Professional Documents
Culture Documents
Ushindi Dhidi Ya Kujichua Na Pornografia - Pastor Eskaka
Ushindi Dhidi Ya Kujichua Na Pornografia - Pastor Eskaka
HAKIMILIKI
Baruapepe: chaulaeskakaa@gmail.com
Instagram: pastoreskakachaula
@2024.
YALIYOMO
UTANGULIZI ................................................................. 5
UTANGULIZI
Kijana mmoja alinijia huku akiwa amepoteza tumaini la kushinda jumla
uraibu na kifungo cha uraibu wa ngono. Historia yake kama ilivyo
maelezo yake alianza kusema;
Nikiwa shule ya msingi siku moja niliona marafiki zangu wakiwa na simu
na ni kama kuna kitu wanaangalia kwa shauku huku wakikifurahia. Na nje
ya matamanio [curiosity] ya kibinadamu nikatamani nikatazame nini
wanatazama, bahati mbaya nilipofika walizima simu wakaficha, mmoja
wao akanambia wewe huwa unasema umeokoka, sasa wenzio
wanaangalia watu wanafanya mapenzi.
Kweli nilifanikiwa kuangalia siku moja kwa muda mrefu maana kaka
alikuwa nazo nyingi sana, na sikuishia kuangalia tu bali nilijikuta kila
nikiangalia najichezea sehemu za siri mpaka nikafika mshindo na huo ndio
ukawa mwanzo wa maisha ya uraibu [addiction] wa kutazama picha za
Mara zote mtu akiokoka kweli hawezi kufurahia kuishi kwenye uchafu wa
ngono, maana dhamiri yake ni hai na ina mhukumu.
PORNOGRAFIA NI NINI?
Neno pornografia linatoka kwenye maneno mawili ya kigiriki:
Mara nyingi jambo hili uwakuta vijana walio katika umri wa balehe. Na
wengine walijikuta wananasa baada ya kushawishika na vijana wa umri
wao [peer pressure] kuingia kwenye utazamaji wa picha za ngono.
Kuna watu wengi wameingia kwenye uraibu huu kwa sababu ya msongo
wa mawazo au kukosa utoshelevu wa kihisia. Mabinti/vijana wengi baada
ya kukosa upendo halisi wa wazazi wao au kwa watu walio tegemea
kupata faraja kwao na ikatengeneza maumivu ya moyo /kihisia, na hii
imefanya watu wengi kuingia kwenye uraibu wa pombe, madawa ya
kulevya na wengine kujichua na kutazama picha za ngono.
Upweke [loniliness]
Hisia za kingono kwa mtu sio dhambi, tatizo linakuja pale ambapo hisia
zinaanza kukuendesha [nimeandika vizuri kwenye kitabu, namna ya
kutawala hisia za kimapenzi kabla ya ndoa]
“An idle mind, they say, is the devil’s workshop” Kuna watu walijikuta
wanapata mawazo ya kutazama huu uchafu kwa sababu ya kukaa muda
mwingi bila kuwa na jambo la maana, shetani akapenyeza wazo tu la
kupekua katika mtandao na wakajikuta wamenasa jumla kwenye huu
uraibu wenye sumu ndani yake.
Nadhani umewahi kusikia mtu anajinasibu kuwa yeye wala sio mzinzi ila
starehe yake ni pombe tu, na wengine hudai starehe yao ni kutazama
picha za ngono.
“Pornography can only bring you pressure, not pleasure. Porn will cause you to
burn and boil in the flesh. And, many times, the pressure from porn leads to
self-destruction. Pornography puts people’s emotion and body under pressure”
Kuna watu wengi sana [hadi kwenye ndoa] wanao dai kuwa wanaangalia
pornografia ili kujifunza namna ya kuwaridhisha wenzi wao. Bahati mbaya
sana huwa hawajiulizi mwanzilishi wa wazo la porno ni nani?
Je hao wanao cheza porno nani aliwafundisha hizo style? Kama porno ni
kitu cha kawaida unadhani mtu ana akili zake timamu anaweza kuwa tayari
kushiriki tendo la ndoa huku akiwa ana rekodiwa na watu dunia nzima
wamtazame? Wewe unaweza kufanya hivyo?
Lakini pia Mungu ameweka hekima kwa walimu mbalimbali waliojaa Roho
Mtakatifu, wanaoweza kufundisha jambo hili kwa usafi na utakatifu hasa
Kuna watu walianza kwa utashi wao wenyewe kutazama porno ila baada
ya muda hawakuwa na uwezo tena wa kuhitawala miili yao,
wanaendeshwa na pepo wa porno na zinaa kwenye uchafu huu nje ya
maamuzi yao.
Moja kati ya eneo ambalo lina athirika moja kwa moja kwa utazamaji wa
porno ni eneo la nafsi hasahasa hisia na akili. Kama dhambi zingine za
zinaa zinazo haribu nafsi pia porno ina madhara makubwa sana kwenye
akili ya muhusika.
Mara nyingi watu wanao tazama picha za ngono, ili kushibisha tamaa ya
ngono iliyo inuka uishia kujichua. Tutaangazia kwa undani kuhusu kujichua
kwenye kurasa zinazofuata.
PUNYETO NI NINI?
Baadhi ya maelezo nimechukua kwenye kitabu cha mtumishi wa Mungu
brother evarist koba "ushindi dhidi ya punyeto" nashauri kila kijana
[na kila mtu akisome] na ikiwezekana watokee watu wanaoweza kukilipia
na ku-print na kukisambaza bure mashuleni, vyuoni, makanisani na kila
eneo, ni moja ya kitabu kizuri sana kwa habari ya kuvuka jumla kwenye
shimo la kujichua/punyeto.
Punyeto/puli/kujilipua/kujichua/kujihudumia/kujimaliza/kujirid
hisha [masterbation] Ni kitendo cha mtu kujichezea kimahaba huku
akivuta hisia za mapenzi kwa mtu ambaye yupo mbali naye hadi
anapomaliza haja zake.
Ndivyo ilivyo pia ufalme wa giza, jini mahaba [spiritual husband or wife]
likitaka kushiriki tendo la ndoa linamvaa na kumuendesha mtu kwa kumpa
Usikubali sasa kuwa mjinga [mtu aliyekosa maarifa] ukiona kuna wazo
linakuja la kutazama picha za uchi au kujichua, sasa unajua kabisa kuna
kiumbe cha rohoni kinataka kutumia mwili wangu kufanya mapenzi, fanya
vita na pepo aliye nyuma ya hilo wazo mpaka atokomee na akuache jumla.
lakini kwa kizazi hiki hali ni hatari sana mpaka kwa wadada nao
wamedumbukia na kuzama kabisa kwenye wimbi hili la kujichua na
kutazama picha za utupu...
Sasa mtu akianza kutazama picha za utupu kuna majira atajikuta anaanza
kuvutiwa na za usagaji [au ushoga] na matokeo yake anavaliwa na roho
ya usagaji na ataanza kutamani kujaribu kile ambacho amekiona kwenye
videos na hii ndio maana baadhi ya shule [na vyuoni] kuna usagaji na
ushoga sana.
Ndio maana sio ajabu sana kuona mtu ambaye yupo addicted na
pornography au kujichua kukwambia kuwa mara kwa mara anaota ana
zini na watu mbalimbali ndotoni na kuna wengine wanaota
wanafungishwa ndoa bahari, wengine wanaota wapo bahari ni mamalkia
na wana watoto wana nyonyesha kabisa.
baada ya kumfungua hata kama aangalii tena anaweza jikuta anaota mara
kadhaa akiwa pengine anatazama picha za ngono au anazini.
(Wala msifuate kanuni za dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia
zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza,
na ukamilifu. (Warumi 12:1)
Kama hakuna mtu wa kuwafundisha then uhitaji watu walio jaa pepo
wachafu wakufundishe namna ya kukutana na mke/mme wako.
Unaweza kuigiza mbele za watu wasio yaona maisha yako ya sirini kuwa
uko vizuri na Mungu lakini uwezi idanganya nafsi yako na moyo wako
kujua kuwa ukinaswa na pepo la zinaa unapoteza kabisa hofu ya Mungu
na unagundua hauna ukaribu na Mungu kama ambavyo ulikuwa ujajiingiza
kwenye huo uchafu.
Dawa pekee hapo sio kuwaigizia watu kujifanya upo vizuri na Mungu,
wakati umekufa lazima ukubali kurudi upya na kuanza na Bwana na kuitia
huruma na rehema zake zikutoe jumla.
“Taa ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote
utakuwa na nuru. Lakini jicho lako likiwa bovu, mwili wako wote utakuwa
na giza. Basi ile nuru iliyomo ndani yako ikiwa giza; si giza hilo” (Mathayo
6:22-23 Biblia Takatifu)
Kuna mtu anaweza kuwa ameanza kujichua tokea akiwa ana umri mdogo
na amejichua kwa muda mrefu sana pamoja na kutazama picha za ngono,
then Mungu akamsaidia kutoka jumla hapo, mashaka yake yakawa je
nitawezaje kuyaepuka madhara yote yatokanayo na kujichua kwa kipindi
chote hicho?
Kwa hiyo bado lipo tumaini kwa yeyote ambaye amedhamiria kutoka
jumla na kuwa chombo cha Bwana pia kwa ajili ya kuwatoa wengi kwenye
mashimo hayo na kuishi maisha ya ushuhuda kwa ajili ya Bwana
Mtu amefunguliwa lakini bado yeye mwenyewe ni kama ana subiria ni lini
ataanguka tena na shetani anakuwa anamletea mawazo kila mara asipo
yapinga kwa neno la Mungu basi anaanguka tena.
Tuko kwenye kizazi cha ajabu, yani mtu anasema pastor mimi nahitaji
Mungu anisaidie kutoka kwenye kujichua ila hataki kuokoka na anataka
aendelee na maisha yake kama ya zamani. Haupo makini Mimi huwa
nawaambia ukweli huko ni sawa na kujitekenya halafu unacheka
mwenyewe tena, kwa sababu kama nikikutoa pepo sahivi na ukarudi
kwenye maisha yako ya uchafu ya zamani pepo litarudi na hali yako
itakuwa mbaya.
Sasa watu wengi wanataka Yesu awasaidie kutoka hapo tu, maisha
mengine wamuachie. Unautani! nakuhakikishia baada ya muda utarudi
tena, mpaka siku ukiamua kutoka moyoni kuwa unahitaji maisha yako
yaongozwe na Yesu maisha yako yote yaliyo bakia kwa kumaanisha ndipo
utakuwa kweli salama.
Bwana YESU kwa akili zangu timamu nautoa mwili wangu kama sadaka
na dhabihu kwenye madhabahu ya maombi na neno, uchafu wa ngono
hautatawala kanisa mwili wangu
“Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili
yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo
ibada yenu yenye maana” (Warumi 12:1 Biblia Takatifu)
USHUHUDA #02
Chanzo cha kuingia kwenye huo uraibu ni baada ya kaka yangu mmoja
kutembelea nyumbani na nlipochukua simu yake nikaenda sehemu ya
video nikakuta video za Ngono na nlipozitazama tu kuna roho iliniingia.
Mwaka huohuo nlipewa simu na wazazi japo ilikuwa ya buton lakini
iliweza kusearch Google na kuingia Facebook.
Mwaka 2021 baada ya kumaliza kidato cha 6 nlianza nlianza kuona kama
ule msukumo wakutazama picha unarudi na safari hii uliambatana na
tamaa Kali ya macho zaidi nlipofika chuoni mwaka huohuo. Lakini
namshukuru Mungu alinikutanisha na Baba Pst Eskaka Chaula mwaka
2022 na nikatoka jumla kwenye huo uraibu. Kwahiyo kama Bwana YESU
alinitoa mimi nawewe anaenda kukutoa
USHUHUDA #03
BWANA YESU asifiwe naitwa M.l, nasoma chuo kikuu cha Dodoma
UDOM mimi kwa mara ya kwanza kabisa nilitazama picha za uchi ningali
mdogo mno nakumbuka nikama 2007 baada yahapo nilijikuta nikiwaka
tamaa na kwakuwa nyumbani tulikuwa wafugaji basi hali hii ilinipelekea
kubaka ng'ombe, kuku na mbuzi ningali kijana mdogo sana.
Namshukru sana Mungu mwishoni mwa mwezi wa pili mwaka huu 2024
nikiwaka kwenye maombi Roho Mtakatifu aliniongoza kuomba maombi
ya rehema nikimuomba Mungu anipe tu nafasi ya mwisho, kwakweli
namshangaa sana Mungu ameniokoa cha ajabu baada ya siku mbili hivi
kuna mwenzangu tunaishi naye chumba kimoja akaanza kutazama picha
za ngono chumbani tena hadharani kwakutumia PC yake ndipo nilipo
mkemea kwa hasira. Naomba Mungu azidi kunipigania na nimechoka
kutumikishwa na shetani natamani kumtumikia Mungu kwa amani kabisa,
Mungu anisaide.
KUHUSU MWANDISHI
Kama umeguswa na kuvushwa mahali kwa kupitia kitabu hiki karibu kwa
ushuhuda au sadaka kwa Tigopesa [+255(0)718578313, Eskaka Chaula],
lakini pia kujifunza neon la Mungu kuhusu kila eneo la maisha nifatilie
kupitia mitandao ya kijamii yote, Facebook, Instagram, Telegram, TikTok
na YouTube account zote kwa jina moja la Pastor Eskaka Chaula.