You are on page 1of 2

MAMBO 10 KUHUSU HUDUMA

8. HUDUMA HAIWEZEKANI BILA UJUZI WA UHAKIKA WA KUMSIKIA MUNGU NA KUPATA SIRI KATIKA
NENO ZA KUGEUZA MAISHA YA WATU

Moja kati ya vitu nilisema kwenye mfululizo wa somo hili, nilisema HUDUMA NI MBIO
NDEFU (MARATHON) na sio MBIO FUPI (RELAY)!
Kila mtu anaweza kuanza huduma, na watu wakaona anacho kitu cha kuwafaa na
wakamkusanyikia, LAKINI WATU KUBAKI KWAKO NA KULETANA KWA WINGI KWAKO NI LAZIMA
WAJIRIDHISHE UNAYO MANENO YA UZIMA!

Petro na wanafunzi wenzie walibaki na Yesu wakati baadhi ya makutano wanaondoka, na


baadae huyu Petro na hao waliobaki WALIENDELEZA HUDUMA YA YESU MPAKA IMETUFIKIA
TUNAKIMBIA NAYO NA TUTAIRITHISHA KWA WENGINE kwa sababu moja kuu, Petro alisema, "
TWENDE KWA NANI?, WEWE UNAYO MANENO YA UZIMA WA MILELE"

Yohana 6
67 Basi Yesu akawaambia wale Thenashara, Je! Ninyi nanyi mwataka kuondoka?

68 Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima
wa milele.

Maana yake, ni kwamba

• Hatuwezi kuondoka kwako kwa sababu AINA YA MANENO YA UZIMA tunayopata kwako,
HATUWEZI KUYAPATA HUDUMA YOYOTE NA KWA MHUDUMU YEYOTE

• Twende kwa nani? Maana yake ni kwamba KAMA YESU ASINGEKUWA NA NENO LISILOPATIKANA
KOKOTE, INGEKUWA RAHISI HAWA JAMAA KUHAMIA KWA MWINGINE (MHUDUMU MWINGINE, HUDUMA,
KANISA JINGINE)! Lakini kwa nyakati zao, WALIGUNDUA MUNGU AMEWAPENDELEA KUWAPA YESU
MWENYE NENO LISILOPATIKANA KWA YEYOTE KWINGINE!

Kama mhudumu wa Injili na hasa mchungaji wa kundi;

• Unapaswa kuwa na Neno lako maalum (ujumbe toka kwa BWANA) ambalo washirika hata
wakitoka kwako wakajaribu kuzunguka zunguka kwingine, WAGUNDUE WANAMISS KITU CHAKO
KISICHO KWA YEYOTE

Kama hauna "Maneno ya uzima wa milele" yasiyopatikana kwa yeyote mwingine, UWE NA
UHAKIKA WATU WATAKUHAMA NA KUHAMIA KWA WENYE NENO USILOKUWA NALO!

• Hili Neno la uzima wa milele haulikopi kwa mchungaji au huduma fulani, linatokana
na AINA YA MAONO ULIYONAYO KAMA HUDUMA!
Mfano kama unakumbuka kwenye sehemu mojawapo ya somo, nilizungumzia MAONO KWENYE
HUDUMA na nikajitolea mfano Mimi Askofu Dickson Cornel Kabigumila na ABC GLOBAL,
na kutokea kwenye ujumbe ule UTAONA ILI NIWEZE KUMTEMTENGENEZEA MUNGU WATU WA MOTO,
WATAKATIFU, WENYE KUGUSA NA KUATHIRI MATAIFA AU DUNIA YAO, lazima nitakuwa na
MANENO YA UZIMA KWENYE MAENEO YA;
•Utakatifu (Holiness)
•Ushindi dhidi ya dhambi (Overcoming sin)
•Ukuu (greatness)
•Mguso (Impact)
•Kanuni zinazotawala maisha (Principles that govern life)
•Kutengeneza watu wakuu na siri za watu wakuu (Raising great men and women; The
secrets of greatness)
•Kujitafuta na kuvumbua ulivyobeba ambavyo dunia inavihitaji (Self discovery)
•Ufuasi na uongozi (Leadership and followership)
•Maarifa, ufahamu na hekima (Knowledge, Understanding and Wisdom)
• Ukiroho na nafasi ya kiroho kwenye ustawi au kufeli kwa mtu (Spirituality and
Spiritual realities)
• Maono (Vision)
Na mengine mengi yanayolenga KUTIMIZA AINA YA HUDUMA NILIYOITIWA!

Kama mhudumu wa injili una uhitaji mkubwa kuyaelewa maono ya huduma uliyopewa na
Mungu kwa kina, na kisha ukae sirini kuchimba Neno mno, vitabu vya watumishi wa
Mungu hasa kwenye eneo lako la wito, na yote yanayoweza kukuongezea ufanisi kwenye
huduma na wito wako, ILI UKITOKEA WATU WA MUNGU WALISHWE KWA UFAHAMU NA MAARIFA NA
SI MAHUBIRI MATUPU!

Yeremia 3
15 nami nitawapa ninyi wachungaji wanipendezao moyo wangu, watakaowalisha kwa
maarifa na fahamu.

Tutaendelea kwenye post ijayo,


Askofu Dickson Cornel Kabigumila
ABC GLOBAL DUNIANI
01.12.2023

NB: KAMA UKO DAR ES SALAAM TUKUTANE MKESHA HUU WA DARE TO BE DANIEL, UNAFANYIKIA
ST. ALBAN CATHEDRAL, POSTA PALE OPPOSITE NA HOLIDAY INN HOTEL

You might also like