wa umma warejeshwe makwao ili nafasi hizo
zijazwe na Watanzania wenyewe, chini ya mpango uliojulikana
kama Africanisation (kwa Kiswahili inatamkwa ‘Afrikanaizesheni’).
Viongozi walivyozidi kuonja utamu wa madaraka, ndivyo
walivyojitenga mbali zaidi na wanyonge. Wakawa wakitembelea
magari ya kifahari aina ya Mercedes Benz, wakajenga majumba ya
kupangisha na kupewa zawadi ya hisa katika kampuni za mabeberu.

Kwa ufupi, viongozi wakaanza kutumia nafasi zao kujilimbikizia


mali ilhali wananchi wa tabaka la chini wakiendelea kuishi katika
umaskini. Ndio maana ilianza kuibuka minyukano ya kitabaka
kati ya watu wa tabaka la chini na viongozi walioingia madarakani
baada ya uhuru kupatikana. Wananchi wa kawaida wakaanza
kuwaita viongozi “wabenzi” (kutokana na aina ya magari ya kifahari
waliyotembelea) na “manaizesheni” (kuonyesha kuwa wao pekee,
na sio wanyonge, ndio waliofaidi matunda ya Africanisation).

vi 1
Na wao wenyewe, wananchi wa tabaka la chini, wakasema kuwa Ujio wa Azimio la Arusha
wamechoka kuwa “Baba Kabwela”. Baba Kabwela (maana yake
baba karejea) ni wimbo wenye asili ya Pwani alioimbiwa Mwalimu Haya yote ndiyo yaliyomsukuma Mwalimu Nyerere kuchukua hatua
Nyerere wakati akirejea kutoka Umoja wa Mataifa ambako alikwenda za kimapinduzi zaidi, ili kuuzatiti uhuru wa Tanzania na kuleta
kutoa hoja za kudai uhuru. Baada ya uhuru kupatikana, wananchi usawa miongoni mwa watu wake. Mwaka 1967 alikiongoza chama
wa kawaida pia walikuwa wakikusanywa ili kuwashangilia chake, TANU, kutangaza Azimio la Arusha juu ya Siasa ya Ujamaa
viongozi walipofanya ziara katika maeneo yao. Ni kutokana na hilo na Kujitegemea. Azimio la Arusha lilitangaza vita ya kimapinduzi:
ndio likazaliwa jina “kabwela” (wingi “makabwela”), ambalo lilikuja
kumaanisha wananchi wa tabaka la chini. Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyonywa kiasi cha
kutosha, na tumepuuzwa kiasi cha kutosha. Unyonge wetu
Waraka mmoja wapo wa kuonyesha hasira za makabwela dhidi ya ndio uliotufanya tuonewe, tunyonywe, na kupuuzwa. Sasa
wabenzi ni barua iliyoandikwa na mwananchi mwenye hasira kwenda tunataka mapinduzi; mapinduzi ya kuondoa unyonge ili
kwa Mwalimu Nyerere mwezi Aprili 1963. “Tunasikitika kututawala tusionewe tena, tusinyonywe tena na wala tusipuuzwe
kama ng’ombe kusudi mawazili wote wapate vitambi,” barua hiyo ilisema. tena.
Mwananchi huyo alionyesha kuwa gharama za maisha na huduma
za jamii zinazidi kwenda juu ilhali viongozi wakizidi kuneemeka: Unaweza kufikiria furaha waliyokuwa nayo makabwela, ambao
waliandamana nchi nzima kuliunga mkono Azimio la Arusha. Kwao
Wewe unatutesa wenzio kama sio wanadam ukitudanganya wao, Azimio lilikuwa ni silaha ya ukombozi, kuelekea nchi ya utu,
kuwa nawakomboa utumwani kumbe unatuangamiza. usawa na uhuru.
Kwa mfano, hata wewe mwe[nye]we wakati unasoma
wangemwambia baba yako alipe Shs 900/= sijui kama Azimio la Arusha lilijengwa katika misingi mitano ya kiitikadi.
ungesoma. Sasa watasoma watoto wa mawazili tu1
(1) Kuubomoa ubepari na kujenga ujamaa kwa kuziweka njia kuu za
Barua hii inaonyesha wazi mvutano wa kitabaka kati ya makabwela uzalishaji mali mikononi mwa wakulima na wafanyakazi.
na wabenzi. Kama inavyofahamika, mabepari hawafanyi kazi. Wao
hufanyiwa kazi na hutajirika kutokana na kuwanyonya watu
Tanzania pia ndio ilikuwa makao makuu ya Kamati ya Ukombozi wa wanaofanya kazi. Wafanyakazi huendelea kutaabika kwa
Afrika (African Liberation Committee) na mwenyeji wa mavuguvugu umaskini. Kinachowapa mabepari nguvu ya kuwanyonya
ya kupigania ukombozi Kusini mwa Afrika. Mwalimu Nyerere wafanyakazi ni kwa sababu njia kuu za uzalishaji mali
alichukua msimamo thabiti wa kuunga mkono ukombozi wa Kusini wanazimiliki mabepari. Kwa hiyo, kiini cha ubepari ni umiliki
mwa Afrika, ambako mifumo ya ukaburu na ukoloni mkongwe binafsi wa njia kuu za uzalishaji mali. Ili kuubomoa mfumo huo
ilikuwa ikiendelea. Na ni kutokana na msimamo huo ndio maana wa kinyonyaji ni lazima kuziweka njia kuu za uzalishaji mali
Tanzania ikajikuta katika migogoro ya kidiplomasia na nchi za mikononi mwa tabaka linalovujajasho.
kibeberu, ambazo zilikuwa zikishirikiana na tawala za kikaburu
na kikoloni Kusini mwa Afrika. Hali hii ilipelekea kusitishwa kwa Njia kuu za uzalishaji mali zilizotajwa katika Azimio la Arusha
uwekezaji, mikopo na misaada kutoka kwa mabeberu. ni kama vile viwanda vikubwa, mashamba makubwa, mabenki
makubwa, migodi mikubwa, n.k.

1 Nakala ya barua hii inapatikana katika nyaraka za Mwalimu Nyerere zilizokusanywa na Kavazi la Mwalimu Nyerere.

2 3
(2) Kuubomoa mfumo wa ukoloni mamboleo kimataifa kwa kujenga taifa (4) Msingi wa maendeleo ni wakulima na wafanyakazi.
linalojitegemea kiuchumi na kisiasa. Azimio liliweka bayana kuwa gurudumu la maendeleo sio
tabaka la mabepari bali ni tabaka la wavujajasho, yaani wakulima
Dunia imegawanyika katika makundi makubwa mawili. Kwa na wafanyakazi. Kwa maana hiyo, ni lazima vyombo vyote
upande mmoja zipo nchi KOMBA KOMBA na kwa upande vinavyojenga ujamaa, na hasa chama na serikali, kushikiliwa na
mwingine zipo nchi OMBA OMBA. Nchi komba komba ni nchi tabaka la wavujajasho.
za kibeberu, ambazo zimepiga hatua kubwa katika maendeleo
ya kiuchumi, lakini maendeleo hayo yamepatikana kwa kupora (5) Miiko ya uongozi.
rasilimali za nchi maskini. Nchi omba omba ni tegemezi kiuchumi Miiko ya uongozi ni kati ya misingi muhimu sana ya Azimio la
na watu wake walio wengi ni maskini. Japokuwa nchi omba Arusha. Iliwazuia viongozi kuwa mabepari au makabaila. Ndio
omba nyingi zina utajiri wa rasilimali pamoja na nguvu kazi, maana ikapiga marufuku viongozi kumiliki majumba makubwa
lakini mwishoni nguvu kazi hiyo pamoja na rasilimali hizo ya kupangisha, kuwa na mishahara miwili au zaidi, au kumiliki
huishia kunyonywa na kuporwa na nchi komba komba. Mifumo hisa au wadhifa wa ukurugenzi katika kampuni za kibepari.
mbali mbali ya kiporaji imetengenezwa na kwa kiasi kikubwa Kwa maana nyingine, miiko ya uongozi ililenga kuhakikisha
imehalalishwa kisheria na kulindwa na dola, pamoja na taasisi kuwa viongozi wa chama na serikali wanakuwa ni wakulima na
zingine za kimataifa. wafanyakazi, na sio vinginevyo.

Kwa hiyo, nchi yoyote inayotaka kujikwamua kutoka katika Utekelezaji wa Azimio
mfumo wa kinyonyaji wa kimataifa basi sharti ijenge uchumi
unaojitegemea. Uchumi unaojitegemea huendeshwa kwa Utekelezaji wa ujamaa katika Tanzania ulibadili sana hali ya
sehemu kubwa na mapato ya ndani badala ya kutegemea maisha ya Watanzania. Kwanza, msisitizo mkubwa wa maendeleo
mikopo na misaada ya nchi komba komba, na pia huzichakata uliwekwa vijijini na zikafanyika jitihada za dhati kabisa kuhakikisha
malighafi inazozalisha ili kukidhi mahitaji ya ndani badala ya kuwa huduma za msingi zinapatikana vijijini. Wasomi na wataalam
kutegemea soko la kinyonyaji la nchi komba komba. Mfumo walihimizwa kuishi vijijini ili wawatumikie wavujajasho.
wa utegemezi wa kiuchumi huzalisha pia mfumo wa utumwa
wa kisiasa, ambapo nchi omba omba hulazimishwa kufuata Pili, utoaji wa huduma za jamii kwa raia wote bila malipo, hasa elimu
matakwa ya nchi komba komba. na afya. Tofauti na sasa ambako huduma za kijamii zimegeuzwa
kuwa bidhaa na wanaozimudu ni wenye pesa, wakati wa Azimio
(3) Demokrasia ya wavujajasho. la Arusha huduma hizo zilipatikana bila malipo. Sambamba na
Demokrasia inayozungumziwa katika Azimio la Arusha ni hilo, serikali ilianzisha ruzuku za kila aina, tangu zile za pembejeo
demokrasia ya wavujajasho, yenye lengo la kuwapa nguvu kwa wakulima vijijini hadi za vyakula kwa wakazi wa mjini, jambo
ya kudhibiti uzalishaji wa kijamaa wa kiuchumi na kushiriki ambalo lilisaidia sana kuboresha hali za maisha za wananchi walio
moja kwa moja katika maamuzi ya kisiasa katika maeneo yao wengi.
ya kazi na makazi, na pia katika taifa kwa ujumla. Kwa hiyo,
badala ya kutegemea amri na hisani za watawala, wananchi Tatu, ujenzi wa viwanda na miundo mbinu, zikiwemo reli, barabara,
watajiongoza wenyewe kupitia vyombo vyao vya kidemokrasia, hospitali, vyuo na shule, n.k. Msisitizo mkubwa wa viwanda
kama mkutano mkuu wa kijiji, vyama vya ushirika, vyama ulikuwa ni kuchakata malighafi ndani ya nchi, na kwa sehemu
vya wafanyakazi, n.k. Mwalimu Nyerere aliifafanua vema fulani tulifanikiwa katika hilo. Mashirika ya umma yapatayo zaidi
demokrasia hii katika maandiko yake kadhaa, ikiwemo “Uhuru ya 400 yalianzishwa. Kubwa kuliko yote, ni kwamba sehemu kubwa
na Maendeleo” pamoja na “Ujamaa Vijijini.”

4 5
ya viwanda vikubwa na miradi mingine vilikuwa chini ya mikono kweli, Tanzania iliingia gharama kubwa sana kupigana vita dhidi ya
ya serikali. Kipindi kati ya 1967 na 1979 kilikuwa na mafanikio utawala wa Idi Amin mwaka 1978 na 1979. Ni baada ya vita hiyo
makubwa kiuchumi. Ukuaji wa uchumi ulikuwa kati ya asilimia 4 ndipo nchi ikiwa katika hali ngumu ya kiuchumi, bei za malighafi
na 6 na ulifikia asilimia 9.4 mwaka 19792. zinazozalishwa zikizidi kuporomoka, huku bei za bidhaa toka nje
zikizidi kupanda. Nchi ikaingia katika kipindi kigumu cha kiuchumi,
Nne, Azimio lilikuwa nguzo kuu ya ujenzi wa umoja wa kitaifa wa ambapo bidhaa za msingi zikawa hazipatikani na baadhi ya viwanda
watu walio huru, wenye kujali utu na wenye msimamo thabiti wa kusitisha uzalishaji kutokana na kukosekana kwa fedha za kigeni za
kupambana na ufedhuli popote unapojitokeza – iwe ndani ama nje kuagiza vipuri toka nje.
ya Afrika.
Mabeberu walipata mwanya mzuri wa kuibana Tanzania iachane
Licha ya mafanikio hayo na mengine mengi, yapo maeneo ambayo na ujamaa. Huko Marekani Ronald Reagan alikuwa amechanguliwa
utekelezaji wa Azimio ulikuwa na mapungufu. Pengine kati ya kuwa rais mwaka 1980, na mwaka mmoja kabla hapo, Margareth
mapungufu makubwa ni kwamba kazi ya utekelezwaji iliachwa Tatcher alikuwa amechaguliwa kuwa waziri mkuu wa Uingereza.
mikononi mwa wale wale wabenzi na manaizesheni. Yaani, kabla ya Wawili hawa walikuwa ni wahafidhina, wenye lengo la kurejesha
Azimio hawa ndio waliokuwa wakijilimbikizia mali, je inawezekanaje nguvu zaidi kwa tabaka la mabepari. Katika nchi zao wenyewe,
wao tena ndio wakawa watekelezaji wa Azimio? Kwa hiyo, wabenzi walishambulia vyama vya wafanyakazi, wakabinafsisha mashirika
hawakuachia nguvu ya maamuzi irejee mikononi mwa makabwela. ya umma, wakaongeza kodi kwa wafanyakazi huku wakitoa unafuu
wa kodi kwa mabepari, na wkubidhaisha huduma za jamii. Sera hizi
Pia, japokuwa Azimio lilisisitiza sana juu ya dhana na haja ya ndizo zilijulikana kama sera za soko huria au sera za uliberali mamboleo.
kujitegemea, bado halikuweza kuondoa utegemezi kwa nchi za
komba komba. Bado nchi iliendelea kusafirisha malighafi kwenda nje, Katika Afrika Tanzania ndiyo ilikuwa mlengwa mkuu wa shinikizo
huku ikipokea mikopo na misaada kutoka kwa mabeberu alimradi tu la mabeberu. Ama moja kwa moja au kupitia taasisi za kimataifa,
misaada hiyo isiwe na masharti yoyote. Na japokuwa vilianzishwa mabeberu wakaanza kuibana Tanzania na kuilazimisha itekeleze
viwanda, bado nchi haikuweza kujitegemea kiteknolojia, hivyo sera hizo za kiuaji na kijambazi. Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF)
kuendeleza utegemezi kwa mabeberu. ndilo haswa lililotumika kuibana Tanzania ili iachane na ujamaa.
Mwalimu aliigomea IMF huku akiuliza, “When did the IMF become an
Kupinduliwa kwa Azimio ‘International Ministry of Finance’? When did nations agree to surrender
to it their power of decision making?” (Kwa tafsiri isiyo rasmi, “Tangu
Azimio halikufa lenyewe kama ambavyo mabwanyenye na vijibwa lini IMF imegeuka kuwa Wizara ya Kimataifa ya Fedha? Tangu lini
vyao wanajaribu kutuaminisha. Azimio lilihujumiwa na kuuawa. mataifa yalikubali kusalimisha mamlaka yao ya kujiamulia mambo
Nguvu mbili kubwa za kitabaka zilishirikiana kulihujumu na kuliua yao kwa IMF?”)
Azimio. Ya kwanza, ni nguvu ya kibeberu kutoka kwa nchi komba
komba. Zilitumika nguvu zote, tangu vitisho vya uvamizi wa kijeshi Na hapo ndipo Mwalimu akasisitiza kuhusu msimamo wa Tanzania:
hata vikwazo vya kiuchumi, kuhakikisha kuwa Azimio linauawa.
Tanzania haiko tayari kushusha thamani ya fedha yake eti
Tusisahau kuwa ni mabeberu, hasa serikali za Uingereza na Israeli, kwa sababu hili ndilo suluhisho la kimapokeo la ‘Soko Huria’
ndio waliochangia kumpindua Milton Obote huko Uganda, kisha kwa kila kitu bila kujali usahihi wa msimamo wetu. Tanzania
kupandikiza serikali ya kifashisti ya Idi Amin ili fashisti huyo haiko tayari kusalimisha haki yake ya kudhibiti bidhaa
auangushe ujamaa nchini Tanzania kwa uvamizi wa kijeshi. Na ziagizwazo toka nje, kwa hatua zilizolenga kuhakikisha kuwa
2 Daudi R. Mukangara, “The Development of Anti-Dependence Policies in Tanzania.” The African Review 24, no 1&2 (1997): 1.

6 7
tunaagiza dawa za hospitali badala ya vipodozi, au mabasi wake. Miiko ya uongozi ilipigwa teke rasmi mwaka 1991 na hivyo
badala ya magari ya watu binafsi kwa ajili ya vigogo. Serikali kuruhusu viongozi kujilimbikizia mali, hali iliyosababisha ufisadi
yangu haiko tayari kuachana na jukumu letu la msingi la wa kutisha.
kutoa elimu ya msingi kwa kila mtoto, huduma za matibabu
ya msingi na maji safi na salama kwa ajili ya watu wetu Akiwa nje ya madaraka, Mwalimu aliendelea kuzipinga sera hizo za
wote. kikatili. Sakata la uuzwaji wa NBC lilimpeleka hadi makao makuu
ya IMF, jijini New York, kupinga uuzwaji huo. Akihutubia maelfu
Katika hotuba hiyo, iliyotolewa katika hafla ya kuukaribisha ya wananchi waliokusanyika kumsikiliza mjini Mbeya, Mei 1, 1995,
Mwaka Mpya 1980 iliyoandaliwa kwa ajili ya mabalozi, Mwalimu Mwalimu alisema kuwa ubinafsishaji ni “unyang’anyi tu”, ambao
aliunguruma: “Na juu ya yote hayo tutaendelea na jukumu letu la unapora “mali yetu wote” na kumpatia mtu mmoja au kakundi ka
kujenga jamii ya kijamaa”. watu wachache. “Lazima tufanye tofauti baina ya kutajirisha watu
wachache na kuleta manufaa ya watu wengi”. Alifafanua kuwa sera
Mwalimu hakufanikiwa katika harakati zake za kuizima IMF na ya ubinafsishaji “itazaa mamilionea Tanzania. Lakini watakuwa ni
kuzizika sera za uliberali mamboleo. Ndani ya Chama chake na mamilionea wachache. Lakini itazaa maskini Tanzania, watakuwa
serikalini kulikuwa na kundi kubwa lililoshirikiana na wahujumu wengi sana.”
uchumi kuuteketeza ujamaa. Kundi hili liliungwa mkono na IMF na
nchi za kibeberu lilizidi kupata nguvu zaidi. Ibara ya 52 ya Mwongozo Mapambano ya wavujajasho
wa Chama Cha Mapinduzi wa mwaka 1981 iliweka bayana nguvu Waathirika wakuu wa sera za uliberali mambo leo walikuwa ni
ya kundi hili: makabwela, watu wa tabaka la chini. Wabenzi na manaizesheni
waliendelea kuneemeka katika fungate yao na mabeberu wa nje na
Leo ubepari una vishawishi vingi zaidi kuliko ulivyokuwa vibaraka wao humu nchini. Wavujajasho duniani kote hawakuzikubali
kabla ya Azimio la Arusha kwa sababu pamoja na kwamba sera hizi, bali walipambana kila namna kuziangusha. Nchini Tanzania,
sasa tuna sekta kubwa ya umma lakini kutokana na udhaifu kulikuwepo na mapambano yaliyoongozwa na wafanyakazi, yakiwa
wa kutokupambana nao, ubepari umefaulu kujipanua na na shabaha ya kuzuia ubinafsishaji wa mashirika ya umma. Katika
kujipenyeza hata ndani ya sekta yenyewe ya umma. Na baadhi ya mashirika kama TANESCO, wafanyakazi walifanikiwa
ndiyo maana ubepari sasa unathubutu kujitokeza hadharani kuzuia ubinafsishaji usifanyike – japokuwa hatimae zilibuniwa mbinu
kuukashifu ujamaa, kubabaisha baadhi ya viongozi na za kuyafaidisha makampuni binafsi ya kuzalisha umeme. Katika
kututaka tubadilishe siasa yetu. mashirika mengine, kama Shirika la Reli Tanzania, wafanyakazi
waliweza kulirejesha nyuma gurudumu la ubinafsishaji na hivyo
Japokuwa zilifanyika juhudi ya kuzima nguvu ya kundi hili shirika hilo likarejeshwa serikalini baada ya mapambano ya muda
kupitia vita dhidi ya uhujumu uchumi mwaka 1983 na 1984, lakini mrefu. Kwingineko, ubinafsishaji ulifanyika kwa mabavu ya dola,
muunganiko wa nguvu kati ya mabeberu wa nje na vibaraka ikiwemo benki ya NBC ambayo iliuzwa kwa bei ya kutupa. Kama
wao nchini ndio ulioibuka na ushindi. Mwalimu alipoondoka lilivyoripoti gazeti la Raia Mwema toleo na. 381 la Novemba 26, 2014:
maradakani mwaka 1985, serikali ya Mwinyi ilisaini mkataba na IMF
mwaka uliouatia, ikikubaliana na masharti yote ambayo Mwalimu WAKATI Benki ya NBC ikiuzwa kwa wawekezaji wa Afrika
Nyerere alikuwa ameyakataa hapo awali. Na hapo ndipo zikaanza Kusini mwaka 2000, kwa thamani ya shilingi bilioni 16,
zama mpya za ubinafsishaji wa mashirika ya umma, uporaji wa yenyewe ilikuwa na kiasi cha shilingi bilioni 151 taslimu
machimbo na ardhi ya wachimbaji wadogo na wakulima wadogo, katika akaunti zake mbalimbali duniani... Kiasi hicho cha
serikali kujiondoa katika utoaji wa huduma za msingi kwa wananchi fedha ni mbali na thamani ya majengo na mali nyingine za

8 9
NBC ilizokuwa ikimiliki wakati huo, na kwa maana hiyo, Nguvu ya muungano tunaiona kwa mabepari ambao wameungana
serikali iliuza benki hiyo kwa kiasi cha asilimia kumi ya kiasi kwa ajili ya kututawala na kutunyonya. Wanapokuja nchini,
ilichokuwa nacho kama akiba. wanakuja chini ya chombo kinachoratibiwa, kama SAGCOT, na
sauti yao inakuwa ni moja. Lakini wazalishaji wadogo hawana sauti
ya pamoja. Watu wa Kilosa wanaporwa ardhi, sisi wengine hatusikii.
Mapambano ya wavujajasho pia yalichukua sura ya migomo katika
Tunaona ni tatizo lao. Watu wa shamba la Kidago katika kijiji cha
maeneo ya kazi ili kudai malipo yenye kuwawezesha wafanyakazi
Lukonde wananyanyaswa na kufungwa lakini sauti zao hatuzisikii.
kuishi, pamoja na kulinda ajira zao. Katika maeneo ya migodi,
Tunaona ni tatizo lao wenyewe. Pia, tumegawanywa kwenye nchi.
wachimbaji wadogo walipambana kuyalinda machimbo yao
Hatuzungumzi kama wanyonge wa Afrika. Kumbuka wakoloni
yasiporwe na kampuni kubwa za kibepari kutoka nje ya nchi.
walitugawanya katika nchi ili watutawale na wapore rasilimali zetu
kiurahisi3.
Katika mgodi wa Bulyanhulu, ambao uligunduliwa na wachimbaji
wadogo wenyewe mwaka 1975, kampuni toka ughaibuni iliwaondoa
Halikadhalika, kukosekana kwa dira inayoeleweka ili kuongoza
wachimbaji wadogo wapatao laki tano kwa mabavu ya dola. Katika
mapambano ya wavujajasho kumesababisha mapambano yatekwe
purukushani hizo inasadikika kuwa watu 54 walifukiwa wakiwa hai.
nyara na mabepari, ama wavujajasho wachonganishwe ili wapigane
Hayo sio maneno yangu, bali yamo katika ripoti ya utafiti uliofanywa
wao kwa wao badala ya kuunganisha nguvu dhidi ya adui yao
na Brian Cooksey, iitwayo The Investment and Business Environment
wa kitabaka. Si ajabu kuona wakulima na wafugaji wakiingia
for Gold Exploration and Mining in Tanzania (kwa tafsiri isiyo rasmi
katika mapigano na hata kumwaga damu ilhali wawekezaji
“Mazingira ya Uwekezaji na Biashara kwa ajili ya Utafutaji na
wakubwa waliopora ardhi yao wakiendelea kutamba. Je, mgambo
Uchimbaji Dhahabu Tanzania”).
wanapowapiga mama ntilie au wamachinga na hata kuwanyang’anya
bidhaa zao, wanafanya hivyo kwa manufaa ya nani? Bila shaka
Wazalishaji wadogo vijijini nao walijikuta wakilazimika kupambana
mgambo wanaelewa vema kuwa bila ya kuwepo mama ntilie ndani
dhidi ya wimbi kubwa la uporaji wa ardhi kwa ajili ya uwekezaji au
ya jiji, mgambo, ambae ni askari kibarua tu, hawezi kumudu kula
hifadhi za misitu. Mijini, wamachinga na mama ntilie wamekuwa
katika migahawa mikubwa.
wakipambana dhidi ya uporaji wa maeneo ya kazi. Vyuoni, wanafunzi
walifanya migomo kupingana na sera za ubidhaishaji elimu.
Kwa sehemu kubwa, vuguvugu la wanafunzi wa elimu ya juu
lilihama kutoka vuguvugu la kupigania maslahi ya wavujajasho
Hiyo ni mifano michache tu ya mapambano ambayo yamekuwa
na masuala ya kitaifa hadi kuwa vuguvugu la kupinga tu sera za
yakiendelea kila siku, katika maeneo mbali mbali nchini mwetu.
ubidhaishaji wa elimu. Hata katika uwanda kupinga ubidhaishaji
Hata hivyo, mapambano hayo yameendelea kubaki katika eneo
pia vuguvugu hilo limehama kutoka vuvugugu la kudai elimu bila
husika (mathalani eneo ambalo limeathirika na uporaji wa ardhi)
malipo hadi vuguvugu la kudai mikopo ya elimu ya juu. Wakati
na hayajaunganisha nchi nzima. Hii ni kusema kuwa wavujajasho
nikiingia chuo kikuu mwaka 2008 kulikuwa na mgomo mkubwa wa
wamekuwa wakipambana bila ya kuwa na umoja na mshikamano
wanafunzi katika vyuo vikuu saba vya umma, jambo lililosababisha
wa kitabaka nchini kote dhidi ya adui yao. Hali hii imefanya baadhi
vyuo hivyo kufungwa. Nyakati hizo tulikuwa tukipinga madaraja
ya wavujajasho kudhani kuwa mapambano yasiyo katika eneo
katika mikopo ya elimu ya juu, na ajenda yetu ilikuwa wanafunzi
lao hayawahusu. Marcelina Kibena, ambae ni mkulima kutoka
wote wapewe mikopo kwa 100%. Hivi sasa hilo sio dai tena,
Morogoro, analifafanua vema jambo hili:
wanafunzi wameshakubaliana na uwepo wa madaraja ya mikopo.
Wanachopigania ni fursa ya kupata mkopo, hata kama ni kwa
3 Marcelina Kibena, Demokrasia Inamaanisha Nini kwa Wazalishaji Wadogo Vijijini? Sauti ya Ujamaa, 14 Januari 2018. Imetolewa
kutoka https://sautiyaujamaa.wordpress.com/2018/01/14/demokrasia-inamaanisha-nini-kwa-wazalishaji-wadogo-vijijini/

10 11
madaraja, kwa sababu sehemu kubwa ya wanafunzi hawapati watajikuta wakigawanyika na kuangukia katika udanganyifu
mikopo. Kupata mkopo imekuwa ni bahati, na sio tena hitaji la ufanywao na mafashisti pamoja na walaghai wengine wa kisiasa.
lazima. Tena hali imekuwa mbaya, kwa sababu mikopo imewekewa
riba na kiwango cha makato ya mikopo hiyo kwa waliohitimu ajira Tufanye nini?
kinazidi kupanda.
Wakati umefika kwa wavujajasho kuunganisha nguvu ili wapaze
Nyakati tulizomo sauti zao kupigania madai yao. Kwa kuanzia, madai hayo yapiganie
Tunaishi katika nyakati ambazo mfumo wa uliberali mambo leo kurejeshwa kwa kila kitu ambacho wavujajasho walikipoteza baada
umo katika anguko kuu. Umepita mwongo mmoja tangu anguko ya nchi kukumbatia sera za soko huria.
hilo lijidhihirishe mwaka 2008, ambapo chumi za kibepari zilianza
kuporomoka na kueneza anguko hilo katika nchi za ulimwengu (i) Katika uwanda wa kijamii, ni wakati wa wavujajasho kudai tena
wa tatu. Kisiasa, mfumo huu wa uliberali mamboleo umepoteza urejeshwaji wa huduma bora za kijamii (hasa elimu na afya) bila
uhalali na mamilioni kwa mamilioni ya wavujajasho duniani kote malipo.
wanapambana kuupeleka mfumo huu kaburini.
(ii) Katika uwanda wa kiuchumi, wavujajasho wapiganie ujenzi wa
Hata hivyo, kumeibuka vuguvuvu la kihafidhina la kibepari na uchumi unaojitegemea ili kuondoa unyonyaji na uporaji unaofanywa
lenye mwelekeo wa kifashisti ambalo limefanikiwa kuteka hisia za na nchi komba komba. Halikadhalika, wapiganie ujenzi wa uchumi
baadhi ya watu wa tabaka la chini. Badala ya kuushambulia ubepari, wa usawa kwa kuondoa njia kuu za uzalishaji mali kutoka kwa
mafashisti hawa wanaelekeza hasira dhidi ya makundi mengine mabepari kwenda kwa wavujajasho wenyewe kupitia vyama vya
ya watu, na hasa wahamiaji, watu wenye rangi tofauti ya ngozi na ushirika vya wavujajasho, pamoja na umiliki wa serikali.
watu wa dini nyingine. Mafashisti hujenga ubepari na huchukua
upande wa mabepari katika mapambano ya kitabaka, hivyo mageuzi (iii) Katika uwanda wa kisiasa, wavujajasho sharti wapiganie
wayafanyayo hulenga kuwaongezea mabepari nguvu zaidi. kurejea kwa nguvu ya maamuzi mikononi mwa wavujajasho.
Kwa maana nyingine, nguvu kubwa ya maamuzi irejeshwe katika
Vuguvugu la kifashisti limeshika kasi katika nchini za India na vyombo ambavyo vinawashirikisha wavujajasho moja kwa moja.
Marekani na hata kufanikisha kuchaguliwa kwa Narendra Modi Mojawapo ya vyombo hivyo ni mikutano mikuu ya vijiji na mitaa.
kuwa Waziri Mkuu wa India mwaka 2014 na Donald Trump kuwa Kwa mfano, sheria ya ardhi namba 4 ya mwaka 1999 (ambayo iko
rais wa Marekani mwaka 2016. Nchini Uingereza, vuguvugu mbioni kubadilishwa) inaupatia mkutano mkuu wa kijiji mamlaka
lililoongozwa na UKIP lilifanikiwa kuiondoa nchi hiyo kutoka ya kusimamia na kugawa ardhi ya kijiji kwa wanavijiji wanaohitaji,
Umoja wa Ulaya ilhali huko Ufaransa, Marine Le Pen na chama na utekelezaji wa maamuzi ya mkutano mkuu hufanywa na
chake cha Front National walibakisha kidogo kuingia Ikulu. Kusini Halmashauri ya Kijiji. Kwa maana nyingine, wavujajasho wapiganie
mwa Amerika, mafashisti wameshika kasi katika nchi za Argentina kuwa na uwezo wa kudhibiti rasilimali kuu na nyenzo kuu za
na Brazil ambako vyama vya mrengo wa kushoto vimeondolewa uzalishaji mali, ikiwemo ardhi, pamoja na kushiriki katika maamuzi
madarakani, na viongozi wa mrengo wa kushoto kama Lula da Silva ya msingi katika nchi yao.
wa Brazil kufungwa gerezani kwa hila za mafashisti.
Hayo ni baadhi ya madai ya jumla ambayo wavujajasho wanaweza
Katika nyakati kama hizi, ni vema kwa wavujajasho kuwa na kuyaibua. Madai haya sio mapya kabisa. Yapo madai mengine ambayo
mshikamano baina yao na kuongozwa na dira ya kimapinduzi ni mahsusi kwa wavujajasho wa sekta fulani. Kila wanapotoa madai
katika mapambano dhidi ya mfumo katili wa ubepari. Vinginevyo, mahsusi basi ni vema wavujajasho wakaambatanisha na madai ya

12 13
2
jumla ya tabaka zima la wanyonge. Azimio la Arusha liliyataja madai
haya kama haki za msingi za wakulima na wafanyakazi. Kwa kuwa
haki hizi ziliporwa kutoka wavujajasho basi ni jukumu la msingi
kwa wavujajasho kuzipigania zirudi mikononi mwao.

Kwa hiyo, Mwalimu Nyerere alituachia urithi mzuri wa Azimio la


Arusha, na ndilo linapaswa kuwa dira yetu katika ujenzi wa jamii SURA YA PILI
mpya. Katika kupigania Azimio la Arusha tunapaswa kujihadhari na
matapeli wa kisiasa ambao wanasema kuwa wamelihuisha Azimio ili AZIMIO LA ARUSHA
liendane na nyakati za sasa. Eti wamelihuisha kwa kubomoa misingi
yote ya kijamaa na kuweka misingi ya kibepari! Hawa ni matapeli UJAMAA NA KUJITEGEMEA
tu wanaolenga kuteka hisia za wavujajasho na kupotosha madai yao
ili hatimae wawarejeshe wavujajasho katika mbawa za mabepari. (Lilipitishwa na Halmashauri Kuu ya TANU, mwezi Januari 1967, na
Tujihadhari na matapeli hao. kuthibitishwa na Mkutano Mkuu wa TANU. Lilitolewa rasmi tarehe 5
Februari 1967)
Umoja na mshikamano wa kitabaka hautapatikana bila ya
wavujajasho kuwa na chombo chao cha kuratibu mapambano yao na SEHEMU YA KWANZA
kupaza sauti zao kwa umoja. Ili yafanikiwe, mapambano ya kitabaka IMANI YA TANU
yanahitaji umoja na mshikamano wa hali ya juu. Kama asemavyo
Marcelina Kibena: Siasa ya TANU ni kujenga nchi ya Ujamaa. Misingi ya ujamaa
Tukiunganisha nguvu na kupambana kama wavujajasho imetajwa katika Katiba ya TANU, nayo ni hii:
wa Afrika, hata mabepari wenyewe watatuogopa. Wakienda
kupora ardhi Kilosa, wajue sisi wote tutaungana kupambana Kwa kuwa TANU inaamini:
nao. Basi watatuogopa, wakijua kabisa kuwa wakimpora
mmoja wetu ni sawa na kutupora sisi sote na Afrika nzima (a) Kwamba binadamu wote ni sawa;
tutaungana kupambana nao. Hivyo ni lazima tuachane (b) Kwamba kila mtu anastahili heshima;
na haya masuala ya nchi, tupambane kama wanyonge wa (c) Kwamba kila raia ni sehemu ya Taifa na anayo haki ya
Afrika nzima4. kushiriki sawa na wengine katika Serikali tangu ya Mitaa, ya
Mikoa hadi Serikali Kuu;
Mapambano ya wanyonge kudai haki zao ni magumu. Kuna
wakati yatapitia misukosuko na hata kushindwa kwa muda lakini (d) Kwamba kila raia anayo haki ya uhuru wa kutoa mawazo
kamwe hayapaswi kurudi nyuma. Mwishowe, mapambano haya yake, wa kwenda anakotaka, wa kuamini dini anayotaka na
yatamalizika kwa wavujajasho kuibuka na ushindi. wa kukutana na watu mradi havunji Sheria;
(e) Kwamba kila mtu anyo haki ya kupata kutoka katika jamii
Enyi wavujajasho wote unganeni. Hamna cha kupoteza hifadhi ya maisha yake na ya mali ya aliyonayo kwa mujibu
isipokuwa minyororo ya utumwa mliyofungwa! wa Sheria;
(f) Kwamba kila mtu anayo haki ya kupata malipo ya haki
kutokana na kazi yake;
4 Rejea makala ya Marcelina Kibena iliyonukuliwa hapo awali.

14 15
(g) Kwamba raia wote kwa pamoja wanamiliki utajiri wa asili (i) Kuona kwamba serikali inaondoa kila namna ya dhuluma,
wanchi hii ukiwa kama dhama kwa vizazi vyao; vitisho, ubaguzi, rushwa na upotofu;
(h) Kwamba ili kuhakikisha kuwa uchumi wanchi unakwenda (j) Kuona kwamba Serikali ya nchi yetu inasimamia barabara njia
sawa Serikali lazima iwe na mamlaka kamili juu ya njia kuu za kuzalisha mali na inafuata siasa ambayo itarahisisha
muhimu za kuukuza uchumi; na njia ya kumiliki kwa jumla mali za nchi yetu;
(i) Kwamba ni wajibu wa Serikali, ambayo ni watu wenyewe,
kuingilia kati kwa vitendo maisha ya uchumi ya Taifa ili (k) Kuona kwamba Serikali inshirikiana na dola nyingine katika
kuhakikisha usitawi wa raia wote na kuzuia mtu kumnyonya Afrika katika kuleta Umoja wa Afrika.
mtu mwingine au kikundi kimoja kunyonya kikundi kingine (l) Kuona kwamba Serikali inajitahidi kuleta amani na salama
na kuzuia limbikizo la utajiri kufikia kiasi ambacho hakipatani ulimwenguni kwa njia ya Chama cha Umoja wa Mataifa.
na siasa ya watu wote kuwa sawa.

MADHUMUNI YA TANU SEHEMU YA PILI


SIASA YA UJAMAA
Kwa hiyo basi, makusudi na madhumuni ya TANU yatakuwa
kama hivi yafuatavyo:
(a) Hakuna Unyonyaji
(a) Kuudumisha uhuru wanchi yetu na raia wake; Nchi yenye Ujamaa kamili ni nchi ya wafanyakazi: haina ubepari
wala ukabaila. Haina tabaka mbili za watu: tabaka ya chini
(b) Kuweka heshima ya mwanadamu kwa kufuata barabara
ya watu wanoishi kwa kufanya kazi, na tabaka ya juu ya watu
kanuni za Tangazo la Ulimwengu la Haki za Binadamu;
wanaoishi kwa kufanyiwa kazi. Katika nchi ya Ujamaa kamili
(c) Kuhakikisha kwamba nchi yetu inatawaliwa na Serilali ya mtu hamnyonyi mtu, bali kila awezaye kufanya kazi hufanya
watu ya kidemokrasia na ya kisoshalist; kazi, na kila mfanyakazi hupata pato la haki kwa kazi aifanyayo
na wala mapato ya wafanyakazi mbalimbali hayapitani mno.
(d) Kushirikiana na vyama vyote vya siasa katika Afrika
vinavyopigania uhuru wa bara lote la Afrika; Katika nchi ya Ujamaa kamili watu peke yao ambao huishi kwa
jasho la wenzao, na ni haki yao kuishi kwa jasho la wenzao, ni
(e) Kuona kwamba Serikali inatumia mali yote ya nchi yetu kwa watoto wadogo, wazee wasiojiweza, vilema na wale ambao, kwa
kuondoshea umaskini; ujinga na maradhi; muda, Jumuia imeshindwa kuwapatia kazi yoyote ya kujipatia
riziki kwa nguvu zao wenyewe.
(f) Kuona kwamba Serikali inasaidia kwa vitendo kuunda na
kudumisha vyama vya ushirika;
Nchi yetu ni nchi ya Wakulima na Wafanyakazi, lakini si nchi ya
(g) Kuona kwamba kila iwezekanapo Serikali inashiriki hasa Ujamaa kamili. Ina misingi ya ubepari na ukabaila na vishawishi
katika maendeleo ya uchumi wa nchi yetu; vyake. Misingi hii ya ubepari na ukabaila yaweza ikapanuka na
kuenea.
(h) Kuona kwamba Serikali inatoa nafasi zilizo sawa kwa wote,
wake kwa waume, bila kujali rangi, kabila, dini au hali;

16 17
(b) Njia Kuu za Uchumi ni chini ya Wakulima na Wafanyakazi wa mwana-TANU na hasa kiongozi wa TANU hataishi kwa jasho
la mtu mwingine au kufanya jambo lolote ambalo ni la kibepari
Namna ya pekee ya kujenga na kudumisha ujamaa ni kuthibitisha au kikabaila.
kuwa njia kuu zote za uchumi wa nchi yetu zinatawaliwa na
kumilikiwa na Wakulima na Wafanyakazi wenye kwa kutumia Utimizaji wa shabaha hizo na nyinginezo zinzofuatana na siasa
vyombo vya Serikali yao na Vyama vyao vya Ushirika. Pia ni ya Ujamaa unategemea sana viongozi kwa sababu ujamaa ni
lazima kuthibitisha kuwa Chama kinachotawala ni Chama cha imani na ni vigumu kwa viongozi kujenga siasa ya ujamaa nikiwa
wakulima na wafanyakazi. hawaikubali imani hiyo.

Njia kuu za Uchumi ni: kama vile ardhi, misitu, madini, maji, mafuta SEHEMU YA TATU
na nguvu za umeme; njia za habari, njia za usafirishaji; mabenki, SIASA YA KUJITEGEMEA
na bima; biashara na nchi za kigeni na biashara za jumla; viwanda
vya chuma, mashini, silaha, magari, simenti, mbolea; nguo, na Tunapigana Vita
kiwanda chochote kikubwa ambacho kinatengemewa na sehemu
kubwa ya watu katika kupata riziki zao au kinachotegemewa TANU ina vita vya kulitoa Taifa letu katika hali ya unyonge na
na sehemu kubwa ya watu katika kupata riziki zao au kulitia katika hali ya nguvu; vita vya kuwafanya wananchi wa
kinachotegemewa na viwanda vingine; mashamba makubwa na Tanzania (na wananchi wa Afrika) watoke katika hali ya dhiki na
hasa yale yanayota mazao ya lazima katika viwanda vikubwa. kuwa katika hali ya neema.

Baadhi ya njia hizi na nyingine zisizotajwa hapa hivi sasa Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha,
zinamilikiwa au kutawaliwa na Serikali ya Wananchi. na tumepuuzwa kiasi cha kutosha. Unyonge wetu ndio
uliotufanya tuonewe, tunyonywe, na kupuuzwa. Sasa tunataka
(c) Kuna Demokrasi mapinduzi; mapinduzi ya kuondoa unyonge ili tusionewe tena,
tusinyonywe tena na wala tusipuuzwe tena.
Nchi haiwi ya Ujamaa kwa sababu tu njia zake kuu au zote za
uchumi hutawaliwa na humilikiwa na Serikali. Sharti Serikali
Mnyonge Hapigani kwa Fedha
iwe inachaguliwa na kuongozwa na Wakulima na Wafanyakazi
wenyewe. Serikali ya makaburu wa Rhodesia au Afrika ya Kusini
Lakini ni dhahiri kwamba tumefanya makosa katika kuchagua
ikitawala au kumiliki njia zote za uchumi, hiyo itakuwa ni njia ya
silaha; kwani silaha tuliyochagua ni fedha. Tunataka kuondoa
kukomaza Udhalimu siyo njia ya kuleta ujamaa. Hakuna Ujamaa
unyonge wetu kwa kutumia silaha ya wenye nguvu, silaha ambayo
wa kweli pasipo na Demokrasi ya kweli.
sisi wenyewe hatuna. Katika mazungumzo yetu, mawazo yetu,
na vitendo vyetu ni kama tumekata shauri kwamba bila fedha
(d) Ujamaa ni Imani
mapinduzi yetu hayawezekani. Ni kama tumesema, “Fedha
Lakini Ujamaa hauwezi kujijenga wenyewe. Kwani Ujamaa ni ndiyo msingi wa maendeleo. Bila fedha hakuna maendeleo’!
imani. Hauna budi kujengwa na watu wanaoamini na kufuata
kanuni zake. Mwana-TANU wa kweli ni Mjamaa, na Wajamaa Hii ndiyo imani yetu ya sasa. Viongozi wa TANU mawazo yao
wenzie, yaani waamini wenzie katika imani hii ya kisiasa ni kwenye fedha. Viongozi wa Serikali, wanasiasa na watumishi,
na uchumi ni wote wale wanaopigania haki za wakulima na mawazo yao na matumaini yao ni kwenye fedha. Viongozi
wafanyakazi katika Afrika na popote duniani. Wajibu wa kwanza wa wananchi na wananchi wenyewe katika TANU, NUTA,

18 19
Bunge, UWT, Vyama vya Ushirika, TAPA na makundi mengine Kiongozi wa Chama cha Ushirika akitaja shida yoyote ya
ya wananchi, mawazo na maombi yao na matumaini yao ni mkulima jibu apendalo kusikia ni kuwa Serikali itaondoa shida
FEDHA. Ni kama wote tumekubaliana na tunasema kwa sauti hizo za mkulima – kwa FEDHA. Mradi kila shida inayolikabili
moja, ‘Tukipata fedha tutaendelea, bila fedha hatutaendelea’! Taifa letu wananchi tunawaza Fedha, Fedha, Fedha!

Mpango wetu wa maendeleo ya miaka mitano shabaha zake Mwaka hata mwaka kila Wizara na kila Waziri hufanya makadirio
kwa kifupi ni shibe zaidi, elimu zaidi na afya zaidi. Na silaha yake ya matumizi – yaani fedha wanazohitaji mwaka huo kwa
yetu tuliyotilia mkazo sana ni fedha. Ni kama tumesema, ‘Katika kazi za kawaida na mipango ya maendeleo. Waziri mmoja tu na
miaka mitano ifuatayo tunakusudia kujiongezea shibe, elimu na Wizara moja tu hushughulika pia kufanya makadirio ya mapato.
afya, na ili kutimiza shabaha hizo tunatumia £ 250,000,000’. Kama Ni waziri wa Fedha. Kila Wizara ina mipango mizuri sana ya
tumetaja na tunapotaja vyombo vingine vya kututimizia shabaha maendeleo. Wizara zinapoleta makadirio yao ya matumizi huwa
hizo tunavitaja kama nyongeza tu; lakini chombo kikubwa katika zinaamini kwamba fedha zipo ila mkorofi ni Waziri wa Fedha na
akili zetu, silaha kubwa katika mwazo yetu, ni FEDHA. Wizara yake. Na kila mwaka lazima Waziri wa Fedha na Wizara
yake awaambie Mawaziri wenzake na Wizara zao kwamba
Mheshimiwa Mbunge anaposema kuwa wanachi wa sehemu hakuna fedha. Na kila mwaka Wizara zote huinung’unikia
yake wana shida ya maji, je, Serikali ina mpango gani wa kuondoa Wizara ya Fedha kwa Kupunguza makadirio yao ya matumizi.
shida hiyo? Jibu analotaka ni kwamba: Serikali inao mpango wa
kuwapa maji wananchi wa sehemu hiyo – KWA FEDHA. Kadhalika Wabunge na Viongozi wengine wanapodai Serikali
itemize mipango mbalimbali huwa nao wakiamini kwamba fedha
Mbunge mwingine anaposema kuwa sehemu yake haina zipo ila mkorofi ni Serikali. Lakini kukataa huku kwa Wizara, na
barabara au shule au hospitali au vyote, je, Serikali ina mpango Wabunge na Viongozi wengine hakuwezi kuondoa ukweli; nao
gani? Naye pia jibu ambalo angependa kupewa ni kuwa Serikali ni kwamba Serikali haina fedha.
inao mpango safi kabisa wa kutengeneza barabara au kujenga
shule au hospitali au vyote kwa wananchi wa sehemu ya Mbunge Na kusema kuwa Serikali haina fedha maana yake ni nini?
Mheshimiwa huyo – KWA FEDHA. Maana yake ni kuwa Wananchi wa Tanzania hawana fedha. Kiasi
walichonacho hutozwa kodi, na kodi hiyo ndiyo inayoendesha
Kiongozi wa NUTA anapoikumbusha Serikali kuwa mishahara shughuli za Serikali hivi sasa na maendeleo mengine ya nchi.
ya chini kwa wafanyakazi wengi bado ni midogo mno na nyumba Tunapotaka Serikali ifanye shughuli zaidi za maendeleo kwa
wanazolala si nzuri, je, Serikali inao mpango gani? Jibu apendalo fedha tunataka Serikali itumie fedha zaidi. Na kama Serikali
kusikia ni kuwa Serikali ina mpango maalumu wa kuongeza haina fedha zaidi tunataka izipate, yaani iongeze kodi.
mishahara na kujenga majumba bora – KWA FEDHA.
Ukidai Serikali itumie fedha zaidi unataka izipate; na njia ya
Kiongozi wa TAPA anaposema kuwa wanazo shule nyingi sana kuzipata ni kodi. Kudai Serikali itumie fedha nyingi zaidi bila
ambazo hazipatikani msaada wa Serikali, je, Serikali na mpango kudai kodi zaidi ni kudai Serikali ifanye miujiza; ni sawa na
gani wa kuzisaida shule hizo, jibu analopenda kusikia ni kuwa kudai maziwa zaidi bila kutaka ng’ombe akamuliwe tena. Lakini
Serikali iko tayari kabisa kesho asubuhi kuzipa shule hizo msaada kukataa huku kukiri kwamba tunapodai Serikali itumie fedha
unaotakiwa – wa FEDHA! zaidi nia yetu ni kutaka Serikali iongeze kodi kunaonyesha
kuwa tunatambua ugumu wa kuongeza kodi. Tunatambua
kuwa ng’ombe hana maziwa zaidi; kwamba hata kama ng’ombe

20 21
mwenyewe angependa ayanywe maziwa hayo au yanywewe na hutangaza jambo hilo ili kila mtu ajue kuwa neema imekuja au
ndama wake au yauzwe yamfae yeye na jamaa yake; utashi huo iko njiani inakuja! Tukipata masaada hutangaza; tukipata mkopo
hauwezi kuondoa ukweli kwamba hana maziwa zaidi. hutangaza; tukipata kiwanda kipya hutangaza; tukiahidiwa
msaada, mkopo au kiwand kipya hutangaza. Japo tukianza
Fedha kutoka Nje ya Tanzania, Je? mazungumzo tu na nchi au shirika la kigeni juu ya msaada, mkopo
au kiwanda, mara hutangaza japo hatuna hakika ya matokeo ya
Njia moja tunayotumia kujaribu kuepukana na lazima hii ya mazungumzo hayo. Na kisa? Ni kuwajulisha wananchi kwamba,
kukiri kodi zaidi ikiwa twataka fedha zaidi ni kutilia sana mkazo tunaanza mazungumzo ya neema!
fedha za kutoka nje ya Tanzania. Fedha hizi za kutoka nje ni za
aina tatu:- TUSITEGEMEE FEDHA KULETA MAENDELEO
(a) Zawadi: Yaani Serikali ya nje iipe Serikali yetu fedha
za bure tu kama sadaka kwa ajili ya mpango fulani wa Ni jambo la kijinga kuchagua fedha kuwa ndiyo chombo chetu
maendeleo. Wakati mwingine shirika lolote la nje liipe kikubwa cha maendeleo na hali tunajua kuwa nchi yetu ni maskini.
Serikali yetu au Shirika jingine katika nchi yetu msaada Ni ujinga vilevile, kwa kweli ni ujinga zaidi, tukidhani kuwa
fulani kwa ajili ya maendeleo. tunaweza kuondoa hali hii ya unyonge wetu kwa kutegemea
fedha za kutoka nje badala ya fedha zetu wenyewe. Ni ujinga
(b) Mkopo: Sehemu kubwa ya fedha tunazotazamia kupata kwa sababu mbili.
kutoka nchi za kigeni si zawadi au sadaka, bali ni
mkopo. Serikali ya nje au shirika la nje, kama vile Benki, Kwanza, hatuwezi kuzipata. Ni kweli kwaba zipo nchi ambazo
hukopesha Serikali yetu fedha fulani kwa ajili ya kazi zetu
zaweza na zapenda kutusaidia. Lakini hakuna nchi moja duniani
za maendeleo. Mkopo huo una masharti yake ya kulipa,
ambayo iko tayari kutupa misaada au mikopo au kuja kujenga
kama vile muda wa kulipa, na kima cha faida.
viwanda katika nchi yetu kwa kiasi cha kuwezesha shabaha zake
(c) Raslimali ya Kibiashara: Aina ya tatu ambayo pia ni kubwa zote za maendeleo. Nchi zenye dhiki ni nyingi sana duniani. Na
kuliko ya kwanza, ni ile ya fedha za watu au makampuni hata kama nchi zote zenye neema zingekubali kuzisaidia nchi
yanayotaka kuja katika nchi yetu kuanzisha shughuli zenye dhiki, bado ingekuwa msaada huo hautoshi. Lakini nchi
mbalimbali za uchumi kwa manufaa yao wenyewe. Na zenye neema hazitakubali. hata katika nchi ileile, matajiri huwa
Sharti kubwa walitakalo jamaa hawa wenye fedha zao ni hawatoi fedha zao kwa hiari ili zisaidei Serikali kuondoa dhiki.
kwamba shughuli yenyewe iwe ni ya faida – kwao – na pia
kwamba Serikali iwaruhusu kuondoa faida hiyo Tanzania Njia ya kuzipata fedha za matajiri ili zisisaidie umma ni kuwatoza
na kuipeleka kwao. Hupenda pia kwa jumla Serikali iwe kodi wakipenda wasipende. Hata hivyo huwa hazitoshi. Ndiyo
na siasa wanayokubaliana nayo au ambayo haihatarishi maana japo tungewakamua vipi wananchi na wakazi wa
uchumi wao. Tanzania, matajiri na maskini, hatuwezi kupata fedha za kutosha
kutimiza mipango yetu ya maendeleo. Wala duniani hakuna
Hizo ndizo njia tatu kubwa za kupata fedha kutoka nje ya nchi Serikali ambayo yaweza kuyatoza kodi mataifa yenye neema,
yetu. Kuna mazungumzo mengi ajabu juu ya jambo hili la kupata yakipenda yasipende, ili kusaidia mataifa yenye dhiki. Hata hizo
fedha kutoka nchi za kigeni. Serikali yetu na viongozi wetu wa zisingelitosha. Hakuna Serikali ya Dunia nzima. Fedha ambazo
makundi mbalimbali hawaachi kufikiria njia za kupata fedha nchi zenye neema hutoa huwa kwa wema wao, au hiari yao au
kutoka nje. Na tukizipata au japo tukipata ahadi tu kuzipata kwa manufaa yao yenyewe. Haiwezekani basi, tupate fedha za
fedha kutoka nje. Na tukizipata au japo tukipata ahadi tu ya kutosha kwa njia hiyo.
kuzipata mara magazeti yetu, au radio zetu na viongozi wetu

22 23
MISAADA NA MIKOPO VITAHATARISHA UHURU WETU Wageni hao na Makampuni hayo mpaka yakubali kuanzisha
mipango yote ya uchumi tunayohitaji katika nchi yetu, hivyo
Pili, japo kama tungeweza kuzipata; hivyo ndivyo tunavyotaka ndivyo tunavyotaka kweli?
kweli? Kujitawala ni kujitegemea. Kujitawala kwa kweli
hakuwezekani ikiwa Taifa moja linategemea misaada na mikopo Kama tungeweza kushawishi wenye raslimali wa kutosha kutoka
ya Taifa jingine kwa maendeleo yake. Hata kama pangetokea Taifa Amerika na Ulaya kuja kwetu na kuanzisha Viwanda vyote, na
au mataifa ambayo yako tayari kutupa fedha zote tunazohitaji mipango mingine yote ya uchumi tunayohitaji katika nchi hii,
kuendesha mipango yetu ya maendeleo isingekuwa sawa kwa hivi kweli tungekubali bila kujiuliza maswali? Tungekubali
nchi yetu kuipokea misaada hiyo bila kujiuliza matokeo yake kweli kuacha uchumi wetu wote uwe mikononi mwa wageni
yatakuwa nini kwa Uhuru wetu na uzima wetu. kwa ajili ya kupata faida na kuipeleka katika nchi zao? Hata
kama wasingedai kuhamisha faida na kupeleka makwao, bali
Msaada ambao ni kama chombo cha kuongeza juhudi au nyenzo faida yote watakayopata wataitumia hapa hapa Tanzania kwa
ya juhudi, ni msaada ambao una manufaa. Lakini msaada maendeleo zaidi. Hivi kweli tungekubali jambo hili bila kujiuliza
unaoweza ukawa sumu ya juhudi si msaada wa kupokea bila hasara zake kwa Taifa letu? Huu Ujamaa tunaosema kuwa ndiyo
kujiuliza maswali. shabaha yetu tungeujengaje?
Kadhalika mikopo. Kweli mikopo ni bora kuliko misaada
ya ‘bure’. Mikopo nia yake ni kuongeza jitihada au kuifanya Twawezaje kutegemea nchi za nje na Kampuni za nje kwa
jitihada itoe matunda mengi zaidi. Sharti moja la mkopo huwa misaada na mikopo na raslimali kwa maendeleo yetu bila
ni kuonyesha jinsi utavyoweza kuulipa. Maana yake ni kwamba kuhatarisha uhuru wetu? Waingereza wana methali isemayo
sharti uonyeshe kuwa unakusudia kuufanyia kazi itakayoleta ‘Amlipaye mwimbaji ndiye huchagua wimbo’. Tutawezaje
manufaa ya kukuwezesha kuulipa. kutegemea nchi za kigeni na Makampuni ya kigeni kwa sehemu
kubwa ya maendeleo yetu bila kuzipa nchi hizo na makampuni
Lakini hata mikopo ina kikomo. Sharti upime uwezo wa kulipa. hayo sehemu kubwa ya uhuru wetu wa kutenda tupendavyo?
Tunapokopa fedha kutoka nje mlipaji ni Mtanzania. Na kama Ukweli wenyewe ni kwamba hatuwezi.
tulivyokwishasema Watanzania ni watu maskini. Kuwabebesha
watu maskini mikopo ambayo inawazidi kimo si kuwasaidia Tukariri basi. Tumefanya makosa kuchagua fedha, kitu ambacho
bali ni kuwaumiza. Na hasa inapokuwa, mikopo hiyo ambayo hatuna, kiwe ndicho chombo kikubwa cha mipango yetu ya
wanatakiwa walipe, haikuwafaidia wao, bali ilifaidia watu maendeleo. Tunafanya makosa kudhani kuwa tutapata fedha
wachache tu. kutoka nchi za kigeni. Kwanza, kwa sababu kwa kweli hatuwezi
kupata fedha za kutosha kwa maendeleo yetu. Na pili, hata kama
Na Viwanda vya wenye raslimali zao je? Ni kweli tunavitaka. Hata tungeweza, huko kutegemea wengine kungehatarisha uhuru
tumepitisha katika Bunge sheria ya kulinda rasilimali ya wageni wetu na siasa nyingine za nchi yetu.
wanaonzisha mipango mbalimbali ya uchumi katika nchi yetu.
Nia yetu na matumaini yetu ni kuwafanya waone kuwa Tanzania
ni nchi inayofaa kuingiza raslimali zao. Kwani raslimali yao
itakuwa salama italeta faida. Na faida hiyo wenyewe wataweza
kuiondoa bila vipingamizi. Tunayo matumaini ya kupata fedha
za maendeleo mbalimbali kwa njia hii. Lakini hatuwezi kupata
za kutosha. Lakini hata kama tungeweza kuwaridhisha kabisa

24 25
TUMEKAZANIA MNO VIWANDA Kwa ajili hiyo, basi, fedha zetu huzitumia zaidi katika miji na
viwanda vyetu pia hujengwa katika miji.
Kwa sababu ya kutilia mkazo fedha tumefanya kosa kubwa la
pili. Tumekazania mno viwanda. Kama vile tulivyosema ‘Bila Na zaidi ya fedha hizi huwa ni mikopo. Japo zijenge shule,
Fedha hakuna maendeleo,’ ni kama twasema pia ‘Viwanda ndiyo hospitali, majumba au viwanda ni fedha za mikopo. Hatimaye
maendeleo. Bila viwanda hakuna maendeleo’. Hii ni kweli lazima zilipwe. Lakini ni dhahiri kwamba haziwezi kulipwa kwa
siku tutakapokuwa na fedha nyingi, tutaweza kusema kwamba fedha zinazotokana na maendeleo ya mijini au maendeleo ya
tumeendelea. Tutaweza kusema, ‘Tulipoanza mipango yetu viwanda. Hazina budi zilipwe kwa fedha tunazopata kutokana
tulikuwa hatuna fedha za kutosha na upungufu huu wa fedha na vitu tunavyouza katika nchi za nje. Kutokana na viwanda
ulitupunguzia nguvu za kuendesha maendeleo yetu haraka vyetu hatuuzi na kwa muda mrefu sana hatutauza vitu vingi
zaidi. Lakini leo tumeendelea na tunazo fedha za kutosha’. Na katika nchi za nje. Viwanda vyetu zaidi ni vya kutusaidia kupata
hivyo ndivyo itakavyotupasa kusema, ‘kwa hiyo, tunazo fedha za vitu hapa hapa ambavyo mpaka sasa tunaviagiza kutoka nchi za
kutosha’. Yaani fedha zetu zitakuwa zimeletwa na maendeleo. nje. Itapita miaka mingi kabla ya kuweza kuuza katika nchi za
Kadhalika siku tutakapokuwa na viwanda tuna haki ya kusema nje vitu vinavyotokana na viwanda vyetu.
kuwa tumeendelea. Maendeleo yatakuwa yametuwezesha kupata
viwanda. Kosa tunalofanya ni kudhani kwamba maendeleo Kwa hiyo ni dhahiri kwamba fedha tutakazotumia kulipa
yetu yataanza kwa viwanda. Ni kosa maana hatuna uwezo wa madeni haya ya mikopo ya fedha kwa maendeleo na viwanda
kuanzisha viwanda vingi vya kisasa katika nchi yetu. Hatuna mijini hazitotoka vijijini na zitatokana na KILIMO. Maana ya
fedha zinazohitajiwa na hatuna ufundi unaohitajiwa. Haitoshi ukweli huu ni nini? Ni kwamba wale wanaofaidi maendeleo
kusema kuwa tutakopa fedha na kuazima mafundi kutoka nje yanayotokana na fedha tunazokopa sio kwa kweli watakaozilipa.
kuja kuanzisha viwanda hivyo. Kosa hili jibu lake ni lilelile Fedha zitatumika zaidi katika miji lakini walipaji watakuwa zaidi
kwamba hatuwezi kupata fedha za kutosha nakuazima mafundi ni wakulima.
wa kutosha kutuanzishia viwanda hivyo tunavyotaka. Na pia
kwamba hata kama tungeweza kupata msaada huo kuutegemea Jambo hili linafaa kukumbukwa sana, maana kuna njia nyingi za
huko kunaweza kukapotosha siasa yetu ya Ujamaa. Siasa ya kunyonyana. Tusisahau hata kigogo kwamba wakaaji wa mijini
kualika msululu wa mabepari kuja kuhodhi viwanda katika wanaweza wakawa wanyonyaji wa jasho la wakulima wa vijijini.
nchi yetu ingefanikiwa kutupatia viwanda vyote tunavyotaka, Hospitali zetu kubwa zote ziko katika miji. Zinafaidia sehemu
basi ingefanikiwa pia kuzuia maendeleo ya Ujamaa. Ila labda ndogo sana ya wananchi wa Tanzania. Lakini kama tumezijenga
tuwe tunaamini kwamba bila kujenga ubepari kwanza hatuwezi kwa fedha za mkopo walipaji wa mkopo ni wakulima, yaani
kujengea Ujamaa. wale ambao hawafaidiwi sana na hospitali hizo. Mabarabara ya
lami yako katika miji, kwa faida ya wakaaji wa mijini na hasa
TUMJALI ZAIDI MKULIMA VIJIJINI wenye magari. Kama mabarabara hayo tumeyajenga kwa fedha
za mikopo walipaji ni wakulima; na fedha zilizonunua magari
Vilevile mkazo wa fedha na wa viwanda unatufanya tukazanie yenyewe zilitokana na mazao ya wakulima. Taa za umeme, maji
zaidi maendeleo ya mijini. Tunatambua kuwa hatuwezi kupata ya mabomba, mahoteli na maendeleo mengine yote ya kisasa yako
fedha za kutosha kuleta maendeleo katika kila kijiji na ambayo zaidi katika miji. Karibu yote yametokana na fedha za mikopo na
yatamfaa kila mwananchi. Tunajua pia kuwa hatuwezi kujenga karibu yote hayana faida kubwa kwa mkulima, lakini yatalipwa
kiwanda katika kila kijiji ili kisaidie kuleta maendeleo ya fedha na kwa fedha zitalazotokana na jasho la mkulima. Tusisahau jambo
viwanda katika kijiji; jambo ambalo tunajua kuwa haliwezekani. hili.

26 27
yake, ambayo italeta maendeleo, yaani chakula zaidi na fedha
Japo tunapotaja unyonyaji hufikiria mabepari, tusisahau kuwa zaidi kwa kila mwananchi.
bahari ina samaki wengi. Nao hutafunana. Mkubwa hutafuna
mdogo na mdogo naye humtafuna mdogo zaidi. Katika nchi MASHARTI YA MAENDELEO
yetu twaweza kugawa wananchi kwa njia mbili. Mabepari na (a) Juhudi
Makabaila upande mmoja; na wafanyakazi na wakulima upande
mwingine. Pia twaweza tukawagawa wakaaji wa mijini upande Kila mwananchi anataka maendeleo, lakini si kila mwananchi
mmoja, na wakulima wa vijijini upande mwingine. Tusipoangalia anaelewa na kukubali masharti ya maendeleo. Sharti moja kubwa
tutakuja kugundua kuwa wakaaji wa mijini nao ni wanyonyaji ni JUHUDI. Twendeni vijijini tuzungumze na wananchi kuona
wakulima. kama inawezekana au haiwezekani wananchi kuongeza juhudi.

WANANCHI NA KILIMO Kwa mfano, katika miji, mfanyakazi wa mshahara hufanya kazi
kwa saa saba na nusu au nane kutwa kwa muda wa siku sita
Maendeleo ya nchi huletwa na watu, hayaletwi na fedha. Fedha au sita na nusu kwa juma. Tuseme saa 45 kwa juma, kuondoa
ni matokeo siyo msingi wa maendeleo. Ili tuendelee twahitaji majuma mawili au matatu ya livu, katika mwaka mzima. Ndiyo
vitu vine: (i) Watu; (ii) Ardhi; (iii) Siasa safi na (iv) Uongozi bora. kusema mfanyakazi wa mjini hufanya kazi ya saa 45 kwa juma
Nchi yetu ina zaidi ya watu milioni kumi5 na eneo la eka 362,000. kwa majuma 48 au 50 kwa mwaka.

MAENDELEO YATALETWA NA KILIMO Katika nchi kama yetu muda huu ni mdogo kwa kweli. Nchi
nyingi hata zilizoendelea kutuzidi – hufanya kazi kwa muda
Sehemu kubwa ya eneo hili ni yenye rutuba na mvua ya kutosha. mrefu zaidi kuliko saa 45 kwa juma. Si jambo la kawaida nchi
Nchi yetu inaweza kutoa mazao ya aina mbalimbali ambayo changa kuanza na muda mfupi kama huo. Jambo la kawaida ni
tunayahitaji kwa chakula na kwa fedha. Mazao ya chakula (na kuanza na muda mrefu zaidi na kuupunguza kila nchi inavyozidi
fedha kama tukiyatoa kwa wingi) ni kama vile mahindi, mchele, kuendelea. Sisi kwa kuanza na muda mfupi huo na tunapodai
ngano, maharage, karanga n.k. Mazao ya fedha ni kama vile muda mfupi zaidi kwa kweli tunaiga nchi zilizoendelea. Na kuiga
Mkonge, pamba, kahawa, tumbaku, pareto, chai n.k. huku kunaweza kukaleta majuto. Lakini hata hivyo wafanyakazi
wa mishahara hufanya kazi ya saa 45 kwa juma; livu yao kwa
Pia nchi yetu ni nzuri sana kwa ufugaji wa ng’ombe, mbuzi, mwaka haizidi majuma manne.
kondoo, kuku n.k. Pia twaweza kuvua samaki katika maziwa,
bahari na mito. Yafaa kujiuliza wananchi wakulima hasa wanaume, hufanya kazi
Wakulima wetu wako katika sehemu ambazo zaweza kutoa kwa saa ngapi kwa juma na miezi mingapi kwa mwaka. Ni wengi
mazao haya, kama si yote walau mawili matatu au hata zaidi. Kila mno ambao hawatimizi hata nusu ya wastani wa mfanyakazi wa
mkulima wetu aweza akaongeza mazao haya ili ajipatie chakula mshahara.
kingi zaidi au fedha nyingi zaidi. Na kwa sababu nia kubwa ya
maendeleo ni kupata chakula zaidi na fedha zaidi kwa ajili ya Ukweli wenyewe ni kwamba vijijini kina mama hufanya sana
kujipatia mahitaji yetu mengine, ndiyo kusema kuwa jitihada ya kazi. Pengine hutimiza saa 12 au 14 kutwa. Hawana Jumapili, na
kuongeza mazao ni jitihada, na kwa kweli ndiyo jitihada peke hawana livu. Kina mama wa vijijini hufanya kazi zaidi kuliko
mtu mwingine yeyote katika Tanzania. Lakini kina baba wa
5 Hesabu ya watu wa mwaka 1967 ilionesha kuwa watan- vijijini (na baadhi ya kina mama wa mijini) nusu ya maisha yao
zania ni zaidi ya milioni kumi na mbili. ni livu. Nguvu hizi za mamilioni ya kina baba vijijini na maelfu

28 29
ya kina mama wa mijini ambazo hivi sasa hazifanyi kazi yoyote kujiletea wenyewe maendeleo ya aina mbalimbali. Kama
ila kupiga soga, kucheza ngoma na kunywa pombe, ni hazina wangengoja fedha wasingeyapata maendeleo hayo.
kubwa yenye manufaa zaidi kwa maendeleo ya nchi yetu kuliko
hazina za mataifa matajiri. JUHUDI NI SHINA LA MAENDELEO

Tutafanya jambo la faida kubwa kwa nchi yetu kama tukienda Mipango inayotegemea fedha inakwenda vizuri lakini kuna
vijijini na kuwaambia wananchi kwamba wanayo hazina hii na mingi ambayo imesimama na yumkini mingine haitatimizwa kwa
kwamba ni wajibu wao kuitumia kwa faida yao wenyewe na sababu ya upungufu wa fedha. Lakini kelele zetu bado ni kelele
faida ya Taifa letu. za fedha. Juhudi yetu ya kutafuta fedha inazidi kuongezeka! Sio
kwamba tuipunguze, bali, badala ya safari nyingi, ndefu na zenye
(b) Maarifa gharama kubwa za kwenda katika miji mikuu ya mataifa ya
kigeni kwenda kutafuta fedha za maendeleo yetu, itafaa kufunga
Sharti la pili la maendeleo ni MAARIFA. Juhudi bila maarifa safari kwenda vijijini kuwafahamisha na kuwaongoza wananchi
haiwezi kutoa matunda bora kama juhudi na maarifa. Kutumia katika kujiletea maendeleo kwa juhudi yao wenyewe. Ndiyo njia
jembe kubwa badala ya jembe dogo, kutumia jembe la kuvutwa ya kweli ya kuleta maendeleo kwa kila mtu.
na ng’ombe badala ya jembe la mkono, kutumia mbolea badala
ya ardhi tupu, kunyunyuzia dawa ili kuua wadudu, kujua ni zao Hii maana yake si kwamba tangu sasa hatutajali fedha, wala
gani lifaalo kupandwa na zao gani lisilofaa, kuchagua mbegu hatutajenga viwanda au kufanya mipango yoyote ya maendeleo
vizuri kabla ya kuzipanda, kujua wakati mzuri wa kupanda, inayohitaji fedha. Wala siyo kusema kuwa tangu sasa hatutapokea
wakati wa kupalilia n.k., ni maarifa yanayowezesha juhudi kutoa wala kutafuta fedha kutoka nchi za nje kwa ajili ya maendeleo
mazao mengi zaidi. yetu. LA, SIVYO. Tutaendelea kutumia fedha; na mwaka hata
mwaka tutatumia fedha nyingi zaidi kwa maendeleo yetu ya aina
Fedha na wakati tunaotumia kuwapa wakulima maarifa haya ni mbalibali kuzidi mwaka uliopita. Kwani hiyo itakuwa ni dalili
fedha na wakati uletao faida kubwa zaidi kwa nchi yetu kuliko moja ya maendeleo yetu.
fedha na wakati mwingi tunaotumia katika mambo mengi
tunayoyaita maendeleo. Lakini hii ni kusema kwamba tangu sasa tutajua nini ni shina na
nini ni tunda la maendeleo yetu. Katika vitu viwili hivyo FEDHA
Jambo hili kwa kweli tunalifahamu. Katika mpango wetu wa miaka na WATU, ni dhahiri kwamba watu na JUHUDI yao ndiyo shina
mitano, mipango inayoendelea vizuri na hata kuzidi makisio ni la maendeleo, fedha ni moja ya matunda ya juhudi hiyo.
ile inayotegemea juhudi ya wananchi wenyewe. Pamba, kahawa,
korosho, tumbaku, pareto ni mazao yaliyoongezeka kwa haraka Tangu sasa tutasimama wima na kutembea kwa miguu yetu
sana katika muda wa miaka mitatu iliyopita. Lakini ni mazao badala ya kupinduka na kuwa miguu juu vichwa chini. Viwanda
ambayo yameongezeka kwa sababu ya juhudi na uongozi wa vitakuja, na fedha zitakuja, lakini msingi wake ni WANANCHI
wananchi, siyo kwa sababu ya fedha. na JUHUDI yao na hasa katika KILIMO. Hii ndiyo maana ya
kujitegemea. Kwa hiyo basi, mkazo wetu na uwe:
Kadhalika wananchi kwa juhudi zao wenyewe na maelekezo au
msaada kidogo wametimiza mipango mingi sana ya maendeleo (a) Ardhi na Kilimo.
huko vijijini. Wamejenga shule, dispensari, majumba ya
maendeleo, wamechimba visima, mifereji ya maji, mabwawa, (b) Wananchi
mabarabara, wamejenga mabirika ya kukoshea mifugo na

30 31
(c) Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, na usawa wa kugawana mapato ya nchi ni lazima kila mtu atimize
wajibu wake kwa kufanya kazi kwa bidii zake zote. Asiweko
(d) Uongozi bora. mtu wa kwenda kwa ndugu yake na kukaa kwa muda mrefu
bila kufanya kazi kwa sababu atakuwa anamnyonya yule ndugu
yake. Vilevile mtu yeyote asiruhusiwe kuzurura zurura hovyo
(a) Ardhi
mijini au vijijini bila kufanya kazi ya kumwezesha kujitegemea
Kwa kuwa uchumi wa Tanzania unategemea na utaendelea mwenyewe bila kuwanyonya ndugu zake.
kutegmea kilimo na mifugo, Watanzania wanaweza kuyaendesha
maisha yao barabara bila ya kutegemea misaada kutoka nje kwa TANU inaamini kuwa kila anayelipenda Taifa lake ni budi
matumizi bora ya ardhi hiyo. Ardhi ni ufunguo wa maisha ya aweze kulitumikia kwa kujitolea nafsi yake na kushirikiana na
binadamu kwa hiyo Watanzania wote waitumie ardhi kama ni wananchi wenzake kwa kuijenga nchi kwa manufaa ya watu
raslimali yao kwa maendeleo ya baadaye. Kwa kuwa Ardhi ni wote. Ili kudumisha Uhuru wa nchi yetu na raia zake barabara
mali ya Taifa, Serikali ni lazima ingalie kuwa ardhi inatumiwa kwa ni budi kujitegemea kwa kila hali bila kwenda kuomba misaada
faida ya Taifa zima na wala isitumiwe kwa faida ya mtu binafsi nchi zingine.
au kwa watu wachache tu. Ni wajibu wa TANU kuona kuwa
nchi yetu inalima chakula cha kutosha na kutoa mazao ambayo Kujitegemea kwa mtu mmoja ni kujitegemea kwa nyumba kumi.
yataleta fedha nchini kwa kuuzwa katika nchi za ng’ambo. Ni Kujitegemea kwa nyumba zote kumi za balozi ni kujitegemea kwa
wajibu wa Serikali na Vyama vya Ushirika kuona kuwa wananchi tawi zima. Kujitegemea kwa matawi ni kujitegema kwa Wilaya
wanapatiwa vyombo, mafunzo ya uongozi unaohitajika katika ambayo ni kujitegemea kwa Mkoa. Kujitegemea kwa Mikoa yote
kilimo na ufugaji wa kisasa. ni kujitegema kwa Taifa lote ambalo ndilo lengo letu.

(b) Watu (d) Uongozi bora

Kuiwezesha siasa ya kujitegemea itekelezwe vizuri, wananchi ni TANU inatambua umuhimu wa kuwa na Uongozi Bora. Tatizo
budi wajengewe moyo na shauku ya kujitegemea. Wajitegemee lililopo ni ukosefu wa mipango maalum ya kuwafundisha
katika kuwa na chakula cha kutosha, mavazi ya kufaa na mahali Viongozi na kwa hiyo Ofisi Kuu ya TANU ni budi itengeneze
pazuri pa malazi. utaratibu maalum kuhusu mafundisho ya Viongozi tangu Taifa
zima hadi Mabalozi ili waielewe siasa yetu na mipango ya
Katika nchi yetu kazi iwe ni kitu cha kujivunia. Bali uvivu, ulevi uchumi. Viongozi ni lazima wawe mfano mzuri kwa wananchi
na uzururaji uwe ni jambo la aibu kwa kila mwananchi. Katika kwa maisha yao na vitendo vyao pia.
upande wa ulinzi wa Taifa, wananchi wawe macho na vibaraka
waliomo nchini ambao wanaweza kutumiwa na maadui wa nje
wenye nia mbaya ya kuliangamiza Taifa hili na wawe tayari
kulilinda Taifa inapolazimika kufanya hivyo.

(c) Siasa Safi

Msingi wa siasa ya kujitegemea lazima uambatane na siasa ya


Ujamaa ya TANU. Ili kuzuia unyonyaji ni lazima kila mtu afanye
kazi na aishi kwa jasho lake yeye mwenyewe. Na ili kuleta

32 33
SEHEMU YA NNE Katiba ya TANU, Madiwani, na Watumishi wa Serikali
UANACHAMA wenye vyeo vya kati na vya juu. (Kwa mujibu wa kifungu
hiki kiongozi ni mtu au mtu na mkewe au mke na
Tangu Chama kilipoanzishwa, tumethamini sana kuwa na mumewe).
wanachama wengi iwezekanavyo. Hii ilifaa wakati wa kupigania
vita vya kumng’oa mkoloni. Hivyo ndivyo ilivyobidi TANU
kufanya kwa wakati huo. Lakini sasa Halmashauri Kuu inaona B. Serikali na Vyombo Vingine
kuwa wakati umefika wa kutilia mkazo kwenye imani ya Chama
7. Inaipongeza Serikali kwa hatua zote ilizokwishachukua
chetu na siasa yake ya Ujamaa.
mpaka hivi sasa katika kutimiza siasa ya Ujamaa.
Kifungu cha Katiba ya TANU kinachohusu uingizaji wa mtu
kwenye Chama kifuatwe na ikiwa inaonekana kuwa mtu haelekei 8. Inaihimiza Serikali, bila kungojea Tume ya Ujamaa,
kuwa anakubali imani, madhumuni na sheria na amri za Chama, ichukue hatua zaidi za kutimiza siasa yetu ya Ujamaa kama
basi asikubaliwe kuingia. Na hasa isisahauliwe kuwa TANU ni ilivyoelezwa katika Tamko la TANU juu ya Ujamaa.
Chama cha wakulima na wafanyakazi.
9. Inahimiza Serikali kutengeneza mipango yake kwa
SEHEMU YA TANO kutegemea uwezo wa nchi hii kuiendesha mipanga hiyo na
AZIMIO LA ARUSHA wala isitegemee mno mikopo na misaada ya nchi za ng’ambo
kama ilivyofanya katika mpango wa maendeleo ya miaka
Kwa hiyo basi, Halmashauri kuu ya Taifa iliyokutana katika mitano. Halmashauri Kuua ya Taifa inaazimia mpango huo
Community Centre ya Arusha kuanzia tarehe 26/1/67 mpaka urekebishwe ili ulingane na siasa ya kujitegemea.
29/1/67, inaazimia ifuatavyo:
10. Serikali ione kuwa mapato ya wafanyakazi nje ya Serikali
A. Viongozi hayapitani mno na yale ya wafanyakazi Serikalini.

1. Kiongozi wa TANU au wa Serikali sharti awe mkulima au 11. Serikali itilie mkazo sana njia za kuinua maisha ya wakulima.
mfanyakazi na asishiriki katika jambo lolote la kibepari au
12. Inahimiza NUTA, Vyama vya Ushirika, TAPA, UWT, TYL,
kikabaila.
masharika yote ya Serikali, kuchukua hatua ili kutekeleza
2. Asiwe na hisa katika makampuni yoyote. siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.

3. Asiwe mkurugenzi katika kampuni ya kikabaila au C. Uanachama


kibepari.
Wanachaa wafundishwe kwa ukamilifu imani ya TANU ili
4. Asiwe na misharaha miwili au zaidi. waielewa, na wakumbushwe wakati wote umuhimu wa
kuishika imani hiyo.
5. Asiwe na nyumba ya kupangisha.

6. Viongozi tunaofikira hapa ni wajube wa Halmashauri


Kuu ya Taifa, Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Vyama
vilivyoshirikishwa na TANU, Wakuu wa Mashirika ya
Kiserikali, Viongozi kutokana na kifungu chochote cha

34 35
NYONGEZA

BADO NATEMBEA NALO

Mimi bado natembea nalo [Azimio la Arusha]. Nalisoma tena na tena


kugundua kama kuna cha kubadili. Labda ningeboresha Kiswahili
nilichotumia lakini Azimio lenyewe bado ni thabiti. Nisingebadili hata neno
moja. Muda mfupi tu baada ya uhuru tulianza kushuhudia kukua kwa
mgawanyiko katika nchi yetu kati ya walionacho na wasionacho. Kundi
la walioneemeka lilianza kuibuka miongoni mwa viongozi wa kisiasa na
warasimu. Hawa walikuwa maskini enzi za ukoloni lakini sasa walianza
kujitajirisha wakitumia nyadhifa zao katika chama na Serikali. Hali hii
ingeweza kuleta utengano baina ya viongozi na wananchi. Kwa hiyo
tukatamka lengo jipya la taifa letu: tulisisitiza kwamba maendeleo ni kwa
ajili ya watu wote, sio kwa manufa ya wateule wachache. Azimio la Arusha
ndilo liloitambulisha Tanzania kama taifa. Tuliweka wazi msimamo wetu,
tukatoa mwongozo wa maadili na miiko ya uongozi na kukafanya jitihada
za dhati kutimiza malengo yetu… Bado naamini kuwa mwishowe Tanzania
tutarejea kwenye maadili na misingi ya Azimio la Arusha.

(Maneno haya yalitamkwa na Mwalimu Julius Nyerere akimjibu


Ikaweba Bunting (1999) alipoulizwa maoni yake juu ya Azimio la
Arusha).

36 37
“Bado naamini kuwa mwishowe
Tanzania tutarejea katika maadili na misingi ya
Azimio la Arusha.” Maneno haya yalitamkwa na
Mwalimu Nyerere miezi michache kabla ya kifo
chake mwaka 1999. Hayo hayakuwa maneno
matupu. Sera za soko huria zilizotekelezwa nchini
baada ya Mwalimu Nyerere kutoka madarakani
zilileta madhara makubwa kwa watu wa tabaka
la chini, huku zikiwaneemesha wale wa tabaka la
juu. Katika kipindi hiki, ambapo wanyonge nchini
Tanzania na duniani kote wanapambana kuzizika
sera hizo za kiuaji, ni muhimu kuongozwa na dira ya
mapambano. Na dira hiyo katika mkutadha wetu ni
Azimio la Arusha!

Mradi huu unafadhiliwa na

You might also like