You are on page 1of 135

—1—

BUTI LA
ZUNGU

RAJAB I. ALLY

—2—
USANIFU WA KURASA
Hussein Molito
+255 718 97 56 59
kalamutulivu@gmail.com

USANIFU WA JALADA

Chapa ya Kwanza 2024

© Rajab I. Ally

ISBN:

Kimechapwa Na

KALAMU TULIVU PUBLISHERS


0718 97 56 59/ kalamutulivu@gmail.com

—2—
BUTI
LA ZUNGU

—3—
Hii ni hadithi ya kubuni
Haimhusu mtu yeyote aliye hai wala aliyekufa. Endapo
jina au tukio fulani litafanana na jambo liliwahi kutukia,
linalotukia ama litakalotukia, jambo hilo lichukuliwe kama
sadfa tu, na kuwa halikukusudiwa na mwandishi.

—4—
SURA YA KWANZA

M
aisha ni magumu sana. Binadamu nao hawana
jema, sijui nifanye nini kujitoa kwenye huu mtego.
Ila ngoja mtaji wa maskini ni nguvu zake
mwenyewe.

Katika jumba moja la kifahari zilisikika sauti zilizoleta


taharuki mtaani hapo, ziliwapa shida watu kung'amua
ishara ya sauti hizo. Ukiwa mbali ungedhani ni sauti ya
vigeregere kutokana na mazoea yaliyojengeka kwenye
jumba hilo ya kula bata. Lakini ukisogea kwa karibu zaidi
unagundua kuwa ni sauti za vilio zilizoambatana na
maombolezo.
Majirani wa eneo hilo walifurika kwa wingi kwenye jumba
hilo. Kila mmoja akiwa na dhati yake moyoni. Wapo
waliokuja kuonekana ili nao wasaidiwe wakiwa na shida
zao. Wapo waliokuja kuliona jumba hilo lilivyo kwa ndani.
Wapo na wale waliokuja kufuata minuso.
“Mh shoga yangu mbona kama mimi ndo nitakuwa
mrithi wa hii nafasi ya humu ndani”
“Hangaika tu litakukuta jambo mi simo!..”
Ghafla akaanzisha kilio “Uuwi!.. kwanini umeondoka,
kwanini umeondoka na bado tunakuhitaji. Aaah!.. mungu
huyu jamani”

—5—
“Hee!.. shoga kulikoni mbona hivyo?”
“We nawe nilikuwa nachukua ponti zangu bwana.
Hujamuona Mr Mlimboka akipita hapo. Nishakuambia hili
jumba litanihusu soon”
Mwenzie alimtazama na kumbenjulia midomo bila ya
kusema kitu.
Kikundi cha watu wanne kimesimama kujadili namna ya
kuendesha mazishi pamoja na maziko. Vichwa vyao
vinawaka moto, mwili wa marehemu bado haujafika na
muda wa kwenda kuzika umeshawadia.
“Kwani ukiwauliza wao wanakuambiaje” Aliuliza
mmoja wao.
“Wanashindwa kunipa majibu yaliyonyooka mpaka
sasa. Wanadai kuwa bado hawajamjua muuaji”
Akadakia mwingine.
"Uchunguzi huo uchunguzi gani muda wote huo, wanataka
kutengeneza mazingira yao kama kawaida yao eeh!."
Akadakia mwingine pembeni.
“Huu ni upuuzi sasa familia kubwa hivi tena ya
Mheshimiwa mambo yanaenda kombo, hii ni fedheha.
Kuna maana gani sasa wewe kuwa kiongozi wa serikali"
Aliongea mzee mmoja wa wastani akimnyoshea kidole Mr
Mlimboka.

Wakati wakiendelea kuongea simu iliita. Akasogea


pembeni na kuipokea simu yake.
“Eeh!.. Inspekta Major”

—6—
“Ndiyo Mr Mlimboka”
“Kuna habari gani huko watu wanasubiria mwili
twende kuzika”
“Kazi tumeimaliza, uchunguzi umekamilika na mwili
upo njiani unakuja. Baada ya uchunguzi wa muda mrefu
tumebaini wewe ndio muhusika wa kifo hiki, hivyo upo
chini ya ulinzi kuanzia muda huu”
“Eti nini?” Alisema kwa sauti iliyowashtua wale
aliokuwa nao karibu yake.
Aliiachia simu yake na kuanguka chini.

Wale waliokuwa nao ndio walikuwa wa kwanza kumwona.


Haraka walimkimbilia.
“Mr Mlimboka!.. Mr Mlimboka!..” Waliita bila
mafanikio.
Mr Peresi aliangalia pembeni akaiona simu ya batani ya
Mr Mlimboka, akaichukua na kuangalia mtu wa mwisho
kuongea naye, aliliona jina la Inspekta Major juu ya kioo
cha simu.
Mh mbona nashindwa kuelewa hapa, taarifa gani
aliyoipokea kwa Inspekta Major.
Walimbeba na kumuingiza ndani. Taharuki ikatanda pale
msimbani. Kila mmoja akiwa na hamu ya kutaka kujua
kilichojiri. Walipoingia ndani baada ya dakika tano Mr
Mlimboka akayafumbua macho yake. Alipepesa kulia na
kushoto akaona watu wamemzunguka. Jambo lililomshtua
sana. Aliinuka harakaharaka akakaa kitako. Kichwa
akakiinamisha chini. Akaikumbuka simu yake ndogo.

—7—
Aliiangalia mfukoni haipo. Kumbukumbu zilipomrejea
vizuri alikumbuka mara ya mwisho alikuwa anaongea na
mtu nje. Akataka kuinuka watu wakamkalisha chini.
Walihisi labda ameshapagawa.
"unatafuta nini" Aliuliza mmoja kati ya watu waliokuwa
wamemzunguka.
"Simu yangu ndogo siioni"
Mr. Peres aliingiza mkono wake mfukoni na kuitoa simu
ya Mr. Mlimboka. Aliipokea mkono wake ukiwa
unatetemeka. Alikimbilia kuangalia mtu wa mwisho
kuongea naye, ndipo akaliona jina la Inspekta Major.
Fahamu zinamrejea vizuri na kuikumbuka taarifa ya
mwisho kuipokea kutoka kwa Inspekta Major.
Anapiga kelele na kusema "Hapana!!." Mikono yake
ilishika ile simu yake kwa nguvu mithili ya mtu aliyekuwa
anafanya jaribio la kutaka kuivunja ile simu.
Wakati wanahitaji kumuuliza kilichomkuta wanasikia sauti
ya kishindo kinakuja kwenye uelekeo waliopo. Kila
mmoja aligeuza shingo yake kuangalia ule upande wa sauti
inapotokea. Baada ya sekunde kadhaa wanamuona mtu
mmoja amevaa buti kubwa akiwa amesimama mguu pande.
Walipopandisha macho yao juu kumtazama usoni waliona
nguo za polisi. Walipata shauku ya kuendelea kupandisha
macho yao juu ili kuweza Kimng'amua mtu huyo vizuri.
Wachache kati yao walimtambua, wengine wakaachwa
njia panda.
Mr Peresi alianza kuunganisha matukio. Alikuwa
miongoni mwa wachache wanaomjua Inspekta Major.

—8—
Alikumbuka yeye ndiye mtu wa mwisho kuongea na Mr
Mlimboka kabla hajazimia. Anashangazwa zaidi kumuona
tena Inspekta Major nyumbani kwa Mr Mlimboka.
“Habari zenu wakuu, mwili wa marehemu
umeshawasili tayari, kazi imebakia kwenu”
Watu wote walikaa kimya hakuna aliyemjibu.
Alimuangalia Mr Mlimboka aliyekuwa amezungukwa na
watu. Alimuangalia kwa jicho la kumhusudu,
akamwambia.
“Ninakuomba mara moja Muheshimiwa”
Kisha akatoka nje.
Watu wengi walishangazwa na kujiamini kwa hali ya juu
kwa Inspekta Major. Wengine walimuona ni mtu asiye na
utu. Kwakuwa alishindwa hata kutoa pole kwa wafiwa.
Mr Mlimboka akasimama kumfuata Inspekta Major.
“Mkuu malizia mazishi haya kisha tuonane kituoni
tayari kwa mahojiano kamili”
“Unataka kusema nini Inspekta, hivi kweli mimi
naweza kumuua mke wangu”
“Sura sio roho Mzee, sitaki kuamini hilo na pia sitaki
kutoamini, imani yangu itakuja baada ya kupata mahojiano
na wewe” Aliyatoa macho yake kuonesha msisitizo.
“Na kama kuna njama zozote zinazoendelea dhidi
yangu basi kuanzia wewe na wakubwa wako hamtakuwa
tena na kazi” Alisema Mr Mlimboka.
“Sawa najua huo uwezo unao mkuu, ila siwezi
ipindisha sheria kwa cheo chako. Uwe na siku njema”
Alibakia Mr Mlimboka akipigapiga miguu yake chini na

—9—
kukandamiza ngumi ukutani. Aliona ndo njia sahihi ya
kupoza hasira zake. Tumbo lake liliucheza mziki aliokuwa
anaucheza. Lilitingishika kama fuko la mashine.
Inspekta Major wakati anatoka alimuita mmoja kati ya
mapolisi waliokuwa wakiimarisha ulinzi pale ndani na
kumpa maagizo.
“Afande Jofu!..”
“Ndiyo Afande” Akasimama imara kwa ukakamavu.
Akabana makalio kutoa heshima kwa mkuu wake.
“Hakikisheni ulinzi unaimarika hapa, na kila kitu
kiende kama kilivyopangwa. Wazii!..”
“Wazi Afande” Akajibu Afande Jofu.
Harakati za kwenda kuupumzisha mwili wa marehemu
zilizidi kupamba moto. Awali mwili ulipangwa
kusafirishwa lakini kutokana na ufinyu wa muda ratiba
ilibadilika.
Watu walipanda kwenye vipando vyao na wengine
walipanda kwenye magari ya pamoja kuelekea makaburini.
Watu baada ya kuona jeneza la marehemu vilio
viliongenezeka. Ilikuwa ni ngumu kuwatambua wanafiki
na watu walioguswa kweli na msiba.
Mr Mlimboka alimuona kijana mmoja hivi kwa mbali.
Hakupendezwa na uwepo wake pale msibani. Haraka sana
alimuita Afande Jofu na kumpatia maelekezo.
“Nenda kamtoe yule kijana, sihitaji kumuona hapa”
Kidole chake alikielekeza kwa Innocent.
“Sawa mkuu” Akapiga saluti.

— 10 —
“ Kijana, huhitajiki kuonekana eneo hili” Alisema
Afande Jofu.
“Nimefanyaje tena kamanda?”
“Sidhani kama nina muda wa kukuelewesha zaidi. Tii
amri bila shuruti, toka eneo hili”
Innocent anamtazama Afande Jofu kwa huruma walau
amsikilize. Ilikuwa ni shauku yake kuwa sehemu ya msiba
ule. Alipoigeuza shingo yake alipata kumuona Mr
Mlimboka akiwa anateta na wenzie.
Alirejesha tena jicho lake kwa Afande Jofu. Ni kama vile
alikuwa anaunganisha matukio.
“Afande najua umetumwa kufanya hivi, ila naomba
ufanye jambo nishiriki mazishi haya ni muhimu sana
kwangu” Alisema tena Innocent.
“We kijana usinitafute ubaya, unanijua vizuri wewe?.
Nahesabu moja hadi tatu baada ya hapo nitajua mimi
namna ya kukutoa” Akameza funda la mate. Akaanza
kuhesabu.
“Moja!!.. mbiili”
“Innocent nenda, heri nusu shari” ilikuwa ni sauti ya
Suzi.
"Basi Afande usimalizie mi wala sio mbishi mwenzio"
Alisema Innocent huko akiyapandisha mabega yake juu.
Innocent hakutaka tena hesabu ya tatu ikamilike. Alitimua
mbio na kutoka nje ya geti.
Binti mmoja aliyeitwa Suzi alimtazama Innocent kwa jicho
la huruma. Na kutembea hatua kadhaa ili apande kwenye
gari.

— 11 —
Baada ya Innocent kutoka getini kuna jambo lilimjia
kichwani. Alitimua vumbi kwa mbio kama vile mtu
aliyeacha chakula jikoni. Alitokea mitaa ya Keko
akielekea Kwa Azizi Ali. Kila aliyemuona alishangazwa
sana na mbio zake. Alivua shati na kulishika mkononi.
Alipokaribia nyumbani akapunguza mbio zake. Alimuona
mzee wake ameanikwa nje jua likimpiga kisawasawa.
Machozi yalimbubujika. Alikita goti lake pembezoni mwa
mkeka aliokuwa amelalia baba yake. Jua lilikuwa kali sana.
Magoti yake yaliipata kasheshe yalipokutana na ardhi
iliyoiva kwa jua. Chozi lilizidi kumshuka baada ya
kumtazama baba yake aliyekuwa juani muda wote huo.
Alimbeba na kumuingiza kwenye kijumba chao. Mlango
nao ulikuwa wazi. Hata Athumani mlangoni hakuwepo.
Alimuweka kwenye kigodoro cha nchi 3. Kilikuwa cheusi
kwa nongo. Kiliisha kiasi cha kuondosha utofauti wa
kulala chini na kwenye hicho kigodoro, zaidi ya kukwepa
kulalia michanga tu.
Innocent alishindwa kumtazama baba yake. Alikaa chini
na kumpa mgongo, uso wake akiuelekeza mlangoni.
Kichwa kikajaa mawazo.
hivi huu nilioufanya leo ni upuuzi wa kiasi gani. Hivi
ni kweli nilikuwa nalazimisha kwenda kwenye mazishi ya
mke wa Mr Mlimboka ili hali baba yangu nilimsahau hapa
nje. Sijui nipatiwe adhabu ya aina gani kwa hili.
Moyo wake uliyasema mengi sana, akijutia kwa
alichokifanya. Aliongea na kujijibu mwenyewe.
Akamtazama baba yake, machozi yakashindwa kustahimili

— 12 —
kubaki ndani.
“Baba naomba unisamehe sana, nisamehe sana,
mwanao nilighafirika na nastahili adhabu kwa hili”
Mzee Batasi alimtaza Innocent naye akiwa anatokwa na
machozi. Mdomo wake ulikuwa mzito sana kunyanyuka
kutokana na maradhi aliyokuwa nayo. Alilazimisha kuitoa
kauli kwa mwanae ila mdomo haukupata nguvu ya
kufanya hivyo.
“Baba sema kitu basi mwanao walau nisikie sauti yako. Ni
mwaka wa nane sasa sijawahi sikia neno lako lolote kutoka
kwako, nashindwa kujua kiasi gani nakukosea baba
yangu”
Makamasi yanamtoka Innocent yakisindikizwa na machozi.
Sauti yake ilibebwa na mawimbi ya kwikwi.
“I..i..no!!..” Mzee Batasi alifungua kinywa.
“Baba!.. baba leo umesema baba, niambie kitu baba,
niambie mwanao baba” Machozi yakiendelea kumtiririka
Innocent. Yalichanganyika machozi ya furaha na huzuni
kwa pamoja. Alimuweka vizuri mapajani. Ili amsaidie
sauti itoke vizuri.
“Kwanza naomba unisamehe sana mwanangu, najua
shida ninazokupatia mwanangu” Anaongea kama mtu
ambae ameishiwa na hewa. Pumzi inatoka kwa shida sana.
“Kuna muda naona kabisa mimi ndio kikwazo cha wewe
kufanikiwa. Hufanyi kazi zako kwasababu yangu. Ukipata
nafasi chukua kisu uniue ili nikuondolee mateso
mwanangu” Machozi yanamtoka mzee Batasi. Sauti
inatoka kwa kukoroma.

— 13 —
“Baba usiseme hivyo baba, hata kama dunia nzima
ikikutenga baba mimi nitakuwa na wewe baba yangu”
Alisema Innocent.
“Kuanzia sasa fanya mambo yako ya maendeleo
usihangaike sana na mimi, mimi muda wangu wa kuishi
hapa duniani ni mdogo sana. Tafuta maisha yako. Na kama
nikifa leo urithi wangu upo kwenye hilo boksi hapo” Mzee
Batasi yakawa maneno yake ya mwisho kinywa kikagoma
kunyanyuka tena. Nguvu zilimuishia kutokana na nguvu
kubwa aliyoitumia wakati wa kuongea, ingawa sauti yake
ilitoka kwa shida sana.
Innocent yeye alikuwa mtu wa kulia tu. Ghafla kimya
kikatawala baada ya kuonana baba yake ameishiwa nguvu.
Alimlaza vizuri na kwenda kuangalia kitu kwenye boksi
lililopo pale pembeni yake. Macho yake hayakuweza
kuona kile alichokihitaji. Alitoka nje haraka haraka.
Akauona mkokoteni wake.
Alikumbuka kuwa ana oda za watu za maji. Aliuchukua na
kusambaza maji kwa watu wake. Akapata elfu mbili mia
saba.
Alikaa chini na kuanza kuigawanya ile hela. Mara hii sura
yake ilikuwa na tabasamu sana. Alipiga goti na
kumshukuru Mungu.
Alienda kwenye duka la madawa lililokuwa karibu na pale
nyumbani kwao, kwaajili ya kumchukulia baba yake dawa.
“Dokta naomba zile dawa za baba.” Akatoa noti ya
shilingi elfu moja.
“Ila ndugu unanipa sana majaribu, yani unakuja

— 14 —
kunikopa na deni lako halijaisha, Aah!.. bwanaa this is not
fare” Alisema Dokta.
“Sitaki kuamini kuwa hadi wewe nimeshaanza kuwa kero
kwako. Nivumilie tu ndugu yangu, yatapita tu haya.”
Alijibu Innocent. Dokta hakumjibu chochote. Alimpatia
dawa Innocent bila ya kumuambia chochote.
Baada ya kupatiwa dawa akaenda kuchukua unga nusu,
nyanya na mafuta robo.
Aliporudi nyumbani alimpatia baba yake dawa. Mzee
Batasi akawa anaashiria kwa kidole cha shahada kuwa
hataki dawa.
"Baba kunywa dawa unanitia unyonge mwanao,
ninaamini ipo siku Mungu atakuinua kama zamani na ndio
maana nakupambania baba"
Mzee Batasi akayapiga maji kofi na kuendelea kuonesha
ishara ya kutohitaji zile dawa kwa kidole chake cha
shahada.
Innocent alitoka nje na kuangalia kulia na kushoto.
Alipogundua hakuna mtu yeyote anayemuona, aliyafumba
macho yake kwa nguo aliyokuwa ameivaa. Alifanya hivyo
kwasababu alihisi baba yake akiona machozi yake atamtia
unyonge. Alipohakikisha machozi yake yamekata aliingia
ndani akiwa anatabasamu. Alichukua maji mengine na
kuendelea kumbembeleza baba yake anywe dawa. Jitihada
zilizaa matunda. Mzee Batasi alizimeza zile dawa ingawa
kwa tabu sana. Ni kama vile hakukuwa na mawasiliano
kati ya ulimi, Koo na tumbo. Hata nguvu ya kusukuma
dawa hakuwa nazo tena. Alipoiona hiyo hali akachukua

— 15 —
kijiko cha chakula na kumpondea zile dawa zingine
zilizobaki, kwenye kijiko na vimaji kidogo, hapo ndipo
ulipopatikana mwarobaini wa kunywa ile dawa. Innocent
akachukua mafiga na kuanza kuyapanga ili akoke moto
kwaajili ya kupika. Alipuliza moto ili uwake. Alipuliza
zaidi na zaidi hadi moto ukashindwa kuelewa unapulizwa
ili uwake au uzime. Macho yilitokwa na machozi kwa
moshi wa jikoni. Hata michanga nayo iliyokuwepo pale
chini iliyasulubu macho yake baada ya kuwa anapuliza
moto ule kwa nguvu kubwa sana.
Moto ukawaka na kuanza kupika.

— 16 —
SURA YA PILI

N
yumbani kwa Mr Mlimboka kuna ugeni ulimjia
asubuhi asubuhi. Mr Mlimboka bado kichwa
chake hakipo sawa. Hakuwa na hamu ya
kuzungumza na mtu yeyote. Mr Peresi ndiye alimtembelea
Mr Mlimboka asubuhi hiyo.
"Kaka acha kuchanganyikiwa kiasi hicho tatizo lako ni
dogo sana"
"We una akili sawa" Aliuliza kwa sauti ya ukali.
"Najua unajiuliza vipi kesi ya mauaji inaweza kuwa
ndogo. Ngoja nikuoneshe kitu"
Mr Peresi alinyamaza kimya na kutazama mlangoni. Mr
Mlimboka aliyafuata macho ya Mr Peresi.
Mlangoni anatokea mtu mmoja aliyevalia suti nyeusi na
kiatu cheusi. Mkononi ameshika begi la mkononi.
Halikuwa na utofauti na lile begi la maamuzi la Jaji
mahakamami. Alilishika kwa umakini kana kwamba
amebeba nyaraka nyeti za serikali. Alisogea na kuchukua
nafasi yake kama walivyokuwa wameketi wenzake.
"Mbona unaleta maigizo mdogo wangu" Alisema Mr
Mlimboka.

— 17 —
"Hakuna maigizo hapa, huyo unayemuona hapo ni
advocate aliyewahi kusimamia kesi kubwa zaidi ya hii.
Kwa jina anaitwa Matonya. Mr Matonya kutana na kaka
yangu anaitwa Mr Mlimboka nina imani habari zake
unazo"
"Namjua vizuri sana" Aliweka kituo akimtazama Mr
Peres. Akirejesha shingo yake kwa Mr Mlimboka. "Ni
kweli anachokueleza mdogo wako. Nipe imani yako
niifanye hii kazi" Alisema yule mwanasheria.
Mr Mlimboka moyo wake ulianza kupata faraja. Alianza
kujiambia mwenywewe moyoni mwake.
Hatimaye Mungu kasikia kilio changu.
Hakumjibu chochote mwanasheria. Alichokiweza ni
kutikisa kichwa tu kwa ishara ya kumpa ruhusa.
Mr Matonya alinyanyuka na kuondoka zake.
Wakati anatoka mlangoni anakutana na kijana mwingine
akiingia nyumbani kwa Mr Mlimboka. Hakuna
aliyemsalimia mwenzake. Walipishana kama vile watu
waliokutana kilingeni kwa mganga.
"Enhe!..bora umekuja, nilikuwa nataka kukupigia simu
sasa hivi hapa" Alisema Mr Mlimboka na kuchukua glasi
ya maji iliyokuwepo mezani na kupiga funda moja.
Akaongeza tena kwa kusema.
"Kaa chini sasa mbona unanisimamia"
Yule kijana alikaa kwenye sofa zilizomtia hamu ya kulala.
Mwili wake na uso wake vilitoa taarifa hiyo.
"Mudi mipango inaenda kama tulivyokubaliana?"
Alimuuliza Mr Mlimboka yule kijana.

— 18 —
"Mipango yote umeishika wewe, na..."
"Naa... Nini?" Akadakia Mr Mlimboka kwa sauti ya
juu.
"Namaanisha kuwa, tangu umepatwa na huu msiba
mambo yote yamesimama" Alisema Mudi huko akiwa
anafinyafinya vidole vyake vya mikono.
"Hakuna jambo kama hilo. Mimi mambo yangu yote
nimeyakamilisha. Tayari nimeshakupangia nyumba Goba.
Na mahari nimemtuma mshenga muda mrefu tu aipeleke.
Kwa hiyo kesho kutwa ndoa ipo pale pale"
"Mi sina neno tena nilikuja kujua hatma ya jambo hili"
"Ila mimi kwenye harusi sitakuwepo, kwahiyo shika
hiki kiasi ili na wewe ujiandae na mambo yako"
Alivuta droo iliyokuwa karibu yake na kutoa vitita vitano
vilivyofungwa vizuri na kumkabidhi.
Mudi alipokea kile kiasi mikono yake ikiwa inatetemeka.
Ni kama alikuwa haamini kile kinachotokea.
Mudi alinyanyuka na kuondoka. Alipofika mlangoni alisita
kutoa mguu wake nje na kugeuza shingo yake nyuma.
Alimtazama Mr Mlimboka.
"Lakini boss vipi kuhusu mke wangu" Aliuliza Mudi.
"Utamlisha njaa?" Alijibu kwa kifupi Mr Mlimboka.
Mudi alishindwa kuongeza lolote tena. Miguu yake
ikakuchukua ustaarabu wa kuondoka.

***********
Jua la utosi linazidi kupamba moto. Watu wanaendelea
kusaka riziki zao tonge liende kinywani. Innocent kama

— 19 —
kawaida yake na mkokoteni wake. Alipita katika nyumba
moja iliyokuwa mtaa wa jirani yao kupeleka oda zake
kama ada yake.
"Mama mkwe leo unachukua dumu ngapi?" Aliuliza
Innocent.
"Nipe dumu tano tu. Lakini Jumamosi uje asubuhi na
mapema kuna mapipa uyajaze"
"Eh!..Mama Suzi kuna nini tena mkwe, maana sio
kawaida yako"
"Utasutwa shauri yako, kazi yako si kuteka maji"
Alijibu Mama Suzi aliyekuwa anachambua maharage.
Innocent alicheka na kuendelea kumimina maji katika
ndoo za Mama Suzi. Alipogeuka pembeni alimuona Suzi
akikatiza akielekea chooni. Jicho la Suzi lilibeba ujumbe
kwa Innocent. Kwa mbali machozi yalikuwa yanamlenga.
Mkononi mwake alishika karatasi aliyoikunja kunja kama
pipi. Aliidondosha chini kwa kudhamiria na kumuonesha
Innocent aende kuifata.
Innocent alimtazama Mama Suzi akagundua kuwa akili
yake ipo kwenye maharage. Alijongea mdogo mdogo
kwenye uelekeo wa ile karatasi na kufanikiwa kuiokota.
"Wewe zungu huko umetoka wapi?" Mama Suzi
aliongea kwa kupayuka na kuelekea kule alikotoka
Innocent. Hakufanikiwa kuona chochote.
"Nimetoka chooni mama Mkwe" Akajibu kwa upole
Innocent.
"Ukome kuniita mkwe, usinichulie mchana wote huu"
Innocent alibaki akimshangaa Mama Suzi maana haikuwa

— 20 —
kawaida yake. Lakini hakuuruhusu moyo wake utawaliwe
na maneno yake.
Alichukua mkokoteni wake na kuendelea na Safari. Jua
lilikuwa kali mno. Ngozi yake ilimuiva. Ilimbidi atafute
sehemu kwanza alisubiri jua lipungue ili kuzuia asije
akaathirika zaidi.
Uchakarikaji wa Innocent uliwashangaza sana watu wengi.
Hasa pale walipoutazama ulemavu wake wa ngozi na
mapambano yake ya maisha. Ni mtu ambaye aliogopa vitu
vya watu. Hakuwahi kupenda cha bure. Aliamini sana
katika upambanaji. Wakati akiwa amekaa kwenye gogo
mawazo yalimjia. Aliwaza kufanya mambo makubwa
katika maisha yake ambayo nafsi yake iliyatamani.
Kichwa kakiinamisha chini. Akiwa ameshika tama.
Maisha ni magumu sana. Binadamu nao hawana jema,
sijui nifanye nini kujitoa kwenye huu mtego. Ila ngoja,
mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe.
Ni maneno yaliyokuwa yakipita moyoni mwa Innocent.
Akijaribu kuuwazia ugumu wa maisha anayoyapitia.
Wakati ameshika tama, alishtuka na kuanza kujisachi
mfukoni. Uso wake ulitoa tabasamu baada ya kutoa
karatasi iliyokuwa mfuko wa nyuma.
Aliitazama ile karatasi kwa muda kabla ya kuifungua.
Mapigo ya moyo yalianza kwenda mbio. Mawazo
yakampeleka hadi nyumbani kwa kina Suzi. Swali lake
lilikuwa ule ujumbe unahusu nini.
"Oya Inno mama Kamongo kanipa ujumbe wako"
Ilikuwa ni sauti ya kijana mmoja wa mtaani hapo.

— 21 —
"Dah!!. Nilisahau aisee, ngoja nimpelekee haraka"
Shauku yake ya Kutaka kujua kilicho ndani ilikatwa na
taarifa ya Mama Kamongo. Haraka haraka alichukua
mkokoteni wake na kuelekea mitaa ya kurasini kwa Mama
Kamongo.
Usiku ulipoingia alirejea nyumbani kuupumzisha
mwili wake. Alipoingia ndani alimkuta baba yake amelala.
Aliangalia unga kwenye kindoo akakumbuka kuwa uliisha.
Alikimbia mchakamchaka hadi dukani kwa Mangi
kuchukua unga. Wakati anarudi njiani alipigana kikumbo
na mtu.
"Pole dada yangu usiku sioni vizuri, sijadhamiria
kukupiga kikumbo"
Alipoyainua macho yake juu aligundua aliyepigana nae
kikumbo alikuwa ni Suzi.
"Ahahaha!!. Kumbe muoga eeh, sasa maelezo yote
hayo ya nini" Alisema Suzi.
"Acha utani wako bwana, sipendi" Alijibu Innocent.
"Hebu ngoja kwanza uliusoma ujumbe wangu?"
"Hapana sikupata muda kipenzi ndio nimerejea
nyumbani sio muda"
"Jitahidi uisome" Alisema Suzi na kuondoka. Innocent
alimtazama Suzi hadi ukomo wa macho yake ulipoishia.
Uliporidhika moyo wake alishika njia ya kurejea
nyumbani.
Baada ya kumaliza kupika alimsogelea baba yake na
kumuasha.
"Baba! Baba.."

— 22 —
Aliita kwa sauti ya chini chini bila mafanikio. Aliutikisa
mwili wake nakuendelea kumuita.
"Baba!. Baba" Kila alipokuwa anamtikisa mwili wake
ulikuwa umelegea. Aliweka vidole vyake viwili cha
shahada na cha kati puani kwake kuangalia kama pumzi
inapita. Sura yake ikaanza kubadilika. Aliuweka mkono
wake wa kuume kifuani kwa Mzee Batasi. Mapigo ya
moyo hayakudunda kama kawaida yake. Pumzi ilikata
kabisa. Mwili wake ukawa wa baridi sana. Kijasho
chembamba na machozi vikaongozana pamoja.
"Baba.. Baba.. Baba!" Aliita kwa sauti ya ukunga.
Mikono yake miwili ikiwa inamtikisa mzee Batasi.
Alinyanyuka na kwenda kuchukua kikombe na kukijaza
maji pomoni. Wakati anataka kumwagia yale maji, mzee
Batasi alifungua macho yake.
Innocent akapiga goti harakaharaka na kumshika baba
yake mashavuni.
"Baba umeamka!." Aliuliza Innocent.
Mzee Batasi alitikisa kichwa chake kilichotoa ishara ya
ndiyo huko tabasamu likichanua usoni mwake.
Mzee Batasi alimshika mwanae kichwani kwa mikono
yake miwili kama vile baba mchungaji akitoa baraka zake
kwa kondoo wake.
Aliinuka pale alipolala na kukaa kitako. Innocent akabaki
akimshangaa baba yake. Ni muda mrefu sana hajamuona
baba yake akiwa amekaa kitako.
"Baba, unaweza kukaa mwenyewe?” Mzee Batasi alikuwa
anakazi ya kutikisa kichwa tu na kutabasamu. Hakuongea

— 23 —
chochote kile. Furaha ikawa imetanda ndani humo.
Innocent naye akatabasamu, akaweka chakula wale.
"Ila hiki ulichokifanya sijakipenda baba. Unataka kuniua
kwa presha sio" Alisema Innocent.
Mzee Batasi kazi yake ilikuwa ni kutabasamu tu.
Alikutanisha viganja vyake vya mikono kama masta wa
kichina. Aliomba msamaha kwa mwanae. Siku hiyo kila
mmoja alikuwa na furaha sana. Walitamani siku isiishe
maana kesho yao ilikuwa fumbo la mwelevu kumfumbia
mjinga.

**********

"Mzee huu mzigo ni mzito sana"


"Mzito kivipi na wewe ulisema kazi ni ndogo sana"
"Ni kweli nilisema ila sikuwa najua kama ushahidi
uliokuweka hatiani ni mzito hivi. Nilienda kwa Inspekta
Major nikamuomba ushahidi aliojiridhisha kuwa wewe ni
muhusika wa mauaji, kisu kimepimwa fingerprint
zimekutwa ni zako. Haikutosha hata CCTV camera zako
zinaonesha ukiwa umeshika kisu kikiwa na damu na
kukiachia chini. Hapo unadhani nakutoaje hatiani"
Mh kazi ya wanaume nimempa mvulana akaifanye. Ila
huyu muuaji inaonesha anachokifanya anakijua.
Mr Mlimboka alijisemea moyoni. Alimkodolea macho
yake kwa ukali Mr Matonya.
Miwani iliyokuwa machoni mwake aliiona mzigo. Akaitoa
na kuishika mkononi.

— 24 —
"Nisikilize we kijana, hebu achana na hii kazi mimi
naweza kuimudu" Alisema Mr Mlimboka kwa msisitizo.
Alinyanyua simu yake ya mkononi na kuitafuta namba ya
Mr Peresi. Akampigia.
"Eeh.. Halloo.." Alisema Mr Mlimboka baada ya
kupokelewa simu yake.
"Niambie kaka, mbona usiku sana" Akajibu Mr
Peresi.
"Upo serious kweli na maisha wewe, unaniletea vijana
wa field kuja kufanya kazi kwangu sio" Kisha akakata
simu.
"Pumbavu kweli huyu, mimi nimekaa najiachia hapa najua
mambo yapo sawa kumbe ndio kwanza mambo mabichi"
Aliongea Mr Mlimboka akiwa anazunguka huku na kule.
Trii!!.. trii.. trii!
Ulikuwa ni mlio wa simu yake ya mezani. Aliifata na
kuipokea.
"Inspekta Major hapa, unatakiwa kituo cha polisi
kesho asubuhi na mapema, over?" Kisha akakata simu.
"Halloo.. Halloo.." Mr Mlimboka aliongea mwenyewe.
Baada ya kugundua kuwa simu imekatwa aliipiga ile simu
ukutani kwa hasira. Ile simu ikaenda kupiga ukutani na
kuiangusha picha ya marehemu mke wake . Aligeuka na
kuiangalia, akaachana nayo.
Aliingia kwenye chumba cha CCTV Camera kuingalia
video yenyewe ushahidi wa mauaji.
"Haa!.." alipatwa na mshangao baada ya kuiona ile video.
kuna watu wana njama za kunitoa kwenye kiti changu. Au

— 25 —
wanahisi kuwa waziri wa mambo ya ndani ni raha sana
eeh.. Hapana nisipoangalia huu uchaguzi utakuwa mgumu
kwangu. Chama kitaniaminije, wananchi wataniaminije
nao.
Alijiuliza maswali ambayo hayakuwa na mjibuji
isipokuwa yeye mwenyewe.
"Mwanangu hebu kalale, usiumize sana kichwa kesho
nayo ni siku" Aliongea baba yake Mr Mlimboka. Kisha
akaondoka.

— 26 —
SURA YA TATU

U siku ulikuwa mnene sana jiji limezizima zii!


idadi ya watu barabarani ilikuwa ndogo mara
dufu. Walioamini riziki zao hupatikana usiku
bado walikuwa katika maeneo yao ya kazi wakiendelea
kusaka tonge.

Ndani ya jumba la waziri wa mambo ya ndani ulinzi


uliimarika sana. Kila kona ya nyumba kulifurika
maaskari waliohakikisha ulinzi nyumbani kwa Mr
Mlimboka. Kesi iliyokuwa inamkabili haikumfanya yeye
asipate ulinzi aliokuwa anastahili. Jeshi la polisi
liliendelea kumpatia ulinzi hadi pale kesi itakapofika
mahakamani na kusomwa kwa shitaka.
Nje ya uzio wa nyumba ya Mr Mlimboka kuna mtu
mmoja alionekana akiwa amevalia koti jeusi lililoanzia
juu hadi chini. Kichwani akiwa na kofia ya lile koti
iliyofika hadi katika paji lake la uso. Kabla ya kofia hiyo
ndani alivalia mzura mweusi uliomficha kiasi cha
kutomtambua. Usoni alivalia kinyago chenye rangi
nyeusi. Kabla ya kinyago hicho alivaa miwani
iliyomsaidia kumficha macho yake na kumuongezea

— 27 —
nguvu ya kuona mbali.
Amesimama katika moja ya pembe ya ukuta wa jumba
hilo na kuchungulia upande wa getini. Alimuona askari
akiwa amesimama na silaha yake mkononi, akiangaza
macho yake kuhakikisha ulinzi unaimarika.
Leo mbona ulinzi umekuwa mkali hivi.
Yule mtu alijisemea moyoni.
Alisogeza kidogo glovu alizokuwa amevaa mikononi na
kuangalia saa. Ilimuonesha kuwa ni saa nane kasoro
robo.
Nina dakika 20 tu za kuwepo eneo hili.
Alichungulia tena kumuangalia yule askari, aliuona
umakini aliokuwa nao askari huyo. Alichukua jiwe
akalirusha katika uelekeo aliopo yeye. Yule askari macho
yake yote yakawa kule aliposikia mchakacho wa lile
jiwe. Ilibidi asogee na gobole lake mkononi kwa
tahadhari kubwa. Yule mtu alisikia kishindo cha yule
askari kikija kwenye uelekeo wake. Alitoa mfukoni
spray na kujiandaa kuipuliza. Askari alipofika katika ile
pembe alipeleka uso wake kuchungulia kujua kuna kitu
gani. Palepale alipuliziwa ile spray na kumlewesha papo
hapo. Aliachia gobole lake likataka kudondoka. Yule mtu
alimdaka harakaharaka ili kisije kikasikika kishindo
akawashtua wenzie. Alimburuza pembeni na kumlaza
chali. Akapanda kwenye uzio kuchungulia ndani.
Akamuona askari amekaa kwenye kiti akiota ndoto za
usiku. Aliruka na kuzama ndani ya mjengo. Taa za
kunasa matukio zikawa zinazunguka upande aliopo yeye.

— 28 —
Akajificha kwenye mti mmoja wa kivuli uliokuwa
umejengewa mule ndani. Baada ya taa kuzungukia
upande mwingine alinyanyuka na kumnyatia yule askari.
Alimbana pua na kitambaa kilichokuwa kimepuliziwa
dawa na kupoteza fahamu za askari yule. Alimuweka
sawa shingo yake na kuiweka vizuri kofia yake kama
vile mtu ambae yupo macho.
Alienda moja kwa moja hadi nyuma ya nyumba hiyo na
kuona nyanya za CCTV camera, akachukua mkasi na
kuzikata zile nyaya. Akasogea pembeni kidogo
kulikokuwa na dirisha lililoachwa wazi. Alimuona mtu
mmoja akiwa amelala chali. Akachukua spray yake na
kumpulizia.
Alirudi hadi mlangoni ili aweze kuingia ndani. Akatoa
kitita cha funguo alizokuwa ameziandika namba.
Akachukua funguo aliyokuwa ameiandika namba 11.
Akajaribu kufungua ikashindikana. Akaangalia namba
22 alivyofungua mlango ukafunguka.
Aliingia hadi chumba alichokuwa amelala yule
aliyekuwa amempulizia spray.
Alisimama na kumtazama kwa sekunde 20 kama vile
alikuwa anafikiria maamuzi ya kuyafanya. Alichomoa
kitu mfukoni na kubonyeza sehemu kikatoka kisu.
Alikishika kile kisu na kukizungusha kwenye kiganja
chake cha mkono. Alinyanyua mkono juu akitaka
kumchoma yule aliyelala pale kitandani. Nafsi yake
ilisita kidogo. Wakati akiendelea kujishauri akasikia

— 29 —
sauti nje zilizomshtusha sana. Nafsi yake ikamwambia
inabidi afanye maamuzi ya haraka mno.
Mara hii alikinyanyua kisu juu kwa hasira sana na
kilipotua kitandani kilifikia sehemu ya moyo wa yule
aliyelala pale kitandani. Alikichomoa tena kisu na
kumtoboa toboa kwenye macho yake. Alishusha pumzi
chini. Akaamini kazi kaimaliza.
Akachukua karatasi akaiweka chini ya mto wa
marehemu. Na juu ya ile karatasi akaweka kisu chake
alichofanyia mauaji. Akamfunika shuka vizuri
marehemu kama vile amelala kawaida.
Alitoka nje na kuchukua waya mpya na kuutoa ule
aliokuwa ameukata katika CCTV CAMERA. Akarejesha
zile nyaya kama alivyozikuta ili watu wasije wakabaini
kama nyaya zilikatwa. Kisha akatokea huko huko nyuma
kwa kasi sana. Alikimbia, kuna sehemu alipofika
alikuwa amemuacha boda boda wake na kumuambia
tuondoke. Akampeleka hadi chamanzi kwa mkongo.
Yule boda alifunga breki nakupaki chombo pembeni.
Alishuka yule abiria wake na kumtolea kiasi chake cha
pesa kama sehemu ya malipo ya kazi aliyoifanya.
Aliipokea ile pesa kwa kutetemeka sana. Yule jamaa
alipoona anamchelewesha aliiweka ile pesa yake kwenye
mlango wa kuwekea mafuta wa pikipiki kisha
akaondoka zake. Yule bodaboda aliinua kinywa chake
akitaka kumuita yule jamaa lakini hakuweza kutoa sauti
kwa woga. Akawasha pikipiki na kuondoka.

— 30 —
**************
Jua limeshachomoza. Kutoa taarifa kuwa watu waende
kuchakarika. Innocent amelala pembezoni mwa baba
yake. Macho yake yakitazama juu ya bati. Aliumizwa na
mwanga wa jua uliopenya kwenye matundu yaliyopo
kwenye bati. Waliishi kwenye kibanda kilichowastiri
wasionekane kwamba wanalala nje. Lakini pindi
zilipokuja neema na mungu za mvua stara ilitoweka.
Hata jua lilipokuwa kali zaidi liliwawakia vikali mno.
Walijaribu kuomba misaada kwa serikali lakini
hawakupatiwa. Walituma maombi yakawa mengi mezani
hadi ikawa kero kwa viongozi wao. Zilipokuja pesa za
jimbo lao kwaajili ya kusaidia kaya maskini
hawakuweza kunufaika nazo.
Na hiyo haikuwa kwao tu. Hata watu wengine mtaani
hapo hawakuweza kupata walichokuwa wanastahili
kupata katika pesa zilizokuwa zinaingia katika jimbo lao.
Ulipokaribia muda wa uchaguzi mambo yalianza
kubadilika. Ilianzishwa miradi na kuachwa bila
kumaliziwa. Ili wagombea wapate pakuanzia wakati wa
kampeni.
Innocent na mzee Batasi hawakuwahi kunufaika kipindi
cha kiangazi wala masika.
Innocent aliamka pale alipokuwa amelala na kukaa
kitako. Fikra za mambo yaliyojiri siku ya jana zikamjia
kichwani. Akaikumbuka ile barua ya Suzi. Nguo
alizokuwa ametoka nazo kwenye mizunguko yake ndizo
alizokuwa amelala nazo. Kwahiyo haikumpa shida

— 31 —
kuitafuta barua yake.
Aliikunjua barua kwa unyenyekevu sana kama vile
Imamu aliyekuwa anaongoza sala msikitini.
Mapigo ya moyo yakaanza kwenda kasi. Hofu ikatanda
moyoni mwake. Mawazo yakamjia na kukumbuka pale
mama yake Suzi alivyokuwa mbogo siku ya jana.
Akaanza kuisoma barua.

"Inno babaa!!..
Imani yangu yanituma kwamba unajua kuwa nakupenda
kiasi gani.
Sikuwahi kujua kuwa pesa inaweza kununua utu wa mtu.
Taarifa fupi ni kwamba nimetolewa posa na kesho kutwa
jumamosi naolewa.
Siyafanyi haya kwa kupenda ila mama amenilazimisha
kipenzi.
Nakupenda sana. Natamani kuona unakuwa baba wa
watoto wangu.
Mpenzi wako Suzi"

Innocent aliifinyangafinyanga ile barua kwa hasira,


machozi yakimbubujika. Alichukua kiberiti na kuichoma
moto ile barua. Alichukua kokoteni na kuanza
kusambaza maji kwa wateja wake.

"Mh! Jamani mi mwenzenu nimechoka kuhudhuria


misiba ya Mr Mlimboka, au anawatoa ndugu zake kafara
ili ashinde uchaguzi"

— 32 —
Innocent aliyasikia maneno ya wadada waliokuwa
wamekaa barazani na kupiga domo.
Alichukua njia ya kuelekea keko kwa Mr Mlimboka.
Akaegesha kokoteni lake nje ya jumba la Mr Mlimboka.
Alizama hadi ndani akayakuta maturubai na watu
wachache waliokuwa wamehudhuria msibani.
Kabla hajakaa kwenye kiti alikuja askari mmoja na
kumuita pembeni Innocent.
"We kijana, mbona unapenda sana kuingilia maisha
ya watu" Alisema yule askari.
"Hapana afande, haya ni maisha yangu lakini"
"Una maana gani?"
Innocent alifikiria kidogo.
"Namaanisha hivi, mara nyingi mambo yanayotokea
kwenye jamii huwa napenda kuyavaa kama ya kwangu,
iwe kwa furaha ama huzuni" Alijibu Innocent.
"Lakini mwenyewe huwa hapendi kukuona kwenye
matukio yake"
"Najua" Akajibu tena Innocent.
"Jambo Afande!.." Alidakia yule Afande aliyekuwa
anazungumza na Innocent.
Innocent aligeuka kuangalia nani aliyesemeshwa.
Alimuona Inspekta Major.
"Jambo!. za kazi" Aliuliza Inspekta Major.
"Nzuri Afande"
"Nzuri eeh!.. jana mlikuwa mnafanyakazi gani hapa
ndani hadi mauaji yanatokea"
Kimyaa hakujibu chochote.

— 33 —
"Waite wenzio wote waje hapa, wazii!.." Aliamuru
Inspekta Major.
"Wazi Afande"
"Kijana ondoka eneo hili haraka sana" Alimgeukia yule
kijana baada ya kupokea maagizo kwa Inspekta Major.
Innocent akaondoka.
Askari wote walikusanyika, na kuanza kuhojiwa wale
waliokuwepo lindoni siku hiyo ili watoe maelezo juu ya
mauaji hayo. Kila mtu alijikanyaga, na hakuna
aliyekuwa na jibu sahihi la kwanini yametokea mauaji
hayo na wao walikuwepo.
"Unadhani jeshi la polisi litawafikiriaje, hata mimi
mwenyewe naanza kuwa na mashaka na nyie
haiwezekani askari watano mnashindwa kuweka ulinzi
humu ndani" Alisema kwa hasira Inspekta Major.
"Afande, tunaomba radhi kwa hili, ila nimegundua
kitu juu ya haya mauaji, yanaonekana ni mauaji ya
kisasi" Alijibu Afande Mabu. Moja kati ya maafande
waliokuwepo lindoni usiku wa jana.
"Una maana gani" Aliuliza Inspekta Major.
"Asubuhi baada ya kusikia ukelele kutoka ndani
niliingia hadi chumbani, nikakuta aliyeuawa ameuawa
kikatili sana. Mbali na hivyo nikauona huu ujumbe"
Inspekta Major aliipokea karatasi kutoka kwa Afande
Mabu.
Ujumbe uliomo ndani ulimfanya asadiki maneno ya
Afande Mabu. Wenzie walitaka kujua kilichopo ndani.
Ikabidi awasomee.

— 34 —
MTENDA HUTENDWA.
MUDA WAKO UKIFIKA. YATAKUKUTA ZAIDI YA
HAYA..
Kila mmoja aliusikia ujumbe uliokuwemo ndani ya Ile
karatasi. Wengine waliungana na maneno ya Afande
Mabu juu ya kauli yake ya awali. Wengine ikiwemo
inspekta Major hawakutaka kuamini kwa asilimia mia
moja juu ya jambo hilo.
Idadi ya watu ilizidi kupungu kwenye misiba ya Mr
Mlimboka. Wengine wakiamini kuwa anawatoa ndugu
zake kafara kwa maslahi yake binafsi. Maswali yalikuwa
ni kwanini vifo vinakuja kwa mfululizo kwenye nyumba
yake tu. Walioona umuhimu wa kuhudhuria walifika
msibani. Waliokuwa wamechoka na habari za msiba za
nyumba hiyo waliendelea na mambo yao.
"Endeleeni kuimarisha ulinzi. Wazii!.." Alisema Inspekta
Major.
Wakati anataka kuondoka alimuita Afande Mabu
pembeni.
"Kwanini ulikuwa unamwambia yule kijana Zungu
aondoke ili hali kaja msibani" Aliuliza inspekta Major.
"Yule kijana ni mhudhuriaji mzuri sana wa misiba
hapa mtaani, lakini Mheshimiwa huwa hataki kumuona
hapa kwake" Alijibu Afande Mabu.
"Unajua anapokaa" Akauliza tena Inspekta Major.
"Mh kusema kweli sijui Afande"
"Ok endelea na majukumu yako" Akaondoka.

— 35 —
*******
Vuguvugu la ndoa ya Suzi mtaani limeenea, ikiwa imesalia
siku moja tu kufikia siku ya harusi. Watu wa minuso hii
ilikuwa ni habari njema sana kwao lakini sio kwa Innocent
ambaye alikuwa anatembea njia nzima na kuongea peke
yake. Nguvu ya mapenzi ndio iliyochukua nafasi yake kwa
wakati huo. Anaelekea nyumbani kwa kina Suzi kupeleka
maji aliyoambiwa na mama Suzi. Nguvu za kuelekea kwa
kina Suzi alizitafuta kwa ugumu sana, maana alijua
anaenda kuumiza moyo wake. Huba limemzidia.
Alijilazimisha kwenda walau akamuone Suzi Kwa mara ya
mwisho.
Alipofika kwa kina Suzi aliwakuta wanawake
wametapakaa pale nje. Sare ya vijora ikiwa inatoa
msisitizo juu ya jambo la kesho. Waligawana majukumu.
Wengine wakiwa wanachambua mchele na wengine
walichambua viungo vya chakula.
Ulikuwa ni wakati wa Innocent kuonesha maana halisi ya
mwanaume. Kujikaza kutoonesha maumivu aliyokuwa
nayo moyoni mwake. Machozi yalipojaribu kumtoka
alikimbilia sehemu ya kujificha na kuyafuta machozi yake.
Aliporejea mbele ya waliokuwa pale uwanjani
aliilazimisha sura yake kuwa na furaha.
Aliyapepesa macho yake walau amuone Suzi kwa mara ya
mwisho. Alichobahatika kukiona ni sare tu zilizozidi
kumpa msisitizo wa siku ya kesho. Hiyo ikamfanya azidi
kufadhaika.
"Wewe fanya uende, we siunaona hapa kuna wanawake

— 36 —
tupu" Alisikika Mama Suzi Akisema.
"Sawa mama namalizia"
Mama Suzi alijua kuwa Innocent anajichelewesha ili
amuone Suzi. Jambo ambalo alihisi anaweza kuyatia
maharage mchanga. Tamaa za pesa zilimfanya aupuuzie
ukweli aliokuwa anajua juu ya Suzi na Innocent
wanavyopendana.

*************

Mr Mlimboka alifika kituo cha polisi ili achukuliwe


maelezo. Inspekta Major alihitaji kujiridhisha kwa maelezo
yake. Ingali alishaanza kuwa na wasiwasi wa Mr
Mlimboka kutohusika na mauaji yaliyotokea. Ila Imani
yake ilimtuma kuwa huenda chanzo cha mauaji anakijua.
Mjadala ulikuwa mrefu sana. Jambo lililomtesa Mr
Mlimboka kwenye hiyo kesi ni baada ya yeye kuwa na
kesi ya madai na mke wake. Alikuwa na mgogoro wa ndoa
na mke wake. Ambapo mahakama ili amuru wagawane
sehemu ya mali kabla mwanamke hajaondoka nyumbani
kwa Mr Mlimboka. Kabla jalada la kesi halijafungwa
ndipo yanapotokea mauaji ya mke wake.
Jopo la maaskari likiongozwa na Inspekta Major liliamini
kuwa huenda Mr Mlimboka akawa anahusika na hayo
mauaji ili kuepuka wasigawane mali walizozichuma wote.
Wakati mahakama inatoa uamuzi wa yeye kugawana mali
na mke wake. Alipinga vikali mno na kujaribu kuwatumia

— 37 —
mawakili wa aina mbalimbali walioshinda kesi kubwa za
kutisha lakini aligonga mwamba. Kinachomtesa Mr
Mlimboka kwenye hii kesi, ni kwasababu historia yake
bado inaishi.
"Mheshimiwa, sisi tunaitambua nafasi yako, ni mtu
mkubwa sana serikalini. Ila hiyo haitufanyi tuache kuiinua
haki iliyolala na kuilaza dhulma inayotembea" Alisema
Inspekta Major.
"Fanyeni kilichopo ndani ya uwezo wenu" Akajibu Mr
Mlimboka.
"Baada ya kuusoma ule ujumbe ulioachwa na muuaji
aliyemuua baba yako huna ulichogundua?" Aliuliza polisi
mwingine.
"Kila kinachoendelea mimi nakiona kama fumbo,
mbaya zaidi sijafanikiwa kulifumbua"
"Na ujumbe ulioachwa wakati wa mauaji ya mke wako
je?"
"Hata hilo pia sina nilichofanikiwa kukijua labda
mutekeleze wajibu wenu sasa" Akajibu Mr Mlimboka.
Walipoona hawajapata majibu waliyohitaji walimruhusu
Mr Mlimboka aondoke kuendelea na majukumu yake
mengine.
Alinyoosha moja kwa moja hadi makao makuu ya chama
chake ambacho kilimuingiza madarakani kupitia kura za
wananchi. Zilikuwa nyakati ngumu sana kwa Mr
Mlimboka. Kichwa kilizidiwa uwezo, furaha ilipokuja
kidogo haikupata muda wa kudumu iliondoka tena.
Wakati huu alikuwa kwenye nyakati za hofu sana, akiwaza

— 38 —
kupoteza nafasi yake. Chama chake cha DEMOCRATIC
PARTY walichozoea kukiita DP kilikuwa na mashaka nae
wakihofia kuipoteza nafasi, jambo litakalo wafanya kuwa
na idadi ndogo ya wabunge katika chama chao.
Walipoitazama nguvu na ushawishi wa Bwana Pallangyo
aliyekuwa mgombea kutoka chama pinzani cha FREE
STATE DEMOCRACY vichwa vilizidi kuwaka moto.
Wakati wakiwa wanaendelea kwenye kikao kulikuwa na
mtoa taarifa aliyepewa kazi ya kukusanya maoni kwa
wananchi juu ya uchaguzi wa mwaka huo. Wakampatia na
kazi ya kuwachunguza wapinzani wao na kuangalia uimara
wao pamoja na madhaifu yao. Kidole cha Haidari kilikuwa
juu akitamka neno taarifa.
"Taarifa mkuu" watu wote walimgeukia yeye.
Akaruhusiwa kutoa taarifa.
"Wananchi bado wana imani kubwa na sisi, ila kwa
taarifa nilizonazo zinaeleza Bwana Pallangyo yupo tayari
kuivaa fitna ya siasa. Na ameahidi kufanya hila ili
akuporomoshe katika jimbo lako, mwisho wa taarifa"
Kila mmoja alimsifu kwa kazi yake iliyotukuka.
Amekuwa mletaji taarifa nzuri zinazowapa mbinu za
kumshinda mpinzani wao.
Lakini taarifa hiyo iliwaumiza sana kichwa. Taarifa
ikazua mjadala mwingine. Kila mtu akawa anashuku
huenda hata mauaji yanayotokea kwa Mr Mlimboka ni
moja ya hila zake. Kikao kikaweka maazimio ya kurejesha
jimbo mikononi mwa chama cha DP. Mwenyekiti wa kikao
ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa chama cha DP

— 39 —
aliahirisha kikao hadi wakati mwingine watakapoitana tena.
Akampa moyo Mr Mlimboka na kumtoa hofu kuwa chama
kitampambania. Kikao kikahitimishwa.
Wakati anarejea nyumbani alipitia maeneo ya
Mtongani na kupita karibu na nyumbani kwa kina Innocent.
Aliipaki gari yake pembeni na kushuka kijana aliyevalia
nguo nyeusi kuanzia juu hadi chini pamoja na viatu vyeusi.
Macho yake yakifichwa na miwani myeusi. Mikono yake
aliitanua kama vile alikuwa anamzuia mtu asipite, uso wa
mbuzi uliomuogopesha kila aliyemtazama. Ulipomtazama
usoni unaweza dhani hajawahi kucheka maishani mwake.
Viganja vyake vya mikono vilifunikwa na glovu nyeusi.
Alishukia mbele kwenye usukani wa gari. Akaelekea hadi
kwenye kijumba cha kina Innocent. Akamkuta Innocent
anapika uji kwenye jiko la mafiga. Akihangaika kuupuliza
moto uwake. Alifika na kupiga teke ile sufuria yenye uji.
Ilibaki punje uji ummwagikie.
"Wewe kijana umeshaambiwa uhame hili eneo hutaki
kuelewa. Au unataka kufukua makaburi" Aliongea yule
kijana aliyeshuka kwenye gari.
"Sasa mnataka mimi niende wapi jamani. Hapa ndo
nyumbani kwetu, unadhani nitaenda wapi" Aliongea
Innocent kwa kitete. Uso wake ukiwa umebeba hofu
iliyojaa ndani ya moyo wake.
"Unadhani machozi yako yanaweza kubadilisha hii
amri, sasa sikia una siku tatu tu za kuendelea kubaki hapa,
laasivyo tusilaumiane"
Alipomaliza kusema maneno hayo alipanda kwenye gari

— 40 —
na kutimua vumbi. Majirani walishuhudia kila kitu
kilichokuwa kinaendelea. Ila walikosa nguvu ya kumsaidia.
Na kila aliyejaribu kumsaidia yalimkuta mambo
yaliyomfanya aachane na masuala yanayomuhusu Innocent
na maisha yake.Maisha ya Innocent yalikuwa filamu ya
kuchekesha na ya kuhuzunisha kwa wakati mmoja.
Waliomzunguka waliamua kuyazoea maisha yake. Jambo
hilo lilimfanya hata yeye mwenyewe kuyazoea maisha
yake. Maana hata alipolia hakupata mtu wa kuyafuta
machozi yake.
Watu walijua analia kwa yale wanayoyaona. Kumbe
alikuwa analizwa na mambo mengine aliyoamua
kuyafanya yawe siri yake. Ilimlazimu afanye hivyo, maana
isingekuwa rahisi watu kuisikiliza na kuielewa hadithi
yake ambayo angeamua kuwahadithia watu
waliomzunguka.
Muda wote alipokuwa anapitia adha kama hizi
alijitahidi kumficha baba yake asijue ili asimtie simanzi.
Kwa isiyo bahati nzuri baadhi ya mambo yalikuwa
yanafanyika mbele ya macho yake. Hivyo haikuwa rahisi
kumficha asijue.
"I.. I.. Ino.. cent mwa..nangu" Aliongea mzee Batasi
kwa shida. Akaendelea kuongea tena.
"Haya yo..te, u_unayapitia kwa..kwasa..babu yangu.
Vumilia i_i_ipo siku yata..isha"
Ni maneno ambayo Innocent hakupenda kuyasikia hata
mara moja. Kwani yalikuwa yanamuumiza mara dufu.
Alishajaribu kumwambia baba yake asiongee maneno

— 41 —
hayo, ila ni sawa alikuwa anampigia mbuzi gitaa.
Kwakuwa usiku ulikuwa umeshaingia alichukua nguo
zake kadhaa na kuzitandika chini alale.

— 42 —
SURA YA NNE
" Walisema haolewi mbona kaolewa, walisema haolewi
mbona kaolewa"
"Aiyaiyaa kuolewa utarudi nyumbani kuteembea,
Aiyaiyaa kuolewa utarudi nyumbani kuteembea"
Hizo zilikuwa sauti zilizokuwa zinasikika uwanjani kwa
Mama Suzi. Watu walijaa tele. Vijora vimechomekewa
kwenye nguo za ndani. Wadada wakishindana kuonesha
ufundi wa alivyowapa mungu.
Mziki ulikuwa mkubwa watu wakashindwa kusikilizana.
Mama Suzi uwanja mzima ulikuwa wake akitamba.
"Wapo wapi walosema atazeeka nyumbani" Aliuliza
Mama Suzi kwa sauti ya juu.
"Wamechinaa!!." Walijibu wadada wapatao sita hadi
saba waliokuwa wamevaa sare tofauti na wenzao. Sauti
zao zilikuwa kubwa zilizomeza sauti zote pale uwanjani.
Innocent alifika kwa kujificha akimtazama Mudi
alivyomkamata Suzi. Alitamani asogee walipo
awaachanishe mikono yao lakini haikuwa ndani ya uwezo
wake.
Bibi na bwana harusi wamekaa kwenye kiti wakipokea
zawadi. Innocent akashindwa kujificha. Akaamua
kujumuika na wenzie ilii ashuhudie vizuri kinachoendelea.
Huyu jamaa mbona namfahamu, na ana mke wake.

— 43 —
Anataka kumfanyia nini mtoto wa watu. Au ni njama za Mr
Mlimboka hizi. Aaah!!.. Sasa kwanini afanye hivi lakini
kama ni yeye kweli.
Innocent alishika shavu akiwa anaongea mwenyewe ndani
ya moyo.
"Oya wee!.. Mbona umekaa kihasara hasara hapa
mtoto ndo anaondoka hivyo"
Alikuwa ni jamaa mmoja aliyekuwa amevaa pama nyeusi.
Amesimama kando ya Innocent akimdhihaki kwa maneno
ya kejeli. Innocent aliona jibu la mjinga ni ukimya.
Hakuwa na hamu ya kufanya mizaha kwa wakati huo.
"Jamani Innocent wangu" Alisema Suzi kwa sauti.
Ikatanda taharuki harusini. Kila mmoja aligeuka na
kumtazama Innocent. Haikuwa ngumu kumtambua maana
alikuwa kijana maarufu mtaani hapo.
Wambea wakaanza kuchekea chinichini.
"Oya nyie, sema nini ujue, ngojeni tule kwanza cha
mtume halafu hayo mambo yenu mtayamaliza" Ilikiwa
sauti ya kijana aliyekuwa amejifunga kitambaa chekundu
kichwani. Mashavuni amejiweka bandeji. Tembea yake
ilielemea upande mmoja. Macho mekundu
yaliyosababishwa na sigara alizokuwa ana vuta. Akaweka
sigara mdomoni na kuvuta funda la moshi. Alipumua na
kutoa moshi kwenye matundua ya pua na mdomo. Watu
wakamgeukia. Wengine wakaunga mkono hoja.
Suzi akazidi kuita "Inno.. Inno mpenzi njoo uniokoe
kipenzi"
Mama Suzi akatoka ndani haraka haraka na kuita "Mwizi!..

— 44 —
Mwizii!.. " Kidole chake akimuoneshea Innocent. Watu
wote walimkimbilia Innocent. Kila mmoja alishika silaha
aliyokuwa anaiweza. Ghafla Innocent akawa mwana
riadha. Hazikupita sekunde tano Innocent hakuonekana
eneo lile.
"Mhh!. Shoga una roho ngumu wewe. Mh aah!!. we ni
kiboko" Alinong'ona mama Ashura shoga yake Mama
Suzi.
"Huyu mtoto mwehu sana. Anataka kuniharibia
shughuli" Akaweka Kwanza kituo. Akameza mate.
Akachukua mtandio aliokuwa amejifunga kiunoni na
kujipepea, jasho likimchuruzika.
"Mwenzio nimepokea hela nyingi sana ya mahari ya
mwanangu. Haya anataka kuniharibia hapa, hizo hela
nitazinyea wapi na nimeshakula zote mwenzio. Tena
asinipande kichwani huyu mtoto nilimwambia hapa
asikanyage kabisa kwasababu haya niliyajua" Mama Suzi
anaongea kwa kuhema. Anazunguka huku na kule. Sura
imekuwa nyekundu ghafla kwa hasira.
Huko uwanjani zikaanza kusikika sauti. Upande wa
mwanaume wanadai wamedhalilishwa. Wamechachamaa
wanataka kuisusia ndoa. Mama Suzi presha imepanda
anataka kuzimia.
Wazee wa mtaa wakaanza kuwabembeleza ndugu wa
mume. Ili walii usiingie mchanga. Wakubwa kwa
wakubwa wakaongea na kuyamaliza. Huo ndio ulikuwa
uzima wa mama Suzi. Aliamka kama sio yeye aliyekuwa
ataka kukata roho dakika kadhaa zilizopita.

— 45 —
Kikaingia kigoma. Watu wakaanza kumwaga radhi.
Ukawadia muda wa uliokuwa unasubiria kwa hamu na
watu wengi. Watu wakala na kusaza.
Bwana harusi akaingia kwenye gari na mkewe. Watu
wakawasindikiza na nyimbo za kuwaaga.
"Aiyaiyaa kuolewa utarudi nyumbani kuteembea,
Aiyaiyaa kuolewa utarudi nyumbani kuteembea"

*************

Innocent anarudi nyumbani kwao anaukuta mlango upo


wazi. Anangia ndani hakuti mtu yeyote. Jambo hili
lilimchanganya mno. Anajua kuwa baba yake hawezi
kutembea, halafu hamuoni ndani. Sasa atakuwa ameenda
wapi. Ni swali alilokuwa anajiuliza. Alitoka ndani na
kuzunguka nje ya kijumba chao kuangalia kama atakuwa
amelala uwani, lakini hakukuta mtu. Katika harakati za
kuendelea kumtafuta baba yake, akaziona alama za gari
iliyokuwa imeegeshwa karibu na kijumba chao. Alirudi
ndani akaachana na zoezi la kumtafuta baba yake.
Alichukua boksi moja lililokuwa kwenye pembe ya ukuta,
akakuta shati yenye mikono mirefu. Akabadilisha nguo
aliyokuwa ameivaa na kuivaa ile iliyokuwa kwenye boksi.
Siku hiyo hakuona salama kulala nyumbani kwao. Alihisi
anaweza kupata madhara. Akiamini kuwa dalili ya mvua ni
mawingu.
Akaenda moja kwa moja hadi gongo la mboto kwa rafiki
yake. Siku hiyo hakukuwa na foleni barabarani. Hali hiyo

— 46 —
ilichagizwa pia muda alioianza safari yake. Ilikuwa ni
majira ya usiku. Magari mengi yalikuwa yameshapumzika.
Rafiki yake Innocent alihitaji kujua kilichomleta Innocent
usiku ule maana haikuwa kawaida yake.
Innocent hakutaka kumueleza chochote kile rafiki yake.
Alimuomba walale kisha mengine watayazungumza kesho
kukicha.
"Lazima nijue mwanangu, maana usije ukakinukisha
maskani"
"Oya Pilato, nielewe basi mwanangu. Niache
nipumzike au kosa kuja kwako" Alijibu Innocent.
"Aah!.. Hamna kichaa wangu, ila siunaelewa
mwenyewe mazingira ile namna gani vipi"
Innocent mara hii hakumjibu chochote aligeukia ukutani
na kulala akimuacha Pilato akijiongelesha mwenyewe.
Alipoona hapati ushirikiano wa anayeongea nae, aliamua
nae anyamaze kimya.
Maisha ya pilato yalikuwa yatofauti kidogo na Innocent
japo kwenye ugumu wa maisha walikuwa wanarandana.
Muda wa kufanya kazi wa Pilato ilikuwa ni usiku. Alikuwa
anafanyakazi kwenye kiwanda cha Pepsi Vingunguti.
Maisha yalikuwa magumu sana kwake. Ambacho
hakukipenda ni kuwakiwa na jua. Aliona bora auone
mwezi huenda ungempa tumaini la kesho yake. Jua kwake
aliliona kama nuksi kwenye maisha yake. Kuna muda pia
alihisi chanzo ni shule. Alikataa kusoma pindi wazazi
wake walipotaka kumsomesha. Ngao yake ilikuwa ni
wangapi wamesoma wakafanikiwa.

— 47 —
Kwenye nyakati ngumu alizonazo anatamani kurudisha
muda nyuma ili arudi tena darasani. Mwenda tezi na omo
marejeo ngamani. Hawezi tena kurudisha muda nyuma.
Ikienda imeenda. Alisahau kuwa muda ni hazina isiyo na
mfano. Na zama nazo hudumu kwa matukio.
Alichukua kibegi chake kilichokuwa na na nguo mbili za
kubadilisha akifika kazini. Alipotoka akarudi mbiombio.
Akaangalia chini ya uvungu wa kitanda ambacho mhimili
wake ulikuwa na matofali na juu ikapitishwa mbao pana
iliyoenea sehemu ile. Mkono wake ulitoka na mibuti
mikubwa iliyokuwa ni lazima awe nayo kiwandani kwa
usalama wake.
"Oya mi natoka nikahangaike kidogo" Alisema Pilato.
Innocent alimgeukia Pilato.
"Unaenda wapi sasa?" Akauliza Innocent.
"Naenda kusaka ugali"
"Hivi bado upo kulekule tu"
"Oya we, nimechelewa bwana ngoja niwahi, sawa"
Pilato akatota na kubamiza mlango kwa nguvu. Innocent
alivuta shuka hadi usoni na kuzialika njozi za usiku.

**********

"Wewe mbona umekuja kujilaza hapa asubuhi


asubuhi"
"Nimeamua tu kwani kuna shida yoyote"
"Nitakukanda sasa hivi, maswali gani hayo ya kipuuzi"
"Mudi tafadhali tafadhali nakuomba uniache, fanya

— 48 —
mambo yako"
Maisha ya Mudi na Suzi hayakuwa ya maelewano hata
siku moja. Pesa ilinunua ndoa ikashindwa kununua penzi.
Suzi bado moyoni mwake yupo Innocent. Tamaa za mama
yake ndizo zilizomtenganisha na mpenzi wake.
Mudi aliona atoke nje kumuepusha shetani. Alienda
kufungua kibanda kimoja kilichokuwa ndani ya uzio wa
nyumba yao. Kuna mtu alikuwa ndani ya kile kibanda.
Alimfungua kitambaa cheusi alichokuwa amefungwa
machoni. Akaifungua na kamba aliyokuwa amefungwa
mikononi kwa nyuma. Kisha akamuwekea chakula chini.
"Kula hicho hapo cha mwishomwisho maana siku
zako zinahesabika"
Yule mzee hakumjibu chochote kile. Hata maana ya kula
kile chakula hakuiona. Uso wake unaonyesha ni mtu
aliyekata tamaa. Moyo umekosa tumaini lolote.
"Sikiliza wewe mzee batasi sijui batusi, tatizo
mnapenda sana kubishana na watu wenye mamlaka. Lile
eneo mliambiwa muomdoke mapema mkatafute makazi
mengine hamuelewi. Sasa haya ndo malipo yake" Alisema
Mudi.
Alipoona hajibiwi alichukua ndo ndogo ya maji na
kummwagia yote pale chini.
Alifunga kibanda na kumuacha peke yake mzee Batasi.
Alipogeuka nyuma alikutana na Suzi uso kwa uso. Mudi
uso wake ukaanza kuwa na mashaka, kuwa huenda Suzi

— 49 —
amejua kinachoendelea.
"Wewe huu mlango usije ukausogelea huu hapa" Alisema
Mudi.
Suzi aliitikia kwa kutikisa kichwa. Ila uso wake ukionesha
hamu ya kutaka kujua kilichopo ndani. Maana alimsikia
Mudi akiongea mwenyewe mule ndani.
Mudi alienda kwenye matembezi yake. Suzi nae akaelekea
dukani kununua vitu vya nyumbani.
"Mangi nipimie kama kawaida" Alisema Suzi.
"Usijari bosi wangu"
Alipopatiwa vitu vyake akaondoka kabla hajafika mbali
akasikia sauti ikimuita.
"Aisee!!.. Tajiri yangu"
Suzi akageuka nyuma.
Akaendelea Mangi.
"Njoo bwana tajiri kuna kamzigo kako"
"Halafu Mangi acha utani wako asubuhi asubuhi bwana,
nawahi kupika ujue" Akajibu Suzi.
"Njoo bwana tajiri kuna mjuba kaleta posa"
"Ahahahaha!!.. Halafu Mangi bwana, Sasa ole wako
nije uniambie upuuzi"
Mangi alitoa bahasha aliyokuwa ameiweka kwenye daftari
iliyokuwepo pembeni kidogo mwa mzani wake na
kumkabidhi Suzi.
"We.. Hivi vitu gani tena" Akauliza kwa kutahamaki
Suzi.
"Acha wenge tajiri kajisomee uone mwenyewe"
Suzi aliipokea ile bahasha lakini akiwa haamini kuwa ile

— 50 —
barua ni yake. Maana hakuwa mwenyeji sana pale mtaani.
Na hata ndugu zake hawakuwa na kawaida ya kumtumia
barua. Alipotazama uso wa Mangi alipata ujumbe
uliomjuza kuwa kweli yeye ni muhusika wa ile bahasha.
Ile bahasha ilimfanya akimbie hadi chumbani na
kujifungia mlango na kutaka kujua kilichopo ndani.
Alihakikisha kuwa mlango ameufunga madhubuti ndipo
alipoifungua ile bahasha.
Mapigo ya moyo yakaanza kubadilika. Moyo ukiwa
umetandwa na shauku kubwa ya kumjua mtunzi wa barua.
Dear Suzi.
Furaha yangu.
Uwaridi wangu.
Mwanamke wa ndoto zangu.
Natamani ujue kuwa nakupenda kiasi gani, kuna muda
natamani kukuonesha hilo, ila huba limefunikwa uwezo na
mali. Sina imani sana kama unafurahia ndoa yako.
Kwakuwa najua hiyo ndoa imekaa kimkakati.
Sina mengi sana kwako nilitaka tu utambue kuwa bado
unaishi kwenye ndoto zangu.
Nakupenda sana.
Innocent

Alipomaliza kuisoma sura ikawa imemezwa na furaha


iliyosindikizwa na machozi yaliyoshuka mashavuni
mwake. Aliikumbatie ile barua akizivuta hisia kana
kwamba ile barua ndio Innocent. Alicheka sana peke yake
chumbani.

— 51 —
Kumbe bado Ino ananipenda nilihisi atanichukia kwakuwa
nimeolewa. Mmwaah!!..
Moyo wake ulianza kushindana kujisemesha na kujijibu
wenyewe. Aliichanachana ile barua na vipande
vilivyopatikana aliviteketeza kwa moto.
**********
Mr Mlimboka na chama chake cha Democratic Party
vichwa vinawaka moto. Mleta taarifa mezani anaeleza
kuwa Bwana Pallangyo wananchi wanamkubali zaidi.
Hasa hasa wananchi wamechoshwa na maendeleo ya
kimkakati. Viongozi wao hawaacha mara baada ya kupata
kura za ndio. Zinazowapa mamlaka ya kuwa viongozi.
Ahadi walizoweka hazikutekelezwa kama inavyotakiwa.
Walisubiria wakati wa uchaguzi ufike ndio waanzishe
mradi na kuuacha bila kuumalizia wakitafuta yakusema
katika majukwaa ya kuombea kura.
Sio kwamba wananchi wana imani sana na bwana
Pallangyo ila walikuwa wanahitaji kufanya majaribio ya
kuleta mabadiliko ya kiutawala.
Kila mtu anajaribu kujenga hoja zitakazowafanya
kumshinda mpinzani wao.
Ulibakia mwezi mmoja kuanza kampeni za wazi. Chama
cha Democratic Party kila kilipojaribu kupima kina cha
maji walikiona kina kirefu sana. Walibebwa na uzoefu tu.
"Lakini, mimi nina wazo, kama mpinzani wetu
ameamua kumshughulisha mgombea wetu. Vipi na sisi
tukashughulika nae"
Ilikuwa ni moja ya sauti za wajumbe wa kikao.

— 52 —
"Kumshughulisha aje, unamaanisha" Akauliza
Mjumbe mwingine.
"Yeye alisema kuwa atafanya juu chini kumfanya Mr
Mlimboka ahangaishwe na mambo mengine ili apoteze
nguvu na mvuto wa siasa. Na ni kweli hilo
tumelishuhudia"
Watu wote walikaa kimya. Wakitafakari namna ya kumjibu
mjumbe aliyotoa hoja.
"Enhee.. Kwahiyo ulikuwa una shaurije" Akauliza
mjumbe mwingine kwenye kikao.
"Tumtafutie skendo mbaya itakayomchafua kwa
wananchi"
Idadi kubwa ya watu walikubaliana na wazo la mjumbe wa
pili. Swali lilikuwa ni kashfa gani wanayoweza kumpa.
Wakati wakiendelea na mjadala simu ya Mr Mlimbiko
ikaita na akawaomba wenzake atoke nje kuongea na simu.
Alipomaliza kuongea na simu akarudi kuomba ruhusa
kuna dharura iliyojitokeza. Walijaribu kumueleza avumilie
kikao kiishe. Lakini alidai anaenda kuokoa maisha ya mtu.
Hilo likawa zito kwao. Ikabidi wampe ruhusa.
Mr Mlimbiko alielekea moja kwa moja hadi goba. Kuna
vijana watatu waliokuwa wamevalia suti nyeusi na miwani
iliyoziba mboni zao za macho. Pembeni yao alikuwepo
Mudi pia.
"Kuna shida gani mbona mmeniharakisha hivyo"
Akauliza Mr Mlimboka.
"Mkuu baada ya kupokea simu yako tu ile asubuhi

— 53 —
niliwashtua wenzangu haraka sana na kwenda nyumbani
kwa Mudi. Ila cha ajabu tulipofika hatukumkuta Mzee
Batasi" Aliongea kijana mmoja aliyekuwa kiongozi wa
wale vijana waliokuwa wamevaa nguo nyeusi.
"Eti nini nyie, acheni kunitania kabisa. Niliwaambia
mumchukue mukamuue. Halafu nyie mnaniambia
hammuoni. Msitake mnijue kwenye upande wangu wa pili
wa shilingi mimi sio mtu mzuri kabisa. Hakikisheni
munamtafuta na mummalize haraka iwezekanavyo" Mr.
Mlimbiko aliyatoa macho akiongea kwa msisitizo.
Wakati anameza mate. Wanakuja vijana wawili wakiwa
nao wamevalia suti zenye rangi nyeusi. Wakaita Mkuu.
Wote wakawageukia waliota.
"Taarifa tulizozipata ni kwamba yule mzee
ameshafariki, alikuwa ana jaribu kutoroka lakini njiani hali
yake ikawa mbaya, kuna watu walimchukua na
kumuwahisha hospitali na akafia huko huko hospitali"
"Umeenda hadi hiyo hospitali kuhakikisha" Akauliza yule
kiongozi wao.
"Yeah tulienda lakini mwili hatukuuona maana kuna
watu walienda kumchukua wakidai ndugu yao wakaenda
kuzika"
"Yees!.. This is how I need. Mudi una kesi ya kujibu
kwangu umeonesha uzembe wa hali ya juu sana. Kwenye
hili siwezi kukuacha. Utanieleza huyo mtu alitokatokaje
na wewe ulikuwa wapi"
Akaingia kwenye gari Mr. Mlimbiko na kuwatimulia
vumbi.

— 54 —
SURA YA TANO

I
nnocent aliamkia kituo cha afya kwaajili ya kwenda
kuchukua vidonge vyake ambavyo vilikuwa
vinamsaidia sana pindi anapopata mabadiliko ya ngozi
yake. Jua kali ya Dar es salaam lilikuwa adhabu kubwa
sana kwake. Ngozi yake ilikuwa nyekundu kila pahala.
Uso wake umejawa na vipele vilivyoanza kutunga usaha.
Hali hii ilimfanya hata ufanisi wake wa utendaji kazi
kupungua. Alichoshukuru ni utolewaji wa vidonge hivyo
bure kwenye hospitali za serikali.
Alipofika hospitali alienda hadi kwenye dirisha la dawa.
Akamkuta Nesi akiwa anachapa kitu kwenye kompyuta.
"Karibu, nikuhudumie nini" Innocent aliisikia sauti ya
Nesi Rose.
"Nimekuja kufata dawa zangu Dokta. Maana hii hali
imeshaanza kunisumbua"
"Ooh!!.. Pole sana. Haya kaa pale nitakuita"
Innocent alielekezwa akae kwenye benchi ambalo alikuwa
amelipa kisogo. Alimtii Nesi Rose na kwenda kuketi.
Nesi Rose alitoka na kuelekea stoo kwenda kuangalia
dawa za Innocent baada ya kugundua kuwa pale
zimemuishia.
"We Da Rose. Unaenda wapi muda huu"

— 55 —
Alikuwa ni Nesi mwenzie akimuuliza swali.
"Naelekea stoo kufuata dawa za yule kijana"
Alimnyooshea kidole chake Innocent.
"Hee!.. Wewe unahamu eh" Aliongea kwa sauti ya
chini na kumvuta Nesi Rose sehemu ya faragha. Akalivuta
sikio lake amnong'oneze.
"Unakumbuka ulivyoajiriwa wewe kuna mtu
ulipishana nae kwenye kitengo chako pale"
Akatikisa kichwa Nesi Rose.
"Yule hakuachishwa kazi bure bure. Ni kwaajili ya
yule kijana. Kiufupi ni kwamba yule kijana hatakiwi
kupata huduma ya aina yoyote ile hapa hospitalini na hilo
ni agizo kutoka juu, kuhusu nani kasema si wenyewe
hatujui"
Nesi Rose akamgeukia Innocent kwa jicho la imani. Uso
wake unaonyesha hana hatia. Ni kwanini hatakiwi
kupatiwa huduma hapa hospitalini. Hakupata jibu.
Alitamani kumsaidia ila lilipokuja suala la ugali wake hofu
ilimtanda moyoni. Alipogeuka ili aseme kitu yule Nesi
mwenzie hamuoni ameshaondoka.
Alimfata Innocent pale alipokuwa amekaa. Moyoni
anajiuliza ataanzia wapi. Alikaa kama sekunde thelathini
bila kusema kitu.
"Dokta, vipi mbona uso wako haupo na furaha au na
wewe hakuna vidonge"
"Unamaanisha nini kusema au na wewe" Akauliza kwa
mshangao.
"Hapana mara nyingi hapa huwa nachelewa nakujaga

— 56 —
vidonge vimeisha"
Nesi Rose alisikia sauti ya Innocent iliyobeba huruma
ndani yake. Kila alipohitaji kumjibu kuwa hakuna dawa
nafsi yake ilimkumbusha kiapo alichokula cha kutenda
haki na usawa.
"Unaitwa nani kwani" Akauliza Nesi Rose.
"Naitwa Innocent" Akajibu haraka haraka.
"Ok, sasa sikia hapa dawa kweli zimeisha. Ila kuna
namba nakupatia mpigie simu mwambie umepewa namba
na mimi atakuletea dawa hadi ulipo"
"I.. Ilaa.. Sina hela ya kuzinunua, nimekuja hospitali
ya serikali maana najua zinatolewa bure"
"Usijali kila kitu nita clear mimi"
Siku iliyofuata Innocent bado anahangaika kumtafuta baba
yake. Ingawa akili yake ilikuwa inahisi aliyefanya utekaji
nyara ni Mr Mlimboka lakini kila alipojaribu kufuatilia
taarifa za wapi alipomficho ilikuwa ngumu kuzipata.
Akazipata za chini chini kuwa yupo Goba kwa Mudi.
Hakusita kwenda hadi Goba kutafuta ushahidi wa hilo.
Alimini majirani zake Mudi wanaweza kumpa taarifa
kuhusu baba yake akiamini kuwa huenda walishawahi
kumuona. Baada ya kufuatilia kwa kina akaambiwa baba
yake ameshafariki tayari. Innocent alivurugwa sana.
Alienda moja kwa moja hadi nyumbani kwa Mudi
kujiridhisha juu ya taarifa alizozipokea. Alijua kuwa mida
hiyo Mudi yupo kwa mke wake mkubwa kwasababu alioa
kwa siri bila mkewe kujua. Kwahiyo muda wa usiku
alirejea Goba na kudai ametoka kazini. Na asubuhi

— 57 —
ilipoingia alielekea Magomeni alipokuwepo mke wake
mkubwa akidai usiku alikuwa kazini. Maisha yake
yaliendeshwa na Mr Mlimboka kwa makubaliano ya
kumuoa tu Suzi.
Baada ya kuzama ndani Suzi akasikia sauti ya geti
likifunguliwa. Aliogopa sana kwasababu hakukuwa na
kawaida ya mtu kuja pale mchana. Alifungua pazia na
kutazama ni nani aliyefungua geti. Akamuona Innocent.
Akayafikicha macho yake kuhakikisha kama alichokiona
ndicho chenyewe. Bado mboni za macho yake zilinasa
sura ya Innocent. Baada ya kujiridhisha alitoka nje
harakaharaka na kwenda kumkumbatia.
Wawili hao walishibana sana. Kila mmoja alionesha hisia
za kumkumbuka mwenzake. Suzi akimkumbatia Innocent
bila kumuachia. Innocent kila alipojaribu kumtoa, lakini
Suzi alimng'ang'ania tu.
"Mpenzi, nimekuja tuondoke wote. Upo tayari
kuondoka nami"
Suzi bila kushauriana na moyo wake akajibu ndiyo.
"Kama unachakuchukua kachukue tuondoke"
Suzi aliingia ndani na kuchukua simu yake pamoja na
nguo moja ya kubadilisha aliyokuwa ameiweka kwenye
kimfuko.
Walianza safari ya kuelekea Mtongani kwa kina
Innocent. Innocent alihitaji kujihakikishia kuwa baba yake
amerudi nyumbani au laa. Ilimbidi amsimulie Suzi yote
yaliyojiri siku chache zilizopita. Baada ya kugundua kuwa
baba yake hajarudi nyumbani imani ya kuamini kuwa baba

— 58 —
yake amefariki kweli ilianza kumjaa.
Akili yake haitaki kabisa abaki pale nyumbani. Ilibidi
waelekee tena gongo la mboto kwa rafiki yake Pilato.
Wamekaa kituo cha daladala wanangojea gari. Usafiri
ulikuwa wa tabu sana. Kila gari iliyopita ilikuwa imejaza
watu hadi mlangoni.
"Utaweza kweli kugombania gari" Aliuliza Innocent.
"Kwanini nishindwe na nipo vitani" Alijibu Suzi kwa
upole.
"Oya wee!.. Gongo la mboottoo!.. " Ilisikika sauti ya
kondakta akiita abiria.
"Oya wee nyeupe hiyo, njo upande"
Innocent ilimbidi acheke baada ya kuitazama hiyo gari
nyeupe inayotangazwa na Kondakta. Gari ilikuwa
imeshonana watu. Kila mmoja akipandisha kichwa juu
walau apate pa kupumulia.
"We dada hapo, sogea mbele kidogo nafasi ipo hapo"
Alisema yule Kondakta.
"Njo ukae wewe hiyo sehemu" Akajibu yule abiria.
Innocent na Suzi walikata shauri na kwenda kupanda gari.
Maana walisimama pale stendi hadi miguu ikataka kuingia
ndani.
"Wewe tulia apandwe" Alisema Kondakta baada ya dereva
kutishia kuondosha gari kituoni. huko akigonga bodi ya
gari.

*************
Simu ya mkononi ya inspekta Major inaita. Alipoitazama

— 59 —
aliliona jina na Afande Rose. Aliipokea na kuiweka
sikioni.
"Ndiyo Afande, za kazi" Alisema Inspekta Major.
"Mungu anasaidia. Nina taarifa fupi nataka kukupatia.
Taarifa tulizokuwa nazo zilikuwa ni sahihi, ni kweli yule
kijana haruhusiwi kupata matabibu kwenye huu mtaa wake
anaoishi, ikidaiwa na maagizo kutoka juu. Ila bado
sijamjua mtoa tamko" Alisema Afande Rose.
"Kazi nzuri. Endelea kufuatilia kwa kina hadi tupate
ushahidi wa kutosha. Wazii"
"Wazi Afande"
Akakata simu Inspekta Major.
Alinyanyua simu yake ya mezani ni kumpigia mtu
mwingine.
"Hakikisha hakuna mtu yeyote anayejua kuwa huyo
mtu yupo wapi. Nataka tuimalize hii kazi mapema sana"
Alipomaliza akakata tena simu.
Alichukua faili moja lililokuwa pembeni yake na
kulifungua. Akaikuta kesi ya Mr Mlimboka juu ya
kuhusika na mauaji. Ushahidi wa alama za vidole
unamkamata Mr Mlimboka kama muuaji. Lakini pia
ushahidi wa CCTV camera unamtoa Mr Mlimboka hatiani.
Kabla ya kulifikisha shauri mahakamani ilimbidi awe na
ushahidi wa kutosha ili kuigawa haki na kuipeleka
inapostahili.
Akiwa kituoni anasikia shamrashamra huko nje. Alipotoka
nje akauona msafara wa Bwana Pallangyo ukiwa
unamsindikiza. Kampeni za wazi zilikuwa zimeshaanza.

— 60 —
Bendera za chama cha FREE STATE DEMOCRACY
zilishikwa na kila mmoja aliyekuwepo kwenye msafara ule.
Alirudi ndani kuendelea na shughuli zake baada ya kuona
ulinzi umeimarishwa.
Bwana Pallangyo amesimama jukwaani akiiona imani ya
watu juu yake. Alisimama dakika moja bila kusema kitu.
Watu lukuki wamefurika uwanja mzima wakiimba na
kunengua.
"Pallangyo!.. Pallangyo!.. Pallangyo!.. "
Alikitoa kitambaa chake kwenye mfuko wa koti wa suti na
kujifuta machozi. Hayakuwa machozi ya huzuni ila ya
furaha. Ni kama vile haamini kama ni yeye ndiye watu
waliokusanyika kwaajili yake. Baada ya muda kupita
alikinyanyua kinywa chake. Na kuanza kuwahutubia watu.
"Free State Democracy Oyee!.. Mageuzi Oyee!..
Pallangyo Safiii!!.. "
Watu wakaitikia "Saafii!!.."
"Awali ya yote kipekee nimshukuru Mungu, muumba
wa mbingu na ardhi. Pili nikishukuru chama changu kwa
kuniamini kuwa mgombea wa nafasi ya ubunge, kwangu
mimi huu ni upendo wa agape. Tatu niwashukuru
wananchi wote mliokuwa bega kwa bega kwenye nyakati
zote hadi leo hii katika kampeni za waziri. Na kwa wingi
wenu huu inaonyesha kweli mnahitaji maendeleo.
Maendeleo Oyee!.."
Watu wakajibu "Oyee!.."
"Leo sitakuwa muongeaji sana. Ila nina imani Mungu
amenituma kwenu kama alivyomtuma Mussa kwa wana

— 61 —
wa Israel nije kuondosha dhulma, nije kutetea haki za
wanyonge. Nije kuwapa faraja waliokata na kukatishwa
tamaa. Free State Democracy oyeee!!.."
Wakaitika tena "Oyee!.."
"Mwisho kabisa niwaombe wananchi wote na
kuwanasihi njia ya maendeleo ni moja tu. Ni Pallangyo
basi kwingine utapigwa za uso" Akaweka kituo.
Watu wakazidi kushangilia bila kuchoka. Jua la utosi ila
hakuna aliyeliona.
Kabla hotuba haijaisha kuna kikundi cha watu kiliingia
eneo lile na kupiga risasi juu. Kila mtu alitafuta sehemu ya
kunusuru nafsi yake. Ghafla uwanja ukawa mweupe.
Bwana Pallangyo akajeruhiwa risasi ya bega. Jeshi la
polisi likafanya jitihada ya kudhibiti shambulizi lile na
kuyaokoa maisha ya Bwana Pallangyo kwa kumuwahisha
hospitali ya Temeke ambayo ilikuwa karibu na tukio hilo.
Taarifa zilimfikia Mr Mlimboka na zikawa taarifa nzuri
sana kwake. Siku hiyo alikuwa Serena hotel. Alienda
kupata chakula cha jioni ndipo akazipokea taarifa hizo.
Moja kati ya vitu vilivyompeleka Serena ni mazungumzo
ambayo alikuwa nayo na mwanasheria wake mpya.
Walikuwa wanaisuka mipango ya kumpakazia Innocent
kesi ya mauaji ya baba yake. Na jalada la kesi lilikuwa
limeshapokelewa tayari likiwa chini ya Inspekta Major.
Aliyeenda kufungua kesi alikuwa ni mwanasheria wa Mr
Mlimboka. Zilizokuwa zikiendelea ni jitihada za
kuutengeneza uongo utakaompoteza Innocent.
Haya yote anayoyafanya Mr Mlimboka ni kwasababu

— 62 —
hapendi kumuona Innocent. Anapokuwa anasikia jina la
Innocent nafsi yake inakosa amani kabisa. Na uwezo wa
kumtumia majambazi anao ila hakuhitaji kumuua. Alitaka
tu asiwe karibu na maisha yake.
Walipopata mwafaka wa kufanya juu ya jambo hilo kila
mmoja aliingia kwenye chumba kwaajili ya kupumzika.
Mr Mlimboka alirejea mapokezi na kuomba kama anaweza
kupata mtu wa kumliwaza kwa muda atakaokuwepo hapo.
"Inawezekana, ila huduma hiyo inabidi ulipie dola mia
tatu" Alijibu mdada wa mapokezi.
"Ok nalipia, utamwambia aje chumbani kwangu"
Alitoa kadi ya benki kwaajili ya malipo na kuelekea
chumbani kwake.

********
Innocent na Suzi wameshawasili nyumbani kwa Pilato.
Alijaribu kumuelezea hali halisi ili aweze kumpatia siku
kadhaa za kukaa nae pale kwake huko yeye akiendelea
kuisuka mipango ya sehemu ya kuishi. Pilato muda wote
jicho lake lilikuwa kwa Suzi. Sura yake nyembamba
ilimfanya avutiwe naye sana. Shepu yake ya mbinuko
ilisaidia kuisukumu damu kwenye vyumba vyake vya
vinne vya moyo. Chuchu zake zilizotunga kwenye dera
kama sindano zilizowaamsha wazungu waliolala.
"Oya wewe" Akaita Innocent.
Pilato akashtuka. Alikuwa yupo kwenye bahari pana ya
mawazo yaliyofunikwa na mawimbi ya utashi wa Mungu
alivyomuumba Suzi.

— 63 —
"Unawaza nini kwani" Akauliza tena Innocent.
"Ah we acha tu kichaa yangu, unajua leo niliunganisha
job nimerudi mda sio mwingi. Kwahiyo hapa nahisi
sitaenda job" Akajibu Pilato.
"Sawa haina shida, mimi mida flani hivi nitaondoka
basi utabaki wewe na shemeji yako"
"Hilo limeisha mwanangu" Akajibu Pilato.
"Ila unaenda wapi sasa, maana sio kawaida yako kutoka
usiku" Aliongezea tena kuongea Pilato.
"Kuna mtu alinipigia simu akanambia kuna siri
anataka kunipenyezea. Ila tuonane usiku ndo sharti
alilonipa" Alijibu Innocent.
Pilato alimsisitiza Innocent kuwa makini. Akidai kuwa
usiku una mambo mengi. Ila Innocent hakuonesha kuwa na
mashaka juu ya hilo. Huenda ni kwasababu ya shauku
aliyokuwa nayo juu ya siri aliyokuwa anataka akaambiwe.
Baada ya nusu saa kuondoka kwa Innocent. Pilato na Suzi
walianza kupiga stori. Walipata wasaa mzuri wa
kutambuana vema.
Pilato alitoka nje na kwenda kumnunulia chakula Suzi
baada ya kugundua kuwa ananjaa.
"Kwani huwa hupiki. Maana naona kama unatumia
gharama kubwa" Alisema Suzi.
"Unajua sisi wanaume furaha yetu ni kutimiza mahitaji
yenu. Sasa mtoto mzuri kama wewe unataka nikupe
maugali kweli. Yani hadi kwa Mungu nitapata dhambi"
Alisema Pilato.
"Ahahahah!!! Shemeji bwana" Suzi akacheka huko

— 64 —
akiendelea kula zile chipsi alizoletewa.
Pilato macho yake yalionesha kumhusudu Suzi. Moyo
wake ulikuwa na kitu kilichomkaa kooni. Baada ya muda
kupita alimsogelea Suzi kwa ukaribu sana. Macho yake
yakagongana na ya Suzi.
Suzi alisogea pembeni akimuacha Pilato pale
alipomsogelea.
"Shemeji unafanya nini tena sikuelewi" Aliuliza Suzi.
"Aaah!!.. Bwana shemeji usichoelewa nini hapa.
Ulizani hizo chipsi ni za bure kweli"
"Ahahahaha!!.. Acha utani shemeji bwana"
Pilato alianza kufungua vifungo vya shati lake. Suzi
akaanza kuona kuwa kweli Pilato anamaanisha. Alizifunga
zile chipsi na kujibana pembezoni mwa ukuta. Pilato
alimsogelea Suzi hadi pale alipo. Alivua pama lake
lililokuwa kichwani na kulitupa chini. Akaanza kufungua
batani ya suruali yake huko macho yake akiyakaza kwa
kumtazama Suzi.
"Shemeji unataka kufanya nini" Akauliza tena Suzi.
"Acha upuuzi usichokijua nini hapa. Saula fasta"
"Majiranii!!.. " Kabla hajamalizia kuita Pilato alimziba
mdomo haraka. Akachukua nguo na kuziingiza zote
kwenye kinywa chake. Alichukua kamba na kumfunga
miguuni kama ng'ombe anayetaka kukamkamua maziwa.
Akachukua kisu na kuchana nguo yake ya juu.
Suzi anahangaika akijaribu kujinasua.
"Waaooh!!.. Kumbe kichaa wangu alikuwa anainjoi
hivi" Alijisemea Pilato.

— 65 —
Akachana tena nguo aliyokuwa ameivaa chini. Na
kuichana kwa mkono nguo yake ya mwisho kabisa. Baada
ya hapo akamuingilia kingono kwa nguvu. Suzi anapiga
makelele bila mafanikio yoyote.
Pilato alipomaliza haja zake alikata zile kamba na kisu
tena. Alimuacha Suzi akilia sana pale ndani, yeye
akielekea pasipojulikana.
"Hivi haya maisha ni maisha gani eeh!. Mungu,
nimeamua kuutunza usichana wangu, kwaajili ya Inno hadi
pale tutakapooana halafu leo nakuja kutolewa kwa
kubakwa"
Suzi aliendelea kulia mithili ya mtu anayeomboleza.
Moyo wake una machungu sana. Aliutunza usichana wake
ili iwe tunu kwa kipenzi chake Innocent. Lakini Pilato
aliutoa kikatili.
Inaonesia dhahiri Suzi hakuwahi kushiriki tendo la ndoa na
mwanaume yeyote yule. Hata mwanaume ambaye alimuoa
pia hakumpatia mwili wake kutokana na mapenzi
aliyokuwa nayo dhidi ya Innocent.
Pilato yupo sehemu moja inaitwa Gomzi nature
amekaa akiwaza jambo alilolifanya masaa kadhaa nyuma.
Nafsini mwake ni kama mtu aliyekuwa anajutia juu ya
alichokifanya. Moyo wake ulimuuma zaidi pale
alipogundua Suzi alikuwa ni bikra. Kichwa kilimuuma
zaidi alipowaza Innocent atazipokeaje zile taatifa. Aliwaza
atamtazama kwa jicho gani. Alinyanyuka na kuingia
kwenye kiduka kimoja kilichokuwepo maeneo hayo na
kuagiza Double kick tatu na kuanza kuzibwia kama maji.

— 66 —
Haukupita muda akaanza kuchafua hali ya hewa kwa
makelele yaliyoambatana na nyimbo.
"We.. Unamjua Suzi wewe. Huyo shemeji yangu wewe.
Suzi mtoto mzuri wewe"
Watu wote walianza kumkodolea macho. Walihisi
amechanganywa na mapenzi. Wengine walianza kumcheka
kwa zile nyimbo na mauno aliyokuwa anayamwaga
hadharani.
Pilato alilewa chakari hata hajitambui. Alienda kujilaza
katikati ya barabara. Yupo hoi hajitambui. Wasamalia
wema walienda kumchukua na kumlaza sehemu
iliyosalama kwa wakati huo.

*****

Mida ya usiku sana Mr Mlimboka anarejea nyumbani


kwake akitokea Serena hotel sehemu ambayo alienda
kujipumzisha. Siku hiyo kwenye gari hakuwa na mlinzi
yeyote. Alishuka kwenye gari mwenyewe pamoja na
mwanasheria wake ambaye alikuwa naye Serena hotel.
Walishuka kwenye gari na kuingia wote ndani. Mr
Mlimboka akamuonesha mwanasheria wake chumba cha
kujipumzishia ili kesho asubuhi waelekee kituoni kutoa
ushahidi unaomuonesha Innocent ndo muhusika wa mauaji
ya Mzee Batasi.
Lilipita lisaa limoja, kwenye gari ambalo walishuka
Mr Mlimboka na yule mwanasheria wake kuna mtu mmoja
alifungua mlango wa gari na kushuka na yeye. Uvaaji

— 67 —
wake ulikuwa ni ule ule wa yule muuaji walieshindwa
kumtanbua siku zote. Siku hiyo hakutumia nguvu nyingi
kuingia ndani ya jumba hilo la kifahari. Mr Mlimboka
mwenyewe ndiye aliyemuingiza ndani kwake bila kujua.
Aliangalia pande zote nne za dunia akawaona maaskari
wawili waliokuwa lindoni usiku huo. Kama kawaida yake
alikimbilia kwenye sehemu za CCTV camera kukata
mawasiliano yoyote ya kuchukua matukio yanayoendelea
muda huo.
Alipofanikiwa alizama ndani na kwenda kuingia kwenye
chumba alichokuwepo yule mwanasheria. Alipomuona
alimuangalia kwa sekunde kadhaa bila kuchukua uamuzi
wowote ule. Yule mwanasheria alilala kama pono asiyejua
kinachoendelea kwa muda huo. Alichukua kitambaa
cheupe na kukipulizia dawa. Kisha akamnusisha puani.
Ikamfanya alale usingizi ambao asingeweza kusikia
chochote kile hata kama kungesikika milio ya mabomu.
Akachomuoa kisu chake. Na kukichoma kwa nguvu
kwenye godoro pembeni kidogo ya kichwa chake. Kisha
akachukua karatasi iliyokuwa na maandishi ya wino
mwekundu. Yaliyosomeka hivi.
NJAA ISIKUFANYE UIPINDISHE HAKI UNAYOIJUA
UKWELI WAKE.
Kisha akaenda kuunganisha nyaya za CCTV CAMERA
kama ilivyokuwa ada yake baada ya kumaliza tukio. Siku
hiyo hakufanya mauaji ndani ya jumba hilo. Ni wazi
alitaka kuufikisha tu huo ujumbe aliomuandikia
mwanasheria huyo. Kumuacha kwake ni wazi kuwa yeye

— 68 —
hahusiki kwenye yale yanayoendelea katika jumba hilo.
Na nia yake thabiti ni kutaka kumtoa asijihusishe na kazi
hiyo.
Alipokamilisha jambo lake akaondoka.

***********
Asubuhi na mapema yule mwanasheria anaamka
anakutana na kisu pembeni yake. Kabla hajaanza
kushughulika na kile kisu anauona ule ujumbe uliokuwa
umeachwa pale. Ulimfanya ajifikirie sana. Alichukua simu
yake na kumpigia Mr Mlimboka aone ule ujumbe.
Alipofika Mr Mlimboka naye akawa amepigwa na butwaa.
Alijiuliza ni kwanini yule hakuuawa. Na sio kawaida ya
muuaji huyo. Pia alijaribu kujiuliza mbona anaua watu
wake wa karibu tu halafu yeye hadhuriki. Kila alipojaribu
kuwaza na Kuwazua mawazo yake yaligonga mwamba.
Ilibidi aichukue ile karatasi na kwenda kuichoma moto.
Mwanasheria wake alichukua vitu vyake na kuelekea kituo
cha polisi ili akatimize makubaliano yake na Mr
Mlimboka.
Yeye ndiye aliyekuwa ameshikilia ushahidi ulioonesha
Innocent kuhusika na mauaji ya Mzee Batasi.

********
Innocent anarejea nyumbani asubuhi na mapema. Alipiga
hodi bila mafanikio yoyote. Aliita majina ya watu wote
aliokuwa amewaacha usiku wa jana. Ila hakusikia
chochote zaidi ya mwangwi. Kila alipoita sauti ilijirejea

— 69 —
mara ya pili. Aliusukuma mlango ukafunguka. Aliingiza
kichwa kwanza kuhakikisha kama ndani kuna watu.
Hakuna alichokiona zaidi ya vitu vya ndani tu.
"Suzi!!.. " Aliita kwa mara nyingine tena Innocent.
Hakusikia mtu yeyote akiitika.
Sasa huyu kaenda wapi tena jamani, au katoka na shemeji
yake. Alijiuliza moyoni mwake.
Alienda hadi chooni hakuona chochote kile. Ilimbidi arejee
ndani atulie awasubiri warudi walipoenda. Kabla hajakaa
chini akaiona bahasha ya kaki pale mezani. Juu imendikwa
kwako Innocent. Ikamshangaza kidogo. Akahitaji kujua
kilichopo ndani. Ikabidi aifungue. Na kuanza kuisoma.
Alipouona mwandiko aligundua kuwa ni Suzi.
Aliichukua na kuisogeza juu kabisa usawa na macho yake
ili aone vizuri maandishi yale. Akaanza kuisoma.
Kipenzi changu Innocent.
Mwanaume wa ndoto zangu.
Mwanaume wa maisha yangu. Imani yangu inanituma
ndoa yetu imeandikwa mbinguni japo duniani bado
haijapitishwa. Nilikuahidi mengi sana. Nikakunyima
stahiki yako ambayo bado ilikuwa haikuidhinishwa kuwa
yako. Lakini nimeshindwa kuilinda stahiki hiyo.
Innocent usiku wa jana rafiki yako alinibaka kinguvu. Na
aliutoa usichana wangu niliokunyima kwa kipindi chote
kwa ahadi ya kukupa hadi utakaponioa. Hata Mudi pia
sikumpa kwakuwa nakupenda sana Inno wangu.
Nimeondoka mbali na wewe kwani nahisi sina thamani
tena kwako. Tutaonana kwenye maisha mengine baada ya

— 70 —
haya ya duniani.
Suzi.
Innocent aliijaza ile barua machozi kwa kulia. Muda huo
huo inaingia namba mpya kwenye simu yake. Ilimlazimu
kuipokea na kuiweka sikuoni bila kuongea kwani mdomo
wake haukuwa na uwezo wa kufanya hivyo kwa muda
huo.
"Kuna mtu amepata ajari ya gari hapa tazara.
Tumeangalia simu yake tukaona wewe ni mtu wake wa
karibu. Wahi mapema maiti utaikuta Muhimbili" Kisha
simu ikakatwa.
"Haa Haloo!!.." Innocent aliita kuona kama anaweza
kupata maelezo zaidi. Ila ukimya ulitawala.
Harakaharaka alitoka na kuelekea hospitali ya Muhimbili
alipopatiwa maelekezo ya mwili wa marehemu ulipo.
Alipofika aliingia moja kwa moja hadi chumba cha daktari.
Alimkuta Doctor anaandika taarifa kwenye faili.
"Shikamoo Doctor" Innocent alimsalimia yule Doctor
ambaye alikuwa Mzee wa makamu. Kichwani kulikuwa
kumeshaanza kuota mvi. Alinyanyua macho yake na
kumtazama aliyemsalimia.
"Marahaba!.. Za kwako" Aliuliza yule Doctor huko
akiwa anaiweka sawa miwani yake machoni.
"Nzuri Doctor. Nimekuja Doctor nimeambiwa hapa
kuna maiti imeletwa muda si mrefu" Innocent alisogeza
kiti kidogo na kuketi chini.
"Anhaaa ndo ule mwili ulioletwa ukiwa amepatwa na
ajali na kusagikasagika pale Mfugale" Aliuliza Doctor.

— 71 —
"Nini Doctor!!.." Aliuliza kwa mshangao Innocent.
"Ila sijajua jina la huyo maiti Doctor" Innocent
alikuwa anahangaika kwenye kile kiti kama vile
amemwagiwa upupu. Alikuwa na kiherehere cha
kumtambua maiti huyo.
"Anhaa!!.. Jina lake anaitwaa!!.." Kabla hajamaliza
kuongea simu yake ya mezani iliita. Ikabidi aipokee
kwanza.
"Eeh! Haloo"
"Doctor nakuomba uje Wodi ya wajawazito kuna mtu
uokoe maisha yake haraka"
Yule Doctor alisimama harakaharaka na kuvaa koti lake
jeupe. Akatoka kwenda kutoa msaada.
Innocent alibaki pale ndani kichwani mwake akiwa na
msongo wa mawazo. Anashauku kubwa ya kutaka kumjua
aliyefakiri. Aliunganisha baadhi ya matukio hasa ile barua
aliyotoka kuisoma kabla ya kupokea simu ya taarifa ya
kwenda hospitali ndio iliyomchanganya zaidi.
Suzi ndio umefanya nini sasa. Alisema na moyo wake.
Jasho lilianza kumtoka. Machozi yakiendelea kukimbizana
kwenye njia za mashavu kuja hadi puani na kudondoka
chini.
Eeh!!.. Mungu mlinde Suzi wangu.
Alijisemea mwenyewe moyoni mwake. Wakati
akirandaranda pale ndani. Alirejea tena Doctor na
kuendeleza mazungumzo yao.
Innocent alihitaji kumfahamu huyo maiti aliyepo

— 72 —
hospitalini hapo aliyenasibishwa nae.
Doctor alimwambia, hawakuwa na uwezo wa kulitambua
jina la marehemu huyo kwani hakuwepo mtu wa
kumuuliza na alipelekwa na wasamalia wema tu. Hata
walipojaribu kumpiga picha haikusaidia maana kichwa
chote kilizama kwenye semi iliyokuwa inatoka mbagala
ikielekea uelekeo wa njia ya mawasiliano na marehemu
alikuwa amepakizwa kwenye bodaboda. Dereva wa
bodaboda alifanikiwa kujinusuru ila abiria huyo yeye ndiye
aliyedhurika na ajali hiyo. Kichwa chote kilikuwa kama chapati.
Mwili wake wote ulisagwa na simu ya marehemu ilidondokea
pembeni kidogo,ndipo watu walipopata uwezekano wa
kumpigia simu Innocent.
Hivyo hata madaktari walishindwa kuijua jinsia ya maiti hiyo.
Innocent alizidiwa kiasi cha kutoweza kuzungumza kabisa.
Alijikaza tu kiume kuyaficha maumivu aliyokuwa nayo.
Doctor alimpatia maagizo kuwa familia ya marehemu itashiriki
kwa salama tu kumzika marehemu. Maana kwa namna ilivyo
maiti haiwezi kusafirishwa kwa umbali mrefu. Kwahiyo
marehemu atazikwa kwenye makaburi ya hospitali
yanayozikiwa maiti zilizokosa ndugu wa kuja kuzikomboa.
Alihitaji kuwaomba ili akamzike hivyo hivyo. Lakini
alipokumbu kuwa hana hata hela ya kuikomboa maiti ilibidi
akubaliane na uamuzi uliotolewa.
Lakini alitoa ombi la kupatiwa simu ya marehemu. Jambo hilo
lilikuwa ndani ya uwezo wake Doctor na alifungua droo na
kuitoa simu ndogo ya batani yenye rangi nyeusi. Mfuniko wake
ulishikiziwa na rababendi ili usianguke.

— 73 —
Alipoitazama aligundua kuwa ni simu ya Pilato. Aliiwasha ili
aipigiee kwaajili ya kuhakikisha na ikawa kweli ni simu yake.
Aliumia mno moyoni mwake. Ni rafiki yake aliyekuwa
amemzoea sana.
Mungu ndo ameamua kulipa hapahapa duniani kweli. Swali
alilojiuliza moyoni mwake.
Baada ya muda alifuta machozi na kuianza safari ya kurejea
nyumbani.

SURA YA SITA

M
udi anahangaika kila kona kumtafuta mkewe
Suzi. Alijaribu kwenda kwao kuulizia kama
alirejea nyumbani ila alishangaa kila mmoja
akimtolea macho. Mama Suzi akawa mbogo na
kumsisitiza ahakikishe anampata mwanae laasivyo
wataonana wabaya.
Mudi akapata wazo la kwenda kwa mkewe aliyekuwa
amempa likizo kwa kipindi baada ya kumuoa Suzi.
Ilikuwa ni safari ya kutoka mtongani kuelekea Magomeni.
Alienda hadi magomeni kanisani. Alipofika nyumbani
kwake alimkuta Athumani kasimama mlangoni. Aliangalia
sehemu wanapohifadhia funguo pindi wakiondoka,
hakufanikiwa kuiona funguo.
"Mama Dani" Mudi alimuita jirani yake wa chumba

— 74 —
cha pili.
Lakini hakuitikiwa. Aliita tena mara nyingine. Na kugonga
mlango wake ili asikie kwa haraka. Pia ukimya uliendelea
kutawala.
Mara asikia kishindo cha mtu kikitokea kwenye uelekea
wa getini. Aligeuza shingo yake kumtazama anayekuja.
Akamuona Mama Dani.
Kabla hata ya salamu mama Dani hakutaka kulaza kiporo
kikachacha. Alikitapika chote.
"Mh!.. Huyo mwenzio hayupo hapo ana mwezi sasa.
Karudi kwa mama yake. Maana uliitelekeza ndoa"
"Hiyo ndio salamu" Aliuliza Mudi.
"He shoga yangu ningekusalimia ningesahau. Haya
mambo!.."
Mudi alisonya na kuondoka zake.
"Hahahahaaa!!!!.. Wanaume shikaamoni. Eh!. tutafika
mbinguni tumechoka kweli" Alisema Mama Dani.
Mudi aliondoka na kuelekea Tandale Kwa mtogole.
Nyumbani kwa wakwe zake. Magari yalikuwa ya shida
sana pale magomeni. Alipoona anachelewa alisimamisha
bodaboda ili imuwahishe. Walipofika Tandale Kwa Tumbo
wakasimamishwa na askari kwa kosa la mwendo mkali.
Dereva akajitetea kuwa wanamuwahi mgonjwa. Askari
ndo anazidi kuchachamaa hamuelewi. Alipoona anazidisha
ukali. Dereva aliingia mfukoni na kutazama kama kuna
watu wanashughulika nao.
"Kula gwala basi" Alimpa mkono aliokuwa ameukunja
ngumi iliyoitwa tano. Yule Askari akaelewa.

— 75 —
"Acha upumbavu leo nakusamehe, una bahati una
mgonjwa"
Dereva akawasha pikipiki na kuchafua hewa kwa moshi.
Mudi alifika hadi ukweni kumuulizia mke wake. Alimkuta
mkewe anaandaa chakula cha mchana.
"Umesahau nini kwangu" Aliuliza mke wake.
"Punguza jazba mke wangu. Nilifanya haya yote
kwaajili yetu mke wangu"
"Mudi nakuomba uondoke uniache na familia yangu
please, nimeshaamua ku-move on na maisha yangu. Nenda
kwa mke wako uliyeamua kuwa nae"
Wakati anaendelea kujieleza akapokea simu kutoka kwa
Mr Mlimbika.
"Mudi nataka urejeshe pesa zangu zote kwakuwa
umeshindwa kuifanya kazi yangu. Nakupa siku tatu tu za
kufanya hivyo"
Mudi hakuwa na chakuongea aliwaza ni wapi angeitolea
ile hela. Kabla hajapatana na mke wake alianzisha tena
safari nyingine.
*************
"Una uhakika haya mauaji kayafanya Innocent"
"Ndiyo. Alimuua baba yake ili apate zile mali. Na
nahisi pia alichoka kumlea baada ya kuwa ameumwa kwa
kipindi kirefu"
"Wewe umezileta hizi taarifa kama nani wa
marehemu"
"Mimi ni mwanasheria tu ninayetaka kuona nuru ya
haki inatanda kwenye uso wa dunia. Na pia nililiona jeshi

— 76 —
la polisi likiifatilia hiyo kesi, nikaona niwarahisishie kazi"
"Anhaaa!.. Nashukuru sana Ndugu Wakili. Aah!.. sijui
unaitwa nani"
"Niite Wakili msomi"
"Oooh!, mimi nai....." Akanyamaza.
Akadakia Wakili msomi.
"Nakufahamu unaitwa Inspekta Major"
"Ooh kumbe unanijua" Akauliza inspekta Major.
"Nakujua kama nguo yangu ya ndani"
"Ahahahahah!!.. " Walicheka wote kwa pamoja.
Walisimama kwa pamoja na kupeana mikono ya kuagana
na kutakiana siku njema. Baada ya kuondoka kwa Wakili
msomi, Inspekta Major alitikisa kichwa chake kama vile
mtu aliyekuwa anamsikitikia Wakili Msomi.
Siku iliyofuata ilikuwa ni zamu ya Mr. Mlimboka na
chama chake kunadi sera zao katika kampeni.
Waliwakodi watu kuja kuongeza wingi wa watu na
kuongeza hamasa kwenye kampeni. Kila aliyefika pale
alipatiwa tisheti iliyochorwa picha ya Mr Mlimboka
ikiongezewa na maandishi yaliyosomeka "CHAGUA
MLIMBOKA" na nyingine zikiandikwa "CHAGUA DP".
watu walihamasika kwenda ili wapate tisheti waongeze
idadi ya nguo walizonazo. Japo idadi iliyopo
haikumfurahisha sana Mr Mlimboka. Haikuwa kawaida ya
kampeni zao kuwa na idadi wa watu kama waliokuwepo
siku hiyo. Alikuwa amepanda kwenye gari iliyokuwa na
uwazi juu. Ikambidi ashuke atembee sawa na wananchi.
Lengo ni kutaka kuonekana kuwa ni mtu anayeweza kuishi

— 77 —
mazingira yoyote yale.
Msafara ulitembea ahadi viwanja wa wazi vya kunadi sera.
Kabla ya kupanda yeye, kulikuwa na utangulizi wa wasanii
waliotumbuiza kuwafanya watu wawe makini zaidi.
Baada ya hapo akapanda mwenyewe Mr Mlimboka
jukwaani.
"DP Saafii!" Alisema Mr Mlimboka.
"Saafii" wakajibu wananchi.
Mr Mlimboka alijinadi kwa yale aliyoyafanya awamu
iliyopita. Aliongea sana kiasi hadi watu waliokuwa
wameandaliwa kufanya fujo za hamasa wakapoa. Jua
lilikuwa kali sana. Watu walitawanyika na kwenda
kutafuta vivuli wajifiche. Eneo la mbele yake kukawa na
watu wachache sana. Hali hii ilimfanya aanze kujisikia
vibaya. Matumaini ya kurejesha jimbo alianza kuyakosa
akiwa pale jukwaani. Ghadhabu zikampanda akashuka bila
kuhitimisha mkutano.
Watu wakashangaa imekuaje tena. Baada ya kushuka yeye
ilibidi apande Katibu wa hamasa na kuwaomba radhi kwa
kilichotokea. Alidai kuwa mgombea hali yake ya kiafya
haipo sawa.
Mwisho akatoa wito kwa wananchi wote siku ya uchaguzi
kufanya jambo moja tu. Kumrejesha Mr Mlimboka
jimboni.
Na akaufunga mkutano.

*************
Innocent bado yupo kwenye jitihada za kumtafuta Suzi.

— 78 —
Siku Hiyo ilimbidi amtafute Mudi popote alipo ili
amuulize. Ilikuwa shida sana kumpata maana na yeye
alikuwa na kibarua cha kumkimbia Mr Mlimboka. Baada
ya kuulizia sana alimpata. Alipata mawasiliano yake na
kumtafuta ili waonane. Haikuwa rahisi kwa Mudi
kulikubali hilo. Maana hakuwa na imani na mtu yeyote
tena. Baada ya ushawishi wa hali ya juu uliomuhakikishia
usalama wake alikubali kuonana na Innocent. Sehemu ya
makutano ilikuwa gongo la mboto standi ya daladala za
kuelekea chanika. Walipokutana walitafuta sehemu ya
kutulia ili waweze kuzungumza kilichowakutanisha.

"Bwana we ni mwanaume mwenzangu, wala sijali


yaliyotokea najua njaa ndo zilikupelekea ufanye yale. Na
ndo maana nimekuwa na ujasiri wa kukuelekeza yote
yaliyojiri. Kiufupi namtafuta Suzi" Alisema Innocent.
"Pole sana ndugu yangu, lakini ukweli wangu
nimeshakueleza muda tu kuwa sina taarifa yoyote kuhusu
Suzi hadi mda huu. Na hapa ninavyoongea na wewe
natafutwa na Mr Mlimbika kisa huyo Suzi. Mudi alimjibu
Innocent.
"Unanisaidiaje sasa ndugu yangu"
"Nahisi kila mtu apambane na hali yake"
"Sawa, labda nikuombe kitu ukimuona popote pale
naomba unijuze" Alisema Innocent.
"Hilo limepita mwanangu. Ila jichunge sana Mr Mlimboka
sio mtu mzuri hata kidogo"
"Usijali namjua yule alikuwa jirani yangu, kwahiyo

— 79 —
namfahamu sana tena kuliko hata mtu yeyote yule"

Innocent na Mudi waliachana na kila mmoja kushika njia


yake.

Usiku umeshaingia. Kiza kimetanda. Jiji linapumua.


Majira ya saa nane usiku kila kona ya jiji ilikuwa tulivu
sana.
Katika jumba la Mr Mlimboka ulinzi ulizidi kuimarishwa
mara dufu. Siku hiyo ulinzi ulikuwa mkubwa kama vile
kuna lindwa nyumba ya Rais. Kila askari alikuwa makini
kutekeleza majukumu yake.
Wakati wakiwa kwenye lindo wakamuona mtu mmoja
akiwa amejigubika nguo nyeusi akiwa ananyatia upande
waliopo.
Mkuu wao akawaamuru wamzungukie denge ili
wamkamate. Kila mmoja akiamini kuwa siku za mwizi ni
arobaini. Walisogea na kumkaribia yule mtu. Wakaja
kukutana wote wakiwa wamemzunguka yule mtu.
"Nyoosha mikono juu" Alisema Kiongozi wa lindo siku
hiyo.
"Yule bwana akawa anawashangaa wale maaskari na
kunyoosha mikono"
Alikitoa kitambaa ambacho alikuwa amejifunga usoni. Na
kuwatazama wale maaskari.
Maaskari wote walishusha silaha zao chini.
"Oya nyie mmepagawa na nini, mnataka kuniua au"

— 80 —
Akauliza yule jamaa aliyekuwa amewekwa chini ya ulinzi.
"Unaleta upuuzi utakufa kweli, sasa ulikuwa unanyata nini
hapo" Akauliza mkuu wao wale maaskari.
"Kuna paka hapa nilikuwa namnyatia bwana.
"Halafu sisi tumeshasahau kama kuna mtu alitoka, sema
punguza uzinzi muda wote huo umesema unaenda
kununua chakula ndo unarudi mda huu kweli"

Wakati wakiendelea kupiga soga wanasikia kishindo


kilichowafanya wote wageuke nyuma. Walibahatika
kumuona mtu aliyeruka kwenye fensi akitokea ndani.
Alikuwa na mkoti mkubwa sana. Kila kitu chake kikiwa
cheusi.
Wakashtuka.
Walianza kumkimbiza yule mtu silaha wakiwa
wamezishika bila kuzitumia. Walikimbia kiasi hadi
wakaanza kuchoka. Kamanda wao akawaambia waongeze
morali hadi wamkamate. Walipita chocho kwa chocho.
Kimya kimya bila kumshtua mtu yeyote yule aliyelala.

Yule aliyekuwa akikimbizwa alifika pahala Mabuti yake


yakawa yanambana. Ilibidi ayavue Mabuti yake haraka
haraka kabla maaskari hawajamkaribia.
Safari ya kukimbia ikaanza tena. Walikuwa wanatokea
keko walikimbia hadi kufikia Sabasaba kwa mpili kwenye
uelekeo wa Mbagala. Alipofika mbele zaidi Buti moja
likamponyoka.
Wakati anataka kurudi nyuma na kuliokoto. Aliwaona

— 81 —
maaskari wamemkaribia sana. Akaamua kuwa na nusu
shari kuliko kufikwa na shari kamili. Alizidi kutimua
mbio.
"Stoop!!.. "

Maaskari walipofikia lile buti mkuu wao akawaamuru


wasimame na kumuacha akimbie.
Walichukua uamuzi wa kuchukua lile buti na kwenda
kulifanyia uchunguzi na kubaini muhusika wa lile buti.
Ambapo akipatikana muhusika. Atakuwa sawa na
aliyekamatwa na ngozi.
Kwakuwa yule mtu alitokea kwenye lile jumba basi
waliamini yeye ndio atakuwa muhusika wa mauaji yote
yaliyokuwa yanatokea mule ndani.

Maaskari wengine waliachwa nyuma. Pumzi zimekata kwa


ukubwa wa vitambi vyao. Waligeuza na kumalizia lindo
siku hiyo.

— 82 —
SURA YA SABA
(SAKATA LA KUMSAKA MUHUSIKA WA BUTI)

Jiji limepatakaa askari kila kona. Waliowaona askari


walihisi labda anatafutwa Iddi Amini Dada. Au Jambazi
ambalo limeshindikana huko USA. Waliwakamata watu
wengi waliowashuku na kuwapeleka kituoni kwaajili ya
mahojiano zaidi. Watu walikula vibano sana. Ilikuwa ni
wiki ya moto katika jiji la Dar Es Salaam. Kila
aliyemuona polisi akikatiza mbele ya macho yake alitimua
vumbi. Mapolisi hawakuona ajizi kujiunga kwenye riadha
za waliokuwa wanakimbia ili kujua walikuwa wanakimbia
nini.
Inspekta Major ndio alikuwa mkuu wa kitengo cha
upelelezi wa kesi hiyo. Kichwa kinazidi kuwaka moto.
Alikumbuka baadhi ya matukio ya mauaji aliyoshikilia
ushahidi wake. Ikiwemo ushahidi wa kisu uliomuhusisha
Mr Mlimboka. Alistaajabishwa sana alipowaza
inawezekanaje Mr Mlimboka amuue baba yake au mke
wake.
Kila alipotazama aina ya mauaji yaliyojitokeza alihisi
kuwa muuaji hatokei mbali na familia ya Mr Mlimboka.

Haya ni mauaji ya kisasi, hili linalofanyika lipo jambo


kubwa nyuma ya pazia. Na bila shaka Mr Mlimboka kuna

— 83 —
siri anaijua.

Baada ya kuwaza hivyo alichukua simu yake ya mkononi


na kuangalia namba ya Mr Mlimboka na kumpigia.
Akipiga mara tatu bila simu kupokelewa.
Alijaribu mara ya nne ndipo simu ikapokelewa.
"Nipo kwenye kikao, unaweza kunipigia simu baadae"
Aliisikia sauti ya Mr Mlimboka kisha akakata simu.

Alichukua uamuzi wa kumpigia Bwana Pallangyo. Ili


aweze kupata mahojiano na yeye. Kwa Bwana Pallangyo
haikuwa shida kwake. Alifanya kama alivyoambiwa kuwa
wakutane kituo cha polisi ili awape ushirikiano juu ya kesi
iliyopo mezani.
Baada ya muda mfupi Bwana Pallangyo alifika kituoni
hapo na kuonana na Inspekta Major. Walizungumza
mambo binafsi kwanza kabla ya kwenda kwenye lengo
mama.
"Hongera kwanza Mheshimiwa maana upepo nasikia upo
kwako sasa hivi" Alisema Inspekta Major.
"Ahahah!!.. Asante sana chief. Kila kitu na wakati wake.
Mungu tu kaamua huu uwe wakati wangu" Alijibu Mr
Pallangyo
"Okay, hongera bwana. Naa!..." Akasita kidogo
kuendelea.
"Naa nini tena" Akauliza Bwana Pallangyo.
"Hivi wewe unalitazamiaje swala la Mr Mlimboka"
"Kivipi hapo Afande, sijakuelewa"

— 84 —
"Anhaa!.. Namaanisha hivi. Unayazungumziaje mauaji
yanayotokea kwenye familia yake"
"Mh!. Kwa kweli sijui nisemeje lakini, nimesikia jeshi
la polisi kuna ushahidi mmeukamata kumuhusu muhusika
wa mauaji. Nahisi hilo lingekuwa bora zaidi kama
mkilitilia mkazo"
"We umejuaje hilo"
"Vyombo vya habari vimeripoti hilo juzi"
"Anhaa, ni sawa. Ila je unaweza tusaidia kumpata
muhalifu"
"Mhh.. Mbona huo mtihani na nadhani unaelewa
kipindi nilicho nacho. Ila patakapohitajika ushirikiano
nitawapa. Ila siwezi kuingia kwenye inshu ya upelelezi"
"Sawa nashukuru kwa ushirikiano wako" Alisema
Inspekta Major.

****************

Innocent ametulia sehemu akiwa ameshika kichwa na


kujiinamia. Ni kama alikuwa na msongo wa mawazo.
Kuna mtu alikuja na kumshika bega kwa nyuma.
Akashtuka sana.
"Ahahaha.. Kijana una nini mbona unaruka ruka sana"
Alipogeuka nyuma alimuona Mudi.
"Acha michezo ya ajabu bwana, unaweza ukaua mtu
ujue upate kesi hapa" Alisema Innocent.
"Pole bwana ndugu yangu" Alisema Mudi
Mudi baada ya kukaa chini alimpa fununu zinazoendelea

— 85 —
huko mtaani juu ya kusakwa kwa muuaji aliyekuwa
anafanya mauaji kwa Mr Mlimboka. Lakini Innocent
hakuonesha kujali kwa chochote alichokuwa anakiongea
Mudi. Alimuambia anajua kila kitu ila akili yake
inamuwaza Suzi. Alilalamika akidai amepoteza kila kitu
kwenye maisha yake. Baba yake amefariki bila kupata
baraka zake za mwisho. Mama yake naye alifariki
akimuacha na Baba yake ambae wameamua kufuatana
huko walipo. Hata faraja iliyokuwa imebaki kwake
ambayo ni Suzi pia nayo imetoweka machoni mwake.
Hayo yote yalikuwa ni maneno anayomweleza Mudi.
"Dunia tambala bovu kaka, mi Mwenyewe tamaa
zimeniweka mbali na mke wangu, jitihada zangu
zinagonga mwamba kila uchao. Ila niamini mimi nyakati
ngumu huja kwenye maisha yetu ili kutupa tahadhari kuwa
tukiipata furaha tuitunze" Alisema Mudi.
"Kabisa kaka, japo furaha zimeadimika sana, kiasi
kwamba tukipata furaha tunahisi ni mtego" Alisema
Innocent. Kisha wakacheka kwa pamoja.
Mudi na Innocent wamekuwa marafiki wa karibu sana kwa
muda mfupi. Waliamua kuonesha maana halisi ya
wanaume. Ambao hawawezi kuishi na vifundo kwa muda
mrefu. Mmoja anapolitambua kosa lake basi hurudi wote
mezani na kuweka ajenda mpya za kuendesha maisha yao.
Na ndicho kilichofanyika kwa wawili hawa. Walisaidiana
kila mmoja kuhakikisha upande wa mwenzie unakaa sawa.
Innocent alijivika majukumu ya kwenda kuongea na mke
wa Mudi ili amsamehe na warudiane kulisongesha

— 86 —
gurudumu la maisha. Na Mudi jitihada zake akiziwekeza
kumtafuta Suzi ili kuirejesha furaha ya Innocent rafiki
yake.
Mudi alikuwa ni karata nyingine kwa Innocent iliyokuja
kuleta faraja ingawaje wote wapo kwenye kipindi kigumu
cha mambo yao binafsi. Ila uwepo wa Mudi unamuondolea
upweke Innocent. Walipiga stori nyingi mno. Na kiza
kilipoingia waliagana kila mmoja akatafuta njia yake ya
kuingilia.
*****
Majira ya usiku hivi, Inspekta Major anapokea simu
iliyomfikirisha sana. Hakuipokea haraka haraka kama simu
zingine za kazi. Alikuwa amesimama anachukua maji
kwenye friji. Alisogea taratibu hadi sehemu iliyokuwepo
kochi na kuketi. Akaipokea ile simu. Kabla hajaanza
kuongea ikasikika sauti ya mtu akiongea kama vile
alikuwa anaingojea simu kwa hamu ipokelewe.
"Afande, nimechoka kukaa ndani kama utumbo
bwana. Mambo gani haya lakini"
"Namalizia kazi yangu sio muda. Soon tu utakuwa
uraiani"
"Hizo soon nimezichoka bwana. Halafu haya mambo
mbona wewe hayakuhusu, tuachie wenyewe
tutayamaliza"
"Nakuelewa sana. Lakini mbona upo sehemu salama tu.
Na kila unachokitaka una kipata" Alisema Inspekta Major.
"Nisikilize wewe, tone la maji moja linalopatikana
kwenye amani ni bora sana. Kuliko lita tano za maji

— 87 —
kwenye vita. Namaanisha hivii!.., nahitaji kuwa huru.
Mimi siwezi kufungiwa ndani na kufanyiwa kila kitu kama
mtoto"
"Nimekuelewa nitalifanyia kazi" Alisema Inspekta Major.
Inspekta Major aliikata simu baada ya kufikia mwafaka.
Wakati Anachukua glasi ya maji na kuipeleka kinyani.
Ikaingia simu nyingine. Mara hii alipiga funda moja la
maji na kuiweka ile glasi chini taratibu taratibu.
Akaipokea ile simu.
"Ndiyo Afande Rose"
"Kuna taarifa zimenifikia hapa kuhusu muuaji. Ila bado
zinanipa mashaka"
"Kwanini tena"
"Tumefanikiwa kumbaini muhusika wa lile Buti lilohusika
mara ya mwisho kwenye mauaji" Alisema Afande Rose.
"Jina lake nani"
"Sijapata muda sana wa kuongea nae. Niliwaamuru tu
wameweke ndani kesho tutaendelea na mahojiano"

— 88 —
SURA YA NANE

I
(MWENYE BUTI ATIWA MBARONI)
nspekta Major hakulala usiku wa jana. Aliomba
asubuhi ifike haraka sana kumbaini aliyekuwa
anasumbua jeshi la polisi kwa muda mrefu. Mapema
sana siku hiyo alidamkia kazini kwake. Alipokezana na
Afande Rose ambaye yeye alikesha hapo usiku wa jana.
Kila alipomhoji amtajie muuaji alimlazimisha aingie
rumande amuone.
Afande Rose akachukua vifaa vyake na kuelekea
nyumbani. Inspekta Major akaingia moja kwa moja
kwenye chumba cha mahojiano. Na kumuamuru askari
mmoja amuite mtuhumiwa aliyeletwa jana usiku ambaye
alisadikika kuwa muhusika wa mauaji.
Baada ya kupita dakika chache kuna mtu akagonga
mlango.
"Pitaa" Alijibu Inspekta Major.
Mlango ukafunguliwa. Inspekta Major anainuka kichwa
chake akimngojea kwa hamu mtuhumiwa. Baada kumuona
aliyeingia moyo wake ulipiga Paah!!.. Hakutaka kuamini
kilichopita akilini mwake ndani ya sekunde mbili.
"Innocent kama unashida na mimi unisubiri kidogo.
Kuna mpuuzi hapa namngojea alikuwa analisumbua jeshi
la polisi sana"

— 89 —
Innocent alishangaa moyoni mwake alipoitwa jina lake na
Inspekta Major ili hali hawajawahi kuzungumza nae jambo
lolote. Hakutaka kumuonesha kuwa ameshangazwa na hilo.
Alifungua kinywa chake, akasema.
"Nimeambiwa na kamanda nahitajika huku"
"Unahitajikaje Inno nimekuambia nenda, kuna mtu
nina mahojiano nae" Alisema kwa sauti ya juu kidogo
inspekta Major.
"Huyo unayemngojea hapo ndio mimi Afande"
Akashangaa kidogo Inspekta Major.
"Inawezekanaje sasa" Akauliza Inspekta Major.
Innocent akawa kimya hakujibu chochote.
Akaambiwa asogee na aketi kwenye kiti kilichokuwa
pembeni.
Inspekta Major alisimama na kufunga madirisha yote
na kushusha mapazia. Chumba kikawa na kiza. Kisha
akaiwasha taa iliyokuwa na mwanga hafifu ulioruhusu
wawili hao kuonana kwa mbaali. Hii ilimtengenezea sana
hofu Innocent. Jambo ambalo ndilo alikuwa analitaka
Inspekta Major ili aeleze ukweli kile atakachoulizwa.
Akachukua pasi ya umeme na kuichomeka ukutani ili
ipate moto. Akafungua kikabati kilichokuwa na zana
mbalimbali ikiwemo kisu, bisibisi, nyundo, na praizi kisha
akaviweka vyote mezani. Mwisho kabisa alichukua lile
buti lililobainika kwenye mauaji na kuliweka mezani.
Innocent alijawa na hofu sana. Ghafla jasho likaanza
kumtoka. Yakaanza kuchuruzika maji kwenye kiti
alichokalia. Inspekta Major alipoangalia vizuri aligundua

— 90 —
kuwa ni mkojo. Ilimbidi afanye kama hajaona kitu. Macho
kauzu. Sura ya mbuzi.
Alirudi na kuketi chini.
"Nataka uniambie unalifahamuje hili buti" Aliuliza
Inspekta Major.
"Mi.. Mi.. Mi.... "
"Mii nini" Akadakia Inspekta Major na kuipiga meza
iliyokuwa imewekewa zile zana.
Akashtuka Innocent.
Joto la mwili linazidi kupanda. Hofu inazidi kutanda.
Uwezo wa kujieleza unazidi kwenda mrama.
"Nimesema niambie, unalifahamuje hili buti"
Innocent akawa anapata kigugumizi kuongea. Kila neno
analoongea halimalizikii. Linaishia pale pale mwanzoni.
Inspekta Major akaongeza kasi ya moto wa pasi kisha
akawa anaizungusha mbele ya macho ya Innocent.
Harufu ya chumba ikaanza kubadirika. Hewa ikazidi kuwa
nzito. Innocent muda mrefu alikuwa ameshazishusha haja
zote mbili ndogo na kubwa.
Hii ilimpotezea hamu Inspekta Major kuendelea kumuhoji.
Aliiweka ile pasi mezani na kuzima batani ya ukutani.
Kisha akatoka nje na kumfungia mlango Innocent.
Alipotoka nje aliisikia simu yake ikiita. Akaitoa
mfukoni na kuitazama. Akabonyeza batani ya kijani
iliyounganisha mawasiliano yao.
"Halloo!.." Alisema Inspekta Major.
"Eeh!.. Inspekta Major jioni ya leo uje ofisini kwangu
nina mazungumzo na wewe"

— 91 —
Inspekta Major alikaa kimya asijue nini cha kujibu.
Kigugumizi kikamshika.
"Ku.. Ku kuna nini kwani"
"Ukifika utaelewa ninachokuitia kwenye simu sio
sehemu salama ya mazungumzo"
Kisha simu ikakata.
Aliingia tena kwenye chumba cha mahojiano na Innocent.
Aliukaza moyo wake ili aweze kuutafuta ukweli
anaoutaka.

*************

Mlango unagongwa ofisini kwa Mr Mlimboka. Kabla ya


kujibu chochote alinyanyua sura yake na kutazama saa ya
ukutani kuangalia muda. Akaona ni saa kumi na nusu jioni.
"Pita" Alisema Mr Mlimboka.
Aliyefungua Mlango alikuwa ni Inspekta Major.
"karibu sana inspekta"
Walipiga stori mbili tatu. Kila mmoja akimuonesha
mwenzie sura ya furaha. Baada ya kupita kwa dakika
kadhaa Inspekta Major aliomba aambiwe alichoitiwa pale.
Mr Mlimboka alikuwa anazunguka akitafuta gia ya kuingia
kwenye mada kuu. Ilibidi amuulize kuhusu mtuhumiwa
waliyemkamata na kuhusishwa na mauaji. Inspekta Major
alidai kuwa hawezi kutoa siri kwa mtu yeyote hadi pale
ushahidi kamili utakapokamilika.

"Afande, huyo muhalifu musimsikilize sana.

— 92 —
Mpelekeni mahakamani haraka sana. Maana namjua ni
mjanja mjanja sana”
"Kwani we unamfahamuje yule"
Mr Mlimboka alikaa kimya kidogo. Kisha akafungua
kinywa chake.
"Hapana. Namaanisha hivi. Wahalifu wengi wanapotiwa
mbaroni wanakuwa wazuri sana kwenye kujitetea"
"Anhaaa.." Alisema Inspekta Major. Akanyamaza kidogo
kisha akaendelea.
"Kwenye hilo usiwe na mashaka jeshi la polisi naimani
linatambua wajibu wake. Na muda sio mrefu mbichi na
mbivu zitajulikana"
Hii kauli ilimtia unyonge sana Mr Mlimboka. Alihisi
huenda kuna ukweli ameshaambiwa unaomfanya yeye
kuwa hatiani.
Hapana ila huyu angekuwa anajua kitu angesharopoka.
Namjua hawezi kukaa na kitu. Alijisemea moyoni Mr
Mlimboka.
Mr Mlimboka alisimama na kwenda kuifungua kabati yake
pale ofisini. Akatoa kitita kimoja cha hela chenye pesa
taslimu kama milioni 10. Akaipiga ile pesa mezani kwa
mbwembwe.
"Unataka kufanya nini Mheshimiwa" Aliuliza Inspekta
Major.
"Chukua hiki kiasi kitakusaidia kuimaliza hii kesi mapema.
Huyu dogo aende jela mapema. Halafu hapo kwenye koo
itakusaidia pia kuweka kufuri"
Inspekta Major alimtazama Mr Mlimboka kwa sekunde

— 93 —
kadhaa kisha akasimama.
"Mkuu hapana hii haipo kabisa kwenye maadili yangu ya
kazi. Hii pesa yako baki nayo" Aliibeba ila pesa pale
mezani na kumshikisha mkononi.
"Na naomba pia nikuache uendelee na majukumu yako"
Alitoka nje Inspekta Major na kuondoka.

Mr Mlimboka alibaki akijisonya mwenyewe mle ndani.


Kichwa kinazidi kupata moto.
Siku yake siku hiyo ilikuwa mbaya sana. Nae aliamua kazi
zake ziishie hapo kwa muda huo.
Aliamua kutafuta viwanja ili apunguze mawazo.
Kama kawaida yake aliingia Serena hotel na kuchukua
chumba kimoja ajiliwaze. Siku hiyo alikunywa sana
pombe kama vile mtu aliyepewa ofa ya mwisho kunywa
halafu baada ya hapo afe. Alikuwa kwenye wakati mgumu
sana. Kila alipomuwaza Innocent alizidi kuchanganyikiwa.
Akimfikiria Inspekta Major mtu ambaye ndiye msaada wa
mwisho anayeweza kumsaidia kwenye jambo lake ili
asiingie fedheha ndio anapojiongeza bia zingine.

Alikunywa hadi akapoteza fahamu. Ilipofika majira ya saa


saba usiku mlinzi wake ilimbidi aingie kwenye chumba
alichokuwa amelala Mr Mlimboka ili ahakikishe usalama
wake. Maana alimuona siku hiyo hakuwa sawa kabisa.
Alipoingia ndani akamkuta Mr Mlimboka hajitambui.
Chumba kimetapakaa pombe za kila aina.
Alimbeba na kumpakiza ndani ya gari ili amrejeshe

— 94 —
nyumbani.
**********

Inspekta major amekaa sehemu akipata kinywaji.


Meza aliijaza bia za kutosha. Kuna mtu alikuwa anampigia
simu hapokei. Bila shaka alikuwa anamsubiri huyo mtu.
Baada ya kupiga simu nyingi sana akaingiziwa ujumbe wa
maandishi kwenye simu.

Leo sijisikii kuongea na wewe mwanangu, nimekuona


hapo muda mrefu ila siwezi kutoka kuja hapo. Na hata
huku usije. Zingatia nataka niwe huru.

Alipomaliza kuusoma ule ujumbe aligeuka kulia kwake


kwenye jumba lililokuwa karibu yake akimtazama
aliyemtumia ujumbe. Macho yake hakufanikiwa kuona
chochote isipokuwa uzio wa matofali na nondo pana
zilizoongeza ulinzi kwenye jumba hilo.
Vile vinywaji alivyovijaza pale mezani hakutumia hata
kimoja zaidi ya maji tu.
Alimuita bodaboda mmoja aliyekuwa ameegesha pikipiki
yake pale kijiweni karibu na ile baa.
"Enhe boss unaelekea wapi" Aliuliza yule bodaboda.
"We twende nitakuelekeza mbele ya safari" Alijibu
Inspekta Major.
Aliwasha pikipiki na kutembea kwa mwendo mkali sana.
Walikuwa wanatokea magomeni mwembe chai na safari
yao ikaishia mbagala zakhiem. Alimpatia nauli yake kisha

— 95 —
akaanza kuzitafuta njia za chocho.
"We mtoto, samahani njo mara moja" Inspekta Major
alikaita katoto kwenye umri unaokadirika miaka mitano
hadi sita.
"Shikamoo"
"Marahabaa!!.. Et unapajua kwa Afande Rose"
Wakati anamalizia kuongea kuna mlevi mmoja aliyekuwa
pembeni akaitikia.
"Eeeh!!.. Napajua" Sauti yake ilitoka kwa tabu
ikiambatana na mikwaruzo.
Inspekta Major akamtazama yule mlevi akijishauri amfate
amuelekeze au aendelee na mtoto.
"Haya asante endelea kucheza eeh.." Alisema Inspekta
Major huko akiwa anatabasamu na kumshika yule mtoto
kichwani.
Kisha akamfata yule mlevi.
"Haya naomba unielekeze ndugu yangu"
"Mafalanga yapooo, au unataka kunisumbua tu"
Alisema yule mlevi.
"Mafalanga ndo nini" Akauliza Inspekta Major.
"Aaii!.. Hajui mafalanga. Yani mkwanja upoo" Kila
alipokuwa akiongea kichwa chake kilienda chini. Macho
yake hayakuwa na uwezo wa kumtazama aliyekuwa
anaongea nae.
"Anhaa.. upo, twende basi" Akajibu Inspekta Major.
Akainuka yule mlevi na kumuongoza njia Inspekta Major.
Utembeaji wake ulikuwa wa kunyata sana. Hata
ukakamavu wa mwili hakuwa nao. Upepo ulipokuja

— 96 —
alipepesuka kama karatasi. Nguzo za umeme zikawa
stamina yake.
Walitembea hadi wakaifikia nyumba moja iliyokuwa
imejitenga na nyumba zingine. Ilikuwa ya tofauti na
nyumba zote zilizokuwa maeneo hayo. Ilionesha dhahiri
anayeishi humo uchumi wake ulikuwa mzuri.
"Oya nyumba ile pale" Walisimama kando ya nyumba
hiyo na yule mlevi akisema kwa kuashiria kidole kwenye
ile nyumba iliyokuwa mbele yao.
"Haya nashukuru" Akasema Inspekta Major.
"Acha kushukuru wewe nipe hela hiyo"
Inspekta Major aliingiza mkono mfukoni na kutoa noti ya
shilingi elfu tano. Akampatia yule mlevi.
"Aah.. Hii yote yangu baba.. Asantee, asante sana.
Aah Mungu kaleta malaika wake leo" Mlevi aliongea huku
akiwa amepiga magoti kwa kushukuru. Aliongea kwa hisia
sana. Kiasi cha Inspekta Major kuanza kuvivaa viatu vyake
vya ugumu wa maisha. Aliishia kutikisa kichwa na
kumnyanyua pale chini.
"Yani leo pale kirabuni watanikoma. Naenda
kuwanunulia wote maana walikuwa wananinunulia kwa
masimango" Yalikuwa ni maneno aliyokuwa akiyaongea
yule mlevi huko akiwa anatembea mdogo mdogo kama
kinyonga kurudi alipotoka. Inspekta Major akaishia
kutabasamu tu na kutikisha kichwa chake.
Alielekea hadi kwenye uelekeo wa ile nyumba. Akagonga
geti. Hakukuwa na majibu yoyote. Aliiona batani ya
kengere kuliani kwake ikabidi aibonyeze. Geti likajifungua

— 97 —
lenyewe. Akapita hadi ndani. Kulikuwa na eneo kubwa
sana la wazi nje ya nyumba kulikuwa na gari mbili zenye
hadhi na thamani kubwa. Kulikuwa na Range rover nyeusi
na TX nyeupe zilizokuwa zimejengewa turubai ili kuzuia
zisipigwe na jua.
Simu yake ikawa inaita. Kuiangalia ni Afande Rose.
Aliangalia mbele kulia na kushoto ili amuone hakumuona.
Akaipokea.
"Acha kushangaa zunguka huku nyuma kuna bustani
tuongee huku"
"Sawa" Akaitika inspekta Major.
Alienda hadi bustanini na kumkuta Afande Rose amekaa
akimngojea. Inspekta Major hakuweza kunyamaza namna
alivyoshangazwa na mandhari ya nyumba ya Afande Rose.
Muonekano wake akiwa kazini na nyumba yake ni tofauti
sana. Kazini huwa anaenda kwa daladala na usafiri anao.
Afande Rose alidai huwa hapendi watu wa kazini kwake
watambue anavyovimiliki maana majungu mengi sana.
Watu wakijua unachomilika ndo mwanzo wa chuki na
majungu.
Mada hiyo waliiua na kuianza mada ya Innocent. Ambaye
alikuwa anawaumiza sana kichwa. Hakuna aliyeamini
kama kweli Innocent anaweza kufanya hayo anayodaiwa
kayafanya. Ingawaje hajakiri bado kuwa yeye ni muhusika
wa lile buti. Pia hajakiri kuwa kahusika na mauaji.
"Sura sio roho, inawezekana pia akawa kafanya hivyo"
Alisema afande Rose.
"Kuna muda najaribu kuamini kuwa huenda kahusika.

— 98 —
Ila mbona matukio yaliyokuwa yanafanyika ni ya kikatili
sana"
"Kipi kinachokufanya usitake kuamini" Aliuliza
Afande Rose.
"Ipo siri kubwa sana imejificha kati ya Mr Mlimboka
na Innocent. Na kama kweli alikuwa anaua Innocent basi
yalikuwa mauaji ya kisasi"
"Unamaana gani kusema hivyo. Na hiyo siri ni siri
gani? "
"Muda ukifika utajua sasa hivi bado mapema sana.
Tuhakikishe kwanza tunamjua muhusika sahihi wa lile buti
na mauaji" Alisema Inspekta Major.
Maongezi yao ya mwisho walikubaliana hivyo.
Walikubaliana kufanya kazi ya ziada ili kuhakikisha
hawamuonei mtu kila mtu apatiwe stahiki yake.

*******
Mr Mlimboka ameshazinduka yupo nyumbani kwake.
Amekaa kwenye kochi akiwa na mawazo tele. Siku yake
ya jana ilikuwa mbaya sana. Alikuwa anajaribu kuwaza
chakufanya ili awe sehemu salama. Kuna jambo
linamsumbua kichwa sana na anajaribu kutumia mbinu
mbalimbali kutaka watu wasilijue.
Wakati amekaa kuna mtu anapita ndani bila hodi. Mr
Mlimboka alipomuona uso wake ulikuwa na nuru ya
tabasamu kubwa sana.
"Mbona umenikurupusha hivyo mkuu kuna shida
gani" Alisema yule mtu aliyeingia pale na kusogelea kochi

— 99 —
na kukaa chini.
"Kuna jambo nataka msaada wako na najua lipo ndani
ya uwezo wako"
"Jambo gani mkuu sema"
"Najua wewe ndio mkuu wa kile kituo pale. Nataka ile
kesi umbadilishie mtu wa kuisimamia, mpe mtu
mwingine" Alisema Mr Mlimboka.
"Kwanini tena, na itakuwa ngumu maana yule ndiye
aliyekuwa Anaisimamia ile kesi kuanzia mwanzo hadi leo
hii. Sasa huyo atakayekuja huoni kama ataharibu kazi"
Mr Mlimboka alifungua droo ya meza iliyokuwepo mbele
yake na kutoa kitita cha shilingi milioni kumi.
Akamsogezea mbele yake.
"Afande Mwita, mimi najua hili unalimudu tusiongee
kama watoto basi. Hiyo kesi mkabidhi mtu mwingine na
aikimbize haraka yule muhalifu afungwe ili mimi niwe
free na maswala ya kampeni"
Afande Mwita akawa anapepesa pepesa macho yake kama
vile mtu aliyechochwa na mdudu machoni. Aliichukua ile
hela na kuitia kwenye mifuko ya koti la suti.
"Nimekuelewa, limepita hilo" Alisema Afande Mwita na
kuondoka zake.
"Ahahahaha.. Hatimae nina amani sasa. Kale katoto
kumbe kabaya hivi. Okay ngoja tumnyooshe sasa"

********

Mudi alizipata taarifa za Innocent kuwekwa ndani.

— 100 —
Hakuwa na msaada wowote ule. Alichoamua ni kumpelekea
chakula ili usiku upite vizuri. Askari aliyekuwepo zamu siku
hiyo ilihitaji kumnyima nafasi ya kumpa chakula kwakuwa
muda wa kuonana nae uliisha. Baada ya kuomba sana akapewa
dakika tano.
Alipoingia ndani alimkuta Innocent kalala kifudifudi. Huruma
ilimjaa sana.
Mudi alikuwa ni moja ya watu ambao walikuwa hawaamini
juu ya Innocent kusadikika kuwa ni muuaji. Kwa muda mfupi
aliokaa naye aliuona unyonge uliokuwa ndani ya Innocent.
Kulikuwa na mvurugano wa mawazo akilini mwake kwenye
kuamini na kutoamini.
Aliinama na kumtikisa kwa mkono wake kwenye mguu.
Innocent akainuka taratibu taratibu. Alipogeuka akamuona
Mudi. Alitabasamu na kumkumbatia kwa furaha kwa sekunde
kumi.
"Umejuaje kama nipo hapa" Akauliza Innocent.
"Kaka hili jambo zito sana uwepo wako hapa nchi nzima
hii inajua" Akajibu Mudi.
Alifungua ule mfuko na kumtolea chakula.
Innocent alikuwa na njaa sana baada kuona chakula hakuuliza
maji yapo wapi. Alianza kukifakamia kile chakula bila kuuliza.
Aliyakumbuka maji baada ya kumaliza kula.
Mudi akagundua njaa aliyokuwa nayo Innocent. Wakati
wanaendelea kuongea yule askari alikuja kuwagongea geti na
kumwambia aondoke.
Walikumbatiana kwa mara ya mwisho kisha Mudi akarejea
nyumbani kwake.

— 101 —
SURA YA TISA
(INNOCENT KUPANDISHWA MAHAKAMANI)

Afande Mwita alimuita Inspekta Major na kumvua kesi


aliyokuwa anaisimamia. Ilikuwa ghafla sana kwa Inspekta
Major. Alijitahidi kuililia ile kesi lakini ngoma ikagonga
mwamba. Mkuu wake kila anachomwambiwa kinaingilia
huku na kutokea huku. Inspekta Major alikumbuka jitihada
zote alizozifanya juu ya kesi hiyo. Inamuuma zaidi pale
anapokumbuka muda aliowekeza kwenye kuifatilia kesi
hiyo.
"Kamanda, nakuomba nipe hii kesi nakuahidi
nitaisimamia vizuri" Alisema Inspekta Major.
"Wewe sijakuita hapa tubagein, nimekuita hapa nikupe
oda"
Inspekta Major kila alipotaka kujua sababu ni nini
hakuweza kuambiwa.
Kesi tayari alikuwa ameshakabidhiwa mtu na tayari
ameshapata uthibitisho kuwa Innocent ndio muhusika wa

— 102 —
lile buti. Hapo ikatumika kauli ya mkutwa na ngozi ndio
mwizi wa ng'ombe. Taarifa ya Innocent kuhusika na
mauaji ilimshtua kidogo Inspekta Major. Na hakutaka
kuendelea kuzungumza na mkuu wake maana kauli
iliyotoka ilikuwa amri na sio ombi.
Lakini alifanya jitihada za kwenda kufanya mazungumzo
ya mwisho na Innocent ili aupate ukweli na kujua
atasimamiaje haki zake ili sheria isimbane yeye peke yake.
Akilini mwake alianza kuhisi kuwa hizo zilikuwa hila za
Mr Mlimboka.
Aliangalia kama hakuna mtu anayemuona na kwenda
kuzungumza tena na Innocent. Awamu hii hakwenda kama
askari alienda kumuhoji kama mdogo wake.
Alianza kumtoa hofu kwa kumpatia maneno yaliyomfanya
asihisi kuwa anaongea na askari.
Baada ya mazungumzo marefu Innocent alimwambia
kuwa majibu yote kampatia Afande Pius na alienda
kumhoji asubuhi asubuhi kwahiyo nahisi huyo anaweza
kukueleza kila kitu.
Alikuwa anampa wakati mgumu sana Inspekta Major,
maana hakujua atumie njia gani ili amuelewe. Na alijua
kwenda kumuambia Afande Pius ampe majibu ya Innocent
ingekuwa ngumu.
Innocent alikuwa ameshajikatia tamaa. Hakuhitaji msaada
wa aina yoyote ile kutoka kwa mtu. Maana hata kuishi pia
alishachoka, maisha yake yalikuwa fumbo. Fumbo
lililomshinda kila mfumbuaji. Hakuwa na tumaini lolote
lile. Shabaha yake ya maisha imeshindwa kumlenga ndege

— 103 —
aliyemuwinda kwa muda mrefu. Ufukara wake ulimfanya
awapoteze wazazi wake kwakukosa nyenzo za
kuwahakikishia ulinzi.
Kuna muda alijaribu hata kumkufuru Mungu na kuwaza
huenda labda ni ulemavu alionao ndo unaomfanya ayapitie
yote hayo.
Alilia sana siku hiyo. Machozi yakaisha yakaanza kushuka
makamasi.
Alitamani kesho ifike mapema, apelekwe mahakamani ili
hukumu ipitishwe.
Inspekta Major kuna muda alikuwa anazidiwa na hasira
akishindwa ajue nini cha kufanya.
Mule ndani akaona sio sehemu sahihi pia kwake. Alijua
akikutwa inaweza kumletea shida. Alitoka na kwenda
kutafuta njia nyingine.
Alikumbuka kuwa kwenye ile kesi alikuwa na msaidizi
wake Afande Rose. Ilimbidi amtafute ili amuombe msaada
wa kumtafutia ukweli.
Bahati iliyo nzuri kwake baada ya kumwambia alilipokea
kwa mikono miwili na kuanza kulifanyia kazi.
Mr Mlimboka kichwani ana mambo mawili siku ya kesho
ndio ilikuwa siku ya majibu ya uchaguzi. Lakini pia ndio
ilikuwa siku yake ya kwenda kusikiliza kesi yake
mahakamani akisimama na Innocent.
Suala la Innocent halikumuwazisha sana maana
aliamini ameshalimaliza kwahiyo alienda kusikiliza
uamuzi wa mahakama. Jambo lililomuumiza kichwa ni
kutetea kiti chake kwenye nafasi yake. Upinzani wake

— 104 —
ulikuwa mkubwa sana. Kuna muda alijipa matumaini.
Kuna muda matumaini yakawa yanafifia.
Usiku wa siku hiyo alikuwa na kikao na mwanasheria
wake.
Wakijaribu kuongelea jambo la kesho. Mwanasheria
alimhakikishia kuwa ushindi ni lazima. Maana Innocent
hakuwa na mwanasheria na hata uwezo wa kumlipa
mwanasheria huyo hana.
Majibu ya Mwanasheria wake yalizidi kumtia imani ya
siku ya kesho.
Kwenye kikao hicho hicho alikuwepo meneja kampeni
ambaye naye alimdhihirishia ushindi kwa hali aliyoiona
kwenye vituo vya kupigia kura.
"Yani kama hatutashinda mkuu basi kweli nitaamini
kuwa watu ni wanafiki" Alisema Meneja Kampeni.
Walichukua glasi zao na kuzigonga kwa pamoja.
Wakaanza kunywa.

*******
Hakuchi sasa kumekucha. Watu wametapakaa kwenye
mahakama ya kisutu. Watu wanatoka ndani wengine
wanafuraha ya kushinda kesi na wengine familia zao
zinasaga meno baada ya kiungo chao muhimu kushindwa
kesi. Wapo walioshindwa kiuhalali na wapo walioshindwa
kwa nguvu ya pesa. Mr Mlimboka yupo kwenye gari na
mwanasheria wake wanangojea zamu yao ifike ya
kusomwa kwa kesi yao.
Innocent yeye hakuwa na mtu yeyote siku hiyo. Watu

— 105 —
wote waliofurika mahakamani hapo hakuna aliyepata
kumfahamu. Isipokuwa mama Suzi tu ambaye nae
alishangazwa kuuona uwepo wake pale.

Ilimbidi ageuke pembeni afanye kama hajamuona.


Ingawaje mama Suzi alikuwa tayari alishamuona.
Alitamani amsogelee pale alipo walau aongee nae lolote
ila nafsi yake ikawa na kauzito. Aliamua kuitii nafsi yake
na kutulizana.
Muda unazidi kwenda tu. Anashangaa shangaa tu. Bahati
mbaya hakuambiwa muda wa kesi ni saangapi.
Akamuona Mr Mlimboka anaingia ndani na jopo la watu
wake akiwemo mwanasheria wake.
Mapigo ya moyo yakaanza kwenda mbio. Alijua kuwa
muda umeshawadia. Alianza kusali na kumuomba Mungu
wake kwa dua na machozi.
Alisimama imara na kujifuta machozi yote. Kisha na yeye
akaingia ndani. Alimkuta Mr Mlimboka Amesimama
kwenye kizimba cha mshitaki.
Alimkata sana jicho.
Mdogo mdogo akiingia kwenye kizimba cha mshitakiwa.
Innocent alipoitazama hadhira alitahamaki sana.
Alishangazwa na idadi kubwa ya watu waliokuja kusikiliza
ile kesi. Kwa isiyo bahati hakuna aliyemjua kati yao. Hata
yule mama Suzi nae aliyemuona pale nje hakumuona tena.
Aliangalia kama angejaribu kumuona hata Mudi rafiki
yake lakini hakumuona.

— 106 —
Inamaana Mudi ameshindwa hata kuja kuniaga kwa mara
ya mwisho.

Yalikuwa ni maneno yaliyopita ndani ya nafsi yake.


Kutokana na uvumi wa kesi hiyo watu wengi walifika
mahakamani kumtazama huyo muuaji aliyekuwa
akilisumbua jeshi la polisi kwa kitambo kirefu.
Kila aliyemtazama Innocent hakuamini kama anaweza
kuwa muuaji. Tena mauaji ya kikatili namna hiyo.
Kila mmoja alisubiri kuona karata ya mahakama
itaamuaje.
Alisimama Jaji na kuitazama hadhira. Akamtazama
Innocent kisha akamtazama Mr Mlimboka na mwanasheria
wake.

"Bwana Innocent, mwanasheria wako au mtetezi wako


yupo wapi" Mahakama nzima ilizizima zii!.. Ukimya
ukatawala. Watu wote macho waliyapeleka kwa Hakimu
na kuyarejesha kwa Innocent wakingojea jibu lake.
"Nipo mwenyewe ndugu Hakimu" Akajibu Innocent.
Hakimu akakaa chini na kuandika kitu kwenye nyaraka
alizokuwa nazo pale.
Pembeni yake kulikuwa na karani aliyekuwa anamsaidia
kuandika baadhi ya hoja zitakazowasilishwa na mshtaki na
mshtakiwa.
Hakimu alisonga mbele kidogo ya mahakama
akiwatazama Mr Mlimboka na Innocent.
Kisha akaitazama karatasi aliyokuwa ameishika na

— 107 —
kuisoma.
"Kesi namba DW2001, jeshi la polisi kikosi namba
TU91 linamfikisha mahakamani bwana Innocent Batasi
mwenye miaka 28 mkazi wa Temeke Mtongani Dar es
salaam. Kwa kosa la mauaji ya watu wa tano ndugu wa
karibu wa Mr Mlimboka, akiwemo baba yake Mr
Mlimboka, mkewe na ndugu yake mwingine pamoja na
walinzi wake wawili. Mtuhumiwa huyo Alionekana
akiruka ukuta wa nyumbani kwa Mr Mlimboka akitokea
ndani mnamo tarehe 2/10/1998 siku ya ijumaa akiwa
amevalia mavazi meusi yaliyoshindwa kumtambulisha
kwa haraka. Baada ya jitihada za jeshi la polisi
kumkimbiza alivua mabuti yake na kudondosha buti moja
lililosaidia jeshi la polisi kumbaini muhusika.
Baada uchunguzi wa kina uliochukua mwezi mmoja na
nusu Bwana Innocent alibainika kuwa muhusika wa lile
buti na jeshi la polisi kuendelea na uchunguzi ukabaini
kuwa yeye ndio muhusika wa mauaji yote hayo ya watu
watano.
Mahakama inampisha Mr Mlimboka kutoa maelezo
kidogo juu ya tukio hilo kisha itampatia nafasi mshitakiwa
ya kujitetea na mahakama kutoa hukumu"
Watu walikuwa wametulia kimya wakimsikiliza Hakimu
kwa umakini. Kuna watu walihisi kuna mkono wa mtu juu
ya kichwa cha Innocent uliokuwa ukimkandamiza
Innocent kwenye kesi hiyo.
Alipopatiwa nafasi ya kujielezea Mr Mlimboka.
Alisema mauaji yote yaliyotokea katika nyumba yake.

— 108 —
Japo hakuwa anafahamu awali ila amepokea ushahidi wa
jeshi la polisi na uzuri pia hata muhusika amekiri hilo.
Aliomba mahakama itoe hukumu yake bila kumsikiliza
tena mshitakiwa kwakuwa aliamini hana hoja ya kuiambia
mahakama.
Maneno hayo aliyaongea Mr Mlimboka akimtazama
Innocent kwa jicho la ghadhabu sana. Ni kama vile
alikuwa anampa onyo asiseme jambo fulani.
Hakimu alimuuliza Mr Mlimboka.
"Je unahisi kwanini Bwana Innocent Batasi alikuwa
anafanya mauaji hayo"
Mr Mlimboka alimgeukia Innocent na kumtazama kwa
sekunde chache.
"Sijui ndugu Hakimu" Akajibu Mr Mlimboka. .
"Je kati ya hao marehemu kuna aliyekusimulia kuwa
alikuwa na uhasama na Bwana Innocent" Akauliza tena
hakimu
"Hakuna aliyewahi kuniambia ndugu Hakimu"
Akajibu tena Mr Mlimboka.
Hakimu akamgeukia Innocent.
"Haya Bwana Innocent, jina lako linasema huna hatia.
Uwanja ni wako wa kujitetea"
Innocent aliwatazama tena watu waliokuja kuisikiliza kesi
yake. Alitamani kila mmoja ayajue maumivu aliyoyapitia
na anayoyapitia lakini sanaa ya kuwasilisha hizo hisia zake
hakuwa nayo.
Akamgeukia Hakimu. Akamwambia.
"Sina cha kujitetea"

— 109 —
Kila mmoja akashangaa sana.
Inamaana kumbe yeye ndo muuaji kweli.
Hayo yalikuwa baadhi ya maneno ya watu waliokuwa
wanaifatilia hiyo.
"Upo tayari kwa uamuzi wa mahakama" Akauliza
Hakimu.
"Ndi.. Ndii.." Akaanza kulia Innocent pale kizimbani.
"Kulia kwako hakusaidii kitu. Nakupa nafasi ya
mwisho ya kujitetea. Ukishindwa nitaisoma hukumu"
Alisema Hakimu.
"Ndugu hakimu. Sina ninachojua juu ya hiki
kinachoelezewa hapa. Sijahusika na mauajj ya mtu yeyote"
Watu wote kimyaa!!..

Hakimu alikuwa na mjadala mfupi kati yake na karani


wake.
Akamgeukia tena Mr Mlimboka.
"Je kuna ushahidi unaomtia hatiani Innocent ufikishwa
hapa"
"Ndiyo ndugu hakimu" Alidakia Mwanasheria wa Mr
Mlimboka harakaharaka.
Akasimama na kwenda hadi mbele ya mahakama.
"Ushahidi wa kwanza ndugu hakimu ni Hili buti
lililokamatwa ambalo mtuhumiwa alionekana akitumia
milango isiyo rasmi kutoka kwenye nyumba ya Mr
Mlimboka. Baada ya uchunguzi wa kina wakazi wa
Temeke Mtongani walithibitisha kuwa hilo Buti ni la
Innocent na miongoni mwa mashahidi hao wapo hapa.

— 110 —
Nitaiomba mahakama yako tukufu iniruhusu kuwaleta
watu hapa mbele muwaone"
Wakainuka vijana watatu ambao Innocent alipowatazama
hakuwa anawajua. Hajawahi hata kuwaona.
Walivyosimama walithibitisha kuwa lile Buti ni la
Innocent. Walipoulizwa wanamtambuaje mshitakiwa.
Walidai wanaishi nae mtaa mmoja.

Innocent alikuwa anaona kile kinachoendelea pale mbele


kama sinema.

Akaendelea tena Mwanasheria.

"Kama hiyo haitoshi siku zilizokuwa zinatokea mauaji


Innocent alikuwa ni mtu wa kwanza kabisa kufika msibani
kabla ya watu wengine kujua kama kuna msiba nyumbani
kwa Mr Mlimboka. Mbaya zaidi umbali wa nyumbani kwa
kina Innocent na Mr Mlimboka ni zaidi ya kilometa
zisizopungua saba. Je taarifa hizo alikuwa anazipataje
mapema kuliko watu wengine. Asante ndugu Hakimu"
Akaenda kukaa yule Mwanasheria.

Mahakama imekaa kimya hakuna hata mtu anayetikisa


kiatu. Macho ya watu yakiwa kwa Hakimu.
"Ndugu asiye na hatia, unachakujitetea kutokana na
ushahidi huo" Aliuliza Hakimu.

Innocent machozi yanambubujika. Kila akitaka kunyanyua

— 111 —
kinywa chake maneno hayatoki. Kuongea tena alikuwa
hawezi.
Baada ya kimya cha muda mrefu Hakimu alichukua
nyaraka alizokuwa anaandika karani wake na kuzipitia
tena watu wote wakimtazama yeye.

Hakimu alipomaliza kuzipitia zile nyaraka alisimama tena


mbele ya mahakama ili kuisoma hukumu ya Innocent.
"Kutokana na kosa alilolifanya Bwana Innocent
ambalo ni kinyume na sheria ya kanuni ya adhabu sura ya
16 ya sheria ya Tanzania. Na sheria ya makosa ya jinai
Namba 2 ya 1970. Mahakama inamhukumu bwana
Innocent"
Hali ya ukimya ikazidi kutawala kila mtu akishika kidevu
wengine kichwa kila mtu na kiungo chake kilichotoa hisia
anazozipokea muda huo.
"Mahakama ina mhukumu bwana Innocent hukumu ya
kunyo...." Ghafla kuna sauti ilisikika.
"Stooop"

— 112 —
SURA YA KUMI
( MTETEZI WA INNOCENT MAHAKAMANI)

Kila mtu aligeuka nyuma kumtazama aliyesimamisha


hukumu hiyo isisomwe muda huo. Mr Mlimboka alikuwa
mshangaaji mkubwa kuliko mtu yeyote. Aliiona sura ya
Inspekta Major. Alikuwa anajiuliza maswali mengi sana.
Aliwaza anataka kusema nini mbele ya mahakama. Na
yeye alishavuliwa usimamizi wa ile kesi.
Mawazo yakamrudisha siku za nyuma kidogo, namna
walivyokuwa wanazungumza kana kwamba kuna jambo
analijua ila halitilia maanani.
Hakimu alimtazama aliyeingia. Nguo za jeshi la polisi
alizovaa zilimfanya awe na hamu ya kutaka kusikiliza
anachotaka kuongea.
"Samahani Hakimu, ninaweza kupata nafasi ya
kumtetea Mshitakiwa mbele ya mahakama yako tukufu"
Alisema Inspekta Major.
Hakimu aliduwaa na kumtazama Inspekta Major. Karani
wake alimuita na kuteta jambo. Akamrejea tena Inspekta
Major.
"Hapana huwezi kwani hujui taratibu za mahakama.
Nishaingia na kuanza kusoma kesi hairuhusiwi mtu

— 113 —
mwingine kuingia"
"Najua ndugu Hakimu, lakini hii kesi ni nzito sana
nisingependa utoe hukumu wakati mshitakiwa hana hatia.
Lakini pia kanuni kuna muda zinawezavunjwa iwapo kuna
jambo la kuifanya sheria iwe na nguvu. Na hapo
unasimamia sheria Ndugu Hakimu"

"Haya sawa, nakupatia dakika kumi za kuieleza


mahakama" Alisema Hakimu.
Kila mtu alisubiri kuona huo utetezi ni upi. Jasho likaanza
kumtoka Mr Mlimboka.
"Hakimu, achana nao hao wanakuletea maigizo"
Akasema Mr Mlimboka.
"Tulia hiyo sio kazi yako" Alijibu Hakimu kwa
msisitizo.
Innocent alikuwa haelewi kile kinachoendelea. Kuna muda
alitaka kuamini kuwa yupo kweli mahakamani, kuna muda
akili yake ikawa inakinzana na ukweli huo.
Watu shingo zikaganda zikigeukia nyuma bila kuchoka.
"Haya ingieni" Alisema Inspekta Major.
Utulivu ukazidi kuongezeka wakingojewa walioambiwa
waingie.
Akaanza kuingia wa kwanza ambaye alikuwa Mama Suzi.
Innocent hakushangaa kumuona Mama Suzi pale. Ila
kilichomshangaza alikuwa anajiuliza anataka kuiambia
nini mahakama. Alipita moja kwa moja hadi mblele ya
mahakama.
Akaingia wa pili Mudi. Huyo ndiye aliyevuruga akili

— 114 —
ya Mr Mlimboka. Anataka amuite ili amuambie jambo
lakini macho ya halaiki nzima yalikuwa kwake.
Akafuatia mtu wa tatu ambaye alikuwa ni Mr Matonya
mwanasheria ambaye alimpatia kesi ya kusimamia baada
ya ushahidi wa kisu kumbaini kuwa Mr Mlimboka
anahusika na mauaji ya mkewe na baadae kukataa kuwa
mwanasheria wake.
Innocent akawa anazidi kuona mapicha picha alibadili
kila aina ya mkao akiwaangalia wale watu waliokuwa
mbele yake.
Baada ya watu hao akaingia Afande Rose. Nae
akujumuika na wenzie. Watu wengi walishangazwa na
yeye kwasababu alikuwa amevalia nguo za jeshi la polisi.
Innocent alimkumbuka kuwa ndiye mtu alimsweka
rumande siku ya kwanza kabisa.
Bado akawa anajiuliza hawa watu wanataka kusema
nini. Alimtazama Mudi ili amuulize hata kwa ishara nini
kinachoendelea. Mudi aliunyanyua mkono wake usawa wa
kiuno na kurejesha chini akikweka kiganja chake
kikiangalia chini. Akifanya hivyo mara tatu kwa pamoja.
Akimuashiria atulie.
Wakati wanaendelea kujiuliza maswali na kujijibu
wenyewe. Wanasikia sauti ya viatu vya mchuchumio.
Vilivyotoa taarifa ya jinsia ya mtu anayeingia. Kila mtu
alikuwa anahamu ya kumuangalia nani atakayetokea.
Alipoingia na kumuona Innocent alikimbia kwenye
uelekeo wa kizimba alichokuwepo Innocent.
Innocent hakuamini kile alichokiona.

— 115 —
"Suuzii..." Innocent nae alitoka kizimbani na
kumkimbilia Suzi na kukutana katikati ya mahakama.
Wakakumbatiana machozi yakiwabubujika. Watu walihisi
wanatazama picha la kihindi. Kesi hiyo ilileta msisimko
kwa kila mtu. Hakimu alibaki akiduwaa akiendelea
kutazama yale yanayoendelea mbele ya mahakama.
Mr Mlimboka anataka kuzimia kwa hofu aliyokuwa nayo.
Awali yeye ndiye aliyekuwa na furaha lakini kwasasa
furaha haipo tena upande wake.
Suzi alisimama na kutazama kule alipotokea. Kila mtu
aligeuzia macho yake tena kule mlangoni. Wakamuona
Inspekta Major wakageuza macho yao na kumtazama tena
Suzi. Wakasikia kishindo kama cha wakoma
kilichowakimbiza washami. Kilikuwa kishindo cha ushindi.
Ni mtu ambaye alikuwa anatembea kwa kujiamini.
Wanamuona Mzee mmoja hivi akiwa yupo ndani ya suti
nyeusi. Innocent alipomtazama mzee huyo alimtambua
haraka sana. Nguvu zilimuishia na kukaa chini kwanza.
Furaha aliyokuwa nayo haikuwa na kifano. Alimtambua
kuwa ni baba yake ambaye siku kadhaa nyuma alipata
taarifa kuwa amefariki. Mr Mlimboka alifikicha macho
yake kumtazama mtu aliyekuwa anaingia mda huo.
Alikumbuka kuwa alimtumia majambazi wamuue. Na
wakamletea taarifa kuwa wameshaimaliza kazi.
Kilichomshangaza zaidi hadi picha za. siku ya mazishi
alipelekewa na akaenda kuoneshwa kaburi lake.
Mzee Batasi alisogea hadi pale alipokuwa amekaa
Innocent na kupiga goti kisha wakakumbatiana. Waliwatoa

— 116 —
sana watu machozi. Wawili hao walionesha hisia za hali ya
juu dhidi yao. Kila mtu akiwa haamini anachokiona.
"Baba unatembea" Aliuliza Innocent.
Innocent anakumbuka baba yake alipooza upande mmoja.
Alikuwa hana uwezo wa kufanya jambo mwenyewe
isipokuwa kwa usaidizi wake.
Baba yake alitikisa kichwa kilichosindikizwa na machozi.
Hakimu ilibidi awarejeshe Mahakamani. Maana baadhi
yao walikuwa washazipeleka akili zao mitaani.
"Mmebakiwa na dakika saba za kuileza mahakama" Askari
mmoja alienda kumnyanyua Innocent na kumpandisha
kizimbani kwa mara nyingine tena.
Inspekta Major alimshukuru Hakimu kwa kumpatia ile
nafasi. Na kuendelea na utetezi wake.
"Ndugu Hakimu, awali ya yote nitangulize maneno
haya, utetezi huu unamuonesha ndugu Innocent kuwa yeye
hahusiki na mauaji haya. Awali ya yote niiambie

mahakama hii tukufu kuwa Jina la mtuhumiwa linasomeka


Innocent Batasi. Na huyo mnayemuona hapo kizimbani sio
Innocent Batasi"
Kauli hii ilianza kuwavuruga baadhi ya watu. Wanajiuliza
anataka kusema nini. Mr Mlimboka anataka
kumnyamazisha Inspekta Major. Ila Inspekta Major macho
yake yalikuwa kwa Hakimu na waliokuwa wamekuja
kusikiliza kesi. Akaendelea kusema.
"Huyo hapo mbele yenu ni Innocent Mlimboka" Akaweka

— 117 —
kituo.
"We unataka kumaanisha nini" Akauliza Mr Mlimboka.
Baadhi ya watu walikuwa na maswali mengi sana. Walihisi
labda Inspekta Major anaongea nahau zilizowafanya
kutomuelewa vizuri. Kwasababu kuna watu walimuona
Mzee Batasi akimlea Innocent kuanzia akiwa mdogo.
Hakimu alikuwa makini kusikiliza hoja za mtetezi ambaye
ni Inspekta Major.
"Kwenye hili siwezi kulielezea sana, niiombe
mahakama yako tukufu ndugu Hakimu impatie ridha mzee
Batasi atuthibitishie maneno haya" Alisema Inspekta
Major.
Hakimu alitikisa kichwa kuonesha kuwa ametoa kibali
hicho.
Mzee Batasi alisogea mbele ya mahakama kuthibitisha
maneno ya Inspekta Major. Hadhira iliongeza antena za
masikio ili kuyanasa mawimbi ya sauti vizuri. Mr
Mlimboka hakuwa na hamu ya kusikiliza maelezo
yaliyokuwa yanatolewa na Mzee Batasi.
Ndugu hakimu, miaka 29 iliyopita Mr Mlimboka
alikuwa ni mfanyabiashara mdogo, hawa tunaowaita
wamachinga. Alikuwa anafanyakazi ya kuuza samaki kwa
kutembeza kichwani. Katika pirikapirika za maisha Bwana
Mlimboka alikutana na binti mmoja kigoli aliyetokea
familia maskini huko tandale. Hisia ziliuvua utu wao
wakakutana kimwili na kumpa mimba yule binti.
Wazazi wa yule binti walikuja juu sana, maana binti yule
alikuwa mwanafunzi wa kidato cha pili aliyekuwa

— 118 —
akijiandaa kufanya mtihani wake wa taifa.
Kesi iliishia serikali za mitaa yule mwanamke alimkingia
kifua bwana Batasi asikutwe na adhabu yoyote ile akidai
kuwa alimpenda sana. Familia yake Bwana Mlimboka
ikawa ya kwanza kati ya watu waliofurahi na kushinikiza
kuunga undugu. Walifanya haraka sana kuikamilisha
mipango ya ndoa.
Baada ya ndoa tu Mungu akampatia kazi ya kueleweka
iliyompa heshima kubwa sana kwenye familia na ukoo
wake.
Pesa za kula haikuwa shida yake tena.
Ndugu Hakimu, baada ya kutimu kwa miezi tisa yule mke
wake alijifungua. Gumzo likawa kubwa sana. Bwana
Mlimboka akidai kuwa mtoto sio wake baada ya kumuona
amezaliwa akiwa na hali ya tofauti kidogo na watoto
wengine. Alikuwa na ngozi laini iliyokithiri. Macho yake
yalikuwa kama ya paka. Baada ya kuitwa kwa watalaamu
wakasema kuwa mtoto aliyezaliwa ni Albino.
Baba yake Mr Mlimboka akaingia kwenye ugomvi wa
wanandoa akishinikiza mwanae amuache mke wake.
Haikuwa ombi muda huo kwake ilikuwa ni amri kwani
alikuwa ameshaletewa mwanamke mwingine wa kumuoa.
Kilikuwa kipindi kigumu sana kwa huyo mwanamke. Kila
mumewe aliporudi kazini alirudi akiwa amemnywea
pombe na matusi ya nguoni. Maneno ya kumkashifu kuwa
yeye ni malaya na changu doa. Akidai kuwa ile mimba
alimbambikizia. Wakati huo yule mwanamke aliyechagulia

— 119 —
na wazazi wake wakaungana na kutengeneza timu ya
kumtesa mwanamke huyo.
Alijitahidi kuipambania ndoa yake, akashindwa. Hata
alipowafata wazazi wake kwaajili ya msaada nao
walimkataa maana aliwaambia wazazi wake wasichukue
hatua yoyote kwakudai kuwa wanapendana. Na kuililia
ndoa akikataa kusoma.
Siku hiyo alirudi nyumbani akiwa amechelewa sana.
Alipomuuliza mbona umechelewa kurudi alinaswa vibao.
Bwana Mlimboka alimpa machaguo mawili mkewe kisha
achague moja. Chaguo la kwanza lilikuwa amtupe mtoto
ili yeye abaki pale ndani na chaguo la pili aondoke yeye
na mwanae usiku huo.
Kila alipojaribu kujielezea hakupata nafasi ya kusikilizwa.
Yule mwanamke aliyekuwa amechagulia na wazazi wa
Bwana Mlimboka akaenda kutoa mabegi yake ya nguo na
kumtupia nje na kumfukuza kama mbwa.
Aliondoka yule binti bila kujua anaelekea wapi. Aliporejea
kwao hakuwakuta tena wazazi wake pale walipokuwa
wanakaa. Kila aliyemuuliza hakuna aliyejua.
Maisha yake yakaishia dampo na kula vyakula vichafu.
Jua na mvua vilikuwa vyake. Lilipomkutia jua, usiku
mlikuta akiwa hapo.
Bwana Mlimboka alihitaji ile siri yake isibainike na watu
waliomzunguka alihama bagamoyo na kwenda kuishi Keko.
Aliwatuma watu wamuhamishe yule mwanamke na
kumuhamishia sehemu aliyohamia. Akimuacha mtaani bila
msaada wowote. Siku hiyo baba yake bwana Mlimboka

— 120 —
akamfata na kumjaza maneno ili akamuue yule mwanamke
ili asije akavujisha siri yao. Kwenye nyakati hizo Mr
Mlimboka alikuwa ameshaanza kujiingiza kwenye siasa.
Aliona akiendelea kumuacha yule mwanamke akiwa hai
huenda akawaeleza wanajamii. Ndipo alipowatuma
watumishi wake watatu kwende kumuua yule mwanamke.
Wakimuacha yule mtoto pale dampo.
Na hapo ndipo nililomuokota yule mtoto na kumpa jina la
Innocent ambaye ndio huyo Aliyesimama mbele yenu
kwenye kizimba cha mtuhumiwa" Aliweka kituo na
kumeza mate. Hakimu alikuwa anamfuatilia kwa umakini
wa hali ya juu. Hadhira wakaanza kutekwa na simanzi.
"Ndugu Hakimu mimi niliishi na Innocent kwa muda
mrefu sana kiasi kwamba kila mtu alijua kuwa ni
mwanangu. Baada ya Innocent kufikisha umri wa miaka
kumi na nane. Tulimjuza bayana na kukijua kila kitu lakini
hiyo haikumfanya yeye aache kutuchukulia mimi na mke
wangu kama wazazi wake.
Mke wangu alijaribu mara kadhaa kwenda kumuomba mke
wake Mr Mlimboka ili aweze kumuomba mumewe
amrudishe mwanae nyumbani. Baada ya kufanya jambo
hilo ikawa vita kubwa sana iliyopiganwa kisiri siri baina
ya mke wangu na yule mwanamke.
Mkewe Mr Mlimboka alijaribu kumfata na kumtishia
maisha na kumuambia akae mbali na mali zao. Na
alimwambia akiendelea kuwafatilia angemuondoa dunaini.

— 121 —
Baada ya masiku machache yule mwanamke aliwaagiza
majambazi na kumuua mke wangu. Nikafungua kesi lakini
kila nilipopita kesi lizimwa. Mr Mlimboka akaahidi
kunipoteza kama nikiendelea kufuatilia jambo hilo. Visa
vilikuwa haviishi kwangu baada ya Mr Mlimboka kujua
nayajua mambo yake. Ndipo hapo nilipoamua kudondoka
chooni na kujifanya kama nimepararaizi na kushindwa
kuongea ili mradi yeye aishi kwa amani kwa kuwa alikuwa

anajua kuwa sina uwezo wa kuongea tena. Ndugu Hakimu

kama Mr Mlimboka alikuwa na uwezo wa kuyafanya yote

haya je atashindwa kumsingizia Innocent hii kesi

inayomkabili sasa hivi. Nipende kuiaminishia mahakama

yako tukufu kuwa Innocent hahusiki na haya mauaji.

Asante"
Mzee Batasi aliishia hapo na kusogea sehemu waliyokuwa
wamesimama wenzio na kuungana nao pamoja. Mr
Mlimboka anatamani akimbie pale mahakamani atafute
chaka la kujificha. Uso wake kabla hajaulizwa na Hakimu
ulitoa taarifa kuwa yaliyozungumzwa yana ukweli ndani
yake.
Baada ya hapo alisogea mbele Afande Rose.

— 122 —
Alisimama na kuiambia mahakama namna Mr Mlimboka
alivyokuwa anazuia na kuwapa hongo baadhi ya watu
kwenye vitengo vya huduma za afya kuzuia Innocent
asipatiwe huduma yoyote. Alitoa ushuhuda wa moja kati
vitu alivyovishuhudia yeye Mwenyewe pindi alipotumwa
kwa kazi maalumu kwenda hospitali kufanya uchunguzi
namna ya watumishi wa wanavyofanya kazi zao na
kutekeleza majukumu yao. Alitoa kinasa sauti na
kumsikilizisha hakimu juu ya mambo yaliyokuwa
yakiendelea kwenye hospitali hiyo. Moja ya mambo
aliyoyasikia hakimu ni pamoja na sauti zilizokuwa
zinaonesha kuwa Innocent hakutakiwa kupatiwa huduma
yoyote ya afya kwenye eneo alilokuwa anaishi.
Ikafika zamu ya Mudi akatoa ushahidi wa
alivyotumwa na Mr Mlimboka kumuoa Suzi ili kumfanya
Innocent asiwe na furaha kwenye maisha yake. Aliieleza
mahakama pesa alizolipwa ili kulifanya hilo.
Haikutosha Mudi alibainisha kuwa alipewa kazi ya
kumteka Mzee Batasi na baadae kuwatuma watu kwaajili
ya kumuua. Jitihada za uokoaji zilifanywa na Inspekta
Major ambaye alimchukua na kumuhifadhi sehemu kwa
muda wote akimpatia kila kitu anachokihitaji kama baba
yake.
Innocent ni moja kati ya watu ambao walishangazwa
na unyama wa Mr Mlimboka ingawaje alishamtambua
kuwa sio mtu mzuri. Ila hapo ndio anaipata picha halisi ya
Mr Mlimboka.
Hakimu alimgeukia Mr Mlimboka na kumuuliza.

— 123 —
"Kwenye haya yaliyosemwa kuna lenye ukweli ndani
yake?"
Ukimya ukatawala. Kukaa kwake kimya kulitoa asilimia
kwa Hakimu kuelewa yale yaliyosemwa yana ukweli kiasi
gani.
"Duniani kuna watu wana roho mbaya sana. yani
mwanao wa kumzaa mwenyewe unaweza kumfanyia haya
kweli" Alisikika mtu mmoja akisema kutoka kwenye
wasikiliza kesi.
Hakimu aliomba utulivu uendelee kutawala wakati
waliobakia wakiendelea kutoa ushahidi wao. Hakuna
aliyechoka kusikiliza. Waandishi wa habari walipata
vichwa vya kwenda kuuzia magazeti na stori za kusisimua.
Wale wa udaku vibarazani nao walipata mada ya mwaka
mzima.
Hakimu alimpatia kijiti Mr Matonya ili aeleze anayoyajua
na yaliyomfanya kuwa pale.
"Ndugu hakimu, nataka kuieleza mahakama yako
tukufu juu ya uovu wa Mr Mlimboka. Mimi ni
mwanasheria ninayeijua misingi ya haki na sheria. Baada
ya kutokea kwa mauaji ya mkewe Mr Mlimboka niliitwa
na rafiki yangu Peres ambaye ni mdogo wa Mr Mlimboka
kuisimamia kesi iliyokuwa inamkabili Mr Mlimboka
baada ya alama za vidole kusoma kuwa yeye ndiye
aliyefanya mauaji. Baada ya kuipokea ile kesi nilipatiwa
pesa nyingi sana ili nimuingize Innocent kwenye ile hatia
pasi na kubaini kuwa ni yeye au sio yeye. Nilihitaji
kusimamia misingi yangu ya kazi ipasavyo. Lakini chini

— 124 —
ya Mr Mlimboka haikuwa kazi ya kusimamia sheria.
Ilikuwa kazi ya kuabuse sheria. Nilipoliona hilo nilitafuta
sababu ili nisiendelee na ile kazi pasi na kukwazana na
yeyote kati yao. Nipende kuithibitishia mahakama yako
tukufu ndugu Hakimu Mr Mlimboka hastahili kuishi
inabidi awe mfano kwa watu wote wenye vitendo kama
vyake vya kuwanyanyapaa watu wenye ulemavu hata
kama sio kama wa Innocent, ulemavu wa aina yoyote ule.
Na hii pia itasaidia viongozi wengine kuyatumia madaraka
yao kwa manufaa ya taifa letu na sio kwa manufaa ya
matumbo yao binafsi"
Baada ya kuzungumza wote alibakiwa wa mwisho
Inspekta Major. Ambaye yeye ndio aliyekuwa wa mwisho
kwenye upande wa utetezi wa Innocent.
"Kuna mwingine kati yenu ana cha kuongezea"
Aliuliza Hakimu.
"Ndiyo" Akajibu Inspekta Major.
"Karibu" Hakimu alimkaribisha Inspekta Major.
"Nipende kukushukuru Ndugu hakimu kwa nafasi hii
adhiim. Awali kesi ya Mr Mlimboka kufuatilia muuaji ni
nani nyumbani kwake nilipewa mimi. Nikaifanyakazi
yangu kikamilifu mpaka kumtia mbaroni Bwana Innocent.
Na nilimkamata kwasababu usalama wake uraiani ulikuwa
mdogo sana. Hata yeye kuhusika na lile Buti ni maelekezo
yake kwa waliopewa kesi hii kuisimamia baada mimi
kuporwa kesi hii. Awali kabla ya kumtia mbaroni kuna
baadhi ya matukio niliyaona kwa Mr Mlimboka
akimfanyia Bwana Innocent ikiwemo kutopenda kumuona

— 125 —
akishiriki kwenye matukio yake. Hali hiyo ilinifanye kuanza
kufanya uchunguzi wa kina kujua ni kipi kinachomfanya Mr
Mlimboka kutofurahishwa na kitendo cha kumuona Innocent
kwenye matukio yake. Ndipo nilipomuomba usaidizi askari
mwezangu afande Rose kunisaidia kwenye upepelezi. Mimi
ndiye niliyetambua awali sana kuwa Innocent ni mtoto wa Mr
Mlimboka na niliificha hii siri bila kumwambia yeyote baada ya
kugundua kuwa siri ni ya mtu mmoja tu na sio wawili. Mr
Mlimboka alikuja kuhisi kuwa huenda kuna vitu navijua kuhusu
yeye. Ikabidi anifate na kunipa hela ilimradi nisiendelee
kuifatilia ile kesi na badala yake nimpeleke Innocent
mahakamani bila ya kumhoji.

Uzuri siku niliyokutana nae nilitega kinasa sauti ili


kurekodi mazungumzo yote tutakayoyazungumza" Akaitoa
flashi mfukoni kwake na kwenda kuiweka kwenye laptop ya
Hakimu baada ya kupata ridhaa ya kufanya hivyo. Hakimu
akapata kuyasikiliza yale mazungumzo yao.
Akaendelea kuongea Inspekta Major.
"Baada ya kuikataa pesa yake Mr Mlimboka alimtumia
mkuu wangu wa kituo kwa kumpa pesa ili aniengue mimi
kwenye ufuatiliaji wa ile kesi. Matakwa yake yakafanikiwa.
Lakini sikukata tamaa kwasababu nilikuwa nimemuhifadhi
Mzee Batasi na Suzi kwaajili ya kuwaomba waje kuithibitishia
mahakama maovu ya Mr Mlimboka ili kupinga vitendo kama
hivi. Nao pia waliniunga mkono kwenye hili. Ndugu Hakimu
uwanja ni wako wa kutoa hukumu" Akamaliza Inspekta Major.

— 126 —
SURA YA KUMI
NA MOJA
(HUKUMU INASOMWA NA HAKIMU)

Hakimu na Karani wake wote kazini kwao kulikuwa na


kazi. Siku hiyo ilikuwa ngumu sana kwao.
Anatamani kuisoma hukumu ila nafsi yake inajawa na
uzito.
Hakimu ilimbidi ampe nafasi ya mwisho ya kujitetea Mr
Mlimboka ili kupisha hukumu. Kila alipotaka kuongea
hakuna neno lililotoka mdomoni. Alijihisi kufadhaika sana.
Nafasi ya Mr Mlimboka akapewa mwanasheria wake.
Ambaye naye suti aliyokuwa ameivaa ikaanza kumvaa.
Jasho linamtoka kama maji, anawaza anawezaje kumtoa
kwenye huu mtego. Mbaya zaidi hana alichokuwa anakijua
kwenye baadhi ya mambo yaliyosemwa pale mahakamani.
"Sina cha kumtetea mtuhumiwa" Alisema
mwanasheria wa Mr Mlimboka. Nafasi ya kuwa mshitaki
ilipotea pale pale akiwa amesimama. Na kuvikwa cheo cha
mtuhumiwa. Innocent yeye muda wote alikuwa analia tu.
Muda wote macho yake yalikuwa kwa Suzi. Anaiwaza
hukumu ya Hakimu itaamua nini. Kuwatenganisha au
kuwaunganisha.

— 127 —
Hii subira yavuta heri ni ipi waliyokuwa wanaizungumzia.
Mbona kwangu yavuta shari, kwa kipindi chote hiki
nilichomsubiria Suzi inamaana namuacha duniani peke
yake kweli. Kweli kisicho riziki hakiliki.
Alikuwa anajisemea Innocent moyoni mwake. Mawazo
yake yalikatishwa na kelele zilizokuwa zinasikika nje.
Watu wote walikuwa makini kusikiliza ni kelele za nini.
Makelele yaliambatana na vigoma vya kizaramo. Kelele
zao zilionesha kuwa ni za furaha.
Baadae kwa mbali wanasikia
"Pallangyo, pallangyo, Pallangyo"
Mr Mlimboka alipatwa na mshtuko baada ya kusikia jina
la mpinzani wake likivuma kwenye vinywa vya raia
waliokuwa nje.
Taarifa zikaja kuwafikia kuwa Bwana Pallangyo
ameshinda nafasi ya ubunge kwa kishindo. Akili za watu
zikahamia mahakamani baada ya kusikia kishindo cha mtu
aliyedondoka kule mbele. Kumtazama vizuri walimuona
Mr Mlimboka akiwa amejilalia chini na kuhemea juu juu.
Presha ilikuwa imeshapanda. Pumzi zinatoka kwa shida.
Akapoteza hali ya utulivu wa mule ndani. Hakimu
aliamuru wamuwahishe hospitali mara moja ili apate
matibabu.
"Napenda kuitangazia Mahakama kuwa kesi namba
DW 2001 imeghairishwa hadi pale mahakama itakapotoa
wito mwingine kusikiliza kesi hii. Mahakama inamuachia
huru ndugu Innocent hadi pale tutakapomuhitaji
mahakamani kwaajili ya kusoma hukumu yake"

— 128 —
Taarifa hii ilikuwa nzuri kwa baadhi ya watu na mbaya
kwa baadhi yao. Kuna watu walitamani kuona Hakimu
akiimaliza kesi pale. Innocent na Suzi ulikuwa ni wakati
wao wa kuwa pamoja baada ya kutoonana kwa kipindi
kirefu.
Alitoka kizimbani akamkumbatia Mzee Batasi, Inspekta
Major na kumalizia na Suzi.

*******
Mr Mlimboka alipata ruhusa hospitalini na kurejea
nyumbani kwake. Siku hiyo ilikuwa mbaya sana kuliko
siku yoyote katika maisha yake. Alizijaza bia mezani na
kuzinywa bila mpangilio. Wafanyakazi wake walikuja
kumzuia asilewe sana. Lakini kila aliyemsogelea
alikoswakoswa na chupa ya bia. Ilifikia pahala ikabidi
wamuache na kumtazama tu.
Jumba lilikuwa kubwa sana na hakuwa na mtu
wakubadilishana nae mawazo isipokuwa wafanyakazi.
Hata wale chawa waliokuwa wanamfatafata kila pahali
wote walipeperuka. Hakuna aliyetamani kuwa karibu na
Mr Mlimboka kwa kipindi hicho.
Upweke ulipomzidi aliingia chumbani kwake. Hata
nguvu za kutembea hakuwa nazo. Alitambaa hadi akaingia
chumbani.
Pembeni ya kitanda chake kulikuwa na meza iliyokuwa na
karatasi nyeupe na kalamu ya wino na kisu. Alijikongoja
hadi kwenye meza na kuvuta kiti akaketi.
Alichukua ile peni na karatasi na kuandika. Aliandika

— 129 —
kwa shida sana mkono wake ulikuwa unatetemeka.
Akajikaza ili aandike anachokitaka. Aliinyanyua karatasi
yake na kuyasoma yale maandishi mwenyewe. Maandishi
yalisomeka.
Ni kweli hakuna binadamu mbaya ila wote huwa
tunalazimishwa kuwa wabaya. Nimelichukua hili kama
funzo. Naomba ulimwengu utambue kuwa ni kweli

Innocent ni mwanangu wa kumzaa mimi mwenyewe. Na

ana haki kama watu wengine wanaonihusu kwenye

familia yanguTUTAONANA TENA"


"Ahahahahh" Akacheka sana Mr Mlimboka.
Kisha akachukua kile kisu kilichokuwa pale mezani na
kujichoma cha tumbo. Alidondoka chini na kuanza

kutapatapa. Damu zikamwagika nyingi sana. Hatimaye

akapoteza maisha hapo hapo.


*******
Innocent asubuhi na mapema anazipata taarifa na
kufika kwenye la tukio akiwa na Mzee Batasi pamoja na
Suzi. Alikuta ulinzi umeimarishwa katika nyumba ya Mr
Mlimboka. Aliyekuwa anaongoza oparesheni alikuwa
Inspekta Major. Baada ya kumuona alimkimbilia na

— 130 —
kumuuliza kilichojiri. Ndipo akapata taarifa ya kujiua kwa
baba yake. Kisha akakabidhiwa ile karatasi ya mwisho
aliyoiacha ili aisome. Kisha akairejesha kwa Inspekta
Major tena.
Maneno yaliyoandikwa mule yalimchoma sana.
Yalikuwa na ukweli unamuhusu Mr Mlimboka na
unaomuhusu yeye mwenyewe.
Inspekta Major alimpa taarifa ya wito wa mahakama siku
ya kesho yake uliowataka kufika mahakamani saa tatu
kamili asubuhi.

*******
Mahakamani watu walifurika tena kusikiliza hukumu ya
Innocent. Watu walihisi kesi imeisha baada ya kufariki
kwa Mr Mlimboka. Kwasababu mara mwisho yeye ndio
alikuwa na tuhuma nyingi kuliko mtu yeyote.
Hakimu alisimama mbele ya mahakama. Akiwataka watu
wote watege masikio. Hakimu alitazama upande wa
mshitaki wa mashitaka yanayomkabili Innocent hakukuwa
na mtu. Taarifa za kifo cha Mr Mlimboka zilimfikia.
Alihitaji kujua mwanasheria wake yupo wapi.
Mwanasheria hakufika siku hiyo.
Hakimu ikabidi aisome hukumu kama ilivyoamuliwa na
Mahakama.
"Mahakama imepokea taarifa ya kifo cha Mr

Mlimboka na ushahidi wa karatasi ulioachwa na


— 131 —
marehemu akithibitisha kuwa Innocent ni mwanae.

Kutokana na hivyo. Sheria inatambua kesi yoyote lazima

iendeshe na uwepo wa pande zote mbili. Kwa maana

upande wa mashitaka na mshitakiwa. Kwa kipengele hicho,

Mahakama inamuachia huru Ndugu Innocent Mlimboka

baada ya kukosekana kwa upande wa mshitaki" Alimaliza

Hakimu.
"Uuuwi.. Waaooh" Suzi alipiga sauti ya ukunga na kwenda
kumkumbatia Innocent. Watu walifurahishwa na kitendo
kilichofanywa na Suzi kilichoashiria ninamna gani
anampenda Innocent. Watu wote walisimama na
kuwapigia makofi wakiwa wamekumbatiana.
Mzee Batasi akaja kuungana nao wakakumbatiana wote
kwa pamoja. Kisha walitoka wote na kwenda kumfata
Inspekta Major sehemu aliyokuwa amekaa na
kumkumbatia wote. Machozi yafuraha yakiwatoka wote
kwa pamoja wakiwa wamekumbatiana.
"Huu ushindi ni wako kaka" Alisema Innocent
akimuambia Inspekta Major.
"Hapana huu ni ushindi wetu sote"
Wakacheka tena kwa sauti ya juu machozi yakiendelea

— 132 —
kuwatoka na kukumbatiana kwa nguvu.

************
Asubuhi ya siku iliyofuata Inspekta Major na Innocent
walikutana sehemu moja tulivu kila mmoja akiwa
ameshika glasi wakinywa. Meza ilikuwa imejaa chakula.
Wakipiga stori za hapa na pale.
"Kaka mimi naomba nikushukuru sana kwenye hili, maana
nilikuwa naozea jela" Alisema Innocent.
"Huna haja ya kunishukuru. Nilifanya hivi kwa maana
kubwa sana. Mr Mlimboka alikuwa na makandokando
mengi sana ninayoyajua. Hakustahili kuwa kiongozi wa
kuwaongoza watu. Mara zote kiongozi ni mfano wa
kuigwa. Unahisi alikuwa na kipi cha kuigwa"

"Mh.. Hana" Alijibu Innocent.


"Ila nakupa onyo shukuru Mungu uliniweka bayana kuwa
ni kweli ulihusika na yale mauaji. Lakini ikija kutokea siku
nyingine jambo lolote la kuvunja sheria basi jua mimi
sitakuwa inspekta Major huyu unayemuona hapa.
Nitakubadilikia hadi hutoamini na sheria itafuata mkondo
wake"
"Nimekuelewa kaka. Niamini mimi, nimeshamaliza kisasi
changu chote kuanzia leo nitaisha maisha yangu kwa
kufuata sheria"

Ahahahaha..

— 133 —
Walicheka kwa pamoja.
Walimalizia vinywaji vyao kisha wakaondoka.

MWISHO

— 134 —

You might also like