You are on page 1of 9

KUSIMAMIA

KATIKA
NYAKATI
NGUMU
Somo la 11 kwa ajili ya Machi 18, 2023
“Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru; Mtimizie Aliye
juu nadhiri zako. Ukaniite siku ya mateso;
Nitakuokoa, na wewe utanitukuza” (Zaburi 50:14-15)
Kitabu cha Ufunuo kimetabiri uwepo wa dhiki katika
dunia hasa itawaathiri wale wanaokuwa waaminifu kwa
Mungu (Uf. 13:15-17).
Wale wanaozitii amri za Mungu hawataweza kuuza
wala kununua katika wakati huo. Ni nini kitatokea? Au
ni nini tunaweza kufanya kama tutakumbana na dhiki
kama hizo leo kwa sababu ya majanga mengine?
Je, tunaweza kujiandaa leo kukabiliana na aina hii ya
dhiki?

Ni nani wa kutulinda katika nyakati ngumu?


Nani wa kumwamini?
Nini cha kushikiria?
Vipi ni vipaumbele vyetu?
Tujiandaaje kwa ajli ya nyakati ngumu?
NANI WA KUTULINDA KATIKA NYAKATI NGUMU?
“[…] Mwaminini BWANA, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini
manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa.” (2 Nyakati 20:20)
Mfalme Yehoshafati alikuwa tayari kwa vita (2Nyak. 17:2,
12-13). Hata hivyo, aliielewa mipaka yake.
Hakushughulika na muungano uliokuwa unamtishia
(2Nyak. 20:1-2).
Hakutafuta msaada kutoka kwa watu wengine kukabiliana
na vita hii, lakini aliuelekeza uso wake Kwake Yeye
awezaye hasa kumsaidia: Mungu (2Nyak. 20:3-12).
Huu haukuwa uamuzi ulioongozwa na
hofu au usio na faida. Yehoshafati
alikuwa akimtumikia Mungu (2Nyak.
17:3-4; 19:4). Alijua kuwa angemwamini
Mungu. Je, unao uzoefu wa namna hiyo
na Mungu kwamba atakusaidia
kumwamini katika nyakati za dhiki?
NANI WA KUMWAMINI?
“Msiwatumainie wakuu, wala binadamu ambaye hakuna wokovu kwake.”
(Zaburi 146:3)

Daudi alijua kuwa hakuna mwanadamu awezaye kumwokoa (Zab.


146:3). Alijifunza kupitia uzoefu wa Yonathani kwamba Mungu hahitaji
jeshi lenye nguvu kuwashinda maadui Zake (1Sam. 14:6, 13, 23).
Hata hivyo, alijaribiwa na Shetani na hivo akahitaji kujua ni askari
wangapi alikuwa nao (1Nyak. 21:1-2). Haikuzuiliwa kufanya hivyo,
lakini Daudi alionyesha kuwa alikuwa anaamini nguvu ya jeshi lake
zaidi ya Mungu.
Mungu yuko zaidi ya
kila kitu. Tunapaswa
kuja kwake kwanza
kabla ya kutumia
raslimali za
kibinadamu
NINI CHA KUSHIKIRIA?
“ Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa
watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa.” (2 Petro 3:11)
Tutashikiria nini Yesu atakaporudi?
Wakati wa dhiki ya mwisho hatutaweza kuuza wala
kununua. Ikiwa tuna chochote kilichobaki baada ya hapo,
kitaharibiwa kwa moto (2Pet. 3:10-11).
Kwahiyo tutmie kila kitu tulichonacho sasa kwakuwa
hatuwezi kukitunza?
Hapana, isipokuwa Roho Mtakatifu atuambie kufanya
hivyo. Sisi ni mawakili wa Mungu kwa kila kitu
alichotupatia hadi Yesu atakaporudi. Tunapaswa
kukisimamia vyema na kwa uaminifu.
Lakini bado, tunapasa kukumbuka kuwa kila
tunachohodhi ni cha kidunia; cha muda mfupi; na,
kama hatuko makini, kina fursa ya kutuharibu kiroho.
VIPI NI VIPAUMBELE VYETU?
“Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa
maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama
atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi
kumtumikia Mungu na mali.” (Mathayo 6:24)

Itatupasa kuamua katika nyakati fulani: ni aidha kumtumikia


Mungu na kupoteza mali zetu, au tushikirie mali zetu na
tumtumikie mwingine ambaye hastahili kutumikiwa.
Uamuzi kwa wakati huo utategemea maamuzi tufanyayo leo
(Mt. 6:24).
Mtume Yohana alisema, “Msiipende dunia, wala mambo
yaliyomo katika dunia” (1Yn. 2:15). Ni kipi kibaya katika
“dunia” kinachotutoa kutoka kwa Mungu (1Yn. 2:16)?
Wafilipi 2:12 ni ushauri mzuri wa kuweka vipaumbele sahihi:
“utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na
kutetemeka.” Umilele wetu ujao unategemea hilo.
TUNAJIANDAAJE NA NYAKATI NGUMU?
“Tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana
chapa ile, yaani jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.” (Ufunuo 13:17)
Wakati wa dhiki utakuja kwa kila mmoja (Dn. 12:1). Wale
wote watakaoendelea kuwa waaminifu na kutunza amri
Zake watakumbana na taabu kubwa.
Ikiwa hatuwezi kujitoa wenyewe kwa nguvu zinazotawala
ulimwengu mzima katika wakati huo lakini tukabakia kuwa
waaminifu kwa Mungu, tutapoteza kazi zetu na mali zetu
(Uf. 13:14-17). Hata hivyo, tutakuwa na uhakika kuwa
Mungu atatujali (2Ths. 3:3; Zab. 34:19).
Tunajiandaaje kwa nyakati hizo?
Kujifunza kumtumaini Mungu na kumwegemea Yeye
leo. Jaribio zuri ni kuwa waaminifu kwa zaka zetu.
Ikiwa tutashindwa kwa kitu kidogo hivyo, tutawezaje
kuwa waaminifu katika dhiki ijayo (Yer. 12:5)?
“Mfuasi wa Mungu, mara kwa mara hufika mahali
ambapo huonekana kuwa, kama akiambatana na
mapenzi ya Mungu hatapata riziki yake. Pengine
inaonekana kwamba utii kwa matakwa ya Mungu
ambayo ni dhahiri kabisa kutawaondolea njia yao ya
kujikimu. […] Tutakapojifunza nguvu ya neno Lake,
hatutafuata mapendekezo ya Shetani ili tuweze kupata
chakula au kuokoa maisha yetu. Swali letu pekee
litakuwa, Je, amri ya Mungu inasemaje? Na ahadi yake
ni ipi? Kwa kujua haya, tutatii amri ya Mungu na
kutumaini ahadi yake.”
E. G. W. (Tumaini la Vizazi Vyote, sura. 12, p. 121)

You might also like