You are on page 1of 1

Swahili Bible Anonymous

New Testament

Matthew

Chapter 1

1
Yesu Kristo alikuwa mzawa wa Daudi, mzawa wa Abrahamu. Hii ndiyo orodha ya ukoo wake:
2 3
Abrahamu alimzaa Isaka, Isaka alimzaa Yakobo, Yakobo alimzaa Yuda na ndugu zake, Yuda
alimzaa Faresi na Zera (mama yao alikuwa Tamari), Faresi alimzaa Hesroni, Hesroni alimzaa Rami,
4 5
Rami alimzaa Aminadabu, Aminadabu alimzaa Nashoni, Nashoni alimzaa Salmoni, Salmoni
alimzaa Boazi (mama yake Boazi alikuwa Rahabu). Boazi na Ruthi walikuwa wazazi wa Obedi,
6
Obedi alimzaa Yese, naye Yese alimzaa Mfalme Daudi. Daudi alimzaa Solomoni (mama yake
7
Solomoni alikuwa mke wa Uria). Solomoni alimzaa Rehoboamu, Rehoboamu alimzaa Abiya,
8
Abiya alimzaa Asa, Asa alimzaa Yehoshafati, Yehoshafati alimzaa Yoramu, Yoramu alimzaa
9 10
Uzia, Uzia alimzaa Yothamu, Yothamu alimzaa Ahazi, Ahazi alimzaa Hezekia, Hezekia
11
alimzaa Manase, Manase alimzaa Amoni, Amoni alimzaa Yosia, Yosia alimzaa Yekonia na
12
ndugu zake. Huo ulikuwa wakati Wayahudi walipopelekwa uhamishoni Babuloni. Baada ya
Wayahudi kupelekwa uhamishomi Babuloni: Yekonia alimzaa Shealtieli, Shealtieli alimzaa
13
Zerobabeli, Zerobabeli alimzaa Abiudi, Abiudi alimzaa Eliakimu, Eliakimu alimzaa Azori,
14 15
Azori alimzaa Zadoki, Zadoki alimzaa Akimu, Akimu alimzaa Eliudi, Eliudi alimzaa Eleazeri,
16
Eleazeri alimzaa Mathani, Mathani alimzaa Yakobo, Yakobo alimzaa Yosefu, aliyekuwa mume
17
wake Maria, mama yake Yesu, aitwaye Kristo. Basi, kulikuwa na vizazi kumi na vinne tangu
Abrahamu mpaka Daudi, vizazi kumi na vinne tangu Daudi mpaka Wayahudi walipochukuliwa
mateka Babuloni, na vizazi kumi na vinne tangu kuchukuliwa mateka mpaka wakati wa Kristo.
18
Basi, hivi ndivyo Yesu Kristo alivyozaliwa: Maria, mama yake, alikuwa ameposwa na Yosefu.
Lakini kabla hawajakaa pamoja kama mume na mke, alionekana kuwa mja mzito kwa uwezo wa
19
Roho Mtakatifu. Yosefu, mumewe, kwa vile alikuwa mwadilifu, hakutaka kumwaibisha
20
hadharani; hivyo alikusudia kumwacha kwa siri. Alipokuwa bado anawaza jambo hilo, malaika
wa Bwana alimtokea katika ndoto, akamwambia, "Yosefu, mwana wa Daudi, usiogope kumchukua

You might also like