You are on page 1of 10

KULIPA FADHILA

Somo la 10 kwa ajili ya Machi 11, 2023


“Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika
BWANA tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya
taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao” (Ufunuo 14:13)
Tunapokaribia mwisho wa miaka yenye matatizo, tunaweza kuwa
na mashaka juu ya Maisha yetu ya baadaye. Ellen G. White
alituachia ushairi: “Wanapaswa kuweka pembeni tashwishwi na
mizigo,na kuwa na furaha kwa kadri iwezekanavyo, na kukomazwa
kwa ajili ya mbinguni.” (TC1, p. 424).
Kwa kawaida tunafikia kiwango hiki maishani
tukiwa na rasilimali Zaidi kuliko tulizokuwa
nazo wakati tukizaliwa. Tuzifanye nini? Kama
wasimamizi, tunawezaje kumrudishia
mwenye navyo?
Kurudisha vilivyo vya Mungu
Kujiandaa na maisha ya baadaye
Furahia mibaraka yako
Je ni lini tunapaswa kurudisha?
Kurudisha kwa kuchelewa
Faida za “sasa”
KURUDISHA VILIVYO VYA MUNGU
“Lakini Mungu akamwambia, ‘Mpumbavu wewe! Usiku huu uhai wako unatakiwa.
Sasa hivyo vitu ulivyojiwekea akiba vitakuwa vya nani?’” (Luka 12:20)

Mali alizokuwa nazo yule tajiri zinaongezeka. Alijenga maghala


makubwa Zaidi na akaridhika. Pensheni yake ilikuwa hakika! Je kisa
hiki kilikuwa na shida gani (Luk. 12:13-21)?
Matendo yake hayakuwa na shida. Kama Yesu alivyoonyesha, shida
ilikuwa ni uchoyo wa yule mtu. Hakuwa tayari kushiriki kile Mungu
alichompatia na watu wengine (Luk. 12:15).
Kwa kadri tunavyokuwa na hali nzuri
ya kimwili na kiakili, tunakuwa
tunatenda vema kila ambacho
Mungu ameweka mikononi mwetu:
nguvu, talanta, rasilimali…
Vitu vyote hivi lazima virudishwe
kwa Mwenye navyo. Kwa namna
gani?
MAANDALIZI YA SIKU ZA BAADAYE
“Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi […]” (Mithali 13:22)

Mstakabali wetu ni wazi, “Kwa maana hatukuja na kitu


duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu”
(1Tim. 6:7). Je tufanye nini na vitu tutakavyo viacha?

Bado ni vya Mungu, haijalishi ni kiasi gani. Biblia


inatutia moyo kuhamishia uwakili wetu kwa
watoto wetu na ndugu (Mith. 13:22; 1Tim. 5:8).
Kama hakuna warithi, tunapaswa kuviachia kanisa.

Katika nchi zingine, urithi huwa ni kwa watoto bila swali.


Kama sheria za urithi nchini mwako hazikubaliani na
mipango yako, unapaswa kuandika wosia ili mali zako
ziende kwa watu sahihi.
KUFARAHIA MIBARAKA YETU
“Kwa maana mali haziwi za milele; na taji je! Yadumu tangu kizazi hata kizazi” (Mithali 27:24)

Je umepokea mibaraka kutoka kwa Mungu? Vifurahie! Usiviharibu, vitumie kwa hekima
(Mith. 27:23). Mpe Mungu zaka na sadaka zako (Kumb. 12:11). Timiza mahitaji ya nyumba
yako (Mith. 27:27). Usisahau walio wahitaji (Yakobo 1:27).

Inakuwa juu yetu sasa kuweka sehemu ili vile tulivyo barikiwa navyo kuwa sehemu ya
kuwabariki watu wengine na kusukuma mbele kazi ya Mungu.
“urithi unaokufa ni mbadala wa ukarimu hai. Watumishi wa Mungu wanapaswa
kutengeneza wosia kila siku, katika matendo mema na kutoa sadaka ya hiari kwa Mungu.”
(Counsels on Stewardship, p. 326).
LINI TUNAPASWA
KURUDISHA?
KURUDISHA KULIKOCHELEWA
“tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya
muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.” (2 Korintho 4:18)

Tunapokuwa watu wazima, tunaelekea kushikilia sana mali


zetu. Kamwe haitoshi, jinsi unavyokuwa Tajiri ndivyo
unavyotaka kuwa Tajiri zaidi (Mhu. 5:10). Huu ni mtego kutoka
kwa Shetani kututenga na Mungu.
Biblia inatutia moyo kamwe tusiweke matumaini katika utajiri
(1Tim. 6:17), lakini turidhike na vile tulivyo navyo (Mith. 30:8).

Baadhi ya watu wanaweza kutokumpa Mungu


wanavyoweza leo kwa sababu ya woga wa kutokuwa navyo
wakati wa uzeeni. Tunawanyima watu mibaraka ambayo
wangeweza kuwa nayo sasa, na tunajinyima wenyewe
mibaraka yetu wenyewe.
FAIDA ZA “SASA”
“Lakini mkumbuke Bwana Mungu wako, kwa kuwa ndiye akupaye
nguvu za kupata utajiri […]” (Kumb 8:18 )
Mungu anamiliki kila tulichonacho (Zab. 24:1; Waeb. 3:4). Anatupa uzima,
uwapo, na nguvu za kupata tulivyo navyo.
Je ni faida zipi hupatikana tunaporudisha kwa Mungu wakati tukiwa hai?

Mtoaji anaweza kuona matokeo ya mchango wake: Jengo jipya kwa ajili ya kanisa,
kijana akisoma chuokikuu, kampeni ya injili…
Mtu anayepokea au huduma inaweza kufaidika leo, hitaji linapokuwa kubwa
Inatoa mfano mzuri wa ukarimu na kuwapenda wengine
Inapunguza athari ya kodi ya utajiri
Inakupatia uhakika kuwa mchango wako unakwenda kunakostahili, kwa kuwa hakuna
mahakama au ndugu walalamishi kuhusishwa
Inaonyesha kuwa moyo wa mtoaji umegeuzwa kutoka katika ubinafsi kwenye ukarimu
Tunaweka hazina zetu Mbinguni
“kama wao [wenye umri mkubwa] watachukua nafasi
ambayo Mungu angewapatia, siku zao za mwisho
zinaweza kuwa bora na zenye furaha. Wale walio na
watoto ambao kwa uaminifu na utendaji wao wa haki
wanayo sababu ya kuwaambia siri zao, waache watoto
wafanywe kuwa na furaha. Wasipofanya hivyo, Shetani
atapata mwanya wa kuwatawala kwa sababu ya kukosa
nguvu/uwezo wa kiakili. Wanapaswa kuweka kando
mashaka na mizigo, wautumie muda wao kuwa na
furaha kwa kadri iwezekanavyo, na kukomazwa kwa ajili
ya mbinguni.” E. G. W. (Testimonies for the Church, book 1, cp. 77, p. 423)

You might also like