You are on page 1of 7

WIMBO ULIO BORA

Utangulizi
Jina la kitabu hiki kuitwa, “Wimbo wa Nyimbo,” yaani, “wimbo mzuri kupita zote,” ni tafsiri ya moja kwa moa
kutoka kwenye Kiebrania “Shir hash-shirim” na ya Kiyunani “asma asmaton.” Ile nyongeza “asher li-Shelomoth,”
ambayo imetafsiriwa “Wimbo wa Solomoni”,ndilo chimbuko la jina linalotumika kwa kawaida katika Kiiengereza
“Wimbo wa Solomoni.”, ambapo kwenye Kiswahili kitabu hiki kimepewa jina “Wimbo Ulio Bora” ambalo
limeendana kabisa na lile la Kiebrania. Baada ya mstari wa kufungua tu, Solomoni ametajwa mara sita katika
(1:1,5; 3:7,9,11; 8:11,12 ).Kwa asili Kanisa la Kikristo linamtambua Solomoni kuwa ndiye mwandishi. Lile jina la
kitabu la Kiebrania lililoko hapo juu, ndiyo njia ya kawaida ya kuuelezea uandishi wa mtu katika maandiko ya
kumbukumbu nyingi katika historia ya kawaida na jeografia zinakubaliana na maneno ya kipindi cha Solomoni.

Wazo Kuu
Watu wengine wanafananishia Wimbo Ulio Bora na upendo wa Kristo kwa kanisa lake. Lakini vinavyokubalika
zaidi ni kwamba Wimbo Ulio Bora ni mkusanyo wa mashairi kati ya wawili wapendanao. Picha nzuri ya upendo
wa mume na mke katika ndoa.

Wahusika Wakuu
Mfalme Solomoni, Mwanamke Mshulami na marafiki.

Mwandishi
Solomoni.

Mahali
Israeli – bustani ya mwanamke Mshulami na jumba la Kifalme.

Tarehe
Kama 960 K.K.

Mgawanyo
• Bibi arusi na Bwana arusi. (1:1-2:7)
• Sifa za mpenzi wake. (2:8-3:5)
• Kumsifu bibi arusi. (3:6-5:1)
• Upendo wenye msukosuko. (5:2-7:9)
• Urafiki ambao haujavunjika. (7:10-8:14)

1
WIMBO ULIO BORA
Wimbo ulio Bora wa Solomoni. vyenye kupambwa kwa fedha.
1
Shairi La Kwanza Mpendwa
12Wakati mfalme alipokuwa mezani pake,

Mpendwa. manukato yangu yasambaza harufu yake


2Unibusu kwa busu la kinywa chako, nzuri.
kwa maana upendo wako unafurahisha 13Mpenzi wangu kwangu mimi ni kifuko cha

kuliko divai. manemane kati ya matiti yangu.


3Manukato yako yananukia vizuri, 14Mpenzi wangu kwangu mimi ni kama kishada

jina lako ni kama manukato yaliyomiminwa. cha maua ya mhina


Ndiyo sababu wanawali wanakupenda! yaliyochanua kutoka mashamba ya
4Nichukue twende nawe, na tufanye haraka! mizabibu ya En- Gedi.
Mfalme na anilete ndani ya vyumba vyake.
Mpenzi
Marafiki 15Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu!
Tunakushangilia na kukufurahia, Tazama jinsi ulivyo mzuri!
tutasifu upendo wako zaidi kuliko divai. Macho yako ni kama ya hua.

Mpendwa Mpendwa
Tazama ni jinsi gani ilivyo haki wakupende! 16Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu!
5Mimi ni mweusi, lakini napendeza, O, tazama ni jinsi gani unavyopendeza!
Enyi binti za Yerusalemu, Na kitanda chetu ni cha majani mabichi
weusi kama mahema ya Kedari, mazuri.
kama mapazia ya hema la Solomoni.
6Usinikazie macho kwa sababu mimi ni mweusi, Mpenzi
kwa sababu nimefanywa mweusi na jua. 17Nguzo za nyumba yetu ni mierezi,
Wana wa mama yangu walinikasirikia na mapao yetu ni miberoshi.
na kunifanya niwe mtunza mashamba
ya mizabibu, Mpedwa
shamba mwenyewe langu la mizabibu Mimi ni ua la waridi la Sharoni,
nimeliacha.
7Niambie, wewe ambaye ninakupenda,
2 yungiyungi ya bondeni.

unalisha wapi kundi lako la kondoo Mpenzi


na ni wapi unapowapumzisha kondoo 2Kama yungiyungi katikati ya miiba
wako adhuhuri. ndivyo alivyo mpenzi wangu katikati ya
Kwa nini niwe kama mwanamke wanawali.
aliyefunikwa shela karibu na makundi ya
rafiki zako? Mpendwa
3Kama mti wa mtofaa miongoni mwa miti ya
Marafiki msituni
8Kama hujui, ewe mwanamke mzuri kuliko ndivyo alivyo mpenzi wangu miongoni
wote, mwa wanaume vijana.
fuata nyayo za kondoo na kulisha wana- Ninafurahia kuketi kivulini mwa mwanaume
mbuzi wako huyu,
karibu na hema za wachungaji. na tunda lake ni tamu kwangu.
4Amenichukua mpaka kwenye ukumbi wa

Mpenzi karamu,
9Mpenzi wangu, ninakufananisha na bendera ya huyu mwanaume juu yangu
na farasi jike aliyefungwa katika mojawapo ni upendo.
ya magari ya vita ya Farao. 5Nitie nguvu kwa zabibu kavu,
10Mashavu yako yanapendeza yakiwa na vipuli, niburudishe kwa matofaa,
shingo yako ikiwa na mikufu ya vito. kwa maana ninazimia kwa mapenzi.
11Tutakufanyia vipuli vya dhahabu, 6Mkono wa kushoto uko chini ya kichwa changu,

2
WIMBO ULIO BORA
na mkono wake wa kuume
unanikumbatia.
7Binti za Yerusalemu, ninawaagiza 3 Usiku kucha kwenye kitanda changu
nilimtafuta yule moyo wangu
kwa paa na kwa ayala wa shambani: umpendaye,
Msichochee wala kuamsha mapenzi nilimtafuta huyo mwanaume lakini
hata yatakapotaka yenyewe. sikumpata.
2Sasa nitaondoka na kuzunguka mjini,
8Sikiliza!Mpenzi wangu! kupitia katika barabara zake na
Tazama! Huyu hapa anakuja, viwanjani,
akirukaruka juu milimani nitamtafuta yule moyo wangu umpendaye.
akizunguka juu ya vilima. Kwa hiyo nilimtafuta lakini sikumpata
9Mpenzi wangu ni kama paa au swala kijana. huyo mwanaume.
Tazama! Anasimama nyuma ya ukuta 3Walinzi walinikuta

wetu, walipokuwa wakizunguka mji.


akitazama kupitia madirishani, Nikawauliza, ‘‘Je, mmemwona yule moyo
akichungulia kimiani. wangu umpendaye?’’
10Mpenzi wangu alizungumza na kuniambia, 4Kitambo kidogo tu baada ya kuwapita

“Inuka, mpenzi wangu, nilimpata yule moyo wangu umpendaye.


mrembo wangu, tufuatane. Nilimshika na sikumwachia aende
11Tazama! Wakati wa masika umepita, mpaka nilipomleta katika nyumba ya
mvua imekwisha imekwenda zake. mama yangu,
12Maua yanatokea juu ya nchi, katika chumba cha yule aliyenichukua
majira ya kuimba yamewadia, mimba.
sauti za njiwa zinasikika katika nchi yetu. 5Binti za Yerusalemu, ninawaagiza
13Mtini unatunga matunda yake ya mwanzoni, kwa paa na kwa ayala wa shambani:
zabibu zinazochanua zaeneza harufu Msichochee wala kuamsha mapenzi
yake nzuri. hata yatakapotaka yenyewe.
Inuka, njoo, mpenzi wangu,
mrembo wangu, tufuatane.” 6Ninani huyu anayekuja kutoka jangwani
kama nguzo ya moshi,
Mpenzi anayenukia manemane na uvumba
14Hua wangu penye nyufa za majabali, iliyotengenezwa kwa vikolezo vyote vya
mafichoni pembezoni mwa mlima, mfanyi biashara?
nionyeshe uso wako, 7Tazama! Ni gari la Solomoni

na niisikie sauti yako, lisindikizwalo na mashujaa sitini,


kwa maana sauti yako ni tamu, walio wakuu sana wa Israeli,
na uso wako unapendeza. 8wote wamevaa panga,
15Tukamatie mbweha, wote wazoefu katika vita,
mbweha wadogo wale wanaoharibu kila mmoja na upanga wake pajani,
mashamba ya mizabibu, wamejiandaa kwa ajili ya hofu za usiku.
mashamba yetu ya mizabibu yalichanua. 9Mfalme Solomoni alijitengenezea gari,

alitengeneza kwa mbao kutoka Lebanoni.


Mpendwa 10Nguzo zake alitengeneza za fedha,
16Mpenzi wangu ni wangu nami ni wake, kitako chake kwa dhahabu.
hujilisha katikati ya yungiyungi. Kiti chake kilikuwa kimepambwa kwa
17Mpaka jua linapochomoza, zambarau,
na vivuli vikimbie, gari lake limenakishiwa njumu kwa
rudi, mpenzi wangu, ndani lilifunikwa kwa upendo
na uwe kama paa, wa binti za Yerusalemu.
au kama ayala kijana 11Tokeni nje, ninyi binti za Sayuni,

juu ya vilima vya Betheri. mumtazame Mfalme Solomoni akiwa


amevaa taji,
taji ambalo mama yake alimvika siku ya

3
WIMBO ULIO BORA
arusi yake, 11Midomo yako inadondosha utamu
siku ambayo moyo wake ulishangilia. kama sega la asali, bibi arusi wangu,
maziwa na asali viko chini ya ulimi wako.
Mpenzi Harufu nzuri ya mavazi yako ni kama ile ya

4 Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu!


O, jinsi ulivyo mzuri!
Lebanoni.
12Wewe ni bustani iliyofungwa, dada yangu,

Macho yako nyuma ya shela yako ni bibi arusi wangu,


kama ya hua. wewe ni chanzo cha maji kilichozungukwa
Nywele zako ni kama kundi la mbuzi kabisa, chemchemi iliyofunguliwa.
zikishuka kutoka mlima Gileadi. 13Mimea yako ni bustani ya komamanga yenye
2Meno yako ni kama kundi la kondoo matunda mazuri sana,
waliokatwa manyoya sasa hivi, yenye hina na nardo,
watokao kuogeshwa. 14nardo na zafarani,

Kila mmoja ana pacha lake, mchai na mdalasini,


hakuna hata mmoja aliye peke yake. pamoja na kila aina ya mti wa uvumba,
3Midomo yako ni kama uzi mwekundu, manemane na udi
kinywa chako kinapendeza. na aina zote za vikolezo bora kuliko vyote.
Mashavu yako nyuma ya shela yako 15Wewe ni chemchemi ya bustani,

ni kama vipande viwili vya komamanga. kisima cha maji yatiririkayo,


4Shingo yako ni kama mnara wa Daudi, yatiririkayo kutoka Lebanoni.
uliojengwa kwa madaha,
juu yake zimetundikwa ngao elfu, Mpendwa
zote ni ngao za mashujaa. 16Amka,upepo wa kaskazi,
5Matiti yako mawili ni kama wana paa wawili, na uje, upepo wa kusi!
kama mapacha ya wana paa Vuma juu ya bustani yangu,
wale wajilishao katikati ya yungiyungi. ili harufu yake nzuri iweze kuenea
6Hata papambazuke mpaka ng’ambo.
na vivuli vikimbie, Mpendwa wangu na aje bustanini mwake
nitakwenda kwenye mlima wa manemane na kuonja matunda mazuri sana.
na kwenye kilima cha uvumba.
7Wewe ni mzuri kote, mpenzi wangu, Mpenzi
hakuna hitilafu ndani yako. Nimekuja kwenye bustani yangu, dada

8Twende pamoja nami kutoka Lebanoni, bibi


5 yangu, bibi arusi wangu,
nimekusanya manemane yangu pamoja
arusi wangu, na kikolezo changu,
twende pamoja nami kutoka Lebanoni. nimekula sega langu la asali na asali
Shuka kutoka ncha ya Amana, yangu,
kutoka juu ya Seniri, kilele cha Hermoni, nimekunywa divai yangu na maziwa
kutoka mapango ya simba yangu.
na kutoka mlima wapendapo kukaa
chui. Marafiki
9Umeiba moyo wangu, dada yangu, bibi arusi Kuleni, enyi marafiki, mnywe,
wangu, kunyweni ya kutosha, Ee wapenzi.
umeiba moyo wangu
kwa mtupo mmoja wa macho yako, Mpendwa
kwa kito kimoja cha thamani cha mkufu 2Nililalalakini moyo wangu ulikuwa macho.
wako. Sikiliza! Mpenzi wangu anabisha:
10Tazama jinsi pendo lako linavyofurahisha, “Nifungulie, dada yangu, mpenzi wangu,
dada yangu, bibi arusi wangu! hua wangu, asiye na hitilafu.
Ni mara ngapi zaidi pendo lako linafurahisha Kichwa changu kimeloa umande,
kuliko divai, na nywele zangu manyunyu ya usiku.’’
na harufu ya manukato yako zaidi kuliko 3Nimevua joho langu,

kikolezo cho chote! je, ni lazima nivae tena?

4
WIMBO ULIO BORA
Nimenawa miguu yangu, iliyopambwa kwa Krisolitho.
Je, ni lazima niichafue tena? Mwili wake ni kama pembe ya ndovu
4Mpenzi wangu aliweka mkono wake iliyong’arishwa
kwenye tundu la komeo, iliyopambwa na yakuti samawi.
moyo wangu ulianza kugonga kwa ajili 15Miguu yake ni nguzo za marimari

yake. zilizosimikwa katika vitako vya dhahabu


5Niliinuka kumfungulia mpenzi wangu, safi.
mikono yangu ilidondosha manemane, Sura yake ni kama Lebanoni,
vidole vyangu vikitiririka manemane, mzuri kama miti yake ya mierezi.
penye vipini vya komeo. 16Kinywa chake chenyewe ni utamu,
6Nilimfungulia mpenzi wangu, kwa ujumla yeye ni wa kupendeza.
lakini mpenzi wangu alishaondoka, Huyu ndiye mpenzi wangu, huyu ndiye rafiki
alikuwa amekwenda zake. yangu,
Moyo wangu ulishuka kwa kuondoka Ee binti za Yerusalemu.
kwake.
Nilimtafuta lakini sikumpata. Marafiki
Nilimwita lakini hakunijibu.
7Walinzi walinikuta 6 Mpenzi wako amekwenda wapi,
yule mzuri kupita wanawake wote?
walipokuwa wakifanya zamu za ulinzi Mpenzi wako amegeukia njia ipi,
mjini. tupate kumtafuta pamoja nawe?
Walinipiga, walinijeruhi,
walininyang’anya joho langu, Mpendwa
hao walinzi wa kuta! 2Mpenzi wangu amekwenda bustanini mwake,
8Enyi binti za Yerusalemu, ninawaagiza kwenye vitalu vya vikolezo,
kama mkimpata mpenzi wangu, kujilisha bustanini
mtamwambia nini? na kukusanya yungiyungi.
Mwambieni ninazimia kwa mapenzi. 3Mimi ni wake mpenzi wangu

na mpenzi wangu ni wangu mimi,


Marafiki huyu mwanaume hulisha katikati ya
9Je,
mpendwa wako ni bora kuliko wengine yungiyungi.
namna gani,
ni mzuri sana kupita wanawake wote? Mpenzi
Je, mpendwa wako ni mzuri kuliko wengine, 4Wewe ni mzuri, mpenzi wangu, kama Tirza,
kwa namna gani, upendezaye kama Yerusalemu,
hata unatuagiza hivyo? umetukuka kama jeshi lenye bendera.
5Uyageuze macho yako mbali nami,

Mpendwa yananigharikisha.
10Mpenzi wangu anang’aa tena mwekundu kwa Nywele zako ni kama kundi la mbuzi
afya, wanaotelemka kutoka Gileadi.
wakuvutia miongoni mwa wanaume kumi 6Meno yako ni kama kundi la kondoo

elfu. wanaotoka kuogeshwa.


11Kichwa chake ni dhahabu safi kuliko zote, Kila mmoja ana pacha lake,
nywele zake ni za mawimbi hakuna hata mmojawapo aliye peke
na ni nyeusi kama kunguru. yake.
12Macho yake ni kama ya hua 7Mashavu yako nyuma ya shela yako

kandokando ya vijito vya maji, ni kama vipande viwili vya komamanga.


aliyeogeshwa kwenye maziwa, 8Panaweza kuwapo malkia sitini,

yamepangwa kama vito vya thamani. masuria themanini


13Mashavu yake ni kama matuta ya vikolezo na mabikira wasiohesabika,
yakitoa manukato. 9lakini hua wangu, mkamilifu wangu, ni wa

Midomo yake ni kama yungiyungi namna ya pekee,


inayodondosha manemane. binti pekee kwa mama yake,
14Mikono yake ni fimbo za dhahabu kipenzi cha yeye aliyemzaa.

5
WIMBO ULIO BORA
Wanawali walimwona na kumwita Nywele zako ni kama zulia nene la
mbarikiwa, kutundika ukutani,
malkia na masuria walimsifu. mfalme ametekwa na mashungi yake.
6Tazama jinsi ulivyo mzuri na unavyopendeza,

Marafiki Ee pendo, kwa uzuri wako!


10Ni nani huyu atokeaye kama 7Umbo lako ni kama la mtende,

mapambazuko, nayo matiti yako kama vishada vya


mzuri kama mwezi, mwangavu kama jua, matunda.
ametukuka kama majeshi yenye 8Nilisema, ‘‘Nitakwea mtende,

bendera ? nami nitayashika matunda yake.’’


Matiti yako na yawe kama vishada vya
Mpenzi mzabibu,
11Nilitelemka kwenye kichaka cha miti ya milozi harufu nzuri ya pumzi yako kama
ili kutazama machipuko ya bondeni, matofaa,
kuona kama mizabibu imechipua 9na kinywa chako kama divai bora kuliko zote.

au kama mikomamanga imechanua


maua. Mpendwa
12Kabla sijang’amua, Divai na iende moja kwa moja kwa mpenzi
shauku yangu iliniweka katikati ya magari wangu,
ya kifalme ya kukokotwa na farasi. ikitiririka pole pole juu ya midomo na
meno.
Marafiki 10Mimi ni mali ya mpenzi wangu,
13Rudi,rudi, Ee Mshulami nayo shauku yake ni juu yangu.
rudi, rudi ili tupate kukutazama! 11Njoo, mpenzi wangu, twende mashambani,

twende tukalale huko vijijini.


Mpenzi 12Hebu na twende mapema katika mashamba

Kwa nini kumtazama Mshulami, ya mizabibu


kama kutazama ngoma ya Mahanaimu a ? tuone kama mizabibu imechipua,
kama maua yake yamefunguka,
Ee binti wa mwana wa mfalme, pia kama mikomamanga imetoa maua,
7 tazama jinsi inavyopendeza miguu yako huko nitakupa penzi langu.
katika viatu! 13Mitunguja hutoa harufu zake nzuri,

Miguu yako yenye madaha ni kama vito vya kwenye milango yetu kuna matunda
thamani, mazuri,
kazi ya mikono ya fundi stadi. mapya na ya zamani,
2Kitovu chako ni kama bilauri ya mviringo ambayo nimekuhifadhia wewe, mpenzi
ambayo kamwe haikosi divai wangu.
iliyochanganywa.
Kiuno chako ni kichuguu cha ngano
kilichozungukwa kwa yungiyungi. 8 Laiti ungelikuwa kwangu kama ndugu wa
kiume,
3Matiti yako ni kama wana paa wawili, ambaye aliyanyonya matiti ya mama
mapacha wa swala. yangu!
4Shingo yako ni kama mnara wa pembe ya Kisha, kama ningekukuta huko nje,
ndovu. ningelikubusu,
Macho yako ni vidimbwi vya Heshboni wala hakuna mtu ye yote
karibu na lango la Beth-rabi. angelinidharau.
Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni 2Ningelikuongoza na kukuleta katika nyumba ya

ukitazama kuelekea Dameski. mama yangu,


5Kichwa chako kinakuvika taji kama mlima yeye ambaye angenifundisha.
Karmeli. Ningelikupa divai iliyokolezwa unywe,
Asali ya maua ya mikomamanga yangu.
3Mkono wa kushoto wa huyo mwanaume uko
a13 ‘‘Ngome ya Mahanaimu’’ hapa ina maana ‘‘ngome kati ya
majeshi mawili.’’ chini ya kichwa changu

6
WIMBO ULIO BORA
na mkono wake wa kuume unanikumbatia. Solomoni,
4Bintiza Yerusalemu, ninawaagiza: na mia mbili ni kwa ajili ya wale wanaotunza
msichochee wala kuamsha mapenzi matunda yake.
hadi yatakapotaka yenyewe.
Mpenzi
Marafiki 13Wewe ukaaye bustanini
5Ni nani huyu anayekuja kutoka nyikani pamoja na marafiki mliohudhuria,
akimwegemea mpenzi wake? unisikizishe na mimi sauti yako!

Mpendwa Mpendwa
Nilikuamsha chini ya mtofaa, 14Njoo, mpenzi wangu,

huko mama yako alipotunga mimba yako, uwe kama swala


huko yeye alipata utungu akakuzaa. au kama ayala mdogo
6Nitie kama muhuri moyoni mwako, juu ya milima iliyojaa vikolezo.
kama muhuri kwenye mkono wako,
kwa maana upendo una nguvu kama mauti,
wivu wake ni mkatili kama kuzimu.
Unachoma kama mwali wa moto,
kama mwali mkubwa wa moto wa
BWANA hasa.
7Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo,

mito haiwezi kuugharikisha.


Kama mtu angelitoa
mali yote ya nyumbani mwake kwa ajili
ya upendo,
angelidharauliwa kabisa.

Marafiki
8Tunaye dada mdogo,
matiti yake hayajakua bado.
Tutafanya nini kwa ajili ya dada yetu
wakati atakapokuja kuposwa?
9Kama yeye ni ukuta,

tutajenga minara ya fedha juu yake


na kama yeye ni mlango,
tutazungushia mbao za mierezi.

Mpendwa
10Mimi ni ukuta,
matiti yangu ni kama minara.
Ndivyo ambavyo nimekuwa machoni pake
kama yule anayeleta utoshelevu.
11Solomoni alikuwa na shamba la mizabibu huko

Baal-hamoni,
alikodisha shamba lake la mizabibu kwa
wapangaji.
Kila mmoja angeleta kwa ajili ya matunda
yake Shekeli elfu moja a za fedha.
12Lakini shamba langu la mizabibu ambalo ni

langu mwenyewe ni langu kutoa:


hizo shekeli elfu ni kwa ajili yako, Ee

a11 shekeli 1,000 za fedha ni sawa na kilo 11.5

You might also like