You are on page 1of 28

SEHEMU YA KWANZA

KUCHOCHEA UBUNIFU WA MKIRISTO KIUCHUMI


Maana ya Mkristo
Mkristo ni mtu aliyemwamini Yesu Kristo na kumpokea au kumfanya Bwana na Mwakozi
wa Maisha yake.
Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako
ya kuwa Mungualimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata
kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. (Warumi 10:9-10)
Maana ya Uchumi
Ni namna ya kutumia rasilimali (resources) zilizopo au chache (scarce) ili kutatua mahitaji na
matakwa (neends and wants) kwa Maisha ya mtu, jamii na taifa kwa ujumla.Ni mapenzi ya
Mungu sote tuyafurahie Maisha yetu aliyotupa yeye hapa duniani kama alivyotuhaidi
Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi (isaya 1:19)
Rasilimali zote tunazozihitaji kwa ajili Maisha mazuri ya baraka tunazo hapa hapa. Rasilimali
hizo ni pamoja na: 1. Watu 2. Mali gafi 3. Pesa na 4. Muda. Kama Mkristo unahitaji namna
au jinsi au kanuni za Ki-Mungu kufikia malengo yako kwa kutumia rasilimali hizo.
UCHAMBUZI WA YAKOBO KIUCHUMI
Tujifunza siri na kanuni za kufanikiwa kiuchumi kwa maisha ya tajiri mmoja, aliyeandikwa
katika Biblia, na jinsi alivyofanikiwa sana kimaisha na kiuchumi, japo alianza maisha kwa
shida na taabu. Mtu huyu tajiri anaitwa Yakobo. Habari hii utaipata katika kitabu cha
Mwanzo 28:1-5; 29: 13-30; 30:25-43; 31:1-3; 32:1-18

UCHAMBUZI WA YAKOBO KIUCHUMI


Yakobo alipomkimbia ndugu yake Esau, alifika kwa mjomba Labani akiwa na fimbo tu,
lakini baada ya kukaa huko kwa muda, alirudi katika nchi ya Baba zake akiwa tajiri mkubwa
mwenye wafanyakazi 1,200 (Matuo mawili = Makundi mawili ya watu 600) Soma Mwanzo
32:9-12. Fikiri mwenyewe, mtu mwenye wafanyakazi 1,200 alikuwa ana wanyama wangapi?
Thamanisha mali zake kwa fedha ya sasa. Utakapokwenda kuisoma habari hii, utaona jinsi
Yakobo alivyokuwa tajiri, kwa maana alikuwa na uwezo wa kutoa zawadi kwa mtu, kiasi cha
punda 200, farasi 200, ngamia 200, ng’ombe 200, kondoo 200 na mbuzi 200. Utajiri huu kwa
lugha ya sasa; Punda 200 (kiuchumi, hii inakadiriwa kuwa ni sawa na magari madogo ya
mizigo (pickup) 16; yaani punda 12 wanaweza kubeba mzigo wa pickup 1). Kondoo 200 ni
sawa na maduka 4 ya nguo, ngamia 200 ni sawa na malori madogo ya mizigo 16, farasi 200
ni sawa na pikipiki 50.
Unaweza kuona jinsi Yakobo wa Isaka alivyokuwa tajiri. Mtu anayeweza kukupa zawadi ya
pikipiki 50, maduka 4 ya nguo, malori madogo 16 na magari madogo ya mizigo (pickup) 16;
yeyé anabakiwa na kiasi gani cha utajiri? Na kama alianza akiwa mikono mitupu, alitumia

1|Mch. Jofrey Daudi Dibson = Semina ya Uchumi TAG -Bethel Revival


Temple-kwa Ask.Dkt Barnabas & Gladymary Mtokambali (25-29/04/2022
njia gani kufikia katika mafanikio hayo ya kiuchumi? Hata mimi nataka kujua. Utashangaa
kwamba, Biblia inafundisha uchumi kiasi hiki.
SWALI LA KUJIULIZA LEO
KANISA LIKO UPANDE GANI KWA HABARI YA KUSAIDIA JUU YA JAMII
ILIYOIZUNGUKA, JUU YA WILAYA, MKOA TAIFA NA KIMATAIFA? AMBAO
NI WAHITAJI

KANUNI ZA KIBIBLIA ZA UCHUMI MZURI


1. Maono - Kuona Fursa za kiuchumi
Mafanikio hayaji kwa bahati mbaya au nzuri, bali yanapangwa. Ukiona mtu amefanikiwa
kiuchumi, ujue aliona kwanza fursa hiyo na akaichuchumilia na kuifuatilia mpaka
akafanikiwa. Rejea kwa Mjomba Labani = Yakobo alivyokaa kwa mjomba wake aliona
furasa kwa kujishughurisha na kazi moja ya ufugaji hadi akafikia malengo yake.
Labani akamwambia Yakobo, Kwa sababu wewe ni ndugu yangu, basi, je! Unitumikie bure?
Niambie mshahara wako utakuwa nini? Labani alikuwa na binti wawili, jina la mkubwa ni
Lea, na jina la mdogo ni Raheli. Naye Lea macho yake yalikuwa dhaifu, lakini Raheli
alikuwa mzuri wa umbo, na mzuri uso. Yakobo akampenda Raheli akasema, Nitakutumikia
miaka saba kwa kumpata Raheli, binti yako mdogo. Labani akasema, Afadhali nikupe wewe
kuliko mtu mwingine; kaa kwangu. Yakobo akatumika miaka saba kwa kumpata Raheli.
Ikawa machoni pake kama siku chache tu kwa vile alivyompenda. Yakobo akamwambia
Labani, Nipe mke wangu, maana siku zangu zimetimia; niingie kwake. Labani akakusanya
watu wote wa mahali pale, akafanya karamu. Ikawa wakati wa jioni akamtwaa Lea, binti
yake, akamletea Yakobo, naye akaingia kwake. Labani akampa Lea mjakazi wake Zilpa, awe
mjakazi wake. Ikawa, kulipokuwa asubuhi, kumbe! Ni Lea. Akamwambia Labani, Nini hii
uliyonitenda? Sikukutumikia kwa Raheli? Mbona umenidanganya? Labani akasema,
Havitendeki hivi kwetu, kumtoa mdogo kabla ya mkubwa; timiza siku zake saba, nasi
tutakupa huyu naye kwa utumishi utakaonitumikia, miaka saba mingine. Yakobo akafanya
hivi, akatimiza siku zake saba. Naye akampa Raheli binti yake kuwa mkewe. Labani akampa
binti yake Raheli mjakazi wake Bilha, awe mjakazi wake. (Mwanzo 29:15-29)

1. Maono - Kuona Fursa za kiuchumi


Hivyo muombe Mungu akupe kuziona fursa zilizopo. Tafuta kuona mahitaji mbalimbali ya
jamii, huwezi kukosa kuona fursa kadhaa za kiuchumi.

2. Malengo mahususi – Kujua kwa hakika unataka kufika wapi


Ukijua unachotaka si rahisi kuyumbishwa mpaka upate unachokitaka. Hii ni tabia kila
mjasiliamali aliyefanikiwa. Ni muhimu sana kwa mtu kuwa na makusudio ya moyo
(Malengo). Kazi za malengo.

2|Mch. Jofrey Daudi Dibson = Semina ya Uchumi TAG -Bethel Revival


Temple-kwa Ask.Dkt Barnabas & Gladymary Mtokambali (25-29/04/2022
Malengo hufungulia nguvu za Mungu. (Msaada wa Mungu) ‘Nawe utakusudia neno, nalo
litathibitika kwako; na mwanga utaziangazia njia zako’ (Ayubu 22:28)
•Malengo hukupa nidhamu ya kimaisha(Descipline)
‘Pasipo maono, watu huacha kujizuia (yaani hukosa nidhamu, au msimamo huyumba-yumba)
(Mith 29:18).

3. Mipango Mizuri – Kuwa na njia za kukufikisha katika malengo yako


Ili kufikia mafanikio na maisha mazuri, mtu wa Mungu si tu kwamba anahitaji kuwa na
maono na malengo tu, bali pia anahitaji kuwa na mipango mizuri ya kumfikisha katika
maono na malengo yake. Jiulize, ni kwa njia gani nitaweza kufikia kule ninakotamani kufika?
Hizo njia utakazopata, ndio tunaita mipango.
Katika habari hii ya Yakobo, unaona anapanga kuwachukua wanyama wa mjomba na
kwenda nao umbali wa siku tatu (3) na kukita kambi ya mifugo huko. Na utaona anapanga
kukaa huko kwa miaka mitatu (3). Hizi namba unazoziona hapa, ni mipango madhubuti. Ni
mawazo ya mtu aliyefanya uchunguzi wa eneo zuri la kuweka kambi ya mifugo na ni
mawazo ya mtu aliyepiga mahesabu kuona, ni baada ya muda gani atakuwa ameweza
kutengeneza faida.
Mipango mizuri itazaa matokeo mazuri.
Mipango mibaya itazaa matokeo mabaya.
Kwahiyo, tafuta namna ya kutengeneza mipango mizuri, ikibidi tumia wataalam wa mipango.
.

3|Mch. Jofrey Daudi Dibson = Semina ya Uchumi TAG -Bethel Revival


Temple-kwa Ask.Dkt Barnabas & Gladymary Mtokambali (25-29/04/2022
SEHEMU YA PILI
NI MAPENZI YA MUNGU WALOKOLE TUWE TUWE MASKINI?
UTANGULIZI
Napenda kuanza kukuambia ya kuwa si mapenzi ya Mungu uwe maskini. Kwa sababu tangu
kuwekwa misingi ya ulimwengu huu, Mungu hakupanga kuwa watu wake aliowaumba wawe
maskini; bila kujali rangi, kabila, wala taifa.
Nafahamu ya kuwa katika Mathayo 5:3, Yesu Kristo alisema; “Heri walio maskini wa roho;
maana ufalme wa mbinguni ni wao.” Watu wengi wanapousoma mstari huu, wanadhani Yesu
Kristo alisema “Heri walio maskini wa mahitaji ya MWILI; maana ufalme wa mbinguni ni
wao.” Lakini Kristo hakusema hivyo
Mtu maskini maana yake ni mtu mhitaji. Yesu Kristo aliposema “Heri walio maskini wa roho
…….” Alikuwa ana maana ya kusema ‘Heri walio wahitaji wa mambo ya rohoni; maana
ufalme wa mbinguni ni wao. Ndiyo maana aliongeza kusema, “Heri wenye njaa na kiu ya
haki; maana hao watashibishwa" (Mathayo 5:6).
Tunafahamu ya kuwa mtu aliumbwa kwa mfano wa Mungu na kwa sura ya Mungu. Na
naamini ya kuwa utakubaliana nami nikisema Mungu wetu si maskini kwa hiyo
hatukuumbwa kwa mfano wa kimaskini wala sura ya kimaskini.
SABABU NNE AMBAZO ZINAONESHA KUWA MUNGU HAPENDI WATU WAKE
HASA WALOKOLE TUWE MASKINI.
1. Mungu ndiye atupaye nguvu za kupata utajiri
“ Bali utamkumbuka Bwana , Mungu wako, maana ndiye akupaye NGUVU ZA KUPATA
UTAJIRI; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo” (Kumb. 8:18).
Si mapenzi ya Mungu tuwe maskini kwa kuwa yeye mwenyewe ndiye atupaye nguvu ili
tupate utajiri! Kama basi Mungu anatupa nguvu za kupata utajiri, ina maana ni wazi kwamba
Mungu hapendi tuwe maskini wa mambo ya mwilini. Lakini fahamu ya kuwa si matajiri wote
waliopo duniani wameupata utajiri kutokana na nguvu walizopewa na Mungu. Na ndiyo
maana sehemu nyingi katika Biblia matajiri wa jinsi hiyo wamekemewa. Soma (Amosi
5:11,12)
Hii pia haimaanishi kuwa Mungu yuko upande wa KILA maskini aliopo duniani. La hasha!
Mungu yuko upande wa yule ayafanyaye mapenzi yake awe tajiri au maskini (Mathayo
7:21).
2. Mungu ndiye atufundishaye kupata faida
•Mungu wetu tunayemwabudu na kumtumikia katika Kristo Yesu si Mungu wa hasara bali
Mungu wa faida. Imeandikwa hivi;
“Bwana, Mkombozi wako, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi;Mimi ni Bwana, Mungu wako,
nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye katika njia ikupasayo kuifuata” (Isaya 48:17).
Si mapenzi ya Mungu tuwe maskini, ndiyo maana anatufundisha ili tupate faida ya halali.
Kwa ajili hiyo imeandikwa; “Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi

4|Mch. Jofrey Daudi Dibson = Semina ya Uchumi TAG -Bethel Revival


Temple-kwa Ask.Dkt Barnabas & Gladymary Mtokambali (25-29/04/2022
iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji” (Waefeso
4:28).
Katika Zaburi 24:1 imeandikwa;“Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana; Dunia na
wote wakaao ndani yake”
Na pia ukisoma katika Hagai 2:8 unaona imeandikwa hivi “Fedha ni mali yangu, na
dhahabu ni mali yangu, asema Bwana wa majeshi”
Ngoja nikuulize swali; Je! unadhani vitu vyote hivi Bwana amemwekea nani? Unadhani
alimwekea shetani na watu wanyonyaji wachache?
La hasha! Mungu aliviweka vitu hivi vyote na mali hii yote kwa ajili ya watu wake wote, ili
itumike katika usawa. Kwa nini? Kwa kuwa Mungu hapendi watu wake wawe maskini.
Ndiyo maana mtu alipoumbwa aliwekwa awe wakili wa mali yote ya Mungu hapa duniani.
Utajiri uliomo duniani umetawaliwa na watu wachache na nchi chache siku hizi kwa sababu
ya dhambi za uchoyo, ubinafsi, uonevu,unyonyaji, unyang’anyi na dhuluma zilizoingia ndani
ya mwanadamu.
Na hii imefanya watu wengine kufikiri ya kuwa Mungu ndiye aliyegawa matabaka haya
mawili, ambavyo si kweli. Na si vizuri kumsingizia Mungu katika jambo ambalo
mwanadamu mwenyewe amejiletea uharibufu

4. Yesu Kristo alikuwa maskini ili sisi tuwe matajiri


“Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu,
ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake” (2
Wakorintho 8:9).
Ni kweli kwamba Yesu Kristo alipokuwa hapa duniani alikuwa maskini. Lakini hakuwa
maskini ili sisi tuwe maskini; bali alikuwa maskini ili sisi tuwe matajiri!
“Yesu akasema, Amini, nawaambiaeni, hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au
ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya
Injili, ila atapewa MARA MIA SASA WAKATI HUU, nyumba, na ndugu waume, na ndugu
wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao
uzima wa milele” (Marko 10:29,30).
Majibu haya ya Bwana Yesu, yanazidi kutudhihirishia ya kwamba si mapenzi ya Mungu
tuwe maskini.

5|Mch. Jofrey Daudi Dibson = Semina ya Uchumi TAG -Bethel Revival


Temple-kwa Ask.Dkt Barnabas & Gladymary Mtokambali (25-29/04/2022
SEHEMU YA TATU
MAMBO YALIYOWAFANYA WALOKOLE KUTOKUAMINI JUU
YA UHUSIANO WA UKRISTO WAO NA UTAJIRI
1. TAJIRI NA UFALME WA MUNGU
Nadhani utakuwa umewahi kusikia watu wakisema; “Matajiri hawataurithi ufalme wa
Mungu” Na wanasema ndivyo Bwana Yesu alivyosema baada ya tajiri aliyetaka uzima wa
milele kukataa kuuza mali yake.
“Kwa shida gani wenye mali WATAUINGIA ufalme wa Mungu. Na akaendelea kusema, Kwa
maana ni vyepesi ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme
wa Mungu. Ni nani basi awezaye kuokoka? Yasiyowezekana kwa wanadamu yawezekana kwa
Mungu” (Luka 18:24-26).
Na kwa kuamini kuwa tajiri hawezi kuurithi ufalme wa Mungu, wakristo wengi kwa
kudhamiria kabisa wameamua kuwa maskini ili wasije wakaukosa ufalme wa Mungu. Lakini
hii si sawa na ni kukwepa wajibu wetu tulionao kama mawakili wa mali zote za Mungu.
“Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa….” (Hosea 4:6)

2. MUNGU NA MALI
Kuna uhusiano gani kati ya Mungu na Mali? Kuna uhusiano gani kati ya Mkristo na Mali?
Kuna uhusiano gani kati ya wokovu na mali? Je, ni dhambi kwa mkristo kuwa na mali
nyingi?
Hebu na tuangalie maneno ya Yesu Kristo juu ya Mungu na Mali.
“Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili, Kwa maana atamchukia huyu, na
kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia
Mungu na Mali” (Mathayo 6:24)
Mtu hakuumbwa ili kuitumikia mali. Mtu aliumbwa kwa ajili ya utukufu wa Mungu na
amtumikie Yeye peke yake. Mali ya dunia iliwekwa kwa ajili ya kumtumikia mtu, na siyo mtu
kuitumikia mali! Mtu aliwekwa juu ya mali yote na aliagizwa kuitawala (Mwanzo 1:28 –
30).

2. MUNGU NA MALI…
“Kwa sababu hiyo nawaambieni, msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini;
wala miili yenu, mvae nini… (Mathayo 6:25-32)
Kuna wakristo wengine wameyaelewa vibaya maneno haya ya Bwana Yesu Kristo hata
kufikia kutokufanya kazi kwa kisingizio cha kwamba Yesu Kristo alisema tusiyasumbukie
maisha. Kwao kufanya kazi ina maana kusumbukia maisha. Lakini napenda kukuambia ya
kuwa Yesu Kristo hakuwa ana maana ya kutuambia tusifanye kazi aliposema tusiyasumbukie
Maisha
6|Mch. Jofrey Daudi Dibson = Semina ya Uchumi TAG -Bethel Revival
Temple-kwa Ask.Dkt Barnabas & Gladymary Mtokambali (25-29/04/2022
Paulo akasema, “Ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula (1Wathesalonike 3:10b)

3. FEDHA NA KUPENDA FEDHA...


Nimewahi kumsikia mhubiri mmoja akisema; “Fedha ni shina la maovu, kwa hiyo wakristo
wajihadhari nazo.” Na wakristo wengi wamekuwa wakisikika wakisema hivyo, kwa hiyo
wanaogopa kuwa na fedha za kutosha. Lakini ninaposikia watu wakisema hivi, huwa
najiuliza wanaupata wapi usemi huu? Biblia haisemi; “Fedha ni shina la maovu.”
Badala yake Biblia inasema hivi;“Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda
fedha;ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa
maumivu mengi”(1Timotheo 6:10)
Kupenda fedha ni kuwa na tamaa ya fedha; ni kuzitamani fedha. Na kupenda fedha huku
ndiko shina moja la mabaya ya kila namna. Tamaa ya fedha ndiyo inayoleta wizi, ujambazi,
mauaji, dhuluma, kutokutosheka, uchoyo, wivu, uasherati; nakadhalika. Lakini unaweza
kuwa na fedha bila ya kufungwa na roho ya kupenda fedha.
Shetani anajua kuwa Mkristo asipokuwa na fedha:
➢ Watumishi wa kanisa watalipwa mishahara midogo
➢ Mikutano ya injili na semina hazitafanyika mara kwa mara
➢ Vyombo vya muziki na vipaza sauti havitakuwepo
➢ Familia nyingi zitaingia kwenye migogoro kwani hakuna fedha
➢ Watoto hawataenda shule kwani hakuna ada Na matokeo yake ni kazi ya Mungu
kupoa.
Maswali matatu ya kujiuliza leo:
➢ Je! Unadhani ni nani ambaye anaweza kutoa fedha yake ili ikahubiri injili kama siyo
wakristo wenyewe?
➢ Na wakristo watatoaje fedha kama hawana fedha?
➢ Na watakuwaje na fedha, kama wanadhani kuwa na fedha nyingi ni dhambi?
Kwa hiyo usikubali unaposikia mtu akisema kuwa na fedha ni vibaya; lakini uwe mtu wa
kutokupenda fedha. Kwa kuwa ukizitamani fedha utajikuta unaanza kuzitafuta hata kwa njia
ambazo ni kinyume cha maadili yetu ya Kikristo; na pia kinyume cha utu wa mwanadamu.
4. MASKINI NA TAJIRI
Nafahamu ya kuwa si mpango wa Mungu kwa mtu aliye tajiri kumtawala maskini kwa
sababu ya umaskini wake. Na pia nafahamu si mpango wa Mungu kwa nchi zilizo tajiri
kuzitawala nchi maskini kwa sababu ya umaskini wake.
Lakini ni vizuri tufahamu uhusiano uliopo kati ya matabaka haya mawili:-
Biblia inasema;“Tajiri humtawala maskini, Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye.”
(Mithali 22:7)
Inakisiwa ya kuwa jumla ya madeni yote ya nchi zinazoendelea ni mabilioni ya dola za
Kimarekani na yanazidi kuongezeka.

7|Mch. Jofrey Daudi Dibson = Semina ya Uchumi TAG -Bethel Revival


Temple-kwa Ask.Dkt Barnabas & Gladymary Mtokambali (25-29/04/2022
Ni kweli kabisa kwamba utajiri huu wa nchi hizo si wote uliopatikana kwa njia ya halali. Na
wafuatiliaji wa mambo ya uchumi duniani, wanafahamu jinsi nchi hizi zilizoendelea
zinavyobuni mbinu mbalimbali kuzinyonya nchi zinazoendelea.
Ingawa si mapenzi ya Mungu tuwe maskini, lakini pia si mapenzi ya Mungu tuwe matajiri ili
kuwatawala wengine kwa sababu ya umaskini wao. Ole ni kwa matajiri wanaoutumia utajiri
wao kuonea na kuwafanya wenzao kuwa watumwa. Mungu anapotupa nguvu za kupata
utajiri ndani ya Kristo ni kwa kusudi muhimu la kuimarisha agano lake la kumhudumia mtu
mzima – kiroho na kimwili.
Na kwa upande mwingine viongozi wa Kanisa wanajikuta wameingiwa na hofu na
kushindwa kuwakemea matajiri hao wakati wanapokwenda kinyume na maadili ya kikristo.
Kama siyo ukoloni wa namna yake ulioingia katika kanisa ni nini basi?
Naamini ya kuwa wachungaji na viongozi, wengi wao wangekuwa na hali nzuri kiuchumi,
baadhi ya matajiri wanaotaka kutawala viongozi wengine wangeshindwa katika mbinu zao.
Au wewe unasemaje?
Shetani ametumia mbinu kwa shabaha zifuatazo:
Maneno ya wakristo yasisikilizwe wanapohubiri, kwa kuwa imeaandikwa; “….Walakini
hekima ya maskini hudharauliwa wala maneno yake hayasikilizwi” (Mhubiri 9:19b). Kwa
lugha nyingine maana yake“hayatiliwi maanani.”
Wakristo waendelee kuwa watumwa ingawa wanadai ya kuwa wamewekwa huru. Kumbuka
imeandikwa hivi; “Tajiri humtawala maskini. Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye”
(Mithali 22;7)
Kwa hiyo lazima tuwe waangalifu ili tunayosema yawe sawa na tunavyoishi. Na tuishi sawa
sawa na ahadi za Mungu tunazozisimamia.

8|Mch. Jofrey Daudi Dibson = Semina ya Uchumi TAG -Bethel Revival


Temple-kwa Ask.Dkt Barnabas & Gladymary Mtokambali (25-29/04/2022
SEHEMU YA NNE A
KUCHOCHEA UBUNIFU WA MIRADI NA FURSA ZA KIBIASHARA

UTANGULIZI…
‘BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Angalia, nimemwita kwa jina lake Bezaleli
mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda; nami nimemjaza roho ya Mungu, katika
hekima na maarifa, na ujuzi na mambo ya kazi ya kila aina, ili ABUNI kazi za ustadi, kuwa
fundi wa dhahabu, na wa fedha, na wa shaba, na kukata vito kwa kutiwa mahali, na kuchora
miti, na kufanya kazi ya ustadi iwayo yote’ (Kut.31:1-5)
“Nimekuwa mambo yote kwa watu wa namna zote, ili kwa vyovyote niwaokoe wengine.”
(1Wakorintho 9:22).
Yapo mazingira yanayochochea akili ya binaadamu kuibuka na fikra au mawazo ya ki-bunifu
ambayo yakitiwa katika matendo yanaweza kumletea mtu mafanikio au kuleta mabadiliko
makubwa katika jamii, au kuongeza thamani ya vitu, bidhaa au huduma kwa wateja.
Watu wenye ari ya kuthubutu, wabunifu na wasiojali hatari zozote katika biashara ndio huwa
moyo wa maendeleo ya nchi. Uchumi wa Kanisa unakuwa, wanaofanya kazi watakuwa na
hali nzuri na watakaomua kulala wataendelea kulia kila kukicha
Imedhihirika kuwa hatua ya kwanza ya kuanzisha mradi/ miradi ni KUBUNI NA
KUTHUBUTU.

UBUNIFU NI NINI?
Mara nyingi huchukuliwa kuwa ni matumizi ya njia bora zaidi zinazokidhi kutatua
changamoto mpya, changamoto ambazo tayari zipo lakini hazijapatiwa ufumbuzi bado, au
changamoto zilizopo kwenye soko au jamii kwa kipindi husika. Maryville, S (1992)
Ubunifu linaweza kutafsiriwa kuwa ni kitu fulani halisia na chenye mchango wa wazi katika
jamii na hivyo ni kitu kipya kinachojitokeza katika soko au jamii kwa hali ya upya.
Frankelius, P. (2009)
Ubunifu ni uwezo wa mtu kuanzisha au kuvumbua kitu chochote kipya, chenye utofauti na
ubora zaidi, ambacho kina thamani au kinaongeza thamani ya kitu kilichopo, kwa manufaa ya
mtu mwenyewe, wateja, na jamii kwa ujumla. Anurag, P. (2015)

CHANZO CHA UBINIFU


MunguCHANZO CHA UBINIFUmwenyewe ni mwanzilishi wa ubunifu Kitabu cha Mwanzo
Baada ya hapo aliwatumia watu wake katika kuendeleza ubunifu huo…angalia hapa.
➢ Nuhu. Ubunifu katika kujenga Safina (Mwanzo 6:14-22)
➢ Bezaleli. Ubunifu katika ufundi stadi (Kutoka 31:1-5)
➢ Gidion. Ubunifu katika Vita (Waamuzi 6:12)

9|Mch. Jofrey Daudi Dibson = Semina ya Uchumi TAG -Bethel Revival


Temple-kwa Ask.Dkt Barnabas & Gladymary Mtokambali (25-29/04/2022
➢ Paulo. Ubunifu katika utume wake ( 2 Wakorintho 9:22)

Je, Kwa Nini Ni Muhimu Kanisa la Mungu Kupatapa Maarifa Ya Ubunifu katika
Miradi?
➢ Agizo kuu la Mungu (Mwanzo 1:28)
➢ Kuweza kutatua changamoto zinazoikabili jamii
➢ Kupata Kitu kipya cha kuboresha maisha
➢ Kupata maarifa, ujuzi, na uwezo wa kujaa na ubunifu.
➢ Kuwasaidia watu kufikiri na kutenda ki-ubunifu
➢ Kumtengenezea mtu uwezo wa kuchambua maarifa, uwezo wa ung’amuzi, na uwezo
wa uvumbuzi.
➢ Kuwasaidia watu kupata uwezo wa kujenga kitu kikubwa zaidi, cha ki-bunifu, juu ya
ujuzi walionao wa stadi za kazi
➢ Kuwa na uwezo wa kulitazama soko au jamii yao kiudadisi, wakajua soko linahitaji
nini, lina changamoto zipi, au bidhaa gani inaweza kuongezewa ubora au thamani, au
mchakato upi ufanyiwe maboresho zaidi.
➢ Mtu akishajenga utamaduni wa ubunifu anapata uwezo wa kupambana na mazoea

10 | M c h .
Jofrey Daudi Dibson = Semina ya Uchumi TAG -Bethel Revival
Temple-kwa Ask.Dkt Barnabas & Gladymary Mtokambali (25-29/04/2022
SEHEMU YA NNE B
MIFANO UBUNIFU NA KUANZISHA MIRADI KUTEGEMEA FURSA ZILIZOPO
KATIKA MAZINGIRA YAKO.

.
1. KILIMO
Mfano kilimo cha mahindi
Gharama ya shamba, aina ya udongo, hali ya hewa, Mvua, Joto au baridi Gharama z akulima,
hallow, kupanda, palizi, kuvuna, kusomba, magunia/ mifuko na Ghala Mbegu, mbolea na
madawa mbalimbali Vipimo; mbegu hadi mbegu, mstari hadi mstari
❖ Kilimo cha umwagiliziaji...
Matunda, Mahindi, Mpunga, Maharage, Viazi aina zote, Soya, Mboga mboga, Ndizi,
Machungwa, Maembe, Mananasi, Parachichi, Matikiti, Matango, Bamia, Bilinganya, Pilipili,
Nyanya, Vitunguu, Vitunguu swaumu, Karoti, Maboga, Passion
❖ Kilimo …Mazao ya biashara
Alizeti, Karanga, Ufuta,Dengu, Pilipili, maua, Ngano, korosho Mbaazi, Njegere
2. Ufugaji
•Kuku: wa kienyeji na wa kisasa; wa nyamab na wa mayai Uzalishaji wa vifaranga wa
kienyeji na wa kisasa wa nyama na wa mayai Matumizi ya mashine za kutotolea vifaranga
Kununua na kuuza mayai
Ufugaji wa Kuku: Mfano Mambo ya msingi
Aina ya banda, Aina ya vifaranga, Kiasi cha chakula, Madawa, Uzito, Magonjwa ya kuu,
Idadi ya kufanya faida, Idadi ya kuku kwa, eneo na Tabia za kuku
➢ Ng’ombe
➢ Mbuzi
➢ Bata Mzinga
➢ Nguruwe
➢ Samaki
➢ Nyuki
➢ Sungura

3. Miradi Uzalishaji: Agro-Busines Kuongeza thamani za bidhaa


➢ Mashine za kusaga na kukoboa mahindi na mpunga.
➢ Kufunga unga na mchele ndani ya vifungashio vizuri. Mashine za kukamua
mafuta ya mazo (alizeti, karanga, ufuta, mawese n.k)
➢ Mashine za kukamua juisi za matunda mbalimbali na kuweka ndani ya
vifungashio

11 | M c h .
Jofrey Daudi Dibson = Semina ya Uchumi TAG -Bethel Revival
Temple-kwa Ask.Dkt Barnabas & Gladymary Mtokambali (25-29/04/2022
➢ Mashine za kukaushia mbogamboga, matunda na Samaki
➢ Kutengeneza na kusindika tomato, chili souce n.k
4. Kubuni Viwanda vidogo vidogo
➢ Sabuni za vipande
➢ Sabuni za unga
➢ Sabubi za kuogea
➢ Sabuni za kuosha mikono
➢ Sabubi ya maji
➢ Shampoo
➢ Karanga za mayai
➢ Egg chop
➢ Chips (clips)
➢ Kababu
➢ Batiki
➢ Mkaa
➢ mishumaa
➢ Matofari ya kila aina
➢ Mitambo ya kusafisha asali
➢ Mashine za kuchuja maji
➢ Mashine za kutengeza vifunganishio
➢ Mashine za kutengeza nta
➢ Mashine za kuzalisha umeme wa maji na jua
➢ Mashine za kutengeneza bati
5. Elimu
➢ Ujenzi wa vituo vya kulelea Watoto wachanga (baby care centers)
➢ Shule za awali au chekechea kwa Watoto wadogo
➢ Shule za msingi, sekondari na vyuo
➢ Kufundisha ususi, saloon, upambaji, urembo
➢ Vituo vya elimu ya kazi mbalimbali za mikono
6. Usafiri na Usafirishaji
➢ Boda boda
➢ Bajaji
➢ Baiskeli
➢ Baiskeli za motor
➢ Hiace
➢ Taxi
➢ Basi
➢ Min bus
7. Biashara
➢ Maduka ya rejareja na jumla
➢ Mini supermarkets
➢ Supermarkets
12 | M c h .
Jofrey Daudi Dibson = Semina ya Uchumi TAG -Bethel Revival
Temple-kwa Ask.Dkt Barnabas & Gladymary Mtokambali (25-29/04/2022
➢ Secretaria services
➢ Kuuza bidhaa za ujenzi
➢ Kuuza vyakula
➢ Kuuza na kununua nje
➢ Kuuza samani
➢ Kuuza madini
➢ Kuuza nguo
➢ Kuuzam mapambo
8. Mradi wa madini na vito uchimbaji na uuzaji
➢ Dhahabu
➢ Almasi
➢ Tanzanite
➢ Gemstones
➢ Gypsum
➢ Chumvi
➢ Mchanga
➢ Mawe
➢ Mafuta na ges
➢ chokaa
➢ Shaba
9. Kubuni - Mradi wa ujenzi na Majumba
➢ Hotel
➢ Hostel
➢ Nymba za wageni
➢ Kituo cha mafuta (shell)

13 | M c h .
Jofrey Daudi Dibson = Semina ya Uchumi TAG -Bethel Revival
Temple-kwa Ask.Dkt Barnabas & Gladymary Mtokambali (25-29/04/2022
SEHEMU YA TANO A
MBINU UNAZOWEZA KUZITUMIA KUANZA MIRADI/BIASHARA YAKO
Je, Tunaweza anzisha mradi bila fedha?
TUSIKIE MIFANO MICHACHE…
Ubunifu na uanzishwaji wa mradi bila fedha
➢ Akili na maarifa vinatosha kuanzisha biashara.
➢ Ubunifu pamoja na matumizi mazuri ya akili na maarifa katika kuona fursa na vyanzo
vya biashra vinavyohitaji ujuzi na bidii ya kazi au nguvu.
➢ Anza na kuainisha fursa zote ambazo zimo katika mazingira yanayokuzunguka, rejea
namna mbili za kuchagua na kufahamu fursa.
1. Kutumia taaluma yako
Una taaluma gani ambayo umesomea katika Maisha yako pengine ni Injinia, Mfamasia,
Dakatari wa Binadamu au Mifugo, Mhasibu, Manunuzi, Dreva, Kompyuta n.k
Njia za kutumia ni pamoja na:
➢ Kufanya wewe mwenyewe: ( Mwl. Anzisha Tuition Centre, Mfamasia anzisha
Famasi)
➢ Kujenga timu ambayo unaweza kufanya hiyo kazi kwa ubora zaidi
2. UZOEFU
Aina 3 za Uzoefu:-
1. Uzoefu kwa kupitia maumivu
Uliyoyapitia Mazingira gani ambayo uliyapitia katika Maisha yako ukiwa katika kufanya
kazi… ukiwa umeajiriwa au kujiajiri…Mfano Dada wa ndani alivyofanyishwa kazi kwa
mateso na baadae zikamtengenezea fursa ya biashara.
2. Uzoefu unaotokana na furaha.
Nakumbuka nikiwa Mhasibu Mkuu hospitali ya Rubya – Muleba nilifanya kazi kwa furaha
ambayo imenifanya kuwa mshauri na mfundishaji wa mambo ya fedha kitu ambacho
kinanilipa kwa sasa.
3. Uzoefu kupanga kujifunza:
Hii ni pale unapojitolea kufanya kazi pasipokujali malipo yoyote yale….baada ya miaka 3 au
5 nitafanya nini cha kuniletea fedha…?

3. MTANDAO
Network is Wealth ( Mtandao ni Utajiri) Maswali ya kujiuliza ni:

14 | M c h .
Jofrey Daudi Dibson = Semina ya Uchumi TAG -Bethel Revival
Temple-kwa Ask.Dkt Barnabas & Gladymary Mtokambali (25-29/04/2022
Watu wanaokuzunguka zaidi wana fursa gani…? kuna kitu gani wanachoitaji ili wewe
uzitumie fursa kuuza na ujipatie kipato) Watu wana umri gani? Hapa ni kwamba kila umri
una maitaji yake ufanye ni nini kwa Watoto…? Vijana…? Watu wa kati…? Na wazee…?)
Watu waliokuzunguka wananunua nini zaidi…? oredhesha watu hao, watafute nenda uongee
nao
Maswali ya kujiuliza kabla hatujaendelea…
➢ Una taaluma gani ambayo unaweza kuitumia kuwa fursa kwa eneo
lililokuzunguka…? Jibu:-
………………………………………….
➢ Una uzoefu gani kwa kile unachokifanya…? Je unaitaji uzoefu zaidi..? Jibu
…………………….
➢ Una mtandao wa kutosha wa kukusaidia katika kazi/ biashara yako…? Jibu:-
…………………………………………
4. KIPAJI
Ni namna ya kufanya jambo kuliko mtu mwingine yoyote yule…
Kitu cha kujua ni kwamba kipaji ambacho hakijanolewa hakiwezi kuleta mafanikio yoyote
yale (Kipaji kinakupa nafasi lakini Ujuzi unakupa Pesa…)
Mambo manne ya kuzingatia:
➢ Kungundua / Tambua kipaji chako
➢ Noa kipaji chako (Hapa watu hawakuoni mfano umenipa masaa 6 ya kukata mti tumia
masaa 4 ya kunoa na masaa 2 ya kukata)
➢ Watu kukiona kipaji chako (hapa unaweza kutumia muda mwingi malipo madogo)
➢ Panua kipaji chako ( maeneo yako, kushirikiana na watu wenzako, kutumia mitanda
ya kijamii nk.)
5. KITU AMBACHO UNAKIPENDA
Ukifanya kitu ambacho unakipenda inakufanya uwe mbunifu zaidi, ukawa na furaha zaidi,
amani n.k
Mfano:-
Mtu anayependa Watoto anaweza kaunzisha day care, duka la ngua la Watoto, kuuza viatu
vya Watoto n.k Watu wanopenda vyakula: anaweza anzisha mgahawa, Watu wanoapenda
mpira wa miguu: wanaweza kuanzisha kumbi za mpira. Tambua kwa kila unachopenda kuna
fursa fursa ndani yake. Una kitu gani…? Weka mkakati.
Weka Mkakati ambao umejikita kwa mambo makuu matatu (3):
➢ Kufanya kitu unachokipenda
➢ Kufanya kitu unachokiweza
➢ Kufanya kitu ambacho kinakulipa
Kuna aina ya watu wanne (4) katika kufanya kazi.

15 | M c h .
Jofrey Daudi Dibson = Semina ya Uchumi TAG -Bethel Revival
Temple-kwa Ask.Dkt Barnabas & Gladymary Mtokambali (25-29/04/2022
1.Kundi la kwanza la watu ni wale ambao wanafanya kitu ambacho wana uwezo nacho wana
skill ya kutosha na kinawalipa lakini hawakipendi. Kinachotakiwa hapa ni carrier transition =
kugeuza shauku
2.Kundi la pili ni watu wanaofanya kitu wanachokipenda na kinawalipa lakini wana ujuzi
mdogo sana katika jambo ambalo wanalifanya. Kinachoitajika ni skill development plan =
kujenga uwezo wao wa kifedha na kibiashara.
3.Kundi la tatu wanachokifanya wanakipenda sana wana ujuzi wa kutosha lakini hakiwalipi
kabisa. Kinachotakiwa ni busness skill = mkakati wa kutengeneza ujuzi wa kibiashara
4. Kundi la nne ni watu wanafanya kitu ambacho wanakipenda wana uwezo / ujuzi
nacho na kinawaletea fedha kinawalipa.

SEHEMU YA TANO B
AINA 5 ZA WATU MUHIMU WANAOWEZA KUKUSAIDIA KUKUANZISHA
BIASHARA MIRADI NA KUTIMIZA MAONO KIUCHUMI KATIKA MAISHA
YAKO

1. WATU WANAOKUAMINI
Kwenye Maisha yako utakuwa na maono makubwa zaidi lazima watokee watu wanaoiona
furture yako leo na wanaimini ili wakupe fursa bila kujali hali yako ya sasa hivi.
Shetani anachofanya anawapofusha watu wasione future yako ili wasiambatane na wewe.
Na usipokuwa makini katika maombi yako watu wa muhim utapishana nao. Wakikuangalia
ni kweli unatakiwa kuwa mhubiri mkubwa, kuwa mfanyabiashara mkubwa, lakini shetani
atapofusha macho yao wasione kitu kilicho ndani yako na matokeo yake wanakaa mbali na
wewe na kupelekea kushindwa kufika kusudio lako.
Hao watu hawatakuhukum ulivyo leo badara yake watasema huyu mtu analala chini, hana
fedha, hana biashara, hana nyumba, hana kazi… lakini ana kitu kikubwa ambacho kitatokea
na watakuamini katika ilo na watasimama na wewe ili kufikia kusudi lako. Nakwambia
usipokutana nao itakuwa shida sana kufikia lengo kwa wakati.
Watu wengi wameteseka sana kwa sababu wamekosa watu wanaowamini. Lazima awepo
mtu wa kuweza kukusemea na ili akuseme lazima aamini kitu ulichonacho.
Unaweza kupakwa mafuta na Mungu lakini bado nafasi haujapewa na unaweza kupewa
nafasi lakini haupakwa mafuta na Mungu angalia Daudi kilichomtokea … Samweli alikazana
sana kumpaka mafuta hadi mara ya pili
“Basi Daudi akaondoka huko, akakimbilia pango la Adulamu; na ndugu zake na watu wote
wa mbari ya baba yake waliposikia Habari hiyo, wakamwendea huko. 2 Na kila mtu
aliyekuwa katika hali ya dhiki, na kila mtu aliyekuwa na deni, na watu wote wenye uchungu
mioyoni mwao wakakusanyika kwake; naye akawa jemedari wao; nao waliokuwa pamoja
naye walipata kama watu mia nne.” 1 Samweli 22:1-2

16 | M c h .
Jofrey Daudi Dibson = Semina ya Uchumi TAG -Bethel Revival
Temple-kwa Ask.Dkt Barnabas & Gladymary Mtokambali (25-29/04/2022
Daudi aliishi pangoni lakini watu wengi wakamfuata hukohuko haijalishi hali ya hewa au
mazingira au ufukara wala kazi wala ofisi nzuri n.k. Na hao watu wakafanyika kuwa
mashujaa kwa sababu walimwamini Daudi walitembea nae kuanzia ngazi ya chini hadi
kufikia hatua ya ufalme. Kuna ndoto uliyonayo lakini haiwezi kutimia mpaka upate watu
wanaokuamini wanaoamini kitu ulichobeba ambacho kwa macho ya Roho wanakiona.
Ukikosa watu namna hii utachoka, utakata tamaa, utatumia nguvu nyingi sana, biasahara,
huduma, ndoa itayumba sana.
Mfano wa Maisha yangu Mimi Mch. Jofrey Daudi… nilizaliwa katika familia ya kipato cha
chini, ilifika hatua nimefukuzwa nimetelekezwa sina mbele wala nyuma. Lakini namshukuru
Mungu alinipatia watu ambao waliniamini na kunishika mkono hadi leo nilivyo kufikia hatua
hii na nafasi hii ya kuwa Makam Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Miradi na Maendeleo TAG
– Taifa ni kwa neema ya Mungu. Bwana Yesu ananipeleka mbali na juu zaidi kwa sababu
watu kuniamini.
Ndoto ya njaa alipewa farao si wengine kwa sababu Farao alikuwa ana uwezo wa kutunza
chakula. Watu wanaokuamini wanaweza wakawa wa aina yake yaani wana uwezo wa
kukusemea vizuri au fedha ya mtaji au kazi ya kufanya cha msingi waone kusudi lako
linatimia.
Omba langu:
Bwana Yesu naomba nipate watu wa kuniamini katika Maisha yangu ili nipate kibali
cha kusonga mbele katika kutimiza kusidi lako ambalo umeliweka ndani yangu katika
uso wa Dunia.

2. WATU WATAKAOKUTAMBULISHA
Kwenye kila atua ya Maisha yako kuna watu Mungu amewandaa kwa ajili ya
kukutambulisha na kukuunganisha maali Fulani. Hatua iliyoko kati ya kule unakotaka
kwenda ni mtu mmoja tu kukutambulisha na kukuunganisha.
Kuna vitu ukisema nitafanya mimi mwenyewe utachukua muda mrefu sana. Bali kunaitajika
mtua atakayekutambulisha atakayekusemea atakayekuunganisha. (Habari ya
Yusufu…alivyotambulishwa) Kumbuka tangu atafsiri hiyo ndoto ilipita miaka miwili
Mwanzo 41:9-15 9 “Basi mkuu wa wanyweshaji akamwambia Farao akisema,
Nayakumbuka makosa yangu leo. 10 Farao aliwakasirikia watumwa wake, akanitia nifungwe
nyumbani mwa mkuu wa askari, mimi na mkuu wa waokaji. 11 Tukaota ndoto usiku mmoja,
mimi na yeye; kila mtu kwa tafsiri ya ndoto yake tukaota. 12 Na huko pamoja nasi palikuwa
na kijana; Mwebrania, mtumishi wa mkuu wa askari, tukamhadithia, naye akatufasiria ndoto
zetu; akamfasiria kila mtu kama ilivyokuwa ndoto yake. 13 Ikawa, kama vile alivyotufasiria
ndivyo ilivyotokea; mimi nalirudishwa katika kazi yangu, na yeye alitundikwa. 14 Ndipo
Farao akapeleka watu, akamwita Yusufu, wakamleta upesi kutoka gerezani. Akanyoa,
akabadili nguo zake, na kuingia kwa Farao. 15 Farao akamwambia Yusufu, Nimeota ndoto,
wala hakuna awezaye kunifasiria; nami nimesikia habari zako, ya kwamba, usikiapo ndoto,
waweza kuifasiri”.

17 | M c h .
Jofrey Daudi Dibson = Semina ya Uchumi TAG -Bethel Revival
Temple-kwa Ask.Dkt Barnabas & Gladymary Mtokambali (25-29/04/2022
(Daudi yalimkuta hayahaya…alivyotambulishwa Daudi alikuwa hafikirii wala hana
matumaini ya kuingia Ikuru.)
1 Samweli 16:17-18. 17 “Basi Sauli akawaambia, Vema, nitafutieni mtu aliye stadi wa
kupiga kinubi, mkaniletee. 18 Ndipo akajibu mmoja wa watumishi wake akasema, Tazama,
nimemwona mwana mmoja wa Yese, Mbethlehemi, aliye stadi wa kupiga kinubi, tena ni mtu
shujaa, hodari wa vita, anenaye kwa busara, mtu mzuri, ambaye BWANA yu pamoja naye”
(Habari ya Sauli = Paulo arijaribu kutafuta kazi...Barnaba akamtwaa akampeleka …)
Matendo 9:26-27 26 Na Sauli alipofika Yerusalemu, alijaribu kujiunga na wanafunzi, nao
walikuwa wakimwogopa wote, wasisadiki ya kuwa yeye ni mwanafunzi. 27 Lakini Barnaba
akamtwaa, akampeleka kwa mitume, akawaeleza jinsi alivyomwona Bwana njiani, na ya
kwamba alisema naye, na jinsi alivyohubiri kwa ushujaa katika Dameski kwa jina la Yesu.
Yesu anatambulishwa…
Yohana 1:29-30 29 “Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama,
Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu! 30 Huyu ndiye niliyenena
habari zake ya kwamba, Yuaja mtu nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa
maana alikuwa kabla yangu”.
Tambua ili kwamba baadhi ya watu wanaotaka kukutambulisha ni watu wadogo sana ndani
ya ofisi.
(Habari ya Naamani kuudumiwa na mtu mdogo house girl… alikuwa na shida sana
lakini alitambulishwa na mtu mdogo sana.)
2 Wafalme 5:1-5 1 “Basi Naamani, jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu, alikuwa mtu
mkubwa mbele ya bwana wake, na mwenye kuheshimiwa, kwa sababu kwa mkono wake
BWANA alikuwa amewapa Washami kushinda; tena alikuwa mtu hodari wa vita; lakini
alikuwa mwenye ukoma.2 Na Washami walikuwa wametoka vikosi, wakachukua mfungwa
mmoja kijana mwanamke kutoka nchi ya Israeli; naye akamhudumia mkewe Naamani. 3
Akamwambia bibi yake, Laiti bwana wangu angekuwa pamoja na yule nabii aliyeko
Samaria! Maana angemponya ukoma wake. 4 Mtu mmoja akaingia, akamwambia bwana
wake, akasema, Yule kijana mwanamke aliyetoka nchi ya Israeli asema hivi na hivi. 5
Mfalme wa Shamu akasema, Haya! Basi, mimi nitampelekea mfalme wa Israeli waraka. Basi
akaenda zake, akachukua mikononi mwake talanta kumi za fedha, na vipande vya dhahabu
elfu sita, na mavazi kumi”
Naamani alikuwa na shida sana ya ukoma kwa miaka mingi lakini house girl akamtambulisha
uponyaji ukatokea.

3. WATU WATAKAO KUKUTOA MAHALI ULIPOPAZOEA.


Hapa twaweza kuona mifano ya watu wa Mungu
➢ Musa anawatoa wana wa Israel Misri…
➢ Daudi alitolewa na Goriath …
➢ Habari ya Yona kutumwa Ninawi watu wakamtupa baharini

18 | M c h .
Jofrey Daudi Dibson = Semina ya Uchumi TAG -Bethel Revival
Temple-kwa Ask.Dkt Barnabas & Gladymary Mtokambali (25-29/04/2022
Yona 1:15-17 “15 Basi wakamkamata Yona, wakamtupa baharini, nayo Habari ikaacha
kuchafuka. 16 Ndipo wale wakamwogopa BWANA mno, wakamtolea BWANA sadaka, na
kuweka nadhiri. 17 BWANA akaweka tayari Samaki mkubwa ili ammeze Yona, naey Yona
akawa ndani ya tumbo la Samaki yule muda wa siku tatu, mchana na usiku”.

Siyo kila aliyeletwa kukukosa ni wa shetani…


Mithali 16:4 4 “Bwana amefanya kila kitu kwa kusudi lake, Naam, hata wabaya kwa siku ya
ubaya”
Habari ya Farao kusimamishwa ili ukuu wa MUNGU ujulikane…
Warumi 9:17 Kwa maana maandiko yasema juu ya farao, ya kwamba, Nilikusimamisha kwa
kusudi hili, ili nionyeshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika nchi.
Licha ya kazi uliyonayo, biashara, huduma, nafasi n.k… Mungu ameandaa watu wa
kukuondoa kwenye mahali ulipozoea wapo na watakuja kila mmoja na njia yake.

4.WATU WATAKAOKUSAIDIA
Ili ufikie malengo na maono yako lazima ukutane na watu watakaokusaidia kwa kutoa Vitu,
Muda, Fedha ili kuyafikia makusudi yako. Kazi yao kubwa Mungu amewaweka ili
wakusaidie kutimiza maono yako.
Hakuna maono ambayo mtu anaweza kuyatekeleza peke yake. Ukiona unaweza kutekeleza
maono peke yako hayo hayajatoka kwa Mungu.
Kwa kila mji, kwa kila makabila, kwa kila ofisi, kwa kila huduma, kwa kila biashara n.k…
Mungu ameweka watu wa kukusaidia kutimiza malengo hayo ukiwakosa watu hao itakuwa
vigumu kutimiza malengo yako.
Watu watakaokupa msaada kutimiza maono yako na maono ya Mungu AINA YA WATU
WAPO KATIKA MAKUNDI MAWILI:
➢ Wale ambao watasimama na wewe tangu siku mnayofamiana hadi siku maono yako
yatakayotimia (mwanzo hadi mwisho)
➢ Wale ambao watasimama na wewe kwa majira furani na baadae watakuacha… cha
kuzingatia hapa ni kuomba Roho Mtakatifu ili akuwezeshe kujua nani kamaliza kazi
umtoe na usimkumbatie maana anaweza kubadirika kuwa mwiba na akaleta madhara
makubwa kwenye huduma yako, biashara yako, ofisini kwako n.k.
(Simoni Mkreni… kumsaidia Yesu kwa majira maalum… alitajwa mara moja, afu
akusemwa tena historia yake ilishia hapo. )
Kosa linafanyika pale mtu anapotusaidia mara moja tunataka na kesho atusaidie hii inaweza
kuleta madhara na laana kubwa kwenye Maisha yako.

19 | M c h .
Jofrey Daudi Dibson = Semina ya Uchumi TAG -Bethel Revival
Temple-kwa Ask.Dkt Barnabas & Gladymary Mtokambali (25-29/04/2022
Mfano wa Maisha yangu nikiwa mdogo hali imekuwa mbaya sana ni mtoto wa mtaani
(Chokolaa). Alitokea mtoto ambaye hadi sasa nasema alikuwa Malaika alinishika mkono
akaanza kunitembeza mji wa Bukoba kisha akanipeleka Bandarini nikapanda meli (Kuzamia)
na kufika Mwanza. Simjui najiuliza yupo..? Kwa kipindi hicho ilikuwa hali ya hatari lakini
Mungu alinisaidia.
Njia wanazozitumia kukusadia zimegawanyika katika makundi mawili:
Njia ya kwanza ni ya Kiroho wanatumia njia ifuatayo:
➢ Njia ya Kiroho kukuombea
(Luka 2:36-37 Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, Binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na
umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali
wake. 37 Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu
usiku na mchana kwa kufunga na kuomba.)
Njia ya kukuambukiza neema ya Mungu (Rumi 1:11 Kwa maana ninatamani sana kuwaona,
nipate kuwapa karama ya rohoni, ili mfanywe imara.
Kumbu 34:9 Na Yushua Mwana wa Nuni, alikuwa amejaa roho ya hekima; maana Musa
alikuwa amemwekea mikono yake juu yake; wana wa Israeli wakamsikiliza, wakafanya kama
BWANA alivyomwamuru Musa.
➢ Njia ya pili ni Vitu (Material support)
Kukupa vitu (Luka 8:2-3 “2 na wanawake kadhaa wa kadha ambao walikuwa na pepo
wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalena aliyetokwa na pepo
saba. 3 na Yohana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi,
waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao. Mfano wa Mpanzi”
Yesu alitambua umuhim huu akamteua Yuda na kumpa Jukum la kushika na kutunza fedha.

5. WATU WANAOONA KITU ULICHOKIBEBA


Hawa ni watu ambao wanaona kitu ulichokibeba kitu ulichonacho inawezekana wewe haijijui
lakini kuna watu ambao wanakujua zaidi ya wewe unavyojijua. Hawa ni watu ambao
wanaona kitu ulichokibeba.
Wagaratia 2: 9 “Tena walipokwisha kujua ile neema niliyopewa; Yakobo, Kefa, na Yohana,
(Wazee wakubwa kanisa la Yerusalem) wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba
mkono wa kuume wa shirika; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao waende kwa watu wa
tohara”

20 | M c h .
Jofrey Daudi Dibson = Semina ya Uchumi TAG -Bethel Revival
Temple-kwa Ask.Dkt Barnabas & Gladymary Mtokambali (25-29/04/2022
SEHEMU YA SITA
MAKOSA YA KUEPUKA UNAPOTAKA KUANZA BIASHARA
1. Kukosa ushauri wa Mungu kabla ya kuanzisha miradi
Kati ya makosa ambayo yanawagharimu watu wengi katika eneo la miradi ni kukosa ushauri
wa Mungu kabla ya kuanzisha miradi
“ Mimi ni Bwana, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongazaye kwa njia
ikupasayo kuifuata” Isaya 48:17
Usitegemee Mungu ajibu maombi yako ya kufanikisha mradi ambao umeanzisha nje ya
mapenzi yake.
“Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawana mapenzi yake
atusikia (1 Yohana 5:14)”
2. Kukosa wakina yusuph wa kusimamia miradi
• Biblia inazungumza sifa za Yusufu kwamba yeye alikuwa: Mwanzo 39:2-6
Alikuwa mtu mwenye Hofu kubwa kwa Mungu Alikuwa Mwaminifu mbele za Mungu na
kwa wawatu
Unaweza ukamuweka mtu kwenye mradi wako halafu akawa kikwazo kwa Mungu kupitisha
baraka kuja kwenye hiyo ofisi / mradi/ biashara n.k
3. Kubadilishwa kwa mfumo wa kuendesha miradi, tofauti na ule wa wakati wa
kuanzisha
Mwanzoni kabisa watu wanapoanzisha miradi wanakuwa karibu Zaidi na Mungu. Wanakaa
kwenye maombi, wanafunga kwa ajili ya kuombea mradi. Wanakuwa watoaji wazuri wa
sadaka kutoka kwenye huo mradi.
Baada ya kuona mradi unaanza kusimama vizuri wanabadili mfumo wa uendeshaji. Maombi
yanapungua, mwisho yanakata kabisa. Utoaji wa sadaka unakuwa sio kwa uhaminifu kama
pale mwanzoni.Uzoefu unatawala siyo tena msaada wa Mungu. Mahusiano na Mungu
yanatoweka.
Matokeo yake:
➢ Mungu anaaribu mwenyewe.
➢ Shetani anaaribu kwa sababu hakuna ulinzi tena wa Mungu
➢ Wanaotumia nguvu za giza watakushinda kwa sababu wanatekeleza masharti
kwa miungu yao
4. KUTOPATA MUDA WA KUSIMAMIA
➢ Biashara unapoinzisha ni kama mtoto mdogo inaitaji kulelewa, kutunzwa, kulisha n.k
➢ Usimamizi ni wa muhim sana katika biashara yoyote ili au kazi au huduma usimamizi
ni jambo la kwanza.
➢ Biashara nyingi zinakufa si kwa sababu ya watu hawana fedha hapana. Bali ni kwa
sababu watu hawana muda wa kusimamia biashara hiyo.

21 | M c h .
Jofrey Daudi Dibson = Semina ya Uchumi TAG -Bethel Revival
Temple-kwa Ask.Dkt Barnabas & Gladymary Mtokambali (25-29/04/2022
5. KUTAKA KUPANUKA KWA HARAKA
Namna unavyojifunza kadri biashara inavyoendelea na muda; ndivyo unapopata ufaham zaidi
juu ya biashara hiyo.
Hapa tunaona kuna aina mbili za kujipanua
➢ Vertical = kujipanua kwa juju tu anataka afahamike haraka
➢ Horizontal = kwenda kwa undani zaidi hapa anaenda polepole
Kumbuka ili kuwa kila kitu kipo katika mchakato na mchakato ndo utakusaidia kuvuka kwa
kila hatua unayoipitia.
6. KUANGALIA UNDUGU NA URAFIKI PASIPO KUANGALIA UJUZI ALIONAO
Mtu anaanzisha biashara na anaweka ndugu yake awe msimamizi huyo mtu ana ujuzi
wowote ule juu ya kazi husika ilo ni kosa la kiufundi
Biashara haitaji kuweka mahusiano ya undugu bali inaitaji ujuzi zaidi na hii ndo maana watu
wengi wanashindwa kufikia malengo yao.
7. KUTUMIA PESA YA MAUZO PASIPO KUTUMIA PESA YA KAWAIDA
Pesa ya mauzo si pesa ya matumizi ya kawaida (mitoko, kununua nguo, gari, kujenga
nyumba n.k)
Pesa ya mauzo ni pesa ambayo inabidi irudi ndani ya biashara ili iendelee kukuza biashara
hiyo.
8. TATIZO LA KUTOKUANZA
Watu wengi wanasumbuliwa na tatizo la kutoaWalichonacho ni kidogo (….)
➢ Watu wanaamini ipo siku mambo yatakuwa mazuri
➢ Bado najipanga
➢ Wanasubilia kusaidiwa anza

22 | M c h .
Jofrey Daudi Dibson = Semina ya Uchumi TAG -Bethel Revival
Temple-kwa Ask.Dkt Barnabas & Gladymary Mtokambali (25-29/04/2022
SEHEMU YA SABA
UNYENYEKEVU
UTANGULIZI
" Ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni? Akaita mtoto mmoja, akamweka
katikati yao, akasema, Amini, nawambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia
kamwe katika ufalme wa mbinguni. Majaribu ya Dhambi. Basi yeyote ajinyenyekeshaye
mwenyewe kama mtoto huyu, huyu ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni” (Mathayo
18: 2-4).
UNYENYEKEVU NI NINI:
1. Unyenyekevu ni hali ya mtu kujishusha licha ya hadhi, haki au kiwango alicho
nacho.
2. Unyenyekevu ni hali ya mtu kuonyesha heshima na kujali kwake kwa watu
wengine bila kujali ukubwa wala udogo wa kiwango kiwango chao chao cha maisha
nk.
3. Unyeyekevu ni hali ya kuudhibiti moyo wako usitawaliwe na kiburi, jeuri,
mavivuno wala dharau kwa mtu wa aina yeyote.
4.Unyeyekevu ni hali ya kuinua kiwango cha thamani ya watu wengine na kuwaleta
katika kiwango chako na kuwa ona kuwa wao pia wana thamani kubwa kama wewe
ulivyo.
KWANINI TUNYENYEKEE
1. Tunapaswa kuwa wanyenyekevu kwasababu hatujui kesho yetu.
Yakobo 4:13-15 "13 Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na
kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida; 14 walakini hamjui
yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo,
kisha hutoweka. 15 Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au
hivi."
2.Tunapaswa Kunyenyekea kwasababu Unyenyekevu Unaleta Baraka.
Mithali 18:12 "12 Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna; Na kabla ya heshima
hutangulia unyenyekevu."
3.Tunapaswa Kuwa Wanyenyekevu kwasababu Mungu Huwapinga Wasio na
Unyenyekevu na Huwapa Neema Wanyenyekevu
Yakobo 4:6 "6 Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga
wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu."
4.Tunapaswa Kunyenyekea kwasababu Hatujui sana Kuhusu Madhaifu Yetu na
Tunahitaji Watu Wengine watusaidie kwa Upendo.
Zaburi 141:5 "5 Mwenye haki na anipige, itakuwa fadhili; Anikemee, itakuwa kama mafuta
kichwani; Kichwa changu kisikatae, Maana siachi kusali kati ya mabaya yao."

23 | M c h .
Jofrey Daudi Dibson = Semina ya Uchumi TAG -Bethel Revival
Temple-kwa Ask.Dkt Barnabas & Gladymary Mtokambali (25-29/04/2022
5.Tunapaswa kuwa na unyenyekevu kwasababu bila ya Unyenyekevu hatutauona
ufalme wa mbinguni.
Mathayo 18:3-4 "3. akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto,
hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. 4 Basi, ye yote ajinyenyekeshaye mwenyewe
kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni."

FAIDA ZA UNYENYEKEVU
➢ Unyenyekevu huongeza thamani ya mtu mbele za Mungu. Isaya 57:15,
Mathayo 18:1-4, 1Petro 5:6
➢ Unyenyekevu humsaidia mtu kukubali kosa na kutubu Mwanzo 3:10-
13, Isaya 53:5,
➢ Unyenyekevu unazima hasira hasira haraka na kukupa wepesi wa
kusamehe. Efeso 3:26,
➢ Unyenyekevu unampa mtu Neema ya Mung. Warumi 8:26, Yakobo
4:6,Mithali 3:34
➢ Unyenyekevu unafanya macho ya Rohoni kufunguka. Mathayo 11:12
➢ Unyenyekevu unaongeza kiu ya kujifunza. Efeso 36:26

ZINGATIA ILI KWAMBA SIYO KILA KITU UKINYENYEKEE


SIYO KILA FURSA NI FURSA:
➢ Yesu Kristo alipewa fursa ya kumsujudia Shetani kidogo ili apewe milki yote na
auepuke msalaba; YESU AKAIKATAA FURSA (MATHAYO 4:9-11).
➢ Mtume Paulo alipewa fursa ya kutoka gerezani kimya-kimya; PAULO
AKAIKATAA FURSA (MATENDO 16:36-39).
➢ Yusufu alipewa fursa ya kulala na mke wa Potifa; YUSUFU AKAIKATAA FURSA
(Mwanzo 39:5-20).
➢ Ruthu alipewa fursa ya kurudi kwa "miungu" ya kwao na aache kuandamana na
Naomi; RUTHU AKAIKATAA FURSA.

➢ Nelson Mandela alipewa fursa ya kutoka gerezani na kuachana na harakati za


ukombozi; MANDELA AKAIKATAA FURSA.

ANGALIZO

❌ USIKUBALI KUNYENYEKEA KWA KILE UNACHOONA SI SAHIHI PASIPO


KWANZA KUPIMA ATHARI ZAKE KWA HATMA YAKO. "SIYO KILA FURSA NI
FURSA"

24 | M c h .
Jofrey Daudi Dibson = Semina ya Uchumi TAG -Bethel Revival
Temple-kwa Ask.Dkt Barnabas & Gladymary Mtokambali (25-29/04/2022
SEHEMU YA NANE
WAJIBU WA MUME
Familia ni ikuru ya Mungu na maskani yake ya kutembelea
WAJIBU WA MUME NDANI YA FAMILIA
Efeso 5:22,25
Kumpenda mke wake
Kujitoa kwa ajili ya mke

1. KUOMBEA FAMILIA
➢ Usalama wa wote ndani ya familia na mahitaji yao
➢ Uzima wa kiroho na kimwili na kimwili kwa watu wote ndani ya familia yake
➢ Kuhakikisha kusudi la Mungu ndani ya familia linafanikiwa
➢ Kuhakikisha ndoto zako na za wote ndani ya familia zinafikiwa

2. KUWA NA MAONO YA NA KUYASIMAMIA


➢ Kuweza kufikiria zaidi ya wote ndani ya familia, kwa sababu wengi leo hii
wako tayari kufa kuliko kufikiria. (Habakuki 2:2-3)
➢ Maono yake yaandikwe
➢ Asiwe mwepesi wa kushirikisha wengine maono yake – Yusuph na Marimu.
➢ Hakikisha unapata watu sahihi wa kuwashirikisha – ukishirikisha kila mtu
nguvu ya maono inakufa au wengine watakusahuri vibaya.
➢ Panga maono ya muda mrefu na muda mfupi; haya ya muda mfupi mara
nyingi husaidia kufanikisha maono ya muda mrefu.
➢ Kuwa na maono mapya kila baada ya vipindi fulana vya Maisha yako.
➢ Awe na maono kwa ajili ya huduma pia.
➢ Kuliona hitaji mapema.
➢ Kuachilia fahamu zake kuweza kugundua mambo mapya. – Kutoka 35:30
aliyetayari kuachilia moyo wake kupokea akili na ufahamu na ustadi toka
juu.
➢ Kuwa tayari kuruhusu wigo mpana zaidi – Isaya 54:2
➢ Atamani kuongezewa kozi.
➢ Kuwaza baada ya miaka 1,2,3,4,….familia yake itakuwa wapi.
➢ Kujua kama yeye akifunguliwa familia yake itakuwaje?

3. KUTOFANYA MAAMUZI KWA MAZOEA


➢ Boresha maamuzi yako kabla hujaanza kuyatekeleza.
➢ Kukubaliana na mabadiliko.
➢ Hata maombi yasifanywe kwa mazoea.
➢ Kuwa tayari kufungua ukurasa mpya.
➢ Kuwa tayari kufanya maamuzi magumu ( Ibrahim na Isack).

25 | M c h .
Jofrey Daudi Dibson = Semina ya Uchumi TAG -Bethel Revival
Temple-kwa Ask.Dkt Barnabas & Gladymary Mtokambali (25-29/04/2022
4. KUJUA NYAKATI ZA KUTIA MOYO FAMILIA
➢ Kujua nyakati za kutia moyo familia na nyakati za kutumika maneno magumu.
➢ Kufahamu watu wenye familia yake wana nini na kuwatia moyo.
➢ Kujua familia inapita katika vipindi vipi vya Maisha.
➢ Kujua kusudi la mungu katika kila nyakatiambazo familia inapitia.
➢ Kuzijua huduma na kalama zilizomo ndani ya wanafamiliawake.
➢ Kuweza kukabiliana na changamoto zinazopita ndani ya familia yake.
➢ Kufanya maandalizi ya : 1. Kupata Watoto 2. Kusomesha

5. KUJIHESABU KUWA NI MTUMISHI WA FAMILIA WA UNAYOIONGOZA


➢ Ukomavu wake tuupate kaytika kuwajibika na sio tu katika umri.
➢ Kuweza kufika pale wengine wasipoweza kufika ndani ya familia.
➢ Kuwa kielelezo katika maeneo yote, mstari wa mbele katika kuomba, ibada na
tabia kwa ujumla, Watoto wanatamani kuiga. – Mithali 22:6.
➢ Kuwa mfano wa kuigwa - watu waulize umewazeje..?

6. MWENYE KUWEZA KUJITENGENEZA KWA NDANI


➢ Kuweza kutambua udhaifu wako
➢ Kuweza kujitengeza ili uwe bora.
➢ Kujiweka mwenyewe viwango vya juu.
➢ Kuweza kupitia matarajio yaw engine.
➢ Kutoridhika na mambo madogo madogo.
➢ Mwenye picha ya mambo makubwa: 1. Viwango vya elimu yako na familia 2.
Hali ya Maisha kwa ujumla 3. Biashara/ kazi / Huduma.

7. KUJUA KUZITUMIA FURSA


➢ Kujua kuzitumia fursa kwa faida
➢ Kuwa tayari kukutana na upinzani au changamoto, sio wakati wote
utaeleweka.
➢ Kutokuwepa gharama ya kulaumiwa
➢ Kuona mbalia hata kama halipi leo: italipa kesho.
➢ Kuziona na kuzitumia fursa za :- Masomo, kuziba mapengo, kazi n.k

8. KUWA MBUNIFU
➢ Kuwa na uwezo wa kuweza kufanya tofauti na ulivyozooleka na wengine.
➢ Kuwa na mawazo na mitazamo mipya.
➢ Kuweza kuyaona mengine ambayo wengine wameshindwa kuyaona.
➢ Kufanya kile unachokiona ni hitaji bila kuangalia ulivyooleka.

9. NIDHAMU YA MAISHA
➢ Kuwa na uwezo wa kujiwekea ratiba ya siku, mwezi, mwaka
➢ Kuweza kutafuta nguvu ya kukamilisha ratiba.
➢ Kuwa na nidhamu ya fedha, kazi na mambo ya kanisani; nidhamu izingatiwe.
➢ Nidhamu ya muda wa kurudi nyumbani, sehemu yako ya kazi.
➢ Kila unachokifanya Watoto wako watafanya.
➢ Mungu hadhihakiwi, kila apandacho mtu, ndicho atakachovuna.

26 | M c h .
Jofrey Daudi Dibson = Semina ya Uchumi TAG -Bethel Revival
Temple-kwa Ask.Dkt Barnabas & Gladymary Mtokambali (25-29/04/2022
10. KUTOKUWA NA UPENDELEO (FAIRNESS)
➢ Kushughurikia maswala ya familia au ta ndugu wa pande zote mbili bila
upendeleo.
➢ Husiruhusu mila na desturi kuvuruga mpango wa ndoa.
➢ Mume atamwacha Baba na Mama yake. Mungu alijua kwa Mume kuondoka
katika maeneo mengi.

11. KUWEKA VIZURI MAMBO YA URITHI


➢ Jinsi ya kuwarithisha Watoto – Mithali 13:22
➢ Usalama wa mke kama yeye atatangulia.
➢ Ajuaye kuweka akiba kwa ajili ya nyakati za uhitaji na nyakati za dahrula –
Mithali 30:25; Zaburi 127: 1 – Ikiwa Mungu hayupo katika Maisha yetu,
kazi zetu, malengo yetu,na katika familia zetu, basi yote ni bure na
mwisho wake ni kukata tamaa.
➢ Zitafute baraka za Mungu na uongozi wake katika mambo yote tangu mwanzo
wa Maisha yetu.
➢ Msingi wa Maisha hujengwa na kusindiliwa na maombi na kumwagiliwa na
maji na neno.

CHANGAMOTO ZINAZOTOKEA KWA MUME AKIWA NA FEDHA


KATIKA FAMILIA KULIKO MKE

1. MUME KUANZA KUDHARAU MAHITAJI YA MKEWE


➢ Ubinafsi unaanza, anaanza kujijali yeye mwenyewe, na kudharau mahitaji
ya mkewe.
➢ Mume hapaswi kukwepa kutimiza mahitaji ya mkewe, mke anahitaji
kuvaa, kupendeza, vocha, sadaka, vifaa vya jikoni (vyombo) na mengine
mengi.

2. MUME KUPUUZA MAENDELEO YA MKEWE NA WATOTO


➢ Anaanza kujiendeleza yeye tu.
➢ Mke anahitaji kuendelezwa kieleimu, kibiashara, akipata elimu hata
biashara atafanya vizuri.

3. MUME KUMWONA MKE KAMA MZIGO BADALA YA KUMWONA


KAMA MWENZA.
➢ Usimwone kama mnyonyaji wala usijute kumwoa.

4. KUTOJALI WAZAZI NA NDUGU UPANDE WA MKE


➢ Wanaumwa umetulia tu, nyumba inavuja hujali, hivi husababisha
maumivu kwa mkeo.

5. KIBURI

27 | M c h .
Jofrey Daudi Dibson = Semina ya Uchumi TAG -Bethel Revival
Temple-kwa Ask.Dkt Barnabas & Gladymary Mtokambali (25-29/04/2022
➢ Kujiona wewe ndio wewena kuanza kujitwalia utukufu hivi vinaweza
kusababisha matatizo mengi katika familia.
➢ Pesa ikiongezeka wengi uwa na kiburi ambacho mwanzo hakikuwepo.
➢ Mume kuanza kula hotelini, kuchelewa kurudi nyumbani.
➢ Uungwana wote unaisha kabisa.
➢ Masimango maneno magumu yanaanza.
➢ Pesa inaanza kumfanya asisikilize ushauri wowote.
➢ Hataki kuulizwa, wala kujadili chochote na mke wake.
➢ Anaanza kujinunulia vitu bila hata kuangaliakipaumbele.

6. MUME KUANZA KUFANYA MAAMUZI BILA HATA KUMSHIRIKISHA


MKEWE WALA WATOTO.
➢ Hili ni kosa, usifikiri kuwa unaweza kufanya chochote bila kumhusisha
mkeo, nyie ni mwili mmoja.

7. KUTOMSIKILZA MKEO
➢ Mke anaongea yeye anasoma gazeti au anaangalia TV. Hili ni kosa kubwa
sana maana Mke anaitaji kusikizwa.
➢ Kwa kufanya hivi mke unasababisha masononeko yasiyoisha ndani ya
moyo wa mkeo.
➢ Mke anaanza kujihisi huenda alikosea kukubali kuolewa na wewe, kumbe
ni kirusi tu cha pesa kimevamia ndoa.
➢ Mungu anapoibariki ndoa kwa fedha kupitia mume ni kwa sababu anajua
mume ni kichwa cha mkewe, si kwamba baraka ya fedha ni fimbo ya
kumjeruhi mkeo.

28 | M c h .
Jofrey Daudi Dibson = Semina ya Uchumi TAG -Bethel Revival
Temple-kwa Ask.Dkt Barnabas & Gladymary Mtokambali (25-29/04/2022

You might also like