You are on page 1of 2

MAONO YA PETRO

Katika Matendo ya mitume kumi, Petro aliona chombo kinatelemshwa kutoka mbinguni kwa Mungu,
ambacho ndani yake walikuwamo wanyama wenye miguu minne, ndege wa angani na viumbe
vitambaavyo. Akasikia sauti ikisema,"PETRO AMKA UCHIJE ULE." Petro alikataa na kusema ya kuwa,
"SIJAKULA KAMWE KITU KILICHO KICHAFU AU NAJISI."

Matendo ya mitume 10:12-14

[12] ambayo ndani yake walikuwamo AINA ZOTE ZA WANYAMA WENYE MIGUU MINNE, NA HAO
WATAMBAAO, NA NDEGE WA ANGANI.

[13] Kisha sauti ikamjia, kusema, ONDOKA, PETRO, UCHIJE ULE.

[14] Lakini Petro akasema, HASHA, BWANA, KWA MAANA SIJAKULA KAMWE KITU KILICHO KICHAFU AU
NAJISI.

Hapa tunaona miaka kadhaa baada ya Masihi kusulubishwa na hata kupaa mbinguni, Ndugu Petro bado
alikua anafuata na kushika sheria ya nyama safi na isiyo safi.

Je, maono haya aliletewa Petro ili kumjulisha ya kuwa kutoka wakati huo sasa Mungu amewatakasa
wanyama wote? La, hasha.

Mara tatu, sauti ilimjia kusema, "VILIVYOTAKASWA NA MUNGU, USIVIITE WEWE NAJISI."

Matendo ya mitume 10:15-16

[15]Sauti ikamjia mara ya pili, ikimwambia, VILIVYOTAKASWA NA MUNGU, USIVIITE WEWE NAJISI.

[16]Jambo hili likatendeka mara tatu; KISHA KILE CHOMBO KIKAPOKEWA TENA MBINGUNI.

Tunaona katika mustari wa kumi na saba, Petro akiwaza kuhusu MAANA ya MAONO hayo aliyoyaona.
Kumbe Mungu alichagua kutumia MAONO haya kama mfano ili kumfundisha Petro jambo tofauti kabisa
na uongo ambao umekuwa ukienezwa na kuwapotosha wengi kuwala wanyama ambao Mungu
hakuwaumba wawe chakula cha mwanadamu.
Baada ya Mungu kumjulisha kuhusu wale watu watatu ambao walikuwa wametumwa kwake na
KORNELIO MTU WA MATAIFA, na kumsihi aende nao wala asione shaka, ndipo alipoelewa wazi maana
ya maono aliyoyaona. Alimwambia Kornerio na watu wa Mataifa waliokuwa pamoja naye;

Matendo ya mitume 10:28

[28]Akawaambia, Ninyi mnajua ya kuwa SI HALALI MTU ALIYE MYAHUDI ASHIKAMANE NA MTU ALIYE
WA TAIFA LINGINE WALA KUMWENDEA, lakini Mungu amenionya, NISIMWITE MTU AWAYE YOTE
MCHAFU WALA NAJISI.

Hebu na tuweze kujihadhali sana na tukome kunena kinyume na Roho Mtakatifu kuhusu MAANA ya
maono ya Petro. Petro kupitia kwa yale maono alionywa asimwite MTU awaye yote najisi wala sio
MNYAMA.Kumaanisha sasa watu wa Mataifa sawasawa na Wayahudi wangeweza kukubarika na Masihi.

Hebu na tukome kuwapotosha watu na kuwandanganya ati Mungu kupitia haya maono aliweza
kumfunza Petro kwamba sasa angeweza kula nyama ya Nguruwe, Panya, Nyoka, Sungura,
vikonokono,.............

Isaiya 66:15-17

[15]Maana BWANA atakuja na moto, na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ILI ATOE MALIPO
YA GHADHABU YAKE KWA MOTO UWAKAO, na maonyo yake kwa miali ya moto.

[16]Kwa maana BWANA atateta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga wake; nao
watakaouawa na BWANA watakuwa wengi.

[17]Watu wale wajitakasao, na kujisafisha katika bustani, nyuma yake aliye katikati; WAKILA NYAMA YA
NGURUWE, NA MACHUKIZO, NA PANYA; WATAKOMA PAMOJA, ASEMA BWANA.

You might also like