You are on page 1of 2

MWISHO USIOTARAJIWA

WIMBO:173 & 110


FUNGU:LUKA 13:7-9.”Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu,tazama
miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu,nisipate kitu,uukate mbona
hata nchi unaiharibu?.Akajibu akamwambia,Bwana,uuache mwaka huu nao,hata
niupalilie,niutilie samadi;nao ukizaa matunda baadae,vema!La,usipozaa,ndipo
uukate.”
 Mungu amefungamanisha onyo la hukumu na ujumbe wa rehema
 Kabla ulimwengu haujapatwa na hukumu za Mungu,maonyo mbalimbali yalitumwa
kupitia wajumbe wa kibinadamu.Katika kila kizazi kumekuwepo na rehema za
Mungu,yaani popote unapopata nafasi ya kusikia ujumbe wa kurejea katika maagizo
kumbuka ni kazi ya rehema za Mungu tu.
 Ndivyo ilivyo kwetu leo kabla ya kumwagwa hukumu ya mwisho bado tumepewa
muda wa Rehema wa kurekebisha Maisha yetu ili yalingane sawa sawa na kanuni za
mbingu.
 Mungu ametoa muda kwa kila mdhambi kutubu na kumgeukia Yeye,lakini bado watu
wanaopewa fursa hizi zote za neema hawajali rehema Zake.
 Leo watu wamekuwa ni wajinga tena wasiojali na wasio na hofu juu ya kile
kitakachowapata wadhambi.
 Ingawa wamepokea karama zote za Roho lakini bado hawana muunganiko na kristo
ambaye wamebeba jina lake.
 Sifa njema ,tabia ya kristo ambayo ni tunda la Roho haionekani katika Maisha yao.
 Lakini Mungu bado amewapatia rehema bali wao hawabebi baraka yoyote,ni
waharibifu wa dunia,wanaoiba manufaa ya watu wengine ambao yangemwinua
Mungu.
 Lakini Mungu katika rehema yake kuu hajawakata,bali amewapatia nafasi nyingine
ya kufanya matengenezo ya tabia zao.

“Na shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti,basi kila mti usiozaa matunda
mazuri hukatwa na kutupwa motoni.”(Mathayo 3:10)

Mkazo wa somo: 1Wakorintho 6:9-10 na Wagalatia 5:19-21

 Mashahidi wa uongo
 Wanaonyanyasa maskini
 Wasiotaka kulipa madeni/matapeli
 Wanaowazuia watu kufanya ibada kwa Mungu
 Wanaokula rushwa
 Wasiotunza miili yao
 Wasengenyaji wote
 Wanaoimba nyimbo za upuuzi/dhihaka (zaburi 69:12,Amosi 6:5)
 Wezi wote wa zaka na sadaka
 Wachawi
 Wazinzi,waasherati na mashoga
 Mafisadi wote
 Wazushi wote
 Walevi na wasio na kiasi wote
 Wauaji
 Wanaopenda mizaha wote
“Katika kila kizazi nuru na fursa hutolewa kwa watu,wakati wa matazamio ambao
wanaweza kufanya maafikiano na Mungu.Lakini kuna kikomo cha neema hii.Rehema
inaweza kusihii kwa miaka mingi na ikakataliwa,na unakuja wakati ambao rehema ya
Mungu hukoma kuita.Moyo hufanywa kuwa mgumu na unakoma kuitikia sauti ya
Roho Mtakatifu.Ndipo sauti ya upole ya kuwasihi wenye dhambi watubu
hukoma.”(Tumaini la Vizazi Vyote,sehemu ya pili,toleo la Kiswahili,Uk 192)

You might also like