You are on page 1of 1

Swahili Bible Anonymous

Kafarnaumu, mji ulio kando ya bahari ya Genesareti, mpakani mwa wilaya za Zabuloni na Naftali,
14 15
akakaa huko. Ndivyo lilivyotimia lile neno lililosemwa kwa njia ya nabii Isaya: "Nchi ya
Zabuloni na nchi ya Naftali, kuelekea baharini ng`ambo ya mto Yordani, Galilaya nchi ya watu wa
16
Mataifa! Watu waliokaa gizani wameona mwanga mkubwa. Nao walioishi katika nchi ya giza
17
na kivuli cha kifo, mwanga umewaangazia!" Tangu wakati huo Yesu alianza kuhubiri akisema,
18
"Tubuni, maana ufalme wa mbinguni umekaribia!" Yesu alipokuwa anatembea kando ya ziwa
Galilaya, aliwaona ndugu wawili wavuvi; Simoni (aitwae Petro) na Andrea, ndugu yake; walikuwa
19
wakivua samaki kwa nyavu ziwani. Basi, akawaambia, "Nifuateni, nami nitawafanya ninyi
20 21
wavuvi wa watu." Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata. ic Alipokwenda mbele kidogo,
aliwaona ndugu wengine wawili: Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo. Hao walikuwa ndani ya
22
mashua pamoja na baba yao Zebedayo, wakitengeneza nyavu zao. Basi Yesu akawaita, nao
23
mara wakaiacha mashua pamoja na baba yao, wakamfuata. Yesu alikuwa anakwenda kila mahali
wilayani Galilaya, akifundisha katika masunagogi na kuhubiri Habari Njema juu ya ufalme wa
24
Mungu. Aliponya kila namna ya maradhi na magonjwa waliyokuwa nayo watu. Habari zake
zikaenea katika mkoa wote wa Siria. Wagonjwa wote wenye maradhi ya kila namna na wale
waliosumbuliwa na kila namna ya taabu: waliopagawa na pepo, wenye kifafa na watu waliokuwa
25
wamelemaa, walipelekwa kwake; naye akawaponya wote. Makundi mengi ya watu kutoka
Galilaya, Dekapoli, Yerusalemu, Yudea na ng`ambo ya mto Yordani, walimfuata.

Chapter 5

1
Yesu alipoyaona makundi ya watu, alipanda mlimani, akaketi. Wanafunzi wake wakamwendea,
2 3
naye akaanza kuwafundisha: "Heri walio maskini rohoni, maana ufalme wa mbinguni ni wao.
4 5 6
Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa. Heri walio wapole, maana watairithi nchi. Heri
7
wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu, maana watashibishwa. Heri walio na huruma,
8 9
maana watahurumiwa. Heri wenye moyo safi, maana watamwona Mungu. Heri wenye kuleta
10
amani, maana wataitwa watoto wa Mungu. Heri wanaoteswa kwa sababu ya kufanya atakavyo
11
Mungu, maana ufalme wa mbinguni ni wao. "Heri yenu ninyi watu wakiwatukana,

You might also like