You are on page 1of 1

Swahili Bible Anonymous

mkimbilie Misri. Kaeni huko mpaka nitakapokwambia, maana Herode anakusudia kumwua huyu
14
mtoto." Hivyo, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, akaondoka usiku,
15
akaenda Misri. Akakaa huko mpaka Herode alipokufa. Jambo hilo lilifanyika ili neno alilosema
16
Bwana kwa njia ya nabii litimie: "Nilimwita Mwanangu kutoka Misri." Herode alipogundua
kwamba wale wataalamu wa nyota walikuwa wamemhadaa, alikasirika sana. Akaamuru watoto
wote wa kiume mjini Bethlehemu na kandokando yake wenye umri wa miaka miwili na chini yake
wauawe. Alifanya hivyo kufuatana na muda aliopata kujua kutoka kwa wale wataalamu wa nyota.
17 18
Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyosemwa kwa njia ya nabii Yeremia: "Sauti imesikika mjini
Rama, kilio na maombolezo mengi. Raheli anawalilia watoto wake, wala hataki kutulizwa, maana
19
wote wamefariki." Baada ya kifo cha Herode, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto
20
kule Misri, akamwambia, "Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, urudi tena katika
21
nchi ya Israeli, maana wale waliotaka kumwua mtoto huyo wamekwisha kufa." Basi, Yosefu
22
aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, akarejea katika nchi ya Israeli. Lakini
Yosefu aliposikia kwamba Arkelao mwanawe Herode alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba
yake, aliogopa kwenda huko. Naye baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda katika mkoa wa
23
Galilaya, akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa
njia ya manabii: "Ataitwa Mnazare."

Chapter 3

1 2
Siku hizo Yohane Mbatizaji alitokea, akaanza kuhubiri katika jangwa la Yudea: "Tubuni,
3
maana Ufalme wa mbinguni umekaribia." Huyu Yohane ndiye yule ambaye nabii Isaya alinena
juu yake aliposema: "Sauti ya mtu imesikika jangwani: `Mtayarishieni Bwana njia yake, nyoosheni
4
vijia vyake."` Yohane alivaa vazi lililoshonwa kwa manyoya ya ngamia, na ukanda wa ngozi
5
kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni. Basi, watu kutoka Yerusalemu,
kutoka mkoa wote wa Yudea na sehemu zote za kandokando ya mto Yordani, walimwendea,
6 7
wakaziungama dhambi zao, naye akawabatiza katika mto Yordani. Lakini alipowaona Mafarisayo
wengi na Masadukayo wanamjia ili awabatize, aliwaambia, "Enyi kizazi cha nyoka! Ni nani
8
aliyewadokezea kwamba mnaweza kuiepuka ghadhabu inayokuja? Onyesheni basi kwa matendo,
9
kwamba mmetubu kweli. Msidhani kwamba mtaweza kujitetea kwa kusema, `Baba yetu ni

You might also like