You are on page 1of 311

Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

By richard MWAMBE

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

01
KAMBI YA JESHI KIZUKA
“Mpaka sasa hatujapata ishara yoyote ya kutuonesha mahali
ilipo ndege yetu. Tumejaribu kuitafuta kwa satellite katika anga lote
lakini kazi imekuwa ngumu sana. Taarifa ya mwisho ilituonesha
kwamba mruko wa ndege ile ulikuwa katika anga la katikati ya
India na Pakistan, juu ya jangwa la Kashmir…”
“Ina maana kutoka hapo haijulikani kilichoendelea?” Namba
moja akauliza.
“Haijulikani, kama imedunguliwa au imekuwaje!” mkuu wa
kikosi cha anga Kizuka alikuwa akiwasilisha taarifa ya kupotea kwa
ndege vita ya kisasa kabisa ambayo Serikali ya Tanzania iliinunua
kutoka Urusi ili kuimarisha ulinzi wa anga dhidi ya adui. Ndege
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

hiyo kubwa lakini yenye uwezo wa kubeba makombora mazito,


makubwa kwa madogo ilikuwa ikitoka Urusi kuja Tanzania.
Mheshimiwa Rais ambaye usiku huo alifika kambini hapo, alijikuta
hana la kusema, alibaki kumtazama Brigedia Steven Maumba,
mkuu wa kikosi hicho cha anga cha Kizuka. Pembeni yake
alikuwapo Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Brigedia Jenerali
Hosea Mlawa. Pamoja nao ni walinzi wa Rais waliokuja usiku huo.
“Sielewi…” akasema, “inaniwia ngumu sana kuelewa au ninyi
mnasemaje? Imetekwa, imeanguka au imekuwaje?” Rais au namba
moja akauliza.
“Tunaendelea na uchunguzi, vijana wapo kazini naamini
watapata jibu. Wanajaribu ku-ping namba za siri za mawasiliano ya
satellite ya ndege hiyo, pindi tu iki-respond, basi majibu yote
yatakuwa mezani,” mkuu wa kikosi akaeleza.
Ukimya ukatawala katika chumba kile kwa sekunde kadhaa,
Zaidi ya muungurumo wa kifaa cha kupoza hewa, hakukuwa na
kelele nyingine yoyote ya ziada.
Manunuzi ya ndegevita hivyo moja yaliutkisa uchumi wan chi.
Watu walipiga kelele dhidi ya maamuzi hayo ambayo yalipitishwa
na kuidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa mbinde.
Wapo waliopinga wakidai kuwa haina maana ya kununua ndege
hiyo kwa kuwa Tanzania haina maadui wa kusema tutaitumia leo
au kesho. Wengine wakasema inunuliwe ili nchi jirani ziogope
kutufatafata. Jeshi lenyewe liliihitaji kwa sababu za kiusalama
ambazo wao ndiyo wanazijua.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Wakati mabilioni ya shilingi yameteketea kuinunua silaha hiyo


ya kwanza kufika Afrika, inapotea angani na kuleta sintofahamu
kwa nchi na serikali.
“Masaa thelathini na sita, nitahitaji taarifa kamili na ya
kuridhisha kuhusu hilo,” Rais akatoa amri na kuinuka tayari
kuondoka. Wale viongozi wa jeshi nao wakasimama na kutoa
saluti. Mkuu wa nchi akaiacha kambi hiyo na kuondoka kurudi
Ikulu. Ilikuwa saa tano na nusu usiku alipikuwa barabarani akirudi
mjini.
Nini kimetokea? Tumehujumiwa? Akajiuliza huku akijiweka sawa
kwenye kiti chake. Tutaujua mwisho tu! Akajifariji.
* * *
Katika jangwa la Kashmir, vumbi lilikuwa likitimka, upepo
mkali ulivuma na kulete hali ya sintofahamu. CaptainBakari
Nsazugwako alikuwa chini kimya, nusu mfu. Kilomita kama mbili
hivi CaptainJoel Maganga naye alikuwa hoi katika ya vumbi nene.
Hakuweza kuinuka wala kufanya chochote alitulia tu akisubiri
kudura za M’nyezi Mungu.
Haiwezekani… Mbona mi nilifuata maelekezo yote kama
nilivyofundishwa! Aliwaza. Akiwa katika lindi la mawazo, akasikia
michakacho na sauto za farasi wakifika eneo hilo. Hakukosea.
Farasi wanne waliokuwa na watu wanne juu yake waliwasili,
wakamzunguka. Mmoja aliyekuwa juu ya farasi mweupe alishuka
juu na kusimama mchangani. Hakuonekana sura yake kwa kuwa
alijifunga tabani lililoficha uso na kuacha macho tu.
“Mchukueni!” akawaambia. Wale wengine wakashuka kutoka
kwenye farasi na kumbeba yle mwanajeshi pale chini, wakampakia
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

na kuondoka naye. Ile ndege iliyokuwa umbali mfupi kutoka


alipokuwa CaptainBakari ilifunikwa kwa turubai ambalo usingeweza
kugundua haraka kama kuna kitu kimefunikwa kutokana na rangi
ya lile turubai ilivyoshahabiana na udongo wa jangwa.
Kati ya milima iliyokatikati ya jangwa hilo kulijengwa jumba
kubwa la kisasa ambalo kwalo, Bakari na Joel walifikichwa na
kufungwa humo. Kazi hiyo ilipokamilika wale mabwana
wakapanda ghorofa ya juu na kupeleka ripoti kwa kiongozi wao
mkuu.
“Mmekamilisha?” akawauliza.
“Ndio mkuu! Lakini tuliambiwa kuwa kwenye ile ndege
kulikuwa na marubani watatu, hawa tuliowaleta ni wawili…”
“Ina maana mmoja hajapatikana?” akawauliza.
“Ndiyo, na tumetuma watu wamtafute popote alipo,
wamlete,” akaeleza yule kiongozi wa msafara.
“Hakikisha hilo linafanyika, maana kazi yetu haiwezi
kufanyika mpaka tumpate yeye,” yule kiongozi akawaambia na
vijana wale wakaondoka.
Hussein Al Mansoor alijenga jumba hilo la kifahari katikati ya
milima hiyo na kuweka makazi yake. Mbele ya jumba hilo palikuwa
na barabara kubwa ya lami kwa ajili ya kutua ndege za wateja wake
au wageni wanaokuja kumtembelea. Alimiliki visima vya mafuta
huko Uajemi, aliuza dawa za kulevya kwa jinsi anavyotaka yeye,
lakini baishara kubwa iliyomficha huko Kashmir ilikuwa ni uuzaji
wa silaha. Hakuna serikali iliyomgusa, viongozi wanchi, makundi ya
waasi, wote walikuwa swahiba zake. Waliketi kula na kunywa
watakavyo. Dunia hii ukiwa na pesa hakuna wa kukusumbua. Pesa
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

sabuni ya roho.Simu katika sebule hiyo ya kisasa iliita, akainuka na


kuifuata, akainyakuwa na kuiweka sikioni.
“Yes!” akaitika.
“Kila kitu kimefanikiwa?” sauti ya upande wa pili ikauliza.
“Yeah kwa asilimia sabini, imekamilika lakini kati ya codes
tunazotakiwa kuwa nazo kuna moja imetoweka, ndiyo tunaitafuta,”
Al Mansoor akajibu.
“Bwana Fernades anataka kujua ili apange safari ya kufika huko
kwa ajili ya biashara,” ile sauti ikaeleza.
“Yes, pindi tukiipata code iliyobaki nitawajulisha mfike,”
akawajibu na ile simu ikakatika.Mansoor akarudi na kuketi kimya
akitafakari jambo. Muda kidogo, akachukua simu kutoka katika
mfuko wa kanzu yake ya gharama. Akaichukua na kuivuta antenna
yake, akabofya namba fulani na kuiweka sikioni.
“Tumepata codes mbili bado moja imetoweka,” akamwambia
mtu wa upande wa pili.
“Hapo mtihani, lazima ipatikane code ya tatu, kwa sababu mfumo huo
hauwezi kufanya kazi kabisa kama hiyo ya tatu haipo. Na hizo mbili
haziwezi kujua ya tatu inasomwaje, kwa hiyo juu chini lazima ipatikane,”
akaeleza mtu wa upande wa pili.
“Ok!” Mansoor akajibu na kukata simu. Akashusha pumzi
ndefu na kuubwaga moyo.
* * *
Captain Joel na Bakari walihifadhiwa kwenye vyumba tofauti
vilivyojengwa chini ya ardhi ndani ya kasri la Al Mansoor. Bakari
licha ya kufungiwa ndani ya chumba hicho, alikuwa akipatiwa
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

matibabu kutokana na majeraha aliyoyapata na kupoteza fahamu.


Joel alikuwa kimya kabisa katika chumba chake chenye kitanda
kimoja kidogo, kiti na kijimeza cha duara. Pembeni palikuwa na
henga iliyoning’iniza suti jozi nne, mpya. Alijigeuzageuza pale
kitandani alipojilaza, akifikiri mara kadhaa nini kimetokea,
hakupata jibu. Alichokikumbuka ni hali mbaya ya hewa
iliyolikumba anga. Akakumbuka kuwa aliambiwa na Bakari abofye
batani ya kuiwezesha sensor kuona umbali wa tufani hiyo.
Sikumbuki alibofya au la, hapana alibofya nilimuona akifanya hivyo.
Akajaribu kukumbuka. Sasa nini kilitokea? Bado lilikuwa ni fumbo
kwake. Akainuka kutoka pale alipojilaza, akazunguka kile chumba
huku akijipigapiga kichwa chake labda atakumbuka kitu.
Jamila! Jamila hayupo, yupo wapi? Akajiuliza.
Eject, eject! Bakari akaikumbuka sauti ya Jamila iliyokuwa
ikimwambia neno hilo. Nikabonyeza batani ya eject, na Bakari alifanya
hivyohivyo, Jamila yuko wapi? Haku-eject?.
Captain Jamila, mwanamke pekee wa kwanza katika Jeshi la
Wananchi wa Tanzania kuchaguliwa kuwa rubani wa ndege vita.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka thelathini na tatu
alijifunza kazi hiyo huko US Air Force kwa miaka mitatu na kuwa
mahiri katika kurusha ndege hizo. Jamila alikuwa mshititi kwenye
masomo ya Fizikia, Jografia na Hisabati. Mara tu aliporudi kutoka
Marekani alipangiwa kituo cha kazi huko Kizuka, Ngerengere.
Wakati serikali ilipohitaji kununua ndege hiyo ya kisasa, chaguo la
kwanza kutoka kwa mkuu wa kikosi ni Jamila. Akateuliwa na
wengine wawili. Jumla yao, watatu, wakatumwa huko Urusi kwa
ajili ya kujifunza mifumo ya ndege hiyo mpya na ya kisasa ambayo
ilikuwa ya kwanza kuuzwa Afrika.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Katika tukio hilo lililowakuta wakiwa safarini kurudi


Tanzania, Jamila ndiye alikuwa kiongozi mkuu wa ndege hiyo huku
Joel na Bakari wakiwa wasaidizi. Tufani na mchafuko wa hali ya
hewa waliokutana nao katika anga la Kashmiri liliwafanya wapoteze
mawasiliano hata na uwanja ulio karibu na kupelekea ndege hiyo
kuanguka bila kufanya mlipuko wowote ule. Baada ya wao wote
kuruka na miamvuli, Joel hakumbuki kama Jamila aliweza kutoka
au la.
Hapa tumehujumiwa, lakini kama ni hivyo basi itakuwa heri kama
mmoja wetu kafa maana hawatapata code ya tatu, mpango wao utafeli!
Akawaza na kutabasamu.
Katika chumba kingine, Bakari alirudiwa na fahamu na
kujikuta sehemu tofauti na aliyokuwa mwanzo.
“Tumeshatua au bado, mi nililala,” akasema kwa
muweweseko. Akajitazama mikono, ina bandeji. Nini kimetokea?
Akajiuliza.
“Joel! Joeeellll! Jamila, Captain Jamilla,” akaita lakini hakupata
jibu lolote. Akajitazama nguo alizovaa sizo alizokuwa nazo
mwanzo, akastaajabu. Bakari akajilaza kimya, akili yake ikiendelea
kurudi taratibu.
* * *
Landrover Defender mbili ziliwasili katika jengo hilo majira
ya saa saba mchana. Wanaume walioshiba na kuchafuka kwa vyeo
vya kijeshi wapatao sita waliteremka. Mmoja kati yao alionekana
ndiye mkubwa kwa jinsi alivyokuwa akinyenyekewa. Wengine
watano walionekana wazi kuwa ni walinzi. Wane walining’iniza
bunduki nzito vifuani mwao na mmoja alikuwa na bastola mbili tu;
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

moja ilibanwa upande huu na nyingine upande ule. Daima alikuwa


nyuma ya mkubwa huyo wakifuatana kulielekea jumba lile.
“Karibu sana Jenerali,” Al Mansoor alimkaribisha mgeni
wake.
“Shukran,” yule kiongozi wa jeshi aliitikia na wote pamoja
wakapanda ngazi kuelekea ghorofa ya juu kwa mazungumzo. Mara
tu walipoketi, wakaletewa vinywaji kusuuza makoo yao dhidi ya
vumbi zito la jangwani.
“Ndiyo, Jenerali Kahir…” Mansoor akaanzisah mazungumzo.
“Bwana Mansoor, nimepata taarifa njema sana, kwanza
nikupongeze kwa kazi nzito uliyoifanya,”
“Shukran, nina kikosi imara na kinachojua kazi yake. Sina
wasiwasi,”
“Hata mimi naona,” Kahir akajikohoza kidogo na kurejea
mazungumzoni, “sasa tunafanyaje? Unajua hiyo ni teknolojia ya
kisasa sana, hata sisi katika harakati zetu tunahitaji mfumo wa
naman hiyo,” akamwambia.
“Aaaaah mimi ni mfanyabiashara, mwenye pesa iliyotakata
namuuzia mzigo… basi!” Mansoor akajibu kwa majigambo.
Mazungumzo kati ya watu hao wawili yalidumu kwa takribani saa
mbili kutokana na mvutano kidogo wa bei ya kile kinachotaka
kuuzwa. Mansoor tayari mkononi mwake alikuwa na mteja
mwenye pesa. Fernandes, tajiri kutoka Latino Amerika anyefadhili
makundi ya wanamgambo huko Mashariki ya kati. Yeye baada ya
kupewa taarifa na bwana Mansoor kuwa kuna teknolojia ya kisasa
anayotaka kuiteka na kuiuza, alipomuelezea jinsi ambavyo
teknolojia hiyo inafanya kazi akavutiwa na kutaka kufanya biashara
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

naye. Mansoor tayari alikuwa na wateja wawili mkononi nani


amuuzie na nani asimuuzie? Kitendawili.
“Hata hivyo, kuna kitu bado sijakikamilisha ili biashara hii
iweze kufanyika,” Mansoor akamweleza.
“Kitu gani?”
“Huu mfumo kadiri ulivyotengenezwa, ili ufanye kazi kwa
ufanisi unahitaji kufunguliwa kwa kodi tatu tofauti…”
“Ina maana yoyote kati ya hizo?”
“Hapana… ni zote kwa mara moja,”
“Sasa huna hizo kodi?”
“Injinia wangu alivyoniambia ni kwamba ile ndege iliuwa
inaendeshwa na marubani watatu, kila rubani alipewa kodi moja ya
huo mfumo. Sasa nilipofanikiwa kuiangusha, nimeweza kuwapata
marubani wawili, mmoja sijampata na hatujua kapotelea wapi,”
“Anhaaaa kwa hiyo huyu wa tatu naye ana kodi yake…”
“Haswaa…, na kazi iliyopo sasa ni kumtafuta rubani wa tatu,
yeye akipatikana tu, biashara inafanyika,” Mansoor akaeleza.
“Sasa we hilo niachie mimi, nitatuma vijana wangu na
atapatikana tu…”
“Usihofu, vijana wangu wapo kazini kumsaka. Cha muhimu
ni awe hai maana kama atakuwa amekufa haina faida. Ndiyo maana
tukaiangusha ile ndege nzima nzima, ili tuwapate wakiwa wazima,”
Mansoor akaeleza.
“Dah!”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Nipe muda, saa arobaini na nane nitakupa taarifa ya kila


kitu,”
“Sawa, nakutegemea, achana na huyo muuza dawa za kulevya,
niuzie mimi mfumo,” Kahir akaongea kwa kujiamini akiwa tayari
keshainuka.
“Mwenye kisu kikali atakula nyama,” Mansoor akamwambia
huku akiwa anamsindikiza.

02
DAR ES SALAAM
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Siku Tatu Baadae…


Kamanda Amata aligutushwa usingizini na kelele za simu
iliyokuwa kwenye kikabati kidogo pembeni ya kitanda chake.
Akainuka kwa taabu na uvivu, akajivuta na kuifikia simu hiyo.
Akainyakuwa na kuiweka sikioni.
“Hallo!” akaita kivivu.
Sauti kutoka upande wa pili wa simu ikavuta pumzi kwanza
na baadae ikasema, “Ofisi ndogo Tafadhali, Scoba anakuja
kukuchukua,” ile simu ikakatika. Amata akaitazama na kuiweka
kwenye kitako chake. Akajinyanyua na kuingia kwenye chumba
chake cha mazoezi. Nusu saa ilimchukua kuuweka mwili katika hali
nzuri ili kuikabili siku hiyo. Akiwa katika chumba hicho, akasikia
honi anayoijua, akasitisha. Dakika thelathini nyingine alikuwa
tayari, akafunga nyumba yake na kuupita uwanja mdogo akielekea
nje kumfuata Scoba.
“Karibu kaka, unalala mpaka sasa?” Scoba akauliza.
“Sasa nifanyeje?”
“Kazikazi,”
“Aaaaa kazi za hivihivi tu mdogo wangu,” akajibu wakati
akifunga mkanda na gari lile kuondoka tarataibu, “kuna nini
huko?”
“Hata sijui, mi nipo kijiweni bibi yako ananipigia simu
nikufuate,”
“Ok!”
Scoba akaendesha gari kwa mwendo wa kasi kuelekea mjini,
ukimya uikuwa umetawala katika gari hilo, ni mziki pekee wa Bob
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Marley uliyokuwa ukitumbuiza. Amata akazima na kufungua redio


ya kawaida.
“Aaaaaa bro’ vipi? Mi Napata hisia hapa we unazima?” Scoba
akalalamika.
“Lazima usikilize habari ujue nchi inaelekea wapi?”

“…wote watatu, hawajulikani walipo.


Duru za kiusalama zimesema,
zinaendelea kufanya uchunguzi ili kujua kama ndege
hiyo
imetunguliwa au imeanguka kwa hitilafu za
kiufundi.”

Wapi tena? Amata akajiuliza. Scoba tayari alikuwa kwenye


foleni ya Daraja la Salenda. Baada ya ile taarifa kurudiwa ndipo
Amata alipoisikia taarifa ile vizuri. Akamtazama Scoba kwa
kumkazia macho.
“Vipi?” Scoba akauliza.
“We unataka kuniambia kuwa ndege yetu imepata ajali?”
akauliza.
“Hah! Kamanda, hujui?”
“Hapana, ni habari mpya!”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Wakiwa wanaenda polepole wakapishana na msafara wa gari


za jeshi ukiwa kasi ajabu, ukitoka mjini kuelekea maeneo ya
Upanga.
“Mh! Sijui, ngoja tumsikie Amiri Jeshi mkuu atasemaje…”
Au Madam kaniitia jambo hilohilo? Akajiuliza.
Scoba aliegesha gari nje ya jengo moja dogo la kikoloni
lililojengwa karibu kabisa na ofisi ya hazina jijini Dar es salaam.
Amata akashusha pumzi na kuteremka kutoka katika gari hilo.
Alipopiga kioo kwa kiganja chake, Scoba akaliondoa taratibu na
kuliacha eneo hilo. Hatua chache zikamfikisha katika mlango wa
ofisi hiyo.
“We!” sauti ya kike ikaita kutoka upande wake wa kushoto.
Akageuka na kumuona Gina akiwa katulia ndani ya BMW na
kushusha kioo cha dereva nusu. Gina akampa ishara ya kuwa aingie
kwenye gari. Amata akafanya hivyo. Akaziacha zile ngazi na
kuelekea kwenye lile gari. Akafungua mlango wa nyuma na kuketi.
“Karibu Amata!” Madam S akamkaribisha. Ukiachana na
Gina, ndani ya gari hilo kulikuwamo Madam S na Amata tu. Gina
akaondosha gari na kuingia mjini. Kutoka pale, Gina akachukua
barabara ya Shaban Robert, moja kwa moja mpaka katika
makutano na ile barabara ya Ghana, mbele kidogo kama anaelekea
barabara ya Barack Obama akaegesha gari pembeni.
“Rudi hapa baada dakika mia moja na themanini zijazo,”
Madam S akamwambia Gina na kuteremka akiwa na mkoba wake
begani.
“Kamanda Amata, kuna kikao cha dharula ambacho nataka
na wewe uhudhurie, mkuu wa majeshi ameridhia hivyo mguu huu
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

tunaelekea makao makuu ya jeshi, Upnaga,” Madam S


akamwambia.
“Nini shida?” akauliza.
“Hata mimi sijui, we twende, tutajua hukohuko,” akajibiwa.
Madam S akasimamisha taksi na wote wawili wakajitoma ndani na
safari ikaanza.
“Diamond Jubilee, sh’ ngapi?” Madam S akamuuliza dereva.
“Elfu nane tu bila chenji,” akajibiwa.
Haikuwachukua muda kuwasili katika ukumbi huo, wakalipa
na kuteremka. Kutoka hapo wakatembea kwa mguu kuelekea
katika ofisi hizo za makao makuu ya jeshi.
Kikao cha watu kumi tu kiliitishwa katika moja ya ukumbi
mdogo ndani ya kambi hiyo. Miongoni mwao alikuwamo Amata
na Madam S. wengine wote walikuwa katika mavazi hadhimu ya
JWTZ, wakichafuliwa na vyeo na nishani za kutosha. Ilitisha. Ni
TSA tu waliokuwa katika mavazi ya kiraia na hii ilikuwa na sababu
maalum.Kiti cha mbele kabisa aliketi mkuu wa majeshi na viti
vingine walikuwapo wasaidizi wake kutoka medani tofauti za jeshi.
“Ndugu, tumepatwa na taizo kubwa,” akaanza kwa kusema,
“miezi sita iliyopita, Amiri jeshi mkuu kwa kupokea maombi yetu
ya kijeshi alituagizia ndegevita tatu za kisasa. Ndege hizo zenye
mfumo wa kisasa kiteknolojia ndizo zilikuwa za kwanza
kununuliwa nan chi ya Afrika. Baada maafikiano kati ya Tanzania
na Urusi, uundaji wa ndege ya kwanza ulianza na kukamilika wiki
mbili zilizopita. Ilifanyiwa majaribio na kupasishwa katika viwango
vya kimataifa. Ndege ile ilikuwa na mfumo unaoweza kuzuia
makombora yoyote yanayopigwa eneo ambalo ipo na kuyaharibu
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

bila kuleta madhara. Ilikuwa na mfumo unaoweza kung’amua


silaha ya hatari za nuklia kutoka umbali wa kilomita mia mbili
hamsini na ukiiruhusu itakueleza kwa mfumo wa satellite silaha
hiyo ipo wapi. Kiukweli ni ndege yenye mifumo hatari nay a ajabu
sana,” mkuu wa majeshi akaeleza ili tu kuwaweka tayari kupokea
maagizo kwa uzito mkubwa. Alipojiweka sawa, akaendelea “sasa
siku tatu zilizopita ilikuwa tuipokee ndege yetu ya kivita ya kwanza,
ila kama mlivyosikia, ndege ile imepotea na haijulikana sababu wala
wapi ilipopotelea, na ndiyo maana nimekuiteni hapa,” akamaliza.
Ukimya ukatawala.
Katika kiti kimoja wapo akanyanyuka mtu mwingine aliyevalia
suti ya buluu bahari ya kijeshi. Kwa mavazi yake tu alionekana ni
mtu wa kikosi cha anga. Brigedia Magoti, akaiendea projector, kifaa
ambacho kiliweza kuonesha mambo anuai yaliyorekodiwa.
“Mniazime macho yenu ndugu wajumbe!” akaanza kwa
kusema. Na wote wakamtazama tayari kusikiliza kile
wanachokisikia. Kwa kutumia fimbo yake aliyokuwa ameishika
mkononi alianza kutoa maelezo.
“Kama alivyoeleza mkuu, mimi nitawaeleza nini kilichotokea
kadiri ya taarifa zetu kutoka katika rada yetu kubwa ya
Kizuka.Mikoyan MiG-29 Foxbat, ndiyo ndege tuliyotegemea
kuipokea, yenye mwendo kasi wa kilomita 9500 kwa saa. Hii ni
ndege ambayo rafiki zetu wa Urusi wameifanyia marekebisho
kutoka kwenye ile Mikoyan Gurevich 25PU. Inasemekana ndiyo
ndege yenye kasi kuliko zote duniani, ikiwa imeipiku ile North
American X-15 ambayo ina mwendokasi wa 7200 kwa saa. Mfumo
huu mpya kabisa wa ndege hii ndiyo unaoongeza maadui kwa nchi
ya Urusi hata Tanzania kutokana na kwamba ukiimiliki hakuna mtu

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

yeyote wa kukusumbua,” akaiongezea sifa huku akionesha kwa


picha kila analolisema. Akainua bilauri na kuoiga mafunda kadhaa
ya maji baridi kisha akaendelea. “Ndege yetu iliagwa na kuondoka
kutoka uwanja wa ndege wa jeshi la anga la Urusi huko
Chuguvyeka, ikiongozwa na kepteni Jamila akisaidiwa na Kepten
Joel na Bakari wote kutoka Tanzania. Tulikuwa tukiendelea
kuwasiliana na kepteni Jamila tangu wakiwa wanaondoka pale
Chuguvyeka na alikuwa akitupatia taarifa zote stahiki za safari yao.
Safari yao ilikuwa itumie saa sita tu kufika hapa. Lakini mnamo
majira ya saa tano asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki, tulianza
kupata mwingiliano wa mawasiliano na chombo hicho. Mafundi
wetu walihangaika sana kurudisha mawasiliano, ilipokuwa ngumu,
tukawasiliana moja kwa moja na watu wa Urusi ili nao pia waweze
kuitafuta ndege hiyo. Jibu walilotupatia ni kwamba hawaioni si kwa
mawasiliano tu bali hata kwa satelaiti. Saa tano na dakika arobaini
na nne ndipo mawasiliano hayo yalipokatika kabisa na kukipoteza
chombo hicho. Ndugu wadau tuna kazi moja tu ya kujua ni wapi
chombo na wapiganaji wetu walipo, kama wamekufa basi tuwazike
kiheshima, kama hawajafa wako wapi? Na chombo chetu je?”
akaweka tuo. Akawatazama wajumbe wa mkutano waliokuwa
kimya kabisa.Akajikohoza, na kuwauliza “tupo pamoja?”
“Ndiyo, ukiona ukimya hivi ujue kuna mambo yanazunguka
vichwani mwetu,” mjumbe mmoja akasema.
“Jambo lingine ambalo nilitaka kuwajulisha ni kuwa, awamu
ya kwanza ya mafunzo ya kuiopareti ndege hiyo tuliwapeleka
makepteni watatu; wawili kutoka Ngerengere ambaye ni Kepteni
Jamila na Bakari, na mmoja ni kutoka Airwing Ukonga naye ni
Kepteni Joeli. Mpaka sasa hatujui wapo wapi… na linalotukabili

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

mbele yetu ni kufumbua kitendawili hiki,” akamaliza na kurudi


mahali pake huku pale ukutani zikiwa picha tatu za wale
makepteni. Ukimya ukatawala, hakuna hata mmoja aliyezungumza
chochote. Kamanda Amata alikuwa akiandika vitu fulani kwenye
simu yake aliyoiweka mezani. Madam S muda wote alikuwa
akimwangalia kijana huyo bila kusema chpochote, alijua wazi kuwa
hapo kwa vyovyote akili ya TSA 1 inachemka.
“Kama kuna mtu ana swali au anataka kujua vizuri asisite
kufanya hivyo,” Mkuu wa majeshi akatoa rai. Ukimya ulipozidi na
minong’ono kusikika chinichini, Amata aliinua mkono.
“Ndiyo kijana!”
Akapewa nafasi kusema kitu. Alistahili kuitwa kijana, kwa
kuwa ndani ya ukumbi ule ni yeye tu aliyeonekana kijana lakini
shupavu. Macho yake yaliwafanya wengi wa maofisa hao kutaka
kudadisi Zaidi, kujua kijana huyo ni nani. Wengi walijuana kwa
vyeo vyao, isitoshe kwa majina na kazi zao.
“Umesema makepteni waliokwenda mafunzoni walikuwa
watatu?” akauliza.
“Ndiyo!”
“Wawili kutoka Ngerengere na mmoja Airwing Ukonga,”
“Ndiyo kijana…”
“Kwa nini mliwatoa wawili kwenye kambi moja? Hamuoni
kama hii inaweza kuwa chanzo cha hujuma au…” Amata
aliwashtua wazee wale kwa swali lake ambalo halikufikirika.
Makamanda wale wakatazamana na kuulizana wenyewe kwa
wenyewe.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Samahani kijana,” Brigedia Magoti akasema, “yaani labda


hapo sijakuelewa sawa, uhusiano wa kupotea kwa ndege na
wapiganaji wetu na hilo la wawili kutokea kambi moja…”
“Ndiyo, ni vigumu kuelewa ninachomaanisha hapo… hoja
yangu ni kwamba, kuwatoa watu wawili sehemu moja na
kuwapeleka mafunzoni, hamuoni kwamba urafiki na ukaribu wao
unaweza kuleta matatizo?” akauliza vizuri.
“Jambo ambalo hatukulifikiria, lakini pia tutalifanyia kazi ili
tuone kama linaweza kuwa sababu,” akajibu mkuu wa majeshi.
“Jambo la pili, Kepteni Jamila alipowapa taarifa kuwa anaaza
safari je aliwaambia ndege hiyo itapita anga la nchi ipi na ipi? Ili
tujue kama imeanguka basi tuwatumie watu waliopo katika nchi
hizo kujua kama wana lolote…”
Hili likawaingia, pamoja na yote waliyoeleza kuhusu tukio hilo
hakuna aliyekumbuka kuhusu wapi na wapi ndege hiyo itapita.
Mazungumzo na majadiliano Makali yakachukua nafasi juu ya hilo
lakini yote kwa yote, swali likabakia kuhusu makepteni wale na
chombo chenyewe.
Saa mbili zilikatika ndani ya chumba kile pasi na kufikia
muafaka wa wapi uchunguzi uanzie wala nani apewe kazi hiyo.
“Lazima tutafute maiti za watoto wetu. Achana na hiyo
ndege, maiti lazima zirudi hapa ndani ya siku saba, MI hawana budi
kuingia kazini,” Mkuu akazungumza. Swala lilipofikia hapo, ilibidi
kuundwa timu ya watu watatu tu kati ya wale waliokuwapo kikaoni
ambao wangeweza kuchagua vijana watakaoweza kufanya kazi ile.
Kikao kiamalizika baada ya mijadala mirefu iliyozua hoja ambazo
zingewawezesha hao wanaoandaliwa kupata pa kuanzia. Kila
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

aliyekuwa mle ndani alijikuta anapenda kujua Zaidi kuhusu kijana


huyu raia naliyekuwa na maswali mengi, aliyeibu hoja za msingi
ambazo hata wao na ubobevu wao wa kijeshi walishindwa
kung’amua hayo mapema.
Madam S na kijana wake walitoka nje ya ukumbi huo na
kuagana na mkuu wa majeshi aliyewasindikiza mpaka karibu kabisa
na lango kuu la kambi hiyo. Wakiwa njiani kuelekea upande ule wa
ukumbi maarufu wa Diamond Jubilee, mazungumzo kati ya mtu na
bosi wake yaliendelea.
“Unajua Amata we mchokozi sana!”
“Kwa nini?”
“Kwa nini uliwauliza lile swali la wale makepteni wawili
kutoka kambi moja…”
“Lile lilikuwa swali la msingi sana. Halikuwa na maana ili
nilitaka kuwafanya wanisikilize hoja zangu, si unaona
walivyochanganyikiwa na kutafuta maana ya swali lisilona maana!”
“Hili swala linataka kunikumbusha Somalia mwaka ulee …”
“Ilivyotekwa manowari yetu ikiwa na makombora?”
“Usinikumbushe Madam!”
“Wakati Magoti anaelezea pale, nilikuwa nakumbuka mkasa
ule kwa undani sana, unafanana kwa namna Fulani,”
“Kabisa, hujuma, nakumbuka, dah!” Amata alajibu wakati
wakiendelea kutembea huu mazungumzo yakizidi kutopea.
“We unalichukuliaje hili?” Madam S akauliza.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Yote yawezekana, kuwa ni ajali ya kawaida ya anga,


yawezekana, kuwa kuna jambo limefanyika pia yawezekana,”
akaeleza.
“Kama nimeelewa vizuri yale mazungumzo yalivyoishia, ni
kuwa wanaotumwa huko wanatakiwa tu wakatafute miili ya
marehemu ili wairudishe nyumbani kwa maziko ya heshima…”
Madam akamwambia Amata.
“Ndiyo hapo ndipo tulipoishia, lakini Madam,” Amata
akasimama, na kumtazama boss wake, “kuna kitu mi
kinanizunguka kichwani,”
“…kipi?”
“Ili yote yapatiwe majibu, turudi kwenye umuhimu wa ile
ndegevitasifa zilizoelezwa na ni kuwa ya kwanza kununuliwa
Afrika… huoni kuwa inaweza ikawa imetekwa, au imeuzwa na
kama haya mawili yametokea basi wahusika watakuwa maeneo
mawili tu, ama Tanzania au Urusi…” Amata akaeleza. Madam S
akamkazia macho kumtazama.
“Kazi inaanzia hapo Kamanda…” alipomaliza tu kusema
hayo, mbele yao likasimama BMW jeusi. Hawakuuliza, walivuta
hatua, wakaingia katika kiti cha nyuma na kuketi.
“Kamanda, anzia kazi hapo halafu nipe majibu nini
unakinusa. Harufu utakayoipata nitaihitaji ofisini ili tujue kama wao
wako sawa au la halafu tutaibua hoja…” akamwambia kijana wake.
“Dah!”
“Nini?”
“Mara hii…”
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Ndiyo, lazima ujue mwenye wazo ndo’ ajuaye,” Madam S


akamwambia huku Gina akiendelea kubadili gia kuelekea mjini kati.
“Hiki ni kibarua kigumu sana…” akasema.
“Ni kweli, lakini tulienda pale kwa agizo la Mkuu wa nchi,
alitaka tukasikilize halafu na sisi tuchekeche. Hili swala linaihusu
Ikulu moja kwa moja kwa sababu hapo imeguswa pabaya…”
Madam akaeleza.
“Warusia wenyewe wanasemaje?”
“Hawawezi kuhangaika kwa sababu wameshakuuzia,”
“Ok, wameshatuuzia… na vipi kama wameamua kuichukua
tena? Unajua hii dunia sasa hizi imeshavaa anadasketi, haieleweki,
hakuna wa kumwamini. Yaani jiamini wewe na nafsi yako tu,”
Amata akaeleza.
“Haswa!”
Gina akaegesha gari nje ya jengo la PPF Tower, akavua kofia
aliyokuwa ameivaa na kugeuka nyuma walipo.
“Mmefika,” akawaambia. Madam S na Kamanda Amata
wakateremka garini na Gina akatia gia na kuondoka zake.
Kamanda Amata na Madam S walibaki wamesimama palepale
barabarani.
“Nikuache!” madam akamwambia kijana wake huku tayari
mkono wake ukiwa ndani ya pochi, akatoa noti ya shilingi elfu
moja na kumkabidhi.
“Ya nini?”
“Ya nauli… una nauli hapo?”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Sawa mama!” wakaagana.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

03
Siku tatu baadae…
Unguja
Lukundame aliiacha ofisi ya Posta ya Shangani, mjini
Zanzibar na kuingia katika gari lake, tayari kurudi ofisini. Hatua
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

kama mia moja hivi kutoka pale alipoegesha gari lake, kuliegeshwa
gari jingine aina ya Rav 4 ya kijivu. Ndani ya Rav 4 hiyo kulikuwa
na watu wane waliokuwa wakifuatilia nyendo za mwanamke huyo.
Watu wale hawakushuka bali walimfuatilia kutokea ndani ya gari
hilo lililokuwa na vyoo vyeusi kulizunguka. Aliwasha gari na
kuikamata Barabara ya Nyerere kuelekea ofisini kwake maeneo ya
Uwanja wa ndege. Mara tu baada ya kuondoka, na lile Rav 4
likamfuatia nyuma pasi na yeye kujua.
“Kumbukeni hatutakiwi kumdhuru,” mmoja wao aliyekuwa
nyuma ya usukani aliwapa ujumbe wenzake.
“Sawa!”
“Na wala msitumie nguvu kwa kuwa kazi yetu sisi ni kutaka
tu atueleze Mzee Hasheem yuko wapi… shida yetu kubwa ni huyo
mzee,” yule bwana akaendelea kuwaeleza huku akiwa nyuma ya
magari mawili kati yake na lile la Lukundame. Dakika ishirini
zilimtosha mwanamke huyo kuwasili ndani ya majengo ya Uwanja
wa ndege wa Aman Karume. Akaegesha gari lake na kusalimiana
na watu kadhaa aliowakuta hapo nje. Hakuwa na wasiwasi wowote,
wala hakujua kama anafuatiliwa. Luundame, mwajiriwa wa serikali
katika idara ya mambo ya hali ya hewa. Ofisi yake ilikuwa katika
moja ya majengo ya uwanja huo mjini Zanzibar. Alipoingia ofisini
mwake, dakika tatu baadae, mlango wake ukafunguliwa na vijana
wa wili waliovalia kanzu safi nyeupe, waliingia. Mwanamke huyo
aliwakaribisha, nao wakakaribia na kuketi kwenye viti viwili vya
wageni.
“Nawasikioliza kaka zangu,” aliwaambia pasi na woga.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Samahani kwa kukusumbua au kukujia ofisini muda huu,


najua labda ulikuwa unakuja kufunga tu ofisi uondoke…”
“Upo sahihi, lakini ni wajibu wangu kuwasikiliza,” akawajibu.
“Kama hatujakosea, ni Lukundame binti Hasheem…”
“Haswaa…”
“Sisi tumetumwa na swahiba wa Mzee Hasheem anayeishi
huko Oman,” wakamwambia. Mwanamke yule aliwatazama kwa
macho ya wizi na kuuona weupe wao, asilimia Fulani aliweza
kuamini kuwa ni wakutoka huko au wenye ukweli ndani yao, na
asilimia nyingine alikuwa na wasiwasi kutokana na hali tete
iliyoigubika familia yao ndani ya siku saba za juma hilo.
“Enhe…” Lukundame aliwataka kuendelea kuongea huku
yeye akiwa anatazama mambo Fulani kwenye laptop yake iliyokuwa
juu ya meza.
“Tuna ujumbe wa Mzee Hasheem, tunahitaji kumpatia,”
“Mzee Hasheem hamuwezi kumuona kwa sasa, amegoma
kabisa kupokea mtu yeyote, kama mna ujumbe uacheni hapa
nitamfikishia…” akawajibu.
“Ujumbe huu tunatakiwa tumkabidhi yeye mwenyewe tu na
ndivyo tulivyoelekezwa,” wakasisitiza. Kila mbinu waliyotumia ili
mwanamke huyo akubali kuwakutanisha na mzee huyo. Akilini
mwake alihisi kuna jambo, kwa nini wamlazimishe awakutanishe
naye ilihali amekwishawaambia kuwa haiwezekani.
“Ok, nimewaelewa, sasa tufanye hivi, mnaweza kuja hapa
kesho saa tano asubuhi ili niwapeleke, maana aliko ni mbali na pia
mpaka nimuombe akubali,” akawaambia.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Wale vijana wakatazamana, kisha wakamtazama Lukundame,


“sawa, tutakuja, itakuwa heri sana kuonana naye,” wakajibu na
kusimama. Kisha wakatoka ndani ya ile ofisi. Mara tu mlango
ulipofungwa, Lukundame akaliendea dirisha na kutazama nje,
akawaona wale vijana wakiwa nje tu ya jengo lile. Hakuweza kusikia
wanaongea nini, isipokuwa walionekana kama wanalaumiana
jambo Fulani. Akawatazama mpaka walipoondoka na gari lao,
akarudi kitini na kuketi kwa kujibwaga. Akashusha pumzi ndefu na
kuvuta laptop yake, akatazama picha mbili alizowapiga vijana wale.
Akina nani hawa? Akajiuliza huku mwili wake ukisisimka kila
wakati. Lukundame alijikuta akikosa raha kabisa, hakutamani tena
kutoka ofisini mwake na kurejea nyumbani. Alijuwa wazi kuwa
watu hao si wema.Akainu simu yake ya mezani na kubofya namba
Fulani, akaiweka sikioni.
“Nina shida, naomba tuonane Hakumwambia mtu, akafunga
kila kilicho chake, akatia mkobani. Siku hii akaamua kuicha laptop
yake ofisini na kuiondoa nywila. Akateremka ngazi na kutokea
upande wa pili wa jengo lile. Upande huo kulikuwa na maegesho ya
magari ya ofisi yao. Ndani ya gari mojawapo alimkuta dereva
kasinzia na kuacha domo wazi. Kabla hajamshitua, akatabasamu
kwanza.
“Mzee Ally!” akamgutusha.
“Eh bibiye, dah…” akajifikicha macho.
“Unalala kizembe hivyo…”
“Aaaa uchovu binti yangu…”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Haya nipeleke Pongwe Beach Club,” akamwambia wakati


tayari keshaingia upande wa abiria. Yule dereva akajiweka sawa na
kutia injini moto tayari kwa safari.
“Leo gari ipo wapi?” yule dereva mzee akahoji swali kwa
Lukundame.
“Nimeamua kuiacha ina shida kidogo,”
“Sawa… magari ndivyo yalivyo mwanangu,” yule mzee
akaendelea kuendesha gari kuelekea huko. Kutoka pale uwanja wa
ndege mpaka Pongwe Hotel iliwachukua takribani dakika arobaini
na tano. Lukundame alipoteremka katika gari hilo akampatia Mzee
Isaa pesa kidogo.
“Ya nini mama?”
“Kapate Al Kasusu…”
“Aaaaa asante binti, unataka bibi yako aburudike leo?”
“Kabisa yani,” akamwambia kisha akasimama na kumtazama,
“babu, usimwambie mtu yeyote kama umenileta huku”.
“Sawa! Lazima niheshimu na kutunza siri za mabosi wangu,”
akamjibu. Lukundae akamwonesha dole gumba kama ishara ya
kuwa amekubaliana naye.
Sijui nani anaenda kuufaidi huu mzigo walahi! Mzee Issa akajikuta
akichanganyikiwa ghafla.Lukundame akavuta hatua na kuingia
kwenye baa kubwa ya hoteli hiyo iliyojengwa upande wa peke yake.
Kabla hata hajachukua kiti ili akae, akapigiwa mruzi kutoka kona
nyingine ya baa hiyo. Alipotupa macho, akakutana na mtu yule
aliyemwambia wakutane.
* * *
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Badru Mapinda, kijana mtanashati anayeupenda na kujivunia


ujana wake, alikuwa ameketi katika moja ya kona za baa hiyo.
Kijana huyu mwajiriwa katika Wizara ya Mambo ya Ndani, katika
jeshi la polisi. Badru ni afisa upelelezi katika Mkoa wa Unguja
Kusini. Kijana huyu alimtazama Lukundame kadiri alivyozidi
kumkaribia, naye mapigo ya moyo yalizidi kuchanganya kiasi
kwamba alihisi yanaruka. Akameza mate kwa kuusawili uzuri wa
binti huyo.
“Karibu mrembo,” akamkaribisha, “leo najiona mwenye
bahati sana, kwa kuwa ni miaka karibu miwili sasa unanipiga
chenga,” akamwambia huku akimtazama kwa jicho la huba na
tabasamu la akiba. Mwanamke hyo wa makamo, hakujibu kitu
isipokuwa alitabasamua tu. Tabasamu hujibu tabasamu. Akavuta
kiti na kuketi.
“Badru!” akaita. Sauti yake ya kumtoa nyka pangoni
ikamfanya kijana yule apoteze umakini kwa nukta kadhaa, “nina
shida… nan i wewe tu unayeweza kunitatulia kwa sasa,” akasema
huku akimwita mhudumu.
“Niletee Redds baridi tafadhali,” akaagiza.
“Enhe, shidika mrembo nakusikiliza,”
“Leo nahisi nimevamiwa ofisini, maana hata simini kama
nimefika hapa sama,”
“Nini kimetokea?”
Lukundame alimweleza Badru mkasa mzima uliotokea siku
hiyo ofini mwake na kumwacha kinywa wazi. Badru kwa akili yake
ya kikachero alielewa wazi kuwa vijana wale wana kitu
wanachokitaka kwa Mzee Hasheem.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Mzee Haseem mwenyewe yupo wapi kwa sasa?” akauliza


Badru.
“Yupo, mzima wa afya, ila nimemficha sehemu ya siri sana
asiweze kufikiwa na mtu yeyote,”
“Kwa nini?”
“Sikia Badru, hapa kuna jambo zito sana linaloendelea chini
chini, hata mimi sielewi sawasawa lakini hatua niliyochukua ni
kulinda uhai wa baba yangu kwanza,” akaeleza.
“Unafikiri hao watu wanataka kumuua baba yako?”
“Ndiyo, kuna mambo mawili hapo, ama kumuua au kumteka.
Na hili nimeliona mara tu baada ya sintofahamu ya Da’ Jamila,”
Lukundame akafungua na kuwanza kubwabwaja hata aliyopanga
kutoyasema.
“Kuna kitu hakijakaa sawa kichwani mwangu Luku’,” Badru
akataka kujua Zaidi, maana kachero huwa hapendi kubakizabakiza
vitu njiani. Ukimpa mpe yote.
“Mh! Ipo hivi, we Badru unamjjua Mzee Hasheem kwa
undani?”
“Hapana, nilimwona mara mbili tu nilipokurudisha nyumbani
jioni zile,”
“Sawa! Mzee Hasheem ni msahafu wa jeshi la Tanzania wa
miaka mingi sana…”
“Yaani veteran!”
“Naam… huyu mzee amehudumu kwenye jeshi la Uingereza,
Urusi, China, Vietenam na Tanzania. Huko kote alikuwa kwenye

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

mafunzo lakini pia kufundisha maswala ya mawasiliano ya anga na


mifumpo endelevu ya maswala ya ndege za kivita na mambo kama
hayo…”
“Kumbe babu mtamu namna hiyo…?” Badru akajikuta
akivutiwa na muhtasari huo.
“Miaka mitatu nyuma, mkuu wa majeshi alikuja hapa
nyumbani kwa babu yangu, wakajifungia na kuzungumza mambo
kwa takribani masaa manne. Bahati, mimi babu huwa hanifichi,
akanambia wazi tu uwa alikuja kuomba ushauri wa manunuzi ya
ndege vita za kisasa, ila alipenda babu apendekeze mifumo ya
ndege hiyo,” akaeleza Lukundame.
“Enhe!”
“Sasa Mzee Hasheem hiyo ndo ilikuwa kazi yake kubwa hata
enzi hizo, hata sasa, nchi mbalimbali zinamtumia kuwaundia
mifumo hiyo…” Lukundame akaeleza.
“Enhe nikukatishe, kwa nini unahisi hao wana nia mbaya na
mzee?”
“Kwa sababu, yeye mwenyewe aliniambia kuwa kuna ujumbe
wa vitisho unaomjia ukitaka awauzie mfumo huo mpya ambao
ameudizaini ufungwe kwenye hizo ndege za kisasa
zitakazomilikiwa na Jeshi la Tanzania,”
“Ok! Unafikiri ujumbe huo ulikuwa unatoka kwa maadui wa
Tanzania?”
“Hapana, hata yeye alinihakikishia ni hapana. Alinambia kuwa
kuna watu walishamuomba awafanyie kazi kama hiyo kutoka
Pakistan, akakataa, sasa ana wasiwasi ni wao,”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Masikini…”
“Usiku mmoja hatukulala, mbwa wa mzee alikuwa akibweka
sana kiasi kwamba tkawa na wasiwasi. Kulipokucha tu;ligundua
kuwa kuna watu walikuja usiku pale nyumbani na alama za miguu
yao zinaonekana wazi, ndipo nikaamua kumuondoa mzee
Hasheem nyumbani kwa siri, usiku wa manane pamoja na vifaa
vyake vya kazi,” Lukundame akamwambia.
“Ukampeleka wapi?”
“Siwezi kukwambia… muda bado,”
“Sawa, sasa mimi nikusaidie nini?” Badru akauliza.
“Kutoka kwako, naomba tu unisaidie kuwajua watu hawa,”
akampatia picha alizokuwa ameziprinti kule ofisini. Badru
akazipokea na kuzitazama kwa makini kisha akazikunja na kuzitia
mfukoni.
“Sawa! Kuna lingine?” akamuuliza.
“Ulinzi, ikiwezekana wakamatwe…”
“Kuwakamata ni kazi kubwa sana maana mpaka nijue
nawapata wapi nan i akina nani,”
“Kazi ndogo sana, kesho saa tano asubuhi nimewaahidi
wafike ofisini ili niwapelekea kwa Hasheem,” akaeleza.
“Basi sawa, mi nitapanga vijana na kesho tutakuwa eneo hilo,
tutawakamata na kwenda kuwahoji ili kujua nini hasa nia yao,”
Badru akaeleza.
“Ila mi naogopa hata kurudi nyumbani…” Lukundame
akasema kwa unyonge.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Badru akatabasamu kwa kauli hiyo, akaona windo lake la


miaka mingi sasa linaingia mtegoni.
“Twende ukalale kwangu!”
“Loh! Mkeo anitoe macho…” akang’aka. Badru akabaki
kucheka.
“Nitapanga chumba hapahapa kwa leo, nitalala,” akasema.
“Ok sawa, nitakuja usiku kukupa taarifa ya wapi nimefikia,”
“Usiku, hapana bwana, asubuhi…” Lukundame aliugutukia
mtego wa kijana huyo. Si kwamaba hakuwa anampenda lakini
aliamini watu kama hao wana wanawake wengi, hivyo hakupenda
kuchangia penzi na watu asiyowajua. Nusu saa baadae wakaagana.
Badru aliondoka na gari lake dogo aina ya Toyota Mark X na
kumuacha Lukundame akiwa palepale baa.
Mwanamke huyo alipohakikisha kuwa Badru ameondoka na
kutokomea, alijiinua pale mezani na kulipia kinywaji chake na cha
Badru. Akaiacha baa hiyo na kuchukua taksi kuelekea Bwejuu
mashambani.
Mwendo wa kama saa moja hivi taksi ile ilimfikisha
Lukundame katika kijiji hicho cha Bwejuu. Bwejuu ni eneo la
kilimo zaidi, mashamba makubwa makubwa ya serikali na watu
binafsi yalikuwapo huko. Hoteli ndogondogo zilikuwepo na zile
kubwa kwa uchache. Alipomlipa dereva taksi ujira wake, akachukua
usafiri wa baisikeli na kuelekea anakokutaka. Ndani ya shamba
kubwa la karafuu na spices, kulikuwa na nyumba ndogo, imara,
iliyojengwa kwa matumbawe. Nyumba hii walikuwa wakiitumia
sana kila walipokuja shambani. Ndani ya nyumba hii Mzee
Hasheem alijenga handaki kubwa chini yake na ni yeye na
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Lukundame tu waliokuwa wakilijua. Ndani ya hilo handaki


kulikuwa na kila kitu, umeme, mawasiliano ya simu na internet.
Kulikuwa na jiko dogo ambalo unaweza kujipikia unachotaka.
Lukundame alihakikisha kuwa kila kitu amekwishakiweka sawa
katika handaki hilo kabla ya kuja kumficha baba yake, Mzee
Hasheem.
“Humu utakuwa salama zaidi,” alimwambia baba yake siku
tano zilizopita. Mzee Hasheem, mwanajeshi mstahafu, mtaalam wa
mambo ya mawasiliano anga, mifumo ya ndege vita na mpiganaji
mahiri aliyebobea katika uga huo wa vita vya anga, alianza maisha
mapya katika andaki hilo huku binti yake wa kwanza, Lukundame,
akimhakikishia usalama. Zaidi ya kompyuta zake tatu na redio
zinazonasa mawasiliano mbalimbali duniani, mzee huyu aliingia
kwenye andaki hilo na bastola yake moja kubwa yenye nguvu,
Smith and Wesson na msahafu wake.
Lukundame aliingia kwenye handaki hilo kwa mlango wa siri
na kumkuta baba yake akiwa ametingwa kujisomea vitabu.
Alichukua kiti cha mbele yake na kuketi akimtazama mzee huyo.
“Baba!” akaita.
“Karibu mwanangu… moyo wangu haujatulia kabisa mpaka
nijue Jamila yuko wapi…”
“Utajuaje baba? Vipi kama amekwishakufa?” Lukundame
akauliza.
“Heri awe amekufa, ila kama ni mzima lazima nijue yuko
wapi. Mpaka sasa hata kwenye redio tu hawatangazi chochote
kutokana na ajali hiyo. Masikini Jamila nilimpenda na kumpa ujuzi
mwingi sana katika kazi yake,” akahuzunika. Lukundame aliliona
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

chozi la baba yake lililodondoka mezani, na mzee huyo kulifuta


kwa kiganja chake. Ukiona mtu mzima Analia ujue kuna jambo.
Katika maisha yake, Lukundame alimuona baba yake akilia siku ya
msiba wa mama yake tu, hapa ilikuwa mara ya pili kuliona chozi
hilo hadimu.
“Usijali, nina uhakika kama yupo hai, atapatikana tu. Hapo
unafanya nini?” Lukundame akamuuliza swali baba yake.
“Ninaendelea kusikiliza mawasiliano mbalimbali labda
nitaisikia sauti ya mwanangu, mara ya mwisho nilimsikia akiwa
angani kuja Tanzania, sijamsikia tena,” akasema, “Sikiliza
Lukundame, ni heri Jamila afe kuliko abaki hai kama hiki
kilichotokea na hujuma…”
“Babaaaaaaaa!”
“Unaweza usinielewe, lakini jua kwamba, wale marubani
walikuwa watatu,”
“Ndiyo!”
“Sasa ili kukamilisha mfumo wa ile ndege ufanye kazi
sawasawa, kila mmoja wao ana utambulisho maalum wa kidijitali na
kadi ndogo ambayo anakabidhiwa. Ndani ya ile ndege kuna
sanduku maalumu la chuma lililovikwa ngozi ya ngamia juu yake,
lina funguo tatu, kila mmoja ana funguo yake. Sasa kinachofanyika
ni kuwa lile sanduku linawekwa kama ni Kizuka au Ukonga kwenye
kambi moja wapo ya anga. Siku ikitokea vita, na ile ndege mmoja
wao akairusha, haiwezi kurusha kombola lolote bila ruhusa ya wote
watatu, mifumo yake ya kivita haiwezi kufanya kazi bila ruhusa ya
wote watatu…”
“Kivipi?”
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Mmoja wao ataondoka na ndege hiyo na kadi yake akiwa


ameipachika katika sehemu moja ya siri ndani ya ndege hiyo. Hii
itamruhusu kuruka atakavyo. Huku chini wawili waliobaki inabidi
wawe na lile sanduku, wapachike kadi zao. Wakishapachika kuna
kioo kitakachowaonesha kila anachokiona yule rubani kule juu,
wakiingiza namba zao za siri tu, mifumo yote itawaka na kufanya
kazi. Maana yake watakuwa wamemruhusu yule aliyerusha ndege
kufanya maneuver atakayo huku wao wakimsaidia kufanya target na
kumpiga adui kutoka pande zote…”
“Waoooh!”
“Sasa mwanangu watu wanataka kuuiba huo mfumo, ndiyo
maana nahisi ile ndege imeangushwa ili wachukue hiyo system, sasa
lazima watu wote watatu wapatikane wakiwa hai. Mmoja akifa tu
hawataweza kuutumia huo mfumo. Kama hawa wanaume
watakuwa wamepatikana hai basi mi naomba Jamila awe amekufa
ili kila kkitu kiwaharibikie. Umenielewa?” Mzee Hasheem alimaliza
kumwelekeza binti yake.
“Hapo ndo umenielewesha vyema, na sasa nimeelewa kwa
nini wanakutafuta…” akasema.
* * *
Wale vijana waliomvamia Lukundame ofisini kwake jioni hile
bado walikuwa maeneo hayo wakitaka kumteka mwanamke huyo.
Giza lilianza kuingia na gari lake lilikuwa palepale kwenye megesho
ilhali wao walitondoka na wawili wao wakarudi kwa kutumia taksi
ili kumvizia. Kila walipoangalia saa zao usiku ulizidi kutaradadadi.
Idadi ya watu katika barabara na maduka na mikahawa ya eneo
hilo, ikaanza kupungua.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Unataka kunambia kalala ofisini?” mmoja wao akauliza.


“Wote tuko hapa mi nitajuaje?” mwingine akamjibu.
Wakawasiliana na wenzao waliokuwa upande mwingine.
“Hata nyumbani mwake hajafika,” wakajibiwa.
Ametuweza. Sasa atakuwa wapi? Akajiuliza huyu aliyebaki
kumvizia ofisini na asimwone.
“Ok, abort mission tukutane Forodhani,” aliyekuwa kiongozi
wa kundi hilo akawaambia. Wale vijana wakachukua taksi na kurudi
mahali walipoambiwa na kukutana na mwenzao.
“Tumeshindwa nini?” yule mkiongozi akauliza. Ukimya
ukatawala.
“Tumetumia mbinu za kijinga tu, yule ilibidi tumbebe tutoke
naye,”
“Ina maana hujui kama pale ni uwanja wa ndege na pana
ulinzi mkali. Isitoshe ni mtoto wa mwanajeshi, unajua kajipanga
vipi? Tumia akili…” yule mkubwa akafoka.
“Tumvizie akiwa njiani, tumteke…”
“Hiyo ndo point sasa… lakini yuko wapi?”
“Hapo ndiypo alipotuweza,” mwingine akajibu.
“Niliwaambia, mtoto wa mwanajeshi yule lazima kuna
mambo keshayashtukia, tuna kazi sasa kumpata,” kiongozi wao
akasema.
“Atapatikana tu, tuliza moyo,” mwingine aliyekuwa kimya saa
zote, akasema.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Baada ya ukimya mfupi, yule kiongozi wao akawaambia, “sasa


usiku huu tunaenda kushinda nyumbanai kwake kumsubiri. Muda
wowote atakaoingia sisi nay eye. Kumbukeni, tunatakiwa kesho
kumfikisha Dar es salaam”.
“Sawa!”
Mpango ukapangwa. Wale vijana wakaondoka kutoka pale
walipokuwapo kuelekea nyumbani kwa Lukundame. Ghorofa la
nne kwenye Barabara ya Karume, mara tu ukiiacha ile ya Felix
Moumie ndipo yalipokuwa makazi ya Lukundame. Wale vijana
waliegesha gari lao mita kadhaa mbele katika Barabara ya Felix
Moumie kisha wakagawana pande za kuwapo ili waweze kumnasa
mwanadada huyo. Jingo lile lenye ghorofa nne lilikuwa bado
likiwaka taa ndani ya vyumba vyake isipokuwa tu kwenye ghorofa
ya tatu. Usiku ulizidi kuwa mnene, hakukuwa na dalili yoyote ya
Lukundame kurudi nyumbani.
Katuweza! Yule kiongozi akafikiri.
* * *
ISLAMABAD
Katika nyumba moja ya kulala wageni ya Royal Galaxy
ioliyopo katika jiji hilo la Islamabad nchini Pakistan, watu watatu
wa juu wa kundi la Hizbul Mujahideen walikutana kwa dharula.
Kati ya hao watatu alikuwapo Jenerali Kahir ambaye siku chache
zilizopita alimtembelea mdfanyabiashara mpiganaji Al Mansoor
huko Kashmir. Lengo la kikao hicho cha dharula lilikuwa ni
kuwapa habari watu wake kuhusu ununuzi wa mfumo huo mpya
ambao Mansoor anaumiliki kwa wakati huo.
“Sasa tunafanyaje ili kuupata?” mmoja akauliza.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Mansoor amesema kuwa mwenye pesa nyingi ndiye


ataeupata, na mpaka sasa mshindani wetu ni Bwana Fernades, tajiri
wa mihadarati kutoka Latino Amerika,” Kahir akajibu.
“Ana pesa kutuliko?” mjumbe wa tatu akadakiza.
“Ni ngumu kujua, cha msingi tuweke mkakati wa kumzidi
nguvu. Kama nilivyowadokeza kuwa katika ule mfumo kuna hiyo
code moja haijapatikana,” Kahir akazidi kudadavua huku uso wake
ukionesha wazi kuwa anahamu ya kuumiliki huo mfumo ili
awanyanyase adui zake.
“Huyu Fernades… anataka wa nini?”
Kahir akatulia kimya kwa jozi la sekunde na kuwatazama wale
watu, “nina wazo ambalo nilitaka niwashirikishe kama mtakubali,
nina uhakika tutafaulu kumshawishi Mansoor,”
“Enhe!”
“Tuitafute code ya tatu…”
“Hapohapo…” mwingine akamkatiza, “nilikuwa najiandaa
kusema hilohilo. Hii ndiyo turufu yetu jenerali… tutie nguvu
tuitafute hiyo code, tukiipata, tunaihifadhi sisi,” akasema.
“Umewaza vyema, hapo Mansoor hatoweza kuuza huo
mfumo kwa sababu hatokuwa na code ya tatu. Sisi tutakuwa nayo,
unaona? Tutamnasa kwa mambo mawili, akitaka atuuzie hizo code
mbili, kama hataki anataka Fernades anunue, basi tumuuzie sisi
code ya tatu… Bingo!”
Kikao kile kilikuwa na mafanikio makubwa kwa viongozi
hawa wa juu wa Hizbul Mujahideen. Wakafikia muafaka wa
kuitafuta code ya tatu yaani Jamila. Hizbul Mujahideen
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

walidhamiria, kwa hali na mali kulipigania eneo hilo la Jammu na


Kashmir ili liwe huru chini ya serikali ya Pakistan, jambo ambalo
India hailikubali hata kidogo nayo inalipigania ili liwe huru chini ya
serikali yao. Mgogoro huo uliochochewa na Waingereza tangu enzi
na enzi uliendelea kudumu daima kati ya mataifa hayo makubwa
yenye nguvu za nyuklia.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

04
Jamila alidondoka vibaya katika bonde la Zalwan. Bonde hilo
lilolimwa mpunga lilikuwa na ardhi yenye tope iliyompokea
mwanajeshi huyo na kumficha kwa ule mwanguko wake. Fahamu
zake ziliondoka, akabaki hapo kalala kama mfu. Usiku huo ambapo
ndege yao iliangushwa, Jamila alitafutwa kila kona. Mansoor
alituma watu wake kila mahali kuzunguka uwanda wote wa
Kashmir, kuanzia milimani mpaka mabondeni wakiwa na kila aina
na njia ya kutafuta mtu aliyetoweka. Saa kumi na tatu zilipita,
hawakuweza kumpata. Si kwamba hawakufika katika bonde hilo,
la. Walifika mpaka Zalwan lakini hawakufanikiwa. Giza lilipoingia
walipunguza nguvu ya msako na kuacha watu wachache wakiwa
huku na kule ili tu waweze kupata fununu zake.
Jamila, alichelewa sekunde kadhaa baada ya wenzake
kufyatuka na kurushwa nje ya ndege ile. Mkanda wa kiti chake,
ulikataa kuachia bako yake. Wakati ndege ile ikitaremka chini kwa
kasi, yeye alikuwa akihangaika kuufyatua mkanda ule. Kepteni
Bakari na Joel tayari walikuwa wamekwishafanikiwa kutoka. Naye
alipofanikiwa, aliiongoza vizuri mwamvuli wake kuelekea chini.
Ukungu uliozingira milima na mabonde ya Kashmir, vilimfanya
asijue hata ni wapi anakoenda kuangukia. Baada ya kufanya juu
chini kuuongoza mwamvuli huo, alilitoka anga lenye ukungu na
hapo ndipo akatumia utaalamu wake wote kupata eneo zuri la
kuangukia. Uwanda wa kijani ulimfanya ajue kuwa kwa vyovyote ni
eneo lenye mpunga. Na eneo kama hilo huwa ni chepechepe

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

daima. Hakukosea, lakini ilikuwa ajali, ajali ambayo hakuitegemea.


Parachute alilokuwa akitumia lilichanika vibaya akiwa umbali wa
kama mita hamsini hivi, likamwacha nay eye akaanguka katika tope
na kudidimia kiasi. Jamila alijigeuza upande wa pili na macho yake
yakachukuliwa na giza zito.
* * *
Katika kasri la Al Mansoor, vijana waliopewa kazi walirudi
jioni sana wakiwa hawana kingine zaodo ya kitambaa cha
parachute. Al Mansoor alitikisa kichwa, akauma meno. Hakuongea
kitu, akabaki kashika tama. Hata wale walioleta taarifa na wao
wakabaki kimya. Dakika kama tano baadae, akainua uso wake na
kuwatazama.
“Lazima mumpate, bila huyo biashara itakuwa ngumu sana,”
akawaambia.
“Tumejaribu kila njia mkuu, hatujafanikiwa…”
“Lazima apatikane… na nimeshawaambia mara nyingi, sitaki
kusikia neon ‘hatujafanikiwa’”
Alipotaka mwingine kuongea, akaonesha ishara ya mkono
akimaanisha kuwa hataki mazungumzo yoyote. Ishara iliyofuatia
ilikuwa ya kuwataka waondoke. Mfanyabiashara huyo aliinuka na
kuingia katika chumba kingine. Uso waote ulisawajika, mawazo
yakamtinga na kuanza kufikiri mbinu mpya za kufanya. Akainua
simu yake ya mezani na kubofya namba kadhaa, akaiweka sikioni.
“Fika ofisini mara moja…” akakata simu.
Haikupita hata dakika thelathini, kijana mmoja mrefu,
aliyevalia kanzu safi, aliwasili kwenye ofisi hiyo.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Faizar Rabin!” Mansoor akatamka jina hilo.


“Nimeitikia wito,” Faizar akajibu huku akiketi kitini.
“Tumefanikisha, lakini kuna kitu hakijakaa sawa…”
“Kipi mkuu?”
“Mtu mmoja kapotea, vijana wametafuta sana lakini
hawajampata,”
“Aisee!”
“Walichoniletea hapa, ni kipande cha parachute tu…”
“Sasa, mbona hao walikuwa washamaliza kazi? Maana kutoka
hapo kwenye hicho kipande wangetafuta tu kilomita walau moja ya
mraba, wangempata au wangejua kaelekea wapi…”
“Nahitaji msaada wako…” Mansoor akasema. Faizar akatulia
kidogo, kisha akajikohoza, “msaada wa kumpata huyo mtu?”
“Ndiyo, tusije tukafanyiwa hujuma …”
“Na nani?”
“Hizbul wanataka niwauzie huu mfumo, alikuja mchana huu
Jenerali Kahir, lakini mi tayari nina mteja wangu wa siku nyingi
bwana Fernandes,”
“Hawana madhara hao, nitakuletea huyo mtu ndani ya saa
sabini na mbili,”
“Nakuamini, Faizar…” Al Mansoor, akavuta droo na
kumuwekea picha mezani. Faizar akaitazama kwa tuo.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Mwanamke, kazi ndogo sana! Akajisemea kwa dharau na


kuinuka, “adios amigos!” akaagana na Mansoor na kuondoka zake
kutoka kwenye kasri hilo.
Faizar Rabin, kijana barobaro kama walivyo wengine. Mpenda
starehe, mpole na mwenye huruma. Ndani ya ngozi yake
kulifichwa ukatili na uovu wa hali ya juu. Alikuwa muuaji wa
kukodiwa kwa bei kubwa. Mauaji yake yalikuwa ya siri sana. Kijana
huyu mwenye asili ya Kiyahudi alilowea katika mabonde haya ya
Kashmir miaka mingi nyuma baada ya kuingia katika mikono ya
serikali ya Isarel na kuwatoroka. Hakutaka kabisa dunia ijue kuwa
yupo katika eneo hilo lisilo na taifa. Aliishi peke mlimani, kwenye
nyumba ndogo iliyobeba siri kubwa na nyingi. Alitokea kuwa rafiki
sana wa Mansoor hasa kwa uhodari na umahiri wa kazi yake.
Kazi kama hii ya kumtafuta mtu tena mwanamke, kwake
ilikuwa kama kumpa pesa ya bure tu. Hakuona kazi hiyo kuwa ni
ngumu badala yake alijisemea tu kuwa ‘watu wana hela za
kuchezea’. Taswira ya Jamila aliimeza na kuweka moyoni na akilini
mwake. Alijua ni muda gani wa kuingia mitaani hii amsake
mwanamke huyo.
Kwa kuwa ni mgeni, tena mwafrika, sintochelewa kumpata!
Akawaza wakati akiifikia nyumba yake ndogo aliyokuwa akiishi
peke yake.
* * *
Usiku wa saa tatu, mvua kubwa ikaanza kunyesha kwenye
bonde hilo. Jamila akashtuka kutoka kwenye yale matope. Akili
yake haikuwa sawa kwa muda kama wa dakika nne hivi. Alijigeuza
na kugundua kuwa mwili wake wote umegandwa na matope.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Joel! Joel! Bakari! Beka!” Jamila akaita kwa sauti ya shida.


Kimya. Akatazama mazingira yale, hakuelewa nini kimetokea.
Niko wapi? Akajiuliza. Akili ilipomrudia sawasawa akagundua
kuwa yupo katika tope zito, bonde la mpunga. Akatumia nguvu
zake zote kujitoa hapo. Alipogeuka akahisi maumivu makali sana
shingoni. Nimeumia! Akajisemea moyoni wakati akijishika shingo.
Alipotaka kujinasua katika tope lile, kwa mbali kando yam lima
aliuona mwanaga wa taa za gari. Akatulia palepale kusubiri. Naam
hakukosea, gari moja aina ya Jeep ilijitokeza, na dakika moja tu
baadae ikafika karibu kabisa na eneo lile. Akatulia kutazama nini
kitaendelea. Lile Jeep likapunuza mwendo, na watu watatu
wakateremka kwa kuruka kabla halijasimama. Jamila akaingiwa na
hofu, akawatazama wale watu waliokuwa wakiangazwa kwa
mbalamwezi. Akasikiliza lafudhi wanayoongea ili tu ajue ni watu
gani. Hakuchelewa kujua kwani matamshi yale yanayofanana na
Kiarabu yalimfanya ajue kuwa hao watu watakuwa Waarabu. Kwa
kuwa alikumbuka kuwa kabla hawajapata tatizo hilo, walikuwa
kwenye anga la India kuingia Pakistan. Wale jamaa wakiwa na
bunduki nzito kila mmoja walitawanyika huku na kule
wakiwasiliana kwa redio zao. Dakika thelathini baadae, wakapanda
lile jeep na kuendelea na safari yao.
“Asante Mungu!” akasema kwa sauti ndogo. Jamila akatumia
nguvu zake kutoka kwenye yale matope. Akafanikiwa. Hakuwa na
muda wa kufanya lolote Zaidi ya kutafuta ama sehemu ya kujificha
au njia ya kuondokea. Akatazama upande ambao barabara ile
imeelekea, akafikiri kuifuata kuelekea upande ule ambao lile Jeep
limeelekea. Baada ya kukubaliana na akili yake akaanza kuifuata
kwa kupita pembeni pembeni, mwendo wa dakika tano, akasita, na

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

kusimama. Moyo wake ulisita, silka yake ikamtaka kurudi alikotoka,


akaamua kufanya hivyo. Jamila akaanza tena kutembea haraka
haraka. Moyo wake ulijaa hofu kuu, nini kingemkuta kama
angekamatwa na watu hao. Kwa haraka haraka alijuwa wazi kuwa
hawakuwa wanajeshi, hivyo hawakuwa watu wema. Wataniua,
watanibaka! Akawaza na kuongeza mwendo kuifuata ile barabara.
Jamila alijikuta anakimbia, nguo zake za kirubani zilizoshonwa kwa
mfano wa ovaroli zilimfanya ashindwe kukimbia sawasawa.
Akasimama na kulivua. Mwilini mwake akabaki na taiti iliyofika
karibu kabisa na magoti, juu alikuwa na sidiria iliyoonekana kama
fulana kwa jinsi ilivyotengenezwa. Buti zake za kitambaa ziliendelea
kumsitiri miguu. Jamila akaanza kutimua mbio.
Alipoyzunguka ule mlima, kule lilikotokea lile Jeep. Nyuma ya
ule mlima kulikuwa na mteremko mkali, na upande wa bondeni
kulipendezeshwa na taa nyingi za umeme. Taa zile zilimtia moyo
na kujua kumbe hayuko mbali na mji, akaongeza mwendo na kila
aliposikia muungurumo wa gari au kuona taa zikimulika aliingia
vichakani na kuliruhusu lipite. Ovaroli lake begani, safari
kaendelea. Akiwa katika safari yake hiyo, akakumbuka kitu.
Akasimama na kuanza kulipekuapekua lile ovaroli. Ndani ya mfuko
mmoja uliokuwa umefungwa kwa zipu imara, akatoa kitu kama
simu, lakini haikuwa simu. Akajaribu kukiwasha kikakataa. Hakujali
sana, akaendelea na safari yake kuufuata ule mji.
* * *
Faizar na vijana wake watatu walilizunguka eneo lote la bonfe
la Kashmir kwa kutumia gari lao lenye nguvu aina ya Jeep.
Walitumia takribani saa nne kumaliza kazi yao na kukubaliana kwa

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

pamoja kuwa mtu huyo wala kinachofanana naye hakipo katika


bonde hilo.
“Sasa kama hapa hatujamuona, awamu ya pili inabidi tuingie
hapo kijiji cha Nawal, muhakikishe mnatumia mbinu
nilizowafundisha kumpata. Kumbukeni, ni Mwafrika, kwa namna
moja au nyingine anaweza kushahabiana na wanawake wengine wa
hapa, hivyo basi, nywele zake ndizo ishara kubwa kwetu ya
kumtambua. Mnajua mtindo wa wanawake wetu wa kufunga
vitambaa vyao kichwani, kamwe hawezi kufanana nao katika
ufungaji huo… basi, twendeni…” akatoa maagizo. Wakaingia
kwenye lile Jeep na kurudi mjini, upande ule wa pili alikoelekea
Jamila..
Nawal, mji mdogo katika bonde la Jammu na Kashmir,
ulikuwa kimya usiku huo. Mibwako ya mwbwa tu hapa na pale
ilikuwa ikisikika usiku huo. Zaidi ya hilo, ni wanajeshi wa India tu
waliokuwa wakipiga doria huku na huko kuhakikisha eneo hilo
linakuwa salama dhidi ya vikundi vya Wapakistan ambao nao
wanagombea kuwa hiyo ni sehemu yao. Jeep la akina Faizar liliingia
mjini kwa mwendo wa wastani likikatisha mtaa huu na ule,
likipenya hapa na pale. Askari wale wa India hata
hawakujishughulisha nalo kwani walilijua vyema, na walijua ni nani
aliyemo humo. Faizar, muuaji wa siri anayetumiwa na tajiri
Mansoor. Machoni mwao alikuwa mtu mtulivu, mpole, mwema na
mpenda Amani.
Pambazuko la siku hiyo liliwakuta doro. Faizar na kundi lake
hawakufanikiwa kumpata Jamila. Kajificha wapi, ilikuwa ni siri
kubwa.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Usiku uleule wakati wao wanaingia mjini, Jamila alikuwa


kajibanza kwenye uwa wa moja ya nyumba za wakaazi wa hapo
Nawal. Aliliona Jeep lile likipita. Kwa mbinu zake za kijeshi
alizopata mafunzoni, alijificha vizuri na wao wasimwone. Nyumba
ya pili ndiyo iliyomfurahisha Zaidi. Ilikuwa kubwa ya ghorofa tatu.
Juu kabisa ya ghorofa kulikuwa na uwazi mkubwa na nguo
zilionekana kuning’inia kwenye Kamba. Alizihitaji. Akaizunguka na
kugundua kuwa imefungwa milango yote. Lakini upande mmoja
kulikuwa na mabomba ya chuma yenye ukubwa wa inchi nne. Kwa
ustadi wa hali ya juu, alikwea yale mabomba mpaka akafika juu
kabisa. Akachagua nguo inayomfaa, suruali nyepesi na fulana.
Akachukua mtandio uliokuwa umeanikwa hapo akaviweka pamoja.
Jamila akateremka kwa kutumia bomba lilelile lakini kabla hajafika
chini alisikia mibweko ya mbwa. Alipoangalia chini, akakuta mbwa
watatu wakiwa wanamsubiri kwa shauku huku wakipiga kelele na
kuzungukazunguka. Jamila akasukuti nini cha kufanya kwa kuwa
alijua kwa vyovyote mbwa wale wanaweza kuvuta watu eneo hilo.
Kutokana na mafunzo ya uanajeshi wake, mwanamke huyu alikuwa
anaelewa maana ya mibweko ya mbwa. Alijua mbweko huo ni ule
wa kutaka kumshambulia mtu mwovu.
Vipi kama kuna askari au mtu anaeelewa maana ya mibweko hii?
Akajiuliza. Hakuwa na jinsi, alichotakiwa kufanya ni kupitisha
uamuzi tu. Hakuwa mbali na mawazo yake, sekunde hiyohiyo
akasikia mlio wa gari ukielekea upande huo. Jamila akajiachia
kutoka pale aliposhika lile bomba na sekunde tatu tu, alitua chini
kwa kishindo. Miguu yake miwili ilitu juu ya shingo ya mbwa
mmoja. Na yu le wa pili alipojaribu kumrukia kwa shambulizi
akakutana na pigo moja lililomfanya atoe sauti ya mwisho. Jamila
hakuishia hapo, teke moja lenye kasi likamzimisha yule wa tatu.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Kisha akatokomea upande wa pili wa jengo lile wakati lile gari


likiwasili na kukutana na miilia ya mbwa.
Jamila akaicha ile nyumba na kuingia vichakani, kisha akaanza
kufuata njia ileile aliyokuja nayo kurudi alikotoka, akijua wazi kuwa
huko mambo yameharibika.
* * *
Dar es salaam
Kamanda Amata aliegesha gari lake nje ya ofisi ya Wizara ya
Ulinzi. Akateremka na kuweka tai yake vizuri. Mkononi mwake
alikuwa na simu iliyomsaidia kupata mawasiliano na wenzake
popote walipo. Ndani ya ofisi hizo, Kamanda Amata alikwenda
kuonana na mtu mmoja tu ambaye kwaye alijua atapata chochote
kuhusiana na sakata hilo. Akakaribishwa na kuongozwa mpaka kwa
katibu wa mtu huyo.
“Nahitaji kumuona Kanali Mwambope,” akamwambia katibu
yule aliyekuwa ametingwa mbele ya kompyuta. Yule dada akainua
macho yake na kumtazama huyo anayeongea naye.
“Hajafika!” akajibu kwa mkato na kuendelea kushughulika na
kazi yake.
“Yuko wapi? Nina shida muhimu na ni ya kiofisi pia, nahitaji
kumuona,” akasisitiza.
“Hayupo, hajafika kazini kabisa leo,”
“Jana alifika?”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Ndiyo aliondoka mapema…” akaeleza. Amata akatafakari


kwa sekunde kadhaa. Alijua wazi kuwa kwa kumkosa huyo bwana,
atashindwa kupiga hatua katika uchunguzi wake.
“Sawa!” akajibu.
Amata akatoka ndani ya ofisi ile mpaka kwenye gari yake.
Akainua simu yake na kupiga simu kwa mtu anayemtaka ambaye
kwa vyovyote angejua ni wapi kanali huyo anaishi. Dakika mbili tu
baadaye akawa keshapata jibu kuwa Mwambope anaishi katika
nyumba za jeshi huko Lugalo. Akawasha injini ya gari lake na
kuanza kuitafuta Lugalo. Haikumchukua muda kuwasili katika
nyumba hizo za maofisa zilizopo Makongo Juu. Katika lango la
kuingia katika kota hizo, Amata alielekezwa mpaka namba ya
nyumba ya afisa huyo. Akakanyaga mafuta kuifuata nyumba hiyo.
Akaipata. Amata akazima gari na kuteremka, akavuta hatua
kuiendea nyumba hiyo. Akazikwea ngazi za nyumba hiyo na
kuufikia mlango. Akagonga hodi na kugonga, hakuna jibu.
Akarudia tena kugonga mlango huo, hakuna jibu. Akatazama huku
na kule kama kuna mtu jirani hapo, hakuna. Kutoka nyumba moja
kwenda nyingine kulikuwa na umbali wa kutosha na kutenganisha
na vichaka vifupivifupi vichache. Akachomoa funguo yake na
kuujaribu mlango. Ukafunguka. Amata akausukuma taratibu na
kujitoma ndani ya sebule pana iliyojaa samani nzuri za kuvutia.
Ilikuwa nyumba pweke, hakukuwa na mtu, ukimya wa kuogofya
uliijaza. Amata akatulia kimya akiwa kasimama hatua tatu tu kutoka
kwenye ule mlango. Masikio yake aliyafungua kusikia chochote
kilichopo ndani humo. Akazima fujo na vurugu zote kichwani
mwake na kuruhusu utulivu wa ajabu ndani yake. Zaidi ya matone
ya maji yaliyokuwa yakisikika bafuni hakuna kingine ambacho

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Amata alikisikia. Akaendelea kutulia, kisha taratibu akavuta hatua


kuikagua nyumba ile chumba kimoja baada ya kingine. Mlango wa
kwanza kuufungua, ulikuwa wa jikoni. Katika chumba hichi Amata
alipepesa macho kiufundi kuangalia kila kitu jinsi kilivyo. Juu ya
meza kubwa kulikuwa na kipande cha ubao ulioonekana wazi kuwa
ulitumika kukatia nyama. Pembeni ya kipande hicho cha ubao
kulikuwa na kisu. Amata akaendelea kutazama vitu vingine mle
ndani, hakuona cha maana. Akaamua kutoka na kukifuata chumba
kingine, kabla hajarudishia mlango ule, akasimama kwa sekunde
chache, akageuka na kukifuata kile kisu. Naam kilikuwa na damu,
tena mbichi. Mwili ukamsisimka, akajua wazi kuwa ndani humo
kuna jambo. Akakiendea chumba kingine, kilikuwa cha kulala.
Kitanda kimoja kidogo na meza ya kusomea kilimjulisha hilo.
Hakikuwa na jipya, akapita na vyumba vingine kama vitatu hivi.
Chumba cha mwisho ndicho kilikuwa cha mwenyewe, kitanda
kikubwa kilichovurugika, mshuka yaliyozagaa sakafuni
yalimsisimua Amata.
Hapa palikuwa na kazi kubwa! Akawaza na kuichomoa bastola
yake, akaiweka sawa tayari kwa lolote. Akili yake ilishajua kama si
mapigano basi palikuwa na mtanange mzito wa mtu na mpenzi
wake. Akaangaza macho kuanzi juu mpaka chini huku akiwa
kasimama palepale. Hakunyanyua hata mguu kupiga hatua, alifanya
ukaguzi kwa macho. Alipojiridhisha na ukaguzi huo, akavuta hatu
kuuelekea mlango mwingine ndani ya chumba hicho hicho,
akausukuma taratibu. Alipopiga jicho ndani yake, Amata alipigwa
na butwaa, moyo wake ulipiga samasoti na kuhisi kama umeruka
mapigo matatu hivi.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Mwambope alikuwa mfu, Kamba iliyoifunga shingo yake


ilifungwa vyema katika bomba la mvua la bafu hilo. Katika beseni
kubwa la kuogea, palijaa maji yaliyochanganyika na damu. Akainua
macho na kugundua kuwa mwili ule ulikuwa umetobolewa macho
yote mawili.
Duniani kuna watu makatili sana! Akawaza na kujikuta akipata
kitapitapi. Akachomoa simu yake na kupiga picha ile hali kisha
akarudi pale chumbani. Kabla hajaufikia mlango, akasikia
mfurukuto wa simu mahali Fulani. Akatahayari na kusimama.
Akageuka taraibu na kutazama labda ataiona simu hiyo. Hakuiona.
Mfurukuto ule ukaendelea, akahisi unatokea chini nya kitanda,
akainama kwa tahadhari kubwa kuangalia. Naam! Kulikuwa na
simu upande mmoja na karatasi chakavu upande wa pili,
akarefusha mkono wake na kuvichukua kimoja baada ya kingine.
Akavitia katika mfuko wa ndani wa koti lake. Akaiacha nyumba ile
katika hali aliyoikuta na kuingia katika gari lake.
Mwambope ameuawa kwa sakata hili au hapa kuna jambo
jingine? Akajiuliza. Kwa kuwa mpaka hapo hakuweza kujua nini
kipo mbele au nyuma ya kifo hicho. Akaondoa gari lake kwa kasi
mpaka lango kuu akasimama hapo.
“Umefanikiwa kumuona?” akaulizwa na askari aliyekuwa
lindoni getini hapo.
“Hapana, nimegonga sana hodi, nimezunguka nyumba yote
hakuna dalili ya mtu,” Amata akajibu, “kuna mtu mwingine
aliyekuja kumtafuta leo hii au jana hivi?” akauliza.
“Aaaaaah… ngoja!” yule askari akamjibu na kurudi kibandani.
Dakika kama mbili hivi, akarudi tena kwa Amata.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Hapana kiongozi, mgeni wake wa mwisho hapa alipita siku


tano nyuma, na walionekana kutoka wote,” akampa jibu.
“Ok asante!” Amata akajibu na kuondoa gari. Nusu saa
baadae, aliegesha gari lake nje ya jengo la JM Mall. Akateremka na
kuingia ndani ya jengo hilo. Akachukua lifti mpaka ghorofa ya sita
ambako ofisi yake ya AGI Investment ilikuwapo. Akaingia na
kumpita Gina kama hamuoni, akajitupa kitini na kujiinamia kwa
jozi la sekunde.
“Vipi Amata?” Sauti laini ya Gina ikayapapasa masikio yake.
Akainua uso wake na kumtazama, “mambo yamekuwa magumu,”
akamjibu.
“Kivipi?”
“Mh! Acha tu nitakueleza, naomba kahawa Tafadhali…”
“Cappuccino au espresso?” Gina akauliza kumtaka achague
kati ya kahawa hizo za Kiitaliano ambazo kwazo alizipenda sana.
“Espresso Tafadhali,”
“Ok!”
Mara tu Gina alipoondoka, Amata akaingiza mkono katika
koti lake na kutoa ile karatasi kwanza. Karatasi ile ilikuwa
imefinyangwafingwa na kuchakazwa kwa hali hiyo. Akaikunjua
taratibu na kuiweka juu ya meza yake. Haikuwa na mambo mengi,
iliandikwa maneno machache tu yaliyotanguliwa na jina moja.
Capt. Hasheem Faraj
R.M.-P.o.R

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Karatasi ile iliishia hapo, hakukuwa na maelezo Zaidi. Amata


aliitazama ile karatasi kwa sekunde kadhaa. Aliposikia Gina
anachezea kitasa cha mlango kuingia ndani, akaitoa haraka na kuitia
kwenye droo.
“Hii hapa!” Gina akamwambia Amata huku akitua chano
mezani.
“Asante G’” akamshukuru na kumkatisha jina lake. Gina
alipenda sana kuitwa G’ na Amata. Naye Amata alilijua hilo hivyo
mara nyingi ili kumfurahisha alimwita namna hiyo.Gina alipotoka,
Amata aliendelea na jambo lake.
Hasheem, Hasheem ni nani? Akajiuliza. Na hii R.M-P.oR ina
maana gani? Akazama katika lindi la mawazo. Akainua kikombe cha
kahawa na kupiga funda moja kubwa kisha akakiteremsha. Mkono
wake ukazama tena kwenye koti lake, akachukua ile simu na
kuitazama kwenye kioo chake. Ilikuwa simu kubwa aina ya
SAMSUNG. Alipoibofya katika kitufe cha kuruhusu kioo chake
kiwake, ikaonesha inataka kufunguliwa kwa namba maalumu.
“Shiiit!” akang’aka na kuiweka simu ile mezani. Jina Hasheem
lilimrudia mara nyingi sana kichwani mwake. Akaiandika meseji ile
kama ilivyo na kumtumia Madam S huku akimtaka waonane haraka
iwezekanavyo.
Mkgahawa wa Albasha. 15 minutes
Amata akapokea ujumbe uliomwelekeza mahali. Hakukawia,
akainuka na kutoka.
“Vipi?” Gina akauliza.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Nakuja, kuna mtu nina miadi naye hapo nje,” akamwambia


wakati anarudishia mlango na kutoka nje ya ofisi ile. Dakika kumi
baadae alikuwa tayari katika mgahawa huu wa Kilebanoni
uliojulikana kama Albasha, ulio katikati ya jiji la Dar es salaam.
Amata alichagua kiti alichoona kitamfaa kuuweka ukumbi ule
mbele ya macho yake ili ajue nani anaingia na nani anatoka.
Mhudumu alipomfikia, hakuwa na makuu, sahrubati baridi ya tufaa
na sambusa mbili. Dakika tano baadae, Madam S aliwasili na
kuungana naye katika meza ileile. Wakaketi katika mtindo wa
kutazamana.
“Enhe, kamanda!” akaanzisha mazungumzo pindi tu
alipokuwa akiketi.
“Kuna jambo lina utata kidogo… sasa sijui kama ni sakata
hilihili au ni linguine…”
“Nini tena Amata, mbona waanza kunisisimua?”
“Ndo hivyo!”
“Sema nisikie…”
“Jenerali Mwambope ameuawa…”
“What? Eeen?
Wakati Madam S kashtuka namna hiyo yule mhudumu
alikuwa keshafika katika meza ile akiwa na kile alichoagizwa
mkononi mwake. Akaitua mezani ile chano na kuweka mbele ya
Amata.
“Asante mrembo,” akashukuru na kumruhusu kuondoka.
“Mwambope ameuawa!” Madam S akarudia kauli ile,
“umejuaje? Na mbona hatujasikia? Maana kifo kama hicho kabla
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

hata ya mama yake mzazi kujua ofisi yetu ingefahamu,”


akamwambia.
“Ni kweli. Ila inaonekana wazi kuwa hakuna anayejua kuhusu
kifo hicho,” Amata akamwambia Madam S na kupiga funda moja
la sharubati iliyokuwa katika bilauri ile. Madam S akatingisha
kichwa juu chini kuashiria kuna jambo anatafakari katika hilo.
“Umejuaje watu hawajui?” akauliza.
“Nilifika kumtembelea nikakuta nyumba ipo kimya, nikaingia
kufanya upekuzi, ndipo nilipogundua mwili wake katika bafu la
chumbani mwake ukiwa umetobolewa macho na kunyongwa
kwenye bomba la mvua,” akaeleza.
“Shiiit!”
“Sasa nataka kujua sababu ya kifo chake…” Amata akaeleza.
“Kwa nini ulimtafuta?”
“Jenerali Mwambope yupo kwenye idara ya manunuzi ya mali
zote za jeshi Tanzania, nilikwenda kwake ofisini ili kujua mchakato
wa manunuzi wa hizi ndege vita na washirika waliochangiana nao
kama ni pesa, mawazo au chochote kile ili kuweza na sisi kupenya
mahali Fulani kujua juu ya hili,” Amata akajibu swali la Bosi wake.
“Enhe…”
“Nilipofika pale ofisini kwake, katibu wake akanieleza wzi tu
kuwa bosi wake hajafika kazini na wala hana taarifa yoyote, ndipo
nikapatafuta. Nilipoenda nikakutana na hayo,”
“Umetoa taarifa popote?”
“Hapana, siyo kazi yangu,”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Hujaonekana na mtu ulipoingia?”


“Sizani kwa sababu nyumba yenyewe ilipo ni mahala ambapo
hakuna watu jirani,”
“Ok! Vipi walinzi wa getini?”
“Wao pekee ndiyo wanaojua kuwa nilikwenda kwa
Mwambope. Nilipotoka niliwahoji kidogo kama wanajua au kuna
mtu aliingia hapo kwa minajiri ya kumuona jenerali huyo ndani ya
saa sabini na mbili…”
“Wakasemaje?”
“Hakuna”.
Ukimya ukatawala kati yao. Amata akaendelea kutafuna
sambusa zake na kumimina ile sharubati tumboni mwake huku
akitikiza mguu taratibu.
“Ikigundulika wasije wakasema ni wewe umeua, maana hao
vijana wa getini wamekuona…”
“Usiogope hilo, kwenye uchunguzi wa maiti hujulikana
mpaka mtu kauawa lini,”
“Sasa tunafanyaje?” Madam akauliza.
“Enhee, muda wote nilikuwa nasubiri hilo swali. Ile meseji
yangu umeipatia ufumbuzi?”
“Simple tu, nashangaa we unazeeka kuliko mimi! Kapeni
Hasheem Faraji, Retired Military, Point of Reference,” Madam S
akajibu.
“Dah! Kweli nimezeeka. Sasa… inabidi nimtafute huyu
Hasheem, ama ndiye muuaji au kuna kitu anajua,” Amata akasema.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Hapo upo sawa. Na kama ni mwanajeshi mstaafu, basi


itajulikana haraka ni wapi yupo,”
“Hapo sawa, nah ii kazi nitaifanya kesho, maana leo siku
imekwisha,” Amata akajibu.
“Sawa, kama hakuna jingine, basi tuonane kesho ofisi ndogo
mara baada ya kwenda huko kutafuta habari za huyo mtu,” Madam
S akamwambia Amata huku akinyanyuka tayari kuondoka. Amata
naye akafanya hivyo, wakapeana mikono kuagana.
Mara tu Madam S alipoondoka, Amata akaichukua ile simu na
kuiwasha. Ikawaka, ikamdai kuweka namba fungushi. Akajaribu
mara ya kwanza ikamkatalia, akajaribu mara ya pili, vilevile.
Akaogopa kuingiza mara ya tatu kwani ingejifunga. Akachukua
simu yake binafsi na kuiwasha program maalum inayoweza
kutambua namba hizo. Akabonya tena ile simu na kuiitisha ile padi
ya namba. Akaiskani kwa simu yake ya kisasa nayo ikamwonesha
tarakimu ambazo zinabofywa sana. Alipozikariri, akazibofya na ile
simu ikafunguka. Jambo la kwanza, akaingia kwenye Call History na
kuchukua namba tano za mwisho zilizompigia na alizozipia,
akaziandika kwenye kumbukumbu ya simu yake.Jambo la pili,
akaingia kwenye kisanduku cha ujumbe mfupi wa maandishi na
kuperuzi baadhi ya jumbe hizo kuona kama zitamsaidia chochote.
‘Siwezi kufanya jambo hilo, kwanza najuta kwa nini
nimehusika…’
Ujumbe wa mwisho wa Jenerali Mwambope ulisomeka hivyo.
Amata akaitazama namba iliyotumiwa ujumbe huo, akatazama
mlolongo mzima wa jumbe hizo na kugundua kuwa una jambo
lililokuwa likiongelewa kwa mafumbo. Akainakili ile namba pia.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

‘Mtu pekee wa kutusumbua ni Capt. Hasheem, tunataka ufanye


juu chini ukamuue kwa mkono wako…’
Ujumbe mwingine kutoka kwenye namba ileile ukasomeka.
Ujumbe ule ulionekana wazi kutumwa majuma manne nyuma.
Hapa kuna kitu kati ya marehemu Mwambope, huyu mtu nisiyemjua
na huyu Hasheem. Hasheem ni nani? Madam kanambi wazi kuwa ni Point
of Reference. Ngoja nianze kumtafuta Hasheem kwanza! Alijiuliza,
akajijibu na kujiambia. TSA 1 akapanga mpangokazi wa kulikabili
swala hilo. Mambo mengi alitakiwa kuyategua kwanza ili kuweza
kulikabili swala hilo. Aliitazama saa yake, saa tisa na dakika hamsini
na mbili alasiri. Siku ya kiserikali imekwisha. Kesho ilikuwa kama
mwaka mwingine kwake, alipenda kulifumbua fumbo hilo kabla
jogoo hajawika ili akikutana na Madam S ajue nini atamwambia.
Hii ilikuwa tabia ya Kamanda Amata. Akishaingia msambweni,
hakupenda kutoka kapa. Alipenda kuhakikisha anafika mahali
fulani.
* * *
Saa mbili usiku, Kamanda Amata aliegesha gari nje ya nyumba
moja eneo la Gongo la Mboto. Ilikuwa moja ya nyumba za jeshi
zilizojengwa kwa mstari mrefu. Amata alikuwa ndani ya kambi
nyingine ya jeshi katika jiji la Dar es salaam.
“Da’ Jamila anaishi mlango huo hapo, ila hayupo ameenda
kozi mwezi wa tatu sasa,” mwanamke wa nyumba jirani
akamweleza Amata.
Ina maana hawajui kama Jamila amekufa au amepotea? Akajiuliza.
“Nani anayeishi hapa sasa?” akauliza.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Yupo mtoto wa dada yake, ila hajarudi shuleni,”


“Huwa anarudi saa ngapi?”
“Saa tatu, si unajua usafiri mgumu baba angu…”
Amata akafikiri kwa muda, amsubiri binti huyo au aondoke
zake. Na kama atamsubiri atamuuliza nini maana alihisi hawa watu
hawajui lolote lililotokea, au inakuwaje. Njia panda. Kabla
hajaamua lakufanya, yule aliykuwa akimfikiri akawasili.
“Anko una bahati, huyo amefika!” yule mama jirani
akamwambia Amata.
“Asante,” Amata akajibu na kuanza kumkabili yule msichana
aliyevaa sare za shule ya sekondari ya Zanaki.
“Karibu,” akakaribishwa ndani na yuole msichana. Bila
hiyana, akaingia na kuketi kwenye sofa kubwa lililojaa sebuleni
hapo na yule mwenyeji wake akakaa katika kiti kingine. Amata
akamtazama kwa jicho lililojaa kila aina ya huba. Mara nyingi yule
msichana aliangalia chini, hakutaka kabisa machpo yake yagongane
nay a mwanaume huyo.
“Tumewahi kuonana kabla?” Amata akamauuliza.
“Hapana, sidhani,”
“Unaitwa nani?”
“Naitwa Esha,”
“Esha! Ok… Mimi naitwa Jaffari, umewahi kunisikia?”
“Mmmmh hapana, nikusikie wapi?”
“Dada ako hajawahi kukwambia kuhusu mimi?”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Hajawahi, hata hivyo ni mara chache sana mi na yeye kukaa


pamoja kwa mazungumzo,” Esha akajibu huku bado akitizama
chini. Ni mwanafunzi wa Zanaki, kidato cha sita, mweusi, mfupi,
mwenye mwili uliyojaa. Sketi yake aliyovaa, kwa mtindo
iliyoshonwa iliyasadifu hasa maungo yake aghalabu maeneo ya
nyonga mpaka mapaja. Alivutia, akatamanisha, Amata alimtazama
kwa jicho la husuda, akameza mate mara kadha wa kadha, mate ya
uchu.
“Mimi ni rafiki wa Jamila, tumeachana muda mrefu sana, leo
nikasema nije kumsalimu…”
“Oh! Karibu. Lakini Da’ Jamila hayupo miezi mitatu sasa
kaenda kozi Urusi. Mara ya mwisho nilipoonga naye alinambia wiki
hii anaweza kurudi,” Esha akaeleza.
Hajui kitu! Akawaza. Akatupa macho huku na huku wakati
yule binti akiinuka na kuingia chumbani. Katika ukuta wa nyumba
hiyo palining’inizwa picha kadhaa, moja kati ya picha hizo ilikuwa
na wanajeshi watatu, akiwamo Jamila na wengine wanaume.
Bakari na Joel? Akajiuliza. Akaitazama kwa makini sana,
akazikariri zile sura na kuhifadhi kichwani mwake. Picha nyingine
ilimwonesha Jamila akiwa na watu wengine wane, kati yao
mwanaume mmoja na wanawake watatu. Akiwa katika kuishangaa
picha hiyo, Esha aliinia sebuleni akiwa kavalia jinzi ya kubana na
fulana nyeusi iliyomkaa vizuri.
“Vipi, una mtoko?” akamuuliza.
“Hapana anko. Nipo tu,”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Sasa nisikilize kwa makini, kama Jamila atakuja katika siku


hizi naomba unioe taarifa nina shida naye ya msingi sana,” Amata
akasema.
“Sawa, lakini sijui kama atanikuta, nataka niende likizo kwa
babu,”
“Wapi?”
“Zanzibar,”
“Ina maana we unamwitaje J’? akatamka jina kwa kulikata ili
kuonesha kuwa ana ukaribu na Jamila ilhali hata hamjui.
“Mimi ni mtoto wa dada ake Jamila anaitwa Lukundame,”
“Kumbe upo kwa mama mdogo!”
“Ndiyo!”
“Ok, basi chukua namba yangu, mwandikie kwenye karatasi
akifika atanipigia,” akamwambia, naye akafanya hivyo. Wakaagana.
Saa tatu usiku, Amata aliiacha nyumba ya Jamila na kuondoka
zake. Hakujua hata anaelekea wapi. Baada ya kupambana na
maamuzi yake, akaamua kwenda nyumbani kwake Kinondoni
kujipumzisha ili kusubiri siku inayofuata.
* * *
KASHMIR
Katika kasri la Bwana Mansoor, Joel na Bakari walihifadhiwa
ndani ya chumba kimoja mara baada ya kutolewa kule
walikokwekwa mwanzo. Katika chumba kile kulikuwa na viti viwili
vya chuma. Wakafungwa barabara juu yake. Hawakuwa na nafasi

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

hata ya kujitikisa kwani viti vile vilikuwa vimefungwa kwa bolti


imara katika sakafu ya jengo hilo.
Ukimya ulitawala, ni wao tu wawili waliokuwa humo lakini
hawakuweza kuongea lolote kutokana na matambara waliojazwa
midomoni mwao. Ukuta wa chumba kile ulikuwa wa marunmaru
nyeupe kutoka juu mpaka chini. Vyuma vyenye ncha kali kama vile
vya kuning’inizia nyama buchani vilikuwapo Zaidi ya kumi
vikining’inia kwenye bomba kubwa lenye nguvu, lililopachikwa
ukutani kutoka upnde huu mpaka ule mwingine.
Kila walipokitazama chumba hicho walijikuta kuishiwa nguvu
kila mmoja kwa wakati wake. Hofu ikawajaa. Katika marumaru
zile, kulikuwa na uchafu ambao kwa watu kama hawa walijua wazi
kuwa ni damu iliyoganda. Na sakafuni palikuwa vuvyo hivyo,
harufu kali ilikijaza chumba hicho. Uvundo.Kuwa ndani ya
chumba hicho ni sawa na kuwa kaburini kwa jinsi kilivyo.
Kelele za komeo zito lisilo na kilainishi lilisikika, mlango
ukafunguliwa, watu watatu wakaingia mle ndani. Mavazi yao tu
yaliwatambulisha kuwa ni watu wa majangwani. Suruali za
kitambaa chepesi, nusu kanzu walizovaa juu yake na vitambaa vya
kichwani viliosha kuwatambulisha utamaduni wao. Kila mmoja
alikuwa na bunduki yenye nguvu, ya kivita, ya AK-47 mgongoni
mwake isipokuwa mmoja tu aliyeonekana kuwa ni kiongozi wao.
Kijana jamali, mwenye ndevu nyeusi kwa uchache wake. Nguo
aliyovaa ni ya mtindo uleule kama wenzake lakini yake ilionekana
kuwa ya gharama Zaidi kwa nakshi zake.
Wakaingia. Wale wawili wakasimama huku na kule na yule
kijana akasogea mpaka walipo Joel na Bakari.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Kepteni!” akaita. Wote wakainua vichwa kumtazama, “dunia


ni duara. Maana ya sentensi hii ni kwamba, wewe ukifanya hivi
mwenzio anafanya vile. Sijui kama mmenielewa! Mimi naitwa Al
Mansoor, tajiri, mfanya biashara mkubwa katika ukanda wa Jammu
na Kashmir. Nauza bunduki, nauza dawa za kulevya, nauza roho
za watu. Kila ambacho mteja anakitaka mimi nauza na lazima
nikipate. Na ninapokitaka kile ninachokitaka, sioni kazi kuua. Hiyo
ndiyo siri ya pesa, ukiitaka uwe jasiri usiyeogopa. Safari hii ninyi
mko mbele yangu kama bidhaa, ama niwauze wazima wazima au
mnipe ninachotaka kisha niwaache muende zenu, mtachagua.
Lakini nini ninataka kwenu, mnisikilize kwa makini,” akajikohoza
huku anatembeatembea ndani ya chumba kile. Joel na Bakari
walikuwa kimya wakimtazama na kumsikiliza.
“Biashara yangu safari hii ni ya ushindani na pesa nyingi.
Tajiri mmoja kutoka Pakistan na mwingine Latino Amerika. Wote
wanataka mfumo mpya kabisa wa kudhoofisha makombora mazito
na kumtambua adui akiwa kilomita nyingi kutoka kwao. Na huu
mfumo utambulika kwa jina PT-502-B.PEGAN X,” alipotaja jina
hilo wakamkazia macho maana mfumo huo wa hatari Zaidi
duniani unaofanya kazi kwa satellite ulikuwa umefungwa ndani ya
ndege vita ambayo Jeshi la Tanzania liliinua huko Urusi.
“Enheeee vizuri sana, naona sasa akili zenu zimeamka baada
ya kusikia hili nililotaja. Sasa ninachotaka kutoka kwenu ni how to
operate,” akawasogelea na kusimama jirani nao, “nahitaji codes zote
tatu. Kila mtu hapa anipatie yak wake haraka, hiyo ya tatu najua
nitaipataje,” akawaambia kwa sauti ya upole. Akatoka pale na
kusimama kando karibu kabisa na ule mlango huku wale vijana
wake wakiziweka sawa bunduki zao.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Haya, naanza na wewe,” akamwoneshea kidole Kepteni Joel,


“nipatie code yako haraka kabla sijavunja miguu yako kwa risasi,”
akamwambia mara hii kwa sauti kali isiyo na chembe ya huruma.
Joel hakujibu kitu, alimtazama tu jamaa huyo, wala hakuonesha
dalili ya kutetereka kwa hicho kitisho. Dakika moja nzima ikapita
kwa ukimya kabisa, hakuna yeyote aliyezungumza si upande huu
wala ule.
“Nahitaji mnipatie code za kuuendeshe mfumo huu…
sentensi yangu ya tatu itakuwa mbaya Zaidi,” akasisitiza huku wale
vijana wake wakiendelea kuweka sawa zile bunduki. Joel alikuwa
akitetemeka, hajui afanyeje. Muda wote Bakari alikuwa akimtazama
kwa jicho lake jekundu kama mvuta bangi. Kepteni Joel hakujua
kama jicho hilo lina maana kuwa atoe hiyo code au hasitoe, alibaki
njia panda. Jasho lilimtoririka sehemu zote za mwili. Akiwa bado
kamtazama Bakari akahisi kitu chenye ncha kali kikimchoma
ubavuni. Akashtuka kutazama mbele. Macho yake yakagongana na
Mansoor ambaye alisimama mita moja tu mbele yake. Mkononi
mwake alikuwa na jambi refu lililofanya tao nchani.
“Mara ya mwisho nasema, nahitaji code ya kuendeshea ule
mfumo, nimemaliza… moja… mbili… tatu,” Joel hakusema
chochote isipokuwa alikuwa amekunja uso na kufumba macho
akitetemeka na jasho mwili mzima. Pigo moja la kitako cha
bunduki, ubavuni mwake likamfanya ajikunje upande huo. Pigo la
pili ubavu wa mbili likamrudisha upande wa pili. Hakupewa nafasi.
Joel alitandikwa mijeledi ya kutosja na kumwacha na vidonda
mgongo mzima. Hakusema. Bakari alijawa na hasira, ijapokuwa
asingeweza kufanya chochote kutokana na kufungwa pale kitini.
Hilo kwake lilikuwa ni teso kubwa.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Joel kama mwanajeshi mtiifu aliyekula kiapo, ilikuwa ngumu


kwake kutoa siri hiyo. Aliona ni bora afe ili wakibaki wawili hata
kama watasema bado Mansoor atakosa code moja. Al Mansoor
naye alilijua hilo hivyo aliona wazi kumuua huyo si dawa. Kijana
huyo akamtazama Bakari kwa jicho kali, “jiandae nakuja nani zamu
yako,” akamwambia,
Kepteni Bakari, akamtazama Joel jinsi alivyojiinamia pale
kitini, machozi yakamtoka, akashindwa amsaidie vipi mtu huyo.
Akabaki akisali moyoni mwake, hakuwa na jinsi nyingine.
* * *
Jua la asubuhi lilichomoza katika milima ya Kashmir,
mabonde ya mpunga yalipendezeshwa na ndege wazuri waliokuwa
wakitoka upande huu kwenda ule kule. Jamila alijitulia kichakani,
mita chache kutoka barabarani. Njaa na kiu vilimchonyota haswa,
lakini hakuwa na jinsi. Alivumilia kikike. Kutoka mbali, alisikia
muungurumo wa gari akajitayarisha kuona kama anaweza kupata
msaada. Asingeweza kukaa Zaidi katika maficho yale akiwa na
chochote cha kula wala kunywa.
Lazima nifike mjini, nitafanya kila niwezalo kupata mahitaji
yangu! Akawaza. Mungu si Athumani, loli moja lilikaribia eneo
hilo, akajitpokeza na kulipungia. Likasimama. Dereva akampa
ishara ya kumtaka kuingia ndani upande wa nyuma. Kumbe
lilikuwa gari la abiria lililopachikwa kwenye chasisi ya Bedford.
Akajitanda mtandio kwa kuificha sura yake. Akapanda na kutafuta
nafasi nzuri, akaketi kati ya wanaume wawili. Safari ikaanza. Kila
mtu ndani ya gari lile alikuwa akimwangalia abiria huyu aliyeabiri
muda huo. Hakufanana na wao, japo alivaa kitamaduni kabisa
lakini jinsi tu alivyofunga kitambaa chake kuzunguka kichwa
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

kumwagika shingoni mpaka mabegani havikushahabiana na


waenyeji wa Kashmir.
Katikati ya kijiji cha Nawal lile gari likasimama, Jamila
akaangalia nje na kuona usalama uliopo. Watu walikuwa
wametingwa na shughuli zao za kujitafutia kipato. Akateremka
kinyemela na kupotelea katikati ya watu. Jamila moja kwa moja
aliiendea benki ya J&M. hakuingia ndani. Katika chumba kidogo
cha ATM akadfanikiwa kutumia Visa Card yake na kutoa pesa
ambayo ingemtosha kwa matumizi yake. Jamila alizifutika zile pesa
kwenye sidiria yake na kuwapita akinamama waliokuwa wakichuuza
bidhaa zao nje tu ya jengo hilo. Umakini ulitaradadi katika fikra
zake kujua kama yupo hatarini au la.
Kama kuna mtego ambao Faisar alifanikiwa ni kuweka kijana
wake karibu na benki hiyo kubwa katika eneo hilo. Mara tu Jamila
alipotoka kwenye mashine ile, tayari taarifa zilifika kwa Faisar kuwa
mwanamke anayefanana rangi na huyo wanayemtafuta
ameonekana kwenye benki ya J&K. mwanamke huyo alipowapitra
tu wale akina mama wafanyabiashara, macho yake yaligongana na
kijana ambaye alihisi anamfuatilia. Akili yake ikafanya kazi haraka
haraka kuona nini cha kufanya.
‘Nifuate tuelewane!’ akajisemea huku akiingia kati ya jengo hilo
na lingine. Hakukosea, mara tu alipopenya kwenye ule uchochoro
yule kijana naye alimfuata. Akapita hapohapo kwa minajiri ya
kutompoteza mwanamke huyo. Jamila akasimama kama anataka
kufanya jambo Fulani.
Nitajaribu bahati yangu! Akawaza.Yule kijana akamkaribia
kabisa huku simu yake ikiwa sikioni na kuongea lugha ambayo
Jamila hakuilewa. Jamila alipoona tayari ni umbali wa mita chache
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

afikiwe, kwa ghafla alipeleka pigo moja la hatari la karate ambalo


lilitua sawia kifuani mwa yule kijana. Akakohoa damu. Kabla
hajakaa sawa, Jamila akamzabua teke jingine kali lililomsukumia
kijana yule ukutani. Akajibamiza kwa nguvui ukutani na kuanguka
chini. Kimya. Jamila akachukua simu ya yule jamaa na kutokea
upande wa pili way ale majengo. Akaingia kwenye taksi na kumtaka
dereva ampeleke Ramban. Si kwamba alikuwa anapajua bali alisikia
watu kwenye gari lile wakipataja.\
“Ramban?” yule dereva akauliza.
“Ndiyo,”
“Ndiyo!”
“Rupee 1500!” yule dereva akamwambia abiria wake ambaye
tayari alikuwa amekwishafunga mkanda.
“Twende!” Jamila akamwamuru na yule dereva akaingiza gari
barabarani na kutoko,ea kwa kasi huku akikenua kuwa kaweza
kumwibia mteja kirahisi kwa kuwa umbali huo haukugharimu pesa
hizo. Akiwa njiani kuelekea huko Ramban, Jamila alikuwa
akiichezea ile simu ambayo haikuwa na kifungo chochote cha
usalama. Jakueleza kuelewa arafa zilizotumwa kutokana na lugha
iliyorumika.
Nikifika Ramban kila kitu kitakuwa sawa! Alijisemea moyoni na
kutulia kimya. Dakika arobaini baadae, wakasimamishwa katika
kizuizi cha askari wa jeshi la Pakistan. Ile taksi ikazuiliwa kwa
ukaguzi. Jamila akatulia tuli kitini akisubiri kujua kinachoendelea.
Askari mmoja aliyevalia sare za jeshi, na kuning’iniza bunduki nzito
vifuani mwake, akasogea kwenye ile taksi, akamtaka dereva
kufungua buti, akafanya hivyo. Yule askari akatazama kule kwenye

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

buti, hakuona kitu Zaidi ya tairi ya akiba. Akalizunguka lile gari


mpaka kwenye dirisha la dereva. Akasimama na kumwangalia
Jamila. Moyo wa mwanamke huyo ulikuwa ukidunda kwa kasi ya
ajabu. Akajua sasa atakamatika lakini moyoni mwake bado alijpa
maoyo kwamba kama hao ni wanajeshi basi wasingemdhuru kama
angejieleza sawasawa.
“Huyu ni nani?” yule askari akauliza.
“Mke wangu!” dereva akajibu kwa kujiamini, “nimetoka nae
hospitali Nawal, namrudisha nyumbani...” akaeleza. Yule askari
akamtazama Jamila na kutikisa kichwa juu chini.
“Kitambulisho!”
“Hata nyumbani tumetoka usiku sana hatukubeba
kitambulisho chake, bahati mimi huwa kinakaa kwenye gari,” yule
dereva akaeleza. Jamila alikuwa akisikiliza lakini hakuelelewa hata ni
nini wanachokiongea. Akatulia tuli, palepale alipoketi. Yule dereva
akatakiwa kuteremka, akafanya hivyo. Akafuatana na yule askari
mpaka kwenye ofisi ndogo iliyojengwa pembezoni mwa barabara
hiyo. Nusu saa baadae akarudi na kuingia garini. Safari ikaendelea.
Dakika kama thelathini hivi wakawasili katika ule mji, Ramban.
“Nikushushe wapi?” yule dereva akauliza kwa lugha ya kwao
ambayo Jamila hakuelewa hata kidogo. Walipofika eneo lenye watu
wengi, akamwamuru dereva asimame, naye akafanya hivyo. Jamila
akateremka na kumpa yile dereva Rupee hamsini za India na kisha
yeye kupotea zake mitaani.
* * *
Ramban, moja ya wilaya ishirini katika eneo la Jammu na
Kashmir, India. Mji huu mdogo ulikuwa kati ya milima ya Pir
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Panjal. Jamila mara tu alipoachana na ile taksi, akaingia katika mitaa


ya mji huo. Jambo la kwanza alilolifanya ni kutafuta duka la nguo.
Akalipata. Akanunua nguo chache na begi moja la ukubwa wa
wastani kisha akatafuta hoteli ya kufikia.
Lords Inn Jammu ilikuwa hoteli ya kawaidasana katika mji wa
Ramban upande wa India. Jamila alichukua chumba na kupumzika
katika hoteli hiyo tayari kuanza mchakato wa nini akifanye.Mara
baada ya kutoka bafuni alichagua nguo aliyoona itamkaa vyema
ambayo aliinunua hapohapo Ramban akaivaa na kujiweka sawa.
Jamila akajitupa kitandani kujipumzisha kwa dakika chache.
Katika kijiji cha Nawal, Faizar na kundi lake walihakikisha
wanapita kila kona na uchochoro kumtia mkononi
hawakufanikiwa. Hasira zilimshika Faisar hasa alipomkuta kijana
wake akiwa hajitambui kwenye ule uchochoro na hakuwa na simu.
Alijuwa wazi kuwa wanayemtafuta sasa atakuwa na siri nyingi juu
ya kundi hilo. Akatoa maagizo kwa vijana wake waliobaki kuwa
wahakikishe mwanamke huyo anapatikana huku akiwapa tahadhari
ya kuwa makini. Wale vijana wakatawanyika Nawal yote. Wakapita
mahotelini, kwenye mabaa, stendi za mabasi, masokoni na kila
kwenye mikusanyiko ya watu. Jamila hakupatikana. Katika
upelelezi wao wakapata fununu za mwanamke huyo kutoka nje ya
ule mji. Wakapeleka taarifa kwa Faizar naye bila kuchelewa akaingia
kazini kutaka kujua ni wapi alikoelekea.
* * *
Bwana Danval Kotvich aliinua mkonga wa simu uliokuwa
jirani tu na pale alipokaa. Mara baada ya kuitambua simu hiyo kwa
namba iliyojitokeza kwenye kioo, akafanya hivyo. Akaipachika
sikioni kwa pozi huku akichezesha mguu wake.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Yes,” akaitika.
“Tunafanyaje? Kuna njia nyingine ya kupata zile codes maana mtu wa
kwanza nimemhoji amekuwa mgumu kutoa,” sauti ya upande wa pili
ikasema.
“Haujambana sawasawa…”
“Mpaka tunavyoongea hali yake ni mbaya anaweza asifike kesho,”
“Oh Shit, Mansoor, unakosea. Unajua kupata code hizo
kupitia wao ndiyo njia rahisi sana. Njia ya pili ni ngumu kwa
sababu lazima tuingie kwenye server za jeshi la Rusia. Unafikiri ni
kazi ndogo?” Kotvich akamuuliza Mansoor, “mimi nimeshiriki
kutengeneza hiyo mifumo lakini hizo code walitakiwa wao
wenyewe kwa siri watengeneze. Ina maana mtu anayeweza kuzipata
ni yule anayetunza server ya jeshi hilo. Na hapo ilipo hiyo server
huwezi kufika wala kuingia peke yako… lazima ruksa itoke juu…”.
Mansoor akashusha pumzi kutoka upande wa pili. Hakujua la
kufanya. Inabidi nizipate kupitia hawahawa!Akawaza. Akili yake alihisi
ikiuma ghafla. Akaona ugumu wa biashara hiyo aliyoishadidia kwa
kuwa ilikuwa na pesa nyingi sana.
Danval Kotvich, mwanasayansi aliyebobea katika uundaji wa
mifumo ya kusalama kutoka nchi ya Czech alikuwa miongoni mwa
watu wataalam wa jeshi la Urusi walioshiriki kuunda ndege hiyo.
Mtaalam huyu asiye mwaminifu, alipokea simu miezi kadhaa
nyuma ya kumtaka kuingia katika biashara hiyo haramu. Akalghaika
na kujikuta mikononi mwa Mansoor aliyempatia maelfu ya Pound
za Kiingereza.
“Na vipi kama watabadili codes hizo?”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“No! kubadili hizo codes ni zoezi jingine gumu sana kwa


sababu lazima uwe na zile za zamani. Lakini ujue kuwa, kuna mtu
mmoja tu yupo Tanzania, yeye ndiye pekee anayeweza kuwa nazo
hizo code au kuzibadili. So, ukitaka kuifanya hiyo biashara, una
mawili; ama kumteka au kumuua. Kwa sababu ndiye aliyedizaini
mfumo huu…” Kotvich akasema.
“Come on, lazima tudeal na huyo!” Mansoor akasema,
“anapatikana wapi, unajua?”
“Anaitwa Meja Hasheem, ni mstahafu lakini ni mtu hatari
sana. Anapatikana Zanzibar… najuta ukupa habari hii, kwaheri,”
Kovich akakata samu. Akairudisha kwenye kibweta chake na
kukunja nne. Mawazo yakakinyanyasa kichwa chake. Hakupenda
usumbufu lakini ilimbidi kutokana na kile alichokifanya. Akatulia
kwa jozi la sekunde akifikiri nini cha kufanya. Atamsaidiaje mteja
wake? Kichwani mwake alikuwa na njia tatu tu za kumshauri jinsi
ya kukusanya codes hizo. Mbili kati yazo alikwishamwambia
Mansoor ila ya tatu alikiri wazi kuwa ni ngumu sana.
Utaingiaje kwenye mtandao wa jeshi la Russia? Akajiuliza.
Kitendawili kisicho na mteguaji! Akajijibu na kupiga funda moja la
kinywaji. Lakini kama akiwabana wale vizuri watampa hizo code,
anashindwa nini? Akajiuliza. Kumuua au kumteka Hasheem sijui kama
inawezekana kirahisi. Ila yule mzee mshenzi tu wacha wakamuue!
Akajifariji.
* * *
Ndani ya Hoteli ya Lords Inn Jammu, Jamila aligutushwa
usingizini kwa hodi iliyokuwa ikibishwa. Akafumbua macho
taratibu na kuruhusu damu yake ikae sawa. Mapigo ya moyo

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

yaliongeza kasi kwa kuwa hakuju nani hasa anayegonga na kwa nia
ipi. Jamila alikuwa mgeni katika mji huo, hivyo hakutegemea kabisa
kupata ugeni. Akaijiweka sawa kwa lolote, akajiinua kutoka pale
kitandani na kuketi kabla hajauendea mlango. Baada ya sekunde
kadhaa akainuka kuufuata ule mlango huku akiwa kajipanga kwa
dhoruba yoyote. Akazungusha funguo na kunyonga kitasa, mlango
ukafunguka.
“Habari!” mwanadada mmoja alikuwa kasimama mlangoni
hapo akiwa na vifaa vyae vya kufanyia usafi. Jamila akamtazama na
kumwambia kuwa kwa muda huo hahitaji usafi katika chumba
chake. Akarudi na kujifungia, kimya. Akili yake ilikuwa akifikiri jinsi
gani ataweza kuwasiliana na baba yake wa kufikia, Mzee Hasheem
ili japo amjuze tu kuwa yupo hai. Hakuwa na simu, Zaidi ni kifaa
kidogo ambacho alikuwa akikitumia kwenye mawasiliano ya ndege
ile. Kifaa kile mfano wa simu ndogo kiliweza kufanya kazi ukiwa
umbali wa kilomita kumi hadi kumi na tano kutoka ndege hiyo
ilipo. Kichwa kilimuuma.
“Lazima nirudi… hata hivyo, nahitaji simu… nitapata wapi
laini?” akajiuliza kama anayemwambia mtu. Ooooooh nimepata wazo!
Akafumbuka. Uamuzi aliouchukua ni kutafuta simu za vibandani ili
aweze kuwasiliana na Mzee Hasheem pamoja na mkuu wake wa
kazi huko Tanzania ili kumjuza nini kimetokea. Jamila akajiandaa,
akachukua kile kifaa chake na kukiweka vizuri. Ni yeye alijua kina
kazi gani. Wote watatu walikuwa na vifaa hivyo vya kuwezesha
mawasiliano kupitia mfumo wa ile ndege. Joel na Bakari walikuwa
wamenyang’anywa, na vifaa hivyo kuhifadhiwa na Bwana Mansoor.
Mpaka siku hiyo, vijana wa Mansoor walifanikiwa kuondoa mfumo

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

ule wa ulinzi kwenye ile ndege na kuuweka katika maabara yake


ndani ya kasri lake. Na kule jangwani waliliacha ganda tu.
Jamila alifungua mlango na kuteremka ngazi mpaka
mapokezi. Pale akauliza wapi anaweza kupata simu ya jamii.
“Dah! Nasikitika kukwambia kuwa hapa Ramban na vijiji
vingine vyote katrika ukanda wa Kashmir, hakuna mawasiliano ya
simu. Na hii ni kwa sababu ya hali yetu ya Amani hapa kama
unavyojua,” akajibiwa. Jamila akaishiwa nguvu, akatulia kama
aliyemwagiwa maji.
“Umekuja kutembea au una shughuli nyingine hapa
Ramban?” yule mhudumu akauliza.
“Nimekuja kikazi, ila sasa kuna taarifa natakiwa nipeleke
makao makuu ndo maana natafuta simu,” Jamila akaeleza.
“Oh pole sana, fanya juu chini ufike Islamabad ila ni mbali
sana ni safari ya siku nzima,” akamwambia.
“Sawa, nitafanya hivyo!” Jamila akajibu na kuiacha ile meza ya
mapokezi na kuelekea nje ya hoteli ile. Mara tu alipouacha mlango
mkuu akavaa miwani yake nyeusi na hijab aliyejitanda hakika
ingekuwa ngumu kumgundua.
Nitafikaje Islamabad? Sina pasipoti wala kibali chochote! Akawaza.
Lakini inanipasa nifanye kila mbinu nifike huko halafu nikishapata
mawasiliano na nyumbani, nirudi tena huku kujua hatima ya ndugu zangu!
Akajipanga. Jamila akaingia katika mgahawa, akapata chakula na
kuanza kufanya utafiti wa usafiri kuelekea Islamabad, mji mkuu wa
Pakistan.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

05
Lukundame aliamka mapema sana na kumwandalia kifungua
kinywa baba yake ambaye usiku kucha alishinda kwenye kompyuta
yake akijaribu hiki na hiki ilia pate japo mawasiliano.
“Baba!” akaita kwa sauti ya upole. Mzee Hasheem akageuka
kumtazama binti yake, akapokea kikombe kile cha kahawa na
kupiga funda moja kisha akakitua. “Umefanikiwa?” akamuuliza.
“Hapana! Sasa nagundua kuwa hii ni hujuma kwa sababu
ingekuwa ni ajali ya kawaida, ningeshajua mpaka eneo ambalo
ndege hiyo imeanguka,” akajibu.
“Aisee…!”
“Ina maana hii ndege imeangushwa halafu kuna watu
wameiba Pegan Box,” akamweleza.
“Pegan box, nini?”
“Oh! Pegan box ndiyo huo mfumo ambao tumeuweka
kwenye hiyo ndege vita. Mfumo huu wa kujilinda na mwenye
nguvu katika mawasiliano ya anga ni wa kisasa sana. Nina mashaka
hii ndege imeangushwa, na mtu anayejua vizuri mambo haya,
amezima ule mfumo kisha kauchukua ndiyo maana hapa kwenye
vifaa vyangu kila ninapojaribu kutafuta nakosa. Nimejaribu Zaidi
ya code 1500 lakini imegoma. Oh mwanangu Jamila, heri awe
amekufa…” Hasheem alihuzunika.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Lukundame akajiandaa kuondoka katika maficho yale.


Akajiweka tayari na kila kinachomfaa kwa kuwa alijua kuwa siku
hiyo ni ngumu kwake. Aliwakumbuka wale vijana ambao alipanga
nao miadi saa tano. Mara alipoagana tu na baba yake akatoka kwa
njia ya siri na kutokomea mjini. Tayari alikwishampa taarifa CID
Badru kuwa anaingia kazini ili naye asogee tayari kutia nguvuni
vijana wale. Badru kwa upande wake, aliandaa vijana watatu
waliokuwa na silaha.
Lukundame alichukua usafiri wa baisikeli kutoka Bwejuu
mpaka barabara kuu ambako alipata taksi kuelekea mjini Unguja.
Ndani taksi hiyo aliketi kiti cha nyuma na kumwacha dereva peke
yake katika ile siti ya mbele. Taksi ile ilimfikisha mpaka eneo la
Mizingani mbele tu ya chuo cha muziki cha DCMA. Akateremka
na kumlipa yule dereva. Alipohakikisha ile taksi imeondoka, akapita
katikati ya majengo haya mawili na kutokea upande wa nyuma.
Huko alimkuta Mzee Issa amekwishafika na kumsubiri.
“Eee malkia wangu, nimekusubiri mpaka nimeanza kulala
tena,” yule mzee akasema na wote wakaanza kucheka. Wakati
anajiandaa kupanda katika Cruiser hilo la ofisini kwao, upande wa
pili wa barabara kukatokea Subaru nyeusi iliyokuwa ikija kasi
upande ule.
“Angalia wasije kukugonga wahuni hao!”
Mzee Issa hakumaliza kusema. Lile Subaru likafunga breki
kali. Mlango wa nyuma ukafunguliwa akachomoza kijana mmoja
mwenye misuli, akamkamata mkono Lukundame na kumnyanyua
kama karatasi akamtupia ndani ya lile Subaru, naye akaingia na
kufunga mlango. Mzee Issa akajikuta anashindwa asaidiaje akabaki
kajishika mikono kichwani akilalama ovyo kama mtu alirukwa akili.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Lile Subaru halikuonekana tena. Wapiti njia na majirani walijazana


kila mmoja akiwa na lake la kusema.
Ndani ya lile gari, Lukundame alichomwa sindano ya usingizi.
Haikumchukua hata dakika mbili, akalegea na ucingizi mzito
ukamchukua.
“Ataamka saa ngapi?” dereva akauliza.
“Saa ishirini nan ne zijazo,” akajibiwa.
“Safi!”
Safari iliendelea mpaka eneo la Mbuyuni, hapo wakaingiza lile
gari ndani ya jengo Fulani lililosheheni maduka upande wa juu.
Kule chini kwenye maegesho, walimhamisha Lukundame na
kumuweka kwenye gari jingine huku lile Subaru likibadilisha namba
za utambulisho. Wakatoka na Volks Wagen na kuikamata Barabara
ya Malawi kuelekea mashambani. Kilomita chache mbele
wakakunja kushoto barabara ya vumbi mpaka kwenye Hoteli ya
Abia. Kila kitu kilikuwa kimepangwa. Boti ya mwendo kasi
inayotumika kubebea wagonjwa itokeapo dharula iliandaliwa kwani
aliyekodi alitoa taarifa ya ugonjwa wa mkewe. Lukundame
akapakiwa na yule bwana akaingia. Wale watekaji wakavaa makoti
meupe ili kuwahadaa wafanyakazi wa hapo. Dakika kumi tu safari
ya Dar es salaam ikaanza kwa makubaliano ya kumshusha
mgonjwa huyo kwenye bandari ndogo ya Bagamoyo.
* * *
Asubuhi ya siku hii Amata aliwasili katika makao makuu ya
Jeshi la Wananchi, Upanga. Baada ya kujitambulisha na shida yake
akaomba kuonana na mtunza Masijala ambaye anahifadhi
kumbukumbu zote za watumishi husika. Amata akafikishwa
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

kwenye ofisi maalum ya kazi hiyo. Rafu kubwa zenye vyumba vingi
zilisheheni makabrasha kila kona. Alipepesa macho kutazama,
moyoni akakiri kuwa kama kuna watu wanateseka na kazi
wanayoifanya basi hawa wa masijala wanapitia hilo.
“Karibu kaka, nikusaidie nini?” askari wa kike aliyekuwa
kwenye dawati la ofisi hiyo alimkaribisha Amata kwa ukarimu wa
Kiafrika haswa.
“Asante sana, naitwa Amata Ric, kutoka idara ya Usalama wa
Taifa,” akajitambulisha kwa uwazi bila kificho. Hakika hakuna
mkate mgumu mbele ya chai. Yule mwanadada akapigwa na
mshangao.
“Amata? Huyu Amata ninayemsoma habari na harakati zake
kwenye magazeti na vitabu au mwingine?” akajikuta akibwabwaja
na kusahau kama kuna wateja wengine wa kuhudumia.
“Hakuna mwingine!”
“Naitwa Meja Mwaja… karibu Bwana Amata, siamini kama
nimekutana na mtu kama wewe loh!”
Mwaja alikuwa mwanamke wa makamo, kati ya miaka
thelathini na tano na arobaini, mchezi mwenye maneno mengi.
Hata uongeapo naye lazima uwe makini kwa jinsi anavyoongea kwa
haraka. Mweupe kiasi mwenye vibonyo mashavuni kila
akitabasamu. Macho yake yaliokaa kama taa za Hyundai ndiyo
yalioukamilisha haswa uzuri wake.
“Keti kidogo, nisamehe nitakusikioliza baada ya hawa
wachache,” Mwaja akamwambia Amata. Hata kama alikuwa na
haraka, alisahau, akaliendea kochi lililokuwa katika moja ya kona za
ofisi hiyo na kuketi. Mwaja akafanya haraka kuhudumia wachache
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

waliokuja hapo na alipowamaliza akamkaribisha tena Amata pale


dawatini huku akimwamuru msaidizi wake awape taarifa wengine
ya kusubiri. Mlango ukarudishiwa.
“Mbona wafunga mlango vipi? Unaniogopesha!” akamtania.
“Usiogope bwana, tangu lini kamanda akaogopa?” Mwaja
akamtania huku akipita mbele yake. Amata Ric akahisi kiu cha
dharura. Macho yake yakamsanifisha binti huyo. Sketi ya kijani
aliyoivaa ilimtengeneza umbo lake kadiri Mungu alivyomuumba.
Mtikisiko wa maeneo ya nyuma kila alipopiga hatua ulimfanya
kijana huyu apoteze umakini wa kazi yake, hata alisahau kwa
sekunde chache kuwa ni nini kimemleta.
“Swadakta!” akajikuta karopoka.
Mwaja akageuka kumtazama, akatoa tabasamu lake la akiba,
“ndiyo nini?” akauliza.
Namtukuza Muumba kwa kazi yake. Kuna wanaume
wamejaliwa kumiliki vitu hadimu ambavyo si rahisi kuvipata na
vimeshatoweka kwenye uso wan chi,” Amata akamsifia. TSA 1
alijua vyema kucheza na viumbe hawa, maneno yake yalikuwa na
shabaha aliyoikusudia.
“Yaani wewe, wanavyoviandika ni kweli kabisa,” Mwaja
akasema, “enhe, shida yako Tafadhali…” akaanzaisha
mazungumzo.
“Mbona mmefunga vitambaa vyeusi vipi mna msiba?” Amata
akauliza swali tofauti na shida yake.
“Yaani mwanausalama hujui kinachoendelea?”
“Sijui!”
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Tuna msiba, Jenerali Mwambope amefariki…”


“Oh poleni sana!” akampolesha, “sasa kilichonileta hapa ni
kuomba taarifa za mstaafu wenu anayejulikana kama Kepteni
Hasheem Faraj,” akaeleza shida yake.
“Hasheem Faraj…?”
“Ndiyo,”
Mwaja akavuta kitabu chake kikubwa akachakurachakura
kurasa na kurasa akiwa kimya wakati Amata akipitia gazeti hili na
lile. Hakumwongelesha chochote, alitaka afanye kazi hiyo kwa
umakini. Dakika sita baadae, Mwaja alivunja ukimya kwa kutoa
taarifa aliyotakiwa aitafute.
“Kepteni Hasheem Faraj!” akatamka jina hilo. Amata akainua
uso kumtzama mwanadada huyo.
“Umelipata?”
“Ndiyo,” akajibu na kujikohoza kidogo, “alistahafu mwaka
1999 akiwa kepteni wa jeshi katika kikosi cha anga Ngerengere.
Alikuwa mbobezi katika maswala ya mawasiliano anga, nan i injinia
mahiri wa ndege vita na mifumo yake. Jalada lake linamwelezea
kama mtu hatari sana katika Nyanja hiyo…” Mwaja akatoa
maelezo ya kutosha ambayo yeye bila kujua alikuwa akirekodiwa na
kibanio cha tai ya Kamanda Amata. “Masomo yake amechukulia
wapi na wapi?” akamtupia swali.
“Aaaaa, kwenye jumuia ya Kisovieti, Uchina na kwa miezi
michache amepitia kozi maalumu pale US Airforce,” Mwaja
akamjibu Amata huku akifunga lile kabrasha na kulirudisha mahali
pake.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Na baada ya kustahafu akaenda wapi?”


“Aaaaa kamanda hilo swali gumu sana. Mtu akishastahafu
jeshini akishatoka hapo nje ya geti basi atufatili tena maisha yake
ilimradi tu tunajua yupo hai. Tutakapokuwa na shida naye ndo
tutamtafuta…” akajibu.
“Fununu je?”
“Labda kwao Zanzibar, maana kwenye kumbukumbu hiyo
inasema hivyo. Unamhitaji?” akajibu na kuuliza.
“Ndiyo, nina shida naye ya maana sana,”
“Nitaulizia, halafu nitakwambia,” Mwaja akajibu huku
akisimama kama ishara ya kuagana na mgeni wake. Amata naye
akainuka kutoka pale kochini.
“Asante mrembo nashukuru. Kazi uliyonifanyia ni kubwa,
naweza kukununulia pepsi baadae?”
“Umeanza Amata, hivi watu wa kada yenu mtaacha vipi hiyo
mambo?”
“Mambo gani?”
“Si hayo unayoniitia…”
“Mwaja, pepsi tu… au umewaza vingine…”
“Mmmm pepsi itakuwa pepsi hapo. Haya nitafute kuanzi saa
kumi na moja jioni kabla sijarudi kwa mwanaume mwenzio,”
Mwaja akasema. Amata akahisi kama mapigo ya moyo yameruka
kidogo kusikia ‘mwanaume mwenzio’.
Wakabadilishana namba za simu na Amata akaondoka zake.
Akiwa ndani ya gari lake mawazo lukuki yakakisonga kichwa chake,

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

afanyeje. Akawasha gari na kutia gia akaondoka zake kurudi mjini.


Aliendesha gari kwa kasi huku akiyapita mengine kwa fujo. Saa
katika gari lake ilionesha kuwa saa sita na dakika arobaini na tano.
Akawasili jirani kabisa na ofisi ndogo na kuteremka. Hakuingia
ofisini, moja kwa moja aliingia katika mgahawa wa jengo la hazina
na kuketi hapo. Akaagiza chakula na kuendelea kuzungusha
mawazo yake ya jinsi gani atatua kitendawili hicho. Akiwa
chakulani hapo. Simu yake ikaita, akaitazama na kuiona nmba ya
bosi wake.
Nini tena? Akajiuliza na kuinyanyua.
“Yes Mom!” akapokea.
“Kuna taarifa ya msiba, umeipata?”
“Hapana,”
“Jenerali Mwambope amefariki, inasemekana ameuawa nyumbani
kwake… fika ofisini kwa mazungumzo Zaidi,” ile simu ikakatika.
Amata akaitia mfukoni na kuendelea kula chakula chake. Madam S
kumpatia taarifa hiyo ilikuwa ni sehemu tu ya kutimiza wajibu wa
kiofisi, si kwamba walikuwa hawajui. Kamanda Amata akamaliza
chakula chake na kulipia. Akashika njia kwa kuvuka barabara mbili
tu mpaka Ofisi Ndogo iliyo jirani na jengo hilo.
* * *
Madam S alikuwa kimya kitini kwake. Akamkaribisha Amata,
naye akakrti katika kiti anachotakiwa kuketi.
“Karibu!”
“Asante,”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Enhe nipe taarifa, umefikia wapi katika ufukununu wako?”


Madam akauliza.
“Jana nilikupa ile karatasi…”
“Yenye jina la Hasheem?”
“Ndiyo,”
“Enhe!”
“NImepata taarifa zake kutoka makao makuu ya jeshi lakini
jambo moja nimekwama na ndiyo nafikiri sasa nianzie wapi…”
“Lini?”
“Leo! Huyu bwana amestahafu mwaka tisini na tisa,” Amata
akaeleza na kumuwekea ile rekodi ya sauti. Madam S akasikiliza
kwa makini, na ilipoisha akashusha pumzi na kujiegemeza kitini.
“Safi, sasa nini kinafuata?” akauliza.
“P.o.R…”
“Yes!”
“inabidi nijue wapi anaishi kwa sasa nikamtembelee na kwa
nini ameitwa hivyo na Mwambope,” Amata akaeleza.
“Sawa, kwa vyovyote huyu atakuwa ndiye funguo yetu kwa
sasa,” Madam S akamuunga mkono. Ukimya ukatawala kwa nukta
kadhaa kati ya wawili hao. Amata akavuta gazeti lililokuwa mezani
pale na kulisoma vichwa vya habari. Habari ya kifo cha
Mwambope ilikuwa ukurasa wa juu kabisa. Amata akavutiwa nayo
na kuanza kuisoma nenio kwa neno, sentensi kwa sentensi mapaka
akaimaliza. Kisha akalitua mezani.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Ina maana hawajui kama kauawa au ndo kuficha mambo?”


akauliza.
“Siwezi kukujibu, si unajua tena mambo ya usalama,” Madam
S akajibu na kuendelea kupitia kabrasha lililokuwa juu ya meza
yake pasi na kumwangalia kijana wake. Kamanda Amata
akachukua ile simu aliyoipata kwa Mwambope na kuanza kuiperuzi
kwa utulivu. Arafa za nyuma sana, akajaribu kuzioanisha na tukio
analolifanyia kazi. Bila kutegemea arafa moja kati ya nyingi
ikamshtua kidogo.
Una tenda mbili kubwa za kufanya,
Dar es salaam Makongo Juu,
Zanzibar Jitini plot 203Z.
Amata akainuka kitini na kubaki wima.
“Vipi?” Madam akamuuliza.
“Naomba kwenda, maana naona muda kwangu si rafiki,”
akajibu.
“Sawa kwa lolote unijuze…” akamwambia. Amata akauendea
mlango tayari kwa kuiacha ofisi hiyo. “Amata!” sauti ikaita nyuma
yake. Akasimama pasi na kugeuka. “MI pia wapo kazini, hivyo we
fanya kwa ajili ya baba yako, sawa?”
“Sawa!” akajibu na kuondoka zake.
* * *
Huko Ramban, vijana wa Faizar walipata fununu ya wapi
mwanamke wanayemtafuta yupo. Wakaingia katika mji huo na
kuhakikisha wameweka mtego kila kona muhimu ambayo wanahisi

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

mtu huyo atafika tu. Faizar mwenyewe na kijana mwingine mmoja


waliifikia hoteli ile ya Lords Inn Jammu. Moja kwa moja walifika
katika dawati la mapokezi na kutoa shida yao.
“Ndiyo, mgeni huyo yupo katika hoteli hii, ila ametoka kama
masaa mawili yaliyopita…” wakajibiwa na mhudumu wa ofisi hiyo.
Faizar aliyejitambulisha kuwa yeye ni askari akatakiwa kumsubiri
mgeni huyo. Akakubali lakini kazi hiyo akamwachia kijana wake
nay eye kuendelea kupita hapa na pale ili kuona kama ataambulia
chochote.
Wakati hayo yote yakitokea, Jamila alikuwa njiani kuelekea
Islamabad. Aliamua kutumia usafiri wa lori la mizigo linalotoka
India kuelekea Pakistan. Ijapokuwa barabara ilikuwa na vizuizi
vingi lakini alivumilia ili mradi afike na kutimiza lengo lake. Mara
alipopata taarifa ile pale Lords Inn kuwa akitaka mawasiliano ya
uhakika afike kwenye jiji hilo aliamua kuondoka kimyakimya bila
kurudi pale. Alijuwa wazi kuwa kitendo cha kurudi pale na
kuchukua kitu chochote kingewafanya watu kujua kuwa amesafiri
lakini kwa jinsi tu alivyotoka kila mmoja alijua kuwa atarudi muda
wowote. Kijana wa Faizar aliketi kochini akisoma magazeti
kumsubiri Jamila ili amtie mkononi.
Wakati yote hayo yakiendelea, Jamila alikuwa katika lori la
mizigo kuelekea katika Jiji la Islamabad nchini Pakistan.
Haikumchukua muda kupata usafiri mara tu alipoiacha hoteli ile ya
Lords Inn. Baada ya kuuliza hapa na pale akaelekezwa wapi
anaweza kupata usafiri wa lori kuelekea huko Pakistan. Hakupenda
kutumia mabasi ya abiria kwa kuwa alijuwa wazi hakutakuwa na
usalama kwake kwani hakuwa na kibali chochote cha kuishi katika
nchi hiyo.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Dreva kijana, mara tu alipoombwa msaada huo hakusita


kuutoa. Macho ya Jamila yalimnyong’onyesha na kuamua kuvunja
amri iliyowekwa na serikali ya India ya kutokupakia abiria katika
lori.
“Lakini safari yetu ni ndefu, itatuchukua saa ishirini nan ne
kufika katika jiji hilo. Vilevile, lolote laweza kutokea njiani, kama
kuvamiwa, kukamatwa na askari au wanamgambo wa Mujahideen,
upo tayari? Maana wewe ni mwanamke nisije nikaponzeka…” yule
kijana akampa risala Jamila huku moyoni mwake akiwa na mengine
kabisa. Alihesabu kaokota dodo chini ya mpera kwa kuwa katika
nchi hiyo huwezi kukuta mwanamke anatumia usafiri kama huo.
“Shaka ondoa, ninachotaka mimi ni kufika Islamabad…”
Jamila akajieleza huku akiketi katika kiti cha upande wa pili wa yule
dereva. Volvo, likawashwa injini, ikaunguruma. Taratibu yule kijana
akaliingiaza barabarani na kuondoka. Ilikuwa saa nane ya mchana
walipouacha mji wa Ramban. Mazungumzo ya kawaida yalichukua
nafasi katika safari hiyo huku yule dereva akiendelea kumung’unya
tambuu zake kinywani.
“Leo ajabu sana hatujakutana na askari njiani…” yule dereva
akasema.
“Lakini safari haijaisha…”
“Ndiyo, hapa tunakaribia kizuizi kimoja cha kuingia katika jiji
hilo, tuombe Mungu tupite maana ni pagumu,” akaeleza.
“Usijali tutapita,” Jamila akampa moyo.
Baada ya mwendo wa takribani saa moja hivi tangu
wazungumze jambo lile, wakafika katika kitongoji cha Jangul.
Jangul ni kijiji kidogo tu, kilomita hamsini kabla hujafika ndani ya
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

jiji la Islamabad. Hapa palikuwa na kizuizi cha wanajeshi. Magari


yote yalisimamishwa na kufanyiwa ukaguzi wa kina.
“Sasa mi nashuka, utanikuta kule mbele!” Jamila akamwambia
yule dereva.
“Usithubutu, hili eneo hatari sana, ukikamatika huko
wanakupiga risasi wanakuua… hawana huruma hata kidogo,” yule
dereva akamsihi Jamila abaki kwenye gari, kitendo ambacho
mwanamke huyo hakukubaliana nacho moyoni mwake. Alijuwa
wazi kuwa endapo atagunduliwa kuwa hana vibali, basi ingekuwa ni
kosa kubwa sana na hasilani asingeweza kutimiza azma yake. Lile
lori likaimamishwa, na yule dereva akatii. Askari wawili wenye
bunduki hatarishi waliova kombati za khaki wakasogelea gari hilo
wakiwa na kurunzi zao mikononi. Jamila alimtazama yule dereva
kwa chati, akamwona jinsi anavyochachawa pale kitini, akiingia
mkono katika mfuko huu na mara ule kule.
Mmoja wa wale askari, akamulika tochi ndani ya ile kibini na
kumuona Jamila.
“Huyu ni nani?” akamuuliza yule kijana. Badala ya kujibu
akaanza kubabaika. Huyu hakuwa mtundu kama yule dereva wa
kwanza aliyemchukua Jamila kutoka Nawal mpaka Ramban,
aliyewaambia polisi kuwa yeye mkewe. Wale askari wote wakawa
upande ule wa dereva na kumtaka ateremke chini. Jamila akaona
wazi kuwa hapo mambo yameshaharibika. Wakamchukua kuelekea
kwenye ofisi yao huku wakikusanya dokumenti zote na kumwacha
Jamila ndani, kosa.
Hapa si pa kubaki, lazima watanirudia tu! Akawaza. Alipowaona
wakiingia ndani ya ile ofisi, akateremka taratibu na kuikanyaga

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

ardhi ya Jangul yenye vumbi mithiri ya saruji. Akasimama wima na


kuurudishia ule mlango taratibu bila kufanya kelele. Katika kizuizi
hicho kulikuwa na magari mengine mengi, malori, mabasi na gari
ndogo. Watu walikuwa wamezagaa huku na huko na askari nao
walikuwa wametanda kila kona. Akaangaza huku na kule kuangalia
ni vipi anaweza kuvuka salama eneo lile na kutangulia mbele.
Jamila aliyapita makundi ya watu na kujifanya anaelekea uwani.
Hakuwa anajua nini kimeandikwa kwenye maelekezo mbalimbali
wala hakuwa anajua nini wanaongea watu anaowapita.
Kilichomfanya ajue kuwa huko ni maliwato nia alama za picha tu.
Akavuta hatua na kuzunguka nyuma ya choo kile. Akatazama huku
na kule, watu wote walikuwa upande wa pili alikotoka. Mwendo
kama wa mita thelathini hivi kulikuwa na miti mirefu na vichaka
vya hapa na pale. Jamila akatazama lile eneo kwa makini sana, kitu
kilichomshtua ni kwa nini eneo hilo liachwe wazi na msitu uanzie
umbali huo.
Huchelewi kukanyaga mabomu humu! Akajiwazia hukua kitazama
kwa makini lile eneo na ule mchanga. Akajitoa mhanga na
kutembea haraka haraka kufuata vile vichaka. Moyo wake ulikuwa
ukidunda ovyovyo, alitembea kwa uangalifu akitazama chini kama
kuna hatari yoyote. Jamila akafanikiwa kuingia kwenye vile vichaka,
akatulia kwanza kuyasoma mazingira. Macho yake yalipozoe hali ile
ya udutu wa giza, akaanza kunyanyua nyayo zake na kuelekea
upande wa mbele kwa makini sana. Akilini mwake aliuwa wazi uwa
kosa moja tu litamgharimu maisha yake.
Akavuta hatua fupifupi huku akili na hisia zake zote
akizielekeza chini kwenye miti midogo na nyasi fupi. Kila alipohisi
kama kamba imeugusa mguu wake, alisimama na kutazama kwa

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

makini kuhakiki ni kitu gani. Kutokana na uanajeshi wake, alijua


fika uwa wakati mwingine maeneo kama hayo hutegwa mabomu ya
ardhini. Jamila aliijua Pakistan, aliisikia Kashmir, alijua uhasama na
mapigano yaliyoigubika nchi hiyo. Kwa sababu alijua wazi kuwepo
mabomu ardhini si sadfa bali ni makusudi mazima.
Akaendelea kuvuta hatua kuuvuka msitu ule. Akiwa katika
harakati hizo, Jamila alihisi kama kakanyaga kitu kama mdomo wa
chupa. Akasimama na kutulia tuli, kwa jozi la sekunde.
Nimekwisha! Akawaza. Mguu wake ulikuwa ukitetemeka
huku jasho la ghafla likimtirirka kuanzia utosini kwenda unyayoni.
Akainama tarataibu na kuangalia nini alichokikanyaga. Loh! Macho
yalimtoka. Hakuwa mbali na hisia yake, bomu. Mguu wake wa
kuume ulikuwa juu ya kifuniko cha bomu ambacho hushikiliwa na
pini maalumu. Bomu lle lilikuwa limechimbiwa ardhini kwa ustadi
wa hali ya juu sana. Akageuzageuza macho yake ili kutazama vizuri,
ndipo akaona waya mwembamba ukiwa umening’iniwa na pini ile
ya kulinda usalama wa bomu hilo. Akabaki katoa macho.
Mwisho wangu utakuwa wa kizembe sana! Akawaza huku
akiyakumbuka maneno yay u;e dereva. Hakika, asiyesiki la mguu,
huvunjika guu.
* * *
Katika ofisi ya shirika la simu la DarCom, Amata alimshukuru
mwanadada aliyekuwa akimsaidia kusikiliza baadahi ya simu kutoka
katika ile simu aliyoiokota nyumbani kwa Mwambope. Alipoliacha
tu lile jengo, akaifutika ile simu kwenye mfuko wake wa koti na
kuliendea gari lake aliloliegesha nje tu ya ofisi zile. Akaketi huku
akiwa na uso uliosawajika kwa kile alichokipata kwenye simu ile.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Zanzibar haraka sana kabla mambo hayajaharibika”


akajiseme huku akiwasha gari kana kwamba ni hilo ndilo
litakalomfikisha huko atakako. Akachukua simu iliyokuwa ndani ya
gari hilo na kubofya namba kadhaa kisha akaiweka sikioni.
“Ndiyo Kamanda!” upande wa pili ukamjibu.
“Nahitaji usafiri wa boti inayoondoka sasa kuelekea
Zanzibar,” akamwambia.
“Dakika moja Tafadhali,” ni Gina aliyepokea simu ile kutoka
AGI Investment. Dakika moja na sekunde kadhaa ukaja na majibu
chanya. Tiketi ya kwenda Zanzibar kwa boti ya Azam ilipatikana,
tena ile ya daraja la kwanza. Kamanda Amata akasoma ujumbe ule
kwenye simu kisha akabofya namba ile ya awali na kuiweka tena
sikioni.
“Naomba niletete mwanangu hapa bandarini,” akamwambia
Gina ambaye tayari alikwishaelewa nini maana ya sentensi hiyo.
Nusu saa baadae Gina na Amata walikutana katika bandari ya
Zanzibar.
“Urudi salama mpenzi!” Gina alimwambia akiwa
kamkumbati.
“Usijali!”
Mara tu walipoachana Kamanda Amata akaongoza njia
kuelekea gatini tayari kuabiri boti hiyo kwa safari yake ya dharula.
Kabla hajalifikia gati ile, simu yake ikaita, akaichukua na kutazama
kioo, ‘Madam S’. akaifyatua kwa kubonya kitufe cha kijani kiasha
akaiweka sikioni.
“Wapi?” akaulizwa.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Zenji,”
“Kunanukia?”
“Kabisa, ngoja nikamtembelee mjomba…moyo wangu
hautaki kutulia kabisa,” Amata akajibu.
“Sawa mara ufikapo usisite kunijuza hali yake,” simu ile
ikakatika wakati akikaa katika kiti safi cha boti. Akaitazama saa
yake, ilikuwa yapata saa kumi na nusu jioni wakati kile chombo
kilipokuwa kikiliacha gati la Dar es salaam kuelekea visiwa vya
karafuu, Zanzibar. Alifumba macho kwa sekunde kadhaa na
kujiuliza maswai ambayo alihitaji mtu asiyemjua kuyajibu. Baada ya
kuoanisha majibu ya kule alikotembelea kwa Mwaja, kisha ofisi za
Tume ya Uchaguzi na kampuni ile ya simu, Amata aliweka taarifa
pamoja na kujikuta akiitwa katika visiwa hivyo. Kwamba jibu la
kitendawili lipo huko. Akaendelea kubaki kimya akitafakari wapi pa
kuanzia pindi awapo katika kisiwa hicho. Kumekucha
* * * *

Saa Kumi na mbili jioni, Kamanda Amata alishuka kutoka ile


boti na kuingia katikakisiwa hicho. Kisiwa cha kitalii kilichobeba
historia adhimu ya utumwa. Alikuwa na kazi moja tu kubwa
iliyomkabili, na aliidhamiria kuifanya pasi na kupoteza muda.

Nahitaji kufika Jitini! Akajisemea kwa sauti ya moyoni. Amata


akakatisha Barabara iliyo mbele ya lango kuu la bandari hiyo na
kuwaendea madereva taksi walioegesha magari yao katika ng’ambo
hiyo. Kijana huyu hakupenda kutumia taksi anayoitiwa, daima
huchagua mwenyewe ile anayoitaka.
“Nifikishe Mercury Bar,” akamwambia dereva kijana
aliyevalia balaghashia yake upande.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Elfu mbili na mia tano tu…” yule dereva akamwambia mteja


wake huku akiwasha gari tayari kwa safari.
“Usihofu kuhusu pesa, fanya nilivyokwambia,” akamwambia
na yule kijana akaondosha gari na kushika Barabara ya Mizingani.
“Mwasemaje Bara huko?” yule dereva mcheshi akauvunja
ukimya.
“Huko tupo tu, jua kali kwelikweli mpaka mifukoni,” Amata
akajibu na kuingiza utani kidogo, “sijui wenzetu huku visiwani
mwatunyima nini!”
“Huku visa tu haviishi, watu kutekwa wengine kuuawa
basi…” akamjibu.
“Na huku kuna ‘wasiojulikana’?”
“Watakosekana tena! Wamemteka dada wa watu asubuhi tu
akiwa anaenda kazini,” akaeleza huku akiendelea kuendesha gari
lake kwa mwendo wa wastani.
“Aisee! Kisa nini?”
“Najua kaka yangu! Nasikia tu kuwa yule binti anafanya kazi
hapo uwanja wa ndege na ni mtoto wa mwanajeshi mstahafu…
sasa sijui bwana wanakitaka kitu gani hao…” akasema. Yule kijana
akaegesha gari lake nje ya baa hiyo.
“Hapa ndiyo Mercury Baa, karibu sana Zanzibar na usikose
kutembelea Foro' mida ya saa mbili usiku hivi,”
“Kuna nini?” Amata akauliza.
“Pale utapata urojo na vyakula vingi vya kizanzibari bila
kukosa warembo bwede’…”
Amata akacheka na kuufunga mlango wa gari huku mkononi
tayari akiwa na hela ya kumlipa kijana huyo.
“Mbona wanipa nyingi?”
“Saa mbili usiku uje kunichukua hapa hapa!” Amata
akamwambia huku akiondoka na kupotelea ndani ya baa hiyo na
kumwacha yule dereva akimsindikiza kwa macho.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Baa ya Mercury haikuwa mbali na Barabara hiyo. Ni mita


chache tu zinazohesabika hata na mototo wa chekechea anayeweza
kuhesabu mpaka mia. Baa hii ilichukua jina la mwanamuziki
maarufu Fredy Mercury mwenye asili ya mchanganyiko wa
Waparsia wa uhindi aliyezaliwa Zanzibar kabla ya kuhamia
Uingereza na familia yake mara baada ya mapinduzi visiwani
humo. Huko alipata umaarufu kwa uimbaji wake katika bendi ya
muziki wa rock iliyojulikana kwa jina Queen.
Amata aliingia ndani ya baa hii na kuchagua meza mojawapo
iliyopo kwenye kona na kuketi. Hakukuwa na watu wengi bali
Wazungu wachache na Waafrika wa kuhesabika. Akavuta menu na
kutazama nini kilichopo. Ndani ya baa hii ambayo ni sawa na kuiita
mkahawa kulikuwa na nakshi za kupendeza. Picha mbalimbali za
mwanamuziki huyo ziliupamba ukutawe.
“Juisi na kacholi mbili,” akamwagiza mhudumu aliyekuja
mezani hapo huku yeye akipitisha macho kwenye gazeti la
Zanzibar Jioni. Katika gazeti hill ndipo alipokutana na habari ile
aliyodokezewa na Yule dereva taksi kwa kina. Habari iliyohusu
mwanamke aliyetekwa asubuhi ya Siku hiyo. Jicho la Amata
likagota kwenye picha hiyo. Akaitazama kwa umakini mkubwa na
kujiuliza ni wapi kaona sura inayofanana na hiyo. Akili yake ilianza
kuchakata mambo.
“Karibu kaka, naona umezama kwenye habari hiyo,” yule
mhudumu alikwishafika na vile alivyoagizwa. Amata akagutuka na
kumtazama, akatabasamu.
“Ee, nashangaa hawa watu wanaomteka mrembo kama huyu
jamani, kweli haki?” Amataakamjibu yule Dada.
“Yaani hata sisi tunasikitika sana, alikuwa anapenda kuja
hapa…”Maneno hayo yakamshtua Amata, “unamjua?” akamuuliza.
“Si mimi tu, wote humu tunamjua,” akajibu huku akiwa tayari
kuondoka.
“Atapatikana tu, alikuwa akiishi wapi?”
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Mh sijui kwa kweli… ila kupatikana si rahisi… ”


Maelezo mafupi ya yule mhudumu yalitosha kumpa Amata
picha ya kuwa matukio hayo yana uhusiano. Kichwani mwake
alikuwa na maelekezo ya Jitini, kitalu namba 203Z. Alilisoma jina la
mateka huyo, Lukundame. Sasa akakumbuka sura hiyo ni wapi
ameiona. Kwa Jamila. Ukutani, kwenye kota za jeshi Airwing,
ambapo Jamila aliishi. Amata aliitazama picha yenye mtu huyu.
Ina maana Jamila, Lukundame na huyu Kepeni Hasheem mstahafu
wana uhusiano? Akajiuliza. Hapo akahisi damu inamchemka.
Akajaribu kuipima kazi iliyo mbele yake, na kuuona uzito.
Hasheem ana nini kwenye sakata hili? Na huyu Lukundame je? Amata
akajikuta anaanza kufanya kazi kichwani mwake ya kutafuta
mahusiano ya watu hao watatu.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

06
T.Mi.35, Bomu la kutegwa ardhini lilikuwa limekandamizwa
na mguu wa Jamila. Akiutoa tu basi mlipuko ungetokea na
kumsambaratisha vibaya. Hakulitaka hilo kwani safari ilikuwa bado.
Akiwa bado anatetemeka na jasho likimtoka, alishuhudia lile lori
alilokuja nalo likiendelea na safari. Akatamani alikimbilie lakini
kitendo hicho kingemgharimu uhai wake. Mchakacho wa miguu ya
kiumbe cha miguu miwili ulisikika nyuma yake.
“Tulia hapohapo! Ukijitikisa tu umekwisha kwa kuwa
ulichokikanyaga unakijua ndiyo maana hujakimbia,” sauti ya mtu
huyo ikamwambia. Ni kweli , alichokikanyaga alikijua na ndiyo
maana alitulia palepale. Askari mmoja akifuatiwa na wengine
watatu wenye bunduki nzitonzito mikononi mwao walifika eneo
hilo.
“Ulitaka kwenda wapi?” akauliza akiwa kasimama mbali
kwenye hivyo vichaka.
Kumbe walikuwa wananitafuta! Akawaza Jamila. Hakujibu
chochote.
“Tulia!” sauti nyingine, si ile ya kwanza, ikamwambia.
Mwanajeshi mmoja aliyevalia vazi maalumu akamkaribia Jamila na
kumtaka atulie ili aweze kumsaidia. Mwanamke huyo akatulia bila
kutikisika, ila mwili wote ulitota jasho, maana ilikuwa ni sawa na
kukutana uso kwa uso na Israeli mtoa roho.. Yule askari,
akautazama ule waya ulipoelekea, akaachana nao. Alijua kila kitu.
Akachukua kitu cha bapa, chembamba kama pasi ya mwashi.
Akakipachika taratibu kati ya unyayo wa Jamila na lile bomu.
Akakandamiza kwa nguvu na kumtaka mwanamke huyo kuutoa ule
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

mguu. Jamila akafanya hivyo. Yule mwanajeshi akalichukua kwa


usalama kabisa lile bomu na kulifunga tena kwa pini yake. Wale
wengine wakamchukua Jamila na kumtia pingu, kisha wakamtupa
selo baada ya kumtandika makofi mawili matatu.

* * * *

Ndani ya kile chumba cha mateso, Joel alikuwa na hali mbaya


sana baada ya kipigo kile. Bakari alikuwa katulia kimya, hajui cha
kufanya. Saa kadhaa zilikuwa zimepita, mlango ulipofunguliwà
tena. Bakari akagutuka kutoka katika lindi la mawazo.
Akawatazama waliongia, ni walewale askari isipokuwa sasa
hakuwapo yule mkubwa wao. Hawakuongea kitu, walimchukua
Joel na kuondoka naye kisha chumba kile kikafungwa. Bakari
akabaki peke yake.
Kepteni Joel akapelekwa kwenye chumba kingine. Chumba hiki
kilikuwa tofauti kabisa na kile. Hiki kilikuwa safi kabisa, kizuri,
chenye viti kadhaa vilivyokaliwa na watu walioonekana‘vibopa’.
Yeye akapelekwa moja kwa moja kwenye kiti maalum cha chuma
lakini ukikitazama ni kama kile kinachotumika kwa waganga wa
meno. Akakalishwa hapo na kufungwa vizuri kabisa mikono na
miguu yake. Kiti kile kilitisha, kilikuwa na mitambo ya ajabuajabu
pembeni mwake. Akavalishwa kitu kama kofia ya chuma, nayo
ikafungwa kwa mkanda maalum. Upande aliofungwa Joel aliweza
kuwaona wote waliokuwa katika chumba hicho kikubwa na kizuri.
Aliwahesabu, walikuwa watatu walioketi na kenda waliosimama.
Kwa uharaka alimtambua mmoja wao, aliyeketi katika kiti cha
katikati. Tajiri, Al Mansoor. Pembeni yake, yaani kushoto na kulia
waliketi watu wawili tofauti; Fernandez na upande mwingine
Jenerali Kahir, msuka mipango wa siri wa kundi la Hizbul
Mujahedeen. Wengine waliosimama walikuwa ni walinzi watiifu wa
watu hao. Jenerali Kahir na Fernandez wote walikuwa wateja
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

wanaotaka kununua ule mfumo uliokuwa umefungwa kwenye ile


ndege. Ambao Mansoor na vijana wake walikwishauondoa kwenye
gofu la ndege ile na kuuchukua katika sanduku lake maalumu, Pegan
Box.

Mansoor akainuka na kuwatazama hao wageni wake, “kama


nilivyowaeleza. Kila kitu kinaendelea vyema… huyu mnayemwona
mbele yenu ndiye code mamba moja ya kufanya mfumo huo ufanye
kazi. Hatuna budi kumfanya aiseme code hiyo… maana cha
muhimu hapa si yeye bali hiyo code…” akaeleza.
“Hawa wapo watatu na kila mmoja ana code yake na
zinavyofanya kazi ni lazima wote watatu watimie,” akaeleza.
“Huyo wa tatu yupo wapi na tutampataje?” Kahir akauliza.
Kuuliza kule hakukuwa kwa heri, Kahir alitaka kujua kile kidogo
ambacho Mansoor anafanya katika kumtafuta huyo mtu wa tatu ili
ikiwezekana naye na vijana wake waingie kazini. Kahir alijua wazi
kuwa kumpata mtu huyo wa tatu ingekuwa turufu ya kuupata
mfumo ule kirahisi. Hiyo watoto wa zamani tuliita ‘mkono kwa
mkono’.
“Bado tunamtafuta, lakini ndani ya masaa arobaini na nane
atakuwa hapa na tutakuwa tumeshaiapata hiyo code ya tatu,”
akamjibu. Mansoor akatoa ishara kwa kijana wake mmoja kuwa
awashe ile machine. Sekunde tatu baadae, umeme mkali ukapita
kwenye vile vyuma vya kile kiti. Shoku mbaya ikampiga Joel.
Akauma meno na kutokwa macho. Maumivu makali yalisambaa
mwilini mwake. Sekunde kumi na tano za shoku ile iliyoambatana
na maumivu yale, ilimfanya Joel ajikute akili ikimhama akaanza
kupiga kelele na kuwataja majina wenzi wake yaani Bakari na
Jamila.
“Taja code yako ya siri,” Mansoor akamwambia. Uoni wa Joel
ukaanza kuwa hafifu, nguvu ya akili yake ikaanza kupoteza
muelekeo. Mansoor akampa ishara kijana wake aongeze volteji ya
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

mashine ile. Ikawa hivyo. Joel alihisi kama kuna nyundo ikimgonga
kichwani kwa nguvu sana. Akapiga kelele ili imsaidie kuendelea
kutunza kumbukumbu yake, ikawa ngumu.
“Taja!”
“…X-…”
“Endeleaaaa mpumbavu wewe utakufaaa…” Mansoor alipiga
kelele.
“… 2bPG_”
“Malizia…”
“… **Tz” Joel aliropoka code yote bila kujijua. Akili haikuwa
yake tena. Umeme ukazimwa. Joel akatulia kimya akiwa hana
fahamu. Mwili ulimlegea na kukosa nguvu kabisa. Mansoor
akaiendea meza moja iliyokuwa kando. Juu ya meza huyo kulikuwa
na sanduku jeusi. Akalifungua. Ndani yake palikuwa na kompyuta
kubwa, imara, iliyotengenezwa na kufungwa ndani ya sanduku hilo.
Akaiwasha. Ikawaka. Pale kwenye kioo pakatokea picha ya Joel na
kumdai aweke hiyo code kama nywila. Akaiandika na kubonyeza
batani iliyosomeka ‘ENTER’. Kompyuta ile ikafunguka. Sehemu
ya pili ikamtaka kuweka kiganja cha mkono wa kuume. Mansoor
akaitazama, kisha akageuka kumtazama Joel, yupo kimya.
Akamwamuru kijana wake aibebe ile kompyuta mpaka pale na
kuweka kiganja cha Joel. Ikamkaribisha na kufunguka. Upande wa
kulia wa kioo cha ile kompyuta kukatokea maandishi yaliyosomeka
‘Two more authorised codes needed'. Akairudisha mezani na
kuiweka.
“Bado codes mbili…” akawaambia wageni wake. Nao
wakainuka na kwenda kutazama. Wakaridhika na wanachokiona.
“Sasa bado kidogo tu biashara yetu itafanyika” akawaambia.
“Mimi niko tayari, hata advance nitaacha leo,” Fernandez
akasema. Mabishano makali kati ya Fernandez na Jenerali Kahir
yakataradadi wakati Mansoor akiwaangalia na kutazama tu..

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Mhmh! Pesa inaongea…” Mansoor akawaambia. Wanunuzi


wale wakaanza kushindana kifedha. Huku na huku, huku na kule,
Fernandez akaibuka mshindi. Kahir na kundi lake wakajikuta
hawana pesa ya kushindana na tajiri huyo Mvenezuela. Hasira,
uchungu na inda vikamjaa Kahir. Nsyongo ikamchafuka, damu
ikamnukia. Jenerali Kahir akainuka na kuondoka bila kuaga, vijana
wake wakamfuata. Mansoor akatabasamu, “mwenye kisu kikali
atakula nyama”.
“Vipi mbona mgeni wako anaondoka bila kuaga?” Fernandez
akauliza. Mansoor hakujibu, badala yake akaliendea dirisha kubwa
na kuchungulia kile kinachotolea nje. Jenerali Kahir na vijana wake
wakaingia garini na kutokomea. Mansoor akarudi kwa Fernandez,
“ndiyo shida ya wasio na hela… umeshindwa kupanda dau, sasa
hasira ya nini… waache wenye pesa wapate mambo mazuri
wayatakayo…” Mansoor akamwambia Fernandez.
“Pindi utakapokamilisha mambo yote, nitakuja kuchukua
mzigo wangu…”
“Ulisema unatanguliza advance... Sivyo?” Mansoor
alikumbusha.
“Ndivyo,” Fernandez akamjibu Mansoor kisha akamwagiza
msaidizi wake alete mkoba wake ambao ndani yake kuna kompyuta
ndogo. Akaitoa na kufanya muamala kutoka kwenye akaunti yake
kuelekea ile ya Mansoor.
“Safi sana, hata akija mnunuzi mwingine, wewe utakuwa
umeshajiwekea kete shimoni,” Mansoor akampamba Fernandes.

* * * *

Kamanda Amata akainuka kutoka pale alipoketi. Pesa ya


malipo ya kile alichokula akaiacha pale mezani. Akili yake yote sasa
ilikuwa ni kazi. Akaipapasa bastola yake na kuikuta imetulia kama
alivyoiweka, Berreta Pico. Akatazama saa yake, ikamwonesha ni saa
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

mbili kasoro dakika chache. Akatoka nje ya baa ile bila kumuaga
yeyote. Pindi tu alipofika nje na lile taksi likawasili.
“Unaona! Mi mzungu braza!…” yule kijana akamwambia
Amata wakati akiingia katika taksi hilo, “nikupeleke wapi?”

“Jitini,” Amata akajibu.


“Kuna Jitini mbili hapa kaka…” yule dereva akamwambia
Amata.
“Acha hii ya hapa nyuma…”
“Aaaaa ile ya kuleee barabara ya Kiembe samaki/”
“Ndiyo. Fanya fasta Nina miadi na mtu, ukinishusha tu
uniache uje kesho kunichukua,” Amata akatoa maelekezo. Yule
kijana akaingiza gari barabarani na kuondoka zake.
Dakika kama ishirini hivi, akawasili eneo hilo, “umefika”
akamwambia Amata.
“Asante…” Amata akateremka na kuagana na kijana huyo.
Alipohakikisha lile taksi limepotea akaanza kazi ya kutafuta
nyumba yenye ile namba. Ijapokuwa nyumba zilikuwa nyingi sana,
Amata alifanikiwa kuipata. Akaisaili kwanza kuona kama ina ulinzi
wowote au vipi. Nyumba ile ilijengwa katikati na kuzungukwa na
ukuta mkubwa ambao uliungana na nyumba nyingine za huku na
huko. Lango kubwa la chuma lilikuwa mbele, kufuli lenye nguvu
lilikuwa likining’inia. Amata akalisogelea na kusimama mkabala na
lango hilo. Àina ya lile kufuli hakuwa na funguo ya kulifungua.
Lazima niruke huu ukuta! Akawaza huku akijiweka tayari kwa
zoezi hilo. Akatazama upande huu na ule, hakuna anayemwangalia.
Akahesabu kimoyomoyo moja mpaka tatu. Ni sekunde tatu tu
zilimtosha kuukwea na kutua ndani bila kishindo. Ilikuwa inahitaji
mafunzo maalumu kufanikisha kitendo hicho pasi na kishindo cha
kuwashtua wengine. Ilikuwa nyumba kubwa yenye ghorofa moja.
Akaizunguka na kuichunguza kwa nje. Mbele yà nyumba hiyo,
upande wa lile lango kulikuwa na Maua mengi ya aina mbalimbali.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Amata akaachana na upande huo na kuzunguka ule mwingine.


Zaidi ya mabanda ya sungura hakukuwa na kitu kingine. Nyumba
hiyo ilionesha dalili zote za kukaliwa na watu kwa jinsi ilivyokuwa
safi na mpangilio mzuri. Amata akacheza na mlango wa nyuma,
ukafunguka. Akisaidiwa na aina ya viatu alivyovaa, akaingia ndani
bila kufanya kelele na kuurudishia ule mlango taratibu. Hatua zake
zikamfikisha katika sebule kubwa. Sebule ilikuwa safi iliyopangwa
samani zake kwa mpangilio mujarab. Kwa kutumia krunzi yake
ndogo mfano wa kalamu, ambayo inaweza kumulika tu pale
palipokusudiwa, aliweza kuyaona yote hayo. Alipoinua kurunzi ile,
ukutani macho yake yalikutana na picha kubwa ya rangi. Picha ile
ilikuwa ya mwanaume, mwanajeshi aliyevalia suti maridadi ya jeshi
tukufu la Tanzania. Nyota tatu zilikuwa begani mwake, upande huu
na ule.
Kepteni Hasheem Faraj? Akajiukiza. Hakukuwa na wa kumjibu.
Amata akaendelea na upekuzi wake, chumba baada ya chumba.
Moja kati ya vyumba hivyo ilikuwa maktaba ndogo. Hapa ndipo
haswa palikuwa muhimu kwake. Kabrasha moja la zamani kutoka
katika saraka ya chini ya kabati la vitabu lilikuwa na historia ya
Hasheem kuanzia utoto wake, elimu, mpaka hapo alipofika.
Kabrasha lile lilikuwa na picha zilizosindikiza historia ile. Ndani ya
kabrasha lile licha yà kuwa na maelezo tu ya kumhusu Hasheem,
pia kulihifadhiwa mambo binafsi ambayo labda mwandishi
hakupenda yaonwe na mtu mwingine. Kama mali za zake, watoto
na wanawake aliowahi ama kulala nao kwa mapenzi ya muda au
kuzaa nao kabisa.
Amata akalikamata vizuri mkononi, aliona wazi kuwa
linamfaa sana. Akaendelea na ziara yake. Chumba cha mwisho
kuingia kilionekana wazi kuwa kinakaliwa na mwanamke. Meza ya
kujiremba iliyosheheni vipodozi mbalimbali na vito vya thamani
iliwekwa kwenye kona moja ya chmba hicho. Kitanda kikubwa
kilichotandikwa kwa ufundi kabisa. Amata alipepesa macho huku
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

na kule. Mkoba uilioning’inizwa katika moja ya ubavu wa kabati la


nguo ulimvutia. Akauendea na kutngua. Kilichofuatia ni kumwaga
kitandani vyote vilivyomo mkobani. Kitambulisho cha mkazi
kikamtambulisha mwenye picha kwa jina Lukundame Hasheem.
Amata akatikisa kichwa kukubali anachokisoma. Zaidi ya hapo
hakuona kingine. Akajiandaa kuliacha jumba hilo. Amata tayari
alianza kujenga picha, Lukundame na Hasheem, mt na baba yake.
Sawa.
Akiwa tayari kutoka na kuliacha jmba lile, kutoka nje akasikia
muungurumo wa gari likisimama mbele tu ya lango lile. Amata
akaghairisha zoezi lake, akaweka kabrasha sakafuni taratibu ili
kujiweka tayari kumpokea huyo anayeingia. Mlango wa mbele
ukafunguliwa. Alichokifanya Amata kabla watu wale hawajaingia,
ni kuiwahi swichi kuu akazima fyuzi zote na kuiacha moja tu ya taa
za nje.
“Jumba kubwa halina umeme ndani” sauti ya mmoja wao
aliyejaribu kuwasha taa ikasikika.
“Haina haja, cha muhimu ni kupata hilo faili,” mwingine
akajibu. Amata akawahesabu. Hawakuwa wengi, wawili tu.
Akamkadiria na dereva, watatu. Akawasubiri waingie. Wakaingia
wote. Kwa jinsi tu walivyoingia akajua hakuna chochote
wanachojua kuhusu sanaa hiyo. Akawafuata nyuma upànde ule
walioelekea. Akawatazama tu wakiingia chumba hiki na kile.
Mwisho wakaingia kwenye ile maktaba. Amata akaufikia ule
mlango na kuufunga kwa nje. Wale vijana wakaanza kujaribu
kuufungua wasiweze. Kilichobaki kilikuwa ni kutukana matusi yote
wanayoyajua wao. Amata akaenda nje mpaka kwenye ile gari.
Hakuuliza, alifungua mlango na kumkamata dereva. Kabla
hajafanya chochote akambamiza kwenyedashboard ya lile gari kama
mara tatu hivi. Yule jamaa akazimia. Simu yake kutoka katika
mfuko wa surali aliyovaa ikaanza kuita. Amata akaichukua na
kusoma jina. Ilikuwa namba tupu.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Hello,” akaipokea.
“Sasa mbona umetufungia mlango? We umekuwa mamluki?”
wakamlalamikia wakijua kuwa mwenzao ndiye aliyewafungia. Wale
vijana hawakuwa wamejiandaa. Amata alitua chini na kumtia
ngwala mmoja aliyedondoka vibaya na kujibamiza kichwa kwenye
meza ya mninga. Yule mwingine, akaona ajaribu bahati yake
kukimbia. Hakufanikiwa, Amata akamkama shati na kumrudisha
ndani. Akampiga kichwa kimoja kizito, akatulia. Kamanda Amata
akawapekua na kuchukua vichache vinavyomfaa. Akiwa katika
harakati hizo akasikia gari jingine likisimama kwa fujo huko nje.
Akafanya haraka,akatoka na kulichukua lile kabrasha. Akakimbilia
mlango wa uwani na kuukwea ukuta ule kwa ustadi wa ajabu.
Akajitupa nje. Hakutaka kabisa watu wengine wajue misheni yake.
Kamanda Amata alijikuta akitua juu ya maji machafu yanayotoka
kwenye nyumba za jirani na kufanya dimbwi kubwa. Kutokana na
lile giza, akajikuta tu keshatumbukia kwenye uchafu huo. Akatoa
tusi la nguoni na kujitahidi kujinasua. Kabrasha lake nalo lilikuwa
halitamaniki lakini hakuliacha.

* * * *

Katika mji wa Saddar, kabla hujafika Islamabad, gari lililobeba


wahalifu na kuwapeleka Gereza kuu LA Islamad likasimama. Bado
halikuwa limefikia makazi ya watu, mapori madogomadogo yenye
miti michache ndiyo vilivyofudikiza eneo hilo. Hakuna maelezo
yaliyotolewa na askari hao juu ya kwa nini wamesimama. Jamila na
wengine kama ishirini hivi walitulia kusubiri nini wataambiwa. Giza
totoro ndani ya lile bodi la gari liliwafanya watu hao wasionane
sawasawa. Ulikuwa usiku wa manane wakati lori hilo la jeshi aina ya
Bedford liliposimama. Mlango wa nyuma ukafunguliwa. Askari
wawili, ambao kwanza walisikika wakijadiliana jambo huko nje
waliingia na kuwasha kurunzi lenye mwanga mkali wa kuumiza
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

macho. Wakaanza kuongea kwa lugha ya kwao wakitoa amri.


Jamila alitulia kimya kwa kuwa hakuelewa hata ni kitu gani
kinazungumzwa.
Dakika iliyofuata, baada ya kuona utii kutoka kwa mahabusu
hao haupo, nguvu ikaanza kutumika. Askari mmoja alimshika
mkono mwanamama aliyekuwa jirani na mlango na kumvuta nje,
akambwaga chini. Askari aliyekuwa chini akamuokota na
kumkokota kwenye vichaka. Mwingine akafanywa hivyohivyo.
Kule chini kulikuwa na askari waliokuwa wakiwaokota wanawake
hao na kuingia nao vichakani. Yule askari mwenye kurunzi kazi
yake ilikuwa kumulika tu na kutoa amri, mwingine ni kuwakamata
na kuwarusha nje bila kujali usalama wao.

Katika mulikamulika hiyo akamwona Jamila, mwanamke


mweusi. Hakuweza Kumtambua kama ni mwanaume au
mwanamke. Akatoa amri, na yule askari mwingine akamwendea
Jamila na kumpapasa kifuani pake kwa nguvu. Sonyo kali
likamtoka mwanamke huyo. Alitamani amrarue lakini hakweza
kutokana na mazingira. Yule askari alipojua kuwa aliyemshika ni
mwanamke akamkamata vizuri na kumsukumia mlangoni. Pale
Jamila akajikwaa kwenye miguu ya watu wengine na kuanguka
sentimeta chache toka kwenye ule mlango wa nyuma wa lori.
Alipoangukia ndipo buti la jeshi la yule askari mwenye kurunzi
lilikanyaga. Yule askari akaongea kwa kumkalipia lakini Jamila
hakuelewa chochote.
Kutokea huko vichakani, Jamila alisikia kelele za vilio vya
wale wanawake. Hakuwa na la kujiuliza bali alielewa wazi kuwa
wale askari wanawatenza kwa nguvu wanawake hao. Jamila
akainuliwa na kusushwa nje. Yule askari mwenye kurunzi
akammulika usoni, akamwondoa kitambaa chake kilichoziba uso.
“Waoh! Mwanamke mweusi…” akatamka kwa lugha yao.
Bado Jamila alibaki hewani tu hakuelewa chochote. Akashikwa
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

mkono na yule askari, akamvutia upande wa mbele wa lile lori.


Kurunzi likazimwa, akaanza kutumia nguvu kumvua nguo.
Nabakwa! Jamila akahamaki moyoni. Akajitahidi kujidhibiti,
na alifanya hivyo makusudi. Yule askari akaona ugumu ule.
Akamwita mwenzake mwenye cheo cha chini amsaidie. Yule kijana
akaweka bunduki yake mgongoni na kuanza kazi aliyoagizwa na
bosi wake. Akaikamata nguo ya juu ya Jamila na kuanza kuirarua
kwa nguvu wakati yule bosi wake akishusha zipu ya suruali yake
tayari kwa kazi. Jamila hakukubali kirahisi.
Heri nife kuliko kubakwa! Akawaza. Sasa akaamua, lolote na
liwe. Akaachia kichwa kikali na kumtandika yule askari aliyekuwa
akimchania nguo yake. Yule askari akamwachia Jamila akayumba
kidogo na kutikisa kichwa chake. Bosi wake akatahamaki kwa
kitendo kile, hakuamini. Akasahau kama dhakari yake ilikuwa nje
kama mkuki. Uchu wa ngono. Jamila akamkamata yule askari na
kumpiga kabali maridadi. Akamtumia kama nguzo na kujifyatua
kwa nguvu. Teke lake likatua katikati ya mapaja ya yule bosi.
Akatoa yowe la uchungu huku mikono yake akiifumbata kwenye
dhakari yake. Yule askari aliyekuwa kwenye kabali ya Jamila
hakufurukuta, akalegea. Jamila akaichomoa bastola kwa askari huyo
huyo namkumtwanga yule bosi, kisha akamwacha na huyu
mwingine akianguka katika vumbi la barabara. Akammaliza kwa
risasi moja.
Nimeharibu hali ya hewa! Akawaza na kujitupa chini,
akabiringika na kuingia uvunguni kwa lile lori. Kule vichakani, ile
sherehe ya ngono zisizo na makubaliano ikakatika ghafla mara tu
baada ya mlio wa pili wa risasi. Wale askari wakaanza kujitokeza
kuona kuna nini. Jamila akawahesabu, walikuwa wanne. Kutoka
pale uvunguni akatumia mbinu zake za kijeshi kuweza
kuwasambaratisha. Risasi nne, Moja kwa kila mmoja. Wote
wakalala chini kwa utulivu. Jamila hakuwa na cha kusubiri, akaingia
vichakani na kutoweka. Akawaacha wengine waziokoe nafsi zao.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Azma yake ya kufika Islamabad ikamrejea tena. Akatembea


porini kwa uangalifu. Hakuamini sana kupita barabarni wala
kuomba msaada katika gari lolote. Alichokifanya ni kupita porini tu
lakini kandokando ya barabara ileile. Mbele kidogo akaona magari
kama sita hivi yakiteremka kuja kule aliko. Akajua kwa vyovyote
wameshapata taarifa za vifo vya wenzao. Kumekucha! Mara Yale
magari yalipompita, akaendelea na safari yake.

* * * *

Siku iliyofuata taarifa za tukio la kuuawa kwa wale askari sita


zilitapakaa kila pembe ya dunia. Jenerali Kahir aliipata akiwa
nyumbani kwake huko Islamabad. Mara Moja akaacha kile
alichokuwa anafanya na kuiendea simu yake ya mezani. Akakoroga
namba fulani na kuiweka sikioni.
“Tumeshambuliwa tena?” akauliza bila hata ya salamu.
“Hapana mkuu… ni wahalifu waliokuwa wakiletwa hapa
ndiyo waliofanya hivyo…”
“Ok, nakuja sasa hivi!” Jenerali Kahir akakata simu na
kujiandaa harakaharaka. Safari ya ofisini ikaanza huku kichwa
chake kikiwa hakielewi nini kimetokea mpaka askari wale wauawe
kizembe na mahabusu kutoroka.
Dakika ishirini tu aliwasili katika gereza kuu la Islamabad na
kukutana na viongozi wa gereza hilo. Jambo la kwanza Jenerali
Kahir alitaka kujua taarifa za uchunguzi wa awali. Alipozipata,
akataka kujua idadi na majina ya watuhumiwa waliokuwa katika
gari hilo. Katika kusoma Yale majina, moja likamgonga kichwa.
Halikuwa jina la asili ya watu wa Pakistan au mahasimu wao India.
Akamwita mkuu wa gereza hilo na kumuuliza kuhusu jina jilo.
Taarifa aliyoipata ni kuwa mwanamke huyo si raia wa nchi yoyote
kati ya hizo mbili, bali ni Mwafrika. Taarifa hii ikamsisimua sana.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Anaweza kuwa code namba tatu? Akajiuliza. Alijiaminisha hivyo


kwa sababu alijua wazi kuwa mwanamke huyo ni mwanajeshi hivyo
kuwazidi akili wale askari siyo jambo la kushangaza. Kahir akahoji
zaidi ili kujua mwanamke huyo alikamatiwa wapi na ilikuwaje.
Akaelezwa kila kitu kuwa alikuwa akitokea Ramban kwenda
Islamabad, jinsi alivyowatoroka na mpaka kukamatwa tena.
“Atafutwe haraka sana, huyu ni mwanamke hatari sana na
dunia inamtafuta… pindi mkimpata mniite mara moja,” akatoa
amri na kuondoka zake. Tangu hapo, akili yake haikuwa na utulivu,
aliwaza tu jinsi ya kumpata mwanamke yule.
Nikimpata, Mansoor na Fernandez watanikoma! Akawaza wakati
akiegesha gari nje ya msikiti wa Tabir Markaz tayari kwa ibada ya
Ijumaa.

* * * *

Katika hoteli ndogo ya Mkunazini, Kamanda Amata


alishtuswa na swala ya alafajiri kutoka msikiti wa jirani. Hakuona
haja ya kulala tena. Alijiinua na kuketi. Akayatazama makaratasi
yake aliyoyaweka mezani, karibu kabisa na taa yenye joto ili
kuyakausha. Yalikuwa tayari yamekauka vema. Akapitisha macho
kusoma kilichoandikwa. Jambo pekee lililomfurahisha na
kumuonesha kuwa kabrasha hilo lina umuhimu wa kipekee ni vile
lilivyokuwa limeandikwa. Haikutumika machine ya taipu wala
kompyuta. Kabrasha zima lilikuwa limeandikwa kwa mkono.
Mwandiko mzuri wa kupendeza. Na ilionekana ni mtu mmoja tu
aliyeandika maandiko hayo. Historia nzima ya Hasheem kuanzia
utoto, mpaka utu uzima. Elimu na taaluma yake ya kijeshi,
viliwekwa bayana. Kila andiko lilipoonesha pale alipopita, aliweka
na orodha ya marafiki ambao walikuwa wa karibu kwake.
Amata akasoma kwa utulivu sana. Akagundua mambo mengi
ambayo kwayo yalimfungua macho kuhusu mstahafu huyo.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Taaluma yake ya kijeshi katika maswala ya ndege vita na


mawasiliano anga ndivyo vilimfanya ajue kwa nini merehemu
Mwambope alimwandika kama P.o.R.
Kurasa nyingine ziliandikwa kuhusu familia yake. Hasheem
alikuwa na mke mmoja aliyemzalia watoto wawili, kati ya watoto
hao, Lukundame alikuwa kifungua mimba. Mtoto wa pili, kabrasha
lile lilimweleza kuwa alitoroshwa na mama yake na kwenda
kusikojulikana. Hasheem akamweleza Jamila kuwa ni mtoto wake
wa kumlea si wa kumzaa. Akaeleza vyema, alivyompata huko
mitaani, alivyomsomesha na kumuingiza jeshini, mpaka kuwa
kepteni na rubani mahiri wa ndege vita katika TAF ya JWTZ.
Zaidi akaelezea mali zake anazomiliki ndani na nje ya
Zanzibar. Pamoja na mali hizo akaeleza kuhusu shamba lake
kubwa la Bwejuu ambalo alilitumia kama sehemu ya kupumzikia
nyakati za mwiaho wa juma. Alipofika mwishoni akagundua kuna
karatasi zimenyofolewa kwa kuwa vishina vyake vilibakia. Tena
ilionekana wazi kuwa aliyevinyofoa alikuwa alikuwa na haraka.
Ziko wapi? Akajiuliza. Wacha nikatafute hili shamba, Hasheem
anaweza kuwa huko! Akajiambia.

* * * *

TSA 1 aliwasili Bwejuu asubuhi ya saa nne. Hakujua kutoka


hapo ni wapi anapaswa kuelekea. Hii haikuwa shida kwa kachero
mwenye maarifa makubwa kama huyu. Akashuka kwenye lile Chai
Maharage na kuvuka barabara mpaka ng’ambo kumfuata muuza
madafu aliyekuwa upande huo. Alipomfikia, jambo la kwanza
lilikuwa ni kununua dafu na kuanzisha urafiki. Vicheko na
mazungumzo vikawapotezea kama dakika tano hivi kabla hajaenda
kwenye jambo lake la msingi.
“Aisee hebu nikuulize, unafahamu shamba kubwa la bwana
Hasheem yule mwanajeshi mstahafu liko wapi hapa?”
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Ah… heeee, we mgeni kumbe, nilijua tu maana mi sura za


hapa nazijua fika…” akajibu muuza madafu.
“We unawajuaje watu wa hapa?” Amata akamtupia swali la
kijinga lakini lenye maana kwake.
“Mi mzawa! Nimezaliwa hapa, nimekulia hapa, ninazeeka
hapa na nitafia hapa. Huyo Hasheem huku tunamwita Mjeda…
shamba lake lipo mbele huko, barabara hii moja kwa moja…
wamtakani?”
“Nina shida na hapo mahali, sisi tuna miradi yetu ya
mashamba, sasa tumepata habari kuwa analiuza lile la kwake ndo
maana nimekuja…” Amata akatia uongo.
“Mh! Kuuza shamba? Sijui lakini, fata njia hii kama kilomita
tatu hivi mkono wa kushoto utaliona, limeandikwa ‘Sheem Estate’”
yule muuza madafu akamuelekeza Amata. Hakuchelewa, akaagana
naye na kuondoka zake. Kutoka pale akakodi baisikeli, hakukuwa
na gari kwenda upande huo. Ilimchukua dakika kama thelathini na
tano kufika eneo alilolikusudia. Mara baada ya kumlipa yule
mwendesha baisikeli, Amata akaliendea lango kuu la shamba hilo.
‘Sheem Estate’akasoma kibao chakavu kilichoning’inia kwenye
vyuma vya lango lile lililofungwa kwa mnyororo. Kwa ndani
kulionekana nyumba ndogo katikati ya shamba hilo. Mabanda ya
ng’ombe na josho lakuogeshea mifugo hiyo vilikuwa upande
mwingine wa shamba lile.
Lilikuwa eneo lenye ukimya sana, watu wachache walipita
wakielekea upande huu au ule. Alipojikuta peke yake, Amata
aliruka lile lango na kutua ndani, kisha akaanza kuvuta hatua
polepole kuelekea kwenye yale mabanda. Hakutaka kwenda moja
kwa moja kwenye ile nyumba maana hakujua usalama wa eneo
hilo.
Mabanda yalikuwa wazi kabisa. Hakukuwa na ng’ombe wala
ndama. Mavi makavu ya wanyama hao yaliyoshikana na sakafu
butu yalimjuza kuwa viumbe hao waliishi humo muda mrefu
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

kidogo na si kwamba wameenda machungani. Alipojiridhisha kuwa


hakuna jambo la kuhatarisha usalama wake eneo lile, akavuta hatua
kuelekea ile nyumba kwa kukatisha uwanja. Amata aliuona umahiri
wa Hasheem katika medani yake ya kijeshi. Kwa jinsi alivyoiweka
nyumba yake hiyo. Mtu wa kawaida hasingeweza kuchagua eneo
hilo kuijenga nyumba yake yaani katikati ya shamba. Kila upande
utakaoingilia lazima upite mwendo wa umbali wa takribani mita
mia mbili au mia mbili hamsini kuifikia. Na hapo unapopita hapana
kitu cha kukukinga usionekane. Unajianika.
Volkswagen Beetle, chakavu, liliegeshwa kando tu ya mlango
wa kuingilia ndani. Amata akalitazama vizuri, akalisogelea. Lilikuwa
chakavu haswa! Viti vyake vya ngozi viliharibika na kuruhusu spring
zake kuonekana nje. Milango yake iliyoshika kutu iliotea mimea
midogodogo kwenye pachipachi zake na bodi la gari hilo. Matairi
yalikuwa tayari yameruhusu upepo wote kuondoka. Lilikaa chini
kama kuku jike afanyavyo pindi anapovificha vifaranga vyake.
Amata akavaa miwani yake na kutazama kila kitu kupitia
miwani hiyo. Naam, alichokifikiria ndicho. Kwenye taa za mbele za
lile gari bovu, kwa ndani, iliyoonekana kama balbu ilikuwa kamera
ya usalama inayotazama moja kwa moja lango kuu. Kama kuna
mtu ndani ya nyumba hiyo basi angeweza kumuona mtu anayeingia
katika wigo huo.
Nimeonekana! Akawaza.
Amata hakujali kwa kuwa hakuwa na uhalifu wowote kwa
huyo anayemfuata. Akalipita lile gari na kuzikwea ngazi kuuelekea
mlango. Akasimama kwa muda kuyaruhusu masikio yake yahisi
chochote. Hakuna. Amata akabisha hodi, ya kugonga na kuita.
Hakuna aliyekuja kufungua. Akaingiza mkono mfukoni na kutoa
funguo yake isiyoshindwa. Akaingiza tunduni na kucheza na kitasa
kile kwa sekunde kadhaa. Akafanikiwa. Akausukuma ule mlango na
kuingia ndani kisha akaufunga nyuma yake. Akajikuta jikoni.
Aliligundua hilo kutokana na samani alizozikuta katika chumba
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

hicho. Akapita na kuingia sebuleni. Viti vichache vya kizamani,


rafu ya vitabu na luninga ndogo ya ‘National’ vilikuwa hapo. Ukuta
ulijazwa na picha tofauti tofauti. Kati ya picha hizo, Amata
aliigundua kirahisi ile ya Lukundame na Hasheem mwenyewe.
Nyingine ilikuwa ya familia, yaani Hasheem na watoto wake.
Akaoanisha na yale maelezo aliyokwishayasoma kwenye lile
kabrasha. Akaafiki.
Amata akaendelea kuitalii ile sebule kwa macho. Hakuvuta
hata hatua moja kwenda mbele wala kurudi nyuma. Dakika tano
baadae, kwake ukawa muda muafaka. Akavuta hatua na kuifikia
rafu ya vitabu, akapiga macho kwa umakini sana. Vitabu, asilimia
kubwa vilikuwa vile vya maswala ya anga na medani za kijeshi.
Hakukuwa na aina nyingine ya vitabu. Juu ya meza ndogo kulikuwa
na karatasi iliyoandikwa kwa mkono, na kukatwa mshazari kwa
mstari mwekundu. Hakuigusa, akaitazama kutoka mbali. Haikuwa
na la maana zaidi ya mwandiko wa kike ulioipamba ile karatasi.
Ilikuwa ni kama taarifa hivi, aliyokuwa akiandikiwa na mtu fulani.
Amata akalikamata jina tu la aliyeandikiwa ujumbe huo ‘CID
Badru’.
Katika kazi za kijasusi, hakuna jambo dogo, yote ni makubwa
tu. Amata aliichukua ile karatasi na kuitia mfukoni. Akakagua
vyumba vyote na kuvikuta tupu. Isipokuwa kimoja ambacho
kilikuwa na picha kubwa ya mwanamke, mwanajeshi. Mavazi ya
mwanamke huyo pichani yalimtambulisa kama rubani wa ndege za
kijeshi.
Jamila! Akawaza.

* * * *

Jamila aliingia katika jiji la Islamabad kwa kificho.


Alihakikisha hakuna mtu anayeweza kumgundua kwa kuwa alijua
kuwa kwa vyovyote vile anatafutwa kila kona. Hakuwa mbali na
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

ukweli. Kichwani mwàke alikuwa na jambo moja tu la kufanya


katika jiji hilo. Kupata sehemu anayoweza kupata intaneti ili aweze
kumpa taarifa baba yake mzee Hasheem ya nini kimemsibu.
Akapita mtaa huu na ule akitafuta ofisi anayoweza kufanya kazi
yake.
Katika kitongoji cha Rawat, Jamila aliteremka kwenye gari
alilopanda mara baada ya tukio lile la kuua wale askari. Akiwa kavaa
juba na nikabu ili hasijulikane kirahisi alianza kutafutakile
anachokitaka. Hakuweza kuuliza kwa kuwa hakujua lugha ya
wenyeji na wala hakuwaelewa wanavyoongea. Alipokunja kona ya
kwanza, ya pili, ya tatu akajikuta anapigwa bumbuwazi na mwili
wote kuingia ganzi. Picha inayofanana na yeye kwa kiasi kikubwa
ilibandikwa ukutani na juuye kuandikwa ‘Wanted’.
Kazi ipo! Akawaza huku akitembea harakaharaka kuliacha
eneo lile. Mitaa kama mitano baadae akafanikiwa kupata kile
akacho. Duka kubwa lililosheheni vifaa vya kielektroniki kama
kompyuta, faksi, machine za fotokopi na kadha wa kadha. Kijana
wa makamo akamkaribisha kwa shauku ya kutaka kujua ni nini
mwanamke huyo anahitaji.
“Internet service!” akamwambia. Yule kijana akampa ishara
mteja wake kuwa amfuate. Jamila akafanya hivyo. Ndani ya duka
lile kulikuwa na ofisi nyingine ndogo iliyojazwa na kompyuta
upande huu na ule. Watu wachache walikuwa wakiendelea na kazi
zao katika ofisi hiyo. Jamila akapewa kompyuta moja na kuanza
kutuma barua pepe kwenda kwa baba yake. Katika barua pepe hiyo
alimwandikia kila kitu kilichowatokea, akamtumia code yake siri
ambayo angetumia kwenye ule mfumo na kumwambia wazi kuwa
hajui hatima ya maisha yake.

* * * *

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Taarifa za kuonekana kwa Jamila katika mji ule zikafika katika


kituo cha polisi cha Rawat. Nao kutoka hapo wakatuma taarifa
hiyo kwenda kituo kikuu kwa hatua zaidi. Amri ya kulizingira duka
hilo ikatolewa. Jamila aliendelea na kazi yake bila kujua nini
kinaendela huko nje. Alimaliza kuandika kila alichokitaka tena kwa
furaha kabisa akijua kuwa mpaka hapo tayari taarifa muhimu
zimefika kunakohusika. Jamila aliandika nyaraka tatu; moja
kwenda kwa baba yake yaani kwa Hasheem ambaye alimjuza
kuhusu ajali, mazingira ya jinsi ilivyotokea na kumtumia code ile ya
siri ambayo hakutakiwa mtu mwingine aijue. Ya pili aliandika kwa
mkuu wake wa kikosi pale Airwing Ukonga akimjuza tu kuwa yuko
salama na anahitaji msaada wa haraka kuwa salama zaidi huku
akisema wazi kuwa hajui hali ya wenzake wala wapi walipo. Ya tatu
aliituma kwa Jenerali Mwambope kumpa taarifa na kumlaumu kwa
kile alichokifanya. Jamila alipogonga kidole cha kati cha mkono wa
kuume kwenye ‘Enter’ili kuifunga akauti yake akajikuta kasimamiwa
nyuma na askari mwenye gwanda. Akahisi kutokwa na haja ndogo.
Mwili ulipoteza nguvu. Akajikaza kikike huku akijua sasa ule wakati
wa shuruba na mateso umefika.
Akasimama, ndipo alipohisi kono gumu lenye nguvu
limemkamata bega. Akageuka mzima mzima na kutazamana uso
kwa uso na huyo askari mwenye rangi nyeusi lakini nywele za
kihindi.
“Upo chini ya ulinzi,” yule askari akaongea kwa lugha yao
ambayo ilimpita kushoto mwanamke huyo. Hakuwa na la kufanya.
Hata kama hakuelewa, alijua wazi kuwa amekamatwa. Akakinga
mikono yake na kuvalishwa pingu.
Huko nje ya lile duka palikuwa na magari matatu ya askari
wenye silaha. Muda huohuo likawasili Toyota Hilux Doble
Cabinslililokuwa na watu wanne tu ndani yake. Likasogea polepole
kuelekea maegesho ya lile duka. Vijana wawili kati ya wale wanne
wakateremka na mmoja wao akaingia kwenye lile duka huku
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

mwingine akibaki nje ya lile gari kaliegemea akivuta sigara. Wale


askari walibaki katika sehemu ambazo walitakiwa kuwapo. ‘Lolote
linaweza kutokea’ walikwishaambiwa.
Kule ndani ya lile duka, yule kijana akakutana uso kwa uso na
yule askari akiongozana na Jamila. Kwa makusudi kabisa
akamgonga Jamila na kujifanya kuyumba, akamvaa yule askari na
kuanguka naye mpaka chini sakafuni. Alijua anachokifanya. Kabla
hata mtu hajaja eneo hilo, tayari alikwishamvunja shingo yule askari
kwa stadi wa hali ya juu sana. Akainuka haraka na kumkamata
mkono Jamila. Hakutoka nate upande wa mbele, bali akapita ndani
kwa ndani na kutokea nyuma ya lile jengo. Huko alilikuta gari
jingine kama lilelile alilokuja nalo, akamwingiza Jamila na kufunga
mlango. Lile gari likaondoka kwa mwendo wa kawaida huku yule
bwana akirudi ndani kwa njia ileile aliyotokea.
Ndani ya lile duka tayari mvurugano ulikwishaanza, askari
waliingia na kukuta mwenzao akiwa marehemu. Kila waliyemuhoji
alieleza tu tukio aliloliona na si zaidi ya hapo. Yule jamaa akapita
nyuma ya rafu zilizobeba kompyuta na kuufikia mlango, akatoka
nje na kuingia mwenye lile gari alilokuja nalo. Injini ikatiwa moto
na gari likageuzwa tayari kwa safari.
Hali ya sintofahamu ikatokea nje ya duka lile mara baada ya
kujuzwa kuwa aliyeua askari kaondoka na gari hilo. Askari wa nje
walijitahidi kulifukuza lile gari huku wakitupiana risasi
wasifanikiwe.

* * * *
Chini ya nyumba ile ya Hasheem kule Bwejuu kulikuwa na
andaki kubwa lililojengwa vizuri na lenye mahitaji yote muhimu.
Amata hakujua kitu hicho, baada ya kuizunguka ile nyumba kwa
ndani hakugundua siri yoyote ile. Akakata tamaa na kuamua
kuondoka. Nje ya nyumba ile akasimama tena, nafsi yake ikigoma
kukubaliana naye. Akaamua kuikagua kwa nje. Kutoka pale kwenye
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

lile gari, akavuta hatua kuizunguka huku akikagua kila akionacho.


Nyuma ya nyumba ile alikuta tanki la choo lililomvutia macho. Juu
ya tanki lile kulikuwa na mifuniko mitatu ya chuma.
No! Akajikatalia. Kwa muundo wa tanki hilo lingekuwa na
mifuniko miwili tu. Amata aliling’amua hilo. Kwa mtu mwingine
asingeweza kuiona hiyo tofauti. Lakini ukiwa jasusi inabidi ujifunze
mambo mengi katika Nyanja tofauti. Akaiangalia ile mifuniko.
Akauwendea ule wa mwisho na kuufunua. Pua zake zikapambana
na harufu kali ya kinyesi na mvuke wa joto. Akaurudishia na
kuufuata ule wa katikati, akaufunua. Akatikisa kichwa juu chini.
Akauweka kando na kuingia kwenye lile shimo. Ngazi zikampokea,
aliposhuka kwa urefu wake, akauvuta na kufunika. Mita tatu chini
akafika kwenye ujia mdogo ambao ili upite lazima uiname.
Akawasha tochi yake ndogo inayoangaza eneo dogo alitakalo.
Akaufuata mpaka mwisho akakutana na mlango wa mbao.
Aliponyonga kitasa ukafunguka. Amata akajitoma ndani na kuibuka
kwenye sebule nyingine iliyofanana kabisa na ile ya mwanzo kwa
kila kitu. Tofauti tu ni kuwa katika sebule hii kulikuwa na meza
iliyojaa kompyuta ambazo zote vilikuwa zikifanya kazi huku kiti
kikiwa wazi. Palionekana wazi kuwa palikuwa na mtu na ametoka
muda si mrefu. Akili ya Amata ikapiga samasoti, akajihami. Bastola
mkononi, akatulia pembezoni tu mwa rafu ya vitabu.
Kutoka chumba kingine, alisikia mruzi wa mtu anayekuja
katika sebule hiyo. Akamsubiri.
Mzee wa makamo akaingia. Ngozi yake ilimtambulia hivyo. Amata
akamsadifu kwa macho. Ukakamavu wa mzee huyo ulionekana
dhahiri shahiri katika mwendo na utendaji wake. Akaketi kitini na
kuchukua sigara yake, akaiwasha na kuiweka mdomoni, akapiga
pafu mbili na kuuachia moshi ukienda hewani taratibu.
“Nimekuwa mgeni wako leo Kepteni Hasheem…” Amata
akasema huku akiiendea ile meza, “asalaam aleikum,” akamsabahi.
Mzee Hasheem hakujibu neno wala hakutikisika. Amata akayasoma
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

macho ya mzee huyo akajua kuna hesabu anayoipiga. Alipotazama


vizuri, akaiona bastola iliyokuwa katika kikombe cha udogo. Kabla
Hasheem hajaiwahi tayari Amata, kama umeme akainyakua. Mzee
Hasheem akapiga ngumi mezani kwa hasira. Akamtazama kijana
huyo shababi, asimmalize.
“Mnataka nini kwangu?” akauliza.
“Akina nani?” Amata naye akauliza.
“Nyie… mnaifuatilia sana familia yangu…”
“No! Hasheem mimi ni mtu mwema sana sina madhara
kwako”
“Hizo ni lugha zenu nazijua…” Hasheem akamwambia
Amata. Kijana huyo akabaki kimya kwanza akitazama kompyuta
moja baada ya nyingine.
“Jamila ni nani kwako” Amata akauliza.
“Ni binti yangu…”
“Yuko wapi kwa sasa?” akapiga swali lililompa ukakasi
kidogo.
“Maswali yako siyaelewi wewe ni nani?” Hasheem akauliza.
“Mimi ni mwanausalama kutoka serikalini…”
“Hapana, wewe umetumwa na ‘kina Mwambope…”
Hasheem akasema.
“Mwambope! Mwambope yupi?”
“Kwani kuna Mwambope wangapi jeshini kwenu wanaoratibu
manunuzi ya vifaa vya jeshi?” Hasheem akamtwanga swali Amata
ambalo hakulitarajia.
“Mwambope ameuawa…” Amata akajibu.
“Ah! Wanaharamu nyie… mmemuua? Sasa mnataka kuniua
na mimi?” Hasheem akalalama.
“Sihitaji kukuua… mimi nahitaji kujua mambo machache
kutoka kwako; mosi, wewe una mahusiano gani na Mwambope?
Pili ni akina nani wanaokufuatilia? Je ndiyo hao waliommuua
Mwambope?” Amata akamwagia maswali. Mzee Hasheem akatulia
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

kimya. Akabinua kompyuta moja na kutoa picha ya msichana.


Akampatia.
“Huyu ndiye Jamila. Rubani mahiri wa jeshi, mmeiteka ndege
yake akiwa anarudi kwa minajiri ya kuuiba mfumo uliofungwa
kwenye ndege hiyo… hamtoweza, na hiyo siri hata mimi
sintowapa,” Hasheem akasema huku akiamini kabisa kuwa Amata
ni mmoja wa adui zake.
“Halafu kuhusu Mwambope,”
“Mwambope ni mjinga kama wajinga wengine, alijiingiza
kwenye biashara haramu ya kuihujumu ile ndege matokeo yake
wenzake wamemzunguka. Yaani nyie mnatufanya sisi wapumbavu.
Najua, kama Mwambope kauawa basi ni wewe uliyemuua kwa
sababu ni yeye pekee anayepajua hapa, naye atakuwa
amekuelekeza,” Hasheem akaeleza.
“Nimekwambia mimi nia secretagent waserikali,” Amata
akasisitiza.
“Noo sidanganywi na watoto wadogo… nyie ndege
mmeiangushia Kashmir, mi najua. Mitambo yangu hii inaonesha
kila kitu, hiyo biashara yenu ni biashara kichaa… hamuwezi
kuniingiza kwenye matatizo na serikali yangu... Naipenda nchi
yangu na ndiyo maana nikakubali kuunda mfumo ule wa ulinzi
ambao uliunganishwa katika ile ndege…” Hasheem akalalama.
“Hasheem, mimi nipo upande wa serikali…” akamwambia,
“huniamini? Siwezi kukuua…”. Akamrudishia bastola yake.
Hasheem akaitazama bastola ile ikiwa mkononi mwa Amata, kisha
akamtazama kijana huyo usoni. Akaichukua na kuikamata kiganjani
mwake. Chozi likadondoea mezani kwake.
“Masikini Jamila binti yangu... Nakumbuka email yako ya
mwisho kwangu uliniambia nini, sikuwa na jinsi ya kukusaidia na
huyo mshenzi Kotvich Mungu atamlipa,” Hasheem akasema
maneno hayo huku macho yake yakiwa yamejawa machozi.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Kotvic ndiyo nani?” Amata akauliza. Swali hilo lilimshtua


Hasheem, alikwishajisahau.
“Humjui? Nimeficha siri hii muda mrefu sana ndiyo maana
Mwambope kauawa na sasa ni mimi…”
“Siri gani?” Amata akauliza tenga.
“Unayemwona wewe kuwa anajenga nchi ndiye huyohuyo
anayeibomoa…” Hasheem akamaliza. Akavuta kabrasha moja
jembamba na kumpatia Amata. Naye akalipokea.
“Soma!” akamwambia. Amata akachukua lile kabrasha na
kulifungua. Ndani yake kulikuwa na karatasi tano tu zilizoonekana
wazi zimenyofolewa sehemu. Akiwa katika kusoma nyaraka hizo
akashtuliwa na mlio mkali wa risasi. Alipogeuka akakuta Mzee
Hasheem kajimaliza kwa risasi moja tu na kufumua kisogo chote.
Amata akabaki kapigwa bumbuwazi, macho yamemtoka hajui nini
afanye. Akalifunga lile kabrasha vizuri. Akautazama mwili wa
Hasheem ukiwa pale kitini, damu zikiwa zimetapakaa kila mahali,
ubongo nao ukiwa huku na kule. Kiukweli ilikuwa picha ya
kuogofya kuitazama. Kwa haraka haraka akapekua hapa na pale,
akapachua zile kompyuta na kutoa hard disk zake, akazitia mfukoni.
Laptop iliyokuwa mezani hapo akaibeba. Amata akapiga picha
kiwiliwili cha Hasheem na ile bastola. Kisha akatoka haraka kwenye
ile nyumba na kutokomea nje.
Nje ya lile geti alitembea harakaharaka kuifuata njia aliyokuja
nayo. Akiwa katika mwendo huo, mbele yake aliliona gai linalokuja
kasi. Likampita na kwenda kusimama mbele ya lile geti. Alipoona
hivyo, Amata akasimama kuangalia mini kinaendelea.Kwenye lile
gari, wakashuka watu watatu na kuruka lile geti. Wote wakakimbilia
ndani ya ile nyumba. Amata akabaki kajibanza nyuma ya miti
akitazama. Dakika kumi na tano, wale jamaa wakatoka na kuingia
kwenye gari lao na kuondoka kwa kasi ileile. Wakapita pale alipo
Amata wasimwone.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Hawa ni akina nani? Akajiuliza asipate jibu. Taratibu akaanza


safari yake ya kurudi mjini. Akiwa njiani anatembea, simu
yake ikaita. Alipoitazama akajikuta akitabasamu.
Mwaja! Akatamka jina hilo moyoni mwake. Akaiweka sikioni
na kutulia kidogo.
“Ukaniahidi kunitafuta ukanichunia… mi jana nikabaki bila
liwazo nakumbatia mito,” Mwaja akalalama kwenye simu.
“We ndo uliniahidi kunipigia…” Amata akamwambia Mwaja.
“Sawa, ushamaliza kazi yako?” Mwaja akauliza.
“Kazi gani?”
“Si ulinambia unamtafuta Hasheem! Ushamaliza kazi yako?”
“Ndiyo!” akajibu.
“Mwanaume wewe, sijaona mwanaume katili kama wewe
duniani…” Mwaja akaendelea kulalama.
“Ukatili wangu uko wapi?”
“Utajua mwenyewe…”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

07
KATIKA BANDARI ya Zanzibar, mchana wa siku hiyo
Kamanda Amata alitulia kusubiri boti ya kumvusha kwenda Dar es
salaam. Miongoni kwa wasafiri wengi waliokuwa katika bandari
hiyo tayari kuabiri kweney boti ya adhuhuri, walikuwapo vijana
wawili wenye mchanganyiko wa asili ya Kihindi na Kiarabu.
Walifanana kwa sura na wajihi wao. Walinyoa nywele katika
mtindo unaofanana, walivaa miwani zinazofanana, saa
zinazofanana. Ni vigumu sana kuamini kama ungeambiwa kuwa
vijana hao hawakuwa ndugu. Kila mtu alivutiwa kuwatazama.
Macho ya wengi hayakuwabanduka. Amata alikuwa kimya
kajiinamia. Kichwa chake kilikuwa kikichakata mambo mengi kwa
wakati mmoja. Hakuwa na habari kabisa na watu hao walioingia
katika bandari hiyo.
Wale vijana wakapachika masikioni mwao vifaa vya mawasiliano.
Kupitia vifaa vile wakapewa maelezo ya nani wanatakiwa
kumuweka chini ya himaya yao.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Hamtakiwi kumdhuru bali kumsindikiza mpaka katikati ya


bahari ambako mtakuta boti yetu ndogo, mteremke naye.
Mkishindwa kuteremka naye, muueni mchukue begi lake,. Hilo
begi limebeba siri nyingi hata ile moja tunaoitaka ipo humo”
wakaelekezwa, wakaelewa. Tangazo la abiria kuingia botini
likasikika. Kamanda Amata akainua uso na kukuta watu wakianza
kuingia kwenye boti hiyo. Naye, taratibu, kwa uchovu, akainuka na
kuliweka begi lake upande wa mbele. Akavuta hatua kuingia ndani
ya boti hiyo. Akiwa amekaribia kabisa mlangoni, akahisi kuna watu
nyuma yake ukiachana na abiria wengine. Hawa walikuwa watu
wasio wa kawaida. Mwili wa Amata ulisisimka, akalihisi hilo.
Alipogeuka kushoto akamuona mmoja na alipogeuka kulia, vilevile.
“Usiwe na wasiwasi, upo kwenye mikono salama,” mmoja
wao akasema. Amata akajua tayari yupo tekoni. Hakujali.
Aliendelea kuvuta hatua kuelekea katika vyumba vya daraja la
kwanza. Alipoingia, akaitazama vizuri tiketi yake na kuisoma
namba ya kiti anachotakiwa kukalia. Akaketi, na wale vijana
wakaketi pembeni, huku na kule, Amata akiwa katikati. Begi lake
akalifumbata kwa mbele kwa kuwa alijua wazi kuwa hilo ndilo
liwindwalo. Boti iling’oa nanga na kuanza safari. Amata alikuwa
kimya kabisa kitini huku wale vijana wakiwa kimya pia.
Saa Moja baadae, yule wa kushoto akamwambia Amata,
“tumeshafika, jiandae kushuka!”
“Tumeshafika wapi wakati unaona tupo katikati ya bahari”
Amata akauliza.
“Jiandae, tunateremka!” wa kulia akasisitiza. Amata
akawatazama kwa zamu.
“Sawa!” Akajibu Amata kisha akatulia palepale akipiga hesabu
zake. Boti lile liliendelea kukata maji. Amata akapiga jicho nje aone
kama kuna jambo linalotendeka. Kwa pamoja wakamtazama
Amata wakamwambia, “let's go… ”. Wakamshika huku na huku na
kuinuka naye kuelekea nje. Hakukuwa na dalili ya boti ile
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

kusimama wala kupunguza mwendo. Amata alitulia kama kondoo


aendae machinjoni, tayari akilini mwake alijua nini cha kufanya
pindi akipata wasaa unaomstahili. Wakatoka nae nje ya behewa ile.
Kila mtu ndani mle alikuwa akiwatazama watu hao. Sambamba na
boti ile kulikuwa na boti nyingine ndogo iendayo kasi ikiikaribia hii
kubwa. Wale jamaa wakamkamata sawasawa Amata, naye alijua
nini kitafuatia. Wakafikia katika korido ambayo kutoka hiyo
unafikia ukingo wa boti ile. Ile boti ndogo yenye kasi ikafika karibu
kabisa na ile waliyokuwapo Amata na wale vijana. Ile boti ndogo
ikafunguka paa lake, akajitokeza kijana mmoja aliyetoa ishara kwa
vijana hao. Ni hapo alipokuwa akipasubiri kwa hamu. Kwa nguvu
zote aliwasukuma wale vijana kila mmoja upande wake. Yule wa
kulia akaanguka chini huyu wa kushoto Amata akawahi kumdaka
na kumtandika kichwa chenye kilo nyingi. Alipomwachia
akapepesuka na kujikwaa kwenye kamba ya kufungia boti za
wokozi. Yule aliyeanguka mwanzo akainuka haraka na kumvaa
Amata. Alikosea sana. Konde moja zito likatua tumboni, akaguna
kwa maumivu. Amata akajibetua tik tak na kumtandika teke zito,
alipotua akashuka na yule mwingine. Akamkamata kwa nguvu na
kumbamizia kwenye chuma la ukingo wa boti na kumpasua vibaya.
Akambeba na kumtosa majini. Akageuka kwa yule wa kwanza
aliyekua kasimama tayari kwa mapambano. Alipokuja, akamuepa
na kumdaka tai yake akaivuta kwa nguvu na kumkaba vibaya.
“Nani kawatuma?” akamuuliza. Yule jamaa macho yalikuwa
yamemtoka pima. Hakuweza kujibu zaidi ya kukoroma tu, kifo
kilimkuta. Utulivu katika ile boti ukatoweka kelele za watu zikazua
taharuki. Nahodha akazima injini na ile boti ikapunguza mwendo
na kusimama. Mabaharia huku na huku wakawa wakizuia na
kuwataka watu kuwa watulivu. Ilikuwa ngumu.
Kutoka kwenye ile boti ndogo, walipoona mambo magum
wakatia moto injini na kuondoka. Amata akachomoa bastola yake
na kuweka shabaha maridhawa. Risasi moja tu ilifumua kichwa cha
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

nahodha yule kabla lile paa halijajifunga. Amata akamtazama yule


aliyemkaba, tayari alikwishalegea. Akamshachi na kuchukua kila
alichoona kinamfaa.
“Kijana, tulia hapohapo usilete vurugu,” mzee wa makamo
alisikika kutoka nyuma yake. Amata akageuka kumtazama. Mzee
yule mkononi mwake aliikamata vyema bastola yake. “Mimi ni
mwanausalama,” akasema na kuning’iniza kitambulisho chake,
Amata akakisoma. Naam, alikuwa mstahafu wa idara ya usalama wa
taifa.
“Nini tatizo? Wewe ni nani?” yule mzee akauliza.
“Mimi ni mwanausalama pia,” Amata akaonesha kitambulisho
chake kwa mtu yule. Akaushuhudia mbutwaiko wake pindi tu
macho yake yalipogongana na jina la Amata.
“Is you?” akamuuliza kwa Kiingereza. Amata
hakujishughulisha naye. Akamuinua yule jamaa kutoka pale chini
akaomba maelekezo ya wapi pa kumuhifadhi, akaoneshwa.
Alipohakikisha kila kitu sawa, akarudi na kuketi mahala pake. Kila
mmoja alikuwa akimshangaa. Hakuna aliyeamini kilichotokea.
Amata akachukua simu yake na kubofya namba fulani, na kuiweka
sikioni.
“Ukipiga tu najua kuna jambo” sauti ya Simbeye iliunguruma.
“Na jambo lenyewe siyo jepesi... Nipo safarini kutoka Zenji
kuja Dar, nimevamiwa na watu wasiojulikana bahati mbaya
nimewashinda na wote ni marehemu,” Amata akaeleza.
“Ok, kwa hiyo unatakaje?”
“Hah! Sasa wataendelea kuelea majini?”
“Acha waliwe na samaki,” Simbeye akajibu kwa utani, “Sawa,
ninasughulika, na pindi ukifika uje utoa maelezo kituoni…”.
“Sawa!” akajibu na kutulia kitini kimya mawazo kadhaa
yakimzunguka kichwani mwake. Akiwa kazama katika lindi la
mawazo, coca baridi ikatua kwenye kijimeza chake. Akainuka uso

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

kumtazama huyo aliyemkirimia hilo. Kitambulisho shingoni


mwake kikamtambulisha kama Zulekha Hassan.
“Asante Bi. Zulekha,” akamshukuru na kuishika ile chupa ya
coca, kizibo chake kilikuwa kimelegea, yaani imefunguliwa.
Akaisogeza kando nankuebdelea na mambo yake.
Ile boti bado ilikuwa imesimama palepale, haikusogea hata kidogo,
“samahani kiongozi,” kijana mmoja aliyeonekana ni baharia katika
boti hiyo akamwita Amata nje. Akatoka kumfuata.
“Sasa hii boti ya hawa jamaa tunaifanyeje?” akauliza. Amata
akashangaa kidogo, “ina maana miili yote mmeiopoa?” akawauliza.
“Ndiyo tumepewa oda kutoka kituo cha polisi huko Dar,”
akaeleza.
“Ok! Subirini kidogo,” akawaambia, “niteremsheni mpaka
chini, nitaiendesha,” akasema. Wale mabahari wakatazamana.
“Unaweza kuendesha boti kwenye maji makubwa?”
“Kila kitu naweza isipokuwa ungo tu…”

* * * *

Jamila alifikishwa katika kambi ya wanamgambo wa Hizbul


Mujahedeen .kambi iliyojengwa katikati ya mkusanyiko wa milima,
ilifichwa na kuwekewa ulinzi mkali. Usingeweza kuifikia kabla
hujawa marehemu kama hukuwa na miadi ya kuelekea hapo. Vijiji
vilivyoitangulia kambi hiyo viliwekwa watu maalumu wa
kuchunguza na kutoa taarifa ya kila gari au mtu anayeelekea huko.
Watu hao walijua orodha ya magari yatakayopita kila siku kelekea
huko na ni nani anayekwenda na kwa nini.
Mara baada ya kuwasili kwenye ile kambi, yale magari
yaliingizwa ndani na kufichwa nyuma ya milima ile. Jamila
akateremshwa garini na kuingizwa kwenye handaki kubwa
lililotengenezwa kiufundi sana. Aliligundua hilo kutokana na
taaluma yake ya kijeshi. Jamila akafungiwa ndani ya chumba kidogo
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

kilichozungukwa na nondo pande zote na mlango wa mtindo


uleule. Hawakuongea chochote, walimfungia na kumwacha
akipambana na giza nene. Giza ambalo halikumruhusu Jamila
kuona hata sentimeta thelathini. Mbu walianza kumshambulia kwa
hasira mwanamke huyo kana kwamba waliambiwa kuwa kuna
damu mpya imeingia. Jamila hakujali, alijikunyata kwenye kona
moja, nguo yake akaivuta na kufunika miguu. Akatulia, na dakika
tano baadae, akapitiwa na usingizi.
Usiku wa siku hiyo hiyo, Jenerali Kahir aliwasili kwenye ile
kambi ya waasi aliokuwa akifanya nao kazi kwa siri. Kahir alikuwa
na cheo cha juu sana katika kundi hilo. Ndiye aliyewatafutia waasi
hao silaha za aina aina. Na hata aliposikia kuhusu mfumo huo wa
kujilinda ambao uliunganishwa katika hiyo ndege vita. Alikubali
kufanya biashara na tajiri Mansoor kwa usindani na Bwana
Fernandez.
Kahir alipokewa na vijana wa Hizbul kwa bashasha.
Walimjua, walimhusudu. Ni kundi hili ndilo lilikuwa katika
mapambano na majeshi ya Kihindi kwa minajiri ya kulipatia uhuru
eneo la Jammu na Kashmir. Wapakistan walidai kuwa eneo hilo ni
lao na Wahindi nao wanadai kuwa eneo hilo nia lao. Mzozo.
“Karibu sana jenerali…” kiongozi wa kundi hilo
akamkaribisha na kufuatana naye ndani. Huko kulikuwa na watu
wengine watatu. Ni hawa ndiyo waliokutana siku chache zilizopita
kule Islamabad mjini. Baada ya maamkiano, Jenerali Kahir aliketi
kwenye zuria lilofumwa kwa ngozi safi ya ngamia.
“Hongereni kwa kazi,” akawaambia, “najua kumpata yule
mwanamke haikuwa kazi ndogo. Msako mkali sana unaendelea
mjini, kila njia na kichochoro kinalindwa,” akawaeleza.
“Sisi tumempata lakini mpaka sasa hatujajua ana umuhumu
gani kwetu, mwanamke tena mweusi…” mmoja wao akatia shaka.
“Swali zuri na ndilo lililonileta…” Kahir akawaambia na
kuchukua kikombe cha kahawa kilicholetwa hapo muda mfupi
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

ulopita. “Mleteni!” akatoa amri. Mmoja wao akapiga simu ya upepo


na dakika kama kumi hivi zilizofuata, Jamila akafikishwa pale.
Akawekwa mbali kidogo na jopo lile, lakini aliweza kuonekana
vyema. Kahir akawataka kumfungua pingu ili awe huru. Baada ya
hilo akaamuru apewe chakula na kinywaji ili apate nguvu.
“Huyu ni mtu muhimu sana kwetu kwa sasa, na kwa kupitia
huyu tutapata tunachokitaka,” akawaambia nao wakatikisa vichwa
kukubali. “Mansoor anao wawili, sisi tunae mmoja lakini
Fernandez hana chochote,” akawaambia. “Code tatu za kuufanya
ule mfumo ufanye kazi mojawapo ndiyo hii,” akawaeleza. Jamila
hakuelewa chochote ambacho watu hao walikiongea kutokana na
lugha yao kutokuwa rafiki na yeye. Hakujali, aliendelea kula kile
alicholetewa kwani ni muda mrefu hajala kwa utulivu. Nusu saa
iliyofuata Jamila alikuwa tayari keshamaliza kula na ametulia
palepale alipowekwa. Jenerali Kahir akamtazama kwa jicho lake kali
lililolegea kwa ulevi wa tambuu.
“Unajifahamu wewe ni nani?” akamuuliza jamila kwa
Kiingereza cha kawaida.
“Kivipi?”
“Yaani jina lako, utokako, umefikaje hapa na kadhalika…”
Jamila hakujibu kitu, alitulia akimtazama yule askari bila
kupepesa macho. Kahir akauona ujasiri wa mwanamke huyo. Huyu
kweli mwanajeshi!Akawaza..
“Usiogope! Ningekuwa na nia ya kukudhuru ningekuacha
wakukamate wale askari, lakini ni mimi niliyesuka mpango
mwingine kukuokoa na kukuleta hapa…”
“Kwa nini uliniokoa?” Jamila akataka kujua.
“Ni stori ndefu… Jenerali Kahir ni afisa mkubwa sana katika
jeshi la Pakistan; mzalendo anayeipanda nchi yake. Lakini Kahiri
huyu aliyesimama mbele yako si katili bali upenda kufanya jambo
kwa maslahi yake na taifa lake…”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Kwa hiyo umeniokoa kwenye mikono ya jeshi kwa maslahi


yako…?”
“Ndiyo… na taifa langu pia. Unatafutwa Ja…mil…”
“Hahahaaaa, Jamila,” akamsaidia kujibu.
“Jina lako linafanana na kitu ninachokipenda na kukihitaji
kwa maslahi yangu na taifa langu,” Kahir akasema.
“Kitu gani?” Jamila akahoji. Mara hii woga ulimwondoka.
Alijikuta akiongea huru kana kwamba amefahamiana muda mrefu
na huyo askari.
“Jammu…” Kahir akajibu.
Jamila akatulia kimya kwa jozi la sekunde akijaribu kuchakata
wazo. Kahir akazunguka ile meza na kumfikia Jamila. Mwanamke
huyo akasimama imara kijeshi. Athari ya kuwa mwanajeshi
ilijitokeza wazi pindi alipokuwa karibu na Jenerali huyo.

* * * *

Mansoor alisimama kimya pindi alipokuwa akipata taarifa za


yule mwanamke anayemtafuta. Faisar alikuja kwa tajir wake
kumwambia wazi kuwa jaribio hilo limeshindikana.
“Yaani umeshindwa! Kwa mara ya kwanza Faisar
umeshindwa kazi… ila najua kwa sababu ulimdharau mwanamke,”
Mansoor akatulia, kisha akaendelea, “yule hakutosha tu kumwita
mwanamke, ni mwanajeshi, anayejua mbinu zote za kivita. Hivyo
kukupiga chenga na kukutoroka huku akiua watu wako ni jambo la
kawaida na ulitakiwa kulitegemea…” akamwambia.
“Labda nikwambie tu Mansoor, sikushindwa kumkamata ila
Hizbul Mujahideen wameniwahi…”
“Unasema!…” Mansoor akang’aka.
Kahir anahusika! Akawaza Mansoor. Akajing’ata kidole kwa
hasira na kujitupa kitini, “keti” akamwambia Faisar. Kijana huyo
akaketi mkabala na Mansoor.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Kahir!” akatamka, “fanya upelelezi ujue yupo wapi kisha


uniletee habari. Kama Kahir kahusika basi mwanamke huyu
atakuwa kwa Hizbul…” akamweleza Faizar.
“Nami nilifikir hivyo,”
“Ok! Kazi kwako… kamlete…” Mansoor akatoa maagizo.
Mara tu baada ya Faisar kuondoka zake. Mansoor aliwaita
vijana wake katika chumba maalum ambacho hutumika kwa
mikutano midogomidogo kama hiyo.
“Tunachezewa mchezo mchafu,” akawaambia.
“Kivipi?” mmoja wa wale vijana akauliza.
“Code namba tatu, tunavyoongea inaonekana ipo mikononi
mwa Jenerali Kahir,” Mansoor akawaambia.
“Ina maana amempata?”
“Ndiyo… ila kalizunguka jeshi tukufu la Pakistan,”
“Amelisaliti?”
“Naam! Nitaongea naye, kama amefanya hivyo ili anikomoe
nami nitamkomoa pia,” Mansoor akaongea kwa hasira.

* * * *

SHAMBA
MADAM S alitulia tuli katika ofisi yake ndogo iliyojengwa
ndani ya jumba hilo. Juu ya meza yake palikuwapo na kabrasha
moja tu liliandikwa kwa mkono ‘Jamila’. Wino mnene mwekundu
wa marker pen. Lilikuwa kando ya meza limefunikwa huku juu yake
kukiwa na beji nzito ya TSA. Nusu saa tangu akae kwenye kiti kile,
mlango ukafunguliwa, Amata akajitoma ndani.
“Nilitegemea jana ileile ungefika kwangu, nilikuwa nina hamu
sana na wewe…” Madam S akamwambia Amata aliyekuwa anavuta
kiti ili akae.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Ni kweli, lakini ningekuja vipi kwako bila taarifa


iliyokamilika?”
“Oh! Sawa. Basi natumaini umekuja na taarifa nzuri…”
“No!”
“No?”
“Yes…”
“Hhaa hhaa hhaa aaaa!” wote wakacheka kwa pamoja.
“Nipe habari,” Madam S akamwambia Amata aliyekuwa tayari
kitini.
“Hasheem amekufa!” Amata akamwambia bosi wake.
“Amekufaje?” Madam S akasema.
“Ningefurahi kama ningejua ameishije ili nikueleze alivyoishi
maana amekufaje, amekufa vibaya ambavyo hakustahili…
Hasheem amejiua, hakuamini kabisa kama mimi ni kachero wa
serikali” Amata akaeleza kwa masikitiko. Ukimya kati yao
ukataradadi, kila mmoja alijikuta kwenye huzuni kuu.
“Ana jambo gani kwenye kadhia hii?”
“Hasheem ni baba aliyemlea Jamila, amenambia mpaka siku
ya Jamila kuondoka Urusi na ile ndege kulikuwa na mambo
hayaelewi”
“Aisee, na vipi uhusiano wake na Mwambope mpaka amfanye
P.o.R?”
“Mwambope kama mnunuzi wa vifaa vya kijeshi,
inasemekana alikutana na Hasheem miaka kadhaa nyuma
akiambatana na CDF mwenyewe kwa mazungumzo kuhusu ndege
hizo wanazotaka kununua…”
“Hasheem awasaidie nini?”
“Hasheem kama mtaalam wa mifumo ya ndege vita pamoja
na mawasiliano anga ili aweze kudiazaini kitu cha kipekee katika
hizo ndege,” Amata akaeleza.
“Na ilikuwaje ukataka kutekwa kwenye boti?”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Inaonekana licha ya sisi kwa mema, kuna kundi


linalomtafuta Hasheem kwa ubaya. Mara tu baada ya mimi kutoka
kwenye ile nyumba, kuna gari lilikuja na watu kadhaa halafu
likaondoka labda baada ya kukuta Hasheem akiwa marehemu”
“Oh shit, na haukuweza kujua ni watu gani?” Madam S
akauliza.
“Sijawajua, ndo tangu nilipofika jana nilikuwa nafanya
uchunguzi kuhusu watu hao. Kwanza wamemteka Lukundame…”
“Ni nani huyo?”
“Lukundame ni binti mkubwa wa Hasheem, na Jamila ni binti
aliyemlea,” Amata akaeleza.
“Kuna kitu kinatafutwa…”
“Ndiyo, na sasa naumiza kichwa ni nini…”
“Umechukua chochote?”
“Ndiyo, na ninahisi nimechukua na hicho kitu ndo maana
wamenifuata mpaka kwenye boti… nitajua tu kwani leo nina
operesheni ngumu sana… ya kufa na kupona,” Amata akaeleza
vizuri. “Vipi jeshi limepeleka watu kama walivyosema?” Amata
akauliza.
“Ndiyo, wameondoka kama Siku nne hivi zilizopita…”
“Ok, sasa wameenda wapi?”
“Wameanzia Russia…”
“Madam, katika tafutishi zangu nimegundua kwamba
Hasheem alikuwa akifuatilia mwenendo mzima wa ile project. Na
mawasiliano au kuifuatilia hiyo ndege inaonesha kwenye kompyuta
yake kuwa imeishia maeneo ya Pakistan … hata yeye ameweka
viulizo hapo… Jambo pekee na zuri ni kuwa Jamila ni mzima.
Baada ya Hasheem kujiua nimezipata baruapepe hizi,” Amata
akamwonesha nakala za baruapepe zile. Madam S akazisoma kwa
umakini sana. Kuna maeneo hakuweza kuelewa na mengine
alielewa.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Umefanya kazi kubwa sana, nitampa Chiba ang’amue no


wapi zilipoandikiwa barua hizi. Akishajua sisi tutaanzia hapo…”
“Swadakta ndipo ninapokupendaga, una maamuzi ya makini
na haraka,” Amata akamwambia Madam S.
“Asante! Mwambope anazikwa leo Kinondoni,”
“Nafikiri nitashiriki mazishi,” Amata akajibu.
“Vizuri, tukutane pale saa saba kamili. Mi na wewe
hatujuani…”
“Kabisa”.

* * * *

Hali ya hewa ya utulivu ililigubika eneo lote la makaburi ya


Kinondoni. Umati wa waombolezaji ulikusanyika katika viwanja
vya makaburi hayo tayari kutoa heshima zao za mwisho. Wanajeshi
waliopendeza kwa mavazi yao walijipanga tayari kuupokea mwili
wa kamanda wao.
Ni muda huo, Kamanda Amata aliwasili akiwa na BMW lake la
kisasa kabisa. Mbele yake kulikuwa na gari Moja jeupe Toyota
Mark X ambalo nalo lilikuwa likitafuta maegesho. Lilipoegeshwa
Amata naye akaegesha gari lake kando tu. Akafungua mlango tayari
kushuka. Alipokwishakufanya hivyo, wakati akiufunga mlango wa
gari lake ndipo akaona kitu ambacho hakukitegemea katika lile
Mark X jeupe. Mwaja. Mwaja akiwa katika mavazi yake nadhifu ya
kijeshi. Upande wa pili akateremka kijana mmoja, mrefu, si mnene
wala si mwembamba, chotara aliyeonekana mjuvi wa mambo.
Mwaja hakumwona Amata, ila yule kijana aligongana macho na
Amata. Yule kijana akavaa miwani ya jua na Amata Naye akavaa ya
kwake. Vinyweleo vikamsimama, akajua, kwa kijana huyu kuna
jambo. Alipokwisha kujiweka tayari, akavuta hatua kuelekea kule
kwenye makaburi na hapo ndipo walipogongana macho na Mwaja.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Mwaja akasimama na tabasamu pana likachanua usoni pake.


Akamsogelea na kumtaka yule kijana afanye vivyo hivyo.
“Habari Kamanda, kutana na Mr. Fareed,” Kisha akamgeukia
yule aliyeitwa Fareed, “kutana na Kamanda Amata, najua hujawahi
mwona ila unaweza kuwa umemsikia,” akatambulisha. Yule kijana
akatoa tabasamu butu wakati Amata akihisi ganzi mwilini mwake.

Mara baada ya kuachana pale wote watatu wakaingia katika


uwanja wa makaburi yale tayari kwa taratibu za mazishi. Watu
walikuwa wengi sana, viongozi wa majeshi na serikali nao
walikuwapo. Kamanda Amata akatafuta eneo zuri ambalo daima
angeweza kumuona yule jamaa. Akili yake haikumtulia, alijua kwa
vyovyote vile huyo bwana ana jambo. Kikubwa zaidi kilikuwa ni
jina lake, Fareed.
Fareed! Akajaribu kukumbuka.

‘Kutana na Fareed Tiffany Hotel saa kumi jioni kesho’

Akaukumbuka huo ujumbe aliokuta katika simu ya kijana


mmoja kati ya wale aliokabiliana nao kwenye boti.
Miadi haina mashiko! Akawaza kwa sababu alijua kwa vyovyote
Fareed anajua habari ya vifo vile na anajua kuwa huyo wa kukutana
naye ameshaitwa marehemu. Amata hakuweza kuvumilia, licha ya
kazi, wivu ulimtafuna. Akaichukua simu yake na kutuma arafa kwa
Mwaja.

‘Umepata Shombe hongera… mchanganyiko wenu utatoa kitu


hadimu…’

Mwaja aliisoma ile arafa na kutabasamu. Mpaka muda huo


hakujua kabisa ni wapi Amata ameketi. Kila alipopepesa macho
hakuweza kumuona.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Kwa upande wa Fareed yeye alitulia bila wasiwasi wowote.


Ijapokuwa hakufikiri kama anaweza kuonana na kiumbe huyo kwa
wepesi namna hiyo. Alimsikia, hakuwahi kumuona, hata walipofika
Zanzibar walijikuta wametanguliwa hatua moja na kijana huyo.
Walipotoka, walijua wazi ni nani aliyeingia ndani ya nyumba ya
Hasheem kwa kutazama kwenye kumbukumbu ya kamera za
usalama zilizofungwa humo ndani. Amata yeye hakuwaza hilo
kabisa. Mara baada ya Hasheem kujiua yeye hakutamani kupekuwa
vitu vingine.
Fareed alijuwa wazi kuwa Amata hajaondoka katika kisiwa
kile, akaacha vijana wa kuifanya kazi ile. Wahakikishe wanamtia
mkononi na kumfikisha kwake kwa siri. Lengo kubwa ni kupata
kabrasha moja ambalo Hasheem ameandika vitu hadimu sana
kuhusu ule mfumo wa usalama wanaoutaka. Haikuwa sawa fikra
zake, jioni hiyo aligutushwa na habari za ghafla kwenye luninga
kuhusu watu waliouawa kwenye boti. Fareed alishikwa na hasira na
kujiapiza kumtafuta huyo aliyeyafanya hayo. Katika uchunguzi
wake hasa kwa mwanamke huyo aliyemnasa kimapenzi kwa kusudi
maalumu, Mwaja, ndipo akamsikia Kamanda Amata.
Alipokutana naye siku hii pale makaburini ilikuwa sadfa tu
kwake. Alimwona tangu machoni kuwa ni mtu hatari asiye na mzaa
na anachokifanya.
“Yule jamaa uliyenitambulisha kwake amenivutia sana,”
Fareed akamwambia Mwaja kwa sauti ya chini.
“Achana na yule jamaa, ni mtata kupita maelezo, usije
ukaomba uingie mikononi mwake, huchomoki…” Mwaja akaeleza.
Maneno haya yalimshtua Fareed, akajiuliza kama Mwaja
amemgundua kuwa yeye ni nani. Akapiga moyo konde.
“Aaaah yeye anapambana na wahalifu, na mi sipo kwenye
kundi hilo…”
“Basi usiwe na hofu, siku moja nitakukutanisha naye… ”
Mwaja akajigamba.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Utampataje?”
“Yule ni mwanaume na hakuna mwanaume jeuri kwa
mwanamke. Alishawahi kunitongoza, hivyo kumpata ni rahisi
sana,” Mwaja akaeleza. Kwa Fareed ikawa furaha moyoni mwake.
Akajiapia, siku akikutana naye tu hatompa nafasi.
Upande wa Amata, yeye alitulia kimya akiangalia kila
kinachoendelea mahali hapo.
Lazimamuuaji au shoga yake awepo eneo hili! Amata akafikiri huku
macho yake yaliyofichwa nyuma ya miwani myeusi yakimtathmini
kila aliyepo msibani hapo. Kila wakati macho yake yalipotua kwa
Fareed, mwili wake ulisisimka.
Shughuli za mazishi ziliendelea, saa moja na nusu baadae kila
kitu kilikamilika. Watu wakaanza kutawanyika, Amata hakutaka
kumpoteza Fareed kwenye macho yake. Akainua mkono wake wa
kushoto na kuifyatua saa yake. Akaikaribisha Karibu na kinywa
chake na kuongea maneno machache tu kwa mtu wa upande wa
pili. Alipoushusha alishuhudia Fareed na Mwaja wakiingia garini.
Gari lile lilipoondoka likamwacha Chiba eneo lile.
Good boy! Amata akamsifu kijana wake na kuvuta hatua huku
akiwapita watu pasi na kusalimia. Alipomfikia Chiba pale alipo
akaingia garini moja kwa moja, na Chiba vivyo hivyo.
“Vipi Kamanda! Umehisi kitu?” Chiba akauliza.
“Kama kawaida… huyu bwana lazima nimtembelee usiku wa
leo, nina miadi naye…” Amata akajibu na kuondoa gari kuelekea
mjini.
“Sakata linaendaje?”
“Kazi ngumu Chiba, lakini kitaeleweka tu,” Amata akajibu
huku akibadili gia na kuinghia barabara ya Ally Hassan Mwinyi.
Chiba akabofya nobu fulani. Kwenye dashboard ya gari lile
kukachomoza luninga mdogo. Akawasha na kubonyeza vitufe
kadhaa. Ramani ya Dar es salaam ikajitokeza na barabara zake.
Doti nyekundu ikajionesha maeneo ya Upanga.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Wapo Upanga,” Chiba akamwambia Amata. Naye akajibu


kwa kutikisa kichwa juu chini. Licha ya kuwa alimhitaji sana huyo
Fareed lakini kilichomuuma moyo ni jinsi gani kampata Mwaja.
Wivu.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

08
Majuma Mawili Yaliyopita…
FAREED aliwasili Tanzania akitokea Pakistan na kuingia
kama mtalii. Alijua maneno kadhaa ya Kiswahili ambayo yaliweza
kuuficha ugeni wake. Mwenyeji wake hakupenda kujitokeza
kumpokea, akamtuma mtu ili amkirimie hilo. Likafanyika bila
tatizo. Fareed alifikishwa kwenye hoteli ya Tiffany ambako huko
angekutana na mwenyeji wake huyo. Fareed alipoingia Tanzania,
naye aliingiza watu wake kwa siri. Aliwaleta kwa kazi moja tu.
Usiku wa saa tatu, siku hiyohiyo ndipo mwenyeji wake
alipokuja kwa mazungumzo na kijana huyo. Mwambope, aliwasili
hapo kwa gari binafsi, akateremka na kuongoza moja kwa moja
mahali walipopanga kukutana, ndani ya hoteli hiyo.
“Bwana mkubwa kaniagiza lile kabrasha tu basi,” Fareed
alimwambia Mwambope.
“Yeye bado anataka kabrasha, siyo rahisi kulipata kama
nilivyomwambia” Mwambope akajibu.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Unachosema ni sahihi lakini ili biashara ile iende, injinia


wake kamwambia lazima apate hilo kabrasha, na bahati mbaya
linapatikana sehemu mbili tu, yaani Urusi na Tanzania. Jambo zuri
pekee ni kwamba kwa upande wa Tanzania ndiyo rahisi kulipata,”
Fareed akamwambia Mwambope.
“Sikatai usemacho, ila ni vipi nitapata hilo kabrasha ndo
mchezo mgumu…”
“Lazima ulipate… mlishakubaliana na Mansoor,” Fareed
alisisitiza. Mwambope alitulia kimya akiwaza na kuwazua jinsi ya
kulipata kabrasha hilo ambalo ndani yake kuna melezo ya kutosha
kuhusu uundwaji wa ndege ile, michoro ya mfumo wake na jinsi
unavyofanya kazi. Zaidi ya hilo pia, kulikuwamo na zile code za siri
ambazo Jamila, Bakari na Joel waliziunda wenyewe na kuzihifadhi.
Hazikutakiwa kuonekana na mtu awaye yote. Si kwamba
Mwambope hakujua ni wapi kabrasha hilo lilipo bali ni jinsi gani
atalipata. Aliyakumbuka makubaliano yake na Mansoor baada ya
kuahidiwa donge nono. Donge lile akalipata sasa utekelezaji wa
kazi ukasubiriwa. Hakujua hata mfanyabiashara huyo aliipata wapi
namba yake ya simu. Alijikuta tu anaingia kwenye kitanzi hicho.
Atatokaje! Kabrasha lile liliondolewa mikononi mwake na
kupelekwa makao makuu ya jeshi baada ya hapo likahamishwa tena
na kukabidhiwa kwa Amiri jeshi mkuu yaani Mkuu wa nchi.
Likahifahiwa huko.
Akili ilimzunguka Mwambope, hakujua anaanzia wapi na ataishia
wapi. Mtu pekee ambaye alijua kuwa anaweza kumsaidia kwa hilo
ni Hasheem pekee.
“Nipe wiki moja, najua tu nitalipata…” alimwambia Fareed
naye akakubali kwa masharti.
“Sawa, kwa kuwa nimepewa wiki moja nyingine nitasubiri
lakini mimi siwezi kuishi hapa mjini bila mke wa muda…”
“Unataka kusema nini?”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Nitafutie wa kuniliwaza moyo wangu wakati nasubiri hiyo


wiki moja,” Fareed akasema wazi.
“Sawa, kesho jioni tukutane kwenye kilabu ya usiku
nitakuletea watu wawili ujichagulie. Mmoja ni katibu wangu na
mwingine ni mfanyakazi mwenzangu ila bado msichana na ana
umbo zuri la kuvutia, hawa hawana mashaka dau lako tu utabeba
mzigo,” Mwambope akamwambia Fareed aliyeonekana kufurahia
jambo hilo. Wakaagana. Mwambope akaondoka zake na Fareed
akabaki kwani katika hoteli hiyo ndipo alipoweka makazi
yake.Usiku wa siku hiyohiyo vijana wanne waliingia Dar as salaam
kwa njia tofauti lakini walikuwa na lengo moja tu. Mmoja aliwasili
na ndege ya Qatar, mwingine aliwasili na ndege ya kukodi kutokwa
Nairobi. Watatu na wanne walifika kwa boti kutokea Zanzibar.

Siku iliyofuata ilimkuta Mwambope akiwa na vimwana wawili


warembo wa sura na wazuri wa maumbo. Kama ilivyokuwa ahadi
yao na bwana Fareed, La Cica Buena iliipokea miadi hiyo. Klabu
hiyo ilikuwa katikati ya jiji la Dar as salaam. Wateja wakubwa
kwenye kilabu hiki waligawanyika makundi mawili; wenye pesa
wanaokja kuzitumbuana wale wanaokuja kuzitafuna pesa hizo.
Fareed aliteremka kwenye taksi iliyomleta kilabuni hapo na
kupokelewa na Mwambope ambaye tayari kinywaji kilitangulia
kichwani mwake. Ndani ya kilabu hicho waliketi sehemu ya watu
maalum. Mahali tulivu, muziki laini na huduma za hali ya juu.
“Karibu sana bwana Fareed,” Mwambope alimkaribisha.
“Shukran!”
“Kutana na Mwaja,” akamtambulisha huku kimshika begani
msichana huyo “… na Maua. Hawa ni rafiki wa karibu sana
kwangu, leo hii nimependa kuja nao kwa kuwa nilijua nitakuwa
nawe rafiki yangu. Ukitaka unaweza oa, wote hawa bado
hawajaolewa…” akachombeza. Fareed alitabasamu na kuivua
miwani yake, akaitia mfukoni. Mazungumzo ya hapa na pale
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

yakafanyika huku Fareed akimtazama Mwaja kwa jicho lenye


ujumbe wa mapenzi. Mwaja hakuwa mgeni na mambo hayo,
alielewa, akalegea. Mwisho wa kila kitu katika kilabu kile cha La
Cica Buena, Mwaja na Fareed wakaenda zao Tiffany hoteli
kuumalizia usiku huo.

Baada ya siku mbili, Mwambope alielekea Zanzibar kwa


minajiri ya mazungumzo na Hasheem kuhusu lile kabrasha
kwakuwa alijua wazi mzee huyo ana kila kitu. Baada ya
mazungumzo marefu, Hasheem alimuahidi Mwambope arudi
kumuona siku mbili baadae ambapo angemwandalia kila kitu. Siku
ilipofika, Mwambope alipoenda tena Zanzibar hakumkuta
Hasheem. Kila alivyotafuta mawasiliano nae hakufanikiwa. Ndipo
aliporudi kwa Fareed na kumweleza habari hiyo ambayo
haikumfurahisha hata kidogo.
“Sawa hilo tutalizungumza nyumbani kwako kesho, nitakuja
kukutembelea,” yalikuwa maneno ya Fareed kwa Mwambope.
“Karibu sana!” Mwambope alimkaribisha.

Kesho yake usiku, kama alivyoahidi, Fareed aliwasili kwa


Mwambope ndani ya kambi ya jeshi ya Lugalo kwenye nyumba za
maofisa na kukaribishwa na yeye mwenyewe.
“Jumba lote hili unaishi peke yako?” Fareed akamuuliza.
“Ndiyo, mke na watoto wangu wako Mbeya…”. Lilikuwa jibu
lililomfurahisha sana kijana huyo maana alijua kuwa sasa kazi yake
itakuwa nyepesi kuliko alivyofikiri kabla.
“Sasa tunampataje Hasheem? Maana muda wangu wa kuwa
hapa unakwisha,” akamtupia swali.
“Kwa kweli sijui... Au la tumpate binti yake… yeye anaweza
kutuambia baba yake kajificha wapi au kaenda wapi au nini
kimempata…”
“Yuko wapi?”
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Anaishi Zanzibar anafanya kazi katika ofisi za mamlaka ya


viwanja vya ndege,” akajibu.
“Kwa nini hukwenda kwake?”
“Kwa kuwa nilihitaji kujadili hilo na wewe kwanza, ili siri hii
isiende mbali lazima mimi na wewe tuamue kila hatua inayotakiwa
kufanyika,” Mwambope akajibu.
“Sijapata kuona mtu mwenye akili kubwa kama wewe!”
Fareed akampaka mafuta kwa mgongo wa chupa.
“Binti yake anaitwa nani?”
“Lukundame Hasheem… huyu ni binti kipenzi cha mzee
Hasheem, atakuwa anajua mengi sana,”
“Sawa, twende usiku huu Zanzibar, nitakodi ndege,”
akamwambia Mwambope, kasha akatazama saa yake, “ muda
umeisha. Nenda kajiandae” akamaliza kusema. Naye akanyanyuka
na kuelekea chumbani. Hapo ndipo Fareed alipokamilisha kazi
yake.

Fareed aliacha kama dakika moja ipite, alipohisi maji


yakitiririka bafuni, akajua sasa ndiyo wakati muafaka kufanya
jambo lake. Akainuka na kupita kwenye korido inayoelekea katika
vyumba vya kulala. Mlango wa jikoni ulikuwa wazi, akapiga jicho
na kukiona kisu kikubwa kikiwa kimepachikwa kwenye henga yake.
Akavuta hatua mbili tu na kukinyakua kile kisu. Akakibana sawia
na kuuwania mlango wa chumba cha Mwambope. Alipousukuma,
ulikuwa wazi. Alipoingia tu akajikuta uso kwa uso na Mwambope.
Jenerali huyo wa jeshi aliyekuwa uchi wa mnyama, macho
yalimtoka mara alipomuona kijana yule akiingia chumbani mwake
namna ile. Kabla hajatahamaki, Fareed alimrukia kwa ustadi akiwa
na jisu lile mkononi. Mwambope akajua sasa hatari imemkabili,
naye akajirusha kumkabili kijana huyo. Kwa ustadi wa hali ya juu
aliupiga teke mkono wa Fareed wenye kisu, kikamponyoka.
Wakavaana na kujibwaga juu ya kitanda. Fareed akalitandua shuka
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

na kumfunika Mwambope na kulifunga katika mtindo ambao


jenerali huyo alikuwa ndani yake. Makonde kadhaa yenye kasi
yakalisulubu tumbo lajenerali huyo lililojaa mafuta. Mwambope
alijitahidi na kujiangusha sakafuni, akajifunua lile shuka na
kumkabili Fareed lakini akachelewa. Kijana yule alikuwa mwepesi
kama unyoya. Pigo moja lililotua sikioni mwa Mwambope
lilimpotezea umakini mtu mzima. Kabla hajatafakari alipokea
mapigo mengine ya weledi na kumpeleka chini. Mwambope
alianguka vibaya na kujigonga kisogo sakafuni. Fareed alimuwahi
na kumkaba koromeo lake. Mwambope alitoa macho mpaka roho
ilipouacha mwili.
Fareed alibaki akitweta. Alipokumbuka kuwa yupo eneo LA
hatari, ndani ya kambi ya jeshi, aliinuka na kuuburuza mwili ile
mpaka bafuni. Kwa kutumia kile kisu, akautoa macho na
kuuning'iniza kwenye bomba LA kuogea. Alipohakikisha kazi yake
imekamilika, akatoka na kukiacha kile kisu jikoni kisha akatokomea
kwa njia ileile aliyoijia.

* * * *
Amata aliwasili katika ofisi yake pale kwenye jengo la JM Mall,
ghorofa ya sita. Gina, mara tu alipomkaribisha bosi wake
akamkabidhi bahasha aliyoichukua posta asubuhi ya siku hiyo.
“Imetoka wapi?” akauiliza.
“Ah ntajuaje? Muhuri unasoma Zanzibar,” Gina akamweleza
wakati Amata akiendelea kuichana ile bahasha. Akaifungua karatasi
iliyo ndani, iliandikwa kwa mwandiko mzuri wa kike. Haikuwa
mistari mingi; michache yenye maana.

‘Naomba umlinde baba yangu, mstahafu wa JW Mzee Hasheem kuna


watu wanataka kumuua.
Siwajui. Nimemficha katika nyumba yake ya siri shambani
Bwejuu, Zanzibar.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Maisha yetu kama familia yako hatarini.


Tunahitaji msaada wako wa hali na mali.
……Lukundame!’

Kamanda Amata alijikuta akipatwa ganzi mwili mzima.


Aliigeuza ile karatasi na macho yake yakakutana na picha ya watu
watatu. Mzee Hasheem, Lukundame na Jamila. Chini ya picha ile
kuliandikwa sentensi moja, ‘naomba uilinde familia yetu’. Sentensi ile
iliishia hapo. Akaitua ile barua na kuiweka mezani. Akashusha
pumzi ndefu na kujiegemeza kitini.
“Vipi?” Gina akauiliza.
“Jambo limeshaharibika…” Amata akajibu.
“Kivipi?”
“Hii barua ingefika wiki iliyopita ingekuwa na thamani kuliko
sasa,” Amata akaeleza huku akimpa Gina karasi ile. Gina akaisoma
na kuigeuza nyuma, akaitazama ile picha, “hawa ni nani?” akauliza.
“Dah! Huyo mzee ameshakufa, huyo mwingine haijulikani
kama mzima au la, huyo mrefu ametekwa,” Amata akaeleza.
“Sawa, sasa huyo marehemu hana thamani tena… hapa cha
kufanya ni kumpata huyu aliyetekwa kisha kujua kuhusu huyu
mwingine,” Gina akautoa ushauri. Amata akatikisa kichwa juu
chini kuonesha amekubaliana na ushauri huo. Akainuka kitini na
kuwa wima.
“Ndo kazi imeanza?”
“Yes!” akajibu.
“All the best”
“Asante,” Amata akajibu na kuiacha ofisi hiyo, akatokomea
mjini.
Ndani ya gari lake, aliifungua ile luninga na kuangalia kijana
yule atakuwa wapi ndani ya jiji la Dar es salaam. Ramani yake
ikaonesha kuwa gari analolitumia Fareed lipo jirani kabisa na jengo
la JM Mall.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Amenifuata! Amata akawaza. Akawasha gari na kuingiza


barabarani. Akakamata barabara ya Samora kuelekea mzunguko wa
picha ya askari. Huku bado akitazama ile ramani, aliona lile gari
likiwa katika barabara ileile likifuata uelekeo uleule. Akataka
kuhakikisha kama kweli linamfuata au la. Akazunguka mzunguko
wa askari na kurudi alikotoka huku akiisoma ile ramani yenye GPS
kuona ni wapi gari hilo litaenda. Akiwa tayari kwenye mzunguko
wa mnara wa saa, akakunja kulia na kuingia barabara ya Uhuru.
Sasa akawa na uhakika kabisa kuwa anafuatwa. Hakujua kama
kwenye gari hilo yupo Fareed na Mwaja au Fareed peke yake.
Huku mkono ukiwa katika usukani, akainua simu yake na kupiga
namba ya simu ya Mwaja.
“We si umenipotezea bwana…” sauti ya Mwaja aliyeonekana
kama katoka usingizini iliyafikia masikio ya Amata.
“Sawa, naona huyo bwana wa Kiarabu amekuzuzua,” Amata
akamwambia.
“Niache nifaidi mapigo ya kisultani…”
“Sawa, ila hujui kama umekaribisha nyoka ndani mwako.
Naomba tuonane usiku huu…” Amata aamwambia Mwaja.
“Leo siwezi, niko fungate, njoo kesho ofisini,”
“Leo utakuwa wapi?”
“Nit…”
Kabla hajamaliza kusema alilotaka kusema, ile simu ikaporwa.
Amata alitaka tu kujua kama Mwaja yupo kwenye lile gari au la.
Lakini sasa alihofu kuwa hata Fareed hayupo katika gari lile. Kama
kuna kitu kilimuuma ni alipowaza tu kuwa kimwanaume hicho
kitakuwa kinagalagala na Mwaja jioni hiyo, kikipewa kila raha.
Alipofika njia panda ya Uhuru na Msimbazi, akakunja kushoto na
kushika barabara ya Msimbazi kuelekea ile ya Nyerere. Alipoyafikia
makutano hayo akanyoosha na kuikamata ile barabara ya Kilwa,
akaongeza kasi. Alipopiga Jicho kwenye runinga yake akaona bado
lile gari linamfuata. Hakuumiza kichwa,akatoa gari lake nje ya
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

barabara na kusimama. Akahesabu gari la kwanza, la pili, la tatu, la


nne, la tano lilikuwa Mark X. Naam ndilo. Ndani kulikuwa na
kijana mmoja lakini si Fareed. Lile gari nalo likaiacha barabara na
kusimama nje ya duka moja kubwa la spea za magari. Yule jamaa
hakushuka.
Kamanda Amata akateremka na kuvuka upande wa pili wa
barabara. Akaambaa ambaa na ile barabara mpaka usawa wa lile
gari. Akavuka tena kurudi upande ule, akaibukia palepale kwenye
lile gari. Akagonga kioo cha mlango wa dereva, yule kijana
akageuka na macho yake yakagongana na Amata. Yakagongana na
macho yasiyo na masihara hata kidogo.
Yule bwana akatia gia kutaka kuondoka, akachelewa. Konde
moja likapita na kioo na kutua sawia shavuni mwake. Amata
akafyatua Loki na kufungua mlango. Akamkamata kisogo yule
mjinga na kumbamiza kwa nguvu kwenye usukani, akawa
mwekundu. Watu wakaanza kukusanyika eneo lile wasijue nini
kinaendelea. Akamvuta nje na kumuegemeza kwenye lile gari,
wakatazamana.
“Umenifuata! Umenipata…” Amata akamwambia yule jamaa.
Ghafla, Amata akajikuta chini. Alipigwa ngwala saa ngapi, hajui.
Yule kijana akawahi kuingia kwenye gari lake kwa minajiri ya
kutoroka. Hapana,alivuta bastola yake kutoka kwenye dashboard na
kurudi upande ule. Kamanda Amata alipojinyanyua akakutana na
guu la kifua lililomrudisha chini. Yule jamaa akaweka tayari bastola
yake ili ammalize Amata. Kitendo bila kuchelewa, Amata aliupiga
mguu wa yule jamaa ukatoka pale kifuani. Akajiviringa kidogo tu
na ile risasi ikachimba chini. Watu wakaanza kutawanyika ovyo
huku na huko. Yule bwana alipotaka kufyatua risasi ya pili akajikuta
akipiga yowe la uchungu. Amata alimpelekea pigo la nguvu kwenye
korodani. Akajitoa pale chini na kujiinua kwa ufundi. Teke moja
lililopigwa kwa hasira likampeleka yule jamaa chini. Akajaribu
kuinuka na kukutana teke lingine lililotua sawia usoni pake,
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

likavunja mwamba wa pua. Amata akasimama na kujishika kiuno,


akimpa ishara kijana yule ainuke. Alishindwa. Akamnyanyua na
kumtia pingu iliyokuwa mfukoni mwake. Akamtumbuliza kiti cha
nyuma. Wakati anataka afungue mlango wa dereva ili akaenyuma
ya usukani, mkono mwororo ukamshika kiganja chake na
kukiondoa kwenye kile kitasa.
“One mistake, one goal… chunga mzigo wako”.
Amata alipomtazama mwanamke huyo, akatikisa kichwa,
Gina. Akaingia siti ya nyuma na kumbana sawia mtu wake. Gina
akatia moto gari mpaka kituo cha kati. Wakamteremsha na
kumkabidhi kaunta.
“Huyu vipi?” askari mmoja akauliza.
“Mwekeni shimoni, nitarudi baada ya dakika chache,”
akawapa maagizo na kuondoka zake mpaka kwenye lile gari.
Wakaanza kulipekua hapa na pale. Ndani ya droo ndogo katika
dashboard ya gari hilo, Amata alichukua kadi ya umiliki na kusoma
kujua mmiliki wa gari hilo. Hakuamini macho yake.
Mwaja J. Kalinga! Akalisoma jina lile. Amata akajikuta
anashindwa kumuelewa mwanamke huyu.
Nitamshikisha adabu! Akajisemea na kurudi katika ile kaunta,
“naomba mwenye gari hili akamatwe mara moja,” akatoa amri.
Akarudi na kukusanya vikolokolo kadhaa, akavitia kwenye mfuko
na plastiki ikiwamo bastola ya yule jamaa. Akavikabidhi kaunta
alipoona havina maana kwake.

* * * *

Mansoor aliona jumba lake kubwa kuliko alivyotegemea.


Aliingia huku akatokea kule, akazunguka sebule yote mpaka
mwisho, kichwa chake hakikupata jibu. Kilichomshtua ni sauti ya
simu iliyoita kwa fujo kutoka mezani kwake. Akaiendea na
kuinyakua kwa shauku, akaiweka sikioni na kutulia.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Hahahahahaaaaaa” sauti ya upande wa pili ikaanza kwa


kucheka. Kisha ikaendelea, “nadhani sasa biashara yetu itafanyika”
sauti ile ikasema. Mansoor alitulia kimya akimtafakari huyo
aliyempigia simu, Jenerali Kahir.
“Kahir, ulichokifanya si kizuri hata kidogo… narudia kauli
yangu ileile, mwenye kisu kikali atakula nyama,” Mansoor akamjibu
huku sura yake akiwa kaifinya kwa gadhabu. Aliujua mchezo
ambao Kahir tayari alikuwa akimchezea.
“Najua unayo code namba tatu, lakini hiyo isikufanye uamini
kuwa utapata utakacho, hasilan abadan!” Mansoor akamwambia.
“Ok ngoja tuone, kila kitu utaniuzia na usipoangalia utanipa
bure,”
“Thubutu yako!”
Ile simu ikakatika. Mansoor, akairudisha kwenye kitako chake
na kujitupa kochini. Dakika mbili baadae, akainua tena ile simu na
kupiga mahala pengine.
“Kahir ametuzunguka,” akamwambia Fernandez
“Kivipi?”
“Ameipata code namba tatu” Mansoor akaeleza.
“Ah! Fanculo!!!” Fernandez akajikuta ametukana. Fernandez,
upande wa pili, akajikuta nywele zikimsimama, hakujua afanyeje.
Akairudia tena simu na kuiweka sikioni, “tumfanye nini mshenzi
huyu?” akamuuliza.
“Naendelea kumtafakari, nitahitaji kikao na wewe ndani ya saa
ishirini na nne,” Mansoor akaeleza.
“Sawa, nasubiri kwa hamu… mshenzi huyo hana maana”.
Akang’aka Fernadez.
Mansoor akaweka simu ile chini na kunywa maji funda moja zito.
Nitamshughulikia Kahir na ujeuri wake! Akajisemea moyoni.
Akaita vijana wake na kuwataka sasa kuifungua code ya pili
ambayo anayo Bakari. Ile ya Joel walishaipata, akaona kabla

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

mambo hayajaharibika basi awe tayari na ile ya pili mkononi


mwake.
Bakari alikuwa peke yake ndani ya kile chumba. Hakujua
mwenzake alipelekwa wapi baada ya kutolewa mule ndani siku tatu
zilizopita. Mawazo, njaa, uchovu vilimtafuna. Afanye nini?
Hakuna. Alibaki mpole akisubir Siku ya hatima yake. Akiwa katika
kukabiliana na shida hizo zote mlango ule wa chuma ukafunguliwa.
Watu walewale waliomchukua Joel ndiyo waliingia tena mara hii.
Hawakuongea. Walikiendea kiti alichoketi kepteni huyo na
kukilegeza vifungo vyake, wakamchukua kikondoo na kumpeleka
kwa bwana wao.
Angalau Bakari aliona mwanga baada ya wiki mbili za kuwa
ndani ya chumba kile. Ijapokuwa haukuwa mwanga wa matumaini
lakini ulimtia faraja. Wale jamaa wakambwaga sakafuni mbele ya
Mansoor. Bakari akajaribu kuinua uso wake amwone huyo
aliyeletwa kwake, hakuweza. Mansoor alimtazama Bakari pale
sakafuni.
“Shida yangu ni moja tu kwako,” Mansoor aliongea taratibu
huku akivuta hatua na kuketi kwenye kiti kilichokuwa kando yake.
Bakari aliweza kuinua uso wake na kumtazama tajiri huyo.
“Sina haja ya kurudia, najua unajua nitakacho haya niambie
kabla sijatengenisha kichwa na kiwiliwili chako,” Mansoor akasema
huku akiufuta upanga wake kutoka alani. Wakati yote hayo
yakitendeka, kijana mmoja alisogeza lile sanduku lenye mtambo
maalum waliouondoa katika ile ndege. Mfumo wa kujihami wa
usalama wa anga. Mansoor akalifungua, na kuliwasha. Ijapokuwa
hakuweza kuona sawasawa lakini bip zilizokuwa zikisikia alizielewa.
Wameshapata code moja washenzi hawa! Akawaza wakati akitafsiri
ile milio iliyokuwa ikitoka kwenye ule mtambo.
“Yule ndugu yako nimemwacha huru baada ya kunipatia code
yake. Na wewe ukinipatia ya kwako utakuwa huru, ya tatu hatuna
wasiwasi, tumeshaipata huko Pakistan na leo hii itakuwa hapa, haya
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

kwa haraka taja bila kumumunya maneno…” Mansoor


akamwambia huku akitoa ishara kwa vijana wake wajiandae. Wale
vijana kila mmoja akatoa mjeledi na kuuweka sawia, tayari kwa
kazi. Bakari alitulia kimya hakujibu neno. Moyoni mwake alikuwa
akisali kimyakimya kumuomba Mungu wake. Mjeledi mmoja
ulioshuka mgongoni mwake ulimfanya apige kelele za maumivu.
Kabla hajatulia akatandikwa mwingine na mwingine. Vipigo vya
mijeledi vilimwacha akiwa hoi. Mgongo wote ulichakazwa kwa
kipigo kile.
“Haya, nambie, sipendi kukuua kijana mdogo kama wewe!”
Mansoor akamwambia Bakari aliyekuwa chini kimya. Hakujibu.
Ikaletwa chano yenye vikolokolo tofauti, mkasi, bisibisi, koleo,
misumari, nyundo na vinghine vingi. Bakari akageuzwa chali,
akavuliwa suruali. Macho yake yalikuwa yamefumba yakipoteza
nguvu za kuona sawasawa.
“Usiwe mjinga kijana, utateseka bure, hii biashara imefanywa
na wakubwa wako wa kazi huko Tanzania… ninyi ni chambo tu,”
Mansoor akamwambia Bakari. Maneno hayo yalimfanya afumbue
macho. Akapepesa huku na huko.
“Mkkubwa gani atttafanya haya?”
“Hahahahaaaaa, mkubwa gani! Mkubwa wako aliyekutuma
Urusi ndiye yupo kwenye mpango huu… na kuna mmoja kwa
ujeuri wake amekwishauawa huko Tanzania, sasa wewe ni nani
ujifanye Mzalendo ilhali walio juu yako wanakutoa sadaka? Nipe
hiyo code haraka,”
“No!” Bakari akajibu kwa neno la herufi mbili tu. Akashikwa
vizuri, na Mansoor akachukua koleo na kumbana Bakari kwenye
korodani.
“Nooooooo,aaaaaa weweee, nasema…”
“Semaaaa!”
“Niache kwanza nnnnaaasema..” Bakari Akalia kwa uchungu
kama mtoto. Baada ya kibano cha maana akajikuta akiropoka kitu.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Kwa Mansoor ilikuwa ni kicheko na tabasam. Wakachukua ile code


na kuiingiza kwenye ile kompyuta kujaribu kama ni sahihi.
Haikukosewa, ule mfumo ukaikubali. Baada ya kupakia faili kadhaa
ukadai code ya tatu ili uweze kuanza kazi yake.
“Hahahahhhhh swadakta” Mansoor alifurahi sana, “sasa bado
ya mwisho, nacheza na mjinga Kahir sasa mpaka niipate” akasema.
Akamtazama Bakari pale chini, akaamuru wamwondoe
wakamuweke na mwenzake upande mwingine. Ikawa hivyo.
Katika chumba kingine, tofauti na kile Joel alimpokea Bakari
akiwa hoi hajitambui. Mara baada ya wale vijana kumtupa na
kufunga lile lango, Joel akatambaa kumsogelea swahiba wake,
akamtikisa, hakuamka, akampapasa hapa na pale, kisha akatulia na
kujiegemeza ukutani.
Hakuna marefu yasiyo na ncha! Joel akawaza. Hakuwa na la
kufanya zaidi ya kutulia na kusubiri kudra za Mwenyezi Mungu. Saa
mbili baadae Bakari alijitikisa, Joel akashtuka maana alijua wazi
kuwa mwenzake huyo hatoweza kuinuka tena kutokana na
majeraha aliyoletwa nayo. Joel akamtazama Bakari aliyekuwa
amelala kifudifudi, akamgeuza na kumuweka chali.
“Beka! Beka!”
Hakuitika. Zaidi alikuwa akijitikisa mara kwa mara. Chumba
kile chenye ukubwa wa wastani kilikuwa na harufu nzito, joto, na
hewa pungufu. Siku zote alizokaa Joel Mansoor alijua kwa
vyovyote atakua amekufa. Hata walipomleta Bakari hawakuwa na
haja ya kutazama hilo. Siku ya kwanza aliamini kuwa hatoimaliza
kutokana na hewa chafu ya mule ndani. Katika kuhangaikahangaika
akagundua tundu dogo la kipenyo cha msumari. Alipoweka pua
yake hapo aliweza kuhisi hewa ya ubaridi, hewa safi. Hapo pakawa
mahala pake pa kuketi. Akajivuta na kumfikia Bakari, akatumia
nguvu kidogo alizonazo na kumsogeza karibu na pale alipoketi.

* * * *
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Kamanda Amata aliingia ofisi ndogo na kukutana na Madam


S. Wakasabahiana, na moja kwa moja akaiendea kompyuta ndogo
iliyopo meza ya kando ili kuweka data fulani. Madam S
hakumsemesha chochote kwani alijua kijana wake. Alimsubiri
amalize ndipo amhoji mawili matatu. Kila mmoja aliendelea na kazi
yake kwa dakika kama mbili hivi au tatu. Alipomaliza, akaifunga
kompyuta ile.
“Enhe, maana naona tu mtu kulupu kwenye kompyuta,”
Madam akamwambia.
“Mambo yameanza kunoga,” akamjibu.
“Enhe usinambie…”
“Ndo hivyo, kaa mkao wa kula, wazee mtaumbuka muda si
mrefu”
“Toba! We mtoto we!”
Wakiwa katika kuongea simu ya Amata ikaita. Akaipokea
nakuiweka sikioni. Alikwishaijua namba hivyo hakujiuliza mara
mbili.
“Fika central haraka,” akaambiwa.
“Vipi?” Madam S akauliza kwa shauku.
“Simbeye, ananihitaji central”
“Kuna nini?”
“Nakwambia mambo yameanza kunoga makaburini… pale
central kuna mzigo nimmeuacha,”
“Sawa, fanya yote ila jioni kama kawaida” Madam
akahitimisha mazungumzo yake. Akatoka na kuiacha ile ofisi. Nje
hapo akachukua taksi na uondoka zake.
Alipofika tu kituo cha polisi cha kati, akapokelewa na kufikishwa
katika ofisi ya Simbeye. Ndani ya ofisi hiyo alikuta watu wawili tu.
Simbeye mwenyewe na Mwaja akiwa ndani ya sare zake za jeshi.
Simbeye akamtaka Amata kuketi. Mshtuko wa wazi ulionekana

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

katika sura ya mwanamke huyo. Hakutegemea kukutana na kiumbe


huyo mahala hapo.
“Karibu Kamanda,” akamkaribisha na kumsabahi, “huyu
ndiye mmiliki wa lile gari, amefika,” Simbeye akamwambia Amata.
Amata akamtazama Mwaja kwa tuo. Sura ya Kamanda ilionekana
kutokuwa na mzaha hata kidogo.
“Samahani afande kwa kukusumbua, maana tumekutoa
kazini. Lakini kuna jambo dogo ambalo ninahitaji au idara yangu
inahitaji kujua kutoka kwako…”
“…hujajitambulisha we nani, unatoka idara gani, enh! Lazima
nikujue, mi siwezi kuhojiwa au kuitwaitwa kwenye kiofisi kama
hiki, mimi ni afisa wa jeshi. Kwanza hamjafuata utaratibu, mi
nimekuja hapa kwa sababu tu ya kurahisisha mambo, si kuanza
blah blaha hapa,” Mwaja kajitutumua. Amata akamtazama
mwanamke huyo kwa jicho la hasira na gadhabu. Nitakutia adabu,
kuku wa kike wewe! Akajisemea moyoni.
“Naitwa Kamanda Amata, afisa wa usalama wa taifa
Tanzania, invinsible unit, code 005unstopable human being, TSA 1.
Umeridhika? Mimi ni binadamu pekee ninayeweza kumkamata mtu
yeyote nchi hii nikamhoji popote ninapotaka na nisiulizwe na mtu.
Dharau zako weka kando unaweza usitoke tena humu ndani kama
ilivyo kwa huyo bwege wako niliyemsweka shimoni”. Maelezo ya
Amata yakawa mazito kuliko tambo za Mwaja na uanajeshi wake.
Meja Mwaja alishtushwa na kauli ya Amata.
Nani kaswekwa huku tena? Akajiuliza. Amata akamsogezea kadi
ya gari.
“Unalitambua hilo gari?” akamuuliza.
Mwaja alihisi ganzi mwili mzima. Alielewa kuwaa hill ni swali
LA mtego tu.
“Ndiyo” akajibu.
“Linamilikiwa na nani kihalali?”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Mimi mwenyewe, na ndilo gari langu la kutumia muda wote”


akajibu.
“Leo siku nzima gari lako lilikuwa wapi?”
Mwaja akatulia, angejibu nini wakati Amata alimwona na gari
hilo kule Kinondoni.
“Nilikuwa nalo mpaka saa saba mchana kisha nikamwachia
rafiki yangu aliyeniahidi kunifuata kazini jioni hii lakini sijamwona,
ndipo nikapata wito wa kufika huku,” akajibu kwa ufasaha.
“Sawa, sasa nasikitika kukwambia kuwa gari lako lipo hapa
central, limekamatwa katika uhalifu. Gari lilikuwa likitumiwa na
jambazi mwenye silaha,” Amata akamwambia Mwaja. Mwaja
akalowa kwa mawazo.
“Je una urafiki na watu wa namna hii?” Simbeye akahoji kwa
sauti yake nzito. Mwaja akamtazama mzee huyo, “hapana labda
iliibwa…”.
“Ok!” Amata akakabidhiwa mfuko wa plastiki wenye vitu
vilivyochukuliwa kwenye lile gari pamoja na ile bastola ikiwa ndani
yake.
“Unavitambua vitu hivyo?”Mwaja akavitazama kwa macho na
kutikisa kichwa kushoto kulia kuwa havitambui.
“Asante sana kwa ushirikiano wako. Tutakuhitaji tena
itakapobidi. Kwa sasa gari lako litabaki hapa, tunapeleleza kama
liliibwa au ulilikodisha, tukishapata jibu stahiki tutakuhitaji tena.
Unaweza kwenda afande,” Amata akamruhusu Mwaja wakati na
yeye akiwa wima.
“Mbona mmenihoji kienyeji hivyo? Hakuna pa kundika vipi
mkigeuza maelezo hapo baadae?”
“We nenda, karatasi utaikuta kaunta, saini uende!” Amata
akamtazama Simbeye, “mzee asante!” akamshukuru na kuondoka
zake. Si kwamba alitoka nje ya jengo lile, bali alikwenda kwenye
chumba maalum cha mahojiano. Ndani ya chumba hicho
alikuwamo yeye pekee. Mbele yake kulikuwa na meza moja ndogo
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

na kiti kimoja cha ajabu ajabu hivi. Mlango ukafunguliwa, askari


mmoja aliyevaa kiraia akaingia na yule jamaa aliyetaka kumuua
Amata. Akaketishwa kwenye kile kiti na kufungwa. Yule askari
akasimama pembeni.
“Nahitaji majibu yaliyonyooka ili nikaendelee na kazi zangu”
Alianza kwa kumwambia. Yule jamaa akatikisa kichwa.
“Unaitwa nani na ni raia wa wapi?” akamuuliza.
“Naitwa Nasiyahd, raia wa Kazakhistan…” akajibu.
“Unaweza kunieleza gari namba T 0X5 TTP ulilipata wapi?”
“Nilipewa,”
“Na nani?”
“Na kaka yangu,”
“Kaka yako anaitwa nani?”
“Fareed,”
“Fareed?”
“Ndiyo…”
“Kule Khazakhistan mnafanya shuguli gani?”
Swali hili likamfanya Nasyahd kunyamaza. Akatafakari jambo.
“Nijibu…” Amata akamwambia.
“Biashara…”
Amata akamtazama kijana huyo kwa tuo, hakummaliza.
“Hapa Tanzania mmekuja kufanya nini?”
“Biashara!”
“Ya kuteka watu?”
“No! Hatuteki watu sisi…” Nasyahd akahamaki.
“Ninyi hamteki watu? Mbona ulikuwa unanifuata na gari na
ukadiriki kunishambulia na silaha, hukutaka kuniua?”
“Hapana! Mimi ni mfanyabiashara lazima kujilinda muda
wote… wewe ulikuja kunishambulia na mimi nikajilinda…”
Amata akamsiliza kwa makini kijana huyo, akastahajabu kwa
jinsi anavyojiamini na kujibu pasi na kuteteleka.
“Kule Zanzibar mlifanya nini?”
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Zanzibar? Mi sijaenda Zanzibar…”


“Sijasema kuwa ulienda Zanibar, nimeuliza Zanzibar mlifanya
nini?”Nasyahd macho yalimtoka Pima “sijuiiiii!”
“Unajua… niambie, Lukundame mmemteka mmempeleka
wapi?” Amata akamhoji kwa ukali.
Nasyahd akabaki kimya. Amata akamtazama kijana huyo.
“Niambie, Lukundame yuko wapi?”Nasyahd hakujibu.
“Jeuri siyo?” Amata akainuka na kuzunguka upande ule
ambao kijana yule aliketi. Akampa ishara yule askari ampatie mkasi.
Ukarushwa. Akaudaka. Amata akamtandika Nasyahd kofi la sikio,
kisha akamdaka kichwa na kuupachika mkasi kwenye sikio la kulia.
“Nambie, Lukundame yuko wapi?”
“Si-si-sijui…”. Amata akakata sikio kidogo, damu zikaanza
kutiririka. O-200721-P029021-K
“Nooooooo niache! Niache…”
“Sikuachi mpaka unambie Lukundame yuko wapi?” Amata
akahoji huku akiendelea kulikata sikio. Nasyahd alitoa kilio cha
uchungu huku akiongea maneno yasiyoeleweka. Aliendelea kupiga
kelele za uchungu, damu zilitapakaa katika bega lake mpaka
kifuani. Amata hakujali hilo, aliendelea kuuminya ule mkasi nao
ukaendelea kukata nyama ya sikio.
“Niacheeeee nasema nasema, aaaa!” akapiga unyende.
“Sema!”
“Bagamoyo, Bagamoyo… niache tayari nishasema!”
“Bado… Bagamoyo sehemu gani”
“Nunge… Nunge beach… kuna meli mbovu imeegshwa
ooooooooh aaaaa asss umeniumiza ms*enge wewe!”
Amata Alimwacha Nasyahd sikio likiwa linaning’inia, “mpeni
matibabu, kesho nakuja kukata jingine,” akamwagiza yule askari.
Nasyahd aliposikia kukata jingine akashtuka na kumwangalia
Amata aliyekuwa akivua gloves zake za mpira baada ya kumaliza

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

kazi. Akatoka na kurudi ofisini kwa Simbeye na kumkuta amesinzia


kitini.
“Mwili unakushinda sasa!” akamwambia. Simbeye akagutuka
na kujiweka vema kitini, akajifikicha macho na kumtazama Amata.
“Ah! Nimechoka sana, nyie na bibi yenu mnalala mnakula
maisha wenzenu tunakimbizana na majambazi usiku kucha…”
Simbeye akasema, “enhe, amekunya?” akauliza.
“Hah! Asinye tena? Amekunya, sasa nataka kuchunguza kama
kinyesi chake ni sahihi. Naweza pata chopa?”
“Sasa hivi?”
“Ndiyo!”
“Mh sijui, maana Leo kulikuwa na operesheni maalum kule
Amboni, nilisikia wakizungumzia hizo chopa kuwa zitumike”
“Kuna eneo nataka nilichunguze kutoka juu kabla sijalivamia
kijeshi usiku huu,” Amata akaeleza.
“Nyi' wakubwa bwana, mkimpigia Rais tu atawapa chopa yake
ya Ikulu”
“Ahahahahahhhhh” wakacheka pamoja.
“Yule mwanamke ameondoka?” Amata akauliza.
“Yap…. Afanye nini wakati we umempa karinye hapa…
umeja wote ukampotea…”
“Anadharau ofisi za watu…”
“Ndo hivyo! Pale alipo hajui ana msala mkubwa wa
kumpeleka jela maisha…”
“Aaaaaaa TSA 1! We wa kumpeleka mrembo kama yule jela?
Akikupa tu kiuno utasahau kila kitu, nani asiyekujua…. Hivi yule
meja akiujua tu udhaifu wako umekwisha…”
“Naona ushanichoka, kwaheri!”
“Haya tutaonana, nikipata chopa nitakwambia ngoja niwapige
polisi anga!” Simbeye alimaliza mazungumzo yake na Amata.
Mazungumzo ambayo ungeweza kufikiri ni utani kumbe yalibeba

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

ujumbe mkubwa wa kikazi kati yao. Nje ya kituo hicho Amata


akachukua taksi na kuondoka zake.

* * * *
Mansoor alibaki kimya akimtazama Mwaja aliyekuwa akimpa
habari ya yaliyomkuta jioni hiyo. Mwaja alikuwa akimlalamikia
Mansoor kuhusu gari. Alichojichanganya Mansoor ni kusema tu
kuwa gari lile alimpa rafiki yake. Akaona wazi kuwa sasa muelekeo
wa penzi hilo bandia utapata ukakasi muda si mrefu. Si kwamba
hakujua kama Mwaja ni mwanajeshi, la, alijua vyema. Siri yake yeye
ni kutaka kuchota na kupata habari za kiusalama kutoka upande
huo. Hakujua kuwa swala lile ijapokuwa lilikuwa likifukuta jeshini
lakini uchunguzi wake ulikuwa kwa siri katika mikono ya raia
wema.
Siku zake za kuwapo Tanzania zilikuwa ukingoni, kazi yake
aliyotumwa na matajiri wake Fernandez na Mansoor ilikuwa
ngumu kuliko alivyofikiri. Kupata kabrasha lenye zile code tatu kwa
mara moja. Haikuwa rahisi, akajikuta amemuua Mwambope,
akamteka Lukundame na baada ya hapo mambo yakawa alijojo.
Alipomuona Amata katika kumbukumbu ya kamera za usalama
nyumbani kwa Hasheem akamsaka kwa minajiri ya kuchukua kile
alichochukua. Kabrasha.
Mwambope, marehemu, alimhakikisia Mansoor kulipata kabrasha
lile kupitia Hasheem kwani alimtafsiri mzee hiyo kama ‘Retired but
Extremely Danger’. Siku hii akajikuta akipoteza vijana wake wawili na
kukamatwa kwa boti waliyokuwa wakiitumia. Pigo! Akajikuta ana
hamu ya kumfahamu na kukutana na kiumbe huyo. Hamad! Uso
kwa uso msibani, hakuamini kama anayetambulishwa kwake ndiye.
Akagundua kuwa Mwaja anamfahamu mtu huyo, alipomhoji
kirafiki akathibitishiwa utata wake. Woga ulimwingia jioni hiyo
alipopewa taarifa na Mwaja kuhusu gari lile. Anajua kuwa alimpa
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Nasyahd kati ya vijana wake wawili waliobakia. Alisawajika kwa


mawazo.
Jioni hii akiwa katika mgahawa wa Addis in Dar na kipenzi chake
Mwaja, Mansoor hakuwa na raha hata kidogo. Maswali yasiyo na
majibu aliyojiuliza yalizidi kumdidimiza kwenye shimo la mawazo.
“Hauko sawa leo!” Mwaja akamwambia.
“Jambo ulilonambia limeniweka njia panda, yule kijana
ninamfahamu ameanza lini ujambazi wa silaha? Isitoshe wewe
mmiliki wa gari ni mwanausalama huoni nakuweka pabaya?”
Mansoor alizungumza kwa hisia kana kwamba ni mtu mwema
kumbe lol.
“Usijali, litaisha tu, ndugu yako nitamtoa na gari langu
nutalipata…”
“Lini?”
“Hiyo kazi ya kesho,” akampa faraja na kumficha kama
amekutana na Amata huko kituoni. Kwa upande wa Mwaja
kilichokuwa kikimtia wasiwasi na kumuweka kwenye wakati
mgumu ni kujua kwamba kesi hiyo ipo kwa Amata. Maana yake
haipo polisi isipokuwa chini ya usalama wa taifa, alihaha.
Atamuanzia wapi Amata? Akajiuliza. Ukimya ukapita wakati
wakiendelea na kula na kunywa. Giza lilizidi kutaradadi, Mansoor
aliitazama saa yake, saa mbili kasoro robo.
“Nahitaji kwenda Bagamoyo usiku huu!” akamwambia
Mwaja.
“Kuna nini?”
“Si unajua mambo ya biashara, kuna watu inabidi nikutane
nao kuile,”
“Ningekusindikiza kama kesho ningekuwa siingii kazini…”
“Yeah, lakini basi, nitarudi usiku huu huu…” akamwambia.
“Utarudia kwangu au Tifanny hotel?”
“Chagua” Mansoor akampa uhuru Mwaja.
“Uje nyumbani, nitakuhitaji sana alfajiri ya kesho…”
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Sawa!”

* * * *
Katika anga la Bagamoyo, jioni ya saa kumi na mbili, ndege
moja ndogo ilikuwa ikirandaranda na kuzunguka bahari kisha kuja
tena pwani. Watu waliokuwa ufukweni mida hiyo walikuwa
wakiishangilia hasa watoto kwa kuwa ilikuwa ikipita chini sana.
Ndani ya ndege hiyo alikuwamo Kamanda Amata akiangalia
kile anachokitaka. Scoba alikuwa katulia akikiongoza kwa weledi
mkubwa chombo hicho cha watu wawili tu.
“Zunguka kuelekea Maghalibi,” Amata akamwambia Scoba.
Naye akafanya hivyo, Amata akatazama kwa umakini kwa kutumia
darubini yake huku akichukua picha kadhaa. Aliporidhika akamtaka
Scoba kurudi.
“Umeridhika au nitue kabisa?” Scoba akamtania.
“Ngoja nishuke kwanza halafu utue peke yako!”
Dakika kumi na tano baadae, tayari walikuwa uwanja wa
ndege terminal 1. Wakaingia kwenye gari na kuondoka zao.
“Kwa hiyo, tutarudi tena?”
“Ndiyo, nipitishe nyumbani, kuna vifaa vichache vya
kuchukua, halafu ongea na Simbeye kuwa tunahitaji boti iendayo
kasi…”
“Kwani kuna nini braza?”
“Kuna mateka pale inabidi aokolewe usiku huu kama ni
kweli…”
“Nimekupata, kazi imeisha” Scoba akamjibu wakati
wakiikamata barabara ya Nyerere kuelekea mjini. Saa tatu usiku
iliwakuta katika kituo cha polisi cha wanamaji eneo la Magogoni
ambapo hapo uhifadhi boti zao. Taarifa ya operesheni hiyo fupi
tayari ilisainiwa na HOT kilichobaki kilikuwa ni utekelezaji tu.
BMW jeusi likaegeshwa nje ya kituo hicho. Daktari Jasmini

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

akateremka na mkoba wake. Suruali yake ya mpira na jaketi lake


vilimkaa vyema. Begi dogo lilikuwa mgongoni pake tayari kwa kazi.
“Upo ok?” Amata akamuuliza Jasmini.
“Yap! Scoba vipi?”
“Yupo anatest mitambo, maana haya maboti hatuijayatumia
muda mrefu sana” Amata akamwambia Jasmini.
Kabla hawajafanya lolote, simu ya Amata ikapokea arafa,
akaifungua kuisoma.

‘Nahitaji kukuona, nimekumiss…’ ujumbe kutoka kwa Mwaja.


Amata akausoma na kuurudia, akabaki akitabasamu na
kutikisa kichwa.
‘Kwa Leo itashindikana, nipo kwenye operesheni maalum’Akamjibu.
‘Au ndo ushapata mwingine unaenda kufanya oparesheni?’Arafa zile
zilikuwa zikimkera Amata pasi na mtumaji kujua.
‘We kula maisha na mwarabu wako, ila ujue umelala na nyoka,
atakuuma muda si mrefu’
Mwaja akajikuta anajawa na mawazo juu ya meseji hizo za
Amata. Mafumbo yaliyokuwepo alishindwa kuyatatua.
‘Maneno ya mkosaji’ akaandika.
Kamanda Amata, Jasmin na Scoba wakaketi chomboni tayari
kwa safari. Baada ya kuhakikisha kila kitu cha muhimu wamebeba
Scoba akatia injini moto na ile boti ikaanza kuyakata maji kwa
mwendo wa kasi. Dakika thelathini ziliwatosha kuifikia Bagamoyo.
Scoba akasogeza chombo mpaka usawa wa Nunge na kuizima
injini.
“Vipi?” Amata akauliza.
“Tumefika…” Scoba akajibu.
“Ok, Jasmin, tunaenda kufanya operesheni ndogo ya wokozi.
Kuna binti ametekwa inasemekana yupo ndani ya lile gofu la meli,
so umekuja kama daktari kama itahitajika. Tukifanikiwa breki yetu
itakuwa Shamba…”
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Copy” Jasmin akajibu. Wakavaa mavazi ya kuogelea tayari


kuiendea meli ile.
“Kwanini tusisogeze boti mpaka pale?” Jasmin akauliza.
“Adui hawezi kuwa mjinga akaishi pale bila kutung’amua.
Kwa kupiga mbizi hawezi kutuona kirahisi…” Amata akajitupa
majini. Jasmin naye akashusha mask yake usoni na kuweka ile snokel
vizuri, akajitupa majini.
Meli mbovu ya MV Bagamoyo ilikuwa imeegeshwa mita mia
tano kutoka katika pwani ya Nunge. Meli hiyo iligeuka maficho ya
wanyang’anyi. Fareed na vijana wake waliigundua meli hiyo katika
tafiti zao na walipoichunguza na kuona inafaa kutumika
wakaitumia. Walipomteka Lukundame Kule Zanzibar, wakamleta
katika meli hii na kumfungia katika chumba kimojawapo ambacho
hata ukipiga kelele hakuna wa kukusikia.
Amata na Jasmini waliifikia ile meli. Amata akawa wa kwanza
kuibuka majini na kuangalia kama kuna hatari yoyote. Meli nzima
ilikuwa giza, hakukuonekana hata mwanga wa mshumaa. Jasmini
naye akaibuka kisha kwa kutumia ishara Amata akamwambia
Jasmini kuwa yeye atatangulia halafu Jasmini afuate nyuma. Amata
akazunguka upande wa nyuma. Kwa kupitia huko akaweza kuingia
ndani bila tabu kwa kutumia mlango mdogo ulio karibu kabisa na
pangaboi la kuendeshea chombo hicho. Jasmin naye akaja nyuma
yake. Wakaingia na kujificha mmoja upande huu na mwingine
upande ule. Kisha kila mmoja akavaa miwani yake inayomwezesha
kuona gizani. Amata akatanghulia, bastola mkononi, chumba
kimoja baada ya kingine. Jasmin akamfuata kwa nyuma bastola
moja mkononi nyingine ikiniwa imetulia kiunoni.
Mwendo wa Amata haukufanya ukelele kutokana na viatu
alivyovaa. Akatembea taratibu kila chumba. Baada ya kupita
vyumba kama vinne hivi, akasimama na kumpa ishara Jasmin
asimame na awe tayari.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Mtu aliyekuwa akipiga mruzi alisikika akishuka ngazi kutoka


juu kuja chini. Amata akajibana vizuri sambamba na ukuta wa meli
hiyo na Jasmin pia. Naam alikuwa mwarabu-mwarabu hivi.
Mwembamba, mrefu. Alipita hapo na kufungua chumba kimoja
kati ya vile alivyovikagua Amata. Yule bwana akachukua kitu kama
mfuko. Akiwa katika kazi hiyo simu yake ikaita akainyakua na
kuiweka sikioni. Akaongea maneno machache kwa lugha ya kwao
kisha akavuta hatua na kuipanda ile ngazi. Alipokwishapotelea kule
juu Amata naye akaongoza kwenda hukohuko. Alipofika juu
alijikuta kwenye sebule ndogo yenye viti viwili na kijimeza. Yule
jamaa hakumuona pale.
Kutoka upande wa chini, Amata alisikia watu wawili
wakiongea lugha ambayo ilikuwa ngeni kwake. Japokuwa alitumia
utulivu mkubwa kujaribu kuelewa moja moja, hakuweza. Alipohisi
wanakuja upande wa juu ambao yeye alikuwamo, akampa ishara
Jasmini ya kutafuta mahala pazuri kujificha. Amata naye akavuta
mlango mmoja wa chumba kilicho jirani akaingia na kuurudishia
taratibu huku akiacha uwazi mdogo wa kumwezesha kuona
kinachoendelea.

“Karibu…” sauti ya yule kijana ikasikika kwa ukaribu zaidi


ikisindikizwa na nyayo za kiatu chenye solo ngumu cha watu
wanaopandisha ngazi. Amata akahesabu mikanyago hiyo akajua
wapo wawili. Ni hesabu ngumu ambayo kama huna utulivu wa akili
huwezi kuijua, kusikiliza vishindo vya watu usiowaona na kujua
idadi yao. Mwanga wa kurunzi ukatangulia kisha watu wawili
wakaingia kwenye kile kisebule na kuketi.
“Wanasemaje mjini?” yule kijana akauliza.
“Mjini hakufai, Nasyahd yupo mikononi mwa polisi kitu
ambacho kinanipa shida sana kwa sasa…” akajibu yule mgeni.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Mikononi mwa polisi oh shit!” yule kijana akaonekana


kuchanganyikiwa kwa habari hiyo. Akatulia kimya kwa sekunde
kadhaa kisha akaendelea kuongea na mgeni wake.
“Kwa hiyo?”
“Hapa ni kuondoka tu… mpaka sasa nina uhakika
tumeshajulikana wote na misheni yetu,”
“Na huyu mateka vipi? Kazi yake imeisha? Au tunafanyaje!”
“Kiukweli kwa sasa hana thamani kwetu, tukimwacha hai
itakuwa hatari kwetu…”
“So?”
“Lazima auawe…” yule mgeni akajibu. Ukimya mwingine
ukajidai kati yao. Katika ile sebule ndogo ni mwanga wa kurunzi tu
uliokuwa ukimulika mara upande huu mara ule. Kwa mazungumzo
yao, Amata akapata uhakika kuwa Lukundame yupo ndani ya gofu
hilo la meli. Akajiweka sawa kuanzisha shambulizi la ghafla.
“Sasa Nasyahd tutampata kweli?” yule kijana akamuuliza
Mgeni wake.
“Tunaweza tukampata, yule mwanamke amenihakikisia kuwa
kesho atajaribu kuwasiliana na watu ambao wanaweza kutusaidia.
Na akitoka tu ni moja kwa moja Zanzibar na tutapandia ndege kule
kuelekea Nairobi,” yule Mgeni akaeleza. Amata akaanza kupata
picha ya mgeni huyo ni nani, hivyo akatega sikio kusikiliza
mazungumzo hayo.
“Kama swala lipo polisi na mtu wetu ni afisa wa jeshi, nina
uhakika atatoka tu…” yule kijana akamwondoa hofu Mgeni wake.
“Sikiliza, Nasyahd yupo polisi lakini swala lake lipo chini ya
idara ya usalama wa taifa. Sasa huyu mwanamke anamjua mtu
ambaye yupo na swala la Nasyahd so ameniahidi kuzungumza naye
na kutumia mbinu zote za kike kumshawishi liishe…”
“Ataweza tu, we unamwonaje, figa la kushawishia analo, au?”
“Tunapambana na mtu mmoja hatari sana kwenye medani za
usalama… mtu kama huyu si rahisi kudanganyika hasa kwenye
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

swala nyeti kama hili… jambo la kufanya hapa sasa, ni kumuua


huyu mateka mwache aozee humu…”
“…halafu twende Zanzibar usiku huu?”
“…siyo twende, wewe uwende Zanzibar, mimi lazima nirudi
kwa yule mwanamke kuna ajenda ya kumaliza naye…. Hatutakiwi
kuacha nyayo nyuma. Kama nilivyofanya kwa Mwambope ndivyo
nitavyofanya kwa huyu…”
Hapo Amata akamjua mgeni huyo, Fareed.
Hutoiacha Tanzania ukiwa hai, nyau wewe! Akamwambia kwa
sauti ya moyoni. Yule kijana akainuka kutoka kwenye kile kiti na
kuchomoa kisu kutoka mkanda wa suruali yake. Mwanga wa
kurunzi ulipopita kwenye kile kisu, mng’ao wake ukapiga sawia
kwenye kile kichumba alichomo Amata. Fareed Jicho lake lilikuwa
kule, akatulia kidogo na kutazama kwa makini. Alihisi kuna kitu
kama kimecheza hivi. Akainuka kutoka pale kitini na kuvuta hatua
kuuendea ule mlango. Amata kule ndani akajiweka tayati kwa
shambulizi. Fareed alipofika, aliuvuta mpaka mwisho na kufunga
kitasa chake kwa nje.
Jasmin akauma meno kwa kitendo hicho, akatoa tusi la
nguoni. Akajua sasa kabaki peke yake, akawatazama wale
wanaume, akajribu kuona aanze na yupi akifanikiwa amalize na
yupi. Akatuma taarifa kwa Scoba kumtaka awe tayari na asogee
kumpa msaada ikibidi. Yule kijana alipomwacha Fareed, alivuta
hatua kuelekea upande uleule ambao Jasmin alikuwepo. Akampa
muda kidogo na kumwacha apite ili aweze kumshughulikia vizuri.
Yule bwana alikuwa akipita huku akigusagusa Makali ya kisu chake.
Jasmin alijitokeza na kuchukua sekunde mbili kutafakari baada ya
kumuona Fareed akipotelea upande mwingine. Hatua kama sita
hivi zikamfikisha kwenye mlango aliofungiwa Amata. Alipotaka
kufungua kile kitasa tu alijikuta akipokea pigo moja matata sana la
karate. Hakujua hata Fareed kafika hapo saa ngapi. Pigo la pili na la
tatu yakambwaga chini Jasmini.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Kasi ambayo Fareed alikuwa akipeleka mapigo, ilimshinda Jasmini.


Akajizungusha pale chini kwa haraka nackumchota ngwala Fareed
lakini alihisi miguu yake imekutana na nguzo za chuma.
“Umetoka wapi wewe?” Fareed akamuuliza Jasmin wakati
amemkamata shingo yake na kumuinua.
“Hutakiwi kujua!” Jasmini akajibu kijeuri. Akatumia mtindo
wa ajabu na kujinasua kutoka kwenye mikono ya Fareed. Kijana
hyo akajikuta mikono mitupu.
“What!” Fareed akashangaa hakuelewa mwanamke huyo
amemchomoka vipi. Kwa kasi, Fareed akamwendea Jasmin.
Mwanamke huyo hakutaka mzaa, alijua kucheza na kiumbe huyo
kutamgharimu maisha. Akachomoa bastola na kuiruhusu risasi
moja kuingia chemba, akaachia risasi moja iliyotua sawia kifuani
kwa Fareed na kumbwaga upande wa pili. Jasmin akawahi mlango
na kuufungua.
Amata akatoka akiwa katota jasho, “yuko wapi huyu hanithi?”
akamuuliza Jasmini.
“Nishammaliza, yule kule,” Jasmini akajibu na kumwonesha
Amata kule alipoangukia. Amata akamwebdea Fareed, kwa kuwa
alijua kuwa kijana huyo ameshajeruhiwa kwa risasi ya Jasmini,
hakujiandaa. Fareed alikuwa mjanja sana, daima hupenda kuvaa
fulana isiyoingia risasi. Risasi ya Jasmin ilikuwa imetulia kifuani bila
madhara yoyote. Jasmin aliondoka pale na kuelekea kule ambako
yule kijana ameenda.
Amata alipomkaribia Fareed alijikuta akipigwa kabali hatari
sana. Fareed aliinuka kwa kasi kama upepo na kumvamia Amata.
“Nimekupata leo mpumbavu wewe, umeniulia vijana wangu
na umekuja mpaka huku…. Hutotoka mzima…” Fareed aliongea
kwa gadhabu huku kono lake likiwa limembana Amata na
kumfanya akose pumzi.
Yule kijana kumbe aliposikia mlio wa risasi akabadili uelekeo.
Akazunguka kule chini na kurudi upande wa pili wa ile meli kisha
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

akaanza kukwea ngazi taratibu. Alipojitokeza juu alikuta vurugu


mechi za Amata na Fareed. Amata akajaribu bahati yake ya
mwisho, alipata nafasi na kukanyaga ukuta, akajisukuma kwa nguvu
na kujibetua sarakasi. Fareed alijikuta anakosa uzani akayumba
kidogo huku Amata akimchomoka. Alopotua chini akajikuta
katikati ya vijana wale wawili. Hakupoteza muda, konde moja zito
likatua mbavuni kwa yule kijana, akamkamata na kumzungusha
upande wa mbele. Pigo la Fareed alilonuia kumtandika Amata
likatua kwa kijana wake na kumvunja mifupa ya kifuani. Yule kijana
akajikuta hoi. Fareed akashikwa na hasira alipogundua nini Amata
amefanya, akapiga ukelele. Akaruka kumuwahi Amata, lakini
akajikuta akipamiana na kijana wake, wore wakaenda chini.
Fareed akaona kazi ngumu, akainuka na kukutana pigo moja
zito lililotua mbavuni sawia. Akajikunja kwa maumivu. Pigo la pili
likatua kwenye uti wa mgongo, na la tatu likamshukia kwenye paji
la uso na kujikuta akibwagwa chini. Fareed aliponyanyuka pale
chini, aliutafuta mlango na kujirusha majini huku akimwacha
Amata akitoa sonyo la hatari. Akamtazama akiogelea gizani
kuelekea nchi kavu.
“Hujanikimbia bado!” akasema. Akamwinua yule bwege pale
chini, “haya, mateka yuko wapi?” yule jamaa hakuweza kujibu,
“nipeleke mlipomweka shenzi nyinyi…” Amata akaongea kwa
hasira.

Ndani ya kile chumba, Lukundame alikuwa kimya


kajikunyata. Mwili wake ulionekana umepigwa na kuteswa,
umechoka na hauna nguvu. Alisikia majibizano ya watu upande wa
nje lakini hakuwa na nguvu hata za kusema ‘nipo humu’.
Yule kijana, kwa shida, aliwaongoza Amata na Jasmini mpaka
kwenye kile chumba, wakakifungua. Amata alimtazama yule
mwanamke pale chini. Jasmin akawasha tochi kummulika
Lukundame.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Shit! Wamemtesa sana,” Jasmini akasema. Scoba tayari


alikuwa keshawasiri. Wakasaidiana na kumchukua Lukundame
kwenye boti yao tayari kwa safari.

* * * *

Fareed alipofanikiwa kutoka ufukweni, moja kwa moja


aliliendea gari alilokuja nalo na kujitupia ndani. Maumivu makali
yalikuwa kwenye bega na mguu wake. Alijaribu kujinyoosha mwili
ili mifupa yake ikae sawa lakini kwa maumivu yale alijikuta
anajitesa. Akawasha injini na kujitahidi kuendesha hivyohivyo
kurudi Dar es salaam.
Njia nzima alikuwa akimtafakari Amata. Hakuamini jinsi
jamaa huyo alivyo mwepesi wa kufanya maamuzi apambanapo.
Alitamani ammalize lakini alijikuta anashindwa. Akaijutia nafasi
aliyoipoteza. Akachukua simu yake na kupiga namba ya Mwaja.
“Hello!” Mwaja akapokea upande wa pili
“Hello nahitaji msaada wa haraka…”
“Nini kimetokea?” Mwaja akauliza.
“Nimevamiwa na majambazi ninaporudi, nimeporwa milioni
saba,” Fareed akadanganya.
“Sawa! Sasa niwataarifu polisi,” Mwaja akauliza kwa hamaki.
“Hapana, acha tu… ukiwahusisha polisi jambo litakuwa
kubwa. Unaweza kuja Tiffany hoteli?”
“Usiku huu?”
“Ndiyo, uje na lile begi langu kuna vitu nahitaji humo…”
“Sawa dear!” Mwaja akajibu na kukata simu.
Umekwisha! Fareed akajisemea na kutoa tabasamu. Ilikuwa ni
mbinu tu. Fareed alinuia kummaliza mwanamke huyo ili asiache
alama yoyote nyuma yake. Aliendesha gari kwa kasi.

* * * *
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Amata, Jasmini na Scoba waliwasili katika kituo cha polisi cha


wanamaji. Amata akachukua begi lake na kulitia mgongoni.
“Mpelekeni huyu Shamba, umpatie matibabu, tutaongea naye
akiwa sawa…”
“We’ wapi?” Jasmin akauliza.
“… kuna kazi naenda kumalizia halafu nitaungana nanyi…”
“Ok na hili lingine?” Jasmin akatulia akimaanisha yule kijana
wa Fareed waliyemchukua kule Nunge.
“Mfungeni pingu vizuri, vijana wanakuja kumchukua,”
akawaambia wakati akiingia kwenye gari ndogo aliyoiacha hapo.
Akatia moto injini na kuondoka zake. Jasmin na Scoba nao
wakaingia kwenye gari jingine pamoja na Lukundame,
wakatokomea zao.

* * * *

HOTELI YA TIFFANY
Kamanda Amata aliwasili Hoteli ya Tiffany katikati ya jiji la
Dar es salaam majira ya saa nane usiku. Akapiga macho kutazama
magari yaliyoegeshwa hapo nje, hakuna alilolitilia shaka.
Akateremka taratibu na kujiweka tayari kuvuka barabara ili aingie
katika hoteli hiyo. Kabla hajavuka, upande wa pili kukatokea taksi
na kumpigia honi kali. Akarudi nyuma. Ile taksi ikasimama katika
kibaraza chenye lango kuu la kuingia hotelini humo. Amata akatulia
kwanza kujua nani anateremka kabla hajaingia kwenye harakati
zake.
Mwaja! Akapigwa na butwaa. Hakuamini anachokiona,
akasubiri mwanamke huyo aingie hotelini mle. Alipohakikisha hilo
limekamilika akavuta hatua kulielekea lango hilo. Amata aliingia

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

dakika tatu nyuma ya Mwaja. Akatumia ngazi kuifuata ghorofa ya


tano kama ambavyo anajua.
Korido ndefu yenye milango mitano huku na mitano upande
mwingine ilimpokea. Zuria jekundu la Kiajemi lilimlaki. Amata
akavaa soksi usoni kisha akavuta hatua mpaka katika mlango
alioutaka. Akachomoa bastola na kuihakikisha kuwa ipo sawa.
Akagonga mlango. Kutoka ndani, haraka, Mwaja aliufikia mlango
na kufungua bila hata kuuliza. Mara tu alipojitokeza alijikuta
akitazamana na domo la Beretta Pico huku akipewa ishara ya
kurudi ndani. Akanywea, hakuwa tayari. Mwilini mwake alikuwa na
nguo ya kulalia tu. Alipepesa macho yake huku na huko. Amata
aliyaona yote hayo, akamtazama nini anataka kufanya. Akamtaka
kuingia ndani. Mwaja hakupinga alirudi kinyumenyume na
kutakiwa kuketi kitandani, akafanya hivyo. Amata akavua soksi
aliyoivaa kichwani ili kuificha sura yake.
“Haaaa!” Mwaja akashangaa.
“Tulia, si ulitaka kuonana na mimi, nimekuja…”
“Mi nilikwambia uje hapa?”
“Tulia… namsubiri bwana wako, najua yuko njiani… kuna
jambo lazima tulimalize…” Amata akasema huku bastola ile ikiwa
bado mkononi.
“Una mat….”
“Shhhhh! Lala chini sakafuni, tena kifudifudi, mikono yako
ikutanishe kisogoni…” Amata akaongea kwa mamlaka. Mwaja
akataka kukaidi.
“Mwaja! Fanya nililokwambia kabla sijakuumiza mpumbavu
wewe… unatufugia magaidi hapa! Na safari hii vitakutokea puani,”
Amata akamwambia. Mwaja akaingiwa ganzi mwilini, akafanya
alivyoamriwa. Akalala sakafuni kifudifudi, mikono kisogoni.
Mnyumbuiliko wa mwilini wake ukamfanya kijana wa TSA kuanza
kusindwa uzalendo. Akamtazama na kumeza mate.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Eh! Kuna binadamu wameumbwa loh! Akawaza huku akikaa kitini,


bastola yake bado mkononi. Akatulia kimya kabisa kumsubiri
Fareed. Saa moja iliyofuata, Amata akasikia mlango ukigongwa
taratibu. Akamgusa Mwaja kwa mguu wake na kumtaka kufungua
mlango. Mwaja akainuka akiwa kalowa jasho, akauendea mlango
huku akisindikizwa na Beretta Pico. Hakutakiwa kufanya ujanja
wowote, naye alilijua hilo. Akaufungua mlango na kumkaribisa
Fareed ndani. Kijana huyo alipojitoma ndani na kuufunga mlango
nyuma yake, macho yake yakagongana na Amata.
“Shiiit” akashangaa.
“Utashangaa sana, nimeshafika nakusubiri… tulichokianza
Bagamoyo tutakimalizia hapa,” Amata akamwambia, “keti na
mpenzi wako kitandani,” akamwamuru. Fareed akaketi kitandani
na Mwaja vilevile. Bado Fareed hakuamini kama anayemwona
hapo ni Amata au kivuli.
“Unashangaa nini? Kaeni chini!” akawaamuru. Mwaja na
Fareed wakaketi kitandani huku domo la bastola likiwatazama.
“Ulifikiri utanikimbia? Hakuna mwanadamu aliyewahi
kunikimbia mimi… haya tulimalize tulilolianza Bagamoyo…”
Amata akamwambia Fareed. Kijana huyo alibaki kimya akimtazama
Amata kwa jicho baya na lililojaa gadhabu.“Mwaja! Nilipokwambia
unafuga magaidi nilikuwa namaanisha… huyu bwana ‘ako ni gaidi,
huyu ndo aliyemuua Mwambope kwa msaada wako,” Amata
akamwambia mwanamke huyo aliyesthushwa kwa maneno hayo.
Akamgeukia bwana wake.
“Fareed ulimuua Mwambope?” Mwaja akauliza kwa
tashwishwi huku machozi yakimtoka, “nambieeeee!” akang’aka.
Amata akatulia tu akitazama.
“Nataka unambie, kuna biashara gani ilikuwa ikiendelea kati
yako na Mwambope mpaka ukamuua mzee wa watu halafu bila
aibu unakuja kumzika?” Amata akamuuliza Fareed. Bado kijana
huyo alikuwa kimya.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Si unaulizwa jibu mpumbavu wewe!” Mwaja akajikuta


akibwabwaja. Fareed akamtazama na kisha akarudisha macho kwa
Amata.
“Mwaja! Huyu bwana wako, alipanga leo hii kukuua ili
aondoke zake nchini…”
“Yaani Mimi nimuue mpenzi wang…”
“Kelele… mpenzi wako au ulikuwa unamtumia kwa maslahi
yako!?” Amata akamkata kauli Fareed.
“Hapana, hawezi kuniua mimi, huyu ni bwana wangu
ananipenda,” Mwaja akamjibu Amata, “hat kifo cha Mwambope
unamsingizia, mbona mtu wa mwisho kwenda kwa Mwambope ni
wewe mwenyewe, unafikiri hatujui?” Mwaja akamwambia Amata.
Moyo wa Amata ukaruka chogo chemba, akatahayari kwa maneno
hayo. Akainua mkono wake wa kushoto, akaifyatua saa yake
sehemu ya kitunza sauti, akafungua. Mazungumzo ya Fareed na
kijana wake kule melini yakasikika dhahiri shahiri juu ya kumuua
Mwaja ijapokuwa waliongea kwa mafumbo.
“No no no hiyo umetengeneza…. Mi siwezi kupanga mauaji ya
mpenzi wangu..” Fareed akajitetea.
“Yaani uliniita ili uniue Fareed?” Mwaja akapiga unyende.
Alipomaliza tu alipokea Kofi moja zito usoni kutoka kwa Fareed,
akajibwaga kitandani. Wakati huohuo, Fareed aliipiga teke bastola
ya Amata ikapaa hewani. Amata hakuweka akili yake kwenye
bastola hiyo. Fareed aliruka kutoka pale kitandani ili aikamate ile
bastola kabla hajamaliza mruko wake. Amata akainuka haraka na
kumtandika konde zito la mbavu. Kijana yule akaguna kwa
maumivu. Alipotua chini akapokea mapigo mawili ya karate
yaliyotua kwenye kolomeo na kumfanya akohoe kwa fujo. Ile
bastola ikaanguka kando.
“Na utanieleza nani kakutuma? Mna biashara gani?” Amata
akaunguruma.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Koh! Koh! Koh! Kammmwe hutokuja kujua…” Fareed


akajibu kijeuri. Amata alipotaka kumpelekea shambulizi, yule jamaa
alijirusha kwa ufundi sana na kuikamata ile bastola. Akafyatua
lakini Amata tayari alishahama lile eneo. Ile risasi ikatawanya kioo
cha dirisha na kuliacha wazi. Amata akamchota ngwala Fareed.
Kwa ustadi mkubwa akaruka na mguu wa Amata ukapita chini.
Pigo moja likaitoa bastola mkononi. Fareed akapeleka mapigo ya
judo kama matano kwa haraka na kumtandika vibaya Amata.
Akaenda chini bila pingamizi.
“Nakuua!” Fareed akamwambia Amata aliyekuwa akizoazoa
pale chini.
“Muue huyo, anaingilia mambo ya watu… tena ukimuua
utakuwa shujaa kwelikweli…” Mwaja akasema huku akijitoa
kitandani na kusimama kando. Fareed aliinua kiti kilichokuwa
pembeni mwa meza ya kusomea na kumtwanga nacho Amata pale
chini. Lakini kabla hakijamfikia alikipiga kwa pigo moja
kikatawanyika vipande vipande. Amata akajiinua na kujiweka sawa,
pigo lililokuja kutoka kwa Fareed akalikinga, la pili akalikinga, la
tatu akalikinga kiufundi kabisa. Pigo la nne akalikwepa na kumdaka
mkono, akamzungusha vizuri na kumuweka nyuma yake kisha
akauvunja mkono wake bila huruma. Fareed akapiga yowe la
uchungu. Amata akamgeuza mbele na kumtandika mapigo matatu
murua na kumvunja mifupa ya kifua. Fareed akaanguka chini
akikoroma na kutokwa damu kinywani.
“Mimi si mtu wa kuchezea fala wewe! Haya nambie nani
kakutuma Tanzania?” Amata akamuuliza tena. Hakujibu isipokuwa
alikuwa akitema mabonge ya damu.
“Hhhhhaina maana… uhk, kho, uuummhh…” Fareed
akagugumia. Amata mara moja akajua nini huyo jamaa anataka
kufanya, akambana mdomo lakini akachelewa, Fareed akameza
kidonge cha sumu na povu lililochanganyika na damu likafuatia.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Limejiua….” akasema. Akainuka haraka na kukiruka kitanda.


Mbisho wa hodi na sauti ya kutaka mlango wa chumba ufunguliwe
zilisikika kutoka nje. Mwaja alijikunyata kwenye kona akitetemeka.
“Kaa umwomboleze bwana wako…” Amata akaichukua
bastola yake na kuisweka kiunoni, akafungua kabati la nguo na
kuchukua vitu vichache ikiwamo kompyuta ndogo na simu ya
marehemu. Akainua mkoba ule aliokuja nao Mwaja akautia
kwapani na kuliendea dirisha.
‘hapa kilichobaki ni kuvunja mlango!’ sauti kutoka nje ikasikika.
“Amata usiniache!” Mwaja akalalama huku machozi
yakimtoka.
“Wewe unatakiwa ubaki hapa ukamatwe uende jela…” Amata
akamwambia Mwaja huku akipita kwenye lile dirisha na kukamata
bomba linalotoka chooni akateremka nalo mpaka chini. Mwaja
hakusubiri la kuambiwa, alipoona mlango umeanza
kuchokonolewa, akapita dirishani na kuteremka chini kwa bomba
lilelile. Alipotua tu, Amata akamkamata mkono na kumvuta
kuelekea anakoelekea yeye. Wakavuka barabara mpaka upande wa
maegesho, akafungua mlango na kumtupia kiti cha nyuma. Yeye
akaingia mbele, nyuma ya usukani.
“Unanipeleka wapi?” Mwaja akauliza.
“Gesti” akajibiwa.
Amata akaondoa gari na kuikamata Barabara ya Morogoro
kuelekea Magomeni. Akabofya namba kwenye simu iliyo ndani ya
gari hilo na kumpa ujumbe mtu wa upande wa pili.
“Tiffany Hoteli chumba namba 54 kuna mzigo wenu…”
akakata ile simu na kukanyaga mafuta.

* * * *

“Jamila! Nimeongea na mkuu wako wa kazi amekubali


kushirikiana na sisi kwa kuwakomboa wenzako na pia kuupata ule
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

mfumo wa usalama. Hivyo amesema unipatie code yako ili wataalam


wafanye kuitrace kujua ni wapi lilipo… wamesema bila code
mojawapo kazi itakuwa ngumu…” Kahir akamwambia Jamila.
Jamila akatulia kimya kwa jozi la sekunde akitafakari maneno
hayo. Kwanza alifurahi moyoni kujua kuwa wenzake wapo hai, pili
akajiuliza tangu lini jeshi la Tanzania limeanza ushirkiano na jeshi
la Pakistan? Akajiuliza. Kama ingekuwa hivyo kwa nini
hakupelekwa jeshini na akaletwa mafichoni? Maswali juu ya
maswali. Jamila akashtukia mchezo anaotaka kuchezewa.
“Jenerali…. Naunga mkono hilo, lakini nihakikishie ni kweli
wenzangu wapo hai?” akamuuliza.
“Ndiyo, wapo hai kabisa…” Kahir akajibu.
Amejuaje? Jamila akajiuliza.
“Sawa, ila naomba niongee na mkuu wangu kwanza… kabla
sijachukua hatua ya kuitoa code hiyo,” Jamila akamwambia Kahir.
“Sawa, kwa kuwa alikwishasema atapiga, nitakuunganisha
naye… sasa upumzike!” Kahir akamwambia Jamila huku
akimwacha hapo na yeye kuondoka zake. Jamila akabaki na
mawazo tele. Akaingiza mkono ndani ya nguo yake na kuchomoa
kidubwasha kidogo kama rimoti. Akakitazama na kukibusu. Kazi
ya kidubwasha hicho ilikuwa ni kuiwasha sigino ya like sanduku.
Kila mmoja alikuwa nacho lakini wakati wa ajali ni Jamila tu
aliyekumbuka kukichukua cha kwake. Akataka kukibonyeza, lakini
moyo wake ukasita kwa kuwa kama angekibonyeza huku kwenye
ule mfumo code mbili zimeshawekwa basi mfumo ule ungejiwasha
automatiki na ingekuwa faida kwa Mansoor.

* * * *

Ugeni wa ghafla uliwasili katika kasri la Mansoor katikati ya


bonde la Kashmir. Hakuwa na taarifa na wala siyo desturi yake

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

kupokea ugeni pasipo na miadi. Kwa kuwa aliambiwa ni nani


aliyewasili, hakuwa na budi kumkirimu muda wake.
“Yes… big man!” akampa mkono Fernandez a na
kumkaribisha kiti.
“Usishangae nimekuja ghafla…”
“Ndiyo…”
“Kilichonileta kwako ni hii biashara yetu… sijamuelewa
mnunuzi mwingine maana ananipigia simu na kunipa vitisho kuwa
niachane na hii biashara… mara anasema kuwa wewe
umeshamuuzia code ya tatu… enh! Sielewi…” Fernandez akalalama.
“Kahir ana matatizo… Kahir amefanya unyama kumpata yule
mtu mwenye code ya tatu akiamini kwamba lazima nitamuuzia hii
program…” Mansoor aliinamisha kichwa chini, vidole vyake
vikapenya kwenye nywele zake, “Kahir, Kahir, Kahir… anataka
kuniharibia biashara yangu” akasema. Kisha akainua uso na
kumtazama Fernandez.
“Mimi sijamuuzia hiyo code, mimi mwenyewe ninaihitaji… ila
alichokifanya ni kama nilivyokwambia hapo awali,” Mansoor
akasema.
“Kwani huyu ni nani na ameijua vipi hii misheni?” Fernandez
akauliza.
“Jenerali Kahir ni kiongozi wa siri wa kundi la wanamgambo
la Hizbul Mujahideen ambao wanapigana na majeshi ya India
katika kile wanachokidai kuiweka huru Jammu na Kashmir. Huyu
bwana amekuwa mteja wangu sana, ninamuuzia silaha mara nyingi
tu, nilimdokezea juu ya huu mfumo lakini bei anayotaka kununulia
ni ya kizee… ndiyo katika kutafuta mteja nikakupata wewe. Sasa
naona anataka kutumia njia nyingine ili afanikiwe…”
“Sikiliza Mansoor, misheni yetu kule Tanzania imefeli…”
Fernandez akamkatisha Mansoor.
“Kivipi?”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Vijana niliowakodi kuhakikisha wanapata lile kabrasha lenye


zile kodi wameuawa…” Fernandez akamwambia Mansoor,
“inasemekana intelijensia ya nchi ile si ya kawaida, imeweza
kung’amua mbinu zetu zote na tayari kabrasha lile lipo kwenye
mikono ya serikali,” akaeleza kinagaubaga.
“Mh! Tanzania hii hii au nyingine…” Mansoor akauliza.
“Hiyo hiyo! Kwa maana hiyo sasa tunabaki na turufu moja
tu…”
“Ipi?”
“Inabidi tumpate Kotvich…”
Baada ya Fernandez kutoa wazo hilo Mansoor akatulia
akitafakari kwa sekunde chache.
“Yule bwana tutampataje? Mimi mwenyewe mpaka leo naijua
sauti yake tu…” Mansoor akaeleza.
“Cha kufanya ni kumpata ili aweze kutufungulia hivi vifungo
ili tuipate code ya tatu” Fernandez akaeleza.
“Ni shotcut, ila gharama za kumpata si za mchezo, nani
atagharamia?” Mansoor akauliza.
“Hilo niachie mimi…” Fernandez akamwambia. Mansoor
akainuka pale alipoketi na kumwita Fernandez pembeni.
“Sikiliza Fernandez… huu mzigo lazima nikuuzie wewe,
Kahir keshaniuzi. Sasa nitaitisha mnada watu mbalimbali wafike
dau. Hakikisha unaweka dau la juu kuwazidi wengine lakini mimi
nitakuuzia wewe kwa bei ya kirafiki”.
“Na kuhusu hiyo code ya tatu,” Fernandez akauliza.
“Si umesema utamtafuta Kotvich!”
“Yeah” wakaweka mambo sawa na kurudi mezani.
“Umenishtua sana kwa hilo jambo la Tanzania…” Mansoor
akamwambia Fernandez.
“Aaaaaah Mansoor, Tanzania wanaanza kunitia hofu. Inabidi
tufanye haraka kukamilisha hili maana najua wale kama dola

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

hawataliachia hili jambo njiani…” Fernandez akamwambia


Mansoor. Ukimya ukatawala tena.
“Au tumvamie Kahir tukamtwange tumchukue huyo mtu?”
Fernandez akatoa wazo.
“Siafiki! Kufanya hivyo ni kuamsha vita mpya, BBC
wataripoti, CNN watafanya hivyohiyvo, DW hawatabaki nyuma….
Tutakuwa tumeharibu kila kitu” Mansoor akaeleza.
“Sure! Mi nahitaji hii kitu mapema ili niipeleke kule Saudi
Arabia kwa vijana wangu wajilinde dhidi ya majeshi onevu ya
Magharibi, ya Marekani na washirika wake… wanatuonea sana,
wanataka visima vyangu vya mafuta kila uchao!” Fernandez
akàlalamika.
“Umepata! Usijali…” Mansoor akamtoa hofu.
“Nakuaminia….”

* * * *

Kamanda Amata aliiacha barabara ya Morogoro, eneo la


Magomeni Kagera na kukunja kushoto. Akaendesha gari kama
mwendo wa dakika tano hivi barabara ya vumbi. Akapunguza
mwendo na kusimama mbele ya nyumba moja kuukuu iliyoinama
upande. Nyumba ya udongo, yenye paa la bati chakavu. Amata
akateremka na kila kitu, akamtaka Mwaja naye kuteremka, akafanya
hivyo. Wakaingia kwenye ile nyumba. Mwaja bado alikuwa na vazi
lake la kulalia bila chochote ndani yake. Sebule ndogo, chafu,
ilikuwa na viti vinne vya ‘mkao wa nyani’ na Meza ndogo katikati
ilimlaki Mwanamke huyo. Akainua macho kutazama ukuta
uliokuwa ukimulikwa na mwanga hafifu wa taa. Picha kubwa ya
Nyerere na viongozi wengine wa TANU zilitundikwa. Pembeni
yake kulikuwa na kalenda ya Sunguratex ya mwaka 1985.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Njoo huku…” Amata akamwita kutoka kwenye mshangao


wake. Akamfungulia chumba kimoja na kumtaka kuingia. Mwaja
akamtazama Amata.
“Unashangaa nini? Hapa ndipo utaishi mpaka utakapokuja
kuchukuliwa na vyombo vya usalama!” akamwambia.Mwaja
akasema huku shingo yake akiiweka upande upande, “Amata, mi
nilijua umenisaidia kwenye hili janga!”
“Kazi yangu si kumsaidia mhalifu bali kumkamata na kumtia
mikononi mwa serikali… wewe ni mhalifu…” Amata
akamwambia.
“Nitakupa chochote Amata!”
“Sitaki, rushwa ni adui wa haki…. Kaa humo…” akamjibu na
kuufunga mlango. Mwaja aliutazama ile mlango, akauendea, loh!
Haukuwa na kitasa wala alama yake. Akakigeukia kitanda, cha
mamba, cha kijijini, hakina godoro wala shuka. Akajitazama yeye
alivyovaa na kile kitanda, kulala ni mateso.

Kamanda Amata alipohakikisha amemfungia Mwaja vizuri,


akavuta hatua kuelekea chumba kingine. Hicho kilikuwa chumba
kizuri kuliko unayofikiria. Kitanda kimoja kikubwa na kochi LA
watu wawili lilikuwa kando, huku mbele yake kukiwa na meza
yenye nakshi safi ya kioo. Kompyuta moja, luninga ya wastani na
vitu vichache vya kielektroniki. Akautupia ule mkoba kitandani na
kuingia maliwato. Aliporudi akaufungua na kumwaga kila kilichopo
pale kitandani. Zaidi ya nguo chache kulikuwa na saa kubwa ya
mkononi, modeli ya kisasa kabisa. Akaiweka kando. Ubamba wa
apple, nao akauweka kando. Pesa taslimu za kimarekani,
akazihesabu harakaharaka akakuta ni takribani dola elfu mbili mia
tano sawa na shilingi milioni tano na laki saba na ushei. Nazo
akaziweka kando.
Ndani ya mkoba huohuo akakutana na kiboksi cha heleni,
Pete na bangili, zote za dhahabu safi. Akakichukua na kukiweka
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

kando. Alipohakikisa amemaliza pekuapekua hiyo. Akazirudisha


nguo kwenye ule mkoba na kuutia kwenye kitu kama kabati dogo
lakini halikuwa kabati. Alipokifunga, akawasha swichi ya umeme ya
ukutani nakuteketeza mkoba wote kwa moto uliozalishwa ndani ya
kikabati hicho.
Kutoka mfukoni mwa koti lake akatoa simu na waleti ya yule
mpumbavu alivyovichukua. Akavibwaga mezani.Kisha yeye
akaingia bafuni kuoga na kujiweka sawa kwa kazi nyingine. Baada
ya kujiweka sawa, vile vitu vyote akavitia kwenye mkoba mwingine
na kutoka mpaka kwenye chumba alichomwacha Mwaja.
Akamkuta kajikunyata kitandani.
“Pole, lakini usijali ndiyo ubinaadamu huo!” akamwambia na
kumrushiakitu kama pakiti ya pipi, “mung’unya hiyo upate afya na
nguvu, mpaka watakapokuja kukuchukua”.
“Nani?” Mwaja akauliza kidhaifu.
“Mkuu wako wa kazi…” akamjibu na kufunga mlango.
Amata akaondoka zake na kuiacha ile nyumba.

* * * *

SHAMBA
Jasmini na Scoba waliwasili Shamba usiku wa saa saba na
kumwingiza Lukundame aliyekuwa hana fahamu katika chumba
kidogo cha matibabu. Chumba kilichosheheni kila kifaa tiba
unachokijua wewe. Wakamlaza katika kitanda na Jasmini
akamwekea dripu yenye virutubisho ili kumrudishia kidogo uhai
uliopotea. Walipohakikisha wamemuweka vizuri wakatoka na
kuwasha kamera ya siri kumtazama. Wawili hao kila mmoja
akaingia katika chumba chake kujipumzisha.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Majira ya saa tisa usiku, Kamanda Amata aliwasili katika jengo


hilo na kuingia kwa kupitia moja ya njia zao za siri. Moja kwa moja
akafikia katika chumba kinachotumika kwa mikutano
midogomidogo akaketi na kuweka kila kitu mezani. Hakutaka
kuwaamsha wengine. Kwanza akachukua ule ubamba na
kuuwasha. Kama kawaida, ubamba ule ukadai alama za vidole za
mtumiaji. Akasonya na kujishika kichwa, akausogeza kando.
Akachukua simu na kuishtua maana haikuwa imezimwa. Ikawaka
na kwenye kioo chake alikuta arafa nne zinazosubiri kusomwa.
Alipojaribu kuzifungua zikamdai nywila ya mtindo wa pattern.
Haikumsumbua, akainuka na kuingia chumba kingine. Huko
akatoka na kitu kama unga laini akaumwaga juu ya kioo cha ile
simu na kuuacha kwa sekunde kadhaa. Kwa wakati huo akaendelea
kuzitazama zile bangili, heleni na pete. Akagundua kuwa hazikua za
kawaida bali ni vinasa sauti. Akavichunguza zaidi kujua kama
vinahifadhi sauti au vinatuma mahali fulani. Dakika tano za
uchunguzi akagundua kuwa vifaa vile havijihifadhii chochote bali
vinanasa sauti na kuituma mahali Fulani. Hakutaka kupajua,
akaviweka kando.
Akairudia ile simu na kupuliza lile vumbi aliloliweka kwenye
kile kioo. Lilipotoka likabaki kiasi mle tu ambamo michoro ya
pattern hupita. Akaishtua tena na kuingiza pattern kana kwamba yeye
ndiye mmiliki wa simu hiyo. Arafa ya kwanza haikuwa na maana,
ya pili vilevile. Akapitia kama arafa kama hamsini hivi, zote
zilikuwa za kawaida.
Haiwezekani! Akawaza. Amata akatumia utundu wake na
kuweza kufika kwenye moja ya application ambayo inaficha arafa za
siri. Ikamtaka tena aweke ule mchoro akafanya hivyo, ikafunguka.
Naaam hapa ndipo alipopataka, picha zaidi ya elfu moja zilikuwa
hapo. Akatazama moja baada ya nyingine, baada ya picha kama mia
hivi akakutana na picha ya Mwambope akiwa anambusu msichana
wa makamo. Amata akaitazama ile sura, haikuwa ngeni lakini
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

hakukumbuka ni wapi aliiona. Picha nyingine zilikuwa za Mwaja,


picha za kitandani, za falagha. Picha za Lukundame na watu
wengine asiowajua. Alichokifanya ni kuzipakuwa zile tu ambazo
alizihitaji, alizoziona labda zingemsaidia katika kazi yake juu ya
sakata hilo.

Asubuhi ya siku iliyofuata iliwakuta TSA 1 Kamanda Amata,


TSA 3 Jasmini na TSA 4 Scoba wakiwa ndani ya Safe House au
Shamba kama wao wanavyoita. Amata, Mara baada ya kuweka kila
kitu tayari aliungana na wenzake waliokuwa katika chumba maalum
wanachotumia kusikiliza au kusoma dokumenti mbalimbali.
“Lukundame!” Amata akatamka.
“Ameamka yuko poa kabisa…” Jasmini akajibu.
“Anaweza kuongea?”
“Ndiyo, anaweza,” Jasmini akajibu.
“Ok, mpeleke chumba cha mahojiano, nakuja…”
Jasmini akainuka na kupotelea ndani ya jumba hilo mpaka
kwenye chumba alichomhifadhi Lukundame. Akamkuta
keshajiweka sawa, “kutakuwa na session ya mahojiano, usiogope…
nifuate!” akamwambia. Wakatoka pamoja na kupita ndani kwa
ndani mpaka chumba cha mahojiano, akamkaribisha kisha yeye
akaondoka zake.
Lukundame alibaki peke yake mle ndani. Aliangaza macho
huku na kule kukichunguza chumba hicho. Ukuta ulikuwa tupu na
pweke kabisa. Hakukuwa na kitu zaidi ya meza moja na viti viwili.
Macho yake hayakutulia kudadisi chumba kile kipana chenye
utulivu. Akakohoa kidogo, lakini akajihisi amekohoa kwa nguvu
kutokana na mwangwi uliojitokeza. Mlango ukafunguliwa nyuma
yake, akageuka na kugongana macho na mwanaume asiyemjua.
Yule mwanaume akaketi kiti kingine mkabala na yeye.
“Usiogope, upo mahali salama, unaongea na Mr Spark…”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Lukundame akatikisa kichwa juu chini, “naitwa Lukundame,”


naye akajiyambulisha.
“Lukundame Hasheem!” Amata akataja jina zima.
“Yes!”
“Pole sana kwa kifo cha Mzee Hasheem!” Amata
akamwambia makusudi ili kumvuruga akili na kumtia hasira.
Lukundame alipata mshtuko, Akalia sana tena kwa uchungu
mkubwa. Dakika tano za kumbembeleza zilikuwa ngumu.
“Mwache alie, kilio umpa faraja mfiwa,” Amata akamwambia
Jasmin aliyekuwa akaingia ndani muda ule. Dakika kumi baadae
akatulia na kumtazama Amata aliyekuwa mbele yake.
“Baba yangu amekufaje?” Lukundame akauliza.
“Baba yako ni shujaa na ni mwanaume kwelikweli…”
“Kwanini unasema hivyo?” akauliza huku bado akiwa kwenye
kilio cha kwikwi. Akivuta kamasi jepesi kila muda kulizuia
lisimponyoke.
“Amejiua,” Amata akajibu. Lukundame akaangusha kilio
kingine cha uchungu.
“Aaali-ku-wa baba ya-ngu ppppeke ya-ke… na-ni ata-ni-
ffffarri-ji mimi?”akaliana kulia, safari hii dakika ishirini na tano
zilipita. Alipotulia bado Amata alikuwa palepale.
“Pole!” akamfariji.
“Asante… lakini nani, ni nani kasababisa kifo cha baba yangu
kipenzi?” Lukundame akauliza.
“Ndiyo maana upo hapa ili tushirikiane kujua chanzo na nani
kasababisha. Upo tayari kutoa ushirikiano?” Amata akamuuliza.
“Ndiyo, nipo tayari,” Lukundame akajibu na kufuta machozi
kwa kiganja chake. Amata akaweka mezani picha tano za watu
tofauti kati ya hizo tatu zilandikwa neno ‘Deceased’ na mbili
hazikuandikwa chochote. Picha hizo zilikuwa za vijana kwenye asili
ya Kihindi si Kihindi, Kiarabu si Kiarabu, wapowapo tu.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Unamtambua nani kati yao?” Amata akamuuliza.Lukundame


akazisogeza zile picha na kuzitazama. Picha nne akazitenga
pembeni, mbili kwa mbili na moja akaiacha kando.
“Hawa wawili nawakumbuka,” akamsogezea Amata, “hawa
walikuja ofini kwangu kuomba niwapeleke waonane na Mzee
Hasheem, na ndiyo waliniteka siku iliyofuata,” akaeleza. “Na hawa
wawili nawakumbuka pia, mmoja alikuwa kwenye ile meli
nilipotekwa na huyu mwingine alikuwa akija mara chache…”
akaeleza vizuri.
“Umewahi kuwaona kabla au ni siku hizohizo tu?”
“Ni siku hizohizo tu” akajibu.
“Je uliwaeleza chochote kuhusu baba yako?”
“Ndiyo, kwanza sikutaka kuwaambia, lakini walinitesa sana na
kunipiga mpaka nikaamua kuwaelekeza alipo,” Lukundame
akauliza.
“Walikwenda?”
“Walikwenda… waliporudi siku iliyofuata walikuwa
wamechukia sana, wakanipiga karibu na kuniua…”
“Kwa nini walichukia?”
“Walikuwa wanasema hawakukuta cha maana kwa mzee zaidi
ya mwili wake, nikajua wanaamanisha amekufa lakini sikuwaamini
nilijua watakuwa wamemteka na kumpeleka sehemu…”
Lukundame akajibu kwa ufasaha kabisa.
“Sawa! Unafikiri kwa nini walikuwa wanamtaka Mzee
Hasheem?” Amata akauliza swali lililouchoma moyo wa
mwanamke huyo.
“Kuna jambo ambalo baba alikuwa nalo… nadhani mmesikia
kuhusu kupotea kwa ndege ya kivita ya JW iliyokuwa ikitokea Urusi
kuja Tanzania…”
“Ndiyo…”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Good, sasa wakati mradi huu unaanzishwa na serikali miaka


mitatu iliyopita, walimshirikisha mzee kwa kuwa yeye ni mtaalamu
mbobezi wa mifumo ya ndege za kivita na mawasiliano ya anga…”
“Aisee kumbe alikuwa mtu mzito!” Amata akajifanya
kusangaa sana.
“Ndiyo, amesoma na kutumikia majeshi ya anga zaidi ya kumi
na sita duniani…”
“Akiwa JW?”
“Ndiyo, akiwa JW… sasa mzee Hasheem ndiye aliyedizaini
michoro ya mifumo ya kiusalama ya hizo ndege… nakumbuka
aliwahi kuniambia kuwa ‘kama ndege hizi zikiwepo Tanzania,
hakuna jeshi lolote litakalotusumbua kwa kuwa ni mifumo ya
kisasa sana,’” Lukundame akaeleza.
“Sasa kwa nini walikuwa wanamtafuta?”
“Hapo sasa ndipo kuna kitu kilichojificha ambacho hata mimi
sikijui au naweza kujua kidogo sana…”
“Niambie hicho kidogo…”
“Unajua mdogo wangu mimi anaitwa Jamila alikuwamo
kwenye ile ndege. Huyu Jamila ni kepteni wa jeshi na alikwenda na
wenzake Urusi ili kujifunza zaidi juu ya ndege hizo na mifumo
yake. Wakati wote wa mafunzo yao na uundaji wa ndege zile Mzee
Hasheem alikuwa akifuatilia kwa njia ya mtandao kana kwamba
yuko pale. Rafiki yake wa karibu ambaye amesoma naye raia wa
Serbia anaitwa Kotvich ndiye alikuwa akiwasiliana naye mara nyingi
kwa sababu huyu Kotvich alikuwepo kule Urusi na alikuwa
msimamizi wa kazi hiyo…”
“Enhe…”
“Sasa baba alinambia kuwa kuna aina ya code ambazo ili
mfumo ule ufanye kazi lazima ziingizwe kwanza na hizo code
watapewa wao yaani Jamila na wenzake,kila mmoja code moja”
akadadavua. “Lakini yeye Hasheem aliweza kuzipata code zote
katika mifumo hiyo ya kompyuta na alikuwa nazo,”
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Unataka kunambia walikuwa wanataka hizo code?” Amata


akahoji.
“Naikiri ndiyo, kwa sababu ile ndege ilipotea, kuna tetesi
imetekwa kwa kwasababu baba alikuwa anafuatilia safari nzima ya
ndege ile… siku hiyo akanambia mawasiliano ya ndege hiyo
yamehakiwa yaani yameingiliwa hivyo ndege inapoteza muelekeo,
akawasiliana na Jamila lakini kabla hajafanikiwa kumwelekeza cha
kufanya mawasiliano yakakatika kabisa,”
“Aisee kumbe ndo maana amepata shida zote hizo….” Amata
akasikitika.
“Tangu hapo, baba amekuwa akiandamwa sana, mara ya
mwisho alikuja Jenerali Mwambope mara tatu akimshawishi kumpa
hizo code kama anazijua…”
“Wao walijuaje kama anazijua?” Amata akauliza.
“Nilimuuliza hilo swali, akanambia ana wasiwasi na Kotvich
kuwa amewaambia kwa sababu ni yeye tu anayejua kuwa Hasheem
anafuatilia kila kitu…”
“Na alipokwambia kuwa mawasiliano yameinghiliwa
alikwambia anamhisi nani kafanya uhalifu huo?”
“Alisema asilimia mia na moja ni Kotvich kwa sababu hakuna
binadamu anayeweza kuingilia mifumo hiyo zaidi ya Kotvich na
yeye basi!”
“Kotvich…” Amata akarudia lile jina.
“Je unajua au alikwambia kuwa wakati hayo yote yanatokea
mpaka mawasiliano kukatika ndege ilikuwa wapi?”
“Hakuniambia… jambo pekee ninaloweza kuwaambia ni
kuwa kuna kijana mmoja mwanajeshi pia yupo Kizuka, huyu
alikuwa akija mara nyingi kujifunza kwa baba… huyu anaweza
kutegua kitendawili endapo tungeipata laptop kubwa ya baba
aliyekuwa akiitumia na vifaa vyake. Sasa sijui kama ipo maana wale
washenzi walimvamia mzee…” Lukundame akaeleza.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Sawa, hiyo laptop na vikolokolo vyake vyote vipo hapa!”


Amata akaeleza.
“Sure? Basi atafutwe huyu kijana, simjui jina ila yupo Kizuka,
anaweza kutumia na akatoa jibu sahihi… mmeipataje hiyo laptop?”
akaeleza na kuuliza.
“Nilikwenda mimi nikaonana na Hasheem, tukazungumza
lakini baba yako hakuamini kabisa kama mimi ni mwanausalama
wa serikali…”
“Asingeamini, alikuwa anaogopa hata akimuona mende…”
“Yeah” Amata akasita kidogo, “baba yako alinipa kabrasha
hili, vitu vilivyoandikwa humu vingi sijaelewa,” akampatia.
Lukundame akaliangalia na kulifunua hapa na pale, akaliweka
mezani, “hilo ndilo walilokuwa wanalitaka, hilihili… dah!”
“Baada ya kunipa hili kabrasha wakati nalipekuapekua ndipo
nikasikia kishindo cha risasi kutazama alikuwa kajiua…” Amata
akaeleza.
Lukundame akamtazama Amata, midomo ikaanza
Kumchezacheza, macho yakatona machozi. Amata aliiona hali ile
akajua wazi nini kinataka kutokea pindi tu akiitoa kauli yake
iliyokuwa tayari kwenye kingo za midomo yake.

“Mzee Hasheem alijiua kwa bastola yake mwenyewe.


Nilipogeuza shingo baada ya kishindo kile nilishuhudia mwili
wenye kichwa kilichofumuliwa vibaya kwa risasi. Pole sana
Lukundame,” akamwambia. Tofauti na matarijio yake, mwanamke
yule aliinama tu kidogo kisha akapiga ngumi mezani.

“Hapa kuna mchezo unaoendelea…” akasema.

“Kwa vipi?”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Nahisi hili swala, wapo watu katika serikali yetu hii


wameingia kwenye biashara haramu. Kwa mtazamo wangu hii
ndege imehujumiwa,” Lukundame akazungumza mara hii si kama
yule aliyefiwa na baba yake.
“Kuna kiongozi mwingine wa serikali aliyekuwa akija?”
“Kabla ya Mwambope, CDF mwenyewe alikuwa akifika, mara
mbili nimemuona… na mara tatu amepigiwa simu moja kwa moja
kutoka nyumba kuu…” yule mwanamke akamweleza Amata.
Amata akabaki kimya kabisa, hakuwa na la kusema.
“Unajua CDF alikuja kuzungumza naye nini na hiyo simu ya
nyumba kuu ilihusu nini?”
“Hapana!” akajibu na kutulia kwa jozi la sekunde. Amata
akaandika vitu Fulani kwenye kijitabu chake.

“Mr. Spark!” akaita.

“Niambie…”

“Maiti ya baba yangu ipo wapi?” Lukundame akauliza.

“Imehifadhiwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja,”

“Sawa. Baada ya sakata hili nitamzika baba yangu hata


kama ni miaka kumi, waambie tu wamuhifadhi…” Lukundame
akasema.

Amata akabaki akimtizama na kushangaa ujasiri huo


anautoa wapi ilhali dakika chache tu zilizopita alikuwa tepetepe
kwa chozi la maombolezo.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Sawa!” akamjibu, “sasa tunawezaje kumpata huyo kijana


ili ajaribu kuona kama kuna lolote kwenye ile laptop?” Amata
akamtupia swali.

“Yupo Kizuka, nafikiri jambo muhimu kwa sasa ni kwenda


Kizuka kumuona…” Lukundame akatoa ushauri.

“Sawa,” Amata akajibu na kubonyeza kitufe kidogo kilicho


kwenye sakafu usawa wa mguu wake. Mlango ukafunguliwa.
Daktari Jasmini akaingia na kumchukua Lukundame, wakatoka
pamoja na kumrudisha katika chumba chake.

Kamanda Amata akatoka na kuingia katika chumba


alichomuacha Jasmini na Scoba, “vipi, mmerekodi kila kitu?”

“Ndiyo…”

“Sawa nafikiri sasa tuanze safari ya kwenda Kizuka kumfata


huyo kijana ili aweze kutuambia kitu,” Amata akawaambia.

“Hiyo Laptop unayo kweli?” Scoba akatia shaka.

“Kila kitu kipo yaani ninavyokwambia twende ujue kila kitu


nimekipanga…”

“Tunaenda na huyo mwanamke?” Jasmin akahoji.

“Tuamue sisi, tumuache au twende nae?” Amata akauliza.


Sekunde za ukimya zikajidai kati yao.

“Uamuzi mzuri ni kwenda naye kwa kuwa yeye anamjua


huyo mtu, so atakuwa na uhakika naye akimuona… si mnajua hii
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

ishu ilivyo na huyo Lukundame kasema kuwa kuna uwezekano wa


mchezo wa watu wakubwa…” Jasmin akatoa jibu, safari
ikaandaliwa. Amata akaingia katika ofisi wanayotumia kwa
mawasiliano na kupiga namba ya Madam S kumweleza yaliyojiri
tangu siku iliyopita.

“Kwa hiyo mnaondoka asubuhi hii?” akamuuliza Amata.

“Yes! Lazima tulifikishe hili swala katika hatua ambayo


itatuelekeza nini cha kufanya. Hata hivyo nitaporudi nitahitaji
kunywa juisi na wewe,” Amata akaeleza.

“Sawa, kila la heri kijana nategemea mazuri kutoka kwako,”


Madam S akamtakia mema kijana wake, “mtahitaji msaada wowote
kwangu?” akamuuliza.

“Aaaaaaa hapana,”

“Mtatumia usafiri gani?”

“Nadhani tutatumia helikopta ya jeshi,” Amata akaeleza.

“No. Siwashauri… tumieni barabara, chukueni sweeper


mmoja awasindikize mpaka Mlandizi ili msikae na mafoleni,”
Madam S akatoa maelekezo.

“Sawa”.

Mara baada ya kukata simu hiyo akapiga nyingine kwa


Simbeye na kumtaka kumpatia msaada wa mtu wa kutangulia na
pikipiki ili kazi yao iende haraka zaidi. Ombi likakubaliwa.
Akakusanya ile kompyuta, lile kabrasha na kifaa kingine ambacho
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Lukundame alisema wasikiache. Wakamchukua na mwanamke


huyo wakateremka chini ya jengo hilo na kuingia kwenye Land
Cruiser tayari kwa safari. Kama kawaida, mtu yeyote hatakiwi kujua
uelekeo wa jumba hilo lilipo.

“Samahani Lukundame,” Jasmini akamwambia na kumvika


fuko jeusi kichwani, akamtia pingu mikononi na mnyororo
mguuni, “si kwamba ni mfungwa, ila huu ndiyo utaratibu wetu,”
akamjuza.

“Usihofu, maadam najua nipo sehemu salama,” akajibu na


lile gari likaondoka. Scoba alikuwa nyuma ya usukani akiongoza
chombo hicho kwa usatdi wa hali ya juu mpaka kituo cha polisi cha
kati. Walipofika pale Jasmini akamvua Lukundame lile guo
kichwani, wakachukua askari mwenye pikipiki mmoja na safari
ikaanza kuelekea Kizuka, Morogoro.

* * *

Sajini Mlewele alikuwa ametingwa katika kazi yake ya rada


pale alipofikiwa na simu ya kumtaka kufika ofini kwa mkuu wa
kikosi. Amata na kikosi chake walikuwa wamekwishafika na
kujitambulisha kwa mkuu huyo kama wachunguzi kutoka serikalini.

Sajini Mlewele alikutana na ugeni huo, aliyemtambua katika


kundi hilo ni Lukundame pekee. Usoni mwake tu kijana huyo
alionekana kupata mshtuko wa wazi. Hilo Amata, Scoba na Jasmini
waliligundua.

“Ndiyo afande!” kaitika na kusimama kikakamavu.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Sajini, kuna hawa wageni kutoka serikalini wana


mazungumzo na wewe,” mkuu wake akamweleza.

“Ndiyo afande!” akaitika. Akawaruhusu. Amata akashauri


mazungumzo yale yafanyikie kwenye gari walilokuja nalo.
Haikupingwa. Ndani ya gari lile Amata aliitoa ile laptop na lile
kabrasha na kuviweka juu ya kiti. Akaifungua ile na kuiwasha.
Ilipowaka ikadai nywila, Lukundame akaingiza nywila za baba yake
kwani alikuwa anazijua vyema.

“Martini!” Amata akaita.

“Ndiyo!” akaitikia.

“Tumekuja kwako kwa maelekezo stahiki kabisa ya Mzee


Hasheem, je unamfahamu?” Amata akauliza.

“Ninamfahamu, na huyu ni binti yake,”

“Sawa, unaifahamu hii kompyuta?” Amata akamuuliza.

“Ndiyo naifahamu…”

“Hebu nambie mahusiano yako wewe na mzee Hasheem


nahii kompyuta,” Amata akamwambia.

“Mimi kutokana na kazi yangu, ya uongozaji rada nilijikuta


najenga urafiki sana na kepteni Jamila, Mungu amrehemu. Huyu
Jamila ndiye aliniunganisha na baba yake Mzee Hasheem ambaye
ni mwanajeshi mstahafu, mtaalamu wa mambo ya anga. Hivyo
nikawa kama mwanafunzi wake kila mwisho wa juma nikiwa off
nilikuwa naenda Zanzibar kujifunza machache…” Martin akaeleza.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Sawa! Kwa nini umesema ‘Mungu amrehemu’ Jamila?”


Amata akahoji.

“Aaa Jamila amepotea na ile ndege tuliyokuwa tumejiandaa


kuipokea hapa Kizuka,” Martin akaeleza.
“Ina maana ninyi na utaalam wenu wote mmeshindwa kujua
ndege hiyo imepotelea wapi?”
“Aaaaanh hatuna rada yenye nguvu kuweza kufika umbali
huo. Unajua mataifa makubwa yana rada za kisasa sana ambazo
zimeunganishwa moja kwa moja na satelaiti… hivyo kwao ni rahisi
kujua chombo chao kipo wapi na wakati gani…”
“Ok, tusipoteze muda, naona kwa kuwa wewe umekuwa
mwanafunzi mzuri wa Hasheem basi unaweza kututegulia
kitendawili hiki…”
“Kipi tena?”
“Tulia…” Amata akamwambia na kumwomba Jasmini
ampatie mkoba uliokuwa pembeni yake. Akampatia ile kompyuta
mpakato pamoja na kifaa cha kusikilizia. Ndani ya ule mkoba
akatoa kabrasha moja lenye karatasi kadhaa, vyote akaiweka juu ya
kiti.
Moja kwa moja, Mlewele akaingia katika ukurasa wa tarehe
ambayo ndege ile ilipotea..
“Haya, tumia elimu yako kujua kilichomo humo…” Amata
akamwambia Martin halafu wote wakawa kimya na kumwacha
kijana huyo akichakata ile laptop hapa na pale. Martin akavaa kile
kifaa cha mawasiliano na kuipakata ile laptop. Ni Lukundame tu
aliyekuwa akifuatilia kile kinachofanyika.
“Mmmmm no!” yule kijana aliguna na kuendelea kusikiliza
huku akirudisha hapa na pale na kuendelea kusoma tarakimu nyingi
zilizokuwa zikipita kwenye kioo. Akapiga vidole vyake hewani na
kuomba karatasi na peni. Akapatiwa na kuanza kuandika vitu fulani
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

juu yake. Alipomaliza kuandika, akavua kile kifaa na kuisukuma


kompyuta kando. Akajiegemeza kwenye kiti na kushusha pumzi
ndefu.
“Vipi?” Amata akawa was kwanza kuuliza.
“No!” akajibu kifupi kisha akachukua lile kabrasha na
kulipekua hapa na pale. Akagota kwenye kurasa moja wapo na
kuonekana akisoma kwa makini zile namba zilizoandikwa na
Hasheem.
“Hapa ticha alikuwa akifuatilia safari na taarifa zote za ile
ndege tangu itoke Urusi…”
“Enhe…” Amata akataka kujua zaidi.
“Kuna kitu anamwambia Jemmy”
“Jemmy ndo nani?”
“Oh sorry, Jamila… anamwambia kuwa kuna mawimbi mapya
yanaingilia yale ya mfumo wa ndege yao… sasa hapa kabla
hajamaliza kuzungumza na Jamila mawasiliano ya ile ndege
yamekatika … ikiwa na maana kwamba, kama ilishika moto ndo
hapa, kama ilianguka ndo hapa, kama ilitekwa ndo hapa.”
“Na sisi tunataka tupajue hapo…”
“Ok!” akajipapasapapasa mifukoni kisha akatulia kwa
sekunde, “mna ramani ya dunia hapo?” akauliza.
“Hapana! Tumia kompyuta hapo au hii tablet…” Amata
akajibu na Jasmini akampatia tablet yake ikiwa imewashwa tayari.
Akaipokea na kuingia mtandaoni. Akaingiza mamba fulani
alizochukua kwenye ile kompyuta ya Hasheem. Akachakata hapa
na pale na kutulia “katikati ya China,Pakistan na India… mmmm
Kashmir, yes Kashmir…” akawaambia.
“What?”
“Katika kompyuta hiyo, hesabu za kijiografia zinanambia
kuwa mawasiliano yalikatika wakati ndege hiyo ikiwa kwenye
coordination ya 34.0°Kaskazini na 76.5° Mashairiki… katika ramani

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

hapa pia inaonesa matokeo ya coordination hiyo ni Kashmir” yule


kijana akaeleza vizuri na kueleweka.
“Nina swali moja kabla halijanitoka kichwani…”
“Uliza kaka!” Mlewele akamruhusu Amata.
“Hasheem alimwambia Jammila kuwa kuna mawimbi
yanaingilia mawasiliano yao…”
“Ndiyo…”
“Sasa hayo mawimbi unaweza kutambua ni ya namna gani au
yametokea wapi, yaani kama kuna chochote cha
kuyatambuoisha…” Amata akadodosa.
“Sikufuatilia hilo, lakini kutokana na usalama wa mfumo
uliofungwa kwenye ile ndege naweza kusema kuwa Mzee Hasheem
ndiye mtu pekee ambaye angeweza kuuingilia huo mfumo kutoka
nje ya ndege ile…” akaeleza.
“Basi imetosha!” Lukundame akatamka. Amata akamtazama
mwanamke huyo kwa nukta kadhaa kisha akamgeukia Mlewele.
“Sawa asante sana kwa maelekezo yako. Tutayafanyia kazi lakini
tahadhari usimwambie mtu yeyote kuhusu hili, ukikaidi utajutia
maisha yako. Martin tutakutafuta muda wowote tukikuhitaji…”
akamwambia.
Martin akarudi kuendelea na kazi yake. Amata na kundi lake
wakaagana na yule mkuu wa kikosi kisha wakaondoka zao kurudi.

* * * *

Katika casino ya Red Carpet maeneo ya Upanga, Kamanda


Amata aliketi katika kiti cha peke yake. Bilauri yake ilikuwa imejaa
pomoni kinywaji cha JackDaniel. Alionekana mtu mwenye mawazo
sana. Akiwa katika hali hiyo, meza yake ikagongwa mara tatu,
akainua uso na kukutana na Madam S.
“Naweza kuketi?” Madam S akauliza.
“Bila shaka….”
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Madam S akavuta kiti kilichobaki wazi akaketi, “nipe habari za


Kizuka…” akaanzisha mazungumzo.
“Kitendawili kinateguka…” akaingiza mkono mfukoni na
kutoa karatasi moja ndogo na kumpatia. Madam S akaisoma
harakaharaka.
“Ina kazi?” akauliza.
“Haina…”
Akaitia kinywani na kuitafuna, “Kashmir…” akatamka.
“Pamefanya nini?”
Wakiwa katika mazungumzo hayo mhudumu akafika kutaka
kumhudumia mama huyo.
“Asante, tunaondoka sasa hivi…” akamshukuru. “Ina maana
kazi inatakiwa kuhamia Kashmir… lakini kipi kinathibitika, ndege
imetekwa, imeungua au kitu gani?
“Kwa maelezo ya yule kijana, hii ndege imetekwa
kimfumo…”
“Yaani!”
“Yaani ilitekwa kimawasiliano halafu ikaongozwa vingine,
hivyo itakuwa ipo mahali na watu wetu si ajabu wako hai…”
“Tuanzie wapi?” Madam S akauliza.
“Bado natafakari…. Kashmir hapakai sawa kichwani
mwangu… ni mabonde, milima, watu masikini, migogoro ya eneo
na kadhalika,” Amata akaeleza. Madam S akabaki kumtazama
kijana wake. Simu ya Madam S ikaita kwa fujo, akaiinua na
kuitazama.
“TSA 2” Madam S akatamka na kuiweka simu ile sikioni.
“HOT”
“TSA 2 nipo bandani…”
“Umekuja wakati muafaka kabisa, karibu nyumbani. Kesho
asubuhi uonane na TSA 1 Shamba…”
“Copy!”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Amata na Madam S wakaongea maneno machache tu kisha


wakaagana.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

09
KAMA kuna siku ambayo jiji la Dar as salaam lilikuwa na
foleni ya kutisha, ilikuwa hii. Kamanda Amata alikwama kwenye
foleni zaidi ya saa moja na nusu. Alitamani ashuke na kuliacha gari
barabarani lakini haikuwa hivyo. Mvua kubwa iliyoambatana na
radi ilikuwa ikiendelea. Saa tatu asubuhi ilikuwa kama saa kumi na
mbili alfajiri kutokana na giza lililosababishwa na mawingu mazito.
Wimbo wa Lionel Richie, Stuck on you, ulikuwa ukimtumbuiza.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Muungurumo wa simu yake ukamgutusha kutoka katika burudani


hiyo iliyokuwa ikimkumbusha mpenzi wake Rakhma wa Tandika.
“Yes Chiba!” akaipokea huku akipunguza sauti ya muziki ule.
“Wapi kaka?”
“Nimenasa kwenye foleni hapa Salenda,” Amata akamweleza.
“Pole, achana na hilo gari nakuja kukuchukua, nipo Ofisi
Ndogo…”
“Ok boy!” Amata akajibu na kuanza kutafuta njia ya kulitoa
gari lile barabarani. Alipofanikiwa, akaliegesha kwenye kituo cha
polisi cha hapo Salenda.Dakika kumi hazikupita, Chiba aliwasili
katika kituo hicho akiwa na pikipiki kubwa aina yaHonda 250.
Wawili hawa walisalimiana na kukumbatiana kisha wakaondoka
zao.
“Chiba! Hebu twende nyumba namba kumi na mbili…”
“Kuna nini huko? Maana sijaenda nina kama miezi mitatu”
Chiba akauliza.
“Hata mimi wiki hii ndo nimeingia huko… kuna mzigo
nimeuweka pale nataka unisaidie, au kuna ishu na HOT?”
“Hapana, mi nilikuwa naripoti tu, na nimeshamalizana naye,
amenambia nipumzike siku saba hivi…”
“Ok! Twende namba kumi na mbili,” Amata akamwambia
Chiba. Naye akaliwasha lile pikipiki na kuelekea Magomeni Kagera.
Nyumba namba kumi na mbili ndiko Amata alikomfungia Mwaja
na kuacha baadhi ya vitu kutoka kwa Fareed.Iliwachukua dakika
ishirini na mbili tu kuwasili ilipo ile nyumba. Chiba akaegesha
pikipiki nje na wote wawili wakaingia.
“Misheni imeenda poa huko lakini?” Amata akamuuliza Chiba
kuhusu kazi aliyotumwa kuifanya.
“Tumshukuru Mungu… upande wangu imekamilika
nimemwacha Gina kuna mambo apambane nayo kwanza,” Chiba
akaeleza.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Yule namwaminia,” akakohoa kidogo na kuendelea kusema,


“hapa bwana kuna jambo zito sana.” Wakasimama nje ya chumba
alichomfungia Mwaja. “Humu ndani kuna sapraiz…” akasema na
huku akifungua ule mlango.

* * * *
Mwaja alikuwa kajilaza kwenye kitanda kile cha kamba kama
mtoto mkiwa. Zilikwishapita saa takribani thelathini tangu
afungiwe mule ndani. Aliposikia mlango ule ukifunguliwa akaketi.
Sura yake ilikuwa imekunjamana kwa usingizi.
“Umeinjoi siyo?” Amata akamuuliza Mwaja.
“Mambo unayonifanyia Amata, sawa tu…” Mwaja
akalalamika.
“Mwaja, nimekuweka hapa kwa usalama wako, usilalamike…”
Amata akamwambia.
“Bila chakula Amata, hapana….” Mwaja akalalamika.
“Nilikupa pipi hukula?”
“Yaani mi wa kushindia pipi?”
“Meza hata moja, kwani mi niliyekupa sina akili!” Amata
akang’aka. Mwaja akabaki kimya.
Chiba akasogea kumtazama huyo mwanamke, “huyu ni nani?”
akauliza.
“Huyu ni Meja Mwaja wa JW kitengo cha Masijala pale
Makao Makuu Upanga,” Amata akajibu.
“Mbona yuko hivi?” Chiba akauliza.
“Huyu nilipomchukua alikuwa hivihivi… naakitoka hapa
anaenda kujibu kesi yake…” Amata akaeleza.
“Pole mrembo!” Chiba akampoza.
“Kula hizo pipi. Saa arobaini na nane tangu nimekuweka
humu zikitimia ndo nitakutoa na kukupeleka panapohusika…”
Amata akamwambia Mwaja na kuufunga ule mlango.Katika
chumba kingine, Chiba na Amata waliketi kwenye kiti hiki na kile.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Hapa kuna sakata la upotevu sijui utekwaji wa ndege…”


“Ile ya jeshi?”
“Ndiyo! Sasa huyu mwanamke huyu anahusika kwa namna
moja au nyingine…”
“Sasa mbona hana nguo? Maana pale ni sawa na kutokuwa na
nguo…”
“Nilimchukua hivyohivyo maana nilimuokoa kwenye kifo
akiwa hivohivo…. Chiba, ni stori ndefu sana, maadam umerudi
utaijua tu..” Amata akajibu.
Amata akavuta mtoto wa kabati na kutoa ubamba ule aliouchukua
kwa Fareed, akamkabidhi Chiba, “nisaidie kufungua kuna vitu
nataka kujua humo, halafu kule shamba kuna vitu pia nataka
unisaidie, halafu ndo utaanza likizo…” akamwambia. Chiba
akaugeuzageuza ule ubamba na kuuwasha. Baada ya sekunde
chache, ukamdai alama za vidole. Chiba akamtazama Amata.
“Ndo hapo nimeshindwa…”
“Kamanda, mwenye tablet hii yuko wapi?” Chiba akauliza.
“Nilishamvunja pumzi jana, nahisi yupo mortuary” Amata
akajibu.
“Sawa, kazi ndogo, twende mortuary tukamkate kidole
tuondoke nacho, kitatusaidia kufungua hii tablet kila
tunapohitaji…” Chiba akamwambia Amata.
“Dah! Chiba una roho mbaya namna hiyo? Ukamkate kidole
marehemu!” Amata akashangaa.
“Khaaaa! Sasa nani ana roho mbaya? Wewe uliyemuua au
mimi ninayetaka kidole chake?”
“Haya, nimekuelewa TSA2…” Amata akajibu na kuiinua simu
yake,akapiga namba fulani na kuiweka sikioni.
“Ndiyo mzee, kijana wako hapa…. Nataka kujua tu lile gege
mmelitupa wapi?”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Muhimbili… halafu uje uchukue vitu vingine hapa na


kuwaona wagonjwa wako!” Sauti ya Simbeye ikaunguruma upande
wa pili wa simu ile. Amata akakata simu na kuitua mezani.
“Muhimbili!” Akamwambia Chiba.
“Twende…”
Chiba na Amata wakatoka pamoja na ule ubamba tayari kwa
safari ya Muhimbili.
“Haumuagi mateka wako…”
“Achana naye nitamtoa kesho, kuna mambo nahitaji kujua
kwanza. Nikiyakamilisha nitamwacha. Maana nikimwacha sasa
ataharibu upelelezi…”
“Ni kweli meja wa jeshi?”
“Ee ni meja, si kwamba namtania… mtu mkubwa sana huyo
mwanamke,ofisa wa jeshi.” Amata akajibu kisha wakaondoka zao.

* * * *

Mchana wa siku hiyo, Madam S alikuwa ndani ya chumba


kidogo kinachojulikana kama Kilimanjaro Square katika Ikulu ya
Magogoni. Ndani ya chumba hicho kilichokua ofisi ya siri ya Rais,
walikuwamo watu wawili tu; Madam S na Mkuu wa nchi. Kabrasha
la awali la taarifa ya upotevu wa ndege ambalo Madam S alilipa jina
KASHMIR lilikuwa katikati yao.
“Kwa hiyo unataka kuniambia kuwa hii itakuwa operesheni
Kashmir?” Rais akauliza.
“Mpaka hapa tulipofikia, naweza kusema, ndiyo…”
“Kwanini unasema ‘mpaka hapa tulipofikia’?”
“Kwa sababu tupo kwenye upelelezi wa hatua za mwisho…
tafutishi zote zitakamilika saa arobaini na nane, ninaamini…”
Madam S akajibu. Mheshimiwa Rais akatikisa kichwa kukubaliana
na mwanamama huyo.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Sawa, serikali inaiamini idara yako kutokana na weledi


mkubwa wa kazi yenu… hivyo ninasubiri taarifa yako ya mwisho
halafu tuweke maazimio…” Rais akaeleza. Kikao kikafungwa kwa
miadi ya kukutana baada ya siku mbili. Wakaagana.
“Uwe mwangalifu… maana kuna mambo naona kama
hayaendi sawa!” Rais akamwambia Madam S.
“Bila shaka mheshimiwa…” Madam S akajibu wakati akiingia
katika BMW lililomleta mahala hapo. Akaondoka zake.
Uwe mwangalifu… maana kuna mambo naona hayaendi sawa! Sauti
ya Mkuu wa nchi ikamrudia kichwani mwake. Mambo gani?
Akajiuliza. Akachukua simu yake na kubofya namba ya Amata,
akaiweka sikioni.
“Upo wapi?” akamuuliza.
“Tupo Muhimbili,” Amata akajibu.
“Mpo! Na nani?”
“Alfa na Beta…”
“Kuna nini?”
“Kuna marehemu tunamhoji,”
“Sawa ukimaliza nahitaji kuonana nawe,” Madam S
akamwambka.
“Nafikiri Shamba ni kuzuri zaidi…” Amata akapendekeza.
“Umesomeka!” akajibu na kukata simu.

* * * *

Huko Pakistan katika kambi ya Izbul Mujahedeen, kikao


kizito kilikuwa kikiendelea. Viongozi wa juu walikutana na
makamanda wao kuweka sawa mikakati. Kikundi hicho
kilichokuwa katika mapambano makali na jeshi la India kilihitaji
kujipanga upya kimfumo ili kukabiliana na jeshi hilo hatari katika
kuikomboa Jammu na Kashmir, koloni lililoachwa na Mwingereza

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

bila mwenyewe. Labda walijua nini kitatokea na walipenda kitokee.


Kikatokea.

* * * *

SHAMBA

Chiba na Amata walitingwa kwa kuweka mambo sawa. Mbele


yao kulikuwa na laptop ile ambayo walienda nayo kule Kizuka.
Tayari ubamba ule aliokabidhiwa Chiba ulikwishafunguliwa, kila
kitu kilikuwa kinasomeka bila shida. Mambo mengi waliyoyakuta
kwenye ubamba ule hayakuwa tofauti na yale yaliyokuwa kwenye
simu ambayo Amata aliichukua kule kwa Mwambope. Isipokuwa
mengine machache waliyagundua.
“Fernandez!” Chiba akatamka, “Fernandez ndiye tajiri
aliyemtuma Fareed na ndugu zake kuja Tanzania…” akaendelea
kueleza huku Amata akisikiliza kwa makini.
“Huyo Fernandez yuko wapi?” Amata akauliza. Chiba
akaendelea na kuperuzi hapa na pale kutafuta mile alichoulizwa.
“Huyu Fernandez ni raia wa Venezuela lakini haijaelezwa
yuko wapi, kama Venezuela au wapi! Haijaelezwa…”
“Tutamfuatilia… yeye mpaka sasa ni target namba moja,”
Amata akatamka na kuandika kitu kwenye kitabu chake cha
kumbukumbu. Chiba akautua ule ubamba mezani, akaivuta ile
laptop na kuitazama. Kwanza ikamshangaza kwa muundo wake,
akaigeuzageuza na kisha akaiweka sawa. Akaiwasha, ikadai nywila.
“Password” Chiba akatamka. Amata akatabasamu, akageuza kiti
chake na kuinua mkonga wa simu, akabofya namba kadhaa na
kuiweka sikioni. Simu ikapokelewa katika chumba alichokuwamo
Lukundame.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Hello, yeah tunaomba password ya kompyuta ya Mzee


Hasheem…” akamwambia. Ukimya kidogo ukapita, Lukundame
alihofu jambo.
“Wewe ni nani?” Lukundame, kutoka upande wa pili akauliza.
“Ni mimi niliyekuleta humu ndani, Mr Spark…”
“Ok… umekikalia lakini huwezi kuondoka nacho, mia moja,
asilimia, dash…” akatamka.
“Umekikalia huwezi kuondoka nacho…” Amata akarudia ile
sentensi.
“Oh! Kiti” akatamka na kuandika neno hilo kwenye ile laptop
kisha akamalizia na namba ‘moja, sifuri, sifuri’ akaweka alama ya
‘asilimia’ na kisha akamalizia na ‘dash’. Ile kompyuta ikafunguka.
Chiba akafungua hapa na pale asione kile anachokitafuta. Akaitalii
katika kila kona yake, asione kinachomfaa yeye wala Amata.
Wakapata wazo na kuiunganisha kwenye Wi-Fi. Kompyuta ile
ikapata nguvu ya mtandao, baadhi ya makabrasha yakaanza
kufunguka. Moja ya kabrasha lililowavutia lilikuwa na jina PT-502-
B.PEGANX.
“Fungua hilo folda” Amata akamwambia na Chiba akafanya
hivyo. Ndani ya folda hilo kulikuwa na dokumenti nyingi tofauti
tofauti. Moja wapo ambayo ilibeba jina la folda hilo lilikuwa na
michoro mingi ya ajabu ajabu na kodi nyingi za mtandao. Chiba
akatulia kufuatilia, kuna maeneo alielewa na kuna mengine
yalimwacha peupe.
“Hili ndilo tunalolitaka?” Chiba akamuuliza Amata.
“Nafikiri, hii ni michoro tu ya hiyo ndege… naona tu mifumo
ya kiinjinia, mi siielewi…” Chiba akalifunga na kufunguka jingine.
Hilo nalo akakutana na vitu vinavyofanana na vile ila hivi vilikuwa
ni mifumo ya kompyuta zaidi. Hapa aliambulia mengi sana,
akamdadavulia mengine Amata ambaye wala hakuwa na haja nayo.
Akaendelea kupekua huku na huko. Chiba akafika kwenye
dokumenti nyingine, hii sasa ilimpa jambo kubwa. Wakakaza
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

macho kuitazama na kuisoma. Kilikuwa na maelezo yanayoeleweka


kwa uwazi. Picha kadhaa za kompyuta iliyofungwa ndani ya boksi
na kuwekwa kiufundi kabisa kwenye dashboard ya ile ndege. Kila
kitu kilioneshwa kwa picha na maelekezo ya kuuendesa huo
mtambo.
Amata akahisi kuwa hiki ndicho kilichokuwa kikitafutwa.
Chini ya zile picha kuliwekwa nyingine tatu za watu watatu. Amata
akaigundua haraka ile ya Jamila. Zilikuwa picha za nusu. Chini ya
kila picha kulikuwa na namba maalum ambayo haikufanana na
nyingine.
“Pegan codes… Amata alisoma kwa sauti…” akatikisa kichwa.
Akampigapiga Chiba begani.
“Vipi?” Chiba akauliza.
“Pegan Codes… huu ndo mchezo mzima kaka… hawa
washenzi itakuwa wanataka hizi codes… maana umenambia kuwa
bila hizi, huo mfumo haufanyi kazi… basi wanataka hizi. Ina
maana kama wanataka hizi basi wanalo hilo sanduku… Pegan Box,
ambalo Captain Bakari, Joel na Jamila kila mmoja alikuwa na ya
kwake… ” Amata akaeleza na kuvuta kitabu chake cha
kumbukumbu akaandika yote aliyoyang’amua. Chiba akaendelea
kusoma na vitu vingine. Akafunga lile folda na kuingia kwenye
barua pepe, hakupata tabu kufunguka kwani kikasha cha barua
hizo kilikuwa wazi, hakikufungwa.
“Kamanda! Njoo tafadhali…” Chiba akaita. Amata aliyekuwa
tayari hatua mbili upande mwingine akarudi kwa bashasha
kusikiliza alichoitiwa. Moyo wake ulijawa tashwishwi ya kutaka
kujua. Chiba akainuka kitini, “kaa hapo umalize kazi yako, for your
eyes only…” akamwambia huku akiliendea jokofu na kuchukua coke
baridi sana. Kamanda Amata aliketi kwa utulivu na kusoma zile
barua pepe. Barua zile kilikuwa hazijafunguliwa bado. Amata
aligundua kuwa zilifika ndani ya saa kumi na mbili ambazo mauti
yalimkuta Mzee Hasheem.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Jamila yupo hai! Akajisemea moyoni ni huku akitabasamu.


Akaendelea kusoma na kusoma. Hapo akagundua kitu kingine, Peg-
flash! Akaandika kando. Kisha akachukua dakika kadhaa
kuchunguza barua pepe ile imetumwa kutoka wapi.
Pakistan, Islamabad, akagundua. Jamila yupo Islamabad?
Akajiuliza. Na hii Peg-flash ni kitu gani? Maswali yakamzidi uwezo.

‘…baba nafikir ni mimi tu nimesalimika,


na nimefanikiwa kubaki na peg-flash yangu…’

Akaeedelea kusoma ile sentensi kwenye ile barua pepe.

‘… pindi upatapo ujumbe huu nijulishe kwa


kuiwasha peg-flash yangu kwa kutumia hizo code zangu.’

Ule ujumbe ulikatikia hapo.Amata akamwita Chiba. “Vipi,


umepata cha maana?”
Chiba akauliza.
“Zaidi… lakini nimekwama hapa kwenye peg-flash”
akamwambia Chiba.

Chiba wa Chiba, TSA 2, alikuwa mmoja wa timu hii ya siri


hasa kwenye suala zima laCyber Intelligence. Aliijua tehama kwa
undani na kifuniko chake kilikuwa ni kazi yake kama Mhadhiri
Msaidizi katika masomo ya tehama katika Chuo Kikuu cha Dar es
salaam. Chiba alirudsha nyuma kwenye makabrasha ya awali na
kujaribu kuona kama angeweza kupata maana ya kitu hicho. Ni
pale kwenye ile michoro ya mfumo ule wa PT-502-B.PEGANX
alipokiona kitu hicho.
“Kwa kuoanisha maelezo haya hapa na yale ya kwenye ile
email… ina maana tukikliki hii bluu code ya Jamila basi hii Peg-flash
yake itawaka, na ikiwaka,kisha tuingize namba za huo mfumo, basi
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

itatuonesa moja kwa moja ni wapi hilo Pegan box lilipo…” Chiba
akaeleza.
“Nahisi tumemaliza kazi!” Amata akamwambia Chiba, "kliki
tuone kinachotokea" akamwambia. Chiba akaweka kila kitu sawa
na kuikliki ile bluu code pale chini ya picha ya Jamila.

* * * *

Akiwa ndani ya chumba alichohifadhiwa, Jamila alishtushwa


na bip hafifu iliyokuwa ikisikika kwa tofauti ya sekunde moja moja.
Haraka haraka akaanza kukitoa hicho kidubwasha. Jamila aliificha
Peg-flash yake ndani ya nguo ambapo haikuwa rahisi kwa mtu
mwingine kujua. Akafanikiwa na kukikamata mkononi. Kile
kidubwasha hakikuwa kikubwa sana, ni inchi tatu kwa inchi moja.
Kikiwa mkononi mwake ile bip ilikuwa ikiendelea huku taa ndogo
nyekundu ikiwaka-waka. Yeye akajua nini maana yake,
akatabasamu.
Finally! Akajisemea moyoni kisha akabofya kinobu kidogo
kilichoandika GPS. Alipokibofya akatabasamu na kushusha pumzi
huku akikibana kifuani kile kidubwasha. Jamila hakuamini hicho
kilichotokea. Akazima ule mlio na kukiacha kikiendelea kuwaka
ikiwa ni ishara kwamba kinawasiliana na rada iliyounganisshwa na
mfumo ule wa usalama ndani ya Pegan Box. Ikiwa na maana kuwa
aliye kwenye rada atajua ni wapi katika dunia hii Jamila alipo na
wapi box lile limehifadhiwa.

Matumaini mapya ya maisha kwa Jamila yalirudi. Hakujua nini


kitafuata kutoka kwa hao waliomteka. Swali kubwa alilojiuliza ni
kama kweli Bakari na Joel wapo hai. Alijua wazi kuwa Mzee
Hasheem atafanya lolote katika kuhakikisha binti yake anapatikana
hai na Pegan Box linapaikana. Akiwa na furaha na matumaini,
usingizi ukamchukua katika chumba hicho kidogo.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

* * * *
Macho ya Chiba na Amata yaliikodolea ile kompyuta
kutazama nini inataka kuwaambia. Rada ya kidijitali iliyokuwa
katika kompyuta ile ya Mzee Hasheem ikawaonesha uelekeo wa
wapi pegan box ilipo.
Kashmir! Amata akajisemea kichwani mwake.
“Mzigo upo Kashmir!” Chiba akamwambia Amata. TSA 1
akashusha pumzi ndefu. Akavuta hatua na kulifikia jokofu, yeye
hakuchukua Coke, bali pombe Kali. Akajimiminia kitoti kimoja na
kupiga pafu kavukavu. Aliporudi akaenda moja kwa moja kwenye
ramani kubwa iliyobandikwa ukutani na kutazama wapi Kashmir
ilipo. Si kwamba alikuwa haijui bali alitaka kujiridhisha.
“Sawa, sasa naweza kuwarudisha mateka wangu uraiani,
mmoja baada ya mwingine,” Amata akamwambia Chiba. Akaketi
na kuweka taarifa zake vizuri wakati Chiba akijiandaa kuliacha
jumba lile.
“Vipi?” akamuuliza.
“Naenda zangu kuanza likizo” Chiba akajibu huku tayari
mkoba wake ukiwa begani.
“Wasalimie…”

Saa Tisa alasiri ilimkuta Amata akiwa Ofisi Ndogo huku


Madam S akiwa katulia kitini kwake.
“Vipi?” Madam S akauliza.
“Nafikiri nilipofikia ni pazuri, kwa taarifa hii
nitakayokukabidhi kila kitu kitaeleweka vyema” Amata
akamwambia Madam S na kumpatia kadi mmweko. Mwanamama
huyo akaichomeka katika kompyuta yake ya mezani na kuanza
kusoma jambo moja baada ya jingine.
“Kwa hiyo mpaka sasa tunaamini kuwa Jamila yuko hai,”
“Ndiyo” Amata akajibu.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Unaamini vipi?”
“Jamila alimwandikia email Hasheem masaa kumi na mbili
kabla hajajiua… na inaonekana kuwa hat hakuzisoma barua
hizo…”
Madam S akatikisa kichwa kukubaliana naye, akaendelea kusoma
yale maandishi. “Kashmir…” akatamka. “Naweza kunakili kwenye
laptop yangu?”
“Ndiyo mama!” Amata akajibu.
“Sawa… nitakutana na Rais usiku wa leo… naomba usiwe
mbali sana kwani chochote atachosema kama kinatugusa moja kwa
moja nitakwambia usiku huuhuu,” Madam S akamwambia Amata.
“Halafu, nilikuwa sijakwambia…”
“Kitu gani?”
“Afisa wa jeshi anayetunza kumbukumbu pale Makao Makuu
ametoweka…” akamwabarisha.
“Ninaye mimi!”
“What?”
“Ninaye Mimi…” Amata akarudia jibu lake.
“Kijana una hatari sana wewe! Umemweka wapi na
unamfanya nini huko mpaka anasahau kazi…” Madam akamuuliza
Amata kwa ukali kidogo.
“Sikiliza Madam, yule afisa ni mmoja wa watu ninaowashukia
kwenye sakata hili,”
“Kivipi?”
“Kwanza kabisa, alikuwa hawala yake na Fareed”
“Fareed huyu uliyemuua?”
“Na siku nilipomuua Fareed nilimkuta na huyu mwanamke,
Meja Mwaja, kuna mambo nilikuwa nayataka kutoka kwake ndiyo
maana nikamficha ili niyajue ajuayo…”
“Umepata nini kutoka kwake?” Madam akazidi kuchimba.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Hamna analojua, zaidi yeye ndiye aliyekuwa mtoa taarifa kwa


Fareed bila kujijua. Kupitia yeye ndipo Fareed akajua wapi pa
kumpata Hasheem na kadhalika…”
“Jingine…”
“Fareed baada ya kumaliza kazi yake, alipanga kumuua
Mwaja, hilo nililijua ndiyo maana nikamuwahi na kumteka
mwanamke huyo” Amata akaeleza. Madam S akatulia kimya
kidogo, kisha akamtazama kijana wake.
“Na vipi kuhusu Lukundame, mmemaliza naye…?”
“Ndiyo… anaweza kurudi uraiani sasa…”
“Sawa mfanye hivyo… kwa njia zetu zilezile afike
Zanzibar…”Madam S akamwambia Amata. “Na huyo mwanajeshi
umwachie salama… maana nakujua…”
“Nimeokoka Madam!” Amata akajibu.
“Mh! Hilo kanisa limevamiwa…”
Mkutano huo wa Amata na Madam S ulimalizika kama saa
kumi hivi. Wakaagana kwa miadi ya kukutana baada ya kikao cha
chake na Mkuu wa nchi.

* * * *

Saa moja na nusu usiku, Kamanda Amata aliegesha gari nje ya


ile nyumba kule Magomeni. Akateremka na kuchukua pochi la
Mwaja alilolichukua kwa Simbeye kule kituo cha polisi cha kati.
Akaingia ndani ya ile nyumba na mmoja kwa moja akakiendea
chumba alichomwacha mwanadada huyo. Akaufungua mlango na
kumkuta akiwa kajilaza kwenye kile kitanda. Akamrushia ule
mkoba, “haya jiandae nikurudishe kwenu…” akatazama upande wa
pili, “mlango huu ni bafu, ruksa kutumia…”.
Alipomaliza akaondoka zake na kuingia kwenye chumba kile
alichotumia mwanzo. Akafungua droo yake ndogo na kutoa zile
pesa. Akachukua baadhi na kuziweka kando na nyingine
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

akazifungwa kwa rababendi, akazitia kwenye bahasha. Zitawafaa


watoto yatima! Akawaza.
Dakika arobaini na tano zilipokwisha, akatoka kwenye kile
chumba na kumgongea Mwaja. Mwanamke huyo alikuwa tayari
kavalia suruali yake ya jinzi na fulana iliyomkaa vyema. Nywele
zake alizibana kwa nyuma kwa kimpira cha kuzungusha. Raba safi
ya NIKE ilitulia mguuni mwake. Jicho la Amata likatazama umbo
mujarabu la kiumbe kilichosimama mbele yake. Akakumbuka mara
ya kwanza alipokutana naye. Akameza funda la mate. Mate ya
uchu. Wazo la kwanza lilikuwa kumrudisha nyumbani kwake, lakini
akahisi kama moyo wake unataka kumsaliti.
“Twende!” akamwambia huku yeye akangulia. Walipotoka nje
wakaingia katika BMW jeusi la kisasa. Amata akatoa ile bahasha na
kuchukua noti chache alizozitenga.
“Samahani kwa yote… nilikuwa kazini, sikukutenda kwa
mabaya. Na kamwe sina desturi ya kuwatesa watoto wazuri kama
wewe… hata hivyo nimepigania swala lako lisiende mbali. Hivyo
upo huru toka sasa na hutakiwi kulizungumza popote swala hili.
Hii nyumba wewe hujawahi kufika wala kuiona…” akamwambia
huku akiwasha gari. “Nikupeleke wapi?” akamuuliza.
“Kwa rafiki yangu,”
“Wapi?”
“Kawe…”
“Sawa,lakini unaonaje kama tukienda kwanza kupata chakula
cha jioni halafu nikupeleke huko kwa rafiki yako?” Amata
hakukubali ndege amponyoke kirahisi namna hiyo.
“Mh! Haya! Leo sijui wema umetoka wapi” Mwaja
akazungumza.
“Wema wangu hauuoni?”
“Ungekuwa mwema ungeniacha bila nguo siku tatu? Bila
chakula pia?”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Pole mrembo! Chukua hizi zikufae… uende benki


ukazibadili utumie,” akamwambia huku akimkabidhi fedha za
Kimarekani. Moyo wa Mwaja ukaruka samasoti na kupoteza kama
mapigo mawili hivi kwa kile alichokuwa akikitia mkononi mwake.
Amata akageuza gari na kutokomea mjini. Tayari Mwaja hakuwa na
kauli tena mbele ya kijana huyo jamali. Alitulia garini wakati likikata
barabara kuelekea mjini kama kondoo apelekwaye machinjoni.
Pesa sabuni ya roho.
Amata aliiacha Barabara ya Morogoro na kukamata ile ya Bibi
Titi mpaka makutano na Ally Hassan Mwinyi, akachepuka na
kuikamata ile ya Ohio. Mita chache tu mbele akakunja kushoto na
kuingia katika lango kuu la Hoteli ya Serena. Tayari ilikwishatimu
saa tatu usiku walipoketi kwenye ukumbi mkubwa wa chakula.
“Mbona una mawazo hivyo?” Amata akamuuliza Mwaja
baada ya kuuona ukimya wake.
“Nawaza tu naanzaje kuripoti kazini, maana nitatakiwa
kuandika barua ya maelezo,” Akajibu.
“Usijali, tayari swala lako linashughulikiwa, usiripoti kazini
mpaka utakapopewa taarifa ya kufanya hivyo hata kama ni mwezi
mmoja, we tafuta mahala ukae utulie…”
“Sawa, nitaenda nyumbani kwa wazee…”
“Wapi?”
“Vikindu…”
“Hah! Si kwa rafiki yako tena?”
“Hapana, kwa rafiki yangu ningeenda kukaa siku moja tu
lakini kwa kuwa umenambia mpaka niitwe kazini, basi ni heri
nirnde kwa wazee…”
“Sawa, uamuzi ni wako! Kama utaridhia nitakupeleka usiku
huu kama…”
Wakiwa wanaongea hayo chakula kikawa tayari mezani kama
walivyoagiza. Wawili hao wakaanza kukishambulia kwa fujo huku

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

vicheko vikitawala. Simu ya Amata ikaita pale mezani. Akainyakua


na kuiweka sikioni.
“Yes Mom!” akaitikia.
“Uko wapi?”
“Serena Hotel…”
Ukimya ukatawala kidogo pande zote mbili. “Tukutane saa sita
usiku nyumbani kwangu…” Madam S akamwambia Amata.
“Bila chenga yaani…” akakata simu na kuirudisha mezani.
“Nani?” Mwaja akauliza.
“Mama yangu… yaani yeye akishtuka tu usingizini lazima
usikie ‘uko wapi! Njoo haraka nyumbani’ unaweza kufikiri kuna
jambo kubwaaa ukifika hakuna la maana. Si unajua wazee…”
“Mzee sana?”
“Miaka sabini na saba sasa…”
“Ndiyo maana….”
Amata akatazama saa yake, tayari saa tano usiku ilikuwa
ikiyoyoma, chakula na vinywaji vilikuwa tupu mmezani.
“Sasa, nitakupeleka kwangu ukalale pale nimuone mama
halafu alfajiri nitakupeleka kwenu…” Amata akamwambia Mwaja
aliyeitikia kwa kichwa. Nusu saa baadae waliwasili Kinondoni
yaliko makazi ya Amata, akamwacha hapo akimwonesha chumba
kikubwa na kizuri.
“Utapenda kulala chumba cha wageni au cha mwenye
nyumba…?” Mwaja akamtazama Amata kwa Jicho pembe na
kurudisha usowe kwa kwanza.
“Cha mwenye nyumba hahahahaaa” akajibu. Amata
akamkaribisha kwenye chumba kingine kipana, kizuri chaenye kila
kitu ndani ukikitazama, hakika ni cha mwenye nyumba.
Akamwacha hapo na yeye akaelekea kukutana na Madam S.

* * * *

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Saa sita usiku ilimkuta Kamanda Amata nyumbani kwa


Madam S. Kinywaji kikali cha Captain Morgan kilikuwa kikiteketea
kati yao. Madam S alikuwa tayari katika vazi la kulalia, mida
imeenda.
“Kuna jambo!” Madam S akamwambia Amata wakati
akimmiminia kinywaji katika bilauri yake iliyotindikiwa.
“Lipi?” Amata akahoji.
“Nimezungumza kwa kirefu sana na Mheshimiwa
Rais,kwanza amehoji kwa kina kuhusu kifo cha Mwambope na
mahusiano ya kifo hicho na sakata hili…”
“Mhm!”
“Anataka kujua nini kimejificha ndani yake. Kwa kauli yake
mwenyewe amesema wazi kuwa kuna uwezekano mkubwa wa
hujuma hii kufanyika ndani ya Jeshi. Anafikiri kuanzisha uchunguzi
ndani ya jeshi kuwabaini waliohusika… ”
“No!”
“Nini?”
“Atakuwa amekosea… ni vizuri anyamaze kimya kwa sasa
mpaka tufikie mwisho wa sakata hili…” Amata akashauri.
“Nami nimemjibu hivyo hivyo”
“Sawa! Enhe nambie sasa kiini cha mazungumzo…”
“Namba moja kasema, taifa haliwezi kupata hasara ya asilimia
mia moja, ndege ilinunuliwa kwa pesa za walipa kodi,
imehujumiwa, basi lazima mbivu na mbichi zijulikane. Hajatoa
uamuzi ila amesema Pegan Box lazima ipatikane kwa njia yoyote…”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

akainua kinywaji chake na kupiga funda moja zito, akaishusha


mezani, “kesho kutakuwa na kikao cha baraza la usalama la taifa
pale pale Ikulu, amesema uamuzi wa nini kifanyike atautoa kesho
hiyohiyo,” akaeleza.
“Mh!” Amata akaguna huku akiwa kajishika shavu, “Madam
S… nahisi kama kuna kosa litafanyika endapo kikao hicho
kitapitisha uamuzi wa moja kwa moja. Manunuzi ya ndege hizi
hayajapitishwa na mtu mmoja bali jopo la watu ndani ya jeshi,
hivyo hivyo kama kuna hujuma basi pia imefanywa na jopo la watu
ndani na nje ya jeshi. Jambo la kufanya ni kuangalia nani na nani
ndani ya jeshi walihusika katika mpango mzima wa manunuzi na
pia nani na nani wamehusika nje ya jeshi halafu kutoka hapo
wachunguzwe mmoja baada ya mwingine,” Amata akaeleza.
Madam S alibaki kimya wakati kijana huyo akieleza hayo,
yakamwingia.
“Umesema jambo la msingi sana! Nilikuwa nawaza kitu kama
hicho. Amata, vyovyote watakavyoamua, jiandae kwa safari ya
Kashmir kupitia Islamabad…” akamwambia. Amata akatikisa
kichwa juu chini, “kamtafute Jamila ambaye mpaka sasa tunaamini
yupo hai…” akamalizia.
“Wewe ukisema, mimi ni nani nikatae?” Amata akamjibu,
akainua bilauri yake na kugida mafunda kadhaa, aliposhusha akatia
tena vipande vya barafu katika bilauri ile na Madam S
akammiminia kinywaji.
“Lini?” akauliza.
“Mara tu baada ya kikao cha kesho… jiandae kwa safari”
Madam S akamwambia kijana wake.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Naenda na nani?”
“Peke yako! Sitaki mtu yoyote ajue kuwa umeenda huko zaidi
ya Mimi na wewe mwenyewe!” Madam S akaongea pasi na lepe la
tabasamu.
“Nimekupata, naomba niende,” Amata akajibu na kusimama.
“Kesho subiri simu yangu kwa hamu…”
Wakaagana, Amata akaondoka katika kasri like na kuelekea
nyumbani kwake. Kichwa chake kilishaanza kuichakata safari hiyo.
* * * *
Mansoor alihisi kichwa kikitaka kumpasuka. Akawaita watu
wake wa karibu ili kuzungumza machache. Mbele yake kulikuwa na
vijana watatu aliyowaamini sana.
“Kuna mambo matatu ya kujadili… moja, niwafanye nini
hawa mateka! Mbili, ni wapi nifanyie mkutano na wateja wangu!
Tatu, tunaipata vipi code ya tatu,” akawaeleza. “Maana hali
inapoendelea itakuwa mbaya, hili pegan box limeshaanza kuwatoa
mate watu wengi… na tukizubaa tunaweza kosa kila kitu.
Nimepata tetesi kuwa Jeshi la India limepata taarifa ya pegan box na
leo walikuwa na kikao kuhusu hilo!” akawaambia. “Tufanyeje?”
akawauliza.
“Kama tunachokitaka kwa hawa mateka tumekipata hawana
maana kwetu, tukiwaacha huru itakuwa hatari kwetu,” mmoja
akaeleza.
“So!”
“Wauawe!”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Kikao hicho kikapitisha uamuzi wa kuwaua Joel na Bakari.


Mansoor hakuwa na lingine zaidi ya kupitisha uamuzi huo. Kikao
hicho kikaamua pia kuwa mnada wa Pegan box ufanyike haraka
iwezekanavyo na sehemu ya kufanya shughuli hiyo iwe hapo hapo
kwenye kasri la Mansoor.
“Wanunuzi waje hapa!” kijana mwingine akashauri, “usalama
wa biashara hii utawezekana tu kama itafanyikia hapa na si mahala
pengine…” akaongeza.
“Huyu Kahir, sisi hawezi kutusumbua… tukiamua kumkata
kichwa ni dakika tu…” Mansoor akamwonesha mkono yule kijana
kumtaka asubiri kwanza.
“Kuna kitu tunakihitaji kutoka kwa Kahir kabla ya yeye
mwenyewe. Kahir ana mateka mmoja ambaye ana code ya tatu,”
akawaeleza. “Ninachokitaka mimi ni yule mateka kwanza… halafu
Kahir baadae…” Mansoor akawaeleza. “Farsi,” akamwita kijana
mwingine, “wasiliana na Swahba, mtu wetu aliyepo Islamabad,
awasiliane na wadau ili kuwaalika kwa mnada utakaofanyika
hapa…”
“Sawa Mkuu!”
“Lakini, kabla ya mnada tuwe tumeshampata yule mateka…
andaeni vijana wawekeni tayari muda na saa yoyote lazima tuvamie
kambi ya Izbul Mujaheeden…” akawaeleza. Kikao hicho
kikamalizika kila mmoja akatoka na agizo lake.
* * * *
“Ninachohitaji kutoka kwako ni code moja tu ya tatu…” sauti
nzito ya Fernandez iliyapenya masikio ya Kotvich, “kuna pesa
nyingi sana nitakupatia”.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Kotvich akatabasamu upande wa pili wa simu ile. Akaupeleka


mkono wake mezani na kuchukua karatasi iliyoandikwa maneno
machache tu.
‘Biashara yetu inaonekana kuingia doa,
mwambie mteja afanye haraka,
ndani ya siku kumi hali itakuwa mbaya…’
Ujumbe ule ulikuwa umetoka Tanzania na kumfikia Kotvich
asubuhi ya Siku hiyo. Simu ile iliyofuata ilimweka njia panda,
hakujua afanye nini.
“Cha msingi, fanyeni kwanza biashara… ukishaununua huo
mfumo nitakupatia code iliyobaki kwa sababu kuipata si kazi ndogo
kama unavyofikiri…” Kotvich akajibu kwa sauti ya chini.
“Unaniahidi? Maana nina uhakika wakununua bidhaa ile…”
Fernandez akamwambia Kotvich.
“Nakuahidi, na ukikamilisha biashara hiyo nitakuja
kukuwekea mambo sawa…”
Fernandez akatabasamu upande wa pili wa simu ile. Moyo
wake ulikurupuka kwa furaha, lakini uliingia ganzi pindi tu
alipokumbuka nini kimetokea kule Tanzania. Kusambaratishwa
kwa kikosi alichokituma kumtafutia kabrasha lenye code zile.
Kilichomuumiza kichwa ni nini kilifanyika baada ya kundi like
kusambaratishwa. Kila alipohisi kuwa siri za mawasiliano yao
zitakuwa zimejulikana alihisi kufa na si kingine. Siku nne sasa
hakuwa akimpata Fareed wala vijana wake. Hofu.
* * * *

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Amata aliwasili nyumbani kwake Kinondoni majira ya saa nane


usiku. Kwa kutumia funguo zake alifanikiwa kuingia bila hata ya
kufanya kelele kwa aliyepo ndani. Hatua zake zikamfikisha katika
mlango aliyomwacha Mwaja.
Akaufungua taratibu na macho yake yakapokelewa na taswira
tatanishi ya Mwaja aliyelala fofofo. Umbo lake kitandani
lilinyumbulika kiasi kwamba kama huna moyo wa subira ungeweza
kufanya uharibifu. Amata akapata ashki kali mwilini mwake.
Akaurudishia ule mlango na kwenda katika chumba chake halisi
tofauti na kile. Chumba hiki ni Gina pekee anayekitumia kulala na
Amata.
Baadaya kuufanyia usafi mwili wake na kuchukua nguo za kuvaa
siku ya pili, akarudi kulekuke kwa Mwaja. Alipoiwasha taa ndipo
alipogundua chupa iliyovunjika ikiwa imetapakaa sakafuni.
Nini kimetokea! Aashtuka na kuangalia vizuri. Akaokota kipande
cha chupa hiyo, ilikuwa ya mvinyo wa Chardonnay. Akamgeuza
mwanamke huyo na kumlaza chali. Mwaja alikuwa hoi kwa kilevi,
hajielewi. Akamfumbua macho na kummulika na tochi, hata mboni
yake ilikuwa imekimbilia juu. Akamwacha na kuchukua vifaa vyake
vya kazi ambavyo daima huvitumia kumwamcha aliye katika hali
hiyo. Kwanza akampima mapigo ya moyo, yapo hafifu sana.
Ningechelewa angedanja! Akajisemea. Akachukua sindano na
kunyonya dawa ya kipimo cha kutosha, akamfunua paja ili
kumdunga, lol.
Hii kweli operesheni Kashmir! Akawaza na kucheka mwenyewe,
akamdunga na kusukuma dawa yote.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Dakika tano zilikuwa nyingi sana, Mwaja aliamka na kupiga


mwayo mrefu. Akaamka na kuingia bafuni, kisha akarudi baada ya
dakika kama tatu hivi.
“Kumbe usharudi!” akamwambia Amata.
“Muda mrefu tu…” akamjibu na kumpokea kitandani akiwa
fresh. Mabusu motomoto yakachukua nafasi, nusu saa iliyofuata
wawili hao walikuwa mbingu ya saba wakibadilishana uzoefu wa
maisha.
* * * *

Kilikuwa kikao kizito ndani ya Ikulu ya nchi. Rais na jopo lake


la usalama walijifungia kutafakari jambo. Haikuwa rahisi; hawa
walisema hivi na wale wakasema vile. Maswali yenye utata
yalilikabili jopo hilo, majibu hayakupatikana kirahisi.
“Huu utakuwa ujinga, kwanini tufanye hujuma hiyo? Ni sawa
na baba kuiibia familia yako mwenyewe…” mmoja wa wajumbe
akafoka. Mkuu wa nchi alikuwa kimya akisikiliza kila
kinachobishaniwa. Hoja ya kifo cha Mwambope ikaibuka upya.
“Sanjari na hili, kifo cha Mwambope lazima kifanyiwe
uchunguzi…” Mkuu wa majeshi CDF akatoa tamko.
“Ni kweli, lakini kwani kuna lililojificha? Mbona muuaji
tumeshawapa taarifa… tumeshamjua?” kauli hii ikawashtua wote.
Kwa sababu za kiusalama haikutamkwa hadharani ni nani hasa
anayeshukiwa.
“Marehemu Mwambope, alikuwa anajua kila kinachoendelea
katika ununuzi wa ile ndege… tafutishi zetu zinaonesha kuwa
alifuatwa na watu waliokuwa tayari kuihujumu nchi, akakataa…
kwa sababu hiyo wakatuma muuaji ammalize kabla hajasema
lolote. Watu waliokuwa doria wanakiri wazi kuwa mtu wa mwisho
kuingia getini na kumuulizia Mwambope aliandika jina lake kwenye
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

kitabu cha wageni, Mr. Spark… walipomuuliza alisema hilo ndilo


jina lake, bahati nzuri picha yake ilinaswa kwenye kamera za
usalama, hii ni kwa mujibu wa taarifa ya MI iliyowasilishwa
kwangu…” CDF akaunguruma.
Madam S alihisi moyo ukimwenda mbio aliposikia ‘Mr Spark’
akitajwa. Alijua kila kitu lakini wasiwasi wake ulikuwa ni jinsi gani
ya kuwaaminisha watu hao kuwa muuaji hakuwa Spark yaani
Amata. Ukimya ukarejea ukumbini pale.
“Hapa mezani nina taarifa mbili zinazokubaliana upande
fulani na zinakinzana upande mwingine…” wajumbe wakatega
sikio hasa waliposikia kuna taarifa mbili. Wengi walijua taarifa moja
tu. “Hapa nina taarifa kutoka kitengo cha upelelezi cha jeshi la
wananchi, MI. Wao wanasema aliyemuua Mwambope ni Mr. Spark
na wameweka na picha hapa… lakini taarifa hii haijaniambia kama
mtu huyu amekamatwa au la, maana kama angekamatwa, yeye
angesema ametumwa na nani… Taarifa ya pili imeletwa kutoka
shirika binafsi la kipelelezi ambalo serikali iliamua kuliomba
lichunguze kadhia hii… wao wanasema aliyemuua Mwambope ni
Muuaji kutoka Kuwait anaitwa Fareed,” akatulia kidogo, kisha
akaendelea, “sasa nani mkweli na nani si mkweli katika hili? Hiyo
haijalishi… nataka nisikie kutoka MI nini maamuzi yenu katika
kulishughulikia hili?” Mkuu wa nchi akaeleza na kuuliza.
“Kuna maamuzi tuliyofikia, na tayari kama jeshi, tumeanza
kuyatekeleza… tunatarajia kutuma vijana wakaanzie uchunguzi
kwa kushirikiana na jeshi la Urusi na tayari tumehakikishiwa hilo,
hivyo tulikuwa tunasubiri saini yako tu ili tuingie kazini…”
“Sawa!” Mkuu wa nchi akajibu kwa neno moja tu. Baada ya
mazungumzo yote kumalizika serikali ikatoa tamko juu ya kadhia
hii ikiwemo kukamatwa kwa kila aliyehusika na kuwekwa ndani.
Kikao kikamalizika majira ya saa saba mchana. Baada ya kikao
kumalizika na wajumbe kutawanyika. Madam S akapewa kimemo
kuwa abaki kwa mazungumzo maalumu. Memo kama hiyohiyo
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

ikafika kwa mkuu wa majeshi. Hivyo kilitakiwa kiwepo kikao cha


watu watatu, yaani Rais, Madam S na Mkuu wa majeshi. Nusu Saa
baadae watu hao walikuwa ndani ya chumba kidogo ambacho Rais
hutumia na watu wake kwa mikutano nyeti.
“Nahitaji kila kitu kipatiwe jibu, makepteni wangu yaani
Jamila, Joel na Bakari miili yao ama wao wenyewe warudiswe hapa.
Isitoshe, nahitaji uchunguzi mkali ndani ya jeshi ufanyike kujua
nani amehusika kwenye hili… kila mmoja atapata waraka wa nini
afanye katika hilo…” Namba moja akaeleza msimamo wake.
Mazungumzo yake na wawili hao yalionesha wazi kuwa kuna
jambo limejificha na siyo dogo. Akawataka kutawanyika, kila
mmoja kuendelea na kazi zake za kawaida kusubiri waraka wa
kupewa majukumu ya kufanya.

* * * *
“Kama nilivyokwambia…” Madam akaanzisha mazungumzo
pindi tu alipokutana na Amata katika uwanja mdogo wa mchezo
wa golf pale Ghymkhana.
“Kwamba…”
“Unapaswa kwenda Kashmir katika uwanja wa vita… Pegan
Box linatakiwa nyumbani kwa udi na uvumba” akamwambia.
Amata na Madam S walikuwa wakitembea kwa hatua za
taratibu wakikizunguka kile kiwanja.
“Sawa!” Amata akajibu. Baada ya mazungumzo marefu
wakafikia mahali penye benchi, wakaketi.
“Kazi hii ni ngumu… na ugumu wake unakuja kutokana na
kwamba hatuna mtangulizi huko uwendako, hivyo akili na
maamuzi ya busara yanatakiwa yatumike katika kujua nini cha
kufanya nani wa kumfuata na kwa nini… Pakistan mpaka Kashimir
si eneo salama hata kidogo kwa usalama, mapigano ya muda wote
yanaendelea, hawa wanamlaumu huyu na huyu anamlaumu yule…”
“Nimekupata mom!”
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“So uwe makini sana katika nyendo zako… wanawake wengi


kule ni wapiga mbinja, hivyo hakikisha upanga wako upo alani
muda wote, ukijilegeza watakumaliza…” akaongeza kumwambia.
Kamanda Amata akasikiliza kwa makini na utulivu. Madam S
akampatia bahasha moja ya kaki iliyojaa vizuri, “kila kitu kipo
humo, kazi njema kijana”.
Amata akamtazama bosi wake na kumwitikia kwa kutikisa
kichwa.
“Urudi na roho yako,” akamwambia. Madam S akasimama
tayari kuondoka, na Amata akafanya vivyo hivyo. Wakapeana
mikono na kila mmoja akashika njia yake.
Ndani ya gari lake Amata akatulia kidogo, akachana ile
bahasha na kuangalia vilivyoko ndani. Tiketi ya ndege kwenda
Islamabad kupitia Dubai. Pesa taslimu za Kimarekani zilifungwa
kwenye bandali moja. Zaidi ya hapo kulikuwa na kifaa kidogo cha
kuvaa sikioni. Akakichukua na kuikipachika sikioni.

‘Kutana na Muheeden Dhakar katika kilabu cha usiku cha


Islamabad…
kinajulikana kwa jina hilohilo yaani Club Islamabad katika
barabara kuu ya Muree karibu kabisa na Kashmir Chowk, saa
saba usiku kesho kwa saa za Pakistan,’

Ujumbe ule ukaishia hapo. Akaitazama saa yake, ilikuwa tayari


saa kumi kasoro jioni. Tiketi yake ilionesha ndege ni saa tatu usiku
wa siku hiyo. Akapiga hesabu zake na kugundua kuwa atawasili
Islamabad saa nne asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki ambapo ni
sawa na saa nne usiku kwa saa za Pakistan. Ina maana alipaswa
kufika na kukaa saa tatu tu ili kuonana na mtu huyo. Akakitoa kile
kidubwasha na kukitia kwenye kijidroo maalum katika lile gari.
Akatia injini moto na kuondoka zake.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

* * * *

Jenerali Kahir aliwasili kwenye kambi ya Izbul Mujahedeen


akiwa na nusu kicheko. Akapokelewa na vijana wake na kuelekea
katika ofisi ndogo aliyopenda kuitumia akiwapo katika kambi hiyo.
Akajitupa kitini na kushusha pumzi ndefu.
“Vipi? Naona una furaha leo!” kiongozi wa lile kundi
akamwuliza Kahir.
“Mansoor kaamua kutangaza mnada…”
“What?”
“Pegan box itapigwa mnada tarehe moja August palepale
kwenye ngome yake…!”
“So?”
“Lazima tukaununue huu mzigo, Mansoor hawezi kumuuzia
mtu yoyote huu mfumo. Sisi tuna turufu, tuna code ya tatu hivyo
lazima tu atuuzie au la tutauza sisi code ya tatu kwa huyo mnunuaji
kwa pesa nyingi,” akawaambia na kutoa cheko la dharau

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

10
AMATA aliwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Islamabad saa tano usiku baada ya kuchelewa Dubai kwa saa
nzima. Mara tu baada ya kutoka kwenye uwanja huo alielekea
katika maegesho ya taksi. Akaitazama saa yake, ilikwishatimu saa
sita kasoro robo usiku. Utata ukamjia; aanze kwenda hotelini au
moja kwa moja aelekee kwenye klabu hiyo aliyoambiwa? Akakosa
jibu. Akaitazama saa yake muda ulizidi kuyoyoma. Hakuwa anajua
umbali wa kutoka hapo kwenda kwenye hicho kilabu wala wa
kwenda hotelini. Mlio wa saa yake kuashiria kuwa saa kamili
imetimia ulimgutusha. Akaitazama, ikamwonesha kuwa saa sita
kamili usiku ilikwishatimu na tayari siku ilikuwa
imebadilika. Akavuta hatua na kuiendea taksi iliyokuwa imeingia
muda huo huo, akaketi katika siti ya nyuma.
“Asalam aleikum!” Amata akamsalimu yule dereva kijana.
“Aleikum asalaam… karibu sana Islamabad…” akamjibu na
kumkaribisha.
“Shukran!”
“Waelekea wapi?”
“Club Islamabad…” Amata akajibu.
“Waoh! Club Islamabad… kilabu cha matajiri hicho kaka….
Karibu sana nitakufikisha..”
“Ila utanisubiri pale kwa kuwa ninaonana tu na tajiri mmoja
halafu nitaenda hotelini…”
“Na hoteli gani utapenda kufikia?”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Nikishamaliza mazungumzo na huyo tajiri, nitakwambia


hoteli gani” Amata akamwambia yule dereva wakati akiyaacha
maegesho yale.
Barabara ya Muree, yule dereva taksi akakunja kushoto kama
anaifuata Kashmir Chowk, akakunja kulia na kuifuata barabara
hiyo iliyokuwa ikielekea katika jumba kubwa la kifahari. Jumba hilo
lililopambwa kwa maua mazuri yaliyong’azwa na kupendezeshwa
kwa taa za rangi ya dhahabu. Mbele ya jengo hilo Amata
alipokelewa na kijana aliyevalia suti nadhifu na gloves katika mkono
wake wa kuume.
“Karibu sana Islamabad Club!” akakaribishwa.
“Asante…”
“Kadi ya uanachama tafadhali” yule mlinzi akamwambia
Amata.
“Oh no! Nina miadi hapa saa saba kamili usiku huu…”
“Mgeni wa Dhakar…”
“Oh! Karibu sana…” yule kijana akamwongoza Amata mpaka
ghorofa ya pili. Huko waliingia katika ukumbi mkubwa
uliyopangwa meza na viti kwa ustadi wa hali ya juu. Ulijionesha
wazi kuwa ulikuwa ukumbi wa chakula. Katika ukumbi huo,
kulikuwa na watu wawili tu kwenye kona kabisa ya ukumbi ule.
“Meza namba saba … karibu sana, mwenyeji wako ataungana nawe
muda si mrefu…”
“Shukran” Amata akajibu na kuvuta kiti kabla ya kuketi.
Akaitoa simu yake na kuiweka mezani kisha akaiseti saa yake vizuri.
Sasa aliweza kuunganisha saa yake na kifaa maalum kilichomo
ndani ya mkoba huo. Hivyo aliweza kujua kama gari lile lipo au
limeondoka.
Lipo! Akajihakikishia. Kisha kwenye simu yake akatuma
ujumbe Shamba kwa namba maalum ambayo ingeruhusu tu
ujumbe ule umfikie Madam S pekee.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Karibu tukuhudumie!” mhudumu nadhifu wa kike


alimkaribisha.
“Shukran, nitaagiza baadae kidogo,” Amata akamwambia yule
mhudumu naye akaondoka. Kwa takribani dakika ishirini na kitu
alikuwa akicheza na simu yake. Kama ilivyokuwa miadi ile, saa saba
kasoro dakika tatu, kijana mmoja mtanashati, mwenye ndevu
nyingi na macho madogo aliwasili na kuketi kiti cha mbele yake.
“Asalaam aleikum” akamsabahi mgeni wake.
“Aleikum…”
“Karibu sana Pakistan, Spark, jisikie upo nyumbani…”
“Shukran…”
“Umeshajaribu vyakula yetu?”
“Aaah no! Bado, ndo kwanza nimeingia hata hotelini
sijafika…”
“Oh pole sana Spark, mlichelewa sehemu?”
“Yeah, Dubai…” Amata akajibu. Mara tu mhudumu
alipokuja,Bwana Dhakar akamwagiza kuleta kinywaj kama chaguo
la mgeni wake lilivyokua. Mhudumu alipoondoka, Dhakar akatoa
bahasha na kumpatia Amata.
“Humo ndani kuna picha za watu unaotakiwa kushughulika
nao..” akamwambia.
“Negative au positive?”
“Negàtive”
“Ok!”
“Jambo la msingi na la kuzingaia sana… Pakistan si nchi
yenye amani kama kwenu. Hivyo epuka mambo makubwa mawili;
mikusanyiko ya watu na wanawake, na pia ongeza weledi kwenye
mambo mawili; muda na umakini wa kazi…” Dhakar akatoa
maelekezo.
“Wanawake! Wakati mwingine huwa informer wazuri
kwangu….” Amata akasema.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Na mara nyingi ni informer wazuri kwa adui zako. Kila mmoja
hupenda kutumia mwanamke kupata habari anazotaka… hapa
Islamabad wanawake wengi ni majasusi kutoka vikundi vya
wanamgambo, so chukua tahadhari braza….” Dhakar alipomaliza
kinywaji kilifika mezani. Kikamiminwa kwenye bilauri kubwa, kila
mmoja na ya kwake. “Cheers” wakagonga bilauri zao na kila mmoja
kupiga mafunda kadhaa kabla hajaitua mezani.
“Nipe mwongozo,” Amata akamwambia Dhakar.
“CIA agent…”
“Copy!” Amata akajibu kisha akainuka tayari kuondoka. “Kwa
lolote nitakutafuta…” akamwambia na kutoka zake nje ya kile
kilabu. Alipoifikia ile taksi, akakuta dereva amechapa usingizi.
Akamtikisa bega na kumwamsha. “Usilale ukiwa kazini…”
akamwambia huku akiingia na kuketi. Yule kijana akajifikicha
macho na kutia injini moto. Akaingia barabara ndogo ya Club na
kuikata barabara kuu ya Srinagar, akaikamata ile ya Constitution na
kukanyaga mafuta mpaka kwenye kona ya barabara ya Agha Khan,
akaifuata hiyo na kuwasili Hoteli ya Mariott salama salimini.
“Hapa ndiyo Mariott Hotel, pazuri na utapafurahia…” yule
kijana akainadi hoteli ile.
“Asante,” Amata akashukuru na kutoa pesa kumlipa dereva
huyo. Yule kijana akampa kadi yake ya mawasiliano, “ukinihitaji,
muda wowote unipigie nitakuhudumia,” akamwambia. Amata
akatikisa kichwa na kuondoka zake.
Ilikuwa hoteli mzuri ya nyota tatu, iliyopendezeshwa kwa taa
mzuri na maua ya kuvutia. Kamanda Amata akawasili katika dawati
la mapokezi na kupata chumba anachokihitaji. Ghorofa ya tatu
chumba namba thelathini na tatu.
Safari hii Nina tatu tatu, namba yangu ya bahati! Akajisemea
moyoni na kuufikia mlango wa chumba hicho. Akatazama kushoto
na kulia, hakuna tatizo. Akaipachika kadi yake kwenye kidubwasha
maalumu kilichokuwa pembeni kwa mlango huo. Akafungua
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

mlango na kuingia ndani. Chumba kikubwa, kilichojaa utulivu wa


aina zote kikamlaki. Akaitazama kitanda kikubwa mbele yake
kilichotandikwa shuka kwa umaridadi wote. Maua ya waridi
yalimwagwa kitandani huku yakikijaza chumba hicho kwa harufu
ya kuziburudisha pua. Amata akavuta hatua na kuketi kwenye kiti
kidogo kilicho kando ya kitanda hicho. Alikuwa amechoka kwa
safari, akaichana ile bahasha na kutoa kila kilicho ndani. Havikuwa
vingi, kidubwasha kimoja tu kinachofanana na kamera.
Akakigeuzageuza na kukibonyeza kwenye batani iliyoandikwa
‘power’. Kutoka kwenye lensi ndogo kikatoa mwanga mkali.
Kumbe projector! Akastuka. Akamulika ukuta ulio mbele yake na
kukaa makini kusikiliza na kutazama.

‘Karibu Islamabad Mr Spark… una kazi moja tu ya kuifanya


katika nchi hii na pembeni kidogo. Kazi yenyewe ni kuliokoa
sanduku la Pegan lenye mfumo aghali wa usalama wa anga ambao
serikali ya nchi yako imeununua kwa gharama kubwa. Sikiliza,
Pegan Box imebeba mfumo makini unaojulikana kama PT-502-
B.PEGAN X. Mfumo huu ulifungwa na kuunganishwa katika
ndege ya kivita ya JET Fighter B 502 SS. Ndege hii ilipoteza
mawasiliano ikiwa katika anga la Kashmir na kuanguka. Habari ya
kweli ni kwamba ndege hii haikuanguka bali ilishuwa kwa remote
control iliyoweza kuingiliana kimawasiliano na ndege hiyo. Mhusika
mkubwa nanaliyepanga mpango huo anaitwa Mansoor makazi yake
yapo katika bonde kubwa la Kashmir. Lengo lake ni kufanya
biashara na watu wawili maarufu, wa kwanza ni tajiri Fernandez
kutoka Venezuela ambaye anamiliki visima vya mafuta huko
Uarabuni na ni mfadhili mkubwa wa vikundi vya kigaidi hukohuko
Mashariki ya kati. Mtu wa pili ni Jenerali Kahir, jenerali wa jeshi la
Pakistan ambaye anafadhili kikundi cha Izbul Mujahedeen hapa
Pakistan. Pegan Box lipo kwa Mansoor huko Kashmir, lakini code
mojawapo ipo kwa Jeneral Kahir…. Nafikiri umeelewa kazi
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

inayokukabili mbele yako… all the best. Ujumbe huu utaharibika


baada ya muda mfup.’
Amata akabaki akikitazama kile kidubwasha mpakamkilipotoa
mlipuko hafifu.

Mara baada ya kidubwasha kile kuharibika, Amata alikitia


kawenye mfuko wa nje wa mkoba wake. Akajitupa kitandani na
usingizi mzito ukambeba. Akalala kama mtoto.

* * * *

Saa tano asubuhi, aligutushwa na kishindo kikubwa


kilichosikika toka nje. Amata, akainua uso na kukuta chumba
kikiangazwa na mwanga wa jua la nje. Akainuka haraka kutoka
kitandani na kulielekea dirisha. Moshi mkubwa na mzito ulitanda
angani. Ving’ora vya magari ya polisi na zima moto vilisikika kila
kona. Haraka akawahi na kufungua luninga iliyo ndani ya chumba
hicho. Kituo cha TV cha taifa cha Pakistani kilikuwa hewanj na
‘breaking news’ kuhusu tukio hilo.

‘… inasemekana ni mlipuko wa bomu la kujitoa mhanga


uliofanyika ndani ya basi la abiria. Abiria kumi na wawili
wamepoteza maisha na wengine wamejeruhiwa vibaya.
Taarifa za awali zinasema kuwa kundi la Izbul Mujahedeen
linahisiwa kutekeleza tukio hilo… ’

Taarifa ile iliyokuwa ikiwasilishwa na mtangazaji wa kiume,


mtu mzima, ilieleza.
Suleiman Jabah! Amata alilisoma jina la mtangazaji yule. Habari
ile iliendelea wakati yeye akijiandaa kuanza kazi yake aliyotumwa
nchini humo. Hakujua kiuhakika wapi aanzie lakini moyoni mwake

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

aliamua kuanza na matembezi tu ya kawaida katika jiji hilo.


Ijapokuwa taarifa aliyopewa na Dhakar kwenye ile machine
ilimwambia wazi kuwa Pegan Box liko wapi, ila yeye aliamua kuanza
utafiti wa wapi maskani ya Izbul Mujahedeen ilipo. Alijua kuwa
huko angekutana na vitu viwili vya msingi; Jenerali Kahir na code
namba 3. Ambayo kwa tafutishi alizofanya kule Tanzania code hiyo
ni Jamila.
Mara baada ya kupata kifungua kinywa, Kamanda Amata
alipotelea mitaani ndani ya jiji la Islamabad akitalii kuangalia
majengo na mambo muhimu ya kuvutia, misikiti mikubwa na
tamaduni za watu wa nchi hiyo. Alifanikiwa kufika eneo lile
lililotokea mlipuko asubuhi ya siku ile. Bado maafisa wa polisi na
wanajeshi waliokuwa na magari ya deraya walikuwapo wakifanya
kazi zao. Lugha waliokuwa wakiongea wenyeji wa mji huo
hakuielewa hata kidogo, ilikuwa tabu kwake.
Siku hii, Amata alikuwa mtalii wa jiji hilo, akitafiti hiki na kile.
Mkononi mwake alikuwa na magazeti mawili ya kiingereza;
Pakistan Times na Karachi Post aliyokuwa akiyapitiapitia kila apatapo
nafasi.

* * * *

Jenerali Kahir alikutana na vijana wake huko katika kambi yao


ya siri. Haikuwa wakati wake kufika, lakini jambo la dharula
lilitokea, ikabidi afike mahali hapo.
“Chanzo chetu cha habari kimenipa ujumbe hatari kidogo…”
akawaeleza. “Kuna mtu kaingia Islamabad, Mwafrika…
inasemekana mtu huyo amelala Mariot Hotel lakini kabla ya kufika
katika hoteli hiyo alikuwa na kikao cha siri pale Islamabad Club na
alikutana na yule agent wa CIA bwana Dhakar” Kahir akawaeleza.
Wale jamaa wakaonekana kujiweka umakini kwa habari hiyo.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Unataka kutuaminisha kuwa kaja kutupeleleza?” mmoja


akauliza.
“Inawezekana, si unajua kuwa tunaye mtu wao hapa…” Kahir
akajibu, “vipi kama ndo kaja kumfuata?!” akawasaili. Wale jamaa
wakatazamana.“Unataka kutuambia nini?”
“Atafutwe auawe… ila kwanza mkamhoji Dhakar akileta
ujeuri mkateni Shingo” Kahir akatoa maagizo.
“Kamwe Izbul haiwezi kutikiswa na mtu mmoja!”
aliyeonekana kama kiongozi wao akatoa tamko.
“Huyo mwanamke hakikisheni sasa anaitema hiyo code…
nahisi hapa sasa mambo yanaharibika…” Kahir akatoa amri. Wale
vijana wakatawanyika kila mmoja akichukua jukumu lake.

* * * *

Bhara Kahu Night Club ilikuwa kilabu cha siri cha usiku
ambacho watu wengi walikuwa wakikutanika kwa starehe. Kilikuwa
cha siri kwa sababu sheria kali za nchi hiyo hazikuruhusu hadharani
mambo kama hayo. Kijana mmoja wa Izbul aliwasili kwa siri
mpaka katika kilabu hicho. Wenzake wakiwa wamebaki nje kwenye
gari kumsubiri. Yule mmoja aliingia mpaka ndani ya kilabu kile.
Akaangazaangaza macho kutazama, maana alikwishaambiwa kuwa
Dhakar yupo katika yupo humo. Izbul walimpa taarifa mmoja wa
wanadada wa kilabu hicho kuchunguza kama mtu huyo yupo hapo
au la.
Dhakar alikuwa ameketi katika kaunta akiendelea kunywa
kinywaji chake taratibu, pembeni yake akiwa na mwanamke wa
Kizungu. Mguso katika bega lake ukamshtua. Alipogeuka,
akagongana macho na mhudumu wa kilabu hicho. “Kuna mgeni
wako nje!” yule mwanadada akamwambia. Dhakar akaangalia saa
yake, saa tatu na nusu usiku.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Akatoka na kumfuata yule mwanadada mpaka nje. Kijana


mmoja alikuwa akimsubiri hapo. Dhakar alipokuwa akimwendea
kijana huyo akahisi kupigwa na kitu kizito kisogoni. Akakosa
stamina na kuanguka chini kama mzigo. Akabebwa na kupakiwa
garini, safari ikaanza.
Katika eneo la viwanda la Hattar, kilomita kumi na tatu
kutoka Bhara Kahu iliwachukua takribani dakika ishirini na tano
kuwasili eneo hilo. Hattar lilikuwa eneo lililojazwa na viwanda aina
mbalimbali. Lile gari walilokuwa wakitumia vijana wa Izbul,
likasimama nje ya lango kuu la kiwanda cha nguo cha Hattar
‘Hattar Textile Mills’.Walipofunguliwa lango, gari lile lilishika njia
mpaka upande wa nyuma wa ghala kubwa. Ndani ya wigo huo
kulikuwa na magahala sita yenye kazi tofauti tofauti. Ndani ya moja
ya maghala hayo, Dhakar aliingizwa katika chumba ambacho
hakitumiki, wakamtupa chini kama gunia kisha ndoo za maji baridi
sana zikamwagwa juu yake. Dhakar akashtuka na kurudiwa na uhai
kama kwanza.
“Vizur sana…. Hahahahaaaaa! Mketisheni kitini…” mmoja
wa wale jamaa akawaambia wenzake. Wakamwinua na kumketisha
katika stuli ya chuma. Wale jamaa hawakuwa na huruma hata
chembe. Kwanza wakamtembezea kipigo cha hatari mpaka Dhakar
akabaki hoi, damu zilimtoka kinywani na puani.
“Kkkkwaninnni mnanipiggga?” akawauliza kwa tabu sana.
“Vizuri sana! Nataka utuambie, mgeni uliyekuwa naye jana
Islamabad Club ni nani, katoka wapi na kaja kufanya nini?” yule
kiongozi wa wale vijana akauliza kwa ukali.
“Anaitttwwwa Sparrrkkk, nendeni Marrriot Hottelll m-ta-m-
kkkuttta koh! koh! koh!” Dhakar alijitahidi kujibu na kuwaelekeza.
Wale jamaa wakatikisa kichwa kila mmoja kukubaliana na hilo.
Pigo moja la nguvu likamfyatua Dhakar kutoka kitini mpaka chini,
akapiga kichwa vibaya sakafuni na kupoteza fahamu kwa mara ya
pili. Baada ya kupata jibu ya lile walilolitaka wale vijana
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

wakakubaliana kwenda huko Hoteli yaMariot kumkusanya huyo


mgeni.

* * * *

Kamanda Amata alirudi kutoka matembezini majira ya saa


mbili usiku na kuingia chumbani kwake moja kwa moja. Baada ya
kujiswafi na kujiweka tayari kwa shughuli za usiku huo mojawapo
ikiwemo kumtembelea yule mtangazaji. Alipanga kufanya hayo
usiku kwa kuwa aliaminini kuwa kwake zingekuwa na tija zaidi.
Mara tu alipojitupa kitini akapitiwa na usingizi akiwa ameketi.
Usingizi ule ulikuwa mzito sana uliomchukua saa nyingi pale kitini
pasi na kushtuka.
Katikati ya usiku, Amata alishtuka na akili yake ikawa makini.
Nywele zake zikamsisimama, akajua hatari imemkaribia. Mlango
wa sita wa fahamu ukafanya kazi. Akaivuta bastola yake aliyokuwa
ameiweka mezani hapo na kuifunga kiwambo cha kuzuia sauti.
Tayari akili yake ilikuwa kazini. Alihisi wazi kuna ugeni unaomfikia
muda si mrefu. Hakukosea. Punde si pnde alihisi kitasa kile cha
kidijitali kikichezewa. Akainuka kutoka pale alipo na kuusogelea ule
mlango huku bastola yake akiwa kaipachika kiunoni.
Mlango ukafunguliwa taratibu. Hakuna mtu aliyeingia, na
Amata akatulia kimya palepale nyuma ya mlango. Sekunde kumi
zikapita, hakuna mtu aliyeingia. Baada ya hapo, Amata akaona
mtutu wa Short Gun ukitangulia kuingia ndani. Akasubiri
anachokitaka kitimie, hakujua wako wangapi. Subira huvuta heri.
Akamwacha aingie ndani kiasi cha kutosha ili mshughukikie.
Tofauti na matarajio yake, yule jamaa aliyeficha sura yake kwa
kitambaa kizito, alirudi nje. Minong’ono ya watu waliokuwa
wakiongea ilisikika kwa mbali. Amata aliisikia kwa utulivu mkubwa
ila tu hakuweza kuelewa ni nini watu hao wanachokiongelea.
Akagundua kuwa wapo watatu, akachomoa bastola yake na
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

kuiweka sawa. Haikupita hata sekunde kumi, akaingia mtu wa


kwanza kisha wa pili. Bastola ya Kamanda Amata ikabanja na
kumtandika yule wa kwanza risasi mbili za mgongo, akajibamiza
ukutani na kuanguka chini kama mzigo. Yule wa pili alipogeuka ili
kujua risasi ile imetokea wapi akakutana na konde zito lililotua
usoni pake na kumvunja mwamba wa pua. Hakujitetea, kwani
hakupewa nafasi hiyo baada ya kukutana uso kwa uso na domo la
bastola. Akabaki anahema kama jibwa lililokimbizwa huku bunduki
yake ya AK 47 ikimning’inia kifuani.
Hakuna aliyezungumza, wakabaki wakitizamana tu.
Wangezungumza nini ilhali lugha hawaelewani. Yule jamaa
alipotaka kuleta janja t, akakutana na chuma cha moto kilichopenya
sawia milimita chache tu kutoka moyoni.

‘…ongeza weledi katika mambo mawili; muda na umakini wa


kazi…’

Akaikumbuka sauti ya mwenyeji wake Dhakar aliyekuwa


akimpa mwongozo wa hali halisi ya kujilinda ndani ya Islamabad.
Yule jamaa kwa maumivu makali ya kifua akajikuta akienda chini
bila pingamizi. Macho yalimtoka akiupigania uhai wake, punde si
punde roho yake ikauacha mwili. Amata akasonya na kuanza
kuwapekua haraka haraka. Katika mfuko wa mmoja wao ndipo
alipopata karatasi ndogo iliyoandikwa kwa lugha ya Kiurdu ambayo
ndiyo iliyotumika haswa kama lugha ya taifa hilo. Akachukua simu
yake, akaiwasha na kuskani yale maandishi kisha akayatafsiri katika
softiwea maalumu.

‘Mfikisheni Hattar Textiles Mills ghala namba 5’

Akatikisa kichwa juu chini. Nani amepelekwa katika kiwanda


hicho? Akajiuliza. Lakini hakukuwa na muda wa kupoteza.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Akachukua simu ya mmoja wao kisha akatoka nje ya hoteli ile. Vitu
vyake vyote vya muhimu alivichukua kwenye mkoba wake mdogo,
akaufunga kiunoni. Kule chumbani aliacha begi tu alilokuwa
amebebea nguo zake. Alijua, kuna kurudi au la.

Alipotoka nje ya ile hoteli, akakutana na kijana mwingine


aliyevalia kama wale akielekea lango kuu la hoteli hiyo.
Akamgundua mapema. Alimwona wakati akitoka kwenye Toyota
Hilux moja lililokuwa maegeshoni. Akachomoa bastola na kumtaka
kurudi alikotoka. Yule jamaa akasimama kama sanamu. Akageuka
na kuanza kurudi kama kondoo mpaka kwenye lile gari. Akamtaka
kuingia, akafanya hivyo na Amata akaingia siti ya nyuma yake.
Akamgusisha domo baridi la bastola kwenye uvungu wa kisogo
chake.

“Hattar Textile mills… go! Go! ” akajaribu kumwambia kwa


Kiingereza. Yule jamaa akatia injini moto na kuondoka eneo lile.
Hakuwa mkaidi, dakika chache tu akawa mbele ya lango la kuingia
katika kiwanda hicho kikubwa. Taa Kali zilikuwa zikimulika uwanja
mpana wa kiwanda hicho ambao ndani yake kulikuwa na maghala
kama sita hivi. Malori kadhaa yalikuwa yameegeshwa katika uwanja
huo. Upande mwingine wa kiwanda hicho kulikuwa na ghala
kubwa lililoonekana halina shughuli nyingi. Mlinzi wa lile eneo
akalisogelea lile gari. Hatua tatu kabla hajainua bunduki yake.
Hakufanya lolote kwani kichwa chake kilifumuliwa vibaya kwa
risasi moja. Amata akatoka nje na mateka wake akiwa kamweka
ngao huku bastola yake inkingali kisogoni. Kishindo cha yule mtu
kuanguka kikawashtua wengine waliokuwa katika kona za karibu.
Kumekucha. Watatu wakajitokeza kutoka upande huo.
Amata akaitungua kwa risasi taa kubwa iliyokuwa ikimulika
hapo na kuipasua. Giza. Akamkokota yule mateka wake huku
akiwaangusha wale walinzi kwa risasi. Akamtupia uvungu wa lori
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

kubwa lililoegeshwa hapo.Lugha asiyoielewa ilizungumzwa na wale


wachache waliobakia wakikimbia huku na huko. Akafungua mkoba
wake na kutoa miwani maalumu ya kuweza kuona gizani, akaivaa.
Naam, sasa aliweza kuona vizuri kabisa. Alimsukuma nje yule
mateka wake, alipojitokeza tu risasi kama zote zikammiminikia.
Akaanguika chini huku akiongea lugha yao ya Kiurdu. Wakajua
wamechezewa shere.
Sasa nawaonesha mchezo. Lazima wacheze Sindimba ngoma ya kwetu!
Akajitoa katika uvungu wa lile lori, na kuachia risasi iloyofumua
tenki la mafuta. Lile Lori likashika moto. Kizaazaa. Amata
akakimbilia nyuma ya lile jingo la kiwanda. Alipofika tu kwenye
kona akapigana kikumbo na mlinzi mwingine akamwangusha chini.
Akamuwahi na kumuinua, akamwekea bastola kwenye shingo yake.
Macho wakitazamana.
“Mmemweka wapi ndugu yangu?” akamuuliza. Yule bwana
hakuwa mkwepeshaji maneno. Akaonesha ishara ya mkono
kwenye lile ghala la upande wa pili. “Twende” Amata
akamwambia. Yule kijana hakuwa na la kufanya, akaongoza njia
kama mwanakondoo aendaye machinjioni.

* * * *
Jenerali Kahir alikurupuka kutoka kitandani baada ya kupata
taarifa hiyo. Alihisi BP inapanda na kushuka bila mpangilio.
Hakuamini anachosikia. Nini kimetokea? Akajiuliza. Akapiga simu
za vijana wake, zote hazipokelewi. Akapagawa. Simu aliyoipiga kule
kiwandani kwenye kitengo cha dharula ndiyo iliyompa mwanga.
“Tumevamiwa, kuna mtu kaja hapa na gari letu
tukamfungulia… amefanya uharibifu mkubwa sana, malori zaidi ya
matatu hapa yameshika moto, tunahitaji msaada…”. Kahir akahisi
kuchanganyikiwa. Akatoka taarifa haraka katika vikosi vya usalama,
akitumia cheo chake. Yeye mwenyewe, akavaa haraka haraka na
kumwacha mkewe Bi. Zulekha kitandani. Akakimbilia gari lake na
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

kuingia, safari ikaanza. Mwendo aliokuwa anapita nao barabarani,


tumshukuru Mungu ilikuwa usiku. Akawasili katika eneo la
viwanda la Hattar na kuelekea pale anapotaka. Aaegesha gari nje na
kuteremka. Kahir akabaki kajishika kiuno baada ya kukaribishwa na
moshi mzito uliotanda angani kote.
Ni nani mshenzi huyu? Akajiuliza. Nukta hiyohiyo simu yake
ikaita, akainyakuwa kutoka katika mfuko wa shati lake. Aliyepiga
anamjua, mmoja wa vijana was Izbul, “ndiyo, nipe taarifa!”
akamwambia.
“Watu wetu wawili wameuawa Mariot Hotel chumba namba
thelathini na tatu…”
“Ok, sawa!” Kahir akajibu na kuikata ile simu. Akajisika kiuno
na kusikitika. Wakati akiwa pale nje, kikosi cha zima moto
kilimaliza kazi yake. Hali ya utulivu ilirejea katika lile eneo.

* * * *

Asubuhi ya siku iliyofuatia, Jenerali Kahir alikuwa na kikao


cha dharula katika moja ya nyumba zake za kifahari maeneo ya
Barabara ya Kohiston ndani ya jiji la Islamabad. Watu watano,
wenye wadhifa katika kundi la Izbul Mujahedeen walikutana.
“Huyu mtu anaonekana hatari sana ee?” mmoja was akauliza,
“kwa sababu kuua vijana wa Izbul wawili kwa mara moja si kazi
ndogo…” akaongeza.
“Na usiseme wawili tu, na wale wa kule kiwandani na
uharibifu aliyofanya…. Huyu bwana akamatwe achinjwe kama
kuku…” mjumbe mwingine akaongeza kusema.
“Kabisa kabisa… lakini tunampata wapi kwa sababu mji
mzima huu hajaonekana Leo, kila kwenye chanzo chetu hakuna
habari” .
Kahir akashusha pumzi, akaweka kofia yake mezani,
“nitamkamata tu! Na nitamvunja shingo… taarifazinasema huyu
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

jamaa ni Mtanzania, ni Secret Agent… nafikiri amekuja kwa ajili ya


hili swala la Pegan Box, nahisi sasa atakuwa anatafuta njia ya
kutufikia ili kumwokoa yule mwanamke”
“Mh!” Mjumbe aliyekuwa kimya muda wote akaguna na
kujiweka vizuri kitini, “anajiamini nini huyo mtu kupambana na
kundi hatari duniani kama hili…?” akauliza.
“Atapatikana tu, vijana wametawanyika kote. Na kule kambini
nimewaambia wahakikise yule mwanamke anatema hiyo code. Na
akishaitema kazi moja kwa Mansoor … tunaenda kuteketeza kila
kitu mpaka yeye mwenyewe na tunachukua hilo box” Kahir
akaongea kwa gadhabu na kuitupa picha ya Amata mezani.
“Kunguni tu huyu!” mwingine akamalizia na kuisogeza ile
picha kwa mwenzake. Wote wakafanya hivyo hivyo mpaka
ikamrudia Kahir.

* * * *

Katika mji mdogo wa Al-Haram, nje ya jiji LA Islamabad,


Dhakar alikuwa akipatiwa matibabu na daktari wa siri ambaye
Amata alimjua baada ya kumpekua mtu huyo aliyekuwa kwenye
mzimio na kuikuta kadikazi ya daktari Sajan.
“Atapona?” akamuuliza yule daktari.
“Atapona tu usijali… na ataamka muda si mrefu kwa hii dripu
niliyomwekea. Aaaah by the way, wewe ni nani na umepajuaje
hapa?” yule daktari akauliza.
“Naitwa Spark, Mr. spark… huyu bwana ni rafiki yangu sana,
nimekuja kikazi na nilikuwa naye mpaka haya yalipotokea. Kabla
hajazimia alinielekeza kwako na akanipa namba za simu,” yule
mzee akatikisa kichwa juu chini kukubaliana naye. Amata akainuka
na kuzungukazunguka mule ndani akitazama hiki na kile.
“Samahani dokta, unamjua Jeneral Kahir?” akauliza.
“Ndiyo! Wa nini?”
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Nina ujumbe wake, nahitaji kumkabidhi…”


“Oh, ni mtu mkubwa na hatari sana jeshini… anadhamini
kundi la Izbul Mujahedeen… kumuona si rahisi sana lakini ….”
akasita.
“Lakini….!” Amata akaanzisha palepale.
“Jinnah Avenue mkabala na Fatima Jinnah Park… hapo ndo
makazi yake makuu na utamwona. Sikushauri umfuate pengine
popote…”
“Sawa!”

* * * *
Jinnah Evenue, barabara safi iliyopo mkabala na hifadhi
ndogo ya Fatima Jinnah katikati ya jiji la Islamabad. Ni upande wa
kushoto mwa barabara hiyo kama unaelekea chuo cha mchezo wa
cricket. Kamanda Amata alikuwa kwenye taksi ileile iliyomchukua
siku ya kwanza. “Niache hapo Punjab Criket…” akamwambia yule
dereva. Alipoteremka akamruhusu kuondoka. Alipohakikisha ile
taksi imepotea. Akajiweka sawa tayari kwa kazi inayoikabili. Amata
akatazama kushoto na kulia, akavuka barabara na kuelekea upande
ulipo mgahawa wa Mac Donald. Akatembea taratibu kuifuata
barabara ndogo ya kuelekea Silver Oaks. Upande huo akaifuata
moja ya ofisi iliyokuwa na kibao kuwa inakodisha magari. Hii ndiyo
hasa ilikuwa ikimleta eneo hili kwanza. Ndani ya ofisi hiyo
alipokelewa na mwanamke aliyeketi nyuma ya dawati kubwa lenye
kompyuta moja na simu ya mezani vikiambatana na makablasha
machache.
“Karibu sana nikusaidie…” yule mwanadada akamkatibisha
Amata.
“Yeah, naweza pata gari la kukodi?”
“Inawezekana, aina gani? Pickup, salon au mini bus? Tuna kila
aina ya gari unalohitaji”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Vyema, nahitaji gari inayohimili barabara zenu, ninaelekea


huko majangwani kutembelea kilimo cha mpunga…”
“Sawa! Ipo Jeep inayoweza kuhimili mikiki yote. Utaendesha
mwenyewe?”
“Ndiyo!”
Yule mwanadada akatoa kitabu kikubwa na kumpatia aweze
kujaza taarifa zake. Akafanya hivyo na kulipia gari hilo kwa Siku
saba. Pasipoti yake ilimtambulisha kama raia ya Nigeria, Frederick
Oduoh. Amata akakabidhiwa gari alilolihitaji, alilothibitishiwa kuwa
litamfaa. Akaliwasha, lilikuwa full tank. Akaondoka taratibu na
kuikamata barabara hiyo mpaka ile ya Mangla, akaingia kushoto na
kuifuata barabara ndogo ya Galli 115. Akahesabu nyumba kama
alivyoelekezwa. Alipoifikia nyumba aliyohisi ndiyo kutokana na
namba ya geti. Akapitiliza na kuliweka gari hilo kwenye kona
ambayo ingemtoa kiurahisi kuelekea barabara ya Jinnah. Amata
akateremka na kurudi kwa miguu. Ukimya ulitawala, ukiachana na
taa za kwenye wigo wa nyumba hizo kumulika barabarani, vivuli
vilivyotokana na miti iliyokuwa upande huu na ule wa barabara
hiyo ndogo vilimficha.
Kilichomshangaza katika eneo hili ni ile hali ya ukimya,
hakukuwa na hata sauti ya mbwako wa mbwa. Akaitazama saa
yake, ilikuwa tayari saa saba usiku. Muda mzuri! Akawaza. Akavuta
hatua na kuifikia ile nyumba. Haikuwa kubwa ya kutisha, bali ya
wastani, iliyozungukwa na maua na miti ya vivuli kila upande.
Akaangalia jinsi ya kuingia katika nyumba hiyo. Wigo wake
uliungana na kukatishwa katikati kwa ukuta. Njia pekee ilikuwa ni
kucheza na geti tu. Akavaa miwani yake yenye kioo cha Giza.
Akatazama vizuri upande wa mbele wa ile nyumba. Miwani ile
ilikuwa na uwezo wa kuonesha kila mwali wa infrared ambayo mara
nyingi hutumika kwenye kamera za usalama za siri kabisa.
Alipojiridhisha kuwa hakuna akauendea ukuta wa mbele pembeni

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

tu mwa geti na kutumia sekunde tatu kuukwea na kutua chini


upande wa ndani.
Nyumba ilikuwa kimya kabisa, mwanga hafifu ulionekana
ndani ya nyumba hiyo. Hakukuwa na ulinzi. Amata akachukua
kurunzi yake ndogo yenye ukubwa wa kalamu na kuizunguka
nyumba ile huku akimulika dirisha la kila chumba. Aliporudi
upande wa pili, akatokea mlango wa mbele. Akachukua funguo
zake na kucheza na kitasa hicho. Kikaachia. Akausukuma taratibu
na kuuacha useleleke wenyewe huku tayari bastola yake iliyoshiba
ikiwa katika mkono imara uliyovikwa gloves nzito ya ngozi. Nguo
zake nyeusi na kiatu chenye soli ya mpira vilimfanya asionekane
vyema kwenye giza na kutotoa aina yoyote ya ukelele atembeapo.
Akakagua kila chumba, hakukuwa na mtu.
Amata akaiendea taa ya sebuleni na kuiondoa, kisha
akachukua jaribosi na kulivisha katika kitako cha taa hiyo.
Akairudishia kwenye holda yake na kutulia sehemu anayojua kwa
vyovyote ataweza kufanya shambulizi endapo ikitokea hali ya
sintofahamu. Kiwambo cha kuzuia sauti kilikuwa kimefungwa
barabara katika domo la bastola hiyo.

* * * *

Mansoor aliketi katika kiti chake anachokipenda ndani ya


jumba lake kubwa huko Kashmir. Vijana wake walikuwa
wamesimama upande huu na ule mwingine.
“Usiku wa kazi umefika, inabidi tukamchukue yule
mwanamke kule Izbul. Lakini ninyi mnajua kilichotokea Islamad
Leo… Jenerali Kahir na wadau wake wa Izbul Mujahedeen
washapata pigo, hivyo hawatakuwa na umakini juu ya ulinzi wao,”
akawaambia. “Ngome yao kule Hattar imetikiswa…. Lakini ni nani
aliyeitikisa? Bado namtafuta!” akaongeza kusema.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Inasemekana kuna kikosi cha siri cha makomandoo kutoka


Afrika kimeingia…” mmoja akajibu.
“Sina uhakika! Cha msingi, hakikisha unaweka ulinzi kwenye
himaya yetu, hii ngome haitakiwi kuguswa. Kitakachotokea sasa
kwa Kahir atajua sisi tumemvamia naye atafanya anachojua,”
Mansoor akasikitika. Akiwa katika kikao hicho, simu yake ikaita,
akaifyatua tayari kuipokea.
“Fernandez!” akatamka na kuwataka vijana wake kutulia.
“Comrade Mansoor, umepata habari za Islamabad?” Fernandez
akauliza kutokea upande wa pili.
“Yeah!”
“Weka kambi imara na ushauri wangu lihamishe hilo box…”
“kwa nini?”
“Nimepata taarifa kuwa mpelelezi mashuhuri wa Tanzania yupo
Pakistan na amekwishaanza jukumu lake la kulitafuta Pegan Box…”
“Shiiit… aje tu nitamchinja kama kuku…”
Fernandez akasikika akiguna kutoka upande wa pili, “huyo
bwana ni hatari, sasa inabidi kuchukua tahadhari…” akamliza.
“Hawezi kufika hapa wala kuitikisa ngome hii…” Mansoor
akajigamba. Mazungumzo machache yakafuata kisha simu ile
ikakatika. Akainama kwa muda wa sekunde kadhaa kisha
akawatazama vijana wake. Arafa ikaingia katika simu yake,
akaifungua na kukutana na picha ya kijana Mwafrika, mwenye
macho angavu na aliyeonekana kubeba umbo la kimazoezi na
kipiganaji. Arafa nyingine ikafuata, iliyosomeka.

‘Mtu huyu yuko Islamabad ni jasusi hatari…’

Mansoor akawapa vijana wake ile picha, nao wakaitazama kwa


zamu na kuirudisha.
“Yupo Islamabad, jasusi hatari kutoka Afrika, ameshaanza
kumtikisa Kahir…” Mansoor akawaambia.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Hapa hawezi…” mmoja wa wale vijana akamwambia bosi


wake.
“Panga kikosi, na hili sanduku litabaki hapa…” Mansoor
akamwambia huyo kijana.
“Tunatuma vijana huko Islamabad kumsaka mtu huyu…
atakamatika tu” kijana mwingine akasema.
“Mkimpata mumuue hukohuko hapa mniletee kichwa tu
nikihifadhi kwenye friji” Mansoor akawaambi vijana wake na
kutaka watawanyike na kazi ifanyike. Ngome ya Mansoor, katikati
ya bonde la Kashmir lililozungukwa na milima ilikuwa eneo hatari
lisilopenyeka. Lilikuwa na wanamgambo walioogopwa wakilinda
kila upande. Wengi hawakujulikana, walikuwa walinzi wa siri wa
Mansoor, walijua kila tukio linalotukia katika eneo hilo. Walimtia
jeuri tajiri huyo.

* * * *

Usiku wa saa tisa, magari mawili yalisimama nje ya lango la


kuingilia nyumbani kwa Jenerali Kahir. lango hilo lilifunguka
lenyewe kwa mtambo maalum. Amata akajiweka tayari. Akaivaa
miwani yake inayomwezesha kuona gizani maana alijua ni nini
kitatokea.
“Na tukimkamata atajuta… tunamkata kidole kimoja baada ya
kingine mpaka tunammaliza…” sauti kali na ya kikatili ya Kahir
aliyapenya masikio ya Amata kiasi kwamba ilimsisimua mwili.
Mmoja wa walinzi wake akafungua mlango na kuwasha taa. Badala
ya taa zile kuwaka, kilichotokea ni shoti sakiti iliyosababisha mlipko
hafifu na taa zote kuzimika. Risasi ya kwanza ikambwaga yule
mlinzi aliyefungua mlango. Ya pili ikamfumua mlinzi mwingine.
Jenerali Kahir akajitupa chini kwenye maua na kujiviringa kiufundi
mpaka chini ya ngazi. Wale walinzi wa nje walipoona tu taa
zimezimika ghafla wakajua kuna hatari. Wakaingia ndani haraka.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Giza lile liliwanyima uhuru wa kuona vizuri. Amata alikuwa


kajibana usawa wa kabati la vitabu akisubiri kuona nini kinatokea.
Kahir naye alitulia kimya pale chini huku maua yakimfunika. Wale
walinzi walipoingia tu, Amata aliwaona pasi na tabu. Kwa shabaha
yake maridhawa akawachapa risasi kila mmoja kwa seknde yake na
kuwabwaga chini wakiwa marehemu.

Kamanda Amata aliwafanyia mashambulizi ya kimyakimya


ambayo hawakuyategemea. Alipoona kimya umekuwa mwingia na
kutawaliwa na harufu ya baruti tu, akajua kuwa wamekwisha, sasa
kazi iliyobaki ni kumsaka mbaya wake. Taratibu akaanza kumtafuta
Kahir. Ilikuwa ngumu kutokana na giza mahali hapo. Lakini
miwani yake ilimsaidia kuona.
Kahir akiwa pale chini, hakutikisika, alitulia kama gogo.
Mbinu za kivita. Alikwishamuona Amata akisogea mahali pazuri.
Akamsumbiri afike mahali pazuri zaidi ili ampe shambulizi la
maana. Bastola yake ilikuwa kiunoni, alijua akiichukua tu adui yake
atamuwahi. Afanyeje? Heri ajaribu anachoweza. Alihitaji kasi ya
ajabu kufanikisha shambulizi hilo. Na siku zote, kwenye pambano
la kufa na kupona, kasi ni jambo la maana kuliko yote. Akahesabu
moyoni huku mkono taratibu ukielekea kwenye bastola.

Amata akasimama baada ya mwili wake kusisimka. Hatari.


Kwa mbali akasikia sauti ya bastola inayoondolewa usalama. Kwa
kasi akajirusha kando na risasi mbili zikapita sentimita chache sana.
Akaanguka chini. Kahir, mtu mzima, mpiganaji wa jeshi la
Pakistan, mfadhili wa Izbul Mujahedeen akaonesha uwezo wake.
Alijibetua kiufundi sana na kusimama. Wakati huo Amata
amekwishahama eneo lile. Giza lilimtatiza mpiganaji huyo na maua
marefu yaliyozunguka nyumba hiyo yalisaidia kumficha adui yake.
Kamanda Amata alitumia mbinu za kujificha alizojifunza huko
Japan katika mafunzo ya Ninjutsu. Hakuonekana kiurahisi.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Jenerali Kahir akanyata polepole sana. Akapepesa macho na


kumuona Amata aliyejifanya kama kivuli cha mti mmoja wapo.
Kahir alikuwa amekariri vivuli vya maua na miti hapo kwake ama
ikimulikwa na taa za usalama au mbalamwezi. Siku hii kulikuwa na
mbalamwezi hafifu, Kahir aliitumia hiyo kumtafuta adui yake.

Amata alikuwa na nafasi ya kummaliza Kahir, lakini haukuwa


mpango wake. Alimtaka akiwa hai isipokuwa amlegeze kidogo.
Kwa sababu hii hakutaka kutumia hata silaha ya moto. Aliiandaa
mikono yake kwa kazi. Alimtazama adui yake, akausawili umri
wake, akakadiria kama miaka sitini kwenda sabini hivi. Akijiangalia
na yeye ni miaka arobaini na mmoja. Hakumdharau maana
wanasema utu uzima dawa na pia koti la babu halikosi chawa.
Kutoka pale alipo, kwa kasi ya ajabu, Amata aliruka kwa
mruko hatari kabisa. Risasi za Kahir zikachana jacket la ngozi
alilovaa Amata. Kabla hajafanya kingine Kahir alajikuta akipokea
mapigo mawili kifuani pake na kwenda chini. Mzee yule hakukubali
kufika chini kiurahisi, akajirusha sarakasi ‘beki’ na kutua tena
ardhini kwa migu yake yote miwili salama salimini huku akijipanga
kumkabili Amata aliyekuwa akija kwa kasi ya upepo. Pigo la karate
lililopigwa na Amata likakingwa kiufundi kabisa na mzee hiyo kisha
Kahir akafyatua pigo zito lililomtandika Amata kichwani,
akayumba na kusikia kizunguzungu kikali. Akapepesuka na
kujibamiza kwenye mti mmoja jirani.
Kahir alikuwa keshafika kumaliza mchezo ule. Alijua kwa
vyovyote adui yake huyo hawezi kuwa na uwezo wa kufanya
chochote kutokana na hali aliyokuwa nayo. Amata akatumia nguvu
ya kutuliza akili yake. Alihisi mfumo wa fahamu zake ulishtuliwa na
pigo lile. Kahir alikuwa kama mbogo vidole vyake vyenye nguvu
vilikuwa vimechanua mithili ya miba ya nungunungu. Alikuwa
tayari kushambulia ikiwezekana kumaliza mchezo kabisa. Amata
akampigia hesabu za harakaharaka. Kahir alipomfikia, Amata
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

akauzunguka ule mti haraka na kumtandika pigo takatifu lililotua


kwenye uti wa mgongo. Kahir akajibwaga chini huku akitoa mguno
wa maumivu.
Amata akamuwahi pale chini. Kahir akajigeuza haraka na
kukutana na mapigo matano mazito yaliyomlegeza nguvu.
Kamanda Amata akaichomoa bastola yake na kufyatua risasi
mmoja iliyotua kwenye kanyagio la mguu. Kahir akaguna kwa
maumivu. Alipotaka kujitutuua akakuta kabwanwa kisawasawa.
“Naitwa Kamanda Amata TSA 1 code 005… namtaka dada
yangu Jamila shenzi nyie,” akamwambia. Kahir alikuwa
akitetemeka, damu zikimmwagika. “Yuko wapi Jamila, liko wapi
Pegan Box?” akamuuliza. Amata akachukua waya mwembamba
kutoka kwenye mkoba wake. Akamtandika Kahir mateke ya nguvu.
Alipogeuka kulala kifudifudi akamuwahi na numtia ule waya
shingoni. Akamkaba barabara.
“Utaniambia au la?”
“Nasssema aaaaah koh!koh!koh” akajibu kwa tabu na
kukohoa. Amata akalegeza ule waya kidogo na kumpa nafasi ya
kupumua.
“Yupo kambini, huko milima ha Kanihar…” akaeleza.
“Kambi ya nani?”
“Izbul Mujahedeen!”
“Anhaa ninyi ndo mnalipualipua mabomu hovyo mjini siyo?
Haya wapigie simu, waambie vijana wawili wamlete hapa kwako
haraka. Wewe unajua utadanganya vipi ili wamlete… vijana wawili,
narudia wawili…” akamwamuru na kumchomoa simu mfukoni
mwake, akaiwasha na kumtaka ataje namba za siri. Kahir akataja
bila shaka, simu ikafunguka. Akaweka namba aliyotajiwa na
kumwekea sikioni.

* * * *

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Katika kambi ya Izbul Mujahedeen huko milima ya Kanihar,


simu ilifika ya kuwa Jamila anatakiwa nyumbani kwa Jenerali.
Ilikuwa ngumu kwanza kwa watu hao kuamini hilo agizo.
Wakaulizana mara mbilimbili. Baada ya itifaki za kutosha na
viongozi wao wakaamua kutekeleza jukumu.
Jamila akatolewa kwenye chumba alichofungwa, akiwa
hatamaniki, kachakaa. Akapakiwa kwenye Toyota Hilux na safari
ya kwenda mjini ikaanza. Katika gari hilo alikuwapo Jamila na
walinzi watatu pamoja na dereva.
“Mkuu anataka mzigo hana lolote!” wakaambiana na kuangua
vicheko vilivyomkera mwanamke hyo. Iliwachukua saa moja
kuwasili katika eneo hilo ambalo kiongozi wao wa siri alikuwa
akiishi. Lile gari likapunguzwa mwendo na kusimama jirani kabisa
na yale mengine mawili yaliyomleta Kahir. Giza lililotanda katika
nyumba ile liliwaogofya. Jamila aliweka mambo mawili kichwani
mwake, hakujua kati ya hayo ni lipi litatukia. Ama kpata mateso
mengine zaidi ili aseme kodi yake au kufanyishwa ngono kwa
nguvu jambo ambalo kwake ilikwa ni heri kufa.
“Kuna dalili ya watu humu kweli?” mmoja akahoji wakati
wakiteremka.
“Mh! Yaani hata akina Farouq bado wapo!” mwingine
akashangaa. Wale jamaa watatu wakashuka, kisha wakamshusha
Jamila na kubofya kengele. Lango la nyumba hiyo likafunguka
taratibu na kuruhusu walio nje kuingia ndani. Wale vijana waliokuja
na Jamila wakapata wasiwasi na hali hiyo. Mmoja wao akatangulia
huku akiiweka bunduki yake ya AK 47 sawasawa. Wale wawili
wakabaki na Jamila nao bunduki zao zikiwa tayari kwa lolote.
Kutoka ndani ya nyumba ile, Kamanda Amata alikuwa
amemkalisha Kahir kitini na yeye nyuma yake. Yule
mwanamgambo aliyetangulia alikuwa akitembea kwa hadhari
kubwa. Amata alikuwa tayari na Shot Gun mkononi mwake.
Alijiweka tayari kwa kuwa alijua nini hasa kitatokea.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Yule mwanamke yupo wapi?” Kahir akauliza kwa taabu.


Jamila akaingizwa katika sebule ile iliyotawaliwa na mwanga hafifu
wa taa ya kusomea. Ile taa ikazimika baada ya Amata alipoona
mmoja wa wale wagambo akiiondoa usalama bunduki yake. Mara
tu alipozima ile taa, Amata alijirusha kando huku akikibinua kile
kiti na kumfunika kahir, ile kamba nyembamba aliyomniga nayo
shingoni ilimbana sawasawa ikiwa imefungwa vizuri kwenye mguu
wa meza. Amata akafyatua risasi na kumwangusha yule mgambo.
Kabla hajafyatua tena, risasi za kutosha zikamiminika pale alipo.
Akajivingirisha kuelekea upande mwingine. Risasi zikamfuata
mfululizo kulekule aliko. Alipogota kwenye ukuta akahisi maumivu
makali kwenye nyama ya paja. Amata akafyatua risasi kuelekea
upande wa pili, mguno wa maumivu ukasikika upande huo.
Akajitahidi kuinuka, lakini kabla hajainuka sawasawa alijikuta
akipigwa dafrao na kurudi chini. Juu yake alikuwa akija yule
mwanamgambo akiwa na jisu kubwa mkononi mwake. Amata
akamdaka mkono na kumyumbisha pembeni, akajibamiza ukutani.
Kwa nguvu zote, akamkunja ule mkono na kuuvunja. Yule
mgambo akainua miguu na kumtia kabali maridadi kwa miguu
yake. Akamvumta nyuma. Amata kwa kutumia kisu kilekile
akakiteremsha kwa nguvu. Yule jamaa akajisogeza kidogo tu,
kikatua sakafuni. Yule mgambo kwa ufundi mkubwa kwa mkono
mmoja aliidaka shingo ya Amata na kujiinua, akamtia kabali
nyingine.
Mlio wa risasi ukasikika jirani kabisa na sikio la Amata. Yule
mgambo akaguna na kulegea, akatua sakafuni. Amata akainuka na
kusimama kwa kuchechemea. Akajishika kwenye meza na
kusimama kwa sekunde kadhaa. Damu zilikuwa zimelowesha
suruali yake.
“Jamila!” Amata akaita. Jamila akamwendea Amata na
kumshika kwa mkono mmoja.
“Pole, umeumia sana?” Jamila akamuuliza Amata.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Hapana nilikuwa nakusanya nguvu tu…. Tuondoke” Amata


akamwambia Jamila. Wakatoka nje ya ile nyumba.
Lazima niwaachie maumivu! Amata akawaza. Akachukua bastola
yake na kupiga risasi moja sawa wa tenki la mafuta la moja ya yale
magari. Moto mkubwa ukalipuka na wakati huo ving’ora vya
magari ya polisi vilikuwa vikisikika. Amata na Jamila wakatokomea
gizani mpaka kwenye lile jeep alilokodi. Amata akaketi nyuma ya
usukani huku Jamila akiwa kando. Safari ikaanza kwa mwendo wa
kawaida kana kwamba hakuna kilichotokea.
“Wewe ni nani?” Jamila akauliza. Amata akamtazama
mwanamke huyo aliyechakaa na kuchoka.
“Amata… Kamanda Amata!” akamjibu. Jamila akajikuta
akipigwa na mshangao, hakuamini anachosikia.
“Kamanda Amata?” akauliza.
“Mimi ndiye,” Amata akamjibu huku akiendelea kupanga na
kupangua gia za lile Jeep, akikata barabara kuelekea kule
alikomwacha Dhakar.
“Siamini…” Jamila akajikuta akitamka.
“Utaamini taratibu, usijali…” Amata akamjibu bila
kumwangalia usoni. Jamila akatulia huku mikono take akiwa
amejishika vizuri kwenye vishikio ndani ya gari hilo.
Al Haram, mji mdogo nje ya jiji la Islamabad ndiko alikoamua
kufikia kwanza. Nyumba ileile aliyomwacha Muhedeen Dhakar
ndipo alifikia usiku huu akiwa na Jamila. Akaegesha gari na
kuteremka huku akichechemea. Jamila akawahi kumsaidia kumpa
wenzo kutembea. Ndani ya nyumba hiyo, daktari Sajan alimsaidia
Amata kumtibu jeraha lake, akamshona nyuzi kadhaa.
“Usihofu, utapona…” Sajan alimfariji.
“Kesho nitatembea?”
“Bila shaka…” Sajani akamjibu, “kazi yako umemaliza?”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Bado, nitaondoka muda wowote. Nipatie sindano na dawa


za maumivu…” akamwambia yule daktari. Jamila alikuwa
sambamba na daktari yule kufuatilia kila hatua ya matibabu yake.
Amata akapewa chumba maalum cha kujipumzisha, Jamila naye
hakuwa mbali akajiweka kwenye chumba hichohicho. Wawili hawa
walikutana katika chumba kimoja.
“Jamila,” akaita.
“Bee!”
“Niambie, nini kilitokea kaika safari yenu ya kurudi…” Amata
akataka kujua. Jamila akaeleza kila kitu mpaka alivyokamatwa na
wanamgambo wa Izbul. Kamanda Amata alituliza akili, akasukuti
na kumtazama kepteni huyo wa kike. “Pole sana! Ina maana sasa
hujui kama wenzio wako hai au wamekufa?” akamuuliza.
“Sijui, nina hofu sana na hili…” Jamila akamjibu.
“Inabidi twende Kashmir tukamalize kazi… Nimetumwa vitu
vinne, kimoja nimeshapata bado vitatu…” Amata akasema. Jamila
akabaki kutikisa kichwa. Akainuka na kuingia kwenye bafu dogo
ndani ya chumba hicho. Hakujali yupo na nani. Alichojoa nguo
zake na kuzitupa kando, akaingia kujimwagia maji na kumwacha
Amata akimeza mate akimeza mate kwa kila alichokiona. Macho
hayana pazia!

* * * *

Kituo cha luninga cha SAMAA kilikuwa kikionesha habari ya


Jeneral Kahir. Kupitia luninga yake kubwa, Fernandez alitabasamu
aliposikia kifo cha Jenerali Kahir. Alijua wazi kuwa sasa upinzani
wa kulipata Pegan Box haupo tena. Akainua bilauri yake iliyojaa
pombe kali, akaipunga hewani na kupiga mafunda kama matatu
huku akikunja sura yake. Aliposhusha akainua mkonga wa simu na
kubonyeza tarakimu kadhaa, akaiweka sikioni.
“Umepata habari za Islamabad?” akamuuliza Mansoor.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Nimepata, nipo hapa natafakari…” Mansoor akajibu.


“Unatafakari? Huoni kuwa kazi imekwisha?”
“No! Aliyemuua Kahir kwa vyovyote yupo safarini kuja
hapa…” akaeleza.
“Usiwe na hofu, cha muhimu ni kumjua mapema na kumpa
pesa tu. Kama hujuma hii imefanywa na viongozi wake, yeye ni
nani awe jeuri? Kuna binadamu jeuri mbele ya pesa?” Fernandez
akauliza.
“Inabidi tukutane tulipange hilo… nafikiri ufike hapa
kesho…” Mansoor akakubaliana na mteja wake Fernandez kuhusu
hali hiyo. Fernandez alitoa taarifa kwa vijana wake waliopo
Islamabad kunusanusa ili kujua tu huyo mtu ni wa namna gani
ambaye mpaka dakika hiyo amekwishaitikisa Izbul Mujahedeen
kwa kumuondoa kiongozi wao.
Taarifa alizokuwa akizipata kutoka Islamabad
hazikutofautiana na zile alizozipata Mansoor kuwa muuaji huyo au
mtu huyo hatari hajajulikana bado. Mpaka dakika hiyo, duru za
kiusalama zilikuwa na picha moja tu ya mtu anayesadikiwa. Picha
hiyo ilipigwa kwa kamera za ulinzi katika hoteli ile ya Marriott
ambayo Amata alifikia na pale palitokea mauaji.

* * * *

“Mambo yameharibika!” sauti nzito ilisikika ikiwaeleza


wajumbe watatu waliojifungia chumbani kwa mzungumzo.
“Hii ni hatari sana, haka kamama kanajiamini nini? Maana
tumetafuta undani wake tumeukosa…. Tumefanya kila upekuzi
anaonekana ni mfanyabiashara tu anayemiliki kampuni yake
pamoja na mwanawe wa kiume…” mjumbe mmoja akasikika.
“Hamumjui yule…. Hizo biashara ni geresha tu…. Ni
mwanausalama wa siri was Rais… invinsible” yule kiongozi
akawaeleza. “Yule mama amehudumu Ikulu kwa miaka mingi….
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Kama mnakumbula sakata la wale majinuni waliotaka kumpindua


Nyerere… yeye ndiye aliyelifanyia kazi mpaka tamatike” akazidi
kudadavua.
“Kama ni hivyo, hastahili kuishi… ” mjumbe mwingine
akaeleza.
“Hafai, ni nyoka mbaya, tayari vijana wake wameshaanza
kuharibu mambo huko Pakistan, nimepata taarifa toka kwa mdau”
“Hatupati kitu, kila kitu kinaharibika…. na unafikiri mwisho
wake ni nini sakata hili likimalizika? Siye tutakuwa matatani…”
“Kwa hilo usemalo, lazima tumkomeshe huyu mama, atakula
jeuri yake… watu tunataka kula na kufaidi mema ya nchi, yeye ni
nani hata atubanie?”
Kikao cha watu hawa kilikuwa kizito chenye maamuzi mazito.
Kilidumu kwa takribani saa nne, kikipitisha maazimio
mazitomazito.

SHAMBA

“Habari njema ni kuwa Amata amefanikiwa Kumpata Jamila


ila amemuua kiongozi mkubwa wa jeshi ambaye inasemekana
alikuwa kiongozi wa siri wa kikundi cha wanamgambo hatari cha
Izbul Mujahedeen” Madam S alieleza. Jopo zima la TSA lilikuwa
katika kikao cha siri isipokuwa Amata peke yake.
“Kiukweli, kazi ya hatari sana aliyoifanya ila ametuimia akili ya
ziada kumpaa Jamila…” Chiba akaeleza.
“Sasa inabidi apate like box…”
“Maadam yuko na Jamila, naamini kazi itaenda. Jamila ni
mwanajeshi hivyo Amata hana mzigo, ila msaada… lakini mwisho
wa yote sakata hili linahamia hapa nchini” akawaeleza. “Kuna watu
lazima wachukuliwe hatua za haraka, wakamatwe na wafikishwe
kwenye vyombo vya usalama. Nikitoka hapa naenda kuwasilisha
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

majina hayo kwa Rais... Nawashukuru sana ninyi kwa kazi


mliofanya. Nakabidhi majina na tunaiachia serikali ifanye
inavyoweza…” Madam S. Madam S akamaliza kikao na vijana
wake akainuka tayari kuondoka. Akageuka na kumtazama Chiba,
akambania Jicho. Chiba akasimama na kukiacha chumba kile. Mara
tu alipotaka kutoka, simu ikaita. Gina aliyekuwa jirani na simu hiyo
akainyakua na kuiweka sikioni.
“Ground Zero!” Gina akaitika maana alijua wazi kuwa simu
hiyo ilikuwa ni mmoja wa miongoni mwao.
“Gina!” Sauti ya Amata ikaita, “niunganishe na HOT,”
akamwambia. Gina akagonga vidole vyake na kumtaka Madam S
asikilize simu hiyo. Madam S akarudi na kuichukua ile simu, “TSA
1…” akaita.
“HOT, kazi inaendelea, nimejificha katika kijiji cha Al Haram
kwa marafiki wa Langley. Nipo na Jamila…. Jamila amenipa taarifa
nyingine za siri sana ambazo nitazituma kwako leo hii… kwa
kifupi, nimeumia mguu, nimepata majeraha na usiku huu
ninaondoka na Jamila kuelekea Kashmir ambako Pegan Box lipo.
Mtuombee hatujui kama tutafika salama, maana inabidi tukatishe
jangwa lenye wagambo wakali wasiojua suluhu… ninatafutwa kila
kona,” Amata akaongea.
Madam S akashusha pumzi, “unaweza kupambana na maumivu
hayo?” akamuuliza.
“Bila shaka… nitapambana nao… wasiwasi wangu ni muda.
Kama kule Kashmiri wakijua kilichotokea Islamabad, basi kwa
vyovyote watahamisha box… lazima nicheze na muda. Ila kazi ni
nzito inayonikabili… hawa jamaa hawajui suluhu wanajua kuua tu.
Hata kumpata Jamila ilikuwa ni sawa na kutupa jiwe gizani. Sasa
hatujui kama wale kepteni wengine wapo hai au la!” Amata
akaeleza. Ukimya ukatawala kwa jozi la sekunde “unahitaji msaada?
Au nikutakie kazi njema!” akamtania.
“Wewe wajua….”
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Hahaha haya, mi naenda Kilimanjaro square, napeleka orodha


chafu… kazi huku imekamilika…”
“Sawa,” Amata akajibu. Wakaagana na ile simu ikakatika.
Madam S akaondoka zake.
Ndani ya gari lake alikuwa peke yake akiendesha kwa mwendo wa
kasi kuelekea Kigamboni. Kwa kuwa safari yake ilikuwa ya kwenda
Ikulu aliona kuwa hiyo ndiyo ilikuwa njia pekee ya kufika kwa
urahisi.
Katika eneo la karibu kabisa na kivuko, magari mengi
yalikuwa yakisubiri kuvuka ili kufika upande wa pili.
Yaliporuhusiwa yakaingia kwenye pantoni hicho. Madam S
alipotaka kuingiza gari akapewa ishara kuwa asubiri. Dakika kumi
baadae kivuko kingine kikubwa kiliwasili na gari la Madam S likawa
la kwanza kuingia na kusimama mbele kabisa. Nyuma yake
kulikuwa na gari la jeshi na mengine. Safari ikaanza, kuvuka
kwenda ng'ambo. Walipofika katikati ya maji, ghafla lile gari la
jeshi. Likatoka pale lilipo na kuligonga gari la Madam S na
kulisukumia majini. Kelele za wananchi kwenye pantoni hiyo
zilitaradadi.
Madam S hakutegemea, kishindo kile nyuma yake kikamshtua,
alipogeuka akajikuta tayari gari lake linaelea majini na kuanza
kuzama taratibu. Kila alipojitahidi kufungua mkanda ilishindikana.
Maji yakaingia kupitia kioo kilichokuwa wazi. Akavuta pumzi
nyingi na kuzibana. Mbinu za kukaa majini alizojifunza katika
medani za kivita. Gari lile lilipozama akatumia pumzi hiyo kidogo
kupumua.
Katika kivuko kile, mara tu lile gari lilipozama, mtu mmoja
alionekana akiruka kutoka sehemu ya juu kabisa ya pantoni na
kutua majini. Mbizi ndicho kilichofuata.

* * * *

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Huko Al Haram, usiku wa Siku hiyohiyo Amata na Jamila


waliondoka na lile Jeep kuelekea Jammu na Kashmir ambako
ndiko haswa ndege ile iliangushiwa. Safari ilikuwa ndefu, ukimya
ulitawala. Zaidi ya sauti tulivu ya muziki wa reggae uliosikika humo
ndani hakukuwa na kingine.
Jamila alikuwa akimtazama kijana huyo kwa kuibia na kurudisha
macho mbele kila alipogundua amegundulika. “Hivi ni kweli niko
na Amata au?” akauliza.
“We unaonaje?”
“Siamini… kwanza siamini kama Amata anaexist duniani, mi
najua ni kazi za kubuni tu,” Jamila akasema.
“Ok! Utaamini tu…”
“Sijaona makeke yake ndo maana!” akaendelea kuzungumza.
“Muda utafika…” Amata akajibu huku like Jeep likiendelea
kutimua vumbi na kulikata jangwa kuelekea Kashmir. Kamanda
Amata hakuwahi kufikiri kama ipo Siku atakuja kupambana na
watu wa jamii hii ambao kila siku wanaonekana kwenye luninga
wakijilipua ovyo, na kuwanyima watu amani ya kuishi na
kadhalika.
“Umewahi kufika Kashmir?” Jamila akuliza.
“Hapana ni mara yangu ya kwanza…”
“Mbona unaendesha gari kama unapajua unapokwenda,”
“Ni moja ya kazi yangu kwenda kwa uhakika nisipopajua…”
“Mh! Nikisikia tu Kashmiri mwili unasisimka… sipajui vizuri,
ila panatisha… sijui kwa nini wanapiganapigana!”
“Migogoro ya muda mrefu na haitaweza kwisha kwa sasa,”
Amata akamwambia Jamila.
“Inaonekana unajua mengi Amata,”
“Moja ya kazi yangu…”
“Niambie kidogo na mimi nipafahamu,” Jamila akaongea kwa
deko huku kichwa chake akikilaza begani mwa Amata.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Msemo mmoja ya Wahindi wekundu unasema ‘Ukiona


samaki wawili wanapigana mtoni basi ujue Mwingereza kwenye miguu mirefu
amepita eneo hilo muda si mrefu’. Kashmir ni mji mdogo katikati ya
Pakistani na India unaogombaniwa na mataifa hayo mawili tangu
Waingereza walipoondoka na kuliacha koloni hilo. Uingereza
ilipoliacha koloni hilo ililiacha na mgogoro ili makusudi wapate njia
ya kuliingilia tena. Miaka ya nyuma ya 1857 eneo hilo lilitawaliwa
na masultani wa Kituruki ambao utawala huo uliangushwa na
Waingereza wakati wa utawala wa Sultani Babur Shah na kulifanya
bara Hindi kutwaliwa na Waingereza. Wahindi ambao kwa mamia
ya miaka walikuwa wakiishi pamoja wakiwa na dini Moja, kabila
moja, na lugha yao binafsi bila kubaguana. Baada ya miaka tisini
bara hilo likagawanywa, kwanza Mara mbili, baadae Mara tatu,
yaani India, Pakistan na Bangladesh na Kiingereza kuwa lugha
rasmi inayozungumzwa katika nchi hizo.
Mwaka 1947 India na Pakistan zilipopata uhuru maeneo yote
yaliyokuwa yakikaliwa na Waislamu wengi yakakabidhiwa kwa
Pakistan na Yale yanayokaliwa na Wahindu wengi yalikabidhiwa
kwa India. Kosa walilolifanya Waingereza au makusudi, labda, ni
kuliacha eneo la Kashmir lililokaliwa na waislamu wachache kaika
mikono ya wenyeji yaani Wakashmir wenyewe. Uamuzi huo wa
Uingereza ndicho chanzo cha mgogoro wa eneo hilo. Mapigano,
kutokuelewana na umwagaji damu ndiyo yamekuwa maisha yao
mpaka sasa. Mwaka 1947 ilipopigwa kura ya maoni kwamba eneo
hilo liwe upande gani, wenyeji waliamua Kashmir iwe chini ya
Pakistan lakini mtawala wa eneo hilo wakati huo ambaye alikuwa
Muhindu, Mihrace Hari Singh, aliamua Kashmir iwe chini ya India.
Hapo ndipo vurugu ilipoanza. Mtawala huyo akaomba msaada
kutoka India. Majeshi ya India yakaingia Kashmir. Kwa kitendo
hicho na majeshi ya Pakistan yakaingia Kashmir. Na hapo ndipo
vita ya kwanza baina ya mataifa hayo ilipoanza na kujenga
mgogoro wa kugombea eneo mpaka sasa,” akamaliza kumsimulia,
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

lakini akashangaa ukimya uliotawala. alipomtazama Jamila, amelala.


Akamfinya pajani. Jamila akashtuka na kumtazama kijana huyo.
Alipogeuka mbele akakutana na kibao kilichoandikwa ‘STOP-
Jangul Check Point’. Maandishi hayo yalimfanya Jamila ashtuke.
“Vipi?” Amata akauliza.
“Hapa nilileta kizaazaa, sijui kama hawatanikumbuka…”
“Tulia!” Amata akamwambia Jamila. Lile Jeep likasogea
kabisa karibu na lango. Askari mmoja akajitokeza, kifuani mwake
akiwa na bunduki kubwa ya kivita ya AK47. Amata akatulia kimya
akimtazama yule askari.
“Passport!” yule askari akasema. Amata akaingiza mkono
mfukoni na kutoa bahasha, akamkabidhi. Yule askari akaifungua na
kukutana na noti za Kimarekani zilizojipanga vyema. Akakenua.
Pesa sabuni ya roho. Akavuta hatua na kufungua geti, akawaruhusu
kupita.

* * * *

Ilikuwa shida kwa Madam S. Pumzi ilimwishia, milango ya


gari ilijifunga, haikuwezekana kufunguka. Hatari. Chiba tayari
alikuwa ndani ya maji. Alijirusha kutoka juu kabisa ya pantoni ile na
kuzama majini. Akaogelea mpaka alipolikuta lile gari. Akafyatua
loki kwa namna ya kushangaza mlango kutoka katika dirisha lililo
wazi. Madam S hakukumbuka kabisa kuwa dirisha lile liko wazi
kutokana na mazingira yaliyomzunguka.
Chiba, akafungua mlango kwa tabu na kuukata mkanda kwa
kisu kilichokuwa kiunoni mwake. Akamtoa Madam S. Akalikamata
lile gari sawia na kulifuata tairi la mbele. Akafyatua nali ya upepo
kwa kuibana vizuri kwa vidole vyake. Akampa ishara Madam S
kutumia hewa iliyopo kwenye tairi hilo kupata oksijeni. Wakafanya
hivyo kwa zamu na kupata ahuweni.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Chiba alipopata nguvu na kuhakikisha Madam S yuko sawa,


wakaliacha lile gari na kuanza kukata maji kuogelea. Sambamba
kabisa na Madam S aliyekuwa mahiri kwenye fani hiyo. Dakika
kumi na tatu walifika katika kituo cha polisi cha wanamaji kilicho
mkabala na Ikulu ya Dar es salaam.
Chiba na Madam S wakapokelewa na konstebo aliyekuwa zamu.
Akawaweka kwenye chumba maalum kinachotengeneza joto.
“Nini kimekukuta?” Chiba akamuuliza Madam S aliyekuwa
akipumua kwa nguvu.
“Nimejikuta tu nagongwa na gari la jeshi likanisumia majini,”
akajibu huku bado akipumua kwa nguvu.
“Pole… ajali za kawaida…”
“Sidhani…. Lakini nashukuru kwa kunisaidia”
“Ndiyo wajibu wangu!”
Chiba alijibu huku akijiinamia kuvuta kumbukumbu ya
kilichotokea. Daima huwa hawamuachi Madam S kutembea peke
yake kila alipotoka ofisini, si katika gari lake bali katika gari jingine.
Walinzi wake daima walikuwa Scoba na Chiba kadiri ya upatikanaji
wao.
Nusu saa baadae, Madam S alikuwa tayari Ofisi ndogo, ndani
ya mavazi mengine. Kila kitu kilikuwapo katika ofisi hiyo. Chiba
naye alikuwa katika suti nyingine maridadi kabisa. Madam S
akamtazama kijana huyo akiwa nadhifu kuliko awali.
“Umekuwa kama mcheza kamali…”
“Mpaka hapa nimeshacheza kamali…” Chiba akajibu. Madam
S akamkabidhi kabrasha lingine, “tayari nimeshaprinti dokument
nyingine. Twende, we ndiyo bodyguard wangu leo,” akamwambia.
“Sawa, ngoja niweke ndevu za bandia” Chiba akaingia katika
chumba kingine na alipotoka alikuwa na ndevu na masharafa huku
ngozi yake ikiwa na makunyanzi usoni. Alionekana kama mtu
mzima sana wa miaka kati ya sitini na sabini. Safari ikaanza. Wakati
haya yote yanafanyika kule kivukoni harakati za kumtafuta
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

aliyekuwa ndani ya gari lile ziliendelea. Wanajeshi wa jeshi la maji


walipiga mbizi kwa amri ya mkuu wao wakitakiwa kumuopoa mtu
huyo na kumfikisha katika kituo cha afya cha jeshi hilo pale
Kigamboni.
Majibu yaliyoletwa na vijana hao, hayakuridhisha, “hakuna
mtu zaidi ni hiki kiatu chake tu,” mmoja wa wale vijana aliyekuwa
akiongoza wenzake akatoa jibu.
“Haiwzekani, mmeangalia vizuri?” kiongozi wao akauliza.
“Ndiyo afande, tumezunguka kilomita moja ya mraba lakini
hatujamuona mtu yeyote…”. Mshangao.
Kapotelea wapi? Yule afande mwenye cheo cha luteni usu
akajiuliza. Likafanyika zoezi jingine la kupiga mbizi kutafuta vizuri.
Dakika thelathini ziliisha. Wakaibuka na jibu lilelile. Wakakubali
matokeo. Kilichoendelea ni kuliibua gari lile.

* * * *

Mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Madam


S alikabidhi kabrasha lenye majina ya wanaosadikiwa kufanya
hujuma ile ya uangushaji wa ndegevita ya jeshi na kuiba mfumo wa
usalama anga wa kisasa. Majina hayo yalikuwa ya watu ndani ya
jeshi na raia. Mkuu wa nchi akalitazama lile kabrasha lililoadikwa
juu ‘Operesheni Kashmir’.
“Nitawashughulikia…” akamwambia Madam S na kumpa
mkono. Kisha akatoa taarifa ya operesheni inayoendelea huko
Kashmir. Rais aliipokea kwa furaha na kumtaka Madam S kusonga
mbele bila kuogopa. Macho ya mkuu wa nchi yalikuwa
yakimtazama Madam S kwa udadisi sana kiasi kwamba
mwanamama huyo akatia shaka na tazamo hilo.
“Vipi Mkuu, kuna tatizo?” akamuuliza.
“Hapana, kuna mambo tu yananichanganya… anyway
nitakutafuta wakati mwingine,” akasema na kuagana nao.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Ndani ya gari walilokuja nalo, Madam S akiwa nyuma ya


usukani akageuka kumtazama Chiba, “sometime simwelewi
mkuu!” akamwambia. Chiba akatulia kwanza kabla ya kujibu,
“nimeona lile jicho… nisingeshtuka kama lingekuwa la mahaba,
lakini ni la mashaka, lina wasiwasi na kitu Fulani,” akamjibu.
“Kuna jambo, lazima tuwe makini…”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

11
KAMANDA Amata na Jamila walifika katika mji wa Ramban
alfajiri ya siku hiyo. Hapo hawakukaa bali safari iliendelea kuelekea
Jammu mpaka Kashmir. Jua lilipoanza kupanda, tayari lile jeep
lililowabeba Amata na Jamila lilikuwa kwenye mlima wa mwisho
kuteremkia kwenye bonde lile. Tayari jangwa walikwishaliacha
nyuma na sasa walikuwa kwenye uwanda wa mipunga na uoto wa
nyasi fupi za asili. Kijani kilichotanda huku na kule kilipendezesha
uwanda wote wa bonde hilo. Amata aliegesha gari pembeni na
kuteremka. Jamila naye akafuata.
Katika ukingo wa mlima ule Kamanda Amata alitazama
bondeni na kuuona mji huo wa Kashmir. Nyumba nyingi kubwa
na ndogo, nzuri kwa mbovu zikiwa zimetapakaa. Hali hiyo iliweza
kuleta maana ya moja kwa moja juu ya maisha halisi ya wakazi wa
eneo hilo.
“Ndege iliangukia wapi?” Amata akauliza.
“Siwezi kukumbuka… ila ni jangwani, hakukuwa na hata
nyasi moja kwa jinsi nilivyoliona eneo hilo toka juu…” Jamila
akaeleza huku mkono wake wa kuume ukiwa juu ya bega la
Amata.
“Tutawezaje kujificha katika jiji hilo tusijulikane?” Amata
akauliza.
“Mtihani… tufike tutajua hukohuko”
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Amata akamtazama Jamila, akatikisa kichwa kushoto kulia


kwa jinsi mwanamke huyo alivyojiachia kwa kukilaza kichwa chake
begani kwa nwanaume huyo.
“Twende!” Amata akamwambia Jamila. Wakaingia garini na
kuanza kuuteremka ule mlima. Kilomita kadhaa kabla ya kuingia
katika mji huo walishuhudia moshi mzito angani. Kelele za watu
zikasikika kwa mbali. Akaendelea kubadili gia na kuteremka ule
mlima mpaka alipoanza kuzifikia nyumba za wakazi wa mji huo.
Vishindo vya mabomu ya machozi na risasi zilizokuwa zikipigwa
hewani ziliwakaribisha. Akaingiza gari katika kituo cha mafuta na
kuliegesha. Akateremka yeye na Jamila.
“Kuna hoteli hapa jirani?” Amata akauliza.
“Ndiyo, lakini mji umechafuka huwezi kusonga mbele…”
kijana aliyekuwa mhudumu wa kituo hicho alimjibu Amata.
“Kuna nini?”
“Maandamano makubwa sana huko,”
“Wanataka nini?”
“Oh aisee hili eneo letu ni tata sana, Kashmir haijulikani ni
mali ya nani… sisi Wakashmir sisi tunataka hili eneo liwe huru…
sasa India wanataka, Pakistani wanataka, ni vurugu tu… tunadai
haki za msingi!”
“Poleni sana!” Amata akamwambia, “Umesema hoteli ipo
upande gani?”
“Ukitoka hapa, barabara ile paleee kunja kushoto utaingia
katikati ya mji huo. Mbele yako tu utaona kibao Jammujah Hotel”
akapewa maelekezo. Kamanda Amata akamshika mkono Jamila,
wakaanza kutembea haraka haraka. Barabara ile iliyopita katikati ya
ule mji ilijaa watu wanaokimbia huku na kule. Mabomu ya machozi
yalionekana yakianguka huku na huko. Akina mama, vijana,
watoto, wote walizagaa barabarani. Amata alitumia nafasi na
upenyo wa vurugu hizo.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

‘Free Kashmir’,
‘Kashmir is our home’,
‘Bring back our homeland’

Yalikuwa mabango machache kati ya mengi ambayo wananchi


hao waliyanyanyua. Ilikuwa ni vuta nikuvute ya hali ya juu. Miili
kadhaa ilikuwa chin, barabarani, haina uhai. Askari wale hawakujali,
walifanya kila wanaloweza kutuliza fujo zile. Wananchi nao
hawakukubali, vifo vya ndugu zao viliwafanya wawe majasiri zaidi.
Amata na Jamila walifanikiwa kufika katika ile hoteli ya
Jammujah. Wakaingia ndani ya mapokezi wakihema. Watu walijaa
katika eneo hilo la mapokezi lakini wao hawakujali. Walijipenyeza
na kulifikia dawati la mapokezi hayo. Wakaomba kupata chumba
na kufanikiwa. Amata na Jamila wakapanda ngazi na kuifikia
ghorofa ya tatu. Wakaingia katika chumba walicholipia. Jamila
hakuwa na simile, alipofika tu akajitupa kitandani mzima mzima.
“Tungepata taabu sana kufika hapa kama mitaa ingekuwa
tulivu” Amata akamwambia Jamila wakati akijitupa kitini.
“Tuwashukuru walioanzisa maandamano…” Jamila akajibu.
“Nawaza, sasa hapa tunaanzia wapi…” Amata akasema.
Jamila akaingiza mkono wake sehemu fulani ya nguo zake na
kutoka kidubwasha kidogo kama rimoti, akampatia Amata.
“Nini hiki?” akauliza.
“Hicho ndicho kitatupa uelekeo wa wapi tunatakiwa kwenda”
Jamila akamwambia Amata.
“Kivipi?” akauliza. Jamila akajiinua kitandani na kuelekea pale
alipoketi kijana huyo na kukichukua tena mkononi mwake tayari
kumuelekeza.

* * * *

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Huyu jamaa keshakuwa mwiba kwetu, kaharibu mipango


yetu sasa hivi” Fernandez akamweleza Mansoor walipokuwa
kwenye kikao chao cha siri hapo katika kasri la tajiri huyo. “cha
kufanya ni kwamba hili sanduku lisikae hapa, ili hata akivamia tuwe
tumesevu kitu,” akamalizia.
“Hawezi kufika hapa akiwa hai…. Kila kona nimeweka watu
tena wenye weledi wa juu, akiingia tu hapa Kashmir atajulikana, na
akishajulikana tu hatoliona jua…” Mansoor akamtoa shaka
Fernandez. Mvenezuela huyo akatulia kimya kabisa akitafakari
jambo.
“Umepanga watu wako kuanzia wapi?” akauliza Fernandez.
“Siri za usalama hutakiwi kuzijua” Mansoor akajibu. “We
elewa kwamba huyo mshenzi kamuweza Kahir peke yake… ila
hapa atagonga ukuta. Namsubiri hapahapa nilipoketi. Akifanikiwa
kuliona jua la kesho basi atachinjiwa hapa mbele yangu” Mansoor
akatema cheche.
Fernandez akaingiza mkono katika mfuko wa koti lake, akatoa
karatasi mbili na kumpatia.
“Nini hiki?”
“Mjue unayepambana naye…”
Mansoor akazichukua zile karatasi kwa mtindo wa kupora na
kuzipekua kwa fujo. Akasoma harakaharaka na kuwapa vijana
wake.
“Akifika tu Kashmir nitajua, hakuna hoteli wala mgahawa
ambao sijaweka jicho langu…” Mansoor akamsisitizia Fernandez.
“Ok, kama unajihakikishia hilo unafanya vyema… sasa
kuhusu code ya tatu inakuwaje?” Fernandez akageuza mada.
“Itapatikana tu, vijana wameshaenda kwenye kambi ya Kahir
hukohuko ilikohifadhiwa…”.
Wakati wawili hao wakiongea, mmoja wa walinzi wa Mansoor
alikuwa bado akiitazama ile karatasi. Akaishusha taratibu na
kumtazama bosi wake.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Boss, kama huyu ndiye tunayepambana naye….


Amekwishafika hapa Kashmir” akamwambia.
“Unasemeje we bwege!” Mansoor akashangaa kwa
analoambiwa.
“Nasema kama huyu ndiye, basi keshafika Kashmir. Tena
yupo yeye na mwanamke mmoja…”
“Umewaona wapi?”
“Nilipoenda kushuhudia maandamano kama ulivyonituma
nilimwona mtu huyu akipita katikati ya watu pamoja na huyo
mwanamke, wameingia Jammujah Hotel…”
Baridi yabisi ikapita kwenye mifupa ya Mansoor. Fernandez
akamtazama kwa chati. “Nilikwambia…. Huyu mtu si wa
kucheza naye… si ajabu hapa tunapoongea keshafika kwenye
uwa wa jumba lako…”
Mansoor akamgeukia Fernandez baada ya kuisikia ile kauli,
“chunga kauli…” akamuonya. Kisha akamtazama yule aliyempa ile
taarifa,“una uhakika?” akamuliza.
“Ndiyo”.
“Siku zote usipuuze vitu unavyoviona vidogo… maana
vidogo ndivyo vyenye madhara makubwa” Fernandez
akamwambia Mansoor. Tajiri kijana, Mansoor akageuka taratibu na
kumtazama mteja wake, “tunafanyaje sasa… kama mtu keshaingia
kwenye himaya yetu bila kujulikana anaweza kuleta madhara
zaidi…”
“Nashukuru kwa kulitambua hilo, nakusikiliza…”
“Tulipanga kumnunua…”
“Inawezekana. Tunampata vipi?”
“Tunamwalika hapahapa aje, akileta jeuri anachinjwa!”
Mansoor akasisitiza. Bila kuchelewa akampa maagizo mmoja wa
vijana wake kufanya mawasiliano na hoteli hiyo kujua kama kweli
wageni hao wapo hapo. Akapewa jibu linalofanana na alilolitaka.
Kuwa wapo wageni mke na mume waliofika hapo, Waafrika
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

wametokea Nigeria. Mansoor akamtazama Fernandez. “Ndiyo


haohao, kamwe hawawezi kujitambulisha kwa utambulisho wao
sahihi…” Fernandez akaongeza kusema.
Mansoor akawapa maagizo vijana wake, waende Hoteli ya
Jammujah wakawachukue na kuwaleta hapo. Tajiri huyo akaandika
waraka maalumu wa mwaliko.

* * * *

Katika hoteli ya Jammujah, Jamila na Amata alikuwa


wametulia chumbani kwao. Mwanajeshi yule wa kike akiwa anatoa
maelekezo kwa Amata kuhusiana na ilr flashi.
“Hii inaitwa Pegan Flash… nikiiwasha basi kama mtambo wa
rada wa jeshi upo hai itapeleka signal ya mahali nilipo au pegan box
ilipo,” Jamila akamweleza Amata.
“Kwa hiyo ukiiwasha sasa itatuonesha Pegan Box lilipo?”
“Ndiyo! Ila bahati mbaya imekwisha chaji…”
“Oh! Hatuna bahati, inatumia waya gani?” Amata akahoji.
“Haitumii waya, ina kibweta chake unaipachika inachaji…
tazama…” akamweleza na kumwonesha ilivyo. Amata
akaigeuzageuza na kuitua mezani. “Tutaifanyia modification, itapata
chaji na itatusaidia. Kumbuka hapa Kashmir hatuna muda wa
kupoteza… ndani ya saa ishirini na nne tujue mbichi na mbivu,”
Amata akaeleza.
“Sawa baba!” Jamila akajibu.
Wakiwa katika mazungumzo hayo, simu ya chumbani ikaita
Amata akaipokea na kuiweka sikioni.
“Kuna wageni wako hapa mapokezi wanahitaji kukuona…”
simu ile ikampa taarifa. Amata akamtazama Jamila.
“Tuna ugeni!”
Ugeni ugenini? Jamila akajiuliza, kisha akamtazama Amata.
Mshangao ule uilikuwa na ujumbe ‘ugeni! Nani anatujua?’. Amata
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

alielewa. Akaitua ile simu mahali pake na kutulia kimya kwa


sekunde kadhaa.
“Tumesajulikana, hatuna budi kukubaliana na linalotukia…”
Amata akaeleza.
“Unamaanisha nini?” Jamila Akataka kujua, akauiliza kwa
wahka.
“Wakati mwingine sisi, kutokana na kazi zetu, inabidi ujitoe
sadaka, unajiingiza katika mikono ya adui makusudi ili upate
matokeo chanya…”
“Na ukifa,je?”
“Kifo ni sehemu ya kazi yetu, jasusi kufa kazini ni sehemu ya
kazi…”
“Mh!”
Amata akamgeukia Jamila, akauona wazi uoga wake,
akamkumbatia na kumweka kwenye kifua chake, mwanamke huyo
akatulia kama mtoto atuliavyo kifuani mwa mama yake. “Kwa hiyo
huko ni mawili… kufa au kupona!” akasema mwanamke huyo.
“Kufa ni asilimia kumi na kupona ni tisini…”
“Unaniaminisa kuwa tutarudi na roho zetu?” Jamila akauliza
huku akitabasamu.
“Bila shaka…” Amata akajibu huku akiuendea mlango wa
chumba kile tayari kuteremka chini, mapokezi. Jamila akamfuata.
Wakiwa katika ngazi kuelekea chini, Amata akasimama na
kumtazama mwanamke huyo, “hakuna jeshi imara kama la
Tanzania katika ukanda wa Afrika, unajua hilo?”
“Ndiyo!” Jamila akajibu.
“Basi wewe ni mmoja wa wanajeshi wanaounda jeshi hilo,
hivyo uimara na ujasiri wako wa kijeshi lazima uuoneshe.
Itakapobidi, lazima tuanzishe vita, tumia silaha, tumia mikono
pambana na adui. Kuanzia sasa, jione upo peke yako na unataka
kuwaokoa kaka zako,” akamtia moyo.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Wawili hao, hawakuwa na kitu zaidi ya bastola moja


aliyokuwa nayo Amata na funguo za lile gari. Jamila alikuwa na
Pegan Flash basi. Walipofika mapokezi wakapokelewa na kijana
mmoja shababi aliyevalia vazi la kipunjabi. Mustachi wake uliomea
vizuri ulisokotwa upande huu na ule mwingine na kumfanya
aonekane kama askari wa kikoloni wa Mjerumani. Yule kijana
hakuongea neno, alimkabidhi Amata bahasha. Amata akaichana na
kutoa kadi ngumu ndani yake, akaisoma.

‘Nakualika rafiki,
uje katika himaya yangu japo kunisalimu na
kufurahia pamoja nami chakula cha jioni ya leo…
kuna jambo la kuzungumza nawe…

Wasalaam Mansoor!’

Ujumbe ule ulikuwa umeandikwa kwa Kiingereza


kisichonyooka. Amata akausoma na kuuelewa maana yake ya
ndani. Akampa Jamila karatasi ile. Naye akaisoma na kuirejesha
kwa Amata. Yeye akaitia mfukoni.
Yule kijana akatoka, Amata akakabidhi funguo za gari pale
mapokezi, wakatoka. Nje tu ya hoteli hiyo palikuwa na Landrover
110 likiwasubiri. Ndani kulikuwa na dereva na mtu mwingine
kwenye kiti cha abiria. Wakaingia kiti cha nyuma na kuketi, safari
ikaanza.
Iliwachukua dakika arobaini na tano kufika katikati ya bonde
la Kashmir. Amata alishuhudia jumba kubwa la kisasa, barabara
ndefu ya kutua ndege na ndege moja kubwa la mizigo aina ya
Antonov limeegeshwa kando. Kila upande kulikuwa vumbi tupu.
Milima ya mkusanyiko wa vumbi huku na kule ililifanya jumba lile
lisionekane kirahisi.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Lile landrover liliendelea kupasua jangwa kuielekea ile


nyumba. Kimya. Hakuna mtu aliyekuwa akiongea safari nzima.
Amata alikuwa akiwatazama wale vijana kwa hesabu kali, na wao
wakifanya hivyohivyo. Katika maegesho ya jumba lile walipokelewa
na mwanadada mrembo sana. Aliyevalia suti ya kike ya Kichina.
Pembeni yake palikuwa na kijana mwingine nadhifu aliyeshika kitu
kama sahani mkononi mwake. Mara tu walipoikanyaga ile ardhi,
yule mwanadada akawasalimu na kuwakaribisha. Kabla hawajavuta
hatua, yule kijana alifika na kumwonesha ile sahani Amata.
Alielewa. Akachomoa bastola take na kuiweka juu ya chombo
hicho. Kisha wakafuatana ndani.

* * * *

“Unamwona Amata?” Madam S akamuuliza Chiba


aliyetingwa na kompyuta yake.
“Naendelea kumtafuta, signal iko chini sana,” Chiba akajibu.
“Ok… maana kuna mambo siyaelewi hapa, nisije kumtoa
kafara kijana wangu bila sababu…”
“Madam! Kwa nini unasema hivyo? Kuna jambo umehisi?”
“Tena zito, naomba Mungu afanikishe kazi hii…”
“Atafanikisha tu!” Chiba akamtoa hofu bosi wake.
Siku hii ilikuwa nzito sana kwa Madam S. Mara tu alipoingia
ofisini aliitwa na Mkuu wa Nchi kwa mkutano wa siri wa kuijadili
taarifa aliyompatia jana yake. Siku hii aliingia ofisini kwa
kuchelewa. Mpaka saa sita mchana bado alikuwa hajaripoti. Kati ya
familia ya TSA hakuna hata mmoja aliyejisugulisha kumtafuta, kwa
kuwa walishazoea kuwa si mara zote mwanamke huyo huingia saa
mbili asubuhi. Na hii hutokana na uwajibikaji wake.
“Jana usiku,nyumba yangu ilivamiwa” Madam S akamwambia
Chiba. Taarifa hii ilimshtua kidogo kijana huyu.
“Ilivamiwa?” akauliza.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Usiku wa saa nane, kuliegeshwa gari Subaru Forester


jekundu mita chache kutoka getini kwangu…” Taarifa ile
ikamfanya Chiba kuacha kile anachokifanya na kutega sikio,
“Ulijuaje kama ni wageni wako?”
“Aaaaa Chiba! We mtu anayekutembelea humjui? Mi wale
niliwajua…lile gari limeipita nyumba yangu mara sita mchana na
mara tatu usiku” Madam S akaeleza. Hayo yote aliyajua kutokana
na mfumo wa kamera za siri za usalama zilizoizunguka nyumba
yake. Kamera hizo hutunza kumbukumbu na ukizitaka zikupe
taarifa ya Siku zitakuorodheshea kama ni magari basi yamepita
mangapi na lipi limepita mara nyingi. Na watu vivyo hivyo.
“Wanakutafuta, wamekukosa pale Kivukoni… Kwa hili
naona wazi kuwa hii ishu mzizi mkuu upo hapa hapa nyumbani…”
Chiba akamwambia Madam S.
“Nimewaza hivyohivyo… Kuna watu wamenifuatilia sana
mchana, bahati mbaya au nzuri huyo mfuatiliaji ni bwege
nilimgundua mapema tu…” akamwambia Chiba, “Sasa unajua kwa
nini nimekuuliza kama unampata Amata?”
“Hapana!”
“Kuna ujumbe huu hapa,” akamsogezea simu, “nimeupokea
dakika kama ishirini kabla ya kufika hapa, mchana huu…”

‘Na huyo uliyemtuma Kashmir, tayari yupo mikononi mwetu…


huwezi kuzuia biashara za wakubwa!
Buriani bibi kizee!’

Ujumbe ule ulisomeka namna hiyo, namba ya mtumaji


haikuonekana. Chiba akaurudiarudia kuusoma. Alipoukinai akaitua
simu ile mezani na kuisukuma kwa mwenye nayo.
“Wangapi wanajua kama Amata yupo Kashmir?” Chiba
akauliza.
“Niliyempa taarifa hii ni Namba moja pekee…”
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Ok, naifikiri jibu umejipatia tayari… kama yeye alipopata


taarifa hii kutoka kwako kawapa wengine basi wigo wa adui wa
ndani unaongezeka…” akaeleza.
“Nimejiuliza sana…”
“Huna la kujiuliza, leo amekupokeaje ulipoenda huko?”
“Kwanini unauliza hivo?”
“Nataka kujua tu alikupokeaje… maana jana lile jicho
halikuwa la kawaida. Inaonekana kuna kitu anataraji na kinachokuja
mezani kwake ni tofauti,” Chiba akaeleza.
“Kuna jambo lilinishangaza… alikuwa akiumauma sana
maneno kama mtu asiyejiamini…”
“Basi! Inatosha… kuwa mwangalifu… namba moja anahusika
katika hicho unachonambia,”
“Sure?”
“Asilimia themanini…”

* * * *

“Mtapumzika kwenye chumba hiki hapa kabla hamjaonana na


mwenyeji wenu. Hapo ndani kuna kila kitu, mtaoga, mtafanya
mnachotaka lakini mjue kuwa mna dakika arobaini na tano za
kuonana naye. Muwe huru, hizo nguo ni kwa ajili yenu…” yule
mwanamke aliyewapokea Amata na Jamila aliwapa maelekezo kisha
akawaacha chumbani hapo na kuondoka zake. Jamila alivuta hatua
mpaka kwenye dirisha kubwa na kujaribu kusukuma kioo ili
atazame nje, hakuweza. Kioo kile kilikuwa kizito na kimefungwa
kabisa, hakitembei. Akasonya. Sonyo lile likamfanya Amata ageuke.
Akaivua miwani yake na kuiweka kando.
“Wanaona kila tunachofanya!” Amata akamwambia Jamila.
“Weeee!” Jamila akapigwa mshangao.
“Kawaida tu hiyo, usihofu. Wewe fanya kama hawakuoni
vile… twende tukaoge tujiandae kukutana na huyo mshenzi…”
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Si umesema wanatuona?”


“Ndiyo wanatuona… hatuna pa kujificha” Amata
akamwambia kwa msisitizo. Taratibu akaliondoa shati alilovaa na
kulitupa kando, akabaki kifua wazi. Dakika moja iliyofuata akaingia
maliwato. Huko kulikuwa na beseni kubwa la kuogea. Jamila
akaungana naye. Wote wawili wakatosha kwenye lile beseni huku
maji yenye umotomoto yakiwaficha usiri wa miili yao. Amata
akameza mate baada ya macho yake kuyaona kwa bahati mbaya
matiti ya mviringo ya Jamila. Ukimtazama Jamila unaweza kusema
ni kwanafunzi wa mwaka wa kwanza au wa pili wa Chuo Kikuu.
Akalisanifu umbo zuri na tamu la mwanamke huyo, mfupi,
kibonge wa wastani, aliyejaa vizuri hasa sehemu za chini ya kiuno.
Mwenye matiti mawili ya duara yaliyosimama vema na kutamanisha
kuyanyonya. Akampokea kwenye beseni, Jamila akapokeleka.

* * * *

Kila mmoja alikuwa tayari, nguo mpya kabisa walizozikuta


ndani ya hicho chumba, ziliwakaa vyema kana kwamba walifanyiwa
vipimo. Kengele ya mlango ikalia, Amata akaitazama saa yake,
ilikuwa ni dakika ya arobaini na tano. Akampa ishara Jamila.
Wakaufuata mlango na kutoka nje.
“Mnasubiriwa ukumbini…” mwanadada mwingine alikuja
kuwachukua. Wakamfuata.
Ilikuwa sebule kubwa ya kisasa, iliyosheheni samani za
gharama sana. Sakafu yake ilikuwa safi na ya kung'aa kama kioo.
Ukitembea unaweza kujiona. Katika sebule hii kulikuwa na mtu
mmoja tu, kijana mwenye mwonekano wa pesa. Mtemba wake
kinywani, ulifuka moshi, Suti yake ya gharama iliudhihirisha ukwasi
alo nao. Juu ya bega lake kulikuwa na mjusi wa thamani sana, mjusi
hai anayemetameta magamba ya mwili wake. Hili lilidhirisha wazi
aliye mbele yao ni mtu mwenye ukwasi kiasi gani.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Karibu sana bwana…” akasahau jina.


“Amata, Kamanda Amata…” akamsaidia kujibu. Yule jamaa
kawaonesha sehemu za kukaa, wakafanya hivyo.
Code namba 3 imekuja yenyewe! Mansoor akawaza. Amata
akageuka upande wa kulia wa sebule ile baada ya kusikia
muungurumo wa ndege.
“Usihofu, hapa tuna kila kitu… huyo anayetua sasa ni
swahiba wangu, mfanyabiashara… anakuja hapahapa…” Mansoor
akamwambia Amata. Kweli, dakika tano baadae, akaingia sebuleni
pale, mtu mmoja mwenye mwili wa wastani, kitambi cha kufutia
simu, cheni za gharama zilikuwa zikining'inia shingoni mwake.
Akaketi. Msichana mmoja wa kati ya miaka ishirini na ishirini na
tano, akaingia sebuleni hapo na chano iliyojaa pombe kali.
Akaweka mezani na kuwamiminia vibopa hao kwenye bilauri zao.
Alipokuja kwa Amata na Jamila akachukua chupa nyingine
kuwamiminia. Kamanda Amata akampa ishara kuwa hatumii kilevi.
“Karibu sana Amata… nimekuwa nikikutafuta siku nyingi
sana kijana!” Mansoor akaanzisha mazungumzo, “naitwa Mansoor,
mmiliki wa himaya hii iliyobarikiwa hadhi ya peponi…” akajisifu.
“Nashukuru kukufahamu,” Amata akajibu.
“Na huyu” akamwoneshea mkono Fernandez, “… anaitwa
Fernandez kutoka Venezuela… ni mteja wangu na ni tajiri mmiliki
wa visima vya mafuta huko Arabuni” akamtambulisha. Amata
akatikisa kichwa, ishara ya kukubali.
“Niambieni mlichoniitia, naamini kabisa kuwa hamkuniitia
utambulisho… na mimi kwangu muda ni mali kuliko pesa,” Amata
akawaambia.
“Amata… sisi kwanza tunakupongeza sana kwa kazi nzuri
uliyoifanya kule Islamabad”
“Kazi ipi?”
“Ya kumuua Kahir…”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Kahir hajafa… nilimzima tu basi… nahisi sasa atakuwa


kaamka…”.
Kauli hii ikawafanya Fernandez na Mansoor kutazamana.
“Yaani!” Mansoor akapigwa mshangao.
“Ulivyosikia ndivyo nilivyosema…”
“Anyway… sisi hatuna ubaya na wewe… lengo la kukuita
hapa ni biashara…”
“Biashara?”
“Ndiyo, biashara…” Fernandez akaingilia kati, Amata
akamtazama.
“Ipi?”
“Hiyo uliyokaa nayo!”
Amata akageuka kumtazama Jamila aliyekuwa kimya muda
wote. Akarudisha macho kwa jamaa hao, “sawa, mnanipa Dola
ngapi? Au mnanipa Bakari na Joel mi nawapa huyu, au mnanipa
Pegan Box mi nawapa huyu… sitaki pesa, nimeghairi…”
akawaambia.
“Unasema nini?” Mansoor akauliza.
“Hujasikia, nimesema, nimekuja hapa kufata vitu vitatu tu,
Pegan Box, na makepten wangu wawili…” Amata akawaeleza,
macho yake hayakuwa na hata chembe ya maskhara.
“Hapa hakuna Pegan Box…” Mansoor akajibu.
“Huwezi kunidanganya… nikiwa Tanzania nimeiona ishara
kuwa Pegan Box lipo hapa na ndiyo maana nimefika hapa…”
akang'aka.
“Hiyo jeuri yako itakwisha muda si mrefu…” Mansoor
akamwambia Amata. Mansoor akabofya kitufe kilicho pembeni
mwa kiti chake. Punde tu, vijana wanne wakaingia katika ile sebule.
“Waleteni wale mateka!” akawaambia. Wale vijana
wakaondoka na muda mfupi baadae wakarudi wakiwaburuza
Kapteni Joel na Kapteni Bakari, wakawabwaga sakafuni. Bakari na
Joel walikuwa wamedhoofika sana, wamekonda. Majeraha
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

yalionekana wazi miilini mwao. Jamila alipatwa na mshtuko,


akajikuta akivuta hatua kuwawahi pale chini, hakufika. Ngwala
Moja maridadi ikampeleka chini. Jamila alianguka vibaya sakafuni.
Amata hakuvumilia. Kwa kasi ya ajabu, alimpa pigo moja la
karate yule jamaa. Pigo lile likampeleka yule jamaa chini huku
mikono yake ikikishika kifua. Pigo lile kutoka kwa Amata liliharibu
mpangilio wa mifupa ya kifua cha yule mjinga. Akiwa pale chini
akajikuta anashindwa kupumua sawasawa, akaanza kukohoa damu.
Mansoor akamtazama Amata kwa jicho baya lililojaa hasira,
“una ujeuri gani wa kufanya jambo hili katika himaya yangu?”
akamuuliza Amata huku akimsogelea.
“Naye ana ujeuri gani wa kumfanyia mke wangu hicho
alichomfanyia?” Amata akajibu kijeuri.
“Meshak, Assad, mchukueni huyu mwanamke mumuhifadhi,
huyu bwege nipelekeeni kule kwenye chumba cha mkutano,
muwekeni tayari kwenye kiti chake, nakuja”. Wale vijana
wakamkamata Amata huku na huku na kuondoka naye wakati
Jamila naye akipelekwa upande mwingine.

* * * *
Mara baada ya Amata na Jamila kuondoshwa pale sebuleni,
Mansoor na Fernandez wakarudi vitini na kuketi. “Umefanya nini
sasa?” Fernandez akauliza.
“Tumeshapata code ya tatu, tatizo nini? Kinachofuata ni
kumtemesha tu huyo mwanamke aseme…” Mansoor akamjibu.
Fernandez akatulia kwa jozi la sekunde akitafakari halo nzima
ilivyoenda.
“Kwa hiyo nikuandalie pesa?” Fernandez akauliza.
“Yeah! Tutafanya muamala baadae…. Ngoja kwanza nikamtie
adabu huyu mwendawazimu” Mansoor akamwambia mgeni wake
huku akimalizia funda la pombe iliyobaki kwenye bilauri yake.
Mansoor alionekana wazi kuwa na hasira hasa kutokana na kitendo
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

alichokifanya Amata. Akainuka kutoka kitini. Fernandez


akamtazama swahiba wake, hakumuelewa hasa nini anachotaka
kufanya.
“Unataka kumfanya nini?”
“Namuua… kama ninachotaka, keshaleta” Mansoor akajibu
kwa jazba huku akisonga mbele. Fernandez akabaki kimya
akimtazama. Alipoondoka, naye akamfuata.
Katika kile chumba alichokipa jina ‘chumba cha mkutano’,
Mansoor na Fernandez walilakiwa na maiti mbili za wale vijana
waliomchukua Amata.
“Haaaaaah!” akapiga kelele. Hakuamini anachokiona.
“Hapa mambo yameshaharibika…. Lazima itafutwe njia ya
kulificha Pegan Box…” Fernandez akasisitiza. Mansoor akageuka na
kumtazama Fernandez.
“Acha uoga mwanaume…. Huyu mtu hatakiwi kutoka
hapa…” akajibu. Mansoor akainyakuwa simu iliyopachikwa
ukutani, akabofya namba kadhaa na kuiweka sikioni. Akaitoa na
kuitazama, akairudisha tena sikioni. Hakuna mawasiliano. Akaipiga
ukutani na kuivunja vipande vipande.
“Mshenzi amekata mawasiliano!” Mansoor akasema. Akatoka
kwenye kile chumba na kuelekea upande mwingine. Mbele
akakutana na mwili mwingine wa kijana wake.
“Aaaaaaaaaah!” akapiga kelele na kugeuka kurudi anakotoka.

* * * *

Kamanda Amata alikuwa chini baada ya kupokea kipigo cha


kushtukiza. Alipojaribu kuinuka bado akajikuta kadhibitiwa vilivyo.
“Umeua vijana wangu wanne! Lazima nikufundishe adabu”
sauti ya jamaa aliyemdhibiti Amata ikaunguruma.
Alikuwa mwanaume kwenye miraba minne. Mrefu na kwenye
nguvu. Pembeni yake palikuwa na vijana wengine wawili.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Akanyosha mkono na kupewa upanga mkali, makali kuwili. Wale


vijana wakamwinua Amata. Mara mlango wa eneo hilo
ukafunguliwa Mansoor akaingia pamoja na Fernandez.
“Umekamatika mshenzi wewe!” Mansoor akasema huku
akimwendea Amata pale chini, akapiga teke la mbavu na
kumporomoshea matusi ya nguoni. Mansoor akamnyang'anya
upanga yule jamaa mwenye miraba minne. Akainua juu na
kuuteremsha kukata kichwa cha Amata.
Kwa kasi isiyopimika, Amata akaepa lile pigo na kumpiga Mansoor
ngwala yenye hesabu nyingi.
Tajiri kijana akaenda chini mzimamzima huku ule upanga
ukimtoka mkononi. Amata akajirusha sarakasi na kuunyakuwa.
Jamaa mwenye miraba minne alikuwa tayari kumvamia, hatua zake
mbili akajikuta ana kwa ana na ncha ya upanga. Alipotaka kuleta
makeke yake. Kamanda Amata hakujiuliza mara mbili,
akamdidimiza upanga wa tumbo na kumsukuma kando kwa pigo
moja zito. Akawahi kuinuka na kusimama wima.
“Muueniii!!!” Mansoor akawakaripia vijana wake. Na wao
wasijihami, wakamvamia Amata. Pigo la kwanza lilipotua upande
wa nyuma wa shingo yule jamaa akaguna na kwenda chini. Pigo la
pili likamfikia kijana wa pili na kumpotezea fahamu. Akachomoa
bastola kutoka katika kiuno cha yule jamaa wa pili. Risasi moja
ikatawanya moyo wa kijana mwingine. Akamwachia huyu
aliyemshika akaanguka chini. Jicho likawa kwa Fernandez,
Mansoor hakuwepo.
Kamanda Amata akamtazama Fernandez aliyekuwa
akitetemeka kama mgonjwa wa homa anayepigwa na baridi kali.
Tajiri huyo alitamani kukimbia lakini ukuta ulimzuia. Mahali pale
alibaki yeye na Amata. Kila alipotazama sakafuni, alikutana na miili
isiyo na uhai.
“Ni-a-che… mimi si-hu-si-kkkki” Fernandez akaomba
msamaha kwa kitetemeshi.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Wewe hauhusiki?” Amata akauliza.


“Nddiiiyyooo!”
“Si wewe uliyemtuma Fareed na vibaraka wake kuja Tanzania
kutafuta kodi za Pegan Box?” Amata akauliza. Fernandez hakujibu,
mkojo ukatiririka. Amata akatamani kucheka lakini akakibana
kicheko chake. Kabla hajasema neno jingine, kishindo kikubwa
kikasikika nyuma yake. Amata akajitupa chini na kushuhudia
kipande cha ukuta kikianguka. Akajiviringa na kile kipande cha
ukuta kikamkosa na kumponda vibaya Fernandez. Mirindimo ya
risasi ikasikika. Amata akatambaa na kutoka katika kile chumba.
Alipojitokeza kwenye korido akashuhudia mtu mmoja aliyevalia
kijeshi akijitokeza kwenye mlango wa mbele. Amata hakujitikisa,
akalala sakafuni kimya, akimtazama mtu yule kwa Jicho la wizi.
Yule mgambo akasimama pale mlangoni, akatazama kushoto
na kulia. Bunduki kubwa iliyoshikwa kwa mikono yenye nguvu ya
mgambo yule ilikuwa tayari ikisubiri amri tu. Amata akampigia
hesabu yule mgambo akijua labda yupo peke yake. Yule mgambo
akanyoosha mkono wa kuume na vidole vyake viwili akavipunga
hewani. Kitendo kile Amata akakielewa vyema. Akatulia palepale
huku mbele yake sakafuni akikingwa na mwili mwingine usio na
uhai. Wakaingia wagambo wengine wawili wakapita mlango
mwingine. Wote hao walikuwa na bunduki kubwa zenye mkanda
uliojaa risasi. Wengine wawili wakaingia na kuelekea upande
mwingine. Kisha wawili wengine wakasimama katikati ya ile
korido. Kwa mwendo wa kunyata wakaanza kuelekea upande
uleule aliokuwapo Amata. Naye akatulia vilevile.
Wale wagambo wakamkaribia Amata. Mmoja wao
akamtazama pale chini alipolala, vumbi lililogubika mwili wake na
kuzifanya nguo zake kupoteza uhalisia wake zilimlaghai. Amata
Akabana pumzi na kujua lolote linaweza kutokea, akajiweka tayari.
Yule mgambo, akapita na kukiendea kile chumba kilichobomoka
upande mmoja. Yule wa pili akasimama jirani kabisa na alipolala
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Amata. Yule aliyekuwa kule mlangoni akawa ametingwa na


kuongea na simu yake ya upepo. Nukta chache tu, akarudi ndani ya
mlango aliotokea. Amata akapiga hesabu kali za shambulizi.
Ama zao, ama zangu! Akawaza.

* * * *
Jamila alifungiwa katika chumba kingine peke yake wakati Joel
na Bakari walitupwa katika chumba kilekile walichokuwamo tangu
awali. Hali ya makepeteni hao ilimtesa sana Jamila. Akaumiza
kichwa afanyeje aweze kuwaokoa, ilikuwa ngumu. Kichwani
mwake alikwishajua kuwa Kamanda Amata huko aliko atakuwa
keshaharibu hali ya hewa. Aliamini kuwa kijana huyo hasingeweza
kukubali kufa kijinga, lazima ajitetee. Alikizunguka kile chumba
huku na huku, akaujaribu mlango wake, akagundua umefungwa
kwa nje. Mlango wa chuma. Akakata tamaa. Akajipapasa kiunoni
mwake, akaichomoa ile pegan flash, akaitazama na kuiweka vizuri.
Jamila alihakikisha kidude hicho hakipotei. Akiwa katika kujiweka
vizuri ule mlango ukafunguliwa. Jamila akarudi nyuma na kuzuiwa
na ukuta. Wakaingia watu wawili waliokuwa wakiongea Kikurdu.
Wale jamaa walikuwa na shotgun kila mmoja. Wakamkamata
Jamila huku na huku na kutoka naye nje ya kile chumba.
Wakamkokota kwa nguvu huku mwenyewe akipinga kuchukuliwa
nao. Pamoja na kukuru-kakara zote hizo hakufanikiwa
kuwachomoka kwani mikono ya wale jamaa ilikuwa na nguvu
mithili ya vaisi.
Jamila akaingizwa katika chumba kingine, mandhali ya mule
ndani haikuwa ngeni kwake, alikikumbuka kwani ni kile
alichokaribishwa akiwa na Amata. Ndani ya chumba kile alimkuta
Mansoor na wanawake wale watatu. Juu ya Meza kulikuwa na like
sanduku la Pegan, mfumo wa kisasa wa usalama wa anga.
Pegan Box! Jamila akapigwa mshangao akawachomoka wale
vijana na kutaka kulivamia lile sanduku. Hakufanikiwa. Wale
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

wanawake watatu walikuwa wepesi kama unyoya. Walimuwahi na


kumdaka hata kabla hajafika pale mezani.
“Hahahahaaaa na wewe unataka kumuiga kaka yako?”
Mansoor akamuuliza Jamila, “blood fool, na huyo kaka yako sijui
hawara yako keshakufa… wewe na mimi sasa tunaelekea
Islamabad… kazi ya kufanya huko unaijua…” Mansoor
akamwambia kwa dharau. Jamila akamtemea mate tajiri huyo. Kofi
Kali likamtoka Mansoor na kutua shavuni pa Jamila.
‘Ding! dong!’ sauti kama ya kengele ya mlango ikasikika.
“Twendeni,” Mansoor akawaambia. Wale wanadada, mmoja
akabeba lile sanduku na wawili wakamkusanya Jamila na kuondoka.
“Hakikisheni huyu mshenzi hatoki humu ndani, na kichwa chake
na vya wale wawili nivikute kwenye friji…” akawaapa maagizo wale
jamaa.
Tayari katika ule uwanja wa ndege mdogo ulio mbele tu ya
kasri lile, iliegeshwa Jet binafsi tayari kuwabeba watu hao.

* * * *

Ndani ya lile jumba, yule mwanamgambo alipovuta hatua tu


kumruka Amata ili aende kwa mwenzake, akajikuta akipigwa
mtama mmoja kwa ufundi sana. Akanyanyuliwa juu na kutua
sakafuni kama mzigo. Amata akaiwahi ile bunduki na kuiweka
sawa. Yule mwenzake aliposikia kishindo akarudi haraka koridoni.
Alipojitokeza tu, Amata akamfumua kifua chake kwa risasi.
Akainuka haraka na kuingia mlango mwingine, akajibanza huko.
Sauti za watu waliokuwa wakiongeaongea zikasikika. Akawasubiri.
Mara zikapotea, Amata akajitokeza na kutembea taratibu mpaka
mlango wa chumba kingine, hakuna mtu. Akatoka kwa tahadhàri
na kuuelekea mlango mwingine. Hapo akasikia minong’ono ya
watu wakiongea. Akajipanga kuwavamia. Akasikiliza kwa makini,
walikuwa wawili.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Wanafanya nn? Akajiuliza. Akajitokeza ghafla na ile bunduki


ikakohoa bila huruma. Mmoja wao akaenda chini na yule mwingine
akavunjwa bega vibaya.
“Tulia hivyohivyo!” akamwambia, “mpo wangapi?”
“Sa-ba!” akajibu.
“Wapo wapi?”
Ghorofa ya chini! Akajibu kwa kuonesha kidole.
“Ndugu zangu wapo wapi?”
Ghorofa ya chini! Akajibu tena kwa ishara. Amata akamtaka
kuongoza njia huku mikonoye kisogoni. Wakatoka mpaka upande
wa chini. Yule mateka akamwonesha Amata mlango wa chuma,
uliofungwa madhubuti. Hakutaka kusumbuka, risasi moja tu
ikavunja kitasa. Amata akamsukumia yule jamaa ndani kisha na
yeye akaingia. Kilikuwa chumba kichafu, kinanuka uvundo wa
mchanganyiko wa uchafu. Alitamani kubana pua lakini
haikuwezekana. Aliwaona Joel na Bakari wakiwa sakafuni.
“Twendeni nyumbani” akawaambia. Joel akajitahidi kuinuka
na kufanikiwa. Bakari alikuwa hana nguvu kabisa. Siku walizokaa
humo bila kula ziliwadhoofisha watu hao. Amata akambeba Bakari
begani mwake, Joel akaichukua ile bunduki kubwa na kuikamata
mikononi mwake hata kama hakuwa na nguvu sawasawa. Jambo la
kwanza na hasira alizokuwa nazo, alimwagia risasi yule mateka wa
Amata na kumwacha amechakaa.
Wakatoka taratibu kuitafuta njia ya nje. Mvumo wa injini za
ndege ukamshtua Amata. Joel aliona mwili mmoja uliokuwa
umevaa mabomu ya kutupa kwa mikono, akatabasamu.
Akayachomoa, yalikuwa matano. Walipoupata mlango wa kutokea
nje ya jumba lile. Walishuhudia ile ndege ikiiacha ardhi na
kutokomea angani. Amata akatafuta eneo zuri na kuwaweka Joel na
Bakari.
“Yeyote atakayekusogelea mmalize,” Amata akamwambia
Joel, kisha yeye akarudi kwenye lile jumba. Hakutaka kuamini kama
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Jamila hayupo. Akaingia na kukifikia kila chumba, hakuona mtu


zaidi ya miili isiyo na uhai. Chumba kimoja kilichoonekana kuwa
cha siri sana kilimfurahisha. Chumba kile kilionekana kuwa ndicho
akitumiacho Mansoor. Akakipekuwa kila kona. Mungu si
Athumani na kila mtenda kazi hustahili ujira wake. Sefu lililojaa
noti lilimlaki. Halikufungwa. Dola,Paundi,Yeni, Yuri na nyingine
nyingine. Akavikusanya vile viburungutu na kuvifunga kwenye
foronya ya mto wa kulalia. Akatoka taratibu na kifurushi chake
mkononi. Alipofika mlangoni, lahaula! Hakuamini anachokiona.
Pegan Flash ilikuwa pale. Akaiokota na kuitia mfukoni. Akiwa katika
kufanya hilo akashuhudia vumbi likitimka upande wa barabara.
Wanakuja! Akawaza. Kwa haraka akakimbilia kule
alikowaacha Joel na Bakari. Alipofika akamkuta Joel akiwa kakosa
utulivu. Macho yake yalitona kwa machozi. Amata akaliweka chini
lile furushi, “vipi ?” akamuuliza Joel.
“Hali ya Beka si nzuri, tunaweza kumpoteza” akajibu. Amata
akapiga magoti na kumtazama Bakari. Kweli hali yake haikuwa
nzuri. Mapigo ya moyo yalianza kupotea.
“Shiit!” akang'aka, “inabidi tuondoke haraka,” akamwambia
Joel.
“Tutaondokaje?”
“Inabidi tupate gari” akamjibu juku akijitokeza kutoka
kwenye maficho yale na kutazama yale magari yaliyokuwa yakija.
Tayari yalikuwa yamefika, hayakuwa mengi, mawili tu yaliokuwa na
watu nane, yaani wanne kila moja. Amata alipata kigugumizi kujua
kama ni wanajeshi au wanamgambo. Maana walivalia sare za
kijeshi. Akarudi akaketi tena.
“Vipi?” Joel akauliza.
“Sijui ni wanajeshi au wanamgambo!” Amata akajibu.
“Haijalishi, tunahitaji usafiri, hivyo hatuna budi kufanya
shambulizi…” Joel akatoa uamuzi wa kijeshi. Amata akatikisa
kichwa kukubali.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Ngoja waingie ndani tufanye mauaji ya halaiki… maana bila


ya hivyo hatuwezi pata tutakacho…” Amata akamwambia. Wale
jamaa wakateremka kwenye yale magari kabla hata hayajasimama.
Wote wakateremka na kuingia kwenye lile jengo kwa kulizunguka.
Mmoja wao akabaki nje, bila shaka kuangalia usalama.
“Tunamlaza yule, kisha tunatoka na kutumbukiza vitenesi,”
Amata akamwambia Joel.
“Kwa kuwa we bado una nguvu nenda kwenye field mi
nitakulinda,” Joel akamwambia. Amata. Akainuka na kuchukua yale
mabomu ya kurusha kwa mkono. Joel akalitega lile bunduki vizuri
kabisa. Mara tu Amata alipojitokeza na kuelekea kule kwenye lile
jengo, Joel akaachia risasi moja iliyomtawanya uhai yule jamaa.
Amata akafika katika lile jengo na kutumbukiza yale mabomu
yakiwa yameondolewa kifungo cha usalama. Milipuko mitatu
ikatokea na moto kulifunikiza jengo lile. Ndani ya jumba lile
kulikuwa kumehifadhiwa silaha za aina mbailimbali yakiwemo
mabomu ya aina tofauti. Nayo yakaitika mwito huo na kufanya
mlipuko mkubwa.
Amata alikimbia na kuwahi gari moja lililoachwa funguo
ndani yake. Akatia moto injini na kuondoka mpaka pale
alipomwacha Joel na Bakari. Akashuka na kusaidiana na Joel,
wakampakia Bakari garini na safari ikaanza. Ndani ya gari lile
kulikuwa na chupa zilizojaa maji.
“Mmwagie maji” Amata akamwambia Joel aliyekuwa akinywa
maji kwa fujo. Akafungua chupa nyingine na kummwagia Bakari.
Amata aliendelea kubadili gia na kuzidi kuliacha lile eneo.
Walipoukaribia mjini Kashmir, akapunguza mwendo na kuegesha
gari katika jumba moja kuukuu.
“Joel, kuna sehemu nimeacha gari, ngoja nikalichukue…
mnisubiri hapa….” Amata akawaambia baada ya kuliacha gari
umbali wa mita kadhaa. Akawaficha ndani ya lile jengo na yeye
kuingia mjini. Amata alifika kwenye hoteli ya Jammujah akachukua
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

funguo na kununua vyakula kadhaa. Kila mtu alikuwa akimshangaa


kijana huyo, kwanza kwa uchafu uliozifubaza nguo zake na uharaka
wa kufanya mambo yake. Alipokamilisha aliondoka na kuchukua
taksi mpaka katika kile kituo cha mafuta. Akalikuta lile Jeep
likimsubiri. Yule kijana aliyemwachia hakuwapo kazini, akajieleza.
Bahati nzuri taarifa zilikuwa kwenye maandishi. Akalichukua lile
gari na kurudi mpaka kwenye lile jengo. Akapiga mruzi kwa namna
ambayo Joel angejua kuwa anaitwa yeye au wao. Akajitokeza.
Amata akamwendea na kumsaidia kuchukua Bakari,
wakampakia garini. Hali ya Bakari ilianza kuwa na ahuweni.
Akampa Joel kile kifurushi chenye chakula na dawa yeye akakamata
usukani kurejea Islamabad.
Mwendo wa saa nne uliwafikisha katika mji wa Ramban. Pale
Amata hakuona haja ya kuendelea na safari. Ilikuwa usiku sana.
Akatafuta hoteli ndogo na kuchukua chumba kwa saa ishirini na
nne. Lengo likiwa ni kupata msaada wa matibabu kwa Bakari na
kujiweka sawa kabla ya kuendelea na safari.

* * * *

Ile private Jet moja kwa moja ilimshusha Mansoor katika


Uwanja wa ndege wa Islamabad. Mansoor na wale wanawake
watatu, walinzi wawili na Jamila waliteremka na kuchukuliwa na
gari binafsi. Pamoja nao kulikuwapo like sanduku la mfumo wa
usalama. Mansoor aligadhibika sana pindi alipopata taaifa kuwa
jumba lake la mabilioni ya fedha limegeuzwa uwanja saa chache
zilizopita.
Safari yao ilikuwa nje ya mji ambako tajiri huyo alijenga kasri
lingine kubwa zaidi ya like la Kashmir. Tofauti tu ni kwamba hili
lilikuwa ni jumba la mapumziko zaidi. Saa mbili zaidi ziliwafikisha
katika jumba hilo. Mansoor bado alikuwa na matumaini ya kufanya
biashara yake hiyo.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Muwekeni katika chumba cha peke yake, msimpe chochote


mpaka atupatie code ya tatu” Mansoor akawaambia wale walinzi
wake wakati yeye na wale wanawake wakaingia upande mwingine
wa jumba jilo. Mmoja wa wale wanawake aliyeonekana mshupavu
ndiye aliyebeba lile sanduku.
Ndani ya sebule kubwa nay a kisasa, Mansoor alijitupa kitini na
kujiinamia. Kichwa chake kilisawajika kwa mawazo. Kila kitu
aliona kikienda segemnege. Akachukua simu yake, akapiga namba
ya Fernandez na kutega sikio kusikiliza, simu ile haikuwa
ikipatikana. Kila aliyejaribu kumpigia, hakuna aliyepatikana.
Mansoor akagwaya, akawa mpole. Taswira ya Amata, ikamjia mara
kwa mara kichwani mwake. Akajikuta akimchukia kuliko
anavyomchukia shetani.
Nitamraruararua nikimtia mkononi! Akawaza.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

12
MADAM S alisimama pasi na kusema lolote. Ukuta mdogo
uliojengwa kwenye kibaraza kile ulimkinga asianguke maana
alikuwa juu kabisa ya jengo lenye ghorofa tatu. Ulikuwa mgahawa
mdogo juu ya jengo hilo katika eneo la Bamaga. Bilauri yake
iliyojaa mvinyo ikiwa mkononi, mawazo yalimnyanyua kutoka
kitini mpaka pale na kusimama akitafakari jambo. Upande wa pili
wa jingo lile, ng’ambo ya barabara kuu ya kwenda bagamoyo
kulikuwa na ghorofa refu la kampuni moja ya simu lililozubngukwa
na uwanja mkubwa wa kupendeza.
Dakika kumi hivi zilimpeleka mbali sana kimawazo, mambo
yaliyokuwa yakimtukia katika siku hizo yalimtia hofu. Watu
walikuwa wakiendelea na burudani zao za kula na kunywa katika
jengo hilo huku kaupepo kakiwapa faraja dhidi ya joto kali la Dar
es salaam. Ghafla, kishindo kikubwa cha mtu kuanguka sakafuni
kiliwashtua waliokaa kwenye viti pale mgahawani.
Madam S alikuwa sakafuni, bilauri yake yenye mvinyo
ikitawanyika vipande vipande. Hakuna aliyesogea pale, kila mmoja
alisimama mbali huku akinamama wakipiga kelele za vilio. Hii
iliwavuta watu waliokuwa chini kupanda juu kuona nini
kilichotokea. Yote hayo yakiendelea, mwili wa mwanamke huyo
ulilala kimya, nguo yake aliyovaa ilipambwa kwa doa kubwa
jekundu kifuani pake. Simu yake ilikuwa mkononi ikiita kwa fujo.
Katika kundi lote hilo lililokuwapo, ni mtu mmoja tu
aliyesogea kwenye mwili ule na kuutazama kwa makini.
Akaichukua ile simu inayoita na kusoma ili kujua huyo apigaye.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

‘My Lovely Son’ ile namba ilisomeka. Yule bwana hakuogopa


akaipokea.
“Hello!” akaita. Sauti ya upande wa pili ikabaki kimya.
Upande wa pili, Chiba alisita kujibu, akaangaliaangalia ile namba
kama kakosea au la. Hapana, hakukosea. Kwa nini simu ipokelewe
na mwanaume… akawaza.
“Yes, naweza ongea na mama?” Chiba akamwambia huyo
aliyepokea.
“Aaaan eeeenh sasa, we upo wapi? … uje hapa Zaramo
restaurant, Bamaga, mama yako amepatwa na tatizo kubwa…” yule
bwana akamwambia Chiba.
“Sawa!”

* * * *

Chiba aliwasili eneo la tukio dakika kumi tu tangu akate simu


ile. Chini ya lile jengo kulikuwa na watu wengi magari ya polisi
nayo yalizingira kila upande, hakuna aliyeruhusiwa kuingia eneo
lile. Ndani ya utepe wa zuio la kipolisi kulikuwa na gari la
wagonjwa linalowaka taa zake za rangirangi. Chiba alijikuta anapata
baridi ya ghafla.
Nini kimetokea? Akajiuliza. Akaufikia ule utepe na kuzuiliwa na
polisi wale kuvuka. Chiba akaomba na kuomba, akawaeleza kuwa
yeye ni mtoto wa majeruhi huyo, wale askari ikabidi wajirdhishe na
baadae akaruhusiwa. Chiba alilifikia lile gari, wale wahudumu
wakamfungulia, akaingia na kumkuta Madam S akiwa kafungwa
kwenye kitanda cha gari hilo. Akamtazama kwa uchungu, chozi
likamdondoka. Lile gari likafungwa milango tayari kuondoka.
Kidirisha kidogo kikafunguliwa kilichomwezesha dereva kuweza
kuwasiliana na mtu aliye na mgonjwa.
“Unaweza kukaa na mwili wa mama yako humo ndani?” yule
dereva akauliza.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Nitafanyaje na wakati ni mama yangu?” Chiba akajibu. Kile


kidirisha kikafungwa na lile gari likaondoka…

* * * *

Safari ya Amata, Joel na Bakari ikaishia kwa Daktari Sajan.


Tayari Amata alikwislipenda eneo hili, tulivu lizilo na vurugu.
Wakamshusha Bakari ambaye alionekana kuwa mgonjwa bado.
Wakamuhifadhi katika chumba walichooneshwa. Amata
akamweleza kila kitu mzee yule. Yuole daktari akamtazama Bakari
pale kitandani, kisha akawatazama Amata na Joel.
“Huyu anatakiwa chekup kubwa, mwili wake haupo sawa
kabisa!” akawaambia.
“Sawa, wewe cha kufanya mpe huduma ya kumpa afya
nikirudi tutampeleka India moja kwa moja,” Amata akamwambia.
“Kamanda, kwa nini tusitoe taarifa nyumbani ili jeshi
lishughulike naye?” Joel akauliza.
“Joe’ ya nyumbani ni magumu sana, na hawatakiwi kujua
kuhusu hii misheni hata kidogo. Tupambane wenyewe, tutapoweza
ndipo hapohapo tutakuwa tumefikia,” Amata akamjibu. Bakari
hakuwa hata na uwezo wa kuongea, alionekana ni mtu mwenye
maumivu makali kwa ndani.
Sajan akamtazama kwa makini Amata, akauona ushupavu wa
kijana huyo tangu machoni pake. Akamhusudu.
“Sawa! Mwacheni hapa, naona kama mna safari nyingine
hivi,”
“Ndiyo, tunakwenda Islamabad, tutarudi kesho,” Amata
akamwambia Daktari Sajan.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

* * * *

Amata na Joel waliwasili Islamabad usiku wa manane.


Akagesha gari karibu na kituo cha mafuta cha Shell katika barabara
kuu itokayo Kashmir.
“Vipi?” Joel akamuuliza. Amata akaingiza mkono mfukoni na
kutoa ile Pegan Flash, akampa Joel, “unaijua hiyo?”
“Ndiyo, ndiyo… umeipata wapi?”
“Ya Jamila…”
“Jamila ana akili sana, yangu na ya Beka sijui hata ziko wapi.
Tukiwa na hii tutajua ni wapi bedui yule alipo…” Joel akamwambia
Amata. Akaanza kuifungua ile flash na kupachua hiki na kile,
“inabidi kuichaji” akasema. Akapiga ngumi sehemu Fulani ya like
gari pakafunguka. Akatazama nyaya zilizojaa humo akachagua
mbili na kuzimenya kwa meno kidogo kisha akaunganisha na zile
za ile flash akaiacha ikining'inia.
“Itachukua muda gani?” Amata akauliza.
“Sasa hivi tu… dakika tano tunaweza kuitumia…”
Akamwambia. Dakika tano baade akaichomoa na kuiwasha.
Ikawaka na kuanza kubipbip. Joel akaonekana kufurahi sana.
“Vipi?” Amata akauliza.
“Sasa hapa tunatakiwa kuiunga na radar Kule Tanzania ili
ituoneshe uelekeo wa sanduku lilipo…” Joel akaeleza. Amata
akainua simu yake na kupiga namba za Chiba.
“Kamanda!” Chiba akaitikia upande wapi.
“Vipi? Upo Shamba?” akamuuliza.
“Yap!”
“Washa ile kompyuta ya Hasheem, kisha unganisha flash kama
tulivyofanya siku ile… nahitaji kujua uelekeo utakaoupata ndipo
naka nifike…”
“Copy!”
“Umepiga wapi?” Joel akauliza.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Kizuka…” akamjibu kwa kumdanganya. Akawasha gari na


kuzidi kuingia mjini. Amata na Joel walikuwa tayari kumkabili
Mansoor popote alipo. Hawakutaka kupoteza muda kwani
walijuwa wazi kuwa kupoteza muda ni kumwacha aende mbali
zaidi. Dakika takriban kumi na tano simu ya Amata ikaita.
Akaicjukua na kuiweka sikioni.
“Nakupata!” akamwambia mtu wa upande wa pili.
“Inasoma Lohar Sharfoo…” Chiba akamwambia Amata.
Losar Sharfoo, mji mdogo ulio nje kidogo ya Jiji la Islamabad
ndiko Mansoor alikoweka makazi yake ya muda pindi akiratibu
mambo yake. Aliamini kuwa akiwa huko hakuna mtu yeyote
angeweza kumgusa. Kamanda Amata akawasha gari na kuitafuta
Barabara ya Peshawar. Ilimchukua dakika thelathini na nne
kuikamata barabara hiyo. Saa kumi na moja alfajiri waliwasiri katika
ule mji mdogo wa Losar Sharfoo. Kama alivyoelekezwa, akaiacha
barabara hiyo na kuingia ile ya M1 Bahter na kufuata maelekezo
aliyopewa na Chiba mpaka alipoliona like jumba aliloelekezwa.
Akapita na gari lile na kuliacha lile nyuma. Akaegesha gari karibu
kabisa na shule ya Kiislam ya Shuffah. Akazima gari.
“Tumefika?” Joel akauliza.
“Tumefika ndiyo… jumba lile paleee…” Amata akamwambia.
Joel akafungua mlango na kuteremka, Amata akafuatia. Wote
wawili walikuwa ndani ya Suti safi, nadhifu, nyeusi. Ungewatazama,
ungesema wanaenda harusini lakini haikuwa hivyo.

* * * *

Swala ya alfajir ilisikika katika msikiti wa karibu, wakati Amata


na Joel walipolifikia lile jumba. Hawakuwa na silaha yoyote. Hili
kwao halikuwa tatizo. Silaha zitapatikana hukohuko ikibidi.
Kulikuwa jumba kubwa, zuri, lililopendezeshwa na Taa za aina
aina.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Vipi kama jumba hili lina ving’ora vya usalama?” Joel


akauliza.
“Haliwezi kukosa, lakini ni kawaida kwa ving’ora kuwa off saa
kumi na moja…” Amata akajibu.
Kitu pekee kilichowashangaza ni kuwa lile jumba halikuwa na
ulinzi kabisa. Alipolifikia lango kuu la jumba hilo, likafunguka
taratibu. Amata akahofu, akajua kwa vyovyote kaonekana.
Hakuogopa, akasimama katikati ya lango hilo wakati likifunguka.
Taa kali za gari zikamulika kutokea uvunguni mwa lile jumba.
Sekunde kumi zilizofuata lile gari likajitokeza likiwa linatoka nje ya
jumba lile. Taa zilipommulika Amata pale getini, likasimama.
Inaonekana dereva hakuamini kama aliyesimama ni binadamu au
mzimu. Mlango ukafunguliwa, akateremka mwanamke mmoja na
kusimama palepale mlangoni.
“We ni nani?” sauti ya like, zile azipendazo Amata ikamfikia.
“Amata Ric, TSA 1”
“Shida nini? Hatusaidii masikini sasa hivi…”
“Nina shida na bosi wako Mansoor na siyo wewe
kibaraka…” Kabla yule mwanamke hajasema neno, Mansoor
alitokea mlango wa pili. Amata alihisi kuwa ni yeye kwa kuwa
hakuweza kumuona vizuri kwa kukinzwa na mwanga ule.
“Mimi ni mgeni wa huyu na siyo wewe!” akamwambia yule
mwanamke.
“Umepajuaje hapa?” Mansoor akauliza.
“Sina muda wa kujibu maswali, nahitaji Pegan Box na
ninamuhitaji Jamila uliyemteka haraka iwezekanavyo, ndege
inanisubiri,” Amata akamwambia Mansoor. Muda wote huo Jicho
lake lilikuwa kwa yule mwanamke, likimwangalia kila akifanyacho.
Yule mwanamke mkono wake ukainyakua bastola iliyokuwa juu ya
dashboard ya gari. Kwa kasi ya ajabu akarudisha mkono nje na
kufyatua. Lakini hakufikia kufanya kile alichokikusudia. Jiwe lenye

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

uzito wa kilo kama moja na nusu hivi lilikifikia kichwa chake,


akaanguka huku bastola ikimtoka mkononi.
Joel alikuwa kafanya lake tayari. Amata akasikia mvumo wa
risasi na kufuatiwa na kishindo cha mtu kuanguka. Akajitupa chini
na kujiviringa kutafuta pa kujificha. Risasi kadhaa zikapita pale
aliposimama awali. Lile lango likaanza kujifunga taratibu.
Hakusubiri, akatambaa na kuingia ndani ya ule uzio. Mansoor
tayari alikuwa keshatoweka eneo lile.
“Amataaaaaa” sauti ya Jamila ikayafikia masikio ya Amata.
Akatambaa na kuingia uvungu wa gari, akajirefusha na kuchukua
ile bastola. Risasi ya kwanza akamzimisha yule mwanamke pale
chini. Akarudi na kumpa ishara Jamila atulie.
Jamila alikuwa ametulia katika kiti cha nyuma cha lile Benzi,
kimya, kajilaza. Amata akasogea karibu kabisa na buti la lile gari.
Tayari alikwishamwona yule anayerusha risasi kutoka ndani.
Akamlia timing alipomweka sawa, akaachia risasi moja iliyofumua
dirisha na kukitawanya kichwa cha yule jamaa. Akamshusha Jamila
na kumpa ile bastola.
“Kaa nyuma yangu! Wako wangapi?” akamwambia.
“Wapo wanne, wanawake wawili na wanaume wawili na
mwenyewe…”
“Pegan Box ipo wapi?”
“Lipo humu kwenye buti…”
“Nilinde!” akamwambia Jamila. Amata akaufuata mlango wa
dereva na kufyatua Loki ya buti hilo. Alipoinama tu kulichukua like
sanduku, akajikuta akipigwa dafrao na kuanguka chini.
Alipohamaki, Jamila hakuwa eneo lile. Akajiinua na kuvaana na
yule jamaa aliyemvamia pale. Amata akapeleka makonde
mazitomazito ambayo yote yalimwishia yule bwana. Yule jamaa
Naye hakuwa haba, mapigo kadhaa ya karate yalifika kwa Amata,
yapo aliyoyakinga na yale yaliyompata. Kamanda Amata akaona
akicheza anaweza kupoteza kwani yule bwana hakuwa na masihara
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

kwenye upigaji wake. Alirudi nyuma na kujirusha sarakasi akampita


hewani na kutua nyuma yake. Pigo moja alilopiga kwa nguvu zote
likatua katikati ya uti wa mgongo. Yule jamaa akaguna kwa
maumivu, pigo la pili likamgeuza na kumzungusha, alipokuja
kutulia, Amata alikwishachomoa sime lililokuwa kiunoni kwa huyo
jamaa na kumdidimiza. Akampigapiga mgongoni na kumwacha
aanguke taratibu.
Amata akatazama huku na kule, hakumwona Jamila. Akabaki
njia panda, amtafute Jamila au achukue lile sanduku. Yuko wapi
Mansoor?
Akiwa katika kuwaza hilo, kioo chadirisha kikapasuka na
mwili wa mwanamke ukaanguka kama mzigo. Amata akawahi
kuutazama, siyo Jamila.
“Nimeshamvunja shingo!” sauti ya Jamila ikatokea dirishani.
Akatumia njia hiyo hiyo kutoka nje. Amata akachukua like sanduku
na kulibusu.
“Joel!” akatamka. Ni nukta hiyo alimkumbula Joel. Akawahi
getini na kulikuta limefungwa. Akatafuta wapi kuna mota ya
kuliendesha lile geti, akapapata. Akavunja na kuunganisha nyaya
mbili, lile lango likasogea taratibu.
“Mansoor tunamwacha?” Jamila akauliza.
“Achana naye!” akamjibu huku akitoka nje. Amata akamuona
Joel akiwa chini anagalagala huku mkono wake kajishika ubavuni
mwake, akamuwahi na kumgeuza. Jamila akaanza kulia kwa
kwikwi.
“Tulia, hapa si pa kulia…” Amata akamwambia na kumwacha
pale nje. Akachukua bastola kutoka kwa Jamila na kurudi ndani.
Giza lilikwishaanza kuondoka taratibu naye yeye hakutaka mwanga
umkute hapo. Akatumia nguvu zake na kulisukuma lile gari mpaka
lilipopata ule mteremko na kutumbukia mle gereji. Akatoka nje.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Twende!” akamwambia Jamila. Akainua lile sanduku


wakakimbia mpaka pale alipoegesha lile jeep lake. Wakaliweka
salama lile sanduku na kumtaka Jamila kuingia garini.
“Tunauacha Joel?” Jamila akauliza.
“We panda gari, acha maswali..” akamkaripia, na mwanamke
yule akaingia garini. Amata akaendesha gari mpaka kwenye lile
jumba. Akasimama na kuteremka, akambeba Joel na kumpakia kiti
cha nyuma. Kisha akainua bastola yake na kulilenga lile benzi.
Risasi zake mbili zikafumua tenki la mafuta. Moto mkubwa
ukalipuka na lile jumba likashika moto. Kizazaa. Amata akaingia
garini na kutulia kwanza. Haikupita dakika akaona mtu anatoka
ndani kwa kasi huku akiwa anawaka moto.
“Heeeelllllpppp!” yule mtu akapiga kelele.
“Mansoor!” Jamila akatamka taratibu.
“Yes!” Amata akajibu na kuinua bastola yake. Akaachia risasi
tatu zilizoishia kwa yule mtu aliyekuwa akihangaika na ule moto.
Akaanguka chini na kutulia kimya. Amata akaondoa gari na
kuliacha eneo lile. Nyuma yake alisikia ving’ora vya magari ya polisi
kama si ya zimamoto yakija eneo lile. Alipoifikia barabara
anayoihitaji, akakanyaga mafuta kuwahi kwa yule daktari. Joel
likuwa anahitaji matibabu ya haraka.

Dakika kama mia na kitu hivi walifanikiwa kufika katika kijiji


cha Al haram, ambako Bakari aliachwa hapo akipata matibabu.
Walipoegesha gari tu, daktari Sajani alikuwa wa kwanza kufika pale
nje.
“Mmefanikiwa?” akamwuliza Amata.
“Tumefanikiwa lakini tuna mgonjwa mwingine mahututi,”
akajibu. Sajani akawahi kufungua mlango wakamteremsha Joel
nakumpeleka chumba tofauti. Walipomlaza tu, yule daktari tayari
alisogeza vifaa vyake, akaanza kufanya matibabu ya haraka ikiwa na
kumtoa risasi iliyokwama ubavuni mwake. Nusu saa baadae
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

alikuwa amekamilisha kazi ile akamfunga lile jeraha na


kumwongezea sindano ya usingizi.
“Atapona?” Jamila akauliza.
“Ndiyo!” Sajani akajibu. Alipomaliza kazi ile akawataka
Amata na Jamila kufuatana pamoja naye mpaka katika ofisi yake
ndogo. Walipoketi akachukua rekoda yake ndogo, akamkabidhi
Amata.
“Hapa mambo siyo mazuri rafiki, Bakari ameenda!” Sajani
akamwambia Amata kwa sauti ya chini. Amataka akahisi kama
amechomwa sindano ya ubongo kwa ganzi aliyoipata. Kwa kidole
chake cha gumba, akafyatua rekoda ile na kuisikiliza.

‘Asante kwa kutuokoa,


umefanya kazi kubwa lakini Mungu ana mpango mwingine kwangu.
Natumai umelipata pegan Box,
Nilitamani na nilikuwa na hamu ya kushuhudia kifo cha mshenzi
Mansoor. Haikuwa hivyo. Nahisi
siwezi kupona, lakini maumivu yangu na damu yangu viwe juu ya wote
wanaohusika.
Kamanda, ukifika Tanzania ndani ya jeshi letu tukufu
hakikisha unampata mtu anyejificha kwa jina la Mudfish, umtie
hatiani.
Yeye ndiye anayejua mpango mzima huu!
Fika kwa mke wangu, akupe funguo ya posta, pale pana bahasha kwa
ajili yake, umpatie tafadhali.
Naipenda Tanzania, naipenda nchi yangu!
Salute kwako!
Capt. Bakari’

Amata alikunja sura na kujikuta akitoa chozi la uchungu, akazima


kile kifaa nakuitoa ile kaseti iliyokuwa ndani yakena kuitia mfukoni.
Jamila alikuwa kimya pembeni.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Vipi?” akauliza, lakini Amata hakujibu, akasimama.


“Naomba kumwona Bakari…” akamwambia yule daktari.
Akawaongoza mpaka mile chumba alichokuwepo. Bakari alikuwa
kimya kitandani. Rangi ya sura yake ilikwishaanza kubadilika.
Jamila hakuweza kuyazuia machozi yaliyokuwa yamesogea kwenye
kingo za macho yake. Amata alisimama kimya akiutazama mwili wa
Bakari. Alitamani amrudishe Tanzania akiwa hai lakini nguvu zake
ziliishia hapo. Akavuta kamasi lilizofikia tundu za pua yake.
Akainua mkono na kupiga saluti na Jamila akafanya hivyohivyo.
Wakaufunika ule mwili na kutoka. Yule daktari alikuwa ameketi
palepale.
“Asante kwa kila kitu!” Amata akamwambia Sajani.
“Nilipenda niuokoe uhai wake lakini imeshindikana,” Daktari
Sajana akamwambia Amata. Wakapeana mikono. Amata akaelekea
chumbani ambako Jamila alikwishatangulia. Akamkuta mwanamke
huyo hatamaniki kwa kilio. Amata alisimama mlangoni
akimwangalia binti huyo akiwa hatamaniki kwa kilio. Akaamua
kutoka nje ya nyumba hiyo. Jua lilikuwa tayari limechomoza
vyema, watu walikuwa wakienda kwenye shughuli zao mashambani
na viwandani. Amata alikuwa kaliegemea lile Jeep pale nje.
Nusu saa baadae alirudi ndani na kumkuta Jamila akiwa
ametulia, macho yake yalijaa machozi, alikuwa ameketi kimya
kitandani akionekana wazi kujawa na uchungu machoni. Akavuta
hatua na kuketi kitandani karibu yake. Jamila akajiegemeza begani
pa Amata.
“Usilie sana, bado tupo kwenye uwanja wa vita!”
akamwambia. Jamila akaitika kwa kutikisa kichwa chake, akajiinua
na kuingia maliwato. Amata akalitazama lile Pegan Box, kasha kile
kifurushi chake, akatabasamu. Akakiacha chumba hicho na
kuelekea kwenye ile ofisi ndogo ya Daktari Sajani. Akamkuta.
“Vipi?” Sajani akauliza.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Nahitaji kufika Islamabad, nikaandae usafiri wa kuondoka na


watu wangu,” akamwambia.
“Sawa!”
“Lakini nikikamilisha kila kitu nitahitaji watu wangu wafike
Islamabad salama, itawezekana?” akamwuliza.
“Aaaaanh nafikiri itawezekana. Najua nini cha kufanya, we
nenda ukiwa tayari nipe taarifa,” Sajani akamwambia Amata.
Amata akatoka na kuingia mule chumbani, akamkuta Jamila akiwa
ameketi kitandani.
“Sikiliza Jamila, naenda Islamabad, naenda kuandaa usafiri wa
kurudi nyumbani. Ubaki hapa, mpaka nitakapowapa taarifa ndo
mje… jipe nguvu, ni wewe tu uliye mzima sasa!” akamwambia.
Amata akamkubatia Jamila, wakaagana.

* * * *
Huko Mabwepande, sherehe iliandaliwa, mbuzi wawili
waliangushwa, vinywaji vya kila aina. Wapo waliojua sherehe hiyo
inahusu nini na wapo waliokuwa wakila na kunywa tu bila kujua
lolote.
“Tumemwangusha bibi kizee!” mmoja wa wtu wa heshima
akawaambia wenzake. Wote wakacheka na kugonga cheers wakati
familia zao zikiburudika.
“Hata kama tutakosa hilo box, lakini mshenzi huyu mtibua
mipango ya watu tumemmaliza kuleni na mnywe… hiyo biashara
itafanyika hata kwa siri tu,” mwingine akaongeza kusema.
“Lakini habari za huko zinasemaje?”
“Huko ni maumivu tu, sijui huyo kiumbe aliyetumwa huko
anafananaje! Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote tunayoipata, kwa
kifupi ameharibu kila kitu,” mjumbe mwingine akasema.
“Atauawa hapahapa kama bibi yake!”
“Kabisa na huo ndiyo mpango unaotakiwa kusukwa sasa…!”
mjumbe wa kwanza akawaeleza wenzake.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Tayari tunataka kufanya utaratibu wa kupokea hilo box, na


siku hiyohiyo huyo mshenzi laziama auawe”. Mikakati ikapangwa.
Vigogo hawa wa juu katika jeshi la wananchi waliweka mambo
sawa. Walijua wazi kuwa kijana huyo akirudi lazima kila kitu
kifanyike kwa taratibu za kijeshi hivyo mkakati wa kumuua Amata
kama alivyouawa Madam S ulianza kuandaliwa.

“Vipi, mtego wetu umefanikiwa?” Madam S akamwuliza


Chiba.
“Ndiyo, lile ulilolisema ndilo lililotokea… na nimempiga
picha,” Chiba akajibu huku akiitoa simu yake mfukoni. Akampatia.
Madam S akaitazama kwa makini ile picha, na kumrudishia simu
Chiba.
“Unasemaje?” akamuuliza.
“Tungoje Amata arudi ili tujumuishe yote pamoja,”
“Sawa!”
Madam S alilazwa katika hospitali ya Hindu Mandal, katikati
ya jiji la Dar es salaam akiwa chini ya uangalizi wa Chiba na Daktari
Jasmini. Mara tu baada ya kuchukuliwa kutoka katika eneo la tukio
pale Mgahawa wa Zaramo, lile gari la wagonjwa lilimfikisha katika
hospitali hii. Akawekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Hakuruhusiwa mtu yeyote kuingia humo ndani isipokuwa Jasmini
na Chiba pekee.
Simu ya Madam S ikaita, Chiba akaichukua na kuiweka
sikioni.
“TSA 1”
“TSA 2” Chiba akaitikia.
“Kuna shida yoyote?” akauliza kwa kuwa si kawaida simu hiyo
kupokelewa na mtu mwingine.
“Ndiyo, lakini usalama upo kwa asilimia zote,”

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Mungu akipenda nitawasili kesho na kila kitu. Nitakuja kwa


ndege ya kukodi,”Amata akaongea na Chiba mawili matatu, kisha
wakakata ile simu. Chiba akairudisha mahala pake.
“Vipi?” akauliza.
“Kamanda atawasli kesho…”
“Safi! Sasa hapo ndipo nataka watu waumbuke, shubamit!
Watakapotua tu, wote wafikishwe Shamba,” Madam S akatoa
maagizo.
Maandalizi ya kumpokea Amata yakaanza kuratibiwa na TSA
wenyewe. Mpango mzima ulikuwa ni kuwafanyia.

* * * *
Kamanda Amata aliwasili Islamabad katika hoteli ileile ya
Mariott. Akaegesha lile Jeep upande wa pili wa hoteli hiyo ambapo
palikuwa na uwanja mkubwa wa kuegesha magari binafsi. Akavuka
na kuingia katika hoteli ile. Akapokelewa mapokezi kukabidhiwa
kadi ya chumba chake. Akaingia. Amata alijua vyema kucheza na
hisia za watu. Ndani ya chumba kile akachukua vichache
alivyoviacha. Akaiacha kadi katika sehemu yake, akatokea mlango
wa dharula na kuondoka. Nje ya hoteli ile, akachukua simu yake na
kupiga kwa yule dereva taksi aliyempokea. Wakakutana. Hakuwa
na la kuongea, alipakia mizigo yake, pamoja na lile pegani box.
“Nipeleke uwanja wa ndege!” yule kijana akampeleka. Baada
ya kuagana naye. Amata akafanya utaratibu wa kukodi ndege
maalum kwa kubeba wagonjwa. Akatoa taarifa kuwa ana mgonjwa
mmoja, mabaki ya binadamu na mtu mwingine. Ndege ile ilikuwa
maalum kwa kazi kama hizo. Huduma za ndege hii ni pamoja na
muuguzi na daktari.
Katika ofisi ile, Amata alijaza fomu maalumu za safari hiyo.
Maswali kadhaa yakaweka mambo sawa. Amata akajieleza vizuri na
kuchanganya na uongo wa kutosha. Akiwa hapo ofisini, akashtuka

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

akishikwa bega. Alipogeuka akagongana macho na Dhakar.


Wakakumbatiana.
“Brother!” Dhakar akaita huku akimkumbatia kwa nguvu,
“asante sana kwa kuniokoa bro’ lakini yule mshenzi hajafa, yupo
hoi hospitalini…” Dhakar akamweleza Amata. Baada ya
mazungumzo machache. Amata alimweleza kila kitu. Dhakar
akazungumza na ile kampuni ya ndege na kuiambia kuwa CIA
kitengo cha siri ndiyo wanaikodi kuelekea Tanzania.
Wakakubaliwa. Amata akapiga simu kwa Daktari Sajani na kumpa
taarifa kuwa safari itakuwa saa nne zijazo. Kampuni ileile ikatoa
huduma ya gari la wagonjwa kuelekea huko Al Haram
kuwachukua.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Dar es salaam
13
Saa nane usiku, Scoba na Daktari Jasmini waliwasili uwanja
wa ndege wa kimataifa wa Dar es salaam. Scoba alikuwa
akiendesha gari la wagonjwa la kampuni binafsi ambalo waliliazima
kwa shughuli hiyo. Jasmini alikuwa na Land Rover Defender yenye
vioo vya giza. Katika msafara wao, gari la tatu lilikuwa na Gina
aliyekuwa amekamilika kwa lolote litakalotokea. Bunduki kubwa
aina ya Kalashnikov AK 47 ya kisasa kabisa. Vikinga risasi
viliuzunguka mwili wake, kofia yake ya chuma iliyounganishwa na
chombo cha mawasiliano ilitulia kichwani. Chiba naye alikuwa
katika mavazi hayohayo, waliimarisha ulinzi. Walijua nini kinaweza
kutokea ingawa maandalizi ya safri hiyo yalikuwa siri kubwa
miongoni mwao. Hawakuacha kuchukua tahadhari.
Uwanja walioutumia kuipokelea ndege hiyo haukuwa wa jeshi.
Waliofia siri yao kuvuja. Madam S bado walikwishamhamisha
kutoka Hindu Mandal na kumpeleka Shamba. Yale magari
yakaingia katika eneo la ofisi za kupakulia mizigo za DHL lililopo
katikati ya Uwanja wa Jeshi na ule wa abiria wa kawaida. Saa nane
hiyo, ile ndege ikawasili na kuongozwa kufika katika eneo hilo.
Hakuna mtu yeyote aliyetilia shaka. Ikasogea mpaka jirani kabisa na
jingo hilo ambapo ndege nyingine za mizigo hufanyia upakuaji
wake. Kamanda Amata na Jamila wakawa wa kwanza kabisa
kuteremka. Rubani pamoja na wafanyakazi wake wakasaidiana
kuteremsha mwili wa Bakari uliohifadhiwa vizuri kwenye boxi
maalumu. Kitanda alicholazwa Joel kikateremshwa na
kubadilishwa. Jamila alilichukua Pegan Box mkononi mwake.

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Gina na Chiba hawakuwa wakiongea lolote, macho yao


yalikuwa katika umakini wa hali ya juu sana kuhakikisha usalama
unakuwepo. Katika lile gari la wagonjwa, Joel akapakiwa. Pamoja
naye akapanda Amata na Jasmini.
“Itifaki lazima isingatiwe!” Scoba akamwambia Amata kupitia
kwenye kidirisha kidogo. Akampatia maguo meusi mawili.
“Mtuvumilie ndiyo kazi yetu inavyofanywa. Akamvika Jamila
lile guo usoni, na Joele vilevile. Katika lile landrover, mwili wa
Bakari ukapakiwa. Wale wahudumu wa ndege ile, wakatakiwa
kuondoka usiku huohuo. Safari ya kuelekea shamba ikaanza.
Msafara ule ulikuwa ukienda kasi sana, hakuna aliyekuwa
akiongea. Gina alikuwa akitazama kila upande kuona kama kuna
dalili ya hatari, hakuna. Saa tisa waliwasili katika chimbo lao. Kila
kitu kikawekwa sawa. Kamanda Amata hakuamini kabisa kama
amefika nyumbani, aliwatazama vijana wake, na wao walimtazama
yeye.
“Karibu nyumbani kamanda!” Chiba akamwambia.
“Asante!” akaitika, “Siamini kama nimerudi, naomba nilale…
nina siku kadhaa sijalala usingizi,” akawaambia na kuwaacha.

* * * *
Kama kuna siku ambayo watu walihadhirika na
kuchanganyikiwa ni hii. Madam S aliwasili Ikulu akiwa na
Kamanda Amata, na kepteni Jamila. Siku hii kulikuwa na kikao
maalum cha maafisa wa jeshi kujadiliana kuhusu swala hilo. Ujio
wa Madam S ulikuwa wa ghafla, hata Mkuu wan chi mwenyewe
hakuutegemea.
Alipokuwa katika mkutano huo akapata taarifa ya ugeni huo
wa dharula na muhimu. Akapigwa na butwaa, hakujua nini
kinatukia.
Madam S! akawaza. Hajafa? Akajiuliza. Hakuwa na jinsi,
akakubali ugeni huo uingie ndani ya ukumbi huo. Mara baada ya
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

mwanamama huyo kuijitokeza ukumbini, kila mtu alijikuta akibaki


kinywa wazi. Amata naye aliingia akifuatiwa na Kepteni Jamila
aliyekuwa amelibeba lile boksi.
“Mheshimiwa Rais na Amiri Jeshi mkuu… kwanza unisamehe
kwa kuvuruga ratiba yako na kuja hapa bila taarifa,” akasema. Kila
mtu alikuwa kimya. “Kazi uliyonituma, nimeimaliza… pegan box
lililokuwa limeibwa ili liuzwe na wale maharamia, hili hapa mkuu.
Limefika Tanzania salama kabisa,” kamanda Amata akalikabidhi
boksi lile kwa wanausalama waliokuwapo. Wakalipokea na
kulihakiki harakaharaka.
“Hili ndilo lenyewe?” akauliza.
“Bila shaka, wataalam wa mambo hayo kutoka katika jeshi
letu tukufu watathibitisha,”Madam S akamwambia.
“Asante sana Selina, kwa mara nyingine umedhihirisha
umahiri wa idara yako. Na vipi kuhusu vijana wetu?” Rais akauliza.
“Niseme tu wazi kwamba nimewakosa, hivyo inabidi
kupangwa operesheni nyingine kwa ajili yao. Tumeweza kupenya
kila ngome lakini hatukuweza kuwapata!” akamjibu. Ukimya
ukatawala kile chumba.
“Sawa, asante. Naomba niwe na kikao na wewe kesho
asubuhi,” Rais akamwambia na mwanamama yule akaondoka.
Tumezidiwa kete, mwanamke mshenzi sana huyu! Rais akawaza
kichwani mwake.

* * * *

Wakiwa katika gari lililokuwa likiendeshwa na Scoba, Amata


akamtazama bosi wake, “hivi kwanini umeamua kulikabidhi hili
boksi kienyeji namna hii?” Amata akamuuliza Madam S.
“Nimetumia technic mwanangu… pale kuna watu
wameshapata aibu…” akamjibu.
“Aibu?”
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Ndiyo! Unajua tungekabidhi hili boksi peke yetu tungeweza


kuambiwa limeibiwa tena au feki… lakini pale si umeona waandishi
wachachache waliopo wamepiga picha, wajumbe wa mkutano
wameshuhudia. Kwa mantikia hiyo sisi tumejivua katika hilo…”
akamweleza.
“Unataka kunambia mpango ulisukwa hapa nyumbani?”
“Haswaaa! Na kuna mengi yametukia wakati haupo…”
Madam S akamwambia.
“Mama yako alishadunguliwa huyo! Ungekuta tunakula msiba
tu!” Scoba akadakia.
“Nawe endesha gari huko!” Madam akamwambia Scoba.
“Bado kazi iliyobaki sasa ni kukusanyakusanya kila takataka.
Tukimaliza ndo tutawatoa watu hao, kwa sasa watusaidie
upelelezi,” akamwambia.
“Hakika!” Amata akaunga mkono. Dakika arobaini na tano
waliwasili Shamba.
“Tunatakiwa tujifiche, hatutatoka nje isipokuwa kwa dharula
tu mpaka sakata hili limalizike,” Madam S akamwambia Amata.

* * * *
“Jamani, si mlisema mmemuua?” mmoja wa wanajopo
akauliza.
“Niliuiza mara kumikumi, mkanihakikishia amekufa, yule
aliyeleta Pegan Box pale ni nani? Tunazidiwa akili mpaka na
mwanamke… yaani yunapanga jinsi ya kulirudisha hilo box wakati
tayari limeshafika nchini,” huyu aliyekuwa akiongea, alionekana
miguu tu. Sura yake ilifichwa. Yeye aliketi juu na wajumbe
walikuwa chini. “Mbaya Zaidi, amewasilisha ofisibi kwangu,
orodha ya majina yenu wote kuwa mnahusika. Upelelezi
umefanyika saa ngapi, hata mimi sijui…” akaongeza kusema.
Wajumbe wale wakabaki kimya, hakuna aliyeongea. “Tunaliweka
vipi jambo hili?” akauliza.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

“Mkuu, unachosema ni kweli, mimi ndiye niliyepanga


shambulizi lile, na nilihakikisha kuwa kweli huyu mtu amekufa.
Kijana wangu aliyekuwa katika ule mgahawa alinihakikishia hilo,”
mjumbe mmoja aliyeketi kwenye siti namba sita akajibu.

Juma moja nyuma

Madam S aliketi na Chiba kwa mazungumzo mafupi na


mpango kabambe. “Sikiliza Chiba, mpango wa kuawa kwangu
umevuja. Siku zote si wote wanaokupenda na wala si wote
wanaokuchukia. Ametafutwa mtu wa kunidungua na hilo zoezi ni
keshokutwa,” akachukua pochi lake na kutoa kadi, akampatia.
Chiba akaipokea na kuisoma, kasha akamrudishia.
“Kwa hiyo wamekualika katika cakula cha jioni ili watimize
haja yao?”
“Ndiyo!”
“Huo mpango umeujuaje Madam?”
“Mwanangu, utu uzima dawa! Mimi najua kuwa nawindwa,
hivyo nimeweka masikio sehemu fulani fulani na ndiko Napata
habari. Nimeambiwa mpaka huyo muuaji ni nani na amefikia wapi,
na zoezi lake atalitekelezea wapi…” akaeleza. Chiba akabaki kimya
kabisa akitafakari jambo hilo.
“Kwa hiyo!”
“Nataka nitoweke machoni pao kwa njia hiyohiyo halafu
nitaibuka kama mzimu mbele ya macho yao. Mchezo huu ni mzito,
Kinara anahusika,” Madam akamwambia Chiba. Kijana huyo
akatikisa kichwa juu chini kuwa ameelewa.
“Lengo la kuniita…”
“Nataka uhakikishe unamdhibiti huyo mtu na wewe kutumia
nafasi hiyo kutekeleza mauaji hayo, halafu uje haraka pale Zaramo
Restaurant kuhakikisha mambo hayaharibiki. Mtanilaza Hindu

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Mandal chini ya uangalizi wenu halafu nitahamia Shamba.


Iaminishwe kwa watu kuwa nimekufa,”
“Kazi imeisha hiyo!” Chiba akamjibu Madam S.
Akakabidhiwa karatasi ndogo yenye jina na mahali ambapo muuaji
huyo atapatumia na hoteli anayoishi. Mara alipoachana na Chiba,
Madam S akamtafuta Scoba na kumpa habari ile kwa namna
nyingine kabisa, akimtaka kuandaa gari la wagonjwa litakalofika
hapo haraka mara tu simu ikipigwa kuomba msaada huo. TSA
walipanga mpango wao kabambe na upande wa wauaji walipanga
pia mpango wao.

Siku mbili baadae


Ndani ya hoteli ya Super Star, Mwenge, Chiba aliwasili na
kuegesha gari lake binafsi nje ya hoteli hiyo. Akavuta hatu kulifuata
dawati la mapokezi. Kofia yake ya ‘Mungu usinione’, ilimkaa vyema
na kuuficha uso wake dhidi ya kamera za uslama zilizofungwa
mapokezi hapo. Chiba alifika hapo na kuongopa kuwa amekuja
kumsalimu mgeni wake aliyefika asubuhi ya siku hiyo. Akamtaja na
jina na mahali anapotokea, akaelekezwa, naye akaenda.
Ndani ya chumba hicho, Franco Demis alikuwa peke yake,
ameketi kitini akiendelea kuburudika na pimbe kali huku akitazama
filam za ngono. Kilichomshtua ni mlango uliofunguliwa bila hodi.
Chiba alipachika funguo na kuingia ndani, hakuwa na simile, wala
hakutaka kuuliza. Pigo moja lililotua katika paji la uso
lilimsambaratisha mtu huyo, akajikuta chini akiwa hana fahamu.
Akaliendea kabati lililokuwa jirani na kufungua, akatoa mkoba
mmoja wa ngozi akaubwaga kitandani. Alipoufungua ndani
akakutana na bunduki ndogo, kipisi lakini yenye nguvu. Bunduki
maalum ya kudungulia. Akapekua Zaidi na kuchukua kila
kilichomfaa. Akachukua huo mkoba na kumuinua huyo mtu,
akamweka begani na kutoka naye mlango wa nyuma. Huko Scoba
na Gina walimpokea na kuondoka naye akiwa hana fahamu.
Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K
Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Katika jingo la kampuni ya DarCom, eneo la Bamaga, Chiba


alipanda mpaka ghorofa ya tatu akiwa amevaa mavazi maalu na
pekee aliyoyakuta kwenye mkoba ule. Akaitega ile bunduki yake
tayari kwa kazi. Kama mpango wao ulivyokuwa. Upande wa pili
kwenye mgahawa ule wa Zaramo, Madam S na watu wengine
walikuwa wakipata chakula cha jioni, huku mazungumzo ya hapa
na pale yakiendelea. Vicheko furaha na utani vilitaradadi. Simu
yake ikaita, akainuka na kuuelekea ukuta uliokuwa kando ili aweze
kuipokea. Hapo ndipo risasi moja ilipotua kifuani pake na
kumbwaga chini huku damu zikimwagika.
* * * *

Kikao kile kiliendelea kwa kutupiana lawama. Jopo hilo lilijua


wazi kuwa Madam S ameuawa lakini walishangaa walipomwona
mkutanoni akikabidhi Pegan Box.
“Wewe ndiye mzembe namba moja… hutakiwi kuzungumza
chochote. Sasa nasema hivi, hakikisheni hao vijana wanafia
hukohuko waliko. Itumike gharama yoyote ile, tutume watu
wakapeleleze wawaulie hukohuko… wakirudi hai hapa nchini
tutaumbuka,” yule mtu akasema na mara kile chumba kikawa na
giza. Giza nene likakitawala, wale wajumbe wakajikuta hawajui la
kufanya. Giza lile liliwanyima hata kuona mbele nukta moja.
“Mwisho wa ubaya aibu!” sauti yenye mwangwi ikasikika.
Wajumbe walitulia kimya, hawakujua nini cha kufanya, “mlifikiri
kuwa hatutaweza kuwagundua hata kama ni vigogo wa serikali?
Hujuma mnazolifanyia taifa zote tunazo, tumefkisha orodha chafu
kwa Rais, naamini atawashughulikia na si vinginevyo. Na wewe
unayejiita Mudfish, una saa ishirini nan ne tu za kujisalimisha,
ukikaidi tusilaumiane… siku njema!” ile sauti ikakatika lakini kile
chumba kikabaki giza. Utata!

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K


Written by Richard Mwambe – Call 0672160016/ whatsapp 0734550514

Ф MWISHO Ф

Sold to Agnes Mbatali O-201126-P035021-K

You might also like