You are on page 1of 21

0 More Next Blog Create Blog Sign In

ChuoKenya
Your Gateway to World of Education

Home

Mwogozo Wa Damu Nyeusi Part 3

GILASI YA MWISHO
MAKABURINI
Katika hadithi hii tunapatana na Msoi mwenye utambuzi
wa kipekee ya mamabo yatakayotokea. Msoi alipata hisia
flani yenye kitisho na wasiwasi. Ndoto nyingi ambazo Msoi
aliwahi kuota mara mara hua ingawa marafiki wake
hawakuamini.
Hisia hizo ambazo Msoi alijaribu kuepuka kwa muda kwa
mwezi mmoja hatimaye zilimfanya awe mwoga zaidi yeye

open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
pamoja na marafi zake walikuwa wanaenda katika bar
iliyokuwa kwenye maskani ya mava ili kunywa na
kujiburudisha baada ya kazi. Pia pahali hapo
palipopachikwa jina la kimombo exotic resort.
Siku moja aliamua kutoenda katika mava kwani hisia zake
zilimfanya aogope sana. Kwa sababu aliona kwamba balaa
kubwa itatokea,Semkwa rafikiye Msoi alienda kwake
nyumbani ili kumsihi waende katika mava akaitikia shingo
upande. Walipokuwa wakitokea Msoi aliligonga bakuli la
maua likavunjika vipande vipande ,alikuwa karibu kuanguka
akiteremsha mguu na pia alijibana kidole kidogo kwenye
mlango wa gari. Hizi zilikuwa ishara za kuonyesha kwamba
jambo mbaya litatendeka. Followers

Njiani walisikia mgurumo wa radi ambayo Semkwa aliona Join this site
kuwa jambo la kawaida. Walipofika kwenye daa ya w ith Google Friend Connect
makaburini,walipatana na Asha na Josefina. Walipokaa Members (5)
chini,Msoi aligeuza namna yake ya kukaa. Siku hiyo alitaka
kuyaangalia mava ili jambo likitokea ataweza kutoroka.
Muda ulivyozidi kuyoyoma , Msoi na marafiki wake
walijiburudisha na vinywaji na muziki uliochezwa na bendi.
Already a member? Sign in
Asha na Msoi walipokuwa wakichheza densi, Msoi
alionekana mwenye wasiwasi. Wenzake wakaanza kumtani
hadi ikambidi anyamaze ili angoje kile ambacho kitaendeea. Blog Archive
Msoi alingwa na kuburudika nao ijapokuwa walimtani na 2010 (1)
kumkejeli kuhusu ndoto zake. Asha aliburudishwa na Msoi
2012 (1)
kuhusu matukio yaliyotendeka na Msoi kuhusu matukio
2013 (1)
yaliyotendeka awali ambayo aliona kama ni ya bure tu. Msoi
2015 (4)
aliamua kujinyamazia.
October (4)
open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
October (4)
Wakati ambao kila mtu alikuwa ameshiba walicheza mziki
Oct 12 (4)
huku wakiwa kwani hawakutosheka. Baada ya muda mfupi,
Mwogozo Wa Damu
Msoi aliviona vizuu vimejifufua kwa mtindo wa Thriller wa Nyeusi Part 3
Micheal Jackson, Asha alipiga uyoe ambao uliskika na kila Mwongozo wa Damu
mtu. Watu walipoona yaliyokuwa yakiendelea walitimua Nyeusi Part 2
mbio hadi kwao nyumbani. Wengine walianguka na Mwongozo Wa Damu
kukanyangwa Nyeusi Part 1

Baada ya Asha na Msoi kufika nyumbani waliskia habari Mwongozo wa Damu


Nyeusi Part 4
kwenye televisheni kwamba wale vizuu walikuwa majambazi
ili waibie Baa ya Makaburini pamoja na wateja wao.kwa
mara nyingine marafiki zake Msoi walifahamishwa kwamba About Me
wanafaa kumsikiliza.
DHAMIRA. Kibe Paul

Mwandishi anatuhimiza tusipuuze mambo ambayo Software


tunaonywa na marafiki zetu. developer and
web designer.
MAUDHUI
View my complete profile
ANASA NA STAREHE
Tunaona kwamba Msoi na Asha walikuwa wanaenda kwenye
baa ya makaburini kujiburudisha baada ya kazi na kulewa
kiasi cha kujisahau.
UHALIFU
Majambazi walivamia watu na kuwaibia mali yao kwani
waligundua kwamba watu huogopa wafu
ITIKADI NA USHIRIKINA
Ushirikina ni ile hali ya kuamini nguvu nyingine kuliko
mungu
Msoi aliamini kwamba baa iliyokuwa kwenye mandhari ya
mava ingevamiwa na watu wasiojulikana
open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
URAFIKI NA UTANGAMANO
Akina Semkwa,Msoi,Asha na Josephina waliburudika
pamoja na kutengamana.walifanya m ambo pamoja
UWOGA
Msoi aliota ndoto ambazo zilimfanya awe mwoga.
WAHUSIKA
1.Msoi.
Ni mtu mwenye kipawa utambuzi wa mambo
SIFA
I. Ni mbarazi ,ana mazoea ya kukaa na watu wengine hasa
katika baa.
II. Ni mshiriki anasa,amekuwa akizuru bar ya makaburini ili
kustarehe.
III. Ni mpole,hana mambo mengi.
IV. Ni mwoga.
V. Ni mshirikina,anaamini katika mambo ya ushirikina.
VI. Anashawishika kwa urahisi.
2.Semkwa,Asha na Josefina.
I. Ni wabaraza
II. Wapenda anasa,kila wikendi walikuwa wanakutana katika
baa na kuburudika pamoja.
III. Wabishi,walibishana na Msoi alipowadokezea kuhusu ndoto
yao.
IV. Weye utani ,wanamtania Msoi anapowaeleza kuhusu ndoto
yake.

3.Majambazi.
I. Ni watu wabunifu walivaa kama wafu ili waweze
open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
kuwaogofya watu
II. Ni waoga-hawajitokezi moja kwa moja kukabiliana na
watu.
III. Wahalifu walijaribu mali ya watu baada ya
kuwaibia.

KIKAZA.
Hadithi hii inazungumzia kikaza ambacho ni suruali
spesheli. Kikaza hiki kimetumiwa kusimamia uongozi katika
jamii. Kikaza ni jazanda inayosimamia uongozi. Hadithi
inaanza pale ambapo kuna dalili za mvua kunyesha,lakini
Mzee Babu akawafahamisha wanakijiji kwamba haitanyesha.
Kwanza wanatekede hawakuamini. Kulikuwa na kikao kwa
mzee huyu na miongoni mwa waliohudhuria ni Bi Cherenga
almaarufu Bi Cherehani na Bw Pima,Bw Machupa pia
alikuwepo(msemaji wa kijiji). Wote walitaka Mzee Babu
awafunulie kitendawili.
Washona kikaza ni wananchi wenyewe. Kikaza kilikuwa
kimepasuka. Bw Mtajika(kiongozi) alifanya makosa
kumwacha Bi Mtajika kukiguza kikaza,kwani yeye siye
kiongozi. Mapinduzi ni marekebisho yalihitaji kufanywa.
Kulikuwa nia uongozi mbays. Bw Pima alipima kikaza na Bi
Cherehani kukishona. Bi Cherehani aliwahimiza
wanatekede kwenda kukishona kikaza (kurekebisha
makosa na kumtoa Bw Mtajika mamlakani) . Kikaza
kilihitaji kushonwa. Bi Cherehani alihakikisha kwamba
atapunguza kipimo ili kikaza kikaze. Kikaza (uongozi) ni cha
ushirika.
open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
DHAMIRA.
Mwandishi anataka kuonyesha kwamba uongozi ni ushirika.
MAUDHUI
1.UONGOZI
Hadithi hii inaongea kuhusu swala la uongozi.

Uongozi umewakilishawa na kikaza suruali ya ndani


Uongozi hushonwa na wananchi.
Uongozi ni ushirika.
Uongozi mzuri au mbaya hutokana na mchango wa watu
wenyewe
Mwandishi pia anaguzia swala la uongozi mbaya
Bw Mtajika tunaelezwa kwamba kikaza chake kimeraruka na
basi uongozi umeigiza dosari.
Bi Mtajika amechangia katika uongoza mbaya.
Wanawake walishona kikaza kiliochobana
2.UBINAFSI
Bw Mtajika na wenzake waliochaguliwa waliochaguliwa
waliwasahau waliwasahau wenzao waliowachagua kama vile
kobe alivyowatendea hadithi yake kuenda angani.

3.USHIRIKIANO
Kikaza kilishonwa kwa kushirikiana. Katika uongozi, lazima
pawepo na ushirikiano wa watu wote.
4. MABADILIKO
Baada ya mambo kugonga mwamba, viongozi wanatolewa
mamlakani na kubadili uongozi.
open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
5. USALITI
Bwana mtajika na Bi. Mtajika , anawasaliti wananchi kwa
kuongoza vibaya na kutomzuia mkewe kukigusa kikaza.
6. UKARIMU
Babu na wanakijiji ni wakarimu wanapopeana mavuno.
7. KUTOWAJIBIKA
Viongozi hawakuajibika katika uongozi wao.
8. UTABIRI
Babu anatabiri.

WAHUSIKA
1. MZEE BABU
Ni mtabiri
Mkarimu
Mwenye busara . Anawatetea na kuwashauri watu
Mbaraza. Anapenda kuingiana na watu.
Mtambuzi wa mambo.

2. BW. MTAJIKA
Kiongoziwa tekede.
SIFA

1. Ni mweledi wa kuongea .anapoongea, hawei kubadilisha


ukweli kuwa uongo.
2. Mwenye ubinafsi. Alipopata cheo, aliwasahau wengine.
3. Ni mwanamme anayetawaliwa na mkewe. Alikua amezidiwa
open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
na nguvu za pili.
4. Msailiti. Amewasaliti wananchi wa Tekede kwa kuwasahau
(hadithi ya safar ya mzee kobe kwenda angani. )

3. BI CHEREHANI/ BI CHIRENGA.
Mshonaji kikazi.
Ni mnyamavu kwani hapendi kuzungumza
Ni mwenye soni
Mkweli. Hapiti njia mbili. Hafichi mambo.
Ni mzalendo .hakwenda ikuliuni peke yake.
Mwenye bidii kwani anashona kikaza kama jukumu lake.
Mvumilivu. Amevumilia kukemewa na watu.

4. BI MTAJIKA.
Msaliti anakigusa kikaza ingawa anaelewa itikada ya jamii
ya wana Tekede inayosema kwamba wa pili hafai kugusa
kikaza.
Ni mkoloni kwani anaamua kutawala watu apendavyo yeye.

5. WANAKIJIJI
Ni wakarimu.Walimpa babu mavuno waliyoyapata.
Wenye mapinduzi. Watu walizinduka kuhusu uongozina Bw.
Mtajika.
Ni wenye ushirikiano.Wanashirikiana kumtoa Bi Mtajika
kwenye mamlaka.
Ni wasikivu. Wanamsikiliza babu kwa makini.
Ni wenye utamaduni.Wanatii tamaduni zao.K.m bibi
open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
hakustahili kugusa kikaza.

MBINU ZA LUGHA
a) TASHTITI
Ni mbinu ya kukejeli mtu kwa njia ya kutomuudhi moja kwa
moja.
Hadithi ya kobe ni tashtiti murua inayoonyesha ubadhilifu,
ukaidi na uogozi mbaya wa Bw. Mtajika. Mzee Babu
anawapa watu hadithi badala ya kusema yote aliyoyafanya
kombo Bw. Mtajikana adhabu atakayoipata atakaposhushwa
madaraka.
Ushonaji wa kikaza vibaya kwa Bi. Cherehani na Bw. Pima
pia ni tashtiti. Yaonyesha namna ambavyo wanakijiji wa
Tedeke waliomchagua kiongozi aliyefaa.
Msemo wa nyani haoni kundule ni semi linaloeleza
upambano na kutojali kwa wanakijijij wa Tekede.
b. FUMBO
Kikaza kimetumika kimafumbo kumaanisha uongozi,
upimaji Na kushonwa kwa kikaza ni kumteua na kumtwika
majukumu ya uongozi. Kupima na kushona kikaza ina
maana ya ushirikiano wa jamii katika kumchagua na
kumsimika kiongozi.
Wa pili hakuruhusiwa kushika kikaza ni mke wa kiongozi.
Kutanda Kwa mawingu meusi angani kusha kukosa
kunyesha ni fumbo inayoeleza dhiki ya waakaazi wa Tekede.
open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
c. HADITHI
Hadithi katika hadithi hii inamhusu kobe inayosimuliwa na
mzee Mzee Babu. Musiliko wa karamu angani ilimjulisha
kobe, ndege na kadhalika. Mzee kobe alifanya ujangili na
kudai jina sisi sote.
Kila chakula, kinywaji na starehe zilielekezwa kwake. Ndege
walitababika na kuamua kumnyanyanya kobe. Manyoya yao
na kobe hakuweza kupaa tena ndio maana gamba la
kobelena viraka au mipasuko.
D. MAJAZI
Mbinu za kisanaa.
Baadhi ya wahusika wanapewa majina kulingana na sifa au
hulka zao. K.m. Mzee Babu alikuwa mzee kuliko wengine. Bw.
Mtajika alitojwa mara kwa mara na kila mtu kwa sababu
alikua kiongozi wao. Bw.Machupa pima aliyapima kwa
uangalifu alivyowaambiwa wanakijiji.
Bw Machupa hakuwa na msimamo dhabiti hasa kuhusu
uongozi wa Bw. Mtajika.
e. TAKRIRI
Baadhi ya kauli zimekaririwa ili kutilia mawazo Fulani
mkazo k.m Bw. Cherehani na Bw. Pima walikuwepo kushiriki
na kutoa mchango walikuwepo vilevile.
Kitendawili cha kukaza kikazidi kukazaa.
f. TABAINI
Ni kusisitiza mambo kwa kutumia vikarushi. Baadhi ya semi
zina dhana ya ukinzani lakini kwa hakika hakuna ukinzani
kimaana. K.m si salama si chochote hakuna kilichotaka
open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
kinywani.
g. TASHBIHI
Yaliyopita huja kama nguvu za sunami.(uk 45) Machupa
hutafuna na kupuliza kama panya.
h. BALAGHA
Hayahitaji majibu.
Anasema nini?
Itakuwaje sisi wawili ndio tuwe najibu?

6. MAEKO
Hadithi inapoanza ni usiku wa manene ambapo Hamduni au
Duni anaporejea kwake. Anatoka ulevini kama ilivyokuwa
desturi yake. Ni majira ya usiku wa manane. Anaimba
wimbo wake wa kawaida ambao mwandishi anaita taarabu
njia. Kwani alizoea kuuimba akiwa njiani kuelekea kwake.
Jamila mkewe Hamduni anapomsikia mumewe anamka ili
kumsubiri. Mwanzoni mumewe anamka ili kumsubiri.
Mwanzoni mumewe anaonyesha furaha na bashasha kwa
kupokelewa na mkewe. Lakini anageuka na kuwa mjeuri
mkewe anapojaribu kumsaidia kupanda ngazi za kuingia
kwao puia anampiga mkewe teke kwa kukawia kumpatia
chakula.
Mwandishi anasema ghasia na zogolaukorofi wa duni zilidi
na kukosesha utulivu katika ndoa yao. Majirani na hata
jamaa zake jamila walipoona kipigo kimezidi walimshauri
ajiondoe kwenye ndoa hiyo. Hata kuna kifana kwa jina salim
aliyoyapitia. Alitaka Jamila amwasi duni halafu angetoroka
open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
naye.Alishindwa kuelewa Kwa hakika. Salim alimpenda kwa
dhati au alitaka kujinufaisha kutokana na hali yake Jamila.
Kwa sababu ya madhila aliyofanyiwa na mumewe Jamila ya
kawaida. Alirauka asubuhi na kutayarisha kiamsha kinywa
cha kukata na shoka ambacho alikiagizwa kwa fujo. Kenyoye
Duni alimpumbaza mkewe kwa mapenzi yasiyo ya kawaida.
Alirauki asubuhi na kutayarisha kiamsha kinywa cha kukata
na shoka akakusanya nguo zote chafu na kuziroweka ili
azifue baadaye kasha akaenda kumwita mkewe. Alimuomba
msamaha mkewe kwa yale yote aliyomtendea kasha
wakashebeha.
Baada ya hapa maisha yakawa ni yay ohayo amani na
mapenzi kwa muiezi miwili, kufarakana, kuombana
msamaha, amani na kadhalika.Hta Jamila mwenyewe
alishindwa afanye nini. Lakini kwa kiasi kikubwa
aliridhishwa na ndoa yake licha ya matatizo aliyoyapata
humo.
DHAMIRA
Watu huvimilia mapato wanayoyapata katika ndio hiyo k.m.
jina, pesa, mapenzi na kadhalika.

MAUDHUI
1. ULEVI
Unywaji pombe kupindukia.
Hamduni alilewa kupita kiasi.Mwandishi anataka kukashifu
ulevi.

open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
2. UVUMILIVU
Jamila amevumilia mateso na majirani wanavumilia kero za
hamduni.
3. DHULMA KATIKA NDOA
Hamdunio anamwacha mkewe na kwenda kulevya.
Kumchapa Jamila akiwa amelevya.

4. MAEKO
Namna ambavyo mtu (Jamila) amewekwa.
Jamila anavumilia dhulma za ndoa kwa kuwa anapewa pesa,
mapenzi, anafanyiwa kazi.

WAHUSIKA

1.HAMDUNI
Ni mhusika mkuu katika hadithi hii na ni mumewe Jamila.
SIFA
1. MLEVI
Analewa kila siku
2. Mwenye fujo
Anampiga mkewe.
3. Ni mkaidi
Alikanywa kupiga makelele usiku lakini anazidisha.
4. Ni msumbufu
open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
Aliimba usiku watu wakiwa wamelala.
5. Ni msanii
Alipenda kuimba.
6. Ni mwenye majuto
Hujitia makosa ambayo alitenda akiwa amelala.
7. Ni msahaulifu
Anasahau kwa haraka aliyomfanyia mkewe.
8. Ni mwenye mapenzi.
Anampenda mkewe.

2. JAMILA
Mhusika mkuu ni mkewe Hamduni.
SIFA
1. Mwanamke mwenye umri mdogo.
2. Ni mvumilivu. Anavumilia masaibu ya ndoa.
3. Mwenye mapenzi.
4. Ni mjinga anaishi katika ndoa kwa sababu ya maeko.
5. Ni msamehevu anamsamehe mumewe kwa aliyamfanyia.
6. Ni mwenye kutamani kuishi maisha mazuri.
7. Mwenye matumaini
open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
8. Mwenye msimamo thabiti hakutaka kutoka kwa mumewe
ingawa alishauri afanye hivyo.
3. SALIM
Ni rafikiye Hamduni.
SIFA

1. Ni mnafiki. Alimwahidi Jamila amuasi duni ili angeweza


kutoroka naye.
2. Ni mwenye mawaidha ya kupotosha. Anamhimiza Jamila
atoke kwa duni ili aepuke kuhapo.
3. Ni msaliti. Anamtaka Jamila ambaye ni bibiye rafiki yako.
4.WANAKIJIJI
1. Wanapenda amani
2. Wanamshauri Jamila.
3. Ni wavumilivu.

4. SELA
Ni mhusika mkuu anasomea shule ya Askofu Timotheo
mwanawe mzee Buteli.
A) Ana utu na huruma. Hakuavya mimba pia
alipokutana na Masazu aliyejifanya mgonjwa ,
alimsaidia.
B) Ni mkarimu. Anampeleka Masazu kwenye kliniki.
C) Mwenye mapenzi ya dhati. Anampenda Masazu
open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
kwa moyo mmoja anampenda ata baada ya kumpa
ua uzito.

MBINU ZA SANAA
NYIMBO
Mwandishi ametumia nyimbo kwa nia ya kuwasilisha
ujumbe Fulani kuonyesha hulka ya mhusika.
Wimbo wa kwanza unaimbwa na Hamduni anapotoka
ulevini kuonyesha kuwa hakujali walivyosema wasebuleni.
MAJAZI
Mwandishi amewapa wahusika majina yaliyolingana na sifa
au hulka zao.
Jina la duni halisi lilikuwa Hamduni lakini watu walizoea
kulifupisha na kuwa Duni ili litamkike kwa urahisi. Jina hili
lilimfanya adharauliwe na watu mtaani sebuleni.
Salim alikuwa rafikiya Duni ambaye aliyejitolea kuleta hali
ya utulivu katika maisha ya Jamila kwani alijiona salama na
bora kuliko Hamduni.

MBINU ZA LUGHA.
I. KEJELI
Duni mtiribu sababu alizoea kuwaamsha majirani zake kwa
nyimbo za kilevi. Duni hakuwa mtiribu, hii ni kejeli kwa
sababu aliwaudhi wanakijiji kwa nyimbo zake.
2. METHALI
m.f. tunaambiwa kuwa wenyeji wa Sebleni walitoa maneno
open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
ya kumlaani Duni akini yalikuwa ni dua la kuku haimpati
mwewe yaani Duni, maanake hakubadilika wa
kushughulishwa na hayo.
3. MISEMO
usiku mkubwa (uk 66) usiku sana. kusafiri kwa mapana
na marefu kusafiri sana. mjaliwa laana mtu aliyelaaniwa.
5. BALAGHA
Mwisho wa haya utakuwa lini ya Rabi? (uk 67) alijiuliza
Jamila hakuwa nalo.
6. KINAYA
Walimwonea Jamila huruma walisema kuwa huko nje
kulikuwa wanaume waungwana na majina na staha zao na
ambao wangefanya lolote ili wampate Jamila.
7. UTOHOZI
Baadhi ya maneno yametoholewa kutoka kizungu ili
kuonyesha usasa na pia athari za kizungu kwenye maisha ya
wahusika.
k.m: stimu- steam
Kozi- course
Bendeji- bandage
Hai- high
Dii dear
8. TASHBIHI
Alimpiga mkewe kama ngoma ya kimanga popote apatapo
kuonyesha jinsi Duni alivyimpiga mkewe bila huruma.
9. TAKRIRI
open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
Maneno na semi au kauli zimarudiwa ili kutilia mkazo wazo
Fulani k.m mtiribu.

Posted by Kibe Paul at 9:05 AM


Recommend this on Google

Labels: fasihi, Hadithi Fupi, KCSE, kiswahili, Mwongozo wa Damu Ny eusi

No comments:

Post a Comment

open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
Enter your comment...

Comment as: Select profile...

Publish Preview

open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
Newer Post Home Older Post

Subscribe to: Post Comments (Atom)

Loa din g ...

open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
Simple template. Template images by luoman. Powered by Blogger.

open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com

You might also like