You are on page 1of 4

Yuda

Utangulizi
Mwandishi wa waraka huu ametambuliwa kuwa ni Yuda, ambaye alikuwa nduguye Yakobo. Yakobo
aliyekuwa msimamizi wa baraza la Yerusalemu na ambaye ndiye mwandishi wa waraka wa Yakobo. Yeye
alikuwa ndugu wa Yesu wa kuzaliwa na Maria (Mk.6:3). Mfanano wa yaliyomo na yale yaliyomo kwenye Waraka
wa pili wa Petro yanaashiria kuwa Yuda alikuwa amehamasishwa na ujumbe wa Petro. Katika (Yuda 1:3)
anaonyesha kuwa alikusudia kuandika kuhusu wokovu wao lakini sasa anabadili nasaha zake kuelekea kwenye
mwelekeo wa kukemea mtazamo wa watu fulani wenye tabia mbaya waliokuwa wanazunguka miongoni mwao
wakiwa wanapotosha neema ya Mungu.

Tarehe
Tarehe ya kuandikwa kwa waraka huu inaweza ikawa kati ya mwaka 65 - 70 B.K., au kama miaka kumi
baadaye. Kama waraka huu uliandikiwa Wakristo wa Kiyahudi huko Palestina, tarehe ya awali inakubalika zaidi.

Wazo Kuu
Yuda anasisitiza umuhimu wa kuishindania imani. Upotovu, yaani, uzushi, ni lazima uonyeshwe wazi
kwamba si kweli. Anaonya kwamba hukumu ya Mungu itakuja juu ya wale wanaopotoka katika imani kama vile
ilivyokuja juu ya Kaini, Kora na Balaamu.

Mgawanyo
• Utangulizi (1:1- 4)
• Maonyo dhidi ya uongo (1: 5 -16)
• Marudi na hitimisho (1:17- 25)

1
Yuda
Kaini, wamekimbilia faida katika kosa la
Salamu Baalamu na kuangamia katika uasi wa Kora.
1Yuda, mtumwa wa Yesu Kisto nduguye 12Watu hawa ni dosari katika karamu zenu

Yakobo, za upendo, wakila pamoja nanyi bila hofu,


wakijilisha pasipo hofu. Wao ni mawingu
Kwa wale walioitwa, wapendwa katika yasiyokuwa na maji, yakichukuliwa na upepo,
Mungu Baba na kuhifadhiwa salama miti isiyo na matunda wakati wa mapuputiko
ndani ya Yesu Kristo: ambayo hunyauka iliyokufa mara mbili na
kung’olewa kabisa. 13Wao ni mawimbi makali ya
2Rehema, amani na upendo viwe kwenu bahari, yakitoa povu la aibu yao wenyewe, ni
kwa wingi. nyota zipoteazo, ambao weusi wa giza ndio
akiba yao waliowekewa milele.
Dhambi Na Hukumu Ya Watu Wasiomcha 14Enoki, mtu wa saba kuanzia Adamu alitoa
Mungu unabii kuhusu watu hawa, akisema, “Tazama,
3Wapenzi, ingawa nilikuwa ninatamani sana Bwana anakuja pamoja na maelfu kwa maelfu
kuwaandikia kuhusu wokovu ambao tunaushiriki ya watakatifu Wake, ili kumhukumu kila mmoja
sisi sote, niliona imenipasa kuwaandikia na na kuwapatiliza wote wasiomcha Mungu kwa
kuwasihi kwamba mwishindanie imani matendo yao yote ya uasi waliyoyatenda,
iliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu. 4Kwa pamoja na maneno yote ya kuchukiza ambayo
kuwa kuna watu waliojipenyeza kwa siri katikati wenye dhambi wamesema dhidi Yake.” 16Watu
yenu, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hawa ni wenye kunung’unika na wenye kutafuta
hii, waovu, wapotoshao neema ya Mungu wetu makosa, wao hufuata tamaa zao mbaya, hujisifu
kuwa ufisadi wakimkana Yeye aliye Bwana wetu kwa maneno makuu kuhusu wao wenyewe na
wa pekee, Bwana Yesu Kristo. kuwasifu mno watu wenye vyeo kwa ajili ya
kujipatia faida.
Hukumu Kwa Walimu Wa Uongo
5Ingawa mmekwisha kujua haya yote, Maonyo Na Mausia
17Lakini ninyi wapenzi, kumbukeni yale
nataka niwakumbushe kuwa Bwana akiisha
kuwaokoa watu Wake kutoka Misri, baadaye Mitume wa Bwana Yesu Kristo waliyotangulia
aliwaangamiza wale ambao hawakuamini. 6Nao kusema. 18Kwa kuwa waliwaambia, “Siku za
malaika ambao hawakulinda nafasi zao, lakini mwisho kutakuwa na watu wenye kudhihaki
wakayaacha makao yaliyokuwa yao hasa, hawa watakaofuata tamaa zao wenyewe za upotovu.”
19Hawa ndio watu wanaowagawa ninyi,
amewaweka katika giza, wakiwa wamefungwa
kwa minyororo ya milele kwa ajili ya hukumu wafuatao tamaa zao za asili wala hawana Roho.
20Lakini ninyi wapenzi, jijengeni katika imani
siku ile kuu. 7Vivyo hivyo, Sodoma na Gomora
na pia ile miji iliyokuwa kando-kando, ambayo yenu iliyo takatifu sana tena ombeni katika Roho
kwa jinsi moja na hao, walijifurahisha kwa Mtakatifu. 21Jilindeni katika upendo wa Mungu
uasherati na kufuata tamaa za mwili zisizo za mkitazamia kwa furaha rehema ya Bwana wetu
asili, waliwekwa wawe mfano kwa kuadhibiwa Yesu Kristo ili awalete katika uzima wa milele.
22Wahurumieni wengine wale wenye shaka,
katika moto wa milele.
8Vivyo hivyo hawa waotao ndoto huutia 23wengine waokoeni kwa kuwanyakua kutoka

mwili unajisi, hukataa kuwa chini ya mamlaka na kwenye moto, nao wengine wahurumieni mkiwa
kunena mabaya juu ya wenye mamlaka. 9Lakini na hofu mkichukia hata vazi lenye mawaa na
hata Malaika Mkuu Mikaeli alipokuwa kutiwa unajisi na mwili.
anashindana na ibilisi juu ya mwili wa Mose,
hakuthubutu kumlaumu, bali alimwambia, Dua Ya Kutakia Heri
24Kwake Yeye awezaye kuwalinda
“Bwana na akukemee!” 10 Lakini watu hawa
hunena mabaya dhidi ya mambo msianguke na kuwaleta ninyi mbele za utukufu
wasiyoyafahamu na katika mambo yale Wake mkuu bila dosari kwa furaha ipitayo kiasi,
25Yeye Mungu pekee, Mwokozi wetu kwa Yesu
wanayoyafahamu kwa hisia kama wanyama
wasio na akili, hayo ndiyo hasa Kristo Bwana wetu, utukufu, ukuu, uweza na
yanayowaharibu. mamlaka vina Yeye tangu milele, sasa na hata
11Ole wao! Kwa kuwa wanaifuata njia ya milele! Amen.

2
Yuda

3
Yuda

You might also like