You are on page 1of 781

MAGOGONI HAS FALLEN

(Magogoni Imeanguka)

MAGOGONI
HAS
FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Planet Link Publishers


Dar es Salaam- Tanzania

1 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

MAGOGONI
IMEANGUKA
Kimepigwa chapa kwa mara ya kwanza Tanzania, mwaka 2023
copyright© 2023 Aziz Hashim

Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuiga, kunakili, kupiga


chapa, kuhifadhi au kukibadili kwa njia au mfumo wowote, au
kukitumia kitabu hiki kwa malengo tofauti na yaliyokusudiwa
bila idhini ya maandishi kutoka kwa mwandishi.

Printed and bound in Tanzania by


Planet Link Publishers Ltd
Dar es Salaam

ISBN 978 9987 9334 1 9

2 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

MAGOGONI
IMEANGUKA

Januari 25, 2017


1

Kijitonyama Kisiwani, Dar es Salaam.

MUME wangu, ujue kuna wale majirani zetu


waliohamia kwenye ile nyumba ya Mzee Ngafu
pale karibu na uwanja wa mpira wa shule siwaelewi
kabisa.”
“Huwaelewi kwa nini?”
“Kwanza muda wote mwanamke hatoki nje, anashinda kutwa
nzima akiwa amejifungia ndani, akitoka anavaa baibui na nikabu
juu, yaani unamuona macho tu.”
“Sasa tatizo liko wapi mke wangu? Mjini hapa kila mtu ana mai-

3 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

sha yake.”
“Siyo hivyo, kingine mwanaume wake naye anaonekana usiku
tu, tena anaingia kwa machale kwelikweli na anatoka alfajiri. Huu
ni mwezi wa pili sasa lakini hata sura zao hakuna anayezijua hapa
mtaani.”
“Bado sioni kama kuna tatizo mpaka halo, hapa ni mjini mke
wangu, kila mtu na maisha yake, mambo ya kufuatiliana hayana
maana kabisa.”
“Kwa hiyo ninachokueleza hakina maana si ndiyo?”
“Siyo hivyo, sijaona kama kuna tatizo katika maelezo uliyonipa,
umefanya jambo zuri kuniambia lakini kama nilivyokueleza, sija-
ona tatizo hapo.”
“Tatizo lipo! Juzi usiku nilipotoka kwenda kukinga maji uani,
nimeona kundi la kama watu nane hivi, wanawake kwa wanaume
wakiingia mle ndani. Nahisi kuna jambo linaloendelea ambalo
tunatakiwa kuwa nalo makini sana, pengine siyo watu wazuri.”
“Hebu ngoja kwanza, ulitoka usiku wa saa ngapi?”
“Kama saa nane hivi, si unajua maji yalikuwa yamekatika wiki
yote hii, sasa usiku nikaanza kuyasikia yakitoka, nikaona bora ni-
kakinge vyombo ili hata yakikatika tena tusihangaike, wewe hush-
indi nyumbani huijui shida tunayoipata maji yanapokatika,” wa-
nandoa wawili vijana, walikuwa wakijadiliana jioni moja wakiwa
chumbani kwao ndani ya nyumba ya vyumba viwili walivyokuwa
wanaishi.
Mwanaume, Denis Mtama alikuwa akifanya kazi ya uandishi wa
habari za uchunguzi huku mkewe, Hope akiwa ni mfanyabiashara

4 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ndogondogo aliyefungua genge nje ya nyumba waliyokuwa wakii-


shi.
Kwa kuwa mwanamke huyo alikuwa akishinda muda wote
kwenye genge lililokuwa nje ya nyumba waliyokuwa wamepanga,
alikuwa na nafasi ya kujua mambo mengi yaliyokuwa yanaendelea
katika mtaa huo waliokuwa wanaishi kuliko mtu mwingine yeyote.
“Kwa hiyo unataka kusemaje mke wangu?”
“Wewe si mwandishi wa habari? Unaweza kuitumia taaluma
yako kujua ukweli wa kinachoendelea, dunia imebadilika hii,
unaweza kukuta ni watu wabaya wanapanga mambo yao halafu
sisi tunawatazama tu,” alisema Hope, wazo ambalo Dennis aliliona
kuwa la msingi sana.
“Unisamehe kwa sababu mwanzo nilihisi ni umbea tu unakusum-
bua maana mke wangu na wewe kwa umbea, kila siku mna kazi ya
kusutana hapo kwenye genge lako,” alisema Dennis kimasihara,
wote wakacheka na kujilaza kitandani kwa sababu tayari ilikuwa
ni saa nne za usiku.
Mazungumzo ya hapa na pale yakaendelea mpaka walipopitiwa
na usingizi.
Kesho yake asubuhi, Dennis aliwahi kuamka kuliko siku ny-
ingine zote, kikubwa ilikuwa ni kutaka kufuatilia kwa undani kile
alichoelezwa na mkewe usiku huo kuhusu majirani zao wapya
waliokuwa wamehamia mtaani hapo.
Kwake hiyo ilikuwa ni fursa ambayo ingeweza kumuingizia
kipato, mara kadhaa habari nzito za uchunguzi alizokuwa akizi-
fanya na kuibua mambo makubwa, zilikuwa zinaifanya kampuni

5 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

aliyokuwa akifanyia kazi, ilikuwa ikimlipa fedha nyingi na wakati


mwingine kupokea pongezi ya fedha taslimu kutoka kwa vyombo
vya ulinzi na usalama au viongozi kutokana na jinsi alivyokuwa na
uwezo wa kuibua mambo mazito.
“Naweza kupiga hela hapa nikaenda kuanza ujenzi kwenye
kiwanja changu cha Bunju,” alijisemea Dennis wakati akitem-
bea taratibu kuelekea kwenye ile nyumba ambayo mmiliki wake
alishahamia kwenye nyumba yake mpya na kuipangisha nyumba
hiyo.
Dennis aliendelea kuitazama kwa umakini asubuhi hiyo, hakuku-
wa na dalili zozote za watu kuwepo ndani kwa sababu ya ukimya
uliotawala ingawa mwenyewe alikuwa na uhakika kama kuna watu
ndani kama alivyoelezwa na mkewe.
Aliipita kisha mbele kidogo akageuza na kurudi alikotoka, kwa
mara nyingine akapata nafasi ya kuchunguza vizuri mandhari
yake. Usingeweza kudhani kama kuna watu walikuwa wanaishi
ndani yake kwa jinsi ilivyokuwa kimya, tofauti kabisa na nyumba
nyingine katika mtaa huo.
Wazo alilolipata, lilikuwa ni kwenda kwa mjumbe wa serikali ya
mtaa huo, akiamini huenda anaweza kuwa na taarifa zaidi.
“Ndugu mwandishi, habari za asubuhi kijana, vipi leo umekuja
kupeleleza kuhusu nini maana na wewe kwa upekepeke hujambo,”
alisema Mzee Matola, Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kijitonya-
ma Kisiwani, ambaye alikuwa amezoeana sana na kijana huyo,
wakati mwingine wakicheza drafti pamoja.
“Nimekuija kupeleleza nasikia unakula hela za ulinzi shirikishi,

6 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

nataka nikukamatishe TAKUKURU,” alisema Dennis kwa masi-


hara na kumfanya mzee huyo acheke sana.
“Sikutarajia kama nitacheka kiasi hiki asubuhi yote hii, hakika
leo siku yangu nimeianza vizuri,” alisema huku akitoa viti viwili na
kuviweka chini ya mti, akakalia kimoja na kingine kumpa Dennis
kwa sababu alikuwa na uhakika kwamba ujio wake asubuhi hiyo
lazima ulikuwa na jambo zito.
“Haya unaendeleaje kijana wangu!”
“Sijambo mzee shikamoo!”
“Marahabaa, kabla hujaniambia kilichokuleta, nataka kukuuliza,
eti kinachoendelea huko Kibiti na Mkuranga ni nini maana hat-
uelewi!”
“Hatupo salama mzee wangu, makundi yenye itikadi kali za
kidini na kisiasa yamejipenyeza nchini kwetu na kusambaza itikadi
zao, watu wanauawa kikatili sana, tena bila hatia.”
“Nasikia jana kuna mwenyekiti wa serikali ya mtaa mwingine
kauawa!”
“Ni kweli, wamemvamia nyumbani kwake usiku, wakamchukua
yeye peke yake na kuwaacha mke wake na watoto, wakaondoka
naye na walipofika mita kadhaa kutoka kwenye nyumba yake,
wakamfunga kamba mikononi na kumpigisha magoti, wakampiga
risasi ya kichwa!”
“Mungu wangu! Huu si ni ugaidi kabisa huu? Na kwa nini wa-
nawaua viongozi wa serikali na askari pekee?”
“Bado hatujui ni kwa sababu gani lakini jeshi la polisi na vyombo
vingine vyote vya usalama vinaendelea na kazi yake, tuwaachie

7 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wafanya kazi yao na naamini ndani ya muda mfupi tu ukweli wote


utajulikana,” alisema Dennis, mzee huyo akashusha pumzi ndefu
na kukaa vizuri kwenye kiti chake.
“Enhee, haya niambie!”
“Una taarifa zozote za watu waliohamia kwenye nyumba ya
Mzee Khatib Ngafu?”
“Ndiyo, japo siyo kwa undani! Yule mzee alinipigia simu na
kunieleza kwamba kuna mpangaji amempata na wameshakubali-
ana kila kitu kwa hiyo atahamia na akifika, amemueleza aje kuri-
poti kwangu kama sheria za mtaa wetu zinavyosema! Kwa hiyo
watakapohamia bila shaka watakuja hapa tufahamiane.”
“Mbona wameshahamia miezi takribani miwili sasa inaisha?”
“Acha masihara! Kuna watu wanaishi mle?”
“Ndiyo! Mimi mwenyewe nilikuwa sijui, mke wangu ndiyo aliy-
enieleza.”
“Sasa wanaishije wakati sijawahi kumuona mtu akiingia wala
kutoka na usiku taa zote za ndani na nje zinakuwa zimezimwa?”
“Basi habari ndiyo hiyo, kilichonishtua zaidi, mwenendo wa mai-
sha yao unatia shaka! Mke wangu ameniambia kwamba wanaishi
wawili ambao kwa kuwatazama wanaonesha ni mume na mke.
“Mke huwa hatoki kabisa nje na akitoka basi ujue ni kwa nadra
sana na anakuwa amejiziba mwili wote na kuacha macho tu. Mwa-
naume naye aiarudi usiku na kuondoka alfajiri.
“Yote tisa, kumi ni kwamba mke wangu ameniambia juzi aliwa-
ona watu kama nane hivi wanawake kwa wanaume wakiingia pale
ndani usiku wa manane! Kuna jambo linaloendelea na tunatakiwa

8 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kuwa makini sana.”


“Kwa nini tuandikie mate wakati wino upo, twende mguu kwa
mguu tukahakikishe kinachosemwa,” alisema mjumbe huyo wa
serikali ya mtaa, wakatoka pamoja na kuelekea kwenye nyumba
hiyo na walipofika, mjumbe alibisha hodi.
Licha ya kubisha hodi mara kadhaa na kugonga sana mlango,
hakukuwa na mwitikio wowote kutoka ndani ingawa mlango
ulionesha kufungwa kwa ndani kuashiria kwamba ndani kulikuwa
na watu.
“Mimi ni mjumbe wa serikali ya mtaa, kama kuna mtu ndani
tafadhali fungua mlango,” alisema mjumbe huyo lakini hakukuwa
na majibu yoyote.
Ilibidi waondoke lakini wakati wanageuka na kuipa nyumba
mgongo, kuna kitu kilimtuma Dennis kugeuka nyuma na kutaza-
ma kwenye dirisha lililokuwa pembeni ya mlango, akakutana na
macho ya mtu aliyekuwa akiwatazama ambaye alipoona Dennis
amemuona tu, harakaharaka alijificha.
“Vipi?”
“Nimeona kama kuna mtu alikuwa anachungulia!”
“Mh! Mbona haya mambo yanatia wasiwasi, hebu tujaribu tena
kugonga mlango!” alisema mjumbe huyo, kweli wakarudi na ku-
gonga lakini bado majibu yalikuwa ni yaleyale, hakukuwa na mtu
yeyote aliyeitikia au kufungua mlango.
“Una uhakika umeona mtu kweli?”
“Ndiyo! Nimemuona mtu kwa macho yangu, nina uhakika wa
asilimai 100,” alisema Dennis wakati wakiondoka.

9 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Inabidi tutoe taarifa polisi, kunaweza kuwa kuna jambo zito


hapa!”
“Hapana, tusitoe kwanza taarifa, naomba unipe siku moja
ya leo nifanye kazi yangu halafu kesho ndiyo tutawapa taarifa
polisi,” alisema Dennis kwa msisitizo.
“Hapana, kesho ni mbali! Kwa mambo yanayoendelea huko
Kibiti na Mkuranga unaweza kukuta anayelindwa ni mimi, nisije
nikauawa!” alisema mjumbe huyo kwa hofu.
“Uuawe kwa sababu gani? Umefanya kosa gani?”
“Kwani hao wanaopigwa risasi kila kukicha wamefanya ma-
kosa gani?”
“Acha woga we mzee!” alisema Dennis huku akicheka,
mjumbe naye akajaribu kujichekesha lakini ndani ya moyo wake
alishakuwa na hofu isiyo na kipimo.
Baada ya kubishana kidogo, hatimaye walikubaliana kwamba
mjumbe huyo wa serikali ya mtaa asiende kutoa taarifa polisi
kwanza ili kumpa nafasi Dennis ya kufanya kazi yake kwa sa-
babu tayari alikuwa na uzoefu wa kufanya habari za kiuchunguzi
kwa uwezo wa juu kabisa.
Baada ya mazungumzo hayo, Dennis aliondoka kwenda kwe-
nye majukumu yake ya kila siku lakini kabla ya kuondoka, alirudi
kwanza nyumbani kwake kwenda kumpa taarifa mkewe juu ya
walichokuwa wamekibaini.
“Umekubaliana na mimi sasa eeh, si uliona kama nakuletea
habari za umbea,” alisema mwanamke huyo na kusababisha wote
wacheke, wakaagana kisha Dennis akaondoka kuelekea kazini

10 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kwake.
Baada ya kuwasili kazini, kwa kuwa tayari jambo alilokuwa
analifuatilia lilikuwa na ishara ya kutishia usalama wa taifa, ilibidi
atoe taarifa kwa mtu maalum aliyekuwa anawasiliana naye mara
kwa mara kama ‘informer’ na kumjuza kilichokuwa kinaendelea.
***
Mtihani wangu wa kwanza baada ya kuwa nimerejea maso-
moni kutoka nchini Israel, ilikuwa ni wimbi la matukio ya uporaji
magari, uvamizi wa vituo vya polisi na kuporwa silaha lakini yote
tisa, kumi ilikuwa ni mauaji yaliyokuwa yanatingisha katika mae-
neo ya Mkuranga, Kibiti na Rufiji.
Nasema ulikuwa ni mtihani mkubwa kwa sababu ndani ya muda
mfupi niliofanya kazi, nilitokea kuaminiwa na viongozi wangu wa
ngazi za juu kabisa na kila tatizo lililokuwa linatokea, mimi ndiye
niliyekuwa nafikiriwa haraka kwamba naweza kuwa na mbinu za
kujua nini cha kufanya.
Sina haja ya kujitambulisha sana, wengi tayari mnanijua, Kenny
hapa, au Snox lakini kwa kuwa sasa hivi nilikuwa nimepanda
ngazi, wengi walikuwa wanapenda kuniita Chief na taratibu jina
hilo lilianza kuwa maarufu kuliko hata lile la Snox.
Hatua ya kwanza ilikuwa ni kujaribu kuyatazama matatizo yote
matatu na kujua ni kwa namna gani yalikuwa na uhusiano, na-
maanisha ujambazi wa kupora magari, matukio ya kuvamia vituo
vya polisi na mauaji ya watu yaliyojawa na utata mkubwa yali-
yokuwa yakiendelea Kibiti, Mkuranga na Rufiji.
Waliokuwa wananiamini hawakuwa wanakosea, mafunzo nili-

11 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

yoyapata awali kitengo na yale niliyoenda kuyapata nchini Israel,


yalinifanya kuwa na uwezo mkubwa sana wa kugundua jambo
ambalo kwa akili ya kawaida, ingewachukua wengine muda
mrefu sana kupata picha.
Matukio haya matatu yaliyokuwa yakitokea kwa kasi, kwangu
yalikuwa ni ishara kwamba kuna jambo linaloenda kutokea lakini
ilikuwa kazi ngumu sana kuwaaminisha wenzangu kwamba ma-
tukio haya yalikuwa na uhusiano.
Ilikuwa ni lazima kwanza nipate ushahidi wa kutosha, niwe na
taarifa za kutosha kisha ndipo niwasilishe kwa viongozi wangu
wa juu ili kwa pamoja, tujue nini cha kufanya kumaliza kabisa
matukio yote.
Kwa hiyo, nilichokifanya kwanza ilikuwa ni kuwa macho kuy-
atazama matukio yote, kujua nani na nani wanahusika na uhusika
wao umekaaje. Ni hapa ndipo nilipoamua kwanza kuanza kulifua-
tilia tatizo la uporaji wa magari lililokuwa limeshamiri. Niliamua
kuanzia huku kwanza kwa sababu kuna jambo nilikuwa nimeli-
hisi.
Ndani ya muda mfupi tu, tayari nilikuwa nimeshapata picha
kamili kuhusu nini hasa kilichokuwa kinaendelea kwenye ujam-
bazo wa magari. Nilibaini kwamba kulikuwa na makundi mawili,
kundi la kwanza lilikuwa ni wahalifu wa kawaida lakini kundi
la pili lilikuwa ni watu ambao huwezi kusema ni wahalifu wa
kawaida.
Nitafafanua ni kwa nini nasema hivi na mbinu iliyofanya niujue
ukweli huo ambao wengine hawakuwa wakiujua, ilikuwa ni ku-

12 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

watumia wahusika wenyewe kuwa ‘macho’ yangu.


Kama ambavyo mimi niliweza kugeuzwa kutoka upande mmoja
hadi kwenda upande mwingine, mimi pia nilikuwa naamini zaidi
katika falsafa hii kwamba unapowakamata kwa mfano majam-
bazi, badala ya kuwapiga risasi au kuwapeleka jela wakaenda
kuozea huko, unaweza kuwachukua wachache kati yao ambao
wanaweza kuwa msaada mkubwa kwako kwa kukuonyesha ni
kwa namna gani huwa wanafanya uhalifu huo na huwa wana-
sirikiana na nani.
Nilijifunza kwa undani kuhusu mbinu hii nilipokuwa nchini
Israel na hata niliporudi nchini, niliamua kuwa nitakuwa naitumia
hiyo zaidi kuliko ile iliyokuwa imezoeleka ya ‘kuwanyang’anya’
silaha majambazi kwa kutumia nguvu.
Ninaposema kuwanyang’anya bila shaka utakuwa unanielewa
vizuri kwamba mtu akiwa na bunduki, ni kwa namna gani una-
vyoweza kumnyang’anya kabla hajakudhuru.
Sikuwa naikubali kabisa falsafa hii na niliamua kuja kuonesha
tofauti ili hata siku nikisimama mahali na kuwaelekeza wenzan-
gu, kuwe na ushahidi wa kutosha wa namna nilivyofanikiwa
katika njia tofauti.
Basi katika oparesheni ya kupambana na wezi wa magari, kama
nilivyosema nilibaini kwamba kulikuwa na makundi mawili, wezi
wa magari wa kawaida lakini na kundi jingine lisilo la kawaida.
Nilitumia mbinu shirikishi kwa kuwatumia baadhi ya wahusika
ambao walikamatwa katika oparesheni hiyo ambao walikuja
kugeuka na kuwa msaada mkubwa sana kwangu. Hili pia nitakuja

13 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kulieleza.
Sasa hili kundi la pili, lenyewe lilikuwa na namna ya tofauti
kabisa ya kufanya uhalifu wao. Kwanza, matukio ya uporaji
wao wa magari, yalikuwa yakihusisha mauaji. Yaani wao wa-
likuwa wakilitaka gari, basi hakuna mjadala, ni aidha uwape
wakuache au uuawe kisha walichukue.
Mbinu hii ilikua ngeni kabisa na ile iliyokuwa inatumiwa
na wezi wa kawaida wa magari ambao wala hawakuwa na
shida ya kuondoa uhai wa mtu wala kujeruhi, hawa wenyewe
walikuwa wakiwafunga kamba madereva na kwenda kuwa-
telekeza mafichoni bila kuwadhuru hata kidogo.
Lakini pia kulikuwa na tofauti nyingine kubwa ambayo
ilizidi kunipa wasiwasi ambayo ni aina ya magari yaliyokuwa
yanaibwa. Inafahamika kwamba wezi wa kawaida wa magari,
huwa wanayalenga magari ya kifahari hasa matoleo mapya
yanayopendwa zaidi.
Lakini kundi hili la pili, lenyewe lilikuwa likiyalenga
magari yenye uwezo mkuba wa kupita hata katika maeneo
ambayo hakuna barabara nzuri, yaani wao walikuwa wanazi-
lenga zaidi gari za kazi. Kwa wale wenye uelewa wa magari
watakuwa wanaelewa ninaposema magari ya kazi namaanisha
ya aina gani.
Kwa kifupi ni yale matoleo ya magari kama Toyota Land-
cruiser, Nissan Patrol, Land Rover na ya aina hiyo. Ilikuwa ni
dhahiri kwamba magari hayo hayaendi kuuzwa kwa sababu

14 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

hata soko lake ni gumu, swali likawa ni je, yanapelekwa wapi?


Mpaka hapo tayari nilikuwa nimeshapata mwanzo mzuri na
nashukuru kwamba timu niliyokuw anafanya nayo kazi ilikuwa
makini sana.
Baada ya kupata mwanga katika tatizo la kwanza la uporwaji
wa magari, nilianza pia kushughulikai suala la pili, uporwaji wa
silaha katika vituo vya polisi. Kama nilivyoeleza, ni katika kip-
indi hiki pia kulikuw ana matukio mengi ya watu wenye silaha
kuvamia vituo vya polisi na kupora silaha kisha kutokomea nazo
kusikojulikana.
Wakati nikiwa naendelea kulifuatilia suala hili kwa karibu,
ndipo nilipopigiwa simu kutoka kwa moja kati ya vyanzo vyangu
vya kuaminika kabisa. Ilikuwa ni simu iliyoonesha kwamba kuna
mtu au watu wamepanga nyumba katika eneo moja lililop[o Ki-
jitonyama Kisiwani na nyendo zao zilikuwa ni za kutoa shaka.
Japo kwa mtu mwingine taarifa hizi zinaweza kuonekana kuwa
hazina uzito, nilishajifunza kutodharau taarifa yoyote, hata kama
itaonekana kuwa nyepesi kiasi gani.
Sijui kwa nini nilivutiwa zaidi na taarifa hii ambayo kwa bahati
nzuri zaidi, haikuw aimeripotiwa polisi kwa hiyo ilikuwa mbi-
chi na inayoweza kunifikisha mahali ambapo nitapata majibu ya
maswali mengi yaliyokuwa yanakisumbua kichwa changu.
Hatua ya kwanza ilikuwa ni kuomba kukutanishwa na mtoa
taarifa.
Niliwasiliana na wenzangu wa kitengo cha ‘Information’ am-

15 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

bao ndiyo huwa wanashughulika moja kwa moja na watoa taarifa


wetu wanaoshirikiana nasi kutupa taarifa moja kwa moja kutoka
kwa jamii.
Nilipewa mawasiliano ya mtoa taarifa wetu na muda huohuo ni-
limpigia simu na kujitambulisha, nikaomba kukutana naye. Ndani
ya muda mfupi tu, tayari nilikuwa nimekaa kwenye meza moja na
mtoa taarifa wetu ambaye sura yake haikuwa ngeni kwangu.
“Mimi na wewe tumewahi kukutana?”
“Sina uhakika lakini mimi nakufahamu vizuri tu,” alisema, ni-
kaachia tabasamu hafifu.
“Code number?”
“Eagle 4 MT 72213.”
“Service?”
“Information!”
Ilikuwa ni lazima nimuulize maswali ya kiufundi ili kwanza
kuwa na uhakika kama mtu niliyekuwa naye mbele yangu ndiye
hasa niliyekusudia kuzungumza naye. Maelezo yake yalioana na
maelezo ya kwenye faili lake nililolitazama kwanza ofisini kabla
ya kuamua kumtafuta.
Maelezo haya ni ya kiufundi ambayo mtu ambaye hajui maana
yake hawezi kujibu na hata akijibu, hawezi kukisia, lazima awe
kweli anajua anachokizungumza. Baada ya kujiridhisha na majibu
yake, sasa niligeukia kwenye kazi iliyonifanya nikamtafuta.
“Tumepokea taarifa kutoka kwako lakini kutokana na uzito wake
nimeona ni muhimu mimi na wewe tukikutana ana kwa ana kwa
sababu naamini hili likishughulikiwa kwa mfumo wa kawaida,

16 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

tunaweza kuchelewa.”
“Ni sahihi kabisa, hata mjumbe wa serikali ya mtaa ninaoishi
alikuwa na haraka ya kutaka kuwasiliana kwanza na polisi lakini
nikamzuia kwa sababu kuna jambo kubwa ambalo nimelihisi,”
alisema, nikashusha pumzi ndefu na kuanza kumhoji kwa undani.
Maelezo yake yote yalikuwa yakinaswa moja kwa moja na vifaa
maalum na vya kisasa vya mawasiliano nilivyokuwa nimevivaa
mwilini ambavyo isingekuwa rahisi kwa mtu yeyote kuviona au
hata kuvihisi.
Maelezo aliyonipa yalinifanya nipate shauku kubwa ya kwanza
kufika kwenye nyumba aliyokuwa ananielezea lakini pia kuweka
vijana wa ‘rada’ ambao wangenisaidia kulitazama suala hilo kwa
karibu zaidi.
Baada ya maelezo na mtoa taarifa wangu, tulitoka pamoja na
kwenda mpaka kwenye gari langu, tukaondoka pamoja kuele-
kea ‘field’ nikiwa na maana ya eneo la tukio. Kwa kuwa sikuwa
naifahamu vizuri mitaa ya Kijitonyama, ilibidi yeye ndiyo anion-
goze, nikawa nafuata maelekezo yake na hatimaye tukafika eneo
husika.
Mwonekano wa mazingira ya nje ya nyumba hiyo, ilionesha
dhahiri kwamba kuna jambo lisilo la kawaida lililokuwa linaende-
lea ndani ya nyumba hiyo, tukapita taratibu huku nikiwa makini
kutazama kila kitu.
“Mimi naishi hapo gengeni, nashukuru kwa kunifikisha nyum-
bani!”
“Hapana, hutakiwi kushuka ili usije ukajihatarisha, hatakiwi

17 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

mtu yeyote kujua ni nani aliyepo ndani ya gari,” nilimwambia,


nikaendesha gari mpaka mwisho wa mtaa, nikatafuta sehemu ya
kugeuza kisha tukarudi na njia ileile tuliyokuja nayo.
Safari hii ilibidi nichukue ushahidi wa video ili ikawe rahisi
hata kuwaelekeza vijana wangu nini cha kufanya, nikafanya
hivyo bila hata mtoa taarifa kujua kama nilikuwa nafanya kitu
gani.
“Nikuache wapi? Najua muda huu hukuwa nyumbani, ulikuwa
kwenye kazi zako,” nilimwambia, nikawa ni kama nimemzindua
kutoka kwenye lindi la mawazo, akanitazama na kujaribu kuachia
tabasamu hafifu.
“Unaonesha una hofu?”
“Kuna jambo aliniambia mjumbe wa serikali ya mtaa asubuhi
nikawa ni kama nimepuuza lakini naona kuna kitu kinaniingia
akilini.”
“Jambo gani?”
“Alikuwa na hofu kubwa kwamba huenda watu hawa wanamu-
winda kumuua yeye kwa sababu ni kiongozi, kama wanavyofan-
ya huko Kibiti na Mkuranga.”
“Unafahamu nini kuhusu Kibiti na Mkuranga?”
“Sina cha ziada ninachokifahamu zaidi ya taarifa ambazo watu
wote tunazisikia na kuziona kwenye vyombo vya habari.”
“Usiwe na wasiwasi, hili tutaalishughulikia ndani ya muda
mfupi tu na majibu yatapatikana, vyombo vya ulinzi na usalama
vipo macho saa 24 kuhakikisha tunakomesha haya mambo. Haku-
na waandishi wenzako ambao unafahamiana nao huko ambao

18 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wanaweza kutusaidia?”
“Umejuaje kama mimi ni mwandishi wa habari?”
“Aaah! Dennis, hivi ukisikia neno serikali huwa unalichuku-
liaje?”
“Lakini hata jina langu pia sijakwambia mahali popote katika
mazungumzo yetu! Umelijuaje?”
“Najua kila kitu kukuhusu wewe kwa sababu hii ni kazi yangu,”
nilisema huku nikijaribu kutabasamu kwa sababu ilionesha mtoa
taarifa wangu bado alikuwa mgeni kwenye kazi yake na pengine
hata hakuwa ananijua vizuri kama alivyojinasibu mwenyewe
mwanzo.
Basi nilirudi naye mpaka Mlimani City, nikamuacha palepale
nilipomkuta na kuchomoa noti kadhaa na kumkabidhi. Haukuwa
utaratibu wetu kupeana fedha kienyeji namna hiyo lakini nililaz-
imika kufanya hivyo kama njia ya kutafuta ukaribu zaidi na mtoa
taarifa wangu.
“Muda wowote ukihisi upo kwenye hatari yoyote nipigie simu,”
nilimwambia, akashusha pumzi ndefu na kunishukuru.
Niliondoka na moja kwa moja nilirudi ofisini ambapo kitu cha
kwanza ilikuwa ni kuwaita vijana wangu wawili ambao nilikuwa
nawaamini sana kwenye kazi. Niliwapa maelekezo yote na ku-
waeleza nini kinachotakiwa kufanyika haraka iwezekanavyo.
Kilichofuatia baada ya hapo ilikuwa ni utekelezaji wa haraka,
taarifa za akina nani waliokuwa wanaishi ndani ya nyumba ile
na kwa nini walikuwa wakijifichaficha muda wote. Maelekezo
yangu ilikuwa ni kuhakikisha taarifa zote muhimu zinapatikana

19 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

haraka iwezekanavyo lakini mimi pia sikutaka kuwaachia peke


yao.
Niliwateua vijana wangu wengine wawili kwa ajili ya kuwa
wanawafuatilia wale wawili wa mwanzo niliowapa majukumu
halafu nyuma yao, mimi pia nikawa nawafuatilia wote wanne
walivyokuwa wanafanya kazi niliyowaagiza, huo ndiyo utaratibu
wetu wa kazi.
Ukipewa jukumu la kufuatilia jambo fulani, basi ujue kuna mtu
mwingine ambaye wewe humjui naye ametumwa kukufuatilia
kwa karibu kuangalia namna unavyofanya kazi uliyopewa.
***
“Mume wangu, mbona leo umewahi sana kurudi nyumbani?”
“Aaah, sijisikii vizuri mke wangu, nahisi uchovu sana, nahisi ni
kwa sababu sijapumzika, umeshindaje?”
“Sijambo!”
“Kuna mapya gani?”
“Hakuna mapya, ila kuna yule mdada aliyekaa pale nje ulipotu-
pita akiwa na beseni la kuuzia matunda.”
“Enhee, amefanya nini?”
“Mh! Ananipa wasiwasi kwa sababu ametoka huko akiwa na
beseni lake kichwani limejaa matunda, alipofika hapo gengeni
kwangu akaanza kuniomba eti na yeye anataka awe anauzia
matunda yake pale pembeni ya genge kwa sababu amechoka
kuwa anazungusha juani kutwa nzima, ameniambia yupo tayari
hata kuwa ananilipa lakini nikimuangalia mtu mwenyewe mbona
kama hafanani na kazi ya kuuza matunda? Wewe mwenyewe si

20 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

umemuona?”
“Mh! Hebu nionyeshe vizuri ni yupi?” Dennis alimwambia
mkewe huku wote wakisogea dirishani, wakawa wanachungulia
kule gengeni ambapo mkewe alimuonesha mhusika mwenyewe
aliyekuwa akimzungumzia.
Alikuwa ni msichana ambaye kiumri hakuwa na zaidi ya miaka
26 na mwonekano wake haukuwa ukifanana na kazi aliyokuwa
akiifanya. Japokuwa alijitahidi kuvaa nguo zilizochokachoka
lakini rangi ya ngozi yake ilionesha kabisa siyo mtu anayefanya
kazi za kutembea juani au siyo mtu ambaye alikuwa na maisha
magumu kama mwenyewe alivyokuwa akitaka kuwaaminisha
watu.
“Mkubalie!”
“Nimkubalie kivipi sasa? Yaani mtu anakuja tu huko simjui
halafu nimkubalie, au mnajuana?”
“Hapana sijuani naye kwa chochote!”
“Sasa kwa nini unasema nimkubalie? Au ndiyo mke mwenzan-
gu nini?” alisema mke wa Dennis na kuanza kuchachamaa aki-
taka aeleweshwe.
“Sasa mimi nikueleweshe nini wakati mimi ndiyo kwanza
namuona? Mimi nimekushauri umkubalie kwa sababu sisi bin-
adamu tumeagizwa upendo, kama mtu amekuja kukulilia shida,
na biashara yake haiingiliani na yako kwa nini umzuie? Kwani
wewe huwa unauza matunda?”
“Hapana lakini sijui kwa nini moyo wangu una wasiwasi naye.
Ananihojihoji maswali ambayo siyaelewei.”

21 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Nisikilize, mkubalie kwa moyo mweupe kabisa, huwezi kujua


anaweza kuja kuwa msaada kwetu kwa namna amabayo hatuku-
itegemea kabisa.
“Halafu mbona ananihojihoji sana?”
“Anakuhoji kuhusu nini zaidi?”
“Mambo mengi tu, anakuwa na hamu ya kujua mambo mengi
kuhusu huu mtaa wetu na watu wake,” alisema mwanamke
huyo. Mpaka hapo tayari Dennis alishakuwa na majibu juu ya
kilichokuwa kinaendelea ila hakutaka kuwa mwepesi wa kuzun-
gumza chochote, akitaka ajiridhishe kwanza.
Alichokuwa na uhakika nacho ni kwamba kukutana kwake na
‘Chief’ asubuhi hiyo, kulishaanza kuzaa matunda na alikuwa na
uhakika kwamba ‘muuza matunda’ aliyekuwa anazungumziwa
na mkewe, hakuwa muuza matunda wa kawaida kama ambavyo
watu wengine wote wangeweza kuhisi.
Muda ulizidi kuyoyoma, yule muuza matunda aliendelea kuka
apale gengeni mpaka majira ya saa tatu usiku ndipo alipoaga na
kuondoka lakini aliomba mzigo wake wa matunda ubakie hapo-
hapo gengeni ili kesho yake awahi kuja kuendelea na biashara.
“Naogopa mume wangu!”
“Unaogopa nini mke wangu?”
“Isije kuwa kuna watu wanatuwinda, huku tumepata majirani
wasioeleweka, huku nako anakuja muuza matunda ambaye hata
haeleweki, hii inamaanisha nini?”
“Sidhani kama tunatakiwa kuwa na wasiwasi na maisha yetu,
pengine ni nguvu mbili zinashindana, hasi na chanya!”

22 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Unamaanisha nini?”
“Namaanisha kwamba pengine kile tunachokihofia tayari seri-
kali imeshakiona na sasa inakifanyia kazi kwa karibu.”
“Kwani ulienda kutoa taarifa polisi?”
“Hapana, kwani umeona polisi wamekuja hapa?”
“Sasa ni nini hiki? Najua unajua lakini hutaki kuniambia!”

23 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

24 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

2
K
WA kutumia vijana maalum, niliendelea kufua-
tilia kwa karibu taarifa tulizopewa na mtoa taarifa
wetu asubuhi ya siku hiyo na kitu ambacho niliona
kinaweza kufaa zaidi, ilikuwa ni kuweka watu wa
kufuatilia nyendo za watu waliokuwa wanaishi
kwenye nyumba ile kama walikuwepo, kwa muda wa saa ishirini
na nne.
Hiyo ilikuwa mbinu ya kwanza lakini mbinu nyingine ambayo
hii ilikuwa ya kitaalamu zaidi, ilikuwa ni kufuatilia mawasiliano
yote yaliyokuwa yanatoka au kuingia katika eneo la Mtaa wa Ki-
jitonyama Kisiwani.
Nasema hii ni mbinu ya kitaalamu zaidi kwa sababu hata watu
waliosomea teknolojia ya mawasiliano, hawawezi kuwa na ujuzi
wa kuelewa namna unavyoweza kuchuja mawasiliano ya maelfu
ya watu mpaka kumpata yule uliyekuwa unamtaka kisha ukaanza

25 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kufuatilia kwa makini alikuwa anazungumza nini na anawasiliana


na nani.
Kwa sababu mbinu hii ilikuwa inahitaji maarifa makubwa zaidi
na kulikuwa na wataalamu wachache waliokuwa na uelewa wa
nini cha kufanya, ilibidi niisimamie mwenyewe kwa kushiriki-
ana na vijana wawili wa ‘Intel’ au ‘Com Dep’ kama wenyewe
walivyokuwa wanapenda kujiita.
Kwa lugha nyepesi, hawa ni wataalamu wa teknolojia ya ma-
wasiliano waliobobea katika ukusanyaji wa taarifa za kiintelijen-
sia (intels) kwa kupitia mawasiliano ya kidijitali na hii inahusisha
kuanzia simu za mkononi, laptop, kompyuta na vifaa vingine
vyote vinavyoweza kutumika kwenye mawasiliano ya kisasa.
Wakati wale vijana wengine wakiendelea na kazi yao, na mimi
nilikuwa naendelea na majukumu yangu kwa kushirikiana na
wale vijana wawili wa Intels. Tulianza kwa kufanya kitu kina-
choitwa ‘mapping’ ambapo kwa lugha nyepesi ni kuchora ramani
ya mahali mnapotaka kupachunguza.
Mifumo mwili ya kijasusi ya kufuatilia mawasiliano, Android
API (Application Program Interface) na GNSS ambayo ni kifupi
cha Global Navigation Satellite System ndiyo ambayo tuliitumia
katika hatua za awali za kufuatilia mawasiliano ambazo kama
majina yake yalivyokuwa, zilikuwa zikitumia mifumo ya simu za
mkononi (androids) na satelite katika kufanya kwake kazi.
Maelezo haya yasikuchanganye kwa sbabau yamekaa kitaalam
zaidi lakini kwa kifupi ni kwmaba tulikuwa tukifuatilia ma-
wasiliano ya watu wote waliokuwa wanaishi eneo la Kijitonyama

26 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Kisiwani kwa lengo la kutaka kujua kama kuna mawasiliano


yoyote ambayo yanatilia mashaka.
Unaweza kushangaa inawezekanaje kufuatilia mawasiliano ya
simu ya mtu bila hata kugusa simu yake? Inawezekana kabisa,
maendeleo ya sayansi na teknolojia yamefanya taarifa za watu
kupatikana kwa urahisi zaidi pengine kuliko wakati mwingine
wowote katika historia ya binadamu.
Hii ndiyo sababu nchi zilizoendelea, zimebadilisha kabisa mi-
fumo ya ulinzi na usalama na kuachana na kutegemea matumizi
ya nguvu kama ilivyokuwa awali na badala yake kuwekeza nguvu
zote kwenye teknolojia.
Badala ya askari kujazana kwenye makutano ya barabara waki-
wa na silaha, magari na pikipiki kwa lengo la kufanya doria kama
ilivyo kwenye nchi zetu nyingi za Kiafrika, wenzetu wanafunga
kamera za barabarani zenye nguvu ya kuona umbali mrefu.
Kamera hizi zinaunganishwa katika kila sehemu na mwisho
unakuta mji mzima unaweza kuonekana kwenye kompyuta kwa
urahisi kuliko kawaida na kufanya hata kupambana na kuzuia
uhalifu iwe rahisi kwa sbaabu kamerfa zinamulika kila mahali na
kuna watu ambao kazi yao ni kuzifuatilia kamera hizo.
Naamini ipo siku na sisi tutafiki ahatua hiyo, basi tukiachana na
maelezo hayo, turudi kwenye suala letu lililokuwa mezani.
Tuliendelea kuzichuja simu zote zilizokuwa zinaingia na kutoka
katika eneo lile kwa kutumia ramani ya mtandaoni (google map)
tukilinganisha na ramani ya mitandao ya simu kwa maana ya
minara na mawasiliano ya satelite, tukazidi kushuka chini mpaka

27 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

tukafikia kwenye kipenyo cha nyumba kumi na tano.


Kwa kuwa nilishafika kwenye nyumba husika na nikiwa pale
nilirekodi picha za video pamoja na ‘location’ kwa maana ya lon-
gitudo na latitudo, niliweza kuinasa kwa urahisi nyumba tuliyoku-
wa tunataka kuiweka kwenye mchujo wa mawasiliano yake kwa
urahisi na hatimaye, tulishuka na kufika kwenye ngazi ya nyumba
husika.
Mwanzo nilihisi ni kama nilikuwa nimechanganya kwenye
mbinu nilizokuwa nazitumia lakini nilipotuliza kichwa vizuri,
niliwekza kupata majibu ya uhakika. Wahusika waliokuwa ndani
ya nyumba hiyo, walikuwa wakitumia laini tofautitofauti za simu
zisizopungua saba kufanya mawasiliano.
Kulikuwa na laini za Tanzania, lakini pia kulikuwa na laini za
simu za Kenya na Msumbiji na ilionesha ni kama laini zilikuwa
zikiwekwa na kutolewa kwenye simu baada ya mawasiliano.
Tuliweza kubaini kulikuwa na simu tatu ambazo ndizo zilizokuwa
zinatumika kubadilishia laini hizo na kufanya mawasiliano hayo.
Kilichozidi kunipa uhakika kwamba wahusika hawakuwa watu
wazuri, ni jinsi simu zilivyokuwa zinapigwa kwa mahesabu ya
hali ya juu, nyingi zikiwa zinapigwa kwenda au kutoka Mom-
basa, Lamu, Tanga, Mkuranga, Mtwara, Lindi, Cabo del Gado na
Pemba kwa upande wa Msumbiji.
Mpaka hapo tayari akili yangu ilishaniambia kwamba asil-
imia hamsini ya maswali ambayo nilikuwa nahitaji majibu yake,
yangeweza kupatikana kwa kuwaweka nguvuni watu waliokuwa
wanaishi kwenye nyumba ile.

28 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Sijui ni kwa nini lakini nilijikuta mapigo ya moyo wangu yaki-


nienda mbio kuliko kawaida kwa kadiri nilivyokuwa naendelea
kugundua mambo mengi zaidi kuhusu watu waliokuwa wanaishi
kwenye nyumba ile.
Kwa bahati mbaya, mbinu tulizokuwa tunazitumia, zilikuwa
zinaweza kutusaidia kuonesha tu simu zilizopigwa na zilizoin-
gia sambamba na ujumbe wa sauti au meseji lakini hazikuwa
na uwezo wa kufanya tuweze kusikia mazungumzo au kusoma
meseji.
Hilo halikuwa tatizo kubwa kwa sababu kama nilivyosema,
hatua ya kwanza ilikuwa ni ‘mapping’ kwa maana ya kuchora
ramani. Hatua ya pili ilikuwa ni ufuatiliaji au kwa kitaalamu
inaitwa ‘tracking’.
Ambacho kilikuwa kikitakiwa kufanyika hapa, kwa sababu
tayari tulishajua kwamba simu zinazotumika ni tatu, ilikuwa ni
kuziwekea ‘tracking’ simu zote kwa maana ya kutaka kujua mtu
anayezibeba anakwenda maeneo gani na gani na kwa utaratibu
gani.
Hatua hii ya pili ilikuwa muhimu zaidi sambamba na hatua ya
tatu kwa sbabau ingeweza kutupa picha kama tuliokuwa tunawa-
fuatilia kweli ni wahalifu, walikuwa wanashirikiana na nani,
walikuwa wakienda kukutana na nani na walikuwa wakitembelea
maeneo gani?
Kila kitu ilibidi kifanywe kwa kasi kubwa kwa sababu sasa taa
nyekundu ilishawaka kwenye kichwa changu na kujua kilichoku-
wa mbele yetu ilikuwa ni hatari kubwa kwelikweli.

29 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Kazi zote mbili ziliendelea kufanyika kwa pamoja, ile timu ili-
yokuwa ikifuatilia kila kitu eneo la tukio kwa usiri wa hali ya juu,
iliendelea kusonga mbele kuelekea kwenye hatua ya kukamilisha
kazi lakini pia upande wa pili mimi na vijana wangu pia tulikuwa
tunaendelea na kazi ya kuhakikisha tunaweza kuzi-track simu zote
tatu zilizokuwa zinatumika kufanyia mawasiliano.
Kitu ambacho watu wengi hawakijui, kuna tofauti kubwa kati
ya matukio ya ujambazi na matukio ya ugaidi na hata namna ya
akuyashughulikia kuna tofauti kubwa pia.
Naweza kusema kwamba kwetu sisi tuna bahati kubwa sana
kwamba matukio ya kigaidi ambayo yameshatokea ni machache
na hata madhara yake siyo makubwa sana ukilinganisha na nchi
kama Kenya, Somalia, Sudan, Libya na nchi nyingine kwa bara la
Afrika.
Hata hivyo, bahati hiyo inakwenda sambamba na ukweli
mwingine mchungu kwamba kwa sababu matukio kama hayo ni
nadra sana kutokea, hata utayari wa vyombo vya ulinzi na usala-
ma kuyashughulikia huwa ni wa kiwango cha chini mno.
Utayari uliopo mara nyingi huwa ni ule wa kupambana na ma-
tukio ya ujambazi au uvamizi wa mipaka ya nchi na hili ni tatizo
kubwa sana ambalo watu waliopata nafasi ya kwenda kusoma na
kupata mafunzo nje, huwa wanakumbana nalo wawapo mafun-
zoni kwa sababu wanakuwa hawaelewi chochote!
Hicho ndicho kilichonikuta hata mimi nilipokuwa masomoni
nchini Israel lakini namshukuru Mungu kwamba niliweza ku-
pata mafunzo ya vitendo kutoka kwa wataalam wa masuala ya

30 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ugaidi ambao wamefanyakazi kwenye maeneo hatarishi kama


Afghanistan, Mogadishu, Iraq, Yemen na kwingineko ambako
kwao magaidi ni kama tunavyosema huku kwetu wapiga ngeta au
wakaba roba kama wengi walivyozoea kuwaita.
Nimeanza kwa kukueleza haya kwa sababu mambo tuliyoku-
tana nayo katika oparesheni hii ndogo ya kuwafuatilia wapangaji
hawa waliokuwa na mwenendo wa kutia shaka, ilikuwa ni mwan-
zo tu, mengi na mazito yalikuwa njiani.
Basi tuliendelea na kazi ya kufanya ‘tracking’ na kwa kutumia
teknolojia ya hali ya juu, tulifanikiwa kuanza kuzifuatilia simu
zote tatu kwa maana ya kwanza sasa tulikuwa na uwezo wa kuona
mtu aliyezibeba anakwenda wapi na kwa muda gani. Kwa wakati
huo, simu zote zilizonekana kuwa ndani ya nyumba husika.
Ilibidi niwaweke maafisa wengine wawili ‘standby’ kwamba
endapo simu zitaonekana zikihama kutoka sehemu moja kwenda
nyingine, basi wafuatilia haraka ili kuweza kubaini ni nani ali-
yekuwa anazibeba kwa maana ya mwonekano wa sura na umbo
na mambo mengine ya aina hiyo.
Ajabu ni kwamba, siku hiyo ilipita simu zote zikionekana
zikiwa palepale tulipoanzia kuzifuatilia, kwa lugha nyepesi simu
zote zilikuwa bado mle ndani na ilionesha kwamba zilikuwa zina-
fanya kazi kwa sababu mawasiliano yaliendelea kufanyika kutoka
sehemu mbalimbali kama nilivyoeleza mwanzo.
Matarajio makubwa ambayo tulikuwa nayo ni kwamba kwa
sababu mtoa taarifa alishatueleza kwamba mhusika mmoja huwa
anaonekana kwa nadra usiku sana akirejea na alfajiri na mapema

31 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

akitoka, basi lazima asubuhi tungeanza kupata matokeo tuliyoku-


wa tunayatarajia.
Mambo hayakwenda kama nilivyokuwa nimetarajia, mpaka in-
afika saa tano asubuhi ya siku ya pili, simu zilionesha kuwa eneo
lilelile! Yote tisa, lakini kumi ni kwamba vijana waliokuwa eneo
la tukio au ‘field’ kama inavyofahamika, hawakuwa wamefani-
kiwa kuona pilikapilika za aina yoyote, kila kitu kilikuwa kimya
kabisa.
“Haiwezekani!” nilijisemea muda mfupi baada ya kupokea
ripoti ya awali kutoka kwa vijana wangu niliokuwa nimewapanga
‘standby’ kwenye eneo la tukio. Niliona kwamba ni kitu ambacho
hakiwezekani kwamba nyumba iwe na watu ndani halafu kusiwe
na purukushani zozote zinazoonekana! Ina maana watu hawali,
hawaendi maliwatoni? Kwa nini kila kitu kilikuwa kimya kwa
kiasi hiki?
Ilibidi kwanza nirudi kwa mtoa taarifa wangu ili kupata uhakika
zaidi, nilimpigia simu kwa namba ya kazi na muda mfupi baadaye
akapokea.
Nilirudia kumhoji baadhi ya mambo, akanijibu kama alivyoku-
wa amenijibu jana yake, ilionesha dhahiri kwamba mle ndani
kulikuwa na watu kwa sababu hata ripoti ya awali ya vijana
waliokuwa eneo la tukio, walithibitisha kwamba ushahidi wa
kimazingira unaonesha kwa asilimia kubwa kwamba ndani kuna
watu.
Ushahidi huo ukichanganya na ule ushahidi niliokuwa nao
wa mawasiliano yaliyokuwa yanaendelea kupitia zile simu tatu

32 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

zilizokuwa mle ndani, vyote vilionesha wazi kwamba kulikuwa


na mtu au watu! Sasa kwa nini wanajificha kwa kiasi kile?
Nilipatwa na shauku ya kuingia mwenyewe ‘field’ kwa sababu
nilihisi ni kama vijana wangu wanazidiwa akili.
Pengine unaweza kuwa unajiuliza kwamba kwa nini tusingeen-
da tu kuivamia nyumba na kuwakamata wahusika?
Tulichokuwa tunakitafuta hapa ilikuwa ni ‘picha kubwa’ am-
bayo inahitaji utulivu mkubwa sana kuweza kuipata, ingekuwa
polisi pengine wao wangeweza kufanya hivyo moja kwa moja
lakini kwa kuwa sisi tulikuwa na mbinu nyingi zaidi, hiyo in-
gekuwa hatua ya mwisho kabisa na tungeshirikiana na polisi kwa
sababu kuna baadhi ya sheria zilikuwa zikitubana.
Kilichokuwa kinatakiwa, ilikuwa ni kuendelea kuchunguza kwa
umakini wa hali ya juu ili hata inapofikia hatua ya kumtia mtu
nguvuni, mnakuwa mmeshapata picha kubwa ya kuzuia madhara
makubwa ambayo pengine yalikuwa mbioni kuweza kutokea.
Sikutaka kupoteza kabisa muda, nikaingia mwenyewe mzigoni
na sitaeleza kivipi lakini elewa tu kwamba nilijiweka kwenye
mazingira ambayo nilikuwa na uwezo wa kuzunguka kila sehemu
kwenye nyumba hiyo na zile za jirani bila mtu yeyote kuwa na
wasiwasi na mimi pamoja na vijana wangu niliokuwa nao.
***
“Mume wangu!”
“Naam mke wangu!”
“Ujue kuna sarakasi zinaendelea hapa mtaani yaani hata sielewi
kabisa!”

33 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Vipi tena?”
“Umechelewa kidogo kuna mafundi wa Dawasco walikuja hapa
mtaani eti wanakagua watu wanaojiunganishia maji kinyemela.”
“Kwani mpaka leo kuna watu wanajiunganishia maji?”
“Mh! Sidhani kwa sbabu sijawahi kusikia, kila mtu mwenye
bomba analipa bili, sasa unaweza kujiunganishia maji halafu
ukawa unalipa bili?”
“Enhee, kwa hiyo hapo sasa stori ni nini?”
“Ujue hayo maswali yako ya kuwa unanihoji kama upo kutafuta
habari huwa siyapendi,” alisema mke wa Dennis na kusababisha
wote wacheke. Kazi yake ya uandishi wa habari za uchunguzi
ilikuwa imemuathiri kisawasawa.
“Sasa si wakawa wameenda hapo nyuma kwa mzee Msomali,
wakawa wanataka kwenda kukagua mita, mzee akawa mkali
kama pilipili, kukatokea bonge la ugomvi watu wakajaa!”
“Khaa! Yaani sijaelewa! Mafundi wa Dawasco wamekuja ku-
kagua mita, halafu mzee Msomali akawa hataki!”
“Wewe naye, mi ninapokusimulia akili zako huwa unaziweka
wapi? Ndiyo! Wamekuja kukagua mita, wameanzia nyumba
nyingine ambapo walikuwa wanakagua vizuri tu, walipofika kwa
Msomali kabla hawajahamia huu upande wetu huku ndiyo timb-
wili likatokea.”
“Sasa kwa nini huyo mzee alikuwa hataki waingie?”
“Kila mtu amebaki na mshangao maana amechachamaa vibaya
mno, eti anasema hapo nyumbani kwake wezi wamekuwa waki-
ingia na kumuibia spea za magari yake uani ndiyo maana hamua-

34 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

mini mtu yeyote kuingia ndani kwake.”


“Sasa kwani hao mafundi si walikuwa na vitambulisho?”
“Siyo tu vitambulisho, walikuwa wamevaa sare zao za kazi na
walikuja na Bajaj yao, si unazijua zile Bajaj wanazotembelea?
Tukahisi labda mzee amejiunganishia maji na ndiyo hayo anayotu-
mia.”
“Kwa hiyo ikawaje?”
“Kumetokea fujo kubwa sana mpaka polisi wakaja, wakam-
chukua mzee Msomali na wale mafundi wakaingia mpaka ndani
kwake lakini ajabu wamekuta hajajiunganishia maji na hakuna
tatizo lolote.”
“Mh! Mbona makubwa!”
“Lakini nasikia wamekuta kuna geti limetobolewa huko ndani
kwa ndani linakuja kutokea kwenye hii nyumba hapa!”
“Haiwezekani! Kwa hiyo unataka kusema kwamba hawa watu
wanaoishi kwenye hiyo nyumba wanaweza kuwa wanaingia na
kutoka kupitia kwa mzee Msomali?”
“Sijui kwa kweli lakini katika mazingira kama haya unaweza
kusemaje?”
“Kwani hilo geti lipo tangu lini?”
“Inavyoonekana siyo la muda mrefu!”
“Haya mambo mbona yanachanganya sana, kwa hiyo imeku-
waje?”
“Wamemchukua mzee Msomali na kuondoka naye, sijui kama
ameshaachiwa au laah!”
“Hebu ngoja kwanza nikajaribu kumuulizia kama yupo nimsikie

35 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

na yeye anasema nini.”


“Hapana mume wangu, unaweza kuonekana pengine wewe
ndiye uliyehusika kumchoma, sikushauri kabisa.”
“Hapana mke wangu, hii ni sehemu ya kazi yangu, matukio
yanapotokea hapa mtaani mimi kama mwandishi wa habari nina
wajibu wa kuyafuatilia kwa kina na kuyaripoti kwa undani ili hata
waliokuwa hawajui chochote nao waelewe.”
“Nakushauri unisikilize, yule mzee alivyokasirika leo anaweza
kukuchukia bure akadhani ni wewe ndiye uliyeenda kuwaleta hao
Dawasco, nakuomba sana unisikilize.”
“Nimekuelewa mke wangu, basi naomba niende kuzungumza
na mjumbe pengine na yeye anaweza kuwa na majibu.”
“Kama ni kwa mjumbe hakuna shida!”
“Sikawii, nakuja sasa hivi! Vipi yule muuza matunda?”
“Kaja, tena leo kaja na mwenzake anauza karanga na korosho,
wako hapo nje!”
“Khaa! Umempa hifadhi na yeye ameenda kumleta mwen-
zake?”
“Watajijua wenyewe, cha msingi wananilipa kodi yangu kila
siku!”
“Unawalipisha fedha?”
“Ndiyo, kila siku lazima walipie ushuru,” alisema mwanamke
huyo na kumfanya Dennis acheke, akatoka kwa kupitia mlango
wa nyuma, simu yake ikiwa mkononi.
Alichokuwa anakitaka kwa mkewe ilikuwa ni nafasi ya kutoka
tu, hakuwa na mpango wa kwenda kuzungumza chochote na

36 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

mzee Msomali wala mjumbe, alitaka nafasi ya kupiga simu ili


kueleza kilichokuwa kinaendelea.
Muda mfupi baadaye tayari alikuwa kwenye ‘line’ ya simu aki-
zungumza moja kwa moja na Chief.
Tofauti kabisa na ambavyo mwenyewe alitegemea, habari hizo
zilionesha kutokuwa mpya kabisa kwa Chief ambaye sanasana
alimtaka awe mtulivu na asije akaonesha dalili zozote ambazo
zinaweza kuwafanya watu wanaomzunguka kuhisi kwamba yeye
ndiye mtoa taarifa.
***
Kama nilivyoeleza, mazingira ya kila kilichokuwa kinatokea
yalinipa wasiwasi mkubwa sana ndani ya moyo wangu na ikabidi
niingie mwenyewe ‘field’ kwa sababu ilionesha kwamba vijana
wangu walikuwa wakizidiwa maarifa.
Njia nyepesi ambayo niliona inaweza kufanya tukakamilisha
kazi yetu bila kushtukiwa na mtu yeyote na kutufanya tuwe na
uwezo wa kuingia mahali popote, ilikuwa ni kujifanya kuwa
maafisa wa Dawasco.
Niliwaandaa vijana wangu, tukawasiliana na mamlaka husika
ambao walitoa ushirikiano kwa kutupa vitendea kazi tulivyokuwa
tunavitaka na wafanyakazi wawili waliokuwa wanaujua vyema
mtaa husika.
Kwa hiyo katika timu ya watu sita tuliyofika pale mtaani, ni
wawili tu ndiyo waliokuwa wafanyakazi halisi waidara ya maji,
sisi wengine tulikuwa kwenye kazi maalum kwa kivuli cha Da-
wasco.

37 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Oparesheni ilifanyika kwa umakini mkubwa, lengo letu lili-


kuwa ni nyuma moja lakini ili kuondoa wasiwasi kwa wananchi,
tulifanya sehemu kadhaa kwenye mtaa huo zikiwemo nyumba
zilizokuwa zinapakana na ile tuliyokuwa tunaifanyia kazi. Lengo
lilikuwa ni kuisogelea kwa karibu iwezekanavyo kutoka pande
zote mbili.
Vijana wetu wengine wawili waliokuwa wamepandikizwa jirani
na nyumba hiyo wakifanya shughuli nyingine tofauti kabisa, nao
walikuwa wakifuatilia kila kilichokuwa kinaendelea, wakitokea
upande wa wananchi.
Katika mazingira ambayo hakuna aliyetegemea, bomu jingine
likalipuka na hii ilikuwa ni baada ya kuingia kwenye nyumba
iliyokuwa inapakana na nyumba tuliyokuwa na mashaka nayo.
Mmiliki wa nyumba hii alikuwa ni mwanaume mmoja wa
makamo, siyo mzee wala siyo kijana, yupo katikati, mwenye asili
ya Kisomali ambaye pale mtaani alikuwa akifahamika zaidi kwa
jina la Msomali ingawa hilo halikuwa jina lake halisi.
Awali tulipotaka kuingia kwenye nyumba yake, alileta upinzani
mkali ambao ulimshangaza kila mmoja na kutufanya tumuweke
kwenye kundi la washukiwa. Isingewezekana kwa mtu ambaye
hana kosa lolote akatae wafanyakazi wa taasisi ya umma kama
Dawasco kuingia ndani ya nyumba yake kufanya ukaguzi ambao
ulikuwa wa kawaida kabisa.
Ni hapo ndipo tulipolazimika kutumia nguvu na kuingia mpaka
ndani ambapo katika hali ya kushangaza, tulibaini kwamba
kulikuwa na geti lingine dogo lililokuwa limetobolewa kuingia

38 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kwenye ile nyumba ambayo ndiyo hasa tuliyokuwa tukiichunguza.


Ulikuwa ni ugunduzi mkubwa na muhimu sana ambao ulitoa ma-
jibu ya maswali mengi kwa wakati mmoja. Kumbe watu waliokuwa
wakiishi ndani ya nyumba ile tuliyokuwa tukiichunguza, walikuwa
wakiingia na kutoka kwa kupitia geti la nyumba nyingine kwa hiyo
isingekuwa rahisi kwa mtu yeyote kugundua kilichokuwa kinaende-
lea.
Nilijiuliza maswali mengi sana yaliyokosa majibu lakini mpaka
hapo ilishakuwa wazi kwamba mwanaume huyu wa makamo ali-
kuwa anashirikiana na watu hawa ambao mpaka muda huo hakuna
aliyekuwa anawajua ni akina nani na walikuwa na malengo gani.
Vurumai ilikuwa kubwa sana eneo la tukio, Msomali akifanya kila
kilicho ndani ya uwezo wake kuzuia tusigundue alichokuwa anaki-
ficha lakini tulimzidi ujanja na ili kutoleta sintofahamu, ilibidi polisi
wapewe taarifa na kuja kumchukua, kisha baadhi yetu tukiongozwa
na mimi mwenyewe, tukaendelea na uchunguzi wa ndani zaidi.
Niliwapa maagizo vijana wangu wawili kwenda upande wa mbele
wa nyumba tuliyokuwa tunaichunguza ili hata kama waliokuwemo
ndani ya nyumba ile watataka kutoroka iwe rahisi kuwadhibiti.
Wengine tulibaki kule ndani kwa Msomali, ambapo kwa kush-
irikiana na polisi watatu waliobaki eneo la tukio baada ya wenzao
kumchukua mzee Msomali, pamoja na mjumbe, tulianza kazi ya
kutafuta njia ya kuingia kwenye nyumba ile.
Mke wa yule mwanaume wa Kisomali, alipoona polisi wakimchu-
kua mumewe, akijawa na hofu kubwa kwa hiyo hata tulipomtaka
akalete funguo ya geti hilo la chuma, alifanya hivyo mara moja

39 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

huku akiwa na wasiwasi mkubwa ndani ya moyo wake.


Mlango ulifunguliwa, mimi ndiyo nikatangulia mbele huku
wenzangu wakinifuata kwa nyuma.
Baada ya kuhakikisha kwamba tupo kwenye eneo ambao raia
wa kawaida hawatuoni tena, nilichomoa bastola kiunoni mwangu,
nikamuona yulemjumbe wa serikali ya mtaa akishtuka kuliko
kawaida, inakuwaje fundi wa Dawasco anatembea na bastola?
Nadhani hakuwa na majibu.
Tusingeweza kuingia kichwakichwa na niliwapa tahadhari watu
wote kwamba eneo lile ni kama uwanja wa vita, lolote linaweza
kutokea ndani ya muda wowote kwa hiyo tuwe makini, nikawa-
ongoza mpaka kwenye korido ndefu iliyokuwa ndani ya nyumba
hiyo, tukaanza kukagua chumba kimoja baada ya kingine, kwa
tahadhari kubwa kuliko kawaida.
Nilianza na chumba cha kwanza kilichokuwa upande wa kushoto
wa korido, nikashika kitasa na kujaribu kufungua, mlango uka-
funguka, nikatanguliza bastola mbele na kujitokeza kwa haraka,
nikiwa tayari kukabiliana na chochote kilichokuwa mbele yangu.
Hakukuwa na chochote mle ndani zaidi ya majamvi kadhaa
yaliyokuwa yametandikwa sakafuni, nikatoka na kusogea kwenye
chumba cha pili bastola ikiwa mkononi. Waliokuwa nyuma yangu
nao walikuwa wamejiweka tayari kwa ajili ya kutoa msaada au
kujibu mashambulizi endapo kungekuwa na ulazima wa kufanya
hivyo.
Tukatoka na chumba kikafungwa huku mlangoni kukiwekwa
utepe maalum wa kuzuia mtu mwingine yeyote asije akaingia kwa

40 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

sababu kulikuwa kunatakiwa kufanyika uchunguzi wa kina zaidi ili


kupata ushahidi ambao ungeweza kutusaidia baadaye.
Chumba cha pili kilikuwa kimefungwa, nikajaribu kuusukuma
bila mafanikio, uamuzi tuliokubaliana ikawa ni kukiacha kwanza
chumba hicho na kuendelea na vingine ili kiwe cha mwisho. Tulijua
endapo tungeanza kuvunja mlango, tungeweza kuharibu kazi yote.
Nikasogea kwenye chumba cha tatu, nikafungua mlango kwa
tahadhari kubwa, ukafunguka kisha nikaingia ndani, hakukuwa na
mtu lakini kulikuwa na bidhaa mbalimbali za vyakula ikiwemo mi-
kate, sukari, tambi, maji ya chupa na tende.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, tukatoka na kufunga chumba
hicho huku nacho kikiwekewa utepe maalum mlangoni, nikawaon-
goza wenzangu kwenda kwenye chumba cha nne na cha mwisho
kwa sababu nyumba nzima ilikuwa na vyumba vinne, sebule na jiko
dogo la ndani.
Nilijaribu kugusa kitasa lakini ilionesha kama nacho kilikuwa
kimefungwa kwa ndani, nilipochunguza vizuri nilibaini kwamba
mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani kwa sababu kulikuwana
funguo inaning’inia kutokea ndani.
Ilibidi hiki nacho tukiweke akiba kwanza, kijana mwingine aka-
simama pembeni ya mlango ili kuhakikisha hata ikitokea aliyepo
ndani akataka kutoka basi asiweze.
Nilitangulia kuelekea sebuleni, hakukuwa na chochote zaidi ya
mazulia yaliyokuwa yametandikwa sebule nzima lakini pia kuliku-
wa na mito ya kukalia kuonesha kwmaba watu waliokuwa wakiishi
humo, walikuwa na utaratibu wa kukaa chini kwenye mazulia na

41 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

siyo kwenye viti au masofa kama wengi wetu wanavyofanya.


Hiyo pekee ilitosha kuonesha kwamba watu waliokuwa wakii-
shi humo ndani walikuwa wakifuata mila na desturi kutoka nchi
za Kiarabu ambazo nyingi wakazi wake hupendelea zaidi kukaa
kwenye mazulia badala ya viti kama ambavyo nchi nyingine zin-
azofuata tamaduni za Kimagharibi zilivyo.
Hakukuwa na kitu kingine chochote zaidi ya mazulia na mito
pale sebuleni lakini hata mazulia yenyewe kwa kuyatazama
yalionesha kuwa ni ya bei ghali na sebule ilikuwa safi kila seh-
emu.
Tulisogea upande wa jiko dogo na hapo nilibaini jambo jingine.
Jiko la gesi lilikuwa likiwaka ingawa halikuwa limebandikwa
kitu na nilipotazama vizuri pembeni, nilibaini kwamba kulikuwa
na maandalizi ya mapishi yaliyofanyika muda mfupi uliopita na
pengine ujio wetu ndiyo uliovuruga.
Niliwaonesha wenzangu lile jiko lililokuwa linawaka na sasa
kila mmoja akawa na uhakika kwamba mle ndani kulikuwa na
watu. Hakukuwa na vitu vingi pale jikoni zaidi ya jiko la gesi,
jiko la umeme, ndoo za maji na friji dogo.
Nililifungua friji na nikagundua kwamba lilikuwa limesheheni
vyakula vya kila aina kuanzia mbogamboga, matunda, nyama,
samaki na kadhalika.
Ni hapo ndipo nilipoanza kupata majibu kwamba kwa nini
waliokuwa wakiishi humo hawakuwa wakionekana kwenda
gengeni wala dukani, kila kitu kilikuwepo ndani na ilionesha
vilikuwa vinanunuliwa kutoka kwenye maduka makubwa (super-

42 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

market).
Picha ambayo niliipata kwa haraka ni kwamba watu waliokuwa
wakiishi mle ndani, japokuwa walikuwa wakiishi maisha ya
ukimya na kujifichaficha, lakini walikuwa na uwezo mkubwa wa
kifedha kutokana na mazingira ya mle ndani.
Kulikuwa na choo na bafu ambavyo vilijitenga lakini vyote vi-
kiwa ni vya ndani kwa ndani, nikahakikisha kote kwamba hakuna
mtu kisha nikarudi na kuanza kuchunguza vizuri dari kuanzia
kule tulikoingia, kwenye vile vyumba tulivyokagua, sebuleni
mpaka chooni.
Ilikuwa ni muhimu kwanza kuchunguza kila kitu kwa ukaribu
kabla ya kwenda kumalizia katika vile vyumba viwili vilivyoku-
wa vimefungwa. Baada ya kujiridhisha, sasa tulirudi kwenye vile
vyumba viwili na niliona ni vyema kuanza na kile chumba amba-
cho kilikuwa kimefungwa mlango kwa ndani.
Kabla ya kutumia nguvu, nilijaribu kwanza kutumia diplomasia
kwa kugonga taratibu na kuwataka waliokuwa ndani wafungue
na kujisalimisha wenyewe. Nilizungumza kwa mara ya kwanza
kwa sauti ambayo nilikuwa na uhakika kwamba inasikika vizuri
kabisa hata kwa mtu aliyepo ndani lakini hakukuwa na majibu
yoyote.
Niligonga kwa mara ya pili lakini bado hakukuwa na majibu,
nikagonga mara ya tatu na ya mwisho huku nikiwaandaa vijana
wangu kwa ajili ya kuvunja mlango. Ajabu ni kwamba tulisikia
mlango ukifunguliwa kutoka ndani, wote tukarudi nyuma na
kukaa ‘standby’.

43 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Mwanamke aliyekuwa amejifunika ushungi na kuvaa baibui


refu lililoacha uso wake tu, alifungua mlango huku akionesha
kuwa na hofu isiyo ya kawaida.
“Mikono juu!” nilisema kwa sauti ya mamlaka, kweli akatii
amri na kuinua mikono juu. Kwa bahati mbaya sana, tulioingia
ndani ya nyumba hiyo tulikuwa wanaume watupu na katika sheria
za ukamataji wa wahalifu, huwa askari wa kiume hatakiwi kum-
kamata mtuhumiwa wa kike.
Hata akimkamata na kumuweka chini ya ulinzi, haruhusiwi
kumpekua kwa sababu ya mikataba ya haki za binadamu ambayo
nchi yetu pia imeisaini. Kwa mazingira ya mle ndani, akili zangu
zilinituma kuamini kwamba lazima mwanamke huyo atakuwa na
silaha, asingeweza kutoka na kujisalimisha kirahisi namna hiyo.
Inapotokea mazingira kama hayo, njia nyepesi inakuwa ni kum-
taka mtuhumiwa mwenyewe alale chini na kuinua mikono juu
kisha unamfunga pingu, hapo kidogo unakuwa salama kwenye
suala la haki za binadamu. Hicho ndicho kilichofanyika, nilimua-
muru kulala chini kisha nikatoa ishara kwa vijana wangu kum-
funga pingu, hilo likafanyika.

44 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

3
K
WA umakini wa hali ya juu, niliingia ndani ya
chumba hicho bastola ikiwa mkononi, nikawa
naangaza kitu kimoja baada ya kingine kwa
umakini mkubwa, hakukuwa na kitu chochote cha
kutia mashaka zaidi ya kitanda, kabati la nguo na
meza ndogo ya kujipambia lakini pia kama ilivyokuwa sebuleni,
chumba chote kilikuwa kimetandikwa mazulia.
Nilihakikisha pia kama uvunguni mwa kitanda hakukuwana
mtu, nikakagua pia kwenye dari ili kuwa na uhakika kama haku-
namtu aliyepanda na kujificha lakini hakukuwa na dalili zozote.
Nilitoka na kutoa ishara kwamba chumba hicho nacho kifun-

45 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

gwe na kuwekewa utepe maalum mlango, asiingie mtu yeyote


mpaka uchunguzi wa kina utakapofanyika. Kwa muda wote huo
nilikuwa na shauku kubwa sana ya kuziona zile simu ambazo
tulinasa mawasiliano yake kwa kutumia mbinu za kisasa lakini
hakukuwa na dalili zozote mpaka wakati huo.
“Chief, una uhakika nyumba ni hii kweli? Mbona mpaka muda
huu hakuna chochote cha kutia mashaka?”
“Hakuna cha kutia mashaka? Akili zako zinafanya kazi sawa-
sawa?”
“Inaonekana ni watu wa kawaida tu, au mmewatilia mashaka
kwa sababu ya dini yao? Hii siyo sawa!” alisema Miraji, mmoja
kati ya vijana niliokuwa nimeongozana nao. Sikuwa nimewahi ku-
fanya kazi na Mirahi hapo awali lakini kwa alichokuwa anakisema
muda huo, niliweza kuisoma saikolojia yake.
Huyu alikuwa ni muumini wa dini ya Kiislam aliyekuwa
anatekeleza matakwa ya dini yake kwa ukamilifu kiasi cha kuwa
na alama usoni, wenyewe wanaita sijda kuonesha kwamba ali-
kuwa akiswali sala tano.
Akili zake zilishamtuma kuhama kutoka kwenye kile tulichoku-
wa tunakifanya na kuhamia kwenye misimamo ya kidini, kama
ambavyo watu wengi huwa wanakosea.
“Unahisi tunawaonea kwa sababu ya dini yao? Umejuaje dini
yao wakati hata mahojiano hayajafanyika?”
“Kila kitu kipo wazi chief, kuna ubaguzi hapa!” alisema na kauli
hiyo nikaichukulia kwa uzito mkubwa kiasi cha kuagiza Miraji
atolewe eneo la tukio haraka kwa sababu angeweza hata kuvuruga

46 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ushahidi akiamini pengine kilichokuwa kinafanyika ilikuwa ni


ubaguzi wa kidini wakati hata haikuwa hivyo.
Baada ya sintofahamu hiyo kuisha, niliamuru yule mwanamke
anyanyuliwe kwa umakini pale chini ili atusaidie kufungua
mlango wa chumba cha mwisho ambacho bado hatukuwa tumeki-
kagua.
Kweli alisimamishwa kwa kuzingatia sheria zote za haki za
binadamu, mikono yake ikiw ana pingu, nikamsogelea na kuanza
kumtazama usoni.
Nilishtuka kugundua kwamba uso wake ulikuwa umevilia damu
na alikuwa na majeraha yaliyokuwa yanaanza kukauka, kuonesha
kwamba aliumia ndani ya siku mbili au tatu zilizopita, jicho lake
moja nalo lilikuwa jekundu sana likionesha kuvilia damu kwa
ndani.
“Samahani kwa kukuvamia namna hii, naomba sana ushirikiano
wako na na kuhakikishia endapo ukitusaidia kupata tunachoki-
taka, hakuna atakayekugusa na tutaondoka kwa amani,” nilisema
kwa sauti ya upole, nikiwa natazamana na yule mwanamke.
Hakujibu kitu.
“Tunaomba funguo za kile chumba,” nilimwambia lakini
akatingisha kichwa kwa nguvu kuonesha kukataa, nikapigwa na
mshangao.
“Tafadhali toa ushirikiano, sisi ni maafisa wa jeshi tupo kazini,
usijaribu kutuzuia kufanya kazi yetu,” nilisema lakini akawa
anaendelea kutingisha kichwa na safari hii alianza kuangua kilio
kwa nguvu, wote tukabaki tumepigwa na butwaa.

47 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Hebu sogeeni pembeni, naomba kuzungumza naye wawili tu,”


nilisema, kweli wenzangu wote wakasogea pembeni na kuniacha
nikiwa na yule mwanamke. Wakati mwingine unatakiwa kujifun-
za kutumia kitu kinachoitwa ‘diplomasia’ katika kutatua changa-
moto zilizopo mbele yako badala ya kutumia nguvu.
Unaweza kushangaa kwamba niliwezaje kuomba kuzungumza
tukiwa wawili tu na mwanamke yule wakati alikuwa miongoni
mwa watuhumiwa na mpaka hapo bado hatukuwa tumepata ma-
jibu ni nini kilichokuwa kinaendelea ndani ya nyumba ile.
Kwa kuwa nilishapitia mafunzo ya saikolojia, nilipomtazama
kwa mara ya kwanza tu, niligundua kwamba kuna kitu hakipo
sawa kwenye maisha yake na hata nilipoendelea kumchunguza
kwa makini, ndipo nilipobaini kwamba alikuwa na majeraha
kwenye uso wake.
Hiyo pekee ilitosha kuonesha kwamba alikuwa akipitia ukatili
fulani ambao mpaka muda huo sikuwa nimegundua ni wa aina
gani lakini akili yangu ilinituma kuamini kwamba pengine ali-
kuwa akinyanyaswa na mwanaume aliyekuwa anaishi naye.
Hiyo pekee ilikuwa ni ‘point’ ya msingi sana katika kuelekea
kufahamu mambo mengi kuhusu kilichokuwa kinaendelea na njia
pekee ilikuwa ni kumtumia huyu aliyeonesha wazi kunyanyaswa
na kitu cha kwanza ilikuwa ni kumhakikishia usalama wake.
“Nisikilize kwa makini, ipo sheria ambayo inaruhusu maafisa
wa serikali kutoa msamaha kwa mtu yeyote hata kama alikuwa
na kesi kubwa kiasi gani kwa sharti moja tu, kukubali kutoa ush-
irikiano!

48 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Ukikubali kushirikiana na sisi, nakuhakikishia kwanza utapewa


ulinzi, utakuwa salama muda wote lakini kama hiyo haitoshi,
utafutiwa mashtaka yoyote ambayo utakuwa unakabiliwa nayo,
bila kujali ni mazito kiasi gani!
“Naomba uniamini, tutakulinda! Nipe funguo za kile chumba
na unieleze ni nini kinachoendelea,” nilimwambia kwa upole,
nikamuona akijifuta machozi na kunitazama kwa macho ya wiz-
iwizi.
“Unaitwa nani!”
‘Sanipha!”
“Vizuri Sanipha! Nipe kwanza funguo,” nilimwambia kwa
upole, akashusha pumzi ndefu na kuingiza mkono ndani ya
mavazi aliyokuwa amevaa, akachomoa funguo tatu zilizokuwa
zimefungwa pamoja, kisha akachagua mojawapo na kunioneshea
kwamba ndiyo itakayofungua kile chumba.
Nilipokea na kumtazama kisha nikatingisha kichwa kuonesha
shukrani zangu kwake, kisha nikamtaka akae palepale na kuni-
subiri, kweli akatii. Nilisogea kule kwenye kile chumba, watu
wote wakasogea pembeni na kunipisha, nikausogelea mlango
lakini kabla sijaingiza ile funguo, nilimsikia yule mwanamke
akiongea maneno ambayo sikuyaelewa, akija mbiombio pale
nilipokuwepo.
“kabla hujafungua naomba tuzungumze pembeni,” alisema kwa
sauti ya chini, ikabidi nitii alichokisema kwa sababu alishaanza
kuonesha hali ya kuniamini, tukasogea tena pembeni kwa mara
nyingine.

49 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Ni wadogo sana, tafadhali msiwadhuru!”


“Akina nani!”
“Hao waliopo humo ndani, hawana hatia yoyote na pengine
hawajui wanachokifanya! Nimepigwa na kuumizwa kwa sbaabu
yao wakati nikiwatetea, naomba mimi ndiyo nikawafungulie
mlango,” aliniambia, nikamtazama kwa kumkazia macho kama
ishara ya kupima kile alichokuwa anakisema. Sikuona nia yoyote
ovu kwenye uso wake, nikampa funguo.
Alisogea mpaka pale mlangoni kisha akagonga mlango mara
tatu akifuatisha ishara maalum, kisha tukamsikia akizungumza
lugha ambayo hatukuwa tunaielewa lakini kwa harakaharaka
nilihisi kwamba inawezekana ikawa ni kisomali.
Baadaya kumaliza kuzungumza maneno yake, alichomeka
funguo kwenye tundu la kitasa kisha akafungua mlango taratibu!
Lahaulaa!
Tulichokiona ndani kilitushangaza kuliko kawaida! Wasichana
takribani watano ambao kiumri walionesha kuwa na kati ya umri
wa miaka 16 hadi ishirini, wakiwa wamevaa Hijab kubwakubwa
za rangi nyeusi na nikabu zilizoacha macho tu, walikuwa wame-
kaa juu ya zulia kwa kukunja miguu yao, wakionesha kutulia
kabisa.
Ni jambo ambalo hakuna aliyelitegemea hata mmoja, mle
ndani ya kile chumba kulikuwa na vitanda viwili pamoja na zulia
kubwa la kisasa pamoja na meza ndogo iliyoonesha kuwa ni ya
kulia chakula.
Tulishindwa kuelewa wasichana wote wale walikuwa wakiishi

50 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

vipi kwenye chumba kama kile na kwa nini muda wote milango
ilikuwa imefungwa. Ambacho hakuna kati yetu ambaye alikuwa
amekigundua ni kwamba kumbe hawakuwa wasichana wadogo
kama ambavyo ungeweza kuwaona kwa harakaharaka.
Nitaeleza vizuri zaidi kwa nini nasema hivyo lakini kilicho-
fanyika pale, ilikuwa ni kwa yule mwanamke kuzungumza nao
kwa lugha waliyokuwa wanaelewana, kisha akageuka na kunio-
neshea ishara mimi, nadhani alikuwa anawatambulisha kwangu,
nikatingisha kichwa kama ishara ya kukubali utambulisho huo.
Yule mwanamke akanisogelea na kunisemesha kwa sauti ya
chini:
“Hawa ni mabinti zangu, hawana baya lolote, wanatumika bila
ridhaa zao, nakuomba sana kama ambavyo umesema utanilinda
mimi, uwalinde na wao! Walikuwa na silaha tayari kupambana
lakini nimewaomba wazishushe chini, naomba wakukabidhi kama
ishara ya uaminifu kati yetu,” alisema yule mwanamke kwa sauti
ya chini akiwa amenisogelea.
Nilishtuka mno aliponiambia kwamba kumbe walikuwa na si-
laha na walishakuwa tayari kwa chochote ili kujilinda, akawageu-
kia kisha akawapa ishara wainuke na kuweka chini silaha zao.
Kila mmoja alikuwa na bunduki ya AK47 iliyokatwa kitako na
kuifanya ibebeke kirahisi na kwa jinsi walivyokuwa wamevaa,
isingekuwa rahisi kwa mtu yeyote kugundua kwamba walikuwa
na silaha.
Japokuwa nilikuwa na ujasiri wa hali ya juu, nilijikuta mapigo
ya moyo wangu yakinienda mbio kuliko kawaida kwa sababu

51 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

endapo tungejaribu kuvunja mlango pale awali, tungekutana na


mvua ya risasi ambayo hatukuitegemea na hata sijui ni maafa
makubwa kiasi gani yangetokea.
Naweza kusema miongoni mwa siku ambazo nilifanya kazi kwa
uzembe mkubwa, ilikuwa ni siku hiyo na sababu kubwa ni kwam-
ba nilipuuza vitu vingi sana ambavyo vilishanionesha kuanzia
mwanzo kwamba watu tunaoshughulika nao, siyo wa kawaida au
pengine siyo aina ile ya wahalifu tuliozoea kushughulika nao.
Nilibaki nimepigwa na butwaa, nikizitazama silaha zile, mapigo
ya moyo yakiendelea kunidunda kuliko kawaida.
Niligeuka nyuma na kuwatazama wenzangu, roho ikaniuma
sana kwa sababu nilikuwa nimewahatarisha lakini kwa upande
mwingine, nikajipongeza sana kwa kuamua kutotumia nguvu na
badala yake kuongozwa na weledi wa kazi kwa sababu tuliepusha
janga kubwa sana lililokuwa mbele yetu.
Mpaka hapo, nyumba yote ilishakuwa ‘crime scene’ kwa maana
ya eneo la tukio la uhalifu kwa sababu kupatikana kwa bunduki
tano, tena AK45 halikuwa jambo la kitoto. Ilibidi niwaombe
wenzangu wote watoke nje, nikabaki na yule mwanamke, Sanipha
na wale mabinti ambao bado mpaka muda huo walikuwa wakio-
nesha sura zao tu.
“Nashukuru kwa ushirikiano wako!”
“Naomba utimize ahadi zako, hawa walitakiwa kuwa shuleni
hivi sasa lakini tazama wako hapa.”
“Naomba tuwachukue wote mpaka kwenye sehemu salama am-
bapo tutawahoji kwa undani, mmoja baada ya mwingine na kila

52 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kitu kikikamilika, basi mtaachiwa.”


“Wakitukosa hapa lazima watatufuatilia mahali popote mtaka-
potupeleka, hapa ni salama zaidi!”
“Akina nani!” nilimuuliza huku nikimtazama usoni, akanitaza-
ma kisha akawageukia wale wasichana waliokuwa wamekaa kwa
kutulia.
“Its complicated!” (Mambo ni magumu!), alisema kwa Kiinger-
eza kizuri na kunifanya nimtazame kwa makini usoni kwa sababu
sikuwa nahisi kama anaweza kuzungumza Kiingereza kizuri na
fasaha namna hiyo.
“How!” (Kivipi?)” nilimuuliza, naye akanitazama na kunisoge-
lea.
“Sielewi nini cha kufanya, kuendelea kuwepo hapa ni hatari
zaidi,” alisema kwa sauti ya chini na kunifanya nikose cha kum-
jibu kwa wakati huo.
Kitu pekee nilichoendelea kumsisitiza ni kwamba anatakiwa
kukubali yeye na wale mabinti tuondoke nao kwenda kwenye
sehemu salama kisha tuweke mtego maalum wa kuwanasa watu
wengine waliokuwa wakiishi kwenye nyumba hiyo.
Baada ya ushawishi mkubwa, hatimaye alikubali na kwa kuwa
nilishafanya mawasiliano na makao makuu kuomba ‘backup’,
tayari magari kadhaa yalikuwa jirani kabisa na eneo la tukio in-
gawa kwa macho ya kawaida usingeweza kubaini chochote.
“Tunatokea mlango wa mbele!” nilimwambia kwa sauti ya
chini, akashusha pumzi ndefu na kuwapa ishara wale wasichana,
wote wakatoka na kuanza kumfuata, mimi na timu yangu tu-

53 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kawa makini kuhakikisha zoezi hilo linakwenda kwa ufanisi kwa


sababu japokuwa yule mwanamke alionesha kutoa ushirikiano,
bado tulipaswa kuwa naye makini pamoja na wale mabinti.
Alifungua mlango wa mbele kwa kutumia funguo nyingine
alizokuwa nazo, tayari gari la kwanza lilikuwa limefika na kusi-
mama usawa wa mlango, mmoja kati ya vijana wangu alitangulia
mbele na wale wengine ambao walikuwa kwenye ‘cover’ nao
tayari walishafika eneo lile wakiwa wamejichanganya na wanan-
chi wa kawaida.
Yule mwanamke akatangulia kuingia kwenye gari, akafuatiwa
na mabinti wawili, gari likawa halina tena nafasi maana ilikuwa
ni Nissan Double Cabin, likaondoka na muda huohuo gari jingine
likawa limeshasogea.
Wakaingia wale watatu na gari hilo nalo likaondoka, likaja gari
jingine, vijana wangu wakaingia na kuondoka na kutuacha mimi
na vijana wangu wawili pale eneo la tukio. Tayari nilishaagiza
kikosi cha pili kije kuongeza nguvu wakati tukiumiza vichwa ni
kwa namna gani tunaweza kuwanasa wahusika wote bila kuhari-
bu misheni yetu.
Kitu cha kwanza ambacho nilikisimamia ni kuhakikisha kwam-
bahakuna yeyotekati ya wale mabinti na yule mwanamke tuliy-
emchukua pamoja na yule mzee wa Kisomali, mkewe na wana-
familia wote wanaofanya mawasiliano ya aina yoyote na ndiyo
maana hata yule mke wa yule mzee nilimuweka chini ya uangal-
izi wa kijana wetu mwingine aliyekuwa eneo la tukio.
Baada ya wao kuondoka, tulirudi ndani na kufunga mlango kwa

54 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ndani na sasa kazi iliyokuwepo mbele yetu ilikuwa ni kufanya up-


ekuzi wa kina ndani ya nyumba hiyo. Kwa kuwa vyumba vingine
tulishafanya upekuzi, tulielekeza nguvu kwenye kile chumba
walichokuwemo wale mabinti.
Tulianza kwa kuzichunguza vizuri zile bunduki walizokuwa
nazo, kama nilivyoeleza awali, zilikuwa ni silaha za kivita, AK47
zikiwa na magazine mbilimbili ambazo zimefungwa kwa kupis-
hanishwa, moja inageukia juu na nyingine inageukia chini.
Kwa waliowahi kutumia silaha hizi watakuwa wananielewa
vizuri ninapozungumzia magazine mbili zinazofungwa kwa mpira
na kupishanishwa. Kwa kawaida, magazine moja ya AK47 inakaa
risasi 30 mpaka 32 kutegemeana na ukubwa wa risasi ingawa
kiwango kamili ni risasi 30.
Magazine zinapokuwa mbili maana yake ni risasi sitini, sasa
hebu fikiria mtu mwenye bunduki ya AK47 halafu ana risasi 60
kwa mpigo ni madhara kiasi gani anayoweza kuyaleta, na huyo ni
mmoja tu, wakiwa watano au sita? Kwa kifupi mle ndani mliku-
wa na kama kikosi cha jeshi na kazi kubwa iliyokuwa mbele yetu
ilikuwa ni kutaka kujua walikuwa wanajopanga kufanya shughuli
gani.
Tulizitoa bunduki zote risasi pamoja na kuchomoa magazine
zake kisha tukaziweka kwenye begi maalum kwa ajili ya uchun-
guzi wa kina zaidi ikiwa ni pamoja na kuangalia alama za vidole
za wote waliokuwa wakizitumia na kufanya ukaguzi maalum
kugundua zilikuwa zimetumika kwenye matukio gani na gani.
Baada ya kumaliza kazi hiyo, upekuzi uliendelea ndani ya kile

55 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

chumba, hatua moja baada ya nyingine. Ndani ya kabati zilikuwepo


simu nne, tatu zikiwa ni simu ndogo za kawaida na moja ikiwa ni
‘satellite phone’, simu maalum zinazotumia satellite moja kwa moja
ambazo ni ngumu kunaswa na mitambo ya kawaida ya kufuatilia
mawasiliano.
Mpaka hapo nilishapata picha nyingine kubwa zaidi, kumbe
wakati sisi tukiona kwamba kulikuwa na simu tatu zilizokuwa zina-
fanya mawasiliano kutoka ndani ya nyumba ile, kulikuwa na simu
nyingine ya nne ambayo kama nilivyoeleza haikuwa ikionekana
kwenye mitambo ya kufuatilia mawasiliano.
Si jambo la kawaida kwa mwananchi wa kawaida kumiliki satel-
lite phones, mara nyingi zinakuwa zinatumika jeshini au na baadhi
ya watu wanaofanya shughuli zao kwenye maeneo ambayo ni mbali
na makazi ya watu na yasiyo na minara ya simu ya mawasiliano.
Sasa kwa eneo kama hilo, Kijitonyama, mtu anawezaje kuwa ana-
tumia satellite phone? Kwa nini anaficha mawasiliano yake? Ana-
wasiliana na nani na yupo wapi? Hayo yalikuwa ni maswali ambayo
yaliendelea kupitandani ya kichwa changu na kuzidi kunifungulia
picha kubwa zaidi iliyokuwa mbele yangu.
Niseme wazi tu kwamba mpaka wakati huo, nilikuwa bado siami-
ni jinsi mambo yalivyokuwa yanaendelea kufunguka kwa ukubwa
zaidi, hatua moja baada ya nyingine na kuzidi kuniduwaza.
Tuliendelea na upekuzi mle ndani, tukagundua kwamba kulikuwa
na sanduku la chuma lililokuwa ndani ya kabati, likiwa limefungwa
kwa makufuli mawili. Tulilitoa na kujaribu kulifungua, kwa kuwa
vifaa tulikuwa navyo, haikuwa kazi ngumu.

56 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Kwa mara nyingine nikapigwa na mshangao mkubwa kuliko


kawaida! Ndani ya sanduku hilo kulikuwa na malighafi za kuten-
genezea mabomu mazito ambapo kwa kuwa nilishajifunza mambo
yote hayo nikiwa mafunzoni Israel, nilipoona tu vifaa vilivyoku-
wemo, niligundua ni nini kilichokuwa kinafanyika au kilichokuwa
kinatarajia kufanyika.
“Mungu wangu!” nilijikuta nikishindwa kujizuia na kusema kwa
sauti, wale vijana wangu wakapigwa na butwaa na kutaka kujua ni
kwa sababu gani nilikuwa nimeshtuka kiasi kile.
“Vifaa vya kutengenezea mabomu na inaonekana vilishaanza
kuunganishwa, si unaona hizi nyaya, zi unaona huu ungaunga,”
nilisema na kuwafanya nao wapatwe na hofu isiyo na kifani.
Mpaka hapo ilishaonesha kwamba kumbe ishu tuliyokuwa tun-
aifuatilia, haikuwa uhalifu wa kawaida bali ugaidi na kama nilivyo-
sema tangu awali, miongoni mwa dosari kubwa tulizonazo katika
nchi nyingi zenye amani na utulivu, ni utayari wa kupambana na
matukio makubwana mazito ya kigaidi.
Sikuwahi kufikiria hata mara moja kwamba ndani ya mipaka
ya nchi yetu kunaweza kuwa na watu wanaoendesha mipango ya
kigaidi tena katika kipindi ambacho vyombo vya ulinzi na usalama
vilikuwa macho kwelikweli kupambana na matukio yote ya ki-
halifu.
Ilibidi nisogee pembeni na kutimiza itifaki za kazi yangu kama
masharti yalivyokuwa yananitaka ambapo ilikuwa ni kutoa taarifa
moja kwa moja kwa mkurugenzi ambaye kimsingi ndiye aliyekuwa
bosi wa ‘kitengo’ nchi nzima.

57 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Kuna mipango ya tukio la kigaidi!”


“Wapi!”
“Bado hatujajua!”
“Umejuaje kama ni tukio la kigaidi na siyo uhalifu mwingine wa
kawaida?”
“Nakutumia picha sasa hivi uangalie mwenyewe! Tupo location
Z,” nilisema kisha nikakata simu, nikasogea kwenye lile sanduku
na kupiga picha ya video kisha muda huohuo nikaituma, ikapokele-
wa na bila kupoteza muda, bosi alinipigia.
“Mungu wangu! Umesema ni location Z?”
“Ndiyo!”
“Hapo unapopafanyia kazi tangu jana?”
“Ndiyo!”
“Tunafanyaje? Tulete kikosi maalum?”
“Ndiyo! Haraka iwezekanavyo lakini kiwe kwenye ‘cover’, tu-
nataka kuwanasa wahusika maana wakituchomoka ni hatari kubwa
zaidi.”
“Sawa! Dakika chache!”
Akili yangu ilikuwa inanienda mbio kwelikweli, nimeshawahi
kusikia sana na kuona kwa wenzetu kuhusu masuala ya ugaidi la-
kini haijawahi kutokea hata mara moja nikajikuta mstari wa mbele
kabisa katika sakata zito kama hilo.
Narudia tena kwamba tatizo kubwa linalotusumbua sana katika
nchi nyingi duniani ukiachilia mbali zile ambazo zipo kwenye
machafuko kwa muda mrefu, huwa ni kukosa uzoefu wa namna ya
kushughulika na dharura zinazohusianana masuala ya ugaidi.

58 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Mimi mwenyewe nilikuwa nimepitia mafunzo ya kutosha lakini


hiyo ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kukutana na tukio kama
hilo na nikiri kwamba hofu ilikuwa imeingia kwenye moyo wangu!
Haukupita muda mrefu tayari kikosi maalum kikawa kimesha-
wasili eneo la tukio na nashukuru kwamba ushauri wangu uli-
tekelezwa kwa sababu walikuja vijana ambao isingekuwa rahisi
kugundua kama wapo kazini.
Sababu kubwa ni kwamba kwanza hawakuwa kwenye aina yoy-
ote ya sare lakini pia hata ‘mishemishe’ zao ilionesha kama vile
kila mtu yupo kivyake wakati kiuhalisia wote walikuwa kazini na
walikuwa wakipokea amri moja kwa moja kutoka makao makuu,
kila kitu kilikuwa kikifanyika kimyakimya.
Kwa kuwa sasa nilikuwa na uhakika kwamba kikosi maalum
kimefika eneo la tukio na kinaweza kusimamia vizuri kazi hiyo
kwa wakati huo, niliona huo ndiyo muda muafaka wa mimi ku-
ondoka haraka kwa ajili ya kwenda kufanya mahojiano na yule
mwanamke pamoja na wale wasichana kwa sababu kwa wakati huo
silaha ambayo ingekuw ana nguvu zaidi, ilikuwa ni taarifa ya nini
kilichokuwa kinataka kufanyika.
“Utasimamia shoo, lengo ni kuhakikisha tunawatia nguvuni
wakiwa hai! Nitarejea muda mfupi baadaye!”
“Sawa chief!” aliitikia Jerry, miongoni mwa vijana niliokuwa
nawaamini na kuwategemea sana kwenye oparesheni za ‘field’.
Kabla ya kuondoka, nilitaka kwanza kufanya jambo moja la
muhimu ambalo lilikuwa ni kukusanya ushahidi wote na kuuondoa
eneo la tukio kwa sababu kama ungeendelea kuwepo hapo, hatari

59 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

bado ilikuwa palepale.


Niliwasiliana na makao makuu na idhini ikatoka, baadhi ya wale
maafisa wa kikosi maalum wakaingia kwa umakini wa hali ya juu,
mmoja baada ya mwingine mpaka mle ndani, wengine wakitumia
mlango wa mbele na wengine wakitumia mlango ule uliokuwa
umetobolewa kutoka kwenye nyumba ya yule mzee wa Kisomali.
Hawa walioingia, walikuwa kwenye kitengo maalum cha ‘Crime
Scene Investigation’ au CSI ambao kazi yao ya kwanza huwa ni
kuhakikisha ushahidi wa awali wa eneo la tukio hauharibiwi na
unahifadhiwa vizuri kwa ajili ya hatua nyingine za kisheria.
Waliingia mpaka ndani na bila kupoteza muda waliaqnza kazi
yao ya kuvipa vidhibiti vyote namba kisha kuvipiga picha na ku-
chukua sampuli mbalimbali na kuziweka kwenye makasha maalum
kwa ajili ya ushahidi.
Wakatyi mwingine makosa madogo mnayoweza kuyafanya
eneo la tukio, yanaweza kupoteza kabisa nguvu ya ushahidi na
kusababisha hata mtu ambaye anafahamika kabisa kuwa na hatia,
anakwenda kuwashinda mahakamani na kuachiwa kurudi uraiani
kuendeleza uhalifu wake.
Nilishafanya sana kazi katika kitengo hiki kabla sijaenda kuonge-
za maarifa na nilikuwa miongoni mwa maafisa waliokuwa wanat-
egemewa sana kutegua mafumbo kwenye kesi ngumungumu kwa
kutumia utaalamu wa hali ya juu wa kipelelezi.
Basi walifanya kazi yao kikamilifu, mimi kazi yangu ikawa ni
kuwaonesha maeneo muhimu ambayo niliamini yanaweza kuwa-
saidia kutokana na uzoefu wangu na wakati wakiendelea na kazi

60 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)
yao, akili yangu ilitua kwenye picha iliyokuw aimetundikwa uku-
tani ndani ya kile chumba walichokuwemo wale wasichana.
Sijui ni machale au ndiyo kuiva kwenye medani kwa sababu
nilipoitazama tu ile picha, kuna kitu kiliniambia akilini mwangu
kwamba niishushe pale ilipokuwa imetundikwa na kuichunguza
zaidi.
Ilikuwa ni picha iliyochorwa kwa mkono ikionesha mandhari ya
kama jangwa hivi pamoja na ngamia kadhaa, picha ambazo watu
wengi hupenda kuzibandika ukutani kwa jinsi zinavyovutia.
Nilipoishusha pale ukutani, akili ya haraka ilinituma niigeuze
upande wa nyuma, nikakutana na kitu ambacho sikuwa nime-
kitegemea kabisa.
Kulikuwa na karatasi nyingine kadhaa zote zikiwa na ukubwa
kama ile picha lakini zikiwa zimewekwa kwa mfumo maalum un-
aowezesha kufunua ukurasa mmoja baada ya mwingine.
Ile iliyokuwa juu kabisa, ilikuwa na mchoro kama wa ramani
ya jengo fulani kubwa, ukiwa na maelezo yote muhimu kama
ambavyo ramani za majengo makubwa zinavyokuwa, ikionesha
milango ya kuingilia na kutokea, madirisha, mifumo ya mabomba
ya maji safi pamoja na maji taka na taarifa nyingine muhimu.
Niliitazama kwa makini, akili yangu ikanituma kwamba haukuwa
mchoro mgeni kwenye macho yangu ingawa kwa harakaharaka
sikuweza kukumbuka ni mchoro wa nini. Nikafungua ukurasa wa
pili! Lahaula, nilikutana na picha iliyochorwa kwa mkono ya jengo
la Ikulu ya Magogoni ya jijini Dar es Salaam.
Ninaposema Ikulu ya Magogoni namaanisha ikulu hiihii ambayo
ndipo anapoishi mheshimiwa rais! Inaitwa Ikulu ya Magogoni kwa
61 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

sababu ule mtaa ilipo, unaitwa kwa jina hilohilo na wengi wa-
napoitaja Magogoni, huwa wanamaanisha ikulu.
Nilishindwa kuelewa picha ya ikulu, tena ikiwa imechorwa kwa
mkono na kwa ustadi wa hali ya juu, ilikuwa inafanya nini ndani
ya nyumba hiyo waliyojaa watu hatari? Kabla sijafunua ukurasa
uliokuwa unafuatia, ilibidi nirudie kwanza kutazama ule mchoro
kwenye ukurasa wa kwanza!
Kile nilichokuwa nimekihisi mwanzo ndicho kilichokuwa kime-
tokea, ulikuwa ni mchoro wa ramani ya ikulu, ukiwa na taarifa zote
muhimu kuhusu sehemu hiyo nyeti na inayolindwa zaidi ukiachana
na benki kuu!
Kwa kawaida, picha na michoro yoyote ya ikulu huwa ni mion-
goni mwa vitu ambavyo kwa kitaalamu huitwa ‘classified docu-
ments’ ikiwa na maana ya nyaraka za siri ambazo ni kundi fulani
dogo la watu wachache ndilo pekee linaloruhusiwa kuziona!
Sasa kama ni hivyo, watu hawa waliweza kupata nyaraka nyeti
na muhimu kiasi hicho? Tena ikiwa na maelezo ambayo mengine
hata mimi mwenyewe sikuwa nayajua? Na kwa nini walikuwa na
michoro hii? Walikuwa wanapanga kufanya nini? Sikupata majibu,
ikabidi niendelee kuzipekua zile karatasi.
Kulikuwa na mchoro mwingine wa kutokea juu ambao nao uli-
kuwa unaonesha eneo lote la ikulu na maeneo ya jirani, ukiwa na
majina ya mitaa na barabara zote kuizunguka ikulu.
Kama hiyo haitoshi, kulikuwa pia na picha zilizokuwa zinaone-
sha mandhari ya ndani ya ikulu na zilikuwa takribani nane, zikiwa
zimekuwa ‘scanned’ na kuunganishwa kwenye karatasi moja.

62 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Karatasi ya mwisho, ilikuwa inaonesha taarifa kibao za usalama,


kuanzia uelekeo wa kamera za ulinzi kuizunguka ikulu kuanzia
kwenye fensi ya nje kabisa mpaka eneo la kuingilia, lakini pia kuli-
kuwa na alama za ‘station’ walizokuwa wanakaa maafisa wa kikosi
maalum cha ulinzi wa rais (Presidential Security Unit).
“Wanataka kuivamia ikulu,” nilijisemea huku nikijaribu kumeza
mate lakini mdomo wangu ulikuwa mkavu kabisa, nadhani ni kwa
sababu ya hofu iliyokuwa imenijaa ndani ya moyo wangu!
Sikuwahi kufikiria hata mara moja kwamba kuna watu wanaweza
kuwa na mpango hatari kama kwenda kuvamia ikulu! Kwanza
unaanzaje kwa mfano, yaani unaanzaje kuvamia ikulu? Sikupata
majibu lakini kwa mazingira tuliyoyakuta ndani ya nyumba hiyo,
ni dhahiri kwamba watu hawa walikuwa wamedhamiria kisawa-
sawa.
Ilibidi muda huohuo nipige simu na kuzungumza na kiongozi
wetu namba moja ambaye kimsingi ndiye mkurugenzi wetu, nika-
mweleza suala lile, kama ilivyokua mara ya kwanza, akashtuka ku-
liko kawaida na safari hii akasema nimsubiri hapohapo nilipokuwa
anakuja mwenyewe!
Kweli haukupita muda mrefu mkurugenzi wetu aliwasili katika
eneo lile ambalo kwa lugha zetu tuliliopa jina la ‘Location Z’,
akaja na walinzi wake wawili na kwa sababu tulishakubaliana
kwamba kila kitu kinatakiwa kufanyika kwa usiri mkubwa bila
kuamsha taharuki yoyote kwa wananchi, ilibidi mimi ndiyo nitoke
kwenda kukutana naye.
Alifikia upande wa mbele wa nyumba ile na kupaki gari mita

63 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kadhaa kisha akateremka nakuanza kusogea mbiombio akiwa


na walinzi wake. Nilishatoka kwa hiyo nilikuwa naona kila kili-
chokuwa kinaendelea, tukasogeleana ambapo bila kupoteza muda
nilianza kumueleza kila kitu kilichokuwa kinaendelea.
“Nataka kushuhudia mwenyewe kwa macho yangu, nataka kuu-
ona ugaidi kwa macho yangu,” alisema akionesha kuwa na ‘kitete’
kuliko kawaida. Nilielewa ni kwa sababu gani alikuwa na hofu kub-
wa namna hiyo ndani ya moyo wake, ugaidi unatisha kisawasawa!
Basi bila kupoteza muda nilimpa ishara, nikatangulia na baada ya
kuingia mle ndani kimyakimya, na yeye aliingia akiwa na walinzi
wake, watu wote wakatulia maana ‘bosi’ alikuwa ameamua kuja
mwenyewe eneo la tukio, mimi ndiyo nikawa mwenyeji wake.
Nilianza kwa kumuonesha kitu kimoja baada ya kingine na safari
yetu ikaishia ndani ya kile chumba walichokuwemo wale wasi-
chana, nikamuonesha bunduki tulizowakuta nazo, nikamuonesha
‘malighafi’ za kutengeneza mabomu pamoja na ile ramani ya ikulu.
Hofu ilijionesha waziwazi kwenye uso wake na nikiri kwamba
sijawahi kumuona mkurugenzi akiwa na hofu kubwa namna hiyo
ndani ya moyo wake.
Akanipa ishara ambayo niliielewa haraka, nikatoa amri kwa vi-
jana wangu kuendelea na kazi kisha mimi na yeye tukatoka mpaka
nje kwa kupitia mlango uleule wa mbele tulioingilia.
“Siamini ninachokiona! Watu wanawezaje kuingia na silaha na
malighafi za kutengeneza mabomu mpaka ‘chumbani’ kabisa?
Unaelewa hii tafsiri yake ni nini? Tafsiri yake ni kwamba idara zote
za ulinzi na usalama zimeshindwa kufanya kazi yake na kutimiza

64 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

majukumu yake lakini kubwa zaidi, ni kwamba sisi ambao tu-


lipaswa kuwa ya kwanza kubaini kilichokuwa kinaendelea, tu-
meshindwa kazi na ninaposema sisi namaanisha mimi kiongozi
wenu nimeshindwa kazi!”
“Lakini mkuu, sisi ndiyo tumekuwa wa kwanza kulibaini jambo
hili, sidhani kama tumechelewa!”
“Kenny! Tumechelewa sana, unawezaje kuelezea jinsi hivi vitu
vyote vilivyosafirishwa na kufikishwa hapa? Tulikuwa wapi? Kwa
nini hatukushtukia kila kitu mapema? Tunajua mbali na hiki tuna-
chokiona, ni mangapi mengine yanayoendelea bila sisi kuwa na
uelewa? Hii ni aibu kwetu!” alisema mkurugenzi na kweli nika-
baini kwamba alikuwa na hoja ya msingi.
“Naamini bado hatujachelewa sana, tunaweza kufanya jambo!”
“Hata sijui tunafanyaje lakini kaa ukijua kwamba hiki ni kama
kitanzi kwenye shingo yangu, jambo lolote litakapotokea na kusa-
babisha madhara basi mimi ndiyo nitakuwa mtu wa kwanza ku-
wajibishwa na najua siyo mimi, viongozi wenzangu kwenye idara
yetu na idara nyingine pia watawajibishwa!
“Tumefanya uzembe wa hali ya juu!” alisema huku akiendelea
kuonesha wazi jinsi alivyokuwa na hofu ndani ya moyo wake kwa
sababu kijasho chembamba kilikuwa kinamtoka.
“Nakuelewa lakini nashauri kuwa hatupaswi kutanguliza hofu tu-
naposhughulikia suala kama hili, hofu inaweza kuwa adui mwing-
ine mbaya zaidi atakayetukwamisha vibaya!”
“Unaujua ugaidi vizuri? Achana na ugaidi wa kusoma kwenye
vitabu! Nilikuwepo wakati ubalozi wa Marekani ulipopigwa ma-

65 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

bomu! Nilikuwa kijana mdogo kama wewe, niliuona ugaidi kwa


macho yangu, niliunusa kwa pua zangu! Naelewa ninachokizung-
umza!” alisema mkurugenzi kwa sauti ya chini huku akiwa ameni-
tolea macho yake mekundu na makali kwa karibu kisha akashusha
pumzi ndefu.
“Tutashinda, unatakiwa kuniamini!”
“Nakuamini sana Kenny! Lakini hili siyo tukio la ujambazi wala
uhalifu wa kawaida! Hujawahi kufanya kazi kama hii hata mara
moja, huujui ugaidi! Nawezaji kukuamini?”
“Basi tuache muda uzungumze!” nilisema huku nikigeuka na
kuanza kurudi kule ndani kwa sababu hakuna kitu ambacho nili-
kuwa sikitaki kama kukatishwa tamaa katika mazingira magumu
kama hayo!
“Snox!” aliniita na kufanya nishtuke, sikuwahi kumsikia mku-
rugenzi akiniita kwa jina hilo, siku zote alikuwa akiniita kwa jina
langu la Kenny lakini siku hiyo aliniita kwa jina langu maarufu
lenye historia ndefu sana! Nikageuka na kumtazama, akapiga hatua
ndefu na kunisogelea kwa sababu nilikuwa nimeshapiga hatua kad-
haa nikiwa nimeanza kuondoka.
“Wewe ndiye utakayesimamia oparesheni hii! Kikosi maalum
cha kuzuia na kupambana na ugaidi kitakuwa kikipokea maelekezo
kutoka kwako! Nataka upambane kufa na kupona, nakuamini na
nakutegemea sana katika hili,” alisema mkurugenzi na kunyoosha
mkono wake mgumu na kunipa, na mimi nikampa wa kwangu,
ikawa ni kama vyuma vimekutana, tukatazamana machoni kwa
sekunde kadhaa kisha wote tukashusha pumzi.

66 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Sikumjibu kitu, nikageuka na kutembea harakaharaka kuelekea


kule ndani, naye akaondoka na walinzi wake mpaka kwenye lile
gari lake walilokuja nalo.
“Vipi Chief!”
“Fresh!”
“Naona mkurugenzi amechachawa ile mbaya!”
“Lazima achachawe, anadai alikuwepo kipindi cha ubalozi wa
Marekani unashambuliwa na anakumbuka hali ilivyokuwa!”
“Daah! Mungu atuepushie mbali! Tunakusikiliza wewe kaka,
naamini tutalimaliza hili mapema kabisa!”
“Kila mmoja akitimiza wajibu wake tutalimaliza hili!” nilisema
huku nikiwahimiza kumalizia haraka zoezi la kufungasaha vile
vifaa vyote hatari na baada ya hapo, silaha zilitolewa na kupelekwa
kwenye magari yaliyokuwa yanatusubiri nje.
Ilikuwa ni lazima kutenganisha, zile bunduki zilipakizwa kwenye
gari lake na yale malighafi ya mabomu nayo yalipakizwa kwenye
gari jingine.

67 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

68 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

4
W
AKATI nikisimamia hilo, nilipokea simu
kutoka kwa kiongozi wa Kikosi cha Kudhibiti
na Kupambana na Ugaidi (Anti Terror Squad-
ron- ATS) akinitaarifu kwamba nimechaguliwa
kuwa ‘field commander’ wa kikosi hicho, ikiwa
na maana sawa na kile alichoniambia mkurugenzi, kwamba mimi
ndiye nitakayekuwa kiongozi wa oparesheni hiyo kwa jumla.
Nilishusha pumzi ndefu kwa sababu mambo yalikuwa yakienda
na kubadilika kwa kasi kubwa mno kiasi kwamba ungeweza
kudhani upo kwenye ndoto ya kutisha! Sikuyaogopa majukumu
makubwa niliyokuwa nimepewa, akili zangu zilikuwa ni kwa
namna gani nitaweza kukimbizana na kasi ya mambo.
Kama nilivyokuwa nimepanga, jambo la msingi kabisakwa

69 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wakati huo ilikuwa ni kwenda kuwahoji yule mwanamke na wale


wasichana ili nipate picha kamili ya kilichokuwa kinaendelea in-
gawa picha kubwa iliyokuwa inaonekana wazi mpaka wakati huo,
ni kwamba kulikuwa na mipango ya kwenda kufanya shambulio la
kigaidi ikulu!
Nani aliyekuwa nyuma ya mipango hiyo, ni kwa jinsi gani
mipango hiyo ilikuwa inapangwa na sababu kubwa ilikuwa ni
nini, hayo ni maswali ambayo ilikuwa ni lazima niyapatie majibu
haraka iwezekanavyo.
Ili kutolewa taharuki pale kwenye ile nyumba, niliagiza kwamba
maafisa wachache pekee ndiyo wanaotakiwa kubakia eneo hilo
tena wakiwa kwenye ‘cover’, wengine wote walikuwa wanatakiwa
kukaa kwenye ‘station’ maalum ambazo nilizipanga harakaharaka
ndani ya kichwa changu na utekelezaji wa suala hilo ukaanza mara
moja.
Baada ya kuhakikisha kila kitu kimekaa sawa, niliondoka na
baadhi ya vijana wangu tukiwa na ule ushahidi wote tulioupata
eneo la tukio zikiwemo zile bunduki za kivita na yale malighafi
ya kutengenezea mabomu na breki ya kwanza ilikuwa ni ‘getini’
kama ambavyo tulikuwa tunapenda wenyewe kupaita, ikiwa na
maana ya ofisini kwetu.
Palikuwa panaitwa ‘getini’ kutokana na jinsi mandhari yake
yalivyo, ofisi zetu zilikuwa barabarani kabisa lakini kama una-
vyofahamu shughuli zetu nyingi huwa ni za siri na hatakiwi mtu
yeyote kujua ni nini kinachoendelea ndani, eneo lote lenye uku-
bwa wa kama mita mia tano hivi kwa urefu, lilikuwa limejengwa

70 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ukuta mrefu.
Ukuta huo ulikuwa umezibwa kwa miti mingi iliyopandwa nje na
ndani ya ukuta na kitu pekee ambacho kilikuwa kikionekana kwa
urahisi, lilikuwa ni geti kubwa jeusi kwenye lango kuu la kuingilia
na ndiyo maana wengi tulipenda kupaita getini.
Kumbe tayari taarifa juu ya tulichokibaini zilikuwa zimeshaenea
kila sehemu na vikosi vyote vilikuwa vimewekwa kwenye hali ya
utayari, wenyewe huwa tunaita ‘Alert’.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, lile gari lililokuwa na silaha
kwa maana ya bunduki, lenyewe ndilo lilikuwa la kwanza kuwasili,
likafuatia lile lililokuwa na malighafi za kutengeneza mabomu na
la mwisho ndiyo lile nililokuwa naliendesha mimi ambalo nilikuwa
nimepanda na vijana wangu na breki ya kwanza ikawa ni nje ya
ofisi za kitengo cha Kikosi cha Kudhibiti na Kupambana na Ugaidi
(Anti Terror Squadron- ATS).
Kitengo hiki ndicho kilichokuwa kinahusika na masuala yote
yanayohusiana na masuala ya ugaidi na kiliundwa rasmi baada ya
tukio la shambulio la ugaidi lililotokea Ubalozi wa Marekani jijini
Dar es Salaam na Nairobi.
Kwa wanaokumbuka vizuri matukio hayo ya mashambulizi ya
kigaidi ubalozini yalitokea Agosti 7, 1998 na kusababisha Afrika
Mashariki na dunia nzima kuzizima, wahusika wakuu wakiwa ni
kundi la kigaidi la Al Qaeda.
Watu 213 walifariki na wengine 4,500 kujeruhiwa jijini Nairobi,
Kenya wakati kwa Tanzania watu 11 waliaga dunia na wengine 85
walijeruhiwa vibaya na huo ndiyo ukawa mwanzo wa marekebi-

71 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

sho makubwa ya sheria za makosa ya jinai na hapo ndipo kikosi


hiki maalum kilipoundwa kwa ajili ya kazi hiyo ya kupambana na
kudhibiti ugaidi.
Baada ya kuwasili, kama zilivyo itifaki za kazi yetu kunapotokea
jambo kubwa kama hilo linalohatarisha usalama wa taifa kwa
kiasi kikubwa namna hiyo, jambo la kwanza lilikuwa ni kukutana
wakuu wote wa idara zote na kupeana taarifa za jumla kuhusu
kinachoendelea, kwa kitaalamu huwa tunaita ‘briefing’.
Ndani ya muda mfupi tu tayari wote tulikuwa tumejaa kwenye
ukumbi wa siri wa mikutano na kila mtu alikuwa na shauku kubwa
ya kutaka kusikia ni nini kilichokuwa kimetokea na kilichozidisha
shauku kubwa ni kwa sababu hata mkurugenzi naye alikuwepo na
ndiye aliyekuwa akiongoza kikao hicho.
“Nobody is safe!” (Hakuna ambaye yupo salama) alianza kuse-
ma mkurugenzi na kuonesha msisitizo akaanza kwa maneno ya
Kiingereza, watu wote tukawa kimya kabisa kumsikiliza, ukumbi
ukiwa na watu wasiopungua 16 ambao kama nilivyosema, wote
walikuwa ni viongozi na wakuu wa idara.
“Kuna tishio la ugaidi, na kibaya zaidi sehemu inayolengwa
ni Magogoni,” alisema, miguno ya chinichini ikasikika ukumbi
mzima, watu wote wakionesha kupigwa na taharuki.
“Agent Kenny atatupitisha kwenye sakata zima kuanzia jinsi
alivyopata taarifa na kilichokuwa kimebainika mpaka wakati huu
lakini kubwa zaidi, nimemteua yeye kuwa kiongozi wa oparesheni
hii kubwa na ya hatari ya kuhakikisha tunalizima tukio lililopo
mbele yetu,” alisema mkurugenzi kisha akanipa ishara nisogee

72 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

mbele kwenye sehemu maalum ya kuzungumzia, watu wote waka-


nigeukia wakiwa na shauku kubwa ya kutaka kujua kwa undani ni
nini kilichokuwa kinaendelea.
Nilianza kueleza jinsi taarifa zilivyotufikia kutoka ‘Information
Desk’ kwa maana ya dawati la taarifa ambalo huhusisha watoa
taarifa (informers) ambao tunafanya nao kazi. Nilieleza jinsi
nilivyoamua kuingia mwenyewe kazini na kufuatilia taarifa hizo
ikiwa ni pamoja na kukutana ana kwa ana na mtoa taarifa ambaye
alinipeleka mpaka eneo la tukio kisha nikaeleza kila kitu kilichoua-
tia baada ya hapo.
Kila mtu alibaki ananitazama akiwa ni kama haamini alichokuwa
anakisikia kwa sababu kama nilivyosema kuanzia mwanzo, ni
kwamba matukio yalikuwa yanafuatana kwa kasi kubwa mno kiasi
kwamba kuna wakati hata mimi mwenyewe nilikuwa najihisi ni
kama nipo ndotoni.
“Bila shaka nyote mmesikia na hapa ndipo tunapoona umuhimu
wa kuwa makini na taarifa zinazotufikia kutoka kwa wasiri wetu!
Mmeona jinsi taarifa ambayo ingeweza kudharauliwa kwa kuon-
ekana kuwa ya kawaida jinsi ilivyotufumbua macho wote na kutuz-
indua kutoka kwenye usingizi mzito?
“Binafsi nakupongeza sana kijana, hakika serikali ilikuwa sahihi
kabisa kukupeleka masomoni nje ya nchi! Ukilitazama suala hili
utagundua kwamba kuna uzembe mkubwa umefanyika kwenye
idara zote kuanzia juu mpaka chini.
“Nilizungumza na Kenny na nikamweleza kwamba mzembe wa
kwanza katika suala hili ni mimi mkurugenzi wenu kwa sababu

73 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

nimeshindwa kuwasimamia matokeo yake watu wanaingia mpaka


chumbani na kupanga mipango ya hatari ya kuhatarisha usalama
wa taifa letu na sisi tupo tumelala usingizi wa pono!
“Najua nitawajibishwa na waliopo juu yangu lakini kabla ya
mimi kuwajibishwa, na mimi nitawawajibisha wote mliozembea
lakini hii itakuwa ni baada ya kulizima tukio hili! Kenny, hebu
tueleze unafikiria nini cha kufanya kwa sasa!”
“Asante mkurugenzi, kama nilivyokueleza naomba pia niwaam-
bie viongozi wangu wote mliokusanyika humu ndani! Lengo la
kwanza la matukio huwa ni kupandikiza hofu, kisha uharibifu
hufuatia na baadaye hofu huongezeka zaidi na uharibifu utaendelea
kwa mfuatano kama huo.
“Kitu cha kwanza tunatakiwa kuishinda hofu, nikiwatazama
wote humu naiona hofu ndani yenu, tukienda namna hii hatut-
aweza kufanikiwa! Tuweke hofu pembei, tuweke lawama pembeni
kisha wote tuingie vitani! Hii siyo vita kama ambazo mmezoea
kuzishuhudia sehemu nyingine yoyote, adui tunaye ndani mwetu,
ameshaingia na kuweka makazi ndani ya vyumba vyetu vya kulala
kwa hiyo haitakuwa kazi nyepesi kumshinda.
“Kitu cha kwanza ni taarifa, kila mmoja kwa nafasi yake ashiriki-
ane nasi kwa kadiri ya uwezo wake wote, kwenye idara yake. Nita-
kutana na kila mmoja kwa nafasi yake lakini kikubwa ni kwamba
hatuna muda wa kupoteza, lazima tujue ni akina nani wapo nyuma
ya tukio, walipanga kufanya nini na nini, wapi na kwa nini kisha
ndipo tutakapojua namna ya kuwadhibiti!
“Kwa heshima yako mkurugenzi naomba kikao kiahirishwe tuin-

74 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

gie kazini haraka! Tayari tunao washukiwa tuliowakuta ‘Location


Z’ na wameahidi kuta ushirikiano, tunao hapa ndani na kinachofua-
tia hapa ni kwenda kuanza kuwahoji! Tutapeana taarifa kwa kila
kinachoendelea,” nilisema, mkurugenzi akatingisha kichwa kuon-
esha kukubaliana na nilichokisema.
Watu wote wakainuka na kuanza kutawanyika na mimi moja kwa
moja nikaongozana na vijana wangu kuelekea kule kwenye vyum-
ba vya chini ya ardhi walikokuwa wamehifadhiwa yule mwanamke
na wale mabinti zake.
Niliongozana na vijana wangu ambao ndiyo waliokuwa
wametangulia na yule mwanamke na wale wasichana wake,
wakanipeleka mpaka kwenye vyumba walivyokuwa wamewekwa,
kila mmoja aliwekwa kwenye chumba cha peke yake ili kutovu-
ruga ushahidi.
“Inabidi nianze na huyu kwanza,” niliwaambia vijana wangu
wakati tukiwatazama wote kwenye kamera maalum zilizokuwa
zimefungwa kwenye kila chumba. Baada ya kuwaeleza, walipeana
ishara na kuniacha mwenyewe kwenye chumba maalum cha maho-
jiano ambacho nacho kilikuwa na kamera.
Muda mfupi baadaye, yule mwanamke aliletwa, nikamkaribisha
kwa uchangamfu kwenye kiti, akakaa kisha na mimi nikakaa kwe-
nye kiti kingine, katikati yetu kukiwa na meza ya chuma iliyotuten-
ganisha.
Kwa jinsi tulivyokuwa tunashughulika nao, wala usingeweza
kudhani kama walikuwa ni watu hatari kiasi kile, nilishawaelekeza
vijana wangu kwamba wanatakiwa kushughulika nao kwa ukarimu

75 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kwa sababu yule mwanamke alishaonesha nia ya kutaka kutoa


ushirikiano vizuri.
“Sanipha! Sijakosea jina lako?”
“Upo sahihi! Hujakosea!”
“Nataka kwanza kukujua, unaweza kunieleza historia yako kwa
kifupi?” nilimuuliza huku nikilazimisha tabasamu kwenye uso
wangu ili kutoamsha hofu zaidi kwenye moyo wake kwa sababu
alishaonesha kukosa kabisa utulivu, nadhani mazingira ya mle
ndani yalimtisha.
“Ulisema kama tutatoa ushirikiano tutakuwa salama, kwa nini
walituziba macho kwenye gari wakati wanatuleta huku? Hapa ni
wapi?”
“Usiwe na wasiwasi, mimi ni mtu wa kutimiza ahadi zangu.
Nimekuahidi na narudi atena kukuahidi kwamba kila kitu kitakuwa
sawa endapo mtatoa ushirikiano! Kuzibwa macho ni taratibu za
kawaida za kazi zetu.”
“Hapa ni wapi?”
“Ni sehemu salama! Usiwe na wasiwasi,” nilimwambia, akashu-
sha pumzi ndefu.
“Mimi ni mzaliwa wa Chakechake, Pemba! Ile nimekulia na
kuishi Kilwa! Baba yangu alikuwa anafanya kazi Makumbusho ya
Kilwa!” alisema, nikawa namtazama machoni kama njia ya kum-
soma kama alichokuwa anazungumza ilikuwa ni ukweli.
Akaendelea kunieleza kwamba alisoma mpaka darasa la saba tu,
baada ya hapo akaendelea na masomo ya dini.
Akazidi kunieleza kwamba baba yake alifariki miaka kadhaa

76 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

iliyopita na kusababisha familia yao kuanza kupitia hali ngumu ya


kiuchumi na mwisho akalazimika kuolewa na mwanaume mmoja
kutoka Mombasa ambaye ndiye huyo aliyekuwa anaishi naye
mpaka wakati huo.
Aliendelea kunieleza kwamba baada ya kuolewa, alihamia
Mombasa, Kenya na mume wake na huko ndiko makazi yao rasmi
yalipokuwepo.
“Una watoto wangapi?”
“Wawili!”
“Wako wapi?”
“Wako Mombasa!”
“Mlikuja lini Dar es Salaam?”
“Kama miezi miwili iliyopita! Kabla ya kuja Dar es Salaam
tuliishi kidogo Tanga Raskazone kwa muda wa kama miezi mitatu
hivi!”
“Mume wako anashughulika na nini?”
“Ni mfanyabiashara!”
“Biashara gani?”
“Sijui lakini yeye huwa ananiambia ni mfanya biashara na huwa
anasafiri mara kwa mara! Siyo mtu wa kukaa nyumbani!”
“Ni nini kilichowatoa Mombasa mkahamia Tanga na baadaye
mpo hapa Dar es Salaam.”
“Mume wangu aliniambia kuwa kuna watu alifanya nao biashara
sasa wakashindwa kuelewana kwa hiyo wanamuwinda ili wamuue!
Ndiyo maana tunaishi kwa kuhamahama na kujificha!”
“Pale mlipokuwa mnaishi, kuna watu walikuwa wakija nyakati za

77 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

usiku na kuondoka kabla hakujapambazuka! Ni akina nani?”


“Ni ndugu zake mume wangu! Mimi siwajui ila huwa ananiam-
bia ni ndugu zake kutoka Somalia!”
“Mumeo ana ndugu kutoka Somalia?”
“Ndiyo, wakati ananiona nilikuwa sijui lakini baada ya kuishi
naye ndiyo nimejua kwamba asili yao ni Mogadishu, Somalia na
Mombasa alihamia kwa ajili ya biashara zake tu!”
“Kwa hiyo mumeo ni raia wa Somalia si ndiyo?”
“Ndiyo!”
“Mmeishi pamoja kwenye ndoa kwa muda gani?”
“Miaka mitatu!”
“Unataka kusema miaka yote mitatu hujawahi kujua mumeo ana-
fanya biashara gani?”
“Sijawahi kujua! Mume wangu ni msiri sana! Huwa ananificha
mambo yake mengi tu!”
“Hao ndugu zake kutoka Somalia umeanza kuwajua lini?”
“Nimeanza kuwajua baada ya kuhamia hapa Dar es Salaam.”
“Huwa wanazungumza nini na mumeo?”
“Sielewi kwa sababu huwa wanazungumza kilugha cha kwao!”
“Silaha zilizokutwa ndani kwenu zimetoka wapi?”
“Ni hao ndugu zake mume wangu ndiyo waliozileta tulipohamia
hapa Dar es Salaam!”
“Mumeo amewahi kukueleza kwamba hizo silaha ni za kazi
gani?”
“Hapana, hajawahi kunieleza chochote na kila nikimuuliza ame-
kuwa akiwa mkali sana kwangu! Wiki iliyopita alinipiga sana usiku

78 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

na kunijeruhi kama unavyoniona!”


“Sababu ya kukupiga ilikuwa ni nini?”
“Hao ndugu zake waliwaleta hao wasichana mlionikuta nao pale
nyumbani, wakawa wanawafundisha kitu fulani kilichonipa wasi-
wasi, nilipokuwa namhoji akawa hataki kuniambia ukweli zaidi ya
kunifokea. Nilipomshupalia na kumtaka aniambie ukweli wana-
panga kufanya nini ndiyo akanipiga sana!”
“Kwa jinsi unavyomjua mumeo, unahisi anapanga kufanya nini
na hao ndugu zake?”
“Wanataka kuvamia ikulu!”
“Wewe umejuaje?”
“Niliwasikia hao ndugu zake wakati wakiwafundisha hao mabin-
ti! Na tena hata hao mabinti nilimsikia mume wangu akisema
watavalishwa mabomu ya kujitoa muhanga!”
“Unasemaje?” alisema mwanamke huyo na kunifanya nipigwe na
bumbuwazi nikiwa ni kama siamini nilichokuwa nakisikia! Liliku-
wa ni jambo la hatari pengine kuliko tulivyokuwa tunahisi awali.”
“Nimewasikia wakisema hivyo! Na kuna mzee mmoja huwa
anakuja naye usiku ndiyo anayefanya kazi ya kuwafundisha kutu-
mia silaha.”
“Mume wako huwa anarudi saa ngapi nyumbani?”
“Yeye ni mtu wa usiku wa manane, anaingia usiku wa manane na
anaondoka alfajiri na mapema!”
“Huwa anakwenda wapi?”
“Kwa kweli sijui, na hapa Dar es Salaam mimi ni mgeni na ame-
nizuia kutoka nje, kila kitu ananiletea yeye mwenyewe!”

79 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Tukitaka kumpata mumeo tutampata wapi tofauti na pale nyum-


bani mnapoishi?”
“Sijui, mtu anayeweza kuwa anajua ni yule mzee wa nyumba
jirani ambaye wageni huwa wanapitia kwake.”
“Huyo mzee Msomali?”
“Ndiyo! Yeye ndiye mwenyeji wake na nadhani huwa wanaon-
doka pamoja kwa kutumia gari yake na hata kurudi yeye ndiyo
huwa anamrudisha!”
“Hebu nisubiri kidogo, nakuomba uwe na amani! Upo kwe-
nye mikono salama,” nilimwambia yule mwanamke na kuinuka.
Niliposimama tu, wale vijana wangu waliingia, nadhani walikuwa
wanasikiliza kila kilichokuwa kinaendelea kwa sababu kama nili-
vyosema, ndani ya kile chumba kuna kamera za siri na vinasa sauti
kiasi kwamba kila kinachozungumzwa, watu waliopo kwenye
chumba kingine maalum wanakuwa wanasikia.
“Mrudisheni kwanza kwenye chumba chake na hakikisheni wan-
apewa chakula,” nilisema kisha nikatoka na kuwaacha wakitekele-
za maagizo yangu! Mapigo ya moyo yalikuwa yakinienda mbio
kuliko kawaida huku kijasho chembamba kikitiririka makwapani!
Nikatembea harakaharaka kuelekea kwenye kile chumba kingine
ambacho ndiyo huwa watu wengine wanakaa wakati mahojiano
yakiwa yanaendelea mle ndani ya kile chumba nilimokuwemo!
Kumbe timu nzima ya wale viongozi tuliokaa nao kikao ilikuwa
ndani ya chumba kile kufuatili amahojiano ambayo nilikuwa nam-
fanyia yule mwanamke.
“Tumekwisha!” alisema mkurugenzi huku akiinuka pale alipoku-

80 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wa amekaa na kunifuata mbiombio!


“Tumesikia wenyewe kila kitu, ilibidi niwaite viongozi wote wa-
sikilize mahojiano! Tunafanya nini sasa!”
“Huyo mzee wa Kisomali anatakiwa kuletwa haraka iwezekana-
vyo!” nilisema huku na mimi nikihema juujuu.
“Akakamatwe haraka iwezekanavyo!”
“Tayari anashikiliwa Mabatini, ni suala la kwenda kumchu-
kua tu!” nilisema, nikaona kila mtu ameshusha pumzi ndefu kwa
sababu sasa mwanga ulishaanza kuonekana. Hakukuwa na muda
wa kupoteza, nilitoka mwenyewe nikiwa na vijana wangu watatu,
tukaondoka mbiombio mpaka Kituo cha Polisi cha Kijitonyama au
kama wengi wanavyokiita, Mabatini.
Wakati zile purukushani zinatokea kule Kijitonyama Kisiwani
tulipojichanganya na mafundi wa Dawasco na kufanikiwa kubaini
kwamba kumbe kulikuwa na mlango mwingine uliokuwa unatu-
mika na wale watu waliokuwa wanaishi kwenye ile nyumba, nilitoa
maagizo ya yule mzee wa Kisomali kwenda kuwekwa chini ya
ulinzi kwanza mpaka nitakaposema vinginevyo kwa sababu nilihisi
kuanzia mwanzo kwamba anaweza kuwa ndiyo mwenyeji wa wale
watu.
Kama angeachwa nje angeweza kuvuruga ushahidi na kumbe nili-
chokuwa nimekihisi, ndicho kilichokuwa sahihi! Nimewahi kueleza
na narudia tena kueleza kwamba vita dhidi ya ugaidi ni ngumu kwa
sababu huwezi kumjua gaidi kwa kumtazama, bora hata majambazi
ni rahisi kuwabaini.
Mtu yeyote anaweza kuwa gaidi au anaweza kushirikiana na

81 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

magaidi! Viongozi wa dini wanaweza kuwa magaidi, wanawake


wanaweza kuwa magaidi, watoto wanaweza kutumika na magaidi
kama silaha lakini pia ugumu ni kwamba magaidi wanaishi katikati
yetu na inakuwa ngumu sana kuwashtukia mapema mpaka ufanye
kazi ya ziada.
Tayari tulikuwa barabarani na kwa kuwa Mabatini hapakuwa
mbali sana na Getini, ndani ya muda mfupi tu tulikuwa tayari
tumewasili huku nikijitahidi mno kudhibiti hisia za hofu ndani ya
moyo wangu!
Hakuna kitu cha hatari kama kupambana na watu wanaotumia
akili kubwa kuandaa uhalifu wao kwani huwa wanakuwa wame-
shapima na kuiona hatari kabla haijatokea na kuchukua hatua za
haraka kuzuia wasije wakaingia matatizoni.
Tulipofika pale Mabatini, wale askari waliokuwepo pale walin-
ichangamkia kwa sababu wengi tayari tulikuwa tunafahamiana
na moja kwa moja nikaingia kwenda kuonana na mkuu wa kituo
ambaye naye tulishakuwa watu wa karibu.
“Chief! Eti ni nini kinachoendelea?” alisema mkuu wa kituo
huku akiinuka haraka na kutoka upande wa nyuma ya meza ali-
pokuwa amekaa kwenye kiti chake na kuja upande wa pili.
“Ni oparesheni za kawaida!”
“Unasemaje oparesheni za kawaida wakati tumeshawekwa kwe-
nye ‘red alert’ na kamishna?” aliniuliza. Niliona kama kukaa na
kuanza kumuelezea nitazidi kupoteza muda, ikabidi nimueleze kwa
kifupi tu kwamba kulikuwa na tishio la ugaidi na mahali palipo-
lengwa ilikuwa ni Ikulu ya Magogoni.

82 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Ni sisi ndiyo tumesababisha uzembe? Wanasemaje wakubwa


huko kwenu?”
“Hapana, hakuna aliyesababisha uzembe, nadhani ni makosa
madogomadogo tu ya kushindwa kunusa taarifa kwa wakati. Usiwe
na wasiwasi!” nilimwambia lakini nadhani akawa bado na wasiwa-
si na kikubwa ni kwamba tukio lilianzia katika eneo ambalo katika
mamlaka za kipolisi, yeye ndiye aliyekuwa anawajibika moja kwa
moja pengine hata kabla ya kamanda wa polisi wa eneo husika.
“Kama kuna hochote nitaarifu tafadhali, tupo tayari kutoa msaada
wa hali na mali, tayari magari yote ya doria yapo ‘standby’ na vi-
jana wetu wote hata ambao hawakuwa kazini wameitwa na tunasu-
biri maelekezo tu kutoka juu!”
“Hakuna tatizo, tupo pamoja!” nilisema kisha nikaomba kupewa
yule mtuhumiwa wangu. Huwezi kuamini mkuu wa kituo alitoka
mwenyewe na kwenda mpaka kule mahabusu, akamtoa mwenyewe
chini ya ulinzi mkali na kumleta kule kwenye ofisi yake huku
mpaka vijana wake nao wakimshangaa kwa sababu hayakuwa
majukumu yake, angeweza kuwaagiza tu askari wake wakafanya
hivyo.
Alimuingiza mle ndani ya ofisi yake akiwa na pingu zake miko-
noni, akawa anamtazama akiwa ni kama haamini! Nadhani na yeye
alikuwa na shauku kubwa ya kutaka kuona mtuhumiwa wa ugaidi
anafananaje.
“Unahitaji escort ya vijana?”
“Hapana, nina vijana wangu! Nashukuru!” nilisema huku ni-
kimpokea yule mzee wa Kisomali, nikamshika nyuma ya suruali

83 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kwenye mkanda, nikatoka naye mpaka pale kaunta ambapo vijana


wangu walimpokea juujuu, wakamkokota mpaka kwenye gari. Kila
kitu kilikuwa kinafanyika kwa kasi kubwa kwelikweli.
“Tuwasiliane chief, najiona kabisa kwamba kazi yangu ipo
mashakani!” alisema mkuu wa kituo akionesha dhahiri kujawa na
hofu kubwa ndani ya moyo wake, nikamtoa wasiwasi kisha tuka-
ondoka na kuwaacha yeye pamoja na wale askari wote wakiwa
wametulia kabisa.
Ukiona mtuhumiwa anatolewa na askari shupavu waliopitia ma-
funzo wananywea kiasi kile, basi ujue hofu iliyopo ndani ya mioyo
yao ni kubwa kiasi kisicho cha kawaida.
Aliingizwa kwenye siti ya nyuma ya gari tuliloenda nalo, lili-
lokuwa na vioo vya tinted, akawekwa katikati chini ya ulinzi mkali
na muda huohuo alivalishwa kitambaa cheusi usoni, tukaondoka
kwa kasi kubwa huku mimi nikiwa nyuma ya usukani.
Nililazimika kuwasha taa za mbele ili kutoa ishara kwa madereva
wengine watupishe na kwa kuwa gari letu lilikuwa maalum, likiwa
na taa za ving’ora kwa upande wa mbele, mtu yeyote anayefahamu
mambo angeweza kuelewa kwa urahisi kwamba ‘wanaume wapo
kazini’.
Ajabu ni kwamba, wakati watu wengine wote wakionesha kuwa
na taharuki kubwa, yule mzee wa Kisomali yeye alikuwa ametulia
kabisa, akiwa kimya! Yaani hakuwa anauliza wala kuhoji kitu cho-
chote, ni kama alikuwa anajua kila kinachoendelea.
Tuliwasili ofisini, wote tukateremka kijeshi kwenye lile gari na
kusaidiana kumtoa mtuhumiwa wetu, watu wa idara zote walio-

84 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kuwa kwenye pilikpilika za hali ya juu, waliacha kila walichokuwa


wanakifanya na kuanza kutushangaa. Hakukuwa na muda wa
kupoteza, akakokotwa mbiombio mpaka kwenye humba cha maho-
jiano, hakukuwa na muda wa kupoteza hata dakika moja.
Japokuwa tulimchukua kwenye mikono ya polisi, ilibidi kwanza
tujiridhishe kuhusu usalama wetu kwa kumpitisha kwenye chumba
maalum kilichokuwa na mashine maalum za kufanya ukaguzi kwe-
nye mwili wa mtu bila kumpekua au kumpapasa kwa mikono.
Ni mashine kama zile zinazotumiwa kwenye viwanja vya ndege
ambapo unapita kwenye mashine kisha inaonesha kila kitu kilicho-
po mwilini wako kwa maana ya silaha au kitu kisicho cha kawaida.
Alipopitishwa tu, mashine ilipiga kelele za milio mingi kuonesha
kwamba alikuwa na vitu kwenye mwili wake.
“Vua mkanda na viatu na kama una chochote mwilini toa!” nilim-
uamuru, kweli akafanya hivyo huku akiwa bado amevalishwa kile
kitambaa usoni. Akavua mkanda na viatu, mfukoni hakuwa na kitu
chochote zaidi ya kitambaa cha kujifutia jasho. Akapita kwa mara
ya pili lakini bado mashine zikapiga kelele kama mwanzo.
Hapo sasa ilibidi niagize apekuliwe kwa mashine zile ndogo za
kupitisha mwilini ili kujua ni nini alichokuwa nacho kwenye mwili
wake na kilikuwa wapi. Ilipitishwa kuanzia juu mpaka maeneo ya
kiunoni, ikapiga kelele. Nikaamuru ainue mikono yake, akafanya
hivyo, mashine ikapita bila kupiga kelele.
“Itakuwa ni kwenye mikono yake,” nilijisemea huku nikisogea
mwenyewe na kurudia kuipitisha ile mashine, kweli ilionesha
alikuwa na kitu kwenye mkono wake wa kushoto lakini ajabu ni

85 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kwamba hakuna chochote kilichokuwa kinaonekana kwa macho,


hakuwa amevaa pete wala saa ambacho tungesema kwamba ndi-
cho kilichosababisha.
“Una nini kwenye mwili wako we mzee!”
“Kwani wewe unaona nini?” alitoa sauti yake kwa mara ya
kwanza tangu alipoleta fujo kule nyumbani kwake. Sikuona sa-
babu ya kujibizana naye, nikaamuru arudishwe kwenye ile mash-
ine kubwa na safari hii, mkono wake upitishwe kwenye ‘scanner’
maalum iliyokuwa na uwezo wa kuona mpaka mifupa.
Nilisogea mwenyewe kwenye ‘screen’ kubwa iliyokuwa upande
wa nyuma wa ile scanner, nikautazama mkono wake kwa makini
na kugundua jambo ambalo lilizidi kunitia hofu.
Alikuwa amepandikizwa ‘chip’ maalum ya mawasiliano katika
eneo la katikati ya kidole gumba na kidole cha pili. Nitakuja kue-
leza baadaye kuhusu ‘chip’ hii na niliweza kuitambua kwa urahisi
kwa sababu kama nilivyosema, nilikuwa nimeiva kimafunzo.
Niliibonyeza ile ‘screen’ kwenye sehemu maalum, ‘ikaprint’
picha ya kile kilichokuwa kinaonekana, nikaichukua ile karatasi
kisha nikawaamuru vijana wangu wampeleke kwenye kile chumba
maalum cha maojiano.
Alikalishwa kwenye kile kiti alichokuwa amekalishwa yule
mwanamke wakati nikimhoji na kwa kuwa huyu sasa alikuwa
mtuhumiwa hatari, ilibidi afunguliwe pingu na kufungwa na pingu
nyingine maalum zilizokuwa zimeunganishwa kwenye ile meza ya
chuma kwa upande wa chini kwa sababu za kiusalama.
Alivuliwe kile kitambaa cheusi alichokuwa amefungwa kuziba

86 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

uso wake, nikakaa kwenye kiti changu kisha tukawa tunatazamana


uso kwa uso.
“Najua kila kitu kuhusu wewe lakini nitataka kusikia kutoka
kwako mwenyewe! Tupo kwenye wakati mgumu sana kwa sababu
ya mambo mnayoyataka kuyafanya wewe na mwenzako.
“Ushirikiano wako ndiyo utakaokuweka upande mzuri au upande
mbaya! Tumeelewana?” nilisema kwa sauti ya chini lakini iliyo-
jawa na mamlaka huku nikiwa namtazama kwenye macho yake.
Hakujibu chochote zaidi ya kuendelea kunitazama, nikamuu-
liza tena kama amenielewa lakini bado hakunijibu kitu chochote.
Nikatoa simu yangu na kuibofyabofya kisha nikairudisha mfukoni.
Nilikuwa nawasiliana na vijana wangu.
Muda mfupi baadaye, faili dogo jeusi lililetwa mezani kwangu na
mmoja wa wasaidizi wangu, nikaliweka vizuri na kulifungua.
“Asad Burhan! Hili ndiyo jina lako?” nilimuuliza yule mwa-
naume lakini kama ilivyokuwa mwanzo hakunijibu kitu zaidi ya
kubaki akinitazama tu usoni.
“Uliingia nchini Tanzania miaka mingi iliyopita lakini hakuna
mahali popote panapoonesha kwamba uliomba uraia na kuukana
uraia wako wa awali wa Somalia, ukiwa umezaliwa Mogadishu na
kusomea elimu ya msingi na sekondari huko! Unalielezeaje hili?”
nilimuuliza, nikamuona uso wake ukibadilika.
Nadhani pengine hakuwa ametegemea kwamba tunaweza kuwa
na taarifa zake za ndani kiasi hicho, midomo ikawa inamtetemeka
kama anayetaka kusema jambo lakini hajui aanzie wapi.
“Ulizaliwa Cabdulcasiis, nje kidogo ya Jiji la Mogadishu na

87 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ulipata elimu yako ya msingi Shule ya Dharkeynley. Majina ya


wazazi wako, baba yako anaitwa...”
“Kijana wangu!” alinikatisha kabla sijaendelea kwa sababu lile
faili lilikuw ana taarifa zake zote muhimu ambazo tulizikusanya
kwa kutumia vyanzo vyetu ndani ya muda mfupi tu tangu lile seke-
seke lilipotokea, tukishirikiana na mamlaka nyingine za ndani na
nje ya nchi.
“Hakuna sababu ya kuyazungumza yote hayo, niambie tu uli-
chokuwa unataka nikusaidie, nakuomba tafadhali!” alisema,
nikashusha pumzi ndefu na kumtazama tena usoni kwa kumkazia
macho, ule ujeuri wake wote ulionekana kuyeyuka ghafla mithili
ya donge la mafuta liyeyukavyo juani.
“Unafahamu kwa nini upo hapa?”
“Ni kwa sababu wafanyakazi wa Dawasco walikuja nyumbani
kwangu kutaka kukagua lakini nikajaribu kuwazuia.”
“Kwa hiyo hilo ndiyo kosa lako si ndiyo?”
“Ndiyo, nilikamatwa kwa kosa hilo! Ni kweli kwamba pengine
naweza kuwa naishi hapa nchini bila vibali lakini mimi ni raia
mwema, nimeishi Tanzania kwa zaidi ya miaka 30 na siku zote
hizo sijawahi kukutwa na kosa lolote la jinai! Mimi ni raia mwe-
ma,” alisema kwa sauti iliyoonesha dhahiri kwamba alikuwa na
hofu kubwa ndani ya moyo wake.
“Unakumbuka neno langu la kwanza nilipofumbua mdomo
wangu baada ya kuingia ndani ya hiki chumba?”
“Nikumbushe kijana wangu!”
“Narudia tena! Najua kila kitu kuhusu wewe lakini nitataka

88 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kusikia kutoka kwako mwenyewe! Ukitoa ushirikiano pengine


hata makosa yako yanaweza kupunguzwa au kufutwa kabisa lakini
ukileta ujuaji, mwisho wako utakuwa mbaya sana!”
“Nimekuelewa kijana wangu!”
“Ni akina nani wanaoishi kwenye ile nyumba inayopakana na
nyumba yako?”
“Unamaanisha nyumba ipi kiongozi!”
“Nyumba unayopakana nayo ambayo ndani kumetobolewa
mlango wa kupitia kwenye nyumba yako!”
“Ni jamaa zangu!”
“Nataka kuwajua hao jamaa zako ni akina nani, wako wangapi,
wametoka wapi na wanapanga kufanya nini!”
“Kiongozi, kiukweli nashindwa hata kujua naanzia wapi!”
“Anzia popote!”
“Ni kweli mimi asili yangu ni Somalia kama ulivyosema lakini
kabla ya kufika Tanzania na kuja kuweka makazi yangu, nilipata
kuishi kwenye maeneo kadhaa nchini Kenya ambako kuna ndugu
zangu!” alisema kisha akajiinamia na ukimya ukatanda, nikatulia
nikiendelea kumsikiliza.
“Endelea! Hatuna muda wa kupoteza!”
“Miongoni mwa hao ndugu zangu wa Kenya, mmoja wao ndiyo
huyo aliyekuja hapa Tanzania na mimi ndiyo nilikuwa mwenyeji
wake, tukamtafutia nyumba hiyo unayoisema.”
“Anaitwa nani?”
“Abdulwaheed Jabal.”
“Anafanya shughuli gani?”

89 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Ni mfanyabiashara kutoka Mombasa!”


“Anafanya biashara gani? Mbona unanipotezea muda?”
“Anafanya biashara za bidhaa mbalimbali za nyumbani kama
vyakula, mavazi na kadhalika. Pia huwa ananunua mazao kama
korosho na kuyasafirisha kwenda nje ya nchi.”
“Nini kilichomleta Tanzania?”
“Ni hayohayo masuala yake ya biashara! Kwa kifupi mimi najua
tu kwamba ni mfanyabiashara! Mengine siyajui.”
“Anaishi na nani?”
“Na mkewe na mabinti zake!”
“Una uhakika na unachokisema?” nilimuuliza huku nikimkazia
macho, akakwepesha macho yake na kutazama chini!
“Sikia, naona bado haujawa tayari kutoa ushirikiano!”
“Hapana kijana wangu! Haya ninayokueleza ni kweli japokuwa
kuna mengine naweza kuwa nakosea lakini ni kweli.”
“Nataka kujua huyo ndugu yako huwa akitoka alfajiri anakwenda
wapi na tunawezaje kumpata sasa hivi!”
“Huwa anakwenda Rufiji, anasema ananunua korosho kwa sa-
babu huu ndiyo msimu wake, huwa anaondoka alfajiri na kurudi
usiku!”
“Najua kwamba huwa mnawasiliana naye mara kwa mara, sasa
nataka umpigie simu yake sasa hivi umuulize mahali alipo.”
“Simu zangu mbili zilichukuliwa nilipokamatwa na polisi!”
“Tunazo hapa, zimeletwa!” nilisema huku nikitoa simu yangu
na kuibofyabofya na muda mfupi baadaye, mlango ulifunguliwa,
akaingia msaidizi wangu akiwa na zile simu.

90 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Ambacho hakuwa anakijua ni kwamba alipokamatwa tu baada ya


lile sekeseke la watu wa Dawasco, nilitoa maagizo kwamba simu
zake zichukuliwe na zikakabidhiwa kwetu, kwa hiyo hazikuwa
kwenye mikono ya polisi kama mwenyewe alivyokuwa anadhani
na sababu kubwa ilikuwa ni kutaka kufuatilia mawasiliano yake
kwa karibu kabisa na kujua ni nini kilichokuwa kinaendelea.
Ndani ya muda huo tangu alipokamatwa, vijana wetu wa kitengo
cha ‘Cyber’ walikuwa wakiendelea na kazi yao na nilikuwa na
uhakika kwamba tayari wameshafanya kazi yao kwa ukamilifu,
kwa hiyo kilichokuwa kinatakiwa kwa wakati huo, ilikuwa ni
yeye kupiga tu simu ya huyo mtu aliyekuwa anamsema kisha kwa
kutumia mitambo maalum tutaweza kunasa ‘location’ ya mahali
alipokuwa huyo mwanaume tunayemsaka kwa udi na uvumba.
“Simu zako si ni hizi?”
“Ndiyo kiongozi!”
“Haya chukua umpigie!” nilisema huku nikibofya kifaa maalum
cha mawasiliano nilichokuwa nimekivaa kutoa ishara kwa watu
wa ‘cyber’ wafanye kazi yao ingawa nilikuwa najua pia kwamba
wanasikiliza kila kilichokuwa kinaendelea.
“Weka loud speaker,” nilimwambia kumpumbaza. Nilikuwa
na uhakika kwamba simu itakapopokelewa tu, atakachokifanya
itakuwa ni kumpa tahadhari huyo mwenzake kwamba amekamatwa
lakini hiyo isingetosha kumuokoa kwa sababu mitambo ilishawe-
kwa ‘standby’ kunasa mawimbi ya sauti na kujua ni wapi alipo.
Kweli simu iliita na muda mfupi baadaye, ilipokelewa.
Kama nilivyokuwa nimetarajia, simu ilipopokelewa tu, yule mzee

91 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wa Kisomali kuna maneno ambayo hakuna kati yetu aliyeelewa


mara moja, aliyasema harakaharaka kisha akajifanya ni kama ame-
paliwa na mate.
Nilitulia nikimtazama kwa sababu nilishakuwa nimeelewa ujanja
wake hata kabla hajaufanya, wakati akiamini yeye ni mjanja tayari
vijana wangu wa Cyber walikuwa wameshafanya yao na kufani-
kiwa kunasa ‘location’ ya huyo aliyekuwa anaongea nae.
Kifaa changu cha mawasiliano nilichokuwa nimekiingiza sikioni,
ndicho kilichofanya nielewe kwamba tayari walikuwa wamefani-
kiwa kunasa ramani ya mahali alipokuwa.
“Muulize yuko wapi!” nilisema kwa sauti ya chini nikimwambia
yule mzee wa Kisomali ambaye bado alikuwa akiendelea kujiko-
holesha wakati simu ikiwa hewani.
“Uko wapi ndugu yangu!”
“Niko shambani!” ilisikika sauti ya upande wa pili, kuonesha
kwamba ndiyo yule tuliyekuwa tukimsaka na Kiswahili chake ki-
likuwa na lafudhi ya tofauti kuonesa kwamba kweli ni yeye ndiye
tuliyekuwa tunamsaka.
“Basi sawa,” alisema kisha akawahi kuikata simu kisha akani-
tazama, bado nilikuwa nimemkazia macho, mapigo ya moyo
wangu yakinienda mbio kuliko kawaida.
“Unajifanya mjanja si ndiyo?”
“Hapana kiongozi, nimefanya kama ulivyoiagiza, na umemsikia
mwenyewe hapa akisema yupo shambani, kama nilivyokwambia
yupo kununua korosho Rufiji,” alisema huku eti akijifanya kunika-
zia macho ili niamini alichokuwa anakisema.

92 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)
Nilichokigundua harakaharaka, ni kwamba mzee huyu wa Ki-
somali naye alikuwa na mafunzo na alikuwa akishirikiana kwa
karibu na watu waliokuwa nyuma ya pazia kwa sababu hata namna
alivyokuwa akijikoholesha pale, ni kwamba kuna ujumbe alikuwa
akiufikisha kwa njia ya kikohozi kumpa taarifa yule aliyekuwa ana-
zungumza naye.
“Sasa kwa kuwa umekataa kutoa ushirikiano kwa hiyari yako,
tutakulazimisha utoe ushirikiano kwa shuruti na na kuhakikishia
utafurahi na nafsi yako,” nilisema huku nikisimama kwa jazba.
Sikutegemea kama anaweza kuleta masihara kiasi hicho katika
suala nyeti kama lile na moyoni nikajiapiza kwamba nitamfunza
adabu, tena kwa mikono yangu mwenyewe kwa sababu ilishaone-
sha wazi kwamba hakuwa tu akishirikiana na magaidi, bali yeye
mwenyewe alikuwa gaidi na ndiyo maana hata alikuwa amepan-
dikizwa ‘chip’ ya mawasiliano kwenye mkono wake.
Niliposimama tu, vijana wangu wawili waliingia na nikawapa
maelekezo kwamba kitu cha kwanza inatakiwa ‘chip’ yake ya mko-
noni ikatolewe na kuhifadhiwa kisha apelekwe kwenye mahabusu
ya chini ya ardhi mpaka nitakaporejea.
Nilitoka kwenye kile chumba na kuwaacha vijana wangu waki-
tekeleza kile nilichowaambia na moja kwa moja nikaingia kwenye
kile chumba cha pili walichokuwa wamekaa viongozi wa idara
mbalimbali wakisikiliza kila kilichokuwa kinaendelea.
“Tunafanyeje!”
“Tumehafanikiwa kunasa location ya mahali alipo huyo ali-
yekuwa anazungumza naye, anatakiwa kwenda kukamatwa haraka

93 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)
iwezekanavyo,” nilisema huku nikikiweka vizuri kifaa changu cha
mawasiliano sikioni ili kuzungumza na vijana wa Cyber ambao
ndiyo waliokuwa wakifanya kazi ile.
“Weka location kwenye ‘screen 2’,´nilisema wakati nikiungumza
nao, nadhani wote mle ndani hawakuwa wamenielewa harakaharaka
nilimaanisha nini na muda mfupi baadaye, ‘screen’ kubwa iliyokuwa
upande wa juu kabisa wa kile chumba, iliwaka, nikawataka watu
wote waitazame kwa makini.
Ilifungua ramani, zile zinazotumika na ‘satelite’, watu wote
wakatulia wakiitazama, mimi pia nikatulia kwa sababu bado sikuwa
nimeelewa yuko wapi. Ramani iliendelea kujifungau huku wote
tukitupia macho na mwisho ikatulia. Mawasiliano yalionesha kwam-
ba simu ile ilikuwa katika eneo la Kibiti mkoani Pwani.
“Ngoja kwanza kuna kitu sijakielewa hapa,” alisema mkurugenzi
huku akisimama, akionesha kushangazwa na kile kilichokuwa kina-
onekana pale kwenye ramani.
“Eneo lote la Mkiru kuna mauaji yasiyoeleweka yanayoendelea
kwa kasi,” alisema, akiwa na maana kwamba Mkiru ni kifupisho
cha Mkuranga, Kibiti na Rufiji, hivyo ndivyo eneo hilo tulivyokuwa
tunaliita kwa lugha za kioparesheni.
Akaendelea: “Halafu hapa tunaoneshwa mtuhumiwa tunayemsaka
yupo Kibiti muda huu! Kwa hiyo inamaanisha wale wanaofanya
matukio ya kihalifu kule ikiwa ni pamoja na kuwaua viongozi wa
serikali wa vijiji na mitaa na kuvamia vituo vya polisi wapo kwenye
‘misheni’ moja na hawa wanaotaka kuvamia ikulu?”
“Siyo kwamba wapo pamoja, bali ni kwamba ni watu haohao, ni

94 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kundi moja lenye lengo moja, picha kubwa imeanza kufunguka


sasa,” nilisema, kila mtu akabaki amepigwa na butwaa.
“Tueleze nini cha kufanya!”
“Tunaondoka sasa hivi kuelekea Kibiti, lazima tumpate leo-
leo, nimeshatoa maelekezo kwamba ‘location’ yake iwe ‘pinned’
ili asitupotee, hata akizima simu tutakuwa na uwezo wa kuona
mahali alipo mpaka tumpate,” nilisema lakini kila mtu nadhani
hakuamini kama nilichokisema kinawezekana.
Walihisi pengine tunakwenda kupoteza muda na kamwe hat-
utafanikiwa kumpata, moyoni nikajiapiza kwamba nitawaonesha
kwamba inawezekana. Teknolojia tuliyokuwa tunatumia katika
kunasa mawasiliano, ilikuwa mpya kabisa na ndiyo iliyokuwa
inatumika katika mataifa yaliyoendelea.
Kilichofuatia baada ya hapo ilikuwa ni utekelezaji, harakaharaka
magari sita yakaandaliwa na timu ya kutosha kutoka kikosi cha
kupambana na ugaidi pamoja na vijana wangu wengine nilioona
watatusaidia lakini pia timu ya Cyber ilitakiwa itoe watu wawili
na wengine wabaki pale makao makuu ili waendelee kufuatilia
kwa karibu ‘location’ ya yule mtu ili asije akatupotea.
Ndani ya dakika kumi tu, tayari maandalizi yote yalikuwa yame-
kamilika, tukatoka kwa kasi ya kimbunga pale getini na safari ya
kuelekea Kibiti ikaanza. Ilibidi mbele tusindikizwe na pikipiki ya
askari wa usalama barabarani ili tusichelewe kwenye foleni za Jiji
la Dar es Salaam.
Tukaondoka kwa kasi kubwa huku mimi nikiwa kiongozi wa
msafara, nikiendesha gari la mbele kabisa katika msafara, pem-

95 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

beni yangu nikiwa na kijana mmoja kutoka Cyber akiwa na vifaa


yake, akiwasiliana moja kwa moja na wenzake waliokuwa kule
ofisini na nyuma ya gari wakiwa wamekaa vijana wangu wawili
niliokuwa nawaamini zaidi.
Kasi tuliyokuwa tunakwenda nayo ilikuwa kubwa kwelikweli,
kama ile inayotumiwa kwenye misafara ya viongozi, ile pikipiki
ya mbele ilitusaidia sana kufungua njia kwa sababu ile pikipiki ili-
kuwa ikiwasiliana moja kwa moja na askari wa usalama barabarani
waliokuwa kwenye vituo mbalimbali, magari yakawa yanazuiwa
sehemu mbalimbali kutupisha.
Ndani ya dakika zisizopungua kumi na tano, tayari tulikuwa
tumeshatoka nje kabisa ya Jiji la Dar es Salaam, tukawa tunaipasua
barabara kuu ya kuelekea kusini kwa kasi ya kimbunga. Tulien-
delea kuchanja mbuga kwa kasi ambapo baada ya yule trafiki
kujiridhisha kwamba hakukuwa tena na chochote kinachoweza
kutukwamisha, aliwasiliana na vijana wangu kwa kutumia simu za
upepo na tukamruhusu arudi.
Aliitoa pikipiki yake pembeni ya barabara, tukampita kama
mshale mimi nikiwa mbele kabisa na safari ikaendelea, yeye aka-
rudi ake mjini.
Tukiwa tumebakiza takribani kilometa ishirini kuingia Kibiti,
yule mtaalamu wa Cyber, aliongea jambo ambalo lilinishtua
kidogo.
“Chief, inaonekana ‘target’ ana-move kwa kasi kubwa kuja
uelekeo huu, anatoka Kibiti kuelekea Dar es Salam kwa kutumia
barabara hiihii,” alisema, akili za haraka zikanituma kusimamisha

96 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

msafara wote kisha tuweke mtego hapohapo.


Nilitoa taarifa kupitia vifaa vya mawasiliano kwa madereva
wote kisha taratibu nikaan kupungua spidi, magari ya nyuma nayo
yakawa yanapunguza spidi kunifuata na mwisho wote tulisimama,
ikabidi kwanza nijiridhishe mwenyewe kile alichokuwa ameni-
eleza.
Ni kweli ramani ya satelite kwenye laptop ya kisasa ya yule afisa,
ilionesha kwamba ile simu tuliyokuwa tukiifuatilia, ilikuwa ikija
kwa kasi ya takribani kilometa 80 mpaka 100 kwa saa kuja upande
wetu, jambo ambalo lilitosha kuonesha kwamba pengine anaweza
kuwa kwenye gari au pikipiki.
Nilijiridhisha mara tatu tatu ili kuhakikisha kama hatuchezewi
akili na baada ya kuwa na uhakika, niliwataarifu viongozi wangu
na tukakubaliana kwamba tuweke kizuizi cha barabarani eneo lile
kwa lengo la kumnasa mtuhumiwa kiulaini kabisa.
“Yupo umbali gani?”
“Inaonesha ni kama kilometa sita kutoka hapa!”
“Piga mahesabu ya kasi anayotumia na muda atakaoutumia ku-
fika hapa!” nilimwambia yule kijana wa Cyber, harakaharaka akaf-
anya mahesabu yake na kunipa majibu. Niliona tunatakiwa kusubiri
kidogo kabla ya kuweka kizuizi kwa sababu endapo tukiweka
mapema, mhusika anaweza kupata taarifa akabadilisha mawazo.
Kilichofanyika ni kwamba tulisogea kama kilometa moja hivi
mbele, mahali ambapo kulikuwa na miti mingi kando ya barabara,
nikaamrisha magari yote yaingizwe vichakani na pale barabarani
libaki gari moja tu, lile ambalo mimi ndiye niliyekuwa naliendesha.

97 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Harakaharaka hilo lilifanyika, nikawakusanya haraka vijana


wangu na kuanza kuwapa maelekezo ya nini kilichokuwa kinat-
akiwa kufanyika.
Ilikuwa ni lazima tumkamate huyo Abdulwaheed Jabal ingawa
nilikuwa na uhakika kwamba lazima atakuwa anatumia majina
mengine ya bandia kama ilivyo kwa magaidi wengi na pengine
hata hilo halikuwa jina lake halisi.
Niliwapa maelekezo yote, kila mmoja akaiweka tayari silaha
yake, nikachomoa bastola yangu kiunoni na kuhakikisha kama ipo
sawa, tayari kwa kilichokuwa mbele yetu na baada ya kuhakikisha
kila kitu kipo sawa, nilirudi barabarani, watu wote wakawa wana-
subiri kusikia kutoka kwangu.
Kwa muda huo pia nilikuwa nawasiliana na makao makuu moja
kwa moja kwa kutumia vifaa vya mawasiliano nilivyokuwa nime-
vivaa mwilini, mkurugenzi akaonesha kuwa na mchecheto usio wa
kawaida.
‘Rada’ ziliendelea kusoma, yule kijana wa Cyber akawa bize
kwelikweli kuhakikisha anatimiza majukumu yake kikamilifu na
mimi nikawa naye bega kwa bega. Magari mengine mengi yalien-
delea kupita kuelekea kila upande, tukawa tumeikazia macho ile
kompyuta ya kisasa yenye uwezo mkubwa aliyokuwa nayo yule
kijana wangu.
‘Location’ iliendelea kusoma, ikionesha chombo cha moto ali-
chomo yule mtuhumiwa wetu ikisogea kwa kasi kubwa kuja pale
tulipokuwepo na alipobakiza kilometa chache, ilibidi niliwashe
gari na kuliingiza barabarani.

98 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Nikawasha taa za ‘double hazard’, zile zinazotumika kuwataarifu


madereva wengine kama kuna tatizo kwenye gari husika, mapigo
ya moyo wangu yakawa yananienda mbio kwelikweli, nikib-
adilisha macho harakaharaka baina ya ile kompyuta na usawa wa
barabarani.
“Ameshafika chief, inaonekana ni hilo gari linalokuja mbele
yetu,” alisema yule kijana na bila kupoteza muda, nilikanyaga
mafuta na kulizungusha gari kwa kasi kubwa, likasimama kiubavu
na kuziba barabara, nikawapa taarifa na wale vijana wangu ambao
wote waliwasha magari yao wakisubiri nitakachowaeleza.
Niliteremka haraka, nikazunguka ule upande ambao ndiyo lile
gari lilikuwa likija, nikachomoa bastola na kuikoki, sekunde
chache baadaye likatokea gari aina ya Toyota Canter, wengi tu-
mezoea kuyaita ‘kenta’ la rangi ya bluu, nikanyoosha mkono juu
huku nikisogea mbele kama ishara ya kumtaka dereva asimame.
Nikatoa ‘signal’ kwa wale vijana wangu, nao wakayatoa magari
kule vichakani kwa kasi kubwa na kuja kuiziba barabara yote,
hakukuwa na uwezekano wowote kwamba dereva anaweza kutuk-
wepa na kukimbia.
Kwa kuwa alikuwa mwendo wa kasi, aliwasha taa kubwa za
mbele na kuzizima kama anayetoa ishara kwamba hawezi kusi-
mama ghafla, nikamuelekezea bastola huku nikiendelea kunyoosha
mkono kumtaka asimame.
Alibadili gia kwa kasi kubwa, akazipangua na kuanza kufunga
breki, gari likawa linajiburuza kwenye lami kiasi cha tairi kutoa
moshi wakati zikisuguana na lami na hatimaye alisimama.

99 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Aliposimama tu, moja kati ya yale magari lilipita pembeni kwa


kasi na kwenda kuzuia kwa nyuma na mengine mawili yakaja na
kusimama ubavuni, moja kushoto na jingine kulia, tukawa tumeli-
weka katikati.

100 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

5
K
ILA kitu kilifanyika kwa kasi kubwa na umakini
wa hali ya juu, vijana wangu wote wakawa wame-
shatoa ‘mabomba’ kuelekeza kwenye lile gari. Kwa
umakini mkubwa nikasogea mpaka upande wa
dereva, nikamuona akiwa amenyanyua mikono juu
huku akionesha kuwa na wasiwasi usioelezeka.
“Teremka!” nilitoa amri, kweli akatii na kuteremka huku mikono
yake ikiwa juu, nikampokea juujuu na kumlaza kwenye lami huku
nikimuwekea goti mgongoni, nikafanikiwa kumdhibiti na kum-
funga pingu kwa nyuma.
Vijana wangu nao walikuwa ‘sharp’ kwelikweli, wakawaterem-
sha watu wengine wawili waliokuwa upande wa pili wa dereva

101 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

na kuwasogeza pale nilipokuwa nimemdhibiti yule dereva, wote


wakalazwa chini na kufungwa pingu.
Gari likakaguliwa, hakukuwa na mtu mwingine zaidi ya dereva
na wale vijana wawili, gari lenyewe lilikuwa limebeba mihogo kwa
wingi upande wa nyuma. Ilionesha dhahiri kwamba ilikuwa ina-
tolewa shamba kuelekea sokoni.
Baada ya kujiridhisha kwamba hakukuwa na mtu mwingine
yeyote, niliamuru dereva ambaye alikuwa akiendelea kutetemeka
pale chini ainuliwe, vijana wangu wakafanya hivyo, akasimamish-
wa akiwa ameshikwa huku na kule, tukawa tunatazama naye.
Alikuwa ni kijana mwenye kati ya umri wa miaka 35 mpaka aro-
baini, akawa ananitazama kwa hofu, akitetemeka kuliko kawaida.
Alipekuliwa pale, hakuwa na kitu kingine mfukoni zaidi ya pakti
ya sigara, leseni yake ya udereva na noti kadhaa.
Bila kumsemesha chochote, niliitazama leseni yake, nikasoma
jina na kutazama sura kuhakiki kama ndiyo iliyokuwepo kwenye
leseni, baada ya kujiridhisha kwamba yeye ndiye mmiliki wa ile
leseni, nilianza kumhoji.
“Unaitwa nani?”
“Sadick Dule bosi wangu, kuna tatizo lolote afande?”
“Unatakiwa kujibu ninachokuuliza siyo kuanza kuhoji tena!”
“Sawa afande!”
“Unatoka wapi na unakwenda wapi?”
“Tumetoka shamba kuchukua mihogo ya mteja wetu, tunaipeleka
sokoni Buguruni!”
“Hawa ulionao ni akina nani?”

102 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Ni wasaidizi wangu afande!”


“Una uhakika?”
“Ndiyo, mmoja anaitwa Jofu na mwingine Said, ni vijana wangu
wa siku zote ninaofanya nao kazi!” alisema, nikaamuru apigishwe
magoti, hilo likafanyika na wale wenzake wakaenda kuinuliwa pale
walipokuwa wamedhibitiwa.
Nilipowatazama sura zao, nilibaki nimepigwa na bumbuwazi,
walikuwa ni vijana wadogo ambao kweli walionesha kuwa ni wa-
saidizi wa yule dereva na wote walionesha kuwa wanashughulika
na kazi ya kusafirisha mazao. Niliwauliza majina yao, kila mmoja
akataja lake kama yule dereva alivyowatambulisha.
Ilibidi nirudi kwenye gari na kumuuliza yule kijana wa Cyber
kama alikuwa na uhakika gari husika ndiyo hilo.
“Ni lenyewe chief, si unaona hapa ‘location’ inasoma mbele yetu
haapa na haitembei tena!”
“Inawezekanaje!”
“Kwa nini bosi!”
“Sidhani kama hawa ndiyo watu tunaowatafuta!” nilisema huku
nikirudi haraka pale tulipokuwa tumewapigisha magoti.
“Kila mmoja atoe simu yake!”
“Hawa vijana wangu hawana simu, huwa wanatumia ya kwangu
afande!” alisema yule dereva huku akionesha mfuko ambao simu
yake ilikuwepo, vijana wangu wakaitoa mfukoni, wale wengine
wakapekuliwa upya na kweli hawakuwa na simu.
Niliichukua ile simu na kurudi kwenye gari haraka, nikamwam-
bia kijana wa Cyber ahakikishe kama ndiyo yenyewe. Ajabu ni

103 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kwamba ilionesha kuwa siyo ile simu tuliyokuwa tumenasa ‘loca-


tion’ yake na kuanza kuifuatilia.
“Kuna uwezekano wa kuipiga hiyo simu inayosoma location
hapa!”
“Ndiyo chief, dakika sifuri,” alisema huku akiibofyabofya laptop
kwa kasi kubwa na muda mfupi baadaye ikaonesha kuwa imeanza
kuita.
“Kuna simu inaita huku chief,” alisema mmojakati ya vijana
wangu akionesha kule nyuma ya lile gari kulikokuwa na shehena
ya mihogo, nikasogea mwenyewe kwenda kuhakikisha. Ni kweli
kulikuwa na simu (smartphone) iliyokuwa inasikika ikiita.
“Mleteni huyo dereva,” niliagiza huku nikiendelea kusikiliza kwa
makini mlio wa ile simu, kweli dereva akaletwa, naye akawa ni
kama anashangaa kusikia simu inaita kwenye shehena ya mihogo.
“Ni simu ya nani hiyo inayoita?”
“Sijui afande, labda tuitafute!”
“Hujui vipi wakati wewe ndiyo dereva wa hili gari?”
“Haki ya Mungu tena sijui afande!” alisema huku na yeye akien-
delea kusikiliza kwa makini mlio wa ile simu.
Tayari magari kadhaa yalikuwa yamefika eneo lile kutokea pande
zote mbili na yakalazimika kusimama kwa sababu barabara ili-
kuwa imefungwa, vijana wangu wengine wawili wakafanya kazi ya
kuhakikisha wanasimama mbali na eneo lile wakati ukaguzi ukien-
delea.
“Itafute mpaka uipate,” nilimuamuru yule dereva, nikamfungua
pingu kwa sababu hakuwa na uwezo tena wa kutukimbia, akapanda

104 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kule kwenye shehena ya mihogo na kuanza kupekua na haukupita


muda akawa ameipata.
“Hii hapa!” alisema huku akiitoa simu hiyo iliyokuwa imefungwa
kwenye mfuko maalum, ilionesha wazi kwamba tulikuwa atume-
chezewa akili.
“Haiwezekanii!” nilisema huku nikilipiga teke tairi la gari kwa
nguvu, sikutaka kuamini kama tumezidiwa akili kizembe namna
ile, ilionesha ile simu iliwekwa kwenye lile gari kwa makusudi
baada ya mhusika kujua kwamba alikuwa anafuatiliwa.
“Hawa watakuwa wanajua kinachoendelea na wameshiriki
kutuchezea akili, sasa nawaambia hivi, mmeingia anga mbaya,
mtaijutia sana siku mliyozaliwa kutoka kwenye matumbo ya mama
zenu?” nilisema kwa kufoka nikiwa nimemsogelea yule dereva
karibu kabisa na uso wake.
“Bosi, utakuwa unatuonea tu afande, ndugu zako tunafanya kazi
ngumu sana ili kuendesha maisha yetu, huu mzigo wa watu tume-
shakula pesa, unafikiri mkitukamata na mzigo ukaharibika tutapata
wapi fedha za kumlipa mhusika?”
“Hayo siyo matatizo yangu! Ni matatizo yenu ambayo hakuna
yeyote kati yetu anayehusika, unafikiri sisi ni wajinga kuja kuwa-
zuia na kuwakamata? Kwa nini tusikamate gari lingine lolote kati
ya yale? Kwa nini tumewakamata nyie?”
“Lakini kamanda mi bado sijaelewa kinachoendelea, kwamba
kuna mtu ametuchoma au? Lakini hatuna kosa lolote tulilolifanya,
tunafanya kazi zetu katika mazingira magumu sana.”
“Hivi unaelewa unachokizungumza kweli? Hebu njoo huku,”

105 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

nilisema huku nikimvuta yule dereva pembeni. Nikiri kwamba kwa


wakati huo akili hazikuwa zangu kwa sababu sikuwa najua nitajibu
nini kwa viongozi wangu kwani nilishawaaminisha kwamba tunak-
wenda kumnasa mhusika, iweje atuzidi akili kirahisi namna hiyo?
Niliona kabisa jinsi ambavyo ningedharaulika na kushusha heshi-
ma yangu kwa viongozi wangu, tena katika nyakati za hatari kama
hizo kwa hiyo hata matendo yangu yalikuwa ni ya kiwendawazimu.
Nasema hivyo kwa sababu njia niliyotumia kumsogeza pem-
beni yule dereva haikuwa sawa, nilimkunja kwenye shati chakavu
alilokuwa amevaa lakini kwa wakati huohuo nikawa nimempiga
‘Tanganyika jeki’, japokuwa alikuwa mtu mzima na alikuwa na
mwili mkubwa, nilimnyanyua kama kifurushi na kumzogeza pem-
beni, vijana wangu waliokuwa wananijua wakawa wameshaelewa
kwamba mashetani yameshanipanda.
Nilimsogeza pembeni kabisa, kule vichakani, nikamkokota mpa-
ka kwenye mti mkubwa na kumkandamiza kwa kutumia mkono
mmoja, mwingine nikachomoa bastola ambayo tayari ilishakuwa
imekokiwa.
“Nataka uniambie unajua nini kuhusu hii simu, vinginevyo ni-
takumwaga ubongo sasa hivi,” nilisema huku midomo ikinicheza,
mapigo ya moyo wangu yakinienda mbio kwelikweli, sikuwa mimi
tena.
Yule dereva ni kama alikuwa haamini kilichokuwa kinatokea,
huku akitetemeka sana akaniomba anieleze anachokijua.
Wakati tumetoka shamba, kuna jamaa mmoja kama Msomali hivi
alitusimamisha na kuomba lifti, akadai anakwenda Dar es Salaam,

106 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kwa kuwa tulikuwa tumeshajaa huku mbele tukamwambia kama


ataweza akae nyuma kwenye mihogo kwa sababu hatuna sehemu
ya kumuweka.
“Akakubali na kupanda nyuma, tukaendelea na safari mpaka
tulipofika sehemu inaitwa Jaribu Mpakani, akagongagonga kioo na
kuniambia kwamba amepigiwa simu kuna matatizo huko shamba
alikotoka kwa hiyo inabidi arudi, kwa hiyo tukamshusha pale Ja-
ribu Mpakani sisi tukaendelea na safari yetu.
“Naamini yeye ndiye aliyeangusha hii simu yake!”
“Yupoje?”
“Mrefu wa wastani, mwembamba na ana sura na nywele za ki-
somali, siyo mweupe wala siyo mweusi.”
“Ukimuona unaweza kumtambua?”
“Vizuri kabisa kwa sababu nilimuangalia vizuri na sidhani kama
ni mara ya kwanza kumuona kwenye yale maeneo, alisema wana
kambi yao ya kununua korosho kule shamba,” alisema kwa ku-
tetemeka, nikashusha pumzi ndefu na kuirudisha bastola kiunoni.
“Usalama wako ni mpaka mtu huyo atakapopatikana, ni mtu
hatari sana kwa usalama wa taifa letu na kwa usalama wa mimi na
wewe, ni lazima apatikane haraka iwezekanavyo.”
“Niko tayari kutoa ushirikiano kamanda, mimi siyo mhalifu
na isitoshe nina familia kubwa inanitegemea, nikipata matatizo
watakaoumia ni wengi, nakuomba sana,” alisema, nikawa bado
namtazama ndani ya macho yake kupima kama alichokuwa
anakisema kilikuwa kinatoka ndani ya moyo wake na kilikuwa ni
kweli.

107 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Nilibaini kwamba alikuwa anazungumza ukweli na kweli ali-


maanisha kile alichokuwa anakisema, moyoni nikawa na ahueni fu-
lani kwamba angalau naweza kueleza ni hatua gani ambayo niliku-
wa nimeifikia mpaka wakati huo na kweli kulikuwa na matumaini
ya kumpata.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, moyoni nikawa nimempania
sana yule mzee wa Kisomali ambaye alikuwa kwenye mikono yetu
kwa sababu ni yeye ndiye aliyevuruga kwa makusudi mpango wa
kumpata mtuhumiwa huyu hatari tuliyekuwa tunamtafuta, nika-
jiapiza kwamba muda wake wa kushughulika naye utakapofika,
atajua kwamba hajui.
Harakaharaka tulirudi kule barabarani, ikabidi kwanza niwape
maelezo vijana wangu ili nao wawe wanajua ni nini kinachoende-
lea, baada ya kila mmoja kuelewa, hakukuwa na muda wa ku-
poteza. Kitu cha kwanza ilikuwa ni kwenda kwenye yale magari
yaliyokuwa yanatokea upande wa kusini kuelekea jijini Dar es
Salaam na kukagua moja baada ya jingine kama yule mtuhumiwa
wetu alikuwemo.
Ilikuwa ni lazima kufanya hivyo kwa sababu Waswahili wa-
nasema unapomulika nyoka lazima uanzie kwenye miguu yako,
isingeleta maana kwenda kuanza msako huko Jaribu Mpakani huku
tukiacha watu wengine waendelee kupita.
Kwa kuwa magari hayakuwa mengi, ndani ya muda mfupi tu tu-
likuwa tumeshamaliza kwa hiyo tukaifungua barabara lakini kabla
ya kuifungua, niliwasiliana na makao makuu na kuwaeleza kila
kilichokuwa kinaendelea ikiwa ni pamoja na wajihi wa mtuhumiwa

108 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

tunayemtafuta kama nilivyoelezwa na yule dereva ambaye alieleza


kwamba hata akimuona anaweza kumtambua.
Vizuizi vya barabarani vilianza kuwekwa kuanzia palepale tulip-
okuwa tumesimama, ambapo lile gari la mihogo ilibidi libaki pale
pamoja na vijana wangu wawili ambao walitakuwa kusubiri mpaka
wenzao watakapokuja kuwapokea.
Kwa kuwa suala lenyewe lilikuwa linahusisha masual aya us-
alama barabarani, askari maalum wa kikosi cha usalama barabarani
walipewa maagizo kutoka juu na haukupita muda mrefu wakaanza
safari ya kuja kutusaidia.
Wakati hayo yakiendelea, mimi na timu yangu ukiacha wale
waliobaki pale kwenye kizuizi cha barabarani, tulikuwa tukiipasua
lami kwa kasi kubwa kwelikweli kuelekea Jaribu Mpakani.
Yule dereva wa lile gari la mihogo ilibidi nikae nae kwenye gari
langu, akawekwa katikati siti ya nyuma wakati nikiendelea ku-
wasiliana kwa karibu na yule kijana wa Cyber ambaye alikuwa na
umuhimu mkubwa sana kwenye timu yetu.
“Hujasema chochote mpaka muda huu!”
“Ni kweli, najaribu kufanya kitu kinachoitwa ‘Triangulation’.”
“Naelewa kuhusu intel triangulation, unataka kubaini nini!”
“Nilichokielewa mpaka sasa ni kwamba huyu mtuhumiwa baada
ya kupigiwa simu kutoka hapa, yeye akiwa hapa, ndipo alipoamua
kubadili uelekeo wake lakini katika masuala haya ya kunasa
uhalifu wa kimtandao wa aina hii, lazima kuwe na mtu wa tatu
anayekamilisha pembe tatu.”
“Unataka kusemaje?”

109 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Huyu alipopigiwa simu lazima na yeye atakuwa amepiga simu


sehemu nyingine, hiyo pembetatu ndiyo ninayohangaika kuikamili-
sha hapa kujua aliwasiliana na nani mwingine ambaye yupo wapi
na kwa nini aliwasiliana naye.”
“Nitegemee nini kutoka kwako?”
“Tutapata majibu ndani ya muda mfupi sana!” alisema kwa sauti
ya chini yule kijana wa Cyber kiasi kwamba ndani ya lile gari ni
mimi na yeye pekee ndiyo tuliokuwa tunaelewana.
Safari iliendelea, nikawa naendesha gari kwa kasi kubwa kwe-
likweli kwa sababu kuna wakati mshale wa kusoma spidi ulikuwa
unacheza kati ya 160 mpaka 180, kwa madereva watakuwa wa-
naelewa jinsi kasi hii ilivyokuwa kubwa kiasi kwamba ukifanya
kosa dogo tu, unaweza kujikuta umesababisha ajali mbaya kupin-
dukia.
Haukupita muda mrefu tukawa tumeshafika Mkuranga, tukapita
kwa kasi ya mshale na kusababisha watu wote wabaki wanatushan-
gaa kwa sababu yale magari yaliyokuwa nyuma yangu yalikuwa
yanafuata moto ninaoenda nao.
Changamoto kubwa ambayo nilikumbana nayo, ni kwamba
barabara ya kusini kwa kawaida huwa inakuwa na malori mengi
yanayobeba saruji au malighafi kwenda au kutoka katika kiwanda
cha Dangote na kwa kawaida madereva wa malori haya huwa wa-
nakuwa wakaidi wawapo barabarani.
Hali hiyo ililazimika niwashe taa kubwa za mbele na kila nili-
pokuwa naona lori mbele, nilikuwa nikiwasha zile taa za vimulim-
uli zilizokuwa mbele na upande wa juu wa gari, kwa hiyo wakawa

110 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wanapisha wenyewe ingawa haikuwa rahisi.


Tuliendelea kupasua lami kwa kasi kubwa, tukaingia sehemu
inayoitwa Mwalusembe, napo tukapita kwa kasi ya kimbunga, tu-
kaingia Kimanzichana na sasa tukawa tumebakiza kilometa chache
kuingia Jaribu Mpakani.
Bado mawasiliano ya karibu yalikuwa yakiendelea na viongozi
wangu waliokuwa jijini Dar es Salaam, nao wakawa wanaendelea
kunisisitiza kwamba mimi ndiye mtu pekee ninayeweza kutegua
kitendawili kile.
Uzuri ni kwamba hakuna aliyekuwa ananilaumu baada ya ku-
ingizwa ‘mkenge’ na yule mhalifu alipoweka simu kwenye gari
lililobeba mihogo, kila mtu alikuwa nyuma yangu, nikapata moyo
wa kuzidi kupambana.
Vikosi vingine vya wanausalama, kuanzia wale wenzetu wa
kikosi maalum cha kupambana na ugaidi, askari wa jeshi la polisi
pamoja na wale wa usalama barabarani, wote walikuwa wameele-
keza macho na masikio yao kule tulikokuwa tunakwenda kwa
sababu suala lililokuwa mbele yetu, lilikuwa linatuhusu wote.
Haikuwa kawaida kwa sisi kufanya kazi kwa karibu na vikosi
vingine lakini kutokana na hali halisi, ilibidi tushirikiane kwa hali
na mali ili kuzuia kilichokuwa kinaenda kutokea.
“Chief nimepata majibu ya ‘triangulation’,” alisema yule kijana
wa Cyber, ikabidi nipunguze mwendo kidogo ili niweze kumuele-
wa alichokuwa anataka kukimaanisha.
“Inaonesha baada ya kupigiwa simu, huyu mtuhumiwa alipiga
simu Kibiti!” alisema, nikashusha pumzi ndefu na kuongeza

111 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

mwendo.
Kile nilichokuwa nakihisi kuanzia mwanzo sasa kilikuwa kinaan-
za kujidhihirisha! Mpaka hapo nilishakuwa na uhakika kwamba
yale matukio ya mauaji na uporaji wa silaha kwenye vituo vya
polisi yalikuwa na uhusiano na ule mpango wa kuivamia ikulu na
mpaka hapo ilionesha kwamba waliokuwa wanafanya matukio
hayo, ndiyo haohao waliokuwa wanapanga kuvamia ikulu.
Nilihisi kichwa kikiwa kinapata moto, nikamuelekeza kutuma
taarifa hizo makao makuu na muda huohuo na mimi nikawa na-
wasiliana na viongozi wangu na kuwaeleza mambo tuliyokuwa
tunaendelea kuyabaini ili kuweka rekodi sawa.
Haukupita muda mrefu tukawa tayari tumeshaingia Jaribu Mpak-
ani, nikaanza kupunguza mwendo wakati tukianza kuingia kwenye
mji huo mdogo uliochangamka kiasi.
Kilichonipa matumaini makubwa, ni kwamba wakati tukiingia
kwenye mji huo, tulikuta kuna kizuizi cha askari wenye silaha
wakiwa wamezuia magari yote yaliyokuwa yanatokea upande wa
kusini, wakifanya ukaguzi gari moja baada ya jingine.
Tulipokaribia kile kizuizi, nilitoa ishara kwa kutumia taa, askari
wenye silaha waliokuwa wametanda barabarani wakiendelea na
ukaguzi wakafungua upande mmoja wa kizuizi ili tupite, vijana
wangu waliokuwa nyuma nao wakapunguza mwendo na badala ya
kupita, niliwasha taa nyingine kuonesha kwamba tunasimama.
Muda mfupi baadaye msafara wetu ukawa umesimama kando ya
barabara, nikateremka na kutembea kikakamavu kuwaelekea wale
askari.

112 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Chief Snox! Afadhali umeingia mwenyewe mstari wa mbele,”


alisema mmoja kati ya askari wale aliyeonesha kuwa kiongozi eneo
lile, akanipigia saluti, nikaipokea ingawa mimi sikupiga lakini kwa
ishara akawa ameshanielewa.
Tulipeana mikono huku tukitazamana usoni, akarudia tena kuse-
ma maneno yake kwamba eti afadhali nimeingia mwenyewe mstari
wa mbele. Kilichonishangaza ni kwamba mimi sikuwa nikimfa-
hamu lakini kwa jinsi yeye alivyonichangamkia, ilionesha kwamba
ananifahamu vizuri.
Tukasogea pembeni ambapo nilimuuliza kama kuna chochote
walichokibaini, akaniambia kwamba wamepokea maagizo kutoka
juu kuweka kizuizi na kuendesha msako mkali wa kutafuta mtu au
watu wenye asili ya Kisomali, nikatingisha kichwa kukubaliana
naye.
Nilimuuliza wameweka kizuizi hicho kwa muda gani, akanitajia
muda ambapo nilipopiga mahesabu yangu nilibaini kwamba ni
ndani ya muda uleule ambao nilitoa taarifa ya kuzidiwa akili na
mtuhumiwa wetu, nikatafakari kidogo huku nikitazama huku na
kule.
Kwa hesbau zangu, walikuwa wameweka kizuizi muda muafaka
kabisa na hakukuwa na uwezekano kama mtuhumiwa anaweza
kuwa amevuka, niliamini bado atakuwa upande ule wa Jaribu
Mpakani ingawa sikuwa na uhakika wa asilimia 100.
“Kwani ni nini kinachoendelea maana taarifa tulizonazo wanao-
fanya mauaji huku ni wananchi wenzetu, hao Wasomali wanain-
giaje?” alinihoji kimtego, sikutaka kumfungulia ‘code’ zaidi ya

113 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kumwambia kwamba hata mimi nimepewa maelezo kama hayo


kutoka juu.
“Wanatusumbua sana hawa watu, kuna tukio jingine limetokea
Kibiti muda siyo mrefu, mwenyekiti wa serikali ya mtaa ameuawa
kwa kupigwa risasi, wenzetu wengine wameelekea huko,” alisema,
hizo zikawa ni taarifa nyingine mpya kwangu, nikachanganya na
maelezo aliyonipa yule kijana wangu wa Cyber kwamba mtuhu-
miwa wetu alifanya mawasiliano na simu iliyopo Kibiti, kichwa
kikawa kinazidi kupata moto.
“Simamieni kwa makini maelezo mliyopewa, kama kuna cho-
chote unaweza kunipigia kwenye namba yangu binafsi,” nilim-
wambia huku nikiingiza mkono mfukoni na kutoa simu yangu ya
kawaida, achana na vile vifaa vingine vya mawasiliano nilivyoku-
wa navitumia.
Na yeye alitoa simu yake, tukabadilishana namba kisha nikarudi
kwenye gari, kabla sijaingia na kukaa nyuma ya usukani, niliagiza
yule dereva wa lile gari la mihogo aliyekuwa amewekwa ‘mtu kati’
kule nyuma ateremshwe.
“Sikiliza ndugu yangu, tumefika Jaribu Mpakani, ukileta michezo
yoyote ya kitoto msimamo wangu uko palepale, nataka unyooshe
maelezo sasa.”
“Nilishakuahidi kamanda, siwezi kukuangusha!”
“Mlimshusha wapi?”
“Kule stendi, hatujafika bado.”
“Na wewe na wenzako mlikuwa mmetoka kuchukua mzigo wapi
kama ulivyosema?”

114 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Kuna kijiji kule mbele kinaitwa Mahege, ukifika Bungu unaia-


cha barabara ya lami unaingia ndanindani huko!”
“Nataka ukae siti ya mbele na mimi,” nilisema na kumuagiza
yule kijana wa Cyber ambaye alikuwa bize kwelikweli na laptop
yake ahamie siti ya nyuma, kweli akafanya hivyo, yule dereva
akaingizwa siti ya mbele na kukaa pembeni ya siti yangu, na mimi
nikaingia kisha tukaanza kuondoka eneo hilo la kizuizi kwa mwen-
do wa taratibu.
Tulikipita kizuizi ambacho kama nilivyosema kilikuwa mwan-
zomwanzo mwa mji huo mdogo wa Jaribu Mpakani, tukawa tuna-
songa mbele tukiwa kwenyemwendoo wa taratibu, macho yangu
yakiwa hayatulii.
Nilijua kwa kuwa kizuizi cha polisi kimewekwa muda muafaka,
mtuhumiwa wetu hawezi kuwa amekimbia kuelekea upande wa
Dar es Salaam na kwa sababu mtu wa Cyber alishasema kwamba
ilionesha kwamba mtuhumiwa aliwasiliana na simu inayoonesha
kuwa Kibiti, basi lazima bado alikuwa kwenye ukanda uleule.
“Tulisimama pale,” alisema yule dereva akionesha kwa kidole
mahali walipomshusha yule mtu, kando ya barabara katika eneo
lililochangamka zaidi kwenye mji huo.
“Akaelekea wapi?”
“Sijajua lakini kwa kuwa hapa mimi nafahamika na wakati
namshusha kuna watu waliniona, wanaweza kutusaidia,” alisema,
matumaini mapya yakaamka kwenye moyo wangu.
Ilibidi nitoke kwenye barabara kuu na kuingia sehemu palipoku-
wa na uwazi wa kuenea magari yote, nikawaamuru vijana wangu

115 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wote kutulia wakiwa ‘standby’, mimi na yule dereva tukateremka


huku nikijitahidi kuwa kwenye mwonekano ambao hautaamsha
wasiwasi kwa wenyeji.
“Ngoja niwaulize hawa jamaa zangu,” alisema huku akioneshea
mahali kwenye duka la spea za magari na pikipiki, tukaongozana
naye mpaka eneo lile. Wenzake walianza kumchangamkia kwa
kumuita jina la Mzee wa Yanga, naye akawa anajitahidi kujichan-
gamsha, basi wakawa wanataniana kuhusu mambo ya ushabiki wa
mpira huku tukiendelea kusonga mbele mpaka kwenye lile duka.
“Mzee wa Yanga umeshafikisha mzigo mara hii?” alimuuliza
yule muuzaji ambaye alionekana kuwa kijana mdogo, akamuita
pembeni huku na mimi nikiwepo.
“Ebwana nimepata matatizo kidogo, kuna yule jamaa nilimshu-
sha hapa muda ule, unamkumbuka?”
“Yule kama Msomali hivi!”
“Huyohuyo!”
“Amekaa muda mrefu sana pale kwenye drafti, nadhani bado
yupo, hebu twendeni,” alisema yule kijana akiongoza njia kwenye
kijiwe cha bodaboda kilichokuwa kando ya kijiwe cha kahawa
ambapo pia walikuwa wanacheza bao na drafti.
“Eti Mudy! Yule jamaa Msomali aliyekuwa amekaa hapa ameen-
da wapi!”
“Alikuwepo sasa hivi hapa, sasa hivi!” alisema kijana ambaye
kwa kumtazama alionesha kuwa ni dereva bodaboda wakati akim-
jibu yule muuzaji wa duka la spea ambaye ndiye aliyetupeleka pale
kwenye kile kijiwe.

116 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Eti wazee, yule jamaa Msomali aliyekuwa amekaa hapa anaku-


nywa kahawa ameelekea wapi?” aliuliza yule bodaboda, kila mtu
akawa anageuka. Hiyo pekee ilitosha kuonesha kwamba mtuhu-
miwa alikuwepo maeneo yaleyale na pengine alituona ndiyo maana
akaamua kutukimbia.
Akili ilinicheza kwa kasi kubwa nikiwa najaribu kuangalia nini
cha kufanya kwa wakati huo kwa sababu kadiri ambavyo tungeen-
delea kupoteza muda ndivyo mtuhumiwa angezidi kwenda mbali.
“Sikilizeni ndugu zangu!” nilisema baada ya kuwa nimeshapata
wazo la haraka la nini cha kufanya, watu wote wakatulia na kuni-
tazama.
“Najua hamnifahamu, mimi ni askari na huyu jamaa tunayem-
tafuta ni mhalifu mkubwa anayesakwa. Nyote si mnajua jinsi
mauaji yasiyoeleweka yanavyoendelea huku kwenu na ukanda
wote wa Kibiti, Rufiji na Mkuranga?” nilisema, wote wakaitikia
kwa kutingisha vichwa huku wakiwa na shauku kubwa ya kutaka
kusikia nataka kusema nini.
“Yeyote atakayetusaidia kumpata huyo Msomali, natangaza dau
la shilingi milioni moja taslimu! Tusaidiane katika hili, nawaom-
ba!” nilisema, wote wakapigwa na butwaa kwa jinsi nilivyotangaza
dau kubwa kama hilo kirahisi.
“Shilingi milioni moja taslimu, tutawanyikeni mpaka apatikane
kabla hajatoroka, ila asipigwe, akamatwe tu,” nilisema, vijana
takribani kumi na nne waliokuwa pale kijiweni wakatawanyika
kwa kasi ya kimbunga, wengine wakawasha bodaboda zao.
Pale tukabaki watatu tu, mimi, yule dereva na yule mwenyeji

117 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wetu aliyetupokea. Bado yule dereva alikuwa akinitazama kwa


hofu, akawa anaangalia sana kiunoni nilikokuwa nimechomeka
bastola.
Lile tangazo nililotoa lilisambaa kwa kasi, vijana wengine ambao
hawakuwepo nao wakawa wanaambiana, basi ikawa ni mtafutano
kwenye mji huo mdogo. Niliondoka na yule dereva na kwenda
mpaka pale nilipokuwa nimewaacha vijana wangu, kila mmoja
akawa anashangaa nini kimetokea kwa sababu ghafla mji wote
umekuwa bize.
Ilibidi niwaeleze wenzangu, wote wakanipongeza sana kwa
uamuzi huo, nikawapa maelekezo wote kuingia mtaani na silaha
mikononi kuhakikisha mtuhumiwa wetu anapatikana.
“Wewe utabaki hapa kwenye gari, Jerry kazi yako hii!” nilisema
nikimkabidhi yule dereva kwa kijana wangu mmoja, wengine wote
wakajiweka tayari na kusogea pale nilipokuwa nimesimama kwa
ajili ya kuwagawanya.
Niliwaweka kwenye makundi ya wawiliwawili kisha nikawaga-
wa kuhakikisha tunafika kona zote za mji ule na haukupita muda
wote wakatawanyika. Mimi pia sikubaki nyuma, nikaingia mtaani
nikiwa peke yangu huku nikiendelea kuwasiliana na makao makuu.
Kijana wa Cyber yeye alibaki ndani ya gari akiendelea kuumiza
kichwa na laptop yake, msako wa nyumba kwa nyumba ukaende-
lea na haukupita muda, kundi la vijana likachomoza kutoka mtaani
likiwa na mwanaume aliyekuwa amebebwa mzobemzobe.
“Huyu hapa afande!” alisema kiongozi wao wakimkabidhi
kwangu, ninachoshukuru ni kwamba hawakuwa wamempiga kama

118 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

nilivyoagiza.
“Haya tupe chetu tugawane!”
“Ngojeni kwanza tujiridhishe kama ndiyo yeye!” nilisema huku
nikimuinamia yule mwanaume aliyekuwa amekalishwa chini, akio-
nesha kuwa na hofu kubwa isiyo na kifani.
Kwa kuwa binafsi sikuwa namjua mtuhumiwa anafananaje,
ilibidi nimnyanyue pale chini, nikamfunga pingu kisha nikaanza
kumkokota kuelekea kule tulikokuwa tumepaki magari yetu. Lengo
lilikuwa ni kutaka yule dereva athibitishe kama ndiye yule tuli-
yekuwa tunamtafuta.
“Siyo mwenyewe!” alisema yule dereva wa gari la mihogo, wale
vijana wakawa ni kama hawaamini, wakarudia kumtazama vizuri.
Ni kweli naye alikuwa na asili ya Kisomali lakini yeye hakuwa
mrefu kama maelezo ya awali yaliyotolewa na hata kiumri huyu
alionesha kuwa bado kijana mdogo.
“Kweli jamani, niliwaambia lakini!” alisema mmoja kati yao, ha-
rakaharaka wakatawanyika na kuingia tena mitaani, wakamuacha
yule mtuhumiwa pale kwenye mikono yangu, nikaanza kumchun-
guza kwa umakini bila kumsemesha chochote.
Sijui kwa nini akili yangu ilinituma kwamba hata kama yule de-
reva amesema siyo yule mtuhumiwa ambaye tulikuwa tunamsaka
kwa udi na uvumba, bado huyu naye anaweza kuwa ni walewale.
“Unaitwa nani!”
“Naitwa Ishmael afande!”
“Unaishi wapi?”
“Naishi Temeke!”

119 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Huku umefuata nini?”


“Tumekuja kununua korosho afande, mimi siyo mhalifu!”
“Upo na nani?”
“Na wenzangu! Wamepeleka mzigo mjini wameniacha mimi
naendelea kutafuta wakulima wenye mashamba ya korosho watu-
uzie.”
“Una kitambulisho chochote kinachokutambulisha kama mfanya-
biashara!”
“Hapana afande!”
“Kitambulisho chochote?”
“Sina!” alisema lakini wakati akizungumza niligundua kwamba
hata lafudhi yake haikuwa ya Kitanzania japokuwa alikuwa anaon-
gea Kiswahili.
“Wewe na Abdulwaheed Jabal mna uhusiano gani?” nilimuuliza
huku nikiwa nimemkazia macho, nilikuwa nataka kusoma hisia
zake.
“Sim... simfahamu!” alisema kwa kubabaika huku akionesha ku-
patwa na mshtuko usiokuwa wa kawaida. Mpaka hapo nilishapata
picha kwamba kuna jambo alikuwa analificha na pengine hakuwa
mfanyabiashara wa korosho kama alivyosema.
“Unajua kwamba kuongea uongo ni kosa?”
“Najua afande, sijaongea uongo!”
“Simu yako iko wapi?”
“Sina simu!” alisema, ikabidi nimfanyie upekuzi ili kuangalia
kama hakuwa na simu kweli. Nilimpekua kwenye mifuko yake
lakini sikukuta simu, badala yake nikagundua kwamba alikuwa na

120 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

‘flash disc’ ndogo. Flash disc ninayoizungumzia hapa, ni kama zile


zinazotumiwa na wengi kuwekea muziki au ‘movie’, tumezoea
kuziita ‘flashi’.
“Hii ni ya nini?”
“Nimewekea muziki,” alijibu harakaharaka, nikampa yule kijana
wetu wa ‘Cyber’ ajaribu kuangalia kulikuwa na nini mle ndani.
“Hapana, ni hatari bosi! Inaweza kuwa na kitu kibaya kikaharibu
mawasiliano yetu!”
“Wewe iweke tujue ndani kuna nini, unaweza kutumia laptop
yangu angalia hapo kwenye droo ya ‘dashboard’, nilimwambia.
Kweli akafanya hivyo na kutoa laptop yangu ndogo ambayo huwa
natembea nayo kwenye gari.
Kweli alifanya hivyo, akaiwasha ile laptop lakini ajabu alipotaka
kuichomeka, yule kijana wa Kisomali alimkataza huku akiteteme-
ka.
“Usiichomeke tafadhali! Nakuomba sana, afande, asiichomeke!”
“Unamaanisha nini? Si umesema umeweka muziki ndani yake?”
“Hapana!” alisema huku akitetemeka, tukiwa bado tumepigwa
na butwaa, tulisikia kelele za wale vijana zikitokea kwenye mtaa
mmoja uliokuwa unakuja kule barabarani.
“Hebu subiri kwanza,” nilisema huku nikichomoa bastola!
Wale vijana walikuwa wakija mbiombio wakiwa wamemtangu-
liza mwenzao mmoja, wakaja mpaka pale tulipokuwepo.
“Afande, jamaa anasema alimbeba huyo Msomali kwenye boda-
boda amempeleka shamba huko na siyo mara ya kwanza kum-
beba,” alisema mmoja wao, ikabidi nimvute pembeni yule kijana

121 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ambaye ndiye niliyekuwa napewa maelekezo yake.


“Unaitwa nani?”
“Abalkassim ila hapa kijiweni wamezoea kuniita Abal!”
“Unashughulika na nini Abalkassim.”
“Umesema umembeba huyo mtu tunayemtafuta kwenye boda-
boda?”
“Ndiyo, huwa ni mteja wangu wa mara kwa mara!”
“Ulipombeba hapa umempeleka wapi”
“Kuna sehemu huwa nampeleka, kuna kama kambi hivi, sijui ni
kambi au ni shule, sijui vizuri.”
“Unaweza kutupeleka sasa hivi?”
“Hapana, miongoni mwa makubaliano yetu ni kwamba sitakiwi
kumpeleka mtu yeyote kule, huwa ananilipa fedha kubwa na alis-
hanionya kwamba endapo nitajaribu kumpeleka mtu nitaijutia nafsi
yangu,” alisema, nikashusha pumzi ndefu, nikawa natafakari nini
cha kufanya.
“Sikiliza, unajua mimi ni nani? Unajua huyu anayetafutwa ni
nani?”
“Hapana!” alisema, ikabidi nianze kumshawishi kwa kujitambuli-
sha upya kwake, nikamueleza kwa yule mtu anayetafutwa ana
hatari kiasi kwa taifa zima na mambo mengine kama hayo. Niliona
akitingisha kichwa kuonesha kuelewa kile nilichokuwa namwam-
bia na mwisho akakubali.
Baada ya kumaliza kuzungumza naye, tulirudi pale kwenye
magari ambapo wale vijana wengine walikuwa wakisubiri kwa
shauku kubwa kutaka kusikia ni nini ambacho kilikuwa kimefiki-

122 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wa.
Lakini ghafla, yule kijana alishtuka akiwa ni kama haamini
alichokuwa anakiona mbele yake. Kilichomshtua ilikuwa ni baada
ya kumuona yule kijana mwingine wa Kisomali ambaye tulikuwa
tumesaidiwa kumpata na wale vijana wa pale.
“Vipi, mbona umeshtuka?”
“Huyu hapa ni ndugu yake, yeye anakujua vizuri zaidi kule ku-
liko hata mimi,” alisema kwa msisitizo akimnyooshea kidole yule
kijana ambaye alikuwa amedhibitiwa vizuri na vijana wangu.
“Una uhakika?”
“Nina uhakika afande, muulize mwenyewe kama nadanganya!”
alisema, nikashusha pumzi ndefu, nikaikamata vizuri bastola am-
bayo kwa muda wote huo ilikuwa mkononi.
“Kwa hiyo kumbe muda wote unaniektia hapa si ndiyo?” nilise-
ma huku nikimkamata yule kijana kwa nguvu na kumsukuma
mpaka kwenye ‘bodi’ la gari, nikamkaba kwa nguvu huku mkono
mmoja nikimgusisha bastola.
“Utasema ukweli, iwe ni kwa hiyari yako au kwa lazima, hau-
wezi kutupotezea muda hapa,” nilisema kwa jazba huku nikizidi
kumkandamiza kwa nguvu nikiwa nimemkaba.

123 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

6

KWENYE flash kuna nini?” nilisema huku nikiwa bado
nimemkaba kwa nguvu, akaonesha ishara kwamba
nimuachie atasema mwenyewe.
“Kuna kazi nilitumwa kuja kuprint.”
“Kazi gani?”
“Sijui ni kazi gani, mimi nimetumwa tu na nimeambiwa hatakiwi
mtu yeyote kujua zaidi ya mtu wa steshenari tu.”
“Umetumwa na nani?”
“Kiongozi wetu!”
“Kiongozi wenu? Kiongozi wenu wewe na nani?” nilizidi kum-
bana lakini alionesha kutokuwa na majibu, nikaona tusizidi kupo-
teza muda, ilitakiwa tuondoke haraka kuelekea huko wanakosema

124 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kuna kambi yao.


Ilibidi tugawane pale, gari moja lilitakiwa kubaki palepale kwe-
nye ule mji mdogo, kisha yale magari mengine ndiyo ambayo tung-
eyatumia kwa safari ya kuelekea huko kijijini.
“Kule magari hayafiki, kuna sehemu yanaishia na baada ya hapo
itabidi tutumie bodaboda.”
“Chukua wenzako watano unaowaamini, kila mmoja na pikipiki
yake,” nilisema wakati nikizungumza na yule dereva bodaboda ali-
yedai kumbeba yule mtuhumiwa na kumpeleka kule kijijini. Ilibidi
yule dereva wa gari la mihogo aliyetufikisha mpaka kwenye mji
huo mdogo wa Jaribu Mpakani.
Ndnai ya muda mfupi tu tayari pikipiki zaidi ya kumi zilikuwa
pale mbele yetu, ilibidi kuwapunguza wengine kuwaahidi kwamba
kama kazi ikikamilika kila mmoja aliyeshiriki atapewa mgao wake,
nadhani lile dau bado lilikuwa linawachanganya vichwa vyao.
Haukupita muda safari ikaanza, wale bodaboda ndiyo wakiwa
mbele wakiongoza njia, ndani ya gari langu nilikuwa na yule
Msomali mwingine akiwa kwenye pingu, katikati ya vijana wangu,
pale pembeni yangu akiwa amekaa yule kijana wetu wa Cyber
ambaye nilimpa kazi ya kuwa anatuma ‘live feeds’ za kila kili-
chokuwa kinaendelea makao makuu iwe rahisi viongozi kuangalia
kila kitu moja kwa moja.
Lakini pia nilimpa kazi ya kuifanyia kazi ile ‘flash’ kutaka kujua
kulikuwa na nini ndani yake, safari ikaanza.
Mpaka hapo kila mtu alikuwa na uhakika kwamba kazi kubwa
tuliyoifanya inakwenda kuzaa matunda na hata kama hatutampata

125 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Abdulwaheed, kitendo cha kumpata mshirika wake wa karibu na


kujua mahali walikokuwa wanafanyia shughuli zao, tyari ulikuwa
ni ushindi kwetu.
Tulielekea upande wa Kibiti kutokea pale Jaribu Mpakani, na
baada ya kilometa kadhaa, wale bodaboda waliokuwa mbele, nao
wakiongozwa na Abalkassim, waliwasha taa kuonesha kwamba
wanaiacha barabara ya lami na kuingia upande wa kushoto ukiwa
unaelekea Kibiti.
Nilipunguza mwendo kwa sababu gari langu ndiyo lililokuwa
mbele na kufuatiwa na vijana wangu, tukazidi kupunguza mwendo
kisha tukatoka barabara kuu na kuingia kwenye ile njia waliyotan-
gulia wale bodaboda.
Haikuwa na hadhi ya kuitwa barabara, kilikuwa ni kinjia chem-
bamba ambacho hakina alama yoyote inayoweza kukuonesha
kwamba huko unakokwenda kunaweza kuwa na kitu chochote cha
maana. Ama kwa hakika usidharau kitu chochote unachokiona.
Safari iliendelea na kutokana na njia yenyewe ilivyo, tulikuwa
tukienda kwa kasi ndogo ambayo hakika ilikuwa inanikasirisha
sana, nilishazoea kukimbizana na muda. Safari iliendelea tukizidi
kuingia ndanindani kabisa.
Mwanzo tulikuwa tukipita kwenye mashamba ya mihogo na
korosho lakini baadaye tuliyapita mashamba yote na sasa tukawa
tunapita kwenye mapori. Safari yetu ilienda kuishia mahali pali-
pokuwa na mto mdogo ambapo wale bodaboda walisimama na
kutupa ishara kwamba tupaki magari kwa sababu njia inayopitika
hapo ndiyo mwisho wake.

126 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Ilibidi tufanye ujanja wa kuyachomeka magari vichakani, ki-


sha tukateremka tukiwa tumekamilika kama tunakwenda vitani.
Niliwaagiza vijana wangu wote kuvaa ‘bullet proof vest’, vizibao
maalum vinavyoweza kuzuia risasi kupenya.
Ilibidi tuondoke watano tu kwa maana kila bodaboda moja in-
ambeba dereva na mtu wetu mmoja, na mimi ya kwangu niliamua
kupanda mshikaki kwenye ile ya Abalkassim pamoja na yule kijana
wa Kisomali na sisi ndiyo tuliotakiwa kutangulia mbele.
Nilichagua nani na nani wa kwenda, wengine wakabaki pale
kwenye magari na bila kupoteza muda safari ikaendelea.
Njia ilikuwa mbovu kwelikweli, kuna wakati bodaboda zilikuwa
zikitaka kutuangusha kutokana na ubovu wa njia, tukaendelea
kuchanja mbuga na hatimaye, tukatokezea mahali ambapo palion-
esha kuwa na shughuli za kibinadamu kwa mbali.
Madereva wote wa bodaboda wakasimama wakiongozwa na
yule aliyekuwa amenibeba mimi pamoja na yule kijana mdogo wa
Kisomali ambaye tulikuwa tumepanda naye ‘mshikaki’ kwenye
bodaboda moja.
“Bosi, mahali penyewe ni pale, mimi na wenzangu hatuwezi
kufika kwa sababu za kiusalama, kama nilivyokwambia tangu
mwanzo, najua hapa tumejiweka kwenye hatari kubwa lakini
Mungu atatusimamia,” alisema yule dereva bodaboda, Abalkassim,
nikamuondoa wasiwasi.
Tuliteremka wote kwenye bodaboda, nikamkamata vizuri yule
kijana mdogo wa Kisomali ambaye muda wote alikuwa na pingu
mkononi na kuanza kumkokota kwenda mbele, nikimtanguliza

127 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

yeye mbele, bastola ikiwa mkononi.


Wale vijana wangu nao walikuwa wanakuja nyuma yangu kwa
‘formation’ ambayo kila mmoja alikuwa anaijua. Hapa kuna jambo
ambalo pengine unaweza kuwa umewahi kuliona au kulisikia lakini
hujawahi kulielewa.
Mnapokuwa kwenye ‘misheni’ za kijeshi, hasa katika mazingira
ambayo mna wasiwasi kwamba maadui wanaweza kuwa na silaha
au kunaweza kuwa na vitu vilivyotegwa ardhini kama mabomu, ni
kwamba wote mnatakiwa kusonga mbele kwa mstari ulionyooka.
Maana yake ni kwamba mwenzako anapoweka mguu, akitoa basi
na wewe unaweka hapohapo, yule anayekuwa mbele ndiyo anaku-
wa kama kinga na kwa kawaida lazima awe ni mwenye uzoefu
kuliko wengine.
“Ni hatari, afande ni hatari sana huku tunakokwenda!” alisema
yule kijana wa Kisomali akitetemeka.
“Kuna nini?”
“Hii kambi yetu inalindwa kwa silaha, wataniua!” alisema, moyo
ukanilipuka ‘paah’! Siyo kwamba moyo ulinilipuka kwa sababu
ya hofu, la hasha! Ni kwa sababu sasa niligundua kwamba kumbe
watu tunaoenda kukabiliana nao, siyo wa kawaida.
Muda huohuo, nilitoa ishara kwa wenzangu waliokuwa nyuma
kusimama na kuchuchumaa kwanza, na kweli wote wakafanya
kama nilivyowapa ishara. Ilikuwa ni lazima kwanza kupata msaada
wa kujua ni nini kilichokuwa mbele yetu kabla ya kuingia kichwa-
kichwa.
Harakaharaka niliwasiliana na yule kijana wetu wa Cyber ali-

128 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

yekuwa amebaki pale Jaribu Mpakani, nikamwambia aingie kwe-


nye picha za ‘satellite’ haraka kwa kutumia mitambo yake aliyoku-
wa nayo pale kisha anitumie taarifa haraka iwezekanavyo.
Sikuishia hapo, niliwasiliana pia na makao makuu, kwa kutumia
‘codes’ na kutoa taarifa za kilichokuwa kinaendelea.
Haukupita muda mrefu, nikapokea majibu kwa kutumia simu
yangu kutoka kwa kijana wetu wa Cyber ambapo alinitumia picha
za ‘satellite’, nikafungua harakaharaka na kuangalia kwa makini.
Japokuwa kwa mbali ilikuwa inaonekana ni kama nyumba moja
tu ambayo bati lake linang’aa, ukweli ni kwamba kulikuwa na
majengo mengi yaliyojengwa kama kambi katika eneo hilo na
ilionesha kwamba kulikuwa na idadi kubwa ya watu tofauti kabisa
na tulivyokuwa tumefikiria.
Nikiwa bado nimepigwa na bumbuwazi, nilipokea simu kutoka
kwa mkurugenzi wetu kupitia vifaa vya mawasiliano kutoka makao
makuu ambaye aliniambia kitu kilichozidi kunichanganya kichwa.
“Nguvu mliyonayo ni ndogo kuliko nguvu ya mnaoenda kupam-
bana nao, vijana wa IT hapa wanatuthibitishia kwamba hata mtuhu-
miwa tunayemtafuta yupo ndani ya eneo hilo, abort the mission!”
alisema na kumalizia kwa maneno ya Kiingereza akimaanisha
tunatakiwa kusitisha misheni yetu.
Nilishusha pumzi ndefu na muda huohuo nikatoa ishara kwa
wenzangu, ikabidi turudi nyuma haraka mpaka kwenye eneo
salama kusubiri maelekezo kutoka makao makuu.
Niliendelea kupokea maelekezo na nikaambiwa kwamba kwa
kuwa kikosi maalum cha kupambana na ugaidi kilikuwa njiani,

129 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

tunatakiwa kuendelea kulisoma eneo hilo kimyakimya bila kusa-


babisha taharuki ya aina yoyote.
Tulirudi mpaka pale tulipokuwa tumewaacha wale vijana wa
bodaboda ambao walikuwa wametulia, wakifuatilia kila kilichoku-
wa kinaendelea.
Niliwapa maelekezo ya kuzificha bodaboda zao vichakani,
mahali ambapo hakuna mtu yeyote anayeweza kuziona kisha ni-
kawaelekeza sehemu ya kukaa na kutulia, wakati tukisubiri msaada
wa wenzetu.
Ilibidi pia niwaelekeze vijana wangu kitu kilichokuwa kinat-
akiwa kufanyika kwa wakati huo na kabla ya kufanya hivyo, ilibidi
kwanza nianze kumhoji yule kijana wa Kisomali undani wa ile
kambi iliyokuwa mbele yetu.
Kwa hali aliyokuwa nayo, hofu ikiwa imetanda kwenye moyo
wake, alikubali kutoa ushirikiano.
“Ni kambi!”
“Kambi ya nini!”
“Ya mafunzo ya dini!”
“Kama ni mafunzo ya dini, kwa nini kunalindwa na silaha?”
“Ni utaratibu ambao mimi niliukuta, sijui!”
“Imeanzishwa lini hii kambi?”
“Siyo muda mrefu, mimi hapa nina mwezi mmoja na nilipofika
ilikuwa na kama miezi miwili nyuma.”
“Wanaolinda na silaha ni akina nani?”
“Sisi sote tunajilinda!”
“Mnafundishwa kutumia silaha pia?”

130 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Ndiyo!”
“Silaha mnapata wapi?”
“Sijui lakini huwa zinaletwa!”
“Kuna njia nyingine ya kuingia au kutoka zaidi ya hii?”
“Ndiyo, kuna njia ya upande wa pili, hiyo ndiyo hutumika sana
nyakati za mchana, hii hutumika nyakati za usiku!”
“Sasa nataka uniongoze twende mpaka huo upande wa pili!”
“Wataniua! Wakishajua nipo na nyinyi wataniua!”
“Tutakulinda!”
“Hamna uwezo wa kunilinda, wakiamua jambo lao hakuna
anayeweza kuwazuia!”
“Ilikuwaje ukafika huku na kujiunga nao?”
“Ni habari ndefu ambayo siwezi kuielezea hapa, walikuja kutu-
chukua Mombasa mimi na wenzangu.”
“Wenzako akina nani?”
“Vijana wenzangu, tuliletwa kama kumi!”
“Jumla kuna watu wangapi?”
“Ni wengi, wanafika arobaini!”
“Kiongozi wenu ni nani?”
“Kwa hapa ni Abdulwaheed lakini kuna viongozi wengine wa juu
ambao huwa wanakuja na kuondoka!”
“Si ulisema humfahamu wewe?”
“Nisamehe! Niliogopa kueleza ukweli.”
“Kwa hiyo mwanzo uliogopa kusema ukweli lakini sasa hivi
huogopi tena si ndiyo?”
“Siyo hivyo! Sasa hivi najua kama nisipowaeleza ukweli sote

131 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

hapa tunaweza kuuawa nikiwemo mimi pia!” alisema yule kijana


wa Kisomali. Miongoni mwa vitu ambavyo nilijifunza nikiwa nchi-
ni Israel, ni kwamba hutakiwi kumwamini mtuhumiwa, hususan
wa kesi za kigaidi kirahisi namna hiyo.
Sikutaka kuamini kama yule kijana wa Kisomali yote aliyokuwa
anayasema yalikuwa na ukweli, kulikuwa na uwezekano kwamba
baadhi ya aliyokuwa anayasema yalikuwa ni ya kweli lakini hicho
hakikutakiwa kuwa kigezo cha mimi kumuamini.
Wakati pekee ambao unaweza kumuamini mtuhumiwa wa kesi
nzito kama ugaidi, ni pale anapokuwa amekufa pekee, kinyume na
hapo ilikuwa ni makosa makubwa kumuamini.
Japokuwa mwenyewe alikuwa hataki kwenda kuonesha mwe-
nyewe upande wa pili wa ile ngome yao kwa kisingizio kwamba
anaogopa kuuawa na wenzake, nililazimika kutumia mabavu na
kumlazimisha atupeleke kwa nguvu.
“Sasa utafuata ninachokisema mimi, utakwenda kutuonesha,
umenielewa?” nilisema huku nikimkamata kwa nguvu mikono
yake iliyokuwa imefungwa pingu na kumnyanyua. Lengo langu
nilitaka avalishwe ‘bullet proof vest’ kwa maana ya lile vazi
maalum linalovaliwa kifuani kama kizibao lenye uwezo wa kuzuia
risasi kupenya.
Hata hivyo, pale nilipomkamata kwa nguvu mikono yake,
niligundua kitu kisicho cha kawaida. Mkono wake wa kushoto
ulionesha kuwa na kitu kwa ndani jirani kabisa na mahali kiganja
kinapoanzia.
“Nini hiki!” nilisema huku nikipaminyaminya pale kwenye

132 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

mkono wake, akawa ananitazama kwa hofu. Akili ya haraka ilini-


tuma kuamini kwamba lazima na yeye atakuwa na ‘chip’ maalum
ya mawasiliano kama ile tuliyomkuta nayo yule mzee wa Kisomali
kule ofisini kwetu baada ya kumkamata.
Hivi ni vifaa maalum ambavyo kitaalamu huitwa RFID Chip au
wengine huviita Human Implanted RFID Chip, RFID kikiwa ni
kifupisho cha maneno ya Kiingereza ya ‘Radio-Frequency Identifi-
cation’.
Niliahidi kuja kuielezea kwa kina teknolojia hii hapo baadaye
lakini kwa kifupi ni kwamba hivi ni vifaa fulani ambavyo ukubwa
wake unaweza kuwa kama punje ya mchele ingawa vingine huwa
vikubwa kidogo, ambavyo hupandikizwa chini ya ngozi ya binad-
amu kwa lengo la mawasiliano na utambuzi.
Mtu akishaunganishwa na kifaa hiki kwa kupitia upasuaji mdogo
unaofanywa kwenye ngozi ya mwili, taarifa zake huunganishwa
kwenye kompyuta ambayo huanza kusoma taarifa zote muhimu
kuhusu mtu aliyepandikizwa kifaa hiki.
Miongoni mwa taarifa zinazoweza kuonekana kwa urahisi, ni
kama mtu yupo hai au amekufa lakini kubwa zaidi kusoma taarifa
zote za mizunguko na ‘location’ alipo mhusika.
Nilijiona kuwa mzembe sana kwa kutohisi jambo hilo tangu ki-
jana yule anakamatwa kule Jaribu Mpakani kwa sababu tafsiri yake
ni kwamba hata hapo vichakani tulipokuwa tunaamini tumejificha,
tayari mifumo ya wale magaidi ilikuwa inasoma ‘location’ alipo
yule mtuhumiwa kwa hivyo wangeweza kufuatilia kwa karibu na
kutaka kujua ni nini kinachoendelea, jambo ambalo lingekuwa la

133 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

hatari kubwa mno kwetu.


“Ni nini hiki!” nilisema, safari hii kwa ukali, yule kijana akawa
anatetemeka ambapo nilipousogeza mkono wake karibu na macho
yangu, niliweza kubaini alama ndogo za kushonwa, jambo ambalo
sasa lilinipa uhakika kwamba ni kweli alikuwa amewekewa kifaa
hicho.
Nilimgeuza na kumbinua kama mcheza miereka, nikamkandam-
iza ardhini na kumuwekea goti mgongoni hiki nikimtisha kwamba
asiposema ukweli namfyatulia risasi.
“Ni chip ya mawasiliano!” alisema huku akitetemeka. Japokuwa
wenzangu hakuna aliyekuwa anaelewa kwa nini nimebadilika
ghafla, mimi ndiyo niliyekuwa najua ni kwa namna gani tumeji-
weka kwenye hatari kubwa.
Nilitoa ishara kwa wenzangu ambao wote walikuwa wameacha
kila walichokuwa wakikifanya, nikiwataka tuondoke eneo hilo
haraka iwezekanavyo. Kwa kasi ya kimbunga nilimnyanyua yule
kijana pale chini, nikachomoa kisu kidogo nilichokuwa nacho
kwenye ‘holder’ ya funguo, nikamchana pale kwenye mkono na
kuingiza vidole viwili.
Nikafanikiwa kukikamata kifaa kile na kukivuta kwa nguvu, ki-
kachomoka kisha nikakirusha vichakani. Ajabu ni kwamba japoku-
wa kitendo kile kilisababisha maumivu makubwa kwa yule kijana,
hakupiga kelele wala kulia zaidi ya kuonekana akigugumia ndani
kwa ndani, damu nyingi zikawa zinamtoka.
Hicho kilikuwa kipimo kingine cha kuonesha kwamba kumbe
tulikuwa tumeingia sehemu mbaya kwelikweli kwa sababu vijana

134 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

waliofuzu kwenye mafunzo ya ugaidi, huwa na uwezo mkubwa


sana wa kuvumilia maumivu, hata yawe makali kiasi gani.
Nilitoa kitambaa na kufunga kwa nguvu pale kwenye mkono
wake ili damu zisiendelee kutoka, tulikuwa tukimhitaji kijana huyu
akiwa hai kwa hiyo ilikuwa ni lazima kumlinda.
Vijana wangu tayari walikuwa wameshakaa mkao wa kuondoka
kwa kasi, basi nikamuinua yule mtuhumiwa na kuanza kukimbia
naye, vijana wangu nao wote wakafanya kama mimi, tukarudi
mpaka pale tulipowaacha wale bodaboda waliotupeleka.
Harakaharaka nikawapa ishara,w akawasha pikipiki zao, tukapan-
da huku mimi nikiwa na mtuhumiwa wangu, tukaanza kuondoka
kwa kasi kubwa kurudi kule tulikokuwa tumetokea, safari hii mimi
nikiwa nyuma kabisa kwa sababu za kiusalama.
Naweza kusema ilikuwa ni kama Mungu tu kwa sababu muda
mfupi tu tangu tulipotoka mbio eneo lile, milio ya risasi mfululizo
ilianza kusikika kule nyuma, vijana wangu wakawa wanataka kusi-
mama ili wapambane lakini nikawazuia na kuwahimiza bodaboda
wazidi kukimbiza pikipiki zao.
Nitaeleza kwa nini nilichukua uamuzi huo na kwa nini nili-
wakataza wasijibu mapigo. Saikolojia nyepesi niliyoibaini baada
ya kugundua kwamba kijana yule alikuwa na ‘chip’ ya mawasilia-
no mwilini, ni kwamba alikuwa anatuchelewesha kwa makusudi
eneo lile.
Alikuwa akijifanya amekubali kutoa ushirikiano na kueleza kila
kitu, lengo likiwa ni kuvuta muda ili wenzake waje kwa sababu
alikuwa anajua kwamba lazima wenzake watamuona na kuja kum-

135 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

saidia hasa baada ya kuona amekaa eneo lile kwa muda mrefu.
Ndiyo maana baada tu ya kugundua kwamba alikuwa na kifaa
hicho, hatua ya kwanza ilikuwa ni kukichomoa na kukitupa lakini
kwa kuwa tayari tulishapoteza muda eneo lile, nilikuwa na uhakika
kwamba lazima wenzake watakuwa wameshatukaribia.
Hicho ndicho kilichotokea kwa sababu milio ya pikipiki iliposiki-
ka tu, wale wenzake ambao ilionesha walikuwa wanatulia ‘timing’
ya kutuzunguka, walichomoka kutoka mafichoni na kuanza kufyat-
ua risasi lakini walikuwa tayari wamechelewa.
Kingine kilichofanya nizuie vijana wangu wasijibu mapigo ni
milio ya silaha zilizokuwa zinatumika. Kwa uzoefu niliokuwa nao,
kabla sijaenda masomoni na baada ya kurudi, nilikuwa na uwezo
wa kutambua aina ya silaha kwa kusikia mlio wake tu hata kama ni
kwa mbali.
Ilionesha wazi kabisa wale wenzake walikuwa wamejihami
kwa bunduki za kivita na kanuni ni kwamba unapopambana na
mtu anayetumia silaha ya kivita, tena kwa kukushtukiza, hutakiwi
kuzubaa eneo hilo kwani sekunde moja tu inaweza kubadilisha kila
kitu.
Uzuri ni kwamba wale bodaboda wote walikuwa ‘sharp’ kwelik-
weli, wakawa wanavuta mafuta kwa nguvu na kusababisha boda-
boda ziwe zinakimbia kwa kasi kubwa kwelikweli, wakati mwing-
ine tukinusurika kugonga miti au kuanguka kutokana na ubovu wa
barabara.
Dakika chache tu baadaye tayari tulikuwa tumefika pale kwenye
kile kijito ambacho tuliyaacha magari yetu. Tukashuka kwenye

136 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

bodaboda kikomandoo na kukimbilia kwenye magari yetu huku ni-


kiwataka wale bodaboda kuendelea kukimbia kwa kadiri ya uwezo
wao mpaka watakapofika kwenye barabara ya lami.
Tukaingia kwenye magari yetu na kwa kusaidiana na wale wen-
zetu waliokuwa wamebaki pale, tuliondoka kwa kasi ya kimbunga.
Unaweza kushangaa inakuwaje mtu aliyebobea kwenye medani
kama mimi naweza kuchukua uamuzi wa kukimbia badala ya ku-
pambana. Ilikuwa ni lazima kufanya hivyo.
Tuliendelea kukimbia na magari yetu kwa kasi kubwa, tukawa tu-
meshatoka eneo lenye misitu mingi na kuingia kwenye eneo lenye
mashamba ya mihogo, mikorosho na mazao mengine.
Safari iliendelea huku nikiendelea kuwasiliana kwa karibu na
vikosi vingine pamoja na kule ofisini ambako kila mtu alikuwa
kwenye hali ya taharuki kwa sababu tulichokuwa tumekidhani
ilikuwa tofauti kabisa!
Watu tuliokuwa tunapambana nao hawakuwa watu wa mchezom-
chezo na endapo tusingekuwa makini, kulikuwa na hatari kubwa ya
kutusababishia madhara makubwa sana. Yaani ndani ya muda mfu-
pi tu kila kitu kilikuwa kimebadilika, mwindaji akawa anawindwa!
Baada ya muda tayari tulishakuwa tumewasili barabarani, pale
tulipoiacha barabara ya kuelekea Kusini. Kwa hali ilivyokuwa,
ilikuwa ni hatari kuendelea kukaa na wale madereva bodaboda kwa
sababu hawakuwa na mafunzo yoyote kwa hiyo endapo tunge-
shambuliwa ghafla, wangeweza kupata madhara makubwa ambayo
yanaweza kuepukika.
“Sikilizeni, huku ni haari kwenu kuendelea kukaa! Tulikubaliana

137 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

dau kwa atakayefanikisha kupatikana kwa yule mtuhumiwa wetu si


ndiyo?”
“Ndiyo boss!”
“Mtuhumiwa hajapatikana lakini hautapita muda mrefu atapati-
kana tu, juhudi zenu zimetufanya tukagundue jambo kubwa na la
hatari sana ambalo lingeweza kuhatarisha usalama wa taifa letu.
“Kwa hiyo kama shukrani yangu na wenzangu kwenu, mtape-
wa kiwango kile nilichowaahidi lakini itabidi mgawane wote
mlioshiriki lakini mtapewa tukishamaliza kazi, nendeni mkajipange
vizuri, Abalkassim ndiyo utakuwa kiongozi, andika majina ya
wenzako wote na mkubaliane ili kusijetokea malalamiko yoyote.
Tumeelewana?”
“Tumeelewana afande!” walisema wote, nikawatajia namba yan-
gu ya simu ya mkononi na kuwataka kutoa taarifa kwangu endapo
kutatokea jambo lolote ambalo litakuwa na kiashiria cha uhalifu,”
wakafurahi na kuwasha bodaboda zao, wakaondoka kwa pamoja na
kutuacha tukiwa pale barabarani, tukiendelea kuumiza vichwa na
wenzangu.
Tukiwa tunaendelea kujadiliana na kupongezana jinsi tulivyochu-
kua uamuzi wa haraka wa kukimbia eneo la tukio, magari ya kikosi
cha kupambana na ugaidi (Anti Terrorism Squadron) au ATS kama
kilivyokuwa kikiitwa kwa kifupi, yalianza kuwasili kwa kasi ya
kimbunga.
Kikosi kilikuwa kipana kwelikweli, kikiwa na karibu magari
kumi, kila gari likiwa na takribani maafisa saba waliokuwa wame-
kamilika kwa kila kitu, kuanzia mavazi ya kuzuia risasi na silaha

138 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

nzito.
Kama nilivyowahi kueleza kuwa kikosi hiki ni miongoni mwa
vikosi ambavyo huwa havionekani sana mitaani na siku waki-
onekana, basi ujue kuna jambo zito! Tayari nilishapewa mamlaka
ya kukiongoza kikosi hicho tangu tukiwa Dar es Salaam kwa
sababu kilikuwa kinatoka ndani ya kitengo ingawa pia kilikuwa na
maafisa wengine kutoka jesi la polisi hususan kitengo cha FFU.
Muda mfupi baadaye kikosi chote kilikuwa kimeshawasili na
magari kupaki pembeni ya barabara, mengine upande wa kushoto
na mengine upande wa kulia. Kwa kuwa walishapewa maelekezo
ya kupokea maagizo kutoka kwangu, walipofika tu, viongozi
wanne waliokuwa na vyeo vya juu kuliko wenzao, walikuja na
kunipigia saluti.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, kwa msaada wa vijana wa
Cyber na teknolojia ya mawasiliano, tulianza kuzipitia picha za
satellite ili kuisoma vizuri ile kambi walikokuwa wamejichimbia
wale wahalifu, wakiongoza na Abdulwaheed.
Niliwaelekeza kila kitu tulichokutana nacho, nikawaonesha yule
kijana wa Kisomali ambaye bado alikuwa kwenye mikono yetu
na kuwaeleza mambo mengi ambayo hawakuwa wakiyajua kisha
baada ya hapo, nikaanza kuwapa mipango ya nilichokuwa nimeki-
panga.
Kwa kuwa ilishaonesha kwamba wale wahalifu walikuwa wame-
jipanga kisawasawa na hatutakiwi kuingia kichwakichwa, nil-
ishauri kwamba tunatakiwa kuendelea kuisoma ile kambi mpaka
usiku kisa ndiyo tutaivamia.

139 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Hata ivyo, wazo langu lilipata upinzani mkali kwa kuonekana


eti tunapoendelea kusubiri tutakuwa tunapoteza muda na huenda
wakapeana taarifa na kutoroka.
“Hawa siyo majambazi kwamba mnavamia, mnapambana,
mnawazidi nguvu kisha mnawakamata! Mambo hayapo ivyo ni sid-
hani kama kuna yeyote kati yenu aliyewahi kushiriki kwenye vita
ya ugaidi,” nilisema baada ya wazo langu kupata upinzani mkali.
Niliwafafanulia kwa nini ilikuwa ni lazima tutumie intelijensia
ya hali ya juu kupambana na magaidi wale badala ya nguvu kwani
ilishaonesha kuanzia mwanzo kwamba wamejipanga kisawasawa
na hawawezi kutolewa kwenye mpango wao kwa mashambulizi
mepesi.
“Inatakiwa tukipiga mara moja tunamaliza kazi, ni hatari sana
kizembezembe, nani anataka kufa kati yenu? Tunatakiwa kuwaka-
mata wote wakiwa hai na sisi wote tukiwa hai,” nilisema na anga-
lau kila mmoja akaanza kunielewa sasa.
Kilichofuatia baada ya hapo, ilikuwa ni kila mmoja kunisikiliza
kwa makini nilichokuwa nakisema. Nilitaka kwanza tuanze na kitu
kinachoitwa recconaisance, ni neno gumu lakini maana yake huwa
ni nyepesi sana katika medani za kivita.
Hii ni mbinu ya kwenda kumpeleleza adui kwa karibu na kupima
nguvu aliyonayo, ambao taarifa zinazopatikana ndiyo zinazoweza
kuwapa picha kwamba kama mnamvamia adui mnatumia nguvu ya
kiasi gani ili kumzidi.

140 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

7
N
ILITAKA recconasance ifanyike kwa njia zote mbele,
kwa kutumia teknolojia kama vile kwa kutazama picha
za satellite na kunasa mazungumzo ya simu ya eneo
husika, lakini pia ilikuwa inatakiwa watu waende eneo
la tukio na kufanya ujasusi.
Nilipowaeleza kuhusu suala hilo, niliona wote wakitazamana, hapa
ndipo linapokuja tatzo.
Nimeeleza na naendelea kueleza kwamba nchi nyingi za ulimwengu
wa tatu zinapata sana shida kupambana na ugaidi kwa sababu hazina
watu wenye uzoefu wa kupambana na magaidi na kwa bahati mbaya
sana wengi huwa wanashindwa kuwatofautisha magaidi na majambazi

141 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

na matokeo yake wanatumia mbinu za kuwadhibiti majambazi


kupambana na magaidi, jambo ambalo ni hatari kwelikweli.
“Nitaongoza mwenyewe hiyo oparesheni, lazima tufanye kitu
kinachoeleweka, maisha ya Watanzania wote, maisha ya viongozi
wetu na maisha yetu sisi yenyewe, yote yanatutegemea sisi, hapa ni
kufa na kupona!”
Baada ya makubaliano hayo, kilichofuatia baada ya hapo, ilikuwa
ni utekelezaji ambapo tulikubaliana kwamba ili tusije tukaleta hali
ya wasiwasi kwa wahusika, magari yote yanatakiwa kuondolewa
pale kando ya barabara, mengine yapelekwe Jaribu Mpakani, men-
gine Kibiti na machache yafichwe vichakani.
Nikiwa naendelea kutoa maelekezo hayo, kuna mwanaume
alipita akiwa anaendesha baiskeli kwa mwendo wa taratibu, huku
akiwa anazungumza na simu. Sijui kwa nini nilipomuona tu,
japokuwa alikuwa na mwonekano wa kawaida kama mwanakijiji
wa kawaida, akili yangu ilihisi kwamba siyo mtu wa kawaida.
Nilimkazia macho, akawa anaendelea kupiga peda taratibu huku
akiendelea kuongea na simu.
“Haloo, hebu simama tafadhali!”
Nilisema kwa sauti ya mamlaka na kumfuata yule mwanaume
ambaye alishakuwa ametupita kwa mita kadhaa, ajabu eti nilipom-
taka asimame, aliongeza mwendo wa basikeli yake na kuiweka
simu mfukoni, akawa anajaribu kunikimbia.
Alishachelewa kwani na mimi nilishakuwa nimejiweka tayari,
nikatimua mbio kwa kasi na muda mfupi baadaye nilishamfikia,
nikaikamata ile baiskeli yake kwenye kiti cha nyuma na kuivuta

142 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kwa nguvu ili isimame na muda huohuo nikawa nimeshamkwida


sehemu ya nyuma ya suruali yake.
Nikamnyakua kama mwewe anavyonyakua kifaranga cha kuku
na kumshusha mpaka chini, nikamlaza chini na kumkandamiza, ha-
rakaharaka nikaingiza mikono mfukoni mwake na kutoa ile simu.
Nikashangaa kugundua kwamba kumbe hakuwa anazungumza na
simu bali alikuwa akiturekodi video.
Nilimtazama kwa macho makali nikiwa ni kama siamini nili-
chokuwa nakiona. Nasema nilikuwa siamini kwa sababu kama
nilivyosema, mtu mwenyewe alikuwa na mwonekano wa kawaida
kabisa kama wanavijiji vingine, sasa iweje awe anashirikiana na
watu hatari kiasi kile?
Picha niliyoipata kichwani mwangu ilikuwa inatisha sana, inapo-
tokea unapambana na maadui ambao wanashirikiana na wananchi
wa kawaida, hakika ni vigumu sana kushinda vita ya aina hiyo
mpaka nguvu kubwa kisawasawa zitumike.
Ipo mifano ya makundi ambayo mpaka leo yanaendelea kuz-
isumbua nchi za wenzetu, mfano mwepesi ukiwa ni Kundi la Boko
Haram la Nigeria.
Kinachofanya iwe vigumu kulimaliza kundi hilo ni kwamba
tayari limeshashaota mizizi mpaka kwenye jamii kiasi kwamba
wakazi wa maeneo yanayoshikiliwa na kundi hilo, wapo tayari wa-
toe taarifa juu ya uwepo wa wanajeshi, polisi au walinda usalama
kwa mapiganaji wa Boko Haram kuliko kutoa taarifa za wapiganaji
hao kwa vyombo vya ulinzi na usalama.
Bado sikuelewa kundi hilo limetumia muda gani kujiimarisha

143 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kiasi cha kuwatumia wananchi wa kawaida kwenye kuwapatia


taarifa.
Bado nilibaki nimepigwa na butwaa, nikiitazama video ndefu ali-
yokuwa ameturekodi mwanaume yule tangu akiwa mbali, ikituone-
sha vizuri jinsi tulivyokuwa tunapeana maelekezo pale barabarani!
Hakika ilikuwa ni hatari kwelikweli.
Ilibidi nitumie vitisho kutaka kujua ukweli kutoka kwa mwa-
naume yule kwa hiyo nilichokifanya, ilikuwa ni kuchomoa bastola,
nikaikoki kisha nikamnyanyua kwa nguvu na kumuegamiza kwe-
nye bodi la gari, nikamgusisha bomba la bastola kichwani huku
nikiwa nimemkwida.
Kila kitu kilikuwa kinatokea kwa kasi kubwa kiasi ambacho hata
yeye mwenyewe hakutegemea, akawa anakiona malaika mtoa roho
akimlia ‘taiming’.
Napenda sana kuitumia njia hii pale ninapokuwa nahitaji taarifa
za haraka kwa sababu mafunzo ya kisaikolojia yanaonesha hakuna
binadamu ambaye hajapitia mafunzo ya kijeshi au ya kiuhalifu
anayeweza kuvumilia kuona amegusishwa na bastola, tena ikiwa
imeshakokiwa tayari, lazima atasema ukweli tu kwa hofu ya kifo.
“Waliokutuma wako wapi?”
“Wapo kambini!”
“Kambini wapi?” nilimuuliza kwa sauti ya ukali, akanyoosha
kidole kuonesha kule kwenye ile kambi tulikotoka muda mfupi
uliopita baada ya kukurupushwa na wale wahalifu.
“Wamekupaje taarifa?”
“Nimepigiwa simu na kupewa maelekezo!”

144 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Onyesha namba iliyokupigia,” nilisema huku nikimkabidhi


simu, huku akitetemeka akaipokea ile simu na kutoa password kwa
sababu ilikuwa ni simu ya kisasa, hizi smartphones, akanionesha
namba na nilipotazama niligundua ni kweli alipigiwa simu dakika
kadhaa zilizopita.
Niliitoa ile bastola kwenye kichwa chake kisha nikamlaza tena
chini na kutoa ishara kwa vijana wangu ambao walimfunga pingu
na kumuingiza kwenye moja kati ya magari yaliyokuwepo eneo
lile.
Ile simu nikamkabidhi yule kijana wetu wa Cyber aifuatilie ile
namba na kuangalia ni watu gani wengine walikuwa wakiwasili-
ana. Nilihisi kichwa kinazidi kupata moto kwa sababu kadiri muda
ulivyokuwa unasonga mbele ndivyo mambo yalivyokuwa yanazidi
kuwa magumu.
“Tunawindwa, kwa hiyo hatakiwi yeyote kati yetu kufanya uzem-
be wa aina yoyote, tunapaswa kuwa macho muda wote, lazima
tuwazidi akili hata kama wanaonekana kujipanga kisawasawa!”
nilisema, vikosi vyote vikawa vinanisikiliza.
Kilichofuatia baada ya hapo ilikuwa ni utekelezaji wa maagizo
ambayo tayari nilikuwa nimeshayatoa, vikosi vikagawanyika kama
nilivyokuwa nimetoa maagizo, magari yaliyotakiwa kubaki pale
yaliingizwa kwenye vichaka vilivyokuwa kando ya barabara, wen-
gine wa kurudi Jaribu Mpakani wakaondoka, wa kuelekea Kibiti
nao wakafanya hivyo na sisi tuliokuwa tunatakiwa kwenda kuende-
lea kufanya uchunguzi kwenye ile kambi tuliondoka, safari hii kwa
miguu, mimi mwenyewe nikiwa kiongozi.

145 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Tuliendelea kusonga mbele, tukifuatisha ile njia tuliyokuwa tumei-


tumia awali, silaha zikiwa mikononi huku nikiwa naendelea kuwasili-
ana na vikosi vyote na kupokea taarifa zilizokuwa zinaendelea kuingia
kwa wingi kupitia vifaa vya mawasiliano nilivyokuwa nimevivaa.
Wale watuhumiwa wawili, yule kijana wa Kisomali pamoja na yule
mwanaume aliyekuwa anaturekodi video, niliagiza warudishwe Dar
es Salaam haraka ili kitengo cha interogation kwa maana ya wapele-
lezi wa ndani ya kitengo waendelee kuwahoji kuangalia kama tu-
naweza kupata taarifa zinazoweza kutusaidia.
Baada ya kutembea kwa karibu dakika sitini, tayari tuliwasili kwe-
nye lile eneo lililokuwa na ile kambi, nikawagawa vijana wangu kisha
tukatengeneza mfumo wa kama duara wa kulizunguka eneo lote na
kuendelea ‘kuwachora’ maadui zetu.
Kila kitu kilikuwa kinafanyika kwa usiri wa hali ya juu, hatuku-
takiwa kuwashtua kwa kitu chochote na kwa sababu walishaamini
kwamba tumekimbia, wasingeweza kuhisi kwamba tunaweza kurudi
haraka kiasi hicho.
Mimi na vijana wangu wawili tulienda upande wa pili, kule alikose-
ma yule kijana wa Kisomali kwamba ndipo lilipo lango kuu, tukawa
tunaendelea kuwasiliana kimyakimya kwa kutumia vifaa vya ma-
wasiliano ambavyo kila mmoja wetu alikuwa navyo mwilini.
Haikuwa kambi ndogo kama ambavyo ungeweza kudhani kwa
kuitazama kwa mbali na kilichozidi kunifanya nizidi kuumiza kichwa,
ni kwamba karibu kila mtu aliyekuwa akiingia na kutoka kwa kupitia
lango la upande ule tuliokuwepo, alikuwa na silaha begani.
Mwili ulikuwa unanisisimka kuliko kawaida, inawezekanaje kikundi

146 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

cha wahalifu wenye silaha kijijenge mpaka kufikia kuwa na kambi


bila vyombo vya ulinzi na usalama kugundua chochote, tena katika
nchi ambayo inasifika kwa jinsi vyombo vya ulinzi na usalama
vilivyokuwa imara, kuanzia kwenye mipaka ya nchi mpaka mitaani
wanakoishi wananchi wa kawaida.
Kwa hesabu za harakaharaka, kulikuwa na watu karibu arobaini
au hamsini kama alivyosema yule kijana wa Kisomali na hapa
kuna jambo jingine nililibaini. Kwanza wote walikuwa ni wanau-
me lakini pia kulikuwa na watu wachache waliokuwa na asili ya
Kisomali lakini wengine wengi walikuwa ni Washahili kabisa, tena
vijana wadogo walikuwa wengi kuliko watu wazima.
Kwa jinsi walivyokuwa wakibeba silaha, jinsi walivyokuwa
wakitembea na jinsi walivyokuwa wakipokea amri zilizokuwa zi-
natolewa, ilionesha wazi kwamba walikuwa na mafunzo ya kijeshi.
Basi tuliendelea kuwachora kimyakimya, vijana watatu wakiwa
na kazi ya kupiga picha kila kilichokuwa kinaendelea upande wa
kule getini ingawa ilikuwa ngumu kuona kwa karibu kilichokuwa
kinaendelea mle ndani lakini pilikapilika zilikuwa nyingi kisawa-
sawa.
Nilibaini pia kwamba usafiri mkubwa uliokuwa ukitumika,
zilikuwa ni pikipiki ambazo kwa muda ule pekee, tuliweza kuzi-
ona karibu saba zikiingia na kutoka. Nilijipongeza ndani ya moyo
wangu kwa uamuzi ule wa kwenda eneo lile kufanya ujasusi
kwanza kwa sababu sasa nilishakuwa na picha kamili ya namna ya
kuvamia bila upande wetu kupata madhara.
Baada ya kutulia kwa takribani saa mbili tukiwa tumejificha

147 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

vichani, hatimaye nilitoa ishara kwa vijana wangu kwamba tuanze


kurudi nyuma, tayari kwa kuondoka eneo hilo mpaka usiku tutaka-
porudi kwa ajili ya kazi moja tu, kuvamia.
Tulirudi nyumanyuma kwa ukimya wa hali ya juu na hatimaye
tukarudi mpaka pale tulipotawanyikia, vijana wote walikuwa salama
ingawa hofu za waziwazi zilionekana kwenye uso wa kila mmoja.
“Hii kazi wanatakiwa waje jeshi bakabaka,” nilimsikia mmoja kati
ya wale vijana niliokuwa nao akizungumza kwa sauti ya chini, aki-
ongea na mwenzake. Nilimkariri vizuri kwa sababu ni hatari kwenda
kwenye ‘misheni’ na watu wa aina hiyo ambao tayari mioyo yao
imeshainama kwa hofu.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, tukaianza safari ya kurudi
barabarani. Tayari ilikuwa inakwenda kwenye saa kumi na moja
jioni na mpaka tunafika barabarani, tayari ilikuwa ni saa kumi na
mbili za jioni.
Sikuwa nimekula kitu siku hiyo tangu asubuhi na vijana wangu
nao walikuwa na hali kama yangu ingawa wale kutoka kikosi
maalum walionesha kuwa walipata muda wa kula kabla ya kuja
kuungana nasi. Tulifanya utaratibu wa chakula na kwa bahati nzuri
ni kwamba tayari gari maalum lilikuwa limeshawasili Jaribu Mpak-
ani likiwa na vyakula kutokea Dar es Salaam kwa ajili yetu.
Tuliingia kwenye magari yetu, safari ya kurudi Jaribu Mpakani
ikaanza, nikawasiliana na wale waliokuwa Kibiti ambao nao walita-
kiwa kurudi ili tukutane pamoja na kupanga namna ya kukabiliana
na wahalifu usiku wa siku hiyohiyo.
Wakati vijana wanaendelea kujisevia chakula, tukiwa tumeenda

148 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kuweka kambi ya muyda kwenye shule ya msingi iliyopo kwenye mji


huo mdogo, mimi nilikuwa naendelea kuwasiliana na viongozi wangu,
tukiendelea kubadilishana mawazo kuhusu namna bora inayoweza
kutuopa ushindi haraka.
Bado kuna mtu mmoja muhimu sana sikuwa nimewasiliana naye
mpaka muda huo, ambaye kwangu naweza kumuita kwamba ndiye
aliyekuwa ‘mastermind’ anayeweza kunipa mwanga wa nini cha ku-
fanya! Baba mkwe wangu, baba wa mke wangu kipenzi Saima.
Kwa jinsi tulivyokuwa tunafanya kazi, baba yake Saima japokuwa
alikuwa ni kiongozi wa juu wa ‘kitengo’, mimi sikuwa nawajibika
moja kwa moja kwake na yeye pia kutokana na uzoefu wake, hakuwa
akishughulika tena na oparesheni bali alikuwa akishughulikia zaidi
masuala ya utawala.
Japokuwa nilikuwa najua kwamba lazima atakuwa anajua kila kitu
kilichokuwa kinaendelea, nililazimika kumtafuta kwanza ili nim-
shirikishe kwenye suala lililokuwa mbele yangu kwa sababu mara
kwa mara yeye ndiye aliyekuwa akinipa mwongozo wa nini cha
kufanya na kwa kuwa alikuwa na uzoefu wa miaka mingi, ilikuwa kila
akikupa mwongozo wa jambo fulani, basi lazima mafanikio yapati-
kane.
Kikazi sikuwa na ‘ruksa’ ya kumpigia simu moja kwa moja kwa
sababu huwa tunabanwa na itifaki linapokuja suala la kazi, lakini kwa
kuwa mimi yule alikuwa ni baba mkwe, nilikuwa na uwezo wa ku-
wasiliana naye muda wote kwa kigezo hicho.
Ilibidi nisogee pembeni, wakati vijana wakiendelea kula, mimi
nikaingia kwenye gari na kutoa simu yangu, nikatafuta namba yake

149 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

niliyokuwa nimeisevu kisha nikaipiga na muda mfupi baadaye,


alipokea.
Nilianza kwa kumsalimu kwa adabu, kama kawaida yake akawa
ananitania mambo ya hapa na pale kisha kabla hata sijamuuliza
nilichotaka kumwambia, akaanza yeye.
“Ilikuwa nikupigie muda si mrefu, tulikuwa na vikao vingi leo na
viongozi wa nchi kuhusu suala hilohilo mnalolishughulikia. Nime-
furahi kusikia kwamba wewe ndiyo umepewa kazi ya kuongoza
misheni lakini nina hofu ndani ya moyo wangu!” alisema, nikatulia
na kuendelea kumsikiliza.
Akaniambia taarifa za ndani zilizopatikana, zinaonesha kwamba
watu tuliokuwa tunapambana nao, wanaungwa mkono na mtandao
mkubwa wa magaidi unaosumbua eneo lote la pembe ya Afrika
kuanzia Somalia.
“Tunaposhughulika na watu wa aina hii, tunapaswa kuwa makini
sana kwa sababu hawana cha kupoteza. Mtu anayeweza kuvaa
bomu na kwenda kujilipua katikati ya watu, hana cha kupoteza kwa
hiyo unatakiwa kuwa makini na namna ya kushughulika naye.
“Nimefurahi kusikia kwamba ulilazimika kusitisha uvaizi wa
hiyo jkambi yao ambao ulikuwa ufanyike leo! Hizo ndizo akili
zinazotakiwa, huwezi kuvamia kichwakichwa, serikali imetumia
fedha nyingi sana kuwapa mafunzo, wewe mwenyewe utakuwa
shahidi wa jinsi ulivyoenda kupata mafunzo ya daraja la kwanza
nchini Israel.
“Sisi viongozi wenu hatupo tayari kuona tunampoteza yeyote kati
yenu kwa makosa ya kushindwa kufikiri vizuri tunapokabiliana na

150 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

matishio, sijui kama unanielewa!”


“Nakuelewa baba!”
“Unajua kwamba mimi baba yako nakutegemea, unajua kwamba
mkeo Saima anakutegemea na unajua kwamba wewe ndiyo kion-
gozi wa familia lakini yote tisa, kumi ni kwamba taifa linakutege-
mea sana wewe na wenzako! Sijui kama unanielewa!” alisema
baba yake Saima, nikashusha pumzi ndefu kwa sababu alichokuwa
anakisema kilikuwa ni ukweli mtupu.
“Nakuelewa baba!”
“Sasa nisikilize kwa makini! Lazima mnapofikiria kwenda kuiv-
amia hiyo kambi, uvamizi uanzie ndani!” alisema, nikawa sijamu-
elewa amemaanisha nini.
“Kama mnaona bado hamuwezi kuvamia kutokea ndani, hutakiwi
kuruhusu misheni ianze, utanishukuru baadaye!” alisema na kunia-
cha kwenye mataa. Uvamizi wa kuanzia ndani kwenye kambi kama
ile, ungewezekanaje?
“Umewahi kujiuliza hao watu wote waliopo kwenye hiyo
kambi wanapata wapi chakula? Anzia hapo na ukishapata majibu,
pandikiza watu ambao muda misheni itakapoanza, wao ndiyo
watakaoanzisha mashambulizi kutokea ndani,” alisema kisha aka-
kata simu na kuniacha nikiwa bado sijamuelewa.
Ilikuwa ni kawaida yake kutoa mwanga wa jambo fulani kisha
baada ya hapo anakuacha mwenyewe utafute majibu kwa kile
mwenyewe alichozoea kusema kwamba ni kukomaza ubongo.
Nilishusha pumzi ndefu na kuegamia ile siti nilipokuwa nimekaa
ndani ya gari, nikajaribu kutuliza akili zangu.

151 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Harakaharaka nilifungua mlango wa gari na kuteremka, nikatem-


bea harakaharaka kuelekea kule ndani ambako vijana walikuwa
wakiendelea kupata chakula, nikamfuata yule mmoja ambaye
nilimkabidhi jukumu la kuwalinda wale watuhumiwa wawili tulio-
kuwa tumewapata.
“Wameshafikishwa Dar es Salaam kama ulivyokuwa umeagiza.”
“Safi! Sasa nahitaji mimi na wewe tuondoke sasa hivi kurudi Dar
es Salaam, kuna jambo la msingi sana tunatakiwa kwenda kumhoji
yule kijana wa Kisomali!”
“Sawa kiongozi!” alinijibu huku akiacha kila alichokuwa anaki-
fanya, japokuwa niliona mshangao aliokuwa nao kwenye uso
wake.
Niliwapa taarifa viongozi wangu kwa kupitia vifaa vya ma-
wasiliano na kwa kuwa bado tulikuwa na saa kadhaa kabla ya
kuanza kwa misheni, nilipewa ruhusa ya kuendelea na nilichokuwa
nimekipanga.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, mimi na yule kijana wangu
tuliingia kwenye gari na safari ya kurudi Dar es Salaam ikaanza.
Lengo kuu lilikuwa ni kwenda kumbana yule kijana wa Kisomali,
hata ikibidi kwa mateso makali ili anieleze vizuri ni wapi wali-
pokuwa wakipata vyakula vyao na utaratibu wa kuingiza vyakula
ulikuwaje.
Mwendo tuliokuwa tunaenda nao ulikuwa siyo wa kawaida, bado
kulikuwa na vizuizi vingi vya barabarani kila baada ya kilometa
kadhaa, jambo ambalo lilinipa nguvu ya kuamini kwamba vikosi
vyote vinashiriki kikamilifu kwenye jambo lile.

152 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Majira ya saa tatu usiku tayari tulikuwa tumeshawasili ‘getini’ na


kwa kuwa nikiwa njiani nilikuwa nawasiliana na wenzangu, tulipo-
fika tulikuta tayari mtuhumiwa ameshaandaliwa kwenye chumba
maalum cha mahojiano.
Nikapitiliza moja kwa moja mpaka kwenye chumba hicho, am-
bacho awali ndicho kilichotumika kwa mahojiano ya wale watuhu-
miwa wa awali, akiwemo yule mzee wa Kisomali.
Kwa bahati nzuri, yule kijana wa Kisomali aliponiona tu, ali-
kubali kutoa ushirikiano na akaniomba sana nimsaidie kwa sababu
alikuwa ameingizwa kwenye mkumbo ambao hakuwa anajua ni
hatari kiasi gani.
Nadhani baada ya kufikishwa pale, alitambua kwamba kumbe
hatukuwa tunacheza kama alivyofikiria awali na tulijipanga kika-
milifu kusambaratisha mtandao wote kabla hawajatimiza malengo
yao.
Msaada wangu kwako utatokana na jinsi mwenyewe utakavyotoa
ushirikiano, ukileta ujuaji kama ule wa mwanzo mwisho wako ni
mbaya sana!” nilimwambia kwa upole wakati nikifungua ‘note-
book’ yangu, nikaanza kumuuliza nilichokuwa nakitaka.
“Kila asubuhi na jioni kuna vijana huwa wanatumwa kwenda
kuchukua maandazi na mikate kwa mama mmoja pale Jaribu
Mpakani ambaye amepewa ‘tenda’ ya kuwa anatupikia vitafunwa!”
alisema, nikawa ni kama siamini alichokuwa ananiambia.
Akaniambia kwamba mahitaji mengine huwa yanafuatwa Kibiti
na kuna watu maalum ambao kazi yao pale kambini huwa ni kufua-
ta vyakula kwa kutumia bodaboda.

153 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Tunaondoka wote mguu kwa mguu ukanioneshe, upo tayari?”


“Nipo tayari kamanda!” alisema huku nikiwa naendelea kum-
soma saikolojia. Safari hii alikuwa akizungumza ukweli mtupu.
Viongozi wangu na wakuu wengine wa idara waliokuwa
wakisikiliza kila kilichokuwa kinaendelea, nadhani walielewa sasa
umuhimu wa mimi kurudi haraka kiasi hicho. Hakukuwa na muda
wa kupoteza, idhini ya kuondoka na mtuhumiwa ikatolewa.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, tuliondoka kwa kasi kubwa na
mpaka inafika majira ya saa tano usiku, tayari tulikuwa tumewasili
Jaribu Mpakani. Vijana walikuwa wameshajiandaa kwa kazi kwa
sababu maelekezo ya awali ambayo hayakuwa yamebadilishwa, ni
kwamba tulitakiwa kwenda kukamilisha misheni hiyo usiku huo-
huo.
Baada ya kuwasili Jaribu Mpakani, ilibidi mimi na viongozi
wawili wa kitengo cha kupambana na ugaidi, tuingie mtaani tuki-
ongozwa na yule kijana wa Kisomali mpaka mtaa mmoja tulivu
uliokuwa pembeni kidogo, tukapokelewa na harufu ya mikate na
maandazi yaliyokuwa yanapikwa, yule kijana wa Kisomali akanio-
nesha nyumba husika kwa kidole.
Tukiwa tunajipanga nini cha kufanya, tulisikia muungurumo wa
pikipiki zikija upande ule tuliokuwepo, ikabidi tuwahi kujificha,
pikipiki nne zikatupita mbiombio na kwenda kupaki nje ya ile
nyumba. Muda mfupi baadaye, tukashuhudia mifuko ile inayotumi-
ka kuwekea unga wa kilo hamsini, ikitolewa na kuanza kufungwa
kwenye zile bodaboda.
“Ni wenyewe, wamefuata mzigo!” alisema yule kijana wa Ki-

154 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

somali.
Harakaharaka niliwasiliana na wale wenzetu tuliokuwa tumewaa-
cha pale kwenye ile shule ya msingi wakiwa wanajiandaa. Tuli-
hitaji kuongeza nguvu haraka iwezekanavyo ili kuwadhibiti wale
wanaume ambao tungewatumia kama chambo kutekeleza zoezi
lile kuanzia ndani kama nilivyokuwa nimeelekezwa na baba yake
Saima.
Kwa kuwa vikosi vyote vilikuwa tayari, hakukuwa na muda
wa kupoteza, takribani vijana wangu sita na wengine sita kutoka
kitengo cha kupambana na ugaidi walichomoka na ndani ya muda
mfupi tu, wakawa tayari wamefika usawa wa barabarani kutokea
pale tulipokuwepo.
Ilikuwa ni lazima wakae kwa kule mbali ili wasije wakaamsha
hofu kwa wale watuhumiwa na kuharibu mpango mzima.
“Wewe utabaki hapahapa, ukijaribu kutoroka kitakachokukuta
tusilaumiane,” nilisema huku nikichomoa funguo ya pingu na ku-
fungua upande mmoja, nikamfungua mkono mmoja kisha nikam-
funga kwenye mguu mmoja.
Nilifanya hivyo kwa sababu katika hali ya kawaida, hakuna mtu
ambaye angeweza kukimbia akiwa amefungwa mkono na kuun-
ganishwa na mguu, na hata kama angejaribu, asingeweza kufika
mbali.
“Chief, anaweza kutoroka huyu,” alisema mmoja kati ya wale
vijana wa kikosi kazi niliokuwa nao, nikatingisha kichwa kum-
hakikishia kwamba hawezi kwa sababu hata sisi tukiwa mafunzoni,
tulikuwa tukipewa mafunzo hayo na ilikuwa ni mpaka mtu aliye-

155 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

fuzu kwa kiwango cha juu kabisa ndiyo anayeweza kutoroka akiwa
amefungwa mkono na mguu kwa pingu.
Pikipiki zilikuwa nne ikiwa na maana kwamba wale vijana nao
walikuwa wanne, lakini sisi tulikuwa watatu, mimi na wale vijana
wawili wa kikosi maalum, kwa hiyo ilitakiwa umakini mkubwa ku-
hakikisha kwamba hakuna yeyote kati yao anayetoroka kwa sababu
kwa kufanya hivyo, tungeharibu mpango mzima.
Niliwapa ishara wenzangu kwamba kila mmoja ashughulike
na mmoja na mimi nitashughulika na wawili na kitu cha kwanza
tulichotakiwa kukifanya, ilikuwa ni kuwaweka chini ya ulinzi kwa
kushtukiza.
Baada ya kila mmoja kunielewa nilichomaanisha, tulianza kuso-
gea kwa mwendo wa kunyata, tukiwa tumekaribia pale, mmoja kati
yao aliingia ndani kwenda kuchukua mzigo, jambo ambalo lilirahi-
sisha kazi kwa sababu sasa kila mmoja alitakiwa kushughulika na
mtu mmoja.
Kwa kasi ya kimbunga tuliwavamia pale, silaha zikiwa mikononi
na kuwaweka chini ya ulinzi kimyakimya. Kwa jinsi tukio lilivyo-
fanyika kwa haraka, kila mmoja alijikuta akiwa chini, tukawapiga
pingu na kuwatuliza chini.
Kufumba na kufumbua yule mmoja aliyekuwa ameingia ndani,
baada ya kusikia purukushani alitoka mbio nje na kutaka kuleta
upinzani lakin naye alijikuta akichotwa mtama na kuanguka chini
kama mzigo, akafungwa pingu na kulazwa pale chini kama wen-
zake.
“Msaada! Majambazi, jamani tumeva...” mmoja kati yao alijaribu

156 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kupiga kelele, uzalendo ukamshinda mmoja kati ya wale vijana


wangu ambaye alimfumua teke kwa nguvu na kusababisha ash-
indwe kumalizia alichotaka kukisema.
“Atakayepiga kelele tutamfumua ubongo sasa hivi,” nilisema
kisha bila kupoteza muda, tukaanza kuwapekua mmoja baada ya
mwingine.
“Ana silaha! Huyu ana silaha alisema mmoja kati ya wale vijana
baada ya kugundua kwamba kumbe mmoja kati yao alikuwa na
bunduki ya AK47 iliyokatwa kitako, aliyokuwa ameificha ndani ya
koti alilokuwa amevaa, upande wa kifuani.
Alinyang’anywa haraka, tukawapekua wengine wote na ku-
chukua simu zao zote, nikaziweka kwenye kimfuko maalum,
harakaharaka nilirudi kule tulikokuwa tumemuacha yule kijana
wa Kisomali, nikamkuta akiwa ametulia palepale nilipomuacha,
nikamfungua pingu mguuni na kuirudishia kwenye mkono wa pili,
nikamkokota na kumrudisha mpaka pale wenzake walipokuwa
wamepigwa ‘tanchi’ na kulazwa chini kwa kuwapanga.
“Kwani kuna ni...” sauti ya mwanamke wa makamo ilisikika
akiwa anatoka mlangoni lakini alipofika mlango na kuchungulia
nje, alishindwa kumalizia kauli yake kwani alikutana na mtutu wa
bunduki na kutakiwa ainue mikono juu.
“Mungu wangu!” alisema kwa sauti iliyojawa woga, ikabidi naye
afungwe pingu kwa sababu hatukuwa tunajua yeye ni nani mpaka
ashirikiane na watu wale.
“Ndani yupo nani?”
“Wapo wanangu tu, hakuna mtu mwingine?”

157 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Kweli?”
“Ndiyo!”
“Twende!” nilisema huku nikimpa ishara ya kuingia ndani. Kwa
kuwa nyumba haikuwana umeme, ilibidi nichomoe tochi ndogo
lakini yenye mwanga mkali na kumulika ndani.
Kule ndani kweli kulikuwa na watoto watatu wa kike na wawili
wa kiume wakiwa wanamsaidia mmwanamke huyo kupika maan-
dazi na mikate. Sebule ilikuwa kama ‘bakery’ ya mikate, wakash-
tuka kuona mama yao akiingia na mimi akiwa amefungwa pingu,
nikatoa amri ya wote kutoka nje, kweli wakatii huku wakitetemeka.
Kule nje walipokelewa na vijana wangu, mimi nikamtaka yule
mwanamke anipitishe chumba kimoja baada ya kingine kuhakiki-
sha kama kweli hakukuwa na mtu mwingine mle ndani.
Nilipekua kila sehemu mpaka uvunguni mwa vitanda lakini haku-
kuwa na mtu, nikatoka naye mpaka nje na kumtaka afunge mlango
mkubwa kwa funguo. Alifanya hivyo na kwa kuwa tayari wale
wenzetu walishapewa maagizo ya kusogea eneo la tukio, tayari
walishafika na kuzingira eneo lote.
Niliagiza nyumba yote ifanyiwe upekuzi wa kina ili kuanga-
lia kama kuna chochote ambacho kinaweza kutusaidia, wale
watuhumiwa wanne pamoja na yule kijana wa Kisomali, niliagiza
wapelekwe pale kwenye ile kambi ya muda pale shuleni kwa ajili
ya mahojiano ya kina, yule mwanamke na wanaye nikaapizwa
wapelekwe kwenye kituo kidogo cha polisi kilichokuwa kwenye
mji ule, kwanza kwa ajili ya usalama wao lakini pia kwa ajili ya
mahojiano ya kina.

158 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Niliagizwa viongozi wa serikali ya mtaa wawepo wakati wa ule


upekuzi wa mara ya pili, jambo ambalo lilitekelezwa haraka, tu-
kagawana majukumu, ile mizigo ya maandazi na mikate ikachuku-
liwa pamoja na zile bodaboda zote nne, zikapelekwa pale shuleni
vikosi vilipokuwa vimeweka kambi ya muda.
Wengi hawakuwa wamenielewa nilichokuwa nakikusudia kwa
wakati huo. Baada ya kurudi pale shuleni, nilianza kuwafanyia
mahojiano vijana wale tuliowakamata, mmoja baada ya mwingine
ambapo hakuna aliyekuwa tayari kuzungumza kitu chochote.
Watatu kati yao walikuwa ni Waswahili wenzetu na yule mmoja
aliyekutw ana bunduki, yeye alikuwa na asili ya Kisomali. Baada
ya kuona wamegoma kuzungumza chochote, sikutaka kushughu-
lika nao kwa chochote kwa wakati huo kwa sababu mambo yali-
kuwa mengi na muda haukuwa unatosha.
Nilimfuata yule kijana wa kwanza wa Kisomali tuliyetoka naye
Dar es Salaam na kumtaka anipe maelezo ya jinsi vyakula hivyo
vilivyokuwa vikiwasilishwa kwenye kambi ile na nikamhakikishia
kwamba ahadi yangu ya kumtoa kwenye matatizo kama atatoa
ushirikiano wa kutosha, ipo palepale.
Alikubali kunieleza kila kitu, akakubali pia kuongoza msafara
wa kwenda kwenye ile kambi, tukitumia pikipiki za wale vijana ili
tuingie mpaka ndani, tayari kwa misheni.
Muda huo ilikuwa tayari saa sita za usiku, niliagiza wale watuhu-
miwa waondolewe haraka na kupelekwa Dar es Salaam chini ya
ulinzi mkali lakini wakati huohuo, vikosi vyote vikae tayari kwa
ajili ya kwenda eneo la tukio! Ilikuwa ni lazima kazi ifanyike usiku

159 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

huohuo.
Baada ya kila kitu kukamilika, ndipo nilipoanza kuwafafanulia
watu wote waliokuwa wanahusika kwenye misheni ile, mpango
uliokuwa ndani ya kichwa changu na jinsi tutakavyovamia.
Kwa jinsi nilivyochora mpango mzima, kila mmoja alikuwa
anatingisha kichwa kuonesha kuniunga mkono kwa sababu kila
kitu kilikuwaakimepangiliwa kwa ufasaha wa hali ya juu. Mimi
na vijana wawili niliokuwa nawaamini kwa ushupavu, tulitakiwa
kuondoka kwa zile pikipiki wakati vikosi vingine vikiondoka kwa
magari kupita njia tofauti na yetu ili kwenda kuizingira kambi
kisha kusubiri amri kutoka kwangu. Safari ikaanza.
Nilikuwa makini kuhakikisha vikosi vyote vinafanya kazi kwa
kufuata maelekezo yangu na kwa umakini mkubwa kwa sababu
kama alivyokuwa ameniambia baba yake Saima, hatukutakiwa
kumpoteza yeyote kati yetu katika misheni ile.
Ili kuhakikisha kwamba hakuna anayeleta uzembe, nilikuwa
nawasiliana na vikosi vyote kila baada ya muda mfupi, na mimi pia
nikawa nawasiliana na watu wa teknolojia ya mawasiliano (IT) na
wale wa Cyber ili kuhakikisha tunapata taarifa za kila kilichokuwa
kinaendelea.
Kama nilivyoeleza awali, vikosi vyote vilikuwa vimegawa-
nywa kwa mfumo maalum wa kwenda kuizunguka kambi yote
ili mashambulizi yatakapoanza, basi yaanzie kutokea ndani kama
tulivyokubaliana kisha yafuatie kwenye pande zote za kuizunguka
kambi ile.
Majira ya kama saa saba hivi, tayari vikosi vyote vilikuwa tayari

160 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

vimewasili na kukaa ‘standby’ kusubiri amri kutoka kwangu. Sisi


pia tulikuwa tumeshawasili lakini tulilazimika kujificha kwanza vi-
chakani na bodaboda zetu, tukisubiri kila mtu awe tayari kwa kazi
iliyokuwa mbele yetu.
Ninachoshukuru ni kwamba yule kijana wa Kisomali alionesha
ushirikiano wa hali ya juu kwani yeye ndiye aliyekuwa akituon-
goza njia, akiwa anaendesha ile pikipiki ya mbele kabisa ambapo
nililazimika kumfunga pingu kwenye mkono wake na kumuungan-
isha na pikipiki ili asije akapata upenyo wa kukimbia.
Njia aliyotuongoza, awali nilikuwa na wasiwasi nikihisi ana-
taka kwenda kutuchuuza kwa sababu ilikuwa inakatiza kwenye
mashamba na baadaye kwenye pori, huku ikiwa nyembamba am-
bayo huwezi kugundua kwa haraka kama huwa inatumika na watu
wengi kiasi kile.
Ni mpaka tulipoikaribia kambi na kuanza kuiona kwa mbali
ndipo nilipoamini kwamba ni kweli alikuwa ameamua kutoa ush-
irikiano.
Baada ya kuhakikisha kila kitu kipo sawa, nilitoa ishara ya sauti
ya kuonesha kwamba misheni imeanza rasmi ambapo nilitumia
‘code name’ ya ‘Rosemarry’ ambayo tulishakubaliana kwamba
nitakapoitaja basi kila mmoja ajue kwamba kazi imeanza.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, nilimuamuru yule kijana wa
Kisomali aongoze msafara wa kwenda kuingia ndani na kweli aka-
fanya hivyo, akaondoa pikipiki yake kwa kasi, mimi nikiwa nyuma
yake nikawa namfuata kwa kasi, mkono mmoja ukiwa kwenye
‘bomba’, tayari kwa chochote huku wale wenzangu wawili nao

161 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wakiwa na silaha mikononi.


Tuliingia kwa kasi kubwa mpaka kwenye geti dogo la miti
lililokuwa kule upande wa kuingilia na kwa sababu nilishatoa
maelekezo, yule kijana wa Kisomali aliendelea kuvuta mafuta kwa
nguvu, pikipiki yake ikawa inakimbia kwa kasi kubwa huku mimi
nikimfuatia kwa mita chache tu nyuma yake.
Tofauti kabisa na tulivyokuwa tumeelezwa mwanzo kwamba
kwenye geti hilo huwa kunakuwa na walinzi wenye silaha ambao
lazima watatusimamisha kwanza kabla ya kuruhusu tuingie, tuli-
kuta geti likiwa wazi na hakukuwa na dalili yoyote ya kuwepo kwa
walinzi.
Akili yangu ilinituma kuamini kwamba kwa sababu ni usiku,
pengine wamepitiwa na usingizi, tukalipita kwa kasi ya kimbunga
mpaka eneo la katikati ambalo lilikuwa na uwazi huku likiwa lim-
ezungukwa na nyumba kadhaa zilizojengwa kwa mabati, maturubai
na mbao kuonesha kwamba ilikuwa ni kambi ya muda.
Kwa kasi ya upepo niliruka kwenye ile pikipiki ambayo ilikuwa
kwenye kasi kubwa, nikabiringika kikakamavu na kwenda kujilaza
chini na kuegamia msingi wa mawe uliokuwa katikati ya eneo lile,
wenzangu nao wakafanya hivyohivyo lakini yule kijana wa Ki-
somali yeye hakuwa na mafunzo hayo kwa hiyo akawahi kuzima
pikipiki na kwa kuwa nilikuwa nimemfunga pingu kwenye usu-
kani, ilibidi alale nayo chini akihofia kupigwa risasi.
Nikafyatua risasi moja juu utoa ishara kwa vikosi vyote vili-
vyokuwa vimeizingira kambi yote, kuingia kutokea kila upande,
tayari kwa mapambano.

162 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Hata hivyo, kuna kitu hakikuwa sawa! Eneo lote lilikuwa kimya
kabisa na hakukuwa na upinzani ambao ulioneshwa. Ndani ya
muda mfupi tu, vikosi vyote vilikuwa vimeshaingia eneo hilo huku
vingine vikibaki kulinda usalama kuizunguka kambi yote ili ku-
hakikisha hakuna mtu hata mmoja anayetoroka.
Harakaharaka niliinuka pale chini nilipokuwa nimejiegamiza na
kutoa ishara, vikosi vyote vikajipanga katika namna ya kuwekeana
kitu kinachoitwa ‘cover’, nikatoa ishara ya kugawanyika kwenye
makundi na kuingia kwenye nyumba zote zilizokuwa eneo lile,
mimi nikiongoza kuelekea kwenye nyumba ambayo ilionekana
kuwa kubwa kuliko zote.
Bado ukimya ulikuwa umetawala, nikaukanyaga mlango wa
lile jengo kubwa na kujibana pembeni kwa sekunde kadhaa kisha
nikawa wa kwanza kuingia, bunduki ikiwa mkononi huku tochi
yenye mwanga mkali niliyokuwa nimeivaa ikimulika mle ndani.
Hakukuwa na mtu yeyote! Nikatoa taarifa kupitia vifaa vya
mawasiliano na kutaka majibu kutoka kwa vikosi vingine, majibu
yakawa ni yaleyale! Hakukuwa na mtu yeyote kwenye jengo hata
moja!
“Haiwezekani! Haiwezekani!” nilisema nikiwa ni kama siamini
kabisa kilichokuwa kinatokea! Inawezekanaje misheni iliyopan-
giliwa kwa umakini mkubwa kiasi hicho ifeli kizembe namna
hiyo? Viongozi wangu wangenionaje? Lilikuwa ni doa kubwa sana
ambalo lilinifanya mapigo ya moyo yawe yananienda mbio kuliko
kawaida.

163 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Niliwasiliana na vikosi vilivyokuwa nje ambavyo navyo vilikuwa


namajibu yaleyale, hakuna mtu yeyote aliyeonekana akitoka katika
eneo hilo, nikawa ni kama nimechanganyikiwa.
Ilibidi nitoe amri ya kufanyika upekuzi wa kina kuangalia kama
kuna njia yoyote ambayo inaweza kuwa imetumiwa na watu wote
waliokuwa eneo hilo kutoroka na wakati huohuo nikaviagiza vikosi
vilivyokuwa upande wa nje, kugeuka na kuanza kufanya msako
kuelekea uelekeo wa tofauti na ile kambi.
Nilihisi ni kama kichwa kinataka kupasuka, kama watu wote
waliokuwa ndani ya kambi ile walikuwa wamefanikiwa kuto-
roka, maana yake ni kwamba wangeweza kutusubiri tuingie kisha
wakaanza kushambulia kutokea nje na ndiyo maana niliagiza viko-
si vya nje kugeuza upande wa oparesheni haraka iwezekanavyo.
Kwa unyonge mkubwa ilibidi nitoe ripoti kwa viongozi wa juu
akiwemo mkurugenzi kuhusu tulichokutana nacho, kumbe nao wa-
likuwa wameshajua kupitia mawasiliano tuliyokuwa tunayafanya,
kila mmoja akawa ni kama haelewi ni nini kilichotokea.
“Chief, you need to see this!” (Kiongozi, unatakiwa kuona hiki!)
alisema mmoja kati ya wale viongozi wa kikosi maalum, akinione-
sha kwa ishara upande wa pembeni kidogo ya ile kambi.
Kulikuwa na rundo la udongo mwekundu uliotengeneza kama
tuta, tukasogea kwa tahadhari na hakika sikuamini nilichokuwa
nimekiona. Kumbe kulikuwa na kitu kama handaki au mfereji
uliochimbwa, ambao ulikuwa ukianzia kwenye eneo hilo kuelekea
upande wa bondeni.
Mpaka hapo nilishapata picha kwamba lazima watu wote walio-

164 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kuwa eneo hilo lazima wametoroka kupitia shimo hilo lililochimb-


wa kienyeji na kufunikwa na matawi ya miti kwa juu. Ndani yake
kulikuwa na alama nyingi za miguu kuthibitisha kile nilichokuwa
nimekibaini.
Harakaharaka nilitoa amri kwa baadhi ya vijana kuanza kufua-
tilia kuangalia ni wapi handaki hilo lilikuwa limeelekea. Mapigo
ya moyo wangu yalikuwa yakinienda mbio kuliko kawaida na
nikaamua kuingia mwenyewe kwenye shimo hilo na kuongoza
msako huku wengine wakifuatia kwa nyuma na wengine wakipita
kwa juu.
Lilikuwa ni shimo lililochimbwa kwa usawa wa ardhi likiwa
na urefu wa kama mita 100 hivi na lilienda kuishia kwenye mto
mdogo uliokuwepo eneo hilo.
Kumbe wakati sisi tukijipanga kuvamia, wahalifu hao nao
walishakuwa na njia mbadala ya kutoroka na kwa jinsi shimo
lilivyokuwa limechimbwa, ilikuwa vigumu sana kubaini ni nini
kilichokuwa kimefanyika kwani lilizibwa kwa umakini mkubwa
kuanzia mwanzo mpaka mwisho.
Harakaharaka nilitoa amri ya vikosi vyote kuelekea nguvu kule
kwenye ule mto mdogo, mimi mwenyewe nikiwa mstari wa mbele,
nyayo nyingi zikaonekana kuvuka mto na kutokomea upande wa
pili kulikokuwa na msitu mkubwa. Sikutaka kabisa kuamini kama
wahalifu hao walikuwa na mbinu kali kiasi hicho.
Huwezi kuamini, tuliendelea na msako huku tukitanguliza tahad-
hari kubwa lakini mpaka kunaanza kupambazuka, hakukuwa na
chochote cha maana tulichokipata, nikajikuta nikiwa na ‘presha’

165 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kubwa isiyo na mfano.


Kwa mara nyingine nilikiri kuzidiwa mbinu, kilichoniuma zaidi
ni kwamba nilizidiwa katika kipindi ambacho kila mtu alikuwa aki-
nitegemea mimi kutegua kitendawili kilichokuwa mbele yetu.
Wakati sisi tukikesha porini tukiendelea na msako, kule ofisini
nako viongozi na wakuu wa idara mbalimbali walikesha wakiwa
wanafuatilia kwa makini kila kilichokuwa kinaendelea na muda
wote tulikuwa tukiwasiliana kwa karibu kabisa kupitia vifaa vya
mawasiliano.
Japokuwa mwenyewe nilikuwa najua kabisa kwamba nimemuan-
gusha kila mtu aliyekuwa nyuma yangu, mkurugenzi wetu yeye
aliendelea kunitia moyo mara kwa mara na kueleza kuwa hata pale
tulipokuwa tumefikia, ilikuwa ni mafanikio makubwa.
Ilipofika majira ya saa kumi na mbili asubuhi, kukiwa tayari
kumepambazuka, maagizo yalitoka juu kwamba tunatakiwa kui-
simamisha misheni ile kwa sababu hakukuwa na uwezekano wa
kufanikiwa katika kile tulichokuwa tunakifanya.
Muda huo tulikuwa tumefika mbali sana tukiendelea kufuatilia
njia walizopita watu wale ambapo kitu ambacho niliweza kukibaini
harakaharaka, ni kwamba uelekeo wao ulikuwa ni kwenye Hifadhi
ya Taifa ya Selous.
Nafsi yangu ilikuwa inaniambia kwamba tunatakiwa kuendelea
kuwafuatilia mpaka mwisho, nikajaribu kumshawishi mkurugenzi
lakini alishikilia msimamo wake na kunifanya nisiwe na cha ku-
fanya.
Ilibidi nitii kile nilichoambiwa, nikatangaza kusitisha oparesheni

166 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ile na kuvitaka vikosi vyote turudi mpaka kwenye ile kambi kisha
maelekezo mengine yatatolewa kuanzia hapo. Kila mmoja alikuwa
amechoka kisawasawa, kwanza uchovu wa kutolala usiku kucha,
kutembea umbali mrefu maporini lakini kubwa ilikuwa ni kush-
indwa kufanikisha misheni ile.
Basi ilibidi kila mmoja atii, tukaanza kurudi ambapo mpaka in-
afika saa mbili za asubuhi, vikosi vyote vilikuwa vimerejea kwenye
ile kambi tuliyoivamia usiku ule. Wale niliowapa jukumu la ku-
fanya upekuzi eneo lile, walikuwa wamefanya kazi yao kwa weledi
wa hali ya juu.
Ushahidi wa kila aina ulikuwa umekusanywa na kuwekwa kwe-
nye masanduku maalum kwa ajili ya uchunguzi wa kitaalamu zaidi
ikiwa ni pamoja na kujaribu kuwatambua baadhi ya watu walio-
kuwa kwenye kambi ile.
Nikiwa naendelea kuangalia ushahidi uliokusanywa, nilipokea
simu ya moja kwa moja kutoka kwa mkurugenzi. Kitendo cha simu
yake kuita moja kwa moja kwenye simu yangu, kilinishtua kwa
sababu kwa kawaida tunapokuwa kwenye misheni kama hizo, ma-
wasiliano huwa yanafanyika kwa kupitia mfumo wa mawasiliano
kupitia vifaa maalum ambapo wote mliopo kwenye misheni husika
mnakuwa mnasikia kila kinachoendelea.
“Unatakiwa kurudi haraka na timu yako! Huko wabaki watu
wachache kwa ajili ya kuendelea kufanya ‘monitoring’ kwa
karibu,” alisema mkurugenzi, huku sauti yake ikionesha kuwa na
mchecheto usio wa kawaida.
Kwa kuwa neno lake lilikuwa ni amri, kilichofuatia baada ya

167 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

hapo ilikuwa ni utekelezaji. Bila kupoteza muda nilitoa maagizo,


nikawachagua vijana wachache wa kubaki na sisi wengine wote tu-
kaianza safari ya kurudi Jaribu Mpakani ambako tungeenza kuun-
gana na wenzetu wengine, tayari kwa safari ya kurudi jijini Dar es
Salaam.
Moyoni mwangu nilikuwa najisikia vibaya kuliko kawaida,
hakuna kitu ambacho kilikuwa kinaniumiza moyo wangu kama
kushindwa kukamilisha oparesheni yoyote ninayopewa kuiongoza
na nikiri kwamba siku zote nilikuwa nimezoea kupata ushindi kiu-
rahisi kwenye kazi lakini misheni hiyo ilishaonesha kunielemea.
“Nitapambana mpaka tone langu la mwisho,” nilijisemea ndani
ya moyo wangu, tukiwa tumepakizana kwenye pikipiki na kijana
wangu mmoja, tukielekea mahali vijana walipokuwa wameacha
magari usiku uliopita.
Tulipofika, niliingia kwenye gari langu ambalo lilikuwa mion-
gioni mwa magari yaliyowapeleka vijana usiku huo, wakati mimi
na wenzangu kadhaa tukitumia bodaboda. Ndani ya muda mfupi,
vijana wote walikuwa wameshafika, tukaingia kwenye magari na
kurudi mpaka Jaribu Mpakani.
Kila nilipokuwa nikifikiria jinsi nilivyopigwa chenga ya mwili
na wale wahalifu, mwili ulikuwa unaishiwa nguvu kabisa. Tulifika
Jaribu Mpakani, ambapo kama ilivyokuwa kwa kule kwenye ile
kambi, nilichagua vijana wachache wa kubaki kisha wengine wote
tukaianza safari ya kurudi Dar es Salaam ingawa bado sikuwa na-
jua ni nini kilichofanya mkurugenzi aagize turudi haraka.
Bado vizuizi vya barabarani vilikuwepo na askari walikuwa

168 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wakiendelea na majukumu yao, tukaendelea na safari na tukiwa


njiani, simu ya baba yake Saima iliita. Niliichukua kwenye dash-
board ya gari nililokuwa naendesha na kuiweka sikioni kwa kutu-
mia mkono mmoja huku ule mwingine ukiwa umeshikilia usukani,
gari likiwa kwenye kasi kubwa kisawasawa.
“Umesikia kilichotokea huku?”
“Hapana baba!”
“Katika kipindi ambacho unatakiwa kutuliza kichwa chako basi
ni hiki! Mlifanya vizuri usiku na japokuwa hamjafanikiwa kuwaka-
mata wote lakini angalau tumepata mwanga wa nini kinachoende-
lea,” alisema baba yake Saima, kauli ambayo ilinifariji sana moyo
wangu lakini bado nikawa na shauku kubwa ya kutaka kusikia ni
nini kilichokuwa kimetokea.
“Tumepokea ‘intels’ kutoka Ubalozi wa Marekani!” alisema
kisha akatulia kidogo, akimaanisha kwamba walikuwa wamepokea
taarifa za kiintelijensia kutoka ubalozini.
“Ni nini?”
“Wamesema kuna hatari ya kutokea kwa shambulio la kigaidi
jijini Dar es Salaam ndani ya siku nne au tano kuanzia leo na ndiyo
maana wote tunatakiwa kukutana haraka iwezekanavyo!”
“Unasema?” nilimuuliza baba mkwe nikiwa ni kama siamini
nilichokuwa nakisikia.
“Kama nilivyokwambia, unatakiwa kutuliza kichwa chako kisa-
wasawa kwa sababu unategemewa, uwezekano mkubwa ni kwam-
ba utapewa jukumu la kuwaongoza wenzako kutegua kitendawili
hiki ambacho kina uhusiano mkubwa na kazi uliyoifanya.”

169 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Target?” nilimuuliza nikiwa na lengo la kutaka kujua hizo ta-


arifa za kiintelijensia walizopewa zinaonesha ni sehemu gani tukio
hilo litatokea?
“Classified!” alisema akimaanisha kwamba ni siri kubwa na
hawezi kuniambia.
“Mungu wangu!” nilisema kisha akakata simu, nikasikia tumbo
likinivuruga kuliko kawaida. Nilishaelewa ni nini alichokuwa ame-
maanisha kwa kunijibu kwa neno hilo la Kiingereza, ‘Classified’.
Jibu nililokuwa nimelipata ni kwamba lazima sehemu ambayo
ilikuwa inakwenda kushambuliwa ni Magogoni. Nasema hivyo
kwa sababu kama ingekuwa ni sehemu nyingine yoyote, lazima an-
geniambia kwa sababu mimi na yeye tunazungumza mambo mengi
sana, tena kwa uwazi mkubwa.
Niliamini kwamba ni Magogoni kwa sababu tayari tulishabaini
kwenye ile nyumba tuliyoivamia kule Kijitonyama Kisiwani
kwamba mipango ilikuwa inafanywa kuvamia ikulu na ndiyo
maana kukawa na picha zilizokuwa zinaonesha kuanzia ramani,
mwonekano wa nje, mwonekano wa ndani mpaka mwonekano wa
kutoka angani wa ikulu, jambo ambalo mimi ndiye niliyekuwa wa
kwanza kulibaini.
Kwa jinsi watu hao walivyokuwa wanaendesha mambo yao kwa
umakini wa hali ya juu, nilijua haitakuwa kazi nyepesi kubaini
mpango wote kisha kuuzima, hasa katika kipindi ambacho mhusika
mkuu alikuwa ametoroka katika mazingira ya ajabu, tena yeye na
kundi lake lote.
Akili walizokuwa wanazitumia zilikuwa ni za hali ya juu kwelik-

170 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

weli, mapigo ya moyo yakawa yananienda mbio kuliko kawaida.


Japokuwa mshale kwenye ‘speedometer’, kile kifaa kinachosoma
spidi ya gari pale kwenye ‘dashboard’ ulikuwa unacheza kwenye
140 hadi 160, niliona ni kama ninazidi kuchelewa.
Nikazidi kukanyaga mafuta nikiwa ni kama nimechanganyikiwa,
vijana wangu niliokuwa nao kwenye gari wakawa wanatazamana
kisha kunitazama kwa macho ya chinichini, nadhani walishagun-
dua kwamba kuna jambo halikuwa sawa.
Sikutaka kuzungumza chochote, mawazo mengi yakawa yanazidi
kupita ndani ya kichwa changu kiasi cha kunifanya niwe ni kama
nimechanganyikiwa. Hatimaye tuliwasili jijini Dar es Salaam na
kwenda moja kwa moja mpaka ofisini.
Tayari ilikuwa ni majira ya saa tano, tukateremka kwenye magari
na kupokelewa na wafanyakazi wenzetu wengi waliokuwa na
shauku kubwa ya kutaka kujua ni nini kilichokuwa kimeendelea.
Yule kijana wa Kisomali alirudishwa kwenye chumba alichoku-
wepo awali kisha mimi na maafisa wawili waliokuwa na nyadhifa
za juu katika kile kikosi maalum cha kuzuia na kupambana na
ugaidi niliokuwa nao eneo la tukio, tukatakiwa kupitiliza moja kwa
moja kwenye chumba cha siri cha mikutano.
Mimi ndiyo angalau nilikuwa na ahueni, wenzangu walionesha
kuchoka kisawasawa, tukaenda moja kwa moja mpaka kwenye
chumba cha siri cha mikutano ambako maafisa wote wa ngazi za
juu, wakiwemo wengine kutoka kitengo cha Presidential Security
Unit (PSU) ambao kazi yao ilikuwa ni kumlinda namba moja, nao
walikuwepo.

171 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Hata wale maafisa wa ngazi za juu kabisa ambao walikuwa


wanashughulikia masuala ya utawala, akiwemo baba yake Saima,
wote walikuwemo kwenye chumba hicho cha mikutano.
Tulipoingia, tulikuta ni kama walikuwa wanatusubiri sisi kwa
sababu kila mmoja alikuwa kimya kabisa. Mkurugenzi wetu ndiye
aliyekuwa akiendesha kikao ambapo baada ya kila mmoja kwenda
kukaa kwenye kiti chake, alivunja ukimya.
Alinitaka nisogee mbele kwenye ‘podium’, kwa maana ya kile
kama kijukwaa kidogo kinachotumika kwenye mikutano, nikaso-
gea mpaka pale. Licha ya uchovu, lakini pia nilikuwa nimechafuka
kisawasawa.
Nilifika pale mbele kwenye podium na kabla sijazungimza
chochote, aliwaeleza watu wote waliokuwepo kwenye chumba
hicho kwamba mimi ndiye niliyekuwa ‘incharge’ wa misheni ile,
akanipongeza kwa kazi nzuri na kutaka nieleze ni nini kilichokuwa
kimetokea, kuanzia mwanzo wa oparesheni mpaka wakati huo.
Ni maelezo ambayo nilikuwa nimeshayatoa mara kadhaa awali
na hata kilichotokea usiku uliopita nilikuwa nimekieleza kwa njia
za kimawasiliano lakini nadhani kwa sababu kuna watu wengine
pale hawakuwa miongoni mwetu, ndiyo maana alitaka nianze upya
kuanzia mwanzo.
Basi ilibidi nianze upya kueleza kila kitu kuanzia jinsi tulivyopa-
ta taarifa kuhusu watu wanaotia mashaka waliokuwa wakiishi kwa
kificho Kijitonyama Kisiwani. Nilieleza kila kitu kwa ufasaha na
utulivu mkubwa, watu wote wakawa wananisikiliza kwa makini.
Nilieleza jinsi tulivyoianza safari ya kuelekea katika ule ukanda

172 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wa Kibiti na kila kitu tulichokutana nacho kuanzia mwanzo mpaka


mwisho. Sehemu iliyokuwa ngumu zaidi kwangu kuielezea ilikuwa
ni jinsi wahalifu hao walivyofanikiwa kututoroka hata baada ya
kuwa tumeizingira kambi yao.
Tofauti kabisa na ambavyo nilitegemea kwamba pengine nita-
kutana na maswali makali na lawama kuhusu uzembe uliofanyika
mpaka tukashindwa kumtia mikononi mtuhumiwa mkuu na kundi
lake lote, kila mmoja alipiga makofi baada ya kuwa nimemaliza
kuzungumza na kwa heshima, watu wote wakasimama huku
wakiendelea kupiga makofi.
Nilibaki nimeduwaa nikiwa ni kama siamini, moyoni nikajiam-
bia kwamba nilikuwa na kazi kubwa zaidi ya kufanya kwa sababu
watu wote walionesha kukubaliana na kila nilichokifanya, jambo
ambalo kwangu lilikuwa ni kama deni.
Mkurugenzi alinionesha ishara kwamba nirudi nikakae, makofi
yakaendelea kisha watu wote wakakaa na kikao kikaendelea.
“Kwa hiyo kama nilivyowaeleza mwanzo, hii taarifa iliyotolewa
na Ubalozi wa Marekani siyo mpya kwetu kwa sababu tayari
tulishajua na kama mlivyomsikia kijana wetu hapo, kama mambo
yangeenda kama yalivyopangwa, usiku wa jana tulikuwa tunamali-
za mchezo wote,” alisema kisha ukimya ukapita.
“Akili na mbinu wanazozitumia hawa watu ni kubwa sana na
inatakiwa umakini mkubwa katika kushughulika nao lakini nataka
niwahakikishie watu wote hapa ndani kwamba tutafanya kila kili-
cho ndani ya uwezo wetu kulizima jaribio hilo.
“Tayari mikononi tunao watu kadhaa ambao ni muhimu sana ka-

173 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

tika kutupatia taarifa zitakazofanya tujue kwa umakini mkubwa ni


nini kinachoenda kufanyika, lini na kwa namna gani. Hata hivyo,
watu wenye taarifa muhimu wamepitia mafunzo kwa hiyo haita-
kuwa kazi nyepesi kuwafanya watoe taarifa lakini nina uhakika
kwamba tutafanikiwa.
“Naomba nisikie mawazo ya kila mmoja wenu ambaye anadhani
anaweza kuwa na majibu ya maswali tuliyonayo,” alisema mkuru-
genzi kisha wajumbe ambao kama nilivyosema, wote walikuwa ni
maafisa wa ngazi za juu, wakaanza kutoa mawazo yao.
Katika mawazo yote yaliyotolewa, wajumbe wote walikuwa
wakizungumzia zaidi mbinu za kuwatesa watuhumiwa wote tulio-
kuwa nao mikononi mpaka watueleze kwa undani nini walichoku-
wa wamepanga.
Baba yake Samia alipopewa nafasi ya kuchangia, yeye alikuwa
na wazo jingine ambalo lilitufumbua macho.

174 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

8
K
WANZA alianza kwa kuichambua ile ripoti iliyo-
tolewa na ubalozi kwa kina na kwa utaalamu wa
hali ya juu, mambo mengi ambayo hayakuwa yame-
bainika awali, yakawekwa wazi.
Akaendelea kuchambua maelezo niliyoyatoa na
mwisho akaja na hitimisho kwamba tunatakiwa kujua ni wapi
kilipo kitovu cha shughuli za watu hao na tukishalijua hilo, itakuwa
ni rahisi zaidi kuwazidi akili.
Ilibidi atumie ubao maalum uliokuwa mle ndani, akawa anachora
kwa kutumia ‘marker pen’ akijaribu kuonesha kile alichokuwa
anakihisi.
Alianza kwa kuanisha njia kuu zinazoingia Dar es Salaam aki-

175 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

fuatisha maelekezo yaliyokuwa yametolewa na ubalozi katika taar-


ifa zao za Kiintelijensia. Ikaonekana kwamba wakati sote tukiamini
kwamba lazima watuhumiwa waliokuwa na nia ovu ya kusham-
bulia Magogoni watatokea upande wa Kusini, yeye alikuja na jibu
tofauti ambalo lilionekana kuendana na ile taarifa ya ubalozi.
Ikaonekana watuhumiwa au vifaa kwa ajili ya shambulio hilo,
vitaingia kutokea Barabara ya Morogoro na hapo ndipo mawazo
yake yakaja kuungana na ya kwangu.
Watuhumiwa wote wakati tukiwasaka usiku, walionekana kuele-
kea kwenye Hifadhi ya Taifa ya Seolous na hifadhi hiyo, ilikuwa
imechukua eneo kubwa la Mkoa wa Morogoro, kwa hiyo ilikuwa
inalea picha kamili kwamba huenda ngome kuu ya watuhumiwa
hao, ipo katika Hifadhi ya Selous na ndiyo maana kila watuhumiwa
wanapofanya matukio ya mauaji au wakikurupushwa, uelekeo wao
wa kukimbia huwa ni kwenye hifadhi hiyo.
“Kwa hiyo tunatakiwa kwanza kuifumua Selous nje ndani kwa
kushirikiana na wenzetu wa wanyama pori, tukishafanikisha hilo,
ndipo tutakapokuwa na uhakika kwamba tunaweza kulizima jaribio
hilo, kisha vijana wetu wajipange kwa layers kuanzia kwenye
target na kuuweka mji wote kwenye uangalizi wa hali ya juu,”
alisema baba yake Saima, kila mtu akawa anatingisha kichwa.
Ninaposema kwamba baba yake Saima ni miongoni mwa vion-
gozi ambao ni hazina kwa taifa, huwa namaanisha kwa sababu
amejaliwa uwezo fulani wa kipekee wa kuyaona mambo ambayo
wengine hawawezi kuyaona kwa urahisi.
Baada ya uchambuzi wa kina alioutoa, majukumu ilibidi yagawi-

176 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

we upya, mimi na kikosi changu tukatakiwa kupanga upya misheni


nyingine ya kuelekea Seolous kutafuta mahali yalipokuwa maficho
ya watuhumiwa wetu.
Nilipewa muda wa saa 48 pekee niwe nimeikamilisha kazi hiyo,
maafisa wengine wakapewa majukumu kila mmoja kwa nafasi
yake na kikosi cha PSU chenyewe kikatakiwa kuhakikisha namba
moja anaondoka Magogoni haraka iwezekanavyo na kupelekwa
sehemu salama ambayo hakuna mtu yeyote atakayejua na ataende-
lea kukaa huko mpaka tutakapolizima kabisa tukio zima.
Mambo yote haya yalitakiwa kufanyika bila kuamsha taharuki
yoyote kwa wananchi, yaani kwa kifupi misheni nzima ilikuwa
‘classified’ na hakuna mtu yeyote asiyehusika aliyetakiwa kujua
chochote kinachoendelea.
Kabla ya kuanza upya misheni iliyokuwa mbele yetu, niliomba
nipewe saa kadhaa za kuwahoji upya watuhumiwa wote tuliokuwa
tunawashikilia kwa sababu niliamini wao ndiyo wanaoweza kura-
hisisha kazi yangu.
Mtu wa kwanza kurudia kumhoji alikuwa ni Sanipha, yule mwa-
namke tuliyemkamata akiwa na wale mabinti Kijitonyama Kisi-
wani kwenye ile nyumba iliyokuwa inatumika kama maficho ya
wahalifu hawa.
“Nimerudi tena kwako kwa mara nyingine kama nilivyokuahidi!”
nilisema kwa upole baada ya kuwa ameletwa kwenye kile chumba
cha mahojiano. Moyo wake ulikuwa na wasiwasi mkubwa na hata
alivyokuwa akinitazama, ni kama alikuwa na jambo ndani ya moyo
wake.

177 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Ulikuwa unajua kwamba mumeo na wenzake wana kambi zao


Kibiti?”
“Ndiyo lakini alikuwa akiniambia kwamba ni kambi za kununua
korosho!”
“Kwa nini hukunieleza kuhusu hili?”
“Hukuniuliza!”
“Abdulwaheed Jabal ndiyo jina la mumeo si ndiyo?”
“Ndiyo! Lakini anavyo vitambulisho vingine ambavyo vina picha
yake lakini vina majina tofauti!”
“Tukisema mumeo ni gaidi tutakuwa sahihi!” nilimuuliza, akani-
tazama kwa mshtuko kidogo kisha akajiinamia.
“Tukisema wewe pia ni gaidi na unashirikiana na mumeo ni
sawa?” nilimbana, akanitazama tena kwa mshtuko kisha akatingi-
sha kichwa kwa nguvu kukataa.
“Unajua adhabu ya mtu anayekutwa na hatia ya kufanya matukio
ya ugaidi au kushirikiana na magaidi?” nilizidi kumbana.
Ilikuwa ni lazima nimfanye awe na hofu ndani ya moyo wake ili
atoe ushirikiano kikamilifu kwa sababu ilionesha kwamba kumbe
kuna mambo mengine mengi alikuwa akiyajua lakini kwa kuwa
sikuwa nimemuuliza, alibaki nayo moyoni mwake.
“Nilikuahidi kuanzia mwanzo kwamba nitakulinda wewe na
hawa mabinti zako, si unaikumbuka ahadi yangu?”
“Ndiyo naikumbuka!”
“Sasa kuna vitu vichache vimebadilika kwenye ahadi hiyo!
Mumeo na wenzake wanapanga kufanya tukio kubwala kigaidi
ndani ya siku chache zijazo kama ambavyo mwenyewe uliniambia.

178 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Sasa ushirikiano ambao unatakiwa kunipa, siyo tu wa kujibu mas-


wali ninayokuuliza, bali ni wa kuzuia shambulio hilo lisitokee!
“Usipofanya hivyo na kweli shambulizi likatokea, sitakuwa tena
na namna ya kukusaidia, wewe na binti zako mtahesabika kuwa
magaidi na sheria itachukua mkondo wake, kwa hiyo uamuzi ni
wako!” nilisema, nikamuona akitetemeka kuliko kawaida, akajiin-
amia chini kwa sekunde kadhaa.
Alipoinuka, macho yake yalikuwa mekundu huku akiwa analeng-
walengwa na machozi.
“Niulize chochote nitakueleza!”
“Bila shaka ulishasikia mipango iliyokuwa inapangwa kuhusu
hili tukio lililopo mbele yetu. Nataka uniambia japo kwa kifupi ni
nini walichokuwa wanapanga!”
“Hili pia naamini nilishakujibu! Nilisikia wakizungumzia kuhusu
washambuliaji wa kujitoa mhanga ambao miongoni mwao walita-
kiwa hawa mabinti!”
“Hilo ulishanieleza, nataka kujua kuhusu mipango, wataanzia
wapi na itakuwaje!”
“Nilisikia wakizungumzia sana neno Selous lakini mimi sijui
maana yake ni nini!”
“Uliishi Kilwa, unashindwaje kujua Selous ni nini?”
“Kwamba ni mbuga za wanyama? Sidhani lakini ni neno
walilokuwa wanalitaja sana.”
“Kingine?”
“Kariakoo!”
“Kariakoo imefanyaje?”

179 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Kuna nyumba moja ipo Kariakoo, nilisikia wakisema huko


ndiyo kuna vifaa vingine na watu wa kufanya hiyo kazi!”
“Kwa nini hukuniambia haya yote?”
“Unisamehe tu, kichwa kilikuwa kimechanganyikiwa!”
“Kariakoo ni kubwa!”
“Sijui ni wapi lakini Kariakoo, kuna sehemu wanauza vifaa vya
ujenzi!” alisema, mapigo ya moyo yakanilipuka kuliko kawaida.
Kumbe adui alikuwa jirani pengine kuliko tulivyokuwa tunafikiria
kwa sababu ukweli ni kwamba kutoka Kariakoo mpaka Magogoni
ni jirani sana.
“Kuna kingine chochote ambacho unadhani kinaweza kuwa
muhimu kwangu kukijua?” nilimuuliza, akashusha pumzi ndefu
kisha akawa anaangalia upande wa juu wa chumba kile, mahali
kulipokuwa na kamera za siri ambazo zilikuwa zimefungwa kwa
utaalamu wa hali ya juu.
Akili yangu ilinicheza haraka, nikahisi kuna kitu anataka kunia-
mbia lakini pengine anaogopa kukisema akiamini kabisa kwamba
kamera zilikuwa zikirekodi kila kitu.
Nilichokifanya ilikuwa ni kumgeuzia ile ‘diary’ yangu na kumpa
kalamu, akanitazama usoni kisha akashusha pumzi ndefu, akai-
sogeza ile ‘diary’ kisha akawa anaandika kitu huku mara kwa mara
akinitazama usoni. Alipomaliza alinisogezea ile ‘diary’, nikawa
nataka kusoma lakini alinizuia kwa ishara.
Niliifunga ile ‘diary’ huku kalamu ikiwa kwenye ule ukurasa ali-
poandika kile alichokiandika, nikabonyeza kifaa cha mawasiliano
na muda huohuo, maafisa watatu waliingia, wawili wakiwa ni wa

180 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kike na mmoja wa kiume, nikawapa ishara ambapo walimuinua na


kumtoa.
Ni hapo ndipo nilipopata nafasi ya kusoma kile alichokuwa ame-
andika, moyo ukanilipuka kuliko kawaida lakini nikajitahidi kufi-
cha hisia zangu, nikashusha pumzi ndefu na muda mfupi baadaye,
yule mzee wa Kisomali aliingizwa mle ndani kwa sababu niliagiza
baada ya yule mwanamke, yeye ndiyo afuatie.
“Nataka jina la nyumba na mtaa Kariakoo!” nilimuuliza baada ya
kuwa wale vijana waliomleta wametoka.
“Sielewi unazungumzia nini!”
“Huu siyo muda wa mchezo mzee!” nilisema huku nikiinuka pale
nilipokuwa nimekaa, nikiwa tayari nimeshapanic kwa sababu ali-
kuwa anataka kuleta masihara katika muda ambao kila mtu moyo
wake ulikuwa ukimuenda mbio.
“Nani anayejua kama upo hapa?” nilimuuliza huku nikichomoa
bastola kiunoni na kumsogelea.
“Naweza kukumwaga ubongo na ukafa hapahapa na hakuna mtu
yeyote atakayejua nini kilichokutokea na hata mwili wako hautaku-
ja kupatikana mahali popote, unanielewa?” nilisema nikiwa nime-
shamfikia mwilini na kumkaba kooni kwa kutumia mkono mmoja
huku ule mwingine nikimkandamiza na ‘bomba’ kichwani.
Akili hazikuwa zangu tena, muda uliokuwa mbele yangu hauku-
tosha kabisa kufanya michezo na mtu yeyote, nikazidi kumkaba
kwa nguvu mpaka akaanza kutapatapa kama anayetaka kukata
roho.
“Kenny! Unafanya nini?” ilisikika sauti ya mkurugenzi kwenye

181 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kifaa cha mawasiliano lakini sikuijali.


“Utasema, utake usitake!” nilisema na kumsukuma kwa nguvu,
kwa kuwa alikuwa amefungwa pingu mikononi kwa nyuma,
alikosa balansi na kuanguka na kiti mpaka chini, akawa anakohoa
mfululizo kwa sababu nilikuwa nimemkaba kisawasawa kabla ya
kumsukuma.
“Leo utaeleza kila kitu,” nilisema huku nikiirudisha bastola
kiunoni, nikabonyeza kifaa cha mawasiliano na muda huohuo
mlango ukafunguliwa.
“Mpelekeni ‘basement’, naona analeta mchezo huyu, leo tutajua
kati yangu na yeye nani mjanja,” nilisema huku midomo ikiteteme-
ka.
‘Basement’ lilikuwa ni jina la chumba cha mateso kilichokuwa
chini ya ardhi, mahali ambapo wahalifu wanaojifanya manunda
walikuwa wakipelekwa kwenda kuteswa mpaka waseme ukweli.
Tayari nilishapandwa na jazba kali na nilikuwa tayari kwa kazi,
moyoni nikawa najisemea ‘hanijui vizuri huyu’.
Alinyanyuliwa harakaharaka na kuanza kukokotwa kuelekea
‘basement’, na mimi nikawa nafuata nyuma huku nikiwa ni kama
nimechanganyikiwa kwa hasira.
Haukupita muda mrefu tukawa tayari tumeshuka mpaka kule
chini, nikawataka watu wote watoke na kuniacha na yule mzee wa
Kisomali, akawa anatazama huku na kule akiwa haelewi ni nini
kinachoenda kumtokea.
Mazingira ya chumba pekee yalitosha kumvuruga kwa sababu

182 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kulikuwa na zana za kila aina za kushughulika na watu wa dizaini


yake.
“Bila shaka sasa tutazungumza lugha moja na naamini tutaelewa-
na,” nilimwambia huku nikivua saa niliyokuwa nimeivaa mkononi,
nikakunja mikono ya shati maalum la kazi nililokuwa nimelivaa.
Nilichomoa pia vifaa vya mawasiliano nilivyokuwa navyo mwil-
ini, nilitaka nibaki mwepesi kwa kazi moja tu iliyokuwa mbele
yangu. Baada ya kuhakikisha kila kitu cha muhimu nimekitoa kwe-
nye mwili wangu na kubaki mwepesi, nilimsogelea pale kwenye
kiti cha chuma alichokuwa amekalia, akiwa amefungwa pingu.
“Nataka jina la nyumba na mtaa Kariakoo!” nilirudia maelezo
yangu, safari hii kwa sauti ya ukali.
Kwa kumtazama, yule mzee alikuwa na umri wa kukaribia kulin-
gana na marehemu baba yangu kama angekuwa hai lakini kwenye
kazi hakuna kitu kama hicho. Mazoezi magumu na yanayoleta uc-
hungu mkali kwenye moyo, yalifanya nisiwe na moyo wa kuwaza
mambo hayo kabisa ninapokuwa kwenye kazi.
Nadhani hali hii pia wanayo watu wote waliopitia mafunzo ma-
gumu, unapokuwa kwenye kazi hata kama mhusika ni baba yako
mzazi, unavaa roho fulani ya ajabu kabisa ambayo inakufanya uwe
unawaza jambo moja tu, kupata kile unachokitaka!
“Sijui chochote kijana wangu, utaniua bure! Nina matatizo mengi
ya kiafya.”
“Utakufa kweli, wewe endelea kuleta mchezo,” nilimwambia
kwa ukali zaidi, huku nikianza kupanga vifaa vyangu vya kazi.
Kwa jinsi nilivyokuwa nakusanya vifaa utafikiri fundi wa ku-

183 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

chomelea vyuma, aliingiwa na hofu kubwa ndani ya moyo wake,


hofu ambayo niliweza kuiona waziwazi kwa sababu kwanza
mazingira ya chumba chenyewe yalikuwa ya kutisha kisawasawa,
ukisikia ‘basement’ basi ujue ni ‘basement’ kwelikweli.
“Simama!” nilisema huku nikimkwida nguo aliyokuwa amevaa
na kumnyanyua pale alipokuwa amekaa. Mazoezi niliyokuwa
nayafanya, yalitosha kunifanya niwe na nguvu kama faru dume, ni-
kamnyanyua kwa urahisi na kumkokota mpaka katikati ya chumba,
mahali ambapo palikuwa na ‘hook’, chuma kama vile vinavyotu-
mika kuning’iniza nyama buchani, kikiwa kimechomoza kutokea
kwenye ukuta wa juu wa kile chumba.
Nikamfungua pingu kwenye mikono yake kwa nyuma kisha nika-
mfunga pingu nyingine maalum ambazo zilikuwa kubwa na nzito
kuliko zile za kawaida, zikiwa zimeunganishwa kwa mnyororo.
Nilisogea ukutani, mahali ambapo palikuwa na kifaa maalum
cha kuishusha ile ‘hook’, nikabonyeza, ikashuka mpaka usawa wa
kichwa chake, nikasogea na kuchomeka mnyororo wa pingu nili-
yokuwa nimemfunga.
“Kijana wangu, naomba tusifike huku! Nionee huruma mzee
wako nina kisukari!” alisema lakini nikawa ni kama sijamsikia.
Nilirudi kwenye ile swichi, nikabonyeza na ile ‘hook’ ikaanza ku-
panda juu taratibu na haukupita muda mrefu, akawa ananing’inia,
nikabonyeza tena swichi na ile hook ikaganda palepale.
Yule mzee sasa akawa ananing’inia huku akizungushwa kwenda
huku na kule kama yupo kwenye bembea, mikono yake iliyofung-
wa pingu ngumu ikiwa ndiyo iliyobeba uzito wote wa mwili wake,

184 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

akawa anaendelea kunisihi sana nisiendelee na chochote na yupo


tayari kutoa ushirikiano.
Sikuonesha kama nilikuwa namsikiliza, nikasogeza meza ya chu-
ma jirani naye, nikachukua vifaa kadhaa pamoja na kiboksi kidogo
kilichokuwa na zana zote za kumlazimisha mtu atoe maelezo kwa
njia ya mateso na kukifungua.
Nilichomoa ‘gloves’ kama zile zinazotumika hospitali na kuz-
ivaa, akawa anaendelea kunisihi safari hii akianza kulia.
Kwa kuwa nilishajua kwamba lazima amepitia mafunzo ya
kigaidi, ilikuwa ni lazima kuhakikisha kiwango cha hofu kimefika
juu kabisa kwenye moyo wake ndipo angeweza kutoa ushirikiano
na kama ingeshindikana, pia ilikuwa ni lazima kumsababishia
maumivu makali zaidi ambayo yangevuka kiwango anachoweza
kustahimili.
Hizo mbinu mbili ndiyo msingi mkubwa katika kitu ambacho
kitaalamu huwa tunakiita ‘The Art of Torture’ ambacho tafsiri yake
kwa Kiswahili ni sanaa ya kutesa. Haya ni mambo ambayo watu
kama sisi tunafundishwa kabisa darasani kiasi kwamba hata kama
mtu alikuwa mgumu kutoa ushirikiano kwa kiasi gani, ukitumia
mafunzo vizuri, mwenyewe atanyoosha maelezo.
Kama nilivyoeleza hapo juu, mbinu ya kwanza huwa ni kupan-
dikiza hofu kwenye moyo wa mtu na kiwango cha hofu kinatege-
meana na makosa anayokabiliwa nayo mtu, kiwango cha mafunzo
alichonacho na utimamu wa mwili.
Nilichokuwa nakifanya kwa wakati huo, ilikuwa ni kupandisha
kiwango cha hofu ndani ya moyo wake kwanza kisha baada ya

185 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

hapo, ningepima mwenyewe kama niendelee na hatua ya pili au la!


“Najua kila kitu kuhusu wewe, ninapokuwa nakuuliza jambo usi-
fikiri nacheza hapa, ukifanya mzaha huu unaweza kuwa mwisho wa
maisha yako. Hutatoka humu ndani leo ukiwa hai mpaka unyooshe
maelezo,” nilisema huku nikiendelea kuweka zana zangu sawa.
Nikachomoa kitu kama mkasi mkubwa, ile inayotumika kukatia
mabati, nikamsogelea huku nikiendelea kuujaribu makali yake.
“Nitaondoa kiungo kimoja baada ya kingine kwenye mwili wako,
nitaanza na vidole vya miguuni, kimoja baada ya kingine, nitaha-
mia kichwani kuanzia mdomoni mpaka machoni kisha nitamalizia
na sehemu zako nyeti,” nilisema kwa sauti ya ukali.
Huwezi kuamini, hata kabla sijamgusa yule mzee, tayari alikuwa
analia kama mtoto akinisihi sana nimuonee huruma.
“Nataka jina la nyumba na mtaa Kariakoo!”
“Nyumba namba 320 Mtaa wa Aggrey!”
“Unanidanganya!”
“Hapana, namaanisha ninachokisema! Mtaa wa Aggrey!”
“Nyoosha maelezo vizuri!”
“Kuna duka la simu linaitwa Tawheed Phone Accessories! Ndani
ya hilohilo duka kuna njia ya kutokea upande wa ndani!”
“Ni nini kinachofanyika huko?”
“Sitakiwi kusema, wataniua!”
“Usiposema pia nitakuua vilevile, kwa hiyo uchaguzi ni wako!”
“Ndiyo assembling point!”
“Ukimaanisha nini?”
“Ndipo shughuli zote zinapofanyikia!”

186 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Magogoni ni lini?”
“Usiku wa Ijumaa.”
“Ijumaa ipi?”
“Ya keshokutwa!”
“Unafahamu nini kuhusu Selous?”
“Ngome kuu!”
“Location?”
“ Mashariki mwa Stiglers Gorge, Kilometa nne kutoka kwenye
maporomoko!”
“Utabaki ukiwa unaning’inia mpaka nitakapaoenda kuhakiki-
sha kwanza Kariakoo kama ulichokisema ni sahihi na kama siyo
sahihi, utabaki hivyohivyo mpaka tutakapoenda na kurudi Selous!”
nilimwambia, akatingisha kichwa harakaharaka kukubali. Mpaka
hapo nilikuwa na uhakika kwamba alichokisema kilikuwa ni kweli.
Nilisogea kwenye ile swichi, nikabonyeza ile swichi, ‘hook’
ikashuka kidogo chini na kumuwezesha miguu yake kukanyaga
sakafuni, nikamsikia akishusha pumzi ndefu akiwa ni kama haami-
ni kama nimemfanyia ‘fair’ kiasi kile.
Harakaharaka nilikusanya vitu vyangu kikiwemo kifaa maalum
cha kurekodia sauti kilichokuwa kinarekodi maelezo yote ali-
yokuwa akiyatoa yule mzee wa Kisomali. Nilizima taa na kufanya
chumba chote kiwe na giza totoro, nikamuacha palepale na kutoka
nje.
Niliona ni kama hatua ninazopiga zinanichelewesha, nikawa
nakimbia huku nikiendelea kuvaa vizuri vifaa vyangu vya ma-
wasiliano, nikielekea kwenye ile ofisi walipokuwepo mkurugenzi

187 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

na timu nzima.
“Uko sawa?”
“Niko sawa chief! Kuna taarifa mpya,” nilisema baada ya kuin-
gia kwenye chumba hicho na kudakwa juujuu na mkurugenzi wetu
ambaye alionekana kuwa na shauku kubwa kuliko wengine wote
waliokuwepo ndani ya chumba hicho.
“Nyumba namba 320 Mtaa wa Aggrey! Kuna duka la simu liit-
walo Tawheed Phone and Accessories,” nilisema huku nikihema.
Watu wote wakatulia wakiwa wamenizunguka, wakiwa na
shauku kubwa ya kutaka kusikia nitakachokisema.
“Hicho ndiyo kituo mipango yote inapofanyika, ikiwa ni pamoja
na kukusanya na kuunda silaha zitakazotumiwa na walipuaji wa
kujitoa muhanga ambao ndiyo waliopangwa kufanya shambulizi
Magogoni,” nilisema, nikaona kila mtu amepigwa na butwaa.
“Tukio limepangwa kufanyika usiku wa Ijumaa, maana yake ni
kwamba tuna siku nne tu kuanzia leo kama taarifa za kiintelijensia
zilivyoeleza,” nilisema, hofu ikazidi kutanda kwenye moyo wa kila
mmoja.
“Kuhusu Selous, kama tulivyobaini awali, huko ndiko ilipo
ngome yao kuu. Mashariki mwa Stiglers Gorge, kilometa nne
kutoka kwenye maporomoko ya Mto Rufiji!” nilisema na kuhitimi-
sha, ukimya ukapita mle ndani, kila mtu akitafakari yake.
“Nashauri kikosi kilichotakiwa kwenda Selous, kianzia kwanza
Kariakoo Mtaa wa Aggrey!” alisema baba yake Saima huku akini-
tazama, mkurugenzi naye akaunga mkono hoja hiyo na karibu kila
aliyekuwa mle ndani akakubalianana kilichosemwa.

188 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Nilishajua kwamba kila mmoja alikuwa akinitegemea mimi


kusimama mstari wa mbele kwa hiyo sikutaka kuwaangusha, ni-
kakubaliana na maagizo mapya lakini pia nikaomba vikosi vina-
vyohusika na masuala ya hifadhi ya wanyamapori kwa maana ya
TFS, TANAPA na TAWA, vyenyewe ndiyo vituongoze kwenda
mstari wa mbele kwa sababu wao ndiyo wanaoielewa zaidi Hifadhi
ya Taifa ya Selous.
Wazo hilo pia liliungwa mkono na kila mmoja lakini tahadhari
ikatolewa kwamba wao wanachotakiwa kukifanya, ni kuzingira
eneo lote kuzuia mtu asiingie wala kutoka lakini hawatakiwi kuin-
gia kwenye mapambano ya aina yoyote kwa sababu hawana ujuzi
wa masuala ya ugaidi, japo nao ni askari.
Hakukuwa na muda wa kupoteza na safari hii, nilishangaa kuona
hata mkurugenzi mwenyewe pamoja na viongozi wengine wa juu,
akiwemo baba yake Saima, wakianza kuelekea ‘changing room’,
chumba maalum cha kubadilishia nguo za kiofisi na kuvaa nguo
za mapambano kwa maana ya kombati, vizibao vya kuzuia risasi
pamoja na kukabidhiwa silaha, tayari kuingia uwanja wa mapam-
bano.
“Niliona anakuandikia kitu kwenye diary yako! Ni nini?” alini-
uliza baba yake Saima tukiwa tunaendelea kubadilisha nguo kule
‘changing room’.
“Nakifanyia kazi kwanza nitakujibu nikishamaliza uchunguzi
wangu,” nilimjibu na kwa bahati nzuri akanielewa kwa haraka.
Ni kweli Sanipha aliwa ameniandikia kitu mle ndani wakati
nikimhoji lakini suala lenyewe lilikuwa zito kidogo kwa hiyo

189 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

niliamua kulifanyia uchunguzi wa chinichini mpaka nipate majibu,


kisha ndiyo nije kutoa ripoti.
Mimi ndiyo nilikuwa wa kwanza kumaliza kubadilisha mavazi ya
awali ambayo kiukweli yalikuwa na hali mbaya kutokana na puru-
kushani za siku nzima ya jana, ikiwemo kukesha kule porini.
Baada ya kumaliza, nilitoka nje harakaharaka ambapo vijana
wangu wote niliopewa jukumu la kuwaongoza, walikuwa wame-
shakaa ‘standby’, wakisubiri maelekezo kutoka kwangu.
“Mtaa wa Aggrey si mnaufahamu?” niliwauliza wakiwa wameni-
zunguka, nikawapa maelekezo ya nini cha kufanya na baada ya kila
mmoja kuwa ameelewa, niliwagawa kwa makundi.
Ilikuwa inatakiwa tuuzingire mtaa huo kutokea pande zote kabla
ya kuvamia duka husika na safari hii sikuwa nataka kosa lolote
litokee tena na kusababisha watuzidi akili na kutoroka.
Mpaka tunatoka na kuianza safari ya kuelekea Kariakoo, ilikuwa
ni takribani saa tano za asubuhi, vikosi vyote vikaondoka kama
nilivyotoa maelekezo, na huku nyuma viongozi nao wakaondoka
kwenda kutupa usaidizi endapo tungezidiwa.
Kichwa changu hakikuwa kimetulia hata kidogo, nilikuwa najua
jinsi Mtaa wa Aggrey ulivyokuwa na pilikapilika nyingi hususan
muda wa asubuhi na mchana, nikawa naendelea kutafakari njia
nyepesi zinazoweza kufanya wananchi wa kawaida wasiohusika,
wasijue chochote kinachoendelea.
Hatimaye tuliwasili Kariakoo huku nikiendelea kuwasiliana na
vijana wangu wote kwa karibu kabisa, kila mmoja akawa anafuata
maelekezo kwa usahihi kabisa.

190 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Baada ya kuhakikisha kwamba kila mmoja ameshafika kwenye


eneo alilopangiwa kuwepo kabla ya kuanza rasmi kwa oparesheni
hiyo, nilitoa maagizo ya kuanza rasmi kwa oparesheni hiyo.
Kitu cha kwanza, ilikuwa ni kuweka vizuizi visivyoonekana
kwenye maeneo yote ambayo yalikuwa yakiingia na kutoka kwe-
nye mtaa ule, vikiwemo vichochoro vinavyotumiwa na mafundi wa
simu kuingia na kutoa kwenye Mtaa wa Aggrey. Kwa wazoefu wa
Kariakoo watakuwa wananielewa vizuri.
Wakati hayo yakiendelea, shughuli za kawaida zilikuwa zikien-
delea Kariakoo kama kawaida, baadhi ya watu ambao wapo makini
wakaanza kushtuka kutuona tukisonga mbele tukiwa na silaha
nzitonzito.
Ndani ya dakika chache, tayari tulikuwa tumefika kwenye duka
tuliloelekezwa, mimi nikiwa mbele. Tulivamia kama nyuki, nikan-
yanyua silaha juu na kupaza sauti kuwataka watu wote waliokuwa
ndani ya duka hilo, kunyanyua mikono yao juu na kulala chini
taratibu.
Mwanzo purukushani kubwa ilitokea, wengi wakidhani pengine
kulikuwa na tukio la ujambazi lakini nikajitahidi kutoa maelekezo
ya watu wote kutulia kwani tulikuwa kazini.
Lilikuwa ni duka kubwa na la kisasa la simu za mkononi na vifaa
vingine vya kielektroniki, ambalo hakuna mtu angeweza kudhani
kwamba kuna shughuli zozote za kihalifu zinaendelea mle ndani.
Kwa kuwa ramani nzima mimi ndiye niliyekuwa nayo, niliso-
gea mpaka upande wa wauzaji ambako kulikuwa na madirisha na
milango ya vioo kwa nje lakini kwa ndani kulikuwa na mageti na

191 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

madirisha ya chuma.
“Fungua tafadhali,” nilisema huku nikitoa kitambulisho, wale
wauzaji waliokuwa wamejifungia upande wa ndani, wakawa
wanatetemeka, nao wakiwa ni kama hawajui ni nini kilichokuwa
kinaendelea.
Binti mmoja mdogo ambaye alionekana kuwa ndiye aliyekuwa
akihusika na kupokea fedha kwa wateja na kuwapa risiti, alifungua
mlango mkubwa huku akitetemeka kuliko kawaida, nikawa wa
kwanza kuingia kule ndani walikokuwa wakihifadhia fedha.
“Simama!” nilimuamuru yule binti aliyefungua geti, akasimama
huku akitetemeka kuliko kawaida.
“Hakikisha mauzo yako yote na vitu vya thamani vimefungiwa
kwenye droo zake, sisi siyo majambazi kama nilivyokueleza,”
nilisema, harakaharaka yule binti akafanya kama nilivyomuele-
keza, maburungutu ya fedha yaliyokuwa yamekaa kihasarahasara
yakafungiwa kwenye droo kisha nikatoa ishara kwa vijana wangu
nao kuingia upande ule.
“Najua kuna mlango wa kutokea upande wa pili, nataka ufungue
haraka,” nilimwambia huku bunduki yangu ikiwa mkononi.
“Haturuhusiwi, ni bosi mwenyewe ndiye anayejua namna ya
kuufungua!”
“Nimekwambia fungua, unataka nitumie nguvu?” nilimtisha
kwa kumnyooshea bastola, akiwa anatetemeka akanionesha kwa
kidole kwenye kabati kubwa la vioo lililokuwa upande wa ukutani,
nikawapa ishara vijana wangu walisogeze.
Walipolisogeza, wote tulipigwa na butwaa kugundua kwamba ni

192 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kweli kulikuwa na mlango mwingine ambao ulitengenezwa kwa


namna ambayo huwezi kudhani ni mlango, nikamgeukia yule binti
na kumpa ishara aufungue.
Akatoa funguo kwenye moja ya droo za pale ndani na kuusoge-
lea, akachagua funguo na kuufungua, nikamnyooshea tena bunduki
na kumtaka yeye ndiyo atangulie kuingia ndani, akatingisha kich-
wa kukataa huku akianza kulia.
“Wataniua!” alisema huku akiendelea kutingisha kichwa, kufum-
ba na kufumbua kikasikika kishindo kikubwa kutokea kule ndani.
Mambo yalikuwa mazito kuliko nilivyokuwa nimefikiria,
kishindo kilichosikika kilikuwa ni kishindo cha mlipuko ambao
kwa harakaharaka sikuelewa ni nini ingawa akili na uzoefu wangu
vilinifanya niamini kwamba lilikuwa ni bomu la kutegwa. Baada
ya kishindo hicho, umeme ulizimika jengo zima.
“Hakuna atakayekuua, nitakulinda,” nilisema huku nikimuweka
mgongoni kwangu kisha mimi nikatangulia, nikawa nataka aniele-
keze namna ya kuingia.
Kuna ngazi upande wa kulia za kushuka chini,” alisema, haraka-
haraka nikaingiza mkono kwenye mfuko wa ‘kombati’ niliyokuwa
nimevaa na kutoa tochi ndogo yenye mwanga mkali ambayo muda
wote huwa natembea nayo.
Nikaiwasha baada ya kuwa nimeshaingia kule ndani kulikokuwa
na giza totoro baada ya umeme kukatika, nikawa namulika huku
na kule na kweli nilifanikiwa kuziona ngazi zilizokuwa zinaele-
kea upande wa chini wa jengo hilo, nikazima tochi kwa sababu
nilishakadiria uelekeo wake, nikatoa amri kupitia vifaa vya ma-

193 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wasiliano ya vikosi vyote kukaa kwenye hali ya tahadhari kubwa.


Vijana wangu nao tayari walishakuwa wameingia, wakajipanga
kama ambavyo tulishapeana maelekezo, mimi nikiwa mbele.
Nikiwa nimeshashuka ngazi kama tatu, nilishtukia kitu kama
moshi mzito ukifuka kutokea kule chini, ikabidi niwashe tena tochi
lakini kwa umakini mkubwa, kweli ulikuwa ni moshi mzito mwe-
upe, nikawa nimeshaelewa ni nini kilichokuwa kinaendelea.
Ulikuwa ni moshi wa vifaa maalum vya kijeshi ambavyo kita-
alamu huitwa ‘smoke grenade’ au kwa lugha nyepesi ‘bomu la
moshi’ ingawa kiufasaha haikuwa sahihi kuviita bomu. Kwa
mwonekano wake, ni kweli vinafanana na bomu lakini utendaji
kazi wake huwa tofauti.
Kazi yake kubwa huwa inakuwa ni kutoa moshi mwingi ambao
huweza kuficha kabisa usione kinachoendelea kwenye eneo kifaa
hicho kilipolipuliwa, hata kama ni mchana. Tofauti yake na ma-
bomu ya machozi ni kwamba haya yenyewe moshi wake huwa
hauwashi wala kupalia.
Kwa mafunzo niliyokuwa nayo, vifaa hivi vilikuwa vinatumika
sana pale mnapokuwa mnataka kufanya jambo kwenye eneo am-
balo adui anaweza kuwaona vizuri, kwa mfano mnapotua kwe-
nye helikopta, mnapotaka kuwaokoa wenzenu waliojeruhiwa au
mnapokuwa mnataka kumtoroka adui.
Moshi huwa ni mwingi kiasi ambacho hata ukimulika kwa tochi
au ukivaa vifaa maalum vya kukusaidia kuona, huwezi kuona cho-
chote kinachoendelea. Akili za haraka zikanituma kugundua ni nini
kilichokuwa kinafanywa na watu waliokuwa kule chini.

194 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Kwa lugha nyepesi ni kwamba walikuwa wanataka kutoroka


baada ya kugundua kwamba tayari walishavamiwa, mapigo ya
moyo wangu yakawa yananienda mbio kuliko kawaida kwa sababu
sikuwa tayari kuona tena tunazidiwa akili kirahisi namna hiyo.
Harakaharaka niliwasiliana na vikosi vyote kwa kutumia vifaa
vya mawasiliano nilivyokuwa nimevivaa na kuomba msaada wa
kuhakikisha hakuna mtu yeyote anayetoka na kutoroka kwa aina
yoyote.
“Kuna mlango mwingine wa kutokea humu zaidi ya huu?” nilim-
uuliza yule msichana wa pale kaunta ambaye nilikuwa nashuka
naye, akiwa mgongoni kwangu, akitetemeka kuliko kawaida.
“Hapana, mlango ni mmoja tu, hakuna mwingine,” alisema kwa
sauti ya kunong’ona, akiwa amenishikilia kwenye mkanda kwa
nguvu. Niliongeza kasi ya kushuka na umakini wa hali ya juu,
nikafanikiwa kuwa wa kwanza kushuka kule chini.
Ilikuwa ni kama stoo ya kuhifadhia mizigo kwani kulikuwa na
maboksi mengi yakiwa yamepangwa, moshi nao ukawa unazidi ku-
ongezeka na kufanya niwe natumia zaidi mkono mmoja kupapasa
huku mkono mwingine ukiwa umeikamatia vizuri bunduki yangu.
Ilivyoonesha ni kama lile bomu la moshi lilikuwa limerushwa ule
upande wa ngazi za kushukia kule chini tu kwani kadiri nilivyoku-
wa nazidi kusonga mbele huku vijana wangu nao wakiwa wanani-
fuata, ndivyo moshi ulivyokuwa unazidi kupungua.
Baada ya kama dakika mbili hivi za kusonga mbele kwa tahad-
hari kubwa, hatimaye ule moshi ulipungua kabisa kiasi cha kutu-
fanya tuweze kuona vizuri kule chini.

195 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Mungu wangu!” nilisema baada ya kusonga mbele mpaka kuu-


fikia ukuta wa upande wa pili wa chumba kile kikubwa cha chini
ya ardhi. Ukuta ulikuwa umebomoka na kuweka shimo kubwa.
Ni hapo ndipo nilipogundua kile kishindo kilimaanisha nini!
Kumbe baada ya kuwa wameshagundua kwamba tumevamia lile
jengo, walitega bomu ukutani kisha kulilipua, kishindo chake
kikasababisha ukuta ubomoke na kuachia tundu hilo kubwa ambalo
ndiyo walilolitumia kutorokea.
“Haiwezekani!” nilisema kwa sauti ya jazba huku nikisogea kwa
umakini mkubwa kwenye lile shimo, nikimulika kwa tochi. Nili-
chokiona ndani yake kilinimaliza nguvu kabisa. Kulikuwa na kama
handaki kubwa lililoenda kuungana na ile mitaro mikubwa ya chini
ya ardhi ya kupitishia maji machafu.
“They have escaped through sewage system chambers!” (Wame-
toroka kwa kupitia chemba za kupitishia maji machafu!) nilijikuta
nimezungumza kwa Kiingereza, nikarudia tena kwa Kiswahili
kutoa taarifa kwa vikosi vyote, ikawa ni taharuki kubwa isiyo na
kifani, nikamsikia mkurugenzi akitukana matusi ya nguoni akiwa
amechanganyikiwa kabisa.
Akili ni kama zilikuwa zimeniruka na sasa sikujali tena kuhusu
usalama wangu, nikaingia kwenye lile lile shimo kwa kuchuchu-
maa na kuanza kumulika huku na kule. Nikawa nazidi kusonga
mbele kwa kuchuchumaa, vijana wangu nao wakawa wananifuata
huku tukiwa hatujali kabisa harufu kali ya chemba hizo.
Uzuri ni kwamba mvua haikuwa imenyesha kwa sababu kwa
jinsi chemba za Kariakoo zilivyo, mvua ikinyesha zinafurika maji

196 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

machafu ambayo inabidi uwe na roho ya kipekee kuvumilia harufu


yake.
Niliendelea kusonga mbele mpaka nilipofika kwenye kitu kama
‘junction’ hivi, mahali ambapo mabomba makubwa ya chini ya
ardhi, yanakutana sehemu moja. Nilipotokeza tu eneo hilo, nili-
pokelewa na mwanga kutokea juu, kuonesha kwamba mfuniko wa
chemba ulikuwa umefunuliwa kwa juu.
Kwa wasioelewa, mifuniko mikubwa ya chemba za mabomba
makubwa, kama ile unayoiona pembeni au wakati mwingine ka-
tikati ya barabara, huwa inakuwa ni kwenye maeneo yenye ‘junc-
tion’, mahali ambapo mabomba yanakutana na maeneo haya huwa
na aukubwa wa kutosha ili kuwawezesha mafundi kuingi na ku-
toka, hususan pale wanapokuwa wanazibua chemba zilizoziba.
Kama nilivyosema mabomba haya huwa makubwa, mfano wa
‘makaravati’ yanayopitisha maji kutoka upande mmoja wa baraba-
ra kwenda upande mwingine Harakaharaka nikajivuta na kudandia
ngazi zilizokuwa zinapanda juu kuelekea kwenye ule mfuniko wa
chemba.
Sekunde chache tu, tayari nilikuwa nimeshafika juu, nikajivuta na
kutoka, nikashtuka kugundua kwamba kumbe chemba ile ilikuwa
upande wa nyuma wa Mtaa wa Aggrey ambao kwa wakati huo hata
sikuwa najua unaitwaje, nao ulikuwa na pilikapilika nyingi kuliko
kawaida.
Kitendo cha mimi kutoka kwenye chemba nikiwa na silaha, kili-
washtua watu wengi waliokuwa wamepigwa na butwaa katika eneo
hilo, muda mfupi baadaye, vijana wangu nao wakawa wanatoka

197 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kama nyuki, wote tukiwa tumelowa miguuni kwa maji machafu


yenye harufu kali.
Akili ilinituma haraka kutafuta mtu ambaye pengine alikuwepo
eneo hilo kwa muda mrefu ambaye anaweza kuwa ameshuhudia
wakati wale wahalifu wetu wakitoroka kupitia njia hiyo.
“Bosi samahani, mimi ni askari, kuna wahalifu tunawasaka
wametutoroka kupitia huu mfuniko wa chemba,” nilimwambia
mwanaume mmoja wa makamo, aliyekuwa amepaki baiskeli yake
akiuza madafu, akawa ananitazama kwa hofu.
“Bila shaka umewaona!”
“Ndiyo nimewaona.”
“Wameelekea wapi?”
“Kuna Canter ilikuwa imepaki hapo, wamepanda wote na kuon-
doka kwa kasi, tulidhani labda ni mafundi wa kuzibua chemba.”
“Walikuwa wangapi?”
“Kama saba au nane hivi!” alisema.
“Canter ya rangi gani!”
“Ina rangi nyeupe na bluu kwa mbali, imeelekea huku, sasa hivi!”
alisema huku akinionesha kwa kidole, muda huohuo nikatoa taarifa
kwenye vifaa vya mawasiliano na kutaka mitaa yote ya kuzunguka
eneo lile ifungwe haraka iwezekanavyo.
Japokuwa mwanzo watu hawakuwa wakielewa kilichokuwa
kinaendelea, kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele, ndivyo hali
ya taharuki ilivyoanza kuwa kubwa, watu wakiwa hawaelewi ni
nini kilichokuwa kinaendelea.
Kwa kuwa hali ilishafikia hatua ya kuwa tete, ilibidi askari wa

198 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

vikosi mbalimbali wakiwemo FFU wamwagwe kwa wingi kuja


kuongeza nguvu, mitaa ya Kariakoo ikawa ni taharuki isiyo na
mfano, askari wengi wenye silaha wakiwa wanakimbizana huku na
kule.
Foleni ilikuwa kubwa kuliko kawaida kwa sababu ilibidi baraba-
ra zifungwe ghafla ili kuzuia lile gari lisije likatoka na kutokomea
kusikojulikana, ikawa ni mshikemshike wa nguvu.
Licha ya jitihada kuwa zilizotumika, hakukuwa na mafanikio
yoyote ya kuwapata watuhumiwa waliotoroka kutoka kwenye
nyumba ile, baadaye tukaja kufanikiwa kulikuta gari ambalo kwa
mujibu wa mashuhuda ndilo lililotumiwa na wale watuhumiwa
takribani saba au nane kutoroka kutoka Mtaa wa Aggrey, likiwa
limetekelezwa Jangwani, jirani na Makao Makuu ya Klabu ya
Yanga.
Harakaharaka niliwaongoza vijana wangu mpaka eneo gari hilo
lilipokuwa limetelekezwa, tukalizingira na kuwaweka chini ya
ulinzi watu kadhaa waliokuwa eneo hilo, ili watusaidie kupata
taarifa sahihi za mahali walipokimbilia watuhumiwa hao.
Hayo yote hayakuweza kubadilisha ukweli kwambakwa mara
nyingine, oparesheni niliyokuwa nikiiongoza, ilikuwa imefeli.
“Hatujafeli Kenny! Bado tumefanikiwa ingawa siyo kwa asilimia
mia moja, unatakiwa kuongoza upekuzi wa nguvu kwenye lile
duka kule Mtaa wa Aggrey, pia taarifa za gari walilotumia kuto-
rokea mpaka Jangwani zikipatikana, kuanzia usajili wake, mmiliki
wake na mambo mengine, zitatusaidia.
“Hutakiwi kusikitika, kazi iliyopo mbele yetu bado ni kubwa na

199 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kaa nilivyokueleza, wewe ndiye tunayekutegemea,” alisema mku-


rugenzi kupitia simu yangu binafsi baada ya kunipigia muda mfupi
tangu nilipotoa taarifa za kilichotokea pale jangwani.
Kauli yake ilinipa nguvu kwani kabla ya hapo nilikuwa ni kama
nimepagawa, nikashusha pumzi ndefu baada ya kumaliza kuzun-
gumza naye, ikabidi niwakusanye vijana wangu, pale tukawaacha
kikosi cha CSI (Crime Scene Investigation) wakiendelea na zoezi
la kukusanya ushahidi wote kutoka kwenye gari lile sambamba na
kuwahoji watu mbalimbali walioshuhudia gari lile likiwasili eneo
lile.
Taarifa za awali zilionesha kwamba watu hao baada ya kuwasili
eneo hilo wakiwa na gari hilo, waliteremka wakijifanya kuna
mzigo walikuwa wanataka kuusafirisha kwenye magari ya mizigo
yanayopaki eneo hilo kisha wakapotea katika mazingira ya ku-
tatanisha na kuliacha gari hilo palepale.
Maelezo ya mashuhuda, yalionesha pia kuwa kulikuwa na
mchanganyiko wa watu wenyewe, baadhi yao wakiwa ni Waswa-
hili huku wengine wakionesha kuwa na asili ya Kisomali.
Tuliondoka mbiombio na kurudi mpaka Mtaa wa Aggrey na kwa
kuwa sasa hakukuwa tena na uwezekano wa kuwakamata watuhu-
miwa hao, hasa ukizingatia idadi ya watu waliopo Kariakoo, ilibidi
nitoe amri ya vizuizi kuondolewa na sasa kazi ya msako iendelee
kimyakimya ili kupunguza taharuki iliyokuwepo kwa wananchi.
Niliagiza pia askari waliokuwa wamevalia gwanda kutoka FFU,
nao waondolewe na badala yake, tubaki sisi na askari waliokuwa
wamevalia nguo za kiraia. Haikupita muda mrefu, hali ikarudi

200 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kuwa shwari Kariakoo ingawa bado watu wengi walionekana


wakiwa kwenye makundi wakijadiliana kuhusu kilichotokea.
Ilikuwa ni oparesheni ya siri kwa hiyo hakutakiwa mtu yeyote
ambaye hajui chochote, kuambiwa kilichokuwa kinaendelea kwa
sababu za kiusalama, wengi wakawa wanahisi pengine kulikuwa na
tukio la ujambazi ambalo tumefanikiwa kulizima.
Tulirudi kwenye lile duka pale Mtaa wa Aggrey, upekuzi wa kina
ukaendelea kuanzia ndani ya duka ambako sasa watu wote wali-
kuwa wametolewa na kubaki wahusika wa duka hilo ambao wote
walikuwa wamewekwa chini ya ulinzi.
Kwa harakaharaka, tulibaini kwamba taarifa tulizokuwa nazo
zilikuwa na usahihi kwa asilimia kubwa na kilichotushtua zaidi,
ilikuwa ni baada ya kufanikiwa kukuta shehena ya silaha za kivita
kule chini, zikiwemo bunduki, mabomu ya kurushwa kwa mkono,
mabomu ya kutega ardhini, malighafi za kutengeneza mabomu
hatari ya TNT ambayo ndiyo hutumika sana na magaidi pamoja na
vifaa vya kiutengenezea mabomu ya kuvaa mwilini kwa walipuaji
wa kujitoa mhanga.
Alichokuwa amekisema mkurugenzi wetu kilikuwa sahihi kwa
kiasi fulani kwamba hata kama watuhumiwa wamefanikiwa ku-
kimbia, kitendo cha kuwavamia kwenye maficho yao nacho kili-
kuwa ni mafanikio makubwa.
Wote tulibaki tumepigwa na bumbuwazi kwamba inawezekanaje
tukio kubwa la kihalifu namna hiyo linaweza kuwa linaratibiwa ka-
tika eneo lenye pilikapilika nyingi namna hiyo halafu vyombo vya
ulinzi na usalama tukawa hatujui chochote kilichokuwa kinaende-

201 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

lea! Ilikuwa ni kitu cha hatari mno ambacho tusingeweza kukwepa


lawama.
Baada ya upekuzi wa awali, silaha zote ilibidi zitolewe na ku-
pakizwa kwenye magari maalum yaliyofika eneo hilo na kupele-
kwa sehemu husika kwa uchunguzi zaidi, watu wa ‘Forensic’ nao
wakawa wanaendelea na uchunguzi wa ndani zaidi.
Ilibidi mimi na avijana wangu, tuondoke eneo hilo tukiwa tume-
wasomba watu wote ambao tulihisi wanaweza kutusaidia katika
uchunguzi wa kina zaidi, safari ya kurudi ‘kitengoni’ ikaanza.
Kwa muda wote huo nilikuwa najitahidi sana kutuliza kichwa
changu, muda mwingi nikiwa kimya kabisa nikiendelea kutafakari
mambo mengi yaliyokuwa yanaendelea kutokea kwa kasi ya ajabu.
Kuna muda nilikuwa nahisi pengine ni kama nipo ndotoni.
Nikiwa katika hali hiyo ya utulivu, tukirejea ‘getini’, ndipo suala
aliloniandikia Sanipha, yule mwanamke aliyenipa ushirikiano
mpaka kugundua kwamba kumbe kuna ‘chimbo’ lingine la magaidi
Kariakoo, lilipopita ndani ya kichwa changu.
Niliachia mkono mmoja kwenye usukani na kufungua ‘dash-
board’ ya gari nililokuwa naendesha, nikatoa ile ‘notebook’ na
kurudia kusoma alichokuwa ameniandikia mwanamke huyo.
Kwa kifupi ni kwamba alinidokeza kwamba mumewe alikuwa
akishirikiana na baadhi ya maafisa wa vyombo vya ulinzi na usala-
ma ambao ndiyo waliokuwa wanampenyezea taarifa za kila kitu tu-
lichokuwa tukikipanga, kwa malipo ya dola nyingi za Kimarekani.
Hilo lilikuwa ni tatizo lingine kubwa na nilijikuta nikianza
kuamini kwamba pengine watu wanaoshirikiana nao, wanatoka

202 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kitengoni kwa sababu mara nyingi tunapopanga misheni, watu wa


vyombo vingine vya ulinzi na usalama, huwa hawaambiwi moja
kwa moja ni nini kinachofanyika zaidi ya kutakiwa kutupa ush-
irikiano.
Nilianza kuhisi kwamba tukio la yule mtuhumiwa wetu mkuu ku-
toroka katika mazingira ya kutatanisha na kuishia kutuachia simu
yake kwenye gari lililokuwa limebeba mihogo, ilikuwa ni kwa
sababu kuna mtu kutoka ndani yetu alimtonya kwamba tumemu-
wekea mtego.
Nilitafakari pia kuhusu tukio la watuhumiwa wetu kututoroka
katika mazingira ya kutatanisha tulipoenda kuvamia kambi yao ya
muda iliyopo kule Jaribu Mpakani na niliamini pia lazima kutaku-
wa kuna mtu amevujisha taarifa za ile oparesheni tuliyotoka kui-
fanya muda huo Kariakoo pengine ndiyo maana watuhumiwa wote
walifanikiwa kuwa mbele yetu hatua moja na kututoroka.
Kama huo ndiyo ungekuwa ukweli, maana yake ni kwamba
kulikuwa na tatizo kubwa zaidi pengine kuliko hata kila mtu
alivyokuwa anahisi na kama tungeenda kwa mwendo huo, nilikuwa
na uhakika kwamba hatutaweza kufanikiwa kuwadhibiti wahalifu
hao na mwisho wangeweza kutimiza azma yao.
“Haloo chief!”
“Kenny!”
“Naam baba! Tunarudi kitengoni, nilikuwa naomba kuzungumza
na wewe ana kwa ana kuhusu kile ulichoniuliza kabla hatujaon-
doka kwenda Kariakoo.”

203 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Tuzungumze tu kwa simu haina shida!”


“Hapana! Nataka tuzungumze ana kwa ana!”
“Okay sawa, sisi pia tupo njiani tunarudi, tukutane ofisini
kwangu,” ilisikika upande wa pili kisha simu ikakatwa. Nilikuwa
nazungumza na baba yake Saima ambaye nikiri kwamba ndiye mtu
pekee niliyekuwa namuamini kwa asilimia mia moja.
Haukupita muda mrefu tayari tulikuwa tumewasili ‘getini’, moja
kwa moja nikaenda kwenye ofisi ya vijana wa Cyber kujua kama
kulikuwa na chochote kipya walichokibaini kule Selous kwa kutu-
mia teknolojia.
“Tumefanikiwa kuona mahali ilipo kambi yao, tazama hii,” alise-
ma kiongozi wao, akinioneshea kwenye ‘screen’ kubwa iliyokuwa
ukutani, picha za satellite zilizokuwa zinaonesha mahali fulani
katikati ya mapori makubwa.
Picha ziliendelea kuvutwa kwa karibu kutokea angani na kweli
ilionesha kuwa kulikuwa na shughuli za kibinadamu zilizokuwa zi-
naendelea, kukiwa pia kumejengwa vijumba vingi kwa mfumo wa
kutengeneza kama duara kubwa, huku katikati kukiwa na uwazi.
“Inaonesha hii ndiyo ngome yao, kuna shughuli nyingi zinazo-
endelea katika eneo hili,” alisema kiongozi wao, nikatulia huku
nikiendelea kuzitazama picha zile.
Akilini mwangu nilikuwa nawaza mambo tofauti kabisa na kile
kilichokuwa kinaonekana kwenye ile skrini. Mara zote tulikuwa
tukipanga misheni zetu kwa umakini wa hali ya juu lakini mambo
yalikuwa yakiharibika katika dakika za mwisho.
Isingekuwa na maana yoyote kuingia tena kwenye misheni hiyo

204 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wakati tatizo la msingi halijashughulikiwa kwa sababu walengwa


wangevujishiwa siri na tungewakosa kwa mara nyingine huku siku
zikizidi kuyoyoma kuelekea usiku wa siku ya tukio.
“Njoo ofisini kwangu haraka,” meseji ilisomeka kwenye simu
yangu, ilikuwa imetoka kwa baba yake Saima, harakaharaka
nikaacha kila nilichokuwa nafanya, nikatoka na kuanza kutembea
kwa hatua ndefundefu kuelekea upande wa utawala ambako ndiko
ilipokuwepo ofisi ya baba yake Saima ambayo huwa anaitumia
anapokuwa ‘getini’.
Kama nilivyoeleza, baba yake Saima kwa wakati huo alikuwa
anashughulikia masuala ya utawala zaidi kwa hiyo alikuwa na ofisi
nyingine makao makuu ambako huko ndiko alikokuwa akitumia
muda mwingi na mara mojamoja kunapotokea ‘ishu’ muhimu kama
hiyo ndiyo anakuja ‘getini’.
Muda mfupi baadaye, tayari nilikuwa nimefika kwenye mlango
wa kuingilia ofisini kwa baba yake Saima. Ilivyoonesha ni kama na
yeye alikuwa ananisubiri kwani wakati nikijiandaa kugonga mlan-
go, ulifunguliwa na yeye mwenyewe.
Tukaingia mpaka ndani, yeye akakaa kwenye kiti chake na akani-
pa ishara kwamba nikae kwenye kiti kilichokuwa kinatazamana na
meza yake, akaniinamia, uso wake ukionesha wazi jinsi alivyoku-
wa na shauku kubwa ya kutaka kusikia nilichotaka kumwambia.
“We have a mole!” nilimwambia kwa Kiingereza, nikimaanisha
kulikuwa na msaliti kati yetu. Kauli hiyo ilimshtua sana, akavua
miwani yake ya mwacho ambayo huwa anaivaa mara mojamoja,
akaifuta vumbi kwa kitambaa maalum kisha akairudisha mahali

205 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

pake, midomo ikawa inamchezacheza.


“Thats a reason!” (Hiyo ndiyo sababu!) alisema akionesha ku-
kubaliana na kile nilichokisema, akasimama na kuanza kuzunguka
huku na kule kama anayetafakari jambo.
“Kitendo cha Abdulwaheed kukwepa mtego mliokuwa mmem-
tegea barabarani, akaacha simu kwenye gari ili kuwapumbaza ni
jambo ambalo nimekuwa nikilitafakari kwa undani sana bila kupata
majibu lakini kwa hiki unachoniambia sasa napata majibu.
“Pia kitendo cha kuvamia ile ngome yao kule Jaribu Mpakani ki-
sha wakawatoroka katika mazingira ya kutatanisha, nacho kinapata
majibu sasa! Kuna msaliti kati yetu, tena ‘high profile’,” alisema
baba yake Saima, akimaanisha kwamba msaliti huyo lazima ataku-
wa kwenye ngazi za juu za uongozi pale kitengoni.
“Hata hili tukio la Kariakoo nimesindwa kuelewa imekuwaje
likavurugika dakika za mwisho na kuwapa nafasi hawa washenzi
ya kutoroka! Haya yote sasa yamepata majibu.”
Alichokuwa anakisema ndiyo hichohicho nilichokuwa nimeki-
fikiria ndani ya kichwa changu, akarudi kwenye kiti chake kisha
akawa anachorachora kwenye karatasi iliyokuwa pale mezani
kwake, kisha akaniuliza swali ambalo sikulielewa kwa muda huo
lilikuwa linamaanisha nini.
“Mkiwa kule Jaribu Mpakani, uliongoza misheni ya kwenda
kuvamia kwa yule mwanamke aliyekuwa anawapikia maandazi na
mikate hawa washenzi. Ulimshirikisha nani kwenye misheni hiyo?”
“Sikumshirikisha yeyote!”
“Na ikafanikiwa?”

206 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Ndiyo, naweza kusema hivyo!”


“Siyo unaweza kusema hivyo, ndivyo ilivyo kwa sababu watuhu-
miwa wote walikamatwa.” Alisema baba yake Saima, nikawa
naendelea kutafakari kwa kina alikuwa anamaanisha nini kuniuliza
swali lile.
“Nenda kwanza ngoja nitafakari nini cha kufanya,” alisema
baba yake Saima huku akiendelea kuchorachora pale kwenye lile
karatasi. Wakati natoka wala hata hakuinua uso wake kunitazama,
alionesha kuzama kwenye tafakuri nzito.

207 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

208 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

9
N
ILIRUDI ofisini kwangu na kwa mara ya kwanza
tangu asubuhi ya siku iliyopita, nilipata muda wa
kukaa kwenye kiti changu. Uchovu niliokuwa nao
ulikuwa siyo wa kawaida kwa sababu kama nili-
vyoeleza, sikuwa nimepata muda wa kupumzika
hata kidogo usiku kucha kutokana na suala lililokuwa mbele yetu.
Kichwa kilikuwa kinawaka moto kwelikweli, ni hapo ndipo
nilipokumbuka jambo ambalo huwa linaniokoa sana pale kichwa
kinapokuwa kimechoka kiasi hicho lakini bado nikawa majukumu
mazito yanayonihotaji nitulize akili mbele yangu.
Tahajudi! Wazungu wanaita ‘meditation’. Hii ni mbinu ambayo

209 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

imekuwa ikinisaidia sana na inaweza kumsaidia mtu yeyote, cha


msingi ujue tu namna ya kuifanya.
Basi nilikaa vizuri pale kwenye kiti changu, nikafumba macho
na kuanza kupumua kwa uhuru, nikivuta pumzi ndefu na kuiachia
taratibu, huku nikijitahidi kuacha kuwaza kitu chochote ndani ya
kichwa changu, akili zangu nikazipelekea kwenye kufuatilia pumzi
tu.
Nilifanya hivyo kwa takribani dakika ishirini, simu yangu ya
mkononi ndiyo iliyonizindua kutoka kwenye hali ya utulivu mkub-
wa wa nafsi, mwili na roho niliyokuwa nimeifikia ndani ya muda
ule wa dakika zile chache kabisa.
Nilifumbua macho na kuinuka, nikaisogelea simu yangu, ilikuwa
ni baba yake Saima ndiyo ananipigia, harakaharaka nikapokea.
“Nimeshapata majibu ya nini cha kufanya! Unatakiwa kuelewa
kwamba mipango yote itabaki vilevile kama ilivyo licha ya mab-
adiliko utakayoyasikia, just focus, tutampata tu anayetuvuruga na
safari hii tutamvuruga yeye kwanza,” alisema baba yake Saima na
kabla haa sijajibu kitu, simu ikakatwa.
Mpaka hapo nilishakuwa nimeelewa ni nini kinachoendelea na
haukupita muda mefu, taarifa zilianza kusambaa kupitia vfaa vyetu
vya mawasiliano kwamba oparesheni zote za kuwatafuta watuhu-
miwa wa ugaidi zilikuwa zimesimamishwa rasmi mpaka taarifa
zitakapotolewa tena.
“Vikosi vyote vinatakiwa kurudi kwenye majukumu yao ya
kawaida mpaka itakapotolewa taarifa nyingine,” alisikika mkuru-
genzi akitoa maelekezo kwa kupitia vifaa vya mawasiliano. Nili-

210 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

jikuta nikitabasamu kwa sababu ama kwa hakika akili iliyotumika


ilikuwa kubwa sana.
Basi taarifa ziliendelea kusambaa kwa kasi na ndani ya muda
mfupi, watu wote wakawa wameshapata taarifa.
Kama alivyokuwa ameniambia baba yake Saima, mimi niliende-
lea na maandalizi ya kimbinu kwa sababu nilikuwa najua kwamba
katika uhalisia ratiba zote zipo kama zilivyokuwa zimepangwa
isipokuwa taarifa zilitolewa vile ili kumchanganya mtu au watu
waliokuwa wakipenyeza taarifa nyeti kwa wahusika.
Baada ya maandalizi yangu yote kuwa yamekamilika, watuhu-
miwa wote tuliofanikiwa kuwakamata wakiendelea kuhojiwa na
kikosi maalum cha ‘Interogation’ kwa maelezo yangu, niliwaku-
sanya vijana wote ambao ndiyo nilitaka tuwe nao mstari wa mbele
kwenye misheni ya kule Selous na nilichowaambia ni kwamba
tunatakiwa kwenda kufanya mazoezi ya kimbinu, kitaalamu tunaita
‘drill’ ili kujiweka tayari kwa kazi siku itakapotangazwa tena.
Kitu cha kwanza nilichokifanya, ilikuwa ni kuchukua simu ya
mkononi wa kila mmoja, kisha nikahakikishawote wamepitishwa
kwenye mashine maalum ya kuscan mwili mzima ili kuwa na
uhakika kama hakuna yeyote kati yao atakayeweza kufanya ma-
wasiliano tofauti na yale ya ndani tunayoyafanya kupitia vifaa
maalum vya kuvaa mwilini.
Hatua hiyo ilimshtua kila mmoja lakini kwa kuwa mimi ndiye
niliyekuwa kiongozi wa misheni ile, hawakuwa na cha kufanya
zaidi ya kukubaliana na mimi. Simu zote ziliwekwa kwenye boksi
maalum kisha nikaagiza vijana wangu wa Cyber wawe wanafua-

211 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

tilia kwa karibu kama kuna chochote kisichokuwa cha kawaida


kwenye simu zile.
Basi tulianza na mafunzo ya darasani, nikawa nawaelekeza
kwamba siku itakapowadia ya kwenda kuvamia ile ngome kule
Selous, tunatakiwa kwanza kuwa tumeshaiva kinadharia, yaani
tulifahamu eneo husika kabla hata ya kufika, tuwajue maadui zetu
kabla ya kukutana nao.
Kwa jinsi nilivyokuwa nawapa ‘lecture’, ilikuwa ni kama tukio
lenyewe lipo mbali yaani siku kadhaa mbele wakati ukweli am-
bao hakuna kati yao aliyekuwa anaujua ni kwamba ‘misheni’ hiyo
ilikuwa inatakiwa kufanyika usiku wa siku hiyohiyo.
Niliendelea kuwapa darasa, nikitumia michoro, ramani na picha
za satellite ambazo zilikuwa zimekusanywa na vijana wa Cyber
wakishirikiana na wenzao wa Information Technology (IT).
Lakini pia niliwapa maelekezo tuliyopewa na wale maafisa wa
vikosi vinavyohusika na masuala ya hifadhi ya wanyamapori kwa
maana ya TFS, TANAPA na TAWA, kila mmoja akawa ananisikili-
za kwa umakini.
Kikosi nilichokuwa nacho, kilikuwa ni cha takribani watu ishirini
pamoja na mimi mwenyewe, ambao walikuwa ni mchanganyiko
kutoka kwa kikosi cha kupambana na ugaidi (Anti Terrorism
Squadron), maafisa vipenyo na maafisa wa kikosi maalum (Special
Task Force) watatu kutoka Ngerengere.
Nilikuwa nimeamua kuwa na kikosi kidogo ambacho itakuwa ni
rahisi kukiongoza na kuzuia taarifa kuvuja na kiukweli, safari hii
nilikuwa na matumaini makubwa kuliko wakati mwingine wowote

212 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

na moyoni nilikuwa najiambia kwamba hii ndiyo kete yangu ya


mwisho ya kuonesha mimi ni nani.
“Kuna mwenye swali?” nilisema baada ya kumaliza kutoa ‘lec-
ture’ ya nguvu, nikawaona wote wakitingisha vichwa kuonesha
kwamba wameelewa kwa kina kile nilichowafundisha.
“Kama tumeelewana, basi niwataarifu kwamba tutaingia ‘field’
muda mfupi kuanzia sasa kwenda kuyafanyia majaribio yale tuli-
yofundishana na tutakwenda ‘Selous’ ingawa mazoezi tutafanyia
sehemu tofauti na ilipo kambi ya wale maadui zetu waliokuwa na
mpango wa hatari sana mbele yao.
Baada ya kumaliza, niliwasiliana na watu wa kitengo cha maaku-
li, vyakula vikaletwa humohumo ndani ya ‘mesi’ ndogo ya maafisa
tulimokuwemo. Sikutaka yeyote kati yao awasiliane kwa namna
yoyote na mtu asiyehusika.
Wakati wakiendelea kula, nilitoka na kwenda moja kwa moja
kwa mkurugenzi ambaye hatukuwa tumezungumza kwa kina tangu
tulipotoka Kariakoo. Aliponiona tu naingia ofisini kwake, aliinuka
kwenye kiti chake alipokuwa amejiinamia, akionesha kuchangan-
yikiwa kabisa.
“Nimezungumza na baba yako, ameniambia kila kitu mlichozun-
gumza, nasikitika sana kugundua kwamba kuna watu wanaotuk-
wamisha,” alisema bila kituo huku akinisogelea, akajiapiza kwam-
ba siku atakapomgundua mtu aliyekuwa anatuhujumu, ataziona
rangi zake halisi.
Ilibidi nitabasamu kwa sababu alikuwa na ‘tension’ kubwa kuliko
kawaida, akanipa ishara ya kukaa, nikakaa ingawa yeye aliendelea

213 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kusimama, akizunguka huku na kule, utulivu ukiwa umemuisha


kabisa.
“Umefikiria nini?”
“Naondoka na ‘special elites’, tunakwenda Selous na nina uhaki-
ka kabla jogoo hajawika alfajiri ya kesho, Abdulwaheed na genge
lake lote watakuwa kwenye mikono yetu,” nilimwambia kwa
kujiamini.
Niliposema special elites nilimaanisha kikosi kazi maalum cha
watu ishirini na mimi nikiwemo, kile nilichokuwa nacho kule
ndani nikiendelea kufundisha mbinu za medani tutakazotumia.
“Una akili sana Snox!” alisema mkurugenzi na kunisogelea, aka-
wa ananipigapiga begani. Huwa ni nadra sana kwake kuniita jina
langu lisilo rasmi la Snox tunapokuwa kwenye mazungumzo ya
kazi, nikaona ni kwa namna gani mpango niliokuwa nao ulivyom-
kosha.
“Mnahitaji nini?”
“Hatuwezi kuondoka kwa magari, tutachelewa sana. Naomba
‘chopper’ mbili za jeshi, zinatosha kabisa,” nilimwambia, muda
huohuo akanyanyua simu yake na kuzungumza na upande wa pili,
nikawa nimetulia nikimsikiliza. Muda mfupi baadaye, alikuwa
ameshamaliza kuzungumza na simu.
Hilo limeisha, mtaondokea Kunduchi, mashine zinawekwa tayari
kwa ajili yenu, sema kingine,” alisema mkurugenzi huku akikaa
kwenye kiti chake, akashusha pumzi ndefu na kuendelea kunitaza-
ma. Nikamuelezea kwa kifupi nilichokuwa nimekipanga, akani-
unga mkono na kunipongeza sana kwa moyo wa kutokata tamaa

214 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

niliokuwa nao.
Ukweli ni kwamba yeye ndiye aliyenipa nguvu kule Jangwani,
Kariakoo kwa kuniambia kwamba hata kama tulishindwa kuwaka-
mata wahusika, lakini kitendo cha kugundua maficho yao pekee
ulikuwa ni ushindi.
Nilimweleza kuwa sitaki mtu mwingine yeyote asiyehusika ajue
ni nini kilichokuwa kinaendelea, akakubaliana na mimi kwa asil-
imia mia moja kwa sababu halikuwa jambo geni ‘kitengoni’ kuwa
na misheni za siri ambazo kitaalamu huitwa ‘classified ops’.
Baada ya kupata baraka zake zote, nilirudi kule ukumbini, vijana
wakawa tayari wameshamaliza kula, na mimi nikala harakaharaka
na baada ya hapo, wote tulielekea kwenye chumba cha kubadilishia
nguo.
Wote tukapiga kombati maalum ambazo zingefaa sana kwa maz-
ingira ya hifadhini, baada ya hapo tukachukua vifaa vyote muhimu,
zikiwemo silaha, majaketi ya kuzuia silaha na vifaa vya huduma
ya kwanza na nikawa nawasisitiza kila mmoja kuchukua vifaa vya
kutosha kwa sababu mazoezi yanaweza kuwa marefu na yanayohi-
tahi vifaa halisi vya mapambano.
Baada ya kumaliza kila kitu, tulitoka kwa kupitia mlango wa
nyuma ambako magari matatu yalikuwa yanatusubiri kwa ajili ya
kutupeleka Kunduchi. Kila kitu kilikuwa kinafanyika kimyakimya
kiasi kwamba kuna watu wengi tu pale ndani hawakuwa wanajua
ni nini kinachoendelea.Waliofanikiwa kujua, waliambiwa kwamba
tunakwenda kwenye ‘drill’ na kwa kuwa tayari matangazo ya
kusitisha oparesheni yalikuwa yameshatolewa na uongozi, kila mtu

215 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

aliamini kwamba ni kweli tunakwenda kwenye mazoezi.


Hata vijana wangu nao kama nilivyosema, wote walikuwa wa-
najua kwamba tunakwenda kwenye mazoezi na nilipanga kwenda
kuwaambia ukweli mara baada ya kushushwa na helikopta ndani
ya hifadhi ya Selous.
Magari yalitoka kupitia mlango wa nyuma na safari hii hata
mimi sikuwa naendesha, madereva maalum ndiyo waliotupeleka
mpaka Kunduchi. Tulipofika, kweli tulikuta helikopta mbili za
kijeshi zikiwa zinatusubiri kwenye viwanja vya chuo, tukateremka
kwenye magari na moja kwa moja tukaelekea kwenye helikopta
ambapo niliwagawa vijana kwenye makundi ya watu kumikumi
nikiwemo na mimi.
Kila helikopta ilibeba watu kumi na marubani wawili, safari ya
kuelekea Selous ikaanza, huku nikijitahidi kutuliza akili yangu kwa
kadiri iwezekanavyo. Kama nilivyosema, sikuwa tayari kuzidiwa
tena ujanja na moyoni nilikuwa najiapiza kwamba safari hii, liwake
jua inyeshe mvua lazima kieleweke.
Helikopta mbili za jeshi zilikuwa zikipasua anga kuelekea Sel-
ous, kila mmoja akiwa kimya kabisa. Safari iliendelea na hatimaye
tukawa tumewasili mkoani Morogoro, marubani wakafuata uelekeo
wa hifadhi hiyo ya taifa inayojumuisha mikoa kadhaa.
Kwa kufuata ramani ambayo tuliwapa kwa msaada wa watu wetu
wa Cyber na IT, tulifanikiwa kutua salama kwenye eneo la wazi
ndani ya hifadhi hiyo.
Ni hapa ndipo nilipanga kumwambia kila mtu ukweli kwamba
hatukuwa kwenye mazoezi au drill kama tunavyoita kitaalamu bali

216 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

tulikuwa kwenye uwanja halisi wa vita.


Helikopta zilianza kushuka kwa zamu, ilianza ya kwanza ambayo
mimi nilikuwepo ndani yake, ikashuka chini na kusababisha vumbi
jingi litimke huku miti na vichaka navyo vikipulizwa kwa nguvu
na upepo kutoka kwenye mapangaboi ya helikopta hiyo.
Wakati hii moja ikitushusha, ile nyingine ilikuwa bado angani
ikizunguka, baada ya wote kumalizika kwenye helikopta ya kwan-
za, muda huohuo ilipaa kisha ile nyingine nayo ikasogea na kutua.
Wakati hii nayo ikishusha, ile nyingine nayo ilikuwa angani iki-
zunguka na baada ya kumaliza kuwashusha wote, ilipaa kisha kwa
pamoja zikaondoka haraka eneo hilo.
Ilikuwa ni lazima zitushushe kwa mbinu hiyo ili hata kama kuna
mtu alikuwa anazifuatilia, asigundua kwamba zimeshusha watu,
bora zionekane zimepita tu eneo hilo ili kutoleta hali yoyote ya
wasiwasi kwa maadui zetu.
Baada ya hapo, tulikaa kwenye ‘formation’ maalum ya kujificha
na kusubiri kuona kama kuna kitu chochote kingetokea.
Baada ya kama dakika tatu hivi za ‘kusikilizia’, tulipata uhakika
kwamba usalama upo kwa hiyo kilichofuata baada ya hapo ilikuwa
ni kutoka kwenye maficho na kuanza kupeana darasa na nikautu-
mia muda huo kuwaambia ukweli.
“Nikiwatazama wote hapa, ukiwaondoa ndugu zetu watatu wa
‘task force’ kutoka Ngerengere, wengine wote tulikuwa pamoja
kuanzia tulipoianza misheni ya kuwasaka wahalifu wanaotishia
kufanya matukio ya kigaidi katika ardhi ya nchi yetu, awiiii!”
nilisema, wote wakaitikia: “Awaaaa!”

217 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Misheni za mwanzo hazikufanikiwa kama tulivyopanga, mtuhu-


miwa wetu namba moja, Abdulwaheed alifanikiwa kutuzidi akili
mara ya kwanza tulipomuwekea mtego barabarani, akafanikiwa
tena kutuzidi ujanja yeye na wenzake tulipoenda kuvamia ngome
yao kule Jaribu Mpakani.
“Kama hiyo haitoshi, saa chache zilizopita genge lake lime-
fanikiwa tena kutuzidi akili Kariakoo na kutoroka katika hatua
za mwisho kabisa! Nani anajua kwa nini haya yote yametokea?”
niliuliza, kila mmoja akabaki kimya kabisa.
“Ni kwa sababu kuna watu wetu wa ndani walikuwa wakiuza
siri za kambi!” nilisema na kusababisha wote wapigwe na butwaa,
wakiwa ni kama hawaamini kile nilichokisema.
“Hiyo ndiyo sababu iliyofanya tangazo likatoka kutoka ngazi
za juu likieleza kwamba oparesheni na misheni zote zimesitishwa
mpaka tutakapopewa taarifa nyingine. Lengo la yote hayo ilikuwa
ni kujaribu kuwapoteza maboya watu wote waliokuwa wakiuza siri
zetu,” nilisema, ukimya ukaendelea kutanda.
“Baada ya kuyasema hayo, nataka niwaeleze ukweli! Hii sio
drill! Hatupo kwenye mazoezi hapa, tupo kwenye classified op
(oparesheni ya siri) na tunakwenda kuivamia ngome ya Abdulwa-
heed na wenzake waliojificha ndani ya hifadhi hii!” nilisema, wote
wakabaki kutazamana.
Ulikuwa ni ukweli wenye kushtua kwelikweli, nikaendelea
kuwajenga kisaikoloji ana kuwajaza ujasiri ndani ya mioyo yao
na nikawahakikishia kwamba safari hii kwa kuwa mambo yote
yamefanyika kwa usiri mkubwa, tunakwenda kushinda vita iliyopo

218 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

mbele yetu!
Baada ya kuzungumza na kikosi kizima kwa takribani dakika
kumi, morali ya kila mmoja ilikuwa imepanda kisawasawa, tu-
kagongesheana mikono pale, kila mmoja akiwa na uhakika kwam-
ba tunakwenda kushinda kimyakimya na baada ya hapo, nilianza
kutoa maelekezo ya jinsi oparesheni hiyo itakavyofanyika.
Mbinu zilikuwa ni zilezile, kwanza kuizunguka kambi yote
kimyakimya kisha kuendelea kusubiri mpaka nitakapotoa maele-
kezo ya kuvamia! Nilihakikisha kila mmoja anazo risasi za kutosha
kupambana muda mrefu zaidi kwa sababu nilikuwa najua kazi
haiwezi kuwa nyepesi.
Tukagawana makundi manne kisha tukaanza kusonga mbele
huku tukiwasiliana kwa karibu, kila mmoja akitoa taarifa ya kila
alichokuwa anakiona mbele yake. Kila kitu kilikuwa kinafanyika
kimyakimya, tukawa tunazidi kusonga mbele kuelekea kwenye lile
eneo ambalo taarifa za kiintelijensia zilionesha kwamba ndipo ilipo
kambi yao ndani ya hifadhi hiyo.
Kazi haikuwa nyepesi kwa sababu kama unavyojua, Selous ni
hifadhi ya taifa yenye wanyama wengi wakali, wakiwemo nyoka
wenye sumu kali, simba, chui, tembo wengi achilia mbali fisi we-
nye njaa.
Mpaka inafika saa kumi na mbili jioni, tulikuwa tumeizunguka
kambi yote kwa takribani umbali wa kilometa moja kutoka kila
upande. Tukawa tunazidi kusonga mbele kwa tahadhari kubwa
huku tukiendelea kusubiri giza liingie kwa sababu oparesheni
ilitakiwa kufanyika usiku ili iwe rahisi kwetu kutimiza kile tuli-

219 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

chokuwa tumekipanga.
Tuliendelea kusonga mbele, giza likaanza kuingia na kufanya iwe
ya kutisha kwelikweli, fikiria ni usiku na upo kwenye mbuga yenye
wanyama wakali lakini kama hiyo haitoshi, unaenda kupambana na
magaidi!
Mpaka inafika saa tatu za usiku, tulikuwa tumeisogelea kambi ile
kwa umbali wa mita mia moja, umbali ambao sasa ulituwezesha
kuweza kuona kilichokuwa kinaendelea kwenye lile eneo. Kuliku-
wa na pilikapilika nyingi zinazoendelea, moto ukiwa umewashwa
kwenye maeneo kama manne hivi.
Unaweza kusema ni kama zile picha za satelite zilikuwa zimetu-
potosha kidogo kwa sababu picha zilikuwa zinaonesha kama ni
sehemu ndogo tu yenye vibanda kadhaa vya mabati lakini kumbe
haikuwa hivyo.
Eneo zima lenye kambi lilikuwa na ukubwa kama uwanja wa
mpira, kukiwa na vibanda vingi vilivyojengwa kwa miti na nyasi
ingawa vichache ndiyo vilivyokuwa vimejengwa kwa mabati na
hivi ndivyo vilivyoonekana kwenye picha ya satelite.
Kwa jinsi nilivyokadiria ukubwa wa eneo lile, niliamini lazima
idadi ya watu iwe kubwa na harakaharaka nilikadiria kwamba ku-
naweza kuwa na watu zaidi ya 100, tena wenye silaha.
Sisi tupo ishirini, maadui wapo 100, kwa hesabu za harakaharaka
kila mmoja wetu alitakiwa kupambana na si chini ya watu watano!
Haikuwa kazi nyepesi hata kidogo.
Hata hivyo nilipiga moyo konde, nikawa naendelea kuwafafanu-
lia vijana wangu kila kinachoendelea na mbinu za kutumia, tukawa

220 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

tunaendelea kutambaa kama nyoka tukisonga mbele huku nikim-


tahadharisha kila mmoja kuwa makini kutosababisha kelele za aina
yoyote.
Kwa uzoefu wangu, shambulio pekee ambalo lingeweza kutupa
ushindi wa haraka, ilikuwa ni ‘ambush’. Ambush kwa Kiswahili ni
shambulio kubwa na la nguvu la kushtukiza.
Tulizidi kusogea na sasa tukawa tumebakiza kama mita hamsini
hivi kutoka kila upande, eneo ambalo sasa tuliweza kusikia na
kuona baadhi ya vitu vilivyokuwa vinaendelea.
Hakika wendawazimu hawa walikuwa wamejipanga kisawasawa,
kwa kifupi kilikuwa ni kama kikosi kizima cha jeshi na muda huo
wa usiku, walikuwa wakifanya mazoezi ya nguvu ya kivita, tukawa
tunasikia jinsi wanavyopigishwa kwata kwa nguvu.
Tuliendelea kusogea na hatimaye tukawa tumeikaribia kabisa ile
ngome, mapigo ya moyo wangu yakawa yananienda mbio kuliko
kawaida kwa sababu ilikuwa dhahiri kwamba kazi inayokwenda
kufanyika, si ya mchezo hata kidogo na umakini mkubwa ulikuwa
unatakiwa.
Sikutaka kumpoteza yeyote kati yetu, nikabonyeza kitufe maalum
kwenye kifaa changu cha mawasiliano na kuruhusu kila mmoja
kuwa ananisikia kwa wakati mmoja, nikawapa maneno ya mwisho
ya kuwapa morali, nikatoa maelekezo ya nini kinatakiwa kufanyika
na nikawaambia wote kwamba risasi yangu ya kwanza nitakayo-
fyatua itaashiria kuanza rasmi kwa mashambulizi, nikataka kila
mmoja ajibu mahali alipo kama ameelewa.
Wakaanza kujibu, mmoja baada ya mwingine na baada ya ku-

221 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

hakikisha kwamba wote tulikuwa tumeelewana, nilisimama baada


ya kuwa nimetambaa kwa umbali mrefu, kidole kikiwa kwenye
‘trigger’ ya bunduki yangu, nikafyatua risasi moja juu na kutamka
neno ambalo tulishafundishana kwamba litaashiria kuanza rasmi
kwa mashambulizi makubwa ya kushtukiza.
“Kinetic!” nilisema kwa sauti! Hilo ndiyo neno tulilokubaliana
kwamba litakaposikika baada ya kusikika mlio wa risasi, kinacho-
fuata ni mapambano ya kufa na kupona na neno hili pia lilikuwa ni
kama kutoa taarifa makao makuu kwamba kazi imeanza kwa hiyo
vikosi vyote vya kuja kutoa msaada vikae tayari.
Kama kawaida yangu, huwa napenda kuwa kiongozi kuliko bosi!
Kiongozi ni yule anayeongoza kwa vitendo na bosi ni yule ambaye
huwa anaamrisha wakati yeye akiwa amekaa pembeni.
Nilikuwa mstari wa mbele kabisa, bunduki ikiwa mkononi,
‘nikimwaga moto’ kuliko kawaida. Kwa kuwa ilikuwa ni usiku na
tulikuwa tukishambulia kutoka pande zote, tulitakiwa kuwa makini
sana tusije kuishia ‘kushonana’ wenyewe risasi.
Kwa hiyo nikawa natoa maelekezo ya kila mmoja kuzingatia
alama aliyonayo mwenzake ambayo ilikuwa ni kitochi kidogo
kinachotoa mwanga wa kijani ambacho kila moja alikuwa ame-
kivaa kifuani, achilia mbali zile tochi kali zenye mwanga mkali
ambazo kila mmoja alikuwa nayo kwenye kofia yake ya chuma.
Ujasiri niliokuwa nao wa kusonga mbele kwa kasi kubwa kwa
staili ya kuruka, kufyatua risasi na kujibingirisha chini kisha kusi-
mama tena na kuendelea kufyatua risasi kwa kasi kama mashine,
uliwapa nguvu vijana wangu ambao niliona nao wakifuata kile

222 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

nilichokuwa nakifanya, tukawa tunazidi kusonga mbele.


Kwa muda wote huo, hatukuwa tumepata upinzani wa aina
yoyote, ilionesha kama ile ‘ambush’ iliwakuta maadui zetu katika
muda ambao hawakuwa wametarajia hata kidogo, wakawa wa-
naanguka mmoja baada ya mwingine huku idadi kubwa ikikimbilia
kwa kasi kuelekea upande wa Magharibi.
Kwa hesabu za harakaharaka, tayari tulikuwa tumewaangusha
kama maadui kumi na saba mpaka ishirini hivi, nikisema kumwan-
gusha adui simaanishi kumpiga mtama, namaanisha kumdondosha
mtu kwa kumpiga risasi, eneo lote likageuka na kuwa uwanja wa
vita.
Ndani ya sekunde chache tu za mashambulizi ya nguvu, tayari
wote tulikuwa tumefika katikati ya eneo la kambi hiyo, mahali
ambapo palikuwa na kama kigema kilichochongwa na kupangwa
mawe kukizunguka na kuwa kama jukwaa. Nadhani eneo hili ndiyo
lililokuwa linatumika kwa viongozi wao kusimama pale wanapotoa
maelekezo kwa sababu lilikuwa juu kuliko maeneo mengine.
Nikatoa amri ya kuweka ‘cover’ palepale katikati kwanza kwa
sababu kuna jambo nilikuwa sijalielewa.
Ninapozungumzia ‘cover’ kwenye uwanja wa mapambano
makali kama hayo, namaanisha kile kitendo cha askari kujipanga
kwa kupeana migongo, kila mmoja anatazama upande wake ku-
hakikisha hakuna mtu anayesogea.
“Wote wanakimbilia upande mmoja, lazima tuwe makini,” nilise-
ma huku nikihema kwa nguvu kutokana na zile purukushani, nika-
toa amri ya sisi sote kuanza kusogea kwa tahadhari kubwa upande

223 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wa pili wa kigema kile ili kuwe na kitu kinachotutenganisha.


Akili zangu zilinituma kuamini kwamba pengine kule walikoku-
wa wanakimbilia ndiko walikokuwa wamehifadhi silaha zao kwa
sababu kama nilivyosema wakati tunavamia walikuwa kwenye
mazoezi ya kupiga kwata kama jeshini, kwa hiyo tulitakiwa kuwa
makini sana.
Vijana wangu walikuwa wameshapandisha ‘mizuka’ kuliko
kawaida, wakawa wanaona ni kama kuwaambia wote tuweke ‘cov-
er’ pale katikati ni kama nawachelewesha, nikasimamia msimamo
wangu kwa sababu nilishahisi kuna hatari kubwa mbele yetu.
Nilichokuwa nimekihisi ndicho kilichotokea, kumbe ni kweli
kule walikokuwa wanakimbilia, kwenye kibanda kilichoonekana
kuwa kikubwa kuliko vyote kikiwa kimejengwa kwa mabati kuan-
zia juu mpaka chini, ndipo kulipokuwa na ghala lao la silaha.
Kufumba na kufumbua, mwanaume mmoja aliyekuwa amevalia
‘nusu kanzu’ na kujifunga kilemba kichwani huku kwa nje akiwa
amevalia kizibao chenye mabakabaka kama yale ya kwenye mag-
wanda ya sare za wanajeshi, alichomoza akiwa na bunduki kubwa
ya kivita.
Wote tulipigwa na butwaa kutokana na ukubwa wa bunduki
aliyokuwa ameibeba, akazungumza maneno kwa lugha ambayo
hatukuielewa mara moja kwa sauti kubwa kisha akaanza kufyatua
risasi kuelekea pale katikati tulipokuwa tumejipanga.
Kama isingekuwa machale yangu ya kukitaka kikosi kizima
kukaa upande wa pili wa kigema kile, hakika maafa makubwa
sana yangetukuta, ikabidi wote tulale chini huku wote wakisubiri

224 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

niwape maelekezo ya nini cha kufanya kwa sababu vijana wengine


wengi walianza kuchomoza nyuma ya yule mwanaume, wote waki-
wa na bunduki za kivita.
Ukisikia mwindaji anapogeuka na kuanza kuwindwa yeye, basi
hicho ndicho kilichokuwa kinatokea. Ilikuwa ni zamu yetu kush-
ambuliwa na moto tuliokuwa tunawashiwa, haukuwa wa kitoto.
Yale mawe yaliyotumika kujengea kile kigema tulichojificha,
yakawa yanapasuliwa na risasi utafikiri kuna mtu anatengeneza
kokoto.
“Hand grenade!” nilisema kwa sauti ya chini, nikimaanisha
kwamba tunatakiwa kuanza kutumia mabomu ya kurushwa kwa
mikono ili kuwazuia wasizidi kutusogelea mbele kwa sababu wali-
kuwa wanakuja kama nyuki.
Nilichomoa bomu lililokuwa kwenye mifuko ya suruali langu, ni-
katoa kipini kwa kutumia meno kisha nikalivurumisha kwa nguvu
kuelekea kule walikokuwa wanatokea.
Kishindo kikubwa kilichosikika kiliwachanganya, wakapoteza
mwelekeo na wakiwa bado hawaelewi nini cha kufanya, bomu
lingine lilirushwa na hapo sasa ndiyo tukawa na nguvu ya kusi-
mama na kuanza kujibu mashambulizi kwa mfumo uleule wa
‘cover’.
Kwa nguvu waliyokuwa wameitumia, ilikuwa ni lazima tu-
rudi nyuma kwanza kwenda kujipanga upya na kuwapunguza,
vinginevyo tusingeweza kuwashinda kwa sababu walikuwa na
silaha ambazo hata sijui nisemeje! Kwa kifupi kilikuwa ni kikosi
cha kijeshi kilichojikamilisha.

225 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Mabomu yale mawili ya kurushwa kwa mkono, yaliwapotezea


mwelekeo kabisa, tukaendelea kufyatua risasi kwa kasi kubwa
huku tukirudi nyuma kutafuta sehemu nzuri ambayo ingetumika
kama sehemu ya kujificha dhidi ya mashambulizi yao.
Ndani ya muda mfupi tu, tayari tulikuwa tumesharudi nyuma um-
bali ambao ungetosha kutufanya tupambane nao kufa na kupona!
Tukawa tunawaona jinsi wanavyokimbizana huku na kule kuwao-
koa wenzao waliokuwa wamecheza muziki wa yale mabomu, tuka-
ongeza nguvu zaidi mpaka wote wakarudi kule ndani ya lile ghala.
Haukupita muda mrefu wakaanza kutoka tena kwa kasi kubwa
mithili ya nyuki, wakifyatua risasi mfululizo. Kwa kuwa sasa
tulikuwa sehemu salama, kazi yetu ilikuwa ni kulenga shabaha tu,
tukawaangusha kwa kasi kubwa na baada ya kuona sasa tumeanza
kuwazidi nguvu, nilitoa amri ya kuinuka tena kutoka pale tulip-
okuwa tumejibanza na kuanza kusonga mbele.
Hilo lilikuwa ni kosa kubwa sana, kumbe wakati tukiamini
kwamba tumewazidi nguvu, wao walikuwa wakijipanga kwa
namna nyingine ya kupambana na sisi, kufumba na kufumbua
risasi zikaanza kupigwa kutokea nyuma yetu, wengine wakawa
wanashambulia kutokea upande wa juu, kwenye paa la lile ghala na
nadhani wengine walikuwa wameshapanda juu ya miti.
Kwa bahati nzuri, pale tulipokuwa ‘tume-take cover’ palikuwa na
kama bonde lililotengeneza kama duara, tukalala ndani ya bonde
hilo huku na sisi tukigawana, kila kundi na upande wake.
Tulibananishwa kisawasawa, risasi zikawa zinarindima vibaya
sana, kila wanapopiga na sisi tunajibu mapigo, wakijaribu kutu-

226 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

sogelea tunawarudisha nyuma na sisi tukijaribu kusogea wanatu-


rudisha nyuma! Sijawahi kukutana na eneo la tukio lenye masham-
bulizi makali kama ilivyokuwa usiku huo.
Kama nisingesisitiza kila mmoja kuhakikisha anachukua risasi
za kutosha, hakika tungemalizwa kirahisi sana kwa sababu ilifika
mahali tumezungukwa kila upande, risasi zinapigwa kama mvua,
na sisi tunajibu mapigo, magazine ikiisha unaichomoa na kuitupa,
unachomeka nyingine.
Wakati majibizano makali yakiendelea, akili zilinituma kugeuka
upande wa pili, nikamuona wanaume wawili wakiwa wamebeba
RPG (Rocket Propelled Grenade), yale makombora yanayofyatuli-
wa na zile bunduki za kubeba mabegani ambayo huwa yanatumika
sana kutungulia ndege au helikopta!
Walikuwa wakilengesha pale kwenye lile bonde tulipokuwa
tumejibanza na endapo wangefanikiwa kulifyatua, hakuna ambaye
angesalimika na kibaya zaidi ni kwamba kikosi kizima cha watu
ishirini tulikuwa sehemu moja.
Kwa kasi ya ajabu, nilielekeza bunduki yangu kwa yule aliyeku-
wa amejitwisha ile bunduki kubwa ikiwa na guruneti kwa mbele,
nikafyatua risasi kumlenga kifuani. Nilifanikiwa kumlenga lakini
naweza kusema ni kama nilikuwa nimechelewa kwa sababu ali-
kuwa ameshavuta ‘trigger’ kulifyatua lile guruneti.
Kilichosaidia ni kwamba risasi niliyomlenga ilimfanya atingi-
shike kidogo kabla ya kuanguka, kule kutingishika kukafanya
apoteze shabaha kidogo.
“Rpgggggg!” nilipaza sauti kuwashtua wenzangu kwa sababu

227 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

guruneti hilo linapopigwa, kuna namna ya kufanya ili kuzuia


madhara, wote tukaing’ang’ania ardhi na kuziba masikio, kishindo
kikubwa kikasikika mita chache kutoka pale tulipokuwa tumelala
na kusababisha vumbi jingi litimke eneo lote.
Japokuwa guruneti lilikuwa limeangukia pembeni kidogo na pale
tulipokuwa tumelala, bado madhara yaliweza kutupata kwa sababu
mabomu ya aina hii huwa yanakuwa na uzito fulani ambao likip-
igwa sehemu, linasababisha madhara kwenye eneo kubwa kuzun-
guka eneo lilipolipukia.
Kwa sekunde kadhaa akili zilikuwa ni kama zimetengana na
mwili, masikio yakawa ni kama yameziba kutokana na kile kishin-
do. Ukimya ulipita, nikaanza kuwasikia vijana wangu wakikohoa
huku wengine wakiugulia maumivu.
Muda ambao tulikuwa tunajitafuta baada ya shambulio lile, wale
‘maharamia’ waliokuwa wamejipanga kisawasawa, waliendelea
kutuwashia moto kisawasawa.
“Retreat! I repeat, retreat!” nilisema kwa sauti ya chini, niki-
waelekeza vijana wangu kurudi nyuma kutoka kwenye uwanja wa
mapambano kwa sababu hali ilishakuwa tete na hali ingeendelea
hivyo, muda mfupi baadaye tungezungukwa na kusababisha tush-
indwe kujitetea.
Kwa kawaida, mnapokuwa kwenye uwanja wa mapambano,
inapotolewa amri ya kurudi nyuma, huwa kuna mbinu za kufanya
ili kuhakikisha wote mnaondoka salama kutoka kwenye mstari
wa mapambano, hata kama kuna waliojeruhiwa au hata kupoteza
maisha.

228 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Mimi ndiyo nilikuwa wa kwanza kuinuka, nikaanza kujibu mapi-


go kwa kasi, nikazichekecha kisawasawa, wenzangu nao wakapata
mwanya wa kusimama na kuanza kujibu mapigo, tukawa tu-
nashambulia kwa nguvu pengine kuliko wakati mwingine wowote
huku tukijipanga kwenye mpangilio maalum wa ku-retreat.
Kama nilivyosema, japokuwa guruneti lilikuwa limepiga mita
kadhaa kutoka pale tulipokuwepo, lakini bado tulipata madhara
japo hayakuwa makubwa, wenzetu wengine wakawa wamejeruhi-
wa na mawe yaliyorushwa kutoka pale bomu lilipolipukia.
Tuliendelea kushambulia huku tukirudi nyuma, wenzetu wawili
walikuwa wamejeruhiwa kiasi cha kushindwa hata kutembea, nika-
toa amri ya nani na nani wawasaidie kuondoka eneo hilo huku sisi
wengine tukiendelea kujibu mapigo.
Dakika kama tatu hivi, zilitosha kutufanya tuwe tumeshatoka
kabisa katika eneo la kambi na kurudi mafichoni, wakawa wa-
naendelea kutushambulia kwa kasi.
“Alpha Team! Do you copy!” nilisikia sauti ya mkurugenzi wetu
kupitia vifaa vya mawasiliano wakati tukiendelea kujibu mapigo
ili kutoa nafasi ya wale wenzetu waliojeruhiwa kupewa huduma ya
kwanza kwa sababu katika kundi letu, kulikuwa na wenzetu wawili
ambao walikuwa na taaluma ya udaktari.
Maneno aliyoyasema mkurugenzi wetu kwa lugha ya kijeshi, ya-
likuwa yanataka tujibu kama tunamsikia na kwa kuwa mimi ndiye
niliyekuwa kiongozi, nilijibu harakaharaka! Kitendo cha sauti yake
kuweza kusikika kwenye vifaa vyetu vya mawasiliano, maana
yake ni kwamba alikuwa jirani na pale tulipokuwepo, nikaona kila

229 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

mmoja akipata matumaini mapya.


Nilimjibu, nikamueleza hali ilivyo kwa kutumia lugha za kijeshi,
naye akanijibu kwamba wapo jirani kabisa na eneo hilo wame-
kuja kutusaidia. Kauli ile ilinifurahisha mno kwa sababu ukweli ni
kwamba mpaka wakati huo tulikuwa tumezidiwa kwa idadi, wen-
zetu walikuwa wengi na walikuwa na silaha zilizokamilika kisawa-
sawa.
Muda mfupi baadaye, ilisikika milio ya helikopta kadhaa zikija
kwa kasi eneo lile kutokea kila upande, kila mmoja akapata nguvu
mpya, helikopta zikapita kwa juu eneo la kambi, nadhani ilikuwa
ni kutengeneza hofu kwa maadui zetu, nikatoa taarifa kupitia vifaa
vya mawasiliano kwamba wanatakiwa kuwa makini kwa sababu
maadui zetu walikuwa na RPG za kutungulia ndege.
Muda mfupi baadaye, tayari vikosi vya ardhini navyo vilikuwa
vimeshawasili, wale wenzetu waliokuwa wamejeruhiwa wakapewa
msaada na kuchukuliwa harakaharaka, wakapandishwa kwenye
helikopta iliyotua mita kadhaa kutokea eneo lile na baada ya
hapo, kazi ikaendelea huku mimi nikitakiwa kuendelea kuongoza
mashambulizi kwa sababu tayari nilikuwa naelewa mazingira.
Kiukweli nilipata nguvu kubwa kuliko kawaida, kwa mara ny-
ingine nikasimama mstari wa mbele, tukawa tunasonga kwa kasi
kwenda mbele, safari hii tuliwa tumezingira kambi yote, tukaende-
lea kushambulia kwa kasi kubwa, maadui wakaanza kuishiwa
nguvu na haukupita muda mrefu, wakaacha kujibu mapigo.
Kwa kutumia kipaza sauti maalum, nilisimama pale katikati
tulipoishia mara ya kwanza na kutangaza kwamba watu wote

230 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wanatakiwa kusalimu amri kama wanataka kuendelea kuishi na


kujitokeza kutoka mafichoni.
Kwa kuwa tulikuwa tumeshawachakaza kisawasawa, wengi
wakiwa wamepigwa risasi sehemu mbalimbali za miili yao,
walianza kusalimu amri, mmoja baada ya mwingine. Kila ali-
yekuwa akisalimu amri, alikuwa akipekuliwa, kufungwa pingu na
kulazwa chini.
Ndani ya muda mfupi tu, watu takribani arobaini walikuwa
wamesalimu amri, tukawa tunawafuata kulekule kwenye maficho
yao na kuendelea kutangaza amri ya kuwataka wasalimu amri. Tu-
kafanikiwa kuwatoa wote waliokuwa wafichoni, wakaweka silaha
chini na kuungana na wenzao.
Kwa muda wote huo, mimi nilikuwa na kazi moja tu, kumtafuta
Abdulwaheed, akiwa hai au akiwa amekufa. Nilikuwa namtazama
kwa makini kila aliyesalimu amri, wengi walikuwa na asili ya Ki-
somali lakini pia kulikuwa na vijana wa Kiswahili wa kutosha.
Madaktari wetu waliendelea pia kuwahudumia watu wote walio-
kuwa wamejeruhiwa kwenye mapigano hayo kwa sababu hiyo
ndiyo kanuni pale mnapokuwa kwenye oparesheni, mnatakiwa
kuwakamata wengi wakiwa hai kadiri iwezekenavyo.
Katika waliokuwa wamepigwa risasi, ni watu saba tu waliokuwa
wamefariki dunia, wengine walikuwa na majeraha yanayoweza
kutibika, wakawa wanaendelea kupewa huduma ya kwanza na
wale waliokuwa na hali mbaya, nao walipakizwa kwenye helikopta
na kuondolewa eneo hilo.
Upekuzi uliendelea kila mahali lakini bado Abdulwaheed haku-

231 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

onekana, akili nyingine zikanituma kuamini kwamba huenda


alikuwa amejeruhiwa kwa risasi kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa
wa kwanza kusimama kwenye mstari wa mbele wa mapambano na
kutoa amri.
Unaweza kushangaa kwamba nilijuaje kama yule mwanaume ali-
yekuwa wa kwanza kuanza kutushambulia ndiye Abdulwaheed tu-
liyekuwa tunamsaka kwa udi na uvumba! Nitalieleza hili baadaye
lakini uhakika ni kwamba yule ndiye Abdulwaheed mwenyewe na
ilikuwa ni lazima apatikane, akiwa hai au amekufa.
Haukupita muda mrefu, mkurugenzi wetu na viongozi wengine,
wakatua na helikopta, wakawa wanakuja kule tulipokuwepo kwa
hatua za harakaharaka, nao wakiwa ni kama hawaamini jinsi tu-
livyofanikiwa kuwazida watu wengi wenye silaha kiasi kile.
Alikuja moja kwa moja mpaka mbele kabisa ambako mimi na
viongozi wa vikosi vingine vilivyokuja kutusaidia tulikuwa tuki-
jadiliana kuhusu Abdulwaheed.
“Kenny!” alisema huku akinisogelea mwilini, akinitazama kwa
makini kama nilikuwa salama. Nilikuwa salama salmini ingawa ni-
likuwa nimechafuka kama kinyago, huku magwanda yangu yakiwa
hayatamaniki.
“Chief!” nilisema, akanisogelea na kunikumbatia kwa nguvu kwa
sekunde kadhaa.
“Tunashukuru mlifika kwa muda muafaka, tulikuwa tumesha-
zidiwa!”
“Tulikuwa tunafuatilia kila kitu kilichokuwa kinaendelea!”
alisema huku akinyoosha kidole juu, nikaona kitu kilichokuwa

232 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kinawakawaka taa ambapo harakaharaka niligundua kwamba ni


‘drone’, zile kamera zinazopaishwa angani na kurekodi kila kina-
choendelea na kutuma taarifa kwenye mashine maalum anayokuwa
nayo mtu anayeziongoza.
“Abdulwaheed bado hajapatikana!” nilimwambia, akaniambia
nisiwe na wasiwasi, nikabaki nashangaa kwa nini anasema tusiwe
na wasiwasi, akanioneshea tena kidole upande wa pili, mwanaume
mmoja akawa anakokotwa na vijana wawili wenye miili mikubwa
akiletwa pale tulipokuwepo, akionesha kujeruhiwa vibaya.
Niliona ni kama wale wenzetu waliokuwa wanamleta yule mwa-
naume wanachelewa, nikapiga hatua ndefundefu kuwafuata, wali-
pogundua kama ni mimi, walisimama, nikamuinua kichwa yule
mwanaume ambaye alikuwa ameloa damu mwili mzima, ikionesha
ni kutokana na majeraha ya risasi.
“Tumempata chief! Huyu ndiyo Abdulwaheed!”
“Hapana! Siyo yeye! Siyo mwenyewe huyu,” nilisema kwa sauti
kubwa, nikarudi harakaharaka kule walipokuwepo wale viongozi
wetu, nikawaambia kwamba mtu yule hakuwa Abdulwaheed.
“Haiwezekani! Wewe unajua Abdulwaheed kwa sura?”
“Ndiyo! Siyo huyu!” nilisema na kuwafanya wote wabaki
wamepigwa na butwaa. Muda ambao kila mmoja alikuwa akiamini
kwamba kazi imeisha, kusikia habari kama hizo lilikuwa ni jambo
la kushtua.
“Subiri!” alisema mkurugenzi wetu, akabonyeza kifaa chake
cha mawasiliano, akageukia juu akiwa anatazama angani. Alitoa
maelekezo kisha muda huohuo, zile kamera za ‘drone’ zilizokuwa

233 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

zinawakawaka taa za rangi ya kijani na nyekundu, zikaanza kuzun-


guka huku na kule kwa kasi.
Uzuri wa kamera hizo za kisasa, ni kwamba zilikuwa na kitu
kiitwacho UV Light, miale maalum ambayo ilikuwa inaziwezesha
kunasa picha hata kwenye giza, zikawa zinaendelea kuzunguka
huku na kule.
“Una uhakika siyo mwenyewe?” alisema mkurugenzi kwa sauti
ya chini baada ya kunisogelea.
“Siyo mwenyewe, nina uhakika wa asilimia 100, kama huamini,
tujaribu kuwatumia hawahawa vijana wake kupata uhakika!”
nilisema, akashusha pumzi ndefu na kuniambia kwamba kikosi cha
wataalamu wa teknolojia ya mawasiliano waliokuwa wakiziongoza
kamera zile, walishapewa maelekezo kwa hiyo watatoa majibu.
“Kwa sasa naomba uelekeze nguvu kuimaliza oparesheni hii!
Wapange vijana wako kuhakikisha watu wote wanaondolewa eneo
hili na linabaki chini ya uangalizi mkali kwa saa ishirini na nne,
siku saba!” alisema, na mimi nikashusha pumzi ndefu.
Ilibidi nifanye kama alivyoniagiza lakini nilikosa kabisa utulivu
kwenye nafsi yangu! Endapo Abdulwaheed angefanikiwa kutoroka
na asipatikane, maana yake ni kwamba bado kungekuwa na tishio
kubwa la yeye kwenda kujipanga upya na kutekeleza kile alichoku-
wa amekipanga.
Nilitoa maelekezo ya nini cha kufanyika na muda mfupi baadaye,
watuhumiwa wote waliokamatwa kwenye kambi ile walianza ku-
ondolewa kwa awamu kwa kutumia helikopta za kijeshi.
Ndani ya muda usiopungua dakika ishirini, tayari wote walikuwa

234 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wameondolewa na maagizo yangu ni kwamba walitakiwa kwenda


kuwekwa kwenye nyumba maalum zilizopo chini yetu jijini Dar
es Salaam kwa sababu kwa idadi yao, isingewezekana kuwaweka
wote sehemu moja.
“Vipi! Kuna taarifa zozote?”
“Ndiyo! Hebu zungumza na huyu kijana wetu hapa!” alisema
huku akitoa simu yake ya mkononi na kubofya namba fulani,
akanipa simu.
Ilikuwa ni sauti ya Eddiville, mmoja kati ya vijana wanaoaminika
sana kwenye suala zima la teknolojia ya mawasiliano. Aliposikia
sauti yangu tu, aliweza kunitambua mara moja.
“Kamera zetu zimeweza kunasa tukio la mwanaume mmoja aki-
wa kwenye pikipiki, akiondoka kwa kasi kubwa kuelekea upande
wa Kibiti,” alisema, nikashtuka kuliko kawaida.
“Mmefikia wapi?”
“Kwa bahati mbaya kamera zetu haziwezi kwenda umbali mrefu
kutoka mahali alipo mtu anayeziongoza, kwa hiyo tumempoteza
lakini uelekeo wake ni kama nilivyosema, anaelekea upande wa
Kibiti kwa kutumia njia za porini, yupo kwenye pikipiki na tume-
fanikiwa kupata picha na video zake, natuma sasa hivi kwenye
simu ili umtazame kama unaweza kumtambua,” alisema, nikaishi-
wa kabisa nguvu.
Muda huohuo, ziliingia picha tatu zilizopigwa kutoka kwenye
‘drone’. Nilipozifungua tu, niliweza kumtabua Abdulwaheed kuto-
kana na mavazi aliyokuwa amevaa.
Kichwani alikuwa amejifunga kiremba na chini alivaa nusu

235 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kanzu na kizibao cha kijeshi juu yake.


“Bila shaka unaniamini sasa!” nilisema huku nikimuoneshea
zile picha, na yeye akabaki amepigwa na butwaa, akiwa ni kama
haamini.
“Tunafanyaje?”
“Lazima apatikane, haraka iwezekanavyo!” nilisema kwa msisiti-
zo, na mimi nikiwa hata sijui naanzia wapi kwa sababu eneo lile tu-
lilokuwepo ilikuwa ni ndani kabisa ya Hifadhi ya Selous na tayari
ulikuwa ni usiku na mtuhumiwa wetu alikuwa akitumia pikipiki,
jambo ambalo lingefanya iwe vigumu kumfikia kwa haraka.
“Mimi nashauri turudi tukajipange upya! Kama jeshi lake lote
tumelisambaratisha, hawezi kuwa na nguvu tena! Kwa kuwatumia
hawa vijana wake, tunaweza kupanga misheni mpya ya kumsaka
kuanzia asubuhi, kwa sasa tunatakiwa kurudi ofisini kwanza na
kuandika ripoti ya oparesheni hii na anayetakiwa kuandika ripoti
hiyo ni wewe!
Namba moja anafuatilia kila kinachoendelea,” alisema mkuru-
genzi, nikawa sina cha kusema zaidi ya kukubaliana naye kwa
sababu neno linalotoka kwa mkubwa wako, kwa itifaki za kijeshi
linakuwa ni amri.
“Umeshajua ni nani na nani wanaobaki?”
“Ndiyo! Nimeshawapanga!”
“Vizuri! Fanya ukaguzi wa mwisho, helikopta inakuja kutuchu-
kua baada ya dakika tatu,” alisema, ikabidi niwakusanye vijana
wangu ambao niliwapangia jukumu la kubaki kule porini! Jumla
walikuwa sita, nikawapa maneno yangu ya kuwatia morali na ku-

236 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

waeleza kuwa kwamba tunawategemea sana.


Niliwaeleza pia habari za Abdulwaheed kufanikiwa kutoroka kwa
kutumia pikipiki, wote wakashtuka kwa sababu walichokuwa wa-
nakijua wote ni kwamba tulikuwa tumefanikiwa kuwakamata wote
huku wachache wakipoteza maisha.
“Nataka tufanye njama! Amekimbilia Kibiti, uwezekano mkubwa
ni kwamba hawezi kufika Kibiti salama kwa sababu amejeruhiwa
kwa risasi na mimi ndiye niliyempiga! Kwa hiyo kama inaweze-
kana, wawili kati yenu mnaweza kujigawa na kumfuatilia, lazima
atachemka tu njiani!
Ni na uhakika hawezi kufika mbali, mnachotakiwa kufanya
ni kufuatilia kwa makini michirizi ya damu” niliwaambia, wote
wakakubaliana na mimi na tukakubaliana kwamba suala hilo libaki
kuwa siri kati yetu. Angalau sasa moyo wangu ulitulia kwa sababu
nilikuwa nawaamini vijana wangu!
“Snooox!” nilisikia sauti ya mkurugenzi ikiniita kwa nguvu, ni-
kageuka na kumuona akinipungia mikono, tayari helikopta ilikuwa
inasikika kwa mbalai ikija.
Nikagongesheana mikono na vijana wangu na kuwaambia kwam-
ba tuendelee kuwasiliana kwa karibu kwa kila kinachoendelea,
nikakimbia kikakamavu kuelekea kule walipokuwa wamesimama
viongozi wetu wa juu waliokuwa wamesalia, akiwemo mkuru-
genzi.
Tayari helikopta ilikuwa inaonekana angani, ikishuka taratibu
jirani na eneo lile, upepo mkali ukawa unapuliza kutoka kwenye
mapangaboi ya helikopta hiyo na muda mfupi baadaye, tayari ili-

237 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kuwa imeshatua.
Harakaharaka tukawa tunakimbia kuelekea pale ilipotua huku
kila mmoja akijitahidi kuinama chini kama sheria zinavyoelekeza
unapoisogelea helikopta ambayo haijazima injini na mapangaboi
yanaendelea kuzunguka.
Mimi nilikuwa wa mwisho kupanda, muda huohuo ikanyanyuka
na kuanza kuondoka kwa kasi.
“Kazi nzuri Snox!” ilisikika sauti kutoka upande wa marubani,
ikabidi nitazame vizuri, sikuamini macho yangu kumuona baba
yake Saima akiwa ndiye anayeiendesha helikopta hiyo. Sikuwahi
kujua kama baba yake Saima ni rubani, nikajikuta nikitabasamu.
“Snox nusu mtu nusu chuma,” alisema mkurugenzi na kusa-
babisha wote tuliokuwa ndani ya ile helikopta tucheke. Walikuwa
ni viongozi wangu, tena wa ngazi za juu kabisa lakini kwa jinsi
walivyokuwa wakizungumza na mimi, utafikiri nalingana nao
kuanzia umri mpaka vyeo.
Stori za hapa na pale ziliendelea wakati helikopta ikipasua anga
kwa kasi kubwa, kila mmoja akawa na shauku kubwa ya kutaka
kusikia jinsi tulivyoianza oparesheni ile mpaka muda ule walipoku-
ja kutupa msaada.
Nilikuwa najitahidi kuwafafanulia kwa kina kwa sababu kama
nilivyosema, wote waliokuwa ndani ya helikopta hiyo, walikuwa ni
viongozi, tena wa ngazi za juu!
Akili yangu kwa wakatu huo ilikuwa haijatulia kabisa na japoku-
wa kila mtu alikuwa ananipongeza, bado sikuwa na amani kabisa.
Kitendo cha kumkosa Abdulwaheed, kilinifanya nione ni kama

238 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

hakuna kitu chochote kilichofanyika.


Safari iliendelea na hatimaye tukawasili Kunduchi, helikopta
ikatua na sisi kushuka, tukaingia kwenye magari yaliyokuwa
yanatusubiri na kwa sababu kama nilivyosema, wote walikuwa ni
viongozi wa ngazi za juu, kila mmoja alikuwa na gari na dereva
wake akimsubiri.
“Tutaondoka pamoja!” alisema baba yake Saima akiniambia
kwa sauti ya chini, basi pale tukawa tunaendelea kupokea pongezi,
maafisa wengi wa kijeshi wakawa wanawapongeza viongozi wetu
lakini pia wakawa wananipongeza na mimi kwa kuongoza oparesh-
eni iliyoisha kwa mafanikio, nikawa sina namna zaidi ya kupokea
pongezi zao.
Misafara ya viongozi ilianza kuondoka, baba yake Saima ambaye
kama nilivyoeleza kwamba ndiye aliyekuwa rubani wa helikopta
iliyotuchukua kutoka eneo la tukio, yeye alikuwa wa mwisho
kuondoka kwa sababu kulikuwa na makabidhiano yanafanyika
kwanza, nikawa namsubiri kwenye gari lake, dereva wake akinipi-
gisha stori za hapa na pale.
“Watu wote tulikuwa tunajua mmeenda kwenye mazoezi, mara
tunashtukia inaingia taarifa ya dharura ya kutaka vikosi vyote
vijiandae kuja kuwapa nguvu, tukabaki tunashangaa,” alisema
yule dereva ambaye naye ni miongoni mwa vijana wa ‘kitengoni’,
ikabidi nicheke.
“Una mbinu kali sana kaka! Pengine usiri ndiyo uliofanikisha
mara ii oparesheni ikakamilika! Nakukubali sana mzee, siku ny-
ingine unichukue na mimi kwenye misheni zako,” alisema, kabla

239 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

sijamjibu mazungumzo yetu yakakatishwa na baba yake Saima am-


baye alifungua mlango wa gari wa nyuma na kuja kukaa na mimi.
Nilishangaa kwa sababu kiitifaki, alipaswa kukaa mbele na
dereva wake lakini akaja kukaa na mimi, nikajikuta nikitabasamu.
Alipoingia tu, alinikumbatia kwa nguvu huku akinipigapiga mgon-
goni na mkono wake mgumu kama kipande cha mti, akawa anani-
pongeza sana.
“Nashukuru sana lakini naamini kama bado kazi haijaisha!”
“Najua! Najua vizuri sana na hivyo ndivyo roo ya kipambanaji
inavyotakiwa kuwa! Lazima umalize kila kitu ndiyo roo yako
itulie!” alisema, akaniambia kwamba katika kila hatua ninayopiga,
hasa katika kazi za hatari kama zile, natakiwa kujipongeza.
“Vijana wote ulioondoka nao wamerudi salama, ni wachache
waliopata majeraha madogomadogo, mmeweza kukiangusha kikosi
chote cha wale wahuni, tena wakiwa na silaha nzito! Kwa nini
uelekeze akili zako kwa mwendawazimu mmoja aliyekimbia?”
alisema baba yake Saima, nikaona ni kama kwa kiasi fulani ana
pointi, nikashusha pumzi ndefu.
“Tunawashikilia miongoni mwa vijana wako wawili ambao tu-
nahisi kuwa ndiyo waliokuwa wanavujisha taarifa,” alisema, kauli
ambayo ilinishtua kidogo na kunifanya niwe na shauku ya kutaka
kuwajua ni akina nani.
“Kama isingetumika mbinu iliyotumika ya kufanya kila mmoja
aamini kwamba ni ‘drill’, pengine yangeweza kutokea kama
yaliyotokea awali, tulitumia akili kubwa sana,” alisema baba yake
Saima, safari ikaendelea na hatimaye tuliwasili ofisini.

240 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Mapokezi niliyopewa usiku huo, yalikuwa ni ya kipekee sana,


kila aliyekuwa ananiona, alikuwa akija na kunikumbatia na kuni-
pongeza kwa kazi nzuri iliyofanyika, nikajikuta nikiwa na furaha
isiyoelezeka.
Nilikwenda moja kwa moja mpaka kwenye ofisi ya mkurugenzi
ambaye naye nilipofika, alikuja kunikumbatia tena kwa nguvu
wakati muda mfupi tu uliopita tulikuwa naye kwenye helikopta.
“Umeniokoa kijana wangu! Najua kazi haijakamilika lakini
umeniheshimisha sana! Umetuheshimisha viongozi wako na
kila mmoja usiku wa leo atalala vizuri! Tulikuwa kwenye wakati
mgumu sana sema mambo mengi tunayafanya kuwa siri tu sisi
viongozi wenu!
“Namba moja alikasirika sana na kuona hatutimizi majukumu
yetu lakini kwa hili ulilolifanya usiku huu wa leo, utamfanya
arejeshe imani kwetu kitengi kizima,” alisema mkurugenzi, akani-
taka nikaandike ripoti haraka kwa sababu usiku huohuo walikuwa
wanatakiwa kwenda kuonana na namba moja na kumpa mrejesho
wa kila kitu kilivyofanyika.
Ni hapo ndipo nilipopata picha kamili ya kwa nini viongozi wote
awali walionesha kuchanganyikiwa kabisa na kwa nini baada ya
kukamilika kwa oparesheni hiyo walikuwa na furaha kubwa mno
kiasi cha kufanya waone kutoroka kwa Abdulwaheed kutokuwa
tatizo kabisa.
Nilikuwa naelewa vizuri jinsi namba moja alivyokuwa hapendi
masihara kabisa linapokuja suala la kazi! Niliikumbuka siku nili-
yoenda kukutana naye ana kwa ana kabla sijasafiri kwenda maso-

241 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

moni, na jinsi alivyonipa nasaha nzito.


Kwa kifupi hakuwa mtu wa mchezo kabisa kwenye kazi na hilo
kila mmoja alikuwa analijua ndiyo maana ikitokea kuna jambo am-
balo mwenyewe analitaama kwa karibu, watu wote wa chini yake
wanakuwa matumbo joto muda wote mpaka kazi ikamilike.
Basi nilitoka ofisini kwa mkurugenzi, harakaharaka nikaenda ofi-
sini kwangu, nikakuta wasaidizi wangu wameshaniandalia kahawa
chungu kwa ajili ya kuchngamsha akili kwa sbabau sasa ilikuwa
inaingia siku ya pili bila kulala hata sekunde moja.
Nilipiga kahawa karibu nusu nzima ya chupa ya chai, tena mfulu-
lizo, nikawa naendelea kuandika ripoti, mahali nilipokuwa nahitaji
usaidizi, vijana wangu walikuwa pembeni yangu kunisaidia, huku
wakiendelea na stori za hapa na pale, wakisimuliana jinsi kazi
ilivyokuwa ngumu kule porini.
Nikiwa naendelea na kazi hiyo ya kuandika ripoti, simu yangu
ilianza kuita! Muda huo ilikuwa ni takribani saa nane za usiku,
ilikuwa ni namba ya mmoja kati ya wale vijana wangu waliobaki
kule porini, ambaye alikuwa miongoni mwa wale wawili niliowapa
jukumu ya kuendelea kumuwinda Abdulwaheed.
Ilibidi nisimame na kusogea pembeni kwa sababu sikutaka mtu
mwingine yeyote ajue chochote kilichokuwa kinaendelea. Haraka-
haraka nikapokea simu.
“Haloo!”
“Chief!”
“Nipe ripoti!”
“Tumemfuatilia jamaa mpaka alipotoka nje kabisa ya hifadhi!”

242 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Enhee! Imekuwaje?”
“Inaonesha alikuwa anavuja damu nyingi sana kwa sababu kote
alikopita tumekuta michirizi ya damu!”
“Twende kwenye point! Amepatikana hajapatikana?”
“Hajapatikana, tumefanikiwa kuikuta pikipiki aliyoitumia kuto-
rokea lakini eneo tulipoikuta, tumeona matairi ya gari. Inaonesha
alikuja kuchukuliwa na gari lakini akiwa na hali mbaya maana hata
pikipiki yenyewe imelowa damu!”
“Mungu wangu! Kwa hiyo amefanikiwa kutoroka?”
“Ametoroshwa! Amechukuliwa na gari!” ilisikika sauti upande
wa pili, nikajikuta nimeduwaa nikiwa hata sijui niseme nini tena!
Zilikuwa ni habari ambazo kiukweli zilinichanganya na sasa ni-
kawa najua kabisa kazi haijaisha!
Kama kuna watu wameweza kuwasiliana naye na kwenda kum-
chukua na gari huko maporini, maana yake ni kwamba bado mtan-
dao wao hatukuwa tumeumaliza.
“Tunaendelea na uchunguzi wetu kama kuna chopchote tutata-
arifiana,” ilisikika sauti ya yule kijana wangu, nikabaki nimeiweka
simu sikioni, hata sikujua ilikatwa muda gani.
Nilipokuja kurudi kwenye hali yangu ya kawaida, nilitembea
harakaharaka kurudi pale kwenye meza yangu, nikaendelea kuan-
dika ripoti na baada ya kumaliza, ilibidi niongeze na yale maelezo
kwamba Abdulwaheed alikuwa ametoroka. Nilijua hayatawafurahi-
sha viongozi lakini ilikuwa ni lazima kila kitu kisemwe kwa ukweli
na usahihi.
Baada ya kumaliza, niliichukua ile ripoti kwa kutumia ‘USB

243 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Disk’, wengi wanaziita flash, hizi zinazotumiwa kuhamishia ma-


faili mbalimbali kutoka kwenye kompyuta moja kwenda nyingine,
wengine wanazitumia kuwekea nyimbo.
Nilitoka kwa hatua za harakaharaka kuelekea ofisini kwa mkuru-
genzi, nikamkuta na yeye akiwa bize kuandika kwenye kompyuta
yake pale mezani kwake.
“Umeshamaliza?”
“Ndiyo kiongozi,” nilisema na kumkabidhi ile flash, akaichome-
ka kwenye kompyuta yake kisha akatulia, nadhani alikuwa anasu-
biri mafaili yaliyopo ndani yake yafunguke. Ilipomaliza, nilimuona
akiisogelea zaidi kompyuta yake na kuvaa miwani vizuri, akaanza
kuipitia ile ripoti, neno moja baada ya jingine, kwa umakini mkub-
wa.
“Hii nini tena!” alisema huku akigeuka ‘laptop’ yake na kunio-
neshea ile sehemu ya mwisho niliyokuwa nimeweka hitimisho
kwamba Abdulwaheed ametoroka.
“Aah, nime...”
“Umefanya nini Snox? Hii hawawezi kuipenda, nimekwambia
tunakwenda kuonana na namba moja! Unafikiri nani anayeweza
kufafanua kuhusu hili?
“Tumekubaliana kwamba hili tuliweke chini ya kapeti kwanza,
sisi ndiyo tunajua kwamba katoroka na tunajua ni kwa namna gani
tunaweza kumpata! Naifuta,” alisema, ‘aka-highlight’ kile kip-
engele chote kisha akabonyeza kitufe kwenye laptop yake kilicho-
andikwa ‘delete’, kipengele chote kikafutika.
“Tusifanye mambo yawe mengi, lazima tuhakikishe kwamba

244 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

tunatuliza presha kwanza kisha mambo mengine yataendelea,”


alisema kwa sauti ya chini, nikatingisha kichwa kuonesha kum-
uelewa.
“Unaweza kwenda kupumzika, tukutane asubuhi!” alisema,
nikainamisha kichwa kwa adabu kuonesha kukubaliana na ali-
chokisema, nikageuka na kuanza kupiga hatua za taratibu, kichwa
nikiwa nimekiinamisha.
Nilitoka na kurudi ofisini kwangu, nikakaa kichovu nikiendelea
kutafakari mambo mengi ndani ya kichwa changu! Ni kweli nili-
kuwa nahitaji kupumzika kwa sababu kama nilivyoeleza, nilikuwa
na zaidi ya saa arobaini na nane sijakigusa kabisa kitanda!
Lakini katika hali kama hiyo, ningewezaje kulala? Kilichokuwa
kinafanyika, ilikuwa ni kama kuficha moto kwa blanketi. Abdulwa-
heed alikuwa mtu hatari kwelikweli na hatukutakiwa kumdharau
hata kidogo.
Baada ya kutafakari kwa kina, niliona pengine suala la kwenda
kupumzisha kichwa changu hata kwa saa mbili tu kinaweza kunid-
saidia sana kunifanya nirudishe umakini kwenye kichwa changu.
Ilibidi niwaage vijana wangu kwamba nakwenda kupumzika
kidogo na kama kuna chochote, basi wanifuate kwenye chumba
maalum cha mapumziko!
Sikutaka kutoka kwenda nyumbani kwa sababu kama nilivyo-
sema, japokuwa kila mtu alikuwa anaamini kwamba kazi imekwi-
sha, ndani ya kichwa changu nilikuwa najua kwamba haijaisha na
chochote kinaweza kutokea wakati wowote.
Muda mfupi baadaye, tayari nilikuwa kwenye chumba cha

245 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

mapumziko pale ofisini, nikajitupa kwenye kitanda kimoja kati


ya vitanda vinne vilivyokuwa ndani ya chumba hicho, kikiwa ni
moja kati ya vyumba karibu vitano ambavyo hutumika kwa ajili ya
mapumziko mafupi hususan mnapokuwa kwenye misheni nzi-
tonzito.
Sikutaka hata kuvua chochote, sikuvua hata viatu, kwa kifupi
nililala kama nilivyotoka kule porini. Nilichokumbuka na kuzinga-
tia, ilikuwa ni kuweka ‘alarm’ kwenye simu yangu, muda mfupi
baadaye nikapitiwa na usingizi zito.

246 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

10
N
ILIKUJA kuzinduliwa na alarm kwenye simu
yangu, nikaamka harakaharaka na kitu cha kwanza,
ilikuwa ni kwenda bafuni, nikavua nguo zote na
kujimwagia maji ya baridi. Japokuwa usingizi
haukuwa umeisha, lakini angalau nilijihisi kuwa
mwepesi sana, nikatumia takribani dakika kumi bafuni, maji ya
baridi yakiendelea kunimwagikia mwilini kutoka kwenye ‘bomba
la mvua’.
Nilijikausha vizuri, nikavaa nguo zangu kisha nikatoka harakaha-
raka kuelekea ofisini kwangu. Niliwakuta vijana wangu bado wapo
macho, wakawa wananishangaa.

247 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Chief si ulisema unaenda kupumzika?”


“Tayari nimepumzika! Au nyie huwa mnaelewaje kuhusu ku-
pumzika?” nilisema, nikawaona wote wakitazamana, nadhani
walishangazwa na jinsi nilivyotumia muda mfupi pengine tofauti
kabisa na walivyokuwa wamefikiria. Kwangu mimi ninapokuwa na
jambo linalokisumbua kichwa changu, kulala kwa saa moja huwa
ni mapumziko tosha kabisa.
Nilichukua ‘diary’ yangu kisha nikawataka wawili kati yao tu-
ongozane! Wakainuka harakaharaka, nikawaongoza kuelekea kule
kwenye vyumba vya chini au basement kama tulivyokuwa tuki-
kuita.
Akili mpya niliyoipata, ilikuwa ni kurudi kwa yule mzee wa
Kisomali kwa sababu hata mwanzo, ni yeye ndiye aliyenipa taarifa
zilizonisaidia sana kuikamilisha oparesheni ile kule porini.
“Mtanisubiri hapa!” niliwaambia vijana wangu, baada ya kuwa
tumeshafika kule chini, wao wakabaki nje ya mlango wa chumba
maalum nilichokuwa nimemfungia yule mzee wa Kisomali.
Nilifungua mlango kimyakimya, nikawasha taa, yule mzee
akashtuka na kuanza kuangaza macho huku na kule. Bado alikuwa
amefungwa vilevile kama nilivyomuacha, akashtuka zaidi kugun-
dua kwamba ni mimi.
“Nisaidie kijana wangu, nahisi sukari imeshuka!” alisema kwa
sauti ya kukauka, kwa ule muda aliokuwa amefungwa pale, nili-
kuwa na matumaini kwamba sasa atakuwa tayari kutoa ushirikiano
zaidi.
Nikamsogelea bila kusema chochote, nikawa namtazama, na

248 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

yeye akawa ananitazama kwa macho ya huruma.“Najua kwenye


kile misheni mnayopanga huwa mnakuwa na plan B! Nataka
uniambie, ni nini mlichokuwa mmekipanga kufanya endapo mbinu
ya kwanza ya kuingia mjini kwenda kufanya tukio lenu imeshindi-
kana?” nilimuuliza, nikamuona akipepesa mdomo wake, akiwa ni
kama anayetafakari nini cha kujibu.
“Sijui!”
“Unakiuka makubaliano yetu si ndiyo?” nilisema huku nikim-
sogelea.
“Snox mimi unanionea tu!” alisema, nikashtuka sana kumsikia
akinitaja kwa jina hilo. Ni kweli hilo lilikuwa ni jina langu la utani
au jina maarufu lakini ni watu wachache sana waliokuwa wanali-
jua, wakiwemo wafanyakazi wenzangu na baadhi ya watu ambao
nimewahi kushirikiana nao huko nyuma kabla sijafungua ukurasa
mpya wa maisha yangu.
Kitendo cha yeye kuniita kwa jina hilo kilinifikirisha sana na
kulikuwa na mambo mawili yaliyokuwa yanapita kwenye kichwa
changu.
Moja niliwaza kwamba pengine anaweza kuwa amesikia wenzan-
gu wakiniita kwa jina hilo, nikajaribu kuvuta kumbukumbu, haku-
kuwa na mahali popote ambapo alilisikia jina hilo kuanzia siku ya
kwanza tunakamata mpaka siku hiyo.
Nikawa pia nawaza kwamba pengine anaweza kuwa amelisikia
jina hilo kutoka kwa watuhumiwa wenzake waliokuwa wakishi-
kiliwa pale kwa sakata lile! Hilo pia liligoma kuniingia akilini kwa
sababu tangu afikishwe, alikuwa kwenye chumba cha peke yake na

249 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

watuhumiwa wote walikuwa wakitenganishwa, kila mmoja akiwa


kwenye chumba cha peke yake ili kutoharibu uchunguzi.
Kama hayo yote yalikuwa hayawezekani, basi hapo ndipo nilip-
owaza kuhusu jambo la pili; kwamba alikuwa ananijua na pengine
hata wenzake walikuwa wananijua. Nilitafakari kwa kina, tangu
tulipoanza misheni ile, hakunamahali popote nilipowahi kuhisi
kwamba pengine Abdulwaheed na wenzake wanaweza kuwa wa-
nanijua. Nilihisi kichwa kinaanza kupata moto tena.
“Unafahamu nini kuhusu Snox?”
“Sihafahamu chochote, nalijua jina tu!”
“Umelijulia wapi hilo jina?”
“Nimelijua tu!”
“Sikiliza! Hatuna muda wa kupoteza. Bila shaka umelisikia vy-
ema swali langu na kama hujalisikia, ngoja nilirudie tena.
“Najua kwenye kile misheni mnayopanga huwa mnakuwa na
plan B! Nataka uniambie, ni nini mlichokuwa mmekipanga ku-
fanya endapo mbinu ya kwanza ya kuingia mjini kwenda kufanya
tukio lenu imeshindikana?”
“Mimi sijui chochote Snox! Viongozi huwa hawaelezi Plan B
ya wanachokipanga mpaka muda wake ukifika!” alisema, mapigo
ya moyo yakanilipuka kuliko kawaida. Unaweza kushangaa kauli
kama hiyo inawezaje kufanya mapigo ya moyo wangu yalipuke?
Ni kwa sababu kuu mbili! Ya kwanza ni kwamba endapo vion-
gozi hususan wa haya makundu ya kihalifu wasiposema chochote
kuhusu ‘Plan B’, maana yake ni kwamba lazima kilichopangwa
awali kitatimia kwa namna yoyote ile na pengine katika namna

250 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ambayo hakuna aliyeitegemea na ndiyo maana wameamua kuli-


fanya suala hilo kuwa siri.
Lakini kubwa zaidi, msemo huo haukuwa mgeni masikioni
mwangu! Nilishausikia sana kipindi hicho nikiwa bado sijauanza
ukurasa mpya wa maisha yangu na mtu pekee aliyekuwa anapenda
kuutumia, hakuwa mwingine bali Mutesigwa! Bosi Mute! Mtu
hatari kuliko kawaida.
Kitendo cha mzee huyo wa Kisomali kwanza kuniita kwa jina
la Snox ambalo nilikuwa nalitumia sana nikiwa chini ya Bosi
Mute enzi hizo, na muda huohuo kuja kutumia nukuu aliyokuwa
anapenda kuitumia Bosi Mute, kilinifanya niishiwe nguvu! Hali-
kuwa jambo la bahati mbaya, ni kama alikuwa anajaribu kufikisha
ujumbe fulani kwangu.
Wakati nikiwa naendelea kutafakari kwa kina, yule mzee wa
Kisomali alikuwa ananitazama kwa kunikazia macho akiwa ni
kama anayetaka kuzisoma hisia zangu! Ambacho hakuwa anakijua
ni kwamba mafunzo niliyoyapitia mpaka wakati huo, yalifanya
nisiwe kama binadamu wengine ambao unaweza kuzisoma hisia
zao kwa kuwatazama machoni.
“Kwa kuwa umekiuka makubaliano yetu, nadhani sasa ni wakati
sahihi wa mimi kuendelea kuanzia pale nilipokuwa nimeishia!”
nilimwambia, mapigo ya moyo yakiwa yananienda mbio kwelik-
weli! Kwa kifupi nilikuwa ‘nime-panic’ nikiwa ni kama siamini.
Jina la Bosi Mute lilinifanya niwe ni kama nimechanganyikiwa
ingawa sikutaka kabisa kuonesha hisia zangu. Sikutaka kabisa kua-
mini na wala sikuwahi kuwa nimefikiria kabisa kwamba jina hilo

251 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

linaweza kuja kusikika masikioni mwangu katika hali tete kama ile
tuliyokuwa nayo kwa wakati huo.
Nilisogea kwenye ile swichi ya ukutani, nikaiwasha, kile chuma
alichokuwa ananing’inia yule mzee wa Kisomali kikawa kinapanda
juu na kusababisha na yeye avutwe juu na kuanza kuning’inia,
kilipofika katika kiwango nilichoona kinatosha, miguu yake ikiwa
haijagusa kabisa chini, nilisogea kwenye lile boksi la vifaa vya
kutesea lililokuwa kwenye meza ya chuma iliyokuwa pembeni.
Harakaharaka nilivaa ‘gloves’ maalum, nikachagua vifaa
nilivyoona vinafaa kwa sababu ilishaonesha dhahiri kwamba
mwendawazimu huyu alikuwa anataka kucheza na akili yangu.
“Nakuomba unisikilize kidogo, dakika yako moja tu ya ku-
nisikiliza inatosha kabisa na baada ya hapo nitakuwa tayari kwa
hatua yoyote utakayoona inafaa!” alisema lakini sikutaka kum-
sikiliza kabisa, ‘kichaa’ kilishaanza kunipanda.
“Usitumie hasira, unaweza kupata majibu ya unachokitafuta bila
hata kutumia nguvu, mimi ni mkubwa kwako kiumri na nilishaku-
onesha utayari wa kukupa ushirikiano na nimekusaidia kuyajua
mengi ambayo hukuwa unayajua, kwa nini hutaki kunisikiliza
kijana wangu?” alisema, nikawa tayari nimeshachukua zana zangu
zote na kumsogelea.
“Sijui chochote kuhusu Plan B lakini naweza kukusaidia kuku-
onesha ni nani anayeweza kuwa anaijua na mahali alipo! Nisikilize
tafadhali kijana wangu!
“Sukari imepanda na nisipopata matibabu ndani ya muda mfupi
tu naweza kurudi kwa Muumba wangu, itakusaidia nini kumtesa

252 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

mtu ambaye anajua kwamba ndani ya muda mfupi baadaye ataku-


fa?
“Nadhani jukumu lako kubwa la kwanza ni kuhakikisha naende-
lea kuwa hai! Nisaidie dawa zangu nami nitakuelekeza unapoweza
kupata unachokitaka,” alisema yule mzee! Kwa kipindi chote tangu
tulipomkamata, sikuwahi kuhisi kwamba mzee huyu anaweza
kuwa bna nguvu ya ushawishi kwenye maneno yake kama ali-
chokionesha wakati huo.
Alichokisema ilikuwa ni kweli kwamba endapo ni kweli alikuwa
na tatizo la kisukari, kwa muda wote ambao nilikuwa nimemfunga
akiwa ananing’inia pale kwenye kile chuma, lazima hali yake ili-
kuwa imefikia katika hatua mbaya zaidi.
Ni kweli nilikuwa nimepanic na nilikuwa na hasira kali ndani ya
moyo wangu lakini hiyo haikuwa sababu ya mimi kukiuka maadili
ya kazi yangu!
“Hivi unanijua vizuri we mzee! Mimi ni mwendawazimu kuliko
wendawazimu wote unaowajua, ninapotaka jambo langu huwa
hakuna cha kunizuia!” nilisema kwa jazba, akawa ananitazama,
safari hii kwa macho ya hofu yaliyokuwa yamechanganyikana na
kutia huruma ndani yake.
“Ni wapi ninapoweza kuipata hiyo Plan B?”
“Nimekwambia unipe dawa zangu kwanza kisha na mimi nitaku-
pa unachokitaka,” alisema kwa kutetemeka, nikajikuta nikishusha
pumzi ndefu.
“Nikikupima na kugundua kwamba huna Kisukari nitakumaliza
kwa mikono yangu mwenyewe.”

253 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Sikudanganyi kijana wangu! Nisaidie nami nitakusaidia,”


alisema, nikarudisha vile vifaa pale kwenye boksi na kutoa simu,
nikapiga kwa mmoja kati ya vijana wangu ambaye pia alikuwa na
taaluma ya udaktari, nikamtaka afike haraka pale nilipokuwepo,
akiwa na kifaa maalum cha kupimia kiwango cha sukari kwenye
damu, kinachotumiwa na wagonjwa wa Kisukari.
“Hakuna vita unayoweza kushinda peke yako kijana wangu! In-
awezekana wewe ukawa na moyo wa kuipambania nchi yako lakini
watu wako wa karibu na unaowaamini wakawa tofauti kabisa na
wewe!
“Unapaswa kuwa na upeo mpana zaidi wa kufikiria, maadui zako
hawako mbali na wewe na ndiyo maana taarifa zinavuja kirahisi
kwenda upande wa pili!” alisema, nikazidi kupigwa na butwaa.
Ilionesha mzee huyu alikuwa na mambo mengi ambayo yangeni-
saidia kama ningeenda naye vizuri kuliko kutumia nguvu, nikaji-
pongeza kwa kuzidhibiti hisia zangu.
Muda mfupi baadaye, yule daktari wetu niliyempigia simu tayari
alikuwa amewasili, nikasikia mlango ukigongwa. Ilibidi kwanza
nikabonyeze tena swichi ukutani, yule mzee ambaye alikuwa
ananing’inia kama nyama buchani, akashushwa chini taratibu
mpaka miguu yake ilipogusa chini, mikono bado ikiwa imefungwa
vilevile kwenye kile chuma.
Nilienda kufungua mlango, mtaalamu wetu akaingia akiwa na
kigbegi chake kidogo kilichokuwa na vifaa tiba muhimu. Nikamu-
elekeza nini cha kufanya, akashauri kwamba mhusika afunguliwe
kwanza mikono pale nilipokuwa nimemfunga kwa sababu miiko

254 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ya kidaktari ilikuwa inazuia mtu kuchukuliwa vipimo akiwa katika


hali kama ile.
Alitoa kifaa maalum kiitwacho Glucometer ambacho ni maalum
kwa kupima kiwango cha sukari kwenye damu kwa wagonjwa wa
Kisukari, akatoa na vifaa vingine wakati mimi nikimfungua yule
mzee pale nilipokuwa nimemfunga.
Nilipomaliza, nilimkokota mpaka kwenye kiti cha chuma kili-
chokuwa mle ndani, nikamkalisha kisha nikazunguka upande wa
pili wa meza na kukaa, nikampa ishara yule daktari wetu aendelee
na kazi yake, huku nikiwa makini kutazama kila kilichokuwa
kinaendelea.
Aliandaa vifaa vyake vizuri na muda mfupi baadaye, alianza
kumpima, nikamuona akitingisha kichwa kwa masikitiko. Mpaka
hapo tayari nilishapata majibu kabla hata daktari hajasema cho-
chote, akanisogelea ule upande niliokuwa nimekaa nikiwatazama
kwa karibu.
“Ni kweli ana kisukari, na kiwango chake cha sukari kimepanda
sana, hii ni hatari,” aliniambia kwa sauti ya chini.
“Nini kinatakiwa kufanyka?”
“Achmwe sindano za Insulin kushusha sukari lakini pia baada ya
hapo anatakiwa kuwa anapewa chakula maalum ili kudibiti kiwan-
go cha skai kwenye mwili wake. Wagonjwa wa aina hii wanahitaji
uangalizi wa kipeee,” alisema kisha nikampa jukumu la kuendelea
naye.
Alimsogelea, akawa anamuuliza baadhi ya maswali na baada ya
hapo, alimchoma sindano, akakusanya vitu vyake na kuondoka

255 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

zake akinieleza kwamba anakwenda kuwasiliana na wapishi ili


kuangalia namna ya kumsaidia.
Alipoondoka, nilisogeza kiti changu izuri, tukawa tunatazama
na yule mzee, akashusha pumzi ndefu na kunishukuru kwa kile
nilichokifanya.
“Najua wakati mwingine inakuwa vigumu kuwa na utu ka-
tika mazingira magumu kama haya. Najua jinsi ulivyo na wakati
mgumu wa kuongoza oparesheni ambayo hata wewe mwenyewe
huijui lakini kwa kuwa umeonesha ubinadamu kwangu, kama nili-
vyokuahidi basi nipo tayari kutoa ushirikiano,” alisema, na mimi
nikashusha pumzi ndefu huku nikiwa nimemkazia macho.
“Mikocheni B, karibu na Kanisa la Mlima wa Moto,” alisema,
akanitajia namba ya nyumba na kunieleza kwamba kuna mtu
muhimu sana ambaye ni miongoni mwa viongozi wa juu wa kundi
lao ambaye ndiye anayejua kwa undani mipango yote ilivyokuwa
imepangwa na ndiye aliyekuwa akiratibu kila kitu.
“Ila angalizo ni kwamba huwa anawasiliana na baadhi ya viongzi
wenu humu ndani na ndiyo wanaomvujishia kila kinachoendelea
kwa hiyo unatakiwa kuwa makini, usimuamini mtu yeyote, fanya
kwanza uchunguzi kwa sababu sidhani kama unao mud wa kutosha
wa kuwea kuzuia hiki kinachokwenda kutokea.
“Kwa nini Magogoni na si sehemu nyingine yoyote?”
“Ni kwa sababu ya anayeishi hapo!”
“Amefanya nini?”
“Mimi pia sijui na sidhani kama kuna yeyote kati ya sisi watu wa
kawaida anayejua, ni viongzi ndiyo wanaojua.”

256 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Kwa nini unashirikiana na watu wa aina hii!”


“Wanalipa vizuri sana, wewe hushangai mpaka vongozi wako
wanaamua kushirikiana nao? Ile ni fursa kama zilivyo fursa
ningine, mtu yeyote akipata nafasi ya kujua jinsi wanavyolipa,
hawezi kukataa hata kidogo! Hili jambo siyo dogo kama ambavyo
unaweza kufikiria,” alisema, nikashusha pumzi ndefu huku nikien-
delea kumkazia macho.
“Kwa nini unaniambia yote haya!”
“Ni kwa sababu umeyaokoa maisha yangu, nilishakata tamaa ya
kuendelea kuishi na pengine kama leo usingekuja na nisingepata
dawa, ungekuwa mwisho wangu,” alisema, nikawa naendelea kuta-
fakari mambo mengi kuhusu kile alichokuwa ameniambia.
“Mna wanachama wangapi?”
“Kwa hapa nchini au?”
“Kwani mpo na wapi kwingine?”
“Tupo kila mahali!”
“Kwa hapa nchini?”
“Ni wengi, siwezi hata kukadiria idadi yake.”
“Wengi ndiyo wangapi?”
“Kweli tena siwezi kukadiria idadi lakini elewa kwamba ni
wengi,” alisema, nikaona nisiendelee kupoteza muda kwa sababu
taarifa alizokuwa amenipa zilikuwa zinatosha kwa wakati huo.
Nilitoka na moja kwa moja nikaenda kuzungumza na mku wa
kitengo cha interrogation ambaye kimsingi ndiye aliyekuwa ki-
ongozi wa shughuli ya kuwahoji watuhumiwa wote waliokuwa
wamekamatwa kwenye oparesheni ile tangu ilipoanza.

257 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Nilitaka kujua kama kuna chochote cha maana ambacho wa-


naweza kuwa wamekipata katika kuwahoji watuhumiwa wote,
wale waliokuwa pale ofisini na wale waliotawanywa kwenye ‘safe
house’ zetu baada ya kujisalimisha kule Selous.
“Bado hakuna chochote cha maana, wote wanaonesha wazi
kabisa kwamba wamefundishwa kutozungumza chochote, nadhani
tutalazimika kutumia mbinu nyingine za kijasusi kuwalazimisha
waseme ukweli,” alisema, nikashusha pumzi ndefu na kumweleza
kwamba muda haukuwa rafiki, walipaswa kuwa tayari wameanza
kutumia mbinu nyingine za kuwalazimisha kuzungumza.
Nilitoka na bila kumweleza yeyote chochote, niliingia ndani ya
gari na kuaga kwamba nakwenda kupumzika. Nilichokigundua ni
kwamba watu karibu wote walikuwa wanaamini kwamba shughuli
imeisha na tumefanikiwa kulizima jaribio lile la kigaidi.
Kwangu hiyo ilikuwa ni kama taa nyekundu kuwaka ndani ya
kichwa changu kwa sababu nilikuwa na uhakika wa asilimia moja
kwamba kazi haijaisha na haitaisha mpaka tuwapate viongozi wa
juu wa kundi lile la wahalifu pamoja na kuelewa kwa kina ni nini
kilichokuwa nyuma ya pazia.
Lengo la safari yangu ilikuwa ni kwenda mpaka Mikocheni
kuanza kuchunguza kwa kina pale nilipoelekezwa na yule mzee
wa Kisomali kwamba ndipo anapoishi mmoja kati ya viongozi wa
kundi hilo hatari.
Niliendesha gari kwa kasi na haukupita muda mrefu nikawa
tayari nimeshafika Mikocheni. Ili kutoamsha taharuki yoyote,
nilienda kulipaki gari langu sehemu ambayo ni mbali kidogo na

258 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

eneo nilipoelekezwa.
Nikasogea mpaka kwenye kituo cha Bajaj kilichokuwa jirani na
pale nilipopaki gari, nikamchukua dereva Bajaj mmoja na ku-
muomba anipeleke katika Kanisa la Mlima wa Moto, tukakubali-
ana bei kisha safari ikaanza.
Niliamua kuchagua Bajaj na siyo bodaboda kwa sababu nilikuwa
na uhakika kwamba kama alichokisema yule mzee wa Kisomali ni
kweli, lazima mahali anapoishi mtu huyo patakuwa na kamera za
ulinzi ambazo zinarekodi kila kinachoendelea kwa hiyo njia nyepe-
si ni kujificha kwenye Bajaj.
Haukupita muda mrefu tukawa tumeshafika kwenye mtaa
nilioelekezwa, mtihani ukawa ni kusoma namba za nyumba kwa
sababu kwa kawaida vibao vya namba za nyumba huwa zinaandik-
wa kwenye vbao vidogo ambavyo ni lazima usogee karibu ndipo
unapoweza kuziona.
“Kaka hebu simama kwanza mara moja,” nilimwambia yule
dereva tukiwa ndiyo kwanza tumeanza kuingia kwenye mtaa huo,
kweli akasimama.
Nikamwambia nimeelekezwa na mwenyeji wangu namba ya
nyumba, nikamuomba akanisaidie kusoma namba za nyumba mbili
zilizokuwa zinafuata ili nipate njia sahihi ya kuhesabu mpaka kwe-
nye nyumba husika.
Bila hata kutafakari kwa kina na kuelewa nilichokuwa nakitaka,
yule dereva alipaki Bajaj yake na kuteremka, akavuka upande wa
pili na kusogea kwenye geti la kwanza, akaisoma namba kwa sauti,
akasogea kwenye geti la pili, napo akaisoma kwa sauti, nikawa

259 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

nimeshapata picha kamili kwani nilifananisha na ile namba aliyo-


nipa yule mzee, nikagundua kwamba kumbe zilikuwa zinaongeze-
ka kwa kwenda mbele kwa hiyo nyumba husika lazima ilikuwa
upande uleule laini mbele zaidi.
“Njoo tuondoke zetu!” nilisema, akarudi kwenye Bajaj na kuion-
doa, nikamwambia twende kwa mwendo wa taratibu wakati tukien-
delea kuzihesabu nyumba kuelekea kwenye ile namba niliyokuwa
nimepewa na yule mzee wa Kisomali.
Alifanya kama nilivyomuelekeza, na mimi nikawa makini kuen-
delea kuhesabu nyumba.
Karibu nyumba zote kwenye mtaa huo zilikuwa ‘mijengo’ ya
maana kisawasawa, ile namba ikaenda kuangua kwenye bonge la
jumba la ghorofa moja lililokuwa na uzio mrefu ambao juu yake
kulikuwa na nyaya za umeme kuzuia mtu yeyote asiruke uzio.
Lakini pia kama nilivyokuwa nimehisi, kulikuwa na kamera
kubwa na za kisasa kwa ajili ya ulinzi (CCTV), nikawa naendelea
kulisoma jumba hilo kwa umakini mkubwa. Niliona kama haitoshi,
nikatoa simu yangu na kuwasha kamera, nikawa napiga picha kwa
umakini wa hali ya juu ili nisije kuamsha taharuki ya aina yoyote.
Tulilipita jumba hilo bila yule dereva Bajaj kuwa amegundua
chochote, tukaenda mpaka mwisho wa mtaa, nikamwambia ageuze
turudi tulipotoka kwa sababu ni kama nimekosea maelekezo nili-
yopewa na mwenyeji wangu.
“Huu mtaa una mijengo ya hatari sana!” nilianzisha mjadala na
yule dereva Bajaj nikitaka kujua kama kuna chochote alichokuwa
anakijua.

260 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Watu wana mawe braza, acha kabisa!” alisema kwa Kiswahili


cha vijana akimaanisha kuna watu wana fedha nyingi sana.
“Hebu angalia mjengo kama huu! Hivi nani anaumiliki huu!”
nilisema nikimuoneshea ile nyumba ambayo ndiyo niliyokuwa
nimeelekezwa na yule mzee wa Kisomali, nikawa na shauku
kubwa ya kusikia ni nini ambacho angenijibu.
“Aah! Hapo si ndiyo anapoishi .... (akamtaja jina), si unam-
jua?” aliniuliza, kiukweli taarifa zile zilinishtua sana kwa sababu
nilikuwa namjua mhusika aliyetajwa na pengine mtu yeyote
anayefuatilia mambo ya mjini anaweza kumjua akisikia jina hilo
alilokuwa amenitajia.
“Hapana simjui, ndiyo nani kwani?” nilizidi kumtega ili nipate
uhakika.
“Si yule mfanyabiashara anayemiliki vituo vya mafuta vya ...
(akataja jina ambalo nalo ni maarufu sana!), moyo ukanifyatuka
paah!
“Duh! Anaishi maisha kama yupo peponi aisee!”
“Mzee ana mawe yule balaa! Hayo magari anayotembelea sasa
ndiyo balaa zaidi!” alisema, nikawa nazidi kulitazama jumba hilo
kwa umakini zaidi, mapigo ya moyo yakizidi kunienda mbio.
Ni hapo ndipo nilipoelewa yule mzee wa Kisomali aliposema
jambo hilo halikuwa dogo wala jepesi kama ambavyo watu wali-
kuwa wanalichukulia. Kama taarifa alizokuwa amenipa zilikuwa
na ukweli, basi hakika lilikuwa jambo zito sana na uzito wake
ulikuwa unaonekana wazi kwa kumtazama mtu aliyekuwa nyuma
ya mambo yote yaliyokuwa yanaendelea.

261 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Pengine unaweza kuwa na shauku kubwa ya kutaka kumjua


mfanyabiashara niliyeoneshwa jumba lake ni nani na alikuwa na
nguvu kubwa kiasi gani. Nitakuja kulieleza kwa undani suala hilo
lakini itoshe tu kusema alikuwa ni mtu mwenye nguvu kubwa ya
kifedha pamoja na nguvu kubwa sana ya ushawishi.
Bado mapigo ya moyo wangu yalikuwa yakizidi kunienda mbio
kuliko kawaida, japokuwa tulikuwa tumeshalipita jumba hilo, bado
nilikuwa naendelea kulitazama kwa kupitia kidirisha kidogo cha
turubai la Bajaj kwa nyuma.
Tukiwa tunakaribia kuumaliza ule mtaa, nikiwa hata sijui nini
cha kufanya, niliona ni kama kuna mtu ametoka kwenye lile geti,
nikamwambia yule dereva Bajaj asimame na kupaki pembeni,
kweli akafanya hivyo, nikawa naendelea kutazama kwa makini.
Ni kweli kuna mtu alikuwa ametoka kwenye lile jumba na mtu
mwenyewe alikuwa amevalia sare kuonesha kwamba alikuwa ni
mlinzi na mkononi alikuwa na bunduki. Akasogea mpaka katikati
ya barabara ya lami iliyokuwa inapita eneo lile, kisha akawa ana-
punga mkono kama anayeita kitu fulani.
Muda mfupi baadaye, nikashuhudia gari moja la rangi nyeusi
likitoka na kuingia barabarani, yule mlinzi akarudi upande wa lile
jumba, gari likaingia barabarani. Kwa bahati nzuri, lilipotoka nje
ya geti, lilianza kuja upande ule tuliokuwepo.
“Vipi kwani braza!”
“Tulia mdogo wangu, unaona hilo gari linalokuja, sasa tangulia
mbele kisha uwe unaenda kwa kasi ndogo, likikupita tu, unatakiwa
kulifuata nyumanyuma na nitakuelekeza nini cha kufanya!”

262 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Hatujakubaliana bei sasa!”


“Usiwe na wasiwasi, nitakupa kiwango chochote unachokitaka,”
nilimwambia, kweli akafanya kama nilivyomueleza, akaingiza
Bajaj barabarani na akawa anaenda kwa mwendo wa taratibu, lile
gari likazidi kuongeza mwendo na baada ya muda mfupi, likawa
limeshakolea, likatupita kwa kasi kubwa.
Nilijaribu kutazama ni nani aliyekuwepo ndani yake lakini kwa
ile kasi nilishindwa kuona chochote, ukizingatia pia kwamba liliku-
wa na vioo vya ‘tinted’.
Jambo pekee ambalo nilifanikiwa kuliona kwa ufasaha, zilikuwa
ni namba zake za usajili na kilichonichosha zaidi ni kwamba zili-
kuwa ni namba za kiserikali, tena za taasisi moja nyeti sana.
“Braza! Una uhakika kweli na ulichokisema?”
“Kwa nini mdogo angu?”
“Si umeona namba hizo? Usije ukaniingiza matatizoni broo! Nina
familia mwenzio,” alisema yule dereva Bajaj, ikabidi nijichekeshe
kama njia ya kutaka kumtoa wasiwasi kwa sababu kwa mtu yeyote
lazima angeogopa kwa sababu kama nilivyosema, zilikuwa ni
namba za taasisi moja nyeti sana na ilivyoonesha, ni kwamba hata
aliyekuwemo ndani yake, alikuwa kiongozi wa juu ndani ya taasisi
hiyo kutokana na aina yenyewe ya gari.
Aliendelea kulifuata lile gari nyumanyuma, tukatoka kabisa
kwenye ule mtaa na haukuopita muda mrefu, tukawa tumeshafika
mahali nilipokuwa nimeacha gari langu.
“Simama hapo!” nilimwambia, nikimuoneshea kusimama kando
la gari langu ambalo nilikuwa nimeliingiza ndani kidogo kutoka

263 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

barabarani. Kweli alifanya hivyo na ninachoweza kumsifu ni


kwamba alikuwa ‘sharp’ kwelikweli.
Tayari nilikuwa nimeshachomoa noti mbili za shilingi elfu
kumikumi, nikamshikisha harakaharaka, nikakimbia mpaka kwe-
nye lile gari na ndani ya sekunde chache nikawa nimeshaingia na
kuliwasha, nikaliondoa kwa kasi na kumpita yule dereva wa Bajaj
ambaye bado alikuwa amesimama pale akiwa haelewi kilichokuwa
kinaendelea.
Nikawa tayari nimeshingia barabarani na uzuri ni kwamba bado
lile gari lilikuwa kwenye upeo wa macho yangu, likawa linakata
mitaa huku na mimi nikizidi kuongeza kasi ili lisije kunipotea,
nikaliona likiingia kwenye barabara ambayo wengi huwa wanaiita
Barabara ya Cocacola, ile inayotokea Mwenge kwenye mataa
kuelekea upande kilipo kiwanda cha Cocacola na baadaye mpaka
kilipo kituo cha redio moja maarufu.
Lilipoingia kwenye barabara hiyo, lilianza kuelekea upande wa
Mwenge, na mimi nikawa nalifuata lakini ili kuzuia kushtukiwa,
ilibidi niache umbali fulani katikati yetu, tukawa tunatenganishwa
na magari kama mawili hivi.
Niliendelea kulifuatilia huku nikiwa makini kwelikweli. Lili-
pofika kwenye taa za kuongozea magari za Mwenge, nilishangaa
kugundua kwamba kumbe kulikuwa na magari mengine mawili
pamoja pikipiki, zile zinazotumika kuongozea misafara ya vion-
gozi.
Gari lilipunguza mwendo, pikipiki ya kuongozea misafara ika-
washwa na kuingia barabarani, gari moja kati ya yale mawili

264 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

likaifuata pikipiki hiyo na kuingia barabarani, lile gari nililokuwa


nalifuatilia likaunga msafara nyuma ya lile gari la kwanza kisha
lile lingine likafuata kwa nyuma.
Ving’ora vya ile pikipiki vikaanza kupigwa kuashiria magari
mengine yapishe njia, askari wa usalama barabarani nao wakaji-
tokeza na kuanza kusaidia kupangua magari eneo hilo, msafara
ukapata njia na kuondoka kwa kasi eneo hilo, na mimi nikaunga
kwa nyuma, nikiwa ni kama siamini kilichokuwa kinaendelea.
Msafara ulikuwa katika kasi kubwa na japokuwa inafahamika
kwamba kuvamia msafara ni kosa, sikujali! Nilikuwa nataka kujua
kwa undani ni nini kilichokuwa kinaendelea.
Basi niliendelea kuufukuzia kwa nyuma na kwa bahati nzuri
sikupata upinzani wa aina yoyote, safari ikaenda kuishia Kurasini,
yalipo makao makuu ya taasisi hiyo. Kikubwa nilichokuwa naki-
taka, ilikuwa ni kuona ni nani aliyekuwa ndani ya gari hilo.
Yale magari mengine yaliyokuwa yakisindikiza msafara, yalipaki
pembeni, nikaona mlinzi mmoja akienda kufungua mlango, macho
yangu yakawa makini kutazama aliyekuwa anafunguliwa mlango.
“Mungu wangu!” nilijisemea baada ya kumuona bosi wa juu
kabisa wa idara ile akiteremka kwenye gari, akasalimiana na
baadhi ya watu kisha akaongozwa na mlinzi wake kuingia ofisini
kwake.
Kwa sasa naomba nimtambulishe kigogo huyu kwa jina la Ka-
mishna! Kama nilivyoahidi, nitakuja kufafanua kwa undani ni nani
na wadhifa wake ni upi lakini kwa kifupi, alikuwa ni miongoni
mwa viongozi wa juu na wa muhimu wa vyombo vya ulinzi na

265 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

usalama.
Nilibaki nimepigwa na butwaa nikiwa ni kama siamini, kama
yule mfanyabiashara wa kule Mikocheni ndiye kiongozi wa mpan-
go hatari uliokuwa mbele yetu, na bado viongozi wa juu kama
huyu Kamishna wanakutana naye, tena nyumbani kwake, kulikuwa
na tatizo kubwa pengine kuliko mtu yeyote alivyokuwa anafikiria.
Kwa mara nyingine, nilihisi ni kama jambo hilo limekuwa kubwa
kuliko uwezo wangu, nikawasha gari langu nililokuwa nimelipaki
mita chache kutoka kwenye ofisi za ile taasisi, nikaondoka taratibu
huku nikiwa hata sijui nini cha kufanya.
Swali ambalo bado nilikuwa sijalipatia majibu, yule mzee wa Ki-
somali aliniambia kwamba baadhi ya viongozi wetu, tena wa ngazi
za juu kabisa kwa maana ya Kitengo walikuwa wanawasiliana kwa
karibu na viongozi wa misheni ile ya kuiangusha Magogoni.
Niliyemuona, hakuwa anatoka Kitengo japo alikuwa kiongozi wa
juu kabisa, yaani wale viongozi ambao namba moja anapokuwa na
jambo lolote linalohusu masuala ya ulinzi na usalama, basi ndiyo
anaokaa nao meza moja kujadiliana nini cha kufanya.
Sasa hawa viongozi aliowataja huyu mzee wa Kisomali kutoka
Kitengo ni akina nani na uhusika wao ulikuwaje? Ni nani hasa
aliyekuwa anavujisha taarifa za misheni yetu kwa kundi hili hatari
la magaidi? Maswali yalikuwa mengi kuliko majibu na mtu pekee
ambaye niliona anaweza kuwa msaada kwangu kwa wakati huo,
alikuwa ni baba yake Saima.
“Haloo chief!”
“Naam!”

266 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Upo ofisini?”
“Ndiyo! Nipo.”
“Naomba kuonana na wewe haraka iwezekanavyo! Naomba iwe
nje ya ofisi.”
“Ulitakiwa kuwa nyumbani kupumzika muda huu! Wewe siyo
mashine, unatakiwa kupumzika, mkeo na familia yako inakuhitaji
pia.”
“Baba, siwezi kupumzika na sitapumzika mpaka nitakapoki-
maliza nilichokianza. Ni wewe ndiye uliyenifundisha falsafa hii!”
nilisema, nikasikia baba yake Saima akishusha pumzi ndefu kisha
akaniuliza mahali nilipo.
“Niko njiani natokea Kurasini!”
“Coco Beach!”
“Roger that sir!” nilimjibu kwa ‘code’ za kijeshi nikimaanisha
kukubali kile alichokuwa amekisema, nikakaa vizuri kwenye
usukani na kuanza kukanyaga mafuta kwa kasi kubwa kuelekea
Ufukwe wa Coco.
Baada ya takribani dakika ishirini hivi, tayari nilikuwa nimefika
Coco Beach, nikawa naangaza macho huku na kule, hususani seh-
emu ambayo mimi na baba mkwe wangu, baba yake Saima tulisha-
wahi kukutana kama mara mbili hivi siku za nyuma kwa masuala
ya kikazi.
Niliangaza huku na kule lakini sikumuona na ufukweni hapo
palikuwa na watu wachache kwa muda huo. Nikaenda kupaki gari
kwenye maegesho, ile nateremka tu, nikashtukia mtu ananigusa
begani.

267 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Lilikuwa ni tukio ambalo sikulitegemea kwa hiyo hata geuka


yangu ilikuwa ni ya kujihami kwelikweli, nikiwa tayari kwa cho-
chote! Nikakutana na baba yake Saima, akiwa kwenye uso wa kazi
kwelikweli.
Hakunisemesha kitu zaidi ya kunipa ishara kwamba niingie ndani
ya gari lake, nikafanya hivyo, na yeye akaingia ndani ya gari lake,
akawasha na kuondoka eneo hilo, nikawa hata sielewi tunaelekea
wapi.
Katika kila alichokuwa anakifanya baba yake Saima, alikuwa aki-
tanguliza umakini wa hali ya juu mno, na mimi nikawa naendelea
kujifunza mambo mengi kutoka kwake. Tulitoka kwenye maegesho,
tukaelekea upande ule wenye miamba mingi mikubwa, kwa wenyeji
wa Coco Beach watakuwa wananielewa vizuri zaidi.
Tulipita na gari kwenye njia nyembamba chini ya miti, tuka-
tokezea kwenye kimlima kidogo cha miamba, tukapanda na gari
mpaka juu kabisa. Uzuri ni kwamba gari alilokuwa analitumia,
lilikuwa na nguvu ya kupita mahali popote.
Tulipofika upande wa juu kabisa wa miamba ya matumbawe pale
Coco Beach, alifunga breki na kupaki gari kwenye eneo la wazi,
akafungua mlango na kuteremka, na mimi nikafanya hivyohivyo.
Tukasogea mbele ya gari, akanigeukia na kunitazama machoni.
“Ni nini?”
Ilibidi kwanza nishushe pumzi ndefu, nikamueleza kuanzia mwan-
zo, kuanzia kile nilichokuwa nimeelezwa na yule mzee wa Kisomali
kule ‘basement’, nikamueleza jinsi nilivyofuatilia nyumba aliyon-
ielekeza, jinsi nilivyomuona Kamishna akitoka ndani ya jumba

268 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)
la mfanyabiashara huyo na jinsi nilivyomfuatilia mpaka makao
makuu.
“Umefanya jambo la hatari sana lakini la kishujaa!” alisema huku
akianza kupiga hatua fupifupi kuelekea mbele, akiwa amekiinami-
sha kichwa chake chini.
Nikarudia kumsisitiza kwamba yule mzee wa Kisomali ameni-
hakikishia kwamba kuna viongozi wetu ambao wanashirikiana na
kundi lile la kigaidi na kwa jinsi walivyokuwa wamejipanga, ni
lazima Magogoni itaangushwa katika siku na muda uliopangwa.
“Vipi kama ukigundua kwamba miongoni mwa viongozi hao na
mimi nipo?” alisema na kunigeukia, nikamtazama kwa mshtuko
mkubwa, akatabasamu. Kwa jinsi nilivyokuwa namjua, kamwe
asingeweza kununulika, hata iweje kwa hiyo nilikuwa na uhakika
kwamba ananitania, na mimi nikajikuta nikiachia tabasamu hafifu.
“Hapa ndipo ile kanuni ya kutomuamini mtu yeyote inapokuja!”
alisema huku akivaa tena uso wa kazi, akaniambia kwamba jambo
la baadhi ya viongozi wasiokuwa na maadili kushirikiana na wa-
halifu, siyo jambo geni Kitengo japokuwa mara zote waliokutwa
na hatia ya kufanya jambo hilo, walishughulikiwa kikamilifu.
“Shida inakuja pale kunapokuwa na zaidi ya mtu mmoja ambaye
anashirikiana na watu hatari kama hao!” alisema, akiwa ni kama
bado anaendelea kutafakari kwa kina ndani ya kichwa chake.
“Mbinu tulizozitumia kukamilisha misheni ya mwisho kule Sel-
ous, ndiyo inayotakiwa kutumika kwa muda huu ili kuwanasa watu
wanaohusika na mchezo huu na nakuhakikishia kwamba hata kama
mtu ana cheo kikubwa kiasi gani, atashughulikiwa kisawasawa,”

269 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

akaendelea kuniambia kwamba Kamishna ni miongoni mwa watu


waliokuwa kwenye kikao na namba moja usiku wa siku iliyopita.
Akaniambia kwamba, mkutano na namba moja usiku uliopita,
umejadili mambo mengi lakini jambo kubwa lililojadiliwa ni
kwamba hofu ya shambulio hilo imekwisha kabisa na namba moja
anatakiwa kuendelea na ratiba zake kama kawaida.
“Kwa hiyo kama umemuona akitoka kwa huyo kigogo, maana
yake ni kwamba amekwenda kumpa ripoti ya kila kitu kilichozun-
gumzwa katika kikao hicho. Hii ni zaidi ya uhaini na huyu anat-
akiwa kuanza kuchunguzwa mara moja na kwa kupitia yeye, ndipo
tunapoweza kujua nyoka ni nani ndani yetu,” alisema huku akitoa
simu yake.
Alibonyeza namba fulani kisha akaiweka simu sikioni, nikam-
sikia akizungumza maneno matatu ambayo ndiyo ilikuwa mara
yangu ya kwanza kuyasikia, yakionesha kuwa na maana iliyojifi-
cha, kitaalamu tunaita ‘code’ kisha baada ya hapo, alikata simu.
“Jukumu la kwanza ni kwenda kushirikiana na watu wa Cyber na
IT kufuatilia mawasiliano yake, inatakiwa tujue huwa anawasiliana
na nani miongoni mwetu na hapo ndipo tunapoweza kujua wapi
pa kuanzia, kumbuka hatuna muda wa kutosha,” alisema baba
yake Saima akiwa ananitazama machoni, na mimi nikamjibu kwa
kutingisha kichwa kuonesha nimekielewa kile alichokuwa anakise-
ma.
Akageuka na kuanza kutembea kwa hatua ndefundefu kurudi
kwenye gari lake, na mimi nikawa namfuata, akafungua mlango na
kuingia, na mimi nikataka kufanya hivyo lakini akatingisha kichwa

270 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)
chake kunizuia, nikajikuta natabasamu.
Kwa lugha nyepesi alikuwa anataka nitembee kwa miguu mpaka
kule kwenye maegesho nilikokuwa nimeacha gari langu, aka-
geuza gari lake harakaharaka, akionesha umahiri mkubwa kwenye
udereva kisha akasimama karibu yangu, akanipa ishara kwamba
nimsogelee, akashusha kioo cha gari lake.
“Namba moja amehakikishiwa kwamba jaribio limezimwa. Awali
kulikuwa na ratiba ya dhifa ya kitaifa kati ya namba moja na wa-
fanyabiashara wakubwa na baadhi ya viongozi ambayo ilipangwa
kufanyika usiku wa siku ambayo hawa maharamia walipanga
kutekeleza shambulio lao na kwa kuwa amehakikishiwa kwamba
jaribio limezimwa, ameagiza ile dhifa iendelee kama ilivyokuwa
imepangwa awali.”
“Haiwezekani! Jaribio bado halijazimwa!”
“Mimi na wewe ndiyo tunaolijua hili lakini wengine wote wa-
naamini kwamba kazi imemalizika,” alisema, nikajikuta nikiishiwa
nguvu kuliko kawaida.
“Kwa hiyo lazima ujue kwamba kazi imezidi kuwa ngumu na
hivi tunavyozungumza, tayari amerudi Magogoni na anaendelea
na shughuli zake kama kawaida,” alisema kisha akafunga vioo na
kuondoka kwa kasi.
Ilikuwa ni taarifa nyingine iliyozidi kunipagawisha na kufanya
kichwa changu kiwe ni kama kimemwagiwa maji ya moto.
Inawezekanaje taarifa za Kiintelijensia zioneshe kabisa kwamba
shambulio limepangwa kufanyika siku fulani, mpaka ubalozi wa
taifa kubwa kama Marekani nao wakatoa taarifa kama hiyohiyo,

271 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)
halafu kirahisirahisi tu watu wote waamini kwamba jaribio li-
mezimwa na ratiba ziendelee kama kawaida? Lilikuwa ni jambo
lililoashiria kwamba kuna tatizo kubwa linakwenda kutokea mbele
yetu.
Kibaya zaidi ni kwamba kama alivyosema baba yake Saima, uli-
kuwa umebakia muda mfupi sana kabla ya kuufikia usiku wa tukio
na ilitakiwa kazi kubwa, nzito na ngumu ifanyike haraka iweze-
kanavyo kabla ya siku husika haijafika.
Niliendelea kuwaza huku kichwa changu kikiendelea kuchemka,
nikawa natembea kwa hatua ndefundefu kutoka kule juu kwenye
miamba ya matumbawe, kurudi kwenye ukumbi maarufu wa Coco
Beach, mahali nilikokuwa nimeacha gari langu.
Kuna muda nilikuwa naona ni kama nachelewa kufika, nikaonge-
za mwendo huku nikitamani hata nikimbie, nikateremka kutoka
kule juu, nikapita kwenye mchanga wa ufukweni na muda mfupi
baadaye tayari nilikuwa nimeshafika kwenye ule ukumbi, nikatoka
harakaharaka mpaka kule nje kwenye maegesho, nikiwapita wa-
hudumu kadhaa waliokuwa wakinikaribisha, wakidhani pengine
nilikuwa mteja.
Muda mfupi baadaye, tayari nilikuwa nimeshaingia kwenye gari,
nikawasha na kuondoka kwa kasi kubwa kiasi cha kuwafanya watu
wengine waliokuwepo eneo lile wabaki wamepigwa na butwaa, un-
geweza kudhani ni gari lililoibiwa na sasa majambazi wanajaribu
kukimbia mkono wa sheria.
Kiukweli zile taarifa zilikuwa zimenichanganya kisawasawa,
muda mwingine mapigo ya moyo wangu yakawa yananienda mbio

272 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kwa sababu kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele ndivyo


kichwa changu kilivyokuwa kinazidi kuelemewa na mambo mengi
ambayo hata sikuwa najua mwisho wake utakuwaje.
Uchovu niliokuwa nao, ulionekana unaweza kuwa kikwazo
cha akili yangu kufanya kazi kwa ufasaha, nikaona njia nzuri ni
kusimama kwenye ‘supermarket’ iliyokuwa jirani na barabara ya
kutokea kule Coco Beach.
Jinsi nilivyotoka barabarani na kuingia kwenye supermarket
hiyo, bado ilikuwa inaonesha ni kwa kiasi gani kichwa changu
hakikuwa sawa. Wakati walinzi wakija kutaka kunikataza nisipaki
eneo lile, tayari nilikuwa nimeshashuka na kuingia ndani, nikasikia
tu wakiita kwa nguvu lakini hata sikugeuka.
Nilienda kuchukua vikopo viwili vya ‘energy drink’ za baridi,
nikatoa noti ya shilingi elfu tano na kumkabidhi msichana aliyeku-
wa pale kaunta, wakati anahangaika kuandika risiti kama ujuavyo
manunuzi ya ‘supermarket’ na kurudisha chenji, tayari nilikuwa
nimeshatoka nje, nikakuta wale walinzi wakiwa wananisubiri kwa
shauku.
“Bosi, mbona unaleta dharau kwenye kazi za watu?” alisema
mmoja wao wakiwa ni kama wanataka kunizuia nisiingie kwenye
gari kwa kile walichoona ni kama nimewadharau. Sikutaka kubis-
hana nao, kwa hali niliyokuwa nayo, ningeweza kusababisha tukio
lingine eneo lile kwa mtu yeyote ambaye angeonekana kutaka
kunichelewesha.
Nilichokifanya, ilikuwa ni kuonesha uungwana wa kutoa kit-
ambulisho changu cha kazi, nikamuonesha yule aliyekuwa ana-

273 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)
onekana ‘kuchonga’ zaidi, nikamuona akiufyata mkia na kunipisha
kwa adabu.
Nikaingia ndani ya gari na kuwasha, nikaondoka kwa kasi ya
mshale, wakawa wananishangaa huku akiwa anamuelezea mwen-
zake jambo, nadhani alikuwa anamfafanulia kuwa mimi ni nani.
Niliendelea kukanyaga mafuta kwa kasi kubwa, na haukuoita
muda mrefu nikawa nimeshaingia kwenye Barabara ya Ali Hassan
Mwinyi, safari ikaendelea na haukupita muda mrefu nikawa nime-
shafika ‘getini’.
Kwa hali niliyoingia nayo, kila mtu alibaki kunishangaa, nadhani
ni kwa sababu kila mmoja alikuwa akiamini kwamba kazi imeisha.
Lakini kama kazi imeisha, mbona mimi bado niko ‘wanguwangu’
kiasi kile? Nilipita moja kwa moja mpaka ofisini kwangu, nikawa-
kuta vijana wangu wakiwa wamejipumzisha, wakiendelea na kazi
ndogondogo, nao wakashangaa kwa jinsi nilivyoingia mbiombio.
Niliwasha kompyuta yangu na kukaa, nikijitahidi kwa kadiri
ya uwezo wangu kutuliza kichwa changu, nikawa naendelea ku-
jimiminia ‘energy drink’. Kiafya huwa hutakiwi kuzinywa kwa fujo
kiasi hicho lakini kwa hali niliyokuwa nayo, ilibidi suala la afya
yangu lisubiri kidogo.
Nikanyanyua simu ya mezani na kupiga kwenye kitengo cha
Cyber, nikamuomba mkuu wa idara aje haraka ofisini kwangu,
nikapiga pia kwa watu wa IT kwa maana ya Kitengo cha Teknolojia
ya Mawasiliano, muda mfupi baadaye wote wakawa wameshafika.
Bado nilikuwa nasumbuliwa na tatizo la kujua nani natakiwa kum-
wamini na nani sitakiwi kumwamini kwa sababu bado hatukuwa

274 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

tumepata jibu la nani anayetuzunguka na kutoa siri kwa maadui zetu


lakini pia kwa wakati huo, sikuwa na cha kufanya zaidi ya kujilazi-
misha kuwaamini wawili hawa ingawa ndani ya kichwa changu
nilishapanga kuwa nawafuatilia kwa karibu kwa kuwatumia watu
wengine!
Mara zote hivyo ndivyo tunavyofanya kazi zetu, ukitumwa kazi
fulani, basi lazima ujue pia kwamba kuna mtu mwingine pia ame-
tumwa kukufuatilia kama unatekeleza kile ulichotumwa, na mambo
yakiwa magumu kama ilivyokuwa kwa wakati huo, tunalazimika
pia kumuongeza mtu wa tatu ambaye naye atakuwa akiwafuatilia
hawa wawili kwa karibu kama wanatekeleza majukumu yao.
Niliwatoa vijana wangu wote, tukabaki watu watatu tu mle ndani,
nikawaeleza nilichokuwa nimewaitia na nilijitahidi sana kuficha
lengo kuu la kile nilichokuwa nawaagiza. Kazi iliyokuwa mbele
yetu, ilikuwa ni kufuatilia mawasiliano ya Kamishna kwa karibu na
kuangalia ni watu gani aliokuwa akiwasiliana nao mara kwa mara
na kuwafuatilia kwa karibu watu hao.
Niliwaeleza kwamba tuna muda wa saa 12 pekee kuikamilisha
kazi hiyo, kwa lugha nyepesi ni kwamba ilikuwa inatakiwa kabla
siku haijaisha tuwe tumeshapata majibu. Uzuri ni kwamba teknolo-
jia iliyokuwa inatumika, ilikuwa kubwa na ya kisasa inayoweza
kufanya kazi kubwa ndani ya muda mfupi.
“Lengo kuu la misheni hii ni nini?”
“Mimi mwenyewe sijui, nimepewa maagizo kma ninavyowapa
nyie?” “Ni kuhusu ile oparesheni ya hawa wendawazimu?”
“Ile si imeshamalizika? Hakuna uhusiano wowote,” nilidanganya

275 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)
waziwazi wakati mkuu wa Cyber akiniuliza. Nikawaambia wote
wawili kwamba kazi hiyo inatakiwa kuhusisha watu wachache kadiri
iwezekanavyo na inatakiwa kufanywa kwa usiri mkubwa.
Uzuri ni kwamba paka mtu upewe nafasi ya ukuu wa kitengo pale
kwetu, ni lazima wewe mwenyewe uwe umebobea kwenye kazi in-
ayohusu kitengo husika.
“Sawa chief!” waliitikia kwa pamoja, wakainuka na kutoka, ni-
kawaita vijana wangu wawili na kuwapa jukumu la kuwafuatilia kwa
karibu wakuu wale wa vitengo kuona kama wanafanya nilichowaa-
giza na uzuri ni kwamba kwenye kila idara nilikuwa na ‘majembe’
yangu ninayoyaamini.
Ngazi ya tatu nikaamua kusimama mwenyewe, kuwafuatilia wote
kama wanafanya kile nilichowaagiza bila wao wenyewe kujua kama
nawafuatilia. Najua unaweza kujiuliza sana hilo lingewezekanaje,
lakini kama nilivyosema, huo ndiyo mfumo wetu wa kufanya kazi
na kwa sababu mimi nilikuwa na mafunzo kuliko wote, nilikuwa na
uhakika kwamba hakuna anayeweza kunizidi akili.
Kazi ilianza kufanyika na jukumu la kwanza likawa ni kujua Ka-
mishna anatumia simu ya aina gani, kama ni zaidi ya moja, mitandao
ya laini alizokuwa anazitumia lakini pia kama anazo simu nyingine
anazozitumia kwa siri kuwasiliana na watu wake.
Wakati haya yote yanaanza kufanyika, yeye hakuwa akijua cho-
chote na hata sikuwa na uhakika kama ananijua kwa undani na anajua
kwamba ninamfuatilia kwa jicho la karibu.
Wakati sisi tukiendelea na hayo, jambo lingine la ajabu lilitokea!
Nasema ni la ajabu kwa sababu halikuwa na ukweli wowote na hali-
kuwa na ulazima wa kufanyika kwa muda huo.
276 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

11
J
AMBO lenyewe ni kwamba jeshi la polisi liliitisha mku-
tano na waandishi wa habari makao makuu. Katika mku-
tano huo, kiongozi mmoja wa juu katika jeshi hilo kupitia
kwa waandishi wa habari, alilitangazia taifa kwamba ile
hofu iliyokuwapo ya tetesi za kuwapo na mipango ya
shambulizi la ugaidi, lilikuwa limezimwa.
“Napenda kutumia nafasi hii kuwatangazia watu wote kwamba
nchi yetu ipo salama! Kulikuwa na tetesi zilizosambaa kwa kasi
kwenye mitandao ya kijamii na kwenye baadhi ya vyombo vya

277 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

habari kuhusu kuwepo kwa mipango ya shambulizi la kigaidi.


“Habari hizo hazikuwa na ukweli wowote na sisi kama jeshi
tumejiridhisha kwamba nchi ipo salama na tutaendelea kuhakiki-
sha kwamba wananchi na mali zao wanaendelea kuwa salama,”
alisema kamanda.
Kibaya zaidi ni kwamba baada ya kumaliza kuzungumza, haku-
ruhusu maswali kutoka kwa waandishi wa habari na mkutano
ukawa umeishia hapo.
Kama nilivyosema, lilikuwa ni jambo la ajabu kwelikweli kwa
sababu kwanza, kwa maelezo aliyoyatoa kamanda, ni kama aliku-
wa akikanusha taarifa zilizotolewa na ubalozi kuhusu mipango ya
magaidi kufanya shambulio katika siku iliyokuwa imetajwa.
Lakini pia, hakuwa amesema ukweli kwa sababu si kweli kwam-
ba hakukuwa na tishio hilo au kwamba taarifa hizo zilikuwa ni za
uongo. Ukweli ni kwamba taarifa zilizotolewa na ubalozi zilikuwa
ni ukweli mtupu na uzuri ni kwamba kabla hata wao hawajatoa
tamko hilo, sisi tayari tulikuwa tumeshashtukia kila kitu na tuli-
kuwa kwenye ufuatiliaji.
Kingine ni kwamba, tulikuwa tumejaribu kulizima jaribio hilo la-
kini hatukuwa tumefanikiwa kulizima kabisa na ushahidi wa hayo
yote ni kutoroka kwa Abdulwaheed katika mazingira ya kutatani-
sha lakini pia kuhusika kwa mfanyabiashara mkubwa nchini am-
baye alikuwa nyuma ya kundi hatari lililokuwa linapanga kufanya
jaribio hilo.
Baada ya kusikiliza kile alichokuwa amekisema, nilifikiri kwa
jicho la tatu na jibu la haraka ambalo nililihisi, ni kwamba pengine

278 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

viongozi wa juu wa jeshi hilo nao walikuwa wakihusika katika


‘mchongo’ huo kwa namna moja au nyingine, ingawa sikuweza
kuthibitisha hilo kwa wakati huo.
Ilibidi nimpigie tena baba yake Saima na ilibidi nimuombe radhi
kwanza kwa sababu mimi mwenyewe nilishajiona kwamba sasa
nimeanza kuwa msumbufu.
Uzuri ni kwamba alinielewa na akanisikiliza kwa makini, nikam-
ueleza kile kilichosemwa na viongozi wa polisi, akanikanya kwam-
ba sitakiwi kuingilia mambo yanayofanywa na vyombo vingine
vya usalama kwa sababu hayanihusu.
“Viongozi wao walikuwepo kwenye mkutano na namba moja,
kwa hiyo hicho walichokisema siyo kwamba wamekitoa kwenye
vichwa vyao, ni makubaliano ya vyombo vyote vya ulinzi na us-
alama.”
“Lakini si tunafahamu kwamba siyo kweli?”
“Kazi yako isiwe kuhoji kama ni kweli au si kweli! Nimeshak-
wambia wapi unatakiwa kusimamia, unatakiwa kuonesha kwa
vitendo kwamba hicho kilichosemwa siyo kweli! Usizungumze
wala kubishana, unatakiwa kuonesha!” alisema baba yake Saima,
nikashusha pumzi ndefu.
Alichokuwa amekisema kilikuwa na mantiki kubwa kwelikweli,
nadhani ni ule mchecheto niliokuwa nao ndiyo uliofanya hata ku-
fikiri kwangu kusiwe kwa namna ambayo watu wengine wanaweza
kunielewa.
Baada ya kumaliza kuzungumza na baba yake Saima ambaye
alinitaka nirudi kwenye maelekezo aliyokuwa amenipa, sikuwa na

279 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kingine cha kufanya zaidi ya kurudi kwenye kazi yangu ya msingi,


ya kuendelea kumchunguza Kamishna na kuujua ukweli, ikiwa pia
ni pamoja na kuwajua watu kutoka kwenye idara yetu waliokuwa
wanauza siri zetu na kutusaliti.
Wakati hilo halijatulia, ikaja taarifa nyingine ambayo ilizidi ku-
nichanganya mpaka nikawa sielewi nini cha kufanya.
Waziri anayehusika na viwanda na biashara, naye aliitisha mku-
tano na waandishi wa habari. Yeye hakuzungumzia kuhusu ishu
ya usalama, isipokuwa alikuwa akaiwataarifu wananchi hususan
wafanyabiashara kuhusu kuwepo kwa dhifa kubwa ya kitaifa kati
ya namba moja na wafanyabiashara wakubwa, ambayo ingefanyika
Ikulu.
Akaeleza muda ambao shughuli hiyo ingefanyika, ambao
kimsingi ndiyo usiku wa siku ileile ambayo tulikuwa tunajua
kwamba kuna shambulio linapangwa kufanyika ikulu. Akatumia
nafasi hiyo kueleza kwamba maandalizi yalikuwa yakiendelea
vizuri na kwamba baadhi ya wafanyabiashara ndiyo watakaow-
awakilisha wenzao nchi nzima.
Kwa taarifa ile, ilionesha dhahiri kwamba kuna jambo kubwa
sana halikuwa sawa! Pengine namba moja alikuwa akipewa taarifa
ambazo hazina ukweli na wasaidizi wake, au pia pengine kulikuwa
na wasaidizi ambao walikuwa wanajua ni nini kinachokwenda ku-
fanyika na sasa walikuwa wakishiriki kwa namna nyingine kabisa
ambayo itawafanya waendelee kuwa salama wakati nchi ikiingizwa
kwenye tatizo kubwa zaidi.
Nilikumbuka swali ambalo nilimuuliza yule mzee wa Kisomali

280 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kule ‘basement’ kwamba kwa nini shambulio lilikuwa limepangwa


kufanyika Magogoni, nikayakumbuka na majibu yake, nikazidi
kuchanganyikiwa.
“Unatakiwa kusimama imara, usalama wa nchi unakutegemea
wewe, uhai wa namba moja unakutegemea wewe, uhai wa mamia
kama siyo maelfu ya wananchi unakutegemea wewe!
“Unatakiwa kupambana kwa kadiri ya uwezo wako wote ku-
hakikisha shambulio hilo halitokei! Hakuna anayeweza kukuamini
au kukuelewa kwa sasa, hutakiwi kukata tamaa, endelea kupam-
bana na ukweli utafahamika,” nilisikia sauti ikiniambia ndani kwa
ndani.
Nadhani hali hii huwa inamtokea kila mtu, unaweza kuwa kwe-
nye mkanganyiko fulani mzito wa mawazo lakini kuna ile sauti in-
ayotoka ndani yako, ukiisikiliza huwa inasaidia sana! Basi ndicho
kilichonitokea, nilikuwa nazungumza na nafsi yangu.
Baada ya sauti hiyo kusikika kutokea ndani ya nafsi yangu, nili-
jikuta nikipata nguvu mpya na sasa nikaamua kulibeba suala hilo
kwa uzito zaidi, bila kutegemea ushauri wa watu wengine.
Nilirudi kwenye suala la msingi lililokuwa mezani kwa wakati
huo, tayari vijana walikuwa wakifanya kazi yao kwa ukamilifu na
taarifa za awali za muhimu kumhusu Kamishna zilikuwa zime-
shaanza kupatikana.
Jambo lililozidi kunipa uhakika kwamba sikuwa nimekosea kum-
hisi vibaya Kamishna, ni jinsi taarifa za awali zilizoibua mambo
yasiyo ya kawaida kabisa. Kamishna alikuwa akimiliki simu
takribani tano, zikiwa na laini takribani nane za mitandao tofautito-

281 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

fauti, tena zikiwa zimesajiliwa kwa majina ya watu wengine tofauti


kabisa.
Ni laini moja pekee ndiyo iliyokuwa imesajiliwa kwa jina lake,
nyingine ilikuwa imesajiliwa kwa jina la taasisi aliyokuwa anaion-
goza lakini zile nyingine zote zilikuwa na majina tofauti kabisa.
Hilo pekee lilitosha kumfanya mtu yeyote akuhisi vibaya,
inakauwaje kiongozi wa taasisi nyeti kama ile anakuwa na mpan-
gilio wa mawasiliano wenye kutia shaka kiasi kile? Nikawa na
shauku kubwa ya kutaka kujua katika hizo namba, alikuwa ana-
wasiliana na watu gani?
Wakati hilo likiendelea kufanyiwa kazi, nilipatwa na shauku pia
ya kufuatilia akaunti zake za benki pamoja na utajiri aliokuwa
anaumiliki kwa sababu tayari taa nyekundu ilikuwa imewaka kwe-
nye kichwa changu.
Ikabidi nimuombe mwenzetu mwingine ambaye alikuwa mkuu
wa kitengo cha uchumi, ambaye ndiye aliyekuwa akihusika na
kufuatilia utajiri au fedha zozote ambazo zilikuwa zinatia mashaka.
Naye nikamueleza kwamba kila kitu kinatakiwa kufanyika haraka
iwezekanavyo lakini kwa usiri wa hali ya juu bila mtu yeyote kufa-
hamu chochote, kazi ikawa inaendelea kimyakimya.
Ndani ya muda mfupi tu, tayari alishanipa mwanga wa kile
nilichokuwa nimemuagiza kufanyia kazi. Kulikuwa na kiwango
kikubwa cha fedha kwenye akaunti ya Kamishna ambazo kiuha-
lisia hazikuwa zikiendana na kipato chake na ilionesha kwamba
zilikuwa zimetumwa kwenye akaunti hiyo ndani ya siku chache
zilizopita.

282 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Katika mambo ambayo alikuwa amefanya uzembe, ilikuwa ni


kuruhusu miamala hiyo kufanyika kwenye akaunti yake, nadhani
hata yeye mwenyewe hakuwa ametegemea kwamba anaweza kush-
tukiwa kirahisi namna hiyo.
Baada ya kupata taarifa hizo, niliagiza kwamba akaunt zilizoku-
wa zinatuma fedha kwenye akaunti ya Kamishna nazo zifuatiliwe
ili nijue ni nani na nani waliokuwa wanatuma fedha hizo na kama
kulikuwa na maelezo yoyote kuhusu matumizi yake.
Wakati kazi hiyo ikiendelea, ilibidi nitume vijana wengine wawili
kwenda mpaka makao makuu kwenye ofisi za Kamishna kwa ajili
ya kufuatilia nyendo zake, nikawatuma wengine wawili kwenda
kuwafuatilia wenzao kama wanafanya kazi kama tulivyokubaliana
na kama kawaida, mimi nikawa mtu wa mwisho kuangalia kama
kila mmoja anafanya kazi zake kama tulivyoelekezana.
Kila kitu kilikuwa kinafanyika kwa usiri wa hali ya juu, niki-
taka mtu yeyote ambaye hahusiki asijue chochote kilichokuwa
kinaendelea. Mtu pekee ambaye nilikuwa naendelea kumpa taarifa
za kila kilichokuwa kinaendelea, alikuwa ni baba yake Saima.
Uchunguzi wa chini kwa chini uliendelea kwa kasi kubwa na
wakati hayo yakiendelea, upande wa pili maandalizi ya dhifa
ya kitaifa kati ya namba moja na wafanyabiashara wakubwa na
wawakilishi wa vyama vya wafanyabiashara yalikuwa yakiendelea
kwa kishindo.
Bado niliendelea kupata majibu ya kila kilichokuwa kinaendelea
kwa vijana wangu niliokuwa nimewapa kazi na kwa kuwa mimi
mwenyewe nilikuwa namfuatilia kila mtu kwa karibu kabisa,

283 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

taarifa zote nilizokuwa nazipokea, nilikuwa na uhakika kwamba


zilikuwa ni za kweli na za uhakika.
Miongoni mwa watu ambao namba zao zilionekana kuwasiliana
mara kwa mara na Kamishna, alikuwa ni yule mfanyabiashara
mkubwa ambaye asubuhi ya siku hiyo nilimuona kwa macho
yangu akitoka kwenye jumba lake la kifahari.
Ilionesha kwamba walikuwa wakiwasiliana mpaka usiku wa
manane na mazungumzo yao yalikuwa yakichukua muda mrefu.
Namba nyingine alizokuwa anawasiliana nazo sana, zilikuwa ni za
kutoka nje ya nchi, ikiwemo nchini Kenya na Somalia.
Niliagiza namba hizo zifuatiliwe moja baada ya nyingine na hapo
jambo lingine likaibuka. Miongoni mwa watu aliokuwa akiwasili-
ana nao, alikuwepo mfanyabiashara mkubwa wa Mombasa, Jabir
Abdillah almaarufu Jalango.
Huyu Jalango aliwahi kuingia kwenye matatizo makubwa na
Serikali ya Kenya, akitajwa kuwa miongoni mwa watu waliofadhili
shambulio la kigaidi kwenye Ubalozi wa Marekani nchini Kenya
na alilazimika kutoroka nchini humo na kukimbilia mafichoni
ambako alikaa kwa miaka mingi kabla ya kuja kufutiwa mashtaka
yake.
Sikuwa najua vizuri ni nini kilichosababisha akafutiwa mashtaka
kwa sababu nimewahi kufuatilia suala hilo na ilionesha wazi
kwamba alihusika kufadhili shambulio hilo kwa kutoa fedha zilizo-
tumika kununua silaha.
Nilishtuka sana kugundua kwamba mtu mkubwa na anayeam-
inika kwenye serikali kama Kamishna, anaweza kuwa na ma-

284 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wasiliano na mtu anayetuhumiwa kufadhili ugaidi. Hiyo ilikuwa


ni taa nyekundu iliyowaka kwenye kichwa changu na mpaka hapo
nikawa na uhakika kwamba kumbe Kamishna alikuwa anahusika
na njama za kutaka kuiangusha Magogoni.
Swali ambalo sikuwa nimelipatia majibu bado ambalo nilikuwa
na shauku kubwa ya kutaka kulijua, ilikuwa ni watau waliokuwa
wanawasiliana na Kamishna kutokea kwenye ofisi yetu, ambao
kimsingi ndiyo waliokuwa wakivujisha taarifa za oparesheni tu-
lizokuwa tunapanga.
Wakati hayo yakiendelea, nilipata majibu ya swali lingine
muhimu sana kwa wakati huo kuhusu watu waliokuwa wakimtu-
mia Kamishna fedha nyingi kwenye akaunti yake.
Majina matatu yalionekana kwenye taarifa za kibenki, wa kwan-
za alikuwa ni yuile mfanyabiashara mkubwa niliyemshuhudia
Kamishna akitoka nyumbani kwake asubuhi hiyo. Wa pili alikuwa
ni Jalango ambaye kama nilivyosema, alikuwa akiishi Mombasa na
wa tatu alikuwa ni mfanyabiashara mwingine mkubwa wa mafuta
kutoka Falme za Kiarabu, Kadar Murtaza.
Sikuwa nafahamu mambo mengi kuhusu mfanyabiashara huyu
zaidi ya kujua kwamba alikuwa akifanya biashara za mafuta, akim-
iliki visima kadhaa vya mafuta! Bado sikuwa najua anahusika vipi
kwenye kilichokuwa kinaendelea.
Zilikuwa ni taarifa nyingi nilizozipata ndani ya muda mfupi sana,
angalau sasa nikaanza kupata matumaini mapya kwamba tunaweza
kuzuia kilichokuwa kinataka kwenda kutokea.
Ilibidi niandike kila nilichokuwa nimekibaini kwenye ‘diary’

285 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

yangu, nikawa najaribu kuunganisha ‘dots’ ili kupata picha kubwa


ya mtandao mzima wa kundi hilo.
Niliendelea kuandika kila kitu, nikawa najaribu kuandika hata
kile nilichokuwa nakihisi, nikaona ni kama diary hainitoshi, nika-
omba karatasi kubwa ambalo nilihamishia kile nilichokuwa naan-
dika na kuchora kwenye ‘diary’.
Kwa kuwa maandalizi ya dhifa ya namba moja na wafanyabi-
ashara yalikuwa yanaendelea, ilibidi pia niwe natazama kwa ma-
kini kila kilichokuwa kinapangwa, ili kujua kama kinaweza kunipa
picha ya tukio zima.
Kwa kuwatumia vijana wetu waliokuwa Magogoni, niliomba
kupata orodha kamili ya wafanyabiashara wote ambao walitara-
jiwa kuhudhuria kwenye dhifa hiyo. Ndani ya muda mfupi nikawa
nimeshatumiwa majina takribani arobaini ya wafanyabiashara hao.
Nilianza kuyapitia, moja baada ya jingine, nikabaini jambo
lingine la kushtua mno. Katika orodha hiyo, alikuwepo yule mfan-
yabiashara mkubwa wa mafuta aliyekuwa anawasiliana na Ka-
mishna mpaka kufikia hatua ya kiongozi huyo kwenda nyumbani
kwake.
Lakini pia kulikuwa na jina la Jalango, mfanyabiashara mkubwa
kutoka Mombasa aliyekuwa na kashfa ya kudhamini ugaidi na
kubwa kuliko yote, kumbe hata Kadar Murtaza kutoka Falme za
Kiarabu naye alikuwa miongoni mwao.
Nilipigwa na butwaa nikiwa hata siamini, ama kwa hakika kuli-
kuwa na uzembe mkubwa sana uliokuwa unaendelea kwanza kwa
kuanzia na kikosi cha ulinzi wa namba moja pamoja na vyombo

286 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

vingine vya ulinzi na usalama kwa sababu walikuwa wanaenda


kumkutanisha namba moja na watu hatari kwelikweli.
Ikabidi nimpigie simu baba yake Saima na kumweleza nilichoku-
wa nimekibaini, na yeye akashtuka kuliko kawaida na kunitaka
niende ofisini kwake haraka iwezekanavyo.
Nilikusanya kila kitu changu na kutoka, nikaelekea mpaka ofisini
kwake, nikamkuta akiwa ananisubiri kwa shauku kubwa kwelik-
weli. Ilibidi nianze kumueleza mbinu nilizotumia na majibu nili-
yokuwa nimeyapata mpaka muda huo, akawa ni kama haamini.
Utulivu ulimuisha kabisa na swali aliloniuliza lilikuwa ni kama
tayari nilikuwa nimeshawapata watu waliokuwa wanavujisha siri
zetu kutokea ndani.
“Bado lakini naamini ndani ya muda mfupi tutapata majibu!”
“Ni lazima kwanza tuwapate kwa sababu kwa haya
uliyoyabaini,kama hatujawajua, ndani ya muda mfupi tu siri zi-
tatoka na kuwafikia wahusika na kwa jinsi walivyojipanga, tut-
akuwa tunahatarisha sana maisha yetu kwa sababu inaonesha kweli
wamedhamiria kufanya wanachotaka kukifanya.
“Inabidi baada ya kumalizana na wewe hapa, mimi niende kuon-
ana na namba moja ana kwa ana nimueleze kuhusu tulichokibaini
ili na yeye awe anajua kinachoendelea. Hatuwezi kukaa kimya na
taarifa nzito kama hizi!” alisema na kunitaka nikaelekeze nguvu
kubwa zaidi kwenye kuwajua wahusika waliokuwa wanatuzun-
guka.
Tuliachana na baba yake Saima kila mmoja akiwa mbiombio,
nikamuona akiingia kwenye gari lake na kuondoka kwa kasi wakati

287 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

mimi nikirudi kule ofisini kwangu.


Ni kweli kwamba bila kuwabaini watu waliokuwa wakituzun-
guka na kwenda kutoa siri, tungekuwa ni kama tunatwanga maji
kwenye kinu kwa sababu lazima wangevujisha siri ya kilichokuwa
kinaendelea.
Ilibidi nifanye kama baba yake Saima alivyonishauri, nikaele-
keza nguvu zaidi katika ile timu ya Cyber na IT katika kuhakikisha
tunajua undani wa waliokuwa wanatuzunguka. Uzuri ni kwamba
nilikuwa na timu imara ambayo haikuwa inahitaji kusukumwa ili
kutekeleza majukumu yake.
Ndani ya muda mfupi tu, taarifa nyingine mpya zilikuwa zimepa-
tikana. Kulikuwa na mfanyakazi mwenzetu mmoja, Berthany
kutoka kwenye dawati la siasa ambaye ilionesha kuwa alikuwa aki-
wasiliana sana na mtu ambaye naye alikuwa na uhusiano wa karibu
na wale wafanyabiashara ambao tulikuwa tumeshawaweka kwenye
listi ya watu hatari.
Harakaharaka nikaagiza Berthany aanze kufuatiliwa kwa karibu,
mawasiliano yake yote yakaanza kuchunguzwa kwa kina, kili-
chokuja kubainika kikamshangaza kila mmoja.
Berthany ambaye ni mwenzetu kama nilivyoeleza, yeye akiwa
kwenye dawati la siasa, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na
kijana mmoja aitwaye Chriss Walusanga. Huyu Chriss Walusanga
alikuwa ni dereva ambaye alikuwa ameajiriwa na kampuni moja
ya kuuza mafuta, akiwa anamuendesha mmoja kati ya viongozi wa
kampuni hiyo.
Uchunguzi wa kina tulioufanya, ulionesha kwamba Chriss na

288 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Berthany walikuwa na uhusiano ambao haukuwa umefikisha hata


miezi mitatu lakini muda mwingi walikuwa wakiutumia pamoja na
walikuwa wakiwasiliana mno, usiku na mchana.
Kibaya zaidi ni kwamba, kwa kuwa Berthany alikuwa kwenye
dawati la siasa, akiwa amefikia ngazi ya ‘field officer’ alikuwa
anashiriki kwa karibu kwenye misheni zote kubwakubwa zilizo-
kuwa zinaendelea, kwa kifupi alikuwa anajua mambo mengi sana
yaliyokuwa yanaendelea.
Jambo ambalo sasa tulitaka kuwa na uhakika nalo kabla ya
kuchukua hatua, ilikuwa ni kujua ni nini ambacho Berthany huwa
anazungumza na Chriss, na baada ya mazungumzo yao, Chriss
naye alikuwa anakwenda kumwambia nani.
Endapo hili lingefanikiwa, basi mchezo mzima ungejulikana
wazi na tungekuwa na uhakika juu ya mtu anayevujisha taarifa
zetu.
Ilikuwa ni lazima kila kitu kifanyike kwa haraka kwa sababu
hatukuwa na muda wa kutosha, nikaagiza mbali na Berthany
kuanza kufuatiliwa bila mwenyewe kujua, lazima pia simu zake
zote ziwe ‘tracked’ na kurekodiwa ili kusikia ni nini walichokuwa
wanawasiliana na Chriss, nje ya uhusiano wao wa kimapenzi.
Waswahili wanasema penzi ni kitovu cha uzembe, hakika hiki
ndicho kilichokuwa kinatugharimu na pengine inawezekana hata
Berthany mwenyewe alikuwa anashiriki kwenye mchezo huo
hatari bila mwenyewe kujua kinachoendelea kwa sababu alishapo-
fushwa na mapenzi.
Baada ya kuyajua hayo, ilibidi tena nirudi ofisini kwangu, ni-

289 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kakaa chini na kuanza kuandika na kuchora kwenye ile ‘diary’


yangu na lile karatasi, nikijaribu kuunganisha ‘dots’. Hivyo ndivyo
nilivyokuwa nikifanya kazi zangu kwa ufanisi na urahisi, nikipata
taarifa mnpya nakwenda kuzitafutia namna ambayo zinawiana na
taarifa zilizokuwepo.
Katika kuunganisha matukio, niligundua jambo lingine la
muhimu sana. Nimeeleza kuhusu huyu dereva aitwaye Chriss
Walusanga ambaye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na ‘mwa-
nakitengo’ mwenzetu, Berthany.
Sasa jambo jipya ni kwamba, kampuni aliyokuwa anaifanyia
kazi, ambayo ilikuwa ikisambaza na kuuza mafuta, ilikuwa na uhu-
siano wa karibu sana na yule mfanyabiashara mkubwa wa mafuta
wa Mikocheni na ilionesha pia hata umiliki wake ulikuwa na ‘ma-
gumashi’ mengi na uwezekano mkubwa ni kwamba nayo ilikuwa
ikimilikiwa na mfanyabiashara yule lakini kwa kutumia nyaraka za
uongo.
Hiyo pekee ilitosha kutoa picha kubwa kwamba kumbe uhusiano
wa kimapenzi kati ya Chriss na mweetu Berthany, haukuwa uhu-
siano halisi bali kijana huyo alikuwa amepandikizwa maalum kwa
mwenzetu, ili amchote akili kwa kisingizio cha mapenzi.
Picha kubwa ilianza kufunguka sasa, nikawa nawahimiza vijana
wangu kuendelea kufuatilia taarifa moja baada ya nyingine, Berth-
any akawa anafuatiliwa kwa karibu, Kamishna akawa anafuatiliwa
kwa karibu na sasa Chriss Walusanga naye akawa anafuatiliwa
kwa karibu kutaka kujua taarifa alizokuwa anzichota kutoka kwa
Berthany alikuwa anazipeleka kwa nani.

290 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Lakini pia, wakati hayo yakiendelea, nilikuwa naendelea kufua-


tilia kwa karibu kilichokuwa kinaendelea ikulu, huku pia nikiwa na
shauku ya kutaka kujua kama ni kweli baba yake Saima anakwen-
da kuonana na namba moja na kuzungumza naye.
Katika ile orodha ya watu ambao watahudhuria kwenye mku-
tano kati ya wafanyabiashara na namba moja, kulikuwa na majina
mengi ambayo yalikuwa yananipa wasiwasi na miongoni mwa ma-
jina hayo, nilikutana na jina lingine ambalo lilinishtua mno, Gilbert
Mutesigwa.
Akili zangu zilinituma kuamini kwamba huenda mtu huyu
anaweza kuwa ni Bosi Mute kwa sababu ni kawaida yake kuwa
anabadilibadili majina hasa kwenye jina la kwanza na nimewahi
kumshuhudia akijiita Gilbert Mutesigwa kipindi cha nyuma.
Hii ilikuwa ni mara ya pili sasa jina lake linaonekana kwenye hizi
njama zilizokuwa zinaendelea. Sikutaka kuamini kwa haraka kama
ni yeye na sikutaka pia kuamini kwamba anaweza kuwa anahusika
kwa namna yoyote kwenye hili lakini Waswahili wanasema wasi-
wasi ndiyo akili. Niliamua kuliacha suala lake kama kiporo kwanza
kwa sababu lingeweza kunitoa kwenye mstari.
Taarifa ziliendelea kumiminika kwa kasi kubwa, ushahidi wa
alichokuwa anakizungumza Berthany na huyo mwanaume wake
ukawekwa wazi kupitia simu zilizokuwa zinarekodiwa bila mwe-
nyewe kujua.
Baada ya kupata ushahidi huo, ilibidi kwanza niwasiliane na baba
yake Saima kwa kutumia meseji kwa sababu sikuwa na uhakika
kama anaweza kuwa kwenye mazingira yanayoweza kumfanya

291 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

akawa huru kuzungumza na simu.


Uzuri nilipomtaarifu tu kwamba tumegundua Berthany ndiye
anayevujisha taarifa zetu kupitia kwa mwanaume ambaye yupo
naye kwenye uhusiano wa kimapenzi, muda huohuo alinipigia.
Akataka nimpe maelezo ya jinsi nilivyolibaini suala hilo, nika-
mueleza mbinu tulixotumia mpaka kumfikia Berthany, nikam-
sikia akiguna. Nadhani hata yeye mwenyewe hakuwa amefikiria
kwamba mbinu hiyo ingeweza kuzaa matunda kirahisi namna hiyo,
akawa anaendelea kunisikiliza kwa makini nikimfafanulia kila kitu.
“Mna uhakika ni yeye peke yake ndiye anayetoa taarifa zote? Ni-
kimuangalia huyo binti sidhani kama atakuwa analifanya hili peke
yake, labda abanwe anaweza kueleza kwa undani zaidi.”
“Inaonekana hata yeye mwenyewe hajui kama anatumika! Mwa-
naume aliyenaye, amepandikizwa kwa makusudi kwa lengo la
kupata taarifa za kila kinachoendelea ndani.”
“Ni sawa lakini kama nilivyosema, sidhani kama anaweza ni
yeye peke yake, endeleeni kuumiza vichwa, nahisi kuna mtu
ambaye ni mkubwa tu ndiye anayefanya yote hayo, angalieni kwa
karibu Berthany huwa anawasiliana na wafanyakazi au mabosi
gani kisha chimbeni kwa kina,” alisema baba yake Saima, nikashu-
sha pumzi ndefu.
Baada ya kumalizana naye, nilimpigia mkurugenzi ambaye hatu-
kuwa tumezungumza kwa muda kidogo, nikampa maelezo kwa
kina, naye akabaki amepigwa na butwaa na kunitaka niende ofisini
kwake haraka iwezekanavyo.
“Tulikubaliana kwamba ungekwenda kupumzika!” alinihoji mku-

292 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

rugenzi mara tu baada ya kuingia ofisini kwake na kumkuta akiwa


ananisubiri kwa shauku kubwa.
“Nitapumzika nikifa!” nilimjibu kwa kujiamini kwa sababu siku-
ona mantiki ya yeye kuniuliza swali kama hilo katika muda ambao
hali ilikuwa tete kiasi kile.
“Napenda sana jinsi unavyoipenda kazi yako!” alisema huku
akiachia tabasamu, nikawa namtazama kwa makini machoni kwa
sababu alichokuwa amekisema kilikuwa kimeenda kuivuruga akili
yangu.
“Karibu uketi,” alisema huku akinioneshea kiti, nikakaa na kush-
usha pumzi ndefu, yeye akawa anaendelea kuzungukazunguka mle
ofisini kwake, akiwa hata haijulikani alikuwa anatafuta kitu gani.
“Nieleze ulichokibaini!” alisema, nikakaa vizuri na kumtazama,
na yeye tayari alikuwa amekaa kwenye kiti chake, tukawa tuna-
tazamana.
Nilianza kumuelezea kuanzia mara ya mwisho mimi na yeye tuli-
pozungumza na kuniambia nikapumzike baada ya kuwa tumefani-
kisha ile misheni kule Selous. Nikamueleza jinsi ambavyo sikuwa
nimeridhishwa na taarifa za jumla kuwa oparesheni ile imekami-
lika wakati tulikuwa tunajua wazi kwamba kiongozi namba moja
alikuwa amefanikiwa kutoroka.
Nikaendelea kumueleza hatua nilizozichukua mimi binafsi
kuanzia pale tulipokuwa tumeishia kama taasisi, nikaona uso wake
ukianza kubadilika, sasa akawa ‘serious’ kama nilivyokuwa mimi.
Nikamueleza kwamba nilifanikiwa kugundua kwamba Abdul-
waheed alitoroka kwa kutumia pikipiki na baadaye akaenda ku-

293 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)
chukuliwa na gari akiwa ameshatoka nje kabisa ya hifadhi hiyo na
kutelekeza pikipiki aliyokuwa ameitumia, akashusha pumzi ndefu.
Niliendelea kumueleza jinsi nilivyoendelea kuumiza kichwa
kutaka kujua ni nini ambacho walikuwa wamepanga kukifanya
wale wahalifu baada ya kuwa tumeenda kusambaratisha ngome
yao kule Selous, nikamueleza jinsi nilivyobaini kwamba wanaye
kiongozi wao mwingine ambaye ndiyo yule mfanyabiashara
mkubwa wa mafuta aliyekuwa na ushawishi mkubwa serikali.
Nilipofika hapo, alisimama na kuanza kuzungukazunguka mle
ndani, ikabidi nitulie kwanza maana ilionesha ni kama kuna kitu
alikuwa anakijua.
“Nani mwingine anajua kuhusu hili?”
“Hakuna! Ni mimi mwenyewe!”
“Haiwezekani! Unataka kusema haya yote ulikuwa unayafanya
peke yako? Si lazima kuna watu ulikuwa unashirikiana nao?”
“Ni kweli lakini nadhani ungenisikiliza kwanza kwa sababu sija-
maliza!”
“Hapana nataka kujua kwanza nani mwingine anayeyajua haya?”
“Majibu yangu ni kama nilivyokujibu kwamba hakuna!”
“Umeshirikiana na nani? Mbona unashindwa kujibu swali rahisi
namna hii?”
“Wapo walionisaidia lakini hawajui ni nini ninachokifanya! Kila
mmoja ameshiriki kwenye sehemu ndogo ambayo hata hawezi
kujua picha kubwa ni nini!”
“Unafikiri wewe peke yako ndiyo ‘genious’ hapa kitengoni?”
alisema mkurugenzi, nikabaki nimepigwa na butwaa kwa sababu

294 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

hakuwahi hata mara moja kuniongelesha kwa namna aliyokuwa


anaitumia siku hiyo, utulivu ukionesha kumuisha kabisa ndani ya
nafsi yake.
“Au na yeye anahusika? Kwa nini amenibadilikia kiasi hiki?”
nilijiuliza huku nikimtazama kwa kumkazia macho. Nadhani al-
igundua kwamba nilikuwa najaribu kuzisoma hisia zake, harakaha-
raka akakwepesha macho yake.
“Unachokifanya ni kama kuchokoza mzinga wa manyigu Ken-
ny!”
“Kwa nini chief!”
“Umeenda kuwagusa watu hatari sana! Watu wenye ushawishi,
ambao wanaweza kufanya chochote wanachokitaka kwenye nchi
hii!”
“Unamaanisha wapo juu ya sheria? Au mimi ndiyo sijaelewa,”
nilimuuliza kimitego, nikamuona akishusha pumzi ndefu na kurudi
kwenye kiti chake, kijasho chembamba kikawa kinamtoka.
“Hebu endelea!” alisema, nikakaa tena vizuri kwenye kiti changu
na kuendelea kumsimulia kila kitu, huku nikijiuliza maswali mengi
ndani ya kichwa changu ambayo yote yalikosa majibu.
Taa nyekundu ilikuwa imewaka kwenye kichwa changu kuhusu
uadilifu wa mkurugenzi wetu na uhusika wake katika sakata hilo!
Mungu atanisamehe kama nilikuwa nimemhisi vibaya!
Nilipomuelezea kuhusu jinsi nilivyofuatilia makazi ya mfanyabi-
ashara huyo na kuliona gari la ‘Kamishna’ likitoka kwenye makazi
ya mfanyabiashara huyo, nilimuona akipatwa na mchecheto
mwingine, akasimama na kuanza kujifuta kijasho chembamba.

295 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Japokuwa ofisi yake ilikuwa na kiyoyozi, huwezi kuamini alikuwa


akitokwa na jasho.
Nikaendelea kumueleza jinsi nilivyoamua kumfuatilia mpaka
ofisini kwake, jinsi nilivyopandikiza watu wa kuanza kufuatilia
mawasiliano yake pamoja na kumfuatilia nyendo zake bila mtu
yeyote kujua.
“Kazi hazifanywi hivyo Kenny, daah! Unataka kunigombanisha
sasa! Unafikiri akigundua kwamba unamfuatilia si atajua moja kwa
moja kwamba mimi ndiyo niliyekutuma? Hivi unajua ngazi ya
uongozi aliyopo yeye na mimi hatupishani na wote tunaripoti moja
kwa moja kwa namba moja?”
“Najua chief lakini si inafahamika kwamba hakuna aliyepo juu
ya sheria?”
“Ni sawa lakini mambo kama haya hayashughulikiwi hivyo, ni
hatari sana kwa sababu lazima mwenyewe atajua na akijua, hili
linakuwa ni kama jaribio la kuyakatisha maisha yake.
Unafikiri akijua tunataka kumkaanga yeye atachukua hatua
gani? Atakaa asubiri tumkaange au atatafuta namna ya kutuwahi?”
alisema mkurugenzi, nikawa bado sijaelewa ni nini alichokuwa
anakiogopa wakati yeye ndiye aliyekuwa kiongozi wetu na alipas-
wa kuwa mfano kwetu katika kusimamia ukweli hata kama utaha-
tarisha maisha kiasi gani.
Tuliendelea kuvutana lakini japokuwa alikuwa ni bosi wangu, na
mimi nikawa naendelea kumhoji kuhusu ubaya wa kile nilichoki-
fanya wakati tayari namba moja alikuwa kwenye hatari kubwa ya
kuuawa.

296 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Ilibidi atulie, nikaendelea kumsimulia kila kilichoendelea mpaka


nilipokuja kubaini kwamba mwenzetu, Berthany alikuwa anatu-
mika kutoa taarifa za kila kilichokuwa kinaendelea kwa kutumiwa
na dereva wa mfanyabiashara mwingine wa mafuta aliyekuwa na
uhusiano wenye kutoa shaka na yule mfanyabiashara mkubwa wa
mafuta.
“Kijana una hatari kubwa sana wewe! Huogopi kufa?”
“Kufa kila mmoja atakufa chief! Ni heshima kufa ukiwa unali-
pambania taifa lako kuliko kukaa pembeni na kufumbia macho
mambo kama haya,” nilisema, akasimama na kunisogelea, ikabidi
na mimi nisimame.
“Nimekuzidi kila kitu, kuanzia umri, uzoefu wa kazi, vyeo,
maisha na kila kitu! Lakini umenizidi kwenye kitu kimoja amba-
cho naamini nimekuwa nikikikosa kwenye maisha yangu,” alisema
huku akinyoosha mkono wake na kunipa, na mimi nikanyooosha
wa kwangu, tukashikana kikakamavu.
“Jambo gani?”
“Uthubutu!” alisema huku akinitazama machoni, na mimi ni-
kawa namtazama.
“Uthubutu wako ni wa kiwango cha hali ya juu sana na pen-
gine kuna jambo ambalo watu wote wanatakiwa kujifunza kutoka
kwako,” alisema huku akinipigapiga mgongoni kisha akaniachia na
kurudi kwenye kiti chake.
“Maelezo yako yamenifungua macho kwa kiasi kikubwa sana!
Nataka unieleze kwa huo uchunguzi wako ulioufanya, unadhani
ni nini kinachokwenda kufanyika na tunatakiwa kufanya nini ili

297 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kuzuia kwa sababu usiku wa kuamkia leo tulikuwa na kikao na


namba moja kama nilivyokuambia.
“Tumemhakikishia kwamba kila kitu kipo sawa ndiyo maana
unaona ratiba nyingine zinaendelea kama kawaida. Ambacho
hata mimi sikuwa nakijua, ni kwamba kumbe hatari iko palepale,
pengine imeongezeka zaidi na muda wa kukabiliana nao ni mdogo
sana na sidhani kama tutafanikiwa!” alisema huku akiwa amekaa
kwenye kiti chake, akionesha kuishiwa nguvu kabisa.
“Unamaanisha nini chief?” nilimuuliza, akashusha pumzi ndefu
na kunitazama.
“Hata kama mimi sihusiki kwa chochote, lolote ambalo litatokea
itaonesha kwamba mimi nilikuwa najua na nimeshiriki,” alisema
mkurugenzi, akazidi kunichanganya kichwa changu kwa sababu
ni kweli hata mimi nilishaanza kuwa na mashaka naye makubwa
kutokana na jinsi alivyokuwa anajkanyaga kwenye mazungumzo
yake.
“Ulitumia njia gani kumshawishi yule mzee wa Kisomali ayazun-
gumze haya yote aliyokwambia?”
“It was just a coincidence!” (Ni matukio tu yaligongana!)
“There’s no such thing as coincidence! Tell me what exactly
happened!” (Hakuna matukio mawili yanayoweza kutokea kwa
pamoja bila sababu! Niambie ni nini hasa kilichotokea!) alinihoji
mkurugenzi wetu na kunifanya nishushe pumzi.
Hapa labda nifafanue kidogo kuhusu falsafa za kazi yetu ambazo
inatumiwa sana duniani kote. Coincidence ni neno la Kiingereza
ambalo huwa linamaanisha kutokea kwa matukio mawili yanayofa-

298 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

nana kwa namna ya kufuatana wakati hakuna aliyekuwa amepanga


mambo hayo yatokee kwa kufuatana au kwa wakati huohuo mmo-
ja.
Yaani kwa mfano rahisi, unataka kwenda sehemu fulani kumfuata
mtu fulani lakini kabla hujaanza safari yako, unakutana na mtu
huyo, naye akiwa anakuja kwako katika mazingira ambayo huku-
tegemea kabisa kabla hata hujaanza safari yako.
Katika maisha ya kawaida, huwa ni kawaida kabisa kwa matukio
ya aina hii kutokea! Au unamfikiria mtu fulani lakini ghafla, simu
yako inaita na kutazama anayekupigia, unagundua ni yule ambaye
ulikuwa unamfikiria.
Nimesema kwamba katika maisha ya kawaida, hali hii huwa ni
ya kawaida na inatokea sana lakini katika ulimwengu wa kipele-
lezi, kijasusi na hata kiroho, wataalamu huwa wanasema kwamba
jambo hilo huwa siyo la kawaida na ukiona limetokea, ujue kuna
kitu nyuma ya pazia ambacho kinaweza kuwa na maana kubwa.
Hata nikiwa mafunzoni, nilifundishwa sana kuhusu msemo huo
wa ‘there’s no such thing as coincidence’. Pengine unaweza us-
ielewe kwa haraka kwa sababu inahitaji fikra pana kidogo kuliele-
wa hili lakini itoshe tu kusema kwamba kwenye kazi zetu, huwa
tunafundishwa, tena kwa herufi kubwa kabisa kwamba hakuna kitu
kinachoweza kutokea kama ‘coincidence’.
Tunafundishwa kwamba kila kinachotokea huwa kinakuwa na
sababu na maana yake. Sasa alichokuwa anakimaanisha mkuru-
genzi ni kwamba, mimi nilimueleza kwamba yule mzee wa Ki-
somali aliamua kutoa ushirikiano kwangu kwa sababu alikuwa

299 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

na hali mbaya ya kiafya baada ya Kisukari kumpanda na kwamba


tulikubaliana kwamba nimpe dawa za kutuliza hali yake kisha atan-
ieleza ukweli.
Hoja yake ni kwamba matukio ya yeye kupandwa na kisukari
mpaka kuzidiwa, kisha kuniomba nimpe dawa ndiyo anieleze uk-
weli, hayakuwa yametokea kwa bahati mbaya.
Ukweli kutoka ndani ya moyo wangu ni kwamba sikuwa
nimepanga chochote kuhusu kile kilichotokea, ‘coincidence’
ilitokea kama inavyotokea tu katika maisha ya kawaida kwa hiyo
sikuwa nimefanya chochote kufanya hilo litokee.
“It was just a coincidence!” nilirudia kumueleza kilekile nili-
chomueleza mwanzo lakini eti ajabu ni kwamba na yeye akaanza
kuonesha wasiwasi kwamba pengine kuna mambo niliyokuwa
nayajua.
“Unajua nini kuhusu mimi kuhusika na hiki kinachotokea!”
“Hakuna ninachokijua chief! Ningekuwa najua ningekueleza!”
“Unafikiri naweza kuasi kiapo changu cha kuitumikia nchi yangu
kwa moyo wangu wote na kwa uadilifu wa hali ya juu?”
“Hayo yanatokea wapi kiongozi?”
“Nikikutazama macho yako napata ujumbe mkubwa sana! Mimi
ni mtu mzima na nilianza kazi kabla hata haujazaliwa kwa hiyo
naweza kujua mtu anapokuwa na mashaka na uadilifu kwangu!”
“Chief, nilikuwa naomba kama inawezekana, hii mada tuiache
kwanza kwa sababu kama ulivyosema hatuna muda wa kutosha
wa kupambana na hawa wahalifu! Kama umenihisi vibaya naomba
unisamehe lakini sijawahi kuwa na wasiwasi na wewe hata mara

300 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

moja.”
“Ikitokea umegundua kwamba na mimi nahusika, utachukua
uamuzi gani?” aliniuliza swali lingine lililozidi kunichanganya
kichwa changu.
“Haiwezi kutokea!”
“Usiseme haiwezi kutokea, nakuuliza sasa hivi, ikitokea umegun-
dua hivyo utachukua hatua gani?” alisema, safari hii akinitazama
kwa macho yaliyokosa kabisa utulivu, pumzi zikimuenda mbio.
“Nitasimama upande wako, nitakulinda na kukutetea!” nilim-
danganya waziwazi kwa sababu hali aliyokuwa nayo, haikuwa ya
kawaida kabisa!
“Naomba dawa zangu!”
“Dawa zako? Zipi?”
“Naomba dawa zangu za moyo!” alisema huku akianza kutapa-
tapa na kujishika kifuani!
“Chief! Chief!”
“Naomba dawa zangu,” alisema huku akinioneshea kwa kidole
kule kwenye meza yake. Alishindwa kuendelea kusimama, akakaa
kwenye kiti kilichokuwa pembeni ya kile nilichokuwa nimekalia
huku akiendelea kuugulia maumivu makali.
Ilibidi nifanye kama alivyoniambia, nikakimbia upande wa pili
wa meza yake, nikakuta kuna kikopo kilichokuwa na vidonge
ndani yake, nikasoma haraka maelekezo yake na kugundua kwam-
ba vilikuwa ni vidonge vya kuzuia shambulio la moyo na alitakiwa
kuwa anakunywa kimojakimoja kila anapopata shida kwenye moyo
wake.

301 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Uzuri ni kwamba kulikuwa na chupa ya maji palepale, ndani ya


sekunde chache tu nikawa nimeshatoa kidonge kimoja na kumpa
pamoja na maji.
Sikuwa daktari lakini angalau nilikuwa na uelewa wa nini cha
kufanya mtu anapokumbwa na hali kama ile, nikawasha kiyoyozi
na kukichochea, kikawa kinatoa ubaridi utafikiri tupo Makete au
Makambako.
Nilimsaidia kulegeza tai aliyokuwa amevaa na kufungua ki-
fungo cha juu cha shati lake, nikamlegeza na mkanda pamoja na
kumvua viatu na soksi. Ilibidi nikafunge mlango kwa ndani kwa
sababu kama mtu yeyote angetokea, ningekosa majibu ya nini
kilichotokea.
Niliendelea kumpa huduma ya kwanza na ndani ya muda mfupi,
alianza kurejea kwenye hali yake ya kawaida, nikamsaidia kuinuka
pale alipokuwa amekaa na kwenda kumkalisha kwenye masofa
yaliyokuwa upande wa wageni, nikamkalisha vizuri huku nikien-
delea kufuatilia maendeleo yake kwa karibu.
Dakika kumi baadaye, aliweza kuinuka mwenyewe pale nili-
pokuwa nimemlaza, akasimama na kuanza kutembea kwa kujivuta
kuelekea kule kwenye kiti chake, akawa anajiweka vizuri nguo
zake.

302 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

12

AHSANTE! Jambo ambalo sina wasiwasi nalo ni kwam-
ba una moyo mzuri sana! Najivunia kuwa bosi wako!”
alisema kisha akanywa maji kwa wingi kutoka kwenye ile
chupa iliyokuwa pale mezani.
Akaendelea kujiweka vizuri, nikamsogezea viatu vyake
na soksi, nikamsaidia ambapo baada ya muda, alikuwa amerudi
kabisa kwenye hali yake ya kawaida.
“Najua umepatwa na mshtuko kwa sababu siamini kama ulikuwa
unajua kwamba huwa nina matatizo ya moyo!”
“Nilikuwa najua!” nilisema huku nikililazimisha tabasamu kwe-

303 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

nye uso wangu ili ajisikie vizuri, na yeye akatabasamu.


“Umeahidi kwamba hata ukiujua ukweli kuhusu mimi utakuwa
upande wangu, naichukulia kauli hiyo kama kiapo!” alisema, ika-
bidi nijilazimishe kicheko, nikatingisha kichwa.
“I have been framed!” alisema, kauli ambayo ilinishtua kuliko
kawaida.
“Unamaanisha nini kiongozi!” nilimuuliza huku nikivaa uso wa
kazi.
“Its a long story!” (Ni habari ndefu!) alisema kisha akashusha
pumzi ndefu, akawa ni kama anavuta kumbukumbu zake. Bado ali-
kuwa amenichanganya kichwa changu kiasi ambacho sasa sikuwa
najua hata wapi pa kuanzia.
“Hakuna kinachowezekana kama hutanieleza angalau kwa
kifupi.”
“Nitakueleza lakini nina uhakika hakuna chochote unachoweza
kufanya kuzuia hili lisitokee.”
“Hatuwezi kuacha haya yatokee, ni lazima tutafute njia na naku-
hakikishia kwamba ukinipa mwanga wa unachokijua, hili litaweze-
kana.”
“Usinielewe vibaya, siyo kwamba najua mambo mengi kuhusu
suala hili, nilichokisema ni kwamba ‘I was framed’,” alisema
mkurugenzi, akiwa ni kama anataka kujitoa. Aliirudia kauli hiyo ya
Kiingereza, ambayo huwa inamaanisha kwamba mtu ametengene-
zewa mazingira ya kuoekana kwamba ni yeye ndiye aliyefanya
uhalifu fulani wakati uhalisia ni tofauti.
“Nimekuelewa vizuri sana, ninachotaka kujua ni ‘how was you

304 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

framed’ nikimaanisha kwamba nilitaka kujua kwamba kama anas-


ema ametengenezewa mazingira ya kuonekana kwamba na yeye
anahusika, ni mazingira gani hayo aliyokuwa amejengewa?
Swali hilo lilionekana kuwa gumu sana kwake na kwa kuwa
maswali a maelezo yangu ya awali yalisababishwa azidiwe ghafla,
sikutaka kuendelea kumbana kwenye kipengele hicho, nikaamua
kuacha mwenyewe ndiyo anieleze anachoona kinaweza kutusaidia
kwa wakati huo.
“Berthany!” alisema, kauli ambayo ilinishtua kuliko kawaida.
“Unamaanisha nini chief!”
“Kila mtu huwa anakuwa na zile siri zake ndogondogo na kub-
wakubwa.”
“Nakuelewa vizuri.”
“Nipo kwenye uhusiano wa kimapenzi na Berthany na baadhi ya
watu wanafahamu kuhusu hilo licha ya kuwa nimekuwa nikijita-
hidi sana kulifanya kuwa siri.”
“Lakini umeoa na una familia chief!”
“Wewe pia ni mwanaume Kenny na uzuri ni kwamba umeoa
pia! Ndoa zina mambo mengi sana ambayo utakuja kujionea
mwenyewe. Usione mwanaume anakuwa na mke mzuri, familia
bora lakini bado anakuwa na mpango wa kando! Maisha ni fumbo
kubwa sana Kenny!” alisema mkurugenzi kwa sauti ya upole,
akionesha kuwa na mengi sana ndani ya moyo wake.
Bado nilikuwa nimepigwa na butwaa, nikiwa ni kama siamini
kile alichokuwa ameniambia. Inawezekanaje mtu mwenye wadhifa
mkubwa kama yeye, awe na uhusiano wa kimapenzi na mfanyaka-

305 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

zi wake wa chini, tena ambaye wamepishana sana umri?


“Najua kitendo cha wewe kugundua kwamba Berthany ndiye
aliyekuwa akitoa siri za misheni zetu kwa maadui zetu, kitafanya
kila mmoja aamini kwamba mimi ndiye niliyekuwa nikitoa siri
zote na kumpa Berthany ili azipeleke kwa hao wahusika! Hakuna
mtu yeyote ambaye anaweza kuja kuamini kwamba sikuwa najua
chochote kilichokuwa kinaendelea.”
“Nashinda nishike lipi na niache lipi kiongozi! Kwa hiyo unataka
kusema kwamba ushiriki wako katika hili ni wewe kuwa na uhu-
siano wa kimapenzi wa siri na Berthany pekee?”
“Exactly! Ni hivyo! Lakini ni nani anayeweza kuamini haya?
Ameniingiza kwenye matatizo makubwa sana huyu mtoto.”
“Ukweli huwa una kawaida moja ya kutojificha! Watu wanaweza
kukuelewa vibaya, kila mmoja akakutafsiri vile anavyotaka yeye,
unaweza pia hata kuwajibishwa kwa uhaini lakini kama una-
chokisema ni ukweli kutoka ndani ya moyo wako, ipo siku itakuja
kujulikana.”
“Naamini hivyo pia lakini mpaka ukweli uje kutoka nitakuwa
nimeshapoteza kila kitu changu na pengine naweza kuwa hata
nimepoteza maisha yangu! Nambva moja huwa hana mchezo
kabisa katika michezo kaa hii, kibaya zaidi nimemhakikishia
kwamba kila kitu kipo sawa!” alisema mkurugenzi, ukimya ukapita
kati yetu.
“Ni nani mwingine anayejua kuhusu haya uliyonieleza?”
“Wapo baadhi ya watu wachache wakiwemo marafiki zake lakini
wanachojua ni kwamba mimi na Berthany tuna uhusiano wa siri

306 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wa kimapenzi. Hakuna zaidi ya hapo.”


“Sasa kama ni hivyo mbona mimi sioni tatizo?”
“Tatizo lipo, tena kubwa sana!”
“Hapana kiongozi, hebu nisikilize kwa makini ninachotaka kuk-
wambia,” nilisema huku nikikaa vizuri kwenye kiti changu, nika-
muona mkurugenzi naye akikaa vizuri kwenye kiti chake. Alikuwa
ni bosi wa juu kabisa lakini jinsi alivyokuwa amekaa kwa umakini,
ungeweza kudhani kwamba pengine mimi ndiyo bosi wake.
“Nilichokibaini ni kwamba Berthany amekuwa akitumika bila
yeye kujua chochote. Amekuwa akimwambia huyo mwanaume
wake kila kitu kinachoendelea, akiamini ni mpenzi wake na msiri
wake wakati ukweli ni kwamba hana mapenzi naye na amepan-
dikizwa kwa kazi maalum.
“Ninachotaka kukisema ni kwamba, kama ikithibitika kwamba
Berthany hakuwa anajua kilichokuwa kinaendelea, au hakuwa aki-
jua kwamba taarifa anazompa mwanaume wake zinakwenda wapi,
wewe unaingiaje kwenye matatizo?”
“Na isitoshe, bado matokeo ya uchunguzi huo nilioufanya ni siri!
Hakuna mwingine anayejua zaidi yangu.”
“Hakuna namna ambayo naweza kukwepa hili kwa sababu hicho
unachokizungumza kinaweza kweli kufanyika lakini bado kuna
bomu lingine kubwa zaidi.
“Bomu gani?”
“Ni kuhusu huyo anayepelekewa taarifa!”
“Kwani vipi?”
“Ni rafiki yangu wa karibu na mimi pia ni miongoni mwa watu

307 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ambao huwa wanakwenda kumtembelea nyumbani kwake na yeye


pia huwa anakuja nyumbani kwangu.”
“Sijakuelewa!”
“Ni rafiki yangu lakini kamwe sijawahi kuhisi kwamba anaweza
kuwa anahusika na mambo kama hayo.”
“Urafiki wenu umejengwa na nini zaidi?”
“Yaani hata sijui nikuelezeje! Lakini kwa kifupi ni yeye ndiye
aliyenitafuta na kujenga ukaribu naye. Na kiukweli amekuwa
msaada mkubwa sana kwangu, kila tunapoonana, amekuwa akinipa
kiasi kikubwa cha fedha na zawadi nyingine nyingi.”
“Mungu wangu!” nilisema kwa sababu hakika mambo yalikuwa
mazito.
“Sasa hizo fedha ulikuwa unazipokea kwa ajili ya nini?”
“Aah! Unajua ukiwa kwenye nafasi kama hii, wafanyabiashara
wengi na watu maarufu huwa wanapenda kujiweka karibu na njia
kubwa wanayokuwa wanaitumia huwa ni kwa kutoa kiasi kikubwa
cha fedha kama zawadi, tena mara kwa mara lakini wengi wao
huwa wanakuwa wanafanya hivyo kwa kutaka tu ukaribu, wa-
naamini wakiwa karibu na sisi basi wako salama.”
“Fedha alizokuwa anakupa, alikuwa anatumia njia gani?”
“Cash!”
“Hakuna miamala ya kibenki wala simu?”
“Ipo pia!”
“Sasa huoni kama huo ni ushahidi mwingine unaoweza kuku-
weka kwenye matatizo makubwa zaidi?”
“Ndiyo maana nimekwambia kwamba nimekuwa ‘framed’. Nim-

308 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

etengenezewa mazingira nionekane nimeshiriki katika hili.”


“Ukweli kutoka ndani ya moyo wako ni upi kuhusu hili? Watu
wengine wote wanaweza kuhisi hivyo lakini je, moyo wako unas-
emaje?”
“Moyo wangu? Si nimeshakwambia? Siwezi kukiasi kiapo
changu hata iweje. Nilikunywa maji ya bendera,” alisema na kusa-
babisha nitabasamu.
Nilikuwa na uwezo mkubwa wa kumsoma mtu kwa kupitia ma-
cho, yaani nikikutazama tu na macho yetu yakagongana, naweza
kujua moja kwa moja kama unachosema ni ukweli au uongo.
Hata hivyo, wakati tukifundishwa kusoma hisia za mtu kwa
macho, tulifundishwa pia namna ya kumpotosha mtu kwa macho,
yaani nikiwa namtazama mtu anayesema uongo naweza kumgun-
dua kupitia macho lakini mimi nikiwa nazungumza uongo, naweza
kumfanya mtu aamini kwamba ninachokisema ni kweli kwa kuni-
tazama machoni.
Nilipomtazama mkurugenzi machoni, ilionesha kabisa kwamba
alichokuwa anakizungumza ni ukweli lakini kwa kuwa na yeye
alikuwa na uwezo huo wa kupotosha kupitia macho, nilishindwa
kuelewa nishike lipi, anasema ukweli au ananidanganya?
Nilichojisemea ndani ya moyo wangu ni kwamba muda huwa
unakawaida ya kuzungumza ukweli. Niliamua kwa moyo mmoja
kuacha muda ndiyo uje uamue kama anachokisema ni kweli au
ananipanga.
“Kama unachosema ni ukweli kwamba hakuna namna yoyote
ya moja kwa moja unayohusika na chochote, nafikiri njia nzuri ya

309 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kuuthibitishia umma itakuwa ni kwa sisi kulizuia hili lililopo mbele


yetu.”
“Ni kweli lakini nimeshakueleza kwamba sidhani kama tunao
muda wa kutosha wa kupambana na hili genge! Sitaki kuamini
kwamba mtu wangu wa karibu kama huyu anaweza kuwa anahusi-
ka kwenye njama chafu kama hii. Ushawishi na nguvu kubwa ya
kiuchumi aliyonayo, inanifanya nione kwamba hakuna kitu kina-
choweza kuwazuia wafanye hicho wanachokitaka.”
“Mimi naamini kwamba tunaoa muda wa kutosha wa kuwadhibi-
ti. Tumeshakula ng’ombe mzima, kilichobakia ni mkia.
“Tukishikamana nina uhakika tutawazidi akili. Hata kama wana
nguvu na ushawishi kiasi gani, hawawezi kutuzidi akili kwa sababu
sisi hii ndiyo kazi yetu. Tumesomeshwa na serikali ili tuje kulisaid-
ia taifa letu na watu wake,” nilisema kwa kujiamini.
“Tunaanzia wapi, hebu labda unieleze mipango uliyonayo kama
naweza kukuelewa.”
“Cha kwanza ni Berthany. Anatakiwa kuwekwa kizuizini lakini
mtu yeyote asijue kinachoendelea. Cha pili ni kumkamata huyo
mwanaume anayemtumia, naye anawekwa kizuizini bila mtu yeyo-
te kufahamu chochote. Tukimminya kisawasawa lazima atatueleza
kinachoendelea.
“Kuanzia hapo sasa tutakuwa na nguvu ya kusonga mbele,
nitaomba pia kamishna awekwe kizuizini kisha baada ya hapo, oro-
dha ya wageni wote wanaotakiwa kukutana na namba moja iangali-
we upya na kumfuatilia mtu mmoja baada ya mwingine lakini pia
kuchomeka watu wetu kwenye hiyo orodha ambao watakuwa na

310 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kazi moja tu, ya kufuatilia kila kitakachokuwa kinaendelea kwenye


hiyo dhifa!
“Lakini kubwa zaidi, tunatakiwa kumtumia ‘double’ wa namba
moja! Nadhani huu ndiyo muda muafaka wa yeye kutumika.
“Namba moja anatakiwa kuondolewa na kupelekwa sehemu
salama kisha ‘double’ wake ndiye atakayekuwa anaendelea ku-
wepo Magogoni,” nilisema, mkurugenzi akasimama na kuanza
kutingisha kichwa chake kuonesha kukubaliana na mimi kuhusu
nilichokuwa nakisema.
“Umejuaje kuhusu ‘double’ wa namba moja?”
“Sikupelekwa Israel kuwashangaa Wayahudi,” nilisema na kusa-
babisha wote wawili wacheke.
Nadhani nilikuwa nimezungumza kitu ambacho hakuwahi kud-
hani kwamba nakifahamu kwa undani kiasi hicho.
“Ninaposema ‘double’ wa namba moja, pengine naweza
nisieleweke kwa haraka lakini duniani kote, kwenye suala la uja-
susi hili siyo jambo geni kabisa.
Kuna jambo moja ambalo pengine huwa tunakutana nalo lakini
wengi huwa tunaishia tu kushangaa na kuona kuwa ni la kawaida.
Waswahili wanao msemo wao kwamba ‘duniani wawili wawili’.
Msemo huu huwa unatumika sana kuelezea watu wawili ambao
hawana uhusiano wowote wa kindugu au wa kifamilia, lakini
wakawa na mwonekano unaofanana sana.
Watu hawa, kwa taaluma yetu huwa tunawaita ‘the doubles’,
yaani mtu mmoja anafanana kwa karibu sana na mtu mwingine
ambaye pengine hata hawafahamiani kwa chochote.

311 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Sasa kinachotokea kiongozi wa taifa anapochaguliwa na kuingia


madarakani, huwa ni kuwatafuta watu ambao wanafanana naye
kwa kiasi kikubwa, na kazi hii huwa inafanywa kwa usiri mkubwa
na maafisa vipenyo.
Akishakidhi vigezo vya ufanano kwa kiwango kinachotakiwa,
basi anakuwa ameula! Kivipi? Huwa anachukuliwa kwa usiri
mkubwa na kukutanishwa na mhusika na endapo akikubaliana
na jinsi ufanano wao ulivyokuwa wa kiwango cha juu, basi huwa
anakabidhiwa kwa ‘kitengo’ ambapo atapewa mafunzo yote ya
msingi kuhusu kujilinda, kufuata itifaki, kuzungumza kama namba
moja, kuvaa na hata kutembea.
Kwa mataifa yaliyoendelea, wengine huwa mpaka wanafanyiwa
upasuaji maalum wa sura ili kumfanya mtu yeyote asigundue to-
fauti kati ya watu hao wawili. Baada ya kufuzu, basi huwa anatu-
mika kama mbadala wa namba moja pale kunapokuwa na uhitaji
wa kufanya hivyo.
Mtu huyu, huwa anapewa matunzo ya hali ya juu na huendelea
kutunzwa mpaka namba moja anapomaliza muda wake au hata
kufariki dunia, baada ya hapo kazi yake inakuwa imekwisha na
anapewa kazi maalum ya kumfanya aendelee kuishi vizuri, yeye na
familia yake.
Mambo haya huwa yanafanywa kwa usiri mkubwa mno kiasi
kwamba hata watu wanaokuwa wanajua kuhusu suala hilo, huwa ni
wachache, tena wale vigogo wanaounda ‘deep state’.
Mimi pia sikuwa najua kuhusu suala hili japokuwa ni kweli tuki-
wa mafunzono tuliwahi kufundishwa lakini sikuwa najua kwamba

312 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

linaweza kuwa linawezekana hata kwenye nchi zetu za Kiafrika.


Ni mpaka siku moja baba yake Saima aliponivijishia siri hiyo,
jambo ambalo alilifanya kwa bahati mbaya halafu nikajifanya ni
kama sijamuelewa wakati ukweli ni kwamba nilikuwa nimem-
uelewa vizuri sana na baada ya kufanya utafiti wangu wa chini kwa
chini, nikaja kuujua ukweli mkubwa zaidi.
“Sasa, huoni kwamba namba moja anaweza kugundua kwamba
tulimdanganya tulipomueleza kwamba hali ni shwari?”
“Hapana, sidhani kama mlimdanganya, isipokuwa ni kwamba
mlimpa taarifa ambazo hazijakamilika. Na mtu yeyote unapom-
pambania maisha yake, ni rahisi kusahau yote ya nyuma na ku-
jenga imani kubwa na wewe,” nilimwambia, nikamuona akikuna
kichwa chake.
“Sina ujasiri wa kwenda kumkabili, labda mkweo atanisaidia,”
alisema, akimaanisha baba yake Saima. Ambacho hakuwa anakijua
ni kwamba tayari baba yake Saima alikuwa ameshaenda kuonana
na namba moja.
“Sawa, basi hili niliache kwenye mikono yako!”
“Sawa, lakini hayo mengine yapo kwenye uwezo wako, Berthany
na huyo mwanaume wake wanatakiwa kuwekwa kizuizini sasa
hivi, hatuna muda wa kupoteza.
“Suala la kamishna na double hayo tutayashughulikia sisi! An-
galizo ni kwamba hii ni misheni ya usiri mkubwa, lazima kila kitu
kifanyike kwa usiri wa hali ya juu vinginevyo tunajihatarishia
usalama wetu, watu waliopo nyuma ni hatari kuliko nyoka mwenye
sumu kali,” alisema huku akijiweka vizuri tai yake.

313 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Alionesha kupandwa na morali kubwa kuliko kawaida, us-


ingeweza kudhani kwamba ni yule ambaye dakika kadhaa zilizo-
pita, alikuwa amepatwa na matatizo ya moyo.
“Umenifanya niwe ni kama nimezaliwa upya,” alisema huku
akinipa mkono, tukashikana kwa nguvu kisha akanitingisha mkono
wangu kama ishara ya kunishukuru, tukaaganana mimi nikatoka
harakaharaka kwenda kuendelea na kile tulichokubaliana pamoja
na yale majukumu yangu mengine.
Nilirudi ofisini kwangu na kiukweli, mambo yalikuwa yanatokea
kwa kasi kubwa mno kiasi kwamba kuna muda nilikuwa naona
ni kama nataka kurukwa na akili. Ilibidi nitulize kwanza kichwa
na kama kawaida yangu, njia nyepesi kwa wakati huo, ilikuwa ni
kufanya meditation au tahajudi japo kwa dakika chache.
Niliwaomba vijana wangu wanipishe mara moja na wao
wakapate muda wa kwenda kula chakula cha mchana. Nilitaka
kubaki peke yangu, kweli wakatoka na kuniacha peke yangu.
Kwa jinsi kichwa kilivyokuwa kimepata moto, niliona kama niki-
fanya meditation ya kwenye kiti, naweza nisifikie utimamu ninaou-
taka, nikasogeza viti na kupata nafasi ya kukaa sakafuni. Nilifunga
mapazia ili kuwe na kama hali ya kigiza fulani hivi kwa ajili ya
kuongeza utulivu ndani ya kichwa changu.
Nilienda kufunga na mlango kwa ndani, nikatoa simu mlio kisha
nikavua viatu na kukaa pale sakafuni, nikakaa kwa kukunja miguu
yangu, nikafumba macho na kuanza kuvuta pumzi ndefu kisha
kuzitoa.
Mambo yalikuwa yakipita kwa wingi ndani ya akili yangu lakini

314 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

nikaelekeza uzingativu wangu kwenye pumzi, nikawa naifua-


tilia jinsi ilivyokuwa inaingia na kutoka, taratibu nikaanza kuona
kichwa kinatulia.
Niliendelea kufanya hivyo na nikawa nimefanikiwa kuufikia
uzingativu na utulivu wa akili kwa kiasi cha juu kabisa. Ingekuwa
ni amri yangu, hili somo kuhusu namna ya kufanya meditation,
lingekuwa linafundishwa kwenye vyuo kabisa kama ilivyo kwenye
nchi za watu kama Japan.
Huwezi kuamini kwamba dakika ishirini zilinitosha kabisa kuni-
fanya niwe mtu mpya kabisa, akili ilikuwa imetulia kisawasawa na
sasa nilikuwa na uhakika wa kuweza kutekeleza majukumu yangu
kwa nguvu na kasi kubwa.
Niliweka kila kitu sawa, nikawafungulia vijana wangu ambao
bado walikuwa kupata chakula cha mchana.
Nilichukua ‘diary’ yangu na kuanza kudadavua kile tulichokuwa
tumezungumza na mkurugenzi. Kulikuwa na mambo mengi am-
bayo nilihitaji kuyatazama kwa jicho la tatu kwa sababu sasa
ilikuwa ni dhahiri kwamba kumbe maadui zetu walikuwa karibu
kuliko tulivyokuwa tunafikiria.
Niliandika na kuchorachora pale nikijaribu kutafuta picha kubwa
iliyokuwa imejificha, nikawa nayakumbuka na kuyatafakari mam-
bo yote aliyokuwa ameniambia mkurugenzi, ikiwa ni pamoja na
kutafakari kwa kina tukio la yeye kutaka kupatwa na shambulio la
moyo baada ya kugundua kwamba kuna baadhi ya mambo nimeya-
jua.
Baada ya dakika kama thelathini hivi za tafakuri ya kina, nili-

315 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

shusha pumzi ndefu na jambo nililoona linafaa kwa wakati huo,


ilikuwa ni kuzungumza na baba yake Saima.
Kwa kuwa alishaniambia kwamba anakwenda kuonana na namba
moja, ilibidi kwanza nimtumie meseji ili yeye ndiyo aniruhusu
kuendelea kumueleza kile nilichotaka kumweleza.
Nilipomtumia ujumbe tu na kumuuliza kama tunaweza kuzung-
umza, alipiga simu muda huohuo, akitumia namba yake nyingine
ambayo ndiyo huwa tunaitumia kuwasiliana hasa katika mazung-
umzo nyeti pamoja na mambo ya kifamilia.
“Kuna mapya nimeyagundua!”
“Safi! Nipo njiani narudi!”
“Umefanikiwa?”
“Ndiyo! Tukutane ofisini kwangu baada ya dakika kumi!” alise-
ma, nikamuitikia kisha simu ikakatwa. Ilionesha kwamba alikuwa
barabarani akiendesha gari.
Dakika kumi zilikuwa nyingi sana kwangu, nikaona wakati
nikisubiri ziishe, ni vizuri kwenda kuangalia maendeleo ya yule
mzee wa Kisomali kule chini kwa sababu ama kwa hakika alikuwa
amenisaidia jambo kubwa mno.
Harakaharaka nilishuka mpaka ‘Basement’, nikafungua kwenye
chumba alichokuwa amehamishiwa kwa maelekezo yangu baada
ya kutolewa kwenye kile chumba cha mateso. Hiki alichokuwa
amehamishiwa, kilikuwa na mazingira mazuri kama vile vyumba
vingine tulivyokuwa tumewahifadhi yule mwanamke, mke wa Ab-
dulwaheed na wale mabinti tuliowakuta kwenye ile nyumba pale
Kijitonyama Kisiwani.

316 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Huo ndiyo ulikuwa utaratibu wetu, mtu ambaye anakubali ku-


toa ushirikiano, anakuwa kwenye mikono yetu lakini mazingira
anayowekwa yanakuwa ni kama yupo nyumbani kwake tu, akipata
huduma zote muhimu isipokuwa anakuwa amezuiliwa kuwasiliana
na mtu yeyote, iwe ni ana kwa ana au kwa kutumia simu lakini pia
anakuwa hawezi kutoka kwenda sehemu yoyote.
Nilienda moja kwa moja kwenye kile chumba, nikafungua
mlango kwa kutumia funguo maalum nilizokuwa nazo.
Macho yangu yaligongana na ya yule mzee ambaye harakaharaka
aliacha kila alichokuwa anakifanya, tukawa tunatazama huku kila
mmoja akiwa kimya.
“Unaendeleaje!”
“Namshukuru Allah kijana wangu! Umeokoa maisha yangu,
sukari imeshuka na sasa nipo vizuri kabisa kama unavyoniona!”
alisema, akionesha uchangamfu ambao sikuwa nimeutarajia.
Usingeweza kuamini kwamba ni huyu ndiye aliyekuwa akinijibu
‘fyongo’ mwanzo, huku wakati mwingine akikataa kuzungumza
chochote. Mambo yalikuwa yamebadilika kwa kasi kubwa na nad-
hani sasa alikuwa ameanza kuwa na imani na mimi hasa baada ya
kumsaidia kumuitia daktari wa kumtibu tatizo lake la Kisukari.
“Umefikia wapi?”
“Bado mambo ni moto lakini nashukuru kwamba msaada ulio-
nipa umenisaidia sana!”
“Mimi huwa ni mtu wa maneno yangu, nikikuahidi kitu lazima
nitimize, hususani nikishajua una ubinadamu ndani yako kama
ulivyo wewe,” alisema na kuachia tabasamu pana.

317 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Una chochote ambacho unadhani kinaweza kunisaidia?”


“Hapana, nadhani nimeshakupa msaada mkubwa sana ambao
pengine utakusaidia kukamilisha kazi yako!
“Sawa!” nilisema huku nikisimama pale nilipokuwa nimekaa
kwa lengo la kutaka kuondoka kwa sababu saa yangu ilikuwa ina-
onesha kwamba zimebakia dakika chache kabla baba yake Saima
hajawasili.
“Labdaa...” alisema huku na yeye akiinuka pale alipokuwa ame-
kaa. Nikatulia, nikawa namtazama machoni kutaka kujua alichoku-
wa anataka kukizungumza.
“Familia yangu! Nina wasiwasi mkubwa sana, najua nao wataku-
wa na wasiwasi mkubwa sana!”
“Wapo salama!”
“Umejuaje?”
“Kuna vijana wetu ambao kazi yao ni kufuatilia mienendo yao na
usalama wao! Wapo salama na watakuwa salama!”
“Wanatakiwa kujua kuwa nipo salama!”
“Uliwezaje kuwa unajihusisha na mambo kama haya wakati un-
ajua kwamba una familia na inakutegemea.”
“Kama kuna jambo ambalo nalijutia katika nafsi yangu basi ni
hili! Nilifanya makosa makubwa sana, sikuwa najua kinachoweza
kutokea! Nayajutia makosa yangu!” alisema, nikageuka kutaka
kuondoka.
“Abdulwaheed!” alisema, nikageuka na kumtazama.
“Najua mahali mnapoweza kumpata!”
“Nitarudi baada ya muda mfupi!” nilisema na kutoka, nikafunga

318 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

mlango kwa funguo na kuanza kutembea harakaharaka kuelekea


ofisini kwa baba yake Saima.
Nikatembea harakaharaka kuondoka kule kwenye ‘basement’,
nikapanda hadi juu na bila kupoteza muda, nikaelekea moja kwa
moja kwenye ofisi ya baba yake Saima. Zile dakika kumi zilini-
kutia nikiwa kwenye mlango wake, kabla sijagonga, akafungua
mwenyewe huku akiitazama saa yake ya mkononi.
Akanionesha kwa ishara kwamba niingie ndani, nikafanya hivyo
na muda mfupi baadaye, tulikuwa tumekaa tukitazamana, yeye
akiwa kwenye kiti chake cha siku zote na mimi nikiwa kwenye
moja kati ya viti vya wageni vilivyokuwa upande wa pili.
“Namba moja ameshtuka kuliko kawaida, nadhani leoleo ana-
rudi tena ‘safe house’, hataki kukaa tena Magogoni wakati anajua
kabisa kwamba anawindwa. Kilichomshtua zaidi ni kugundua
kwamba hata wakuu wa idara za ulinzi na usalama, wanaonekana
hawajui kinachoendelea,” alisema baba yake Saima, kwa sauti ya
chini, ukimya ukapita kati yetu.
“Kwa upande wako nini kinachoendelea!” aliniuliza, ikabidi
nianze kumsimulia kila kitu kilichotokea, kuanzia ugunduzi
mwingine nilioupata, jinsi nilivyoenda kuzungumza na mkuru-
genzi, jinsi alivyonusurika kupatwa na shambulio la moyo na yote
yaliyoendelea baada ya hapo.
Ajabu ni kwamba baba yake Saima hakuonesha kushtushwa sana
na nilichokuwa namwambia, yaani ni kama alikuwa tayari anajua
au alikuwa anategemea jambo kama hilo litatokea. Baada ya kum-
aliza kumsimulia kila kitu, aliniuliza swali moja tu.

319 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Ni picha gani kubwa uliyoipata?”


Nilimueleza kwamba kwa jinsi mambo yalivyotokea, nina
uhakika kwamba mkurugenzi hawezi kuwa anashirikiana na wale
wahalifu isipokuwa alikuwa ameingizwa kwenye ‘mkenge’ bila ya
yeye kujua.
Niliendelea kumueleza sababu zilizonifanya nipate picha ile na
mwisho nikamueleza kwamba kama nilikuwa nakosea kuwaza vile,
basi tuache muda utakuja kuzungumza.
Kwa bahati nzuri, kumbe hata yeye mwenyewe alikuwa aki-
waza hivyo. Mkurugenzi alikuwa ni rafiki yake wa muda mrefu na
walikuwa wakifahamiana kwa undani na miongoni mwa mambo
ambayo alikuwa na uhakika nayo, ni kwamba kamwe mkurugenzi
hawezi kubadilika na kuasi kitengo wala kuliasi taifa lake.
“Mafunzo tuliyokuwa tunapewa sisi enzi zetu ni tofauti kabisa na
siku hizi. Sisi tulifundishwa ule uzalendo wa kutoka ndani kabisa
ya moyo wako. Ni vigumu sana kwa mtu aliyepitia mafunzo kip-
indi chetu na akaiva kisawasawa, kuasi kiapo chake,” alisema baba
yake Saima.
Akaendelea kunieleza kuwa, licha ya yeye kuwa na uhakika na
uaminifu wa mkurugenzi, tayari namba moja alikuwa ameingiwa
na wasiwasi kubwa kuhusu uadilifu wake.
“Kitendo cha mimi kwenda kuzungumza na namba moja kimeku-
wa ni kama nimeenda kumchongea japokuwa kiuhalisia ni kwamba
mimi natimiza majukumu yangu na natakiwa kuripoti moja kwa
moja kwa namba moja kunapokuwa na jambo lolote ambalo halipo
sawa,” alisema baba yake Saima, na hapa nikajifunza kitu kingine

320 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kikubwa kuhusu jinsi wawili hawa walivyokuwa wameshibana.


“Inatakiwa tumsaidie na njia pekee ya kumsaidia, ni kuzuia hiki
kisitokee. Yaani kama mwanzo tulikuwa na sababu elfu moja za
kuzuia jambo hili lisitokee, hivi sasa tuna sababu milioni moja,
lazima tupambane kwa nguvu zetu zote,” alisema baba yake Saima,
akanyanyua simu yake ya mezani na kupiga.
Niligundua kwamba alikuwa anazungumza na mkurugenzi na
ajabu ni kwamba japokuwa baba yake Saima kicheo alikuwa chini
kuliko mkurugenzi, nilimsikia akimuelekeza kufika ofisini kwake
haraka, nikawa bado sijaelewa na nikiwa naendelea kujiuliza
maswali mengi ndani ya kichwa changu, baba yake Saima alivunja
ukimya.
“Tatizo la ndugu yangu huyu ni ‘totoz’. Ni kiongozi wetu, ni bosi
wako na bosi wangu lakini amekuwa na shida kubwa sana katika
maadili hususan katika suala zima la wanawake. Hii si mara ya
kwanza mimi kumuokoa kutoka kwenye majanga kama haya,”
alisema huku akionesha kuwa ‘serious’ kisawasawa.
“Naomba mimi niwapishe kwa sababu sidhani kama ni adabu
kwa mimi kusikiliza mazungumzo yenu, isitoshe sikuwa nimem-
weleza chochote kwamba na wewe unajua,” nilimwambia lakini
akanionesha tu kwa ishara kwamba natakiwa kutulia.
Muda mfupi baadaye, mkurugenzi aliwasili na baada ya kuingia,
alishtuka kidogo kuniona na mimi nikiwa mle ndani.
“Huyu ni kijana wangu na nimetaka na yeye awepo hapa kwa
sababu anajua vitu vingi kutuhusu mimi na wewe! Usiwe na wasi-
wasi,” alisema baba yake Saima, nikamuona mkurugenzi akishusha

321 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

pumzi ndefu, akakaa.


Mazungumzo yalikuwa magumu kwelikweli, sikuwahi kudhani
kwamba baba yake Saima anaweza kuwa na mamlaka makubwa
kiasi kile mbele ya mkurugenzi, alikuwa akimuonya na kumkanya
kuhusu kuwa makini na mambo yake ya kujihusisha kimapenzi na
wanawake hovyo wakati anaye mke wake wa ndoa.
“Kibaya ni kwamba unashiriki hiyo michezo mpaka na wafan-
yakazi wako, unafikiri ni kwa kiasi gani jambo hili linaweza kuja
kukugharimu?” alisema baba yake Saima, aibu nikawa naona
mimi.
Baada ya kumsimanga kisawasawa, tulirudi mezani sasa kwa ajili
ya kupanga mipango ya namna ya kuzuia tukio la ugaidi lililokuwa
mbele yetu.

322 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

13
B
ABA yake Saima alikuwa na mawazo ambayo
kimsingi hayakuwa yakitofautiana sana na kile
tulichokuwa tumekizungumza mwanzo japokuwa
yeye aliongeza mbinu za kimedani zaidi. Akasisiti-
za kwamba lazima tufanye kila kinachowezekana
kuhakikisha tunalizuia hilo na akamueleza mkurugenzi kwamba
hiyo ndiyo itakuwa sababu pekee ya namba moja kurudisha uami-
nifu kwake.
Tulijadiliana pia kuhusu suala la ‘double’ ambapo baba yake Sai-
ma alikuwa na taarifa za ndani zaidi na akatuelekeza nini ambacho
kiliamriwa kwa kushirikisha vitengo viwili, sisi pamoja na kikosi
cha ulinzi wa namba moja.

323 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Mipango ilisukwa kisawasawa na baada ya hapo, majukumu


yaligawanywa kwa kila mmoja na nilichofurahi zaidi ni kwamba
wote wawili, baba yake Saima na kurugenzi, safari hii waliamua
kuingia mstari wa mbele kabisa.
Baada ya kila kitu kukamilika, kilichofuatia baada ya hapo ili-
kuwa ni utekelezaji, tukakubaliana kwamba kila kitu kitafanyika
kwa usiri mkubwa ili kuzuia kuvuja taarifa kwa watu wasiostahili.
Baada ya kutoka ofisini kwa baba yake Saima, moja kwa moja
nilitoka na kurudi kule ‘basement’ kwa sababu kuna jambo ni-
likuwa sijalikamilisha bado na nadhani pengine ndiyo lilikuwa
muhimu zaidi.
Ni kuhusu mazungumzo yangu na yule mzee wa Kisomali am-
bapo aliniahidi kwamba atanieleza sehemu ninapoweza kwenda
kumpata Abdulwaheed.
Harakaharaka nilirudi mpaka kule kwenye kile chumba alichoku-
wepo yule mzee wa Kisomali lakini ajabu ni kwamba, hakuwepo
kwenye kile chumba nilichokuwa nimemuacha.
Ilibidi nirudi kwa msimamizi wa eneo lile ambaye ndiye aliyeku-
wa na jukumu la kusimamia ulinzi wa watu wote waliokuwa chini
ya uangalizi wetu.
“Amepelekwa hospitali, hali yake ya kiafya haiko sawa, sukari
ilipanda ghafla muda mfupi baada ya wewe kuondoka,” alisema
yule msimamizi, nikashtuka sana kwa sababu nilipoondoka muda
mfupi uliopita, nilimuacha akiwa sawa kiafya, na akionesha kuwa
mchangamfu kuliko kawaida.
“Sijakuelewa.”

324 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Chief, ni wewe ndiye uliyetoa ruhusa ya daktari wetu kuwa


anamshughulikia yule mzee, nikosoe kama nimekosea.”
“Ni kweli!”
“Basi daktari ndiye aliyekuja kumchukua akisaidiana na wenzake
na mimi pia nimeshuhudia zoezi zima, kwa hiyo nadhani daktari
atakuwa na taarifa kamili zaidi.
“Sawa, nashukuru!” nilisema huku akili yangu ikinituma kwamba
kuna jambo halikuwa sawa.
Harakaharaka nilitoka na kuelekea kwenye hospitali kubwa
iliyokuwa ndani ya eneo letu, ambayo pia ilikuwa ikitumika kuwa-
tibu watu mashuhuri nchini. Nilimuulizia yule daktari, nikapewa
taarifa kwamba ni kweli alikuwa ameingia na mgonjwa dakika
kadhaa zilizopita, nikataka kujua alikuwa ameenda naye kwenye
wodi gani na hali yake ilikuwaje.
Kwa kuwa nilikuwa nikifahamiana na kuheshimiana na watu wa
idara zote, nilipewa ushirikiano mkubwa na yule dada aliyekuwa
pale mapokezi, akanitaka niongozane naye, tukapita kwenye korido
ndefu na muda mfupi baadaye, tulikuwa tumewasili kwenye moja
kati ya wodi za dharura.
Nilimkuta yule daktari akiwa anahangaika, akishirikiana na ma-
nesi wawili, wakijaribu kuokoa maisha ya yule mzee wa Kisomali.
“Chief!”
“Dokta Cosmas! Nini kimetokea?”
“Hata mimi sielewi!” alisema yule daktari ambaye tulizoea ku-
muita Dokta Cossy ingawa jina lake halisi alikuwa akiitwa Cos-
mas, huku akiendelea kuhaha huku na kule kuhakikisha mgonjwa

325 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

anapata ahueni.
Nilimpa ishara yule dada wa mapokezi aliyenifikisha kwenye
wodi hiyo kwamba arudi kuendelea na majukumu yake, nikamshu-
kuru kwa ishara, akaachia tabasamu hafifu kisha akaondoka haraka.
Mle wodini tukabaki wanne, mimi, dokta Cosmas na wale manesi
wawili, ikabidi nisogee jirani zaidi nikiwa na shauku ya kutaka
kujua ni nini kilichokuwa kimemtokea yule mzee wa Kisomali kwa
sababu mambo yalikuwa yamebadilika ndani ya muda mfupi sana.
“Nilienda kumuangalia kule basement ikiwa ni pamoja na kwen-
da kumpelekea dawa zake za Kisukari.”
“Ulipofika alikuwa na hali gani?”
“Alikuwa na afya njema kabisa na tukawa tunataniana na kuche-
ka wakati nikimpima kiwango cha sukari.”
“Baada ya hapo, nikamchoma sindano ya Insulin kama kawaida
ili kuweka sawa kiwango chake cha sukari kama utaratibu ulivyo,
lakini nikashangaa muda mfupi baadaye hali yake ikibadilika!”
“Mungu wangu!” nilisema, kengele ya hatari ikalia ndani ya
kichwa changu.
“Dawa uliyomchoma iko wapi?” nilimuuliza, akaacha kila
alichokuwa anakifanya na kusogea kwenye mkoba wake, akatoa
kichupa kidogo kilichokuwa na kiasi kidogo cha dawa.
“Ni zilezile ninazomchoma tangu uliponikabidhi kwake!” alise-
ma, akionesha kuchanganyikiwa kabisa.
“Sawa, endelea na kazi!” nilimwambia, harakaharaka akaungana
na wale manesi, wakawa wanaendelea kuhangaika. Yule mzee wa

326 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Kisomali alikuwa amelala akiwa hoi, macho yake akiwa ameya-


geuzia juu kama anayetaka kukata roho, wakawa wanahangaikia
kumtundikia dripu na kumfanyia vipimo vingine.
Kiukweli nilichanganyikiwa kuliko kawaida, nikajilaumu kwa
nini sikumsikiliza alichokuwa anataka kuniambia kabla sijatoka
nilipoenda kumuangalia karibu saa moja iliyopita.
“Najua mahali mnapoweza kumpata!” nilikumbuka kauli yake
ya mwisho aliyoniambia wakati nikiagana naye kwenda kuonana
na baba yake Saima, akimaanisha kwamba alikuwa anajua mahali
tunapoweza kumpata Abdulwaheed, yule mtuhumiwa namba moja
aliyefanikiwa kututoroka katika mazingira ya kutatanisha kule Sel-
ous.
“Lazima kuna kitu, there is nothing as a coincidence!” nilijise-
mea mwenyewe ndani ya moyo wangu huku nikiwa nimekishikilia
kile kichupa cha dawa ambacho Dokta Cossy alinieleza kwamba
ndicho alichokitumia kumchoma sindano yule mzee wa Kisomali.
Mpaka hapo ilishaonesha kuna mchezo mwingine uliokuwa
umefanyika ingawa sikuwa najua ni nani mwingine anayeweza
kuwa amefanya mchezo ule. Kilichozidi kunichanganya zaidi ni
kwamba bado Berthany hakuwa amewekwa chini ya ulinzi kama
tulivyokubaliana.
“Hizi dawa umezichukua wapi na lini?”
“Nilizichukua hapahapa kwenye bohari yetu na nimekuwa na-
tembea nazo kwenye begi langu la kidaktari.”
“Ulipofika leo begi lako uliliweka wapi?”
“Begi huwa naliacha kwenye ofisi yangu, huwa natembea nalo

327 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kwenye dharura tu.”


“Kwa hiyo kabla ya kwenda kumchoma sindano ya Insulin huyu
mgonjwa begi lilikuwa wapi?”
“Ofisini kwangu Chief!”
“Nani mwingine anayeingia kwenye ofisi yako?”
“Huwa ni sisi watu wa kitengo cha medical pekee!” alijibu Dokta
Cossy huku akiendelea na kazi yake, kijasho chembamba kikim-
toka.
Harakaharaka nilitoka na kuelekea ‘control room’, chumba amba-
cho ndicho kilichokuwa na mitambo yote ya CCTV Camera zilizo-
kuwa zimefungwa kila sehemu hapo kikosini kwetu. Hata sikuwa
najua nataka kufanya nini lakini niliamini kwamba naweza kupata
majibu kwenye chumba hicho.
Kwa jinsi nilivyoingia mbiombio ndani ya chumba hicho am-
bacho kwa kawaida ni watu maalum pekee ndiyo wanaoruhusiwa
kuingia, hata wale vijana waliokuwa mle ndani walipigwa na but-
waa, wakaacha kila walichokuwa wanakifanya na kunitazama kwa
mshangao.
“Nataka footage za ofisi ya medical kuanzia asubuhi ya leo ha-
raka iwezekanavyo,” nilisema, harakaharaka wale vijana wakaanza
kazi yao.
Ndani ya muda mfupi tu, tayari picha za video za CCTV kwenye
ofisi hiyo zilikuwa zikionekana kwenye runinga kubwa iliyokuwa
ukutani, nikawataka waanze kuzipeleka mbele harakaharaka, kweli
wakafanya hivyo, nikiwa makini kutazama kila kilichokuwa kimer-
ekodiwa.

328 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Sikuwa na muda wa kutosha lakini ilibidi nijilazimishe, nikiwa


naendelea kutafakari kwa kina, kile kichupa kikiwa mkononi
mwangu, niliona jambo ambalo lilinishtua. Nilimuona Berthany
akiingia kwenye ofisi hiyo iliyokuwa inatumiwa na Dokta Cosmas
na wenzake.
“Pause and zoom!” nilisema nikimaanisha wale vijana waisi-
mamishe ile video kisha waivute kwa karibu. Hakukuwa na shaka
yoyote kwamba aliyekuwa anaonekana kwenye video hiyo alikuwa
ni Berthany.
Nikawaambia waendelee kuicheza ile video, Berthany akaoneka-
na akitoka kwenye ile ofisi kama dakika mbili hivi baadaye, akio-
nesha kuwa na wasiwasi mkubwa ndani ya moyo wake.
“Nakiomba hicho kipande, nitumieni kwenye email yangu,”
nilisema kisha nikatoka bila hata kuaga, nikawa natembea mbiom-
bio kurudi kule wodini.
“Berthany aliingia ofisini kwenu leo?”
“Ndiyo! Alikuja asubuhi akidai alikuwa na maumivu ya mifupa!”
“Ikawaje?”
“Nikampatia kisha akaondoka!”
“Dawa ulikuwa nazo alipofika?”
“Hapana, ilibidi niingie stoo kumtafutia kisha ndiyo nikampa.”
“Alikukuta wewe na nani?”
“Nilikuwa peke yangu.”
“Ulipoingia stoo yeye ulimuacha wapi?”
“Nilimuacha pale kwenye kiti na niliporudi nilimkuta.”
“Muda huo begi lako lilikuwa wapi?”

329 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Lilikuwa pale mezani kwangu!” alisema halafu akawa ni kama


ameshtuka hivi.
“Kuna nini?”
“Berthany huwa ana kawaida ya kuja ofisini kwako?”
“Kwa siku za karibuni hapana ingawa nyuma kidogo alikuwa
anakuja sana kufuata dawa za maumivu,” alisema, nikawa tayari
nimeshapata majibu.
Harakaharaka nikatoka tena huku nikiwa hata sielewi naelekea
wapi. Berthany alishakuwa tatizo kubwa sana ambalo lilitakiwa
kushughulikiwa haraka iwezekanavyo vinginevyo angeendelea
kusababisha madhara makubwa mno.
“Naomba mnitafutie Berthany haraka iwezekanavyo, namhitaji
basement room 20!” niliwaambia vijana wangu baada ya kufika
ofisini kwangu, wakatoka wawili kwenda kufanya kazi niliyowapa.
Muda huohuo nikachukua simu yangu na kumpigia rafiki yangu
na mwenzetu ambaye alikuwa akifanya kazi Maabara Kuu ya
Taifa, Eddy.
“Snox! Umenitenga kaka!” alisema baada ya kupokea simu,
akionesha kunichangamkia sana kama ilivyokuwa kawaida yetu
kila tunapowasiliana. Tukapiga stori mbili tatu kisha nikamwambia
nina shida ambayo inahitaji msadaa wake wa haraka.
“Kuna nini kaka!”
“Usijali nitakueleza tukionana. Nilitaka kujua kama upo ofisini!”
“Nipo nimejaa tele mzee! Hata ningekuwa mapumziko simu yako
moja tu ilikuwa inatosha kunifanya niache kila nilichokuwa naki-
fanya bosi!” alisema na kusababisha wote tucheke. Nikamwambia

330 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

nitafika muda wowote ofisini kwake kisha nikakata simu.


Nilipokata simu tu, nilipokea taarifa kupitia vifaa vyangu vya
mawasiliano kwamba tayari Berthany alikuwa amefikishwa kule
kwenye vyumba vya chini.
Room 20 au chumba namba ishirini, kilikuwa ni maalum kwa
ajili ya sisi wenyewe kwa wenyewe kuhojiana inapotokea kuna
jambo halipo sawa na ilikuwa ukisikia tu unatakiwa kufika ‘room
20’ basi unakosa amani kabisa kwa sababu ilikuwa ni zaidi ya ma-
hakama ya kijeshi.
Harakaharaka niliinuka, kile kichupa cha dawa aliyochomwa
yule mzee wa Kisomali kikiwa mkononi mwangu, nikapita kwenye
korido ndefu na kutokea upande kulikokuwa na ngazi za kuteremka
kuelekea ‘basement’, kule kwenye vyumba vya chini ya ardhi.
Niliongoza mpaka chumba namba ishirini, nikawakuta wale
vijana wangu wakiwa wamesimama mlangoni kwa nje, nikafungua
mlango na kuingia, macho yangu na ya Berthany yakagongana.
Alikuwa amekaa kwenye kiti cha chuma, akionesha kuwa na wasi-
wasi mkubwa mno ndani ya moyo wake.
Niliwapa ishara wale vijana wangu kwamba wanatakiwa kwenda
kuendelea na majukumu yao kama nilivyokuwa nimewapangia.
Nikafunga mlango kwa ndani, nikapiga hatua ndefu na kumsogelea
Berthany huku nikiwa nimemkazia macho.
Alisimama pale alipokuwa amekaa na kutoa salamu ya heshima
kwangu, nikamjibu kwa ishara na kumuelekeza akae, akafanya
hivyo. Nilivuta kiti cha upande wa pili na kukaa, tukawa tunataza-
mana huku nikiwa nimemkazia macho kisawasawa.

331 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Nilitoa kile kichupa kwenye mfuko na kukiweka mezani, nika-


muona jinsi alivyokuwa ameshtuka.
“Sina muda wa kupoteza, nataka maelezo!” nilimwambia huku
nikimuoneshea kile kichupa, nikamuona jinsi alivyokuwa ana-
tetemeka. Berthany na mimi tulikuwa tukifahamiana lakini hatu-
kuwa na mazoea yoyote zaidi ya kushirikiana kwenye kazi tu.
“Maelezo kuhusu nini chief!” alisema kwa sauti ya kutetemeka.
“Najua kila kitu kuhusu wewe na awali nilikuwa nahisi kwamba
unatumika bila mwenyewe kujua lakini majibu yako yanaonesha
jambo la tofauti. Unajua adhabu anayotakiwa kupewa mhaini?”
“Mimi siyo mhaini!”
“Utatoa maelezo au unataka mpaka tutumie njia nyingine ku-
kulazimisha kutoa maelezo?” nilimuuliza kwa sauti iliyoonesha
kutokuwa na masihara hata kidogo. Ajabu ni kwamba, alijiinamia
na kuanza kujiliza, ili ionekane ni kama nilikuwa namuonea.
“Nilitoa simu yangu, nikaingia kwenye upande wa email, nika-
fungua video niliyowaagiza wale vijana wa ‘control room’ wani-
tumie, ikimuonesha Berthany akiingia kwenye ofisi ya watu wa
medical na baadaye kutoka.
Nikamgeuzia simu na kumuonesha video hiyo, akaacha kulia na
kupigwa na butwaa. Nadhani hakuwa ametegemea kwamba nawe-
za kuwa na ushahidi kama ule.
“Huyu ni nani?”
“Ni mimi chief!”
“Ulienda kufanya nini kwenye ofisi za madaktari?”
“Nilienda kuchukua dawa za mifupa, nina tatizo la kuumwa mi-

332 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

fupa hasa kukiwa na baridi kama hivi.”


“Usinipotezee muda. Kadiri unavyonisumbua na kunipotezea
muda ndivyo unavyozidi kujiweka kwenye matatizo makubwa
zaidi. Unajua vizuri nini kitakutokea. Au unafikiri mkurugenzi
atakusaidia kwa kuwa una uhusiano naye wa kimapenzi?” nilimuu-
liza, likawa ni jambo lingine lililomshtua mno kwa sababu pengine
hakuwa anajua kwamba mimi pia najua.
“Sasa sikiliza, ngoja niutafute ukweli mwenyewe kisha mimi na
wewe tutamalizana!” nilisema huku nikisimama, nikamtaka anika-
bidhi kitambulisho chake cha kazi, akafanya hivyo huku akiteteme-
ka kuliko kawaida.
“Una muda mfupi wa kujitafakari kama unaweza kueleza uk-
weli kwa hiyari yako au mbinu nyingine zitumike,” nilisema huku
nikielekea mlangoni.
“Kaka Kenny!” aliita nikiwa nimeufikia mlango, nikageuka na
kumtazama.
“Nitakueleza kila kitu.”
“Andaa maelezo yako, nitarudi baada ya muda mfupi,” nilisema.
Kiukweli nilikuwa na mambo mengi sana ambayo ilikuwa ni
lazima niyapatie majibu haraka iwezekanavyo kwa hiyo niliona ni
kama anazidi kunichelewesha.
Nilitoka mpaka ofisini kwangu kwa lengo la kwenda kujua vijana
wangu wamefikia wapi kwa sababu bado kuna mambo mengi
yaliyokuwa yanatakiwa kufanyiwa kazi chini ya usimamizi wangu
mwenyewe.
Nilipojiridhisha kwamba kila mtu alikuwa anaendelea na kazi

333 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

zake kwa ukamilifu, nilitoka kimyakimya bila kumuaga mtu yeyo-


te. Nikaingia ndani ya gari langu na kuondoka kwa kasi kubwa.
Ilikuwa ni safari ya kwenda Mabibo kwenye maabara kuu ya
taifa kuonana na Eddy. Nilikuwa nataka kujua ni nini kilichokuwa
ndani ya kile kichupa alichokuwa amechomwa yule mzee wa
Kisomali kulikuwa na kitu gani kwa sababu nilikuwa na uhakika
kwamba ndicho kilichosababisha ile hali iliyomtokea.
Dakika kumi na tano pekee zilitosha kunifanya niwe nimeshafika
Mabibo, nikampigia simu Eddy na kumweleza kwamba nilikuwa
nimefika. Harakaharaka akatoka na kuja mpaka kwenye gari langu,
tukasalimiana kwa uchangamfu kisha nikamueleza kilichonipeleka
ingawa sikumwambia kwa undani.
“Nataka kujua hiki kilichopo humu ndani ni nini na inapotokea
kimeingia kwenye mzunguko wa damu wa binadamu nini kinat-
akiwa kufanyika ili kuokoa maisha ya mhusika.”
“Imeisha hiyo!”
“Dakika ngapi?”
“Siyo dakika mzee! Hii ni kazi ngumu na kwa sababu umetaka
pia kujua nini cha kufanya ili kureverse side effects!” alisema
akichanganya na Kimombo, akimaanisha kuondoa madhara yaliyo-
sababishwa na dawa ile.
“Ni dharura kaka! Mgonjwa yupo hoi kitandani na ni mtu
muhimu sana kwenye ishu kubwa iliyopo mbele yetu. Magogoni
Saga!” nilimwambia ili na yeye aone ni kwa kiasi gani kazi ile
ilikuwa muhimu.
“Daah! Sawa, nipe dakika thelathini!” alisema huku akiteremka

334 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kwenye gari, nikamuona akitembea harakaharaka kuelekea ndani


ya ofisi yao, nikatulia kwenye siti yangu ya gari ambayo nilikuwa
nimeitegua ili nipate muda wa kupumzika kidogo.
Dakika thelathini baadaye, Eddy alikuja kugonga kwenye kioo
cha gari langu. Hata sikuwa najua ni muda gani usingizi umenipi-
tia. Harakaharaka nilifungua mlango na kuinua siti, akaingia akiwa
anahema.
“Mzee ni kisanga!” alisema huku akikaa vizuri kwenye siti ya
pembeni yangu, mkononi akiwa na kile kichupa, karatasi lililoku-
wa na maelezo mengo na vichupa vingine vitatu vilivyokuwa na
rangi kama ya kijani hivi kwa mbali.
“Glipizide! Ni kama sumu hasa akipewa mgonjwa wa Kisukari.
Ikiingia mwilini inaenda kushusha presha kwa kasi kubwa na ku-
ongeza kiwango cha sukari kwa kasi kubwa. Ndani ya saa kadhaa
tu mtu lazima arudishe namba!” alisema Eddy akichanganya na
Kiswahili chake cha mtaani.
“Hizi ni dawa zinazoweza kusaidia kupunguza ukali wa dawa hii
ndani ya mwili. Anawekewa kwenye dripu, inatakiwa atundikiwe
mfululizo mpaka vichupa vyote vitatu viishe na haya ni maelezo ya
kitaalamu,” alisema, kabla hata hajamalizia, nikawa nimeshawasha
gari na kuanza kuondoka eneo hilo.
“Kwa hiyo umeamua kunichukua na mimi,” alisema, eti ndiyo
nikakumbuka kwmaba kumbe alikuwa anatakiwa kuteremka, nika-
funga breki kwa ghafla, akafungua mlango na kurukia nje, nikaon-
doa gari kwa kasi kubwa mno huku nikiviweka vile vichupa vya
dawa alizonipa vizuri.

335 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Haikuchukua muda mrefu nikawa nimeshafika ofisini. Kwa


jinsi nilivyoingia kwa kasi pale getini, watu waliokuwa wanani-
jua waligundua kwamba kuna kitu hakipo sawa ingawa ilikuwa
vigumu kujua ni nini hakipo sawa kwa sababu kila kitu kilikuwa
kinafanyika kwa usiri mkubwa huku kwa nje tukiwaaminisha watu
kwamba kila kitu kilikuwa kimemalizika salama.
Niliteremka kwenye gari na moja kwa moja nikaelekea kule
upande wa hospitalini, nikaingia pale mapokezi, nikasalimiana kwa
ishara na yule dada wa mapokezi ambaye aliponiona tu alikuwa
ni kama ameshtuka, nikapita mbiombio na muda mfupi baadaye
tayari nilikuwa kwenye ile wodi aliyokuwa amelazwa yule mzee
wa Kisomali.
Dokta Cossy na wale manesi walikuwa wanaendelea kuhangaika
kuokoa maisha ya yule mzee wa Kisomali na bado hakukuwa na
dalili zozote za yeye kupata ahueni.
“Ulimchoma Glipizide badala ya Insulin,” nilisema huku nikimu-
onesha Dokta Cossy kile kichupa na matokeo ya uchunguzi kutoka
maabara kuu ya taifa.
“Mungu wangu, Glipizide? Kivipi? Haiwezekani!”
“Hii ni serum ya kureverse madhara ya Glipizide mwilini, ina-
takiwa atundikiwe kwenye dripu mpaka chupa zote tatu ziishe,”
nilimwambia Dokta Cossy. Japokuwa yeye ndiye aliyekuwa daktari
akiwa amesomea kabisa fani hiyo, mimi ndiyo nilionekana kuwa
mtaalam kwa jinsi nilivyokuwa naelezea, nikifuatisha maelezo
niliyopewa na Eddy.
Nilimuona Dokta Cossy akipoteza kabisa utulivu ndani ya nafsi

336 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

yake, nadhani alikuwa anajua kwamba yeye ndiye atakayekuwa


mtuhumiwa wa kwanza katika kesi ya jaribio la kutaka kumuua
shahidi muhimu kwa kumchoma sindano ya dawa ambayo huwa
ikikosewa inakuwa sumu hatari kwenye mwili.
Hata hivyo, ukweli ambao nilikuwa naujua mpaka muda huo ni
kwamba yeye hakuwa akihusika kwa chochote, alikuwa ameche-
zewa mchezo na Berthany, lengo likiwa ni moja tu, kutuhujumu
ili tushindwe kupambana na tukio kubwa lililokuwa linatarajiwa
kutokea Magogoni.
“Najua ulikuwa hujui, usingeweza kufanya kitu kama hiki
kwa makusudi. Nakuamini ndiyo maana nilikuchagua wewe,”
nilimnong’oneza sikioni wakati akiendelea kuchanganya kichupa
kimoja kwenye dripu.
Nilimuona akishusha pumzi ndefu, akanigeukia na kunitazama
kama ambaye haamini kusikia maneno kama yale kutoka kwangu,
akaendelea na kazi yake huku uso wake ukionesha ni kama ametua
mzigo mzito uliokuwa unamuelemea.
Nilisimama pembeni nikishuhudia kila kilichokuwa kinaende-
lea, dripu yenye dawa maalum ya kuondoa sumu mwilini ikaanza
kutiririka kwa kasi kuingia kwenye mishipa ya yule mzee wa Ki-
somal, ambaye alikuwa ameunganishwa na mashine ya kumsaidia
kupumua kutokana na jinsi hali yake ilivyokuwa tete.
Dripu iliendelea kutiririka kwa kasi kuingia kwenye mishipa yake
huku Dokta Kessy akiwa makini kusoma mashine nyingine ili-
yokuwa ukutani, ambayo ilikuwa ikifuatilia mwenendo wa mifumo
yote muhimu katika mwili wa mgonjwa.

337 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Presha inaanza kurudi kwenye hali yake ya kawaida,” alisema


Dokta Cossy huku akinionesha mistari ya kitu kama grafu kwenye
ile mashine, ikionekana kuanza kupanda juu.
“Nakushukuru sana kwa kugundua mapema kilichokuwa kime-
tokea, kwa hiyo dawa hakika tungempoteza mzee wa watu na sijui
ningeweza vipi kuikwepa hatia kubwa namna hii. Ni nani? Ber-
thany?”
“Bado hatuna uhakika lakini muda utazungumza.”
“Hata sijui nikushukuru vipi kaka, itoshe kusema umeniokoa
na lazima nilipe fadhila kwako,” alisema kwa upole, grafu ikawa
inaonesha shinikizo la damu likizidi kurudi kwenye hali yake ya
kawaida na ndani ya dakika kumi tu baadaye, mgonjwa alifumbua
macho ingawa bado akili zake zilikuwa hazijatulia.
“Endeleeni naye nitarudi baadaye, bila shaka umeshaona ni kwa
kiasi gani anatakiwa kulindwa, hilo jukumu naomba libakie kwe-
nye mikono yako,” nilimwambia, akatingisha kichwa kwa heshima
kuonesha kuelewa, nikawaona wale manesi nao wakianza kuwa na
nuru kwenye nyuso zao baada ya kumuona mgonjwa amefumbua
macho.
Nilitoka na moja kwa moja nilirudi kule Basement, nilitaka
kwenda kufahamu mambo kadhaa kutoka kwa Berthany ingawa
nilikuwa najua hawezi kuninyooshea maelezo. Kila kitu kilikuwa
kinafanyika kwa kasi kubwa kisawasawa, nikashuka mpaka kwe-
nye chumba alichokuwepo Berthany.
Nilifungua mlango na kuingia, akakurupuka kutoka pale kwenye
kiti alipokuwa amejiinamia, akawa ananitazama kwa wasiwasi

338 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

mkubwa. Nadhani kitendo cha kumuacha kule chini, akiwa chini


ya ulinzi kilimfanya agundue kwamba hatukuwa na utani tena ka-
tika jambo lililokuwa mbele yetu.
“Nataka kujua uliipata wapi hii!” nilimuuliza baada tu ya kuwa
nimekaa kwenye kiti kilichokuwa kinatazama na kiti cha chuma
alichokuwa amekalia yeye, tukitenganishwa na meza katikati yetu.
“Mwanaume wangu!”
“Ndyo aliyekutuma?”
“Ndiyo!”
“Alikupa vichupa vingapi?”
“Kama kumi hivi lakini alinielekeza kwamba nikahesabu kwenye
begi la Dokta Cossy vipo vichupa vingapi vya dawa kisha nibadil-
ishe niweke vile alivyonipa.”
“Alikueleza ni kwa ajili ya nini?”
“Hapana!”
“Na wewe ukakubali bila kuhoji!”
“Nimekosa!”
“Unajua ni nini kilichopo humu ndani na kimesababisha madhara
gani mpaka sasa?”
“Hapana!”
“Berthany! Wewe ni afisa ambaye umepitia mafunzo na ume-
kuwa kazini kwa takribani miaka miwili sasa, si ndiyo?”
“Ndiyo!”
“Unaelewa vizuri kabisa uzito wa kosa la kushirikiana au kula
njama na mtu wa ndani au wa nje ya kitengo kufanya jambo lolote
ambalo ni kinyume cha sheria.”

339 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Kaka Kenny naomba unisaidie kunitoa kwenye huu mtego.”


“Unajua mbali na hiki ulichokifanya ni matatizo gani mengine
umetusababishia idara nzima?”
“Mimi? Hapana! Sina rekodi ya kufanya makosa yoyote, hii
ndiyo mara yangu ya kwanza na nimeifanya kwa sababu sikuwa na
jinsi.”
“Hukuwa na jinsi? Kivipi? Hebu nyoosha maelezo kwanza.”
“Huyu mwanaume niliyenaye.”
“Amefanya nini?”
“Amenirekodi picha za utupu tukiwa tunafanya tendo lakini yeye
haonekani na amekuwa akitishia kuzivujisha endapo sitafanya
anachokitaka.”
“Alikurekodi lini na amekuwa akikuagiza kufanya nini?”
“Alinirekodi siku ya kwanza tu nilipolala naye, wiki kama mbili
hivi baada ya kuwa nimefahamiana naye. Kuanzia hapo ameende-
lea kuwa ananitumia anavyotaka yeye.”
“Nataka kujua amekuwa akikuagiza kufanya nini?”
“Nihakikishie kwamba utanisamehe na mkurugenzi hatajua hili.”
“Mkurugenzi anajua kila kitu!” nilimwambia, nikamuona aki-
ishiwa nguvu kabisa, machozi yakawa yanambubujika. Nilikuwa
mgumu kuamini kile alichokisema kama ni kweli kwa sababu nili-
hisi ni kama anatafuta huruma yangu kwa kucheza na akili zangu.
“Mlianzisha uhusiano wenu lini?”
“Kama miezi mitatu iliyopita!”
“Narudia tena swali la msingi, amekuwa akikutuma kufanya nini
na nini?” nilimuuliza Berthany huku nikimkazia macho kutaka ku-

340 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

jua kama alichokuwa anakisema kilikuwa na ukweli wowote ndani


yake.
“Amekuwa akitaka kujua kuhusu misheni na oparesheni zote
zinazoendelea kila siku,” alisema, nikashusha pumzi ndefu kwa
sababu sasa ilikuwa ni dhahiri kwamba kumbe taarifa za kila tuli-
chokuwa tunakifanya, zilikuwa zinavuja kutokea kwa Berthany.
“Christopher Walusanga! Hilo ndiyo jina lake si ndiyo?”
“Mimi namjua kwa jina la Chriss Ephraim.”
“Anaitwa Christopher Ephraim Walusanga. Field officer kama
wewe unakuwaje kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanaume
ambaye hata jina lake halisi hulijui?” nilimuuliza huku nikimkazia
macho.
“Kiukweli sikupata muda wa kufahamiana naye vizuri, hata jinsi
nilivyokutana naye yaani mazingira yalikuwa hayaeleweki nikaji-
kuta tu nimelala naye.”
“Unawezaje kuwa na uhusiano na mwanaume mwingine wa nje
kizembe namna hiyo wakati unajua pia kwamba upo kwenye uhu-
siano na mkurugenzi wetu?” nilizidi kumbana, akanitazama kwa
macho ya mshtuko kwa sababu sasa alikuwa na uhakika kwamba
kumbe nilikuwa najua kuhusu uhusiano wake wa kimapenzi na
mkurugenzi.
Hakuwa na cha kujibu, akajiinamia chini huku machozi yakiwa
yanambubujika.
“Unajua ni kwa kiasi gani umeigharimu taasisi yetu? Unajua ni
kwa kiasi gani kwa kushirikiana na huyu mhuni umeuweka us-
alama wa nchi yetu hatarini?” nilimuuliza, akawa ni kama haelewi

341 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

nilichokuwa nakizungumzia.
“Taarifa ulizokuwa unamvujishia huyo mwanaume ndizo
zilizofanya mpaka leo tushindwe kuudhibiti mtandao hatari wa
magaidi ambao wanataka kuishambulia Magogoni. Bila shaka
sasa unaelewa makosa yako yana uzito kiasi gani. Kibaya zaidi ni
kwamba umekuwa pia ukipata taarifa nyingine nyeti kutoka kwa
mkurugenzi wetu na wewe ukawa unazipeleka moja kwa moja kwa
huyo mwanaume wako. Huu ni uhaini wa kiwango cha juu kabisa
Berthany na adhabu ya uhaini inafahamika.”
“Nisaidie kaka Kenny!”
“Mara ya mwisho umekutana lini na Chriss?”
“Asubuhi ya leo,” alisema, nikashusha pumzi ndefu.
“Sasa nisikilize, kitu cha kwanza utatakiwa kufanikisha Chriss
kukamatwa, tena sasa hivi. Ushirikiano utakaoutoa ndiyo utaka-
oonesha ni kwa kiasi gani unajutia makosa yako.”
“Nipo tayari chief.”
“Nieleze njia rahisi tunayoweza kuitumia kumchukua bila mtu
yeyote kujua kinachoendelea.”
“Muda huu atakuwa kwenye ‘depot’ yao, Kiwalani. Nashauri
twende mpaka Kiwalani, nitampigia simu na kumweleza aje tuon-
ane mara moja, akija basi itakuwa ni rahisi kwenu kumchukua,”
alisema Berthany, nikatafakari kile alichokuwa amekisema na
kuona kina mantiki.
“Tunaondoka pamoja, mguu kwa mguu, ukileta ujuaji wa aina
yoyote tusilaumiane,” nilisema huku nikiinuka, nikatoka na ku-
muacha mle ndani. Ilikuwa ni lazima niende kwanza kuwapanga

342 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

vijana wangu ambao tungeenda pamoja kukamilisha ‘misheni’ ile.


Niliwapanga vijana wanne ambao nilikuwa nawaamini. Bila
kupoteza muda, nikaagiza Berthany akatolewe kule basement chini
ya ulinzi mkali wa kificho ili mtu yeyote asielewe kilichokuwa
kinaendelea.
Niliichukua simu ya Berthany kutoka kwa vijana wa Cyber
ambao niliwapa kazi ya kunakili taarifa zake zote za mawasiliano
aliyokuwa akiyafanya kwa ajili ya ushahidi. Nikaelekea kwenye
gari yangu na muda mfupi baadaye, Berthany aliletwa, nikaagiza
akae siti ya pembeni yangu dereva.
Wale vijana wanne wao waliingia kwenye gari nyingine binafsi
na bila kupoteza muda, tukatoka kuelekea Kiwalani. Sikuwa naijua
hiyo ‘depot’ yao kama alivyonieleza Berthany, ikabidi yeye ndiyo
awe ananipa maelekezo huku wale vijana wangu wakitufuata kwa
nyuma.
Tulipofika jirani na eneo husika, ilibidi kwanza tupaki magari
yetu mahali ili kuandaa mpango kazi wa nini cha kufanya, nikawa
nawasiliana na vijana wangu kwa kutumia vifaa vya mawasiliano,
ambavyo kila mmoja alikuwa amevaa mwilini.
“Utatakiwa kumpigia simu na kumueleza kwamba aje kwenye
gari kama tulivyokubaliana. Akifika sisi tutamaliza kazi,” nilim-
wambia Berthany huku nikichomoa pingu.
“Hiyo ni ya kazi gani chief,” aliniuliza Berthany kwa mshangao,
nikamuonesha ishara kwamba anatakiwa kuhamia kwenye siti ya
dereva, mimi nikafungua mlango na kuteremka, akahama siti kisha
nikamfunga pingu mkono wake mmoja na kumfunga kwenye usu-

343 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kani wa gari.
“Hakukuwa na ulazima wa kufanya hivi, anaweza kushtuka akija
na kuniona.”
“Nina maana yangu, fanya kama nilivyokuelekeza,” nilimwambia
huku nikiingia kwenye siti ya nyuma ya gari lile ambalo lilikuwa
na tinted, nikamtaka aendeshe mpaka nje ya ile ‘depot’, kweli aka-
fanya hivyo huku nikimfuatilia kwa makini kutokea siti ya nyuma,
vijana wangu nao wakafanya kama tulivyokubaliana.
Berthany aliendesha gari mpaka kwenye maegesho ya nje ya
ile ‘depot’, nikampa simu na kumuelekeza aweke ‘loud speaker’
wakati akizungumza naye. Tayari vijana wangu walikuwa wame-
shajipanga kwenye ‘formation’ kama tulivyokubaliana, tayari kwa
kazi.
“Chriss!”
“Mambo baby!”
“Poaa! Upo kazini?”
“Ndiyo! Vipi kuna jipya?”
“Hamna hata jipya, tunaweza kuonana mara moja, nimekuja huku
mitaa ya kazini kwako nikaona nikupitia japo nikuone. Nipo nje
hapa kwenye ‘parking’,” alisema Berthany huku akijitahidi sana
kutoonesha tofauti yoyote kwenye mazungumzo yake.
“Dakika sifuri baby, tena ndiyo vizuri twende tukapate ‘lunch’
pamoja,” alisema mwanaume huyo bila kujua kwamba kumbe
alikuwa amewekwa kwenye mtego.
Muda mfupi baadaye, kijana mmoja mrefu, maji ya kunde mwe-
nye mwili wa mazoezi, alionekana akitoka kwenye lango kuu la

344 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kuingilia kwenye ‘depot’ ya kampuni yao ya kusambaza mafuta.


“Ni yule pale!” alisema Berthany, harakaharaka nikawapa taarifa
vijana wangu juu ya mwonekano wa mtuhumiwa wetu, akawa
anabofyabofya simu yake kisha akaiweka sikioni, simu ya Ber-
thany ikawa inaita.
“Nimekuona, njoo kwenye hii gari nyeusi hapa kwenye ‘park-
ing’, kushoto kwako.”
“Shuka kwenye gari tuelekee canteen, ni jirani tu,” alisema yule
kijana huku akitembea taratibu kufuata barabara kubwa ya kutokea
kwenye eneo hilo.
“Sawa, ila njoo kwanza kwenye gari nina ‘sapraiz’ yako,” alise-
ma Berthany, nikamuoneshea alama ya dole kwa sababu alifanya
kitu kinachotakiwa katika muda muafaka.
Yule mwanaume alikata simu kisha akawa anasogea kwenye lile
gari, akionesha kutokuwa na wasiwasi hata kidogo, akafika mpaka
kwenye lile gari na kitendo cha kugusa mlango wa mbele pembeni
ya dereva tu, tayari alijikuta mikononi mwa vijana wawili wa kazi.
Mmoja aliwahi kumbana kwa nyuma huku mwingine akimziba
mdomo kwa kitambaa, kwa kuwa na mimi nilishakuwa ‘standby’,
nikaufungua mlango wa nyuma, akasukumiwa ndani ambapo
nilimdaka juujuu na kumkandamiza kwenye siti ya gari na kumgu-
sisha bastola kichwani.
“Unatakiwa kutulia kimya, vinginevyo nitakumwaga ubongo
wako,” nilimwambia kwa sauti ya mamlaka. Vijana wa kazi, mmo-
ja aliingia upande wa mbele na kufunga mlango, mwingine akain-
gia kule nyuma nilikokuwa nimemdhibiti kisawasawa yule kijana,

345 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

akafunga mlango kisha Berthany akalitoa gari kinyumenyume kwa


kasi kubwa, akaligeuza na kuingia barabarani, wale vijana wawili
nao wakawasha gari na kuanza kutufuata.
Kila kitu kilikuwa kimetokea kwa kasi ya kimbunga, sekunde
chache tu zilitosha kukamilisha tukio lile kiasi cha mtu yeyote
kutoelewa ni nini kilichokuwa kimetokea.
Baada ya kuhakikisha tumeondoka kabisa katika eneo lile, ni-
limpa ishara Berthany kwamba anatakiwa kupunguza mwendo na
kusimama, kweli akafanya hivyo na muda mfupi baadaye, alisi-
mamisha gari.
Jambo la kwanza ilikuwa ni kumfunga yule kijana pingu kwa
nyuma kisha nikamkalisha vizuri kwenye siti, nilifungua mlango
na kuteremka, nikafungua mlango wa mbele pale kwenye usukani,
nikamfungua Berthany pingu pale kwenye usukani na kumfunga
mikono yote, nikamteremsha kibabe na kumhamishia kule nyuma.
Nikampa ishara yule kijana wangu aliyekuwa amekaa siti ya
mbele, akateremka na kuja kule nyuma. Kwa hiyo Berthany na
mwanaume wake wakawa wamekaa katikati huku kijana mmoja
akiwa kushoto na mwingine kulia.
Nilitoa ishara nyingine, wote wawili wakavalishwa vitambaa vya
kuziba nyuso zao, wakianza na Berthany. Nilikuwa nafanya yote
hayo kwa sababu maalum, kuna kitu nilikuwa nataka kukipandiki-
za kwenye moyo wa yule kijana.
Niliwasha gari na kuondoka kwa kasi kubwa, kila mtu akiwa
kimya kabisa ndani ya gari, nikawa namtazama yule kijana jinsi
alivyokuwa anatetemeka kwenye moyo wake. Lile gari la nyuma

346 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

yetu nalo likawa linakuja kwa kasi kubwa, safari ikaendelea na


hatimaye tukawasili kitengoni.
Kwa kuwa kila kitu kilikuwa kinafanyika kwa usiri mkubwa,
sikutaka mtu yeyote ambaye hahusiki agundue ni nini kilichokuwa
kinaendelea hivyo ilibidi nilishushe gari mpaka kwenye parking
ya kuingilia kwenye ‘basement’.
Hilo lilifanyika na baada ya kufika eneo hilo, nilizima gari na
kutulia kwa muda mfupi, baada ya mazingira kutulia, niliwapa
ishara vijana wangu wafanye kazi yao, mmoja akateremka na
kufungua mlango, akatangulia kumtoa Berthany akiwa bado ame-
fungwa kitambaa machoni.
Yule kijana wa pili naye akamnyanyua yule kijana na kumterem-
sha, akamuingiza kule kwenye basement, nikaliondoa gari eneo
hilo na kulirudisha kwenye ‘parking’. Nikateremka na kuingia
ofisini kwangu ili kupoteza ‘maboya’ watu waliokuwa wanafua-
tilia ‘movement’ zangu.
Nilikaa kwa muda mfupi pale ofisini nikiendelea kutafakari kwa
makini hatua ya pili ya nini cha kufanya baada ya kumpata kijana
yule.
Baada ya kama dakika tatu, nilitoka na kuelekea kule chini
‘basement’ nikiwa na ‘diary’ yangu. Nilishakuwa nimewaelekeza
mahali pa kumpeleka yule kijana, nikaanzia kwenye chumba
alichokuwemo Berthany ambaye tayari alikuwa ameshafunguliwa
pingu na kuondolewa kile kitambaa usoni.
“Umefanya kazi nzuri, hiyo ni hatua ya kwanza,” nilimwambia
Berthany, akashusha pumzi ndefu na kukaa vizuri.

347 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Huyu kijana anaishi wapi?”


“Anaishi Kijitonyama!”
“Unapafahamu anapoishi?”
“Sifahamu nyumba, nafahamu tu kwamba anaishi Kijitonyama.”
“Huwa mnakutania wapi kufanya mambo yenu?”
“Lodge!”
“Umekuwa mzembe sana Berthany! Anyway sawa!” nilisema
huku nikigeuka na kutaka kuondoka.
“Kaka Kenny!” aliita Berthany, nikageuka na kumtazama.
“Haikuwa malengo yangu kusaliti kiapo changu, naomba sana
unisamehe na unisaidie kutoka kwenye huu mtego.”
“Tutaangalia ila siwezi kukuahidi kwa sasa!” nilisema huku
nikigeuka na kutoka, nikafunga mlango na kuelekea ‘Room 77’
ambako ndiko nilikowaelekeza vijana wangu mahali pa kumpeleka
yule mtuhumiwa.
Nilifika na kushika kitasa, mlango ukafunguka. Vijana wangu
walikuwa wamemkalisha yule kijana kwenye kiti cha chuma na
kumfunga pingu kwa mbele ikiwa imeunganishwa na minyororo
iliyokuwa imeungana na ile meza ya chuma.
Nikawapa ishara ya kutoka na kunipisha, kweli wakafanya hivyo,
nikarudi na kufunga mlango kwa ndani kisha nikasogea mpaka
pale kwenye kiti cha upande wa pili, ukiachana na kile alichokuwa
amekaa yeye.
Nikakaa nikiwa kimya, nikawa namtazama, na yeye akawa anani-
tazama kwa macho ya wiziwizi.

348 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

14

CHRISTOPHER Ephraim Walusanga,” nilimuita kwa
jina lake kamili.
“Ulizaliwa Desemba 24, 1989 katika Hospitali ya
Mbozi Mission mkoani Mbeya, siku hizi ni mkoa wa
Songwe,” nilisema, akashtuka na kunitazama kwa macho
ya mshangao.
“Ulisoma shule ya msingi Mbozi Mission Primary School na
kuhitimu darasa la saba. Ukaenda kusoma Vwawa Day Secondary
School, ukafukuzwa ukiwa kidato cha tatu kwa sababu ya kuka-
matwa ukiwa unavuta bangi, ni kweli siyo kweli?”

349 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Umeyajulia wapi haya?”


“Najua kila kitu kuhusu wewe, nina faili zima lenye taarifa zako
zote muhimu,” nilimwambia na kumkazia macho, nikamuona jinsi
alivyokuwa anababaika.
“Nimeanza na taarifa zako kwa kifupi kuonesha tu kwamba
nakujua kwa undani, kwa hiyo usitake kunisumbua kwa maswali
ambayo nitakuuliza.”
“Nimefanya makosa gani mpaka kutekwa? Hapa ni wapi?”
“Hujatekwa! Umekamatwa! Upo kwenye mikono ya vyombo vya
usalama.”
“Sijakamatwa, mimi nimetekwa!”
“Kwa hiyo unataka kusemaje?”
“Siwezi kujibu swali lolote mpaka kwanza niitiwe mwanasheria
wetu wa kampuni.”
“Una akili timamu kijana?”
“Nina akili timamu na ndiyo nimekujibu hivi. Siwezi kutoa
maelezo kwa mtu ambaye simjui.”
“Nimekwambia upo kwenye mikono ya vyombo vya ulinzi na
usalama, hiki hapa ni kitambulisho changu,” nilisema huku nikitoa
kitambulisho na kumuonesha, akasoma kisha nikamuona ni kama
ameshtuka hivi. Nadhani awali alidhani amechukuliwa na askari
wa jeshi la polisi na pengine ndiyo maana alitaka kuanza kuleta
mambo ya siasa.
“Ulifahamiana lini na Berthany na ilikuwaje?”
“Nilikutana naye miezi kama mitatu minne hivi.”
“Una uhusiano gani naye?”

350 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Ni mpenzi wangu.”


“Unafahamu anafanya kazi gani?”
“Hapana!”
“Kwa muda mrefu umekuwa ukimlazimisha kukupa baadhi ya
taarifa kutoka sehemu anayofanyia kazi huku ukimtishia kwamba
endapo hatafanya hivyo, utavujisha picha zake ulizompiga akiwa
mtupu. Umekuwa unazipeleka wapi taarifa hizo?”
“Siyo kweli, sijawahi kumuuliza chochote kuhusu kazi yake wala
sijawahi kumpiga picha za utupu.”
“Kwa kawaida, mahojiano yetu huwa yanakuwa na hatua mbili,
ya kwanza huwa ni mazungumzo ya hiyari kama hivi, endapo
hatua hiyo ikishindikana hatua ya pili huwa ni kutumia nguvu
kumlazimisha mhusika kutoa taarifa. Nimeanza na hatua ya awali
lakini inaonekana hutaki kutoa ushirikiano, unataka nitumie hatua
ya pili?”
“Mimi sina makosa, kama ni kuniua nyie niueni tu, sijui chochote
kuhusu hayo unayoniuliza,” alisema, nikajikuta nikipandwa na
jazba kali mno ndani ya moyo wangu, nikainuka na kumkamata
koo kwa nguvu.
“Unafanya utani kijana si ndiyo? Nitakuua kweli,” nilisema huku
nikiendelea kumkaba koromeo kwa nguvu kisha nikamsukuma
kwa nguvu, akadondoka na kile kiti mpaka chini huku akiwa anata-
patapa mithili ya mtu anayetaka kukata roho.
Nikiri kwamba, kila kitu kilikuwa kimetokea kwa ghafla kiasi
kwamba nilijikuta nikishindwa kujizuia kwa sababu ni kweli yule
alikuwa mtuhumiwa ambaye alikuwa hatari kwa usalama wa nchi

351 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

lakini kwa kile nilichokuwa nimemfanyia, ilikuwa ni kinyume


kabisa na kanuni za kazi.
Nilimfuata kule alikokuwa ameangukia, nikamnyanyua na
kumkalisha vizuri, bado akawa anaendelea kutapatapa kwa sababu
nilimkaba vibaya kwenye koromeo lake na kuvuruga kabisa mfu-
mo wake wa upumuaji.
Ambacho wengi hawakijui ni kwamba mnapokuwa mafunzoni,
mnafundishwa namna ya kukabiliana na adui hususan katika kujio-
koa au kujilinda na miongoni mwa mambo ambayo watu waliopitia
mafunzo ya kijeshi wanayajua vizuri, ni sehemu za kumgusa adui
na kumsababishia madhara makubwa bila kutumia nguvu kubwa.
Hasira nilizokuwa nazo ndizo zilizosababisha nimkamate yule
kijana koromeo kisha kulibonyeza kwa ufundi maalum, jambo
ambalo linaweza kusababisha mtu akazimia au akapoteza maisha
kabisa ndani ya sekunde chache tu.
Ilibidi nimpe hudumaya kwanza kwa kumpiga mgongoni kwa
nguvu, akashtuka kisha akawa ni kama amezinduka kutoka kwenye
usingizi mzito, macho yakiwa yamemtoka pima.
“Hatupo hapa kucheza, utauawa kweli na hakuna atakayejua ma-
hali ulipo, hata maiti yako haitaonekana, endelea kufanya mche-
zo,” nilisema kwa sauti ya ukali, nikamuona akitetemeka kuliko
kawaida. Kitendo nilichokuwa nimemfanyia, japokuwa kilikuwa
kinyume cha sheria lakini kilikuwa kimesaidia kumshikisha adabu.
“Nani huwa anakutuma?” nilimuuliza kwa ukali, akawa anaba-
baika, hofu ikiwa imetanda kwenye moyo wake, akionesha dhahiri
kwamba endapo nitaendelea kumbana, ataeleza kila kitu.

352 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Mimi simjui ila huwa tunawasiliana tu kwa simu!”


“Unanidanganya! Unajua unazidi kunipandisha hasira? Najua
kila kitu lakini nataka kusikia kutoka kwako,” nilisema huku niki-
simama, nikavua saa niliyokuwa nimeivaa, nikamuona akitetemeka
kuliko kawaida.
“Ni bosi wetu ndiyo aliyenipa hiyo kazi.”
“Bosi wako anaitwa nani?”
“Gilbert.”
“Gilibert Mutesigwa, si ndiyo?” nilimuuliza huku nikijitahidi
kuuficha mshtuko niliokuwa nao, akatingisha kichwa kuonesha
kukubali kile nilichokisema huku naye akishangaa nimelijuaje jina
kamili la bosi wake.
“Ni kazi gani aliyokupa?”
“Ya kuwa na Berthany.”
“Wewe ulimjuaje Berthany?”
“Ni yeye ndiye aliyenioneshea na kunielekeza namna ya kumpa-
ta.”
“Kwa nini Berthany?”
“Hata sijui, mimi nilipewa tu kazi.”
“Anakulipa shilingi ngapi?”
“Kila wiki nalipwa shilingi laki moja.”
“Shilingi laki tatu kwa kila taarifa nyeti ninayompelekea,”
alisema, nikashusha pumzi ndefu na kukaa tena pale kwenye kiti.
Nikawa namtazama usoni.
“Unajua ninao uwezo wa kumgundua mtu anayedanganya?”
“Sidanganyi afande! Nasema ukweli mtupu,” alisema, nikawa

353 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

namkazia macho kwa makini.


Akili yangu ilikuwa imehama kabisa, kitendo cha yule kijana
kuniambia kwamba bosi wake alikuwa anaitwa Gilbert Mutesigwa
kilinichanganya kuliko kawaida. Ni Gilbert Mutesigwa huyuhuyu
ndiye ambaye alikuwepo kwenye orodha ya wageni ambao walita-
kiwa kukutana na namba moja kwenye dhifa maalum ya wafanya-
biashara.
Ambacho sikuwa na uhakika nacho, ni kwamba huyu Gilbert
Mutesigwa ndiyo yule Bosi Mute ninayemjua mimi au ni mtu
mwingine? Kama ni yeye, imekuwaje tena anashiriki kwenye
njama kubwa kama hizi wakati inafahamika mahali alipo? Kama
siyo yeye, ni nani huyo anayeweza kucheza na sharubu za simba
kiasi hicho?
Picha kubwa ambayo ilikuwa imefunguka kwenye kichwa
changu, ni kwamba kumbe mtandao ulikuwa mpana kwelikweli
na hakika walikuwa wamejipanga kisawasawa kufanikisha wali-
chokuwa wanataka kitokee.
Nilichokifanya ni kwamba nilijiapiza kwamba liwake jua inye-
she mvua, nitapambana kwa kadiri ya uwezo wangu wote kupam-
bana nao kuhakikisha lengo lao halitimii. Kila nilipokuwa nawaza
kwamba huyo Gilbert Mutesigwa anaweza kuwa ndiyo Bosi Mute,
nilikuwa nakosa kabisa amani ndani ya moyo wake kwa sababu
‘balaa’ lake nalijua kisawasawa.
“Kwa hiyo laki tatutatu kwa kila taarofa unayopeleka kwa Mute-
sigwa ndiyo zilizokufanya umpige picha za utupu Berthany?”
“Ni yeye ndiye aliyenifundisha kufanya hivyo.”

354 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Sasa sikia, ninao uwezo wa kukusaidia kupunguza uzito wa kesi


yako lakini kwa sharti moja tu, nataka utusaidie kumpata huyo bosi
wako.”
“Afande, bosi wangu mimi huwa simjui kwa sura, huwa nazun-
gumza naye kwenye simu tu hata pale ofisini, sisi wafanyakazi wa
kawaida huwa tunamsikia tu hakuna anayemfahamu kwa sura.”
“Haiwezekani, nimekwambia kama unataka nikusaidie lazima
uonyeshe ushirikiano, unaujua uzito wa makosa yako? Unajua
adhabu yake ni ipi? Kwa kifupi unastahili kuuawa.
Usipouawa kwa kupigwa risasi, mahakama itaamuru unyongwe
hadi kufa. Umehatarisha sana usalama wa taifa letu kwa sababu
ya malipo ya hivyo vi laki tatutatu unavyopewa. Hakuna mtu
anayeweza kuamini kwamba ulikuwa unatumwa, itaonekana wewe
pia ni gaidi na ndiyo unayeshirikiana na hao magaidi kutaka kuit-
ingisha nchi.”
“Magaidi? Magaidi kivipi tena afande?”
“Unajifanya hujui si ndiyo? Basi utajua hujui,” nilisema huku
nikimtazama usoni yule kijana. Kwa jinsi ilivyoonesha, ni kama na
yeye hakuwa anajua kwa undani taarifa alizokuwa anazitoa ziliku-
wa zinaenda kutumika wapi, kwa hiyo na yeye alikuwa anatumika
huku yeye pia akimtumia Berthany!
“Umesema bosi wenu humjui, nani aliyekupa vichupa vya sumu
na kumpa Berthany akaweke kwenye mkoba wa daktari? Unajua
tayari kuna mtu amepoteza maisha na mtuhumiwa wa kwanza
ni wewe?” nilisema, akashtuka kuliko kawaida, nadhani hakuwa
anajua kwamba nilikuwa najua na madhara ya kile walichokifanya

355 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ni yapi.
“Hakuna mtu yeyote ambaye unaweza kumletea maelezo mepesi
namna hiyo halafu akakuamini. Wewe unahesabika kuwa gaidi,
tena gaidi hatari,” niliendelea kumchanganya kichwa ili kuendelea
kumsoma.
“Hapana, mimi siyo gaidi. Mimi nilielekezwa tu kwenda ku-
chukua fedha kwa mhasibu wetu, akanielekeza kuzipeleka mahali
fulani kisha nikapewa huo mzigo wa vichupa vya dawa. Mimi sijui
chochote kinachoendelea zaidi ya kutumika kama dalali tu afande,
sijui nakuapia kwa Mungu.”
“Hivi unafikiri unaweza kunidanganya mtu kama mimi? Hivi
unanifahamu vizuri kweli? Jinsi tulivyokuja kukukamata pekee ku-
napaswa kukufanya ugundue kwamba sisi siyo watu wa kawaida.
“Najua unajua kila kitu ila hapa unatafuta huruma. Nikwambie
tu kwa kifupi ni kwamba taarifa ambazo umekuwa ukimlaghai na
kumtishia Berthany ili akupe, ndizo ambazo zimekuwa zikitumika
na magaidi wanaotaka kuishambulia ikulu. Bila shaka ulisikia
kwamba kuna tukio la ugaidi lilikuwa linataka kutokea, basi wewe
pia umeshiriki kwenye njama zote na ushahidi upo.
“Kwa hiyo kama nilivyokwambia, wewe fikiria uone ni kwa
namna gani utakayoweza kutusaidia kuwapata huyo bosi wako
na wenzake. Ukifanikisha hilo, nakuahidi kwamba nitasimama na
wewe, ukileta ujuaji basi kesi yako ndiyo hiyo na hukumu yake
inafahamika,” nilisema na kutoka, nikamfungia mlango kwa nje na
kurudi ofisini kwangu.
“Nikiwa nimekaribia, akili zangu zilinituma kupitia kwanza kwa

356 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

mkurugenzi kwenda kumweleza nilichokuwa nimekibaini lakini


wakati huohuo nikawa nataka nirudi kule wodini kuangalia maeen-
deleo ya yule mzee wa Kisomali kuona kama anaweza kuzung-
umza kile alichokuwa ametaka kuniambia kabla hajafikwa na lile
balaa.
Nikawa sielewi hata nielekee wapi, jina la Mutesigwa likawa
linaendelea kuzunguka ndani ya kichwa changu.
Mwisho niliamuakwamba niende tu kule wodini kwanza huenda
naweza kupata kitu kinachoweza kunisaidia kwa sababu nilikuwa
na uhakika kwamba yule mzee wa Kisomali tayari ameshapata
nafuu.
Kwa jinsi nilivyokuwa natembea, mtu yeyote angenitazama kwa
makini angegundua kwamba akili yangu haikuwa sawa kwa sababu
hata mwendo wangu, ulikuwa ni katikati ya kutembea na kukimbia,
yaani sitembei wala sikimbii, nipo katikati.
Muda mfupi tu tayari nilikuwa nimeshaingia wodini na kuwakuta
wale manesi waliokuwa wakisaidia na Dokta Cossy wakiendelea
kumhudumia mgonjwa ambaye sasa alionesha kuwa na ahueni
kubwa.
“Pole sana,” nilisema baada ya kumsogelea pale kitandani kwake
na kuwapa ishara wale manesi kwamba wanipishe kidogo kwani
nilikuwa na mazungumzo nyeti na mgonjwa.
“Sijambo! Nini kilitokea? Nilikuwa naendelea vizuri mbona?”
“Muhimu ni kwamba unaendelea vizuri, nadhani sukari yako
ilipanda au kushuka sana ghafla.”
“Hapana, nilikuwa naendelea vizuri kabisa, au daktari kuna ma-

357 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kosa aliyafanya?”
“Hapana, Dokta Cossy ni mtu makini sana, hawezi kufanya
makosa yoyote ya kusababisha uzidiwe ghafla,” nilimtetea Dokta
Cossy kwa lengo la kumtoa wasiwasi yule mzee kwa sababu kama
angegundua ni nini kilichokuwa kimetokea, lazima angeacha kutoa
ushirikiano.
“Amefanya kazi kubwa sana kukupigania, anastahili pongezi,”
nilimwambia, nikamuona akishusha pumzi ndefu na kutuliapale
kitandani.
“Nilijua habari yangu imekwisha,” alisema, nikawa naendelea
kumfariji pale kwa upole.
“Tunaweza kuzungumza?”
“Bila shaka.”
“Mara ya mwisho wakati naagana na wewe uliniambia jambo
kuhusu Abdulwaheed, ukaniambia unajua wapi kwa kumpata.”
“Ndiyo, mambo yanapomuwia magumu, huwa anarudi kujipanga
upya na sehemu zake ni mbili, Kibiti au Mafia.”
“Nawezaje kumpata?”
“Kama unaweza, nenda Kibiti au tuma watu waende, ukifika
stendi ya mabasi, ulizia kwa Ustaadh Fundi, naomba kalamu na
karatasi nikuandikie ujumbe, ataelewa na atakusaidia,” alisema,
nikashtuka nikiwa ni kama siamini kusikia yale aliyokuwa anayas-
ema.
Sikutaka kupoteza muda, nilitoa kalamu, nikajisachi mwilini
kuangalia kama nilikuwa na karatasi, sikuliona, nikaangazaangaza
mle wodini na kuona ‘notebook’ ndogo juu ya droo iliyokuwa

358 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

pembeni, nikaichukua.
Ilikuwa ni ya Dokta Cossy, nikachana karatasi moja na haraka-
haraka nikamsogezea yule mzee wa Kisomali. Akaandika maneno
machache kwa lugha ambayo hata sikuielewa kisha chini akaan-
dika namba fulani hivi.
“Mwambie nimekutuma mimi lakini usimwambie kwamba
mnanishikilia, anaweza kuingiwa na hofu na akakataa kutoa ush-
irikiano. Kubwa zaidi, naomba msimpe kashikashi ya aina yoyote,
ni mtu mzuri,” alisema yule mzee.
“Kwa nini unafanya yote haya?”
“Nimeamua kukusaidia, nitatekeleza nadhiri yangu kwa sababu
nimegundua kwamba kwa miaka mingi sikuwa katika mstari
mzuri wa maisha na sasa nimeamua kubadilika,” alisema, nikashu-
sha pumzi ndefu na kunyoosha mkono wangu wa kulia kumpa,
akaupokea palepale kitandani, tukatazamana kwa sekunde kadhaa.
“Nenda harakam, muda hautoshi.”
“Nashukuru, lakini kabla sijaondoka, naomba nikuulize kitu
kingine.”
“Kitu gani?”
“Gilbert Mutasigwa ni nani?”
“Unaniuliza mimi? Nadhani mimi ndiyo nilipaswa kukuuliza
wewe swali hilo,” alisema, akazidi kunichanganya.
“Umemsahau bosi wako?”
“Bosi Mute?” niliuliza kwa mshtuko nikiwa ni kama siamini,
nikamuona akicheka.
“Siku hizi siyo binadamu wa kawaida, mambo mliyomtendea

359 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

yamemfanya kuwa zaidi ya mnyama.”


“Hapana, haiwezekani. Bosi Mute yupo gerezani.”
“Ndiyo, yupo gerezani lakini pia yupo uraiani, kwa kifupi ni
kwamba yupo kila mahali,” alisema, nikageuka haraka na kutaka
kutoka lakini akaniita, tena kwa jina lilelile aliloniita siku chache
nyuma na kunifanya nibaki na maswali mengi ndani ya kichwa
changu.
“Snox!”
Niligeuka na kumtazama, akanionesha ishara kwa kidole kwamba
nimsogelee, nikafanya hivyo. Akaniomba kile kikaratasi alichoku-
wa ameniandikia, nikampa. Akaniomba na kalamu, nikampa. Ali-
kifungua kwa sababu nilikuwa nimeshakikunja, akaongeza maneno
machache pale chini kisha akanipa na kunipa ishara kwamba
niondoke.
Nilitoka kwa kasi ya kimbunga, muda mfupi baadaye, tayari ni-
likuwa ofisini kwangu, vijana wangu wakawa wananishangaa kwa
sababu ama kwa hakika nilikuwa nimepagawa.
“Haiwezekani!” nilisema huku nikipiga meza kwa nguvu, ni-
kainuka na kutoka tena mbiombio. Akili zilinituma kwenda kwa
baba yake Saima kumweleza jambo zito nililokuwa nimeligundua.
Niliamini yeye ndiye mtu pekee anayeweza kunielewa kwa wakati
huo.
“Vipi, mbona mbiombio,” alisema baba yake Saima huku akii-
nuka kwenye kiti chake na kuacha kila alichokuwa anakifanya,
akanisogelea na kunitazama machoni, na mimi nikawa namtazama,
akashusha pumzi ndefu.

360 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Kaa,” alisema huku akinishika begani, akafungua friji dogo


lililokuwa mle ndani na kutoa chupa ya maji, akamimina kwenye
glasi kisha akanirudia pale nilipokuwa nimekaa, akanipa kisha na
yeye akakaa. Niligida ile glasi yote, nilipoishusha, ilikuwa tupu.
Nikashusha pumzi ndefu na kukaa vizuri.
“Kumetokea nini?”
“Mutesigwa!”
“Amefanya nini?”
“Anahusika kwenye hili. Gilbert Mutesigwa aliyemo kwenye
orodha ya wafanyabiashara watakaokutana na namba moja, ni Bosi
Mute,” nilisema, nikamuona akivua miwani yake na kusimama,
akaifutafuta kisha akaivaa upya na kuanza kuzungukazunguka mle
ofisini kwake.
“Umejuaje?” aliniuliza, ikabidi nimfafanulie kila kitu, kuanzia
nilivyoanza kuhisi mwanzo kuhusu uhusika wake baada ya kum-
sikia yule mzee wa Kisomali akiniita kwa jina la Snox na kila
kilichoendelea baada ya hapo.
“Haiwezekani,” na yeye alisema na kuinuka tena, akazunguka-
zunguka kisha akarudi na kukaa.
“Tatizo ni kubwa kuliko tunavyofikiri,” alisema. Nadhani na
yeye alipatwa na hofu kubwa ndani ya moyo wake kwa sababu
kama nilivyowahi kueleza, Bosi Mute hakuwa mtu wa mchezo hata
kidogo.
“Mutesigwa si yupo gerezani Mafia, tena kwenye gereza maalum
la siri lenye ulinzi mkali?”
“Ndiyo lakini nimeambiwa kwamba yupo gerezani, yupo uraiani

361 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

na yupo kila mahali. Lakini pia nimeelekezwa sehemu ninapoweza


kumpata Abdulwaheed, nimeambiwa maficho yake huwa ni Kibiti
na Mafia.”
“Abdulwaheed, Mafia, Mutesigwa, Mafia! Naanza kupata picha
sasa. Hii kazi inataka nguvu kubwa kuliko kawaida, nadhani ni
muda muafaka sasa wa mimi kuvaa gwanda,” alisema huku akirudi
kule kwenye kiti chake, akavua koti la suti alilokuwa amelivaa
kisha akaja mbiombio huku akikunja mikono ya shati lake nadhifu.
“Nifuate!” alisema.
Tulitoka huku baba yake Saima akipiga hatua ndefundefu, na
mimi nikawa namfuata kwa nyuma nikiendelea kutafakari mambo
mengi ndani ya kichwa changu. Safari yetu iliishia kwenye ofisi
ya mkurugenzi wetu ambaye kwa muda wote alikuwa amejifungia
ofisini kwake.
Ilibidi baba yake Saima agonge mlango na muda mfupi baadae
ukafunguliwa, akashtuka kutuona mimi na baba yake Saima.
“Kuna nini,” alisema huku akirudi kwenye kiti chake, akionesha
kupatwa na mshtuko.
“Mambo yanazidi kuwa magumu,” alisema baba yake Saima,
akalegeza tai aliyokuwa ameivaa na kufungua kifungo cha juu
cha shati lake. Ilibidi aanze kumuelezea kuhusu kile nilichokuwa
nimemueleza huku mara kwa mara akinigeukia kunitazama ili
kuhakikisha kama alichokuwa anakisema kilikuwa sahihi, na mimi
nikawa natingisha kichwa kukubaliana naye.
“Mungu wangu, Mutesigwa kwa mara nyingine tena,” alisema
huku akisimama, nadhani kiti kilikuwa cha moto kwa wakati huo.

362 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Kuna mambo siyaelewi hapa, huyu bwana si yupo gerezani?”


“Hebu mueleze alichokueleza mtoa taarifa wako.”
“Yupo gerezani, yupo uraiani na yupo kila mahali,” nilisema,
mkurugenzi na baba yake Saima wakatazamana kisha wote
wakanitazama.
“Kila tatizo lazima lina njia ya kutokea. Kulibaini hili ni hatua
ya kwanza lakini kulishughulikia ni hatua nyingine ambayo ndiyo
tunayotakiwa kuelekeza nguvu zetu kwa sasa kuifanyia kazi,”
alisema baba yake Saima, mkurugenzi akarudi kwenye kiti chake
na kushusha pumzi ndefu.
Akaeleza kwamba lazima tuondoke haraka na kikosi maalum
kuelekea Kibiti na Mafia lakini katika safari hiyo, lazima Kamish-
na wa Magereza awepo na watu wake.
“Vipi pia kama kamishna huyu anajua kila kinachoendelea na
anashirikiana na wahalifu kucheza michezo ya hatari na Mutesig-
wa? Kama ambavyo yule kamishna mwingine anafanya?” nilise-
ma, wazo likaonekana kuwa la msingi sana.
“Unashaurije?”
“Nashauri na yeye achunguzwe nyendo zake kwa kina, kuanzia
mawasiliano yake na kila kitu chake kisha ushahidi uwekwe, tuta-
jua kama alikuwa anajua au laa,” nilisema, wazo ambalo lilikuba-
lika na viongozi wangu, mkurugenzi akanyanyua mkonga wa simu
muda huohuo, akazungumza na upande wa pili na hata sikuelewa
alikuwa anazungumza na nani.
“Kuhusu breach of information (kuvuja kwa taarifa), tumejiridhi-
sha kwamba tuko salama?”

363 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Berthany na mwanaume wake tayari wako kizuizini kwa hiyo


nadhani tatizo tutakuwa tumelimaliza lakini kwa tahadhari tunat-
akiwa kuendelea na utaratibu uleule wa kufanya mambo kimyaki-
mya.”
“Ni sawa lakini kwa jinsi oparesheni hii itakavyokuwa, sidhani
kama tutaweza kuifanya kuwa siri.”
“Kwa nini?”
“Kwa sababu tutahitaji timu kubwa na maafisa kutoka nje.”
“Hapana, mimi nashauri timu ileile iliyoenda na Kenny Selous
ndiyo hiyohiyo itumike kutekeleza oparesheni hii na sisi viongozi
tuongeze nguvu, mipango na kila kitu viwe sawa na ilivyokuwa
Selous,” alisema mkurugenzi, wakawa wanabishana kwa hoja na
baba yake Saima.
“Hizi misheni hazifanani, kule Selous walikuwa wanaenda
kuvamia kambi, lakini Kibiti na Mafia siyo kuvamia kambi, ni
‘manhunt’ ya Abdulwaheed na Mutesigwa,” alisema akimaani-
sha kwamba oparesheni hii ilikuwa ni ya kwenda kuwasaka watu
wawili na siyo kama ilivyokuwa mwanzo.
“Kwa jinsi unavyomfahamu Mutesigwa unafikiri atakuwa anaya-
fanya haya mwenyewe? Ni fundi sana wa kuunda makundi makub-
wa ya kiuhalifu na huwa anaweza kucheza mno na akili za wafuasi
wake kiasi kwamba huwa wapo tayari kupambana kufa na kupona
kumtetea,” alisema mkurugenzi huku akinitazama, nikainamisha
kichwa chini.
Niliinamisha kichwa chini kwa sababu ni kama mkurugenzi
alikuwa ananitazama mimi kama anayesema ‘au nadanganya?’

364 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kwa sababu mimi pia nimetokea kwenye mikono ya Mutesigwa na


kama isingekuwa miujiza iliyonitokea maishani mwangu, pengine
ningeshakuwa nimeuawa kwa kupigwa risasi au ningekuwa naozea
jela.
“Ni kweli anachokisema mkurugenzi.”
“Kwa hiyo tunafikia muafaka gani?”
“Timu iliyoenda Selous ndiyo hiyohiyo itumike kwenye oparesh-
eni hii na Kenny ndiyo aongoze kama ilivyokuwa awali, naamini
tutapata mafanikio makubwa na ya haraka, hatuna muda wa ku-
tosha,” alisisitia mkurugenzi, muafaka ukafikiwa na kilichofuatia
baada ya hapo ilikuwa ni utekelezaji.
Nilipewa saa chache za kuwakusanya vijana wangu na kuangalia
kama kuna mtu anaweza kuongezwa kuziba pengo la yule mwen-
zetu mmoja ambaye alikuwa amejeruhiwa vibaya kule Selous,
nikarudi ofisini kwangu na kuanza kuchekecha kichwa.
Mambo yalikuwa yanatokea kwa kasi kubwa mno kiasi amba-
cho ilitakiwa nitulize sana kichwa changu ili kuhakikisha hakuna
makosa ya kizembe yanayoweza kutokea.
Ilikuwa ni lazima kulizima shambulio baya lililokuwa limepang-
wa kutokea Ikulu ya Magogoni ndani ya muda mfupi ujao ambao
nao ulikuwa unazidi kuyoyoma, mkitatua changamoto hii mnash-
tukia nyingine inaibuka.
Baada ya kutuliza kichwa kwa kama dakika kumi hivi, nilianza
kukikusanya kikosi changu. Changamoto iliyokuwepo ni kwamba
wengine nilikuwa nimewapa majukumu mengine ya kunisaidia
kwenye kazi mbalimbali ambazo zote zilikuwa zinatuhitaji kwa

365 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

lengo lilelile la kuzuia shambulio lile la kigaidi.


Nilichokifanya ilikuwa ni kuchukua vijana wengine niliokuwa
nawaamini kisha nikawapa yale majukumu waliyokuwa nayo wale
vijana wangu wa kikosi kazi, kisha nikawapa taarifa kila mmoja
kukutana kwenye chumba cha mikutano haraka iwezekanavyo.
Wengine walikuwa mapumzikoni lakini kama ilivyo kanuni yetu
ya ‘always be prepared’ iliwalazimu kurudi haraka iwezekanavyo
na kama ilivyokuwa mwanzo, sikutaka kuwaeleza ni nini hasa
kinachoenda kufanyika zaidi ya kuanza kwa kuwapongeza kwa
kazi nzuri tuliyoifanya Selous.
“Tumefanya kazi kubwa na hakika tumeweza kulitetea taifa letu,
lakini bado tunatakiwa kwenda kufanya ‘drills’ nyingine Kibiti.,
Mkuranga na Mafia, bila shaka nyote mnajua jinsi tunavyopi-
tia kwenye wakati mgumu kutokana na matukio ya kila kukicha
yanayofanywa na hawa wahuni.
“Aaah chief, we tuchane tu ukweli, ni drill au misheni nyingine?”
alisema Danny, mmoja kati ya vijana wangu niliokuwa nawaamini
sana, jina lake halisi akiitwa Daniel Mjema.
Kauli yake ilifanya wenzake wacheke sana, ikabidi na mimi
nicheke kwa sababu siri kubwa ya kuwafanya vijana wangu wawe
wanajituma sana ni kwamba tulikuwa tunaishi ‘kishkaji’ sana.
“Kweli Chief, we tuambie tu, hakuna anayeweza kuvujisha
taarifa kati yetu na si tumesikia tayari ‘snichi’ ameshafahamika?”
alisema kijana wangu mwingine, Clement Mtawa, tulizoea kumuita
Kile Sniper kwa jina la utani, basi wote wakaendelea kucheka kwa
nguvu.

366 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Kwa kuwa wenyewe walikuwa wanataka kuambiwa ukweli,


ilibidi nifanye kama walivyokuwa wanataka, nikawaona nao wak-
ishtuka sana kusikia kwamba Mutesigwa alikuwa nyuma ya kila
kilichokuwa kinaendelea na wakafurahi kusikia kwamba hatimaye
nilikuwa nimeweza kujua mahali Abdulwaheed alikokimbilia.
“Si tunaruka na chopa tena kama kawaida,” alihoji Danny, wen-
zake wakacheka sana, mimi pia nikacheka. Kiukweli mshikamano
uliokuwepo kwenye timu yangu ilionesha wazi kwamba safari hii
tunakwenda pia kufanikisha oparesheni yetu kwa urahisi zaidi.
“Sina uhakika lakini nafikiri itakuwa hivyo, tuachane na hayo
nataka kila mmoja atulize akili yake nataka tuichore oparesheni
nzima ubaoni kwanza kabla ya kwenda eneo la tukio,” nilisema, ni-
kaanza kuwaelewesha kwa kina ni nini tunachokwenda kukifanya.
Tulijadiliana kwa kina kuhusu kinachokwenda kufanyika, kila
mmoja akawa ameelewa vizuri jambo zito lililokuwa mbele yetu na
kilichofuatia baada ya hapo, ilikuwa ni maandalizi ya mwishom-
wisho, wote tukatoka na kuelekea ‘dressing room’ na baada ya
hapo, tulielekea ‘armoury’, kule kwenye chumba maalum ndani ya
dressing room ambako ndiko silaha zote zilikokuwa zinahifadhiwa.
Tukiwa tunaendelea kujiandaa, baba yake Saima aliingia akiwa
na Chief Mwaipopo na maafisa wengine wa ngazi za juu wapatao
sita. Chief Mwaipopo alikuwa ni mkuu wa oparesheni na mafunzo
na kwa kipindi kirefu alikuwa nje kimasomo.
Kwa kuwa hatukuwa tumeonana kwa muda mrefu, ilibidi niso-
gee kwenda kumsalimia, aliponiona tu, akatabasamu na kuja kule
nilikokuwa natokea.

367 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Tulipeana mikono migumu, tukatingishana kikakamavu huku


kila mmoja akiwa na tabasamu usoni. Nilikuwa namheshimu sana
kwa sababu kipindi kile napelekwa mafunzoni na baba yake Saima,
Mwaipopo alikuwa miongoni mwa walimu wangu wa mwanzo
kabisa ambao nikiri kwamba alinifunza mambo mengi sana.
“Tangu utoke Israel hatujawahi kukutana!”
“Ni kweli kabisa, na wewe tangu utoke Vietnam hatujawahi
kukutana,” nilisema na kumfanya acheke sana. Ilikuwa ni kweli
kwamba kipindi ambacho mimi nilikuwa narejea kutoka Israel
mafunzoni, yeye alikuwa ameshaondoka nchini kwenda Vietnam
kwenye kozi maalum.
“Kwa hiyo leo tutakuwa na mbinu za Kiisrael na Kivietnam
kwenye uwanja wa vita,” alisema baba yake Saima ambaye kumbe
alikuwa anatusikiliza mazungumzo yetu, wote tukacheka sana.
Tuliendelea na stori za hapa na pale, kila mmoja akivaa gwanda,
akiwemo baba yake Saima na baada ya muda, sote tulikuwa tayari.
Kitendo cha baba yake Saima kuvaa gwanda na kubeba silaha,
lakini pia uwepo wa Mwaipopo, mwalimu wangu wa medani,
naye akiwa kwenye kombati na kubeba silaha, yalikuwa ni mambo
yaliyonipa nguvu kubwa na kuamsha morali kubwa mno ndani ya
moyo wangu.
Baada ya kila mmoja kuwa ameshamaliza kujiandaa, ilibidi tu-
rudi tena bwaloni na safari hii kwa kuwa tulikuwa na viongozi wa
juu kabisa, ilibidi na wao wapate nafasi ya kuzungumza na vijana
wangu.
Awali nilidhani kwamba kwa sababu baba yake Saima na Chief

368 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Mwaipopo tulikuwa tunakwenda nao, yeyote kati yao ndiyo an-


gekuwa kiongozi wa oparesheni lakini haikuwa hivyo, Chief
Mwaipopo aliwaambia watu wote kwamba mimi ndiyo kiongozi
wao, akiwemo na yeye, baba yake Saima naye akakazia kwamba
yupo tayari kupokea maelekezo kutoka kwangu.
Watu wote walipiga makofi kisha baada ya hapo, tukasogea
pembeni na kuteta mawili matatu na viongozi wangu, wakanieleza
kwamba tunaondoka mpaka Kunduchi ambako helikopta za kijeshi
zilikuwa zinatusubiri na tukitoka tukakwenda moja kwa moja
mpaka Kibiti ambapo tutaweka kambi ya muda na kundi lingine
litaondoka kuelekea Mafia.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, baada ya makubaliano hayo,
nilirudi na kuwatangazia vijana wangu kuhusu mpango wa safari
jinsi ulivyokuwa na baada ya hapo, tulitoka tukiwa kwenye mstari
mmoja na kwenda mpaka kwenye maegesho ya magari ambako
tayari ‘Coaster’ mbili zilikuwa zinatusubiri.
Staili ambayo tulitoka nayo, ilikuwa ni ya kipekee na ya kuwa-
fanya watu waamini kwamba tulikuwa tunakwenda kwenye ‘drill’
au mazoezi ya kimedani wakati uhalisia ni kwamba tulikuwa
tunakwenda kwenye kazi.
Lengo la kufanya hivyo, lilikuwa ni lilelile la kuzuia taarifa zisije
zikavuja kwa sababu licha ya kwamba Berthany alikuwa kizuizini,
bado hatukuwa na uhakika kama ni yeye pekee ndiye aliyekuwa
tatizo.
Magari yalitoka taratibu mpaka nje ya geti na kuingia barabara
kuu, safari ikachanganya. Kwa nje usingeweza kujua ni nini kili-

369 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

chokuwa ndani ya Coaster hizo mbili, ungeweza kudhani zime-


kodiwa kupeleka watu sehemu fulani kwenye shughuli ya kijamii
kama harusi au msibakwa sababu zilikuwa na usajili wa kawaida
lakini pia zilikuwa na vioo ‘tinted’ ambavyo vilikuwa vikizuia mtu
wa nje kuona chochote kilichokuwa ndani.
Wakati safari ikiendelea, nilikuwa natafakari mambo mengi ndani
ya kichwa changu. Kimsingi kazi nyingi zilikuwa hazijakamilika
na zilikuwa zinanihitaji sana kuzikamilisha kwa lengo lilelile moja
la kuzuia kilichokuwa mbele yetu lakini kubwa na muhimu zaidi
ilikuwa ni hicho tulichokuwa tunakwenda kukifanya.
Nilitafakari kwa kina kuhusu kile kilichokuwa kimemtokea yule
mzee wa Kisomali, nilitafakari kuhusu Berthany na yule mwa-
naume wake na jinsi Mute alivyofanikiwa kutuzidi akili na kumpe-
nyeza yule mwanaume wa Berthany mpaka ndani kabisa ya himaya
yetu.
“Mute anatakiwa kukomeshwa kisawasawa vinginevyo ataende-
lea kutusumbua vichwa kila kukicha,” niliwaza huku nikiendelea
kutafakari jinsi alivyofanikiwa kupata ushawishi na kushirikiana na
watu hatari kiasi kile.
Sikuwahi kudhani hata mara moja kama Bosi Mute anaweza kuja
kuhusika na mambo hatari kiasi kile, jambo ambalo nilikuwa najua
kwamba hawezi kuacha, ilikuwa ni kumiliki magenge ya majam-
bazi lakini kamwe sikuwahi kudhani kwamba anaweza kuingia
kwenye ugaidi.
Safari iliendelea, nikawa pia naendelea kumtafakari yule mfan-
yabiashara mkubwa wa mafuta na jinsi alivyokuwa akitumia fedha

370 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

zake kuwanunua maafisa wa ngazi za juu kabisa serikalini na ku-


watumia kwa maslahi yake binafsi, hakika mambo yalikuwa mengi
na muda haukuwa unatosha.
Nilikuja kuzinduka kutoka kwenye lindi zito la mawazo na
kushtukia tukiwa tunaingia Kunduchi kwenye geti kubwa la pale
chuo cha mafunzo. Magari yalielekea mpaka ndani kabisa kwenye
uwanja mkubwa wa michezo, palepale ambapo tuliondokea mara
ya mwisho wakati tukielekea Selous.
Helikopta mbili kubwa na za kisasa zilizokuwa na rangi za
kijeshi, zilikuwa zimepaki zikitusubiri. Hizi zilikuwa tofauti na zile
tulizozitumia awali. Tukateremka na moja kwa moja tukajipanga
kama ulivyo utaratibu, nikamtazama baba yake Saima, akanipa
ishara kwamba niwagawe vijana wangu katika makundi mawili
tayari kwa safari.
Nilifanya hivyo na haukupita muda mrefu tukawa tayari tume-
shaingia kwenye helikopta. Tofauti na mara ya mwisho ambayo
baba yake Saima alikuwa mmoja wa marubani, safari hii alikaa na
sisi, tukawa tunaendeshwa na marubani wawili wa jeshi.
Tulipaa na safari ya kuelekea Kibiti ikaanza, moyoni nikiwa na
ari kubwa kuliko kawaida, nikawa najisemea kwamba lazima Ab-
dulwaheed na wenzake wapatikane, tena wakiwa hai na lazima pia
Bosi Mute achukuliwe, akiwa hai au amekufa pamoja na mtandao
wake wote.
Tuliendelea kupasua mawingu, tukipita juu ya mapori makubwa
na hatimaye tuliwasili Kibiti. Mpango mkakati ulivyokuwa, ili-
kuwa inatakiwa tushuke kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari

371 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Kibiti na tungetumia baadhi ya majengo ya shule hiyo kama kambi


ya muda wakati oparesheni ikiendelea.
Baada ya muda, tayari tulikuwa tumeshafika Kibiti, helikopta
zikatua uwanjani, tukateremka kijeshi na bila kupoteza muda, kazi
ikaanza.
Uzuri ni kwamba mpaka tunafika kwenye shule hiyo, wanafunzi
wote walikuwa wameshatawanyika kwa sababu mawasiliano yali-
shafanyika na ilikuwa ni lazima wote waondoke ili tusije kuhatari-
sha maisha yao.
Jambo lingine zuri ni kwamba vikosi vingine vya majeshi ya
ulinzi na usalama, yalikuwa yameweka kambi katika ukanda wa
Kibiti, Mkuranga na Rufiji ili kukabiliana na matukio ya mauaji
yaliyokuwa yanaendelea, ambayo picha kubwa niliyokuja kuipata
ni kwamba mauaji hayo yalikuwa na uhusiano wa moja kwa moja
na kilichokuwa kinataka kwenda kutokea Magogoni.
Baada ya kutua Kibiti, hakukuwa na muda wa kupoteza, nikawa-
panga vijana wangu ‘mkao wa kula’ kisha mimi na Chief Mwaipo-
po tukatoka na kuelekea mpaka Kibiti Stendi, mahali nilipoelekez-
wa na yule mzee wa Kisomali.
Magwanda tuliyokuwa tumevaa, yaliwafanya watu wengi wawe
wanatushangaa kwa sababu hayakuwa yakifanana na magwanda ya
wanajeshi wa kawaida wala polisi, yalikuwa ni maalumkwa ajili ya
oparesheni zetu nzitonzito kwa hiyo hata mwonekano wake hau-
kuwa wa kawaida.
“Samahani, tunamuulizia Ustaadh Fundi,” tulimuuliza mzee
mmoja aliyekuwa na meza ya kuuza samaki, jirani na stendi ya

372 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Kibiti. Jinsi alivyotutazama na majibu aliyoyatoa, ilionesha wazi


kwamba alikuwa anamjua lakini akawa anaogopa kutoa ushirikia-
no.
“Najua una wasiwasi na sisi,” nilimwambia huku nikitoa kit-
ambulisho na kumuonesha, nikamhakikishia kwamba atakuwa
salama na hatukuwa na lengo lolote baya.
“Nifuateni,” alisema huku akionesha kuwa na hofu kubwa ndani
ya moyo wake, tukawa tunamfuata wa tahadhari kubwa kwa saba-
bu mambo yaliyokuwa yakiendelea katika ukanda huo, hayakuwa
ya kawaida hata kidogo.
Safari yetu ilienda kuishia kwenye kibanda cha wastani kilicho-
jengwa kwa mabati na mbao na kukifanya kionekana kama kara-
kana ndogo lakini iliyokuwa na mpangilio nadhifu kisawasawa,
tukamkuta mwanaume wa makamo, akiwa bize kushona viatu kwa
kutumia mashine ndogo, akisaidiwa na vijana kama wanne hivi,
wote walipotuona tukiingia, waliacha kila walichokuwa wanaki-
fanya.
Yule mwenyeji wetu alimfuata yule mwanaume wa makamo
ambaye kwa kumtazama ilionesha dhahiri kwamba ndiyo Ustaadh
Fundi kwa jinsi alivyokuwa amevalia, akamnong’oneza jambo
kisha wote wawili wakawa wanatutazama.
Tukamuona yule Ustaadh Fundi naye akimnong’oneza jambo
kisha harakaharaka yule mwenyeji wetu alisogea upande tulioku-
wepo, akanisogelea.
“Yupo tayari kuwasikiliza lakini amesema hapa siyo vitani kwa
hiyo wekeni silaha zenu chini,” alisema, nikatingisha kichwa kwa

373 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

adabu na kuvua ‘chuma’ iliyokuwa begani, nikamgeukia Chief


Mwaipopo na kumpa ishara afanye kama mimi, nikamuona akini-
tazama kwa jicho la mshangao lakini baadaye akakubali.
Nadhani alikubali kwa sababu sote tulikuwa tunajua kwamba
ukiachilia bunduki kubwa za kivita tulizokuwa tumezibeba shin-
goni, kila mmoja wetu alikuwa na bastola mbili kiunoni mwake
pamoja na visu maalum vya kijeshi kwa ajili ya kujihami.
Baada ya sisi kuweka silaha chini, yule Ustaadhi Fundi alitoa
ishara kwamba tuingie kule alikokuwepo na wakati huohuo, yule
mwenyeji wetu akawa anataka kuondoka kwenda kuendelea na
shughuli zake, nikamzuia kwanza.
Niliingiza mkono kwenye kombati langu na kutoa noti tano za
shilingi elfu kumi kumi na kumkabidhi na nilitaka Ustaadh Fundi
aone nikiwa namkabidhi kwa lengo la kujenga imani kwao.
“Umetusaidia sana! Hii ni kama shukrani yetu kwako,” nilisema
huku nikinyoosha mkono kumpa zile fedha, nikamuona akini-
tazama kwa macho ya hofu, akamgeukia Ustaadh Fundi ambaye
alimpa ishara kwamba apokee, kweli akapokea na kutoa shukrani
kwa ishara kisha harakaharaka akatoka.
Nilimgeukia Chief Mwaipopo na kumpa ishara kwamba yeye
anatakiwa kubaki palepale kwa lengo la kulinda bunduki zetu tu-
lizokuwa tumeziweka kwenye jamvi pale chini. Ungekuwa uzembe
wa hali ya juu kwa sisi kuingia kule ndani na kuacha silaha zetu
pale mlangoni.
Baada ya kuwa tumeshakubaliana, nilianza kupiga hatua za tara-
tibu nikiwa makini kisawasawa, nikiwatazama kwa zamu Ustaadh

374 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Fundi na wale vijana wake wanne ambao kama nilivyosema, wa-


likuwa wameacha kila walichokuwa wanakifanya baada ya kuona
tukiingia eneo lile.
Chumba chote kilikuwa katika mpangilio nadhifu kwelikweli
na kama nilivyosema, ilikuwa ni kaa karakana fulani au kiwanda
kidogo cha kutengeneza viatu. Nilishangaa kugundua kwamba ku-
likuwa na mashine ndogondogo za kisasa kwa ajili ya kutengene-
zea viatu vya kila aina na kulikuwa na mzigo wa ‘sendozi’ nyingi
zilizokuwa tayari zimetengenezwa.
“Ustaadh Fundi,” nilisema baada ya kuwa nimemfikia, hakujibu
kitu akawa ananitazama usoni kwa makini.
“Huu ni ujumbe wako!” nilisema huku nikiingiza mkono mfu-
koni na kutoa kile kikaratasi nilichokuwa nimepewa na yule mzee
wa Kisomali kule ‘kitengoni’ na kutaka kumpa. Ajabu ni kwamba
hakupokea yeye, badala yake msaidizi wake mmoja akasogea ha-
raka na kwa kushtukiza na kukipokea.
Kila kitu kilikuwa kinafanyika kwa mtindo wa kama kuviziana
hivi kwa sababu hata jinsi yule msaidizi wake alivyokuwa ameni-
sogelea, nisingekuwa na utulivu pengine jambo baya lingetokea
kwa sababu ungeweza kudhani anataka kunivamia.
Baada ya kukipokea kile kikaratasi, alikifungua na kumsogezea
Ustaadh Fundi, akakitazama harakaharaka kisha akashusha pumzi
ndefu na kunitazama tena usoni kisha akamtazama Chief Mwaipo-
po, akashusha tena pumzi ndefu na kuwageukia vijana wake,
akawapa ishara ambapo muda huohuo, waliendelea na majukumu
yao huku wakitutazama kwa macho ya chinichini.

375 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Ustaadh Fundi alisimama na kunipa mkono huku akiendelea


kunitazama usoni, na mimi nikanyoosha mkono na kumpa wa
kwangu, nikamuona akishtuka baada ya mikono yetu kugusana,
nadhani ni kutokana na jinsi mkono wangu ulivyokuwa mzito.
“Ndugu yangu yuko wapi?”
“Yuko salama! Yupo sehemu salama.”
“Nimekuwa nikihangaika kwa siku kadhaa sasa kutafuta ma-
wasiliano naye bila mafanikio, mkewe anasema alienda kukamat-
wa na polisi.”
“Ni kweli lakini yuko salama na yeye ndiye aliyetuelekeza kuja
kwako,” nilimwambia kwa sauti ya mamlaka, akanitazama tena
machoni.
“Unanihakikishiaje usalama wake?”
“Amini ninachokwambia, kwangu pia namchukulia kama ndugu
yangu na tumeshirikiana mambo mengi mpaka leo, nakuhakikishia
kwamba yupo salama na atakuwa salama kwa sababu amekubali
kushirikiana nasi.
“Abdulwaheed na wenzake ni mashetani, wametuingiza kwenye
matatizo makubwa sana,” alisema huku mikunjo ya ndita ikioneka-
na waziwazi kwenye uso wake.
“Nifuateni,” alisema na kuanza kutembea kuelekea upande wa
pili, tofauti na ule tulioingilia, nikampa ishara Chief Mwaipopo
ambaye harakaharaka alibeba bunduki zote mbili, ya kwake
akaivaa shingoni na kuishika ile ya kwanza.
Tulitokea upande wa pili ambako kulikuwa na nyumba ya maka-
zi, iliyoonesha kwamba ndiyo yeye na familia yake walipokuwa

376 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wanaishi.
“Karibuni,” alisema huku akituoneshea ishara kwenda kukaa
kwenye viti vilivyokuwa vimepangwa vizuri pembeni ya mti wa
mkorosho, akaingia ndani kwake na muda mfupi, kundi la wan-
awake na watoto kama nane hivi, wote wakiwa wamejistiri vizuri
walitoka na kutusalimu.
“Hii ni familia yangu, nimewaita wawasalimu kwa sababu
ukarimu ni jadi yetu, mtatumia nini, maji, juisi au maziwa?”
alisema Ustaadh Fundi ambaye nyumba yake ilikuwa inatosha
kuonesha kwamba alikuwa anaishi maisha fulani ya kujiweza sana
kiuchumi kwa sababu hata wake zake wawili aliotutambulisha,
walikuwa na afya njema, achilia mbali watoto wake.
“Tunashukuru, tumekula tulikotoka!”
“Hapana, lazima mtie baraka kwenye nyumba yangu, mimi
mgeni yeyote akija hapa lazima ale au kunywa chochote, huo ndiyo
utaratibu wangu,” alisema na kuwageukia wake zake waliokuwa
wamesharudi ndani na kusimama mlangoni kwa ndani.
Akasogea na kukaa kwenye moja kati ya vile viti vilivyokuwa
pale chini ya mkorosho, akatutazama tena mmoja baada ya mwing-
ine.
“Nitawasaidia kwa sababu ya chuki yangu kwa Abdulwaheed
na kundi lake, walikuja kama watu wazuri lakini mwisho wame-
tuingiza sisi wenyeji kwenye matatizo makubwa sana. Wanafanya
mambo tofauti kabisa na maelekezo ya dini yetu ya haki,” alisema
kwa upole, akionesha kuwa na ustaarabu wa hali ya juu unaoletwa
na mtu mwenye hofu ya Mungu.

377 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Naitwa Jamal Kandauma, wengi wananiita Ustaadh Fundi kwa


sababu mimi ni fundi, kama mnavyoona nina karakana yangu
ndogo hapa natengeneza viatu na kwenda kuuza sehemu mbalim-
bali, ndani na nje ya nchi,” alisema, ikabidi mimi nijitambulishe na
kumtambulisha pia Chief Mwaipopo.
Akawa anaendelea kutueleza kwamba kitendo cha wenyeji,
akiwemo yeye kuwapokea Abdulwaheed na kundi lake, kime-
fanya kila mtu ahisi kwamba nao wanashirikiana nao, na akaeleza
kwamba yeye binafsi hakubaliani kabisa na matendo yaliyokuwa
yanafanywa na Abdulwaheed na wenzake na kwamba kama ange-
jua mwanzo lengo lao, kamwe asingekubali kushirikiana nao.
“Ni wateja wangu wazuri sana wa Makubazi la Kisomali ambayo
mimi pia natengeneza hapa kwenye karakarana yangu, wamekuwa
wakinunua mzigo mkubwa mara kwa mara lakini tangu nilipojua
uhalisia wao, nimekuwa nao makini sana, ni watu wabaya ambao
hawastahili kuwepo kwenye jamii yetu.
“Wamewaponza watu wengi sana, akiwemo ndugu yangu huyo
ambaye amewaelekeza kuja hapa,” aliendelea kueleza mambo
mengi, tukawa makini kumsikiliza huku kifaa changu maalum
kikirekodi mazungumzo yote.
Licha ya maelezo yake yote hayo, shauku yetu kubwa ilikuwa ni
kutaka kusikia akitueleza ni wapi tunapoweza kumpata Abdulwa-
heed.
“Alipigwa risasi akiwa kwenye uhaini wake ambao wanaufanya
na kujificha kwenye kivuli cha dini, hakuna dini inayoruhusu haya,
wanatuchafulia dini yetu, wanafanya wote tuonekane kama wao,”

378 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)
alisema kisha ukimya ukapita.
“Yuko wapi kwa sasa?” nilimuuliza, akawa ni kama anatafakari
kitu kisha akawa ni kama amezinduka kutoka kwenye lindi zito la
mawazo.
“Nisubirini!” alisema huku akielekea ndani ya nyumba yake kwa
hatua ndefundefu, mimi na Chief Mwaipopo tukatazamana.
Alipoingia ndani, muda mfupi wakeze wawili walitoka wakiwa
na sahani na chupa ya chai, wakasogeza meza ndogo pale katikati
yetu na kuweka vikombe viwili, wakatumiminia maziwa fresh na
vitafunwa vya kiasili, ukiwa ni mchanganyiko wa mihogo, mag-
imbi na karanga za kuchemsha zilizomenywa vizuri.
Baada ya kumaliza kuandaa, harakaharaka waliondoka na kurudi
ndani, tukawa tunatazamana na Chief Mwaipopo, ‘itifaki’ zetu
zilikuwa zinatuzuia kula au kunywa chochote tunapokuwa kwenye
misheni kwa sababu za kiusalama.
Chief Mwaipopo alinionesha ishara kwamba tuendelee tu ili
kujenga imani kwa yule mwenyeji wetu ambaye alishaonesha
kwamba yupo tayari kutoa ushirikiano.
Basi tulinawishana mikono pale, tukaanza kushughulikia mchan-
ganyiko ule wa vyakula vya kiasili, moyoni nikafurahia sana
kwa sababu sikuwa nakumbuka mara ya mwisho kula maboga na
mihogo ya kuchemsha ilikuwa ni lini. Mfumo wa maisha ulikuwa
umebadilika mno.
Ndani ya muda mfupi tu, tayari tulikuwa tumeshafuta kila kitu,
Ustaadh Fundi alipotoka nje, akabaki kushangaa baada ya kukuta
tunanawishana mikono kuashiria kwamba tulishamaliza kupata

379 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

‘staftahi’.
Kumbe alikuwa ameenda ndani kubadilisha nguo, akatoka akiwa
amevaa tofauti kabisa na jinsi tulivyomkuta awali, miguuni akawa
amevaa mabuti kama ya kijeshi, kofia pana iliyoziba sehemu
kubwa ya kichwa chake na koti refu! Kwa kumtazama tu, ilionesha
kwamba kweli amedhamiria jambo.
Tulimshukuru kwa ‘staftahi’ kisha tukainuka, yeye akatangulia
mbele. Tulitokea kwenye geti kubwa lililokuwa upande wa mbele
wa nyumba ile, tukapata nafasi ya kuitazama vizuri.
Kama nilivyosema, kwa mazingira yale ya kule, ilikuwa ni
nyumba unayoweza kuiita bora, ikiwa imejengwa kwenye eneo
kubwa lenye mandhari nzuri.
Tulitoka mpaka nje, yule mzee akatoa simu na kupiga ambapo
muda mfupi baadaye, Bajaj ilikuja na kusimama kando yetu.
Akatuonesha ishara kwamba tuingie, kisha na yeye akaingia wa
mwisho.
“Ni mbali kidogo na kwa jinsi mlivyovaa, haitaleta picha nzuri
kuonekana mkiwa mmeongozana na mimi mitaani,” alisema Usta-
adh Fundi, tukakubaliana na wazo lake ingawa bado ilibidi tuwe
makini sana na kila kilichokuwa kinaendelea.

380 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

15
T
ULITOKA mpaka nje kabisa ya Kibiti, tukaiacha
barabara ya lami na kuingia kwenye barabara ya
vumbi, upande wa kushoto wa Barabara ya Kusini.
Baada ya umbali mrefu, alimpa ishara dereva kwam-
ba asimame na atusubiri hapohapo mpaka tutaka-
porudi.
Akikuuliza mtu yeyote mwambie upo na mimi lakini usiseme
kama nipo na wageni,” alisema Ustaadh Fundi, yule kijana akai-
tikia kwa adabu na safari ikaendelea, safari hii tukitembea kwa
miguu.
Tulipita kwenye mashamba mengi ya korosho na minazi yasiyo-

381 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

hudumiwa na baada ya muda, tulitokezea kwenye kijiji kilichoku-


wa na nyumba chache, tena nyingi zikiwa ni za makuti huku zile
zilizokuwa zimeezekwa kwa mabati, zikionekana kuchakaa sana.
“Yupo kwenye ile nyumba iliyopakwa chokaa, amekuwa akitibi-
wa huku kwa siri tangu alipopigwa risasi, hali yake ni mbaya, hata
kutembea hawezi lakini analindwa na vijana wake waaminifu.
Haitakuwa rahisi kumfikia,” alisema Ustaadh Fundi tukiwa mita
chache kabla ya kuzifikia zile nyumba.
Kwa jinsi kijini chenyewe kilivyokuwa, nyumba zilikuwa zimet-
engana kwa umbali mkubwa kwa hiyo hata alipotuelekeza nyumba
yenyewe, tuliweza kuiona kwa urahisi, ikabidi tujadiliane kwanza
namna ya kuingia na kama kulikuwa na ulazima wa kuongeza
nguvu.
“Sisi ni jeshi kubwa, hakuna haja ya kuongeza nguvu, lazima tu-
oneshe ukubwa wetu kwa vitendo, tunaingia na kumchomoa akiwa
hai na yeyote atakayeleta ukaidi, lazima ashikishwe adabu. Njia
nyepesi ni ‘ambush’,” alisema Chief Mwaipopo, nikakubaliana na
alichokuwa amekisema.
Ilibidi kwanza tuhakikishe Ustaadh Fundi anabaki salama, tu-
kamuelekeza kukaa nyuma ya mti wa mkorosho na kumweleza
kwmaba akisikia risasi, njia nyepesi ya kujilinda ni kulala chini
kwa usalama wake na kutulia mpaka tutakapoenda kumchukua,
akatingisha kichwa kuonesha kukubaliana na tulichokuwa tunak-
isema.
“Sitaki mtu yeyote ajue kwamba mimi ndiye niliyemchomesha
huyu mwendawazimu, vijana wake wanaweza kuja kunifuata usiku

382 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kulipa kisasi.
“Usiwe na wasiwasi,” nilimwambia na bila kupoteza muda, tu-
kagawana njia za kupita kuelekea kwenye ile nyumba.
Chief Mwaipopo yeye alichagua kusogea moja kwa moja kuele-
kea mbele, mimi nikatakiwa kuzunguka na kutokea upande wa pili
ili asipate mtu yeyote nafasi ya kutoroka. Nilianza kusonga mbele
kuelekea upande tofauti, nikawa najibanza kwenye miti na kuta za
nyumba chakavu kuzuia nisije kuonekana na mtu yeyote.
Niliendelea kusonga mbele na ndani ya dakika zisizozidi tatu ni-
kawa tayari upande wa pili, nikiitazama nyumba ile kutoka kwenye
maficho niliyoyachagua, mita kama ishirini hivi kutoka kwenye ile
nyumba.
Nilimpa ishara Chief Mwaipopo kwa kutumia vifaa maalum vya
mawasiliano, muda huohuo naye akatoka pale alipokuwa ametega
akisubiri ishara kutoka kwangu.
Sijui nini kilitokea lakini ghafla nilisikia filimbi ikipulizwa, kama
zile zinazotumiwa jeshini, nikashtuka sana kwa sababu ilionesha
ni kama tayari wasaidizi wa Abdulwaheed walikuwa wameshtukia
uwepo wetu eneo hilo.
Baada ya filimbi, kilichofuatia ilikuwa ni milio ya risasi lakini
ajabu ni kwamba hazikuwa zinarushwa upande wangu, nikajua
Chief Mwaipopo na Ustaadh Fundi tayari wameingia matatizoni.
Kwa jinsi risasi zilivyokuwa zinarindima, kwanza ilionesha
waliokuwa wakifyatua risasi hizo walikuwa na mafunzo ya ku-
tumia silaha lakini kama hiyo haitoshi, ilionesha kwamba silaha
walizokuwa wanatumia, zilikuwa ni za kivita, mafunzo yangu

383 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

yakanifanya nihisi kwamba inawezekana ni AK47 lakini zilizokat-


wa mitutu kutokana na jinsi zilivyokuwa zinapiga kelele.
Kwa kutumia vifaa maalum vya mawasiliano, nilijaribu kumuuli-
za Chief Mwaipopo kama yupo salama, lakini akawa hajibu cho-
chote, sanasana milio ya risasi ikawa inazidi kuongezeka, nikaona
ni lazima nifanye jambo, siwezi kuendelea kukaa eneo lile wakati
sijui mwenzangu ana hali gani pamoja na yule mzee aliyejitolea
kutusaidia.
Nilianza ‘ku-crawl’ kwa kasi kubwa kusonga mbele, kwa walio-
wahi kupitia mafunzo ya kijeshi watakuwa wanaeleza nikisema
ku-crawl’ namaanisha nini, wengine huwa wanarahisisha na kuita
‘kukroo’.
Hii ni mbinu ya kutambaa kwa kutumia mikono na miguu kwa
kasi kubwa kumfuata au kumkimbia adui bila mwenyewe kujua
chochote.
Ndani ya muda mfupi tu, tayari nilikuwa nimeshaisogelea ile
nyumba kiasi cha kuweza kuona na kusikia kila kilichokuwa
kinaendelea.
Nikiwa natafakari nini cha kufanya, nilisikia Chief Mwaipopo
akinijibu kupitia vifaa vya mawasiliano kwamba alikuwa ame-
zidiwa na anahitaji msaada wangu, akaniambia kwamba alikuwa
akishambuliwa kwa kasi lakini alikuwa sehemu salama akiendelea
kujibu mashambulizi.
Inapotokea hali kama hiyo, kila mmoja alikuwa anajua nini cha
kufanya ili mwisho tusije kuishia kushonana risasi wenyewe kwa
wenyewe. Nilichokifanya, ilikuwa ni kuwachanganya watu walio-

384 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kuwa wakifyatua risasi, nikapiga risasi tatu hewani kwa kuzichek-


echa mfululizo, ukimya ukapita.
Nadhani walishtuka sana kusikia risasi zikitoka upande mwing-
ine, tena nyuma yao, wakawa wanahaha na nikiwa naendelea
kusikilizia kabla ya kuinuka, nilishtuka kuona mlango wa ule
upande niliokuwepo ukifunguliwa, wakatoka wanaume wawili
wakiwa na bunduki, wakawa wanaangaza huku na kule kama wa-
naotafuta kujua ni wapi milio ile imetokea.
Walipoona kupo kimya, walitoka wengine wawili wakiwa wame-
beba kitu kama machela, ikionesha kulikuwa na mtu juu yake.
Kwa kuwa yule Ustaadh Fundi alishatueleza kwamba Abdulwa-
heed hana uwezo wa kutembea baada ya kujeruhiwa kwa risasi,
akili zangu zilinituma moja kwa moja kuamini kwamba ni yeye
ndiye aliyekuwa amebebwa kwenye machela na sasa vijana wake
walikuwa wanataka kumtorosha, nikamueleza Mwaipopo nili-
chokuwa nakiona na nilichopanga kukifanya.
“Tunawahitaji wakiwa hai,” alisema Mwaipopo na muda huohuo
nikaanza ‘kukiwasha’. Hatua ya kwanza ilikuwa ni kuwachang-
anya kwa kufyatua risasi zilizopiga ukuta pale walipokuwepo.
Kwa jinsi nilivyokuwa nafyatua risasi mfululizo, nilifanikiwa
kuwachanganya, wakambwaga Abdulwaheed kwenye ile machela
yake pale chini kisha kila mmoja akawa anatafuta sehemu ya kujik-
inga asipigwe risasi.
Sikufanya makosa, nikamtwanga wa kwanza risasi ya begani,
bunduki aliyoishika ikadondoka, na yeye akadondokea upande wa
pili.

385 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Kufumba na kufumbua nilimlenga wa pili kwenye paja, akadon-


doka chini kama mzigo ingawa bado aliendelea kufyatua risasi,
yule wa tatu akafanikiwa kuzunguka upande wa pili wa nyumba na
kufanya nisiweze kumpata kwenye shabaha, nikasikia risasi zikilia
kulekule alikokimbilia zikifuatiwa na yowe, nikajua tayari Chief
Mwaipopo ameshamaliza kazi.
Niliendelea kupambana na yule aliyeanguka chini ambaye kama
nilivyoeleza bado alikuwa akiendelea kufyatua risasi hovyo. Nili-
piga risasi nyingi kuzunguka eneo alilokuwepo, akachanganyikiwa
kabisa na mwenyewe akaitupa bunduki yake na kuinua mikono
juu.
Kufumba na kufumbua nilichomoza kutoka pale nilipokuwa
nimejificha na kwenda kuwadhibiti wote watatu, Abdulwaheed
ambaye alikuwa akijaribu kutaka kuinuka kutoka pale kwenye ma-
chela bila mafanikio pamoja na wale vijana wake wawili niliokuwa
nimewashona risasi, mmoja begani na mmoja kwenye bega.
Nilipowakaribia, kitu cha kwanza ilikuwa ni kuhakikisha hakuna
anayeweza kuendelea kufyatua risasi, nikaipiga teke bunduki ya
yule niliyempiga risasi kwenye paja ili asije akanigeukia, nikam-
sogelea huku nikimnyooshea ‘bomba’.
“Lala kifudifudi,” nilisema kwa amri, akatii nilichomwambia,
harakaharaka nikamfunga pingu kwenye mikono yake kwa nyuma,
damu nyingi zikimtoka pale kwenye paja. Muda huohuo nikam-
fuata yule wa pili niliyemshona begani ambaye alikuwa anatapata
kama anayetaka kukata roho, damu nyingi zikimtoka pale kwenye
jeraha la risasi.

386 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Nilimlaza kifudifudi na kumfunga pingu mikono kwa nyuma na


sasa nikawa na uhakika kwmaba hawawezi kuleta madhara, nikam-
sogelea Abdulwaheed ambaye nilipomtazama tu, niliweza kumtam-
bua haraka.
Ni huyu ndiye aliyekuwa akiongoza mashambulizi kule kwenye
kambi yao ya Selous tulipowavamia, akawa ananitazama kwa hofu,
akionesha kuchoka sana kutokana na majeraha ya risasi aliyoy-
apata kule porini.
“Ulidhani unaweza kutuzidi ujanja? Tulia hivyohivyo,” nilisema
huku nikimsogelea kwa tahadhari, nikiwa nimemnyooshea bun-
duki.
Nilichomoa pingu kutoka kwenye magwanda yangu, ile nainama
nataka kumfunga, nilishtukia milio mfululizo ya risasi ikitokea
ndani ya ile nyumba kunilenga. Kama isingekuwa ‘usharp’ wangu
wa kuwahi kujirusha chini na kutambaa kama nyoka nikitafuta seh-
emu ya kujibanza, huenda tungekuwa tunazungumza mengine.
Zilipigwa risasi kama sita mfululizo kutokea ndani, nikawa
nashindwa kujibu mapigo kwa sababu aliyekuwa anafyatua sikuwa
namuona.
Nilichokifanya, ilikuwa ni kutulia kwa sekunde kadhaa, nad-
hani ukimya wangu ukamfanya aliyefyatua risasi aamini kwamba
amenimaliza. Kufumba na kufumbua wakatoka wanaume wawili
waliokuwa wameziba nyuso zao kwa vitambaa, wote wakiwa na
bunduki, wakawa wanaangaza huku na kule kuangalia nimean-
gukia wapi.
Lilikuwa kosa kubwa sana kwao, nilifyatuka kama mshale pale

387 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

nilipokuwa nimejibanza, nikamrukia mmoja wao mwilini na


kumkaba shingoni kwa nguvu kisha nikamuweka kwa mbele ili
awe kama ngao kwa yule mwenzake.
“Weka silaha chini, piga magoti kisha nyanyua mikono juu
vinginevyo nakutwanga risasi,” nilisema kwa sauti ya amri.
Kumbe ile milio ya risasi mfululizo ilimfanya Mwaipopo na yeye
aamini kwamba nimepigwa, nikiwa namtazama yule mmoja aki-
tekeleza amri huku nikiendelea kumkaba shingo kwa nguvu yule
niliyekuwa nimemdhibiti, Chief Mwaipopo naye alitokeza kutokea
upande wa pili wa ile nyumba, akiwa amemkaba yule mtuhumiwa
ambaye alifanikiwa kunikimbia wakati nilipowashambulia kwa
kushtukiza.
Naye alikuwa amemkaba kwa staili ileile kama nilivyofanya
mimi na kumgeuza kuwa ngao yake huku akiwa amemfunga pingu
mikononi kwa nyuma.
“Piga magotiii,” alipaza sauti Mwaipopo kukazia amri niliyoitoa,
yule mwanaume akawa hana ujanja zaidi ya kuweka silaha chini na
kufanya alichoamrishwa.
Kufumba na kufumbua, Chief Mwaipopo alimsukuma yule ali-
yekuwa amemkata na kumkata mtama, akadondoka kama mzigo na
kumuwahi yule aliyekuwa amepiga magoti, akamkandamizia ard-
hini na kumfunga pingu huku akimpekua kama alikuwa na silaha
nyingine.
Muda huohuo na mimi nilimtegua miguu yule niliyekuwa
nimemkaba kwa namna ya kumlazimisha kupiga magoti, akadon-
doka mzimamzima, nikamuwahi na kumkandamiza mgongoni kwa

388 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

goti kisha nikamfunga pingu na kumpekua mwilini. Alikuwa na


bastola pamoja na kisu kiunoni, nikavichukua na kumuacha kwani
hakuwa tena na ujanja.
“Are you okay?” aliniuliza Chief Mwaipopo kwa Kiingereza
huku akihema akitaka kujua kama nilikuwa salama.
“Positive!” nilimjibu kwa lugha za kijeshi, nikimaanisha niko
sawa, wote tukawa tunahema kwa nguvu kwelikweli, bunduki
zikiwa mikononi, tayari kwa chochote.
“Nilimsogelea tena Abdulwaheed ambaye hakuwa na cha kufan-
ya, akiwa amedhoofika sana kutokana na majeraha yake.
Safari hii sikutaka kupoteza muda, nilimnyanyua kutoka pale
kwenye machela na kumfunga pingu kwenye mikono yake kwa
nyuma. Kwa jinsi alivyopiga yowe wakati nikimnyanyua kwa
nguvu pale chini, ilionesha kwamba alikuwa kwenye maumivu
makali kisawasawa.
Wakati nikimfunga pingu, Mwaipopo yeye alikuwa akiwakusan-
ya mateka wote ambao jumla yao walikuwa watano, ukichanganya
na Abdulwaheed, jumla walikuwa sita.
Tukiwa tunaendelea kuwapanga, tulishtukia purukushani kubwa
ikiibuka kutokea ndani, tukaziweka silaha zetu ‘standby’ kukabili-
ana na chochote ambacho kingetokea.
Kufumba na kufumbua tukashtukia kumuona Ustaadh Fundi
akimtoa mwanaume mwingine mwenye mwili mkubwa kutokea
ndani, akiwa amemkaba roba na kumgusisha bastola kichwani.
“Kaa chini,” alifoka Ustaadh Fundi akimuamrisha yule mwanau-
me, tukabaki tumepigwa na butwaa. Kwanza hakuna yeyote kati

389 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

yetu aliyefikiria kwamba Ustaadh Fundi anaweza kuwa na bas-


tola na anajua kuitumia lakini kubwa zaidi, tulishangaa kwa jinsi
alivyoweza kulidhibiti jitu la miraba minne kama lile, tena kutokea
ndani.
Kweli alifanikiwa kumkalisha mwanaume yule chini, akamlaza
kifudifudi kisha akatupa ishara kwamba tuendelee naye, Chief
Mwaipopo akasogea na kumsaidia kumfunga pingu yule mwa-
naume, ambaye naye ni kama alikuwa amepigwa na butwaa, akiwa
haamini kilichotokea.
Ustaadh Fundi alianza kuwakagua wale mateka wetu, mmoja
baada ya mwingine, akiwa ni kama anamtafuta mtu, macho yake
yakatua kwa Abdulwaheed ambaye tulikuwa tumemlaza kifudifudi
kwenye mstari mmoja na wale wenzake.
Kufumba na kufumbua alimrukia na kumgeuza pale chini kisha
akamuinua na kumkalisha, bastola ikiwa mkononi mwake.
“Umetusababishia matatizo makubwa sana mwanaharamu
wewe,” alisema kwa hasira kisha akamzaba kofi kwa nguvu, akai-
weka bastola yake kiunoni na kurudia kumzabamakofi mfululizo,
safari hii akitumia mikono miwili.
Mpaka namrukia kumtoa, alikuwa ameshamzaba makofi mazito
kama matano hivi, ikabidi nimuinue kwa nguvu na kumsogeza
pembeni.
“Niache nimshikishe adabu, ametusababishia matatizo makubwa
sana mwendawazimu huyu, inatakiwa auawe,” alisema Ustaadh
Fundi akiendelea kutweta kwa hasira.
“Nakuomba utulie tafadhali, bado kazi haijaisha!” nilisema,

390 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

tukashtukia kelele za watu wengi wakipaza sauti kutaka nimuachie


Ustaadh Fundi amshikishe adabu Abdulwaheed. Kumbe tayari
wanakijiji walikuwa wamekusanyika eneo la tukio, kila mmoja
akionesha kuwa na hasira kali na Abdulwaheed na wenzake.
“Auaweeee! Auawee!” wanakijiji ambao walikuwa wanazidi
kuongezeka walikuwa wakipiga kelele, nikaona kama tusipokuwa
imara, kweli Abdulwaheed anaweza kuuawa na kusababisha tupo-
teze ushahidi muhimu sana.
Niliinyanyua bunduki yangu na kuielekeza juu, nikapiga risasi
moja juu na kufanya watu wote wapatwe na hofu ya ajabu, aki-
wemo Ustaadh Fundi mwenyewe.
“Hakuna sheria inayoruhusu mtuhumiwa kuuawa hasa kama
tayari ameshakamatwa, ukiachana na sheria, huyu akiuawa hapa
hatutaweza kuwajua anaoshirikiana nao, naomba mtulie tufanye
kazi yetu,” nilisema kwa sauti ya ukali, nikamuona Ustaadh Fundi
akishusha pumzi ndefu na kutulia, wananchi nao ikabidi watulie,
wakawa wanaangalia kinachoendelea katika eneo lile ambalo lili-
kuwa limetapakaa damu.
Nilimgeukia Chief Mwaipopo, akatingisha kichwa kuonesha
kukubaliana na nilichokuwa nimekifanya, akanisogelea huku akiwa
bado anahema kwa nguvu, kama ilivyokuwa kwangu.
“Tunafanyaje?”
“Tunatakiwa kuondoka na hawa wendawazimu haraka iweze-
kanavyo kabla wananchi hawajatuzidi nguvu,” nilimwambia,
akatingisha kichwa kisha akawa ni kama anatafakari.
“Tunaondokaje?”

391 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Piga simu tuwajulishe wenzetu labda wanaweza kuwa na ma-


jibu!”
“Wewe ndiyo kiongozi wa hii misheni, wewe ndiye unayetakiwa
kupiga simu na kutoa taarifa ya kilichotokea,” alisema, nikashusha
pumzi ndefu na kuishusha bunduki chini, nikabonyeza kifaa cha
mawasiliano nilichokuwa nimekivaa, nikawa hewani.
Kwa jinsi mfumo wa vifaa vyetu vya mawasiliano vilivyokuwa
vikifanya kazi, ni kwamba watu wote waliokuwa wanahusika kwe-
nye oparesheni ile, wakiwemo tuliowaacha jijini Dar es Salaam,
walikuwa na uwezo wa kusikia kila kinachozungumzwa.
Nilieleza hali tuliyokutana nayo, nikaeleza kwamba hatimaye tu-
likuwa tumefanikiwa kumpata Abdulwaheed na vijana wake walio-
kuwa wakimlinda kule mafichoni, taarifa ambazo zilipokelewa
kwa furaha kubwa na viongozi, akiwemo baba yake Saima ambaye
yeye tulikuwa naye kule ingawa wenyewe walibaki kwenye ile
kambi ya muda.
Mkurugenzi naye akafurahi sana kusikia taarifa hizo, nikawasikia
wakizungumza wenyewe kwa wenyewe, wakiulizana kama he-
likopta zilizotupeleka zilikuwa zimeshaondoka. Majibu yakawa ni
kwamba zimeshaondoka kurudi Dar es Salaam.
Mjadala ukawa ni kwamba tunaondokaje eneo lile? Muafaka
uliofikiwa, ni kwamba kulikuwa na magari mengi ya polisi walio-
kuwa wakiendelea na oparesheni maalum katika ukanda wote wa
Kibiti, Mkuranga na Rufiji. Amri ikatolewa kwamba wao ndiyo
watusaidie kuondoka na watuhumiwa wetu kutoka eneo hilo.
Mkurugenzi akawasiliana na viongozi wa jeshi la polisi na

392 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

haukupita muda mrefu, tayari magari matatu ya polisi yaliyokuwa


jirani na mahali tulipokuwepo, yalianza safari ya kutufuata haraka
iwezekanavyo.
Nilieleza pia kuhusu tishio lililokuwepo la wananchi kutaka
kujichukulia sheria mkononi, tukatakiwa kuendelea kuwa makini
wakati tukisubiri polisi wafike kutusaidia kuondoka eneo hilo.
Kwa bahati nzuri, ndani ya dakika kumi tu, tayari magari yalian-
za kusikika yakija kwa kasi kwenye kile kijiji, mawasiliano yaka-
wa yanaendelea kufanyika na hatimaye, askari kama kumi na mbili
wenye silaha, waliwasili wakiwa ndani ya magari matatu ambyo
kwa jinsi yalivyoingia kwenye kijiji kile, ungeweza kusema kuna
mashindano ya mbio za magari.
Kabla hata magari hayajasimama, tayari askari wengi wenye
silaha walikuwa wamesharuka, wakaja mpaka pale tulipokuwa
tukiwasubiri, tukasalimiana kijeshi na kwa kuwa walishaelekezwa
kwamba wanatakiwa kuripoti kwangu, wakawa wanasubiri maele-
kezo.
Nilimuona kiongozi wao akipigwa na butwaa kuona kumbe
tuliokuwa tumefanya kazi ile tulikuwa wawili tu. Nikawaelekeza
nini cha kufanya na muda huohuo wale askari walianza kusaidiana
kuwabeba watuhumiwa wote na kuwapakiza kwenye gari moja.
Kabla hatujaondoka, nilizungumza na wananchi ambao walikuwa
wametulia wakifuatilia kwa makini kila kilichokuwa kinaendelea,
nikawaambia ni makosa kuona kuna matukio ya uhalifu yanaende-
lea maeneo yao halafu wakashindwa kutoa taarifa, nikawapa
namba yetu ya dawati la taarifa na kuwaeleza kwamba kama kuna

393 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

chochote kitatokea, wapige simu haraka.


Baada ya hapo, mimi na Chief Mwaipopo tulipanda kwenye lile
gari lililokuwa limewabeba wale wahalifu, Mwaipopo yeye ali-
panda mbele lakini mimi nikataka nikae nyuma pamoja na baadhi
ya askari kwa ajili ya ulinzi wa watuhumiwa wetu.
Msafara ukaanza kuondoka kwa kasi kubwa huku askari wawili
wakibaki eneo la tukio kwa ajili ya kuendelea kuimarisha ulinzi
pamoja na kuchukua maelezo kutoka kwa wanakijiji.
Ustaadh Fundi yeye alipanda kwenye gari la mbele, nikasikia
wanakijiji wakipiga makofi wakati msafara wetu ukiondoka kwa
kasi eneo hilo.
“Saluti kwako kamanda,” alisema mmoja kati ya askari tulio-
kuwa tumepanda nao kwenye lile gari lililowabeba wale watuhu-
miwa, nikatingisha kichwa kukubali pongezi zake. Sikuwa na-
jua kwamba askaari hao walikuwa wakinifahamu, nikawasikia
wakinong’onezana huku wakilitaja jina langu la Snox, tabasamu
hafifu likachanua kwenye uso wangu.
Safari iliendelea, haukupita muda mrefu tukawa tumefika pale
tulipomuacha yule dereva Bajaj, gari la mbele likasimama na ku-
fuatiwa na yale mengine mawili, likiwemo lile la kwetu, nikamu-
ona Ustaadh Fundi akiteremka na kutaka kwenda kupanda kwenye
ile Bajaj.
Ilibidi nishuke haraka na kumfuata Ustaadh Fundi, nikamzuia ku-
panda kwenye ile Bajaj na kumtaka aongozane na sisi kwanza kwa
sababu za kiusalama. Alikubali na kumpa ishara yule dereva Bajaj
awe anatufuata kwa nyuma, nikamuona jinsi alivyokuwa na hofu.

394 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Tulirudi kwenye magari na safari ikaendelea. Japokuwa njia


ilikuwa mbovu, mwendo ambao magari yote matatu yalikuwa nao,
ulikuwa si mchezo. Dakika kadhaa baadaye tukawa tumeshafika
kwenye barabara ya lami, safari ikaendelea na hatimaye tuliwasili
kwenye ile shule ambapo tuliweka kambi yetu ya muda.
Harakaharaka kazi ya kuwateremsha watuhumiwa wote ikaanza,
wenzetu ambao tayari walikuwa wanatusubiri kwa shauku kubwa,
wakaifanya kazi ile kwa kushirikiana na wale askari tuliokuja nao.
“Kazi nzuri sana! Siamini kama huyu mwendawazimu amekama-
tika kirahisi namna hii,” alisema baba yake Saima na kunikumbatia
kwa nguvu, nikatabasamu na kumshukuru kwa pongezi, akamfuata
na Chief Mwaipopo, wakakumbatiana kwa nguvu wakipongezana.
Kwa kuwa kazi ya wale askari ilikuwa imekwisha, nilimfuata
kiongozi wao na kumshukuru kisha nikamtaka aondoke na vijana
wake wakaendelee na kazi zao na endapo tukihitaji msaada wao
basi tutawasiliana.
“Nitakuwa mnafiki kama sitakupongeza mkuu, mmefanya kazi
kubwa ambayo sisi ingetuchukuamuda mrefu sana kuikamilisha,”
alisema yule kiongozi wa polisi, nikapokea pongezi zake na hau-
kupita muda mrefu magari yote matatu yakaondoka eneo hilo kwa
kasi.
“Tumeshazungumza na wenzetu, helikopta moja inakuja kuwa-
chukua watuhumiwa wetu, nashauri kwamba wewe pia unatakiwa
kuondoka nao kwa ajili ya kwenda kumhoji kwa kina huyu Abdul-
waheed, au unaonaje?” alisema baba yake Saima wakati tukizung-
umza pembeni sisi watatu, mimi, yeye na Chief Mwaipopo wakati

395 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

vijana wetu wakiwaingiza watuhumiwa wetu kwenye chumba


maalum.
“Hapana, bado tuna kazi kubwa mbele yetu, tunatakiwa kwenda
kumalizana na Mutesigwa Mafia,” nilisema, wazo ambalo liliung-
wa mkono pia na Chief Mwaipopo.
“Kwa hali yake ya kiafya ilivyo, inatakiwa kwanza akapatiwe
matibabu asije akafa na kufanya kazi izidi kuwa ngumu,” alisema
Chief Mwaipopo, nikamuona baba yake Saima akitingisha kichwa
kukubaliana na kilichokuwa kimesemwa.
Tukaanza kujadili kuhusu kinachokwenda kufanyika Mafia, baba
yake Saima akawa anatuelekeza alichokuwa anakifikiria na akaele-
za kwamba ni lazima tuwe na uhakika kwanza kwamba watuhu-
miwa wote wameshafikishwa sehemu salama kisha ndiyo mipango
mingine iendelee.
Mazungumzo yakiwa yanaendelea, tukasikia mlio wa helikopta
ya kijeshi ikipasua anga kwa kasi kubwa, ikija kule tulikokuwepo.
Haukupita muda mrefu ikawa imeshawasili, ikaanza kushuka chini
ili kutua na kusababisha vumbi kubwa litimke eneo hilo.
Tuliendelea kutazama wakati helikopta ile ikitua mpaka ilipogusa
ardhi, maafisa wawili wa jeshi ambao ndiyo waliokuwa marubani,
wakateremka baada ya kuwa helikopta imeshazimwa, wakaja moja
kwa moja kule tulikokuwa tumesimama.
Tulisalimiana nao kisha baba yake Saima akasogea pembeni na
kuanza kuzungumza nao, ni hapo ndipo na mimi nilipokumbuka
kuhusu suala la Ustaadh Fundi, akili yangu na ya Chief Mwaipopo
zikawa ni kama zinafanya kazi sawasawa, naye akaniuliza kuhusu

396 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

suala hilohilo.
“Umemfahamu vipi Ustaadh Fundi?”
“Sikuwa namfahamu kabla ya leo, ila niliunganishwa na yule
mzee wa Kisomali kama nilivyokueleza.”
“Inaonesha anajua mambo mengi sana huyu, ulikuwa unajua
kwamba anamiliki silaha?”
“Siyo tu kumiliki, sikuwa najua pia kwamba anajua kuitumia
lakini pia sikuwa najua anazijua medani za kivita! Hakika amenis-
hangaza sana.”
“Ukimtazama unadhani ni mtu mwema?”
“Mimi pia nilitaka nikuulize swali hilohilo.”
“Nafikiri tunatakiwa kuzungumza naye kwa kina, siyo mtu wa
kawaida ingawa akili zangu zinaniambia kwamba ni mtu mwema.”
“Kwa ushirikiano aliotupa, mimi pia akili zangu zinaniambia
kwamba ni mtu mwema ingawa jambo ambalo bado sijalielewa ni
jinsi alivyokuwa na hasira na Abdulwaheed, inaonesha kuna jambo
kubwa sana alifanyiwa na huyu mwendawazimu.”
“Yote tutayajua baada ya kuzungumza naye na nashauri kwamba
lazima mazungumzo kati yetu na yeye yawe ya kirafiki,” alise-
ma Chief Mwaipopo, nikakubaliana naye kwa kila alichokuwa
anakisema na muda huohuo, ilibidi mimi nitoke na kumfuata Usta-
adh Fundi ambaye alikuwa amekaa pembeni akiwa amejitenga,
akionesha kuwa na mawazo mengi ndani ya kichwa chake.
“Mbona umejiinamia Ustaadh Fundi!”
“Mawazo! Mawazo kijana wangu.”
“Nashindwa nikushukuru kwa namna gani kwa jinsi ulivyoweze-

397 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

sha kukamatwa kwa Abdulwaheed na vijana wake. Tumehangaika


sana kabla lakini baada ya kuja kwako, kila kitu kimeenda vizuri
na kukamilika ndani ya muda mfupi sana. Umetuheshimisha,”
nilimwambia, nikaona akiachia tabasamu hafifu na kukaa vizuri.
“Naomba uniwie radhi kama nilifanya makosa kule eneo la
tukio.”
“Hapana! Ulikuwa sahihi, najua ni kwa kiasi gani unamchukia
Abdulwaheed lakini lazima uelewe kwamba chuki humchoma zaidi
anayeihifadhi. Bila shaka hata maandiko matakatifu yanatuzuia
kujenga chuki ndani ya mioyo yetu.”
“Ni sahihi kwa unachokisema lakini kwa mambo aliyotufanyia
Abdulwaheed, hata ungekuwa wewe kwenye nafasi yangu, lazima
ungefanya kama nilivyofanya mimi.”
“Kwani ni nini hasa alichokifanya Abdulwaheed?” nilimuuliza,
akanitazama machoni kisha akashusha pumzi ndefu.
“Nilikutana na Abdulwaheed miaka takribani mitatu iliyopita. Al-
iletwa kwangu na madalali wa korosho, na kunieleza kuwa alikuwa
ni mfanyabiashara mkubwa kutoka Kenya ambaye alikuwa anataka
kuwekeza katika biashara ya korosho. Ninayo mashamba makubwa
ya korosho ambayo nilirithishwa na wazee wangu na kwa muda
mrefu nimekuwa nikiendesha kilimo na biashara ya korosho.
“Baada ya kukutanishwa naye, tulisalimiana na huo ndiyo ukawa
mwanzo wa mimi kufahamiana naye, msimu wa kwanza tulifanya
biashara vizuri, akaomba nimtafutie pia mashamba ya kukodi au
hata ya kununua kama itawezekana pamoja na vijana wa kumsaidia
kuyahudumia mashamba hayo.

398 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Nilifanya hayo kwa moyo mkunjufu, nikamkutanisha na vijana


kadhaa, nikamsaidia pia kupata mashamba ya korosho ya kukodi,
akawa anaendelea na shughuli zake huko mashambani. Taratibu
akaanza kuwaleta watu wageni sijui kutoka wapi huko, akawa
anasema ni wafanyakazi wa kumsaidia kazi zake za shambani
pamoja na biashara ya kununua korosho.
“Kumbe haikuwa hivyo, alikuwa anawafundisha vijana wetu
hapa imani kali na kuwabadilisha kabisa mawazo, akawa anawapa
mafunzo ya kutumia silaha na mambo mengine mengi ya hovyo-
hovyo, kwa kifupi ni kwamba alikuwa anaunda jeshi lake.”
“Kibaya zaidi, alikuwa akinipa tenda ya kutengeneza viatu,
hususan makubazi na sendoz kwa wingi akinidanganya kwamba
zinatumiwa na vijana wake huko mashambani na vingine anaenda
kuza kwao Kenya kumbe yalikuwa ni kama sare kwa wanajeshi
wake hao.
“Ushahidi wa hilo ni kwamba wengi wanaokamatwa na vyombo
vya usalama, wanakutwa wakiwa wamevaa viatu, sendozi au
makubazi ambayo mimi ndiye niliyekuwa natengeneza na kumuu-
zia Abdulwaheed kwa idadi kubwa.
“Kwa kifupi ni kwamba Abdulwaheed na wenzake ni magaidi na
anawafundisha vijana wetu kuwa magaidi kama yeye.”
“Uliyajua lini haya?”
“Nimekuja kuyajua baada ya kuanza kuibuka kwa mauaji huku
kwetu, bila shaka unaelewa ni kwa kiasi gani watu wasio na hatia
wamekuwa wakiuawa na hawa wahuni, nashukuru baada ya jesi la
polisi kuingilia kati angalau sasa yanaenda yakipungua. Nimekuwa

399 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

nikishirikiana kwa karibu na jeshi la polisi tangu mauaji yalipoan-


za.
“Kinachoniuma zaidi, ni kwamba vijana ambao mimi ndiyo niliy-
emuunganisha nao, ndiyo hao waliogeuka na kuwa wauaji ambao
nao wamekuwa wakikamatwa au kuuawa na vyombo vya ulinzi na
usalama.
Kwa kuwa mimi ndiye niliyewaunganisha, familia zao zote zime-
kuwa zikinichukulia kama mimi pia ni mshirika wa Abdulwaheed
na nilikuwa najua kila kilichokuwa kinaendelea. Roho inaniuma
sana,” alisema kisha akajiinamia, ukimya ukapita kati yetu.
“Na vipi kuhusu silaha uliyonayo, uliipata wapi na je, unaimiliki
kihalali? Usinielewe vibaya tafadhali nataka kukusaidia.”
“Nilijua lazima utaniuliza hili. Hii bastola naimiliki kihalali, nili-
fuata taratibu zote za kumiliki silaha na sababu kubwa ni kujilinda.
“Kama nilivyosema, mimi ni mfanyabiashara wa korosho, kila
msimu nauza kiasi kikubwa sana lakini msimu wa mavuno ukiisha,
nakuwa naendelea na kazi ya kutengeneza viatu kwenye karakana
yangu. Kwa hiyo nikutoa wasiwasi kuhusu hilo na nitakuonesha
pia nyaraka zangu za umiliki,” alisema.
“Ulijifunzia wapi medani za kivita?”
“Nilipita Jeshi la Kujenga Taifa, usinione hivi, mimi pia ni ka-
manda,” alisema na kusababisha nicheke, na yeye akacheka.
Mazungumzo yetu yalikatishwa baada ya Chief Mwaipopo kuja
na kuniambia kwamba nilikuwa nahitajika na baba yake Saima.
“Maandalizi tayari?”
“Ndiyo, nadhani tutaondoka ndani ya mud mfupi,” alisema, nika-

400 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

muomba nimalizane na Ustaadh Fundi kwanza.


“Unafahamu nini kuhusu mtu aitwaye Mutesigwa?”
“Huyo si ndiyo anayeshirikiana na huyu Abdulwaheed na wen-
zake? Yeye ni kama mfadhili wao na shughuli zao wanazifanyia
Mafia Kisiwani.”
“Lakini unafahamu kwamba huyu mtu yupo gerezani?”
“Gerezani wapi wakati hata hapa Kibiti nasikia alikuwa anakuja
nyakati za usiku ingawa mimi sijawahi kumuona? Wamewanunua
viongozi wa gereza, wanaishi kama wapo huru na wakati mwing-
ine askari wanamsaidia kwenye mipango yake,” alisema, jambo
lililotushangaza mno.
“Nafikiri tunatakiwa kuongozana na wewe maka Mafia, unaweza
kuwa msaada muhimu sana kwetu.”
“Siwezi kuondoka na kuiacha familia yangu, wanahitaji sana
ulinzi wangu kwa sababu sasa hivi tunaishi kwa kulipiziana visasi.
Hawa wendawazimu wakishajua tu kwamba unashirikiana na poli-
si, watakuwinda wewe na familia yako mpaka wawaue,” alisema,
tukatazamana na Chief Mwaipopo.
“Vipi kama tutaweka vijana wa kuilinda familia yako kutoka
miongoni mwetu?”
“Ikiwa hivyo nipo tayari kuondoka nanyi hata sasa hivi!”
“Basi sawa!” nilimjibu huku nikiinuka haraka na kutaka kuon-
doka lakini akaniita tena.
“Kuna binti yangu mmoja mnaye!”
“Binti yako?”
“Ndiyo! Alichukuliwa na huyu Abdulwaheed na kudai anakwen-

401 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

da kumuunganisha na ndugu yake mwingine aliyepo Dar es Salaam


kwa ajili ya kumtafutia kazi kwa sababu ndiyo kwanza alikuwa
amehitimu kidato cha nne.
“Taarifa nilizonazo ni kwamba kumbe alienda kumuunganisha
kwenye mpango wao mwingine wa kutaka kuwatumia wasichana
wadogo kama walipuaji wa kujitoa mhanga,” alisema, akili yangu
ikanituma haraka kuamini kwamba lazima atakuwa miongoni mwa
wale mabinti tuliowakamata kwenye nyumba ya kule Kisiwani B,
Kijitonyama kwenye nyumba aliyokuwa akiishi Abdulwaheed na
mkewe, Sanifa.
“Anaitwa nani?”
“Zuleikha Jamal Kandauma! Ni mwanangu kabisa wa kumzaa,”
alisema huku akilengwalengwa na machozi.
“Atakuwa salama, niachie mimi!” nilimwambia kisha harakaha-
raka nikaondoka na kumuacha akiwa amejiinamia, Chief Mwaipo-
po akiwa pembeni yake, mimi nikaenda kuitikia wito wa kiongozi
wangu.
“Yule ni nani?”
“Anaitwa Jamal Kandauma almaarufu Ustaadh Fundi! Ni ‘in-
former’ wetu aliyetu...” nilisema lakini kabla sijamalizia, akadakia.
“Nimeshakuelewa, anatakiwa kulindwa sana! Anafahamu nini
kuhusu Mafia?”
“Anafahamu mengi na nimefikiria kwamba tunatakiwa kwenda
naye mpaka Mafia, anajua vitu vingi sana na uzuri zaidi ni kwamba
anamchukia sana Abdulwaheed na kundi lake,” nilimwambia,
akawa ananisikiliza kwa makini.

402 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Tunaweza kumuamini?”
“Asilimia mia moja! Kumbe miongoni mwa wale mabinti tu-
naowashikilia, mmoja ni mwanaye wa kumzaa na alirubuniwa na
Abdulwaheed kwamba anakwenda kumtafutia kazi mjini,” nilise-
ma, baba yake Saima akawa anatingisha kichwa kuonesha kuelewa
nilichokuwa namueleza.
“Hatuna muda wa kupoteza, tuna dakika kumi kabla ya kupaa
kwenda Mafia!” alisema kisha akanipa ishara kwamba nikaendelee
na majukumu yangu ya kuwaandaa vijana wangu, tayari kwa safari
hiyo.
Harakaharaka niliwakusanya vijana wangu, tukapeana maelekezo
ya mwisho ambapo pia nilimtambulisha kwao Ustaadh Fundi na
kuwaeleza kwamba tutakuwa naye kwenye misheni yetu mpaka
mwisho.
Baada ya kumaliza kuwapa maelekezo ya mwisho, niliwataka
wakae ‘standby’ kwa ajili ya kuondoka, nikamtafutia Ustaadh Fun-
di ‘bullet proof vest’, kizibao maalum kwa ajili ya kuzuia risasi.
“Hujaniambia chochote kuhusu familia yangu!”
“Usijali kuhusu hilo, ipo salama na itakuwa salama, nimeshatoa
maelekezo maana kuna wenzetu wanakuja kwa njia ya barabara
kuongeza nguvu, kila kitu kitakuwa sawa,” nilimwambia ili kumri-
dhisha lakini ukweli ni kwamba sikuwa nimeshafanya mawasiliano
na wenzangu kuhusu kuimarishwa kwa ulinzi nyumbani kwake.
Ilibidi nimfuate baba yake Saima, nikaenda kumueleza kuhusu
suala hilo lakini tofauti na nilivyokuwa nafikiria mimi, alishauri
kwamba suala hilo tuzungumze na jeshi la polisi kwa sababu

403 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

isingewezekana kumpunguza yeyote kati yetu wakati hatujui ni


upinzani wa kiasi gani tutakaoenda kukutana nao Mafia.
“Hebu ngoja!” alisema huku akitoa simu yake, akazungumza na
upande wa pili kwa kutumia lugha za kificho kisha akakata simu
na kunitaka nimtajie ramani ya mahali ilipo nyumba ya Ustaadh
Fundi. Nikamuelekeza kwamba alikuwa maarufu sana Stendi ya
Kibiti, wakifika na kumuuliza mtu yeyote, anaweza kuwapeleka
mpaka nyumbani kwake.
Akapiga tena simu na kuzungumza maneno machache, akanigeu-
kia na kunionesha alama ya dole gumba kwamba kila kitu kimeen-
da sawa. Nilirudi kwa Ustaadh Fundi na kurudia kumhakikishia
kwamba kila kitu kitakuwa sawa, nikamsaidia kumvalisha vizuri
ile ‘bullet proof vest’ na kumpa maelekezo kadhaa ya kiusalama
pindi tutapokuwa Mafia.
Tukiwa tunaendelea na mazungumzo, muungurumo wa helikopta
ilisikika angani, wote tukainua vichwa vyetu juu kuitazama. Ili-
kuwa ni ile helikopta ya pili ambayo tulikuwa tunaisubiri, am-
bayo ndiyo iliyowapeleka akina Abdulwaheed na wenzake Dar es
Salaam.
Mpaka hapo sasa mambo yalishakuwa yameiva, nikawapa is-
hara vijana wangu ambao nao tayari walishakuwa wanasubiri kwa
shauku kubwa kuondoka eneo hilo kuelekea kisiwani Mafia kuka-
milisha kazi yetu.
Helikopta ilitua pembeni kidogo ya ile ya awali ambayo ilikuwa
imeshafika kitambo kidogo, nikawagawa vijana wangu kama tu-
livyosafiri wakati tukitoka Dar es Salaam na wote wakapanda.

404 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Mimi, Ustaadh Fundi, Chief Mwaipopo na baba yake Saima,


tulikuwa wa mwisho, tukakubaliana kwamba mimi nipande na
Ustaadh Fundi na Chief Mwaipopo na baba yake Saima wakapanda
kwenye ile nyingine, safari ikaanza.
Tulipaa kutoka Kibiti, safari ikapanda moto, tukawa tunapasua
mawingu kwa kasi kubwa, tukawasili Mafia na kama ilivyokuwa
kwa Kibiti, tulifikia pia kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari
Kitomondo, kwa wenyeji wa Mafia watakuwa wananielewa vizuri.
Tulitua kwenye uwanja wa shule hiyo na tukaweka kambi ya
muda katika eneo hilo, wakati tukijipanga nini cha kufanya kwa
sababu wote tulikuwa wageni. Muda mfupi baadaye, wenyeji wetu
wawili ambao nao ni ‘kitengo’ walikuja kutupokea, wakashangaa
kwa jinsi tulivyowasili kimyakimya bila hata wao kuwa na taarifa.
Nakumbuka kwamba walipigiwa simu na baba yake Saima
tukiwa tumeshafika na kuweka kambi kwenye shule hiyo.
Baada ya hapo, kilichofuatia ilikuwa ni kuanza upyakuchora
ramani ya nini kinatakiwa kufanyika na hapa kuna baadhi ya vitu
sitaviweka wazi sana. Itoshe kusema kwamba kulikuwa na gereza
ambalo ndiko watu ambao huonekana kuwa tishio kwenye mager-
eza mengine, hupelekwa.
Ulinzi wake ni tofauti na magereza mengine na hata idadi ya
wafungwa ni ndogo ili iwe rahisi kwa wafungwa hao kuwekwa
chini ya uangalizi maalum. Ili kufika kwenye gereza hilo, ilikuwa
ni lazima kusafiri tena kwa njia ya maji kwa sababu gereza lilikuwa
kwenye kisiwa kingine cha pembezoni.
Tulipanga mipango yote katika kambi hiyo ya muda, tukakubali-

405 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ana kwamba muda mzuri wa kuingia, inatakiwa kuwa usiku ili


tusije tukavuruga mipango lakini kubwa, ilikuwa ni lazima kwanza
kupata taarifa kamili juu ya nini kilichokuwa kinaendelea mitaani
mpaka kumfanya Mutesigwa awe huru kupanga mipango hatari
kama hiyo.
Kwa kuwatumia wale wenyeji wetu wawili, pamoja na Ustaadh
Fundi, tulipata picha ya kitu kilichokuwa kinafanyika kwenye
kisiwa hicho kwanza kabla ya kutaka kujua ni nini kilichokuwa
kinafanyika kule gerezani.
Jambo ambalo lilitushangaza sana ni kwamba, Mafia ni mji
mdogo na hata idadi ya wakazi wake ni ndogo lakini Mutesigwa
alikuwa na ushawishi mkubwa mno.
Kulikuwa na vijana wengi, wakijifanya kama wanafanya kazi ya
uvuvi lakini kiundani, walikuwa ni wafuasi waaminifu wa Mute-
sigwa na genge lake na ndiyo aliokuwa akiwatumia kufanikisha
mipango yao. “Tunafanyaje?”
“Inatakiwa kuwakusanya wote kwanza, tukiendelea kuwaacha,
taarifa zitasambaa kwa haraka na tutashindwa kufanya mambo
yetu,” alisema Ustaadh Fundi na kwa kuwa alikuwa anafahamu
mtandao mzima, ilibidi yeye na wale wenyeji wetu, ndiyo watuon-
goze katika oparesheni hiyo.
Kikwazo kingine kikawa ni kwamba sisi tulikuwa kwenye mag-
wanda kwa hiyo kuonekana mitaani tukiwa na magwanda, ingewe-
za kuibua hali ya sintofahamu na kuvuruga mipango yote.
“Nilikuwa na wazo ambalo naona linaweza kutusaidia sana,”
nilisema, Chief Mwaipopo na baba yake Saima wakawa wanan-

406 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

isikiliza kwa makini.


“Hivi hatuoni kwamba hawa watu wanaweza kuwasiliana kwa
kupigiana simu na kuvuruga misheni yetu?” nilisema, kila mmoja
akawa ni kama amezinduka kutoka kwenye lindi zito la mawazo.
”Unataka kusemaje?”
“Tunatakiwa kwanza kuhakikisha tunazima mawasiliano ya aina
yoyote kwenye mji huu wote na kwa sababu mji wenyewe ni mdo-
go hilo litawezekana kwa urahisi,” nilisema, wote wakatingisha
vichwa vyao kuonesha kukubaliana na nilichokuwa nimekisema.
“Wazo zuri sana, ngoja niwasiliane na makao makuu, vijana wetu
wa Cyber na IT wanaweza kulifanya hili kirahisi sana, wala siyo
kazi kubwa,” alisema baba yake Saima kisha akabonyeza kitufe
kwenye kifaa chake cha mawasiliano.
Alikuwa akizungumza na mkurugenzi na kumueleza tulichokuwa
tumekiwaza, mkurugenzi naye akaunga mkono wazo hilo kisha
akawa anasikika akitoa maelekezo kwa vijana wa Cyber na IT
muda huohuo.
Kwa jinsi mazungumzo yalivyokuwa yakifanyika, ni sisi wa-
husika pekee ndiyo tuliokuwa tunaweza kuelewa kinachozung-
umwa kwa sababu kila kitu kilikuwa kikizungumzwa kwa lugha ya
kificho au ‘codes’ kwa lugha ya kitaalamu.
Mawasiliano yaliendelea, watu wa kitengo cha teknolojia ya
mawasiliano wakawa wanasikika kupitia mfumo wa mawasiliano
wakipeana maelekezo na haukupita muda mrefu, mawasiliano yote
ya simu kuingia au kutoka kwenye Mji wa Mafia yalizimwa, ikawa
huwezi kupiga simu, kutuma meseji wala kutuma ujumbe wa barua

407 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

pepe.
Pengine unaweza kujiuliza hili linawezekanaje? Nikutoe wasi-
wasi kwamba ni mbinu ya kawaida ambayo huwa inatumika sana
kwa watu maalum kwa sababu za kiusalama.
Hata zinapotokea ziara za viongozi wakubwa duniani kote,
mfano Rais wa Marekani anapokuwa kwenye nchi nyingine kwa
ziara, maafisa usalama wa nchi hiyo huwa wanakawaida ya kuzi-
ma mawasiliano yote ya simu na internet kwa kutumia teknolojia
maalum na hufanya hivyo kwa lengo la kuzuia watu wenye nia
ovu kufanya mawasiliano na kupanga njama zao.
Hata namba moja anapokuwa anafanya ziara kwenye maeneo
korofi hususan kwenye mipaka ya nchi, teknolojia hii pia huwa
inatumika sana, mnashtukia tu simu za mitandao yote haziwezi
kutoka wala kuingia mpaka shughuli inapokamilika.
Hicho ndicho kilichofanyika na baada ya hilo kuwezekana,
tulitakiwa sisi ndiyo tuwe wa kwanza kuhakikisha kama kweli kila
kitu kimeenda sawa. Nilitoa simu yangu ya mkononi, kwenye lile
eneo ambalo ‘network’ ya simu ya mtandao husika husoma, zil-
ionesha kutokuwa na alama yoyote inayoonesha kwamba mtandao
unapatikana eneo hilo.
Kil ammoja alijaribu na majibu yalikuwa yaleyale, mawasiliano
pekee ambayo yalikuwa yanapatikana, ilikuwa ni kupitia mifumo
yetu ya mawasiliano ambayo yenyewe ilikuwa inategemea zaidi
mawasiliano ya ‘satelite’ na siyo minara ya kawaida ya simu za
mikononi au za mezani.
Kwa kuwa sasa tulikuwa na uhakika kwamba hakuna mtu

408 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

anayeweza kupiga wala kupokea simu, suala la sisi kuingia mitaani


tukiwa na sare zetu za kazi halikuwa tatizo tena.
Wale wenyeji wetu wawili kwa kushirikiana na Ustaadh Fundi
wakaanza kutupa maelekezo ya mahali tunapoweza kuwapata
vijana wote wanaoshirikiana na Mutesigwa na genge lake kwenye
njama walizokuwa nazo.
Kwa kuwa hakukuwa namagari ya kutosha, ilibidi tugawane,
wengine wabaki pale kwenye ile kambi ya muda kisha sisi wach-
ache ndiyo tuingie mitaani kwa kutumia msafara wa magari matatu
ambayo yalikuwa yakiongozana.
Tulipita kwenye maeneo yote tuliyoelekezwa na wenyeji wetu
wakiongozwa na Ustaadh Fundi ambaye alionesha kuwa anaujua
zaidi mji huo, tukawakusanya vijana wengi ambao tuliwahisi kuwa
wanaweza kuwa wanahusika na alama kubwa ambazo tulikuwa
tunazitumia kuwanasa, ilikuwa ni aina ya mavazi na mwonekano
wa jumla wa mtu.
Sitafafanua kwa undani lakini ifahamike kwamba mafunzo tuli-
yokuwa nayo na ushirikiano tuliopewa, ulifanya tuweze kuwabaini
kwa urahisi kabisa watu wote ambao walikuwa na chembechembe
za uhalifu au kujihusisha na makundi ya uhalifu.
Tukiwa tunaendelea na kazi yetu, tukabaini pia kwamba kila
tulipokuwa tunapita, baadhi ya vijana wachache waliokuwa waki-
fanikiwa kuchoropoka na kuukimbia mkono wa dola, walikuwa
wakishindwa kutoa taarifa kwa wenzao kwa sababu ya kuzimwa
kwa mitandao yote ya simu.
“Ulitoa wazo la msingi sana kuhusu kuzimwa kwa mitandao,

409 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kazi ingekuwa ngumu sana,” alisema baba yake Saima. Mpaka


zoezi linakamilika, tulikuwa tumewakusanya takribani vijana sitini,
wengi wao wakiwa na umri wa kati ya miaka 18 hadi 35 na mion-
goni mwao, walikuwepo wachache ambao walikuwa na asiliya
Kisomali na wengine asili ya Kiarabu.
Jambo baya sana alilokuwa analifanya Mutesigwa na genge lake,
lilikuwa ni kulilenga kundi hili la vijana na kuwatumikisha kwa
maslahi yao, wakati mwingine bila hata vijana wenyewe kuelewa
ni nini hasa kilichokuwa kinaendelea.
Wengi walikuwa ni vijana wazaliwa wa eneo hilo, wengine wali-
kuwa wakitokea maeneo ya Kibiti, Rufiji, Mtwara na Mkuranga na
wengine kama nilivyoeleza, walikuwa ni wageni kabisa.
“Sikilizeni, nyie wote ni watuhumiwa tu, hakuna mwenye usha-
hidi kwamba mnajihusisha na uhalifu lakini matendo yenu ndiyo
yatakayofanya wengine muachiwe huru na wengine mfikishwe
mbele ya vyombo vya usalama.
“Mtakaokuwa tayari kutoa ushirikiano, mtaachiwa huru bila
masharti kwa sababu tunajua wengi wenu hamjui ni nini mna-
chokipigania, lakini mtakaoleta ujuaji, mtahesabiwa kuwa wa-
halifu.
“Kila mmoja kuanzia sasa atahojiwa na maafisa wetu na
unachotakiwa kukieleza ni ukweli kwa sababu sisi tunajua kila
kitu, hatujafika eneo hili kwa bahati mbaya,” nilisema kwa sauti ya
mamlaka tukiwa tumewakusanya wote kwenye bwalo la chakula
la shulehiyo ya sekondari, chini ya ulinzi mkali.
Baada ya kuwaeleza hayo, wengi wakiwa na hofu kubwa ndani

410 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ya mioyo yao, wakijiuliza sisi ni akina nani kwa sababu hatukuwa


kwenye sare za kipolisi wala za askari magereza, zoezi lililofuata
lilikuwa ni kuanza kuwahoji na hapa tulitumia dodoso maalum la
kutaka kujua mambo kadhaa ya msingi.
Miongoni mwa maswali ambayo tulikuwa tukiwauliza, ilikuwa
ni pamoja na utambulisho wa kila mmoja wao lakini pia kuwahoji
kama wanamfahamu Mutesigwa, kama wamewahi kumuona mtu
huyo mitaani, kama walikuwa wanamfahamu Abdulwaheed.
Lakini pia kuwahoji kama walikuwa wamepewa mafunzo yoyote
ya kijeshi au medani za kimapigano na kama walikuwa wanajua
wanachokisimamia au kukipigania na akina nani wengine walio-
kuwa wanashirikiana nao.
Kila mmoja alikuwa akihojiwa peke yake na kwa kuwa tulikuwa
wengi, haikuchukua muda mrefu tukawa tumepata taarifa muhimu
sana ambazo zilitupa picha kamili ya kilichokuwa kinaendelea.
Tatizo lilikuwa kubwa kuliko kawaida, vijana wengi walikiri
kumfahamu Mutesigwa na wakakiri kuonana naye mara kadhaa
hususani majira ya usiku ambapo walikuwa wakikutana naye na
wapambe wake kwenye maeneo ya mafichoni.
Wakaeleza pia kwamba karibu wote walikuwa wakipewa ma-
funzo ya medani za kimapigano ‘martial arts’, Judo na mazoezi
mengine huku wakiahidiwa kwamba watakuwa wakilipwa fedha
nyingi baada ya kumaliza mafunzo ikiwa ni pamoja na kutafutiwa
ajira nje ya nchi.
Jambo ambalo hawakuwa wanalijua, ni nini hasa walichokuwa
wanakipigania kwa sababu wengi walichokuwa wakikisema ni

411 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kwamba wanaandaliwa kwa ajili ya kwenda kuajiriwa kwenye


makampuni ya kulinda visima vya mafuta nje ya nchi, makampuni
ambayo yalikuwa yakimilikiwa na Mutesigwa na wafanyabiashara
wenzake lakini pia walikuwa wakiandaliwa kwa ajili ya kwenda
kulinda shehena za korosho ambazo waliambiwa eti kampuni ya
Mutesigwa na wenzake walikuwa wakijiandaa kuzinunua na kuz-
isafirisha kwenda nje ya nchi.
Hakuna aliyekuwa anajua kwamba Mutesigwa alikuwa gerezani
na kwamba alikuwa akishirikiana na makundi hatari ya ugaidi,
tukajikuta tukichanganyikiwa kuliko kawaida. Kazi ya mwisho ili-
yokuwa imesalia, ambayo tulikuwa tunasubiri giza liingine, iliku-
wa ni kwenda kwenye gereza alilokuwa anashikiliwa Mutesigwa.
Taarifa za tulichokuwa tumekibaini Mafia zilimshangaza kila
aliyezisikia na nakumbuka baba yake Saima alinidokeza kwamba
taarifa zimemfikia namba moja na amekasirishwa sana na uzembe
wa vyombo vya ulinzi na usalama na kumpa taarifa zisizo na
ukweli kwamba hali ya ulinzi na usalama ni shwari wakati ukweli
ulikuwa tofauti.
“Watu pekee ambao tumeonekana kufanya kazi kwa weledi,
ni sisi na kiukweli, wewe ndiye uliyetuheshimisha na kumfanya
namba moja atuamini kwa kiasi kikubwa sana.
“Umemheshimisha mkurugenzi wetu, umetuheshimisha sisi vion-
gozi wako na umemheshimisha kila mmoja ‘kitengoni’, tunajivunia
uwepo wako na mimi najivunia zaidi uamuzi wangu wa kuamua
kukusaidia na kukubadilisha kutoka kule ulipokuwa na kuja huku.
Kubwa zaidi najivunia kuwa mkwe wangu,” alisema baba yake

412 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Saima na kunifanya nicheke kwa furaha.


“Naamini mpaka hapa tulipofika, tutafanikiwa kulizima kabisa
tukio hili kwa sababu tumechagua kushughulika na mzizi wa
tatizo, kama tungebaki kuilinda Magogoni pekee na kuacha haya
yaendelee huku, ingekuwa ni sawa na kuzuia watu wasiogelee
baharini eneo moja wakati bahari ni kubwa na watu wanaweza
kuhamia eneo lingine na kuendelea kuogelea,” alisema.
“Akili yangu itatulia tutakapoumaliza mtandao mzima, naamini
tumefanya kazi kubwa lakini bado kuna kazi nyingine kubwa zaidi
ambayo ni lazima tuikamilishe ndani ya muda huu mfupi tulionao,”
nilisema, tukawa tunaendelea kuvuta muda kusubiri giza liingie
tukamalize kazi kule gerezani.
Muda uliendelea kuyoyoma kwa kasi na hatimaye giza likaanza
kuingia na taarifa tulizokuwa tunazipata kupitia vifaa vyetu vya
mawasiliano ni kwamba vikosi vingi zaidi vilikuwa njiani kuja
kuongeza nguvu kwa sababu kwa idadi yetu, isingewezekana
tukaendelea kuwaweka chini ya ulinzi vijana takribani sitini kwa
wakati mmoja na wakati huohuo tukijiandaa kwenda kulifumua
genge la Mutesigwa ndani ya gereza na kuzima jaribio zima
walilokuwa wanalipanga.
Maandalizi ya mwishomwisho yaliendelea na muafaka wa
mwisho ambao tuliufikia, ni kwamba kwa sababu vikosi vingine
bado havijafika na sisi tunakimbizana na muda, kikosi maalum
nilichokuwa nakiongoza kigawanywe mara mbili, nusu ya kwanza
ibaki kuendelea kuwashikilia wale vijana wote tuliowaweka chini
ya ulinzi katika Mji wa Mafia na nusu ya pili ndiyo ivuke maji

413 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kwenda gerezani.
Baada ya hilo kukamilika, sisi tuliotakiwa kwenda kule gerezani,
tuliondoka pale kambini na kuelekea kwenye eneo la bandari
ndogo ambapo hapo ndipo ingekuwa kituo chetu cha kuondokea
kwa kutumia usafiri wa boti za mwendo kasi ambazo tayari zili-
kuwa zimeandaliwa kwa ajili ya kutuvusha.
Ikumbukwe kwamba wakati haya yakiendelea, bado hakukuwa
na mawasiliano yoyote yaliyokuwa yanapatikana katika eneo lote
la Mafia kwa sababu mitandao ya simu zote za mikononi, simu za
mezani na intaneti ilikuwa imezimwa.
Saa mbili kamili juu ya alama, safari ilianza. Kulikuwa na boti
tatu ambazo zilituchukua mimi, baba yake Saima, Chief Mwaipo-
po, Ustaadh Fundi aliyeendelea kuwa mtu muhimu kwenye msafa-
ra wetu, wale maafisa wawili wa kitengo waliokuwa wenyeji wetu
pamoja na vijana kumi, jumla tukawa watu 15 pamoja na mana-
hodha watatu ambao kila mmoja alikuwa akiiongoza boti moja.
Hawa manahodha walikuwa ni kutoka kikosi maalum cha askari
wanaofanya kazi ya kulinda rasilimali za bahari ikiwa ni Pamoja na
kupambana na uvuvi haramu.
Bahari ilikuwa tulivu, safari ikaendelea huku boti zote tatu zikiwa
zimeongozana, tukapasua mawimbi na kama baada ya dakika kumi
na tano, tayari tulishawasili kwenye gati maalum lililokuwa linatu-
miwa na maafisa wa gereza, ikiwa ndiyo njia ya kuingia na kutoka
kwenye kisiwa hicho kidogo kilichokuwa sehemu ya Visiwa vya
Mafia, kulipokuwa na gereza maalum la siri alikokuwa anashikili-
wa Mutesigwa.

414 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Kuwasili kwetu eneo hilo, kulikuwa ni kama ‘sapraiz’ kubwa


kwa askari magereza waliokuwa wakililinda eneo lote la kisiwa
hicho ambao hawakuwa na taarifa zozote za ujio wetu, hasa katika
nyakati za usiku kama ule.
Ilibidi wenyeji wetu wale wawili kutoka kitengoni pamoja na
wale manahodha wa boti zilizotubeba, ndiyo watangulie mbele na
kuwapa maelezo askari wale ambao awali walikuwa wamezuia
tusivuke kwenye lile eneo la gati na kuingia kwenye kisiwa kile.
Walipopewa utambulisho wetu na sababu iliyotufanya tufunge
safari ile, walipatwa na hofu kubwa ambayo iliweza kuonekana
vizuri kwenye sura zao kisha wakakubali kuta ushirikiano lakini
wakataka kwanza tukaripoti kwa mkuu wa gereza ambaye ndiye
aliyekuwa na mamlaka ya kisheria ya kutoa idhini ya sisi kuende-
lea na shughuli zetu.
“Kwa nini asipigwe simu aje hapa? Sidhani kama tuna muda wa
kutosha.”
“Tuna shida ya mawasiliano tangu mchana wa leo, simu zote
hazitoki, siyo simu za kawaida wala simu za upepo (radio call),
alisema mmoja kati yao, akiwa amevalia magwanda ya magereza,
mkononi akiwa na bunduki.
“Anapatikana wapi?”
“Siyo mbali kutoka hapa, nyumba yake ipo ndani ya eneo la ger-
eza na kwa muda huu anaweza kuwa bado yupo kwenye ofisi yake
ndani ya gereza.”
“Ataondoka askari wenu mmoja na kiongozi wetu kwenda kuon-
ana naye, kazi yetu inatakiwa kuanzia hapahapa, hatuwezi kuongo-

415 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

zana wote,” nilimwambia yule askari kisha nikamgeukia baba yake


Saima na kumpa ishara, akatingisha kichwa kuonesha kukubaliana
na nilichokisema, nikamgeukia Chief Mwaipopo ambaye naye alit-
ingisha kichwa kuonesha kukubaliana na nilichokisema.
Tulipeana ishara na tukakubaliana kwamba baba yake Saima
ndiyo anayetakiwa kwenda kuzungumza na mkuu wa gereza, bila
kupoteza muda akaikamata bunduki yake vizuri na kuanza safari
ya kuelekea ndani ya eneo la gereza, akiwa ameongozana na yule
askari magereza ambaye alionesha kuwa na cheo kuliko wenzake,
sisi tukabaki na askari wengine kama sita hivi wa magereza, ambao
kila mmoja alikuwa na bunduki mkononi.
“Mkuu!” aliita askari magereza mmoja huku akinisogelea, nika-
jitenga pembeni kidogo ili kumsikiliza alichokuwa anataka kukise-
ma.
“Kuna ishu gani kwani?”
“Ni ukaguzi wa kawaida wa gereza, mbona una wasiwasi?”
“Hapana, sina wasiwasi lakini ni muda mrefu sana umepita hatu-
japata ugeni wa kutisha kama huu. Kuna mtu mnamhitaji?”
“Hapana, ni ukaguzi wa kawaida,” nilimwambia huku nikijaribu
kumsoma kwa kumkazia macho, mwanga wa taa kali zilizokuwa
pale kwenye lile gati na eneo lote la gereza, zikafanya kazi yangu
iwe nyepesi kwa sababu niliweza kumuona jinsi alivyokuwa na
hofu kwenye uso wake.
“Mna jumla ya wafungwa wangapi?”
“Huwa wanaongezeka na kupungua, lakini huwa tunakuwa na
wafungwa wachache, gereza letu ni dogo na huwa tunaletewa

416 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

watu walioshindikana kwa hiyo lazima wawe wachache ili tuweze


kuwadhibiti.”
“Kwa sasa wapo wangapi?”
“Tuna wafungwa ishirini na saba.”
“Basi vizuri, unaweza kwenda kuendelea na majukumu yako,”
nilimwambia huku nikirudi pale nilipokuwa nimesimama awali,
pembeni ya Chief Mwaipopo.
Kwa muda wote huo, vijana walikuwa wamejipanga kwa mfumo
maalum kama tulivyokuwa tumeelekezana, kila mmoja bunduki
yake ikiwa mkononi, tayari kwa chochote.
Ustaadh Fundi alikuwa amesimama pembeni akiwa na wale
manahodha watatu waliotusafirisha huku wale maafisa wawili wa
‘kitengo’ ambao ndiyo waliokuwa wneyeji wetu, wakiwa wamesi-
mama pembeni, wakiwa ni kama wanazungumza jambo kwa sauti
za chinichini, nao kila mmoja akiwa na silaha yake mkononi,
tukawa tunaendelea kusubiri baba yake Saima arudi na mkuu wa
gereza Pamoja na yule askari aliyeondoa naye.
Kwa muda wote huo, akili yangu ulikuwa haitulii kabisa, nikawa
naendelea kulisoma eneo lote la kisiwa kile na mwonekano wa
mbele wa gereza ambalo lilikuwa kama mita mia moja kutoka pale
kwenye gati tulipokuwa tumesimama, upepo wa bahari ukiendelea
kutupuliza, eneo lote likiwa kimya kabisa.
Baada ya kama dakika tano hivi kupita, tuliwaona baba yake
Saima, yule askari magereza aliyeondoka naye wakiwa na mtu
mwingine wa tatu, wakija kwa hatua ndefundefu, baba yake Saima
akionesha ni kama anabishana na yule mtu wa tatu waliyekuwa

417 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wakija naye ambaye akili zangu zilinituma kuamini kwamba


huenda ndiyo mkuu wa gereza.
Waliendelea kusogea kwa hatua za harakaharaka, watu wote tu-
kawa makini kuwatazama, wakasogea mpaka hatua kadhaa mbele
yetu, yule mwanaume na yule askari magereza wakasimama kisha
baba yake Saima akapiga hatua ndefu na kusogea hadi pale tulip-
okuwa tumesimama mimi na Chief Mwaipopo, tukawa tunamtaza-
ma kwa makini kutaka kusikia ni nini anachotaka kutuambia.
“Hataki kutoa ushirikiano!”
“Kivipi? Kwa nini hataki kutoa ushirikiano?”
“Anasema lazima apewe maelekezo na kamishna mkuu wa mag-
ereza kwa sababu hajui nia yetu ni nini, tunaweza kuwa na nia ya
kuwatorosha wafungwa.”
“Haiwezekani! Kuna jambo anataka kulificha!” nilisema huku ni-
kionesha kupandwa na jazba, nikawa namtazama pale aliposimama
kwa hasira kali, na yeye akawa ananitazama, tukiwa tumetengan-
ishwa na hatua kadhaa kati yetu.
“Ni sawa, anasimamia sheria za kazi yake ingawa pia angeweza
kutumia busara kwa sababu japokuwa sisi ni vyombo tofauti vya
ulinzi, lakini linapokuja suala la kulipigania taifa letu lazima tuwe
kitu kimoja.”
“Tunafanyaje?”
“Amesema ni lazima kwanza tuwasiliane na kamishna mkuu,
kisha kamishna yeye ndiyo ampigie simu na kumpa maelekezo.”
“Kwa nini yeye asimpigie mkuu wake na kumueleza kuhusu ujio
wetu? Nadhani kiongozi wake naye anajua ni nini kinachoendelea

418 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kwa sababu kwenye mkutano wa namba moja na wakuu wa idara


za ulinzi na usalama na yeye alikuwepo.”
“Anasema tangu mchana hawezi kupiga wala kupokea simu.”
“Nahitaji kuzungumza naye na kumhoji mambo kadhaa.”
“Hapana! Kenny, unapaswa kutulia, hili ni jambo ambalo lipo
ndani ya uwezo wetu,” alisema baba yake Saima ambaye bado
alikuwa akipumua kwa nguvu, nikawa simuelewi kabisa.
“Huyu anacheza na akili zetu, anataka kututoa kwenye reli.”
“Tulia, hii ni kazi ndogo sana,” alisema baba yake Saima na
kubofya kitufe kwenye kifaa cha mawasiliano alichokuwa amevaa,
wote tukawa tunamsikia akizungumza moja kwa moja na mku-
rugenzi wetu na kumueleza kinachoendelea kwa kutumia lugha
maalum ya kificho.
Katika mazungumzo yao, kulitokea mvutano kidogo kwa sababu
mkurugenzi naye alikuwa na akili kama zangu, akawa hataki ka-
mishna mkuu aambiwe chochote kwa sababu yeye pia nyendo zake
zilikuwa zinachunguzwa.
Sababu kubwa ya kuchunguzwa kwake,ilikuwa ni uzembe ulio-
kuwa unafanyika kwa kuruhusu mfungwa hatari anayeshikiliwa
kwenye moja kati ya magereza anayoyasimamia, kuweza kuwa
anatoka na kurudi gerezani kama nyumbani kwake na kushiriki-
ana na makundi ya magaidi kupanga njama hatari za kuiangusha
Magogoni.
Walivutana kidogo na mwisho wakakubaliana kwamba lazima
namba moja aambiwe kinachoendelea kisha yeye ndiyo atoe amri
kwa kamishna kuruhusu oparesheni ile kuendelea ndani ya gereza

419 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

hilo la siri.
“Itachukua muda gani?” nilimuuliza baba yake Saima baada ya
kuwa ametoka kwenye laini na mkurugenzi.
“Hili ni suala la dharura kwa hiyo naamini ndani ya dakika
chache tu agizo litatoka juu.”
“Sasa huyu atapewaje taarifa wakati tumezima mawasiliano?”
“Tunaweza kuzungumza na wataalamu wetu waachilie ma-
wasiliano kwa dakika chache kisha mitambo izimwe tena.”
“Hapana! Ni hatari sana kwa sababu hizohizo dakika chache wa-
naweza kuzitumia wafuasi wa Mutesigwa kumpa taarifa juu ya kila
kinachoendelea. Lakini pia, suala la kuzima mitambo na kuwasha,
siyo kitu cha papo kwa hapo, ni mchakato unaoweza kuchukua
mpaka dakika arobaini na tano kwa mujibu wa vijana wetu wa
Cyber na IT.”
“Kwa hiyo unashauri nini?” baba yake Saima aliniuliza, tukawa
tunatazamana kwa sababu hata mimi sikuwa na majibu ya haraka-
haraka ya nini cha kufanya.
“Nafikiri amri ikishatoka juu, tunaweza hata kutumia nguvu kuin-
gia, hawawezi kutuzidi nguvu hawa.”
“Hapana! Kazi hizi haziendi hivyo Kenny, unataka kuharibu
mambo sasa,” alisema Chief Mwaipopo ambaye muda wote ali-
kuwa kimya akisikiliza jinsi ninavyolumbana na baba yake Saima.
“Hii inaweza kutusaidia,” alisema Chief Mwaipopo huku akitoa
‘satellite phone’ ndogo aliyokuwa nayo kwenye magwanda yake na
kuiwasha. Nimewahi kueleza kidogo kuhusu hizi simu za satellite
au SAT kama ambavyo tulizoea kuziita.

420 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Sifa ya kwanza ya simu hizi ni kwamba zenyewe huwa hazitumii


‘signal’ za minara ya simu kama zilivyo simu nyingine za kawaida.
Hizi huwa zinatumia mawasiliano ya satellite moja kwa moja na
ndiyo maana hata ukiwa sehemu ambako hakuna kabisa network,
unaweza kupiga na kupokea simu ukiwa na SAT.
Sifa ya pili ni kwamba zilikuwa ni simu ambazo mtu yeyote
hawezi kuingilia mawasiliano yake na hii ndiyo sababu huwa raia
wa kawaida hawaruhusiwi kuzimiliki bila kibali maalum kwa
sababu hata kama watu wanapanga njama zao, vyombo vya ulinzi
na usalama haviwezi kufuatilia mawasiliano ya wanaopanga njama
hizo kama wanatumia simu za aina hii.
“Tukishakuwa na uhakika kwamba tayari amri imetoka kwa
namba moja kwenda kwa kamishna, itabidi tumpe hii awasiliane na
kamishna moja kwa moja!”
“Wazo zuri sana!” alisema baba yake Saima, mimi pia nikatingi-
sha kichwa kuonesha kukubaliana na kilichokuwa kimezungumz-
wa.
Kilichoendelea baada ya hapo ikawa ni kuendelea kusubiri huku
tukiwa tunawindana wenyewe kwa wenyewe, mkuu wa gereza
akionesha kutokuwa na imani na sisi kwa sababu tunakwenda kuto-
boa siri kubwa aliyokuwa anaificha, lakini sisi pia tukiwa hatuna
imani naye kwa kuona ni kama anataka kutuletea ‘kauzibe’.

421 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

422 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

16
B
AADA ya kama dakika kumi hivi za kuendelea
kusubiri, vifaa vyetu vya mawasiliano vilitoa ishara
kwamba kuna mtu yupo kwenye laini. Alikuwa ni
mkurugenzi ambaye alikuwa akimuita kwenye laini
baba yake Saima, harakaharaka akajibu kwamba
yupo kwenye laini, maelekezo yakaanza kutolewa kwa kutumia
lugha ya uficho.
Niliweza kuelewa vizuri alichokuwa anakisema, akaeleza kwam-
ba namba moja alikuwa ametoa maagizo kwa kamishna kuhusu
sisi kuruhusiwa kuendelea na kazi yetu lakini tatizo ni kwamba
kamishna alirudisha majibu kwamba hampati mkuu wa gereza

423 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kwenye simu.
Wote tulishusha pumzi ndefu kwa sababu sasa kile tulichokuwa
tumekipanga kilikuwa kinaenda kutimia, Chief Mwaipopo akamka-
bidhi ile SAT baba yake Saima ambaye aligeuka haraka na kuele-
kea pale alipokuwa amesimama mkuu wa gereza ambaye alionesha
kukosa utulivu kabisa.
Walizungumza kwa kifupi kisha akampa ile simu, tukamuona
akibofya namba fulani kisha akaiweka simu sikioni na haukupita
muda, simu ikapokelewa upande wa pili. Akawa anazungumza na
upande wa pili na baada ya kama sekunde arobaini hivi, alimrud-
ishia simu baba yake Saima kisha wakawa ni kama wanajadiliana
jambo tena.
Baada ya kujadiliana kwa kifupi, mkuu wa gereza aliwaita askari
wake waliokuwa eneo lile na wakati huohuo baba yake Saima aka-
geuka na kurudi pale tulipokuwa tumesimama.
“Permission granted!” alisema kwa Kiingereza, akimaanisha
kwamba ruhusa ilikuwa imetolewa.
Hakukuwa tena na muda wa kupoteza, harakaharaka tukaanza
kujadiliana namna ya kuifanya kazi ile, tukakubaliana kwamba
vijana sita watabaki nje ambapo watalizunguka gereza kwa upande
wa nje ili kuhakikisha kwamba hakuna mtu anayetoka na sisi wen-
gine tutaingia ndani kwa kuongozana na mkuu wa gereza mwe-
nyewe pamoja na wale askari wake.
Kilichokuwa kinatakiwa kwenda kufanyika ndani, ilikuwa ni
kwenda kumchomoa Mutesigwa ili akajibu tuhuma zilizokuwa
zinamkabili.

424 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Baada ya kukubaliana, niliwakusanya vijana wangu wote, ni-


kagawa majukumu na kuwaeleza ni nini hasa ambacho kinakwenda
kufanyika ndani, nikawataka kila mmoja kuwa makini kwa sababu
watu waliokuwa ndani ya gereza hilo, hawakuwa wafungwa wa
kawaida kwa hiyo lazima tutulize vichwa kisawasawa.
Baada ya kumaliza kupeana majukumu, mkuu wa gereza na
vijana wake walitusogelea na kwa mara ya kwanza tukawa tuna-
tazamana kwa karibu kabisa. Nikashangaa kuona mkuu wa gereza
ananikazia mimi macho huku midomo yake ikimchezacheza.
“Huyu anaitwa Chief Kenny, wengi wamezoea kumuita Snox,
ndiye kiongozi wa misheni hii,” alisema baba yake Saima, akim-
weleza mkuu wa gereza ambaye alinisogelea kisha akanyoosha
mkono wake, na mimi nikanyoosha wa kwangu na kumpa.
“Niite Kilasi, Elius Kilasi, mkuu wa gereza!” alisema huku akini-
tazama machoni, na mimi nikawa namtazama machoni, nikatingi-
sha kichwa kuonesha kwamba nilikuwa nimeuelewa utambulisho
wake.
“Mimi na wewe tunatakiwa kuzungumza kwa kifupi pembeni,”
alisema huku akiwa bado ameushikilia mkono wangu, akanivuta
tukasogea pembeni, watu wote wakawa kimya kabisa wakituta-
zama. Tulipiga hatua kadhaa na kusogea pembeni.
“Nimekuwa nikisikia sana taarifa zako kutoka kwa mmoja kati
ya wafungwa tulionao hapa, Mutesigwa! Amekuwa akinieleza
kwamba wewe ni kijana wake ambaye alikutoa kwenye mazingira
magumu sana na akakupa nafasi ya kuwa mtu mwingine kabisa,”
alisema yule mkuu wa gereza, nikawa naendelea kumsikiliza kwa

425 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

makini.
“Kwa kuwa wewe ni kijana wa Mutesigwa, na mimi na Mutesig-
wa tumekuwa na uhusiano mzuri sana baina yetu, nitakuwa sahihi
nikisema kwamba wewe pia ni mmoja kati yetu?”
“Sijakuelewa!”
“Utanielewa usiwe na wasiwasi! Najua ni nini kilichowaleta
huku na ni jambo ambalo tulikuwa tunalitarajia, hata asubuhi ya
leo nilizungumza na Mutesigwa na akaniambia kwamba kwa jinsi
anavyokuja, lazima utakuja hapa gerezani na timu yako. Ambacho
hatukuwa tunakijua ni lini na saa ngapi mtakuja!” alisema, nikawa
naendelea kumtazama kwa makini jinsi alivyokuwa anababaika.
“Bado sijakuelewa!”
“Sikiliza kijana wangu! Ni wewe pekee ndiye unayeweza kuni-
saidia kutoka kwenye huu mtego hatari nilionasa ndani yake,
ukinisaidia mimi utakuwa pia umemsaidia Mutesigwa, tupo tayari
kukupa chochote unachokitaka lakini nakuomba sana utoe ripoti
kwamba huku kilakitu kipo sawa.”
“Kitu gani ambacho kipo sawa?”
“Mlichokuja kukifuata.”
“Unajua tumefuata nini?”
“Najua, najua kwamba...” alisema mkuu wa gereza akiwa anaba-
baika na hofu kubwa iliyokuwa inajionesha dhahiri kwenye uso
wake ilionesha wazi kwamba ni yeye ndiye aliyekuwa akimpa
Mutesigwa nafasi ya kufanya aliyokuwa akiyafanya, huku waki-
udanganya ulimwengu kwamba Mutesigwa alikuwa gerezani.
“Chief Kenny!” sauti ya baba yake Saima ndiyo iliyokatisha

426 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

mazungumzo yetu, wote tukamgeukia na kumtazama, akanionesha


kwa ishara kwamba muda ulikuwa unaenda na hakuna tena muda
wa majadiliano.
“Nijibu swali moja tu kwanza!” nilisema kwa sauti ya chini huku
nikimtazama kwa makini usoni.
“Swali gani?”
“Mutesigwa yupo humu gerezani au hayupo?” nilimuuliza, ajabu
ni kwamba alishindwa kulijibu swali langu, akawa anababaika,
akili za haraka zikanituma kuamini kwamba alichokuwa anakifan-
ya pale ilikuwa ni kupoteza muda kwa makusudi kwa sababu zake
binafsi.
“Naomba mimi na wewe tuzungumze tukishamaliza kazi ili-
yotuleta, naamini tutafikia muafaka mzuri tu,” nilimwambia huku
nikigeuka na kuanza kupiga hatu andefu kurudi kule nilikowacha
wenzangu ambao walikuwa wakisubiri maelekezo kutoka kwangu
ili kazi ianze.
Mkuu wa gereza akawa ananifuata nyuma huku na yeye akipiga
hatua ndefu, nikawakagua vijana wangu kwa mara ya mwisho na
baada ya kujiridhisha kwamba kila kitu kipo sawa, ilitoa ishara ya
kuonesha kwamba kazi imeanza rasmi.
Kwa kuwa kila mmoja alikuwa ameshaelewa maelekezo ya
anachotakiwa kufanya, tuligawanyika, wale waliokuwa wanat-
akiwa kulizunguka gereza kwa nje walitawanyika kwa utaratibu
maalum, wakiongozana na askari magereza kadhaa kisha sisi wen-
gine tukawa tunaelekea kwenye lango kuu la kuingilia gerezani.
Ndani ya muda mfupi tu, tayari tulikuwa tumelifikia lango la ge-

427 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

reza, nikamgeukia mkuu wa gereza kumpa ishara kwamba awape


amri vijana wake watufungulie, kweli akafanya hivyo huku jasho
jingi likimtoka licha ya kwamba kulikuwa na upepo mkali ulio-
kuwa unapuliza kutokea baharini.
Kituo cha kwanza, ilikuwa ni kwenye ofisi ya mkuu wa gereza,
nikamtaka atufungulie ofisi yake, kweli akafanya hivyo, mimi,
baba yake Saima, Chief Mwaipopo na baadhi ya askari magereza,
wakiongozwa na mkuu wa gereza mwenyewe, tuliingia mpaka
ndani ya ofisi yake.
Nikaomba kupatiwa ‘counter book’ kubwa lililokuwa na taarifa
za wafungwa wote ndani ya gereza lile, akafanya kama nilivyo-
muagiza, nikalichukua daftari lile kubwa kisha nikamueleza kwa
sauti ya chini kwamba anatakiwa kutuongoza mpaka kwenye
mabweni ya wafungwa walipokuwa wafungwa wote kama ili-
vyokuwa inaonesha kwenye daftari lile.
Kama nilivyoeleza awali, gereza hilo lilikuwa ni la siri na hata
wafungwa waliokuwa wakishikiliwa, walikuwa ni wale watukutu,
wenye kesi nzito ambao kuwachanganya na wafungwa wengine
ingekuwa ni jambo la hatari.
Tofauti na magereza mengine, gereza hilo kila mfungwa alikuwa
akiishi kwenye kichumba chake peke yake, vyote vikiwa na mi-
lango ya chuma, vikiunganishwa na korido ndefu ambayo nayo
ilikuwa na mageti ya chumakila baada ya mita kadhaa.
“Naomba uwe unatoa maelezo kwenye kila hatua tunayoipi-
tia, nataka kuwajua wafungwa wote waliopo humu kwa kutumia
mwongozo wa hiki kitabu,” nilimwambia huku nikimrudishia kile

428 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kitabu maalum chenye taarifa za wafungwa wote, akanitazama kwa


macho ya hofu.
Ilibidi afanye kama nilivyokuwa nimemuelekeza, akawa anatuta-
jia mfungwa mmoja baada ya mwingine kuanzia jina lake, namba
yake ya gerezani na makosa yaliyofanya akafungwa kwenye gereza
hilo.
Wafungwa kumi wa mwanzo ambao ndiyo waliokuwa kwenye
jengo la kwanza tuliloanzia kufanya ukaguzi, taarifa zao zilikuwa
zikifanana na taarifa zilizoandikwa kwenye kitabu kile na wote
walikuwepo kwenye selo zao.
Tulielekea kwenye jengo la pili, ambapo kulikuwa na wafungwa
sita tu huku selo nyingine zikiwa tupu, nako maelezo yao yalikuwa
yakifanana na taarifa zilizokuwepo kwenye kitabu kile.
Alitupitisha kwenye miundombinu mingine ya gereza hilo kabla
hatujapita kwenye uwanja mpaka uliokuwa katikati ya gereza na
kuelekea upande wa pili ambako nako kulikuwa na majengo men-
gine kama manne hivi, likiwemo jengo moja ambalo lilikuwa ni
maalum kwa viongozi au watu wakubwa serikalini ambao walikut-
wa na makosa mbalimbali. Nitafafanua kuhusu hili baadaye.
Tuliingia kwenye jengo la kwanza, kulikuwa na wafungwa sita
tu, ambao kama wale wenzao, nao walikuwa wamefungiwa kwe-
nye selo maalum, tukawakagua mmoja baada ya mwingine, nao
taarifa zao zilionesha kuwa sawa na zile zilizokuwa kwenye kile
kitabu maalum chenye taarifa za wafungwa.
Tukaingia kwenye jengo la pili kwenye upande huo, kulikuwa
na wafungwa watatu tu ambao nao taarifa zao zilikuwa zikiendana

429 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

na taarifa za kwenye kitabu, kengele ya hatari ikaanza kugonga


kwenye kichwa changu.
Taarifa nilizopewa na yule askari magereza mmoja kule nje, zil-
ionesha kwamba kwa wakati huo, kulikuwa na wafungwa ishirini
na saba ndani ya gereza, taarifa ambazo pia zilikuwa zinaendana na
taarifa zilizokuwa ndani ya kile kitabu cha wafungwa.
Mpaka wakati huo, hesabu zilikuwa zinaonesha kwamba tume-
wakagua wafungwa 25 pekee, jengo la kwanza kabisa lilikuwa na
wafungwa kumi, jengo la pili kulikuwa na wafungwa sita, jengo
la tatu wafungwa sita na jengo la nne wafungwa watatu, kwa hiyo
jumla yao ni wafungwa 25.
Mpaka muda huo, hatukuwa tumemfikia Mutesigwa na mfungwa
mwingine mmoja na tulikuwa tumemaliza majengo yote ya wa-
fungwa wa kawaida, isipokuwa kwenye lile jengo moja tu la wa-
fungwa viongozi au wanasiasa mashuhuri.
Wasiwasi niliokuwa nao, ulikuwa sawa na aliokuwa nao baba
yake Saima na Chief Mwaipopo, tukaondoka upande huo na kuele-
kea kwenye lile jengo maalum la wafungwa maalum.
Milango ya chuma ilifunguliwa, tukaingia huku tukimfuata mkuu
wa gereza, akatupeleka mpaka kwenye chumba cha ndani kabisa
ambako kulikuwa na mfungwa mmoja.
“Huyu ni nani? Kwa nini amewekwa kwenye jengo hili la wa-
fungwa maalum na vipi kuhusu mfungwa mwingine ambaye ndiye
hasa tuliyekuwa tunamtafuta? Mutesigwa yuko wapi,” nilimuuliza
mkuu wa gereza kwa sauti ya mamlaka.
“Atakuwepo, alikuwepo, eti afande Johnson, atakuwa ameenda

430 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wapi?” alisema mkuu wa gereza huku akionesha kuchanganyikiwa


kuliko kawaida kiasi cha kuanza kujiumauma, akiwa hata haelewe-
ki ni nini alichokuwa anakizungumza.
Tulitazamana, kila mtu akawa haamini kama mwisho wa jitihada
zote ungeweza kuwa ni kile tulichokutana nacho. Ilibidi tuanze ku-
kagua chumba kimoja baada ya kingine, hakukuwa na mtu mwing-
ine yeyote zaidi ya yule mzee ambaye naye alionesha kutokuwa na
habari na ujio wetu eneo lile.
Wakati tukiendelea kukagua selo moja baada ya nyingine, tu-
libaini kwamba kulikuwa na mazingira ambayo hayafanani na ge-
reza ndani ya jengo lile. Kwa kifupi ni kwamba ilionesha ni kama
kuna mtu au watu ambao wanaishi maisha yao wakiwa ni kama
wapo uraiani wakati wapo gerezani.
Kulikuwa na vyumba kadhaa ambavyo vilikuwa safi kabisa,
vikiwa na vitanda vyenye magodoro kama ya nyumbani, kulikuwa
na samani kama za nyumbani yakiwemo masofa na kulikuwa na
mpaka runinga na redio, vyote vya kisasa.
Kulikuwa na majiko mawili, moja la umeme na lingine la gesi,
kulikuwa na friji kubwa na vitu vingine kadhaa mbavyo vilitu-
fanya wote tupigwe na butwaa kuliko kawaida. Hakuna aliyeamini
kwamba mambo kama hayo yanaweza kufanyika ndani ya mager-
eza yetu.
“Bila shaka humu ndimo anamoishi Mutesigwa! Tunachotaka ku-
jua ni wapi alipo, mengine tutajua mbele ya safari,” nilimwambia
mkuu wa gereza ambaye alikuwa akitufuata nyumanyuma wakati
tukiendelea kushangaa hali halisi ya kila kilichokuwa kinaendelea

431 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

gerezani humo.
“Mutesigwa yuko wapi?” nilirudia kumuuliza mkuu wa gereza,
akawa hana majibu.
Mutesigwa alikuwa mfungwa ambaye vyombo vyote vya ulinzi
na usalama vilikuwa vinajua kwamba yupo gerezani, tena kwenye
gereza maalum lililopo Mafia, tena kisiwani.
Inakuwaje tena tumefika kwenye gereza husika halafu tunakutana
na mapichapicha kama yale, ikionesha wazi kwamba mtuhumiwa
alikuwa akiishi maisha ya kifahari kiasi kile? Lakini yote tisa, kumi
ni wapi alipokuwa Mutesigwa kwa wakati huo? Hakuna aliyekuwa
na majibu.
Ilibidi sisi watatu tusogee pembeni kwanza kwa sababu tuliona
ni kama mkuu wa gereza anataka kutuletea mchezo wa kitoto.
Tulianza kujadiliana pale kuhusu nini cha kufanya, tukakubaliana
kwamba kitu cha kwanza ni lazima tufanye upekuzi wa kina ndani
ya lile jengo ambalo ndilo tuliloelekezwa kwamba Mutesigwa
alikuwa akishikiliwa.
Nilitoa wazo kwamba awali alipokuwa gerezani jijini Dar es
Salaam, Mutesigwa na genge lake walikuwa na kawaida ya kuingia
na kutoka gerezani nyakati za usiku kwa kutumia njia maalum ya
chini ya ardhi, kupitia kwenye chemba za maji machafu.
Kila mmoja alikubaliana na nilichokuwa nimekisema, tu-
kakubaliana kwamba tutachunguza kila kitu hatua kwa hatua ili
tupate majibu kamili.
Lakini pia tulikubaliana kutoa taarifa kwa uongozi wa juu na ku-
toa mapendekezo ya nini kifanyike ambapo jambo la kwanza na la

432 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

muhimu, ilikuwa ni sisi kumuweka chini ya ulinzi mkuu wa gereza


na kuondoka naye ili akatueleze kwa kina ni nini hasa kilichokuwa
kinaendelea.
Akili yangu ilikuwa ikienda mbio kuliko kawaida, yale matarajio
makubwa ambayo nilikuwa nayo ndani ya mopyo wangu kwamba
tunakaribia kuhitimisha kazi kubwa na ngumu iliyokuwa mbele
yetu, yaliyeyuka mithili ya theluji iyeyukavyo kwenye jua kali.
Kwa jinsi nilivyokuwa namfahamu Mutesigwa, shughuli yake
haikuwa nyepesi hata kidogo na kibaya ni kwamba muda tulio-
kuwa tumebakiwa nao ulikuwa unaelekea mwishoni tukiwa bado
hatujafanikiwa kuzima mpango huo.
“Naona umeamua kutuchezesha mchezo wa kitoto, si ndiyo?”
“Kenny! Nilishakuomba kuanzia mwanzo kwamba hili suala
tunakutegemea wewe ndiyo unisaidie, na hata kama utashindwa
kunisaidia mimi, basi fanya kwa ajili ya Mutesigwa,” alisema yule
mkuu wa gereza, nikajikuta nimepandwa na jazba kiasi ambacho
kama nisingejizuia, pengine ningemsababishia madhara makubwa
sana palepale.
“Hivi una akili timamu kweli? Unalipwa mshahara na serikali,
lakini kumbe hiki ndicho unachokifanya huku! Huu ni zaidi ya
uhaini,” nilimtolea maneno makali sana kwa sauti ya chini kiasi
ambacho ni mimi na yeye pekee ndiyo tuliokuwa na uwezo wa
kusikia nilichokuwa nakisema.
“Sasa sikiliza, kwa kuwa unataka kucheza mchezo wa kitoto, sisi
tutakuonesha mchezo wa kikubwa! Upo chini ya ulinzi,” nilisema
huku nikiikoki bunduki yangu na kumnyooshea.

433 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Kwa kuwa nilikuwa nimeshawapa taarifa wenzangu wote kuhusu


kinachotakiwa kufanyika, kila mmoja alikuwa ‘standby’ kusubiri
kuona ni nini kinachokwenda kutokea.
Kitendo cha mimi kumnyooshea bunduki mkuu yule wa gereza,
hakikupokelewa vizuri na wale askari magereza ambao yeye ndiye
aliyekuwa kiongozi wao, wakawa ni kama wamepigwa na butwaa,
wakiwa hawaamini walichokuwa wanakiona.
“Inua mikono juu kisha geuka nyuma,” nilisema kwa sauti ya
mamlaka, nikiwa sina hata chembe ya masihara, tayari nilishavaa
ile sura yangu kamili ya kazi. Huku akinitazama kwa macho yali-
yojawa hofu kubwa, alitekeleza kile nilichomwambia, akageuka.
Kwa tahadhari kubwa nilimsogelea kisha nikamkamata mikono
yake na kumfunga pingu kwa nyuma. Unaweza kushangaa mamla-
ka ya kufanya jambo kama hilo tuliyatoa wapi wakati kile kilikuwa
ni chombo kingine kilichokuwa kinajitegemea?
Tulishapewa mamlaka na namba moja mwenyewe kwamba
tufanye kila kinachowezekana na yeye ndiye atakayewajibika, cha
msingi ni kuhakikisha tunawakamata wahalifu wote na kuzima
jaribio lile.
Baada ya kufanikiwa kumuweka chini ya ulinzi, nilimwambia
anatakiwa kuwatuliza vijana wake na kufuata maelekezo ambayo
nitakuwa nampa.
“Unatakiwa kuongoza njia kuelekea ofisini kwako, vijana wako
wote pia wanatakiwa kuongozana na wewe.”
“Hapana! Hilo haliwezekani, wafungwa wanaweza kutoroka!”
“Kwa hiyo hawa wafungwa wengine wakitoroka ndiyo inaoneka-

434 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

na tatizo, lakini Mutesigwa akitoroka ni kawaida kabisa.”


“Hajatoroka!”
“Yuko wapi?” nilimuuliza mkuu wa gereza, akawa hana majibu
ya kunipa, nikarudia kumuonya kwamba hatutaki mchezo wa ki-
toto kwa sababu hatukuwa na muda kwa ajili ya michezo hiyo.
Ilibidi akubali, akazungumza maneno fulani hivi kisha askari
wake ambao walikuwa wameinua silaha zao, wakazishusha na
kuanza kutoka kwa tahadhari kubwa, wote tukatoka mpaka nje,
pale katikati kwenye uwazi mkubwa mle gerezani.
Vijana wangu kwa muda wote huo nao walikuwa ‘standby’ na
muda wote silaha zilikuwa mikononi, kwa ajili ya kutekeleza amri
yoyote ambayo ingetolewa.
Tuliwasogeza askari magereza wote waliokuwa mle ndani mpaka
kwenye ofisi ya mkuu wa gereza ambaye tayari alikuwa na pingu
mikononi huku mimi nikiwa naye bega kwa bega.
Baada ya kuingia kwenye ofisi ya mkuu wa gereza, kama tu-
livyokuwa tumekubaliana, ilibidi wenzangu waendelee na kazi
kule nje na baadhi wabaki na mimi kama ‘backup’, nikamueleza
mkuu wa gereza kwamba nahitaji tuzungumze sisi wawili tu, mimi
na yeye.
Aliwapa maelekezo askari wake ambao ilibidi wasogee pem-
beni, na mimi nikawapa maagizo vijana wangu, nao wakasogea
pembeni. Kilichokuwa kinaendelea, ilikuwa ni kutunishiana misuli
hadharani baina ya vikosi viwili, sisi tukionesha kujikamilisha kwa
kila kitu.
“Yatakufika mambo mabaya sana endapo utaendelea kutuficha

435 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kuhusu Mutesigwa, tunayo idhini kutoka juu ya kufanya chochote


ilimradi kazi ikamilike. Nataka kujua Mutesigwa yuko wapi?”
“Yupo!”
“Wapi!”
“Ametoka kidogo lakini yupo.”
“Ametoka kwenda wapi? Ni sheria gani zinazoruhusu mfungwa
kutoka usiku gerezani?”
“Haya mambo yanazungumzika chief!”
“Yanazungumzika? Unawezaje kutoa majibu mepesi namna hii
wakati unajua kabisa nchi ipo kwenye hatari? Hujui ni nini kina-
choendelea Magogoni si ndiyo?”
“Chief, nayatambua makosa yangu lakini ukiendelea kunikan-
damiza namna hiyo, hatuwezi kufanikisha chochote, mimi ni mtu
mzima, huwa wanasema mtu mzima hakosei lakini mimi nakiri
kwamba nimekosea!
“Naomba nafasi ya kurekebisha makosa yangu, niko chini ya
miguu yako,” alisema mkuu wa gereza, huku akitaka kunipigia
magoti, nikamzuia.
“Mimi sihitaji kusujudiwa! Kampigie magoti Mungu wako, mimi
nasimamia kazi yangu, siwezi kukubali mtu mmoja aniharibie kazi,
siwezi kukubali mtu mmoja ashiriki kulihujumu taifa ukategemea
nitakaa kimya, hapana!” nilisema kwa sauti ya mamlaka.
“Naelewa Kenny, tafadhali sana naomba unisaidie na mimi nita-
kusaidia!” alisema, safari hii machozi yakiwa yanamlengalenga.
“Nakusikiliza!”
“Unajua mimi nimebakiza miaka michache tu kabla ya kustaafu,

436 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

mwakani mwezi kama huu nitakuwa tayari nimestaafu. Kwa bahati


mbaya, sikuwa nimejipanga vizuri, mwisho nikajikuta nikiangukia
kwenye tamaa mbaya!” alisema mkuu wa gereza kwa sauti ya
chini, huku akionesha kuwa na hofu kubwa mno ndani ya moyo
wake.
“Mutesigwa alipoletwa hapa gerezani, siku za mwanzo alikuwa
akijaribu sana kunishawishi niwe namsaidia katika baadhi ya
mambo yake na yeye atakuwa akinilipa fedha za kutosha lakini
nikawa sipo tayari kukubaliana naye kwa sababu naijua miiko ya
kazi yangu.
“Hali iliendelea hivyo, ikawa kila anapopata nafasi ya kuzung-
umza na mimi, anaongeza dau tu, mwisho nikajikuta nikiingiwa na
tamaa na kuamua kuwa namsaidia katika mambo yake kwa usiri
mkubwa.
“Tangu wakati huo, nimekuwa nikimsaidia na kiukweli naye
amekuwa akinilipa vizuri, pengine kuliko hata kile ninacholipwa
katika kazi yangu. Nakiri nimefanya makosa, nimeikosea taaluma
yangu, nimelikosea taifa langu na nimemkosea Mungu wangu,”
alisema, ukimya ukapita kati yetu.
“Umekuwa ukimsaidia kufanya nini na nini?”
“Kwanza nimekuwa nikimruhusu kuonana na wageni wake wa-
naokuja mara kwa mara hapa gerezani, jambo ambalo ni kinyume
na gereza hili. Lakini pia nimekuwa nikimruhusu kutoka nyakati za
usiku na kurejea alfajiri. Nimemhamisha kutoka kwenye selo aliyo-
pangiwa awali na kumpeleka kule kwenye jengo maalum ambako
amekuwa akiishi kama yupo nyumbani kwake.”

437 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Amekuwa akitoka mara ngapi kwa wiki?”


“Mara mbili mpaka tatu, mara nyingi siku za mwisho wa wiki
ndiyo huwa anatoka na mara mojamoja katikati ya wiki kama hivi
leo.”
“Aliondoka saa ngapi leo?”
“Saa moja jioni, mara nyingi huwa anatoka saa tatu mpaka saa
nne usiku na kurejea saa kumi au saa kumi na moja alfajiri.”
“Kwa nini leo ameondoka saa moja jioni?”
“Sijajua lakini aliniambia kuna dharura.”
“Amekuwa akitumia simu akiwa gerezani, kweli au si kweli?”
“Ni kweli!”
“Anazo simu ngapi?”
“Anazo simu mbili.”
“Namba zake unazijua?”
“Hapana.”
“Alizipataje hizo simu wakati aliletwa hapa akiwa hana simu?”
“Alinituma nikamnunulie.”
“Kwa hiyo ulienda kuzinunua wewe si ndiyo?”
“Ndiyo!”
“Anapokuwa anatoka hapa gerezani, huwa anakwenda wapi?”
“Kwa mujibu wa vijana wangu, huwa anakwenda Kibiti.”
“Kwa mujibu wa vijana wako gani?”
“Askari wangu ambao huwa wanamsindikiza.”
“Unasemaje?” nilimuuliza kwa mshangao mkubwa. Kumbe licha
ya mkuu wa gereza kuwa anamruhusu Mutesigwa kutoka nje ya
gereza kinyume cha sheria, kumbe pia huwa anampa na ulinzi wa

438 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

askari magereza ambao huondoka nao na kurudi nao.”


“Nataka majina ya askari ambao wamekuwa wakimsindikiza,”
nilimwambia, akashusha pumzi huku akionesha bado kuwa na
wasiwasi mkubwa sana ndani ya moyo wake.
“Ni wawili tu, hao ndiyo ambao wamekuwa wakiongozana naye
kwenye safari zake zote na ni yeye ndiye aliyewachagua.”
“Majina yao tafadhali na nataka kujua wako wapi kwa sasa,”
niliendelea kumshikia bando, akanitajia majina yao na kunielezak-
wamba kwa wakati huo, walikuwa wameondoka na Mutesigwa.
“Namba zao za simu?” nilimuuliza, akasogea upande wa nyuma
wa meza yake, akafungua kwenye kabati kubwa la mbao lililokuwa
ukutani na kutoa faili moja, akalipekua kisha akaandika namba
mbili za simu na majina yake kisha akanikabidhi.
“Nataka uniambie tunampataje Mutesigwa!”
“Mimi nashauri tuendelee kusubiri kwa sababu lazima atarudi
tu.”
“Hapana! Hatuwezi kumsubiri mpaka alfajiri, akipewa taarifa
huko aliko unadhani atarudi?”
“Hakuna mtu wa kumpa taarifa, leo hakuna mawasiliano kabisa
tangu mchana, simu haziingii wala hazitoki.”
“Huko anakokwenda si anaweza kukutana na watu wakam-
tonya?”
“Hata wakimtonya, vijana wangu lazima wamrudishe hapa, hayo
ndiyo makubaliano yetu na hajawahi kuyavunja hata mara moja.
Atarudi tu.”
“Usalama wako ni kupatikana kwa Mutesigwa, kwa hiyo kama

439 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

unataka kuleta ujanja wa aina yoyote ili kumsaidia, tambua kwam-


ba unajikaanga kwa mafuta yako mwenyewe.”
“Naelewa hilo! Lakini samahani nilikuwa na ombi.”
“Ombi gani!”
“Vijana wangu wananiheshimu sana, kuniona nikiwa nime-
fungwa pingu namna hii ni jambo ambalo linaniumiza mno ndani
ya moyo wangu, nakuomba kama inawezekana, unifungue, siwezi
kukimbia na naahidi kutoa ushirikiano wa kutosha.”
“Hapana! Hilo haliwezekani, labda kwa kukusaidia, kaa kwe-
nye kiti chako na kutulia,” nilimwambia, akawa bado anaendelea
kunisihi.
“Kaa kwenye kiti chako nijadiliane na wenzangu kwanza, in-
awezekana lakini lazima kwanza utii ninachokueleza,” nilimwam-
bia, kweli akasogea kwenye kiti chake na kuketi, akashusha pumzi
ndefu akinitazama.
“Mutesigwa amekuwa akikutaja sana, sijawahi kumsikia akimho-
fia mtu kama anavyokuhofia wewe. Sasa nimeanza kuelewa ni kwa
nini!” alisema mkuu wa gereza, nikatulia kama sijasikia chochote.
Bado nilikuwa nikiendelea kuzunguka huku na kule ndani ya ofisi
yake, nikiyachuja kwa makini yale yote aliyonieleza, nikahisi
kichwa kinapata moto. Ilikuwa ni lazima Mutesigwa apatikane
kabla jogoo la kwanza halijawika.
Baada ya kuzunguka kwa kama dakika nzima hivi, nilipata wazo,
ikabidi nitoke, nikawapa ishara vijana wangu wawili waingie kwa
ajili ya kuendelea kumlinda mkuu wa gereza asije akafanya mambo
ambayo yataifanya kazi yetu izidi kuwa ngumu.

440 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Baba yake Saima na Chief Mwaipopo walikuwa wakinisubiri


kwenye korido, nao wakionesha kuwa na shauku kubwa ya kutaka
kujua ni nini kilichokuwa kinaendelea, tukaondoka eneo lile la
korido na kuwaacha baadhi ya vijana wetu wakiwa na wale askari
magereza, wengine tukatoka mpaka kwenye lile eneo la katikati
kwenye uwazi mkubwa.
Vijana wengine walipewa amri ya kujipanga pale kwenye ule
uwazi, sisi watatu tukasogea pembeni na kuanza kujadiliana, kila
mmoja akionesha kuwa na shauku kubwa ya kutaka kujua ni nini
kilichokuwa kimejiri mle ndani ya ofisi ya mkuu wa gereza.
Ilibidi niwaeleze kila kitu alichonieleza mkuu wa gereza, kila
mmoja akawa anatingisha kichwa chake kwa masikitiko makubwa.
Zilikuwa ni habari ambazo wakati mwingine unaweza usiziamini
kirahisi.
Baada ya kujadiliana kwa kina, suala moja baada ya jingine,
tulikubaliana kwamba pengine tumuite Ustaadh Fundi pengine
anaweza kuwa na wazo la nini cha kufanya kwa wakati huo.
Nilitoa ishara kwa vijana wangu ili wamuite Ustaadh Fundi
ambaye alikuwa amebaki kule kwenye korido na wale vijana wetu
wengine pamoja na askari magereza. Hakutakiwa kujua kila kitu,
kwa hiyo nikamueleza yale ambayo tulikubaliana kwamba hata
akiyajua hayawezi kuwa na athari zozote kwetu.
Baada ya kumueleza kwa kifupi, tulitaka kusikia na yeye ana
mawazo gani, kwamba tuendelee kusubiri mpaka alfajiri Mute-
sigwa atakaporejea ndiyo tumtie nguvu au tufanye nini.
“Kwa Jografia ya huku jinsi kulivyo, hata tukisema tuingie

441 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

mtaani kwenda kumsaka, itakuwa vigumu sana, kama mnavyoona


eneo lote hili limezungukwa na bahari, nashauri tusubiri tu mpaka
huo muda akirejea ndiyo mambo mengine yaendelee,” alisema,
tukaanza kujadiliana kwa pamoja.
Mawazo ya baba yake Saima, Chief Mwaipopo na Ustaadh
Fundi, yalikuwa ni kwamba tusubiri mpaka alfajiri, mimi peke
yangu ndiyo nikawa siamini kama hiyo inaweza kuwa njia sahihi
kwa wakati huo.
Hoja zangu nilizoziweka mezani ni kwamba tayari tulikuwa
tumewakamata vijana wengi kule kwenye Mji wa Mafia, vijana
ambao walikuwa ni sehemu ya mtandao hatari wa Mutesigwa. Ki-
tendo cha Mutesigwa kuingia uraiani usiku huo, ilikuwa ni lazima
kwamba ataenda kupewa taarifa za vijana wake wengi kusombwa
na kupelekwa kusikojulikana.
Hiyo pekee ingeweza kuwa sababu ya kumfanya Mutesigwa
asirudi tena gerezani kwani angejua kwamba tumeshamshtukia na
tupo mbioni kumkamata kwa mara nyingine kwa hiyo lazima ange-
tafuta njia ya kutoroka moja kwa moja.
Hoja zangu zilitokana na ukweli wa jinsi nilivyokuwa namfa-
hamu Mutesigwa, kipindi chote nilichokuwa chini yake, nilishamt-
ambua ni mtu wa aina gani. Muda wote alikuwa ni mtu anayependa
sana kufikiri kwa kutumia akili nyingi na pengine hiyo ndiyo
iliyokuwa sababu ya yeye kuendelea kuwa tishio kwa taifa hata
wakati yupo gerezani.
“Hata akijua kwamba tumewakamata vijana wake, sidhani kama
anaweza kuhisi kwamba tayari tupo huku gerezani tunamsubiri.

442 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Kwa akili yake lazima anajua kwamba sisi tunajua yeye yupo ge-
rezani kwa hiyo hahusiki na chochote kinachoendelea uraiani kwa
hiyo hata akijua, pengine ndiyo itakuwa sababu ya yeye kuwahi
kurudi gerezani kwa sababu anaamini yupo salama zaidi akiwa
gerezani kuliko akiwa uraiani,” alisema baba yake Saima, maneno
ambayo kwa mbali yalianza kunishawishi nibadili mawazo yangu.
Tuliendelea kujadiliana mambo mengi, mwisho tukakubaliana
kwamba tukae kwa kusubiri lakini ni lazima tujue akiwa anarudi,
huwa anapitia wapi kuingia gerezani na kuwa makini asije akash-
tukia mchezo kabla hajaingia ndani ya eneo la gereza.
Baada ya muafaka huo kufikiwa, tulikubaliana kwamba mimi
nirudi tena kwa mkuu wa gereza kwenda kuendelea kumdadisi.
Wakati nikitaka kugeuka na kuondoka, Chief Mwaipopo alizung-
umza jambo la maana sana.
“Si amekupa namba za simu za askari ambao ameongozana
nao?”
“Ndiyo, hizi hapa,” nilisema huku nikitoa kikaratasi alichonian-
dikia mkuu wa gereza na kukishika mkono.
“Kwa nini wasipewe vijana wetu wa Cyber na teknolojia ya ma-
wasiliano ili wajaribu kuzitrack hizo namba tujue ni wapi walipo?”
“Lakini si mitandao imezimwa?”
“Vipi kama wametoka nje ya eneo mitandao ilipozimwa?” aliika-
zia hoja yake, wote tukakubaliana kwamba alikuwa amezungumza
kitu cha muhimu sana, harakaharaka hilo likafanyika ambapo baba
yake Saima ndiye aliyewasiliana na wenzetu waliokuwa jijini Dar
es Salaam. Akawatajia namba husika na kazi ya kuzifuatilia namba

443 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

hizo ikaanza mara moja.


Wakati hilo likiendelea, wote tukiwa makini kusikiliza ma-
wasiliano yaliyokuwa yakifanaywa kupitia vifaa maalum, mimi
niliondoka nikiwa nimeongozana na Ustaadh Fundi kuelekea kule
kwenye korido ya kuingilia ya kuingilia kwenye ofisi ya mkuu wa
gereza.
Nikamuacha Ustaadh Fundi pale koridoni na vijana wetu wen-
gine pamoja na wale askari magereza, mimi nikaingia ndani ya
ofisi, wale vijana niliowaacha walipoona nimeingia, ilibidi wao
watoke, tukabaki wawili tu ofisini.
Mazungumzo kati yetu yakaendelea, bado akiendelea kunisihi
sana nimsaidie kumnasua kwenye ule mtego.
Kwa kuwa nilikuwa nataka ushirikiano wake wa asilimia mia
moja, nilimwambia nitafanya hivyo endapo na yeye atafanya kazi
yake kwa ukamilifu na kutusaidia kujua hata mambo ambayo hatu-
kuwa tunayajua kumhusu Mutesigwa na maisha yake ya gerezani.
Wakati mazungumzo yakiendelea, mimi nilikuwa makini pia
kufuatilia mawasiliano yaliyokuwa yakiendelea kwenye mifumo
yetu ya mawasiliano. Kwa kuwa nilikuwa nimevaa kifaa maalum,
mkuu wa gereza hakuweza kugundua kwamba kuna kitu nilikuwa
nikikisikiliza kwa makini kwenye kifaa changu cha mawasiliano
nilichokuwa nimekivaa.
Vijana wa teknolojia ya mawasiliano, walikuwa wamefanikiwa
kuziona simu za wale askari waliokuwa wameondoka na Mute-
sigwa na taarifa za awali, zilionesha kwamba walifika Kibiti kisha
baada ya hapo, wakaondoka tena kuelekea upande wa Lindi na

444 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ilionesha walikuwa kwenye gari ambalo lilikuwa likikimbia kwa


kasi kubwa sana.
“Kutoka Kibiti mpaka Lindi kuna umbali gani?” nilimuuliza
mkuu wa gereza, mapigo ya moyo wangu yakinienda mbio kuliko
kawaida. Kama kilometa 300 hivi, ni mwendo wa kati ya saa tatu
mpaka nne kwa mwendo wa gari wa kawaida,” alisema mkuu wa
gereza.
“Unajua kwamba Mutesigwa huwa anakwenda mpaka Lindi?”
“Ndiyo, mara kadhaa vijana wangu wamewahi kuniambia kuhusu
hilo.”
“Anafuata nini Lindi?”
“Sina uhakika lakini vijana wangu wamewahi kunieleza kwamba
kuna watu kutoka Msumbiji huwa wanakutania Lindi kuzungumza
mambo yao ingawa vijana wangu huwa hawaruhusiwi kuingia
wala kusikiliza mazungumzo yao.
“Kwa hiyo huwa anakwenda Lindi na kurudi Kibiti kisha ndiyo
anarudi gerezani?”
“Ndiyo!” alisema, nikawa natafakari kwa kina, bado nikawa sija-
pata kitu kinachounganisha ili kupata picha kubwa zaidi. Nilitoka
tena na kwenda kujadiliana na viongozi wenzangu, nao wakawa
wameshasikia kila kitu kwenye vifaa vya mawasiliano.
Kila mmoja alikuwa na kimuhemuhe kikali ndani ya moyo wake,
tukiwa hatujui kama atarudi kweli au la. Muda ulizidi kuyoyoma,
nikawa na kazi ya kujadiliana na viongozi wenzangu na kurudio
kwenye ofisi ya mkuu wa gereza huku pia tukifuatilia taarifa zilizo-
kuwa zinaingia kupitia vifaa vyetu vya mawasiliano.

445 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Kwenye kama majira ya saa nane hivi za usiku, taarifa mpya


ziliingia kuonesha kwamba simu za wale askari zilikuwa zinaone-
sha kwamba wameondoka Lindi na sasa walikuwa wakirudi Kibiti,
nikashusha pumzi ndefu, nikijua sasa ule muda tuliokuwa tunau-
subiri, umekaribia.
Majira ya kama saa kumi hivi alfajiri, taarifa mpya zilionesha
kwamba tayari ‘location’ ya zile simu ilikuwa haionekani tena
lakini uelekeo wao ulikuwa ni kurudi gerezani, sasa kila mmoja
akawa na uhakika kwamba Mutesigwa anarejea gerezani na ndani
ya muda mfupi atakuwa ameshafika gerezani.
Harakaharaka tulikusanyana upya, tukapeana mipango mipya ya
namna ya kumnasa Mutesigwa, tukatawanyika na sasa kilichokuwa
kinasubiriwa, ilikuwa ni ishara maalum ambayo mimi ndiye nilita-
kiwa kuitoa baada ya kuona msafara wa Mutesigwa ukiwa umek-
aribia gerezani kwa kutumia njia ya maji.
Kila mmoja alikaa kwenye nafasi yake, mimi, baba yake Saima
na Chief Mwaipopo ndiyo tukatangulia mstari wa mbele kabisa
na kujibanza kwenye eneo ambalo boti aliyokuwa anakuja nayo
Mutesigwa na walinzi wake, tulielekezwa kwamba ndipo mahali
ambapo ingefikia, upande wa nyuma wa gereza.
Tulijipanza kwenye mawe na fensi ya michongoma iliyokuwa
upande ule, tukawa tunatazama kwa makini kule baharini, hauku-
pita muda mrefu mlio wa boti ndogo iendayo kwa kasi ukaanza
kusikika, ikija kwa kasi upande ule tuliokuwepo.
Ajabu ni kwamba tulikuwa tunasikia tu muungurumo lakini
hakukuwa na mwanga wowote uliokuwa unaonekana, akili za hara-

446 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ka zikanituma kuamini kwamba lazima walikuwa wamezima taa za


boti ili wasionekane, harakaharaka nikatoa taarifa kwa wenzangu
wote kupitia vifaa vya mawasiliano, kila mmoja akaendelea kutu-
lia.
Muungurumo uliendelea kuongezeka, baada ya muda, boti ndogo
ilionekana ikija, ikiwa na watu wanne ndani yake, mmoja akiwa
amekaa kwa nyuma kuonesha kwamba ndiye aliyekuwa akiiende-
sha boti hiyo.
Mahali nilipokuwa nimejibanza, paliniwezesha kuona vizuri
kwa msaada wa taa za nje ya gereza, nikawa natoa taarifa kwa
kunong’ona kuhusu kila nilichokuwa nakiona na muda mfupi baa-
daye, injini ya boti ilizimwa, ikiwa tayari imeshafika ufukweni.
Wanaume wawili waliteremka na kutangulia mbele, akafuata
mtu wa tatu ambaye kwa kumtazama tu, niligundua kwamba ndiye
Mutesigwa au Bosi Mute kama ambavyo wafuasi wake walikuwa
wakimuita.
Walipotoka kabisa kwenye maji, injini ya boti iliwashwa tena
kisha nikashuhudia kwa macho yangu ikigeuza na kurudi ilikotoka,
ikiwa na mtu mmoja tu ndani yake, nikagundua kwamba pengine
huyo mtu ndiye aliyekuwa akimfuata Mutesigwa kumchukua kisha
kumrudisha alfajiri.
Nilitazama saa yangu ya mkononi, tayari ilikuwa imegonga
saa kumi na dakika ishirini na tano za alfajiri, giza likiwa bado
limetanda, nikawa makini kuendelea kufuatilia kila kilichokuwa
kinaendelea.
Wale wanaume wawili walimuongoza Mutesigwa kuelekea kwe-

447 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

nye lango kuu la kuingilia gerezani, wakiwa hawajui kabisa kwam-


ba tayari walikuwa wanaingia kwenye mtego. Kama tulivyokuwa
tumekubaliana, tuliwaacha wasogee mpaka wafike kwenye eneo la
mbele ya gereza kisha ndiyo tuwapige ‘ambush’.
Kweli walijaa kwenye mtego kirahisi kabisa mpaka nikawa
siamini macho yangu Mutesigwa anaweza kunasa kirahisi namna
hiyo.
Walipofika tu kwenye eneo la wazi la mbele ya gereza, nilitoa
ishara maalum ya kazi kuanza, vijana waliokuwa wameshajipanga
eneo hilo wakajitokeza ghafla na kuwaweka chini ya ulinzi wote
watatu, wakawa wamepigwa na butwaa wakiwa ni kama hawaami-
ni kilichotokea.
Ndani ya sekunde chache, tayari na sisi tulikuwa tumeshafika
eneo lile, nikatoa amri ya wote watatu kunyoosha mikono yao juu,
Mutesigwa akashtuka sana kusikia sauti yangu, akanitazama kwa
mshtuko, mimi na yeye tukawa tunatazamana.
“Nimesema mikono juu kisha taratibu pigeni magoti,” nilisema,
safari hii nikiikoki bunduki yangu ambayo ilikuwa ‘standby’ miko-
noni, tayari kwa chochote.
Mutesigwa aliendelea kunitazama kwa mshangao, akageuka huku
na kule na kujikuta akiwa amenyooshewa zaidi ya mitutu kumi ya
bunduki, nikamuona akishusha pumzi ndefu, akawageukia vijana
wake ambao walikuwa bado hawaamini walichokutana nacho.
Kuna jambo walinong’onezana, Mutesigwa akawa wa kwanza
kuinua mikono juu, akapiga magoti, wale vijana wake nao waka-
fanya hivyohivyo, nilitoa ishara kwa vijana wangu kuwasogelea

448 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kwa makini na kuwafunga pingu, kweli hilo likafanyika kisha


nikaamuru wote walazwe chini, kifudifudi.
Mutesigwa alikuwa amebadilika sana, usingeweza kuamini kama
ni mfungwa, tena anayeshikiliwa kwenye gereza maalum. Ali-
kuwa amenawiri vizuri huku mwili wake ukiwa umejengeka vizuri
kimazoezi, tofauti kabisa na kipindi nilichofahamiana naye ambapo
alikuwa na mwili wa kawaida kabisa.
Baada ya kuhakikisha wote wamelazwa chini, niliagiza wapeku-
liwe, mmoja baada ya mwingine. Wote watatu walikuwa na bastola
kwenye viuno vyao, nikagundua ni kwa nini Mutesigwa alichelewa
kutii amri ya kuinua mikono juu.
Nadhani alikuwa amepanga kuleta upinzani lakini alipotazama
idadi yetu, akajua bastola zao haziwezi kuwasaidia chochote.
Baada ya kuhakikisha hatua zote za kiusalama zimefuatwa, nili-
toa taarifa kupitia kifaa changu cha mawasiliano, kuwaeleza watu
wote kwamba zoezi la kumuweka nguvuni Mutesigwa lilikuwa
limefanikiwa kirahisi kabisa, bila madhara yoyote kutokea, tofauti
kabisa na tulivyokuwa tumefikiria awali.
Mkurugenzi ndiye aliyekuwa wa kwanza kujibu, akatupongeza
na kutueleza kuwa tunatakiwa kumpeleka sehemu salama na alfa-
jiri hiyohiyo anatakiwa kusafirishwa mpaka jijini Dar es Salaam.
Miongoni mwa maelekezo mengine yaliyotolewa, ilikuwa ni ku-
hakikisha gereza linaendelea kuwa chini ya ulinzi mkali na mkuu
wa gereza aendelee kushikiliwa na tuondoke naye mpaka kikosi
maalum kutoka Jeshi la Magereza kitakapowasili kwa ajili ya kui-
marisha ulinzi.

449 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Ilibidi tugawane, vijana saba wenye silaha wakatakiwa kuende-


lea kubaki kwa saa kadhaa kusubiri kikosi maalum kitakapowadia
kisha sisi wengine tuondoke tukiwa na watuhumiwa wetu wanne,
Mutesigwa, askari magereza wawili waliokuwa wakimsindikiza
kwenye shughuli zake kinyume cha sheria na mkuu wa gereza.
Boti tulizozitumia wakati wa kuja, ndizo hizohizo tulizozitumia
kuondoka nazo, Mutesigwa akawa ndiyo mtu ambaye tunapaswa
kumcgunga zaidi katika safari hiyo. Boti ziliwashwa na safari
ikaanza, vijana tuliowaacha kule gerezani wakatoa ishara maalum
ya kutuaga, safari ikapamba moto.
Japokuwa kulikuwa na giza, Mutesigwa alikuwa akinitazama
kwa macho makali sana, na mimi nikawa najifanya sina habari
naye kabisa, safari ikapamba moto. Tukiwa katikati ya safari yetu,
giza likiwa limeanza kupungua kidogo na kufukuzwa na mwanga
wa mapambazuko, kitu kisicho cha kawaida kilitokea na kutufanya
wote tutulie.
Milio ya boti kama tatu hivi ilisikika ikionesha ni kama ilikuwa
inakuja kufuata uelekeo tuliokuwepo. Tulijaribu kuangaza huku na
kule, hakuna chochote ambacho tuliweza kukiona zaidi ya kuende-
lea kusikia miungurumo hiyo ikizidi kuja kwa kasi kule tulikoku-
wepo.
Ilibidi nimsogelee baba yake Saima ambaye alikuwa amekaa na
Chief Mwaipopo, wakiwa wamemzunguka Mutesigwa mle ndani
ya boti.
“Itakuwa yule aliyewaleta amegundua kitu na sasa ameenda
kutoa taarifa kwa wenzake,” nilisema kwa sauti ya chini, wote

450 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wakanitazama.
“Hatushindwi kupambana nao, nguvu yetu ni kubwa!” alisema
Chief Mwaipopo na harakaharaka tukashauriana nini cha kufanya.
Hatua ya kwanza ilikuwa ni kuzima injini za boti zote pamoja na
taa zake, hilo likafanyika, injini zikazimwa pamoja na taa, tukawa
tunaelea kwenye maji huku boti zikitingishwa na mawimbi ya
bahari.
Ajabu ni kwamba, muda mfupi baada ya injini zote kuzimwa
na sisi kumezwa na giza la alfajiri, ile milio ya boti nayo iliacha
kusikika, tukawa tunaendelea kujadiliana nini cha kufanya.
Nilimtazama Mutesigwa, na yeye akanitazama, macho yetu yak-
agongana, nikamuona akitabasamu.
Mpaka hapo nilishapata picha kwamba ni kweli wale walikuwa
ni vijana wengine wa Mutesigwa ambao walikuwa wanatufuatilia
na kitendo cha sisi kuzima boti zetu, kiliwafanya washinddwe kue-
lewa tupo upande gani kwa sababu kulikuwa kimya kabisa, upepo
wa bahari ukiendelea kuvuma.
Niliwatazama vijana wangu, mmoja baada ya mwingine. Ni kwe-
li kwamba wote walikuwa wameiva sana katika medani za kimapi-
gano na ndiyo maana nikawachagua, lakini hakukuwa na yeyote
kati yao ambaye alikuwa na anazijua mbinu za medani kwenye
maji, kwa kifupi ni kwamba wao walikuwa wanajua mapambano
ya nchi kavu zaidi.
Ni sisi watatu pekee, mimi, baba yake Saima na Chief Mwaipopo
ambao angalau tulikuwa na mafunzo ya mapigano ya kwenye maji,
moyo wangu ukaingiwa na wasiwasi kwamba endapo hao walio-

451 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kuwa wakitufuatilia walikuwa wanajua mbinu za mapigano ya


kwenye maji, basi wangeweza kutuzidi nguvu kirahisi.
Nikamsogelea tena baba yake Saima na Chief Mwaipopo, tukawa
tunajadiliana jambo. Ghafla ile milio ya boti ilianza kusikika upya,
safari hii zikionesha kuwa karibu kabisa na pale tulipokuwepo,
apigo ya moyo wa kila mmoja yakawa yanaenda mbio kuliko
kawaida.
Ilitakiwa tuchukue uamuzi wa haraka kadiri iwezekanavyo
vinginevyo tungejikuta kwenye matatizo makubwa na kazi yote
tuliyoifanya yasingekuwa na maana. Wazo ambalo niliona linafaa
kwa wakati huo, ilikuwa ni kukabiliana na kile kilichokuwa mbele
yetu, niliwaamrisha manahodha wote kuwasha njini za boti zao
kisha wawashe taa kumulika kule ile milio ilikokuwa inatokea.
Wakati huohuo, niliwaamrisha vijana wangu wote kukaa tayari
kwa mapambano, kila mmoja akaweka silaha yake tayari kwa kazi.
Injini za boti zote ziliwashwa kisha zinageuzwa, zikawashwa taa
na kuanza kumulika kule ile milio ilikokuwa inatokea.
Boti kama tatu hivi zilikuwa zinakuja kwa kasi, huku zote zikiwa
zimezima taa, kwa msaada wa taa za zile boti zetu, tuliweza kuzi-
ona vizuri boti hizo. Hazikuwa boti kubwa wala za kisasa, ni zile
zinazotumiwa na wavuvi lakini ndani yake zilionesha kuwa na
watu wengi.
Kitendo cha sisi kuzimulika zile boti, ni kama ziliwashtua walio-
kuwa kwenye boti hizo, nao wakawasha taa zao na kutumulika,
kila mmoja bunduki ikiwa mkononi, tayari kujibu mashambulizi
yoyote ambayo yangetokea kwa sababu ilionesha ujio wao siyo wa

452 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

heri.
Nadhani walipoona kila mtu ameshika ‘chuma’, mimi nikiwa
mbele kabisa, walipata hofu ndani ya mioyo yao, wakazima ha-
raka taa za boti zao zote kisha milio ikawa inasikika kuonesha boti
zimebadili uelekeo na kuacha kuja kule tulikokuwa tukiwasubiri na
kurudi kulekule zilikotoka.
Wote tulishusha pumzi ndefu, nikawaamrisha manahodha tu-
endelee na safari, kwa kasi kubwa kuliko iliyokuwa ikitumika
mwanzo. Nilimgeukia Mutesigwa, nikamuona akiwa ameinamisha
kichwa chake, nadhani kuna jambo alitarajia litatokea lakini hali-
kutokea.
Safari ikaendelea, boti zote zikawa zinafukuzana kwa kasi kub-
wa. Ilikuwa ni lazima tufike nchi kavu haraka iwezekanavyo ili ku-
jihakikishia usalama kwa sababu kama nilivyoeleza, kikosi changu
hakikuwa na utaalamu wa kupambana kwenye maji.
“Watakuwa ni akina nani hawa washenzi wanaotaka kutujaribu?”
alisema baba yake Saima huku akiishusha bunduki yake chini,
watu wote wakashusha bunduki zao, ukimya ukapita, hakukuwa na
aliyekuwa na majibu kwa baba yake Saima.
Safari iliendelea kwa kasi kubwa, giza la alfajiri nalo likawa
linazidi kukimbizwa mbali na nuru ya mapambazuko na hatimaye
tulianza kuona taa kutokea upande wa pili, kuashiria kwamba tu-
libakiza umbali mfupi kabla ya kufika nchi kavu.
Tukiwa tumekaribia kufika ufukweni, milio ya boti ilianza
kusikika tena zikija kwa kasi, nikawahimiza manahodha kuongeza
kasi na kwa bahati nzuri, tulifanikiwa kuwasili kwenye gati ambalo

453 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ndilo tulilotumia kuondokea.


Harakaharaka nikaamrisha watuhumiwa wetu wote waondolewe
haraka kwenye boti na kupelekwa sehemu salama, huku kazi
ya kumdhibiti Mutesigwa nikiiacha kwenye mikono ya Chief
Mwaipopo, tukateremka harakaharaka kwenye boti, mimi nikawa
makini kuziangalia zile boti ambazo kwa kuwa sasa kulikuwa
kumeshaanza kupambazuka, zilionekana vizuri zikiwa mbali
kidogo.
Niliwapanga vijana wangu kwa ajili ya kujibu mashambulizi
endapo wakijaribu kutushambulia kwa sababu akili zangu zilini-
tuma kuamini kwamba safari hii kwa kuwa walikuwa wameshaona
tupo wangaopi na tuna silaha nzito kiasi gani, lazima watakuwa
wameenda kujipanga upya.
Nilichokiamini ni kwamba tayari walikuwa wameshachelewa
kwa sababu kama kulikuwa na sehemu ambayo wangeweza kutu-
zidi nguvu kwa urahisi, ilikuwa ni kule katikati ya bahari.
Watuhumiwa wote waliteremshwa chini ya ulinzi mkali na kuon-
gozwa mpaka pale magari tuliyoyatumia kutoka kule tulikokuwa
tumeweka kambi mpaka kwenye bandari hiyo ndogo. Mimi na vi-
jana wangu kadhaa tukawa bado tupo palepale kwenye gati kuwa-
soma wale wendawazimu waliokuwa wakitufuata na boti.
Wakati hayo yanaendelea, tulikuwa tukiendelea kutoa taarifa
kupitia vifaa vyetu vya mawasiliano, moja kwa moja kwa kutu-
mia vifaa vyetu vya mawasiliano. Baada ya Mutesigwa kuingizwa
kwenye gari chini ya ulinzi mkali pamoja na wale vijana wake,
akiwemo na mkuu wa gereza, tulipeana ishara kwamba hatuwezi

454 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kuendelea kupoteza muda kupambana na wale watu waliokuwa


wanakuja kwenye boti.
Nikawapa ishara vijana wangu ambapo harakaharaka wote
tuliondoka na kukimbilia kwenye magari, safari ikaanza muda
huohuo kuelekea Shule ya Sekondari Kitomondo, Mafia, maha,li
ambapo tulikuwa tumeweka kambi yetu ya muda.
Ilikuwa ni lazima kila kitu kifanyike haraka kwa sababau kama
nilivyokuwa nimeeleza, tuliweka kambi kwenye madarasa ya shule
hiyo ya sekondari na siku hiyo ilikuwa ni siku ya kawaida kwa
hiyo lazima wanafunzi wangeanza kuwasili baada ya kuwa kume-
shapambazuka kabisa.
“Ulisema kabla jogoo la kwanza halijawika tutakuwa tumempata
Mutesigwa, na hilo limetimia. Itakuwa sawa kama nikikuita Sheikh
Yahaya?” alisema baba yake Saima katikati ya ukimya uliokuwa
umetawala ndani ya gari tulilokuwa tumepanda, sisi tukiwa mbele
kabisa.
Kauli hiyo ilisababisha wote tucheke ndani ya gari, safari
ikaendelea ambapo dereva wa gari letu lililokuwa mbele ya msa-
fara, alikuwa akipangua gia kwa umahiri wa hali ya juu. Hatimaye
tuliwasili kwenye shule hiyo, ikiwa ni kama saa kumi na moja na
nusu hivi.
Kilichonifurahisha sana baada ya kufika kwenye shule hiyo, ni
kwamba maandalizi yote yalikuwa yameshakamilika, helikopta
zilikuwa zikitusubiri eneo hilo, gari maalum la kubebea wafungwa
au watuhumiwa, nalo lilikuwa limeshawasili kwa ajili ya kuwachu-
kua wale vijana wote tuliokuwa tumewakamata lakini pia kulikuwa

455 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

na magari mengine kadhaa kutoka Jeshi la Polisi, ambayo yalikuwa


yamefika kutuongezea nguvu.
Tulipowasili tu, kazi kubwa ya kwanza ilikuwa ni kwa mtuhu-
miwa namba moja, Mutesigwa na wale wenzake, kupandishwa
kwenye helikopta kwa ajili ya kusafirishwa haraka iwezekanavyo
kupelekwa jijini Dar es Salaam.
Lakini pia kuwasafirisha wale watuhumiwa wote mpaka Kibiti,
sehemu ambapo taratibu nyingine zingeendelea. Kwa hiyo tu-
lichokifanya, ilikuwa ni kugawana majukumu, mimi nilitakiwa
kuendelea kubaki kuhakikisha kila kitu kinakwenda vizuri, Chief
Mwaipopo na baba yake Saima walitakiwa kusafiri na watuhumiwa
wote mpaka jijini Dar es Salaam kwa kutumia helikopta moja na
ile helikopta nyingine ingetumika kutusafirisha mimi na vijana
wangu ambao tungesalia, mpaka Kibiti.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, Mutesigwa akakokotwa mpaka
kwenye helikopta na watuhumiwa wenzake, mara kwa mara akawa
ananigeukia na kunitazama kwa macho makali lakini sikuwa nam-
jali kabisa.
Haukupita muda mrefum, helikopta ya kwanza ikapaa na safari
ya kuelekea jijini Dar es Salaam ikaanza.
Mimi na vijana wangu, tulisaidiana na askari wengi waliokuja
kutuongezea nguvu, tukawatoa watuhumiwa wote waliokuwa
wamekamatwa mchana wa jana yake, wakapandishwa kwenye
karandinga, wengine wakapandishwa kwenye magari ya polisi na
safari ya kuelekea Kibiti ikaanza.

456 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

17
B
AADA ya msafara huo kuondoka, ndipo mimi na
vijana wangu waliokuwa wamesalia, pamoja na Usta-
adh Fundi, tukapanda kwenye helikopta ya mwisho
na safari ikaanza.
Tukiwa angani, nilianza kuwaona wanafunzi wach-
ache wakiwa wanaelekea shuleni, moyoni nikajipongeza kwa sa-
babu kila kitu kilikuwa kimefanyika kwa ustadi wa hali ya juu kiasi
kwamba hata wanafunzi wasingeweza kujua ni nini kilichokuwa
kimetokea.
Kasi ya kuusindikiza msafara wa wale watuhumiwa wote, ilibaki
kwa wale vijana wa kitengo ambao ndiyo waliotupokea.
457 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Safari iliendelea, helikopta ikawa inapasua mawingu kwa kasi na


haukupita muda, tukawa tayari tumeshawasili Kibiti na moja kwa
moja tukaenda mpaka kwenye kambi yetu nyingineya muda katika
Shule ya Sekondari Kibiti.
Tulikamilisha taratibu zote za pale na kwa kuwa tayari wanafunzi
walishaanza kufika, pia tulitakaiwa kuondoka haraka kurudi jijini
Dar es Salaam kuendelea na taratibu nyingine katika oparesheni
ile.
Jukumu la kuwasubiri na kuwapokea watuhumiwa wengine tu-
liowasomba Mafia, tuliikabidhi kwa Jeshi la Polisi, mimi na kikosi
changu chotekilichosalia, tukaondoka na helikopta kuelekea jijini
Dar es Salaam. Furaha niliyokuwa nayo ndani ya moyo wangu,
ilikuwa kubwa kuliko kawaida, sikuamini kwamba Mutesigwa
angeweza kupatikana kirahisi namna ile.
Tukiwa angani, helikopta ikiendelea kupasua mawingu kwa kasi,
niliendelea kutafakari mambo yote tuliyokutana nayo kwenye opa-
resheni hiyo, kuna muda nilijikuta nikiwa nasisimka mwili kuliko
kawaida.
Ungeweza kufananisha kila kilichokuwa kinaendelea na ndoto ya
kusisimua, iliyojawa na visa na mikasa vya kutosha. Nilitafakari
kwa kina kumhusu Ustaadh Fundi, hakika alikuwa mtu muhimu
sana ambaye alipaswa kulindwa kwa hali na mali.
Japokuwa nilikuwa nimemuacha kwenye mikono salama kwa
kumkabidhi yeye na familia yake kwenye mikono ya kamanda
wa polisi aliyekuwa akisimamia eneo la Kibiti, bado niliona kama
anastahili kuongezewa ulinzi kwa sababu wabaya wake wangewe-

458 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

za kwenda kulipiza kisasi kwa jinsi alivyowachoma na kutupa


msaada mkubwa.
Nilijiapiza kwamba baada ya kumaliza kabisa kila kilichokuwa
mbele yetu, lazima nitarudi tena Kibiti kwenda kuonana naye,
tukae na kuzungumza mambo mengi zaidi ikiwa ni pamoja na ku-
peleka shukrani zetu kwake.
Safari iliendelea na hatimaye, tuliwasili Kunduchi, helikopta
ikatua na bila kupoteza muda tuliteremka na kwenda eneo maalum
ambalo viongozi wetu, akiwemo mkurugenzi walikuwa wamekuja
kutupokea.
Nilishangaa kwa nini safari hii tunapokelewa na viongozi kwa sa-
babu haikuwa kawaida, moyoni nikawa najiambia kwamba huenda
ni kwa sababu ya kazi kubwa tuliyokuwa tumeikamilisha Kibiti na
Mafia.
Kila mmoja alikuwa na furaha sana kutuona tena, kila mmoja
akionesha kuwa na uchovu wa hali ya juu kwa sababu tangu opa-
resheni ilipoanza, hakukuwa na muda wa kupumzika hata mara
moja.
“Umeniokoa kijana wangu! Naamini sasa kila kitu kitaisha
kabisa, sijui namna ya kukushukuru,” alisema Mkurugenzi na
kunikumbatia kwa nguvu, nikamwambia kwamba bado akili yangu
ilikuwa inaniambia kwamba kazi haijaisha mpaka tutakapowamal-
iza wahusika wote, wakiwemo viongozi wa ngazi za juu serikali
kama ‘kamishna’ pamoja na watu mashuhuri akiwemo yule mfan-
yabiashara mkubwa.
“Ukitaka kuukata mti kwa urahisi, unachimba kuanzia kwenye

459 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

mizizi na siyo kukata matawi pekee! Upo sahihi kabisa,” alisema


huku tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wake.
Tuliingia kwenye magari na bila kupoteza muda, safari ya kuele-
kea ofisini ilianza. Ndani ya magari, stori za hapa na pale zilikuwa
zinaendelea kupigwa, kilammoja akionesha kuwa na furaha kuliko
kawaida.
“Mmewezaje kulipata lile gaidi kirahisi namna hiyo? Abdulwa-
heed ni gaidi kisawasawa, ukimtazama tu sura yake lazima ush-
tuke, siyo binadamu wa kawaida!” alisema mkurugenzi, tukacheka
sana.
Akasema madaktari wamebaini kwamba alikuwa na risasi tatu
kwenye kifua chake, tena zote zikiwa zimepiga sehemu mbaya la-
kini bado alikuwa hai, jambo ambalo huwa siyo la kawaida. Tuka-
baki kutazamana kwa mshangao.
“Na huyu mwingine naye amebadilika kutoka kuwa jambazi
sugu na kuwa gaidi, Mutesigwa ni tishio kwa usalama wa taifa
letu! Watu kama hawa dawa yao huwa siyo kuwafunga gerezani,
inatakiwa wauawe! Hii ni mara ya ngapi Mutesigwa anatuletea
matatizo makubwa kiasi hiki,” alisema mkurugenzi, tukawa tunam-
sikiliza.
Safari iliendelea na hatimaye tuliwasili ‘kitengoni’, japokuwa
oparesheni ilikuwa ya kimyakimya, mapokezi tuliyoyapata yali-
tushangaza kisawasawa, tulipokelewa kama mashujaa wanaorejea
kutoka uwanja wa vita.
Ulikuwa wakati mzuri sana kwetu sote, tukawa tunapokea
pongezi nyingi na moja kwa moja tulielekea ‘mess’ kwa ajili ya

460 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

chakula kwa sababu tangu tulipoondoka jana yake, chakula kili-


kuwa ni cha kuvizia kwelikweli.
Tulikuta kila kitu kimeshaandaliwa, kifungua kinywa na chakula
cha mchana kwa pamoja, tukala na kusaza kisha tukaenda kuoga
na kubadilisha nguo na fursa ya kwenda kupumzika ikatolewa,
japokuwa huwa nakuwa mgumu sana kupumzika mpaka nimal-
ize ninachokifanya, niliona naweza kuwehuka kwa sababu kichwa
kilikuwa kimechoka kuliko kawaida.
Tulielekea kwenye bwalo maalum la kupumzikia lililokuwa
palepale ofisini, nikawaambia vijana wangu wote kwamba hakuna
anayeruhusiwa kwenda kupumzika nyumbani bali tunatakiwa
kupumzika palepale kwa saa kadhaa kisha baada ya hapo tutapan-
giana majukumu mapya.
“Chief utatuua!” alisema mmoja kati yao na kusababisha wote
tucheke sana, nikawaambia hakuna muda wa kupoteza mpaka tum-
alize kabisa ile kazi iliyokuwa mbele yetu.
Nilikuwa nimejenga utaratibu fulani kwamba vijana wangu tu-
napokuwa nje ya kazi, naishi nao kirafiki, tukitaniana na kucheka,
jambo ambalo liliwafanya wengi wawe wananiheshimu sana hata
tunapokuwa kwenye kazi.
Tuliingia mpaka kwenye bwalo hilo, kila mmoja akachagua
kitanda chake na haukupitamuda mrefu, nilianza kuwasikia vijana
wangu wakikoroma kwa uchovu. Mimi ilibidi nipate kwanza muda
wa kufanya tahajudi (meditation) kwanza na baada ya kama dakika
thelathini hivi, ndipo nilipopanda kitandani.
Nilitegesha simu yangu kwamba iniamshe baada ya saa mbili tu

461 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kwa sababu kama nilivyosema, bado kulikuwa na kazi kubwa na


muda haukuwa unatosha. Haukupita muda mrefu na mimi nika-
pitiwa na usingizi mzito.
Simu yangu ndiyo iliyoniamsha kutoka usingizini baada ya kuwa
saa mbili zimekwisha, nikaamka na kujinyoosha, angalau sasa akili
yangu ilikuwa imekaa vizuri. Muda huo ilikuwa ni kama saa nne
hivi za asubuhi, nikatoka na kwenda ‘changing room’, nikaoga na
kubadilisha tena nguo, nikaelekea ofisini kwangu.
Nilipofika, mafaili mengi yalikuwa yakinisubiri, yakiwa na ripoti
za kazi mbalimbali nilizokuwa nimewapa vijana wangu, nikaanza
kupitia moja baada ya jingine. Hakika kazi zilikuwa nyingi na zote
zilikuwa muhimu sana kwangu kiasi kwamba kama nisingejipanga
vizuri, ningeweza hata kuchanganyikiwa na kuwa mwendawazimu.
Wakati nikiendelea na kupitia ripoti za kazi, nilikumbuka kwam-
ba hatukuwa tumetoa amri ya kuwashwa upya kwa mawasiliano
kule Mafia, nikachukua simu ya mezani na kubofya namba fulani,
simu ikawa inaita. Niliwapa vijana maelekezo na yakafanyiwa
kazi.
Nilipiga simu za mkononi kwa wale wenzetu wa Mafia kutaka
kujua ni nini kilichokuwa kinaendelea, wakanihakikishia kwamba
vijana wote waliosombwa Mafia wamefikishwa salama katika eneo
salama na kilichokuwa kinaendelea ilikuwa ni kuwahoji, mmoja
baada ya mwingine kisha kuandaa utaratibu mzuri wa kuwaachia
kwa dhamana.
Baada ya kujiridhisha, niliendelea kupitia mafaili ya zile ripoti na
baada ya muda, nilikuwa tayari nimeshamaliza. Nikataka kwenda

462 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kuzungumza na yule mzee wa Kisomali kwanza kujua maendeleo


yake lakini pia kumshukuru kwa ushirikiano aliokuwa ametupa.
Baada ya hapo pia ilitakiwa kwenda kuzungumza na Sanipha
na kufuatilia taarifa za wale mabinti tuliowakamata kwenye ile
nyumba, Kijitonyama Kisiwani na kikubwa nilikuwa nataka kumu-
ona mtoto wa Ustaadh Fundi ambaye alinieleza kwamba alikuwa
amechukuliwa kienyeji na Abdulwaheed akijifanya anakwenda
kumtafutia kazi jijini Dar es Salaam.
Yote tisa, kumi ni kwamba nilikuwa nataka kwenda kuzungumza
ana kwa ana na Mutesigwa na kumhoji baadhi ya mambo kuanga-
lia kama anaweza kutoa ushirikiano, ingawa ndani ya moyo wangu
nilikuwa najua kwa jinsi alivyokuwa mjeuri, anaweza asikubali
kabisa kutoa ushirikiano.
Nilitaka pia kwenda kuzungumza na Abdulwaheed na kusikia ku-
toka kwake kwa sababu sikuwa nimewahi kuzungumza naye kitu
chochote na pengine hakuwa anajua kwamba najua nini kumhusu
yeye.
Niliandika kila kitu kwenye ‘diary’ yangu ili kuhakikisha hakuna
ninachokisahau, ilikuwa ni lazima kujipangia ratiba iliyokamilika
kwa sababu kama nilivyosema, bado muda haukuwa rafiki na mimi
sikuwa mwepesi wa kuamini kwamba tayari kazi imeisha wakati
muda wa tukio uliopangwa bado haujafika, ilikuwa ni lazima niwe
na uhakika na kila kitu.
Baada ya kupangilia vizuri mambo yangu, niliinuka na breki ya
kwanza ilikuwa ni kwenye chumba cha yule mzee wa Kisomali.
Nilipofungua tu mlango, alijifunua shuka alilokuwa amejifunika

463 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

na kuinuka pale kitandani alipokuwa amekaa, akasimama huku


akinitazama, akionesha kuwa na shauku kubwa ya kutaka kujua ni
nini kilichotokea.
“Kijana wangu!”
“Mzee wangu!” nilisema huku nikimsogelea, akawa ananitazama
huku akitetemeka, nikamshika begani na kumtuliza kisha nikataka
akae kwanza.
“Unaendeleaje!”
“Sijambo, nashukuru nimepewa huduma nzuri sana, hapa nina
uchovu wa dawa tu lakini wamenihakikishia kwamba sumu yote
imeshadhibitiwa mwilini na nitaendelea kupata ahueni taratibu.”
“Pole sana!”
“Umeonana na jamaa yangu?”
“Ndiyo, ametusaidia sana na tumefanikisha kila kitu!”
“Mmempata Abdulwaheed?”
“Ndiyo! Tupo naye hapa, anaendelea kutibiwa! Tumempata
Mutesigwa pia, nakushukuru sana kwa ushirikiano wako uliotu-
onesha,” nilimwambia, akashusha pumzi ndefu huku akiendelea
kunitazama, kama anayetaka kusikia mengi zaidi kutoka kwangu.
“Mmerudi salama wote?”
“Salama salmini! Japokuwa tulipata ugumu kidogo wa kum-
kamata Abdulwaheed na ililazimika risasi zirindime kisawasawa
lakini tumempata,” nilimwambia.
“Ustaadh Fundi anasemaje?”
“Ametusaidia sana, ametupa ushirikiano mzuri sana na bado tut-
aendelea kushirikiana naye hatua kwa hatua.”

464 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Mmemhakikishia usalama wake? Wanaweza kumdhuru yeye na


familia yake.”
“Hawawezi, tumempa ulinzi wa kutosha kwa sababu hata yeye
alilizungumzia hilo,” nilimweleza kisha nikawa ni kama nimekum-
buka jambo.”
“Unamfahamu Zuleikha Jamal Kandauma?”
“Ndiyo, ni binti wa Ustaadh Fundi! Alikuwa akiishi na Abdulwa-
heed pale kwenye ile nyumba mlipokuja kunikamatia, kule uani!”
“Unajua alifikaje pale na aliletwa kwa ajili ya kazi gani?” nilim-
uuliza swali la kimtego, akashusha pumzi ndefu kisha akainua
kichwa chake akiwa ni kama anavuta kumbukumbu.
“Kwa kuwa nimeamua kuwa mkweli kwa nafsi yangu na kwa
Mungu wangu, ngoja nikueleze ukweli,” alisema, ukimyaukapita
kati yetu.
“Kabla sijakueleza, naomba kujua Ustaadh Fundi ananizungum-
ziaje!”
“Bado anakuchukulia kama ndugu yake ambaye kwa pamoja
mmeingizwa kwenye mtego hatari na Abdulwaheed na genge
lake!” nilimwambia, akashusha tena pumzi ndefu.
“Nashukuru kusikia hivyo! Zuleikha na mabinti wengine wali-
chukuliwa kwa wazazi wao kwa ulaghai kwamba wanakuja kutafu-
tiwa kazi, ikiwa ni pamoja na kupelekwa kwenye miradi mbalim-
bali ambayo Abdulwaheed alijitapa kuwa nayo. Lakini baadaye
nikaja kugundua jambo lingine tofauti kabisa. Naomba Mwenyezi
Mungu anisaidie sana kwa kushindwa kuchukua hatua za kumnus-
uru binti huyu na wenzake,” alisema kisha akajiinamia, alipoinuka,

465 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

uso wake ulikuwa umelowa kwa machozi.


“Alikuwa anawafundisha kuja kutumika kama walipuaji wa kuji-
toa mhanga!”
“Uliyajua lini hayo?”
“Siku moja kabla ya kukamatwa kwangu! Nilimfuma akiwa
anawafundisha kutumia silaha pamoja na kuwaelekeza ramani
nzima ya mahali wanapotakiwa kwenda kufanya kazi ya kujilipua
kwa kujitoa mhanga!”
“Wapi?”
“Magogoni!” alisema. Sikushtuka kwa sababu tayari nilikuwa
nayajua hayo na aliyenifanya nikayajua alikuwa ni Sanipha, mwa-
namke aliyejitambulisha kama mke wa Abdulwaheed ambaye
tulimkamata kwenye ile nyumba pale Kijitonyama Kisiwani.
“Unajua sasa hivi yuko wapi?” nilimuuliza kwa kumtega,
akatingisha kichwa kuonesha kwamba alikuwa hajui. Ni kweli
hakuwa akijua kwamba wote walikuwa wakishikiliwa chini ya
uangalizi maalum palepale kitengoni, wakiwa wametenganishwa.
“Basi nashukuru kwa ushirikiano wako, kuna chochote kingine
ambacho ungependa kunieleza?”
“Hapana sina, nakuomba endelea kupambana kwa sababu naami-
ni walikuwa wamejipanga kwa kila namna kuhakikisha wanatimiza
shambulio lao la Magogoni, kuwakamata Abdulwaheed na Mute-
sigwa siyo kumaliza kazi! Shughulika na hao watu wakubwa mna-
okula na kunywa nao huko kwenu, hao ndiyo hatari zaidi,” alise-
ma, nikashusha pumzi ndefu na kuinuka, nikawa nataka kutoka.
“Ahadi yangu bado haujaitimiza!” alisema, nikamgeukia na ku-

466 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

muonesha ishara kwamba atulie na asiwe na wasiwasi.


Baada ya kutoka kwenye kile chumba alichokuwa akishikiliwa
mzee yule wa Kisomali, nilitoa diary yangu, nikaandika baadhi
ya vitu kisha nikaelekea kwenye chumba alichokuwa amefungiwa
Sanipha.
Vijana wetu waliokuwa wameimarisha ulinzi, waliponiona,
walinipisha na kunifungulia mlango baada ya kuwa nimewaonesha
ishara kwamba nataka kwenda kuzungumza na Sanipha.
Mlango ulipofunguliwa, Sanipha ambaye alikuwa amekaa juu
ya kitanda kidogo kilichokuwa mle ndani akiwa amejikunyata,
alishtuka kusikia mlango unafunguliwa lakini aliponiona ni mimi,
nilimuona akishusha pumzi ndefu, akajiweka vizuri na kukaa
kitako, akionesha kuwa na shauku kubwa ya kutaka kunisikiliza.
“Unaendeleaje?”
“Alhamdullilah! Hofu tu ndani ya moyo wangu, sijui haya yatai-
sha lini!”
“Yamekaribia kuisha!” nilimwambia huku nikikaa kwenye kiti
kilichokuwa mle ndani, akawa ananitazama kwa shauku kubwa.
“Nini kinaendelea!”
“Mume wako Abdulwaheed tumefanikiwa kumpata!”
“Mungu wangu, yupo hai?”
“Yupo hai ingawa alipata majeraha ya risasi lakini anaendelea
kutibiwa.”
“Naomba nafasi ya kumuona tafadhali!”
“Utaipata lakini siyo kwa sasa, nakuahidi kwamba nitakusaidia
muonane, najua nafsi yako itatulia!”

467 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Nitashukuru sana!”
“Lakini hilo litawezekana kama utaendelea kutoa ushirikiano
vizuri kama unavyofanya kuanzia mwanzo.”
“Haina shida baba, kwanza nashukuru kwamba japokuwa nipo
chini ya ulinzi lakini napata huduma zote muhimu, nakushukuru
kwa kutimiza ahadi zako na nakuahidi nitaendelea kutoa ushiriki-
ano.”
“Vizuri! Nataka kujua kuhusu binti aitwaye Zuleikha!” nilimuu-
liza, akawa ni kama ameshtuka kidogo kisha akakaa vizuri.
“Ni miongoni mwa wale mabinti mlionikuta nao mlipokuja
kutukamata!”
“Unafahamu ametokea wapi?”
“Hapana sifahamu kama nilivyokueleza mwanzo, waliletwa pale
na nikapewa jukumu la kuwa nawahudumia na kuwapa huduma
zote muhimu!”
“Ukiacha hao mabinti tuliokukuta nao, kuna wengine ambao
umewahi kuletewa pale ndani?” nilimuuliza, akashusha pumzi
ndefu na kuinua kichwa chake, akiwa ni kama anavuta kumbu-
kumbu, kisha akanigeukia na kunitazama, tukawa tunatazamana.
“Unisamehe sikuwa nimekueleza kila kitu mwanzo!”
“Usijali, unao muda wa kurekebisha hayo yote na wakati wako
ni huu!”
“Ukweli ni kwamba hawa wasichana hawakuwa wa kwanza
kuletwa pale na mume wangu. Kulikuwepo na awamu nyingine
mbili nyuma, kila awamu ilikuwa na wasichana kumikumi la-
kini wenyewe walikuwa wakija kulala tu, hawakuwa wakishinda

468 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

pale!”
“Unasema?” nilisema kwa mshtuko. Nikakaa vizuri na kuendelea
kumsikiliza nikiwa ni kama siamini kile alichokuwa amekisema.
“Walikuwa wakija kuchukuliwa usiku, mida ya kuanzia saa tatu
hadi saa nne, kisha wanarudishwa alfajiri wakiwa wamechoka na
kuchafuka sana, wakati mwingine miili yao ikiwa na majeraha
kwenye maeneo mbalimbali.
“Nilipokuwa nawauliza, walikuwa wananiambia kwamba wa-
metoka kwenye mazoezi na hilo lilikuwa linathibitika kwa jinsi
walivyokuwa wakionekana.”
“Mazoezi ya nini?”
“Awali walikuwa wakiniambia kwamba ni mazoezi tu ya kuweka
miili timamu na niliamini lakini walipokuja hawa wa mwisho, ndi-
po nilipoelewa kuwa hayakuwa mazoezi ya kuweka utimamu wa
mwili bali mazoezi ya kijeshi ikiwa ni pamoja na kutumia silaha.”
“Umewahi kuwauliza walikuwa wanaenda kufanyia wapi hayo
mazoezi?”
“Hawakuwa wakijua kwa sababu wote walikuwa ni wageni,
wengine wakiwa ni kutoka nje ya nchi,” alisema, nikashusha pumzi
ndefu, kijasho chembamba kikawa kinanitoka makwapani.
“Sasa hivi wako wapi?”
“Sijui wako wapi? Ilikuwa wakimaliza mafunzo yao wanaondoka
wanaletwa wengine,” alisema, taa nyekundu ikawa imewaka kwe-
nye kichwa changu.
Niliamini kwamba watu wanaoweza kuwa na taarifa hizo, ni
wawili au watatu. Wa kwanza alikuwa ni Abdulwaheed mwe-

469 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

nyewe, mwingine alikuwa ni Mutesigwa na mwingine, alikuwa


ni Ustaadh Fundi, hao ndiyo ambao nilikuwa na uhakika kwamba
wanaweza kuwa wanajua kila kilichokuwa kinaendelea.
Nilishangazwa sana na mbinu ambayo ilikuwa imetuka na Ab-
dulwaheed na genge lao lote, la kuwatumia mabinti wadogo katika
kukamilisha nia yao ovu. Ukimya ulipita kati yetu, nikawa najaribu
kuumiza kichwa kutaka kujua ni nini hasa kilichokuwa kimepang-
wa kuhusu wasichana hao na jinsi watakavyotumika katika mpan-
go huo.
Nilijiuliza kwa nini kila muda ambao watu wote wanaamini
kwamba mambo yameisha kunaibuka jambo lingine, tena kubwa
zaidi? Muda uliokuwa umesalia ulikuwa mfupi sana, usiku wa Iju-
maa, muda ambao ndiyo tukio lilipangwa litokee, ulikuwa umek-
aribia muda kiasi ambacho, nilihisi kichwa kinachemka.
“Sawa, endelea kutafakari kama kuna jambo lingine lolote am-
balo hujaniambia na unahisi litanisaidia, unatakiwa kunieleza, usi-
subiri mpaka nikuulize mimi kwa sababu mwisho wa siku, endapo
tukio hilo likitokea, nitashindwa namna ya kukunasua kutoka
kwenye tuhuma zinazokukabili, njia pekee ni kuzuia tukio lisito-
kee,” nilimwambia kwa msisitizo, akatingisha kichwa kuonesha
kukubaliana na nilichokuwa nimekisema.
Niliinuka na kupiga hatua ndefu kuelekea mlangoni, kichwa
kikiwa kinachemka kisawasawa. Kumbe nilipoinuka, nilisahau
hata kuchukua ‘diary’ yangu, nilipofika mlangoni ndipo nilipokum-
buka, nikarudi na kuichukua.
“Nilikuwa nikisikia wakiitwa kwa jina la CAT GIRLS, labda

470 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

unaweza kupeleleza zaidi,” alisema yule mwanamke, nikamtazama


na kutafakari kile alichokuwa amekisema. Nikajua lazima kwa vy-
ovyote vile, Cat Girls ni jina la kificho ambalo lilikuwa na maana
tofauti iliyojificha, au kwa kitaalamu ‘code name’.
Nilitingisha kichwa kuonesha kuelewa alichokuwa amekisema,
nikatoka na akili zilinituma kurudi kwanza kwa yule mzee wa
Kisomali kwa sababu hakuwahi kunieleza chochote kuhusu wa-
sichana hawa na makubaliano yetu yalikuwa ni kutoa ushirikiano
kwa asilimia mia moja.
“Kuna jambo la muhimu nilisahau kukuuliza,” nilisema baada ya
kuingia kwenye chumba cha yule mzee wa Kisomali. Kasi nili-
yoingia nayo ilimshtua, akainuka tena kitandani na kukaa kitako,
akawa ananitazama kwa wasiwasi.
“Jambo gani kijana wangu!”
“Tumekubaliana kwamba utoe ushirikiano kwa asilimia mia
moja, si ndiyo?”
“Ndiyo kijana wangu!” aliitikia kwa sauti ya kutetemeka.
“Kwa nini unatoa taarifa nusunusu na nyingine unazificha?”
“Mimi? Nimekuficha nini tena kijana wangu?”
“Kuna makundi mawili ya wasichana yaliletwa pale kwenu kwa
nyakati tofauti ukiachana na wale waliokutwa eneo la tukio,”
nilisema kwa sauti ya mamlaka, nikamuona akishusha pumzi
ndefu.
“Nisamehe nilisahau, ni kweli! Cat Girls!” alisema na kulitaja
jina lilelile nililotajiwa na Sanipha.
“Nakusikiliza,” nilisema huku nikifunua ‘diary’ yangu na kukaa

471 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kwani kwa muda wote huo nilikuwa nimesimama.


“Ni kweli kuna wasichana wadogo ishirini waliletwa kwa awamu
mbili tofauti. Sikuwa nimekueleza kwa sababu sikuwa nimefikiria
kama nao pia wanaweza kuwa wanahusika kwenye huu mpango.”
“Uliambiwa ni akina nani?”
“Niliambiwa ni watumbuizaji wa majukwaani, wakiruka sarakasi,
kucheza ngoma na kucheza michezo mbalimbali ya kuburudisha.”
“Walikuwa wakichukuliwa usiku na kurudishwa alfajiri, ni
kweli?”
“Ndiyo, ni kweli kabisa!”
“Walikuwa wakipelekwa wapi?”
“Abdulwaheed alinieleza kwamba wanaenda kufanya mazoezi
ya michezo yao na hawataki watu wajue wanachokifanya ndiyo
maana walikuwa wakipelekwa mazoezini usiku.”
“Walikuwa wakifanyia mazoezi wapi?”
“Sijui ni wapi lakini kwa mazungumzo ya Abdulwaheed, ilion-
esha ni hii njia ya Bagamoyo ingawa sijui ni wapi.”
“Narudia tena kukukumbusha kwamba unatakiwa kutoa ush-
irikiano wa asilimia mia moja kuhakikisha tukio hili halitokei.
Likitokea sitakuwa na namna ya kukusaidia, utaingizwa kwenye
orodha ya watuhumiwa na adhabu yake haiwezi kuwa nzuri.
“Haya makosa yanaangukia kwenye kifungu cha makosa ya
uhaini na adhabu yake huwa ni kifo au ukiwa na bahati sana basi
unafungwa jela maisha,” nilisema na kuinuka, nikamuacha akiwa
amejiinamia. Sikujali kwamba sukari yake inaweza kupanda tena
kwa vitisho vile.

472 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Nimekuelewa na kama nilivyokuahidi kuanzia mwanzo, nita-


toa ushirikiano kwa kadiri ya uwezo wangu wote. Angazia zaidi
kwenye vipengele viwili, makundi ya burudani yaliyoalikwa
kwenye dhifa ikulu pamoja na watoa huduma za vyakula,” alisema,
nikajifanya ni kama sijamsikia au sijatilia maanani alichoniambia,
nikatoka.
Ilibidi kwanza nirudi ofisini kwangu kwenda kutafakari kwa kina
kuhusu taarofa hizo mpya nilizokuwa nimezipata.
“Makundi ya burudani yaliyoalikwa na watoa huduma za vyaku-
la!” maneno hayo yalijirudia ndani ya kichwa changu, nikaona
hapo ndipo ninapoweza kuanzia uchunguzi wangu.
Sikutaka kumshirikisha yeyote mpaka kwanza nipate mwanga.
Mtu pekee ambaye niliona anaweza kunipa mwanga kwa zile
dondoo chache nilizokuwa nimezipata, niliona ni baba yake Saima
kwa sababu yeye alikuwa anazijua vizuri taarifa za Magogoni,
nilipokaa tu kwenye kiti changu, nikampigia simu.
Haukupita muda mrefu akapokea, sauti yake ikionesha kuchoka,
nadhani ulikuwa ni uchovu wa ile misheni ya Kibiti na Mafia.
“Samahani, naweza kupata ratiba ya makundi yaliyoalikwa kwe-
nye dhifa ya namba moja na wafanyabiashara?”
“Kuna nini tena?”
“Kuna jambo nalifuatilia hapa! Naomba pia kujua kuhusu mipan-
go ya watu watakaotoa huduma za vyakula kwenye dhifa hiyo!”
“Suala la vyakula vya wafanyakazi wetu wote huwa linasimam-
iwa na sisi, sijajua kuhusu vyakula vya wageni. Subiri nakupigia
simu muda siyo mrefu,” alijibu baba yake Samia kisha akakata

473 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

simu, nikashusha pumzi ndefu.


Haukupita muda mrefu, akapiga tena simu, safari hii alikuwa na
taarifa kamili, akanieleza kwamba vyakula vya wageni pamoja na
vinywaji, vitashughulikiwa na moja kati ya kampuni zilizoingia
ubia na serikali kwenye masuala la kuhudumia kwenye dhifa na
sherehe za kiserikali.
Alinieleza pia kwamba kutakuwa na burudani za muziki wa ‘live’
na maonesho ya jukwaani, akanitajia vikundi vyote ambavyo vilita-
kiwa kushiriki, nikamuomba anitumie kwa maandishi kampuni
itakayofanya kazi ya kuhudumia vyakula pamoja na makundi ya
burudani na wasanii watakaokuwepo.
Ndani ya dakika zisizozidi mbili, tayari alikuwa amenitumia kila
kitu kupitia barua pepe (email) yangu, nikafungua na kuanza ku-
soma kwa umakini, nikitazama kila kitu kwa jicho la tatu.
Orodha ya wasanii ambao walitarajiwa kushiriki, walikuwa ni
walewale ambao huwa wanaalikwa kwenye dhifa za kitaifa na
hakukuwa na chochote ambacho kingeweza kuleta mashaka.
Kwa upande wa vikundi vya maonesho ya jukwaani, pia ku-
likuwa na vikundi vya siku zote kutoka jeshini ambavyo ndiyo
huwa vinatumbuiza kwenye shughuli za kiserikali, nikahisi kichwa
kinapata moto.
Nilirudi kwenye kampuni ambayo ilikuwa ikitarajiwa kufanya
kazi ya kuhudumia vyakula, nayo ilikuwa ni ile ambayo huwa
inatumika mara zote na haikuwahi kuwa na rekodi yoyote mbaya,
nikaishiwa nguvu.
Niliamua kuliweka kwanza suala hilo pembeni kwa sababu haku-

474 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kuwa na chochote ambacho kingenipa mwanga kwa wakati huo,


nikalazimika kuendelea na ratiba yangu kwanza ya kwenda kuwa-
hoji watu ambao niliona wanaweza kuwa wanajua chochote.
Niliona ni vyema nikaanze kwanza kwa binti wa Ustaadh Fundi
ambaye alikuwa akishikiliwa pale kitengoni na wale wasichana
wenzake tuliowakuta kwenye ile nyumba kule Kijitonyama Kisi-
wani.
Niliwahoji vijana wangu ambao ndiyo waliokuwa na jukumu la
kuwasimamia watuhumiwa wote wanaoshikiliwa, wakanielekeza
mahali walipokuwa wamehifadhiwa kwa sababu tangu walipoka-
matwa, sikuwa nimeshughulika nao kwa chochote kutokana na
kubanwa na ratiba.
Niliagiza waletwe mmoja baada ya mwingine kwenye chumba
maalum cha mahojiano, mimi nikatangulia huku nikiendeleakuta-
fakari mambo mengi ndani ya kichwa changu. Niliagiza yule binti
wa Ustaadh Fundi ndiyo awe wa mwisho, ili hata nitakapokuwa
namhoji, niwe nimeshapata mwanga kutoka kwa wale wenzake.
Aliletwa wa kwanza, akakalishwa kwenye kiti kilichokuwa
kinatazama na kile nilichokuwa nimekaa mimi, tukitenganishwa
na meza ya chuma katikati yetu. Alikuwa ni binti mdogo ambaye
kiukweli nilisikitika sana aliponieleza jinsi alivyoingizwa kwenye
mtego huo.
Alikuwa ni mwenyeji wa Kibiti na alinieleza kwamba alikuwa
amechukuliwa kwa wazazi wake na watu ambao waliahidi kwamba
anakwenda kupatiwa mafunzo kisha kutafutiwa ajira kwa sababu
alikuwa amehitimu kidato cha nne na hakuwa amefaulu vizuri kue-

475 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ndelea na masomo ya kidato cha tano au hata kwenda chuo.


Alinieleza kwamba wakati anachukuliwa kwao, hakuwa ana-
jua chochote kilichopo mbele yake zaidi ya kufurahia kwamba
anakwenda kupatiwa kazi. Nilimhoji kwa kina kutaka kujua
walianzaje kupewa mafunzo ya kijeshi ikiwemo kutumia silaha,
akanieleza kila kitu. Nilikuwa nimetumia kigezo cha kumhakiki-
shia kwamba kama atatoa ushirikiano, basi nitamsaidia na atafu-
tiwa kesi iliyokuwa inamkabili.
Nilichokibaini katika mazungumzo yake, ni kwamba hakuwa
anapenda kile kilichokuwa kinaendelea lakini hakuwa na cha ku-
fanya wala hakuwa na uhuru wa kuchagua kama atekeleze anacho-
ambiwa au akatae, akinieleza kwamba walipewa vitisho vikali.
Alinisimulia mafunzo waliyokuwa wanapewa, hakika walikuwa
wanaandaliwa kuwa watu wabaya kuliko maelezo, wakipewa
mafunzo mazito katika medani za mapambano ya kutumia silaha
pamoja na kujilinda.
Nilimhoji kuhusu ile ramani ya Magogoni niliyoikuta mle ndani,
akaonesha kutoelewa lilikuwa ni jengo la nini na linapatikana wapi
lakini alionesha kwamba tayari ameshaielewa vizuri kabisa. Kila
alichokuwa ananieleza nilikuwa namrekodi bila yeye kujua huku
nikiandika kwenye ‘diary’ kila nilichokuwa naona kinaweza kuwa
na manufaa.
Yalikuwa ni maelezo nyeti kwelikweli. Nilipomalizana naye,
niliwaambia vijana wangu wamlete mwingine, naye maelezo yake
yalikuwa yakifanana na yule wa kwanza. Kwa kifupi, niliendelea
kuwahoji mmoja baada ya mwingine na wote simulizi zao zilikuwa

476 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

zikifanana na hatimaye, ikawadia zamu ya mtoto wa Ustaadh


Fundi.
Kwanza alishtuka kusikia nikimuita kwa majina yake kamili na
kumueleza kila kitu kuhusu familia yao, akawa ananitazama kwa
mshangao uliochanganyikana na hofu. Baadaya kumaliza kumhoji,
ilibidi nimueleze kwamba nilikuwa nimekutana na baba yake na
ndiye aliyenieleza kuhusu yeye.
Nilipomueleza kuhusu baba yake alivyokuwa na hofu juu ya
usalama wake na kinachoendelea kwenye maisha yake, alilia sana
mbele yangu na akawa ananiomba nimsaidie akaungane na familia
yao.
Nilijaribu kumdadisi mambo mengine mengi lakini alionesha
kutokuwa na ufahamu wa mambo mengine, tofauti na yale nili-
yoelezwa na wenzake. Kwa kifupi, walikuwa ni kama wamechu-
kuliwa mateka, wakiwa hawajui kwa nini wanafundishwa mafunzo
ya kijeshi ikiwemo kutumia silaha pamoja na kuisoma ramani ya
Magogoni na kuielewa vizuri kabisa.
Baada ya kuona hakukuwa na chochote cha ziada ambacho
ningekipata, niliagana naye na kumhakikishia kwamba atakuwa
salama na kuungana na familia yake. Vijana wangu wakaingia
kumtoa, na mimi nikaondoka kwenda kuendelea na majukumu
yangu mengine.
Nilikwenda kwenye wodi maalum aliyokuwa anatibiwa Abdul-
waheed, nikakuta tayari ameshafanyiwa upasuaji wa kuondolewa
zile risasi alizokuwa anaishi nazo mwilini na kwa hali aliyokuwa
nayo, hakuwa na uwezo wa kuzungumza chochote.

477 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Ilionesha wazi kwamba alipata madhara makubwa sana kutokana


na zile risasi tulizomshona tulipoenda kuvamia ngome yao kule
kwenye Hifadhi ya Taifa ya Selous. Niliwapa maelekezo madaktari
waliokuwa wakimtibu kwamba wafanya kila kinachowezekana
kuhakikisha anapona na anarudi kwenye hali yake ya kawaida,
mapema iwezekanavyo.
Baada ya hapo, mtu muhimu ambaye nilitakiwa kwenda kum-
fanyia mahojiano, alikuwa ni Mutesigwa au Bosi Mute kama
ambavyo tulikuwa tukimuita awali. Kila nilipokuwa nawaza namna
ya kumuingia ili kama kuna anachokijua atupe ushirikiano, moyo
wangu ulikuwa ukiishiwa nguvu kwa sababu nilikuwa namjua.
Isingekuwa rahisi kwa yeye kuzungumza kitu chochote ambacho
kingetusaidia, iwe ni kwa hiyari yake au kwa kulazimishwa na
mateso makali. Nilikuwa nakijua vizuri kichwa chake, kwa kifupi
alikuwa ‘jiwe’ kwelikweli.

478 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

18
B
AADA ya kutafakari sana, niliamua kupiga moyo
konde, nikaenda mpaka kwenye chumba chenye
ulinzi wa juu zaidi, alichokuwa ameshikiliwa, nikain-
gia na kuwaagiza vijana wangu wafunge mlango kwa
nje.
Nilipoingia tu, aliinuka haraka sakafuni alipokuwa amekaa,
mikono na miguu yake vikiwa vimefungwa kwa pingu na minyor-
oro. Ilikuwa ni lazima afungwe kwa mtindo huo kwa sababu ali-
kuwa ni ‘high profile criminal’ kwa maana ya mtuhumiwa mwenye
matukio mengi, makubwa na ya kutisha ya kihalifu.
Watu wa namna yake, walikuwa wakiwekwa kwenye vyumba
tofauti na watuhumiwa wengine na kama nilivyoeleza, hata ulinzi

479 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wao ulikuwa ni wa hali ya juu tofauti na watuhumiwa wengine.


“Mutesigwa!”
“Kenny!” aliitikia kwa sauti iliyoonesha kutokuwa na hofu hata
kidogo.
“Hatimaye tumekutana tena!”
“Unafikiri utaweza kuniangusha tena safari hii?” alisema kwa
dharau, nikamsogelea huku tukitazamana mithili ya majogoo
yanayotaka kupigana.
“Nikipata nafasi, nitakuua kwa mkono wangu na nitataka ufe
taratibu, uyasikie vizuri maumivu mpaka roho yako itakapotengana
na mwili wako.
“Mimi ndiye niliyekutengeneza, sishindwi kukuharibu, hao
unaowatumikia walikukuta tayari ukiwa umeshakamilika, hawa-
jui ilinigharimu kiasi gani kukufanya uwe vile walivyokukuta!”
alisema Mutesigwa, safari hii midomo yake ikiwa inachezacheza
kwa hasira, akinitazama kwa macho makali, na mimi nikawa nam-
tazama machoni wakati akiendelea kunitolea vitisho vikali.”
“Hujui kama dhamana ya uhai wako ipo mikononi mwangu?”
“Mimi nilishakufa siku nyingi, kabla hata ya kukutana na wewe!
Huwezi kunitisha kwa kitu chochote mbwa wewe!” alifoka huku
akionesha kuzidi kupandwa na jazba, macho yakamtoka pima
kama anayetamani angekuwa na uwezo wa kunikabili.
“Cat girls ni akina nani?” nilimuuliza, akajifanya ni kama haja-
sikia swali langu, akawa anaendelea kunitolea maneno ya vitisho
na matusi mengi, huku akijaribu kujivua pingu na minyororo ali-
yokuwa amefungwa mikononi na miguuni.

480 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Naona unanipotezea muda wangu, narudia kwa mara ya pili,


Cat Girls ni akina nani?” nilisema huku nikionesha wazi kwamba
maneno makali aliyokuwa ananitolea hayakuwa yakiuchoma moyo
wangu kwa chochote.
Licha ya kurudia kumuuliza swali lile, tena kwa sauti ya mam-
laka, bado Mutesigwa aliendelea kunipaka kisawasawa.
Nimesema kwamba nilionesha kwamba maneno yake hayakuwa
yakiuchoma moyo wangu, lakini hiyo ilikuwa ni kile nilichokuwa
nakionesha kwa nje kwa sababu sikutaka kuonesha udhaifu lakini
ukweli ni kwamba maneno yake yaliupasuapasua moyo wangu
vibaya mno.
Mutesigwa alikuwa akinifahamu, pengine kuliko mtu mwingine
yeyote kwa sababu nilikutana naye nikiwa katika hali ya uhi-
taji mkubwa mno katika maisha yangu. Nimewahi kueleza huko
nyuma kwamba kipindi ambacho nakutanishwa na Bosi Mute kwa
mara ya kwanza, nilikuwa kwenye matatizo makubwa mno.
Kila mmoja anayo historia ya maisha yake ambayo kamwe huwa
hapendi kuikumbuka au hapendi kabisa kukumbushwa. Bosi Mute
aliamua kutumia historia ya maisha yangu kuninyong’onyesha ki-
sawasawa na pengine hii ndiyo sababu ambayo ilinifanya hata pale
wakati najiandaa kwenda kumhoji, moyo wangu usite sana.
Haikuwa mara ya kwanza kwa yeye kunichoma moyo wangu
kwa kunikumbusha nilikotoka na nadhani alishaona kwamba hiyo
ndiyo silaha pekee inayoweza kunivunja nguvu zangu na akawa
anapenda sana kuitumia pale ambapo anakuwa hana tena mbinu.
Sina sababu ya kurudia kuelezea ni kwa namna gani nilikutana na

481 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Bosi Mute miaka hiyo, jinsi alivyotokea kuwa mtu muhimu sana
kwenye maisha yangu, jinsi alivyokuja kunibadilisha na kunifanya
niwe mhalifu anayeogopwa na kila kilichoendelea kwenye maisha
yangu, naamini bado kila mmoja anakumbuka.
Kwa hiyo kilichoendelea baada ya hapo, ilikuwa ni yeye kuen-
delea kunitukana na kunikumbusha mambo mengi kuhusu maisha
yangu na mwisho nikaona imetosha sasa.
“Nitakuuliza kwa mara ya tatu na ya mwisho, baada ya hapo
naomba tusilaumiane, Cat Girls ni akina nani?”
“Huna cha kunifanya! Najua unajua kwamba hakuna unachowe-
za kukipata kwangu, na hakuna unachoweza kunitisha nacho,”
alisema kisha akaachia msonyo mkali huku akiendelea kunitazama
kwa macho makali kwelikweli, midomo yake ikimchezacheza kwa
hasira.
“Utaujutia huu muda, utayajutia maneno yako yote unayoni-
tolea,” nilisema huku nikigeuka na kutaka kuondoka.
“Kilichopangwa lazima kitatimia, uliniangusha mara ya kwanza,
ukaniangusha mara ya pili lakini safari hii hutaweza! Siyo wewe
wala serikali ya kidhalimu unayoitumikia, safari hii lazima tuwa-
shikishe adabu,” alisema na kuendelea kunipaka kisawasawa.
Nilitoka moyo wangu ukiwa umenyong’onyea sana, maneno ya
Mutesigwa yalikuwa yamenitonesha donda ndani ya moyo wangu
kwa kunikumbusha mambo mengi katika maisha yangu ambayo
sikuwa nataka kabisa kuyasikia wala kuyakumbuka.
Hali niliyotoka nayo ndani ya chumba alichokuwa amefungiwa
Mutesigwa, iliwashtua mpaka vijana wangu ambao siku zote

482 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

walikuwa wanaamini kwamba mimi ni mtu imara sana ambaye


siyumbishwi na chochote.
Ukweli ni kwamba hakuna binadamu yoyote ambaye hana ud-
haifu, ni suala la kuujua tu, Mutesigwa alikuwa ameamua kuutumia
udhaifu wangu kisawasawa.
Nilirudi ofisini kwangu, maneno makali ya Mutesigwa yakiende-
lea kupita ndani ya kichwa changu na kunifanya niendelee kujisikia
vibaya sana. Niliingia ofisini kwangu na kwenda kukaa kwenye
kiti changu, nikawa naendelea kutafakari kwa kina yote aliyokuwa
ameniambia.
Mtu pekee ambayenilion anaweza kunisaidia kunirudisha kwenye
hali yangu ya kawaida kwa wakati huo, alikuwa ni kipenzi changu,
mke wangu, Saima. Ubize wa kazi ulisababisha niwe napata muda
mchache sana wa kukaa na familia yangu, kuna wakati nilikuwa
nasahau kabisa kwamba nimeoa na nina familia.
“Mke wangu!” nilisema baada ya kuchukua simu yangu na kum-
pigia Saima.
“Mume wangu! Pole na kazi baba!”
“Ahsante! Mnaendeleaje?”
“Hatujambo! Tunakumiss tu baba, tumekukumbuka sana ila na-
jua upo bize na kazi!”
“Ni kweli niko bize lakini nimepata muda wa kupumzika, nakuja
muda siyo mrefu,” nilimwambia, furaha aliyoionesha Saima ili-
kuwa ni kubwa kuliko kawaida, akawa anachekacheka mwenyewe
mpaka simu ilipokatika.
Miongoni mwa mambo ambayo namshukuru sana Mungu wan-

483 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

gu, ni kunikutanisha na Saima. Japokuwa tulikutana naye katika


mazingira magumu sana, lakini siku zote huwa nasema kwamba ni
kama Mungu alikuwa amepanga mimi nikutane na Saima na tangu
nilipokutana naye, ndipo maisha yangu yalipoanza kubadilika kwa
kasi mpaka kufikia kuwa mtu ambaye naweza kutegemewa na taifa
langu.
“Natoka kidogo, nikiweza nitarudi baadaye, nikishindwa basi
tukutane asubuhi na mapema,” niliwaambia vijana wangu, kila
mmoja akawa anatingisha kichwa kuonesha kukubaliana na nili-
chokuwa nimekisema.
“Unahitaji kupumzika, bila shaka unaenda kwa shemeji yetu,
atakuwa amekumiss sana,” alisema mmoja kati ya vijana wangu na
kusababisha wote tucheke.
Nilichukua vitu vyangu muhimu, nikampa taarifa mkurugenzi
kwamba naenda nyumbai kupumzika, naye akaniunga mkono na
kuniambia angekuwa na uwezo angeniruhusu nichukue hata likizo
ili nipate muda wa kukaa na familia yangu.
Basi baada ya hapo, nilihakikisha kila kitu kipo sawa na kazi
zinaendelea hata nisipokuwepo, nikatoka mpaka kweny maegesho
ya magari na kuingia ndani ya gari langu binafsi, tofauti na lile nili-
lokuwa nalitumia kwa kazi.
Nikiwa ndani ya gari, nilikumbuka kwamba sikuwa nimemuaga
baba yake Saima, nikampigia simu na kumweleza kwamba na-
kwenda nyumbani kupumzika, kauli yangu ikamshtua sana.
“Kumetokea nini?”
“Hakuna, najihisi kukaa na familia yangu kidogo kisha nitarudi

484 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kuendelea na kazi, sipo sawa!”


“Kabla hujaondoka nakuomba ofisini kwangu mara moja,”
alisema baba yake Saima, nikajua lazima kuna kitu amekigundua
kutoka kwangu. Nilikuwa nimeshawasha gari, ikabidi nilizime na
kushuka kwa sababu nisingeweza kukaidi chochote kinachosem-
wa na baba yake Saima.
Nilitembea kwa hatua za harakaharaka kuelekea ofisini kwa
baba yake Saima huku nikijitahidi kuvaa uso wa kichangamfu ili
kuficha hisia kali na chungu zilizokuwa ndani ya moyo wangu.
Ndani ya muda mfupi tu, tayari nilikuwa nimefika ofisini
kwake, nikamkuta akiwa amesimama na kugeukia dirishani,
akiwa anatazama nje huku akiwa ameshikilia kikombe kidogo
cha kahawa, akanionesha ishara kwamba na mimi nijisevie.
Nilifanya kama alivyonielekeza, nikachukua kikombe kidogo
kilichokuwa kwenye meza ndogo ya kahawa iliyokuwa pembeni,
nikajimiminia kahawa kisha nikasogea pale alipokuwa amesi-
mama baba yake Saima, akiendelea kunywa kahawa yake, akio-
nesha kuwa ndani ya tafakuri nzito.
“Uliingia kumhoji Mutesigwa?”
“Ndiyo chief!”
“Na baada ya kutoka unataka kwenda kuonana na mke wako!”
“Ndiyo!”
“Mmezungumza nini na Mutesigwa mpaka ukapata wazo la
kwenda kuonana na mkeo na familia yako?”
“Hakuna chochote cha ziada, ni mahojiano ya kawaida!” nilim-
jibu, akanigeukia na kunitazama.

485 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Amezungumza kitu chochote kuhusu familia yako?”


“Hapana!”
“Amezungumzia chochote kuhusu historia ya maisha yako?”
aliniuliza, nikashindwa cha kumjibu kwa sababu ni kama alikuwa
amezisoma hisia zangu, nikababaika kidogo.
“Kwa nini unamruhusu atumieudhaifu wako kukunyong’onyesha
muda wote?” alisema baba yake Saima huku akinitazama, nikash-
indwa cha kumjibu.
“Nilishakueleza sana kuhusu hili suala, wewe siyo yule wa
kipindi kile, kila mmoja ana historia ya maisha yake lakini kamwe
mambo yaliyopita hayana chochote cha kufanya kwenye maisha
yako ya leo.
“Sikiliza, yaliyopita yamepita, unatakiwa kuishi maisha yako ya
leo na kamwe usikubali kabisa mtu atumie udhaifu wako wa nyu-
ma kukuvurugia maisha yako ya leo,” alisema baba yake Saima,
nikashusha pumzi ndefu.
“Unatakiwa kwenda nyumbani kwa sababu umemkumbuka
mkeo, umeikumbuka familia yako, jambo ambalo halina ubaya
wowote lakini siyo kwa sababu Mutesigwa amekuchanganya
kichwa chako.
“Wewe ni mtu imara sana na sisi sote tunakutegemea, umefani-
kisha mambo makubwa sana kwenye hii oparesheni ambayo kama
usingekuwepo sijui ingekuwaje. Usikubali kuchezewa kihisia na
mwendawazimu kama Mutesigwa. Umemzidi mbinu na ndiyo
maana leo yupo kwenye mikono yetu, wewe ni mshindi, sisi ni
washindi na hakuna kinachoweza kutuzuia kuendelea kushinda,”

486 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

alisema.
Maneno yake yalinipa nguvu kubwa mno ndani ya moyo wangu,
nilishusha pumzi ndefu na kupiga funda la kahawa chungu, nikawa
angalau najisikia vizuri, ni kama alikuwa amenitua mzigo mzito
kichwani.
“Nenda kaonane na mkeo lakini unatakiwa kurudi haraka, bado
tuna kazi kubwa ya kuifanya na wewe ndiyo tunayekutegemea.
Msalimu Kamami, mwambie anipigie simu nimemkumbuka?”
alisema na kunifanya nicheke. Kamami ni jina ambalo alikuwa
anapenda kumuita Saima wakiwa nyumbani na alianza kumuita
tangu akiwa binti mdogo.
“Kuhusu huyu mwendawazimu niachie nitashughulika naye,
umesahau kwamba mara zote mimi ndiyo namshughulika naye?
Wewe nenda, ukirudi utayakuta majibu yako yote mezani,” alisema
baba yake Saima, wote tukacheka.
Alichokuwa amekisema ilikuwa ni ukweli, yeye ndiye aliyekuwa
anammudu linapokuja suala la kumhoji, nakumbuka mara ya
mwisho Mutesigwa alipokuwa anacheza na vichwa vyetu, aliin-
gia kwenye chumba alichokuwa amefungiwa na ndani ya dakika
chache, alitoka huku shati lake likiwa limelowa damu, Mutesigwa
akiwa hoi kwa kipigo.
Kwenye suala la kushughulika na wahalifu sugu, baba yake Sai-
ma alikuwa mbobezi na hilo sikuwa na wasiwasi nalo hata kidogo,
japo kwa kumtazama kwa nje usingeweza kudhani kwamba ndani
yake ana roho kama ya simba.
Basi nilimalizia kahawa yangu, nikatoka uso wangu ukiwa na

487 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

tabasamu, tofauti kabisa na wakati nikiingia ndani ya ofisi hiyo.


Nilinyoosha moja kwa moja mpaka kwenye gari langu, nikaingia
na kuliwasha, nikatoka na safari ya kuelekea nyumbani kwangu
ikaanza.
Njia nzima nilikuwa nikimuwaza Saima, ubize wa kazi hakika
ulikuwa ukitutenganisha sana. Baada ya kama dakika ishirini,
tayari nilikuwa nimewasili nyumbani, nikapiga honi getini ambapo
mlinzi alikuja kufungua, nikaingiza gari mpaka ndani.
Tukasalimiana na mlinzi ambaye naye alionesha kufurahi baada
ya kuniona, nikiwa naendelea kupiga naye stori mbili tatu, Saima
alitokeza akiwa amembeba mtoto, tabasamu pana likiwa limecha-
nua kwenye uso wake.
Niliachana na mlinzi, nikapiga hatua ndefundefu mpaka pale
alipokuwa amesimama, nikawakumbatia wote kwa pamoja kisha
nikampokea mtoto ambaye naye alionesha kuwa na hamu sana ya
kuniona.
Tulikumbatiana tena na Saima, akanishika mkono na kuniongoza
kwenda ndani, moyo wangu ukawa umejawa na furaha kubwa sana
kumuona jinsi Saima wangu alivyokuwa anazidi kupendeza na
kunawiri, huku mwanangu naye akizidi kukua vizuri akiwa na afya
njema.
“Unaonekana umechoka sana baba,” alisema Saima huku akitaka
kunipokea mtoto ili nipate muda wa kupumzika, ajabu ni kwamba
mwanangu akawa hataki kuchukuliwa na mama yake, akawa anata-
ka kuendelea kubebwa na mimi, tukajikuta tukicheka sana.
“Amemmisi sana baba yake ndiyo maana hataki kukuachia,

488 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

anajua utaondoka tena!” alisema, tukawa tunaendelea kuchoka.


Ilibidi tupitilize mpaka chumbani, mke wangu akanisaidia kunivua
nguo zangu, tukatumia ujanja wa hali ya juu kumtoa mtoto kwenye
mikono yangu, nikaenda kujimwagia maji ya baridi bafuni.
Nilipata nguvu mpya, nilipotoka, Saima alikuwa amemuacha
mtoto kitandani akicheza, yeye akawa ameenda kuleta chakula
ambacho alikuwa ameshakiandaa baada ya mimi kumpa taarifa
kwamba naenda nyumbani.
Tulikula wote chumbani huku mazungumzo ya hapa na pale
yakiendelea, kila mmoja akionesha kuwa na furaha kubwa ndani ya
moyo wake. Baada ya kumaliza, tulipumzika kitandani tukiendelea
kucheza na mtoto wetu ambaye utundu wake ulikuwa umeongeze-
ka maradufu.
Kwa kuwa alikuwa ameshashiba, hukupita muda mrefu akapitiwa
na usingizi, nikamsaidia mke wangu kumlaza vizuri na sasa tu-
kapata muda mzuri wa kuzungumza mambo yetu.
Ilibidi nimsimulie kwa kifupi Saima kila kilichokuwa kinaende-
lea. Sheria za kazi huwa haziruhusu kabisa kumweleza mtu yeyote
asiyehusika siri za kazi lakini kwa jinsi nilivyokuwa naishi na
Saima, mara nyingi nilikuwa nikimueleza huku na yeye akitoa
ushauri wa nini cha kufanya.
Alionesha kufurahishwa sana na ufanisi niliouonesha kwenye
kazi, akawa ananipongeza kwa mabusu motomoto na maneno
matamu, akinieleza jinsi alivyokuwa anajivunia kuwa na mimi
kama mumewe.
Kwa kuwa kila mmoja alikuwa amemmisi sana mwenzake, hau-

489 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kupita muda mrefu tukajikuta tukiwa kwenye maandalizi ya ku-


timiza mahitaji muhimu ya ndoa kwa wanandoa, ukawa ni wakati
mwingine mzuri sana kwetu wote wawili.
Kazi ilifanyika kikamilifu, Saima akawa wa kwanza kupitiwa na
usingizi mzito baada ya kazi kuwa imekamilika katika kiwango
kinachotakiwa, mimi nikawa najaribu kupambana na usingizi
mzito lakini kutokana na uchovu wa muda mrefu niliokuwa nao,
nilishindwa kuendelea kujizuia, tukalala tukiwa tumegandana
kama ruba.
Saima ndiye aliyekuwa wa kwanza kuamka na aliamshwa na
mtoto wetu ambaye aliamka na kuanza kufanya fujo kama kawaida
yake, na mimi nikajikuta usingizi ukiniisha, nikaamka.
Japokuwa ilikuwa ni jioni, nilijisikia furaha kubwa ndani ya
moyo wangu kuamka na kujikuta nikiwa pembeni ya familia
yangu. Wote tulienda kuoga, tukarudi na kuendelea kupumzika
na ilipofika saa kumi na mbili jioni, ilibidi nianze maandalizi ya
kuondoka kurudi kazini.
“We nenda tu mume wangu, tunajua umuhimu wa kazi unayoi-
fanya ingawa huyu jamaa hapa najua hawezi kukubali kukuona
ukiondoka nakumuacha,” alisema Saima, tukacheka sana, mtoto
naye akawa anacheka utafikiri anaelewa kinachozungumziwa.
Saima aliniandalia kila kitu, nikabadilisha nguo na kuvaa ny-
ingine safi, nikambeba mtoto na kutoka mpaka nje, mke wangu
naye akawa anatufuata kwa nyuma. Ilibidi tumdanganye mtoto
kwa kuingia naye ndani ya gari kwanza, akiendelea kucheza na
mimi kwa furaha, kisha nikamkabidhi kwa mama yake kijanja.

490 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Walipoteremka kwenye gari na mimi kuliwasha kwa lengo la


kuondoka, mtoto aliibua zogo kubwa, akiwa ananililia kwa nguvu
mpaka nikajisikia vibaya. Ilikuwa ni lazima niondoke, nikaliondoa
gari taratibu mpaka nje, nikawaacha wakiwa wanaendelea kubem-
belezana.
Saa moja juu ya alama, tayari nilikuwa nimeshawasili kazini,
nikiwa na nguvu mpya na morali ya hali ya juu, ikabidi niende
kwanza kwa baba yake Saima kumtaarifu kwamba nimesharudi,
nikamuona akitabasamu japo na yeye alionesha kuwa na uchovu.
“Nimemkabili Mutesigwa kisawasawa, haya ni baadhi ya mambo
aliyonieleza kama nilivyomhoji,” alisema baba yake Saima huku
akinisogezea faili mezani, macho yangu yakatua kwenye ngumi
zake, nikagundua kwamba zilikuwa zimebadilika na kuwa nyekun-
du, nikajua kweli kazi iliyofanyika siyo ya mchezo, nikalifungua
lile faili.
Nilisoma kitu kimoja baada ya kingine, nikashusha pumzi ndefu
nikiwa ni kama siamini kama Mutesigwa angeweza kutoa taarifa
nzito kiasi hicho kwa urahisi namna hiyo. Ilibidi nirudie tena ku-
soma baadhi ya maeneo niliyoyaona kuwa muhimu.
Mutesigwa alikuwa amekiri mwenyewe kwamba ni kweli wali-
kuwa wamepanga kufanya shambulizi kubwa Magogoni na kwam-
ba mhusika mkubwa aliyekuja na wazo hilo alikuwa ni Abdulwa-
heed kwa kushirikiana na ‘washirika’ wake kutoka nje ya nchi.
Alikiri pia kwamba walikuwa wakiwahonga viongozi kadhaa wa
ngazi za juu serikalini ili kufanikisha tukio hilo na kueleza kwamba
mpango uliopo, ilikuwa ni kutumia vikosi viwili kutekeleza sham-

491 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

bulio hilo.
Kikosi cha kwanza kilikuwa ni wasichana waliopewa mafunzo
ya mashambulizi ya kujitoa mhanga na kundi la pili walikuwa ni
vijana wapiganaji waliopewa mafunzo makali ya kijeshi.
Alieleza kwamba mpango uliokuwepo, ni kwamba walipuaji wa
kujitoa mhanga ndiyo ambao walitakuwa kuwa wa kwanza kuanzi-
sha mashambulizi muda utakapowadia, kisha baada ya kufanya
mashambulizi mfululizo, ndipo kundi la pili litakapoingia na kum-
alizia kazi.
Hata hivyo, baada ya kuyasoma maelezo yote, nilibaini kwamba
kuna mambo ya msingi sana Mutesigwa hakuwa ameyazungumza.
Hao vijana waliopewa mafunzo ya kivita ni akina nani na wali-
kuwa wapi kwa sababu akili yangu ilikuwa inanituma kuamini
kwamba tayari tulikuwa tumeivuruga ngome yote, kuanzia kule
Kibiti, Selous mpaka Mafia.
Lakini swali lingine, lilikuwa ni kuhusu hao wasichana waliope-
wa mafunzo ya kushambulia kwa kujitoa mhanga. Nilitaka kujua ni
akina nani na kama ndiyo hao Cat Girls niliokuwa nikiambiwa au
kulikuwa na kundi jingine?
Na kama wapo kweli, wapo wapi na wamepanga kutumia mbinu
gani kuingia Magogoni? Nilishusha pumzi ndefu na kumgeukia
baba yake Saima, naye kumbe alikuwa ametulia akinitazama jinsi
nilivyokuwa napitia taarifa zilizokuwa ndani ya faili lile.
“Una lipi la kusema?”
“Bado vitu vingi havijaelezwa kwa undani lakini kubwa zaidi
haijaelezwa kwamba licha ya oparesheni zote tulizofanya, bado

492 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ratiba yao ipo palepale?” nilimwambia baba yake Saima, akawa


anatingisha kichwa kuonesha kukubaliana na nilichokisema.
“Jambo ambalo yule mwendawazimu amelisisitiza sana ni kwam-
ba safari hii hakuna tunachoweza kufanya kuwazuia, lazima wali-
chopanga kitatimia tu, iwe isiwe,” alisema baba yake Saima.
“Nilichogundua ni kwamba kazi ndiyo kwanza imeanza, tunat-
akiwa kuyafanyia kazi haya yote aliyoyaeleza ndani ya hizi saa 48
za mwisho zilizosalia, tuna siku ya kesho na keshokutwa pekee,”
alisema, nikashusha pumzi ndefu.
Siku ambayo ilipangwa kwamba tukio hilo litatokea, ilikuwa ni
Ijumaa usiku na siku hiyo ambayo tunayazungumza hayo, ilikuwa
ni Jumatano, tena jioni! Hakukuwa na muda wa kutosha kabisa
kukamilisha kile kilichokuwa mbele yetu.
“Hivi kuna ulazima gani wa hiyo dhifa ya namba moja na wafan-
yabiashara kufanyika wakati tumeshaona kuna hatari kubwa kiasi
hiki na muda hautoshi? Kwa nini isiahirishwe au kufutwa kabisa?”
“Matatizo hayatatuliwi kwa kuyaahirisha! Tutakapoahirisha maa-
na yake ni kwamba tutakuwa tunatoa muda wa hawa wendawaz-
imu kujipanga upya na safari hii sijui watakuja na mpango gani.
“Ni lazima tulishughulikie tatizo na siyo kuliahirisha kwa hiyo
dhifa lazima itafanyika kama ilivyopangwa, cha msingi ni kuzima
jaribio hili,” alisema baba yake Saima, nikatingisha kichwa kuon-
esha kumuelewa.
Alichokuwa amekisema kilikuwa ni ukweli mtupu kwa sababu
hata jinsi njama za tukio hilo zilivyogundulika, naweza kusema
ilikuwa ni kama muujiza na miujiza huwa haitokei mara kwa mara.

493 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)
“Nafikiri hatutakiwi kuogopa chochote, taarifa tayari zipo kwe-
nye vyombo vyote vya ulinzi na usalama, kila mmoja amekaa
‘standby’ kukabiliana na kilichopo mbele yetu kwa hiyo bado
tunayo nafasi ya kulizima jaribio hili!
“Mpaka hapa tulipofikia, naweza kusema tumelizima kwa asil-
imia kubwa sana, hatutakiwi kurudi nyuma,” alisema, ukimya
ukapita kati yetu.
“Kazi kubwa iliyopo mbele yetu kwa sasa, ni kufuatilia kwa kina
kugundua hayo makundi mawili yaliyopewa hiyo kazi, yako wapi,
yanajipanga kufanya nini kwa kutumia mbinu gani na mwisho ni
kutafuta njia za kuyakabili haraka iwezekanavyo,” alisema.
“Unatakiwa kuendelea na mipango yako kama ulivyokuwa
umeipanga, endelea kuchimba kuhusu Cat Girls, endelea kufuatilia
mawasiliano ya kila mtu ambaye tuna wasiwasi naye, mimi kwa
upande wangu naendelea na nilichokipanga na viongozi wenzangu
nao wataendelea na mipango yao, hawawezi kutushinda nguvu,”
alisema baba yake Saima, tukaagana kisha nikatoka ofisini kwake.
Ninachomshukuru Mungu ni kwamba muda niliopata wa ku-
kaa na familia yangu, ulikuwa umenisaidia sana kutuliza kichwa
changu na sasa nilikuwa na uwezo wa kutafakari kwa kina zaidi
kwa sababu sikuwa na uchovu wa aina yoyote.
Nilitoka na kabla ya kurudi ofisini kwangu, ilibidi kwanza niende
kwenye chumba alichokuwa anashikiliwa Mutesigwa kwenda
kujionea hali aliyokuwa nayo baada ya kukabiliana uso kwa uso na
baba yake Saima.
Vijana waliokuwa doria, waliponiona tu, walinipa ushirikiano

494 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

mkubwa na muda mfupi baadaye, nilikuwa ndani ya kile chumba


cha Mutesigwa. Mlango ulipofunguliwa tu, nilipokelewa na harufu
kali ya damu, nikashtuka kidogo.
Niliingia ndani na kufunga mlango haraka, nikapigwa na butwaa
kwa hali niliyokutana nayo. Mutesigwa alikuwa ametundikwa
juu mithili ya nyama inavyotundikwa buchani, akiwa amefungwa
mikono yake na minyororo ambayo ilikuwa imeunganishwa kwe-
nye vyuma maalum vilivyokuwa upande wa juu wa chumba kile.
Mwili wake ulikuwa hautamaniki, nguo alizokuwa amevaa zili-
kuwa zimelowa damu kiasi kwmaba usingeweza hata kujua rangi
yake halisi ni ipi. Kila mahali kulikuwa na damu, nyingine zikiwa
zimeanza kukauka.
Ungeweza kudhani pengine Mutesigwa alikuwa amekutana na
mnyama mkali aliyemrarua kisawasawa. Nilisogea taratibu nikiwa
namtazama kwa makini usoni. Ilionesha wazi kwamba hakuwa na
fahamu zake, uso ulikuwa umevimba kiasi kwamba kama ulikuwa
humjui kwa sura, usingeweza kumtambua kwa wakati huo.
Japokuwa nilikuwa na roho ngumu, nilijikuta nikimsikitikia na
kujiuliza ni mbinu gani au zana gani ambazo baba yake Saima
alikuwa amezitumia kumchakaza kiasi kile.
“Haya yote umeyasababisha wewe, utayalipia,” sauti ya Mute-
sigwa ilinishtua kuliko kawaida. Nilipomtazama awali niliamini
kwamba alikuwa amepoteza fahamu kwa jinsi alivyokuwa amewe-
ka kichwa chake lakini kumbe haikuwa hivyo.
“Haya yote umeyasababisha wewe, utayalipia,” sauti ya Mute-
sigwa ilinishtua kuliko kawaida. Nilipomtazama awali niliamini

495 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kwamba alikuwa amepoteza fahamu kwa jinsi alivyokuwa amewe-


ka kichwa chake lakini kumbe haikuwa hivyo.
Alikuwa ananitazama tangu nilipokuwa naingia ila aliamua tu
kuniigizia.
“Hatimaye umekutana na kiboko yako!”
“Huyo mzee wako hana akili na siku itakapowadia, nitawaua
wote wawili kwa mikono yangu, mtayalipia haya mateso mliyonipa
na nikuhakikishie tu na wewe kwamba mipango ilishapangwa.
“Hata mkiniua lazima jambo letu litatimia tu, tumejipanga kisa-
wasawa na tukishamalizana na Magogoni, tutaanza kushughulika
na nyinyi, mmoja baada ya...,” alisema Mutesigwa lakini kabla
hajamalizia alichotaka kukisema, alianza kukohoa damu mfululizo.
Kwa jinsi alivyokuwa mjeuri, eti akawa anatafuta namna ya
kunitemea zile damu alizokuwa anakohoa, ikabidi niwahi na ku-
fungua mlango, nikatoka huku nikiwa natingisha kichwa kwa ma-
sikitiko. Sikuwahi kukutana na mtu mwenye roho ngumu maishani
mwangu kama Mutesigwa.
“Kumetokea nini?” niliwauliza vijana wangu ambao kila mmoja
alikuwa akinitazama huku akiwa ni kama anataka kucheka.
“Amekutana na treni ya umeme!” alisema mmoja kati yao na
kusababisha wenzake wote wacheke. Nadhani walikuwa wanache-
ka kwa jinsi baba yake Saima alivyokuwa amemchakaza nunda
Mutesigwa.
Hata hivyo, mimi sikucheka kwa sababu nilikuwa najua bado
tuna kazi kubwa ya kuifanya mbele yetu vinginevyo yote ambayo
tulikuwa tumeshayafanya, yangekuwa kazi bure.

496 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Nikaondoka na kuwaacha wakiwa bado wanacheka chinichini,


nikaongoza kuelekea kwenye wodi maalum aliyokuwa amelazwa
Abdulwaheed, nikiwa na matumaini makubwa kwamba atakuwa
tayari amezinduka kutoka kwenye usingizi wa kifo.
Nilipokelewa na vijana wetu waliokuwa wakiilinda ile wodi
aliyokuwa amelazwa, waliponiona tu, kila mmoja akawa ni kama
amepata ahueni kubwa ndani ya moyo wake, wakanifungulia
mlango ili niingie.
Kabla sijaingia, nilitaka kusikia kutoka kwao kama kuna cho-
chote walichokuwa wanataka kuniambia hususan kuhusu maende-
leo ya mtuhumiwa wetu namba moja.
“Anaendeleaje?”
“Amezinduka lakini amekuwa akifanya fujo mara kwa mara,
akitaka kuyakatisha maisha yake. Ilibaki kidogo ajichome shingoni
na mkasi,” alisema mmoja kati yao, nikaelewa ni kwa nini wali-
poniona tu walionesha kupata ahueni kubwa kwenye mioyo yao.
“Daktari anayeongoza matibabu yake yuko wapi?”
“Yuko ndani!” alisema mmoja wao, nikaingia ndani ya wodi
hiyo na kukutana na daktari pamoja na manesi wawili waliokuwa
wakiendelea kumchukua vipimo vya hapa na pale. Waliponiona,
wote waliacha kila walichokuwa wanakifanya, wakanipisha.
Nilisogea mpaka kwenye kitanda alichokuwa amelazwa Abdul-
waheed, aliponiona tu, aligeuzia kichwa chake upande wa ukutani,
akiwa ni kama hataki kuzungumza chochote na mimi.
Mikono yake ilikuwa imefungwa kwa mikanda maalum na kuun-
ganishwa na vyuma vya kitanda alichokuwa amelazwa. Miguu

497 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

yake nayo ilikuwa imefungwa kwa mtindo huohuo, nikamtazama


kuanzia kichwani mpaka miguuni, nikawaomba wamfunue kwenye
majeraha yake ya risasi.
Ilionesha kwamba majeraha yoteyalikuwa yameshughulikiwa ki-
kamilifu na sasa alikuwa akiendelea vizuri, ingawa bado kuna jera-
ha moja ya pembeni ya tumbo, lilikuwa likitoa damu zilizolowani-
sha bandeji aliyokuwa amefungwa.
Nilimgeukia daktari na kumpa ishara fulani, akanisogelea na
kuanza kunieleza maendeleo ya mgonjwa. Alinieleza kama nili-
vyokuwa nimeelezwa pale mlangoni kwamba Abdulwaheed ali-
kuwa akijaribu kuyakatisha maisha yake na ndiyo maana walikuwa
wamemfunga mikono na miguu.
Akaniambia pia kuwa hata jeraha lake la pembeni ya tumbo lili-
kuwa likiendelea kuvuja damu kwa sababu alikuwa amenyanyuka
kwa nguvu kitandani na kukiuka maelekezo aliyokuwa amepewa.
Baada ya maelezo hayo, niliwaomba wote watoke nje na kunia-
cha naye ili nizungumze naye, muda mfupi baadaye wote wakatoka
na kutuacha tukiwa wawili tu mle ndani.
“Abdulwaheed Elmi-Dihoud! Ulizaliwa April 8, 1972 katika Mji
wa Baidoa! Baba yako alifariki Desemba 20, 2006 katika mapi-
gano yaliyotokea kati ya kundi la wanaharakati wa kundi lenye
msimamo mkali la Somali Court Union na majeshi ya serikali ya
Somalia na wanajeshi wa Ethiopia!
Baba yako alikuwa miongoni mwa viongozi wa kundi hili amba-
lo lilitangazwa kuwa ni la kigaidi na serikali ya Somalia,” nilisema
kwa sauti ya utulivu, Abdulwaheed ambaye awali alijifanya kugeu-

498 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kia ukutani, akanigeukia na kunitazama. Nadhani hakutegemea


kama naweza kuwa namjua kwa undani kiasi hicho.
Nikaendelea kumsomea historia yake ambayo mwenyewe ali-
kuwa anajua kwamba hakuna anayeijua, nikamueleza jinsi alivyo-
kimbia Somalia baada ya mapambano kuwa makali na kuhamia
nchini Kenya, ambako nako alilazimika kukimbia baada ya serikali
ya Kenya kumkosakosa kumkamata, akitajwa kuwa mmoja kati
ya watu waliokuwa wakifadhili ugaidi, kutoa mafunzo ya kigaidi
kwa vijana wa Kenya pamoja na kusafirisha silaha huku akijificha
kwenye kivuli cha kufanya biashara.
Nikaendelea kumueleza jinsi alivyoingia nchini Tanzania na
sehemu zote alizowahi kuishi, pamoja na watu wa karibu aliokuwa
akishirikiana nao kwenye mipango yao ya kigaidi, ikiwemo tukio
la kutaka kuiangusha Magogoni.
“I know who you are!” (Najua wewe ni nani!) alifumbua mdomo
wake na kutamka maneno hayo huku akiwa amenitolea macho
makali.
“Kwa makosa yanayokukabili kuanzia Tanzania, Kenya na
Somalia, bila shaka unajua kwamba adhabu pekee unayostahili ni
kifo!”
“Mimi nilishakufa miaka mingi iliyopita! Mimi ni mfu!” alisema
kwa Kiswahili chenye lafudhi ya Kisomali. Nikaendelea kumtingi-
sha kisaikolojia, nikamtajia jina la mkewe na majina ya watoto wao
na mahali walipokuwa. Nikamtajia majina ya ndugu zake wa damu
na mahali walipokuwa, ule ujeuri aliokuwa nao mwanzo ukaanza
kupungua taratibu.

499 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Sikia, sijaja hapa kucheza michezo ya kitoto na wewe! Tunao


uwezo wa kuifuta familia yako na ukoo wako wote chini ya jua
lakini pia mimi ninao uwezo wa kukusaidia ukaepuka adhabu ya
kunyongwa hadi kufa lakini pia kuilinda familia yako,” nilisema,
nikamuona akichezeshachezesha midomo yake kama anayetaka
kusema neno lakini hajui aanzie wapi.
Wenzako wote ambao unashirikiana nao wapo mikononi mwetu
na wale wachache ambao bado hawajapatikana, watakamatwa
ndani ya saa ishirini na nne zijazo! Mutesigwa, swahiba wako wa
karibu, tunaye kwenye mikono yetu na hii ndiyo hali aliyonayo
kwa sasa,” nilisema huku nikimsogezea simu yangu ya mkononi na
kumuwekea picha niliyoipiga kwa siri kule kwenye chumba ali-
chokuwa ameshikiliwa Mutesigwa.
Akaitazama picha ile kwa mshtuko akiwa ni kama haamini kama
aliyekuwa anamuona ni Mutesigwa. Nadhani pia hakuwa anatarajia
kwamba Mutesigwa tulishashughulika naye kikamilifu.
Nilimuonesha picha ya mkewe, Sanipha ambaye naye pia tuli-
kuwa tunamshikilia, yeye akiwa kwenye hali nzuri, akavuta pumzi
ya moto na kuishusha.
“Unachotakiwa kukifanya ni kutoa ushirikiano kwangu na kujibu
maswali yote nitakayokuuliza. Narudia kukuhakikishia kwamba
ukijibu maswali yangu na kutoa ushirikiano, nitakusaidia kupata
nafasi ya pili maishani mwako! Nitakusaidia pia kuilinda familia
yako.
“Muda wowote ukiwa tayari, utamweleza daktari anipe taarifa,”
nilisema huku nikisimama pale kwenye kiti nilipokuwa nimekaa,

500 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

pembeni ya kitanda alichokuwa amelazwa na kufungwa.


“Muda wowote ukiwa tayari, utamweleza daktari anipe taarifa,”
nilisema huku nikisimama pale kwenye kiti nilipokuwa nimekaa,
pembeni ya kitanda alichokuwa amelazwa na kufungwa.
Sikutaka kugeuka nyuma, nikatoka mpaka pale nje, nikampa
ishara yule daktari, akanisogelea kunisikiliza.
Nikamweleza kwamba muda wowote Abdulwaheed atakapotaka
kuzungumza na mimi, anipigie simu yangu ya mkononi moja kwa
moja, akainamisha kichwa kwa utii, nikamtaka aendelee kuwa
makini kwa sababu tulikuwa tunamhitaji Abdulwaheed akiwa hai
ili kufanikisha kazi nzito iliyokuwa mbele yetu.
Baada ya hapo niliondoka na kurudi ofisini kwangu, nikakaa
kwenye kiti changu na kuanza kutafakari hatua ambayo ingefuatia.
Maelezo aliyoyatoa Mutesigwa kwamba vyovyote tukavyofanya ni
lazima lengo lao litatimia, yalinifanya niwe na wakati mgumu sana
wa kuchanganua mambo ndani ya kichwa changu.
Kama kawaida yangu, nilichukua karatasi na kalamu, nikaanza
kuchorachora huku nikijaribu kuunganisha nukta kujua ni wapi
tunapoweza kuanzia kazi ya kuyasaka kwa udi na uvumba yale
makundi mawili ambayo kwa maelezo ya Mutesigwa, ndiyo yali-
yokuwa yakitarajiwa kukamilisha kazi ile ya kuiangusha Magogo-
ni.
Kwa wakati huo, nilijiapiza kwamba nitatumia uwezo na akili
zangu zote kutegua mtego uliokuwa mbele yetu. Nilipata wazo la
kurudi kwenye orodha ya wageni ambao walitarajiwa kukutana na
namba moja kwenye dhifa hiyo maalum ambayo ndiyo iliyopang-

501 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wa kutumika na wendawazimu hao kutimiza malengo yao.


Nilirudia kuyatazama majina yote, moja baada ya jingine. Kwa
kuwa tayari nilishawapa kazi vijana wangu kuhakikisha wanapekua
taarifa za kila mmoja kwa kina, haikuwa kazi kuujua undani wa
kila mmoja. Nilifuatilia ‘details’ mojamoja, hata zile ndogo kabisa
ili kujiridhisha kwa kina.
Baada ya kupata nilichokuwa nakitaka, nilirudi tena kwa mara
nyingine kuchunguza kwa kina ni nani na nani ambao wanataraji-
wa kufika Magogoni kuanzia asubuhi ya siku ya tukio, kwa sababu
nilihisi kuna wengine wanaweza kutumia ujanja wa kuingia kwa
kisingizio kingine chochote.
Niliingia kwenye ‘portal’ maalum ya shughuli za kiofisi za Ma-
gogoni na kujaribu kuangalia ratiba zote za siku ya tukio kuanzia
asubuhi mpaka jioni, bado sikuona chochote ambacho kinaweza
kunipa mwanga, nikashusha pumzi ndefu.
Niliendelea kutafakari kwa kina, bado sikuwa najua nini kina-
choweza kunisaidia kwa wakati huo. Nikiwa naendelea kuwaza
kwa kina, nilikumbuka jambo ambalo niliona linaweza kuongeza
nguvu kwenye timu yangu, harakaharaka nikanyanyua simu ya
mezani na kubofya namba kadhaa na kuiweka sikioni.
“Chief, samahani kwa usumbufu! Kuna wazo nimelipata hapa
ambalo naamini linaweza kutusaidia.”
“Endelea!”
“Naomba Jackson Mashewa aongezwe kwenye timu yangu, bila
shaka alishamaliza mafunzo.”
“Jackson Mashewa ni nani?”

502 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Ni yule kijana wa Shamte!”


“Shamte wa kikosi cha kudhibiti wizi wa magari?”
“Ndiyo Chief! Anajua mambo mengi yule kijana na pia ni msomi
wa chuo kikuu, naamini atatusaidia sana!”
“Wazo zuri! Ngoja niangalie hapa taarifa zake na mahali alipo
kwa sasa!”
“Nitashukuru sana!” nilisema kisha nikakata simu. Historia ya
kijana huyu ilikuwa inafanana kwa mbali na historia ya maisha
yangu, utofauti wetu ni kwamba yeye alichukuliwa kutoka mtaani
katika namna ya tofauti kabisa.
Huwa zipo njia nyingi ambazo ukionekana unafaa kwenye kazi
zetu, zinaweza kutumika kukufanya uingie, wakati mwingine hata
bila mwenyewe kutaka au kuridhia.
Kijana huyu alikuwa amesomea Bachelor Degree in Electronic
Engineering au kwa Kiswahili Shahada ya Kwanza ya Uhandisi wa
Vifaa vya Kielektroniki na alikuwa miongoni mwa wanafunzi wa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliofaulu kwa kiwango cha juu
kabisa.
Uelewa wake mkubwa wa masuala ya kielektroniki, kuanzia
simu, kompyuta, mifumo ya ulinzi zikiwemo CCTV Camera, vifaa
vya GPS na mambo mengine mengi, zilikuwa ni sifa zilizowavu-
tia viongozi wetu kumuona kama ‘bidhaa adimu’ anayeweza kuja
kuwa msaada muhimu kwenye kazi zetu.
Hata hivyo, ilikuwa ni lazima kumchunguza kwa kina kwa
kumpitisha kwenye mambo magumu kupima ukomavu wake na
uaminifu wake kwa sababu vijana wengi waliokuwa wakisomea

503 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

masomo kama yake, huwa wanatumika vibaya na makundi ya wa-


halifu, wakati mwingine wakitumiwa mpaka na majasusi wa nchi
jirani kwa manufaa yao.
Hizo ni miongoni mwa sababu zilizofanya kijana huyu apitishwe
kwenye tanuri la moto kwanza kabla ya kuja kupelekwa mafunzoni
na njia iliyotumika, ilikuwa ni kumtengenezea kesi bandia, akaten-
genezewa kesi nzito iliyomtingisha kisawasawa, akidaiwa kumuua
kwa kumchoma kisu mpenzi wake.
Kuna wakati nilikuwa namuonea huruma sana wakati akipitishwa
kwenye tanuri la moto kwa sababu nilikuwa najua kila kilichokuwa
kinaendelea lakini ilikuwa ni lazima kumuacha kwanza ayapitie
aliyoyapitia ili mwishoni, aje kuwa mtu wa kutegemewa.
Baada ya safari yake ndefu ya kupitishwa kwenye milima na
mabonde, hatimaye aliunganishwa na kikosi maalum cha siri cha
kudhibiti wizi wa magari na akiwa huko, akaonesha uwezo mkub-
wa sana, ikiwemo matumizi ya mifumo ya ‘GPS Tracking’ ambayo
ilikuwa ikihusisha vifaa maalum vinavyofungwa kwenye vyombo
vya moto kama magari na pikipiki, kwa ajili ya kufuatilia mwenen-
do wa chombo husika bila mtu yeyote kujua.
Jackson Mashewa alikuwa na uwezo wa kuunganisha au kucho-
moa mifumo ya GPS kwenye gar ndani ya sekunde chache kabisa,
alikuwa pia na uwezo wa kufunua mifumo ya ‘alarm’, zile zinazo-
tumiwa kwenye magari kutoa taarifa endapo kuna uhalifu wowote
unaofanyika kwenye gari husika.
Kwa kifupi alikuwa ni kijana mdogo lakini anayejua mambo
mengi sana, tena muhimu kwenye suala la ulinzi au ufuatiliaji wa

504 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

vifaa mbalimbali kwa kutumia teknolojia.


Baada ya kuwa wote tumeridhishwa na uwezo wake, ndipo nili-
potumwa kwenda kumchukua na kumpeleka mafunzoni, nikakuta-
na naye akiwa hajui chochote kilichokuwa kinaendelea na mwisho
akapelekwa mafunzoni ambako aliendelea kunolewa na kumfanya
awe mtu muhimu sana kwenye masuala ya kiteknolojia.
Sisemi kwamba yeye alikuwa bora kuliko vijana wangu wa
kitengo cha teknolojia ya mawasiliano na Cyber, hapana! Nina-
chokisema ni kwamba ujuzi wake, endapo ungechanganywa
kwenye ile timu ya wale vijana wengine, ingeweza kutufanya kuwa
na ufanisi mkubwa sana kwenye masuala ya usalama na upelelezi
wa kiteknolojia kwa sababu dunia yote sasa imehamia kwenye
teknolojia.
Haukupita muda mrefu, simu yangu ya mezani ilianza kuita, ni-
kajua moja kwa moja ni baba yake Saima, nikapokea harakaharaka.
Sikuwa nimekosea, akanipa mrejesho na kunieleza kwamba Jack-
son Mashewa alikuwepo jijini Dar es Salaam, akiwa ameungan-
ishwa kwenye dawati la Data Science! Nitakuja kueleza baadaye
kuhusu dawati hili na jinsi lilivyokuwa likifanya kazi.
Sikuwa nimekosea, akanipa mrejesho na kunieleza kwamba
Jackson Mashewa alikuwepo jijini Dar es Salaam, akiwa ameun-
ganishwa kwenye dawati la Intercom! Nitakuja kueleza baadaye
kuhusu dawati hili na jinsi lilivyokuwa likifanya kazi.
Aliendelea kunieleza kwamba tayari ameshatoa maelekezo
aletwe ofisini hapo haraka iwezekanavyo hivyo nijiandae kwenda
kumpokea.

505 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Nilifurahi sana kwa jinsi baba yake Saima alivyolishughulikia


suala hilo kwa uharaka na uzito wa aina yake, nikashusha pumzi
ndefu na kurudisha simu mezani, tabasamu hafifu likachanua kwe-
nye uso wangu.
Niliendelea kuwaza kwa kina jinsi tunavyoweza kumtumia Jack-
son Mashewa au Jack kama alivyokuwa akitambulika zaidi, nikawa
na uhakika kwamba atakapofika, tukikaa pamoja na nikamueleza
nilichokuwa nakitaka, anaweza kuwa na majibu ya nini cha ku-
fanya.
Baada ya kama dakika arobaini hivi, simu ya baba yake Saima
iliita tena, nikapokea haraka, akanieleza kwamba niende ofisini
kwake kwani tayari mgeni wangu alikuwa amewasili, harakaharaka
nikainuka na kuelekea ofisini kwake.
Nilimkuta Jack akiwa amekaa kwenye kiti mle ndani ya ofisi
ya baba yake Saima, aliponiona nikiingi atu, nikamuona akiachia
tabasamu pana kwenye uso wake. Nadhani alikuwa amekumbuka
mambo mengi sana baada ya kuniona.
Baba yake Saima hakuwa na maneno mengi, akanioneshea tu
kwa ishara kwamba mgeni wangu ndiyo huyo niendelee naye.
Nilimsogelea pale alipokuwa amekaa, akasimama kikakamavu,
tukawa tunatazamana.
Nilichoweza kukibaini harakaharaka, ni kwamba mwili wake
ulikuwa umedhoofika sana, hakuwa kama nilivyomuona mara ya
mwisho, nikajua ni kwa sababu ya msoto wa mafunzo kwa sababu
mafunzo yetu yalikuwa siyo ya mchezo.
Nilinyoosha mkono wangu na kumpa, naye akanyoosha wa

506 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kwake na kunipa! Japokuwa alikuwa amedhoofika kimwili, lakini


alikuwa na nguvu kisawasawa, mkono wake ulikuwa umebadilika
kutoka ule ulaini wa mwanzo aliokuwa nao na kuwa kama chuma,
nikatabasamu huku nikiwa nimemshika mkono, na yeye akiwa
amenipa wa kwake, tukiwa ni kama tunapimana nguvu.
Nilimsogeza kifuani kwangu na kumkumbatia kikomandoo,
naye akafanya hivyo, tukagonganisha vifua, kila mmoja akiwa na
furaha.
“Siamini kama nimekuona tena Chief,” alisema, nikatingisha
kichwa kumtoa wasiwasi, tukawa tunaendelea kutazamana macho-
ni. Hakika alionekana kuiva kisawasawa! Nilimgeukia baba yake
Saima na kumpa ishara ya kuonesha shukrani zangu kwake, naye
akatingishatu kichwa, nikatoka na Jack mpaka nje.
“Unaendeleaje!”
“Niko fit Chief! Imara kama simba,” alisema huku akichekacheka
kwa furaha, alionesha kushindwa kabisa kuificha furaha aliyokuwa
nayo baada ya kukutana na mimi.
Tulipiga hatua ndefundefu utafikiri tupo kwenye gwaride na
muda mfupi baadaye, tukawa tayari tumeshafika ofisini kwangu,
nikamkaribisha na kumuelekeza sehemu ya kukaa, akafanya hivyo.
Ilibidi niache kila kitu kwanza, tuzungumze kwa kina na kubadil-
ishana mawazo juu ya nini cha kufanya na kabla ya yote, nilitaka
kwanza kujua historia yake tangu siku ya mwisho tulipoachana,
nikamuona akishusha pumzi ndefu na kuvaa uso wa ‘userious’ na
kunitazama, tukawa tunatazamana.
“Wewe ni shujaa wa maisha yangu kaka Kenny! Umeyabadili-

507 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

sha maisha yangu na ya familia yangu, sijui nitakushukuru vipi,”


alisema Jackson Mashewa huku akitaka kunipigia magoti, nikamu-
wahi na kumzuia, akawa anaendelea kuniambia mazito aliyokuwa
nayo moyoni kutokana na wema niliokuwa nimemtendea.
“Mshukuru zaidi Mungu wako mdogo wangu! Mimi pia nime-
tokea kwenye familia maskini, najua jinsi ufukara unavyotesa,
naelewa uchungu anaokuwa nao kijana kutoka kwenye familia
maskini anapokuwa anaipambania familia yake. Ni Mungu ndiye
aliyekuonyooshea mapito yako na kamwe usiache kumshukuru
nakuwafanyia wengine mema.
“Mimi pia nilisaidiwa kama ulivyosaidiwa wewe na ndiyo maana
leo unaniona hapa. Pengine ningeshakuwa nimefariki dunia kwa
sababu nilikuwa naishi maisha ya hatari sana,” nilimwambia kisha
tukakumbatiana kikakamavu, nikawa nampigapiga mgongoni
kwani hisia zake zilikuwa zimemzidi kiasi cha kuwa anatokwa na
machozi.
“Jukumu kubwa ambalo unatakiwa kulitimiza maishani mwako
kwa yote yaliyokutokea ni kulitumikia taifa lako kwa moyo wako
wote na uaminifu wa hali ya juu! Tunakutegemea sana na ndiyo
maana nimeomba uletwe kuja kuongeza nguvu kwenye misheni
yetu inayoendelea na nitaendelea kukutumia kila nitakapoona ina-
faa,” nilimwambia.
Ilibidi nianze kwanza kumpigisha stori za tofauti ili kumtoa kwe-
nye ile hali aliyokuwa nayo, nikawa namuuliza kuhusu msoto wa
mafunzoni, akawa ananieleza kila kitu na mwisho tuliishia kuwa
tunacheka, hasa alipokuwa ananielezea kuhusu matukio ambayo

508 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

hatakuja kuyasahau maishani mwake, aliyokutana nayo akiwa


mafunzoni.
Baada ya kuona ametulia na kurudi kwenye hali yake ya
kawaida, nilimrudisha kwenye sababu kuu ya yeye kuwepo pale
wakati ule, nimkamfafanulia baadhi ya mambo na kutaka kusikia
kutoka kwake kwamba ni nini ambacho tungeweza kukifanya kwa
wakati huo ili kukabiliana na hatari iliyokuwa mbele yetu.
Nilimuona akiinamisha kichwa chake chini, akawa ni kama ana-
jaribu kutafakari kwa kina, akabadilisha mkao na kuinua kichwa
chake, akawa anatazama juu kama anayeendelea kutafakari mambo
kwa kina.
“Nina wazo! Kwa uelewa wangu mdogo nilionao, najua lazima
mitaa yote ya kuzunguka Magogoni itakuwa na kamera za usala-
ma,” alisema, akawa ni kama amenifumbua macho jambo ambalo
nilikuwa nalijua vizuri lakini sikuwa nimefikiria kama linaweza
kuwa msaada kwetu.
“Ndiyo! Zipo nyingi na siyo Magogoni tu, katikati ya mji kote
kuna kamera za kificho ambazo zinafanya kazi saa ishirini na nne.”
“Basi itakuwa vizuri sana! Najaribu kuwaza kwa sauti, nimeji-
funza kwamba watu wanapotaka kwenda kufanya tukio mahali,
ni lazima kwamba kuwepo na wale wanaotumwa kwenye eneo la
tukio kwanza kufanya utafiti au kitaalamu recconaissance! Nipo
sahihi?”
“Hakika umekwiva! Ndivyo ilivyo, enhee! Endelea,” nilimwam-
bia huku nikiachia tabasamu hafifu kuoneshwa kukoshwa na jinsi
akili zake zilivyokuwa zinafanya kazi kwa haraka.

509 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Najua kwa siku kadhaa hizi, lazima kuna watu watakuwa wakii-
fanya kazi hiyo, tukifanikiwa kuwabaini watu hao na kuwafuatilia,
tutafanikiwa kuwapata wahusika wa hayo makundi mawili.”
“Tunawezaje kuwabaini?”
“Ni kwa kupitia hizihizi kamera, lazima tufuatilie na kuchunguza
kwa kina kila kitu kilichokuwa kinatokea kwenye mitaa ya kuzun-
guka Magogoni kwa siku hizi tatu mpaka nne zilizopita lakini pia
lazima tuendelee kufuatilia kila kinachoendelea mpaka muda wa
tukio,” alisema.
Kiukweli lilikuwa ni wazo la msingi sana alilolitoa lakini hatu-
kuwa na muda wa kutosha kupitia video zote hizo. Muda tuliokuwa
nao haukuwa unatosha kabisa na ilibidi nimueleze kuhusu hilo.
“Inawezekana kwa kutumia teknolojia. Ni suala la kujua namna
ya kucheza na kamera zote pamoja na servers na kompyuta zinazo-
tumika kuhifadhi taarifa hizo.”
“Unafikiri inaweza kuchukua muda gani?”
“Ikizidi sana ni saa sita!”
“Saa sita? Una uhakika?”
“Ndiyo! Teknolojia imerahisisha sana mambo, nikipewa nafasi
ya kuingia kwenye servers naweza kukuonesha ni kwa namna gani
hilo linawezekana! Ila itabidi niwe na watu wa kunisaidia pamoja
na kompyuta zenye uwezo mkubwa,” alisema, akaniacha nikiwa
nimepigwa na butwaa nikiwa ni kama siamini alichokuwa ameni-
elezea.
Hata hivyo, kwa kuwa yeye alikuwa amebobea kwenye fani hiyo
kuliko mtu mwingine yeyote, ilibidi nikubaliane naye lakini nili-

510 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

taka kwanza anieleze kwa nadharia, Waingereza wanaita ‘theory’,


yaani kukidadavua kitu kwa maneno na maelezo ya kutosha kwan-
za kabla ya kuanza kufanyia kazi wazo husika.
Nilinyayua simu yangu na kupiga kwa vijana wangu wa IT na
Cyber, nikaomba wawasiliane na wenzao wa Intercom kuona kama
tunaweza kupata ‘access’ ya CCTV Camera zote za kuanzia Ma-
gogoni mpaka katikati ya mji.
Ndani ya muda mfupi nilirudishiwa maelezo kwamba inatakiwa
ruhusa kutoka juu, nikajilaumu kwa kutofuata hatua stahiki haraka
bila kupoteza muda. Nilimpigia simu baba yake Saima na kum-
weleza nilichokuwa nakihitaji, akaniambia nisubiri kidogo.
Dakika chache baadaye, alinipigia simu ya mezani na kuniambia
kwamba tayari ruhusa ilikuwa imeshatoka kuanzia juu kwa hiyo
tunaweza kuendelea, akanitumia namba ya mtu wa Intercom wa
kuwasiliana naye moja kwa moja.
Haukupita muda mrefu, kompyuta yangu kubwa na ya kisasa
iliyokuwa mezani kwangu, ilipewa ruhusa ya kuingia kwenye
‘servers’ kuu za Magogoni, nikampisha Jack pale kwenye kiti kisha
mimi nikakaa pembeni na kuanza kufuatilia kwa makini alichoku-
wa anakifanya.
Alibofyabofya kompyuta kisha CCTV Camera zikaanza kufun-
guka, moja baada ya nyingine. Kwa lugha nyepesi, tukiwa palepale
ofisini, tukawa na uwezo wa kuona eneo lote kuanzia katikati ya
mji mpaka Magogoni huku upande wa pili tukiwa na uwezo wa
kuona mpaka umbali wa mita kadhaa baharini, katika eneo lote la
kuzunguka Magogoni, nikashusha pumzi ndefu kwa sababu hicho

511 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

hakikuwa kitu kigeni kwangu, nilishafanya kazi na vijana wangu


waliokuwa wanajua vizuri namna ya kucheza na kamera hizo.
Baada ya kamera zote kufunguka, kila moja ikiwa na jina lake na
mahali ilipo, nilibaki na shauku kubwa ya kutaka kusikia ni hatua
ipi ambayo ilikuwa ikifuatia.
“Kuna teknolojia inaitwa Facial Recognition! Hii ni maalum
kwa ajili ya kutambua sura za watu wanaoonekana kwenye kamera
na kuangalia taarifa zao muhimu zinazoweza kuwa zinapatikana
mtandaoni.
“Kwa nchi zilizoendelea, kwa kuwa kila raia huwa anasajiliwa na
taarifa zake zote kujazwa kwenye database ya taifa, huwa inakuwa
ni rahisi sana kujua kila kitu kuhusu kila mtu anayeonekana kwe-
nye kamera hizi.
“Ila kwa kuwa sisi bado teknolojia haijawa kubwa, ni taarifa
chache zinazoweza kupatikana kwa haraka. Kitu kinachoweza
kufanyika kwa haraka, ni kuchanganya teknolojia tatu mpaka nne
kwa wakati mmoja.
“Ya kwanza itakuwa ni kutambua sura za watu ambao wame-
onekana mara nyingi zaidi katika kamera zote, ya pili itakuwa ni
maalum kwa ajili ya kuangalia namba za magari ambazo zime-
onekana sana katika maeneo ya kuzunguka Magogoni, ya tatu
itakuwa ni kujaribu kutafuta taarifa za tutakaowabaini kuwa wame-
onekana mara nyingi zaidi na hapo tunaweza kuwa tumepata pa
kuanzia,” aliniambia, nikashusha pumzi ndefu na kukaa vizuri.
Yalikuwa ni mambo yanayohitaji uelewa mkubwa wa kiteknolo-
jia ili kuyaelewa kwa kina, nikamtaka aoneshe kwa vitendo. Ali-

512 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

bofyabofya ‘keyboard’ ya kompyuta, akaivuta kamera ya kwanza


kwa karibu, akabofyabofya tena, vitu kama viboksi vikatokea kwe-
nye sura za kila mtu aliyekuwa anaonekana kwenye ile kamera.
Akabofyabofya tena kisha kompyuta ikawa ni kama inatafuta
taarifa fulani muhimu kwenye ‘servers’ na ‘database’, ikawa inatoa
mlio usio wa kawaida, sekunde chache tu baadaye, sura za watu
zinaanza kuonekana kwenye kompyuta kwa wingi. Hakika ilikuwa
ni teknolojia iliyonishangaza sana. Picha zikawa zinaendelea ku-
funguka kwa kasi.
Aliendelea kubofyabofya, akaivuta kwa karibu picha moja kisha
akabofya ‘keyboard’ kwa sekunde kadhaa, zile picha zikawa zinaji-
panga kwa mfuatano maalum unaoonesha watu wanaofanana na
mwisho zikajipanga picha zote zinazomuonesha mtu mmoja.
Akashusha pumzi ndefu na kunigeukia, tukawa tunatazamana
huku na mimi nikishusha pumzi ndefu.
“Hivi ndivyo tutakavyokuwa tunafanya, huyu ni mtu mmoja
ambaye kama unavyoona hapa amenaswa na kamera akiwa kwe-
nye uelekeo wa Magogoni kwa siku nne mfululizo na ndiyo maana
unaona amebadilisha nguo,” alisema huku akizivuta karibu zile
picha.
Alichokuwa anakisema ni kweli, mwanaume wa makamo,
alionekana kwenye kamera hizo huku pia ikionesha ni mara ngapi
alionekana katika maeneo hayo kwa muda wa siku nne kwa nyaka-
ti tofautitofauti.
“Lakini si hivyo tu, tunaweza pia kujua magari ambayo yame-
onekana mara nyingi zaidi katika maeneo yote yenye kamera,”

513 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

alisema huku akibofyabofya kompyuta kisha akatafuta picha ya


gari ambalo namba zake za usajili zilikuwa zinaonekana kwa
mbele.
Akazivuta karibu zile namba kisha akabofyabofya tena! Kwa
jinsi alivyokuwa akibofyabofya kompyuta kwa kasi, ungeweza
kudhani alikuwa mashine, na muda wote wala hakuwa akiitaza-
ma ‘keyboard’, yeye macho yote yalikuwa kwenye ‘screen’ ya
kompyuta, kuonesha ni kwa namna gani alikuwa na uzoefu wa
kutumia kompyuta.
Baada ya kubofyabofya, zile namba za gari zilisogea kwa karibu
kiasi cha kuweza kusomeka vizuri, akaendelea na kazi yake, zile
namba zikazungushiwa kama kiboksi hivi kwa juu yake, akaende-
lea kubofyabofya kompyuta ikaanza tena kusearch na muda mfupi
baadaye, zilionekana picha tofautitofauti zikilionesha gari lilelile,
katika nyakati tofautitofauti.
Nilishusha pumzi ndefu tena na kuachia tabasamu hafifu, nika-
mgeukia na kumtazama. Kwa mwonekano wake na mambo ali-
yokuwa anayafanya, vilikuwa ni vitu viwili tofauti kabisa.

514 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

19
K
AMA nilivyoeleza mwanzo, Jackson Mashewa
alikuwa bado ni kijana mdogo, ukichanganya na
msoto alioupata mafunzoni, alizidi kuonekana
kuwa mdogo lakini alikuwa na akili na ujuzi
mkubwa mno.
“Unadhani hiki unachokifanya kinaweza kutusaidia vipi kuwa-
nasa wahusika kabla hawajaleta madhara?” nilimuuliza.
“Lazima tuwe na ‘keywords’ kwa maana lazima tujue tunatafuta
nini. Inaweza kuwa labda tunajaribu kuangalia nyendo za mtu
fulani ambaye tunamtilia mashaka, lakini pia tunaweza kuwa labda

515 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

tunatafuta mtu mwenye jina fulani au gari zenye namba fulani.


“Kwa mfano unaweza kuwa na orodha ya majina ya watu ambao
unataka kujua kama wameonekana kwenye kamera. Utakachoki-
fanya kwanza itakuwa ni kuingiza jina mojamoja, kisha unatafuta
taarifa zao mitandaoni, ikiwemo sura zao kutokea kwenye ‘data-
base’ ya mfumo wa utoaji leseni za barabarani, leseni za biashara
au hata vitambulisho kama kitambulisho cha uraia au hata hati ya
kusafiria.
Ukishaipata sura ya mhusika, unafanya kitu kinachoitwa ‘facial
matching’ kwenye kumbukumbu za picha zilizonaswa na kamera
zetu ambapo ndani ya muda mfupi tu, utaweza kuona picha za
mhusika kama alionekana maeneo hayo na kama hakuonekana,
basi itakurudishia majibu kwamba mtu huyo hajaonekana kwenye
kamera yoyote,” alisema.
Hapohapo nikawa nimeshapata mwanga wa jinsi tunavyoweza
kuifanya kazi hiyo kwa urahisi na akili zangu zilinituma kwanza
kuangalia katika ile orodha ya wageni wote ambao walitakiwa
kuhudhuria dhifa maalum na namba moja Magogoni.
“Hatuna muda wa kupoteza, hebu tuanze na haya majina,”
nilisema huku nikisogea kwenye kompyuta na kutafuta email am-
bayo nilitumiwa na baba yake Saima ya orodha ya wageni ambao
walitarajiwa kuwepo kwenye dhifa ile.
Tulipoingiza jina la kwanza tu, kitu kisicho cha kawaida kilion-
ekana. Jina lenyewe lilikuwa ni Alpha Mutakingirwa ambaye
taarifa zake kwenye ile orodha ya wageni, zilionesha kuwa ni
mfanyabiashara.

516 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Alipoanza kutafuta taarifa zake, haraka sana picha zake zilion-


ekana kwenye mfumo wa idara ya uhamiaji wa hati za kusafiria
(passport). Tulipoipata picha yake na kuanza kuitafuta kwenye
kamera, ilionesha kwamba ameonekana mara tatu kwa siku tofauti
na mara zote alikuwa ndani ya gari.
Katika mara zote alizoonekana kwenye kamera, alionekana
akipita karibu kabisa na lango la Magogoni, upande wa mbele.
Nikamtaka tufuatilie zile namba za gari zilizokuwa zinaonekana na
kutaka kujua mmiliki ni nani kabla hatujaendelea.
Ndani ya muda mfupi tu, tayari alikuwa ameingia kwenye mfumo
wa usajili wa magari wa mamlaka ya ukusanyaji wa mapato, tu-
kafanikiwa kugundua kwamba gari lilikuwa limesajiliwa kwa jina
lake lakini pia taarifa zilionesha kwamba alikuwa akimiliki magari
mengine matatu.
Nilimtaka tujaribu kuyatafuta hayo magari mengine kama nayo
yanaweza kuonekana kwenye kamera kwa kutumia zile namba za
usajili. Kati ya hayo matatu, ni moja ndilo lililoonekana kwenye
kamera na tulipofuatilia, ilionesha kwamba nalo lilikuwa lime-
onekana mara tatu kwa nyakati tofauti na kilichotushangaza ni
kwamba nalo lilionekana katika muda uleule kama ambao lile gari
la yule mfanyabiashara lilionekana.
Kwa kifupi ni kwamba magari yote mawili yalikuwa yamepita
kwenye njia zinazofanana, kwa muda unaofanana, jambo lililoone-
sha kwamba walikuwa kwenye msafara wa pamoja.
Nilisimama huku jasho likinitoka makwapani, sikuwa nimetarajia
kwamba kwa kutumia teknolojia, kazi in aweza kuwa nyepesi kiasi

517 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

hicho na tunaweza kubaini mambo mengi namna hiyo. Nilimuom-


ba anikusanyie kwanza ushahidi wote na kuutuma kwenye email
yangu kuhusu huyo mtu mmoja tu kwanza, kisha baada ya hapo
ndiyo nijue nini cha kufanya.
Wakati akiendelea na kazi hiyo, mimi nilikuwa nazunguka-
zunguka tu mle ofisini kwangu, nikiwaza na kuwazua. Kipupwe
kilichokuwepo, hakikusaidia chochote kuzuia kijasho chembamba
kisinitoke.
Baada ya kuwa ameshanitumia, nilimtaka aendelee na majina
yote, moja baada ya jingine kwa namna ileile kama ambavyo
tulifanya kwa jina lile la kwanza, nikatoka na kuelekea ofisini kwa
baba yake Saima.
Aliponiona nikiingia mbiombio hata bila kubisha hodi wala kum-
pigia simu, aligundua kwamba kuna jambo haliko sawa, akaacha
kila alichokuwa anakifanya na kusimama, nikamtaka akae na kuin-
gia kwenye email yake kuangalia nilichokuwa nimemtumia baada
ya mimi kuwa nimetumiwa na Jack.
“Ni nini hiki!” alinihoji huku na yeye akiwa ni kama amepigwa
na butwaa, ikabidi nianze kumueleza, jambo moja baada ya jingine
ili tuelewane vizuri.
Nilimweleza kile alichokuwa amenieleza Jack na nikamwambia
kwamba tulijaribu kufanya kwa majaribio kwenye jina moja kati
ya wageni waliotakiwa kukutana na namba moja kwenye mkutano
wake na wafanyabiashara wakubwa nchini.
“Hili jina na hii sura siyo vigeni kwangu,” alisema, nikaendelea
kumsimulia kila kitu tulichokibaini, nikamuona na yeye akipoteza

518 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kabisa utulivu.
“Kumbe maadui zetu wapo karibu yetu kuliko tulivyokuwa
tunafikiria! Nakubaliana na wewe sasa kwamba kumbe kazi bado
ndiyo kwanza imeanza,” alisema huku akivua koti la suti alilokuwa
amevaa, akalegeza na tai aliyokuwa ameivaa.
“Huyu kijana ana akili kubwa sana! Anaweza kutusaidia kutegua
hiki kitendawili kilichopo mbele yetu!” alisema, nikamweleza kila
alichokuwa anakihitaji na yeye akaniambia kwamba tunatakiwa
kumsaidia na kuhakikisha kila anachokitaka kinatimia na kazi ina-
fanyika haraka iwezekanavyo.
“Tunaanzia wapi?” aliniuliza, swali ambalo hata mimi nilikuwa
nataka kumuuliza. Nadhani alikuwa ameniwahi, nikashusha pumzi
ndefu.
“Nafikiri kwanza tumalizie kuwachunguza wageni wote walioa-
likwa kisha kutokea hapo ndipo tunapoweza kuanza kuunganisha
nukta moja hadi nyingine ili kupata picha kubwa iliyojificha,”
nilimwambia.
“Hawa wendawazimu wamejipanga kisawasawa na tukiwachekea
kweli Magogoni itaanguka, inabidi kwanza tuitishe kikao cha
dharura cha viongozi wote ili tujadiliane kwa pamoja nini cha
kufanya. Naamini kila mmoja akitumia akili zake kisawasawa,
tutafanikiwa kuwawahi na kuwadhibiti. Hii ni hatari sana,” alisema
huku akichukua simu yake ya mezani na kuanza kuibofyabofya,
akaniambia nirudi ofisini kwangu na atakaponipigia simu, nielekee
kwenye chumba cha mikutano ya siri bila kupoteza hata dakika
moja, nikatingisha kichwa kukubaliana na alichokisema, nikatoka

519 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

na kumuacha akiwa anazungumza na simu, huku na yeye akione-


sha kabisa kupoteza utulivu.
Ilibidi nielekee moja kwa moja kwenye ofisi ya vijana wangu wa
IT na Cyber, nikawakuta wakiwa wanaendelea na majukumu yao,
kila mmoja akionesha kuwa bize kisawasawa.
Kama nilivyosema awali, narudia tena kusema kwamba siyo
kwamba sikuwa nawaamini vijana wangu wa vitengo vya IT na
Cyber, tulifanikisha mengi sana na timu hii iliyojawa vijana wado-
go wenye ujuzi mkubwa wa masuala ya teknolojia.
Kwa hiyo kila nilipokuwa nikipata nafasi ya kuzungumza nao,
nilikuwa nawaeleza ni kwa namna gani naheshimu mchango wao
katika kuitumikia idara lakini kubwa zaidi katika kuitumikia nchi.
“Mnaendeleaje wapambanaji!” nilisema baada ya kuingia, wote
wakaacha kila walichokuwa wanakifanya na kunisikiliza maana
ujio wangu ulionesha kwamba kuna jambo nakwenda kuwaeleza.
“Tumepata ugeni! Kuna ingizo jipya!” nilisema huku nikizun-
guka huku na kule. Nikawatajia jina la Jackson Mashewa na ni-
kawafafanulia kwamba kijana huyo amekuja kuongeza nguvu kwa
sababu yeye anao utaalamu wa tofauti kidogo kwa hiyo anaweza
kutusaidia.
Ilikuwa ni lazima kwanza niwajenge kisaikolojia ili wasije waka-
ona kama tumewadharau kiasi cha kuwatafutia mtu mwingine wa
kuongeza nguvu!
Unaposhughulika na vijana, unatakiwa kuwa makini sana na
japokuwa mimi pia nilikuwa kijana, nilikuwa nimejifunza mambo
mengi sana mafunzoni juu ya namna ya kufanya kazi na timu ya

520 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

vijana, tena ambao damu zao zinachemka.


Baada ya kuhakikisha kwamba wote wamenielewa, niliwaambia
wanisubiri kidogo nitarejea nikiwa na Jackson Mashewa lakini
pia nitakuja na mpango kazi mpya! Kwa muda huo nikawataka
waendelee kwanza na majukumu yao.
Nilirudi mpaka ofisini kwangu, nikamkuta Jack akiwa anaende-
lea na ile kazi aliyokuwa ameianza, akionesha kuwa bize kwelik-
weli, nikakaa pembeni na kufuatilia alichokuwa anakifanya.
“Mambo ni mengi sana Chief!” alisema huku akiinua uso wake
na kunitazama, na mimi nikawa namtazama.
“Kuna watu kadhaa ambao wanaonekana ni kama wana lengo
linalofanana,” alisema, sikutaka kumkatisha kwanza alichokuwa
anakifanya, nikataka amalize kwanza kisha ndiyo anielee kwa
kina.
Alifanya hivyo kisha baada ya kama dakika mbili za kubofy-
abofya sana kompyuta yake, alisimama na kujinyoosha, akanitaka
nikae pale alipokuwa amekaa yeye ili nijionee mwenyewe ali-
chokuwa amekibaini.
Kulikuwa na picha kadhaa zikiwaonesha watu tofautitofauti,
wakiwa ndani ya magari, wakiipiga picha Magogoni kutokea
pande tofautitofauti.
“Inawezekanaje watu wakawa wanapiga picha bila kushtukiwa
na vyombo vya ulinzi?”
“Inaonekana walikuwa wanatumia kamera za kisasa zenye
uwezo wa kuvuta picha hata ikiwa umbali mrefu, ukitazama
hapa utagundua kwamba hawa walikuwa wakipiga picha kutokea

521 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

mbalikabisa na Magogoni, mahali ambapo hakuna anayeweza ku-


washtukia,” alisema, akawa anazivuta zile picha kwa karibu, kweli
wakawa wanaonekana wakipiga picha kutokea ndani ya magari.
“Hawa wakifuatiliwa kwa haraka, tunaweza kupata picha kubwa
iliyojificha, tunatakiwa kuwapata mmoja baada ya mwingine,
haraka iwezekanavyo,” nilimwambia, akashusha pumzi ndefu,
akaniambia kwamba tunatakiwa kusubiri kwanza tumalize kazi
ya kukusanya taarifa kisha ndiyo mambo mengine yatakapofuata,
tukiwa tayari tumeshapata picha inayoeleweka.
Niliona ni kama ananichelewesha, tayari damu ilikuwa inachem-
ka kisawasawa ndani ya mwili wangu na ilikuwa ni lazima kila kitu
kifanyike haraka iwezekanavyo.
Nikiwa naendelea kujadiliana naye, simu ya mkononi iliita,
ilikuwa ni namba ya simu ya baba yake Saima, harakaharaka ni-
kaipokea.
Kwa kuwa tayari alishanielekeza nini cha kufanya, niliiinuka
na kuiweka sikioni huku nikipiga hatua ndefundefu kuelekea kule
kwenye chumba cha mikutano ya siri, nikamuonesha ishara Jack
kwamba yeye aendelee na kazi.
Ndani ya dakika zisizozidi mbili, tayari nilikuwa nimeshafika
kwenye lango la kuingilia kwenye chumba hicho, nikakutanana vi-
ongozi kadhaa nao wakielekea ndani, kila mmoja akionesha kuwa
na haraka kwelikweli.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, kila mmoja aliingia kimya-
kimya na kwenda kukaa kwenye eneo lake, meza kuu kukiwa na
watu wawili, mkurugenzi na baba yake Saima. Mkurugenzi ndiye

522 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

aliyefungua kikao baada ya kuwa watu wote wameshafika na


milango kufungwa, akatueleza kwamba tumekutana kwa kikao cha
dharura kwa sababu kuna taarifa mpya zilikuwa zimepatikana.
Akamkaribisha baba yake Saima ambaye naye bila kupoteza
muda, alinitaka nisogee kwenye ‘podium’ ndogo iliyokuwa mbele
ya ukumbi, kwa pembeni kidogo. Podium ni neno la Kiingereza
ambalo huwa linamaanisha kile kijukwaa kidogo kinachotumika
mtu anapozungumza kwenye mkutano.
Nilisogea pale na kuwasalimu watu wote kisha nikaanza kue-
leza kwa kifupi, nikigusia maeneo muhimu ya nilichokuwa
nimekibaini. Kila mmoja alionesha kushangazwa sana na jinsi
nilivyopata wazo kama lile na kulifanyia kazi, nadhani hakuna
aliyekuwa amewaza kama mimi.
Baada ya kueleza kila kitu, ikiwa ni pamoja na mapendekezo ya
nini cha kufanya, ulifika muda wa wajumbe wengine nao kuchan-
gia mawazo yao, mimi nikarudi kukaa. Kila aliyekuwa akisimama
pale mbele, kwanza alikuwa ananipongeza sana kwa jinsi nili-
vyokuwa ‘sharp’ kichwani, moyoni na mimi nikawa nampongeza
Jack kwa sababu kazi kubwa ilikuwa imefanywa na yeye.
Nilichokibaini, watu waliokuwa wamekusanyika kwenye kikao
hicho cha dharura, walikuwa na uwezo mkub wa sana wa kufikiri
kwa sababu mipango iliyokuwa inatolewa na kila mmoja, ilikuwa
siyo ya kitoto.
Nikawa bize kuandika mawazo ya kila mmoja kwa umakini
mkubwa na baada ya wote kuzungumza, baba yake Saima naye
alisimama na kutoa mjumuisho wa pamoja, ikiwa ni pamoja na

523 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kueleza mbinu ambazo zitatumika kuikamilishakazi iliyokuwa


mbele yetu, haraka iwezekanavyo.
Alichokiagiza ni kwamba viongozi wote wanatakiwa kushiriki
kwa asilimia 100 na hakuna atakayeruhusiwa kuondoka kazini
mpaka tuhakikishe tumefanikiwa kuwadhibiti wendawazimu wale.
Mimi nilitakiwa kwenda kuwapanga vijana wangu na ku-
hakikisha kazi ile inafanyika ndani ya saa sita kama ilivyokuwa
imepangwa, na wakati mimi nikiendelea na kazi hiyo, viongozi
wengine nao watakuwa wakinisaidia kwa karibu pamoja na kue-
ndelea na majukumu mengine, kila mmoja kama ambavyo ange-
pangiwa.
Nguvu ilikuwa kubwa na kwa kiasi fulani nilijihisi kuutua mzigo
mzito niliokuwa nao, baada ya kuona sasa kila mmoja anaingia
uwanjani kuongeza nguvu. Kikao kiliahirishwa na tukakubaliana
kukutana baada ya saa sita kuisha kwa ajili ya kujua maendeleo ya
kilichokuwa kinafanyka.
Nilipotoka tu, moja kwa moja nilirudi ofisini kwangu, nikamkuta
Jack akiwa anaendelea na kazi, akiwa bize kwelikweli.
“Sasa kuna mabadiliko kidogo!” nilimwambia, akaacha kila ali-
chokuwa anafanya na kunitazama.
“Tunatakiwa kuhamia kwenye ofisi yenye vifaa bora zaidi na
timu ya kushirikiana nayo ili kuifanyakazi hii!” nilimwambia,
nikamuona akiachia tabasamu pana kwa sababu pale mazingira ya-
likuwa magumu kwake kufanya kazi kwa kasi aliyokuwa anaitaka
kama mwenyewe alivyokuwa anasema.
“Nakwenda kukukutanisha na timu ya vijana wenzako, wapo

524 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

waliobobea kwenye IT lakini pia wapo waliobobea kwenye Cy-


ber, hawa ndiyo utakaokuwa ukifanya nazo kazi kwa karibu, mimi
nikiwa pembeni yako! Ndani ya saa sita lazima kazi iwe imekami-
lika kama ulivyonieleza.
Jack alitingisha kichwa kuonesha kukubaliana na nilichomwam-
bia, akamalizia alichokuwa anakifanyakisha tukainuka, nikatangu-
lia na yeye akawa ananifuata kwa nyuma.
Tulitembea kwa hatua ndefundefu na muda mfupi baadaye tayari
tulikuwa tumewasili kwenye ofisi za vijana wetu wa IT na Cyber.
Kama ilivyokuwa mwanzo, tulipoingia tu, vijana wote waliacha
kila walichokuwa wanakifanya na kutulia, wakawa wanatutazama,
zaidi wakimtazama Jack.
“Guys! Habari za kazi?” niliwasalimia tena, wote wakaitikia,
nikarudia kuwatambulisha kwa Jack kisha nikamtambulisha pia
Jack kwao.
Nikarudia kuwaeleza kuhusu Jack pamoja na ujuzi aliokuwa nao,
nikawaeleza ni kwa sababu gani tumeamua kumuongeza kwenye
timu yetu na kuwaomba watu wote wampe ushirikiano ili kwa
pamoja tukamilishe kazi iliyokuwa mbele yetu.
Nilimpa nafasi ya kuzungumza mawili matatu, akawasalimu
wote kwa adabu, akarudia kujitambulisha kisha akaeleza kwa kifu-
pi kuhusu ujuzi wake. Hakukuwa na muda wa kupoteza, nikamua-
giza mmoja kati ya wale vijana, amuwekee vizuri meza iliyokuwa
tupu, nikamuelekeza akakae.
Kilichofuata baada ya hapo, ilikuwa ni mimi kuanza kwa ku-
waeleza jinsi mpango kazi ulivyokuwa. Kila mmoja alibaki

525 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

amepigwa na butwaa kwa sababu hawakuwa wamefikiria kama


ambavyo mimi nilikuwa nimefikiria.
Lakini pia hakuna ambaye alikuwa anaelewa ni kwa namna
gani misheni ile ingewezekana kwa kutumia teknolojia. Baada ya
kuwaeleza kwa kina kuhusu mpango mzima wa kuzifuatilia kwa
kina kamera zote za ulinzi zilizokuwa katika eneo lote la kuanzia
katikati ya mji mpaka Magogoni.
Baada ya kumaliza kuwaeleza kuhusu mpango kazi wote, uli-
wadia muda wa Jack kusimama na kueleza mbinu za kiteknolojia
ambazo alipanga kuzitumia ili kufanikisha kazi hiyo nzito iliyoku-
wa mbele yetu, ya kuhakikisha tunafuatilia nyendo za watu wote
ambao katika siku chache zilizopita wameonekana maeneo yote ya
kuzunguka Magogoni.
Alisimama na kusogea mbele, nikamuonesha kwa kidole kwamba
asogee kwenye ubao mweupe na kueleza kwa maandishi na micho-
ro jinsi kazi hiyo itakavyofanyika, ili kitu mtu aelewe vizuri.
Alifanya kama nilivyokuwa nimemuelekeza, akarudia kutoa sal-
amu kisha akaanza kueleza, hatua moja baada ya nyingine. Alieleza
kuhusu kamera za CCTV jinsi zilivyokuwa zimefungwa katika
maeneo yote muhimu kuanzia katikati ya jiji mpaka Magogoni.
Akaendelea kutoa darasa utafikiri ni mhadhiri wa chuo kikuu,
akawa anafafanua hatua moja baad aya nyingine jinsi kazi itaka-
vyofanyika. Wakati akiendelea kutoa maelekezo, mimi nilikuwa
naset vizuri ‘projector’ ili akishamaliza kuelekeza kwa nadharia,
tuhamie kwenye vitendo.
Kwa ambao hawajui ‘projector’ ni nini, hiki ni kifaa cha kisasa

526 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kinachotumia teknolojia kama ile iliyokuwa inatumika miaka ya


nyuma kuonesha sinema zile za kwenye matambara yanayofungwa
uwanjani hususan nyakati za usiku.
Tofauti yake ni kwamba hizi projector za kisasa, zinakuwa zi-
naweza kusoma taarifa za picha au video kutoka kwenye kompyuta
kisha kuzielekeza kwenye ukuta mweupe au ubao maalum ambapo
kile kinachoonekana kwenye kompyuta kinakuwa kinaonekana kwa
ukubwa pia kwa kutumia ukuta au ubao maalum.
Hata kwenye baadhi ya kumbi za starehe au kumbi za mikutano,
teknolojia hiyo inatumika sana siku hizi kuonesha picha na video
kwa ukubwa kupitia ukuta safi au ubao maalum. Wengine wanatu-
mia hata kuoneshea mechi za mpira wa miguu kwenye eneo lenye
watu wengi.
Baada ya kueleza kwa nadharia, uliwadia sasa muda wa kuon-
esha kwa vitendo, Jack akarudi kukaa pale kwenye ile meza yake,
kompyuta mpakato niliyokuwa nimemuandalia nikawa nimeshai-
unganisha na ‘projector’ na sasa alianza kuonesha kwa vitendo,
akitumia baadhi ya taarifa nilizokuwa nimempa kutoka kwenye
‘server’ zinazotunza kumbukumbu ya taarifa zote za kamera za
ulinzi zilizokuwa zimefungwa kuanzia katikati ya mji mpaka eneo
lote la kuzunguka Magogoni.
Kwa jinsi alivyokuwa akifafanua kila kitu kwa lugha rahisi, kila
mmoja aliweza kuelewa vizuri kabisa, moyoni nikawa nachekelea
kwa sababu alionesha kwamba kweli yeye ni mtu muhimu sana
anayeweza kutusaidia kisawasawa kukabiliana na ile changamoto
kubwa iliyokuwa mbele yetu.

527 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Alifanya kama alivyokuwa amenionesha kule ofisini kwangu, ni-


kawa namsaidia kufafanua kwenye maeneo ambayo pengine aliku-
wa akiyaruka au kuelezea kwa kifupi, kila mtu akawa anashangaa
kwa sababu alionesha kuwa na uelewa mkubwa kuliko kawaida.
Alieleza jinsi tunavyotakiwa kwanza kuwa na ‘keywords’ za ku-
jua ni nini tulichokuwa tunakitafuta, akaeleza pia kuwa teknolojia
ile ilikuwa na uwezo wa kufuatilia kuanzia sura za watu na kuzit-
ambua lakini pia kufuatilia namba za magari na kuyafuatilia kujua
mmiliki wake ni nani na kama anamiliki magari mengine.
Kwangu mimi kila kitu kilikuwa ni marudio kwa sababu alisha-
nionesha kule ofisini tukiwa wawili tu.
Alirudia mfano wa kutafuta jina la mtu na kuangalia kama ame-
onekana mara ngapi kwenye kamera, akatumia jina la Alpha Mu-
takingirwa ambaye alikuwa miongoni mwa wafanyabiashara am-
bao walialikwa kwenye dhifa maalum na namba moja Magogoni.
“Sijaelewa hapo, imewezekanaje kupata taarifa zote hizi za huyo
mtu ndani ya muda mfupi?” aliuliza kijana mmoja, miguno ikasiki-
ka mle ndani kutoka kwa wenzake kwa sababu ilionesha ni kama
yeye anachelewa kuelewa.
Ilibidi nimsaidia kufafanua eneo hilo na kueleza jinsi tuna-
vyoweza kutumia ile teknolojia ya Facial Matching kwa maana
ya kufananisha sura za mtu mmojammoja kutoka kwenye mifumo
mbalimbali, ikiwemo ule wa hati za kusafiria, mfumo wa vit-
ambulisho vya taifa mpaka mfumo wa leseni za udereva pamoja na
leseni za biashara.
Baada ya kuhakikisha kila mmoja ameelewa, Jack aliendelea

528 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kuonesha kwa vitendo jinsi kazi inavyotakiwa kufanyika, nikawa


nawasikia vijana wangu wakishusha pumzi ndefu, mmoja baada ya
mwingine.
Baada ya kumaliza mfumo wa kutambua sura, alirudia mfano
mwingine wa namna ya kutambua alama za magari na kuwajua
mpaka wamiliki wake kwa kutumia mfumo wa mamlaka ya mapa-
to, akawa amemaliza kuonesha kwa vitendo. Katika hali ambayo
sikuitegemea, vijana wangu wote walisimama na kumpigia makofi,
nikamuona Jack akiachia tabasamu hafifu.
Baada ya kumaliza kumpigia makofi, nilisogea pale mbele na
kuanza kuwaeleza sasa jinsi tutakavyojigawa kwa ajili ya kuanza
utekelezaji wa vitendo haraka iwezekanavyo.
“Jack amenieleza kwamba kazi hii inaweza kuchukua muda wa
mpaka saa sita kuimaliza, kwa hiyo naomba kila mtu aache kila
alichokuwa anakifanya kisha kwa pamoja tufanye kazi hii iliyopo
mbele yetu.
Niliwapanga vizuri vijana wangu na kwa kuwa ofisi nzima
ilikuwa na mashine za kisasa, kazi ilionesha kuwa inaweza kumal-
izika kabla ya hata muda husika tuliokuwa tumepanga.
Tulipita kwenye kompyuta ya kila mmoja na kufanya kazi ya
kuwaunganisha kwenye ‘servers’, mmoja baada ya mwingine na
baada ya kuhakikisha kila kitu kimekamilika, kazi ilianza huku
Jack akiwa ndiye kiongozi wa kazi hiyo.
Nilichokuwa nakifanya, ilikuwa ni kuwasimamia kwa karibu ili
kuhakikisha kila mmoja anafanya kazi ile kwa ufasaha na kuweka
kumbukumbu kwenye ‘folders’ maalum ambazo zilikuwa zimeten-

529 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

genezwa maalum kwa ajili ya kazi hiyo.


Baada ya kuhakikisha kila mmoja ameelewa kinachotakiwa ku-
fanyika, nilitoka kwa dakika chache kwenda kuzungumza na baba
yake Saima kuona na wao walikuwa wamefikia wapi kwa sababu
kila mmoja alikuwa amepangiwa majukumu yake.
“Unazidi kuniheshimisha Kenny, ulichokionesha leo kimefanya
viongozi wetu wazidi kukuheshimu kuliko kawaida na tayari
namba moja ameshaambiwa kila kinachoendelea na ameahidi
kukutana tena na wewe hili likipita salama,” alisema, nikatabasamu
kwa furaha.
Aliniambia kwamba kwa sasa namba moja mwenyewe amekubali
lile wazo letu la kutumia ‘double’ wake kwa sababu ameshagundua
ni kwa namna gani maadui zetu wamejipanga kuhakikisha wa-
natimiza lengo lao la kuiangusha Magogoni.
Akaniambia kuwa ‘deep state’ walikuwa wameingia kazini na ni
wao ndiyo walioshauri kwamba kwa sababu imeshindikana kuia-
hirisha hiyo dhifa yake na wafanyabiashara, basi lazima tahadhari
zichukuliwe mapema.
Nilishusha pumzi ndefu kwa sababu kiukweli sikuwa nimewahi
kufanya kazi mstari wa mbele na ‘double’ hata mara moja zaidi ya
kujifunza tu nilipokuwa Israel mafunzoni.
Nilijikuta nikiwa na shauku kubwa sana ya kushuhudia mwe-
nyewe jinsi mambo yatakavyokuwa yanakwenda lakini kubwa
zaidi nilikuwa na shauku kubwa ya kuona jinsi tunavyokwenda ku-
wazidi akili hawa wendawazimu na kuzima shambulio walilokuwa
wanataka kulifanya la kuiangusha Magogoni.

530 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Tulizungumza mambo kadhaa na baba yake Saima, akanieleza


mambo mengine makubwa kabisa yaliyokuwa yanaendelea ku-
fanyika chini kwa chini katika kuhakikisha kwamba jaribio hilo
linazimwa na mwisho akanisisitiza kwamba natakiwa kuhakikisha
nafanikiwa kuyajua yale makundi mawili ambayo ndiyo haswa
yaliyopangwa kutekeleza kwa vitendo shambulio hilo.
“Kila mmoja anakutazama wewe, mpaka Deep State wamekubali
uwezo wako na wamekuvulia kofia, kwa hiyo hii inaweza kuwa
ni kama penalti ya mwisho kwenye mechi ya fainali, hakikisha
unatumia akili zako zote kuwajua Cat Girls ni akina nani lakini pia
kulijua hilo kundi la pili la hao wanaume ambao ndiyo wataka-
okuja na silaha kufanya walichokusudia kukifanya,” alisema baba
yake Saima.
Akaendelea kunipa ushauri wa jinsi ninavyotakiwa kulishughu-
likia suala hilo, akanipa sana motisha na kuonesha ni kwa namna
gani anavyoheshimu uwezo mkubwa niliokuwa nao.
Baada ya kumaliza kuzungumza naye, ilibidi nitoke na kumua-
cha aendelee na kazi kwa sababu alionesha kuwa na ratiba ngumu
kwelikweli, nikarudi ofisini kwangu na kuendelea kutafakari nini
cha kufanya.
Nilishaeleza kwamba miongoni mwa watu ambao nilikusudia
kwenda kuzungumza nao kwa mara nyingine, ilikuwa ni Ustaadh
Fundi wa Kibiti ambaye kwa hakika alikuwa ametusaidia sana
kwenye misheni ya kumsaka Abdulwaheed na Mutesigwa.
Kuna jambo moja ambalo niliamini kwamba nikilifanya, ni-
tamfanya Ustaadh Fundi awe tayari kupambana kufa na kupona,

531 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

yaani kumfanya asiwe tu mtu anayetusaidia lakini pia aone kwam-


ba kazi iliyokuwa inatakiwa kufanyika, ilikuwa inamhusu pia.
Ni hapo ndipo nilipopata wazo jipya, nikachukua ‘tape recorder’,
kifaa maalum cha kurekodia sauti na kutoka ofisini kwangu, ni-
kaelekea kule kwenye chumba cha mahojiano na lengo lilikuwa ni
kwenda kuonana na Zuleikha Jamal Kandauma, mtoto wa Ustaadh
Fundi ambaye alikuwa miongoni mwa mabinti waliorubuniwa na
Abdulwaheed.
Niliwapa maelekezo vijana wangu wakamtoe kule kwenye chum-
ba maalum alikokuwa anashikiliwa na wenzake, hilo likafanyika na
muda mfupi baadaye, yule binti aliletwa kwenye kile chumba cha
mahojiano.
Aliponiona tu, alianza kuangua kilio kama kawaida yake, akione-
sha jinsi alivyokuwa anahitaji msaada kutoka kwangu.
“Kinachokuliza ni nini?”
“Nataka kwenda nyumbani!” alisema huku akiendelea kulia kwa
kwikwi, nikamwambia asiwe na wasiwasi nitamsaidia kama nili-
vyokuwa nimemuahidi tangu mwanzo na hakuna chochote kibaya
kinachoweza kumtokea.
“Muda si mrefu nakwenda Kibiti kuonana na baba yako, niliku-
wa nataka kama kuna chochote ambacho ungependa kumwambia,
ukiseme na nitakurekodi kwa hii ‘tape recorder’ kisha nitakwenda
kumsikilizisha.
Naamini na yeye akikusikia, atazungumza jambo kwa ajili yako
na nikirudi nitakuja kukusikilizisha,” nilimwambia, nikamshauri
kwamba kama nilivyokuwa nimemuahidi, nitamsaidia kutoka

532 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

salama lakini hiyo itategemea na kama tutafanikiwa kulizuia sham-


bulio lililokuwa mbele yetu.
Nikamwambia kama kuna chochote anachoweza kumwambi
ababa yake ambacho kinaweza kutusaidia kwenye kazi ya kuwata-
futa watu wote anaohisi wanaweza kuwa wanahusika, basi am-
weleze. Nikamhakikishia kwamba hakuna mtu mwingine yeyote
anayeweza kujua chochote kuhusu atakachokizungumza zaidi ya
sisi watatu kwa maana ya mimi, yeye na baba yake.
Baada ya kumaliza kumweleza, nilimuona akishusha pumzi
ndefu, akafuta machozi na kukaa vizuri kwenye kiti chake, nikai-
bonyeza ile tape recorder kuruhusu ianze kurekodi kisha nikam-
sogezea kwenye ile meza iliyokuwa inatutenganisha.
Akaanza kwa kumsalimu baba yake, akamsimulia kila kitu kili-
chokuwa kimetokea tangu siku ya mwisho alipokuja kuchukuliwa
nyumbani kwao na wasaidizi wa Abdulwaheed, akasimulia mambo
mengi sana, mengine yakiwa ni ambayo hata mimi mwenyewe
sikuwa nayajua.
Alizungumza kwa karibu dakika kumi nzima, wakati mwingine
akilia, wakati mwingine akizungumza kikabila na mwisho alimal-
iza. Niliichukua ile tape recorder na kuibonyeza tena, nikaisave ile
sauti yake kisha nikajaribu kuicheza palepale mbele yake ili kuwa
na uhakika kama ilikuwa imerekodi kama inavyotakiwa.
Ilisikika vizuri sana, nikazungumza naye mambo machache kisha
nikarudia kumpa moyo na kumtaka asiwe na wasiwasi, nikainuka
na kuagana naye, nikatoka ambapo vijana wangu waliingia na
kumtoa, wakamrudisha kule walikokuwa wamehifadhiwa.

533 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Nilirudi ofisini kwangu, nikajaribu kuicheza tena ile sauti yake,


nikitaka kujiridhisha kwenye baadhi ya mambo aliyokuwa ameya-
zungumza. Kulikuwa na dondoo nyingi kwenye mazungumzo
yake, ambazo niliamini baba yake kwa maana ya Ustaadh Fundi
akienda kuzisikiliza, anaweza kuwa na majibu yatakayotusaidia.
Baada ya kuisikiliza yote, niliizima ile tepa recorde, nikainua
mkonga wa simu ya mezani, nikamtaarifu baba yake Saima kwam-
ba nilikuwa nataka kwenda Kibiti mara moja lakini nitarejea ha-
raka iwezekanavyo kwa sababu kuna taarifa za muhimu nilikuwa
nakwenda kuzifuata kwa Ustaadh Fundi.
Alikubaliana na mimi na kunitaka nikitoka nisiondoke peke
yangu, lazima niende na mmoja kati ya vijana wangu kwa ajili
ya usalama wangu lakini pia akataka nisitumie gari langu ambalo
huwa nalitumia kazini bali nichukue gari la kiraia ili mtu yeyote-
asije akanigundua nikiwa njiani.
Nilimshukuru, nikampigia simu mkurugenzi ambaye pia alin-
ieleza mambo kama yaleyale ambayo alinieleza baba yake Saima
na kunipa baraka zote.
Baada ya kumaliza kuzungumza naye, nilirudi kule kwa vijana
wangu, nikawapitia mmoja baada ya mwingine na baada ya ku-
jiridhisha kwamba kazi zilikuwa zinaenda kama zilivyopangwa,
nilitoka bila kuwaeleza kwamba ninakwenda wapi kufanya nini.
Nilifanya hivyo ili nisije nikawavunja moyo kwa sababu kama
wangejua kwamba nimeondoka, wangeweza kupunguza kasi ya
kutekeleza majukumu yao. Mtu pekee ambaye nilimdokeza, ali-
kuwa ni Jack ambaye nilimtaka ahakikishe kila kitu kinakwenda

534 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kama kilivyopangwa, na ndani ya muda tuliokubaliana.


Baada ya hapo, nilitoka na kwenda kwa mtu aliyekuwa anahusika
na masuala ya kusimamia masuala yote ya usafiri kuanzia magari
mpaka mafuta. Nilimueleza kwamba nilikuwa nahitaji gari zuri la
kiraia ambalo lipo kwenye hali nzuri.
Harakaharaka akaenda kuchukua funguo, akanipeleka kule
magari ya ofisini yanakohifadhiwa, akanipeleka mpaka kwenye
gari aliloona litanifaa. Alijaribu kuliwasha, akalikagua kila sehemu
na baada ya kujiridhisha alinikabidhi, nikamshukuru sana na kuin-
gia, nikalitoa mpaka kule getini.
Sikuwa nimemchagua mtu wa kuondoka naye, kwa hiyo nikat-
eremka na kwenda kwenye ofisi ya vijana wetu wa ‘field officers’,
nikamchagua Nelson Mtafya au Nelly kama wenzake walivyokuwa
wanapenda kumuita.
Nilimchagua kwa sababu maalum na bila hata kumueleza tu-
nakwenda wapi, nilimtaka anifuate, tukatoka mpaka kwenye gari,
tukaingia na safari ikaanza.
Mimi ndiye niliyekuwa nimekaa nyuma ya usukani, tukawa
tunaendelea kupiga stori za hapa na pale na Nelly, wakati mwing-
ine tukicheka. Baada ya kuwa tumeshavuka Mbagala, nilimweleza
kwamba safari yetu ni ya Kibiti, akashtuka kidogo lakini nikam-
toa wasiwasi kwamba haikuwa misheni ngumu bali ni mambo ya
kawaida tu.
“Hata ingekuwa ni misheni ngumu, nikiwa na wewe sina wasiwa-
si wowote!” alisema na kusababisha wote tucheke, safari ikaende-
lea huku mara kwa mara tukisimamishwa kwenye ‘checkpoints’

535 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

za ukaguzi zilizokuwa na mchanganyiko wa askari wa kawaida


pamoja na wanajeshi. Vituo vya ukaguzi vilikuwa vingi sana kwe-
nye barabara yote ya kuelekea kwenye ukanda huo.
Jambo hilo lilinifurahisha sana kuona jinsi vikosi vyote vya ulinzi
na usalama vilivyokuwa vikifanya kazi yake ipasavyo. Hakuna gari
wala chombo chochote cha moto ambacho kiliruhusiwa kupita bila
watu wote waliokuwepo ndani yake kukaguliwa.
Japokuwa hilo lilisababisha safari iwe ndefu kidogo kutokana
na kusimama mara kwa mara kukaguliwa, kwangu ilinipa moyo
kwamba kila mmoja katika nafasi yake sasa alikuwa macho ku-
hakikisha nchi inaendelea kubaki salama dhidi ya watu wote walio-
kuwa na nia mbaya na taifa letu.
Baada ya kupita kwenye vituo vya ukaguzi karibu sita, hatimaye
tuliwasili Kibiti, kwa kuwa tayari nilikuwa naifahamu ramani ya
kuelekea kwa Ustaadh Fundi, nilitoka kwenye barabara kuu na
kuingia kwenye barabara ya mtaa.
Sikuwa nimemwambia Ustaadh Fundi kwamba nakwenda ku-
onana naye, nilitaka kila kitu kifanyike kimyakimya kwa sababu
nilitaka kwenda kujionea mwenyewe kama alikuwa akipewa ulinzi
kama tulivyokuwa tumekubaliana.
Niliendelea kuendesha gari kwa mwendo wa taratibu nikielekea
kule kwenye ule mtaa kulipokuwa na ofisi yake pamoja na nyumba
yake ya kuishi na baada ya muda mfupi, nilisimamisha gari nje ya
ofisi yake.
Mtu wa kwanza kutupokea, alikuwa ni askari kanzu aliyekuwa
amevaa nguo za kiraia, hatukuwa tukifahamiana naye na kwa

536 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kuwa tulikuwa kwenye nguo za kiraia, alitupokea kwa maswali


ya kutaka kujua sisi ni akina nani, tumetoka wapi na tulikuwa na
shida gani.
Ilibidi mimi nikae kimya nikiendelea kutazama huku na kule,
kijana wangu ndiyo akafanya kazi ya kujitambulisha pamoja na
kunitambulisha mimi. Alipogundua kwamba mimi ni nani, alipiga
saluti ya utii kisha akanisogelea na kuniomba radhi kama nilikuwa
nimekasirishwa na maswali yake.
“Sijakasirika, sanasana nimefurahi kwa sababu unafanya kazi
yako kikamilifu! Huyu mzee ni mtu muhimu sana, anatakiwa
kulindwa kikamilifu,” nilisema, nikasikia vishindo vya mtu akija
harakaharaka kutokea ndani.
Alikuwa ni Ustaadh Fundi ambaye aliponiona tu, alikuja moja
kwa moja mwilini, akanikumbatia kwa uchangamfu mkubwa huku
tabasamu pana likichanua kwenye uso wake.
Tulipeana mikono pale, akasalimiana na kijana wangu na haraka-
haraka akatukaribisha ndani, kwenye ile karakana yake ya kuten-
genezea viatu. Kulikuwa na vijana wake kadhaa ambao walikuwa
wakimsaidia kazi zake, akawatambulisha kisha tukapita na kutokea
upande wa pili kulikokuwa na nyumba yake aliyokuwa anaishi.
“Bila taarifa sheikh? Au ndiyo kila kitu kinafanyika kijeshijeshi,”
alisema huku tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wake,
tukacheka kwa pamoja.
“Mnaendeleaje?” alisema huku akituonesha sehemu ya kukaa,
kwenye viti maalum vilivyokuwa pale nje ya nyumba yake ya
kisasa, mahali ambapo mara ya mwisho ndipo tulipokuwa tumekaa

537 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

naye nikiwa na Chief Mwaipopo.


Sikuwa na muda wa kutosha, kwa hiyo nilimuonesha kijana
wangu kwa ishara kwamba anatakiwa kuinuka na kuelekea upande
wa mbele wa ile nyumba ya yule mzee kwa lengo la kuhakikisha
usalama.
“Anakwenda wapi tena, si mpate kwanza chochote kitu?”
“Hapana, usiwe na wasiwasi, tuko na muda mfupi sana,” nilise-
ma huku nikimuonesha ishara kwamba akae ili tuzungumze, akawa
ni kama hakubaliani na mimi, nadhani ukarimu ulikuwa umemzidi
kiasi cha kunichukulia kama ndugu yake.
Alielekea ndani na muda mfupi, alitoka akiwa ameongozana na
wake zake, mmoja akiwa amebeba chupa ya chai na mwingine
akiwa na sahani ndogo. Walinisabahi kwa uchangamfu, mmoja
akanimiminia maziwa kwenye kikombe na yul mwingine akaweka
sahani iliyokuwa na mihogo ya kuchemsha na karanga za kukaan-
ga.
Wakaninawisha kisha wakaondoka na kurudi ndani, nikajikuta ni-
kitabasamu mwenyewe, nikamuuliza Ustaadh Fundi kama alikuwa
anategemea ugeni wowote au alishajua kama nakwenda kumtem-
belea.
“Hapana, mimi siku zote huwa nahakikisha ndani kuna kitu cho-
chote cha kuwakirimu wageni wangu, imani yangu ya dini inani-
fundisha kufanya hivyo kwani ni sadaka kubwa kwa Mungu wetu,”
alisema kwa utulivu wa hali ya juu, nikawa namtazama huku
nikiendelea kufurahia vitu vya asili nilivyokuwa nimeandaliwa,
ambavyo mjini huwa nakula kwa nadra.

538 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Najua upo bize sana na kazi lakini najua kwamba umeona na


mama naye anahitaji huduma yako! Vitu kama hivi vinasaidia sana
kuleta heshima ndani ya ndoa, huko mjini nyie mnashindia vyakula
vya supermarket na chipsi, sisi huku ndiyo vitu vyetu hivi, kijana
wako naye anatakiwa tukimaliza hapa apate shea yake,” alisema na
kunifanya nicheke sana.
Ukiachilia mbali ukarimu, Ustaadh Fundi alikuwa mcheshi sana
hasa akiwa ameshaanza kukuzoea. Kwa kuwa sikuwa na muda wa
kutosha, nilikula harakaharaka huku tukiendelea na mazungumzo
ya kawaida, akinieleza jinsi mambo yalivyokuwa yakienda hapo
Kibiti tangu tulipoondoka.
“Mji umetulia, yule mwendawazimu Abdulwaheed ndiye ali-
yekuwa anatuharibia amani na utulivu wetu! Hakuna tukio lolote la
mauaji ambalo limeripotiwa tangu alipochukuliwa, na nasikia Ma-
fia nako kumetulia kwa sababu wale vijana wakorofi wote wame-
shikishwa adabu,” alisema, nikawa namsikiliza kwa makini.
Baada ya kumaliza kula, nilitoa ‘tape recorder’ mfukoni mwan-
gu, nikamtaka anisogelee ili asikie mwenyewe ujumbe wake nilio-
kuwa nimemletea. Ilikuwa ni sauti ya mwanaye, Zuleikha ambayo
nilimrekodi kwa ajili ya kuja kumhakikishia kwamba binti yake
yuko salama kabisa.
Alipogundua kwamba ni sauti ya mwanaye, alitulia na kutega
masikio kwa makini, akawa anamsikiliza alichokuwa anasema.
Kwa kadiri mwanaye alivyokuwa akiendelea kuzungumza kupitia
sauti ile niliyomrekodi, ndivyo Ustaadh Fundi alivyokuwa anazidi
kuzamakwenye dimbwi zito la hisia za uchungu.

539 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Kuna wakati alishindwa kuvumilia, machozi yakawa yanam-


bubujika kwa uchungu wa hali ya juu. Nilimuacha asikilize mpaka
mwisho, alipomaliza, alitoa kitambaa kwenye nusu kanzu aliyoku-
wa ameivaa na kujifuta machozi, akajishika tama na kujiinamia.
“Nakuomba sana wake zangu na familia yote waje wasikilize
wenyewe, maana nakosa hata usingizi, wake zangu wanataka
kujua alipo Zuleikha, wakimsikia najua watatulia,” alisema Usta-
adh Fundi, ikabidi nimruhusu japokuwa nilikuwa najua kwamba
navunja sheria.
Aliinuka na kuelekea ndani na muda mfupi alikuja na wake zake
na wanaye wengine, wakatandika jamvi na kukaa kwa kutulia,
wote wakiwa wamejistiri vizuri, nikaibofya ile ‘tape recorder’ na
sauti ya Zuleikha ikaanza kusikika.
Wote walitulia na kutega masikio kwa makini, kama ilivyokuwa
kwa baba wa familia, nao ilifika mahali wakawa wanalia mithili
ya watu waliopokea taarifa za msiba. Walisikiliza mpaka mwisho
kisha Ustaadh Fundi akawataka warejee ndani, wakaondoka kila
mmoja akiwa analia.
“Msiwe na wasiwasi, atakuwa salama na nitahakikisha nalisi-
mamia hilo kwa vitendo,” nilimwambia, akawa anatingisha kichwa
kuonesha kukubaliana na nilichokuwa nimemwambia, macho yake
yakiwa yamebadilika rangi na kuwa mekundu.
“Kuna kitu chochote umekibaini kwenye alichokisema mwa-
nao?”
“Ndiyo, kuna mambo amenieleza hata mimi sikuwa nayajua,”
alisema huku akionesha ni kama anatafakari jambo kwenye kichwa

540 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

chake.
“Kuna binti mmoja walichukuliwa pamoja ingawa yeye alitangu-
lia kwenda mjini. Amesema kwa mafumbo kwamba wamekutana
naye lakini amemueleza kwamba akipata nafasi akamuagie kwao
kwa sababu anajua hatarudi tena na hataendelea kuishi,” alisema,
nikashangaa kidogo kwa sababu sikuwa nimesikia kitu kama
hicho.
Akanifafanulia kwamba kwenye kile kipengele ambacho binti
yake alizungumza kilugha, ndipo alipoyasema maneno hayo,
akanitaka nikirudie kipande hicho, nikarudia na kweli niligundua
kwamba kuna kitu alikitaja lakini sikuwa nimekielewa au pengine
sikuwa nimekitilia maanani.
Alinieleza kwamba hata yeye hakuwa amepata taarifa kamili
lakini kwa kifupi hicho ndicho alichokuwa amemaanisha, nika-
muuliza kama tukimpa nafasi ya kwenda kuoanana na binti yake
anaweza kumhoji zaidi kuhusu hicho alichokisema?
“Zuleikha hana shida, hata wewe anaweza kukueleza lakini ni
mpaka asikie mimi nimeruhusu akwambie,” alisema, wote tu-
kashusha pumzi ndefu, nikawa natafakari cha kufanya kwa sababu
mpaka muda huo bado sikuwa nimemueleza Ustaadh Fundi ni nini
hasa kilichonifanya nikafunga safari.
“Ningeweza kuondoka na kuongozana na wewe lakini bado sid-
hani kama itakuwa salama kwangu na kwa familia yangu, naamini
kila kitu kinaweza kufanyika bila hata ya mimi kusafiri,” alisema
Ustaadh Fundi.
Nilikubaliana naye na kama nilivyokuwa nimepanga, nilitaka na

541 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

yeye nimrekodi sauti yake akiwa anazungumza na mwanaye ili ni-


kifika nikamsikilizishe Zuleikha kwa lengo la kuzidi kujenga imani
yake kwangu.
Nilikuwa naamini kwamba mtu anapokuamini kutoka ndani
ya moyo wake, anaweza kukusaidia mambo mengi na makubwa
mpaka mwenyewe ukashangaa. Ni mbinu hiyo ndiyo niliyokuwa
nimeitumia kuanzia mwanzo na hakika ilikuwa imeleta matokeo
makubwa sana kwangu.
Alikubaliana na mimi lakini akaomba kwanza akachukua kalamu
na karatasi ili apangilie vizuri mambo ambayo alitaka kuyazung-
umza lakini pia akataka kwenda kuwauliza wake zake kama nao
wanacho chochote ambacho wangetaka kumweleza binti yao huyo.
Muda mfupi baadaye alirejea akiwa na kalamu na karatasi,
akaanza kupangilia mambo ya muhimu ambayo alitaka kuzung-
umza na binti yake. Baada ya kumaliza kupangilia, alinipa ishara
kwamba yupo tayari, nikachukua ile ‘tape recorder’ na kuibofya,
akaanza kuzungumza.
Nilifurahishwa kwa jinsi alivyokuwa akizungumza kwa utulivu.
Usingeweza kuamini kama ni yeye ndiye ambaye muda mfupi ulio-
pita, alikuwa akimwaga machozi baada ya kumsikia mwanaye.
Kikubwa alichomwambia mwanaye, ni kwamba kila kitu kita-
kuwa sawa na akamhakikishia kwamba mimi ni mtu mzuri na
nafanya kazi kubwa ya kuhakikisha nchi yetu inabaki salama.
Akamwambia anieleze kila kitu ambacho naamini kitasaidia kuzuia
shambulio ambalo lilipangwa kufanyika Magogoni, likimlenga
namba moja.

542 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Alimhakikishia kwamba wao wapo salama na Mungu akipenda


wataungana tena na kuwa pamoja kama zamani. Akamueleza uovu
wa Abdulwaheed na jinsi alivyopata nafasi ya kumzaba makofi
kadhaa baada ya kumkamata kutokana na mambo yote aliyokuwa
ameyafanya.
Kuna muda nilitamani kucheka kwa sababu alikuwa amenikum-
busha tukio lililotokea tulipofanikiwa kumkamata Abdulwaheed,
akiwa mafichoni ambapo mwanaume huyo alimzaba makofi kad-
haa kwa hasira kali huku akimfokea vikali.
Alipomaliza, aliniomba niwape hata dakika mojamoja wanafa-
milia wengine wakiwemo wake zake na wanaye nao wamsalimu
ndugu yao, ikiwezekana kila mmoja ampe salamu zake.
Nilikubali, akaenda kuwatoa wanafamilia kadhaa wakiongozwa
na wake zake, nikawarekodi mmoja baada ya mwingine ambapo
wote ni kama walikuwa wameshaelekezwa nini cha kuzungumza,
kikubwa ikiwa ni kumhakikishia kwamba wao wapo salama na
yeye atakuwa salama lakini kubwa kwamba mimi ni ndugu yao na
kama ana tatizo lolote aniambie nitamsaidia.
Nilijikuta nikitabasamu mwenyewe kwa sababu ilionesha ni kwa
namna gani Ustaadh Fundi alikuwa amefanikiwa kujenga familia
iliyokuwa bora, ikiwa na hofu ya Mungu na yenye ushirikiano wa
hali ya juu.
Baada ya wote kumaliza, waliondoka na kurudi ndani, wote
wakionesha ni kama wametua mzigo mzito kwenye mioyo yao,
wakiwa na nyuso za furaha, nikabaki na Ustaadh Fundi.

543 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

544 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

20
U
KIMYA ulipita kati yetu, nikiwa najaribu kutafuta seh-
emu ya kuanzia kumweleza kile ambacho ndicho hasa
kilichonifanya nifunge safari kuja kuonana naye.
“Taarifa za kiintelijensia zinaonesha bado shambu-
lio la Magogoni lipo palepale, hawa wendawazimu
wamejipanga kisawasawa kuhakikisha wanaiangusha,” nilimwambia,
akawa ni kama hajasikia vizuri nilichokuwa nimekisema, akanitaza-
ma kwa mshangao.
“Inawezekanaje? Abdulwaheed, Mutesigwa wote wapo kwenye
mikono yenu, inawezekanaje tukio likatokea kama lilivyokuwa
limepangwa/”
“Tulichokibaini ni kwamba walikuwa wameshatengeneza mpango

545 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kazi wa hali ya juu kwamba vyovyote itakavyokuwa, lazima siku,


muda na saa iliyopangwa ikitimia, shambulio litokee. Muda tulio-
bakiwa nao ni mdogo sana na taharuki inazidi kuwa kubwa.”
“Taarifa mlizozibaini zinaonesha nini?”
“Kuna makundi mawili ambayo ndiyo hasa yaliyopangwa
kutekeleza shambulio hilo. La kwanza ni la wasichana, hawa
mabinti wadogo wanaitwa Cat Girls na kundi la pili ni la washam-
buliaji wenye mafunzo makubwa ambao hawa ndiyo watakaokuja
kumaliza kazi ambayo itaanzishwa na Cat Girls.
“Kichwa kinauma, sijui mwisho wa haya yote ni nini. Kama
kuna chochote ambacho unakijua, hata kama ni kidogo kiasi gani,
kitatusaidia kuwakabili kabla hawajafanya walichopanga kuki-
fanya,” nilimwambia, akashusha pumzi ndefu kisha akawa ni kama
anatafakari.
“Umezungumzia kuhusu Cat Girls! Nimewahi kulisikia hilo
neno,” alisema, nikainua uso wangu na kumkazia macho, nikiwa
na shauku kubwa ya kutaka kusikia anachotaka kukisema.
“Ulilisikia wapi?”
“Kwa Abdulwaheed.”
“Ni kitu gani? Nataka kujua ni kitu gani hicho?”
“Kuna kampuni inaitwa Martisoor Catering and Hospitality
Company! Hawa ni jamaa zake Abdulwaheed ambao huwa wana-
fanya shughuli za kuandaa vyakula kwenye hafla na dhifa mbalim-
bali, lakini pia huwa wanapamba kumbi za maharusi, kufanya usafi
maofisini na sehemu nyingine.
“Asili yao ni nchini Somalia lakini wamesambaa sana kwenye

546 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

nchi nyingine kadhaa ikiwemo hapa nyumbani, huwa wanabadil-


ishabadilisha majina tu lakini ndiyo haohao.
“Hizo kazi zote nilizokutajia ni kazi wanazotumia kujifichia, la-
kini uhalisia ni kundi la wauaji hatari waliopewa mafunzo ya kazi
hizo nilizokutajia awali lakini kubwa zaidi ni mafunzo ya ujasusi,
mauaji na uharibifu.
“Amewahi kunieleza hili yeye mwenyewe, sijui alifurahi nini
siku hiyo lakini hakuniambia kwamba na yeye ni mshirika wao.
Silaha kubwa wanazotumia kuingia mahalipopote wanapopataka,
kwanza ni kuwatumia wasichana warembo kisawasawa lakini pili
ni kutoa rushwa ya mamilioni ya fedha kila wanapotaka jambo
lao,” alisema, nikawa ni kama hata sielewi kama Ustaadh Fundi
anaweza kuwa na taarifa muhimu kama hizo.
“Sasa unafikiri hawa wanawezaje kupenya mpaka Magogoni?”
“Kwani si umesema kutakuwa na dhifa sijui sherehe Magogoni?”
“Ndiyo!”
“Si lazima kutakuwa na shughuli za kupamba lakini pia kuhudu-
mia vyakula na vinywaji?” alisema kitu ambacho sasa kilinifanya
nipate picha kamili kwenye kichwa changu.
Nasema hivyo kwa sababu hata nilipompeleleza baba yake
Saima kuhusu kampuni ambayo itahudumia vyakula na vinywaji
kwenye dhifa hiyo, alinieleza kwamba kwa upande wa namba
moja na viongozi, huwa wanahudumiwa na maafisa maalum lakini
kwa kuwa kutakuwa na wageni wengi, kutakuwa na kampuni am-
bayo ndiyo iliyopewa hiyo tenda.
Ukimya ulipita katikati yetu, nikawa naendelea kutafakari kwa

547 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kina, mate yakanikauka kabisa mdomoni. Hakika hawa wendawaz-


imu walikuwa wamejipanga kisawasawa.
“Vipi kuhusu hilo kundi la pili?”
“Sidhani kama kutakuwa na makundi mawili, linaweza kuwa ni
kundi hilohilo moja lakini kwa sababu kuna mchanganyiko wa wa-
naume na wanawake, wanaume wanaweza kuwa ndiyo hilo kundi
la pili. Sina uhakika lakini nahisi hivyo,” alisema Ustaadh Fundi,
akazidi kunifumbua macho.
“Unahisi tunawezaje kuwatambua?”
“Mimi naweza kuwatambua, unajua nimeshakaa kidogo na hawa
watu, nakuwa na uwezo wa kugundua kwamba mtu huyu au yule
anahusika na jambo fulani kwa sababu sura zao huwa zimebeba
ujumbe ambao kama unajua vizuri haya mambo, unaweza kuwat-
ambua kwa urahisi.”
“Huoni kwamba sasa ni muhimu mimi na wewe kusafiri pamoja
ili tukasaidiane kazi kwa karibu zaidi kama ulivyotusaidia kuanzia
mwanzo?”
“Wewe nenda, kesho asubuhi nitakuja mapema kabisa, siwezi ku-
lala nje na hapa kwangu! Nitakupigia simu nikifika, wewe usinipi-
gie,” alisema, nikainuka na kumkumbatia kwa nguvu.
Hakika uamuzi wangu wa kuamua kusafiri na kwenda kuoana
naye, ulikuwa umezaa matunda makubwa mno pengine kuliko hata
nilivyokuwa nimetegemea.
Nilimshukuru sana kwa taarifa muhimu alizokuwa amenipa,
nikamsisitiza kwamba kesho anatakiwa ahakikishe anafika asubuhi
na mapema na kama kutatokea changamoto yoyote anatakiwa ku-

548 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wasiliana na mimi nijue namna ya kumsaidia.


Niliingiza mkono mfukoni na kutoa noti kadhaa za shilingi elfu
kumikumi, nikataka kumpa ili zimsaidie kwa nauli lakini akakataa
na kunieleza kwamba alikuwa anajitosheleza kwa kila kitu.
Basi sikutaka kubishana naye kwa sababu alishaonesha ni mtu
wa misimamo ya aina yake, nikamshukuru sana kisha tukaagana,
nikawasiliana na kijana wangu aliyekuwa upande wa mbele wa ile
nyumba, kuhakikisha kwamba kila kitu kinakwenda sawa.
“Huyu bwana amesema eti wewe umeshiba hutakiwi kula viru-
tubisho vya huku shamba,” alisema Ustaadh Fundi akimwambia
kijana wangu wakati akitusindikiza, tukacheka sana kisha akawa ni
kama amekumbuka kitu.
“Mkanisubiri kwenye gari, msiondoke kwanza,” alisema huku
akirudi haraka ndani kwake, mimi na kijana wangu tukatoka na
kuagana na askari wawili waliokuwa wakisimamia ulinzi kwenye
makazi ya Ustaadh Fundi kisha tukaenda mpaka kwenye gari.
Muda mfupi baadaye, Ustaadh Fundi alikuja akiwa ameongozana
na mwanaye mdogo wa kiume, aliyekuwa amebeba mfuko ulioku-
wa umefungwa vizuri pamoja na chupa ya maji iliyokuwa imewe-
kwa maziwa ndani yake.
“Kwa kuwa wewe hujapata nafasi ya kula, basi utakula hata nji-
ani lakini pia kwa kuwa najua kilichopo kinawatosha nyote wawili,
na wewe utakula tena ili mama akafurahi nyumbani,” alisema
Ustaadh Fundi na kusababisha tucheke sana kwa furaha.
Ukarimu wa Ustaadh Fundi ulikuwa ni wa kipekee mno, basi
tuliagana pale huku kila mmoja akiwa na furaha kubwa ndani ya

549 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

moyo wake, tukatoka na gari na safari ya kurudi mjini ikaanza.


“Mnaiva sana na huyu mzee,” alisema kijana wangu, akiwa
ni kama anataka kusikia kama nimetoa ruhusa ya yeye kula kile
kilichokuwa kwenye kifurushi alichopewa na Ustaadh Fundi kama
ulivyokuwa utaratibu wetu wa kazi.
“Huyu mzee ana roho safi sana na isitoshe ametusaidia kwa kiasi
kikubwa sana kwenye hii kazi yetu! Wakati mwingine nawaza
kwamba kama isingekuwa yeye sijui kama tungefanikiwa kutegua
kitendawili kilichopo mbele yetu,” nilimwambia kijana yangu.
Nikachukua kipande cha mhogo wa kuchemsha kutoka kwenye
kile kifurushi na arangakidogo, nikawa nakula taratibu, kijana
wangu naye akawa anashambulia kilichokuwemo kwenye kile
kifurushi, akionesha kufurahishwa mno na vyakula vya asili,
kuanzia mihogo ya kuchemsha, magimbi, viazi na maboga, vyote
vikiwa vimechemshwa vizuri, huku pembeni kukiwa namaziwa
fresh kwenye chupa ya maji na karanga mbichi za kutosha.
“Ndiyo maana hawa wazee wa huku wanakuwa na uwezo wa
kuwa hata na wake wanne na kuzaa nao watoto wengi, wanakula
vyakula vinavyotakiwa, siyo kama sisi,” alisema kijana wangu,
akasababisha nicheke sana kwa sababu alichokuwa amekisema,
kilikuwa kimesemwa pia na Ustaadh Fundi.
Tatizo la vyakula au lishe, limesababisha wanaume wengi kupata
matatizo kwenye ndoa zao kwa sababu wanapoteza nguvu zao
kama wanaume na mwisho wanaishia kudharauliwa au kusalitiwa
na wake zao kwa sababu hawawezi tena kutimiza majukumu yao
ya kindoa kutokana na matatizo ya nguvu ambayo kwa kiasi ki-

550 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kubwa yanasababishwa na aina ya vyakula tunavyokula.


Basi safari iliendelea tukipiga stori za hapa na pale, mimi nikiwa
nyuma ya usukani, tukapita kwenye vituo vya ukaguzi barabarani
kama mwanzo na kwa kuwa sasa askari waliokuwepo walikuwa
wanajua sisi ni akina nani, hatukupata usumbufu.
Wakati wote wa safari, japokuwa nilikuwa nikicheka na kupiga
stori na kijana wangu, akili zangu zilikuwa mbali, nilikuwa niki-
tafakari kwa kina kile nilichokuwa nimeelezwa na Ujstaadh Fundi
ambacho kwa hakika, kilikuwa ni kama kete ya mwisho mche-
zoni, au penalti ya mwisho kwenye fainali.
Kitendo cha kupata mwanga kuhusu Cat Girls, ilikuwa ni zaidi
ya ushindi na niliamini mpaka tukirudi kitengoni, vijana wangu
wakiongozwa na Jack, watakuwa wamesogea mbele sana kwenye
kazi waliyokuwa wanaifanya.
Nilikuwa na shauku kubwa mno ndani ya moyo wangu ya
kuijua kwa kina kampuni ya Martisoor Catering and Hospitality
Company ambayo kumbe ndiyo iliyokuwa imepangwa kutekeleza
tukio la kuiangusha Magogoni, wakijificha kwenye kivuli cha
kampuni ya kutoa huduma za vyakula, vinywaji na mapambo
kwenye sherehe.
Safari iliendelea na hatimaye tukawasili ofisini, nikamshusha
kijana wangu pale kwenye maegesho kisha nikalirudisha gari
kulekule nilikokuwa nimekabidhiwa awali kama utaratibu wa kazi
ulivyokuwa.
Baada ya kukabidhiana na mhusika, nilirudi mpaka pale kwenye
maegesho ambako kijana wangu alikuwa ananisubiri, akiwa ame-

551 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

shika kile kifurushi tulichopewa ambacho sasa kilikuwa kimefika


nusu, tukaelekea mpaka ofisini ambapo tuligawana kisha nikam-
ruhusu akaendelee na majukumu yake mengine.
Nilikaa na kuanza kutafakari upya wapi pa kuanzia kwa sababu
taarifa mpya zilizokuwa mikononi mwangu zilikuwa za moto
kwelikweli. Nilitaka kwenda kumpa taarifa baba yake Saima lakini
nikaona haitakuwa sawa kutoa taarifa ambazo hazijakamilika.
Niliamua kuanza kwa kwenda kuzungumza na Zuleikha, mtoto
wa Ustaadh Fundi ambaye kama nilivyoeleza, tulikuwa tukimshi-
kilia pamoja na wenzake.
Ukarimu mkubwa aliokuwa ametuonesha, ulitakiwa kulipwa kwa
mimi kumfikishia salamu zake mwanaye haraka iwezekanavyo la-
kini pia, hiyo ilikuwa nafasi ya mimi kujiweka karibu zaidi na binti
huyo ambaye ilionesha kwamba kuna taarifa ambazo alikuwa nazo
zingeweza kutusaidia sana.
Nilitoka na kwenda moja kwa moja kwenye chumba cha mahoji-
ano, nikawapa taarifa vijana wangu kwamba nahitaji kuzungumza
kwa mara nyingine na yule binti, kweli dakika chache tu baadaye
akaingizwa kwenye kile chumba na kukalishwa palepale ambapo
huwa anakaa kila ninapozungumza naye. Alipogundua kwamba ni
mimi, nilimuona akiwa na shauku kubwa ya kutaka kusikia ni-
tamwambia nini.
“Nimetoka nyumbani kwenu, nimezungumza na baba yako,
mama zako, wadogo zako na ndugu zako wote, wamekukumbuka
sana na wanakusalimu sana,” nilimwambia, nikamuona akiachia
tabasamu hafifu, nikabonyeza ‘tape recorder’ na kuchagua zile

552 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

sauti za ndugu zake, nikaanza kumsikilizisha.


Nilitaka baba yake awe wa mwisho kumsikiliza kwa sababu ku-
likuwa na mambo ya msingi sana ambayo nilikuwa nataka kuzun-
gumza naye, kutokea kwenye kile ambacho alikuwa ameelezwa na
baba yake.
Sauti zilianza kusikika moja baada ya nyingine, kwa mara ya
kwanza nikaliona tabasamu pana likichanua kwenye uso wake,
baada ya kusikia sauti za ndugu zake. Nilimuona akifurahi mpaka
machozi yakawa yanamtoka.
“Unajisikiaje?”
“Nimefurahi sana! Allah akubariki sana afande,” alisema huku
akijifutamachozi ya furaha. Hakika nilikuwa nimefanikiwa kuzigu-
sa hisia zake kwa sababu hata namna alivyokuwa akinitazama na
kuzungumza na mimi, vilibadilika kabisa. Alishaonesha kuniamini
kuliko kawaida.
“Kwa hiyo unapajua mpaka nyumbani kwetu?”
“Ndiyo! Tumepikiwa mihogo, maboga, viazi, magimbi, karanga
na maziwa, tumekula na kufurahi sana,” nilisema huku nikijilazi-
misha kutabasamu, akacheka sana kusikia maneno hayo, akawa
anaendelea kujifuta machozi ya furaha.
“Kuna salamu zako pia kutoka kwa baba yako,” nilisema huku
nikiibofyabofya ile tape recorder, nikachagua sauti ya baba yake
na kuanza kumsikilizisha, nikamuona akitulia na kutega masikio
kwa makini.
Alisikiliza kuanzia mwanzo mpaka mwisho, kwa mara nyingine
akawa anajifuta machozi, safari hii hayakuwa machozi ya furaha

553 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

tena, bali machozi ya hisia za ndani kabisa kutokana na ujumbe


mzito ambao alikuwa amepewa na baba yake. Nikamuacha atulie
kwanza, dakika kama mbili za ukimya zikapita kati yetu kisha
nikainua uso wangu na kumtazama.
“Unaamini kwamba hizo ni sauti za baba yako na ndugu zako?”
“Naamini kwa asilimia zote. Naijua sauti ya baba, nazijua sauti
za ndugu zangu, ni wenyewe! Nakushukuru sana,” alisema, ni-
katingisha kichwa huku nikitafakari wapi pa kuanzia kumhoji kwa
undani zaidi.
“Ulipomtumia baba yako ujumbe wa sauti, kuna sehemu ulizun-
gumza maneno ya kilugha. Ulikuwa umemaanisha nini?” nilim-
uuliza kwa mtego kwani niliona hiyo ndiyo sehemu nzuri ambayo
naweza kuanzia kumhoji.
“Sikumbuki vizuri,” alisema kisha akainamisha kichwa chake
vizuri.
“Baba yako amenihakikishia kwamba utanieleza kila kitu kwa
undani! Amenieleza kwamba ulimwambia kwamba sijui kuna rafiki
yako ulikutana naye na akakupa ujumbe uufikishe kwao. Nataka
kujua ni nani na ni ujumbe gani alikwambia,” nilimuuliza kwa
sauti ya upole.
Nadhani licha ya yote ambayo nilikuwa nimeyafanya, bado si-
kuwa nimefanikiwa kumfanya Zuleikha aniamini kwa asilimia zote
mia moja.
“Nakuhakikishia hakuna mtu yeyote ambaye atajua kama ni
wewe ndiye uliyenieleza na lengo langu siyo baya, ni kuhakikisha
kwamba tunategua kitendawili kilichopo mbele yetu kabla mambo

554 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

hayajaharibika!
“Kama unakumbuka nilikuambia kuanzia mwanzo kwamba ili
nitimize ahadi yangu ya kukusaidia,lazima tuhakikishe shambulizi
lililopo mbele yetu halitokei! Likitokea maana yake wewe na wen-
zako wote mnakuwa matatizoni na utanipa wakati mgumu sana wa
kutimiza ahadi yangu ya kukusaidia,” nilisema kwa upole huku
nikiwa nimemkazia macho Zuleikha, mtoto wa Ustaadh Fundi ili
anieleze ukweli.
Nilipomkumbusha makubaliano yetu hayo, alishusha pumzi
ndefu kisha akainua uso wake na kunitazama, alipogundua kwam-
ba nilikuwa nimemkazia macho, aliyakwepesha macho yake kisha
akashusha pumzi ndefu.
“Ni kweli!”
“Ni kweli kuhusu nini?”
“Kwamba nilimwambia baba hicho ulichokisema!”
“Ulimwambia nini? Nataka unieleze mwenyewe ili nipate picha
kamili.”
“Kuna rafiki yangu anaitwa Zahara, tumesoma pamoja, wazazi
wake na wazazi wangu wanafahamiana vizuri kwa hiyo amekuwa
kama ndugu yangu,” alisema kwa sauti ya chini, nikakaa vizuri
kwenye kiti nikimtegea sikio kwa umakini.
“Yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kuja mjini na tuliambiwa
kwamba na wao wamekuja kupewa mafunzo kisha watafutiwe
kazi. Yeye na wasichana wenzetu wengine walitangulia kuja
mjini na tulipoona hawarudi, tukaamini kwamba mambo yao
yanawaendea vizuri ndiyo maana hata sisi ikawa rahisi kukubali

555 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kushawishika,” alisema.
“Enhee, ikawaje?”
“Baada ya mimi na wenzangu wengine kuwa tumechukuliwa na
kuletwa mjini, tulishangaa kuona mafunzo tunayopewa hayafanani
na kile tulichokuwa tumeambiwa mwanzo. Kuna sehemu tulikuwa
tunapelekwa kufanya mazoezi ya kijeshi na siku moja ndipo nili-
pofanikiwa kukutana na Zahara!”
“Mlikuwa mnapelekwa wapi kufanya mazoezi?”
“Sipajui, mimi hii ndiyo mara yangu ya kwanza kuja mjini!”
“Enhee, ulipokutana naye akakwambiaje?”
“Akaniambia kwamba yeye na wenzake hawana matumaini ya
kurudi tena nyumbani kwa sababu walikuwa ni kama wametekwa,
wakifundishwa mazoezi ya kijeshi pamoja na kutumia silaha.
Akaniambia wamesikia habari za chinichini kwamba watapelekwa
vitani kwa hiyo haamini kama watarudi salama. Akanitaka nikipata
nafasi nikawape taarifa wazazi wake.”
“Walisikia kwamba wanapelekwa vitani?”
“Ndiyo! Akaniambia wamekuwa wakifundishwa misimamo
mikali ikiwa ni pamoja na kufundishwa ujasiri wa kuvaa mabomu
mwilini na kwenda kujilipua watakapotakiwa kufanya hivyo.”
“Mungu wangu! Enhee, ikawaje?”
“Aliniambia maneno hayo akiwa analia sana, alikuwa na hofu
kubwa ndani ya moyo wake na kuanzia hapo sijawahi kuonana
naye tena!”
“Unampenda rafiki yako?”
“Ndiyo! Nampenda sana.”

556 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Upo tayari kuona anafariki dunia?”


“Hapana!”
“Upo tayari kufanya jambo ambalo litamuokoa na kifo?”
“Ndiyo! Nipo tayari! Hata sasa hivi!”
“Wewe na wenzako pia mlikuwa mmeshafundishwa kutumia
silaha si ndiyo?”
“Ndiyo! Silaha za aina tofautitofauti.”
“Ikiwemo mabomu ya kuvaa mwilini?”
“Hapana, hatukuwa tumefikia huko! Ndiyo mkaja kutukamata!”
“Unafikiri huko vitani alikokuambia rafiki yako Zahara ni wapi?”
“Sikujui, sisi tulikuwa tunafundishwa kuhusu Magogoni!”
“Umewahi kufika Magogoni?”
“Tulipelekwa kupaona, tulipitishwa tu kwa mbali tukiwa ndani
ya gari!” alisema, nikahisi ni kama ubongo wangu unachemka
ndani ya fuvu la kichwa.
“Unaweza kukumbuka kitu chochote ambacho ulikiona kina-
choweza kutusaidia kujua ni wapi ulipokutana na Zahara? Naamini
ukitaja vitu vichache unavyovikumbuka unaweza kutusaidia kwen-
da kuwaokoa wenzako. Nataka kujua huko mlikokuwa mnafanyia
mazoezi ni wapi. Jaribu kuvuta kumbukumbu! Chochote ambacho
unakikumbuka kinaweza kutusaidia!” nilimwambia, akashusha
tena pumzi ndefu na kuinua kichwa chake juu, nikaona kwamba
machozi yalikuwa yanamlengalenga.
“Kwanza ni karibu na bahari kwa sababu tulikuwa tunausikia
upepo wa baharini pamoja na sauti za mawimbi ya bahari.”
“Enhee! Kingine?”

557 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Kuna minazi ambayo ni kama imepakwa rangi. Kuna uwanja


mkubwa na upande wa mwisho kuna kama pori hivi ambalo nad-
hani ndiyo limeenda mpaka baharini.”
“Kingine?”
“Kuna nyumba kama kota ambazo hazitumiki, zimejengwa kwa
namna inayofanana lakini inaonesha zilijengwa zamani zimebaki
kama magofu, zipo pande mbili, huku na huku halafu katikati
ndiyo kuna huo uwanja.”
“Ni umbali gani kutoka barabarani?”
“Sikumbuki vizuri lakini kwa makadirio yangu, tulikuwa tuki-
iacha barabara ya lami nakuingia barabara ya vumbi na kwenda
umbali wa kama dakika tano hivi ndiyo tunafika.”
“Mazingira ya eneo la kuingilia yapoje?”
“Kwa mwanzo kuna kama makaburi mengi ambayo yapo
ndanindani ya miti mikubwa, baada ya hapo tunapita kwenye
barabara nyembamba inayokatiza kwenye mapori au vichaka
ndiyo unafika kwenye geti la kuingilia.”
“Kuna alama yoyote unayoweza kuikumbuka getini?”
“Hapana, alama yangu kubwa ninayoikumbuka ni makaburi
yenye misalaba, mengine yamejengewa kama vijumba hivi. Ina-
onesha ni makaburi ya miaka mingi.”
“Kipi kingine unachokikumbuka?” nilimuuliza, akawa ni kama
anajaribu tena kuvuta kumbukumbu.
“Hakuna kingine kwa sababu tulikuwa tunapelekwa usiku bna
kurudishwa usiku. Ila kuna sehemu ukikaa, kwa mbali unaona taa
zinawaka ng’ambo ya pili ya bahari kwa mbali,” alisema.

558 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Kwa muda wote huo wakati akinieleza, nilikuwa najaribu kujen-


ga picha fulani ndani ya kichwa changu na ndiyo maana nilikuwa
namtaka aendelee kukumbuka lakini alipoeleza tu kuhusu kuona
taa ng’ambo ya pili ya bahari, nikawa tayari nimeshapata picha
kamili.
Nilikuwa nalifahamu eneo lililokuwa linazungumziwa! Nasema
hivyo kwa sababu katika kipindi ambacho nilikuwa chini ya Bosi
Mute, tulikuwa tukipelekwa mara kwa mara kwa ajili ya kujifua
zaidi katika medani za mafunzo ya kijeshi yasiyo rasmi.
Sikuwahi kuwa nimefikiria hata mara moja kwamba hata baada
ya Bosi Mutesigwa kukamatwa na mtandao wake wote kusam-
baratishwa, bado eneo hilo linaweza kuwa linatumika kuwapa
mafunzo wahalifu hususan wanaofanya matukio ya kihalifu kwa
kutumia silaha za moto.
Nilishusha pumzi ndefu na kuinua kichwa changu juu, nikawa
nalitazama dari la kile chumba cha mahojiano. Japokuwa macho
yangu yalikuwa yakitazama dari, akili zangu zilikuwa zimenirudi-
sha miaka kadhaa nyuma, nikawa nakumbuka mambo yote yali-
yokuwa yanafanyika eneo hilo kipindi cha utawala haramu wa
Bosi Mute, mimi na wenzangu tukiwa wafuasi wake.
Baadaye nilishusha pumzi ndefu na kumtazama Zuleikha ambaye
kumbe na yeye alikuwa akinitazama nilipokuwa najenga tafakuri
ndani ya kichwa changu.
“Kuna kingine chochote ambacho ungependa nikijue kwa sasa?”
nilimuuliza, akatingisha kichwa chake kuonesha kwamba hakuwa
na chochote kwa muda huo. Nikamshukuru na kumuahidi kwamba

559 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

nitarudi tena kama nitakuwa na chochote ambacho ningehitaji


kujua kutoka kwake.
Nikainuka na kutoka, vijana wangu wakaingia na kumchukua,
wakamrudisha kwenye chumba alichokuwa akiishi tangu tulipow-
akamata yeye na wenzake. Niliongoza moja kwa moja mpaka kwe-
nye ofisi za vijana wa Cyber ambako Jack na wenzake walikuwa
wakiendelea na kazi nzito iliyokuwa mbele yao.
“Mnaendeleaje?” nilimuuliza Jack kwa sauti ndogo, nikivuta kiti
na kukaa pembeni yake.
“Safi Chief,” alijibu kwa kifupi, nikashuhudia mwenyewe jinsi
alivyokuwa ‘bize’ kuendelea kuchambua picha za CCTV Camera
na kuoanisha taarifa kutoka kwenye vyanzo vingine muhimu.
Kwa jinsi alivyokuwa bize, sikutaka kumuondolea utulivu,
nikawa natazama jinsi anavyochapa kazi, nikainuka na kuanza
kuwapitia vijana wengine, mmoja baada ya mwingine.
Wengi kijasho chembamba kilikuwa kikiwatoka, kazi ikiwa
inapigwa kisawasawa. Nilimpitia mmoja baada ya mwingine,
nilichokigundua kwa haraka ni kwamba kila mmoja alikuwa anajua
nini anachokifanya, nikaishia kutabasamu kwa sababu ilionesha
Jack amefanya kazi yake kikamilifu kuwaelekeza vijana wote
kuhusu kilichokuwa kinatakaiwa kufanyika.
“Unaweza kupata dakika chache tukazungumza?” nilimwambia
Jack baada ya kuwa nimerudi kwa mara ya pili kwenye kompyuta
yake. Hakunijibu, akaendelea kubofyabofya kompyuta yak haraka-
haraka kisha akashusha pumzi ndefu na kunigeukia.
“Ndiyo Chief!”

560 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Unaweza kutumia kamera zinazojiendesha zenyewe?”


“Drone?”
“Ndiyo!”
“Naweza mkuu!”
“Mtakapomaliza kazi hii, baadaye sana kuna mahali tutakwenda
nataka tukafanye misheni ndogo kwa kutumia drone,” nilimwam-
bia, akatingisha kichwa kuonesha kukubaliana na nilichokuwa
namwambia kisha akarudisha akili yake kwenye kazi, akaendelea
namajukumu yake.
Kwa wasioelewa, ‘drone’ niliyokuwa naimaanisha hapa, ni zile
kamera ambazo zinakuwa zimeunganishwa na kifaa ambachho
kinakuwa na mapangaboi madogo, zikiwa na uwezo wa kuruka
angani na kwenda umbali fulani huku zikipiga picha za mnato na
video.
Siku hizi zimekuwa nyingi mitaani kiasi kwamba hata kwenye
maharusi au matukio ya kawaida yanayohitaji kamera za kisasa,
zimekuwa zikitumika sana achilia mbali kwenye video za wasanii
mbalimbali wa muziki.
Jinsi mfumo wake ulivyo, ni kwamba unakuwa na kitu kama
rimoti ambayo inakuwa na screen kama simu za mkononi, ambayo
ndiyo inayotumika kuiongoza ‘drone’ kwa maana kuiruhusu iruke
kwenda juu, kuiruhusu iende mbele, igeuka au irudi nyuma, izidi
kwenda juu au ishuke chini kulingana na kile unachokitaka, kisha
unakuwa unaona kinachorekodiwa na ile kamera kwa kutumia hii
rimoti unayokuwa umeishika mkononi! Mambo ya kiteknolojia
hayo!

561 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Unaweza kushangaa kwa nini nilimuuliza Jack kama anao uwezo


wa kutumia drone! Japokuwa hapa kwetu inaweza kuonekana
kama ni teknolojia mpya, kwa wenzetu teknolojia hii ilianza kutu-
mika miaka mingi nyuma.
Miaka ya nyuma kidogo, mashirika makubwa ya kijasusi, yaliku-
wa yakiwatumia ndege kama njiwa, kwa kuwafunga kamera ndogo
za siri kisha kuwaachia waruke na kamera hizo zikawa zinapiga
picha na kurekodi mambo yote yanayoonekana kwenye maeneo
yote ambayo ndege husika amepita.
Maendeleo ya sayansi na teknolojia, yakawezesha kutengenezwa
vifaa vingine vingi, vikiwa katika maumbo mbalimbali, ambavyo
vinao uwezo wa kuongozwa kwa rimoti na kuruka umbali mrefu,
vikikusanya taarifa mbalimbali za kiintelijensia na kijasusi.
Taarifa hizi zilikuwa zikitumika na majasusi na maafisa wa jeshi
tu lakini kwa sasa, mambo yamebadilika ambapo vifaa hivyo
vinapatikana kwa urahisi na vinatumika hata kwa shughuli ambazo
siyo za kijeshi.
Ukiachilia mbali ‘drone’ hizi ndogo ambazo zinapiga picha
katika eneo dogo, lakini pia kwenye nchi zilizoendelea, wamekuja
na uvumbuzi mwingine wa ndege ambazo zinajiongoza zenyewe,
yaani bila kuwa na rubani.
Hizi pia zinatumika kwa kazi zilezile za kukusanya taarifa za
kiintelijensia kwa kupiga picha kutoka umbali mrefu angani na
wakati mwingine kubeba mabomu na silaha za kivita, kisha zi-
nakuwa zinafuatiliwa na watu ambao wako mbali kabisa na eneo
husika.

562 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Tuachane na hayo, ninachotaka kueleza hapa ni kwamba, kwa


kuwa eneo ambalo Zuleikha alikuwa amelitaka nilikuwa nalifaha-
mu kama nilivyoeleza, njiapekee ambayo ingeweza kufanya tujue
ni nini kinachofanyika kule ndani, ilikuwa ni kwa kutumia ‘drone’
kwa sababu nilikuwa najua kwamba eneo hilo huwa linalindwa
vikali na wanaume wenye silaha nzito, isingekuwa rahisi kujipe-
nyeza na kuingia ndani bila kusababisha machafuko.
Uwezo wa kuvamia na silaha ulikuwepo lakini hilo lisingekuwa
na msaada wowote katika kile ambacho tulikuwa tunakihitaji kwa
wakati huo. Ilikuwa ni lazima tukusanye taarifa za siri kwanza ku-
jua ni nini kilichokuwa kinaendelea na jinsi tunavyoweza kulizima
tukio lililokuwa limebakiza saa chache tu mbele yetu.
Kwa hiyo, njia pekee ambayo ingerahisisha, ilikuwa ni kwa
kutumia drone za kisasa ambazo tulikuwa tunazimiliki kwa ajili ya
kazi zetu, ambazo zina tofauti kidogo na hizi zinazotumiwa mita-
ani, zenyewe zikiwa na uwezo wa kufanya kazi bila kugundulika
kirahisi.
Kwa kutumia drone, tungeweza kuona kila kilichokuwa
kinaendelea mle ndani, tukiwa mbali na eneo la tukio kwa sababu
za kiusalama lakini pia kutovuruga uchunguzi wa kina uliokuwa
unaendelea.
Basi nilirudi ofisini kwangu, nikachorachora kwenye makaratasi
na baada ya kupata mpango kazi wa jinsi kazi hiyo itakavyoenda
kufanyika, niliiweka pembeni ratiba hiyo ili kutoa nafasi ya kushu-
ghulikia kazi kubwa iliyokuwa inafanywa na Jack na wenzake kwa
wakati huo.

563 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Nilitoka na kurudi tena kule walikokuwepo akina Jack, nikaende-


lea kuwafuatilia kwa karibu katika kila walichokuwa wanakifanya.
Kama alivyokuwa ameeleza Jack, kwamba kazi ile ingechukua
takribani saa sita kukamilika au chini ya hapo, baada ya kupita saa
tano na dakika kadhaa hivi, tayari kazi ilikuwa imekamilika.
Kilichofuatia baada ya kazi hiyo kukamilika, ikawa ni Jack kuku-
sanya taarifa zote walizozipata katika kazi hiyo, na kuzipanga ka-
tika namna ambayo, ingekuwa rahisi kwa mtu wa kawaida kuelewa
ni nini hasa kilichokuwa kimefanyika, na matokeo yake yalikuwa
ni yapi.
Haikuwa kazi ngumu kwake, akaifanya na baada ya kama dakika
ishirini tu, akawa ameshamaliza, na sasa ukawadia muda wa kupi-
tia kwenye taarifa zote zilizokuwa zimepatikana.
Kilichokuwa kimebainika, ni kwamba tulibaini watu kama
ishirini hivi wa rika tofauti na jinsia tofauti, ambao ndani ya siku
hizo chache, walikuwa wametembelea mitaa ya Magogoni mara
nyingi zaidi bila kuwa na sababu ya msingi.
Nasema bila kuwa na sababu ya msingi kwa sababu ilibidi kuwa-
chuja, mmoja baada ya mwingine, wapo ambao tulibaini kwamba
walikuwa wakifanya kazi maeneo ya mjini jirani na Magogoni kwa
hiyo kuonekana kwao mara kwa mara kwenye kamera hakukuwa
kukilea maswali ya aina yoyote.
Tulibaini pia kwamba wapo wengine ambao ni wafanyabiashara,
wakubwa kwa wadogo ambao ili kwenda au kurudi kutoka kwenye
biashara zao, ilikuwa ni lazima wapite katikati ya mji au jirani na
Magogoni, hao nao hatukuwa na tatizo nao.

564 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Baada ya kuwachuja wote, ndipo sasa walipobakia hao takribani


ishirini hivi, ambao kwanza walikuwa wameonekana mara nyingi
zaidi katika maeneo ya Magogoni, wakiwa hawana sababu zozote
za msingi za kuonekana eneo hilo.
Lakini pia, kulikuwa na kundi lingine la watu kama tisa mpaka
kumi, ambao kwa kutumia magari tofauti, walikuwa wakionekana
wakipiga picha kutokea kwenye magari, mandhari ya Magogoni.
Kundi hili ndiyo ambalo tuliamua kuanza nalo kwa sababu ina-
fahamika kwamba ni kosa kisheria kupiga picha kwenye maeneo
nyeti kama Magogoni tena bila kuwa na sababu yoyote maalum
wala kuwa na kibali!
Tena picha zenyewe zinapigwa kwa kuibia, kutokea mbali kwa
kutumia kamera za kisasa, lengo likiwa ni kuonesha mandhari ya
Magogoni.
Tulipofuatilia usajili wa magari husika kwenye mfumo wa mam-
laka ya mapato, tulibaini kwamba magari matatu yalikuwa yakim-
ilikiwa na mfanyabiashara mmoja, kisha hayo mengine yaliyosa-
lia, kila moja lilikuwa likimilikiwa na mtu mmoja mmoja, lakini
miongoni mwao akiwepo mtu mwingine mkubwa sana ambaye
sasa ushahidi ju yake ulikuwa umeshaanza kupatikana.
Kama unakumbuka nimewahi kueleza kuhusu mfanyabiashara
mmoja mkubwa wa mafuta anayeishi Mikocheni, ambaye bado
tulikuwa tukiendelea kumchunguza kutokana na jinsi alivyokuwa
akishiriki kufadhili matukio ya kihalifu ikiwa ni pamoja na kutoa
rushwa kubwakubwa kwa watumishi wa serikali ili afanikishe
malengo yake.

565 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Ni huyu ndiye aliyekuwa amempandikiza kijana ambaye naye


bado tulikuwa tunamshikilia, kwa lengo la kumtongoza Berthany
na kuanzisha naye uhusiano wa kimapenzi, kwa ajili ya kuwa
anatumika kuvujisha taarifa za siri na kuzifikisha kwenye mikono
ya wabaya wetu.
Basi huyu naye alikuwa miongoni mwa watu ambao magari yao
yalionekana maeneo ya kuzunguka Magogoni, yakiwa yamebeba
watu waliokuwa wanapiga picha za video za mandhari ya kuzun-
guka eneo lote la Magogoni.
Hizi zilikuwa ni taarifa muhimu sana kwa sababu kuanzia
mwanzo, tulikuwa tunakwama kumuingia moja kwa moja mfan-
yabiashara huyu, kwa sababu hakukuwa na ushahidi wa moja kwa
moja ambao ungeweza kumbana, hasa ukizingatia kwamba tayari
alikuwa amewaweka mfukoni baadhi ya maafisa wa ngazi za juu
serikali, kwa hiyo angeweza kuchomoka kirahisi.
Lakini kupatikana kwa ushahidi huu, ilikuwa ni hatua muhimu
ambayo inaweza kuja kutumika kumwajibisha kisheria siku chache
mbele.
Kwa hiyo baada ya kuhakikisha tumeshawajua wamiliki wa
magari yote, hatua iliyofuatia ilikuwa ni kuanza kuwatafuta,
mmoja baada ya mwingine isipokuwa kwa wale wafanyabiashara
wawili ambao tuliamini kuwaweka nguvuni au kuwahoji kwa
namna yoyote, kunaweza kuvuruga uchunguzi wetu.
Kikosi kazi kilipewa jukumu la kuhakikisha wanapatikana
haraka iwezekanavyo na ndani ya muda mfupi tu, watu wanne
wakawa wameshakamatwa na kuwekwa kizuizini ambapo taratibu

566 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

za kuwahoji zilianza bila kupoteza muda.


Wakati hayo yakiendelea, kikosi kazi kingine pia kilipewa
jukumu la kuhakikisha wale watu takribani ishirini walioonekana
sana kwenye kamera, wanafuatiliwa mmoja baada ya mwingine na
kukamatwa haraka iwezekanavyo.
Ni kwa kupitia watu hawa, ndipo tungeweza kuyajua mengi zaidi
ambayo hatukuwa tunayajua. Kutokana na idadi kubwa ya watu
ambao walikuwa wanatakiwa kukamatwa, ubize uliongezeka ku-
liko kawaida pale ofisini, kila alipewa jukumu lake akawa anajita-
hidi kuhakikisha analikamilisha haraka iwezekanavyo kwa sababu
kama nilivyokuwa nimeeleza, hatukuwa na muda wa kutosha
uliobakia.
Kwa upande wangu, na mimi kichwa kilikuwa kinafanya kazi
kama kompyuta kuhakikisha kila kitu kinaenda kama kilivyopang-
wa. Japokuwa viongozi wote na wakuu wa idara walikuwa wame-
ingia kuongeza nguvu, bado ilikuwa inatakiwa sana akili yangu
ndiyo itumike zaidi kwa sababu mimi nilikuwa nayajua mengi
pengine kuliko mtu mwingine yeyote.
Mpaka kufikia majira ya saa kumi na mbili jioni, takribani
watuhumiwa 14 kati ya wale ishirini, walikuwa wameshapatikana
na kuanza kuhojiwa. Sikutaka sana kuhusika kwenye kuwahoji
kwa sababu nilihisi kichwa changu kinaweza kuzidiwa, nikaacha
watu wa kitengo cha ‘interrogation’ ndiyo wafanye kazi hiyo kisha
mimi nije kupewa ripoti ya jumla.
Kwa jinsi akili ya binadamu inavyofanya kazi, unapokuwa na
taarifa nyingi tofautitofauti kwa wakati mmoja, kichwa kinakuwa

567 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ni kama kinazidiwa na matokeo yake, unaweza kujikuta ukiyaacha


yale mambo ambao ni ya msingi zaidi na badala yake kuyashughu-
likia yale ambayo akili imeweza kuyaelewa vizuri na kwa haraka.
Hii ndiyo sababu inayofanya wakati mwingine unashauriwa
kutopendelea kutazama runinga kwa muda mwingi au kukaa
mitandaoni kwa muda mrefu kwa sababu akili ya binadamu huwa
inachoshwa na taarifa nyingi zinazoingia kwa wakati mmoja.
Wakati kikosi cha interogation’ kikianza kazi ya mahojiano, huku
kikosi kazi kikiendelea kuwaska wale watu wengine wote ambao
tulikuwa tunawatafuta, niliona huo ndiyo muda mzuri kwa mimi na
Jack kutoka mpaka kule nilikoelekezwa na Zuleikha, yule binti wa
Ustaadh Fundi kwamba ndiko walilokuwa wakipewa mafunzo ya
kijeshi.
“Naomba dakika chache nipumzike kiongozi!”
“Utapumzika ukifa kijana, jiandae tuondoke! Kuna kahawa
ofisini kwangu, nenda kajihudumie mwenyewe utakuta nakusubiri
kwenye gari,” nilimwambia Jack ambaye kiukweli alikuwa ana-
onesha kuchoka kuliko kawaida, muda mwingi akiwa anajifikicha
macho yake yaliyobadilika rangi na kuwa mekundu.
Ilikuwa ni sahihi kabisa kwa yeye kuchoka kwa sababu kwa
muda wa takribani saa sita mfululizo hakuwa amepumzika hata
kidogo, tena akishughulikia mambo mengi, makubwa na magumu
kwa wakati mmoja.
Nilikuwa namuelewa lakini kama ambavyo mimi pia nilifundish-
wa ukomavu, ndivyo na mimi nilivyotaka kumkomaza kwa sababu
nilikuwa najua kwamba bado hana uzoefu wa kufanya mambo

568 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

mengi kwa wakati mmoja bila kupumzika kama vile.


Aliondoka akiwa anajivuta kuelekea ofisini kwangu nilikom-
wambia akajihudumie kahawa, kisha mimi nikaelekea stoo kwa
ajili ya kuandikisha na kuomba kupewa ‘drone’ ambayo ndiyo
tuliyokuwa tunakwenda kuitumia usiku huo kwenye ile kambi
iliyopo kandokando ya bahari.
Vifaa hivyo vilikuwa vinatoka kwa utaratibu maalum kwa hiyo
ilikuwa ni lazima kwanza ueleze kwa maandishi unakwenda ku-
fanyia nini na itakuchukua muda gani.
Kutokana na jinsi nilivyokuwa nafahamika na kuheshimika pale
ofisini, nilipofika kule kwenye ofisi ya stoo keeper, aliponiona tu
kama ni mimi, hakutaka niandike maelezo kwanza, akaniuliza tu
kuhusu nilichokuwa nakihitaji na bila kupoteza muda, alinitolea
‘drone’ ya kisasa kabisa ikiwa kwenye boksi lake la plastiki,
akaniambia nitakuja kujaza maelezo nikimalizila kazi.
Nilimshukuru sana kwa sababu kama nilivyosema, sikuwa na
uda wa kutosha. Ndani ya dakika chache tu, nikawa nimeshafika
kwenye gari langu na kuanza kuikagua ile ‘drone’ kama ilikuwa
sawa. Muda huhuo, nikamuona Jack naye akija, safari hii akiwa
amechangamka tofauti na dakika chache zilizopita.
“Uko tayari?”
“Ndiyo chief! Nilikuwa sijui kama kahawa ni dawa, naona
uchovu wote umeyeyuka kabisa,” alisema, tukacheka kisha nika-
mtaka aikague na yeye ile drone kabla hatujaondoka.
“Ni toleo la kisasa kabisa hili!,” alisema Jack akiishangaa.
“Mambo ya teknolojia hayo!” nilimwambia, akawa anashan-

569 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

gaashangaa!
“Lakini mfumo wake wa uendeshaji ni kama zile nyingine isi-
pokuwa hapa kuna vitu vichache vilivyoongezeka,” nilimwambia,
eti na mimi nikawa mwalimu kwake kwenye vifaa vya kiteknolo-
jia.
Nilikuwa na ujuzi wa kawaida kwa sababu tukiwa mafunzoni
nchini Israel, namna ya kuongoza ndege zisizo na rubani, kuanzia
ndege kubwa mpaka hizo drone za kupigia picha yalikuwa ni ma-
somo ambayo tulijifunza, ingawa ambacho sikuwa nacho ilikuwa
ni uzoefu kwa sababu hata niliporudi sikupata muda wa kutosha
wa kufanyia mazoezi nilichojifunza na hiyo ndiyo sababu iliyoni-
fanya nimchukue Jack.
Basi baada ya kuzungumza mawili matatu na Jack, tuliingia kwe-
nye gari na safari ikaanza. Hakuwa anajua tunaelekea wapi lakini
mimi tayari nilikuwa na ramani yote kichwani.
Yale maelezo yaliyotolewa na Zuleikha, mtoto wa Ustaadh Fundi
kuhusu lile eneo walilokuwa wakifanyia mazoezi ambako ndiko
alikokutana na yule mwenzake na kumueleza kile alichokuwa
amenielekeza, yalikuwa yakishabihiana na eneo ambalo nimesha-
wahi kulielezea siku za nyuma na nilikuwa na uhakika kwamba
ndiyo penyewe.
Safari iliendelea tukiwa tunapasua lami ya Barabara ya Baga-
moyo au Ali Hassan Mwinyi. Mwendo niliokuwa naendesha, kama
ilivyo kawaida yangu, haukuwa wa kawaida, nikawa nayapita
magari mengine kwa kasi na baada ya takribani dakika ishirini
hivi, tukawa tumeshafika eneo linaloitwa Mbuyuni, njia panda ya

570 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Kunduchi.
Nikaiacha Barabara ya Bagamoyo na kukata kulia na kuingia
Barabara ya kuelekea Kunduchi. Safari iliendelea mpaka eneo
linaloitwa Mtongani, kwa wenyeji wa maeneo ya Kunduchi
watakuwa wanalijua eneo hilo, nikakata tena kulia na sasa tukawa
tunaendelea Kunduchi Mwisho.
Tulifika mpaka kwenye kituo cha daladala cha Kunduchi, jirani
na geti la hoteli moja kubwa na maarufu iliyopo eneo hilo, nikakata
kushoto na kuingia kwenye barabara ya vumbi, taratibu tukaanza
kuyaacha makazi ya watu.
Dakika kadhaa baadaye, tuliwasili kwenye eneo lenye maka-
buri ya kale ambayo inaelezwa kwamba walizikwa mabaharia wa
Kigiriki miaka mingi nyuma. Haya ndiyo makaburi aliyoyaeleza
Zuleikha na japokuwa mwenyewe hakuwa akijua yapo sehemu
gani, maelezo yake yaliendana kabisa na mwonekano wake.
Ilibidi nitafute sehemu ya kupaki gari kwa sababu sikutaka
uwepo wetu ujulikane na mtu yeyote na eneo hilo barabara yake
ilikuwa mbovu sana, ikiwa imejawa na mchanga mwingi lakini pia
kukiwa na vichaka vingi.
“Huku ni wapi tena?” aliniuliza Jack, akiwa anashangaashangaa,
nikamuonesha ishara kwamba atulie. Kama siyo mwenyeji wa Dar
es Salaam, unaweza kudhani upo mkoani huko kwa jinsi eneo zima
lilivyokuwa.
Nilizima gari baada ya kuwa nimelichomeka vichakani, mahali
ambapo isingekuwa rahisi kwa mtu yeyote kuliona.
Nikamtaka Jack achukue boksi lake lililokuwa na ile ‘drone’,

571 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

nikaichukua bastola yangu iliyokuwa kwenye ‘dashboard’ ya


gari, nikaikagua na baada ya kujiridhisha iko sawa, niliteremka na
kuichomeka kiunoni, nikafungua buti la gari na kwenda kuchukiua
vizibao viwili vya kuzuia risasi kupenya (bullet proof).
Kimoja nikavaa mimi na kingine nikampa Jack, naye akavaa
kisha akabeba boksi lake lenye drone, nikatangulia mimi mbele na
kumpa ishara kwamba anifuate. Tulipenyapenya kwenye vichaka
na mwisho tukatokea kwenye yale makaburi.
Kwa jinsi eneo hilo lilivyokuwa linatisha, hasa ukizingatia
kwamba tayari giza lilishakuwa limeingia, ilibidi nichomoe bastola
yangu na kuishika mkononi, tayari kwa chochote. Tukapita kwenye
makaburi hayo ambayo yalikuwa yamezingirwa na miti mikubwa
ya mibuyu na vichaka vikubwa.
Sikupata sana shida kujua njia za mkato kwa sababu kama nili-
vyoeleza, nilikuwa nalijua vizuri eneo hilo, Jack akawa ananifuata
kwa nyuma, tukaendelea kupenya na mwisho tukawa tumeyavuka
makaburi hayo, tukatafuta sehemu palipokuwa na kama mwinuko
hivi, nikampa ishara Jack kwamba aitoe ile drone.
Kutokana na giza, ilibidi nitoe tochi yenye mwenye mkali, nika-
muwashia, akaliweka lile boksi chini na kulifungua, akaanza kuun-
ganisha ile drone, kuanzia kwenye mapangaboi madogo yanayoi-
wezesha kuruka mpaka kwenye lenzi ya kamera.
Baada ya kuhakikisha kila kitu kipo sawa, nilimpa ishara kwam-
ba ajaribu kuiwasha, ikawaka bila tatizo, akawa bado anaishangaa
na nadhani ni kwa sababu ya muundo wake.

572 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

21
D
RONE za kawaida zinazotumika mitaani, huwa
zikiwashwa, taa za rangi ya kijani, nyekundu na
kijani zikawaka lakini hii ilikuwa inawaka sehemu
moja tu, tena mwanga mweupe ambao ni hafifu
kiasi kwamba ukiwa mbali kidogo, huwezi kuuona.
Ilitengenezwa hivi ili hata ikiwa inafanya kazi angani, isiwe
rahisi kwa mtu yeyote kuigundua. Aliishika rimoti yake, akaibofy-
abofya na yale mapangaboi yakaanza kuzunguka kwa kasi lakini
bila kutoa mlio wowote, nikamuona akizidi kushangaa kwa sababu
zile za mitaani, huwa zinatoa mlio fulani ambao ukiwa mita kad-
haa pembeni unausikia.
Nikampa ishara kwamba ajaribu kuipaisha, kweli akabofyabofa
ile rimoti, ikaanza kupanda juu taratibu, kama helikopta inavyopaa.
573 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Aliendelea kuipandisha juu taratibu huku akiwa makini kusikiliza


maelekezo ninayompatia.
Ilipofika umbali wa kama mita mia moja juu, nilimpa ishara
kwamba aigandishe kwanza hapohapo, nikasogelea ile rimoti
aliyokuwa ameishika, nikamtaka awashe kamera, kweli akafanya
hivyo na sasa tukawa tunaweza kuona eneo lote kutokea juu.
Kingine kilichomshangaza ni kwamba ilikuwa imetengenezwa
kwa teknolojia maalum iitwayo UV-Light, ikiwa na maana kwam-
ba inakuwa na uwezo wa kupiga picha hata kwenye giza na kufan-
ya vitu vyote vionekane vizuri bila kuhitaji mwanga wa ziada.
Nikamtaka aigeuze ikiwa hapohapo huku nikiwa makini kuan-
galia picha zilizokuwa zinaonekana pale kwenye kioo cha rimoti
ambacho kama nilivyoeleza, kilikuwa kama simu hizi za kisasa za
mkononi.
Nilichokuwa nakifanya hapo, ilikuwa ni kuangalia vizuri uelekeo
wa ile kambi ilipokuwepo, baada ya kupata uhakika, nilimuele-
keza kwamba aanze kuipeleka mbele kuelekea kwenye eneo la ile
kambi, ikiwa umbali uleule kutoka ardhini kwa maana ya mita mia
moja.
“Anza kurekodi,” nilimwambia baada ya kuwa tayari imeshaingia
kwenye eneo la ile ngome, kweli akabofyabofya kwenye rimoti,
ikaanza kuonesha kwamba inarekodi video. Mara ya kwanza nilim-
uelekeza kwamba apite juu mpaka mwisho wa lile eneo la ndani ya
kambi, mpaka upande wa baharini.
“Imefika mbali, inaweza kupoteza mawasiliano na rimoti tu-
kaipoteza,” alisema kwa sauti ya hofu, nikamwambia asiwe na wa-

574 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

siwasi kwa sababu ilikuwa na uwezo wa kwenda mbali zaidi bila


kupoteza mawasiliano kama zilivyo ‘drone’ za kawaida kutokana
na teknolojia yake.
Akawa anazidi kushangaa, kweli akaipitisha eneo lote la kambi
mpaka mwisho, kisha nikamuelekeza aigeuze na aipeleke upande
wa pili wa kambi. Ilivyopita mara ya kwanza, hatukuona chochote
kwenye rimoti kwa maana hatukumuona mtu yeyote.
Alivyoigeuza upande wa pili, ndipo tulipobaini kwamba kumbe
kulikuwa na watu kama kumi hivi, waliokuwa wamekaa chini,
mmoja akiwa amesimama, ikionesha ni kama alikuwa anawaele-
keza jambo. Nikamtaka aishushe chini kidogo ili tuweze kuwaona
vizuri watu hao kwa karibu, nikakazia macho kwenye ile ‘screen’
ya rimoti.
Kwa jinsi picha zilivyokuwa zinaonekana kwa ubora, tuliweza
kubaini kwamba aliyekuwa amesimama alikuwa ni mwanaume na
wote waliokuwa wamekaa wakimsikiliza, walikuwa ni wasichana,
tena wa umri mdogo. Nilitamani sana kamera ingekuwa na uwezo
wa kunasa mpaka mazungumzo yao lakini hilo halikuwezekana.
Akawa anaizungusha eneo lile kama nilivyokuwa namuelekeza,
tukafanikiwa kuzinasa sura za wote waliokuwa eneo lile, nikamu-
elekeza kuipaisha juu na kuendelea kuzunguka maeneo mengine,
tukawaona walinzi kadhaa waliokuwa na silaha, wakiwa wanazun-
guka huku na kule kuhakikisha hakuna mtu asiyehusika anasogelea
eneo hilo.
Aliendelea kuizungusha, tukafanikiwa pia kuyaona magari
mawili yaliyokuwa yamepaki kwenye maegesho maalum ambayo

575 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

nayo yalikuwa yanalindwa. Kwa kama dakika thelathini nzima,


drone ilikuwa angani ikiendelea kurekodi matukio yote.
Katika hali ambayo hakuna aliyeitarajia kati yetu, tulishtuka
kusikia bunduki ikikokiwa nyuma yetu na kufuatiwa na sauti kali:
“Tulieni hivyohivyo!” Mapigo ya moyo wangu yakanilipuka na
kuanza kunienda mbio kuliko kawaida.
Nilichokifanya, niliinua mikono juu taratibu huku nikiwa nata-
fakari nini cha kufanya kwa sababu hakuna aliyekuwa amemuona
mtu huyo aliyekuwa nyuma yetu.
Kila kitu kilikuwa kimetokea ghafla mno, nikawa najilaumu
kwamba inawezekanaje adui atusogelee kiasi hicho bila kushtuka
mapema? Haikuwa kawaida yangu.
“Mnafanya nini hapa?” alihoji yule mwanaume kwa sauti ya
mamlaka, safari hii akinisukuma mgongo kwa mtutu wa bunduki
akiwa ni kama ananizuia nisigeuke na kumtazama.
“Samahani afande, tunarekodi kaklipu ka kuposti Youtube!”
nilisema na muda huo nikawa nimeshafanikiwa kugeuka, tukawa
tunatazamana uso kwa uso na yule mwanaume, ambaye kwanza
kwa mwonekano wake, niligundua kwamba hakuwa askari bali
mlinzi, tena mlinzi wa kampuni binafsi kwa sababu hata umri uli-
kuwa umeenda kidogo.
“Mnafanya nini?” alirudia kuuliza, nikaitazama vizuri ile bun-
duki aliyokuwa ameishika, kwa harakaharaka niligundua kwamba
ni gobole!
“Tusaidie mzee wangu, kuna elfu kumi hapa,” nilisema nikiingi-
za mkono mfukoni na kuchomoa noti ya shilingi elfu kumi. Ilikuwa

576 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ni lazima nitumie mbinu hiyo kwa sababu kutumia nguvu kubwa


kwa mtu kama yule, isingekuwa uamuzi sahihi ingawa uwezo huo
nilikuwa nao.
“Iko wapi!” alihoji huku akishusha bunduki yake chini, nikamka-
bidhi shilingi elfu kumi na kumuomba atuache tumalizie tulichoku-
wa tunakifanya.
Ajabu ni kwamba alikubali, na yeye akawa anashangaa ni nini
hasa kilichokuwa kinafanyika, ikabidi nitumie ujanja wa kumsoge-
za pembeni ili Jack aweze kufanya kazi yake kikamilifu bila yule
mlinzi kujua ni nini hasa kilichokuwa kinafanyika.
“Afande, eti hapa huwa kuna shughuli gani zinazofanyika kwe-
nye haya makaburi usiku?” nilimuuliza huku nikiahidi kumuon-
geza shilingi elfu kumi nyingine endapo atanipa ushirikiano mzuri.
“Mambo ya kichawi tu! Unajua maeneo ya Kunduchi kuna wa-
vuvi wengi wanaofanya shughuli zao baharini! Shughuli za uvuvi
huwa zinaendana sana na shughuli za kishirikina! Kwa hiyo huwa
wanakuja sana kuwanga hapa makaburini ndiyo maana nikaajiriwa
mimi kwa ajili ya kazi ya kuwadhibiti.
“Nilijua na nyie mmekuja kuwanga!” alisema huku akitoa kip-
ande cha sigara, akakiwasha na kuvuta funda kubwa kisha akatoa
moshi kwa kutumia pua na mdomo,” nikawa natingisha kichwa
kuonesha kumuelewa alichokuwa anakisema.
“Hivi kumbe mambo ya uvuvi yanahitaji ndumba eeh?”
“Ndiyo, si unajua tena baharini kuna mengi? Ili mpate samaki
lazima mzunguke kwa wataalamu. Ili kuwa salama mkiwa baharini
dhidi ya majini wabaya pia inatakiwa kutumia uchawi,” alisema,

577 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

nikawa natingisha kichwa, nikachomoa noti nyingine ya shilingi


elfu kumi na kumpa.
“Kwani huku ukiacha haya makaburi kuna nini kwa upande ule,”
nilisema huku nikionesha kidole upande kulipokuwa na ile ngome.
“Kuna kampuni ya ulinzi hii ndiyo kama ngome yao ya kufanyia
mazoezi.”
“Ooh! Kwa hiyo kuna watu mle ndani?”
“Watu wa kila aina, ila wote huwa wanakuja na kuondoka! Mimi
nashinda sana maeneo haya kwa hiyo huwa nawaona, usiku ndiyo
mida yao! Inaonesha bosi wao ni tajiri maana huwa wanakuja mpa-
ka Wasomali sijui Waarabu wale,” alisema, nikauficha mshtuko
ndani ya moyo wangu.
“Duh! Basi sawa, nakushukuru sana kwa kuturuhusu maana tuli-
posikia bunduki tumeshtuka sana!”
“Miye nimewaona tangu mlipokuwa mnapaki gari lenu kule,
nikawa nawafuatilia kimyakimya! Ningewakuta mnawanga hakika
mngekiona cha mtema kuni leo,” alisema huku akicheka, nikagun-
dua kwamba hata uelewa wake wa mambo ulikuwa mdogo sana in-
gawa alikuwa na taarifa muhimu sana kuhusu kile kilichotupeleka
eneo lile usiku ule.
Kwa kuwa tayari tulikuwa tumeshafanya kazi yetu kiasi cha
kutosha, niliona kuendelea kukaa eneo lile, tungeweza kuharibu
mambo maana kwa muda wote nilikuwa namkwepa yule mlinzi
asije akaanza kunihoji jambo lolote kuhusu sisi ni akina nani kwani
angeweza kusababisha kizaazaa.
“Jack! Inatosha kwa leo, tutakuja siku nyingine,” nilimwambia

578 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Jack ambaye alikuwa anaendelea na kazi yake, akaitikia kuonesha


kwamba amenielewa, akaigeuza ile drone kule angani ilikokuwa
ikiendelea kurekodi, akairudisha mpaka usawa wa pale tulipoku-
wepo, akaishusha chini na kuipokea kwa mkono mmoja kisha
kuizima.
“Hiki ni nini?”
“Ni kamera zenye uwezo wa kupaa, si unaona hapa!” nilisema
nikijibu swali la yule mlinzi ambaye alipigwa na butwaa kuiona ile
drone.
Nilimzugazuga pale, akaonesha kuwa na shauku kubwa ya
kutaka kujua zaidi, na mimi nikawa namjibu kwa namna ya kuzidi
kumpumbaza ili asijue kwa undani ni nini hasa kilichokuwa kime-
fanyika eneo lile.
Jack aliifungua drone kama ilivyokuwa mwanzo, akaiweka kwe-
nye boksi lake kisha tukamuomba yule mlinzi atusindikize kurudi
kule tulikokuwa tumepaki gari. Kwa kuwa kulikuwa na giza, ilibidi
yeye ndiyo awashe tochi yake, akatuongoza kupenya kwenye vi-
chaka mpaka kwenye gari letu.
Harakaharaka tukaingia kisha nikawasha gari, nikawa nampungia
mkono mlinzi ambaye naye alikuwa akikenua meno, akionesha ku-
furahia shilingi elfu ishirini nilizompa, tukaondoka kwa kasi eneo
hilo.
“Daah, umetumia akili kubwa sana kucheza na yule mlinzi!
Ningekuwa mimi pale hata sijui ningefanyaje!” alisema Jack, akiji-
futa kijasho chembamba kilichokuwa kinamtoka.
“Ukomavu ni pamoja na kujua nini cha kufanya kwa wakati gani!

579 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Huwezi kuua mende kwa nyundo,” nilisema na kusababisha acheke


sana.
“Hawa jamaa ni watu hatari sana, nimesikia pale anasema huwa
wanakuja Wasomali au Waarabu, itakuwa wanatoa mafunzo ya
kigaidi!”
“Ni hivyo! Tuna kazi kubwa sana mbele yetu!”
“Lakini inawezekanaje haya yanatokea bila vyombo vya ulinzi na
usalama kugundua?”
“Hawa watu huwa wanakuwa na mbinu nyingi sana! Si umesikia
hapo mlinzi anasema ni kampuni ya ulinzi? Wanawahadaa watu
kwamba ni kampuni ya ulinzi lakini kumbe ni kitu tofauti kabisa.
“Na utashangaa hata ukifuatilia kwa undani, utakuta ni kweli
wamejisajili kama kampuni ya ulinzi na wanavyo vibali vyote
kumbe wanafanya mambo tofauti kabisa,” nilisema, akawa
anatingisha kichwa kuonesha kusikitika.
“Tunachotakiwa kwenda kukifanya tukifika tu, ni kutoa hizi vid-
eo zote kisha kuangalia zile sura za wale mabinti tuliowakuta eneo
la tukio kisha tuangalie kama kuna yeyote kati yao ametembelea
maeneo ya Magogoni katika siku za hivi karibuni. Nina wasiwasi
mkubwa kwamba huenda hawa ndiyo Cat Girls wenyewe,” niliji-
kuta nimetamka jambo ambalo Jack hakuwa na uelewa nalo.
“Cat Girls ndiyo akina nani?”
“Aah! Achana nao, cha msingi ni kuhakikisha tunawadhibiti!”
nilisema kisha ukimya ukapita kati yetu, safari ikaendelea na baada
ya muda, tukawa tumewasili ofisini.
Nilisimamisha gari kwenye maegesho kisha tukateremka na moja

580 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kwa moja tukaongozana mpaka ofisini kwangu.


Nilitaka ile kazi ifanyike muda huohuo, kweli tulipoingia tu, kazi
aliyoanza nayo Jack ikawa ni kuhamisha video kutoka kwenye
drone kwenda kwenye kompyuta kubwa na ya kisasa ili baada ya
hapo ndiyo kazi ya kuwafuatilia wote walionaswa kwenye ile video
ianze.
Ilichukua karibu dakika ishirini video yote kuwa imeingia kwe-
nye kompyuta, Jack akakaa vizuri kisha akaanza kazi yake ya
kufananisha sura kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu. Ndani ya
muda mfupi tu, tayari majibu yalianza kupatikana, majibu ambayo
yalitushtua kuliko kawaida.
Miongoni mwa wale watu ambao kama nilivyoeleza awali, wa-
likuwa wamenaswa kwenye kamera za CCTV mara nyingi zaidi
wakizengeazengea Magogoni, watatu kati yao walikuwa ni wale
wasichana ambao tulifanikiwa kuzinasa sura zao kwenye video
tuliyoenda kuirekodi usiku ule Kunduchi.
Wengine wawili kati yao, walikuwa wamenaswa na kamera za
CCTV wakiwa wanapiga picha kutokea ndani ya magari kama nili-
vyoeleza awali. Kwa lugha nyepesi, maadui walikuwa karibu yetu
kuliko tulivyokuwa tukifikiria.
Hakukuwa na wasiwasi tena kwamba wale waliokuwa wakiitwa
Cat Girls miongoni mwao ndiyo wale wasichana tuliowakuta kule
Kunduchi, wakiwa wanapewa maelekezo huku nao wakisikiliza
kwa umakini mkubwa.
Ulikuwa ni ugunduzi mwingine ambao hakika ulituchosha
vichwa kuliko kawaida, nikamuona Jack akiwa anabofyabofya

581 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kompyuta yake huku akitetemeka vidole! Hofu ilikuwa imeingia


na kwenda kuota mizizi ndani kabisa ya moyo wake.
Mimi pia nilikuwa na hali hiyohiyo lakini badala ya kuogo-
pa, moyoni nilikuwa naendelea kujipongeza kwa jinsi mambo
yalivyokuwa yanaendelea kufunguka, moja baada ya jingine na
kuzidi kutoa picha kubwa zaidi.
“Kwisha habari yao! Hawawezi tena kutuzidi akili,” nilimwam-
bia Jack, akaacha kubofyabofya kompyuta na kunigeukia, akawa
ananitama usoni, akionesha kukosa kabisa utulivu.
“Usiwe na wasiwasi, hakuna jiwe ambalo halitaachwa bila
kugeuzwa! Niprintie picha za hawa watano pamoja na ile picha
tuliyowapiga kule Kunduchi wakiwa wanaonekana wote sura zao
haraka kisha endelea kuchimba taarifa za kila mmoja kati ya hawa
wasichana watano.
“Angalia familia zao, angalia wazazi wao, namba zao za simu na
kila taarifa inayoweza kutusaidia,” nilimwambia, akashusha pumzi
ndefu na kuendelea kupambana na ile kompyuta kwa kasi kubwa.
Aliniprintia picha za wale wasichana watano, nikazikagua vizuri
na kushusha pumzi ndefu. Sasa nilikuwa najua hata nikienda ku-
zungumza na baba yake Saima, nitakuwa na ushahidi uliokamilika
mkononi.
Nilitoka ofisini na kumuacha Jack akiendelea na kazi, nikatoka
na akili zangu zilinituma kwanza kwenda kwa Zuleikha, mtoto wa
Ustaadh Fundi kwenda kumuonesha zile picha kama kuna yeyote
anayeweza kumtambua.
Nilipanga pia kwenda kwa Sanipha, yule mwanamke tuliyem-

582 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kamata na wale wasichana kule Kijitonyama Kisiwani ili na yeye


akawatambue kama kuna anayemjua au kama walishapita kwenye
mikono yake.
Nilipanga pia kwenda kuzungumza na yule mzee wa Kisomali
ambaye kwa hakika aligeuka na kuwa msaada mkubwa sana kwe-
nye oparesheni iliyokuwa mbele yetu. Ilikuwa ni lazima nikusanye
taarifa zote muhimu haraka iwezekanavyo kwa sababu kama
nilivyoeleza, muda ulikuwa unayoyoma kwa kasi kubwa kuliko
kawaida.
Nilianzia kwa Zuleikha, japokuwa ilikuwa ni usiku, niliagiza
akaletwe kwenye chumba cha mahojiano haraka iwezekanavyo,
vijana wangu wakaenda kumtoa na muda mfupi baadaye, nilikuwa
nikitazamana naye, akionesha ni kama alikuwa ameenda kuamsh-
wa usingizini.
Baada ya salamu, niliweka zile picha mezani na kumtaka azi-
tazame. Alipoichukua ya kwanza tu, alionesha mshtuko mkubwa
kisha akawa ni kama ameduwaa.
“Vipi?”
“Zahara! Huyu ndiyo Zahara!” alisema, ikabidi nisimame na
mimi nimtazame vizuri huyo Zahara aliyekuwa akimzungumzia.
Nifafanue kidogo kuhusu huyu Zahara!
Huyu ndiye msichana ambaye alizungumza na Zuleikha na kum-
weleza kwamba akamuagie kwa wazazi wake kwa sababu hadhani
kama atarudi akiwa salama kwa sababu walikuwa wakipewa ma-
funzo ya kuvaa mabomu na kujitoa mhanga.
Niliichukua ile picha na kumtazama vizuri! Nilijikuta na mimi

583 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

nikishtuka kuliko kawaida. Alikuwa miongoni mwa wale wasicha-


na tuliowakuta kule Kunduchi.
“Una uhakika?”
“Ndiyo! Namfahamu vizuri kwa sababu tulisoma naye na wazazi
wake na wazazi wetu wanafahamiana vizuri. Ni mtu ninayemjua
vizuri,” alisema huku na yeye akiwa anatetemeka mikono.
Nikaiweka pembeni ile picha, nikamtaka aendelee kuziangalia
zile nyingine. Ajabu ni kwamba, ni wachache ambao hakuwa aki-
wafahamu na maelezo yake ni kwamba wengi kati yao walikuwa ni
kutoka Kibiti na Mkuranga na wengine alikuwa amesoma nao.
Baada ya kuchukua maelezo yote, nilimshukuru na kumtaka
akapumzike na kama nitakuwa nina shida na jambo lolote, nitaenda
tena kumuamsha hata kama ni usiku wa manane.
Nikatoka na kuwaagiza vijana wangu wamrudishe kwenye chum-
ba chake. Nikaongoza moja kwa moja mpaka kwenye vyumba vya
upande wa chini ambavyo vilikuwa na ulinzi mkali zaidi. Lengo
langu lilikuwa ni kwenda kuonana na Sanipha kama nilivyokuwa
nimepanga.
Naye nilimuonesha zile picha, kama ilivyokuwa kwa Zuleikha,
naye alikiri kwamba anawafahamu wasichana wote hao kwani
waliletwa kwake na mumewe na walipita kwenye mikono yake.
Baada ya kuchukua maelezo yote, nilitoka na kwenda kwa yule
mzee wa Kisomali ambaye sikuwa nimeonana naye kwa muda
kidogo. Nilifungua na kuingia ndani ya chumba chake, nikamkuta
akiwa anasali. Aliponiona tu, alimalizia harakaharaka alichokuwa
anafanya kisha akanisogelea akiwa na shauku kubwa ya kusikia

584 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

chochote kutoka kwangu.


“Mmefanikiwa? Mmefanikiwa kuwadhibiti?”
“Bado, ila naamini tutawadhibiti! Nataka unisaidie kuwatambua
hawa wasichana,” nilisema huku nikimkabidhi zile picha, akazi-
tazama moja baada ya nyingine, nikamuona akitingisha kichwa
chake kwa masikitiko.
Alinieleza kwamba wasichana wale wote walikuwa wamechuku-
liwa makwao na kuletwa jijini Dares Salaam kwa ajili ya kupewa
mafunzo ya kutumika kama silaha kwa maana ya walipuaji wa
kujitoa muhanga.
“Kinachokusikitisha ni nini?”
“Najihisi kuwa na hatia kubwa ndani ya moyo wangu! Nimey-
atambua makosa yangu, namuomba sana Mungu anisamehe kwa
yote niliyoyatenda! Sikuwa najua nafanya nini lakini yote haya
ameyasababisha Abdulwaheed! Nawaombea mfanikiwa kuzima
hili tukio kabla hizi damu za hawa mabinti wasio na hatia hazi-
jamwagika!” alisema huku akijifuta machozi.
Niliendelea kumhoji lakini alionesha kutokuwa na taarifa
nilizokuwa nazihitaji, zaidi akawa anamlaumu sana Abdulwa-
heed kwamba hakuwa amewaeleza kuanzia mwanzo malengo ya
alichokuwa anakipanga.
Sikutaka kuendelea kupoteza muda, nilitoka na moja kwa moja
nikaongoza kwenye ofisi ya baba yake Saima. Tayari ilikuwa
inaelekea saa sita za usiku. Nilipofika, nilimkuta baba yake Saima
akiwa bize kuliko kawaida.
Haikuwa kawaida kuona ofisi nzima watu wako bize mpaka

585 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

usiku kama huo. Aliponiona tu, aliacha kila alichokuwa anakifan-


ya, akainuka haraka na kunisogelea.
“Mambo ni magumu sana Kenny! Nahisi hatutakuwa na muda
wa kutosha kuwadhibiti hawa wendawazimu,” alisema baba yake
Saima na kunieleza kwamba alikuwa amekabidhiwa mafaili yote
kutoka kwa watuhumiwa waliokuwa wamekamatwa siku hiyo
wakiwa wanachora ‘raketi’ Magogoni na kunieleza kwamba walio-
wahoji wamegundua mambo mengi ambayo hayana majibu.
Alinifafanulia kila kitu, mwisho na mimi nikamweleza nili-
chokuwa nimekibaini mpaka wakati huo.
“Mungu wangu! Una akili sana kijana wangu! Sikuwa nimewaza
kama ulivyokuwa umewaza wewe na sidhani kama kuna yeyote
kati yetu aliyekuwa amewaza kama wewe ulivyowaza.
“Sasa naamini kwa kutumia taarifa hizo mpya tunaweza kuwad-
hibiti kabla hawajaleta madhara!” alisema kisha na yeye akatoa
wazo kama nilivyokuwa nafikiria mimi kwamba wale wasichana
watano ambao tulishapata uhakika kwamba ni miongoni mwa
waliopangwa kwenda kufanya tukio hilo, wafuatiliwe taarifa za
familia yao haraka iwezekanavyo.
“Tayari hilo linafanyika na naamini mpaka muda huu tayari
kijana wangu atakuwa ameshapata taarifa zote muhimu,” nilisema,
baba yake Saima akanisogelea na kunikumbatia kwa nguvu, nika-
mshauri tuongozane mpaka ofisini kwangu kuona ni wapi alipoku-
wa amefikia Jack, harakaharaka tukatoka huku baba yake Saima
akiwa anazungumza mwenyewe wakati tukipiga hatua ndefundefu.
“Hebu subiri kwanza,” alisema baba yake Saima na kusimama

586 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ghafla, ikabidi na mimi nisimame, akawa ni kama anatafakari


jambo.
“Hivi kwa nini tusiende kupiga ‘ambush’ hapo kwenye hiyo
kambi ya Kunduchi mlipowaona? Si wanaweza kuwa bado mpaka
muda huu?” alihoji, nikagundua tayari mambo yalishaanza kum-
zidia ndani ya kichwa chake.
Nilikuwa nimempa taarifa nyingi na za muhimu ndani ya muda
mfupi kwa hiyo nadhani akili yake ilikuwa inaenda mbio kuliko
kawaida kujaribu kuchanganua mambo.
“Hapana! Hautakuwa uamuzi wa busara, itakuwa sawa na kuvu-
ka barabara ukiwa umefumba macho! Hatujui kuhusu uimara wao,
hatujui ulinzi upo kwa kiasi gani, hatujui wanazo silaha za aina
gani na kubwa kuliko yote, hatulijui eneo hilo vizuri.”
“Lakini wewe si umesema unapajua vizuri na ulishawahi kuingia
mara kadhaa miaka ya nyuma?”
“Ni muda mrefu umepita, siwezi kusema kama napajua tena jinsi
palivyo leo lakini hapo umezungumzia kuhusu hoja moja tu kati ya
nne nilizozisema.”
“Hawawezi kutuzidi nguvu kwa namna yoyote ile! Labda useme
kuhusu madhara tutakayoyapata!” alisema baba yake Saima huku
akishusha pumzi ndefu, tukaendelea kutembea haraka haraka kue-
lekea ofisini kwangu.
“Nahisi kichwa changu kimepata moto,” alisema baba yake
Saima na kusababisha nicheke. Nilichokuwa nimekihisi ndicho
alichokuwa amekisema mwenyewe, alipoona nacheka ikabidi na
yeye acheke.

587 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Nadhani hii ndiyo inaweza kuwa misheni ambayo imeniumiza


kichwa kuliko zote tangu nilipoanza kazi. Hakuna kazi ngumu
kama kupambana na adui ambaye ameshaingia mpaka chumbani
kwako na kujitawala,” alisema,
Tuliingia ofisini na kumkuta Jack akiwa anapambana kwelikweli,
tayari alikuwa ameshakusanya taarifa nyingine nyingi ambazo
zingetusaidia, zikiwemo baadhi ya namba za simu za wanafamilia
wa wale mabinti.
“Tunafanyaje?”
“Vijana wa Cyber kwa kushirikiana na Jack wanaweza kuwa
msaada mkubwa sana kwetu. Lazima tutumie teknolojia ya ma-
wasiliano ya simu, kuchunguza nani na nani wamekuwa waki-
wasiliana na namba za hawa wazazi wa hawa mabinti.”
“Huoni kama hapo tutazidi kupoteza muda zaidi? Kwa nini
tusiwapigie wazazi ambao namba zao zimepatikana na kuwauliza
kama kuna yeyote ambaye amepigiwa simu na mwanaye?”
“Unafikiri kwa jinsi wanavyochungwa kuna yeyote anayeweza
kuwa na simu au hata muda wa kupiga simu?”
“Kwa jinsi ninavyowajua watoto wa kike, hata ufanye nini hu-
wezi kuwadhibiti kwenye suala la kumiliki simu. Amini ninachok-
wambia, huwa wanakuwa wajanja sana. Mtoto wa kike hawezi
kukaa bila kuwasiliana na wazazi wake au mpenzi wake, atafanya
kila kinachowezekana,” alisema baba yake Saima wakati tukiwa
tunaendelea kujadiliana.
Alichokisema pia kikaungwa mkono na Jack akieleza kwamba
endapo hilo litashindikana, ndipo tutakapolazimika kutumia ile

588 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

njia niliyokuwa nimeisema mimi, ambayo alieleza kwamba nayo


inahitaji muda wa kutosha.
“Hili litafanyika asubuhi, si ndiyo?”
“Hapana! Inatakiwa lifanyike sasa hivi na mimi ndiye nitakayei-
fanya hiyo kazi.”
“Lakini ni saa sita za usiku tayari! Ni vigumu simu kupokelewa
muda huu!”
“Wewe ukipigiwa simu usiku wa manane na namba ngeni uta-
pokea au hutapokea?” baba yake Saima alinihoji, nikakosa cha
kujibu zaidi ya kushusha pumzi ndefu. Kichwa chake kilikuwa
kimepata moto kwelikweli, nadhani uchovu pia ulikuwa wa ki-
wango cha juu sana.
Alitoa simu yake, nikamsaidia kuwa namuandikia zile namba
alizozipata Jack za wazazi na ndugu wa wale wasichana tuliowa-
ona Kunduchi, moja baada ya nyingine.
Alipiga namba ya kwanza, ikawa haipatikani, tukaiwekea alama.
Akapiga ya pili, ikaita kwa muda mrefu na ikiwa inakaribia ku-
kata, ikapokelewa, wote tukawa na shauku kubwa ya kusikia baba
yake Saima atazungumza nini.
“Samahani kwa kupiga simu usiku mwingi kama huu, kuna
dharura ambayo inahitaji msaada wa haraka. Bila shaka unamfa-
hamu Sauda Ismail Kingu!” alisema baba yake Saima, simu akiwa
ameiweka ‘loud speaker’, wote tukawa tunasikia.
“Ndiyo! Mimi ni baba yake, ni binti yangu! Kumetokea nini?”
“Unafahamu binti yako yuko wapi?”
“Yuko Dar es Salaam anafanya kazi!”

589 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Mara ya mwisho kuzungumza naye ilikuwa lini?”


“Asubuhi ya leo alinipigia, tukazungumza japo kwa kifupi, aka-
zungumza na mama yake pia.”
“Mlipozungumza amesema anaendeleaje?”
“Amesema wameshamaliza mafunzo na wanatarajia kuanza kazi
muda wowote!”
“Kabla ya kuzungumza naye leo ulizungumza naye lini?”
“Sijawahi, tangu alipoondoka hakuwahi kupiga simu, ni leo tu
ndiyo ametupigia na sote tukafurahi sana japo alikuwa anaonesha
kama ana haraka sana!”
“Binti yako yupo matatizoni! Unaweza kunipa namba aliyoku-
pigia nayo? Alikuambia ni ya nani?”
“Matatizo? Matatizo gani? Namba ninayo nimeisevu ngoja ni-
kutajie, alisema ni ya rafiki yake!” alisema mwanaume aliyekuwa
akizungumza na baba yake Saima na muda huohuo akataja namba
alizotumia binti yake kumpigia, harakaharaka tukaziandika.
Akamuaga yule mwanaume na kumwambia kwamba atapigiwa
simu asubuhi na akaambiwa asimwambie mtu yeyote kilichotokea
wala asiipige tena ile namba aliyotumia binti yake kuwasiliana
naye.
Nilikoshwa sana na jinsi baba yake Saima alivyoweza kutoa
wazo la msingi kama lile na kulifanyia kazi muda huohuo.
“Sasa hapa kinachotakiwa, ni hii namba kufuatiliwa kujua
anayeimiliki ni nani, alipowasiliana na hii namba ya huyu mzazi
wake alikuwa eneo gani na sasa hivi yupo eneo gani.
“Tukipiga namba kama tano tu, zitatosha kutupa mwanga kwam-

590 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ba hawa mabinti wamefichwa wapi hapa mjini. Tukishajua hilo tu,


basi mchezo wote utakuwa umeisha,” alisema, wote tukatingisha
vichwa kukubaliana naye, akili kubwa sana ilikuwa imetumika.
Tuliendelea na kazi ya kupiga zile namba, moja baada ya ny-
ingine, baadhi zikawa hazipatikani huku nyingine zikiita bila
kupokelewa. Ni jumla ya simu nne tu ndizo ambazo zilipokelewa,
na wote waliopokea walikuwa ni wazazi wa wale mabinti.
Ajabu ni kwamba kama alivyokuwa amesema baba yake Saima,
wote kwa nyakati tofauti walikuwa wamewahi kuwasiliana na wa-
zazi wao, mara moja au mara mbili tangu walivyoondoka.
Pia maelezo ya wazazi na walezi wao, yote yalikuwa yakifanana,
kwamba wapo Dar es Salaam wanapewa mafunzo kisha baada ya
hapo wataajiriwa. Nadhani wengi wao walishaharibiwa akili kiasi
cha kuamua kuficha kilichokuwa kinaendelea huko walikokuwepo.
“Hizi zinatosha kuanzia, nyingine tutaendelea nazo asubuhi lakini
kwa sasa, kazi iendelee, kama kuna vijana waliolala wakaamshwe
haraka, hatuna muda wa kupoteza,” alisema baba yake Saima, bila
kupoteza muda nikainuka na kumpa Jack ishara kwamba anifuate,
baba yake Saima naye akawa anatufuata.
Tulienda mpaka kwenye ofisi ya vijana wa Cyber na Teknolojia
ya Mawasiliano (IT). Nilikuwa nimeshawapa maagizo tangu muda
tunaondoka kwenda Kunduchi kwamba hakuna anayeruhusiwa
kuondoka kwenda mahali popote, kama ni kulala kila mmoja alale
humohumo ofisini.
Kwa bahati nzuri sana, wote walikuwa wametii nilichowaambia,
wengine wakawa wamelala kwenye viti vyao na wengine wakawa

591 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wanapiga stori za hapa na pale. Walipoona tumeingia, wote walia-


cha kila walichokuwa wanakifanya na kwa kuwa tulikuwa tumeon-
gozana na baba yake Saima, wote walisimama huku wakiwaamsha
na wenzao ambao walikuwa wamelala.
Mimi ndiye niliyekuwa wa kwanza kuvunja ukimya, nikawataka
wote kuwa makini kuna kazi ya dharura ambayo inatakiwa ifanyike
haraka iwezekanavyo.
Nikamkaribisha baba yake Saima aeleze, ajabu ni kwamba
aliwasalimu tu vijana, akatoa maneno mawili matatu ya kuwatia
moyo na kuonesha namna uongozi unavyofurahishwa na jinsi
walivyokuwa wakijituma.
Baada ya hapo, alitaka mimi ndiyo nitoe maelekezo ya kazi,
ikabidi nifanye kama alivyoagiza. Nikaanza kwa kuwaeleza kwa
kifupi ni nini ambacho tulikuwa tumekibaini mpaka muda huo
kisha nikawaeleza ni nini kinachotakiwa kufanyika.
Niliwaeleza kwamba Jack ndiye atakayekuwa anasimamia kwa
vitendo kwa sababu yeye alikuwa anajua zaidi kuhusu nini kili-
chokuwa kinahitajika, nikawaona vijana wangu wakitingisha
vichwa vyao kuonesha kwamba wameelewa vizuri nilichokieleza.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, Jack alianza kutoa maelezo
ya kitaalamu wakati mimi nikiziandika zile namba kwenye ubao
mweupe uliokuwa mbele ili kila mtu azione. Wakaanza kazi, mimi
na baba yake Saima tukawa tunazungukazunguka mle ndani tuki-
watazama wanavyofanya kazi.
“Kizazi chenu kipo tofauti kabisa na kizazi chetu! Inshangaza
sana kuona kijana mdogo kama Jack akiwa anajua mambo mengi

592 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

mno kuhusu teknolojia wakati sisi wengine kompyuta tulikuja


kuzijulia ukubwani,” alisema baba yake Saima na kusababisha
wote tucheke chinichini.
“Dunia ya sasa imehamia kwenye teknolojia ya kidijitali! Nyie
mlikuwa mnaishi zama za analojia,” nilisema, tukazidi kuangua
vicheko vya chini kwa chini.
“Hii kazi tukiimaliza salama, itabidi mimi, mama yenu, wewe,
mkeo na familia, tusafiri kwenda ‘vacation’ maana nimechoka
mwili, roho na akili, naamini hali ni hivyohivyo pia kwako lakini
kubwa zaidi hatupati muda wa kutosha wa kuwa na familia zetu,”
alisema baba yake Saima, kauli ambayo ilinikosha sana moyo
wangu.
Ni kweli kabisa kwamba ilikuwa inahitaji mke au mume mwele-
wa na mwenye uvumilivu wa kipekee kuishi na watu wa aina yetu!
Muda mwingi tunautumia zaidi kwenye kazi, akili zetu muda wote
zinawaza kazi kiasi kwamba tunakosa kabisa muda wa kukaa na
familia.
Basi tuliendelea kuwa tunapiga stori za hapa na pale, za kazi na
za kifamilia wakati tukiendelea kuwasimamia vijana ambao kila
mmoja alikuwa amezama kwenye kazi kuhakikisha tunachokitaka
kinapatiwa majibu haraka iwezekanavyo.
Baada ya kazi ngumu ya kama dakika arobaini hivi, Jack alii-
nuka pale alipokuwa akifanyia kazi zake na kuja pale tulipokuwa
tumesimama mimi na baba yake Saima, mlemle ndani.
“I think you need to see this!” alisema Jack kwa Kiingereza, aki-
maanisha kuna jambo alikuwa anataka tukajionee wenyewe.

593 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Harakaharaka tulimfuata huku tukitazamana mara kwa mara


kutaka kujua ni nini alichokuwa amekibaini yeye na wenzake.
Teknolojia ya kisasa waliyokuwa wakiitumia Jack na wenzake,
ilibaini kwamba katika wale wasichana ambao tulipata taarifa zao
kwamba wamewahi kuwasiliana na familia zao, simu zote zilikuwa
zimepigwa kutokea sehemu moja.
Tafsiri yake ni kwamba, mahali ambapo simu zilikuwa zimepig-
wa kwenda kwa wazazi wa mabinti hao kwa nyakati tofauti,
ilikuwa ni sehemu moja.
“Hii maana yake ni nini?” nilimuuliza Jack nikimtaka afafanue
ili niwe na uhakika na ile tafsiri ambayo nilikuwa nayo kichwani.
Alichokieleza ndiyo kilekile nilichokuwa nimekielewa lakini
yeye alikuja na ufafanuzi wa ndani zaidi, akieleza kuhusu minara
iliyotumika, ‘location’ iliyosoma kwenye GPS, muda ambao kila
simu ilipigwa, namba ambayo ilipokelewa na muda wa maongezi
walioutumia.
“Pin down the location!” nilimjibu kwa Kiingereza, nikimaanisha
aikuze hiyo sehemu ambayo simu hizo zilikuwa zimetoka, ikabidi
akae na kubofyabofya kwenye kompyuta yake, majibu yakaanza
kuonekana, tena kwenye ramani ya satelite ambayo ilikuwa ina-
onesha vitu vingi kwa wakati mmoja.
Ramani ilianza kwa kuonesha picha ya kama dunia yote ku-
tokea angani, kisha ikaanza kukuza eneo moja ambalo lilikuwa
limewekewa alama ya kiduara kidogo cha rangi nyekundu kwenye
il ramani, ikajivuta haraka na kuonesha ramani ya Bara la Afrika,
ikaendelea kujivuta mpaka ikaonesha ramani ya Tanzania.

594 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Haikuishia hapo, ikawa inaendelea kujivuta kwa kasi, ikaonesha


ni ndani ya Jiji la Dar es Salaam, ikaendelea kusogea karibu kwa
kasi, ikaonesha ni Wilaya ya Kinondoni, ikaendelea kujivuta nam-
wisho ikaonesha ni Masaki.
“Hebu tulia kwanza,” nilisema huku mapigo ya moyo wangu
yakinienda mbio kuliko kawaida, nikashusha pumzi ndefu na
kumgeukia baba yake Saima, naye akashusha pumzi ndefu, tukawa
tunatazamana.
Ilikuwa ni taarifa ya kushtua mno kugundua kwamba kumbe
yawezekana wale wasichana walikuwa wakihifadhiwa Masaki,
eneo ambalo kwa akili za kawaida ni vigumu sana kuhisi kwamba
kuna watu hatari kiasi kile wanaweza kuwa wamejificha, wakien-
delea na mpango hatari kama ule.
“Endelea,” alisema baba yake Saima, nadhani ni baada ya kuona
ni kama bado nimepigwa na butwaa, nikiwa sijui nini cha kufanya.
Jack aliendelea kuivuta ile ramani, ikaendelea kusogea karibu
huku ikiendelea kutoa taarifa zaidi kuhusu mitaa, barabara mpaka
namba za ‘Plots’. Ikaenda kuishia kwenye jengo la ghorofa moja.
“Simu zote zimepigwa kutokea ndani ya jengo hili!” alisema
Jack, tukageukiana na baba yake Saima na kutazamana, wote tu-
kashusha pumzi kwa pamoja.
“Print hiyo image na nyingine itume kwenye email haraka,”
nilimwambia, ikabidi tusogee pembeni na baba yake Saima, tu-
kawa tunajadiliana nini cha kufanya.
“Kwa nini msitumie ujanja kama mliofanya kule Kunduchi,
mkaenda na ile kamera ya drone kuangalia kuna nini kinachoende-

595 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

lea mle ndani?”


“Ni sawa ingawa sidhani kama itakuwa rahisi kutokana na jinsi
eneo lenyewe lilivyo, nashauri kwamba hatua ya kwanza kabla ya
kufanya chochote, ni kuiweka nyumba yote kwenye uangalizi wa
karibu ili kujua ni nani anayeingia na kutoka, na kwa wakati gani!
Lazima iwekwe chini ya ulinzi, muda siyo rafiki kwetu,” nilim-
wambia baba yake Saima.
“Watakapoona shughuli zisizo za kawaida wanaweza kushtuka!”
“Hawawezi kuona, tutafanya kwa usiri mkubwa kama kawaida
yetu! Lazima kwanza tufike eneo la tukio kuangalia namna tuna-
vyoweza kupandikiza watu wetu haraka iwezekanavyo,” nilisema,
tukaendelea kujadiliana pale na mwisho, baba yake Saima akasema
ni lazima mkurugenzi na baadhi ya viongozi wa juu washirikishwe
ili hata chochote kikitokea, isionekane kama sisi wawili ndiyo
tuliosababisha.
Nilimuelewa kwa nini amesema hivyo, hoja ikawa ni je, itaweze-
kana kuwapata watu wote hao ndani ya muda huo? Kwa sababu
ilikuwa inaendelea kama saa nane kasoro hivi usiku.
“Inawezekana! Waruhusu vijana wakapumzike kwanza kisha
mimi na wewe twende chumba cha mikutano ya siri! Utanikuta
nakusubiri,” alisema baba yake Saima, akaniacha mimi mle ndani
ya ile ofisi.
Nilianza kwa kuwashukuru wote waliohusika na kuwaeleza
kwamba kwa muda huo wanaruhusiwa kwenda kupumzika lakini
saa kumi na mbili asubuhi juu ya alama, wawe wamesharejea ofi-
sini.

596 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Hakukuwa na muda wa kupoteza, kila mmoja alizima kompyuta


yake na kutoka kwenda kupumzika, nikabaki na Jack ambaye
alikuwa anamaliziamalizia kuprint ile ramani na kuituma kama
nilivyokuwa nimemuelekeza.
“Unafikiri nini kifanyike ili kujua ni nini kinachoendelea mle
ndani?”
“Tupandikize kamera za siri lakini pia tunaweza kufunga GPS
kwenye gari au chombo chochote cha usafiri kinachoingia au
kutoka kwenye hilo jengo. Hiyo inaweza kutusaidia kujua sehemu
nyingine ambazo wanapangia mipango yao mbali na ndani ya
jengo hilo. Tunatakiwa kujua kila kitu kabla ya kuchukua uamuzi
wowote!”
“Hilo linawezekanaje na muda hautoshi?”
“Inawezekana. Na lingine muhimu zaidi, ni kwamba ule ni mtaa
wanaoishi watu wenye maisha bora! Wengi lazima wamefunga
kamera za ulinzi kwenye nyumba zao kama siyo wote! Tunaweza
kuzidukua baadhi ya kamera tukaona kila kilichotokea na kinacho-
endelea kutokea.
“Tunaingia kwenye kikao nitakuja kuzungumza na wewe nikito-
ka! Najua umechoka sana lakini usilale tafadhali. Usingizi ukiku-
zidi kanywe kahawa ofisini kwangu,” nilimwambia Jack ambaye
macho yake yalikuwa yanaonesha ni kwa kiasi gani amechoka na
ana usingizi.
“Sawa kaka, nashukuru kwa kuniamini, nimepata uzoefu mkub-
wa sana kwa hiki tunachokifanya!” alisema, nikamuonesha alama
ya dole gumba, wote tukatabasamu na bila kupoteza muda, nilitoka

597 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

na kuelekea kule kwenye chumba cha mikutano ya siri ambako


baba yake Saima aliniambia nitamkuta.
Nilipoingia, nilimkuta baba yake Saima ameshakaa kwenye kiti
meza kuu, pembeni yake akiwa na mkurugenzi ambaye hata siku-
jua ameingia saa ngapi. Ndani ya dakika mbili zilizofuatia, tayari
viongozi wote muhimu, wakiwemo wakuu wa idara mbalimbali,
walikuwa wameshakaa kwenye viti vyao.
Tayari ilikuwa ni saa nane za usiku lakini kila mmoja alionesha
kutokuwa na hata chembe ya usingizi! Suala lililokuwa mbele yetu
lilikuwa kubwa na muhimu zaidi kuliko hata kulala, baba yake
Saima akafungua kikao.
Alianza kwa kueleza kila kitu kilichotokea tangu mara ya
mwisho tulipokaa kwenye kikao na kwa hakika, mambo yalikuwa
yakienda mbio kwelikweli. Ndani ya muda mfupi tu uliopita, tayari
kulikuwa na matukio mapya mengi kwelikweli.
Aliwaeleza wajumbe wote kila kitu kwa ufafanuzi mzuri kabisa,
matukio mengine yakiwa ni yale ambayo mimi ndiye niliyekuwa
nimempa taarifa zake. Aliendelea kufafanua tukio au taarifa moja
baada ya nyingine mpaka alipohitimisha na taarifa za ile nyumba
iliyopo Masaki ambayo ilionesha kwamba wale wasichana walio-
kuwa wakiandaliwa kwa tukio la kuiangusha Magogoni walikuwa
wakihifadhiwa.
Alipofika hapo, alifungua mjadala ili kila mmoja achangie
kuhusu nini cha kufanya kwa sbaabu mpaka muda huo, tulikuwa
tumesaliwa na saa chache kabla ya muda wa tukio kuwadia, usiku
wa Ijumaa.

598 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Wakati mnachangia, naomba niwakumbushe kwamba hivi sasa


ni saa nane na dakika arobaini na saba, saa tisa kasoro. Tayari siku
imebadilika, tayari tupo ndani ya Ijumaa na tukio limepangwa
kufanyika usiku wa Ijumaa,” alisema baba yake Saima kisha aka-
ruhusu mjadala uendelee.
Nadhani kitendo cha kutukumbusha wote kwamba tayari Ijumaa
imewadia na tukio limepangwa kufanyika siku hiyohiyo ya Ijumaa,
kiliwaamsha watu wote kwamba kumbe tupo ukingoni kabisa mwa
muda.
Mkurugenzi wetu ndiye aliyekuwa wa kwanza kuchangia am-
bapo alianza kwa kutupongeza kwa jinsi tulivyopambana mpaka
kufikia hatua hiyo, akatoa mawazo yake ambayo naweza kusema
yalikuwa ni ya msingi sana.
Alichokisema ni kwamba hatutakiwi kukurupuka na pengine
kwenda kuivamia ile nyumba kwani tutaharibu kila kitu, tu-
nachotakiwa kufanya, ni kuwahadaa maadui zetu ili wasijue kwam-
ba tunajua mambo mengi ya msingi kuhusu mipango yao.
Tukishafanikiwa kuwahadaa, tutaenda kuwapiga ‘ambush’ muda
sahihi ukiwadia, wakiwa wameshajiandaa kwa kila kitu.

599 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

22
N
ILIONA kila mtu mle ndani akitingisha kichwa
chake baada ya mkurugenzi kuwa amemaliza
kuchangia, jambo la msingi akisisitiza kwamba
kuanzia muda huo, eneo lote la Magogoni linataki-
wa kuwa ‘zero ground’ kwa maana macho, masikio
na akili zote za vikosi vyote vya ulinzi na usalama vinatakiwa
kuelekeza nguvu zao hapo.
Wajumbe wengine waliendelea kuchangia, ikaibuka ishu ya
usalama wa namba moja, ikabidi baba yake Saima asimame tena
kutoa ufafanuzi. Alieleza kwamba tayari namba moja alishaon-
dolewa Magogoni na kupelekwa sehemu salama na badala yake,
‘double’ wake ndiye aliyekuwepo na ndiye atakayekuwepo mpaka
muda wa tukio.
Nimeshaeleza sana kuhusu maana ya ‘double’ katika masuala ya

600 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ulinzi na usalama kwa hiyo sidhani kama natakiwa kutumia muda


mrefu kufafanua upya, itoshe tu kusema ‘double’ ni mtu ambaye
alikuwa ametengenezwa kufanana kwa kila kitu na namba moja,
kuanzia mwonekano wa jumla, jinsi anavyotembea, jinsi anavyo-
zungumza na kila kitu.
Alipoeleza kuhusu suala la ‘double’ wa namba moja, mjadala
uliibuka kidogo lakini baada ya kutoa ufafanuzi wa kutosha, kila
mmoja akawa ameridhika. Tukaendelea kujadiliana mambo men-
gine kwa kina, nikawa makini kuandika mawazo ya kila mmoja ili
nisije nikasahau.
Mipango ya nini kinachotakiwa kufanyika kuanzia wakati huo,
hatua kwa hatua mpaka mwisho. Jambo ambalo lilisisitizwa kwa
mara nyingine, ni kwamba mimi ndiye nitakayesimamia opareshe-
ni hiyo mpaka mwisho kama ambavyo nilikuwa nimefanya kuanzia
mwanzo.
Niliuona kama msalaba mzito sana lakini viongozi wote wakani-
hakikishia kwamba watakuwa bega kwa bega na mimi kuhakikisha
tunalizima shambulio hilo, muda muafaka.
Hata sijui ni nini kilikuwa kinaendelea ndani ya kichwa changu
kwa sababu licha ya viongozi wote kunihakikishia nao watakuwa
mstari wa mbele pamoja nami, bado moyo wangu ulikuwa umepig-
wa na baridi kali ya hofu! Inawezekana sikuwahi kuwa na hofu
kama nilivyokuwa nayo wakati huo.
“Calm down! Everything is going to be okay!” nilijiambia mwe-
nyewe huku nikivuta pumzi ndefu na kuzitoa taratibu kwa sababu
mikono ilikuwa inatetemeka kiasi kwamba sikuweza tena kuende-

601 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

lea kuandika.
Kikao cha dharura na cha siri kilimalizika, viongozi wote waka-
wa wanakuja kwangu na kunipa maneno ya kunitia nguvu, yakawa
yanaingilia sikio moja na kutokea sikio jingine.
“Tunahitaji kuzungumza!” alisema baba yake Saima ambaye
ndiye aliyekuwa wa mwisho kunifuata, akanishika begani na kuni-
tazama.
“Umeingiwa na hofu!” alisema huku akitabasamu, ikabidi na
mimi nizuge na kutabasamu kwa sababu ni yeye pekee ndiye aliy-
enisoma kwa usahihi.
“Usiruhusu hofu ikuingie ndani ya moyo wako! Hutakiwi kuogo-
pa kwa sababu hauna sababu ya kuogopa! Umekuwa imara kuan-
zia hatua ya kwanza nakufahamu, naamini utaendelea kuwa imara
mpaka mwisho wa uhai wako! Nikwambie tu miongoni mwa watu
ambao hawana wasiwasi na wewe hata kidogo, ni mimi! Nakuami-
ni kwamba uwezo aliokujaalia Mungu, ni mkubwa sana na utatu-
vusha salama katika hili! Tuliza akili, tuliza moyo wako, tayari hii
vita tumeshaishinda mezani!
“Vita huwa haipiganwi katika uwanja wa vita! Huwa inapiganwa
mezani kwa hiyo kushinda au kushindwa huwa kunaanzia mezani!
Sisi tumeshaishinda hii mezani,” alisema baba yake Saima kwa
busara za hali ya juu.
“Unatakiwa kurudi nyumbani, ukatumie saa hizi chache na
familia yako, saa kumi na moja na nusu unatakiwa uwe hapa!
Tuondoke!” alisema baba yake Saima huku akinishika mkono, kwa
kiasi fulani nikajihisi kuanza kupata nguvu.

602 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Kafunge ofisi yako, utanikuta ‘parking’ alisema baba yake


Saima, baba mkwe wangu na kiongozi wangu aliyenifanya nikawa
kama nilivyo baada ya kuniokoa kutoka kwenye mdomo wa mam-
ba.
Nilielekea ofisini kwangu huku nikiendelea kujikaza kuificha
ile hofu niliyokuwa nayo isionekane kwa nje. Nikaenda mpaka
ofisini kwangu, nikamkuta Jack akiwa amekaa kwenye kiti, akiwa
anasinzia.
“Itabidi ulale hapahapa ofisini kwa saa mbili tatu ili upunguze
uchovu! Mimi natoka mara moja, nitarejea alfajiri,” nilimwambia,
akanishukuru na kuinuka pale kwenye kiti, akaelekea kwenye viti
vilivyokuwa pembeni, nikamuona akijinyoosha na kuuchapa usin-
gizi.
Niliweka vitu vyangu vizuri kisha nikatoka na kuelekea mpaka
kwenye maegesho ya magari, nikamkuta baba yake Saima akiwa
ameegamia gari nililokuwa nalitumia, akanionesha ishara kwamba
nimpe funguo.
Nilifanya hivyo, akaingia na kukaa nyuma ya usukani, mimi
nikakaa pembeni yake, akawasha gari kisha tukatoka. Akawa
anaendelea kunipa maneno ya kuamsha morali ndani ya moyo
wangu, akaniendesha mpaka nyumbani kwangu, jambo ambalo
halikuwa kawaida yake hata kidogo.
“Niitie huyo mrembo wako nimsalimie,” alisema akimaanisha
mwanaye Saima baada ya kuwa tumeshafunguliwa geti na mlinzi
na kuingia mpaka ndani. Saima aliposikia tu geti linafunguliwa,
alaishtuka usingizini na kama kawaida yake, akatoka kuja kuni-

603 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

pokea, akishangaa kwa nini sijampa taarifa kwamba nitarudi.


“Imekuwa ghafla, nimekuja na mzee anataka akusalimu!” nilim-
wambia, Saima akashtuka kwa furaha, harakaharaka tukaongozana
mpaka pale kwenye gari, baba yake akafungua mlango na kuter-
emka, wakakumbatiana kwa furaha kwa sababu zilipita siku nyingi
bila kuonana zaidi ya kuwa wanawasiliana kwenye simu.
“Nitaondoka na gari lile, kaniletee funguo,” alisema baba yake
Saima akinioneshea gari letu dogo ambalo huwa tunalitumia kwa
safari za kifamilia. Nikatabasamu tu kwa sababu hata yeye alikuwa
anajua huwa haendeshi mtu mwingine yeyote gari hilo zaidi ya
mimi au Saima.
Nilielekea ndani na kuwaacha wakiwa wanazungumza na Saima,
sikutaka kuingilia mazungumzo yao, nikaingia mpaka chumbani
na kuchukua funguo, kabla sijatoka akili ikanituma nifungue diri-
sha na kuchungulia nje, kule nilikowaacha Saima na baba yake.
Nilimuona baba yake Saima akiwa anazungumza na binti yake
kwa misisitizo usio wa kawaida. Akawa anamuelekeza wakati
mwingine akitumia lugha za ishara ili kuonesha msisitizo, Saima
naye akawa anatingisha kichwa kwa adabu kuonesha kuelewa
somo alilokuwa anapewa.
Sikuweza kuelewa ni nini hasa alichokuwa anamwambia kwa
muda ule, ila akili zangu zikanituma kwamba lazima atakuwa
anamfundisha mwanaye namna ya kunisaidia ili nitulize akili.
Nilishusha pumzi ndefu, nikajikuta nikijisikia amani ndani ya
moyo wangu kwa sababu nilikuwa nimezungukwa na watu walio-
kuwa wananijali kisawasawa na kunipa umuhimu mkubwa sana.

604 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Nilitoka mpaka nje, nilipofungua tu mlango, baba yake Saima


akapunguza sauti na wote wakawa wananitazama. Nilijua tu
lazima Saima wangu atanieleza kila kitu baba yake akishaondoka.
“Hii hapa funguo baba!”
“Sawa, nashukuru!” alisema baba yake Saima, akamgeukia mwa-
naye na kumpa ishara fulani, nikamuona Saima akitingisha kichwa
kwa adabu. Harakaharaka akaelekea kwenye lile gari, akabonyeza
rimoti, taa za pembeni zikawaka na milango kujitoa ‘lock’, akain-
gia na kuliwasha.
“Mbaki salama!” alisema baada ya kutusogelea, akafungua kioo
na kutuaga kisha akasogea getini, mlinzi akamfungulia, akatoka na
kwenda zake, wote tukashusha pumzi ndefu. Hata sijui Saima ali-
kuwa amenisogelea muda gani, nilishtukia tu akiwa ameniegamia
begani.
“Pole na kazi mume wangu!”
“Ahsante sana mke wangu! Mnaendeleaje?”
“Hatujambo, tulikuwa tumeshalala nyie ndiyo mmeniamsha,”
alisema huku akifikicha macho yake kwa uchovu, nikamsogeza
na kumbusu kwenye paji la uso wake, naye akanibusu, nikapitisha
mkono kwenye kiuno chake na kumshika, nikamsogeza karibu
yangu na kumbana kifuani, tukawa tunatazamana.
Asikwambie mtu, kuoa, hasa kuona mwanamke mrembo unay-
empenda, huleta furaha kubwa mno ndani ya moyo! Ule uchovu
wote niliokuwa nao, ile hofu niliyokuwa nayo, vyote viliyeyuka
mithili ya donge la mafuta liyeyukavyo kwenye kikaango jikoni.
“Nilikumiss mume wangu! Nashukuru umerudi,” alisema huku

605 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

akipitisha mkono wake nyuma ya shingo yangu, tukagusanisha


ndimi na kugandana kama ruba. Tulishasahau kama tupo nje,
kelele za mlinzi akifunga geti ndiyo zilizotuzindua kutoka kwenye
dimbwi la hisia tamu za mapenzi.
Saima alinishika mkono, kisha akatangulia mbele kidogo hivi,
nadhani alifanya kusudi ili niione vyema hazina iliyokuwa ime-
fichwa nyuma yake, akawa ananikokota kuelekea ndani mithili ya
mbuzi anayepelekwa machinjioni.
Tuliingia mpaka ndani, akahakikisha amefunga vizuri milango,
akanipeleka mpaka chumbani, akanisaidia kuvua nguo zangu, na
yeye akavua zake, akanipeleka mpaka bafuni ambapo aliseti vizuri
maji na kupata uvuguvugu fulani mzuri sana.
Aliniogesha kama anavyomuogeshaga mtoto wetu, huku mara
kwa mara akinimwagia mvua za mabusu motomoto, alipomaliza
na mimi nilimuogesha vizuri, tukarudi kitandani huku kila mmoja
akionesha kuwa na ‘shauku’ kubwa na mwenzake.
Haukupita muda mrefu, tukawa tunaogelea kwenye bahari ya
kina kirefu cha huba, tukiifurahia tunu ya ndoa kikamilifu. Hata
sijui nilipitiwa na usingizi saa ngapi, nilikuja tu kushtuka na kuji-
kuta mwili wangu ukichuliwa taratibu kwa maji ya moto na mafuta
yenye manukato mazuri.
“Umeamkaje kipenzi changu,” alisema Saima na kuniinamia,
akanipiga busu zito, nikawa najihisi ni kama nipo ndotoni.
“Najua leo una kazi nzito sana! Najua kwamba hujapata muda
wa kupumzika kwa muda mrefu sasa ndiyo maana nimekufungia
kazi,” alisema Saima kwa sauti laini, tabasamu pana likiwa

606 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

limechanua kwenye uso wake.


“Ulilala saa ngapi na umeamka saa ngapi?”
“Wakati mnakuja mie nilikuwa nshalala sana tu, na hata uki-
ondoka nitapata muda wa kutosha wa kulala, kwa hiyo usiwe na
wasiwasi na mimi,” alisema Saima huku akiendelea kunichua tara-
tibu, mgusano wa mikono yake laini ukichanganya na yale mafuta
na maji ya uvuguvugu, vilinifanya nijihisi ni kama naimiliki dunia
nzima.
Alinigeuza na kuniweka alivyokuwa anaona yeye inafaa, kisha
akatoa mtandio laini aliokuwa amejifunga na kumfanya abaki
kama alivyo, akawa ananitazama kwa macho yake mazuri kama
anayetaka kuniambia jambo fulani hajui wapi pa kuanzia.
Hata sijui kulitokea nini, tulijikuta tu tayari tupo uwanjani tukili-
sakata kabumbu kwa mara nyingine. Baada ya hapo tulikokotana
mpaka bafuni, huko nikaogeshwa kwa mara nyingine na kusaf-
ishwa kila kona ya mwili wangu, huku tukipiga stori za hapa na
pale na kucheka kwa sauti za chinichini kwa sababu bado ilikuwa
ni mapema sana.
Baada ya kumaliza kuoga, tulirudi chumbani kwetu, Saima wan-
gu akawa ananiandaa mithili ya mama anavyomuandaa mwanaye
anayewahi alfajiri kwenda shule. Nilijikuta moyo wangu ukiwa na
furaha kubwa isiyo na kifani.
Baada ya kumaliza kuniandaa, tulienda sebuleni na kukaa kwa
ajili ya kupata kifungua kinywa ambacho hata sijui Saima wangu
alikuwa ameniandalia saa ngapi maskini ya Mungu! Ndani ya
zile saa chache tu alikuwa amefanya mambo mengi sana kwa ajili

607 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

yangu, tena kwa mahaba mazito ambayo yalinifanya niwe mtu


mpya kabisa.
“Baba ameniambia kwamba leo mna kazi nzito sana!”
“Ni kweli!”
“Na wewe ndiyo wanayekutegemea si ndiyo?”
“Ha... hapana!”
“Najua kila kitu,” alisema huku akitabasamu, ikabidi na mimi
nitabasamu kisha nikatingisha kichwa kumjibu kile alichokuwa
ameniuliza.
“Najisikia fahari sana kuwa na wewe Kenny! Tangu nikufahamu,
umenifanya kila siku inayopita kwenye maisha yangu, iwe bora
kuliko jana. Umenifanya kuwa mwanamke mwenye furaha sana,”
alisema, akaendelea kunipa maneno matamu kama asali, wakati
mwingine akinisaidia kunilisha na kunisindikiza kwa mabusu
motomoto.
“Nakutakia kazi njema, naamini utaishinda mitihani yote mbele
yako! Pale utakapojihisi kuishiwa nguvu au kupungukiwa ujasiri,
kumbuka kwamba familia yako inakupenda sana!
“Utakapohisi hofu ndani ya moyo wako ikumbuke tu sura yangu
utapata nguvu mpya! Si unaniambiaga mimi ni mrembo sana
kiasi kwamba sura yangu huwa inaishi ‘rent-free’ kwenye kichwa
chako?” alisema Saima na kunifanya nicheke sana.
Hayo ni baadhi ya maneno ambayo huwa nampamba na kum-
chombeza tukipata muda wa kupiga stori, na yeye akacheka kwa
furaha! Tayari nilikuwa nimeshamaliza kupata kifungua kinywa,
saa ya ukutani ikawa inasoma saa kumi na moja kasoro dakika

608 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kumi na tano alfajiri.


Alitoa vyombo, kisha akaja tena mwilini mwangu, akajilaza
kama mtoto anavyojilaza kwenye mikono ya mama yake, akawa
anaendelea kunipa maneno matamu kama asali ambayo yaliamsha
morali kubwa mno ndani ya moyo wangu!
Kama ni kazi, Saima alikuwa amefanya kazi kubwa mno ambayo
ilinifanya nijihisi kubaki na deni kubwa ndani ya moyo wangu,
deni ambalo malipo yake ilikuwa ni ushindi tu kwenye mtihani
uliokuwa mbele yetu.
Aliniaga kwa bashasha kubwa mno kiasi cha kunifanya hata nili-
poingia ndani ya gari na kuondoka kurudi ofisini, nibaki namfikiria
tu ndani ya kichwa changu huku tabasamu pana likiwa limetawala
kwenye uso wangu.
Waliosema utu uzima dawa walikuwa na akili sana! Utu uzima
wa baba yake Saima ulimfanya ajue kwamba kwa mud ule mfupi
uliokuwa umebakia tangu tulipomaliza kikao, ni kitu gani nilikuwa
nakihitaji ili kuishinda hofu iliyokuwa ndani ya moyo wangu na
kuamsha upya morali ndani ya moyo wangu na nadhani ndiyo
sababu iliyomfanya anirudishe mwenyewe nyumbani kisha kuzun-
gumza kwa msisitizo na mke wangu!
“Lazima tutashinda! Magogoni haiwezi kuanguka, leo ndiyo
watajua mimi ni nani! Nitawaonesha shoo wendawazimu hawa,”
nilijikuta nikijisemea ndani ya moyo wangu, huku nikiendesha gari
kwa kasi kuelekea ofisini. Morali niliyokuwa nayo, ilikuwa siyo ya
kawaida, nilipania kuliko kawaida kuhakikisha tunakwenda kuwa-
zidi akili, maarifa na nguvu maadui zetu.

609 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Niliwasili ofisini mapema, dakika ishirini kabla ya muda tulio-


kuwa tumekubaliana na baba yake Saima. Saa ilikuwa inaonesha
kwamba ni tayari saa kumi na moja na dakika kumi.
Nikapaki gari kwenye maegesho na harakaharaka nikatembea
kuelekea ofisini kwangu. Nilimkuta Jack akiwa amelala palepale
nilipomuacha, akiwa anakoroma. Nilimtazama kwa sekunde kad-
haa, nikajikuta namuonea huruma kwa sababu kasi ya kumkomaza
ilikuwa kubwa kwelikweli.
“Heey! Amkaaa,” nilisema huku nikimtingisha kwa nguvu Jack,
akakurupuka kutoka usingizini na kusimama kiukakamavu, ajabu
eti akanipigia saluti! Niliishia kucheka tu kwa sababu nilijua bado
ana ‘wenge’ la usingizi na hakuwa anaelewa anachokifanya.
“Dakika kumi uwe umeshaoga na kurudi hapa! Tuna kazi kub-
wa sana leo,” nilimwambia, akatoka kwa mwendo wa kwata na
kunifanya nizidi kucheka. Niliwasha vifaa vyangu vyote vya kazi,
nikaipitiapitia ‘diary’ kisha nikaanza kuchorachora, nikijaribu
kuangalia njia sahihi tunazoweza kuzitumia kukabiliana na tishio
kubwa lililokuwa mbele yetu.
Nikiwa naendelea kuchorachora pale kwenye diary yangu,
nilisikia mtu akiingoa ofisini kwangu, akili zangu nilijuwa kuwa ni
Jack anarudi kutoka kuoga lakini haikuwa hivyo, alikuwa ni baba
yake Saima.
“Unaendeleaje?” aliniuliza huku akiwa anajaribu kunisoma, ajue
nimeamkaje. Uchangamfu niliomuonesha, ulimfanya atabasamu,
nikasimama, tukawa tunatazamana huku nikijisikia aibu fulani
ndani ya moyo wangu kutokana na kile alichokuwa amemuagiza

610 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

mke wangu saa chache zilizopita.


“Bila shaka umekuja na nguvu mpya! Nakuona ukiwa na morali
kubwa!” alisema huku akinipa mkono wake, tukashikana kikaka-
mavu huku tukiendelea kutazamana kwenye macho, nikijitahidi
kuificha aibu niliyokuwa naihisi.
“Mkeo hajambo?” aliniuliza swali ambalo lilinifanya nipoteze
ujasiri wa kuendelea kumtazama machoni, nikaangua kicheko na
yeye akacheka sana mpaka tukagongesheana ngumi kama wana-
vyofanya vijana wakiwa wenyewe kwa wenyewe.
“Bado tuna dakika kama dakika kumi ana tano hivi, jiandae na
mimi nakwenda kuweka mambo sawa, saa kumi na moja na nusu
tunatakiwa kukutana kwenye chumba cha mikutano ya siri kwa
ajili ya kuanza utekelezaji wa mipango yetu,” alisema, akatoka na
kuniacha nikiwa bado nachekacheka mwenyewe.
Kilichokuwa kinaniganya nimpende sana mzee huyu, ni kwam-
ba alikuwa zaidi ya kila kitu kwangu! Alikuwa zaidi ya rafiki,
zaidi ya bosi, zaidi ya mzazi na zaidi ya baba mkwe! Nadhani
damu zetu zilikuwa zimetokea kuendana kwa sababu sikumbuki
kama nimewahi kumuona akiwa anacheka na mtu mwingine
yeyote zaidi yangu, mkurugenzi na familia yake.
Alipotoka tu, nilikumbuka kwamba nilimuamsha Jack peke
yake na sikuwa nimempa majukumu ya kwenda kuwaamsha na
wenzake wote kwa sababu niliamini bado wamelala kutokana na
uchovu wa jana yake.
Harakaharaka nikatoka na kuelekea kwenye ofisi yao, nikawa-
kuta baadhi wameshaamka na wanafanya mazoezi mepesi mlemle

611 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ndani ofisini, nikawapa maelekezo ya kwenda kuamshana wote na


kujiandaa kwa ajili ya kazi.
Wakati natoka, niligundua kwamba pia wakuu wa idara mbalim-
bali, wote walishaamka na kila mtu alikuwa na vijana wake
wakiendelea na mazoezi ya kuweka sawa viungo, kwa ajili ya kazi
nzito iliyokuwa mbele yetu.
Nilirudi ofisini na kukuta tayari Jack amesharejea, naye akawa
anafanya mazoezi mepesi mepesi, eti huku akiwa ananishangaa
nimefika saa ngapi? Nilijikuta nikicheka tena na kumsimulia vituko
alivyovifanya nilipomuamsha, naye akawa anacheka akiwa ni
kama haamini.
Kwa kuwa sasa alikuwa na akili zake timamu, nilimtaka anieleze
kama yeye ndiyo angekuwa kiongozi wa oparesheni ile, angefanya
nini na nini ili kuhakikisha kwamba mambo yote yanadhibitiwa na
shambulio halitokei.
Alinieleza kwa mtazamo wake, nikagundua kwamba alikuwa
na akili sana kwa sababu mengi kati ya aliyoyasema, tulishaya-
jadili kwenye kikao cha siri saa chache zilizopita. Nikamuuliza pia
kuhusu teknolojia, akanieleza kuhusu mambo sijui ya ‘signalling’
ambayo kimsingi mengi sikuwa nayajua kwa sababu yalikuwa
yakihitaji elimu kubwa na ubobezi kwenye masuala ya vifaa vya
kielektroniki.
Aliniambia kwamba kuna vifaa ambavyo kama vinaweza ku-
patikana na kufungwa kwenye maeneo muhimu ndani ya ‘zero
ground’, vinao uwezo wa kuzuia mabomu yanayotegemea mawim-
bi ili kulipuka, kwa maana yake ambayo yanategwa kisha mtu

612 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

anakuwa na rimoti mahali, akiibofya ndiyo yanalipuka.


Akawa amenikumbusha jambo moja la msingi sana ambalo hata
sijui kwa nini sikuwa nimelikumbuka mpaka wakati huo.
Ni suala ambalo pengine linaweza kuwa gumu kumfafanulia
akalielewa, lakini naamini baada ya ufafanuzi wa juujuu, kila mtu
anaweza kupata picha ya nilichokuwa nimekikumbuka kwa wakati
huo.
Katika misafara ya viongozi hususan marais wa nchi, huwa
kunakuwa na magari mengi lakini kuna moja huwa lipo tofauti
kidogo na mengine. Nazungumzia lile gari ambalo huwa na rangi
nyeusi mara nyingi, likiwa na vitu kama machumachuma, antenna
na madishi kwa upande wa juu.
Bila shaka utakuwa umeanza kunielewa. Basi gari hili kitaal-
amu huwa linaitwa linaitwa Convoy Protection Jammer ambalo
kazi yake kubwa huwa ni ulinzi wa kiongozi husika kwa kutumia
teknolojia.
Huwa na uwezo kudhibiti mawasiliano ya aina mbalimbali,
kuanzia mawimbi ya redio, mawimbi ya simu, mawimbi ya GPS
mpaka simu za satelite na kubwa zaidi, huwa linakuwa na uwezo
wa kuzuia mlipuko wowote wa kutumia rimoti usitokee kwa
kukata mawasiliano kati ya bomu au mlipuko husika na rimoti ya
kufyatulia.
Unaweza kuelewa sasa ni kwa kiasi gani Jack alikuwa ameni-
saidia kukumbuka jambo la msingi ambalo lingeweza kutusaidia
kwa kiasi kikubwa kwa sababu nilikuwa najua kwamba Magogoni
yapo magari mawili ya aina hii na yote yanafanya kazi.

613 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Ukiachana na hicho ulichokisema, ni nini kingine kinaweza


kufanyika?”
“Drone! Turushe drone ambazo zitakuwa zinapiga picha na ku-
rekodi kila kinachoendelea kwenye eneo lote la Magogoni.
“Kwa namna hii tunaweza kuzuia tatizo kabla halijatokea na
kulipatia ufumbuzi wa haraka lakini kubwa zaidi ni kuzima ma-
wasiliano yote ya simu kisha tukatengeneza chaneli moja tu am-
bayo simu zote zinazotumika na wanausalama ndiyo zitakapokuwa
zinapitia,” alisema Jack, muda huohuo ‘alarm’ ikapiga kwenye
simu yangu.
Alarm hiyo ilikuwa ikinikumbusha kwamba zilikuwa zimesalia
dakika tano kabla ya muda ambao tunatakiwa kukutana kwenye
chumba cha mikutano ya siri kwa ajili ya mipango ya mwisho
kabla ya kuanza kwa oparesheni hiyo.
“Endelea kutafakari kwa kina, nikirudi nitataka pia kusikia
mbinu nyingine unazodhani zinaweza kutusaidia,” nilimwambia
Jack huku nikiandika harakaharaka kuhusu yale mambo makubwa
mawili aliyokuwa ameniambia.
Nilichukua diary yangu na moja kwa moja nikaongoza kwenye
chumba cha mikutano ya siri. Viongozi wengi tayari walikuwa
wameshakaa kwenye viti vyao, kila mmoja akionesha kuwa mtu-
livu kabisa, akisubiri maelekezo mapya kama yalikuwepo.
Baba yake Saima na mkurugenzi ndiyo waliokuwa wa mwisho
kuingia, nadhani kuna jambo walikuwa wakijadiliana na bila ku-
poteza muda, ilipogonga saa kumi na moja na nusu juu ya alama,
kikao cha siri kilianza rasmi.

614 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Kubwa tulilokuwa tukijadiliana, ni namna ya kila mmoja kushiri-


ki kikamilifu kwenye oparesheni hiyo, ambayo kama nilivyoeleza,
mimi ndiyo nilikuwa kiongozi wake.
Tukaelezwa kwamba tayari eneo lote la Magogoni na mitaa yote
ya kuizunguka, ilikuwa imeshafungwa, kwa Kiingereza wanaita
‘cordon’, kwa maana mnazuia mtu yeyote asitoke wala kuingia
kwenye eneo hilo mpaka kuwe na sababu maalum.
Ilikuwa ni lazima hicho kifanyike, ili wasije kupata madhara
watu ambao hawahusiki, au maadui wasije wakapata muda wa
kujipenyeza mapema na kwenda kusababisha madhara.
Tulielezwa pia kuwa wafanyakazi wote wa kawaida pale Ma-
gogoni ambao kimsingi huwa ni wasaidizi wa namba moja kwe-
nye nyanja tofautitofauti, nao wote walikuwa wamechukuliwa na
kupelekwa mahali salama na kwamba kwenye kila eneo ambalo
mfanyakazi wa kawaida alitolewa, aliwekwa amtu wa kitengo ili
kuhakikisha tunaishika Magogoni yote mkononi.
Zilikuwa ni taarifa ambazo zilikuwa zinaniongezea morali kadiri
muda ulivyokuwa unaendelea, tukaelezwa pia kwamba ‘double’ wa
namba moja alikuwa akiendelea kufanya ‘rehersal’ ya jinsi shughu-
li ya usiku itakavyokuwa, jinsi atakavyokuwa akiwapokea wageni,
jinsi atakavyotoa hotuba na vitu vingine vingi.
Kimsingi mambo yote yalikuwa yamepangwa na yakapangika
kisawasawa, nikaelewa kwa nini baba yake Saima alikuwa anania-
mbia kwamba ile vita tulikuwa tayari tumeishinda mezani.
Tulielezwa pia kwamba tayari kuna wadunguaji nane wenye sifa
na uzoefu wa kimataifa, ambao walishajitegesha vyema kwenye

615 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

paa la Magogoni, katika maeneo yote muhimu, wakiwa tayari ku-


pokea maelekezo.
Uliwadia muda wa wajumbe wengine kuchangia mawazo yao
juu ya nini ambacho kinatakiwa kufanywa ili kuhakikisha hatuachi
upenyo wowote unaoweza kuwapa njia maadui zetu.
Mtu wa kwanza ambaye alitakiwa kuchangia mawazo, nilikuwa
ni mimi ambapo kwa kuwa tayari akili yangu ilikuwa imetulia, nili-
kuwa nawaza kwa kasi kubwa, kwa upana na kwa umakini wa hali
ya juu.
Nilisimama na kuwasalimu wajumbe wote kisha nikaeleza
kwamba mawazo yangu yatalenga maeneo kadhaa muhimu. Ni-
kaanza kwa kueleza kuhusu nini kinachotakiwa kuongezwa Ma-
gogoni ambayo sasa tulikuwa tumeibatiza jina la ‘ground zero’.
Nilipongeza kwa hatua zote ambazo zilikuwa zimefanyika mpaka
wakati huo, lakini nikaongeza mawazo kuhusu kurushwa kwa
‘drone’ ambazo zitakuwa na kazi ya kufanya doria kwenye anga
lote la Magogoni na maeneo ya kuzunguka, mpaka baharini.
Nilieleza pia kwamba tunatakiwa kuzima mawasiliano kama am-
bavyo Jack alikuwa amenishauri na badala yake, kuwe na ‘chaneli’
moja tu ya mawasiliano ambayo itakuwa inatumika na watu wote
waliopo kwenye oparesheni hiyo ili iwe rahisi kuwasiliana bila mtu
mwingine yeyote kujua kinachoendelea.
Nikaeleza pia kuhusu kutumika kwa magari maalum ya Convoy
Protection Jammer kwa ajili ya kukata mawasiliano yoyote ya
mawimbi kuanzia ya redio mpaka ya satelite.
Nadhani nimeshaeleza kuhusu magari haya na namna yanavyo-

616 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

fanya kazi, nikukumbushe tu kwamba ninapozungumzia Convoy


Protection Jammer, nazungumzia yale magari maalum yanayotu-
mika kulinda misafara ya viongozi wa juu katika mataifa mbalim-
bali, ambayo huwa na vifaa maalum vinavyoweza kuzuia vilipuzi
yakiwemo maomu ya kutegwa, yashindwe kulipuka kwa kuwa
linakuwa na teknolojia inayokata kabisa mawasiliano katika eneo
linapokuwepo mpaka mita kadhaa kuzunguka eneo hilo.
Nilipoeleza kuhusu suala hilo, nadhani nikawa nimemfumbua
macho kila mmoja, nadhani hakuna aliyekuwa amefikiria kwa
upana huo, nikiri kwamba hata mimi mwenyewe sikuwa nime-
fikiria mwanzo mpaka Jack aliponikumbusha kuhusu kutumia vifaa
maalum vya kukata mawasiliano ndiyo nikakumbuka.
Majadala uliibuka, wajumbe wakawa wanataka kujua kama kuli-
kuwa na magari ya aina hiyo mangapi na kama yalikuwa yakifanya
kazi kisawasawa, mkurugenzi akatoa ufafanuzi kwamba yapo
mawili na yote yanafanya kazi kisawasawa.
Baada ya kuwa tumemaliza hoja hiyo, niliibua suala lingine,
nikaeleza kwamba uzoefu unaonesha kwamba magaidi huwa wana-
penda kutumia mashambulizi ya anga pale wanapoona mipango
yao yote imebanwa na hawana njia ya kupenya.
Nikaeleza kwamba lazima vijana wetu wawepo kwenye mfumo
wa rada pale uwanja wa ndege, na maafisa wote wanaohusika na
usalama wa anga, wawekwe kwenye hali ya dharura ya kufuatilia
kwa karibu chombo chochote ambacho kitaonekana kikipaa kwe-
nye anga la katikati ya jiji mpaka Magogoni lakini pia jeshi la anga
likae ‘standby’ kwa ajili ya kuzuia shambulizi lolote kabla hali-

617 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

jatokea.
Hoja hiyo pia iliamsha gumzo lingine, nikawaona ‘washua’
wakiwa wanatingisha vichwa na kunipongeza kwa jinsi nilivyoku-
wa nawaza nje ya boksi, nadhani hakuna yeyote kati yao ambaye
alikuwa amewaza namna hiyo kama ambavyo mimi nilikuwa
nimewaza.
Mwisho nikaeleza kuhusu ile nyumba kule Masaki ambayo
taarifa za kiintelijensia zinaonesha kwamba ndipo wanapohifad-
hiwa mabinti ambao ni miongoni mwa watu waliopangwa kufanya
shambulio hilo, tena wakiwa na mafunzo ya kujilipua na kujitoa
muhanga, watu wote wakakaa na kutulia kutaka kusikilia nilikuwa
na mawazo gani.
Niliwaeleza kama ambavyo Jack alikuwa amenishauri kwamba
lazima maafisa ambao tayari walishakuwa eneo la tukio, waongez-
we maradufu kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila mtu anayetoka
kwenye jengo hilo, lakini pia kazi ya kudukua kamera za usalama
(CCTV) ambazo zipo kwenye majengo ya jirani na eneo hilo,
iendelee ili kuchunguza kwa makini ni nini ambacho kimekuwa
kikifanyika kwenye eneo hilo.
Nikaeleza pia kwamba magari yanayoingia au kutoka kwenye
jengo hilo, yatanasishwa vifaa maalum vya GPS ambavyo vimeun-
ganishwa na sumaku, ili kufuatilia nyendo zake, kuona huwa
yanakwenda wapi na wapi.
Nilihitimisha mchango wangu na kukaa, wajumbe wakanipigia
makofi, wengi wakionesha kufurahishwa na mchango wangu, ni-
kawa nimetulia huku nikiwa nimevaa sura ya kazi kwelikweli.

618 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Wengine waliendelea kuchangia mawazo yao lakini mambo


yote ya msingi yalikuwa yameshaangaziwa, na baada ya hapo kila
mmoja akakumbushwa majukumu yake na tukatakiwa kutawanyika
kuelekea kwenye maeneo yote ambayo kila mmoja amepangiwa
lakini pia kuripoti moja kwa moja kwangu.
Kwa kuwa mimi ndiye niliyechaguliwa kuongoza misheni hiyo,
nilikuwa na kazi kubwa pengine kuliko wote, ya kuhakikisha
mambo yote yaliyozungumzwa na kupangwa mezani, yanaenda
kutekelezwa kikamilifu ‘field.
Nilirudi ofisini kwangu, nikaweka kila kitu sawa kisha nikatoka
na kuelekea ‘dressing room’ ambako niliwakuta maafisa wengine
wa ngazi za juu nao wakiwa wanajiandaa, tayari kuelekea maeneo
wanayotakiwa kuyasimamia.
Nilivua nguo nilizotoka nazo nyumbani, nikavaa nguo za kazi,
nikahakikisha kila kitu kipo timamu, nikazikagua silaha zangu
tatu, bunduki kubwa ya mkononi na bastola mbili, niliporidhishwa
kwamba zote zilikuwa kwenye hali timamu, nilizichukua, bastola
mbili nikazichomeka kwenye mikanda yake, moja kushoto na ny-
ingine kulia na ‘chuma ya kazi’ nikaishika mkononi.
Mawasiliano yalikuwa yakiendelea kufanyika kupitia vifaa vya
mawasiliano na kila ambaye alikuwa amekamilisha kila kitu, ali-
kuwa akiripoti moja kwa moja, ndani ya kama dakika ishirini hivi,
timu ya maafisa kama arobaini hivi, ilikuwa tayari kwa kuondoka.
Miongoni mwao walikuwepo waliokuwa wanatakiwa kwenda
kuongeza nguvu Masaki, ambao hawa wengi walikuwa kwenye
mavazi ya kawaida, kulikuwa na timu inayotakiwa kwenda ‘ground

619 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

zero’ ambayo hii kila mmoja alikuwa amejikoki kisawasawa na


kulikuwa na timu inayotakiwa kwenda uwanja wa ndege.
Wengine walitakiwa kuwa kwenye doria za kawaida kwenye
maeneo mbalimbali ya mji, kufuatilia kila kitu kinachoweza kuleta
mashaka.
Mimi nilikuwa natakiwa kwanza kwenda Masaki na vijana
wangu wa Cyber na IT kwa ajili ya kuanza kazi sambamba na wale
wapambanaji wengine waliokuwa kwenye nguo za kawaida, kisha
baada ya hapo nilikuwa natakiwa kwenda ‘ground zero’ kuhakiki-
sha kama kila kilicozungumzwa, kilikuwa kinaenda kama kilivyo-
pangwa.
Jack alikuwa pembeni yangu, muda wote akionesha kuwa na
wasiwasi mkubwa mno kwenye moyo wake kwa sababu hiyo
ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza ya kufanya kazi za nje, akawa
ananiganda muda wote, nadhani aliamini yupo salama zaidi akiwa
pembeni yangu.
“Lazima ujifunze kusimama kwa miguu yako mwenyewe na
kujiamini, ishinde hofu ndani ya moyo wako,” nilimwambia Jack,
akanitazama kwa hofu kisha akameza funda la mate na kutingisha
kichwa kuonesha kunielewa.
Tuliendelea kutoka kwa makundimakundi, tukitumia magari ya
kiraia na baada ya kuhakikisha makundi yote yameshatoka, mimi
na vijana wangu wachache, akiwemo Jack, tukatoka.
Mimi ndiye niliyekaa nyuma ya usukani, nikawa naendesha gari
huku pembeni yangu akiwa amekaa Jack na vijana wengine waki-
wa wamekaa siti za nyuma, kila mmoja akiwa bize kwenye laptop

620 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

yake, kuhakikisha hakuna taarifa yoyote inayoweza kutupita.


“Kuna sehemu naona kama tumepasahau lakini panaweza kuwa
muhimu sana kutupa taarifa ya kila kinachoendelea.”
“Wapi?”
“Kule Kunduchi,” alisema Jack, akawa amenikumbusha jambo
la msingi sana ambalo hata sijui ilikuwaje wote hatukulizungumzia
kabisa katika vikao vyetu viwili vya siri.
“Unashaurije?”
“Tunaweza kugawana, kule nako wakawepo watu hata wawili
au watatu kuangalia kila kinachoendelea kutokea mbali,” alisema,
nikatingisha kichwa kuonesha kukubaliana na alichokuwa ame-
kisema.
Muda huohuo, nilibofya kitufe kwenye kifaa cha mawasiliano
nilichokuwa nimekivaa, nikazungumza kwa ‘code’ na baba yake
Saima ambaye muda huohuo alinijibu, akitaka niendelee kuzung-
umza nilichopanga kukisema.
Kwa kutumia lugha za kificho, nikamueleza kile nilichokuwa
nimekumbushwa na Jack, naye akashtuka na kubaki akijiuliza
tuliwezaje kusahau jambo la muhimu kama hilo. Muda huohuo,
alitoa maagizo kwa ‘surveilance team’, kikosi maalum cha wapele-
lezi kutoka kitengoni kupeleka maafisa wawili haraka iwezekana-
vyo, ambao watakuwa wanaripoti moja kwa moja kwangu kuhusu
kinachoendelea.
Kwa kuwa ni mimi na Jack pekee ndiyo tuliokuwa tunalijua eneo
husika, ilibidi Jack ndiyo afanye kazi ya kutafuta ‘coordinates’
kwa kutumia laptop yake. Neno coordinates lisikuchanganye, ni

621 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

lugha za kitaalamu katika masuala ya teknolojia ya mawasiliano


ambayo humaanisha ramani au uelekeo wa sehemu husika kwenye
mfumo wa latitudo na longitudo kutoka kwenye satellite.
Kama ulikuwa vizuri kwenye somo la Jiografia, basi hapa utaku-
wa umerudishwa darasani kidogo. Kwa kawaida ‘coordinates’
huwa katika mfumo wa namba na ili kuweza kuzisoma na kuziele-
wa, ilikuwa ni lazima uwe na ujuzi wa namna ya kuzisoma ambapo
ukizijulia, unaweza kufika mahali popote bila kupotea wala kuuliza
hata kama hujawahi kabisa kufika.
Ndani ya sekunde chache tu, tayari Jack alikuwa ameshazipata
‘coordinates’ za eneo husika, akanipa na mimi moja kwa moja
nikazituma kwa wahusika ambao walitakiwa kwenda eneo hilo,
nikawaeleza tahadhari ambazo wanapaswa kuzichukua ili wasije
wakaangukia kwenye mikono ya wale wendawazimu.
Ilibidi gari lingine liondoke pale ofisini kuelekea Kunduchi, na
sasa roho yangu ikawa imetulia. Tuliendelea kupasua mitaa, Jack
akiwa ndiye anayeniongoza kwa kutumia GPS kuelekea kule
Masaki kwenye lile jengo walikokuwa wanahifadhiwa wale wasi-
chana.
Haukupita muda mrefu tukawa tumeshakaribia kwenye mtaa
husika, ikabidi nilichomeke gari kwenye uchochoro ili tusije kuon-
ekana na kuharibu mipango yote, vijana wakaanza kazi ya kujaribu
kudukua kamera za CCTV zilizokuwa kwenye mtaa huo.
Mimi niliteremka na kuanza kuyasoma mazingira na kwa kuwa
bado ilikuwa mapema sana, isingekuwa rahisi kwa mtu yeyote
kunishtukia. Bunduki kubwa niliiacha ndani ya gari na kubaki na

622 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

bastola zangu mbili ambazo isingekuwa rahisi kwa mtu yeyote


kujua kama nina silaha.
Nilitokeza kwenye barabara iliyokuwa inapita nje ya jengo lile,
nikagundua kwamba kuna watu kadhaa waliokuwa wakikimbia
barabarani, wakiwa wanafanya mazoezi, ikabidi na mimi nivunge
kama nafanya mazoezi, nikawa nakimbia kwa mwendo wa tara-
tibu, huku nikiwa makini kuyasoma mazingira yale.
Nilipita nje ya jengo hilo, nikagundua kwamba mazingira yake
ungeweza kudhani ni nyumba ambayo haikaliwi na mtu kwa sa-
babu kwanza taa za nje hazikuwa zimewashwa kama zilivyokuwa
nyumba nyingine kwenye mtaa huo lakini pia, eneo lote la nje
halikuwa likifanyiwa usafi kiasi cha nyasi kuota kwa wingi kando
ya fensi.
Niliendelea kukimbia huku nikiwa makini kisawasawa, nika-
gundua pia kwamba ndani ya fensi, kulikuwa na maeneo ya uwazi
kila upande na nyumba ilikuwa katikati ya eneo ambalo kwa
hesabu za haraka, niligundua kwamba ni viwanja viwili vilivy-
ounganishwa.
Nilijaribu sana kutazama kwa ndani lakini sikuweza kuona cho-
chote kwa sababu pande zote kulikuwa na fensi ndefu za matofali
ambazo juu yake kulikuwa na nyaya za umeme, zile zinazotumika
kuzuia wezi au wahalifu wasiweze kupanda na kuingia.
Nilikimbia mpaka mwisho wa mtaa, nikagundua kwamba
upande wa pili wa jengo lile, kulikuwa na mgahawa mdogo
ambao ulikuwa ukitazamana na jengo hilo, nikajua hiyo inaweza
kuwa sehemu muhimu sana ya kupandikiza vijana wetu ili wawe

623 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wanasoma kila kinachoendelea.


“Za asubuhi bosi,” nilimsalimu kijana ambaye alikuwa kwenye
mgahawa huo, akiwa anahangaika kuandaa mazingira ya kufungua
biashara.
“Safi, karibu kaka!” aliitikia yule kijana kwa uchangamfu.
“Hapa mnauza nini?”
“Tunauza kuanzia chai, supu na maziwa freshi na vitafunwa kwa
asubuhi lakini mchana kuna vyakula pamoja na chipsi na jioni
pia,” alisema.
“Nini kipo tayari kwa muda huu?”
“Bado ndiyo kwanza tunafungua, labda kama utasubiri kidogo,
maziwa freshi yako jikoni,” alisema huku akiendelea kupangapan-
ga viti na kufanya usafi.
“Kuna vijana wangu wana njaa sana usiku hawakula, ngoja
nikawalete waje kusubiria hapahapa,” nilisema, akanijibu kwamba
haina shida kabisa. Ili kumjengea imani, nikatoa noti ya shilingi
elfu kumi na kumpa, wakati anapokea nikamuona akikitazama
kizibao cha kuzuia risasi nilichokuwa nimevaa.
“Nyie ni walinzi eeh!”
“Ndiyo, tunafanya kazi na kampuni inayolinda nyumba kadhaa
kwenye huu mtaa!”
“Sijawahi kukuona, walinzi wengi ni wateja wangu na wengine
usiku huwa wanakaa sana hapa mpaka tunapofunga.”
“Aah! Kampuni yetu ni mpya na ina kawaida ya kuhamisha
walinzi kila baada ya muda, kwa hiyo sisi ni wageni,” nilisema,
nikamuona akitingisha kichwa kuonesha kunielewa kwa nilichom-

624 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ueleza.
“Basi freshi kaka, karibuni sana muwe wateja wangu!”
“Haina shida kabisa,” nilisema huku nikiendelea na kukimbia
taratibu kurudi kule nilikokuwa nimetokea. Sikutaka kukatisha
kurudi pale nilipowaacha vijana wangu kwanza kwa kuogopa
kushtukiwa, nikakimbia mpaka mwisho wa mtaa upande wa pili,
nikapenye kwenye njia za ndani ya mtaa, nikazunguka na kutokea
pale nilipokuwa nimewaacha vijana wangu.
“Mnaendeleaje?”
“Tumeshafanikiwa kupata ‘access’ ya kamera nne mpaka sasa,
kazi inaendelea!”
“Safi, sasa kuna jambo nataka tujadiliane wote,” nilisema baada
ya kupokea majibu kutoka kwa Jack, wote wakaacha kazi yao na
kunisikiliza.
“Nimepita mtaa mzima, nimebaini kwamba kuna cafe moja ina-
tazama na lile jengo, ni sehemu nzuri ambazo wachache wanaweza
kujibanza na kujifanya wateja wakati mkiendelea kufuatilia kila
kinachoendelea. Mnaonaje?” nilisema, kila mmoja akaunga mkono
hoja niliyoitoa, lakini maswali yakawa ni kutaka kujua kama eneo
hilo linaweza kuwa salama?
“Unaulizia usalama kwenye uwanja wa vita? Usalama wako ni
umakini wako,” nilisema, wote wakakaa kimya. Niliwateua vijana
wawili kwa ajili ya kazi hiyo lakini nikawaeleza kwamba wata-
baki na Jack kwanza mpaka baadaye tutakaporudi kuja kuangalia
wamefikia wapi, Jack akakubali kwa moyo mkunjufu, wale vijana
wawili nao wakakubali.

625 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Ili kutozua taharuki, niliagiza wote wavue mavazi rasmi wali-


yokuwa wamevaa ili waonekane kuwa wa kawaida ikiwemo kuvua
vizibao vya kuzuia risasi kupenya kwa maana ya ‘bullet proof
vests’.
Ndani ya muda mfupi tu, tayari wote walikuwa wameshabadi-
lika, tukateremka kwenye gari ambapo niliwataka tutumie mbinu
ileile ya kujifanya tunafanya mazoezi, tukawa tunakimbia taratibu
mpaka kwenye ule mgahawa. Yule kijana niliyezungumza naye
akatupokea kwa uchangamfu na kutukaribisha ndani.
“Mimi nitarudi baadaye, utawahudumia bila haraka yoyote,”
nilisema huku nikitoa noti nyingine ya shilingi elfu kumi na kumk-
abidhi, akanishukuru sana na kuwaongoza akina Jack mpaka ndani.
Bila kupoteza muda, mimi nilirudi nikiwa nakimbia vilevile
mpaka kwenye gari, nikaingia na kuliwasha, vijana waliosalia bado
walikuwa bize na mambo yao, nikawasha gari na safari ya kuele-
kea ‘ground zero’ ikaanza.

626 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

23
K
ILA mtu alikuwa kimya kabisa ndani ya gari, kitu
pekee kilichokuwa kinasikika, ilikuwa ni ‘keyboard’
zikigongwagongwa na vidole vya vijana wangu kwa
kasi ya cherehani.
Nilipiga gia na baada ya dakika kadhaa, tukawa
tayari tumewasili ‘ground zero’, kama nilivyoeleza awali, jina
hilo lilikuwa ni la kificho kumaanisha Magogoni kwa wakati huo.
Kabla hatujafika eneo la tukio, nilikuwa makini kujaribu kuangalia
maeneo mengine muhimu yanayoizunguka Magogoni.
Jambo ambalo nililibaini ni kwamba oparesheni ile ilikuwa in-
aendeshwa kwa utaalamu wa hali ya juu kwa sababu wananchi wa
kawaida walikuwa wakiendelea na majukumu yao kama kawaida

627 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kwenye maeneo ya katikati ya jiji bila kujua ni nini kilichokuwa


kinatarajiwa kutokea.
Lakini pia, katika maeneo yote muhimu, nilibaini kwamba kuli-
kuwa na vijana wengi wa ‘kitengo’ wakiwa katika nguo za kiraia,
wakiwa wamejichanganya na wananchi wa kawaida, kuhakikisha
wananasa taarifa zote za kila kilichokuwa kinaendelea.
Maeneo ambayo yalikuwa na tofauti kidogo, ilikuwa ni maeneo
ya jirani na Magogoni ambayo yalikuwa kimya kabisa, barabara
zote za kuingia na kutoka, zilikuwa zimefungwa au kwa kitaalamu
‘cordoned’ kwamba hakukuwa na mtu yeyote anayeruhusiwa kuin-
gia au kutoka bila ruhusa maalum.
Hata hivyo, kufungwa kwake hakukumaanisha kwamba kuli-
kuwa na vizuizi vya barabarani vinavyoonekana kwa macho, la
hasha! Kulikuwa na maafisa wengi waliokuwa kwenye nguo za
kiraia, ambao ndiyo waliokuwa wakifanya kazi ya kuzuia mtu asi-
yehusika asiingie wala kutoka bila ridhaa na usingeweza kugundua
kama kuna chochote kilichokuwa kinaendelea.
Kwa kuwa sheria ilikuwa msumeno, hata gari letu lilipoonekana
kunyoosha kwenye barabara ya kuelekea kwenye geti kubwa la
Magogoni, tulisimamishwa, nikatii na kusimama na baada ya kujua
kama nilikuwa ni mimi na vijana wangu, ndipo tuliporuhusiwa ku-
ingia, lakini ni baada ya gari kukaguliwa ili kusije kuwa kuna kitu
cha hatari kimepandikizwa bila sisi kujua.
Tulifika getini, tukakaguliwa tena ndipo tuliporuhusiwa kuingia
ambapo ndani, vijana walikuwa ‘bize’ kwelikweli, wakishirikiana
na PSU, kikosi maalum cha ulinzi wa namba moja. Tulionyeshwa

628 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

sehemu ya kupaki gari, nikafuata maelekezo kisha nikalipaki gari


vizuri.
Harakaharaka niliteremka na kwenda kuripoti kwa wakuu wangu
wa kazi, nikapokelewa na baba yake Saima ambaye siku hiyo ali-
kuwa amevalia tofauti kabisa. Hakuwa amevaa suti kama kawaida
yake, bali alikuwa ndani ya kombati, chuma kizito kikiwa begani
kwake.
Ni yeye ndiye aliyeanza kunipa maelekezo ya nini ninachotakiwa
kufanya, mimi ndiye niliyekuwa kiongozi wa oparesheni lakini hilo
halikubadili ukweli kwamba ninao viongozi wangu wa juu, akiwe-
mo baba yake Saima na mkurugenzi ambao wote tayari walikuwa
eneo la tukio.
Nilianza kwa kumuelezea tulichokikuta kule Masaki, kisha na
yeye akanieleza kwa kifupi hatua zote ambazo zilikuwa zimechu-
kuliwa kwa muda ule ambao sikuwa nimefika, akanitambulisha
kwa kiongozi wa kikosi cha PSU, tukapeana mikono huku tuki-
tazamana machoni.
Ni kiongozi huyu wa PSU ndiye aliyekuwa anatakiwa kunizun-
gusha kwenye maeneo yote muhimu ya Magogoni, pamoja na
sehemu ambazo tulikuwa tumekubaliana kuwaweka vijana wetu.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, harakaharaka nilipelekwa mae-
neo yote muhimu, haikuwa mara yangu ya kwanza kuingia Ma-
gogoni lakini nikiri kwamba mambo mengi sikuwa nayajua mpaka
asubuhi hiyo, tukapitia maeneo yote ya ndani na nje na mwisho
nikapelekwa kwenda kuonana na ‘double’ wa namba moja ambaye
alikuwa akiendelea kufanyishwa mazoezi.

629 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Nikiri pia kwamba nilikuwa najua tu kw anadharia kuhusu ku-


wepo kwa ‘double’ wa namba moja lakini sikuwa nimewahi kumu-
ona kwa macho yangu, au pengine niliwahi kumuona lakini sikuwa
nimejua kwamba ndiye huyo ‘double’ mwenyewe kutokana na jinsi
alivyokuwa akifanana na namba moja.
Kwanza nilibaki nimepigwa na bumbuwazi baada ya yule ki-
ongozi wa PSU (Presidential Security Unit) kunitambulisha kwa
kunionesha kwa mbali kisha akaninong’oneza kwa sauti ya chini.
Alikuwa amefanana kwa kila kitu na namba moja kiasi cha
kunifanya nifikiche macho yangu, nikiwa najihisi kwamba pengine
naweza kuwa nipo ndotoni. Ili kujiridhisha kwamba hakuwa namba
moja halisi, nilitaka kuona namna ambavyo angenipokea ninapo-
enda kusalimiana naye.
Nilishawahi kuelewa kwamba baada ya kazi kubwa niliyoifanya
kipindi kile, namba moja aliagiza nipelekwe kwake tukazungumze
ana kwa ana na akanipa zawadi siku hiyo, kwa hiyo alikuwa akini-
fahamu vizuri na tulizungumza mengi.
Kitu pekee ambacho kingenifanya niwe na uhakika kama kweli
yule ni ‘double’ na siyo namba moja mwenyewe, ilikuwa ni jinsi
atakavyonipokea.
“Mheshimiwa Rais,” aliita kiongozi wa PSU kwa adabu, akaa-
cha kila alichokuwa anafanya, wale wasaidizi wake waliokuwa
wakiendelea kumuelekeza baadhi ya mambo, nao wakaacha kila
walichokuwa wanakifanya na kutugeukia.
“Ooh! Umefika?” alisema ‘double’ wa namba moja huku akiinu-
ka na kunisogelea, akanipa mkono huku akiwa ameachia tabasamu

630 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

pana, na mimi nikaachia tabasamu la uongo huku nikimtazama


machoni.
“Karibu sana!” alisema tukiwa tumeshikana mikono, na yeye
akawa ananitazama machoni. Nilikuwa na shauku kubwa ya
kusikia atasema nini baada ya salamu hiyo.
“Huyu ndiye atakayeongoza oparesheni yetu ya leo,” alisema
Mkuu wa PSU, nikawa bado namtazama ‘double’ machoni.
“Safi sana! Nikumbushe jina lako?” alisema, moja kwa moja
nikawa nimepata majibu. Hakuwa namba moja mwenyewe bali
‘double’ wake, nikashusha pumzi ndefu na kumtajia jina langu
kwa ukamilifu, akawa anatingisha tu kichwa.
“Basi nbi hilo tu mheshimiwa,” alisema yule kiongozi wa PSU
na kuinamisha kichwa kwa utii, na mimi nikafanya hivyo kisha
tukageuka na kuondoka, akaendelea na wasaidizi wake.
Nilibaki najiuliza maswali mengi sana ndani ya kichwa changu,
ama kwa hakika serikali inazo siri nyingi sana ambazo mtu wa
kawaida kamwe hawezi kuzijua hata kidogo.
Tuliendelea kuzungukia maeneo yote muhimu, nikawa natam-
bulishwa kwa maafisa wengi wa ikulu ambao nilikuwa nawajua
kwa majina tu, na wao wakawa na shauku kubwa ya kuonana na
mimi na kuona jinsi ninavyofanya kazi, nadhani walikuwa wame-
shasikia sifa zangu.
Jambo ambalo wengi walikuwa wakishindwa kujizuia kulione-
sha, ni mshangao wa jinsi umri na mwonekano wangu ulivyokuwa
na majukumu niliyokuwa nimewahi kuyafanya siku za nyuma
pamoja na ambayo yalikuwa yakiendelea.

631 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Jambo ambalo pia watu wanapaswa kuwa nalo makini, ni kuhusu


mwonekano wa mtu! Mara nyingi watu huwa wanaamini kwamba
kazi kubwa, nyeti na za kutumia akili, hufanywa na watu wenye
miili mikubwa, yaani mtu akisikia jasusi wa kimataifa pengine
anajenga taswira kichwani mwake kwamba ni bonge la jitu wakati
uhalisia unakuwa ni tofauti kabisa.
Mwonekano wangu kama ambavyo nimekuwa nikijieleza mara
kwa mara, ulikuwa wa kijana mbichi, kijana wa kawaida kabisa
ambaye pengine unaweza kupishana naye barabarani na usigeuke
mara mbili kumtazama wala usihisi chochote.
Pengine kitu ambacho kingeweza kukushtua katika mwonekano
wangu wa nje, ni jinsi ambavyo mwili wangu ulikuwa umejen-
geka vizuri kimazoezi pamoja na ukakamavu niliokuwa nao. Sifa
nyingine zote ambazo nilikuwa nazo, zilikuwa hazionekani kwa
urahisi kwa nje.
Baada ya kama dakika arobaini hivi, nilikuwa tayari nimesha-
tembezwa kwenye maeneo yote muhimu na sasa niseme kwamba
Magogoni ilikuwa kwenye mikono yangu, nilikuwa naijua vizuri
pamoja na vichochoro vyake vyote.
Nikarudi kule nje ambako vikosi vilikuwa vikiendelea kujipanga,
kwa kufuata maelekezo kama ambavyo tulikuwa tumekubaliana,
nikawa naongoza mawasiliano ya nani akae wapi na kama kuna
marekebisho ya aina yoyote. Nilihakikisha nawasiliana moja kwa
moja kwa kupitia kifaa cha mawasiliano na watu wote muhimu,
wakiwemo vijana wetu ambao walikuwa wamejipanga kisawasawa
kuhakikisha tunatetea heshima yetu.

632 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Muda ukawa unazidi kusonga mbele, huku ‘pressure’ ikizidi ku-


ongezeka kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele.
Mara kwa mara nilikuwa nikiwasiliana na vijana wangu, kuanzia
wale niliowaacha Masaki wakiongozwa na Jack, wale waliokuwa
wameenda Kunduchi, wale waliokuwa wameweka kambi katikati
ya mji na kujichanganya na raia mpaka wale waliokuwa juu ya paa
la Magogoni, wakiwa wameshajipanga kwa kazi moja tu iliyokuwa
mbele yao.
Nilikuwa pia nikiwasiliana na wenzetu waliokuwa Uwanja wa
Ndege kwenye rada, pamoja na viongozi wangu wote. Kimsingi,
nilionekana kuwa bize kuliko mtu mwingine yeyote, muda wote
nikawa na kazi ya kutoa maelekezo.
Jack na wenzake waliokuwa kule Masaki, nje ya lile jengo
walilokuwa wakihifadiwa wale wasichana, ndiyo niliokuwa
nawatazama kwa karibu zaidi na uzuri ni kwamba miongoni mwao
alikuwepo Jack, ambaye naye kichwa chake kilikuwa kikifanya
kazi kwa haraka kuliko kawaida.
Ndani ya muda mfupi tu, walikuwa wamefanikiwa kukusanya
taarfa nyingi kutoka kwenye vyanzo vikuu viwili, kwanza kutoka
kwenye zile kamera za CCTV walizozidukua, lakini pili kutoka
kwa yule kijana aliyekuwa akifanya kazi kwenye ule mgahawa
pamoja na wafanyakazi wenzake.
Taarifa za uhakika, zilikuwa zinaonesha kwamba, kulikuwa na
wasichana wapatao ishirini na tano waliokuwa wakiishi ndani ya
jengo lile, karibu wote wakiwa na umri wa rika moja, isipokuwa
wanawake wawili ambao walikuwa watu wazima na ilionesha

633 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kama ndiyo waliokuwa wakiwasimamia.


Kila siku, walikuwa wakija kuchukuliwa na magari kuanzia saa
moja jioni, saa mbili mpaka saa tatu na walikuwa wakirudishwa
usiku mwingi, wakati mwingine wote kwa pamoja, wakati mwing-
ine kwa makundi makundi.
Majirani waliokuwa wakiishi eneo hilo, walitengenezwa kua-
mini kwamba, wasichana wale walikuwa ni wanafunzi wa Chuo
cha Kodi na pale ilikuwa ni hosteli yao. Hata hivyo, kwa mujibu
wa wale wafanyakazi wa ule mgahawa, wasichana hao walikuwa
wakiishi maisha tofauti kabisa na wanachuo wa kawaida.
Kwanza ilikuwa ni marufuku kwa wao kutoka nje bila ruhusa,
kulikuwa na walinzi wenye silaha ambao walikuwa wakikaa ndani
ya geti, hawakuwa wakiruhusiwa kujichanganya mitaani kama
wanafunzi wengine wa vyuo wanavyofanya.
Vyakula walivyokuwa wanakula, vilikuwa vikiletwa vikiwa
vimeshapikwa, kuanzia asubuhi, mchana na jioni, hawakuwa
wakipika wenyewe wala hawakuwa wakishinda kwenye vibanda
vya chipsi na mihogo kama wanavyuo wengine.
Lakini kubwa zaidi, kila walipokuwa wakitoka au kuingia ndani
ya nyumba hiyo, walikuwa wakivaa mavazi maalum yaliyokuwa
yakiziziba nyuso zao, kama wanavyovaa wanawake wa Kiarabu au
Mashariki ya mbali, kwa hiyo hakuna ambaye alikuwa akifahamika
mtaani hapo kwa maana ya mwonekano wa sura.
Kupitia CCTV kamera, tulifanikiwa kupata namba za usajili za
magari yaliyokuwa yakitumika kuwachukua na kuwarudisha wasi-
chana hao, tukafanikiwa kuwajua wamiliki wake na kazi ya kuwa-

634 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

fuatilia, mmoja baada ya mwingine, ikawa inaendelea kimyakimya.


Namba na aina za magar hayo, zilitangazwa kwa maafisa wote
waliokuwa doria kwamba popote yatakapoonekana, yanatakiwa
kusimamishwa na kukaguliwa kwa kina.
Ilipofika majira ya saa tano za asubuhi, ilibidi Jack na wenzake
waende kuchukuliwa kutoka pale walipokuwa, Masaki na kuletwa
‘ground zero’ kuongeza nguvu lakini niliwasiliana na Jack na kum-
taka ahakikishe kablas hajaondoka, ajenge urafiki na yule kijana
aliyewapokea asubuhi na ampe kazi ya kumjulisha muda ambao
wale wasichana wataenda kuchukuliwa kwa sababu hakukuwa na
uwezekano wowote wa wao kutoka asubuhi au mchana, ilikuwa ni
mpaka giza liingie.
Hilo lilifanyika, Jack na wenzake wakaenda kuchukuliwa na wa-
kaja kuongeza nguvu Ground Zero ambapo walipofika tu, nilitaka
kwanza kuzungumza na Jack faragha.
Nikamhoji kwa kina kuhusu kila kitu ambacho nilihisi kinaweza
kuwa na msaada kwetu, na nikamtaka kuhakikisha zile video zote
walizozidukua kutoka kwenye zile CCTV camera za mtaani, zina-
hifadhiwa vizuri kwa ajili ya ushahidi.
Baada ya hapo, nilimtaka Jack akaungane na maafisa wa pale, ka-
tika kufuatilia kamera za usalama zilizokuwa zimefungwa kuanzia
katikati ya mji katika barabara zote zilizokuwa zinaelekea ‘ground
zero’.
Kwa upande wa vijana ambao walikuwa wameelekea Kunduchi,
wao pia hawakubaini kitu chochote kisicho cha kawaida, eneo lote
lilikuwa limetulia kabisa na hakukuwa na shughuli zozote zilizo-

635 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kuwa zikiendelea.
Tofauti na akina Jack, hawa walitakiwa kuendelea kubaki eneo
hilo kutwa nzima. Shughuli za hapa na pale zikawa zinaendelea
ndani ya eneo la Magogoni, kuhakikisha hakuna chochote kibaya
kinachotokea usiku huo.
Baadhi ya watumishi wa Magogoni, walitakiwa kuendelea na
shughuli zao kama kawaida ili kutomshtua mtu yeyote kuhusu kili-
chokuwa kinaendelea, wakatakiwa kuhakikisha kwamba maandal-
izi yote ya dhifa maalum kati ya namba moja na wafanyabiashara
wakubwa, yanakamilika kwa wakati.
Majira ya saa saba za mchana, maandalizi ya mkutano huo,
yalianza kufanyika na ili kuzidi kuwapumbaza zaidi maadui zetu,
taarifa za kufanyika kwa dhifa hiyo, zilitangazwa kwenye vyombo
mbalimbali vya habari, kuonesha kwamba namba moja atakutana
na kufanya mazungumzo na wafanyabiashara wakubwa nchini.
Taarifa kwenye vyombo vya habari, zilieleza kwamba lengo la
mkutano huo, ni kuangalia namna ya kujenga ushirikiano imara
utakaowezesha taifa kupiga hatua kimaendeleo na wafanyabiashara
hao nao kupata mafanikio makubwa.
Kwa kuwa ilikuwa ni ‘mpango mkakati’, taarifa hiyo pia ilisam-
bazwa kwenye mitandao ya kijamii, gumzo likawa kubwa kuhusu
mkutano huo. Muda ulizidi kusonga mbele, maandalizi ya mkutano
nayo yakazidi kupamba moto.
Kama nilivyoeleza awali, kadiri muda ulivyokuwa unazidi ku-
songa mbele, ndivyo ‘presha’ ilivyokuwa inazidi kupanda ndani ya
mioyo yetu. Haikuwa kwangu peke yangu, nilimuona pia mkuru-

636 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

genzi wetu naye akiwa hana utulivu kabisa.


Mtu ambaye alionekana kuwa na utulivu wa kutosha, alikuwa ni
baba yake Saima pekee, yeye muda wote alikuwa ‘bize’ kuhakiki-
sha kila kitu kinakwenda sawa. Saa nane mchana, saa tisa, hati-
maye ikagonga saa kumi za jioni, habari mpya zikaingia.
Zilikuwa ni habari kutoka kwa yule kijana wa kule mgahawani,
Masaki ambaye alimpigia simu Jack na kumueleza kwamba, kuna
magari matatu, aina ya Coaster yalikuwa yamewasili eneo lile
kwenda kuwachukua wale wasichana.
Taarifa hiyo ilieleza pia kwamba, tofauti na siku zote ambazo
huwa wanatoka wakiwa wamevalia mavazi ya kuziba nyuso zao,
siku hiyo walikuwa wamevalia sare nadhifu ingawa wote wali-
kuwa wamevaa barakoa na miwani ya rangi nyeusi, hivyo kufanya
iwe vigumu kuwatambua.
Harakaharaka tulipeana taarifa, namba za magari zikawekwa
hadharani na vijana waliokuwa mitaani kwenye doria, wakaanza
kuyatafuta. Wakati hayo yakiendelea, baada ya kama dakika
ishirini hivi, zilikuja taarifa nyingine kutokea Kunduchi ambapo
vijana wetu waliripoti kwamba kuna magari matatu aina ya Coast-
er, yameonekana yakiingia katika eneo hilo.
Tulipojaribu kuuatilia kwa karibu, tulibaini kwamba namba za
usajili zilikuwa ni zilezile, kwa hiyo tukawa na uhakika kwamba
wasichana wale wamechukuliwa kutoka kwenye makazi yao na
kupelekwa kwenye kambi ya mafunzo, macho na masikio yakaele-
kezwa Kunduchi kutaka kujua ni nini kilichokuwa kinaendelea, na
ipi ilikuwa hatua yao iliyokuwa inafuatia.

637 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Ilibidi tukubaliane kwamba timu iongezwe Kunduchi na wakati


tukiwa tunajipanga, zilikuja taarifa nyingine ambazo sasa ziliya-
fanya mapigo ya moyo ya kila mmoja, kuanza kwenda mbio.
Zilikuwa ni taarifa za boti zilizokuwa zinaingia na kutoka pale
kwenye kambi ile upande wa baharini, ikionesha ni kama zilikuwa
zinabeba aina fulani ya mzigo kuuingiza kwenye ile kambi kutokea
kusikojulikana. Taarifa za kiintelijensia zikaonesha kwamba kili-
chokuwa kinaingizwa kwenye eneo lile, zilikuwa ni silaha, tena za
kivita.
Taharuki iliyotokea ilikuwa haielezeki, kila mtu alichanganyiki-
wa kuliko kawaida, tukiwa hatujui ni nini kinachotakiwa kufanyika
kwa wakati huo.
“Hapa njia nyepesi ni kulizingira eneo lote, kuanzia nchi kavu
mpaka baharini kuhakikisha silaha hazitoki.”
“Hilo sidhani kama ni wazo sahihi, kama tukiwazuia wanaweza
kubadili mbinu.”
“Hoja hupingwa kwa hoja, usiishie tu kupinga wazo la mwen-
zako bila kutoa wazo lako!” mkurugenzi na Chief Mwaipopo
walikuwa wakivutana kwa hoja. Mkurugenzi alikuwa anataka
tukalizingire eneo lote la ile kambi ili wasije kufanikiwa kuziingiza
zile silaha mitaani lakini Chief Mwaipopo akawa anaona hiyo siyo
njia sahihi.
“Hapa kinachotakiwa, ni kuendelea kuwapumbaza kwamba hatu-
jui chochote wanachokifanya, kisha tuendelee kuwafuatilia kwa
karibu, tuhakikishe tunajua silaha zote zikitolewa hapo zinapele-
kwa wapi, tunatakiwa kuwa hatua moja mbele yao,” alisema Chief

638 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Mwaipopo, mvutano ukazidi kuwa mkubwa.


“Unawezaje kuruhusu silaha za kivita ziingie mitaani, tena
kwenye mikono ya watu wenye mafunzo ya namna ya kuzitumia
kisawasawa, huoni tutakuwa ni kama tunacheza na moto?”
“Tunao uwezo mkubwa kuliko wao, tunayo timu ya wataalam
wa kutumia silaha kuliko wao na kubwa zaidi, tunazo silaha za
kisasa zaidi kuliko wao, tunaweza kuwamudu kwa namna yoyote
ile,” alisema Chief Mwaipopo, mimi nikawa hata sijui nisimamie
upande gani.
“Unachokisema mkurugenzi ni sahihi na uko sawa zaidi lakini
pia tunatakiwa kufikiria kwa kina kwamba endapo tukifanya kama
anavyoshauri Mwaipopo nini kitatokea? Ni kweli tunao uwezo wa
kuwadhibiti wendawazimu hawa pamoja na silaha zao?” aliingilia
kati baba yake Saima.
Nilichokuwa nimekielewa, ni kwamba alikuwa ameona wazo la
Chief Mwaipopo kuwa bora zaidi ingawa hakutaka kumfanya mku-
rugenzi ajisikie vibaya kwa wazo lake kukataliwa.
“Au kiongozi wa oparesheni wewe unasemaje?” aliniuliza mimi,
bila kumung’unya maneno nikakazia palepale kwamba kama suala
ingekuwa ni kuwadhibiti, tungeshawadhibiti kuanzia mwanzo
wasifanye chochote lakini lengo letu lilikuwa ni kuwaingiza kwe-
nye mtego kisha tuwafyatue dakika chache kabla hawajatekeleza
walichokuwa wanakipanga.
“Ukitaka kuukata mti na kuumaliza kabisa, haushii kukata ma-
tawi pekee, lazima tung’oe mizizi yote,” nilisema na kuendelea
kufafanua nilichokuwa nimemaanisha, wazo la Chief Mwaipopo

639 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

likaonekana kufaa zaidi.


Hata hivyo, ili kufanikisha kile kilichokuwa kimeshauriwa,
ilitakiwa tuongeze kikosi cha wataalam wengi zaidi kwa ajili ya
kufuatilia nyendo za wendawazimu wale, hatua kwa hatua mpaka
tufanikishe kuwajaza kwenye ‘kumi na nane’ zetu.
Harakaharaka taarifa zilisambaa kwa watu wote waliokuwa kwe-
nye oparesheni ile, kikosi cha vijana wengine thelathini, kikaan-
daliwa haraka kikiwa na mchanganyiko wa vijana kutoka kiten-
goni, askari kutoka jeshini, polisi wachache na askari maalum wa
kitengo cha ‘Navy’, kwa lugha nyepesi hawa ni askari wa majini.
Kikaelekea Kunduchi na kujipanga kwa namna ambayo mtu
yeyote hawezi kugundua kilichokuwa kinaendelea. Vijana wali-
pangwa katika maeneo yote muhimu ili kufuatilia ni nini hasa
kilichokuwa kinaendelea na kila mmoja akatakiwa kuwa macho
kisawasawa.
Wapo ambao walipangwa kwenda kukaa baharini, mbali kidogo
kutoka kwenye kambi ile ili kuendelea kufuatilia jinsi silaha
zilivyokuwa zinaingizwa, lakini pia wapo waliopangwa kujipanga
kwenye barabara kuanzia Kunduchi mpaka kwenye Barabara ya
Bagamoyo ili kufuatilia mzigo ukitoka Kunduchi utapelekwa wapi.
Lakini pia, walikuwepo askari ambao walitakiwa kuvaa nguo za
askari wa kuongoza magari barabarani, ambao hawa sasa ndiyo
wangekuwa na kazi ya kutupa taarifa za karibu kabisa kuhusu kita-
kachokuwa kinaendelea barabarani kwa sababu tulikuwa na uhaki-
ka kwamba lazima zingesafirishwa kwa njia ya barabara kuelekea
eneo lililopangwa.

640 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Ndani ya muda mfupi tu, tayari vijana walikuwa wameshafika


kwenye maeneo waliyopangwa, tukahakikisha kila mmoja anaele-
wa vizuri majukumu yake, angalau sasa tukashusha pumzi ndefu
kusubiri kuona ni nini ambacho kingetokea.
Ni katika kipindi hichohicho, ndipo nilipopokea simu kutoka kwa
Ustaadh Fundi, yule msiri wetu kutoka Kibiti ambaye alitusaidia
sana kumtia nguvuni Mutesigwa na Abdulwaheed.
Nilishasahau kama tulikuwa na miadi naye ya kuja mjini kuonana
na mimi ili tujadiliane kwa kina kuhusu taarifa zilizokuwa zime-
tolewa na binti yake. Nilipoona simu yake ndiyo nikakumbuka.
“Unaendeleaje kijana wangu!”
“Sijambo mzee, sijui wewe!”
“Sijambo, nimefika mjini, nimeenda nje ya makubaliano yetu
kwa sababu kuna taarifa mpya na nyeti nilikuwa nazifuatilia,”
alisema, nikamuuliza yuko wapi? Akaniambia ndiyo ameteremka
kwenye gari maeneo ya Mbagala Rangi Tatu.
“Ni taarifa gani mpya ulizonazo?”
“Hatuwezi kuzungumza kwenye simu, ni nyeti na zinatakiwa
kufanyiwa kazi harakaiwezekanavyo,” alisema, nikatazama saa
yangu. Kitu pekee ambacho niliona kinaweza kusaidia kunikutani-
sha naye haraka iwezekanavyo, ilikuwa ni kumuelekeza kwmaba
achukue bodaboda kisha anipe nizungumze naye.
Kweli alifanya hivyo na muda mfupi baadaye, nikawa nazung-
umza kwenye simu na kijana aliyejitambulisha kwamba ni dereva
bodaboda anayepaki Mbagala Rangi Tatu.
“Unakujua Magogoni?”

641 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Ndiyo, si huko Feri?”


“Ndiyo! Sasa mlete huyo mzee haraka iwezekanavyo. Hakikisha
amevaa helmet na wewe pia umevaa kisha kimbia kwa kadiri ya
uwezo wako wote. Zingatia usalama wenu, kadiri utakavyofika
mapema ndivyo niakavyokulipa fedha nyingi zaidi,” nilimwambia,
tukawa tumekubaliana, nikakata simu.
Nilibaki kuwa na shauku kubwa sana ndani ya moyo wangu kwa
sababu kwa jinsi nilivyokuwa namjua Ustaadh Fundi, lazima ali-
kuwa na taarifa za muhimu sana.
Baada ya kukata simu, niliendelea kusimamia mambo mengine
yote kuhakikisha yanakwenda kama yalivyokuwa yamepangwa.
Hayo yakiwa yanaendelea, nilipokea taarifa nyingine kutoka kwa
kiongozi wa PSU ambaye alinitaarifu kwamba maandalizi ya hafla
ya usiku huo kati ya wafanyabiashara na namba moja, yanaenda
vizuri kwa asilimia kubwa lakini kuna jambo bado halijakamilika.
“Jambo gani?”
“Wahusika wanaotakiwa kuja kuwahudumia wageni waalikwa
vyakula na vinywaji pamoja na waliokuwa wanatakiwa kuupamba
ukumbi itakapofanyika hafla hiyo, bado hawajafika mpaka muda
huu,” alisema, kengele ya hatari ikalia ndani ya kichwa changu,
ingawa sikutaka kuonesha waziwazi hali hiyo.
Nilitazama saa yangu ya mkononi, kisha nikamgeukia na kumuu-
liza kwamba makubaliano yalikuwaje?
“Walitakiwa wawe wamefika kuanzia saa tisa alasiri,” alisema,
nikamwambia tunatakiwa kuendelea kusubiri, ikifika saa kumi na
mbili jioni, ndipo tunapoweza kuamua nini cha kufanya, akakubali-

642 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ana na wazo langu.


Alipoondoka tu, nilimpigia simu baba yake Saima na kumweleza
nilichokuwa nakihisi, naye akawa ni kama amezinduka kutoka
kwenye lindi la usingizi, ila akaniambia sitakiwi kumweleza
yeyote kwanza kuhusu nilichokuwa nakihisi.
Nilimaliza kuzungumza naye, nikawa najaribu kuunganisha ma-
tukio ili kupata picha kubwa zaidi iliyokuwa mbele yetu.
Nikiwa naendelea kutafakari, simu ya Ustaadh Fundi iliita,, ni-
katazama saa yangu kabla ya kuipokea. Zilikuwa zimepita dakika
ishirini tangu nilipozungumza naye, harakaharaka nikaipokea.
Akaniambia tayari wameshafika na walikuwa wamesimama mita
chache kutoka Feri, nikapigwa na butwaa nikiwa ni kama siamini!
Imewezekanaje kufika ndani ya muda mfupi kiasi hicho?
Nikamuelekeza wanisubiri hapohapo, nikawaaga viongozi wangu
na kuingia ndani ya gari, nikaruhusiwa kutoka na kuingia baraba-
rani kwenda kuonana na Ustaadh Fundi huku mapigo ya moyo
wangu yakiwa yananienda mbio kuliko kawaida.
Sikuwa najua ni wapi hasa walipokuwa wamepaki, ikabidi nitoe
simu na kujaribu kuipiga namba ya Ustaadh Fundi, harakaharaka
akaipokea, nikamuuliza kuhusu mahali walipokuwa wamesimama
lakini kwa kuwa yeye hakuwa mzoefu sana wa mitaa ya Dar es
Salaam, ilibidi ampe dereva wa bodaboda aliyemleta.
Akanielekeza na kwa bahati nzuri, walikuwa jirani kabisa na pale
nilipokuwa nimefika, ikabidi nilitoe gari barabarani na kusimama
pembeni, nikamuelekeza jinsi gari lilivyokuwa na kwa uhakika
zaidi, nikawasha taa za mbele na kuzizima, akaniambia ame-

643 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

shaliona niwasubiri.
Dakika mbili tu baadaye, tayari walikuwa wamepaki nyuma ya
gari langu, Ustaadh Fundi akateremka kama nilivyomuelekeza na
kuja mpaka kwenye mlango wa dereva, nikashusha kioo na kumpa
ishara kwamba azunguke upande wa pili na kuingia kwenye gari.
Alifanya hivyo, akaingia kwenye gari huku akiwa anahema kwa
kasi mithili ya mtu aliyetoka kukimbia mbio za mita mia moja.
Tulisalimiana kisha nikafungua ‘dashboard’ ya gari, nikatoa
kibunda na kuhesabu noti kadhaa za shilingi elfu kumikumi kwa
lengo la kumlipa dereva. Ajabu ni kwamba Ustaadh Fundi aliniam-
bia ameshamalizana naye, nikataka nimrudishie fedha zake lakini
pia akagoma.
Nilishusha pumzi ndefu na kutazama kwenye ‘side mirror’, nika-
muona yule dereva bodaboda akiondoka zake, kuonesha kwamba
ni kweli alikuwa ameshalipwa chake na Ustaadh Fundi.
“Kwa nini umekataa nisimlipe bodaboda na hutaki nikurudishie
fedha zako?”
“Achana na hayo, hebu tuzungumze mambo ya maana!” alisema
na kunifanya nitabasamu kwa sababu aliyazungumza hayo kwa
lugha ya kimasihara ingawa uso wake haukuwa ukionesha masi-
hara hata kidogo.
“Naomba tuongozane tutaenda kuzungumza vizuri huko tunak-
okwenda!”
“Ni wapi? Sitaki kuonekana kwa namna yoyote ile,” alisema, ni-
kamwambia asiwe na wasiwasi, nikawasha gari na kuingia baraba-
rani, nikazunguka na kuanza kurudi Magogoni.

644 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Wakati nikiendelea kupiga gia, nikazungumza kwenye vifaa vya


mawasiliano kuwataarifu viongozi wangu kwamba nilikuwa na
mtoa taarifa wa muhimu kwa hiyo naomba idhini ya kuingia naye
Magogoni, mkurugenzi akanijibu muda huohuo na kunipa ruhusa
ingawa alinitaka kuzingatia taratibu zote za kiusalama.
Dakika chache baadaye, tayari tulikuwa kwenye geti la Ma-
gogoni, gari likakaguliwa tena, nikapewa ruhusa ya kuingia ndani,
Ustaadh Fundi akawa anashangaashangaa tu akiwa haelewi kina-
choendelea.
“Usiwe na wasiwasi,” nilimwambia, nikamuona bado ame-
kosa kabisa utulivu, nadhani ni kwa sababu ilikuwa mara yake ya
kwanza kuingia Magogoni japo hakuwa ameniambia kwamba hiyo
ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza.
Niliingiza gari mpaka kwenye maegesho na kupaki lakini siku-
lizima, nikaliacha likiwa ‘on’, nikafungua mkanda na kusogeza siti
nyuma kidogo na kumgeukia Ustaadh Fundi.
“Utakuwa ‘comfortable’ kuzungumza hapahapa ndani ya gari?”
“Ndiyo! Haina shida kabisa!” alisema huku na yeye akikaa vi-
zuri, akakohoa kidogo kulainisha koo lake kisha akaanza kunieleza
kilichomfanya atake kuonana na mimi muda huo.
“Leo ndiyo fainali, si ndiyo?”
“Naam! Ni suala la muda tu!”
“Mmeshajua ni akina nani watakaokuja kutekeleza lile jambo?”
“Ndiyo, kwa kiasi kikubwa tumeshawajua na tunasubiri waingie
kwenye mtego tu,” nilimjibu, akawa anatingisha kichwa kukubali-
ana na nilichokuwa namuelezea.

645 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Itakapofika saa moja na nusu jioni, umeme utakatika mji mzi-


ma! Hapa huwa kuna majenereta ya ‘standby’ si ndiyo?”
“Ndiyo!”
“Nayo yataharibika ghafla! Giza nene litatanda!” alisema huku
akinitazama kwa makini, akaendelea kueleza:
“Watakuja mafundi umeme wakiwa kwenye magari rasmi na
hao ndiyo watakaokuja kutekeleza walichokipanga! Hawatakuwa
mafundi umeme, watakuwa ni vijana wa Abdulwaheed na genge
lao, wataingia na silaha nzito zitakazokuwa zimefichwa kwenye
masanduku ya kubebea vifaa vya ufundi umeme kwa hiyo hata
mkiwakagua, mtafikiri ni vifaa vya ufundi!
“Watakapoingia tu, wenzao ambao watakuwa tayarai wames-
haingiza silaha nyingine humu ndani, nao wataungana nao, kitaka-
chofuata baada ya hapo mimi na wewe hatujui!” alisema Ustaadh
Fundi na kunifanya nijaribu kumeza mate lakini muda huohuo
nikagundua kwamba mate yalikuwa yamekauka mdomoni.
Japokuwa ndani ya gari kulikuwa na kipupwe, kijasho chembam-
ba kilianza kunitoka, mikono ikawa inatetemeka mithili ya mlevi
wa pombe kali aliyekubuhu.
“Sijakuelewa!” nilisema huku nikijaribu kukaa vizuri kwenye
siti ya gari, nikajipapasa kidogo kisha nikawa nimebonyeza kifaa
maalum mwilini mwangu cha kurekodi mazungumzo kwa sababu
niliamini kile alichonieleza Ustaadh Fundi, kama nikiwaeleza vi-
ongozi wangu, nao wanaweza wasinielewe, wanaweza wasiniamini
na wanaweza kushindwa kujua kama taarifa hizo zina ukweli kiasi
gani.

646 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Hujaelewa nini?”
“Sijaelewa kila kitu, hebu naomba rudia kunieleza, taratibu,
hatua kwa hatua!” nilimwambia Ustaadh Fundi, akanitazama
machoni, na mimi nikawa namtazama, akashusha pumzi ndefu na
kuanza upya kunielezea kile alichonieleza, safari hii akifafanua
vizuri zaidi.
“Wewe umezipata wapi taarifa hizi?”
“Ina maana huniamini si ndiyo?”
“Sijamaanisha hivyo, nataka tu kujua,” nilimwambia kwa sauti
ya upole, akashusha pumzi nyingine ndefu na kunieleza kwamba
amezipata kutoka kwenye vyanzo vyake vya kuaminika.
“Inawezekanaje umeme ukatike mji mzima mpaka hapa? Hili ni
eneo maalum ambalo limepewa kipaumbele namba moja! Umeme
huwa haukatiki hapa?”
“Leo utakatika! Ikifika saa moja na nusu juu ya alama utakatika!
Kama huamini basi sawa!”
“Hata ikitokea umekatika, taarifa nilizonazo zinaonesha majen-
ereta yanayotumika hapa ya kisasa kabisa na yanakaguliwa mara
kwa mara! Inawezekanaje nayo yakazimika na kusababisha giza
totoro?”
“Swali zuri! Ni kwa sababu kuna nyoka ndani! Kuna mtu au
watu wameuza utu wao! Kuna wasichana ambao wataingia mape-
ma au inawezekana wakawa wameshaingia, naamini hao ndiyo
ambao umeniambia taarifa zaio mnazo! Wataingia kwa gia ya kuja
kupamba pamoja na kutoa huduma za vyakula na vinywaji.
“Hao ndiyo watakaokuja kuchora mchoro wote wa kuharibu

647 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

majenereta ambayo baadaye yatatumika kama mabomu! Na hao


ndiyo watakaofungua mashambulizi baada ya wenzao kuingia!”
alisema, mpaka hapo nikawa na uhakika kwamba alichokisema ni
kweli kwa sababu hata sisi tulishakuwa tunajua kwamba zile silaha
zilizoonekana zikishushwa Kunduchi, ndizo zilizopangwa kuletwa
Magogoni ingawa bado hatukuwa tumejua zitaingizwa kwa njia
gani au zitatumika wakati gani.
“Nikuombe kitu! Naomba unisubiri hapahapa ndani ya gari!
Usitoke kwenda popote,” nilisema huku nikipumua kwa kasi, safari
hii ilikuwa zamu yangu kuhema kama mtu aliyetoka kukimbia
mbio za mita mia moja.
Nilishuka kwenye gari na moja kwa moja nikaenda mahali
alipokuwepo baba yake Saima, alipoona tu ujio wangu, alijitenga
pembeni, nadhani alishakuwa ameisoma sura yangu.
“Kuna nini?” aliniuliza lakini badala ya kumjibu, nilichomoa ile
tape ‘recorder’ na kuibofya, sauti niliyomrekodi Ustaadh Fundi
akifafanue lile jambo ikaanza kusikika, nikamuona na yeye amesh-
tuka baada ya kusikiliza sekunde chache tu.
“Haiwezekani!” alisema huku akigeuka na kutazama huku na
kule, akionesha kuchanganyikiwa kabisa.
“Hebu iweke ianze upya,” alisema akinikabidhi ile tape recorder,
nikaipokea na kuibofyabofya, sauti ya Ustaadh Fundi ikaanza
kusikika upya kuanzia mwanzo, akieleza kila kitu.
Aliendelea kusikiliza yale maelezo, akiwa anatingisha kichwa
chake na kunifanya nishindwe kumuelewa kwamba alikuwa
anabishana na kilichokuwa kinasemwa na Ustaadh Fundi au ali-

648 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kuwa anasikitika.
Aliisikiliza mpaka mwisho, akawa ni kama amepigwa ganzi
mwili mzima, akabaki ametulia kwa sekunde kadhaa kisha akavuta
pumzi ndefu na kuzishusha.
“Tunahitaji kukutana kwa dharura haraka iwezekanavyo!” alise-
ma, nikajaribu kumkumbusha jambo la muhimu.
“Kuna nyoka kati yetu! Tunawezaje kukutana wote tena? Maana
yake si taarifa zitavuja kwamba tayari tumejua?”
“Unashaurije?”
“Tuitane wachache tu, ikiwezekana watatu au wanne tu, mimi,
wewe, mkurugenzi na Chief Mwaipopo!”
“Haitakuwa na maana kama hatutawashirikisha PSU,” alisema
akimaanisha wale maafisa wa kikosi cha ulinzi wa namba moja.
“Hatuwezi kuwaamini, kwa sababu kama ni nyoka, safari hii
yupo upande wao!”
“Kiongozi wao ni mtu mwenye maadili sana! Nimefanya naye
kazi kwa kipindi kirefu, ni mtu unayeweza kumuamini bila tatizo
lolote,” alisema, nikatingisha kichwa kuonesha kumkubalia.
“Na mtoa taarifa wako lazima awepo ili atufafanulie kwa kina
zaidi, najua kila mmoja ana maswali mengi sana,” alisema, ni-
katingisha kichwa kuonesha kukubaliana na alichokuwa anakise-
ma.
Harakaharaka akabonyeza kigaa chake cha mawasiliano, akazun-
gumza kwa lugha ya kifico (code) akiwataka mkurugenzi na Chief
Mwaipopo kuelekea kwenye ofisi ndogo iliyokuwa ndani, akanipa
ishara na mimi nikamchukue Ustaadh Fundi.

649 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Tuliachana, yeye akawa anaelekea kule alikokuwa kiongozi wa


PSU akiendelea kuwapanga vijana wake, mimi nikawa napiga
hatua ndefundefu kuelekea kule kwenye gari nilikokuwa nimemua-
cha Ustaadh Fundi.
Muda mfupi baadaye, wote tulikuwa ndani ya ofisi ndogo ya
mikutano, baba yake Saima akaniomba nimtoe nje kwanza Ustaadh
Fundi atusubiri wakati tukijadiliana. Nikafanya hivyo na kwenda
kumkabidhi kwa mmoja kati ya maafisa waliokuwa kwenye mlan-
go mkubwa.
“Mgeni wangu huyu, naomba anisubiri hapahapa,” nilimwambia,
akatingisha kichwa kuonesha kunielewa, tukatazamana na Ustaadh
Fundi ambapo nilimpa ishara kwamba asiwe na wasiwasi, naye
akatingisha kichwa kuonesha kunielewa.
Harakaharaka nikapiga hatua ndefundefu kurudi ndani, nikakuta
kila mmoja akiwa ametulia kabisa, wakiwa wananisubiri mimi.
Baba yake Saima alionesha kujikuna kichwa muda wote.
“Tumeitana hapa kwa dharura! Kuna taarifa nyingine mpya na
za muhimu sana, naomba kila mmoja asikilize kwa umakini wa
hali ya juu!” alisema baba yake Saima kisha akanigeukia na kunipa
ishara kwa macho. Nikaitoa ile ‘tape recorder’ na kuiweka mezani,
nikaibonyeza kisha Ustaadh Fundi akaanza kusikika, akiwa ana-
zungumza na mimi.
Kila mmoja alitulia kimya wakati sauti ikianza kusikika, yaliyo-
sikika yakawafanya wote wapigwe na butwaa, wakiwa ni kama
hawaamini kile walichokuwa wanasikia. Kama ilivyokuwa kwangu
na kwa baba yake Saima, baada ya kumaliza kuisikiliza, wote

650 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

waliomba tuirudie tena, nikafanya hivyo! Tukarudia tena kuisikili-


za kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Ilipoisha, kila mmoja alishu-
sha pumzi ndefu, utulivu ukionesha kupotea kabisa, nikatakiwa
nitoe ufafanuzi kuhusu kilichosikika.
“Ustaadh Fundi ndiye aliyetuletea taarifa hizi!”
“Ustaadh Fundi ni nani?” aliuliza kiongozi wa PSU kwa sa-
babu yeye pekee ndiye ambaye alikuwa hamjui, baba yake Saima
akanipa ishara kwamba nikamlete. Wakati nataka kutoka, mkuru-
genzi akanipiga swali lingine.
“Unamuamini kwa kiasi gani?”
“Kwa asilimia 100! Taarifa zake ndizo zilizotusaidia kufanikisha
kwa kiasi kikubwa misheni hii, ni yeye ndiye aliyetuelekeza alipo
Abdulwaheed, ni yeye ndiye aliyetuelekeza kuhusu Mutesigwa! Ni
mtu wetu ambaye anaaminika,” nilisema, wote wakashusha tena
pumzi ndefu na nikaruhusiwa nimfuate.
Muda mfupi baadaye nilirejea nikiwa nimeongozana na Ustaadh
Fundi, nikamuelekeza sehemu ya kukaa.
“Viongozi wanataka kujua kwa undani kuhusu maelezo uliyonipa
na jinsi wewe ulivyopata taarifa,” nilisema baada ya kuwa nimeru-
dia kumtambulisha Ustaadh Fundi, akaanza kueleza jinsi alivy-
opata taarifa hizo.
Maelezo yake yalikuwa yamenyooka kiasi kwamba hakuna
yeyote kati yetu aliyebaki na wasiwasi kuhusu taarifa zile.
“Unaweza kujua huyo nyoka ni nani?”
“Hapana! Lakini i mtu wa ndani!” alisema Ustaadh Fundi baada
ya kuhojiwa na kiongozi wa PSU, tukabaki kutazamana kwa zamu-

651 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

zamu.
“Nafikiri tunatakiwa kuzifanyia kazi taarifa hizi haraka iweze-
kanavyo,” alisema mkurugenzi na tukiwa tunatafakari kila mmoja
kwa nafasi yake, taarifa nyingine mpya ziliingia.
Zilikuwa ni taarifa kutoka kwa wale vijana wetu waliokuwa
wamepangwa kuanzia kule Kunduchi na kwenye barabara zote za
eneo lile.
Zilikuwa ni taarifa kwamba, kuna magari mawili aina ya Coaster,
yametoka kwneye ile kambi kule Kunduchi yakiwa yameongozana,
kila mmoja akajua sasa kazi imeanza.
“Nashauri tuahirishe kikao hiki kwa muda, tujue kwanza ni nini
kinachoendelea,” alisema baba yake Saima, wazo ambalo kila
mmoja alilikubali, tukainuka na kutawanyika, mimi ikabidi kwanza
nimrudishe Ustaadh Fundi kwenye gari ili nipate nafasi ya kufanya
kazi kwa umakini zaidi.

652 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

24
T
AARIFA ziliendelea kuingia, hatua kwa hatua. Baada
ya magari yale mawili kutoka Kunduchi, kila afisa
aliyepangwa kwenye eneo lake alikuwa akitoa taarifa
ya kila kinachoendelea, magari manne ya vijana wetu,
yakaanza kuwafuatilia kwa nyuma kwa namna ambayo
isingekuwa rahisi kwa wao kujua kwamba wanafuatilia.
Taarifa zilionesha kwamba baada ya kutoka Kunduchi, waliele-
kea moja kwa moja mpaka eneo liitwalo Mbuyuni ambapo ndipo
ilipo njia panda inayozikutanisha barabara mbili, ile ya Kunduchi na
Barabara ya Morogoro.
“Wameingia Barabara ya Bagamoyo, wakielekea upande wa
Mwenge,” ilisikika taarifa kwenye mfumo wetu wa mawasiliano.

653 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Muda huohuo, zikaingia taarifa nyingine kwamba magari men-


gine matatu yalikuwa yameonekana yakitoka kwenye ile kambi,
moja lilikuwa ni Coaster na mengine mawili yalikuwa ni Land-
cruiser moja na Nissan Patrol ambayo nayo yalikuwa yameongo-
zana.
Nayo yakaanza kufuatiliwa, ikaonesha nayo yanafuata njia ileile
kama yale mawili ya mwanzo, macho na masikio ya kila mtu yaka-
wa ni kwenye magari hayo matano. Zile Coaster mbili za kwanza
ziliripotiwa kuwa tayari zimeshafika Mwenge kwenye mataa na
zilikuwa zinaendelea na safari kwa kufuta Barabara ya Ali Hassan
Mwinyi.
Dakika kadhaa baadaye, zikaja taarifa kwamba magari yote yali-
kuwa yakiendelea kupasua lami kwa kasi kwenye Barabara ya Ali
Hassan Mwinyi, yakielekea katikati ya mji, hapo sasa kila mmoja
akawa na uhakika kwamba safari ile ni ya kuelekea Ground Zero.
Nilitazama saa yako, ikawa inaonesha ni tayari saa kumi na mbili
jioni, tukawa tunajadiliana kwa mafumbo kuhusu nini ambaco
kinatakiwa kufanyika kwa sababu ilishakuwa wazi kwamba magari
hayo, yanakuja pale tulipo.
“Tunatakiwa kuwapanga vijana wetu wa maeneo yote ya baraba-
ra za kuingia Magogoni, huu ndiyo muda wetu wa kumaliza kazi,”
nilisema wakati nikizungumza na baba yake Saima, akaniuliza ni
nini ambacho nilikuwa nakiwaza ndani ya kichwa changu? Wa-
ruhusiwe kuingia au tuwazuie kwanza?
“Nadhani tulishakubaliana kuhusu hilo, tunatakiwa kuwaacha
wao wafanye kile walichokipanga ili waingie kwenye mtego,”

654 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

nilisema kwa kujiamini, baba yake Saima akashusha pumzi ndefu.


“Hapana, tunatakiwa tuwe na uwezo wa kubadilisha mipango
yetu kwa kadiri taarifa mpya zinavyotufikia! Mwanzo tulikubali-
ana kwa sababu tulikuwa hatujajua kwamba kutakuwa na suala la
umeme! Unadhani silaha zote zikiingizwa kisha ikatokea kweli
umeme ukazimwa kama walivyopanga, si eneo lote hili litageuka
kuwa bwawa la damu?” alisema, ikawa ni zamu yangu kushusha
pumzi ndefu.
“Nafikiri tufanye kitu kimoja, tuwacheleweshe kwa makusudi
kuingia na baadaye tukiwaruhusu, itabidi watangulie wao kwanza
kisha magari yote yenye silaha tuyaweke chini ya uangalizi wetu!”
“Hebu fafanua!” alisema baba yake Saima, akili yangu ikawa
inafanya kazi kwa kasi kubwa kwelikweli.
“Jambo la kwanza tunalotakiwa kulifanya, wakishaingia tu
kwenye barabara za kuelekea hapa tulipo, kwa maana ya barabara
ambazo tayari tumeshawapanga vijana wetu, mawasiliano ya simu
yazimwe kwanza!
“Hii itawazuia kuwasiliana na wenzao, kisha tutatengeneza mi-
tego ya magari makubwa kuharibika katikati ya barabara na kuten-
geneza foleni mita chache kutoka hapa! Kwa hiyo magari yote
yatabaki yamenasa kwenye foleni!
“Baada ya hapo, tutawataka watu wote wateremke kwenye
magari ili wasizidi kuchelewesha ratiba za maandalizi ya dhifa
yanayoendelea! Kwa kuwa kutakuwa na walinzi waliojipanga,
tena wenye silaha, watalazimika kuteremka kwenye magari yao na
kuziacha silaha ndani ya magari.

655 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Baada ya hapo, tukishakuwa na uhakika kwamba wameter-


emka wote, tutawaweka madereva chini ya uangalizi, tutayapeleka
magari yote kwenye maegesho ya nje na tutazuia mtu yeyote asiin-
gie wala kutoka,” nilisema.
“Hujafikiri vizuri! Hujui kwamba msafara umegawanyika katika
sehemu mbili? Maana yake ni kwamba hawatawasili kwa wakati
mmoja kwa hiyo hata hiyo foleni tutakayoitengeneza, itawashtua
wale ambao watakuwa bado hawajafika, hasa ukizingatia kwamba
watakuwa wanashindwa kuwasiliana na wenzao waliotangulia kwa
hiyo lazima watashtukia kwamba kuna kitu kinaendelea,” alisema
baba yake Saima.
“Mimi nina wazo lakini halitofautiani sana na alichokisema
kijana hapa,” alisema mkurugenzi, wote tukawa tunamsikiliza kwa
makini alichokuwa anataka kukisema, ambacho kama alivyosema
mwenyewe, hakikuwa kikitofautiana sana na nilichokuwa nime-
shauri.
“Tutengeneze foleni kama alivyoshauri, tena kwenye njia zote,
kisha tusubiri kidogo, tusizime mawasiliano kwanza mpaka kundi
la pili nalo litakapokuwa limeingia kwenye foleni, kisha baada ya
kuwa na uhakika kwamba kundi lote limeingia kwenye mtego,
ndipo tutakapozima mawasiliano yote na kuwalazimisha water-
emke kwenye magari na kutembea kuingia hapa ndani na kwa
kuwa watakuwa wameshakaribia sana, hakuna atakayepinga!
Baada ya hapo, tutaenda kuwaweka wote kwenye chumba
maalum, ambapo hakuna atakayeweza kuwasiliana na mtu mwing-
ine yeyote kwa sababu mawasiliano yatakuwa yameshazimwa!

656 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Tutawapandikiza vijana wetu ambao ndiyo watakaofanya kazi za


upambaji wa ukumbi na kuwahudumia wageni waalikwa wakati
tukisubiri kazi ianze,” alisema mkurugenzi, wote tukatingisha vi-
chwa kuonesha kukubaliana na alichokuwa amekisema.
Swali likabaki kuwa moja! Je, huyo nyoka aliyepo katikati yetu,
hawezi kutoa taarifa kuhusu kinachoendelea?”
“Hataweza na kama akijaribu, tutambaini kwa urahisi kwa sa-
babu tayari tulishakubaliana kwamba simu pekee zitakazoruhusiwa
kuingia na kutoka, zitakuwa ni za kwetu na zitapitia kwenye chane-
li maalum kwa hiyo kila kitu kitakuwa kinasikilizwa na vijana
wetu wa Cyber!” nilisema, wote tukakubaliana kuhusu hilo.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, kilichofuatia baada ya hapo,
ilikuwa ni kufanya mawasiliano na vikosi vyote vilivyokuwa doria
katikati ya mji, malori makubwa matatu yalitafutwa na ndani ya
muda mfupi tu, yakawa yameshaelekezwa kwenye barabara kuu
tatu zilizokuwa zinaelekea ‘ground zero’.
Kwa kuwa vijana wetu ndiyo waliokuwa wakiyaendesha baada
ya ‘kuyachukua’ kutoka kwa madereva na wamiliki wake kwa
makubaliano maalum, kila kitu kilienda kama kilivyopangwa.
Lori la kwanza, lilitegeshwa na kuziba barabara yote ya kwanza,
dereva na vijana wake wakateremka na kuanza kufungua matairi
ili ionekane walikuwa wamepata dharura, lori la pili nalo likafunga
barabara ya pili kwa mtindo uleule, la tatu nalo likafanya hivyo-
hivyo.
Kwa kuwa kila kitu kilikuwa kinafanyika kwa ‘taiming’ kubwa,
ndani ya muda mfupi tu, zile ‘coaster’ mbili zilikuwa zimeshajaa

657 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kwenye mtego, zikanasa kwenye foleni ‘feki’, katikati ya magari


ya vijana wetu, mbele kabisa kukiwa ndiyo kuna lile lori lililote-
geshwa.
Nadhani waliwasiliana na wenzao kwa sababu yale magari men-
gine yaliyokuwa yanafuatia, hayakupita kwenye njia ile waliyopita
wenzao, yakajaribu kupita kwenye njia ya pili ambako nako wali-
kutana na hali ileile.
Baada ya kuwa sasa tumeshahakikisha kwamba magari yote
yamenasa kwenye foleni, ndipo amri ya kuzima mawasiliano ya
mitandao yote ya simu ilipotoka, magari maalum ya Convoy Pro-
tection Jammer ambayo nayo yalikuwa yameshapangwa kwenye
maeneo muhimu, yakawasha mitambo yao ili hata kama kulikuwa
na mtu anayetumia simu za sattelite, naye asiweze kupata ma-
wasiliano.
Ile njia ya tatu ambayo haikuwa na tatizo, lori liliondolewa na
barabara ikafunguliwa kwa ajili ya matumizi maalum pekee.
Tuliwaweka kwenye foleni kwa takribani dakika ishirini, vijana
wetu wakizidi kuongezeka eneo lile, wakijifanya ni kama wanataka
kujua kumetokea nini mpaka kukawa na foleni, tukawa tunawasili-
ana kwa karibu kupitia vifaa vyetu vya mawasiliano ambavyo
kwa kuwa vyenyewe vilikuwa vimeunganishwa kwenye ‘channel’
maalum, mawasiliano hayakukatika.
Baada ya hapo, kilichofuatia ilikuwa ni amri ya watu wote kuter-
emka kwenye magari na wale ambao walikuwa wakielekea ndani
kwa maana ya Magogoni, watembee kwa miguu wakati vijana
wakiendelea kushughulikia lile suala la foleni.

658 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Kwa jinsi akili nyingi zilivyokuwa zimetumika, tuliweza ku-


wazidi akili kirahisi sana kwa sababu ni kweli waliingia kwenye
mtego mwingine, wakaanza wale mabinti waliokuwa kwenye zile
‘coaster’ mbili za mwanzo, ambao waliteremshwa, mmoja baada
ya mwingine.
Ni kweli walikuwa wamevalia sare kama wahudumu maalum
ingawa kila mmoja alikuwa amevaa ‘barakoa’, wakaongozwa na
maafisa wetu mpaka kwenye lango kuu la kuingilia ‘ground zero’,
wakawa wanakaguliwa, mmoja baada ya mwingine.
Pale getini tulikuwa tumeshaandaa kamera za siri, kwa hiyo kila
aliyekuwa akikaguliwa, alikuwa akitakiwa kwanza kuvua barakoa,
wakati anakaguliwa kamera zinawa zinafanya kazi yake ya ku-
wapiga picha zilizoonesha vyema sura zao wakiwa hawana bara-
koa.
Hakuna aliyeruhusiwa kuingia na chochote na walioshuka na
mizigo, walitakiwa kurudisha mizigo yao kwenye gari, huku
wakipewa maelekezo kwamba magari yataingia ndani ya muda
mfupi. Coaster ya kwanza ilikuwa na mabinti kumi na tano, coast-
er ya pili nayo ikawa na mabinti kumi na tano pamoja na wan-
awake wawili ambao walikuwa watu wazima kidogo.
Walipoingia ndani, walipokelewa na maafisa wa kike ambao wa-
likuwa wamevaa nguo rasmi ili waonekane kama na wao ni wafan-
yakazi wa pale wanaofanya kazi ya kuwapokea wageni, wakawa-
chukua wote na kuwapeleka kwenye chumba maalum chini ya
ulinzi mkali ambao haukuweza kuonekana kwa macho.
Baada tu ya kuwa wameshaingizwa, lori la kwanza nalo lili-

659 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kuwa limeshapona, likawashwa na kuondoka eneo hilo, maafisa


wetu wakalisimamisha na kumuelekeza dereva kupaki pembeni ili
asiendelee kusababisha foleni.
Madereva wote wawili wa Coaster wakawekwa chini ya ulinzi
bila mtu yeyote asiyehusika kuelewa chochote, magari yakaingiz-
wa ndani na kupelekwa kwenye maegesho maalum ya chini kwa
ajili ya ukaguzi.
Upande wa pili, taratibu kama zilezile zilikuwa zinafanyika
kwenye yale magari mengine yaliyokuwa yamenasa kwenye foleni
ya pili na tofauti na coaster mbili za mwanzo, yenyewe yalikuwa
yamewabeba wanaume watupu.
“Hatuwezi kuteremka, tutasubiri foleni iishe tuingie na magari,
kuna vitu vya thamani humu hatuwezi kuteremka,” alisema mwa-
naume mmoja mwenye mwili ulioshiba, aliyekuwa kwenye ile
Coaster nyingine iliyokuwa kwenye foleni ya pili.
“Haya ni maelekezo, bila shaka mnajua mpo sehemu gani!
Maelezo ya hapa ni amri, hakuna anayetakiwa kuhoji wala kup-
inga!”
“Haiwezekani! Hakuna atakayeteremka!” alifoka yule mwanau-
me, wakati akijibizana na vijana wetu, mazungumzo yao yakawa
yanasikika moja kwa moja kwenye vifaa vyetu vya mawasiliano,
akilini nikajiambia sasa kazi imeanza rasmi.
Akili zilinicheza haraka, nikajua lazima kuna jambo halijaenda
sawa! Haiwezekani mtu yeyote alete ubishi mbele ya maafisa us-
alama, tena akiwa katika eneo nyeti kabisa la nchi, nikajua lazima
kuna mchezo ulikuwa umefanyika na sasa kilichokuwa kinaende-

660 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

lea, ilikuwa ni kuhamisha mawazo na nguvu eneo ambalo siyo


sahihi ili wapate muda wa kufanya walichokuwa wanakipanga.
Harakaharaka nilimpigia simu baba yake Saima na kumweleza
kwamba nahisi kuna mchezo ambao umefanyika, ambao hatujau-
gundua na sasa ni sisi ndiyo tuliokuwa tunataka kuingizwa kwenye
mtego. Nilipomueleza hivyo tu, na yeye ni kama alichekecha akili
yake kwa haraka, akakubaliana na mimi na kunitaka niwazuie wale
vijana wetu waliokuwa wanataka kuwateremsha wale watu kwe-
nye gari.
Nikabonyeza kifaa changu cha mawasiliano na sasa nikawa
nasikika na kila mtu aliyekuwa amevaa vifaa vya mawasiliano,
nikatoa amri kwamba kama wamekataa kushuka kwenye gari kwa
hiyari yao, waachwe kwanza wakati tukitafakari nini cha kufanya.
Baada ya maagizo yale, kweli vijana wetu ambao tayari wali-
kuwa wameshaanza kupandisha jazba, ilibidi watulie.
“Kuna jambo hatujalifanya kwa umakini na pengine ndiyo lili-
lowashtua.”
“Jambo gani?”
“Haya maroli yaliyotumika kufunga barabara na kutengeneza
foleni bandia yamepatikanaje?” nilihoji wakati tukiwa tumekutana
tena kwa dharura, kujadiliana nini cha kufanya!”
“Swali gani hilo? Si tulishakubaliana kwamba kuna vijana wetu
ambao ndiyo walioifanya kazi hiyo?” alijibu mkurugenzi, nadhani
alikuwa amejibu bila kufikiria kwa kina kuhusu ambacho nilikuwa
nimemaanisha.
“Nadhani humjaelewana,” baba yake Saima aliingilia kati na

661 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kunitaka nizungumze nilichokuwa nakiwaza.


“Malori kama haya hayaruhusiwi kuingia huku mjini, si ndiyo?”
nilisema, nikawa ni kama nimemfungua macho kila mmoja, watu
wakawa wanatazamana.
“Jibu ni ndiyo! Hayaruhusiwi! Sasa kama hivyo ndivyo, unafikiri
kwa watu wanaotumia akili kubwa kama hawa, wanaweza kuona
malori kadhaa, tena siyo moja, yote yakielekea kwenye barabara
za kuingilia Magogoni wasishtuke?” niliendelea kuhoji, hakuna
ambaye alinijibu lakini nikawaona ni kama wanatafakari kwa kina.
“Sote hapa tunajua kwamba mabinti waliopangwa kwa ajili ya
kazi hii, wamepewa mafunzo ya kutosha kwa muda mrefu tu! In-
awezekanaje tuwanase kirahisi namna hii?
“Hakuna upinzani wowote waliouleta! Inawezekana kweli ku-
wakamata magaidi kirahisi namna hii na kuwaswaga kama kondoo
wanaopelekwa machinjioni?” niliendelea kuhoji, bado kukawa
hakuna aliyeweza kunijibu, nikawa ni kama namewafumbua ma-
cho wote.
“Hebu tueleze unachokiona kwenye akili yako maana wewe
ndiyo kiongozi wa misheni hii!”
“Kabla sijaeleza ninachokiwaza, nataka kwanza sote tujiridhishe
jambo moja! Yule mtoa taarifa wetu, Ustaadh Fundi anawafahamu
baadhi ya mabinti waliokuwa wakipewa mafunzo kwa sababu
walichukuliwa Kibiti na miongoni mwao alikuwepo binti yake
ambaye tunamshikilia.
“Kwa sababu tumefanikiwa kuwapiga picha watuhumiwa wote
tuliowashusha kwenye zile Coaster mbili, nataka twende naye

662 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

mpaka kwenye ‘control room’ haraka iwezekanavyo, aoneshwe


sura zao wote kisha atueleze kama kuna yeyote anayemjua!
Ikitokea amewatambua, basi nitafuta kauli yangu lakini kama
asipowatambua, nitaeleza ni nini ninachokiona,” nilisema, wote
wakakubaliana na mawazo yangu.
Harakaharaka nilimfuata Ustaadh Fundi kwenye gari nilikokuwa
nimemuacha na kumpa maelekezo ya kunisubiri, nikamkuta akiwa
amekaa kwa kutulia kwenye siti yake.
Nikampa ishara anifuate, tukatoka mpaka ‘control room’ ambapo
tayari mkurugenzi, baba yake Saima, Chief Mwaipopo na yule
kiongozi wa PSU walikuwa wameshatangulia.
Harakaharaka nikamuelekeza Ustaadh Fundi nini anachotakiwa
kukifanya na bila kupoteza muda, picha zote zikaanza kupita kwe-
nye screen kubwa, moja baada ya nyingine. Wote tukawa tumetu-
lia, tukimtazama Ustaadh Fundi ambaye naye alikuwa akizitazama
kwa makini.
Ajabu ni kwamba picha za mabinti kumi na tano waliokuwa kwe-
nye Coaster ya kwanza, zilipita zote lakini Ustaadh Fundi haku-
weza kumtambua hata mmoja kati yao, zikapita picha nyingine za
mabinti wengine kumi na tano waliokuwa kwenye coaster ya pili,
napo hakuweza kumtambua hata mmoja.
Wakati akimalizia kutazama picha za wanawake wawili walio-
kuwa kwenye Coaster ile ya pili, akashtuka na kutaka zirudishwe
azitazame vizuri.
“Huyu mmoja namfahamu! Huyu mwanamke... namfahamu!”
alisema, wote tukatazamana.

663 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Kwa hiyo katika wote hawa umeweza kumtambua huyu mwa-


namke mmoja tu si ndiyo?” nilimuuliza, akatingishwa kichwa
kuonesha kukubaliana na nilichokuwa nimekizungumza, nikawa-
geukia viongozi wangu, nikawa nawatazama usoni mmoja baada
ya mwingine.
“Mungu wangu! Unaweza kuwa upo sahihi,” alisema baba yake
Saima, kwa mara ya kwanza nikamuona akikata kucha za vidole
vya mikono yake kwa kutumia meno.
Nilimtaka Ustaadh Fundi amuelezee yule mwanamke kwa jinsi
alivyokuwa anamjua, akaeleza kwamba amewahi kumuona akiwa
na Abdulwaheed ambaye alimtambulisha kama mfanyabiashara
mwenzake.
“Tukutane tena haraka!” alisema baba yake Saima, nikamrudisha
Ustaadh Fundi kwenye gari kisha tukarudi kwenye chumba cha
mikutano ya siri.
“Wametuzidi akili, hawa wasichana tunaowashikilia, siyo wale
tuliowatarajia. Nimetazama jambo lingine la muhimu ambalo sid-
hani kama kuna mwingine aliyelibaini!
“Hizi gari mbili tulizowashusha, zinatofautiana namba za usa-
jili na zile gari ambazo ndizo hasa zilizoonekana kuanzia Masaki
mpaka Kunduchi ingawa kwa nje zote zinafanana rangi,” nilisema,
nikazidi kuwavuruga vichwa kwa sababu ilikuwa ni kweli.
“Lazima walipoona malori yanaingia katikati ya mji, walijua
kuna mtego tumeuandaa, kwa hiyo wakabadilisha mbinu na kusa-
babisha sisi ndiyo tuingie kwenye mtego wao.
“Wahusika bado hawajaingia kwenye hili eneo lakini nina uhaki-

664 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ka mkubwa kwamba wapo jirani kabisa na hapa na pengine sasa


wataingia kwa kutumia njia nyingine tofauti kabisa,” nilisema,
kisha nikashauri kwamba kwa kuwa mbinu hiyo ya kwanza ilikuwa
imefeli, tuyaruhusu yale magari mengine yaingie lakini tuweke
tahadhari kubwa kufuatilia hatua kwa hatua.
Mwanzo wazo hilo lilipingwa vikali lakini baada ya kutetea
hoja yangu, wote walikubaliana na mimi, ikabidi lile lori lingine
liondolewe, foleni ikafunguka na magari yakaanza kupita kama
kawaida.
Ajabu ni kwamba yale magari matatu baada ya foleni kuruhusu,
yaliondoka kwa kasi na baada ya kukaribia kwenye lango kuu,
yalibadilisha mwelekeo na kuingia kwenye barabara iliyokuwa
inaenda kuungana na barabara inayoelekea feri, wote tukabaki
tumepigwa na butwaa, tukiwa hatuelewi nini cha kufanya.
“Tuwakimbize na kuwatia nguvuni!”
“Hapana! Hiyo siyo njia sahihi, wafuatilie tu kujua wanakwenda
wapi,” nilisema na baada ya wazo langu kukubaliwa, nilitoa amri
kwa vijana wetu kuwafuatilia kwa makini kutaka kujua wanaelekea
wapi.
“Wameteremka wote kwenye magari na kujichanganya na abiria
wanaoingia na kushuka kwenye pantoni,” aliripoti mmoja kati ya
vijana wetu kupitia mawasiliano yetu, tukabaki tunatazamana, kila
mmoja akionesha sura iliyojawa na hofu isiyo ya kawaida.
“Sasa itakuwaje?”
“Achana nao, wasitutoe kwenye mstari! Walitumwa makusudi
kuja kutuvuruga na kama tusingekuwa makini, tungeingia kwenye

665 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

mtego wao,” nilisema wakati nikizungumza na Chief Mwaipopo


ambaye ilibidi anifuate baada ya kuwa tumemaliza kikao kifupi
cha siri.
“Uliwezaje kunusua kama tumezidiwa ujanja?”
“Machale tu, nilihisi kuna kitu hakipo sawa!”
“Au unatumia ndumba nini?” alisema Chief Mwaipopo na kusa-
babisha wote tucheke japokuwa tulikuwa kwenye wakati mgumu
kwelikweli.
“Kama wale wasichana wote siyo wahusika, hii inaweza kuwa
kashfa kubwa kwetu.”
“Kwenye kupambania usalama wa taifa letu hakuna kashfa, ni
bora tumejaribu na kubaini mapungufu katika maamuzi yetu.”
“Nini cha kufanya maana nahisi kichwa kimepata moto. Vion-
gozi wetu wote nao naona wamechanganyikiwa, kila mtu amepan-
iki.”
“Hakuna kitu kibaya kama kupaniki katika maingira kama haya.
Tunatakiwa kuanza na hawa wanawake wawili kwanza, lazima tu-
jue wao ni akina nani lakini pia lazima tujue hawa mabinti ni akina
nani,” nilisema, nikawa ni kama nimemzindua Chief Mwaipopo
kutoka kwenye lindi la usingizi.
Nilichokuwa nimekiwaza, kumbe kilikuwa sawa na alichokuwa
amekiwaza baba yake Saima ambaye hata sijui alitokea upande
gani, tukashtukia tu ameshaingilia mazungumzo yetu.
“Kuna mchezo uliofanyika hapa na tusipokuwa makini, kweli
Magogoni itaanguka usiku wa leo. Wale wanawake wawili lazima
watengwe na kupelekwa kwenye chumba maalum cha mahojiano

666 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

lakini pia yale magari mawili waliyokuja nao hawa mabinti inabidi
yakaguliwe kisawasawa, hatuna muda wa kupoteza,” alisema baba
yake Saima.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, nilitoa maagizo kupitia vi-
faa vya mawasiliano kwamba wale wanawake wawili watengwe
haraka na ningependa kwenda kuwahoji mimi mwenyewe wakati
magari yote mawili nayo yakikaguliwa.
Kabla ya kwenda kuwahoji wale wanawake, nilielekea kwanza
kwenye kile chumba maalum walipokuwa wale wasichana wadogo
ambao kama nilivyosema, idadi yao ilikuwa ni thelathini.
“Kiongozi wenu ni nani?” nilivunja ukimya, wasichana wawili
wakanyoosha mikono, nikawapa ishara kwamba wasogee pale nili-
pokuwa nimesimama, wakasogea huku wote tukiwa tumezunguk-
wa na maafisa usalama waliokuwa wamewaweka chini ya ulinzi
mle ndani ya chumba kile kikubwa.
“Ni nini kilichowaleta jioni hii?”
“Tumeambiwa kuna kazi ya kupamba ukumbi wa mikutano la-
kini pia kuwahudumia wageni.”
“Vitambulisho vyenu tafadhali,” nilisema, kila mmoja akatoa kit-
ambulisho chake. Vilikuwa ni vitambulisho vilivyoonesha kwamba
walikuwa wanatoka kwenye kampuni ya ‘cartering’ iitwayo Marti-
soor Catering and Hospitality Company.
Ni kampuni hii ndiyo ambayo duru za kiintelijensia, zilionesha
kwamba ndiyo iliyopangwa na Abdulwaheed na wenzake, ku-
tumika kama njia ya kupenya Magogoni. Ni hawa ndiyo ambao
tulielezwa kwamba ndiyo kwa kifupi wanaitwa ‘Cat Girls’.

667 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Mmewahi kuja kufanya shughuli yoyote hapa ndani?”


“Ndiyo, mara nyingi tu huwa tunakuja,” alisema mmoja kati ya
wale wasichana wawili viongozi.
“Wale wanawake watu wazima wawili mliokuja nao ni akina
nani?”
“Mimi siwajui, tuliambiwa tu kwamba ndiyo watakaotusimamia
leo kwa sababu wao ni wazoefu.”
“Mliambiwa na nani?”
“Na viongozi wetu ofisini.”
“Ofisi zenu ziko wapi?”
“Upanga!”
“Kwa hiyo wakati mnakuja mmetokea Upanga si ndiyo?”
“Ndiyo!” alisema mmoja kati yao, nikashusha pumzi ndefu.
“Viaa vyenu vya upambaji viko wapi?”
“Kwenye magari tuliyokuja nayo!”
“Kwa nini mmechelewa kuja na ratiba inaonesha mlitakiwa ku-
fika hapa tangu saa tisa jioni?”
“Labda viongozi wetu ndiyo watakuwa wanajua, tulikuwa tume-
jiandaa tangu mapema lakini tukaambiwa tusubiri.”
“Viongozi wenu wanaowasimamia siku zote wako wapi?”
“Wanakuja, sisi tumeambiwa tutangulie na kuanza kazi chini ya
usimamizi wa wale akina mama wawili,” alisema mmoja kati ya
wale mabinti, ambaye alionesha kuwa mzungumzaji kuliko wen-
zake.
“Sawa! Subirieni kidogo wakati tukikamilisha taratibu za kiusal-
ama.”

668 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Sawa, lakini muda umeenda sana na tumeambiwa shughuli


inaanza saa mbili za usiku,” alisema yule msichana, sikuwa na
cha kumjibu, harakaharaka nikatoka na kuelekea kwenye chumba
walichokuwa wamepelekwa wale wanawake wawili watu wazima,
wakiwa chini ya ulinzi.
“Ilibidi niagize kwamba mmoja atolewe kwanza kwa sababu
nilikuwa nataka kuzungumza nao mmoja mmoja.”
“Unaitwa nani?”
“Bella Mwakazi!”
“Kitambulisho chako tafadhali,” nilimwambia yule mwanamke
ambaye ndiye hasa niliyekuwa nataka kuzungumza naye, ambaye
Ustaadh Fundi alitueleza kwamba anamfahamu.
“Ooh, samahani, nimesahau kitambulisho, samahani kwa hilo.”
“Kampuni yenu inaitwaje?”
“Aah, ni cartering service.”
“Jina! Zipo kampuni nyingi zinazofanya shughuli hiyo, nataka
kujua hii ya kwenu unaitwaje?”
“Aah, kiukweli mimi bado ni mgeni kwa hiyo silijui vizuri jina la
kampuni.”
“Inawezekanaje ufanye kazi kwenye kampuni ambayo huijui jina
lake? Una muda gani kazini?”
“Nina mwezi wa pili sasa.”
“Unamfahamu Abdulwaheed?” nilimuuliza swali ambalo pen-
gine hakuwa amelitegemea kabisa, nikamuona akishtuka kuliko
kawaida, kisha akawa anatafuta jibu la uongo la kunipa.”
“Hapana!”

669 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Umewahi kufika Kibiti?”


“Mimi? Aaa... eeh! Ndiyo! Nimewahi kufika.”
“Ulienda kufanya nini?”
“Tulienda kwenye shughuli ya ndugu yetu, alikuwa anamcheza
mwali.”
“Una uhakika na unachokisema?”
“Ndiyo! Ndiyo! Ni kweli kabisa baba.”
“Hebu sogeza mikono yako,” nilimwambia, akawa anasitasita.
Nilikuwa nataka kujua jambo fulani ambalo lingeweza kunipa
picha kamili yule mwanamke ni nani hasa.
Aliisogeza mikono yake mezani, nikaitazama kwa makini,
mapigo yamoyo wangu yakanilipuka kwa sababu ilionesha kuwa
ni mtu wa kazi kwelikweli. Mikono yake ilikuwa imekomaa na ku-
weka sugu kwenye eneo la vifundo vya mikono, kuonesha kwamba
alikuwa akifanya mazoezi makali ya viungo ikiwemo kupiga
‘pushapu’.
“Huwa unafanya mazoezi si ndiyo?”
“Hapana, ni mafuta ninayopaka ndiyo yamenikataa, sifanyi
mazoezi mimi,” alisema, nikajua wazi kabisa ananidanganya.
Nilibofya kifaa changu cha mawasiliano, nikaagiza wataalamu wa
kuscan mwili wa binadamu kwa kutumia vifaa maalum waingie
ndani ya chumba kile haraka.
Nilishahisi jambo lingine kubwa, nikamuona yule mwanamke
akiwa anatetemeka kuliko kawaida. Muda mfupi baadaye, vijana
wawili waliingia, nikawataka wamchunguze yule mwanamke kwe-
nye mikono ake kwa kutumia ‘scanner’ maalum.

670 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Nilichokihisi ndicho kilichotokea, alikuwa amepandikizwa ‘chip’


ya mawasiliano katikati ya kidole gumba na kidole cha pili kwenye
mkono wake wa kushoto.
“Hapo kwenye mkono wako pamewekwa nini?”
“Hata sijui! Sielewi chochote,” alisema huku akibabaika kuliko
maelezo.
“Una uhakika?”
“Ndi...ndiyo!” alisema, nikawapa ishara vijana wanu wafanye
kazi yao, wakafanikiwa kutoa chip ndogo kwenye ngozi yake.
“Uko chini ya ulinzi,” nilisema huku nikisimama, akafungwa pin-
gu muda huoho, nikaagiza atolewe na kupelekwa kwenye chumba
maalum kwa ajili ya kusubiri hatua nyingine za kiusalama.
Niliagiza yule mwanamke mwingine aingizwe, naye nikamhoji
maswali yaleyale, naye akawa anababaika na baada ya kumchun-
guza kwa kina, tulibaini naye alikuwa na sugu kwenye mikono
lakini kubwa zaidi, alikuwa amepandikizwa ‘chip’ ya mawasiliano,
ikaolewa kisha naye akatolewa chini ya ulinzi mkali na kupelekwa
kwenye chumba maalum, kusubiri hatima yake.
Muda huoho, niliwataarifu viongozi wangu kuhusu nilichokuwa
nimekibaini, ikabidi tukutane tena kwenye chumba cha siri cha
mikutano, kila mmoja akaonesha kuzidi kuchanganyikiwa kuliko
kawaida.
“Mbona mambo yanakuwa magumu kiasi hiki?” alisema mkuru-
genzi, huku akipumua juujuu, nikajua anaweza kurudiwa na tatizo
lake kama siku ile alipopandwa napresha ofisini kwake tukizung-
umza.

671 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Tunatakiwa kutuliza vichwa! Hawa mabinti waruhusiwe kuen-


delea na maandalizi ya ukumbi kama ratiba ilivyo,” nilisema, wazo
ambalo lilikutana na upinzani mkali kwelikweli.
“Haiwezekani! Hata kama hawa siyo wale tuliokuwa tunawata-
rajia, kwa kuwa walikuwa wameongozana na hawa wanawake am-
bao umesema ushahidi wote unaonesha nao ni magaidi, hauwezi
kuwatoa kwenye kundi, nao ni magaidi tu!” alisema mkurugenzi
huku kasi ya kupumua kwake ikizidi kuongezeka.
“Nimejaribu kuwahoji viongozi wao na wamenieleza kwamba
hawa wanawake wawili hawawafahamu zaidi ya kuwa waliletwa
tu ofisini kwao na wakaambiwa kwamba watakuja kuwasimamia
kwenye shughuli ya upambaji pamoja na kuhudumia vyakula.
“Na isitoshe, inaonesha hawa siyo mara yao ya kwanza kuingia
hapa kuja kufanya shughuli kama hizi!”
“Hiyo pekee haitoshi kuwaamini na kuwaruhusu wajichanganye!
Tutakuwa tunacheza na moto na chochote kitakachotokea, itaone-
sha hatukuwaza vizuri,” alisema mkurugenzi. Muda wote huo tu-
liokuwa tukibishana tulikuwa ni sisi wawili, mimi na mkurugenzi
lakini baba yake Saima alikuwa kimya kabisa, vivyo hivyo kwa
Chief Mwaipopo na kiongozi wa PSU.
“Labda tuwasikie na wengine wanasemaje,” nilisema baada ya
kuona mkurugenzi ni kama haamini kuhusu mbinu niliyokuwa
nimeitoa.
“Nafikiri tuwaruhusu waendelee lakini wawe wanafuatiliwa kwa
ukaribu kabisa! Magari yao yakakaguliwe kisawasawa, vifaa vyote
watakavyokuwa wanavitumia vikaguliwe, naamini bado tunayo

672 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

nafasi ya kuwazidi akili,” alisema baba yake Saima.


“Mpaka hapa wameshatuzidi akili, badala ya wao kuingia kwe-
nye mtego wetu, tumejikuta sisi ndiyo tunaingia kwenye mtego
wao. Tusipotumia akili kweli Magogoni itaanguka,” alisema Chief
Mwaipopo, kiongozi wa PSU akamkatiza maelezo yake na kum-
taka na yeye atoe mawazo yake.
Hakuwa na majibu, ikabidi wazo nililolitoa ndiyo lipite, cha
kwanza ikawa ni kwenda kukagua magari yote mawili kwa vifaa
maalum vilivyokuwa na uwezo wa kubaini uwepo wa silaha yoyote
hata kama ilikuwa imefichwa mbali kiasi gani.
Kikosi maalum cha milipuko na silaha ndicho kilichopewa kazi
hiyo, magari yakakaguliwa kitaalamu na majibu yaliyotoka, ni
kwamba hakukuwa na silaha wala kitu chochote chenye kutia
shaka kwenye magari hayo.
Ikabidi mimi nikasimamie zoezi la kuwatoa wale wasichana kule
kwenye kile chumba maalum nikiwa na vijana wangu, tukawasi-
mamia wakati wakiteremsha vifaa vyao vyote vya kazi na kuele-
kea kwenye ukumbi maalum ambao dhifa kati ya namba moja na
wafanyabiashara ilikuwa ifanyike.
Kazi ya kupamba ukumbi ikaanza huku tukiwa macho kwelik-
weli, vijana wangu walikuwa wamezagaa kila sehemu, wengine
wakiwa wamevalia kama wahudumu wa kawaida, kuhakikisha
kwamba tunafuatilia kila kilichokuwa kinaendelea.
Wakati hayo yakiendelea, tulikubaliana kwamba wale wan-
awake wawili ambao ushahidi wote ulikuwa unaonesha kwamba
ni washirika wa Abdulwaheed, wanaondolewa eneo lile chini ya

673 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ulinzi mkali na kupelekwa mpaka ‘kitengoni’ kwa ajili ya maho-


jiano ya kina na tulikubaliana kwamba mbinu zote zitumike mpaka
waeleze ukweli wa walichokuwa wamekipanga.
Kwa kutumia mlango wa siri, wanawake wale walitolewa kimya-
kimya chini ya ulinzi mkali, wakaingizwa kwenye magari mawili
tofauti na wakaondolewa eneo lile kupelekwa kitengoni, wakiwa
wamefungwa pingu na vitambaa machoni mwao.
Mpaka inagonga saa moja kamili, tayari kazi ya upambaji ilikuwa
imekamilika, ukumbi ukawa umepambwa na kupendeza na baada
ya kwenda kuukagua, tulijiridhisha kwamba kila kitu kimeenda
sawa.
Ilibidi wale wasichana wote wachukuliwe na kurudishwa kwenye
kile chumba walichokuwa wamewekwa awali, wakisubiri taratibu
nyingine kwa sababu kazi yao ya kwanza walikuwa wameimaliza
na tusingeweza kuwaacha waendelee kuzagaa wakati bado wageni
hawakuwa wameanza kuwasili.
Kwenye majira ya kama saa moja na dakika kumi, ziliingia
taarifa kwamba kuna gari lilikuwa getini likisubiri kuruhusiwa
kuingia ndani kwa maelezo kwamba eti ndiyo lililokuwa limebeba
vinywaji na vyakula kwa ajili ya wageni.
“Msiliruhusu kwanza, nakuja mwenyewe,” nilisema kupitia kifaa
changu cha mawasiliano na taarifa zikawa zimemfikia kila mmoja.
Ilikuwa ni lazima niende mwenyewe kujiridhisha kuhusu gari
hilo na kubwa zaidi nilikuwa nataka kujua ni akina nani waliokuwa
ndani yake. Tulijadiliana tena na wenzangu, uamuzi wangu ukawa
umepewa baraka zote, huku timu nzima ikiwa nyuma yangu kuan-

674 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

galia ni nini kilichokuwa kinaendelea.


Nilitoka mpaka getini na kusogelea mahali gari hilo lilipokuwa
limeelekezwa kupaki kwa upande wa nje, kitu cha kwanza nikata-
ka kujua ndani yake kulikuwa na akina nani.
Ajabu ni kwamba, ndani ya gari hilo kulikuwa na watu watano,
wote wakiwa wamekaa mbele wakati uwezo wa gari lile ilikuwa ni
kubeba watuwawili tu mbele, dereva na mtu mwingine mmoja. Ni-
kaagiza wote wateremke, kweli wakatii, nikataka kwanza kuzung-
umza na dereva pembeni.
“Mmebeba nini?”
“Vyakula na vinywaji.”
“Mmetokea wapi?”
“Kisutu, tumeelekezwa kwamba tuvilete hapa kwa sababu kuna
shughuli!”
“Mmeelekezwa na nani?”
“Na Madam!”
“Madam gani?”
“Bosi wa hii kampuni ya cartering! Silijui vizuri jina lake tu-
mezoea kumuita Madam.”
“Leseni yako tafadhali!” nilisema, akaingiza mkono mfukoni na
kutoa leseni yake, nikaikagua na baada ya kujiridhisha kwamba
kweli picha iliyokuwa inaonekana kwenye leseni inafanana na sura
yake, niliendelea na mahojiano naye.
“Hawa ulioongozana nao ni akina nani?”
“Ni vijana wangu wa kunisaidia kushusha mizigo!”
“Kwa hiyo wewe ni mwajiriwa wa huyo Madam wako?”

675 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Hapana, huwa ananikodi tu kumbebea vifaa vyake wakiwa na


shughuli kama hivi!” alisema, nikatingisha kichwa na kumruhusu
arudi pale walipokuwa wenzake, nikaendelea kuwahoji wale vijana
wake, mmoja baada ya mwingine, lengo likiwa ni kutaka kujua
walikuwa wanahusikaje na ile kampuni.
Nilibaini kwamba maelezo yao wote yalikuwa yakifanana, wao
walikuwa wakikodiwa tu kubeba vyakula na vinywaji na huyo
kiongozi wa ile kampuni ambayo tulishakuwa na uhakika kwamba
ina uhusiano na Abdulwaheed.

676 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

25
B
AADA ya mahojiano ya awali kumalizika, niliwaita
vijana wangu walionisaidia kuwapekua wale wan-
awake kule ndani mpaka kubaini kwamba walikuwa
na ‘chip’ zilizopandikizwa kwenye mikono yao.
Ndani ya muda mfupi tu waliwasili, wakawakagua
wote kwa kuanzia na dereva na hawakubaini chochote, gari nalo
likakaguliwa kisawasawa, hakukuwa na chochote chenye kutia
shaka.

677 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Gari liliruhusiwa kuingia ndani, wakaanza kupakua mizigo yao


chini ya uangalizi mkubwa, muda wote nikawa naendelea kuumiza
kichwa kutaka kujua ni nini walichokuwa wamepanga wendawaz-
imu wale, nikawa natazama saa yangu mara kwa mara.
Muda huohuo, zikaingia taarifa kwamba kulikuwa na magari
mengine matatu yaliyokuwa yamewasili kule getini, maelezo
yakawa eti ni wageni waliolikwa na namba moja ndiyo wameanza
kuwasili, nikashusha pumzi ndefu.
Ilibidi tutoke viongozi wote na kuelekea kule getini kwa sababu
sasa kama ni kazi, hakika ilikuwa imeanza rasmi.
Katika ile orodha ya wale wageni, baada ya kuwa tumeipitia na
kuichuja, kuna baadhi ya watu ambao tulilazimika kuwaondoa na
walikuwa wameshapewa taarifa kwamba watapata nafasi ya kuon-
ana na namba moja wakati mwingine.
Ilikuwa ni lazima kuwa nao macho ili wasije wakajipenyeza
na kuingia kwa sababu tayari duru za kiintelijensia zilishaonesha
kwamba wanahusika moja kwa moja na Abdulwaheed kwa hiyo
kitendo cha kuwaruhusu waingie, ingekuwa ni sawa na kucheza na
sharubu za simba.
Tulifika getini na baada ya kukagua magari yote matatu ambayo
yalikuwa ni ya kifahari kisawasawa, tulijiridhisha kwamba kweli
walikuwa ni wageni ambao walikuwepo kwenye orodha ya wa-
geni waliokuwa wakitakiwa kukutana na namba moja jioni ya siku
hiyo.
Licha ya kuwa tumejiridhisha, ilibidi kwanza tuitane tena pembe-
ni kujadiliana maana mambo hayakuwa yakienda kama yalivyoku-

678 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wa yamepangwa kwa upande wetu.


Mipango ya awali ambayo tulikuwa tumeipanga, ilitakiwa kuwa
mpaka wakati huo, tuwe tumeshawatia mikononi karibu robo tatu
nzima ya watu wote ambao walikuwa wakihusika katika tukio
lililokuwa linatarajiwa kutokea usiku huo lakini mpaka wakati huo,
tulikuwa tumefanikiwa kuwakamata wale wanawake wawili pekee
na muda ulikuwa ukizidi kuyoyoma.
“Jambo la msingi ambalo kila mmoja wetu anatakiwa kulielewa
kama ambavyo tumekuwa tukikumbushana mara kwa mara, ni
kwamba hatutakiwi kuruhusu hofu ituingie, tunatakiwa kupambana
mpaka tone la mwisho la damu!”
“Ni sawa, lakini hujasema nini tunachotakiwa kukifanya mpaka
muda huu!”
“Si kila kitu kuhusu maandalizi yote kwa upande wetu kimeka-
milika?”
“Ndiyo! Kila kitu kimekamilika kwa asilimia mia moja! Kila kitu
kipo sawa!”
“Basi turuhusu shughuli ziendelee wakati na sisi tukiendelea
kutafuta namna ya kuwanasa watuhumiwa wote ambao bila shaka
kila mmoja atakuwa anajua kwamba watakuwa karibu sana na sisi
kwa muda huu na pengine wanafuatilia kila kinachoendelea,” alise-
ma baba yake Saima, katika mjadala mkali uliokuwa ukiendelea.
“Unachotakiwa kukisimamia ni kuhakikisha hakuna mianya
yoyote ya kiusalama inayoachwa ili wasije wakajipenyeza bila sisi
kujua, tunatakiwa kuwa tunatazama kila kinachoendelea, tena kwa
jicho la tatu,” alisema mkurugenzi, akinipa maelekezo mimi, nikai-

679 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

tikia kwa adabu kile alichokuwa amekiagiza.


Kabla wageni wale hawajaruhusiwa kuanza kuingia kwa sababu
mpaka muda huo bado walikuwa wamezuia pale nje ya geti, ilibidi
niombe dakika chache za kujiridhisha kwa mara ya mwisho kama
kila kitu kipo sawa, nikaruhusiwa.
Kitu cha kwanza, ilikuwa ni kuanza kupita kwenye ‘points’ zote
za ulinzi kama ambavyo nilikuwa nimewapanga vijana wangu.
Nilianzia ndani kabisa ya ukumbi ambako ndiko namba moja ali-
kuwa anatarajiwa kuzungumza na wafanyabiashara wale.
Vijana wote waliokuwa wamepangwa, kila mmoja alikuwa
kwenye eneo alilopangwa, wakiendelea kufuatilia kwa makini kila
kinachoendelea lakini pia kila mmoja akiwa ‘standby’ kwa cho-
chote kinachoweza kutokea.
Nilitoka na kuelekea upande wa maliwatoni, kamera za siri zili-
kuwa zimefungwa kwenye kila eneo muhimu ili kuzuia mtu yeyote
asije kuingia na kufanya jambo linaloweza kuhatarisha usalama.
Nilipita kwenye ‘points’ nyingine zote muhimu za ndani, kila
mtu alikuwa amekaa mahali alipopangwa. Baada ya hapo, ni-
kaenda kwenye chumba cha kufuatilia mawasiliano, ambako nako
vijana walikuwa macho kwelikweli, wakifuatilia kila kilichokuwa
kinaendelea kwenye kamera zote za ulinzi kuanzia nje mpaka
ndani ya Magogoni.
Nilitoka na kuanza kufuatilia ‘points’ zote za nje, kwa maana ya
kuanzia juu ya paa la Magogoni ambako nako vijana walikuwa
wamejipanga kila mmoja kwenye eneo alilokuwa amepangwa.
Baada ya kujiridhisha, nilishuka na kwenda mpaka getini na

680 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

baada ya kuwa nimejiridhisha kwa asilimia mia moja, ndipo nili-


poruhusu sasa shughuli nyingine ziendelee.
Wageni wote walikuwa wakitakiwa kupita kwenye geti na ku-
kaguliwa, ikiwa ni pamoja na kupigwa picha bila wao kujijua,
kisha baada ya hapo, walikuwa wakitakiwa kupelekwa kwenye
chumba maalum cha kusubiria kisha ndiyo wapelekwe ukumbini,
chini ya uangalizi wa karibu kabisa kwa mfumo ambao tuliuba-
tiza jina la ‘man to man’, yaani kila mgeni mmoja asindikizwe na
afisa mmoja kwenye kila hatua alizokuwa anapita mpaka kufika
ukumbini.
Kwa mfumo huo, nilikuwa na uhakika kwamba hakuna mtu
yeyote anayeweza kuingia akiwa na silaha au kitu chochote cha
hatari, na hakuna njama zozote ambazo zingeweza kufanyika ndani
ya ‘ground zero’ na kusababisha hatari.
Kazi ilianza, magari yalikuwa yakikaguliwa kisawasawa am-
bapo vijana kutoka jeshi la polisi kitengo cha mbwa na farasi, nao
walikuwepo eneo lile wakiwa na mbwa maalum waliokuwa wame-
fundishwa kunusa harufu za milipuko ya aina yoyote.
Ukaguzi ulikuwa ni wa kiwango cha juu kabisa, wageni wa
kwanza takribani saba waliokuwa kwenye yale magari matatu,
wakasindikizwa mpaka ndani. Muda mfupi baadaye, magari men-
gine mawili yaliwasili, yakaongezeka mengine manne mwisho
yakawa yanawasili kwa mfululizo.
Kwa muda wote huo, akili yangu ilikuwa inafanya kazi kwa
kasi kubwa kuliko kawaida, nilikuwa macho pengine kuliko mtu
mwingine yeyote kuhakikisha vijana wetu wanafuata maelekezo

681 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

bila kufanya kosa hata moja, wageni wakawa wanazidi kumimini-


ka eneo lile na kupelekwa ndani kwa kufuata utaratibu uleule.
Muda wote nilikuwa makini sana kutazama saa yangu maana saa
moja na nusu, muda ambao tuliambiwa kwamba ndiyo umeme uta-
zimika, ulishapita bila kitu chochote kutokea.
Mpaka inafika saa mbili kasorobo za usiku, wageni wote walio-
kuwa wanatakiwa kuwepo, walikuwa wameshafika na kwa sababu
za kiusalama, ikabidi barabara zote za kuingia na kutoka eneo lile,
ziongezewe ulinzi na vizuizi, ambapo safari hii tuliweka vizuizi
vya barabarani vinavyoonekana, kuanzia mabomba maalum ya
chuma, nyaya za kutandaza kwenye lami pamoja na vifaa vingine
vyote vya kisasa vya ulinzi.
Muda wote mimi nikawa nacheza na kifaa changu cha ma-
wasiliano, huku mara kwa mara nikielekea kwenye chumba cha
kuongozea kamera kuona kama kuna chochote hakiendi kama
kinavyotakiwa kuwa.
Saa mbili kamili, ni muda ambao namba moja alikuwa anatakiwa
kuingia ukumbini, yeye akiwa ndiyo mtu wa mwisho kulingana na
itifaki kwa sababu ilikuwa inatakiwa akishaingia yeye, basi mila-
ngo mingine yote inafungwa kiasi kwamba hakuna mtu ambaye
angeweza kuingia wala kutoka mpaka mwisho wa shughuli hiyo.
Ni hapo sasa ndipo nilipoona umuhimu wa kwenda kuhakiki-
sha kama ‘double’ wa namba moja, naye yupo tayari kwa kazi
iliyokuwa mbele yake. Kwa sababu za kiitifaki, sikuwa na ruhusa
ya kwenda mahali alipo bila kupitia kwa kiongozi wa PSU, kikosi
maalum cha ulinzi wa namba moja.

682 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Kwa muda wote tuliokuwa tumefanya kazi pamoja tangu tu-


lipowasili, nilishakuwa nimezoeana na kiongozi huyo muhimu
na yeye alionesha kujenga imani kubwa na mimi kwa hiyo hata
nilipomueleza kwamba nataka kwenda kuzungumza na ‘double’ wa
namba moja kwa mara ya mwisho kuona utayari wake, hakuwa na
pingamizi.
“Tangu nianze hii kazi, sijawahi kupitia wakati mgumu kama
huu, mimi ni jasiri lakini moyo wangu unadunda kuliko kawaida,”
aliniambia wakati tukitembea kikamavu kwenye korido ndefu,
kuelekea kule alikokuwa ‘double’ wa namba moja.
“Unatakiwa kuishinda hofu ndani ya moyo wako,” nilimwam-
bia na kumpa moyo. Japokuwa nilitamka maneno hayo, ukweli ni
kwamba haya mimi nilikuwa natetemeka kuliko kawaida, nikiwa
sijui ni nini ambacho kingetokea dakika chache mbele.
Tulienda mpaka kule kwenye chumba maalum alichokuwepo
‘double’ wa namba moja, akiendelea kuifanyia mazoezi hotuba
aliyotakiwa kuitoa usiku huo.
Ilibidi tusimame pembeni kwanza na kumtazama jinsi alivyoku-
wa akiendelea kuifanyia mazoezi, akiwa anasimamiwa na wasaid-
izi wa namba moja. Kwa jinsi alivyokuwa akiendelea na mazoezi,
wote tuliridhika kwamba kila kitu kitaenda sawa.
Alipomaliza, ndipo tuliporuhusiwa sasa kwenda kuzungumza
naye, nikawa wa kwanza kumsogelea, kiongozi wa PSU naye akaf-
uatia nyuma yangu.
“Mheshimiwa rais!”
Niliita huku nikiwa namtazama, nikamuona amesita kidogo

683 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kuitikia, nadhani ni kwa sababu hakuwa amezoea kuitwa hivyo,


akaitikia huku akijichekesha kidogo kuficha makosa yake ya
kuchelewa kuitikia.
“Maandalizi yote yamekamilika na wageni wote wameshawasili,
unasubiriwa wewe tu,” nilimwambia, akatabasamu kwa mbali na
kutingisha kichwa kuonesha kukubaliana na nilichokuwa nakise-
ma.
“Unatakiwa ku-relax na usioneshe kitu chochote kitakachoweza
kuwashtua watu,” nilimwambia kwa sauti ya chini, nadhani bado
alikuwa anajiuliza ndani ya kichwa chake mimi ni nani na kwa nini
namwambia maneno yake?
Ilibidi nirudie tena kujitambulisha kwake na nikamueleza kwam-
ba mimi ndiye kiongozi wa oparesheni iliyokuwa inaendelea.
“Oparesheni gani?” alisema kwa mshtuko, nikagundua kwamba
kumbe hakuwa ameambiwa ni kitu gani kilichokuwa kinatarajiwa
kutokea au ni kwa sababu gani alichukuliwa yeye kwenda kuzung-
umza na wafanyabiashara na siyo namba moja mwenyewe.
Kabla sijajibu chochote, kiongozi wa PSU alinigusa kwa umakini
wa hali ya juu akiwa ni kama ananipa ishara fulani, nikawa nime-
shaelewa kinachoendelea.
“Oparesheni ya kusimamia ulinzi na usalama usiku wa leo,” nili-
jibu boila kubabaika hata kidogo.
“Ooh, sawa, haina shida kabisa!”
“Bila shaka umeshaelezwa kunapotokea dharura unatakiwa ku-
fanya nini.”
“Nimeelezwa na nimefanya mazoezi ya kutosha, huyu kamanda

684 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

amefanya kazi yake vizuri kwa hiyo usiwe na wasiwasi,” alisema


akimgusa begani kiongozi wa PSU, wote tukatabasamu.
“Nakutakia kazi njema!” nilisema huku nikimpa mkono, naye
akanipa wa kwake, tukashikana na kutazamana usoni.
“Nawe pia! Naamini mtanilinda vyema mimi kiongozi wenu,”
alisema huku akitanua mabega na kusababisha tucheke bila
kutarajia. Namna alivyokuwa ameiva kwa maelekezo aliyokuwa
amepewa, tulikuwa na uhakika kwamba kila kitu kitaenda kama
kilivyopangwa.
Baada ya kuzungumza naye, tuliruhusu ratiba nyingine ziendelee,
wasaidizi wa namba moja wakawa wanaendelea kumuandaa.
“Kwa nini hajaambiwa ukweli?”
“Hawezi kuhimili hofu kubwa kiasi hicho! Akiujua ukweli
anaweza kuungua picha nzima,” alisema kiongozi wa PSU.
“Hamuoni kwamba mnahatarisha maisha yake?”
“Hapana! Tumejipanga kisawasawa kumuokoa, chochote kita-
kapotokea, tupo tayari kukabiliana nacho,” alisema kiongozi wa
PSU, nikashusha pumzi ndefu huku tukiwa tunatazamana machoni
kama majogoo yanayotaka kupigana.
“Una uhakika?”
“Unataka kunifundisha kazi yangu sasa si ndiyo?”
“Sijamaanisha hivyo! Bila shaka unajua kwamba mimi ndiyo
nitakayejibu kila kitu endapo mambo yakienda ndivyo sivyo.”
“Bila shaka na wewe unajua kwamba mimi ndiye nitakayejibu
endapo jambo lolote likimtokea mheshimiwa!” alisema yule kion-
gozi wa PSU, hata sikuelewa ni nini kilichokuwa kimemkasirisha

685 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ghafla namna ile, ikabidi nishushe pumzi ndefu, tukawa tunaende-


lea kutazamana.
Tukiwa katika hali ile, taarifa mpya iliingia kupitia vifaa vy-
etu vya mawasiliano. Ilikuwa ni kutoka kwa maafisa waliokuwa
kwenye moja kati ya barabara za kuingilia ‘ground zero’ wakieleza
kwamba namba moja alikuwa amewasili akiwa na walinzi wake
wawili na walikuwa wanataka kuingia ndani.
Zilikuwa ni taarifa za kushtua mno kwa sababu tayari ilikuwa
imeshaamriwa tangu mapema kwamba kwa sababu za kiusalama,
namba moja hatakiwi kabisa kuwepo eneo hilo na alikuwa ame-
shapelekwa mafichoni kwenye moja kati ya ‘safe house’ zinazotu-
mika kwa ajili ya ulinzi wake.
Kwa kuwa mimi na kiongozi wa PSU wote tulisikia taarifa hiyo
kwa pamoja wakati tukiwa bado tunatazamana, tulijikuta wote
tukitoka kwa pamoja mpaka nje ambako tuliwakuta viongozi wote
nao wakikusanyana kwa dharura.
Kwa sababu za kiitifaki, hakuna yeyote kati yetu ambaye ali-
kuwa na uwezo wa kumzuia namba moja kwa wakati ule kwa hiyo
ndani ya muda mfupi tu, alikuwa tayari ameshapita kwenye vizuizi
vyote na sasa alikuwa kwenye geti kubwa.
Geti lilifunguliwa na gari alilokuwemo, likaingizwa mpaka kwe-
nye maegesho maalum ambayo huwa yanatumiwa na yeye tu.
Kila mmoja alikuwa amepigwa na bumbuwazi, tukiwa ni kama
hatuamini kilichokuwa kinaendelea.
“Nini kinaendelea?”
“Hata mimi sielewi! Labda tusubiri kumsikia mwenyewe anas-

686 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

emaje,” alisema baba yake Saima, mkurugenzi naye akakazia


hapohapo, ikabidi wote tusogee mpaka kule kwenye gari alilokuja
nalo, ambalo bado lilikuwa likiendelea kunguruma bila ya mtu
yeyote kuteremka.
Mara kioo kimoja cha upande wa dereva, kiliteremshwa kidogo,
mmoja kati ya walinzi wake akatoa ishara kwa mkono, akimuita
kiongozi wa PSU ambaye alikuwa miongoni mwetu, wote tukiwa
tunashangaa tu.
Alisogea mpaka pale kwa yule dereva, wakazungumza maneno
machache, akasogea kwenye mlango wa nyuma wa gari, ukafungu-
liwa, akaingia kisha mlango ukafungwa. Hatukuwa na uwezo wa
kuona chochote kwa sababu gari alilokuwa ametumia siku hiyo,
lilikuwa na vioo vya ‘tinted’ kila upande, mpaka mbele.
Muda mfupi baadaye, aliteremka, akasogea mpaka kwa mkuru-
genzi wetu, akamnong’oneza jambo, muda huohuo akasogea kwe-
nye mlango uleule aliokuwa ameteremka yule kiongozi wa PSU,
mlango ukafunguliwa, akaingia kisha ukafungwa.
“Ni hatari sana kwa yeye kuwepo hapa muda huu,” nilisema kwa
sauti ya chini, nikimwambia baba yake Saima ambaye alikuwa
amesimama pembeni yangu, akaishia tu kushusha pumzi ndefu.
Muda mfupi baadaye, mkurugenzi aliteremka kwenye gari, akaja
moja kwa moja pale tulipokuwa tumesimama.
“Ratiba zote inatakiwa zisimame mara moja!” alisema, kwa kuwa
yeye ni kiongozi na hali ilishakuwa tete, hakuna aliyeweza kum-
hoji chochote, akabonyeza kitufe maalum kwenye kifaa chake cha
mawasiliano, kisha akatoa maelekezo kwamba ratiba zote inataki-

687 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wa zisimame kwa muda mpaka itakapoelezwa vinginevyo.


Nilitazama saa yangu ya mkononi, ikaonesha ni tayari saa moja
na dakika hamsini na tisa, saa mbili kasoro dakika moja, muda
ambao ndiyo ‘double’ wa namba moja alitakiwa kuwa anaelekea
ukumbini kwenda kuzungumza na wale wafanyabiashara.
Baada ya agizo hilo, ilibidi mimi niwaache na kuelekea kule
ndani, kwenda kuhakikisha kama maagizo yanafuatishwa, nikaan-
zia ukumbini ambapo wageni walikuwa wamekaa kila mmoja
kwenye sehemu yake, wakiendelea kusubiri kwa shauku kubwa
kuzungumza na namba moja.
Hakuna yeyote kati yao aliyekuwa anaelewa ni nini kilichokuwa
kinaendelea. Nikatoka na kuelekea kwenye chumba alichokuwemo
‘double’ ambaye naye aliponiona tu, alisimama pale alipokuwa
amekaa.
“Nini kinaendelea? Mbona nimeambiwa nisubiri? Kuna nini?”
“Ni taratibu za kawaida, unatakiwa usubiri kama ulivyoelezwa,”
nilimwambia na muda huohuo, taa za mle ndani zikawa ni kama
zimecheza kidogo, umeme ukawa ni kama umepungua nguvu
kidogo kisha ukarudi kwenye hali yake ya kawaida, wote tukainua
macho kutazama taa, kufumba na kufumbua zote zikazima.
Nilitoka mbiombio mpaka koridoni, nikagiundua nako taa zi-
likuwa zimezima, nikakimbia mpaka nje, nako taa zote zilikuwa
zimezimwa, Magogoni yote ikawa giza tupu. Harakaharaka nili-
panda kwenye ngazi za kuelekea juu ya jengo zilizokuwa upande
wa pembeni, nikapanda juu na kutazama maeneo ya jirani, umeme
ulikuwa umekatika mji mzima.

688 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Harakaharaka niliteremka kule juu mpaka chini, kupitia vifaa vya


mawasiliano, maelekezo yakatolewa kwamba viongozi wote tuku-
tane kwenye moja kati ya bustani zilizokuwa mle ndani.
Wakati hayo yakiendelea, bado namba moja alikuwa ndani ya
gari lake, nadhani na yeye alishtuka mno baada ya kuona umeme
umekatika mpaka Magogoni, jambo ambalo halikuwa kawaida hata
kidogo.
“Nini kimetokea?” aliuliza baba yake Saima, akiwa anamtazama
kiongozi wa PSU.
“Majenereta yote yameshindwa kuwaka! Kwa kawaida huwa
umeme ukizima, yanajiwasha yenyewe kwa hiyo umeme huwa
haukatiki kabisa na hata huwezi kujua kama umeme umekatika.”
“Vijana wako wanasemaje?”
“Wanashughulikia, litakuwa ni tatizo la kiufundi!”
“Nadhani kuna shida mahali! Unawezaje kujibu kirahisi namna
hiyo kwamba ni matatizo ya kiufundi wakati mtoa taarifa ameletwa
mpaka mbele yetu na alishatueleza kuhusu hili suala la umeme
kukatika?”
“Mambo mengine yanakuwa nje ya uwezo wangu! Bila shaka
nyote mnaona jinsi mambo yalivyo magumu na muda huu nataki-
wa kubadilisha kabisa ratiba zote za kazi na kuelekeza nguvu kwa
namba moja,” alisema kiongozi wa PSU wakati akihojiwa, naye
akionesha kuchanganyikiwa kabisa.
Tukiwa bado hatujapata majibu, mara umeme ulirudi, wote tuka-
wa tunatazama huku na kule na tulibaini kwamba ulikuwa umerudi
mji mzima.

689 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“We are loosing this battle!” (Tunashindwa hii vita!) alisema


Chief Mwaipopo kwa Kiingereza, akionesha kuanza kukata tamaa.
“Imekuwaje namba moja ameingia mpaka huku ndani? Ina
maana vijana waliopo doria mji mzima hawakuweza kugundua
mapema ili tujue nini cha kufanya?”
“Gari alilotumia siyo gari ambalo huwa anatakiwa kutumia, hapa
hatutakiwi kulaumiana, bila shaka nao walijua ni maafisa wetu
wapo kazini! Si mnaona gari yenyewe ina namba za kiraia na vioo
vyote vipo tinted? Hapa kama kuna mtu wa kumlaumu, basi ni
namba moja mwenyewe na sote tunajua hakuna anayeweza kuml-
aumu.”
“Kwani yeye amesema kwa nini amerudi?”
“Mimi alichonijibu ni kwamba nyoka akiingia ndani ya nyumba,
baba wa familia huwezi kukimbia na kuiacha familia yako! Lazima
wewe ndiyo uwe mstari wa mbele kupambana mpaka kumuua
nyoka huyo!”
“Hata mimi pia ameniambia hivyohivyo,” alidakia mkurugenzi
wakati baba yake Saima akiwa amemkalia kooni kwelikweli kion-
gozi wa PSU.
“Uwepo wa namba moja eneo hili, muda huu, unafanya hili jam-
bo lizidi kuwa zito na gumu, tusipotumia uwezo wetu wote, hakika
tutashindwa vita hii kama alivyosema Mwaipopo. Tunachotakiwa
hapa sasa hivi, ni kujadiliana nini cha kufanya,” alisema baba yake
Saima.
Kila mtu akashusha pumzi ndefu, tukiwa bado tunatazamana,
umeme ulicheza tena na haukupita muda mrefu, ukazima kwa mara

690 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

nyingine, mji mzima ukawa giza.


“Hapa jambo la kwanza lazima tuhakikishe namba moja yuko
salama! Ni hatari sana kwa yeye kuendelea kukaa eneo la wazi
kama alipo, akishafika eneo salama ndipo tunapoweza kushughu-
likia mambo mengine,” alisema baba yake Saima, wazo ambalo
kila mmoja aliliafiki kwa sababu ni kweli kwamba mpaka wakati
huo, bado alikuwa ndani ya lile gari alilokuja nalo, akiwa na
walinzi wake.
Kiongozi wa PSU aliwasiliana na vijana wake, kwa maana ya
maafisa maalum ambao kazi yao ilikuwa ni kumlinda namba moja,
ambao walikuwa eneo hilo.
Ikumbukwe kwamba wakati namba moja anatolewa na kupele-
kwa mahali salama, aliondoka na kikosi chake chote cha ulinzi
kinachojumuisha maafisa kutoka kitengoni, maafisa kutoka PSU,
wanaovaa suti pamoja na wale wanaovaa kombati wakiwa na
silaha.
Lakini pia aliondoka na mabodigadi wake pamoja na mpambe
wake lakini aliporejea, alikuwa na watu wawili tu, bodigadi mmoja
ambaye ndiye aliyekuwa anasimama kama mlinzi wa kwanza
lakini pia alikuwa na mpambe wake.
Hilo nalo lilikuwa ni tatizo lingine kubwa sana katika usalama
wake kwa sababu, kwa kawaida viongozi wa mataifa duniani kote
huwa wanalindwa na vikosi vya watu wengi, ambao wengine wan-
aonekana na wengine hawaonekani au hata wakionekana, unakuwa
huwezi kujua kama nao ni walinzi.
Kwa pamoja, hawa huwa wanatengeneza kitu ambacho kitaal-

691 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

amu huitwa ‘layers of protection’ au ‘security rings’ na idadi ya


hizi hutegemeana na sera za nchi husika ambapo kwa nchi kama
Marekani, huwa zinakwenda mpaka nane kutegemea ni mahali
gani kiongozi yupo na jinsi mazingira yenyewe yalivyo.
Kinachofanyika ni kwamba walinzi wanakuwa wamejipanga na
kutengeneza kama miduara fulani kwa mpangilio wa kificho na
kila duara linakuwa na watu tofauti wenye kazi tofauti na katikati
kabisa ya miduara yote ndipo anapokuwepo namba moja mwe-
nyewe akifuatiwa na bodigadi mkuu ambaye anakuwa karibu zaidi
kuliko wote akifuatiwa na wasaidizi wake lakini pia kunakuwa na
mpambe wake, ambaye mara zote hukaa nyuma yake.
Sitafafanua sana jinsi wanavyojipanga, lakini kwa kifupi elewa
kwamba unapomuona kiongozi wa nchi akiwa mahali popote, jua
kwamba kuna idadi kubwa ya walinzi wake wanafanya kazi ku-
hakikisha hakuna jambo lolote baya linaloweza kutokea na hata
likitokea, wanakuwa wanajua ni nini cha kufanya kwa wakati gani.
Kwa hiyo unaweza kuona ni kwa namna gani kitendo cha namba
moja kurudi ‘ground zero’ kienyeji, kulifanya misheni ile iwe
ngumu kuliko kawaida.
Uzuri ni kwamba, walikuwepo maafisa wengine wengi ambao
nao hiyo ndiyo kazi yao, kwa hiyo kiongozi wa PSU hakupata
shida sana kuwakusanya na baada ya dakika zisizozidi tatu, kikosi
cha maafisa kutoka PSU wasiopungua kumi na mbili, walikuwa
wameshajipanga kwa kazi moja tu, ya kuhakikisha namba moja
anakuwa salama!
Mawasiliano yalifanyika kwa pande zote huku mimi nikiwa

692 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ndiyo kiungo muhimu kati ya pande zote na baada ya kila kitu ku-
kamilika, namba moja aliteremshwa kimyakimya kwenye kwenye
gari lake, akaongozwa gizani kuingia ndani.
Makubaliano maalum ya siri ilikuwa ni kwamba hatakiwi mtu
yeyote asiyehusika kujua kilichokuwa kinaendelea kisha apelekwe
kwenye sehemu maalum iitwayo ‘vault’ mpaka tutakapokuwa
na uhakika ni nini kilichokuwa kinaendelea. Nitakuja kufafanua
‘vault’ maana yake ni nini na hutumika wakati gani.
Nadhani hata mwenyewe hakuwa ametegemea kwa alichokutana
nacho na ndiyo maana akalazimika kuwa mpole na nahisi kabisa
ndani ya moyo wake alikuwa anajutia uamuzi wake wa kuvunja
makubaliano kwa sababu eneo hilo halikuwa salama tena!
Nililibaini hilo wakati nikipishana naye koridoni ambapo ali-
poniona, japokuwa ilikuwa ni gizani tukiongozwa na tochi kali
zilizokuwa zinawashwa na kuzimwa, alinionesha ishara fulani am-
bayo niliweza kuilewa vizuri kabisa. Hili pia nitakuja kulifafanua
baadaye.
Basi alipelekwa mpaka ‘vault’, muda wote mimi nikawa na kazi
ya kuingia na kutoka kuhakikisha nakuwa macho na kila kili-
chokuwa kinaendelea, jengo zima bado likiwa gizani huku tukiwa
tunawasiliana kila baada ya sekunde chache kuhakikisha kwamba
kila kitu kinakwenda kama kilivyopangwa.
Muda mfupi tu baada ya kuwa amefikishwa ‘vault’, ziliingia ta-
arifa nyingine ambazo zilizidi kutuchanganya! Zilikuwa ni taarifa
za vijana waliokuwa wamejipanga kwenye barabara zote za kuin-
gia na kutoka, ambao walituarifu kwamba eti kulikuwa na mafundi

693 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

umeme wakiwa kwenye magari mawili walikuwa wanataka kwen-


da kushughulikia hitilafu ya umeme iliyokuwa imetokea.
“Nani amewaita? Kuna yeyote aliyetoa taarifa kwamba kuna hiti-
lafu ya umeme?” niliuliza kwenye vifaa vya mawasiliano, haku-
kuwa na majibu! Swali likawa, ni mafundi gani hao na wameitwa
na nani? Shida ya umeme ipo mji mzima, kwa nini wao wapange
kuelekea eneo lile pekee? Maneno ya Ustaadh Fundi sasa yalianza
kutimia!
Huo ulikuwa ni mtego mwingine wa hatari kwelikweli, na mbaya
zaidi ni kwamba namba moja alikuwepo eneo la tukio na yeye
ndiye aliyekuwa mlengwa wa kila kilichokuwa kinaendelea.
Akili yangu ilinituma kuamini kwamba, kilichokuwa kina-
fanyika, ilikuwa ni kutuchezea akili, nikatoa maagizo kwamba
‘mafundi’ hao wazuiliwe kulekule walikokuwa wamesimamishwa
na kamwe wasiruhusiwe kusogea kule ‘ground zero’.
“Unaposema wasiruhusiwe kuingia, je, kama ni mafundi kweli?”
“Kwa hiyo wewe unaona ni busara watu hawa wakaruhusiwa
kuingia? Unajua kwamba mifumo yote ya kiusalama inategemea
umeme? Vipi kama ni wahalifu? Si wanaweza kuingia na silaha za
hatari humu ndani?”
“Tumeulizana hapa kwamba kama ni mafundi, wamepewa na
nani taarifa kwamba umeme umekatika huku wakati siku zote
inafahamika kwamba hata umeme ukatike nchi nzima, Magogoni
lazima uwepo?”
“Sidhani kama ni sawa kuanza kubishana! Tupo gizani, hatuwezi
kuendelea kukaa gizani, lazima taratibu za haraka zifanyike ku-

694 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

tatua hili tatizo na mimi naona njia nyepesi kwa sasa, ni kumpigia
simu mkurugenzi wa shirika la umeme, yeye ndiye anayeweza ku-
tuambia tatizo ni nini na kipi kifanyike,” alisema baba yake Saima,
akiingilia majibizano yaliyokuwa yanaendelea kati yetu.
“Ulichokisema ni sawa lakini kwa sababu tunajua itachukua
muda, kwa nini vijana wetu waliosomea ufundi wa umeme wa
majumbani na viwandani wasiitwe haraka kuja kuangalia namna
ya kushughulikia haya majenereta? Tena ikiwezekana waje na jen-
ereta lingine kubwa la ziada haraka iwezekanavyo,” alisema Chief
Mwaipopo, wote tukakubaliana na alichokuwa amekisema kwa sa-
babu alikuwa amefikiri ‘nje ya boksi’ kama wanavyosema vijana.
“Lakini huu pia ni uzembe! Kiongozi wa oparesheni, ulishakuwa
na taarifa kwamba kutatokea hitilafu ya umeme na majenereta
yatashindwa kufanya kazi.
“Kwa nini hukuwasiliana na hao vijana wakafika hapa mapema
na kukaa ‘standby?’, kwa hiyo tulikuwa tunasubiri mpaka tatizo
litokee,” alisema kiongozi wa PSU ambaye ndiyo kwanza alikuwa
amerejea kutoka kumpeleka namba moja sehemu salama kule
ndani.
Lilikuwa ni swali gumu ambalo lilikuwa limeelekezwa kwangu
na kwa sababu alichokuwa amekisema kiongozi wa PSU kilikuwa
ni ukweli ambao upo wazi hata kama alikuwa na chuki dhidi yangu
ambayo hata sijui ilikuwa imesababishwa na nini, nilishindwa cha
kujibu.
“Huu siyo muda wa kulamiana! Narudia tena kusisitiza, huu siyo
muda wa kulaumiana kwa sababu tukianza kuchunguzana hapa,

695 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kila mmoja ana makosa yake!


“Suala la majenereta kushindwa kuwaka, linakuhusu wewe zaidi
kwa sababu wewe ndiyo kiongozi wa kikosi cha ulinzi wa namba
moja na unajua kabisa kwamba kukosekana kwa umeme ni hatari
kubwa kwa ulinzi wake,” alisema baba yake Saima, wote tukashu-
sha pumzi kwa sababu alikuwa amelenga sehemu sahihi kabisa.
Mkurugenzi alitoa simu yake ya mkononi, nadhani alikuwa
ameshasahau kwamba tulikuwa tumezima mawasiliano yote ya
kawaida na njia pekee ilikuwa ni kupitia ‘chaneli’ moja tu ya vifaa
vya mawasiliano.
Alibofyabofya simu yake na kuiweka sikioni, baba yake Saima
akamkumbusha, akaitoa simu sikioni na kuanza kuzungukazun-
guka, nadhani na yeye kichwa kilikuwa kimeshapata moto.
“Hatuna sababu za kuchanganyikiwa, hebu naomba kila mmoja
atulize kichwa chake,” alisema baba yake Saima, akabofya kifaa
chake cha mawasiliano, akawa anazungumza na ofisi kuu kwa
sababu kule nako walikuwa wameunganishwa kwenye ile ‘chaneli’
pekee ya mawasiliano iliyokuwa wazi.
Sote tulisikia alichokuwa akikizungumza na ofisi kuu, aliagiza
kuletwa haraka iwezekanavyo kwa jenereta la akiba pamoja na
mafundi sita kutoka kitengoni lakini pia akataka mkurugenzi wa
shirika la umeme apigiwe simu na kuelezwa kuhusu kilichokuwa
kimetokea.
Wote tulishusha pumzi ndefu baada ya baba yake Saima kum-
aliza kutoa maagizo, tukawa tumeganda palepale tulipokuwa tu-
mesimama, kila mmoja akionesha ‘kupagawa’ na kila kilichokuwa

696 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kinaendelea.
Tukiwa katika hali ile, ghafla tulishtushwa na milio ya risasi,
ambayo ilionesha kurindima kutoka mbali kidogo na pale tulipoku-
wepo, ikitokea upande wa mitaa iliyokuwa jirani na ‘ground zero’,
harakaharaka nikabofya kifaa changu cha mawasiliano kwa lengo
la kutaka kusikia kutoka kwa vijana wangu waliokuwa eneo milio
ile ilikosikika.
Kabla hata sijazungumza chochote, mmoja kati ya vijana wetu
walioripoti kuhusu kuwasili kwa mafundi waliokuwa wanadai
wanakwenda kushughulikia suala la umeme Magogoni, aliripoti
kwamba mafundi wale walikuwa wametoa silaha na kuanza ku-
fyatua hovyo, wakitaka waruhusiwe kupita vinginevyo watawapiga
risasi.
“Permission to engage granted!” alisema baba yake Saima,
nadhani ni baada ya kuona siyo mimi, mkurugenzi wetu wala yule
kiongozi wa PSU anayetoa amri ya nini kifanyike.
Msemo huo wa Kiingereza, huwa unamaanisha kwamba sasa
mnaruhusiwa kuanza kufyatua risasi kujibu mashambulizi pale
mnaposhambuliwa, risasi zikaanza kurindima, safari hii mfululizo.
Milio ile ya risasi ilizua taharuki kubwa si tu kwa wageni walio-
kuwa kule ndani bali kwa kila mtu aliyeisikia. Halikuwa jambo la
kawaida kabisa kusikia milio ya risasi jirani na ‘ground zero’.

697 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

698 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

26
A
KILI ya haraka ilinicheza kwamba sitakiwi kuen-
delea kuzubaa eneo lile bali kwenda mpaka mstari
wa mbele kuongeza nguvu kwa sababu hiyo ndiyo
ilikuwa maana halisi ya uongozi.
Nilitoka mbio pale tulipokuwa tumesimama na
kukimbilia mpaka getini, vijana wetu kadhaa waliokuwa na silaha,
nao wakawa wananifuata kila mmoja akikimbia huku akiiweka
vizuri silaha yake mkononi.
Tulitoka nje ya geti na kuanza kukimbia kwa tahadhari kubwa
kuelekea kule milio ile ilikokuwa inasikika na kadiri nilivyokuwa
nazidi kusikia milio hiyo, ndivyo ile ‘roho ya kazi’ ilivyokuwa
699 AZIZ HASHIM
MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

inazidi kunipanda.
Muda wote nilikuwa makini kusikiliza ni nini kilichokuwa kinar-
ipotiwa kupitia vifaa vyetu vya mawasiliano, mara ikaingia taarifa
mpya kwamba wale ‘mafundi’ wamevunja kizuizi cha barabarani
na kupita kwa nguvu na magari yao huku wakiendelea kufyatua
risasi.
Sikuwa na wasiwasi kwa sababu nilikuwa na uhakika kwamba
hawatachukua raundi kwa sababu kulikuwa na vizuizi vingine
viwili mbele, nikatoa maelekezo ya vijana wangu kutoruhusu
wendawazimu hao wapite kwenye vizuizi hivyo kwa namna yoy-
ote ile, mimi na vijana wangu tukawa tunazidi kukimbia kuelekea
kule risasi zilizokuwa zinatokea, kila mmoja silaha ikiwa miko-
noni.
Tukiwa tunakaribia kufika kwenye kizuizi cha kwanza kutokea
geti kuu, jambo lisilo la kawaida lilitokea na kunifanya nijihisi ni
kama nataka kuchanganyikiwa.
Zilikuwa ni taarifa nyingine mpya kwamba kuna boti mbili zili-
kuwa zinaonekana kuja kwa kasi kutokea baharini kuja upande wa
nyuma wa Magogoni na maafisa wa kikosi cha wanamaji walipo-
jaribu kuzisimamisha, waliokuwa ndani yake walianza kufyatua
riasi.
“Zinakuja kwa kasi kubwa na taa zote zimezimwa,” alisema afisa
mmoja wa kikosi cha wanamaji kupitia vifaa vya mawasiliano, ni-
kajikuta nimefunga breki za ghafla, vijana wangu nao wakasimama
nyuma yangu na kwa kuwa nao walikuwa wamesikia kinachori-
potiwa, walibaki wakinitazama kusikia nitatoa uamuzi gani, kila

700 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

mmoja akiwa anahema kutokana na kukimbia kwa kasi.


Ilibidi niwagawe kwa ishara, wengine waendelee kwenda kuon-
geza nguvu kisha mimi nikageuza na wengine kadhaa na kuanza
kutimua mbio kuelekea upande wa nyuma wa Magogoni, kule
tulikoambiwa kwamba zile boti ndiko zinakotokea.
Muda huohuo, zikaingia tena taarifa nyingine kwamba moja
kati ya chemba za maji taka upande wa kushoto wa ‘ground zero’,
zilikuwa zimefunuliwa na ilionesha ni kama kuna watu wameingia
kupitia chemba hizo na sasa walikuwa ndani ya uzio.
Zilikuwa ni taarifa za kushtua na mbaya pengine kuliko habari
nyingine zote zilizokuwa zimeingia kwa muda huo! Maadui ku-
ingia ndani ya uzio wa Magogoni, tena namba moja akiwa ndani?
Hakika mambo yalikuwa yameharibika.
Nilijikuta ni kama nimepagawa, nikiwa sielewi nikimbilie wapi
muda huo. Nilichekecha akili ndani ya sekunde kadhaa, wazo
nililoona bora kwa wakati huo, ilikuwa ni kuwagawa kwa mara
nyingine vijana wangu waliokuwa nyuma yangu, wengine waende
kule tulikuwa tunaelekea na sisi wengine turudi haraka Magogoni
kwenda kushughulika na kilichokuwa kimetokea.
Ndani ya dakika chache tu, tayari tulikuwa tumeshafika kwe-
nye geti kubwa, tukaingia ndani ambako taharuki kubwa ilikuwa
imetanda, maafisa wakikimbizana huku na kule, wakiwa na tochi.
“Mambo yameharibika! Wameingia ndani!”
“Akina nani?”
“Vijana wa Abdulwaheed!”
“Inawezekanaje? Yaani ulinzi wote huu inawezekanaje wapenye

701 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

na kuingia ndani?”
“Njoo ujionee mwenyewe,” alisema baba yake Saima ambaye
aliponiona tu nimeingia, licha ya giza lililokuwa limetanda kila
upande, alinifuata na kunisimamisha.
Alipiga hatua ndefu, mikononi mwake akiwa na bunduki na tochi
ndogo yenye mwanga mkali, na mimi nikawa namfuata kwa hatua
ndefundefu, mapigo ya moyo yakidunda mithili ya ngoma.
Alinipeleka mpaka upande wa kushoto wa jengo kubwa, tu-
katembea umbali wa mita kadhaa kwenye bustani nzuri zilizokuwa
zikihudumiwa vizuri, safari yetu ikaishia kwenye chemba ya maji
taka, ambayo mfuniko wake ulikuwa umefunguliwa.
Akamulika ndani na kunitaka nitazame vizuri. Kulikuwa na ngazi
ya chuma ambayo hata sijui iliwekwaje ndani ya chemba hiyo.
Kubwa zaidi, kulikuwa na nguo kadhaa zilizokuwa zimechafuka
na maji taka, zikiwa zimerundikwa kwenye moja ya kona za shimo
hilo.
“Wamebadilisha nguo zao na inaonesha wametoka wakiwa
wamevaa kama maafisa wa humu ndani, na pengine tayari wame-
ingia ndani kabisa mpaka kwenye ukumbi wa mikutano,” alisema
baba yake Saima, nikatingisha kichwa nikiwa ni kama siamini
alichokuwa anakisema.
“Tazama!” alisema huku akimulika na tochi yake na kunionesha
alama za viatu kutoka pale kwenye mfuniko wa ile chemba.
“Huu ni uzembe mkubwa sana umefanyika! Watu wanawezaje
kuingia kirahisi namna hii? Yaani ulinzi wote huu tuliokuwa nao?”
“Na sio tu kuingia, lakini pia kuingia wakiwa na silaha,” alisema

702 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

huku akimulika pembeni kidogo, macho yangu yakatua kwenye


‘magazine’, makasha maalum ya kuhifadhia risasi ambayo hu-
chomekwa kwenye bunduki. Kwa uzoefu wangu wa harakaharaka,
nilitambua kwamba ni magazine ya AK-47, silaha hatari za kivita.
Mwili wote uliniisha nguvu, kibaya zaidi ni kwamba milio ya ri-
sasi ilikuwa ikiendelea kusikika kutokea pande mbili, kule upande
wa baharini na kule upande wa barabara moja ya kuingilia, ambako
wale waliojifanya kuwa mafundi umeme walikuwa wakitumia
nguvu kutaka kuingia mpaka ‘ground zero’.
“Tunafanyaje? Si... sielewi! Sijawahi kushindwa lakini safari hii
nadhani nimeshashindwa mapema kabisa!”
“Tuliza kichwa chako!”
“Nawezaje kutuliza kichwa wakati inaonesha tumeshashindwa?”
“Hatujashindwa na hatuwezi kukubali kushindwa kirahisi namna
hii!”
“Nyoka wameingia chumbani kwetu, familia nzima ikiwa ndani!”
“Namba moja amefanya kazi imekuwa ngumu sana, sijui ni nani
aliyemshauri arudi katika wakati mgumu kama huu,” alisema baba
yake Saima. Akanitaka nitoe taarifa kwa timu nzima kwamba
kuna wavamizi walikuwa wamefanikiwa kuingia mpaka ndani
na uwezekano mkubwa, ni kwamba watakuwa wameingia mpaka
kwenye chumba cha mikutano, tena wakiwa na silaha.
“Kwa nini usitoe taarifa wewe?”
“Wewe ndiyo kiongozi wa oparesheni, unatakiwa kutuliza kich-
wa chako na kuonesha ukomavu! Kila mtu anakutazama wewe,
tukishinda, sifa zitakuwa kwako, tukishindwa pia lawama zitakuwa

703 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kwako,” alisema, nikameza funda la mate na kushusha pumzi


ndefu.
“Huu ndiyo muda wa kuonesha ukomavu wako!” alisema baba
yake Saima, nikashusha pumzi nyingine ndefu.
Njia pekee ambayo niliona inaweza kutusaidia kwa wakati huo,
ilikuwa ni kuwakusanya vijana wangu wote haraka iwezekanavyo
na kujipanga upya kwa sababu ilionesha kwamba mipango tuli-
yokuwa tumeipanga awali, yote ilikuwa imevurugika.
Wale waliokuwa wamepangwa kwenye ‘station’ maalum pale
ndani, na wale ambao walikuwa wakiendelea na mapambano ya
kuwazuia wavamizi zaidi wasiweze kupenya na kuingia ndani, nili-
wapa maelekezo ya kuendelea na walichokuwa wanakifanya, kwa
nguvu na kasi kubwa zaidi.
Ndani ya dakika mbili tu, vijana walikuwa wameshakusanyika
mbele ya mlango kubwa wa kuingilia ndani, kila mmoja akiwa na
silaha. Nikarudia kuwaeleza kilichokuwa kimetokea na kuwaeleza
kwamba kwa wakati huo, kitu cha kwanza ambacho tulikuwa
tunatakiwa kukifanya, ilikuwa ni kuwatoa nyoka ndani ya nyuma
kwanza.
Niliwaeleza kwamba mimi ndiye nitakayekuwa kiongozi na seh-
emu ambayo tutaanzia, itakuwa ni ndani ya ukumbi wa mikutano,
kisha kwenye maeneo mengine yote ambayo tunahisi wanaweza
kuwa wamejificha lakini baada ya hapo, tutatakiwa kuwanza kuwa-
sogeza nyuma wale waliokuwa wakijaribu kuingia, kwa nguvu zetu
zote.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, niliwagawa vijana wangu

704 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

na kazi ikaanza mara moja. Kwa bahati nzuri zaidi, tayari vijana
wa ‘kitengoni’ walikuwa wameshawasili na jenereta la akiba,
wakaunganisha mitambo na ndani ya dakika zisizozidi tan, tayari
umeme ulirudishwa kwenye jengo zima.
Nikaagiza milango yote ambayo ilikuwa ikilindwa kwa mifumo
ya umeme, ‘ilokiwe’ ili asiwepo mtu yeyote ambaye angeweza
kuingia au kutoka bila kutambulika.
Kuwashwa kwa umeme kulitusaidia kuliko maelezo, wale wa-
huni waliokuwa wanajifanya ni mafundi, walidhibitiwa wote na
kufungwa pingu, wakaletwa ndani na kupelekwa kwenye ‘selo’
maalum ya chini ya ardhi iliyokuwa ‘ground zero’.
Lakini pia, kwa kuwa sasa umeme ulikuwepo, taa kubwa zenye
nguvu ziliwashwa upande wa kule baharini ambako wale wahuni
waliokuwa wakijaribu kusogea na boti zao, nao waliweza kud-
hibitiwa kisawasawa na vijana waliokuwa wameapa kufia nchi yao.
Kazi iliyobakia, ikawa ni kwa upande wangu na vijana wangu
wa ndani, kuhakikisha tunawatoa nyoka kabla hawajaleta madhara.
Tulianzia ukumbi wa mikutano ambapo nilitangaza kwamba watu
wote wanatakiwa kutulia sehemu walizokuwa wamekaa na hat-
akiwi mtu yeyote kunyanyuka.
Niliamini kwa wakati huo, teknolojia inaweza kutusaidia kuwa-
baini wahusika kwa haraka bila kutumia nguvu nyingi. Eneo lote la
Magogoni, lilikuwa na kamera maalum ambazo zenyewe zilikuwa
na uwezo wa kufanya kazi hata kwenye giza totoro.
Nikabonyeza kifaa changu cha mawasiliano na kuzungumza na
vijana waliokuwa kwenye ‘control room’, nikawakata watazame

705 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kwa makini ni nini kilichokuwa kimetokea kwenye chemba ili-


yokuwa imefunuliwa upande wa kushoto wa ‘ground zero’.
Ndani ya muda mfupi tu, taarifa zikawa zimeshapatikana, ika-
bidi nitoke mwenyewe mpaka ‘control room’ kwenda kujionea
kilichokuwa kimenaswa na kamera muda ule umeme ulipokuwa
umekatika.
Ndani ya muda mfupi tu, tayari nilikuwa mbele ya kompyuta
kubwa nikitazama kila kilichokuwa kimerekodiwa ndani ya dakika
zile chache ambazo umeme ulikatwa, nikashtuka kuliko kawaida
kwa kile nilichokuwa nakiona.
Kundi la takribani watu saba, wanaume wa miraba minne, ambao
miili yao ilikuwa imejengeka kimazoezi kisawasawa, walionekana
wakitoka kwa kusaidiana kutoka kwenye ile chemba, wote wakiwa
wamevalia mavazi maalum kama yanayovaliwa na maafisa wa
Magogoni wanaohusika na masuala ya ulinzi na usalama.
Nilijaribu ‘kuzoom’ picha moja kwa karibu, na kubaini kwamba
nao walikuwa na vifaa vya mawasiliano masikioni mwao, jambo
ambalo pengine lingefanya iwe vigumu sana kuwatofautisha wao
na maafisa halisi wanaofanya kazi Magogoni.
Kilichozidi kunishtua zaidi, ni kwamba baada ya kutoka kwenye
ile chemba, walijipanga kwa umakini wa hali ya juu kama am-
bavyo maafisa wetu huwa wanafanya wanapokuwa wakidumisha
ulinzi na usalama na walikuwa na tochi zenye mwanga mweupe
mkali kama ambazo vijana wangu walikuwa nazo.
Nikawa nazidi kufuatilia kwa makini nyendo zao, kumbe baada
ya kutoka upande ule, walijichanganya na maafisa wetu waliokuwa

706 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wakiendelea na doria na mara kwa mara walikuwa wanaonekana


wakizungumza kuhusu vifaa vya mawasiliano.
Yote tisa, kumi ni kwamba, walisogea kwa ujanja wa hali ya juu
na wakafanikiwa kuingia mmoja baada ya mwingine kwa kupitia
lango kuu, wakionesha kuwa wazoefu kabisa wa mazingira yale
kiasi kwamba haikuwa rahisi kwa mtu yeyote kushtukia chochote.
“Mungu wangu!” nilisema na kutoka haraka kwenye kile chumba
maalum cha kufuatilia mawasiliano na kamera zote, nikakimbia
mpaka kwenye ukumbi wa mikutano, vijana wangu wakawa wa-
nanishangaa kwa jinsi nilivyokuwa natweta.
Kila mtu alikuwa amekaa na kutulia kama nilivyokuwa nime-
agiza, kuanzia wageni mpaka wale wasichana wahudumu na vijana
wangu pamoja na maafisa wa Magogoni, walikuwa wakipita huku
na kule kuhakikisha hakuna yeyote ambaye atakaidi amri ile.
Nilianza kwa kuanza kuwapitia maafisa wote waliokuwa waki-
dumisha ulinzi mle ndani, nikawa namtazama kila mmoja usoni,
nadhani hawakuwa wameelewa ni nini nilichokuwa nakifanya, nao
wakawa wananishangaa. Nadhani kuna wengine walihisi pengine
nimeanza kurukwa na akili.
Hakukuwa na sura ngeni hata moja, nikaanza kupita kwenye
viti vya wageni, bunduki ikiwa mkononi na kidole kikiwa kwenye
‘trigger’, kitufe cha kufyatulia risasi.
Niliwatazama mmoja baada ya mwingine na kwa kuwa niliku-
wepo wakati wote wakiingia, nilikuwa na uhakika kwamba endapo
kungekuwa na sura ngeni yoyote, ningeweza kuitambua lakini
haikuwa hivyo.

707 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Wote walikuwa ni walewale walioingia mapema kabla mambo


hayajaharibika na kila mmoja alikuwa ametulia kwenye siti yake.
Nikazidi kuchanganyikiwa, nikarudia kuwatazama wote harakaha-
raka, hakukuwa na yeyote ambaye ningeweza kumtilia mashaka.
Nikawa napiga hatua ndefundefu kuelekea kwenye mlango wa
ndani, ambao ‘double’ wa namba moja alitakiwa kuingilia ukumbi-
ni pale, ambao ulikuwa ni tofauti na mlango unaotumiwa na watu
wengine wa kawaida.
Mlango ulikuwa umefungwa kama nilivyokuwa nimetoa maelezo
na kwa kawaida, milango yote muhimu huwa inafunguliwa kwa
kadi maalum za ‘kuswipe’. Nilitoa kadi niliyokuwa nayo, nikaja-
ribu kuswipe lakini mlango haukufunguka, nikajaribu mara ya pili
na ya tatu, ikawa vilevile.
Akili za haraka zikanituma kuwasiliana na vijana waliokuwa
‘control’ room na kuwapa maelekezo kwamba wau-unlock mlango
huo kwa sababu nilihisi pengine ulikuwa umelokiwa kama nili-
vyokuwa nimetoa maelekezo.
Kwa kuwa kila mlango ulikuwa na namba, haikuwa kazi ngumu
kutoa maelekezo lakini ajabu ni kwamba, majibu ambayo nili-
yapokea kutoka kwa vijana wa ‘control’ room, mlango huo uli-
kuwa umeharibiwa ‘sensor’ kwa ndani, ambayo ndiyo hutumika
kuweka na kutoa ‘lock’ kwa hiyo hakukuwa na uwezekano wa
kuufungua kwa kutumia ‘system’ labda kwa kuuvunjwa kwa ku-
watumia mafundi wetu.
Taa nyekundu iliwaka kwenye kichwa changu, nikarudi haraka
na kutumia mlango uliokuwa unatumika na watu wengine, ile

708 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

naufungua tu, nilikutana na baba yake Saima na Chief Mwaipopo


ambao nao walikuwa wakija kule kwenye chumba cha mikutano,
tukakutana mlangoni.
Kwa jinsi ilivyoonesha, ni kama walikuwa wakinifuata mimi,
kila mmoja akiwa anatweta kwelikweli, baba yake Saima akanipa
ishara ya kumfuata, tukatoka na milango ikajifunga, tukapiga hatua
kadhaa kwenye korido.
“Kuna tatizo kubwa!”
“Milango ya chumba alichokuwemo ‘double’ yote imeharibiwa
‘sensors’ kutokea ndani na hatuwapati watu waliokuwa wakimuan-
daa,” alisema baba yake Saima, wote tukasimama kwa sababu sasa
ilionesha mambo yanazidi kuwa magumu.
“Lakini si namba moja yupo kwenye ‘vault’, si ndiyo?”
“Inabidi tukahakikishe, wewe nenda ‘vault’ haraka wakati sisi
tunaendelea kutafuta njia ya kufungua milango!”
“Hapana, kwa nini mmoja kaati yenu ndiyo aende ‘vault’? Nahisi
kazi kubwa na ya muhimu ipo hapa zaidi!”
“Kwani wa muhimu ni nani? Double au namba moja? Na ki-
ongozi wa oparesheni ni nani?” alisema baba yake Saima, ubishi
ukaniisha kwa sababu alichokuwa amekisema kilikuwa ni ukweli
mtupu.
“Ipatikane ramani ya jengo zima na nahisi tuelekeze nguvu zaidi
kwenye mifumo ya maji safi na maji taka! Kama wameweza kuin-
gia kwa kupitia chemba, lazima watakuwa wameshaisoma ramani
vizuri na watataka kutumia njia hiyohiyo kutoka au kuzidi kuingia
kwa wingi,” nilisema, wote wakatingisha vichwa vyao, tukaachana

709 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

na mimi nikaanza kukimbia kuelekea kwenye ‘vault’.


Nilidokeza kidogo kuhusu ‘vault’ na kueleza kwamba nitakuja
kufafanua zaidi ni kitu gani. Kwa kifupi, ikulu zote duniani, huwa
zinakuwa na chumba maalum cha chini ya ardhi, ambacho huwa
ndiyo sehemu salama zaidi kuliko zote ndani ya ikulu.
Kwa mfano, Ikulu ya Marekani, The White House, ‘vault’ yake
imepewa jina la ‘The Situation Room’ na hapa ndipo sehemu ya
mwisho ambayo rais wa nchi hiyo hupelekwa, inapotokea kume-
tokea shambulio lolote linalohusu ikulu.
Njia zote za kuingia kwenye ‘vault’ huwa zinafungwa kwa mi-
lango maalum ya chuma na mizito, kama ile inayotumika kufunga
kwenye ‘safe’ za benki, mahali kunakohifadhiwa fedha au dha-
habu.
Kwa hiyo, kabla hata hujafika kwenye ‘vault’ yenyewe, ni lazima
kwanza upite kwenye milango hiyo ambayo huwa inafungwa na
kufunguliwa kwa namba maalum ambazo huwa ni watu wachache
sana wanaozijua.
Baada ya kuingia kwenye mlango wa kwanza wa Vault, huwa
kunakuwa na korido nyembamba ambazo zimejengwa kwa chuma
kizito pande zote na inategemeana na nchi husika, huwa kunakuwa
na milango migumu na mizito ya chuma kadhaa mpaka kufikia
kwenye mlango wa kuingilia ndani kabisa ya ‘vault’ ambao huo
ndiyo huwa mkubwa na mzito zaidi, ukiwa umetengenezwa kwa
chuma kigumu.
Ndani kabisa ya ‘vault’, huwa kunakuwa na ofisi ndogo ambayo
inaweza kuchukua watu kadhaa kwa wakati mmoja, kukiwa na vi-

710 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

faa vya kisasa vya mawasiliano na vifaa vingine vyote muhimu vya
mawasiliano ya namba moja, hiyo ni kwa mataifa yote duniani na
kadiri taifa linavyokuwa na nguvu za kijeshi na kiusalama, ndivyo
ambavyo hata ‘vault’ zao huwa zinakuwa kubwa na imara zaidi.
Kuta za ‘vault’, hufanya iwe vigumu kwa silaha ya aina yoyote
kupenya. Unaambiwa hata ikitokea ikulu husika ikapigwa kwa
makombora mazito, ndani ya ‘vault’ huwa hakuna kinachoweza
kupenya kwa hiyo usalama wa kiongozi wa nchi, huwa unakuwa
salama kwa asilimia mia moja.
Tukija kwa Magogoni sasa, sitaeleza zaidi kuhusu jinsi ‘vault’
yake ilivyo kwa sababu za kiusalama, lakini kwa kifupi, elewa
kwamba ndiyo sehemu salama zaidi anapoweza kupelekwa namba
moja kunapotokea tatizo lolote lakini pia siyo kila mtu anaweza
kuingia huko. Wengine hufanya kazi kwa miaka mingi bila kujua
kama kuna kitu kama hicho.
Kwa hiyo nilichokifanya, ilikuwa ni kuwasiliana na vijana wa
‘control room’ na kwa kuwa suala lenyewe lilikuwa nyeti, ilibidi
kiongozi wao ndiyo atoe ruhusa ya mimi kuingia kule ndani amba-
po pia ilibidi kiongozi wa PSU naye aidhinishe na yeye ndiye aliy-
etakiwa kuniongoza, nikawa naliona tatizo lingine mbele yangu.
Baada ya kama dakika tatu, mimi na kiongozi wa PSU tulikuwa
kwenye geti la kwanza la kuingia kwenye korido ya kushuka chini
kuelekea kwenye ‘vault’. Hakuna aliyekuwa anamsemesha mwen-
zake, hata sijui hii chuki ilikuwa imetokea wapi.
“Unajifanya mjuaji sana wewe!” alisema kiongozi wa PSU
wakati tukisubiri mlango ufunguliwe huku akinitazama kwa macho

711 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

makali. Sikumjibu kitu zaidi ya mimi pia kumkazia macho, mlan-


go mgumu wa chuma ukafunguka.
Tulitazamana tena kama majogoo yanayotaka kupigana, akatan-
gulia kuingia kwenye mlango ule, na mimi nikamfuatia kwa nyu-
ma kisha mlango ukafungwa kwa nyuma yetu, tukawa tunashuka
kwenye ngazi kuelekea chini.
Tulipita kwenye korido ndefu, tukipita kwenye milango kadhaa
na hatimaye, tukawa tayari tumefika kwenye mlango wa mwisho,
ukafunguliwa kwa kutumia namba maalum kisha tukaingia ndani
ambako tuliwakuta maafisa kadhaa wakiwa wamekaa kwa kum-
zunguka namba moja, kila mmoja akionesha kuwa na shauku
kubwa ya kutaka kujua ni nini kilichokuwa kikiendelea.
Nilipowatazama wale maafisa waliokuwa wamemzunguka yule
aliyekuwa katikati yao, mapigo ya moyo wangu yalinilipuka ku-
liko kawaida, nikiwa ni kama siamini nilichokuwa nakiona.
Hawakuwa wale walinzi waliomchukua namba moja kutoka
kwenye gari na kuingia naye kule chini bali walikuwa ni wale
maafisa waliokuwa wakimlinda ‘double’ na kumfanyisha maele-
kezo ya jinsi anavyotakiwa kwenda kuzungumza na wageni.
Nilirudia kuwatazama mmoja baada ya mwingine, mapigo ya
moyo wangu yakinienda mbio kuliko kawaida, nikamgeukia kion-
gozi wa PSU ambaye naye alikuwa amepatwa na mshtuko kama
niliokuwa nimeupata mimi.
“Nini kinaendelea hapa!” alisema yule kiongozi wa PSU kwa
sauti iliyoonesha wazi kwamba alikuwa anatetemeka kwa hofu,
mmoja kati ya wale maafisa akamweleza kwamba walikuwa

712 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wamepewa maelekezo ya kushuka kule chini na kubadilishana na


namba moja ambaye aliingia na walinzi wake kule kwenye chum-
ba walichokuwa wakiendelea kumuandaa ‘double’.
“Mungu wnagu!” alisema kiongozi wa PSU akiwa anahaha,
akiwa hata hajui nini cha kufanya. Sikutaka kuamini kwa haraka
kile kilichosemwa na kile nilichokuwa nakishuhudia, ikabidi nim-
sogelee yule waliyekuwa wakimlinda, ili nijihakikishie mwenyewe
kama kweli hakuwa namba moja.
Nilimsogelea mpaka nikamkaribia kabisa, tukawa tunatazamana
ana kwa ana, nikajikuta mwili wote ukiishiwa nguvu baada ya
kubaini kwamba hakuwa namba moja kama ambavyo kila mtu
kule nje alikuwa anajua, bali ni ‘double’.
Ni kweli kwamba makosa mengi yalikuwa yametokea jioni hiyo
na kusababisha wale wendawazimu kupenya mpaka ndani lakini
kosa kubwa kuliko yote lililokuwa limetokea, lilikuwa ni lile nili-
lokuwa nalitazama mbele ya mboni za macho yangu.
Nilisogea pembeni haraka huku mapigo ya moyo wangu yakien-
delea kudunda kuliko kawaida, nikabonyeza kifaa changu cha ma-
wasiliano na kutoa taarifa kwa timu nzima kwamba namba moja
hakuwepo kwenye ‘vault’ na badala yake, ‘double’ wake ndiye
aliyekuwa amepelekwa ‘vault’.
Taharuki kubwa iliibuka, baba yake Saima akawa mtu wa kwan-
za kunitaka nifafanue ni nini hasa nilichokuwa namaanisha. Muda
huohuo, kabla hata sijamjibu, mkurugenzi naye akaja na swali
hilohilo.
Nilirudia kuwaeleza kile nilichokuwa nimemaanisha, kila mtu

713 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

akachanganyikiwa kuliko kawaida.


Nilimgeukia kiongozi wa PSU, nikamuona akiwa amezubaa,
akiwa hata hajui nini cha kufanya, nikamgusa begani, akashtuka
mithili ya mtu aliyeguswa na nyoka mwenye sumu kali.
“Tunatakiwa kutoka haraka iwezekanavyo,” nilimwambia,
akawa ni kama amezinduka kutoka kwenye lindi la usingizi mzito,
mimi nikatangulia na kuanza kutimua mbio kutoka nje. Naye
akawa ananifuata, akiwa anakimbia na kuhema kwa nguvu.
Kwa kuwa milango yote tuliyokuwa tumeipita mwanzo, baada tu
ya sisi kupita ilikuwa imefungwa tena, ilibidi mawasiliano ya ha-
raka yafanyike na vijana wa ‘control room’, ambao nao kwa bahati
nzuri, walikuwa ‘sharp’ kisawasawa, milango yote ikawa inafun-
guliwa, mmoja baada ya mwingine bila kupoteza hata sekunde
moja.
Wakati tukizidi kusonga mbele kuelekea juu, vishindo vya hapa
na pale vilikuwa vinasikika kutokea juu ikiwa ni pamoja na milio
ya risasi, nikazidi kuchanganyikiwa. Ndani ya muda usiozidi
dakika mbili tu, tayari tulikuwa tumeshafika kwenye mlango wa
mwisho kabisa, ambao nao ulifunguliwa.
Nikawa wa kwanza kutoka huku nikihema, kiongozi wa PSU
naye akatoka akitweta, akiwa hata haelewi nini cha kufanya,
akawa ananifuata nyumanyuma. Tukawa tunakimbia kuelekea kule
ndani.
Baba yake Saima alisikika kwenye vifaa vya mawasiliano akini-
ulizia nilikuwa nimefika wapi, nikamjibu kwamba tayari nilikuwa
nimeshatoka na sasa nilikuwa koridoni, nikielekea kule nilikowaa-

714 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

cha. Akanielekeza mahali walipokuwepo.


Ndani ya muda mfupi tu, tayari nilifika mahali walipoku-
wepo wote watatu, baba yake Saima, mkurugenzi wetu na Chief
Mwaipopo, wakawa wanatutazama kwa shauku kubwa, kila
mmoja akionesha kupagawa kabisa, wakawa wanataka kusikia
upya kilichotokea.
Nilirudia tena kuwafafanulia, wote wakamgeukia kiongozi wa
PSU ambaye alikuwa amesimama nyuma yanguy.
“Wakati yote haya yanatokea, wewe ulikuwa wapi? Inaweze-
kanaje vijana wako wapewe amri ya hatari kama hii halafu wewe
kiongozi wao ukawa hujui chochote?” mkurugenzi alimpiga
maswali mfululizo kiongozi wa PSU, akawa anajiumauma tu kwa
sababu hakuwa na majibu.
“Huu siyo muda wa kulaumiana, tushughulikie kwanza tatizo
lililopo mbele yetu,” alisema baba yake Saima, nikamuona mkuru-
genzi akimkata jicho kali kwelikweli yule kiongozi wa PSU.
“Mafundi wapo tayari,” alisema baba yake Saima, wote tukageu-
ka kutazama kule alikokuwa anatazama baba yake Saima. Vijana
watatu waliokuwa na vifaa maalum mikononi mwao, walikuwa
wakija kwa kasi kule tulikokuwa tumesimama, harakaharaka
akawaonesha mlango wa kwanza ambao wanatakiwa kuuvunja.
“Tunaingia ndani, namba moja atakuwa kwenye wakati mgumu
sa...” alisema baba yake Saima na kabla hajamalizia kauli yake,
tulishtushwa na kishindo kikubwa kilichosikika kutokea kule nda-
ni ya kile chumba, taharuki ikazidi kuongezeka kuliko kawaida.
“Tumeshawapanga vijana wetu kwenye mlango wa pili kwa hiyo

715 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

hakuna njia wanayoweza kuitumia kutoroka, tunatakiwa kuingia na


kumuokoa namba moja na kuwashikisha adabu hawa wendawaz-
imu,” alisema baba yake Saima akinitazama mimi.
Nadhani alishaona kwamba majukumu ya kuongoza oparesheni
ile, yalikuwa yameshakuwa makubwa kuliko mimi.
Tulijipanga vizuri, wale vijana wakasogea kwenye mlango,
wakahesabu mpaka tatu kisha wakawasha mashine zao mbili za ku-
katia vyuma, wakaanza kukata ule mlango kwa kasi ya kimbunga.
Ndani ya muda mfupi tu, tayari walikuwa wameshamaliza kazi
yao, wakarudi nyuma na kukaa kwenye migongo yetu, baba yake
Saima akanipa ishara kwamba mimi ndiye ninayetakiwa kutoa
maelekezo ya nini cha kufanya.
Nikaonesha ishara ya vidole, kila mmoja akaikamata vyema bun-
duki yake, nikahesabu kwa ishara mpaka tatu kisha nikaukanyaga
ule mlango kwa nguvu.
Kwa kuwa tayari ulishakatwa kwenye vyuma vilivyokuwa
vinaushikilia, teke moja tu lilitosha kuurusha mlango mpaka ndani,
nikawa wa kwanza kuingia ndani huku bunduki ikiwa ‘standby’,
nikageuza macho kwa kasi kubwa kila upande, nikiwa tayari
kumkabili mtu yeyote aliyekuwa mbele yangu lakini nilipokelewa
na moshi mwingi mweupe ambao ulinizuia kuona chochote mle
ndani japo taa zilikuwa zinawaka.
Wenzangu wote nao wakawa wameshaingia na tukapangana kwa
mfumo wa ‘pair’. Huu ni mfumo ambao mnajipanga wawili wawili
na mnapeana migongo, huyu anatazama upande huu na mwingine
anatazama upande mwingine, kila mmoja bunduki ikiwa tayari kwa

716 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

chochote.
Tuliangaza huku na kule lakini hakuna tulichoweza kukiona,
tukawa tunasogea kwa tahadhari kubwa, moshi ukizidi kupungua.
Ghafla niliona kitu kilichozidi kunichanganya kabisa.
Kwenye kona ya chumba kile, mahali kulipokuwa na mlango
wa kuelekea kwenye vyoo vya ndani, kulikuwa na alama za damu
ukutani na pamoja na matundu mengi ya risasi, nikawapa ishara
wenzangu kisha wote tukaanza kusogea kuelekea kwenye mlango
ule, ambao nao ilionesha kwamba umevunjwa.
Tukiwa tunaendelea kusonga mbele kwa tahadhari kubwa, nil-
ishtuka tena baada ya kuona damu zikiwa zinachuruzika kutokea
nyuma ya makabati ya kuhifadhia vitabu na nyaraka mbalimbali
ndani ya chumba hicho.
Nikawapa tena ishara wenzangu, ikabidi tugawane, wawili
waendelee kusogea kule kwenye mlango wa kuingilia chooni
ambao ni mimi na baba yake Saima ambao tulikuwa ‘pair’, kila
mmoja akiwa amemgeuzia mwenzake mgongo, tukisogea mbele
kwa pamoja.
Mkurugenzi ambaye alikuwa ‘pair’ na Chief Mwaipopo, wao
walielekea nyuma ya yale makabati.
“One officer down! I repeat, one officer down!” sauti ya mkuru-
genzi ilisikika kwenye vifaa vya mawasiliano, ikitutaarifu kwamba
afisa mmoja wa usalama alikuwa amepigwa risasi, baada ya kuwa
wamefika kule nyuma ya yale makabati.
Sijui kwa nini lakini akili yangu ilinituma kuamini kwamba
aliyekuwa ameangushwa hawezi kuwa ni miongoni mwetu wala

717 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

miongoni mwa walinzi wa namba moja. Niliamini hivyo kwa sa-


babu nilikuwa najua ni mafunzo makubwa kiasi gani ambayo kila
mmoja alikuwa nayo, kiasi cha kufanya aangushwe kirahisi namna
hiyo, tena katika uwanja wa nyumbani.
“Confirm his identity!” nilimjibu mkurugenzi wetu baada ya
kuwa ametoa taarifa ile, kupitia kwenye vifaa vya mawasiliano
ambavyo wote tulikuwa tumeunganishwa navyo.
Nilichokuwa nimekihisi ndicho kilichokuwa kimetokea, aliyeku-
wa amepigwa risasi, alikuwa ni miongoni mwa wale wanaume
waliovamia Magogoni na pengine ambacho kilimfanya mkurugen-
zi aamini haraka kwamba anaweza kuwa miongoni mwetu, ni jinsi
alivyokuwa amevaa.
Kama nilivyoeleza, wanaume wale walikuwa wamefanikiwa
kupenya na kuingia mpaka ndani bila kugundulika kirahisi kwa
sababu walikuwa wamevalia sawa kabisa na maafisa wa Magogoni
pamoja na maafisa wa kitengoni.
Baada ya kuwa na uhakika kwamba hakuwa miongoni mwetu,
harakaharaka walirudi kuungana na sisi ambao muda huo tayari
tulikuwa tumeshafika kenye ule mlango, tukawa tunasubiri kuingia
kwa kasi ya kimbunga na kukabiliana na chochote kilichokuwa
mbele yetu.
Walipofika pale tulipokuwepo, nilitoa ishara kwa vidole, tukahes-
abu mpaka tatu kisha wote tukaingia kwa kushtukiza, tukapigwa na
butwaa kwa tulichokiona.
Pembeni ya sinki la choo cha kukaa, kulikuwa kumetobolewa
shimo kubwa kwenda chini ya ardhi, tukabaki tunashangaa hayo

718 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

yote yanawezekanaje ndani ya muda mfupi kiasi hicho?


Lilikuwa ni shimo lenye upana kama wa kisima cha kuchotea
maji, tukatazamana kisha tukasogea kwa tahadhari kwa sababu
ilionesha kwamba kuna jambo halikuwa sawa. Nasema hivyo kwa
sababu hakukuwa na udongo wowote ndani ya choo kuonesha
kwamba shimo limechimbwa kutokea ndani.
Kilichoonekana, ni kama shimo hilo lilikuwa tayari lime-
shachimbwa na kilichokuwa kinazuia lisigundulike, ni marumaru
zilizokuwa mle chooni. Tulisogea na kumulika na tochi zetu zenye
mwanga mkali kuangalia kule chini.
Kulikuwa na ngazi moja ndefu ya chuma ambayo ilionesha ndiyo
iliyotumika kwa watu wale kushuka chini, kila mmoja akazidi
kupagawa.
Mapaka kufikia hapo, nilikuwa na uhakika mkubwa kwamba
mpango wa kuingia Magogoni ulikuwa umeandaliwa kwa muda
mrefu, kwa kutumia akili kubwa mno na lazima watu wa ndani
walikuwa wanahusika.
Sikutaka kusikia ushauri wa mtu, harakaharaka nilirukia kwenye
ile ngazi na kuanza kushuka chini, hata sikufikiria nini kitanipata
endapo kutakuwa na watu wenye silaha kule chini wakisubiri mtu
yeyote ajichanganye.
Lilikuwa ni shimo lenye urefu wa kama futi kumi na mbili kwen-
da chini, nikashuka ngazi kwa kasi kubwa na hatimaye nikajiru-
sha mpaka chini, bunduki yangu nikiwa nimeishika kwa kutumia
mkono mmoja, na mkono mwingine nikiwa nimeshika tochi.
Wenzangu nao walinifuata na sekune chache baadaye, wote

719 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wanne tukawa kule chini ya shimo. Tulipomulika vizuri, tulibaini


kwamba kulikuwa na michirizi mingi ya damu, kuanzia kwenye
ngazi mpaka kule chini.
Tulipotazama vizuri, tuligundua kwamba kumbe shimo lile
lilikuwa limeungana na shimo lingine ambalo lenyewe lilikuwa
limechimbwa kwa ulalo kama handaki, ambalo huwezi kupita
ukiwa umesimama, lazima uiname au utambae kama nyoka. Ku-
mulika vizuri, tukabaini kwamba kulikuwa na mwili mwingine wa
mwanaume kwa upande wa ndani wa shimo lile.
Kwa tahadhari kubwa tukamvuta na kumtoa pale kwenye seh-
emu yenye upana kisha tukammulika. Alikuwa ni mwanaume
mwingine kati ya wale wavamizi, akiwa amepigwa risasi ya kwe-
nye paji la uso.
“Watakuwa wameingia kwenye bomba kubwa linalopeleka maji
taka baharini, tukienda kwa mwendo huu watatuzidi kasi,” alisema
baba yake Saima, wazo ambalo liliingia kabisa akilini.
Yale mashimo yote mawili, yalikuwa yamechimbwa kwa ufanisi
wa hali ya juu na ilionesha kwamba waliyoyachimba, walikuwa
wanaijua vyema ramani yote ya eneo hilo.
Uzuri ni kwamba, baba yake Saima alikuwa na ramani yote ya
mifumo ya maji taka kama ambavyo nilikuwa nimeagiza tangu
mwanzo baada ya kubaini kwamba wale wendawazimu walikuwa
wameingia kwa kupitia kwenye chemba ya majitaka.
“Hatuna muda wa kupoteza, hatuwezi kwenda wote kwa namna
hii, wengine lazima watoke haraka na kwenda kuwapanga vijana
kwenye njia zote za mifumo ya maji taka.,” nilisema, baba yake

720 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Saima akaongezea kwamba mabomba yote makubwa ya maji


taka, yalikuwa yameelekezwa baharini kwa ndani kabisa kwa hiyo
nguvu zote lazima zielekezwe huko.
Ilibidi mkurugenzi na Chief Mwaipopo ndiyo waendelee na kazi
ya kuwafuatilia wale wendawazimu ambao mpaka muda huo nikiri
kwamba walikuwa wametuzidi akili kwelikweli, mimi na baba
yake Saima tukapanda haraka na kurudi juu, harakaharaka nikatoa
maagizo kwa maafisa kadhaa ambao nao walikuwa wakitufuata
kwa nyuma, waingie ndani ya shimo lile kwenda kuongeza nguvu.
Watu kumi wenye silaha walishuka harakaharaka, wengine nikaa-
giza watufuate, tukatoka ndani ya kile chumba na kuanza kukimbia
kwenye korido, kuelekea upande wa nje.
Wakati yote hayo yakiendelea, ndani ya ukumbi wa mikutano,
ulinzi ulikuwa umeimarishwa na kila mtu alikuwa ametulia, wage-
ni wakiwa wanashangaa ni nini hasa kilichokuwa kinaendelea kwa
sababu kila kitu kilikuwa kikifanyika kwa usiri mkubwa.
Ndani ya muda mfupi tu, tayari tulikuwa tumeshatoka nje, mimi
nikiwa mbele kabisa. Nikawakusanya vijana wote waliokuwa
wakiendelea na doria kule nje na kuwaeleza kila kilichokuwa ki-
metokea.
Nikiwa naendelea kuwaeleza mipano ambayo tunatakiwa kuifan-
ya, kuna jambo nililibaini. Tangu tulipoenda kuvunja ule mlango
wa kile chumba ambacho ‘double’ alikuwa akiandaliwa, sikumu-
ona tena kiongozi wa PSU, kwa kifupi alikuwa ni kama ameyeyu-
ka, taa nyekundu ikawaka ndani ya kichwa changu.
Harakaharaka nikabonyeza kifaa changu cha mawasiliano,

721 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

nikatoa taarifa kwa vijana wote na kuwaelekeza kwamba nguvu


zote kwa wakati huo, zinatakiwa kuelekezwa upande wa baharini
na nikatoa amri kwa vijana wa ‘marine’ waliokuwa kwenye boti
wakifanya doria kule baharini, wahakikishe wendawazimu wale
hawatoki hata iweje.
Harakaharaka tulitawanyika, kila mmoja kuelekea eneo alilo-
pangiwa, huku wale wengine wakitakiwa kuendelea kuimarisha
ulinzi ndani na nje ya eneo hilo, nikawa nawaongoa vijana wangu
kwa kukimbia kuelekea kwenye geti dogo lililokuwa linafungukia
upande wa baharini.
Ndani ya muda mfupi tu, tayari mimi na vijana wangu tulikuwa
tumeshafika kule upande wa baharini, magari mengi ya doria nayo
yakawa yanawasili kutokea kila upande, sambamba na boti za
askari wa majini zilizokuwa zinaendelea na doria kali.
Kwa jinsi nilivyolitazama eneo lote la bahari jinsi lilivyokuwa
wazi, na jinsi boti za doria zilivyokuwa zikiendelea kurandaranda
huku na kule, niliamini kwamba kama wale wendawazimu waliwe-
za kutumia akili kubwa ya kuingia kupitia chemba za maji taka na
baadaye kuchimba chini kwa chini, hawawezi kuwa wajinga kiasi
cha kutoka kienyeji na kuibukia baharini.
Niliamini lazima wanaweza kuwa pia wametafuta njia ambayo
wataweza kutoka kupitia yale mabomba na kuendelea na safari yao
chini kwa chini bila kuibuka kwenye usawa wa maji ya bahari.
Harakaharaka nikabonyeza kifaa cha mawasiliano na kumtaka
baba yake Saima atoe ramani kamili ni wapi mabomba hayo yali-
kuwa yanaishia kule ndani ya bahari ili vijana wa Marine wazamie

722 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

na kwenda mpaka kwenye maeneo ambayo mabomba hayo yali-


kuwa yakiishia.
Uzuri ni kwamba, kumbe ramani ilikuwa inaeleza vizuri kwamba
kila bomba limeenda umbali gani kutoka nchi kavu.
Kwa ambao hamkuwa mkijua, mabomba mengi ya maji taka,
japo siyo yote, yameelekezwa baharini lakini kwa sababu za ku-
zuia uharibifu wa mazingira, huwa yanapelekwa mbali na fukwe,
yaani yanaopita chini kwenye sakafu ya bahari mpaka umbali
fulani na kule ndiko yanakoenda kumwaga maji taka ambayo
huchanganyikana na maji ya bahari bila kusababisha uchafu
wowote kurudi kwenye fukwe za bahari.
Ndani ya muda mfupi tu, tayari alikuwa ameshatoa maelekezo,
na mimi nikayahamishia maelezo hayo kwa vijana wa Marine
ambao wengine walienda kuzamia kwenye ‘point’ husika ambako
mabomba ya kutoka ‘ground zero’ yalikuwa yakimwaga maji taka.
Lakini pia akili nyingine zilinijia ndani ya kichwa changu! Si-
kuwa mtaalamu wa mambo ya mifumo ya maji taka baharini lakini
nilihisi lazima mabomba hayo yatakuwa na ukubwa tofautitofauti.
Ikabidi niulize tena kwa baba yake Saima.
Naye hakuwa na majibu ya haraka, ikabidi tutafute majibu kwa
maafisa waliokuwa wakishughulikia idara hiyokutoka Magogoni.
Majibu yaliyotolewa, yalizidi kufanya kazi iwe ngumu.
Tulielezwa kwamba, kwa sababu za kiusalama, mabomba hayo
huwa yanapungua kipenyo kadiri yanavyoingia zaidi baharini. Ni-
kisema kipenyo, namaanisha lile eneo la ndani la bomba, kwamba
huku yalikokuwa yakianzia, yalikuwa na upana mkubwa lakini

723 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kadiri yanavyoingia baharini, yalikuwa yakienda yakipungua tara-


tibu mpaka mwisho kabisa na yalitengenezwa kuruhusu uelekeo
mmoja tu.
Hiyo iliwekwa kwa sababu maalum, kwamba mtu au kitu cho-
chote kisiweze kupenya kutokea baharini na kurudi mpaka ndani
ya chemba lakini lakini pia kuzuia maji ya baharini, hasa kipindi
cha maji kujaa, yasiweze kurudi mpaka kwenye chemba na kwen-
da kuharibu miundombinu.
Tafsiri yake ni kwamba, hata kama wendawazimu wale walifani-
kiwa kuingia kutokea upande wa Magogoni ambako kipenyo chake
ni kikubwa, wasingeweza kwenda mpaka mwisho wa mabomba
kwa sababu kule mabomba yalikuwa membamba na isingeweze-
kana kwa mtu yeyote kupita, nikagundua kwamba kwa mara
nyingine ile akili ya kwenda kuwasubiria mwisho wa mabomba,
isingeweza kuzaa matunda.
Ambacho lazima watakuwa wamekifanya, itakuwa ni kutoboa
lile bomba ambalo walikuwemo katika eneo ambalo lina kipenyo
kikubwa na kutokea baharini, ikabidi nitoe amri nyingine ya ma-
bomba yote kufuatiliwa kuanzia kule mwisho walikokuwa wa-
mezamia wale vijana wa marine mpaka ufukweni.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, kazi ikaanza na mara taarifa
mpya zikaingia kwamba kulikuwa na milio kutokea ndani ya
bomba moja, kuonesha ni kama lilikuwa likikatwa kutokea ndani,
hapo sasa ikabidi na mimi niingie baharini.
Tulifanya mawasiliano haraka, moja ya boti za doria ikasogea
kwenye maji mafupi, nikawachagua vijana wanne wa kuongo-

724 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

zana na mimi, tukajichanganya na wale waliokuwa ndani ya boti,


tukaingia na kuanza kukimbia kwa kasi kuelekea eneo ambalo
ndipo taarifa zilipokuja kwamba kuna milio ya bomba inasikika,
lilikatwa kutokea ndani.
Jambo ambalo bado nilikuwa najiuliza mpaka wakati huo, ni
wapi walipokuwepo wale maafisa maalum waliokuwa wakimlinda
namba moja ambao ndiyo walioingia naye kwenye ‘vault’?. Kwa
nini wote walikuwa hawajibu chochote kwenye vifaa vyao vya
mawasiliano? Alikuwa wapi kiongozi wa PSU na kwa nini naye
hakuwa akijibu chochote kwenye kifaa chake cha mawasiliano?
Ndani ya muda mfupi tu, tayari tulikuwa tumeshafika kwenye
eneo lile, boti kadhaa za doria nazo zilikuwa zimelizunguka eneo
hilo, askari wa majini wakawa wanavaa vifaa vyao harakaharaka
kwa ajili ya kuzamia kwenda chini kuongeza nguvu.
“Na mimi nataka kuzamia, siwezi kubaki kwenye boti wakati
sijui ni nini kinachoendelea!”
“Hapana mkuu, vifaa vyetu ni tofauti na hata silaha zetu pia ni
tofauti, vijana watafanya kazi yao ipasavyo. Hapo itabidi uvue
kila kitu kwa sababu kila ulichovaa hakiwezi kufanya kazi chini
ya bahari, utaharibu kila kitu,” alisema kiongozi wa wale askari
wa majini, nikawa sina cha kufanya kwa sababu ni kweli kila
nilichokuwa nacho, hakikuwa rafiki kwa maji, kuanzia kifaa cha
mawasiliano mpaka silaha.
“Unaweza kuwa unasikiliza na kufuatilia kila kinachoendelea
tukiwa hapahapa,” alisema, moyoni nikawa najilaumu kwa nini
sikuwa nimepata mafunzo ya ‘marine’ na mimi kwa sababu katika

725 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

muda kama huo ndipo ujuzi wangu ungeweza kutumika kisawa-


sawa.
Hata hivyo, kwa jinsi tulivyokuwa tumejipanga, nilikuwa na
uhakika kwamba hakuna atakayefanikiwa kutoka salama eneo hilo,
ilikuwa ni ama zao, ama zetu.
Wakati hayo yakiendelea, niliendelea kuwa natoa taarifa kwa kila
mtu kupitia vifaa vya mawasiliano, mkurugenzi, Chief Mwaipopo
na vijana wao walioingia kule kwenye ile chemba, nao wakawa
wanatoa taarifa na kueleza kwamba wanazidi kuwakaribia maadui
ingawa kazi ilikuwa ngumu kutokana na hewa ndogo iliyokuwa
ndani ya mabomba yale.
Mimi pia nikawa nawaambia kilichokuwa kinaendelea kule baha-
rini, huku baba yake Saima naye akitujuza kilichokuwa kinaende-
lea kule ‘ground zero’ kwa sababu yeye alilazimika kubaki pale.
Nadhani wakiwa mle ndani ya bomba, wale wendawazimu
walipata taarifa kwamba tayari tulikuwa tumezingira eneo wali-
pokuwa wanajaribu kutoboa ili waingie baharini.
Bado sijajua hasa ni nani aliyekuwa anavujisha taarifa hizo kwani
muda mfupi baadaye, wale vijana waliokuwa wamezamia, walitoa
ripoti kwamba zile kelele za bomba kukatwa kutokea ndani ziliku-
wa zimeacha kusikika na hakukuwa na eneo lolote ambalo lilikuwa
limetobolewa.
Wakati taarifa hizo zinaingia, muda huohuo zikaja taarifa ny-
ingine kutoka kwa mkurugenzi ambaye aliongea kupitia kifaa
chake cha mawasiliano huku akikohoa sana, akieleza kwamba kuna
hewa ya sumu ilikuwa imepulizwa ndani ya bomba na vijana wake

726 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

walikuwa wakianza kulegea na kuishiwa nguvu mmoja baada ya


mwingine.
“Mungu wangu!” nilisema, sikuwa nimewaza kama wendawaz-
imu wale wanaweza kuwa wamejipanga kiasi hicho. Kilichooneka-
na, ni kwamba baada ya kujua kwamba hawawezi kutoka salama
kupitia lile bomba, waliamua kurudi nyuma lakini kwa kuwa tayari
walikuwa wanafuatiliwa kwa karibu, waliamua kutumia mbinu
mbadala za kuwarudisha nyuma waliokuwa wanawafuatilia na
ndipo hapo walipoamua kutumia sumu.
Nikiwa hata sijui nini cha kusema, baba yake Saima alisikika
kwenye kifaa chake cha mawasiliano, akitoa ushauri kwamba wa-
natakiwa kurudi nyuma haraka na kutoka kabla sumu haijawaathiri
zaidi, akaeleza kwamba lazima wahalifu wale baada ya kukosa
njia, waliamua kurudi ndani kwa hiyo njia bora ni kwenda kuwasu-
biri kutokea ndani.
Watu wa huduma ya kwanza waliandaliwa haraka kwa ajili ya
kuwahudumia wote waliokuwa wamevuta hewa ya sumu, tukawa
tunazidi kuchanganyikiwa kwa sababu kama maafisa wetu wlaivu-
ta hewa ya sumu, vipi kuhusu namba moja ambaye wote tulikuwa
na uhakika kwamba yupo kwenye mikono ya wale wendawazimu?
Kwa wakati huo, mimi nilikuwa natakiwa kuondoka haraka
kutoka kula baharini ili kwenda kuongoza oparesheni kule ‘ground
zero’ lakini sijui kwa nini nafsi yangu ilikuwa inagoma.
Kwa mbinu za hali ya juu walizokuwa wamezionesha wale
wendawazimu, ilikuwa ni vigumu sana kutabiri ni hatua gani wa-
napanga kuichukua kwa hiyo kila kitu kilitakiwa kufuatiliwa kwa

727 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ukaribu na umakini wa hali ya juu.


Mpaka muda huo, ilikuwa inakwenda kama saa mbili na nusu za
usiku, tukiwa bado tunaendelea kuhaha huku na kule kuhakikisha
tunamuokoa namba moja, tena akiwa salama.
Wazo lililokuwa ndani ya kichwa changu kwa wakati huo, iliku-
wa ni kutumia nguvu za ziada kuwafuata wale wendawazimu kule
chini kutokea upande wa baharini kwa sababu hata kama tungese-
ma tuendelee kuwasubiri watoke wenyewe, hatukuwa na uhakika
ni kipi ambacho wangeweza kumfanyia namba moja kule ndani ya
lile bomba.
Kitendo cha wao kufanikiwa kumfikia namba moja na kumshi-
kilia kwa muda wote huo, kilikuwa ni zaidi ya kashfa kwetu na
serikali nzima kwa hiyo ilikuwa ni lazima hatua za haraka zichu-
kuliwe, tena kwa nguvu kubwa zaidi kabla mambo hayajazidi
kuharibika.
“Tunatakiwa kutoboa bomba na kuwafuata hukohuko ndani!”
nilisema kupitia vifaa vya mawasiliano.
“Hapana! Ukitoboa bomba maana yake unaruhusu maji yaingie
ya baharini yaingie kwa nguvu ndani ya bomba hilo ambalo namba
moja yupo ndani yake, tutakuwa tunazidi kuhatarisha zaidi usalama
wake kuliko kumuokoa,” alisema mkurugenzi na muda huohuo
Chief Mwaipopo naye akadakia:
“Ni hatari kutoboa bomba na kama hiyo haitoshi, maji yatarudi
kwa kasi na kuingia ndani ya Magogoni, siyo uamuzi sahihi hata
kidogo!”
“Mimi ndiyo kiongozi wa oparesheni, nasema lazima tutoboe

728 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

bomba na kuwafuata hukohuko ndani! Hatuwezi kuendelea ku-


subiri wakati namba moja yupo hatarini! Nipo tayari kubeba la-
wama endapo jambo lolote baya litatokea,” nilisisitiza nilichokuwa
nimekisema, hakuna aliyenibishia tena.
Nilikuwa nimesema hivyo kwa sababu nilikuwa nimeshazun-
gumza na kiongozi wa kikosi cha Marine ambaye nilianza kwa
kumuuliza mbona kina cha maji kilikuwa kinaendelea kupungua
kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele?
Akaniambia kwa kuwa mwezi ulikuwa umeandama, huo uli-
kuwa ni muda wa maji kupwa, akaniambia kwa uzoefu wake, maji
yanaweza kuja kuanza kujaa baada ya kama saa nne au tano baa-
daye.
Kwa watu wenye uelewa na bahari, watakuwa wananielewa
vizuri ninaposema kupwa! Hata kama huna uelewa wa bahari, basi
bila shaka umewahi kusikia kuhusu maji kupwa na maji kujaa.
Ile hali ya maji ya bahari kupungua kina hasa maeneo ya jirani
na ufukweni mpaka kufikia hatua ya mchanga kuonekana kwenye
maeneo ya karibu na fukwe, ndiyo huitwa ‘kupwa’ ambapo bahari
inakuwa ni kama inasogea kurudi nyuma.
Baada ya maji kupwa, huwa yanaanza tena kurudi kwa kasi ufuk-
weni na mara nyingi huwa yanarudi yakiwa na kasi kubwa inayo-
tokana na mawimbi makubwa ya bahari.
Sina uhakika na sababu hasa zinazofanya ratiba za maji kupwa
na kujaa ziwe tofauti kipindi mwezi unapoandama lakini ambacho
nina uhakika nacho ni kwamba maji kupwa na maji kujaa huwa
kunasababishwa na nguvu za uvutano kati ya dunia na mwezi.

729 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Ni jambo hilo ndiyo lililowa limenipa ujasiri wa kuamuru bomba


litobolewe kutokea nje kwa sababu nilikuwa na uhakika kwamba
japokuwa maji hayakuwa yamepungua mpaka mwisho, bado yas-
ingeweza kuwa na nguvu inayoweza kuleta madhara kwa sababu
ulikuwa ni muda wa maji kupwa.
Ndani ya muda mfupi tu, vijana niliokuwa nimewachagua kwa
kazi hiyo, ambao ndiyo waliotusaidia kuvunja ile milango kule
ndani, walikuwa wamewasili wakiwa na boti ndogo inayokwenda
kasi, wakisindikizwa na maafisa wa jeshi la majini au Marine.
Niliagiza nipewe vifaa maalum vya kuzamia ndani ya maji na
safari hii sikutaka kusikia tena suala kwamba sijui nikizamia nita-
sababisha mifumo yote ya mawasiliano na vifaa vyangu kushindwa
kufanya kazi kwa sababu ya kuingia maji.
Nilikuwa tayari kuhatarisha kila kitu ilimradi niingie mwenyewe
na kuwaongoza vijana wangu kwenda kumuokoa namba moja.
Uzuri ni kwamba safari hii yule kiongozi wa Marine ambaye tuli-
kuwa naye kwenye boti moja alinielewa na akaniambia atakuwa na
mimi bega kwa bega.
Harakaharaka alitoa maelekezo kwa wasaidizi wake, nikapewa
nguo maalum za kuzamia kwenye maji pamoja na vifaa vyote
muhimu. Sikutaka kuvaa mavazi yale maalum, nilichokitaka kwa
wakati huo ilikuwa ni mtungi wa gesi pamoja na ile ‘mask’ yake
ya kuvaa usoni unapokuwa chini ya maji kwa ajili ya kukusaidia
kuona vizuri na kupumua.
“Itabidi vifaa vyako vya mawasiliano uvivue, tunaweza kuvi-
fungia vizuri sehemu salama ndani ya boti.”

730 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Hapana! Hakuna uwezekano wa kuviweka kwenye kitu amba-


cho hakitaruhusu maji kuingia?”
“Wazo zuri,” alisema kiongozi wa Marine, nikaletewa kimfuko
maalum cha plastiki, nikatoa vitu vyote vinavyoweza kuharibika
na maji, nikaviweka kwenye kimfuko hicho na kukifunga vizuri,
nikakiweka kwenye mfuko wa chini wa gwanda langu.
Kitu pekee ambacho nilikubali kukiacha, ilikuwa ni bunduki ya-
nagu ambayo kama nilivyoeleza awali, yenyewe haikuwa na uwezo
wa kufanya kazi ikiingia maji, tena yenye chumvi kama yale ya
baharini, nikabadilishana na mmoja kati ya vijana wa Marine, ni-
kampa ile na yeye akanipa ya kwake ambayo ilikuwa na uwezo wa
kufanya kazi hata ikiingia maji.
Kila kitu kilifanyika kwa kasi ya kimbunga, dakika chache tu
maandalizi yote yakawa yameshakamilika, kikosi cha watu saba,
mimi, yule kiongozi wa Marine na vijana wake watatu na wale
vijana wetu wawili wa kwenda kukata bomba kwa kutumia mash-
ine maalum, tulirukia kwenye maji na kuanza kuelekea kwenye
bomba, chini kabisa ya bahari.
Nimeeleza kwamba sikuwa na mafunzo ya ‘marine’ kwa maana
ya mapigano ya kwenye maji lakini hiyo haikuwa na maana kwam-
ba sikuwa najua kuogelea. Nilikuwa naweza kupiga mbizi vizuri tu
kwa hiyo wala sikuwa na wasiwasi.
Uzuri ni kwamba zile mask zilikuwa na tochi kwa mbele kwa
hiyo japokuwa kulikuwa na giza, tulikuwa na uwezo wa kuona
mbele, tukashuka mpaka tulipolifikia bomba, kiongozi wa Navy
akiwa ndiye anayetuongoza.

731 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Kwa eneo hilo tulilokuwepo, bomba lilikuwa na kipenyo kidogo,


ikabidi tuanze kutambaa chini kwa chini mpaka tulipofika eneo
ambalo bomba lilikuwa na upanakama wa pipa, mapipa haya ya
kuwekea mafuta au yanayotumika kuhifadhi maji majumbani.
Tukaoneshana kwa ishara kwamba eneo hilo lilikuwa sahihi
kutoboa kwa sababu ndani kulikuwa na nafasi inayoweza kuruhusu
mtu kupita na kuanza kuogelea kurudi nyuma.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, kazi ya kutoboa ilianza mara
moja, wale vijana kwa kutumia mashine zao wakafanikiwa kukata
bomba lile lililokuwa limetengenezwa kwa zege ngumu na nondo
pamoja na nyavu za chuma.
Baada ya kukakikisha kwamba sehemu ilipotobolewa ilikuwa
inatosha kwa mtu kupenya kuingia ndani, mimi ndiyo nilikuwa wa
kwanza kuingia. Bomba lilikuwa na kila aina ya uchafu kwa ndani
lakini kwa kuwa nilikuwa nimevaa mtungi wa gesi, ile harufu hai-
kuniathiri chochote.
Maji yaliyokuwa yanaingia kwa kasi kutokea nje, yakawa yanan-
isukuma kwa kasi kurudi ndani. Ilibidi niizime ile tochi kwenye
mask yangu ili nisije kuonekana kwa urahisi, ndani ya muda mfupi
tu watu wote wakawa nao wameshaingia na wakawa wanakuja
nyuma yangu.
Kwa jinsi bomba lilivyokuwa, ilikuwa ni vigumu kugeuka nyuma
kwa sababu ya kipenyo chake, kumbuka nimeeleza kwamba katika
eneo tulilokata na kuingia, kipenyo chake kilikuwa sawa na kip-
enyo cha pipa.
Maji yalizidi kuingia kwa kasi, nikawa najivuta kuelekea mbele

732 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kwa kupiga mbizi kwa kutumia mkono mmoja huku mkono


mwingine nikiwa nimeshika bunduki, kidole kikiwa kwenye kitufe
cha kufyatua risasi, tayari kukabiliana na chochote ambacho kin-
getokea mbele yangu.
Kwa wanaofahamu jinsi mabomba ya maji taka yanavyojen-
gwa, watakuwa wanaelewa kwamba huwa kunakuwa na ‘point’
za maungio, mahali ambapo mabomba kutoka huku na kule yana-
kutana na kumwaga maji kwenye sehemu moja ambayo inakuwa
imechimbwa kwa upana na kina kirefu na kutengeneza kama ngazi
hivi.
Basi baada ya kuhaha kwenye maji taka ambayo sasa yalikuwa
yamechanganyikana na maji ya bahari, nilitokea kwenye eneo le-
nye maungio, kulekule chini. Ilibidi niwashe tochi ili niweze kuona
vizuri kilichokuwa mbele yangu.
Baada ya kuhakikisha kwamba hakukuwa na mtu eneo hilo, ili-
bidi nijivute kutoka kwenye bomba na kutokezea kwenye eneo am-
balo sasa nilikuwa na uwezo wa kusimama, maji machafu yakawa
anatiririka kutokea juu, usawa wa kichwa changu.
Nikisema maji machafu, namaanisha machafu kwelikweli, maji
kutoka kwenye vyoo na masinki, yote yakawa yananimwagikia
kuanzia kichwani kushuka chini. Harakaharaka nilijivuta pembeni
kidogo, nikagundua kulikuwa na vyuma kadhaa ambavyo vilikuwa
vimechomekwa na kutengeneza kama ngazi ndogo ndani ya bomba
lile.
Nadhani wakandarasi walitengeneza hivyo ili kuwarahisishia
mafundi kufika kwa urahisi eneo hilo endapo kungetokea tatizo la

733 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

mabomba kuziba. Baada ya kujiridhisha kwamba eneo hilo liliku-


wa salama, nilitoa ishara kwa wenzangu kwamba waanze kuingia
kwa awamu kwa sababu upana wa eneo hilo ulikuwa unawezesha
watu watatu kusimama kwa wakati mmoja.
Kilichonishtua kuliko kawaida kutoka ndani ya moyo wangu, ili-
kuwa ni baada ya kugundua kwamba eneo hilo lilikuwa limetapak-
aa damu na palikuwa na purukushani fulani kuonesha muda mfupi
uliopita, kulikuwa na watu kwenye eneo hilo.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, nilishika vyuma vya upande
mmoja na kuanza kupanda kuelekea juu kwa tahadhari kubwa
kuliko kawaida, mapigo ya moyo wangu yakawa yanadunda kwa
kasi kwelikweli.
Kiongozi wa marine ambaye ndiye aliyekuwa nyuma yangu,
naye akashika vyuma vya upande wa pili, tukawa tunapanda kwa
tahadhari huku tukipeana ishara, naye akionesha kushtukia kila
kilichokuwa kinaendelea, damu nyingi zikiwa zimetapakaa kwe-
nye bomba lote na nyingine zikiwa zinashuka zikiwa zimechang-
anyikana na maji taka.
Eneo lenyewe lilikuwa na kama mita tatu au nne kwenda juu,
yaani usawa wa kutoka kwenye sakafu mpaka kwenye dari kwenye
nyumba za kawaida na wakati tukipanda, tulianza kuona mwanga
kutokea juu, nikampa ishara mwenzangu azime tochi, tukawapa
ishara wengine wote waliokuwa nyuma yetu kuzima tochi zao, tu-
kawa tunapanda kwa kukisia tu mahali kulipokuwa na vile vyuma
vya ngazi.
Kuna muda nilisikia kijana wetu mmoja akiteleza na kurudi chi-

734 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ni, akajikaza na kutotoa kelele yoyote zaidi ya kishindo cha kuan-


gukia kwenye maji machafu kilichosikika. Nadhani aliteleza kwani
vile vyuma vilikuwa vimeota ukungu wenye kuteleza kutokana na
maji machafu yaliyokuwa yanatiririka muda wote.
Mimi ndiyo nilikuwa wa kwanza kufika juu ambapo ilibidi nitu-
mie akili ya ziada kuchungulia, nisingeweza kutokeza mzimamzi-
ma kwa sababu hatukuwa tunajua ule mwanga unatokea wapi wala
zile damu zilikuwa zinatokea wapi.
Nilijishikilia vizuri na kujivuta taratibu bila kusababisha kelele
ya aina yoyote, nikafanikiwa kuchungulia upande wa juu ambako
sasa bomba lilikuwa pana na likiwa limelazwa kama lile tulilo-
ingilia kutokea baharini, nikagundua kwamba tulikuwa tumefika
uwanja wa vita sasa.
Kulikuwa na watu kibao wakiwa wamejibanza kwenye bomba
kwa kushonana, wote wakiwa wamegeukia upande ule ambao
bomba lilikuwa linatokea kwa maana ya ‘ground zero’, wakiwa ni
kama wanasikilizia kitu.
Harakaharaka nilirudisha kichwa chini, nikampa ishara kiongozi
wa marine ambaye naye kwa umakini mkubwa alitoa kichwa na
kuchungulia, naye akashtuka na kurudisha kichwa harakaharaka,
tukawa tunatazamana kwa hofu na kwa kuwa macho yalikuwa
yameshazoea giza na kutiririkiwa na maji taka, tuliweza kuonana
vizuri.
Wakati hayo yakiendelea, yale maji ya baharini yalikuwa yanazi-
di kuingia kwa kasi na sasa yakaanza kujaa kwenye eneo hilo na
kuyazuia maji taka yasielekee tena baharini zaidi ya kutuama eneo

735 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

hilo, yakawa yanazidi kuongezeka kwa kasi kubwa.


Ilikuwa inatakiwa tufanye maamuzi ya haraka kwa sababu maji
yalikuwa yanaendelea kujaa kwa kasi na kama tungeendelea
kuchelewa, maana yake ni kwmaba baada ya kujaa kwenye eneo
lote lile la maungio, yangeanza kuelekea ndani ya ‘ground zero’ na
kile nilichokuwa nimeonywa mwanzo kingetimia na kuifanya kazi
iwe ngumu kuliko kawaida.
Kibaya zaidi ni kwamba kama nilivyoeleza kuanzia mwanzo,
kabla ya kuzamia baharini, nilivua kifaa changu cha mawasiliano
kwa hiyo sikuwa najua ni nini kilichokuwa kinaendelea kule juu na
sikuwa na uwezo wa kuwasiliana na wenzangu.
Akili ilinicheza haraka, eneo nililokuwa mimi, maji yaliyokuwa
yakitiririka kutokea juu, hayakuwa mengi, nikajivuta pembeni
kidogo kwa kutumia mkono mmoja na sasa nikawa sehemu am-
bayo maji hayanigusi kabisa.
Ilibidi niiachie bunduki yangu, ikawa inaning’inia, kwa kutumia
mkono ambao ndiyo awali nilikuwa nimeshika bunduki, nilivua ile
mask iliyokuwa inanisaidia kuvuta oksijeni kutoka kwenye mtungi
niliokuwa nimeubeba mgongoni, nikapokelewa na harufu kali kwe-
likweli ya maji taka.
Sikujali, harakaharaka nilitoa kimfuko kilichokuwa na vifaa vy-
angu nilivyovivua, kikiwemo kifaa cha mawasiliano. Huku nikiwa
nimening’inia kwa mkono mmoja kwenye vile vyuma vya ngazi,
nilikivaa kifaa cha mawasiliano na kukibonyeza, moja kwa moja
nikawa hewani.
Kitendo cha kubonyeza tu kifaa hicho, muda huohuo nilim-

736 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

sikia baba yake Saima akitaka nijibu kama nipo salama, nadhani
walishajaribu kunitafuta mara kadhaa bila mafanikio. Kwa jinsi
alivyokuwa anazungumza, sauti yake ilikuwa ikitetemeka ikione-
sha kuwa yupo kwenye pilikapilika za hali ya juu.
“Kiongozi wa PSU ameasi! Anashirikiana na hawa wendawaz-
imu, wanatushambulia vikali kutokea kwenye chemba, wamemteka
namba moja na inavyoonekana wamemjeruhi,” alisema baba yake
Saima huku akiwa anaonekana ni kama anakimbiakimbia, milio ya
risasi ikawa inasikika zikirindika kwa kasi kubwa.
Yaani ule muda mfupi tu niliokuwa ndani ya bomba, kumbe
mambo yalikuwa yamebadilika kuliko kawaida, nikawa natamani
nimjibu lakini nikawa naogopa kwamba nikifumbua mdomo tu,
nitawashtua wale wendawazimu waliokuwa ndani ya bomba, mita
chache tu kutoka pale tulipokuwepo.
Ilibidi nijaribu kutumia njia ya dharura ya mawasiliano ambayo
haihusishi sauti, nikawa nagonga kwenye spika ya kifaa changu
cha mawasiliano kwa utaratibu maalum, harakaharaka akawa ame-
shanielewa.
Hali ambayo tulikuwa tumefikia sasa ilikuwa ni ile kufa na
kupona kwa sababu risasi zilikuwa zinarindima kisawasawa, kule
kwenye bomba zilikuwa hazisikiki lakini kwenye kifaa cha ma-
wasiliano zilikuwa zinasikika vizuri kabisa.
Harakaharaka nilikivua kile kifaa cha mawasiliano na kuvaa
mask yangu, angalau sasa nikawa napata hewa safi, nikavuta pumzi
ndefu nikiwa bado sijui nini cha kufanya kwa wakati huo.
Nilichokiamua ni kwamba sasa liwalo na liwe, lazima tuwakabili

737 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kwa sababu kama nilivyosema maji yalikuwa yakizidi kuongezeka,


nikampa ishara kiongozi wa marine kwamba sasa tunajitosa, naye
akawapa ishara wenzake, nikahesabu kwa vidole moja mpaka tatu,
nikajivuta kwa kasi na kujitosa kwenye lile bomba kimyakimya,
bunduki ikiwa mbele, kidole kikiwa kwenye trigger, tayari kwa
chochote.
Kiongozi wa marine naye alikuwa ‘sharp’ kwelikweli, naye aka-
wa ameshajivuta na kuingia kwenye bomba, mita chache nyuma
yangu. Nikahesabu tena mpaka tatu, tukawasha tochi zetu.
Kitendo cha kuwasha tochi, kiliwashtua kuliko kawaida wale
wendawazimu, nadhani hawakuwa wametarajia kabisa kwamba
tunaweza kuwafuata kule chini na kutokea nyuma yao.
Jambo ambalo tulikuwa nalo makini, ni kwamba tulitakiwa kuto-
fyatua risasi kiholela mpaka itakapotulazimu kwa sababu hatukuwa
tunajua namba moja yuko kwa upande gani na ni yupi kati yao kwa
sababu kama nilivyosema, tulikuwa tumetokezea kwa nyuma yao,
tena ndani ya bomba ambalo huwezi hata kugeuka nyuma haraka.
“Tulia hivyohivyo, yeyote atakayegeuka tutammwaga ubongo,
usalama wenu ni kutii kila mtakachokuwa mnaambiwa,” nilisema
kwa sauti ya mamlaka ambayo kwa sababu tulikuwa ndani ya
bomba ilikuwa ikisikika kwa mwangwi!
Amri yangu ilifuatiwa na milio ya bunduki kama tano hivi ku-
kokiwa, kutoka kwa wale vijana tuliokuwa tumeongozana.
“Songa mbele bila kugeuka nyuma,” nilisema, bado wakawa
wamepigwa na butwaa, lilikuwa ni tukio ambalo nadhani hakuna
aliyekuwa amelitegemea kati yao, ikabidi waanze kusukumana ku-

738 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

songa mbele, na sisi tukawa tunazidi kusogea mbele kwa tahadhari


kubwa kuliko kawaida.
Muda huohuo, mimi nilikuwa naendelea kuwasiliana na wenzan-
gu kwa kutumia kifaa changu cha mawasiliano, nikamjibu baba
yake Saima kwa lugha ya kificho nikimjibu swali ambalo aliniuliza
awali lakini nikawa siwezi kumjibu.
Wakati tukizidi kuwasukuma mbele taratibu na kwa tahadhari
kubwa, maji ya bahari yalikuwa yameshajaa kwenye lile eneo la
‘joint’ na sasa yakawa yanaanza kuja kwenye lile bomba. Sikujali
kwa wakati huo kwa sababu nilichokuwa nimekikusudia, kilikuwa
tayari kimeshaanza kutimia.
Kila mmoja alishangaa sana nilipowaeleza kwamba tulikuwa
ndani ya bomba, mgongoni mwa wale wendawazimu, nikamsikia
baba yake Saima akishusha pumzi ndefu na kuniuliza ni nini hasa
nilichokuwa nimekikusudia.
Nilimweleza kwamba tutaendelea kuwasukuma kusonga mbele
mpaka pale kwenye lile shimo walilokuwa wamelichimba na ku-
fanikiwa kulitumia kujaribu kutorokea.
Nikaendelea kuwaeleza kwa lugha ya kificho kwamba nguvu
zote zinatakiwa kuelekezwa kwenye eneo hilo kwa sababu ndipo
kitakapokuwa kitanzi chao cha mwisho.
“Kule ndani hakuingiliki, kama nilivyokwambia kiongozi wa
PSU ameasi na yeye ndiye anayetumika kutusogeza nyuma ili hao
wendawazimu wapate njia ya kutokea,” alisema baba yake Saima,
nikawa ni kama sijamuelewa kile alichokuwa anakisema.
“Tunawezaje kurudishwa nyuma na mtu mmoja? Maisha ya

739 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

namba moja yapo hatarini, hata ikilazimu kumuangusha aangush-


we kwa sababu dawa ya msaliti huwa inafahamika.”
“Siyo mmoja, nimekueleza kuhusu yeye lakini huku nje hali
imechafuka! Wanaongezeka mmoja baada ya mwingine, hata sijui
wanatokea wapi, tumeshawaangusha kama wanne hivi, vijana
wetu kadhaa wamepata madhara kiasi,” alisema, kauli yake ikazidi
kunichanganya.
Kwa maelezo hayo, sasa ilikuwa ni lazima kila tulichokuwa
tunakifanya, kiongezwe kasi zaidi kwa sababu kwa jinsi mambo
yalivyokuwa yanakwenda, tungeweza kupata madhara zaidi na
hofu ya kila mmoja ilikuwa ni kwa namba moja.
Baba yake Saima akanieleza kwamba walikuwa wamefuatilia ki-
faa maalum ambacho namba moja huwa anatembea nacho kila seh-
emu kwa ajili ya kujua mahali alipo na kilikuwa kinaonesha bado
yupo ndani ya bomba ingawa hawakuwa wanajua ana hali gani.
Nilimsisitiza kwamba naamini namba moja alikuwa ameshikiliwa
na wale watu ambao tulikuwa tukiwaswaga kule kwenye bomba na
ndiyo maana nataka nguvu kubwa ielekezwe huko kwa muda huo.
Nashukuru baba yake Saima alinielewa na muda huohuo nikawa
namsikia akiwapanga vijana kwa ajili ya kuingia kwa nguvu kule
ndani kwa ajili ya kumkabili kiongozi wa PSU ambaye nilielezwa
alikuwa amebadilika na kuwa kama mnyama mkali wa mwituni,
akiwafyatulia risasi mpaka vijana ambao yeye ndiye aliyekuwa
kiongozi wao kabla hajaasi.
Tulikuwa tukiendelea kuwaswaga wale wendawazimu kusonga
mbele, nao wakawa wanaendelea kutii kila tulichokuwa tunawaam-

740 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

bia, akili yangu ikanituma kwamba lazima kuna jambo walikuwa


wanalisubiria litokee ili watugeuzie kibao kwa sababu isingekuwa
rahisi nanma hiyo kuwanasa watu walioweza mpaka kumteka
namba moja na kujaribu kutoroka naye.
Ni sababu hiyo ndiyo iliyonifanya niamini kwamba lazima
watakuwa wanasubiri wafike kwenye lile shimo walilolitumia
kutoroka na namba moja! Niliifikiria familia yangu, nikawa nata-
fakari ni vipi Saima wangu ataishi endapo itatokea jambo lolote
baya likanipata!
Hata sijui ni kwa nini nilifikiria hayo lakini nadhani yale maz-
ingira tuliyokuwepo kwa wakati huo ndiyo yaliyonifanya niwaze
hivyo kwa sababu uhai na kifo vilikuwa vinatenganishwa na mstari
mwembamba sana, na zile damu zilizokuwa zimetapakaa kwenye
bomba ndiyo zilizidi kufanya akili zangu ziwe zinanienda mbio
kuliko kawaida.
Tulizidi kuwasukuma mbele, maji ya bahari nayo yakawa
yanazidi kupanda, na baada ya kama dakika kumi hivi za kutam-
baa kwenye bomba, hatimaye tulifika kwenye lile shimo ambalo
ndiyo lililotumika kumtorosha namba moja kutokea kwenye moja
kati ya vyoo vya ndani kwenye vyumba vya ndani ya ground zero!
Nilichokuwa nimekihisi mwanzo ndicho tulichoenda kukutana
nacho, baada ya wahalifu wote kuwa wametoka kwenye bomba na
kuwa na uwezo wa kusimama, sisi tukiwa bado ndani ya bomba,
walitugeuzia kibao.
Risasi zilianza kufyatuliwa kama mvua kuelekea kule kwenye
bomba ambako sisi bado tulikuwa ndani, ikabidi na sisi tusipoteze

741 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

muda na kuanza kujibu mashambulizi muda huohuo, lakini hapo-


hapo nikabaini tatizo lingine kubwa.
Kabla sijaelezea ni tatizo gan ambalo tulikutana nalo, nilitaka
kufafanua kwa nini licha ya risasi kumiminwa kama mvua haziku-
weza kuleta madhara kwetu, hasa kwa sisi tuliokuwa mbele kabisa.
Kitaalamu ni kwamba, mtu akiwa amelala chini au akiwa ana-
tambaa, ni vigumu sana kwa mtu aliyesimama kumpiga risasi na
kumlenga. Lakini mtu akiwa amelala au akiwa anatambaa kwa
kutumia tumbo, anaweza kumpiga risasi mtu yeyote bila kukusoea.
Hiyo ndiyo sababu wanajeshi au watu wote wanaopitia mafunzo
ya kijeshi, huwa wanafundishwa zoezi muhimu sana la kutambaa
kwa kutumia tumbo lakini pia kupiga risasi wakiwa wamelala.
Hii pia ndiyo sababu ambayo watu huwa wanashauriwa kwamba
unaposikia risasi zinarindima, kitu cha kwanza siyo kutimua mbio
kwa sababu unaweza kupigwa hata kama aliyekuwa analengwa
siyo wewe, badala yake unatakiwa kuwahi kulala chini haraka
iwezekanavyo, tena unalalia tumbo na kujinyoosha kabisa! Ukifan-
ya hivyo unakuwa kwenye nafasi ya kusalimika hata kama risasi
zitarindima saa zima.
Hicho ndicho kilichotokea, wao walikuwa wamesimama, sisi
bado tupo ndani ya bomba tukitambaa kusonga mbele, kwa hiyo
risasi zote ziliishia kutoboa kingo za bomba.
Nilichokuwa nimekibaini, kumbe walikuwa wamemteka namba
moja na walinzi wake kama watano hivi na wote walikuwa wame-
fungwa pingu na kuvalishwa vitambaa usoni halafu wakawe-
kwa mbele, yaani wao ndiyo watumike kama kinga endapo sisi

742 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

tutafyatua risasi au endapo risasi zitafyatuliwa kutokea upande


wowote.
Niliweza kuona vyema kwa sababu kama nilivyosema, mimi
nilikuwa mbele zaidi, kwa hiyo hapohapo nikatoa ishara kwamba
hatutakiwi kufyatua risasi kwa sababu tungekuwa tunajikaanga
wenyewe kwa mafuta yetu.
Baada ya kuona timu yangu yote tuliokuwa kwenye bomba
tumeelewana, nilibonyeza kifaa changu cha mawasiliano na ku-
waeleza watu wote tuliokuwa kwenye oparesheni mahali ambapo
tulikuwa tumefikia.
Kama kawaida, nilizungumza kwa lugha ya kificho lakini am-
bayo ilifikisha ujumbe kwa kila mmoja, taharuki nyingine ikaibuka
kwa sababu niliwaeleza kwamba kati ya watu waliokuwa wame-
chukuliwa mateka na kutumika kama ngao, alikuwemo namba
moja.
Nilipotakiwa kueleza kama nina uhakika wa kiasi gani kama
namba moja alikuwepo wakati nimeshaeleza kwamba wame-
fungwa vitambaa vya kuziba kabisa nyuso zao, nilieleza kwamba
mavazi aliyokuwa ameyavaa jioni hiyo nilikuwa nimeyaona na
yalikuwa yakifanana na mavazi ya mmoja kati ya wale mateka
waliokuwa wanashikiliwa.
Baba yake Saima aliingilia kati na kueleza kwamba hiyo haitoshi
kuwa uthibitisho wa kuonesha kwamba niliyekuwa namuona kweli
alikuwa ni namba moja kwa sababu kwa jinsi wendawazimu hao
walivyokuwa na mbinu kali, huenda wakawa wamembadilisha
nguo na kumvalisha za mtu mwingine ili kutupoteza maboya.

743 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Baada ya kueleza kile alichokisema, niliona ni kweli anaweza


kuwa na hoja, hata sijui ni kwa nini sikuwa nimefikiria jambo lile.
Ilibidi nijivute kwa umakini wa hali ya juu kusogea mbele kidogo
ili niweze kuwatazama wote vizuri.
Uzuri ni kwamba baada ya kuona sisi tumeacha kufyatua risasi,
nao waliacha kufyatua risasi, wakawa ni kama wanatusikilizia.
Niliwatazama vizuri, mmoja baada ya mwingine, nilishindwa
kupata picha kamili kwa sababu kule chini kulikuwa na mwanga
hafifu ila nilichoweza kukibaini haraka, ni kwamba yule aliyekuwa
amevaa nguo za namba moja ambaye akili za mwanzo zilinituma
kuamini kwamba ndiye mwenyewe, chini alikuwa amevaa mabuti.
Sikuwa najua vizuri ratiba za mavazi za namba moja lakini ki-
tendo cha kuona tu kavaa mabuti, nilijua lazima kile alichokisema
baba yake Saima ndicho kilichokuwa kimefanyika, akili kubwa
kwelikweli!
Nilijaribu kuwafuatilia wale wengine kwa umakini, nikagundua
kwamba miongoni mwao, ni mmoja tu ndiyo alikuwa amevalia
viatu ‘casual’, wengine wote walikuwa na mabuti, tena yale ya kazi
kama ambayo nilikuwa nimevaa mimi, mabuti ya jeshi!
Kwa umakini wa hali ya juu nilirudi nyuma taratibu, nikabonyeza
kifaa changu cha mawasiliano na kutoa taarifa kwamba kuna
uwezekano mkubwa namba moja alikuwa amebadilishwa nguo ili
kuzidi kutuchanganya.
Ushauri alioutoa Chief Mwaipopo, ni kwamba kwa hatua tuli-
yokuwa tumefikia, kwa kuwa tumeshawabananisha kwenye kona,
tuwaamrishe wajisalimishe wenyewe, jambo ambalo lilipingwa na

744 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

kila mmoja.
Hoja iliyotolewa na wote waliokuwa wanapinga, ni kwamba
kama shida yao ilikuwa ni kumteka namba moja, jambo ambalo
walikuwa wamefanikiwa, suala la kujisalimisha lilikuwa haliweze-
kani na pengine wangeweza hata kumdhuru.
Mkurugenzi alitoa hoja ambayo hakuna yeyote kati yetu ambaye
alikuwa ameifikiria kwa wakati huo. Alitaka kwamba vijana wa
Cyber wajiridhishe kwanza kama ni kweli namba moja alikuwa
miongoni mwa wale mateka kwa kutumia teknolojia.
Nilieleza awali kwamba miongoni mwa vifaa vya ulinzi alivyo-
navyo namba moja, ni kifaa maalum ambacho kitaalamu kinaitwa
‘transponder chip’, kifaa kidogo sana ambacho lazima namba moja
awe nacho mwilini muda wote.
Kifaa hiki, huwa kinasoma ‘GPS’ kwa ajili ya kujua namba moja
yupo wapi hasa kunapotokea dharura za kiusalama kama hizo.
Awali walikuwa wameshascan na kutoa majibu kwamba alikuwa
ndani ya bomba lakini kwa kuwa sasa tulikuwa tumeshawarudisha
nyuma mpaka kwenye shimo lile, ilikuwa ni lazima warudie tena
kuscan ili tuwe na uhakika kwa asilimia mia moja.
Akaendelea kueleza kwamba endapo tukishapata uhakika, ndipo
sasa tutumie njia ya majadiliano, kwa kitaalamu tunaita ‘negotia-
tion’. Mjadala mwingine ukaibuka kwamba sera za kiusalama,
zilikuwa haziruhusu majadiliano ya aina yoyote na wahalifu hatari
kama magaidi.
Ilibidi nikae kimya kusikiliza mjadala, moyoni nikawa najisemea
kwamba endapo watu wote wangejua ni mazingira ya hatari kiasi

745 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

gani ambayo tulikuwa nayo kule chini, kamwe wasingeendelea


kupoteza muda kwenye mijadala kama ile!
Ni kama baba yake Saima alikuwa amesoma ukimya wangu,
akaingilia kati na kueleza kwamba kwa kuwa tulikuwa kwenye
dharura, jambo hilo pia lilitakiwa kufanyika kwa dharura, hata
kama itabidi kuvunja baadhi ya sheria.
Hicho ndicho nilichokuwa nampendea baba yake Saima, kuna
wakati alikuwa anakuja na maamuzi magumu kabisa hata kama
anajua wazi kwamba kufanya jambo fulani ni kinyume cha sheria,
kanuni na taratibu zilizopo.
Ilibidi kila mmoja akubaliane na alichokisema, mkurugenzi
akaendelea kueleza kwamba ipatikane njia ya kuwasiliana na
magaidi hao na waelezwe kwamba tulikuwa tumewazingira kila
mahali kiasi kwamba hakuna namna yoyote wanayoweza kutoka
salama, kisha baada ya hapo tuwape ‘options’ za kuchagua ili
wamuachilie namba moja hata kama ni kwa ahadi za uongo kwam-
ba tutawaruhusu waondoke salama bila kuwakamata.
Ungeweza kuona kama lilikuwa ni wazo la kipuuzi kwa wakati
huo lakini ukweli ni kwamba, hiyo ndiyo njia pekee ambayo in-
geweza kutusaidia kwa wakati huo na mimi niliiunga mkono kwa
asilimia mia moja.
Pengine kama ulikuwa hujui, suala la ‘negotiation’ ni taaluma
kabisa katika vyombo vya ulinzi na usalama, yaani kuna watu
ambao wamesomea kabisa kufanya majadiliano na wahalifu kwa
lengo la kupata kile mnachokitaka na wao kuwapa wanachokitaka,
ingawa mara nyingi huwa wahalifu wanapewa ahadi tamu ambazo

746 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

huwa ni za uongo.
Ahadi tamu ambazo huwa zinatumika ni kama kuwapa usafiri
wa kuwawezesha kuondoka salama bila kukamatwa kutoka eneo
la tukio, au kufutiwa mashtaka yote yanayowakabili na wakati
mwingine kuwaahidi kiasi kikubwa cha fedha ili kuwahadaa na
kuwajaza tamaa ili mwisho wa yote wafanye kile ambacho nyie
mnakitaka.
Basi baada ya majadiliano ya hapa na pale, hoja ilipita, ikatakiwa
itafutwe namna ya kuwasiliana kwa sauti na wale wahalifu kuanzia
waliokuwa wamejifungia kule ndani mpaka wale waliokuwa kule
chini, ikakubaliwa kwamba wale waliokuwa na namba moja kule
chini ndiyo ambao wanatakiwa kufanya nao majadiliano.
Nilishaeleza kwamba miongoni mwa waliokuwa wamejifungia
kule ndani, alikuwa ni kiongozi wa PSU ambaye hata sijui nini
kilitokea mpaka akaasi na kuungana na watu waliokuwa wanataka
kuiangusha Magogoni! Yaani mtu ambaye jukumu lake kubwa
ilikuwa ni kuhakikisha usalama wa namba moja, ndiye aliyekuwa
amekengeuka na kuwa mtu hatari kuliko kawaida, akishirikiana na
wale wendawazimu.
Harakaharaka vijana wa Cyber na wale wa IT walifanya mautun-
du yao, mtaalamu wa majadiliano ya kiusalama ambaye kiukweli
sikuwa namjua ni nani, akaanza kuzungumza na sauti yake ikawa
inasikika mpaka kule chini akitumia vifaa maalum vya kiteknolojia
kuzungumza ambapo sauti yake ilikuwa inasikika vizuri kabisa.
Alianza kwa kujitambulisha, akaeleza kwamba tayari wamesha-
wajua watu wote waliokuwa wamevamia Magogoni usiku ule na

747 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wale waliokuwa wakimshikilia namba moja, akaeleza kwamba


tayari tumewazingira kila upande na hakuna namna yoyote wanay-
oweza kufanya ili kutoka salama.
Njia pekee ilikuwa ni kwa vikosi vya ulinzi kufanya nao mabadil-
ishano, wao wamkabidhi kwetu namba moja akiwa salama pamoja
na walinzi wake, kisha sisi tutawapa nafasi ya kipekee ya kuondo-
ka salama eneo hilo bila kukamatwa wala kufunguliwa mashtaka.
Akaeleza kwamba tayari gari maalum lilikuwa limeandaliwa kwa
ajili ya kuwawezesha kuondoka Magogoni salama bila kuguswa
na mtu yeyote, isipokuwa kwa masharti kwamba lazima wakubali
kumwachilia namba moja! Ukimya mrefu ukapita kwa sababu
kama ni kusikia, kila mmoja alikuwa amesikia vizuri kabisa, hata
sisi kule kwenye bomba japokuwa maji yalikuwa yakizidi kuon-
gezeka, tuliweza kusikia vizuri kabisa.
Kila mmoja kati yetu alikuwa na shauku kubwa ya kutaka kusikia
ni nini watakachokisema wendawazimu wale na ni nani kati yao
ndiyo atazungumza kwa niaba ya wenzake.
Jambo ambalo halikutarajiwa kabisa likatokea, kiongozi wa PSU
ambaye alikuwa ameasi, eti ndiyo akawa anajibu kwa niaba ya
wenzake.
“Ananias Mtafya, Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi wa Rais, wewe
si miongoni mwao, wewe ni mwenzetu na nakuhakikishia kwamba
kilichotokea leo ni mambo yetu ya ndani na kinaweza kumalizwa
na ukaendelea na kazi kama kawaida,” alisema yule ‘negotiator’
wetu ambaye baadaye nilikuja kugundua kwamba ni mtu ambaye
tunafahamiana vizuri kabisa.

748 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Mimi siyo miongoni mwenu, mimi si mwenzenu!”


“Labda kama unasema kuanzia leo wewe siyo mwenzetu basi
hapo tunaweza kukuelewa lakini tunaamini kuanzia mwanzo wewe
ni mwenzetu na tumefanya mambo mengi pamoja!” alisema yule
muongoza majadiliano, watu wote tukawa tunasikia kila kilichoku-
wa kinaendelea, tukawa kimya kabisa.
Waliendelea na majadiliano, negotiator akijaribu kucheza na akili
za Ananias Mtafya, akawa ni kama kuna kitu fulani hivi anakita-
futa, kwa kuwa taaluma hiyo haikuwa yangu, nilitulia nikiwa na
shauku kubwa ya kutaka kujua ni nini hasa alichokuwa anakwenda
kukifanya.
Ananias Mtafya ndiye huyu ambaye leo alikuwa amegeuka na
kuwa muasi! Kachero mbobezi aliyepitia mafunzo ya kijeshi kwa
ngazi moja baada ya nyingine, akipanda vyeo kutokana na umahiri
wake katika medani za kivita, baadaye akapewa mafunzo maalum
ya ukachero, akapelekwa nchi mbalimbali kwa mafunzo na alipore-
jea akateuliwa kwenye kitengo maalum cha ulinzi wa namba moja,
PSU ambako nako alikuwa akipanda cheo hatua kwa hatua hadi
kufikia kuwa kiongozi wa juu kabisa.
Akiwa na uziefu wa takribani miaka kumi na saba kwenye kazi,
hakuna mtu hata mmoja ambaye angeweza kuwa na mashaka na
uadilifu wa kiongozi huyu wa PSU! Kwa awamu tofauti, alikuwa
wamewatumikia viongozi wakuu wa nchi watatu, awamu moja
akiwa kama afisa wa kawaida na awamu akiwa kiongozi mwan-
damizi na kiongozi mkuu.
Kila mmoja alikuwa akimuamini sana kiongozi huyu wa PSU,

749 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

nakumbka hata baada ya kikosi kazi chetu kuwasili Magogoni na


kuanza kazi, nilizungumzia ishu ya kuwepo kwa ‘nyoka’ ndani ya
Magogoni, ambao ndiyo waliokuwa wakitumiwa kutoa siri za kila
kilichokuwa kinaendelea na nikataka tujitenge kabisa na maafisa
wote wa Magogoni ili siri zetu zisivuje lakini baba yake Saima
pamoja na mkurugenzi wakamtetea.
Lakini ni huyuhuyu ndiye aliyekuja kugeuka na kuwa kikwazo
kikubwa kwenye kazi yangu na mwisho nikajikuta tumejenga
uhasama ambao hata sijui chanzo chake ni nini, eti akidai kwamba
mimi nilikuwa najifanya mjuaji.
Kila kitu sasa kilikuwa kinafunguka na kutoa picha kubwa zaidi
na ambacho nilihisi, ni kwamba pengine hata uamuzi wa namba
moja kutoka kwenye ‘safe house’ alikokuwa amehifadhiwa kwa
sababu za kiusalama na kurudi Magogoni, tena muda ambao hali
ilikuwa tete kwelikweli, yawezekana ni yeye ndiye aliyemshawi-
shi.
Majadiliano yaliendelea, yule mtaalamu wetu wa majadiliano
naye akawa anazidi kumjaza kiongozi wa PSU ili asijione kama
amefanya makosa ambayo hayawezi kusameheka.
Baada ya kama dakika ishirini hivi za majadiliano, watu wote
tukiwa kimya kabisa tukisikiliza majadiliano yaliyokuwa yakien-
delea, hatimaye kiongozi muasi wa PSU alikubali ofa iliyokuwa
imetolewa kwake na wale wendawazimu wenzake ingawa bado
alikuwa anasitasita sana, nadhani ni kwa sababu alikuwa anajua
kwamba mara nyingi ahadi hizo huwa ni feki.
Alikubali kuweka silaha chini, akakubali yeye na wenzake ku-

750 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

waachia namba moja na walinzi wake lakini kwa masharti kadhaa.


Sharti la kwanza, eti alitaka umeme uzimwe wakati wakitoka, la-
kini pia walitaka wapewe fedha kwa ajili ya kufanikisha safari yao
ya kuondoka na mwisho, walitaka gari ambalo watapewa, lijazwe
mafuta ‘full tank’ na asitokee mtu yeyote wa kuwafuatilia.
Mwisho kabisa, eti alitaka kati ya watu wote waliokuwa waki-
washikilia, watamuachia namba moja pekee lakini wale wengine
ambao kimsingi ni maafisa wa kikosi cha PSU waliokuwa chini
yake, wataondoka nao kama dhamana ya usalama wao mpaka eneo
watakalohisi kwamba sasa wapo salama.
Yalikuwa ni masharti ya kipuuzi, ambayo hakuna mtu yeyote
mwenye akili timamu angeweza kuyatoa wala angeweza kuyakub-
ali, labda kama ni mtego.
Ajabu sasa, ‘negotiator’ wetu alikubaliana na kila walichokuwa
wanakitaka na muda huohuo, mipango ikaanza kufanyika. Wakati
hayo yakifanyika, upande wa pili na sisi ni kama oparesheni ili-
kuwa imeanza upya.
Licha ya ‘negotiator’ wetu kukubali kile alichokuwa anaambiwa
na kiongozi muasi wa PSU, Ananias Mtafya, ukweli ni kwamba
ahadi zote alizokuwa anapewa zilikuwa ni feki na zisizotimilika.
Kwa walichokuwa wamekifanya, kisheria ni kosa la uhaini na
kosa hilo, hukumu yake huwa ni kuhukumiwa kunyongwa mpaka
kufa, duniani kote ndivyo ilivyo! Uhaini linatajwa kuwa kosa
hatari zaidi ambalo yeyote anayelifanya, hukumu yake ipo wazi
kabisa.
Nadhani, Ananias Mtafya alikuwa anajua kwamba kosa waliloli-

751 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

fanya halina msalie mtume na ndiyo maana akataka waondoke na


wale maafisa wa PSU waliokuwa wamewateka kama dhamana ya
usalama wao! Ukijua hili, wenzako wanajua lile, ndivyo Waswahili
wanavyosema na kwa kiongozi huyo wa PSU na wendawazimu
wenzake, hakika walikuwa wamejichanganya.
Tulichokuwa tumekubaliana, ni kwamba baada tu ya namba moja
kuachiwa na wote tukajiridhisha, ambacho kingefuatia ingekuwa
ni mapambano ya kufa na kupona kwa sababu ingekuwa ni kashfa
kubwa mno kwetu kwa wendawazimu wale kuja kutuchezea
mpaka sehemu nyeti kama ile kisha watoke salama.
Ilikuwa ni lazima wote wakamatwe, tena wakiwa hai, ilikuwa ni
lazima kiongozi wa PSU akamatwe akiwa hai, hapo ndipo udhaifu
wetu ungeweza kuonekana siyo kosa kubwa tena bali ushujaa!
Hata katika maelezo, ingekuwa rahisi zaidi kueleza kwamba
kiongozi wa PSU aliyewasaidia magaidi kuingia ikulu na kujaribu
kumteka namba moja, alikuwa amekamatwa lakini yote tisa, kumi
ni kwa namba moja mwenyewe!
Kwa yaliyotokea,ilikuwa wazi kwamba alikuwa anakihitaji
kichwa cha Mtafya kuliko kitu kingine chochote kwa hiyo makosa
yoyote ambayo yangesababisha atoroke, yangetugharimu kuliko
kawaida.
Kwa hiyo tulichokubaliana, ilikuwa ni kuhakikisha kwanza
namba moja yuko salama kisha ndiyo mambo mengine yafuatie.
Mipango ikafanyika bila kupoteza muda na eneo lote la ‘ground’
zero likawekwa kwenye hali ya hatari.
Ilibidi mimi na vijana wangu tubakie kulekule chini kwanza

752 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

mpaka makubaliano yatakapoanza kutekelezwa ambapo mimi


ndiyo nilikuwa na jukumu la kwanza la kuhakikisha namba moja
anakabidhiwa akiwa salama.
Baada ya kila kitu kuwa kimekaa sawa, umeme ulizimwa kama
Mtafya na wenzake walivyokuwa wanataka na muda huohuo, mimi
na vijana wangu kule chini ya bomba, tukajiweka katika hali ya
utayari.
Baada ya umeme kuzimwa na Mtafya kujiridhisha kwamba
makubaliano yalikuwa yakienda kama walivyokubaliana, alitoa
amri kwa wale wendawazimu kule chini waanze kutoka, kwa
utaratibu maalum, tukawa tunafuatilia kwa makini kila kilichoku-
wa kinaendelea na baada ya kuwa wamepanda ngazi ya chuma
iliyokuwepo eneo hilo kuelekea juu, na sisi tulijitokeza kutoka
kwenye bomba mpaka kwenye shimo lile, tukawa tunaangaza huku
na kule, kwa tahadhari kubwa.
Baada ya kujiridhisha kwamba eneo hilo lilikuwa salama, tu-
lianza kupanda ngazi kuelekea kule ndani, mimi nikiwa mstari wa
mbele kabisa, bunduki yangu ikiwa mkononi, tayari kwa chochote.
Baada ya kufanikiwa kupandisha mpaka kule ndani ya kile choo,
nilitafuta sehemu salama na kujibanza, wenzangu nao wakawa wa-
napanda mmoja baada ya mwingine na kujibanza, wakati Mtafya
na wenzake wakiwa wanaamini kwamba sasa kile walichokuwa
wanakitaka kinaenda kutimia, hawakuwa wakijua kwamba kumbe
tulikuwa tukiwafuatilia tena kwa karibu kabisa.
Baada ya yule kiongozi wa GSU, Ananias Mtafya na genge lake
kujiridhisha kwamba ni kweli tulikuwa tumekubali kuwaachia

753 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

salama, walianza kutoka, mmoja baada ya mwingine, wakiwa na


wale mateka wao.
Makubaliano yao kama nilivyoeleza awali, yalikuwa ni kwamba
eti lazima waondoke na wale walinzi wa namba moja ambao wa-
likuwa wamewateka ili iwe ni kama kinga yao na baada ya ku-
hakikisha kwamba wameshaondoka na kutoka nje ya mji, eti ndiyo
wangeenda kuwaachia wakiwa salama mbele ya safari.
Wakataka eti wakati wakiwa wanatoka, mmoja kati yao ambaye
ndiye aliyekuwa amemshikilia mateka namba moja, ndiyo atakuwa
wa mwisho kutoka baada ya kuwa wenzake wote wameshatoka
na atatoka akiwa na namba moja ambapo ataenda kumuachia huru
baada ya kuwa ameshaungana na wenzake.
Ambacho hawakuwa wakikijua ni kwamba safari hii tulikuwa
tumejipanga kuhakikisha tunarekebisha makosa yetu yote kwa
kuwadhibiti kabla hawajatoka kwenye geti la ‘ground zero’ na amri
ya siri ilikuwa imeshatolewa kwamba yeyote ambaye angeleta
ubishi, basi kifo kingekuwa haki yake.
Hakuna ambaye alikuwa tayari kuona wendawazimu wale wa-
naendelea kutamba hata baada ya kuwa wametutoa jasho kwa
muda wote huo tangu walipovamia Magogoni na sasa muda wao
ulikuwa ukihesabika.
Kweli kila kitu kilienda kama tulivyokuwa tumepanga, kitendo
cha mimi na timu yangu kuhakikisha tunaziba tena njia ya wao ku-
rudi ndani ya bomba, ilikuwa ni hatua muhimu sana ambayo kikosi
kizima kilikuwa kinakisubiria ili kazi ianze.
Baada ya kuhakikisha tayari mimi na wenzangu tuliokuwa ndani

754 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ya bomba tumeshatoka na kuingia ndani ya chumba ambacho awali


ndicho walichokuwa wamekitumia kumteka namba moja, nilitoa
taarifa kupitia kifaa changu cha mawasiliano.
Wakati huo, wale wendawazimu ambao sasa ilikuwa wazi kwam-
ba aliyekuwa anawaongoza alikuwa ni kiongozi wa GSU, Ananias
Mtafya, nao walikuwa wameshatoka na sasa walikuwa wakisonga
mbele kwenye korido ndefu za Magogoni, wakielekea kwenye
mlango mkubwa wa kutokea nje.
Tuliendelea kuwafuata nyumanyuma kwa tahadhari kubwa na
kwa sababu wao tayari walishakuwa na uhakika kwamba wametu-
zidi ujanja, hawakuwa wakichukua tahadhari za kutosha, akili zao
kwa wakati huo ilikuwa ni kutoroka tu.
Baada ya kuwa na uhakika kwamba sasa walikuwa wakielekea
nje, ilibidi mimi nitumie medani zangu za mafunzo kuwahi kutoka
nje kabla yao. Kwa kutumia dirisha la dharura ambalo lilikuwa
likifunguka zimazima kutoka ndani, nilijirusha mpaka nje, nikat-
ambaa kwenye bustani za maua na sasa nikawa kwenye eneo zuri
ambalo nilikuwa naweza kumuona kila aliyekuwa anatoka.
Ni hapo sasa ndipo kazi ilipoanza rasmi, umeme uliwashwa
ghafla kama tulivyokuwa tumekubaliana, wakabaki wamepigwa na
butwaa kwa sababu hawakuwa wametegemea kama makubaliano
waliyokuwa wamefikia na sisi kwa kumtumia ‘negotiator’ wetu
yanaweza kuvunjwa kirahisi namna hiyo.
Kikosi cha walenga shabaha (sniper) ambao kwa muda mrefu
walikuwa wamepangwa kwenye paa la Magogoni, kilipewa amri
ya kutekeleza kazi yao na kufumba na kufumbua, tulianza ku-

755 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wafyatulia risasi kutoka kila upande.


Kwa kuwa lilikuwa ni tukio la kushtukiza ambalo hawakuwa
wamelitegemea, walijikuta wakikosa mbinu zaidi ya kutaka kurudi
kule ndani ambako awali walikuwa wamejificha wakiwa wanam-
shikilia mateka namba moja na walinzi wake.
Walipojaribu kurudi nyuma, walikutana na moto mwingine ulio-
kuwa unawashwa kutokea ndani, wakakosa cha kufanya zaidi ya
wote kulala chini wakiwa na mateka wao kwa sababu sasa walisha-
gundua kwamba hatuna mchezo tena.
Baada ya kuona wote wamelala chini, baba yake Saima ambaye
alikuwa na kipaza sauti, akiwa upande wa kule getini, aliwasha
kipaza sauti chake na kuanza kutoa maelekezo.
Maelekezo yenyewe aliyoyatoa kama ambavyo tulikuwa tume-
kubaliana, ilikuwa ni kuwalazimisha wasalimu amri kwa sababu
hicho ndiyo kitu pekee ambacho kingeweza kunusuru maisha yao
kwa wakati huo.
Ni kama maelekezo hayo ya baba yake Saima yalikuwa yamem-
kasirisha sana Ananias Mtafya ambaye kwa akili zake alikuwa
akiamini kwamba ametuzidi maarifa, akainuka pale alipokuwa
amelala chini. Hakuinuka peke yake, aliinuka na yule mtu ambaye
walikuwa wamembadilisha nguo na kumvalisha nguo za namba
moja.
“Mmekiuka masharti tuliyokubaliana, sasa mtachagua, turudi
kwenye makubaliano au nimwage ubongo wa namba moja,” alise-
ma huku akiwa amemgusisha bastola yule mtu ambaye wengi wetu
walikuwa wakiamini kwamba ndiyo namba moja kwa sababu kama

756 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

nilivyoeleza, walikuwa wamewavalisha vitambaa vyeusi usoni na


kuwafunga pingu.
Ilibidi muda huohuo nitoe angalizo kwenye kifaa changu cha ma-
wasiliano kwamba yule hakuwa namba moja na nikaeleza ni kwa
sababu gani nilikuwa nasema hivyo. Mtafya aliendelea kusonga
mbele akimtumia yule aliyetraka kutuaminisha kama ndiyo namba
moja kama ngao yake.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, amri ilitolewa kwa walenga
shabaha, kufumba na kufumbua Mtafya alipigwa risasi ya kichwa
na kusababisha adondoke kama mzigo, damu nyingi zikimwagika
mithili ya bomba lililopasuka.
Yule mtu aliyekuwa amemkamata, naye muda huohuo alijivua
kile kitambaa alichokuwa amejifunga usoni na wote tukaweza
kuiona sura yake vizuri, alikuwa mmoja kati ya walinzi wa namba
moja, akiwa amebadilishwa nguo.
Kwa kuwa naye alikuwa ameiva kwenye mafunzo, alijua kuen-
delea kusimama katikati ya uwanja wa vita ni hatari kwake, aka-
jirusha upande alikoangukia Mtafya, akaokota ile bastola yake na
huku mikono yake ikiwa imefungwa pingu, akaanza kufyatua risasi
kuelekea pale wale wendawazimu walipokuwa wamejibanza, wote
tukawa ni kama tumepata nguvu.
Zilimiminwa risasi za kutosha lakini kwa uangalifu wa hali
ya juu ili tusije kuwaua walinzi wa namba moja na namba moja
mwenyewe, wawili kati yao wakafanikiwa kunyanyuka wakiwa na
mateka mmoja.
Nadhanai hawakuwa wamefikiria kwamba kule walikokuwa

757 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wanakimbilia ndiko nilikokuwa nimejibanza mimi, nikasubiri kwa


sekunde kadhaa kisha nikainuka kikomandoo na kusimama mbele
yao, risasi zikiendelea kurindima.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, nilijirusha kikomandoo na ku-
wafyatua mtama wote wawili kisha nikawahi kumdaka yule mate-
ka waliyekuwa naye kwa sababu naye alikuwa akielekea kuanguka
chini na kujibamiza. Uzuri ni kwamba nilimuwahi vizuri, nikam-
daka na kuangukia naye upande wa pili, mimi nikiwa chini yeye
akiwa juu.
Walijarinu kuinuka na kutaka kukimbia lakini walikuwa tayari
wameshachelewa, vijana wa kulenga shabaha waliifanya kazi yao
kikamilifu, eneo lote likatapaa damu kama machionjioni.
Harakaharaka nilimvua kitambaa yule mateka, katika hali am-
bayo hata mimi mwenyewe sikutegemea, nilishtuka kugundua
kwamba alikuwa ni namba moja, akihema mithili ya mtu aliyetoka
kukimbia mbio za mita mia moja.
Sikuwahi kumuona namba moja akiwa na hofu kama siku hiyo,
macho yalikuwa yamemtoka, akiwa ni kama haelewi ni nini kili-
chokuwa kinaendelea.
“Kenny!”
“Mheshimiwa!”
“Walikuwa wanataka kuniua!”
“Usijali uko salama!” nilisema na muda huohuo nikaanza kutam-
baa naye kuelekea ukutani kwa sababu risasi zilikuwa zinaendelea
kurindima kuliko kawaida.
Ambacho kilikuwa kimenipita nikiwa kule chini kwenye bomba,

758 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ni kwamba kumbe kulikuwa na kundi linginela wanaume wenye


silaha walikuwa wamevamia Magogoni na ndiyo hao ambao wa-
likuwa wakijibizana risasi na maafisa wetu wakiongozwa na baba
yake Saima na mkurugenzi.
Baada ya kufika ukutani, ilibidi nimbane namba moja, yeye akae
ukutani na mimi nibaki kama kinga yake, harakaharaka nikawa
taarifu wenzangu wote kupitia kifaa cha mawasiliano kwamba
nilikuwa nimefanikiwa kumuokoa namba moja.
Risasi zilikuwa zikiendelea kurindima kwelikweli, uamuzi uka-
tolewa kwamba natakiwa kufanya kila kinachowezekana nimu-
ingize ndani kwa sababu kule nje hakukuwa salama, huo ukawa
mtihani mwingine mgumu kwangu.
“Nguo zako zinanuka sana, nini shida,” alisema namba moja kwa
sauti ya kutetemeka akijilazimisha kucheka nikiwa nimembana
pale ukutani, nadhani hakuwa anajua kwamba nilitoka kwenye
bomba la maji taka muda mfupi uliopita!
Sikuwa na cha kumjibu kwa wakati huo kwa sababu akili zangu
zilikuwa zinaenda mbio kuliko kawaida, nikiwaza ni kwa namna
gani naweza kumrudisha ndani ambako kutakuwa salama kama
nilivyokuwa nimeelekezwa.
Nilipiga mahesabu ya kukimbia naye kutoka pale tlipokuwepo
mpaka kwenye lango kuu kisha ndiyo tuingie ndani lakini kwa jinsi
risasi zilivyokuwa zikirindima, tena kutoka kila upande, niliona
naweza kutwanga maji kwenye kinu.
Ningekuwa peke yangu, ile isingekuwa kazi ngumu hata kidogo
kwa sababu ninayo mafunzo ya kutosha ya kukimbia kwa mwendo

759 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wa ‘zig zag’ kukwepa risasi, au kutambaa kwa kasi kama ya nyoka


kwa kutumia tumbo na kupita sehemu yoyote hata kama kuna miba
au ‘senyenge’ kwa sababu hayo ni mambo ambayo kila mpiganaji
lazima ayapitie awapo mafunzoni, wenyewe wanaita ‘ku-crawl’ au
kukroo kwa Kiswahili.
Tatizo lilikuwa kwa namba moja, hakuwa na ujuzi wowote wa
masuala ya kijeshi kwa hiyo isingewezekana kukimbia naye kwa
mtindo wa zigzag wala kukroo. Nikiwa bado nawaza nikiwa sijui
nifanye nini, nilisikia mtu akiniita kwa sauti ya kunong’ona, nika-
geuka haraka bunduki ikiwa mkononi.
Alikuwa ni Ustaadh Fundi ambaye mkononi alikuwa amebeba
bunduki ambayo hata sijui alikuwa ameipata wapi, naye akiwa
amelala kwenye bustani za maua na kujikausha kama nyoka.
“Ustaadh Fundi?” niliita kwa mshtuko, huwezi kuamini katika
purukushani zilizokuwa zinaendelea kwa muda wote huo, nili-
shasahau kama nilikuwa nimemuacha ndani ya gari langu.
“Niko tayari kukusaidia, nieleze ni nini unachotaka!”
“Huyu ni nani?” alihoji namba moja, naye akiwa amepigwa na
butwaa, akizidi kujibanza ukutani akiwa nyuma yangu, pale chini
tulipokuwa tumelala.
“Ni msamaria mwema na mtoa taarifa wetu, ametusaidia sana
kuanzia mwanzo wa oparesheni yetu!” nilimfafanulia namba moja
kwa sauti ya chini, nikamuona akiwa anamtazama kwa macho ya
wasiwasi, nadhani kilichokuwa kimetokea kilimfanya sasa asiwe
anamuamini mtu yeyote kirahisi, akashusha pumzi ndefu.
“Sogea karibu, kuwa makini!” nilimwambia, kweli akasogea pale

760 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

tulipokuwepo huku akihema kuliko kawaida.


“Wanaingia kupitia kule kwenye chemba, nimepambana nao
sana lakini wanazidi kuongezeka,” alisema, nikashtuka kwelikweli
kwa sababu ni kweli ni chemba hiyohiyo ndiyo walioingilia wale
wendawazimu wa mwanzo kabisa na hakuna aliyefikiria kwamba
kumbe kuna wengine wanaendelea kuingia na hao ndiyo walio-
kuwa wanafyatuliana risasi na wenzetu kwa muda wote ambao
tulikuwa kule chini.
Muda huohuo ilibidi nibonyeze kifaa changu cha mawasiliano na
kutoa taarifa kwamba kumbe bado wale wendawazimu walikuwa
wakiendelea kuingia kupitia njia ileile waliyoitumia wenzao wa
mwanzo.
Baba Saima akajibu muda huohuo kwamba kumbe ndiyo maana
kila walipokuwa wakipambana nao, walikuwa wakizidi kuongeze-
ka huku ikiwa haifahamiki wanaingilia kutokea wapi kwa sababu
njia zote zilikuwa zimefungwa huku maafisa wenye silaha wakiwa
wametanda kila sehemu.
Muda huohuo amri ikatoka kwamba nguvu kubwa ielekezwe
upande ule na tukapeana neno la siri la namna ya kutambuana
wenyewe kwa wenyewe kwa sababu wale wendawazimu walikuwa
wakiingia wakiwa katika mavazi kama wanayoyatumia maafisa wa
Magogoni pamoja na kitengo.
Baada ya amri hiyo, kazi iliendelea, milio ya risasi ikawa in-
aendelea kusikika huku na kule. Usingeweza kuamini kwamba
eneo linalolindwa vikali saa ishirini na nne, tena na maafisa wenye
uwezo mkubwa wa medani za ulinzi na usalama, lilikuwa limegeu-

761 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ka na kuwa kama uwanja wa vita.


“Tunamuingiza namba moja ndani, ndiyo kazi iliyopo mbele
yetu!” nilimwambia Ustaadh Fundi, nikamuona akigeuka huku na
kule akiwa ni kama anasema hilo jambo haliwezekani kwa wakati
huo kutokana na hali halisi.
“Hapana! Ni salama zaidi hapa kuliko kuhatarisha usalama
wa mheshimiwa kukimbia mpaka kwenye lango kuu, si unaona
mwenyewe?” alisema, nikamuonesha kwa ishara kwenye dirisha
nililokuwa nimelitumia kuruka kutokea kwenye korido za ndani
mpaka kule nje bila kupitia kwenye lango kuu.
“Tunaingia kupitia pale dirishani!” nilisema, namba moja naye
akageuka na kulitazama lile dirisha, akatingisha kichwa akiwa ni
kama hataki kwa sababu dirisha lilikuwa juu kutokea nje na eneo
lenyewe lilikuwa wazi, taa kali zenye mwanga zikiwa zinamulika.
“Nitasimama chini, utanipanda mabegani kisha utamsaidia
kupanda! Ukifika juu unatakiwa kuruka haraka kwenda ndani,
hauwezi kuumia! Akishaingia, utaning’inia kwa mkono mmoja
na kunivuta!” nilimwambia Ustaadh Fundi na namba moja, wote
wakawa ni kama hawaamini kama hicho nilichokisema kilikuwa
kinawezekana.
Nadhani urefu wa mahali dirisha lilipokuwa kutokea chini
kwa nje, uliwatisha! Muda huohuo nilibonyeza kifaa changu cha
mawasiliano na kutoa taarifa ya nilichokuwa nataka kukifanya na
kuomba nipewe ‘backup’, baba yake Saima akaitikia haraka bila
hata kusubiri kusikia wengine watasema nini.
Cha kwanza nilichofanya, ilikuwa ni kuzizima taa zilizokuwa zi-

762 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

nawaka na kumulika eneo lile kwa mwanga mkali! Nilichokifanya,


ilikuwa ni kulenga shabaha kwenye taa ya kwanza, nikapiga risasi,
taa ikatawanyika na kupasukapasuka. Nikalenga taa ya pili, nayo
ikapasukapasuka, nikamalizia na ya tatu, eneo hilo likawa na giza.
Harakaharaka niliinuka na kuanza kusonga mbele, namba moja
akiwa mgongoni kwangu ili hata ikitokea mtu yeyote akishambu-
lia, basi aanze kupambana na mimi kwanza, Ustaadh Fundi akawa
anafuatia kwa nyuma, yeye akitembea kinyumenyume kutazama
nyuma kama nilivyomuelekeza.
Ndani ya sekunde chache tu, tayari tulikuwa tumefika kwenye
lile dirisha, tukalala chini kwanza kupima upepo, hakuna yeyote
aliyekuwa akishambulia ule upande tuliokuwepo.
Nikarudia kutoa maelekezo kwa vitendo, nikapiga goti moja chi-
ni, bunduki ikiwa mkononi, baba yake Saima akanipanda mabegani
na kutafuta balansi kwenye ukuta, kisha akanyoosha mkono kumpa
namba moja, tukasaidiana kumpandisha, wote wawili wakapanda
kwenye mabega yangu na Ustaadh Fundi akawa anaendelea kum-
saidia namba moja apande kwenye mabega yake.
Walifanikiwa, kwa ukakamavu wa hali ya juu nikaanza kujivuta
ili kuinuka kwa sababu bado nilikuwa nimepiga goti, uzito mkub-
wa wa watu wawili walioshiba ukinielemea mabegani.
Haikuwa kazi nyepesi kwa sababu kwa hesabu za harakaharaka,
Ustaadh Fundi alikuwa na kama kilo sabini hivi na namba moja ali-
kuwa na kama kilo tisini hivi. Nilijivuta kikomandoo na hatimaye
nikafanikiwa kusimama, nikawa nahisi ni kama mifupa ya kwenye
mbavu na kiuno inataka kupishana kutokana na uzito.

763 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Ilibidi nibane pumzi ili nisije nikaishiwa nguvu, namba moja aka-
fanikiwa kushika vyuma vya dirisha na bila kupoteza muda aliji-
rushia kwa ndani, uzito ukapungua mabegani. Kasi ikawa Ustaadh
Fundi ambaye hakuwa akifikia kwenye lile dirisha, ikabidi niiachie
bunduki na kuinua mikono yangu miwili kwa ukakamavu, Ustaadh
Fundi akawa ameshaelewa nini cha kufanya.
Alikanyaga kwenye mikono yangu ambayo nilikuwa nimeiten-
geneza na kuwa kama daraja, akafanikiwa kulishika dirisha, akaji-
vuta na kupanda kwa juu, nikashusha pumzi ndefu, sasa ikawa ni
zamu yangu. Ilikuwa inatakiwa nipande haraka iwezekanavyo ili
kuhakikisha namba moja anaendelea kubaki mgongoni kwangu.
Nikiwa najiandaa kurukia kwenye mkono wa Ustaadh Fundi
ambaye alikuwa ameshajitengeneza na kupata balansi kwenye lile
dirisha, tulishtuka baada ya tochi yenye mwanga mkali kuwashwa
na kunimulika machoni.
Ilibidi nijirushe kwa sababu nilikuwa najua kinachofuata, risasi
mfululizo zikanikosakosa na kutoboatoboa ukuta, Ustaadh Fundi
akajirusha kwa ndani kwa usalama wake.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, niliikamata vyema bunduki
yangu na kuanza kujibu mashambulizi, nikafanikiwa kuwaangusha
wanaume watatu wenye miili mikubwa waliokuwa wakija kasi pale
nilipokuwepo huku wakifyatua risasi.
Kukatulia, nikaangaza macho huku na kule na baada ya kujiridhi-
sha, nilimuita Ustaadh Fundi ambaye kumbe alishajiongeza, akawa
ameshafunga kamba pale dirishani, ambayo hata sijui aliipata wapi
kisha akanirushia.

764 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Nikaikamata kikamavu na kuanza kujivuta kwenda juu, sekunde


ishirini tu zilitosha kunifanya niwe nimeshafika juu, nikajirushia
kwa ndani, huku nyuma risasi nyingine kadhaa zikapiga ukuta.
“Uko salama?” namba moja aliniuliza huku akiwa anahema kwe-
likweli, akiwa mgongoni kwa Ustaadh Fundi!”
“Niko sawa, vipi wewe?”
“Niko sawa, nimejigonga bega wakati naruka lakini niko sawa,”
alisema, nikabonyeza kifaa changu cha mawasiliano na kutoa ta-
arifa kwamba tayari tulikuwa tumeshaingia ndani na namba moja,
maelekezo yakawa ni kwamba natakiwa kumfikisha namba moja
kwenye ‘vault’ haraka iwezekanavyo.
Mkurugenzi alishauri eti kikosi cha ulinzi wa rais kije kisaidiane
na mimi kuhakikisha suala hilo linatimia lakini kabla hata mimi
sijajibu, baba yake Saima aliingilia kati na kueleza kwamba tus-
ingeweza kumuamini mtu mwingine yeyote kutoka kwenye kikosi
hicho kutokana na kile kilichokuwa kimetokea, cha kiongozi wa
PSU kuasi.
Hicho ndicho nilichokuwa nimekiwaza hata mimi kwamba
hatutakiwi tena kuwaamini wale maafisa wote wa PSU kwa sa-
babu kama kiongozi wao alikuwa ameasi, kulikuwa na uwezekano
mkubwa kwamba kuna waliokuwa wanamtii na walikuwa tayari
kuendelea kushikilia msimamo wa kile alichokuwa akikiamini
ndani ya kichwa chake.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, nilimuelekeza Ustaadh Fundi
nini cha kufanya, ilibidi yeye ndiyo ashirikiane na mimi kuunda
‘pair’. Nilishaeleza huko nyuma kuhusu ‘pair’ maana yake ni nini

765 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

katika medani za kimapigano na huwa zinafanyaje kazi kwa hiyo


sitarudia tena.
Kwa kifupi ni kwamba Ustaadh Fundi alitakiwa kushirikiana na
mimi, yeye akiwa nyuma wakati tukimpeleka namba moja kwe-
nye ‘vault’ kwa mara nyingine. Nilimuelekeza namba moja nini
anachotakiwa kufanya, kwa kuwa naye alikuwa ameshaonja joto ya
jiwe akawa anaitikia kwa adabu.
Tuliinuka pale tulipokuwa tumejibanza, mkono wangu mmoja
nikawa nimeshika bunduki, kidole kikiwa kwenye ‘trigger’, tayari
kwa chochote na mkono wangu mwingine nilimshika namba moja
na kumuweka nyuma yangu.
Ustaadhi Fundi naye alimshika mkono mmoja namba moja huku
yeye akitembea kinyumenyume kuhakikisha anazidhibiti hatari
zozote ambazo zingeweza kutokea upande wa nyuma, tukamu-
weka namba moja katikati kisha tukaanza kusonga mbele kwa kasi
kubwa.
Baba yake Saima yeye alikuwa akitoa maelekezo kwa vijana wa
‘control room’ ambao ndiyo waliokuwa wakihusika na kufungua
na kufunga milango ya kuelekea kwenye ‘vault’.
Ndani ya muda mfupi tu, tayari tulikuwa tumefika kwenye mlan-
go wa kuingilia kwenye korido ndefu ya chini kwa chini iliyokuwa
inaelekea kwenye ‘vault’, katika hali ambayo sikuitarajia, nikam-
kuta baba yake Saima na mkurugenzi nao wakiwa wameshafika.
Wakaungana na sisi, tukawa tunavuka kiunzi kimoja baada ya
kingine na hatimaye tulifanikiwa kufika salama kwenye ‘vault’,
milango ikafunguliwa na tukaingia mpaka ndani ambapo tuli-

766 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

pokelewa na wale wasaidizi wa namba moja ambao walikuwa


wamepewa kazi ya kumuandaa ‘double’ kabla mambo hayajahari-
bika, namba moja na ‘double’ wake wakakutana ana kwa ana.
“Wewe itabidi ubaki huku, sisi acha tukapambane kurudisha utu-
livu juu,” alisema mkurugenzi, eti akimaanisha mimi ndiyo nibaki
kule chini, nikaona ni kama analeta masihara.
“Hapana, mimi ndiyo kiongozi wa hii misheni, nawezaje kubaki
huku?”
“Misheni imeshaisha, namba moja yuko salama,” alisema, ika-
bidi baba yake Saima aingilie kati nakushauri kwamba kwa kuwa
tayari namba moja alikuwa kwenye mikono salama, sisi wote tuka-
ongeze nguvu kule nje, wazo ambalo hata namba moja mwenyewe
aliliunga mkono.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, Ustaadh Fundi naye akagoma
kubaki kule chini na kueleza kwamba alikuwa anataka kwenda
kutusaidia, tukatoka mbiombio na kuanza kukimbia kwenye korido
ndefu kupanda juu.
Nakumbuka wakati tukitoka namba moja alionesha ni kama ana-
taka kuzungumza jambo na mimi lakini kwa jinsi hali ilivyokuwa,
ilikuwa ni lazima kwanza tukamalize kazi ndiyo mambo mengine
yafuatie, tukapeana ishara ambayo wote tuliielewa vizuri.
Ndani ya muda mfupi tayari tulikuwa tumeshatoka kwenye
‘vault’, tukakimbia kwenye korido za juu na muda mfupi baadaye,
tukawa tumeshafika kwenye lango kubwa la kutokea nje.
Moto ulikuwa unawaka kwelikweli na vijana wetu wote ni kama
walikuwa wamepagawa kwa sababu walikuwa ‘wakikiwasha’ sa-

767 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

wasawa, tukajichanganya nao na kuongeza nguvu na ndani ya da-


kika zisizozidi tatu, tayari tulikuwa tumeshamaliza mchezo mzima,
hakukuwa na adui aliyebaki amesimama hata mmoja.
Wote walikuwa wameshaangushwa na kusafirishwa kwenda ku-
onana na muumba wao na waliokuwa na bahati, walikuwa wame-
shawekwa chini ya ulinzi, wengi wakiwa na majeraha ya risasi.
Baada ya kuhakikisha kazi imemalizika, kama ilivyokuwa
utaratibu, ilibidi vijana wetu wote waliohusika kwenye misheni
hiyo waanze kutafutwa mmoja baada ya mwingine ili kukagua ni
madhara kiasi gani tulikuwa tumeyapata.
Kazi ilianza kufanyika, nikawa nawasiliana na mmoja baada ya
mwingine, vijana wetu sita walikuwa wamejeruhiwa ingawa wote
walikuwa kwenye hali nzuri, harakaharaka mipango ya kuwakim-
biza kwenye hospitali ya kitengo kwa ajili ya kwenda kupatiwa
matibabu ikaanza.
Vijana wawili kutoka PSU pia walikuwa wamepata majeraha ya
risasi, nao wakaunganishwa na kukimbizwa haraka hospitali.
Miili kumi na nne ya wale wendawazimu akiwemo kiongozi
wa PSU ambaye alipigwa risasi ya kichwa na kufa papo hapo,
ilikusanywa na kupakizwa kwenye gari jingine, nayo ikapelekwa
hospitali kwa ajili ya taratibu nyingine huku majeruhi watano kati
yao, nao wakipelekwa hospitali baada ya kuwa wameshakaguliwa
kikamilifu.
Kilichofuatia baada ya hapo, ilikuwa ni kuanza kushughulika na
wale wageni ambao bado walikuwa ndani ya chumba cha miku-
tano. Kutokana na hali ilivyokuwa katika eneo lote la Magogoni,

768 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

tulikubaliana kwamba hawatakiwi kushuhudia kilichotokea kwa


sababu za kiusalama.
Baba yake Saima ndiye aliyeenda kuzungumza nao, akawaeleza
kwamba kulikuwa kumetokea changamoto ya kiusalama kwa hiyo
hakuna atakayeruhusiwa kutoka usiku huo mpaka watakapoele-
kezwa vinginevyo.
Upande wa pili, tayari kikosi cha mafundi kutoka jeshini kiliku-
wa kimeshawasili kwa ajili ya kufanya marekebisho ya haraka na
kuondoa ushahidi wowote ambao ungeonyesha kwamba Magogoni
ilikuwa imevamiwa na kugeuka uwanja wa vita.
Vijana wetu wote ambao walikuwa salama, nao walitakiwa kuen-
delea na doria usiku kucha ili kuhakikisha mpaka kunapambazuka,
kila kitu kiwe kimerudi kama kilivyokuwa. Kwa upande wa askari
wa majini, nao walitakiwa kuendelea na doria katika eneo lote la
bahari.
Kazi kubwa ilifanyika usiku huo, kila ushahidi ulikusanywa
kwa ajili ya kuhakikisha mtandao mzima wa wote waliohusika na
mchezo huo hatari wanakamatwa na kufikishwa mbele ya mkono
wa sheria.
Pilikapilika ziliendelea usiku kucha na mpaka kunapambazuka,
usingeweza kuamini kama ni eneo hilo ndipo damu ilipomwagika
usiku uliopita.
Wale mafundi kutoka jeshini walikuwa wamesharudishia kila
kitu kama kilivyokuwa, vioo na milango iliyokuwa imevunjwa,
ikabadilishwa na kuwekwa mipya, kuta zilizokuwa na matundu ya
risasi zikakarabatiwa na kupakwa rangi vizuri.

769 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Namba moja yeye bado alikuwa kwenye ‘vault’ kwa sababu za


kiusalama na ilipofika saa kumi na mbili asubuhi, ndipo wageni
wote waliokuwa kwenye ule ukumbi wa mikutano waliporuhusiwa
kuanza kutoka, mmoja baada ya mwingine, tena chini ya ulinzi
mkali.
Kwa kuwa marekebisho makubwa yalikuwa yameshafanyika, ili-
kuwa ni vigumu kwao kuelewa ni nini hasa kilichokuwa kimetokea
usiku uliopita zaidi ya kubaki na maswali mengi ndani ya vichwa
vyao kuhusu risasi zilizorindima usiku uliopita.
Kila mmoja aliyekuwa akitoka, alikuwa akisainishwa fomu
maalum ambayo ilikuwa na maelezo muhimu kumhusu kila mmoja
lakini pia kukiwa na kipengele cha yeyote kati yao kutoeleza ma-
hali popote kuhusu alichokisikia au kukiona usiku huo walipokuwa
eneo hilo.
Ilikuwa ni lazima kufanya hivyo ili kutunza siri, ukiambiwa
serikali inabeba siri nzito, basi ni pamoja na siri za matukio hatari
kama hayo.
Baada ya wote kuwa wametolewa, wale wasichana wote ambao
walikuwa wakitoa huduma usiku uliopita, tulikubaliana kwamba
hawatakiwi kuachiwa na kurudi uraiani kwa sababu kampuni wali-
yokuwa wakiifanyia kazi ilikuwa imehusika kwa kiasi kikubwa na
kilichokuwa kimetokea, wote wakapeleka kwenye nyumba maalum
(safe house) ambako wangeendelea kuhojiwa kwa kina, mmoja
baada ya mwingine.
Wengi walionesha kutoelewa chochote kilichokuwa kinaendelea
zaidi ya kuwa wafanyakazi wa kawaida tu ambao walikuwa waki-

770 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

fanya kazi ili kupata kipato cha kuweza kuendesha maisha yao na
familia zao.
Hata hivyo, walikuwepo wachache ambao walikuwa wana jua ni
nini kilichokuwa kinaendelea ingawa nao hawakuwa wakihusika
moja kwa moja. Ni ushahidi huo uliotolewa na wasichana hao
ndiyo uliofanya kazi iwe rahisi.
Wamiliki wa kampuni hiyo iliyokuwa na ofisi zake Kisutu jijini
Dar es Salaam walienda kukamatwa na kuunganishwa na wenzao
waliokuwa wakiendelea kushikiliwa ‘kitengoni’ na kwenye nyum-
ba maalum.
Ni baada ya saa arobaini na nane kuisha, ndipo tulipotangaziwa
kumalizika rasmi kwa oparesheni ile ambayo kama nilivyoeleza,
kuanzia mwanzo mimi ndiye niliyekuwa kiongozi ambapo bila
msaada mkubwa kwa viongozi wangu, hakika isingewezekana
kabisa.
Mkurugenzi ndiye aliyetutangazia sisi viongozi kwamba oparesh-
eni imekamilika na mimi nikatakaiw andiyo niwatangazie vijana
wangu wote kuhusu taarifa zile. Hakukuwa na muda wa kupoteza,
nilitoa taarifa kupitia kifaa cha mawasiliano na kuwataka vijana
wote walioshiriki kwenye oparesheni ile, kukusanyika kwenye
bustani zilizokuwa Magogoni.
Hata wale waliokuwa wakiendelea na doria kwenye maeneo
mengine yote, walitakiwa kuacha kila walichokuwa wakikifanya
na kufika haraka eneo nililokuwa nimewaelekeza.
Walioachwa, ni wale waliokuwa wakiendelea na matibabu pekee,
lakini wengine wote waliitikia wito na ndani ya dakika kadhaa,

771 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

‘jeshi’ la vijana wapambanaji, kila mmoja akionesha kuchoka kisa-


wasawa kutokana na kazi ngumu iliyofanya tukose hata muda wa
kulala, lilikuwa limekusanyika kwenye viwanja vya Magogoni.
Niliwapanga wote vizuri na baada ya hapo, nilitangaza rasmi
kwamba kazi yetu imefika mwisho, nikawashukuru wote walio-
kuwa wamehusika na kupambana kisawasawa kuilinda nchi yetu.
Maneno yalikuwa machache lakini yaliyoonesha ni kwa kiasi
gani kila mmoja alikuwa muhimu kwenye kazi ile, nikaona nyuso
za vijana zikianza kuchanua matabasamu hafifu, nikahitimisha kwa
salamu yetu ambapo wote waliitikia kwa sauti ya juu.
Baada ya mimi kumaliza, nilitoa nafasi kwa viongozi kuzung-
umza. Mkurugenzi wetu ndiye pekee aliyezungumza, akatushukuru
sana kwa kazi kubwa, ya hatari na ya kujitoa sadaka tuliyokuwa tu-
meifanya na akaahidi wote walioshiriki, watapewa zawadi mbalim-
bali, kila mmoja kulingana na jinsi alivyoshiriki lakini pia akaahidi
kwamba wapo watakaopandishwa vyeo.
Akaeleza kwamba hata ambao hawatapandishwa vyeo kwa
wakati huo, waelewe kwamba kazi kubwa waliyoifanya, itabaki
kwenye kumbukumbu ya mashujaa wa taifa na kuwataka kuende-
lea kuipenda nchi yao na kujitoa kama walivyofanya.
Tukiwa tunaendelea kumsikiliza mkurugenzi, tulishtuka kuona
maafisa wa kitengo cha ulinzi wa namba moja, wengine wakiwa ni
wapya, wakianza kusogea kule tulikokuwa tukiendelea kumsikiliza
mkurugenzi, tukawa tumeshaelewa kwamba namba moja alikuwa
anakuja kuzungumza na sisi.
Mkurugenzi akiwa anaendelea kuzungumza, namba moja aliibu-

772 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ka, uso wake ukiwa umejawa na bashasha kubwa, akasogea mpaka


pale alipokuwa amesimama mkurugenzi, kwa kuzingatia itifaki,
ikabidi mkurugenzi asitishe kile alichokuwa anakisema.
“Malizia tu, nataka kuzungumza na vijana wangu,” alisema,
mkurugenzi akaonesha kubabaika kidogo kisha akamalizia na kum-
karibisha.
Alianza hotuba yake fupi kwa kicheko, ikabidi na sisi wote
tucheke! Namba moja alikuwa ni mtu fulani hivi ambaye akiwa na
furaha, anapenda masihara lakini akiwa kwenye kazi, muda wote
uso wake nao unakuwa wa kikazi kwelikweli.
Kitendo cha sisi kumuona akicheka, na sisi wote tulicheka.
“Walifikiri hapa panaingilika kirahisi, walifikiri wanaweza kuni-
angusha kirahisi! Hawakuwa wanajua kwamba ninalo jeshi imara
la vijana wenye nguvu na akili,” alisema kisha akacheka sana, wote
tukawa tunacheka.
Haukupita muda mrefu, akavaa sura ya kazi, alianza kwa ku-
tushukuru sana kwa jinsi tulivyopambana kumuokoa yeye pamoja
na kuilinda nchi yetu dhidi ya uvamizi ule wa kigaidi. Akaeleza
kwamba awali alikuwa hajui ni ugumu kiasi gani tunaokutana nao
kuilinda nchi yetu na viongozi wake lakini baada ya tukio lile,
alikuwa amejifunza mambo mengi sana.
“Kenny yuko wapi?” alisema wakati akiendelea kuzungumza,
harakaharaka nikasogea mbele na kumpigia saluti ya utii, akanio-
nesha ishara kwamba nimsogelee, kweli nikafanya hivyo.
“Mnamuita Snox eeh!” alisema na kusababisha wote tucheke
sana, nikamuona mpaka baba yake Saima akicheka kwa nguvu

773 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)
kwelikweli.
“Niwape siri moja! Huyu bwana si mnaona huu mwili wake,
alitubeba watu wawili kwenye mabega yake, yaani tulimfanya
kama ngazi, yule mzee yuko wapi?” alisema, akimaanisha Ustaadh
Fundi, nikamjibu kwamba alikuwa ameenda kitengoni kupumzika.
“Angekuwepo angesimulia mwenyewe, tulipanda kwenye haya
mabega, nikawa siamini kama kweli tutafanikiwa, akatunyanyua
wote wawili, tena mwili wake ukiwa unanuka maji taka mpaka
nikawa natamani kuziba pua zangu,” alisema, tukaangua kicheko
kwa mara nyingine, safari hii kwa nguvu zaidi.
“Mkurugenzi, mzee mwenzangu,” alisema akiwageukia mkuru-
genzi na baba yake Saima ambao walikuwa wamesimama pembeni
yake, wakainamisha vichwa vyao kwa utii.
“Mnafanya kazi kubwa sana ya kuwaibua na kuwaandaa vijana
kama hawa ambao ni hazina kubwa ya taifa, nawashukuru sana!”
alisema, wakainamisha tena vichwa vyao kwa utii, ukimya ukapita,
kisha akaendelea.
“Leo sikupanga kuzungumza nanyi lakini nilipoona mnahiti-
misha kazi yenu, nikaona nije kujumuika nanyi. Nataka tuandae
siku maalum tukutane, wote mje na familia zenu kwa wale wenye
familia, ambao hamna familia haiwahusu!” alisema kisha akawa
anacheka, wote tukawa tunacheka.
“Niandalieni siku maalum ya kuka ana vijana wangu, tule,
tunywe na kucheza muziki pamoja, najua mkono wangu utakuw
aumeshapona,” alisema huku akijishika begani huku akicheka,
wote tukacheka sana.

774 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Akatuaga na kusisitiza kwamba siku hiyo ikishapangwa,


hataki mtu yeyote akose kwa sababu atakuwa na zawadi kubwa
kwa ajili yetu,” alisema kisha akamsogelea mkurugenzi, sijui
alimnong’oneza nini, akawa anatingisha kichwa kuonesha kuelewa
alichokuwa anaambiwa.
Akamsogelea na baba yake Saima, naye akamnong’oneza jambo
kisha wote wakanigeukia na kunitazama, nikashangaa wanaangua
vicheko kisha akaondoka na walinzi wake, wote tuukabaki kuche-
ka.
Basi tulipeana maelekezo ya mwisho kisha tukaelekea kwenye
magari ambayo yalikuwa yanatusubiri, tukaingia na kuondoka.
Kwenye gari vijana wangu wakawa wanajitania na kucheka sana
kutokana na masihara ya namba moja aliyowaambia.
Japokuwa tulikuwa tumechoka sana, lakini mioyo yetu ilikuwa
na furaha kubwa, hasa baada ya kusikia maneno ya namba moja.
Tulielekea mpaka kitengoni ambako tulipokelewa kwa shangwe
kubwa na wenzetu ambao hawakushiriki kwenye oparesheni ile.
Baada ya shamrashamra za hapa na pale, kila mmoja sasa
aliruhusiwa kutawanyika kwa ajili ya mapumziko ya siku tatu, wa
kukabidhi vifaa wakafanya hivyo, wa kubadili nguo nakuoga nao
wakafanya hivyo.
“Namba moja amekupenda sana, nadhani kuna jambo kubwa
linaenda kutokea kwenye maisha yako ndani ya siku hizi chache,”
alisema baba yake Saima ambaye alinivuta pembeni baada ya
kunikuta nikiwa najiandaa kwa ajili ya kurudi nyumbani kupumzi-
ka.

775 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

“Alisemaje pale mbona mlinigeukia na kucheka?” nilimuuliza


baba yake Saima, akaishia kucheka bila kunipa majibu yoyote,
tukaagana pale na baada ya mimi kukamilisha kila kitu, ikiwemo
kuandika ripoti, nilitoka na safari ya kurudi nyumbani kwnagu
ikaanza, akilini nikimuwaza kipenzi cha moyo wangu, Saima!
Niliendesha gari langu nikiwa nawaza mambo mengi kwa
wakati mmoja lakini kubwa kuliko yote, nilikuwa nawaza jinsi
oparesheni ile kubwa na nzito ilivyofanikiwa, japo ilitugharimu
jasho na damu.
Nilimfikiria Ustaadh Fundi ambaye kwa hakika alikuwa ame-
fanya kazi kubwa mno ya kutufumbulia mafumbo mengi ambayo
hatukuwa na majibu yake. Moyoni nikajiapiza kwamba hata kama
mamlaka hazitaona umuhimu wake, nitatafuta namna ya kumuun-
ganisha ili na yeye awe katika sehemu ambayo itamfanya atambu-
like na serikali kutokana na mchango wake.
Nilimfikiria kijana wangu Jack, ambaye naye kwa hakika ali-
kuwa amefanya kazi kubwa mno upande wa ‘Cyber’ na teknolojia
ya mawasiliano, nikajikuta nikitabasamu baada ya kumfikiria.
Kwa uwezo mkubwa aliokuwa nao, niliona sasa kuna umuhimu
wa kumhamishia moja kwa moja kitengoni ili tufanye kazi kwa
karibu zaidi na kufanikisha mambo mengi na makubwa.
Mawazo yaliyokuwa yakiendelea kupita kwa kasi ndani ya
kichwa changu, yalinifanya hata nisiwe nazingatia kuhusu safari
yangu, nikaja kushtukia tu tayari nimekaribia nyumbani kwangu,
nikapunguza mwendo na muda mfupi baadaye, tayari nilikuwa
getini, nikapiga honi na kufunguliwa geti na mlinzi.

776 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Japokuwa sikuwa nimemwambia Saima kitu chochote nikitaka


kwenda kumfanyia ‘sapraiz’, kumbe baba yake alishamueleza
kwamba tumemaliza kazi na nitarudi nyumbani muda wowote,
nadhani ni baada ya kunikosa mimi hewani ndipo alipoamua kum-
pigia baba yake.
“Nilikuwa nakusubiri kwa hamu mume wangu!” alisema Saima
baada ya kuwa amenirukia mwilini kwa nguvu, akionesha kuni-
miss kisawasawa, na mimi nikamdaka na kumbeba juujuu, tukawa
tunaelekea ndani huku akiwa ameniganda kama ruba.
“Nilikuwa na wasiwasi sana, muda wote roho ilikuwa juujuu,
pole kwa kila kitu,” alisema Saima wangu, machozi yakiwa yana-
mlengalenga, nikawa naitikia kwa kugunaguna tu kwa sababu hata
mimi nilikuwa nimeimisi sana familia yangu, hasa mke wangu
kipenzi Saima.
Basi baada ya kuwa tumeingia ndani, yaliyoendelea huko mengi
hayaelezeki, itoshe tu kusema kama ni maisha ya ndoa, nilikuwa
nayafaidi kisawasawa nikiwa na mrembo wangu Saima.
Siku hiyo ilipita, kesho yake nikapumzika nyumbani pamoja na
siku iliyofuatia, nikiendelea kufurahi na familia yangu. Baada ya
siku tatu kuisha, wote tulirudi kazini na kama ambavyo namba
moja aliahidi, tulipewa taarifa kwamba mwishoni mwa wiki tut-
aenda tena Magogoni, safari hii siyo kuipigania nchi yetu tena bali
kwenda kupongezana na kuburudika.
Maandalizi yalifanyika na hatimaye siku husika ikawa imewadia,
‘jeshi’ lote lililohusika na oparesheni ile, tukaelekea Magogoni am-
bako siku hiyo tulipokelewa kama Wafalme. Ilikuwa ni sherehe ya

777 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)
aina yake, viongozi karibu wote wa ngazi za juu serikalini wakiwa
wamehudhuria kwa ajili ya kutupongeza.
Tulikula, kunywa mpaka kusaza, tulifurahi na viongozi wetu,
ikiwemo kulisakata rhumba na namba moja kwa zamuzamu, mwe-
nyewe akionesha kuwa na furaha kubwa kuliko kawaida siku.
Tulipewa pia nishani maalum ambazo tulivishwa na namba moja
mwenyewe, tukapewa cheki za shilingi milioni thelathini kila
mmoja kama asante huku pia tukipandishiwa mishahara yetu kwa
maelekezo ya namba moja.
“Nimezungumza na viongozi wako, kuna kazi nataka kukupa!
Wao wameridhia na naamini wewe pia utaridhia,” aliniambia
namba moja tukiwa tunaendelea kufurahi pamoja.
“Kazi gani mheshimiwa?”
“Siwezi kukwambia kwa sasa, utapewa taarifa rasmi kwa mujibu
wa sheria!”
Upande wa pili, kamatakamata ilikuwa ikiendelea kwa kasi
kubwa, viongozi wa serikali ambao nao walithibitika kuhusika,
akiwemo Kamishna wa Uhamiaji, nao waliwekwa nguvuni, wafan-
yabiashara wakubwa watatu, akiwemo mfanyabiashara mkubwa
wa mafuta, mwenye vituo vingi vya mafuta nchi nzima, naye
alikamatwa, orodha ikaendelea kuwa kubwa na ya kushangaza.
Hata watu ambao walikuwa hawategemewi kabisa kuhusika kwa
namna moja au nyingine, nao walikamatwa na kuunganishwa na
wenzao na baada ya kuwa tumeshawamaliza wote, tuliwakabidhi
kwa jeshi la polisi ambao kimsingi ndiyo waliokuwa na mamlaka
ya kufungua mashtaka na kuwafikisha mahakamani.

778 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Zoezi hilo lilienda sambamba na kuwaachia watuhumiwa wote


ambao walikubali kutoa ushirikiano na kufanikisha oparesheni ile
kubwa lakini walikuwa wakiachiwa mmoja baada ya mwingine
baada ya taratibu nyingi za kisheria kufanyika ili kuwaondolewa
makosa waliyokuwa wakikabiliwa nayo.
Miongoni mwa watu wa mwanzo kabisa kuachiwa, alikuwa ni
Sanipha, yule mwanamke tuliyemkamata mwanzoni kabisa akiwa
kwenye ile nyumba pale Kijitonyama Kisiwani.
Aliachiwa kwa sababu ilionesha yeye hakuwa mhalifu bali
alikuwa akishirikiana na mumewe, Abdulwaheed ambaye alikuwa
miongoni wa viongozi wa juu kabisa wa genge lile la kigaidi.
Ushirikiano aliokuwa ameutoa kuanzia mwanzo, ulitosha kuonesha
kwamba alikuwa raia mwema.
Masharti aliyopewa, ilikuwa ni kuendelea kuwa mtoa taarifa
wetu wa siri kuhusu jambo lolote linalohusu usalama wa nchi yetu,
endapo akipata taarifa hizo. Wa pili kutoka, alikuwa ni yule mzee
wa Kisomali ambaye naye aliachiwa kwa sababu kuu mbili.
Sababu ya kwanza ni kwamba japokuwa alikuwa na hatia ya
kushirikiana na Abdlwaheed kupanga njama za kutenda uhalifu,
baada ya kukamatwa, alikubali kutoa ushirikiano kubwa na ta-
arifa alizokuwa akitupa, zilisaidia mno kujua nini kilichokuwa
kimepangwa na kujua namna ya kuzizuia.
Sababu ya pili ilikuwa ni hali yake ya kiafya, kitendo cha yeye
kupewa sumu akiwa kwenye mikono yetu, lilikuwa jambo baya
sana la kuhatarisha usalama wake kwa hiyo ilikuwa inatakiwa
aachiwe ili akaendelee kupata matibabu ya kitaalamu zaidi.

779 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

Kama ilivyokuwa kwa Sanipha, huyu naye alitakiwa kubaki


kuwa mtoa taarifa wetu na alitakiwa kuwa anatujuza kuhusu jambo
lolote ambalo angeona ni hatari kwa usalama wa nchi.
Wengine walioachiwa, walikuwa ni wale mabinti waliokamatwa
nyumbani kwa Abdulwaheed wakiwa na Sanipha, ambao miongoni
mwao alikuwepo mtoto wa Ustaadh Fundi.
Hawa kuachiwa kwao, kulikuwa tofauti kidogo. Kwa sababu
walikuwa tayari wameshapitia mafunzo makali ya kivita pamoja
na kutumia silaha, kuwaachia warudi mtaani lilikuwa ni jambo la
hatari kwa hiyo makubaliano yaliyofikiwa, ilikuwa ni kwa wao
kupelekwa jeshini ambako wangeendelea kufuatiliwa kwa karibu,
hatua kwa hatua.
Wengine kadhaa pia waliachiwa lakini wengine wote ambao
walikutwa na hatia ya kuhusika kupanga njama, kutekeleza au ku-
fadhili ugaidi, wakitaka kuiangusha Magogoni, moto uliwawakia
kisawasawa. Makosa yao yalikuwa yakiangukia kwenye vipengele
vitatu, uhaini, ugaidi na mauaji.
Kama sheria ilivyo, makosa yote hayo, kifungo cha chini kabisa
ni miaka thelathini jela. Kwa hiyo kesi ziliendeshwa harakaharaka
na baada ya ushahidi kukamilika, kila mmoja alihukumiwa kuloin-
gana na jinsi alivyohusika. Mutesigwa na Abdulwaheed, wao wali-
hukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa sababu makosa yao yalikuwa
makubwa na mazito kisawasawa.
Wale vijana wao, ukiwemo mtandao mzima kuanzia kule Mafia,
Kibiti, Rufiji, Mkuranga mpaka jijini Dar es Salaam, wengi wa-
lihukumiwa kifungo cha miaka thelathini kila mmoja, huku wale

780 AZIZ HASHIM


MAGOGONI HAS FALLEN
(Magogoni Imeanguka)

ambao walibainika kutokuwa raia, wakisafirishwa na kurudishwa


kwenye nchi zao kwenda kutumikia vifungo vyao.
Kuanzia hapo, utulivu, amani na usalama vikawa vimerejea upya
katika ukanda wa Mkiru ambao kama nilivyoeleza, ulikuwa ukihu-
sisha Mkuranga, Kibiti na Rufiji.
Yale mauaji ya wenyeviti wa vijiji na viongozi wa serikali za
mitaa, yaliisha kabisa na sasa ikawa imefahamika wazi kwamba
kumbe Mutesigwa na Abdulwaheed pamoja na wafadhili wao,
ndiyo waliokuwa nyuma ya mauaji hayo yaliyoitingisha nchi kisa-
wasawa.

MWISHO.

781 AZIZ HASHIM

You might also like