You are on page 1of 10

SOMO LA KWANZA 2017.

ELIMU KWA JAMII


TUJIKUMBUSHE: VIELELEZO VYA TAIFA

1. Lengo la somo la leo ni kuelimisha Jamii ya Watanzania kuwakumbusha


kuhusu, vielelezo vya Taifa ambavyo ni:-
i. Bendera ya Taifa
ii. Nembo ya Taifa
iii. Wimbo wa Taifa

2. TUJIKUMBUSHE: CHANZO MATUMIZI NA UMUHIMU

Bendera ya Taifa

Mwanzo Bendera ya Taifa mwaka 1961 ilijulikana kama Bendera ya


Wananchi ikiwa na rangi tatu; Kijani kibichi, Nyeusi na Dhahabu. Bendera
ya wananchi ilipandishwa rasmi Tanganyika ilipopata uhuru tarehe
09/12/1961. Siku hiyo ilishushwa bendera ya Wakoloni na kupandishwa
Bendera ya Wananchi wa Tanganyika.

Muasisi wa Taifa letu, Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage


Nyerere siku inapandishwa Bendera ya Wananchi aliwahutubia wananchi
na kutoa ufafanuzi ufuatao kwa nini imepandishwa Bendera ya Wananchi,
alisema:

Wananchi wenyewe kwa maelfu wamekata shauri kushirikiana


kufanyakazi kwa juhudi na kwa umoja bila kujali faida za Nafsi zao
wenyewe ili wapandishe Bendera yao wenyewe kupandishwa kwa
Bendera ni kusherekea Uhuru, uhuru wa kujitumikia wenyewe, uhuru wa
kupanga na kuendesha mambo yetu ya Baadaye sisi wenyewe.

3. Tarehe 26/04/1964, Tanganyika iliungana na Zanzibar na Bendera ya


Wananchi wa Tanganyika ikibadilika rangi na jina pia. Kuanzia mwaka
1964 Bendera ya Wananchi ikaitwa Bendera ya Taifa; na badala ya rangi
tatu (Kijani, Nyeusi na Dhahabu) ikawa na rangi nne, (Bluu, Dhahabu,
Nyeusi na Kijani). Rangi zote zikiwa na maana (Bluu bahari na mito ya
nchi); Nyeusi (watu), Dhahabu (madini utajiri) Kijani (mimea ardhi)

4. Sheria inayosimamia Bendera ya Taifa ni Sheria No. 15 ya mwaka 1971.


Awali ilikuwa na Sheria ya mwaka 1962 na kurekebishwa 1965 na rasmi
ikawa 1971 ikijumuisha Bendera na Nembo ya Taifa (The National Flag
Page 1 of 10
and Court of Arms of 1971). Kutundika Bendera mbele ya Ofisi ya Serikali
ni utekelezaji wa wajibu wa Utiifu kwa Serikali, hivyo hakuna sababu ya
kutokuweka Bendera ya Taifa mbele ya Ofisi yako. Unaogopa nini? Hutaki
ujulikane kama wewe ni Ofisi ya Serikali? Nawasihi wenye mamlaka
kuzingatia hilo ili hata asiyejua kusoma au mgeni atambue mahali pa
msaada.

5. Matumizi ya Bendera ya Taifa

Hakuna mtu yoyote anayeruhusiwa kufanya marekebisho


(modification) bendera ya Taifa zaidi ya Mh. Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania
Bendera ya Taifa hairuhusiwi kutumiwa kama Kivutio au urembo
wa kibiashara.
Bendera ya Taifa itumike mahali sahihi na kwa bendera sahihi, ni
marufuku kutundika au kutumia bendera iliyopauka, iliyotoboka
toboka, iliyochakaa na chafu kimwonekano. Kwa kuwa tumefafanua
umuhimu wake basi atakayechukuliwa hatua za kisheria afahamu
kuwa tendo lake la kudharau Bendera ya Taifa ni sawa na kudharau
Wananchi wa Tanzania.

6. Taratibu za uwekaji na utundikaji Bendera katika milingoti


Bendera ya Taifa inapandishwa mlingotini saa 12 asubuhi na
kushushwa saa 12 jioni.
Katika uwekaji kwenye magari, Mh. Rais ( bendera ya Rais),
Makamu wa Rais na Mheshimwa Waziri Mkuu ( Bendera za Taifa)
huwekwa upande wa KULIA. Viongozi Waandamizi wote huweka
bendera ya Taifa upande wa kushoto na hupeperusha maeneo yao
ya Utawala pekee.

B.WIMBO WA TAIFA: MUNGU IBARIKI AFRIKA


Maana ya Wimbo: Ukombozi wa Mwafrika. Wimbo unasisitiza kuwa
Waafrika ni wamoja, wanapitia magumu na magumu hayo yanahitaji
kutatuliwa hivyo Waafrika wanapata faraja kuwa juhudi zao

Page 2 of 10
zitafanikiwa kwa msaada wa Mungu. Kwa hiyo Wimbo wa Taifa ni
dua maalum la kitaifa kuombea ustawi wa nchi na Wananchi wa
Nchi husika.

Chimbuko la kihistoria, zinaonyesha kuwa mtunzi wa Wimbo wa


Wimbo Mungu Ibariki Afrika alikuwa mmoja wa kwaya master
maarufu miaka ya 1880s aitwaye ENOCK SONTONGA. Enock
awali aliuimba Wimbo huu ukiwa na heading ya God Bless Afrika
yaani Mungu Ibariki Afrika yaani NKOSI SIKALELI mwaka 1897
kanisani kwao na ukaonekana una maana kubwa kwa Waafrika
wanaoteseka. Kutokana na hali halisi ya Afrika kusini wakati huo,
mwaka 1912 kulianzishwa chama cha kugombea HAKI ZAO za
WAAFRIKA kwa ujumla kiitwacho SOUTH AFRICAN NATIVE
CONGRESS, mwaka 1925 waliuchagua Wimbo wa Nkosi Sikeleli
Afrika(Mungu Ibariki Afrika) kuwa Wimbo wa Taifa.

Kutokana na dhana ya Ukombozi wa Afrika, wimbo huo umekuwa


wimbo wa Taifa kwa nchi za Tanzania na Zambia na Afrika Kusini. Ni
wimbo bora katika Afrika kwani unafahamika katika nchi nyingi hata
bara la Ulaya.

Yapo maswali na mitazamo inayowachanganya wananchi kwamba


Tanzania imeiga na wengine wanatajwa kuwa ndio walioleta wimbo
huo hapa Tanzania. Usahihi ni kwamba mwaka 1954 wakati Chama
cha Ukombozi wa Watanzania kinazaliwa, yaani Tanzania National
Union (TANU) wimbo wa Nkosi Sikeleli Afrika ulishika hatamu Afrika
yote kutokana na vuguvugu la ukombozi Tanganyika ikiwa mstari wa
mbele, hivyo, Mpambanaji wetu Hayati Baba wa Taifa J.K Nyerere
alishiriki kikamilifu ukombozi wa Afrika na ndiye Muasisi sahihi wa
Mungu Ibariki Tanzania hapa nchini.

UMUHIMU NA MAHALI PA MATUMIZI


Wimbo wa Taifa unatoa tafsiri ya utaifa, ni dua pekee la kitaifa
linalobainisha Mungu katika kupata Amani, Umoja na kuwaombea
Hekima kwa Watawala. Ni Heshima ya Kitaifa kwa Mungu
kusimamia Ustawi wa Taifa na Raia wake. Wimbo huu umekaa
kimaombi katika mfumo wa DUA.
Wimbo unaweza kuimbwa kwenye mikusanyiko ya shughuli za
Kitaifa, Mashuleni (kuandaa vijana), michezo ya kimataifa (Taifa au
Uwakilishi wa klabu kwa Taifa), Mikutano ya Kitaifa awapo Mhe.
Rais.
Page 3 of 10
Kwa kawaida unapoimbwa wimbo huu redioni, tunatarajia
kitakachofuata ni HOTUBA au TAMKO litakalotolewa na Mhe. Rais.
Wimbo unaweza kuimbwa inapopandishwa BENDERA YA TAIFA
kwani wakati huo hutakiwa kusimama kwa utii na nidhamu.
Wimbo wa Taifa hauruhusiwi kuimbwa katika Vilabu, Baa, Mkutano
ya Kivyama au kuwa sehemu ya nyimbo za kusherehesha ibada
makanisani au msikitini. Huko tuna miongozo yetu ya Kiimani au
kivikundi. Hata hivi, madhehebu ya dini yamepata fursa pekee
kuimba wimbo huu katika Ibada za kufunga mwaka na kuanza
mwaka mpya.

C. NEMBO YA TAIFA
Tarehe 23/11/1962, Bunge la Tanganyika, The Constituent Assembly
of Tanganyika lilipitisha The Public Seal ambayo ilihesabiwa kuwa ni
mali ya Mtukufu Rais. The Public Seal ni aina yaMuhuri wenye
Nembo ya Taifa (wakati huo Tanganyika). Katika Transitional
Decree, 1964, para ya 10 iliridhia Public Seal ya mwaka 1962
iendelee kutumika hadi marekebisho yatakapofanyika.

Nembo ya Tanganyika ilikuwa na Bendera ya Tanganyika, Mwenge


wa Uhuru uliozungushiwa minyororo na umesimamishwa juu ya
kilele cha mlima Kilimanjaro, picha ya Adam na Hawa wamesimama
juu ya Msitu wa Kahawa (Adam) na Msitu wa Pamba (Hawa) wote

Page 4 of 10
wameshika Kipusa cha Tembo kulia na kushoto.Pia katika nembo
yapo Maandishi Uhuru na Umoja.

Mwaka 1964 baada ya Tanganyika kuungana na Zanzibar, Vielelezo


muhimu vya Taifa vilibadilika, hii ni pamoja na Nembo ya
Tanganyika. Mabadiliko yaliyofanyika katika Nembo ya Tanganyika
ni kwanza, Mkuki na Minyororo iliondolewa; pili imewekwa Bendera
ya Taifa badala ya bendera ya Tanganyika. Tatu,kumeongezwa
Jembe na Mundo vilivyopishana katikati ya Mlingoti wa Mwenge wa
Uhuru. Na hii ndiyo NEMBO SAHIHI YA TAIFA ambayo imepitishwa
kwa Sheria ya National Flag and Court of Arms No. 15 ya mwaka
1971.
MATUMIZI:
Nembo ya Taifa hutumiwa kama MUHURI WA TAIFA. Muhuri wa
Taifa unaitwa The Public Seal. Huu hutumiwa na Mheshimiwa Rais
kwa maamuzi au maelekezo muhimu kitaifa. Na ipo mihuri ya Umma
inayotumiwa na Ofisi muhimu kugonga katika vibali, Hati za Umiliki
wa Ardhi na Hukumu za Mahakama. Nembo haitumiki ovyo wala
hairuhusiwi kushikwa na Maafisa wasioidhinishwa kushika au
kuhifadhi. Nembo za aina hii huhifadhiwa katika safe Maalum.

Hairuhusiwi kabisa mtu yeyote, mfanyabiashara, mjasiriamali au


mtumishi wa Serikali kukaa na MUHURI WENYE NEMBO YA TAIFA
nyumbani kwake au Ofisini kwake bila ya idhini ya Mamlaka
iliyokasimiwa madaraka ya kushika Nembo ya Taifa kama Muhuri.
Muhuri wenye NMembo ya Taifa ni mali ya jamhuri na kuna
utaratibu wake wa kushika. yeyote atakayebainika kuwa na Nembo
au Muhuri wa Nembo ya Taifa atachukuliwa hatua kali kwa mujibu
wa sheria za nchi.

Page 5 of 10
MASWALINAMAJIBU
6.1Swali la Kwanza
Kwa nini Mwenge wa Uhuru umewekwa katika Nembo ya Taifa?

Jibu la Mpigachapa Mkuu wa Serikali

Mwenge wa Uhuru umewekwa katika nembo ya Taifa kwa sababu


Mwenge wa uhuru ni miongoni mwa nyenzo za kuleta maendeleo ya
nchi. Katika Nembo ya Taifa zipo nyenzo nyingine kama Jembe na
mundo, karafuu, Pamba mkonga wa tembo ukiwakilisha maliasili
zetu.Menge umewekwa kileleni Kilimanjaro siku ya kupandisha
bendera yetu ya kupata Uhuru ili Umulike hata nje ya Mipaka yetu,
ulete matumaini, upendo na hekima zaidi ya yote umulike kusaidia
kuondoa maadui wakubwa wan chi yetu ambao ni ujinga, maradhi
na umaskini.
Tarehe 22/10/1059 Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa
Mwenyekiti wa TANU wakati akihutubia Baraza la kutunga Sheria
(LEGICO) na pia akiwa Mjumbe wa Baraza hilo alisema Sisi
(Watanganyika), tunataka kuwasha Mwenge na kuuweka juu ya
Mlima Kilimanjaro, Umulike hata Nje ya Mipaka yetu, Ulete Tumaini
pale Ambapo Hakuna Matumaini, Upendo pale ambapo pana Chuki,
Heshima ambapo pamejaa Dharau.

Mwenge wa Uhuru uliwashwa kwa mara ya kwanza kwenye kilele


cha Mlima Kilimanjaro mwaka 1961.

Maneno haya ndio dhima ya kuwasha Mwenge, ni falsafa


iliyowafanya Watanganyika kujikusanya, kuungana na kupigania
haki zao, kupigania ukombozi wa watanganyika na wa nchi za nje
kupitia chama cha TANU. Hivyo Vijana wa TANU, waliojulikana
kama TANU YOUTH LEAGUE waliutumia Mwenge kuhamasisha na
Dira ya Maisha bora.

Toka mwanzo Vijana wamepewa Jukumu la kusimamia na kulinda


Uhuru wenye Matumaini, Upendo na Heshima. Na ili kuleta
matumaini hayo yatupasa kupambana na Maadui Wakubwa Watatu,
Ujinga,Maradhi na Umaskini. Mbio za Mwenge zinalenga
uhamasishaji wa Vita hivi Vikuu Vitatu.

Wito wangu hapa ni kwa Vijana wetu wanaopewa dhamana ya


kukimbiza Mwenge kutoa tafsiri ya malengo ya Mwenge ya kuondoa

Page 6 of 10
Ujinga, Umaskini na maradhi, watamke bayana kila mradi umegusa
eneo lipi la malengo ya Mwenge. Maadui Ujinga, Maradhi na
Umaskini, kila adui anayo tafsiri pana, mfano Ujinga, Inagusa
kufunguliwa kwa vyuo, shule za sekondari na vikundi vya elimu ya
watu wazima n.k. Kwa hiyo nawasisitiza wakimbiza Mwenge kutoa
tafsiri ya kila mradi waufunguao na kwamba umetokana na dhima ya
kuwasha mwenge.

Kwa ufafanuzi huu mfupi, muuliza swali na Watanzania kwa ujumla


sasa wataelewa umuhimu wa Mwenge na Mbio za Mwenge na kwa
nini Mwenge umekuwa kwenye Nembo ya Taifa. Kila kilichokwekwa
kwenye Nembo ya Taifa kina maana kubwa kwa maisha huru ya
Mtanzania. Msingi wa kuanzisha Mwenge wa Uhuru una ujumbe wa
kuendelezwa.

6.2 SWALI LA PILI


Kwa nini Mabalozi wa Nchi za nje hawafuati taratibu za Matumizi ya
Bendera ya Taifa? Masharti yao yakoje katika uwekaji Bendera
kwenye Magari yao?

MAJIBU YA MPIGACHAPA MKUU WA SERIKALI


Kwanza napenda kuweka sawa kuhusu hoja zinazohusu Wana-
diplomasia, mtendaji sahihi wa kujibu hoja hii ni Mkuu wa Itifaki au
tumezoea kumwita Chief of Protocol ambae yuko Wizara ya
Mambo ya Nchi na Uhusiano wa Kimataifa. Mimi nimepewa
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Nyaraka za Serikali na ndiko
Mheshimiwa Rais alikonipa dhamana, hivyo siwezi kutoa majibu
mazuri ya swali hili.

Hata hivyo, naweza kutoa ufafanuzi kwa mujibu wa elimu ya


darasani. Kwani nimebahatika kusomea mambo ya Diplomasia na
Sheria ya Mahusiano Kidiplomasia na kutunukiwa Shahada ya
Uzamili, hivyo nitafafanua kama Mwanadiplomasia msomi (a
diplomat graduate).

Jibu: Mabalozi wa Nchi za Nje wanatekeleza majukumu yao kwa


mujibu wa Mkataba wa Kimataifa uitwao Vienna Convention.
Mabalozi katika nchi ni miongoni mwa Wanadiplomasia.
Kumbukumbu zinaonyesha kuwa mwaka 1949 Umoja wa Mataifa
kupitia TUME YAKE iliyoitwa International Law Commission
ilipendekeza mada iliyojulikana kwa jina la Diplomatic Intercourse

Page 7 of 10
and Immunities na kupewa uzito mkubwa kiasi kwamba Katibu
Mkuu wakati huo, mwaka 1961 aliitisha Mkutano kule Vienna
(Vienna Conference). Katika Mkutano huo nchi mbalimbali duniani
zilishiriki na kujadili suala la Mashirikiano na Mahusiano na
kukubaliana kuwepo kwa utaratibu maalum wa kimahusiano Baada
ya makubaliano hayo yanayojukiana kw jina la Vienna Convention,
1961, tarehe 24 April, 1964, The Vienna Convention ikapitishwa
rasmi (came into force) na kuwepo kwa Aya (Articles) mbalimbali za
kuzingatiwa kama miongozo ya utendaji wao wa kazi mfano; Nchi
inayopokea Mabalozi wana jukumu kubwa la kuwalinda watumishi
wa ubalazi katika nchi wanazotumikia., hii imo katika Aya ya 22
(Article 22 of the Vienna Convention). Taratibu za utendaji kazi za
mabalozi zinazingatia makubaliano yao ya Vienna Convention of
1961 na sio sheria za nchi wanayoishi (Receiving State)

Pili, kuhusu uwekaji wa Bendera


Balozi zinaruhusiwa kupeperusha Bendera za Taifa lao kwenye
makazi wanayoishi na kufanyia kazi. Bendera za Kibalozi
zinapeperushwa kuanzia saa mbili asubuhi na kuteremshwa jua
lizamapo (kwa Tanzania saa 12 jioni). Kwa kuwa bendera ni
kielelezo cha Taifa, nayo inasisistizwa kuwa iwe safi na isiyopauka.
Kama kuna maombolezo ya Kitaifa kwao, bendera itapeperushwa
nusu mlingoti. Balozi hupeperusha bendera zao pekee. Isipokuwa
endapo Mhe. Rais atatembelea Makazi ya Balozi kwa shughuli za
kikazi, basi bendera ya Rais itapeperuswa mara tu afikapo huko na
kuondoa atokapo. Vienna Convention of 1963 imeidhinisha
Consulates kupeperusha Bendera kwenye Ofisi zao na sehemu zao
za kazi.

Balozi hupeperusha bendera kwenye gari yake atembeapo kwa


safari za kikazi na huwekwa juu upande wa kushoto wa mudguard
ya gari yake. Lakini wageni binafsi wa nchi za nje hawaruhusiwi
kupeperusha bendera za Taifa lao kwenye makazi yao. Hii imo
kwenye Vienna Convention of 1963 sehemu ya Diplomatic Protocol
and the Rules of Courtesy.

Balozi anaruhusiwa kutumia bendera kwenye gari yake mara tu


baada ya kukabidhi hati yake ya Utambulisho kwa Rais wa
Receiving State. Hata miezi sita, kabla ya hapo haruhusiwi kutumia
hiyo bendera wala kuhudhuria Official functions zozote. Hizo

Page 8 of 10
zitaendelea kuhudhuriwa na CHARGE DAFFAIRES aliyeachiwa
Ofisi na Balozi aliyeondoka. Huyu anaweza kutumia bendera
kwenye gari. Najua hilo linawasumbua wengi lakini ukweli ndio huu
na hii ndiyo DIPLOMACY AT WORK.
Bendera ina maana kubwa sana katika utambulisho wa nchi,
bendera inaheshimu sana Taratibu, Mila na Desturi ya nchi husika.

Naona nimewavuruga wengine niliposema Charge DAffaires.


Mpangilio wa ukubwa wa kiutawala katika balozi, umeainishwa
katika Mkataba wa Vienna, Article 14 of the Vienna Convention ume-
establish a hirachykatika kategori tatu ambazo ni
Ambassodors;Envoys na Charge Daffaires. O.K tumalizie hapa
ila ninavyokumbuka Profesa wetu alituonya na akasisitiza maadili ya
kazi kuwa ukiwa Balozi huruhusiwi kwenda na gari ya Kibalozi
kwenye makamuzi usiku au kwenye safari ambazo siyo Officials.
Nadhani hata kwa watendaji wetu wenye hadhi ya kuweka bendera
kwenye magari yao, hayo ni maadili mtambuka.

6.3.SWALI LA TATU
Mpigachapa Mkuu wa Serikali, unaweza kutupatia tathimini ya Vita
vyako ulivyoanzisha dhidi ya Wachapishaji wa Nyaraka Bandia?

Jibu la Mpigachapa Mkuu wa Serikali


Naona swali hili limewahi somo langu lifuatalo ambalo litazungumzia
Mkakati wa Serikali kukabiliana na Wachapishaji wa Nyaraka
Bandia. na Tafsiri ya Nyaraka muhimu (Classified Documents).
Somo lenye manufaa makubwa kwa Watumishi Serikalini na
Wananchi kwa ujumla, Vikundi, Mashirika na Makampuni. Nichukue
fursa hii kuwakaribisha tena katika kipindi hiki kwenye mwendelezo
wa kuelimisha jamii kwenye kujivunia uzalendo wao.

Hata hivyo, Kiufupi, vita dhidi ya wachapishaji wa nyaraka bandia


imekuwa ya mafanikio makubwa ingawaje wapo wasiotaka kuacha.
Kumekuwepo na mwitikio mzuri toka kwa Wananchi, Taasisi na
Mamlaka mbalimbali. Upo ushirikiano mzuri na makundi hayo ya
Kiraia na Dola, na nitoe tu tahadhari kuwa hivi sasa Mikakati mipya
imeandaliwa kutokomeza biashara hii jamii itambue kuwa
kuchapisha nyaraka bandia ni janga kwa jamii ya Watanzania.Ofisi
yangu itafuata nyayo kama walivyofanya Ofisi ya Rais, Utumishi,
tutakuwa na msako wa nyumba kwa nyumba kwa Kampuni

Page 9 of 10
zinazojihusisha na uchapishaji. Uchapishaji ni wito na una maadili
yake hivyo lazima kuyazingatia na kama huyawezi tafuta biashara
nyingine. Wito wangu, nawaomba wachapishaji wote kujiorodhesha
katika Ofisi za Mpigachapa Mkuu wa Serikali ili tukutambue na
umma ukutambue siyo kujificha ficha kama wale wanaoogopa
kujulikana kuwa wanaitumikia Serikali kwa kutoweka bendera ya
Taifa mbele ya Ofisi zao (za Serikali) Tujiandikishe hadi ifikapo
tarehe 30/03/2017 ambapokutakuwa na Mkutano ujao ambao
wachapishaji halali wote watakaojiorodhesha watakaribishwa ili nao
watoe mawazo ya kuiweka nchi mahali salama kupitia nyaraka.

Imeandaliwa na Ofisi ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali

13/02/2017 Chibogoyo, K.C.


Mpigachapa Mkuu wa Serikali

Page 10 of 10

You might also like