You are on page 1of 19

A THREAD BY FORTUNATUS BUYOBE

FBI IN TANZANIAN SOIL

Tarehe 7 August 1998 jiji la la Dar lilitikisika.

Majira ya saa 4:45 asubuhi,Maafisa wawili wa Polisi wakiwa katika


kituo cha polisi Salender Bridge, walishtuliwa na Kishindo
Kikubwa.

Maafisa hawa ni SSP Mohamed Stambuli na ASP Valentino


Mlowola

Naam!

Fuatana nami!

Kwa maelezo ya maelezo ya SSP Stambuli, alieleza kwamba


majira hayo alisikia kishindo kikubwa ambacho kililifanya anga
kuwa jeusi kwa wangu mazito ya moshi, vumbi na vyuma
vikiruka angani kutoka majengo ya jirani na ofisini kwake.

Haikuchukua muda mrefu kwa maafisa hawa kubaini kuwa,


kishindo kile kilitokea katika jengo la ubalozi wa Marekani
ambalo halikuwa mbali toka pale kituoni mwao.

Ilikuwa ndio mara ya kwanza kwa taifa hili kuonja machungu ya


uhalifu mpya kwa jina la “Ugaidi”

Achana na ugaidi wa mchongo wa Kina Mbowe au ule wa Kibiti,


Amboni na Mkuranga!

Huu ndio ulikuwa ugaidi ambao ulilenga moja kwa moja kwa
aliyeanzisha vita vya ugaidi yaani Taifa la Marekani.

Magaidi hawakujali kama wanapambana na Mmarekani nje ya


ardhi yake.

They didn’t care!


Tukio hili lililikuta taifa letu likiwa halijajiandaa kabisa
kukabiliana na janga hili.

Hii ni baada ya Idara yetu ya “Crime Investigation Department”


CID kubaini kuwa wasingeweza kufua dafu kupeleleza kisa kile
kilichohitaji wataalamu wa Forensic science na Engineering.

Yes!

Kwa wakati ule idara yetu haikuwa imepiga hatua kwenye


mambo ya Forensic science au kutatua uhalifu wa kiinjinia.

Kutokana na hilo Idara yetu ilibidi isalimu amri na kuwaomba


wataalamu wa FBI wasaidie upelelezi ule.

Sote tunajua jinsi ilivyo vigumu kwa taifa moja kuruhusu


wapelelezi wa nje kuchunguza visa vya ndani.

Katika sakata hili hakukuwa na njinsi.

Ombi la Tanzania kwa FBI likapokelewa kwa furaha kubwa kwani


taifa la Marekani lilikuwa lina maslahi kwenye tukio lile.

Kwa upande wa Tanzania ikaundwa timu maarumu ya kikachero


wakiwemo SSP Stambuli, ASP Mlowola, SSP Samson Kassala na
wengineo,

Hawa walikuwa wakipokea maelekezo kutoka kwa maafisa wa


FBI moja kwa moja.

Timu hii ikasogela eneo la tukio ambapo walikuwata RPC RCO


na wengineo

Pale kazi ya kwanza ilikuwa ni kuwapeleka majeruhi Muhimbili,


kuopoa maiti 11 na kupunguza taharuki.

Mpaka muda huo hakuna yeyote aliyekuwa na tetesi yoyote juu


ya nani hasa anaweza kuwa mshukiwa/washukiwa wa tukio lile.

Baada ya hali kutulia, ikaanza Crime scene Investigation


Maafisa hawa wakashuhudia uharibifu ulioachwa na kishindo
cha mlipuko ule.

Magari mengi yakiwa yameharibiwa “beyond repair”

Moto ulikuwa bado ukiwaka na akskari mmoja wa kitete


akasikika akisema “Hili ni bomu la Hiroshima”

Hii ni kutokana na jinsi Bomu lilivyochimba ubalozi

Vitu vingi vikaokotwa eneo la tukio na kuanza kuchunguzwa kwa


umakini.

Maafisa wa FBI wakavutiwa na kipande kimoja cha Chuma

Kipande hiki cha Chuma ndicho kilikuja kuwa muongozo wa


muhimu sana katika kutatua fumbo la juu ya nani hasa alilipua
bomu lile.

Kipande kile cha Chuma, Kiliaminika kuwa ni cha Chassis ya gari


iliyotumika kubeba bomu lililolipuka kwenye ubalozi ule.

Baada ya uchunguzi wa kimaabara wa maafisa wa FBI kwa


Laboratory Photographic Enlargement, walifanikiwa kupata
namba fulani kutoka kwenye chuma kile

Namba hiyo ilikuwa ni MH40-06050 (Kielelezo namba 6 cha FBI)

Msako ukaanza kwa kuyahoji Makampuni mbalimbali


yanayohusika na kuingiza Magari nchini kama walishaingiza gari
lenye ile namba ya Chassis.

Wakafanikiwa kuipata kampuni moja!

Naam!

It was JABA MOTORS COMPANY!

Ndiyo!
Kampuni ile ndiyo iliingiza nchini gari aina ya NISSAN ATLAS,ya
tani mbili,yenye Model namba MH40, Engine namba ED 33-
50626 na Chassis No. MH40-06050

Naam!

Gari ile ilisajiliwa kwa namba TZH 6134 na iliuzwa kwa AMANI
JUMA KASINYA

Mnunuzi wa gari ile akakamatwa na kuwekwa Makwaya.

And upon a gentle interrogation that involved a promise of free


testicles surgery, Mnunuzi akaeleza mambo kinagaubaga!

Alieleza kuwa ni kweli alinunua gari ile, lakini alishaiuza.

Akaeleza kuwa gari ile ilikuwa ina friji kubwa kwa nyuma ambayo
alikuwa akiitumia kusafirishia samaki kutoka Tanga mpaka Dar

Akatoa mkataba wa Mauziano wa tarehe 17 June 1998 kuwa


alimuuzia mtu aitwaye Mohamed Sultan Said kwa bei ya Tshs
milioni 3.5

Ikawa ni msako wa nyani ngedere haponi!

Na yamkutayo Mamba na Boko yatamkuta

A manhunt now launched towards the said Mohammed Sultan


Saidi

Naye Mohamed Sultan alipodakwa akaeleza jinsi alivyouza gari


ile kwa watu wawili wenye asili ya Kiharabu kupitia kwa dalali
SLEIYUM SULEIMAN SALUMU JUMA

Dalali naye akadakwa

Katika mahojiano, dalali huyu akaeleza kuwa tarehe 27 July 1998


akiwa katika hotel ya AL-NOOR mnazi mmoja alifatwa na vijana
wawili mmoja mrefu na mwingine mfupi wenye asili ya kiarabu
wakitaka awauzie gari ambayo ilishapelekwa kwake kutafuta
mnunuzi.
Gari hii haikuwa nyingine bali ile NISSAN ATLAS yenye Friji.

In a nutshell,anunuzi hawa waliitaka gari hii na si nyingineyo


kimkakati zaidi!

Gari ile ilikuwa inasifa za kiinjinia walizozitaka.

Gari ile ikauzwa kwa watu hawa kwa Tshs Mil. 4.3 ambao
tutawajua huko mbeleni

Gari ile baada ya kununuliwa ikatakiwa ifanyiwe modifications


mbalimbali kwa wataalamu na mafundi mbalimbali,Locations
mbalimbali kwa nyakati mbalimbali zilizoratibiwa kiufundi
kuhakikisha hata mafundi wenyewe hawajui walifanyalo.

Kwanza gari ile ikapelekwa Kidongo Chekundu kwenye gereji ya


mtu aliyeitwa ANOLD KESSY

Fundi huyu akatakiwa aifanyie gari ile Service kuhakikisha


alternator, mfumo wa brake, engine oil ziko sawa.

Akaambiwa abadili tairi kisha atoe mfumo wa friji kwenye gari ile

Fundi Anold Kessy akatoa compressor na storage chambers


kwenye gari lile ambazo zilikuwa “built in”

Kazi yake ikaishia hapo akalipwa ujira wake waarabu wale


wakaondoka na gari.

Wakaingia nayo Nyumba No. 15 mtaa wa Amani, Ilala

Baada ya siku 2 gari ile ikatolewa na kupelekwa mafundi wawili


wa welding

Mafundi hawa ni kijana mmoja wa kichaga Frank Marley na


Julius Kaloli Kisingo

Waarabu wale wakawapa mchoro ya jinsi wanavyotakiwa


kuichomelea gari ile kwa nyuma

Mchoro uliwataka watumie flat bars za nchi 3’ Kutengeneza


vyumba vinne kama mashelf nyuma ya gari ile lilipokuwepo friji
Kisha wakaambiwa kwa chini kwenye floor wachomelee vyuma
vidogo wiwili vinavyotosha kukaa batteries mbili za gari

Kazi yao ikaishia hapo wakalipwa

Waarabu wale wakachukua gari yao na kupotele katika


makutano ya barabara ya Nyamwezi na Ilala na ndio ukawa
mwisho wa mafundi hawa kuiona tena gari ile machoni kwao.

Kule ndani ya nyumba ya ilala kulikuwa kunaendelea zoezi fulani


la kimyakimya

Kijana mmoja mwenye asili ya Unguja alijivika sura ya kinyonge


kila jioni akionekana akiingia kwenye nyumba ile akiwa amebeba
kiroba cha mbolea

Kijana huyu alijulikana kama KHALFANI HAMIS MOHAMMED


maarufu kama Bwana Somba (Samaki)

Huyu ndiye alijulikana kama Ahmed Mrefu.

Hii ni kwa kuwa alikuwa akigawa samaki bure katika mitaa ya


Magomeni Makuto kila boti yao ya uvuvi ikiingia kutoka
mombasa.

Kihalisia kutokana na mbolea ile, ilikuwa ikitengenezwa Kemikali


ya aina mbili yenye uwezo mkubwa wa kusababisha mlipuko.

Kemikali hizo ni TriNitroToluene (TNT) na Pentaerythitol Tentra


Nitrate (PENT)

Hapa ndipo wakaingia kwenye picha wachaga watatu


Yes!

Ni kwa kuwa kemikali hizi zilihitajika kuwekwa kwenye mitungi


mitupu ya gas

Kwa kuwa walihitaji mitungi 10 wakawa wanaenda kununua kwa


muda tofauti mitungi yenye gas na mitupu kutoka kwa FLENAN
ABED SHAYO, FELIX JOHN LEKULE na FRED LYIMO waliokuwa
wanasupply mitungi hiyo

Shayo aliyeanza kupata mashaka baada ya kuwauzia mitungi 7


akaamua kuwauliza vijana wale kama wanahitaji mitungi kwa
kazi gani?

Akajibiwa kuwa wao wanafanya biashara ya vyuma chakavu


hivyo wanahiitaji kwa biashara hiyo.

Hadi wakati huu wapelelezi walikuwa bado gizani

Lakini FBI ni FBI

Kwa kuwa mlipuko wa bomu wa Dar es salaam ulienda


sambamba na wa Jijini Nairobi, kutokea Nairobi ndipo zilianza
kufunguka details zilizowaelekeza wapelelezi kuwabaini
waliohusika pia na shambulio la Dar Es Salaam.

Ni kwamba walishafanikiwa kuwajua washirika walioshiriki tukio


la Nairobi! (Nilishaelezea katika uzi zilizopita jinsi walivyofungua
kampuni ya vito na biashara ya uvuvi)

Kwa kutumia kampuni hii ya uvuvi wakitumia boti ya engine,


ndivyo walivyoweza kuwa wanaenda Tanga, Mombasa, Zanzibar
na Dar.

Baada ya FBI kuibaini kampuni zao za BLACK GIANT (ya vito) na


HELP AFRICA PEOPLE (Ya Charity) wakaanza kutrace
movements za wamiliki wake

Yote haya yalijulikana baada ya kukamatwa kwa gaidi AL-


OWHALI siku tano tu baada ya shambulizi la Nairobi.
Gaidi huyu kwa kuwa alikiwa karibu na eneo la mlipuko,
hakuweza kutoka salama kwani naye alijeruhiwa.

Akaenda kutibiwa hospitali za vichochoroni

Likawa kosa lake la kwanza

Kisha akapiga namba fulani Nchini Yemen kuomba msaada wa


fedha

Namba hiyo ilikuwa ni

967-1-200578

Namba hii ilikuwa ikimilikiwa na mtu aitwaye AL-HADA

Hili lilikuwa kosa la pili!

Makachero katika kufatilia simu zote zilizoingia na kutoka Kenya


kabla na baada ya shambulia, wakanasa mazungumzo yale.

Kisha madaktari waliomtibu gaidi yule nao wakamuuza


akadakwa.

Focal pont ikapatikana kwa wapelelezi

Ikabainika kuwa watu hawa walikuwa wakitembelea sana kati ya


Zanzibar, Tanga na Dar es salaam.

Wakiwa Dar ikatokea tu just a coincidence watu hawa walikuwa


na mwenyeji mmoja ingawa walikuwa wanakuja watu tofauti
kwa nyakati tofauti.

Kwa wapelelezi makini kama FBI this was not just a coincidence

Macho makali ya FBI yakaanza kummulika mtu huyu ambaye


alishafahika kwa jina lake halisi la RASHID SALEHE HEMED
aliyekuwa akimiliki duka la vipuri vya magari la SERA AUTO
PARTS

Neno Sera lilisimama kama kifupisho cha wabia wawili ambao ni


Seifu na Rashidi tunayemzungumzia
Ni kama Coincidence tena, mtu huyu naye ingawa alikuwa na
asili ya Kisiwani Pemba, naye alikuwa ni muarabu kama wenzake
ambao tayari walishaingia kwenye radar ya FBI

Duka na makazi ya mtu huyu yakajulikana kupitia upelelezi wa


kimya kimya.

Wapelezi walishajua kuwa Rashid aliingia Jijini Dar es salaam


akitokea Pemba mwaka 1995 na mwanzoni akafungua biashara
ya nguo.

Baadae akaingia ubia kwenye biashara ile na mtu aitwaye ABEID

Baada ya muda mfupi huyu mmbia mwenzake aitwaye Sued


anamuaga Rashid kuwa anakwenda Saud Arabia hivyo
anamtambulisha kijana ambaye atakuwa anasimamia maslahi
yake pale dukani.

Kijana huyu aliitwa Suleman Abdalah

Biashara inaendelea huku wakifata nguo za kuuza Dubai na


Zanzibar.

Katika safari moja ya Zanzibar, ndipo suleiman akarudi pale


dukani akiwa ameambatana na kijana aitwaye AHMED
KHALFANI GHAILANI

Huyu ndiye aliyekuwa akifahamika kama mwarabu mfupi au


Ahmed Mfupi.

Naam!

Huyu ndiye aliyekuja kuwa engineer wa bomu la Dar Es Salaam

Suleman akamtaka Rashid ampe makazi na kibarua

Rashid kwa kujua au kutojua ndio akawa anaishi naye pale


nyumbani kwake mtaa wa Amani nyuma namba 15 Ilala.

Zaidi ya yote, akampatia kazi pale kwenye duka lake la nguo.


Mwaka mmoja baadaye, baba mdogo wa Rashid ambaye
alikuwa ni mwalimu wa Primary huko Pemba (toka 1971 mpaka
1994) akapunguzwa kazini hivyo akaamua kuja jijini Dar Es
Salaam kuungana na mwanae Rashid kwenye biashara.

Mwalimu huyu aliitwa KHASIM JUMA ABDALAH

Hawa wote wakawa wanafanya kazi pale kwenye duka.

Kikatokea kitu cha hajabu kwenye biashara!

Ni kwamba Suleiman akamtambulisha tena Rashid kwa


mfanyabiashara wa Mombasa aitwaye Mohammed Blazari!

Rashid na huyu mfanyabiashara wa Mombasa wakakubaliana


kuanzisha biashara fulani lakini Rashid hakuwa na mtaji.

Mfanyabiashara huyu akamwambia atampatia yeye huo mtaji.

Lakini biashara hii haikufanyika

Kwa nini?

Just hold on!

Eti huyu aliyetakiwa kutoa mtaji akamkopa anayetakiwa kupewa


mtaji.

Yes!

Bwana Blazari alipata Safari ya kwenda Dubai na akamuomba


Rashid amwazime dola elfu 10

Rashidi akampa kwa makubaliano kuwa atampatia pesa hizo


agent wa Rashid aitwaye Jakubu ambaye naye anaishi Dubai
mara tu atakapofika.

Haikuwa hivyo!

Na haikuwa kwa bahati mbaya.


Kwenye maswala ya Ugaidi huwa kuna mambo mengi ya
kupimana imani kabla mtu hajaamua kukuingiza kwenye
channel

Uhondo wote huu mtaufaidi mkijiunga kwenye channel yetu


inayofundisha mambo ya Criminology hasa tukianza kudadavua
mada ya Counter terrorism and a terror mind (Tunakaribia
kumaliza mwezi tangu tuanze)

Tuendelee,

Bwana BLAZAR hukutuma pesa kama alivyoahidi

Radhid baadaye akajulishwa kuwa Mohamed Blazar amefariki.

Lakini siku tatu tu baada ya kujulishwa juu ya kifo cha Blazar,


mke wa Blazar akampigia simu Rashid

Akamtaka akutane na ndugu wa Blazar aliye jijini Dar ampatie


pesa zake zote.

Ndugu huyu aliitwa Abdula Blazar!

Kweli jamaa akapewa fedha zake.

Lakini baadaye akaenda dukani kwake kijana aitwaye Fahadi na


cha hajabu akamuuliza kama ameshapewa mzigo wake.

Kuanzia hapa kijana huyu akaanza kumzoea Rashid na akawa


anafika hadi nyumbani kwake.

Huyu Fahadi akawa rafiki mkubwa sana na Ahmed Mfupi na


akawa anasafiri naye sasa kwenda Mombasa.

Biashara ya Rashid ikazidi kukua kwa kasi!

Rashidi Akafungua duka la spare Mtaa wa sikukuu Kariakoo


akiwa na mbia mwingine aitwaye Seif (SERA AUTO PARTS)

Fahadi na Ahmed mfupi wakapanga chumba kingine Ilala Boma


nyumba namba 17
Lakini hawakuacha kwenda kukaa katika nyumba kula au hata
kulala kwa nyakati tofauti.

Huku safari zao za Mombasa zikishika kasi.

Naam!

Maelezo haya ndivyo yalivyosomeka katika file la FBI kumhusu


Rashid ambalo walishakuwa nalo mezani.

Sasa wapelelezi walishakusanya ushaidi wa kutosha dhidi ya mtu


huyu kuhusiana kundi lililofanya mashambulizi haya.

Hasa baada ya kuwa na uhakika alikuwa na ukaribu na Ahmed


Mfupi aka AHMED KHALFANI GHAILANI

Hivyo ikaonekana sasa muda wa kumface na kumhoji


ulishawadia

Tarehe 26 August 1998 Assistant Superintendent wa polisi bwana


Valentino Mlowola sasa akapewa green light ya kuhakikisha
anamyakua.

Zikiwa zimepita siku 20 tangu shambulio lile.

Kama mna kumbukumbu vizuri huyu ndiye baadaye alikuja


kuwa mkuu wa taasisi ya kuzuia rushwa.

Wakati mkasa huu unatokea alikuwa na cheo cha nyota tatu tu.

Tuendelee,

ASP Mlowola akaanza kwa kwenda kumuona mshukiwa huyu


kwenye dula lake la spare lililokuwa mtaa wa Sikukuu Kariakoo
lakini hakumkuta.

Akaelekezwa nyumbani kwake ambapo ilikuwa ni nyumba ile ile


namba 15 ya mtaa wa Amani Ilala.

Kule nako hakumuta lakini alimkuta mfanyakazi wake wa ndani


aliyeitwa Amina Rashidi
Naam!

Amina Rashid binti wa miaka 17 huyu.

Amina akaombwa namba za simu za mwajiri wake naye bila


kusita akampatia Kachero Mlowola.

Afande Mlowola akapiga namba ile.

Ikapokelewa na Rashid Salehe Hemedi.

Yes!

Rashid Salehe Hemedi yule yule aliyekuwa akimtafuta

Afande Mlowola akamjuza Rashidi kuwa anamtafuta sana na


alimfata dukani akamkosa.

Hivyo akamuomba afanye juu chini aende pale nyumbani kwake


anamsubiri kwani ana mazungumzo naye.

Haikuwa hivyo!

Ulishapita muda wa kutosha bila Rashidi Salehe Hemedi


kutokea.

Njagu Mlowola akaamua kuipiga tena namba ile ya simu.

Safari hii ikapokelewa na mtu mwingine ambaye alimweleza


Mlowola kuwa mwenye simu yupo msikitini anaswali.

Akiwa ameshachoka kusubiri, Afande Mlowola akawa anataka


kuondoka

Mara akafika pale mtu aliyejitambulisha kama rafiki wa Rashid

Mtu huyu aliitwa Hamis Said Hamis na alifika pale akiwa


anaendesha gari aina ya Suzuki Samurai yenye namba TZG 7575

Mtu huyu akadai kuwa ametumwa na Said amwambie(Afande)


kuwa yeye Rashid yupo Boma.
Kachero Mlowola akaagiza mmoja wa askari aende kumchukua
Rashid pale Boma.

Lakini alipoondoka tu yule askari, akaenda pale mtu mwingine


ambaye naye alijitambulisha kama rafiki wa Rashid akitumia gari
ya Saloon ambaye alijitambulisha kama Issa Salum Mattra.

Huyu akadai Rashid hayuko kule Boma bali yuko sehemu


nyingine.

Afande akamwambia huyo kijana aitwaye Issa, aende akamfate


na kumleta pale walipo.

Ilikuwa imeshafika saa 4 usiku Rashid akiwazungusha


makachero hivyo Ikaamuliwa msako kwenye nyumba ya Rashid
uanze usiku uleule.

Kwanza Ikakamatwa ile gari Suzuki Samurai ambayo alikuja nayo


yule mpambe wa kwanza.

Ndani ukafanyika msako wa juujuu siku ile ambapo walikuta


mabetri ya gari, Detonator cap, Diary ya Ahmed Mfupi, Alminium
foil, Carbon switch brushes etc

Vyote hivi vikachukuliwa.

Muda huu Maafisa watatu maalumu nao wakawa wameshawasili


jijini Dar

Maafisa hao ni Agent Gregory Carl, Agent Robert Fricke na Agent


Michael Gough

Maajenti hawa wakaamuru ufanyike upekuzi wa pili kwenye


nyumba hii

Upekuzi huu ulifanyika tarehe 29 August 1998 siku tatu tu baada


ya ule wa kwanza.

Kwenye upekuzi maagent hawa wakaanza kukwangua rangi za


kwenye nyumba ile hasa milangoni, wakachukua vitambaa vya
masofa kisha wakakwangua rangi za kwenye ile gari aina ya
Suzuki.

Wakachukua seat cover za gari

Kisha wakaomba wapewe nguo zilizochukuliwa awali

Kisha maagent hawa wa FBI wakaomba wapewe wapewe access


ili wafatilie miamala ya kifedha ya watu mbalimbali katika
mabenki mbalimbali kabla na baada ya tukio

Hii ni kwa sababu waliamini ili kufanikisha tukio hili kulihitaji


matumizi ya pesa.

Katika kufatilia, likaibuka jina la Thomas Lyimo.

Huyu alikuwa akiishi Kimara Bucha akimiliki vioski sehemu


mbalimbali vya kuuza maziwa na pia alimiliki garage pamoja na
kuuza gas za kuchomelea.

Biashara za Mzee Thomas Lyimo hazikurandana na kiasi fulani


kikubwa alichoingiziwa siku chache kabla ya siku ya kulipuliwa
ubalozi wa Marekani Dar es Salaam

Kama mnakumbuka, mmoja wa watu aliyewauzia watu hawa


mitungi ya gesi, aliitwa Fred Lyimo na alikuwa ni mtoto wa mzee
Thomas Lyimo.

Baada ya kazi hii na kulipwa dau nono, kijana huyu akadeposit


pesa zile kwenye account ya mzee wake.

Ndipo ikawavutia FBI

Naye akadakwa.

Maagenti hawa wakarudi zao Marekani.

Kule vitu vile akakabidhiwa Mkemia wa FBI bwana Robald Kelly


afanyie uchukuzi zile specimens

Kwenye rangi zilizobanduliwa milangoni na kwenye gari


zikapatikana alama nyingi za vidole
Mojawapo ikiwa ni ya Ahmed Mfupi, Fahadi na KHALFANI HAMIS
MOHAMMED maarufu kama ODEH au Magomeni wakimjua
kama Bwana Samaki

Kwenye nguo na siti za gari yakakutwa mabaki ya unga wa


vilipuzi aina ya PENT na TNT

Duru za kipelelezi zikabaini kuwa Ahmed Mfupi aliondoka nchini


tarehe 11 August 1998 siku tatu tu na Kukimbilia Yemen

Lakini zikapatikana taarifa za mshirika mzanzibari mwenzake


KHALFANI SAID MOHAMED kuwa ametoka Tanzania tarehe 16
August 1995 siku tano tu baada ya Ahmed Mfupi kuondoka.

Kuwa aliingia nchini Msumbiji na kisha akavuka mpaka kuingia


Afrika kusini akitua nyaraka bandia kuomba hifadhi nchini humo
akitumia jina bandia la Zairon Nassor Maulid

Akapewa hati ya muda kuishi nchini humo wakati akisubiri ombi


lake lijibiwe.

Akatakiwa kila mwezi awe anaenda kuripoti kwenye ofisi ya


Uhamiaji.

Makachero wa FBI wakanasa taarifa kuwa KHALFANI HAMIS


MOHAMMED anafanya kazi kama mkanda ngano katika bakery
fulani jijini Pretoria.

Ikabidi afisa mmoja wa CIA aliyepo Pretoria atumwe kuhakikisha


anapata alama za vidole za mshukiwa wao ili kwanza
kuthibitisha taarifa zao

Ndipo kwa mbinu za kijasusi afisa huyu akafanikiwa kuchukua


alama za dole gumba za Mshukiwa kwenye moja ya ngano
aliyokuwa amekanda

Akatuma sampuli Marekani na majibu yakasoma Positive

Hapa ndipo akatumwa Afisa wa FBI bwana Stephen Gaudin


aende akawasiliane na Idara ya Uhamiaji SA
Pale akakutana na mkuu wa Idara ya uhamiaji bwana Christo
Terbranche na akamfahamisha kuwa wana mshukiwa wao
ambaye alifika katika idara yao akitumia nyaraka bandia kuomba
ifadhi ya kisiasa.

Akaomba apatiwe alama zake za vidole ambazo nazo zilisoma


positive.

Ukawekwa mtego kuwa mshukiwa akirudi kuhuisha kibali chake


cha muda atiwe nguvuni.

Ndivyo ilivyofanyika.

Tarehe 5 Mwezi October mwaka 1999, baada ya kujificha zaidi ya


mwaka mzima, KHALFANI MOHAMMED KHAMIS aliporudi
uhamiaji kuhuisha kibali akatiwa nguvuni na kusafirishwa mpaka
Marekani.

Turudi kwa bwana Rashid,

Rashid alienda mwenyewe kuripoti kituo kikuu cha polisi baada


ya siku 20 za kuwakwepa

Alipofika pale alitoa ushirikiano kwa kukubali kumjua Ahmed


Mfupi na wenzake lakini hakujua waliyokuwa wakifanya.

Akatoa hadi mkataba wa manunuzi ya gari aina ya Suzuki


Samurai ambao FAHADI aliungia na mzee wa kihaya bwana A.J
RUTAHIRWA wa tarehe 9 June 1998 ambapo Fahadi alilipa kiasi
cha milioni 2.3

Akaeleza kinagaubaga jinsi alivyojuana na washukiwa pasipo


kujua mipango yao.

Alipoulizwa ni kwa nini alikuwa anawakimbia polisi akaeleza


kuwa alikuwa na matatizo na TRA Tanga ambapo aliingiza gari
aina ya Mitshubishi Canter kutoka kenya kupitia Horohoro lakini
ndani yake alijaza vipuri ambavyo havikulipiwa kodi.

Kwamba gari hiyo ilikamatwa lakini agent wake akafanikiwa


kuitorosha kutoka kwa maafisa wa forodha na kuileta Dar hivyo
alikuwa anatafutwa.
Kutokana na hilo, aliposikia polisi wanamtafuta, akajua
anatafutwa kwa sababu hiyo.

Akaulizwa kwa nini siku ya tukio alirudi nyumbani mapema


tofauti na ratiba yake kuwasha TV kufatilia habari ya tukio la
mashambulizi?

Akajibu hakurudi ili kuwasha TV bali alirudi kuangalia kama kaka


yake Husein aliyekuwa anapaswa kufika kutokea Zanzibar
amefika lakini hakumkuta

Hivyo taarifa za mashambulizi zikamkuta akiwa nyumbani ndio


akawasha TV.

Kuhusu nguo kukutwa na mabaki ya vilipuzi akajibu kuwa polisi


wakati wanapekua hawakutenganisha kati ya nguo zake na
washukiwa bali walizikusanya sehemu moja

Hawakutofautisha kati ya nguo zake na zile za washukiwa na


wala hawakumuuliza kuhusu hilo.

Kwa kuwa alikuwa na vielelezo vyote, ndugu Rashid hata


alipofikishwa mahakamani hakukutwa na hatia.

In fact watu wengi waliodakwa kama Rashid, mfano mzee


Thomas Lyimo, Dalali Sleyum aliyeuza gari, baba mdogo wa
rashid, dalali aliyewapangisha nyumba kina Fahadi kule Ilala
Boma nk, walikuja kuwa mashaidi wa FBI na walisafirishwa
mpaka marekanai kutoa ushaidi uliowatia hatiani Ahmed Mfupi
na Bwana Samaki ambao mpaka leo wanatumikia vifungo vya
maisha

MWISHO

You might also like