You are on page 1of 25

AGANO LA KALE

Mwanzo 1:24
24 Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho
kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo.
Mwanzo 2:19
19 Bwana Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa
angani, akamletea Adamu ili aone atawaitaje; kila kiumbe hai, jina alilokiita Adamu likawa ndilo
jina lake.
Mwanzo 3:20
20 Adamu akamwita mkewe jina lake Hawa; kwa kuwa yeye ndiye aliye mama yao wote walio
hai.
Mwanzo 6:19
19 Na katika kila kilicho hai chenye mwili, wawili wa kila namna utawaleta ndani ya safina,
kuwahifadhi pamoja nawe; wawe mume na mke.
Mwanzo 7:3, 4, 23
3 Tena katika ndege wa angani saba saba, mume na mke; ili kuhifadhi hai mbegu juu ya uso wa
nchi yote.
4 Kwa maana baada ya siku saba nitainyeshea dunia mvua, siku arobaini mchana na usiku; na
kila kilicho hai nilichokifanya juu ya uso wa nchi nitakifutilia mbali.
23 Kila kilicho hai juu ya uso wa nchi kikafutiliwa mbali tangu mwanadamu hata mnyama wa
kufugwa, na kitambaacho, na ndege wa angani; vilifutiliwa mbali katika nchi, akabaki Nuhu tu,
na hao walio pamoja naye katika safina.
Mwanzo 8:1, 17, 21
Na Mungu akamkumbuka Nuhu, na kila kilicho hai, na wanyama wote waliokuwamo pamoja
naye katika safina; Mungu akavumisha upepo juu ya nchi, maji yakapungua;
17 Utoe pamoja nawe kila kilicho hai kilichomo pamoja nawe, chenye mwili, ndege, na
mnyama, na kila kitambaacho, chenye kutambaa juu ya nchi; wajae katika nchi, wawe na uzazi,
wakaongezeke katika nchi.
21 Bwana akasikia harufu ya kumridhisha; Bwana akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada
ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu
ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya.
Mwanzo 9:3, 10, 12, 15, 16
3 Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani,
kadhalika nawapeni hivi vyote.
10 tena na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, ndege, na mnyama wa kufugwa, na kila
mnyama wa mwitu katika nchi pamoja nanyi; wote wanaotoka katika safina, hata kila kilicho hai
katika nchi.
12 Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano nifanyalo kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai
kilichoko pamoja nanyi, kwa vizazi vyote hata milele;
15 nami nitalikumbuka agano langu, lililoko kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai katika wote
wenye mwili, wala maji hayatakuwa gharika tena kuwaharibu wote wenye mwili.
16 Basi huo upinde utakuwa winguni; nami nitauangalia nipate kulikumbuka agano la milele
lililoko kati ya Mungu na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili kilichoko katika nchi.
Mwanzo 12:12
12 basi itakuwa, Wamisri watakapokuona watasema, Huyu ni mkewe; kisha wataniua mimi na
wewe watakuacha hai.
Mwanzo 43:7, 27, 28
7 Wakasema, Mtu yule alituhoji sana habari zetu na za jamaa yetu, akisema, Baba yenu angali
hai? Mnaye ndugu mwingine? Nasi tukamjibu sawasawa na maswali hayo. Je! Tuliweza kujua ya
kwamba atasema, Shukeni pamoja na ndugu yenu?
27 Akawaulizia hali yao, akasema, Je! Baba yenu, yule mzee mliyemnena, hajambo? Angali hai?
28 Wakasema, Mtumwa wako baba yetu hajambo, angali hai; wakainama, wakasujudu.
Mwanzo 45:3, 26, 28
3 Yusufu akawaambia ndugu zake, Mimi ndimi Yusufu; baba yangu angali hai bado? Wala ndugu
zake hawakuweza kumjibu, maana waliingiwa na hofu mbele yake.
26 Wakampasha habari, wakisema, Yusufu angali hai; naye ndiye mtawala katika nchi yote ya
Misri. Moyo wake ukazimia, kwa sababu hakuwasadiki.
28 Israeli akasema, Yatosha! Yusufu mwanangu angali hai; nitakwenda, nionane naye kabla
sijafa.
Mwanzo 46:30
30 Israeli akamwambia Yusufu, Na nife sasa, kwa kuwa nimekuona uso wako, ya kuwa ungali
hai.
Mwanzo 47:25
25 Wakasema, Umetulinda hai, na tuone kibali machoni pa bwana wetu, nasi tutakuwa watumwa
wa Farao.
Kutoka 1:17, 18, 22
17 Lakini wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, wasifanye kama walivyoamriwa na huyo
mfalme wa Misri, lakini wakawahifadhi hai wale wanaume.
18 Basi mfalme wa Misri akawaita wale wazalisha na kuwauliza, Kwa nini kufanya jambo hili,
na kuwahifadhi watoto waume wawe hai?
22 Kisha huyo Farao akawaagiza watu wake, akisema, Kila mtoto mwanamume atakayezaliwa
mtamtupa mtoni, na kila mtoto mwanamke mtamhifadhi hai.
Kutoka 4:18
18 Basi Musa akaenda na kurejea kwa Yethro mkwewe, na kumwambia, Nipe ruhusa niende,
nakusihi, niwarudie hao ndugu zangu walioko Misri, nipate kuwaona kwamba wako hai hata
sasa. Yethro akamwambia Musa, Haya, nenda kwa amani.
Kutoka 21:35
35 Ng'ombe wa mtu akimwumiza ng'ombe wa mtu mwingine hata akafa; ndipo watamwuza
huyo ng'ombe aliye hai na kugawanya thamani yake; na ng'ombe aliyekufa pia watamgawanya.
Kutoka 22:4
4 Kama hicho kitu kilichoibwa chapatikana hai mkononi mwake, kama ni ng'ombe, au punda, au
kondoo; atalipa thamani yake mara mbili.
Walawi 11:46, 47
46 Hii ndiyo sheria katika hao wanyama, na ndege, na kila kiumbe kilicho hai, kiendacho ndani
ya maji, na kila kiumbe kitambaacho juu ya nchi;
47 ili kupambanua kati ya hao walio najisi na hao walio safi, na kati ya kiumbe kilicho hai
ambacho chaliwa, na hicho kilicho hai ambacho hakiliwi.
Walawi 14:4, 6, 7, 51, 52, 53
4 ndipo huyo kuhani ataagiza kwamba watwae kwa ajili yake atakayetakaswa ndege wawili
walio hai, ambao ni safi, na mti wa mwerezi, na sufu nyekundu, na hisopo;
6 kisha huyo ndege aliye hai atamshika, na huo mti wa mwerezi, na hiyo sufu nyekundu, na
hisopo, naye atavichovya hivyo, pamoja na yule ndege aliye hai, katika damu ya huyo ndege
aliyechinjwa juu ya maji ya mtoni;
7 kisha atamnyunyizia huyo atakayetakaswa na ukoma mara saba, naye atasema kwamba yu safi,
kisha atamwacha yule ndege aliye hai aende zake nyikani.
51 kisha atatwaa huo mti wa mwerezi, na hisopo, na sufu nyekundu, pamoja na huyo ndege aliye
hai, na kuvichovya vyote katika damu ya huyo ndege aliyechinjwa, na katika hayo maji ya
mtoni, na kuinyunyiza nyumba mara saba;
52 naye ataitakasa hiyo nyumba kwa damu ya ndege, na kwa maji ya mtoni, na kwa huyo ndege
aliye hai, na kwa mti wa mwerezi, na kwa hisopo, na kwa sufu nyekundu;
53 lakini ndege aliye hai atamwacha atoke mle mjini aende nyikani; ndivyo atakavyofanya
upatanisho kwa ajili ya hiyo nyumba; nayo itakuwa safi.
Walawi 16:10, 20, 21
10 Bali yule mbuzi aliyeangukiwa na kura kwa ajili ya Azazeli atawekwa hai mbele za Bwana ili
kumfanyia upatanisho, ili kumpeleka jangwani kwa ajili ya Azazeli.
20 Naye akiisha kufanya upatanisho kwa ajili ya mahali patakatifu, na hema ya kukutania, na
madhabahu, atamleta yule mbuzi aliye hai.
21 Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na
kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli, na makosa yao, naam, dhambi zao zote; naye
ataziweka juu ya kichwa chake yule mbuzi, kisha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa
mtu aliye tayari.
Walawi 18:18
18 Wala usitwae mwanamke pamoja na nduguye, awe mtesi wake, na kufunua utupu wake, huyo
wa pili atakapokuwa yu hai.
Hesabu 4:19
19 lakini wafanyieni neno hili, ili kwamba wawe hai, wasife, hapo watakapovikaribia vile vitu
vilivyo vitakatifu sana; Haruni na wanawe wataingia ndani, na kuwawekea kila mtu utumishi
wake, na kila mtu mzigo wake;
Hesabu 14:38
38 Lakini Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, wakabaki hai miongoni mwa
wale watu waliokwenda kuipeleleza nchi.
Hesabu 16:30, 33, 48
30 Lakini Bwana akiumba kitu kipya, na hiyo nchi ikifunua kinywa chake na kuwameza, pamoja
na wote walio nao, nao washukia shimoni wali hai; ndipo mtatambua ya kwamba watu hawa
wamemdharau Bwana
33 Basi wao, na wote waliokuwa nao, wakashukia shimoni wali hai; nayo nchi ikawafunika
wakaangamia kutoka mle mkutanoni.
48 Akasimama kati ya hao waliokufa na hao waliokuwa wakali hai; tauni ikazuiwa.
Hesabu 22:33
33 punda akaniona, akageuka upande mbele zangu mara tatu hizi; kama asingejiepusha nami,
bila shaka ningalikuua wewe, nikamwacha yeye hai.
Hesabu 31:15, 18
15 Musa akawauliza, Je! Mmewaponya wanawake wote hai?
18 Lakini hao watoto wote wa kike ambao hawakumjua mume kwa kulala pamoja naye,
mtawaweka hai kwa ajili yenu.
Torati 5:3, 26, 33
3 Bwana hakufanya agano hili na baba zetu, bali na sisi, yaani, sisi sote tuliopo hapa, tu hai.
26 Maana katika wote wenye mwili ni nani aliyeisikia sauti ya Mungu aliye hai, akisema toka
kati ya moto, kama vile sisi, asife?
33 Endeni njia yote aliyowaagiza Bwana, Mungu wenu, mpate kuwa hai, na kufanikiwa,
mkafanye siku zenu kuwa nyingi katika nchi mtakayoimiliki.
Torati 6:24
24 Bwana akatuamuru kuzifanya amri hizi zote, tumche Bwana, Mungu wetu, tuone mema
sikuzote ili atuhifadhi hai kama hivi leo.
Torati 11:6
6 na alivyowafanya Dathani, na Abiramu, wana wa Eliabu mwana wa Reubeni; nchi ilivyofunua
kinywa chake, ikawameza, na walio nyumbani mwao, na mahema yao, na kila kitu kilichokuwa
hai kikiwafuata, katikati ya Israeli yote;
Torati 19:4, 5
4 Na hii ndiyo hukumu ya mwenye kuua mtu, atakayekimbilia huko awe hai; atakayemwua
mwenziwe pasipo kukusudia, wala hakumchukia tangu hapo;
5 kama aingiapo mtu na mwenziwe mwituni kwenda kukata kuni, akapeleka mkono wake na
shoka ili kukata mti, likatoka shoka katika mpini, likampiga yule mwenziwe hata akafa; basi na
akimbilie katika miji hii mmojawapo awe hai;
Torati 20:16
16 Lakini katika miji ya mataifa haya akupayo Bwana, Mungu wako, kuwa urithi, usihifadhi
kuwa hai kitu cho chote kipumzikacho;
Torati 30:6, 16, 19
6 Bwana, Mungu wako, atautahiri moyo wako, na moyo wa uzao wako, ili umpende Bwana,
Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, upate kuwa hai.
16 kwa hivi nikuagizavyo leo kumpenda Bwana, Mungu wako, kuenenda katika njia zake, na
kushika maagizo yake, na amri zake, na hukumu zake, upate kuwa hai na kuongezeka; Bwana,
Mungu wako, apate kukubarikia katika nchi uingiayo kuimiliki.
19 Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na
mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;
Torati 31:27
27 Kwa kuwa uasi wako naujua, na shingo yako ngumu; angalieni, mimi nikali hai pamoja nanyi
leo, mmekuwa waasi juu ya Bwana; siuze nitakapokwisha kufa!
Yoshua 2:13
13 ya kwamba mtawaponya hai baba yangu na mama yangu, na ndugu zangu wanaume na
wanawake, na vitu vyote walivyo navyo, na kutuokoa roho zetu na kufa.
Yoshua 3:10
10 Yoshua akasema, Kwa jambo hili mtajua ya kuwa Mungu aliye hai yu kati yenu, na ya kuwa
hatakosa kuwatoa mbele yenu Mkanaani, na Mhiti, na Mhivi, na Mperizi, na Mgirgashi, na
Mwamori, na Myebusi.
Yoshua 8:23
23 Kisha wakamshika mfalme wa Ai ali hai, nao wakamleta kwa Yoshua.
Yoshua 9:15, 20, 21
15 Naye Yoshua akafanya amani pamoja nao, na kufanya agano nao, ili kwamba waachwe hai;
na wakuu wa mkutano wakawaapia.
20 Tutawafanyia neno hili, kisha tutawaacha wawe hai; hasira isije juu yetu, kwa ajili ya hicho
kiapo tulichowaapia.
21 Wakuu waliwaambia, Waacheni wawe hai; basi wakawa wenye kupasua kuni, na wenye
kuteka maji, kwa ajili ya mkutano wote; vile vile kama hao wakuu walivyowaambia.
Yoshua 14:10
10 Sasa basi, angalia, yeye Bwana ameniweka hai, kama alivyosema, miaka hii arobaini na
mitano, tangu wakati huo Bwana alipomwambia Musa neno hilo, wakati Israeli waliokuwa
wakienenda barani; na sasa tazama, hivi leo nimepata miaka themanini na mitano umri wangu.
Waamuzi 8:19
19 Naye akasema, Watu hao walikuwa ndugu zangu, wana wa mamaangu mimi; kama yeye
Bwana alivyo hai, kwamba mliwaokoa hai watu hao, mimi nisingewaua ninyi.
Waamuzi 21:14
14 Basi Benyamini wakarudi wakati huo; nao wakawapa wale wanawake waliowaponya wali hai
katika hao wanawake wa Yabesh-gileadi; lakini hawakuwatosha.
Ruthu 2:20
20 Naye Naomi akamwambia mkwewe, Na abarikiwe huyo na Bwana, ambaye hakuuacha wema
wake, wala kwa hao walio hai wala kwao waliokufa. Kisha Naomi akamwambia, Mtu huyu ni
wa mbari yetu, mmojawapo wa jamaa yetu aliye karibu.
1Samweli 1:28
28 kwa sababu hiyo mimi nami nimempa Bwana mtoto huyu; wakati wote atakaokuwa hai
amepewa Bwana. Naye akamwabudu Bwana huko.
1Samweli 2:6
6 Bwana huua, naye hufanya kuwa hai; Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu.
1Samweli 15:8, 9, 15
8 Akamkamata Agagi, mfalme wa Waamaleki, yu hai, akawaangamiza hao watu wote kwa
upanga.
9 Lakini Sauli na watu wake wakamwacha Agagi hai, na katika kondoo walio wazuri, na
ng'ombe, na vinono, na wana-kondoo, na cho chote kilicho chema, wala hawakukubali
kuwaangamiza; bali cho chote kilichokuwa kibaya na kibovu, ndicho walichokiangamiza kabisa.
15 Sauli akasema, Wamewaleta kutoka kwa Waamaleki; maana watu waliwaacha hai kondoo na
ng'ombe walio wazuri, ili wawatoe dhabihu kwa Bwana, Mungu wako, nao waliosalia
tumewaangamiza kabisa.
1Samweli 17:26, 36
26 Daudi akaongea na watu waliosimama karibu, akisema, Je! Atafanyiwaje yeye atakayemwua
Mfilisti huyo, na kuwaondolea Israeli aibu hii? Maana Mfilisti huyu asiyetahiriwa ni nani hata
awatukane majeshi ya Mungu aliye hai?
36 Mtumishi wako alimwua simba na dubu pia; na huyu Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa kama
mmoja wao, kwa sababu amewatukana majeshi ya Mungu aliye hai.
1Samweli 20:31
31 Maana wakati mwana wa Yese akiwa hai juu ya nchi, wewe hutafanikiwa, wala ufalme wako.
Basi, sasa peleka, ukamlete kwangu, maana hakika yake atakufa huyu.
1Samweli 27:9, 11
9 Tena Daudi akaipiga nchi hiyo, asimhifadhi hai mume wala mke, akateka nyara kondoo, na
ng'ombe, na punda, na ngamia na mavazi; kisha akarejea na kufika kwa Akishi.
11 Tena Daudi hakumhifadhi hai mume wala mke, ili kuwaleta Gathi maana alisema,
Wasituchongee kusema, Ndivyo alivyofanya Daudi, tena ndivyo ilivyokuwa desturi yake wakati
wote alipokaa katika nchi ya Wafilisti.
2Samweli 1:9
9 Akaniambia, Tafadhali simama karibu nami, ukaniue, maana shida imenipata; kwa sababu roho
yangu ingali hai ndani yangu.
2Samweli 8:2
2 Akapiga Moabu, akawapima kwa kamba hali wamelazwa chini; akapima kamba mbili za
kuuawa, na kamba moja nzima ya kuhifadhi hai. Wamoabi wakawa watumwa wa Daudi,
wakaleta zawadi.
2Samweli 12:18, 21, 22
18 Ikawa siku ya saba, yule mtoto akafa. Nao watumishi wa Daudi wakaogopa kumwambia ya
kuwa mtoto amekufa, maana, walisema, Angalieni, yule mtoto alipokuwa angali hai, tulisema
naye, asitusikilize sauti zetu; basi hatazidi kujisumbua, tukimwambia ya kuwa mtoto amekufa?
21 Watumishi wake wakamwambia, Ni neno gani hili ulilolitenda? Ulifunga na kulia kwa ajili ya
mtoto, alipokuwa hai; lakini mtoto alipokuwa amekufa, uliinuka ukala chakula.
22 Akasema, Mtoto alipokuwa hai, nalifunga, nikalia; kwa maana nalisema, Ni nani ajuaye
kwamba Bwana atanihurumia, mtoto apate kuishi?
2Samweli 18:14, 18
14 Ndipo Yoabu akasema, Siwezi kungoja na kusema nawe hivi. Akachukua vyemba vitatu
mkononi mwake, akamchoma Absalomu moyoni, alipokuwa akali hai katikati ya ule mwaloni.
18 Huyo Absalomu alipokuwa yu hai alikuwa ameitwaa na kujiinulia ile nguzo iliyoko bondeni
mwa mfalme; kwa maana alisema, Mimi sina mtoto wa kulikumbusha jina langu; akaiita hiyo
nguzo kwa jina lake mwenyewe nayo inaitwa ziara la Absalomu hata hivi leo.
2Samweli 22:47
47 Bwana ndiye aliye hai; Na ahimidiwe mwamba wangu; Na atukuzwe Mungu wa mwamba wa
wokovu wangu;
1Wafalme 3:22, 23, 25, 26, 27
22 Ndipo yule mwanamke wa pili akasema, Sivyo hivyo; bali mtoto wangu ndiye aliye hai, na
mtoto wako ndiye aliyekufa. Na mwenzake akasema, Sivyo hivyo; bali mtoto wako ndiye
aliyekufa, na mtoto wangu ndiye aliye hai. Ndivyo walivyosema mbele ya mfalme.
23 Ndipo mfalme akasema, Huyu anasema, Mtoto wangu yu hai, na mtoto wako amekufa. Na
huyu anasema, Sivyo hivyo; bali mtoto aliyekufa ni wako, na mtoto aliye hai ni wangu.
25 Mfalme akasema, Mkate mtoto aliye hai vipande viwili, kampe huyu nusu, na huyu nusu.
26 Ndipo mwanamke yule, ambaye mtoto aliye hai ni wake, akamwambia mfalme kwa maana
moyoni mwake alimwonea mtoto wake huruma, akasema, Ee bwana wangu, mpe huyu mtoto
aliye hai, wala usimwue kamwe. Lakini yule mwingine akasema, Asiwe wangu wala wako; na
akatwe.
27 Ndipo mfalme akajibu, akasema, Mpe huyu wa kwanza mtoto aliye hai, maana yeye ndiye
mama yake.
1Wafalme 12:6
6 Mfalme Rehoboamu akataka shauri kwa wazee waliokuwa wakisimama mbele ya Sulemani,
baba yake, alipokuwa hai, akasema, Mwanipa shauri gani ili niwajibu watu hawa?
1Wafalme 17:23
23 Eliya akamtwaa mtoto, akamchukua toka orofani mpaka chini ya nyumba ile, akampa mama
yake. Eliya akanena, Tazama, mwanao yu hai.
1Wafalme 18:5
5 Ahabu akamwambia Obadia, Pita katika nchi, kwenye chemchemi zote za maji, na vijito vyote;
labda tutapata majani, tuwahifadhi hai farasi na nyumbu, tusipate hasara ya hao wanyama wote.
1Wafalme 20:18, 32
18 Akasema, Kwamba wametoka kwa amani, wakamateni wa hai; au kwamba wametoka kwa
vita, wakamateni wa hai.
32 Basi wakajifungia magunia viunoni, na kamba vichwani, wakamjia mfalme wa Israeli,
wakasema, Mtumwa wako Ben-hadadi asema Roho yangu, nakusihi, iishi. Akasema, Je! Yu hai
bado? Ni ndugu yangu yeye.
1Wafalme 21:15
15 Ikawa Yezebeli aliposikia ya kwamba Nabothi amepigwa kwa mawe na kufa, Yezebeli
akamwambia Ahabu, Inuka, ulitamalaki shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli, alilokataa
kukupa kwa fedha, maana Nabothi hako hai, lakini amekufa.
2Wafalme 7:4, 12
4 Tukisema, Tutaingia mjini, mjini mna njaa, nasi tutakufa humo; nasi tukikaa hapa, tutakufa vile
vile. Haya! Twende tukaliendee jeshi la Washami; wakituhifadhi hai tutaishi; wakituua, tutakufa
tu.
12 Mfalme akaondoka usiku, akawaambia watumishi wake, Sasa nitawaonyesha ninyi
walivyotutendea Washami. Wanajua ya kuwa tuna njaa; basi wametoka kituoni, ili kujificha
kondeni, wakisema Watakapotoka mjini, tutawakamata hai; tena tutapata kuingia mjini.
2Wafalme 10:14
14 Akasema, Wakamateni wa hai. Wakawakamata wa hai, wakawaua penye birika ya nyumba ya
kukatia manyoya kondoo, watu arobaini na wawili; wala hakumsaza mtu wao awaye yote.
2Wafalme 19:4, 16
4 Yamkini Bwana, Mungu wako, atayasikia maneno yote ya amiri huyu, ambaye mfalme wa
Ashuru ,bwana wake,amemtuma ili amtukane Mungu aliye hai,naye atayakemea hayo maneno
aliyoyasikia BWANA ,Mungu wako;kwa sababu hii inua dua yako kwa ajili ya mabaki
yaliyobakia.
16 Tega sikio lako, Ee Bwana, usikie; fumbua macho yako, Ee Bwana, uone; uyasikie maneno ya
Senakeribu, ambayo amemtuma mtu aje nayo ili kumtukana Mungu aliye hai.
2Nyakati 10:6
6 Mfalme Rehoboamu akataka shauri kwa wazee, waliosimama mbele ya Sulemani baba yake,
alipokuwa hai bado, akasema, Mwanipa shauri gani la kuwajibu watu hawa?
2Nyakati 25:12
12 Na elfu kumi wengine, ambao wana wa Yuda waliwachukua wali hai, wakawaleta juu ya
jabali, wakawaangusha toka juu ya jabali, hata wakavunjika-vunjika wote.
Ayubu 12:10
10 Ambaye nafsi ya kila kilicho hai i mkononi mwake, Na pumzi zao wanadamu wote.
Ayubu 14:14
14 Mtu akifa, je! Atakuwa hai tena? Mimi ningengoja siku zote za vita vyangu, Hata
kufunguliwa kwangu kunifikilie.
Ayubu 19:25
25 Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya
nchi.
Ayubu 27:6
6 Haki yangu naishika sana, wala sitaiacha; Moyo wangu hautanisuta wakati nikiwapo hai.
Ayubu 28:21
21 Kwa kuwa imefichwa mbali na macho ya wote walio hai, Na kusitirika na ndege wa angani.
Ayubu 33:30
30 Ili kurudisha roho yake itoke shimoni, Ili atiwe mwanga kwa mwanga wa walio hai.
Zaburi 18:46
46 Bwana ndiye aliye hai; Na ahimidiwe mwamba wangu; Na atukuzwe Mungu wa wokovu
wangu;
Zaburi 27:13
13 Naamini ya kuwa nitauona wema wa Bwana Katika nchi ya walio hai.
Zaburi 41:2
2 Bwana atamlinda na kumhifadhi hai, Naye atafanikiwa katika nchi; Wala usimtie katika hali
wamtakiayo adui zake.
Zaburi 42:2
2 Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai, Lini nitakapokuja nionekane mbele za
Mungu?
Zaburi 49:18
18 Ajapojibariki nafsi yake alipokuwa hai, Na watu watakusifu ukijitendea mema,
Zaburi 52:5, 15
5 Lakini Mungu atakuharibu hata milele; Atakuondolea mbali; Atakunyakua hemani mwako;
Atakung'oa katika nchi ya walio hai.
Zaburi 55:15
15 Mauti na iwapate kwa ghafula, Na washuke kuzimu wangali hai, Maana uovu u makaoni
mwao na katikati yao.
Zaburi 56:13
13 Maana umeniponya nafsi yangu na mauti; Je! Hukuizuia miguu yangu isianguke? Ili nienende
mbele za Mungu Katika nuru ya walio hai.
Zaburi 63:4
4 Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai; Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu.
Zaburi 84:2
2 Nafsi yangu imezionea shauku nyua za Bwana, Naam, na kuzikondea. Moyo wangu na mwili
wangu Vinamlilia Mungu aliye hai.
Zaburi 104:25, 33
25 Bahari iko kule, kubwa na upana, Ndimo mlimo viendavyo visivyohesabika, Viumbe hai
vidogo kwa vikubwa.
33 Nitamwimbia Bwana maadamu ninaishi; Nitamshangilia Mungu wangu nikiwa hai;
Zaburi 116:9
9 Nitaenenda mbele za Bwana Katika nchi za walio hai.
Zaburi 124:3
3 Papo hapo wangalitumeza hai, Hasira yao ilipowaka juu yetu
Zaburi 142:5
5 Bwana, nimekuita nikasema, Ndiwe kimbilio langu, Fungu langu katika nchi ya walio hai.
Zaburi 143:2
2 Wala usimhukumu mtumishi wako, Maana kwako hakuna aliye hai mwenye haki.
Zaburi 145:16
16 Waufumbua mkono wako, Wakishibisha kila kilicho hai matakwa yake.
Zaburi 146:2
2 Nitamsifu Bwana muda ninaoishi, Nitamwimbia Mungu wangu ningali ni hai.
Mithali 1:12
12 Tuwameze hai kama kuzimu, Na wazima, kama wao washukao shimoni.
Mhubiri 4:15
15 Nikawaona wote walio hai waendao chini ya jua, ya kwamba walishikamana na huyo kijana,
huyo wa pili aliyesimama badala ya yule.
Mhubiri 6:8
8 Kwa maana mwenye hekima hupata faida gani kuliko mpumbavu? Au maskini ana nini kuliko
yeye ajuaye kwenda mbele ya walio hai?
Mhubiri 7:2
2 Heri kuiendea nyumba ya matanga, Kuliko kuiendea nyumba ya karamu. Kwa maana huo ndio
mwisho wa wanadamu wote, naye aliye hai atautia moyoni mwake.
Mhubiri 9:3, 4, 5
3 Baa hilo ni katika mambo yote yanayofanyika chini ya jua, ya kuwa wote wanalo tukio moja;
naam, zaidi ya hayo, mioyo ya wanadamu imejaa maovu, na wazimu umo mioyoni mwao wakati
walipo hai, na baadaye huenda kwa wafu.
4 Kwa kuwa liko tumaini kwa yule aliyeambatana na wote walio hai; (maana ni afadhali mbwa
aliye hai kuliko simba aliyekufa);
5 kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala
hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.
Wimbo Ulio Bora 4:15
15 Wewe ndiwe chemchemi ya bustani yangu, Kisima cha maji yaliyo hai, Vijito vya Lebanoni
viendavyo kasi.
Isaya 4:3
3 Tena itakuwa ya kwamba yeye aliyebaki katika Sayuni, na yeye aliyeachwa ndani ya
Yerusalemu, ataitwa mtakatifu; yaani, kila mmoja aliyeandikwa miongoni mwa hao walio hai
ndani ya Yerusalemu;
Isaya 37:4, 17
4 Yamkini Bwana, Mungu wako, atayasikia maneno ya huyo amiri ambaye mfalme wa Ashuru,
bwana wake, amemtuma ili amtukane Mungu aliye hai; na Bwana, Mungu wako atayakemea
maneno aliyoyasikia; basi, inua dua yako kwa ajili ya mabaki yaliyobakia.
17 Tega sikio lako, Bwana, usikie; funua macho yako, Bwana, uone; uyasikie maneno ya
Senakeribu, aliyopeleka ili kumtukana Mungu aliye hai.
Isaya 38:11, 19
11 Nalisema, Sitamwona Bwana, yeye Bwana, katika nchi ya walio hai; Sitamwona mwanadamu
tena pamoja na hao wakaao duniani.
19 Aliye hai, naam, aliye hai, ndiye atakayekusifu, kama mimi leo; Baba atawajulisha watoto
kweli yako.
Isaya 53:8
8 Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa; Na maisha yake ni nani atakayeisimulia? Maana
amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai; Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu.
Yeremia 10:10
10 Bali Bwana ndiye Mungu wa kweli; Ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele; Mbele za
ghadhabu yake nchi yatetemeka, Wala mataifa hawawezi kustahimili hasira yake.
Yeremia 11:19
19 Lakini mimi nalikuwa kama mwana-kondoo mpole, achukuliwaye kwenda kuchinjwa; wala
sikujua ya kuwa wamefanya mashauri kinyume changu, wakisema, Na tuuharibu mti pamoja na
matunda yake, na tumkatilie mbali atoke katika nchi ya walio hai, ili jina lake lisikumbukwe
tena.
Yeremia 17:13
13 Ee Bwana, tumaini la Israeli, wote wakuachao watatahayarika. Wao watakaojitenga nami
wataandikwa katika mchanga, kwa sababu wamemwacha Bwana, kisima cha maji yaliyo hai.
Yeremia 23:36
36 Na mzigo wa Bwana hamtautaja tena; maana neno la kila mtu ndilo litakalokuwa mzigo
wake; maana ninyi mmeyapotosha maneno ya Mungu aliye hai, ya Bwana wa majeshi, Mungu
wetu.
Yeremia 49:11
11 Waache watoto wako wasio na baba, mimi nitawahifadhi hai, na wajane wako na wanitumaini
mimi.
Maombolezo 3:39
39 Mbona anung'unika mwanadamu aliye hai Mtu akiadhibiwa kwa dhambi zake?
Ezekieli 1:5, 13, 14, 15, 20, 21, 22
5 Kukatokea katikati yake mfano wa viumbe hai vinne. Kuonekana kwao kulikuwa hivi;
walikuwa na sura ya mwanadamu.
13 Kwa habari za kuonekana kwao vile viumbe hai; kuonekana kwao kulikuwa kama makaa ya
moto yawakayo, kama kuonekana kwa vinga vya moto; moto ule ulikuwa ukienda juu na
kushuka chini, katikati ya vile viumbe hai; na ule moto ulikuwa na mwangaza mwingi, na katika
ule moto ulitoka umeme.
14 Na vile viumbe hai walipiga mbio, kwenda na kurudi, kama kuonekana kwa kumulika kwa
umeme.
15 Basi, nilipokuwa nikivitazama vile viumbe hai, tazama, gurudumu moja juu ya nchi, karibu
na kila kimoja cha vile viumbe hai, pande zake zote nne.
20 Kila mahali ambako roho hiyo ilitaka kwenda, walikwenda; walikuwa na roho ya kwenda
huko; nayo magurudumu yaliinuliwa karibu nao; kwa maana roho ya viumbe hai ilikuwa ndani
ya magurudumu.
21 Walipokwenda hao, yalikwenda hayo nayo; na waliposimama hao, yalisimama hayo nayo; na
walipoinuliwa hao juu ya nchi, magurudumu yaliinuliwa karibu nao; maana roho ya viumbe hai
ilikuwa ndani ya magurudumu.
22 Tena juu ya vichwa vya viumbe hai palikuwa na kitu mfano wa anga, kama rangi ya bilauri,
lenye kutisha, limetandwa juu ya vichwa vyao.
Ezekieli 3:13
13 Nikasikia mshindo wa mabawa ya vile viumbe hai, walipogusana, na mshindo wa yale
magurudumu kando yao, mshindo wa radi kuu.
Ezekieli 7:13
13 Kwa maana auzaye hatakirudia kilichouzwa, wajapokuwa wangali hai; kwa sababu maono
haya yawahusu wote jamii; hapana mmoja atakayerudi; wala hapana mtu atakayejitia nguvu
katika uovu wa maisha yake.
Ezekieli 10:15, 17, 20
15 Makerubi wakapaa juu; huyo ndiye kiumbe hai niliyemwona karibu na mto Kebari.
17 Waliposimama hao, hayo nayo yalisimama; na walipopaa juu hao, hayo nayo yalipaa juu
pamoja nao; maana roho ya huyo kiumbe hai ilikuwa ndani yao.
20 Huyu ndiye kiumbe hai niliyemwona, chini ya Mungu wa Israeli, karibu na mto Kebari;
nikajua ya kuwa hao ni makerubi.
Ezekieli 13:18
18 useme, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wanawake wale, washonao hirizi katika viungo
vyote vya mikono, wawekao leso juu ya vichwa vya kila kimo, ili wawinde roho za watu; je!
Mtaziwinda roho za watu wangu, na kuzihifadhi hai roho zenu wenyewe?
Ezekieli 16:6
6 Nami nilipopita karibu nawe, nikakuona ukigaagaa katika damu yako, nalikuambia,
Ujapokuwa katika damu yako, uwe hai; naam, nalikuambia, Ujapokuwa katika damu yako, uwe
hai.
Ezekieli 26:20
20 ndipo nitakapokushusha pamoja nao washukao shimoni, uende kwa watu wa kale; nami
nitakukalisha pande za chini za nchi; mahali palipokuwa ukiwa tangu zamani, pamoja nao
washukao shimoni; ili usikaliwe na watu, wala usiweke utukufu wako katika nchi yao walio hai.
Ezekieli 32:23, 24, 25, 26, 27, 32
23 ambao makaburi yao yamewekwa pande za shimo zilizo mbali sana, wote jamii
wamezunguka kaburi lake; wote pia wameuawa, wameanguka kwa upanga, waliofanya utisho
katika nchi yao walio hai.
24 Elamu yuko huko, na watu wake wote jamii, pande zote za kaburi lake; wote pia wameuawa,
wameanguka kwa upanga, walioshuka hali hawana tohara hata pande za chini ya nchi; ambao
waliwatia watu hofu katika nchi ya walio hai, nao wamechukua aibu yao, pamoja nao washukao
shimoni.
25 Wamemwekea kitanda kati ya hao waliouawa, pamoja na watu wake wote jamii; makaburi
yake yamzunguka; wote pia hawakutahiriwa, wameuawa kwa upanga; maana maogofyo yao
yalifanyika katika nchi ya walio hai, nao wamechukua aibu yao, pamoja nao washukao shimoni;
amewekwa kati ya hao waliouawa.
26 Mesheki yuko huko, na Tubali, na watu wake wote jamii; makaburi yake yamzunguka; wote
pia hawakutahiriwa, wameuawa kwa upanga; maana walifanya utisho wao katika nchi ya walio
hai.
27 Je! Wasilale pamoja na mashujaa wao wasiotahiriwa, walioanguka, walioshuka kuzimu
pamoja na silaha zao za vita, ambao wameweka panga zao chini ya vichwa vyao, na maovu yao
mifupani mwao? Maana waliwatisha mashujaa katika nchi ya walio hai.
32 Kwa maana nimeweka utisho wake katika nchi ya walio hai; naye atalazwa kati yao
wasiotahiriwa, pamoja na hao waliouawa kwa upanga; yeye Farao na watu wake wote jamii,
asema Bwana MUNGU.
Ezekieli 33:10
10 Na wewe, mwanadamu, sema na nyumba ya Israeli; Ninyi mwasema hivi, kwamba, Makosa
yetu na dhambi zetu ni juu yetu, nasi tumedhoofika katika dhambi hizo; basi tungewezaje kuwa
hai?
Ezekieli 47:9
9 Tena itakuwa, kila kiumbe hai kisongamanacho, kila mahali itakapofika mito hiyo, kitaishi;
kutakuwapo wingi mkubwa wa samaki, kwa sababu maji haya yamefika huko maana maji yale
yataponyeka, na kila kitu kitaishi po pote utakapofikilia mto huo.
Danieli 2:30
30 Lakini mimi, sikufunuliwa siri hii kwa sababu ya hekima iwayo yote niliyo nayo zaidi ya
watu wengine walio hai, bali kusudi mfalme afunuliwe ile tafsiri, nawe upate kujua mawazo ya
moyo wako.
Danieli 4;17
17 Hukumu hii imekuja kwa agizo la walinzi, na amri hii kwa neno la watakatifu; kusudi walio
hai wapate kujua ya kuwa Aliye juu anatawala katika ufalme wa wanadamu, naye humpa
amtakaye, tena humtawaza juu yake aliye mnyonge.
Danieli 5:19
19 na kwa sababu ya ule ukuu aliompa, watu wa kabila zote, na mataifa, na lugha, wakatetemeka
na kuogopa mbele yake; aliyetaka kumwua alimwua; na aliyetaka kumwacha hai, alimwacha hai;
aliyetaka kumtukuza, alimtukuza; na aliyetaka kumshusha, alimshusha.
Danieli 6:20, 26
20 Naye alipolikaribia lile tundu, akamlilia Danielii kwa sauti ya huzuni; mfalme akanena;
akamwambia Danielii, Ee Danielii, mtumishi wa Mungu aliye hai, je! Mungu wako,
unayemtumikia daima, aweza kukuponya na simba hawa?
26 Mimi naweka amri, ya kwamba katika mamlaka yote ya ufalme wangu watu watetemeke na
kuogopa mbele za Mungu wa Danielii; maana yeye ndiye Mungu aliye hai, adumuye milele, na
ufalme wake ni ufalme usioharibika, na mamlaka yake itadumu hata mwisho.
Danieli 12:7
7 Nami nikamsikia yule mtu aliyevikwa nguo za kitani, aliyekuwa juu ya maji ya mto, hapo
alipoinua mkono wake wa kuume na mkono wake wa kushoto kuelekea mbinguni; akaapa kwa
yeye aliye hai milele na milele, ya kwamba itakuwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati;
tena watakapokuwa wamekwisha kuvunja nguvu za hao watu watakatifu, ndipo mambo hayo
yote yatakapotimizwa.
Hosea 1:10
10 Tena itakuwa ya kwamba hesabu ya wana wa Israeli itafanana na mchanga wa bahari,
usioweza kupimwa wala kuhesabiwa; tena itakuwa, badala ya kuambiwa, Ninyi si watu wangu,
wataambiwa, Ninyi ndio wana wa Mungu aliye hai.
Zekaria 14:8
8 Tena itakuwa siku hiyo, ya kwamba maji yaliyo hai yatatoka katika Yerusalemu; nusu yake
itakwenda upande wa bahari ya mashariki, na nusu yake upande wa bahari ya magharibi; wakati
wa hari na wakati wa baridi itakuwa hivi.

AGANO JIPYA
Mathayo 16:16
16 Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.
Mathayo 22:32
32 Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu
wa wafu, bali wa walio hai.
Mathayo 26:63
63 Lakini, Yesu akanyamaza. Kuhani Mkuu akamwambia, Nakuapisha kwa Mungu aliye hai,
utuambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu.
Mathayo 27:63
63 wakasema, Bwana, tumekumbuka kwamba yule mjanja alisema, alipokuwa akali hai, Baada
ya siku tatu nitafufuka.
Marko 12:27
27 Yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. Hivyo mwapotea sana.
Marko 16:11
11 Walakini hao waliposikia kama yu hai, naye amemwona, hawakusadiki.
Luka 20:38
38 Naye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai; kwa kuwa wote huishi kwake.
Luka 24:5, 23
5 nao walipoingiwa na hofu na kuinama kifudifudi hata nchi, hao waliwaambia, Kwa nini
mnamtafuta aliye hai katika wafu?
23 wasiuone mwili wake; wakaja wakasema ya kwamba wametokewa na malaika waliosema
kwamba yu hai.
Yohana 4:10, 11, 50, 51, 53
10 Yesu akajibu, akamwambia, Kama ungaliijua karama ya Mungu, naye ni nani akuambiaye,
Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo hai.
11 Yule mwanamke akamwambia, Bwana, huna kitu cha kutekea, na kisima ni kirefu; basi
umeyapata wapi hayo maji yaliyo hai?
50 Yesu akamwambia, Enenda; mwanao yu hai. Mtu yule akalisadiki lile neno aliloambiwa na
Yesu, naye akashika njia.
51 Hata alipokuwa akishuka, watumwa wake walimlaki, wakisema ya kwamba mtoto wake yu
hai.
53 Basi babaye akafahamu ya kuwa ni saa ile ile aliyoambiwa na Yesu, Mwanao yu hai.
Akaamini yeye na wote wa nyumbani mwake.
Yohana 5:25
25 Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa
Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai.
Yohana 6:57
57 Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye
kunila atakuwa hai kwa mimi.
Yohana 7:38
38 Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani
yake.
Yohana 14:19
19 Bado kitambo kidogo na ulimwengu haunioni tena; bali ninyi mnaniona. Na kwa sababu
mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai.
Matendo 1:3
3 wale aliowadhihirishia nafsi yake, kwa dalili nyingi, baada ya kuteswa kwake, ya kwamba yu
hai, akiwatokea muda wa siku arobaini, na kuyanena mambo yaliyouhusu ufalme wa Mungu.
Matendo 9:41
41 Akampa mkono, akamwinua; hata akiisha kuwaita wale watakatifu na wajane akamweka
mbele yao, hali yu hai.
Matendo 10:42
42 Akatuagiza tuwahubiri watu na kushuhudia ya kuwa huyu ndiye aliyeamriwa na Mungu awe
Mhukumu wa walio hai na wafu.
Matendo 14:15
15 wakisema, Akina bwana, mbona mnafanya haya? Sisi nasi tu wanadamu hali moja na ninyi;
twawahubiri habari njema, ili mgeuke na kuyaacha mambo haya ya ubatili na kumwelekea
Mungu aliye hai, aliyeumba mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo;
Matendo 25:19
19 bali walikuwa na maswali mengine mengine juu yake katika dini yao wenyewe, na katika
habari ya mtu mmoja Yesu, aliyekuwa amekwisha kufa, ambaye Paulo alikaza kusema kwamba
yu hai.
Warumi 6:11, 13
11 Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika
Kristo Yesu.
13 wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni
wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha
za haki.
Warumi 7:1, 2, 3, 9
Ndugu zangu, hamjui (maana nasema na hao waijuao sheria) ya kuwa torati humtawala mtu
wakati anapokuwa yu hai?
2 Kwa maana mwanamke aliye na mume amefungwa na sheria kwa yule mume wakati
anapokuwa yu hai; bali akifa yule mume, amefunguliwa ile sheria ya mume.
3 Basi wakati awapo hai mumewe, kama akiwa na mume mwingine huitwa mzinzi. Ila mumewe
akifa, amekuwa huru, hafungwi na sheria hiyo, hata yeye si mzinzi, ajapoolewa na mume
mwingine.
9 Nami nalikuwa hai hapo kwanza bila sheria; ila ilipokuja ile amri, dhambi ilihuika, nami
nikafa.
Warumi 8:10
10 Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i
hai, kwa sababu ya haki.
Warumi 9:26
26 Tena itakuwa mahali pale walipoambiwa, Ninyi si watu wangu, Hapo wataitwa wana wa
Mungu aliye hai.
Warumi 12:1
Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai,
takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.
Warumi 14:9
9 Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hai pia.
1Wakorintho 7:39
39 Mwanamke hufungwa maadamu mumewe yu hai, lakini ikiwa mumewe amefariki, yu huru
kuolewa na mtu ye yote amtakaye; katika Bwana tu.
1Wakorintho 15:45
45 Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni
roho yenye kuhuisha.
2Wakorintho 3:3
3 mnadhihirishwa kwamba mmekuwa barua ya Kristo tuliyoikatibu, iliyoandikwa si kwa wino,
bali kwa Roho wa Mungu aliye hai; si katika vibao vya mawe, ila katika vibao ambavyo ni
mioyo ya nyama.
2Wakorintho 4:11
11 Kwa maana sisi tulio hai, siku zote twatolewa tufe kwa ajili ya Yesu, ili uzima wa Yesu nao
udhihirishwe katika miili yetu ipatikanayo na mauti.
2Wakorintho 5:15
15 tena alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe,
bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao.
2Wakorintho 6:9, 16
9 kama wasiojulikana, bali wajulikanao sana; kama wanaokufa, kumbe tu hai; kama
wanaorudiwa, bali wasiouawa;
16 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la
Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao
nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
Wagalatia 2:20
20 Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani
yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye
alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.
Wakolosai 2:13
13 Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili
wenu, aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote;
1Wathesalonike 1:9
9 Kwa kuwa wao wenyewe wanatangaza habari zetu, jinsi kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu;
na jinsi mlivyomgeukia Mungu mkaziacha sanamu, ili kumtumikia Mungu aliye hai, wa kweli;
1Wathesalonike 4:15, 17
15 Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata
wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.
17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana
hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
1Timotheo 3:15
15 Lakini nikikawia, upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu,
iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli.
1Timotheo 4:10
10 kwa maana twajitaabisha na kujitahidi kwa kusudi hili, kwa sababu tunamtumaini Mungu
aliye hai, aliye Mwokozi wa watu wote, hasa wa waaminio.
1Timotheo 5:6
6 Bali, yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa ingawa yu hai.
1Timotheo 6:13
13 Nakuagiza mbele za Mungu anayevihifadhi hai vitu vyote, na mbele za Kristo Yesu,
aliyeyaungama maungamo mazuri yale mbele ya Pontio Pilato,
2Timotheo 4:1
Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na
waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake;
Waebrania 3:12
12 Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa
kujitenga na Mungu aliye hai.
Waebrania 4:12
12 Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote
ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo
ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
Waebrania 7:8, 25
8 Na hapa wanadamu wapatikanao na kufa hutwaa sehemu ya kumi; bali huko yeye
ashuhudiwaye kwamba yu hai.
25 Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai
sikuzote ili awaombee.
Waebrania 9:14, 17
14 basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa
Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate
kumwabudu Mungu aliye hai?
17 Kwa maana agano la urithi lina nguvu palipotukia kufa kwa mtu; kwa kuwa halina nguvu
kabisa, akiwa yu hai yeye aliyelifanya.
Waebrania 10:20, 31
20 njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani, mwili wake;
31 Ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai.
Waebrania 12:22
22 Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni,
na majeshi ya malaika elfu nyingi,
Yakobo 4:15
15 Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi.
1Petro 2:4, 5, 24
4 Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye
heshima.
5 Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu,
mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.
24 Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa
mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.
1Petro 4:5, 6
5 Nao watatoa hesabu kwake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa.
6 Maana kwa ajili hiyo hata hao waliokufa walihubiriwa Injili, ili kwamba wahukumiwe katika
mwili kama wahukumiwavyo wanadamu; bali wawe hai katika roho kama Mungu alivyo hai.
Ufunuo 1:18
18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo
funguo za mauti, na za kuzimu.
Ufunuo 2:8
8 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika; Haya ndiyo aneneyo yeye aliye wa kwanza
na wa mwisho, aliyekuwa amekufa, kisha akawa hai.
Ufunuo 3:1
Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho
saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe
umekufa.
Ufunuo 4:10
10 ndipo hao wazee ishirini na wanne huanguka mbele zake yeye aketiye juu ya kile kiti cha
enzi, nao humsujudia yeye aliye hai hata milele na milele, nao huzitupa taji zao mbele ya kile kiti
cha enzi, wakisema,
Ufunuo 7:2
2 Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye
hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari,
Ufunuo 10:6
6 akaapa kwa yeye aliye hai hata milele na milele, yeye aliyeziumba mbingu na vitu vilivyomo,
na nchi na vitu vilivyomo, na bahari na vitu vilivyomo, ya kwamba hapatakuwa na wakati baada
ya haya;
Ufunuo 19:20
20 Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo
ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo
mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la
moto liwakalo kwa kiberiti;
Ufunuo 20:4, 5
4 Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho
zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao
wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya
nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.
5 Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu.

You might also like