Professional Documents
Culture Documents
Mwalimu Oscar Samba KISIMA CHA TATU Rehobothi.
Mwalimu Oscar Samba KISIMA CHA TATU Rehobothi.
TATU
Toleo la 1
Kitabu hiki hakiuzwi, ila ukiguswa kuichangia huduma hii unaweza kutumia namba
zifuatazo za M-Pesa
Angalizo
Pia kumbuka au fahamu kitabu hiki kimetolewa kwa njia ya “ki-elektroniki” kwa hiyo
ubadilishwaji “convert” kwa njia au namna yoyote ile, au uzaji wowote ule na kwa nia
yoyote ikiwemo ya nia ya wizi ama kujinufaisha ni kosa kisheria na kiroho pia.
2. Unapaswa Kuwa na Imani Dhabiti, lakini pia na Nia au Utayari wa Urejesho ...................................... 9
2. Mukutadha wa Kugombaniwa kwa Visima na Ushindi Katika Kisima cha Tatu. ..................................... 12
Kanuni ..................................................................................................................................................... 18
Mawasiliano ................................................................................................................................................ 35
1. Mukutadha wa Kufukuwa Visima.
Inawezekana kwenye maisha yako kuna vitu vimefukiwa na adui kama Wafilisti
walivyofukia visima vya Ibrahimu. Mwanzo 26:15 Na vile visima vyote walivyochimba
watumwa wa baba yake, siku za Ibrahimu babaye, Wafilisti walikuwa wamevifukia, wakavijaza
kifusi.
18 Isaka akarudi akavichimbua vile visima vya maji walivyovichimba siku za Ibrahimu
babaye; maana wale Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kufa kwake Ibrahimu;
naye akaviita majina kufuata majina alivyoviita babaye.
Yamkini hukuchimba wewe na hata yawezekana aliyevichimba ni wewe pia; la muhimu hapa
ni kufahamu ya kuwa vipo visima katika familia yako, au kwenye maisha yako binafsi
vilivyopaswa kukupatia riziki lakini vimefukiwa.
Ipo miradi mbalimbali ambayo enzi za baba au mzazi wako, au zama fulani ilikuwa ikifanya
kazi lakini kwa sasa imefukiwa. Usijali, upo upako wa kifukuwa visima siku ya leo. Kitabu hiki
kimekuwa kama sehemu ya huo upako. Umesota vya kutosha, lazima sasa ifike mahali uanze
kufukuwa visima. Umeishi maisha ya taabu vya kutosha sasa ni wakati wa kunywa maji ya
kisima chako mwenyewe.
Umenyanyasika na ajira za watu vya kutosha, sasa ni wakati wa kufukuwa kisima au visima
vya kale ambavyo zama hizo vilitumika kama njia ya kupitishia kipato kwa familia, wazazi
na hata wewe binafsi.
Lakini pia inawezekana ni eneo la kihuduma; kipawa au karama fulani iliyokuwa ikifanya
vyema sana hapo zamani lakini sasa imeuawa na adui, au ulishindwa kuichochea na mwenye
kufukia akapata mwanya akaifukia: nayo au navyo pia huhitaji kufukuliwa.
Yamkini ni mahusiano yako na ndugu, mzazi, jamaa; rafiki na hata mtu wako wa karibu sana
kikazi au kihuduma; nacho kisima hicho kinahitaji kufukuliwa. Kufilisika, au mtu aliyesimama
kama mchonganishi na mashitaka yake ya uongo na kukuvurugia mahali. Hata kama ni kweli
ulikosea, ninachofahamu ni kwamba kwa Mungu kuna msamaha; na kisha tunakifukua hicho
kisima.
Mwana mpotevu alipotapanya mali, aliona ni jambo jema tu. Ila njaa ilipoingia, naye
kuteseka ndipo akili zilipomjilia na kuamua sasa kururea nyumbani. Kwa hiyo, taabu
ilikuja ili kumjulisha umekosea! Unaishi chini ya kiwango cha maisha uliyopaswa kuishi
hapo awali; unaishi maisha yasiyo yako.
Maana roho ya kufukia visima haifukii tu visima vya mwili, bali huwa inavifukia rohoni;
kwa maana kwamba akili nazo huwa zinakamatwa. Roho inayokufunga jela, haiishi tu
kukufunga ikakuacha bali huwa inakulinda ili usije ukatoka!
Wakati na Petro au Petro, Paulo na Sila walipokuwa jela bado kulikuwa na ulinzi
maalumu dhidi yao. Na alikadhalika visima vikifukiwa, uwe na hakika na akili au fahamu za
muhusika nazo huletewa usingizi mzito. Ndio maana utamuona ni mtu mwenye furuksa kubwa
tu, lakini shamba lake amelitelekeza kijijini. Wakati angeweza hata kulilima akiwa mjini, na
bado maisha yake yakaenda sawa. Kasoma lakini ukimshauri atafute kazi kwenye "fani" au ujuzi
aliosomea bado anakuwa mkali. Sasa Mungu akitaka kukusaidia, huwa ana ruhusu dhoruba zije
ili kukufanya ufikiri kwa upya moyoni mwako; Luka 15:15 Akaenda akashikamana na mwenyeji
mmoja wa nchi ile; naye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe.
16 Akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe, wala hapana mtu
aliyempa kitu. 17 Alipozingatia moyoni mwake, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba
yangu wanaokula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa.
Nawe usikubali kutazama kila tatizo kwa sura hasi, kama kikwazo au vita. Bali mengine
yanakuja yakiwa na sababu ya kunuia kuzisaidia akili zako ili kufanya marejesho kwa
ulivyopoteza. Ukiweza kusoma kitabu chetu cha USIFIE JANGWANI, basi nenda moja kwa
moja kwenye ujumbe unaoitwa Majira ya Farao Asiyemjua Yusufu. Utakutana na ujumbe na
somo litakalokusaidia kuyaona haya majira kwa sura pana zaidi.
Miaka hiyo ya 390 ndipo Musa alipokuwa akiibukia. Alikuwa na nia ya kuwakomboa,
alipokuwa akimua au tukio lile la kumuamua Mwebrania mwenzake dhidi ya mzawa liloishilia
na hatua ya kumuua huyo Mmisri lilikuwa na maana ya ukombozi wao. Lakini wakamkataa
kama Stefano anavyotuambia kwenye Matendo ya Mitume; 7:35 Musa huyo waliyemkataa,
wakisema, Ni nani aliyekuweka kuwa mkuu na mwamuzi? Ndiye aliyetumwa na Mungu kuwa
mkuu na mkombozi, kwa mkono wa yule malaika aliyemtokea katika kile kijiti.
Katika kumkataa huko kulionyesha dhairi ya kuwa akili zao hazikuwa tayari kutoka
utumwani. Hawakuwa tayari kufukuwa kisima cha ahadi ya nchi ya Kanani kama Bwana
alivyowahaidia wazee wao. Utumwa ule ulifunika akili zao. Ilibidi Musa akae utumwani
miaka 40.
Mungu alipoona sasa imepita miaka kadhaa toka ahadi iachiliwe, ndipo akayaruhusu
haya majira ya Farao asiyemjua Yusufu ili kuhuisha akili zao. Danieli aliyaomba maombi ya
urejesho kwa wakati kabla ya muda kuzidi na bila utumwa kuzidishiwa makali, ni Daniel 9.
Wakati Wengine walilazimika kuyaomba baada ya taabu kukazwa; Kutoka 1:8 Basi akainuka
mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu.
10 Haya! Na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, ikitokea vita, wao nao
wasije wakashikamana na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi hii. 11 Basi
wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji
ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi.
Kutendwa kwa akili maana yake ni jambo ambalo lilihusha fahamu au akili zao pia!
Ashukuriwe Mungu aliyeliruhusu hilo, hata kama adui hakufahamu moja kwa moja alichokuwa
akikifanya, ila Mungu alilitumia kama sehemu ya kuziamsha akili zao. (Wakati wa taabu usione
haya au aibu kumkumbuka Mungu. Usiseme mimi huwa "namtafutaga" mtumishi wakati na
shida tu! ) Huwa "nawaambiaga" sisi ni kama hosipitali; sasa ukiwa unakuja wakati ukiwa
mgonjwa tu hatuwezi kushangaa! Na usipokuja pia hatuna kazi. Furaha na ajira yetu ni kuona
tunatatua matatizo ya watu. "Lakini pia unaweza kwenda hosipitalini kwa ajili ya kufanya
'chekapu' ya afya. Kwa hiyo, wakati mwingine nikutie moyo kuwakumbuka wakufunzi au
walimu wako na kuwashirikisha mema yako wakati wa mafanikio. Japo imizo hapa ni kwamba
ukikwama au kubanwa usiache kurudi kwao kwa kuona haya.
Taabu yao iliamsha akili zao; Kutoka 2:23 Hata baada ya siku zile nyingi mfalme wa
Misri akafa; wana wa Israeli wakaugua kwa sababu ya ule utumwa, wakalia; kilio chao
kikafika juu kwa Mungu kwa sababu ya ule utumwa.
Kutoka 2:24 Mungu akasikia kuugua kwao, Mungu akakumbuka agano lake alilolifanya
na Ibrahimu na Isaka na Yakobo. 3 Musa akasema, Nitageuka sasa, niyaone maono haya
makubwa, na sababu kijiti hiki hakiteketei.
6 Tena akasema, Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na
Mungu wa Yakobo. Musa akaficha uso wake; kwa maana aliogopa kumwangalia Mungu. 7
Bwana akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia
kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao;
8 nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi
njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori,
na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi. 9 Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikilia; tena
nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa.
Sijui kama umeona jambo hapo? Hii ni faida kubwa sana ya haya majira. Ninakutaka
kuwa makini maana hata wao kidogo wangekwama hapa. Badala ya kutazama faida ya hili pito
kama ninavyokufunza kwenye kile kitabu chetu cha MUONE MUNGU NYUMA YA PITO
LAKO, wao waliishilia kuwa na uchungu na maumivu yaliyotaka kuziba maskio yao ya ndani;
hawajui Mungu amenuia kutumia kilio hicho kama sehemu ya kuwatoa utumwani. Kwa hiyo
Musa alipowaendea ugumu ukajidhiirisha; Kutoka 6:6 Basi waambie wana wa Israeli, Mimi ni
YEHOVA, nami nitawatoa ninyi mtoke chini ya mizigo ya Wamisri, nami nitawaokoa na
utumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyoshwa, na kwa hukumu kubwa;
7 nami nitawatwaeni kuwa watu wangu, nitakuwa Mungu kwenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ni
YEHOVA, Mungu wenu, niwatoaye mtoke chini ya mizigo ya Wamisri. 8 Nami nitawaleta hata
nchi ile ambayo naliinua mkono wangu, niwape Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo; nitawapa iwe
urithi wenu; Mimi ni YEHOVA. 9 Musa akawaambia wana wa Israeli maneno haya; lakini
hawakumsikiliza Musa kwa ajili ya uchungu wa moyo, na kwa ajili ya utumwa mgumu.
Kuwa makini uchungu wa jaribu lako usijekufanyika kikwazo, au kwazo katika safari
yako. Mungu anaweza akaja na ujumbe wa kukutoa kifungoni lakini ukajikuta
unasukumia mbali sauti yake. Fikra zako mwenyewe za kukata tamaa zikakuzuilia
kufukuwa kisima. Ukaanza kujisema lakini hii biashara nimeifanya miaka mingi bila
mafanikio, nimeingia hasara na kujikuta nakuwa mtu wa madeni tu. Nimeomba au
nimetuma barua za maombi ya kazi hadi mwenyewe nimechoka: kwa hiyo sioni haja au
sipo tayari. Uwe na hakika kuna mahali unajikwamisha. Lazima uweze kutambua
kubadilika kwa majira. Muda wa kukaa utumwani umeshapita, sasa ni wakati wa kutoka.
Japo kwenye kutoka nako sio kwepesi, lazima uwe tayari kupambana na askari
waliowekwa kaburini kukulinda ili usifufuke kutoka kwenye kaburi la uchumi, kwenye kaburi
lililozika ndoa au kibali chako kihuduma. Lazima uwe na huo utayari. Niposa tukakuwekea
mada ya pili ili kukupa mukutadha au picha hii kiwazi zaidi. Maarifa ni muhimu sana, ili uweze
kutenda vyema katika kila hatua ya maisha yako.
Isaka alilitambua hilo, kufukuzwa kwake na Wafilisti katika mji au eneo alilokwapo
ilikuwa furuksa ya kufukua visima. Nawe tazama mambo kwa jicho kama hilo. Kuna muda
kufukuzwa kazi, kusimamishwa huduma, kuondolewa kwenye nyumba ya kupanga ni sehemu ya
kuinuliwa. Sio kuzalilishwa na kuabishwa, bali ni ngazi na mwanzo wa kufufua karama na
vipawa, ni mlango wa kazi nzuri na hata ajira yako, pia ni mlango wa kupata nyumba yako.
Hukuwahi kusikia ule msemo usemao ya kwamba mlango mmoja ukifungwa mingine
saba inafunguliwa! Unafikiri ni maneno ya kawaida tu! Tunapaswa kutazama mambo
kwa jicho chanya! Katikati ya tatizo unatakiwa kuuona utukufu wa Mungu nyuma yake!
Ndiposa ninakutaka kuendelea kumuabudu Mungu au kuendeleza uhusiano wako na
Mungu vyema unapokuwa upo mahali pagumu katika kitabu chetu kile cha KATIKATI
YA SHIMO MKUMBUKE MUNGU.
Muone Isaka; Mwanzo 26:16 Abimeleki akamwambia Isaka, Utoke kwetu, maana wewe una
nguvu sana kuliko sisi. 17 Basi Isaka akatoka huko akapiga kambi katika bonde la Gerari,
akakaa huko. 18 Isaka akarudi akavichimbua vile visima vya maji walivyovichimba siku za
Ibrahimu babaye; maana wale Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kufa kwake Ibrahimu;
naye akaviita majina kufuata majina alivyoviita babaye.
Neno ondoka wakati mwingine huwa na maana ya nenda kafanikiwe zaidi. Huwa na
maana ya kwa nini unakaa hapa na unaendelea kuteseka na maisha haya magumu wakati
zipo nafasi nyingi za kukufanikisha! Ndio maana wanakufukuza kazi ili sasa ukanzishe
kampuni yako itakayo ajiri maelufu ya watu.
Uliwahi kulielewa hili andiko? Kutoka 1:12 Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa ndivyo
walivyoongezeka na kuzidi kuenea. Nao walichukiwa kwa sababu ya wana wa Israeli.
Lazima ujiulize kwa nini hapo awali ulikiwa huyakumbuki hayo yote? Ile umekumbuka
ni kwamba ni ishara ya msimu mpya. Ni ishara ya kwamba kuna jambo linapaswa
kuzaliwa. Kwa kifupi ni kwamba roho ya manung'uniko itapofusha fikra zako na kuziba
maskio yako yasiweze kusikia na kusikia.
Alitamani ajaye imani, awe na utayari pamoja na nia dhabiti ya kufufuka kwa ndugu yake.
Na aliwekeza kwa Martha zaidi hata ya kwa Miriamu; japo inafahamika Martha ndiye mkubwa,
lakini funzo moja wapo hapa ni kwamba Mungu muda mwingi hutafuta mtu, na sio sana sana
watu wengi; kuna muda huhitaji mtu mmoja tu ili asimame kwenye nafasi yake.
Hii ikupe kuniona ya kuwa wewe ni mtu muhimu katika kuisaidia familia, kanisa au hata
ukoo wako ama timu yako ya kwaya kanisani. Acha kulalamika bali simama sasa kwenye nafasi
yako. Nikutie moyo kupitia tukio zima, ila hapa nakumegea tu mara haya ya ufufuo; Yohana
11:39 Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana,
ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne.
44 Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake
amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.
Unajua ni kwa nini Yesu alikuwa akiuliza maswali kama haya alipokuwa akihitaji
kumuombea mtu! Ama hata kuibua changamoto fulani!
29 Akamwambia, Kwa sababu ya neno hilo, enenda zako, pepo amemtoka binti yako. (Neno
hilo! Lilibeba ni imani yake. Unanijliza najuaje, twende huku;Mathayo 15:28 Ndipo Yesu
akajibu, akamwambia, Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona
binti yake tangu saa ile.)
Nia ilimsukuma kung'ang'ania mujiza. Lakini pia utayari ulimzulia kukata tamaa.
Alikuwa radhi kuvuka kila kikwazo.
Marko 7:30 Akaenda zake nyumbani kwake, akamkuta yule kijana amelazwa kitandani, na yule
pepo amekwisha kumtoka.
Unaenda hata sasa kwenye maombi lakini kiukweli ndani kumepunguka..na moyoni
unamwambia Yesu kupitia muhubiri wake ya kwamba ukiweza waweza tusaidia..! Maana hata
ukiambiwa uelezee tatizo linalokusibu unajikuta unaelezea tu kushindwa kwa waombaji
waliotangulia...Juwa sana yule kiwete wa mlango mzuri alikaa pale muda mwingi...na Yesu
alimfahamu...lakini hakumponya kipindi hicho...maana wakati wake ulikuwa ni kipindi cha
Yohana na Petro...tazama pale jinsi muujiza ule ulivyoleta badiliko la kiinjili ndipo utakapoona
umuhimu wake kwa muda ule. Maana ulitikisa baraza zima la mji. Maana yake kuna namna
misingi ya mji ilitikisika. (Ukiona umefanya jambo la kiroho na eneo fulani kutikisika uwe na
hakika kuna jambo limetokeo. Usiwaone viongozi wanaokuinukia bali ona vitu vilivyotikiswa
vilivyokuwa chini yao.)
Tujione nilipoanzia msingi wa nasaha hii; Marko 9:22 Na mara nyingi amemtupa katika moto,
na katika maji, amwangamize; lakini ukiweza neno lo lote, utuhurumie, na kutusaidia. 23 Yesu
akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye. 24 Mara babaye yule kijana
akapaza sauti, akasema, Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu.
2. Mukutadha wa Kugombaniwa kwa Visima na Ushindi Katika
Kisima cha Tatu.
Kuna mambo kadhaa na muhimu unayohitaji kufahamu kwanza kuhusu kisima cha tatu.
Ni kwamba ni kisima cha ushindi, katika hili hakuna anayeweza kukupokonya au
kukunyanganya tena. Maana kisima cha kwanza walikigombania, hakufa moyo
akafukuwa cha pili nacho wakakipigania, napo hakukata tamaa bali aliendelea kufukua
na cha tatu ambacho hawakukiweza tena. Mwanzo 26:19 Watumwa wa Isaka
wakachimba katika lile bonde, wakapata kisima cha maji yanayobubujika.
21 Wakachimba kisima kingine, wakagombania na hicho tena. Akakiita jina lake Sitna. 22
Akaondoka huko akachimba kisima kingine, wala hicho hawakukigombania. Akakiita jina lake
Rehobothi, akasema, Kwa kuwa sasa Bwana ametufanyia nafasi, nasi tutazidi katika nchi.
Mukutadha mkuu wa kitabu hiki nikukutaka kutokukata tamaa. Maana inawezekana huyo
mchumba ni kisima tu cha pili, wala usijione una mkosi, maana yamkini alikuwa haonekani, ila
kwa maombi yako akaanza kuonekana machoni pa watu, ndipo wakamuona na kumnganyania.
Kwani kabla yako hakuwa hata na kibali, ila baada ya kuwa naye kwenye mahusiano ni kama
vile nyota imeanza kung'aa ama kung'ara. Wala usijiulize maswali mengi, maana waliogombania
visima hawakujua tena kama vilikwepo hapo? Ninaamini kabisa historia waliijua, hata kufukia
inawezekana walihusika kabisa. Lakini macho yao na fikra au akili zao zilifukiwa pamoja na
kisima. Lakini vilipoanza kufukuliwa ndipo waliposhituka na kuanza kusema hivi ni vyetu,
mashindano yakazaliwa hapo.
Na wewe u sawa na mtu aliyefukuwa kisima au visima, awali hakusifika wala kuuona
uzuri wake. Kwa nini? Ni kisima chenye kifusi, lakini sasa kwa kuwa kinatoa maji ndipo
wanaanza kuona uzuri wake na kuanza kugombania. Wala usiwasuate na kuwauliza kwani hapo
awali mlikuwa hamumuoni? Wala usitake kumuuza huyo mpenzi wako wa zamani ya kwamba
ni kwa nini asijliuze hapo awali walimchukia na kumuona wa kawaida ila sasa iweje ang'ae
machoni pao? Wewe fahamu ni kisima kilichofukuliwa. Kila akionaye atakipenda tu. (Zamani
walikikanyaga nakupita juu yake, wakaona ni njia. Na pengine kilipofukiwa kikawekwa na jiwe;
kwa hiyo wakisafiri na kuchoka walikaa juu yake. Lakini wewe ukawa sawa na wale wenye
mashine za kupima aridhi kama chini kuna madini au maji yanapatikana; ukaona na kuanza
kufukuwa.) "Songa mbele kisima chako cha tatu kipo."
Usijiulize sana kwamba eneo hilo lilikaa muda mrefu bila biashara, iweje sasa umeanza
tu wewe kila mtu ameanza kulipigania. Kwani hapo awali walikuwa hawalioni? Uliwahi kupita
aneo mjini ukatamani kama ungefungua hapo biashara; kisha baada ya muda ukakuta kuna mtu
kashawahi! Uwe na hakika kuna namna ulifukuwa kisima, ile uliona na kwenda kuombea, au
kutamka neno; rohoni umefukuwa kisima. Na ukitaka kujua utakuta biashara ile ile uliyoitaka
kuifanya ndiyo iliyokuja kufunguliwa. (Kweli adui anaweza kukuibia wazo, ndio maana
unahitajika kujifunza kufunika mawazo yako kwa damu ya Yesu, ila yote katika yote kufukuwa
visima kupo.)
Hutakiwi kukata tamaa kisa adui amegombania kisima chako, fahamu kuna visima
vinakuja na hataweza kuvigombania tena. Kubwa zaidi ni kuhakikisha unakaza katika
kuvifukuwa.
Kisima cha tatu kina mambo makuu mawili, ambapo Isaka aliyabainisha na kutujuza,
mosi ni nafasi na pili ni baraka za kuzidi au baraka za maongezeko. Rehobothi yako imebeba
nafasi, na kisha baraka za maongezeko, ukishindwa kufukuwa kisima cha pili ni unanizuilia
kuipata Rehobothi yako, usikubali kukwamia Eseki ambacho ni kisma cha kwanza wala Sitna
ikiwa ni chapili bali nenda hadi katika Rehobothi yako ili ujipatie nafasi pamoja na roho ya
maongezeko; Mwanzo 26:22 Akaondoka huko akachimba kisima kingine, wala hicho
hawakukigombania. Akakiita jina lake Rehobothi, akasema, Kwa kuwa sasa Bwana
ametufanyia nafasi, nasi tutazidi katika nchi.
Kuna mambo mengine yanaachiliwa ili kukutoa Eseki yako au Sitna kwa nia njema
kabisa ya kukufikisha Rehobothi kwako. La muhimu ni macho yako ya ndani kuwa tayari
kumsikia Mungu. Akikwambia hapa ni Edeni usitoke hicho ni kitu kingine. Ila kama ni jambo tu
la ubishi wako, na upofu wako wa kutokuona mbele kuna Rehobothi yako; uwe na hakika
utakwama.
Narudia tena ya kwamba, ni lazima kujifunza kumuona Mungu katika mambo magumu,
macho yako yaone uchanya wa mapito na matukio magumu maishani mwako. Kuna
muda unasalitiwa na mchumba kumbe Mungu ameshajua mbele kuna Rehobothi yako.
Kwa hiyo usikubali kuumia sana, ila jifunze kuisubiria na kuipigania Rehobothi yako.
Najua ujumbe huu hautakupa kuachilia kila kitu kizembe. Maana hata Isaka
hakuachilia kizembe, alijua vipo visima viwili mbele. Na ole wao wangesubutu
kumfutilia tena akiwa Rehobothi! Uwe na hakika angewatoa kwa makali ya
upanga hapo. Adui akikufuata Edeni au katika Rehobothi yako lazima uwe mkali.
Na mlango wa vita au upako wa ukali utauona tu. Ila wakija Eseki ama Sitna
wewe kuwa muungwana tu na usonge mbele. Watashangaa walitarajia kukuona
umekonda, umenywea umepoteza matumaini kumbe ndo kwanza unanawiri na
kuchanua. Kwa nini? Unajua Rehobothi yako ipo.
Kwa Isaka maneno Bwana ametufanyia nafasi, nasi tutazidi katika nchi yalikuwa na
maana gani? Ni utimizwaji wa Ahadi ya kiagano juu yao. Kuhusu kumiliki, na kuzaana. Nafasi
maana yake kwa mara ya kwanza anapata eneo ambalo ataishi bila bugudha. Fahamu huko awali
alikuwa akihamishwa na kukimbizwa na mfalme na hata wenyeji wa nchi kumbugudhi yeye au
babaye. Lakini sasa anapokea hakikisho la kuwa na umiliki wa kisehemu chakekwa wakati ule;
na nchi yao kwa wakati ujao.
Kwa hiyo, havikuwa vita vya urithi vya kawaida, haikuwa vita vya kugombania
mali vya kawaida au vya kumfilisi tu. Bali kiroho alikuwa anafukuzwa katika nchi.
Ili nini? Asiwe na makao wala asizae na kuongezeka.
Hawakuwa wanafukia visima tu, kama visima bali walikuwa wanazika ndoto zake au za
uzao wao wa kuja kuishi hapo. (Hii ikufungue macho sana, usije kutazama vita unavyokutana
navyo kama vya kawaida, kwa kuona ni jambo dogo kumbe kiroho unazuiliwa jambo kubwa
sana.) Ndio maana alipopata cha tatu kichoitwa Rehobothi hakuna namna aliendelea
kunyanyaswa tena. Na ndipo mkuu wa nchi alipomfuata na kufanya naye mapatano.
Hii inatupa kufahamu ya kuwa walipokuwa wanafukia visima vya baba yake Ibrahimu
hawakuwa wanafukia mali za marehemu bali walikuwa wanafukia ahadi za Mungu au
mbaraka wa Mungu kwa uzao wake. (Japo walisahau ya kwamba katika baraka hizo
walihaidiwa nao pia: kama mataifa kufaidi pale kwenye Mwanzo 22 ndiyo maana
Eseki..na Tasna... yaani kisima cha kwanza na cha pili vilikuwa vyao.)
Visima vile vilikuwa ni ishara ya mbaraka wa Mungu kwa uzao wa Ibrahimu. Na adui
akijua kuwa kwako kuna baraka ya namna hii, vita vyake sio vidogo. Kwa wengine ndoa ni hii
ishara, na ukiwa na ndoa ya namna hiyo uwe na hakika utakutana na vita vikali sana. (Hii ikupe
pia kupigania visima vyako, wala usikubali kuvipoteza kirahisi.)
Baraka za uzao na kumiliki nchi zisingeweza kuwa kwa Isaka mpaka amefukuwa visima.
Na kwa mataifa ikiwemo taifa la Filisti baraka hizi zisingeweza kuwa hai hadi visima
vimefukuliwa.
Hukuwahi kuona hata ndugu waliokupiga vita nao wamefanikiwa mara tu baada ya wewe
kuanza kufanikiwa? Uwe na hakika walifukia na visima vyao; (wapokufukuza, walifukuza
mbaraka! Ulipokaza na kufanikiwa: nao pia wakaanza kula matunda ya mbaraka) yaani kile cha
kwanza na cha pili. Sema tu hawakujua wanajua. Na adui tabia yake ni moja, yupo tayari
asababishe ajali itakayouwa watu wote kwenye ndege au basi, akinuia kumua mtu mmoja tu
ambaye ni muhubiri wa injili. Kama Mungu alivyokuwa radhi kufanya lolote bila kujali kuna
wafanya biashara wenye mkopo wa Kabaila au benki kwenye melikebu aliyopanda Yona
akimtafuta tu Yona!
Sasa Shetani yu radhi kuhakimisha na wao visima vyao vinafukiwa akinuia tu kukuzuilia
wewe usiifikie Rehobothi yako. Ndio maana kupenya kwako ni muhimu ili na ndugu
zako nao waweze kupokea mpenyo. Nje ya hapo utasalia unalalamika tu mbona ndugu
zako nao wamekwama eneo ulilokwama wewe! Wenyeji wa nchi hawezi pata visima
vyao viwili hadi wewe umeamua kuvifukuwa; kuna muda wataweza kufukia lakini
wasiweze kufukua. Adui kuna muda anajua kuloga lakini hajui kuagua. Kule Misri
kipindi cha Musa waganga wa Farao walitengeneza na wao vyura ili kumuiga Mungu
wetu, na wakashindwa kuwaondoa ikabidi Musa aje kuwasaidia. Kwa hiyo usishangae
kushindwa kwao.
Ikupe kufahamu pia ya kwamba kipindi kama hiki usikubali kikupite, maana upako huu
huja ili kukuwezesha kupokea mpenyo. Vita vya namna hii bila Mungu kuingilia kati huwezi
penya maana adui anafahamu thamani yake, hawezi kukuachilia kirahisi.
Kikifukiwa na fimbo yao ya enzi, uwe na hakika kuwa inahitajika mamlaka ya fimbo ya
enzi ya Rohoni pia ili kupambana na fimbo yao ya rohoni. Ikupe kufahamu kuwa unaopigana
nao hupigani nao kikawaida, hushindani nao kikawaida. Bali nyuma yao ipo roho, kuna fimbo ya
enzi pia. Sasa rehema itawanyima uhalali tu lazima.
Kwa hiyo, kama angekwama ni ishara ya kukwama kwa jambo kubwa sana. Maana ahadi
za Mungu kwa Ibrahimu zilihusisha pia wokovu kwa uzao wake. Uzao kama mchanga wa bahari
ni watu kweli wa kwake, lakini zaidi ni uzao hata kwa wale ambao watakuja kuunganishwa naye
kumpitia Yesu Kristo kama Isaka wa pili; kama Wagalatia 3 inavyotujiza. Mimi na wewe tulio
okoka ni sehemu ya kisima kilichofukuliwa.
Sasa kama hujaokoka, tafadhali hii iwe ni nafasi yako ya kumuamini huyu Yesu sasa ili
uweze kunufuka na dhima hii ya womovu. Hayo maandiko niliyokupatia hapo
"commentary" moja wapo ya Matthew Henry imeunganisha hayo maandiko ya Hesabu
21:10-20 na kisima kama wokovu, uzima wa milele, ikitupeleka kwenye maji ya Yohana
7:38-39 (huwakilisha Roho Mtakatifu) na hata hiyo Isaya 12:3 inayonena habari za
wokovu.
Kitabu hiki kimenikumbusha mbali sana! Miaka fulani nilishangaa (nikiwa mdogo
kwenye miaka kumi naa..) nilitoka safarini na kukuta ndugu yangu mmoja au mtu wa karibu
kang'oa maua yangu. Na anatoa sababu fulani tu japo ni za kiroho. Sasa leo ndo ufahamu
unanijia kumbe na mimi nilikuwa nang'olewa kwenye urithi! "Sikuhitajika juu ya nchi."
Kingine nilipotaka kufuga kuku upinzani ulikuwa mkubwa sana kutoka kwa mtu mmoja,
anadai hawana faida. Mara ukienda chuo utamuachia nani, sijui unamtwisha mama mzigo. Mtu
anakuwa mkali hadi unashanga! Sasa ukimya ukanisaidia. Japo haikuishia hapo...uwe na hakika
ya kwamba vita kama hivi havitaki uwe sehemu ya urithi wa familia. Havitaki kukuona ukiwa
unatumia rasilimali za kifamilia kupiga hatua.
Kuna kipindi nilikuwa nachukiwa mimi pamoja na mauwa yangu. (Maana sikuja kuchoka
kupanda mengine.) Unafikiri ni maua ndo yalikuwa yanachukiwa la! Kwani hili sio kwa mtu
mmoja. (Sasa usiulize ni wakina nani!) Ila fahamu ya kuwa lilikuwa ni jambo la kiroho.
Hukuwahi kupitia mahali pagumu kwenye kilimo na ufugaji hadi maua nyumbani yakakauka!
Hadi ukifuga paka aidha wafe au wakimbie, ama wadumaye! Jaribu kufuga mbwa utakutana na
kesi kama hiyo hiyo! Zinakufa biashara na paka nao wanakufa na maua yananyauka tu bila
sababu ya msingi. Lazimisha bustani ndo utaelewa au miti ya matunda.
Upinzani mwingine ni ishara ya kukufahamisha ya kuwa upo vitani, na vita hivyo kuna
kitu vinanuia kufanya. Alipokufa baba ndipo nilipoanza kuelewa maana ya vile vita. Sasa
bahati nzuri nilishapambana navyo toka mapema, ila adui alikusudia jambo gumu kweli
kweli.
Fahamu:
Uchimbaji wa Ibrahimu kama mvumbuzi, au mwanzilishi; na "strago" au kuteseka ama
kupambana kwa Isaka katika kufukuwa vilivyofukiwa kulikuwa ni mtaji kwa ajili ya uzao wake
ujao. Nawe usiache kupambana maana ni nani ajauye kuwa mapambano yako ni mbegu kwa ajili
ya washirika wako au watu ambao Mungu atakupa kuwachunga ama kuwaongoza na hata uzao
wako; Kumbukumbu la Torati 6:10 Tena itakuwa atakapokwisha Bwana, Mungu wako,
kukuleta katika nchi aliyowaapia babu zako, Ibrahimu na Isaka na Yakobo, ya kuwa atakupa;
miji mikubwa mizuri usiyoijenga wewe; 11 na nyumba zimejaa vitu vyema vyote usizojaza
wewe, na visima vimefukuliwa usivyofukua wewe, mashamba ya mizabibu na mizeituni
usiyoipanda wewe, nawe utakula na kushiba.
Msaada: Ukipanda Mua Panda na Majivu. Sijui aridhi ya kwenu, ila huku kwetu
nilijikuta naingia hasara mara kadhaa. Niliwahi kuleta mbegu ya mua kutoka Singida, nikiipokea
Dodoma na kuifadhi kisha kuja kuipanda huku Rombo-Kilimanjaro nayo cha ajabu ikaliwa.
Sikujua maana mbegu kadhaa nazo zilikuwa zikiliwa.
Afadhi ioteshwe kipindi ambacho sicho cha mvua nyingi, au eneo husika liwe halina maji
mengi. Likiwa tu na maji mengi ni kosa. Maana kuna aina fulani ya wadudu ambao hushambulia
sio mbegu au kipande kilichopandwa bali chipukizi likiwa teke, yaani bado changa.
Lakini, ukiotesha na majivu, hakika hawawezi kusogelea. Hii ni siri hata kwa wale
bacteria au wadudu wanaoshambulia migomba hususani maaeneo ambayo siyo ya mvua nyingi
na unapoamua kuimwagilia basi hujirundika hapo. Na kuna aina fulani ya migomba
hushambuliwaga zaida katika maeneo mbalimbali (tunaita ndizi kisukari.)
Usikubali kuanza mradi bila maombi ya kutosha. Maombi ni majivu kwa muwa na
ndizi kisukari. Maombi ni ulinzi kwa hilo wazo. Hata unapochipuza endelea kuhakimisha
unauzingira kwa maombi. Asubuhi na mchana. Uwe na tabia hii hadi pale majira
yatakapobadilika. Ni kweli majira hubadilika, lakini hata kabla ya kubadilika unaweza
kupanda mbegu jangwani au eneo la ukame na ukavuna kama Isaka.
Isaka katika sura hiyo hiyo ya kufukuwa visima, alitokewa na Mungu na kuonywa
kuwa asielekee Misri kusaka chakula bali atafanikiwa akiwa hapo hapo. Alipotii,
ndipo alipokuja na kufukuwa visima. Maandiko hutujuza kuwa alipanda mbevu
na kuvuna sana. Ni nchi kame lakini kwake ikapandwa. Na wewe ukipanda weka
na majivu.
Kanuni
1. Omba Rehema. Rehema ni sawa na kufungua njia ya kupita kwenye eneo ambalo njia
haikwepo. Rehema humpatia Mungu uhalali wa kukupigania, rehema hurejesha neema
uliyowahi kuipoteza au ambayo iliondoka kutokana na uzembe wa kutokuitumia. Lakini pia
rehema huwa na kazi ya kuachilia ama hata kuongeza nguvu za Mungu ambazo hukusaidia
katika kufukuwa visima. Rehema huondosha uhalali wa adui au ile haki ya adui katika kuvifukia,
kuvilinda visifukuliwe na kadhalika.
Kwa hiyo hakikisha unafanya toba kwa muda. Kufa kwa Ibrahimu kuliwafanya
Wafilisti kufukia visima! Sio jambo la kawaida maana Isaka tu fahamu ndiye mrithi pekee wa
Ibrahimu, kivyovyote vile ipo sababu iliyopelekea ucheleweshaji wa urithi huu juu yake.
Kuna vitu tunaitaga zuio kwenye upande wa urithi. Zuio hili huweza kuwa ni laana,
au aina fulani ya maneno yaliyowahi kuachiliwa ama ni aina pia ya kifungo kwa watu ambao
wapo kwenye aridhi au eneo husika ama ni swala la kifungo kinachotembea kizazi na kizazi.
Lakini pia kama mali hiyo haikuwa halali, nikimaanisha ilitokana na msaada wa miungu ya
kigeni, uwe na uhakika kuna uwezekano wa kuwepo kwa mashariti ya mganga au ya kishirikina
hapo. Mashariti hayo yanaweza kuwa na vigezo kadhaa, ambavyo mtapaswa kuvitimiza. Na
nyingine huwa na agizo au zuio la kutokurithiwa na yeyote kabisa, ama ikachagua mrithi, yaani
kubagua wengine.
Wakati Joshua anaibomoa Yeriko aliweka mashariti kwa atakayetaka kuja kuijenga upya.
Mashariti hayo yalihitaji sadaka ya mtoto wa kwanza katika misingi yake. Na malango yake ni
sadaka ya mtoto wa mwisho. Kwa hiyo, ukitoa sadaka moja ya mtoto wa kwanza utafanikiwa
kuujenga mji, au ukuta wake. Lakini usipotoa ya mtoto wa mwisho maana yake malango yake
hayawezi jengwa.
Kwa hiyo, kama malango hayajajengwa ni mji usio na ulinzi, na ni mji ambao hauwezi
kupenyeza baraka maana hauna malango au mafanikio hayawezi patikana kwa watu wa mji huo.
Maana Isaya 60:11-13 hutaumbia kuhusu malango ya kwamba yawe wazi ili watu waweze
kumuletea utajiri wakiongozwa na wafalme wao.
Swala la ukiwa pia litatawala maana ni mji ambao hakuna anyeutaka. Kwa sababu
malango yake hayajajengwa. Haya ni mambo muhimu sana ya rohoni unapaswa kuyajua. Kwa
hiyo kama ni fedha au mali zenye mashariti kadhaa ya marehemu kama ilivyokuwa kwa Yoshua,
lazima ajaye yaani mfalme Ahabu akitaka kujenga ayajue na ayatimize hayo mashariti. Nje ya
hapo hiyo mali ya marehemu itapuputika tu au itapotea tu! Sikwambii haya bure maana hata
Isaka alichimbua visima baada ya Mungu kumtokea kiagano kama Mungu wa Ibrahimu babaye.
(Na mali ya mashiriti ya upande wa pili huhitaji kujua namna ya kutembea kiagano au katika
agano la marehemu ili naye Mungu wa marehemu akutoke kiagano; ila ni kama hujaamua
kuokoka au kumkabidhi Yesu hiyo kesi).Hii ina maana kwamba swala la visima kama urithi
halikuwa la kawaida kama alivyorithi mali nyingine kirahisi.
Tuanze na Yoshua dhidi ya Ahabu kama aliyekuja kupaswa kutimiza mashariti. Yoshua;
Yoshua 6:26 Naye Yoshua akawaapisha kiapo wakati ule, akasema, Na alaaniwe mbele za
Bwana mtu yule atakayeinuka na kuujenga tena mji huu wa Yeriko; ataweka msingi wake kwa
kufiliwa na mzaliwa wa kwanza wake, tena atayasimamisha malango yake kwa kufiliwa na mtoto
wake mwanamume aliye mdogo.
Nathani umeona! Ndio maana kama umeokoka, na unataka kurithi mali ambayo hujui vyanzo
vyake kiuhalisia. Hunabudi kuwekeza muda wa kutosha kwenye rehema; ( ya namna
ilivyopatikana). Pili inunue hiyo mali kwa Damu ya Yesu, na katika kuinunua hakikisha
unaitumia hiyo damu kufuta mashariti yoyote yaliyowekwa kama sehemu ya kuirithi hiyo mali.
Kisha vunja maagano yote yanayoambatana na hiyo mali. Pangua kila kafara iyowahi kuyolewa
au sadaka kwa miungu mingine. Ondoa zui juu yako kuihusu, kisha tangaza wewe ndiwe
mmiliki mpya na halali wa hiyo mali. Yaombe kwa muda na usiache kuambatanisha na sadaka
maombi haya. Maana sadaka huwa na tabia ya kupambana na sadaka nyingine.
Ukifeli hapa au nje ya hapo, ujiandae kusota na kesi hiyo mahakamani sana huku
mali ikipuputika yenyewe. Na wengine wanakosa kabisa utayari wa kufuatilia hizi mali hadi
zinapotea kabisa. Utakuta tu hajui ni kwa nini hataki kuifuatilia, au kila akipanga anakutana na
kikwazo, atakosa hata nauli au udhuru wowote utamkwamisha tu. Akilazimisha anajikuta
ugomvi mkubwa umeibuka baina yake na ndugu zake kiasi cha kutokuwapa mwanya wa kulijadi
kwa muda huo. Uonapo dalili hizo huna budi kuliweka magotini.
Sio kiroho hata kidogo kukataa kurithi mali za unayostahi kurithi kwa kujisemea kuwa
hujui chanzo chake! Huku nako ni aina fulani ya kulogwa akili. Unaweza kujiona upo
kiriho sana na ikawa ni kweli ni kiroho lakini ni kiroho kile cha giza. Kuna giza
limefukia akili zako katika huo urifhi kwa kubana fahamu au fikra zako mahali.
Unawezaje kurithi jina la baba alafu ugomee kurithi mali zake? Hata kama una
uhakika sio halali, chukua hatua ya kuziombea na kuzihalalisha ili uweze kuzimiliki. Narudia
tena ni kulogwa akili kugoma na hata kuzembea kurithi mali za mzazi. Ukishindwa pia
kuzigombania au kuzipambania/kuzipigania kwa njia ya maombi na mhakama kwa kusema
unaachilia nako pia ni kufungwa fahamu. Isaka angeachilia visima vyake bila kuvifukuwa
angekwama tu. Na huwezi pata kisima cha tatu kama hukufukua cha kwanza na cha pili. Hili
lishike daima.
Sijui sana ila nijualo ni kwamba mambo ya rohoni ni lazima tujifunze kufukuwa visima
vilivyofukiwa na Wafilisti, Isaka angewaza hivyo angekwama tu. Na hayo maandiko
yanatumiwa vibaya na hila ya adui kama nyoka amekaa hapo. Fahamu hata alipomtokea Yesu
alimsomea maandiko tena kwa usahihi, lakini Yesu aligundua hila yake na kumpa tafsiri sahihi
kimaandiko pia. Yakwamba hakubisha malaika huweza kuagizwa kweli ili kumuokoka, ila
inategemea na mazingira, kama itakuwa yu hatarini kuangushwa na adui sawa. Ila sio katika
mazingira ya Yesu kujiangusha, huko ni kumjaribu Mungu. Na wewe lazima uwe na maandiko
ya kukinzana na hizi hila.
Na maandiko ya Isaka kuchimbua visima ni jibu tosha kwa fikra kama hizi. Ni lazima
kuhakikisha ya kuwa adui hapewi mwanya wa kutuzuilia mibaraka yetu.
Nasikia mtu kwenye ulimwengu wa roho akisema ya kuwa lakini kuna migogoro!
Nisikilize, Damu ya YESU iingize vitani. Omba, na baada ya muda urithi utakufuata. Migogoro
mingine ni matokeo ya zuio lililokaa kwenye urithi.
3 Kaa ugenini katika nchi hiyo, nami nitakuwa pamoja nawe, na kukubariki, maana nitakupa
wewe na uzao wako nchi hizi zote. Nami nitakifanya imara kiapo nilichomwapia Ibrahimu baba
yako. 4 Nitazidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, nami nitawapa uzao wako nchi hizi zote,
na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia.
Mwanzo 26:6 Isaka akakaa katika Gerari....18 Isaka akarudi akavichimbua vile visima vya maji
walivyovichimba siku za Ibrahimu babaye; maana wale Wafilisti walikuwa wamevifukia baada
ya kufa kwake Ibrahimu; naye akaviita majina kufuata majina alivyoviita babaye.
Hapo awali nilikwambia pia uenda zuio hilo ni laana au aina fulani ya maneno
yaliyowahi kuachilia. Huku kwetu na jirani yetu kuna aridhi moja iliyonenewa maneno kwa
kichagga ya kwamba, "nelaa mwesha." Ya kwamba atalala au ataishi hapo mtu mgeni, "wakuja."
Kwa hiyo kuna zuio la mwenyeji kuishi hapo. Yaani ndugu au mtu wa damu. Sababu ni
kwamba huyo bibi aliyekuwa anaishi hapo walimtesa na njaa, akafa njaa, katika kuelekea nakufa
aligundua kuwa urithi ule utatwaliwa tu na watu ambao walipaswa kumtunza; ndiposa akaachilia
hilo zuio. Sasa wewe unakuja kama mjukuu, au hata ndugu mwingine tu na ukapewa hiyo aridhi
iwe urithi wako, ghafula unashangaa kila unachokifanya hapo hakiendi. Wanakuja watu
wanakwambia hapa bibi yako au ndugu huyu alisema hivi na hivi na ukitazama ni kweli hakuna
kinachoenda. Utafanyaje? Na ukijaribu kuuza uwe na hakika fedha ya namna hiyo hailiki.
Mungu aliwahi kughadhabishwa na maisha ya watoto na malezi ya baba yao kuhani Eli.
Akaachiliana laana kama hii juu ya uzao wao (kama kuna laana huwa siipendi, kuiogopa ni ile ya
uzao, maana inaadhiri hata watu ambao kiuhalisia wanazaliwa hatiani au wanaingia hatiani kwa
kosa la mwingine). 1 Samweli 2:30 Kwa sababu hiyo, Bwana, Mungu wa Israeli, asema, Ni
kweli, nalisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele;
lakini sasa Bwana asema, Jambo hili na liwe mbali nami; kwa maana wao wanaoniheshimu
nitawaheshimu, na wao wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu.
31 Angalia, siku zinakuja, nitakapoukata mkono wako, na mkono wa mbari ya baba yako, hata
nyumbani mwako hatakuwako mzee. 32 Nawe utalitazama teso la maskani yangu, katika utajiri
wote watakaopewa Israeli; wala nyumbani mwako hatakuwako mzee milele.
33 Tena mtu wa kwako, ambaye sitamtenga na madhabahu yangu, atakuwa mtu wa kukupofusha
macho, na kukuhuzunisha moyo; tena wazao wote wa nyumba yako watakufa wapatapo kuwa
watu wazima. 36 Kisha itakuwa, ya kwamba kila mtu atakayesalia katika nyumba yako
atakwenda kumsujudia, apate kipande kidogo cha fedha, na mkate mmoja; na kumwambia,
Tafadhali unitie katika kazi mojawapo ya ukuhani, nipate kula kipande kidogo cha mkate.
Hapo kuna paka laana ya watu kutokuwa wazee. Kuna mchungaji mmoja ambaye mama
(36), dada (20’s) na baba (56) walifariki wakiwa tu na umri wa kawaida, hawakufikilia uzee,
tena kama mama na dada ndo mapema zaidi. Anasema kabla ya baba kufa roho ya mauti
ilimuwinda yeye, na aliikemea ndotoni: ndipo baba yake akaja kufa. Alipoona hivyo likawa
ishara kwake baada ya kuokoka, (mama alifariki akiwa bado hajaokoka) na kuwa na huu
ufahamu. Aliamua kuingia kwenye maombi ya muda na kuikomesha hii hali huko kwao. Baba
alikuwa mganga kwa hiyo huwezi juwa sana kuna damu nyingi kiasi gani zilikuwa zikipiga
kelele juu yao, na wengineo walisema baba ndo alimuua mama. Nakujuza haya ili kama na
kwako kuna vitu vya namna hiyo ujifunze kuvishughulikia.
Jambo mojawapo ninalotaka ulione hapo ni hili la kuachiliwa laana kwenye eneo la
kutokurithi nafasi ya ukuhani. Mungu anasema maneno magumu ya kuwa mkono wa Eli
utakatwa, na ule wa baba yake yaani urithi na baraka za kiurithi au uweza huo utakatwa.
Ukuhani ulikuwa ni kisima cha baraka kwa uzao huu wa Eli kuhani; ambapo naye aliridhi
ikitokea kwa Haruni babu yao. Ni njia na mkondo wa baraka pia. Lakini kwa bahati mbaya
kisima hiki kinafunikwa. Sasa hapa mfunikaji ni Mungu, kwako inawezekana mfukiaji ni Shetani.
Lakini hata kama mfukiaji ni Mungu bado kuna nafasi ya matengenezo! Tazama jambo
hili lilivyokuja kutimia hata mikaa kadhaa baadae, sijui ni baada ya uzao wa ngapi ila
inawezekana ni wa tatu hata wa nne baada ya kuhani Eli, ilipita hesabu ya miaka au kipindi cha
kutoka utawala wa kuhani na mwamuzi Samweli, kisha Sauli aliyetawala miaka 40 na Daudi 40,
unaweza kupata miaka hiyo au uweza kutafuta kwa kufuatilia pia uzao huo zaidi. Kipindi cha
mwanzo cha utawala wa mfalme Sulemani mambo huja kujidhiirisha; 1 Wafalme 2:27 Hivyo
Sulemani akamtoa Abiathari asiwe kuhani wa Bwana; ili alitimize neno la Bwana, alilonena juu
ya nyumba ya Eli katika Shilo.
Kwa hiyo kuna nafasi unaweza kuondolewa na kumbe kwenye ulimwengu wa roho kuna
maneno au zuio la kilaana limesababisha. Ni muhimu ujue cha kufanya unapopitia nafasi
kama hii. Kumjua Mfilisti wako ni jambo muhimu sana.
Kijana mmoja alifukuzwa kazi, kumbe ni matokeo ya mke wake kusimama kama Mfikisti na
kinywa kibaya. Mke huyu alikuwa amemkosea mumewe vya kutosha, na mumewe kumrudisha
kwa wazazi kwa muda ili wamfundishe na kumsaidia ili ajue kuishi na mume. Usiku mmoja
akaota anamuuza mumewe kwa "bosi" au muajiri wake mumewe kwa shinlingi elufu 30 za
kitanzania. Babaye alikuwa ni mchungaji na alimuonya. Tafsiri yake ilikuwa ni roho ya usaliti
kwa mumewe katika eneo la kazi au nafasi, maana fedha hiyo iliwakilisha vipande thelathini vya
fedha alivyopewa Yuda. Sio jambo la kawaida, bali kuna roho ilimpa majukumu hayo ya usaliti,
(kwani hata Yuda hizo fedha alipewa na Wakuu wa Makuhani na baraza lao.) Haikuchukuwa
siku kadhaa mumewe alifukuzwa kazi na kupita sana kiuchumi.
Siku moja kijana huyu naye akaja akaota ndoto babu yake ambaye ni marehemu
anamkabithi huyu mwanamke pochi ya kiume yaani ya huu mume, "waleti" lakini iliyochaka
chakaa. Na aliiota baada ya muda akiwa kwenye mapambano ya kiuchumi.
Kuna kitu kingine kimenihuzunisha hapa kwa Eli na kuniongezea pia ufahamu. “..
atakuwa mtu wa kukupofusha macho, na kukuhuzunisha moyo;..” Unajua maana yake? Kuna
familia ambazo huko kwao au jamii zao, lazima kuwe na mtoto ambaye ni teso kwa mzazi au
wazazi ama jamii. Tumezoea kuwaita “pasua kichwa.”
Ndio chanzo hata cha ugonjwa au magonjwa ya moyo ama kisukari kwa mzazi.
Amekuwa sehemu ya huzuni kwenye familia. Shule akatae yeye, kesi mtaani na polisi ni yeye,
magomvi pia ufujaji wa mali ni yeye. Kutukanana na kupiga wazazi pia ni huyu huyu.
Hapa tunajuzwa ni aina ya laana. Ukiona boma au jamii ama kaya na hata ukoo wenye
uzao wa namna hii. Tazama sasa kwa jicho la laana au kifungo fulani ama kama adhabu ya
kiungu au miungu imekaa hapo. (Adhabu za miungu sijui kama unazielewa. Mara nyingi ni
matokeo ya uzao ujao kuasi mashariti ya namna ya kuishi na mizimu au miungu ya baba zao.
Nikutie moyo kuwa ukiiasi, basi amua kuokoka. Na ukiokoka; simama au maanisha. Lakini pia
ukiyaona haya yashughulikie kwa haraka maana hupaswi kuonewa nayo kwani wewe
ulishahama kihalali kutoka kwenye miliki yao.)
Roho Mtakatifu ananijulisha ya kuwa, kuna mtazamo usio wa Kibiblia miongoni mwa
wapendwa wengi kuhusu laana,.. Ni kama vile laana haiwezi kuwa juu yao. Unapaswa
kubadilika. Utofauti ni kwamba tuliokoka tuna nafasi nzuri na bora ya kushuhulika nazo kuliko
walio nje. Ukibisha, tazama matatizo yanayozunguka familia za ndugu zako utayaona na kwako.
Ukiona haya iwe ni ishara kwako. Ingia katika mombi ya rehema na uanze kujitoa kwenye hivyo
vifungo wewe na wanao au na watu wa kwenu kumbuka hata Lazaro alivyotoka kaburini
alipaswa kufunguliwa sanda.
Alipomfufuka Yesu hakuondoa kila kitu. Mengine tunaachiwa ili tujifunze vita. Ndiposa
ulipookoka kuna mambo yaliondoka papo hapo, na kuna mengine ni hatua kwa hatua. Andiko la
ya kale kupita na tazama yamekuwa mapya; unapaswa kulielewa kwa upana wake. Epuka
kuokoka kuliko Biblia. Na kial andiko la kwenye Biblia linapaswa kushikamana na mengine. Hii
ni kanuni ya kutafsiri maandiko, kwa walioenda vyuo vya Theoojia huweza kunielewa kirahisi.
Kuna watu wamejitengenezea misimamo yao na kulazimisha iwe ya Kibiblia. Hii ndo
imewazuilia wengine kupuuzia ndoto. Wakati hata babaye mlezi wa Yesu kwenye gano Jipya
aliongozwa au alipewa mara kama tatu hivi maelekezo muhimu kumuhusu Yesu na mamye kwa
kupitia ndoto! Tunahitaji kuwa na fundisho sahihi kutoka katika msimamo wa Kibibia sio
msimamo na mtazamo wa mtu au dhehebu ama Imani na hata mrengo fulani. Tuendee pale
ulipoishia ka kuhanu Eli;
Kuna mfalme mmoja kipindi kile cha Yeremia aliwahi kutamkiwa maneno kama haya,
sio kwake yeye tu, bali hata manaye hataketi hapo. Na nchi yaani aridhi ikaambiwa iandike hayo
maneno. Bi lia ya kingereza imetumia neno aridhi. Yeremia 22:29 Ee nchi, nchi, nchi, lisikie
neno la Bwana.
30 Bwana asema hivi, Andikeni habari za mtu huyu kwamba hana watoto, kwamba mtu huyu
hatafanikiwa siku zake zote; maana hapana mtu katika wazao wake atakayefanikiwa, akiketi
katika kiti cha enzi cha Daudi, na kutawala tena katika Yuda.
Hata akiketi hapo huyo mtoto hatafanikiwa! Ni muhimu kutaka kujua ugumu au tatizo
fulani limeanzia wapi na lini? Mengine yameanza tu toka uliporithi kiwanja au nyumba fulani.
Lazima utake kujua ya kuwa kuna maneno yatakuwa yalisemwa au kusemewa ama lipo zuio la
ulimwengu wa roho katika hiyo nafasi. Nalo sio jepesi, panahitaji matengenezo makubwa, sasa
rehema ninavyokufunza humu kitabuni itakusaidia.
Jana nilikumbuka mambo muhimu sana, chanzo cha kuandika vitabu ni matokeo ya aina
fulani ya kisima cha urithi. Ni kweli toka nikiwa mdogo (hata kabla ya kumaliza chuo cha
uandishi wa habari) nilikuwa nasema mimi ni mwandishi wa vitabu, lakini kiukweli sikuwahi
kuanza kuandika.
Siku niliyoanza kuandika niliota ndoto baba yangu mzazi (kipindi hicho bado akiwa hai)
akinipa kitu kama kashata eneo la huku nyumbani kwetu Rombo, katika aridhi ambayo zamani
ilimilikiwa na wazee wetu wa karibu kabisa, japo kwa sasa bado ipo mikononi mwa ndugu wa
ukoo. Nipoamka tu upako wa kuandika ukanizukia.
Sasa maana yake ni nini? Baba yangu alikuwa ni mpenzi wa vitabu, japo sio mwandishi
ila ni msomaji mkubwa sana alikuwa. Baba yangu mdogo ambaye alifariki mwaka 1985 akiwa ni
msomi wa kwanza huku kwetu wa chuo kikuu, alikuwa mwandishi wa vitabu; waliniambia.
Lakini pia kwa upande wa bibi mzaa baba kwao wapo au yupo mwandishi. Ambapo vitabu
vyake vikitajwa hapa vinaweza kufahamika maana serekalini nimewahi somwa mashuleni.
Sasa kwako wewe ambaye unateseka na familia ya namna hii hujui hujinashueje kutoka
katika vifungo vya kilaana au maneno ya namna hii ni muhimu kwako kujua umuhimu wa
rehema. Tubia kosa lao, tubia sababu za kuachiliwa kwa laana au kifungo hicho. Kikatae kwako
au jitoe kwenye orodha ya watu wanatamkwa kuwa chini ya hivyo kifungo. Kataa jina lako
kuwepo, kisha tangaza mujiondoa kwenye maisha au huo uruthi wako mbaya.
Ununue huo urithi au hiyo nafasi kwa damu ya Yesu. Ukitaka kusaidia na wengine basi
waombee pia hivyo. (Kitabu au vitabu vyetu vya Namna ya kutoka kwenye vigungo
vitakusaidia.)
Sasa ukitaka kuamini kuwa ni kweli jambo hili la visima lilihusisha nguvu ya kiagano,
basi nenda toka enzi za Ibrahimu na huyo mfalme wa Wafilisti. Utagundua kuwa yalikwepo
mapatano, kiapo na sadaka. Ambapo sadaka hiyo inabebwa na ishara ya kondoo saba wa wakike.
Mambo hayo manne hukamilisha agano, moja ni ishara, pili ni mapatano, tatu ni sadaka na nne
ni kiapo. Alafu mwishowe Ibrahimu tunamuona akimfanyia Mungu ibada au madhabahu. Kwa
hiyo ni dhairi kuwa ni Agano kati yake na Mungu lakini na nchi, aridhi ikiwakilishwa na mkuu
wa nchi au mkuu wa hiyo aridhi pamoja na mkuu wa majeshi.
Mwanzo 21:25 Kisha Ibrahimu akamlaumu Abimeleki kwa sababu ya kisima cha maji ambacho
watumwa wa Abimeleki wamekinyang'anya. 27 Ibrahimu akatwaa kondoo na ng'ombe akampa
Abimeleki, na hao wawili wakafanya mapatano.
28 Ibrahimu akaweka wana kondoo wa kike saba peke yao. 29 Abimeleki akamwambia
Ibrahimu, Hawa wana kondoo wa kike saba, uliowaweka peke yao, maana yake nini?
30 Akasema, Hawa wana kondoo wa kike saba utawapokea mkononi mwangu, wawe ushuhuda
ya kuwa ni mimi niliyekichimba kisima hiki. 31 Kwa hiyo akapaita mahali pale Beer-sheba, kwa
sababu waliapa huko wote wawili.
32 Basi wakafanya mapatano huko Beer-sheba. Abimeleki, na Fikoli mkuu wa jeshi lake,
wakaondoka wakarudi hata nchi ya Wafilisti. 33 Ibrahimu akapanda mkwaju Beer-sheba,
akaliitia huko jina la Bwana Mungu wa milele. (Kuliitia jina la Bwana kunawakilisha ibada, na
hakuna ibada kipindi kile bila madhabahu.) Mti wa mkwaju uliopandwa hapo uliwakilisha
madhabahu, eneo la kiibada. Kamusi moja wapo katika tafsiri moja wapo ya huo mti huo
imetumia neno Ashera. :34 Ibrahimu akakaa hali ya ugeni katika nchi ya Wafilisti siku nyingi.
2. Fukuwa Malango Watu Waliofukiwa Kama Kisima. Kuna muda adui huwa
anatutenga na watu muhimu sana ambao walipaswa kutusaidia au kutuvusha mahali au watu
ambao wanapaswa kufanyika baraka kwenye maisha yetu. Mtunga Zaburi anasema kuwa
ametengwa na mpenzi wake. Akimaanisha rafiki wake wa karibu sana. Zaburi 88:8 Wanijuao
umewatenga nami; Umenifanya kuwa chukizo kwao; Nimefungwa wala siwezi kutoka.
Hayo maandiko ni magumu sana, mosi ametengwa nao, pili wametupiwa roho ya
kumchukia, yaani hali ya kukataliwa. Tatu amefungwa wala hawezi kutoka ili yamkini
aweze kujipigania ili kuchomoka hapo.
Tazama msitari mwingine katika sura hiyo hiyo; 18 Mpenzi na rafiki umewatenga nami, Nao
wanijuao wamo gizani.
Hapa tunapata jambo la nne ya kwamba wamo gizani. Muhusika kafungwa (jambo la 3)
kwa hiyo hawezi kujipigania, alafu ambao yamkini wangemuona ili waweze kumsaidia
nao wapo gizani. Kwa maana hawawezi muona; alafu usisahau wanamchukia.
Hii ikupe kuwa makini sana unapojikuta ghafula watu wako muhimu wameamua
kukuchukia, wamejikuta wanakuchukia tu bila sababu. Umakini unahitajika sana tena mno. Watu
ambao walikuwa wakikusaidia, au ambao unafahamu fika ya kwamba walipaswa kukusaidia
alafu wanakupita kama vile hawakuoni uwe na hakika ya kuwa wapo gizani. Hawawezi kukuona.
Ni muhimu kuyajua haya maana watu wengi hawajui ni kwa nini wanatengwa au
marafiki huwa wanawasahau wanapopita katika njia au mahali pagumu. Mara nyingi huwa ni
vita vya namna hii. Na adui hukutenga nao kwa makusudi ili kukuzuilia kuvuka.
Fahamu sana kuwa hata uwe ni mtu mzuri, mwenye uwezo au ubora mkubwa kiasi gani
bado unawahitaji watu watakaokusemea vizuri. Watu watakao kuvusha mahali. Narudia tena ya
kwamba kila mtu anahitaji mtu ili kutimiza ndoto zake, sio watu kama wasaidi tu, bali watu
kama wakina Yohana Mbatatizaji. Watu ambao watajitoa ili wewe uvuke. Yesu na Uungu wake
alimuhitaji Yohana Mbatatizaji. Sasa jaribu kufikiri nini kitatokea kama Yohana wako
amekwamishwa mahali!
Paulo alimuhitaji Barnaba. Nawe pia kuna mtu unamuhitaji. Wakati nasoma maandiko
haya mwaka jana muda ama mwezi kama huu na juma kama lijalo niliamua kuingia kwenye
maombi ya siku nne, nilipoyahitimisha tu katika tarehe 24 ya mwezi wa 12 ndipo kesho yake ya
25 nilipokea majibu yangu. Nilikuwa kwenye vita kali na uongozi wangu wa sehemu, na hapo
awali nilipoteza maelewano na mchungaji wangu wa zamani.
Yusufu alipokuwa jela igundua kabisa huyu ni lango mtu, huyu ni mtu kama mlango wa
mimi kutoka gerezani. Ndio maana aliweza kumwambia haya maneno; Mwanzo 40:14 Ila
unikumbuke mimi, utakapopata mema, ukanifanyie fadhili, nakuomba, ukanitaje kwa Farao, na
kunitoa katika nyumba hii. 15 Kwa sababu hakika naliibiwa kutoka nchi ya Waebrania, wala
hapa sikutenda neno lo lote hata wanitie gerezani.
Akili kama hizi za Yusufu tunazihitaji sana! Ili zikupe kunufaika na haya malango watu.
Wapo kila mahali, na katika kila hatua ya maisha. Sema tu adui huwa ana tabia ya kutangulia
mbele na kututenga nao. Ndio maana unapochukiwa na mtu muhimu wako bila sababu huna budi
kuhitaji matengenezo. Maombi ni njia muhimu sana, tengeneza kwa njia ya maombi na utaona tu
mlango mwilini wa kutengeneza pia.
Hata kama hujui sababu, huwajui kwa majina wewe omba tu kama mimi, ya kwamba
ninarejesha au ninarejesha mlenzi ama rafiki au mtu wangu wa muhimu niliyetengwa naye.
(Ukisoma hayo maandiko kwenye Biblia mbalimbali za kingereza utagundua maneno
yaliyotumika hapo pa mpenzi au rafiki ni yenye maana kubwa sana katika mahusiano.)
Kwa Yusufu huyu mtu alifukiwa au kufunikwa na roho au hali ya kumsahau Yusufu. Ila
Bwana alihakikisha analeta uhitaji uliomfanya Yusufu kukumbukwa. Nawe ukikaza kuomba
utakuta tu unakumbukwa; Mwanzo 41:8 Hata asubuhi roho yake ikafadhaika; akapeleka watu
kuwaita waganga wote wa Misri, na watu wote wenye hekima walioko. Farao akawahadithia
ndoto yake, wala hakuna aliyeweza kumfasiria Farao mambo hayo.
9 Basi mkuu wa wanyweshaji akamwambia Farao akisema, Nayakumbuka makosa yangu leo.
12 Na huko pamoja nasi palikuwa na kijana; Mwebrania, mtumishi wa mkuu wa askari,
tukamhadithia, naye akatufasiria ndoto zetu; akamfasiria kila mtu kama ilivyokuwa ndoto yake.
14 Ndipo Farao akapeleka watu, akamwita Yusufu, wakamleta upesi kutoka gerezani. Akanyoa,
akabadili nguo zake, na kuingia kwa Farao.
Wengine wameamua kutokuomba tena maana kila wakiomba vita huibuka kubwa zaidi.
Kwa hiyo, anaamua kuacha kabisa kuomba ili kuepuka hivyo vita. Wengine wakiomba na
wakikaribia kumaliza hahelewi anapolala na kuota ndoto au kuona maono kuwa kuna mtu
alikuwa anapigana au kuna kitu alikuwa anapambana nacho na aliamka akiwa bado hajamaliza
mapambano. Njozi au maono hayakuisha na ushindi. Mwingine yanaisha akiwa amejeruhiwa au
amelemewa na vita.
Ukiona umelemewa hakikisha unaongeza "gia" au omba msaada kwa waombaji wengine.
Kuongeza "gia" kunakutaka kuhakikisha kama yalikuwa ni maombi ya masaa 24 basi unaingia
magumu zaidi. Kama mlikuwa wawili, ongeza waombaji wengine, usipowapata basi huna budi
kuongeza muda zaidi wa maombi na uzito wa mfungo.
17 Nikazishika zile mbao mbili, nikazitupa kutoka katika mikono yangu miwili, nikazivunja
mbele ya macho yenu. 18 Nikaanguka nchi mbele za Bwana siku arobaini usiku na mchana,
kama pale kwanza; sikula chakula wala kunywa maji; kwa sababu ya makosa yenu yote
mliyokosa, kwa kufanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, kwa kumkasirisha.
Kuna wakati unaombea jambo la ndoa kwa muda wa siku tatu, na ukimaliza tu
mwenzako anachachamaa kana kwamba ndo Shetani kashuka mzima-mzima kutoka kuzimu!
Suluhu ni kurudi tena mlimani kwa siku nyingine tatu tena.
Kwa kifupi sana ni kwamba unapopambana vita hakikisha unaipigana hadi inaisha. Usifanye
vita kwa muda uliouweka tu! Uwe na nia na akili zakupigana vita hadi viishe. Sio hadi siku
40 ziishe, ni hadi upate usbindi.
Siku moja nikiwa kanisani, na muhubiri mmoja mgeni alisoma au alihubiri kutoka kwenye
jambo lile la Wafilisti kuiba sanduku la Agano la Bwana, yule mgeni akanitaka nisome akisema;
Mwalimu tusomee..wakati nasoma, alikuwa akiniwekea kituo na kusemea mstari kabla ya mimi
kuendelea... nikiwa nimesimama huku nasoma na muda ule wa kituo Roho Mtakatifu
alinifunulia jambo zuri sana na mimi kutikisa kichwa.
Ni kuhusu Dagoni yule mungu wao, kuna pigo la kwanza alipigwa la kuanguka kifudifudi na
kumsujudia Mungu aliye hai, ikiwa ni ishara kwao kukubali kusalimu amri kabla ya lile la pili la
kukatika baadhi ya viungo...makuhani wa ile dini hawakumuacha, hawakukubali kuwa
wameshindwa vita dhidi ya Mungu wa Waebrania bali walimsimamisha tena!
Roho Mtakatifu akaniambia kuwa vita dhidi ya miungu mara nyingi huwa na hatua au "face"
zaidi ya moja. Na tatizo kubwa la wapendwa huishia ile ya kwanza. Ndugu yangu ni kwamba
ukiingia siku arobaini wakati mwingine ni umepigana hatua ya kwanza, na makuhani
wamemsimamisha tena Dagoni hata kama wameshapwa isara a ni yupi n Mungu mkuu, kati ya
Mungu wa Waebrani na Dagoni. Hapa ndipo pale ambapo vita vikali huibuka na kushamiri sana.
Na kwa bahati mbaya walio wengi huvunjika moyo na hata kukata tamaa kabisa.
Ukiwa hapa, epuka kutumia midomo, nguvu au akili zako kujipigania. Tuliwahi maliza
maombi ya simu 40 kanisani zamani ningali tu kijana mdogo, na kuliibuka vita vikali
vilivyoacha majeraha hadi leo. Kanisa hadi leo imepita miaka zaidi ya kumi natumai; lakini
halijakaa sawa! Mzee wa kanisa Kiongozi alishindwa kuelewana na mchungaji. Wakatofautiana.
Baya zaidi kilichofuata ni kutupiana maneno. Na kwa vita vya maneno adui akapata pakukaa.
Laiti tungekuwa na akili hizi leo! Kitu ambacho kingefuata ni ukimya, alafu tunarudi tena
mlimani kwa siku 40, labla Mungu mwenyewe aseme kwa kweli kipande kilichosalia ni siku
21: _tungeweza kuimalizia ile vita.
Kuna mzungu mmoja ambaye alikuwa ni mwindaji hapa nchini, siku moja akampiga simba
risasi kadhaa. Simba akajifanya amekufa, "wazoefu wanasema wanyama kama hao huwa na hiyo
mbinu." Mzungu akamfuata ili kuendelea na nia yake, simba alipoona amemkaribia alimrukia na
kumrarua kifuani. Walimkimbiza mzungu wa watu Nairobi na helkopta kwa haraka lakini
alifariki. Naye simba alikufa tu punde maana alikuwa amezidiwa sana.
Lazima uwe na akili ya kujua huyu adui amemalizika! Simba alikuwa amezidiwa, ila alisalia
na nguvu ambapo angeachwa mwenyewe muda angejifia. Kwa kuwa alisogelewa kwa haraka,
aliweza kujilipizia kasasi. Mzungu angejua angemuongeza risasi nyingine moja. Inawezekana
alishazoea simba wengine huuawa kwa risasi kama kwa huyo kiidadi. Ni kweli hata wewe vita
vingine umeshinda kwa maombi ya siku 21, lakini hivi usiishi au usiingie kwa kukarili.
Tazama maandiko haya ya Dagoni; 1 Samweli 5:1 Basi Wafilisti walikuwa wamelichukua
sanduku la Mungu, wakaenda nalo kutoka Eben-ezeri hata Ashdodi. 2 Wafilisti wakalichukua
sanduku la Mungu, wakalitia katika nyumba ya Dagoni, wakaliweka karibu na Dagoni.
3 Na watu wa Ashdodi, walipoamka alfajiri siku ya pili, kumbe! Dagoni imeanguka chini
kifudifudi, mbele ya sanduku la Bwana. Wakaitwaa Dagoni, wakaisimamisha mahali pake tena.
(Unaona hapo!) Ni ni hatua. Hapa ndo panachemshaga vita sana. 4 Hata walipoamka kesho yake
asubuhi, kumbe! Dagoni ilikuwa imeanguka chini kifudifudi, mbele ya sanduku la Bwana; na
kichwa chake Dagoni na vitanga vya mikono yake vyote viwili vimekatika, vipo vimelala
kizingitini; Dagoni ikasalia kiwiliwili chake tu.
5 Kwa hiyo makuhani wa Dagoni, na mtu awaye yote aingiaye nyumbani mwa Dagoni,
hawakanyagi kizingiti cha nyumba ya Dagoni huko Ashdodi, hata leo.
Amen.
a
Orodha ya Vitabu Vyetu
Vya Ndoa/Familia:
Vya Uongozi:
18. Hekima ya Uongozi Kihuduma, 19. Nafasi Ya Ulimwengu Wa Roho Katika Uongozi. (Kiti
Cha Enzi.) 20. Siasa, na Uongozi Uliotukuka, 21. Wito wa Kitumishi. 22. Ujuwe Wito na
Huduma ya Mwinjilisti. 23. Ujuwe Wito na Huduma ya Mchungaji. 24. Ujuwe Wito na Huduma
ya Mtume. 25. Ujuwe Wito na Huduma ya Mwalimu. 26. Ujuwe Wito na Huduma ya Nabii. 27.
Ijuwe Huduma ya Uimbaji. 28. Usizike Ndoto Zako 29. Utumishi na Mtumishi, 30.Uwe Hodari
Shujaa na Mwenye Moyo Mkuu,
Utoaji:
Faraja:
33. Usifie Jangwani, 34. Neno la Faraja, 35. Mtu wa Nne. 36. Ipo Nguvu kwa Mwenye Tumaini.
37. Jipe Moyo. 38.Usiogope, 39.Katikati ya Shimo Mtafute Mungu, 40. Usikate Tamaa. 41.
JANGWANI MAJI YAPO. 42. Bwana Yu Pamoja Nawe, 43 . Katikati ya Shimo Mtafute Mungu,
44. Nguvu ya Kuomba Bila Kukoma. 45. Mungu Ni Kimbilio na Msaada ! 46. Mungu
Amekusamehe na Kusahau, 47. Mungu Anakupenda, 48. Nguvu ya Kuomba Bila Kukoma, 49.
Mwaka wa Urejesho. 50. Majaribu ni Mtaji 51. Imani Ya Kusubiria Na Kupokelea Majibu 52.
Namna ya Kuishi wakati wa Majaribu au Mapito.
53. Cha Kufanya Unapokuwa Njia Panda 54. Muone Mungu Nyuma ya Pito au Jaribu Lako. 55.
Vumilia Wamjue Mungu Wako, 55. YESU NI RAFIKI WA KWELI WAKATI WA TAABU
57. Hata Jela Yesu Yupo 58. CHAKUFANYA UNAPOLEMEWA NA MZIGO AMBAPO
MUNGU BADO ANATAKA UENDELEE KUUBEBA. 59. Kesho Yako Ni Bora Kuliko Leo
Yako. 60. Siku Ya Tatu. 61. Nina Siri Kwa Waliao. 62. Kisima cha Tatu
b
Mfumo wa Fahamu:
63. Saikolojia ya Mtu wa Ndani. 64. Moyo Wa Fahamu, 65. Nguvu ya Fikra Katika Kukufanya
Uishi na Utakavyo Ishi, 66. Nafasi ya Akili Katika Kukunufaish Aua Kukufanikisha Kimaisha,
67. Nafasi ya Hekima Katika Kukufanikisha Kimaisha. 68. Thamani ya Muda wa Uanafunzi au
Elimu kwa Mwanafunzi. 69. Maana Yakumpenda Mungu kwa Akili Zako Zote.
Ukuaji:
70. Namna Ya Kuomba, 71. Nafasi ya Imani Katika Kukufanikisha Maishani . 72. Kuwa Kiroho.
73. Maana ya Mbegu Iliyodondoka Kando ya Njia, 74. Ukulie Wokovu, 75. Muongozo Maalumu
wa Kiroho kwa Waalimu wa Waongofu Wapya, 76. Kwa Nini Unapaswa Kuokoka. 77. Kwa
Nini Kusamehe Ni Muhimu 78. Nguvu Ya Neno La Mungu Kwenye Maisha Ya Mwanadamu.
79. Sauti ya Mungu
Uungu/Utumishi:
80. Moyo Safi, 81.Tunu za Tunda la Roho 82. Utumishi Wenye Matunda Mbele za Mungu,
83. Thamani ya Muda Katika Kufanikisha Ndoto Zako. 84. Sababu Za Damu ya Yesu Kuwa na
Nguvu Iliyo Nayo, 85. Mjuwe Yesu Kristo. 86. Kweli na Neema Kama Kristo. 87. Nafasi Ya
Roho Mtakatifu Katika Kukufanikisha Kimaisha Au Kihuduma ( Siri Ya Upako). 88. Hila za
Shetani. 89. Thamani ya Kukaa Kwenye Mapenzi ya Mungu. 90. Zijuwe Ajenda Muhimu za
Maombi kwa Mtumishi na Utumishi. 91. Ijuwe Thamani na Mamlaka Uliyo Nayo kwa Mungu,
(Jione kama Mungu Anavyokuona.) 92 . Nafasi ya Viungo vya Mwili wa Mwanadamu katika
Ulimwengu wa Roho. 93. Maana ya Kumuabudu Mungu Katika Roho na Kweli. 94. Mtumikie
Mungu. 95.Nafasi Ya Roho Mtakatifu Katika Kufanikisha Ndoto au Maono Yako. 96. Zijue na
Uzishinde Roho za Maajenti wa Kuzimu Makanisa 97. Karama Na Neema Za Roho Mtakatifu
98. Wasifu Wa Yesu Kristo. 99. Fikra Sahihi Katika Shamba la Bwana.
Uchumi/Mafanikio:
100. Tajirika Kibiblia. 101. Utumishi na Mali au Fedha. 102. Nafasi ya Fedha Katika
Kukufanikisha au Kukuangamiza Kiroho na Kimaisha ( Faida na Hatari ya Fedha). 103. Timiza
Maono Kibiblia. 104. BARAKA 105. Msaada Wa Kimaarifa Kwa Anayemuona Mungu
Amechelewa Kumbariki 106. Kwa Nini Mungu Anataka Umkabidhi Njia Zako
Vifungo/Ukombozi:
107. Msaada kwa Waliokosa Mpenyo Kihuduma na Kimaisha, 108.Namna ya Kutoka Kwenye
Vifungo (Kuvunja Nira), 109. Namna ya Kutoka Katika Kifungo au Hali ya Kukataliwa,
110.Teka, Miliki na Utawale, 111. Zijuwe na Uzishinde Roho za Kaburi na Mauti. 112.Ondoa
Zuio. 113. Ijuwe Na Uishinde Hasira, 114. Nguvu ya Ndoto Kwenye Ulimwengu wa Roho.
c
115. Malango kwenye Ulimwengu wa Roho. 116. Nguvu ya Agano Kiroho,
117. Uponyaji wa Mtu wa Ndani. 118. Nguvu ya Ukiri wa Kinywa. 119. Zijue na Uzishinde
Roho za Mapepo Mahaba. 120. Nguvu ya Kinywa au Maneno, 121. Mambo Muhimu ya
Kufanya au Kuzingatia Kunapokuwa na Adhabu ya Kiungu Inyoijumuisha Eneo Ulilopo au
Jamii.
Matendo ya Miujiza:
Vinginevyo:
123. Uzuri wa Mbinguni, 124. Ole Wafu Wafao Nje ya Bwana. 125.Furuksa, 126. Jiandae na
Uishi Vyema katika Msimu Wako Mpya wa Kiroho, 127.Wanatheolojia Wanapokesea, 128.
Mjuwe Mwalimu Oscar Samba.
E-Book:
d
Mawasiliano
http://www.ukombozigospel.blogspot.com
Telegram https://t.me/+fft3GHXC9xIzYjhk