You are on page 1of 30

MAFUNDISHO YA TAMAA ZA UTAJIRI KIRAHISI

‘’Katika kufanikiwa lazima ushughulikie jambo moja kwa umakini na


kuhakikisha unalimaliza vizuri bila papala’’.

-Donald Trump

Duniani hakuna taifa lolote lililoendelea kirahisi. Usidanganyike na ukaingia katika


orodha ya wapumbavu wawazavyo hivyo. Nenda Amerika wakupe siri ya mafanikio
yao mpaka wakafika kwenye sayari ya venus wanasayansi wakaweka makazi na
kuishi huko. Nenda Amerika ushangae tu! Waliwezaje kuunda ndege zisizohitaji
rubani na zajipeleka tu automatikali. Nenda Japani uwaulize waliwezaje kuunda redio
za panasoniki na soni. Nenda uchina uwaulize basi hata njiti ya kusukutua meno kisha
kula kitoweo chako. Waulize wanyarwandwa wamewezaje kufikia maendeleo mpaka
hapo walipo, walifanya nini? Jibu sina. Tafuta wewe mwenyewe.

Nenda Taiwan waliwezaje kuunda Tablet Samsung galaxy table 4, Ipad, Trekta? Kwa
kulala? Waulize akina Padre Simon Liberio Muha wa Kigoma mwisho wa reli wa milima
mabonde kuinama na kuinuka Mabamba waliwezaje kuandika miswada Tisa ya Vitabu Tisa
wakiwa masomoni Segerea? Na sasa Kitabu hiki cha Mahangaiko kinachofanya
nitimize Vitabu kumi na tatu katika safari ya kuandika vitabu mia moja kabla sijafa
Mungu akinihurumia, akipenda nitimize ndoto hiyo. Penye nia pana njia. Mungu
anaweza yote. Kwa Mungu hakuna linaloshindikana, ili mradi lisipingane na utukufu
wake.

Muulize Padre Titus Amigu mmakonde amewezaje kuandika Vitabu zaidi ya 40 na


makala elfu na maelfu. Muulize Rais Mstaafu wa Marekani Bill Clinton aliwezaje
kusoma vitabu elfu thelathini kabla hajatimiza miaka thelathini ya umri wake. Muulize
Rais Mstaafu George Bush alivyofanikiwa kusoma vitabu 95 kuanzia mwishoni mwa
mwaka 2006 mpaka mwaka 2008 alipokuwa akijiandaa kumaliza kipindi chake cha
urais wa Amerika. Muulize Rais Obama muamerika mweusi mwenye asili ya wajaruo
wa Kenya aliwezaje kutoboa mpaka akaingia White House Washington (Ikulu). Unafikiri
alishinda Urais wa marekani kimchezomchezo? Aliitwa nyani, lakini hakukata tama.
Aliitwa sokwe lakini akasema katika kampeni zake huko Illinoia, Yes I can! Maana
yake Ndio Ninaweza!

Muulize Mwandishi Nguli wa Nigeria na Afrika na Dunia kwaujumla, Chinua Achebe


alifanikiwaje kuitwa Profesa. Kwa kulala? Muulize Chinua Achebe aliwezaje kuandika
vitabu mamia na Riwaya nyingi katika medani za Fasihi ya kiafrika. Kwa kulala?
Muulize Ngungi wa Thiong’o aliwezaje kutoboa maisha mpaka kuwa mwandishi
maarufu toka Kenya mpaka dunia yote inamtambua kwa vitabu vyake maarufu kama
Songs of Lawino, The River Between, This Time Tomorrow, Kwa maombi ya wachungaji
hewa? Au kwa kumwambia Mungu atende miujiza?

Waulize akina Mao Ze Dong wa uchina waliwezaje kuwa na maendeleo mpaka hivi sasa
kila baada ya hatua ya mguu utaona bidhaa za wachina zimetapakaa kama uyoga
duniani kote, huku Afrika imebaki kuwa dampo la wachina. Waulize watu wa Urusi
wamefanyaje mpaka wakawa bingwa katika tasinia ya utabibu. Waulize madaktari
bingwa wa India wamewezaje kuwa mbali sana katika mahesabu, uchumi, uandishi wa
vitabu na ubingwa uliobobea katika tasnia ya udaktari wa kutibu magonjwa
mbalimbali, kasoro ukimwi. Kila maendeleo yanaendana na ubunifu na jitihada za
makusudi katika kufikia lengo madhubuti.

Lengo madhubuti ndilo linalokufikisha kwenye tarajio lako. Mara nyingi matunda
tuyaonayo katika maisha yetu huwa ndio majibu ya haki za jitihada zetu za tangu
mwanzo. Henry David Thoreau anasema, “Mwisho wa siku tunafanikiwa pale
tulipolenga.’’ Hauwezi ukagonga pale ambapo haujalenga. Hauwezi kushuka baharini
huku usafiri wako ni wa ndege. Hauwezi kushuka stesheni (kituo cha gari moshi) huku
umesafiri kwa kutumia meli. Hauwezi kumsubiri abiria uwanja wa ndege huku
amesafiri kwa meli.

Siri ya mafanikio yoyote inaendana na kupambana. Unaweza kufanikiwa tu, kwa kuwa
mchapa kazi na sio kwa kuombewa pepo Au kwa kushinda kwenye masinagogi na
mahekalu. Hauwezi kufaulu kwa kushinda umeshika majuzu, koroani wala biblia bila
kuweka ubunifu maridhawa uliopambwa kwa sala za kila siku.

Lazima utambue kuwa maisha si kula sambusa tu au vitumbua tu bali kuna pilipili,
kuna kahawa dawa, kuna alovela n.k. Maisha si kwenda mbele tu, bali kuna kurudi
nyuma na kurudishwa nyuma na wenzako pia. Mafanikio katika maisha yako
hayapimwi na shahada zako wala magari yako mengi wala nyumba yako nzuri ila
kinacholeta maana ya mafanikio ni pale unapoishi maisha uliyopenda kuishi yaani
furaha na amani ya kweli kutoka moyoni. Usiishi maisha ya wengine itakula kwako. Pia,
usifanye kitu usichokipenda katika maisha yako.

“Hatuwezi kutengeneza historia katika maisha yetu bali, historia ndiyo inayotutengeneza.”
Aliyasema hayo Dr.Marthin Luther King Jr.
Ni lazima katika maisha yetu tuishi na ndoto zetu kubwakubwa. Ndoto zetu
kubwakubwa zitatufanya tuongeze bidii katika yote tunayotaka kuyafanya. Kamwe
usikubali ndoto zako zinyeshewe na zipotee. Pia Mwanaharakati Dr. Marthin Luther
King Jr. alisisitiza siri ya mafanikio ya kutimiza ndoto zako katika maisha yako.
Anasema, “Hakuna yeyote mwenye haki ya kutokomeza ndoto zako au kuzififisha ndoto zako.”
Siku zote katika maendeleo yako, usiogope figisufigisu za watu.

Mafanikio yako na kushindwa kwako kuko mikononi mwako. Mafanikio yako ni sasa.
Maendeleo yako ni sasa. Asiyetumia fursa za leo atashindwa pia kutumia fursa za maendeleo
za kesho, wahenga wa Afrika walifundisha hivyo katika methali za kiafrika. Siku zote
usichoke kufanya kazi zako hata kama zitakuumiza kwani wahenga katika falsafa za
kiafrika zinasema machozi yanayotililika usoni hayakufanyi uwe kipofu.

Maisha yetu ni kuchagua, kwamba kama unataka kwenda haraka nenda peke yako
huku ukitaka kwenda mbali nenda na wengi, waafrika tulisisitizwa na wahenga wetu.
Pia, lazima uso wa mwanume uwe na makovu. Mwanadamu anapaswa kukomaa na
maisha yake mwenyewe. Mwanadamu ni mabadiliko yenyewe. Mwanadamu ni
mabadiliko mwenyewe. Mwanadamu anapaswa kufanya mabadiliko mwenyewe.
Mwanadamu anapaswa alete mabadiliko mwenyewe asingoje yajilete au yaletwe na mwingine
alisema Barack Obama Rais wa marekani miaka ya 2008 -2012. Mwanadamu
mpambanaji lazima awe na makovu usoni, hiyo ni methali pia ya kiafrika.

Dini zote duniani zinasisitiza kufanya kazi. Dini ya Kiislamu inawaambia jamii ya
kiislamu kuwa kisha ibada zao hata ijumaa salati, waende kufanya kazi. Ni matumaini
yangu kuwa hayo ndiyo mafundisho ambayo mashekhe na maulamaa wanawasisitiza
waamini wa kiislamu. Uvivu ni dhambi hata mbele ya Mungu. Mungu hambariki
mvivu. Maisha ni ushujaa unaopaswa kuushinda. Maisha ni ushindi uyashinde. Maisha
ni chaguo sahihi chagua. Maisha ni mbio, kimbiza kijiti chako. Kamwe usikate tamaa,
kwani hata mayai kwa uvumilivu hutembea kwa miguu, ndio kuku. Mtu hupimwa na
kazi, akili, busara na ueledi wake. Yafanyie kazi hayo ili uyaishi na uone kama Mungu
hatamimina neema zake katika maisha yako.

Mhandisi anapochimba shimo ili apate maji kutoka kisimani lazima atoke jasho. Je,
naye anahitaji aombewe na wachungaji kanjanja kufanya hivyo? Mtoto anayejifunza
shuleni kwa utulivu na bidii kubwa na kisha kuwa wa kwanza darasani, naye anahitaji
unenaji wa lugha ili afaulu hivyo? Kwenye mbio za marathoni tunawaona kwa uzoefu
wakenya na waethiopia kidogo na waetria wakipeperusha bendera za kuwa washindi.
Je, nao wamefuzu kwa karismatiki isiyotulia.
Je, aliyefanikiwa kutengeneza roboti naye aliombewa. Aliyefanikiwa kuwa tajiri wa
dunia Bill Gate naye aliombewa ndipo akawa tajiri? Je, mapambio tu bila jitihada na
bidii tungeweza kupata Computer? Tungewezaje kupata Microsoft? Je, watu wetu
tuwasaidieje sasa? Wanaumwa nini? Wanaumwa uvivu, wanaumwa umasikini wa
mawazo? Wanaumwa umasikini na uchu wa utajiri bila kutoka jasho. Wanaumwa
mahangaiko ya njaa. Njaa imetoboa mifuko yetu. Ugumba nao usiseme. Utasa ndio
gumzo mitaani? Uuaji ndio hausemeki tena. Watu kuuana na kujiita watu
wasiojulikana, si serikali haiwajui wala wananchi nao hawawajui. Nani atamfunga
paka kengere. Yote haya ni mahangaiko katika maisha ya mwanadamu wa sasa?
Tukimbilie wapi? Tukimbilie kwa Yesu Kristo kwa njia ya sakramenti zake mbalimbali.
Tujielimishe elimu na maarifa juu ya magonjwa yetu na tujitahidi kukwepa magonjwa
hayo kwa nidhamu ya chakula na mazoezi ya viungo. Baadhi ya wachungaji
wamegeuka matapeli. Baadhi ya wachungaji wamewadanganya mabinti zetu kwamba,
wangepata wachumba kwa maombi yao tu, bila kujali kuishi maisha ya haiba na
desturi njema.

Vikundi vya maombi miongoni mwa wakatoliki vimebaki kuwa magenge ya kumnadi
pepo. Ubishi kwa makrelo. Dharau kwa sakramenti na visakramenti kwa baadhi. Pepo
amesingiziwa mpaka kwa walevi. Pepo ulevi. Pepo uzinzi. Pepo wa ngono. Pepo wa
wizi. Pepo wa uongo. Pepo wa uchawi. Pepo wa uchafu. Pepo uvivu. Pepo wehu. Pepo
uchawi n.k. Haya yote ni majina ya kumnadi pepo. Pepo ametafutwa na kuwindwa
badala ya kumtafuta Yesu Kristo Mwanzo na Mwisho, Alpha na Omega.

Badala ya kufanya mageuzi ya maisha yetu, kila dhambi tumebaki tukimsingizia pepo.
Pepo amepanda bei mpaka ametajwa mara nyingi wakamsahau baunsa Yesu Kristo
mwenyen uwezo wa kuyaangamiza mapepo. Sio, marahaba utamkuta pepo akinadiwa
kwenye majukwaa ya wasakatonge tangu asubuhi mpaka usiku. Pepo amenadiwa na
kuimbwa mara zote, amebaki ni wimbo wa zilizopendwa. Hapo lazima pepo aote
mbawa kwani anawachachafya wenye uoga, wasiotaka kuishi maisha ya toba,
msamaha, kuungama, kupokea ekaristi mara kwa mara nk.

Binadamu amekuwa mgonjwa akifikiri maombi ya kanisani yanatosha tu kumtoa


katika hali yake ya uhohehahe. Muulize Bakhresa kama alibaki kuombewa na
wachungaji kanjanja mpaka akafikia ubilionea huo kama sio utirionea. Muulize Dangote
tajiri mkubwa mnaijeria, tajiri wa kwanza Afrika yote. Unafikiri kuwa wa kwanza
katika utajiri wake barani Afrika alimsubiri Yesu Kristo atende miujiza. Unafikiri
alihitaji kwenda kwa mnaijeria mwenzake Mchungaji TB Joshua? Aaaah wapi!!! Amka
mwafrika.

Piga kazi. Acha hadithi za akina Abunuwazi na Buricheka. Si kweli, mafanikio ya hao
hayakutokana na kuombewa maombi ya kupata utajiri, isipokuwa walimwomba
Mwenyezi Mungu abariki kazi zao na wakaongeza jitihada kubwa. Mwenyezi Mungu
hufanya kazi na wote wenye jitihada. Mwenyezi Mungu hafanyi kazi na
wavivu.Tuache maisha ya vichekesho kama tuvionavyo katika sinema na Bongo movie.
Tuache maisha ya vichekesho kama tunavyoviona katika michezo ya Isidingo ya Afrika
Kusini.

Aliyegundua ndege aina ya Bormbadier watanzania wanaifurahia. Unafikiri aliivumbua


na kuiunda bila kuumiza kichwa? Aliyegundua simu yako na yangu pia unafikiri
hakuumiza kichwa? Mbaya zaidi, simu “imeabudiwa” na kuwa “mungu kitu’’
imethaminika hata zaidi ya Biblia miongoni mwetu. Wewe ni shahidi wangu, itokee
abiria amepoteza simu au imedondoka utaona aliyepoteza au kuibiwa simu
atakavyohaha. Atajipapasa kama vile ameingiliwa na siafu nguoni. Tujiulize ni
wakatoliki wangapi wana Biblia Takatifu? Pia, tujiulize ni wakatoliki wangapi
wanamiliki simu za mkononi hata kama ni simu dizaini ya mche wa sabuni?

Fika Dar es salaam, uone daraja la Nyerere la Kigamboni, unafikiri lilikuwa vile
kimiujiza au ni uhalisia wa nguvu, jasho, kodi za wananchi na mifuko mbalimbali
imetumika kulijenga daraja la mfano na la kuvutia hata macho yangu na yako. Au rejea
barabara za juu kwa juu (flyovers( zilizotengenezwa chini ya usimamizi wa Muhandisi
Mfugare mkoani Dar es Salaam nchini Tanzania, unahisi hakuumiza kichwa? Je,
alisubiri miujiza?

Hakuna muujiza hapo. Nenda Japan, viwanda vya magari navyo unafikiri vimekuwa
hivyo kwa kunena kwa lugha. Yote yamewezekana kwa sala na kazi. Hata kama Japani
wengi wanaabudu dini nyingi za miungu, lakini kuna wanaomfahamu na kumwabudu
Mungu YESU KRISTO. Maombi tu, bila kazi ni upinga Kristo. Tunaifahamu sote
anghalabu kuwa imani bila matendo imekufa. Si kitu. Ni sawa na sauti iliayo kama
debe tupu.

Kazi yenyewe ni ngumu na wala haivutii masikioni mwetu ila matunda ya kazi
yanavutia kwelikweli. Ndio maana baadhi ya miti ina mizizi michungu lakini matunda
yake ni matamu. Hakuna utukufu bila usumbufu ndugu yangu. Kukuruka mwanangu.
Pambana na hali yako kama kizazi cha magulification kinavyosema. Acha kudeka. Acha
kusaka mafanikio kwa njia nyepesi. Utachekwa duniani, tena katika Lugha ya
Kiswahili kuna maneno kama kazi, bidii, jitihada, ubunifu, ueledi, kujituma, kujitoa,
kujiumiza, kujisadaka nk. Maneno haya na vitenzi, vyote vinasisitiza juu ya kupiga kazi.
Maneno haya yanampa moyo mwanadamu aweze kufikia mafanikio chanya ambayo
mtu anapaswa kuyafikia bila kukata tamaa.

Vipi Waafrika wenzangu tunagoma kuamshana? Kivipi tupeane elimu na maarifa? Je,
tuamshwe kwa kufungwa kamba miguuni na kisha tuburuzwe kwa matrekta? Hebu
ndugu zanguni tuelewe walau kidogo. Afrika nzima iamke. Lakini mambo bado kabisa
kati yetu wanyonge. Hivi kwanini tunabishania vyombo vinavyoweza kuongeza kulala
kwetu. Tunagombania “klorofomu?’’ Tumelaaniwa kiasi gani, Afrika imesheni madini,
ardhi yenye rutuba, mvua, bahari, maziwa, mito na watu wenye nguvu kwelikweli?
Kulialia, kusali kwa makelele, kufunga na mikesha isiyokwisha, vinavyoufedhehesha
Ukristo vinatuongezea kubweteka kwetu. Vyanini hivyo? Tuyagutukie mambo na
vyombo “vinavyotulofaza’’ na “kutuvivusha’’ kwa kutungojesha na kutusubirisha
miujiza. Zamani hizo Wakatoliki hatukuwamo katika “mibweteko,’’ mambo ya
“kulofazana’’ na “kuvivushana,’’ lakini siku hizi na SISI NI WALEWALE! Tofauti kati
ya Kanisa Katoliki na makanisa ya “private’’ inazidi kupotea. Sauti na hadhi vya Kanisa
Katoliki poleple vinakwenda na maji. Yaonekana tumeamua kujiunga kwenye michezo
ya watoto. Toba, Mungu tuhurumie!1

4. MAFUNDISHO YA KUWA WATUMWA WA KULOGWA

“Usiogope kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako,
nitakutia nguvu naam nitakusaidia naam nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu’’
(Isa 41:10).

Dunia imejaa mambo ambayo daima yanatuletea hofu na mashaka, woga na wasiwasi
katika maisha yetu ya kila siku. Kutokana na hali hiyo watu wengi sana wanaishi
maisha ya hofu na kutawaliwa na wasiwasi mkubwa katika maisha yao ya kila siku. 2

Hofu hutuondolea amani mioyoni mwetu. Hofu ni kizuia maendeleo. Hofu hutufanya
sisi wanadamu kuwa watumwa wa hisia zetu. Hofu hutukwamisha maendeleo. Hofu
hutuondolea ujasiri. Hofu hutukatisha tamaa katika jitihada zetu. Hofu ni mlango
mkubwa wa kushindwa kufikia malengo yetu katika maisha. Kimsingi, hofu ni
1
TITUS AMIGU, MAJIBU YAKE, KATIKA UKURASA WAKE WA KIJAMII FACEBOOK, Septemba,
24,2019.
2
ELEUTER A. MANGE, TIBA YA HOFU, Utangulizi wa Kitabu, uk. X.
ugonjwa wa sononi. Hofu huteletea masononeko na mwisho kuwa mbali na Mungu
wetu. Mwenyezi Mungu anatupatia moyo kupitia kalamu ya Mtume Paulo
anapomwandikia barua Timoteo kuwa, “Maana Mungu hakutupa Roho ya woga, bali ya
nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.” (2 Tim 1:27).

Hofu ni hisia zinanazomwandama mwanadamu, huenda kwa kushitushwa, au kwa


kusimuliwa hadithi zenye matukio ya kutisha au ya kuhuzunisha. Hofu huondoa
ujasiri. Palipo na hofu hapana ujasiri. “Bado tuliweza kuthibitisha kuwa tu watu wenye
uwezo wa kufanya mambo makubwa ili kuzikabili changamoto zetu kubwa.’’ Aliyasema
maneno hayo Barack Obama, Rais wa Amerika katika moja ya hotuba zake wakati akiwa
Rais wa Taifa kubwa duniani Amerika. Hofu ni kukosa moyo mkubwa, kama mithali
ya kiafrika inavyosema, “Watu mashuhuri wana mioyo mikubwa.’’ Hofu imemfanya
mwanadamu awe masikini na mashaka nayo yakamfanya mwanadamu ajisaidie ndani ya
nyumba yake, hiyo ni methali ya kiha kwa maneno (Ubhutinyi bhutera ubhukene nabwo
ubwobha bhukakunyesha munzu).

“Mwanadamu anahitaji magumu katika maisha yake, kwani ni muhimu katika kufurahia
mafanikio yake.’’ Aliyasema maneno hayo Dr. Abdul Kalaam, Rais na mwanasayansi wa
India. Ndiye aliyekuwa akiwapatia ujasiri wananchi wake wa India, kwamba, “Ni
mpaka India itakapojisimamia yenyewewe katika maamuzi yake, ndipo itaheshimika mbele ya
ulimwengu. Katika ulimwengu huu uoga hauna nafasi, nguvu mara zote huheshimu nguvu.’’

Ndugu msomaji wangu unaona namna hofu ilivyo kipingamizi cha maendeleo ya
mwanadamu wa bara lolote hapa duniani. Tuachane na hofu zisizokuwa na msingi,
Martin Luther King Jr aliwahi kusema; Maendeleo ya mwanadamu hayajiletii tu automatiki,
japo ni ya lazima. Kila hatua kuelekea mbele kwenye malengo ya haki, inahitaji sadaka, mateso,
na jitihada, kupambana bila kuchoka na uvumilivu wa hali ya juu na kujitoa kwelikweli.’’

Hofu hii ndio Baba Mtakatifu Benedikto XIV anayotuomba Waafrika tuiache katika
AFRICAE MUNUS 93. Kati yetu Waafrika weusi, mtu akiwa anakushinda na kufanya
mambo yake kwa kujiamini wengi wetu hukimbilia kumtuhumu mtu huyo anatumia
nguvu zisizo za kawaida. Katika karne ya 21, tuupuuze utamaduni huu anaousema
Baba Mtakatifu Benedikto XVI “Kujifunga kwa Waafrika pingu poozeshi’’ (Africae
Munus 93). Hii karne ya 21 iwe aibu kwa Mkristo Mkatoliki kuamini katika uchawi. Na
iwe aibu kubwa sana kwa vijana. Baba Mtakatifu Benedikto XVI, anatusikitikia Waafrika
kwa sababu wakati wa mabara mengine wanasonga katika utaalamu na juhudi za
kuutawala ulimwengu, sisi tunatawaliwa na fikra na hofu zilizopitwa na wakati.
Wakati wenzetu wanatumia vyombo angani kutafuta Sayari zingine za kuishi.
Wamarekani wametuma ‘curiosity Skycrane’ kwenye Mars na ‘Juno’ kwenda Jupiter,
Wahindi wametuma mangalian kwenda Mars na wanasayansi wa kiarabu wanaandaa
chombo cha kupeleka Mars, vijana Waafrika weusi wanasema eti mtu anayeandika
dhidi ya Karismatiki anatumia nguvu zisizo za kawaida. Huu ni “unyuma’’ wa
kuonewa haya. Kama fikra kama hizi zinatoka kwa vijana, Waafrika weusi
tutakombolewa na nani? Nani atupaishe kwenye anga za fikra mpya na utafiti? Nani
atusaidie kuzikata “pingu poozeshi?’’3

Dhambi kubwa ya mshirikina ni kuvipa nguvu na uwezo wa pekee vitu, watu, na


viumbe visivyo na nguvu wala uwezo huo hata kidogo, na kisha akaviaminia vitu
hivyo, kuvitumainia na kuvitegemea katika kufanikisha mambo yake. Tumesema
mahali pengine kuwa tofauti kubwa kati ya uchawi na ushirikina ni hii kwamba kila
mchawi ni mshirikina, lakini si kila mshirikina ni mchawi. Ni hakika kwamba
washirikina ni wengi zaidi kuliko wachawi, kama vile wanafunzi walivyo wengi kuliko
walimu. Yote mawili, uchawi na ushirikna, husukumwa na kuchochewa na hofu ya
kudhurika, hofu ya kukosa jambo fulani tunalolitaka kwa udi na uvumba, mfano
utajiri, ukuu na mamlaka, ushindi, mapenzi na kadhalika.4

Mwenyezi Mungu anapinga kuunadi ushirikina, kwani ni kuabudu miungu. Mwenyezi


Mungu amemkataza mwanadamu asijiingize katika pilikapilika za ushirikina. Ni
dhambi. Mungu huwapatiliza washirikina. Ndio maana kati ya watakaoikosa mbingu
ni pamoja na washirikina wote. Zifuatazo ni nukuu chache kutoka katika Biblia
Takatifu zinazoonesha namna Mungu asivyopenda ushirikina na mahangaiko ya
hirizi na waganga wa kienyeji.

(1 Sam. 22:23, Eb 19:31, Eb. 20:6, Uf. 18:23, Gal. 5 :19 -21, Micah. 5:10 -12, Mdo. 19:17
-20; Isa. 8 :19-22, Isa. 19:1-4, Mdo. 8:9-13, Isa. 47: 8-14).

Imani za kishirikina na hadithi mbalimbali za kichawi katika maisha ya mwafrika,


zimemfanya mwafrika abaki mtumwa wa hofu zisizo na kichwa wala miguu. Imani ya
kishirikina imemwacha hoi mwafrika. Mwafrika hayuko huru tena amebaki hana
raha.Kwakuwa penye mizoga ndipo tai hutua. Wahubiri huchukua fursa hiyo
kuwahadaa watu wetu. Hofu ikizidi kwa kila jambo maisha hayaendi.

3
TITUS AMIGU, MAJIBU YAKE, KATIKA UKURASA WAKE WA KIJAMII FACEBOOK, KAMATA
KIPIMO UMBAINI “MPAGANI’’ NA ANAYEMPINGA KRISTO,’’ OKTOBA 21, 2019
4
NZABHAYANGA SEBASTIAN MPANGO, JIPENI MOYO MSIOGOPE (Isaya 35:4), Hofu kama wa
uchawi,uk. 118
Dhana hii inatokana na uoga uliopitiliza. Uoga ni hali ya kutokuwa na uhakika wa usalama
na mazingira, alisema Profesa wangu wa somo la Falsafa Kibosho Seminari Kuu ya Falsafa,
Moshi Kilimanjaro, Padre Beda Ishika PhD wa Jimbo Katoliki Same, Tanzania.

Ndio maana kila penye uoga, ushirikina au dhana ya kujikinga kwa ndumba zozote au
hirizi zinakuwapo. Binafsi naona tangu utoto wangu nimekua nikisikia mengi, lakini
sijawahi kuyathibitisha hata mojawapo ya hayo yasemwayo na waafrika wenzangu.
Mimi padre, wachungaji, na mashekhe tutapata chamoto tukiwadanganya waamini wa
Mungu wetu kwa kuwahadaa kuwa kila kiwasumbuacho ni kulogwa.

Zama zetu tumeshuhudia wengi wa wachungaji na hata viongozi wengine wa dini


mbalimbali wakiunadi ushirikina. Hata katika Karismatiki isiyotulia utawakuta
wenyewe wakisontana vidole na kutuhumiana kulogana wao kwa wao. Kesi hizo
nimeziona na kuzisikia kwa macho na masikio yangu. Wewe ndiyo chanzo cha furaha
yako. Wewe ndiyo chanzo cha huzuni yako. Dalai Lama XIV, alisema “Furaha sio kitu
ambacho kimekwishatengenezwa. Inakuja kutoka ndani ya matendo yake.” Hapo ndipo
mawazo hayo yanaendana na Bill Gates tajiri wa kwanza wa dunia anasema,
“ukishindwa kufanya jambo liwe zuri basi lifanye lionekane na watu kuwa zuri.” Tunakuwa vile
tunavyowaza kama Budha asemavyo.

Tuache kuwajingisha waamini nao wakawa na ugonjwa wa kubeba dhana hizo mpaka
wakakosa amani na kuanza kuunadi ushirikina badala ya kumtangaza Kristo. Tuihubiri
injili ya Kristo. Tumuhubiri Kristo.Tukiunadi ushirikina kuwa sababu ya kukosa
mafanikio ya miongoni mwa wakristo, Kristo anatatushangaa. Hayo hayatakuwa
mahubiri ya Yesu. Hayo sio mafundisho ya Bwana wetu Yesu Kristo. Bwana wetu
Yesu Kristo hatarajii kuyasikia kwetu tukionesha kuyaogopa na kuyaweka kwenye
mioyo ya waamini wake. Atatuchapa mboko. Suala sio kutoyaogopa tu bali tusiwe na
ushirika nayo. Kamwe, tusiwadanganye wakristo kwa kuwawekea sumu ya uoga na
kujikuta wanakuwa wadau wa kuishi maisha ya uoga na hata kutafuta ulinzi kwenye
manyoya ya kuku. Maisha ya mwanadamu hayawezi yakanyoka siku zote. Kuna
mabonde. Si kila mambo yako yanapokwenda kombo ukadhani kuna mkono wa mtu.
Jichunguze je, mimi naogopa wachawi? Naogopa watu wanaoroga? kwanini naogopa
wakati neno la Mungu linaniambia kuwa, “Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, wala
hapana uganga juu ya Israeli.’’ (Hes 23:23). Tena mwambie Mungu “akulinde kama
mboni ya jicho lake, akufiche chini ya uvuli wa mbawa zake, Wasikuone wasio haki
wanaokuonea, adui za roho yako wanaokuzunguka.’’ (Zab 17:8- 9).5

5
ELEUTER A. MANGE, TIBA YA HOFU, N0.17, Hofu ya Wachawi, Uk.17
Kuna visiki. Kuna makorongo. Kuna mifereji. Kuna utelezi. Kuna tope hasa kwetu sisi
ambapo barabara zetu za kijijini kwa mama na baba yangu. Kuna kubomoka kwa
madaraja. Kuna ajali za kizembe. Hayo nayo yametokana na kurogana. Kuna ebora
nayo watu wamelogwa? Kuna ukimwi. Je, watu wamelogwa ukimwi? Kuna UTI nayo
watu hulogwa UTI? Kuna ugonjwa wa Tezi dume. Eti, watu wamelogwa Tenzi dume.
Tuache mbwembwe za kuunadi ulozi.

Kuna magonjwa pia, kaswende, malaria, tezi za dumu, saratani ya damu, kizazi, na ya
mifupa, madonda ya tumbo, ukichaa. Jamani haya nayo tumwite mchungaji ayaombee
haya akijinadi kuwa magonjwa haya yanatokana na uchawi. Ni uchochezi kusema,
jirani yako ndiye aliye kuloga. Na hivi, Mungu ampatilize mbali. Haya si mafundisho
ya Kikristo. Sio mafundisho ya Kristo. Wewe unayejidai kuwa umelogwa na
wafanyakazi wenzako. Fanya kazi, acha kujibwetesha kwa fikra finyu. Fanya kazi acha
migogoro na wenzako. “Tafuta amani na furaha kutoka ndani mwako mwenyewe, usiitafute
amani na furaha nje yako.” Guatama Budhaa alisisitiza hayo kwa wafuasi wake.

Mang’amuzi ya Padre Sebastian Mpango Nzabhayanga wa Jimbo Katoliki Kigoma, Tanzania,


katika Kitabu chake JIPENI MOYO MSIOGOPE (Isaya 35:4) ukurasa wa 114, anasema
juu ya hofu kama mama wa [dhana ya] uchawi.

Ni rahisi kuona jinsi hofu ilivyo mama wa [dhana ya] uchawi. Bahati mbaya mama
anaweza akafa na mtoto akabaki, na hili linasababisha tuwe na aya [kifungu]
inayofuata, ikielezea hofu kama mtoto wa uchawi, maana mtoto naye hukua akaanza
kuzaa watoto na wajukuu wakafanana na bibi yao. Je, tuseme kuwa kwa vile hofu ni
mama wa uchawi basi hofu itakapotokomezwa na kutoweka kati ya watu basi
tutakuwa tumeondokana kabisa na uchawi? Hapana, ndiyo jibu langu kwa kadiri ya
ufahamu wangu kuhusu uchawi na ainisho lake. Katika Kitabu pacha na hiki (Uchawi
na Ushirikina) uchawi umeelezwa kwa kirefu, na katika maelezo yake unapata kuona
kuwa uchawi una chimbuko lake katika uovu wa mwanadamu. Hata hivyo tunaweza
kusema kuwa pasipo hofu uchawi unabaki kuwa mazingaombwe zaidi na michezo ya
kuigiza.6

Ndugu msomaji wangu, kwakuwa ushirikina nao ni moja ya mahangaiko


yanayotuchachafya sisi wana wa dunia hii lukumbalukumba, ni lazima nalo niliingize
kati ya mahangaiko ya mwanadamu katika dunia hii ili kitabu changu kieleze
mahangaiko mengi. Hata kama hakitayamaliza yote basi itanibidi niandike matoleo
pacha ya kitabu hiki. Uzoefu wangu binafsi mimi Padre Simon Liberio J. Bahanza
6
Rejea, Maelezo yaliyonukuliwa katika Kitabu , uk.114
Bavugubusa, mwana wa Buha wa Mabamba Kibondo, mkoani Kigoma, mwandishi
wenu wa Kitabu hiki, naweza kusema; Tukiwa watoto wadogo tuliaminishwa
kwamba kuna watu wenye uwezo wa kuruka usiku tena kwa nyungo. Huku nafahamu
fika nyungo ni kwa ajili ya kupepeta nafaka na sio kwa usafiri. Sijawahi kuona dreva
huyo na usafiri wake wa ungo mpaka leo hii mwaka 2019 natimiza miaka 36 ya
kuzaliwa. Naamini kuwa tulidanganywa, na uongo huu siwezi kuukubali hata kidogo
leo hii. Tuache usiku, basi waruke mchana tuwaone tuwazawadie bilioni 40. Kwani,
watakuwa wametuletea ukombozi wa usafiri, na kuturahisishia adha tunazozipata
barabarani hasa sisi wana Kigoma, Tabora, na jirani zetu wa Nyakanazi n.k.

Nani mwenye picha na video ya kudhihirisha uongo huu. Au naomba niwe abiria wako
wa kwanza kama unaweza kunibeba kwa ungo wako. Mbona wengi wetu tunatembea
mpaka miguu inapinda. Kwanini tujichoshe kama kuna usafiri unaoitwa ungo trans au
nyungo trans waafrika tuache ujinga.

Kama ni kweli, kwanini tununue bombardier kama ya Rais Magufuri na watanzania wake,
kwanini tununue Kilimanjaro Air ways, Tanzania air ways. Tufanye kazi tuache
kudanganyana kwa hadithi za kijiweni. Mataifa ya Ulaya, Amerika na Asia wanaumiza
vichwa katika mbio za maendeleo ya Sayansi na tekinolojia, wewe mwafrika
mwenzangu unakomaa na vibuyu, nyungo, vichwa vya panya na ngozi ya kakakuona.
Aibu tupu kwangu na kwako.

Wenzetu wa Ulaya, Amerika na India wanafika mwezini, wanafika mpaka kwenye


sayari za Venus na kuweka makazi. Wenzetu wanafika angani wakituma satellite huko
na kurekodi shughuli mbalimbali za huko na kutufikishia huku duniani kwa
wamatumbi wenzetu. Miaka ya nyuma, wakazi wa Ujiji na Gungu mkoani Kigoma wengi
wa wakazi wa huku waliogopa kujenga nyumba nadhifu na kubwa kisa wasije
wakalogwa. Wengi wao waliogopa kufanya mambo ya maendeleo wakihisi huenda
watalogwa.

Hiyo ndio hofu iliyokuwa imejengeka kuwa wangelogwa kama wangeonekana ni


matajiri. Hayo ndiyo yaliyo waogofya wengi wasijiendeleze kielimu wakihofia
kulogwa. Lakini, ama kweli! Zama zimebadilika tembelea Mwasenga, Ujiji, na Bulega
utaweza kuwa shahidi wangu kuwa Buzebazeba ya sasa sio sawa na ya zamani.
Tumetigita kweli wana Kigoma, Kigoma leka tutigite wishavu ameneke.!!!!![Kigoma
tunafurahia maendeleo mwenye wivu apasuke] Rejea, Wimbo wa Kigoma All Stars, uitwao
Kigoma leka tutigite. Hofu ni nguvu inayokwamisha na kuzuia maendelea ya
mwanadamu. Hofu inamaliza munkari wa kazi za maendeleo. Hofu hutufanya tubaki
walalamishi tu bila kutenda.

Sehemu hizi, siku hizi wakazi wamejitahidi kujenga nyumba zenye ubora. Wengi
wamejenga bila hofu tena ya kulogwa. Nenda Mwasenga, Mji mwema, Kagera ya Ujiji
Kigoma na Bangwe. Utayaona mabadiliko ya kifikra. Ama kweli, ukale unatudumaza.
Ukale unaturudisha nyuma. Ukale unatubwetesha. Ukale unatubakiza nyuma
tunashangaana na njaa zetu za kifikra. “Hakuna umasikini mkubwa kama umasikini wa
fikra.” Nyerere, Rais wetu wa kwanza wa Tanganyika kabla na baada ya muungano wa
Zanzibar na Tanzania alituambia, tumkumbuke ili tusibaki kulala tongo macho. Fikra
zetu hasi na duni ndizo zitakazotuzika tusipoamka.Fikra zetu chanya ndizo zitakazo
tukwamua katika ujinga wetu. Tumkumbuke tena Budhaa aliyefundisha kuwa, “Amani
ya moyo wako usiitafute nje yako, amani ya moyo wako iko ndani ya moyo wako.’’

Tembelea maeneo ya pwani yote, yametekwa na fikra hizi za kudumazana tupende


kazi. Kazi ituweke “bize’’ hata dhana za kudanganyana kwenye vijiwe zitapungua kwa
kiasi kikubwa ka. Kwanza, waafrika ma sio kuisha kabisa. Waafrika tuachane na ndoto
za kutaka kupaa bila mbawa. Pia, ujumbe kwa mtoto wa Afrika, ningemshauri apende
elimu. Ajiboreshe kielimu. Asome kwa bidii kama anayesomeshwa na halmashauri ya
walei Kigango cha; Mabamba, Mazimavyagwa, Burimanyi, Kabhuranzwili, Titye, kishapu.
Jionee mwenywe, Mabama, Usinge, Nyabitaka, Kibuye, Rusohoko, Songambele, Kazuramimba,
Rusesa, Rusaba, Nyarubanda nk.

Mtoto wa Afrika, kamwe asilete mchezo shuleni. Akumbuke ushauri wa Mwalimu


Julius Kambarage Nyerere, aliomshauri mwana wa Mtanzania aendapo shuleni;
“Mwanafunzi anapokuwa shuleni akumbuke amefananishwa na yule mtu aliyetumwa na
nduguze kuleta chakula nchi ya ng’ambo baada ya janga kubwa la njaa kali. Na hivi, wenzake
wanamtarajia arudi na chakula ili kiwasaidie na kuwaokoa waliobaki katika nchi ya njaa. Ndugu
zake watamsubiri kwa hamu kubwa. Asiporudi atakuwa muhaini na hafai kwa Taifa letu la
Tanzania wala popote.’’7

Viongozi wa dini, tusiwahadae wakristo kwa kuwabwetesha na mahubiri ya furaha tu,


tuwaambie pia kuna msalaba. Wabudha wanaamini juu ya umuhimu wa mateso katika
maisha ya mwanadamu; wao wanaamini kuwa, “Mateso yapo ili yaweze kumnyenyekesha
mwanadamu dhidi ya kiburi chake.’’ Kwakweli, hayo ndiyo Mt. Yustino Mfia dini
anayozungumza katika kuonesha kwanini mateso ni ya lazima kwa mwanadamu hapa

7
NYERERE JULIUS KAMBARAGE , Moja ya Nukuu zake, Inapatikana Shule ya Wavulana Tabora (Tabora
Boys/ Tabora School kwenye moja ya Ubao wa matangazo.
duniani. Anasema: “Mungu huruhusu mateso yatupate ili tusije tukajisahau tukadhani sisi
wenyewe tu bila yeye tunajitosheleza kana kwamba hatumhitaji Mungu katika maisha yetu.’’

“Tunakuwa kile tunachofikiria” alisema Budha pia. Waafrika “tuzinduke’’ ndio, tuamke.
Tufanye kazi. Karne zinabadilika na zama pia hivyo hivyo. Shida inayokuja hapa wengi
wetu waafrika tunaishi kwa mazoea. Kuna mambo mengi ambayo nimezaliwa
nayakuta na nimekua nayasikia, niache mwenyewe niyaite “uongo’’ au ukipenda
waweza kuyaita dhana potofu miongoni mwa waafrika wengi.

Moja, kwamba mtu anaweza kujigeuza kuwa fisi. Huu ni uongo namba moja. Naomba
unipatie ushahidi wa matukio kama haya. Hata mawili au matatu ili niweze kuzidi
kudadisi juu ya uongo huu. Hapa, hata maelezo ya kisayansi ya wataalamu kamu
Charles Dawn, wa mabo ya mabadiliko ya viungo (evolution) atakubishia kama
angekuwa hai. Huu ni usanii na upandikizo wa uoga miongoni mwetu waafrika
mapara bongo.

Pili, ni kule kuamini kuwa mtu mwenye nia mbaya nawe ana uwezo wa kukutumia radi
ikudhuru. Huu nao ni uongo na dhana potofu zinazoisonga jamii yetu ya kiafrika katika
baadhi ya sehemu. Huu nao ni uongo na fikra za kijinga ambazo nami Padre Mtunzi na
mwandishi wa kitabu hiki cha “Mahangaiko Duniani‘’ nimezaliwa na kukuta dhana hizi
katika mazingira yangu. Naamini hata nikifa, ujinga huu utabaki mwa wengi.

Dhana hizo potofu zinabaki vichwani mwa wengi . Mimi fanani mwandishi, lazima
nichukue kipaza sauti kukemea ujinga huu, ili kuwakomboa hadhira yangu ya wasomaji
wa Kitabu hiki. Waambiwe wazi kuwa, hatutaendelea kama tutabaki
tukijishikamanisha na ndoto za mchana. Hatutaendelea kama waafrika wenzangu
tutabaki tumejifunika gubegube blanketi zito usoni. Afrika simama, jikomboe kifikra, kihaki,
kielimu, kiuchumi aliimba Bob Marley katika wimbo wake uitwao “Africa stand up’’.

Tatu, kuwa mtu anaweza kuichukua bahati yako kwa kuchukua udongo ambapo miguu yako
imeacha nyayo.

Huu nao ni uongo unaomtesa mwafrika. Kama ulicheza shuleni. Unatarajia nini? Kama
unaishi bila mipango kama mbuzi unatarajia nini? Kama unaishi bila malengo
unatarajia nini? Ninayaandika haya ili yabaki katika historia. Nisije nikalaumiwa kuwa
sikuyasema wala kuyaandika vitabuni. Tumejikuta waafrika tukiogopa hewa.
Tumejitwika “mizigo- fikra’’. Tumejikuta tukiishi bila raha kwani tumejitwika
mahangaiko hata ambayo si yetu. Watu wengi miongoni mwa jamii zetu bado
wanaogopa hata kupoteza vyeo, ofisi, na madaraka kwa njia ya ushirikina. Ndio maana
baadhi ya viongozi wa Afrika wanapojiandaa na nafasi mbalimbali katika chaguzi huku
Afrika hujikuta nao wamedanganyika katika ushirikina.

Hofu ni ugonjwa. Hofu hutudumaza katika kuleta maendeleo. Hofu ni kikwazo cha
mafanikio. Katika Kitabu cha “IS IT POSSIBLE?” yaani INAWEZEKANA?
kilichoandikwa na HR Ole Kuret, anapoonesha namna jamii nyingi za kiafrika
zilivyokuwa zina uoga katika mabadiliko. Mwandishi anamtaja Lerionka kijana wa
kiume wa kimasai anavyoogopeshwa na baba yake, kwamba asiende shule kwani eti
tu, haiwezekani kusoma shule huku akiendelea na shughuli za uchungaji au ufugaji wa
mifugo.

Mwisho wa siku, kijana Lerionka anatoroka nyumbani kijijini katika tembe za kimasai na
kwenda shuleni mjini Arusha. Na anapomaliza shule, anarudi nyumbani kuwa mfugaji
bora, mifugo hawafi hovyo hovyo kwani anafahamu kuwatibu, wanapata maziwa ya
kutosha kwani wanahudumiwa kiutalaamu kwa kutumia elimu aliyoipata shuleni.
Mwisho wa siku baba yake Lerionka anafurahia matunda ya elimu aliyoipata mwanae.
Kwani, hapo awali aliogopa kumpeleka mwanae kuwa angeharibiwa na elimu ya
kizungu au kikoloni na kupoteza mila na desturi za kabila lake la kimasai. Mwisho
mwishoni, baba wa Lerionka anakuja kukubali na kusema INAWEZEZEKANA
KUSOMA BADO UKABAKI NA MILA ZAKO, DESTURI ZAKO, NA TAMADUNI ZAKO
NJEMA NA UKAWA MFUGAJI HODARI WA MIFUGO KAMA LERIONKA KIJANA WA
KIMASAI.

Uongo namba nne, kamwe sisi viongozi wa dini mbalimbali kanisani, misikitini, na
masinagogini; tusiungane na mawazo kuwa kuna waganga wa kienyeji wanaoweza kutengeneza
mvua. Tusiunadi ushirikina Kanisani wala misikitini, kwani tunamwaaibisha Mungu wetu
Mweza yote.

Katika jamii zetu bado watu wanadanganywa kuwa kuna watengeneza mvua. Hawa
tungeweza kuwaita “wataalamu’’ wa kusoma alama za nyakati kwa kutambua na
kusoma majira na nyakati. Baada ya kuisoma tabia ya mazingira na mahali na vielelezo
vyake kwa mfano kipindi cha mvua kinapokaribia, wataalamu hawa huona viashiria
kama vichuguu kutoa wadudu kama kumbikumbi, mchwa kutokea shimoni, uyoga wa
kuliwa na uyoga sumu, wadudu kadhaa kutoka ardhini na vyura pia. Hivyo, ni
viashiria namba moja vya kutambua kuwa mvua iko usoni inakuja mara. Miaka ya
1996, nyumbani Mabamba nilishuhudia wazee waliojichokea wakisurubiwa kwa
kuwekwa juu ya paa (bati) na kupigwa viboko eti wao ndio waliokwamisha mvua. Huo
ni ujinga namba nne kweli unaomwelemea mwafrika wa leo. Tuache kudanganyana.
Tupande misitu minene. Tutunze miti. Tutunze vyanzo vya mito.Tuache shughuli zote
kwenye vyanzo vya mito. Tutapata mvua ya kutosha mpaka kuikimbia. Tuwaulize
wachina na wathailand wanachanganya kemikali zipi na kishapo mvua hupatikana?
Japo huo ni uharibifu nao wa mazingira na tabia ya nchi.

Uongo namba tano, kwamba usiku wa manane ndio wachawi na mashetani hufanya kazi kwa
kasi. Huu nao ni uongo tuukemee.

Uoga hutuendekeza katika ujinga. Wengi wameshindwa kufanya maendeleo kisa uoga
wa wachawi na hata pepo.

1. HOFU DHIDI YA PEPO MIONGONI MWA WAKRISTO

‘’Tunaogopa kesho kwasababu tuko tunaipoteza leo’’.


- Mama Terezia wa Kalkuta

Kwanza kabisa, ni ajabu lakini ya kweli. Je ni wakristo tu wanaoogopa mapepo?


Tungeweza kujibu, hapana hata wasio wakatoliki nao huogopa mapepo. Ni lazima
kumpinga shetani. Pepo aliye mwovu na adui wa Mungu lazima awe adui pia wa rafiki
wa Mungu. Pepo ndiye shetani aliye nyanganywa umalaika wema, kwa kukosa utii
kwa Mungu Mwenyezi. Kwa maneno mengine, Shetani ni malaika muasi kwa Mungu.
Swali jingine, ni kwanini suala la pepo limepamba moto miongoni mwa wakristo?
Kwamba, wakristo ni dhaifu kwa sala zetu? Kwamba, wakristo tuna nguvu za soda tu?
Kwamba, wakristo tunavivutio vya mapepo zaidi ya waislamu, wabudha, watao na
wankofusia?

Kwa kuwa dhana ya hofu dhidi ya shetani imepamba moto miongoni mwa wakristo,
wengi wa wakristo wamegeuzwa kuwa mradi na magenge ya vikundi vya sala na
maombi kama tunavyoona wakristo wetu wengi wasivyo na utulivu.

Katika sala ya “Baba Yetu’’ ambayo ni Sala kuu na ya kielelezo cha sala zote,
tunapoisali sala hiyo, tunamwomba Mwenyezi Mungu, “Usitutie kishawishini lakini
utuopoe maovuni.”

Hiyo ndiyo kauli mbiu ya mkristo yeyote kwa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu
anatambua kuwa ana kiumbe chake ambacho atakilinda siku zote dhidi ya uvamizi wa
shetani. Mwenyezi Mungu anatoa ahadi zake kamili za ulinzi wetu. Zifuatazo ni nukuu
zinazoonesha ulinzi wa Mwenyezi Mungu kwa mwanadamu (2Thes 3:3, Zab 5:11, Mith
2:11, Zab 34:19, Zab 20:1, Zab 57:1, Zab 138:7, Zab 91, Zab 34:7-9).

Mwenyezi Mungu ametuahidi tukimkimbilia hatatuacha kwani ndiye kimbilio letu.


(Zab 91). Atatupatia nguvu tukisali kwa imani, na hivi tutamchapa mboko shetani wala
hata asifue dafu, tutabaki imara. ( 2Thes 3:3-5). Ametuhakikishia kuwa hatatujaribu
zaidi ya uwezo wetu. (1Kor 10:13). Kwamba mara zote Mwenyezi Mungu ni
mwaminifu na atatukinga na mwovu. (2Thes 3:3). Mwenyezi Mungu amekwisha
tuambia tujiamini na tuwe na matumaini makubwa, tuwe imara kwani atakuwa nasi,
hatatuacha kamwe. (Kumb 31:6). Mzaburi anatuambia tuufurahie ulinzi wa Mwenyezi
Mungu wala hatutaaibika. (Zab 5:11). Mwenyezi Mungu atatuhifadhi salama (Zab
140:4). Twaona shaka bali hatukati tama. (2Kor 4:8). Bwana Mungu wetu ni ngome yetu
na ulinzi wetu katika maisha yetu. (2Sam 22:3-4). Mbele ya Mungu hakuna
kitakachotushinda. (Yoh 10:28 -30). Bwana ndiye mchungaji wangu sitapungukiwa na
kitu … yeye ni ngome yangu, fimbo yake na gongo lake vyaniongoza. (Zab 23). Bwana
wetu Yesu Kristo amekuja kumharibu shetani (1Yon 3:8).

Katika tukio moja Yesu alipomponya mtu mwenye pepo, kipofu na bubu, watu
walishangazwa na uwezo wake. Wafarisayo, wakitaka kubeza uwezo huo, walisema,
“Huyu hatoi pepo, ila kwa uwezo wa Beelzebul mkuu wa pepo ’’.Tamko la Wafarisayo
lilithibitisha ukweli kuwa Yesu alitoa pepo, ila waliamini ya kuwa Yesu alifanya hivyo
kwa uwezo wa mkuu wa pepo. Yesu alijibu kuwa kuamini hivyo ni kichekesho kitupu
na ni kupungukiwa akili. (Mt 12:22-28). Katika majumuisho ya kazi ya Yesu, kazi ya
kutoa pepo inatajwa hivi: “Basi [Yesu] alitembea nchi yote ya Galilaya akihubiri katika
masinagogi yao na kuwatoa mapepo wabaya.’’ (Mk 1:39). Injili zinaripoti matukio
yafuatayo ya Yesu kutoa pepo: Mwenye pepo wa Kapernaumu (Mk 1:21-28), mwenye
pepo wa Gerasi (Mk5:1-20), bubu mwenye pepo (Mk. 9:32-34), binti wa mama
Msirofonike (Mk 7:24-30), mtoto mwenye pepo bubu (Mk.9:14-28). Licha ya Yesu
mwenyewe kuwa na uwezo wa kutoa pepo, aliwapa mitume wake uwezo huo nao
waliutumia kwa mafanikio. (Mk 3:15; 6:7; Lk 10:17 -20).

Ingawa alikuwa na uwezo juu ya pepo, hali kadhalika juu ya magonjwa na juu ya
nguvu za maumbile, Yesu hakujitangaza wala kujigamba kama wafanyavyo
“waponyaji” wengi wa leo. Kama tusemavyo “Si kila king’aacho ni dhahabu,’’ pia si
kila tatizo chanzo chake ni pepo. Yesu atuondolee pepo watu, pepo mawazo na pepo
malaria. Tumsifu Yesu Kristo … Milele. Amina.8
8
CHRISTIAN L. MHAGAMA, BIBLIA KWA WOTE, Katekisimu Katoliki, Yesu mtoa pepo, no.239, uk.188,
Paulines Publications, 2014
Lakini mtu atabainishaje kesi za mapepo (mashetani) na za kisaikolojia?

Njia halisi ni ya mazungumzo na uchunguzi wa karibu wa mtu anayeonesha dalili za


ugonjwa wa ajabu ajabu. Katika hili, hakuna haraka ya kuhitimisha tatizo kwa kusema
tu amepagawa au “ana majini’’ na kuanza mara kumwagia mtu maji ya Baraka. Kanisa
Katoliki linaamini katika uwepo wa mapepo kwa maana mashetani, yaani malaika
wabaya. Katu haliamini katika uwepo wa majini. Hiyo ni imani ya kiislamu, tuwaachie
wenyewe kama wao wanavyotuachia imani yetu. Kesi ya mapepo yaani mashetani
kimsingi itakutikana kwa mtu mwenye dhambi kubwa asiyetaka kuiungama naye
atakuwa na tabia za kukataa matakatifu kwani shetani atakuwa anataka
kumwangamiza mtu huyo. Halafu kesi za kisaikolojia zitagugundulikana kwa mtu
kueleza taabu nyingi za maisha binafsi au ya familia na mara nyingi katika maisha ya
ndoa. Hata umri wa watu wenye matatizo ya kisaikolojia utakuwa mkubwa na mara
nyingi ni akina mama kwani wao si waonjaji maalumu wa matatizo ya kisaikolojia,
yaani good conductors of social heat.

Lakini kwa vyovyote kesi za kupagawa na mapepo siku hizi lazima ziwe chache kati ya
Wakristo kwa sababu mbili. Mosi, kwasababu shetani ni kiumbe naye hawezi
kutokuwa na mpaka katika maajabu yake ya kughilibu wanadamu na pili kwa sababu
Yesu ameshinda na kumpiga bao. (Mt 12:29 na Ufu 20: 1-10). La sivyo, Yesu angekuwa
amefanya kazi ya Pwagu na Pwaguzi. Tena tusisahau kwamba ni siku hizi tunapofaidi
ile miaka 1000 ya utawala pamoja na Kristo, yaani wakati ule ambapo shughuli na
shetani zilipopunguzwa kabisa. Unajua sisi Wakatoliki hatutazamii utawala wa miaka
1000 pamoja na Kristo kama Walokole au Waprotestanti. Wao wanautazamia utawala
huo kwa namna ya pekee na wanasubiri utaanza siku fulani hapo siku za mbele. Wapi
na wapi !9 Uoga mara zote unaanzia kichwani, na baada ya hapo huleta hisia nyingi za
uoga na kujikuta watumwa wa uoga hewa.

Kumtafuta shetani mpaka kwenye “mashuka’’ ni upagani. Kumtafuta pepo mpaka


kwenye kuta na dali za nyumba zetu ni kupungukiwa imani kwa ulinzi wa Bwana
wetu Yesu Kristo. Hii ni dalili wazi kuwa Kristo hatujamwalika katika maisha yetu na
familia zetu. Tungeweza kusema, kizazi hiki kina mnadi pepo, hivi kwamba pepo
amesababisha hata ajira kwa wachungaji wasakatonge. Nenda kwenye makongamano
mengi ya kilokole utakuta pepo anawindwa mpaka “kwapani’’. Nenda kwenye vikundi
vya sala Karismatiki ambayo haijatulia hivyo hivyo utawakuta wanalialia kama
9
TITUS AMIGU, HOFU JUU YA MAPEPO NA MAJINI, Mafundisho ya Mkopo, (Kitabu no.5)
makinda ya ndege. Yote hayo ni mahangaiko ya kutaka wepesi wa maisha. Ni
mahangaiko ya kutaka majibu ya haraka haraka kutoka kwa Mungu wetu
asiyeshindwa.

Kwavile maisha yanatuchachafya tunataka kila tatizo na mahangaiko yetu yajibiwe na


mikesha ya maombi. Kwa vile maisha yanatuchachafya tunataka suluhisho zake ziwe
ni kulialia na kusaka miujiza hewa kwa wachungaji “feki’’. Utawasikia watu wakilialia
na kuimba kuwa Bwana “atende miujiza,’’ “Bwana anajibu maombi.’’ Yesu Kristo kwa
mateso, kifo na ufufuko hiyo yote ni muujiza tosha. Unataka uamini kama ni miujiza
mpaka utembelee ulimi!
Kwavile, hata uchumi wetu nao si rafiki, wavivu wamemgeuza Mwenyezi Mungu
kuwa “Saccos’’ na kujikuta sala zimewabwetesha watu wakikimbia kazi
ngumungumu. Wamegeuza sala kuwa panadol. Kizazi chetu, sehemu kubwa ya vijana
wengi hawapendi kuishi vijijini. Wengi hukimbilia mjini na kujikuta hawana kazi,
unawakuta wengi wako jobless. Watu “wakidijitali’’ hawataki kujiumiza. Hawataki
kuumiza kichwa. Hawataki kazi za suluba. Wamejilealea kimayaimayai.

Mtakatifu Augustino, anatuambia kwa maneno ya busara kuwa yeye aliyekuumba


pasipo wewe hawezi kukukomboa bila wewe. Mkristo hata usiye mkristo jikomboe na
dhana za kubweteshana kuwa kila ugonjwa ulionao au unakusumbua ni pepo.

Kimsingi, jina walilopewa malaika waovu hujulikana kama “shetani,’’ likimaanisha


“Lusifa’’ au ’’ Lusifero’’. Ndiye kiongozi wa mashetani yote. Kama tunavyosoma
katika Maandiko Matakatifu (Mat 25:41) inayotujuza Shetani na malaika wake. Kumbe,
Lusifa ana wafuasi wake na mashetani wenzake.

Shetani aliye pepo ametajwa sehemu nyingi katika maagano yote, Agano la kale na
Agano jipya. Shetani ameoneshwa ubaya wake dhidi ya mwanadamu tangu kitabu cha
Mwanzo mpaka kitabu cha Ufunuo. Kanisa Katoliki limetoa mafundisho juu ya uovu
wa shetani aliye pepo mwovu. Mafundisho hayo tunayapata katika Mtaguso wa Nne
wa Laterano, Mtaguso huo unasema kwamba, Mwenyezi Mungu aliumba viumbe wa
aina mbili, vitu vya Roho na vingine vya mwili, ndio kusema malaika, dunia,
ulimwengu na mwisho mwanadamu aliyeumbwa mwili na Roho. Mtaguso unaendelea
kusema;

“Diabolus enim et alii daemones a Deo quidem natura create sunt boni, sed ipsi per se facti
sunt mali.” Maneno haya ya kilatini yakimaanisha kwamba, “Kwa asili haya
tuyaonayo, mintarafu Shetani na mashetani mengine, yaliumbwa na Mungu hapo
awali wakiwa ni malaika wema. [Hapo mwanzo waliumbwa na Mungu wakiwa ni
malaika wema, wao [mashetani] ndio waliojifanya kuwa waovu wenyewe. Japo Mungu
tangu awali aliwaumba wakiwa ni malaika wema”].10

Maneno hayo, naomba yaeleweke vizuri kwamba Mwenyezi Mungu aliumba malaika
wema. Kukengeuka kwao ndiko kulikowafanya wapoteze utakatifu na kuwa
mashetani. Hivyo basi, baada ya kukengeuka kwa malaika hao wazuri wakawa malaika
wabaya yaani “maibilisi’’, na hapo yakawa maadui wa Mungu na mwanadamu. Uadui
wa shetani ulipanuka kwa Mungu na kwa mwanadamu. Kwa kutambua uadui huo wa
shetani dhidi ya marafiki wa Mungu wote. Mwenyezi Mungu ametengeneza silaha za
kivita dhidi ya shetani. Neno la Mungu linatuhamasisha kuwa tumpinge shetani naye
atatukimbia (Rejea). Mwenyezi Mungu anatuambia tubaki imara tukimpinga shetani
kwani ni lazima tukeshe, shetani huzunguzunguka akitafuta mawindo kama simba ili
atung’ate (Pet).

Ieleweke kuwa mwanadamu alitenda dhambi kwa ushawishi wa shetani na hivi katika
ulimwengu ujao watenda dhambi au wenye dhambi wataadhibiwa milele wao na
shetani pia. Pamoja na wanaokengeuka kwa malaika hao waasi kuwa mashetani
yalibaki na “roho’’.

KIBURI

‘’ Kiburi hupofusha akili za mwanadamu’’ Simon R.Liberio (Mwandishi wa


Kitabu hiki)

Kiswahili chatuambia kwamba kiburi ni ugumu wa kichwa unaomfanya mtu akaidi


jambo au ushauri au ang’ang’anie msimamo wake hata kama hauna misingi mizuri.Ni
10
KENT WILLIAM, The Catholic Encyclopaedia, Devil, vol.4. ,New York, Robert, Appleton Company.
ukichwa ngumu. Ni kinyume cha unyenyekevu. Kiburi kinaweza kusonga mbele kwa
namna mbili tofauti na kugeuka na kuwa makossa mengine. Kwa upande mmoja
kiburi huweza kusonga mbele kwa ugumu na kuwa ukaidi wa wazi, ubishi wa moto na
hatimaye kuwa ugomvi na ukatili.Kumbe kwa upande mwingine kiburi huweza
kusonga mbele kwa ulaini na kugeuka kuwa majivuno na majigambo. Kiburi ni
kujikuza kutokana na lugha mama katika misamiati ya Lugha mama ya Biblia
Takatifu yaani Kiebrania.Misamiati hiyo ya kiburi kwa kiebrania ni kama ataq, gaal,
geah,geeh, gaavah, gaon, geuth, geva. Kigiriki kinakiita kkiburi kuwa ni hyperephania,
neno ambalo maana zake ni mbili; Kiburi na Majivuno.11

Msomaji wangu, neno Kiburi si geni katika maisha yetu ya kila siku. Naomba tutupie
darubini yetu kwenye Kamusi Sanifu ya lugha ya Kiswahili (TUKI). Kamusi ya
Kiswahili, inataja neno Kiburi kuwa ‘’ni hisia za mtu kujiona kuwa yeye ni bora au
mkubwa kuliko wengine ‘’. Kiburi kimefananishwa na maneno kama majivuno,
ujeuri.12 Katika jamii za wakristo, mfano wa watu waliojaa kiburi ni pamoja na wazazi
wetu wa kwanza Adam una Eva. Hutajwa kama waliobebeshwa kiburi baada ya
ushawishi wa mwovu shetani (Mwanzo 3). Pia, wakristo tuseme Wakatoliki huamini
kuwa dhambi ya asili ndio kiburi . Mungu alimwumba mtu kwa sura yake na
akamfanya rafiki yake. Kama kiumbe cha kiroho,mtu hawezi kuuishi urafiki huu bila
kujinyenyekea kwa hiari mbele ya Mungu. Hiyo ndiyo maana ya amri aliyopewa mtu
asile matunda ya Mti wa Ujuzi wa Mema na Mabaya ‘’ kwa maana siku utakapokula,
hakika utakufa’’. ‘’ Mti wa ujuzi wa mema na mabaya’’ huonesha kwa mifano mipaka
ambayo mtu, kwa vile ni kiumbe amewekewa asiivuke. Tena aikubali mipaka hiyo kwa
hiari na aiheshimu kwa ujasiri.Mtu anamtegemea muumbaji wake, na yuko chini ya
sharia za uumbaji na taratibu za maadili zinazoiratibu matumizi ya uhuru.13

Kiburi kwa chenyewe ni ukaidi. Na ukaidi hauwezi kuwa kitu chema. Mwenyezi
Mungu aliumba Malaika wema tu. Baadaye mwovu Ibilisi aliwashawaisha Adamu na
Eva. Wakafukuzwa bustanini. Malaika hao kwa kukengeuka wakawa malaikawabaya

11
TITUS AMIGU, BIBLIA NA MAKOSA YA BINADAMU (SEHEMU YA KWANZA), KIBURI, UK.58
12
Kamusi ya Kiswahili Sanifu (TUKI), Oxford, neno Kiburi, Uk. 217
13
Katekisimu ya Kanisa Katoliki No.114, Dhambi ya Asili, Paulines Publications Afrika, Nairobi, Kenya,
Uk 115
ndio mashetani yanayo uchachafya ulimwengu. Kumbe sasa ,ukaidi ni kazi ya
kishetani. Jeuri ni kazi ya kishetani. Kiburi ni kazi ya kishetani. Kiburi kwa bahati
mbaya ni dhambi ambayo sio rahisi kujigundua kama unayo. Ni kwasababu ya ugumu
wa kujigundua,ndio maana imemaliza watu wengi n ahata watu wakubwa nav yeo
vyao. Kuna mambo ambayo kila msomaji ujitathimini kwa KUJIPIMA SOTE KAMA
TUNA DALILI KUBWA SANA ZA MTU MWENYE KIBURI.

1.Ukiona, KILA UKIONYWA UNAKASIRIKA NA KUNUNA AU KUSUSA, HIYO


NI DALILI KUBWA SANA YA MTU MWENYE KIBURI.

Yaani unaona karipio au onyo badala ya kuona tatizo lako, huwezi kujizuia
KUKASIRIKA AU KUNUNA UKIONYWA.

2.Ukiona, KILA MKIKOSANA NA MTU, HUONI KOSA LAKO, UNAONA


MAKOSA YA MWINGINE TU, HIYO NI DALILI KUBWA SANA YA MTU
MWENYE KIBURI.

- Kiburi siku zote NI KIDOLE KUKUONESHA KOSA LA MWINGINE.

-Nilichojifunza, kwenye kila wawili au zaidi kukosana na kutokuelewana. Kila


mmoja ana mahali pa kujirekebisha kwa kujikosoa mwenyewe.

3. Ukiona, KILA UNALOFANYA, UNATAKA KUJILINGANISHA NA WENGINE,


AU KILA WANACHOKIFANYA UNAJILINGANISHA NAO, HIYO NI DALILI
KUBWA SANA YA MTU MWENYE KIBURI.

- Kiburi siku zote KINATAKA WEWE UJIONE UKO JUU YA WENGINE.

Wewe mzuri zaidi ya wengine.Wewe msomi kuliko wengine. Wewe mjuaji kuliko
wengine. Unapesa kuliko wengine. Unafundisha vizuri zaidi kuliko wengine. Wewe
ndiye unayehubiri vizuri Zaidi yaw engine. Wewendiye mwenye vitu vizuri tu Zaidi
ya wengine. Wewe ni mwema sana kuliko wengine.

4. Ukiona, KILA UNALOFANYA, UNAFANYA KWA LENGO LA KUSHINDANA.

- Unafanya jambo zuri ndio, lakini adhma (motive) yako ni mashindano, hata kama
hujasema hivyo.

- Unafanya ili kumshinda Fulani hata kama Fulani hajui, yaani utoshelevu wako wa
ndani sio kutimiza jambo Fulani, bali ni kugundua KWA KUTIMIZA HILO
UMEMSHINDA FULANI.
5. Ukiona, UNAPENDA KUSIFIWA KWA KILA UNALOLIFANYA, Kwa lugha
nyingine KUTAMBULIKA (RECOGNIZED) na KUSIFIWA KATIKA KILA KITU
(APPRECIATED). Sijambo baya kabisa, lakini ukiona ukikosa hicho kitu unakosa
amani kabisa na unatumia gharama yoyote utambulike na kushukuriwa. HICHO NI
KIBURI KINACHOKUSUKUMA.

6. Ukiona, KILA ZURI UNALOLIFANYA SIRINI, UNATAKA LIJULIKANE NA


WATU HATA KAMA SI MUHIMU KWAO na si kwa lengo la KUJIFUNZA, hiyo ni
dalili ya KIBURI.

- Ukisali, hauridhiki mpaka watiu wajue kuwa ulisali, UKIFUNGA mpaka watu
wajue kuwa ulifunga au huwa unafunga. UKIFANYA JAMBO ZURI KWA MUNGU
WAKO, mpaka watu wajue ndio unasikia kuridhika. Kinachokusukuma ndani ni
KIBURI.

7. Ukiona, HAUKO HURU (COMFORTABLE) KABISA KUTUMIA LUGHA YA


PAMOJA .Kwa mfano.Tutajenga Kanisa Jipya.Tutakarabati soko. Tumekamilisha
zoezi la kujikinga na ugonjwa wa Corona. UNAPENDA ZAIDI KUTUMIA LUGHA
YA BINAFSI.Kwa mfano. Nitajenga Kanisa. Nitakarabati soko. Nimekamilisha zoezi
la kujikinga na ugonjwa wa Corona (COVID 19). UNAPOONGELEA MAMBO AU
UMILIKI WA VITU, hiyo yaweza kuwa dalili ya KIBURI.

- Hupendi kutumia lugha kama vitu vyetu, jambo letu, huduma yetu sisi n.k.
Unapoongelea jambo ambalo na wengine wana mchango hata kama ni mdogo
sana,hasa kama wewe ni mwanzilishi wa jambo au nuna mchango mkubwa juu ya
jambo hilo.14

SIFA NA TABIA 10 ZA MTU MWENYE KIBURI

1.Hupenda kujulikana na wengine wasijulikane.

2.Anapenda kusikilizwa ila yeye hapendi kusikiliza wengine. Kutoka 5:2, ‘’ Farao
akasema,’’Bwana ni nani hata nisikilize sauti yake na kuwapa Israeli ruhusa waende
zao’’ Mimi simjui Bwana, wala sitawapa Israeli ruhusa waende zao’’. Hii ni roho ya
kiburi na huyu farao alishushwa.

Pia, Methali 12:15, inasema ‘’Njia ya mpumbavu imenyoka machoni pake mwenyewe;
Bali yeye aliye na hekima husikiliza shauri’’.

14
Kwa msaada wa Mtandao wa Kijamii (Facebook) , Makala, Mkristo Mtakatifu katika kushinda KIBURI.,
26.04.2020
3.Hapendi kushauriwa na wengine ila yeye anapenda kushauri wengine. Mithali
29:1-2, ‘’Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, atavunjika ghafla, wala hapati
dawa. Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi, Bali mwovu atawalapo, watu
huugua.”

4.Hapendi kukosolewa, ila yeye hupenda kukosoa kwa kila jambo. Mithali 13:10,
inasema, ‘’Kiburi huleta mashindano tu, Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana’’.

5. Anapenda kutiwa moyo lakini yeye hawezi kuwatia moyo wengine. Mtu kama
huyu akiugua anapenda watu wamtembelee na kumpelekea zawadi lakini yeye
hajawahi kumtembelea mgonjwa hata mmoja. Hii ni roho ya kiburi.

6.Anapenda kulaumu wengine ila yeye hapendi kulaumiwa.

7. Hupenda kudharau wengine lakini yeye hapendi kudharauliwa. Mtume Paulo


kwa (Wakolosai 3:13 – 14). ‘’Mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu
ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi. Zaidi ya hayo yote
jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu. Pia, Mithali 14:21 inasema ‘’Amdharauye
mwenzake afanya dhambi, bali amhurumiaye maskini ana heri.

8.Hudai heshima kwa nguvu lakini yeye hataki kuheshimu wengine. Mithali 3:34 -35
inasema ‘’Hakika yake (Mungu) huwadharau wenye dharau, Bali huwapa
wanyenyekevu neema. Wenye hekima wataurithi utukufu, Bali kukuzwa kwa
wapumbavu ni fedheha’’. Na Pia Mithali 14:15 nayo inasema ‘’ Mjinga huamini kila
neno , Bali mwenye busara huangalia sana aendavyo’’.

9.Hupenda kumiliki mali isiyo yake. Ndugu msomaji hata fungu la kumi ni la
MUNGU hivyo kuacha kutoa zaka na matoleo mengine Kanisani ni kumwibia
MUNGU. Malaki 3:8 – 9, inasema ‘’Je mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi
mnaniibia mimi, Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia
zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana, maana mnaniibia mimi, naam, taifa
hili lote.’’

10. Hufurahi kuwaonea wengine na kuwasimanga lakini yeye hataki kuonewa wala
kusimangwa. Obadia 1:12, ‘’Lakini usiitazame siku ya ndugu yako, siku ya mashaka
yake, wala usisimange juu ya wana wa Yuda siku ya kuangamizwa kwao; wala
usinene maneno ya kiburi katika siku ya shida yao’’. Ndugu msomaji hata shetani
aliangushwa kwa sababu ya kiburi. Maana alisema nitafanana na MUNGU. Na kwa
sababu ya kiburi chake alishushwa. Nabii Isaya 14:14 – 15,’’ Nitapaa kupita vimo
vya mawingu, Nitafanana nayeye Aliye juu. Lakini utashushwa mpaka kuzimu;
mpaka pande za mwisho za shimo.15

1. KIBURI KITOKANACHO NA OFISI, CHEO NA UONGOZI

Hiki ni kiburi kitokanacho na ofisi ambayo mwanadamu anakabidhiwa. Hiki ni kiburi


kitokanacho na ngazi au cheo katika jamii. Maandiko Matakatifu yanasema mwanangu
uwe mnyenyekevu kadiri unavyofanikiwa. Maandiko Matakatifu yamekemea kiburi
miongoni mwa wanadamu (Mithali 16:18 -19).
Wapo watu wapatapo vyeo huwasahau wenzao na kubadilika. Hao huwa akina Nicolo
Machiavel wa Italia. Ndio kusema hupoteza unyenyekevu(simplicity). Kundi la watu wa
namna hii hujiona wamefika mwisho. Hukosa unyenyekevu.Hutaka waonwe kama
akina Mao Ze Dong wa uchina. Waonwe kuwa ni ‘’nusu mungu’’. Tunaalikwa kuwa
wanyenyekevu sana katika uongozi na madaraka tuliyoaminishwa na Mungu na watu.
Mwanafalsafa Plato anasema ‘’Si kila mtu anaweza kuwa kiongozi.Kiongozi anapaswa
afahamu maana ya uongozi. Na anaongezea kwa kusema kuwa ili uwe kiongozi unapaswa
kuwa mwanafalsafa. Unapaswa uone mbali kuliko wale unaowaongoza. ‘’Kadiri unavyofahamu
jambo ndivyo unavyfanikiwa ‘’ alisema Robin Sharma mwandishi wa Vitabu vingi
kikiwemo ‘’Kiongozi asiye na Cheo’’(The Leader Who had no Title).
Uongozi ni dhamana, kwa mwanafalsafa Socrates anasema ‘’ moja ya sifa za msingi za
kiongozi ni ‘’umoja’’ miongoni mwa wale anaowaongoza’’.Kiburi katika uongozi hutawanya
umoja. Uongozi ni haki yako ya kuzaliwa alisema Mwandishi nguli mkanada nimpendaye
Robin Sharma.
Pia, ukipenda kuongoza vema tumia njia ya kugawa wajibu kama vile unatoa
pendekezo. ‘’Kwa asili mwanadamu hapendi kupewa maelekezo kama amri anaweza kutimiza
wajibu huohuo kwa kuwashirikisha wale unaowaongoza kwa kuwauliza mnaonaje hili jambo
tulifanyeje. Mnaonaje tukifanya hivi, natumai mambo yatakwenda vizuri’’. Njia hii ya kugawa
wajibu aliishauri Mwandishi nguli Dale Carnegie katika Kitabu chake maarufu kiitwacho
HOW TO WIN FRIENDS AND INFLUENCE PEOPLE (NAMNA YA KUWASHIKA
MARAFIKI NA KUWAVUTIA WATU).

15
Kwa njia ya Mtandao wa Kijamii (Facebook) JOHN SHABANI, MAFUNDISHO,03.05.2020
2.KIBURI KITOKANACHO NA MAFANIKIO

‘’Jamii haipendi mtu mwenye kiburi,jamii inapenda mtu mnyenyekevu’’.


Simon R. Liberio (Mwandishi wa Kitabu hiki)

Kamwe usiwabeze watu kutokana na mafanikio yako. Kamwe usiwadharau wenzako


kwa ‘’kutusua ‘’ maisha. Katu usijione kuwa wewe ndio kila kitu. Maandiko Matakatifu
yanasema wazi ‘’
Mafanikio ni haki ya kuzaliwa ya kila mwanadamu. Hakuna duniani aliyezaliwa kuja
kushangaa mafanikio ya wenzake.Kila mmoja ana haki ya kufanya vizuri. Kila mmoja
anapaswa ajione kuwa hakuna atakaye muwakilisha katika kutimiza ndoto zake. Ni
kweli kila mmoja ni wa pekee. Kila mmoja amepewa mzigo wake aubebe vizuri na
kuufikisha salama hapa duniani na kurudisha ripoti iliyokamilika kwa Mungu Baba.
Kila mmoja wetu hapa duniani amepewa kibarua chake lazima akifanyie kazi. Hapa
duniani hakuna kuwakilishana. Ndio maana baada ya Kitabu changu nilichokiita
USIKATE TAMAA, nitatoa Kitabu kingine kinachoitwa ULIKUJA HAPA DUNIANI
KUTAFUTA NINI?. Ni Kitabu kikubwa ambacho nimekwisha kukiandika ninamalizia
kuhariri ili nacho kiweze kukubadilisha mawazo chanya, fikra chanya, mitazamo
chanya kwa maendeleo yako mwenyewe. Usikikose Kitabu hicho ili kikukumbushe na
kukupatia hamasa na changamoto ili ujue nafasi yako katika ulimwengu huu wenye
Mazuri mengi na Mahangaiko mengi ya kukatishana tamaa kwingi.

Marthin Luther King Jr. muamerika mweusi na mwanaharakati wa haki za watu weusi
na waliokandamizwa kwa ubaguzi, unyanyasaji huko Amerika aliwahi kusema ‘’
Wakati mwingine inafika hatua unajitetea mwenyewe kwa kujisemea mwenyewe kwani hakuna
atakaye kutetea wala kukusemea ‘’. Je, tusifurahie mafanikio katika Maisha hapa duniani?
Kuna sababu ya kufurahia mafanikio yetu na ya wenzetu. Tuna kibarua kikubwa cha
kunyenyekea. Tuna kibarua cha kuwa watu wa msaada kwa wengine. ‘’Hakuna masikini
duniani’’ alisema Mt.Therezia wa Calcuta, ‘’umpatie mwenzako tabasamu, hiyo ni zawadi
kubwa’’. Mafanikio ya mwanadamu yawe kwa faida ya mwanadamu mwenzake.
Tusifiche vipaji vyetu wala tusiue vipaji vya wenzetu kwa wivu. Robin Sharma
mwandishi nguli na maarufu Mkanada, aliyeandika vitabu kama ‘’Who Will Cry when
you die?’’ (Nani atakayelia siku utakapofariki) , na vingine kama ‘’A monk who Sold
his Ferrari’’, ‘’The Leader Who had no Title’’ anasema, Asilimia karibu 95 ya mambo
tunayoyafanikiwa yametokana na michango ya watu. Penye mafanikio yako, kuna wenzako
wamekufikisha hapo. Uwe mpole usiwaringie watu.
-Tutamkumbuka Shakespear kwa uandishi wake mahili.
- Tutamkumbuka Michelo Angelo, mcharaji matata wa picha , vinyago na msanifu
mbobezi wa majengo muitaliano.
- Tutamkumbuka Ronaldihno Gaucho, na Ronaldo De Lima mbrazili, Christiano
Ronaldo wa Ureno, Lionel Messi wa Argentina ,Samuel Etto wa Kameruni, Didie
Drogba wa Ivory Coast, Maradona Diego wa Argentina, Zinedine Yazid Zidane wa
Algeria kwa asili, Abed Ayew Pele Mbrazili mweusi, Samatta mtanzania wote na
wengine wengi kwa umaarufu katika soka.
-Tutamkumbuka Jane Goodall mwingerezi mtafiti wa tabia za wanyama kwa utafiti
wake wa miaka 50 nchini Tanzania na kuwa Profesa wa utafiti wa tabia, maisha ya
Wanyama waitwao sokwe katika Mbuga ya Sokwe Mtu huko Gombe Mkoani Kigoma,
Tanzania na kwingine kwingi Afrika na dunia.
- Profesa Marie mwanasayansi aliyegundua ULTLA SOUND atakumbukwa daima.
- Mwanasayansi Thomas Edson atakumbukwa kwa ugunduzi wa bulb.
- Jean Piaget, Sigsmund Freud, ni wanasaikolojia na wengi wengi ambao ulimwengu
hautawasahau.
- Mark Zubeck atakumbukwa kwa uvumbuzi wa mitandao ya kijamii kama Facebook,
Whatsaap, Twiter nk.
- Bill Gates hatasahaulika katika vichwa vya wat na maendeleo ya ‘’MICROSOFT.’’
- Steve Job, hawezi kusahaulika katika mapinduzi ya maendeleo ya Sayansi na
Teknolojia ya ‘’APPLE’’.
- Fold atakumbukwa kwa kuunda gari la kwanza hapa chini ya jua.
Mimi na wewe unayesoma ninayezungumza nawe kwa njia ya Kitabu hiki nikuulize
tutakumbukwa kwa lipi? Kazi ni kwangu na kwako. Tulikuja duniani kutafuta nini?

Viburi vingingine vinajidhihirisha katika mazingira mbalimbali kama:


Kiburi kitokanacho na urafiki na “bosi’’kiburi kitokanacho na udugu na “bosi’’
Kiburi kitokanacho na umri , Kiburi kwa kukaa ofisini muda mrefu, Kiburi
kitokanacho na elimu kubwa mtu aliyoipata, Kiburi cha kipato kikubwa cha pesa,
utajiri na mali nyingi ,Kiburi kitokanacho na utaalamu wa taaluma fulani ,Kiburi
kinachotokana na kulewa madaraka, Kiburi cha kusahau kesho
Kiburi cha kusahau jana,Kiburi cha kufanya utakavyo.Wengine kwa kiburi hutoa
majibu ya ajabu kama ‘’niache nilivyo’’,“Wewe ni nani kwangu?’’ “Niache
bwana’’?“Unanilisha’’? au “Unanivika’’.

DAWA YA KIBURI NI UNYENYEKEVU


‘’Dawa ya kiburi ni unyenyekevu’’.
- PADRE SIMON R.LIBERIO, MWANDISHI WA KITABU HIKI.

Unyeyekevu ni fadhila na fadhila ni kuwa na mazoea na mwelekeo thabiti wa kufanya mema.


Fadhila ni tabia ya kudumu ya akili, dhamira au vionjo ambayo kwayo mtu aweza kutenda
analotakiwa kimaadili katika nafasi fulani, au kutenda kwa njia sahihi, yaani akiwa na msukumo
wa kufaa.
- Mtakatifu Thomaso wa Akwino
‘’ Unyenyekevu utatuinua pale tutakapojishusha bila shuruti’’
PADRE PASCHAL IGHONDO, VATICAN, ROMA

Unyeyekevu ni fadhila na fadhila ni kuwa na mazoea na mwelekeo thabiti wa kufanya


mema.
Fadhila ni tabia ya kudumu ya akili, dhamira au vionjo ambayo kwayo mtu aweza
kutenda analotakiwa kimaadili katika nafasi fulani, au kutenda kwa njia sahihi, yaani
akiwa na msukumo wa kufaa. Hivyo fadhila hutusaidia kutenda mema kwa wepesi,
kwa urahisi, kwa kudumu na kwa furaha zaidi.
Karibu ndugu msikilizaji wa Radio Vatican, katika tafakari ya Liturujia ya Neno la
Mungu, dominika ya 22 ya mwaka C wa Kanisa, kipindi cha kawaida. Masomo ya leo
yamebeba ujumbe wa unyenyekevu, fadhila ambayo kwayo mtu hujitambua kuwa
hajitoshelezi bali anamhitaji binadamu mwenzake ili amsaidie kujikamilisha na zaidi
sana anamhitaji Mungu aliye ukamilifu wote. Somo la kwanza kutoka kitabu cha
Yoshua bini Sira latufundisha kuwa unyenyekevu upo katika kujua kuwa Mungu peke
yake ni mkubwa na mwenye nguvu na ndiye ukamilifu wote. Mtu mnyenyekevu
hajikuzi mbele ya wengine bali yupo tayari kuwahudumia wote wanaohitaji msaada
wake ndiyo maana anasema, mwanangu, wakati wa kufanikiwa uendelee katika
unyenyekevu; hivyo utapendwa kuliko mwenye ukarimu. Kadiri ulivyo mkuu uzidi
kujinyenyekesha, nawe utapata kibali machoni pa Bwana; kwa maana rehema zake
Bwana ni kuu, na siri yake ni kwa wanyenyekevu.
Somo la pili kutoka waraka kwa Waebrania linalinganisha Ufunuo wa Agano Jipya
na Agano la Kale. Agano Jipya halikufanyika kwa vitisho kama lile la Kale bali katika
utii na unyenyekevu wa Bwana wetu Yesu Kristo, utii na unyenyekevu hata mauti ya
msalaba. Agano hili halikufanyika hapa duniani bali lilifanyika patakatifu mbinguni,
kati ya Mungu Baba na Yesu Kristo, Mjumbe wetu; na tena sisi wakristo tumekwisha
kushiriki maisha ya Kimungu na heri ya Watakatifu kwa Agano hilo. Injili ya leo
ilivyoandikwa na Luka imegawanyika katika sehemu kuu mbili. Sehemu ya kwanza
inatufundisha kwamba tukitaka kuufaidi ufalme wa Mungu lazima tuwe wanyofu,
wanyenyekevu na tutegemee msaada wa Mungu. Kristo anatuasa tusijikweze ili
tusijedhiliwa, bali tuwe wanyenyekevu ili katika unyenyekevu wetu tuweze
kukwezwa. Na sehemu ya pili inatuambia kuwa mapendo ya kweli ni kuwasaidia wale
ambao hawawezi kutulipa kitu chochote. Tukifanya wema kwa maskini, vilema, viwete
na vipofu ambao hawana uwezo wa kutulipa tunakuwa na heri ya kulipwa katika
ufufuo wa wenye haki, yaani kuuridhi ufalme wa mbinguni.
Unyenyekevu ni nini? Unyeyekevu ni fadhila na fadhila ni kuwa na mazoea na
mwelekeo thabiti wa kufanya mema. Mtakatifu Thomaso wa Akwino anasema fadhila
ni tabia ya kudumu ya akili, dhamira au vionjo ambayo kwayo mtu aweza kutenda
analotakiwa kimaadili katika nafasi fulani, au kutenda kwa njia sahihi, yaani akiwa na
msukumo wa kufaa. Hivyo fadhila hutusaidia kutenda mema kwa wepesi, kwa urahisi,
kwa kudumu na kwa furaha. Kuwa mwenye fadhila humaanisha kujisahau mwenyewe
kwa ajili ya upendo wa Mungu unaojimimina kwetu.  Ni kuiga upendo wa Kristo,
kujikana nafsi kabisa na kuwa mwanga wa upendo kwa Mungu na jirani. Mtume Paulo
anapowaandikia Wafilipi anasema, ndugu zangu jazeni fikira zenu kwa mambo mema
na yanayostahili kusifiwa, mambo ya kweli, bora, haki safi, ya kupendeza na ya
heshima" (Wafil. 4:8). Ili kudumu kuwa mkristu mwema lazima kuamua kwa makusudi
kujijengea mazoea yanayoendana na imani.
Mazoea hujenga tabia, mazoea yanayotokana na kurudiarudia hali, mwenendo au
matendo safi na maadilifu. Mazoea yanayoendana na Injili huitwa fadhila. Kama
fadhila nyingine zilivyo unyenyekevu unajengwa kwa matendo mema madogo
madogo ya kila siku pasipokutegemea sifa na mtu yuko tayari kukosolewa anapokosea
na kujirekebisha, mtu huyu daima anajitafakari kila mara juu ya udhaifu wake,
anajikosoa na kujirekebisha na pia yuko tayari kusifia mafanikio ya wengine wala
hajikwezi daima. Faida za kuwa mnyenyekevu. Unyenyekevu ni mama wa fadhila zote,
humfanya mtu kuwaheshimu wengine na kumtegemea Mungu. Unyenyekevu
unampatia mtu kibali cha kuonekana wa maana na wa muhimu na hivyo kupewa sifa
na majukumu zaidi. Ni katika namna hii Yesu anasema, kwa maana kila ajikwezaye
atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa,” Lk 14:11. Kinyume cha unyenyekevu ni kiburi.
Kiburi ni kupenda makuu, kuwa na dharau, kujiona bora kuliko wengine, kupenda
ufahari.
Mwenye kiburi hujikweza hata kwa sifa asizokuwa nazo na kuwadharau wengine,
ana majivuno kuwa yeye ni bora kuliko wengine wote. Mwenye kiburi hayuko tayari
kuwa chini ya Mungu au kuwa chini ya wenye mamlaka halali au wale wanaotawala
na kuongoza kwa niaba ya Mungu katika mambo muhimu na halali (Rum 1:29-32).
Yakobo anasema, mwenye kiburi humpinga Mungu na Mungu anampinga mwenye
kiburi (Yak 4:6) daima anajiona mkamilifu mbele za wat una mbele za Mungu kama
Mfarisayo aliyeenda hekaluni kusali (Lk 18:11-12). Athari za kuwa na kiburi ni kukosa
unyenyekevu. Kiburi ni mzizi mkuu wa dhambi, kwani mwenye kiburi ukaidi
hamuachi salama. Mwenye kiburi hawathamini wengine, mwenye kiburi hamtegemei
Mungu, mwenye kiburi hujiona anajua yote, yeye ndiye kipimo cha ukweli, hivyo
hawezi kutii sheria yoyote. Jamii yenye kiburi, inajiona kuwa inajitosheleza katika yote,
inamwondoa Mungu kuwa ndiye chanzo cha ukweli hasa kuhusu maadili, inajifanya
yenyewe ndiyo chanzo na kipimo cha maadili, inamwondoa Mungu kuwa ndiye lengo
la maisha.
Jamii yenye kiburi haitambui kwamba furaha tunayoihitaji kama binadamu
itakamilishwa kwa kumwona Mungu, kwa kuwa watu wake daima wanaitafuta
furaha ndani mwao, kwa ajili ya hiyo watu wake hawawezi kutenda mema kwa
sababu jamii imeondoa chanzo cha mema. Jamii ya namna hii haiwezi kuwa na furaha
watu wake daima wanaishi katika kilindi cha huzuni. Ndiyo mtakatifu Agustino baada
ya kuikosa furaha ya kweli katika viumbe alimwongokea Mungu na kusema, ee Mungu
umetuumba kwa ajili yako na roho zetu hazitatulia kamwe mpaka pale zitakapotulia
ndani mwako. Yoshua bin Sira anatuambia kuwa, “Msiba wa mwenye kiburi hauleti
kupona, mche wa uovu umepandika ndani yake,” YbS 3:28. Kushindwa kwa wengi
katika maisha na hata kile walicho kadiri ya wito na nafasi zao hutokana na kiburi.
Mshahara wa kiburi ni anguko lako mwenyewe. Kumbe nisichoke kuiomba hekima ya
Mungu kila siku ili iniongoze katika busara. Na “moyo wa busara utatambua mithali,
na sikio sikivu ni tamaa ya mtaalamu,” YbS 3:29. Unyenyekevu utatuinua pale
tunapojishusha pasipo shuruti kwani Yesu anasema, “kila ajikwezaye atadhiliwa, naye
ajidhiliye atakwezwa,” Lk 14:11. Basi tumwombe Mungu atujalie fadhila ya
unyenyekevu ili kwayo tuweze kutambua ukuu wake na kumtegemea yeye. 16

PADRE PASCHAL IGHONDO, MAHUBIRI YA DOMINIKA YA 22 MWAKA C, KIPINDI CHA


16

KAWAIDA CHA MWAKA (KUTOKA UKURASA WA MTANDAO WA RADIO VATICAN,,


VATICAN, ROMA, 27.08.2019

You might also like