KUJITAMBUA NI NINI ? Neno KUJITAMBUA linatokana na neno TAMBUA lenye
maana ya KUJUA UKWELI WA KITU FULANI KWA KINA , kwahiyo KUJITAMBUA ni hali ya KUJIJUA VILIVYO KWA KINA . Ingawa watu wengi sana WANAISHI lakini HAWAJITAMBUI KWA KINA. HUWEZI kuwa MJASIRIAMALI mwenye MAFANIKIO bila ya KUJITAMBUA. Wakati huo huo HUWEZI KUJITAMBUA BILA KUMJUA MUNGU. JIULIZE MASWALI HAYA :-- {1}. Kwanini Ulizaliwa ? {2}.Umekuja hapa duniani kufanya nini ? {3}.Umetokea wapi na unaenda wapi ? AMINI USIAMINI MATAJIRI ( Watu wenye MAFANIKIO ) duniani kote wanajua kwanini walizaliwa ? Kwa nini Wanaishi lakini pia wanajua wanakokwenda. Kwahiyo ili UFANIKIWE ni lazima UJUE UMETOKA WAPI ? NA UNAKWENDA WAPI ? NA KWANINI UPO HAPA DUNIANI ? Katika MAISHA YA MAFANIKIO ni lazima SIO OMBI kuwa ili Uweze KUFANIKIWA katika kiwango kikubwa ni lazima uwe umeyapata majibu ya maswali ya hapo ju
Maama, faida na hasara ya kutojitambua
#KUJITAMBUA NI SOMO LISILOJULIKANA KWA WENGI Karibu wana FB Kujitambua ni uelewa wa mtu binafsi kungamua yeye ni nani,anapaswa kufanya nini, kwa sababu ipi.lini na katka muktadha upi. Elimu hii ya kujitambua ni adimu mno! Kwani hujikita ndani ya nafsi ya mtu na kumfanya kuonekana mwenye busara na hekima katika uongeaji ,kimaamuzi na kimatendo pia bila kufanya hivyo kiunafiki.Pia wapo ambao hujitia ukiziwi,ububu na wengine kuwa waropokaji ili waonekane wenye elimu ya kujitambua kumbe hamna kabisa hata chembe ya kujitambua. Na si wasomi wote hapa duniani na Tanzania ikiwemo ambao hubahatika kuipata elimu ya kujitambua pamoja na kwamba husoma vitabu mbalimbali ,sehemu mbalimbali nchi moja na nyingine na kupata vyeti rukuki (stashada,shahada,shahada ya udhamili n.k) lakini bado hushindwa kupata elimu ya kijitambua ndio maana baadhi ya watu hutenda matendo ambayo hayaendani na unavyowaona na unavyowategemea wafanye . Mfano 1. -Humu FB kuna baadhi ya watu bado hawana uelewa binafsiri matokeo yake huchangia hoja kwa maslahi binafsi na si kwa manufaa ya jamii na wengine huchangia kwa kutumia matusi kwa kudhani wanawakomoa watu ambao hata hawawafahamu wala hawajawahi kuwaona na hawatakaa wawaone! Mfano2 Baadhi ya mabosi kutokana na kutojimbua hupenda kumiliki wafanyakazi wote(hasa wa kike) waliowaajili na kuwatumia kingono bila hata kufikiri faida na hasara na sababu ya kufanya hivyo na ukioji utaambiwa mapenzi ni upofu wakati wanaotenda vioja hivyo ndio hujitia upofu. Pia waweza kuangalia baadhi ya watu wanachosema sicho wanachokifanya mfano baadhi ya wanaopinga imani za kishirikina ndio watambikaji maarufu! Baadhi ya watungaji sheria ndio wavunjaji mfano mtu anaua makusudi wala sheria haichukui mkondo wake na mwingine akiiba kuku hata kama ni mmoja anafungwa miaka saba (sheria ya wizi wa mifugo).n.k FAIDA KUU YA KUJITAMBUA. -Kila akifanyacho mtu anayejitambua hulenga kuchochea na kuleta maendeleo katika jamii husika. Ø Kuwa jasiri Au msimamo dhabiti kwa analoamini ni sahihi bila kuyumbishwa na mtu yoyote. Ø Kufikia malengo chanya. Ø Huwa kioo cha jamii (unakuwa barua isomwayo na kila mtu katika jamii). Ø Kutenda matendo mema (kutetea haki za wanyonge,kupinga ufisadi,n.k) katika jamii Ø Hutambua nafasi aliyonayo na jamii humuheshimu bila kushinikizwa mfano utamskia mtu anamwambia mwenzake “unajua unaongea na mheshiwa?wengine hulalamika eti pamoja na kutoniita mh, n.k Ø Mtu huyu huwa sio tegemezi katika jamii.. Ø Huwa ni mtu asiyekuwa na makuu, huwa na matumizi mazuri ya rasliamali.mfano raslimali watu,ardhi,pesa n.k Ø Huwa ni mtu wa watu. Ø Huwa mbunifu (Creative) husoma nyakati. Ø Huwa anatoa suruhu na sio kulalamika au kulalamikiwa na yeye kuanza kulaumu na huwa hakati tamaa mpaka siku ya kufa n.k MADHARA YA KUTOJITAMBUA -Hathari ni kinyume cha faida tajwa na mjumuisho wa hili; -Kutojitambua huzorotesha maendeleo kwani mlengwa hufanya mambo hovyo hovyo).Na hii hupelekea miigogoro kuongezeka katika jamii (Mtu asiyejitambua huwa chanzo cha migogoro na kero kubwa katika jamii).n.k HITIMISHO. Cha kushangaza watu wasiojitambua huwa hawataki msaada wa kuwatoa katika utumwa wa kutojitambua ndio maana huwa wakali wa kutokubaliana na mkakati wa anayetaka kuwasaidia ,huku wengi wakibeza na kuweka mbele vyeo,elimu,umri,pesa,uzuri,umb o n.k japo wengine hukimbilia kujitetea kuwa binadamu hajakamilika wakati hawako tayari kukamilishwa na wale wenye kujitambua.Hivyo ni vyema mtu akibahatika kujigundua kuwa ana dalili za kutojitambua yambidi kujitafakari na kuanza kuchukua taratibu taratibu ili arudi kwenye mstari