You are on page 1of 4

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFSI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA MAANDALIZI KABLA YA MTIHANI WA TAIFA


SHULE ZA VIPAJI MAALUMU
KIDATO CHA SITA
KISWAHILI 1
121/1

MUDA: SAA 3 Jumanne 27-March-2024 Asubuhi

MAELEKEZO
1. Karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali nane (08)
2. Jibu maswali yote ya sehemu A na maswali matatu (3) kutoka sehemu B.
Swali la Tano (05) ni la lazima.
3. Zingatia maagizo ya kila sehemu na ya kila swali.
4. Simu za mikononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba
cha mtihani.
5. Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu cha kujibia.

1
SEHEMU A (alama 40)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
1. Soma kifungu cha habari kifuatacho kwa makini kisha jibu kwa usahihi maswali
yanayofuata.
Baadhi ya wananchi walianza kuamini kuwa huo ndio ulikuwa mtindo wa maisha, wakaanza
kujivunia na kufurahia vitendo vyao vya uovu. Wakaanza kudhihaki uadilifu na wema.
Wanawake vimulimuli wakaanza kuvaa mavazi yasiyo nadhifu bila kimuyemuye. Wakaanza
kukosa huruma na kutamani honoraria kwa kila kazi wanayopewa kuitekeleza, iwe kwa
watoto yatima au kanisani. Ubinafsi umeshamiri, wanawake walioteuliwa na Mungu ili wazae
na kulea watoto wamekuwa ndio watu wasio na huruma: mitaroni, makorongoni, mtoni na
vichakani vichanga kutupa.

Ufisadi ukajiheshimisha kwa mwanamke na kuufafanya kuwa kifufumkunye ndani ya jamii.


Kiumbe ambaye kwaye huonekana ni mnyenyekevu na farisi machoni pa watu. Mshauri na
kiongozi wa familia, hidi katika maamuzi mbalimbali. Uchu wa madaraka ukatawala ofisini
na sehemu mbalimbali hata kusahau mqjukumu aliyopewa na Mungu ya kuwa mshauri na
msaidizi mkuu wa Adam. Kuvalia junju kichwani wakati wote huku akijinasibu kuwa yeye ni
kimulimuli wa mjini.
Woga wa kuficha wala rushwa ukaigubika jinsia hii. Rushwa ikahamia kwao,
wamenyamazishwa kwa kipande cha neno "Haki sawa" kumbe hizo ni chenga za jinsia ya
kiume. Mkweche wa mawazo ya jinsia ya kiume umekuwa ukiwala taratibu taratibu huku
wakipoteza utu bila mjibizo. Ni bora wakaondokana na maasia hayo.
Ujasiri wa kudai haki zao ukafifia na kuanza kudai haki za nyongeza. Haki za kuzaa salama
na kulea mtoto, kumwandalia hababi wake, haki ya kuwa mshauri wa familia na haki ya
kutoongozwa na viongozi wa ovyo ikapuuzwa. Uchu wa madaraka umewamea na
kusababisha kundi hili muhimu kuingia katika makundi yasiyo aminika na jamii.
Mahakamani enzi hizo ilikuwa haiwezekani kwa mwanamke kuwa na shitaka lolote lakini
sasa hivi imekuwa ni desturi. Mara nataka talaka hanipi, hatunzi watoto, kamwagia mtoto uji
wa moto mwili mzima kwa kosa la kuiba shilingi 200 na kadhalika. Kwcli chenga za jinsia
ya kiume ni nzito. Huko ni kupoteza muda, mwanamke hakuletwa duniani kulalamika.
Mwanamke ameletwa duniani kuunganisha palipokatika. Siku hizi mambo mengi kila pishi
mpikalo ni mbatata haliliki mithili ya shubiri.

Ufisadi kwa mwanamké hufanyä yasiyowezekäna, hualalisha haramu na kuharamisha halali.


Huingilia harakati za uchumi na kuyakaba na kuyabana maendeleo. Mwanamke maridadi
huchukia ufisadi kwani ukikithiri huwasamehe matajiri kulipa kodi na makabwela ndio
hukandamizwa zaidi. Huwafanya matajiri kutoguswa na sheria kutokana na kwamba ufisadi
ni adui wa haki. Ufisadi husababisha maghala yaliyofurika ukiritimba na usipong'olewa
bila huruma hakuna tumaini la aina yoyote ya maendeleo isipokuwa kurudi nyuma.
Ikumbukwe kuwa maendeleo ni ya watu wote na si ya watu wa chache matajiri tu.

2
Maswali
a) Andika kichwa cha habari kisichozidi maneno matano.
b) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyolumika katika habari uliyosoma.
i. Vimulimuli
ii. Kimuyemuye
iii. Honoraria
iv. Akajinasibu
v. Ukiritimba

c) Kutokana na habari uliyosoma, taja madhara matatu ya ufisadi.


d) Mwandishi anamaanisha nini katika aya ya sita

2. Kwa kutumia mifano kutoka katika lugha ya kiswahili, toa hoja tano kubainisha tofauti
kati ya mofimu na silabi.

3. Fafanua kwa mifano maridhawa dhana zifuatazo kama zinavyotumika katika lugha ya
kiswahili
i. Umilisi wa lugha
ii. Chagizo
iii. Uambishaji wa kisarufi
iv. O-rejeshi
v. Kitenzi kishirikishi

4. Eleza kwa mifano kuntu mambo matano (5) yanayoweza kupelekea mtu kuwa mlumbi
wa lugha katika jamii.

3
SEHEMU B (ALAMA 60)
Jibu maswali matatu (03) kutoka sehemu hii. Swali la tano (05) ni la lazima.
5. Ukiwa kama mtaalamu mbobevu wa taaluma ya tafsiri na ukalimani eleza kwa mifano
kuntu mbinu sita (6) za kutathmini matini.

6. Wewe kama mdau wa elimu, andika insha yenye maneno yasiyopungua 350 na
yasiyozidi 400 kuhusu umuhimu wa Mtaala Mpya wa Elimu ambao jamii itanufaika
endapo utatekelezwa kikamilifu nchini Tanzania kuanzia mwaka 2024. Toa hoja tano
(5).

7. Kwa kutumia mifano kutoka katika Lugha ya Kiswahili, eleza ni kwa namna gani lugha
moja inaweza kusababisha kuibuka kwa utofauti katika lugha hiyo hiyo miongoni mwa
watumiaji. Tumia hoja sita (6) zenye mifano madhubuti.

8. Waarabu walikuwa na mchango mkubwa katika kukuza lugha ya Kiswahili nchini


Tanganyika kabla ya uhuru ila kwa kiasi kikubwa wanalaumiwa na wazawa kwa
kudumaza lugha ya Kiswahili. Jadili madai hayo kwa kutoa hoja sita (6) zenye mashiko.

You might also like