You are on page 1of 2

Select Menu

HABARI MPYA

SERIKALI YASIMAMISHA KAZI VIONGOZI WOTE UWANJA WA MKAPATANESCO YAJISAFISHA TATIZO LA


TAA UWANJA WA MKAPAYANGA SC WATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHOROBERTINHO
AELEKEZA NGUVU ZAKE UBINGWA WA LIGI KUU YA TANZANIA BARAMAN UNITED WAIZABA ASTON
VILLA 1-0 OLD TRAFFORDWENYE TAJI LAO MAN CITY YAREJEA KILELENI LIGI KUU ENGLANDNUSU
FAINALI LIGI YA MABINGWA NI AL AHLY V ESPERANCE NA MAMELODI V WYDADTFF YASHUTUSHWA NA
TUHUMA ZA RUSHWA LIGI YA CHAMPIONSHIPMAZOEZI YA MWISHO YANGA KABLA YA KUMALIZANA NA
WANIGERIA KESHOMASHUJAA SIMBA SC MAPEMA KESHO ASUBUHI WAPO DARMAYELE APEWA JEZI YA
HESHIMA YA MABAO 50 YANGAJKT, KITAYOSCE NA PAMBA ZOTE ZATOA SARE CHAMPIONSHIPWYDAD
CASABLANCA 1-0 SIMBA SC (PENALTI 4-3, LIGI YA MABINGWA)SIMBA WALIVYOIANZA SAFARI YA
KUREJEA NYUMBANI LEONABI ASEMA DHAMIRA YA YANGA NI KUWAFUNGA TENA RIVERSTWAHA
KIDUKU AONGEZA MKATABA WA UBALOZI BAKHRESA GROUPSIMBA SC YAFA KIUME MOROCCO,
YATOLEWA KWA MATUTAWIKIENDI YA SHANGWE MERIDIANBETRAIS SAMIA SASA KUZAWADIA SH
MILIONI 10 KILA BAO SIMBA NA YANGA CAFSERIKALI KUANGALIA UPYA MGAWANYO WA MAPATO YA
MECHI ZA KLABU

MWANZO

>UNTAGGED

ULIKUWA MWAKA WA SIMBA SC...

ULIKUWA MWAKA WA SIMBA SC...

UNAPOANZA kuzungumzia makali ya klabu za soka Tanzania, basi Simba itatajwa kama hodari namba
moja, kutokana vitu vyake ilivyowahi kufanya kihistoria, kuanzia mwaka 1974.

Mwaka 1974, kwanza Simba ilianza kwa kutwaa Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, katika
michuano iliyofanyika mjini Dar es Salaam.
Kama wahenga walisema nyota njema huonekana asubuhi, basi hizo zilikuwa dalili njema kwa Simba
kutikisa soka ya Afrika mwaka huo.

Mwisho wa msimu, Simba iliingia kwenye orodha ya klabu nne bora zaidi barani Afrika, kutokana na
kufika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika mwaka huo 1974.

Mwaka huo, Wekundu hao wa Msimbazi walianza Raundi ya Kwanza kwa kumenyana na Linare ya
Lesotho na katika mchezo wa kwanza ugenini, waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 kabla na ushindi wa 2-
1 nyumbani, hivyo kusonga mbele kwa ujumla ya ushindi wa mabao 5-2.

Katika Raundi ya pili, Simba ilimenyana na Zambia Army na katika mchezo wa kwanza mjini Lusaka,
iliibuka na ushindi wa 2-1 kabla ya kumalizia na ushindi wa 1-0 nyumbani, Dar es Salaam, hivyo kusonga
mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-1.

Hatimaye Simba ikaingia Robo Fainali ambako ilikutana na Hearts of Oak ya Ghana na kwenye mchezo
wa kwanza ugenini Wekundu wa Msimbazi waliustaajabisha ulimwengu kwa kuibuka na ushindi wa 2-1,
mabao yakifungwa na Adam Sabu (sasa marehemu) na Abdallah Kibadeni na kwenye marudiano, timu
hizo zilitoka sare ya bila kufungana mjini Dar es Salaam.

Kwa matokeo hayo, Simba ilikata tiketi ya kuinga Nusu Fainali, ambako ilikutana na Mehallal El Kubra ya
Misri na kwenye mchezo wa kwanza Dar es Salaam, Wekundu wa Msimbazi walishinda bao 1-0 na
kwenye marudiano, Waarabu walilipa kisasi cha ushindi wa 1-0.

Kwa matokeo hayo, mchezo huo ulihamia kwenye mikwaju ya penalti na ndipo Simba ilipong’olewa kwa
penalti 3-0. Tena siku hiyo, aliyekuwa kipa wa Simba, Athumani Mambosasa (sasa marehemu)
alilalamikwa kupigwa na vitu akiwa langoni, jambo ambalo lilimfanya ashindwe kuelekeza akili yake
vyema kwenye kuokoa michomo ya Waarabu.

Huu ni kati ya miaka miwili ya kihistoria kwa Simba kwenye soka ya Afrika, mwingine ukiwa ni mwaka
1993, timu hiyo ilipofika fainali ya Kombe la CAF na kufungwa na Stella Abidjan mjini Dar es Salaam 2-0,
baada ya kulazimisha sare ya bila kufungana ugenini.

You might also like