You are on page 1of 4

KOZI YA KISWAHILI, MWAKA WA 3 – MUHULA WA 2 S/Y:

2023-2024
MWALIMU: Jean Pierre Niyongabo
Email: pniyongabo@villagehealthworks.org
FASIHI ANDISHI: HADITHI FUPI

Hadithi fupi ni mtungo wa kubuni ambao hueleza hadithi au kisa kwa ufupi. Maelezo ya hadithi huwa ya
lugha ya kawaida. Ni kisa kifupi cha kubuni ambacho kinahusu watu na wanyama. Ili mtu aweze
kwandika hadithi fupi anapaswa kuzingatia hatua zifuatazo:

1. Mwandishi awe na wazo anataka kuwasilisha kwa msomaji (kwa mfano uovu wa kula rushwa),
2. Awe anaielewa kwa undani mada anayotaka kuiandika,
3. Kuteua wahusika,
4. Mfululizo wa matukio (fikira) ya hadithi,
5. Aanze kuandika nakala ya kwandika kisha baadaye aisome na kuimarisha.
6. Hadithi fupi iliondikwa ipewe anuani,
7. Mwandishi azingatie fundisho kwa kila msomaji

Mfano wa hadithi fupi:

Mwaka mmoja ilitokea njaa kali sana na majani yote yalikauka. Alikuako kapera mmoja tu mwenye
shamba la mahindi. Kulikuwa na nyani. Hao nyani wakifikiria namna ya kuyapata mahindi yale kwa
urahisi. Walimchukua mwali wao mmoja mzuri sana na kumgeuza awe mtu ili akaombe mahindi. Walijua
kuwa mwenye mahindi akimwona tu, atamtamani na akitaka kumuoa akubali. Kama akiolewa na yule
mwenye mahindi basi nyani wote watapata urahisi wa kwenda kuvunja mahindi bila kufukuzwa. Basi
wakamgeuza mtoto mmoja wa nyani kuwa mwali katika umbo la binadamu mrembo na akaenda
kuomba mahindi.

Alipofika tu, mwenye shamba kamtamani. Alipomwambia anataka kumwoa, nyani alikubali, Basi
wakaona yule mtu hakufahamu ya kuwa anaoa nyani. Ikawa asubuhi na jioni yale manyani wanakuja
wanakuja kuvunja mahindi bure.

Mwanamke yule alikuwa hawafukuze maana ni ndugu zake. Lakini siku moja akawaambia, « Akina nyani
nyie, mimi, sasa nimechoka kuwapa mahindi ya bure. »

« Wewe tumekugeuza sisi kuwa mtu, lakini kama sasa unatukataa sisi kwa sababu ya mikia yetu, haya ».
Lakini tukikasirika sisi wewe hukai na mumeo, maana tutakubadili tena uwe nyani kama sisi.

Yule mwali ndipo aliwaambia ya kwamba hawawezi tena kumugeuza nyani na tangu siku ile hataki tena
kuwaona nyani nyumbani kwake. Basi nyani walikasirika na kurudi nyumbani. Waliipofika nyumbani
waliitana mkutano na wote wakajaa n kuanzakusimulia aliyaongea yule mwali waliyemgeuza mtu ili
wapone njaa. Wote wakakubaliana kuwa wampelekee mkia wake na kumrudisha kwenye umbo la nyani.
Basi wakakutana wote na kwenda nyumbani kwa ule mwali huku wakiimba.
Ukimwona Loda, mpelekee mkia wake huo.

Walipofika karibu na nyumba yake akaanza akaanza kusikia wimbo ule. Mme wake akaanza
kushangaakuumwa huko kumemuanza lini? Nyani walivyozidi kuja huku wakiimba ndivyo yule mwali
alivyoanza kugeuka miguu. Alipomaliza kugeuka na kuwa nyani alikimbilia porini kwa nyani wenzake.

A. Maswali ya ufahamu:

1. Kwa nini nyani aliolewa kwa bianadamu?


2. Nyani walikuwav na shida gani?
3. Kitu gani kilichofanyika ili nyani aolewe kwa binadamu
4. Hadithi hii inatufunza nini katika maisha yetu?

Ufafanuzi wa msamiati:

- Kapera: mvulana (mtu mzima) ambaye hajafunga ndoa


- Nyani : mnyama anayefanana na tumbiri mkubwa Zaidi mwenye rangi ya kaki ya kijivu na
jekundu matakoni.
- Mwali/mwari: msichana bado bikira ama msichana aliye kwisha vunja ungo ambaye hajaolewa.
Maharusi wanakuwa harusi
- Fungate: Kiini cha siku saba za mwanzo baada ya maharusi kuolewa (siku harusi
wakijipumukisha)
- Kutamani: kuwa na hamu ya kitu, kutaka sana kitu.
- Mwanamke mrembo: mwanmke mwenye umbo mzuri
- Kusimulia: kutoa maelezo juu ya tukio Fulani

VIRAI VYA KISWAHILI

KIRAI

Ni kipashio cha lugha ambacho huwa na muundo wa neno moja au zaidi lakini huwa hakina muundo wa
kiima na kiarifu. Muundo wa kirai huwa ni wa neno moja au zaidi ambayo huwa pamoja katika mpangilio
maalumu wenye kuzingatia uhusiano wa maneno hayo na neno kuu ambalo ndio huwa linabeba aina ya
kundi hilo la maneno.

AINA ZA VIRAI

A. Kirai nomino (KN)

Hili ni kundi la maneno ambalo hutawaliwa na nomino. Kirai nomino huundwa na maneno yafuatayo:-

o Nomino pekee. Mfano; Asha anapika, Carine anaimba, Maria anacheza (N)

o Nomino mbili au zaidi zinazounganishwa. Mfano; Mhindi na Paul wanacheza. (N+U+N)

o Nomino na kivumishi. Mfano; Mtoto mnene amekuja, Mzee mfupi ameondoka. (N+V)

o Kiwakilishi pekee. Mfano; Yule ameondoka, Wewe umenena, Wale waliokuja. (W)

o Kiwakilishi na kivumishi. Mfano; Yule mvivu amerudi, Wewe mpole njoo. (W+V)
o Nomino na kitenzi jina. Mfano; Mchezo wa kusisimua, Wimbo wa kupendeza. (N+Ktj)

o Nomino na kishazi tegemezi kivumishi. Mfano; Mjukuu aliyepotea, Mheshimiwa aliyeondoka.


(N+βV)

B. Kirai kivumishi (KV)

Hiki ni kirai ambacho muundo wake umejikita katika kivumishi na maneno yanayohusiana na kivumishi
katika tungo tungo hiyo. Virai hivi kwa kawaida hujibainisha zaidi kimuundo kama sehemu ya virai
nomino. Virai hivi huundwa na:-

o Kivumishi na Kirai nomino. Mfano; Mwenye mali nyingi, Wenye watoto wengi.

o Kivumishi na kielezi. Mfano; Mzuri sana, Mweupe pee ! Mweusi tii!, Mbaya sana.

o Kivumishi na kirai kitenzi. Mfano; Mwenye kupiga gitaa, Mwenye kupenda sana.

o Kivumishi na kirai kiunganishi. Mfano; Nzuri ya kupendeza, Mpungufu wa akili.

C. Kirai kitenzi (KT)

Neno kuu katika kirai hiki ni kitenzi. Kirai kitenzi kimeundwa na vipashio vifuatavyo:-

o Kitenzi pekee. Mfano; amekuja, amekula, ameoga. (T)

o Kitenzi kisaidizi na kitenzi kikuu. Mfano; Alikua anacheza(Ts+T), Alikua anaweza kuimba. (Ts+Ts+T)

o Kitenzi, jina na kielezi. Mfano; Nimepika uji asubuhi

D. Kirai kielezi

Kirai kielezi huelezea namna, wakati, mahali na kinachofanya tendo hilo litendeke.

Mifano:
o Anaenda sokoni mara nyingi.
o Anampenda Sana sana.
o Wanatembea polepole
o Jana asubuhi nilienda shuleni
o Tutaonana kesho mchana, n.k.

E. Kirai kihusishi

Kirai kihusishi ni kikundi ambacho neno lake kuu ni kihusishi.

Ni kirai ambacho muundo wake umekitwa katika mahusiano baina ya vihusishi kwa, na, katika,au
kwenye na fungu la maneno linaloandamana nacho.

Mifano
o Nimewaona katika kituo cha mabasi.
o Ameenda kwa baba yake.
o Wanaishi chini ya barabara.
Fasihi Simulizi – Hadithi Fupi
Hadithi za kale – Jogoo na Kondoo

Hapo zamani za kale, kulikuwa na jogoo na kondoo ambao walikuwa wanaishi pamoja katika familia
moja. Siku moja, wenye nyuma walitarajia wageni wengi kuja kwa ajili ya sherehe. Kwa sababu ya idadi
kubwa ya wageni, hao watu wakapanga kumchinja kondoo ili kuandaa chakula cha kutosha. Jogoo,
ambaye alikuwa na kiburi na tabia ya kuwadharau wengine, alimcheka kondoo na kumfanyia mzaha kwa
sababu alijua kuwa yeye hatakuwa mmoja wa wale wanaochinjwa.

Hata hivyo, mambo yalibadilika ghafla. Wageni waliofika walikuwa wachache sana kuliko ilivyotarajiwa.
Wenye nyumba waliamua kumchinja jogoo badala ya kondoo ili kuandaa chakula cha kutosha kwa
wageni hao wachache. Jogoo alishangazwa na hali hiyo na akageuka kuwa wa kuchinjwa.

Hadithi hii inatufundisha umuhimu wa kutokuwa na kiburi na kutojionyesha mbele ya wengine.


Tunapaswa kuheshimu na kuthamini kila mtu bila kujali nafasi yetu au jinsi tunavyojiona. Kwa sababu
maisha yanabadilika na mambo yanaweza kugeuka kwa ghafla, ni muhimu kuwa na unyenyekevu na
kujifunza kutokana na uzoefu wetu.

You might also like