You are on page 1of 5

MTIHANI WA USHIRIKIANO USIO NA MIPAKA

KIDATO CHA NNE

015 ELIMU YA DINI YA KIISLAMU

(Kwa Watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni)

MUDA: SAA 3 Ijumaa, 21 Julai 2023 mchana

Maelekezo

1. Mtihani huu una sehemu tatu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na moja (11).
2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali mawili (2) kutoka sehemu C.
3. Hakikisha unasoma maelekezo ya kila swali kwa umakini.
4. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
5. Hakikisha unaandika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha
kujibia.

Page 1 of 5
SEHEMU A (Alama 16)
Jibu maswali yote katika sehemu hii

1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x) kisha andika herufi ya jibu hilo
kwenye kijitabu chako cha kujibia.

(i).Umetakiwa kueleza aina mbili za elimu zinazokubalika kwa mujibu wa uislamu. Ni


aina zipi mbili za elimu utakazozitumia kuwasilisha mada uliyotakiwa kueleza?

A. Elimu dunia na Elimu akhera


B. Elimu ya muongozo na Elimu ya mazingira
C. Elimu ya Dini na elimu dunia
D. Elimu ya faradhi na elimu ya sunnah
E. Elimu ya ibada maalum na Elimu ya ibada mbalimbali.

(ii).Firauni katika Maisha yake alikanusha kuwepo kwa MwenyeziMungu lakini siku ile
Allah (s.w) anamzamisha baharini alikiri kumjua Mwenyezi Mungu. Ni jambo gani
lilomfanya kumtabua Allah (s.w) wakati huo?

A. Malaika wa kutoa roho alimpa mawaidha


B. Muda ule aliona alama za kuwepo Allah (sw)
C. Fitra -hisia za kumjua Allah alizopandikizwa na Allah
D. Ile hali ya sakaratul mauti aliyokuwa nayo
E. Ile hali ya mateso aliyoipata wakati anaangamia.

(iii). Watu wa kaumu ya Nabii Lut waliangamizwa kwa udongo wa motoni kutokana na
maovu yao. Ni madhambi gani utakayoyalenga kuwaonya watu wako ili wasijepata
adhabu kali kama ilivyokuwa kwa watu wa Lut?

A. Zinaa na kujihusisha na kamari


B. Mauaji na kupunja vipimo
C. Kuingiliana kinyume cha maumbile na ujambazi
D. Kupunja vipimo na kuzika watoto wa kike wakiwa hai
E. Kunyonya wanyonge na kumshirikisha Allah (s.w)

(iv). Juma ni kijana ambaye amejitenga na jamii kwa ajili ya kufanya ibada na amesema
hataoa na muda mwingi atafunga na anajitenga na mambo haya ya maendeleo ya
dunia ili apate pepo. Kwa mujibu wa uislamu yeye tunamuweka katika kundi gani?

A. Kundi la Wapagani B. Kundi la Makafiri


C. Kundi la washirikina D. Kundi la watawa.
E. Kundi la wacha Mungu

(v).Babu yako ni mgonjwa na imefika zamu yako kukaa naye, ghafla amekata roho. Ni
mambo gani kati ya haya utakayomfanyia mara baada ya kutokea hali hiyo?

Page 2 of 5
A. Kufumba mdomo, macho na kumnyoosha viungo vya mwili.
B. Kumpa maji ya kunywa na kumuogesha
C. Kumtamkisha shahada na kumtawadhisha
D. Kumpaka manukato, kuvukiza ubani na kumpa maji ya kunywa
E. Kumlaza ubavu kuelekea qibla na kumtamkisha Laillaha ila lla.

(vi). Kaku alidai kuwa anaweza kuishi akiwa muislamu kamili kwa kufuata Qur’an tu bila
sunnah ya Mtume (s.a.w). Je, ni kwa nini dai hili la Kaku sio sahihi?

A. Mtume (s.a.w) ndiye aliyeitafsiri Qur’an kivitendo.


B. Hakuna tofauti kati ya Sunnah na Qur’an
C. Qur’an na sunna vyote ni wahyi.
D. Tabia ya Mtume (s.a.w) ilikuwa Qur’an.
E. Qura’n ndio uislamu wenyewe

(vii) Ni ipi faida unayoipata katika Maisha yako ya kila siku unapotekeleza nguzo tano za
kiislamu kikamilfu?

A. Ndio utekelezaji kamili wa uislamu katika maisha ya kila siku


B. Nguzo tano ni kifutio cha madhambi ya kila siku
C. Nguzo tano za uislamu hutusaidia kufikia lengo la kuumbwa kwetu kirahisi.
D. Nguzo tano za uislamu ndio uislamu wenyewe.
E. Nguzo tano za uislamu humfanya mtu kupata thawab na kuingia peponi.

(viii) “Bali hii ni Qur’an tukufu iliyotolewa katika Lawhi Mmahfuudh (huo ubao
uliohifadhiwa)…” (85:21-22). Baada ya hatua hii ni hatua gani ilifuata katika
ushukaji wa Qur’an?

A. Ilishuka kidogo kidogo kwa Mtume (s.a.w).


B. Ilishuka yote mpaka uwingu wa kwanza.
C. Ilishuka kwa Jibril (a.s) kabla ya Mtume (s.a.w)
D. Ilihifadhiwa na maswahaba wa Mtume (s.a.w)
E. Iliandikwa katika karatasi, magome, mawe na ngozi.

(ix). Mzee Said alimuusia mwanae kutoa sadaka kwa siri. Kwa nini Mzee Said alimuusia
mwanae hivyo?

A. Ili makafiri wasijue.


B. Ili aepukane na ria.
C. Ili pasitokee unyang’anyi .
D. Allah (s w) ndivyo anavyopenda.
E. Ili watu wasimjue kuwa yeye ni tajiri

(x) Kabla ya kuzaliwa mtume (s.a.w) hali ya maadili katika bara Arabu ilikuwa sio ya
kutamanika. Ni tabia zipi kwa sasa zinaweza kutumika kuelezea hali hizo?

Page 3 of 5
A. Kukithiri kwa kamari, ulevi na uzinifu
B. Uvaaji modo na kunyoa kiduku
C. Liwati na usagaji
D. Kusuka rasta na kuzika watoto wa kike hai
E. Kuvuta bangi na madawa ya kulevya

2. Oanisha aina za mazao kutoka orodha A na nisaab za mazao hayo kutoka orodha B kisha
uandike herufi ya jibu sahihi katika kijitabu chako cha kujibia.
ORODHA A ORODHA B
i. Mazao ya shambani A. Tola 7.5
ii. Dhahabu na vito B. Kilo 666
iii. Mali ya kuokotwa C. Thamani yoyote
iv. Ng’ombe D. Kilogram 66.6
v. Ngamia E. Arobaini
vi. Kondoo F. Thelathini
G. Watano
H. Ishirini

SEHEMU B (Alama 54)


Jibu maswali yote katika sehemu hii

3. Baada ya ndoa kufungishwa walii amekupa jukumu la kumuelimisha muoaji juu ya


wajibu wake kwa mke aliyemuoa. Bainisha majukumu matatu utakayotumia katika
kufafanua jukumu ulilopewa.

4. Makadiani wameitisha mhadhara mtaani kwenu na wanahubiri kuwa baada ya Mtume


(s.a.w) yupo mtume mwingine atakayekuja. Ni hoja zipi tatu utakazozijenga kufuta dhana
hiyo potofu?

5. Katika kuadhimisha siku ya Watoto duniani sheikh Jarufi alialikwa kueleza haki za
Watoto kwa mujibu wa uislamu. Ainisha haki zipi tatu ambazo ungemshauri Jarufi
kuzitumia katika kuwasilisha mada yake?

6. Umewakuta watu wasio waislam wakidai kuwa katika dini sheria hazina umuhimu wala
kazi yoyote. Tumia dondoo tatu kuwaonesha kuwa katika dini ya uislamu hilo sio sahihi.

7. “Mkataba wa hudaibya una mafunzo mengi ya namna ya kuishi na wasiokuwa waislamu


na huku unatekeleza jukumu la kusimamisha uislamu.” Thibitisha kauli hii kwa kutoa
mafunzo matatu kutoka katika mkataba huo.

Page 4 of 5
8. Kuna madai kuwa kuenea kwa uislamu Tanganyika na Afrika ya mashariki kwa ujumla
kulisaidiwa na biashara. Fafanua ukweli wa suala hili kwa dondoo tatu.

SEHEMU C (Alama 30)


Jibu maswali mawili tu katika sehemu hii

9. Utafiti uliofanyika katika jiji la Dar es Salaam umebaini kuwa wapo waislamu
wanaoswali swala tano lakini bado wanashiriki katika kufanya maovu mbalimbali. Toa
sababu nne zinazoweza kuwa sababu za hali hiyo kutokea.

10. Uandishi wa hadith za Mtume (s.a.w) ulipitiwa na vipindi vinne lakini katika kipindi cha
Mtume (s.a.w) uandishi ulikuwa mdogo sana au haukuwepo. Toa ufafanuzi uliopelekea
hali hiyo kutokea (dondoo nne)

11. Qur’an ilishushwa kwa Mtume (s.a.w) akiwa Makka na baadae Madina, hali ambayo
ilisababisha utofauti wa sura zilizoshushwa katika maeneo hayo. Onesha tofauti nne (4)

Page 5 of 5

You might also like