You are on page 1of 5

SEFANIA

Utangulizi
Sefania maana yake “Yeye ambaye Yehova amemficha”.Sefania ni wa ukoo wa Hezekia (Sef 1:1). Inawezekana
huyu babu anayetajwa akawa ni Mfalme Hezekia, mfalme wa Yuda, kutokana na ukweli kwamba ukoo huu
umefuatiliwa kutoka mbali na muda husika unakubalika. Nabii Sefania alitumika wakati wa utawala wa Mfalme Yosia
(639-609 K. K.). Sefania alionya kwamba siku ya BWANA ingeleta hukumu kwa Yuda pamoja na Yerusalemu, hivyo
akawashauri Wayahudi watu na kumrudia Mungu (2:1-3). Uvamizi wa kuiteka Yuda kutoka kaskazini ulikuwa unakuja
juu yao, nao ungekumba pia mataifa yanayoizunguka. Ingawa wasomi wengi wanahusianisha uvamizi huu na ule wa
wa Wasinthia kuelekea kusini kutoka jimbo la Kaukaukasia uliotokea 630 K.K. kama ulivyoelezwa na Herodota.
Inawezekana Sefania alikuwa anasema juu ya Wakaldayo, ambao ndio waliotimiza unabii huu wa huku kuharibiwa
kwa Yuda mnamo mwaka 605-586 K.K. Ingawa hukumu ya Yuda umeainishwa, ahadi ya kufanywa upya ni
yakini.Mtaifa yatahukumiwa na kutiishwa na Mfalme wa Israeli, anayetawala katika Sayuni.

Wazo Kuu
Dhambi ambazo Sefania anazitaja juu ya Yuda na Yerusalemu zinaonyesha alizitabiri kabla ya uamsho wa
matengenezo ya Yosia, wakati ambapo dhambi za waliomtangulia kutawala , yaani, Manse na Amoni, zilikuwa
zinaendelea kutendwa katika jamii hiyo. Uamsho huo wa matengenezo haukutokea hadi mwaka wa 12 wa kutawala
kwake Yosia ( 627 K.K.) ndipo mfalme alipotuma jeshi kwenda kulipatiliza taifa kwa ajili ya ibada ya sanamu na
kurejeshwa tena kwa ibada ya kumwabudu Mungu wa kweli, yaani, Yehova. Baadaye Mika naye akaamuru kujengwa
tena kwa hekalu la Solomoni na kulitakasa kipindi nakala ya Sheria ya Bwana ilipogunduliwa (ling.2wafalme 22:1-10).
Kwa hiyo Sefania akatabiri kwamba mataifa yaliyokuwa jirani na Yuda yangeangamizwa pia. Aliwapa watu matumaini
kwamba Mungu angewarudisha watu wake nyumbani.

Dhumuni
Kuwaonya watu wa Yuda waepukane na kutosheka na maisha, waache kuabudu sanamu na wamrudie Mungu wao
(YEHOVA).

Mambo Muhimu
Mfalme Yosia wa Yuda alikuwa anajaribu kurekebisha hali ya uovu iliyosababishwa na tawala za wafalme wawili
(Manase na Amoni) waliomtangulia katika Yuda. Yosia aliweza kupanua himaya yake kwa sababu kwa wakati wake
hakukuwa na taifa jingine ambalo lilikuwa na nguvu.zaidi kwa maana nguvu za Ashuru zilikuwa zinafifia kwa kasi.

Mwandishi
Sefania

Mahali
Yerusalemu

Tarehe
Maelezo ya Sefania kuhusu kudidimia kiroho na kimaadili kwa Yuda inawezekana yaliandikwa mwaka 630 K.K.,
lakini kuna uwezekano kkwamba mahubiri ya kinabii yalimgusa sana mfalme na kusababisha mageuzi ya kiroho
aliyoyafanya. Tarehe hii ya 630K.K. inazidi kuthibitishwa na ukweli kwamba Sefania hakutaja habari za
Babeliiliyokuwa dola inayotambuliwa kimataifa.Babeli iliinuka mnamo mwaka 625 K.K. wakati Napolasa alipotwaa
madaraka. Hata hivyo Sefania anatabiri juu ya kuharibiwa kwa Ashuru, jambo ambalo lilitokea mwaka 612 K.K.,
Ninawi ilipoanguka. Sefania aliishi wakati mmoja na Yeremia lakini wakati huo Yeremia alikuwa mdogo kwa Sefania.

Mgawanyo
• Kutangazwa kwa hukumu ya Mungu. (1:1-2:3)
• Hukumu dhidi ya mataifa. (2:4-15)
• Maisha ya baadaye ya Yerusalemu. (3:1-20)

1
SEFANIA
Neno la BWANA ambalo lilimjia Sefania na mshindo mkubwa kutoka vilimani.
1 mwana wa Kushi, mwana wa Gedalia, 11Ombolezeni, ninyi mnaoishi katika eneo la
mwana wa Amaria, mwana wa Hezekia, wakati wa sokoni,
utawala wa Yosia mwana wa Amoni mfalme wa wafanyabiashara wenu wote wataangamizwa,
Yuda: wote ambao wanafanya biashara ya fedha
wataangamizwa.
Onyo la Maangamizi Yanayokuja
2BWANA asema, 12Wakati huo nitasaka katika mji wa Yerusalemu
‘‘Nitafagia kila kitu kutoka kwenye uso wa kwa taa
dunia.’’ na kuwaadhibu wale ambao wanakaa
3“Nitafagilia mbali watu na wanyama, katika hali ya kuridhika,
nitafagilia mbali ndege wa angani na samaki ambao ni kama divai iliyobaki kwenye
wa baharini. machicha,
Wafanyao waovu wajikwae, ambao hudhani, ‘BWANA hatafanya lo
pamoja na hao waovu, lote, jema au baya.’
13Utajiri wao utatekwa nyara,
nami nitamkatilia mbali mwanadamu atoke
katika dunia,’’ nyumba zao zitabomolewa.
asema BWANA. Watajenga nyumba, lakini hawataishi ndani
yake,
Dhidi ya Yuda watapanda mizabibu lakini
4“Nitaiadhibu Yuda na wote wakaao hawatakunywa divai yake.
Yerusalemu.
Kutoka mahali hapa nitakatilia mbali kila Siku Kubwa Ya BWANA
14‘‘Siku kubwa ya BWANA iko karibu,
mabaki ya Baali,
majina ya wapagani na makuhani waabuduo iko karibu na inakuja haraka.
sanamu, Sikilizeni! Kilio katika siku ya BWANA
5wale ambao husujudu juu ya mapaa kitakuwa kichungu,
kuabudu jeshi la vitu vya angani, hata shujaa atapiga kelele.
15Siku ile ni siku ya ghadhabu,
wale ambao husujudu na kuapa kwa BWANA
siku ya fadhaa na dhiki,
na ambao pia huapa kwa Malkamu, siku ya uharibifu na ukiwa,
6wale ambao wanaacha kumfuata BWANA siku ya giza na utusitusi,
wala hawamtafuti BWANA wala kutaka siku ya mawingu na giza nene,
16siku ya tarumbeta na mlio wa vita
shauri lake.
7Nyamazeni mbele za BWANA Mwenyezi, dhidi ya miji yenye ngome
kwa maana siku ya BWANA iko karibu. na dhidi ya minara mirefu.
17Nitawaletea watu dhiki
BWANA ameandaa dhabihu,
amewaweka wakfu wale aliowaalika. nao watatembea kama wasio na macho,
8Katika siku ya dhabihu ya BWANA kwa sababu wametenda dhambi dhidi ya
nitawaadhibu wakuu na wana wa mfalme BWANA.
na wale wote wanaovaa nguo za kigeni. Damu yao itamwagwa kama vumbi na
9Katika siku hiyo nitaadhibu wote matumbo yao kama taka.
18Fedha yao wala dhahabu yao haitaweza
ambao hukwepa kukanyaga kizingiti,
ambao hujaza hekalu la miungu yao kuwaokoa katika siku hiyo ya ghadhabu
kwa jeuri na udanganyifu. ya BWANA.
Katika moto wa wivu wake
10BWANA asema, dunia yote itateketezwa,
‘‘Katika siku hiyo kilio kitapanda juu kwa maana ataleta mwisho wa wote
kutoka lango la Samaki, wanaoishi katika dunia ghafula.’’
maombolezo kutoka mtaa wa pili,
2
SEFANIA
2 Kusanyikeni pamoja, kusanyikeni pamoja,
enyi taifa lisilo na aibu,
mahali pa magugu na mashimo ya chumvi,
nchi ya ukiwa milele.
2kabla ya wakati ulioamuriwa haujafika Mabaki ya watu wangu watawateka nyara,
na siku ile inayopeperusha kama makapi, mabaki ya taifa langu watarithi nchi yao.’’
kabla hasira kali ya BWANA haijaja juu
yenu, 10Hiki ndicho watarudishiwa kwa ajili ya kiburi
kabla siku ya ghadhabu ya BWANA chao,
haijaja juu yenu. kwa kutukana na kudhihaki watu wa
3Mtafuteni BWANA, BWANA Mwenye Nguvu zote.
enyi nyote wanyenyekevu wa nchi.
Ninyi ambao hufanya lile analoamuru. 11BWANA atakuwa wa kutisha kwao
Tafuteni haki, wakati atakapoangamiza miungu yote ya
tafuteni unyenyekevu, nchi.
labda mtahifadhiwa siku ya hasira ya Mataifa katika kila pwani yatamwabudu,
BWANA. kila moja katika nchi yake lenyewe.

Dhidi ya Ufilisti Dhidi ya Kushi


4Gaza utaachwa 12“Ninyi
pia, Ee Wakushi,
na Ashkeloni utaachwa magofu. mtauawa kwa upanga wangu.’’
Wakati wa adhuhuri Ashdodi utaachwa mtupu
na Ekroni utang'olewa. Dhidi ya Ashuru
5Ole wenu ninyi ambao mnaishi kando ya bahari, 13Mungu atanyoosha mkono wake dhidi ya
Ee watu wa Wakerethi, kaskazini na kuangamiza Waashuru,
neno la BWANA liko dhidi yenu, akiiacha Ninawi ukiwa
Ee Kanaani, nchi ya Wafilisti. na pa kame kama jangwa.
14Makundi ya kondoo na ng’ombe yatajilaza pale,

‘‘Mimi nitawaangamiza, viumbe vya kila aina.


wala hakuna atakayebaki.’’ Bundi wa jangwani na bundi waliao kwa sauti
nyembamba
6Nchi kando ya bahari, mahali ambapo wanaishi wataishi juu ya nguzo zake.
Wakerethi, Mwangwi wa kuita kwao utapita madirishani,
patakuwa mahali pa wachungaji na mazizi ya kifusi kitakuwa milangoni,
kondoo. boriti za mierezi zitaachwa wazi.
7Itakuwa mali ya mabaki ya nyumba ya Yuda, 15Huu ndio mji uliotukuka na kuishi kwa furaha

hapo watapata malisho. wakijisikia salama.


Wakati wa jioni watajilaza chini Ulisema moyoni mwako,
katika nyumba za Ashkeloni. “Mimi ndimi, na wala hapana mwingine ila
BWANA Mungu wao atawatunza, mimi.’’
naye atawarudishia wafungwa wao. Jinsi gani umekuwa gofu, mahali pa kulala
wanyama pori!
Dhidi ya Moabu na Amoni Wote wanaopita kando yake
8“Nimeyasikia matukano ya Moabu wanauzomea na kutikisa mkono kwa
nazo dhihaka za Waamoni, dharau.
ambao waliwatukana watu wangu
na kufanya vitisho dhidi ya nchi yao. Hatima ya Yerusalemu

3
9Hakika, kama niishivyo,” Ole wa mji wa wadhalimu,
asema BWANA Mwenye Nguvu zote, waasi na waliotiwa unajisi!
Mungu wa Israeli, 2Hautii mtu yeyote,

“Hakika Moabu itakuwa kama Sodoma, haukubali maonyo.


Waamori kama Wagomora, Haumtumaini BWANA,
3
SEFANIA
haukaribii karibu na Mungu wake. wale wote wanaoshangilia katika kiburi chao.
3Maafisa wake ni simba wangurumao, Kamwe hutajivuna tena katika kilima changu
watawala wake ni mbwa mwitu wa jioni, kitakatifu.
ambao hawabakizi chochote kwa ajili ya 12Lakini nitakuachia ndani yako

asubuhi. wapole na wanyenyekevu,


4Manabii wake ni wenye kiburi, ambao wanatumaini jina la BWANA.
ni wadanganyifu. 13Mabaki ya Israeli hayatafanya kosa,

Makuhani wake hunajisi patakatifu hawatasema uongo,


na kuihalifu sheria. wala udanganyifu hautakuwa katika vinywa
5BWANA aliye ndani yake ni mwenye haki, vyao.
hafanyi kosa. Watakula na kulala wala hakuna ye yote
Asubuhi kwa asubuhi hutoa haki yake, atakayewaogopesha.”
kila kukipambazuka huitimiza,
14Imba, Ee Binti Sayuni,
bali mtu dhalimu hana aibu.
Paza sauti, Ee Israel!
6‘‘Nimeyafutilia mbali mataifa, Furahi na kushangilia kwa moyo wako wote,
ngome zao zimebomolewa. Ee Binti Yerusalemu!
15BWANA amekuondolea adhabu yako,
Nimeziacha barabara ukiwa,
hakuna anayepita humo. amewarudisha nyuma adui zako.
Miji yao imeharibiwa, BWANA, Mfalme wa Israeli,
hakuna mmoja atakayeachwa, hakuna yu pamoja nawe,
hata mmoja. kamwe hutaogopa tena madhara yo yote.
7Niliuambia huo mji, 16Katika siku hiyo watauambia Yerusalemu,

‘Hakika utaniogopa na kukubali maonyo!’ “Usiogope, Ee Sayuni,


Ndipo makao yake hayatafutiliwa mbali, Usiiache mikono yako ilegee.
17BWANA Mungu wako yu pamoja nawe,
wala adhabu zangu zote hazitakuja juu
yake. yeye ni mwenye nguvu kuokoa.
Lakini walikuwa bado na shauku Atakufurahia kwa furaha kubwa,
kutenda kwa upotovu katika yote atakutuliza kwa pendo lake,
waliyofanya. atakufurahia kwa kuimba.’’
8BWANA anasema,
18“Huzuni katika sikukuu zilizoamriwa nitaziondoa
‘‘Kwa hiyo ningojee mimi,
siku nitakayosimama kuteka nyara. kwenu,
Nimeamua kukusanya mataifa, hizo ni mzigo wa fedheha kwenu.
19Katika wakati huo nitawashughulikia
kukusanya falme na kumimina ghadhabu
yangu juu yao, wote waliokudhulumu, nitaokoa kilema
hasira yangu kali yote. na kukusanya wale ambao wametawanywa.
Dunia yote itateketezwa Nitawapa sifa na heshima
kwa moto wa wivu wa hasira yangu. katika kila nchi ambamo waliaibishwa.
9“Ndipo nitatakasa midomo ya mataifa, 20Wakati huo nitawakusanya,

kwamba wote waweze kuliitia jina la BWANA wakati huo nitawaleta nyumbani.
na kumtumikia kwa pamoja. Miongoni mwa mataifa yote ya dunia
10Kutoka ng'ambo ya mito ya Kushi wakati nitakapowarudishia mateka yenu
watu wangu wanaoniabudu, watu wangu mbele ya macho yenu hasa,’’
waliotawanyika, asema BWANA.
wataniletea sadaka.
11Siku hiyo hutaaibishwa kwa ajili ya makosa yote

ulionitendea,
kwa sababu nitawaondoa kutoka mji huu

4
SEFANIA

You might also like