You are on page 1of 36

HISTORIA YA MUZIKI WA RAP TANZANIA TANGU 1980's by theostell59

Utangulizi.
Muziki wa rap ni aina ya muziki ulioanza kunako miaka ya 1970, ukiwa umeanzishwa
na Wamarekani weusi katika miji mikubwa ya Marekani. Hip hop mara nyingi inatumia
staili moja ya kuimba iitwayo kurap au kufokafoka.
Kurap ni staili ya uimbaji ambayo mwimbaji anatoa au anaimba maneno-mashairi
yaambatanayo na vina. Mashairi mengi yaliyoimbwa katika muziki wa hip hop yalikuwa
yakizungumzia maisha halisi ya watu weusi.
Real Hip-Hop sio R&B. Real Hip-Hop sio Jazz.Real Hip-Hop sio Neo Soul. Real Hip-Hop
sio techno au EDM nyingine yoyote (muziki wa densi ya elektroniki). Uchezaji wa Real
Hip-Hop unaweza kutoa matokeo mazuri ya usawa lakini sio mfumo wa mazoezi ya
mwili.Real Hip-Hop sio tu kuvaa nguo za mkoba, bandannas au kofia Real Hip-Hop sio tu
ya kuvutia kwa muda wote kwa uchezaji maarufu au wa mitaani au muziki kwa mpigo.
Real Hip-Hop Ni utamaduni wa mitindo, lugha / misimu, muziki, harakati, sanaa ya kuona
na kujieleza.Real Hip-Hop ina historia maalum na mageuzi na wabaya wake, mashujaa,
hadithi, ushindi na maporomoko.
Kama utamaduni wa watu wowote wa asili, Hip Hop inastahili kuheshimiwa na
kuwakilishwa kwa usahihi na watu ambao ni wenyeji wa tamaduni hiyo au wamechukua
muda kusoma kwa undani na vizuri. Kamwe hautarajii mgeni kufundisha densi ya watu wa
kizaramo au kihaya bila kuwekeza wakati mzito katika masomo ya kitamaduni na mazoezi
ya mwili katika tamaduni husika, sio muhimu sana kwamba mtu yeyote anayefundisha
Real Hip-Hop afanye vivyo hivyo.
Pia ni vema kutambua utamaduni wa Real Hiphop katika Misingi na nguzo zake
zinazopelekea kusimikwa ama kusimama kwa sanaa ya utamaduni wa Real Hip-hop tangu
enzi na enzi za uwepo wa Real Hip-hop na mifumo yake:
1. Nguzo ya kwanza ya Real Hiphop ni (GRAFFITI ART) -Aerosol, Mwandishi,
Kichoma moto, Kuweka alama, Mtindo wa mwitu, Kutupa-Juu
Hii Sanaa ya Michoro au machata ilikuwepo tangu enzi kabla ya kuja ukoloni Afrika mfano
Michoro ya Kondoa ni kundi la michoro ya miambani katika wilaya ya Kondoa, mkoa wa
Dodoma nchini Tanzania. Mapango au nusumapango haya zaidi ya 150 yanapatikana
mfululizo kwenye vilima vinavyotazama mtelemko wa Bonde la Ufa la Afrika ya
Mashariki. Pia mababu wa Wasandawe na Wahadzabe wa leo, ambao
walihifadhi desturi ya kuchora mwambani hadi miaka ya hii ya sasa.
Inasemekana kuwa, zaidi ya miaka 3000 iliyopita, jamii ya mbilikimo ya Batwa iliishi hapa.
Kadhalika kuna mchoro wa “ngazi” kwa sababu jamii hiyo walikuwa wafupi, walihitaji
ngazi ili kufikia maeneo ya juu. Jamii hiyo ilichonga michoro iliyoashiria au kuangazia hali
yao ya maisha.
Baadhi ya michoro hiyo ni mviringo, ama mduara, ikiwakilisha jua ambalo waliabudu
kama “Mungu” wao. Pia kuna mchoro wa Mamba, ambaye anasemekana alikuwa katika

1
ziwa la karibu na eneo hilo, aliyewaua wengi wa wakaazi wao pia wakati wa ukoloni
watumwa walitumia michoro au machata kutuma au kufikisha taarifa katika jamii zao au
kuamasisha mshikamano au mwamko katika harakati zao za kujikwamua na ukoloni.

Katika nguzo ya michoro au machata hapa Tanzania kuna kundi linaloitwa wachata crew
ambao ni wabobevu wa sanaa ya Graffit tangu mwaka 2007 linaloundwa na Mejah
Mbuya,Mwila Khamsini,Kalasinga,Ahmed Mohamed"Meddy"
Kiasilia, graffiti ni michoro au maandishi yanayochorwa kiustadi katika sehemu mbalimbali
kwa lengo la kuwasilisha ujumbe au hisia za mtu au jamii husika ndani ya wakati
uliotarajiwa. Maandishi hayo huchorwa sehemu tofauti tofauti kulingana na lengo la
mhusika mfano kwenye kuta, magari mabovu, miti mikubwa, mawe na miamba mikubwa,
pia ata kwenye mapango kama ilivyokuwa enzi za kale mfano ndani ya Piramidi za Misri
Huku wengine wakienda mbali zaidi kwa kuchora graffiti katika miili yao kama 'tattoo'.
Hivyo ndio maana tunaona hata wadau wa utamaduni wa Hip Hop wakiwemo wasanii,
wamekuwa wakichota tattoo kwenye miili yao kwa ajili ya kuwasilisha hisia au ujumbe
fulani kwa watu au jamii husika.

2
2. Nguzo ya pili ya Real Hip-Hop Ni Dj (Turntablist, Turntablism, Kuchanganya, Kukata,
Kukwaruza na Kusokota,
Katika muziki wa hip hop, DJs wanaweza kuunda beats, kwa kutumia mapumziko ya
sauti, basslines na yaliyomo kwenye muziki yaliyokadiriwa kutoka hapo awali ... Mbinu
kadhaa hutumiwa na DJs kama njia ya kuchanganya na kuchanganya muziki uliorekodiwa.
Hapa Tanzania tuna madj wengi ikiwamo Dj John Dilinga Matlow,Dj Rico,Dj Venture,Dj
Boni Luv,Dj Mackay,Dj Saydou,Dj Raph Kuti,Dj Boucha,Dj Niga Jay,Dj Ommy,Dj Super
Deo,Dj Godfather,Dj Joe Holela,Dj Junior Challenger,Aboubakar Sadiki
sebastian magang,dj steve b,Dj Kim,Dj Rommy Jones,Dj Mafuvu,dj

3
3. Nguzo ya Tatu ya Real Hiphop ni (Breaking dance) Bboy/Bgirl Break Girl ,Break Boy,
Bong-Yong, Break Dance,

Hii sanaa hapa kwetu ilikuwepo tangu miaka ya 80s ilikuwa ikiitwa mabreka
ikiwaskilishwa na wasanii kama Othman Digadiga, Sammy Cool na Bob Rich, Mzee
Bachu, Ommy Sidney, Black Moses , Maganga, Hafidh, Ali Baucha na mpaka leo sanaa hii
imeendelea kukuwa kupitia matamasha mbalimbali kama dance 100 mia.
4.Nguzo ya Nne ni (EMCEE / M.C) - Mwandishi wa Nyimbo, Rhyming, Msanii, emcee
ni msanii anayerap juu ya midundo, midundo yenye kishindo cha nguvu midundo yenye
mpangilio wa sauti ikiambatana na kick na snare, miaka ya 80's Tanzania kulikuwa na
MaeMcee wa Real HipHop kama wakina
Coneway Francis, DJ Young Milionea, DJ.Danny Star, Mukama Muganda GTRM,
KG 40 ,G Pupple(George Kusila) KBC (Kibacha), Makili, Chief Rymson, Eddy
Cox, Dika Sharp, Fanani (Trigga F),Ibony ,Fresh XE , Saleh Jabry ,Kool Moe Cee, Kool X,
MGM, Tough Jam, Big Money, DJ Edy Cox, Nigga One (Adili Kumbuka),Chief Rymson,
Lady Tassy, Killa B, Easy B na, P Funk , Mukamuganda GTRM, Mahadia Kumbuka.D-
Rob(zomba), Kr- Mullar,2proud,Nigger J,Sos B,Hashim Dogo,Imamu Abbas,Balozi Doul
Soul,Y-Thang,Lindu,Kimya,Kala Pina,Gwalu Fuluda,Nash Mc, JCB,Chindo Man,Fid
Q,Father Nelly,Stopa The Rymecca,Ibra Da Hustla,Jay Mo, Nikki
Mbishi,Saigon,Mapacha, Rado,Abc-ujamaa,Lugombo,hao ni Ma-eMcee wa apa
wakiwakilisha wengine wengi wanaofanya utamaduni wa Real Hiphop

4
Emcee wengi walianzia shule kwenye mabonanza mbalimbali kama Jitegemee secondary,
Twiga, New Chox,Silent Inn Mwenge,Imasco Temeke,Lang'ata,Kinondoni Club,Kiringe
Msasani Club,Wapi British Council, Coco Beach.

5
6
5.Nguzo ya Tano ya Real Hiphop ni (Knowledge) Wisdom and Over-standing yani
maarifa na hekima ni nguzo muhimu ndani ya utamaduni wa Real Hiphop kwani ni
maarifa na hekima vinavyomwongoza Real Emcee na kumpelekea kuandika au
kuwasilisha tungo zenye funzo,zenye kukanya ama kukemea yaliotokea au yajao kwa
kuinyoja jamii na kuiangazia muktadha wa yajao, (Lost Element in Hip Hop ) hii nguzo
ya Knowlege imefifia ama kupotezwa na kizazi cha Hiphop matokeo yake sanaa ya Real
Hiphop inapelea maudhui na dhima halisi ya utamaduni wa sanaa yenyewe ya Real
Hiphop kwa sababu ili upate uelewa wa sanaa ya Real Hiphop huna budi kuelewa nguzo
na vipengele vinavyopelekea kuwepo kwa Real Hiphop kupitia Elimu ya jamii Husika na

historia ya jamii husika .


The Don @unju bin unyuku son of uchu

7
MLALE PEMA ADILI KUMBUKA, D-ROB, FATHER NELLY, DONII, GEEZ-
MABOV NA MC's wote M.A.P
Baada ya kupata utambulisho kwa ufupi nini maana halisi ya utamadumi pamoja na mila
na desturi za muziki ama sanaa ya muziki wa kurap ama kufokafoka( Real Hiphop)
pamoja na Nguzo zake tano sasa tunaitazama Historia ya Muziki wa Rap hapa nchini
kwetu Tanzania mwanzo jinsi harakati zake zilivyochipukia na kupelekea kuenea na
kukua na kusambaa kwa utamaduni huu wa Real Hiphop..
Hip-hop ya 'Tanzania,Hip hop ya Tanzania ilianza katika miaka ya 1980 wakati huo vijana
wa Kitanzania walikuwa na mapenzi ya juu na muziki wa hip hop wa Marekani. Hapo
awali, walichukua biti za rap na hip hop za Kimarekani na kuimbia juu yake.
Wakati vijana wakirap, polepole ikaanza kujitengeneza katika maudhui ya muziki wa asili
ya Kitanzania kwa kuunda muziki wa aina yake yenyewe. Matokeo yake, ikaanza
kuonesha shauku kutoka kwa vijana wengine kutoka katika maeneo ya Afrika Mashariki.
Real hip-hop kupitia nguzo ya graffti/machata ilikuwepo tangu Tanganyika kama
nilivyoelezea kwenye utangulizi kule kondoa Irangi ila katika nguzo ya Emcee utamaduni
huu wa Real Hiphop Tanzania ilianza tangu miaka ya 80's ambapo rap ilikuwa ikifanyika
kwa emcee kurap nyimbo za kimarekania ambazo zilikuwa kwa lugha ya kimombo
nyimbo izo walikuwa wakitumiwa kanda au CD za muziki kutoka kwa
ndugu,jamaa,marafiki waliokuwa uko Nje mfano nyimbo kama zakina Grandmaster
flash,Run DMC,Eric B,Rakim,Doug E Fresh,Public Enemy,LL Cool J,Biggy Daddy
Kane,Boogie Down Productions,N.W.A,Slick Rick,Ice T,
Tanzania kulikuwa na Emcee akiitwa Fresh X E - jina halisi ni Edward Mtui na ndiye
hasa mwanzilishi wa kurap kwa Kiswahili katika miaka ya 1980 na alikuwa akiimba wimbo
wake kwa kiitikio cha "Piga Makofi" ambao aliubadilisha wa Run-D.M.C. Clap Your

8
Hands, lakini hajaurekodi. Kwa kuenzi uwepo wa Fresh na mchango wake katika
tasnia, Professor Jay akatengeneza wimbo wa Piga Makofi kwa kutumia kiitikio kilekile cha
Fresh kisha kutaja hazina kubwa ya wasaniii walioanzisha hip hop ya Tanzania, akiwepo
Young Millionaire na Conway Francis.
ilipoingia miaka ya 90's marapa wa Tanzania walibadili muziki kwa kuchukua sampuli
ya midundo ya rap ya Kimareni, na kutia maneno ya Kiswahili ata ivyo baadae
maproducer wa Tanzania wakimo wakina Dj Boni Lovu,Master J,P-Funk, walihamua
kutumia midundo yenye mahadhi ya kitanzania na kuanza kutengeza mizani, sauti na
midundo ya kinyumbani ikiwa na twisti ndipo wasanii wa Real Hiphop Tanzania
walipoanza kuandika mashaiiri yenye vina,mizani, na hoja zenye kuburudisha na
kuelimisha kuhusu, magonjwa, umaskini na rushwa, au kuhusu maisha, mahusiano, fedha,
wivu na mapenzi na majigambo ndani yake.
Sehemu kubwa ya hip hop ya Tanzania ilianza na watu ambao siku hizi hawatajwi
kabisa au mchango wao unaonekana hafifu. Baadhi ya wasanii walioanzisha hasa
gurudumu la muziki wa hip ho ya Tanzania. Kifupi, hip hop ya Tanzania, sehemu kubwa
ya wasanii walianza kwenye miaka ya 1985 hadi 1987. Zama hizi kulikuwa na mashindano
ya kurap katika maeneo mbalimbali hasa majumba ya starehe na masheleni. Ukikutana na
mtu anayeweza kuchana kwa Kiingereza lazima ushindane nae mtu kwa mtu hadi
kieleweke (Battle)
Saleh Jabri ndo msanii wa kwanza wa hip hop ya Tanzania kurekodi na kusambaza kazi
zake. Japo mwenyewe hakuonesha kutaka kusambaza kazi zile bali alikuta tayari mzigo
uko sokoni na baadaye kukamia ili apate chochote kitu. Inaaminika ndiye hasa
aliyechochea kurap kwa Kiswahili, hasa kwa kufuatia shindano la Yo Rap Bonanza la
mwaka 1992 na kuibuka mshindi.
Saleh Jabri hutazamika kama ndiye chachu aliyesabisha wasanii wengine wa muziki wa
hip hop ya Tanzania kuanza kuimba kwa Kiswahili,Kabla ya Saleh J kushiriki kwenye
tamasha la Yo Rap Bonanza, lugha kuu ilikuwa Kiingereza kwenye ilo tamasha, lakini
Saleh alitumia Kiswahili katika tungo zake. Hasa alifanya kunakili nyimbo za Kimarekani,
Kama vile Ice Ice na kuimba kwa Kiswahili.
Wimbo wa Ice Ice wa Blake feat DDG‟‟ aliurekodi mwishoni mwa mwaka 1991,
Wimbo haukupendwa sana na marapa wa Tanzania bara kwa sababu wakati huo watu
kitambo walishaanza kuchana katika kumbi mbalimbali jijini Dar kama vile Twiga, New
Chox, Coco Beach na nyingine kibao tangu 1987. Pamoja na yote, bado hakukuwa na
rekodi rasmi zilizotolewa.
Kwa vile walifanya Kwa kujifurahisha, watu walikuwa wanakutana chini ya uangalizi
WA Bonny Luv, Na makundi yakaanza kuundwa kwa kasi ya ajabu kuanzia mwanzoni
mwa miaka ya 1993. Hata rekodi za awali ilianza tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990,
lakini sehemu kubwa ya nyimbo hizo ilikuwa kwa Kiingereza japokuwa kulikuwa na
baadhi ya wasanii waliokuwa wanakinukisha kwa Kiswahili japo si sana.
Kwa kipindi kile ilikuwa aidha uende kwa watayarishaji huko Masaki au studio za Clouds
na rap ilikuwa inakua kwa kasi. Nilipewa upendeleo wa kipekee kwa kudondosha wimbo

9
wa "Oya Msela"' na Clouds Ent 1991 lakini sikuwa wa kwanza kuimba kwa Kiswahili,
kulikuwa na wajuvi zaidi yangu kabla ya mimi.
Lakini umaarufu wa wimbo ulishika hatamu na kupigwa sana kwenye vyombo mbalimbali
vya habari kama vile ITV ulitazamiwa kama wimbo wa kwanza wa rap wa video kurushwa
katika runinga hiyo. Kwa hakika ilimaliza nyimbo za rap ya Kiingereza kwa sababu tangu
hapo wengi walitamani nao kuimba kwa Kiswahili. Baada ya kibao hiki, nilipata simu
kutoka kwa Mr II lakabu Sugu akisema, "ahsante kwa kufunifungua macho".

SAIGON PFUNK

1. Conway Francis (1990) Rapper 2. Samia X, Cool Moe Cee, Ibony Moalim, Kim, Adili
Kumbuka
Conway alikuwa mwanachama wa kundi la "Three Power Crew" ambalo ndani yake
alikuwa anakuja Fresh XE, Young Millionaire na Con mwenyewe. Con alikuwa
machachari Sana.
Adili Kumbuka, lakabu Nigga One. Alikuwa mchanaji maarufu sana kwa watoto Ilala.
Katika shindao la Yo Rap Bonanza la mwaka 1992, Nigga One alichukua nafasi ya pili, na

10
ya kwanza ikaenda kwa Saleh Jabri. Kundi lake lilikuwa Raiders Posse kabla kuundwa KU
Crew. Alikuwemo KBC, D-Rob, Eddy Cox, James Paul Wamba na wengine wengi.

Kwa baadhi ya waghani vijana kama Dolasoul, au Balozi, (Ahmed Dola), "walifanya rap
kwa kujifurahisha tu, sio kwa ajili ya kujipatia kipato,miaka ya 90's rekodi zikaanza
kufanywa, unakili na usambazaji wa hip-hop , Kwa mujibu wa mwanahabari Henry
Bukuru (a.k.a. Cxteno Allstar), mzuki wa rap ulikuwa hasa ndiyo uliyoleta athira ya
utamaduni wa hip hop nchini Tanzania. Mponjika aliwahi kuelezea elementi nne za
utamaduni wa nchini Tanzania: break dancing (b-boying), graffiti, DJing, na rapping.
Mashindano ya UDJ yameleta kuzaliwa kwa hip hop, hasa huko Zanzibar, ambapo
kulikuwa na televisheni inarusha mashindano haya yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja
visivyo rasmi kwa ajili ya mashindano hayo.
From:theostell1986@yahoo.com or theostell1986@gmail.com (0712055981)
@1959.61.2021.jan.84.theostell1986@Elizeus Jerad Mushobozi"I AM REAL HIPHOP"

*Mawingu Band lakabu the Clouds - ilikuwa bendi iliyotamba na wimbo wa "Oya
Msela" wimbo ambao unatoka katika albamu yao ya mwaka wa 1994, Msela. pia kuna
Cool James lakabu Mtoto wa Dandu
*Adili Kumbuka lakabu Nigga One - alikuwa mmoja kati ya wasanii mahairi sana katika
rap ya Tanzania. Vilevile alishiriki vilivyo katika kuanzishwa kwa Kwanza Unit mwanzoni
mwa miaka ya 1990 bahati mbaya hakuona matunda yake kwani alikuja kufa katika ajali ya
gari mnamo mwaka wa 1993(M.A.P). Kulingana na duru, Nigga One inasemakana alikuwa

11
hatari sana kwa kufoka. Wasanii wengi walimhofia kupambana nae katika mashindano ya
rap,Sindila Assey anamwelezea Nigga One
"To be honest, a lot of icons where with Kwanza Unit, One, Ramzy, KBC, Easy B just to
name a few. One aka Adili was the most stubborn influence behind every stage. He never
shies away from an empty instrumental. He will annoy any DJ to get the piece of his lyrics
out anytime anywhere. A very humble dude he was. He would always share a stage with his
crew (KU) and anyone who's willing to try him. That's the interview you would have loved
to have. I instantly became a friend when KBC introduced me to all (KU) one afternoon
day at Twiga when DJ Bonny Luv asked of me. I was nervous; KBC was telling them I can
do Treach all day... my gf was there too. In front of KU I did prove myself. Adili was
jumping up n down. We then set for a New Chox cinema show. „One‟ was unique on the
microphone. He flowed like the late Guru and would get on any track".

*Kwanza Unit - miongoni mwa makundi ya kwanza kabisa katika hip hop ya Tanzania.
Kiufupi, KU ndiyo kundi la kwanza kuundwa katika tasinia nzima ya muziki wa hip hop
ya Tanzania. Kuundwa kwa kundi ni juhudi kubwa na za dhati kutoka kwa Zavara
Mponjika na hayati Nigga One. Kabla ya muungano, kulikuwa na mabifu kibao yasomana
na ilibidi waungane li kuondoa mabifu na kukuza muziki kwenda kiwango kingine.
Kuungana kwao, kulifanikisha mambo mengi kama wasanii waasisi wa rap ya Tanzania.
Pia kulikuwepo na Hard Blasters - kundi ambalo hutazamiwa kuleta mabadiliko katika
muziki wa hip hop ya Tanzania likiundwa na Fanani,Terry,na Nigger J

12
Pia kundi la Da Young Mob - kundi ambalo II Proud alipanda nalo katika kinyang'anyiro
cha Yo Rap Bonanza, 1993
Pia kuna kundi la Deplowmatz - Wakati wanaanza harakati ilibidi kwanza wamuone
Sindilla Assey kwa ushauri zaidi. Muda mfupi baadaye wakarekodi nyimbo zao mbili za
kwanza "Turuke kwa Furaha" na "Word is Born".izo nyimbo ziliipa umarufu kundi ilo na
kujulikana na wengi.
Kuna kundi likiitwa No name likiundwa na P-Funk na Mchizi karabani, makundi
mengine yaliowakilisha sanaa ya Real Hiphop ni Wagumu Weusi Asilia lakabu W.W.A
Black Houndz,Bantu Pound,Niggaz with Power (NWP),Full Soldiers,Rough Niggaz,Kibo
Flava,The Mac Mooger,Mabaga Fresh,KNT Squad ,Ras Pompidue,Sos B,Niggaz 2 Public,
pia kulikuwa na kundi la Xplastaz na Underground Souls,GWM,Big Dogg
Pose,L.W.P,Gangwe Mobb,Afro Reign,Pyscho Tak, na kundi la Ugly Faces likiundwa na
Mac D,Dj Rich Maka,Eazy Daz walifanya ngoma moja kali ndani ya Mawingu Band chini
ya Bonny Luv mwaka 1997 ngoma ikiitwa"wapambe Nuksi" kuna kundi la Hardcore
Unit,Imeditation Kingdom,Fun with Sense,wachuja Nafaka,Watengwa, pia kuna
Watulutumbi,Kikosi cha Mizinga,Naco2Naco,Vatoloco Soldier,Mapacha,Boys from the
Army,EastCoastTeam,TMK Crew,Tamaduni Music,Kikosi Kazi,River Camp Soldier,Pia
kuna kundi la Isanga Family,Vinega,Dox Family,U'Clan,
Emcee wengine waliochangia kukua kwa utamaduni wa Real Hiphop ni pamoja na
2Proud a.k.a Mr II a.k.a Sugu a.k.a Jongwe, pia King Crazy Gk,Bugsy Malone,Kool X,
Big Money pia kunaE-Attack,Hashim Dodo vogo Mwendawazimu Kitimtim,Mack
Malik"Mac2B"Solo Thang, Juma nature,Jay Mo,Dataz,Squezer,Bu-Naco,Afande
Sele,Bonta,Adili Hisabati,Soggy Doggy,pia kuna D-wa Ghetto,Coin,Suma G,Prof.Ludigo,
Adili, Joh Makini, Mansu-Li, Blac, Salu-Te, Saigon, Magazijuto, Geez Mabovu,G-
nako,Lord Eyes,P-The Mc,Zaidi,One da Incredible,Nikki Mbishi, Godzilla,Criff-
mitindo,Andaki,Mteganda,Imamu Abbas,"bwax"Dudu Baya,Dnob,Ommy G,Mansu
Li,KadGo,Azma,Kimya,Chidi Benzi,Ibra da hustle,Abou Gaidi,RuffMc,
Wakazi.Complex.Rah P,Zay B,Witness,Sister P,Langa,Dark Master.Zaharan.
Rage, YoungKiller, Songa, Sasho, Ras Omega, Rambo-fidovato, Yuzzo, Dwee.

13
M.A.P mtoto wa dandu da Legend PFunk Master J
Mwanzoni mwa harakati za kukua kwa utamaduni wa Real Hiphop Tanzania kulikuwa na
mabonanza pamoja na matamasha yaliochangia kuibua na kukuza sanaa ya Real Hiphop
Shindano la kwanza la muziki wa rap nchini Tanzania lilianzishwa na marehemu
Shaban Sato mnamo 1989/90 katika ukumbi wa Lang’ata. Kupitia mashindano haya,
ndipo marehemu Kim and the Boyz (Abdulhakheem Magomero) na Ibony
Moalim walipopata wazo la kuanzisha mashindano makubwa ya rap maarufu kama Yo
Rap Bonanza katika ukumbi uleule wa Lang‟ata Kinondoni..
Emsii usiku huo alikuwa DJ Junior Challenger almaarufu Amani Misana (Mzee wa
Pillow Talk). Usiku wa shindano uliambatana na kudansi (wakati huo waliita B Boying)
akina Othman Digadiga, Sammy Cool na Bob Rich, Mzee Bachu, Ommy Sidney, Black
Moses , Maganga, Hafidh, Ali Baucha wengine wengi walionesha uwezo mkali wa "Break
Dancing". Kwa upande Ma-emsii walikuwa wengi sana ikiwa ni pamoja na Coneway
Francis (wakati huo alionekana kuwa tishio katika rap na alivutia wengi kuingia katika
shindano). Inasemekana Conway alikuwa na suati zito ambalo lililkuwa kivutio wakati huo
na aliimba na dada mmoja aliyefahamika kama Janeth (Janet Jackson)
Ma-emsii wengine ni pamoja na DJ Young Milionea, DJ.Danny Star, Mukama
Muganda GTRM, KG 40 (Kelvin Ndunguru) na kundi lao la the Raports akiwa na
wakina G Pupple(George Kusila) KBC (Kibacha) na Makili, Chief Rymson na kundi zima
la Villian Gangster (baadaye ikaungana na kundi lingine la rap na kuunda Kwanza
Unit), Eddy Cox, Dika Sharp, Fanani (Trigga F) na Ibony Moalim (ambaye wakati huu
alikuwa ana floo na kurap), na wengine wengi. Katika usiku huu, Coneway Francis alitisha
kupita maelezo. DJ Danny Star (aliiimba Summer Holiday Rap) KG 40 na Fresh
XE ambaye kwa nyimbo hiyo hiyo ya “Piga Makofi Tafadhali ndiye aliyeibuka mshindi wa
taji la Rap. Kwa bahati mbaya kukatokea vurugu, hasa kutoka kwa vijana wa Illaa na watu
wengine wanaompenda Coneway Francis wakafanya fujo na kudai kuwa ushindi uende
kwa Coneway hata hivyo matokeo hayakuweza kubadilishwa.

14
Shindano la pili la Yo! Rap Bonanza, ambalo lilifanyika katika ghorofa ya saba katika
hoteli ya New Africa. Safari hii, makundi ya rap yaliongezeka mno kupita wale wa
kwanza. Hii sasa ilivutia hata watu kutoka nje ya Dar es Salaam, na ndiyo ilikuwa mara ya
kwanza kwa Saleh Jabry kushiriki katika mashindano ya Yo Raps. Upande wa majaji
alikuwepo Ibony Moalim - kama Chief Jaji, DJ Saydow, Mark (Mzungu wa Holiday
Hotel),na Slim (Check Bob Maarifa).
Upande wa wasanii walioshiriki ni pamoja na Kool Moe Cee, Kool X, MGM, Tough Jam,
Big Money, DJ Edy Cox, Nigga One (Adili Kumbuka) na kundi zima la Raiders Posse,
Chief Rymsom, Lady Tassy, Killa B, Easy B na kundi lao la the Bad Mother's, KG 40
(Kelvin Ndunguru), KBC (Kibacha), Saleh Jabry, P Funk na kundi lake la No Name,
Mukamuganda GTRM, Mahadia Kumbuka. Upande muongozaji wa tamasha alikuwa DJ.
Rusual na lugha iliyotumika ilikuwa Kiingereza. Rusual (wa Jetset Discotheque - Msasani
Beach) ndiye aliyendeshsha shindano, aliweza kurap kidogo kwa Kiswahili na hata alitia
na Kidigo kuboresha na watu walipenda sana.
Wakati shindano linaendelea, mmoja kati ya majaji usiku huu uzalendo ulimshinda na
kuanza kuingia stejini na kuanza kuruka majoka wakati zamu ya Saleh Jabry (jaji
mwenyewe alikuwa Slim - Check Bob Maarifa). Alifanya hivyo kila alipokuwa anaingia
Saleh Jabry. Suala hili lilipelekea shindano hilo kusimama kwa muda hadi hapo
walipopatana na majaji wenzie asifanye hivyo. Zogo lilikuwa kubwa, lakini hatimaye
waliyamaliza kikubwa.
Mtindo aliokuwa nao Saleh Jabry ni ule wa kuchanganya maneno ya msimu ya Kiingereza
na Kiswahili kidogo. Inasemekana katika usiku huo, ni watu wawili tu ndio waliongea
Kiswahili, DJ Rusual na Saleh Jabry tu, lakini wengine wote walikuwa wanamwaga
Kiingereza tu (hii ikiwa kama mwigo wa mtindo halisi wa rap ya Kimarekani). Hata matusi
aliyokuwa anatukanwa Slim yalikuwa kwa maneno ya msimu ya Kiingereza cha
Kimarekani. Pamoja na kushiriki wasanii wengi na mazogo ya hapa na pale, mshindi wa
usiku huo akawa Saleh Jabry.
Tamasha/shindano hili la Yo Raps! Bonanza ilifanyika Mara sita. Tamasha hili lilileta
hamasa kwa watu wengi baadaye. Miongoni mwao akina Issa Michuzi waliokuwa
tayari kutoa taarifia hizi katika magazeti nchini. Akina DJ Jummane (Mzungu Mholanzi
maarufu DJ J4 au Jumanne Thomas). DJ huyu ambaye baadaye kaja kuwa kama
mwanaharakati halisi wa muziki wa hip hop ya Tanzania. Kaenda mbali zaidi kwa kuwa
kama meneja wa kundi zima la Xplastaz na mwaka wa 1997 akaanzisha wavuti ya Rhumba
Kali (baadaye na hadi sasa inaitwa “African Hip Hop.com). DJ J4 ana nafasi kubwa katika
muziki wa hip hop ya Tanzania, kwanza akiwa kama mshabiki nambari moja kutoka nchi
za nje, na mtunza kumbukumbu mkuu wa muziki huu wa hip hop ya TZ.[16]]]

"REAL HIPHOP" ILIPEWA NGUVU NA KUNDI LA KWANZA UNIT AMBAO


MWAKA 1994 WALITOA ALBUM YAO YA KWANZA ILIYOITWA KWANZA-
UNIT,PIA MWAKA 1995 WALITOA ALBUM YA PILI ILIYOITWA TROPICAL
TECHNIQUES NA ALBUM YA TATU ILITOKA MWAKA 1999"KWANZANIANS,
Members na foundation wa Kwanza Unit ni Chief Rhymson(Ramadhan A.
Mponjika),KBC aka K-Singo (Kibacha Singo),Adili "Nigga One" Kumbuka – amekufa
15
1993,D-Rob(Robert Mwingira) – amekufa 2001, Eazy-B (Bernard Luanda),Papa Sav
(Makanga Lugoe),Abbas Maunda,Balbo,Baraka,Fresh-G
Y-Thang, Gaddy GrooveBugzy Malone (Edward Margat),Richard Mwingira,Totoo,
Base One aka KK (Khalid Kumbuka), Lenana na Sundeo

"harakati kazi ngumu wengi wamezikimbia" by Kalama Masudi"Kala Pina" in Umoja ni


Nguvu
Ngumu kumeza; LINDU, MAJANI.PARA.DUKE
.KIMYA.DAZKNOWLEDGE.MUJWAHUKI.TEXAS.QTHEDON.
PROF.LUDIGO.DUNGA.LAMAR.DX,CASTRO, ,Bonny P,Ray Technohammer,Wille
Hd
SALUTE TO RECORD LEBO SOUND CRAFTERS''ENRICCO,JCEE" PIA DON-
BOSCO"MALLEN RANGES"
MJ-RECORD"MASTER J",BONGO RECORD"PFUNK",MAWINGU STUDIO"BON
LUV"M-LAB''DUKE''

16
2proud na Master J Duke Tuchez Daz Knowledge

Pfunk na stopa Ryme Prof.Ludigo Jumanne Mchopanga"Jay Mo"


Muziki huu ulianza kujengwa katika miaka ya 1980 wakati vijana wa Kitanzania
walipoanza kuvutiwa kuimba muziki wa hip hop wa Marekani.Haraka wakaongeza.
Aina hii ya muziki imekuwa maarufu kwa haraka sana; umekuwa miongoni mwa muziki
unaouza vizuri katika Afrika ya Mashariki, na tayari ushapata mafaniko katika nchi za
jirani kama vile Kenya na Uganda, na kusambaa maeneo mengine ya Afrika na duniani
kwa ujumla. Mwaka wa 2004, studio ya Kijerumani Out Here Records ilitoa kompilesheni
ya CD iliyoitwa Swahili Rap from Tanzania.[6] CD hiyo yenye dakika 70 ambayo ndani
yake kuna wasanii kama X Plastaz, Juma Nature, na Gangwe Mobb wamefurahia
usambazaji huo wa kimataifa.

BEEF NDANI YA GAME YA REAL HIPHOP BONGO.

17
Katika ulimwengu wa tamaduni ya Real Hiphop kulikuwa na migongano ya
mawazo,tofauti za kiitikadi, au tambo na majigambo ambayo yalipelekea labda sanaa ya
Real Hiphop kupendwa na kutambulika na jamii kwa wingi au kupelekea kushuka kwa
sanaa husika,
hapa tunazungumzia malumbano au Beef ndani ya tamaduni ya Real Hiphop ambazo
zilitokea katika kundi na kundi au msanii kwa msanii na kupelekea shauku au taharuki
katika tasnia ya Hiphop.
1. BEEF KATI YA KWANZA UNIT VS DIPLOWMATS-bifu iliyodumu kwa muda
mrefu kiasi cha kwamba mashabiki wenyewe kutoka kundi moja kuwa na chukidhidi ya
wengine kuwa na chuki na ilifikia mpaka kushikana mashati na kulushiana ngumi
wakikutana mitaani na ilikuwa ni bifu ya mistari na bifu ya mitindo huru na ushindani wa
kutoa ngoma kali, yani kundi ili likitoa single hii na kundi ili linaingia studio kujibu na
makundi yote yalikuwa chini ya Lebo ya Maste J,
mpaka ikatokea kushindanishwa ndani ya kipindi cha radio One cha "Nani Zaidi" ambapo
kundi la Diplowmatz waliibuka kidedea,"ila kwanza unit walikuwa hardcore na
deplowmatz walikuwa commercial" kwanza unit waliimba kama nilivyosema sasa nakuja
na deplowmatza wakajibu wakasema vyovyote utakavyokuja utachezea msuli, kwa iyo bifu
ilikuwa bifu kindakindaki.

KWANZA UNIT VS DIPLOWMATS

2. BEEF KATI YA EASTCOAST TEAM VS TMK WANAUME-hii ilikuwa bifu ya


majigambo na pia ilikuwa bifu ya kuoneshana uwezo wa kurap na kughani mashairi kati ya
vijana wa temeke na wale ambao maskani yao ilikuwa upanga, bifu hii kati ya Eastcoast
team iliyokuwa na vijana machachari wa kugani mashairi ya rap kama
Ay,FA,GK,Snare,Buff G,sharrif,Oten na wengine pia Temeke TMK walikuwa na
wakongwe wa game ya hiphop katika kujibu mashambulizi wakiongozwa na KR
Mullar,Juma Nature,Doro,Mzimu,Doto, na wengine. Bifu ili lilikuwa kubwa kiasi cha

18
kuanza kuwekeana mipaka ya maeneo ya kupita mtaa kwa mitaa, pia ilikuwa imejaa tambo
za uyu kusifia maisha ya kishua na hawa wakitamba na maisha ya uswaz. ingawa bifu ili
lilipelekea kuchochea kukua kwa muziki wa rap pia kwenye soko la muziki ilichachusha
soko na matamasha yakawa yanafulika na sanaa ikaongeza kipato.

EASTCOAST TEAM VS WANAUME TMK FAMILY


3. BIFU KATI YA KIKOSI CHA MIZINGA NA NACO2NAKO-katika historia ya
muziki wa Real Hiphop Tanzania beef ambayo ilikuwa serius kuliko kawaida ilikuwa bifu
ya aya makundi, bifu ilikuwa ya mistari,bifu ya mitindo huru,iliingia mpaka kwenye staili
za maisha ya kawaida, ilikuwa kwenye punchline wanachanana kinomanoma na kila
kundi likuwa linajiona lenyewe ndo linafanya Real Hiphop, na pia kila kundi lilikuwa
likijigamba kwamba hiphop ipo sehemu flani uyu anasema Real Hiphop ipo Arusha na
kikosi wanasema Real Hiphop ipo Dar, hii bifu ilipelekea member mmoja wa kundi la
Naco2naco aliyeitwa Bu-Naco kukutana na uvamizi na kipigo kilichomsababishia
majeraha makubwa, ata ivyo naco2naco nao walijibu kwa mistari punchline beef na pia na
wao kulipiza kwa kuvamia maskani ya kikosi cha mizinga iliyopo maeneo ya block 41
kinondoni na kuleta noma ya hatari kikosini, hii bifu ilipelekea Emcee wa Kikosi cha
Mizinga Kalama Masudi-kalapina kuwa wanted ndani ya Chuga.na Naco2naco kuwa
wanted Dar na hii ni bifu iliyodumu muda mrefu ikiwa ni serious kinoma sio kama zile bifu
nyingine za kibiashara na mashairi hii ilienda kwenye bifu la kinoma noma.
Pia kikosi walikuwa na bifu na wasanii bongofleva kwa ujumla kulikuwa na diss track
kibao dhidi ya bongofleva kama track ya "Beef" "tunalipua" "wasaliti" track ya mstari wa
mbele" uwezo,"wabishi wa dar es salaam" na track nyingine kibao wao Naco2naco
walikuwa na Hawatuwezi,HipHop,machafuko, izi track nazo zilikuwa na punchline za diss
dhidi ya bongofleva kwa iyo haya makundi ukiacha bifu lao pia walikuwa na bifu na
wasanii wa muziki wa bongofleva.
''MJESHI ANAPOKUFA NDO MJESHI ANAZALIWA HAKUNA CHA
KUCHEKESHA ATA UCHESHI UNGETAKIWA"HASHIMU DOGO
MWENDAWAZIMU"

19
NACO2NACO VS KIKOSI CHA MIZINGA
4.BIFU KATI YA VINEGA VS CLOUDS MEDIA-hii bifu katika tamaduni ya Hip Hop
Tanzania naizungumizia kwa sababu chanzo chake ilikuwa ni wasanii wa muziki wa
Hiphop walikosa platform ya kuwasilisha kazi zao za sanaa katika media house mbalimbali
na ata kukutana na vizingiti ata nje ya media mfano ata wakati wa uandaaji wa matasha ya
tamaduni za hiphop ulikuwa unakutana na vizingiti lakini kila ukifatilia vile vizingiti
chanzo unakuwa ni clouds media ambaye alikuwa amekamata wadau wote wa muziki na
kupelekea tamaduni ya Real Hiphop kizidi kukandamizwa.
Japo kuwa wadau wanasema hii ilikuwa inshu binafsi za kinega Jongwe na Ruge,lakini
ukweli ni kwamba mvutano wa tamaduni ya hiphop ulikuwa ukigonga ukuta wa uyu
mshikadau clouds media ,sasa maujanja saplayaz mapacha,sugu,Adili Hisabati,Prof.Ludigo
wakina Rama D,Soggy,Coin,D-wa Ghetto,Suma G na wenzao wakaamua kujilipua ki-
mullah omar kupigania sanaa ya Real Hiphop chini ya Ant-virus mixtape ikiwa na joint
kama "Huu mziki",Hellow wafu Fm"Clouds Get Money From Us"
Clouds media nao wakajibu mapigo kwa kufungia kucheza nyimbo za Vinega zikiwemo
kutocheza nyimbo za Rama D,Sugu,Mapacha,Dani Msimamo,Soggy,Suma G
na kwenda mbali mpaka bungeni kumshtaki Mbunge Sugu kwa Ant-virus
Lakini Clouds Media walikuja kusanda na kuanza kuomba usuluhishi baada ya kuona mix-
tape zinazidi usambaa na kuungwa na mkono na legends Emcee Kama wakina Juma
Nature,Inspector Haroun wakaona ngoma itakuwa ngumu na hatimaye bifu likapoa na
kuendelea kuunguruma kimya kimya kwani wale wasanii ambao nyimbo zao zilipigwa
marufuku katika iyo media bado zilipigwa lupango.

20
Kwa iyo pamoja na media hii ya clouds iliyochangia kukuza sanaa hii ya hiphop pia ndo
iliyopelekea kushuka kwa sanaa hii ya Real hiphop kwa kutozipa Airtime tena kazi za
hiphop kama ilivyokuwa hapo awali na kupelekea huu mgongano wa maslahi na fikra.

From:theostell1986@yahoo.com or theostell1986@gmail.com (0712055981)


@1959.61.2021.jan.84.theostell1986@Elizeus Jerad Mushobozi"I AM REAL HIPHOP"

21
PIA KULIKUWA NA LYRICS AMBAZO ZILIKUWA ZA BIFU AU DISS KWENYE
GAME YA HIPHOP EMCEE KWA EMCEE AU EMCEE KWA MEDIA STREAM
AU WADAU WA MUZIKI;
Verse ya Crazy Gk- ama zao ama zangu"...iwe mtaani ama maskani,home au popote,amiri
jeshi mkuu sasa naitangaza vita,siku ile kuu ya tatu bali hii ni ya kiviet-nam bali mtaa kwa
mtaa,mmoja mmoja nawakamateni alafu nazaa nao...."
Verse ya KR Mullar - Kamua"kruu kuaah Yes Pfunk nipe beat kimakusudi machizi GWM
tumeshaludi,na mwaka huu lazima ma&%v yagonge chupi,wananiita Kr jibaba mziki
mkubwa CD700 njoo kichwa kichwa kula za uso vaba,huu ndo ujio na haina fagio ni
majitu ya mistari toka awali,majabali yenye asili ya kimentari na hisia kali..
Verse ya Hashim Dogo-mitindo huru"waniita dogo ngale mi-si-vogo nasizi kama nimekula
mjani si kidogo,nipe kipaza nipate kuharibu taratibu mamc mistari inawasibu,nawaharibu
mamc si ki#%nge niko kijenge kama vile kiberenge,nasonga kwenye reli nazungumza
ukweli si uongo wabongo wamejawa tongotongo,longolongo kibao ndo maana mimi
natafuta mafao,.....",
Verse ya Kala Pina -Mstari wa Mbele"...zimaa zima mziki Halfan Majani wazaramo
wameshapanda kichwani,wanataka kifo wakati kinakuja bila hodi,wanatamani kiama hali
ni kesho,hii ndo hiphop sio bongofleva wala komesho...."......mnaongea mnatetemeka
sanaa wapi mnaipeleka sisi sio watu wa kucheka cheka.."
Verse ya Chindo Man-Sio Lazima"Hiphop imeanza Arusha,Dar Mnatuyayusha mala
Maemcee mashoga mamcee waoga,battle kwa sana Hiphop ndo itarudi sio mnatetereka
kama wakurdi,Hiphop ya mtaa inaitaji akili sana,huwezi ukakurupuka..."
Verse ya Hashim Dogo"mistari inaunguza kama tindi kali, ma MC wanajifunza hakuna
cha ushindi shwari, Emcee freestail ziko kama za aina tatu ambazo ukizipiga zinaweza
kuchanganya watu ya kwanza ni ile ya papo kwa papo juju kwa juu maemcee wape kichapo
alafu atanukuu,ya pili ni ile ambayo umeshaijadili ambayo mwenyewe unasafiri alafu
unakili,alafu ya tatu ni ile ambayo umeshaiandika alafu unakwenda kuitandika dakika
iyoiyo maMcee washike maskio harafu wenyewe wataona bora kutoka mbio.."
Verse ya Nash Mc-Zima" Hiyo mistari inayoitwa taarifa ya Habari oya ZIMA!
Ile ya ku unga unga mibovu ya kizushi sijui nini ''Gorge anarudi Bush ZIMA!''
Wachanaji wasio na vina hizo ngoma zote ZIMA
DJ unataka hela, aisee sina kwenye kipindi chako wimbo wangu zima,
Hata Redio yenu kucheza kazi zangu wala sio lazima
Oya nanii P the MC washa TV bunge la katiba huwa siangalii ZIMA !
Weka ata Mieleka Ya John Cena
Good Music sitaki ZIMA Kwaito ZIMA, Kiduku ZIMA!
Nyimbo za Mapenzi zenye mambo ya Kishenzi siziwezi ZIMA (eeeh)
PIA UTAMADUNI WA REAL HIPHOP UMEPITA KWENYE HARAKATI ZA
KUPIGANIA SANAA YA HIPHOP AMBAYO IMEKUWA IKIPIGWA VITA
KWENYE MEDIA INDUSTRY KWA MUDA MREFU KWA IYO ILIPITIA
KWENYE HARAKATI MBALIMBALI :

22
harakati izo zilipitia kwenye njia tofautitofauti kupitia matamasha na media ambazo
zilizokuwa zikisapoti harakati za tamaduni za Real Hiphop; Okoa Hiphop ya Adili
kulikuwa na Anti-Virus ya Vinega,Hiphop Base ya Saigon,Wapi ya Zavara,Kiringe ya
Tamaduni,S.U.A ya Daz Knowlege,Cheusi dawa ya Fid Q.
OKOA HIPHOP -
okoa hiphop ni harakati zilizoanzishwa kwa ajili ya kuinua harakati za hiphop kupitia
matamasha kwa ajili ya mapinduzi ya muziki huo.
Okoa Hip hop ni mradi maalum uliobuniwa na msanii Adili a.k.a Hisabati ambaye
amekuwa akipigana vilivyo kuhakikisha muziki huo unasimama na kufanya vizuri kama
ilivyo aina nyingine za miziki hapa nchini. Mradi unawahusha wakali wa hip hop akiwemo
Jay Moe, Adili, Joh Makini, Mansu-Li, Mapacha, Blac, Salu-Te, Saigon, Magazijuto, Nako
2 Nako, Geez Mabovu na wengine kibao.

ANT-VIRUS MIXTAPE
Harakati za Ant-virus zilianzishwa na maujanja saplyaz"mapacha wakiwa na
Sugu"Jongwe" wakishirikiana na Adili Hisabati,Prof.Ludigo wakina Rama
D,Soggy,Coin,D-wa Ghetto,Suma G na wenzao wakaamua kujilipua kupigania harakati za
hiphop dhidi ya wasaliti wa Hiphop wakishirikiana na Clouds media kutaka kutokomeza
Hiphop industry ,
vinega na harakati za Ant-virus walikuwa na record lebo ambayo waliitumia kurecord
mixtape ya Ant-virus chini ya Producer Prof.Ludigo na kufanya matamasha mbalimbali ya
kuhamasisha Hiphop na kuwafumbua wadau wa muziki macho kwamba sanaa
inadidimizwa na media kwa kubagua wasanii na kuchagua aina ya muziki wa kucheza
radio bila kujali maudhui, dhima ya sanaa ya msanii wa muziki katika jamii husika.
HIPHOP BASE.
Hiphop Base ilikuwa ni kipindi cha luninga kilichokuwa kikiluka hewani kupitia television
ya EAST AFRICA TV(EATV) chini ya mtangazaji machachari mwenye mizuka ya
harakati ya kimapinduzi ya Hiphop Saleh Daudi Suleiman"SAIGON" Hoi hoi hoi hoi
kalinyekalinye....HOI HOI... ambaye ni Legend Emcee kutoka kundi la Deplowmatz,

23
HIPHOP BASE ilipata umaarufu kwa kasi sana na ata kupelekea kupata mashabiki wengi
sana waliovutiwa na utangazaji wake lakini pia ilichochea na kukuza utamaduni wa Real
Hiphop katika jamii kwa kasi na jamii kuanza kuelewa tamaduni za muziki wa Hiphop
katika nguzo zake, kwani Saigon alikuwa akitembele maskani za Hiphop na kufanya nao
vipindi na kupelekea watu kuwafahamu wasanii wengi wa Hiphop amabo walikuwa
hawapati muda wa kuchezwa kazi zao kwa radio ama luninga.

CHEUSI DAWA NA FIDYSTYLE FRIDAY


Cheusi dawa tv ni kipindi kinachokuza na kuchochea harakati za tamaduni Real Hiphop
kilichoanzishwa na Freed Kubanda"FidQ" katika kukuza na kuvumbua na kuendeleza
tamaduni ya sanaa ya Hiphop ambayo haipati airtime ya kutosha katika vipindi vingine vya
radio ama luninga .Fidystyle Friday ilikuwa inawapa Maemcee nafasi ya kuonesha vipaji
na taaluma yao katika ulimwengu wa Hiphop na baadae kutambulika na jamii ya Hiphop
kupitia Cheusidawa tv.salute kwake FidQ kwa hizi harakati halisi za kukuza na kuendeleza
tamaduni za hiphop.

S.U.A(Support Underground Arts) BACK2SUA Kaakijanja OKOA MTAA PROJECT.


S.U.A ni harakati za tamaduni ya Real Hiphop chini ya Producer Daz Knowledge, ambayo
uwa inaandaa matamasha ambapo Emcee wanapata jukwaa la kutambulika kwa
kuwakilisha mitaa yao na hisia zao katika jamii wanayotokea,pamoja na kujifunza nguzo

24
na misingi ya tamaduni za hiphop (Emcee, Graffiti, Dj, Break-dance na maarifa) ambapo
ufanyika mara moja kwa mwezi- iniyoitwa SUA Free-stage (tangu 2012) hii project
inawezesha Maemcee kujenga ujasiri kwa wasanii, kuonekana na matumizi ya lugha, na
pia mkusanyiko wa vijana kutoka mitaa tofauti ya Arusha kushiriki maarifa. Kila mwaka
kikundi cha wasanii 3-4 huchaguliwa kushiriki katika Mradi wa Okoa Mtaa. Mradi huo ni
muundo wa kuunganisha msanii kwenye sherehe tofauti, studio, mradi na programu za
mafunzo,Mamcee ambao wanashiriki katika harakati izi kwa uchache ni pamoja na
Montra-The Future,Toxic Man,Edo G,Biznea,Pacha the Great, 21, Sight Mo ', 28, na
Uchebe Chatta,Nchama, 20. wakiwakilisha mitaa ya Kijenge, Ngalimi na Sekei, vitongoji
vitatu maarufu jijini Arusha.

WAPI.
Wapi ilikuwa ni harakati za tamaduni ya Hiphop zilizokuwa zikiandaliwa na kuongozwa
na gwiji wa tamaduni ya Real Hiphop Zavara Mponjika wa Kwanza Unit, tamasha ili la
Wapi lilikuwa likifanyika kila mwezi maeneo ya British Council Dar-es-salaam ambapo
tamaduni mbalimbali za Hiphop zilikuwa zikifanyika ikiwa ni pamoja na Emcee kufanya

25
michano na mitindo huru na pia michoro ya graffit ilikuwa ikifanyika pale. lengo la WAPI
ilikuwa ni kuvumbua na kukuza vipaji mbalimbali vya sanaa na tamaduni ya Hiphop pia
kuwapa jukwaa la kuwakilisha na kuelimisha jamii kupitia michano na pia ilisaidia Emcee
kuja uwezo wa kujiamini ata pia kujulikana na kusikika na kutambulika kwa sababu lile
lilikuwa ni jukwaa kubwa kwani Emcee wakubwa kutoka Afrika na Magharibi walikuwa
wakialikwa kuja kutoa changamoto mfano Emcee kama Tariq Trotter a.k.a Blackthought
kutoka Philadelphia wa kundi la The Roots walikuwa wakiibuka. kwa iyo WAPI ilikuwa ni
jukwaa muhimu kwenye chachu ya Hiphop salute Zavara.

HIPHOP KILINGE CYPHER (TAMADUNI MUZIKI)HISIA ZA MTAA.


KILINGE ni sehemu ambayo jamii ya tamaduni ya Real Hiphop ilikuwa ikikutana kila ya
jumamosi ya mwisho wa mwezi kuanzia saa 8:00 mchana mpaka saa 4:00 usiku ili
kujadiliana mawazo kuhusiana na muziki wa HIP-HOP,KILINGE kinaandaliwa na
tamaduni muzik ambao ni umoja wa wasanii wa HIP-HOP.
Kimsingi kilinge kilisaidia kugundua na kuendeleza vipaji vya wa sanii wachanga
wasiokuwa na uwezo wa kurekodi ikiwa ni pamoja ya kuandaa project kwa wasanii wote
waio onesha uwezo katika kilinge,
prodyuza wa muziki wa hip hop Tanzania "Duke" mwanzilishi wa M Lab Records,
Tamaduni Muzik, na ambaye pia ni mmoja wa waasisi wa Hip Hop Kilinge (cypher).
Kwenye Kilinge, vijana wengi walikuja kusikiliza muziki uliochezwa na DJs, kusikia sauti
ya MC, kushiriki katika cyphers, kununua bidhaa za mitindo ya hip hop,kama
Tshirt,CD.Mixtape,na pia kupata elimu ya masuala ya hakimiliki na sanaa ya sampling na
kufahamu jukumu la prodyuza katika hip hop. producers wa kilinge ambao walifanya kazi
na kilinge ni Duke, Bonny P,Ray Technohammer,Wille Hd,Texas, Mujwahuki, AK47,
PALLA na wengine kadha, pia kilinge kilikuwa na Emcee waliokuwa wakitoa elimu na
kuwakilisha michano na mitindo huru katika jukwaa la kiringe kama wakina Azma,Nikki
Mbishi,Wakazi,Jan B,Bonny P,Danny Laizer,P the Mcee, kadgo, ghetto ambassador,
songa, mansuli,Nash Mc, na wengine wengi tu

26
FREESTYLE RAP BATTLE/CITY RAP BATTLE(CRB).
Mwasisi wa City Rap Battle (CRB) walikuwa ni wamiliki wa MICASA Lounge
wakishirikana na Legend Sinza Star Mansuli, wakiwa na lengo la kuamsha harakati za
hihop katika msingi wa Rap Battle/Emcee, iliuwa ikifanyika ndani ya MICASA LOUNCE
iliyopo Ubungo ambapo Judges walikuwa wakina P THE MC,SONGA,ONE
INCREDIBLE na wadau wengine wa Hiphop kama Djs
Rap Battle-ni aina moja ya nguzo ya Hiphop ambayo ni mitindo huru,ambapo ni pamoja
na kujisifu,majigambo,na kuonesha uwezo wa nani zaidi katika kughani mashairi na
misemo adhimu ya mitaa ikiamabtana na umaili wa kushuka mashairi kwa kufatana na
vina na mizani, kwenye battle iyo ambapo MCs watatumbuiza kwenye jukwaa moja kuona
ni nani aliye na aya bora anaibuka kidedea, rap battle pia uweza kupelekea magomvi na
bifu kutokana na maneno makali ya mtaa ambayo yanaweza kutumika kumcholesha
Emcee mwenza katika battle. EMCEEs waliokuwa wakishiriki katika Rap City Battle
walikuwa ni wakina Black Mc,Mteganda(kibabu cha mistari),stan rhymes,Barz writer,Dibo
Mc,Jaco Geezy,Abo master,pizzaro,na wengine kibao

27
DAKIKA KUMI ZA MAANGAMIZI
ni kipindi cha radio cha East Africa Radio Fm 88.1 kinacholushwa hewani siku ya
jumatatu na East Africa Television(EATV) chini ya mtangazaji machachari Dulla akiwa
pamoja na MaDJs kama Dj Fantastic,Dj Dare,kinachoitwa Planet Bongo,ambapo Emcee
wanapata nafasi ya kuonesha uwezo wa kuchana mistari ndani ya Midundo tofutitofauti
ndani ya dikika kumi, ambapo Rappers wanapewa nafasi ya kuonesha uwezo wa kunata na
midundo na kupata nafasi pia ya kutambulika katika ulimwengu wa Hiphop na muziki kwa
ujumla baadhi ya EMCEE ambao wameshapata nafasi ya kushusha mistari ndani ya dakika
kumi za maangamizi kwenye planet bongo ni Dizasta Vina, Fikra vina,toxic,chuma boy
mbeya,nyenza,bando Mc,Rapcha,Werre mullah,James Moto,kitwana Hisabati,Boshoo
Ninja,Shakir G.I.G,Michano kuntu,Element,Mo Rymes,Q-Girl, na EMcee wengine kibao
wameshawakilisha dakika kumi za maangamizi.

REAL HIPHOP LYRICS OF ALL THE TIME WHICH INSPIRE THE REAL HIPHOP
VIBES

28
BONGO HIPHOP By Fareed Kubanda FID-Q

VERSE 1:
Ulianza wewe.. wakaja waimbaji na wabana pua/
Wale mwewe.. Franga wawindaji wakatusua/
Kwakuwa.. wanajua mshikaji unaishi kwa miko/na zako itikadi.. ziko kimziki na sio
mshiko/
Kama haileti hela..basi haimake sense.. no sweat kisela mie nikakomaa tu na lako penzi/
Sikusound garbage au kuchange suddenly../
Mie ni mjeshi so naweza fight savagely/
Hiphop ya ukweli.. ukapigwa radioni/sometimes malaika wa heri nao hutembelea motoni/
Penzi ni kipofu na anayemuona halioni/ sikuwa na hofu.. mama alinipenda tangu nikiwa
tumboni/
I started young.. I made my mother's womb a drum/
My umblirical chord a guitar.. muhoji aliyenizaa/
BONGOFLAVA mzuri kiasi.. hiphop we ndo my queen/ my 1st.. my last & everything in
betweenjj

UTAMADUNI By NIKKI MBISHI


Verse I:
Yo, vina punch na midundo, mafumbo na temithali
Za semi, zisome tungo, ni gumzo, jiweke mbali
Mi ni fundo we ni mwali nishike udumishe ndoa
Bila mishe niko poa nipishe nisafishe doa
Nadharia kwa kilinge, ninge hazitambi tena
Nishinde mbilinge, Mungu hazijui dhambi njema
Gongo La Mboto msoto hainyweki gongo ya moto
Maisha vitisho, mwisho wanaujua hadi Mrisho Mpoto
Kafara za kuchinja fake wanachimba
Kila napo timba wanapotea ki mazingara kama ninja
Choir master bubu, rasta choma kaya, fire
Si husudu mabaya, hii ni saa mbaya, muhaya tubu
Napanga mistari mithili watoto wa kaya za kipemba
Mashairi ka riwaya za Andanenga
Nafunza kwa Kilingi
Kama tenzi ni hela ubongo wangu ni benki, so nazitunza ka shilingi
Blow kiss kama jada, makada ndio sisi
We radar police, snitch vipi unidiss bila mada?
Wonder kama Stevie na hii flow ndiyo yenye mwali
Inayokubamba kama mwizi na siku hizi Emcees hawalali

29
NINI DHAMBI by FATHER NELLY from X-PLASTAZ
VERSE 1;
Piga magoti, tuombe Mungu
Hii ni siasa, dini, vita, ubwana, utwana, au kiama ghalika, sodoma na gomora?
Simama imara, zunguka kila kona, kila anga angaza
Kushoto, kulia, mbele, nyuma kote pitia
Na hapo ulipojishikiza g'ang'ania, sikilizia, vumilia baadae usije jutia
Hii ni mahususi na maalum kwa watu wangu
Walemavu, vipofu, zeruzeru na wendawazimu
Watoto wa mitaani, fukara, masikini na wenye akili zao timamu
Hii kamba ngumu,Mjue tunavutana na wenye nguvu
Vitambi na mashavu,Hakuna tena fair game
Refarii kauzu,Uwanja wenyewe mkavu
Ujira mgumu, malipo finyu,Kilichobaki kucheza rafu
Tumechoshwa na ukabaila, ubepari na ubeberu
Wakati ndo huu,Ukombozi ndo huu
Na sasa naamuru mliopo chini wote mpate divai ya vinibu
Mtetezi wenu nikaze gidamu,Nimwage sumu ya upupu juu yao
Wajikune bila aibu,Kwanza saluti kwa waliyotangulia kuzimu
Pili tuombe Mungu,Baba yetu, utupe mkate wetu wa kila siku
Utujaze nguvu,Tupate kudumu ndani ya game
Tutakapofika kuzimu siku ya hukumu,Utupe nafasi tupate kutubu
Kwani tunajua tunatenda maovu,Tunakula haramu
Tunatumia kila mbinu,Juju, uhalifu, upanganyifu
Ili tuweze kujikimu,Lakini isiwe kisingizio kwa wanadamu wengine kunyimwa haki
zetu,Kutuzibia riziki zetu,Kutuita makafiri, dharau na kutukashifu
Kwani nini dhambi.

XPLASTAZ
From:theostell1986@yahoo.com or theostell1986@gmail.com(0712055981)
@1959.61.2021.jan.84.theostell1986@Elizeus Jerad Mushobozi"I AM REAL HIPHOP"

30
31
32
GANGSTER WITH MATATIZO G.W.M KR MULLER ,DOTO

33
DEPLOWMATS CREW.

SHUKRAN KWA WANA UTAMADUNI WOTE WA REAL HIHOP


WANAODUMISHA NA KUHESHIMU MILA ,DESTURI,MIIKO,NA TAMADUNI
ZA HII SANAA YA REAL HIPHOP KWA KUGHANI MASHAIRI YENYE TENZI
ELIMISHI,VINA VYENYE MIDONDOKO INAYOFATA MIDUNDO YENYE
UZITO KAMA RADI ZA BARAGUMU, TANGU WATANGULIZI WA REAL
HIPHOP BONGO 1980''s wakina Conway Francis,Adili Kumbuka,Saleh Jabri,K-
single,Chief Ramson,Balozi,Saigon, 2proud,Sos B,Kr Muller,Hashim Dogo,Soggy
Doggy,Inspector Haroun ,FiQ,Squezer,Complex,Dudu baya, Dataz,Bad gear,father
Nerry,Kala Pina,Solo Thang,Jay Mo,Dark Master,Mchizi Mox,JCB,Chindo Man, Bou
Nako,Ibra da husler,Lord Eyes,Gwalu Fuluda,Mteganda,Nikki
Mbishi,Godzillah,Azma,Stoppa R,Bonta na Memcee wengine wengi ambao mpaka leo hii
wamesimamisha misingi ya Real Hiphop kupitia nguzo mbalimbali ukiwa kama Producer
kama Duke,ama ukiwa Dj wote kwa pamoja tunasonga kama kikosi cha Dogo
Mwendawazimu na wakibana tunazima kama Nash Mc.
@1959.61.84.86.theostell1986@Elizeus Jerad Mushobozi"I AM REAL HIPHOP"

34
@unju bin unyuku.elizeus jerad mushobozi .20012021 35
Shout-out 2crazycrew,state crew,pdd,u‟clan,kwetu bantu my home boy Andaki culture and
all real hiphop icon of all da time from block 41 Hashim dogo,kalapina,Yuzzo and boys
from da hood of kijenge ya juu Chindo Man and Jcb,

Shout-out to Hiphop Base icon Cygon,shout-out to WAPI by Zavara, shout-out to Kilinge


and Midundo instrument Beat from Lindu,Duke,Texas,Mujwauki,Majani P-funk,Ludigo

Salute to Wachata my Home-Boy Kalasinga, Localism, Meddy, Mejah himself

Salute to Bube, Kaija, Gagarino, Mutiu Adepoju, Quan, and Shauri John3:16, and all street
soldiers who live Hiphop Real

@theostell1986@gmail.com-0712055981-I AM HIPHOP

36

You might also like