You are on page 1of 1

Ujitokezaji wa udrama katika ngano, Mulokozi (1996) anasema kuwa Ngano ni hadithi za kimapokeo

zitumiazo wahusika kama wanyama, mazimwi, miti na watu kuelezea au kuonya kuhusu maisha. Pia
Wamitila (2004) anaeleza kuwa Ngano ni hadithi za kimapokeo ambazo huwatumia wahusika wa aina
mbalimbali (wanyama , miti ,au watu) kusimulia tukio au kisa fulani chenye mafunzo. Anaendelea
kusema kuwa kuna aina mbalimbali za ngano kama vile: Ngano za mazimwi, Ngano za usuli, Ngano ya
kishujaa, Ngano za hekaya, Ngano za hurafa au wanyama, Ngano za mtanziko, Ngano za kimafumbo
(kuna ngano za Istiara, mbazi/vigano, mchapo/ kidahizo), Ngano za kichimba kazi/ kudhubahi na Soga.
Udrama katika ngano unaweza kujitokeza kupitia matukio au migogoro inayowakumba wahusika
kuonesha hisia na changamoto wanazopitia. Kwa mfano katika ngano ifuatayo

Katika kijiji kimoja kulikuwa na jogoo mweusi aliyekuwa na sauti Nzuri sana

Jogoo huyo alikuwa maarufu sana kwa kuwika kila asubuh na kuwap nguvu

Wakazi wote wa kijijini hapo. Lakini siku moja mbwa mwitu mjanja alimuona

Jogoo alikuwa peke yake na akapanga njama ya kumashinda. Mbwa mwitu

Akatafuta washiriki wawili Sungura na Kasa na wote wakaanza mpango wao

Wa kumvizia Jogoo na kuanza kumpigia kelele. Jogoo akachanganyikiwa na

Kutishwa sana ndipo Sungura akatumia ujanja wake kumshawishi jogoo kuwa

anauwezo wa kumuokoa lakin I wanahitaji msaada wake. Jogoo akawa na

moyo wa ujasili akakubali kuwaongoza walipofika kwenye lango la kijiji

Jogoo alianza kuwika kwa nguvu zote sauti yake ikawavunja moyo Mbwa mwitu

na washiriki wake wakaamua kikimbia na kijiji kilikuwa Salama tena.

Hapa udrama unajitokeza wazi kupitia changamoto za Jogoo na jinsi anavyopambana na hatari iliyokuwa
inamkabili udrama huo huongeza kipengere cha kusisimua katika ngano na kutoa mafunzo kuhusu ujasili
na ushirikiano

Malejereo

Mulokozi M.M (1996), Fasihi Ya Kiswahili. Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania. Dar es salaam.

Wamitila K.W. (2004), Kichocheo Cha Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi.English press. Nairobi.

You might also like